Ngoswe

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 5

UHAKIKI WA TAMTHILIYA

Fasihi andishi ni tawi la fasihi linalotumia sanaa ya maneno kufikisha


ujumbe kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Zipo aina nyingi za fasihi
andishi, miongoni mwa hizo ni pamoja na hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na
mashairi.
Fani katika Tamthiliya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe
JINA LA KITABU: NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE
MWANDISHI: EDWIN SEMZABA
WACHAPISHAJI: NYAMBARI NYANGWINE PUBLISHERS
MWAKA:2006
UTANGULIZI
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe ni tamthiliya maarufu sana ambayo
imewahi kuigizwa katika redio Tanzania na katika majukwaa mbalimbali
hapa nchini. Ni tamthiliya ambayo imeundwa vyema katika vipengele vya
fani na maudhui. Ameteua lugha nzuri na yenye mvuto kwa wasomaji
yenye mbinu za kifasihi zilizosheheni, muundo wenye mtiririko mzuri,
unaoakisi kuanza kuchipuka kwa matukio mpaka kilele cha matukio.
Wahusika wamebeba vyema uhusika wao mfano Ngoswe.
Ameibua dhamira kuhusu mambo yanayoigusa jamii ya leo kama vile
uzembe, madhara ya ulevi, uzembe kazini, suala la matabaka kati ya mjini
na vijijini. Mtazamo, falsafa na msimamo wake ni kulenga kuibadilisha jamii
na kuleta maendeleo.
JINA LA KITABU
Jina la kitabu “Ngoswe penzi kitovu cha uzembe” ni jina ambalo limesawiri
vyema yaliyomo ndani ya kitabu hicho, kwani Ngoswe ndio jina la mhusika
mkuu anayebeba dhamira kuu ya tamthiliya. Pia penzi limeonekana kuwa
ni kitovu cha uzembe kwani ndio yaliyopelekea kuteketezwa kwa karatasi
za takwimu za sensa. Hivyo jina la kitabu si tu kwamba limesawiri yaliyomo
katika kitabu bali pia katika jamii.
MTINDO
Mtindo alioutumia mwandishi ni dayalojia au majibizano. Mwandishi
amepanga visa na masimulizi kwa kutumia majibizano ya wahusika.
Matumizi ya nafsi ya kwanza.Mwandishi ndiye ameyafafanua na kuelezea
baadhi ya matukio. Katika karibu kurasa zote mwandishi ameonekana
kuwa ndiye msimuliaji wa matukio.
Matumizi ya nafsi ya pili.Hapa watu wawili na zaidi wanajibizana. Tamthilya
hii wahusika wanaojibizana kuibua dhamira na migogoro. Kuna majibizano
baina ya mzee Mitomingi, Ngoswe na Mazoea nk.unaweza kupata mfano
uk. wowote kwani ndio mtindo uliotawala.
MUUNDO
Muundo uliotumika ni muundo wa mojakwamoja au sahili. Kwani
ameonesha tangu mwanzo wa mambo mpaka mwisho, anajenga visa
vidogo mpaka visa vikuu au kileleni.Amepanga visa na matukio yake katika
maonesho matano. Kila kichwa kina maelezo yaliyojadiliwa katika onesho
hilo.
KIJITO:
Hapa yanaeleza jinsi mambo yanavyoanza. Jinsi Ngoswe anavyoingia
kijijini anavyopokelewa na kuanza kufahamiana na wenyeji wake.
VIJITO:
Hapa Ngoswe anaanza kufanya kazi iliympeleka kijijini na tunaanza
kuoneshwa changamoto anazokumbana nazo.
MTO:
Ni mwendelezo wa matukio ya mwanzo hapa visa vinazidi kukua.
JITO:
Hapa Ngoswe anakumbana na changamoto nyingi zaidi katika kazi yake.
Na hapa anazidi kuanguka kwani anajiingiza katika mapenzi na msichana
Mazoea, anaendekeza ulevi na kuharibu kazi kabisa.
BAHARINI:
Hapa inaoneshwa mwisho wa mambo jinsi yalivyokuwa. Yanaonekana
mahojiano baina ya Serikali na Ngoswe na Mitomingi juu ya uzembe
uliofanyika wa kupoteza takwimu na hapa ndipo suluhisho linapotolewa juu
ya matatizo hayo.
WAHUSIKA
NGOSWE
Kijana wa kiume umri kati ya miaka 20-25
Ameelimika na amestaarabika
Anatumwa na serikali kufanya sensa kijijini
Anajihusisha na mapenzi na msichana mazoea
Ni mlevi
Hana umakini katika kazi
Aliharibu kazi ya serikali
Hafai kuigwa na jamii
MAZOEA
Ni msichana mwenye umri kati ya miaka 18-20
Ni binti wa Mzee Ngengemkeni Mitomingi
