Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 4

Draft

MAKUBALIANO YA HIARI YA KUKATISHA MKATABA WA UPANGISHAJI


WA BAADHI YA VYUMBA

Makubaliano kukatisha Mkataba wa Kupangisha baadhi ya vyumba yanafanyika leo


tarehe ………………. mwezi wa ……………………... 2020

Kati ya

SEKUNDA MOSARD NJIGE ambaye ni Msimamizi wa Mirathi ya Marehemu Cyprian


Mosard Njige na katika Mkataba huu atajulikana kama “Mwenye Nyumba” neno ambalo
litajumuisha Mke na Watoto wa Marehemu Cyprian Mosard Njige, warithi wao na wote
watakaodai haki kutokana na mkataba huu, kwa upande mmoja.

Na

ABDUEL FAHAMUEL MMASA ambaye hapa ataitwa “Mpangaji”, neno ambalo


litajumuisha yeye binafsi, warithi wake na yeyote atakayedai haki kutokana na mkataba huu kwa
upande mwingine.

UTANGULIZI

A. KWAMBA, Tarehe 02.07.2016 Wahusika katika mkataba huu walisaini mkataba wa


kupangisha vyumba Vinne na vyoo viwili vya ndani (self-contained) ambavyo
vinatumika kama chumba, sebule na choo mara mbili, katika nyumba iliyopo Plot
No. 713, Block 7 Kijitonyama, Dar es salaam, ambayo ni Mali halali ya Mwenye
Nyumba.

B. KWAMBA, katika Mkataba huo, pande zote mbili zilikubaliana kwamba Mkataba huo
utakuwa wa miaka kumi na tano (15) na kwamba malipo ya awamu ya kwanza ya kodi
katika Mkataba huo yalifanyika kama wahusika walivyokusudia, ambapo awamu ya
kwanza malipo ya kodi ya miaka mitatu yalilipwa na Mpangaji na Mwenye nyumba
anakiri kupokea malipo hayo ya kodi

Page 1 of 4
Draft

C. KWAMBA, Kodi ya miaka mitatu iliyolipwa wakati wa kusaini Mkataba huo imeisha
tangu tarehe 30 mwezi Mei Mwaka 2019 na Mpangaji hajalipa kodi nyingine mpaka
sasa.

D. KWAMBA, kwa kupitia makubaliano haya pande zote zimeridhia kusitisha Mkataba wa
Upangishaji wa baadhi ya vyumba kwa ajili ya Biashara uliosainiwa tarehe 02.07.2016

E. KWAMBA, kwa kupitia makubaliano haya pande zote zimeridhia hapo baadae kuingia
Mkataba mpya wa upangishaji nyumba hiyo kwa ajili ya Makazi ambao hautahusiana
kwa namna yeyote na Mkataba wa Upangishaji wa tarehe 02.07.2016 baina ya wahusika.

SASA BASI, MAKUBALIANO YA HIARI YA KUKATISHA/KUVUNJA MKATABA


YANASHUHUDIA YAFUATAYO

1. Mkataba wa Upangishaji baadhi ya vyumba kwa ajili ya Biashara uliosainiwa tarehe


02.07.2016 utasitishwa ifikapo tarehe 31/07/2020.

2. Kwamba, Mpangaji kwa muda wa miaka minne ya upangaji wa baadhi ya vyumba kwa
ajili ya Biashara hakuweza kutumia baadhi ya vyumba kufanya Biashara na badala yake
alitumia vyumba hivyo kwa ajili ya Makazi.

3. Kwamba, Mwenye Nyumba na Mpangaji wamekubaliana kufuta deni lililopo la kodi ya


pango ya mwaka mmoja na miezi miwili yaani miezi kumi na minne (14) kuanzia tarehe
31/05/2019 hadi tarehe 31/07/2020 sawa na shilingi milioni saba na laki saba (TShs
7,700,000/=) hata hivyo, mpangaji atatakiwa kulipa kodi ya pango ya shilingi laki mbili
(TShs 200,000/=) ya makazi kwa mwezi kuanzia tarehe 31/05/2019 hadi tarehe
31/07/2020 sawa na shilingi milioni mbili na laki nane (TShs 2,800,000/=).

4. Kwamba, Malipo ya Kodi ya Pango ya TShs 2,800,000/= yatafanyika kwa njia ya pesa
taslimu ambazo zitalipwa kwa Mwenye Nyumba na yatafanyika siku ya kusaini
Makubaliano haya.

5. Kwamba, Kodi ya Mkataba wa kupangisha baadhi ya vyumba (Vinne na vyoo viwili vya
ndani (self-contained) ambavyo vinatumika kama chumba, sebule na choo mara mbili)

Page 2 of 4
Draft

ambavyo vitatumika kwa ajili ya Makazi itakuwa TShs Laki tano (500,000/=) kwa
mwezi sawa na Tsh. Milioni Sita (6,000,000/=) kwa mwaka, malipo hayo yatafanyika
kwa utaratibu ulioainshwa hapa chini;

a) Kodi yote ya Mwaka (yaani Tsh. Milioni Sita) italipwa kwa mkupuo mmoja na
Malipo hayo yatafanyika kwa njia ya pesa taslimu ambazo zitalipwa kwa
Mwenye Nyumba siku ya kusaini Mkataba huu.

6. MKATABA huu unapaswa kusainiwa na kutekelezwa na pande zote mbili kabla ya au


tarehe 31.07.2020, endapo Mkataba huu hautasainiwa na kutekelezwa na pande zote
kabla ya tarehe tajwa, basi Mpangaji atapaswa kuhama na kurudisha vyumba
alivyopangishiwa kwa Mwenye Nyumba ndani ya siku saba(7) baada ya kuvunjika kwa
Mkataba wa awali ambao pande zote zimekubaliana ufikie ukomo tarehe 31.07.2020

7. MKATABA huu utasimamiwa na kutafsiriwa kwa Sheria za Mikataba za Tanzania na


kwamba mgogoro wowote utakaotokea kuhusu MKATABA huu, Mahakama zitakuwa
na mamlaka ya kuamua mgogoro huo.

NA INASHUHUDIWA kwamba wahusika wameingia makubaliano ya kukatisha Mkataba wa


Upangishaji kwa ajili ya biashara na kuingia makubaliano ya upangishaji kwa ajili ya makazi,
siku hii kama inavyoonekana hapo chini:

Makubaliano haya YAMESAINIWA na

SEKUNDA MOSARD NJIGE


Kama Msimamizi wa Mirathi ya Marehemu
CYPRIAN MOSARD NJIGE
Ambaye ametambulishwa kwangu na ..........................................
…………………………………… MWENYE NYUMBA
Ambaye ninamfahamu,
Leo Tarehe: …............mwezi............2020.
Hapa Dar es salaam.

MBELE YANGU

Page 3 of 4
Draft

Sahihi ………………………………………………………….

Jina ……………………………………………………………..

Anuani: ………………………………………………………..

Wadhifa: WAKILI

Makubaliano haya YAMESAINIWA na

Ndugu ABDUEL FAHAMUEL MMASA


ambaye ametambulishwa kwangu na ..........................................

………………………………………….. MPANGAJI

Ambaye ninamfahamu katika siku hii ya


Leo. Tarehe: …………………………
Hapa Dar es salaam.

MBELE YANGU

Sahihi: ………………………………………………………………………

Jina……………………………………………………………………………

Anuani: …………………………………………………………………….

Wadhifa: WAKILI

Page 4 of 4

You might also like