Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 15

KATIBA YA KIKUNDI CHA UJIRANI MWEMA TARAKWA

1
KATIBA YA KIKUNDI CHA UJIRANI MWEMA TARAKWA.
UTANGULIZI:                                                        
           
(UJIRANI MWEMA TARAKWA) - Ni kikundi cha hiari chenye lengo la kusaidiana katika shida na raha pia kufanya
shughuli mbalimbali za kijamii kwa ustawi wa wanachama wake. Kikundi hiki kimeanzishwa rasmi tarehe 02/08/2020
Kwa pamoja wanachama wanaahidi  kuilinda na kuitekeleza katiba hii.
Pamoja na Katiba hii, Kikundi hiki kitaendeshwa kwa mujibu wa kanuni mbalimbali ambazo zitawekwa na wanachama.

SURA YA KWANZA

1.        JINA LA KIKUNDI,  ANUANI  YA KIKUNDI  NA TAFSIRI


1.1.  Jina la Kikundi
Kikundi hiki kitajulikana kama UJIRANI MWEMA TARAKWA.
Anuani ya kikundi hiki itakuwa ni sanduku la barua ................. S.L.P Arusha.
Anuani ya makazi ambayo ni Makao Makuu ya Kikundi hiki yatakuwa ni KATA- TARAKWA. Mtaa wa SAITABAO
Wilaya-ARUMERU.

1.2  Tafsiri
Kwa mujibu wa Katiba hii, maneno yafuatayo yatakuwa na maana ifuatayo;
i) Mwanachama: Mtu yeyote atakayekidhi vigezo vya kuwa mwanachama
ii) Mwanachama hai : Mwanachama anayetimiza masharti ya kuwa mwanachama kwa mujibu wa katiba hii.
iii) Kanuni: Muongozo wa jinsi ya uendendeshaji wa kikundi
iv) Kikundi: Taasisi hii inayoanzishwa kwa mujibu wa katiba ambayo inatambulika kuwa ni UJIRANI MWEMA
TARAKWA.
v) Matatizo:Ina maana ya misiba, na ugonjwa wa muda mrefu kwa mujibu wa katiba hii.
vi) Nidhamu: Kitendo chochote kile kinacho kinzana na Katiba hii pamoja na kanuni zake.

SURA YA PILI

2.1   Aina ya Kikundi
UJIRANI MWEMA TARAKWA ni Kikundi cha Kijamii cha kusaidiana katika shida na raha pamoja na maendeleo ya
Kiuchumi na elimu.
  
2.2    Madhumuni na Malengo ya Kikundi.
2
Kikundi hiki kipo kwa kutimiza au kutekeleza yafuatayo:-
i) Kuanzisha mfuko wa kikundi wa kuweka na kukopa.
ii) Kushirikiana na kusaidiana nyakati za shida na raha kama misiba, magonjwa ya muda mrefu na sherehe.
iii) Wanakikundi kuwezeshana katika kuimarisha hali zao za Kipato ili kuweza kuwa    na maisha yaliyo bora zaidi.
iv) Kuanzisha miradi mbalimbali ya kukuza mfuko wa kikundi pale kikundi kitakapokuwa kikubwa na fedha za kutosha.

2.3.      Matarajio ya Kikundi
            Ili kuweza kufikia matarajio ya Kikundi kitafanya yafuatayo:-
i) Kuweka utaratibu mahsusi MICHANGO YA FEDHA kwa wanakikundi ikiwa ndio msingi wa chanzo cha mapato.
ii) Kubuni Miradi mbalimbali itakayosimamiwa na kuendeshwa Wanakikundi wenyewe au hata kwa msaada wa kiufundi
kutoka nje ya kikundi.
iii) Kuimarisha ushirikiano na wanakikundi wenye changamoto mbalimbali kama vile; Maradhi, Misiba,Harusi, Elimu na
Sherehe, Majanga ya Kiasili na matukio mengine yanayolingana na hayo.
iv) Taratibu hizo zitakuwa ni sehemu ya Katiba hii.

