Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

Bwana Yesu asifiwe mwaka huu wa 2021, kuliko alivyosifiwa mwaka jana wa 2020.

Heri ya mwaka
mpya.
Ujumbe nilionao kwako,toka madhabahuni pa Mungu kwa mwaka huu ni: Irudishe na Iweke imani
yako mahali inapostahili’! Au kwa muhtasari kwa kiingereza –
‘Reposition your faith to its right place’!
Hii ni kwa sababu,ulimwengu wote,tupo katika msimu mpya. Na mambo yanayotokea katika
mwanzo wa misimu mipya, huwa yana tabia ya kuyumbisha imani za watu.
Je, imani yako ipo mahali inapotakiwa kuwapo? Je, imani yako ikiyumba utajuaje? Na unairudishaje
imani iliyoyumba,na kuiweka mahali inapostahili kuwapo? Dalili za imani iliyoyumba ni zipi? Ngoja
nikupe mifano michache ya dalili hizo:
Dalili ya 1: ‘Kufikiri moyoni mwako ya kwamba, kwa kuwa jambo limekushinda wewe, na
limewashinda watumishi wa Mungu, basi, hata Mungu wao limemshinda!’
Ukiona umefikia mawazo ya namna hii, katika kupata utatuzi wa jambo linalokusumbua, ujue imani
yako haiko tena kwa Mungu, hata kama unaomba! Soma Marko 9:14 – 27. Huyu baba wa
mtoto,aliyekuwa na pepo bubu,alifikia mawazo kama haya!
Rudisha imani yako kwa Mungu,kwa kutubia kutokuamini kwako (Marko 9: 22 – 24); na anza tena
kutafakari,na kuamini mistari ya biblia,inayotujulisha kuwa, hakuna lisilowezekana kwa Mungu
(Luka 1:37, Yeremia 32:12,27, Mathayo 19:26).Na ya kwamba Mungu anajibu maombi (Waebrania
11:6).
Dalili ya 2: ‘Unapoanza kulalamika moyoni mwako,kana kwamba Mungu amekusahau, na unadhani
ndio maana hajibu maombi yako, na kutoyaondoa matatizo yako!’
Ukiwaza namna hii, ni dalili ya kuwa, imani yako imeondoka, mahali inapotakiwa kuwapo! Ndicho
kilichompata Habakuki. Soma Habakuki 2:1 – 4.
Habakuki alijikuta analalamika mbele za watu (Habakuki sura ya 1), na mbele za Mungu (Habakuki
2:1); kwa sababu alipoteza imani inayokuja na maono ya Mungu juu ya eneo lao. Na kwa kuyumba
kwa imani yake, alijikuta uwezo wake wa kuendelea ‘kumsubiri’ Mungu unapotea! Uvumilivu
unapotea!
Na ile Mungu kumwambia Habakuki,mwenye haki ataishi kwa imani yake (Habakuki 2:4),ina maana
alitaka ajue ya kwamba,kulalamika kwake ilikuwa ni ishara ya kuwa,imani yake haikuwa mahali
ilipotakiwa kuwapo.
Ikiwa unapitia hali ya imani yako kuyumba kama ya Habakuki, hata kama wewe ni mwombaji kama
Habakuki,rudisha imani yako mahali inapostahili, kwa kutafakari Ahadi ya Mungu inayokupa
“maono” ya Mungu, yaliyobeba jibu la mazingira mabaya yanayokuzunguka! Soma tena Habakuki
2:1 – 4. Na msome pia Ibrahimu katika Warumi 4:18 – 21 na Waebrania 6:11 – 18.
Dalili ya 3: ‘Unapojikuta unapoteza utulivu, na amani moyoni mwako, kwa sababu unapita mahali
pagumu kimaisha, au kiutumishi, au kikazi, au kibiashara, au kimahusiano, au kiuchumi, au kisiasa!’
Hali hii,iliwapata wanafunzi, wakiwa na Yesu ndani ya boti, huku bahari ikiwa imechafuka sana. Ni
dhahiri walipoteza utulivu,na amani mioyoni mwao. Yesu aliwauliza: “Imani yenu iko wapi?” (Luka
8:22 – 25).
Swali hilo lilionyesha ya kuwa, imani yao haikuwa mahali ilipotakiwa kuwapo! Ingawa walikuwa na
Yesu ndani ya boti, bado wali – “panic” – maana yake walikosa utulivu,na amani mioyoni –
wakidhani watazama!
Kumbuka: Unaweza ukawa na Yesu, lakini imani yako isiwe,mahali ambapo anaweza kuitumia
kukusaidia.
Imani yao waliiweka kwenye ‘uzoefu’ wao,katika kusafiri baharini. Na ‘uzoefu’ uliposhindwa
kuwasaidia, wakapoteza amani, na utulivu.
Ikiwa unapitia hali kama ya namna hii, ujue imani yako imepigwa dhoruba, na haipo mahali
inapotakiwa. Irudishe imani hiyo mahali pake,kwa kukua katika kumjua Yesu, na neno lake linasema
nini juu ya uwezo wake,juu ya mazingira mabaya unayopitia.
Ukisoma Luka 8:25 – utaona wanafunzi wakiulizana: “ni nani huyu basi hata anaamuru pepo na
maji, navyo vyamtii?” Ni dhahiri walimjua Yesu na uwezo wake katika maeneo mengine, lakini
