Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 25

SOMO: FAHAMU AINA ZA WATU WANAOKUJA, UNAOKUTANA

NAO, UNAOAMBANA NAO AU UTAKAOKUTANA NAO KWENYE


KIPINDI FULANI CHA MAISHA

Mithali 16:4

“BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam hata wabaya kwa
siku zake”

Lengo la somo: Somo hili lina lengo la kutusaidia au kumsaidia mtu ili
awe na uwezo wa kuishi kwa upendo wa dhati na kila mtu kwenye
maisha pasipo kujali udhaifu wake au hali yake ya maisha.

Utangulizi: Kila mtu aliyeumbwa na Mungu, ameumbwa kwa kusudi,


kwa sababu hiyo mtu yeyote anayekuja kwenye maisha yako huja kwa
kusudi. Zingatia Si kila mtu anayekuja, unayekutananaye amekusudiwa
na Mungu aje kwenye mfumo wa maisha yako, Lakini pia kama
tumeumbwa kwa kusudi basi elewa kuwa mtu yeyote yule anayekuja
kwako huwa na athari chanya au hasi.

Mwl Fredrick Kapaya Page 1


Sisi wanadamu tumeumbwa na Mungu mmoja lakini tunatofautiana
katika mambo mbalimbali kwenye maisha haya, kwa mfano: Tabia zetu
hutofautiana toka mtu hadi mtu.

Mwanzo 1:27

“Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, Mungu alimwumba


mwanamume na mwanamke aliwaumba”

Tofauti zetu zitufanye tuheshimiane na kuthaminiana kuliko


kudharauliana, kwa sababu kila mtu anakitu ndani yake alichopewa na
Mungu kimsadie yeye na kiwasaidie na wengine.

Wafilipi 2:3

“Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa
unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa ni bora kuliko
nfsi yake”

Andiko hili linapotumia neno Kushindana Tafsri yake ni kuwa


tunauwezo tofauti tofauti katika kutenda mambo (Kama tunauwezo
tofauti basi kila mtu amwone mwenzake kuwa ni bora kwa sababu
tumepewa kwa sehemu tu, kuna mambo ambayo utaweza kufanya
lakini yapo ambayo utahitaji mtu au watu wakusaidie kufanya.

Hakuna mtu ambaye hana udhaifu kwa sababu hiyo watu wote ambao
huja, unaokutana nao au kuambatana nao huwa na udhaifu fulani lakini
pia hukukuta nawe pia una udhaifu fulani ndani yako.

Hakuna mtu anayeweza au mwenye uwezo wa kufanya kila jambo


pasipo kuwa hitaji watu wengine (Ili ufanikiwe unahitaji watu). Ni kweli
tunahitaji watu lakini elewa kuwa si kila mtu anafaaa kuambatana
nawe. Omba Mungu akupe au akuletee watu sahihi wa kuambatana

Mwl Fredrick Kapaya Page 2


nao ili wakufikishe kwenye maono yako, ukiambatana na watu wasio
sahihi ndani yao huwa na uwezo wa kuua maono yako.

Kumbuka: Mtu yeyote yule aliye katika dunia hii huwa na thamani
kubwa sana, hata kama hautaona leo thamani yake ila ipo siku utajua
thamani yake hasa akiondoka kwenye mfumo wa maisha yako. Jifunze
kumheshimu kila mtu unayekutana naye kwa sababu haujui kesho yake.
Namna unavyomuona mtu leo inaweza kuwa sivyo atakavyokuwa
kesho. Hakikisha kila iitwapo leo unagusa maisha ya wtu kwa kadri
Roho Mtakatifu atakavyokuongoza.

Twende ndani kidogo tuanze kuchambua vizuri aina ya watu au


makundi ya watu. Wapo watu wa aina tofauti tofauti unaweza
kukutana nao katika maisha. Na tofauti kubwa hapa tutakazoenda
kuziangalia ambazo zitatupa aina tofauti za watu zinatokana na tabia
zao, walichokibeba ndani yao, sababu za kuja kwako. Utofauti huu
huweza kuchangiwa na mambo mbalimbali kwa mfano: Malezi,
mazingira mtu aliyokulia, elimu, imani, nk. Ufahamu huu utakusaidia
namna ya kuishi na watu wa aina tofauti tofauti kwa upendo, akili na
kwa hekima.

