Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERI KALI ZA MITAA
Anuani ya Simu "TAM/SEMI" DODOMA Mji wa Serikali - Mtumba,
Simu Na: +255 26 2321607 Mtaa wa TAM/SEMI,
Nukushi: +255 26 2322116 S.L.P. 1923,
Barua pepe:ps@tamisemi.go.tz 41185 DODOMA.
Unapojibu tafadhali taja:-

Kumb.Na. DC. 20/507/01/10 2 Novemba, 2020

Makatibu Tawala wa Mikoa,


TANZANIA BARA.

Yah: UJAZAJI WA "FORM FOUR {F4) SELFORM" MWAKA 2020 KWA


WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI

Tafadhali rejea soma tajwa hapo juu.

2. Wanafunzi wa Kidato cha Nne mwaka 2020 wanatarajiwa kuanza mitihani ya


Kuhitimu Kidato cha Nne kuanzia tarehe 23 Novemba hadi 11 Disemba, 2020.
Wanafunzi wote wa Kidato cha Nne, kama ilivyo utaratibu wanatakiwa kujaza "F4 Sel
form" kwa ajili ya kuomba kuchaguliwa kuendelea na masomo ya Kidato cha Tana,
Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Vyuo vya Ualimu. Fomu hiyo ndiyo inayomsaidia
mwanafunzi kuchagua tahasusi (combination) au utaalamu. Fomu hiyo inatakiwa
ijazwe kwa umakini na kwa kuwashirikisha wazazi, walezi pamoja na walimu
washauri wa masomo.

3. Kwa sababu hiyo, waelekezeni Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa


kusambaza fomu hizo kwenye shule zote za Serikali na zisizo za Serikali iii kila
mwanafunzi ajaze nakala mbili. Kati ya nakala hizo, moja itabaki shuleni kwa rejea
na nyingine iwasilishwe kwa Afisaelimu wa Sekondari wa Halmashauri kabla ya
tarehe 28 Disemba, 2020 ambako taarifa zote zitaingizwa kwenye mfumo wa
uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha Tana na Vyuo vya Elimu ya Ufundi na
Ualimu. Baada ya kukamilisha ujazaji kwenye mfumo, nakala ngumu zitolewe na
kurejeshwa shuleni kwa ajili ya uhakiki.

4. Aidha, Ofisi ya Rais -TAMISEMI itaendelea kutoa fursa kwa wanafunzi


kufanya mabadiliko ya tahasusi kwenye tovuti (www.tamisemi.go.tz) baada ya
matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2020 kutangazwa. Hivyo, wanafunzi
wote wapewe taarifa hiyo na kutunza namba zao za mtihani ambayo ni namba ya siri

"password" ya kuingilia kwenye mfumo

5. Pamoja na barua hii, naambatisha nakala ya "F4 Sel Form" orodha ya shule
zote za Kidato cha 5 na 6 yenye tahasusi husika, Vyuo vya Ualimu na orodha ya
Vyuo vya Elimu ya Ufundi yenye fani zinazotolewa katika vyuo hivyo .
.~
6. Ninawashukuru kwa ushirikiano wenu.

1iJ.s. '-"-~
Eng. Joseph M. Nyamhanga
0-
KATIBU MKUU
..

wote wapewe taarifa hiyo na kutunza namba zao za mtihani ambayo ni namba ya siri
"password" ya kuingilia kwenye mfumo

5. Pamoja na barua hii, naambatisha nakala ya "F4 Set Form" orodha ya shule
zote za Kidato cha 5 na 6 yenye tahasusi husika, Vyuo vya Ualimu na orodha ya
Vyuo vya Elimu ya Ufundi yenye fani zinazotolewa katika vyuo hivyo .
.~
6. Ninawashukuru kwa ushirikiano wenu.

~,._,._.. C-
Eng. Joseph M. Nyamhanga
KATIBU MKUU

You might also like