Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 4

Sisi waanzilishi wa kikundi cha Ngome Imara, kutokana na kuliangalia suala la majanga

yanapotokea miongoni mwa jamii zetu, wengi wetu tunakuwa katika wakati mgumu wa
kuyakabili majanga hayo, ambayo aidha hutokea kwa uasili wake au kwa bahati mbaya. Hivyo
basi tumeamua kuanzisha mfuko huu ili kukabiliana na hali hiyo.
HomeAboutEditEditEditEditEdit Wednesday, September 26, 2012 MUHTASARI WA KIKAO
CHA KWANZA CHA KUANZISHA MFUKO WA KUSAIDIANA KILICHOFANYIKA
SIKU YA IJUMAA TAREHE 15/6/2012 MUHTASARI WA KIKAO CHA  KWANZA CHA
KUANZISHA MFUKO WA KUSAIDIANA KILICHOFANYIKA SIKU YA IJUMAA 
TAREHE 15/6/2012 KWENYE HOTEL YA SERENA DAR ES SALAAM 1.0      
MAHUDHURIO          
A:      WALIOHUDHURIA S/N JINA WADHIFA
1. ESTHER DAFFA MJUMBE
2. EMMA SIZYA MJUMBE
3. SAUDA RAJABU MJUMBE
4. ESTER MSECHU MJUMBE 5. ASHA WAHINDI MJUMBE 6. NEEMA ABDALLAH
MJUMBE 7 JOYCE SAMWEL MJUMBE 8 FATUMA KILENGA MJUMBE 9 DEVOTA
ELISAE MJUMBE 10 LUSAJO MWAKASEGE MJUMBE 11 SUBIRA WADDA MJUMBE
12 SHABANI KALUSE MJUMBE 13 FLOLENCE MAREALE MJUMBE 14 ALICE
KASHILILILA MJUMBE 15 GETRUDA FLORIAN MJUMBE 16 FATUMA MSIGALA
MJUMBE B:  WASIOHUDHURIA  -  S/N JINA WADHIFA 1 JOSEPH MWITA MJUMBE 2
JACKSON MUMBII MJUMBE 3 SAADA MUYINGA MJUMBE 4 VICTORIA GUNZE
MJUMBE 2.0       UFUNGUZI WA KIKAO Mjumbe aliyeitisha kikao Sauda Rajabu
aliwashukuru wajumbe wote kwa mahudhurio yao kwenye  kikao hicho na alitangaza
kukifungua rasmi kikao cha kwanza. 3.0       AGENDA KULIKUWA NA AGENDA TATU ZA
KUJADILIWA KATIKA KIKAO HICHO 1.   Kujadili juu ya kuanzishwa kwa mfuko wa
kusaidiana 2.   Kujadili jina la kikundi 3.   Kuteua kamati ya muda ya kuandaa rasimu ya katiba
ya kikundi 4.   Mengineyo 3.1  AGENDA NAMBA 1 Kujadili juu ya kuanzishwa kwa kikundi
cha kusaidianana na kutungwa kwa katiba: Wajumbe tulikubaliana juu ya kuanzisha mfuko wa
kusaidiana wakati wa majanga yanapotokea miongoni mwa jamii zetu. Kutokana na mazingira
yetu ya kazi, kwani muda mwingi tunautumia hapa kazini na kushiundwa kushirikiana na jamii
iliyotuzunguka huko mitaani tunapoishi tumejikuta tunakuwa katika wakati mgumu wa
kuyakabili majanga hayo, ambayo aidha hutokea kwa uasilia wake au kwa bahati mbaya. Pia
tumeangalia hali ngumu ya maisha inayo zikabili jamii nyingi hapa Dar es Salaam na Nchini
kwa ujumla na kwamba   Jamii nyingi kukosa mitaji ya kuanzisha biashara ndogo ndogo kwa
kujiongezea kipato na kukidhi baadhi ya mahitaji muhimu ya kibanadamu. Pia tulijadili juu ya
kutungwa kwa katiba ya kikundi ambayo itazingatia mambo yafuatayo: -          mwanachama
kuacha kazi/kujitoa -          Mwanachama akiuguliwa atasaidiwaje (atapewa fedha kiasi gani)
-          Mwanachama akifunga ndoa atasaidiwaje na kikundi -          Mwanachama akifiwa na
watu wake wa karibu au msiba kuwepo nyumba anayoishi. -          Kufungua Account ya kikundi
-          Jinsi ya kuunganisha Chama na uongozi wa hoteli ili michango yetu ikatwe moja kwa
moja kutoka kwenye mshahara na kwenda bank moja kwa moja badala ya kushikana mashati.
-          Mahudhurio ya kikao, wanachama wajitahidi kuhudhuria, hakuta kuwa na lawama kwa
wasio hudhururia kwa lolote litakaloamuliwa na kikao au wanachama waliokuwepo. -         
Kuwezeshana kimtaji ianze haraka iwezekanavyo kwa lengo la kukuza kikundi hasa upande wa
riba. -           Kuanzia siku ya leo mwanachama yoyote atakaye patwa na tatizo kubwa wanachana
wanawajibu wa kuwajibika kama kikundi kumsaidia ikiwa ndio dhana kubwa ya kuanzishwa
kwa kikundi hichi. -          Ikitokea mwanachama amepatwa na tatizo kubwa kabla ya mfuko
kutuna wanachama watatakiwa kuchanga kutoka kwenye mifuko yao kwaajili ya kumsaidia
mwanachama mwenzao. -          Fain itatolewa kwa watakao kuwa wanachelewa kwenye kikao
au kutohudhuria mara kwa mara kwenye vikao pasipo sababu maalum. -          Maendelea