Aina ya kwanza:

 Wapo watu ambao wamekusudiwa na Mungu waje kwako au


ukutane nao katika kipindi fulani au katika hali fulani ngumu ili
wafanyike au afanyike msaada au daraja ili kupitia mtu huyo
wewe upate kuvuka au kutoka kwenye hiyo shida kisha ufike
unakotakiwa kufika ukiwa salama.

Mwl Fredrick Kapaya Page 3


Muhimu: Si kila mtu au rafiki yako au zako wanaweza kukusaidia au
kukubari kufanyika daraja (kutumia mda wao au mali zao nk) ili wewe
uvuke mahali ulipo ila ni yeye tu au watu waliokusudiwa na Mungu tu.

Upo uwezekano kabisa katika maisha yako, ukapata shida na moyo


wako ukategemea kabisa rafiki yako au ndugu yako akusaidie katika
wakati huo mgumu lakini cha ajabu wanaweza wasikusaidie
wakakumbia kisha mtu mwingine kabisa ambaye haukumtegemea
ndiye akakusaidia.

Sifa za watu ambao hufanyika daraja kwa ajili yako

 Huwa na shauku au kiu ya kukutia moyo na kukupa matumaini ya


kuendelea mbele lakini pia uhakika wa kufika unapoenda.
 Wako tayari kutumia gharama zao pasipo kuhitaji au kutegemea
malipo yoyote kwako ( gharama, kutumia mda wao kwa ajiri ya
shida zako, mali zao nk)
 Huwa na huruma yaani hawapendi kuona unateseka.

Aina ya pili:

 Watu ambao huja kwenye maisha yako wakiwa wamebeba vitu


vya kukusaidia wewe kwenye kipindi fulani au kiwango fulani tu
yawezekana ni kwenye elimu, biashara nk. Muda wao tu ukiisha
huondoka kwenye mfumo wa maisha yako na hata ukiendelea
kuwang’ang’ania hawataweza kukusaidia chochote kwa sababu
kiu yao ya kukusaidia imeondoka kutokana na muda kuisha.

Usiumie ikiwa ndugu wamekusahau, hawakutafuti au siku hizi


hawakusaidii kama zamani ila elewa kuwa yawezekana muda wake wa
kukusaidia umeisha anatakiwa ainuke mtu mwingine kwa ajili yako ili
umalizie kipande cha safari kilichobaki.
Mwl Fredrick Kapaya Page 4
Yoshua 1:1-3

“Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa BWANA, BWANA


akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa,
akasema, Musa mtumishi wangu amekufa; haya basi, ondoka, vuka
mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hata nchi
niwapayo wana wa Israeli. Kila mahali zitakapokanyaga nyayo za
miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa”

Wana wa Israeli walipokuwa wanasafiri kutoka Misri kwenda kanani,


katika safari waliongozwa na Musa. Musa alipofariki haikuwa na maana
ya kuwa safari ya wana wa Israeli iliishia hapo. Ila Mungu alimwinua
mtu mwingine (Yoshua) ili awaongoze katika kipande kilichobaki
hatimaye wafike kanani. Kuna watu wakiondoka kwenye maisha yako
haimanishi kuwa safari imefika mwisho jipe moyo Mungu atainua kina
Yoshua wakusaidie ufike salama.

Angalizo: Weka kwenye fikra zako, tumia hekima na akili ndani yako
katika kutekeleza ili usitengeneze chuki.

Mfano:

Mwanzo 13: 8-9

“Abramu akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati ya


mimi na wewe, wala kati ya wachungaji wako; maana sisi tu ndugu.
Je! Nchi hii yote haiko mbele yako? Basi ujitenge nami, nakusihi;
ukienda upande wa kushoto, nitakwenda upande wa kuume; ukienda
wa kuume nitakwenda upande wa kushoto”

Mwl Fredrick Kapaya Page 5


Abrahamu na lutu walisafiri katika nchi yote ya kanani. Lakini kwa
sababu ya njaa walienda katika nchi ya Misri ambako waliishi kwa
muda.

Kwa tafsri rahisi ni kuwa Abrahamu na Lutu waliishi pamoja katika


kipindi fulani cha maisha. Ila viwango vyao au utajiri wao ulipoongezeka
eneo halikuwatosha ikabidi watengane.

