GodianNewton KaziYako

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 2

Do you want to log in to or join Facebook?

Join

or

Log In

Gordian Newton Friends Who Like Christopher & Diana Mwakasege(Mana Ministry)

15 August at 05:22 ·

"ACHA KAZI ZAKO ZIKUTAMBULISHE"


Yohana 14:12 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye
atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya,kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
Ukisoma hili neno utaona mambo mawili jambo la Kwanza ni Yesu anataka wanaomwamini waamini kazi
zake ...(HUDUMA YAKE)...
Watu wanatamani kuona kazi zako...siyo maneno yako ..siyo cheo chako Bali KAZI ZAKO. Yesu
alipojitambulisha kuwa yeye ni mwana Wa Mungu hakuna aliyemwelewa lakin wengi walimwamini kwa
kazi alizozifanya ..ishara za uponyaji ndizo zilizomtambulisha...Hata alipokufa wakakiri HAKIKA HUYU
ALIKUWA NI MWANA WA MUNGU.....
Mathayo 27:54 Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la
nchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.
Kitu gani umekifanya kinachoweza kukutambulisha wewe ni nani?alama gani umeiweka
inayokutambulisha?...
Nakumbuka nikiwa sekondari academic master alituambia ili uweze kufahamika shuleni lazima uwe na
sifa unique... Kama ni msafi uwe msafi saaaana watu wakiwa wanakutafuta waseme humjui yule kaka
msafi?..au uwe mchafu saaanaaaa waseme hulijui lile likaka lichafuuu jambo hii si nzuri
kwetu...akasema uwe na akilii saaanaaaa waseme hujui hule jamaaa mwenye akili saaanaa?au uwe
mjinga saaana waseme hujui yule anayekuwaga Wa mwishoo hii nayo siyo nzuri kwetu japo ni
utambulisho...uwe mkimyaa saaanaa au mcheshi saanaaaa...sijui wewe ulikuwaje shuleni ulitambulikaje?
..HAKIKISHA UNA SIFA NJEMA ...KAZI ZAKO NJEMA
Nachotaka kusema hakikisha popote ulipo acha alama itakayokutambulisha...usifanye kwa mazoea
..kama ni kazi ya Mungu Fanya kwa bidii iache alama..kwenye ndoa yako..kwenye ofisi yako...kwenye
huduma yako...kila mahali....
Usilazimishe utambulisho wako wakati hakuna kazi inayokutambulisha...Adui na watesi wako washinde
kwa kazi uzifanyazo siyo kwa maneno yako mengi..BALI WASHINDE KWA KAZI..
TAFAKARI NI KIPI KINACHOKUTAMBULISHA? WHO ARE YOU?
Wanadamu wanaweza kukuua wewe lakin hawawezi kuziua kazi zakoo ulizozifanya....wanaweza
kusahau Maneno yako hawaweza kusahau matendo yako
Nawatakia siku njema na baraka za Bwana ziwe juu yenu
By Gordian Newton
Do you want to log in to or join Facebook?

Join

or

Log In

Like Share

You might also like