Ulu Ul Azmi Minna Rusul Juzuu Al Awwal أُوْلُواْ ٱلْعَزْمِ مِنَ ٱلرُّسُلِ

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 965

1

﴾ِ‫﴿أُوْﻟُﻮاْ اﻟْﻌَﺰْمِ ِﻣﻦَ اﻟﺮﱡ ُﺳﻞ‬


‫اﻟﺠﺰء اﻻول‬
‫ﺗﺠﻤﻴﻊ واﻧﺘﺎج‬

‫اﻟﻤﺴﺘﻜﺸﻒ أﺑﻮﻣﻨﺎل داﻧﺎ‬


UuLU AL A’AZMI MINA ALRRUSUL
AL JUZUI AL AWWAL
WENYE AZMA THABIT ZAIDI
MIONGONI MWA MITUME
SEHEMU YA KWANZA

KIMEKUSANYWA NA KUTAYARISHWA NA AL MUSTAKSHIF ABU MANAL DANAH


KIMECHAPISHWA NEW DELHI – INDIA.
MWAKA 1442 AL HIJRA – 2021 C.E
3

﴾‫اﻟﺮ ِﺣ ِﯿﻢ‬
‫ـﻦ ﱠ‬ِ ‫اﻟﺮ ْﺣ َﻤ‬ ‫﴿ ِﺑ ْﺴ ِﻢ ﱠ‬
‫ا�ِ ﱠ‬
‫اﳊَ ْﻤ َﺪ ِﱠﻪﻠﻟِ َْﳓ َﻤ ُﺪﻩُ وﻧَ ْﺴﺘَﻌِﻴﻨُﻪُ َوﻧَ ْﺴﺘَـ ْﻐ ِﻔُﺮﻩُ َوﻧَـﻌُﻮذُ ِﺎﺑ ﱠﻪﻠﻟِ ِﻣ ْﻦ ُﺷُﺮوِر أَﻧْـ ُﻔ ِﺴﻨَﺎ َوِﻣ ْﻦ‬
ْ ‫إ ﱠن‬
ِ ِ ْ ‫ﻀ ﱠﻞ ﻟَﻪ وﻣﻦ ﻳ‬ ِ ‫اﻪﻠﻟ ﻓَ َﻼ ﻣ‬ ِِ ِ ِ
‫ي ﻟَﻪُ َوأ ْﺷ َﻬ ُﺪ‬ َ ‫ﻀﻠ ْﻞ ﻓَ َﻼ َﻫﺎد‬ ُ ْ ََ ُ ُ ُ‫ َﻣ ْﻦ ﻳَـ ْﻬﺪﻩ ﱠ‬،‫َﺳﻴِّﺌَﺎت أ َْﻋ َﻤﺎﻟﻨَﺎ‬
ُ‫ﻳﻚ ﻟَﻪُ َوأ ْﺷ َﻬ ُﺪ أ ﱠن ُﳏَ ﱠﻤ ًﺪا َﻋْﺒ ُﺪﻩُ َوَر ُﺳﻮﻟُﻪ‬ َ ‫اﻪﻠﻟُ َو ْﺣ َﺪﻩُ َﻻ َﺷ ِﺮ‬ ‫أ ْن َﻻ إِﻟَﻪَ إِﱠﻻ ﱠ‬
Inna Al-hamda Lillaahi nahmaduhu wanasta’eenahu wa nastaghfiruhu, wa
na’oodhu billaahi min shuroori anfusinaa wa min sayi’aati a’maalinaa. Man yahdih
- Illaahu falaa mudhilla laahu wa man yudhlil falaa haadiya lahu. Wa ashhadu an
laa ilaaha ill-Allaahu wahdahu laa shareekallahu, wa ashhadu anna Muhammadan
‘Abduhu wa Rasooluhu.

Tafsir: Kwa jina la Allah, ambae anastahiki shukrani zote, tunaemuomba msaada na
msamaha wake. Tunajilinda kwa ulinzi wa Allah na kila maovu ya Nafsi zetu na
mambo mabaya yetu. Kwani kwa hakika mtu yeyote yule alieongozwa na Allah basi
hakuna atakaempotoa, na aliepotoshwa na Allah basi hakuna atakaemuongoa.
Nnashuhudia kua hakuna anaepaswa kuabudiwa isipokua Allah pekee asiekua na
mshirika, na nnashuhudia kua Muhammad (Salallahu A’layhi wa Salam) ni Mja wake
na ni Mtume wake.

‫ﻳﻘﻮل ﷲ ﻋﺰ وﺟﻞ ﰲ ﻛﺘﺎﺑﻪ اﻟﻌﺰﻳﺰ‬


﴾‫اﻪﻠﻟَ َﺣ ﱠﻖ ﺗُـ َﻘﺎﺗِِﻪ َوﻻَ َﲤُﻮﺗُ ﱠﻦ إِﻻﱠ َوأَﻧﺘُﻢ ﱡﻣ ْﺴﻠِ ُﻤﻮ َن‬
‫ﻳﻦ ءَ َاﻣﻨُﻮاْ اﺗﱠـ ُﻘﻮاْ ﱠ‬ ِ‫ﱠ‬
َ ‫﴿�َﻳـﱡ َﻬﺎ اﻟﺬ‬
Ya ayyuha alladhina amanoo ittaqoo Allaha haqqa tuqatihi wala tamootunna illa
waantum muslimoona (Surat Al Imran 3:102)

Tafsir: Enyi mlioamini! Muogopeni Allah (kwa kutekeleza maamrisho yake na


kuachana na makatazo yake) kama anavyostahiki kuogopewa. [Mtiini, mshukuruni
na daima mkumbukeni], na msife isipokua mkiwa katika hali ya kua ni Waislam.
4

ٍ ‫ﱠﺎس اﺗﱠـ ُﻘﻮاْ َرﺑﱠ ُﻜ ُﻢ اﻟﱠ ِﺬى َﺧﻠَ َﻘ ُﻜ ْﻢ ِﻣ ْﻦ ﻧـﱠ ْﻔ‬


‫ﺲ َو ِﺣ َﺪةٍ َو َﺧﻠَ َﻖ ِﻣْﻨـ َﻬﺎ َزْو َﺟ َﻬﺎ‬ ُ ‫﴿ﻳَـﺄَﻳـﱡ َﻬﺎ اﻟﻨ‬
‫اﻪﻠﻟَ اﻟﱠ ِﺬى ﺗَ َﺴﺂءَﻟُﻮ َن ﺑِِﻪ َو ْاﻷ َْر َﺣ َﺎم إِ ﱠن َﱠ‬
‫اﻪﻠﻟ‬ ‫ﺚ ِﻣْﻨـ ُﻬ َﻤﺎ ِر َﺟﺎﻻً َﻛﺜِﲑاً َوﻧِ َﺴﺂءً َواﺗﱠـ ُﻘﻮاْ ﱠ‬ ‫َوﺑَ ﱠ‬
﴾ً‫َﻛﺎ َن َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ َرﻗِﻴﺒﺎ‬
Ya ayyuha alnnasu ittaqoo rabbakumu alladhi khalaqakum min Nafsin wahidatin
wakhalaqa minha zawjaha wabaththa minhuma rijalan kathiran wanisaan
waittaqoo Allaha alladhii tasaaloona bihi waal-arhama inna Allaha kana
AAalaykum raqeeban (Surat An Nisaa 4:1)

Tafsiri: Enyi Watu! Mcheni Mola wenu aliekuumbeni kutokana na Nafsi moja
(Adam), na kutokana nae (Adam) akamuumba mke wake (Hawwa), na kutokana nao
(Adam na Hawa) akawaumba Wanaume na Wanawake wengi na muogopeni Allah
ambae ana haki juu yenu, na msivunje udugu, kwani kwa Hakika Allah ni mwenye
uangalifu mkubwa juu yenu.

‫ﺼﻠِ ْﺢ ﻟَ ُﻜ ْﻢ أ َْﻋ َﻤـﻠَ ُﻜ ْﻢ َوﻳَـ ْﻐ ِﻔْﺮ‬ ِ


ْ ُ‫اﻪﻠﻟَ َوﻗُﻮﻟُﻮاْ ﻗَـ ْﻮﻻً َﺳﺪﻳﺪاً ۞ ﻳ‬‫ﻳﻦ ءَ َاﻣﻨُﻮاْ اﺗﱠـ ُﻘﻮاْ ﱠ‬ ِ‫ﱠ‬
َ ‫﴿�َﻳـﱡ َﻬﺎ اﻟﺬ‬
﴾ً‫اﻪﻠﻟَ َوَر ُﺳﻮﻟَﻪُ ﻓَـ َﻘ ْﺪ ﻓَ َﺎز ﻓَـ ْﻮزاً َﻋ ِﻈﻴﻤﺎ‬
‫ﻟَ ُﻜ ْﻢ ذُﻧُﻮﺑَ ُﻜ ْﻢ َوَﻣﻦ ﻳُ ِﻄ ِﻊ ﱠ‬
Ya ayyuha alladhina amanoo ittaqoo Allaha waqooloo qawlan sadeedan, Yuslih
lakum aAAmalakum wayaghfir lakum dhunoobakum waman yutiAAi Allaha
warasoolahu faqad faza fawzan AAadhiman (Al Ahzab 33:70-71)

Tafsir: Enyi Mlioamini! mcheni na muogopeni Allah, na (daima) semeni kauli za


ukweli ulionyooka, atakuongozeni kufanya mema na kukusameheni dhambi zenu. Na
kwa hakika yeyote yule ambae anaemtii Allah na Mtume wake (Salallahu A’layhi wa
Salam) basi atakua ni miongoni mwa waliofuzu.

Allahuma Ij’Aalna minna al faizin fawzan A’adhimah…Aamin

‫أ ََﻣﺎ ﺑَـ ْﻌ ُﺪ‬


5

‫ﱠﱯ ﺻﻠﱠﻰ ﷲُ ﻋﻠﻴﻪ وﺳﻠﱠ َﻢ‬


‫ﻗﺎل اﻟﻨ ﱠ‬

ُ‫ َو َﺧْﻴـَﺮ اﻟْ ِﻤﻠَ ِﻞ ِﻣﻠﱠﺔ‬،‫ َوأ َْوﺛَ َﻖ اﻟْﻌُْﺮي َﻛﻠِ َﻤﺔُ اﻟﺘﱠـ ْﻘ َﻮى‬،ِ‫اﻪﻠﻟ‬
‫ﺎب ﱠ‬ ِ ِ ِ ْ ‫ﻓَِﺈ ﱠن أَﺻ َﺪ َق‬
ُ َ‫اﳊَﺪﻳﺚ ﻛﺘ‬ ْ
‫ﺚ ِذ ْﻛُﺮ‬ ِ ‫اﳊ ِﺪﻳ‬ َ ‫ َوأَ ْﺷَﺮ‬،‫ﺻﻠﱠﻰ ﷲُ َﻋﻠَْﻴ ِﻪ َو َﺳﻠﱠ َﻢ‬ ٍ ِ
َْ ‫ف‬ َ ‫ َو َﺧْﻴـَﺮ اﻟ ﱡﺴﻨَ ِﻦ ُﺳﻨَ ُﻦ ُﳏَ ﱠﻤﺪ‬،‫إِﺑْـَﺮاﻫ َﻴﻢ‬
‫ﺺ َﻫ َﺬا اﻟْ ُﻘْﺮآ ُن‬ ِ ‫ﺼ‬ َ ‫َﺣ َﺴ َﻦ اﻟْ َﻘ‬ َ ‫اﻪﻠﻟِ ﺗَـ َﻌ‬
ْ ‫ َوأ‬،‫ﺎﱃ‬ ‫ﱠ‬
Qala An Nabiyya Salallahu A’alayhi wa Salam: Fa'inna 'asdaqa alhadith kitab alllahi,
wa'awthaq al’aAuryi kalimat alttaqwaa, wakhayr almilal millat 'Ibrahima, wakhayr
alssunan sunan Muhammad Sala Allahu Aalayhi wa Salam, wa'ashraf alhadith dhikr
allah taalaa, wa'ahsan alqasas hadha al Quran.

Amesema Rasul Allahi Salallahu Alayhi wa Salam kua: Kwa hakika hadith za kweli
kabisa ni za Kitabu cha Allah Subhanah wa Ta’ala, na kauli nzito ni kauli zenye
Taqwa, na Mila bora ni Milat Ibrahima, Na Sunna bora ni Sunna za Muhammad
(Sala Allahu Alyhi wa Salam) na Maneno Matukufu ni Dhikr Allah Ta’ala na Visa
bora ni hii Qur’an.

‫ﻮل ﷲ ﻋﺰ وﺟﻞ‬
ُ ‫َوﻳَـ ُﻘ‬
ِ ِ ِ ِ َ ‫ﭑﳊ ِﻖ ﻧـَﺰَل وﻣﺂ أَرﺳ ْﻠﻨ‬ ْ ِ‫﴿ َوﺑ‬
َ ً‫ﺎك إﻻﱠ ُﻣﺒَ ّﺸﺮاً َوﻧَﺬﻳﺮا‬
ُ‫۞وﻗُـْﺮآ�ً ﻓَـَﺮﻗْـﻨَﺎﻩُ ﻟﺘَـ ْﻘَﺮأَﻩ‬ َ َ ْ َ َ َ ّ َْ ِ‫ﭑﳊَِّﻖ أَﻧْـَﺰﻟْﻨَﺎﻩُ َوﺑ‬
ْ‫ﻳﻦ أُوﺗُﻮا‬ ِ ‫ﺚ وﻧَـﱠﺰﻟْﻨﺎﻩ ﺗَـْﻨ ِﺰﻳﻼً۞ﻗُﻞ ِآﻣﻨﻮاْ ﺑِِﻪ أَو ﻻَ ﺗـُﺆِﻣﻨـ ۤﻮاْ إِ ﱠن ٱﻟﱠ‬
‫ﺬ‬ ٍ ِ ‫َﻋﻠَﻰ ٱﻟﻨ‬
َ ُْ ْ ُ ْ ُ َ َ ‫ﱠﺎس َﻋﻠَ ٰﻰ ُﻣ ْﻜ‬
‫ﺎن ُﺳ ﱠﺠﺪاً۞ َوﻳَـ ُﻘﻮﻟُﻮ َن ُﺳْﺒ َﺤﺎ َن َرﺑِّﻨَﺂ إِن‬ ِ َ‫ٱﻟْﻌِْﻠﻢ ِﻣﻦ ﻗَـﺒﻠِ ِﻪ إِ َذا ﻳـْﺘـﻠَ ٰﻰ ﻋﻠَﻴ ِﻬﻢ َِﳜﱡﺮو َن ﻟِﻸَ ْذﻗ‬
ْ َْ ُ ْ َ
ْ‫ﻳﺪ ُﻫ ْﻢ ُﺧ ُﺸﻮﻋﺎً۞ﻗُ ِﻞ ْٱدﻋُﻮا‬ ِ َ‫َﻛﺎ َن و ْﻋ ُﺪ رﺑِﻨَﺎ ﻟَﻤ ْﻔﻌﻮﻻً۞وَِﳜﱡﺮو َن ﻟِﻸَ ْذﻗ‬
ُ ‫ﺎن ﻳَـْﺒ ُﻜﻮ َن َوﻳَِﺰ‬ َ ُ َ َّ َ
َ‫ﻚ َوﻻ‬ َ ِ‫ﺼﻼَﺗ‬ َ ِ‫َﲰَﺂءُ ٱ ْﳊُ ْﺴ َ ٰﲎ َوﻻَ َْﲡ َﻬْﺮ ﺑ‬ْ ‫ٱﻪﻠﻟَ أَ ِو ْٱدﻋُﻮاْ ٱﻟﱠﺮ ْﲪَـٰ َﻦ أ َّ�ً ﱠﻣﺎ ﺗَ ْﺪﻋُﻮاْ ﻓَـﻠَﻪُ ٱﻷ‬
‫ﱠ‬
6

ِ ‫ٱﳊﻤ ُﺪ ِﱠﻪﻠﻟِ ٱﻟﱠ ِﺬى َﱂ ﻳـﺘ‬ ِ ‫ُﲣﺎﻓِﺖ ِﻬﺑﺎ وٱﺑـﺘ ِﻎ ﺑـ‬


‫ﱠﺨ ْﺬ َوﻟَﺪاً َوَﱂ ﻳَ ُﻜ ْﻦ‬ َْ ْ َْ ‫ﻚ َﺳﺒِﻴﻼً۞ َوﻗُ ِﻞ‬ َ ‫ﲔ ٰذﻟ‬ َْ َ َْ َ َ ْ َ
ِ
﴾ً‫ﻚ وَﱂْ ﻳَ ُﻜ ْﻦ ﻟﱠﻪُ وِﱄﱞ ﱠﻣﻦ ٱﻟ ﱡﺬ ِّل وَﻛِّْﱪﻩُ ﺗَ ْﻜﺒِﲑا‬ ِ ٌ ‫ﻟﱠﻪُ َﺷ ِﺮ‬
َ َ َ َ ‫ﻳﻚ ﰱ ٱﻟْ ُﻤ ْﻠ‬
Wabialhaqqi anzalnahu wabialhaqqi nazala wama arsalnaka illa mubashshiran
wanadheeran, Waqur-anan faraqnahu litaqraahu AAala alnnasi AAala mukthin
wanazzalnahu tanzeelan, Qul aminoo bihi aw la tu/minoo inna alladheena ootoo
alAAilma min qablihi idha yutla AAalayhim yakhirroona lil-adhqani sujjadan;
Wayaqooloona subhana rabbina in kana waAAdu rabbina lamafAAoolan;
Wayakhirroona lil-athqani yabkoona wayazeeduhum khushooAAan; Quli odAAoo
Allaha awi odAAoo alrrahmana ayyan ma tadAAoo falahu al-asmao alhusna wala
tajhar bisalatika wala tukhafit biha waibtaghi bayna dhalika sabeelan, Waquli
alhamdu lillahi alladhee lam yattakhidh waladan walam yakun lahu shareekun fee
almulki walam yakun lahu waliyyun mina aldhdhulli wakabbirhu takbeeran (Surat
Al Isra 17:105-111)

Tafsir: Na kwa haki tumeiteremsha chini (Hii Qur’an) na kwa haki imeshuka, na
tumekutuma wewe (Muhammad) si kwa chochote isipokua kwa ajili ya kuweka wazi
na kuonya. Na hii Qur’an ambayo tumeigawa (katika aya na sura tofauti) ili upate
kuisoma kwa watu kwa makusudio. Na tumeishusha hii (Qur’an) kwa vituo (tofauti).
Sema (Ewe Muhammad): ‘Iaminini au msiiamini. Kwani kwa hakika wale waliopewa
Ilm kabla yake (Ilm ya Ahl Al Kitab kina Abd Allah Ibn Salam, Salman Al Farsi n.k)’
waliposomewa, walianguka chini kwa nyuso zao kwa Unyenyekevu wa Kusjudu. Na
wakasema: ‘Utukufu ni Wa Allah Pekee. Ahadi ya Mola wetu ni lazime iwe ni yenye
kutekelezwa’. Na wakaanguka kwa nyuso zao wakilia machozi na hii ilizidisha
Unyenyekevu wao. Sema (Ewe Muhammad) Muombeni Allah, au muombeni Ar
Rahmani, au kwa jina lolote (Katika Majina yake Matukufu), kwani kwake yeye ndio
kwenye umiliki wa Majina Matukufu, na Salini bila ya kufanya kelele au kwa sauti ya
chini, bali fuateni njia ya baina yake (hali hizo mbili). Na semeni, shukrani zote
anastahiki Allah ambae hana mtoto, na wala hana mshirika katika Ufalme wake, na
ni asiekua (na uhitaji wa) Msaidizi wala Mlinzi. Na Mkuzeni kwa Takbir.

ALLAHU AKBAR!
7

YALIYOMO

YALIYOMO ........................................................................................................... 7
VITABU VILIVYOTANGULIA VYA AL MUSTAKSHIF ABU MANAL
DANAH: .............................................................................................................. 12
UTANGULIZI...................................................................................................... 13
SURA YA KWANZA ............................................................................................ 19
MUONGOZO, MANUFAA, TIBA NA REHMA ZILIZOMO NDANI YA
QUR’AN. ............................................................................................................. 20
HIKMA NA BARAKA NDANI YA QUR’AN ........................................................ 28
MAFUMBO NA MITHALI ZILIZOMO NDANI YA QUR’AN. ........................... 34
AINA ZA KALIMAT (KAULI) NDANI YA QURÁN ............................................ 52
MANUFAA YA KUTAWANYIKA NA KUTEMBEA ARDHINI KULINGANA NA
QUR’AN. ............................................................................................................. 56
UMUHIMU WA HIJRA KATIKA ISLAM ........................................................... 66
MAUMBILE YA NYOYO ZA IBN ADAM: AL QALB, AL FUAD, AL LUBB, AL
SADR NA AN NAFS KATIKA QURÁN ............................................................... 74
AL QALB ............................................................................................................. 75
AL FUAD ............................................................................................................ 88
AL LUBB ............................................................................................................. 89
AL SADR ............................................................................................................. 90
MAANA YA AQL, HIJR, HILM, NNUHA NA BALU. ......................................... 95
NAFSI – MAUMBILE YAKE NA UHIBITI WAKE. .......................................... 102
KUSUDIO LA ALLAH SUBHANAH WA TA’ALA KUTUMA MITUME KWA
WAJA WAKE. .................................................................................................... 105
MITUME NA MANABII WALIOTAJWA KATIKA QURÁN. ............................ 115
MAANA YA MIUJIZA. ...................................................................................... 128
SURA YA PILI ................................................................................................... 136
ULUU AL A’AZMI MINA AL RUSUL .............................................................. 137
NAJIYYU ALLAH NUH AÁLAYHI SALATU WA SALAAM.............................. 142
8

MASIKITIKO YA NABII NUH KWA MOLA WAKE DHIDI YA WATU


WAKE........................................................................................................... 151
KUGHARIKISHWA KWA WATU WA NABII NUH ............................... 173
AL FULKA - SAFINA YA NABII NUH. ..................................................... 176
UMMAH MPYA WA NABII NUH BAADA YA GHARIKA. .................. 197
SIFA KUU ZA NABII NUH AMBAZO HAKUWAHI KUA NAZO IBN
ADAM MWENGINE ................................................................................... 211
KUVUKA MIPAKA KWA DHAMBI ZA WATU WA NABII NUH ........ 218
KHALILU ALLAH IBRAHIM AÁLAYHI SALATU WA SALAAM..................... 239
HIJRA YA NABII IBRAHIM KUTOKA KATIKA MJI WA UR
KUELEKEA FALESTINA........................................................................... 286
HIJRA YA NABII IBRAHIM KUTOKA JERUSALEM KUELEKEA
MISRI............................................................................................................ 294
KHALIL ALLAH IBRAHIM NA WATU WA NABII LUT....................... 305
KHALIL ALLAH NA DHABIHU ALLAH ................................................ 356
KHITAN YA WANAWAKE KATIKA UISLAM. ..................................... 361
GHIRA NA HASAD KATIKA UISLAM. ................................................... 365
KHALIL ALLAH NA MJI WA MAKKAH AL MUKARRAMAH. .......... 385
UJENZI WA BAYTU ALLAH AL HARAM .............................................. 405
MILLAT IBRAHIMA .................................................................................. 424
SIRI NA HIKMA YA IBADA YA HIJA KULINGANA NA MITIZAMO
YA WANAZUONI. ...................................................................................... 439
SIFA KUU ZA NABII IBRAHIM................................................................ 461
KALLIMU ALLAH MUSA IBN AMRAN AÁLAYHI SALATU WA SALAAM .... 466
SURAT TA-HA, HARFU MUQATTAA’AT NA KISA CHA NABII
MUSA. .......................................................................................................... 470
ASILI YA FIR’AWN NA HAMMAN. ........................................................ 496
KUZALIWA KWA NABII MUSA. ............................................................. 502
KULELEWA NABII MUSA NA ASIYAH BINT MUZAHIM NA
FIR’AWN...................................................................................................... 507
9

HIJRA YA KWANZA YA NABII MUSA KUTOKA MISRI KUELEKEA


MADYAN. .................................................................................................... 520
MAISHA YA NABII MUSA KATIKA MJI WA MADYAN. .................... 534
FIMBO YA NABII MUSA........................................................................... 544
HIJRA YA PILI YA NABII MUSA KUTOKA MADYAN KUELEKEA
MISRI............................................................................................................ 546
UKARIBU WA ALLAH SUBHANAH WA TA’ALA KWA NABII MUSA
NABII HARUN NA VIUMBE WAKE KWA UJUMLA. ........................... 588
UTUKUFU WA AYAT AL KURSIY.......................................................... 592
FADHILA ZA AYAT AL KURSIY ............................................................ 605
NABII MUSA NA NABII HARUN WAKABILIANA NA FIR’AWN. ..... 609
MAKABILIANO BAINA YA NABII MUSA NA NABII HARUN DHIDI
YA WACHAWI WA FIR’AWN. ................................................................. 635
MAANA NA TOFAUTI BAINA YA MUUJIZA, UCHAWI NA
KARAMA. .................................................................................................... 646
VIFO VYA MSUSI WA BINTI FIR’AWN NA ASIYAH BINT
MUZAHIM. .................................................................................................. 660
KISINGIZIO CHA FIR’AWN CHA KUMTAFUTA MUUMBA. ............. 663
AYAT KAWNIYAH NA UTHIBITISHO WA KUWEPO KWA
MUUMBA. ................................................................................................... 668
1-DALILI KATIKA KUUMBWA MBINGU NA ARDHI ......................... 670
2-DALILI KATIKA KUUMBWA USIKU NA MCHANA ........................ 680
MAANA YA LIBAS KATIKA USIKU, KATIKA NDOA NA KATIKA
TAQWA ........................................................................................................ 690
3-DALILI KATIKA UUMBWAJI WA BAHARI. ...................................... 704
4-DALILI KATIKA UNYESHAJI WA MVUA. ......................................... 710
5-DALILI KATIKA UUMBWAJI WA WANYAMA MBALI MBALI. .... 719
6-DALILI KATIKA MAUMBILE YA HALI YA UPEPO WA
ALRIYYAH .................................................................................................... 724
DALILI KATIKA MAUMBILE YA HALI YA UPEPO WA RIHAN ....... 727
10

USAWIA WA MIZANI KATIKA MAUMBILE YA VILIVYOMO


ULIMWENGUNI. ........................................................................................ 738
MIUJIZA TISA YA NABII MUSA KWA FIR’AWN NA WATU
WAKE........................................................................................................... 742
HIJRA YA TATU YA NABII MUSA – MUUJIZA WA KUPASUKA KWA
BAHARI NA KUANGAMIA KWA FIR’AWN NA JESHI LAKE. ........... 756
MUNAJAT NABI MUSA KATIKA KUKABIDHIWA TAWRAT. ............ 778
MUNAJAT NABI MUSA: MITHILI YA TAWRAT NDANI YA
QUR’AN. ...................................................................................................... 788
SAMIRII, ATHARI RASULI NA NDAMA WA DHAHABU WA BANI
ISRAIL .......................................................................................................... 802
QARUN, MALI ZAKE NA KIBRI CHAKE. .............................................. 824
WATU WA BANII ISRAIL NA FADHILA WALIZOPEWA NA MOLA
WAO ............................................................................................................. 838
UHAI NA MAISHA YA AL KHIDHR. ...................................................... 850
QISA AL MUSTAQILLA - NABII MUSA NA AL KHIDHR ................... 868
NABII MUSA NA BAQARATUN SAFRAU - KISA CHA NG’OMBE WA
BANI ISRAIL. .............................................................................................. 896
MADHARA YA UBAKHILI NA FAIDA YA KUTOKUA NA UBAKHILI
KATIKA JAMII. ........................................................................................... 912
AMRISHO LA KWANZA LA BANII ISRAIL KUINGIA KWENYE
ARDHI TAKATIFU. .................................................................................... 920
MAUTI YA NABII HARUN NA NABII MUSA ........................................ 927
AMRISHO LA PILI LA BANII ISRAIL KUINGIA KWENYE ARDHI
TAKATIFU NA NAMNA WALIVYOBADILISHA AMRISHO. .............. 930
NAMNA MAYAHUDI NA MANASARA WALIVYOBADILISHA
MANENO NDANI YA VITABU VYAO ASILIA. ..................................... 948
KAULI, WASIA NA MAFUNZO YALIYOMO NDANI YA KISA CHA
NABII MUSA. .............................................................................................. 954
HITIMISHO LA JUZUU YA KWANZA. ................................................... 963
MARUDIO YA VITABU VILIVYOTUMIKA KATIKA KITABU HIKI: 963
11

MARUDIO YA MTANDAO VILIVYOTUMIKA KATIKA KITABU


HIKI .............................................................................................................. 965
12

VITABU VILIVYOTANGULIA VYA AL MUSTAKSHIF ABU MANAL DANAH:



1- IJTIHAD NA TAQLID HISTORIA YA UISLAM: MAIMAMU NA MADHHAB


YAO KATIKA UISLAM - TOLEO LA KWANZA - MWAKA - 1435 AL HIJRA
(2014).

2- IJTIHAD NA TAQLID HISTORIA YA UISLAM: MAIMAMU NA MADHHAB


YAO KATIKA UISLAM - TOLEO LA PILI - MWAKA - 1437 AL HIJRA
(2016).

3- IJTIHAD NA TAQLID HISTORIA YA UISLAM: MAIMAMU NA MADHHAB


YAO KATIKA UISLAM - TOLEO LA TATU - MWAKA 1439 AL HIJRA
(2018).

4-TAFSIR SURAT YUSUF – AHSAN AL QASAS - MWAKA 1441 AL HIJRA


(2020).

Vitabu hivyo vyote vilivyotangulia pamoja na hiki vinapatikana bure Mtandaoni,


ukiandika kwenye Google na kutafuta basi utavipata.

13

UTANGULIZI



‫ﺎب َﻣﺎ َﻛﺎ َن َﺣ ِﺪﻳﺜﺎً ﻳـُ ْﻔﺘَـَﺮ ٰى َوﻟَـٰﻜِﻦ‬ِ ‫ﺼ ِﻬﻢ ِﻋْﺒـﺮةٌ ﻷُوِﱃ ٱﻷَﻟْﺒ‬
َ ْ َ ْ ‫ﺼ‬
ِ َ‫﴿ﻟََﻘ ْﺪ َﻛﺎ َن ِﰱ ﻗ‬
َ
﴾‫ﻴﻞ ُﻛ ِّﻞ َﺷ ْﻲ ٍء َوُﻫ ًﺪى َوَر ْﲪَﺔً ﻟَِّﻘ ْﻮٍم ﻳـُ ْﺆِﻣﻨُﻮ َن‬ ِ ِ ِ ‫ﺗَﺼ ِﺪ‬
َْ َ‫ﻳﻖ ٱﻟﱠﺬى ﺑـ‬
َ ‫ﲔ ﻳَ َﺪﻳْﻪ َوﺗَـ ْﻔﺼ‬ َ ْ
Laqad kana fee qasasihim AAibratun li-olee al-albabi ma kana hadeethan yuftara
walakin tasdeeqa alladhee bayna yadayhi watafseela kulli shay-in wahudan
warahmatan liqawmin yu/minoona (Surat Yusuf 12:111)

Tafsir: Kwa Hakika katika Visa vyao, kuna mafunzo kwa watu wenye kufahamu,
Haikua (hii Quran) Hadith ya kughushi, bali ni Usadikisho wa Vitabu (Zabur,
Tawrat, Injil n.k vilivyopo vya Allah) wenye maelezo ya kina juu ya kila kitu na
Muongozo na Rehma kwa Ummah wa Walioamini.


ِ ِِ ْ ﴿
﴾‫ﲔ‬ ِّ ‫ٱﳊَ ْﻤ ُﺪ ﱠﻪﻠﻟ َر‬
َ ‫ب ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬
Alhamd Lillah Rabbi Al Aálamin!

Awali namshukuru Allah Subhanahu wa Ta’ala na kumuombea Rehma na Amani M-
bora na Mtukufu wa viumbe, Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam.

Pili namshukuru Allah Subhanahu wa Ta’ala kwa kutujaalia kua ni wenye kuingizwa
kwenye Rehma zake kwa kujaaliwa kupata Muongozo wake na hivyo kua ni wenye
kumuamini yeye na Mtume wake Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam, na kwa
kunineemesha nafasi hii yenye manufaa na kisha kuniwezesha kua ni mwenye uwezo wa
kujaribu kuandika kwa mara nyengine tena. Namuomba Allah Subhanahu wa Ta’ala
atunufaishe kwa yale mambo yenye manufaa ndani ya kitabu hiki na pia yale
yaliyokuwemo katika maisha yetu na pia atuepushe na yale yasiyokua na manufaa
nasi..Aamiin.
14

Tunapoiangalia Qurán ambayo ni kitabu kitukufu cha Allah Subhanah wa Ta’ala basi
tunaona kua ndani yake imezungumzia mambo mengi sana yenye manufaa katika maisha
ya Ibn Adam, ikiwemo maamrisho, makatazo na pia visa kadhaa ndani yake, na pale
iliposhuka na kuelezea baadhi ya visa vya Manabii na Mitume basi ilikua na ujumbe wa
kumpa nguvu, utulivu na kumliwaza mpokeaji wake ambae ni Nabii Muhammad
Salallahu A’layhi wa Salam na vile vile Waislam wote kwa ujumla na hivyo tuweze
kutafakkar na kua na ustahmilivu na subra katika mitihani tutakayo kumbana nayo katika
kipindi cha mpito cha uhai wa hapa Ulimwenguni kwa ujumla, ambapo hatukuletwa kwa
ajili ya kucheza, kwani tumeletwa kwa ajili ya kumuabudu Mola wetu na kua katika
mapigano dhidi ya Iblis na pia dhidi ya Matamani ya Nafsi zetu.

Kwani ukweli ni kua katika kipindi cha karne yetu tunayoishi basi Waislam wengi
wamekua ni wenye kuishi kimazoea badala ya kua ni wenye kuishi kulingana na Ilm ya
dini yao kwa kutumia njia na mifano iliyoainishwa ndani ya Quran na Sunnah, na
Waislam hivyo kua katika hali na mazingira yanayosikitisha Kidini, Kielimu, Kiafya,
Kiufahamu, Kimamlaka, Kiuchumi, n.k na hivyo ni kuonekana kua ni dhalili na wenye
kukosa subra, ustahmilivu mkubwa pale inapokosekana msaada wenye manufaa kwao
katika kutatua matatizo yao ambayo mengi hua ni yenye kutokana na mapambo ya
kidunia kiasi ya kua wanafikia kuitumia Dini yao kwa ajili ya manufaa yao ya kidunia na
hivyo kua ni wenye kukaribia kuingia katika ile hali ambayo imeelezewa na aya ifuatayo:

‫َﺻﺎﺑَﻪُ َﺧْﻴـٌﺮ اﻃْ َﻤﺄَ ﱠن ﺑِِﻪ ۖ َوإِ ْن‬ ٍ ِ ‫﴿ َوِﻣ َﻦ اﻟﻨ‬


َ ‫ﱠﺎس َﻣﻦ ﻳَـ ْﻌﺒُ ُﺪ اﻟﻠﱠـﻪَ َﻋﻠَ ٰﻰ َﺣْﺮف ۖ ﻓَِﺈ ْن أ‬
ِ ِ
‫اﳋُ ْﺴَﺮا ُن‬ْ ‫ﻚ ُﻫ َﻮ‬ َ ‫ﺐ َﻋﻠَ ٰﻰ َو ْﺟ ِﻬ ِﻪ َﺧ ِﺴَﺮ اﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ َو ْاﻵ ِﺧَﺮ َة ۚ َٰذﻟ‬
َ َ‫َﺻﺎﺑَـْﺘﻪُ ﻓْﺘـﻨَﺔٌ اﻧ َﻘﻠ‬
َ‫أ‬
﴾‫اﻟْﻤﺒِﲔ‬
ُ ُ
Wamina alnnasi man yaAAbudu Allaha AAala harfin fa-in asabahu khayrun
itmaanna bihi wa-in asabat-hu fitnatun inqalaba AAala wajhihi khasira alddunya
waal-akhirata Dhalika huwa alkhusranu almubeenu.(Surat Al Hajj 22:11)

Tafsir: Na miongoni mwa watu ni wale ambao Wanamuabudu Allah wakiwa


Ukingoni, hivyo kama akifikwa na Mema basi hua ni mwenye kuridhia, lakini
akifikwa na Mitihani basi hua ni mwenye kugeuza uso wake (hua na shaka na hivyo
hua ni mwenye kukosa Imani na Mola wake) hula hasara hapa Duniani na Akhera.
Huko hua ni kula hasara sana kuliko wazi.

Ama kuhusiana na ayah hii basi anasema Jarra Allah, Sultan Al Balagha Imam Abu Al
Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Neno ‘Harfin’ lililotumika katika ayah hii linamaanisha
15

hali ya mtu ambae hayupo katikati ya dini, yaani yupo pembeni kabisa kama vile
mtu anaeenda vitani kisha akakaa kwenye mstari wa nyuma kabisa huku akisubiri
watu wakishinda basi akimbilie ngawira na wakishindwa basi awe ni wa mwanzo
kukimbia’

Yaani hawa ni watu ambao Imani zao zimekua dhaifu na ingawa wanamuabudu Allah
Subhnah wa Ta’ala lakini hata hivyo hawana Imani thabit katika nyoyo zao kwani Nuru
ya Dini yao katika nyoyo zao ni dhaifu kiasi ya kua akipata mtihani mdogo tu basi
anaweza kua ni mwenye kuangukia katika hali mbaya ya kuiuza dini yake na hivyo kua
ni miongoni mwa wenye sifa ya unafiq.

Allah Subhanah wa Ta’ala ni mwenye kuwapima waja wake kwa kuwapa mitihani katika
mazingira tofauti kama alivyotuonesha kupitia katika viza vilivyomo ndani ya Qur’an
hivyo unapofuatilia njia na mifano iliyomo ndani ya Qurán basi unaona kua ingawa
Qurán imezungumzia visa vingi katika sura zake mbali mbali ambapo hapo hapo hakuna
kujirudia rudia kwa visa hivyo wala kupingana kwa visa hivyo katika kuvielezea kwake,
lakini kuelezewa kwa visa hivyo kamwe hakukuwa ni kwa ajili ya kutuelezea historia au
kutuburudisha kwa hadith zake tu, bali ni kwa ajili ya kutoa mifano yenye mafunzo na
pia yenye maonyo kwa kutuonesha namna Allah Subhanah wa Taála anavyowapenda,
anavyowahurumia na kuwajali waja wake wanaomtii kumshukuru na namna
anavyowaonya kabla ya kuwaadhibu wale wenye kumuasi na kumkufuru na ndio maana
akawa ni mwenye kutuhimiza kumtii kwa kutuambia:

‫ﺖ ﻟِﻐَ ٍﺪ َوٱﺗﱠـ ُﻘﻮاْ ﱠ‬


‫ٱﻪﻠﻟَ إِ ﱠن ﱠ‬
َ‫ٱﻪﻠﻟ‬ ْ ‫ﱠﻣ‬
َ ‫ﺲ ﱠﻣﺎ ﻗَﺪ‬
ٌ ‫ﻔ‬
ْ ‫ـ‬
َ‫ﻧ‬ ‫ﺮ‬ُْ‫ﻈ‬ ‫ﻨ‬َ‫ﺘ‬ْ‫ﻟ‬‫و‬َ ‫ٱﻪﻠﻟ‬
َ ‫ﱠ‬ ‫ا‬
ْ‫ﻮ‬‫ﻘ‬ُ ‫ﱠ‬
‫ـ‬‫ﺗ‬ ‫ٱ‬ ‫ا‬
ْ‫ﻮ‬ُ‫ﻨ‬‫آﻣ‬
َ ‫ﻳﻦ‬
َ ‫ﺬ‬ِ ‫﴿ ٰ�َﻳـﱡﻬﺎ ٱﻟﱠ‬
َ
﴾‫َﺧﺒِﲑٌ ِﲟَﺎ ﺗَـ ْﻌﻤﻠُﻮ َن‬
َ
Ya ayyuha alladheena amanoo ittaqoo Allaha waltandhur nafsun ma qaddamat
lighadin waittaqoo Allaha inna Allaha khabeerun bima taAAmaloona (Surat Al
Hashr 59:18)

Tafsir: Enyi Mlioamini! Muogopeni Allah na tekelezeni majukumu yenu juu yake. Na
kila mmoja wenu aangalie ni nini Nafsi yake imetanguliza kwa ajili ya kesho. Na
Muogopeni Allah. Kwani Kwa Hakika Allah ni mwenye habari juu ya kila
mnachokifanya.

Hivyo mbali ya kua Allah Subhanah wa Taála ni mwenye kutuonya na kutuhimiza


kutekeleza majukumu yetu juu yake kupitia katika kitabu chake kitukufu lakini pia ni
mwenye kutuongoza ndani yake kama alivyosema:
16

‫ٱﻪﻠﻟَ ﺑِ ُﻜ ِّﻞ‬ ِ ِ ‫﴿وﻣﺎ َﻛﺎ َن ﱠ‬


َ ِّ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻟﻴُﻀ ﱠﻞ ﻗَـ ْﻮﻣﺎً ﺑَـ ْﻌ َﺪ إِ ْذ َﻫ َﺪ ُاﻫ ْﻢ َﺣ ﱠ ٰﱴ ﻳـُﺒَـ‬
‫ﲔ َﳍُﻢ ﱠﻣﺎ ﻳَـﺘﱠـ ُﻘﻮ َن إِ ﱠن ﱠ‬ ََ
﴾‫َﺷﻲ ٍء َﻋﻠِﻴﻢ‬
ٌ ْ
Wama kana Allahu liyudhilla qawman baAAda idh hadahum hatta yubayyina
lahum ma yattaqoona inna Allaha bikulli shay-in AAaleemun (Surat At Tawba
9:115)

Tafsir: Na si juu ya Allah kuwapotosha watu baada ya kuwaongoza hadi


akawabainishia ni jambo gani la kujiepusha nalo. Hakika Allah ni mwenye kujua juu
ya kila kitu.

Anasema Imam Ibn Al Mundhir Al Nishapuri kua: ‘Ilikua ni kawaida ya Sahaba Abd
Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu, kuwasomesha darsa wanafunzi wake katika
kila siku ya Alkhamis na kisha baada ya kumaliza darsa basi hua ni mweye kusema:
‘Yeyote yule miongoni mwenu anaetaka kua Mwanazuoni basi na aombe dua juu
ya hilo. Na asiombe chochote baada ya hilo kwa sababu Mwanazuoni na
Mwanafunzi wako sawa kimalipo. Enyi watu mimi sikhofu kua nyie mtaulizwa juu
ya kile ambacho Allah Subhanah wa Taála amekuwekeeni wazi juu yenu, kwani
amesema: ‘Wama kana Allahu liyudhilla qawman baAAda idh hadahum hatta
yubayyina lahum ma yattaqoona inna Allaha bikulli shay-in AAaleemun’ yaani, Na si
juu ya Allah kuwapotosha watu baada ya kuwaongoza hadi akawabainishia ni
jambo gani la kujiepusha nalo. Hakika Allah ni mwenye kujua juu ya kila kitu.’ ’

Hivyo ni wajibu wetu kuachana na kuepukana na kuishi kimazoea na badala yake


tujitahid kushikamana na njia na mifano iliyomo ndani ya Qur’an, na Sunnah za Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam na pia kushikamana na ufafanuzi wa Wanazuoni wa
skuli za Madhhab na mitazamo yao juu ya Vitu viwili hivyo ambavyo ndio vyanzo vya
Hukmu na Sharia vinavyotuongoza kidini katika njia iliyonyooka na hivyo kua ni wenye
kudumu katika njia ya uongofu.

Mpangilio wa Kitabu hiki kimegawika katika sura mbili ambapo katika Sura ya Kwanza
inazungumzia juu umuhimu wa kuisoma, kuifahamu na kuizingatia Qur’an kwa kina ili
kuweza kua ni wenye kunufaika na Mafunzo, Hikma na Busara zilizomo ndani yake na
nimeyaelezea haya kabla ya kuingia katika Sura ya Pili ambamo ndani yake ndio mna
Visa vya Manabii na Mtume Watano Waliokua na Azma kubwa zaidi katika Maisha yao
na kujaribu kufafanua historia zao, mitihani yao, subra na ustahmilivu wao uliotokana na
17

kua na Nuru ya Iman kwa Mola wao katika Vifua, Nyoyo na Nafsi zao na kua na
misimamo imara na hivyo kua ni mifano bora kwetu kutokana na yaliyomo ndani yake.

Na ingawa Mitume hao wako watano ambao ni Nabii Nuh Alayhi Salam, Nabii Ibrahim
Alayhi Salam Nabii Musa Alayhi Salam, Nabii Isa Ibn Mayram Alayhi Salam na
Muhammad Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, lakini hata hivyo katika kitabu hiki
sikuweza kuwaeleza Mitume hao wote, kwani nimewaelezea Mitume watatu tu ambao ni
Nabii Nuh Alayhi Salam, Nabii Ibrahim Alayhi Salam Nabii Musa Alayhi Salam.

Na hii ni kwa sababu ya kua kama ningewaelezea wote kwa pamoja katika kitabu kimoja
basi Kitabu kingekua kikubwa sana yaani kingekaribia kurasa 2000, hivyo nimeona bora
nikigawe mara mbili kwa kutoa juzuu ya kwanza ili kurahisisha usomaji, na uzingatiaji
wa ujumbe uliomo ndani yake kwanza, na bila ya shaka kama Allah Subhanah wa Ta’ala
akiniwezesha Isha In-shaa Allah basi nitatoa Juzuu ya pili ambayo ndani yake
nitamuelezea Nabii Isa Ibn Maryam Alayhi Salam na Nabii Muhammad Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam na hivyo namuomba Allah Subhanah wa Ta’ala aniwezeshe
kutekeleza ahadi yangu hio.

Hivyo kama tukizingatia mafunzo yaliyomo ndani yake basi tutakua ni wenye kunufaika
na mengi sana hususan katika wakati huu wa mitihani ndani ya Uhai wetu, kwani
kitatuongezea Imani kwenye Nafsi na Nyoyo zetu na kutupa Muongozo stahiki katika
kupigana vita dhidi ya uadui wa ndani kutoka katika Nafsi zetu na uadui wa nje
unaotokana na Shaytan na wafuasi wake wanaotuzunguka katika mazingira yetu kwani
anasema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

‫ﻳﻦ َﳜْ َﺸ ْﻮ َن‬ ِ ‫ﻳﺚ ﻛِﺘﺎﺎﺑً ﱡﻣﺘﺸ ِﺎﻬﺑﺎً ﱠﻣﺜ ِﺎﱏ ﺗَـ ْﻘﺸﻌِﱡﺮ ِﻣْﻨﻪ ﺟﻠُ ﱠ‬ ِ ِ ‫﴿ﱠ‬
َ ‫ﻮد ٱﻟﺬ‬
ُ ُ ُ َ َ َ َ َ َ ‫َﺣ َﺴ َﻦ ٱ ْﳊَﺪ‬ ْ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻧَـﱠﺰَل أ‬
‫ٱﻪﻠﻟِ ﻳَـ ْﻬ ِﺪى ﺑِِﻪ َﻣﻦ‬
‫ﻚ ُﻫ َﺪى ﱠ‬ ِ ِ‫رﺑـﱠﻬﻢ ﰒُﱠ ﺗَﻠِﲔ ﺟﻠُﻮدﻫﻢ وﻗُـﻠُﻮﺑـﻬﻢ إِ َ ٰﱃ ِذ ْﻛ ِﺮ ﱠ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟ ٰذﻟ‬ ْ ُُ َ ْ ُ ُ ُ ُ ُْ َ
﴾‫ٱﻪﻠﻟ ﻓَﻤﺎ ﻟَﻪُ ِﻣ ْﻦ َﻫ ٍﺎد‬ ِ ْ ‫ﻳﺸﺂء وﻣﻦ ﻳ‬
َ ُ‫ﻀﻠ ِﻞ ﱠ‬ ُ ََ ُ َ َ
Allahu nazzala ahsana alhadeethi kitaban mutashabihan mathaniya taqshaAAirru
minhu juloodu alladheena yakhshawna rabbahum thumma taleenu julooduhum
waquloobuhum ila dhikri Allahi dhalika huda Allahi yahdee bihi man yashao
waman yudlili Allahu fama lahu min hadin (Surat Az Zumar 39:23)

Tafsir: Allahu ameshusha hadithi bora kabisa, Kitabu (Quran) chenye sehemu ndani
yake zinazofanana kwa wema na usahih. Ngozi za wale wenye kuomuogopa Allah
zinatetemeka (Wanapoisikia Qurán). Na kisha Nyoyo zao na ngozi zao hulainika
18

kutokana na kumkumbuka Mola wao. Huo ni Uongofu wa Allah. Ambae humuongoza


amtakae na anaepotoshwa na Allah basi hakuna atakaemuongoza.

Namuomba Allah Subhanah wa Ta’ala awe ni mwenye kunifanikishia malengo yangu


ya kuvielezea Visa vya Ulu ul Azmin Minna Rusul Juzuu ya Kwanza na kuinufaisha Nafsi
yangu na kuwanufaisha Waislam wengine wote kwa ujumla kutokana na Mafunzo,
Hikma, Busara na Miongozo inayopatikana ndani yake kulingana na Aya za Quran
Tukufu, Sunnah na Hadith za Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na pia kulingana
na Mitizamo ya Wanazuoni tofauti waliotumia mda wao na Ilm yao katika kuelezea
namna walivyofaham juu ya visa vya Mitume hao husika na hivyo kua ni wenye
kutunifaisha nasi. Na muomba Allah Subahanh wa Ta’ala awalipe kwa jitihada zao na
awazidishie ziada katika amali zao.

Na vile vile namuomba Allah Subhanah wa Ta’ala anisamehe kwa makosa na kasoro
zitakazojitokeza katika jitihada yangu hii kwani ukamilifu ni wake yeye tu, na ni yeye
pekee ndie mwenye kuijua nia yangu katika utekelezaji wa haya nnayoyafanya.

Amiin ya Rabb!

19

SURA YA KWANZA

20

MUONGOZO, MANUFAA, TIBA NA REHMA ZILIZOMO NDANI YA QUR’AN.



Bila ya shaka katika aya za Qur’an nilizoanza nazo ndani ya kitabu hiki na nyenginezo
nyingi zilizomo ndani ya Qura’an tumeona kua Allah Subhanah wa Taála ametuwekea
wazi kua ndani ya kitabu chake mna muongozo wa kina wa kila kitu katika maisha yetu,
ikiwemo pia Muongozo dhidi ya matatizo mbali mbali ya kidunia na kiakhera, lakini hata
hivyo kamwe hatutoweza kuikimbia hali ya matatizo tuliyokua nayo wakati bado tukiwa
ni wenye kuutupa ufunguo unaofungua mlango wa utatuzi wa matatizo hayo, ufunguo
ambao si mwengine bali ni Qurán yenyewe ambayo ndani yake hamna Muongozo tu,
lakini pia mna Kinga, Rehma na Tiba pia ya maradhi tofauti kuanzia ya Kimwili,
Kinyoyo, Kinafsi, Kiroho n.k kama inavyoweka wazi aya ifuatayo:

ِ ِ ُ ‫آن ﻣﺎ ﻫﻮ ِﺷ َﻔﺂء ور ْﲪﺔٌ ﻟِّْﻠﻤ ْﺆِﻣﻨِﲔ وﻻَ ﻳ ِﺰ‬


ِ ِ
َ ‫ﻳﺪ ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
‫ﲔ إَﻻﱠ‬ َ َ َ ُ َ َ َ ٌ َ ُ َ ‫﴿ َوﻧـُﻨَـِّﺰُل ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻘْﺮ‬
﴾ً‫َﺧﺴﺎرا‬
َ
Wanunazzilu mina alqur-ani ma huwa shifaon warahmatun lilmu/mineena wala
yazeedu aldhdhalimeena illa khasaran (Surat Al Isra 17:82)

Tafsir: Na tumeiteremsha hii Qur’an ndani yake mkiwa na Tiba na Rehma kwa
Walioamini, lakini kwa Madhalimu haiwanufaishi na chochote isipokua Hasara.

Naam aya imetumia neno Shifaun ambalo ni lenye kutokana na neno Shafa. Na kwa
kilugha basi neno Shafa hua ni lenye kumaanisha Kuponya, Kutibu, Kurudisha Afya,
Kuridhisha, Kurudisha katika hali yake ya Asili au ya Kimaumbile,na ndio maana wenye
Lugha yao hua wanasema: ‘Shaf’ahu aAn Al Mas-alati’ kumaanisha kua
Amemuondolea Mashaka na kumridhisha Nafsi yake juu ya Jambo fulani.

Anasema Sultan al Mutakallimin Mujaddid ud Din Imam Abu Abd Allah Muhammad
Ibn Umar Ibn Al Husayn Al Taymi Al Bakri Al Tabaristan Fakhr Ad Din Al Razi Al
Shafii kuhusiana na ayah hii kua: ‘Quran ni Tiba ya Kitabia, Kijamii, Kiroho na
Kiafya pia. Na bila ya shaka baadhi ya Aya zake zimebainika kua ni Tibba ya
Maradhi tofauti ya Kimwili’

Ama kwa upande mmoja basi Hujjat Ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Ibn
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii anatuambia
kua miongoni mwa manufaa yanayohitajika kupatikana katika Quran basi ni kujua darja
21

za usomaji wake katika hali tofauti kwa kusema kua: ‘Amesema Amir ul Muuminina
Ali Ibn Abi Talib kua: ‘Yeyote yule atakaesoma Qur’an wakati akiwa amesimama
kwenye Sala basi anapata thawabu 100 kwa kila herufi moja ya Qur’an, na
atakaesoma Qur’an wakati akiwa amekaa kitako ndani ya Sala basi hua ni mwenye
kupata thawabu 50 kwa kila herufi, yeyote yule atakaesoma Qur’an nje ya Sala
akiwa katika hali ya kua na udhu basi hua anapata thawabu 25 kwa kila herufi, na
kwa kila atakaesoma Qur’an bila ya udhu kutokana na kua ni mwenye kuihifadhi
Moyoni mwake basi atapata thawabu 10 kwa kila herufi’

Na kwa Upande mwengine basi Hujjat ul Islami Mujadid Ad Din Imam Abu Hamid
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii basi
anatuwekea wazi namna ya kunufaika na Muongozo, Tiba na Rehma zilizomo ndani ya
Qur’an kwa kutubainishia umuhimu wa kuzifaham siri za ndani na za nje zinazotakiwa
kupatikana katika kisomo cha Qur’an ambazo ni:

1 – Unapoanza kusoma basi inatakiwa uhisi ukubwa na uwezo wa mwenye maneno


hayo ambae ni Allah Subhanah wa Ta’ala. Na athari hio unaweza kuihisi ndani ya
Moyo wako pale unapoanza kuhisi ukubwa wa Arshi na Mamalka yake Duniani na
Mbinguni a kila kilichomo ndani yake wakiwemo viumbe vyake, Ibn Adam, Majini,
Wanyama, na Miti. Unatakiwa ukumbuke kua Muumbaji wa vitu vyote hivyo ni
Mmoja, na Vitu vyote hivyo vimo ndani ya mamlaka yake na uwezo wake. Kuhisi
Neema zake na Reha zake basi kunakupelekea kua ni mwenye kutaka kuzisoma aya
zake na kuona ndani yake Sifa zake, Majina yake, Uzuri wake, Ilm yake na Hikma
zake.

Faham kua kama ilivyokua Qur’an inawezekana kuguswa na wale waliotoharika –


na hivyo kua ni iliyofichikana kwa wasiokua tohara – kwa kimaana na kisiri basi
ndio hivyo hivyo inavyofichikana kutokana na Nyoyo zisizokua Nadhifu.

2 – Unatakiwa utafakkar na kuzingatia maana yake wakati unapokua unaisoma


kama ukitaka kua ni miongoni mwa watu wenye kuisoma Qur’an. Unatakiwa
urudie kila ulichokisoma kwa ulimi wako wakati akili yako ilipokuwa haipo kwenye
kisomo cha aya husika. Kwani haitakiwi kuhesabu kisomo ambacho hakina
mazingatio ndani yake kua ni sehemu ya kufanya amali njema. Kwa sababu ubora
wa kisomo cha Qur’an hua ni katika kuzidisha mazingatio yake. Amesema
Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu kua: ‘Hakuna Ubora katika Amali
njema pale inapokua hakuna ufahamu juu ya Amali hio, na pia katika kisomo
kisichokua na Mazingatio.’
3 – Unatakiwa uwe ni mwenye kuvuna Matunda ya Ilm kutoka katika Matawi yake
na kuyatafutia kutoka katika asili yake zinakopatikana, huku ukiwa ni mwenye
kutafakkar. Usitafute Kinga kutoka katika sehemu ambayo unatafutia hazina, na
22

usitafute Hazina katika sehemu ambayo unatafutia Miski na harufu yake nzuri,
kwani katika kila Tunda basi hua lina tawi lake na kila hazina ina chanzo chake.
Jambo hili hua linarahisika pale unapojua kua kuna aina za aya za Quran
kulingana na kusudio la ujumbe wake kwa mfano:-

A - Aya ambazo zinazomzungumzia Allah Subhanah wa Ta’ala, Sifa zake na


Vitendo vyake. Hivyo tafuta ndani ya haya Ilm ya kujua Ukubwa na Ufalme wa
Allah Subhanah wa Ta’ala.

B – Aya ambazo zinazungumzia Muongozo wa njia iliyonyooka: Hivyo tafuta ndani


ya haya Ilm ya Rehma zake, Neema zake na Hikma zake.

C – Aya ambazo hua ni zenye kuzungumzia Maangamizo: Hivyo tafuta ndani yake
Ilm ya Uwezo, Ujabari na Utukufu wake Allah Subhanah wa Ta’ala.

D – Aya ambazo hua ni zenye kuzungumzia Maish ya Mitume: hivyo tafuta ndani
yake Ilm ya Huruma na Ukarim wake, Baraka, Neema na Misaada yake kwa waja
wake.

Hivyo kwa kila kusudio basi tafuta manufaa yaliyomo ndani yake kwa kadiri
inavyowezekana.

4 – Inakubidi ujilinde na kila kitu kinachozuia ufahamu wako kwa sababu kitu
hicho hua ndio pazia linalokuzuia kufaham kama alivyosema Allah Subhanah wa
Ta’ala:

‫﴿إِ ﱠ� َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ َﻋﻠَ ٰﻰ ﻗُـﻠُﻮﻬﺑِِ ْﻢ أَﻛِﻨﱠﺔً أَن ﻳَـ ْﻔ َﻘ ُﻬﻮﻩُ َوِﰱ آ َذا�ِِ ْﻢ َوﻗْﺮاً َوإِن ﺗَ ْﺪﻋُ ُﻬ ْﻢ إِ َ ٰﱃ ٱ ْﳍَُﺪ ٰى‬
﴾ً‫ﻓَـﻠَ ْﻦ ﻳَـ ْﻬﺘَ ُﺪ ۤواْ إِذاً أَﺑَﺪا‬
Inna jaAAalna AAala quloobihim akinnatan an yafqahoohu wafee adhanihim
waqran wa-in tadAAuhum ila alhuda falan yahtadoo idhan Abadan (Surat Al Kahf
18:57)

Tafsir: Na kwa hakika sisi tumejaalia katika nyoyo zao mapazia ili wasiifahamu
(Quran), na katika masikio yao uziwi. Na hata kama wewe ukiwaita katika uongofu
basi hawatoongoka Abadan.
23

Faham kua mtu mwenye ufahamu unaomtafuta Mola wake hua unapewa mitihani
ya aina mbili: Aidha hua unakua na mtihani wa kua na shaka na kukanusha ambao
hua ni wenye kuwajaribu wale ambao ni wenye Imani dhaifu. Au hua na mtihani
wa pazia linalojaa matamanio ya Moyo ambalo hua ni lile linalomfunika yule Mtu
mwenye kuiendekeza Dunia.

Ama kuhusiana na Mja ambae ni mwenye Iman na hivyo hua ni mwenye kua na
umakini katika Njia ya Mola wake, basi nao hua na Mapazia ya aina mbili. Ambapo
la kwanza ni vishawishi vya wasi wasi vinavompelekea kutofikiria hata juu ya kutia
katika Ibada husika, kwa mfano jee mwanzo wake ulikuaje Ibada hii, au bado niko
katika Ikhlas?, n.k. Aina ya pili ya vishawishi vya wasi wasi ni vile ambayo hua
vinakutoa katika umakini wa kutamka kwa usahih, na hivyo hukupelekea kua na
wasi wasi na kurudia tena kauli husika katika Ibada. Jambo hili hutokea ndani ya
Sala na nje ya Sala pia.

Jee itakuaje siri za Ufalme wa Allah Subhanah wa Ta’ala zipatikane na Moyo ambao
umakini wae upo katika kuhisi ni namna gani Midomo inafunga na kufunguka na
ni vipi Ulimi na Taya zinafanyakazi na hewa inapitaje baina yake?

Aina ya pili ya pazia linalokuwepo kwa Mja mwenye Imani ni pale mtu anapokua
hajui maana ya ndani ya kina cha aya za Qur’an. Kwani hali hii huuzuia ufaham
wake, kwani Allah Subhanah wa Ta’ala amemuamrisha Mja wake kua ni mwenye
kumuamini kulingana na hali ya vigezo tofauti ambavyo hua vipi katika ufahamu
wa juu juu na ufaham wa kina zaidi kama mfupa na nyama nyama iliyomo ndani
ya Mfupa kwa mfano: Allah Subhanah wa Ta’ala amewataka waja wake wawe ni
mwenye kuamini kua ni anaweza kuonekana, lakini hata hivyo kuonekana hua
kuna aina mbili ambazo ni:

Kama mtu atakua anaamini kua kumuona Allah Subhanah wa Ta’ala ni sawa na
kuoa kwa kutumia macho kama tunavyoona Ibn Adam Ulimwenguni basi
anategemea kujua nini juu ya siri ya Allah Subhanah wa Ta’ala pale aliposema:

ۤ ِ ‫ﺎل ر‬ ِ ِ ِ ‫﴿وﻟَ ﱠﻤﺎ ﺟﺂء ﻣ‬


‫ﺎل ﻟَﻦ ﺗَـَﺮ ِاﱏ‬ َ َ‫ﻚ ﻗ‬ َ ‫ب أَِرِﱐ أَﻧﻈُْﺮ إِﻟَْﻴ‬ ّ َ َ َ‫ﻮﺳ ٰﻰ ﻟﻤﻴ َﻘﺎﺗﻨَﺎ َوَﻛﻠﱠ َﻤﻪُ َرﺑﱡﻪُ ﻗ‬
َ َُ َ َ
‫ف ﺗَـَﺮ ِاﱏ ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ َﲡَﻠﱠ ٰﻰ َرﺑﱡﻪُ ﻟِﻠْ َﺠﺒَ ِﻞ‬ ِ ْ ‫َوﻟَـٰ ِﻜ ِﻦ اﻧْﻈُْﺮ إِ َﱃ‬
ْ ‫اﳉَﺒَ ِﻞ ﻓَِﺈن‬
َ ‫اﺳﺘَـ َﻘﱠﺮ َﻣ َﻜﺎﻧَﻪُ ﻓَ َﺴ ْﻮ‬
‫ﻚ َوأ ََ�ْ أَﱠو ُل َﺟ َﻌﻠَﻪُ َد ّﻛﺎً َو َﺧﱠﺮ‬ َ ‫ﺖ إِﻟَْﻴ‬
ُ ‫ﻚ ﺗُـْﺒ‬َ َ‫ﺎل ُﺳْﺒ َﺤﺎﻧ‬َ َ‫ﺎق ﻗ‬َ َ‫ﺻﻌِﻘﺎً ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺂ أَﻓ‬
َ ‫ﻣﻮﺳ ٰﻰ‬
َ
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ٱﻟْ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬
24

Walamma jaa moosa limeeqatina wakallamahu rabbuhu qala rabbi arinee andhur
ilayka qala lan taranee walakini ondhur ila aljabali fa-ini istaqarra makanahu
fasawfa taranee falamma tajalla rabbuhu liljabali jaAAalahu dakkan wakharra
moosa saAAiqan falamma afaqa qala subhanaka tubtu ilayka waana awwalu
almu/mineena (Surat Al Araf 7:143)

Tafsir: Na kisha akaja Musa katika eneo na mda maalum tuliompangia na


akazugungumza na Mola wake, (Nabii Musa)akasema : ‘Ewe Mola wangu Nioneshe
nipate Nikuone’ Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Huwezi kuniona, lakini
angalia Mlima, kama utabakia katika sehemu yake. Basi nawe utaweza utaniona’
Kisha alipouonesha Utukufu wake Mola wake kwa Mlima, akaujaalia kua ni wenye
kupukutika na kua vumbi. Na akaanguka nakupoteza faham Musa. Kisha
alipozindukana akasema: ‘Utukufu ni wako, Mimi Natubu kwako na hakika mimi ni
wa awali miongoni mwa Walioamini’

Na jee mtu huyo atafaham vipi kua haiwezekani kumuona kwa macho kama
tunavyoona katika Ulimwengu huu kwani jicho la kutizamia Ulimwengu hua
haliwezi kuona kila kitu, kila sehemu na kila upande, na jee atafaham vipi maana
ya maana ya maneno ya Allah Subhanah wa Ta’ala pale aliposema:

﴾‫ٱﳋَﺒِﲑ‬ ِ
ُ ْ ‫ﻴﻒ‬ ُ ‫ﺼ َﺎر َوُﻫ َﻮ ٱﻟﻠﱠﻄ‬ َ ْ‫﴿ﻻﱠ ﺗُ ْﺪ ِرُﻛﻪُ ٱﻷَﺑ‬
َ ْ‫ﺼ ُﺎر َوُﻫ َﻮ ﻳُ ْﺪ ِرُك ٱﻷَﺑ‬
La tudrikuhu al-absaru wahuwa yudriku al-absara wahuwa allateefu alkhabeeru
(Surat 6:103)

Tafsir: Hakuna Mtizamo utakaoweza kumuona yeye, lakini Mtizamo wake yeye huona
kila kitu. Kwani kwa hakika yeye ni Mpole na mwenye kujua kila kitu.

Aya ambayo inaenda sambamba na kauli yake isemayo:

ِ ٍِ
﴾ٌ‫ﱠﺿﺮةٌ۞ إِ َ ٰﱃ رِّﻬﺑَﺎ َ� ِﻇﺮة‬ ﴿
َ َ َ � ‫ُو ُﺟﻮﻩٌ ﻳَـ ْﻮَﻣﺌﺬ‬
Wujoohun yawma-dhin nadhiratun, Ila rabbiha nadhiratun (Surat Al Qiyamah
75:22-23)

Tafsir: Baadhi ya Nyuso siku hio zitang’ara, kutokana na kumuangalia Mola wao.
25

5 – Hutakiwi kua ni mwenye kufuatilia juu ya kupata Nuru ya Qur’an tu, lakini pia
unatakiwa upate hisia na athari zinazotakiwa kupatikana katika kuisoma Qur’an.
Hivyo usiisome aya bila ya kua si mwenye kujipamba na sifa zake. Kutokana na
kua na hali hio basi utakua ni mwenye kufaham na kuhisi athari ya kila aya
unayoisoma, kiasi ya kua rehma na usamehevu unapotajwa basi unakua unahisi
utulivu na furaha, na inapotajwa adhabu basi unahisi maumivu na khofu, kutokana
na kutajwa kwa Allah Subhanah wa Ta’ala, na Ukubwa wake na Sifa zake basi wewe
hua ni mwenye kuinamisha kichwa chako kutokana na Unyenyekevu unaouhisi
ndani ya mwili wako, kama vile mtu ambae unaetoweka kutokana na kumuona
Mola wako. Na wanapotajwa Makafiri na Utukufu wa Allah Subhanah wa Ta’ala
wa kua mbali sana na sifa ya kua na Mke na Mtoto basi wewe hua ni mwenye
kuiamisha kichwa chako na kupunguza sauti yako kama vile mtu anaejificha
kutokana na kuona haya isiyokua na kifani.

Athari hisi huonekana wazi kwenye viungo vya mwili wako kama vile kutokwa na
kilio kwa huzuni, kutokwa na jasho kwenye paji la uso kwa kuona aibu mbele ya
Mola wako, kutetemeka kwa furaha ya kuuona Utukufu wa Allah Subhanah wa
Ta’ala na kujisikia raha ndani ya viungo vyako, ulimi wako na sauti unapoona
habari njema ndani ya maneno yake Allah Subhanah wa Ta’ala na kua na khofu
unapoona ndani yake habari zenye kuonya. Kama ikiwa ni mwenye kufanikiwa kua
na hali ya hisia kama hivyo basi utakua ni mwenye kufanikiwa kupata Baraka za
Qur’an.

Kwa upande mwengine basi Shifaa na Rehma za Qur’an sio kua zinapatikana kutokana
na kuisoma na kuifanyia kazi tu lakini pia hua zinapatikana kwa kuisikiliza Qur’an
yenyewe pale inapokua inasomwa na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akasema
katika Qur’an:

ِ ‫ئ ٱﻟْ ُﻘﺮآ ُن ﻓَﭑﺳﺘَ ِﻤﻌﻮاْ ﻟَﻪ وأ‬


﴾‫َﻧﺼﺘُﻮاْ ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜﻢ ﺗـُﺮ َﲪُﻮ َن‬ ِ﴿
ْ ْ َُ ُ ْ ْ َ ‫َوإذَا ﻗُِﺮ‬
Wa-idha quri-a alqur-anu faistamiAAoo lahu waansitoo laAAallakum turhamoona
(Surat At Aaraf 7:204)

Tafsir: Kwa hivyo inaposomwa Quran isikilizeni, na mkae kimya kwa umakini ili
mpate kua ni wenye kurehemewa.

Abd Allah Ibn Masoud Radhi Allahu Anhu, anasema kuhusiana na ayah hii kua:
‘Inaposomwa Quran basi mnatakiwa mkae kimya huku mkiisikiliza kwa umakini
na kuitafakkari.’
26

Mtizamo wa Sahaba Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu ni mtizamo ambao
haujaachana na mtizamo wa Hujjat ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn
Muhammad Al Ghazali. Hivyo tuiangalie ayah hii kulingana na mtizamo mwengine
ambao unatuthibitishia athari ya Qur’an katika miili yetu pale unapotulia na kuisikiliza,
na ili kufaham vizuri zaidi basi kwanza inabidi tufahamu kuhusiana na mawimbi ya
umeme yanayosambaza hisia za mawasiliano katika Ubongo wa miili yetu.

Katika kusafirisha hisia mbali mbali ndani ya miili yetu basi Ubongo hua unazalisha
nguvu ya mawimbi ya umeme ambayo nayo yamegawika katika aina nne. Aina ya
kwanza ni ilie inayoitwa Beta, aina hii huzalishwa pale mtu anapokua yuko katika hali
ya pirika pirika za kazi au jambo ambalo linahitaji umakini sana katika utekelezaji wake,
mawimbi haya hua na kasi ya mizunguko 15-40 kwa sekunde kulingana na namna
Ubongo unavyofanya kazi kwa ari katika wakati huo.

Aina ya pili ni ile iitwayo Alpha ambayo hua ni yenye kuzalishwa baada ya mtu husika
kumaliza jambo lililokua likimshughulisha akili yake, na hivyo kua kwenye hali ya
mapumziko ya ubongo na mwili, mawimbi haya ya Alpha hua yanatofautiana na Beta
kutokana na kua ni ya utulivu na hivyo hua ni yenye kasi ya mizunguko 9-14 kwa
sekunde, hali hii hua anayo pia mtu ambae amekaa na kutafakkari kitu kwa utulivu, au
akiwa anatembea taratibu kwa ajili ya kupata hewa nzuri na hivyo hua ni mwenye
kuridhika.

Aina ya tatu ya mawimbi hua ni ile inayoitwa Theta ambayo hua na kasi ya mzunguko
wa kati kwani hua na mizunguko 5-8 kwa sekunde, hali hii hua nayo yule ambae
ameshamaliza kazi, ameshapoa na kutulia na hivyo anakua ni mwenye kufikiria au
kukumbuka mambo mazuri mazuri yaliyopita au atakayoyapata baada ya yale
aliyoyafanya.

Aina ya mwisho ambayo ni aina ya nne ya mawimbi hua inaitwa Delta ambayo hua na
kasi ya mzunguko mdogo zaidi kwani hua na mizunnguko 1-4 kwa sekunde, na hali hii
hua nayo mtu pale anapokua anasinzia hadi anapoingia katika hali ya usingizi na kulala
fofofo!

Hivyo Mtu unaposikia Qur’an, ukanyamaza na kuisikiliza kwa umakini basi mzunguko
wa mawimbi ya Ubongo wako hua ni wenye kutoka katika hali iliyokuwepo na kuingia
katika hali ya Alpha ambayo ni ya kua mwenye kuridhika Kimwili, Kinafsi, Kiufaham
na Kiakili. Na hivyo kukupelekea kua na Muongezeko wa Imani ya Kiroho, ongezeko la
Uwezo wa Nguvu ya Kinga ya mwili, na ongezeko la uzalishaji wa seli mbali mbali za
mwili na hivyo kua ni tiba kwa Maradhiya Saratani, huzidisha nguvu ya Akili katika
sehemu ya Ufahamu na kuhifadhi, Huimarisha mishipa ya Moyo na sambamba na hayo
27

basi usikilizaji wa Qur’an hukupunguzia Hisia za Khofu, Mshtuko, Wasi wasi, Uzito wa
mkusanyiko wa mawazo na hukupa utulivu wa kiakili kukupunguzia uvamizi wa maradhi
yanayotokana na mshtuko wa Moyo na mzunguko wa damu na utulivu wa kimwili pia
kwa ujumla kwani hata wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji basi hua ni wenye kupona
haraka maumivu yao pale wanapokua wanasikiliza Qur’an mara kwa mara.