Ninachotaka kukuonesha hapa si kwamba ukipata mali utengane na


ndugu zako hapana ila ninataka uone kuwa kama kuna eneo
umewekewa muda wa kuwepo, muda huo ukiisha ile radha ya kuwa
pamoja au eneo hilo huondoka.

Aina ya tatu:

 Wapo watu ambao unaweza kukutana nao au huja kwenye


maisha yako kisha wakatengeneza urafiki na wewe. Nawe
ikatokea au inaweza tokeo ukawaamini sana kisha ukawaeleza
siri zako baada ya muda mfupi hao marafiki huweza kugeuka
kuwa maadui wa ndani na kuanza kukuangamiza polepole.

Mathayo 10:36

“Na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake”

Kumbuka kuwa: Mtu anayekufahamu vizuri ndiye atakayeweza


kukuangamiza vizuri.

Mika 7:5-6

“Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya


midomo ya kinywa chako ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue
habari”

Mwl Fredrick Kapaya Page 6


Angalizo: Usiwe mwepesi sana wa kumuamini kila mtu anayekuja
kwenye maisha, jifunze kumuuliza Roho Mtakatifu juu ya ujio wa huo
mtu kwenye maisha yako.

Aina ya Nne:

 Wapo watu wanaokuja kwenye maisha yako kisha hukubana au


hufanyika ukuta katika namna ya rohoni au kwa lugha nyepesi
huwa kama kizuizi cha wewe kuendelea mbele, wakati
mwingine hufanyika kizuzi cha wewe kumwabudu Mungu katika
viwango unavyotakiwa kumwabudu.

Kumbuka kuwa: Mungu hutafuta na kutumia watu katika kufanya kazi


yake lakini pia shetani naye hutumia watu katika kutimiza kile
anachokitaka hapa duniani.

Isaya 6:1

“Katika mwaka ule alio kufa mfalme uzia nalimwona Bwana ameketi
katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za
vazi lake zikalijaza hekalu”

Uzia alikuwa kizuizi cha Isaya kuweza kumuona Mungu katika viwango
alichotakiwa kuona. Yawezekana pia katikati ya maisha yako wapo kina
uzia wanaosimama kama kizuizi cha wewe kumuona Bwana.s

Aina tano:

 Watu ambao huambatana na wewe kila mda lakini pia huitaji


kukaa karibu nawe ni kweli kabisa wanaweza kuwa
wanakupenda kwa dhati ila sio wote wengine huwa karibu
nawe kwa sababu huvutwa na ulichonacho (Ulichonacho ni
kama sumaku inayovuta uwepo wa watu, rafiki). Watu wa

Mwl Fredrick Kapaya Page 7


namna hii utawagundua tu pale utakapofika au kupoteza ulicho
nacho nao huondoka kisha upendo wao au thamani yako kwao
hupotea.

Aina ya sita

 Watu ambao mioyo yao huambatana na moyo wako. Watu au


mtu wa namna hii ni lazima mtapendana nao sana.

1 Samweli 18:1

“Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani,


ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake
mwenyewe”

Kuna wakati unaweza kujikuta ghafla moyo wako unatokea tu


umempenda mtu kiasi ambacho unaweza kuwa na mzigo wa
kumuombea sana katika hali hiyo elewa kuwa Mungu kakupa mzigo wa
kumuombea mtu huyo ili avuke eneo fulani katika maisha.

Aina ya saba

 Wapo watu ambao huja au walikuja kwenye kipindi fulani cha


maisha nawe ukawapokea/ kumpokea kisha ukamuami sana
kiasi ambacho ulimfungulia mlango wa moyo wako nao
wakaingia. Baada ya muda watu hao au mtu huyo aliuchezea
na kukuusababishia moyo wako maumivu makubwa sana.

Watu wa namna hii huweza kumsababishia mtu huyo aliyeumizwa


kubadili mtazamo juu ya watu fulani huku ndani yake. Ni ngumu sana
mtu kubadili na kuanza kuwaamini watu kama aliyemwamini sana
kwenye kipindi fulani cha maisha alimfanyia jambo ambalo hakutarajia
kama atafanyiwa na mtu huyo.

