Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 18

KIKUNDI CHA YES WE CAN SOCIAL CLUB

(YCSC)

KATIBA

YA

KIKUNDI

(YCSC)

FOUTH DRAFT
YALIYOMO

1. SEHEMU YA KWANZA ......................................................................................................4

1.1 TAARIFA YA KIKUNDI:............................................................................................................. 4

1.2 UFAFANUZI WA MANENO: ...................................................................................................... 4

2. SEHEMU YA PILI................................................................................................................5

2.1 MADHUMINI YA KIKUNDI: ...................................................................................................... 5

3. SEHEMU YA TATU .............................................................................................................5

3.1 UANAKIKUNDI ........................................................................................................................... 5

3.1.1 Sifa za kuwa Mwanakikundi ....................................................................................................... 5

3.1.2 Haki za Mwanakikundi ............................................................................................................... 6

3.1.3 Wajibu wa Mwanakikundi kwa Kikundi ...................................................................................... 6

3.1.4 Maadili ya Mwanakikundi........................................................................................................... 7

3.1.5 Ukomo wa Uanakikundi.............................................................................................................. 7

4. SEHEMU YA NNE ...............................................................................................................8

4.1 Michango ...................................................................................................................................... 8

4.1.1 Mchango wa Kiingilio................................................................................................................. 8

4.1.2 Michango (Ada) ya kila mwezi ................................................................................................... 8

4.1.2 Michango Mingine ...................................................................................................................... 8

4.2. Faini (Penalty) na Adhabu Nyingine ............................................................................................. 8

4.3 Kuhifadhi Fedha na Akiba za Kikundi............................................................................................ 9

5. SEHEMU YA TANO .......................................................................................................... 10

5.1 Vyanzo vya Fedha ....................................................................................................................... 10

6. SEHEMU YA SITA ............................................................................................................ 11

6.1 Mikutano ya Kikundi ................................................................................................................... 11

6.1.1 Mkutano Mkuu wa Wanakikundi .............................................................................................. 11


6.1.2 Mkutano wa Kawaida wa kila mwezi ........................................................................................ 11

6.1.3 Mkutano Mkuu wa Dharura ................................................................................................ 11

6.1.4 Mkutano Maalum wa Uchaguzi .......................................................................................... 11

6.2 Utoaji wa Taarifa za Mikutano au Vikao. ............................................................................... 12

6.3 Uongozi wa Kikundi .................................................................................................................... 12

6.3.1 Mfumo wa Uongozi (Kamati Kuu) ya kikundi .......................................................................... 12

6.3.2 Wajibu na kazi za viongozi wa kikundi ..................................................................................... 12

6.3.3 Muda wa Uongozi wa Kikundi .................................................................................................. 13

6.3.4 Kusitishwa kwa Uongozi .................................................................................................... 13

7. SEHEMU YA SABA ........................................................................................................... 14

7.1 Kamati za Kikundi ................................................................................................................. 14

7.1.1 Kamati Tendaji................................................................................................................... 14

7.1.2 Kamati ya Nidhamu na Maadili .......................................................................................... 14

7.1.3 Kamati ya Fedha na Mikopo ............................................................................................... 14

8. SEHEMU YA NANE........................................................................................................... 16

8.1 Utaratibu wa Kutoa Maoni/Mapendekezo .................................................................................... 16

8.2 Utatuaji wa Migogoro au Malalamiko .......................................................................................... 16

8.3 Mialiko ya Kikundi ...................................................................................................................... 16

8.4 Marekebisho/ Mabadiliko ya Katiba ............................................................................................. 16

9. SEHEMU YA TISA ............................................................................................................ 17

9.1 Kufutwa kwa Kikundi .................................................................................................................. 17

9.2 Kuthibitishwa na Kusainiwa ........................................................................................................ 17