Hana elimu na hajastaarabika
Ana nidhamu ya woga
Ana tama
Hana msimamo alikubali kuchukuliwa na Ngoswe hali akijua alishatolewa
mahari
Hafai kuigwa na jamii.
NGENGEMKENI MITOMINGI
Ni balozi katika kijiji chake
Ni baba mzazi wa Mazoea
Ameoa ndoa ya mitara, ana wake wawili
Hajaelimika
Anashikilia mila na desturi za kale
Mlevi
Mkali sana
Anateketeza karatasi za takwimu
MZEE JIMBI
Mwanakijiji
Hajaelimika kwani hajui hata umri wake
Ni mlevi
Ana wake wawili
Anashikilia ukale
MAMA MAZOEA
Mke mkubwa wa Mitomingi
Mama yake Mazoea
Mlezi wa familia
Hapewi nafasi ya kutoa maamuzi katika familia
MAMA INDA
Mke wa pili Mzee Mitomingi
Mama yake Huzuni
Hapewi nafasi ya kutoa maamuzi
Ni mlezi wa familia.
MANDHARI
Mandhari ya tamthiliya hii imechorwa katika mazingira ya kijijini. Mambo
yanayoelezwa ni ya kijijini mfano kilimo, hali ya watu kimaisha, huduma
duni sana za kijamii kama vile shule, umbali wa makazi toka nyumba moja
hadi nyingine. Haya yanatudhihirishia vyema mandhari hiyo ambayo kwayo
imeibua dhamira mbalimbali kama vile umaskini, ukosefu wa elimu,
huduma duni za afya vijijini, masuala ya imani potofu nk.
MATUMIZI YA LUGHA
Lugha aliyotumia mwandishi ni lugha fasaha na rahisi kueleweka kwa
wasomaji. Pia kuna matumizi ya lugha nyingine mfano uk. 1 “bell bottom”
Matumizi ya semi
Methali:Uk.22 “Penye nia pana njia”.Uk.27 “Waona vyaelea vyaundwa.”
Misemo:Uk.14 “Akuwaniae ujovu haji kweupe”
Nahau:Uk.11 “hebu keti tutupe mawe pangoni” –tule chakulaUk.7 “mbongo
zimelala”-ana maarifa Uk.14 “pombe na yeye ni pete na chanda”-
anapenda pombe sana.
Matumizi ya tamathali za semi
Tafsida:Uk.21 “Wala hajarudi, kama ingekuwa ni kujisaidia si angekuwa
amekwishamaliza?”
Tashbiha:Uk.1 “vumbi jekundu kama ugoro wa subiana”Uk.8 “sarawili yake
miguuni kama kengele ya bomani”Uk.17 “wanaondoka huku wakitazamwa
kama vile mizuka”
Sitiari:Uk.7 Mama Mazoea : “kiziwi mkubwa wee!”Uk.14 “pombe na yeye ni
pete na chanda!”Uk.26. “karatasi? za takwimu? Ndio wanyama gani hao?”
Mubaalagha:Uk.11 Mama Mazoea : “kupeleka chakula ndio umefanya
makao!”Mama mazoea : “Kujibu swali ndio ukachukua mwaka mzima!”
Mbinu nyingine za kisanaa
Mdokezo:Uk.22 Mazoea : “sijui….. siwezi….. namuogopa baba”Uk.16
Ngoswe : “huyo mtoto wenu wa kwanza anaishi hapa au…..”
Takriri:Uk.9 “Mama Masikio! We Mama Masikio!”Uk.13. “Hodi! Hodi!”Uk.2
“karibu karibu”
Tashtiti:Uk.5 Ngoswe: “hivyo waitwa nani?”Mazoea: “mie?”Uk.22 Ngoswe:
“mchumba? Kwani mchumba ni kitu gani?”Uk.26 Mitomingi: “karatasi? Za
takwimu? Ndio wanyama gani hao?Hapa wahusika waliuliza maswali
ambayo majibu yake waliyaelewa ila kutokana na kutaka kudhihirisha
hasira, msisitizo nk. Ndio maana wametumia tashtiti.
Onomatopea/tanakali sauti:Uk.7 Kifaruhande anacheka “Ha! ha! ha!
Ujenzi wa taswira
Mwandishi ametumia taswira ya mto kuelezea visa vyake. Sehemu ya
kwanza ni sehemu ya kijito, kijito ni kimto kidigo mwandishi hapa anaanza
kueleza mambo yakiwa machanga kabisa ndio yanaanza.
Sehemu ya pili ni vijito. Huu ni muunganiko wa vijito vidogovidogo hapa
mwandishi anaanza kueleza visa vidogovidogo. Sehemu inayofuata ni
sehemu ya Mto. Hii inaashiria mambo yameanza kuwa mazito, visa
vinakua zaidi na Ngoswe anazidi kuingia katika changamoto kubwa zaidi.
Pia Jito ni taswira ambayo mwandishi ameitumia kuashiria hatari zaidi
mambo makubwa zaidi na hapa ndipo tunaona Ngoswe anaanguka kabisa
katika kazi yake kwani Jito ni lenye maji mengi na yanayoenda kwa kasi
hivyo huhitaji umakini mkubwa zaidi.
Mwisho sehemu ya Bahari ambapo hapa ndipo hatima ya mambo
inaelezwa Ngoswe anazama na kupotea kabisa! Hafanikiwi kutoa takwimu
kwani karatasi zilichomwa moto.

You might also like