Kwa upande mwengine basi tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala anatuthibitishia
haya tena pale aliposema:

﴾‫ﻮب‬ ِ ِ‫ٱﻪﻠﻟِ أَﻻَ ﺑِ ِﺬ ْﻛ ِﺮ ﱠ‬


‫ﻳﻦ َآﻣﻨُﻮاْ َوﺗَﻄْ َﻤﺌِ ﱡﻦ ﻗُـﻠُﻮﺑـُ ُﻬ ْﻢ ﺑِ ِﺬ ْﻛ ِﺮ ﱠ‬ ِ ‫﴿ٱﻟﱠ‬
ُ ُ‫ٱﻪﻠﻟ ﺗَﻄْ َﻤﺌ ﱡﻦ ٱﻟْ ُﻘﻠ‬ َ ‫ﺬ‬
Alladheena amanoo watatma-innu quloobuhum bidhikri Allahi ala bidhikri Allahi
tatma-innu alquloobu (Surat Ar Rad 13:28)

Tafsir: Wale walioamini na wakazipatia utulivu Nyoyo zao kutokana na kumkumbuka


Allah. Kwani kwa hakika ni katika kumkumbuka Alla ndiko kunakoupa Nyoyo
utulivu.

Ambapo anasema Imam Abu Muammad Abd Allah Al Tustari kua: ‘Katika kufanya
(dhikr) huku ukiwa na (ʿilm) basi hua unapata utulivu (sukūn), na katika kufanya
Dhikr kwa Ufahamu (ʿaql) basi hua kunakuletea Utulivu mkubwa (ṭutmaʾīna).
Katika kufanya Dhikr huku ukiwa na (ʿilm) basi hua kunakuletea mapumziko ya
utulivu (sukūn), na Katika Kufanya Dhikr kwa ufahamu (ʿaql) Basi hua kuna
Utulivu mkubwa (ṭutmaʾīna) ’

Allah Subhanah wa Ta’ala anatuambia haya kwa sababu ni maumbile ya Nafsi za Ibn
Adam kua kila Nafsi zinapofikiria ya mapambo ya Kidunia, basi hua ni yenye kutaka
kuikimbilia na kujitumbukiza ndani yake na kutaka chengine zaid ya kile ambacho
kishaingia ndani yake. Lakini unapokua unamfikirira Allah Subhanah wa Ta’ala ambae
ndie Muumba basi hua hakuna kitu chengine chochote bora zaidi yake, hivyo kwako
wewe hua hakuna unachohitaji kwani kwake yeye kuna kila unachokihitaji na zaidi ya
utakachokihitaji kutoka kwake. Na hivyo hukupelekea kuyakimbia yasiyofaa na
kutokukukaribisha karibu yake, jambo hili hukupelekea kujawa na Imani na ari zaidi ya
kutekeleza maamrisho yake na kua ni mwenye kumtegemea yeye tu katika kila jambo
lako, na huo hua ni muongozo tosha kwa moyo na Nafsi yako, kama inavyosema aya
ifuatayo juu ya hayo.
28

‫ﱠﺎس ﻗَ ْﺪ َﺟﺂءَﺗْ ُﻜ ْﻢ ﱠﻣ ْﻮ ِﻋﻈَﺔٌ ِّﻣﻦ ﱠرﺑِّ ُﻜ ْﻢ َو ِﺷ َﻔﺂءٌ ﻟِّ َﻤﺎ ِﰱ ٱﻟ ﱡ‬


‫ﺼ ُﺪوِر َوُﻫ ًﺪى‬ ُ ‫ٰ�َﻳـﱡ َﻬﺎ ٱﻟﻨ‬
﴿
﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ
َ ‫َوَر ْﲪَﺔٌ ﻟّْﻠ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬
Ya ayyuha alnnasu qad jaatkum mawAAidhatun min rabbikum washifaon lima fee
alssudoori wahudan warahmatun lilmu/mineena (Surat Yunus 10:57)

Tafsir: Enyi Watu! Kwa hakika yamekujieni Mawaidha kutoka kwa Mola wenu na
Tiba kwa ajili ya Vifua (Nyoyo) vyenu, na Muongozo kwa Walioamini.

Bila ya shaka tunapozungumzia Muongozo kwa Waumini wanaoishi katika hali ya


maisha ya Kiislam basi hatuwezi kukamilisha bila ya kugusia Hikma na Baraka
zinazopatikana ndani ya Muongozo huo kutoka kwa Mola wetu tuliobainishiwa ndani ya
kitabu kitukufu cha Qurán.


HIKMA NA BARAKA NDANI YA QUR’AN

Neno Hikma limetokana na asili ya neno Hakama ambalo kwa lugha ya Kiarabu hua ni
lenye kumaanisha Kuzuia, Kudhibiti, Kuamrisha, kua na Mamlaka, Kuhukumu, kua na
Hikma au Busara, kua na Uadilifu na kua na l’lm. Neno Hikma pia kimaana ndani yake
hua linajumuuisha tabia njema na kila sifa zilizo njema.

Tunapoiangalia Qurán basi tunaona pia kua ina sifa ya kua ni Uhkimat, yaani yenye
Kulindwa na Kudhibitiwa kutokana na Upotovu, na hivyo hua ni yenye kuweka bayana
kila lenye manufaa na kuweka bayana kila lisilokua na manufaa kwa kila Ibn Adam tena
bila ya kua na shaka yeyote ndani yake kutokana na asili yake. Kwani anasema Allah
Subhanah wa Taála kua;

‫ﲔ۞ إِ ﱠ� َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎﻩُ ﻗُـْﺮآ�ً َﻋَﺮﺑِﻴّﺎً ﻟﱠ َﻌﻠﱠ ُﻜ ْﻢ ﺗَـ ْﻌ ِﻘﻠُﻮ َن۞ َوإِﻧﱠﻪُ ِ ۤﰲ أُِّم‬ ِ َ‫﴿ﺣ ۤـﻢ۞ وٱﻟْﻜِﺘ‬
ِ ِ‫ﺎب ٱﻟْﻤﺒ‬
ُ َ
﴾‫ﺎب ﻟَ َﺪﻳْـﻨَﺎ ﻟَ َﻌﻠِ ﱞﻲ َﺣﻜِﻴﻢ‬ ِ َ‫ٱﻟْ ِﻜﺘ‬
ٌ
29

Ha-meem, Waalkitabi almubeeni, Inna jaAAalnahu qur-anan AAarabiyyan


laAAallakum taAAqiloona, Wa-innahu fee ommi alkitabi ladayna laAAaliyyun
hakeemun (Surat Az Zukhruf 43:1-4)

Tafsir: Ha Mim. Na (Naapa) kwa kitabu chenye kubainisha. Kwa hakika tumekijaalia
Qurán kua katika Lugha ya Kiarabu ili mpate kuzingatia. Na kwa Hakika hii (Quran)
imo ndani ya kitabu Mama mbele yetu, ni Kitukufu kilichojaa Hikma.

Anasema Imam Abu Al Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Qurán kimeitwa Umm ul Kitab
yaani Kitabu Mama kwa sababu hiki ni Kitabu ambacho ndio kilichotoa vitabu
vyote vya Mitume waliotangulia hapo kabla. Hivyo vitabu vyote vilivyotangulia
vimetokana na Kitabu Mama Qurán - Umm ul Kitab’

Umm ul Kitab si kitabu ambacho kilichojaa Hikma tu lakini pia ni kitabu ambacho
kimejaa Baraka ndani yake na juu ya hili basi linabainishwa na Qurán yenyewe pale
iliposema:

ِ ‫﴿وﻫـٰ َﺬا ﻛِﺘﺎب أَﻧﺰﻟْﻨﺎﻩ ﻣﺒﺎرٌك ﱡﻣﺼ ِّﺪ ُق ٱﻟﱠ ِﺬى ﺑـﲔ ﻳ َﺪﻳ ِﻪ وﻟِﺘ‬
‫ﻨﺬ َر أُﱠم ٱﻟْ ُﻘَﺮ ٰى َوَﻣ ْﻦ‬ُ َ ْ َ ََْ َ َ َُ ُ َ َ ٌ َ َ َ
﴾‫ﺻﻼَﻬﺗِِﻢ ُﳛَﺎﻓِﻈُﻮ َن‬ ِِ ِ ِ ِ ِ ِ ‫ﺣﻮَﳍﺎ وٱﻟﱠ ِﺬ‬
ْ َ ‫ﻳﻦ ﻳـُ ْﺆﻣﻨُﻮ َن ﺑﭑﻵﺧَﺮة ﻳـُ ْﺆﻣﻨُﻮ َن ﺑﻪ َوُﻫ ْﻢ َﻋﻠَ ٰﻰ‬
َ َ َ َْ
Wahadha kitabun anzalnahu mubarakun musaddiqu alladhee bayna yadayhi
walitundhira omma alqura waman hawlaha waalladheena yu/minoona bial-
akhirati yu/minoona bihi wahum AAala salatihim yuhafidhoona (Surat Al AnAam
6:92)

Tafsir: Na hiki ni Kitabu (Qurán) ambacho kimeshushwa kikiwa kimejaa Baraka,


kuthibitisha vilivyotangulia kabla yake, ili upate kuuonya mji Mama (wa Makkah) na
iliyo pembeni yake, Wale ambao wanaamini juu ya Akhera wanaiamini (Qurán) na
wale ambao juu ya Sala zao wanahifadhi.

Neno Baraka kwa Lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kuongezeka, Kukua na pia
humaanisha Furaha. Neno Barakah linatokana na neno linalomaanisha sehemu ya mbele
ya Ngamia ambae amekaa chini na kuididimiza miguu ndani ya mchana bila ya kutaka
kuondoka sehemu hio, na pia humaanisha msimamo thabiti wa mtu au kitu bila ya kurudi
nyuma kama vile anavyokua mtu shujaa anapobakia peke yake katika uwanja wa vita
dhidi ya maadui wote hivyo huamua kupigana hadi mwisho bila ya kukimbia mapigano,
Kua na msimamo, Kuishi, Kupewa heshima.
30

Hivyo Baraka hua ni muendelezo au muongezeko wa milele wa jema kutoka kwa Allah
Subhanah wa Taála wenye faida ndani yake ambalo hua halionekani kupungua kwake
bali hua linaonekana katika kuongezeka kwake bila ya kujua chanzo cha muendelezo au
muengezeko huo. Kwa mfano pale mtu anapotoa Sadaka na hivyo Baraka huingia katika
mali yake na kuonekana kwa muongezeko wa wingi wa Mali hio.

Anasema Allamah Abu Qasim Ibn Husein Ibn Mufadal Ibn Muhammad Raghib Al
Isfahani kua: ‘Baraka hua ni tofauti na Neema ambayo hua inamaanisha kitu au
jambo fulani maalum liwe kidogo au kikubwa kingi, na hua ni neema pale mtu
aliepewa anapokua na akili na ufahamu.’ Allah Subhanah wa Ta’ala amesema
katika Qurán:

‫ﻮﻫﺎ إِ ﱠن ٱﻹﻧْ َﺴﺎ َن‬ ِ‫آﺎﺗ ُﻛﻢ ِﻣﻦ ُﻛ ِﻞ ﻣﺎ ﺳﺄَﻟْﺘﻤﻮﻩ وإِن ﺗَـﻌ ﱡﺪواْ ﻧِﻌﻤﺔَ ﱠ‬ ﴿
َ‫ﺼ‬ ُ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻻَ ُْﲢ‬ َ ْ ُ َ ُ ُ ُ َ َ ّ ّ َ ‫َو‬
﴾‫ﻮم َﻛ ﱠﻔ ٌﺎر‬
ٌ ُ‫ﻟَﻈَﻠ‬
Waatakum min kulli ma saaltumoohu wa-in taAAuddoo niAAmata Allahi la
tuhsooha inna al-insana ladhaloomun kaffarun (Surat Ibrahim 14:34)

Tafsir: Na amekupeni nyinyi kila mlichotaka, na kama mkitaka kuzihesabu Neema za


Allah basi kamwe hamtoweza kuzihesabu. Kwa Hakika Mtu ni mwenye kujidhulumu
na mwenye kukufuru.

Hivyo tunapozungumzia kuhusiana na Allah, basi hua inazungumziwa kwa ujumla, na


kwa umoja kumaanisha: ‘Misaada ya Allah' anayoitoa kwa Waja wake. Na hua
inajumuisha dalili zake, malipo yake, manufaisho yake kwa Viumbe wake, Neema zake,
Rehma zake, n.k.

Neno Barakah pia hua ni lenye kumaanisha al Ziyadah yaani Ziada, al Sa’adah yaani
Furaha, Al Du’a yaani Dua. Al Manfaáh yaani Manufaa, Al Baqah yaani Kinachobaki
Milele, Al Taqdis yaani Kitu kitukufu. Kwa hivyo Allah Subhanahu wa Taála anapotia
Barakah ndani ya kitu basi hata kama mwanzoni kitu hicho kilikua si chochote, lakini
baada ya kutiwa Barakah basi kitu hicho huanza kubadilika wingi, thamani yake,
manufaa yake na hata uzuri wake hupelekea kuzidisha idadi ya wingi wake. Barakah
kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala hua inakuja kutoka katika upande usiotegemewa
wala kufikirika na haihitaji wingi wa kitu.
31

Ama tunapozungumzia Barakah ndani ya Qurán kama ilivyoelezewa katika aya


tuliyoanza nayo ya Surat Al An Aam 6:92 na pia katika aya ifuatayo:-

﴾‫َﻧﺰﻟْﻨَﺎﻩُ ُﻣﺒَﺎرٌك ﻓَﭑﺗﱠﺒِﻌُﻮﻩُ وٱﺗﱠـ ُﻘﻮاْ ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜﻢ ﺗُـﺮ َﲪُﻮ َن‬ ِ
ْ ْ َ َ ٌ َ‫﴿ َوَﻫـٰ َﺬا ﻛﺘ‬
َ ‫ﺎب أ‬
Wahadha kitabun anzalnahu mubarakun faittabiAAoohu waittaqoo laAAallakum
turhamoona (Surat Al AnAam 6:155)

Tafsir: Na hiki ni Kitabu (Qurán) ambacho kimeshushwa kikiwa kimejaa Baraka,


hivyo kifuateni na kuweni na Taqwa, ili muwe ni wenye kupata rehma.

Basi tunaona kua anasema Mujaddid ud Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Maana
ya Kitabun Mubarakan hua linamaanisha Kitabu chenye Rehma na Neema za Milele
kwa sababu hua ni chenye kuusia mema, malipo mengi zaidi na msamaha mkubwa
sana, na hapo hapo hua ni chenye kuonya kwa wanaomuasi Allah Subhanah wa
Ta’ala kwa kufanya Dhambi na Maovu’.

Ama kwa upande wa Imam Abu Al Thana’ Shihab Ad Dīn Sayyid Maḥmūd Ibn ‘Abd
Allāh Al Ḥusaynī Al Alusi Al Baghdadi basi yeye anasema kua: ‘Maana ya Kitabun
Mubarakan hua kunamaanisha Kitabu kilichojaaliwa kua na baraka nyingi ndani
yake, kwani kinajumuisha manufaa ya hapa Duniani na manufaa ya kesho Akhera
na kuweka wazi Ilm ya mambo ya sasa na yaliyotangulia’ (Ruh al-Ma'ani fi Tafsir al-
Qurán Al 'Adhim wa Sab'a Al Mathani)

Qurán imetumia aya zaidi ya 10 zenye kuzungumzia juu ya Baraka za Allah Subhanah
wa Taála katika vitu na mambo mbali mbali muhimu kwa Waislam kwa mfano: Mji wa
Makkah kama sehemu yenye nyumba ya awali ya kufanyia Ibada katika Surat Al Imran
3:96, Mji wa Jerusalem ulipotajwa Masjid Al Aqsa katika Surat Al Isra 17:1, Jangwa la
Sinai ambalo ni lenye Mlima Tur sehemu ambayo Allah Subhanhah wa Ta’ala
aliyozungumza na Nabii Musa, Ardhi ya Mji wa Sham sehemu ambayo waliozaliwa na
pia kuishi Mitume wengi zaidi katika Surat Al Anbiyah 21:71, Usiku wa Barakah
ulioshushwa Qurán katika Surat Ad Dukhan 44:3 na Surat Al Qadr.

Mti wa Mzaitun pia umetajwa kua na sifa ya kua Mubaraka katika Surat An Nur 24:35
ambapo matunda yake yanatoa mafuta ambayo hua ni yenye kutoa Nuru kali ya aina ya
Infra Red isiyoonekana kwa macho ya kawaida ya Ibn Adam lakini huweza kuonekana
32

kwa kutumia darubini maalum si hapa ulimwenguni tu lakini pia Nuru yake huweza
kuonekana hata kutoka katika kituo cha uchunguzi wa kisayansi cha angani. Mitume nao
pia ni miongoni mwa waliopewa sifa ya kua Mubaraka kama Nabii Nuh alipotajwa katika
Surat Hud 11:48, Nabii Ibrahim na Nabii Is-haq kama walivyotajwa katika Surat Saffat
37:113, Nabii Isa Ibn Maryam katika Surat Maryam 19:31. n.k

Neno Barakah ndio lililotoa neno Mubarik ambalo hua ni Isim fa'il yaani ni sifa ya
mweye kutoa Barakah ambae ni Allah Subhanah Allahu wa Taála pekee na ndio maana
Allah Subhanah wa Taála akawa na sifa ya kua na Tabarak ambayo ipo katika hali ya Al
Taqdis yaani ya Utukufu wa Kutoa Barakah pale aliposema katika Qurán:

﴾‫ﻚ وُﻫﻮ َﻋﻠَ ٰﻰ ُﻛ ِﻞ َﺷﻲ ٍء ﻗَ ِﺪﻳﺮ‬ ِِ ِ ِ ‫ﱠ‬ ﴿


ٌ ْ ّ َ َ ُ ْ‫ﺗَـﺒَ َﺎرَك ٱﻟﺬى ﺑﻴَﺪﻩ ٱﻟْ ُﻤﻠ‬
Tabaraka alladhee biyadihi almulku wahuwa AAala kulli shay-in qadeerun (Surat
Al Mulk 67:1)

Tafsir: Ametukuka yule ambae ndani ya mikono yake kuna Mamlaka, na ni yeye
ambae ni mwenye uwezo wa juu ya kila kitu.

Neno Tabaraka limetajwa ndani ya Qurán mara 9, ambapo aya zilizotaja na kutumia sifa
hii zimemsifia yule ambae tu ni pekee anaestahiki kua na sifa hio ya Al Mutabarik pekee,
ambae anatuwekewa wazi juu ya hilo pale aliposema katika aya nyengine iliyotumia neno
Tabarakah Allahu ambayo inasema:

ٍ ِ ِ َ ‫ات وٱﻷَر‬ ِ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ ٱﻟﱠ‬ ِ﴿


ْ ‫ض ِﰱ ﺳﺘﱠﺔ أ ﱠَ�م ﰒُﱠ‬
‫ٱﺳﺘَـ َﻮ ٰى َﻋﻠَﻰ‬ ْ َ ‫ٱﻟﺴ َﻤ َﺎو‬ َ ‫ﻖ‬
َ ‫ﻠ‬
َ ‫ﺧ‬
َ ‫ى‬ ‫ﺬ‬ ُ‫إ ﱠن َرﺑﱠ ُﻜ ُﻢ ﱠ‬
ٍ ‫ٱﻟْﻌﺮ ِش ﻳـ ْﻐ ِﺸﻰ ٱﻟْﻠﱠﻴﻞ ٱﻟﻨـﱠﻬﺎر ﻳﻄْﻠُﺒﻪ ﺣﺜِﻴﺜﺎً وٱﻟﺸﱠﻤﺲ وٱﻟْ َﻘﻤﺮ وٱﻟﻨﱡﺠﻮم ﻣﺴ ﱠﺨﺮا‬
‫ت‬ َ َ ُ َ ُ َ ََ َ َ ْ َ َ ُُ َ َ َ َ ْ ُ َْ
﴾‫ب ٱﻟْﻌﺎﻟَ ِﻤﲔ‬ ْ ُ‫ِﺄﺑ َْﻣ ِﺮﻩِ أَﻻَ ﻟَﻪ‬
َ َ ‫ٱﻪﻠﻟُ َر ﱡ‬ ‫ٱﳋَْﻠ ُﻖ َوٱﻷ َْﻣُﺮ ﺗَـﺒَ َﺎرَك ﱠ‬
Inna rabbakumu Allahu alladhee khalaqa alssamawati waal-ardha fee sittati
ayyamin thumma istawa AAala alAAarshi yughshee allayla alnnahara yatlubuhu
hatheethan waalshshamsa waalqamara waalnnujooma musakhkharatin bi-amrihi
ala lahu alkhalqu waal-amru tabaraka Allahu rabbu alAAalameena (Surat Al Araf
7:54)

Tafsir: Hakika Mola wako ni Allah ambae yeye ndie alieumba Mbingu na Ardhi kwa
siku sita kisha akasimama juu ya Arshi, ni yeye ambae anauleta usiku kwa kuufunika
33

mchana kwa utaratibu usiosita, na Jua, na Mwezi, na Nyota zikiwa chini ya amri yake,
kwa hakika ni vyake viumbe na amri. Utukufu ni wake Allah Mola wa Ulimwengu.

Katika aya tuliyoianisha hapo juu ya Surat Al Araf 7:54 tunaona kua Allah Subhanah wa
Tabarak anatuwekea wazi kua Utukufu ni wake yeye tu kwani yeye ndie alietuumba sisi
viumbe na kila kitu kinachotuzunguka ulimwenguni na kuainisha Utukufu wake kwa kua
ndie mwenye Mamlaka ya kila kitu Mbiguni na Ardhini na kua ni yeye tu ndie aijuae
Siku ya Malipo na kutuhakikishia kua kwake yeye ndio marejeo yetu kama anavyosema
katika aya inayofuatia:

‫ﺎﻋ ِﺔ‬ ِ َ ‫ض وﻣﺎ ﺑـﻴـﻨَـﻬﻤﺎ و ِﻋ‬ ِ ِ


َ ‫ﻨﺪﻩُ ﻋ ْﻠ ُﻢ ٱﻟ ﱠﺴ‬ َ َ ُ َْ َ َ ِ ‫ﻚ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤ َﺎوات َوٱﻷ َْر‬ ُ ‫﴿ َوﺗَـﺒَ َﺎرَك ٱﻟﱠﺬى ﻟَﻪُ ُﻣ ْﻠ‬
﴾‫وإِﻟَْﻴ ِﻪ ﺗُـﺮ َﺟﻌُﻮ َن‬
ْ َ
Watabaraka alladhee lahu mulku alssamawati waal-Ardhi wama baynahuma
waAAindahu AAilmu alssaAAati wa-ilayhi turjaAAoona (Surat Az Zukhruf 43:85)

Tafsir: Na Utukufu ni wa yule ambae mwenye mamlaka ya Mbiguni na Ardhini na


kila kilichomo baina yake, na yeye ndie mwenye kujua saa ya kiama na kwake yeye
ndio marudio yenu.

Hivyo ayah hii ya Surat Az Zukhruf 43:85 iko wazi kua ni jambo lisilokua na shaka kua
mwisho wetu Ibn Adam ni kufika tulikotoka yaani kwa Mola wetu lakini wakati bado
tupo safarini hapa ulimwenguni ndani ya Mamlaka yake kuelekea kwa Mola wetu basi
tunaweza kunufaika baada ya kufuata Muongozo wake na hivyo kupata Baraka na
Fadhila nyingi sana na za aina tofauti kutoka kwake Allah Subhanah wa Taála kama
inavyosema aya ifuatayo:

‫ﻳﻦ َآﻣﻨُـ ۤﻮاْ إِن ﺗَـﺘﱠـ ُﻘﻮاْ ﱠ‬


‫ٱﻪﻠﻟَ َْﳚ َﻌﻞ ﻟﱠ ُﻜ ْﻢ ﻓُـْﺮﻗَﺎ�ً َوﻳُ َﻜ ِّﻔْﺮ َﻋﻨ ُﻜ ْﻢ َﺳﻴِّﺌَﺎﺗِ ُﻜ ْﻢ‬ َ
ِ ‫﴿� أَﻳـﱡﻬﺎ ٱﻟﱠ‬
‫ﺬ‬ َ َ
﴾‫ﻀ ِﻞ ٱﻟْ َﻌ ِﻈﻴ ِﻢ‬ ‫َوﻳَـ ْﻐ ِﻔْﺮ ﻟَ ُﻜ ْﻢ َو ﱠ‬
ْ ‫ٱﻪﻠﻟُ ذُو ٱﻟْ َﻔ‬
Ya ayyuha alladheena amanoo in tattaqoo Allaha yajAAal lakum furqanan
wayukaffir AAankum sayyi-atikum wayaghfir lakum waAllahu dhoo alfadhli
alAAaDheemi (Surat Al Anfal 8:29)
34

Tafsir: Enye Mlioamini! Kama mtamcha Allah basi atakujaalie Furqan na


kukufutieni Madhambi yenu na atakusameheni, na kwa hakika Allah ndie mmiliki
wa fadhila Kubwa.

Tunapoitafakkar ayah hii basi tunaona kua ayah imetumia neno Furqan ambalo maana
yake hua ni muongozo unaotofautisha baina ya jema na ovu, na bila ya shaka neno hili
hua linafasirika vizuri zaidi pale tunapoiangalia maana ya aya ifuatayo ya Surat Al
Furqan:

﴾ً‫ﲔ ﻧَ ِﺬﻳﺮا‬ ِ ِ ِ ِِ ِ
َ ‫﴿ﺗَـﺒَ َﺎرَك ٱﻟﱠﺬى ﻧَـﱠﺰَل ٱﻟْ ُﻔْﺮﻗَﺎ َن َﻋﻠَ ٰﻰ َﻋْﺒﺪﻩ ﻟﻴَ ُﻜﻮ َن ﻟ ْﻠ َﻌﺎﻟَﻤ‬
Tabaraka alladhee nazzala alfurqana AAala AAabdihi liyakoona lilAAalameena
nadheeran (Surat Al Furqan 25:1)

Tafsir: Ametukuka yule ambae ameishusha Furqan (Qurán) kwa mja wake ili awe ni
muonyaji kwa viumbe.

Naam, neno Furqan linatokana na neno Faraqa ambalo kwa kiarabu hua linamaanisha
Kubagua, Kutofautisha, Kuamua au Kugawa, hivyo Furqan hua ni Uthibitisho, Hoja au
kitu kinachotofautisha baina ya Jema na Ovu, Nuru na Kiza, n.k.

Hivyo Qurán imepewa jina la sifa ya Furqan kwa sababu Quran ni yenye muongozo
wenye kubainisha na kutofautisha baina jema na ovu kwa kutumia njia tofauti za
kubainisha mambo kwa moja kwa moja, kwa mafumbo na njia ya mithali za aina tofauti
zenye mafunzo ndani yake.


MAFUMBO NA MITHALI ZILIZOMO NDANI YA QUR’AN.

Neno Mathala kwa kiarabu hua ni lenye kumaanisha Mithili ya kitu, Mfano, Mfanano,
Mfananisho, Sawasawa na kitu fulani, Muwakilisho, Msemo, Mithali n.k na baadhi ya
wakati neno hili hua linatumika kumaanisha Hoja!

Tunapoiangalia Qurán basi tunaona kua imetumia neno Mathala katika hali mbali mbali
mara 114 katika kutoa mafunzo yake ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala ameamua
35

kutumia pia njia za mithali au mifano ili sisi walengwa wenye kupewa ujumbe huo tupate
kutafakkar, kuzingatia na kufahamu kwa kina zaidi mafunzo yanayotakiwa kupatikana
kutoka ndani ya kile kinachoelezewa juu yake kama anavyotueleza Allah Subhanah wa
Taála pale aliposema:

‫ﱠﺎس ِﻣﻦ ُﻛ ِّﻞ َﻣﺜَ ٍﻞ َوَﻛﺎ َن ٱ ِﻹﻧْ َﺴﺎ ُن أَ ْﻛﺜَـَﺮ َﺷ ْﻲ ٍء‬ ِ ‫آن ﻟِﻠﻨ‬ ِ ‫﴿وﻟََﻘ ْﺪ ﺻﱠﺮﻓْـﻨَﺎ ِﰱ ﻫـٰ َﺬا ٱﻟْ ُﻘﺮ‬
ْ َ َ َ
‫ﱠﺎس أَن ﻳـُ ْﺆِﻣﻨُـ ۤﻮاْ إِ ْذ َﺟﺂءَ ُﻫ ُﻢ ٱ ْﳍَُﺪ ٰى َوﻳَ ْﺴﺘَـ ْﻐ ِﻔُﺮواْ َرﺑـﱠ ُﻬ ْﻢ إِﻻﱠ أَن‬
َ ‫َﺟ َﺪﻻً۞ َوَﻣﺎ َﻣﻨَ َﻊ ٱﻟﻨ‬
﴾ً‫اب ﻗُـﺒُﻼ‬ ِ ِ ِ
ُ ‫ﲔ أ َْو َ�ْﺗﻴَـ ُﻬ ُﻢ ٱﻟْ َﻌ َﺬ‬
َ ‫َﺄﺗْﺗﻴَـ ُﻬ ْﻢ ُﺳﻨﱠﺔُ ٱﻷَﱠوﻟ‬
Walaqad sarrafna fee hadha alqur-ani lilnnasi min kulli mathalin wakana al-insanu
akthara shay-in jadalan; Wama manaAAa alnnasa an yu/minoo idh jaahumu
alhuda wayastaghfiroo rabbahum illa an ta/tiyahum sunnatu al-awwaleena aw
ya/tiyahumu alAAadhabu qubulan (Surat Al Kahf 18:54-55)

Tafsir: Na kwa hakika tumeelezea ndani ya hii Qur’an kila aina ya mithali kwa ajili
ya Watu. Lakini mtu hua ni mwenye kupenda kuliko (kiumbe) yeyote kujadili. Na
hakuna kinachowazuia watu kutokana na kutoamini wakati uongofu umewafikia na
kuomba msamaha kwa Mola wao. Isipokua ni kua na hali ya kufuata njia za watu
waliotangulia au wapewe adhabu itakayokabiliana nao uso kwa uso.

Bila ya shaka Ibn Adam ni kiumbe mwenye kupenda kujadili juu ya kila kitu kuliko
kiumbe mwengine yeyote yule wa Allah Subhanah wa Ta’ala, na hivyo hua si wenye
urahisi wa kujifunza kutokana na wanayoambiwa na mifano wanayoelezewa, na hivyo
hua ni wenye kuishi kwa kufuata mazoea ya wazee wao na waliowatangulia kabla yao,
kiasi ya kua kwa wengi wao inakua vigumu kwao kufumbuka macho kutokana na mazoea
hayo mpaka uwafikie ujumbe wenye kuonya na baadhi ya wakati hadi watu iwashukie
adhabu ya Mola wao juu yao. Allah Subhanah wa Ta’ala anaendelea kutumithilishia
mifano kwa kutuambia kua:

ً‫آن ِﻣﻦ ُﻛ ِّﻞ َﻣﺜَ ٍﻞ ﻟﱠ َﻌﻠﱠ ُﻬ ْﻢ ﻳَـﺘَ َﺬ ﱠﻛُﺮو َن۞ ﻗُـْﺮآ�ً َﻋَﺮﺑِﻴّﺎ‬
ِ ‫ﱠﺎس ِﰱ ﻫـٰ َﺬا ٱﻟْ ُﻘﺮ‬ ِ
ْ َ ‫﴿ َوﻟََﻘ ْﺪ‬
َ ِ ‫ﺿَﺮﺑْـﻨَﺎ ﻟﻠﻨ‬
﴾‫َﻏْﻴـﺮ ِذى ِﻋﻮ ٍج ﻟﱠ َﻌﻠﱠ ُﻬﻢ ﻳَـﺘﱠـ ُﻘﻮ َن‬
ْ َ َ
36

Walaqad dharabna lilnnasi fee hadha alqur-ani min kulli mathalin laAAallahum
yatadhakkaroona; Qur-anan AAarabiyyan ghayra dhii AAiwajin laAAallahum
yattaqoona (Surat Az Zumar 39:27-28)

Tafsir: Na kwa hakika tumepiga kwa ajili ya watu ndani ya hii Qurán mithali za kila
aina ili (Watu) wawe ni wenye Kukumbuka. Qurán ya Kiarabu ambayo haina ubaya
wowote ndani yake ili wapate kua ni wacha Mungu.

Ingawa aya ya Surat Al Kahf 18:54 imetumia neno Sarafna ambalo hua ni lenye
kumaanisha Kuweka, kuelezea lakini ayah inayofuatia baada ya hio ambayo ni ya Surat
Zumar 39:27 na aya nyenginezo nyingi ambazo zimetumika katika njia ya kufunza kwa
kutoa Mithali hua zimetumia neno Dharaba ambalo kwa lugha ya Kiswahili hua
linamaanisha Dharuba. Hivyo Allah Subhana wa Taála ametumia neno Dharaba kwa
sababu kwa lugha ya Kiarabu neno Dharaba hua linamaanisha Kupiga kitu kwa nguvu
hadi kikatoa sauti, Kuponesha, Kutaja, Kufananisha, Kutafuta njia, Kufunga safari,
Kupigania kitu kwa ajili ya kupata faida au manufaa.

Hivyo aya zimetumia neno Dharaba kwa sababu zinatutaka tupiganie manufaa yaliyomo
ndani ya mithali hizo kama tukiwa hatujalala kiakili, na kama tumelala kiakili basi aya
zinatutaka tuzindukane kama vile watu waliopigwa dharuba yaani kibao usoni na hivyo
kua ni wenye umakini wa kuzingatia mithali tunazopigiwa na Mola wetu alietuumba
ambae ndie anaetujua maumbile yetu ndani nje.

Ndio maana ikawa mbali ya kua Qurán ni kitabu kilichojaa Baraka lakini pia ni kitabu
ambacho tumeshushiwa Waislam kupitia kwa Rasul Allahi Salallahu A’layhi wa Salam
ili kitupe muongozo kwa ajili ya kumkumbuka Mola wetu na hivyo kutuwezesha kufuzu
katika maisha yetu ya hapa Duniani na ya kesho Akhera, hivyo hali hii ya kuletewa
muongozo kutoka kwa Muumba kwa ajili yetu ili tuufuate na kua na Ucha Mungu ni
fadhila kubwa sana kwa kila mmoja miongoni mwetu ambae atauamini na kuufuata
muongozo huo, kwani Allah Subhanah wa Taála alieuleta muongozo huo na kumpa kila
amtakae anatuambia katika Qurán kwa kusema:

﴾‫ﻀ ِﻞ ٱﻟْ َﻌ ِﻈﻴ ِﻢ‬ ‫ٱﻪﻠﻟِ ﻳـُ ْﺆﺗِ ِﻴﻪ َﻣﻦ ﻳَ َﺸﺂءُ َو ﱠ‬
ْ ‫ٱﻪﻠﻟُ ذُو ٱﻟْ َﻔ‬ ‫ﻀ ُﻞ ﱠ‬ ِ
َ ‫﴿ ٰذﻟ‬
ْ َ‫ﻚ ﻓ‬
Dhalika fadhlu Allahi yu/teehi man yashao waAllahu dhoo alfadhli alAAadheemi
(Surat Al Jumuah 61:4)

Tafsir: Hio ni Fadhila ya Allah ambayo humpa amtakae, ama kwa hakika Allah ni
mwenye fadhila kubwa sana.
37

Hivyo tusipotafakkar na kutoizingatia Qurán basi hatutonufaika na fadhila hizo zilizo


bora na tutakua kama watu waliotangulia kabla yetu waliotajwa katika aya inayofuata
baada ya hio ambayo nayo inasema kwa kumithilisha kua:

‫ﺲ َﻣﺜَ ُﻞ‬ ‫ﺌ‬


ِْ‫َﺳ َﻔﺎراً ﺑ‬‫أ‬ ‫ﻞ‬ ‫ﻤ‬ ُِ ‫﴿ﻣﺜَﻞ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ‬
ِ ‫ﲪﻠُﻮاْ ٱﻟﺘـﱠﻮرا َة ﰒُﱠ َﱂ َﳛ ِﻤﻠُﻮﻫﺎ َﻛﻤﺜَ ِﻞ ٱ ْﳊِﻤﺎ ِر َﳛ‬
َ ْ ُ ْ َ َ َ ْ ْ َْ ّ َ ُ َ
﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ ‫ٱﻪﻠﻟِ َو ﱠ‬ ِ �‫ٱﻟْ َﻘﻮِم ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ َﻛ ﱠﺬﺑﻮاْ ِﺂﺑ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻻَ ﻳـَ ْﻬﺪى ٱﻟْ َﻘ ْﻮَم ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬ ‫ت ﱠ‬ َ ُ َ ْ
Mathalu alladheena hummiloo alttawrata thumma lam yahmilooha kamathali
alhimari yahmilu asfaran bi/sa mathalu alqawmi alladheena kadhdhaboo bi-ayati
Allahi waAllahu la yahdee alqawma aldhdhalimeena (Surat Al Jumuah 62:5)

Tafsir: Mithili ya wale ambao wale waliopewa (Majukumu ya) Tawrat, lakini hapo
hapo wakashindwa kuyabeba (Majukumu hayo kwa kutekeleza amri zilizomo ndani
yake) hua ni kama mithili ya Punda aliebeba shehena za vitabu, Ni m-baya sana mfano
wa wale ambao wamekadhibisha aya za Allah na kwa hakika Allah hawaongozi watu
madhalimu.

Naam, hapa tunaona kua aya imetumia maneno Kamathali alhimari yahmilu asfaran –
Kama mithili ya Punda aliebeba Asfara, ambapo neno Asfara ni neno linalotokana na
neno Sifr la Kiarabu ambalo limetokana na neno Safara ambalo mbali ya kua hua
linamaanisha Safari lakini pa hua linamaanisha Kufagia, Kutawanyika, Kutembea,
Kufunua, Kupambazuka, Kuweka wazi kwa Maandishi yaani kwenye Kitabu na hivyo
neno Asfara lililotumika hapa hua linamaanisha Vitabu vikubwa vyenye kufunua macho
na ufahamu wa mtu kutokana na yaliyomo ndani yake kama ikiwa mtu huyo atavisoma,
atazingatia na kutafakkari yaliyomo ndani yake.

Na Alhamd Lillah sisi Waislam tumejaaliwa kua ni miongoni mwa waliochaguliwa


kupata fadhila bora kutoka kwa Allah Subhanah wa Taála hivyo tusipotafakkar na
kuzingatia Qurán basi hatutokua sawa na Punda tu aliebeba mzigo wa vitabu vyenye
thamani kubwa lakini asiejua thamani iliyomo ndani ya uzuito wa mzigo wake, bali
tutakua pia ni sawa na wale watu ambao wanaelezewa katika aya ya mithali ifuatayo:
38

ْ‫ﺖ ِّﲡَ َﺎرﺗُـ ُﻬ ْﻢ َوَﻣﺎ َﻛﺎﻧُﻮا‬ ِ ‫﴿أُوﻟَـٰﺌِ ﱠ‬


ْ َ‫ﻀﻼَﻟَﺔَ ﺑِﭑ ْﳍَُﺪ ٰى ﻓَ َﻤﺎ َرِﲝ‬ ‫ﻳﻦ ٱ ْﺷﺘَـُﺮواْ ٱﻟ ﱠ‬
َ ‫ﻚ ٱﻟﺬ‬
َ ْ
ِ ‫ﻣﻬﺘ ِﺪﻳﻦ۞ﻣﺜـﻠُﻬﻢ َﻛﻤﺜ ِﻞ ٱﻟﱠ‬
ُ‫ٱﻪﻠﻟ‬
‫ﺐ ﱠ‬ َ ‫ﻫ‬
َ ‫ذ‬
َ ‫ﻪ‬
ُ ‫ﻟ‬
َ‫ﻮ‬ْ ‫ﺣ‬
َ ‫ﺎ‬ ‫ﻣ‬
َ ‫ت‬ْ ‫ﺎء‬
َ ‫َﺿ‬
َ ‫أ‬ ‫ﺂ‬‫ﻤ‬‫ﱠ‬ ‫ﻠ‬
َ ‫ـ‬
َ ‫ﻓ‬ ‫ا‬
‫ر‬
ً �َ ‫ﺪ‬َ ‫ﻗ‬
َ‫ﻮ‬ْ ‫ـ‬َ‫ﺘ‬ ‫ٱﺳ‬
ْ ‫ى‬ ‫ﺬ‬ َ َ ْ ُ ََ َ َ ْ ُ
﴾‫ﺼﺮو َن‬ ِ ‫ﺎت ﻻﱠ ﻳـﺒ‬ ٍ ‫ﺑِﻨُﻮِرِﻫﻢ وﺗَـﺮَﻛﻬﻢ ِﰱ ﻇُﻠُﻤ‬
ُ ُ ْ َ ُْ َ َ ْ
Ola-ika alladheena ishtarawoo aldhdhalalata bialhuda fama rabihat tijaratuhum
wama kanoo muhtadeena, Mathaluhum kamathali alladhee istawqada naran
falamma adhaat ma hawlahu dhahaba Allahu binoorihim watarakahum
fee dhulumatin la yubsiroona (Surat Al Baqara 2:16-17)

Tafsir: Hawa ni wale watu ambao, wameununua upotovu kwa bei ya uongovu, hivyo
biashara yao imekua haina faida, na hawakuongozwa. Mithili yao watu hao ni mithili
ya wale ambao wamewasha moto, kisha ukawamurikia katika maeneo yao, na kisha
Allah akauchuchukua mwangaza wao nao wakawa ni waliobakia katika kiza.

Yaani mithili yetu itakua sawa na watu ambao wamewekewa wazi uongofu lakini badala
ya kuutafakkar na kuufanyia kazi basi wao wakaachana nao hivyo kuendelea kupotoka
kwa kutokua na Shukrani, Yaqini na Ikhlas katika mambo yao, na hivyo kua ingawa
wamepata Nuru ya muangaza baada ya kua gizani, lakini kwa kutoujali muangaza huo
basi muangaza huo ukazimika na kutoweka kwani kila mtu unapokua na Shukran, Yaqini
na Ikhlasi kwa Mola wako basi ndivyo Nuru ya muangaza inavyozidi kuongezeka katika
Moyo wako, na unapokua na shaka na wasi wasi basi ndivyo inavyozidi kufifia nuru ya
muangaza huo na hivyo hutoweza kuongoka na hutoweza kua huru kutokana na
Matamanio ya Nafsi yako na upotovu wa Iblis.

Qurán inayaweka wazi haya pale Allah Subhnah wa Taála alipotoa mithali husika katika
aya ifuatayo:

ً‫ٱﻪﻠﻟُ َﻣﺜَﻼً َﻋْﺒﺪاً ﱠﳑْﻠُﻮﻛﺎً ﻻﱠ ﻳَـ ْﻘ ِﺪ ُر َﻋﻠَ ٰﻰ َﺷ ْﻲ ٍء َوَﻣﻦ ﱠرَزﻗْـﻨَﺎﻩُ ِﻣﻨﱠﺎ ِرْزﻗﺎً َﺣ َﺴﻨﺎ‬ ‫ب ﱠ‬ َ﴿
َ ‫ﺿَﺮ‬
َ‫ٱﳊَ ْﻤ ُﺪ ِﱠﻪﻠﻟِ ﺑَ ْﻞ أَ ْﻛﺜَـُﺮُﻫ ْﻢ ﻻ‬
ْ ‫ﻓَـ ُﻬ َﻮ ﻳـُْﻨ ِﻔ ُﻖ ِﻣْﻨﻪُ ِﺳّﺮاً َو َﺟ ْﻬﺮاً َﻫ ْﻞ ﻳَ ْﺴﺘَـ ُﻮو َن‬
ٍ
‫َﺣ ُﺪ ُﳘَﺂ أَﺑْ َﻜ ُﻢ ﻻَ ﻳَـ ْﻘ ِﺪ ُر َﻋﻠَ ٰﻰ َﺷ ْﻲء َوُﻫ َﻮ َﻛﻞﱞ‬ َ‫ﲔأ‬ ِ ْ َ‫ٱﻪﻠﻟ َﻣﺜَﻼً ﱠر ُﺟﻠ‬
ُ‫ب ﱠ‬ َ ‫ﺿَﺮ‬ َ ‫ﻳَـ ْﻌﻠَ ُﻤﻮ َن۞ َو‬
39

ِ ْ� َ‫ﻋﻠَﻰ ﻣﻮﻻﻩ أَﻳـﻨَﻤﺎ ﻳـﻮِﺟﻬﻪﱡ ﻻ‬


‫ت ِﲞٍَْﲑ َﻫ ْﻞ ﻳَ ْﺴﺘَ ِﻮى ُﻫ َﻮ َوَﻣﻦ َ�ْ ُﻣُﺮ ﺑِﭑﻟْ َﻌ ْﺪ ِل َوُﻫ َﻮ‬ َ ّ َُ َ ْ ُ ْ َ ٰ َ
﴾‫اط ﱡﻣﺴﺘَ ِﻘﻴ ٍﻢ‬ ٍ ‫ﻋﻠَﻰ ِﺻﺮ‬
ْ َ ٰ َ
Dharaba Allahu mathalan AAabdan mamlookan la yaqdiru AAala shay-in waman
razaqnahu minna rizqan hasanan fahuwa yunfiqu minhu sirran wajahran hal
yastawoona alhamdu lillahi bal aktharuhum la yaAAlamoona, Wadharaba Allahu
mathalan rajulayni ahaduhuma abkamu la yaqdiru AAala shay-in wahuwa kallun
AAala mawlahu aynama yuwajjihhu la ya/ti bikhayrin hal yastawee huwa waman
ya/muru bialAAadli wahuwa AAala siratin mustaqeemin (Surat An Nahl 16:75-76)

Tafsir: Anakupigieni Allah mfano wa Mja ambae anamilikiwa na (Mja) mwenzake, na


hivyo akawa hana uwezo wowote, na Mtu mwengine ambae tumemjaalia riski nyingi
kutoka kwetu na hivyo akawa anatumia kwa siri na kwa uwazi, jee watakua sawa watu
hawa? Shukrani zote anastahiki Allah, lakini wengi wao hawajui. Na Allah anatoa
mfano wa watu wawili, ambapo mmoja wao ni bubu ambae hana uwezo wowote, na
hivyo kua ni mzigo kwa bwana wake, kwa kila upande amuelekezao hua hana faida
yeyote juu yake. Jee huyu hua ni sawa na yule anaeamrisha mema wakati mwenyewe
akiwa katika njia iliyonyooka.

Hayo ni maneno ya Muumba wa kila kitu na ndie pia alietuumba sisi na ndie anaetumiliki
na hivyo anatupa mithali zilizowazi kua bila ya shaka kitu ambacho kinamilikiwa na
hakina mamlaka yeyote basi hakiwezi pia kua na maamuzi yeyote isipokua kutekeleza
maamrisho ya Mmiliki na hivyo kuthibitisha kua Mwenye Mamlaka ya kila kitu
ulimwenguni ni Allah Subhanah wa Ta’ala na yeye pekee ndie anaestahiki Kuabudiwa
na Kushukuriwa kwani yeye ndie Muumba. Na juu ya hili basi kila mtu mwenye akili na
kutafakari hua ni mwenye kujua kua kuna tofauti baina ya Muumba na Kiumbe, pia baina
ya Mwenye uwezo na Asiekua na uwezo, Mwenye Nguvu na asiekua na nguvu, hivyo ni
ujinga ulio wazi pale inapokua Mtu hawezi kuona tofauti baina ya vitu viwili hivyo.

Kwa kua Allah Subhanah wa Ta’ala yeye ndie Muumba na Mmiliki wa kila kitu
Ulimwenguni iwe kikubwa au kidogo basi anawawekea wazi waja wake, kua yeye haoni
shida kututolea mifano hata kama ya mdudu Mbu, na zaid ya Mbu kiukubwa na pia zaidi
ya mbu kiudogo pia, pale aliposema katika Qurán:
40

ِ‫ﱠ‬ ‫﴿إِ ﱠن ﱠ‬
َ ‫ﻮﺿﺔً ﻓَ َﻤﺎ ﻓَـ ْﻮﻗَـ َﻬﺎ ﻓَﺄَﱠﻣﺎ ٱﻟﺬ‬
ْ‫ﻳﻦ َآﻣﻨُﻮا‬ َ ُ‫ب َﻣﺜَﻼً ﱠﻣﺎ ﺑَـﻌ‬ َ ‫ﻀ ِﺮ‬
ْ َ‫ٱﻪﻠﻟَ ﻻَ ﻳَ ْﺴﺘَ ْﺤ ِﻰ أَن ﻳ‬
ً‫ٱﻪﻠﻟُ ِﻬﺑـَٰ َﺬا َﻣﺜَﻼ‬ ِ ‫ٱﳊ ﱡﻖ ِﻣﻦ ﱠرﻬﺑِِﻢ وأَﱠﻣﺎ ٱﻟﱠ‬
‫ﻳﻦ َﻛ َﻔُﺮواْ ﻓَـﻴَـ ُﻘﻮﻟُﻮ َن َﻣﺎذَآ أ ََر َاد ﱠ‬
َ ‫ﺬ‬ َ ّْ َْ ُ‫ﻓَـﻴَـ ْﻌﻠَ ُﻤﻮ َن أَﻧﱠﻪ‬
ِِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ﻳُﻀ ﱡﻞ ﺑِﻪ َﻛﺜﲑاً َوﻳَـ ْﻬﺪى ﺑِﻪ َﻛﺜﲑاً َوَﻣﺎ ﻳُﻀ ﱡﻞ ﺑِﻪ إِﻻﱠ ٱﻟْ َﻔﺎﺳﻘ‬
Inna Allaha la yastahyee an yadhriba mathalan ma baAAoodhatan fama fawqaha
faamma alladheena amanoo fayaAAlamoona annahu alhaqqu min rabbihim
waamma alladheena kafaroo fayaqooloona madha arada Allahu bihadha mathalan
yudhillu bihi katheeran wayahdee bihi katheeran wama yudhillu bihi illa
alfasiqeena (Surat Al Baqara 2:26)

Tafsir: Hakika Allah haoni haya kukupigieni mifano hata ya Mdudu Mbu au juu yake
zaidi wakati unapokua uko juu (mfano wa ukubwa wa huyo mbu). Ama wale wenye
kuamini, basi wanajua kua ni ukweli kutoka kwa Mola wao, ama kwa wale wasioamini
basi husema: ‘Ah Allah amekusudia nini juu ya mfano huu.’ Kutokana na mfano huo
basi huwapotosha wengi na kuwaongoza wengi. Na huwapotosha wale tu ambao ni
wenye kumuasi.

Naam, anasema Sultan al Mutakallimin Mujaddid ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi
kua: Allah Subhanah wa Taála haoni haya kutoa mfano wa kile alichokiumba, lakini
hapo hapo hua ni mwenye kuona haya juu ya kutojibu dua ya maombi ya mja wake
aliemuomba kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: Allah
Subhanah wa Taála ni Hai na ni Mkarimu, kiasi ya kua anaona Haya kua mja wake
amenyanyua juu mikono yake kwa ajili ya kumuomba dua kisha yeye asimjibu dua
hio.

Katika kufafanua sehemu ya pili ya aya hii basi Sultan Al Balagha Imam Abu Al Qasim
Al Zamakhshari kua: Upotoshwaji hapa umenasibishwa na Allah Subhanah wa Taála
kwa sababu yeye ndie mwenye kutoa Mithali ambazo ndani yake hua kuna
muongozo kwa watu. Hivyo kwa wale watakaoufuata basi watakua ni wenye
kuongoka kutokana nao na wale watakaoukataa basi watapotoka. Anasema Malik
Ibn Dinar kua Siku moja alimtembelea mfungwa ambae alikua amefungwa
kutokana na kua na madeni mengi, na hivyo mtu huyo akamwambia Malik Ibn
Dinar kua: Hebu angalia namna tulivyofungiwa na kudhulumiwa haki zetu. Hivyo
Malik Ibn Dinar, akaangalia juu, na kuona kua kuna mkoba unaning’inia.

Hivyo nae akauliza: Jee ule ni mkoba wa nani? Ambapo yule mfungwa akajibu kwa
kusema: Ni wangu mie. Hapo Malik Ibn Dinar akaushusha mkoba ule chini ili
41

kuangalia mna nini ndani yake, na akaona kua mna Kuku na Halua, Hapo Malik
Ibn Dinar akasema: Ama hiki ndio kilichokufungisha. Yaani kuendekeza matamnio
ya Dunia na ya Nafsi.

Kwa upande mwengine basi, tunaona kua ayah hii ya mithali ya mdudu Mbu imetumia
neno BaAAoodhatan ambalo maana yake hua ni Mbu lakini mwishoni mwa jina hilo
kuna harfu Ta ambayo ni yenye kuonesha kua Mbu huyu si mbu yeyote yule, bali
ni Mbu jike kwani aya pia imetumia neno fawqaha yaani juu zaidi yake mbu jike.

Tunaweza kujiiuliza kwa nini labda Allah Subhanah wa Taála akatumia mfano wa
Mdudu mdogo huyu huku akibainisha kua haoni haya kummithilisha, kwa mtizamo wa
ghafla basi tunaweza kusema kua labda kutokana na uwezo wake Mbu jike wa kumdhuru
Ibn Adam na baadhi ya wakati kuweza kumsababishia hata kifo, kwani Mbu jike ndie
anaenyonya damu na kuitumia kwa ajili ya Mayai yao.

Lakini huo ni mtizamo wa juu juu tu, kwani mdudu Mbu ingawa ni mdogo kiumbo lakini
ana Miujiza mikubwa zaid inayostaajabisha. Kwani miongoni mwa sifa zao ni pamoja
na:

1-Kuna aina 2700 za Mbu.


2-Uzito wa Mbu hua ni baina 2-2.5 Milligram.
3-Mbu Jike katika uhai wake anaweza akanyonya lita milioni za Damu.
4- Mbu Dume huishi kwa muda wa siku 10-20 lakini Mbu Jike huishi kwa mda wa
siku 10-100.
5-Katika siku za kungára Mwezi basi Mbu huongezeka kwa mara 500 zaidi.
6-Mbawa za Mbu hua ni zenye kupiga mara 500 kwa kila sekunde moja.
7-Mbu ndio wadudu wanaoongoza kwa kuusababisha vifo Ulimwenguni.
8-Mbu hua wanapendelea damu ya watoto zaidi kuliko ya Watu wazima.
9-Mbu wanachukia mafuta ya ndimu kwa sababu hua yanawaumiza miguu yao.
10-Mbu anaweza akamfuatilia Mtu anaemtaka kumnyonya damu yake kwa umbali
wa futi 18.
11-Mbu wana Nyoyo tatu ambazo hufanya kazi sambamba.
12- Mbu wana Macho zaidi ya 100 kwenye kichwa chao.
13-Mbu wana Meno 48 katika midomo yao.
14-Mbu wana mbawa 3.
15-Mbu wana Sindano 6 katika pua zao, na kila Sindano ina kazi yake maalum.
16-Mbu wanaona kwa kutumia mionzi ya X-Ray na hivyo huweza kuona na
kuitofautisha ngozi ya Ibn Adam na vitu venyine katika kiza.
17-Mbu wanauwezo wa kupima aina ya Damu wanayoihitaji kwa sababu hua
wanapenda zaidi damu ya Group O, na hua hawapendi damu ya Group A.
18-Mbu wanaweza kusikia harufu ya Ibn Adam kutoka umbali wa futi 100.
42

19-Mbu huwa wananyonya damu za viumbe wengine lakini hupendelea zaidi damu
ya Ibn Adam kwa sababu hua ni rahisi kuwanyonya, na hua wanaweza kugundua
harufu ya hewa ya Carbon Dioxide tunayoitoa mwilini ambayo hua imechanganyika
na Lacti Acid, Octenol, Uric Acid na Fatty Acid na hivyo hua wanajua kua kuna Ibn
Adam katika maeneo ya karibu.
20-Mbu hua wana chanjo ya ganzi ya kuondoa maumivu ambayo humpiga mtu
wanaetaka kumyonya damu mara tu wanapotua juu ya ngozi ya mtu ili mtu huyo
asihisi maumivu ya kutobolewa na kuingizwa sindano ya mbu na kisha kunyonywa
damu huyo.
21-Mbu hua wana pampu ambayo huwaongezea kasi ya kunyonya damu nyingi
zaidi pale wanapoifungua na kuanza kunyonya damu wnayoitaka.

Hio ni baadhi tu ya Miujiza mikubwa ya Mithali ya Mdudu Mbu, na bila ya shaka Qurán
haikutumia Mithali ya mdudu Mbu tu bali pia imetumia mithali ya Mdudu Nzi pale
iliposema katika aya ifuatayo:

ْ‫ٱﻪﻠﻟِ ﻟَﻦ َﳜْﻠُ ُﻘﻮا‬


‫ون ﱠ‬ ِ ‫ﺿ ِﺮب ﻣﺜَﻞ ﻓَﭑﺳﺘَ ِﻤﻌﻮاْ ﻟَﻪ إِ ﱠن ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﺗَ ْﺪﻋﻮ َن ِﻣﻦ د‬
ُ ُ َ ُ ُ ْ ٌ َ َ ُ ‫ﱠﺎس‬ ُ ‫ٰ�َﻳـﱡ َﻬﺎ ٱﻟﻨ‬
﴿
ِ ِ
‫ﻒ‬ َ ُ‫ب َﺷْﻴﺌﺎً ﻻﱠ ﻳَ ْﺴﺘَﻨﻘ ُﺬوﻩُ ﻣْﻨﻪ‬
َ ُ‫ﺿﻌ‬ ُ ‫ٱﺟﺘَ َﻤﻌُﻮاْ ﻟَﻪُ َوإِن ﻳَ ْﺴﻠُْﺒـ ُﻬ ُﻢ ٱﻟ ﱡﺬ َﺎﺑ‬
ْ ‫ذُ َﺎﺑﺎﺑً َوﻟَ ِﻮ‬
﴾‫ﻮب‬ ِ
ُ ُ‫ﺐ َوٱﻟْ َﻤﻄْﻠ‬ُ ‫ٱﻟﻄﱠﺎﻟ‬
Ya ayyuha alnnasu dhuriba mathalun faistamiAAoo lahu inna alladheena
tadAAoona min dooni Allahi lan yakhluqoo dhubaban walawi ijtamaAAoo lahu wa-
in yaslubuhumu aldhdhubabu shay-an la yastanqidhoohu minhu dhaAAufa
alttalibu waalmatloobu (Surat al Hajj 22:73)

Tafsir: Enyi watu! Mnapigiwa mfano, hivyo usikilizeni kwa makini: Wale ambao
mnawaomba badala ya Allah, hawawezi kuumba hata Mdudu Nzi, hata kama
wakijikusanya pamoja kwa lengo hilo, na kama huyo Nzi akipokonya kitu kutoka
kwao, basi kamwe hawatokua na uwezo wa kumnyang’anya, wako dhaifu sana
waombaji na wanaoomba.

Hii ni mithali ambayo ndani yake Allah Subhanah wa Ta’ala anawapigia wale watu
wasiomuamini, mfano wa mdudu Nzi, mdudu ambae ni mdogo, asie na thamani,
asiependezesha sehemu anayotua kwa sababu hua ni sehemu yenye uchafu, na hata kama
haina uchafu basi Nzi akitua katika sehemu basi huwacha uchafu pale anapoondoka
katika sehemu husika, na pia huchukua kitu katika sehemu husika kiasi ya kua hakuna
Ibn Adam anaeweza kuona kwa macho yake kile alichokiwacha mdudu huyo wala
43

alichochukua mdudu huyo na hivyo hua haiwezekani kumpokonya alichochukua, kwa


sababu Nzi anapotaka kuchukua kitu fulani basi hutoa maji yenye kemikali ambayo
hukilainisha kitu hicho na kisha yeye hunyonya kilichomo ndani ya kitu husika na
kuondoka nacho kile cha ndani tu na hivyo hubakisha bua tupu yaani kile
kinachoonekana kwa mizamo wa nje na hivyo hua haonekani ni nini alichokichukua,
hivyo hua hakuna na uwezekano wa kupokonyeka kile alichokichukua.

Hapa haina haja ya kuzungumzia wingi wa wadudu Nzi, kwani kiaina tu basi kuna aina
90,000 za mdudu Nzi, ambao hua wanazaana kila baada ya wiki 2 huku kila Nzi jike hua
ni mwenye kutaga mayai 100. Na pia haina haja kuainisha juu ya maumbile ya Mbawa
zake mdudu Nzi ambapo kimaumbile hua zina hali ya upekee, ya kua na uwezo wa
kudhuru na uwezo wa kutibu.

Ambapo anasema Mujaddid ud Din Imam Shah Waliyu Allah Al Dahlawi katika Hujjat
Allah Al Baligha kua: Allah Subhanah wa Ta’ala anaweka wazi Hikma na Busara
zake katika kumuumba kwake Mdudu Nzi kua kila mdudu mwenye sumu basi hua
ni mwenye kujaaliwa kua na dawa ya kuondoa sumu hio kwa ajili ya kuulinda na
kuendeleza uhai wa mdudu huyo.

Ama kwa upande wa Shaykh al Akbar Imam Muhyi ad Din Abu Bakr Ibn Al Arabi basi
yeye anasema kua: Nzi mara zote hua ni mwenye kuliweka juu bawa lake lenye dawa
ili lisiguse kile kitu chenye umaji maji alichotulia juu yake, ili aweze kutumia Ubawa
huo kwa ajili ya kurukia anapotaka kuondoka kwa haraka katika sehemu hio, na
hii pia ni miongoni mwa Maumbile aliyojaaliwa kua nayo kutoka kwa Muumba,
ambapo sifa hii pia wanayo Sisimizi, Nyuki na Ndege wa aina ya Hud Hud. (Imam
al-Tahawi, Sharh Mushkil (8:343-344) Imam al-Khattabi, Ma`alim al-Sunan (4:459))

Ama hizi mithali za mdudu Nzi, Mbu na mithali nyenginezo zinathibitisha kua Allah
Subhanah wa Taála ndie Nuru ya kila kitu ulimwenguni yaani ni mwenye kuweka wazi
kile ambacho kilichokua hakijulikani na viumbe wake kama anavyosema yeye
mwenyeye katika aya ifuatayo:

‫ﺎح ِﰱ‬ ِ ‫ض ﻣﺜَﻞ ﻧُﻮِرﻩِ َﻛ ِﻤ ْﺸ َﻜﻮاةٍ ﻓِﻴﻬﺎ ِﻣﺼﺒ‬ ِ ِ ‫﴿ﱠ‬


ُ َ‫ﺼﺒ‬ ْ ‫ﺎح ٱﻟْﻤ‬
ٌ َْ َ ُ َ ‫ﻮر ٱﻟ ﱠﺴ َﻤ َﺎوات َوٱﻷ َْر‬ ُ ُ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻧ‬
َ‫ي ﻳُﻮﻗَ ُﺪ ِﻣﻦ َﺷ َﺠَﺮةٍ ﱡﻣﺒَ َﺎرَﻛ ٍﺔ َزﻳْـﺘُﻮﻧٍَﺔ ﻻﱠ َﺷْﺮﻗِﻴﱠ ٍﺔ َوﻻ‬ ‫ﺐ ُد ِّر ﱞ‬ ٌ ‫ﺎﺟﺔُ َﻛﺄَﻧـﱠ َﻬﺎ َﻛ ْﻮَﻛ‬
ٍ ‫زﺟ‬
َ ‫ﺎﺟﺔ ٱﻟﱡﺰ َﺟ‬َ َُ
‫ٱﻪﻠﻟُ ﻟِﻨُﻮِرﻩِ َﻣﻦ‬
‫ﻮر َﻋﻠَ ٰﻰ ﻧُﻮٍر ﻳَـ ْﻬ ِﺪى ﱠ‬ ِۤ ٍ
ُ ‫َﻏْﺮﺑِﻴﱠﺔ ﻳَ َﻜ‬
ٌ ‫ﺎد َزﻳْـﺘُـ َﻬﺎ ﻳُﻀﻲءُ َوﻟَ ْﻮ َﱂْ ﲤَْ َﺴ ْﺴﻪُ َ�ٌر ﻧﱡ‬
﴾‫ٱﻪﻠﻟ ﺑِ ُﻜ ِﻞ َﺷﻲ ٍء َﻋﻠَﻴِﻢ‬ ِ ‫ﺎل ﻟِﻠﻨ‬ ُ ‫ﻀ ِﺮ‬
ٌ ْ ّ ُ‫ﱠﺎس َو ﱠ‬ َ َ‫ٱﻪﻠﻟُ ٱﻷ َْﻣﺜ‬
‫ب ﱠ‬ ْ َ‫ﻳَ َﺸﺂءُ َوﻳ‬
44

Allahu nooru alssamawati waal-Ardhi mathalu noorihi kamishkatin feeha


misbahun almisbahu fee zujajatin alzzujajatu kaannaha kawkabun durriyyun
yooqadu min shajaratin mubarakatin zaytoonatin la sharqiyyatin wala
gharbiyyatin yakadu zaytuha yudee-o walaw lam tamsas-hu narun noorun AAala
noorin yahdee Allahu linoorihi man yashao wayadribu Allahu al-amthala lilnnasi
waAllahu bikulli shay-in AAaleemun.(Surat Al-Noor 24:35).

Tafsir: Allah ni Nuru ya Mbingu na Ardhi, mithli ya Nuru yake ni kama Mishkat
(Mishkat ni sehemu kama kidirisha ambacho hujengwa maalum kwa ajili ya kuwekea
taa ukutani na hivyo kufanya muangaza wa taa hiyo uwe mkubwa zaid pale taa
inapokua ndani ya kidirisha hicho kuliko taa hiyo ikikaa katika sehemu iliyo wazi), na
ndani yake mna taa, na taa hiyo imo ndani ya kioo. Kioo ambacho kinang’ara kama
nyota ya Durriyun (aina ya nyota yenye kung’ara sana kama Lulu), (taa) ambayo
imewashwa kutokana na mti mtakatifu wa Mzaituni usio wa Mashariki wala
Magharibi, ambao mafuta yake hutoa mwangaza bila ya kuguswa (kuwashwa) na
moto wowote. Nuru juu ya Nuru! Allah humuongoza katika mwangaza wake yeyote
yule amtakae. Na Allah anaweka wazi mifano kwa Bani Adam, Na hakika Allah ni
mwenye kujua kila kitu.

Hapa tunaona kua aya hii imetumia kiunganishi ‘ka’ kinachotafsirika kwa lugha ya
Kiswahili kama ‘kama’ ambacho hujulikana kama Kaf at tashbih ambayo inayoleta
maana ya kushabihisha kitu kimoja kua kinafanana tu na kitu chengine lakini hata hivyo,
kitu hicho si kitu chenyewe kilichokusudiwa. Kutumika kwa Kaf at Tashbih katika aya
hii kunaonesha kutokuwepo uwezekano wa kuelezea sifa za Majina ya Allah Subhanah
wa Ta’ala hata kupitia kwa njia za kufananisha kwani yeye mwenyewe anasema kua:

﴾ٌ‫ﺲ َﻛ ِﻤﺜْﻠِ ِﻪ َﺷ ْﻰء‬


َ ‫﴿ﻟَْﻴ‬
Laysa kamithlihi shay-un (Surat Ash Shuraa 42:11)

Tafsir: Hakuna kitu chenye mithli yake.

Na vile vile akasema:

َ ‫﴿وَﱂْ ﻳَ ُﻜ ْﻦ ﻟﱠﻪُ ُﻛ ُﻔﻮاً أ‬


﴾‫َﺣ ٌﺪ‬ َ
Walam yakun lahu kufuwan ahadun (Surat Al Ikhlas 112:4)

Tafsir: Hakuna anaefanana nae.


45

Hivyo ufananisho huu wa Sifa ya ‘Nuru ya Allah’ hauwezi kuonesha ukweli halisi
ulivyo, bali ufafanisho huu umetumika ili kufafanua kimaana kutokana na ufahamu wa
walengwa waliokusudiwa, kwa sababu ukweli halisi wa ‘Nur ya Allah’ ni ukweli ambao
hauwezi kufikirika kwa hali yeyote ya kiumbe yeyote yule na wala hauwezi kuelezeka
kwa lugha ya kiumbe chochote.

Hujjat ul Islami Mujaddid ud Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn
Muhammad Al Ghazali katika kuielezea maana ya Al Nur anasema kua: Al Nur ni yule
anaeonekana kutokana na kuvifanya vitu vyote vionekane, kwani kila kitu
kinachoonekana chenyewe na kusababisha vitu vyengine vionekane hua kinaitwa
Nuru. Tukiangalia kwa mtazamo wa kua kila kilichokuwepo hupingana na
kisichokuwepo, basi kile kinachoonekana hakiwezi kulinganishwa na kitu chengine
isipokua tu na kile kilichokuwepo. Kwani hakuna kiza kilichokua cheusi zaidi
kuliko kile kiza cha kitu kisichokuwepo.

Kile kilichokua huru kutokana na giza la kutokuwepo, na kua na uwezekano wa


kutokuwepo, na huondoa kila kitu kutoka katika kiza cha kutokuwepo na
kukiingiza katika udhihirisho wa kuwepo, basi hua kinastahiki kuitwa Nuru.
Kuwepo ni Nuru iliyohuru isiyotegemea kitu inayomurika kila kitu kutokana na
asili ya Nuru yake Allah Subhanah wa Ta’ala, kwani Allah Subhanah wa Ta’ala ni
Nuru ya Mbingu na Ardhi. Na kama ilivyokua hakuna hata muale mmoja wa
muangaza wa Jua ambo huonesha kua hio ndio chanzo cha muangaza wa Jua hilo,
basi vile vile hakuna hata chembe moja ya kitu kutoka katika vitu vilivyomo ndani
ya Mbingu na Ardhi, ambacho hakimpelekei mtu kukosa uhakika wa kutokana na
uwezekano wa kuwepo kwake bila ya kuhitaji kuwepo kwa yule aliesababisha
kuwepo kwa kitu hicho.

Hivyo kutokana na Nuru, hususan Nuru ya Allah, basi kila kitu hua kiko wazi, chenye
kuonekana, chenye kufahamika na hivyo kua ni chenye uhakika na chenye kua na yakini.

Ama kwa upande mwengine basi anasema Hasan Al Basr kua: ‘Mithali ya Nuru ya
Qurán ni Misbah (Taa). Misbah ambayo Sirajan (Moto au Muangaza) yake ni
Maarifah (Maarifa ya kuokoka Kinafsi) na Fatil (Utambi) yake ni Faraidh (FArdhi
za Dini) ambao Dhuhn (Mafuta) yake ni Ikhlas na Nuru yake (Ya Kiroho) ni ya
Ittisal (Kufikia Darja inayotakiwa kufikiwa). Hivyo kila Ikhlas ikizidi kiusafi basi
mwangaza wa Taa ndio hua unazidi zaidi. Na kila faradhi za dini zinapozidi basi
ndio unapopatikana uhakika (Haqiqa) na ndivyo Nuru inavyozidi.’

Allah Subhanah wa Taála anatupigia mifano myengine juu ya wale watu ambao
hawatomuamini yeye na hivyo kua ni wenye kumshirikisha kua ni wasiojua udhaifu
mkubwa sana wa kile wanachokiamini na kuona kua kinawanufaisha kwa kusema:
46

ِ ِ ِ‫ون ﱠ‬ ِ ‫﴿ﻣﺜَﻞ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﱠٱﲣَ ُﺬواْ ِﻣﻦ د‬


ْ ‫ٱﻪﻠﻟ أ َْوﻟﻴَﺂءَ َﻛ َﻤﺜَ ِﻞ ٱﻟْ َﻌﻨ َﻜﺒُﻮت ﱠٱﲣَ َﺬ‬
‫ت ﺑـَْﻴﺘﺎً َوإِ ﱠن‬ ُ َ ُ َ
﴾‫ﻮت ﻟَﻮ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳَـ ْﻌﻠَﻤﻮ َن‬ِ ِ
ُ ْ ُ‫ﺖ ٱﻟْ َﻌﻨ َﻜﺒ‬ ُ ‫أ َْوَﻫ َﻦ ٱﻟْﺒُـﻴُﻮت ﻟَﺒَـْﻴ‬
Mathalu alladheena ittahadhoo min dooni Allahi awliyaa kamathali alAAankabooti
ittakhadhat baytan wa-inna awhana albuyooti labaytu alAAankabooti law kanoo
yaAAlamoona (Surat Al Anqabut 29:41)

Tafsir: Mithili ya wale ambao wanaoichukua Miungu myengine zaidi ya Allah, hua ni
mithli ya Buibui ambae hujijengea nyumba. Lakini kwa hakika! Hakuna nyumba
dhaifu kama nyumba ya Buibui, lau kama wao wangejua.

Katika aya hii ya Surat Al Anqabut ambayo ndio aya iliyotoa jina la Sura hii, basi tunaona
kua Allah Subhanah wa Taála anatutolea mfano wa Al Anqabut yaani mdudu Buibui
ambae anaelezewa Nyumba yake anayoijenga na kuishi kwa kutumia uzi laini wa Hariri
ambao anautoa ndani ya mdomo wake tena kwa wingi sana kiasi ya kua anaweza
akajenga nyumba baina ya miti miwili kwa kuurusha uzi huo kwa umbali mita 25 kutoka
upande mmoja hadi mwengine bila ya kuonekana kwa dalili ya kuishiwa kwa uzi wake
huo wa Hariri wenye kutokana na Protein ambayo inatokana na madini ya Carbon,
Hydrogen, Oxygen na Nitrogen zinazozalishwa kwa wingi sana na mwili wake, na hadi
hii leo Wanasayansi na utaalamu wao wote bado hawajapata jibu juu ya uwezo wa Buibui
katika kuzalisha kwa wingi uzi huo bila ya kuishiwa na madini hayo hususan
ukilinganisha na ukubwa wa mwili wa mdudu Buibui.

Tunapoiangalia aya hii basi tunaona kua imetumia neno ‘Ittakhadha’ ambalo kwa kiarabu
hua ni lenye kumaanisha: Afanyae Kitu, Mwenye kuchukulia Kitu au Mwenye Kitu.
Lakini sasa neno Ittakhadha lililotumika hapa mwishoni mwake limeishia na harfu
‘ta’ na hivyo limekua katika hali ya Ittahadhat ambayo ni yenye kumaanisha jinsia
ya Kike.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala hapa anatuwekea wazi kua Buibui anaejenga nyumba
hua ni Buibui jike, na hivyo ni Buibui jike ndie anaedumu katika nyumba husika na wala
si Buibui dume. Jambo ambalo limethibitishwa pia na Wanasayansi wa Kijerumani
mnamo mwaka 1984 pale walipochapisha matokeo ya uchunguzi wao huo katika gazeti
la Cosmos Magazine la Ujerumani ambao umethibitisha hivyo. Hii ni kuthibitisha
miongoni mwa Miujiza mingi ya Qurán.