1. SEHEMU YA KWANZA

1.1 TAARIFA YA KIKUNDI:


(a) Jina la kikundi litakuwa: YCSC (YES WE CAN SOCIAL CLUB).
yaani kikundi kamili kwa watu waishio ndani ya Tanzania
(b) Anuani ya Kikundi: S.L.P 0000 Dar es salaam
(c) Tarehe ya kuandikishwa: ……………..
(d) Nambari ya kuandikishwa: ……………
(e) Wanakikundi waanzilishi: ……………..
(f) Eneo la shughuli za Kikundi litakuwa: Ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(g) Makao makuu ya kikundi yatakuwa: Dar es salaam
(h) Lugha rasmi ya kuendesha shughuli za kikundi itakuwa: Kiswahili au Kiingereza

1.2 UFAFANUZI WA MANENO:


Maneno yafuatayo yanapotumika katika masharti haya yatakuwa na maana kama inavyoelezwa
hapa chini:-
(a) “Kikundi” lina maana ya Kikundi cha YES WE CAN SOCIAL CLUB.
(b) “Mwanakikundi” ni mtu yeyote aliyejiunga na kikundi na anayeshiriki kikamilifu kutimiza
kanuni na taratibu za kikundi.
(c) ”Viongozi” ni wanakikundi waliochaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa katiba hii au
kanuni za kikundi, kusimamia mali au uendeshaji wa shughuli yoyote ya kikundi.
(d) “Mtoto” ni mtu mwenye umri chini ya miaka 18.
(e) “Kitega uchumi” (Investment) ni uwekezaji wenye kuleta tija kwa kikundi
(f) “Kanuni” za kikundi ni taratibu zote zilizopitishwa na wanakikundi kutumika kwenye
kikundi katika kuitekeleza katiba hii na kufanikisha madhumuni/malengo ya kikundi.
(g) “Ndani ya Tanzainia” Ndani ya nchi ni mipaka ambayo kijiografia inahusisha maeneo yote
ndani ya jamhuri ya muungana na nje ya nchi itamaanisha maeneo yote yasiyokuwa ya
Tanzania
(h) “Mkutano halali” ni kikao chochote au mkutano wowote wa wanachama ulioitishwa
kulingana na katiba hii au kanuni za kikundi na uliofanywa kwa utaratibu uliowekwa.
2. SEHEMU YA PILI

2.1 DHUMUNI KUU KIKUNDI


a. Kushirikiana kijamii na kiuchumi

Malengo mahususi:
(a) Kushirikiana na kusaidiana wakati wa shida na raha.nk
(b) Kuwezesha wanakikundi kuimarishana kiuchumi na hali ya maisha kwa:-
i. Kupokea na kuweka michango ya fedha za wanakikundi
ii. Kuanzisha na kuendeleza shughuli zozote halali za kiuchumi kwa manufaa ya
wanakikundi kama itakavyokubaliwa katika mkutano halali wa wanakikundi
iii. Kuwezesha kifedha shughuli binafsi za wanakikundi kwa masharti yaliyokubaliwa na
wanakikundi
iv. Kuhamasisha ushirikiano na wanakikundi wenye changamoto mbalimbali kama ulemavu,
uzee, uyatima, uathirika wa ukimwi na watoto wa mitaani.

3. SEHEMU YA TATU

3.1 UANAKIKUNDI

3.1.1 Sifa za kuwa Mwanakikundi


(a) Awe raia wa Tanzania.
(b) Awe ni mtu mwenye akili timamu na wa kuaminika.
(c) Awe anayefanya kazi iliyo rasmi ama isiyo rasmi au shughuli zinazokubalika kisheria
(d) Awe ametimiza umri wa miaka 18.
(e) Awe ni mtu aliye tayari kuiheshimu, kuitetea na kuongozwa kwa katiba ya kikundi na
kanuni zake
(f) Awe ametimiza taratibu zote za kujiunga na kikundi:
i. Kujaza fomu ya maombi na kukubaliwa na uongozi kisha kupitishwa na mkutano
mkuu kuwa mwanachama.
ii. Kulipa kiingilio kama inavyoonyeshwa katika kanuni za kikundi, au kama itakavyo
amuliwa na Mkutano halali wa kikundi.
iii. Ili kuondoa tofauti ya michango kati ya mwanakikundi ambaye yupo na yule
anayetaka kujiunga, wanakikundi watakubaliana kiasi cha fedha atakachotakiwa
kuchangia mtu anayetaka kijiunga na muda wa kukamilisha mchango huo.
3.1.2 Haki za Mwanakikundi
Mwanakikundi atakuwa na haki zifuatazo:-

