Kilimo Cha Vitunguu PDF

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 5

KILIMO CHA VITUNGUU MAJI

UTANGULIZI
Vitunguu maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi
duniani zenye hali ya hewa ya ubaridi wastani. Zao hili lina wapatia
watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye
nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Nchini Tanzania,
vitunguu maji hulimwa kwenye mikoa ya Iringa wilaya ya Kilolo
mpakani mwa mkoa wa Morogoro na kwenye maeneo ya mto Ruaha,
mkoani Arusha sehemu za Mang’ora na Babati, Kilimanjaro, na
Morogoro wilayani Kilosa sehemu za Lumuma na Malolo na baadhi
ya sehemu za Mkoa wa Singida.

Kipato kikubwa na hivyo huinua uchumi

Hali ya Udongo
Vitunguu maji huhitaji udongo wenye rutuba, usiopasuka,
usiotuamisha maji na wenye mboji ya kutosha. Hali ya udongo katika
kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0.
Unaweza kuuza mara moja au kuhifadhi
Hali ya hewa Uoteshaji miche na Upandaji
Hali ya hewa ifaayo ni ile ya ubaridi wastani. Joto linalohitajika ni Vitunguu maji huoteshwa zaidi kwa kutumia mbegu kwenye kitalu
kati ya nyuzi joto 13 hadi 24°C ingawa kwa miche iliyoko kwenye na kisha kupandikizwa shambani. Kiasi cha kilo 3.5 cha mbegu hutoa
kitalu joto zuri ni la nyuzi 20 hadi 25°C. Joto la juu hufanikisha miche ya kutosha kupandikiza eneo la hekta moja ya shamba.
utengenezaji wa kitunguu na ukaukaji.
Kusiha mbegu kwenye kitalu
Aina ya Vitunguu maji Mbegu zinasiwa kwenye kitalu kilichoandaliwa vizuri. Mbegu
Kuna aina nyingi ya vitunguu maji. Aina hizi zinaweza hupandwa kwenye kina cha sentimita moja kwa kumiminwa polepole
kutofautishwa kulingana na: kwenye mistari/mifereji iliyoandaliwa vizuri. Kisha mbegu hufukiwa
(i) rangi ya ganda la nje la kitunguu kilichoishavunwa; kwa kunyunyizia udongo juu ya mbegu zilizoko kwenye mifereji.
(ii) radha (utamu au ukali) wa kitunguu chenyewe; Mbegu huota baada ya siku 7 hadi 10. Lakini hii hutegemeana na hali
(iii)mahitaji ya mwanga katika uzaaji: kuna aina yenye kuhitaji ya hewa. Kwani mbegu huweza kuechelewa kuota hadi mpaka siku
siku fupi (mwanga wa saa 10 hadi 12 kwa siku) na aina 21 udongo unapokuwa wa baridi. Hali ya hewa ikiwa nzuri, mbegu
ihitajio siku ndefu (saa 13 hadi 14 za mwanga kwa siku) ili uota mapema zaidi, hata ndani ya siku 4.
kuweza kuweka kitunguu. Aina ya kwanza ndiyo ilimwayo
katika nchi za tropic.