Ni maumbile ya Mdudu Buibui kua na uwezo wa kuzalisha uzi huu wa kujengea nyumba
yake ambapo nyumba hio hua na nyuzi aina tano tofauti, kuna nyuzi pana ambazo ndio
hua msingi wa nyumba na ndio anazotumia yeye katika kuzunguka na kuisimamia
47

nyumba hio, ingawa uzi huu ambao ndio msingi wa nyumba yake hua ni mpana lakini
upana wake haufiki hata upana wa milimita moja, Buibui pia hua anazalisha Uzi maalum
kwa ajili ya kuhifadhia Mayai yake, Uzi maalum kwa ajili ya kujilinda, na Uzi maalum
kwa ajili ya Kuhifadhia chakula chake na wadudu anaowakamata, na pia huzalisha uzi
mwengine ambao ni mwembemba zaidi kwa ajili ya hujenga ukuta ambao hua pia kama
mtego kwa ajili ya maadui zake na hapo hapo kwa ajili ya wadudu ambao hua ndio
chakula chake, na hivyo Buibui hua ni mwenye kusubiri katikati ya nyumba yake hado
pale nyuzi nyembamba zinapotetemeka na hivyo hujua kua upande fulani kuna mdudu
ameshaganda tayari, hivyo Buibui kwa kutumia nyuzi nene basi huelekea upande
uliotokea mtetemeko huo kwa kutumia nyuzi nene na kutembea hadi katika sehemu
aliyoganda mdudu kwenye mtego wake.

Kwa kimaumbile nyuzi zote hizi za aina mbili ingawa ni laini na nyembamba ambapo
nyuzi zenye uzito wa gramu 320 hua na uwezo wa kuzungushwa dunia nzima kutoka
pande moja hadi nyengine, lakini ni nyuzi ambazo hazina mfano wake katika uimara
wake, kwani nyuzi hizi hua na umadhubuti wa mara 100 zaidi ukilinganishwa na
umadhubuti wa uzi wa chuma cha pua ambacho ni chuma kigumu zaidi, mbali ya kua
Uzi wa Buibui ni madhubuti lakini pia uzi huo hua na uwezo wa kuvutika kwa mara nne
zaidi ya urefu wake wa kimaumbile bila ya kukatika na ukikusanywa pamoja hua na
ugumu mkubwa sana kwa mara 10 zaidi ya materiali ya Kevla ambayo hutumika kwa
ajili ya kutengenezea mavazi ya Bullet Proof yaani yanayovaliwa ili kuzuia risasi isitokee
upande wa pili na hivyo kuzuia zisiingie mwilini mwa Ibn Adam.

Si hivyo tu bali pia uzi huu wa Buibui hua ni wenye kujivuta na kupunguza urefu wake
kwa 50% unaponyeshewa na mvua na pia una uwezo wa kupitisha nguvu za mawasiliano
ya umeme haraka na kwa wingi zaidi kuliko kitu chochote kile kwani hata waya wa shaba
ambao ndio unaotumika kusafirishia umeme majumbani hua haufikii uwezo wa uzi wa
Buibui. Mbali ya kua na sifa zote hizo na nyenginezo lakini hapo hapo Allah Subhanah
wa Ta’ala anasema kua:

ِ ِ
﴾‫ﻮت ﻟَﻮ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳـَ ْﻌﻠَﻤﻮ َن‬
ُ ُ ‫﴿ َوإِ ﱠن أ َْوَﻫ َﻦ ٱﻟْﺒُـﻴُﻮت ﻟَﺒَـْﻴ‬
ْ ُ‫ﺖ ٱﻟْ َﻌﻨ َﻜﺒ‬
Wa-inna awhana albuyooti labaytu alAAankabooti law kanoo yaAAlamoona (Surat
Al Anqabut 29:41)

Tafsir: Lakini kwa hakika! Hakuna nyumba dhaifu kama nyumba ya Buibui, lau kama
wao wangejua.

Kua hii ni nyumba ambayo mbali ya kua ni nyumba iliyojengwa kwa nyuzi zenye
umadhubuti wa hali ya juu kwa mdudu Buibui mwenyewe na wadudu wengine ambao
48

hua ndio chakula chake, lakini hapo hapo basi tunaona kua hakuna nyumba iliyo dhaifu
ndani na nje kama ilivyo nyumba ya Buibui, kwani mbali ya kua kwa nje inaweza
kuvunjwa na kuteketezwa mara moja na wale wenye uwezo zaidi ya Buibui na haiwezi
kumzuia Buibui huyo na madhara ya mvua wala ya jua kama tunavyojua lakini pia kwa
ndani ya nyumba hio basi hua na mazingira ya kutoishika kwa Buibui dume ambae yeye
kufariki kwake hutokea mara tu baada ya kumnyatia taratibu na kumuingilia Buibui jike
ambapo Buibui jike nae humgeuza Buibui dume huyo kua ni chakula chake huku wakiwa
katika hali ya kuingiliana. Jambo hili humpelekea Buibui jike kupata mayai ya akiba zaidi
kutoka kwa Buibui dume.

Na kwa baadhi ya Buibui basi pia Buibui jike hua ni mwenye kufariki mda mfupi tu mara
baada ya mayai kutoa watoto kwani watoto hao humgeuza mama kua ndio chakula chao
na ndio maana Buibui hutaga mayai takriban 3000 kwa mkupuo mmoja.

Bila ya shaka Allah Subhanah wa Ta’ala anatupigia mithali ili tupate kutafakkar ambako
nako kutatupelekea kufaham maana na makusudio ya mithali hizo kama alivyosema:

﴾‫ﱠﺎس وَﻣﺎ ﻳَـ ْﻌ ِﻘﻠُ َﻬﺂ إِﻻﱠ ٱﻟْ َﻌﺎﻟِﻤﻮ َن‬ ِ ْ َ‫ﺎل ﻧ‬
َ ‫﴿ َوﺗِْﻠ‬
ُ َ ِ ‫ﻀ ِﺮﺑـُ َﻬﺎ ﻟﻠﻨ‬ ُ َ‫ﻚ ٱﻷ َْﻣﺜ‬
Watilka al-amthalu nadhribuha lilnnasi wama yaAAqiluha illa alAAalimoona
(Surat Al Anqabut 29:43)

Tafsir: Na tunaipiga mifano hii kwa watu, lakini hakuna atakaefahamu isipokua wale
wenye kujua.

Allah Subhana wa Ta’ala anamalizia kuweka wazi juu ya aina mbali mbali za mifano na
mithali kwa ajili ya kuwanufaisha viumbe wake kwa kusema:

‫آن ِﻣﻦ ُﻛ ِّﻞ َﻣﺜَ ٍﻞ َوﻟَﺌِﻦ ِﺟْﺌـﺘَـ ُﻬ ْﻢ ِﺂﺑﻳٍَﺔ ﻟﱠﻴَـ ُﻘﻮﻟَ ﱠﻦ‬
ِ ‫ﱠﺎس ِﰱ ﻫـٰ َﺬا ٱﻟْ ُﻘﺮ‬
ْ َ ِ ‫ﻨ‬ ‫ﻠ‬ِ‫﴿وﻟََﻘ ْﺪ ﺿﺮﺑـﻨﺎ ﻟ‬
ََْ َ َ
﴾‫ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ َﻛ َﻔﺮ ۤواْ إِ ْن أَﻧﺘُﻢ إِﻻﱠ ُﻣْﺒ ِﻄﻠُﻮ َن‬
ْ ُ َ
Walaqad dharabna lilnnasi fee hadha alqur-ani min kulli mathalin wala-in ji/tahum
bi-ayatin layaqoolanna alladheena kafaroo in antum illa mubtiloona (Surat Ar Rum
30:58)
49

Tafsir: Na bila ya shaka, tumeipiga kwa ajili ya watu ndani ya hii Quran kila mifano,
lakini kama ukiwaletea wao vithibitisho basi wasioamini watasema kua: Hakika nyinyi
hamkua isipokua ni wenye kujishughulisha na mambo ya kipuuzi.

Hivyo bila ya shaka mifano na mithali hizo wamepigiwa Ibn Adam ili watumie akili zao
wapate kujiokoa na adhabu za Mola wao, kwani wasipotafakkar basi watakua ni watu
waliopotoka na wataingia Motoni, na hua si sawa watu Motoni na watu wa Peponi, kwani
watu wa Peponi hua si watu waliopotoka bali hua ni watu waliofuzu. Allah
anatukumbusha haya na kutuwekea wazi, thamani, uzito na umuhimu wa Qurán kwa
kutuambia:

‫ٱﳉَﻨ ِﱠﺔ ُﻫ ُﻢ ٱﻟْ َﻔﺂﺋُِﺰو َن۞ ﻟَ ْﻮ‬


ْ ‫ﺎب‬ ‫ﺤ‬ ‫َﺻ‬ ‫أ‬ ِ ‫ٱﳉﻨ‬
‫ﱠﺔ‬ ْ ‫ﺎب‬ ‫ﺤ‬ ‫َﺻ‬ ‫أ‬‫و‬ ‫ر‬ِ ‫ﱠﺎ‬
‫ﻨ‬ ‫ٱﻟ‬ ‫ﺎب‬ ‫ﺤ‬ ‫َﺻ‬ ‫أ‬ ۤ ‫﴿ﻻ ﻳﺴﺘ ِﻮ‬
‫ي‬
ُ َ ْ َ ُ َ َ ْ ُ َ ْ َْ َ َ
ِ‫ﺎﺷﻌﺎً ﱡﻣﺘﺼ ِّﺪﻋﺎً ِﻣﻦ ﺧ ْﺸﻴ ِﺔ ﱠ‬
‫ﻚ‬َ ‫ٱﻪﻠﻟ َوﺗِْﻠ‬ َ َ ّْ َ َ
ِ ‫أَﻧﺰﻟْﻨَﺎ ﻫـٰ َﺬا ٱﻟْ ُﻘﺮآ َن ﻋﻠَﻰ ﺟﺒ ٍﻞ ﻟﱠﺮأَﻳـﺘَﻪ ﺧ‬
َ ُ ْ َ ََ ٰ َ ْ َ َ
ِ ‫ٱﻪﻠﻟ ٱﻟﱠ ِﺬى ﻻَ إِﻟَـٰﻪ إِﻻﱠ ﻫﻮ ﻋ‬
‫ﺎﱂ‬ ‫ﻮ‬ ‫ﻫ‬ ۞ ‫ن‬ ‫و‬ ‫ﺮ‬ ‫ﱠﺎس ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻬﻢ ﻳَـﺘَـ َﻔ ﱠ‬
‫ﻜ‬ ِ ‫ﻨ‬ ‫ﻠ‬ِ‫ﻀ ِﺮﺑـﻬﺎ ﻟ‬
ُ َ َ ُ َ ‫ﱠ‬
ُ َ ُ َ ُ ْ َ ُ ْ َ‫ﺎل ﻧ‬ ُ َ‫ٱﻷ َْﻣﺜ‬
ِ ِ ‫ﺐ وٱﻟﺸﱠﻬﺎدةِ ﻫﻮ ٱﻟﱠﺮ ْﲪـٰﻦ ٱﻟﱠﺮِﺣﻴﻢ ۞ ﻫﻮ ﱠ‬
‫ﻚ‬ُ ‫ٱﻪﻠﻟُ ٱﻟﱠﺬى ﻻَ إِﻟَـٰﻪَ إِﻻﱠ ُﻫ َﻮ ٱﻟْ َﻤﻠ‬ َُ ُ ُ َ َ ُ َ َ َ ‫ٱﻟْﻐَْﻴ‬
ِ
‫ٱﻪﻠﻟِ َﻋ ﱠﻤﺎ‬ ْ ‫ﱡوس ٱﻟ ﱠﺴﻼَ ُم ٱﻟْ ُﻤ ْﺆِﻣ ُﻦ ٱﻟْ ُﻤ َﻬْﻴ ِﻤ ُﻦ ٱﻟْ َﻌ ِﺰ ُﻳﺰ‬
‫ٱﳉَﺒﱠ ُﺎر ٱﻟْ ُﻤﺘَ َﻜِّﱪُ ُﺳْﺒ َﺤﺎ َن ﱠ‬ ُ ‫ٱﻟْ ُﻘﺪ‬
‫ٱﳊُ ْﺴ َ ٰﲎ ﻳُ َﺴﺒِّ ُﺢ ﻟَﻪُ َﻣﺎ ِﰱ‬ْ ُ‫َﲰَﺂء‬ْ ‫ﺼ ِّﻮُر ﻟَﻪُ ٱﻷ‬ َ ‫ئ ٱﻟْ ُﻤ‬ ُ ‫ٱﳋَﺎﻟِ ُﻖ ٱﻟْﺒَﺎ ِر‬
ْ ُ‫ٱﻪﻠﻟ‬‫ﻳُ ْﺸ ِﺮُﻛﻮ َن۞ ُﻫ َﻮ ﱠ‬
﴾‫ٱﳊَ ِﻜﻴﻢ‬ ِ ِ ‫ات َوٱﻷ َْر‬ ِ ‫ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬
ُ ْ ‫ض َوُﻫ َﻮ ٱﻟْ َﻌﺰ ُﻳﺰ‬ ََ
La yastawee as-habu alnnari waas-habu aljannati as-habu aljannati humu alfa-
izoona;Law anzalna hadha alqur-ana AAala jabalin laraaytahu khashiAAan
mutasaddiAAan min khashyati Allahi watilka al-amthalu nadribuha lilnnasi
laAAallahum yatafakkaroona; Huwa Allahu alladhee la ilaha illa huwa AAalimu
alghaybi waalshshahadati huwa alrrahmanu alrraheemu; Huwa Allahu alladhee la
ilaha illa huwa almaliku alquddoosu alssalamu almu/minu almuhayminu
alAAazeezu aljabbaru almutakabbiru subhana Allahi AAamma yushrikoona;
Huwa Allahu alkhaliqu albari-o almusawwiru lahu al-asmao alhusna yusabbihu
lahu ma fee alssamawati waal-Ardhi wahuwa alAAazeezu alhakeemu; (Surat Al
Hashr 59:20-24)
50

Tafsir: Hawako sawa watu wa Motoni na Watu wa Peponi, kwani Watu wa Peponi
watakua ni waliofuzu. Lau kama tungeishusha hii Qurán kwa ajili ya Majabali, basi
kwa hakika ungeona namna Majabali yanavyonyenyekea na kumomonyoka kutokana
na kumuogopa Allah. Na hizi ni Mithali ambazo tunawapigia watu ili watafakkari!
Hakika yeye ni Allah ambae hakuna Mungu isipokua yeye. Mjuzi wa yasiyoonekana
na yanayoonekana. Yeye ni mwingi wa Rehma na Huruma. Yeye ni Allah ambae
hakuna Mungu isipokua yeye, yeye ndie Mfalme, Mtukufu, Asiekua na Kasoro,
Mwenye kuwahakikishia Usalama viumbe wake, Msimamizi wa Amani ya viumbe
wake wote, Muangalizi wa vitendo vya Viumbe wote, Mwenye uwezo Mkubwa sana wa
kulipa kwa kuadhibu kwa adhabu kali kabisa, Mwenye Uwezo Mkubwa wa kusimamia
mambo ya viumbe na kuwaweka chini ya khiari yake kama atakavyo, Mwenye Ukubwa
wa pekee usiokua na Kifani katika kila kitu. Utukufu ni wake yeye Allah ambae hana
mshirika. Yeye ni Allah ambae ndie Muumbaji, Muanzishaji wa kila kitu bila ya
kuhitajika kuwepo kwa kitu chengine katika kuanzisha kwake huko, Mwenye Kuumba
kwa namna na aina ya vitu atakavyo, kwake yeye ndio kwenye Umiliki wa Majina
Yenye Sifa Bora ambae anatukuzwa na kila kilichomo Mbinguni na kilichomo
Ardhini, na ni Mwenye Uwezo wa kila kitu na mwenye Hikma katika kila kitu
akifanyacho.

Baaada ya kutuwekea wazi hayo basi Allah Subhanah wa Taála anatupa mithali nyengine
hapo hapo kutuwekea wazi kua Viumbe walioumbwa na kupewa ukubwa wa mara 1000
zaidi yetu, yaani Milima basi hua inafahamu jukumu lake mbele ya Mola wake kiasi ya
kua kama ingeshushiwa Qurán basi bila ya shaka ingetetemeka na kububujika kutokana
na kua na khofu kwa Mola wake, lakini Ibn Adam asietumia akili yake na kutafakkar juu
ya Qurán basi basi hua ni mjinga mwenye kuipuuza na kutokua na khofu yeyote mbele
ya Mola wake kutokana na ujinga wake na kutojua majukumu yake.

Hivyo, basi Allah Subhanah wa Ta’ala anatoa mithali na visa ndani ya Qurán ili angalau
tupate kujifunza pale tutakapozingatia na kutilia maanani visa, mifano na mithali hizo na
ni kutokana na kutafakkar na kuzingatia kwake basi ndio tunapopata uongofu kwa
kufuata njia sahih tunazoelekezwa ndani yake na kuachana na njia potovu tunazokatazwa
kuzifuata kulingana na mifano hai tunayooneshwa kupitia katika njia zilizomo ndani ya
Kitabu chake Qurán na Sunnah za Nabii wake Muhammad Salallahu Aálayhi wa Salam
ikiwemo Mithali zinazoainisha kanuni za mawasiliano ya kauli kama isemavyo aya
ifuatayo:

ٍ ِ
ٌ ِ‫َﺻﻠُ َﻬﺎ َﺎﺛﺑ‬
‫ﺖ َوﻓَـْﺮﻋُ َﻬﺎ‬ ْ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻣﺜَﻼً َﻛﻠ َﻤﺔً ﻃَﻴِّﺒَﺔً َﻛ َﺸ َﺠﺮةٍ ﻃَﻴِّﺒَﺔ أ‬
‫ب ﱠ‬ َ ‫ﺿَﺮ‬ َ ‫ﻒ‬َ ‫﴿ أََﱂْ ﺗَـَﺮ َﻛْﻴ‬
‫ٱﳊَﻴَﺎةِ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ َوِﰱ‬
ْ ‫ﺖ ِﰱ‬ ِ ِ‫ٱﻪﻠﻟ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ آﻣﻨُﻮاْ ﺑِﭑﻟْ َﻘﻮِل ٱﻟﺜﱠﺎﺑ‬ ِ
ْ َ َ ُ‫ﺖ ﱠ‬ ُ ِّ‫ِﰱ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤﺂء ۞ ﻳـُﺜَـﺒ‬
51

ٍ‫ٱﻪﻠﻟ َﻣﺎ ﻳَ َﺸﺂء۞ وَﻣﺜﻞ َﻛﻠِﻤ ٍﺔ َﺧﺒِﻴﺜٍَﺔ َﻛ َﺸ َﺠﺮة‬ ِ ِ ‫ﻀ ﱡﻞ ﱠ‬


َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
ِ
ِ ‫ٱﻵﺧﺮةِ وﻳ‬
َ َ ُ َ ُ ُ‫ﲔ َوﻳَـ ْﻔ َﻌ ُﻞ ﱠ‬ َُ َ
﴾‫ض َﻣﺎ َﳍَﺎ ِﻣﻦ ﻗَـﺮا ٍر‬
ِ ‫َر‬‫ﻷ‬‫ٱ‬ ِ ‫ﺧﺒِﻴﺜٍَﺔ ٱﺟﺘُـﺜﱠﺖ ِﻣﻦ ﻓَـﻮ‬
‫ق‬
َ ْ ْ ْ ْ َ
Alam tara kayfa dharaba Allahu mathalan kalimatan tayyibatan kashajaratin
tayyibatin asluha thabitun wafarAAuha fee alssama/-I, Tu/tee okulaha kulla heenin
bi-idhni rabbiha wayadribu Allahu al-amthala lilnnasi laAAallahum
yatadhakkaroona, Wamathalu kalimatin khabeethatin kashajaratin khabeethatin
ijtuththat min fawqi al-Ardhi ma laha min qararin (Surat Ibrahim 14:24-26)

Tafsir: Jee hujaona namna Allah anavyopiga mifano, kauli nzuri hua ni kama mti
ambao asili yake (mizizi yake) iko thabit (imekomaa ardhini) na umechipua kuelekea
juu angani, huzaa matunda kila msimu kwa idhini ya Mola wake, na Allah anatoa
mifano kwa watu ili wapate kukumbuka. Na mithili ya kauli mbovu hua ni sawa na
mti uliong’oka na kua juu ya Ardhi ukiwa hauna uimara.

Bila ya shaka mfano wa Mti usiokua na mizizi imara au Mti ambao upo juu juu hua ni
Mti usiokua na faida yeyote kwani hautoweza kutoa Matunda, huu ni mfano mzuri ambao
pia unatuonesha kua amali za mtu asiekua ni mwenye kuamini basi hua hazina faida
kwake isipokua hapa hapa Duniani kwani Akhera hua hana malipo yeyote isipokua
hasara.

Anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi
wa Salam alienda kwa Masahaba akawakuta wanazungumzia juu ya Kalimatan
Tayyibatan ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Kalimatan
Tayyibatan ni kama Muumini ambae mizizi yake, imezama ardhini na Matawi yake
yako Mbinguni.’

Yaani amali zake hua zinanyanyuliwa mbinguni na zinakubaliwa Hivyo hii mithali
ambayo Allah Subhanah wa Taála amemithilisha kwa Waumini na Makafiri. Na
akasema Kalimatan Tayyibatan hua ni kauli za kweli zenye Ikhlasi ndani yake, hua
ni Shajaratin Tayyibatin yaani kama Mtende ambao mizizi yake ni madhubuti
ardhini na majani yake yamefikika Mbiguni.

Vile vile ndivyo ilivyo amali za Muumini ambazo zimepatikana kutokana na


kuthibitisha kwa Kalimat at Tawhid ambayo ni mzizi madhubuti wenye matawi yake
Mbinguni yaani amali zake zimenyanyuliwa juu Mbinguni na ni zenye kukubaliwa,
isipokua labda ziwe ni zenye kasoro (Ihdath) ndani yake. Lakini hata hivyo Mzizi
wa amali zake katika kumpwekesha Mola wake hauondolewi, hivyo hii inakua
52

kama vile ambavyo upepo unapovuma na kuyumbisha majani ya Mtende tu, huku
mizizi yake ikiwa madhubuti ardhini.

Na amezimithilisha kauli za Mtu asieamini na Shajara al Khabitha kwa kusema kua:


‘Wamathalu kalimatin khabeethatin kashajaratin khabeethatin’ kumaanisha mti wa
aina ya Hanzal (Matikiti ya Jangwani yasiyolika) ambao hakuna mti wenye ladha
mbaya sana kama huo, kwani hauna mizizi chini yake. Kama vile ilivyokua Kufr na
Unafik ambao haustahmiliwi kesho Akhera. Hivyo katika hazina ya Allah
Subhanah wa Taála hakuna hazina nzito kama Kalimat Tawhid!’



AINA ZA KALIMAT (KAULI) NDANI YA QURÁN


Neno Kalimatan ni neno lililotokana na neno Kalama ambalo kwa Lugha ya Kiarabu hua
ni lenye kumaanisha Kutoa Kauli, Kuzungumza, Kusema, Kuelezea kwa maneno, Kutoa
Mtizamo juu ya jambo Fulani, Kutoa habari au Amri, Ahadi, Kuwasilisha Ujumbe na pia
humaanisha Mtizamo au mawazo ambayo yamo ndani ya Ufahamu lakini bado
haujatamkwa.

Hivyo Qurán inatutolea mithali ya kauli njema kwa kutufunza pia umuhimu wa kanuni
za mawasiliano ya kufikisha ujumbe baina ya Mitume na watu wanaowapelekea ujumbe
katika jamii zao, Viongozi, Watawala, Wenye I’lm na wasiokua na I’lm, wafuasi wao na
wapinzani wao na kadhalika, kwa sababu kanuni za mawasiliano ya kufikisha ujumbe
kwa wahusika ni sehemu ya Iman na Ihsan ya dini ya Kiislam.

Kwani anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘Al Islam
(Uislam) ni Hukm, Al Iman ni Wasl (Kuiwasilisha kwa Allah Subhanah wa Taa’la)
na Ihsan ni Thawab (Malipo). Hivyo Uislam ni Iqrar (kuthibitisha) ambako hua ni
wenye kuonekana, lakini Iman hua haionekani, wakati Ihsan hua ni Taábud
(Ufanyaji Ibada)’

Hivyo ingawa neno Kalimah hua ni lenye kumaanisha pia Qawl (Kauli) lakini pia hapo
hapo hua linatofautiana kimaana pale tunapoona kua neno Kalimah hua linamaanisha pia
Mtizamo ambao umo ndani ya ufahamu wa Ibn Adam lakini haujatamkwa na ulimi, wala
kuoneshwa kwa njia yeyote ya ishara na hivyo hua ni mtizamo ambao haujaingia katika
hali ya Qawl.
53

Neno Qawl hua ni lenye kutokana na neno Qulu ambalo kwa kilugha hua linamaanisha
Kutoa kauli, Kusema, Kuzungumza, Kutamka, Kuelezea, Kuhadithia, Kunukuu na hua
pia linatumika katika kuainisha kitu au tukio halisi linalotokea bila ya kusikika sauti ya
maneno, kwa mfano pale mtu anaposema: ‘Qalat laha al aynayn samaAna wa ta’Atan’
yaani: ‘Yalimwambia yeye macho yangu nimesikia na nitatii’. Au pale wanaposema:
‘Imta'a ala hawdhu wa qala qatni’, yaani: ‘Lilijaa Hodhi hadi likasema imetosha’.

Neno Qala ndio lililotoa neno Qawlan ambalo humaanisha kutoa Kauli, Kusema,
Kuashiria au Kuelezea kwa kutumia njia ya kutoa sauti kama inavyosema aya ifuatayo
ambayo inakataza utumiaji wa kauli mbovu zisizokua na maana na hususan inapokua ni
kwa kupaza sauti, pale iliposema:

‫ٱﻪﻠﻟُ َﺷﺎﻛِﺮاً َﻋﻠِﻴﻤﺎً ۞ ﻻﱠ ُِﳛ ﱡ‬


‫ﺐ‬ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﺑِ َﻌ َﺬاﺑِ ُﻜ ْﻢ إِن َﺷ َﻜْﺮُْﰎ َو َآﻣْﻨـﺘُ ْﻢ َوَﻛﺎ َن ﱠ‬
‫﴿ ﱠﻣﺎ ﻳَـ ْﻔ َﻌ ُﻞ ﱠ‬
﴾ً‫ٱﻪﻠﻟ َِﲰﻴﻌﺎً َﻋﻠِﻴﻤﺎ‬ ِ ِ ِ ِ ِۤ ِ
ُ‫ٱﻪﻠﻟُ ٱ ْﳉَ ْﻬَﺮ ﺑﭑﻟ ﱡﺴﻮء ﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻘ ْﻮل إﻻﱠ َﻣﻦ ﻇُﻠ َﻢ َوَﻛﺎ َن ﱠ‬ ‫ﱠ‬
Ma yafAAalu Allahu biAAadhabikum in shakartum waamantum wakana Allahu
shakiran AAaleeman, La yuhibbu Allahu aljahra bialssoo-i mina alqawli illa
man dhulima wakana Allahu sameeAAan AAaleeman (Surat An Nisaa 4:147-148)

Tafsir: Kwa nini Allah Subhanah wa Taála akuadhibuni nyinyi wakati Mmemshukuru
na Kumuamini. Na hakua Allah isipokua ni mwingi wa Kukubali, kuridhia na
kuthamini na Mwenye kujua kila kitu. Hapendi Allah uovu unaowekwa wazi kwa njia
ya kauli ya kupaza sauti, isipokua kwa yule aliedhulumiwa. Na hakika Allah ni mwingi
wa kusikia na mwingi wa ujuzi.

Naam aya mbili hizi zimetumia neno Shakartum na neno Jahara ambapo Hali ya
kuonesha Shukrani mbele ya Allah Subhanah wa Taála ni katika kumjua kwake na
Rehma zake ndani ya Nyoyo zetu, na kuthibitisha kwa njia ya Kauli na katika vitendo
vyetu. Sasa tunapozungumzia neno Shakartum ambalo ni lenye kutokana na Jina la Sifa
Tukufu ya Allah Subhanah wa Taála ambalo ni Shakir ambalo hua linamaanisha Mwingi
wa kukubali, kuridhia na kuthamini yale anayofanyiwa na Waja wake wanaompenda,
yaani hapa tunazungumzia kulingana na uhusiano baina ya Muumba kwa Kiumbe wake.
Ama tunapozungumzia kuhusiana na Kiumbe kwa Mja wake basi neno Shakir hua
linamaanisha Kukubali na kushukuru Rehma za Muumba juuu yake.

Hivyo aya inayofuatia ambayo ndio imetumia neno Jahara ambalo hua linamaanisha
kusema kwa Kupaza Sauti. Hivyo Allah Subhanah wa Taála anaweka wazi kua
hakubaliani na kauli mbovu zinazotolewa kwa kupaza sauti na Wanafiq, lakini hata hivyo
54

baadhi ya wakati mtu anapopandishiwa sauti basi inaruhusika kurudisha majibu ya kauli
hizo, hivyo aya hii inaweka wazi kua Allah Subhanah wa Taála anachukia Kauli mbovu.

Ambapo Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al
Qurtubi basi yeye anasema juu ya maana ya ayah hii ni kua: ‘Hapa kwanza inabidi
tuiangalie hali ya sharti la Illa yaani ‘Isipokua’, kisha ndio tunaangalia maana ya
aya yote kwa ujumla na hivyo kuona kua Ni mwenye kufanya Dhulma tu ndie
ambae hua ni mwenye kupaza sauti katika uovu.’

Allah Subhanah wa Taála anahoji kuhusiana na utumiaji bora wa mawasiliano ya kauli


katika Surat Fusilat kua:

﴾‫ﲔ‬ ِ ِ‫ﺎل إِﻧﱠِﲎ ِﻣﻦ ٱﻟْﻤﺴﻠ‬


‫ﻤ‬ َ ‫ﻗ‬
َ‫و‬ ‫ﺎ‬
ً ِ ‫ٱﻪﻠﻟِ وﻋ ِﻤﻞ ﺻ‬
‫ﺎﳊ‬ ‫ﱠ‬ ‫ﱃ‬
َ ِ
‫إ‬ ‫ﺂ‬ ‫ﻋ‬ ‫د‬ ‫ﱠﻦ‬
‫ﳑ‬ِّ ً‫﴿وﻣﻦ أَﺣﺴﻦ ﻗَـﻮﻻ‬
َ ُْ َ َ َ َ َ َ َ َ ْ ُ َ ْ ْ ََ
Waman ahsanu qawlan mimman daAAa ila Allahi waAAamila salihan waqala
innanee mina almuslimeena (Surat Fusilat 41:33)

Tafsir: Na ni nani mwenye kauli bora, zaidi ya yule anaewaita watu kwa Allah, na
akafanya mema na akasema: Hakika mimi ni Miongoni mwa Waisalam.

Katika kuilezea ayah hii basi anasema Hasan Al Basri kua: ‘Huyu hua ni mtu
anaependwa na Allah Subhanah wa Taála, ni mtu aliechaguliwa, na ndie
anaependwa na Allah Subhanah wa Taála zaid ya watu wote hapa duniani, kwani
yeye hua ni mwenye kuitikia wito wa Allah Subhanah wa Taála, na hivyo hua ni
mwenye kufanya mema na kusema kua: ‘Mimi ni miongoni mwa Waislam’ huyu
hua ndie Khalifa wa Allah hapa Ulimwenguni.’

Ama kwa upande wa Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari basi yeye
anasema kua: ‘Alie bora kwa Kauli ni yule ambae, anaewaongoza watu kumuelekea
Mola wao. Ibada zake na Sunna zake, na mwenye kujilinda juu ya makatazo ya
Mola wake, na anaeongoza katika Idama (Msisitizo) na Istiqama (Msimamo Thabit)
mbele ya Allah, na hivyo hua ni mwenye msimamo kutokana na khofu ya Khatma
yake. Na hua ni mwenye kua katika Tariqat al Wusta (Njia ya kati na kati), na kua
katika Jadda Mustaqima (Njia ilinyooka) ambayo ila atakaeifuta basi atakua
Salama, ambayo ni njia itakayompelekea kila atakae kua mbali nayo na kujawa na
Nadama (Majuto)’

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari ametumia neno Tariqat Wusta
yaani Njia ya Msimamo wa Kati na Kati, kwani Ummah wa Kiislam unajulikana kwa
kua na sifa ya Ummatan Wasatan yaani Ummah wenye kufuata misimamo ya kati kati
55

bila ya kua ni wenye Ghuluw yaani kuvuka mipaka kwa kua na misimamo mikali katika
mambo yao na bila ya kua ni wenye Tafrit yaani kuvuka mipaka kwa kudharau mambo
yao.

Kwani Waislam ni wenye kutumia kauli nzuri, Allah Subhanah wa Ta’ala


anatuthibitishia kua walioamuamini yeye na wakawa wanafanya mema watakua ni wenye
kulipwa Pepo kwani wao ndio wale ambao walioongozwa kutokana na kauli njema kwa
kusema:

ٍ ‫ﺎت ﺟﻨ‬
‫ﱠﺎت َْﲡ ِﺮي ِﻣ ْﻦ َْﲢﺘِ َﻬﺎ ْاﻷَﻧْـ َﻬ ُﺎر‬ ِ ِ ‫اﻪﻠﻟ ﻳ ْﺪ ِﺧﻞ اﻟﱠ ِﺬﻳﻦ آﻣﻨُﻮا وﻋ ِﻤﻠُﻮا اﻟ ﱠ‬
َ َ‫ﺼﺎﳊ‬ َ َ َ َ ُ ُ ‫﴿إِ ﱠن ﱠ‬
‫ﺎﺳ ُﻬ ْﻢ ﻓِ َﻴﻬﺎ َﺣ ِﺮ ٌﻳﺮ ۞ َوُﻫ ُﺪوا إِ َﱃ‬‫ﺒ‬ِ‫ﺐ وﻟُﺆﻟُﺆا وﻟ‬
ٍ ‫ﻫ‬ ‫ذ‬
َ ‫ﻦ‬ ِ ‫ُﳛﻠﱠﻮ َن ﻓِﻴﻬﺎ ِﻣﻦ أَﺳﺎ ِور‬
‫ﻣ‬
َ
ُ َ َ ً ْ َ ْ َ َ ْ َ َْ
ِ ‫اﳊ ِﻤ‬
﴾‫ﻴﺪ‬ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ‫اﻟﻄﱠﻴ‬
َْ ‫ﺐ ﻣ َﻦ اﻟْ َﻘ ْﻮل َوُﻫ ُﺪوا إ َﱃ ﺻَﺮاط‬ ّ
Inna Allaha yudkhilu alladheena amanoo waAAamiloo alssalihati jannatin tajree
min tahtiha al-anharu yuhallawna feeha min asawira min dhahabin walu/lu-an
walibasuhum feeha hareerun; Wahudoo ila alttayyibi mina alqawli wahudoo ila
sirati alhameedi (Surat Al Hajj 22:23-24)

Tafsir: Hakika Allah atawaingiza wale waliomuamini na wakafanya mambo mema


katika Bustani (Peponi) ambazo chini yake kuna mito ambamo watapambwa ndani
yake kwa makoja ya Dhahabu na Lulu na nguo zao zitakua za Hariri. Na
Wameongozwa kutokana na (utumiaji wa) bora miongoni mwa kauli na wakaongozwa
katika njia iliyonyooka.

Hivo ni baadhi tu ya mifano ya umuhimu wa kauli nzuri, iliyotajwa katika Qurán, lakini
tukifuatilia kwa makini basi tunaona kua Qurán imetumia asili ya neno Qulu katika hali
tofauti mara 1726 ikiwemo pale ilipotilia mkazo umuhimu wa kutovuka mipaka katika
mawasiliano baina yetu kwa njia ya kauli na kututaka kua na misimamo bora ya kati na
kati hata katika mazungumzo yetu na hivyo kuzijumuisha kauli tofauti katika aina 6 za
kauli bora ambazo ni:-

1. Qawlan Sadida
2. Qawlan Baligha
3. Qawlan Ma'rufan
4. Qalan Karima
5. Qawlan Layyina
6. Qawlan Maysura.
56

Katika kipindi ambacho Waislam tumezungukwa na mitihani katika kila upande ambayo
inayotupelekea kuhitaji kuthibitisha zaidi Imani na kumtegemea zaidi Allah Subhanah
wa Ta’ala katika maisha yetu na hivyo kuwa na uwezo wa kujilinda na madhara ya
viumbe na mitihani katika mazingira yetu na pia katika mazingira ya waliotangulia kabla
yetu, basi Qur’an haikutufunza namna ya kua na kauli nzuri tu bali pia Qur’an
imetuamrisha pia kujifunza kwa vitendo kwa kutumia njia ya kutembea katika maeneo
mbali mbali ardhini, kwani amesema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

﴾‫اب ﰒُﱠ إِ َذآ أَﻧﺘُﻢ ﺑَ َﺸﺮ ﺗَﻨﺘَ ِﺸﺮو َن‬


ٍ ‫﴿وِﻣﻦ آ�ﺗِِﻪ أَ ْن َﺧﻠَ َﻘ ُﻜﻢ ِﻣﻦ ﺗُـﺮ‬
ُ ٌ ْ َ ّْ َ ْ َ
Wamin ayatihi an khalaqakum min turabin thumma idha antum basharun
tantashiroona (Surat Rum 30:20)

Tafsir: Na Miongooni mwa Dalili mwake ni kua amekuumbeni nyie kutokana na


Udongo kisha mkawa katika Maumbo ya Watu Mliotawanyika na kutembea.


MANUFAA YA KUTAWANYIKA NA KUTEMBEA ARDHINI
KULINGANA NA QUR’AN.

Ni jambo lililowazi kua bila ya shaka Qurán imebeba kila aina ya ujumbe wenye manufaa
kwa ajili yetu ndani yake, na miongoni mwa mambo hayo yenye manufaa ni namna ya
kutembea ardhini kwa ajili ya kuzingatia hali na maumbile ya vitu mbali mbali vilivyomo
ndani yake na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akatutaka kutokua na Kibr katika
wakati wetu hapa Ulimwenguni kwani kufanya hivyo hakutotunufaisha wala
hakutotupelekea kuzingatia malengo ya kuumbwa kwetu na vinavyotuzunguka katika
mazingira yetu kama zinavyosema aya:

َ َ‫ٱﳉِﺒ‬
﴾ً‫ﺎل ﻃُﻮﻻ‬ َ ‫ض َﻣَﺮﺣﺎً إِﻧﱠ‬
َ ‫ﻚ ﻟَﻦ َﲣْ ِﺮ َق ٱﻷ َْر‬
ْ ‫ض َوﻟَﻦ ﺗَـْﺒـﻠُ َﻎ‬ ِ ‫ﺶ ِﰱ ٱﻷ َْر‬
ِ َْ‫﴿ َوﻻَ ﲤ‬
Wala tamshi fee al-Ardhi marahan innaka lan takhriqa al-ardha walan tablugha
aljibala toolan (Surat Al Isra 17:37)
57

Tafsir: Na msitembee juu ya Ardhi kwa madaha, kwani kwa hakika kamwe hamtoweza
kudidimia ndani ya ardhi, na wala hamtoufikia urefu wa milima.

Tunapoiangalia aya hii basi tunaona inatuonesha kua Ibn Adam tunatakiwa kua
wanyenyekevu na kamwe hatutakiwi kuishi maisha ya kujiona kwa kutembea kwa
madaha, kudunda au kwa ubabe kwani kufanya kwetu hivyo hakuto ipelekea Ardhi kua
ni yenye kutoboka na sisi kudidimia ndani yake na wala hakutopelekea kua warefu kiasi
ya kuufikia urefu wa milima, kwani kuna wengi waliokuja kabla yetu ambao nao walikua
wakijiona na kua na Kibr, lakini hata hivyo nao wakawa ni wenye kuacha kila kitu
Duniani kama walivyokikuta.

Na haya pia ndio maneno ambayo Luqman Al Hakim alitumia kumuusia Mtoto wake
kama inavyoelezewa katika Surat Luqman na aya zifuatazo:

‫ٱﻪﻠﻟَ ﻻَ ُِﳛ ﱡ‬
‫ﺐ ُﻛ ﱠﻞ ﳐُْﺘَ ٍﺎل‬ ‫ض َﻣَﺮﺣﺎً إِ ﱠن ﱠ‬ ِ ‫ﺶ ِﰱ ٱﻷ َْر‬ ِ ‫ﱠك ﻟِﻠﻨ‬
ِ َْ‫ﱠﺎس َوﻻَ ﲤ‬ َ ‫ﺼ ّﻌِْﺮ َﺧﺪ‬
َ ُ‫﴿ َوﻻَ ﺗ‬
ِ ‫ﻚ إِ ﱠن أَﻧ َﻜﺮ ٱﻷ‬ َ ِ‫ﺻ ْﻮﺗ‬ ِ ‫ﻚ وٱ ْﻏﻀ‬ ِ
‫ت‬ُ ‫ﺼ ْﻮ‬ َ َ‫َﺻ َﻮات ﻟ‬
ْ َ َ ‫ﺾ ﻣﻦ‬ ْ ُ َ َ ِ‫ﻓَ ُﺨﻮٍر۞ َوٱﻗْﺼ ْﺪ ِﰱ َﻣ ْﺸﻴ‬
﴾‫ٱﳊَ ِﻤ ِﲑ‬
ْ
Wala tusaAAAAir khaddaka lilnnasi wala tamshi fee al-ardhi marahan inna Allaha
la yuhibbu kulla mukhtalin fakhoorin, Waiqsid fee mashyika waoghdud min
sawtika inna ankara al-aswati lasawtu alhameeri (Surat Luqman 31:18-19)

Tafsir: Na usigeuze uso wako kwa kujiona, na wala usitembee kwa madaha. Kwani
kwa hakika Allah hawapendi wenye kujivuna kwa fakhari. Na usiwe ni mwenye
haraka katika kutembea kwako, na punguza sauti yako, kwani sauti kubwa
inayochukiza ni sauti ya Punda.

Hivyo kabla ya mtu kua na Kibr na hivyo kutembea kwa madaha kutokana na uzuri wako,
mamlaka yako, mali zako, Ilm yako n.k basi inabidi kutafakkar ni nini kilichowafika wale
waliotangulia kabla yetu na hii ndio miongoni mwa sababu ambazo Allah Subhanah wa
Ta’ala akatuhimiza kutembea ardhini kwa unyenyekevu ili kupata kuona na kuzingatia
mazingira ya Ulimwengu katika aya takriban 14 ambazo zimetumia neno Nadhara.

Neno Nadhara kwa Lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kuona, Kuangalia, Kutizama
kwa kituo, Mtizamo, Kuchunguza, Kufikiria, Kusubiri, Kusubiri ili upate kuona au
kuthibitisha, Kufuatilia kwa umakini kwa kutumia macho, Kutafuta, Kuzingatia na pia
58

humaanisha Kutafakkar. Wenye Lugha yao hua wanasema Nadharat FiiHi yaani Angalia
Uone!

Neno Nadhara ndio lililotoa neno Undhuru ambalo ni lenye kumaanisha Angalia
Uzingatie, Ili kufahamu zaidi basi na tuangalie mfano unaofafanua wazi maana ya neno
Undhuru katika ifuatayo ambayo imetumia neno Undhurna:

ِ ِ ْ ‫اﻋﻨﺎ وﻗُﻮﻟُﻮاْ ٱﻧْﻈُﺮَ� و‬ِ ِ‫ﱠ‬


‫اب‬ َ ‫ٱﲰَﻌُﻮاْ َوﻟﻠ َﻜﺎﻓ ِﺮ‬
ٌ ‫ﻳﻦ َﻋ َﺬ‬ َ ‫َ�أَﻳـﱡ َﻬﺎ ٱﻟﺬ‬
َ َ ‫ﻳﻦ َآﻣﻨُﻮاْ ﻻَ ﺗَـ ُﻘﻮﻟُﻮاْ َر‬
﴿
َ ْ
﴾‫أَﻟِﻴﻢ‬
ٌ
Ya ayyuha alladheena amanoo la taqooloo raAAina waqooloo undhurna
waismaAAoo walilkafireena AAadhabun aleemun (Surat Al Baqara 2:104)

Tafsir: Enyi Mlioamini! Msiseme (Kumwambia Rasul Allah Salallahu A’layhi wa


Salam) Raina semeni Undhurna na Sikilizeni! Na kwa Waliokufuru ni juu yao
Adhabu kali.

Ambapo tunaona kua anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Waarabu
walikua wakipenda kutumia neno Raina (lenye kumaanisha kua Tuangalie), hivyo
Mayahudi waliposikia Waarabu wakitumia neno hilo pamoja na Rasul Allah
Salallahu A’layhi wa Salam, basi nao wakalipenda, kwa sababu neno Raina hua ni
lenye kumaanisha matusi kwa lugha ya Kiyahudi, (Ambapo kwa Lugha ya Kiarabu
pia hua linamaanisha Mchungaji wa Wanyama wetu, na pia Mtu Mjinga na Laghai)
Hivyo Mayahudi wakasema: ‘Zamani tulikua tukimtukana Muhammad kisiri siri,
hivyo sasa hivi tunaweza kumtukana wazi wazi kwa kutumia hili neno Raina
ambalo limo katika Lugha yao.

Hivyo wakawa wanakuja mbele ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na


kusema: ‘Ya! Muhammad Raina!’ kisha wanaanza kucheka! Siku moja walipokuja
akawepo Sa’ad Ibn Ubadah Radhi Allahu Anhu ambae ni miongoni mwa Ansari
mwenye kujua maana ya neno Raina kama walivyokua wakikusudia Mayahudi.
Hivyo Sa’ad Ibn Ubaidah Radhi Allahu Anhu akawaambia: ‘Enyi Maadui wa Allah!
Allah akulaanini nyie. Hakika mimi nnaapa kwa yule ambae ndani ya Mamlaka
yake imo Roho ya Muhammad Rasul Allah Salallahu Alyhi wa Salam. Kua kama
nikimsikia mtu yeyote yule anatumia tena neno hilo, basi Wa Allahi nitamkata
kichwa chake!’
59

Mayahudi hao nao wakapinga na kusema: ‘Lakini jee nyinyi hamtumii neno hilo?’
hivyo basi baada ya majibishano hayo ndio Allah Subhanah wa Taála akashusha
aya hio.’’

Hivyo neno Raina lina maana zenye utata ndani yake kwani hua halina maana ya
kutizama kwa ulazima wa kuona tu pekee. Lakini neno Undhurna maana yake ni kua:
‘Tuangalie kwa kituo ili Utuone au Tusubiri’, na ukweli ni kua kutokana na kua na
maana hio ya Kuangalia au Kutizama kwa ajili ya Kuona kwa kituo na mazingatio kwa
ajili ya kupata mafundisho na manufaa yaliyomo ndani ya kinachoangaliwa, basi Qurán
imetilia mkazo Kuangalia kwa ajili ya Kuona na Kutafakkar katika aya nyingi ndani yake
na kwa kuzungumzia mambo mengi ndani yake na hivyo kuzijumuisha pamoja aina tatu
muhimu za Safari kwa ajili ya Kuona ambazo ni:

Aina ya kwanza: Ni ile iliyoainishwa katika aya ambazo zimezungumzia Safari lakini
hazikutumia neno Undhuru, na hizi ni zile aya ambazo zinazungungmzia habari na Visa
vya Mitume na Manabii wakiwemo Nabii Nuh, Nabii Ibrahim, Nabii Musa, Dhul
Qarnayn, Al Khidhr, Nabii Yaqub, Nabii Yusuf, Nabii Sulaiman, Malqia Bilqis, Nabii
Yunus, Maryam Bint Imran, Nabii Isa, As-hab Al Kahf, Uzayr n.k.

Ambapo ndani yake zimewazungumzia watu wema hawa ambao ni miongoni mwa
mifano ya kuigwa mbele yetu. Haina haja kwetu sisi kuzianisha aya hizi kwa sababu
tutazizungumzia baadhi yake katika kurasa za mbele za kitabu wakati tukielezea maisha
ya Ulu ul Azmi Minna Rusul ambayo ndio mada kuu ya Kitabu chetu.

Aina ya Pili: Ni ile iliyoainishwa katika aya ambazo zinatuamrisha sisi kutembea ardhini
kwa malengo na makusudio ya kujifunza mambo mbali mbali tangu kuanzia kwa Viumbe
vya Ulimwenguni, Uwezo na Maajabu yao ya hadi kufikia katika kuona Uwezo Mkubwa
na Maajabu ya Muumba wa Ulimwengu wote na kila kitu kilichomo ndani yake. Aya hizi
hua zina malengo ya kututanua kiakili na kututayarisha kiufahamu na kutufunza juu ya
namna ya kukabiliana na mitihani na mambo mengine yaliyo mbele yetu kwa kua na
subra na ustahamilivu kama vile walivyokua wale waliotangulia kabla yetu ambao ni
miongoni mwa Waliomuamini Allah Subhanah wa Taála na pia miongoni mwa wale
ambao hawakumuamini, kwa mfano katika Surat Al Imran pale aliposema:

ُ‫ﻒ َﻛﺎ َن َﻋﺎﻗِﺒَﺔ‬ ِ ‫ﺖ ِﻣ ْﻦ ﻗَـْﺒﻠِ ُﻜ ْﻢ ُﺳﻨَ ٌﻦ ﻓَ ِﺴﲑُواْ ِﰱ ٱﻷ َْر‬


َ ‫ض ﻓَﭑﻧْﻈُُﺮواْ َﻛْﻴ‬ ْ َ‫﴿ﻗَ ْﺪ َﺧﻠ‬
ِ
﴾‫ﲔ‬َ ِ‫ٱﻟْ ُﻤ َﻜ ّﺬﺑ‬
60

Qad khalat min qablikum sunanun faseeroo fee al-Ardhi faondhuroo kayfa kana
AAaqibatu almukadhdhibeena (Al Imran 3:137)

Tafsir: Kwa hakika yamewafika mengi waliokuja kabla yenu (Walioamini na


Wasioamini), hivyo tembeeni katika Ardhi ili mpate kuona ni upi ulikua mwisho wa
wale waliokadhibisha.

Na mfano wa aya zinazohimiza kusafiri ili kupata vithibitisho juu ya Ukubwa wa Allah
na Uwezo wake katika Kuumba kwake ni pamoja ile isemayo:

ِ َ‫ﻨﺸﺊ ٱﻟﻨﱠ ْﺸﺄَة‬


‫ٱﻵﺧَﺮَة إِ ﱠن‬ ِ ‫ٱﳋ ْﻠﻖ ﰒُﱠ ﱠ‬ ِ ‫﴿ﻗُ ْﻞ ِﺳﲑُواْ ِﰱ ٱﻷ َْر‬
ُ ُ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻳ‬ َ َْ َ‫ﻒ ﺑَ َﺪأ‬َ ‫ض ﻓَﭑﻧﻈُُﺮواْ َﻛْﻴ‬
﴾‫ٱﻪﻠﻟ َﻋﻠَ ٰﻰ ُﻛ ِﻞ َﺷﻲ ٍء ﻗَ ِﺪﻳﺮ‬
ٌ ْ ّ َ‫ﱠ‬
Qul seeroo fee al-Ardhi faondhuroo kayfa badaa alkhalqa thumma Allahu yunshi-
o alnnash-ata al-akhirata inna Allaha AAala kulli shay-in qadeerun (Al-Ankabut
29:20)

Tafsir: Sema: Tembeeni katika Ardhi na mpate kuona (namna Allah) alivyoanzisha
Uumbaji wake, na kisha Allah atawafufua viumbe kesho Akhera. Kwa Hakika Allah
ni muweza juu ya kila kitu.

Bia ya shaka Allah Subhanah wa Ta’ala hamuamrishi tu kila Ibn Adam kutembea ili
apate kujifunza kwa kuona lakini pia anatutilia mkazo zaidi sisi Waislam, tuliomuamini
juu ya jambo hilo. Aya inayofuatia pia ni miongoni mwa mifano mwa aya hizo.

‫ﻳﻦ ِﻣﻦ ﻗَـْﺒ ُﻞ َﻛﺎ َن أَ ْﻛﺜَـُﺮُﻫ ْﻢ‬ ِ‫ِ ﱠ‬ ِ ‫﴿ﻗُ ْﻞ ِﺳﲑُواْ ِﰱ ٱﻷ َْر‬
َ ‫ﻒ َﻛﺎ َن َﻋﺎﻗﺒَﺔُ ٱﻟﺬ‬ َ ‫ض ﻓَﭑﻧْﻈُُﺮواْ َﻛْﻴ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ
َ ‫ﱡﻣ ْﺸ ِﺮﻛ‬
Qul seeroo fee al-ardi faondhuroo kayfa kana AAaqibatu alladheena min qablu
kana aktharuhum mushrikeena (Ar-Rum 30:42.)

Tafsir: Sema (Ewe Muhammad): Tembeeni katika Ardhi na mpate kuona ni upi ulikua
mwisho wa wale waliokuja kabla yenu. Walikua wengi wao ni Washirikina.
61

Aina ya Tatu: Ni ile iliyoainishwa katika aya ambazo zinawahoji wale ambao
hawatembei ardhini wakaona yaliyowafika wale walikuja kabla yao, ama kwa ujumla
basi aya za kundi hili la tatu zinawashutumu wale ambao hawakumuamini Allah
Subhanah wa Ta’ala, Mitume wake na vitabu vyake na hivyo kua ni wenye kupingana
na mamrisho ya Mola wao kutokana na ujinga wao kwa mfano pale Qurán iliposema:

ْ‫ﻳﻦ َﻛﺎﻧُﻮاْ ِﻣﻦ ﻗَـْﺒﻠِ ِﻬ ْﻢ َﻛﺎﻧُﻮا‬ ِ‫ِ ﱠ‬


َ ‫ﻒ َﻛﺎ َن َﻋﺎﻗﺒَﺔُ ٱﻟﺬ‬ ِ ‫ﲑواْ ِﰱ ٱﻷ َْر‬
َ ‫ض ﻓَـﻴَﻨﻈُُﺮواْ َﻛْﻴ‬
ِ ﴿
ُ ‫أ ََوَﱂْ ﻳَﺴ‬
ِ‫ٱﻪﻠﻟ‬
‫ٱﻪﻠﻟُ ﺑِ ُﺬﻧُﻮﻬﺑِِ ْﻢ َوَﻣﺎ َﻛﺎ َن َﳍُﻢ ِّﻣ َﻦ ﱠ‬
‫َﺧ َﺬ ُﻫ ُﻢ ﱠ‬ ِ ‫َﺷ ﱠﺪ ِﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ ﻗـُ ﱠﻮةً َوآ َﺎﺛراً ِﰱ ٱﻷَْر‬
َ ‫ض ﻓَﺄ‬ َ ‫ُﻫ ْﻢ أ‬
﴾‫ِﻣﻦ و ٍاق‬
َ
Awa lam yaseeroo fee al-ardhdhi fayandhuroo kayfa kana AAaqibatu alladheena
kanoo min qablihim kanoo hum ashadda minhum quwwatan waatharan fee al-
Ardhi faakhadhahumu Allahu bidhunoobihim wama kana lahum mina Allahi min
waqin (Surat Ghafir 40:21)

Tafsir: Jee hawakutembea juu ya Ardhi na wakaona, yalivyokua mabaki ya


waliotangulia kabla yao? Walikua na wingi wa kinguvu na kiathari walizoacha
ardhini zaidi yao. Lakini akawapa adhabu Allah kwa dhambi zao na hawakua na wa
kuwasaidia dhidi ya Allah.

Na vile vile ikasema tena katika Sura hio hio:

‫ﻳﻦ ِﻣﻦ ﻗَـْﺒﻠِ ِﻬ ْﻢ َﻛﺎﻧـُ ۤﻮاْ أَ ْﻛـﺜَـَﺮ‬


َ
ِ ‫ض ﻓَـﻴﻨﻈُﺮواْ َﻛﻴﻒ َﻛﺎ َن ﻋﺎﻗِﺒﺔُ ٱﻟﱠ‬
‫ﺬ‬ َ َ َ ْ ُ َ ِ ‫َر‬
ْ ‫ﻷ‬ ‫ٱ‬ ‫ﰱ‬ ِ ْ‫﴿أَﻓَـﻠَﻢ ﻳَ ِﺴﲑوا‬
ُ ْ
﴾‫ن‬ َ ‫ض ﻓَ َﻤﺂ أَ ْﻏ َ ٰﲎ َﻋْﻨـ ُﻬﻢ ﱠﻣﺎ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳَ ْﻜ ِﺴﺒُﻮ‬ َ ‫ِﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ َوأ‬
ِ ‫َﺷ ﱠﺪ ﻗُـ ﱠﻮةً َوآ َﺎﺛراً ِﰱ ٱﻷ َْر‬
Afalam yaseeroo fee al-Ardhi fayandhuroo kayfa kana AAaqibatu alladheena min
qablihim kanoo akthara minhum waashadda quwwatan waatharan fee al-Ardhi
fama aghna AAanhum ma kanoo yaksiboona (Surat Ghafir 40:82)

Tafsir: Jee hawakutembea juu ya Ardhi na wakaona, yalivyokua mabaki ya


waliotangulia kabla yao? Walikua wengi zaid yao na wenye uwezo mkubwa kinguvu,
na katika athari zao walizoacha katika ardhi, lakini hata hivyo kila kitu chao
walichokua nacho hakikua ni chenye kuwasaidia.
62

Hapa wale wasioamini wanatakiwa kutafakkar yale mambo ambayo yaliwafika watu
waliotangulia kabla yao ambao wao walikua ni wakubwa kimaumbile na kinguvu pia
kiasi ya kua athari zao walizoacha hadi hii leo bado zipo na zimekua ni miongoni mwa
maajabu ya Dunia, kwa mfano: Piramidi za Misri, Makasri, Ngome na Majumba
waliyoyajenga kwa kuchonga Milima ya mawe nchini Afghanistan, Iran, Iraq, Syria,
Jordan, Yemen n.k kwa kutumia utaalamu na zana ambazo hadi hii leo bado Wanasayansi
wa karne yetu hawajajua ni zana gani za karne hizo zinazochonga mawe kama zana za
karne yetu, kiasi ya kua ukiona athari zake basi lazima utastaajabu, kutokana na ukubwa
na umadhubuti wa Matofali, Mawe na Urefu wa Nguzo na Minara waliyojenga
kimpangilio kulingana na mpangilio wa nyota na sayari za angani, ambapo uzuri wa
Nakshi na mapambo yake baadhi miongoni mwa Majengo hayo hua ni kama yenye
kuonekana kama yamechongwa kwa kutumia mashine maalum za katika kipindi chetu
cha wakati wa maendeleo.

Lakini hata hivyo Ukubwa wao, Nguvu zao, Maarifah yao, Ujuzi wao, Utaalamu wao,
Mali zao, Majumba yao, Mafanikio ya athari zao walizokua nazo na kubakia hadi hii leo
basi vyote hivyo havikuwasaidia kitu, kwani kumsahau kwao Mola wao na kuenda
kinyume na maamrisho yake ndiko kulikosababisha kushushiwa adhabu kwao kupata
maangamizo yao kama inavyosema aya inayofuatia ya Surat Muhammad 47:10 ambayo
pia ni miongoni mwa mifano ya aya za Fayandhuru:

‫ﻳﻦ ِﻣﻦ ﻗَـْﺒﻠِ ِﻬ ْﻢ َد ﱠﻣَﺮ ﱠ‬


ُ‫ٱﻪﻠﻟ‬
ِ‫ِ ﱠ‬
َ ‫ﻒ َﻛﺎ َن َﻋﺎﻗﺒَﺔُ ٱﻟﺬ‬ َ ‫ض ﻓَـﻴَﻨﻈُُﺮواْ َﻛْﻴ‬ِ ‫﴿أَﻓَـﻠَ ْﻢ ﻳَ ِﺴﲑُواْ ِﰱ ٱﻷ َْر‬
﴾‫َﻋﻠَْﻴ ِﻬﻢ وﻟِْﻠ َﻜﺎﻓِ ِﺮﻳﻦ أ َْﻣﺜَﺎ ُﳍَﺎ‬
َ َْ
Afalam yaseeroo fee al-ardi fayandhuroo kayfa kana AAaqibatu alladheena min
qablihim dammara Allahu AAalayhim walilkafireena amthaluha (Surat Muhammad
47:10)

Tafsir: Jee hawajatemea ardhini, na hivyo wakaona ni upi ulivyokua mwisho wa wale
ambao waliotangulia kabla yao (Waliokua wakifanya maovu) hakika aliwashushia
Allah juu yao maangamizo, na kwa makafiri yatawakuta mithili yake.

Ingawa Allah Subhanah wa Ta’ala anawataka Ibn Adam katika aya hizo za Safari zenye
malengo ya kujifunza lakini wale wajinga wasiojua miongoni mwetu wamekua katika
mstari wa mbele katika jitihada za kufuta athari za watu hawa waliotangulia kabla yetu
na ambao tumetakiwa kujifunza kutoka kwao tena kupitia katika aya zilizowazi kama
tunavyoona katika mifano ya aya hizo.
63

Inasikitisha kuona kua Watu wanaojiita Waislam tena walioamini kua wanavamia
miji ya Zamani ya Kihistoria na kisha kuvunja na kubomoa Majengo na Athari
mbali mbali za Kihistoria zilizozungumziwa kwenye Qurán, hususan katika Ardhi
ya Mashariki ya Kati kwani Miskiti mingi ya Kihistoria za watu Watukufu, kama
Mawalii, Masahaba, Maiamamu n.k imeripuliwa kwa mabomu kwa mfano Masjid
Khalid Ibn Walid wa Mjini Homs nchini Syria, Mji wa Palmira, nchini Iraq mji wa
Nimrudh, nchini Libya mji wa Cyrene uliojengwa na Warumi miaka 630 kabla ya
Nabii Isa, nchini Yemen katika mji wa Barqaish, nchini Afghanistan, Lebanon,
Palestina, Miskiti na Maktaba za Mji wa Timbuktu, nchini Mali n.k

Watu hawa wasiojua hua wanatumia kisingizio cha ile hadith ya Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam isiemayo kua: ‘Msifunge safari kwa malengo ya kutembelea Miskiti
isipokua katika Misikiti Mitatu, Misikiti huu (Masjid An Nabbawi wa Madina),
Masjid Al Haram wa Makkah na Masjid Al Aqsa’(Sahih Bukharin a Muslim)

Huku ni kutofaham maana halisi ya Hadhith hio kwani anasema Al Hafidh Imam Al Iraqi
kua: ‘Miongoni mwa maana nzuri iliyobebwa na Hadith hii, ni kukatazwa kwa
malengo ya kutembelea Miskiti husika. Lakini, kutembea kwa malengo ya Kutafuta
I’lm, Kumtembelea Mtu Mtakatifu, Rafiki au Jamaa, au kwa Malengo ya kufanya
Biashara, Kuuburudisha Moyo, Kujizidishia Iman n.k basi inaruhusiwa kwani
hayo hayajajumuishwa ndani ya Hadith hii, na hili linafafanulika vizuri zaidi na
Hadith nyengine ya Said Al Khudri ambae anasema kua: ‘Amesema Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam kua : ‘Hairuhusiki kwa mtu, kutembelea Miskiti kwa
malengo ya Kusali ndani ya Msikiti huo, isipokua kwa ajili ya Miskiti mitatu: Masjid
Al Haram (Makkah), Masjid Al Aqsa na Misikiti wangu huu (Masjid An Nabbawi wa
Madina),’’’’((Musnad Imam Ahamd, Musannaf Ibn Shaybah) Al Hashiyah Minhaj Al
Tulab – Imam Al Jamal Shaykh Sulaiman Ibn Mansur)

Na akasema Mujaddid Ad Din Imam Taj Ad Din Al Subki kua: ‘Hakuna sehemu juu
ya mgongo wa Ardhi ambayo iliyokua haina Utukufu wake, kwa ajili ya mtu
kutembelea sehemu hio kutokana na Utukufu husika, isipokua sehemu hizi (Masjid
Al Haram, Masjid Al Aqsa na Masjid An Nabbawi wa Madina). Na nnaposema
Utukufu wa sehemu husika, basi hua nnakusudia juu ya ule Utukufu uliothibitishwa
na Sharia za Kiislam. Ambapo Mtu hatakiwi kutembelea sehemu kwa ajili ya
Utukufu wa Sehemu hio husika, bali kwa sababu ya kutafuta I’lm, kwa kutembea,
au kwa sababu nyengine yeyote ile inayokubalika Kisharia. Wale ambao
wanaopinga juu ya hilo basi hua ni wenye kukosea katika Imani yao, kwani
kutembelea Msikiti husika hua kunatokana kwa ajili ya wale waliomo ndani ya
Msikiti husika, na si kwa ajili ya Msikiti husika.

Hivyo Hadithi hii imepinga kutembelea Miskiti kama Miskiti isipokua kwa ajili ya
Miskiti Mitatu hio husika. Lakini kufunga safari kwa sababu ya kumtembelea Mtu,
64

au kwa sababu ya kutafuta I’lm, basi hua si kwa sababu ya Msikiti huo, bali hua ni
kwa ajili ya wale waliomo kwenye Msikiti huo) (Hashiyah Minhaj Al Tulab – Imam Al
Jamal Shaykh Sulaiman Ibn Mansur)

Tumalizie sehemu hii kwa kuangalia aya ya Fayandhuru inayofuata ambayo kutokana
na ujumbe wake basi tunaona kua, Allah Subhanah wa Ta’ala anatuainishia tena
umuhimu wa kutembea pia kwa ajili ya kuona na kufahamu madhara yaliyowafika wale
waliokua ni wenye kupingana na Ujumbe wa Mitume wake kwani kupinga kwa watu hao
baada ya kuwekewa vithibitisho vilivyowazi hakukua na faida yeyote kwao wao na
badala yake ilikua ni kujitia maangamizo na hivyo kua ni wenye kujidhulumu wao
wenyewe, kama inavyoweka wazi aya ifuatayo:

ۤ ِ ِ‫ِ ﱠ‬
َ ‫ﻳﻦ ِﻣﻦ ﻗَـْﺒﻠ ِﻬ ْﻢ َﻛﺎﻧـُﻮاْ أ‬
‫َﺷ ﱠﺪ‬ َ ‫ﻒ َﻛﺎ َن َﻋﺎﻗﺒَﺔُ ٱﻟﺬ‬ َ ‫ض ﻓَـﻴَﻨﻈُُﺮواْ َﻛْﻴ‬ِ ‫﴿أ ََوَﱂْ ﻳَﺴﲑُواْ ِﰱ ٱﻷ َْر‬
ِ َ‫ِﻣْﻨـﻬﻢ ﻗـُ ﱠﻮةً وأَ َﺎﺛرواْ ٱﻷَرض وﻋﻤﺮوﻫﺂ أَ ْﻛﺜَـﺮ ِﳑﱠﺎ ﻋﻤﺮوﻫﺎ وﺟﺂءﺗْـﻬﻢ رﺳﻠُﻬﻢ ﺑِﭑﻟْﺒـﻴِﻨ‬
‫ﺎت‬ َّ ُ ُ ُ ْ ُ َ َ َ َ ُ َ َ َ َ ُ َ َ َ َ ْ ُ َ ْ ُ
﴾‫ٱﻪﻠﻟ ﻟِﻴَﻈْﻠِﻤ ُﻬﻢ وﻟَـٰ ِﻜﻦ َﻛﺎﻧـُ ۤﻮاْ أَﻧ ُﻔﺴ ُﻬﻢ ﻳَﻈْﻠِﻤﻮ َن‬
ُ ْ َ َ ْ َ ُ‫ﻓَ َﻤﺎ َﻛﺎ َن ﱠ‬
Awa lam yaseeroo fee al-Ardhi fayandhuroo kayfa kana AAaqibatu alladheena min
qablihim kanoo ashadda minhum quwwatan waatharoo al-ardha waAAamarooha
akthara mimma AAamarooha wajaat-hum rusuluhum bialbayyinati fama kana
Allahu liyadhlimahum walakin kanoo anfusahum yadhlimoona (Surat Rum 30:9)

Tafsir: Jee hawatembei ardhini na kuona mwisho wa wale ambao waliotangulia kabla
yao, walikua wakubwa zaidi yao kinguvu, na wakawacha athari zao katika ardhi, na
wakaijaza Ardhi kuliko walivyofanya hawa, na wakaja kwao wao Mitume wenye
vitibitisho vilivyowazi. Hakika Allah hakuwadhulumu, bali wao ndio waliokua
wakijidhulumu.

Hakika watu hao waliotangulia walikua ni kama sisi yaani wenye Nyoyo, Macho na
Masikio lakini na kadhalika lakini hata hivyo wao walikua ni miongoni mwa
waliojidhulumu kutokana na kutumia sivyo neema za viungo vyao hivyo muhimu
walivyopewa na Mola wao aya inayofuatia inaweka wazi juu ya jambo hilo.

‫ﻮب ﻳَـ ْﻌ ِﻘﻠُﻮ َن ِﻬﺑَﺂ أ َْو آذَا ٌن ﻳَ ْﺴ َﻤﻌُﻮ َن ِﻬﺑَﺎ‬ ِ ‫﴿أَﻓَـﻠَ ْﻢ ﻳَ ِﺴﲑُواْ ِﰱ ٱﻷ َْر‬
ٌ ُ‫ض ﻓَـﺘَ ُﻜﻮ َن َﳍُْﻢ ﻗُـﻠ‬
ِ
﴾‫ﺼ ُﺪوِر‬ ‫ﻮب ٱﻟﱠِﱴ ِﰱ ٱﻟ ﱡ‬ ُ ُ‫ﺼ ُﺎر َوﻟَـٰﻜﻦ ﺗَـ ْﻌ َﻤ ٰﻰ ٱﻟْ ُﻘﻠ‬َ ْ‫ﻓَِﺈﻧـﱠ َﻬﺎ ﻻَ ﺗَـ ْﻌ َﻤﻰ ٱﻷَﺑ‬
65

Afalam yaseeroo fee al-Ardhi fatakoona lahum quloobun yaAAqiloona biha


aw adhanun yasmaAAoona biha fa-innaha la taAAma al-absaru walakin taAAma
alquloobu allatee fee alssudoori (Surat Al Hajj 22:46)

Tafsir: Jee hawakutembea wao juu ya ardhi? Hawakua wao na nyoyo ambazo ni za
kufahamu na masikio ya kusikilizia? Kwa hakika sio macho yao yanayokua na upofu
wa kutoona bali ni nyoyo ndani ya vifua vyao ndio vilivyokua na upofu.

Moyo wa Ibn Adam unafahamu kulingana na mitizamo ya aina mbili aina ya kwanza ni
ya kuona kwa mtizamo wa ndani ya Moyo ambao ni kwa kupitia kwa njia ya hisia za
kuhisi kwa Moyo na mtizamo wa pili ni mtizamo wa kuona kwa mtizamo wa nje ya
Moyo, hivyo kutembea na kuona kwa mitizamo yote miwili hii, hua kuna manufaa zaid
kwani hupelekea kuuelimisha na kuupumzisha Moyo, Ufahamu na Akili ya Ibn Adam
kama anavyosema Mujaddid ad Din Imam Muhammad Idris al Shafii katika kitabu chake
cha Al Diwan kua:

Uache Mji wako kwa ajili ya kutafuta


Darja kwa kuelimika ‫ﺗﻐﺮب ﻋﻦ اﻷوﻃﺎن ﰲ ﻃﻠﺐ اﻟﻌﻠﻰ‬
Na Safiri. Kwani katika kusafiri kuna
faida Tano. ‫وﺳﺎﻓﺮ ﻓﻔﻲ اﻷﺳﻔﺎر ﲬﺲ ﻓﻮاﺋﺪ‬
Kuiwepesishia Mzigo Nafsi na kujitafutia
Maisha yako.
ٍ
‫ﻣﻌﻴﺸﺔ‬ ‫ﺗﻔﺮﻳﺞ ﻫﻢ واﻛﺘﺴﺎب‬
Na I’lmu na Adabu na Marafiki bora.
ٍ ‫وﻋﻠ ٍﻢ‬
‫وآداب وﺻﺤﺒﺔ ﻣﺎﺟﺪ‬
Kama ikisemwa kua kusafiri ni Madhila
na Ugumu wa mambo. ‫ﻓﺈن ﻗﻴﻞ ﰲ اﻷﺳﻔﺎر ذل وﳏﻨﺔ‬
Na urefu wa kuvuka Majangwa, ugumu
na matatizo. ‫وﻗﻄﻊ اﻟﻔﻴﺎﰲ وارﺗﻜﺎب اﻟﺸﺪاﺋﺪ‬
Basi Kifo ni bora kwa Mtu kuliko
kubakia sehemu moja. ‫ﻓﻤﻮت اﻟﻔﱴ ﺧﲑ ﻟﻪ ﻣﻦ ﻗﻴﺎﻣﻪ‬
Katika Manyanyaso baina ya Usaliti na
Husda. ‫ﺑﺪار ﻫﻮان ﺑﲔ واش وﺣﺎﺳﺪ‬
Naam neno Undhur basi limetumika pia tena katika Quran pale iliposema:
66

َ‫ٱﻪﻠﻟ‬ ‫ﺖ ﻟِﻐَ ٍﺪ َوٱﺗﱠـ ُﻘﻮاْ ﱠ‬


‫ٱﻪﻠﻟَ إِ ﱠن ﱠ‬ ْ ‫ﱠﻣ‬
َ ‫ﺲ ﱠﻣﺎ ﻗَﺪ‬ ‫ﻳﻦ َآﻣﻨُﻮاْ ٱﺗﱠـ ُﻘﻮاْ ﱠ‬
ٌ ‫ٱﻪﻠﻟَ َوﻟْﺘَﻨﻈُْﺮ ﻧَـ ْﻔ‬
ِ‫ﱠ‬
َ ‫ٰ�َﻳـﱡ َﻬﺎ ٱﻟﺬ‬
﴿
﴾‫َﺧﺒِﲑٌ ِﲟَﺎ ﺗَـ ْﻌﻤﻠُﻮ َن‬
َ
Ya ayyuha alladheena amanoo ittaqoo Allaha waltandhur nafsun ma qaddamat
lighadin waittaqoo Allaha inna Allaha khabeerun bima taAAmaloona (Surat Al
Hashir 59:18)

Tafsir: Enyi Mlioamini, Muogopeni Mola wenu, na Nafsi ijichunguze juu ya kile
ilichokitanguliza kesho, na Mcheni Allah kwani kwa hakika Allah ana habari juu ya
kila mnachokifanya.