1. Kutumia na kupata huduma zote za kikundi bila ubaguzi.


2. Kupokea taarifa za kikundi, kuona taarifa au kumbukumbu za kikundi kwa utaratibu
unaokubalika
3. Kuchagua (yaani kupiga kura) na kuchaguliwa (yaani kupigiwa kura) kwenye nafasi
yoyote katika kikundi
4. Haki ya kura moja kwa kila mwanakikundi bila kujali kiasi cha michango aliyoweka
kwenye kikundi.
5. Haki ya kujitetea dhidi ya jambo lolote litakalomkabili katika uhusiano wake na
wanakikundi wengine.

6. Haki ya kutoa hoja yoyote inayohusu mwenendo wa wanakikundi ndani ya mikutano ya


kikundi

7. Haki ya kujitoa kwa hiari kwenye kikundi

8. Mwanakikundi ambaye uanakikundi wake umekoma kwa sababu zilizoanishwa katika


kifungu 3.1.5 hapo chini, atarudishiwa fedha zake kulingana na mgawanyo wa thamani
za kikundi kwa wakati huo kwa wanachama wote ndani ya siku tisini (90) baada ya
kikundi kupata taarifa ya maandishi kwa kuzingatia yafuatayo:-
i. Marejesho yatafanyika baada ya kuzingatia matumizi (pamoja na hasara) ya
kikundi yaliyotokea kwa kipindi chote alichokuwa mwanakikundi
ii. Mwanakikundi hatarejeshewa fedha zake mpaka madeni yake na ya wanakikundi
wote aliowadhamini yawe yamelipwa yote au kupata mdhamini mwingine.
iii. Asilimia ishirini (20%) ya kiasi kilichobaki baada ya kipengele (i) na (ii) hapo juu
kutumika, itabaki kwenye mfuko wa kikundi. Kiasi hiki kitatumika kadiri ya
kanuni za kikundi kwa maendeleo ya kikundi.
iv.

3.1.3 Wajibu wa Mwanakikundi kwa Kikundi


Mwanakikundi atakuwa na wajibu ufuatao kwa kikundi:-

1. Kuchangia fedha kila mwezi (ada) na michango mingine yoyote kama itakavyoanishwa
kwenye kanuni au iliyopendekezwa na kuidhinishwa na wanakikundi

2. Kuhudhuria na kushiriki katika mikutano yote halali ya kikundi.

3. Kuwa mtu Mwaminifu, Mwaadilifu, na Mwenye Kujitolea kwa ajili ya kikundi


4. Kufuata kanuni, sheria na masharti ya kikundi yaliyo kubaliwa

5. Kutii na kufuata maazimio yote ya Mkutano wowote halali hata ikiwa hakuwepo kwenye
mkutano huo, au kutoshiriki katika kupitisha azimio hilo

6. Kueneza sifa nzuri za kikundi

7. Kuwa na nidhamu wakati wa vikao au mkutano

8. Kushiriki kikamilifu kubuni miradi ya kuendeleza na kuimarisha kikundi

9. Kutunza siri zote za kikundi

3.1.4 Maadili ya Mwanakikundi


Kila mwanakikundi atapaswa kufuata maadili yafuatayo:
(a) Kupendana na kuheshimiana
(b) Kukubali kukosolewa endapo maadili yamekiukwa
(c) Mwanakikundi haruhusiwi kupokea wala kutoa rushwa
(d) Kuepuka dharau, kiburi, chuki na hasira
(e) Kutoshiriki mikutano yoyote itakayofanyika kinyume na katiba na kanuni za kikundi
(f) Mwanakikundi anapokwenda kinyume na maadili ya kikundi ataonywa mara ya kwanza
kwa mdomo, tatu kwa maandishi na Kamati tendaji; asipobadilika kipengele cha
kumwachisha uwanakikundi kitatumika