Mwl Fredrick Kapaya Page 8


Mithali 4:23

“Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; maana ndiko zitokako


chemchemi za uzima”

Biblia inasema linda sana moyo wako, maana yake unatakiwa uwe na
makini na kinachoingia ndani au unachokiruhusu kuingia ndani ya moyo
wako ili kisije kuuharibu moyo wako.

Mtu ambaye moyo wake umeharibika au kubeba uchungu huwa na


tabia ya usikivu kuondoka ndani yake.

Kutoka 6:9

“Musa akawaambia wana wa Israeli maneno haya; lakini


hawakumsikiliza Musa kwa ajili ya uchungu wa moyo, na kwa ajili ya
utumwa mgumu”

Aina ya nane

 Watu ambao wanapenda sana kukuona unaendelea kubaki


kwenye kifungo au hali ngumu ya kimaisha uliyo nayo, watu wa
namna hii huweza kuwa kimya nyakati upo kwenye kifungo au
hali ngumu ila siku ukifunguliwa au kufanikiwa watu hawa wivu
huwajaa ndani yao kisha huanza kuongea maneno ya
kutofurahishwa na mafanikio yako.

Mambo ya msingi sana kuyaelewa kwenye hili kundi:

 Watu hawa wanaweza wakawa wanajua kabisa hali ngumu


unayopitia au kifungo ulichonacho
 Uwezo wa kukusaidia wanaweza kuwa nao kabisa ila hawataki
kukusaidia kwa sababu furaha yao ni kukuona unateseka

Mwl Fredrick Kapaya Page 9


 Wakati mwingine hujifanya kama vile hawakuoni au hawajui kuwa
unateseka.

Mfano wa 1

Luka 19:30-31

“Akisema, Nendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mtakapoingia


ndani mtaona mwana punda, amefungwa, ambaye hajapandwa na
mtu yeyote bado, mfungueni mkamlete hapa. Na kama mtu
akiwauliza, Mbona mnamfungua? Semeni hivi, Bwana anamhitaji. Na
wale waliotumwa wakaenda wakaona kama alivyowaambia. Na
walipokuwa wakimfungua mwana-punda, wenyewe waliwaambia,
mbona mnamfungua mwanapunda?”

 Ndani ya hili andiko kuna mambo kadhaa tunaweza kuyaona

Jambo la kwanza: Huyu punda alikuwa amefungwa (Alikuwa kwenye


kifungo)

Jambo la pili: Kama punda alikuwa amefungwa basi kuna aliyekuwa


amemfunga.

Jambo la tatu: Kwenye hilo eneo kulikuwa na watu lakini pia


yawezekana kabisa kulikuwa na watu waliokuwa wakipita mahali punda
alipokuwa amefungwa.

Jambo la Nne: Wale watu waliokuwa eneo punda alipofungwa


walipenda kumuona punda anaendelea kuwepo kwenye hicho kifungo,
ndio maana hakuna aliyeangaika kwenda kumfungulia huyo punda.

Mwl Fredrick Kapaya Page 10


Jambo la Tano: Walipojitokeza watu wa kwenda kumfungua ndipo
wakaanza kusema juu ya kufunguliwa kwa punda huyo. Kwa sababu
hiyo hawakupenda punda yule afunguliwe.

Pamoja na watu kutopenda utoke hapo ulipo (shida, mateso) maadamu


unamwamini Mungu. Mungu atahakikisha kuwa anaweka neno juu ya
watu/ mtu aliyemkusudia ili lije kukusaidia kisha uvuke hapo ulipo
maana maandiko yanaonesha wazi kuwa Mungu hutuwazia yaliyo
mema.

Yeremia 29:11

“Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni


mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu
za mwisho”

Mfano wa 2:

Matendo ya Mitume 16:16

“Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja


aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake
faida nyingi kwa kuagua”

Kijakazi huyu alikuwa na pepo (Alikuwa kwenye kifungo). Kuwa kwake


kwenye kifungo hiki kulikuwa kunawapa faida bwana zake kwa hiyo
kijakazi huyu alitumika kama chanzo cha uchumi kwa watu wale.

Mwl Fredrick Kapaya Page 11


Kama alitumika kama chanzo cha uchumi tafsri yake ni kuwa hawa
matajiri wake hawakutaka afunguliwe ila walipenda awe kwenye hicho
kifungo ili wao waendelee kupata faida. Hawakumjali huyu kijakazi wala
kufikili juu ya maisha yake ya badae ila wao walijiangalia wenyewe na
kutaka wanufaike.