SURA YA TATU

3.0     UANACHAMA. 
Ni mtu yeyote yule ambaye ametimiza taratibu zote za kujiunga na Kikundi au Umoja huu kwa mujibu wa Katiba na
Kanuni zake ikiwa ni pamoja na kulipa ada na Michango stahiki.

3.2.1           Sifa za kuwa Mwanachama
i) Awe na Umri usiopungua miaka 18.
ii) Awe mwenye nia na awe tayari kuwa mwanachama
iii) Awe tayari kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kikundi
iv) Awe na akili timamu.
v) Awe tayari kutii na kufuata masharti ambayo yameainishwa kwenye Katiba na Kanuni za kikundi
vi) Awe tayari kulipa kiingilio, adhabu pale ambapo ataenda kinyume na taratibu, michango itakayo ainishwa
kwenye kanuni ya ada, michango na adhabu pamoja na ada ya uanachama ya kila mwezi
vii) Awe anaishi kata ya Tarakwa au maeneo ya karibu ya Tarakwa pamoja na yeyote ambaye ana nia ya kuwa
mwanachama na ananidhamu ya kuwa mwanachama ila haishi maeneo ya Tarakwa.

3.3.1      Haki za Mwanachama
3
i) Kutoa maoni yake kwa uhuru
ii) Kuchagua au kuchaguliwa katika nafasi yoyote ile ya Uongozi katika Kikundi au Umoja huu.
iii) Kuwasiliana na Uongozi/Viongozi ikiwa ni pamoja na kupokea na kutoa taarifa zinazohusu Kikundi au Umoja
huu.
iv) Kuhudhuria na/au kuwakilisha katika jambo lolote lile linalohusu Kikundi au Umoja huu kwa kufuata taratibu na
kanuni zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba hii.
v) Kupewa nafasi ya kujieleza na kujitetea pindi anapokabiliwa na tuhuma zozote zile dhidi yake katika umoja
huu.
vi) Kutumia Mali za Kikundi kwa kufuata utaratibu na Kanuni za Umoja huu.
vii) Ana haki ya kutoa hoja yake na kusikilizwa wakati wa kushiriki majadiliano kwenye vikao.
viii) Kufahamu mapato na matumizi ya Kikundi kwa kutumia na kuzingatia Kanuni.
ix) Kusaidiwa linapomtokea tatizo.
x) Kusaidiwa kimawazo au kiuchumi kulingana na hali itakavyo ruhusu.

3.3.2           Wajibu wa Mwanachama.
i) Kuilinda na kuitetea katiba hii wakati wote.
ii) Kutekeleza majukumu atakayopewa na viongozi au wanachama wenzake.
iii) Kushiriki katika shughuli zote za kikundi kwa mujibu wa katiba hii ikiwa ni pamoja na vikao halali vya Umoja
huu.
iv) Kulipa ada pamoja na michango mbalimbali itakayo pitishwa na Kikundi au Umoja  huu.
v) Kueneza sifa nzuri za Umoja huu.
vi) Kutii na kufuata maagizo na maazimio ya Mkutano/Mikutano halali ya Umoja huu, hata ikiwa hatakuwepo
kwenye Mkutano huo, au hakushiriki katika kupitisha azimio hilo.
vii) Kuwa na nidhamu wakati wa Mikutano ama shughuli nyingine zozote za Kikundi.
viii) Kutunza siri zote za Umoja huu

3.4.1             Kujiunga na Kikundi.
a) Kujaza Fomu ya maombi itakayotolewa kwa ada itakayokuwa imepangwa.Maombi haya ni lazima yapitiwe na
kukubaliwa na Uongozi.
b) Baada ya kukubaliwa Mwombaji atatakiwa kulipa Ada ya kiingilio cha kiasi kitakachokuwa kimepangwa na
Mkutano Mkuu.
c) Pamoja na Ada ya kiingilio Mwanachama mpya atalazimika kulipa Michango ambayo itahainishwa kwenye
kanuni.

       3.4.2    Michango

            (a)     Ada ya Uanachama

4
 Kila Mwanachama atalazimika kulipa ada ya Uanachama kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 3.4.1.(b) na (c) ya Katiba
hii.