3.1.5 Ukomo wa Uanakikundi


(a) Kifo
(b) Kushindwa kuchangia michango ya kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu (3) mfululizo
kwa sababu zozote zile bila taarifa ya mdomo au kwa maandishi
(c) Mwanakikundi kujiuzulu au kuomba kuacha uanakikundi yeye mwenyewe kwa sababu
zozote zile
(d) Kutoa au kupokea rushwa kwa viongozi au mwanakikundi yeyote
(e) Kuachishwa uanakikundi kwa azimio litakaloungwa mkono na Wanakikundi
wasiopungua theluthi mbili (2/3) ya Wanakikundi waliohudhuria katika Mkutano halali
(f) Kushiriki katika kuiba au kuhujumu mali za kikundi (ikiwa ni pamoja na fedha)
(g) Mtu aliyeacha au kufukuzwa uanakikundi anaweza kuomba kujiunga tena kwa mujibu
wa masharti ya uanakikundi kama yalivyo lakini atatakiwa kuwa na wadhamini wawili
(2) ambao ni wanakikundi hai.
(h) Mwanakikundi anaweza kurithisha uanakikundi kwa wale wanaomtegemea; na yule
anayerithishwa kama inavyoonyesha kwenye fomu na awe na sifa zilizoanishwa katika
kifungu namba 3.1.1
4. SEHEMU YA NNE

4.1 Michango

4.1.1 Mchango wa Kiingilio


(a) Mwanakikundi mwanzilishi anawajibika kulipa kiingilio cha shilingi laki moja (Tshs
100,000) kabla ya tarehe 31/01/2015.
(b) Mwanakikundi atakeyejiunga baada ya tarehe 31/01/2015 hatakuwa mwanzilishi na
atatakiwa kulipa mchango kulingana na kanuni za kikundi.
(b) Mtu aliyejiunga na kikundi atastahili haki za Mwanakikundi pale atakapokuwa amelipa
mchango wa kiingilio.
(c) Kila atakayejiunga na Kikundi atapatiwa fomu ya usajili ambayo itaonyesha kiasi
anachotakiwa kulipa kuwa Mwanakikundi, kiasi alicholipa na utaratibu wa kukamilisha kiasi
kilichobaki.

4.1.2 Michango (Ada) ya kila mwezi


(a) Mwanakikundi atatakiwa kulipa kwa wakati kiasi kilichopitishwa kama ada ya kila mwezi
kama ilivyoainishwa katika kanuni na taratibu za kikundi.

(b) Endapo mwanakikundi atachelewa kulipa kiasi hicho, au asipolipa kabisa, utaratibu wa faini
(penalty) na adhabu nyingine zilizokubaliwa katika kanuni za kikundi zitatumika.

(c) Mtunza fedha wa kikundi atatoa taarifa sahihi za michango yote iliyokusanywa siku ya
mkutano akionyesha wale waliolipa, wanaodaiwa, aina ya michango iliyokusanywa na habari
nyingine inayofaa kadiri ya utaratibu wa hesabu za fedha.

4.1.3 Michango Mingine


(a) Kikundi kitakuwa na michango mingine kadiri itakavyopitishwa katika kanuni, ikiwa ni
pamoja na michango ya msiba, harusi, ugonjwa au matukio mengine.

(b) Kila mwanakikundi atatakiwa kulipa kiasi cha fedha kilichopitishwa kwa wakati sahihi, na
kwa utaratibu uliowekwa; na atakayekiuka, kipengele cha faini kitatumika.

