BARAZA LA WATU WANAISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA
TANGAZO LA UCHAGUZI WA KONGA NGAZI YA WILAYA
Balaza la watu wanaoishi na VVU Tanzania NACOPHA kwa kushirikiana na Ofisi ya maendeleo ya Jamii Kitengo cha Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, inapenda kuwatangazia watu wote wanaoishi na virusi vya UKIMWI kuwa tunatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wa Konga ngazi ya Halmashauri, hivyo kwa yeyote mwenye nia ya kugombea nafasi yoyote anaombwa kufika ofisi ya Konga au Ofisi ya Mratibu wa UKIMWI (CHAC) Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro ili aweze kuchukua fomu ya kugombea na baada ya kuijaza atapaswa kuirudisha kwa muda atakao ambiwa ili kuruhuru taratibu nyingine za uchaguzi kufanyika. Nawatakia uchaguzi mwema