ILI MRADI IELEWEKE KWAMBA:-


Mwanachama ambaye alikuwa na taarifa juu ya uanzishwaji wa kikundi na hakujiunga wakati huo, endapo atataka
kujiunga baadae, atatakiwa kulipa kiingilio na michango yote tangu kikundi kilipoanza mpaka kilipofikia, ndipo ataweza
kukubaliwa kuwa mwanachama. 

Kiasi atakacho lipa mwanachama mpya ambaye alikuwa hana taarifa kabisa ya uanzilishi wa kikundi hiki, kitahainishwa
kwenye kanuni za ada ana michango.   
   
           
            (b)    Michango Mingine.
Kila Mwanachama atawajibika kuwasilisha mchango mwingine wowote ule   utakaoamuliwa kuchangishwa kwa azma
ya kukidhi miongoni mwa matarajio ya Umoja huu kama yalivyoainishwa katika ibara 2.3 ya Katiba hii na kima
kitakachokuwa kimeamuliwa.

(c ) Michango ya Misiba kwa Ajili ya Kumfariji Mwanakikundi aliyefiwa au aliye fariki


Kiasi cha kuchangia michango hii kitatokana na kanuni inayohusu michango ya misiba.

( d) Adhabu
Mwanachama akichelewa kikao baada ya mwenyekiti kufungua kikao atapaswa kulipa adhabu, ambayo itaainishwa
kwenye kanuni ya ada, michango na adhabu.
Atalipa adhabu hiyo kwa muda wa vikao vitatu mfululizo kama atashindwa kufika kwenye vikao ivyo mfululizo, baada
yah apo kiasi kikubwa zaidi kitatozwa dhidi yake, kiasi hicho kitahainishwa kwenye kanuni ya ada, michango na
adhabu.

(e ) Ugonjwa
Michango kwa ajili ya ugonjwa itachangwa kutokana na taratibu zitakazo hainishwa kwenye kanuni ya ada,michango
na adhabu.

(f ) Sherehe
Aina ya sherehe inayopaswa kuchangiwa, kiwango cha kuchangia, wanaopaswa kuchangiwa yatahainishwa kwenye
kanuni ya ada, michango na adhabu.

3.4.3     Kukoma Uanachama.

Mwanachama anaweza kukoma kuwa mwanachama katika mazingira yafuatayo:-


i) Kujitoa kwa hiari yake kwa kutoa taarifa ya maandishi kwa mwenyekiti miezi mitatu kabla na kama ana mali za Kikundi
atalazimika kurudisha ndipo atakubaliwa kutoka,
ii) Mwanachama atakaye ondoka kwa amani atapewa kiasi cha michango yake kama itavyo hainishwa kwenye kanuni ya
kukoma uanachama.
iii) Mwanachama ambaye atakuwa na utovu wa nidhamu ataondolewa kutokana na maamuzi ya mkutano mkuu, kufuata
mapendekezo ya kamati ya nidhamu pamoja na kanuni za nidhamu.

5
iv) Kushindwa kulipia ada ya kila mwezi kwa miezi mitatu mfululizo bila sababu yoyote ya msingi.
v) Kupuuza taarifa zinazotaka ushiriki wake katika shughuli za wanachama.
vi) Kupoteza sifa kutokana na mambo ya kinidhamu
vii) Ikiwa mwanachama atafariki.
viii) Kushidwa kufuata Katiba na Kanuni za Kikundi.

ILI MRADI IELEWEKE KUWA


Mtu aliyeacha au kufukuzwa Uanachama(uanakikundi) anaweza kuomba kujiunga tena kwa mujibu wa masharti ya
uanakikundi baadae na atatakiwa kuwa na wadhamini wasiopungua WATATU ndani ya Kikundi ambao ni hai.
                             

SURA YA NNE.