Tukisoma vizuri maandiko tunaona kabisa alipofunguliwa huyu kijakazi


walikasilika sana hawa bwana zake, kwa sababu hawakufurahishwa
lakini pia kufunguliwa kwake kulisababisha kuua chanzo chao cha
uchumi.

Matendo ya Mitume 16:18-20

“Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka


akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke
huyu. Akamtoka saa ile ile. Basi bwana zake walipoona ya kuwa
tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila,
wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji;
wakawachukua kwa makadhi, wakasema, Watu hawa wanachafua
sana mji wetu, nao ni Wayahudi”

Katika maisha watu wa namna hii wapo, hawataki kukuona


unafunguliwa kwenye hicho kifungo au kwenye hiyo shida uliyo nayo
kwa sababu kuna faida wanayoipata kwa kuwa kwako wewe kifungoni
siku ukifunguliwa/kufanikiwa basi upo uwezekana wakafanya vita na
wewe lakini pia juu ya wale walikufungua au kusababisha ufanikiwe”

Mwl Fredrick Kapaya Page 12


Mfano wa 3

 Farao hakutaka wana wa Israeli waondoke Misri ila alitaka


waendelee kumtumikia yeye, lakini Mungu hakutaka kuwaona
wana wa Israeli wanaendelea kuteseka huko Misri.

Kwa hiyo, Farao alipenda kuwaona wana wa Israeli wanaendelea


kuwepo kifungoni (Kwenye mateso) kwa sababu walimpatia faida.

Kutoka 5:2

“Farao akasema, BWANA ni nani, hata niisikilize sauti yake, na


kuwapa Israeli ruhusa waende zao”

Kutoka 5:5-8

“Kisha Farao akasema, Tazameni, watu wa nchi sasa ni wengi, nanyi


mnawapumzisha, wasichukue mizigo yao. Na siku ile ile Farao
akawaamuru wasimamimamizi wa watu, na wanyapara wao,
akisema, Msiwape watu tena majani ya kufanyia matofali, kama
mlivyofanya tangu hapo; na waende wakatafute majani wenyewe.
Lakini hesabu ya matofali waliyokuwa wakifanya tokea hapo,
wawekeeni iyo hiyo, msiipunguze hata kidogo, kwa maana ni wavivu
hao; kwa hiyo wanapiga kelele, wakisema, Tupe ruhusa twende
kumtolea Mungu wetu dhabihu”

Mungu hakutaka wana wa Israeli waendelee kuteseka (kuwepo


kifungoni).

Kutoka 3:7-8

“BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko


Misri, name nimesikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao;

Mwl Fredrick Kapaya Page 13


maana nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na
mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema,
kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanani, na
Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi”

Wapo watu kwenye maisha yako wanafurahia sana wewe uendelee


kuwa kwenye shida au uteseke, ikitokea unatafuta upenyo wa kutoka
kwenye hiyo shida huongeza juhudi za kuhakikisha hautoki kwenye hilo
eneo, kwa sababu wanajua ukitoka tu hapo kuvuka hatua nyingine
utafanikiwa kimaisha.

Mfano wa 4

1 Samweli 1:2

“Palikuwa na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima


ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa
Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, Mwefraimu naye alikuwa na
wake wawili; jina lake mmoja akiitwa Hana, na jina lake wa pili aliitwa
Penina; naye huyo Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na
watoto”

Katika hili andiko tunawaona wake wawili wa Elkana ambao ni Hana na


Penina. Lakini pia Hana alikuwa amefungwa tumbo (Alikuwa kifungoni).
Penina alifurahia kuona mwenzie yupo kwenye hicho kifungo/
anaendelea kuwepo kwenye hiyo hali.

Laiti kama Penina angekuwa hataki au hafurahishwi na hali aliyokuwa


nayo Hana, Penina angefanyika faraja kwa ndugu yake ila yeye alikuwa

Mwl Fredrick Kapaya Page 14


chanzo cha Hana kujisikia vibaya. Dalili mojawapo ya kuwa mtu
anafurahia wewe kuwepo kwenye hali ngumu ni kutokutaka kufanyika
faraja kwako.