hawakumjua Yesu na uwezo wake katika jambo gumu walilokuwa wanapitia wakati ule? Je, wewe
unamjua Yesu kwa kiwango gani, na uwezo wake kwa kiasi gani, juu ya eneo hilo ambalo unapita
mahali pagumu?
Dalili ya 4: ‘Unapojikuta unapoteza imani yako ya kuendelea na juhudi zako, za kufanya kile
ambacho huoni matunda ya juhudi zako, hata kama unajua, Mungu amekuamini na amekukabidhi
ukifanye!’
Soma Luka 13:6 – 8. Mtu huyu ni mfano wa mtu aliyekabidhiwa kazi na Mungu, lakini kwa miaka
mitatu mfululizo,kazi ile haikuzaa matunda yaliyotakiwa. Lakini,unaona mtu yule hakupoteza imani
yake,juu ya kuendelea na juhudi za kuifanya kazi ile. Ndipo akaomba aongezewe mwaka mwingine!
Je, umejikuta unakata tamaa, kwa kuwa tu, kazi uifanyayo haikuzalii matunda yanayotakiwa?
Usikate tamaa! Unapokata tamaa kuendelea kulifanya jambo, ambalo Mungu amekupa ulifanye, ujue
imani yako haiko mahali inapotakiwa kuwapo “kiutendaji” (Yakobo 2:17,20).
Rudisha imani yako mahali inapotakiwa kuwapo, kwa kutokuchoka kutenda,au kufanya kile
ambacho,Mungu amekupa ukifanye,kwa sababu utavuna kwa wakati wake (Wagalatia 6:9)!
Dalili ya 5: “Unapojikuta unaikubalia tabia mbaya uliyonayo, kuinyima imani nzuri uliyonayo,fursa
ya kumpa Mungu nafasi akutoe katika maisha uliyonayo, na kukuingiza kwenye msimu wako mpya
kimaisha, au kikazi, au kiutumishi, au kibiashara, au kisiasa, au kimahusiano, au kiuchumi!”
Habari ya Rahabu, yule kahaba, inatupa kujua ya kwamba, mtu anaweza akawa na tabia mbaya
isiyompendeza Mungu, na wakati huo huo akawa na imani nzuri inayompendeza Mungu! Soma
Waebrania 11:31.
Mazingira aliyoishi Rahabu,yalimpa urahisi wa kuona fursa ya kutumia tabia mbaya aliyokuwa nayo,
kuliko kuona fursa nyingi za kuitumia imani yake nzuri aliyokuwa nayo. Lakini moyoni mwake,
aliazimu kutokubali imani yake hiyo, iyumbishwe na tabia mbaya aliyokuwa nayo. Tena, wala
hakukubali imani yake, iyumbishwe na maneno ya waliomzunguka, waliokuwa wanamtuhumu,na
kumshambulia,juu ya tabia yake mbaya aliyokuwa nayo!
Fursa moja ilipotokea ya imani yake kutumika, hakusita kuitumia. Tabia mbaya aliyokuwa nayo,
haikumzuia kuitumia imani yake, kutumia fursa ya ‘kutoa sadaka’ ya kukaribisha ‘watumishi’ wa
Mungu! Mungu akaitumia imani ya Rahabu kumtoa kwenye ukahaba, na kumpa msimu mpya na
maisha mapya.
Je, una tabia ambayo si nzuri machoni pa Mungu, uliyoingia nayo mwaka huu,hata kama si
inayofanana na aliyokuwa nayo Rahabu? Na je inafanya imani uliyonayo kwa Yesu, iwe mahali
ambapo huwezi kuitumia ipasavyo katika msimu huu mpya?
Irudishe imani yako katika nafasi inayostahili kuwapo,ndani ya moyo wako, ili uweze kuitumia kwa
faida.Rahabu aliitunza imani yake, katikati ya tabia mbaya aliyokuwa nayo, kwa kuendelea
kutafakari shuhuda za Mungu wa Israeli, alizokuwa anazisikia. Na wewe fanya vivyo hivyo. Soma
Yoshua 2:1, 8 – 11.
Rahabu aliiweka imani yake mahali ambapo, alipopata fursa ya kumtolea Mungu sadaka, aliitoa bila
kusita, na akiwa na amani. Mungu akaitumia sadaka ile,kumtoa kwenye mazingira ya maisha mabaya
ya msimu wake uliokuwa umetangulia, na kumwingiza kwenye msimu mpya uliokuwa umeandaliwa
na Mungu kwa ajili yake. Soma Waebrania 11:31. Na wewe fanya vivyo hivyo!
Rahabu aliiweka imani yake mahali ambapo, ilikuwa rahisi kujiambatanisha na Mungu wa Israeli
kiagano, kwa njia ya maombi. Na Mungu akaonyesha uaminifu wake wa kushika agano lake, kwa
kujibu ombi la kiagano la Rahabu. Soma Yoshua 2:12 – 21 na Yoshua 6:17, 23. Na wewe fanya
vivyo hivyo.
Na ndani ya maombi hayo ya Rahabu,kulikuwa na toba yake.Na wewe usiache kuitubia tambia
mbaya uliyonayo.
Wewe uliyesoma ujumbe wa salamu hizi, nakuombea, ili kama imani yako haiko mahali pake kwa
ajili ya misukosuko ya msimu mpya, Mungu akujalie na akuongoze cha kufanya ili imani yako,irudi
mahali inapotakiwa kuwapo.
Heri ya Mwaka 2021.

You might also like