  4.0  UONGOZI.

4.1   Kikundi hiki kitakuwa na viongozi wafuatao:-


(i)     Mwenyekiti
(ii)   Makamu Mwenyekiti
(iii)  Katibu
(iv)  Katibu Msaidizi
(v)    Mweka Hazina

4.2 Muda wa kikomo cha uongozi kwa viongozi wote itakuwa ni miaka miwili, baada ya hapo viongozi wapya
watachaguliwa katika kikao cha halmashauri kuu. Kiongozi wa zamani anaweza kuchaguliwa tena upya kwa kipindi
kindine, ila hatapaswa kuchaguliwa kwa zaidi ya awamu mbili.
4.3 Endapo kiongozo ataonesha utovu wa nidhamu kama matumizi amabaya ya fedha za chama, ugombanishi, kuwa
chanzo cha migogoro ambayo itahatarisha uhai wa chama au kuivunja katiba hii kwa makusudi au kwa kutokukusudia,
Kamati ya nidhamu itashughulika na swala hilo ikiwa pamoja na kumuita kiongozi huyo na kumuhoji, endapo
itadhibitika maswala aliyo yafanya kiongozi huyo ni kweli basi mapendekezo ya kumfukuza yatatolewa na kamati ya
nidhamu kwa wanachama. Wanachama watatoa maamuzi ya adhabu hiyo.

4.4    Kikundi kitakuwa na kamati zifuatazo.


4.4.1 Kamati ya Utendaji.
 Itakayoundwa na wajumbe wafuatao:-
1.       Mwenyekiti

6
2.       Makamu Mwenyekiti
3.       Katibu
4.       Katibu Msaidizi
5.       Mweka Hazina
6.       Wajumbe wawili watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu.

4.4.2  Kazi  za Kamati ya Utendaji.


i) Kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya vikao halali vya Kikundi au Umoja huu.
ii) Kukutana wakati wa dharura na kujadili suala lilipo mbele yao na kulitolea uamuzi kwa niaba ya wanachama
wote.
iii) Kuandaa agenda za mkutano mkuu.
iv) Kuandaa taarifa mbalimbali kwenye mkutano mkuu.
v) Kasimamia shughuli zote za kimaendeleo na ukuaji wa kikundi
vi) Kujadili na kuyafanyia kazi mambo mbali mbali yanayohusu wanachama au Kikundi kwa ujumla wake.

4.4.3  Kamati ya Fedha na Mipango


 Kamati hii itaundwa na wajumbe watatu watakao teuliwa na mkutano mkuu wa kikundi. Wajumbe wa kamati hii
watachagua kutoka mingoni mwao na kumpata Mwenyekiti na Katibu siku ya kikao cha kwanza cha kamati hii.

4.4.4   Kazi za Kamati ya Fedha na Mipango


  (i)      Itakayokuwa na kazi ya kubuni, kushauri na kuelekeza juu ya miradi yote ya kimaendeleo ya kikundi hiki.
  (ii)     Itakuwa na kazi ya kusimamia utekelezaji wa miradi na mambo yote ya fedha ya kikundi
  (iii)    Kudhibiti na kusimamia mapato na matumizi ya fedha na mali za kikundi kwa kufuata Kanuni zilizowekwa.
( iv) Kutoa taarifa za fedha

4.4.5  Kamati ya Sheria na Nidhamu


Kamati hii itakuwa na jukumu la kusimamia nidhamu na kushughulikia migogoro ya wanachama. Kamati hii itaundwa
na wajumbe watatu watakaoteuliwa na wana kikundi. Mwenyekiti wake kama itawezekana awe ni mtu mwenye
elimu  ama ufahamu wa sheria. Kama hatakuwepo mtu wa kukidhi kigezo hicho, mtu mwingine yeyote atakayeteuliwa
na wanakamati wenyewe ndio atakuwa  Mwenyekiti.

SURA YA TANO.

5.0    KAZI ZA VIONGOZI
5.1   Kazi za Mwenyekiti.
i) Atakuwa msemaji mkuu wa kikundi.

7
ii) Ataitisha mikutano yote ya kikundi.
iii) Ataitisha mkutano wa dharura pale itakapokuwa inahitajika.
iv) Ataongoza mikutano yote ya wanachama wote.
v) Atakuwa ndio Kiongozi Mkuu wa Kikundi au Umoja huu.
vi) Atakuwa mtuia sahihi kwenye akaunti ya benki

5.2      Kazi za Makamu Mwenyekiti.


i) Atafanya kazi zote za Mwenyekiti pale ambapo Mwenyekiti hatakuwepo.
ii) Atafanyakazi zote atakazoelekezwa na Mwenyekiti.
iii) Atakuwa ndio msaidizi mkuu wa Mwenyekiti.