4.2. Faini (Penalty) na Adhabu Nyingine


(a) Kikundi kitakuwa na mamlaka ya kuweka faini ya fedha au kusitishwa kwa uanachama kwa
mwanakikundi yeyote atakayekiuka utaratibu wa michango, vikao, mikutano, na kanuni
nyinginezo za kikundi.

(b) Kiasi cha faini na utaratibu wa kulipa faini utaratibiwa kadiri ya kanuni za kikundi.
(c) Ikiwa wanakikundi wataona inafaa na wakaridhia kwa zaidi ya theluthi mbili (2/3), na
kutegemeana na kosa, mwanakikundi atasimamishwa uanachama na kushitakiwa kwenye
vyombo vya sheria.

4.3 Kuhifadhi Fedha na Akiba za Kikundi


(a) Fedha za Kikundi zitahifadhiwa katika taasisi HALALI za kifedha Kama vile Benki au
kuwekezwa katika rasilimali inayotoa faida kwa kikundi.
(b) Fedha yote ya kikundi itahifadhiwa katika taasisi za kifedha kama vile Benki. Hata hivyo,
Uongozi unaweza kutenga kiasi kidogo (Petty cash) ili kukidhi matumizi madogomadogo
(c) Fedha za kikundi zilizokusanywa zaweza kutumika kuwasaidia wanakikundi kukabiliana na
dharura au hali za maisha kwa njia ya mkopo kwa utaratibu ulioainishwa kwenye kanuni za
kikundi.

4.4 Kutoa Fedha na Akiba za Kikundi


(a) Fedha za kikundi zinaweza kutolewa wakati wowote kulingana na mahitaji
yatakayopendekezwa na wanakikundi.
(b) Malipo yatafanyika kwa njia ya hundi au taslim (cash) baada ya kukamilika kwa utaratibu
wa utoaji wa fedha za kikundi
(c) Kutakuwa na makundi mawili A na B katika kuidhinisha utoaji wa fedha

(i) Kundi A

Kundi hili litajumisha kamati kuu tendaji yaani Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti, Katibu,
na Katibu Msaidizi. Kama mmoja wa kiongozi hayupo, mfumo utazingatia mtiririko Katika
uongozi kutoka juu kwenda chini.

(ii) Kundi B

Kundi hili litajumuisha Mwenyekiti/Makamu mwenyekiti kutoka kamati za nidhamu na


maadili pamoja na kamati ya mikopo na fedha.

4.4.1 Mgongano wa kimaslahi katika kusaini.

Bila kuathiri matakwa ya kuidhinisha malipo, iwapo watajwa katika ibara 4.4(c) (i) na (ii)
watakuwa na mgongano wa kimaslahi aidha ya kindugu ama kwa namna yeyote ile basi ni
lazima ikaepukwa kwa maslahi ya kikundi.
5. SEHEMU YA TANO

5.1 Vyanzo vya Fedha


i. Fedha ya kiingilio anayotoa kila mwanakikundi wakati anapojiunga.
ii. Ada za kila mwezi na tozo mbalimbali.
iii. Vitega uchumi mbalimbali (Investments), mashamba, Viwanja, biashara nk.
iv. Mikopo kutoka vyombo vya fedha au chombo kingine chochote baada ya kupata idhini ya
wanakikundi kwa idadi ya theluthi mbili ya wanachama au Zaidi.
v. Misaada au Ufadhili kutoka sehemu mbalimbali.
vi. Chanzo kingine chochote halali kwa mujibu wa sheria za nchi na katiba ya kikundi.
6. SEHEMU YA SITA

6.1 Mikutano ya Kikundi

6.1.1 Mkutano Mkuu wa Wanakikundi


(a) Mkutano Mkuu wa Wanakikundi utaitishwa na mwenyekiti na utafanyika kila baada ya
mwaka mmoja.
(b) Uhalali wa mkutano au kikao chochote cha kikundi ni mahudhurio ya wanakikundi kuwa
zaidi ya nusu ya idadi yote.
(c) Mambo yafuatayo lazima yajadiliwe katika Mkutano Mkuu wa mwaka:-
i. Kusoma na kuthibitisha muhutasari wa mkutano uliopita.
ii. Kupokea na kujadili taarifa ya mwaka ya mapato na matumizi.
iii. Kupokea na kujadili taarifa za maendeleo ya kikundi kutoka kwenye kamati
mbalimbali za kikundi
iv. Kuidhinisha makisio ya mapato na matumizi ya mwaka unaofuata
v. Kuzungumzia mikakati inayohusu maendeleo ya Kikundi kwa jumla na kutoa
maelekezo ya utekelezaji kwa watendaji wa kikundi.