Umbile
Siku za Rangi ya Rangi ya
Aina la
kukomaa ganda ndani
kitunguu
Red Nusu Nyekundu -
150 Nyekundu
Creole bapa kahawia
Red Nyekundu Nyeupe -
160 Duara
Bombay angavu kahawia
Texas Njano
165 Duara Nyeupe
Grano (Kaki)
Kupandikiza vitunguu shambani Umwagiliaji:
Miche hupandikizwa inapokuwa na urefu wa sentimita 15 na unene Umwagiliaji mzuri unahitajika ili kupata vitunguu bora. Umwagiliaji
1
/2 au 3/4 ya penseli kwenye shina. Miche hii huwa imetimiza umri wa maji yanayokwenda chini kiasi cha sentimeta moja au zaidi kwa
kati ya wiki 7 hadi 9 kulingana na matunzo. Miche inapandikizwa wiki ni mzuri kwa kupata vitunguu vikubwa. Epuka umwagiliaji
kwenye nafasi ya upana wa sentimita 20 hadi 30 na nafasi ndani ya kupita kiasi au pungufu kwani hali hii huweza kusababisha
mstari ni sentimita 10 hadi 15. mipasuko.
Kuandaa shamba
Kabla ya kupandikiza udongo utifuliwe vizuri na majani yaondolewe Udhibiti wa magugu
kabisa. Kisha matuta au majaruba hutengenezwa ili kurahisisha Ukuaji na mavuno yanaathirika sana endapo magugu hayatadhibitiwa
umwagiliaji. mapema. Magugu yanadhibitiwa kwa kutumia madawa ama jembe
dogo la mkono. Wakati mwingine ni mchanganyiko wa madawa,
Mbolea jembe la mkono na kungolea kwa mkono.
Vitunguu maji vinamahitaji makubwa ya rutuba ya udongo. Hukua
vizuri vinapopata samadi ya kutosha kiasi cha tani 25 hadi 40. Kwa Udhibiti wa magonjwa
hekta. Mbolea isambazwe shambani baada ya kupandikiza, lakini ni 1. Ugonjwa wa doa la pinki (Purple blotch)
vizuri zaidi kama ikichanganywa kwenye udongo kabla ya Uanza kama doa dogo linalozama ndani ya jani na kisha
kupandikiza. Kwa kuzingatia mazao ya tani 18 kwa hekta, vitunguu linaongezeka ukubwa na kufanya rangi ya pinki. Kiini cha ugonjwa
huchukua kutoka katika udongo, kiasi cha wastani wa kilo 66, 11 na huu huanzia kwenye mbegu na pia hubaki kwenye maozo ya majani
70 za virutubisho aina ya Nitrojeni, Fosiforasi na Potasiam. ya vitunguu. Aina ya Red Creole inaonyesha kutoshambuliwa sana
na ugonjwa huu.
Hivyo kiasi cha mbolea kinachopendekezwa ni kilo 450 hadi 565 za
mbolea ya NPK (10-10-20) kwa hekta. Mbolea huwekwa siku 7 hadi
10 kabla ya kupandikiza. Kisha, inapendekezwa kuweka kiasi cha
kilo 13 hadi 18 za Nitrojeni baada ya wiki tatu hadi nne, ili kuongeza
ukuaji wa mimea. Upungufu wa kirutubisho cha Nitrojeni
unaharakisha ukomaaji na unapunguza ukubwa wa kitunguu.
Kirutubisho hiki kikizidi kupita kiasi huongeza ukubwa wa kitunguu
na unene wa shingo ya kitunguu, tabia ambayo upunguza ubora.
Ugonjwa wa doa la pinki Kuoza kwa kitunguu
Mbinu za kudhibiti ugonjwa huu ni kuendesha mzunguko (crop 1. Utitiri wa vitunguu (Onion thrips)
rotation) wa muda mrefu wa mazao pamoja na kuzuia kutuama kwa Hawa ni wadudu wadogodogo sana ambao hula kwa kukwaruza juu
maji shambani. Kupunguza msongamano wa mazao shambani na ya jani na kunyonya majimaji ya kwenye mmea. Hali husababisha
matumizi ya mbolea zenye calcium, phosphate and potassium kutoka kwa mikwaruzo meupe kwenye majani ya vitunguu.
hupunguza kuenea kwa ugonjwa huu. Kwa upande mwingine, Mashambulizi yakizidi majani huanguka na kunyauka. Ukubwa wa
matumizi ya mbolea ya nitrojeni kwa wingi au kwa kiasi pungufu vitunguu hupungua. Hili ni tatizo kubwa zaidi hasa wakati wa ukame
uongeza mlipuko wa magonjwa. Viatilifu kama vile Mancozeb kuliko wakati wa unyevu.
hutumika kuzuia mashmbulizi ya ugonjwa huu.