5.3               Kazi za Katibu.
i) Atakuwa Mtendaji Mkuu wa kikundi.
ii) Kuandaa ajenda za vikao vyote.
iii) Ataandika miniti za vikao vyote vya kikundi.
iv) Atakuwa anatoa taarifa ya maendeleo ya kikundi mara moja kwa mwezi
v) Kwa kushirikiana na Mwenyekiti atakuwa anaandaa yatokanayo na vikao vilivyopita
vi) Atakuwa mtunza kumbukumbu na nyaraka mbalimbali za kikundi.
vii) Atakuwa katibu wa kamati ya utendaji.
viii) Atakuwa mjumbe wa kamati ya Fedha na Mipango.
ix) Atawajulisha wanachama taarifa zote za vikao.
x) Atafanya kazi zote kadri atakavyoelekezwa na Mwenyekiti.

5.4               Kazi za Katibu Msaidizi .


i) Atamsaidia Katibu kuendesha shughuli za kila siku za kikundi.
ii) Atakaimu nafasi ya Katibu pale ambapo Katibu atakuwa hayupo.
iii) Atakuwa Mtunza Hazina msaidizi

5.5               Kazi za Mweka Hazina.


i) Atakuwa mtunza fedha za kikundi.
ii) Atakusanya / atapokea fedha zote za kikundi na  kutoa stakabadhi.
iii) Atakuwa mtunza nyaraka zote zinazohusiana na masuala ya fedha.
iv) Atatoa taarifa ya mapato na matumizi ya kikundi kila mwezi.
v) Atafanya  malipo yote halali ya kikundi.
vi) Atajibu hoja zote zinazo husiana na masuala ya fedha.
vii) Atakuwa mjumbe wa kamati ya utendaji pamoja na kamati ya Fedha na Mipango.

8
SURA YA SITA.

6.0      Vikao

Kikundi hiki kitaongozwa kwa kufanya vikao mbali mbali kama vifuatavyo.
6.1      Mkutano Mkuu
Kutakuwa na mkutano mkuu utakaofanyika mara  moja kwa mwaka. Ili mkutano huu  ufanyike idadi ya wajumbe
watakohudhuria kikao hicho ni lazima iwe siyo  chini ya  mbili ya tatu (2/3) au (67%)  ya  wajumbe wote walio hai

6.2      Kazi za Mkutano Mkuu.


i) Kuchagua viongozi wa kikundi.
ii) Kupokea taarifa za mapato na matumizi kwa mwaka mzima.
iii) Kupokea taarifa ya kazi zote za mwaka.
iv) Kufanya mabadiliko au marekebisho kwenye vifungu mbalimbali vya katiba.
v) Kuidhinisha mipango ya kimaendeleo ya kikundi
vi) Kufanya Uchaguzi wa viongozi ikiwa muda umewadia.

6.3      Mkutano wa Kawaida wa Wanachama Wote.


Mkutano huu utafanyika mara moja kwa mwezi, siku na tarehe zitajulishwa na katibu  wiki moja kabla.
        Ili mkutano huu ufanyike ni lazima idadi ya wajumbe ifikie asililimia 50% ya wajumbe wote walio hai. Endapo kikao
kitasitishwa mara mbili kwa kukosa idadi, kikao cha tatu kitaendelea hata kama idadi  itakuwa haijafikiwa na maamuzi
ya kikao yatakuwa maamuzi halali ya kikundi.