1 Samweli 1:6

“Ila mwenzake humchokoza sana, hata kumsikitisha, kwa sababu


BWANA alikuwa amemfunga tumbo”

Aina ya Tisa:

 Wapo watu ambao Mungu amekuandalia kwenye maeneo fulani


ya kimaisha (Elimu, kazini, Biashara, sehemu ya ugeni
unayoenda) ili wakusaidie kukuonesha njia au kukutunza.

Mfano wa 1:

1 Wafalme 17:3-4

“Ondoka hapa, geuka, uende upande wa mashariki, ujifiche karibu na


kijito cha Kerithi kinachokabili Yordani. Itakuwa utakunywa maji ya
kile kijito; name nimewaamuru kunguru wakulishe huko”

1 Wafalme 17:8-9

“Neno la BWANA likamjia, kusema, Ondoka, uende Sarepta, ulio mji


wa Sidoni ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa
huko akulishe”

Mwl Fredrick Kapaya Page 15


Eliya alipewa agizo na Mungu, aondoke pale kwenye kile kijito ambacho
kilikuwa kimekauka kisha aende Serepta. Huko Serepta tayari Mungu
alikuwa amemwandalia mwanamke mjane ili amtunze.

1 Wafalme 17:13-16

“Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema;


lakini unifanyie kwanza mkate mdogo uniletee; kisha ujifanyie nafsi
yako na mwanao”

Kuna maeneo ya ugeni ambayo unaweza kwenda, Mungu akawa


ameshakuandalia watu wa kukutunza. Hakikisha kila sehemu ya ugeni
unayoenda mwambie Mungu akuandalie watu wenye moyo wa
kukutunza/ kuwa karibu na wewe.

Mfano wa 2

2 Wafalme 4:8-12

“Hata ikawa siku moja, Elisha alikwenda Shunemu; na huko kulikuwa


na mwanamke mmoja mwenye cheo; naye akamshurutisha aje ale
chakula. Ikawa kila alipopita njia ile, huingia kula chakula. Yule
mwanamke akamwambia mumewe, Tazama, mimi naona ya kuwa
mtu huyu apitaye kwetu mara kwa mara ni mtu mtakatifu wa Mungu.
Nakuomba, tumfanyie chumba kidogo ukutani; na ndani yake
tumwekee kitanda, meza, na kiti, na kinara cha taa; na itakuwa,
atujiapo, ataingia humo”

Mwl Fredrick Kapaya Page 16


Elisha alipokwenda Shunemu, huko Shunemu Biblia inasema kuwa
kulikuwa na mwanamke mwenye cheo. Mwanamke huyu ndani yake
alikuwa na moyo wa kumtunza mtumishi wa Mungu Elisha (Tukienda
ndani zaidi ninaweza kusema kuwa huyu mwanamke alikuwa
amekusudiwa au ameandaliwa ili amtunze Elisha katika kipindi na
majira yale). Ndio maana hakujali gharama, ila alitumia gharama
kumtunza mtumishi.

Mungu akikuandaa kwa ajili ya kumtunza mtu fulani na ndani yako


ukaona kabisa msukumo wa kumsaidia mtu huyo basi hakikisha
unakuwa mtii. Yawezekana kupitia kumsaidia mtu huyo nawe pia
Mungu ukukumbuka kisha ukusaidia kwenye shida uliyonayo ambayo
yawezekana umeona kabisa haiwezekani.

2 Wafalme 4:16-17

“Akasema, Panapo wakati huu mwakani, utamkumbatia mwana.


Akasema, la! Bwana wangu, wewe, mtu wa Mungu, usiniambie mimi
mjakazi wako uongo. Yule mwanamke akachukua mimba, akazaa
mtoto mume wakati uo huo mwakani, kama Elisha alivyomwambia”

Mfano wa 3

 Rahabu aliwaficha wale wapelelezi lakini pia aliwaonesha njia ya


kupiti ili adui wasiwapate.

Mwl Fredrick Kapaya Page 17


Yoshua 2:1

“Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu


kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Enendeni mkaitazame nchi hii,
na Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina
lake aliitwa Rahabu, wakalala huko. Mfalme wa Yeriko akaambiwa,
kusema, Tazama, watu wawili wa wana wa Israeli wameingia humu
leo usiku, ili kuipeleleza nchi”

Pamoja na Rahabu kuwa kahaba lakini Mungu alikusudia lakini pia


alimuuandaa Rahabu ili aje kuwatunza watumishi wa Mungu.