Aya inatuwekea wazi kua Ulimwengu tulionao unawakilisha siku ya leo katika Uhai wetu
na Ulimwengu wa Akhera unawakilishwa a siku ya kesho ambayo kwa hakika itakuwepo
kwa kila mmja miongoni mwetu. Hivyo bila ya shaka kuna umuhimu wa kuaziangalia
Nyoyo zetu na kufanya safari ndani yake kama anavyosema Maulana Jalal Ad Din Al
Rumi kua: ‘Safari hukurudishia nguvu ya mwili, na mapenzi ndani ya Moyo wako.
Hivyo hata kama ikiwa huwezi kusafiri kuelekea kokote basi fanya safari ndani ya
sehemu za Moyo wako’

Hivyo amri ya Undhur imetumika kututaka Ibn Adam kutumia ipasavyo viungo vya miili
yetu yaani Miguu, Ufahamu wa Akili, Macho na mtizamo na ufahamu wa Moyo katika
kutafakkar na kuondoka kutoka katika hatua moja ya maisha duni ya kiimani na kuingia
katika hatua nyengine iliyobora zaid kiimani na hivyo kua ni wenye kupata ridhaa ya
Allah Subhanah wa Ta’ala kwa sababu hua ni wenye kufanya Hijra.



UMUHIMU WA HIJRA KATIKA ISLAM



Neno HIJRA liatokana na neno HAJARA la Kiarabu ambalo hua ni lenye kumaanisha
Kunyangánya kutoka kwa, Kupokonya kutoa kwa, Kuficha, Kudhibiti, Kukataza au
Kuzuia kuingia katika sehemu fulani, kuweka Kizingiti, Kusahaulika, Kuachana na kitu.
Neno Hajara ndio ililotoa neno Hijrun ambalo maana yake hua ni Kitu chochote
kilichokatazwa kufanywa, Ufahamu wa Ibn Adam, na pia likatoa neno Hajar ambalo
67

maana yake hua ni Jiwe, hivyo Jiwe limeitwa Hajar kwa sababu ya kutokana na kua na
mumbile ya Ugumu wenye kujidhibiti sana.
Neno Hajara ndio lilotoa neno Hijra ambalo pia hua ni lenye kumaanisha kuhama kutoka
katika sehemu moja isiyokubalika, au isiyowezekana kubakia na kuelekea katika sehemu
nyengine, ambapo hali hiyo ya kuhama hua inagawika katika sehemu mbili, ambapo moja
ni kuhama kwa watu au mtu kutoka sehemu moja kwa ajili ya kuihami nafsi yake au dini
yake kuelekea sehemu nyengine yenye usalama zaid na aina hii ya Hijra inazungumziwa
na Allah Subhanah wa Taála ndani ya Qurán pale aliposema:

‫ض ُﻣَﺮا َﻏﻤﺎً َﻛﺜِﲑاً َو َﺳ َﻌﺔً َوَﻣﻦ َﳜُْﺮ ْج ِﻣﻦ‬ ِ ‫اﻪﻠﻟِ َِﳚ ْﺪ ِﰱ ٱﻷ َْر‬
‫ﺎﺟْﺮ ِﰱ َﺳﺒِ ِﻴﻞ ﱠ‬ِ ‫﴿وﻣﻦ ﻳـﻬ‬
َُ ََ
‫ٱﻪﻠﻟِ َوَﻛﺎ َن ﱠ‬ ِ ِِ‫ٱﻪﻠﻟِ ورﺳﻮﻟ‬ ِ ‫ﺑـﻴﺘِ ِﻪ ﻣﻬ‬
ِ‫ﺎﺟﺮاً إ‬
ُ‫ٱﻪﻠﻟ‬ ‫ﻠﻰ ﱠ‬ َ ُ‫ﻋ‬
َ ‫ﻩ‬
ُ‫ﺮ‬ ‫َﺟ‬
ْ ‫أ‬ ‫ﻊ‬
َ ‫ﻗ‬
َ‫و‬َ ‫ﺪ‬ْ ‫ﻘ‬
َ ‫ـ‬
َ ‫ﻓ‬ ‫ت‬
ُ ‫ﻮ‬ ‫ﻤ‬
َْ ‫ﻟ‬
ْ ‫ٱ‬ ‫ﻪ‬
ُ ‫ﻛ‬
‫ر‬
ْ ‫ﺪ‬
ْ ‫ﻳ‬
ُ ‫ﰒ‬
‫ُﱠ‬ ‫ﻪ‬ ُ ََ ‫ﱠ‬ ‫ﱃ‬َ َ ُ َْ
﴾ً‫َﻏ ُﻔﻮراً ﱠرِﺣﻴﻤﺎ‬
Waman yuhajir fee sabeeli Allahi yajid fee al-Ardhi muraghaman katheeran
wasaAAatan waman yakhruj min baytihi muhajiran ila Allahi warasoolihi thumma
yudrik-hu almawtu faqad waqaAAa ajruhu AAala Allahi wakana Allahu ghafooran
raheeman (Surat An Nisaa 4:100)
Tafsir: Na yule ambae atakaehama kwa ajili ya Allah Subhanah wa Taála, basi atakuta
katika Ardhi sehemu nyingi sana za kuishi. Na yeyote yule atakaehama kutoka katika
nyumba kuhmia kwa Allah na Mtume wake na kifo kikamkuta basi atayakuta Malipo
yake yapo kwa Allah. Na kwa hakika Alllah ni mwingi wa usamehevu na mwingi wa
Rehma.
Neno Hijra halikutumika katika Qurán kumaanisha kuhama kwa ajili ya kujinusuru
kutoka katika Ardhi moja kuelekea katika Ardhi nyengine tu lakini limetumika kuhama
kwa ajili ya kusimamia haki baina ya Mke Muadilifu na Mume Muadilifu pale Allah
Subhanah wa Ta’ala aliposema katika aya ifuatayo:

‫ﺾ َوِﲟَﺂ أَﻧْـ َﻔ ُﻘﻮاْ ِﻣ ْﻦ‬ ٍ ‫ﻀ ُﻬ ْﻢ َﻋﻠَ ٰﻰ ﺑَـ ْﻌ‬ ِ ‫ﺎل ﻗَـ ﱠﻮاﻣﻮ َن ﻋﻠَﻰ ٱﻟﻨِﺴ‬
ِ ‫ﺂء‬ ِ ﴿
َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﺑَـ ْﻌ‬
‫ﱠﻞ ﱠ‬ َ ‫ﻀ‬ ‫ﻓ‬
َ ‫ﺎ‬‫ﲟ‬
َ َ ّ َ ُ ُ ‫ٱﻟﺮ َﺟ‬ ّ
‫ٱﻪﻠﻟُ َوٱﻟﻼﱠﺗِﻰ َﲣَﺎﻓُﻮ َن‬ ‫ﻆ ﱠ‬ َ ‫ﺐ ِﲟَﺎ َﺣ ِﻔ‬ ِ ‫ﺎت ﻟِّْﻠﻐَْﻴ‬ ِ
ٌ َ‫ﺎت َﺣﺎﻓﻈ‬
ِ ِ ‫أَﻣﻮاﳍِِﻢ ﻓَﭑﻟ ﱠ‬
ُ َ‫ﺼﺎﳊ‬
ٌ َ‫ﺎت ﻗَﺎﻧﺘ‬ ْ َْ
ْ‫ﻮﻫ ﱠﻦ ﻓَِﺈ ْن أَﻃَ ْﻌﻨَ ُﻜ ْﻢ ﻓَﻼَ ﺗَـْﺒـﻐُﻮا‬ ِ ‫ﻧُﺸﻮزﻫ ﱠﻦ ﻓَﻌِﻈُﻮﻫ ﱠﻦ وٱﻫﺠﺮوﻫ ﱠﻦ ِﰱ ٱﻟْﻤ‬
ُ ُ‫ٱﺿ ِﺮﺑ‬
ْ ‫ﻀﺎﺟ ِﻊ َو‬ َ َ ُ ُُ ْ َ ُ َُ ُ
﴾ً‫ٱﻪﻠﻟ َﻛﺎ َن َﻋﻠِﻴّﺎً َﻛﺒِﲑا‬ ِ ِ ِ
َ‫َﻋﻠَْﻴﻬ ﱠﻦ َﺳﺒﻴﻼً إ ﱠن ﱠ‬
68

Alrrijalu qawwamoona AAala alnnisa-i bima faddala Allahu baAAdahum AAala


baAAdin wabima anfaqoo min amwalihim faalssalihatu qanitatun hafidhatun
lilghaybi bima hafidha Allahu waallatee takhafoona nushoozahunna
faAAidhoohunna waohjuroohunna fee almadajiAAi waidriboohunna fa-in
ataAAnakum fala tabghoo AAalayhinna sabeelan inna Allaha kana AAaliyyan
kabeeran(Suran An Nisaa 4:34)
Tafsir: Wanaume ni Qawwamoona (wasimamizi) juu ya Wanawake kwa sababu Allah
amewafadhili baadhi yao (Wanaume) juu ya baadhi yao (Wanawake) kutokana na kile
wanachokichuma na kukitumia juu yao. Hivyo Wanawake wema ni watiifu (kwa Mola
wao na kwa Waume zao wenye kuwasimamia) na hujilinda wanapokua Waume zao
hawapo kile walivyoamrishwa na Allah kujilinda. Ama kwa Wanawake ambao
mnaona kua wanafanya maovu, basi waonyeni (kwanza), (kisha kama hawakusikia
basi) Fanyeni Hijra kutoka katika vitanda vyao, (Na kama hio haijazaidia basi)
wapigeni kidogo, lakini kama wakirudi katika utiifu wenu, basi msiitafute njia za
kuwakera. Kwa hakika Allah ni alie Juu zaidi ya Kila kiitu na ni Mkubwa sana.

Hapa tunaona kua kwanza aya imetumia neno Qawwam kwa kilugha hua linamaanisha
kusimamia au kuhudumia kitu kwa muda mrefu, hivyo tunapozungumzia kifamilia basi
neno hili hua linajumuisha jukumu la kusimamia kimwili, kimahitaji, kiheshima na
kimajukumu kwa upande wa kidunia na kiakhera.

Hivyo maana ya neno Qawwam hua kamwe haimaanishi kama vile wanavyofikiria watu
wengi kua maana yake ni kudhibiti, kuweka chini yake au chini ya mamlaka yake, kwani
kufikiria hivyo basi hua ni sawa na walivyokua wakifanya jamii za watu wa Jahiliyyah.

Katika kuielezea maana ya aya hii, basi Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakkalimin Imam
Al Ghazali Al Thani Imam Fakhr al Din Al Razi anasema kua sehemu ya aya hii ya Surat
An Nisaa 4:34 ambayo ni: ‘Alrrijalu qawwamoona AAala alnnisa-i (Wanaume ni
wasimamizi wa Wanawake) ina uhusiano na sehemu ya aya nyengine kabla yake
isemayo:

ِ ‫﴿وﻻَ ﺗَـﺘَﻤﻨـﱠﻮاْ ﻣﺎ ﻓَﻀﱠﻞ ﱠ‬


﴾‫ﺾ‬ َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﺑِﻪ ﺑَـ ْﻌ‬
ٍ ‫ﻀ ُﻜ ْﻢ َﻋﻠَ ٰﻰ ﺑَـ ْﻌ‬
َ َ َْ َ
Wala tatamannaw ma fadhala Allahu bihi baAAdhakum AAala baAAdhin’ (Surat
An Nisaa 4:32)

Tafsir: Na wala msitamani kile ambacho Allah amewafadhili baadhi yenu kuliko
wengine.
69

Imam Fakhr Ad Din Al Razi anaendelea kwa kusema: Aya ambayo tulisema kua
ilishushwa kwa sababu baadhi ya Wanawake walitoa kauli kuhusiana na Allah
kuwapendelea Wanaume katika Urithi. Hivyo Allah ameweka wazi katika ayah hii
kua amewafadhili tu Wanaume juu ya Wanawake kwa sababu Wanaume ni
Wasimamizi wa Wanawake. Kwani ingawa wote Mke na Mume wanafaidika na
matunda na haki zinazotokana na kua pamoja, basi Allah amemuamrisha
Mwanamme kumlipa Mwanamke sehemu ya ndoa yao, na kumhudumia katika
mahitaji ya kila siku, hivyo ongezeko la upande mmoja hukabiliana na ongezeko la
upande wa pili – na hivyo hua kama vile hamna pendeleo baina yao. Jambo hili
linaweka wazi mpangilio wa namna zilivyopangika aya.’

Hivyo darja ya Qawwam aliyokua nayo mwanamme kwa familia yake hua ni kuilinda,
kuisimania na kuwahudumia A’al, Ahl, Zawj au familia yake katika hali ya kiuadilifu, na
hapa msimamizi husika hua anatakiwa kuitumia fadhila hiyo aliyopewa na Allah
Subhanah wa Ta’ala, kwa kua na umakini, huruma, busara na subra katika kutekeleza
majukumu hayo, kwani vyenginevyo itakua ni kuenda kinyume na matakwa ya mfadhili
na mtoaji wa majukumu hayo na hivyo mwanamme husika hupoteza haki ya kua na Darja
hiyo ya Qawwam.
Kwa upande wa pili basi tunaona kua Ayah hii ya Surat al Nisaa 4:34 imetumia pia neno
Hijra kwa kuwapa amri Wanaume wenye sifa ya Qawwam kwa wake zao kufanya Hijra
katika vitanda vya wake zao, pale inapokua Waume hao hawatekelezewi haki zao na
Wake zao wasiokua na utiifu kwao. Hivyo ayah hii inawapa haki Wanaume wenye sifa
ya Qawwam kuwapa adhabu Wake zao hao kwa kuwafanyia Hijra.
Ama juu ya Hijra hii basi kuna mitizamo tofauti kwani kuna wasemao kua Hijra hii
iliyomaanishwa hapa ni Hijra ya kutowaingilia Wanawake kwa muda fulani hadi
watakapojirekebisha. Na pia kuna wasemao kua Hijra hii inaamanisha kua wanaweza
kuwaingilia lakini wajizuie na kuwasemesha, na pia kuwapa mgongo wakati wa kulala
kama ikiwa watalala katika kitanda kimoja.
Hizo ni miongoni mwa aina za Hijra zilizotajwa ndani ya Qurán na ambazo Waislam
tunatakiwa kuzifanya kwa kutumia kiwiliwili katika kipindi cha uhai wetu hapa
ulimwenguni. Ama tunapozungumzia Hijra ya pili basi hua ni ile ya kuhama kutoka
katika hali moja kuenda katika hali nyengine pia, lakini aina hii ya Hijra hufanywa kwa
kutumia njia za Kiroho, Kinafsi, Kiakili na Kifikra kama vile ambavyo Allah Subhanah
wa Taála alipomwambia Rasul Allah Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kua awe
na Subra na anayofanyiwa na Makafiri huku akiwa ni mwenye kuachana nao na
kutoshirikiana nao kwa ukarimu na katika hali nzuri pale aliposema katika Surat Al
Muzzamil:-

َِ ً‫﴿وٱﺻِﱪ ﻋﻠَﻰ ﻣﺎ ﻳـ ُﻘﻮﻟُﻮ َن وٱﻫﺠﺮﻫﻢ ﻫﺠﺮا‬


﴾ً‫ﲨﻴﻼ‬ ْ َ ْ ُ ُْ ْ َ َ َ ٰ َ ْْ َ
70

Waisbir AAala ma yaqooloona waohjurhum hajran jameelan (Surat Al Muzzamil


73:10)
Tafsir: Na kua na Subra (Ewe Muhammad)juu ya kile wanachokisema, na achana nao
kwa muachano mwema.
Hivyo Hijra hii ya aina ya pili yaani ya Kinafsi na Kiroho ni Hijra ambayo inajumuisha
pia kuhama kutoka katika hali ya kiza cha maasi na kuingia katika hali nyengine iliyo
bora zaidi ambayo ni hali ya kuingia katika Nuru, Muangaza na kua na Utiifu kwa Allah
Subhanah wa Taála na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.
Hijra ya aina hii ni Hijra ambayo inahimizwa na kutiliwa mkazo zaid kufanywa kwa kila
mmoja miongoni mwetu katika Dini ya Kiislam. Kwani hii hua ni hali ya kujidhibiti na
matamanio ya Nafsi dhidi ya kuiendekeza Dunia na hivyo kuzirudisha Nafsi katika
kumuelekea na kumtii Allah Subhanah wa Taála na Mtume wake Muhammad Salallahu
A’layhi wa Salam. Umuhimu wa aina hii ya Hijra katika maisha yetu unathibitishwa na
malengo ya Muumba wetu kutuletea Qur’an ili iwe ndio muongozo wa kila kitu katika
Maisha yetu na hivyo kutakiwa kuifanyia kazi kama ipasavyo Qurán bila ya kuihama,
kwani kuihama Qurán hua ni kuenda kinyume na Imani ya Dini ya Kiislam na hivyo
tutakua na masuali ya kujibu mbele ya Mola wetu kama inavyosema Surat Al Furqan:

﴾ً‫ب إِ ﱠن ﻗَـ ْﻮِﻣﻰ ﱠٱﲣَ ُﺬواْ َﻫـٰ َﺬا ٱﻟْ ُﻘْﺮآ َن َﻣ ْﻬ ُﺠﻮرا‬
ِّ ‫ﻮل ٰﻳـَﺮ‬
ُ ‫ﺎل ٱﻟﱠﺮ ُﺳ‬
َ َ‫﴿وﻗ‬
َ
Waqala alrrasoolu ya rabbi inna qawmee ittakhadhoo hadha alqur-ana
mahjooran (Surat Al Furqan 25:30)
Tafsir: Na atasema Rasul, Ya Rabbi! Hakika kaumu yangu wameichukulia hii Qurán
kua ni Mahame.
Tunapozungumzia hali ya Qur-ána Mahjuran basi ingawa tunaona kua aya
inawazungumzia watu wa Kabila la Quraysh ambao ndio waliokua wakilalamikiwa
katika ayah hii kua hawakuiamani na waliichukulia Qurán kua ni kama hekaya za kale
na mashairi yasiyokua na maana yeyote. Lakini pia ayah hii inavizungumzia vizazi
vilivyofuatia baadae vikiwemo vizazi vilivyokuja kabla yetu, vizazi vyetu na vizazi
vitakavyokuja baada yetu. Vizazi hivyo ingawa ni vizazi vya Kiislam lakini hua
vimeifanya Qurán kua Mahjuran yaani iliyohamwa kwa njia nyingi sana ikiwemo,
Kutoisoma kabisa, Kuisoma lakini bila ya Kuitafakkar na Kuifaham, Kutochukua jitihada
yeyote ila ya kutaka kuifaham, Kutosimamia maamrisho yake, hukmu zake na Sharia
zilizomo ndani yake, Kutoitilia maanani n.k
Ukweli ni kua Waislam hatutakiwi kua ni wenye kuifanya Qurán kua Mahjuran bali
tunatakiwa Dunia ndio tuifanye kua ni Mahjuran, hivyo tunapaswa kufanya Hijra kutoka
kwenye matamanio ya Dunia na kuhamia ndani ya Qurán na kua ni wenye kufanikiwa
71

kwa kurudi kwa Mola wetu huku tukiwa ni wenye kufuzu kwa kua na Nyoyo zisizokua
na madoa ndani yake kwani Moyo ndio Msingi wa Mja kumjua Mola wake na hivyo ni
kiungo ambacho kinatakiwa kua kisafi na salama ndani nje na ndio maana Waislam
tukawa ni wenye kutiliwa mkazo wa kufanya Hijra ya kuachana na maasi na kurudi chini
ya utiifu wa Allah Subhanah wa Taála.
Kwani Anasema Allah Subhanah wa Taála kua:

ٌ ‫ﻨﺪ َرﺑِِّﻪ َوﻻَ َﺧ ْﻮ‬


َ‫ف َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ َوﻻ‬ َ ‫َﺟُﺮﻩُ ِﻋ‬ ِ ِ
ْ ‫﴿ﺑَـﻠَ ٰﻰ َﻣ ْﻦ أ‬
ْ ‫َﺳﻠَ َﻢ َو ْﺟ َﻬﻪُ ﱠﻪﻠﻟ َوُﻫ َﻮ ُْﳏﺴ ٌﻦ ﻓَـﻠَﻪُ أ‬
﴾‫ُﻫﻢ َْﳛَﺰﻧُﻮ َن‬
ْ
Bala man aslama wajhahu lillahi wahuwa muhsinun falahu ajruhu AAinda rabbihi
wala khawfun AAalayhim wala hum yahzanoon (Surat Al Baqar 2:112)
Tafsir: Bali yeyote yule ambae atausalimisha uso wake kwa Allah, akiwa ni mwenye
kufanya mema, basi malipo yake yapo kwa Mola wake na haina haja kwake kua na
khofu wala kua na huzuni.
Bila ya shaka aya iko wazi kua yeyote yule ambae atausalimisha uso wake na akajitolea
kwa ajili ya Mola wake pekee, na akajisafisha a kutokua na uchafu wa dhambi, akawa
Mcha Mungu, akawa ni mwenye I’lm ya kujua kila anachokifanya katika Ibada zake basi
hua ni mwenye kufanya mema katika mambo yake, basi hawatakua na khofu ya kua ni
wenye kufanyiwa Hajar (Kuachwa, au kusahaulika) na Mola wao kwani kwa hakika
Malipo yao watayakuta kwa Mola wao.
Ayah hii pia imetumia neno Wajh yaani Uso kwa sababu uso ndio sehemu muhimu ya
mwili wa Ibn Adam inayoonekana wazi na ndio inayomtambulisha mtu husika mbele ya
watu wengine na hivyo basi katika Lugha ya Kiarabu neno Wajh hua linawakilisha
muonekano wa mwili mzima wa Ibn Adam, na limetumika mara nyingi sana katika
Qurán kumaanisha kiwiliwili cha Ibn Adam.
Ayah hii pia imetumia neno Muhsin (Mwenye kuufanya Mema kwa kumtii Mola wale)
ambalo hua ni lenye kutokana na neno la Kiarabu Ihsan ambalo Kisharia maana yake hua
ni Kumuabudu Allah kama unamuona, na kama humuoni basi yeye anakuona, hivyo mtu
mwenye sifa ya Muhsin hua ni mtu ambae tayari ameshafanya Hijra ya kurudi kwa Mola
wake na hivyo katika kila analolifanya basi hua anamuona Mola wake na hivyo hua
hatakiwi kua na khofu ya kufanyiwa Hajar na Mola wake bali hu na ukaribu zaidi na
Mola wake kwa sababu mtu anapomkaribia Mola wake kwa hatua moja basi Allah
Subhanah wa Taála humkaribia mtu huyo kwa hatua mbili zaid, sasa katika hali kama
hii basi mtu huyu hua ni mwenye kufanya kila anachokifanya kwa Ihsan na hivyo hua ni
Muhsin katika matendo yake na hua ni Muhsin katika hali yake ya Kimaumbile kutokana
72

na jitihada zake kwa ajili ya Mola wake zinazotokana na muonekano wa nje wa viungo
vya mwili wake unaojumuishwa na Moyo wake na viungo vyengine vya ndani ya mwili
wake.
Mujaddid ad Din, Sultan al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi anaifafanua maana
ya Muhsin iliyotumika katika ayah hii kwa ile hadith isemayo kua:

ِ ‫ﺎل ِﺎﺑﻟﻨِّﻴﱠ‬
“ ‫ﺎت‬ ْ ‫”إِﱠﳕَﺎ ْاﻷ‬
ُ ‫َﻋ َﻤ‬
Innama al aAmal bi alniyyati
Tafsir: Uhakika wa Amal hutegemea na nia yake.
Kwa kutuambia kua: Nia hua ni kitu ambacho kinatoka ndani ya kina cha Moyo
kutokana na Ikhlas iliyomo katika tendo jema husika, bila ya kuamua kua na
maamuzi juu ya tendo husika. Kwani siku zote mtu alieshiba kamwe hawezi
kuamua tu na kusema kua sasa hivi nna njaa, na akawa na njaa katika wakati
huo huo kama alioamua huku akiwa ameshiba, jambo hili hua haliwezekani, bali
mtu huyu humbidi kutafuta njia ya kukitamani chakula kutoka ndani ya Moyo
wake, na njia hio hujulikana kama Nia Sahih ambayo haipatikani hadi pale mtu
huyu atakapoweza kuuthibitishia Moyo wake na Ufahamu wake.
Hivyo Nia ya Muhsin hutokana na kujua na kufahamu malipo yanayotokana na
kitendo husika, huku kukijumuishwa I’lm iliyokuwemo katika kina cha Moyo
kua Allah Subhanah wa Taála ni mwenye uwezo juu ya kila kitu, na hivyo ndie
mwenye uwezo wa kutoa zawadi au kuadhibu na hakuna mwengine anaeweza
kufanya hivyo isipokua yeye. Kila Uthibitisho huu unapokua mkubwa na kua na
nguvu zaidi katika Nafsi na Moyo wa mtu husika kutokana na I’lm ya kujua
hayo basi ndivyo inavyozidi usafi wa Nia ya mtu husika.
Ama kwa upande wa Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Ibn Muhammad Ibn Muhammad
Al Ghazali basi yeye anasema kuhusiana mambo muhimu yanayohitajika katika
kufanikisha Amali njema za Muhsin ni kua:
1- Kua na Moyo Msafi katika kutekeleza Amali husika.
2- Kua na Ikhlas katika kutekeleza Amali husika.
3- Kuuhudhurisha Moyo na Ufahamu katika kutekeleza wa Amali husika.
4- Kua na Unyenyekevu mbele ya Allah Subhanah wa Taála.
5- Kua na Khofu mbele ya Allah Subhanah wa Taála.
6- Kua na Mapenzi Juu ya Allah Subhanah wa Taála.
7- Kua ni mwenye kuona Haya mbele ya Allah Subhanah wa Taála
73

8- Kua na Matumaini na kua ni mwenye kumuamini Allah Subhanah wa


Taála.
Ambapo mambo manane hayo hua yanafafanulika kwa kujumuishwa katika hali
zifuatazo:
1- Kua na Moyo Msafi na Ikhlas.
2- Kuuhudhurisha Moyo na Ufahamu katika kutekeleza Amali husika.
3- Kua na Unyenyekevu mbele ya Allah Subhanah wa Taála.
4- Kua na Khofu na Mapenzi mbele ya Allah Subhanah wa Taála.
5- Kuaona Haya, kua na Matumaini na Kua ni mwenye Kumtegemea Allah
Subhanah wa Taála baada ya kumaliza Amali husika.
Hujjat Islami Imam Abu Hamid Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali
anayafafanua majumuisho hayo kwa kusema kua:
1- Kua na Moyo Msafi na Ikhlas – Hii ni hali ambayo inajumuisha kuusafisha Moyo
kutokana na kua na Maradhi ya Nafsi na kua na Tabia Mbovu, katika hali pia Moyo
inabidi usafishwe na hivyo usiwe na nia au malengo yeyote ya kufanya jema kwa
ajili ya yeyote au chochote isipokua iwe kwa ajili ya Allah Subhanah wa Taála pekee
na hivyo Moyo wa Mtu husika hautakiwi kua na kitu chochote ndani yake isipokua
Muumba wa Moyo huo ambae ni Allah Subhanah wa Taála. Kiasi ya kua athari ya
Ikhlas ndani ya amali zake hua ni yenye kuonekana kuanzia kwenye Moyo wake na
hivyo hua ni zenye kuthibitishika katika kiwiliwili chake katika utekelezaji wa Amali
njema hizo. Ambapo hali ya juu kabisa ya kua na Moyo Msafi na Ikhlasi katika
matendo ya Mja hufikika pale inapokua Mja anafanya mambo mema kwa ajili ya
Mapenzi kwa Mola wake bila ya kutegemea Malipo kutoka kwake wala kua na khofu
au kutaka kuokoka kutokana na adhabu za Mola wake.
2- Kuuhudhurisha Moyo na Ufahamu katika kutekeleza Amali husika – Hii hua ni
ile hali ambayo inajumuisha ufanyaji wa amali njema huku Moyo na ufahamu ukiwa
unaenda sambamba na kauli na vitendo vya Mtu husika. Ambapo hapa hua
tunazungumzi mfumo mzima wa Ufahamu wa mtu katika kujua umuhimu wa jambo
analilofanya huku akiwa ni mwenye kumkumbuka Mola wake kimawazo, kikauli na
kivitendo katika kila hatua ya utekelezaji wa Amali husika.
3- Kua na Unyenyekevu mbele ya Allah Subhanah wa Taála – Hali hii inajumuisha
hali ya Kumnyenyekea, Kumtukuza, Kumkuza, Kumsifu Mola wako.
4- Kua na Khofu na Mapenzi mbele ya Allah Subhanah wa Taála – Hali hii
inajumuisha Al Taqwa (Taqwa), Al Khawf (Khofu) na Al Mahabbah (Mapenzi) kwa
Allah Subhanah wa Taála katika utekelezaji wa Amali husika. Na haya yote hua
74

yanategemeana na Ilm ya Mja juu ya Uwezo, Ukubwa, Malipo, Adhabu za Mola


wake wake na Wingi wa kasoro zake Mja huyo na wingi wa dhambi zake mbele ya
Mola wake. Kila mtu anaopokua anajua juu ya mambo haya basi ndio Khofu na
Mapenzi yanazvyozidi kuongezeka kwa Mola wake.
5- Kuona Haya, kua na Matumaini na Kua ni mwenye Kumtegemea Allah
Subhanah wa Taála baada ya kumaliza Amali husika – Hali hii hua inajumuisha
Al Raja (Matumaini) na Tawakkul (kumtegemea Allah Subhanah wa Taála tu katika
kila kitu) baada ya kumaliza kutekeleza Amali husika. Kwani Mja anatakiwa kua ni
mwenye kuona haya kutokana na kua na kasoro nyingi katika Matendo yake na hivyo
anatakiwa kua na khofu ya kutokukubaliwa kwa Amali zake njema, lakini hapo hapo
anatakiwa kua ni mwenye kumtegemea Allah Subhanah wa Taála na kua na
matumaini kua atamkubalia amali njema zake hizo.

Ili kufahamu juu ya Hijra inayompelekea Mja kua na sifa ya Muhsin, basi na tuangalie
Maumbile ya Moyo ambacho ni kiungo kinachohusika moja kwa moja na utayarishaji
wa uthibitisho wa mtu husika kufanya Hijra kutoka katika hali ya kua ni mtu wa kawaida
na kuingia kuingia katika hali hio ya Muhsin, kwani tofauti na tunavyodhani sisi mimi na
wewe kua Moyo ni Moyo yaani ni Al Qalb, lakini tunapoiangalia Qurán basi tunaona
kua Moyo ni kiungo muhimu kilichogawika katika hali nne za darja tofauti kulingana na
mazingira ya Maumbile yake kama zilivyotajwa na Allah Subhanah wa Taála ndani ya
Qurán ambazo ni Al Qalb, Al Fuad, Al Lub na Al Sadr.


MAUMBILE YA NYOYO ZA IBN ADAM: AL QALB, AL FUAD, AL
LUBB, AL SADR NA AN NAFS KATIKA QURÁN

Maamrisho yote ya Dini ya Kiislam na Hukmu zake yamewekwa na Allah Subhnaha wa
Taála kwa ajili ya kusimamia Maslahi ya kila kiumbe kilichopo Ulimwenguni, lakini
Maslahi hayo huwezi kuyaona hadi pale utakapoisoma Dini ya Kiislam na kuifaham kwa
kutumia ufahamu wa Moyo na hapo ndipo utakapohisi athari zake ndani ya mwili wako
na pia ndipo utakapopata mantiki ya maamrisho hayo kama isemavyo aya ifuatayo ya
Surat Az Zumar ambao tushaiangalia katika Utangulizi:
75

‫ﻳﻦ َﳜْ َﺸ ْﻮ َن‬ ِ ‫ﻳﺚ ﻛِﺘﺎﺎﺑً ﱡﻣﺘﺸ ِﺎﻬﺑﺎً ﱠﻣﺜ ِﺎﱏ ﺗَـ ْﻘﺸﻌِﱡﺮ ِﻣْﻨﻪ ﺟﻠُ ﱠ‬ ِ ِ ‫﴿ﱠ‬
َ ‫ﻮد ٱﻟﺬ‬
ُ ُ ُ َ َ َ َ َ َ ‫َﺣ َﺴ َﻦ ٱ ْﳊَﺪ‬ ْ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻧَـﱠﺰَل أ‬
‫ٱﻪﻠﻟِ ﻳَـ ْﻬ ِﺪى ﺑِِﻪ َﻣﻦ‬
‫ﻚ ُﻫ َﺪى ﱠ‬ ِ ِ‫رﺑـﱠﻬﻢ ﰒُﱠ ﺗَﻠِﲔ ﺟﻠُﻮدﻫﻢ وﻗـُﻠُﻮﺑـﻬﻢ إِ َ ٰﱃ ِذ ْﻛ ِﺮ ﱠ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟ ٰذﻟ‬ ْ ُُ َ ْ ُ ُ ُ ُ ُْ َ
﴾‫ٱﻪﻠﻟ ﻓَﻤﺎ ﻟَﻪُ ِﻣ ْﻦ َﻫ ٍﺎد‬
‫ﱠ‬ ِ
‫ﻞ‬ ِ‫ﻀﻠ‬ْ ُ‫ﻳَ َﺸﺂءُ َوَﻣﻦ ﻳ‬
َ ُ
Allahu nazzala ahsana alhadeethi kitaban mutashabihan mathaniya taqshaAAirru
minhu juloodu alladheena yakhshawna rabbahum thumma taleenu julooduhum
waquloobuhum ila dhikri Allahi dhalika huda Allahi yahdee bihi man yashao
waman yudhlili Allahu fama lahu min hadin (Surat Az Zumar 39:23)

Tafsir: Allahu ameshusha hadithi bora kabisa, Kitabu (Quran) chenye sehemu ndani
yake zinazofanana kwa wema na usahih. Ngozi za wale wenye kuomuogopa Allah
zinatetemeka (Wanapoisikia Qurán). Na kisha Nyoyo zao na ngozi zao hulainika
kutokana na kumkumbuka Mola wao. Huo ni Uongofu wa Allah. Ambae humuongoza
amtakae na anaepotoshwa na Allah basi hakuna atakaemuongoza.

Naam aya zimesema hivyo kwa sababu Moyo una maumbile ya kua ni kiungo kikamilifu
kinachojitegemea na hivyo kua na ufahamu wake na maamuzi yake yasiyotegemeana na
kiuongo chochote mwilini, na ndio maana Allah Subhanaha wa Taála akawa
ameuzungumzia Moyo katika hali tofauti na mara nyingi sana katika kitabu chake
kitukufu cha Qurán, hivyo na tuanze kwa kuangalia maana na matumizi ya neno Qalb
kama lilivyotumiwa katika Qur’an.

AL QALB

Neno Qalaba kwa Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Kugeuka, Kugeuza kitu Juu Chini
au Mbele Nyuma au Ndani Nje, Kubadilisha, Kubadilika Hali au Muelekeo,
Kubadilishana Mmoja baada ya Mwengine. Neno Qalaba ndio lililotoa neno Qulub
ambalo maana yake hua ni Moyo, na tunapoiangalia Qurán basi tunaona kua imetumia
neno Qalaba mara 168 katika hali tofauti ikiwemo katika hali ya neno Qulubu ambalo
ndio lililotumika katika aya ya Surat Al Araf pale Allah Subhanah wa Ta’ala aliposema:
76

ِ ِ ْ‫ٱﳉِ ِّﻦ َوٱ ِﻹﻧ‬


ْ ‫﴿ َوﻟََﻘ ْﺪ َذ َرأْ َ� ِﳉَ َﻬﻨ َﱠﻢ َﻛﺜِﲑاً ِّﻣ َﻦ‬
ٌ ُ ‫ﻮب ﻻﱠ ﻳَـ ْﻔ َﻘ ُﻬﻮ َن ﻬﺑَﺎ َوَﳍُْﻢ أ َْﻋ‬
‫ﲔ‬ ٌ ُ‫ﺲ َﳍُْﻢ ﻗُـﻠ‬
‫ﻚ‬َ ِ‫َﺿ ﱡﻞ أ ُْوﻟَـٰﺌ‬
َ ‫ﻚ َﻛﭑﻷَﻧْـ َﻌ ِﺎم ﺑَ ْﻞ ُﻫ ْﻢ أ‬ َ ِ‫ﺼُﺮو َن ِﻬﺑَﺎ َوَﳍُْﻢ آذَا ٌن ﻻﱠ ﻳَ ْﺴ َﻤﻌُﻮ َن ِﻬﺑَﺂ أ ُْوﻟَـٰﺌ‬ ِ ‫ﻻﱠ ﻳـﺒ‬
ُْ
﴾‫ُﻫﻢ ٱﻟْﻐَﺎﻓِﻠُﻮ َن‬
ُ
Walaqad dhara/na lijahannama kathiiran mina aljinni waal-insi lahum quloobun
la yafqahoona biha walahum aAAyunun la yubsiroona biha walahum adhanun la
yasmaAAoona biha ola-ika kaal-anAAami bal hum adhallu ola-ika humu
alghafiloona (Surat Al Araf 7:179)

Tafsir: Na kwa hakika tumewaumba kwa ajili ya Jahannam wengi miongoni mwa
Majini na Watu. Wana Nyoyo ambazo hawafahamu kutokana nazo, wana Macho
ambayo hawaona kutokana nayo, na wana Masikio lakini hawasikii. Wao wako kama
Ngo’mbe lakini wao wamedhalilika zaidi, kwani hawa ndio wale ambao wamekumbwa
na Mghafiliko.

Naam tunapoiangalia aya hii basi tunaona kua imetumia maneno yasemayo Walaqad
Dhara/na Li Jahannama yaani Na kwa hakika Tumewaumba kwa ajili ya Jahannam na
neno kwa ajili ya Jahannam limeunganishwa na harfu Laam. Ambayo ni Laam tofauti na
ile Laam ya LiyaAAbuduuni iliyotumika katika aya ifuatayo:

ِ ‫ٱﳉِ ﱠﻦ وٱ ِﻹﻧﺲ إِﻻﱠ ﻟِﻴـﻌﺒ ُﺪ‬


﴾‫ون‬ ُْ َ َ َ ْ ‫ﺖ‬ ُ ‫﴿ َوَﻣﺎ َﺧﻠَ ْﻘ‬
Wama khalaqtu aljinna waal-insa illa liyaAAbudooni (Surat Adh Dhariyyat 51:56)

Tafsir: Sikuwaumba Majini na Ibn Adam isipokua kwa ajili ya kuniabudu mimi tu.!

Kwani Laam iliyotumika katika aya Surat Adh Dhurriyat 51:56 yaani Laam ya
LiyaAabuduuni hua inajulikana kama Laam Al Ghaayah yaani Laam inayoweka wazi
Kusudio la Kitu Fulani na Laam iliyotumika katika aya yetu ya Surat Al Aaraf 7:179
ambayo ni Laam ya Li Jahannama inajulikana kama Laam al Aqibah yaani Laam
inayoweka wazi kinachobakia baada ya tukio fulani.

Na ijapokua Wanazuoni wengi wanasema kua Laam zote mbili katika aya hizi ni Laam
Al Ghayah, lakini Laam ya LiyaAabuduuni hua pia inahesabika kua ni Laam al Tashrii
77

yaani Lam ya Kisharia wakati Laam ya Li Jahannama inahesabika kua ni Laam Al


Takwini yaani Laam ya Mfumo wa Kimaumbile.

Hivyo basi Laam iliotumika katika Li Jahannama ambayo ni Laam al Aqibah na hapo
hapo ikawa ni Lam Al Takwin imetumika ili kuweka wazi kua kutokana na Maumbile
yao viumbe viwili hivi yaani Ibn Adam na Majini basi wengi wataghafilika na
watashindwa kujizuia na matamanio ya Nafsi zao na hivyo kushindwa kwao kuzitumia
ipasavyo neema za Viungo hivyo walivyopewa na Mola wao ambavyo ni Macho,
Masikio na Nyoyo zao basi kutapelekea kutokea tukio la kuingizwa Motoni kwa wengi
miongoni mwao kutokana na makosa ya kutovitumia ipasavyo viungo hivyo kwa
kutokana na kughafilika, na ingawa kughafilika ni sehemu ya Maumbile ya Ibn Adam,
lakini hata hivyo hakuna Kughafilika kubaya kama kughafilika juu ya Mola Wako
aliekuumba!…Allahuma ajirna minna Naar!..Aamiin!

Hivyo tuungalie maumbile ya Al Qalb kulingana na mtizamo wa Kisayansi ili tupate


kujua kwani nini Allah Subhanah wa Ta’ala akasema:

﴾‫ﻮب ﻻﱠ ﻳَـ ْﻔ َﻘ ُﻬﻮ َن ِﻬﺑَﺎ‬


ٌ ُ‫﴿ َﳍُْﻢ ﻗُـﻠ‬
Lahum quloobun la yafqahoona biha – Wana Nyoyo Lakini hawafahamu kutokana
na Nyoyo hizo!

Mara nyingi sana Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qurán amekinasibisha kiungo cha
Moyo na Kuona, Kufaham na Kutafakkari pia kwa sababu kimaumbile Moyo ni kiungo
cha mwili ambacho kinajitegemea kwa kua na ufaham wenye nguvu ya upekee katika
mwili mzima wa Ibn Adam. Ufahamu wa Moyo wa Ibn Adam hua unafanya kazi zake
kimaumbile kwa kuishirikisha mifumo mikuu minne ya usafirishaji wa nguvu za hisia za
mwili wa Ibn Adam ambazo ni:

1- Mfumo wa Usambazaji wa hisia za sehemu tofauti za mwili.


2- Mfumo wa Viasili vinavyodhibiti maumbile ya ufanyaji kazi wa mwili
vinavyozalishwa na Moyo.
3- Mfumo wa Usambazaji Kemikali kupitia katika mapigo ya Moyo na
usambazaji Damu.
4- Mfumo wa Uzalishaji Nguvu za Kimaumbile za mwili za ufanyaji kazi wa
viungo vya Ibn Adam na nguvu za Mawimbi ya Mvutano wa Umeme wa
Sumaku za ndani ya Mwili na nje ya Mwili.
78

Kimaumbile Moyo wa Ibn Adam hua na uwezo wa kuzalisha nguvu za umeme zenye
asili ya mawimbi ya sumaku zenye nguvu mara 5000 zaid na nguvu kama hizo
zinazozalishwa na Ubongo wa Ibn Adam, nguvu hizo ambazo pia huweza kuhisika hata
nje ya mwili wa Ibn Adam kwa takriban umbali wa mita 3 hua na uwezo wa kusambaza
na kupokea na kuwasiliana na hisia mbali mbali kutoka katika ubongo wa mtu husika na
sehemu nyengine za mwili mzima wa mtu huyo na wakati huo hua na uwezo wa
kuwasiliana na nguvu zinazozalishwa na watu wengine zaidi ya wanane waliopo karibu
nae na hivyo hua na uwezo wa kuwaathiri watu hao walio karibu nawe kihisia.

Nguvu hizi zinazozalishwa na Moyo pia huweza kuwasiliana kihisia na kuathiri nguvu
za mvutano wa mawimbi ya umeme ya viumbe wengine waliokuwepo karibu yake mtu
ikiwemo Wanyama na Viumbe wengine wasioonekana wa Ulimwengu wa Al Ghayb. Na
ndio maana baadhi wakati mtu anaweza akakaa peke yake na ghafla akahisi kama mwili
unamsisimka, kwa sababu nguvu hizi za kimaumbile za Moyo hua na uwezo wa kuhisi
kutokea kuwepo kwa Viumbe wengine wasioonekana kama vile Majini ambao wao
Maumbile yao yana asili za nguvu hizi. Na ni kutokana na athari ya nguvu hizi ndio
Viumbe Majini hua na uwezo wa aidha kuwadhibiti Ibn Adam au kuwaogopa na
kuwakimbia Ibn Adam.

Moyo wa Ibn Adam una nyuroni 40000 ambazo kwa pamoja hua zinaunda kitu
kinachoitwa Akili ya Moyo, ambayo hua ni yenye uwezo wa kukumbuka kwa muda fupi
na kwa mda mrefu, kujifunza na kufanya maamuzi yake wenyewe bila kuitegemea akili
na hivyo hua na uwezo wa kuyadhibiti mapigo ya Moyo, athari ya Ufahamu wa Moyo
hua na uwezo wa kuubadilisha hata mtizamo wa ufahamu wa akili kihisia na kimaamuzi
katika mambo mbali mbali.

Kila Moyo unapopiga basi hua ni wenye kuzalisha nguvu za mawimbi ya umeme wa
sumaku na hivyo kusababisha athari mbali mbali za Moyo ikiwemo kuona kwa mtizamo
wa Jicho la Moyo, kuhisi kwa hisia za Moyo, ambapo hisia zote hizi zinapotokea ndani
ya Moyo hua zina athari kubwa zaidi ndani ya mwili wa Ibn Adam na zinazotofautiana
sana na zile zenye kutokea moja kwa moja kupitia katika akili ya Ibn Adam, ambapo
mawasiliano kutoka kwenye Moyo kuelekea kwenye Akili hua ni maradufu zaidi yana
umuhimu zaidi kwa ufanyaji kazi wa Mwili kuliko mawasliano ya kutoka kwenye Akili
kuelekea kwenye Moyo.

Hii inaonekana wazi pale Moyo unapobadilika hali yake kulingana na hisia na vitendo
tofauti vinavyosababishwa na ufaham wa akili na hivyo kuufanya Mwili wa Ibn Adam
kua dhaifu na kuishiwa nguvu, kwa mfano Ibn Adam anapokua na hasira, wasiwasi
mkubwa, mawazo mengi au khofu basi hali ya mapigo ya Moyo hubadilika na hivyo
hufanya mawasiliano na akili ambayo nayo baada ya kupata mawasiliano hayo basi hua
ni yenye kujua kua kuna hisia ambazo sio nzuri kwenye Moyo na mwili mzima kwa
79

ujumla na hivyo kusababisha akili kupungukiwa na uwezo wake wa kufanya kazi kwa
umakini na kufikiria ipasavyo.

Na hivyo kila Ibn Adam akiwa na hali kama hio mara kwa mara basi Moyo wake
hudhooofika, jambo ambalo hupelekea na viungo vyengine muhimu vya mwili
kudhoofika ikiwemo, Mafigo, Ini, Mapafu n.k na kusababisha madhara makubwa sana
mwilini ikiwemo mshtuko wa Moyo.

Mbali ya kua ni Moyo hua ni wenye nguvu za umeme zenye asili ya mawimbi ya sumaku
lakini pia hua ni wenye kusababisha uzalishwaji wa kemikali ambazo husababisha hisia
nzuri kwa Ibn Adam zikiwemo zile zinazojulikana kama Dopamine,Oxytocin,
Endorphines, Seratonin, n.k ambazo hua na jukumu la kukamilisha sifa ya maumbile ya
asili ya kila mtu yanayotokana na maana ya neno Al Ins.

Neno Al Ins linatokana na neno Anisa ambalo maana yake hua ni kua na Mazoea,
Kupenda, Kua na Umoja kijamii, au Kushikamana pamoja.

Hivyo Mtu ameitwa Insan kwa Lugha ya Kiarabu kwa sababu neno hilo hua linamaanisha
Kiumbe ambae Maumbile ya mwili wake yana sifa ya kuzalisha kemikali za Dopamine
na Oxytocin zinazosimamia hisia za Mapenzi, Matamanio, Mshikamano, Kusaidiana,
Kuhurumiana, n.k baina ya Mke na Mume, Baba na Mama, Kaka na Dada, Ndugu na
Familia, n.k kulingana na uhusiano wa hali ya hisia hizo zinazosababishwa kuzalishwa
kutokana na nguvu na uwezo wa Moyo na pia Ubongo wa Ibn Adam.

Kwani tunapozungumzia Oxytocin basi hua tunazungumzia kemikali ambazo kimaarufu


hua zinajulikana kama kemikali za ‘Mapenzi na Uaminifu’ na huzalishwa ndani ya miili
yetu baada ya kupatikana hisia zinazotokana na ufanyaji kazi wa viungo vya hisia za
Mwili za Kuona, Kusikia Sauti, Kuhisi Harufu au Kugusana na hivyo hutupelekea kua
na hali ya kujisikia kua na Raha, Upendo, Utulivu, Usalama, Amani pale tunapokua
karibu na wale tunaowapenda na hivyo kutuzidishia hisia za kutotaka kukosana au
kuachana na watu hao na kuwapenda, kuwajali, kuwafanyia ukarimu na kuwaonea
huruma.

Kemikali za Oxytocin pia hua ndizo zinazosimamia jukumu la kuvitayarisha viungo vya
mwili wa Mwanamme na Mwanamke katika kuingiliana kimwili, kwa ajili ya kuendeleza
vizazi na pia kwa ajili ya kuupa utulivu na kuupumzisha mwili kwa kuupa hisia za Raha
inayotokana na kitendo cha kuingiliana kimwili, ambayo hutegemeana na wingi wa
uzalishwaji wa Oxytocin kwani kila zinavyozidi kuzalishwa kwa wingi zaidi katika
wakati wa tendo hilo basi ndio inavyozidi kupatikana hisia za Raha ambayo haina mfano
wake katika tendo hilo kama anavyoelezea Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu
Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali pale aliposema kua:
‘Raha ya mda mfupi inayopatikana katika kuingiliana kimwili basi hua ni Raha
80

ambayo kamwe haiwezi kufananishwa na Raha nyengine, na kama ingekua ni yenye


kudumu basi ingekua ni moja kati ya dalili ya moja kati ya Raha za Milele
tulizoahidiwa Peponi’

Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn
Muhammad Al Ghazali anatufafanulia zaidi pale aliposema: ‘Hikma ya Allah Subhanah wa
Ta’ala na Rehma zake zinaonekana pale unapoangalia katika kuweka Matamanio ya aina
aina mbili katika Maisha yetu. Matamanio ya kwanza ni ya muonekano wa kimaisha wa nje
pale mtu anapokua anaendeleza kizazi chake kupitia kwa watoto wake. Na muonekano wa
pili ni wa muonekano wa kimaisha ya ndani unaohusiana na maisha ya baadae kesho
Akhera. Kwani raha ya kuingiliana kimwili hua si yenye kudumu katika ulimwengu huu na
ni lazima iwe ni ya mda mfupi, na yenye kikomo kwa kumalizika mara tu baada ya kuihisi
raha hio kiasi ya kua humpelekea Ibn Adam kua na hamu ya kutaka raha hio iwe ni yenye
kudumu, na hivyo hii humfanya Ibn Adam kua ni mwenye kudumu katika Mema kiibada
ambayo yatampelekea kupata Raha kama hizo milele.’

Allah Subhanah wa Ta’ala anaelezea Miujiza ya ufanyaji kazi wa Oxytocin katika


maumbile yetu ambazo kuzalishwa kwake kunasababishwa na Moyo na Ubongo na
kutusababishia kua na hali ya Upendo na Utulivu baina yetu katika maisha yetu
aliposema:

‫آ�ﺗِِﻪ أَ ْن َﺧﻠَ َﻖ ﻟَ ُﻜﻢ ِّﻣ ْﻦ أَﻧ ُﻔ ِﺴ ُﻜ ْﻢ أ َْزَواﺟﺎً ﻟِّﺘَ ْﺴ ُﻜﻨُـ ۤﻮاْ إِﻟَْﻴـ َﻬﺎ َو َﺟ َﻌ َﻞ ﺑَـْﻴـﻨَ ُﻜﻢ‬ ِ
َ ‫﴿ َوﻣ ْﻦ‬
﴾‫ت ﻟَِّﻘﻮٍم ﻳَـﺘَـ َﻔ ﱠﻜﺮو َن‬ ٍ َ‫ﻚ‬ ِ ِ
َ َ ‫ﱠﻣ َﻮﱠد ًة َوَر ْﲪَﺔً إ ﱠن ِﰱ ٰذﻟ‬
ُ ْ �‫ﻵ‬
Wamin ayatihi an khalaqa lakum min anfusikum azwajan litaskunoo ilayha
wajaAAala baynakum mawaddatan warahmatan inna fee Dhalika laayatin
liqawmin yatafakkaroona (Surat Rum 30:21)

Tafsir: Na miongoni mwa alama zake ni kukuumbieni wake kwa ajili yenu kutoka
miongoni mwenu, ili mpate utulivu pamoja nao, na akakuwekeeni baina yenu mapenzi
na rehma. Kwa hakika katika hili kuna dalili kwa wale wenye kutafakkar.
Aya inatuwekea wazi kua: ‘Miongoni mwa Dalili za Utukufu, Uwezo na Rehma
kubwa za Allah Subhanah wa Ta’ala juu yetu ni kutujaalia Ibn Adam kua wa aina
moja lakini hapo hapo kua ni wenye maumbile mawili tofauti baina yetu kwani
kuna umbo la kijinsia ya Kiume na jinsia ya Kike, ambapo mbali ya kua kuna
utofauti wa Muonekano mzuri na wa kuvutia wa Umbo la nje baina ya jinsia mbili
hizo lakini pia kuna utofauti wa maumbile ya ndani ya miili katika mifumo ya
kiufanyaji kazi, kuanzia katika mfumo wa Hisia, Ufaham, Akili, Uzazi n.k.
81

Tofauti zote hizo za kimaumbile ni kwa ajili ya kutufanya kua ni wenye kuendana,
kuvaana, kutegemeana katika kutimiziana mahitaji ya kimwili na hivyo kua ni
wenye kupata utulivu wa nafsi zetu unaopatikana kutoka ndani ya uhusiano
unaokubalika kisharia na Allah Subhanah wa Ta’ala baina ya jinsia mbili hizo za
Kiume na Kike kwa ajili ya kuendeleza kizazi na pia kuistarehesha miili yetu na
akili zetu na hivyo ndani ya uhusiano huo kupatikana Furaha, Mapenzi, Huruma
na kutakiana mema baina ya Mume na Mke.’
Kwa upande mwengine basi, kemikali za Oxytocin zinapozalishwa na kuachiwa ndani ya
mwili wa Mwanamke basi hua pia ni zenye kuzidisha mtetemeko wa kizazi cha
mwanamke na hivyo kurahisisha manii ya Mwanamme kulifikia yai la Mwanamke na pia
hua ni zenye kuutayarisha mwili wa Mwanamke pale anapotaka kujifungua na kupelekea
kutanuka kwa njia ya Uzazi pale Mtoto anapotaka kuzaliwa na pia ndio zenye
kusababisha utayarishaji wa Maziwa baada ya mtoto kuzaliwa na kua tayari kwa ajili ya
kunyonya maziwa.
Ama kwa upande wa Dopamine basi inapozalishwa hua ni yenye kutupelekea kua na
hamu, ari maamuzi ya kutekeleza na kutimiza mahitaji yetu kijamii na matamanio yetu
kimaumbile na kihisia na hivyo hua inajulikana pia kama kemikali inayochangia
kuchochea kupatikana kwa hisia za kujisikia raha na hivyo kutupeleka kutaka kuongeza
bidii zaidi juu ya jambo lililotupa raha au manufaa na hivyo kua ni wenye kuridhika
kutokana na kutimiza malengo, mahitaji na matamanio yetu. Dopamine pia hua na
jukumu la kuhifadhi kumbukumbu ndani ya Ubongo, kusababisha umakini wa mtu katika
jambo husika, n.k

Hivyo basi Dopamine na Oxytocin hua ni zenye kufanya kazi pamoja sambamba ili
kuimarisha mshikamno wa uhusiano baina ya Mume na Mke, Kifamilia na Kijamii, n.k
kiasi ya kua Dopamine inapokosekana au inapokua imezalishwa kidogo basi hata kama
Oxytocin itazalishwe kwa wingi peke yake haitowezi kusababisha mshikamano huo
unaotakiwa kupatikana ili kua na ukaribu baina yetu na pia inapokosekana Oxytocin basi
Dopamine peke yake haiwezi kusababisha mshikamano huo.

Kwa upande wa Seratonin basi hua ni zenye kumfanya mtu kuuona Umuhimu na thamani
yake katika jamii au familia husika, hivyo Seratonin inapokua haijazalishwa mwilini basi
mtu husika hua ni mweye kujisikia mpweke na mwenye huzuni, mfano mtu
unaposhukuriwa baada ya kufanya jambo fulani basi shukrani hio husababishia
uzalishwaji wa Seratonin katika mwili na kumfanya mhusika awe ni mwenye kuridhika
kuona kua ni mwenye thamani na kukubalika, kwa sababu shukrani hua ni hali ya hisia
ya Moyo kuonesha kukubali thamani ya jambo jema ulilofanyiwa kutoka ndani ya moyo
wa mtu uliemfanyia wema huo.
82

Hivyo ushirikiano baina ya kemikali hizi za Oxytocin, Dopamine, Seratonin n.k ambazo
kuzalishwa kwake kunategemeana na mfumo wa ufanyaji kazi wa Moyo basi ndio
unaopelekea kuwepo kwa maingiliano ya watu na mshikamano katika Kifamilia na
Kijamii na hivyo huwapelekea watu unapowakosea kusema: ‘Ah unanitia uchungu
ndani ya Moyo!’ au unapowaambia maneno Qawlan Sadida basi husema ‘Maneno yako
yananigusa ndani ya Moyo!’ au ‘Hakika Mimi nampenda fulani kwa Moyo wangu
wote’ n.k.

Hivyo ukweli ni kua Ibn Adam hua anautaja Moyo pale anapoathiriwa sana na kitu fulani
na hii ni kwa sababu kama kuhisi basi kabla ya kuhisi kwa ufahamu wa akili na Ubongo
basi kiungo kinachohisi kwanza hua ni Moyo, yaani hali ya hisia husika huanzia kwenye
Macho, au Masikio ambayo hupeleka habari kwenye Ubongo ambapo Ubongo nao
hutuma habari kwenye Moyo kisha Moyo hutoa maamuzi sahih juu ya jambo husika kwa
aidha kuzidisha kasi au kuyawacha katika hali yake ya kawaida mapigo ya Moyo na
sambamba hapo hapo Moyo hutoa habari zinazopelekea kuzalisha kemikali na
zinazosababisha mwili wa Ibn Adam kuchukua hatua stahiki kwa ajili ya jambo husika,
iwe kulia, kucheka, kupenda, kuchukia, kupigana, kukimbia, n.k.

Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi anasema kua: ‘Al Qalb na Fuad
vinahifadhiwa ndani ya Sadr, hivyo Fuad inajumuisha Moyo mzima ambao
unajumuisha mishipa ya damu. Hivyo Qalb hua ni sehemu ambayo ndio kiti cha
hisia mbali mbali za upendo, chuki, hasira, ufahamu, n.k.’

Kwa upande mwengine basi tunaona kua Al Qalb yaani Moyo pia hua ni wenye uwezo
wa kuhifadhi hisia hizo na kukumbuka ndani yake tena kwa mda mrefu pia kama vile
ilivyokua kwa upande wa Ubongo, Na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala
akatuelezea katika aya ifuatayo kwa kutuambia kua:

﴾‫ﻮب‬ ِ ِ‫ٱﻪﻠﻟِ أَﻻَ ﺑِ ِﺬ ْﻛ ِﺮ ﱠ‬


‫ﻳﻦ َآﻣﻨُﻮاْ َوﺗَﻄْ َﻤﺌِ ﱡﻦ ﻗُـﻠُﻮﺑـُ ُﻬ ْﻢ ﺑِ ِﺬ ْﻛ ِﺮ ﱠ‬ ِ ‫﴿ٱﻟﱠ‬
ُ ُ‫ٱﻪﻠﻟ ﺗَﻄْ َﻤﺌ ﱡﻦ ٱﻟْ ُﻘﻠ‬ َ ‫ﺬ‬
Alladheena amanoo watatma-innu quloobuhum bidhikri Allahi ala bidhikri Allahi
tatma-innu alquloobu (Surat Ar Rad 13:28)

Tafsir: Wale wenye kuamini, na ambao nyoyo zao zinapata utulivu kutokana na
kumkumbuka Allah. Kwani ni katika kumkumbuka Allah ndio Nyoyo hupata utulivu.

Aya hii imekiambatanisha kiungo cha Moyo wa Ibn Adam na Hisia za Kufaham na
Kukumbuka kwani, imetumia maneno mawili ambayo ni Al Qalb liliopo katika hali ya
wingi ambalo ni Qulubu na kisha ikatumia neno Dhikri lenye kumaanisha Kukumbuka,
Kuhifadhi au kuweka kwenye Ufahamu, Kuonya, Kusifu, Kutukuza n.k hivyo aya
83

inaweka wazi Maumbile ya hali ya Utulivu unaopatikana ndani ya Moyo na Ufahamu


wake kutokana na Moyo husika kua na kumbukumbu ya kumkumbuka Allah Subhanah
wa Ta’ala. Na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akasema tena kumwambia Mtume
wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:

۞‫ﻚ َﳍَُﻮ ٱﻟْ َﻌ ِﺰ ُﻳﺰ ٱﻟﱠﺮِﺣ ُﻴﻢ‬ ِِ ِ


َ ‫ﲔ۞ َوإِ ﱠن َرﺑﱠ‬َ ‫ﻚَ ﻵﻳَﺔً َوَﻣﺎ َﻛﺎ َن أَ ْﻛﺜَـُﺮُﻫﻢ ﱡﻣ ْﺆﻣﻨ‬ َ ‫﴿إِ ﱠن ِﰱ ٰذﻟ‬
‫ﻚ ﻟِﺘَ ُﻜﻮ َن ِﻣ َﻦ‬ َ ِ‫ﲔ۞ َﻋﻠَ ٰﻰ ﻗَـﻠْﺒ‬ ِ
ُ ‫وح ٱﻷَﻣ‬
ِِ
ُ ‫ﲔ۞ ﻧَـَﺰَل ﺑﻪ ٱﻟﱡﺮ‬
ِ
ِّ ‫ﻳﻞ َر‬
َ ‫ب ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬ ِ ِ
ُ ‫َوإﻧﱠﻪُ ﻟَﺘَﻨﺰ‬
﴾ ‫ﲔ۞ وإِﻧﱠﻪ ﻟَ ِﻔﻰ زﺑ ِﺮ ٱﻷَﱠوﻟِﲔ‬ ٍ ‫ٱﻟْﻤْﻨ ِﺬ ِرﻳﻦ۞ ﺑِﻠِﺴ‬
َ ُُ ُ َ ٍ ِ‫ﰊ ﱡﻣﺒ‬ ٍِّ‫ﺎن َﻋَﺮ‬ َ َ ُ
Wa-inna rabbaka lahuwa alAAazeezu alrraheemu, Wa-innahu latanzeelu rabbi
alAAalameena; Nazala bihi alrroohu al-ameenu; AAala qalbika litakoona mina
almundhireena; Bilisanin AAarabiyyin mubeenin; Wa-innahu lafee zuburi al-
awwaleena; (Surat Shu-ara 26: 191-196)

Tafsir: Na kwa hakika Mola wako ni Mwenye uwezo Mkubwa na ni Mwingi wa Rehma,
Na ka hakika hii (Qur’an)ni teremsho kutoka kwa Mola wa Ulimwengu wote.
Imeteremshwa kupitia kwa Ruhi Al Amiin (Malaika Jibril), Kwenye Moyo wako (Ewe
Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) Ili uwe ni mwenye kuonya. Kupitia katika
Lugha ya Kiarabu iliyowazi kabisa. Na Hii (Qur’an) imo ndani ya maandiko
(Zaburi, Tawrat na Injil) yaliyotangulia.

Hivyo kutajwa kwa Moyo katika ayah hii kua Qur’an imeteremshwa na kua ni kama
iliyogongwa muhuri kwenye Moyo wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ili isitoke,
kunatilia mkazo umuhimu wa kiungo hicho cha Al Qalb katika kuhifadhi kumbukumbu
kwake, kiasi ya kua aya imetoa kipaumbele zaidi kwa Ufahamu wa Moyo kuliko kwa
Ufahamu wa Ubongo na Akili.

Wanasayansi wamethibitisha haya ya kua Moyo unahifadhi kumbukumbu pale


walipofanya upasuaji wa upandikizaji wa Moyo uliofanyika mnamo mwaka 1988 nchini
Marekani kwa mgonjwa wa Moyo aitwae Claire Sylvia ambae alipandikizwa Moyo na
kisha baadae aliandika kitabu kinachoitwa A Change of a Heart ambacho ndani yake
anaelezea yaliyomkuta baada ya upandikizwaji wake huo wa Moyo kua alianza kupenda
kunywa vilevi na vyakula visivyokua na lishe na mambo mengine mengi ambayo
yanayopendwa kufanya na vijana walio tofauti na rika lake, kwani yeye alikua ni mtu
mzima anaekarbia miaka 45-50 hivyo alikua hapendi kuyafanya mambo ya ujana ambayo
keshayapita tayari kabla ya kufanyiwa upadikizaji huo wa Moyo, yaani alibadilika tabia
zake zote. Na kufikia wakati ikawa anaota wazi wazi kua ana uhusiano wa kimapenzi na
kijana mdogo kwake kiumri wa Kiume aitwae Tim Lamirande. Claire alikua akihisi hisia
84

za mapenzi makubwa sana juu ya kijana huyu ambae hata hivyo alikua hamjui wala
hajawahi kumuona katika maisha yake, kwani yeye alikua akimuona ndotoni tu.

Hivyo Claire akaamua kufanya uchunguzi ambapo akagundua kua Moyo wake
aliopandikizwa ulikua ni wa Mtu aliekwisha fariki ambae alikua akijulikana kwa jina la
Timothy Lamirade. Alipofuatilia kwa kina na kukutana na wazazi wa Tim basi
alithibitisha kua kijana huyo ndie aliekua akimuona ndotoni pale alipooneshwa picha ya
Tim na wazee wake, na wazee nao wakathibitisha kua Tim ambae alifarikia akiwa na
umri wa miaka 18 alikua ni mwenye kupenda vilevi na vyakula vyote ambavyo Claire
alikua havipendi lakini akaanza kuvipenda baada ya kupandikizwa Moyo wa Tim.

Mfano mwengine ni wa Mwanamme aitwae Sony Grahham wa Marekani pia ambae nae
baada ya kupandikizwa Moyo wa mtu mwengine basi akaanza kua na hisia za mapenzi
na Mwanamke aitwae Cheryl ambae alikua ni Mjane wa Mtu ambae alifariki baada ya
kujiua kwa kujipiga risasi na hivyo Moyo wake ukapandikizwa kwa Sony ambae alikua
na matatizo ya Moyo wake. Baada ya kupandikizwa na kutoka hospitali basi Sony
akamuoa Cheryl, ndoa ambayo ilidumu kwa miaka 12 kisha baada ya hapo, Sony akajiua
kwa kujipiga risasi kama alivyofanya yule mume wa mwanzo wa Cheryl ambae Moyo
wake ulipandikizwa kwa Sony.

Vile vile kuna mfano wa Professor wa Marekani aitwae Benjamin ambae nae alikua na
matatizo ya Moyo na mara tu baada ya kubadilishwa Moyo wake nakufanyiwa
uandikizaji basi akawa ni mweye kuota ndoto zenye kutisha, kwani alikua anaota kua
anapigwa na Radi ambayo inamuunguza na kufikia kuuhisi ujuoto wa moto wake.
Professor Benjamin hakumwambia mtu yeyote juu ya ndoto hii isipokua Mke wake,
ambae nao akamuelezea Mke wa alietolewa Moyo huo baada ya kufariki kwake, na hivyo
Mke huyo akashtuka na akathibitisha kua mume wake alipigwa na Radi na baada ya
kupigwa na radi hio basi alifariki hapo hapo.

Ingawa huo ni mtizamo wa Kisayansi juu ya moyo na Maumbile yake tunapozungumzia


kuhusiana na Maumbile ya Moyo, lakini tunaporudi katika mtizamo wa I’lm ya Dini ya
Kiislam kupitia katika aya za Qurán basi tunaona kua: Mujaddid ad Din Hujjat ul Islami
Imam Abu Hamid Ibn Muhammad Ibn Muhmmad Al Ghazali katika Ihya Ulum Ad Din
kua: ‘Al Qalb una sifa ya Latifah (Ni wenye uwezo na Sifa ya Kuona na Kufaham
mambo ambayo hayako wazi) na Rabbaniyyah (Utukufu wa Kimungu) na Kiroho
na ndio asili ya Ibn Adam. Al Qalb katika mwili wa Ibn Adam hua ni kiungo
kinachofaham, kinachotafakkari, kinachozingatia, kinachozungumziwa pale
unapozungumza na mtu, ndicho kinachoadhibu, ndicho kinacholaumu na ndio
kinachobeba Majukumu yote ya Ibn Adam. Al Qalb ni kama Mfalme wa mwili na
viungo vyengine ni kama Askari na wasaidizi’
85

Imam al Ghazali anaendelea kusema kua: ‘Heshima na Utukufu wa Ibn Adam, ambao
unawapita Viumbe wote walioumbwa na Allah Subhanah wa Taála unatokana na
Kumjua Allah Subhanah wa Taála, Al Qalb ni ndio unaojumuisha Ubora, Ukamilifu
na Uzuri wa Ibn Adam katika Ulimwengu huu na Malipo yake yatakayokuwepo
katika Ulimwengu unaofuatia. Ibn Adam Amejaaliwa kufaham na Kupata I’lm hii
kupitia kwa Moyo wake tu, na wala sika kwa kutumia Viungo vyengine vyote
vilivyabakia. Kwani ni Moyo ndio unaomjua Allah, Unaofanya kazi kwa ajili ya
Allah, Unaojitahidi kwa ajili ya Allah, Unaomkaribia Allah, na kuweka wazi kile
inachokiona mbele ya Allah. Na viungo vyake vyote vya Ibn Adam vilivyobakia hua
ni wafuasi, watumwa na vifaa ambavyo Moyo huvitumia na kuviajiri.

Kwani ni Moyo unaokubaliwa na Allah ndio unaokua uko huru dhidi ya kila kitu
isipokua Allah Subhanah wa Taála, Moyo huwekewa pazia usimuone Allah
Subhnaha wa Taála pale Moyo huo unapokua umejaa kila kitu zaidi ya Allah, Al
Qalb ni ule ambao Mtu akiujua Moyo wake basi hua ameijua Nafsi yake na akiijua
Nafsi yake basi hu ni alimjua Mola Wake. Moyo ndio ule ambao Mtu asipoujua
Moyo wake, basi hatoijua Nafsi yake na hivyo hatomjua Mola wake. Hivyo I’lm ya
kuyajua maumbile ya Moyo na sifa zake ndio mzizi wa Dini na ndio msingi wa njia
ya yule mwenye kutamfuta Mola wake.’

Wenye kua na Ilm hio ya kumjua Mola wao ndio wale wanaoelezewa katika Aya
ifuatayo:

ِ ٍ ِ‫ﺐ ﱡﻣﻨ‬ ِ
َ ‫ﻮﻫﺎ ﺑِ َﺴﻼٍَم ٰذﻟ‬
‫ﻚ ﻳـَ ْﻮُم‬ َ ُ‫ﻴﺐ۞ ْٱد ُﺧﻠ‬ ٍ ‫ﺐ و َﺟﺂء ﺑَِﻘ ْﻠ‬
ِ ِ
َ َ ‫ﱠﻣ ْﻦ َﺧﺸ َﻰ ٱﻟﱠﺮ ْﲪَـٰ َﻦ ﺑﭑﻟْﻐَْﻴ‬
﴿
ِ ُ‫ٱ ُﳋﻠ‬
﴾‫ﻮد‬
ُ
Man khashiya alrrahmana bialghaybi wajaa biqalbin muneebin; Odkhulooha
bisalamin dhalika yawmu alkhuloodi (Surat Qaf 50:33-34)

Tafsir: Yule ambae anamuogopa mwingi wa Rehma katika Ulmwengu wa Ghayb, na


akaja na Moyo wenye kujirudia katika kufaya Toba. Wataambiwa: ‘Ingia ndani yake
kwa usalama, kwani hiya ni maisha ya Milele’

Watu hawa hua ni wenye kumuogopa Mola wao, wanapokua faragha hapa Duniani na
wanapokua mbele za watu pia, kabla ya hata hawajawa mbele ya Mola wao kesho
Akhera, ambapo hua wanamuogopa Mola wao kutokana na Rehma zake zaidi ya kitu
86

chochote, kiasi ya kua mbali ya kua ni mwenye kumjua Mola wake kutokana na Rehma
zake lakini hata hivyo hua si mwenye kufanya dhambi. Bila ya Shaka katika haya kuna
mafunzo mengi kwa kila mwenye Moyo wenye kutaka kuzingatia na hivyo ndivyo yenye
kusema aya ifuatayo:

﴾‫ﺐ أ َْو أَﻟْ َﻘﻰ ٱﻟ ﱠﺴ ْﻤ َﻊ وُﻫﻮ َﺷ ِﻬﻴ ٌﺪ‬ ‫ﻠ‬


ْ ‫ـ‬
َ‫ﻗ‬ ‫ﻪ‬ ‫ﻟ‬
َ ‫ن‬
َ ‫ﺎ‬‫ﻛ‬َ ‫ﻦ‬ ‫ﻤ‬ِ‫﴿إِ ﱠن ِﰱ ٰذﻟِﻚ ﻟَ ِﺬ ْﻛﺮ ٰى ﻟ‬
َ َ ٌ ُ َ َ َ
Inna fee dhalika ladhikra liman kana lahu qalbun aw alqa alssamAAa wahuwa
shaheedun (Surat Qaf 50:37)

Tafsir: Kwa Hakika katika haya kuna ukumbusho kwa yule mwenye Moyo na akatoa
sikio lake kwa kusikiliza huku akiwa ni mwenye kushuhudia.

Kulingana na ufafanuzi huo basi ndio tunaona uzito na umuhimu wa majukumu ya Al


Qalb yaani Moyo pale Qurán ilipokua ikizungumzia siku ya Malipo siku ambayo
hakitomfaa kitu chake isipokua Qalbin Saliimin kwa kusema:

﴾‫ﺐ َﺳﻠِﻴﻢ‬
ٍ ‫ٱﻪﻠﻟَ ﺑَِﻘ ْﻠ‬
‫ﺎل َوﻻَ ﺑـَﻨُﻮ َن۞ إِﻻﱠ َﻣ ْﻦ أَﺗَﻰ ﱠ‬
ٌ ‫﴿ﻳَـ ْﻮَم ﻻَ ﻳَﻨ َﻔ ُﻊ َﻣ‬
Yawma la yanfaAAu malun wala banoona; Illa man ata Allaha biqalbin saleemin
(Surat Ash Shuara 26:88-89)

Tafsir: Katika siku ambayo haitomfaa mtu Mali wala watoto wake, Isipokua yule
atakaempa Allah Moyo ulio Salama.