2. Ukungu wa unga (powdery mildew) na wa chini (Downy


mildew)
Magonjwa haya hushambulia majani ya mimea shamabani na hata
miche michanga. Kwenye majani kunaonekana vidoa vyeupe hasa
kwenye majani makuu ya mimea michanga. Ukungu mweupe
unatokea na kuongezeka kwa haraka kwenye sehemu au nyakati za
baridi. Viini huishi kwenye mabaki ya mimea ya vitunguu na huweza
kupeperushwa mbali na upepo. Kwenye mimea michanga ugonjwa
unaweza kudhibitiwa na madawa kama mancozeb.
Utitiri wa vitunguu Madhara ya utitiri
3. Kuoza kwa vitunguu (bulb rots)
Hali hii inaweza kutokea shambani au wakati wa hifadhi ghalani.
2. Bungua weupe (White grub)
Ugonjwa huu ni hatari zaidi kwenye sehemu za joto na zenye
Huyu ni aina ya funza mkubwa. Hutaga mayai yake kwenye uozo wa
kutuamisha maji. Ni vyema kuhakikisha kwamba shambani hakuna
majani na samadi na hivyo mashamba ya vitunguu yaliyoko karibu
hali ya kutuamisha maji na pia kwenye ghala kunakuwa na hali nzuri
au kwenye maeneo ya jinsi hiyo huwa kwenye hatari zaidi.
ya mzuunguko wa hewa.
Hushambulia mizizi na kusababisha kukauka kwa mimea. Kutifulia
shamba na kuwaweka wazi wadudu hawa kunapunguza idadi yao.
Udhibiti wa wadudu
Utitiri wa vitunguu (Onion thrips), Funza wa vitunguu (Onion
maggots) na Minyoo wa vitunguu (Onion wireworms) ni miongoni
mwa wadudu wasumbufu kwenye zao la kitunguu.
huwa na shingo iliyonywea vizuri na ganda kavu. Kama shingo ya
kitunguu haikukauka sawasawa kutatokea hali ya uozo.

Soko la vitunguu
Ukubwa wa vitunguu ni sifa ingaliwayo na wanunuzi. Vitunguu
vidogodogo sana au vinene sana huwa havipendwi. Vitunguu
vinavyopendwa ni vile vyenye wastani wa unene wa sentimita nne.
Bungua mweupe Funza wa Kitunguu Vitunguu vilivyochubuka, mapacha na vyenye shingo ya chupa huwa
3. Minyoo ya vitunguu (Onion wireworms) havipendwi. Vitunguu vilivyooza na vile vilivyobabuka na jua pia
Hawa ni funza ambao mayai yao hutagwa kwenye maeneo yenye havifai. Kwa Tanzania wakulima wengi wanauza vitunguu kwa
magugu. Wadudu hawa huwa ni tatizo kubwa kwenye sehemu zenye vipimo vya magunia na ama ndoo za plastiki. Kwa miaka kadhaa
kutuamisha maji. Kutifulia udongo ili upitishe maji vizuri pamoja na vitunguu vimekuwa vikiuzwa kati ya shilingi 20,000/= hadi 30,000/=
udhibiti wa maguu ni njia nzuri ya kuwadhibiti wadudu hawa. kwa gunia.

Uvunaji Hifadhi ya vitunguu


Inapowezekana mwezi mmoja kabla ya kuvuna udongo uanze Vitunguu vipya vilivyovunwa huwa havioti upesi. Hifadhi sahihi
kuondolewa polepole ili kuviacha wazi vitunguu kwa ajili ya hurefusha muda wa kutoota. Kwenye hifadhi ni vizuri vitunguu
ukaukaji mzuri. Zoezi hili linalenga kufanya angalau theluthi moja ya vipate hewa yenye mzunguuko mzuri na ndiyo maana maghala ya
sehemu ya kitunguu kiwe hakijafunikwa na udongo kwa siku kati ya kuhifadhia vitunguu yanajengwa kama vichanja ili kuruhusu hewa
7 hadi kumi kabla ya kuvuna ili kuharikisha ukaukaji. Vuna wakati kuzunguuka hata kwa kupitia sehemu za chini. Ndani ya ghala
asilimia 75 ya shingo za vitunguu zimelala. Mara nyingi vitunguu vitunguu humwagwa na kusambazwa kama inavyonyesha kwenye
hung’olewa na kurundikwa kwenye matuta na baadaye kukusanywa picha namba.. Vitunguu vinaweza kuhifadhiwa kwa miezi sita au
na kuwekwa kwa ajili ya kukata shingo. Mizizi pia inapunguzwa na zaidi bila kuharibika.
vitunguu vinajazwa kwenye magunia tayari kwa kusafirishwa
nyumbani kwa ukaushaji zaidi na kisha kuwekwa galani au kuuzwa. Mavuno
Mavuno ya vitunguu yanategeme huduma za shamba pamoja na hali
Ukaushaji ya hewa. Vitunguu pia hutofautiana katika mavuno kulingana na aina
Madhumuni ya kukausha ni kuvifanya vitunguu visiweze kuota kwa ya kitunguu. Kwa wastani vitunguu vinaweza kutoa mavuno kati ya
muda na pia kuvifanya visiharibike. Vitunguu vilivyokauka vizuri tani 10 hadi 18 kwa hekta moja.

You might also like