Yoshua 2:4

“Yule mwanamke akawatwaa wale watu wawili, akawaficha,


akasema, Naam, wale watu walikuja kwangu, lakini sikujua
walikotoka, ikawa kama wakati wa kufungwa lango la mji, kulipokuwa
giza, watu wale wakatoka, wala sijui walikokwenda; wafuateni upesi,
maana mtawaata. Lakini yeye alikuwa amewapandisha darini,
akawaficha kwa mabua ya kitani, aliyokuwa ameyatandika juu ya
dari. Basi hao watu wakawafuata kwa njia iendayo Yordani mpaka
vivukoni; na mara wale watu waliowafuatia walipokwisha kutoka,
wakalifunga lango. Tena kabla hawajalala akawaendea juu darini”
(Mst 16) Akawaambi, Enendeni zenu mlimani, wale wanaowafuatia
wasije wakawapata; mkajifiche huko siku tatu wao wanaowafuatia
watakaporudi; kisha enendeni zenu”

Kuna maadui wanaokufuatilia kwenye maisha yako/ wanakuwazia


mabaya. Lakini wapo watu ambao Mungu amekuandalia na kuna vitu
ameweka ndani yao kwa ajili yako ili wakuoneshe njia ya kupita ili ufike

Mwl Fredrick Kapaya Page 18


salama au uvuke salama katikati ya changamoto unayoipitia. Wao
wanaweza kuwa ni sababu ya adui kutokupata wewe.

 Tukimchukua Rahabu yule kahaba kisha tukamleta katika maisha


yetu ya kawaida tutagundua mambo yafuatayo.

Jambo la kwanza: Kuna watu unaweza kuwadharau kutokana na


namna walivyo kumbe ndani yao wamebeba vitu kwa ajili yako ili uvuke
hapo ulipo. (Usimdharau mtu kwa namna alivyo kwa sababu anaweza
akawa amebeba hatima yako au majibu ya maswali kwa unachokifanya)

Jambo la pili: Rahabu alikuwa na imani ndani yake na imani ndani yake
aliidhihirisha kwa matendo.

Waebrania 11:31

“Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na hao


walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani”

Aina ya kumi

 (a) Watu ambao husitasita katika kufanya maamuzi na hata kama


ikitokea wamefanya maamuzi basi huwa na tabia ya kurudi nyuma
au kuangalia nyuma tena kiasi ambacho huweza kubadili mawazo
au maamuzi yako (Watu wasiokuwa na msimamo).

Mwl Fredrick Kapaya Page 19


Maamuzi mazingira huingiwa na huruma

Hukumbuka mambo ya nyuma

Hugeuza macho yao/ hubadili mawazo yako

1 Wafalme 18:21

“Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasita-sita katikati ya


mawazo mawili hata lini? BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali
ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu
neno”

Eliya alikuwa anawasemesha watu juu ya Eneo la maamuzi/ uchaguzi


wao juu ya kutumika, kwa sababu aliwaona kuwa wanahali ya kusitasita
ndani yao katika kufanya maamuzi, kwa lugha nyepesi walikuwa
hawana msimamo ndani yao. Wapo watu ambao kila siku wao ni wa
kusitasita tu hawawezi kabisa kupiga hatua kwenye maisha yao.

(b) Watu ambao hufikiri sana kisha hufanya maamuzi mara moja, watu
hawa baada ya kufanya maamuzi huwa hawana tabia ya kuangalia
nyuma au kubadili maamuzi yao yaani hawabadilishwi na mazingira
wanauhakika au kuona usahihi wa maamuzi yao (Watu wenye
msimamo)

Mwl Fredrick Kapaya Page 20


Maamuzi mazingira Husimamia kile walichokiamua

Huwa na uhakika wa maamuzi yao

Hawana tabia ya kurudi nyuma

Maamuzi/chaguo

Mfano 1

2 Wafalme 7:3-5

“Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji;


wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe? Tukisema, Tutaingia
mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa
vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi
hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu. Basi wakaondoka kabla ya
mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika
mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu”

Watu hawa wenye ukoma waliokuwa wamekaa penye lango la mji.


Kuna mambo kadhaa tunaweza kujifunza kwao.