Ama kuhusiana na aya hii basi anasema Sultan Al Balagha Imam Al Zamakhshari na pia
Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua, Qalbin Saliimin maana yake
hua ni Moyo ambao uko Salima yaani umejiweka huru na Kumshirikisha Allah Subhanah
wa Ta’ala na hivyo ukawa Aslama yaani na ukawa Salama, na ukawa Salama yaani
ukapata Usalama kutokana na Nyoyo za viumbe wengine, na Moyo huo uka Istaslama
yaani ukajisalimisha kwa Allah.

Ama kwa upande wa Allamah Raghib Al Isfahani basi yeye anasema kua: Al Qalb hua
na maana ya Kugeuza kitu juu chini, au kukizungusha kitu, kama vile ambavyo
mtu unavyoigeuza Nguo, au unapogeukia upande mwengine tofauti na ule
87

ulioelekea. Hivyo maana yake hujumuisha hali ya kugeuka geuka, na ndio maana
Qurán inatumia neno Inqalib kumaanisha wale watu ambao wamegeuza muelekeo
wao, au waliokimbia kutoka katika uwanja wa vita, au hutumika kama jina
kumaanisha kitendo cha kupindua, na pia hutumika kumaanisha kwa mtu kurudi
tena kwa Allah Subhanah wa Ta’ala yaani baada ya kufariki kwa mtu huyo.

Allamah Raghib Al Isfahani anaendelea kufafanua kwa kusema kua: Jina hili la Al Qalb
hutumiwa kumaanisha Moyo wa Ibn Adam kwa sababu ya kua na maumbile ya
kugeuka geuka kila mara, au kama tunavyosema kua mtu yupo katika hali ya
mabadiliko ya Moyo pale anapokua anabadilika kihisia, kimtizamo, kimaamuzi.
Neno lenyewe Al Qalb, hua pia linajumuisha Nafsi, I’lm, Ushujaa, n.k.

Lakini hata hivyo Al Qalb hua si sawa na Ufahamu, bali Al Qalb mara nyingi hua
unajumuishwa na Ufahamu kama vile ambavyo unavyojumuishwa Mto wa maji
usiotembea, wakati ukweli ni kua ni Maji ya Mto ndio yanayotembea, lakini
kutembea huko hua kunajumuishwa na Mto kwa sababu Mto ndio wenye Maji.

Allah Subhanah wa Ta’ala ametumia maneno Nuqallibu af-ida pale aliposema:

‫ﺼ َﺎرُﻫ ْﻢ َﻛ َﻤﺎ َﱂْ ﻳـُ ْﺆِﻣﻨُﻮاْ ﺑِِﻪ أَﱠوَل َﻣﱠﺮةٍ َوﻧَ َﺬ ُرُﻫ ْﻢ ِﰱ ﻃُ ْﻐﻴَﺎ�ِِ ْﻢ‬ ِ ِّ‫﴿وﻧـُ َﻘﻠ‬
َ ْ‫ﺐ أَﻓْﺌ َﺪﺗَـ ُﻬ ْﻢ َوأَﺑ‬
ُ َ
﴾‫ﻳَـ ْﻌﻤ ُﻬﻮ َن‬
َ
Wanuqallibu af-idatahum waabsarahum kama lam yu/minoo bihi awwala marratin
wanadharuhum fee tughyanihim yaAAmahoona (Surat Al Anaam 6:110)

Tafsir: Na tutazigeuza Nyoyo zao na Macho yao (mbali na uongofu), kwani wamekataa
kuukubali kwa mara ya kwanza, na tutawaachia katika kupita kwao wakiwa na upofu.

Hivyo hapa Allah Subhanah wa Ta’ala ametumia neno Nuqallibu Af-ida ambapo
kutokana na mtizamo mwengine basi hua tunaona kua jina jengine la Moyo hua ni Fuad.
88

AL FUAD

Neno Fuad linatokana na neno Fa’ada ambalo kwa Kiarabu hua linamaanisha Kuumizwa
Moyoni, Kupigwa Moyoni, Kuumwa na Moyo. Mbali ya kua neno Fa’ada limetoa neno
Fu’ad lakini pia neno hili ndio pia lililotoa neno Af’idah ambalo humaanisha Moyo au
Ufahamu.

Allamah Al-Raghib Al Isfahani anasema kua Al Fuad hua moja kwa moja linamaanisha
Qalb, likiwa na utofauti wa kua Moyo unaitwa Fuad kwa sababu ya kua pia na Maumbile
ya kua ni wenye kua na hisia ya kuripuka moto, kwani Fuad linatokana na kuoka Moto
nyama kwenye jiko au mkaa yaani juu ya Moto uwakao, kama mishikaki ambapo nyama
hio baada ya kuiva hua ni yenye kuitwa Faiid. Hivyo Moyo huitwa Fuad kwa ajili ya
kuainisha kwa kiasi gani mripuko wa Moyo wa mtu hua na uwezo wa kuathiri mambo
mengi katika maisha yake Ibn Adam.

Wakati Moto unapowaka ripuripu basi hua ni sawa na Moyo unapojaa jazba na hivyo
ndani yake hua na hisia za kutokua na utulivu na kuongezeka kwa mapigo yake na
hamasa, hali hii inawekwa wazi katika aya ya Qurán iliyotumia majina yote mawili ya
Moyo ambayo ni Qalb na Fuad pale Allah Subhanah wa Ta’ala anapotuelezea kisa cha
Nabii Musa baada ya Nabii Musa kutumbukizwa mtoni na kuokotwa na Asia bint
Muzahim Mke wa Fir’awn na kukabidhiwa mama yake Nabii Musa ili amnyonyeshe,
kwa kusema:

ۤ
‫ت ﻟَﺘُـْﺒ ِﺪى ﺑِِﻪ ﻟَ ْﻮﻻ أَن ﱠرﺑَﻄْﻨَﺎ َﻋﻠَ ٰﻰ ﻗَـ ْﻠﺒِ َﻬﺎ‬
ْ ‫ﻮﺳ ٰﻰ ﻓَﺎ ِرﻏﺎً إِن َﻛ َﺎد‬ ِ ْ ‫﴿ َوأ‬
َ ‫َﺻﺒَ َﺢ ﻓُـ َﺆ ُاد أ ُّم ُﻣ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ ِ
َ ‫ﻟﺘَ ُﻜﻮ َن ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬
Waasbaha fu-adu ommi moosa farighan in kadat latubdee bihi lawla an rabatna
AAala qalbiha litakoona mina almu/mineena (Surat Al Qasas 28:10)

Tafsir: Na ukawa mtupu (usiokua na mawazo yeyote isipokua mawazo juu ya Musa)
Moyo wa Mama yake Musa. Kiasi ya kua alikua tayari kuiweka wazi Siri yake (kua
Musa ni Mtoto wake) kama si sisi kuuthibitishia Moyo wake (kwa Iman), ili apate kua
ni miongoni mwa Walioamini.
89

Al Fuad pia hua unaitwa ni ufuniko wa hisia ulio juu ya Al Qalb, na hivyo kumaanisha
kua Al Qalb uko ndani zaidi na una umaalum zaidi kuliko sehemu ya juu ya Al Fuad.
Ingawa huu ni mtizamo wa Kilugha tu, lakini Wanazuoni wa U’lum ul Qurán wanasema
kua Al Fuad hua ni sehemu inayopatikana ndani zaidi ya Moyo kuliko Al Qalb kwani hio
ndio sehemu ambayo Nuru ya I’lm ya kumjua Allah Subhanah wa Taála huanzia na ndio
maana Allah Subhanah wa Taála akasema katika Qurán kua:

َ ِ‫ﺼَﺮ َوٱﻟْ ُﻔ َﺆ َاد ُﻛ ﱡﻞ أُوﻟـٰﺌ‬


ُ‫ﻚ َﻛﺎ َن َﻋْﻨﻪ‬
ِ ِ َ َ‫﴿وﻻَ ﺗَـ ْﻘﻒ ﻣﺎ ﻟَﻴﺲ ﻟ‬
َ َ‫ﻚ ﺑِﻪ ﻋ ْﻠ ٌﻢ إِ ﱠن ٱﻟ ﱠﺴ ْﻤ َﻊ َوٱﻟْﺒ‬ َ ْ َ ُ َ
﴾ً‫َﻣﺴ ُﺆوﻻ‬
ْ
Wala taqfu ma laysa laka bihi AAilmun inna alssamAAa waalbasara waalfu-ada
kullu ola-ika kana AAanhu mas-oolan (Surat Al Isra 17:36)

Tafsir: Na Msifuate kile ambacho hamkijui. Kwani bila ya shaka ya Macho, Masikio
na Nyoyo kila kimoja juu yake mtaulizwa.

Hivyo kwa kua Al Fuad ndio sehemu inayoanzia hisia mbali mbali ikiwemo Nuru ya Ilm
ya kumjua Allah Subhanah wa Taála huanzia basi bila ya shaka ndio tutakayoulizwa juu
ya namna tulivyoutumia, na hivyo hatutoulizwa juu ya Al Qalb, Al Sadr wala Al Lubb.

AL LUBB

Neno Al Lubb linatokana na neno la Kiarabu Labba ambalo hua ni lenye kumaanisha
Kujaaliwa kua na ufahamu wa kina, Moyo wenye huruma. Neno Labba ndio lililotoa pia
neno Albabun ambalo hua na maana ya Moyo, Sehemu ya kati kati ya kitu, Kiini au
Ufahamu wa Kitu, Sehemu ya kitu isiyokua na Doa wala Dosari yeyote, Moyo wa Ibn
Adam au wa Tunda kama vile Moyo wa Nanasi au Fenesi.

Hivyo neno Lubb ambalo wingi wake hua Albaab ambalo humaanisha ufahamu msafi
usiokua na dosari, Al Lubb pia humaanisha aina ya ufahamu ambao ni wenye kuona kitu
kwa kina au kwa mtizamo wa ndani kabisa ya Moyo. Na ukweli ni kua sehemu ya Al
Lubb ndio inayokaa Nuru ya Allah Subhanah wa Taála ndani ya Moyo wa Ibn Adam,
ambapo Ibn Adam mwenye Moyo wenye Nuru hio basi hua ni mtu asiekua na mapenzi
ya kitu chochote ndani ya Moyo wake isipokua mapenzi ya Allah Subhanah wa Ta’ala
90

pekee na hivyo hua na darja ya juu kabisa miongoni mwa Viumbe kiasi ya kua Viumbe
wote hua chini yake, wakiwemo Majini na Malaika.

Hivyo kila Lubb hua ni Ufahamu lakini si kila Ufahamu hufikia darja au uwezo wa
kufahamu wa Lubb na ndio maana Allah Subhanah wa Taála akasema katika Quran kua:

‫اﳊِ ْﻜ َﻤﺔَ ﻓَـ َﻘ ْﺪ أُوﺗِﻰ َﺧ ْﲑاً َﻛﺜِﲑاً َوَﻣﺎ ﻳَ ﱠﺬ ﱠﻛُﺮ إِﻻﱠ‬


ْ ‫ت‬
َ ‫ﺆ‬ْ ‫ـ‬
ُ ‫ﻳ‬ ‫ﻦ‬‫ﻣ‬َ‫و‬َ ‫ﺂء‬
ُ ‫ﺸ‬َ ‫ﻳ‬
َ ‫ﻦ‬‫ﻣ‬َ ‫ﺔ‬
َ ‫ﻤ‬
َ ‫ﻜ‬
ْ ِ‫اﳊ‬
ْ ‫ﻰ‬ِ‫﴿ﻳـﺆﺗ‬
ُّ
َ
﴾‫ﺎب‬ ِ ‫أُوﻟُﻮاْ ٱﻷَﻟْﺒ‬
َ ْ
Yu/tee alhikmata man yashao waman yu/ta alhikmata faqad ootiya khayran
katheeran wama yadhdhakkaru illa oloo al-albabi (Surat Al Baqara 2:269)

Tafsir: Humpa hikma yule amtakae, na yule anepewa hikma nae, basi kwa hakika hua
ni mwenye kupewa Kheri nyingi sana, na hawatokumbuka isipokua ulu albaab.

Kutokana na kua na maana hiyo basi ndio maana Allah Subhanah wa Taála akatumia
neno Ulu al Baab mara kadhaa katika Qurán ili kuweka wazi wale Waumini ambao wana
ufahamu mkubwa wa Kiakili, Kihisia na Kiimani, na hivyo kua ni wenye kujua, kuona
na kuhisi alama za Allah Subhanah wa Ta’ala na katika kila kitu na katika kila jambbo.
Sehemu ya hali ya Moyo ya Al Lubb hua ni sehemu ambayo ina utulivu wa hali ya juu na
hivyo hua haina miripuko kama ya Al Fuad wala uwepezi wa Al Qalb na pia ni tofauti na
Al Sadr.

AL SADR

Neno Sadara kwa Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Kurudi, Kuendelea Mbele, Kupita,
Kutokea, Kufikia, au Kupiga Kifua. Neno Sadara ndio lililotoa neno Sadrun ambalo
humaanisha Kifua, Sehemu ya juu ya mwili, Ufaham, Moyo. Na pia likatoa neno Sudur
ambalo maana yake hua ni Nyoyo au Vifua.
91

‫ﱠﺎس ﻗَ ْﺪ َﺟﺂءَﺗْ ُﻜ ْﻢ ﱠﻣ ْﻮ ِﻋﻈَﺔٌ ِّﻣﻦ ﱠرﺑِّ ُﻜ ْﻢ َو ِﺷ َﻔﺂءٌ ﻟِّ َﻤﺎ ِﰱ ٱﻟ ﱡ‬


‫ﺼ ُﺪوِر َوُﻫ ًﺪى‬ ُ ‫ٰ�َﻳـﱡ َﻬﺎ ٱﻟﻨ‬
﴿
﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ
َ ‫َوَر ْﲪَﺔٌ ﻟّْﻠ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬
Ya ayyuha alnnasu qad jaatkum mawAAidhatun min rabbikum washifaon lima fee
alssudoori wahudan warahmatun lilmu/mineena (Surat Yunus 10:57)

Tafsir: Enyi Watu! Hakika yamekujieni Mawaidha kutoka kwa Mola wenu, na ponyo
kwa yaliyomo ndani ya vifua vyenu. Muongozo na Rehma kwa Waumini.

Allah Subhanah wa Ta’ala anapozungumzia kuhusiana na Al Sadr basi hua anamaanisha


Moyo kuanzia nje yake hadi ndani kwenye kiini chake yaani Al Sadr hua unajumuisha
Ufahamu na Nguvu za uwezo wa Moyo katika kubeba hisia mbali mbali na kama
tunavyoona katika mfano wa aya iliyo hapo juu. Na ndio maana pale Allah Subhana wa
Ta’ala alipozungumzia kisa cha Nabii Musa katika Qurán basi anatuambia kua:

﴾‫ﺻ ْﺪ ِري‬ ِّ ‫ﺎل َر‬


َ ‫ب ٱ ْﺷَﺮ ْح ِﱃ‬ َ َ‫﴿ﻗ‬
Qala rabbi ishrah lee sadree (Surat Ta-Ha 20:25)

Tafsir: Akasema (Musa) Ewe Mola wangu nifunulie Moyo wangu kwa ajili yangu.

Aya inatuwekea wazi kua baada ya Nabii Musa kufahamu kua anataka kubebeshwa
mzigo mkubwa na mzito wa kueneza ujumbe wa Mola wake basi akajua kua atahitaji kua
na kifua kikubwa chenye ustahmilivu wa kubeba siri na kudhibiti hisia tofauti ikiwemo
hasira, huruma n.k yaani Al Sadr hua ni kama Sanduku ambalo ndani yake mna vitu
vilivyofichwa na pia kupingana na vishawishi vinavyotokana na minong’onezo ya
Shaytani kama vile iliyotumika katika aya ifuatayo:

ِ ‫﴿ٱﻟﱠ‬
﴾‫ﱠﺎس‬ ُ ‫س ِﰱ‬
ِ ‫ﺻ ُﺪوِر ٱﻟﻨ‬ ِ
‫ﻮ‬
ُ َ‫ﺳ‬
ْ ‫ﻮ‬ُ‫ـ‬‫ﻳ‬ ‫ى‬‫ﺬ‬
Alladhee yuwaswisu fee sudoori alnnasi (Surat Nas 114:5)
92

Tafsir: Yule ambae anaenong’oneza ndani ya Nyoyo za Watu.

Shaytan kamwe hawezi kuinong’oneza Qulub bali hua ni mwenye kuinong’oneza Al


Sadr, kwa sababu Allah Subhanah wa Taála ameuumba Al Qalb kua ni kitu kitukufu na
kisafi kabisa, yaani hapa tunaona kua mfano wa Al Qalb kua kama sanduku lenye hazina
ndani yake, lakini pia ni kama Ngome ambayo huwezi kuifikia hadi kwa kupitia katika
njia za viungo vyengine vya Mwili kama Macho, Masikio, Ulimi n.k ambazo ni miongoni
tu mwa Neema nyingi zisizohesabika za Allah Subhanah wa Taála juu yetu ambazo mara
nyingi tunakumbushwa katika Qur’an ikiwemo katika aya ifuatayo:

‫ٱﻪﻠﻟِ َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ َوِﻣﻴﺜَﺎﻗَﻪُ ٱﻟﱠ ِﺬى َواﺛـَ َﻘ ُﻜﻢ ﺑِِﻪ إِ ْذ ﻗُـ ْﻠﺘُ ْﻢ َِﲰ ْﻌﻨَﺎ َوأَﻃَ ْﻌﻨَﺎ‬
‫﴿ َوٱذْ ُﻛُﺮواْ ﻧِ ْﻌ َﻤﺔَ ﱠ‬
﴾‫ﺼ ُﺪوِر‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻋﻠِﻴﻢ ﺑِ َﺬ‬ ِ ‫وٱﺗﱠـ ُﻘﻮاْ ﱠ‬
‫ات ٱﻟ ﱡ‬ ٌ َ َ‫ٱﻪﻠﻟَ إ ﱠن ﱠ‬ َ
Waodhkuroo niAAmata Allahi AAalaykum wameethaqahu alladhee wathaqakum
bihi idh qultum samiAAna waataAAna waittaqoo Allaha inna Allaha AAaleemun
bidhati alssudoori (Surat Al Maidah 5:7)

Tafsir: Na kumbukeni Neema za Allah juu yenu, na makubaliano yake ambayo


mlikubaliana nae, pale mliposema: Tumesikia na Tunatii. Na Mcheni Allah kwani
kwa hakika Allah ni mwenye kujua yaliyomo ndani ya vifua.

Hivyo kutokana na Rehma zake Allah Subhanah wa Taa’la juu yetu basi hakumjaalia
Iblis kua ni mwenye uwezo wa kuingia ndani ya Qulub zetu, bali amemjaalia kua na
uwezo wa kuingia ndani ya Sudur, na hivyo ni sisi Ibn Adam kutokana na ujinga, kutojali
na kukosa shukrani kwa Mola wetu basi ndio tunajiachia na hivyo kumpa nafasi Iblis
kuingia ndani ya Qulub zetu kwa kupitia kwenye Sudur na kujaribu kutupotosha kwa
kupingana na Makubaliano tuliyokubaliana na Mola wetu, hili ni kosa ambalo kila mmoja
wetu ataenda kuulizwa juu yake kwani Allah Subhanah wa Taála anatuambia kua:

ِ ِ ِ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ َﻏ ِﲏ ﻋﻨ ُﻜﻢ وﻻَ ﻳـﺮ‬


َ ‫ﺿ ٰﻰ ﻟﻌﺒَﺎدﻩ ٱﻟْ ُﻜ ْﻔَﺮ َوإِن ﺗَ ْﺸ ُﻜُﺮواْ ﻳَـْﺮ‬
ُ‫ﺿﻪ‬ َ َْ َ ْ َ ‫﴿إِن ﺗَ ْﻜ ُﻔُﺮواْ ﻓَِﺈ ﱠن ﱠَ ﱞ‬
‫ُﺧَﺮ ٰى ﰒُﱠ إِ َ ٰﱃ َرﺑِّ ُﻜ ْﻢ ﱠﻣْﺮِﺟﻌُ ُﻜ ْـﻢ ﻓَـﻴُـﻨَـﺒِّﺌُ ُﻜ ْـﻢ ِﲟَﺎ ُﻛﻨﺘُ ْﻢ ﺗَـ ْﻌ َﻤﻠُﻮ َن‬
ْ ‫ﻟَ ُﻜ ْﻢ َوﻻَ ﺗَ ِﺰُر َوا ِزَرةٌ ِوْزَر أ‬
﴾‫ﺼ ُﺪوِر‬ ‫ات ٱﻟ ﱡ‬ ِ ‫إِﻧﱠﻪ ﻋﻠِﻴﻢ ﺑِ َﺬ‬
ٌ َُ
93

In takfuroo fa-inna Allaha ghaniyyun AAankum wala yardha liAAibadihi alkufra


wa-in tashkuroo yardhahu lakum wala taziru waziratun wizra okhra thumma ila
rabbikum marjiAAukum fayunabbi-okum bima kuntum taAAmaloona innahu
AAaleemun bidhati alssudoori (Surat Az Zumar 39:7)

Tafsir: Na kama mkikufuru, basi kwa hakika Allah si mwenye kuhitaji kitu kutoka
kwenu, na haridhii kufuru kutoka kwa Waja wake, na kama mkimshukuru basi
atakuridhieni. Hakuna mwenye mzigo atakaebeba mzigo wa mwenzake. Hivyo kwa
Mola wenu ndio marejeo yenu ambapo atakuambieni mliyokua mkiyafanya. Kwani
yeye ni mwenye kujua yale yaliyomo ndani ya Sudur.

Hivyo Moyo ndio wenye uuwezo wa kuchagua baina ya jema na ovu, jambo lililo sahih
na lisilo sahih kwa sababu kiungo hicho ndio makao makuu ya ufahamu wa Ibn Adam.

Hujjat ul Islami Imam Abu Hamid Ibn Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al
Ghazali anasema kua: ‘Ingawa Moyo, Akili, Roho na Nafsi hua ni vitu vyenye maana
tofauti, lakini viungo hivi vyote kwa pamoja ndivyo vinavyowakilisha kile ambacho
kinachojulikana kama Viungo muhimu visivyoonekana vyenye uwezo mkubwa wa
Ibn Adam aliopewa na Allah Subhanah wa Ta’ala, kwani hivi ndivyo
vinavyoyapadisha darja Maumbile ya Ibn Adam na kumtofautisha yeye na Viumbe
wengine’.
Na ndio maana kukawa kuna makubaliano ya Ijmaa juu ya utukufu, ukubwa na darja ya
Amali zinazofanywa na Moyo hua ziko juu zaidi kulingana na zile zinazofanywa na
kiwiliwili. Hivyo kuna umuhimu wa Ibn Adam kujisalimisha kwa Allah Subhanah wa
Taála kwa kutumia Nyoyo zao, Kumuamini Mola wao kwa kutumia Akili zao na kufanya
Ibada kwa kutumia Miili yao.

Anasema Imam Mahammad Ibn Abd Allah Ibn Sahl Al Tustari kua: ‘Fahamu kua Allah
Subhanah wa Taála alipotaka kuiweka wazi Ilm ya kujulikana kwake basi aliiweka
Ilm hio ndani ya Aql, kisha akaweka sharti kua hakuna Ibn Adam yeyote
atakaeweza kuifikia Ilm hio kwa njia yeyote ile isipokua kwa njia ya kutumia Aql,
Hivyo mtu yeyote yule alienyimwa Aql basi hua pia ni alienyiwa Ilm. Na kua na Aql
basi ni kua na Husn Al Nadhar (Hikma) mtazamo bora ya kujidhibiti juu ya kila
unachokifanya kwa ajili yako na kwa ajili ya Mola wako.’

Na kwa mtizamo huo basi tunaona kua Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al
Tustari anatufafanulia kua maumbile ya ndani ya Ibn Adam yanajumuisha hali ya
Kimaumbile ya Nafsi, Al Qalb, Aql na Al Ruh kama alivyosema katika maana ya aya
ifuatayo:
ِ ‫﴿ﻓَﭑﻟْﻤ ْﻠ ِﻘﻴ‬
﴾ً‫ﺎت ِذ ْﻛﺮا‬َ ُ
94

Faalmulqiyati Dhikran (Surat Al Mursalat 77:05)

Tafsir: Na kwa Malaika Wanaoshusha Ukumbusho.

Ambapo ayah inazungumzia Ujumbe wa Qurán na kwa mtizamo wa Imam Abu


Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari basi tunaona anasema kua: Hii Qurán ni
Wahy, unaopita katika njia ya Ilham, ambayo inajumuisha Nafs Al Ruh, Aql na Qalb
na kuwekwa juu ya Nafsi ya Maumbile. Na hii hua ndio njia ya Dhikr al Khafiy
(Ukumbusho uliyofichikana).

Kwaini Allah Subhanah wa Ta’ala amesema katika Qur’an kua:

ِ ِ ِ ِ ‫﴿ﻓَ َﻤﻦ ﻳُِﺮِد ﱠ‬


َ ‫ﺻ ْﺪ َرﻩُ ﻟ ِﻺ ْﺳﻼَم َوَﻣﻦ ﻳُِﺮْد أَن ﻳُﻀﻠﱠﻪُ َْﳚ َﻌ ْﻞ‬
ُ‫ﺻ ْﺪ َرﻩ‬ َ ‫ٱﻪﻠﻟُ أَن ﻳَـ ْﻬﺪﻳَﻪُ ﻳَ ْﺸَﺮ ْح‬
ِ‫ﱠ‬ ِ ‫ﺼﻌﱠﺪ ِﰱ ٱﻟ ﱠﺴﻤ‬
ِ‫ﺂء َﻛ ٰﺬﻟ‬
َ‫ﻳﻦ ﻻ‬ َ ‫ﺲ َﻋﻠَﻰ ٱﻟﺬ‬ ‫ﺟ‬
ْ
َ ّ
ِ ُ‫ٱﻪﻠﻟ‬
‫ٱﻟﺮ‬ ‫ﱠ‬ ‫ﻞ‬
ُ ‫ﻌ‬
َ ‫ﳚ‬
ْ َ ‫ﻚ‬
َ َ ُ ‫ﺿﻴِّﻘﺎً َﺣَﺮﺟﺎً َﻛﺄَﱠﳕَﺎ ﻳَ ﱠ‬َ
﴾‫ﻳـُ ْﺆِﻣﻨُﻮ َن‬
Faman yuridi Allahu an yahdiyahu yashrah sadrahu lil-islami waman yurid an
yudhillahu yajAAal sadrahu dhayyiqan harajan kaannama yassaAAAAadu fee
alssama-i kadhalika yajAAalu Allahu alrrijsa AAala alladheena la yu/minoona
(Surat Al An Aam 6:125)

Tafsir: Ama kwa yule ambae Allah hutaka kumuogoza basi humfungulia kifua chake
kwa ajili ya Uislam, na kwa yule ambae hutaka kumdhalilisha basi humfungia kifua
chake na kua ni chenye kubana kama kwamba ni mwenye kupanda juu kuelekea
Angani. Hivyo ndivyo Allah anavyotoa adhabu kwa wale ambao hawakuamini.

Anasema Imam Muhammad Ibn Jarir Al Tabari Al Shafii kuhusiana na aya hii kua Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliulizwa: ‘Jee Moyo hufunguka vipi kwa ajili ya
Uislam?’ hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akajibu: ‘Ni Nuru ya Allah
Subhanah wa Ta’ala ndio inayoingizwa ndani ya Nyoyo za Ibn Adam, hivyo Moyo
hua ni wenye kutulia na kufunguka.’

Na ingawa aya imetumia neno Harajan ambalo hua ni lenye kumanisha: Kubana kwa
matawi ya mti kiasi ya kua sehemu ya matawi hayo yaliyobanana haiwezi kufikika
na mtu wala na mnyama, lakini kwa upande wa Sayyidna Umar Ibn Al Khattab Radhi
Allahu Anhu alipoambiwa juu ya maana hiyo na mabedui ambao wao ni wataalamu
wakubwa wa lugha ya Kiarabu, basi Sayyidna Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu
95

akasema: ‘Huo hua ni Mfano wa Nyoyo za Wanafiq, kwani kamwe hakuna jema
linaloweza kuingia ndani ya Nyoyo zao.’

Na anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘Allah
Subhanah wa Ta’ala ametofautisha baina ya Murid (Mja anaemtafuta Mola wake)
na Murad (Mja anaetafutwa na Mola wake) ijapokua Waja wawili hawa wote ni
kutoka kwake yeye mwenyewe Allah Subhanah wa Ta’ala. Lakini yeye Allah
Subhaah wa Ta’ala ni mwenye kutofautisha baina ya Khusus (Wenye sifa hususan
maalum) na Umum (Wenye sifa ya Ujumla) na hivyo kawatofautisha wale Murad
(wanaotafutwa na Allah Subhanah wa Ta’ala) katika ayah hii na nyenginezo’

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari anaendelea kutufafanulia kwa
kusema kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala hua ni mwenye kuziangalia Nyoyo, zote
kwani nyoyo hua ziko mbele yake, hivyo anapoona Moyo fulani una unyenyekevu
juu yake basi huujalia jema atakalo juu yake Moyo huo, Kisha baada ya hapo
hufuata Nyoyo zenye kubadilika haraka na kurudi kwake yeye Allah Subhanah wa
Ta’ala. Hizo ni aina mbili za Nyoyo anazozijaalia mema.’

Na kisha Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari akasema: ‘Kila wakati
Allah anapouangalia Moyo na akauona kua ni wenye kua na hamu ya Ulimwengu
huu, basi huuchukia Moyo huo na kuchukia kwake huko, hua kunajionesha kupitia
katika kuuwachia Moyo huo pamoja na Nafsi ya Mtu huyo. Kwani Moyo
haumilikiwi na yeyote isipokua Allah Subhanah wa Ta’ala, na hivyo hautakiwi
kumtii yeyote isipokua Allah Subhanah wa Ta’ala. Hivyo kama ukiwa unaujali
Moyo wako basi Mfanye Mola wako awe ndie msiri wako.’

Hivyo kama vile ambavyo Quran ilivyotumia maneno Qalb, Fuad, Lubb na Sadr
kumaanisha Moyo basi pia tunapoiangalia neno Aql yaani Akili basi tunaona kua Qurán
imeitaja sehemu ya kiungo hiki katika hali tofauti lakini kimaana kuenda sambamba na
hali za Hijr, Hilm, Nuha na Balu.


MAANA YA AQL, HIJR, HILM, NNUHA NA BALU.

Neno Aql linatokana na neno Aqala la Kiarabu ambalo hua ni lenye kumaanisha.
Kufunga, Kuzuia, Kua na Busara, Kufahamu, Kulipia Fidya Mtu fulani. Kupanda juu ya
Kilele cha Mlima na pia hua ni lenye kumaanisha Kutumuia Ufahamu au Akili.
96

Ingawa kuna tofauti kimaandishi na kimatamshi lakini Quran ilipozungumzia Ufahamu


basi imetumia maneno kadhaa yenye kuenda sambamba kimaana na neno Aql, miongoni
mwao ikiwemo neno Naha ambalo hua ni lenye kumaanisha Kujizuia au Kufaham,
ambapo tunaona kua hali nyengine ya neno hili ni ile hali ya Nuhyatun ambayo hua ni
yenye kumaanisha kile kinachomzuia Ibn Adam kutovuka mipaka na kutofanya mambo
yasiyoingia akilini. Neno Nuha limetumika katika Qurán pale iliposema:

ِ ِ ‫﴿أَﻓَـﻠَﻢ ﻳـﻬ ِﺪ َﳍﻢ َﻛﻢ أَﻫﻠَ ْﻜﻨَﺎ ﻗَـﺒـﻠَﻬﻢ ِﻣﻦ ٱﻟْ ُﻘﺮ‬
َ ‫ون ﳝَْ ُﺸﻮ َن ِﰱ َﻣ َﺴﺎﻛِﻨِ ِﻬ ْﻢ إِ ﱠن ِﰱ ٰذﻟ‬
‫ﻚ‬ ُ َّ ُْ ْ ْ ْ ُْ ْ َ ْ
﴾‫ﱡﻬ ٰﻰ‬ ِ ٍ
َ ‫َﻵ َ�ت ﻷُْوِﱃ ٱﻟﻨـ‬
Afalam yahdi lahum kam ahlakna qablahum mina alqurooni yamshoona fee
masakinihim inna fee dhalika laayatin li-olee alnnuha (Surat Ta-Ha 20:128)

Tafsir: Jee si Muongozo kwao wao (Kujua) kua tumeviangamiza vizazi vingapi kabla
yao. Ambavyo wao wanatembea juu ya makazi yao? Hakika katika haya kuna mafunzo
kwa waliopewa Nnuha (Ufaham).

Quran imetumia pia neno Ahlam ambalo linatokana na neno Halama lenye kumaanisha
Ndoto, Muono na pia hua linamaanisha Ustahmilivu. Neno Ahlam hua pia linamaanisha
Kupea Kiufaham na maana hii inaonekana wazi pale Allah Subhanah wa Ta’ala ilipohoji
juu ya Makafiri kua na ufahamu wa kutafakkari, kutokana na kukanusha kwao lakini
hapo hapo kua na ufahamu tu si hoja bali hoja ni kua na ufahamu uliopea kwani huo ndio
ambao unamsababisha mtu kua na uwezo wa Kutafakari kwa kina na ndio maana Allah
Subhanah wa Ta’ala akauliza:

﴾‫َﺣﻼَ ُﻣ ُﻬﻢ ِﻬﺑـَٰ َﺬآ أ َْم ُﻫﻢ ﻗَـﻮٌم ﻃَﺎﻏُﻮ َن‬ ﴿


ْ ْ ْ ْ ‫أ َْم َﺄﺗْ ُﻣُﺮُﻫ ْﻢ أ‬
Am ta/muruhum ahlamuhum bihadha am hum qawmun taghoona (Surat AT Tur
52:32)

Tafsir: Jee Ahlamuhum (Ufahamu wao) ndio unawaamrisha (kukuzulia ewe


Muhammad) au wao ni watu wanaopenda kuvuka mipaka?

Hivyo bila ya shaka ni kua ufahamu wao watu hao ambao ni Makafiri unaonesha kua
umepea lakini hata hivyo wanafanya hivyo kwa sababu ya kua na Kibri tu kutokana na
maumbile ya baadhi ya Ibn Adam wanapoona kua katika hali ya kua ni wenye
kujitosheleza ambayo hua ni sawa na ile hali inayoelezewa na aya ifuatayo:
97

﴾‫ٱﺳﺘَـ ْﻐ َ ٰﲎ‬ ِ ِ ﴿
َ ‫َﻛﻼﱠ إ ﱠن ٱﻹ‬
ْ ُ‫ﻧﺴﺎ َن ﻟَﻴَﻄْﻐَ ٰﻰ۞ أَن ﱠرآﻩ‬
Kalla inna al-insana layatgha; An raahu istaghna (Surat Al Alaq 96:6-7)

Tafsir: Hakika Ibn Adam hua ni mwenye kuvuka mipaka. Anapojiona kua
anajitosheleza.

Ama kuhusiana na jambo hili la kutotumia Ahlam kutokana na kua na Kibri basi mwisho
wake hua majuto katika siku ya Malipo kama inavyoweka wazi hivyo Quran kwa
kusema:

﴾‫ﺎب ٱﻟ ﱠﺴﻌِ ِﲑ‬


ِ ‫َﺻﺤ‬ ‫أ‬ ۤ ِ ‫﴿وﻗﺎﻟُﻮاْ ﻟَﻮ ﻛﻨﱠﺎ ﻧﺴﻤﻊ أَو ﻧـﻌ ِﻘﻞ ﻣﺎ ﻛﻨﱠﺎ‬
‫ﰲ‬
َ ْ ُ َ ُ َْ ْ ُ َ ْ َ ُ ْ ََ
Waqaloo law kunna nasmaAAu aw naAAqilu ma kunna fee as-habi alssaAAeeri
(Surat Al Mulk 67:10)
Tafsir: Na wao watasema: ‘Lau kama tungesikiliza au tungetumia akili zetu, basi
kamwe tusingekua ni miongoni mwa watu wa Motoni’

Mbali ya kua Neno Hajara ambalo ndio asili ya neno Hijra, lenye kumaanisha Kuhama
na ndio maana ambayo wengi sana ni wenye kuijua kutokana na tukio la Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam kuhama kutoka katika Mji wa Makkah na kuhamia katika Mji
wa Madina, ambapo ndani ya tukio hili basi mna mafuzo mengi ikiwemo lile la Umuhimu
wa Nia katika kila Jambo analolifanya Muislam, kwani amesema Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam kua:

‘Ama kwa hakika Amali Hutegemeana na Nia, na Kwa Hakika Kila mtu atalipwa
Kulingana na Nia yake, Hivyo yeyote Yule aliefanya Hijra kwa Ajili ya Kidunia au
kwa ajili ya Mwanamke Basi Hijra yake hua ni kwa Ajili ya alichokifanyia
Hijra’(Sahih Bukhari)

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliyasema maneno ya Hadith hii kwa
ajili ya kuainisha Umuhimu wa Nia katika Kila Jambo. Na tunapoangalia hadith basi
tunaona kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anazungumzia Hijra kisha ndani
yake akainisha aina za Nia na Madhumuni ya Hijra.

Kwani katika Wakati huo, na hadi katika wakati wa leo pia Kuna watu hua ni wenye
Kufanya Hijra kwa ajili ya Dini yao, na kuna wanaofanya Hijra kwa ajili ya Dunia yao.
Na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kuhusiana na Wanawake kwa sababu
98

kuna Watu walifanya Hijra ya kutoka Makkah kuelekea katika Mji wa Madina si kwa
sababu ya Dini yao wala si kwa sababu ya Mola wao na Mtume wake basi kwa sababu
tu ya Kusikia kua katika Mji wa Madina kuna Wanawake wazuri zaid kuliko Wanawake
wa Makkah.

Ambapo kwa upande mwengine basi anasema Imam Maaruf Al Kharki kua: ‘Kila
kinapotokea Kitendo kinachofanywa na Ibn Adam basi hua ni chenye kutokana na
Nia Ndani yake, Hivyo Kama Nia ni Sahih basi na Kitendo hua Sahih. Na kama Nia
si Sahih basi na Kitendo hia si Sahih

Ambapo Nia Sahih juu ya Kitendo Sahih hua katika hali 3 zifuatazo;

1-Kama ikiwa Nia juu ya Kitendo Husika hua ni yenye kutokana na Kumuogopa
Allah Subhanah wa Ta'ala. Basi Kitendo hicho hua ni sawa na kufanya Ibada kwa
Mja huyo mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala.

2-Kama ikiwa Nia Juu ya Kitendo Hua ni yenye kutokana na Kuikimbilia Pepo ya
Allah Subhanah wa Ta'ala. Basi Kitendo hicho hua ni sawa na kufanya Biashara
kwa Mja huyo mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala. kwa ajili ya Akhera yake.

3-Kama ikiwa Nia juu ya Kitendo hicho hua ni yenye kutokana na Kuona aibu kwa
Mja Mbele ya Mola wake, na hivyo hua ni kutekeleza Wajibu wake na kuonesha
Shukrani kwa Mja huyo mbele ya Mola wake. Basi Kitendo hicho hua ni sawa na
Ibada ya Mtu mwenye Kujikomboa na Kutaka kujitafutia Uhuru unaotokana na
kua na uzito wa Majukumu yake mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala.’

Naam, Inasikitisha kuona kua wengi wetu pia leo hii hua tunafanya Ibada zetu nyingi
huku tukiwa na nia ya hali ya 3 yaani kwa sababu tu ya kujipunguzia Uzito wa
Majukumu.

Yaani kwa Mfano: Watu Wanafanya Ibada fulani kwa sababu tu ya Kumrishwa Na
Muumba kufanya Ibada hio, bila kutilia maanani kua kufanya kwao Ibada husika mbali
ya kua ni Jukumu lao lakini hua ni kwa ajili ya Manufaa yao wao wenyewe.

Na hivyo hatufanyi Vitendo kwa ajili ya Nia ya Aina ya kwanza yaani kwa Ikhlasi au
kwa ajili ya Nia ya Aina ya pili yaani kujitolea kufanya Bishara na Allah Subhanah wa
Ta’ala kwa ajili ya kuwekeza katika Akhera yetu, na hivyo kutokua ni wenye kufanya
Ibada kwa Kutumia Hisia na Ufaham juu ya kile tunachokifanya, na hii ndio maana
nyengine ya Hijr.

Kwani pia neno Hajara ndio asili ya neno Hijrun ambalo maana yake hua ni Kua na hisia
na Ufaham, mfano wa matumizi wa maana hii ni katika aya ifuatayo:
99

﴾‫ﻚ ﻗَﺴﻢ ﻟِّ ِﺬى ِﺣ ْﺠ ٍﺮ‬ِ ِ ﴿


ٌ َ َ ‫َﻫ ْﻞ ﰱ ٰذﻟ‬
Hal fee dhalika qasamun lidhee hijrin (Surat Al Fajr 89:5)

Tafsir: Hakika katika hayo mna vithibitisho kwa wale wenye Hijrin (Ufahamu).

Na tumalizie kwa kuangalia neno Balun ambalo nalo ni linaloenda sambamba kimaana
na neno Aql neno hili limetumika katika Qurán kumaanisha Moyo, Akili, Ufahamu, Nia
au Hali ya Ufahamu, Mawazo, Mtizamo au Jambo muhimu sana, miongoni mwa aya
zilizotumia neno hili ni pamoja na:

ِ َ َ‫ﻮل ﻗ‬ ُ ‫ﻚ ٱﺋْـﺘُ ِﻮﱏ ﺑِِﻪ ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ َﺟﺂءَﻩُ ٱﻟﱠﺮ ُﺳ‬ ِ َ َ‫﴿وﻗ‬
‫ﺎﺳﺄَﻟْﻪُ َﻣﺎ َﺎﺑ ُل‬ َ ِّ‫ﺎل ْٱرﺟ ْﻊ إِ َ ٰﱃ َرﺑ‬
ْ َ‫ﻚ ﻓ‬ ُ ‫ﺎل ٱﻟْ َﻤﻠ‬ َ
﴾‫ٱﻟﻨِّﺴﻮةِ ٱﻟﻼﱠﺗِﻰ ﻗَﻄﱠ ْﻌﻦ أَﻳْ ِﺪﻳَـ ُﻬ ﱠﻦ إِ ﱠن رِّﰉ ﺑِ َﻜْﻴ ِﺪ ِﻫ ﱠﻦ َﻋﻠِﻴﻢ‬
ٌ َ َ َْ
Waqala almaliku i/toonee bihi falamma jaahu alrrasoolu qala irjiAA ila rabbika
fais-alhu ma balu alnniswati allatee qattaAAna aydiyahunna inna rabbee
bikaydihinna AAaleemun (Surat Yusuf 12:50).

Tafsir: Na akasema Mfalme: ‘Mleteni mbele yangu’. Lakini Wajumbe hao walipofika
mbele yake (Yusuf) basi akasema: ‘Rudini kwa bwana wenu na mmuulize: ‘Ni ipi hali
ya ufahamu wao wale Wanawake waliojikata viganja vyao?’ Hakika Mola wangu ni
mwenye kujua juu ya hila zao’

Ambapo aya hio Nabii Yusuf anauliza juu ya hali ya Akili, Ufahamu, Mawazo au
Mtizamo wa wale Wanawake waliompelekea yeye kua ni mwenye kuenda Jela bila ya
kua na makosa. Jee wametafakkar na kuona kua wao ndio wenye makosa? Jee Ufahamu
wao utakubali kua wao ndio wenye makosa? n.k.

Na mfano mwengine ni pale Firáwn alipomwambia Nabii Musa kama inavyoelezewa:

﴾‫ُوﱃ‬ ِ ‫ﺎل ﻓَﻤﺎ ﺎﺑ ُل ٱﻟْ ُﻘﺮ‬


ٰ َ ‫ون ٱﻷ‬ ﴿
ُ َ َ َ َ‫ﻗ‬
Qala fama balu alqurooni al-oola (Surat Ta-Ha 20:51)

Tafsir: Akasema (Firáwn): ‘Jee ni ni hali yao wale waliotangulia kabla yetu?’
100

Yaani Fir’awn anamhoji Nabii Musa kua kama kweli kuna Mungu, alieumba kila kitu na
kukipa muongozo, kwa nini watu hao basi hawakumuabudu Mola wao? Ufahamu wao
na akili zao ilikuaje ukawakoseshea uongofu? Jee walikua hawana Akili na Ufahamu?
Ina maana wameangamia au vipi?

Hivyo ukweli ni kua Qurán inazungumzia mambo mengi sana ambayo bila ya kufuatilia
basi hua ni yenye kuonekana kua ni ya kawaida, na ni pale tu tutakapoyafuatilia, na
kuyatafakkari basi ndipo tutakaponufaika na kupata Baraka zilizomo ndani yake, kwani
vyenginevyo basi tutakua ni miongoni mwa walioingia katika hali ya Sakara.

Neno Sakara kwa lugha ya Kiarabu kwa upande mmoja hua ni lenye maana sawa na neno
Aql ambayo ni Kuzuia, Kufunga, Kudhibiti, Kua katika hali ya kujilinda, n.k. Lakini kwa
upande mwengine wa kimaana basi neno Sakara hua ni lenye kupingana kimaana na neno
Aql, kwani tumeona kua Aql hua inamanisha kua na Akili, Kua na Ufahamu na pia kua
ni mweye Kutumia Akili wakati neno Sakara huani lenye kukanusha mtu kua na Ufaham,
yaani kua katika hali ya Kua ni kizingiti baina ya mtu na Ufahamu wake, Raha kubwa
sana au Maumivu Makali sana yanayotoa Akili, Kutokua na Ufahamu, Kutokua na Akili,
Kulaaniwa kiakili au Kulewa.

Anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘Sakara hua ni
kitu chochote kile ambacho kinachoilevya Nafsi ya Ibn Adam hapa Duniani na
hivyo kumpelekea Ibn Adam huyo kua ni mwenye kuisahau Akhera yake’

Ndio maana Allah Subhanah wa Taála akatuzindua ili tusimsahau yeye na tusiisahau siku
ya mwisho ya Ulimwengu tunaoishi ambayo watu wataonekana kama wamelewa lakini
hawajalewa kama inavyosema aya ifuatayo:

‫ﺎﻋ ِﺔ َﺷ ْﻲءٌ َﻋ ِﻈ ٌﻴﻢ ۞ ﻳَـ ْﻮَم ﺗَـَﺮْوﻧـَ َﻬﺎ ﺗَ ْﺬ َﻫ ُﻞ‬


َ ‫ﱠﺎس ٱﺗﱠـ ُﻘﻮاْ َرﺑﱠ ُﻜ ْﻢ إِ ﱠن َزﻟَْﺰﻟَﺔَ ٱﻟ ﱠﺴ‬
ُ ‫ٰ�َﻳـﱡ َﻬﺎ ٱﻟﻨ‬
﴿
ِ ٍ
‫ﱠﺎس ُﺳ َﻜ َﺎر ٰى‬ َ ‫ﻀ ُﻊ ُﻛ ﱡﻞ َذات َﲪْ ٍﻞ َﲪْﻠَ َﻬﺎ َوﺗَـَﺮى ٱﻟﻨ‬ َ َ‫ﺖ َوﺗ‬ ْ ‫ﺿ َﻌ‬ َ ‫ُﻛ ﱡﻞ ُﻣْﺮ ِﺿ َﻌﺔ َﻋ ﱠﻤﺂ أ َْر‬
﴾‫ٱﻪﻠﻟِ َﺷ ِﺪﻳ ٌﺪ‬
‫اب ﱠ‬ ِ
َ ‫َوَﻣﺎ ُﻫﻢ ﺑِ ُﺴ َﻜ َﺎر ٰى َوﻟَـٰﻜ ﱠﻦ َﻋ َﺬ‬
Ya ayyuha alnnasu ittaqoo rabbakum inna zalzalata alssaAAati shay-on
AAadheemun; Yawma tarawnaha tadhhalu kullu murdhiAAatin AAamma ardaAAat
watadaAAu kullu dhati hamlin hamlaha watara alnnasa sukara wama hum bisukara
walakinna AAathaba Allahi shadeedun (Surat Al Hajj 22:1-2)
101

Tafsir: Enye Watu! Mcheni Mola wenu! Kwani Mtetemeko wa Ardhi wa Saa (Ya
Kiama) ni kitu kibaya sana. Katika Siku hio mtaona kila Mama anaenyonyesha
atamsahau Mtoto wake anaemnyonyesha, na mwenye Mimba ataiangusha (Itatoka
kwa Hamkani) Mimba yake, na Utawaona watu wakiwa katika hali ya kua ni Sukara
(Waliolewa), lakini hakuna atakaekua ni Sakara (kalewa), na kwa hakika Adhabu ya
Allah ni kali sana.

Naam aya inazungumzia hali itakavyokua katika saa ya mwisho ya Ulimwengu ambayo
itakuja kabla ya Siku ya Kufufuliwa, na ndio maana ikazungumzia juu ya kutoka kwa
Mimba kutokana na hamkani na tafrani zake siku hio, kwani hii ni siku ambayo
Ulimmwengu utabadilika Maumbile yake na hivyo Jua litachomoza kutoka katika
upande wa Magharibi, Mfumo wa Nguvu wa Sayari utakwisha nguvu zake za Mvutano
kutokana na amri ya Mola wake alieuumba na hivyo kua ni wenye kusimama kwa ghafla
moja., Sayari, Nyota na Mwezi zitakosa muelekeo na kuanza kupukutika na hivyo Dunia
itashindwa kutulia kwenye mhimili wake nayo pia itakua ni yenye kutetemeka katika hali
nzito, yenye kasi kubwa isiyokua ya kawaida, na hivyo basi huenda baadhi ya Sayari na
vipande vyake vikaangukia Duniani. Hii ni hali ya hatari sana kwa Ibn Adam na ukweli
ni kua ni hali isiyoelezeka wala kufahamika kiufaham kwa ufahamu wa Ibn Adam kwani
hua ni yenye kuonesha kuwepo kwa Muumba na uwezo wake ambae ni Allah Subhanah
wa Taa’la.

Anasema Imam Musa Ibn Jafar Al Sadiq kua: ‘Lam Yakhaf Allaha Man Lam Yaaqil
Aani Allah – Yeyote yule asiemuogopa Allah Basi Hana Akili au Ufahamu juu ya
Allah.’

Kwa kumalizia juu ya hali za Maumbile na hali za Nyoyo na Akili na Ufahamu wa


Viungo hivyo basi na tuangalie hali hizo kulingana na mtizamo wa Imam Abu Abd Allah
Muhammad Ibn Ali Ibn Hasan Ibn Bashir Al Hakim Al Tirmidhi ambae yeye anasema
katika kitabu chake cha Bayan al Farq Bayn Al Sadr al Al Qalb wa Al Fuad wa Al Lubb
kua:

AL SADR – Ndio Sehemu inayokaa Nuru ya Uislam na pia hujulikana kama Nafs Al
Ammarah.
AL QALB – Ndio Sehemu inayokaa Nuru ya Iman na pia hujulikana kama Nafs Al
Mulhimah.
AL FUAD – Ndio Sehemu inayokaa Nuru ya Maarifah na pia hujulikana kama Nafs Al
Lawwamah.
AL LUBB - Ndio Sehemu inayokaa Nuru ya Tawhid na pia hujulikana kama Nafs Al
Mutma’inah.
102

Huo ni mtizamo wa Imam Al Hakim Al Tirmidhi, hivyo ili kuifahamu zaid basi na
tufafanue hizi aina nne za Nafsi zilizonasibishwa na hali nne za Nyoyo, ambapo tunaona
kua Neno Nafsi limetokana na neno Nafasa ambalo kwa lugha ya Kiarabu hua na maana
ya Kitu chenye Thamani, Katika kuomba, Kuliwaza, Kufurahisha.

NAFSI – MAUMBILE YAKE NA UHIBITI WAKE.



Neno Nafs linatoka na neno Nafasa ambao kwa lugha ya Kiarabu hua ni lenye
kumaanisha Kitu Adimu na chenye Thamani Kubwa sana, kiasi ni hsara kubwa sana
kukitupa au kukipotezana kama ukikipoteza basi bila ya shaka pengo lake hua kamwe
haliwezi kuzibika. Neno Nafasa hua pia ni lenye Kumaanisha Kuliwaza, Kuchangamsha
au Omba.

Subhana Allah! Bila ya shaka lugha ya Kiarabu ni lugha yenye kujitosheleza tena sana,
kwani tuunapoangalia maana ya neno Nafasa ambalo ndio lililotoa neno Nafsi basi neno
hilo moja tu kimaana limebeba Uzito mkubwa sana wa maana ya Nafsi kwa kina na
kutuonesha kua Nafsi ni kitu chenye Thamani kubwa sana na kilicho adimu sana kiasi ya
kua ukikipoteza basi hua umekula hasara kubwa sana na kamwe hutoweza kuliziba pengo
lake.

Neno Nafasa ndio lililotoa neno Nafsun ambalo maana yake hua ni Nafsi, Roho, Uhai,
Mtu alie hai, Ufahamu, Hisia za ndani za matamanio. Na pia neno Nasafa limetoa neno
Nafsi ambalo nalo pia maana yake hua ni Mimi mwenyewe Binafsi, Kitu chenyewe,
Damu, Kanuni za Msingi, Nia au Makusudio, Matamanio, Moyo, n,k

Nafsi hua ni kitu ambacho kimo ndani ya Miili ya Viumbe lakini hakionekani wala
hakikamatiki isipokua kwa Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ndie alietuumba. Hivyo
ingawa Nafsi haikamatiki wala haionekani lakini kimaumbile Nafsi hua inadhibitika na
kiumbe husika mwenye Nafsi hio kwani hua inajumuisha hali ya uhusiano wa ufanyaji
kazi wa hisia zote kamilifu za mwili wa kiumbe kwa kutumia Ufaham, Akili, Moyo na
Ubongo, n.k. Na ndio maana akatuusia Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kusema kua:

‫ﻀﱡﺮﻋﺎً َو ِﺧﻴ َﻔﺔً َوُدو َن ٱ ْﳉَ ْﻬ ِﺮ ِﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻘ ْﻮِل ﺑِﭑﻟْﻐُ ُﺪ ِّو‬ َ ‫ﻚ ِﰱ ﻧَـ ْﻔ ِﺴ‬
َ َ‫ﻚ ﺗ‬ َ ‫﴿ َوٱذْ ُﻛﺮ ﱠرﺑﱠ‬
ِِ ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ٱﻵﺻ ِﺎل َوﻻَ ﺗَ ُﻜ ْﻦ ّﻣ َﻦ ٱﻟْﻐَﺎﻓﻠ‬
َ ‫َو‬
103

Waodhkur rabbaka fee nafsika tadharruAAan wakheefatan wadoona aljahri mina


alqawli bialghuduwwi waal-asali wala takun mina alghafileena (Surat Al Isra 7:205)

Tafsir: Na Mkumbuke Mola wako katika Nafsi yako, kwa Unyenyekevu na kwa Khofu,
bila ya kupaza sauti Asubuhi na Jioni na Usiwe miongoni mwa wenye kughafilika.

Na kisha akatoa onyo juu ya watakaoshindwa kuzidhibiti Nafsi zao, na kuwaahidi wale
watakao weza kuzidhibiti Nafsi zao kwa kusema:

‫ٱﳊَﻴَﺎ َة ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ ۞ ﻓَِﺈ ﱠن ٱ ْﳉَ ِﺤ َﻴﻢ ِﻫ َﻰ ٱﻟْ َﻤﺄْ َو ٰى۞ َوأَﱠﻣﺎ َﻣ ْﻦ‬
ْ ‫﴿ﻓَﺄَﱠﻣﺎ َﻣﻦ ﻃَﻐَ ٰﻰ۞ َوآﺛـََﺮ‬
﴾‫ٱﳉَﻨﱠﺔَ ِﻫﻰ ٱﻟْﻤﺄْو ٰى‬ ِ ِِ
َ َ َ ْ ‫ﺲ َﻋ ِﻦ ٱ ْﳍََﻮ ٰى۞ ﻓَﺈ ﱠن‬ َ ‫ﺎف َﻣ َﻘ َﺎم َرﺑّﻪ َوﻧَـ َﻬﻰ ٱﻟﻨﱠـ ْﻔ‬
َ ‫َﺧ‬
Faamma man tagha; Waathara alhayata alddunya; Fa-inna aljaheema hiya
alma/wa; Waama man khafa maqama rabbihi wanaha alnnafsa AAani alhawa; Fa-
inna aljannata hiya alma/wa (Surat An Naziat 79:37-41)

Tafsir: Ama kwa yule atakaevuka mipaka. Na akawa ni mwenye kupendelea Maisha
ya Dunia, Basi kwa Hakika Motoni ndio yatakapokua makazi yake. Ama kwa yule
atakae kua ni mwenye kua na khofu ya kusimama mbele ya Mola wake na akaizuia
Nafsi yake na Matamanio, Basi kwenye Bustani (Peponi) ndio yatakayokua makazi
yake.

Ili kufahamu zaidi juu ya udhibiti wa Nafsi na hali zake basi na tuangalie mtizamo wa
Sultan al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi ambae anatufafanulia kwa kusema
kua: Kimaumbile Nafsi hua ni kitu kimoja, lakini ni chenye hali nyingi
zinazotofautiana. Nafsi inapokua katika hali yake husika ya juu kabisa basi hua
katika hali ambayo ni yenye kusimamia hali yake hio na kuizidishia nguvu kwa
kuzidisha mwamko wake wa kuendelea kua katika hali husika.

Ama kwa upande wa Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad
Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii basi yeye anatuambia kua:

Kimaumbile Nafsi zimegawika katika aina mbili:-


104

1- Al Nufus Al Sahiha – Yaani Nafsi zenye Afya yake ya kimaumbile na hivyo hua
ni zenye kupeka Wahy na Ilham. Aina hii ya nafsi hua ni zenye kuonesha Miujiza
kwa sababu hua hazishuguliki na matamanio ya Kidunia. Hizi Hua ni Nafsi za
Maitume na Manabii ambao wao hua ni Madaktari wa Nafsi.
2- Al Nufus Al Maridha – Yaani Nafsi zenye maradhi ambazo nazo hua katika darja
tatu zifuatazo:
a) Nafsi zenye Maradhi kutokana na Matamanio ya Kidunia, lakini hua ni zenye
kutibika na kurudi katika hali yake ya kiafya ya kimaumbile kupitia katika
njia ya Kutafuta I’lm, Kutafakkar na Kuzingatia.
b) Nasi zenye Maradhi kutokana na hamu na ushawishi wa kuyakumbatia
Matamanio ya Kidunia na hivyo nafsi hizi hua ni zenye kua na Nuru. Ambayo
hua inaisaidida kuipigania Nafsi hii katika maisha yake yote ili kuirudisha
katika hali yake ya afya ya kimaumbile kwa kupitia katika njia ya I’lm
ambayo hua ni yenye kuyaangamiza Maradhi yaliyoikumba Nafsi hio bila
ya kutegemea.
c) Nafsi zenye Maradhi kutokana na kuharibika kwa hali ya kimaumbile ya nafsi
hio. Nafsi hii hua katika halia ambayo haiwezekani kutibika wala
kurekebishika na kurudi katika hali yake ya kimaumbile.

Wanazuoni wanasema kua Nafsi ziko katika hali 7 tofauti, ambazo ni Nafs al Ammara,
Nafs Al Lawwamah, Nafs Al Mulhimah, Nafs Al Mutma’inah, Nafs ar Radhiyah, Nafs Al
Mardhiyah na Nafs al Kamilah, ambapo kulingana na mtizamo wa Imam Al Hakim Al
Tirmidhi basi zinafafanulika kulingana na mifano ya aya zilizotaja hali za Nafsi, ambapo
kuhusiana nazo basi tayari tumeshazizungumzia kwa kina katika kitabu cha Tafsir ya
Surat Yusuf ambacho kinapatikana pia bure mtandaoni, unachotakiwa ni kutafuta tu jina
Al Mustakshif Abu Manal Danah – Tafsir Surat Yusuf katika Google.

Hivyo kutokana na kuwepo kwa utofauti wa Kimaumbile wa Nafsi za Ibn Adam basi
ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ndie Muumba akaamua kutuma Mitume
na Manabii kwa waja wake wenye kusudio maalum.


105

KUSUDIO LA ALLAH SUBHANAH WA TA’ALA KUTUMA MITUME


KWA WAJA WAKE.

Ili kujua nia na kusudio la Allah Subhanah wa Ta’ala kutuma Mitume kwa waja wake
kila baada ya muda fulani ulimwenguni basi kwanza inabidi tukumbuke kua Allah
Subhanah wa Taála amewaumba Ibn Adam kua ndio watawala wa Ulimwenguni na
alipotuumba alituumba katika umbo lililobora kabisa kuliko viumbe wote kama
anavyosema katika aya ifuatayo:

﴾‫َﺣﺴ ِﻦ ﺗَـ ْﻘ ِﻮ ٍﱘ‬


‫أ‬ ۤ ِ ‫﴿ﻟَﻘﺪ ﺧﻠَﻘﻨﺎ ٱ ِﻹﻧﺴﺎن‬
‫ﰲ‬
َْ َ َ َْ َ ْ َ
Laqad khalaqna al-insana fee ahsani taqweemin (Surat At Tin 95:5)

Tafsir: Kwa hakika tumemuumba mtu katika Taqwiim bora kabisa.

Naam aya hii ya Surat At Tin 95:5 ni miongoni mwa aya ambazo zinanukuliwa sana na
Waislam Ulimwenguni lakini ni wachache wenye kuijua maana halisi ya ayah hii, kwa
sababu wengi sana hua wanazungumzia ubora wa muonekano wa nje wa mwili wa Ibn
Adam, lakini ukweli ni kua aya inaweka wazi ubora uliokamilia usiokua na kasoro wa
mwili wa Ibn Adam, ubora ambao unajumuisha mfumo mzima wa ufanyaji kazi
kikamilifu wa umbo la nje la mwili wa Ibn Adam ukishirikiana na ufanyaji kazi wa
mifumo yote kamilifu ya ndani ya mwili wa Ibn Adam ambayo inajumuisha Mfumo wa
Ubongo na Ufahamu wake, Mfumo wa hisia wa Uti wa mgongo na hisia zake tofauti
ikiwemo hisia za njaa, joto, baridi, matamanio, mapenzi, furaha, huzuni, maumivu n.k

Ubora huo unajumuisha pia mfumo kamilifu wa mzunguko wa Damu ndani ya Moyo na
ufahamu wake. Tunapozungumzia Moyo basi hua tunazungumzia kiungo ambacho ni
chenye ufahamu mkubwa na wa kina unaojitegemea kinguvu na kiuwezo kama
tulivyoona hapo kabla ambavyo vyote hivyo ni tofauti na uwezo wa ufahamu wa akili na
ufaham wa viumbe wengine kama Malaika na Majini.

Hivyo kamwe hatukukamilishwa kwa kujaaliwa kua na maumbile bora labda kwa ajili
ya kumhudumikia kwa kumtafutia riski au kumfanyia jambo lolote lile Muumba wetu
ambae ni Allah Subhanah wa Taála kwani yeye ni Muumba hivyo ni mwenye
kujitosheleza juu ya kila kitu na ni mwenye kua na uwezo wa kuwatosheleza viumbe
wake wote aliowaumba, hivyo Ibn Adam tumeumbwa kwa maumbile bora ili tupate
kutafakkar na kumjua, kumuabudu, kumshukuru na kumnyenyekea Allah Subhanah wa
Taála kama alivyotuwekea wazi kwenye Qurán kwa kusema:
106

ُ ‫ﻳﺪ ِﻣْﻨـ ُﻬﻢ ِّﻣﻦ ِّرْزٍق َوَﻣﺂ أُِر‬ ِ ‫ٱﳉِ ﱠﻦ وٱ ِﻹﻧﺲ إِﻻﱠ ﻟِﻴـﻌﺒ ُﺪ‬
‫ﻳﺪ أَن‬ ُ ‫ون۞ َﻣﺂ أُِر‬ ُْ َ َ َ ْ ‫ﺖ‬ ُ ‫﴿ َوَﻣﺎ َﺧﻠَ ْﻘ‬
ِ ‫ﻳﻄْﻌِﻤ‬
﴾‫ﻮن‬
ُ ُ
Wama khalaqtu aljinna waal-insa illa liyaAAbudooni, Ma oreedu minhum min
rizqin wama oreedu an yutAAimooni (Surat Adh Dhariyyat 51:56-57)

Tafsir: Sikuwaumba Majini na Ibn Adam isipokua kwa ajili ya kuniabudu mimi tu.!
Sitaki kutoka kwao Riziki wala sitaki wanipe chakula.

Anasema Allamah Abu Qasim Ibn Husein Ibn Mufadhal Ibn Muhammad Raghib Al
Isfahani kuhusiana na neno LiyaA’Abuduuni lililotumika katika aya hii kua: ‘Ubudiyya –
Utumwa hua ni kuuonesha unyenyekevu. Na Ibada hua ni kutilia mkazo, kwani
Ibada ndio mpaka wa unyenyekevu, na hakuna anaestahiki unyenyekevu au
kuabudiwa isipokua yule ambae ni mwenye uwezo wa kujaalia kila kitu ambae ndie
anaestahiki kuabudiwa ambae ni Allah Subhnahah wa Ta’ala na ndio maana
akasema:

﴾ُ‫ﻚ أَﻻﱠ ﺗَـ ْﻌﺒُ ُﺪ ۤواْ إِﻻﱠ إِ ﱠ�ﻩ‬


َ ‫ﻀ ٰﻰ َرﺑﱡ‬
َ َ‫﴿وﻗ‬
َ
Waqadha rabbuka alla taAAbudoo illa iyyahu (Surat Al Isra 17:23)

Tafsir: Na Mola wako amejaalia kua usimuabudu yeyote isipokua yeye’

Ama tunapozungumzia kuhusiana na LiyaA’Abuduuni basi hua kuna Ibada za aina mbili:

1. Unyenyekevu wa Ulazima – Ambao hua ni hali inayojumuisha kila kitu cha Mja
kinachohusiana na Muumbaji kutokana na kutokua na kitu na hivyo kua na uhitaji wa
Mja kwa Muumba ambae ni Allah Subhanah wa Taála.

2. Unyenyekevu wa Khiari – Ambao hua ni hali inayojumuisha hali moja kati ya mambo
ya matatu yafuatayo:
107

a) Unyenyekevu wa yule mtu ambae hayuko huru (yaani ni mtumwa alie chini ya
mtu mwengine, iwe kiutumwa, kiutumwa wa kileo ambao hua ni wa kikazi au
kifungo)

b) Unyenyekevu wa yule mtu ambae yuko huru lakini hua ni anaemtumikia Allah
Subhanah wa Taála (Ambalo ndio kusudio la uhalisia wa kila Kiumbe)

c) Unyenyekevu wa yule mtu ambae yuko huru lakini hua ni mwenye kumtumikia
Allah Subhanah wa Taála katika kuabudu na kihuduma, yaani anaemtumikia Allah
Subhanah wa Ta’ala kwa Ikhlasi na hivyo utumwa wake ni katika uhai wa Maisha
haya na kila kinachohusiana nayo. [Imam Raghib Al Isfahani, Mufradat Alfadhl Al
Qurán, 542]

Hivyo Allah Subhanah wa Taála anatuwekea wazi kua hakutuumba sisi Ibn Adam na
Majini isipokua kwa ajili ya Kumuabudu na kumnyenyekea yeye peke yake, kwa sababu
yeye ndie Mola wetu alietuumba na kuendelea kutulea tangu tulikotoka, hapa tulipofikia
na hadi tutakapoelekea katika mwisho wetu kwa kutujaalia Afya, Nguvu, Uwezo, Rizki,
Familia na kadhalika kwa kila mmoja miongoni mwetu kabla ya kuufikia mwisho wetu
ambao hakuna anaeujua miongoni mwetu isipokua yeye Mola wetu kama alivyosema
katika aya ifuatayo:

ِ ‫ض وﻣﺂ أَﻣﺮ ٱﻟ ﱠﺴ‬ ِ ِِ ﴿


َ َ‫ﺎﻋﺔ إِﻻﱠ َﻛﻠَ ْﻤ ِﺢ ٱﻟْﺒ‬
‫ﺼ ِﺮ أ َْو ُﻫ َﻮ‬ َ ُ ْ َ َ ِ ‫ﺐ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤ َﺎوات َوٱﻷ َْر‬ ُ ‫َو ﱠﻪﻠﻟ َﻏْﻴ‬
َ‫ﻮن أُﱠﻣ َﻬﺎﺗِ ُﻜ ْﻢ ﻻ‬
ِ ُ‫ٱﻪﻠﻟ أَﺧﺮﺟ ُﻜﻢ ِﻣﻦ ﺑﻄ‬ ِ ٍ ‫ب إِ ﱠن ﱠ‬
ُ ّ َ َ ْ ُ‫ٱﻪﻠﻟَ َﻋﻠَ ٰﻰ ُﻛ ِّﻞ َﺷ ْﻲء ﻗَﺪ ٌﻳﺮ۞ َو ﱠ‬ ُ ‫أَﻗْـَﺮ‬
﴾‫ﺼﺎر وٱﻷَﻓْﺌِ َﺪةَ ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜﻢ ﺗَ ْﺸ ُﻜﺮو َن‬
ُ ْ َ َ َ ْ‫ﺗَـ ْﻌﻠَ ُﻤﻮ َن َﺷْﻴﺌﺎً َو َﺟ َﻌ َﻞ ﻟَ ُﻜ ُﻢ ٱﻟْ ﱠﺴ ْﻤ َﻊ َوٱﻷَﺑ‬
Walillahi ghaybu alssamawati waal-Ardhi wama amru alssaAAati illa kalamhi
albasari aw huwa aqrabu inna Allaha AAala kulli shay-in qadeerun; WaAllahu
akhrajakum min butooni ommahatikum la taAAlamoona shay-an wajaAAala
lakumu alssamAAa waal-absara waal-af-idata laAAallakum tashkuroona (Surat An
Nahl 16:77-78)

Tafsir: Na kwa Allah ndiko kwenye umiliki wa Ulimwengu usioonekana wa Mbiguni


na ardhini, na amri juu ya wakati si chochote bali ni kama kupepesa kwa jicho au
karibu zaidi. Kwa hakika Allah ni mwenye uwezo juu ya kila kitu. Na Allah ndie
108

aliekutoeni katika matumbo ya uzazi wa mama zenu wakati nyinyi mkiwa hamjui kitu,
na akakupeni Masikio, Macho na Moyo ili mpate kua ni wenye kushukuru.

Tunapozungumzia juu ya Ibada ya kumuabudu Allah Subhanah wa Taála katika Dini ya


Uislam basi hua hatuzungumzii tu Kusali, Kufunga kutoa Zakkah na Sadaka bali hua
tunazungumzia utekelezaji wa Majukumu yote tuliyoamrishwa na Allah Subhanah wa
Taála katika wakati wa uhai wetu wote tunapokua hapa Ulimwenguni, tangu kuingia
kwetu hadi kutoka kwetu, kwani sisi tumekuja hapa Duniani kwa ajili ya Mola wetu na
hivyo kua katika hali ya mapigano ya kutafuta mafanikio yetu ya baadae dhidi ya
vichochezi vya Iblis na Nafsi zetu zitakazopelekea kuachana na lengo la kuumbwa kwetu,
hivyo hatukuja Duniani kwa ajili ya mchezo jambo ambalo linawekwa wazi na aya
zifuatazo:

ِ ِ ٍ
﴾‫َﺣ ٌﺪ‬
َ ‫ﺐ أَن ﻟﱠﻦ ﻳَـ ْﻘﺪ َر َﻋﻠَْﻴﻪ أ‬ َْ ‫ﻧﺴﺎ َن ِﰱ َﻛﺒَﺪ ۞ أ‬
ُ ‫َﳛ َﺴ‬
ِ
َ ‫ﻟََﻘ ْﺪ َﺧﻠَ ْﻘﻨَﺎ ٱﻹ‬
﴿

Laqad khalaqna al-insana fee kabadin, Ayahsabu an lan yaqdira AAalayhi ahadun
(Surat Al Balad 90:5-6)

Tafsir: Kwa hakika tumemuumba Ibn Adam katika hali ya Harakati na Mapigano, Jee
anajihesabu kua hakuna mwenye kuweza kumdhibiti juu yake?

Aya zinatuwekea wazi kua Ibn Adam ameumbwa kwa ajili ya kua katika hali ya
mapigano yenye kudumu na kuendelea katika kipindi cha uhai wake wote, harakati na
mapigano ambayo yanaanzia tangu kutafutwa kwake na Wazee wake, hadi kupatikana
kwake anapozaliwa, anapokua kua kwake, anapoidhibiti Nafsi yake na hadi katika wakati
wa kutolewa Roho yake, yeye yupo katika hali ya harakati na mapigano ambayo
yanatakiwa yampelekee kua na unyenyekevu juu ya Mola wake ambae ni Allah Subhanah
wa Ta’ala.

Lakini wapi, kila anavyokua na kupata afya, uwezo, mali na kadhalika basi ndio kwanza
anapozidi kujiona kua hakuna kama yeye. Hivyo jee kweli anafikiria kua hakuna
atakaemdhibiti? Suali hili linatiliwa mkazo kwa kuulizwa tena katika aya ifuatayo pale
Qurán iliposema:

﴾‫َﳛﺴﺐ ٱ ِﻹﻧﺴﺎ ُن أَن ﻳـُْﺘـﺮَك ُﺳ ًﺪى‬ ﴿


َ َ ُ َ َْ ‫أ‬
Ayahsabu al-insanu an yutraka sudan (Surat Al Qiyama 75:36)
109

Tafsir: Hivi anajihesabu mtu kua ataachwa bila kuhukumiwa?