6.1.2 Mkutano wa Kawaida ni kila baada ya miezi miwili


(a) Utafanyika kila Jumapili ya kwanza ya mwezi
(b) Utapokea taarifa mbalimbali za uendeshaji wa kikundi za kila mwezi
(c) Utapokea maoni/mapendekezo ya mipango ya maendeleo ya kikundi
(d) Kuthibitisha kuingizwa na kufukuzwa kwa Wanakikundi
(e) Kupokea wanakikundi wapya kama wapo

6.1.3 Mkutano Mkuu Wa Dharura


(a) Mwenyekiti/Makamu mwenyekiti/Katibu/Katibu Msaidizi/mwanakikundi kwa idadi
isiyopungua theluthi mbili ataitisha/wataitisha Mkutano Mkuu wa Dharura kwa jambo la
dharura linalohusu kikundi kama vile Msiba, Ugonjwa, Kuibiwa mali za Kikundi na
yanayofanana na hayo.

(b) Mkutano wa Dharura unaweza kuendeshwa na idadi isiyopungua nusu ya wanakikundi

6.1.4 Mkutano Maalumu wa Uchaguzi


(a) Mkutano utakuwa ni maalumu kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa kikundi baada ya
viongozi waliopo madarakani kumaliza kipindi chao cha uongozi

(b) Ikiwa kiongozi yeyote atasitishwa uongozi kama inavyoelezwa katika kipengele cha
6.3.4, utaitishwa mkutano maalum wa uchaguzi kwa nafasi yake.
6.2 Utoaji wa Taarifa za Mikutano au Vikao.
(a) Taarifa za mkutano zitatolewa kwa wanakikundi wote kwa kutumia taratibu
zinazokubalika. Taarifa hii itabidi ionyeshe waziwazi tarehe ya Mkutano, Idadi ya
wanakikundi waliohudhuria, muda, mahali pa mkutano na dhumuni la mkutano.
(b) Taarifa yoyote ya dharura inayohusu kikundi itatakiwa kufikishwa kwa uongozi kwanza
na uongozi utatoa utaratibu wa kuwafahamisha wanakikundi wote na taratibu nyingine.

6.3 Uongozi wa Kikundi


Kutakuwa na mfumo rasmi wa kisheria katika uongozi ambao ni Kamati Kuu, Kamati tendaji za
kudumu/Mda kama itakavyoonekana inafaa.

6.3.1 Mfumo wa Uongozi (Kamati Kuu) wa kikundi

(a) Uongozi wa Kikundi utakuwa na watu watano:

i. Mwenyekiti
ii. Makamu Mwenyekiti
iii. Katibu
iv. Katibu Msaidizi
v. Mweka Hazina

(b) Kundi linaweza kuwa na wadhamini mpaka watatu (3) ambao watapendekezwa na
kamati kuu na kuidhinishwa na mkutano mkuu wa wanakikundi. Hawa watakuwa ni
washauri wakuu wa masuala mbalimbali yatakayohusu maendeleo ya kikundi.