6.4      Kazi za Mkutano wa Kawaida wa Wanachama Wote.


i) Kupokea taarifa ya utendaji na uendeshaji kikundi kwa mwezi husika.
ii) Kukusanya michango ya kila mwezi toka kwa wanachama.
iii) Kupata taarifa za utekelezaji wa maagizo na malengo yoyote ya kikundi.
iv) Kupokea taarifa ya fedha ya mwezi husika.
v) Kupitisha maamuzi ya kamati mbalimbali za kikundi.
vi) Kujadili na kulitolea uamuzi suala lolote litakalokuwa limejitokeza.
vii) Kupanga tarehe na siku ya kufanyia mkutano wa mwezi unaofuata.

6.5      Kikao cha Kamati ya Utendaji.


Kutakuwa na vikao vya mara kwa mara vya kamati ya utendaji kadri itakavyohitajika.
Kazi za vikao hivi ni kama ilivyoonyeshwa kwenye kifungu cha 4.2.2  cha katiba. Vikao hivi vitaweza kuendeshwa hata kwa
mitandao kama WhatsApp, Skype n.k, ili kurahisishwa wajumbe kuweza kushiriki kwa urahisi.

9
6.6      Kikao cha kamati ya Fedha na Mipango.
Kamati hii itakua na vikao kadri itakavyohitajika kufanya hivyo.

6.7      Kazi za vikao vya kamati ya Fedha na Mipango.


i) Kuandaa Mpango wa Mkakati wa Kikundi
ii) Kubuni miradi kwa ajili ya kuongeza mapato ndani ya Kikundi.
iii) Kusimamia miradi mbalimbali ya kikundi na kuandaa taarifa za maendeleo.
iv) Kujadili maombi yote ya mikopo na kutoa mapendekezo yake kwa Mwenyekiti.
v) Kuandaa taarifa za ukusanyaji madeni yote toka kwa wanachama.

SURA YA SABA

7.0      Taarifa za Uchaguzi
Kutakuwa na chaguzi mbali mbali za viongozi wa kikundi, ambazo zitafanyika kila baada ya
Miaka miwili (2) katika Mkutano Mkuu wa Kikundi wa mwaka. Kama ifuatavyo:-

7.1      Mwenyekiti na Makamu Mwenyeki wa kikundi.

Kutoka miongoni wa wajumbe wa kikundi yatapendekezwa majina matatu na kupigiwa kura kwa pamoja,  ambapo
Mwenyekiti  na makamu wake watapatikana kutokana na wingi wa kura utakao patikana. Mwenyekiti atachaguliwa
endapo atapata kura zaidi ya asilimia hamsini (50%). Atakae fuatia kwa kura nyingi ndio atakuwa Mwenyekiti Msaidizi.

7.2      Katibu  wa Kikundi

 Kutoka miongoni mwa wajumbe wa kikundi yatapendekezwa majina matatu na kupigiwa kura kwa pamoja. Katibu
atapatikana kwa kupata kura zaidi ya asilimia hamsini (50%) ya kura zote. Atakayefuatia kwa kura nyingi ndio atakuwa
Mwenyekiti Msaidizi.

7.3      Mweka Hazina wa kikundi

Kutoka miongoni mwa wajumbe wa kikundi yatapendekezwa majina matatu na kupigiwa kura kwa pamoja. Mweka
hazina atapatikana kwa kupata kura zaidi ya asilimia hamsini (50%) ya kura zote.

10
SURA YA NANE

8.0      ADA

8.1     Kutakuwa na michango na ada  mbali mbali ambazo zitaainishwa kwenye kanuni za kikundi . Michango na ada hizo ni
kama ifuatavyo:
i) Kiingilio kwa wanachama
ii) Ada ya kila mwezi kwa kila mwanachama,
iii) Misiba,
iv) Sherehe na
v) Magonjwa

SURA YA TISA

9.0      Utunzaji wa Fedha Benki


Kikundi kitatunza fedha zake kwenye benki itakayopitishwa na Mkutano Mkuu.
Fedha zitatolewa kwenye akaunti kwa mujibu wa taratibu zilizo wekwa kwenye kanuni za fedha za kikundi.