Hivi jee kweli inawezekana kiumbe Ibn Adam kiachiwe tu bila ya kudhibitiwa na
Muumba wake juu ya majukumu yake kwa Mola wake na kwa viumbe wenzake? Bila ya
kuamrishwa kua lipi alifanye na kukatazwa lipi asilifanye na jee anafikiria kua
hatohesabiwa na kuhukumiwa kwa kila analolifanya hapa Ulimwenguni? Na kama
anafikiria hivyo basi huyu ni kiumbe ambae hakumuamini Mola wake kwani anaamini
kua Allah Subhanah wa Ta’ala alieumba kila kitu hana habari na kila kiumbe chake na
wala hajui kitu chochote juu yake, jambo ambalo haliingii akilini.

Kwani Allah Subhnah wa Ta’ala ambae ndie alieiumba Dunia na kuipamba kwa ajili ya
Waja wake ili wasipate shida katika mazingira yao na hapo hapo wasighafilike juu yake
basi anasema katika Qur’an kua:

ِ‫ﱠ‬ ِ‫ِ ﱠ‬ ِ ِ ِ﴿
‫ﻳﻦ ٱﺗﱠـ َﻘﻮاْ ﻓَـ ْﻮﻗَـ ُﻬ ْﻢ‬
َ ‫ﻳﻦ َآﻣﻨُﻮاْ َوٱﻟﺬ‬ َ ‫ٱﳊَﻴَﺎةُ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ َوﻳَ ْﺴ َﺨُﺮو َن ﻣ َﻦ ٱﻟﺬ‬ْ ْ‫ﻳﻦ َﻛ َﻔُﺮوا‬َ ‫ُزﻳّ َﻦ ﻟﻠﱠﺬ‬
‫ﺚ‬َ ‫اﺣ َﺪ ًة ﻓَـﺒَـ َﻌ‬ ِ ‫ﺎب۞ َﻛﺎ َن ٱﻟﻨﱠﺎس أُﱠﻣﺔً و‬ ٍ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻳـﺮُز ُق ﻣﻦ ﻳ َﺸﺂء ﺑِﻐَ ِْﲑ ِﺣﺴ‬ ‫ﱠ‬ ‫و‬ ِ ‫ﻳـﻮم ٱﻟْ ِﻘﻴﺎﻣ‬
‫ﺔ‬
َ ُ َ ُ َ َ َْ ُ َ َ َ َ ْ َ
ِ ِ ‫ﭑﳊ ِﻖ ﻟِﻴﺤ ُﻜﻢ ﺑـﲔ ٱﻟﻨ‬ ِ ِِ ِ ِ‫ٱﻪﻠﻟ ٱﻟﻨﱠﺒِﻴ‬
‫ﻴﻤﺎ‬
َ ‫ﱠﺎس ﻓ‬ َ ْ َ َ ْ َ ّ َْ ِ‫ﺎب ﺑ‬ َ َ‫َﻧﺰَل َﻣ َﻌ ُﻬ ُﻢ ٱﻟْﻜﺘ‬ َ ‫ﻳﻦ َوأ‬ َ ‫ﲔ ُﻣﺒَ ّﺸ ِﺮ‬
َ ‫ﻳﻦ َوُﻣﻨﺬر‬ َ ّ ُ‫ﱠ‬
ِ ِ ِ ‫ٱﺧﺘـﻠَ ُﻔﻮاْ ﻓِ ِﻴﻪ وﻣﺎ ٱﺧﺘـﻠَﻒ ﻓِ ِﻴﻪ إِﻻﱠ ٱﻟﱠ‬
ً‫ﺎت ﺑَـ ْﻐﻴﺎ‬ ُ َ‫ﻳﻦ أُوﺗُﻮﻩُ ﻣﻦ ﺑَـ ْﻌﺪ َﻣﺎ َﺟﺂءَﺗْـ ُﻬ ُﻢ ٱﻟْﺒَـﻴِّﻨ‬ َ ‫ﺬ‬ َ َْ ََ َْ
‫ٱﻪﻠﻟُ ﻳـَ ْﻬ ِﺪى َﻣﻦ‬ ‫ٱﺧﺘَـﻠَ ُﻔﻮاْ ﻓِ ِﻴﻪ ِﻣ َﻦ ٱ ْﳊَِّﻖ ﺈﺑِِ ْذﻧِِﻪ َو ﱠ‬ ِ
ْ ‫ﻳﻦ َآﻣﻨُﻮاْ ﻟ َﻤﺎ‬
ِ ‫ﺑـﻴـﻨـﻬﻢ ﻓَـﻬ َﺪى ﱠ ﱠ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ٱﻟﺬ‬ َ ْ ُ َ َْ
﴾‫اط ﱡﻣﺴﺘَ ِﻘﻴ ٍﻢ‬ ٍ ِ ِ
ْ ‫ﻳَ َﺸﺂءُ إ َ ٰﱃ ﺻَﺮ‬
Zuyyina lilladheena kafaroo alhayatu alddunya wayaskharoona mina alladheena
amanoo waalladheena ittaqaw fawqahum yawma alqiyamati waAllahu yarzuqu
man yashao bighayri hisabin; Kana alnnasu ommatan wahidatan fabaAAatha
Allahu alnnabiyyeena mubashshireena wamundhireena waanzala maAAahumu
alkitaba bialhaqqi liyahkuma bayna alnnasi feema ikhtalafoo feehi wama ikhtalafa
feehi illa alladheena ootoohu min baAAdi ma jaat-humu albayyinatu baghyan
baynahum fahada Allahu alladheena amanoo lima ikhtalafoo feehi mina alhaqqi bi-
idhnihi waAllahu yahdee man yashao ila siratin mustaqeemin(Surat Al Baqara
2:212-213)

Tafsir: Yamependezeshewa kwa waliokufuru Maisha ya Duniani na hivyo huwafanyia


maskhara walioamini, na wale wanaomcha (wanaotii maamrisho ya Allah Subhnaha
110

wa Ta’ala na kukaa mbali na makatazo yake), watakua juu yao katika siku ya Kiama,
Na Allah humruzuku amtakae bila ya kiasi. Walikua watu ni Umma mmoja kisha
Allah akawatumia Manabii wenye Kubainisha na Kuusia, na pamoja nao akawatumia
Maandiko kwa haki ili watoe hukumu baina ya Watu katika mambo waliyotofautiana,
na hawakuhitilafiana navyo (Vitabu hivyo) isipokua wale waliokwishapewa baada ya
kubainishiwa kutokana na chuki baina yao, kisha akawaongoza Allah wale
walioamini kutokana na kile walichohitilafiana kuwaelekeza katika haki kutokana na
Idhini yake. Na kwa hakika Allah humuongoza amtakae katika njia iliyonyooka.

Kutokana na maneno ya aya hio basi ndio maana Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
akawa ni mwenye kupenda kuisoma dua ifuatayo katika wakati wa usiku anaposali Salat
Dhuha.

ِ ‫ ﻋ‬،‫ض‬ ِ ‫ﺎﻃﺮ اﻟ ﱠﺴﻤﻮ‬ ِ َ‫ ﻓ‬،‫ب ِﺟﺒـﺮاﺋِﻴﻞ وِﻣﻴ َﻜﺎﺋِﻴﻞ وإِﺳﺮاﻓِﻴﻞ‬


َ‫ﺎﱂ‬ َ ِ ‫َر‬‫ﻷ‬‫ا‬‫و‬ ‫ات‬
ْ َ ََ َ َ َْ َ َ َ َ َ ْ ‫))اﻟﻠﱠ ُﻬ ﱠﻢ َر ﱠ‬
‫ ْاﻫ ِﺪِﱐ ﻟِ َﻤﺎ‬،‫ﻴﻤﺎ َﻛﺎﻧُﻮا ﻓِ ِﻴﻪ َﳜْﺘَﻠِ ُﻔﻮ َن‬ ِ ِ ِ ‫ أَﻧْﺖ َﲢ ُﻜﻢ ﺑـ‬،ِ‫ﺐ واﻟﺸﱠﻬﺎدة‬
َ ‫ﲔ ﻋﺒَﺎد َك ﻓ‬َْ َ ُ ْ َ َ َ َ ِ ‫اﻟْﻐَْﻴ‬
((‫اط ُﻣ ْﺴﺘَ ِﻘﻴ ٍﻢ‬
ٍ ‫ﻚ ﺗَـﻬ ِﺪي ﻣﻦ ﺗَ َﺸﺎء إِ َﱃ ِﺻﺮ‬
َ ُ ْ َ ْ َ ‫ﱠ‬
‫ﻧ‬ ِ‫ إ‬،‫ﻚ‬
َ ِ‫اﳊ ِﻖ ِﺈﺑ ْذﻧ‬
ّ َْ ‫ﻦ‬
َ
ِ ‫اﺧﺘُﻠِﻒ ﻓِ ِﻴﻪ‬
‫ﻣ‬ َ ْ
(Allahumma Rabb Jibrail wa Mikail waI'iisrafila, fatir alssamawat wal'ardhi,
aA’alim alghayb walshshahadati, 'ant tahkum bayn aIibadik fima kanuu fihi
yakhtalifuna, ahdini lima akhtulif fihi min alhaqq bi'idhnika, 'innak tahdi man
tasha' 'iilaa sirat mustaqimin)

Tafsir: Ya Allah Rabbi wa Jibril, na Mikail na Israfil, Muanzilishi wa Mbingu na


Ardhi, Mwenye kujua yaliyofichikana na yaliyowazi, hakika wewe ni mwenye
kuhukumu baina ya waja wako juu ya kile walichokhitilafiana, niongoze kutokana na
kile walichohitilafiana niwe katika Haki kwa idhini yako, kwa hakika wewe ni mwenye
kuwaongoza uwatakao katika njia iliyonyooka.

Hii ni Dua muhimu sana ambayo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua
akimuomba Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ni mola wa Malaika Jibril, Mikail na Israfil
kwa ajili ya uongofu wa Hapa Duniani na kesho Akhera, kwani hakuna usalama katika
siku ya malipo kesho Akhera hadi uwe ni mwenye kujihakikishia kua upo kwenye njia
iliyonyooka ambayo ndio njia ya waliofuzu kama anavyosema Allah Subhanah wa
Ta’ala:
111

ٍ ‫ﺎت ﺟﻨ‬
‫ﱠﺎت َْﲡ ِﺮي ِﻣ ْﻦ َْﲢﺘِ َﻬﺎ ْاﻷَﻧْـ َﻬ ُﺎر‬ ِ ِ ‫اﻪﻠﻟ ﻳ ْﺪ ِﺧﻞ اﻟﱠ ِﺬﻳﻦ آﻣﻨُﻮا وﻋ ِﻤﻠُﻮا اﻟ ﱠ‬
َ َ‫ﺼﺎﳊ‬ َ َ َ َ ُ ُ ‫﴿إِ ﱠن ﱠ‬
‫ﺎﺳ ُﻬ ْﻢ ﻓِ َﻴﻬﺎ َﺣ ِﺮ ٌﻳﺮ ۞ َوُﻫ ُﺪوا إِ َﱃ‬ ِ ٍ ‫َﺳﺎ ِور ِﻣ ْﻦ ذَ َﻫ‬ ِ ِ
ُ َ‫ﺐ َوﻟُْﺆﻟًُﺆا َوﻟﺒ‬ َ َ ‫ُﳛَﻠﱠ ْﻮ َن ﻓ َﻴﻬﺎ ﻣ ْﻦ أ‬
ِ ‫اﳊ ِﻤ‬
﴾‫ﻴﺪ‬ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ‫اﻟﻄﱠﻴ‬
َْ ‫ﺐ ﻣ َﻦ اﻟْ َﻘ ْﻮل َوُﻫ ُﺪوا إ َﱃ ﺻَﺮاط‬ ّ
Inna Allaha yudkhilu alladheena amanoo waAAamiloo alssalihati jannatin tajree
min tahtiha al-anharu yuhallawna feeha min asawira min dhahabin walu/lu-an
walibasuhum feeha hareerun; Wahudoo ila alttayyibi mina alqawli wahudoo ila
sirati alhameedi (Surat Al Hajj 22:23-24)

Tafsir: Hakika Allah atawaingiza wale waliomuamini na wakafanya mambo mema


katika Bustani (Peponi) ambazo chini yake kuna kuna mito ambamo watapambwa
ndani yake kwa makoja ya Dhahabu na Lulu na nguo zao zitakua za Hariri. Na
Wameongozwa kutokana na (kutumia) bora miongoni mwa kauli (Dhikr Allah, Lâ
ilâha ill-Allâh, Alhamdu lillâh, Kusoma Qur’an, Kuamrishana Mema n.k) na
wakaongozwa katika njia iliyonyooka.

Hivyo bila ya shaka Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ametujaalia mahitaji yetu yote
hapa Ulimwenguni ni mwenye kujua na kuona kila kitu juu yetu hivyo ni wajibu wetu
kumuamini na kumtii na kufahamu kua bila ya shaka baadae kuna kuhesabiwa amali zetu
na ambapo kwa watakaoamini na kujichunga basi watakua ni miongoni mwa waliofuzu
na wale wasioamini na kucheza basi watakua ni miongoni mwa waliokula hasara kwani
mwisho wake watafikia mahali pabaya sana kama inavyosema Qurán:

ِ ‫ٱﻵﺧﺮةِ وﻳ‬ ِ ِ ْ ‫ﺖ ِﰱ‬ ِ ِ‫ٱﻪﻠﻟ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ آﻣﻨُﻮاْ ﺑِﭑﻟْ َﻘﻮِل ٱﻟﺜﱠﺎﺑ‬
ُ‫ٱﻪﻠﻟ‬
‫ﻀ ﱡﻞ ﱠ‬ ُ َ َ ‫ٱﳊَﻴَﺎة ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ َوِﰱ‬ ْ َ َ ُ‫ﺖ ﱠ‬ ُ ِّ‫﴿ﻳـُﺜَـﺒ‬
ِ‫ٱﻪﻠﻟ ﻣﺎ ﻳﺸﺂء ۞أََﱂ ﺗَـﺮ إِ َﱃ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﺑ ﱠﺪﻟُﻮاْ ﻧِﻌﻤﺔَ ﱠ‬ ِِ
ْ‫َﺣﻠﱡﻮا‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟ ُﻛ ْﻔﺮاً َوأ‬ َْ َ َ َ ْ ُ َ َ َ ُ‫ﲔ َوﻳَـ ْﻔ َﻌ ُﻞ ﱠ‬ َ ‫ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
‫ﻀﻠﱡﻮاْ َﻋﻦ‬ ِ ‫َﻧﺪاداً ﻟِّﻴ‬
َ ‫أ‬ ِ‫ﻗَـﻮﻣﻬﻢ دار ٱﻟْﺒـﻮا ِر۞ﺟﻬﻨﱠﻢ ﻳﺼﻠَﻮﻧَـﻬﺎ وﺑِْﺌﺲ ٱﻟْ َﻘﺮار۞وﺟﻌﻠُﻮاْ ِﱠﻪﻠﻟ‬
ُ َ َ َ ُ َ َ َ َ ْ ْ َ َ َ َ ََ َ َ ْ ُ َْ
ِ ِ ‫ﺼﲑُﻛﻢ إِ َﱃ ٱﻟﻨﱠﺎ ِر۞ﻗُﻞ ﻟِّﻌِﺒ ِﺎد ﱠ‬ ِ ِ ِِ ِ
َ‫ﺼﻼَة‬ ‫ﻴﻤﻮاْ ٱﻟ ﱠ‬ ُ ‫ﻳﻦ َآﻣﻨُﻮاْ ﻳُﻘ‬ َ ‫ى ٱﻟ ﺬ‬ َ َ ْ َ ‫َﺳﺒﻴﻠﻪ ﻗُ ْﻞ َﲤَﺘـﱠﻌُﻮاْ ﻓَﺈ ﱠن َﻣ‬
َ‫ﺎﻫ ْﻢ ِﺳّﺮاً َو َﻋﻼﻧِﻴَﺔً ِّﻣﻦ ﻗَـْﺒ ِﻞ أَن َ�ْﺗِ َﻰ ﻳَـ ْﻮٌم ﻻﱠ ﺑَـْﻴ ٌﻊ ﻓِ ِﻴﻪ َوﻻ‬ ِ ِ
ُ َ‫َوﻳـُْﻨﻔ ُﻘﻮاْ ﳑﱠﺎ َرَزﻗْـﻨ‬
‫َﺧَﺮ َج ﺑِِﻪ‬ ِ ِ ‫ات وٱﻷَرض وأ‬ ِ ِ ‫ِﺧﻼَ ٌل۞ ﱠ‬
ْ ‫َﻧﺰَل ﻣ َﻦ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤﺂء َﻣﺂءً ﻓَﺄ‬ َ َ َ ْ َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ٱﻟﱠﺬى َﺧﻠَ َﻖ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤ َﺎو‬
112

ِ ‫ات ِرزﻗﺎً ﻟﱠ ُﻜﻢ وﺳ ﱠﺨﺮ ﻟَ ُﻜﻢ ٱﻟْ ُﻔ ْﻠ‬


‫ى ِﰱ ٱﻟْﺒَ ْﺤ ِﺮ ِﺄﺑ َْﻣ ِﺮﻩِ َو َﺳ ﱠﺨَﺮ ﻟَ ُﻜ ُﻢ‬ َ ُ َ َ َ ْ ْ ِ ‫ِﻣ َﻦ ٱﻟﺜ َﱠﻤَﺮ‬
َ ‫ﻚ ﻟﺘَ ْﺠ ِﺮ‬
‫ﲔ َو َﺳ ﱠﺨَﺮ ﻟَ ُﻜ ُﻢ ٱﻟْﻠﱠْﻴ َﻞ‬ ِ ْ ‫ﱠﻤﺲ وٱﻟْ َﻘﻤﺮ َدآﺋِﺒَـ‬
َ َ َ َ ْ ‫ٱﻷَﻧْـ َﻬ َﺎر۞ َو َﺳ ﱠﺨﺮ ﻟَ ُﻜ ُﻢ ٱﻟﺸ‬
‫ﻮﻫﺎ إِ ﱠن‬ ِ‫آﺎﺗ ُﻛﻢ ِﻣﻦ ُﻛ ِﻞ ﻣﺎ ﺳﺄَﻟْﺘﻤﻮﻩ وإِن ﺗَـﻌ ﱡﺪواْ ﻧِﻌﻤﺔَ ﱠ‬
َ‫ﺼ‬ ُ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻻَ ُْﲢ‬ َ ْ ُ َ ُ ُ ُ َ َ ّ ّ َ ‫۞و‬ َ ‫ﱠﻬ َﺎر‬
َ ‫َوٱﻟﻨـ‬
﴾‫ﻮم َﻛ ﱠﻔ ٌﺎر‬ ٌ ُ‫ٱﻹﻧْ َﺴﺎ َن ﻟَﻈَﻠ‬
Yuthabbitu Allahu alladheena amanoo bialqawli alththabiti fee alhayati alddunya
wafee al-akhirati wayudhillu Allahu aldhdhalimeena wayafAAalu Allahu ma
yasha/o; Alam tara ila alladheena baddaloo niAAmata Allahi kufran waahalloo
qawmahum dara albawari; Jahannama yaslawnaha wabi/sa alqararu;
WajaAAaloo lillahi andadan liyudhilloo AAan sabeelihi qul tamattaAAoo fa-inna
maseerakum ila alnnari, Qul liAAibadiya alladheena amanoo yuqeemoo alssalata
wayunfiqoo mimma razaqnahum sirran waAAalaniyatan min qabli an ya/tiya
yawmun la bayAAun feehi wala khilalun; Allahu alladhee khalaqa alssamawati
waal-ardha waanzala mina alssama-i maan faakhraja bihi mina alththamarati
rizqan lakum wasakhkhara lakumu alfulka litajriya fee albahri bi-amrihi
wasakhkhara lakumu al-anhara; Wasakhkhara lakumu alshshamsa waalqamara
da-ibayni wasakhkhara lakumu allayla waalnnahara; Waatakum min kulli ma
saaltumoohu wa-in taAAuddoo niAAmata Allahi la tuhsooha inna al-insana
ladhaloomun kaffarun (Surat Ibrahim 14:27-34)

Tafsir: Allah atawapa msimamo wenye kauli thabit wale wanaomuamini hapa Duniani
na Akhera, na Allah atawapotosha wale wenye kujidhulumu na Allah hufanya kile
akitakacho. Jee hujaowana wale ambao wamebadilisha Neema za Allah kua ni Kufuru
na kuwasababishia watu wao kukaa katika sehemu ya maangamizo? Jahannama ndio
utakaowaunguza! Na kwa hakika ni sehemu mbaya sana kukaa ndani yake, na
wanajaalia Miungu myengine dhidi ya Allah ili kuwapotosha watu kutokana na
muongozo wake, Waambie: Kuleni Raha!kwani kwa hakika mtakapofikia mwisho
wenu ni Motoni. Waambie (Ewe Muhammad) waja wangu walioamini! Kua
wasimamishe Sala, na watoe kutokana na kile tulichowaruzuku kwa siri na kwa
dhahir, kabla ya kuwasili siku ambayo itakua hakuna kupatana wala kupendeleana.
Allah ni yule ambae alieumba Mbigu na Ardhi na akashusha maji kutoka mbiguni,
na kutokana nayo akatoa matunda kua ni rizki kwa ajili yenu, na akazifanya Meli kua
kwa ajili ya matumizi yenu, ili muweze kuelea (kusafiri) juu ya Bahari kutokana na
amri yake na Mito kua kwa ajili yenu. Na akalifanya Jua na Mwezi kua daima ni yenye
kupita katika njia zake kwa ajili yenu, na akajaalia Mchana na Usiku kua ni kwa ajili
yenu. Na akakupeni kila kitu mlichohitaji. Na kama mtazihesabu Neema za Allah juu
113

yenu, basi kamwe hamtoweza kuzihesabu. Ama kwa Hakika Mtu ni mwenye
kujidhulumu na ni mwenye kukufuru

Allah Akbar! Wa Alhamd lillah! wa La Illah Ila Allah! Allah Subhanah wa Ta’ala ambae
ndie Mola wa Ulimwengu wote na kila kilichomo ndani yake, anatuwekea wazi namna
anavyotupenda sana waja wake na hivyo bila ya shaka yeye ni mwenye kutuonea huruma
kutokana na udhaifu wa Nafsi zetu na matamanio ya Ulimwengu huu wa mpito na
kututahadharisha juu ya siku ya Malipo siku ambayo itakua hakuna kupatana wala
kupendeleana.

Naam, kutokana na Ukarimu wake juu yetu kwa kutujaalia kila aina ya Neema
tunazozihitaji basi pia akatujaalia kutumwagia Rehma zake juu yetu Ibn Adam, kwa
kutupa nafasi ya kuomba msamaha wake kwa kila atakaeamua kurudi kwake, na pia kwa
kutuma Mitume kwa kila baada ya mda ili kutukumbusha waja wake juu yake, Mitume
hao ni kutoka miongoni mwa watu wa jamii husika ili watoe muongozo, maonyo na
kuwausia watu juu yake pale watu hao wanapopotoka kutokana na njia iliyosahih ya
kuelekea kwake kabla ya yeye kuamua kuwashushia wanaopotoka adhabu kali isiyoweza
kustahmilika kutokana na maumbile yetu Ibn Adam, kama inavyosema Qurán katika aya
zifuatazo.
ِ ‫ﺿ ﱠﻞ ﻓَِﺈﱠﳕَﺎ ﻳ‬ ِِ ِ ِ
‫ﻀ ﱡﻞ َﻋﻠَْﻴـ َﻬﺎ َوﻻَ ﺗَ ِﺰُر َوا ِزَرةٌ ِوْزَر‬ َ َ ‫﴿ ﱠﻣ ِﻦ ْٱﻫﺘَ َﺪ ٰى ﻓَِﺈﱠﳕَﺎ ﻳَـ ْﻬﺘَﺪى ﻟﻨَـ ْﻔﺴﻪ َوَﻣﻦ‬
ِ ِ
َ ‫ﺚ َر ُﺳﻮﻻً ۞ َوإِ َذآ أ ََرْد َ� أَن ﻧـﱡ ْﻬﻠ‬
�َ‫ﻚ ﻗَـْﺮﻳَﺔً أ ََﻣْﺮ‬ َ ِ‫ُﺧَﺮ ٰى َوَﻣﺎ ُﻛﻨﱠﺎ ُﻣ َﻌ ّﺬﺑ‬
َ ‫ﲔ َﺣ ﱠ ٰﱴ ﻧَـْﺒـ َﻌ‬ ْ‫أ‬
﴾ً‫ُﻣْﺘـﺮﻓِ َﻴﻬﺎ ﻓَـ َﻔﺴ ُﻘﻮاْ ﻓِ َﻴﻬﺎ ﻓَ َﺤ ﱠﻖ َﻋﻠَْﻴـ َﻬﺎ ٱﻟْ َﻘﻮ ُل ﻓَ َﺪ ﱠﻣﺮَ� َﻫﺎ ﺗَ ْﺪ ِﻣﲑا‬
ْ ْ َ َ
Mani ihtada fa-innama yahtadee linafsihi waman dhalla fa-innama yadhillu
AAalayha wala taziru waziratun wizra okhra wama kunna muAAadhdhibeena
hatta nabAAatha rasoolan, Wa-idha aradna an nuhlika qaryatan amarna
mutrafeeha fafasaqoo feeha fahaqqa AAalayha alqawlu fadammarnaha tadmeeran
(Surat Al Isra 17:15-16)

Tafsir: Ama kwa yule atakeongoka basi hua ni mwenye kuiongoa Nafsi yake, na
mwenye kupotoka basi hua ni mwenye kuipotosha Nafsi yake, na hakuna mbebaji
atakaebeba mzigo wa mwenzake. Na sisi kamwe hatuadhibu hadi inapokua tayari
tumeshatuma Mjumbe (kuonya). Na tunapoamua kuuangamiza Mji basi hua
tunatuma amri kwanza (kwa watu husika kua wamtii Allah Subhanah wa Taála) kwa
baadhi miongoni mwao ambao wamepewa vizuri katika uhai huu. Na kisha wakavuka
mipaka kutokana na kupewa huko, basi hapo ndio kauli (ya adhabu) inawahalalikia
114

juu yao. Na kisha baada ya hapo ndio tunauangamiza (Mji au Ummah husika) kabisa
kabisa.

Anasema Sultan al Mutakallimin Mujaddid ud Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi juu ya
ayah hii kua: ‘Wakati Allah Subhanah wa Taála anapotaka kuuangamiza mji
kutokana na dhambi za watu wake, basi hua haharakishi katika kuungamiza mji
husika kwa sababu ya kuwepo kwa madhambi hayo, bali huwaamrisha wenye
uwezo miongoni mwa watu hao kuachana na dhambi husika, kwani wenye uwezo
wanapofanya dhambi hizo wao basi wale wasiokua na uwezo nao huwafuata katika
hayo. Hivyo wanapo kataa kuachana na dhambi husika basi ndio huadhibiwa kwa
adhabu husika, na wamelengwa wenye uwezo kwa sababu wao ndio ambao
wanatakiwa zaid kumshukuru Allah Subhanah wa Taála kwa kuwapendelea kwa
neema alizowajaalia. Hivyo baada ya onyo la kwanza basi huwapa nafasi watu hao
kwa kuwaonya tena mara kadhaa, na wakiendelea kudumu katika dhambi hizo basi
na Adhabu husika huwashukia watu hao.’

Mbali ya kua Allah Subhanah wa Ta’ala anatuambia katika Qurán kua hashushi adhabu
hadi atume Mitume wake kuonya ili wawaonye watu na kuwarudisha watu katika njia
moja ya haki ya kimaumbile ya kumpwekesha Allah Subhanah wa Taála lakini pia hapo
hapo, inatuwekea wazo kua kila Ummah wa wakati husika ulikua ni wenye kutumia
Hukmu na njia tofauti zilizokua zikiendana na Nyakati husika, kwa mfano tunapoiangalia
kitabu cha Zabur cha Nabii Daud basi tunaona kua mbali ya kua kilikua kinabashiria
mambo yatakayotokea katika miaka ya baadae lakini pia kilikua ni kitabu kilichokua
hakina Sharia wala Hukmu ndani yake, lakini kilikua kinazungumzia mambo ya Halali
na Haram tu basi ndani yake.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala katuwekea wazi kua Qurán ndio kitabu kilichokuja
kubatilisha vitabu vyote vya Mitume wengine vilivyokuja kabla yake na hivyo
kumwambia Mtume wake Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam kua Qurán ndio
chenye kauli ya mwisho na chenye uthibitisho juu ya vitabu vyote walivyopewa Mitume
waliotangulia kabla yake, na yaliyoteremshwa ndani ya Qurán ndio yanayotakiwa
kufuatwa badala yake kwa kusema:

‫ﺎب َوُﻣ َﻬْﻴ ِﻤﻨﺎً َﻋﻠَْﻴ ِﻪ‬


ِ َ‫ﲔ ﻳ َﺪﻳِْﻪ ِﻣﻦ ٱﻟْ ِﻜﺘ‬ ِ ِ ‫ﭑﳊ ِﻖ ﻣ‬ ِ َ ‫﴿وأَﻧﺰﻟْﻨَﺂ إِﻟَﻴ‬
َ َ ُ ّ َْ ِ‫ﺎب ﺑ‬
َ َْ َ‫ﺼ ّﺪﻗﺎً ﻟّ َﻤﺎ ﺑـ‬ َ َ‫ﻚ ٱﻟْﻜﺘ‬ ْ ََ
‫ٱﳊَِّﻖ ﻟِ ُﻜ ٍّﻞ َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ‬
ْ ‫ٱﻪﻠﻟُ َوﻻَ ﺗَـﺘﱠﺒِ ْﻊ أ َْﻫ َﻮآءَ ُﻫ ْﻢ َﻋ ﱠﻤﺎ َﺟﺂءَ َك ِﻣ َﻦ‬
‫َﻧﺰَل ﱠ‬ ِ
َ ‫ﭑﺣ ُﻜﻢ ﺑَـْﻴـﻨَـ ُﻬﻢ ﲟَﺂ أ‬
ْ َ‫ﻓ‬
115

‫اﺣ َﺪ ًة َوﻟَـٰ ِﻜﻦ ﻟِّﻴَـْﺒـﻠَُﻮُﻛ ْﻢ ِﰱ َﻣﺂ‬


ِ ‫ٱﻪﻠﻟ َﳉﻌﻠَ ُﻜﻢ أُﱠﻣﺔً و‬ ِ
َ ْ ََ ُ‫ﻣﻨ ُﻜ ْﻢ ﺷْﺮ َﻋﺔً َوﻣْﻨـ َﻬﺎﺟﺎً َوﻟَْﻮ َﺷﺂءَ ﱠ‬
ِ ِ
﴾‫ﲨﻴﻌﺎً ﻓَـﻴُـﻨَـﺒِّﺌُ ُﻜﻢ ِﲟَﺎ ُﻛﻨﺘُﻢ ﻓِ ِﻴﻪ َﲣْﺘَﻠِ ُﻔﻮ َن‬
َِ ‫ات إِ َ ٰﱃ ﷲِ ﻣﺮِﺟﻌ ُﻜﻢ‬
ِ ‫آﺎﺗ ُﻛﻢ ﻓَﺎﺳﺘَﺒِ ُﻘﻮا اﳋﻴـﺮ‬
َ
ْ ْ ُ َْ َ َْ ْ
Waanzalna ilayka alkitaba bialhaqqi musaddiqan lima bayna yadayhi mina
alkitabi wamuhayminan AAalayhi faohkum baynahum bima anzala Allahu wala
tattabiAA ahwaahum AAamma jaaka mina alhaqqi likullin jaAAalna minkum
shirAAatan waminhajan walaw shaa Allahu lajaAAalakum ommatan wahidatan
walakin liyabluwakum feema atakum faistabiqoo alkhayrati ila Allahi
marjiAAukum jameeAAan fayunabbi-okum bima kuntum feehi takhtalifoona
(Surat Al Maidah 5:48)

Tafsir: Na kwako wewe tumetuma Kitabu kwa Haki na Ukweli, kuthibitisha vitabu
vilivyotangulia kabla yake na chenye uongofu na uthibitisho zaidi juu yake. Hivyo toa
hukumu baina yao kutokana na alivyoteremsha Allah, na kamwe usifuate matamanio
yao, yatakayokutoa katika Haki iliyokujia wewe. Kwa kila mmoja miongoni mwenu
amebainishiwa Sharia na njia iliyowazi. Kama Allah angelitaka basi angekujaalieni
nyie kua Ummah mmoja. Lakini (mipango yake) ni kukujaribuni nyinyi juu ya kile
alichokujaalieni, hivyo jitahidini kwa kukimbilia katika kufanya mema. Marejeo ya
kila mmoja wenu ni kwa Allah. Ni yeye ndie ambae atakaekuonesheni ukweli juu ya
kile mnachohitilafiana.

Ama kuhusiana na aya hii basi anasema Qatadah kua; ‘Ingawa watu wa Mataifa yote
ya hapo awali yalikua yakifuata Dini Moja inayompwekesha Allah Subhanah wa
Ta’ala pekee, lakini wote walikua na Shariah tofauti’. Hapa sasa umefika wakati wa
kuwaangalia Mitume na Manabii hao waliotangulia na kutajwa katika Qurán.


MITUME NA MANABII WALIOTAJWA KATIKA QURÁN.


Kwa lugha ya kiarabu neno ‘Nabi’ lina maana ya habari au ripoti. Hivyo mtu huitwa
‘Nabi’ (Nabii) kwa sababu hua anatoa habari kuhusiana na Mola wake na pia hua
anapokea habari kutoka kwa Mola wake kupitia kwa Malaika Jibril. Kwa kishariah
neno ‘Nabi’ yaani Nabii, humaanisha mtu alie na sifa ya ubora ambayo
amehamasishwa kwa kupitia njia za Wahy kufanya vitendo vyake bila ya
116

kuamrishwa kuwafikishia watu wengine ujumbe wa Wahy huo na hivyo mtu huyo
huutekeleza ujumbe huo yeye mwenyewe binafsi.

Na ‘Rasul’ (Mtume) humaanisha mtu alie na sifa ya ubora ambayo amehamasishwa


kwa kupitia njia za Wahy kufanya vitendo vyake na kuamrishwa kuueneza na
kuwafikishia watu wengine ujumbe wa wahy huo. Hivyo kila Rasul (Mtume) hua ni
lazima kua Nabi (Nabii) lakini si lazima kwa kila Nabi (Nabii) kua ni Rasul (Mtume).

Katika kulifafanua zaidi hili basi na tuangalie mtizamo wa Imam Jaffar As Sadiq ambae
yeye anasema kua: Manabii wamegawika katika makundi manne:

1 - Nabii ambae hua anapokea Wahy na Ilham lakini hua hana jukumu la kueneza
ujumbe ulio ndani ya Wahy au Ilham husika kwa watu wengine.

2 - Nabii ambae hua anaona na kusikia ujumbe anaoletewa katika wakati ambao
akiwa macho wazi yaani hajalala na hayuko usingizini au katika wakati macho
yakiwa ameyafunga yaani akiwa usingizini lakini nae pia hua hana jukumu la
kueneza ujumbe huo kwa watu wengine.

3 - Nabii ambae hua ni Nabii Al Mursal ambae yeye hua anapokea ujumbe na
kuamrishwa kuutanaza ujumbe husika kwa baadhi ya watu tu.

4 - Nabii ambae hua ni hua anapokea Wahy na kutumwa kuueneza ujumbe huo kwa
watu wote kwa ujumla.

Anasema Hujjat ul Islami Mujaddid ud Din Imam Abu Hamid Ibn Muhammad Ibn
Muhammad Al Ghazali kua: Kama ilivyokua kwa viumbe Ibn Adam kutofautishwa
na wanyama wengine kwa wao Ibn Adam kupewa Nafsi yenye Ufahamu, basi ndio
hivyo hivyo walivyotofautishwa Ibn Adam wengine na Mitume na Manabii kwani
Nafsi na Roho za Mitume na Manabii hutofautiana na za watu wa kawaida kwa
sababu wao hua ni waliopewa Uongofu na Ufahamu wenye kuongoka zaidi tofauti
na watu wengine, kwani Uongofu wao huwaongoza katika njia ya Allah Subhanah
wa Taála. Kama vile ilivyokua mwendo wa kutembea wa Ibn Adam kua ni tofauti
na ni Miujiza kwa Wanyama wengine basi ndio hivyo hivyo inavyokua kwa miendo
ya Mitume kuelekea kwa Mola wao kwani miendo yao hua ni tofauti na ni Miujiza
kwa Ibn Adam wengine.

Hivyo kushushiwa kwa Mitume na Manabii kwa watu hua ni Rehma kubwa sana kutoka
kwa Allah Subhanah wa Ta’ala. Tukiangalia historia ya Ulimwengu tunaona kua
ustaarabu Ulimwenguni ulianzia katika maeneo ya Mashariki ya kati baina ya nchi za
Misri, Syria, Iraq na Uarabuni, na hii ni kwa sababu maeneo hayo ndio maeneo ambayo
117

yalikua na idadi kubwa ya jamii za watu katika kipindi cha mwanzoni mwa maisha ya
Ulimwenguni kuliko maeneo mengine, hivyo idadi hiyo kubwa ya jamii za watu
waliokua wakiishi katika maeneo hayo kulipelekea kutumiwa kwa Mitume na Manabii
wengi katika maeneo hayo.

Mitume na Manabii hao walikua na miongoni mwa wenye sifa kuu zifuatazo:

1. Mitume na Manabii walitoka miongoni mwa Bani Adam, hawakutoka miongoni


mwa Majini au Malaika.

2. Mitume na Manabii walikua na sifa za uaminifu, ukweli, kutokufanya dhambi.


Hua hivi ili madai yao yakubaliwe na kupandishwa darja ya juu.

3. Mitume na Manabii walikua na sifa za kua na ufahamu uliokamilia, uhakika na


uongofu.

4. Mitume na Manabii walikua ni lazima wafikishe kwa watu wao ujumbe wote wa
Wahyi walioamriwa kuufikisha, hawakuficha kitu chochote.

5. Mitume na Manabii walikua ni Wanaume.

Ama kuhusiana na sifa ya tano, basi kuna kutofautiana kuhusiana na mtizamo wa


waliopewa Unabii kua ni Wanaume tu, kwani kwa mtizamo wa Wanazuoni
wanaofuata mitizamo ya Aqida ya Maturidi basi wao wanaosema kua waliopewa
Utume walikua ni Wanaume tu.

Ama kwa upande wa Wanazuoni wanaofuata mtizamo wa Aqida ya Ashari basi wao
wanasema kua miongoni mwa waliopewa Unabii walikuemo pia Wanawake.

Kwa upande wa wafuasi wa Maturidi ambao ndio wanaosema kua waliopewa Unabii
walikua ni wanaume tu, basi wao wanasimamia katika uthibitisho wa aya ambayo
imetumia neno “Rijalan”, ambapo kwa mtizamo wao basi ni kua neno hilo hua
linamaaisha kua ni Mwanamme, aya hio ni ile isemayo kua:

َ‫ﺎﺳﺌَـﻠُﻮاْ أ َْﻫ َﻞ اﻟ ِّﺬ ْﻛ ِﺮ إِن ُﻛﻨﺘُ ْﻢ ﻻ‬ ِ


ْ َ‫ﻚ إِﻻﱠ ِر َﺟﺎﻻً ﻧﱡﻮﺣﻰ إِﻟَْﻴ ِﻬ ْﻢ ﻓ‬
َ َ‫﴿وَﻣﺂ أ َْر َﺳ ْﻠﻨَﺎ ﻗَـْﺒـﻠ‬
َ
﴾‫ﺗَـ ْﻌﻠَ ُﻤﻮ َن‬
118

Wama arsalna qablaka illa rijalan noohee ilayhim fais-aloo ahla aldhdhikri in
kuntum la taAAlamoona. (Surat al-Anbiya 21:7)

Tafsir: Na hatukutuma kabla yako Rijalan yeyote isipokua watu ambao


tuliwahamasisha, hivyo uliza wenye kujua ikiwa wewe hujui.

Lakini hata hivyo miongoni mwa Wanazuoni wenye I’lm ya Tafsir ambao ni wafuasi wa
Aqida ya Ashari wanasema katika kutafsiri aya hii kua neno 'Rijalan’, lililotumika hapa
linajumuisha Wanaume na Wanawake, hivyo miongoni mwa Manabii pia wapo Manabii
wanawake. Miongoni mwa Wanazuoni wenye mtizamo huo ni pamoja na Imam Abu
Hasan Al Ashari, Imam Fakhr Ad Din Al Razi (Katika Al Durr Al Mukhtari), Imam Al
Suyuti (Katika kitabu chake cha Al Ashbah wal Nazair), Imam Kamal al Humam (katika
kitabu cha Husun al Uswah), Imam Ibn Hazm, Imam Al Mubarkafuri (katika kitabu cha
Tuhfat al Awhathi) n.k.

Wanazuoni hao wanasimamia katika hoja ya vithibitisho ambavyo miongoni mwao ni


pamoja na pale Allah Subhanahu wa Ta’ala aliposema kuhusiana na Yuhanz ambae ni
mama yake Nabii Musa kua: ‘Na tukamshushia Wahyi mama yake Musa’, katika Surat
Al Qasas isemayo:

‫ﺖ َﻋﻠَْﻴ ِﻪ ﻓَﺄَﻟْ ِﻘ ِﻴﻪ ِﰱ ٱﻟﻴَِّﻢ َوﻻَ َﲣَ ِﺎﰱ‬


ِ ‫﴿وأَوﺣﻴـﻨَﺂ إِ َ ٰﱃ أُِم ﻣﻮﺳﻰ أَ ْن أَر ِﺿﻌِ ِﻴﻪ ﻓَِﺈ َذا ِﺧ ْﻔ‬
ْ َٰ ُّ َْ ْ َ
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ِ ِ ‫وﻻَ َْﲢﺰِ ۤﱐ إِ ﱠ� رآ ﱡدوﻩ إِﻟَﻴ‬
َ ‫ﻚ َو َﺟﺎﻋﻠُﻮﻩُ ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻤْﺮ َﺳﻠ‬ ْ ُ َ َ َ
Waawhayna ila Ummi Moosa an ardhiAAeehi fa-idha khifti AAalayhi faalqeehi fee
alyammi wala takhafee wala tahzanee inna raddoohu ilayki wajaAAiloohu mina
almursaleena (Surat Al Qasas 28:7)

Tafsir: Na tukamshushia Wahyi mama yake Musa (kumwambia): ‘Mnyonyeshe


(Musa), lakini ikiwa utakhofia juu yake, basi mtie mtoni na wala usiwe na khofu yeyote
wala huzuni. Kwani kwa hakika sisi tutamrudisha kwako wewe na tutamfanya kua ni
miongoni mwa Mitume yetu’.

Na uthibitisho uliomo katika Surat Maryam, pale Allah Subhanahu wa Ta’ala aliposema:
119

‫ت ِﻣﻦ‬ ‫ت ِﻣﻦ أ َْﻫﻠِﻬﺎ ﻣ َﻜﺎ�ً َﺷﺮﻗِﻴﺎً ۞ ﻓَ ﱠ‬ ِِ ِ ِ


ْ ‫ﭑﲣَ َﺬ‬ ْ َ َ ْ ْ ‫﴿ َوٱذْ ُﻛْﺮ ِﰱ ٱﻟْﻜﺘَﺎب َﻣْﺮَﱘَ إذ ٱﻧﺘَـﺒَ َﺬ‬
ُ‫ﺖ إِِّ ۤﱐ أَﻋُﻮذ‬ ْ َ‫ﱠﻞ َﳍَﺎ ﺑَ َﺸﺮاً َﺳ ِﻮّ�ً ۞ ﻗَﺎﻟ‬
‫ﺜ‬ ‫ﻤ‬‫ﺘ‬
َ ‫ـ‬
َ‫ﻓ‬
َ َ َ ُ َ‫ﺎ‬‫ﻨ‬
َ ‫وﺣ‬ ‫ر‬ ‫ﺂ‬ ‫ﻬ‬ ‫ـ‬‫ﻴ‬
َْ‫ﻟ‬ِ‫إ‬ ‫ﺂ‬َ‫ﻨ‬‫ﻠ‬ْ ‫ﺳ‬‫َر‬
‫ﺄ‬
َْ َ‫ﻓ‬
َ ‫ﺎﺑ‬
ً ‫ﺎ‬‫ﺠ‬ ‫ﺣ‬ِ ‫دو�ِِﻢ‬
ُ
﴾ً‫ﻚ ﻏُﻠَـﻤﺎً َزﻛِﻴّﺎ‬ ِ َ‫ﻚ ﻻًّﻫﺐ ﻟ‬
َ َ ّ‫ﻮل َرﺑ‬
ِ ِ ُ ‫ﺎل إِﱠﳕَﺂ أ ََ�ْ رﺳ‬
َُ َ َ‫ﻨﺖ ﺗَِﻘﻴّﺎً ۞ ﻗ‬ َ ‫ﻨﻚ إِن ُﻛ‬ َ ‫ﺑِﭑﻟﱠﺮ ْﲪَـٰ ِﻦ ِﻣ‬
Waodhkur fee alkitabi maryama idhi intabadhat min ahliha makanan sharqiyyan;
Faittakhadhat min doonihim hijaban faarsalna ilayha roohana fatamaththala laha
basharan sawiyyan; Qalat innee aAAoodhu bialrrahmani minka in kunta taqiyyan;
Qala innama ana rasoolu rabbiki li-ahaba laki ghulaman zakiyyan (Surat Maryam
19:16-19)

Tafsir: Na ametajwa katika kitabu, Maryam, wakati alipojitenga na familia yake katika
sehemu inayoelekea upande wa Mashariki; Akaweka pazia kabla yao, kisha
tukamtumia Ruhi (Malaika) wetu alietokea mbele yake katika umbo la mtu aliejaa
heshima; Nae akasema: ‘Hakika mimi ninajilinda kwako na kwa Mwingi wa Rehma,
ikiwa unamuogopa Allah’; Nae (Malaika) akasema: ‘Mimi ni mjumbe kutoka kwa
Mola wako, (kukupa habari ya kua) utapata mtoto alie mwema’.

Kwani Allah Subhanahu wa Ta’ala alimchagua Maryam bint Imran na akamuamrisha


Malaika Jibril Alayhi Salaam kumshushia Wahyi wa kumbashiria habari njema kama
inavyofafanuliwa zaidi katika Surat Al Imran kwa kusema:

ِ ‫ﺎك ﻋﻠَﻰ ﻧِﺴ‬


‫ﺂء‬ ِ ِ ِ ‫ﺖ ٱﻟْ َﻤﻼَﺋِ َﻜﺔُ ٰﳝَْﺮَﱘُ إِ ﱠن ﱠ‬
ِ َ‫﴿وإِ ْذ ﻗَﺎﻟ‬
َ ٰ َ ‫ٱﺻﻄََﻔ‬
ْ ‫ٱﺻﻄََﻔﺎك َوﻃَ ﱠﻬَﺮك َو‬
ْ َ‫ٱﻪﻠﻟ‬ َ
﴾‫ﲔ‬ ِ
َ ‫ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬
Wa-idh qalati almala-ikatu ya Maryamu inna Allaha istafaki watahharaki
waistafaki AAala nisa-i alAAalameena (Surat Al Imran 3:42)

Tafsir: Na (kumbuka) wakati Malaika aliposema: ‘Ewe Maryam! Kwa Hakika Allah
amekuchagua wewe na kukutakasa, na kukuchagua kua juu zaid ya Wanawake wote
wa Ulimwenguni’.

Na vile vile pale Allah Subhanahu wa Ta’ala alipomjumuisha Maryam bint Imran ambae
ni mama yake Nabii Isa katika hali ambayo amewajumuisha Manabii wengine kwa
kusema katika Surat Al Imran:
120

﴾‫ﲔ‬ ِ ِ َ ‫آل إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ و‬ ‫﴿إِ ﱠن ﱠ‬


َ ‫آل ﻋ ْﻤَﺮا َن َﻋﻠَﻰ ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬ َ َ َ ْ َ ‫آد َم َوﻧُﻮﺣﺎً َو‬
َ ‫ٱﺻﻄََﻔ ٰﻰ‬
ْ َ‫ٱﻪﻠﻟ‬
Inna Allaha istafa adama wanoohan waala ibraheema waala AAimrana AAala
alAAalameena (Surat Al Imran 3:33)

Tafsir: Hakika Allah amemchagua Adam, Nuh, familia ya Ibrahim na familia ya


Imran kua juu ya Alamin (Majini na Bani Adam wa wakati huo).

Na pia katika Surat Maryam pale Allah Subhanahu wa Ta’ala aliposema:

ٍ ُ‫ءاد َم َوِﳑ ْﱠﻦ َﲪَْﻠﻨَﺎ َﻣ َﻊ ﻧ‬


‫ﻮح‬ ِ
َ ‫ﲔ ﻣﻦ ذُِّرﻳﱠﺔ‬
ِ ِ‫ٱﻪﻠﻟ ﻋﻠَﻴ ِﻬﻢ ِﻣﻦ ٱﻟﻨﱠﺒِﻴ‬
َْ ّ َ ّ ْ َ ُ‫ﻳﻦ أَﻧْـ َﻌ َﻢ ﱠ‬
َ َ
ِ ‫﴿أُوﻟَـٰﺌِﻚ ٱﻟﱠ‬
‫ﺬ‬
ِ ْ ‫وِﻣﻦ ذُ ِرﻳﱠِﺔ إِﺑْـﺮ ِاﻫﻴﻢ وإِ ْﺳﺮاﺋِﻴﻞ وِﳑﱠﻦ َﻫ َﺪﻳْـﻨَﺎ و‬
‫ت ٱﻟﱠﺮ ْﲪَـٰ ِﻦ‬ َ ‫ٱﺟﺘَـﺒَـْﻴـﻨَﺂ إ َذا ﺗُـْﺘـﻠَ ٰﻰ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ‬
ُ �‫آ‬ َ ْ ََ َ ََ َ ّ َ
﴾ً‫َﺧﱡﺮواْ ُﺳ ﱠﺠﺪاً َوﺑُ ِﻜﻴّﺎ‬
Ula-ika alladhina anAAama Allahu AAalayhim mina alnnabiyyeena
min dhurriyyati adama wamimman hamalna maAAa noohin wamin dhurriyyati
ibraheema wa-isra-eela wamimman hadayna waijtabayna idha tutla AAalayhim
ayatu alrrahmani kharroo sujjadan wabukiyyan (Surat Maryam 19:58)

Tafsir: Wao ni wale ambao Allah amewaneemesha kutoka katika miongoni mwa
Mitume, kutoka katika kizazi cha Adam, na wale tuliowachukua pamoja na Nuh, na
miongoni mwa kizazi cha Ibrahim na Israel na miongoni mwa wale tuliowaongoza na
kuwachagua. Wakati aya za mwenye wingi wa Rehma zinaposomwa, husujudu na
kulia.

Ambapo miongoni mwa kizazi cha Adam ni Idris, na miongoni mwa wale tuliowachukua
pamoja na Nuh katika Safina ni kizazi cha wazee waliomtoa Nabii Ibrahim, na miongoni
mwa kizazi cha Ibrahim ni Is-haq, Yaqub na Ismai’l na miongoni mwa Bani Israel ni
Mama yake Musa, Musa, Harun, Zakariyah, Yahya, Maryam na Isa Ibn Maryam.

Wanazuoni wanasema kua katika wanawake hao pia yumo Hawa mke wa Nabii Adam,
na vile vile Sarah aliekua mke wa Nabii Ibrahim, kama ilivyoelezewa katika Qurán kwa
kutumia njia ya kauli ya Sarah pale alipozungumza na Malaika walipokuja kumtembelea
Nabii Ibrahim na yeye akiwepo na kuwabashiriwa mtoto kama inavyoelezewa katika aya
ifuatayo:
121

ِ ِ ِ ِ
۞ ‫ﻴﺐ‬ ٌ ‫ﻮز َوَﻫـ َﺬا ﺑَـ ْﻌﻠﻰ َﺷْﻴ ًﺨﺎ إ ﱠن َﻫـ َﺬا ﻟَ َﺸ ْﻰءٌ َﻋﺠ‬ ٌ ‫ﺖ ٰﻳـ َﻮﻳْـﻠَﺘَﺎ ءَأَﻟ ُﺪ َوأ ََ�ْ َﻋ ُﺠ‬
ْ َ‫﴿ﻗَﺎﻟ‬
﴾‫ﲪﻴ ٌﺪ ﱠِﳎﻴ ٌﺪ‬
َِ ‫ﺖ إِﻧﱠﻪ‬
ِ ِ‫ٱﻪﻠﻟِ ر ْﲪﺔُ ﱠ‬ ِ ِ‫ﻗَﺎﻟُ ۤﻮاْ أَﺗَـﻌﺠﺒ‬
ُ ‫ٱﻪﻠﻟ َوﺑـََﺮَﻛﺎﺗُﻪُ َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ أ َْﻫ َﻞ ٱﻟْﺒَـْﻴ‬ َ َ ‫ﲔ ﻣ ْﻦ أ َْﻣ ِﺮ ﱠ‬ َ َْ
Qalat ya waylata aalidu waana AAajoozun wahadha baAAlee shaykhan inna hadha
lashay-on Aaajeebun; Qaloo ataAAjabeena min amri Allahi rahmatu Allahi
wabarakatuhu AAalaykum ahla albayti innahu hameedun majeedun (Surat Hud
11:72-73)

Tafsir: Akasema (kwa kushangaa) ‘Ole wangu! Nitapata mtoto wakati mimi ni
kikongwe, na huyu hapa mume wangu ni kizee’. Nao (Malaika) wakasema: ‘Unaona
ajabu juu ya yale aliyoyakadiria Allah? Rehma za Allah na Baraka zake ziwe juu yenu,
Enyi familia ya Ibrahim. Hakika yeye (Allah) Mwenye kustahiki sifa zote na mwenye
Kushinda.’

Na pia habari hiyo kuelezewa kwa njia ya kuonesha picha ya vitendo katika Surat Adh
Dhuriyyat:

ْ‫ﻮز َﻋ ِﻘ ٌﻴﻢ ۞ ﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻗَﺎﻟُﻮا‬


ٌ ‫ﺖ َﻋ ُﺠ‬ ْ ‫ﺼ ﱠﻜ‬
ْ َ‫ﺖ َو ْﺟ َﻬ َﻬﺎ َوﻗَﺎﻟ‬ َ َ‫ﺻﱠﺮةٍ ﻓ‬
ِ
َ ‫﴿ﻓَﺄَﻗْـﺒَـﻠَﺖ ْٱﻣَﺮأَﺗُﻪُ ِﰱ‬
﴾‫ٱﳊَ ِﻜ ُﻴﻢ ٱﻟْ َﻌﻠِ ُﻴﻢ‬
ْ ‫ﻚ إِﻧﱠﻪُ ُﻫ َﻮ‬ ِ ‫ﺎل رﺑﱡ‬ ِ ِٰ
َ َ َ‫َﻛﺬﻟﻚ ﻗ‬
Faaqbalati imraatuhu fee sarratin fasakkat wajhaha waqalat AAajoozun
Aaaqeemun; Qaloo kadhaliki qala rabbuki innahu huwa alhakeemu alAAaleemu
(Surat Adh Dhuriyyat 51:29-30)

Tafsir: Kisha Mke wake (Sarah) akakabiliana nao, na akajipiga vibao usoni na
kusema: ‘Kikongwe alie Mgumba!’. Nao (Malaika) wakasema: ‘Kadhalika hivyo
ndivyo asemavyo Mola wako. Hakika yeye ni mwingi wa Hikma, na ni Mjuzi wa kila
kitu.’

Na miongoni mwa Wanawake hao pia ni pamoja na Asiyah Bint Muzahim aliekua mke
wa Fir’awn, kutokana na kua ni mfano bora miongoni mwa wenye kuamini kama
isemavyo Qurán:
122

‫ب ٱﺑْ ِﻦ ِﱃ ِﻋﻨ َﺪ َك ﺑَـْﻴﺘﺎً ِﰱ‬ ِ ِِ


ِّ ‫ﺖ َر‬ ْ َ‫ﻳﻦ َآﻣﻨُﻮاْ ْٱﻣَﺮأََة ﻓْﺮ َﻋ ْﻮ َن إِ ْذ ﻗَﺎﻟ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻣﺜَﻼً ﻟّﻠﱠﺬ‬
‫ب ﱠ‬ َ ‫ﺿَﺮ‬
َ ‫﴿ َو‬
ِِ ِ ِ ِ ِِ ِ ِ ِ ِْ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ٱﳉَﻨﱠﺔ َوَﳒِّﲎ ﻣﻦ ﻓْﺮ َﻋ ْﻮ َن َو َﻋ َﻤﻠﻪ َوَﳒِّﲎ ﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻘ ْﻮم ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
Wadharaba Allahu mathalan lilladheena amanoo imraata firAAawna idh qalat
rabbi ibni lee AAindaka baytan fee aljannati wanajjinee min firAAawna
waAAamalihi wanajjinee mina alqawmi aldhdhalimeena. (Surat At Tahrim 66:11)

Tafsir: Na Allah anatoa mfano kwa wale walioamini: Mke wa Fir’awn, pale
aliposema: ‘Mola wangu! Nijengee mimi nyumba kwako wewe Peponi, na uniokoe
kutokana na Fir’awn na amali zake, niokoe kutokana na watu madhalimu’

Ambapo aya inayofuatia baada ya hiyo (Surat At Tahrim 66:12) inamsifia tena Maryam
Bint Imran. Hivyo kutokana na vithibitisho vyao hivyo tunaona kua Wanawake pia kama
Wanaume hua na sifa na uwezo wa kua miongoni mwa wenye kupokea Wahyi na hivyo
hua kuna uwezekano wa kua Manabii na vile vile kua ni miongoni mwa mifano bora
inayofaa kuigwa, ingawa hawakutajwa kua na Unabii kwa majina, kwani Allah
Subhanahu wa Ta’ala anasema kua kuna Mitume aliowataja majina na kuhadithia visa
vyao katika Qurán na vile vile pia kuna Mitume na Manabii ambao hakuwataja kwa
majina katika Qurán, kama inavyoelezea aya ifuatayo:

‫ﲔ ِﻣﻦ ﺑَـ ْﻌ ِﺪﻩِ َوأ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إِ َ ٰﱃ إِﺑْـَﺮِﻫ َﻴﻢ‬ ٍ ُ‫ﻚ َﻛ َﻤﺂ أ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إِ َﱃ ﻧ‬
َ ِّ‫ﻮح َوٱﻟﻨﱠﺒِﻴ‬ َ ‫﴿إِ ﱠ� أ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إِﻟَْﻴ‬
ِ ِ ‫وإِ ْﲰـﻌِﻴﻞ وإْﺳﺤـﻖ وﻳـﻌ ُﻘﻮب و ْاﻷ‬
‫ﺲ َوَﻫ ُـﺮو َن َو ُﺳﻠَْﻴ َﻤ َـﻦ‬ َ ُ‫ﻮب َوﻳُﻮﻧ‬ َ ‫ﻴﺴ ٰﻰ َوأَﻳﱡ‬ َ ‫َﺳﺒَﺎط َوﻋ‬ ْ َ َ ْ ََ َ َ ْ َ َ َ َ
ِ َ ‫وءاﺗَـﻴـﻨَﺎ داوود زﺑﻮراً ۞ ورﺳﻼً ﻗَ ْﺪ ﻗَﺼﺼﻨَـﻬﻢ ﻋﻠَﻴ‬
‫ﺼ ُﻬ ْﻢ‬ْ‫ﺼ‬ ُ ‫ﻚ ﻣﻦ ﻗَـْﺒ ُﻞ َوُر ُﺳﻼً ﱠﱂْ ﻧَـ ْﻘ‬ ْ َ ُْ ْ َ ُ َُ َُ َ ُ َ ْ َ َ
ِ ‫ﻳﻦ ﻟِﺌَﻼﱠ ﻳَ ُﻜﻮ َن ﻟِﻠﻨ‬
‫ﱠﺎس‬ ِِ
َ ‫ﻳﻦ َوُﻣﻨﺬر‬
ِ ِ
َ ‫ﻮﺳﻰ ﺗَ ْﻜﻠﻴﻤﺎً ۞ ﱡر ُﺳﻼً ﱡﻣﺒَ ّﺸ ِﺮ‬ ‫ﻚ َوَﻛﻠﱠ َﻢ ﱠ‬
َ ‫اﻪﻠﻟُ ُﻣ‬ َ ‫َﻋﻠَْﻴ‬
﴾ً‫ٱﻪﻠﻟُ َﻋ ِﺰﻳﺰاً َﺣ ِﻜﻴﻤﺎ‬ ‫ٱﻪﻠﻟِ ُﺣ ﱠﺠﺔٌ ﺑَـ ْﻌ َﺪ اﻟﱡﺮ ُﺳ ِﻞ َوَﻛﺎ َن ﱠ‬ ‫َﻋﻠَﻰ ﱠ‬
Inna awhayna ilayka kama awhayna ila noohin waalnnabiyyeena min baAAdihi
waawhayna ila ibraheema wa-ismaAAeela wa-ishaqa wayaAAqooba waal-asbati
waAAeesa waayyooba wayoonusa waharoona wasulaymana waatayna dawooda
zabooran; Warusulan qad qasasnahum AAalayka min qablu warusulan lam
naqsus-hum AAalayka wakallama Allahu moosa takleeman; Rusulan
123

mubashshireena wamundhireena li-alla yakoona lilnnasi AAala Allahi hujjatun


baAAda alrrusuli wakana Allahu AAazeezan hakeeman (Surat An Nisaa 4:163-165)

Tafsir: Hakika tumekushushia Wahyi wewe kama vile tulivyomshushia Nuh na


Manabii waliofuata baada yake. Na pia tulimshushia Wahyi Ibrahim, Isma`il, Ishaq,
Ya`qub, na Al-Asbat (kizazi cha watoto 12 wa Nabii Ya`qub) `Isa, Ayyub, Yunus,
Harun, na Sulayman; na Daud tukampa Zabur. Na Mitume ambayo tumekutajia wewe
kabla, na Mitume ambayo hatukukutajia, na Musa aliezungumza moja kwa moja na
Allah. Mitume kama wabebaji ujumbe mwema na maonyo pia, ili watu wawe hawana
kisingizio baada ya (kutumiwa) Mitume. Hakika Allah ni mwenye uwezo na ni mwingi
wa Hikma.

Na vile vile akasema tena Allah Subhanah wa Taála:

ِ َ ‫ﻚ ِﻣْﻨـﻬﻢ ﱠﻣﻦ ﻗَﺼﺼﻨَﺎ ﻋﻠَﻴ‬ ِ ِ


‫ﺺ‬
ْ ‫ﺼ‬ُ ‫ﻚ َوﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ ﱠﻣﻦ ﱠﱂْ ﻧَـ ْﻘ‬ َْ ْ َ ُ َ ‫﴿ َوﻟََﻘ ْﺪ أ َْر َﺳ ْﻠﻨَﺎ ُر ُﺳﻼً ّﻣﻦ ﻗَـْﺒﻠ‬
ِ ُ‫ٱﻪﻠﻟِ ﻗ‬
‫ﻀ َﻰ‬ ‫ٱﻪﻠﻟِ ﻓَِﺈ َذا َﺟـﺂءَ أ َْﻣُﺮ ﱠ‬ ٍ ‫ﻚ وﻣﺎ َﻛﺎ َن ﻟِﺮﺳ‬
‫ﻮل أَن َ�ْﺗِ َﻰ ِﺂﺑﻳٍَﺔ إِﻻﱠ ﺈﺑِِ ْذ ِن ﱠ‬ َُ َ َ َ ‫َﻋﻠَْﻴ‬
﴾‫ﻚ ٱﻟْ ُﻤْﺒ ِﻄﻠُﻮ َن‬ ِ
َ ‫ﭑﳊَِّﻖ َو َﺧ ِﺴَﺮ ُﻫﻨَﺎﻟ‬ْ ِ‫ﺑ‬
Walaqad arsalna rusulan min qablika minhum man qasasna AAalayka waminhum
man lam naqsus AAalayka wama kana lirasoolin an ya/tiya bi-ayatin illa bi-ithni
Allahi fa-itha jaa amru Allahi qudhiya bialhaqqi wakhasira hunalika almubtiloona
(Surat Al Ghafir 40:78)

Tafsir: Na kwa hakika sisi tulituma Mitume kabla yako (Ewe Muhammad), ambapo
baadhi yao tumekuhadithia juu yao na baadhi yao hatukuhadithia juu yao, na
haikuwahi kutokea kwa Mtume yeyote yule kupewa aya zetu isipokua kwa idhini ya
Allah, Hivyo inapokuja amri ya Allah basi jambo hilo litaamuliwa kwa haki na
wataofuata vyenginevyo watakua ni waliopotea.

Ama kwa upande mwengine basi Abu Dhar Radhi Allahu Anhu anasema kuhusiana na
idadi ya Mitume na Manabii katika hadith ifuatayo ambayo ni ndefu kidogo lakini yenye
mafunzo mengi ndani yake kua: ‘Siku moja niliingia Msikitini nikamkuta Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam akiwa amekaa peke yake. Hivyo nikamuuliza: ‘Ya Rasul
Allah (Salallahu Alayhi wa Salam) Niambie kuhusiana na Ibada ya Sala ambazo
umetuamrisha?’
124

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Sala ni Ibada bora. Hivyo Sali kwa
wingi zaid kwa kadiri utakavyoweza’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee Ibada ipi ni Bora zaid?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Kumuamini Allah na kupigana


Jihad kwa ajili yake.’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee ni yupi Mumuumini bora?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Muumini bora ni yule alie m-bora
katika tabia zake’

Abu Dhar akauliza; ‘Jee ni Muumini yupi aliekua salama?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Muumini alie salama ni yule ambae
Waislamu wenzake watakua salama kutokana na ulimi wake’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee Ni yupi Muhajirina (Mhamiaji) bora?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Mhamiaji bora ni yule alie yahama
maovu yake’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee ni Sala ipi ndio Bora?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Sala bora ni ile yenye Kisimamo
Kirefu’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee ni Funga ipi ndio Bora?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Funga bora ni Funga za FArdhi
ambazo zinazolipwa kikamilifu. Kwani Allah hutoa Malipo makubwa zaid’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee Kafara ipi ndio bora zaidi?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Ya yule aliechinja na kuimwaga
damu kwa mikono yake’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee Kuachia huru kuopi ndio bora zaid?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Mtumwa alie ghali kuliko wote na
alie m-bora kwa watu wake’
125

Abu Dhar akauliza: ‘Jee Sadaka ipi ndio bora zaidi?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Yenye jitihada za asiekua na kitu
na yenye kutolewa kwa siri kwa mwenye shida’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee ni ipi aya yenye uzito zaidi uliyowahi kushushiwa?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Ayat Al Kursiy’ kisha Rasul Allah
Salallahu Aályhi wa Salam akaongezea kwa kusema: ‘Abu Dhar! Mbingu 7 si chochote
mbele ya Ayat Kursy bali ni kama chembe ya mchanga katika sehemu ya Ardhi na
Kursy si chochote mbele ya Arshi bali ni chembe ya mchanga katika sehemu ya
ardhi’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee Kuna Mitume Mingapi?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Manabii 124000’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee ni wangapi miongoni mwao walikua ni Mitume?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Mitume 313, wengi sana na
wazuri sana’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee ni Nabii gani wa Mwanzo?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Nabii Adam’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee nae alikua ni Mtume pia?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Naam, Allah alimuumba kwa
mikono yake, kisha akampulizia Roho yake, na akamuweka sawasawa’, kisha Rasul
Allah Salallahu A’layhi wa Salam akaongezea kwa kusema: ‘Abu Dhar! Wanne
miongoni mwao walikua ni Wasyria: Adam, Shith, Idris ambae ndie wa kwanza
kuandika kwa Kalamu na Nuh. Wanne miongoni mwao walikua ni Waarabu: Hud,
Shuayb, Salih na Mtume wako (Rasul Allah Salallahu Aályhi wa Salam). Ya Abu
Dhar! Mtume wa Mwanzo miongoni mwa Bani Israil ni Musa na wa Mwisho ni Isa,
Mtume wa Mwanzo ni Adam na wa Mwisho ni Muhammad.’

Abu Dhar akauliza: ‘Ya Rasul Allah! Jee Allah ameshusha vitabu vingapi?’
126

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Vitabu 104: Kwa Shith 50, kwa
Idris 30, kwa Ibrahim 10, kwa Musa 10 kabla ya kumshushia Tawrat, na kisha
akashusha Tawrat, Zabur, Injil na Furqan.’
Abu Dhar akauliza: ‘Jee mlikua mna nini katika Suhufi Ibrahima?’ (Maandiko ya
Nabii Ibrahim)

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Visa vyenye mafunzo na Wasia
kama vile: ‘Enyi Wenye Kibr! Wafalme wenye kufanya dhulma, sikukuchagueni
nyie mjikusanyie mali, nimekuchagueni ili msimamie matatizo ya wenye
kudhulumiwa, mimi mwenyewe sikatai maombi ya mwenye kudhulumiwa, hata
kama aliefanyiwa dhulma huyo atakua ni mtu asieniamini’ na ‘Mtu mwenye akili
huugawa mda wake katika sehemu zifuatazo: Sehemu moja kwa ajili ya
kuwasiliana na Mola wake ambapo ndani yake atachukua sehemu ya amali zake,
Sehemu nyengine kwa ajili ya kutafakari uumbaji wa Allah Subhanah wa Taála, na
sehemu nyengine kwa ajili ya kujitafutia riski yake. Na mtu mwenye akili
hajishughulishi isipokua katika mambo matatu: Matayarisho kwa ajili ya Akhera
yake, Kufanya kazi kwa kujitafutia Riski yake na Kufurahia kile ambacho
hakijaharamishwa. Na mtu mwenye Ufahamu humbidi kuutumia vyema mda wake
kwa kujishughulisha na mambo yanayomhusu, kuulinda ulimi wake, kwani kila
anaegundua kua kauli zake ni sawa na vitendo vyake basi hatozungumza isipokua
mazungumzo yaliyo muhimu na kua na maana’’

Abu Dhar akauliza: ‘Na jee ni nini kilichoandikwa ndani ya Suhufi Musa?’(Maandiko
ya Nabii Musa)

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Ibar (Maneno yenye kuonya) kama
vile: ‘Inashangaza kwa yule mtu ambae ana uhakika wa kifo lakini akwa ni mwenye
kuzikimbilia anasa’’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee na sisi tunayo maneno kama hayo katika kitabu chetu?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Naam!’ Kisha Rasul Allah Salallahu
A’layhi wa Salam akasoma aya zifuatazo:

ْ ‫ﺼﻠﱠ ٰﻰ۞ ﺑَ ْﻞ ﺗُـ ْﺆﺛُِﺮو َن‬


۞‫ٱﳊَﻴَﺎةَ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ‬ ِ
َ َ‫ٱﺳ َﻢ َرﺑِّﻪ ﻓ‬
ْ ‫﴿ﻗَ ْﺪ أَﻓْـﻠَ َﺢ َﻣﻦ ﺗَـَﺰﱠﻛ ٰﻰ۞ َوذَ َﻛَﺮ‬
‫ﻒ إِﺑْـَﺮ ِاﻫ َﻴﻢ‬
ِ ‫ُوﱃ۞ ﺻﺤ‬
ُ ُ ٰ َ ‫ﺼ ُﺤﻒ ٱﻷ‬
ِ ‫ٱﻵﺧﺮةُ َﺧﻴـﺮ وأَﺑـ َﻘ ٰﻰ۞ إِ ﱠن َﻫـٰ َﺬا ﻟَِﻔﻰ ٱﻟ ﱡ‬
ْ َ ٌ ْ َ ‫َو‬
ِ
﴾‫ﻮﺳ ٰﻰ‬َ ‫َوُﻣ‬
127

Qad aflaha man tazakka; Wadhakara isma rabbihi fasalla; Bal tu/thiroona
alhayata alddunya; Waal-akhiratu khayrun waabqa; Inna hadha lafee alssuhufi al-
oola; Suhufi ibraheema wamoosa(Surat Al Aála 87:14-19)

Tafsir: Ama kwa hakika amefuzu yule anaejitakasa, Na akalikumbuka jina la Mola
wake na kisha akasali. Lakini nyinyi mnakumbatia maisha ya Dunia. Ijapokua maisha
ya akhera ni bora na yenye kudumu zaidi. Hakika haya yametajwa katika Suhufi
zilizotangulia, Suhufi za Ibrahim na Musa.(Al Anwaa wa Al Taksim Al Hafidh Imam
Abu Hatim Abd Rahman Muhammad Ibn Idris Al Razi Ibn Hibban Al Basti)

Ama kuhusiana na aya hizi 5 za Surat Al Aála, basi anasema Ikrimah kua: ‘Qad aflaha
man tazakka – Kwa hakika amefuzu yule aliejitakasa, ambapo aliefuzu kwa
kujitakasa ni yule ambae ni mwenye kumpwekesha Allah Subhanah wa Taála tu.’

Na akasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua kua: ‘Wadhakara isma
rabbihi – ‘Na akilikumbuka jina la Mola wake’ - hua kunamaanisha ukamilifu
unaopatikana ndani ya Nafsi ya mtu kutokana na kumjua Allah Subhanah wa
Taála. Na neno fasalla ‘Na kisha akasali’ basi linamaanisha Ukamilivu wa Mwili na
viungo vyake katika kumtii Mola wake’

Ama kuhusiana na ‘Bal tu/thiroona alhayata alddunya; Waal-akhiratu khayrun


waabqa’- basi amesema Muhaqiq Al Faqih Imam Shihab Ad Din Abu Abbas Ahmad
Ibn Muhammad Ibn Ali Ibn Hajar Al Haytami Al Makki Al Shafii kua: Amesema
Abu Musa Al Ashari kua amesema Rasul Allahi Salalahu A’layhi wa Salam kua:
‘Yeyote yule anaeipenda Dunia hii basi ataidhuru Akhera yake, na yeyote yule
anaeipenda Akhera yake basi ataidhuru Dunia hii, hivyo mnatakiwa muipendelee
Akhera yenu ambayo ni ya kudumu dhidi ya Dunia hii ambayo ni ya mpito.’

Na akasema Malik Ibn Dinar kua: ‘Kama ingekua Dunia hii ni Dhahabu lakini ni
yenye kupita na kutoweka na Akhera ni Tambara bovu lenye kudumu, basi Akhera
inatakiwa ipewe kipaumbele zaidi, Jee hali itakuaje pale ambapo Dunia hii ni
Tambara bovu la mpito na Akhera ni Dhahabu ya Milele?’