6.3.2 Wajibu na kazi za viongozi wa kikundi

(a) Menyekiti/Makamu Mwenyekiti wa kikundi

i. Atakuwa ni msemaji mkuu wa kikundi


ii. Ni kiongozi/msimamizi wa shughuli zote za kikundi
iii. Atahakikisha kikundi kinaimarika na kusimamia katiba kikamilifu
iv. Ni mwenyekiti wa vikao vyote vya kikundi

(b) Katibu/Katibu Msaidizi wa kikundi

i. Ni Katibu Mtendaji Mkuu wa kikundi


ii. Ni mwandishi na mwekaji wa kumbukumbu za vikao vyote vya kikundi
iii. Ni mtayarishaji wa taratibu zote za vikao vya kikundi kwa kushirikiana na
mwenyekiti
iv. Mfuatiliaji wa maazimio na mipango ya kikundi.
v. Mwandishi mkuu wa barua au taarifa nyingine zinazokihusu kikundi.
(c) Mweka Hazina wa Kikundi

i. Mtunzaji fedha na taarifa zote za fedha za kikundi


ii. Ni mtoaji wa taarifa zote zihusuzo mapato na matumizi ya kikundi
iii.Ni mtengenezaji/muandaaji wa bajeti ya kikundi
iv. Kufuatilia na kuwakumbusha wanakikundi kuhusu madeni yao kwa barua, simu na/au
barua pepe
v. Kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya kikundi wakati wowote inapohitajika
vi. Kutoa taarifa za dharura zitakazohusu mfuko wa kikundi.

6.3.3 Muda wa Uongozi wa Kikundi


(a) Muda wa uongozi katika kikundi utakuwa ni miaka miwili (2)

(b) Viongozi waliomaliza muda wao wanaweza kuchaguliwa tena lakini wasiwe wamekalia
nafasi hiyo hiyo kwa zaidi ya vipindi vitatu mfululizo.

6.3.4 Kusitishwa kwa Uongozi


(a) Uongozi/Kiongozi unaweza/anaweza kusitishwa wakati wowote kabla ya muda wa
uongozi kuisha iwapo:

i. Uanakikundi wake umefikia ukomo (angalia kipengele 3.1.5 Ukomo wa


Uanakikundi)

ii. Kumekuwa na kutokuwajibika ipasavyo kuleta maendeleo ya kikundi kwa mujibu


wa kikundi za kikundi

iii. Wanachama watakosa imani nao/naye kwa idadi ya thelulthi mbili ya wanachama
wote.

iv. Ataamua kujiuzulu kwa ridhaa yake mwenyewe kwa maslahi ya kikundi; na zaidi
ya nusu ya wanakikundi wamekubaliana na ombi lake la kujiuzulu

(b) Kiongozi aliyesitishwa kuongoza atawajibika kukabidhi mali na taarifa sahihi kwa
kikundi (au kiongozi mwingine aliyechaguliwa) kwa utaratibu ulioanishwa kwenye
kanuni za kikundi.
7. SEHEMU YA SABA

7.1 Kamati za Kikundi


(a) Kikundi kitakuwa na kamati za kudumu zitakazosaidiana na Kamati Kuu kufanikisha
mipango na shughuli za kikundi

(b) Kamati nyingine zozote za Muda zinaweza kuundwa katika mikutano ya kawaida ya
mwezi kulingana na matukio au umuhimu wa kuwepo kamati hizo.

7.1.1 Kamati Tendaji


(a) Itakuwa na viongozi wakuu watano wa kikundi (kifungu 6.3.1 (a)) pamoja na wenyeviti
wote wa kamati mbalimbali zilizoundwa kwa mujibu wa katiba au kanuni za kikundi.

(b) Kamati tendaji itakuwa na kazi zifuatazo:

i. Kupitia na kujadili mapato na matumizi ya kikundi kabla ya kufikishwa kwenye


Mkutano Mkuu wa Wanakikundi

ii. Kujadili na kupitisha maombi ya wanakikundi wapya watakaoomba kujiunga na


kikundi

iii. Kusimamia utendaji na utekelezaji wa mipango na shughuli za kikundi.

iv. Kusimamia masuala yote ya katiba na kanuni za kuendesha kikundi.

7.1.2 Kamati ya Nidhamu na Maadili


(a) Watachaguliwa na wanakikundi wasipungua theluthi mbili ya wanachama katika uchaguzi
mkuu wa kikundi.