Mwl Fredrick Kapaya Page 21


Jambo la kwanza: Hawa wenye ukoma walipogundua kuwa wamekaa
pale lango kwa mda mrefu ndani yao waliaanza kufikiri kwa undani
zaidi.

2 Wafalme 7:4a

“Tukisema, Tutaingia mjini, mjini ni njaa, nasi tutakufa humo; nasi


tukikaa hapa, tutakufa vilevile”

Jambo la pili: Baada ya kufikiri au kujadiliana kwa undani zaidi,


walifanya maamuzi (Walichukua hatua)

2 Wafalme 7:4b

“Haya! Twendeni tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai


tutaishi; wakituua, tutakufa tu”

Jambo la Tatu: Hawakubadili kabisa mawazo yao walifuata kile


walichokiamua /mazingira ya huko walipokuwa wanakwenda
hayakubadili fikra zao (Watu hawa walikuwa na msimamo)

2 Wafalme 7:5

“Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha


Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe!
Hapamna mtu”

Watu wenye uwezo wa kufikiri zaidi au wanaotumia muda kufikiri zaidi


kabla ya kufanya maamuzi ni watu wanao weza kuleta mabadiliko
katika jamii.

Mwl Fredrick Kapaya Page 22


Mfano wa 2

Danieli 3:16-18

“Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu,


wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika
neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza
kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono
wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi
hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya
dhahabu uliyoisimamisha”

Shadraka, Meshaki na Abednego walijitoa kumtumikia Mungu wa


Mbingu/ katika maisha yao walifanya maamuzi ya kumtumikia Mungu,
kwa sababu hiyo walipoambiwa kuiabudu miungu ya mfalme
Nebukadreza hawakukubali. Hawakutaka kurudi nyuma au kubadili
maamuzi yao ila waliendelea kukaa na kufuata maamuzi yao.

Hawakuruhusu mazingira (Uwepo wa tanuru iwakayo moto) yabadili


misimamo au maamuzi yao, ila waliamini kuwa Yupo Mungu ambaye
anaweza kuwaokoa na hayo mazingira magumu.

Mfano wa 3

Marko 5:25-34

“Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi


na miwili, na kuteswa mengi kwa mikono ya matatibu wengi,

Mwl Fredrick Kapaya Page 23


amegharamiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali
hali yake ilizidi kuwa mbaya aliposikia habari za Yesu, alipita katika
mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake; maana alisema, Nikiyagusa
mavazi yake tu, nitapona”

Imani ya mwanamke mwenye kutokwa damu miaka kumi na miwili


ilimsaidia huyu mwanamke kufanya maamuzi yaliyosababisha apige
hatua pasipo kujari mazingira. Hakusitasita kwa alichokiamua.

Aina ya kumi na moja

 Watu ambao huwa na hamasa ya kupata matokeo mazuri kwa


wanachokifanya haijarishi mazingira ni magumu kiasi gani au
yanaonesha kutokupatikana au kuwezekana kwa hilo jambo ila
wao hutumia uwezo wao au huamini katika uwezo aliowapa
Mungu pasipo kukata tamaa mpaka wapate wanachokitaka.

Watu wa namna hii huwa si wepesi kusema neno “Nimeshindwa au


siwezi” Ila huwa na tabia ya kujalibu tena na tena. Lakini pia huwa
hawana tabia ya kuishi kwa kufuata historia ya kushindwa au
kushindikana kwa jambo fulani, ila wao uhakikisha wanabadili historia
yaani hufanya mambo yaliyoshindika ili yawezekane kisha watu
wengine wajue kuwa yanawezekana.

Ili ufanikiwe unahitaji watu sahihi kwenye maisha yako. ili ufanikiwe
zaidi unahitaji umakini katika kutengeneza marafiki wapya wenye
mitazamo mipya itakayokufungua fahamu zako ili uanze kuwaza
mawazo mapya ya kukufanikisha.

Mwl Fredrick Kapaya Page 24


Hizi ni baadhi ya aina za watu zipo nyingi ila nimejaribu kuelezea chache tu, Ili
ndani yako ujengeke ufahamu juu ya hili eneo.

Mungu wa mbinguni akubariki sana

Mwl Fredrick Kapaya

Contants: 0768226595

Aug 2019

Mwl Fredrick Kapaya Page 25

You might also like