Na juu ya ‘Inna hadha lafee alssuhufi al-oola; Suhufi ibraheema wamoosa’ - Basi
anasema Imam Al Shanqiti kua: ‘Maneno haya yanaonesha kua Ibar – Maonyo ni
maunganisho yanayounganisha Vitabu na Maandiko yaliyopita katika mnyororo
mmoja’

Baada ya ufafanuzi huo kuhusiana na maana, sifa na tofauti baina ya Mitume na Manabii
basi na tuangalie kuhusiana na dalili na alama za Mitume wa Allah Subhanahu wa Ta’ala
ambazo hujulikana pia kama Miujiza.
128

MAANA YA MIUJIZA.


Miujiza hua ni maajabu ya Allah Subhanahu wa Ta’ala ambayo hua yanavunja Sharia’h
za kawaida za kimaumbile kupitia katika njia au mikono ya Mitume wake, ili kuthibitisha
Uaminifu na Ukweli wa Mitume wake. Muujiza unaweza kua katika njia ya kauli kama
vile Qurán au kwa njia ya vitendo.

‘Allamah Muhammad Sarfaraz Khan Safdar anasema kua: ‘Kilugha neno Mu’jizat hua
linatokana na neno ‘Ajz (Ajizi, au kutokua na uwezo), ambalo ni kinyume na neno
Qudrah (uwezo), na ‘ta’ [ambayo ni tāʼ marbūṭah kwa kilugha na huashiria kua ni
herufi ya mwisho katika neno na hutamkwa kwa kuhemewa ‘-a’ bila ya ‘t’, kihistori
herufi hii ilikua ikitamkwa kama ‘ha’ na ndio maana ‘ta marbutah hua inaonekana
kama ‘ha’] iliyoko mwishoni mwa neno hilo hua inaonesha msisitizo. Neno Mu‘jizat
hua ni sifa kama lilivyo neno Ayah (Alama, Dalili), n.k. Ni Allah Subhanahu wa
Ta’ala ambae hutengeneza ‘Ajz (Ajizi) ndani ya Mu‘jizat na hivyo kiukweli ni kua
huwaondolea uwezo wale wanaopinga. Mu’jizat hua unatoka kwa Allah Subhanahu
wa Ta’ala pekee, lakini hupitia katika mikono ya Mtume. Mtume hua hana uwezo
juu ya Miujiza yake. (Hidayat al-Murtab Ila Tariq al-Sawab fi Tahqiq al-Mu’jizat)

Mujaddid ud Din Imam Al Ghazali anasema kuhusiana na Miujiza kua: ‘Sababu


inayofanya Mu‘jizat kua inadhihirisha ukweli wa Mitume, ni kua katika kila kitu
ambacho Bani Adam hawezi kukifanya au hawezi kutoa mfano wake basi hua ni
lazima kimefanywa na Allah. Kila jambo hili linapohusishwa na changamoto za
Mtume, basi hua kama Allah Subhanahu wa Ta’ala anathibitisha kwa kusema,
‘Hakika wewe ni wa Kweli.’’(Ihya ‘Ulum al-Din)

Mujaddid ud Din Imam Fakhr Al Din Razi anasema kuhusiana na Miujiza kua,
‘Kutokana na aya nyingi kua zinazounga mkono ukweli tuliouzungumzia basi
tunaona kua, wakati Allah Subhanahu wa Ta’ala alipozungumzia kuhusiana na
Makafiri kua walitaka Miujiza mingi mikubwa mikubwa (Al Mu’jizat Al Qakhirah)
kutoka kwake yeye, Allah Subhanahu wa Ta’ala alisema katika maelezo yake:

ٌ‫ﻚ َﺟﻨﱠﺔ‬ َ َ‫ﻮﻋﺎ ۞ أَْو ﺗَ ُﻜﻮ َن ﻟ‬ ِ ‫ﻚ َﺣ ﱠ ٰﱴ ﺗَـ ْﻔ ُﺠَﺮ ﻟَﻨَﺎ ِﻣ َﻦ ْاﻷ َْر‬
ً ُ‫ض ﻳَـْﻨـﺒ‬ َ َ‫﴿وﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻟَﻦ ﻧـﱡ ْﺆِﻣ َﻦ ﻟ‬
َ
‫ﻂ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤﺂءَ َﻛ َﻤﺎ‬َ ‫ﺐ ﻓَـﺘُـ َﻔ ِّﺠَﺮ ْاﻷَﻧْـ َﻬ َـﺮ ِﺧﻠَـﻠَ َﻬﺎ ﺗَـ ْﻔ ِﺠ ًﲑا ۞ أ َْو ﺗُ ْﺴ ِﻘ‬
ٍ َ‫ِّﻣﻦ ﱠِﳔ ٍﻴﻞ و ِﻋﻨ‬
َ
ۤ ِ‫زﻋﻤﺖ ﻋﻠَﻴـﻨﺎ ﻛِﺴ ًﻔﺎ أَو َﺄﺗْﺗِﻰ ﺑِ ﱠ‬
‫ﺖ ِّﻣﻦ‬ َ َ‫ﭑﻪﻠﻟ َوٱﻟْ َﻤﻼﺋِ َﻜ ِﺔ ﻗَﺒِﻴﻼً ۞ أ َْو ﻳَ ُﻜﻮ َن ﻟ‬
ٌ ‫ﻚ ﺑَـْﻴ‬ َ ْ َ َْ َ َ ْ َ َ
129

‫ﻚ َﺣ ﱠﱴ ﺗُـﻨَـِّﺰَل َﻋﻠَْﻴـﻨَﺎ ﻛِﺘَ ًﺎﺎﺑ ﻧـﱠ ْﻘَﺮءُﻩُ ﻗُ ْﻞ‬ ِِ ِ ٍ


َ ِّ‫ُز ْﺧُﺮف أ َْو ﺗَـْﺮﻗَ ٰﻰ ِﰱ اﻟ ﱠﺴ َﻤﺂء َوﻟَﻦ ﻧـﱡ ْﺆِﻣ َﻦ ﻟُﺮﻗﻴ‬
﴾ً‫ﻨﺖ إَﻻﱠ ﺑَ َﺸًﺮا ﱠر ُﺳﻮﻻ‬ ُ ‫ُﺳْﺒ َﺤ َـﻦ َرِّﰉ َﻫ ْﻞ ُﻛ‬
Waqaloo lan nu/mina laka hatta tafjura lana mina al-Ardhi yanbooAAan; Aw
takoona laka jannatun min nakheelin waAAinabin fatufajjira al-anhara khilalaha
tafjeeran; Aw tusqita alssamaa kama zaAAamta AAalayna kisafan aw ta/tiya
biAllahi waalmala-ikati qabeelan; Aw yakoona laka baytun min zukhrufin aw tarqa
fee alssama-i walan nu/mina liruqiyyika hatta tunazzila AAalayna kitaban
naqraohu qul subhana rabbee hal kuntu illa basharan rasoolan. (Surat Al Isra 17:90-
93)

Tafsir: Na wao husema: ‘Hatutokuamini hadi pale utakaposababisha maji kutoka


ardhini kwa nguvu kwa ajili yetu; Au wewe una bustani ya Mitende na Mizabibu, na
usababishe maji kutoka kwa nguvu baina yao kwa wingi; Au usababishe Mbingu
kutuangukia vipande vipande kama ulivyojidai, au utuletee Allah na Malaika wake
mbele yetu uso kwa uso; Au una nyumba ya Zukhruf (iliyopambwa kwa Dhahabu) au
upae juu mbiguni, na hata hivyo hatutokuamini katika kupaa kwako hadi pale
utakaposhuka na kitabu ambacho tutakisoma’. Sema: Ametukuka Mola wangu! Mimi
sikua yeyote isipokua ni Bashar (mtu), alietumwa kama Rasul.

‘Yaani kwa maneno mengine, Bani Adam kua kiumbe chenye sifa za Utume,
kunamaanisha kua amekamilika katika vitendo vyake na kauli zake, na anaweza
kuwatibu Bani Adam wengine ambao waliokua hawana sifa mbili hizo; lakini si
lazima kua kutokana na kua na sifa hii (ya Utume) basi akawa na uwezo wa
kukutoleeni mambo [Mu’jizat] ambayo nyinyi mnamtaka akutoleeni’. (Matalib
‘Aliyyah, Mawlana Shibli Nu’mani)

Miujiza hua na sifa zifuatazo:

1. Hutokana kwa Allah Subhanah wa Ta’ala.


2. Huvunja Sharia’h za kawaida za kimaumbile katika kutokea kwake.
3. Hua na hali isioweza kuelezeka.
4. Hupitia kwa Mtume husika ili kuthibitisha Utume huo.
5. Hua inayoendana na madai yanayodaiwa.
6. Hua haipingani na madai yanayodaiwa.
7. Hua haizidishi wala haipunguzi kiasi cha madai husika.

A’llamah ‘Abd Al Rahman Ibn Khaldun anasema kuhusiana na Miujiza kua, ‘Miongoni
mwa alama za Mitume ni kufanya Miujiza ambayo huthibitisha ukweli wao.
130

Miujiza hua ni vitendo ambavyo mithili yake hua kamwe haiwezekani kufanywa na
Bani Adam. Na ndio maana ikaitwa Miujiza (Mu’jizat). Kwani hua haimo ndani ya
uwezo wa Bani Adam bali imo nje ya uwezo wao. Kuna utofauti wa mitazamo
kuhusiana na namna gani inavyotokea na namna gani huthibitisha ukweli wa
Mitume. Wachunguzi wa mitizamo ya kidini (Mutakallimun) wamesimamia katika
misingi ya Imani ya kua, Miujiza hua ni mambo ambayo hutokea kwa kutaka, na
hivyo husema kua Miujiza hutokea kutokana na uwezo wa Allah Subhanah wa
Ta’ala, na si kupitia katika vitendo vya Mitume wake. Mu’tazila wao wana mtizamo
wa kua vitendo vyote vya Bani Adam hutokana na Bani Adam mwenyewe, lakini
hata hivyo Miujiza hua haimo katika aina hizo za vitendo vinavyofanywa na watu.
Kulingana na Skuli za Madhhab yote, nafasi ya Mitume katika kufanya Miujiza hua
ndani ya mipaka ya ‘Changamoto zinazoendelea’ (Tahaddi) ambayo yeye huitoa
kutokana na amri ya Allah. Yaani Mtume hutumia Miujiza kabla ya kutokea
kwake, kama kithibitisho cha ukweli wa madai yake. Hivyo wao hua wanachukua
nafasi ya maelezo ya wazi kutoka kwa Allah kudhihirisha kua Mtume fulani ni wa
Kweli’.(Al Muqaddimah)

Ingawa Qurán haikuwataja Mitume wote lakini imetaja na kuhadithia visa na Hadith za
baadhi ya Mitume, ambao idadi yao ni 25 tu, na imefanya hivyo kwa sababu ndani ya
visa na Hadith hizo kuna mafunzo na mifano bora ya kuigwa katika uhai wa kila Bani
Adam, kama vile vile anavyosema mwenyewe Allah Subhanah wa Taála:

ْ ِ‫ﺖ ﺑِِﻪ ﻓُـ َﺆ َاد َك َو َﺟﺂءَ َك ِﰱ َﻫـٰ ِﺬﻩ‬ ِ ِ َ ‫ﺺ ﻋﻠَﻴ‬


‫ٱﳊَ ﱡﻖ‬ ُ ِّ‫ﻚ ﻣ ْﻦ أَﻧْـﺒَﺎء ٱﻟﱡﺮ ُﺳ ِﻞ َﻣﺎ ﻧـُﺜَـﺒ‬ ْ َ ‫﴿وُﻛـﻼًّ ﻧـﱠ ُﻘ ﱡ‬
َ
﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ ِ ِ
َ ‫َوَﻣ ْﻮﻋﻈَﺔٌ َوذ ْﻛَﺮ ٰى ﻟ ْﻠ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬
Wakullan naqussu AAalayka min anba-i alrrusuli ma nuthabbitu bihi fu-adaka
wajaaka fee hadhihi alhaqqu wamawAAidhatun wadhikra lilmu/mineena (Surat
Hud 11:120)

Tafsir: Na vyote tunavyokuhadithia kuhusiana na habari za Mitume ni kwa ajili ya


kuupa nguvu moyo wako kutokana navyo. Na ndani yake hii (Qurán) umekujia ukweli
na pia mawaidha na ukumbusho kwa walioamini.

Sababu nyengine za kutajwa kwa visa vya Mitume na Manabii hao 25 ndani ya Qurán
hua ni pamoja na kuudhibitishia ukweli wa utukufu wa Utume na kazi ya aliyeshushiwa
Qurán hiyo ambae ni Mtume wa Mwisho Muhammad Rasul Allah Salallahu A’layhi wa
Salam, kuthaminisha thamani ya Ummah wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa
Salam dhidi ya Úmma za watu wa Manabii na Mitume waliotangulia, kuzihuisha njia za
131

maisha ya Mitume na Manabii hao walizokua wakipita ili ziendelee kuwepo, kufahamika
na kufuatwa kwa milele.

Tunapoiangalia Qurán basi tunaona kua imewataja Mitume mbali mbali na tofauti
kulingana na mazingira yao waliyokabiliana na mitihani mbali mbali. Kwa mfano
tunapoiangalia Surat Al An Aam basi tunaona kua imetaja Mitume ambao
imewatafautisha kwa kua na sifa zifuatazo:

Nabii Nuh Alayhi Salatu wa Salam basi yeye ametajwa kua ni Nabii na Mtume wa
mwanzo kupingana na Jamii ya watu wanaoabudu Masanamu.

Nabii Is-haq na Nabii Yaqub Alayhim Salatu Salam basi wao wametajwa kua ndio
waanzilishi wa watu wa Bani Israil.

Nabii Daud na Nabii Sulayman Alayhim Salam wote wawili wametajwa kwa
kutofautishwa na Mitume wengine kwa kua na sifa ya Utume, Mali na Utawala wa
Mamlaka ya Kifalme.

Nabii Ayub na Nabii Yusuf Alayhim Salam wametajwa kwa kutofautishwa kwa
kujaribiwa kwa Mitihani na Ustahmilivu wao.

Nabii Musa na Nabii Harun Alayhim Salam wao wametajwa kwa kutofautishwa
kwa kua na uwezo na nguvu za kudhoofisha nguvu za Utawala wenye Nguvu kubwa
sana Kimamlaka.

Nabii Zakariyah, Nabii Yaqub, Nabii Isa Ibn Maryam na Nabii Ilyas Alayhim Salam
basi wao wametajwa kwa kutofautishwa kwa kua ni mfano wa kuigwa katika Ucha
Mungu, Ilm yao ya Kiroho na Kujitolea Muhanga.

Na vile vile tunapoangalia kwa upande wa Shaykh Al Akbar Imam Muhammad Ibn Ali
Ibn Muhammad Abu Bakr Muhyi Al Din Ibn Al Arabi Al Hatimi Al Ta’i Al Andalusi Al
Mursi Al Dimashqi ambae yeye ni mtaalamu wa I’lm Tasawwuf basi tunaona kua yeye
amewataja Mitume, Manabii na watu wengine Watukufu waliotajwa katika Qurán na
Hadith na kuwaainisha kulingana na aina za Hikma za ujumbe wa Allah Subhanah wa
Ta’ala zinazopatikana katika kuhadithiwa habari zao na hivyo tunaona kua:-

1. NABII ADAM – HIKMAH ILAHIYYAH – Hikma ya Uungu.


2. SHITH – HIKMAH NAFTHIYYAH – Hikma ya Matarajio.
3. NABII IDRIS – HIKMAH QUDUSIYYAH– Hikma ya Utukufu.
4. NABII NUH – HIKMAH SUBUHIYYAH – Hikma ya Kupandisha Darja.
5. NABII SALIH – HIKMAH FATIHIYYAH – Hikma ya Ufunguzi wa Kila Jambo.
132

6. NABII HUD - HIKMAN AHADIYYAH – Hikma ya Umoja wa kutokua na


Mshirika
7. NABII IBRAHIM – HIKMAH MUHAYMIYYAH – Hikma ya Upendo.
8. NABII LUT – HIKMAH MALIKIYYA – Hikma ya Uwezo wa Kiutawala.
9. NABII ISMAIL – HIKMAH ALIYYAH – Hikma ya Kujisalimisha.
10. NABII IS-HAQ – HIKMAH HAQQIYAH – Hikma ya Ukweli.
11. NABII YAQUB – HIKMAH RUHIYYAH – Hikma ya Kiroho.
12. NABII YUSUF – HIKMAH NURIYYAH – Hikma ya Nuru.
13. NABII SHUAYB – HIKMAH QALBIYAH – Hikma ya Kimoyo.
14. NABII UZAYR - HIKMAH QADARIYYAH – Hikma ya Makadirio.
15. NABII DAUD – HIKMAH WUJUDIYAH – Hikma ya Kua Hai.
16. NABII SULAYMAN – HIKMAH RAHMANIYYAH – Hikma ya Rehma.
17. NABII YUNUS – HIKMAH NAFASIYYAH – Hikma ya Sehem ya Kuvuta Hewa.
18. NABII AYYUB – HIKMAH GHAYBIYYAH – Hikma ya Ghayb.
19. NABII ILYAS – HIKMAH INASIYYAH – Hikmah ya Ukaribu
20. NABII MUSA – HIKMAH ULUWIYYAH – Hikma ya Mafanikio.
21. NABII HARUN – HIKMAH IMAMIYYAH – Hikma ya Uongozi
22. LUQMAN AL HAKIM – HIKMAH IHSANIYYAH – Hikma ya Tabia Njema.
23. NABII ZAKARIYYAH – HIKMAH MALIKIYYAH – Hikma ya Mamlaka.
24. NABII YAHYA – HIKMAH JALALIYYAH – Hikma ya Sifa Njema.
25. NABII ISA – HIKMAH NUBUWIYYAH – Hikma ya Unabii.
26. KHALID IBN SINAN – HIKMAH AS SAMADIYYAH – Hikma ya Kila kitu
kurudi Kwake.
27. NABII MUHAMMAD SALALLAHU ALAYHI WA SALAM – HIKMAH
FARDIYAH – Hikma ya Umoja wa Upekee

Ambapo anasema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

ِ ‫ﭑﻋﺒ ُﺪ‬
﴾‫ون‬ ِ ِ ۤ ِِ ۤ ِ ِ ٍ ِ َ ِ‫﴿وﻣﺂ أَرﺳ ْﻠﻨَﺎ ِﻣﻦ ﻗَـﺒﻠ‬
ُ ْ َ َْ َ ٰ ُ‫ﻚ ﻣﻦ ﱠر ُﺳﻮل إﻻﱠ ﻧُﻮﺣﻲ إﻟَْﻴﻪ أَﻧﱠﻪ‬
‫ﻓ‬ � َ
‫أ‬ ‫ﱠ‬
‫ﻻ‬ ‫إ‬ ‫ﻪ‬‫ـ‬َ‫ﻟ‬ ‫إ‬ ‫ﻻ‬ ْ َ ْ ََ
Wama arsalna min qablika min rasoolin illa noohee ilayhi annahu la ilaha illa ana
faoAAbudooni (Surat Al Anbiyah 21:25)

Tafsir: Na sisi hatukutuma kabla yako (Ewe Muhammad) Mitume isipokua


tuliwashushia ujumbe kua Hakuna anaestahiki kuabudiwa ila mimi hivyo Niabuduni.

Kwa upande wa Imam Baddiuzzamman Said Nursi basi yeye anasema kua miongoni
mwa sababu nambazo zinamepelekea kuwepo kwa takriri au kurudiwa kwa Visa Vya
Manabii na Mitume katika sura tofauti za Quran hua kunatokana na kuonesha Miujiza
yake Allah Subhanah wa Ta’ala ambayo ni yenye malengo makuu yafuatayo:
133

1-Kuelezea sehemu za visa ambazo zimetajwa katika sehemu nyengine maalumu


kulingana na mazingira maalum, na hivyo ingawa hiii hua si Takriri alkini
huonekana kua kama ni Takriri kwa sababu ya mazingira ya muonekano wake.

2-Kuweka wazi ufasaha na uwazi wa aya za Qur’an, kwani katika baadhi ya sehemu
kisa husika hua kimetajwa kwenye sura husika kwa aya chache lakini katika baadhi
ya sura kimetajwa kwa kina na kwa aya nyingi.

3-Kuweka wazi uthibitisho wa Utume wa Rasul Allah Sallahu A’layhi wa Salam,


kubainisha kuwepo kwake Mungu mmoja tu ambae ni Allah Subhanah wa Ta’ala,
kutoa mafunzo ya kua Allah Subhanah wa Ta’ala ana uwezo juu ya kila kitu
ikiwemo kuwaadhibu wanaomuasi, kuwaonya wasiomuamini kwa kuwawekea wazi
yaliyowafika wale waliotangulia kabla yao. Kiasi ya kua kila takrir iliyotumka basi
hua imetumika kwa ajili mazingira husika na katika wakati husika ili kufikisha
ujumbe husika.

4-Kumliwaza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na pia kuwaliwaza Waislam


ambao walikua wanakumbana na matatizo na mitihani mingi sana katika kipindi
hiki cha mwanzoni mwa Uislam, kwa mfano tunapoangalia kisa cha Nabii Musa na
Nabii Ibrahim basi tunaona kua vilikua vinarudiwa kwa sababu ya kuwaonesha
Waislam waliokua kwenye mitihani dhidi ya Makafiri kua lazima mwanzoni
Mitume na wanaowaamini Mitume hao hua wanapata misukosuko lakini baadae
hua kuna uongofu na uokovu kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala.

Na pia kwa upande mwengine tunapoangalia mifano ya kuangamizwa kwa jamii za


Watu wa Nabii Lut na Fir’awn kutokana na Uasi wao basi hua kunaonesha kua
haina haja na wala haitakiwi kwa Ibn Adam kua ni wenye kufanya dhambi dhidi
ya viumbe wenzao, dhidi ya Mola wao na hawatakiwi kumuuasi Mola wao.

5-Kuwapa Moyo Waumini kujidhibiti dhidi ya adui wao mkubwa ambae ni Shaytan
na dhidi ya Uadui wa Nafsi zao, na kuwawekea wazi malipo watakayoyapata pale
watakapofanikiwa kujidhibiti na maadui zao hao, na hapo hapo kuwavunja Moyo
wasiwe ni wenye kudumu katika dhambi.

6-Kuwafundisha Waumini Dua na namna ya kumkumbuka Mola wao, kufuata


Maamrisho yake, kumpwekesha na kuwasisitizia kua wao ni viumbe na watumwa
wa Allah Subhanah wa Ta’ala. Na hivyo kuwaonesha Malengo na Makusudio ya
kuumbwa kwao na kuumbwa kwa Ulimwengu wanaoishi ndani yake ambao nao
una kila kitu wanachokihitaji katika maisha yao hapa Ulimwenguni.

7-Kuwaponya watu wa kila aina kuanzia wenye ufahamu wa hali ya juu na wenye
134

ufaham mdogo, wenye Taqwa na waliopotoka, wenye kuikimbilia Akhera yao na


wenye kuikumbatia Dunia yao.

Lakini hata hivyo si kila mtu hua ni mwenye bahati ya kusioma Qur’an yote,
ambayo ni ponyo na ni dawa kwa kila mtu. Kwa hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala
aambae ndie mwenye kuweka Lulu, Hikma na Busara katika kila kitu akifanyacho
ndani yake, na ndie ambae mwingi wa Rehma na Huruma kwa waja wake basi
akaamua kuweka ndani yake Sura ambazo ni zenye kubeba malengo makuu ya
Qur’an. Kiasi ya kua kila sura imekua kama ni Qur’an ndogo na hivyo kua ni zenye
kumrahisishia kila mtu kunufaika nayo, ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala
akasema katika Qur’an

﴾‫﴿وﻟََﻘ ْﺪ ﻳَ ﱠﺴﺮَ� ٱﻟْ ُﻘﺮآ َن ﻟِﻠ ِّﺬ ْﻛ ِﺮ ﻓَـ َﻬﻞ ِﻣﻦ ﱡﻣ ﱠﺪﻛِ ٍﺮ‬
ْ ْ ْ َ
Walaqad yassarna alqur-ana lildhdhikri fahal min muddakirin (Surat Al Qamar
54:17)

Tafsir: Na kwa Hakika (kutokana na kuishusha katika Lugha ya Ibn Adam)


Tumeifanya Qur’an iwe ni rahisi kwa ukumbusho. Lakini jee ni nani mwenye
kuufuata ukumbusho huo?

8-Imeelezewa katika hadithi na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: Kila
aya ina kina cha maana kuna Muhkamat na Mutashabihat, yaani maana iliyowazi
na maana ya ndani ambayo inaweza kufahamika na wenye kujua tu. Hii hua ni
kama kina cha mzunguko wa kimaana, na kila kina cha mzunguko wa kimaana
umegawika sehemu nne kimaelezo, kialama, kimatawi na kiainisho. Kwa mtizamo
mwengine basi kila aya ya Qur’an ina matabaka ya kimaana, na mambo mengi
ndani yake, ikiwemo Hukmu, Manufaa na ainisho kwa malengo maalum. Hivyo
kutokana na sababu hio basi ndio maana kisa kimezungumziwa katika sehemu
moja na kisha kikazungumziwa katika seheu nyengine, ambapo katika sura moja
kimeelezewa kwa sababu fulani na katika sura nyengine kwa sababu tofauti.
Kutokana na hali hii basi hua hakuna takrir katika Qur’an, yaani hii ni kama vile
yalivyofanana macho na masikio ya watu, lakini ukweli ni kua yote yapo tofauti.

9-Kama ilivyokua mwili wa Ibn Adam unavyohitaji mahitaji tofauti ambapo baadhi
ya mahitaji hayo hua yanahitajiika kila mara kama uvutaji wa hewa kwa mfano,
na baadhi ya mahitaji huhitajika baada ya mda fulani kama kula, kunywa maji n.k
na baadhi hua ni yenye kuhitajika kila baada ya wiki, mwezi au mwaka mara moja
kama vile matumizi ya dawa. Na hivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa mahitaji ya kiroho
kwa upande wa Ibn Adam kila mmoja hua na njia zake za kufanya Dhikr Allah,
135

kuna kila wakati wasema wasemao Allah! Allah, kuna wasemao Biismi Allahi kuna
wasemao La Illah Ila Allah kila baada ya saa n.k kutokana na kuwepo kwa hali hii
basi Qur’an pia imekua na Takrir ndani yake kwa kutokana na kuhitajika kwake
na umuhimu wake.

Kulingana makusudio hayo na mengineyo mengi ambayo hatukuyataja basi


tunaona kua ingawa ndani ya Qur’an kuna takrir za mara kadhaa lakini hata hivyo
kujirudia huko basi kamwe hakukua ni kwenye kusababisha kukosekana kwa
mvuto wa Qur’an kama vile ambavyo yaliyo maneno au mazungumzo ya Watu,
lakini kwa upande wa Qur’an hali imekua ni kinyume chake, kwani kila ukiisoma
basi ndio hamu yya kuizoma zaidi ndivyo inavyozidi kukua na kuongezeka, vile vile
Qur’an ni Nuru ya kila Muumini katika kila wakati wa maisha yake yote hapa
Ulimwenguni na imekua hivyo kwa karne na karne, na imekua ikisomwa tena na
tena katika sala zao, na imerahisishwa kwa watoto kuihifadhi, Qur’an ni tamu kama
maji ya Zam Zam kwa mtu alie katika wakati wa kukata roho. Na haya yote
yanaonesha miujiza ya Qur’an iliyopo katika kila hali.

Baada ya kuangalia takrir katika Qur’an ambazo zimetumika katika kuelezea visa vya
Mitume tofauti ambapo ingawa Mitume na Manabii wote wanatoka kwa Allah Subhanah
wa Ta’ala kwa ajili ya kuja kueneza ujumbe wake Muumba na kuwaongoza watu katika
njia iliyosahih, na hivyo kukumbana na mitihani mingi sana kutoka kwa watu
wanaowausia juu ya ujumbe huo lakini baadhi miongoni mwao walikua na sifa ya darja
ya juu zaidi kuliko wengine na hii ni kulingana na mitihani waliyoipata na namna
walivyokabiliana na mitihani hio, na hivyo basi kutoka na kua na sifa hizo basi Mitume
hawa walikua wakijulikana kama Ulu al A’zmi mina al Rusul.
136

SURA YA PILI

137

ULUU AL A’AZMI MINA AL RUSUL




﴾‫ﺻﺒَـَﺮ أ ُْوﻟُﻮاْ ٱﻟْ َﻌْﺰِم ِﻣ َﻦ ٱﻟﱡﺮ ُﺳ ِﻞ‬ ِ ْ َ‫﴿ﻓ‬


َ ‫ﭑﺻ ْﱪ َﻛ َﻤﺎ‬
Faisbir kama sabara oloo alAAazmi mina alrrusuli (Surat Al Ahqaf 46:35)

Tafsir: Hivyo kua na Subira kama walivyokua na Subira Ulul A’zmi miongoni mwa
Mitume.


Neno A’zmi linatokana na neno la Kiarabu A’zama ambalo hua ni lenye kumaanisha
Azma, Amuzi lisilotenguka wala kupingika, Kusudio, Lengo au Msimamo thabit
usiotetereka na hivyo kua na thamani ambayo inapelekea kusudio husika
kutoachika njiani na hivyo hua ni lenye kufuatiliwa au kutekelezwa hadi likamilie.

Hivyo Uluu al A’zmi Mina Al Rusul hua ni Mitume na Manabii ambao walikabiliwa
na mitihani mikubwa sana yenye kuvunja Moyo mara kadhaa katika kutekeleza
kazi yao ya kuwaongoza watu na kueneza ujumbe wa Allah, lakini hata hivyo
hawakuvunjika moyo bali waliendelea kufanya jithada za kueneza ujumbe huo kwa
subira na ustahmilivu mkubwa sana.

Allah Subhanahu wa Ta’ala amewataja Ulul A’zmi katika sehemu mbili ndani ya Qurán
ambapo ni katika Surat Al-Ahzab (33:7) na Surat Ash-Shuara (42:13).

Ambapo katika Surat Al Ahzab (33:7) Allah Subhanah wa Ta’ala amesema kua:

‫ﻴﺴﻰ ٱﺑْ ِﻦ‬ ِ‫ﻮح وإِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ وﻣﻮﺳﻰ وﻋ‬ ِ َ ‫﴿وإِ ْذ أَﺧ ْﺬ َ� ِﻣﻦ ٱﻟﻨﱠﺒِﻴِﲔ ِﻣﻴﺜَﺎﻗَـﻬﻢ وِﻣْﻨ‬
َ َ ٰ َ ُ َ َ َ ْ َ ٍ ‫ﻚ َوﻣﻦ ﻧﱡ‬ َ ُْ َ ّْ َ َ َ
﴾ً‫َﺧ ْﺬ َ� ِﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ ِّﻣﻴﺜَﺎﻗﺎً َﻏﻠِﻴﻈﺎ‬
َ ‫َﻣْﺮَﱘَ َوأ‬
Wa-idh akhadhna mina alnnabiyyeena meethaqahum waminka wamin Nuuhin wa-
Ibraheema waMuusa waAAeesa ibni Maryama waakhadhna minhum meethaqan
ghaleedhan (Surat Al Ahzab 33:7)
138

Tafsir: Na kumbuka wakati tulipochukua kutoka kwa Manabii ahadi zao, na kutoka
kwako wewe (Muhammad) na Nuh, na Ibrahim, na Musa na Isa Ibn Maryam. Na
tumechukua kutoka kwao ahadi madhubuti.

Na pale aliposema katika Surat Ash Shuara:

ۤ ِ ‫ع ﻟَ ُﻜﻢ ِّﻣ َﻦ ٱﻟ ِّﺪﻳ ِﻦ َﻣﺎ َو ﱠ‬


‫ﺻْﻴـﻨَﺎ ﺑِِﻪ‬
‫ﻚ َوَﻣﺎ َو ﱠ‬ َ ‫ﺻ ٰﻰ ﺑِِﻪ ﻧُﻮﺣﺎً َوٱﻟﱠﺬي أ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إِﻟَْﻴ‬ َ ‫﴿ َﺷَﺮ‬
ِ ِِ ِ ِ ِ ‫إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ وﻣﻮﺳﻰ و‬
‫ﲔ َﻣﺎ‬ َ ‫ﻳﻦ َوﻻَ ﺗَـﺘَـ َﻔﱠﺮﻗُﻮاْ ﻓﻴﻪ َﻛﺒُـَﺮ َﻋﻠَﻰ ٱﻟْ ُﻤ ْﺸ ِﺮﻛ‬ ُ ‫ﻴﺴ ٰﻰ أَ ْن أَﻗ‬
َ ‫ﻴﻤﻮاْ ٱﻟ ّﺪ‬ ‫ﻋ‬
َ َ ٰ َ ُ َ َ َْ
ِ‫ٱﻪﻠﻟ َﳚﺘَِ ۤﱯ إِﻟَﻴ ِﻪ ﻣﻦ ﻳ َﺸﺂء وﻳـﻬ ِﺪ ۤي إِﻟَﻴ ِﻪ ﻣﻦ ﻳﻨ‬ ِ
﴾‫ﻴﺐ‬ ُ ُ َ ْ ْ َ َ ُ َ َ ْ ْ ُ‫ﻮﻫ ْﻢ إِﻟَْﻴﻪ ﱠ‬ ُ ُ‫ﺗَ ْﺪﻋ‬
SharaAAa lakum mina alddeeni ma wassa bihi Noohan waalladhee awhayna ilayka
wama wassayna bihi Ibraheema wamoosa waAAeesa an aqeemoo alddeena wala
tatafarraqoo feehi kabura AAala almushrikeena ma tadAAoohum ilayhi Allahu
yajtabee ilayhi man yashao wayahdee ilayhi man yuneebu(Surat Ash Shuara 42:13)

Tafsir: Tumekushushieni Sharia katika dini kama vile tulivyomuusia Nuh. Na vile
ambavyo tulivyokushushia wewe na kama tulivyomuusia Ibrahim, na Musa, na Isa
kuwaambia msimamishe Dini wala msisababishe mgawanyiko ndani yake.
Wasichoweza kukistahmilia Makafiri ni kuwaita kwako katika njia ya Allah. Allah
humchagua amtakae na humuelekeza katika upande wake yule anaemgeukia yeye kwa
ustahmilivu na utiifu.

Na igawa Wanazuoni wanakubaliana kua Mitume na Manabii waliotajwa kwa majina


waliotajwa kwenye aya hizi mbili yaani Nabii Nuh, Nabii Ibrahim, Nabii Musa, Nabii
Isa na Nabii Muhammad tu Salallahu A’layhi wa Salam, lakini kwa upande wa Imam
Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari basi yeye anasema kuhusiana na aya
isemayo:

﴾‫ﺻﺒَـَﺮ أ ُْوﻟُﻮاْ ٱﻟْ َﻌْﺰِم ِﻣ َﻦ ٱﻟﱡﺮ ُﺳ ِﻞ‬ ِ ْ َ‫﴿ﻓ‬


َ ‫ﭑﺻ ْﱪ َﻛ َﻤﺎ‬
Faisbir kama sabara oloo alAAazmi mina alrrusuli (Surat Al Ahqaf 46:35)

Tafsir: Hivyo kua na Subira kama walivyokua na Subira Ulul A’zmi miongoni mwa
Mitume.
139

Kua: ‘Aya hii inamaanisha kusema kua: ‘Kua na Subra kama wenye (Sabr) Subra
miongoni mwa watu wenye maarifa (Ahl Al Maarifa) kama vile walivyokua wale
wenye maazimio thabiti (Uluu al Azmi) miongoni mwa Mitume walioonesha Subra,
Subra ambayo ni moja kati ya njia za kua na Maridhio (Ridhaa) na Kujisalimisha
(Taslima) bila ya kua na masikitiko (Shakwa) au kukosa ustahmilivu (Jaza).

Nabii Ibrahim alipewa mtihani wa kuingizwa ndani ya tanuri la moto na mtihani


wa kumtoa Muhanga mtoto wake, lakini alipokea Mitihani hio kwa maridhio na
kujisalimisha, Nabii Nuh alipewa mtihani wa kutokukubaliwa na watu wake lakini
nae akawa ni mwenye Subira (Sabara), wakati Nabii Yunus alipewa mtihani wa
kuishi ndani ya tumbo la Nyangumi lakini akawa ni mwenye kumkumbuka Mola
wake, na kuomba hifadhi kutoka kwake, Nabii Yusuf alipewa mtihani wa
kutumbukizwa Kisimani na kufugwa Jela lakini hakutetereka. Nabi Yaqub alipewa
mtihani wa kupoteza macho yake na kupoteza mtoto wake, lakini alimlamikia Mola
wake na hakulalamika kwa Ibn Adam yeyote. Kuna Mitume 12 ambao Sala na
Salam za Allah ziwe juu yao, waliokua na Subra na ustahmilivu juu ya mitihani yao
iliyowafika na hivyo kua ni wenye kujulikana kama Wenye Misimamo Thabiti (Ulu
al Azmi) miongoni mwa Mitume, lakini Allah Subhanah wa Taála ni mwenye kujua
zaidi’’

Ingawa Nabii Adam alikua ni mtu wa mwanzo na Nabii wa mwanzo lakini Nabii Idris
ambae alikua anatoka katika kizazi cha tano kutoka kwa Nabii Adam alikua ni mtu wa
mwanzo kupewa Utume baada ya Nabii Adam. Nabii Idris alizaliwa na alikulia katika
mji wa Babylon ambao uliokuwepo katika maeneo ya Iraq.

Katika wakati wa uhai wake, Nabii Idris alijaribu kuwarudisha watu wake wale
waliopotoshwa na Iblis na kutolewa kutoka katika njia ya haki lakini ni wachache sana
waliomsikiliza na wengi waliobakia miongoni mwao walimpinga na kumkataa. Hivyo
akaendelea kuwausia mema na kuwakataza mabaya na baadae akaamua kuhama na wale
waliomkubali na kuhamia katika maeneo ya Ardhi ya Misri ambako alikaa huko hadi
kufariki kwake. Qurán inasema kuhusiana na Nabii Idris kua:

ً‫ﻳﺲ إِﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن ِﺻ ِّﺪﻳﻘﺎً ﻧﱠﺒِﻴﱠﺎً ۞ َوَرﻓَـ ْﻌﻨَﺎﻩُ َﻣ َﻜﺎ�ً َﻋﻠِﻴّﺎ‬


َ ‫ر‬ ِ َ‫﴿وٱذْ ُﻛﺮ ِﰱ ٱﻟْ ِﻜﺘ‬
ِ ‫ﺎب إِ ْد‬
ْ َ
ٍ ُ‫ءاد َم َوِﳑ ْﱠﻦ َﲪَْﻠﻨَﺎ َﻣ َﻊ ﻧ‬
‫ﻮح‬ ِ
َ ‫ﲔ ﻣﻦ ذُِّرﻳﱠﺔ‬
ِ ِ‫ٱﻪﻠﻟ ﻋﻠَﻴ ِﻬﻢ ِﻣﻦ ٱﻟﻨﱠﺒِﻴ‬
َ ْ ّ َ ّ ْ َ ُ‫ﻳﻦ أَﻧْـ َﻌ َﻢ ﱠ‬ َ َ
ِ ‫۞أُوﻟَـٰﺌِﻚ ٱﻟﱠ‬
‫ﺬ‬
ِ ْ ‫وِﻣﻦ ذُ ِرﻳﱠِﺔ إِﺑْـﺮ ِاﻫﻴﻢ وإِ ْﺳﺮاﺋِﻴﻞ وِﳑﱠﻦ َﻫ َﺪﻳْـﻨَﺎ و‬
‫ت ٱﻟﱠﺮ ْﲪَـٰ ِﻦ‬ َ ‫ٱﺟﺘَـﺒَـْﻴـﻨَﺂ إ َذا ﺗُـْﺘـﻠَ ٰﻰ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ‬
ُ �‫آ‬ َ ْ ََ َ ََ َ ّ َ
﴾ً‫َﺧﱡﺮواْ ُﺳ ﱠﺠﺪاً َوﺑُ ِﻜﻴّﺎ‬
140

Waodhdkur fee alkitabi idreesa innahu kana siddeeqan nabiyyan; WarafaAAnahu


makanan AAaliyyan ; Ola-ika alladheena anAAama Allahu AAalayhim mina
alnnabiyyeena min dhurriyyati adama wamimman hamalna maAAa noohin
wamin dhurriyyati ibraheema wa-isra-eela wamimman hadayna waijtabayna idha
tutla AAalayhim ayatu alrrahmani kharroo sujjadan wabukiyyan (Surat Maryam
19:56-58).

Tafsir: Na ametajwa katika Kitabu (Qurán) Idris. Hakika yeye alikua ni mtu mkweli
na ni Nabii. Tulimnyanyua katika darja ya juu. Hawa ndio wale ambao Allah
Subhanah wa Ta’ala amewapa fadhila zake miongoni mwa Mitume, waliotokana na
kizazi cha Adam, na wale uliowabeba (katika Safina) pamoja na Nuh, na kizazi cha
Ibrahim, na Israil (Nabii Yaqub) na miongoni mwa wale ambao tumewaongoza na
kuwachagua. Wanaposomewa Aya za mwingi wa Rehma (Allah Subhanah wa Taála)
basi huanguka chini huku wakiwa katika hali ya Kusjudu huku wakibubujikwa na
machozi.

Naam, aya hizi za Surat Maryam 19:56-58 ni aya ambazo zinathibitisha kua Nabii Idris
alikuja kabla ya kuja Nabii Nuh, kwa sababu aya imeanza na kumuelezea Nabii Idrisa na
kumjumuisha kua ni miongoni mwa waliopewa fadhila miongoni mwa kizazi cha Nabii
Adam, kisha vikatajwa vizazi vya Nabii Nuh, Nabii Ibrahim na Nabii Yaqub.

Baada ya kufariki Nabii Nabii Idris A’layhi Salaam, ilipita miaka mingi sana na kama
kawaida yake Iblis akazidi kuongeza jitihada zake za kuwapotosha watu na watu hao
wakaanza kutengeneza masanamu na kuyaabudia na kuamini kua yalikua na uwezo wa
kuwanufaisha na kuwalinda na mengi. Anasema Imam Ibn Jarir kua: ‘Watu wema
walioishi baina ya Adam na Nuh na wale waliokua wakiwafuata walitengeneza
masanamu yao na kusema: ‘Ikiwa tutafanya Masanamu yao, basi itapendeza zaid
katika kufanya Ibada zetu na pia itatukumbusha kuhusiana na wao’ hivyo
wakatengeneza Masanamu, na baada ya kufariki wale waliotengeneza Masanamu
hayo, basi Iblis akawashawishi waliofuatia kwa kuwaambia: ‘Mababu zenu walikua
wakiwaabudu hawa na kupitia katika Ibada zao hizo walikua wakipata mvua.’
hivyo nao wakawa wanayaabudu.’’

Na waliendelea kufanya hivyo hadi pale Allah Subhanah wa Ta’ala alipoamua kumtuma
Nabii wa tatu, ambae ni Nabii Nuh Alayhi Salatu wa Salam.
141

‫ﻧﻮﺡ ﻧﺎﺟﻴﺔ ﺍﷲ‬



142

NAJIYYU ALLAH NUH AÁLAYHI SALATU WA SALAAM




‫ﺎل ﻟَِﻘ ْﻮِﻣ ِﻪ ٰﻳـ َﻘ ْﻮِم إِن َﻛﺎ َن َﻛﺒُـَﺮ َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ ﱠﻣ َﻘ ِﺎﻣﻰ َوﺗَ ْﺬﻛِ ِﲑى‬ َ َ‫ﻮح إِ ْذ ﻗ‬
ٍ ُ‫﴿ َوٱﺗْ ُﻞ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ ﻧَـﺒَﺄَ ﻧ‬
‫َﲨﻌُ ۤﻮاْ أ َْﻣَﺮُﻛ ْﻢ َو ُﺷَﺮَﻛﺂءَ ُﻛ ْﻢ ﰒُﱠ ﻻَ ﻳَ ُﻜ ْﻦ أ َْﻣُﺮُﻛ ْﻢ َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ‬
ِْ ‫ٱﻪﻠﻟِ ﺗَـﻮﱠﻛ ْﻠﺖ ﻓَﺄ‬
ُ َ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻓَـ َﻌﻠَﻰ ﱠ‬
ِ‫ت ﱠ‬ ِ �‫ِﺂﺑ‬
َ
﴾‫ﻨﻈُﺮو َن‬ ِ ُ‫ﱃ وﻻَ ﺗ‬ ‫ﱠ‬ َ ِ‫ﻀ ۤﻮاْ إ‬ُ ْ‫ﻏُ ﱠﻤﺔً ﰒُﱠ ٱﻗ‬
َ
Waotlu AAalayhim nabaa noohin idh qala liqawmihi ya qawmi in kana kabura
AAalaykum maqamee watadhkeeree bi-ayati Allahi faAAala Allahi tawakkaltu
faajmiAAoo amrakum washurakaakum thumma la yakun amrukum AAalaykum
ghummatan thumma iqdoo ilayya wala tundhirooni.(Surat Yunus 10:71)

Tafsir: Na wasomee habari za Nuh. Wakati alipowaambia watu wake: ‘Enyi watu
wangu, kama ikiwa kubaki kwangu pamoja nanyi na kukukumbusheni dalili za Allah
ni kugumu juu yenu basi mimi namtegemea Allah. Hivyo jumuisheni hila zenu, nyie
na washirika wenu, na kisha wala msiwe na shaka juu ya hila zenu hizo na kisha
amueni (mnalotaka kuamua kulifanya) juu yangu na wala msinionye’


Neno Naha kwa Lugha ya Kiarabu hua ni lenye kumaanisha, Kulalamika kwa huzuni,
Kulamamika kwa Maumivu na pia humaanisha Kulalamika kwa Sauti ya Chini nzuri
yenye Unyenyekevu. Neno Naha ndio lililotoa neno Nuh ambalo ndio Jina Nabii na Rasul
wa Allah Subhanah wa Ta'ala ambae ametajwa wazi kwa jina lake la Nuh mara 43 ndani
ya Qur'an. Nabii Nuh ni Miongoni mwa Mitume ambao walikuja katika kipindi ambacho
kwa Ulimwengu hua ni wa Mabadiliko makubwa kwa maisha ya Ibin Adam, na hivyo
basi Nabi Nuh akawa ni mwenye kuleta Mabadiliko hayo makubwa Ulimwenguni na
kuyasimamia. Mabadilko haya yamegawika katika sehemu nne na ndio maana Allah
Subhanah wa Ta'ala akaapa kwa kusema katika Aya zifuatazo:

ِ ‫ﲔ۞ وَﻫـٰ َﺬا ٱﻟْﺒَـﻠَ ِﺪ ٱﻷ َِﻣ‬


﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ ِ ِِ ﴿
َ َ ‫َوٱﻟﺘّﲔ َوٱﻟﱠﺰﻳْـﺘُﻮن۞ َوﻃُﻮر ﺳﻴﻨ‬
Waaltteeni waalzzaytooni, Watoori seeneena, Wahadha albaladi al-ameeni (Surat
Tin 95:1-3)
143

Tafsir: Naapa kwa Tin na Zaytun, Na Mlima wa Sina, Na kwa Mji huu wa Amani.

Katika ayah hii tunaona kua Allah Subhanha wa Ta'ala anaapa kwa Tin, Zaytun, Turi
Sinina na Baladi Al Amin, ambapo mbali ya kua Tin hua ni tunda lakini pia Tin hua
inawakilisha kipindi cha Mwanzoni cha Nabii Adam ambacho ni kipindi Msingi wa
Maisha ya Ibn Adam Ardhini, pia hua ni kipindi cha Nabii Uhai wa Nabii Isa Ibn Maryam
na kwa upande wa Zaytun ambapo pia tunajua kua ni tunda lakini pia hapo hapo hua
inamanisha kipindi cha Nabii Nuh ambae ndicho kipindi kilichosimamishwa Sharia za
Allah Subhanah wa Ta'ala ardhini, na Turi Sinin ambao ni Mlima wa Sinai lakini pia
unawakilisha wakati wa Nabi Musa ambao ni wakati Shariah za Allah Subhnaha wa
Ta'ala zilianza kufafanuliwa na pia aya zimetaja kipindi cha nne ambacho ni kipindi cha
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa kutajwa Baladi Al Amin yaani Mji wa Amani
ambacho kinawakilisha wakati ambao Sharia za Allah Subhanah wa Ta'ala
zilikamilishwa na kumaliziwa na kuamrishwa kua ziwe ni zenye kutumika milele mpaka
mwisho wa Ulimwengu kwa wale wenye kutaka kuongoka, kupata ridhaa za Mola wao
na kua na Mwisho mwema katika maisha yao ya hapa Ulimwenguni.

Inasemekana kua Nabii Nuh alizaliwa miaka 1056 baada ya kuumbwa kwa Nabii Adam
au baada ya kushuka Duniani Nabii Adam, na anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi
Allahu Anhu kua amesema Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kua: ‘Kipindi
baina ya Adam na Nuh ni Qarn (karne) kumi’ (Sahih Bukhari).

Tukiangalia maana ya neno Qarn ambalo kwa kiswahili maana yake hua ni Karne yaani
miaka 100, basi tutaona kua kuna utofauti wa maana yake kitafsir kwani baadhi ya
Wanazuoni wanasema kua Qarn hua inamaanisha miaka 100, wengine wanasema kua ni
miaka 1000 na wengine wanasema kua Qarn maana yake ni mda wa maisha unaoishi
kizazi kimoja, na hakuna anaejua kwa uhakika kua vizazi vya wakati huo vilikua vikiishi
kwa muda wa miaka mingapi.

Nabii Nuh alikua akijulikana kama Tashakkur Ibn Lamik, Ibn Mitoshilkh, Ibn Idris, Ibn
Yard, Ibn Mahlabeel, Ibn Qinan, Ibn Anoush, Ibn Seth, Ibn Adam A’layhi Salaam. Na
mama yake alikua akijulikana kwa jina la Batanush. Tunapoiangalia Qurán basi tunaona
kua inamuelezea Nabii Nuh kua ni miongoni mwa Mitume waliopandishwa Darja pale
iliposema:

ً‫ﲔ ۞ ذُِّرﻳﱠﺔ‬ ِ ِ َ ‫آل إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ و‬ ‫﴿إِ ﱠن ﱠ‬


َ ‫آل ﻋ ْﻤَﺮا َن َﻋﻠَﻰ ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬ َ َ َ ْ َ ‫آد َم َوﻧُﻮﺣﺎً َو‬
َ ‫ٱﺻﻄََﻔ ٰﻰ‬
ْ َ‫ٱﻪﻠﻟ‬
﴾‫ﻴﻊ َﻋﻠِﻴﻢ‬ ٌ
َِ ‫ٱﻪﻠﻟ‬
‫ﲰ‬ ‫ﱠ‬ ‫و‬ ٍ
‫ﺾ‬ ‫ﻌ‬
ْ ‫ـ‬
َ‫ﺑ‬ ‫ﻦ‬
ْ
ِ ‫ﺑـﻌﻀﻬﺎ‬
‫ﻣ‬ َُ َْ
ٌ ُ َ
144

Inna Allaha istafa adama wanoohan waala ibraheema waala AAimrana AAala
alAAalameena, Dhurriyyatan baAAdhhuha min baAAdhin waAllahu sameeAAun
AAaleemun (Surat Al Imran 3:33-34)

Tafsir: Kwa hakika Allah amempandisha darja Adam na Nuh na familia ya Ibrahim
na familia ya Imran juu ya Walimwengu wote. Vizazi vilivyotokana na baadhi yao
miongoni mwao, hakika Allah ni mwingi wa wa Kusikia kila Kitu na ni Mwenye kujua
juu ya kila Kitu.

Aya imewataja Manabii waliopandishwa Darja na Allah Subhanah wa Taála, ambao ni


Nabii Adam, kisha ikamtaja Nabii Nuh, na kisha ikamtaja Nabii Ibrahim na familia yake
na kisha ikaitaja familia ya Al Imran, na wakati huo huo tunapoiangalia Qurán basi
tunaona imeziainisha familia mbili za Imran ambapo familia ya Imran wa kwanza ndio
iliyotoa Nabii Musa na Nabii Harun Ibn Imran na familia ya Imran wa pili ndio iliyotoa
Maryam Bint Imran na Nabii Isa Ibn Maryam. Hivyo wote waliotajwa katika aya hii na
familia zao wanatokana na vizazi Vitukufu ambavyo vinawajumuisha pamoja kwa
kuwaunganisha Kindugu, Kiimani, Kiupendo, Kiutukufu na Kiikhlas katika matendo
yao.

Ama kwa upande wa Nabii Nuh alikua katika mitihani ya kuwausia na kupingana na watu
wake kwa muda wa miaka 950.

۞ ‫اب أَﻟِﻴﻢ‬ ٌ ‫ﺬ‬


َ ‫ﻋ‬
َ ‫ﻢ‬ ‫ﻬ‬
ُ ‫ـ‬‫ﻴ‬
َ
ِ‫ﻚ ِﻣﻦ ﻗَـﺒ ِﻞ أَن �ْﺗ‬
َ ْ َ ‫ﻣ‬
َ‫ﻮ‬ ‫ـ‬
َ ‫ﻗ‬ ‫ر‬
ْ
ِ ‫﴿إِ ﱠ� أَرﺳ ْﻠﻨﺎ ﻧُﻮﺣﺎً إِ َ ٰﱃ ﻗَـﻮِﻣ ِﻪ أَ ْن أ‬
‫َﻧﺬ‬ ََْ
ٌ ْ ْ ْ
‫ﻮن ۞ ﻳَـ ْﻐ ِﻔْﺮ ﻟَ ُﻜ ْﻢ‬ ِ ‫َﻃﻴﻌ‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ وٱﺗﱠـ ُﻘﻮﻩ وأ‬ ‫ا‬‫و‬ ‫ﺪ‬ ‫ٱﻋﺒ‬ ِ‫ﲔ ۞ أ‬
‫َن‬ ِ
‫ﺒ‬ ‫ﻣ‬ ‫ﻳﺮ‬ ِ َ‫ﺎل ٰﻳـ َﻘﻮِم إِِﱏ ﻟَ ُﻜﻢ ﻧ‬
ُ َُ ََ ‫ﱠ‬ ْ ُ ُ ٌ ‫ﱡ‬ ٌ ْ ّ ْ َ َ‫ﻗ‬
‫ﺬ‬
‫ٱﻪﻠﻟِ إِ َذا َﺟﺂءَ ﻻَ ﻳـُ َﺆ ﱠﺧُﺮ ﻟَ ْﻮ ُﻛﻨﺘُ ْﻢ‬
‫َﺟ َﻞ ﱠ‬ ِ
َ ‫َﺟ ٍﻞ ﱡﻣ َﺴ ًّﻤﻰ إ ﱠن أ‬
ِ ِ ِ
َ ‫ّﻣﻦ ذُﻧُﻮﺑِ ُﻜ ْﻢ َوﻳـُ َﺆ ّﺧْﺮُﻛ ْﻢ إ َ ٰﱃ أ‬
﴾‫ﺗَـ ْﻌﻠَﻤﻮ َن‬
ُ
Inna arsalna noohan ila qawmihi an andhir qawmaka min qabli an ya/tiyahum
AAadhabun aleemun, Qala ya qawmi innee lakum nadheerun mubeenun, Ani
oAAbudoo Allaha waittaqoohu waateeAAooni, Yaghfir lakum min dhunoobikum
wayu-akhkhirkum ila ajalin musamman inna ajala Allahi idha jaa la yu-akhkharu
law kuntum taAAlamoona (Surat Nuh 71:1-4)

Tafsir: Ama kwa hakika, tulimtuma Nuh kwa watu wake, kwa kumwambia Waonye
watu wako! Kabla haijawafikia juu yao adhabu kali sana. Nuh akasema: Enyi watu
wangu! Kwa hakika mimi ni muonyaji alie wazi juu yenu, (nnaekuonyeni) Muabuduni
Allah pekee na mumtekelezee majukumu yake na mnitii. Yeye (Allah Subhanah wa
145

Taála) atakusameheni dhambi zenu na kukuakhirishieni (kukuzidishieni katika)


majaaliwa yenu. Kwani kwa hakika, Majaaliwa ya Allah hayaakhirishiki, ya laiti kama
mngelijua.

Naam, Allah Subhanah wa Ta’ala anamsifu Nabii Nuh kutokana na Subra, Ustahamilivu,
Ukarimu na Upendo kwa watu wa jamii yake kiasi ya kua alipandisha Darja ya juu kama
alivyosema katika aya inayofuatia:

ِ ٍ ِ ِ‫﴿وﻟََﻘ ْﺪ أَرﺳ ْﻠﻨﺎ ﻧُﻮﺣﺎً إِ َ ٰﱃ ﻗَـﻮِﻣ ِﻪ ﻓَـﻠَﺒ‬


‫َﺧ َﺬ ُﻫ ُﻢ‬ َ ‫ﻒ َﺳﻨَﺔ إِﻻﱠ ﲬَْﺴ‬
َ ‫ﲔ َﻋﺎﻣﺎً ﻓَﺄ‬ َ ْ‫ﺚ ﻓﻴ ِﻬ ْﻢ أَﻟ‬َ ْ ََْ َ
﴾‫ٱﻟﻄﱡﻮﻓَﺎ ُن َوُﻫ ْﻢ ﻇَـﻠِ ُﻤﻮ َن‬
Walaqad arsalna noohan ila qawmihi falabitha feehim alfa sanatin illa khamseena
AAaman faakhadhahumu alttoofanu wahum dhalimoona. (Surat Al Anqabut 29:14)

Tafsir: Na kwa hakika tulimtuma Nuh kwa watu wake na akakaa pamoja nao
miongoni mwao kwa miaka 1000 ila (toa) miaka 50 (akiwausia kumuamini Mungu
mmoja na kutomshirikisha) na wakakumbwa na Tufani wakati wakiwa ni miongoni
mwa walio madhalim.

Tunapoiangalia ayah hii basi tunaona kua inatuonesha umuhimu wa Subra, Ustahmilivu
na kua na Msimamo katika kufanya kazi ya kusimamia maamrisho ya Allah Subhanah
wa Taála, na kua vyovyote vile itakavyokua basi mtu hata aishi miaka mingapi katika
Ulimwengu huu basi kamwe hatoweza kudumu milele kwani maumble ya mwili wake
hayatoweza kustahamili tena hivyo itabidi mwisho wake kua ni kukumbana na kifo tu
ambacho ndicho kitakacho mrudisha kwa Mola wake kwani anasema Allah Subhanah wa
Ta’ala kua:

﴾‫ٱﳋَِْﲑ ﻓِْﺘـﻨَﺔً وإِﻟَْﻴـﻨَﺎ ﺗُـﺮ َﺟﻌُﻮ َن‬


ْ ‫و‬ ِ
‫ﱠﺮ‬‫ﺸ‬‫ﭑﻟ‬ ِ ‫ﺲ َذآﺋَِﻘﺔُ ٱﻟْﻤﻮ‬
ِ‫ت وﻧَـْﺒـﻠُﻮُﻛﻢ ﺑ‬ ٍ ‫﴿ ُﻛ ﱡﻞ ﻧَـ ْﻔ‬
ْ َ َّ َ َْ
Kullu nafsin dha-iqatu almawti wanablookum bialshsharri waalkhayri fitnatan wa-
ilayna turjaAAoona (Surah Al-Anbiya 21:35)

Tafsir: Kila Nafsi itayaonja Mauti, na tutakujaribuni nyie kwa maovu na mema
kimtihani. Na kwetu sisi ndio marudio yenu.

Ambapo aya imetumia neno Dhaiqat ambalo linalotokana na neno Dhaqa ambalo hua
linamaanisha Kuonja au Kujaribu, na hivyo basi hua ni lenye kuonesha kua Kifo ni kitu
146

kichungu sana ambacho hakuna njia isipokua kuonjwa kwa kila kiumbe kwani ndio njia
pekee ya kuhama kutoka katika maisha ya Ulimwengu wa Kidunia ambapo tumekuja
kwa ajili ya kujaribiwa kwa mema na mabaya yetu na kuingia katika maisha ya
Ulimwengu wa Akhera, na hivyo basi hakuna sehemu ya kujificha kwa ajili ya
kutokumbana na kifo, kwani anasema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

﴾ٍ‫وج ﱡﻣ َﺸﻴﱠ َﺪة‬


ٍ ‫ت َوﻟَْﻮ ُﻛﻨﺘُ ْﻢ ِﰱ ﺑـُُﺮ‬
ُ ‫﴿أَﻳْـﻨَ َﻤﺎ ﺗَ ُﻜﻮﻧُﻮاْ ﻳُ ْﺪ ِرﻛ ﱡﻜ ُﻢ ٱﻟْ َﻤ ْﻮ‬
Aynama takoonoo yudrikkumu almawtu walaw kuntum fee buroojin
mushayyadatin (Surat An Nisaa 4:78)

Tafsir: Popote pale mlipo, Kifo kitakukuteni (huko huko Mliko) hata kama mkiwa
kwenye Makasri Makubwa yaliyo imara.

Tunapoaiangalia aya yetu hii nayo pia tunona kua imetumia neno Yudrikumu linalotokana
na neno Daraka ambalo hua linamaanisha Kufuatia, Kukutia, Kufikia, Kufuata kitu hadi
ukakifikia na kukipita na hivyo kua mbele yake, Kukamata kwa ghafla moja, Kuvamia
kwa kasi ya kutoka juu kuelekea Chini. Hivyo hakuna atakaeweza kukiepuka kifo kwani
hata ajifiche wapi basi atakumbana nacho.

Ama kuhusiana na ufafanuzi zaidi wa ya hii basi anasema Mufassir Imam Mujahid Ibn
Muzahim kua: ‘Kuna mwanamke alijifungua mtoto wa kike, kisha mwanamke huyo
akamwambia Mfanyakazi wake kua: Nenda nje katafute moto (kwa ajili ya kuoka).
Yule Mfanyakazi wake alipokua anatoka nje ya nyumba hio, akakutana na Mtu
mwengine Mwanamme ambae alimuuliza Mfanyakazi huyo, ‘Jee amejifungua
mtoto gani?’ Mfanyakazi akajibu: ‘Mtoto wa Kike’ yule mtu alieuliza suali hilo
akasema: ‘Binti huyo hatokufa hadi pale atakapokua tayari ameshazini na watu
100, na Mfanyakazi wa kiume wa Mama mzazi wa Binti huyu ndie atakaemuoa
Binti huyo na kisha Binti ndio atakufa kwa kutafunwa na Buibui’

Yule mfanyakazi aliposikia maneno hayo akakasirika na kusema: ‘Yaani mimi ndie
nitakaemuoa Mwanamke huyu aliezaliwa ambae atazini na watu mia? Kuna faida
gani?’ Hivyo akarudi ndani kisha akamchoma kisu cha tumbo yule mtoto mchanga
akampasua na kisha akakimbia na kuhama nchi.’

‘Lakini hata hivyo yule Binti hakufariki bali alipatiwa matibabu na akapona,
ikapita miaka na binti akawa mkubwa, akawa anafanya kazi ya kuuza mwili wake
katika Mji ulio karibu na Bahari.
147

Siku moja katika Bandari ya mji huo kuna jahazi limewasili ambalo ndani yake
akashuka Mfanya biashara tajiri sana. Mfanya biashara huyu aliamua kuishi
katika eneo hilo na kutangazia kua anataka kumuoa mwanamke mzuri kuliko wote
wa Mji huo. Hivyo watu wa Mji huo wakampelekea yule Binti mbele yake na
alipomuona akaridhika nae na kumpenda mbali ya kua aliambiwa juu ya sifa ya
Binti huyo. Ambae nae akakiri na kusema kua ataachana na kazi hio kama ataolewa
na Mfanya biashara huyo’

Baada ya kuoana, Mfanya biashara akamuelezea mkewe juu ya historia yake, na


hapo Binti akasema kua Binti aliechomwa kisu ndio yeye, na akamuonesha kovu
yake na kusema kua hana uhakika kama Wanaume aliozini nao wanafika mia ama
zaidi. Kuona hivyo basi yule Mfanya biashara akamwambia mkewe kua yule mtu
alitabiri kua kifo cha Binti huyo kitatokana na Buibui, hivyo wakaamua kujenga
Kasri kubwa sana katika maeneo ya Jangwani ambako ni vigumu kukutana na
mdudu Buibui.

Siku Moja walipokua wamekaa ndani ya Kasri lao baada ya kumalizika kari hilo.
Basi ghafla yule binti akamuona Buibui ananing’inia juu ukutani. Hivyo akashtuka
na kunadia: ‘Buibui huyu ataniua!’ hivyo akaanza kumkimbilia ili amuue kabla ya
kuuliwa yeye, hadi yule Buibui akaanguka chini, yule binti akajaribu kumkanyaga
kwa mguu wake ili amuue, lakini akamkosa na Buibui akamtafuna chini ya kucha
ya kidole chake cha Mguuu. Ghafl, Mguu huo ukabadilika rangi na kua mweusi
kutokana na sumu ya Buibui huyo, na hivyo haukuchukua mda isipokua binti huyo
akafariki Dunia.’

Kwa upande mwengine basi mbali ya kua hakuna kiumbe anaeweza kujificha dhidi ya
kifo lakini pia hakuna atakaeweza kukikimbia kama inavyosema aya ifuatayo:

ِ ‫ت ٱﻟﱠ ِﺬى ﺗَِﻔﱡﺮو َن ِﻣْﻨﻪُ ﻓَِﺈﻧﱠﻪُ ُﻣﻼَﻗِﻴ ُﻜﻢ ﰒُﱠ ﺗُـﺮﱡدو َن إِ َ ٰﱃ َﻋ ِﺎﱂ ٱﻟْﻐَْﻴ‬
‫ﺐ‬ َ ‫﴿ﻗُ ْﻞ إِ ﱠن ٱﻟْ َﻤ ْﻮ‬
َ ْ
﴾‫ﱠﻬ َﺎدةِ ﻓَـﻴُـﻨَـﺒِّﺌُ ُﻜﻢ ِﲟَﺎ ُﻛﻨﺘُﻢ ﺗَـ ْﻌﻤﻠُﻮ َن‬
َ ‫َوٱﻟﺸ‬
َ ْ
Qul inna almawta alladhee tafirroona minhu fa-innahu mulaqeekum thumma
turaddoona ila AAalimi alghaybi waalshshahadati fayunabbi-okum bima kuntum
taAAmaloona (Surat Al Jumuah 62:8)

Tafsir: Sema: Kwa hakika hayo Mauti ambayo mnayakimbia basi kwa hakika
yatakulakini, kisha mtarudishwa (kwa Allah Subhanah wa Ta’ala). Mwenye kujua juu
148

ya kila kitu kisichoonekana na kinachooonekana kisha mtabainishiwa juu ya yote


mliyokua mkiyafanya.

Aya hii pia nayo imetumia neno Mulaqeekum ambalo linatokana na neno Laqiya lenye
kumaanisha Kulaki yaani Kupokea Kitu au Mtu, Kukutana na Mtu au Kitu, Kukipitia
Kitu, Kukitegemea, Kukumbana na Kitu, Kuegemea Kitu, Kuelekea katika Muelekeo
Unaoelekea Kitu au Unaokabiliana na Kitu n.k.

Hivyo basi aya inatuwekea wazi kua Kifo kitamkabili kila kiumbe na bila ya shaka
ukifika mda wake basi kiumbe husika atakikimbilia mwenyewe kama mtoto mdogo
anavyomkimbilia na kumlaki mzee wake ambae hajamuona kwa mda mrefu sana
kutokana na kua na hamu nae.

Tuangalie mfano wa Iman Abu Muhammad Sulaiman Ibn Mihran Al Kahili Al Asad Al
Amash ambae yeye anatuambia kua: ‘Siku moja Nabii Sulayman alikua amekaa na
Mawaziri wake, mbele ya watu wengine, na mara mmoa kati ya Mawaziri wake
akagundua kua miongoni mwa watu waliopo mbele yao basi anamtizama sana yeye
kwa njia ya mshangao mkubwa sana, na kisha mtu huyo akatoweka. Yule Waziri
akamuuliza Nabii Sulayman kwa kumwambia: ‘Miongoni mwa hawa watu mimi
nilimuona mtu mmoja wao ambae alikua akiniangalia sana, hivi jee unamjua alikua
ni nani?’ Nabii Sulayman akajibu: ‘Yule alikua ni Malaika Izrail’ Yule Waziri
akasema: ‘kwa hakika alikua akiniangalia kama kwamba anataka kuichukua Roho
yangu. Hakika mimi nimeingiwa na khofu.’ Nabii Sulayman akamuuliza: ‘Jee
unataka nikusaiidie Vipi?’

Yule Waziri akasema: ‘Basi niondoe haraka ya Nabiyu Allahi Sulayman, Uamrishe
Upepo unichukue hadi katika maeneo ya Ardhi ya India.’ Nabii Sulayman
akauamrisha Upepo umrushe Waziri huyo hadi katika Ardhi ya nchini India.

Ukapita Mda, kisha siku moja Nabii Sulayman akakutana tena na Izrail na
kumuuliza: ‘Hivi ilikuaje siku ile ukawa unamuangalia yule Waziri wangu katika
hali kama ile?’ Malaika Izrail akasema: ‘Hakika mimi niliamrishwa kuitoa Roho
ya Mtu yule katika Ardhi ya India, hivyo nikashangaa kuona kua yeye yupo katika
eneo la Ardhi yako wakati anatakiwa awe kwenye Ardhi ya India.’

Nabii Sulayman akamuuliza Malaika Izrail: ‘Jee wewe hua unajua ni Roho ya Nani
na Nani utakayoitoa leo hii? ’

Malaika Izrail akajibu: ‘Kwa hakika mimi najua kuhiana na hilo kama vile ujuavyo
wewe, kwani mimi hua naletewa Majina tu ya watu wa kuwatoa Roho’
149

Hivyo Waziri wa Nabii Sulayman alitaka kuyakimbia Mauti lakini badala yake akawa ni
mwenye kuyakimbilia, na hivyo alipofika India akayakuta Mauti yakiwa yanamlaki yeye.
Hivyo kila mtu atazaliwa na kuishi kwa wakati wake na atakufa kwa wakati wake
maalum na hakuna atakaewahi wala kujichelewesha kuingia Duniani na pia kuuondoka
Duniani kama anavyosema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qur’an:

‫ﺎﻋﺔً َوﻻَ ﻳَ ْﺴﺘَـ ْﻘ ِﺪ ُﻣﻮ َن۞ َ�ﺑَِ ۤﲏ‬ ِ


َ ‫َﺟﻠُ ُﻬ ْﻢ ﻻَ ﻳَ ْﺴﺘَﺄْﺧُﺮو َن َﺳ‬ ِ ‫﴿وﻟِ ُﻜ ِﻞ أُﱠﻣ ٍﺔ أ‬
َ ‫َﺟ ٌﻞ ﻓَﺈ َذا َﺟﺂءَ أ‬َ ّ َ
ِ ‫ﺼﻮ َن ﻋﻠَﻴ ُﻜﻢ‬ ِ ِ ِ
َ‫َﺻﻠَ َﺢ ﻓَﻼ‬ ْ ‫آ�ﺗﻰ ﻓَ َﻤ ِﻦ ٱﺗﱠـ َﻘ ٰﻰ َوأ‬ َ ْ ْ َ ‫آد َم إ ﱠﻣﺎ َ�ْﺗﻴَـﻨﱠ ُﻜ ْﻢ ُر ُﺳ ٌﻞ ّﻣﻨ ُﻜ ْﻢ ﻳَـ ُﻘ ﱡ‬
َ
ِ‫ﱠ‬
‫ﻚ‬َ ِ‫ٱﺳﺘَ ْﻜﺒَـُﺮواْ َﻋْﻨـ َﻬﺂ أ ُْوﻟَـٰﺌ‬ ِ
ْ ‫ﻳﻦ َﻛ ﱠﺬﺑُﻮاْ ِﺂﺑ َ�ﺗﻨَﺎ َو‬ ِ ٌ ‫َﺧﻮ‬
َ ‫ف َﻋﻠَْﻴﻬ ْﻢ َوﻻَ ُﻫ ْﻢ َْﳛَﺰﻧُﻮ َن۞ َوٱﻟﺬ‬ ْ
﴾‫ﺎب ٱﻟﻨﱠﺎ ِر ُﻫﻢ ﻓِ َﻴﻬﺎ َﺧﺎﻟِ ُﺪو َن‬
ُ ‫َﺻ َﺤ‬ ْ‫أ‬
ْ
Walikulli ommatin ajalun fa-idha jaa ajaluhum la yasta/khiroona saAAatan wala
yastaqdimoona, Ya banee adama imma ya/tiyannakum rusulun minkum
yaqussoona AAalaykum ayatee famani ittaqa waaslaha fala khawfun AAalayhim
wala hum yahzanoona; Waalladheena kadhdhaboo bi-ayatina waistakbaroo
AAanha ola-ika as-habu alnnari hum feeha khalidoona (Surat Al Araf 7:34-36)

Tafsir: Na kwa kila Ummah una majaaliwa yake, na yanapofika majaaliwa yake, basi
hawawezi kuuchelewasha wala kuutanguliza saa yake (Majaaliwa hayo). Enyi Ibn
Adam kama akija Mtume kutoka miongoni mwenu, na akakusomeeni aya zangu, basi
yeyote yuele atakaekua Mcha Mungu na kufanya Mema, basi (Watu hao) hawatokua
na khofu wala hawatohuzunika. Lakini wa wale watakaozikataa aya zetu na kua na
kiburi juu yake basi makazi yao ni Motoni ambamo watakaa milele.

Hivyo ingawa pia Aya zinasema kua Nabii Nuh A’layhi Salaam aliishi kwa miaka 1000
na alikuwa katika mitihani mikubwa na watu wake kwa muda wa miaka 950, na miaka
50 iliyobakia aliishi maisha yaliyokua ya kawaida bila mitihani, hii inamaanisha kua
Nabii Nuh alitumia asilimia 95% ya uhai wake katika mitihani na asilimia 5% tu
iliyobakia katika maisha yake ndio aliitumia katika hali ya kawaida.