yanayolengwa kwa ajili ya baadae yawekwe kabisa katika katiba ili kuondoa usumbufu hapo
baadae, kama ujasiliamali n.k. -          Kwa kuanza ifunguliwa Account  ya kawaida , watu
wawili waijue password kwakuwa pesa haziwezi kuwa zinakaa mfukoni kwa mtu ni” risk”.
-          Kwa sasa jambo litakalo hitaji pesa kama utengenezaji wa katiba n.k uchakavu upitishwe.
-          Baada ya kukamilika kwa katiba kila mwanachama atahitajika kuwa na katiba na aisome
na kuielewa ili tuwe kwenye mstari mmoja. -          Kuwepo na kamati ndogo ndogo ndani ya
kikundi K.M kamati ya misiba,harusi n.k. -          Kamati hizo ndizo zitaleta taarifa ya matumizi
ya pesa na yatakayojiri sehemu husika. -          Kwa baadae atakayetaka kujinga na kikundi
imependekezwa ada iwe ni sh laki mbili, ili kupunguza msongamano wa kuwa na wanachama
wengi. -          Kiingilio kwa wanachama ishirini wa mwanzo ni sh 5000/= na mchango  wa kila
mwezi ni 5000/=, michango inatakiwa kuanza kutolewa June, na kiingilio kinatakiwa kuwa
kimekamilika mwishoni mwa mwezi wa saba. 3.2  AGENDA NAMBA 2 Kujadili jina la
kikundi: Wajumbe walikubaliana kila mmoja apendekeze jina la kikundi ambapo wajumbe
waliomba wapewe muda wa kutafakari, hata hivyo muumbe mmoja Shaban Alipendekeza jina la
kikundi liwe ni NGOME IMARA. Wajumbe wote waliridhia jina hili lipitishwe kwa muda lakini
kama kutakuwa na pendekezo la jina lingine, basi liwasilishwe kwenye mkutano wa pili wa
kikundi kwa ajili ya kupigiwa kura. 3.3  AGENDA NAMBA 3 Kuteua kamati ya muda ya
kuandaa rasimu ya katiba ya kikundi: Wajumbe walipendekeza majina ya wajumbe sita kuingia
kwenye kamati ya muda ya kuandaa rasimu ya katiba ya kikundi na kuiwasilisha kwenye
mkutano mkuu wa pili wa kikundi ambapo kamati hiyo ilipwea mwezi mmoja kukamilisha
rasimu hiyo ya katiba. Wajumbe hao waliochaguliwa na nafasi zao ni hawa wafuatao: Jina la
mjumbe Wadhifa Shaban Kaluse Mwenyekiti Sauda Rajabu Makamu mwenyekiti Emma Sizya
Katibu Devota Elisea Katibu msaidizi Esther Daffa Mweka hazina Ester Msechu Mweka hazina
msaidizi Mwenyekiti wa muda aliyeteuliwa akizungumza na wajumbe wa kikao hicho
aliwashukuru kwa kumuamini na kumteua kuongoza jahazi hilo la kuanza rasimu ya kikundi. Pia
kwa niaba ya wajumbe walioteuliwa katika kamati hiyo, mwenyekiti alieleza hatua za awali za
kuchukua katika utekelezaji wa kuanzishwa kwa kikundi hicho. Mwenyekiti alitaka wajumbe
waanze kutoa michango yao ili pamoja na mambo mengine ituwezeshe kufanikisha uandaaji wa
rasimu hiyo ya katiba na pia kulipia gharama za usajili. Wajumbe walikubaliana na wazo hilo na
mwenyekiti aliwaomba watoe mapendekezo yao. Makamu mwenyekiti Sauda Rajabu alitoa
maoni kwamba kila mwanachama atoe kiingilio cha shilingi 50,000 halafu michango kwa mwezi
iwe ni shilingi 5,000 kila mwezi. Wajumbe waliafiki, lakini waliomba kiasi hicho cha shilingi
50,000 kisitolewe kwa mkupuo kwa sababu ya hali ngumu walizo nazo wajumbe waanzilishi.
Ilikubaliwa kishi hicho kilipwe kwa awamu mbili ikiwa ni sambamba  na mchango wa kila
mwezi wa silingi 5,000. Hivyo basi iloiamuliwa mwisho mwezi wa Juni kila mwanachama atoe
kiasi cha shilingi 25, 000 pamoja na shilingi 5,000 ya mcnago wa mwezi jumla itakuwa ni
shilingi 30,000, halafu na mwisho  wa mqwezi wa Julai wajumbe wote watoe kiashi hicho hicho.
Wajumbe wpte waliafiki wazo hilo na kulipitisha. 3.4  AGENDA NAMBA 4. Mengineyo:
Hapakuwa na hoja zaidi na kila mjumbe aliridhishwa makubalianao hayo. 4.0     KUFUNGA
KIKAO Mwenyekiti aliwashukuru  wajumbe wote kwa michango yao ya mawazo katika kikao
hicho. Aliwakumbusha  wajumbe kuweka vyema kumbukumbu za kikao hicho ili kuepusha
kusahau maazimio waliyoyafanya wakati wa kikao hicho. Kikao kijacho kitakuwa tarehe
15/06/2012. Alitamka kukifunga  rasmi kikao cha 1 cha kikundi cha NGOME IMARA.
Mine coins - make money: http://bit.ly/money_crypto

You might also like