20202508371427tangazo La Kazi Mkurabita PDF

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/ K/268 25 Agosti, 2020

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Kwa niaba ya Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za


Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi
wa Umma inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa
kujaza nafasi moja (01) kama ilivyoainishwa hapa chini.

1. MKURUGENZI WA URASIMISHAJI WA RASILIMALI NA BIASHARA – (NAFASI


1)
1.1 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kuandaa na kufanya Mapitio ya Miongozo ya urasimishaji wa rasilimali na


biashara kwa ajili ya kutekeleza shughuli za urasimishaji Tanzania.
ii. Kuandaa na kufanya mapitio ya vigezo vinavyotumika kuchagua maeneo
ya utekelezaji wa urasimishaji wa rasilimali na biashara kila mwaka kwa
Tanzania.
iii. Kusimamia utekelezaji wa urasimishaji wa biashara kwa Mfumo wa
kuanzisha Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara katika
Malmalaka za Serikali za Mitaa za Tanzania.
iv. Kusimamia utekelezaji wa urasimishaji rasilimali ardhi Mijini na Vijijini
Tanzania.

1
v. Kubuni, Kuandaa na Kutekeleza Programu za kuwajengea uwezo
wananchi waliorasimisha rasilimali ardhi na biashara zao ili kuzitumia katika
kupata mitaji kutoka Taasisi za fedha kwa ajili ya shughuli za kiuchumi
vi. Kuandaa na kutekeleza Mpango na Bajeti ya kila mwaka kwa ajili ya
utekelezaji wa shughuli za urasimishaji wa rasilimali na biashara Tanzania.
vii. Kubainisha na kutoa ushauri wa utatuzi wa changamoto ambazo
zinabainika wakati wa utekelezaji wa urasimishaji wa rasilimali ardhi na
biashara Tanzania;
viii. Kushirikiana na Mtaalam wa Utafiti, Ufuatiliaji na Tathmini kufanya Utafiti,
Ufuatiliaji na Tathimini ya utekelezaji wa shughuli za urasimishaji wa
rasilimali na biashara Tanzania. Aidha, Mkurugenzi wa Urasimishaji, anao
wajibu wa kufanya tafsiri ya matokeo ya utafiti, fuatiliaji na tathmini na
kuandaa mpango kazi wa utekelzaji wa mapendekezo yanayotolewa;
ix. Kushirikiana na Mtaalamu wa Mawasiliano kwa Umma katika kuhamasisha
na kujenga hamasa kwa wamiliki wa rasilimali na biashara ili waweze
kurasimisha na kuzitumia rasilimali ardhi na biashara zao kwa shughuli za
kiuchumi;
x. Kusimamia na kuratibu uaandaji wa taarifa ya utekelezaji wa urasimishaji
wa rasilimali na biashara katika vipindi vya robo mwaka, nusu mwaka na
mwaka Tanzania;
xi. Kubuni na kusimamia utekelezaji wa mambo mbalimbali yanayolenga
kuboresha mchango wa ajenda ya urasimishaji katika kukuza uchumi wa
nchi na kupunguza umaskini wa kipato kwa mtu mmoja mmoja;
xii. Kubuni na kusimamia utekelezaji wa mambo mbalimbali yanayolenga
kuchochea uendelevu wa matokeo ya urasimishaji wa rasilimali na biashara
nchini.
xiii. Kazi zingine ambazo atapangiwa na Mratibu wa Mpango;

1.2 SIFA ZA MWOMBAJI


i. Awe na Elimu ya kiwango cha shahada ya Uzamili katika moja ya maeneo
yafuatayo:- Uchumi, Uongozi wa Biashara, Ujasiriamali na Usimamizi wa
Ardhi.

2
ii. Awe na Uzoefu usiopungua miaka mitano (5) katika kubuni, kuandaa na
kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ajili ya kukuza uchumi na kuondoa
umaskini kwa wananchi wanyonge wa Tanzania.
iii. Awe na uzalendo na uadilifu usio na mashaka na awe tayari kutekeleza
majukumu yake bila usimamizi na mwenye kujituma mwenyewe na awe na
uwezo wa kuongoza na kusimamia wengine.
iv. Awe na uwezo wa kuwasiliana katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza
v. Awe na ujuzi wa komputa kutumia “Microsoft Word, Microsoft Excel na Power
point”
vi. Awe na umri usiozidi miaka 55.

1.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara za MKURABITA.

1.4 AINA YA AJIRA

Mkataba ambao unaweza kurejewa kutegemea na utendaji wa kazi utakaoneshwa


wakati wa utekelezaji.

1.5 KITUO CHA KAZI

Kituo cha kazi ni Dodoma ingawaje utekelezaji wa urasimishaji wa Rasilimali na


Biashara unafanyika katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za Tanzania Bara na
Zanzibar.

MASHARTI YA JUMLA.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 55
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao ni Watumishi wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi
kwa Waajiri wao.
iv. Waombaji waambatishe kupitia mfumo wa maombi ya kazi, maelezo binafsi
yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu zinazopatikana
pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
3
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya kidato cha nne
na sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali
kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE NA/AU NECTA).
viii. Waombaji wa nafasi za Ajira waliostaafishwa/kuachishwa kazi katika Utumishi wa
Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
x. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 08 Septemba, 2020
xi. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.
xii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo;
http://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia
sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

Imetolewa na:

KATIBU
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

You might also like