SURA YA KUMI

10.0            Utatuzi wa Migogoro
Ufuatao ni utaratibu wa kikundi kutatua migogoro itakayo jitokeza ndani ya  kikundi:  
Migogoro yote ya kikundi itatatuliwa Kamati ya Sheria na Nidhamu. Kama Mgogoro huo utashindikana
kutatuliwa  na Kamati ya Sheria na Nidhamu mgorogoro huu utapelekwa
i) Kamati ya utendaji
ii) Na endapo mwanachama/ wanachama  watakataa kufuata makubaliano ya utatuzi wa
shauri, basi watakuwa wamejifukuzisha uwanachama wao wenyewe /mwenyewe.

SURA YA KUMI  NA MOJA


11.0            Kubadli Katiba.
Mabadiliko yeyote ya katiba yatafanyika baada ya kupitishwa na mkutano mkuu wa kikundi wa mwaka
ambao unafanyika mara moja kwa mwaka. Mabadiliko yatapitishwa kwa kupigiwa kura ya wazi na zaidi ya
asilimia 67% ya wanachama wote waliohai. Katiba itakuwa inafanyiwa marekebisho na kupitishwa upya, pale
ambapo itaonekana kuna haja ya kufanya hivyo.
11
SURA YA KUMI NA MBILI
12.0            Kuvunjika kwa Kikundi.

i) Kikundi kitakuwa kimevunjika endapo asilimia 99% ya wanachama hai watapiga kura ya
ndio ya kuvunja kikundi katika mkutano mkuu wa kikundi.
ii) Au endapo kwa mujibu wa sheria ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
iii) Endapo kikundi kitavunjika kila mwanachama atakuwa na haki sawa ya kurudishiwa
michango yake kulingana na hali ya fedha itakavyokua.  Mali yote iliyopatikana itagawanywa sawa kwa kila
mwanachama.

SURA YA KUMI NA TATU


13.0            Hitimisho: 
Katiba hii imesomwa, kujadiliwa na kupitisha na wanachama wote. Na kuweka sahihi kwa niaba yao na:

Mwenyekiti wa kikundi                                                 Katibu wa Kikundi

Jina      ____________________ _____                Jina    _____________________________

Sahihi..................................................               Sahihi …………………….……...............
Tarehe …………………………............                Tarehe ………………………..................

MAJINA YA WANACHAMA WAANZILISHI          SAHIHI YA MWANACHAMA                   


1.       ................................................................................................ -------------------------------
2.  ................................................................................................. ------------------------------
3. .................................................................................................. -------------------------------            
12
4.       ........................................................  ------------------------------
5.       ........................................................ -------------------------------
6.       ........................................................  ------------------------------
7.       ........................................................ -------------------------------
8.       ......................................................... -------------------------------                            
09.   .........................................................  ------------------------------
10.   ......................................................... -------------------------------
11.   ......................................................... -------------------------------
12.   ......................................................... -------------------------------
13.   ......................................................... --------------------------------
14.   ........................................................... --------------------------------
15.   ...........................................................  --------------------------------  
16.   ........................................................... -------------------------------
17.   ........................................................... ---------------------------------
18.   ........................................................... --------------------------------

19. .......................................................... --------------------------------

20. .......................................................... --------------------------------

21. ........................................................... --------------------------------

22. ........................................................... --------------------------------

23. ........................................................... --------------------------------

24. ........................................................... -----------------------------------

25. ........................................................... -----------------------------------

26. ........................................................... -----------------------------------

27. ........................................................... -----------------------------------

28. .......................................................... ------------------------------------


13
29. .......................................................... -------------------------------------

30. ........................................................... -------------------------------------

31.............................................................. .............................................

32.............................................................. ............................................

33.......................................................... ............................................

34........................................................... ............................................

35............................................................. .............................................

36............................................................ ............................................

37................................................................ .............................................

38............................................................ .............................................

39.............................................................. .............................................

40................................................................ .............................................

41.................................................................. ..............................................

42................................................................... ...............................................

43.................................................................... ...............................................

44................................................................... ...............................................

45................................................................... ................................................

46................................................................... ................................................

47................................................................... ................................................

48.................................................................... ................................................

49......................................................................... ................................................

14
50....................................................................... ................................................

15

You might also like