(b) Itakuwa na watu wasiopungua wawili.

(c) Itakuwa na jukumu la kushughulikia masuala ya nidhamu na maadili ya kikundi kwa


viongozi na wanakikundi wa kawaida

7.1.3 Kamati ya Fedha na Mikopo

(a) Watachaguliwa na wanakikundi wote katika uchaguzi mkuu wa kikundi.

(b) Itakuwa na watu wasiopungua wanne

(c) Itafuatilia masuala yote ya fedha na rasilimali nyingine za kikundi


(d) Itaratibu na kupitisha mikopo ya kikundi na wanakikundi kwa mujibu wa katiba au kanuni
za kikundi
8. SEHEMU YA NANE

8.1 Utaratibu wa Kutoa Maoni/Mapendekezo


(a) Maoni , Mapendekezo au Malalamiko yoyote kwa mwanakikundi/wanakikundi yatatolewa
kwa maandishi au kwa kusema kwa viongozi au kwenye kikao halali cha wanakikundi

(b) Ikiwa jambo husika linahitaji maamuzi ya wanakikundi wote, Kamati Tendaji itawasilisha
mapendekezo yao kwenye mkutano wa wanakikundi wote kwa uamuzi wa mwisho.

8.2 Utatuaji wa Migogoro au Malalamiko


(a) Migogoro au malalamiko yoyote yanayohusu kikundi au wanakikundi yatatatuliwa kwanza
na wahusika kwa njia ya udugu (majadiliano na maelewano) kwa msaada wa uongozi wa
kikundi

(b) Ikiwa njia ya kwanza itashindikana, msaada wa mahakama na taratibu za kisheria zinaweza
kufuatwa.

8.3 Mialiko ya Kikundi


(a) Kikundi kitakuwa na fursa na uwezo wa kutuma mialiko kwenye vikundi vingine kwa
lengo la kushirikishana uzoefu, mawazo, michezo, huduma, shughuli za kiuchumi, kijamii
na mengineyo yenye maslahi kwa kikundi.

(b) Utaratibu wa mialiko itakuwa kama ulivyopitishwa katika kanuni za kikundi

8.4 Marekebisho/ Mabadiliko ya Katiba


(a) Mapendekezo ya Mabadiliko ya Katiba ni lazima yajadiliwe katika Mkutano Mkuu na
yaidhinishwe walao na robo tatu (75%) ya wanakikundi wote

(b) Mapendekezo yoyote ya katiba yanayotakiwa kujadiliwa yatakusanywa na Kamati tendaji


katika kipindi chote cha mwaka, kwa ajili ya kuidhinishwa/kutoidhinishwa na wanakikundi
siku ya Mkutano Mkuu wa Mwaka.
9. SEHEMU YA TISA

9.1 Kufutwa kwa Kikundi


(a) Kikundi hiki kitafunga kabisa shughuli zake kwa sababu za msingi zitakazokubalika na
zaidi ya robo tatu (75%) ya wanakikundi wote katika Mkutano Mkuu.

(b) Endapo Kikundi hiki kitavunjwa, Mali zote za kikundi zitafilisiwa ili kulipia madeni
yatakayokuwa yanakikabili kikundi hadi wakati huo

(c) Fedha zitazobakia baada ya kulipa madeni, zitagawanywa kwa wanakikundi wote kulingana
na muda na kiasi cha michango ya kila mmoja.

(d) Endapo fedha zilizopo hazitoshi kulipa deni, salio la deni litagawanywa kwa utaratibu sawa
na wa kipengele 9.1 (c) hapo juu.

(e) Usimamizi wa zoezi la ufilisi utafanywa chini ya Mahakama

9.2 Kuthibitishwa na Kusainiwa


Katiba hii imethibitishwa na kupitishwa na waanzilishi wote wa kikundi ambao ni:

Na. Jina Cheo Mawasiliano Sahihi


1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32

MWISHO.

You might also like