Lakini kuna kutofautiana kwa mitizamo ya Wanazuni juu ya Umri alioishi Nabii Nuh,
kwani mbali ya mtizamo tulioanza nao basi tuaona kua kuna mtizamo wa Imam Qatadah
Ibn Diama al Salusi ambae yeye anasema kua: Mda kamili wa uhai alioishi Nabii Nuh
ni miaka 1000 kasoro 50, na alikaa pamoja na watu wake kwa muda wa miaka 350
kabla ya kuanza kuwausia watu wake juu ya Allah Subhanah wa Taála, na akaishi
nao kwa mda wa miaka 350 akiwa katika hali ya kuwausia juu Mola wao na baada
150

ya Gharika pia aliishi kwa miaka 350 (Tafsir Al Qurán Adhim Imam Ibn Kathir, Tafsir
Imam Ibn Abbi Hatim)

Ama kwa upande wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema kua
‘Allah Subhanah wa Taála alimtuma Nuh kama Mtume wake kwa Watu wake
wakati Nuh akiwa na umri wa miaka 40 na akakaa akiwausia watu wake hao kwa
muda miaka 950, na baada ya Gharika, basi Nuh aliishi kwa muda wa miaka 60,
hadi watu wake walipoongezeka.’ (Dur al Mandhur Imam Al Suyuti)
Ama kuhusiana na neno Sanah na neno Aám ambayo yote mawili ni yeye maana moja
yenye kumaanisha Mwaka basi Wanazuoni pia wametofautiana jua ya kwa nini
yakatumika yote mawili katika aya moja, hivyo maneno haya mawili yametumika katika
aya kutokana na kama anavyosema Sultan al Balagha Imam Abu Qasim Mahmud Ibn
Umar Al Zamakhshari kua: ‘Kama ukihoji jee ni kwa nini aya kwanza imetumia neno
Sanah na kisha ikatumia neno Aám? Basi jibu litakua ni kua kutumia neno moja
katika kauli moja kunatakiwa kuepukwe kutokana na manufaa ya ufasaha wa
lugha, isipokua pale inapokua kufanya hivyo hua ni kwa makusudi kwa ajili ya
kutilia mkazo jambo husika.’(Tafsir Al Kashshaf)
Ama kwa upande Allamah Raghib Al Isfahan basi yeye anasema kua: ‘Kimaana neno
Aám ni sawa na neno Sanah, isipokua neno Sanah hua mara nyingi linatumika
kumaanisha mwaka ambao una shida na matatizo au ukame ndani yake na ndio
maana Ukame ukawa unaitwa Sanah, neno Aám hua linatumika kumaanisha
mwaka ambao ndani yake mna utulivu na neema kama tunavyoona pale Allah
Subhanah wa Taála aliposema katika Surat Yusuf:

ِ ِ ِ ‫ﺎث ٱﻟﻨ‬
﴾‫ﺼﺮو َن‬ ِِ ِ ِ
َ ‫﴿ﰒُﱠ َ�ْﺗِﻰ ِﻣﻦ ﺑَـ ْﻌﺪ ٰذﻟ‬
ُ ‫ﱠﺎس َوﻓﻴﻪ ﻳَـ ْﻌ‬
ُ ُ َ‫ﻚ َﻋ ٌﺎم ﻓﻴﻪ ﻳـُﻐ‬
Thumma ya/tee min baAAdi dhalika AAamun feehi yughathu alnnasu wafeehi
yaAAsiroona (Surat Yusuf 12:49)
Tafsir: Na kisha utakuja baada ya hapo mwaka ambao watu watanufaika na mvua ya
kutosha ambapo watakamua (ndani yake mvinyo na mafuta)’ (Surat Yusuf 12:49)
(Allamah Raghib al-Asfahani Mufradaat Alfaaz al-Qurán 2/140):
Ama Imam Abu Hasan Ibrahim Ibn Umar Burhaan ad Din al Biqaa’i Al Shafii basi yeye
anasema kua:
‘Neno Sanah hapa hua limetumika kuelezea maana mbaya ya siku za Kufr na Aám
hapa hua limetumika kuelezea kua baada ya kukufuru kwao basi wakagharikishwa,
na hapo maisha ya Nabii Nuh yakawa na wepesi na utulivu kutokana na imani ya
Walioamini na Neema katika ardhi.’ (Nazm ad-Durar (14/404))
151

Imam Umar Ibn Ali Ibn ‘Aadil Al Dimashqi Al Hanbali basi yeye anasema kua
‘Mwanzoni aya imetumia neno Sanah na mwishoni ikatumia neno Aám ili
kurahisisha utamkaji na hivyo kusiwe na uzito katika usomaji wa aya hio. Vile vile
neno Aám limetumika kwa kuelezea miaka 50 ili kutilia mkazi kipindi ambacho
Mtume wa Allah Subhanah wa Taála alipoachana na waovu hao, kua katika hali ya
utulivu, Waarabu hutumia neno Aám kumaanisha Neema na neno Sanah
kumaanisha Ukame’ (Al-Lubaab fi 'Ulum al-Kitab, 12/429)


MASIKITIKO YA NABII NUH KWA MOLA WAKE DHIDI YA WATU
WAKE.

Hivyo tunaporudi kwa Nabii Nuh na watu wake basi tunaona kua kutokana na Ujinga na
Kibri cha watu hao basi hawakutaka kurekebisha majaaliwa yao kwa kupitia katika Lawh
Al Ithbati na badala yake waliamua kua bora yambakia kama yalivyo, na hivyo wakaona
kua Nabii Nuh anataka kuwazidi kwa hoja, hivyo wakaamua kumtishia Nabii Nuh kwa
kumwambia kua kama hasikii wanachomwambia, na hawachi juu ya kuwausia wao na
watu wao juu ya kuachana na mambo yao, basi watampa adhabu ambayo hatoisahau
katika maisha yake kwa kusema:

﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ِ ِ ﴿
ُ ُ‫ﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻟَﺌ ْﻦ ﱠﱂْ ﺗَـْﻨـﺘَﻪ ٰﻳـﻨ‬
َ ‫ﻮح ﻟَﺘَ ُﻜﻮﻧَ ﱠﻦ ﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻤْﺮ ُﺟﻮﻣ‬
Qaloo la-in lam tantahi ya noohu latakoonanna mina almarjoomeena (Surat Ash
Shuara 26:116)

Tafsir: Watu hao wakasema (Kumwambia Nabii Nuh): ‘Kama hukusita ewe Nuh! Basi
kwa hakika wewe utakua ni miongoni mwa watakaopigwa mawe’.

Neno Marjummiina linatokana neno Rajama ambalo humaanisha Kufukuza, Kupiga


mawe, Kuua kwa kupiga mawe, Kulaani, Kusingizia na pia Kutukana, hivyo basi
maneno ya watu hawa wa Nabii Nuh walikua wanaweka wazi kuchukiwa kwao na
vitendo vya Nabi Nuh vya kutokana kuwaongoza watu wake kutoka katika upotofu na
kuwavuta katika uongofu kwa jithada zake zisizoonesha kufifia nguvu zake, hivyo basi
152

wakaamua kumzuia kwa kutumia nguvu za vitisho vya kumpa adhabu kali ambayo
hatoisahau maishani mwake.

Baada ya hali kufikia hivyo basi Nabii Nuh akaamua kumuelezea Mola wake juu ya
mitihani yake hio kama inavyosema aya ifuatayo:

‫ت ﻗَـ ْﻮِﻣﻰ ﻟَْﻴﻼً َوﻧـَ َﻬﺎراً ۞ ﻓَـﻠَ ْﻢ ﻳَِﺰْد ُﻫ ْﻢ ُد َﻋﺂﺋِ ۤﻲ إِﻻﱠ ﻓَِﺮاراً ۞ َوإِِّﱏ‬ُ ‫ب إِِّﱏ َد َﻋ ْﻮ‬ ِّ ‫ﺎل َر‬
َ َ‫﴿ﻗ‬
ِ ِِ ۤ ۤ ِ ِ
ْ‫َﺻﱡﺮوا‬ ْ ‫َﺻﺎﺑِ َﻌ ُﻬ ْﻢ ِﰲ آذَا� ْﻢ َو‬
َ ‫ٱﺳﺘَـ ْﻐ َﺸ ْﻮاْ ﺛﻴَﺎﺑـَ ُﻬ ْﻢ َوأ‬ َ ‫ُﻛﻠﱠ َﻤﺎ َد َﻋ ْﻮﺗُـ ُﻬ ْﻢ ﻟﺘَـ ْﻐﻔَﺮ َﳍُْﻢ َﺟ َﻌﻠُﻮاْ أ‬
ۤ ِ ِ ْ‫وٱﺳﺘَ ْﻜﺒـﺮوا‬
‫ت َﳍُْﻢ‬ ْ ‫ﺖ َﳍُْﻢ َوأ‬
ُ ‫َﺳَﺮْر‬ ُ ‫ٱﺳﺘ ْﻜﺒَﺎراً ۞ ﰒُﱠ إِِّﱏ َد َﻋ ْﻮﺗـُ ُﻬ ْﻢ ﺟ َﻬﺎراً ۞ ﰒُﱠ إِِّﱐ أ َْﻋﻠَْﻨ‬ ْ َُ ْ َ
﴾ً‫إِ ْﺳﺮارا‬
َ
Qala rabbi innee daAAawtu qawmee laylan wanaharan, Falam yazid-hum duAAa-
ee illa firaran Wa-innee kullama daAAawtuhum litaghfira lahum jaAAaloo
asabiAAahum fee adhanihim waistaghshaw thiyabahum waasarroo waistakbaroo
istikbaran Thumma innee daAAawtuhum jiharan. Thumma innee aAAlantu lahum
waasrartu lahum israran (Surat Nuh 71:5-9)

Tafsir: Ambapo nae (Nuh) akasema: Ewe Mola wangu! Kwa hakika mimi nimekua
nikiwaita watu wangu usiku na mchana (Kumkubali Allah Subhanah wa Ta’ala,
kutomshirikisha na kutii maamrisho yake) Lakini hakukuzidisha kitu kuwaita kwangu
kote isipokua kuwasukuma mbali zaid (Kutoka katika ukweli wangu), Na kwa hakika
kila ninapowaita ili wapate msamaha wako, basi hutia vidole vyao kwenye masikio yao,
hujificha kwa nguo zao na kujiona kutokana na Kibri chao. Kisha nikawaita kwa sauti,
Kisha nikawaita hadharani na pia kwa faragha.

Aya zinatuonesha kua ingawa Nabii Nuh alikua akitumia vithibitisho vya hoja mbele ya
watu wake, lakini watu hawakutaka kunufaika na vithibitisho hivyo, kwani alikua ni
wenye kuziba masikio yao, na kuzificha nyuso zao na nguo zao ili wasionekane wala
kujulikana na Nabii Nuh kua fulani amepita mbele yake kwa maana hio basi badala ya
Nabii Nuh kua ni mwenye kuonekana kua ni neema kwa watu wake basi watu hao
walimuona kua ni nuksi isiyokua na haja hata ya kuikaribia, kiasi ya kua hata Nabii Nuh
alipokua akienda katika majumba yao kuwausia kisirisiri basi watu hao walikua
hawamfungulii milango kwa sababu ya ujinga na kibri waliokua nao na hivyo basi watu
hao wakawa ni wenye kua mbali na Muongozo wa Allah Subhanah wa Ta'ala kupitia
kwa Nabii Nuh.
153

Anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: 'Kudumu katika
Dhambi kwa watu wa Nabii Nuh kulipelekea watu hao kuingia katika hali ya
Ujinga, na Ujinga ukawapelekea Kua ni wenye kuvuka mipaka na kuzama katika
Upotovu. Na upotovu ukawapelekea kua ni wenye kua na Unafiq na unafiq wao
ukawapeleka kua ni wenye kufanya Kufr, na hivyo hua ni wenye kuona Nuru
wanapokumbushwa tu, lakini wanapoachana na mkumbushaji huyo basi hua kama
hayajasikia kitu na hakuna kilichoinga ndani ya nyoyo zao ndio maana Allah
Subhanah wa Ta'ala akasema:'

ْ‫َﺿﺂءَ َﳍُْﻢ ﱠﻣ َﺸ ْﻮاْ ﻓِ ِﻴﻪ َوإِ َذآ أَﻇْﻠَ َﻢ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ ﻗَ ُﺎﻣﻮا‬


َ ‫ﺼ َﺎرُﻫ ْﻢ ُﻛﻠﱠ َﻤﺎ أ‬
َ ْ‫ﻒ أَﺑ‬ ُ ‫﴿ﻳَ َﻜ‬
ُ َ‫ﺎد ٱﻟْﺒَـْﺮ ُق َﳜْﻄ‬
﴾‫ٱﻪﻠﻟ َﻋﻠَ ٰﻰ ُﻛ ِﻞ َﺷﻲ ٍء ﻗَ ِﺪﻳﺮ‬ ِ ِ َ ْ‫ٱﻪﻠﻟ ﻟَ َﺬ َﻫﺐ ﺑِﺴﻤﻌِ ِﻬﻢ وأَﺑ‬
ٌ ْ ّ َ‫ﺼﺎ ِرﻫ ْﻢ إ ﱠن ﱠ‬ َ ْ ْ َ َ ُ‫َوﻟَ ْﻮ َﺷﺂءَ ﱠ‬
Yakadu albarqu yakhtafu absarahum kullama adaa lahum mashaw feehi wa-idha
adhlama AAalayhim qamoo walaw shaa Allahu ladhahaba bisamAAihim
waabsarihim inna Allaha AAala kulli shay-in qadeerun (Surat Al Baqara 2:20)

Tafsir: Bado kidogo mwangaza uchukue macho yao, kwani unapowamurikia basi hua
ni wenye kuingia ndani yake, na wanapokua katika kiza basi hua ni wenye kusimama.
Na kama Allah angetaka basi angewapokonya usikivu wao na macho yao. Kwani kwa
hakika ana uwezo juu ya kila kitu.

Bila ya shaka ingawa Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari amefafanua
aya kulingana mada inayowazungumzia watu wa Nabi Nuh lakini na sisi aya pia
zinatugusa kwa sababu wengi wetu leo hii tumekua wajinga, na pia tuna Unafiq ndani
yetu na kama inavyosema aya juu ya hatari ya kua na hali hio ambayo huwa ni yenye
kupelekea kwenye maangamizo kama hatutokua na umakini katika Imani ya dini yetu.

Baada ya Nabii Nuh kumlalamikia Mola wake juu ya watu wake hao na njia alizotumia
kuwausia watu wake kwa ajili ya akhera yao na kuona kua hakuna muelekeo wowote
kutoka katika nyoyo na nafsi zao basi akaamua kutumia mbinu nyengine ambazo ni za
kuwaambia kuhusiana na manufaa ya kidunia watakayoyapata kama watakua ni wenye
kumfuata Mola wao. Allah Subhanah wa Taála anatuonesha namna Nabii Nuh alivyokua
akitumia kauli zilizo laini zenye hikma, busara za kujaribu kuwafumbua macho watu
wake ndani yake kutokana na kuwaonea huruma watu wake kwa kusema:
154

۞ ً‫ٱﺳﺘَـ ْﻐ ِﻔﺮواْ رﺑﱠ ُﻜﻢ إِﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن َﻏ ﱠﻔﺎراً ۞ ﻳـُﺮِﺳ ِﻞ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺂء َﻋﻠَْﻴ ُﻜﻢ ِّﻣ ْﺪرارا‬ ُ ‫﴿ﻓَـ ُﻘ ْﻠ‬
َ ْ َ َ ْ ْ َ ُ ْ ‫ﺖ‬
ٍ ِ ِ
﴾ً‫ﱠﺎت وَْﳚ َﻌﻞ ﻟﱠ ُﻜﻢ أَﻧْـ َﻬﺎرا‬
ْ
‫ﱠ‬
َ ‫ﲔ َوَْﳚ َﻌﻞ ﻟ ُﻜ ْﻢ َﺟﻨ‬ َ ‫َوﳝُْﺪ ْد ُﻛ ْﻢ ِﺄﺑ َْﻣ َﻮ ٍال َوﺑَﻨ‬
Faqultu istaghfiroo rabbakum innahu kana ghaffaran, Yursili alssamaa
AAalaykum midraran, Wayumdidkum bi-amwalin wabaneena wayajAAal lakum
jannatin wayajAAal lakum anharan (Surat Nuh 71:10-12)

Tafsir: Nikawaambia: ‘Ombeni msamaha kwa Mola wenu, kwani hakika yeye ni
mwingi wa kusamehe, Atakushushieni juu yenu mvua ya kutosha, na atakuongezeeni
katika mali na watoto, na atakuzidishieni katika mashamba yenu na kukutiririshieni
mito ya maji.’

Allah Subhanah wa Ta’ala anatuwekea wazi kua ili kuepukana na mitihani ya Ukame,
Umasikini na Watoto na barka katika kila kitu chetu basi ni muhimu kua ni wenye
kudumu katika kufanya Istighfar.

Anasema Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Siku moja Hasan Al Basr, alikua
amekaa pamoja na Wanafunzi wake na mmoja miongoni mwao akawa ni mwenye
kulalamika juu ya kukosekana kwa mvua katika mji wao. Hivyo Hasan Al Basr
akasema: ‘Fanyeni Istighfar!’ na mwengine akalalamikia juu ya kutopata Watoto,
na mwengine akalalamikia juu ya Umasikini, na mwengine akalalamikia juu ya
kutokua na barka katika Ardhi yake na hivyo kukosa mazao katika msimu huo.
Ambapo Hasan Al Basr akawaambia wanafunzi wake wote hawa kua wanatakiwa
wafanye Istighfar kwa wingi. Watu hao wakauliza: ‘Hivi inakuaje kua sote
unatushauri tufanye kitu kimoja ingawa tuna malalamiko tofauti?’ ambapo Hasan
Al Basr akawasomea aya za Surat Nuh 71:10-12.’

۞ ً‫ٱﺳﺘَـ ْﻐ ِﻔﺮواْ رﺑﱠ ُﻜﻢ إِﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن َﻏ ﱠﻔﺎراً ۞ ﻳـُﺮِﺳ ِﻞ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺂء َﻋﻠَْﻴ ُﻜﻢ ِّﻣ ْﺪرارا‬ ُ ‫﴿ﻓَـ ُﻘ ْﻠ‬
َ ْ َ َ ْ ْ َ ُ ْ ‫ﺖ‬
ٍ ‫وﳝُْ ِﺪ ْد ُﻛﻢ ِﺄﺑَﻣﻮ ٍال وﺑﻨِﲔ وَﳚﻌﻞ ﻟﱠ ُﻜﻢ ﺟﻨ‬
﴾ً‫ﱠﺎت وَْﳚ َﻌﻞ ﻟﱠ ُﻜﻢ أَﻧْـ َﻬﺎرا‬
ْ َ َ ْ َ ْ َ َ ََ َ ْ ْ َ
Faqultu istaghfiroo rabbakum innahu kana ghaffaran, Yursili alssamaa
AAalaykum midraran, Wayumdidkum bi-amwalin wabaneena wayajAAal lakum
jannatin wayajAAal lakum anharan (Surat Nuh 71:10-12)
155

Tafsir: Nikawaambia: ‘Ombeni msamaha kwa Mola wenu, kwani hakika yeye ni
mwingi wa kusamehe, Atakushushieni juu yenu mvua ya kutosha, na atakuongezeeni
katika mali na watoto, na atakuzidishieni katika mashamba yenu na kukutiririshieni
mito ya maji.’

Na tunapoiangalia ayah kihistoria basi tunaona kua katika kipindi cha Amir ul Muuminina
Sayyidna Umar Ibn Al Khatttab Radhi Allahu Anhu kulitokea ukame mkubwa sana katika
Ardhi za Waislam hivyo Amir ul Muuminina Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu
akatoka na watu wake kwa ajili ya kuenda kusali Sala ya Mvua, na walipofika katika
sehemu waliyokubaliana kukutana basi Amir ul Muuminina Umar Ibn Al Khattab Radhi
Allahu Anhu akawa ni mwenye kufanya Istighfar tu, kwa Allah Subhanah wa Ta’ala.

Hivyo watu wakamuuliza Amir ul Muuminina Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu
kwa kusema kua: ‘Ya Amir ul Muuminina, mbona hatusali?’ Amir ul Muuminina Umar
Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu akajibu: ‘Kwa sababu nimeshagonga katika
Mlango ambao Mvua hua inashushwa kupitia kwake.’ kisha akasoma aya zifuatazo:

﴾ً‫ٱﺳﺘَـ ْﻐ ِﻔﺮواْ رﺑﱠ ُﻜﻢ إِﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن َﻏ ﱠﻔﺎراً ۞ ﻳـُﺮِﺳ ِﻞ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺂء َﻋﻠَْﻴ ُﻜﻢ ِّﻣ ْﺪرارا‬ ُ ‫﴿ﻓَـ ُﻘ ْﻠ‬
َ ْ َ َ ْ ْ َ ُ ْ ‫ﺖ‬
Faqultu istaghfiroo rabbakum innahu kana ghaffaran, Yursili alssamaa
AAalaykum midraran, (Surat Nuh 71:10-11)

Tafsir: Nikawaambia: ‘Ombeni msamaha kwa Mola wenu, kwani hakika yeye ni
mwingi wa kusamehe, Atakushushieni juu yenu mvua ya kutosha’

Bila ya shaka Nabii Nuh alikua akiwajali sana watu wake na alikua akiwaonea huruma
kiasi ya kua alitumia kila njia kuwathibitishia watu wake juu ya njia sahihi na
inayotakiwa kufuatwa kwani walikua ni kama wenda wazimu walioghafilika kabisa juu
ya Mola wao na kuzama katika Kufr kutokana na Kibr na Ujinga wao na mwisho kufikia
kuwahoji kwa vithibitisho vilivyowazi kutokana na maumbile yao na mazingira yao
wanayoishi na hivyo labda huenda wakawa ni wenye kufunguka macho kama
inavyosema Qurán:

ِِ
ُ‫ٱﻪﻠﻟ‬ َ ‫﴿ ﱠﻣﺎ ﻟَ ُﻜ ْﻢ ﻻَ ﺗَـْﺮ ُﺟﻮ َن ﱠﻪﻠﻟ َوﻗَﺎراً ۞ َوﻗَ ْﺪ َﺧﻠَ َﻘ ُﻜ ْﻢ أَﻃْ َﻮاراً ۞ أََﱂْ ﺗَـَﺮْواْ َﻛْﻴ‬
‫ﻒ َﺧﻠَ َﻖ ﱠ‬
﴾ً‫ات ِﻃﺒَﺎﻗﺎ‬ ٍ ‫ﺳﺒﻊ َﲰﺎو‬
َ َ َ َْ
156

Ma lakum la tarjoona lillahi waqaran, Waqad khalaqakum atwaran, Alam taraw


kayfa khalaqa Allahu sabAAa samawatin tibaqan,(Surat Nuh 71:13-15)

Tafsir: Mna nini nyie? (Kua hamumuogopi Allah Subhanah wa Taála) hata hamtarajii
kumtukuza Allah. Wakati ni yeye aliekuumbeni kupitia katika hali tofauti. Jee
hamuoni namna Allah alivyoumba Mbingu saba moja juu ya nyengine. Na akaweka
ndani yake Mwezi kua mwangaza, na Jua kua ni Taa?

Naam hivi inakuaje kwa Ibn Adam kufikia katika hali kama hio ambayo ni ya hatari sana
kwake ya kukataa kumtukuza Mola wale aliemuumba, kwani hili ndilo suali ambalo
Nabii Nuh alikua akiwahoji watu wake. Yaani kwanini wanamuasi Mola wao ambae ndie
aliewalea tangu wakiwa ndani ya tupu za wazee wao, mpaka wakaingizwa ndani ya
tumbo la uzazi, na kuanza kukua kidogo kidogo hatu kwa hatua mpaka wakazaliwa. Na
kua wakubwa kidogo kidogo, hadi kufikia uzeeni akiwa chini ya uangalizi wa Mola wake
kiasi ya kua kama asingetaka basi Ibn Adam huyo asingekuwepo wala asingefikia umri
huo.

Aya imetumia maneno yasemayo Sabaa Samawatin Tibaqan yaani Mbingu Saba
zilikaliana kitabaka. Ambapo neno Samawat limetokana na neno Sama ambalo kwa lugha
ya Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Kua juu, Kua na hali ya kunyayuliwa, Kitu kua
katika hali ya juu ya kupendeza kiasi ya kua kitu hicho kikawa kinastahiki kuangaliwa
kwa mshangao kutokana na maajabu ya uzuri wake.

Neno Sama ndio pia lililotoa neno Ism ambalo hua ni Jina la Kitu au Sifa ya Kitu na hivyo
basi neno Ism hua pia ni lenye kumaanisha Kitu kinachokitofautisha kitu chengine
kutokana na upekee wa uhalisia wa kitu hicho. Na ukweli ni kua mara nyingi Waislam
tumekua tukisema Biismi Allahi katika kuanza mambo yetu mengi, lakini hapo ahopo
tumekua si wenye kujua kua mbali ya kua unaposema Biismi Allahi basi hua unasema:
'Naanza kwa jina Allah' lakini pia unaposema Biismi Allahi basi hua: Unamtukuza
na kumpandisha darja ya juu kabisa Allah Subhanah wa Ta'ala kutokana na sifa
zake za upekee kutokana na kua ni yeye pekee anaestahiki darja hio ya upekee.

Hivyo neno Sama ndio pia lililotoa neno Samawati ambalo humaanisha Mbingu au
Sehemu ya Juu ya kitu yaani kama paa la kitu, au Sehemu ya juu kabisa ya Ulimwengu
ambayo sisi Ibn Adam hua tunaishi chini yake na hivyo kua kama paa lililofunika juu
yetu. Na kama tunavyoona kua aya imetaja Sabaa Samawatin Tibaqan yaani Mbingu
saba zilizo kwenye matabaka saba tofauti. Ama juu ya hili basi kuna mitizamo tofauti
ambapo miongoni mwao ni pamoja na ule wa Ilm Ruhanniya ambao unasema kua Sabaa
Samawati hizi ni Sayari 7 ambazo ni:

1-Mercury - Attarid.
2-Venus - Zuhra.
157

3-Saturn - Zohal.
4-Earth - Duniya.
5-Mars - Mirikh.
6-Jupiter - Mushtara.
7-Moon - Qamar.

Ambapo kulingana na mtizamo huo basi hua tunaona kua Sabaa Samawatin ni Matabaka
yanayozunguka Sayari hizi na nyenginezo kwani neno Saba kwa Lugha ya Kiarabu hua
linamaanisha idadi ya vitu Saba au zaidi.

Kwa upande wa Sahaba Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu basi yeye ni mwenye
kusema kua:‘Umbali wa masafa ya kutoka Duniani mpaka katika Mbingu ya
kwanza (ambayo ni ya juu yetu) basi ni umbali wa safari ya miaka 500 na masafa
baina ya tabaka moja la Mbingu mpaka jengine hua ni miaka 500’
Hapa inabidi tujue kua Allah Subhanah wa Taala kutokana na Hikma zake na Rehma
zake basi ametujaalia kua ni wenye kuishi chini matabaka ya Mbingu saba ambapo tabaka
la Mbingu ya kwanza ni ile iliopo juu yetu ambayo ina jukumu la tulinda sisi wenye
kuishi Ulimwenguni kutokana na madhara ya nguvu za kimaumbile za Jua na sayari
nyengine zilizopo nje ya mazingira ya Dunia ambazo hua ni zenye kutoa mionzi mikali
sana. Hivyo basi tabaka Mbingu zinazotuzunguka hua ni kama Mwamvuli unaozuia
athari hizo kwa sababu vyenginevyo basi hata mionzi ya jua kuchunjwa ingekua sio
yenye kutudhuru sisi tu bali ingekua ni yenye madhara kwa kila kiumbe kilichopo
Duniani, kwa upande mwengine bila ya kuwepo kwa mbigu hizo basi pia ingekua kuna
baridi kali sana katika wakati wa usiku kiasi ya kua kila kitu ardhini kingekua ni chenye
kugeuka na kua barafu.
Miongoni mwa manufaa ya tabaka la Mbingu iliyokaribu nasi basi ni kua ndio sehemu
ambayo hua inabeba maji ya mvua na kuipeleka sehemu inayohitajika kwa ajili ya
kunyesha na kunufaisha maisha yetu hapa Duniani. Na vile vile miongoni mwa manufaa
ya tabaka hilo la Mbingu ya duniani hua pia ni kubeba na kusambaza hewa za aina ya
Nitrogen, Oxygen na Carbon Dioxide ambazo ni muhimu sana kwa uhai wetu na hii si
kwa ajili ya mahitajio ya kuvuta kwetu hewa na kutoa kwa ajili ya uhai wetu lakii pia
kwa ajili mambo mengine, kwa mfano bila ya kuwepo kwa hewa ya Oxygen basi
tusingekua na uwezo wa kuwasha moto kwa ajili ya kupika vyakula vyetu ambavyo
haviwezi kuwiva bila ya kupikwa kwa kutumia moto. n.k
Ama kwa mtizamo wa pili basi pia ni ule unaomaanisha kua ni Matabaka Saba tofauti
moja baada ya jengine kama yalivyo maganda va Kitunguu Maji au Kabichi. Ambayo
hua ni Matabaka ya Mbingu zilizouzunguka Ulimwengu wote kwa ujumla kama
ilivyoelezewa katika kisa cha safari ya Isra na Miraj wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi
wa Salam alipoenda Mbinguni.
158

Na pia kuna wasemao kua hii ni kama ilivyo kulingana na mtizamo wa Ilm ya Jiografia
ambapo hapa tunakutana na Matabaka yafuatayo:

1-Trotosphere - Ambayo ndio sehemu ya chini ya Mbingu ambayo chini yake ndio
tunaishi sisi ambalo kutoka chini ardhini mpaka juu kwenye mpaka wake hua ni 16 km.

2-Stratosphere ambayo ipo juu ya Trotosphere kwa masafa ya kuanzia 15 km na mwisho


wake 50 km kutoka ardhini. Hili hua ndio eneo ambalo linatumiwa sana na ndege za
kivita, eneo hili hua halina upepo wala mawingu.

3-Chemosphere ambayo ipo juu ya Stratosphere hadi kufikia masafa ya 80 km kuelekea


juu.

4-Mesosphere ya kati na kati.

5-Ionosphere ambayo ipo 400 km baada ya Mesosphere, hili hua ni eneo ambalo hewa
yake hua imejaa nguvu za umeme kwa sababu ya mkusanyiko wa gesi na ndio maana
likawa linaitwa Ionosphere kwa sababu kuna electron nyingi sana ndani yake, na hivyo
eneo hili kimaumbile ndio linalohusika na kutumika kusafirisha mawimbi ya umeme wa
sumaku ya masafa mbali mbali ikiwemo ya Redio, Tv, Simu, Enternet n.k

6-Exosphere ambayo ndio eneo ambalo Satelite na kituo cha Kimataifa cha anga za juu
hua zinazunguka ndani yake, kwani eneo hili ni eneo ambalo halina nguvu za mvutano
wala za msuguano hivyo kila kitu hua kinaelea juu yake.

7-Magnetosphere ambayo inajumuisha Exosphere na ukubwa zaid ya 64000 km ambayo


mpaka leo hi hakuna aliefika huko wala kujua habari zake, kwani kuna nguvu kubwa
sana ya mvutano kiasi ya kua, hakuna kinachoweza kustahamili mvutano huo na hivyo
basi kitu kitakachofika huko hakitokua na uwezo wa kurudi tena kwani kitavutwa
kusikojulikana na kitatoweka milele.
W Allahu aAalam!

Ama kwa upande mwengine basi tunaona kua Sabaa Samawati Tibaqan hua pia ni zenye
kutafsiriwa kama ni Mifumo Saba tofauti ya Mbingu na Sayari zake ambayo ndani yake
inajumuishwa mifumo ifuatayo:

1. Solar System hua ni mfumo wa Jua ambao unajumuisha Jua, Nyota, Sayari, Mwezi
na Dunia ambao ndio mfumo tunaoishi Ibn Adam ndani yake.
2. Galaxy hua unajumuisha mkusanyiko wa kundi la Sayari na Nyota 400 Bilioni ndani
yake.
3. Cluster ambayo hua unajumuisha (Galaxy) makundi ya Nyota na Sayari tofauti ndani
yake.
159

4. Supercluster ambao hua unajumuisha (Clusters) makundi Mengi zaidi ya Nyota na


Sayari tofauti ndani yake.
5. Filament ambao hua unajumuisha (Super Cluster) Makundi mengi zaid ya maradufu
ya Super cluster.
6. Universe ambao unajumuisha (Filament) Makundi tofauti ya Filament.
7. Multiverse ambao unajumuisha mchanganyiko wa Universe tofauti.

Na ukweli ni kua Allah Subhanah wa Ta’ala amezungumzia juu ya Matabaka haya Saba
ya Mbingu na kuficha maana yake ndani yake kiasi ya kua hakuna anaejua kwa kina juu
yake hivyo basi kutuwachia sisi Ibn Adam kutafakkar na kuzingatia ukubwa wake yeye
Muumba pamoja na uwezo wake katika kuumba kwake huko kulingana na kila mmoja
miongoni mwetu kwa uwezo wake wa kiufaham na kulingana na I’lm yake. Na ndio
maana ikawa kuna mitizamo tofauti juu ya maana halisi ya Sabaa Samawatin Tibaqan.

Aya zinaendelea kuweka wazi hoja alizotoa Nabi Nuh kwa watu wake kwa kusema:

﴾ً‫ﱠﻤﺲ ِﺳﺮاﺟﺎ‬ ِِ ﴿
َ َ ْ ‫َو َﺟ َﻌ َﻞ ٱﻟْ َﻘ َﻤَﺮ ﻓﻴﻬ ﱠﻦ ﻧُﻮراً َو َﺟ َﻌ َﻞ ٱﻟﺸ‬
WajaAAala alqamara feehinna nooran wajaAAala alshshamsa sirajan.(Surat Nuh
71:16)

Tafsir: Na akaweka ndani yake Mwezi kua mwangaza, na Jua kua ni Taa?

Allah Subhanah wa Ta’ala anatuambia kua amejaalia Mwezi kua ni Nuru ndani yake,
ambapo tunapoangalia maana ya neno Nuru basi tunaona kua limetokana na neno Nara
ambalo hua linamaanisha Kung’ara, kutoa Moto, Nuru au Mwangaza kwa kutegemea
kitu chengine. Na hivyo basi kutuwekea wazi kua Mwezi hua unang’ara kutokana na
Muangaza wa kitu chengine ambacho ni Jua ambalo nalo limetajwa kama Sirajan yaani
Taa kutokana na ku ana Nuru yake wenyewe ya kujitegemea, ambapo vitu viwili hivi
vyote vimo ndani yake hizo Samawat lakini katika sehemu mbili tofauti.

Na kama tulivyosema hapo juu kua katika matabaka hayo kuna nyota zaidi 400 Bilioni,
lakini aya imegusia vitu viwili hivi kwa sababu Jua ndio linalowakilisha Muangaza wa
wakati wa Mchana katika maisha yetu na Mwezi hua ni wenye kuwakilisha mwangaza
wa Usiku.

Na kabla ya kuendelea zaidi basi nadhani kwanza tuzungumzie juu ya maana nyengine
ya Nur kwani neno Nur hua linamaana nyingi tofauti, ambapo baadhi miongoni mwao
hua ni Bi Al Ishtiraq yaani zenye maana zaidi ya mbili, baadhi hua hua ni ya juu juu na
baadhi hua ni yenye kushabihisha kitu, kwa mfano kuna Nuru ya Mwezi, Nuru ya Jua,
160

Nuru ya maumbile ya Malaika, Nuru ya Moyo na ufahamu wa Ibn Adam, Nuru ya Imani,
Nuru ya Taqwa, Nuru ya Almasi, Dhahabu n.k

Hivyo ili watu wasije wakachanganya pale niliposema kua Nur hua inamaanisha
Kung’ara au kutoa Mwangaza unaotegemeana na kitu chengine kama tulivyosema
kuhusiana na Nuru ya mwezi. Kwani kuna baadhi wanaweza wakajiuliza kuhusiana na
jina Tukufu la Allah Subhanah wa Ta’ala ambalo ni la Al Nur kama ilivyosema aya
ifuatayo ya Surat Nur:

‫ﺎح ِﰱ‬ ِ ‫ض ﻣﺜَﻞ ﻧُﻮِرﻩِ َﻛ ِﻤ ْﺸ َﻜﻮاةٍ ﻓِﻴﻬﺎ ِﻣﺼﺒ‬ ِ ‫ات َوٱﻷ َْر‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻧُﻮر ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬ ﴿
ُ َ‫ﺼﺒ‬ ْ ‫ﺎح ٱﻟْﻤ‬
ٌ َْ َ ُ َ َ َ ُ ُ‫ﱠ‬
َ‫ي ﻳُﻮﻗَ ُﺪ ِﻣﻦ َﺷ َﺠَﺮةٍ ﱡﻣﺒَ َﺎرَﻛ ٍﺔ َزﻳْـﺘُﻮﻧٍَﺔ ﻻﱠ َﺷْﺮﻗِﻴﱠ ٍﺔ َوﻻ‬ ‫ﺐ ُد ِّر ﱞ‬ٌ ‫ﺎﺟﺔُ َﻛﺄَﻧـﱠ َﻬﺎ َﻛ ْﻮَﻛ‬
ٍ ‫زﺟ‬
َ ‫ﺎﺟﺔ ٱﻟﱡﺰ َﺟ‬
َ َُ
‫ٱﻪﻠﻟُ ﻟِﻨُﻮِرﻩِ َﻣﻦ‬
‫ﻮر َﻋﻠَ ٰﻰ ﻧُﻮٍر ﻳَـ ْﻬ ِﺪى ﱠ‬ ِۤ ٍ
ُ ‫َﻏْﺮﺑِﻴﱠﺔ ﻳَ َﻜ‬
ٌ ‫ﺎد َزﻳْـﺘُـ َﻬﺎ ﻳُﻀﻲءُ َوﻟَ ْﻮ َﱂْ ﲤَْ َﺴ ْﺴﻪُ َ�ٌر ﻧﱡ‬
﴾‫ٱﻪﻠﻟ ﺑِ ُﻜ ِﻞ َﺷﻲ ٍء َﻋﻠَﻴِﻢ‬ ‫ﱠ‬ ‫و‬ ِ
‫ﱠﺎس‬ ‫ﻨ‬ ‫ﻠ‬ِ‫ﺎل ﻟ‬
َ َ‫ٱﻪﻠﻟُ ٱﻷ َْﻣﺜ‬
‫ب ﱠ‬ ُ ‫ﻀ ِﺮ‬
ْ َ‫ﻳَ َﺸﺂءُ َوﻳ‬
ٌ ْ ّ ُ َ
Allahu nooru alssamawati waal-Ardhi mathalu noorihi kamishkatin feeha
misbahun almisbahu fee zujajatin alzzujajatu kaannaha kawkabun durriyyun
yooqadu min shajaratin mubarakatin zaytoonatin la sharqiyyatin wala
gharbiyyatin yakadu zaytuha yudee-o walaw lam tamsas-hu narun noorun AAala
noorin yahdee Allahu linoorihi man yashao wayadhribu Allahu al-amthala lilnnasi
waAllahu bikulli shay-in AAaleemun(Surat Nur 24:35)

Tafsir: Allah ni Nuru ya Mbingu na Ardhi, mithli ya Nuru yake ni kama Mishkat
(Mishkat ni sehemu kama kidirisha ambacho hujengwa maalum kwa ajili ya kuwekea
taa ukutani na hivyo kufanya muangaza wa taa hiyo uwe mkubwa zaid kuliko taa hiyo
ikikaa katika sehemu iliyo wazi), na ndani yake mna taa, na taa hiyo imo ndani ya
kioo. Kioo ambacho kinang’ara kama Nyota ya Durriyun (aina ya nyota yenye
kung’ara sana kama Lulu), (Taa) ambayo imewashwa kutokana na mti mtakatifu wa
Mzaituni usio wa Mashariki wala Magharibi, ambao mafuta yake hutoa mwangaza
bila ya kuguswa na moto wowote (kuwashwa). Nuru juu ya Nuru! Allah humuongoza
katika mwangaza wake yeyote yule amtakae. Na Allah anaweka wazi mifano kwa Bani
Adam, Na hakika Allah ni mwenye kujua kila kitu.

Naam kwa upande mmoja wa juu juu kimaana basi aya inasema kua Allah Subhanah wa
Ta’ala ni Nuru ya Mbingu na Ardhi kwa sababu yeye ndie alieziumba na kuzidhihirisha
kuwepo kwake kutokana na Nuru yake.
161

Lakini kwa upande mwengine basi aya hii imetumia kiunganishi ‘ka’ kinachotafsirika
kwa lugha ya Kiswahili kama ‘kama’ ambacho hujulikana kama Kaf at tashbih ambayo
inayoleta maana ya kushabihisha kitu kimoja kua kinafanana tu na kitu chengine lakini
hata hivyo, kitu hicho si kitu chenyewe kilichokusudiwa. Kutumika kwa kaf at tashbih
katika aya hii kunaonesha kutokuwepo uwezekano wa kuelezea sifa za Majina ya Allah
Subhanahu wa Ta’ala hata kupitia kwa njia za kufananisha kwani yeye mwenyewe
anasema kua:

﴾ٌ‫ﺲ َﻛ ِﻤﺜْﻠِ ِﻪ َﺷ ْﻰء‬


َ ‫﴿ﻟَْﻴ‬
Laysa kamithlihi shay-un (Surat Ash Shuraa 42:11)

Tafsir: Hakuna kitu chochote chenye mithli yake.

Hivyo ufananisho huu wa Sifa ya ‘Nuru ya Allah’ hauwezi kuonesha ukweli halisi ulivyo,
bali ufafanisho huu umetumika ili kufafanua kimaana kutokana na ufahamu wa
walengwa waliokusudiwa, kwa sababu ukweli halisi wa ‘Nuru ya Allah’ ni ukweli ambao
hauwezi kufikirika kwa hali yeyote ya kiumbe yeyote yule na wala hauwezi kuelezeka
kwa lugha ya kiumbe chochote.

Hivyo maana ya Nuru iliyotajwa kwenye ayah basi hua ni Jina lake na Sifa yake Tukufu
ya Ilm yake na uwezo wake Allah Subhanah wa Ta’ala ambao hua ni wenye kutoa Nuru
inayopelekea kuamsha hisia za muonekano wa kuthibitisha, kuaminisha, kuuridhisha
Moyo na Nafsi juu ya kile kisichokuwepo mbele ya macho na kua ni kisichoonekana na
hivyo kua ni chenye kuwepo na kuoneka kutokana na uwezo wa Nuru yake kua kua ni
wenye kuonesha vithibitisho husika kulingana na ufahamu wa viumbe wake na hivyo
Nuru hio hua ni yenye kuondoa shaka ya kutokuwepo au kutoaminika kwa kitu husika.

Na ndio Hujjat Islami Mujaddid Ad Din Zukhruf Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad
Ibn Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali katika kuielezea maana ya
Al Nur anasema kua: Al Nur ni yule anaeonekana kutokana na kuvifanya vitu vyote
vionekane, kwani kila kitu kinachoonekana chenyewe na kusababisha vitu vyengine
vionekane hua kinaitwa Nuru. Tukiangalia kwa mtazamo wa kua kila
kilichokuwepo hupingana na kisichokuwepo, basi kile kinachoonekana hakiwezi
kulinganishwa na kitu chengine isipokua tu na kile kilichokuwepo. Kwani hakuna
kiza kilichokua cheusi zaidi kuliko kile kiza cha kitu kisichokuwepo.

Kile kilichokua huru kutokana na giza la kutokuwepo, na kua na uwezekano wa


kutokuwepo, na huondoa kila kitu kutoka katika kiza cha kutokuwepo na
kukiingiza katika udhihirisho wa kuwepo, basi hua kinastahiki kuitwa Nuru.
162

Kuwepo ni Nuru iliyo huru isiyotegemea kitu inayomurika kila kitu kutokana na
asili ya Nuru yake Allah Subhanah wa Ta’ala, kwani Allah Subhanahu wa Ta’ala ni
Nuru ya Mbingu na Ardhi. Na kama ilivyokua hakuna hata chembe moja pekee ya
muangaza wa Jua ambayo huonesha kua ndio chanzo cha muangaza wa Jua hilo,
basi vile vile hakuna hata chembe moja ya kitu kutoka katika vitu vilivyomo ndani
ya Mbingu na Ardhi, ambacho hakimpelekei mtu kukosa uhakika wa kutokana na
uwezekano wa kuwepo kwake bila ya kuhitaji kuwepo kwa yule aliesababisha
kuwepo kwa kitu hicho.

Ama kwa upande wa Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari basi yeye
anasema kua: ‘Yaani Allah Subhanah wa Ta’ala ni yule ambae amezipamba Mbingu
na Ardhi kwa Nuru. Mithili ya Nuru yake hua inamaanisha mithili ya Nuru ya Nabii
Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam, kama alivyosema Hasan Al Basr kua: ‘Allah
Subhanah wa Ta’ala hua ni mwenye kuulenga moyo wa Muumini na Nuru ya
Kukubali kumpwekesha Allah Subhanah wa Ta’ala, kwani kwa Nyoyo za Mitume
na Manabii hua ni zenye kung’ara sana kiasi ya kua haziwezi kumithilishwa na
Nuru nyengine. Allah Subhanah wa Ta’ala amesema: ‘Mithili ya Nuru ya Qur’an ni
Misbah, Taa ambayo Mshumaa wake ni Maarifa na Utambi wake ni majukumu ya
Kidini ambapo Mafuta yake hua ni Ikhlas na Nuru yake hua ni Nuru ya Kiroho’.
Hivyo kila Ikhlasi inavyozidi kua safi basi ndivyo unavyozidi Muangaza wa katika
Maarifa, na kila Majukumu ya Kidi yanapozidi basi ndio hua kuna kuzidi na
kupaikana kwa Uhakika unaotakiwa na Taa huzidi kuongeza Nuru yake’

Ama kwa upande wa Sultan Al Balagha Imam Abu Al Qasim Al Zamakhshari basi yeye
anasema kua: Kutokana na kua rahisi kufahamika kiufaham, basi Allah Subhanah
wa Ta’ala amemithilisha sifa yake na Nuru na hii ni kulingana na kauli yake pale
aliposema:

ِ ۤ ِ ‫ﺎت إِ َﱃ ٱﻟﻨﱡﻮِر وٱﻟﱠ‬ ِ ‫ﱃ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ آﻣﻨُﻮاْ ُﳜْ ِﺮﺟﻬﻢ ِﻣﻦ ٱﻟﻈﱡﻠُﻤ‬
‫ﺂؤُﻫ ُﻢ‬
ُ َ‫ﻳﻦ َﻛ َﻔُﺮواْ أ َْوﻟﻴ‬‫ﺬ‬
َ َ َ َ ّ ُُْ َ َ ‫ٱﻪﻠﻟُ َوِ ﱡ‬ ‫﴿ﱠ‬
‫ﺎب ٱﻟﻨﱠﺎ ِر ُﻫ ْﻢ ﻓِ َﻴﻬﺎ‬ ُ ‫َﺻ َﺤ‬ ْ ‫ﻚأ‬
ِ ‫ٱﻟﻄﱠﺎﻏُﻮت ُﳜْ ِﺮﺟﻮﻧـَﻬﻢ ِﻣﻦ ٱﻟﻨﱡﻮِر إِ َﱃ ٱﻟﻈﱡﻠُﻤ‬
َ ِ‫ﺎت أ ُْوﻟَـٰﺌ‬ َ َّ ُْ ُ ُ
﴾‫َﺧﺎﻟِ ُﺪو َن‬
Allahu waliyyu alladheena amanoo yukhrijuhum mina aldhdhulumati ila alnnoori
waalladheena kafaroo awliyaohumu alttaghootu yukhrijoonahum mina alnnoori ila
aldhdhulumati ola-ika as-habu alnnari hum feeha khalidoona (Surat Al Baqara
2:257)
163

Tafsir: Allah ni Msimamizi wa wale walioamini, kwani huwatoa kwenye dhulma (kiza)
na kuwaingiza kwenye Nuru, lakini kwa wale waliokufuru Wasimamizi wao hua ni
Miungu myengine ambao huwatoa kwenye Nuru na kuwaingiza kwenye Kiza. Hao ni
watu wa Motoni ambamo watakaa humo Milele.

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala aliposema kuhusiana na Kutoka kwenye


Dhulma kuwaingiza kwenye Nuru basi alikua akikusudia Nuru ya Mbinguni na
Ardhini katika hali mbili zifuatazo: Kwanza hua ni mwenye kumaanisha ukubwa
wa Muangaza wake (Ishraq) na kuenea kwa Nuru yake na hivyo Mbingu na Ardhi
kua ni zenye Kua na Nuru kutokana nao muangaza huo. Au hua anamaanisha kua
viumbe wake wa Ardhini na Mbinguni kua ni wenye kunufaika kutokana na
kupatikana kwa Nuru yake.

Baada ya kuelezea kuhusiana na maumbile ya Jua na Mwezi kwa watu wake basi Nabii
Nuh akaendelea kwa kusema:

‫ض ﻧَـﺒَﺎﺎﺗً ۞ ﰒُﱠ ﻳُﻌِﻴ ُﺪ ُﻛ ْﻢ ﻓِ َﻴﻬﺎ َوُﳜْ ِﺮ ُﺟ ُﻜ ْﻢ إِ ْﺧَﺮاﺟﺎً ۞ َو ُﱠ‬


‫ٱﻪﻠﻟ‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟُ أَﻧﺒَـﺘَ ُﻜ ْﻢ ِّﻣ َﻦ ٱﻷ َْر‬
‫﴿ َو ﱠ‬
﴾ً‫ض ﺑِﺴﺎﻃﺎً۞ﻟِّﺘَﺴﻠُ ُﻜﻮاْ ِﻣْﻨـ َﻬﺎ ُﺳﺒُﻼً ﻓِ َﺠﺎﺟﺎ‬
ْ َ َ ‫َﺟ َﻌ َﻞ ﻟَ ُﻜ ُﻢ ٱﻷ َْر‬
WaAllahu anbatakum mina al-Ardhi nabatan, Thumma yuAAeedukum feeha
wayukhrijukum ikhrajan, WaAllahu jaAAala lakumu al-ardha bisatan, Litaslukoo
minha subulan fijajan (Surat Nuh 71:18-20)

Tafsir: Na ni Allah ndie ambae aliekufanyeni mkue kutokana na vumbi la Ardhi kwa
ukuaji (mzuri) wa hatua kwa hatua. Na kisha atakurudisheni ndani yake na pia
atakutoeni (atakufufueni kutoka) ndani yake? Na ni Allah aliekujaalieni Ardhi
iliyotandazika? ili mpate kutembea juu yake kwa mapana?

Kwa lugha ya Kiarabu neno Nabata hua ni lenye kumaanisha Kuchipua, Kukua kwa
hatua Kuchomoza. Neno Nabata ndio lililotoa neno Anbata ambalo hua ni lenye
kumaanisha kukua, hivyo aya imetumia neno hilo katika halli zote mbili za Nabata na
Anbata lakini kwa Upande Ibn Adam na hivyo basi kua ni zenye kumnasibisha Ibn Adam
na Mimea kimaumbile kwa sababu Ibn Adam na Mimea vyote hivyo ni vyenye kuumbwa
kutokana na Udongo na kuutegemea udongo katika uhai wake.

Na pia hua ni vyenye kukua kwake hatua kwa hatua, tofauti na Wanyama wengine ambao
wao wanapozaliwa basi hua ni wenye kujiweza hali ambayo ni tofauti na Ibn Adam
ambae yeye hua ni dhaifu kama ulivyokua mmea ambao hua unahitaji mazingira mazuri
ili ukue vizuri basi na hivyo ndivyo alivyo Ibn Adam ambae nae hua ni mwenye kuhitaji
164

muongozo wa Mola wake katika kufanikiwa katika maisha yake ikiwemo pia muongozo
wa I’lm ya kumjua Mola wake.

Na ndio maana Hujjjat Ul Islami Mujaddid Ad Din Zukhruf Ad Din Imam Abu Hamid
Ibn Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali kua: ‘Ilm huwepo ndani
ya Nafsi ya Ibn Adam kama vile ambavyo mbegu inavyokua ndani ya ardhi,
unaposoma basi yale yanayotakiwa yawe hua yanakua kiuhalisia.’
Nabii Nuh akaendelea kuwawekea wazi watu wake kua inawabidi wajue kua wao ni
viumbe wa Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ndie aliewaumba, na hivyo kama alivyokua
na uwezo wa kuwaumba kutokana na udongo basi bila ya shaka mwisho wake watarudi
ndani ya udongo na kisha Muumbaji wao aliewaumba atawafanya wawe ni wenye
kutolewa tena upya kutoka kwenye udongo huo huo na kuhesabiwa waliyoyafanya moja
baada ya moja, hivyo hawana njia nyengine ya kufuata itakayowafikisha sehemu salama
katika safar yao hio ya kurudi kwa Mola wao isipokua kufuata maamrisho ya Mola wao.
Kisha Nabii Nuh anamalizia kwa kusema kua: ‘Hakika Allah Subhanah wa Ta’ala
ameijaalia Ardhi kua pana na tulivu na laini isiyokua ni yenye kusababisa madhara
kwa wanaotembea juu yake ambao ni Ibn Adam na viumbe wengine kwa manufaa
yao ili waweze kuishi maisha ya utulivu ndani yake’
Ukweli ni kua Watu wa Nabii Nuh Alayhi wa Salam walikua na Kibri cha kutotaka
kumuabudu Allah Subhanah wa Taála kwa sababu kutokana na mtizamo wao basi wao
walikua na Miungu yao ya Masanamu ambayo walikua wanaona kua ilikua
inawatosheleza kwa kuwapa yale wayatakayo katika maisha yao ya kidunia kama vile
Heshima, Nguvu, Utulivu, Uzuri, Muono wa mbali na kadhalika, mtizamo ambao ulikua
sio sahihi kwani Masanamu hayo yalikua hayana manufaa yeyote kwao, jambo ambalo
Nabii Nuh alikua kila mara anawabainishia watu wake lakini wapi!!

Walikua hawaoni wala hawasikii yaani walikua katika ile hali ambayo Allah Subhanah
wa Ta’ala anaizungumzia katika Qurán kwa kusema:

﴾‫ﺻ ﱞﻢ ﺑُ ْﻜﻢ ﻋُ ْﻤﻲ ﻓَـ ُﻬﻢ ﻻَ ﻳَـﺮِﺟﻌُﻮ َن‬﴿


ْ ْ ٌ ٌ ُ
Summun bukmun AAumyun fahum la yarjiAAoona (Surat Al Baqara 2:18)

Tafsir: Wao ni Viziwi, Mabubu, na Vipofu na wala hawatorudi (katika njia ya kheri
wanayoongozwa)

Ambapo kwa mtizamo mwengine basi Allah Subhanah wa Taála anasema:


165

‫ﺼﺎراً َوأَﻓْﺌِ َﺪ ًة ﻓَ َﻤﺂ أَ ْﻏ َ ٰﲎ‬ ِِ ِ ‫﴿وﻟََﻘ ْﺪ ﻣ ﱠﻜﻨ‬


َ ْ‫ﻴﻤﺂ إِن ﱠﻣ ﱠﻜﻨﱠﺎ ُﻛ ْﻢ ﻓﻴﻪ َو َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ َﳍُْﻢ َﲰْﻌﺎً َوأَﺑ‬
َ ‫ﺎﻫ ْﻢ ﻓ‬
َُ َ َ
ِ‫ٱﻪﻠﻟ‬
‫ت ﱠ‬ ِ �‫ﻋْﻨـﻬﻢ َﲰﻌﻬﻢ وﻻَ أَﺑﺼﺎرﻫﻢ وﻻَ أَﻓْﺌِ َﺪﺗـُﻬﻢ ِﻣﻦ َﺷﻲ ٍء إِ ْذ َﻛﺎﻧُﻮاْ َﳚﺤ ُﺪو َن ِﺂﺑ‬
َ َْ ْ ّ ُْ َ ْ ُُ َ ْ َ ْ ُ ُْ ْ ُ َ
﴾‫ﺎق ﺑِﻪ ﱠﻣﺎ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﺑِِﻪ ﻳَﺴﺘَـ ْﻬ ِﺰﺋُﻮ َن‬ َ ‫َو َﺣ‬
ْ
WajaAAalna lahum samAAan waabsaran waaf-idatan fama aghna AAanhum
samAAuhum wala absaruhum wala af-idatuhum min shay-in idh kanoo
yajhadoona bi-ayati Allahi wahaqa bihim ma kanoo bihi yastahzi-oona (Surat Al
Ahqaf 46:26)

Tafsir: Na tumewajaalia juu yao (kua na viungo) vya Kusikia, Kuona, na Nyoyo lakini
hawakunufaika na kusikia kwao, wala kwa kuona kwao wala na Nyoyo zao
hazikuwasaidia kitu kutokana na kumkataa kwao Allah Subhanah wa Taála na
walikua wamezungukwa na hicho wanachokifanyia mzaha.

Allah Subhanah wa Ta’ala anawatolea mfano watu kama hao kwa kusema:

َ‫ﺼ ِﲑ َوٱﻟ ﱠﺴ ِﻤﻴ ِﻊ َﻫ ْﻞ ﻳَ ْﺴﺘَ ِﻮَ� ِن َﻣﺜَﻼً أَﻓَﻼ‬


ِ ‫ﲔ َﻛﭑﻷ َْﻋﻤﻰ وٱﻷَﺻ ِﻢ وٱﻟْﺒ‬
َ َ َّ َ ٰ َ ِ ْ ‫﴿ َﻣﺜَﻞ ٱﻟْ َﻔ ِﺮﻳ َﻘ‬
ُ
﴾‫ﺗَ َﺬ ﱠﻛﺮو َن‬
ُ
Mathalu alfareeqayni kaal-aAAma waal-asammi waalbaseeri waalssameeAAi hal
yastawiyani mathalan afala tadhakkaroona (Surat Hud 11:24)

Tafsir: Mithili ya makundi mawili (Ya Walioamini na Wasioamini)ni kama Kipofu na


Kiziwi, na Mwenye kuona na mwenye kusikia. Jee watakua sawia baina yao? Hivi jee
hamtaki kuongoka?

Na ndio maana watu hao wakawa ni wenye kumuona Nabii Nuh kua yeye ndie
aliepotoka, kwa sababu walikua vipofu wa kutouona ukweli na viziwi wa kutousikia
ukweli hivyo Nabii Nuh akamlalamikia Mola wake kama inavyosema aya ifuatayo:
166

۞ ً‫ﺼﻮِﱏ وٱﺗﱠـﺒَـﻌُﻮاْ َﻣﻦ ﱠﱂْ ﻳَِﺰْدﻩُ َﻣﺎﻟُﻪُ ووﻟَ ُﺪﻩُ إِﻻﱠ َﺧﺴﺎرا‬ ِ ِّ ‫ﻮح ﱠر‬ َ َ‫﴿ﻗ‬
َ ََ َ ْ َ ‫ب إﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ َﻋ‬ ٌ ُ‫ﺎل ﻧ‬
ِ
َ ُ‫َوَﻣ َﻜُﺮواْ َﻣ ْﻜﺮاً ُﻛﺒﱠﺎراً۞ َوﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻻَ ﺗَ َﺬ ُر ﱠن آﳍﺘَ ُﻜ ْﻢ َوﻻَ ﺗَ َﺬ ُر ﱠن َوّداً َوﻻَ ُﺳ َﻮاﻋﺎً َوﻻَ ﻳَـﻐ‬
‫ﻮث‬
﴾ً‫ﻮق وﻧَﺴﺮا‬
ْ َ َ ُ‫َوﻳَـﻌ‬
Qala noohun rabbi innahum AAasawnee waittabaAAoo man lam yazid-hu maluhu
wawaladuhu illa khasaran, Wamakaroo makran kubbaran, Waqaloo la
tadharunna alihatakum wala tadharunna waddan wala suwaAAan wala yaghootha
wayaAAooqa wanasran (Surat Nuh 71: 21-23)

Tafsir: Nuh akasema: Ewe mola wangu hakika hawa wameniasi, na wameamua
kuwafuata wale ambao hawawazidishii kitu chochote katika mali zao wala watoto wao
isipokua hasara, Na wamepanga mikakati mikubwa, na kusema: Usiwaache Miungu
wako, na usiachane na Wadd wala Suwa, wala Yaghuth wala Yauúq wala Nasr.

Naam aya inaweka wazi kua watu wa Nabii Nuh walikua wakimuona kua Nabii Nuh
hana akili na hivyo anataka kuusiwa yeye badala ya yeye kuwausia wao hivyo
wakamwambia Nabii Nuh kua asiwachane na Miungu ya wazee wake au cha Moto
atakiona, ambapo kwa upande wa Imam Ibn Jarir At Tabari basi yeye anasema kuhusiana
na watu hao waliokua wakiabudiwa kua:

‘Watu hawa (Wadd, Suwa, Yaghuth, Yauúq na Nasr.) walikua ni watu wema ambao
waliwahi kuishi katika kipindi cha baina ya Nabii Adam na Nabii Nuh na watu
wakawa wanawachukulia kua ni mfano wa kuigwa kwao kiasi ya kua hata baada
ya kufa kwao, basi wale waliokua wakiwathamini wakasema: ‘Kama tukitengeneza
Masanamu yao itakua bora kwetu sisi katika Ibada zetu na wao tutakua
tukiwakumbuka’ Hivyo watu hawa wakatengeneza Masanamu yao watu hao, na
baada ya vizazi vya watu hao kufariki basi Iblis akawalaghai kwa kuwaambia kua:
‘Wazee wenu walikua wakiyaabudu Masanamu haya na katika kuyaabudu kwao
basi walipokua wakiyaomba walikua wakipata Mvua’’.

Ama kwa upande wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema kua:
‘Baada ya kufariki watu hao wema basi, Shaytan akawashawishi watu wao
wawatengenezee masanamu katika sehemu ambazo walikua wakikaa. Na walifanya
hivi lakini Masanamu haya hayakuabudiwa hadi katika kipindi cha vizazi vya
baadae walipotoka kutoka katika njia sahih ya maisha. Na kisha baadae wakawa
wanawaabudu kama Miungu yao’
167

Ama kwa upande wa Imam Abu Hatim Abd Rahman Muhammad Ibn Idris Al Razi basi
yeye anasema kua: ‘Waddan alikua ni mtu mwema ambae alikua akipendwa sana na
watu wake, kiasi ya kua alipofariki basi watu wake hao walihamia katika Mji wa
Babylonia ambako ndiko lilipokuwepo na watu hao walikua wamejawa na huzuni.
Hivyo Iblis akaiona huzuni waliyokua nayo watu hao kutokana na kifo hicho, na
akachukua nafasi hiyo kwa kujiingiza katika umbo la mtu mmoja mzee sana ambae
aliwaambia watu hao: ‘Nakuoneni namna mnavyohuzunika kutokana na kifo cha
mtu wenu, hivyo jee mnaonaje kama, nikikutengenezeeni sanam lake kisha
mkaliweka katika sehemu ambayo mtakusanyika nyote kwa pamoja ili mpate
kumkumbuka?’ watu hao nao wakakubaliana na mtizamo huo na wakasema:
‘Naam kufanya hivyo ni bora zaidi’’
Hivyo Iblis akawatengenezea sanamu linalofanana na Waddan, na kisha watu hao
wakaliweka sanamu hilo katika sehemu ambayo hua wanakutana kila baada ya
muda. Lakini hata hivyo Iblis alipowaona kua watu hao wanavutiwa katika
kumkumbuka Waddan kuliko wanavyomkumbuka Mola wao basi nae akawaambia
watu hao: ‘Jee mnaonaje kama ikiwa katika kila nyumba kutakua na sanam lake?’
ambapo nao wakakubali juu ya wazo hilo na hapa sasa watoto wa watu hawa
wakawa wanawaona wazee wao wanavyomkumbuka Waddan badala ya
kumkumbuka Allah. Hivyo Sanam wa kwanza kuabudiwa baada ya Allah alikua ni
Waddan, yaani huyo sanam waliemtengeneza’
Ingawa Nabii Nuh aliwapatia hoja na vithibitisho vilivyo wazi watu wake, na watu wake
hao kamwe hawakutaka kumsikiliza, na bado wao wakamuonya yeye kua asije akaachana
na miungu wao ambao ni Wadd, Suwa, Yaghuth, Yauu’q na Nasr. Lakini hata hivyo Nabii
Nuh hakuvunjika moyo hata baada ya kupita karne na karne zilizokua ni zenye kudumu
na mitihani hiyo.

Hadi hali ikafikia kama anavyoielezea Imam Ad Dahhak Ibn Muzahim ambae yeye
anasema kua: Amesema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Nabii Nuh
alikua akipigwa na kisha kufungwa kamba na kutiwa ndani ya gunia na kurushwa
ndani ya Nyumba yake, lakini alikua kila akifanikiwa kutoka basi hutoka tena nje
na kuwausia watu kwa ajili ya kumfuata Mola wao. Hali iliendea hivi hadi siku moja
akatokea mzee mwenye mkongojo ambae alikua na mtoto wake ambae alimwambia
mtoto wake huku akimuoneshea kidole Nabii Nuh: ‘Ewe mtoto wangu Jee
unamouna yule mzee? Hivyo nakuonya juu ya Mzee yule kama mimi alivyonionya
mimi Baba Yangu, Yule Mzee ni muovu. Hivyo kua muangalifu nae asije
akakupotosha’ ambapo na yule mtoto nae akamwambia baba yake: ‘Tafadhal Baba
nipe mie huo mkongojo wako.’ Hapo yule Mzee akampa mtoto wake ule mkongojo
na yule mtoto akauchukua mkongonjo huo na kuanza kumpiga nao Nabii Nuh.’
168

Ama baada ya matukio hayo basi Nabii Nuh akamwambia Allah Subhanah wa
Taála: ‘Ya Allah! Unaona namna Waja wako wanavyonifanyia, hivyo kama ikiwa
kweli unawajali waja wako hawa basi waongoze kupitia kwangu na kama ni
vyenginevyo basi nipe mimi ustahmilivu hadi pale utakapojaalia kuhukumu baina
yao na baina yangu, kwani kwa Hakika wewe ni m-bora wa Kuhukumu’ (Sultan Al
Mutakkalimin Mujaddid ud Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi katika Mafatih al Ghayb -
Tafsir al Kabir, Sultan Al Balagha Imam Al Zamakhshari katika Al Kashshaf)

Naam hali ilipofikia hivyo basi Nabii Nuh akaamua kuwawekea wazi watu wake kwa
kuwaonesha kua anawapa onyo la mwisho, na hivyo yeye hajali tena kwani kama
wanaona kua kwao wao ni vigumu kua pamoja nae katika jamii yao, basi hakuna tatizo
kwani yeye anatekeleza jukumu lake juu yao, na wala hatowakimbia au kuachana nao,
hivyo na wafanya watakavyofanya dhidi yake, wao na Miungu yao, tena bila ya hata
kumuonya kwani yeye anamtegemea yule ambae ni mwenye sifa ya upekee ya
kutegemewa ambae ni Allah Subhnah wa Ta’ala pekee, kama ilivyosema aya inayofuatia:

‫ﺎل ﻟَِﻘ ْﻮِﻣ ِﻪ ﻳٰـ َﻘ ْﻮِم إِن َﻛﺎ َن َﻛﺒُـَﺮ َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ ﱠﻣ َﻘ ِﺎﻣﻰ َوﺗَ ْﺬﻛِ ِﲑى‬ َ َ‫ﻮح إِ ْذ ﻗ‬
ٍ ُ‫﴿ َوٱﺗْ ُﻞ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ ﻧَـﺒَﺄَ ﻧ‬
‫َﲨﻌُ ۤﻮاْ أ َْﻣَﺮُﻛ ْﻢ َو ُﺷَﺮَﻛﺂءَ ُﻛ ْﻢ ﰒُﱠ ﻻَ ﻳَ ُﻜ ْﻦ أ َْﻣُﺮُﻛ ْﻢ َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ‬
ِْ ‫ٱﻪﻠﻟِ ﺗَـﻮﱠﻛ ْﻠﺖ ﻓَﺄ‬
ُ َ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻓَـ َﻌﻠَﻰ ﱠ‬
ِ‫ت ﱠ‬ ِ �‫ِﺂﺑ‬
َ
‫ى‬ ِ
‫ﺮ‬ ‫َﺟ‬ ‫أ‬ ‫ن‬ ِ
‫إ‬ ‫ﺮ‬ٍ ‫ﺟ‬ َ‫أ‬ ‫ﻦ‬ ِ ‫ﻨﻈﺮو َن ۞ ﻓَِﺈن ﺗَـﻮﻟﱠﻴـﺘُﻢ ﻓَﻤﺎ ﺳﺄَﻟْﺘُ ُﻜﻢ‬
‫ﻣ‬ ِ ُ‫ﱃ وﻻَ ﺗ‬ َ ِ
‫إ‬ ‫ا‬
ْ‫ﻮ‬ۤ ‫ﻏﻤﺔ ﰒُﱠ ٱﻗْﻀ‬
َ ْ ْ ْ ّْ ْ َ َ ْ َْ ُ َ ‫ﱠ‬ ُ ً‫ُﱠ‬
ِِ ِ ِ ِ‫إِﻻﱠ ﻋﻠَﻰ ﱠ‬
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ت أَ ْن أَ ُﻛﻮ َن ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻤ ْﺴﻠﻤ‬ ُ ‫ٱﻪﻠﻟ َوأُﻣْﺮ‬ َ
Waotlu AAalayhim nabaa noohin idh qala liqawmihi ya qawmi in kana kabura
AAalaykum maqamee watadhkeeree bi-ayati Allahi faAAala Allahi tawakkaltu
faajmiAAoo amrakum washurakaakum thumma la yakun amrukum AAalaykum
ghummatan thumma iqdoo ilayya wala tundhirooni. Fa-in tawallaytum fama
saaltukum min ajrin in ajriya illa AAala Allahi waomirtu an akoona mina
almuslimeena (Surat Yunus 10:71-72)

Tafsir: Na wasomee habari za Nuh. Wakati alipowaambia watu wake: ‘Enyi watu
wangu, kama ikiwa ni kugumu juu yenu kubaki kwangu pamoja nanyi na
kukukumbusheni dalili za Allah basi mimi namtegemea Allah. Hivyo jumuisheni hila
zenu, nyie pamoja na washirika wenu, na wala msiwe na shaka juu ya hila zenu hizo
na amueni (mnalotaka kuamua kufanya) juu yangu wala msinionye. Lakini kama
mkinipa mgongo, basi hakuna malipo niliyokuombeni, kwani Malipo yangu yapo kwa
Allah na mimi nimeamriwa niwe miongoni mwa Waislam.’
169

Naam bila ya shaka, hivi ndivyo wanavyokua wale wenye sifa za kua ni Waislam, kwani
kumtegemea kwao Mola wao hua ni kwenye kuleta matokea stahiki ambayo ni mazuri
zaidi. Tunapoiangalia hali ya Nabii Nuh katika wakati anawawekea wazi watu kwake juu
ya kumtegemea kwake Mola wake na kisha tukajilinganisha na sisi katika wakati wetu,
basi tunnaona kua kuna tofauti kubwa sana baina yetu, na ndio maana tunapomuangalia
Imam Sufyan Al Thawry basi alikua akijisuta Nafsi yake pale tunapozungumzia hali ya
Nafsi ya mja katika kumtegemea Allah Subhanah wa Ta’ala basi kila wakati alipokua
akisali na kusoma Surat Al Fatiha basi alikua akilia sana pale anapofikia katika aya
isemayo:
ِ
ُ ‫﴿إِ ﱠ� َك ﻧَـ ْﻌﺒُ ُﺪ وإِ ﱠ� َك ﻧَ ْﺴﺘَﻌ‬
﴾‫ﲔ‬
Iyyaka naAAbudu wa-iyyaka nastaAAeenu (Surat A Fatiha 1:5)

Tafsir: Ni wewe pekee ndie tunaekuabudu na ni wewe tu ndie tuneokuomba msaada.

Sufyan Ath Thawry alipoulizwa ni kwa nini alikua akilia sana na kuikariri ayah hii wakati
anapoisoma basi alijibu kwa kusema: ‘Kwa hakika mimi hua naalia kwa sababu sisi
hua tunamwambia Allah Subhanah wa Ta’ala kua Ni wewe tu tunae kutegemea na
ni wewe tu ndie tunakuomba msaada lakini ukweli ni kua sisi tunasema tu, lakini
hatuoneshi kua tunamtegemea yeye kwani tunategemea zaidi Dinar na Dirham
kuliko tunavyometegemea Mola wetu.’

Hivyo Nabii Nuh akawawekea watu wake kua wale ambao wanaemfuata na kumuamini
basi hatoachana nao, kwani kama vile alivyokua yeye ni Miongoni mwa Waislam basi
na hao pia ni Waislam na watanufaika kwa kupata malipo ya kukutana na Mola wao
aliewaridhia juu yao na:

ْ‫ﻳﻦ َآﻣﻨُـ ۤﻮا‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟِ وﻣﺂ أ ََ�ْ ﺑِﻄَﺎ ِرِد ٱﻟﱠ‬


‫ﺬ‬ ‫ﱠ‬ ‫ﻰ‬ ‫ﻠ‬
َ ‫ﻋ‬ ‫ﱠ‬‫ﻻ‬ ِ‫إ‬ ‫ى‬ ‫ﺮ‬ِ ‫َﺟ‬ ‫أ‬ ‫ن‬ْ ِ‫إ‬ ‫ﻻ‬
ً ‫ﺎ‬‫ﻣ‬ ‫ﻪ‬ِ ‫﴿وٰﻳـ َﻘﻮِم ۤﻻ أَﺳﺄَﻟُ ُﻜﻢ ﻋﻠَﻴ‬
َ ََ َ َ ْ َ َْ ْ ْ ْ َ
‫ٱﻪﻠﻟِ إِن‬
‫ﻨﺼُﺮِﱏ ِﻣ َﻦ ﱠ‬ ِ ۤ ِ ِِ
ُ َ‫إِﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ ﱡﻣﻼَﻗُﻮ َرّﻬﺑ ْﻢ َوﻟَـٰﻜ ِّﲏ أ ََرا ُﻛ ْﻢ ﻗَـ ْﻮﻣﺎً َْﲡ َﻬﻠُﻮ َن۞ َوٰﻳـ َﻘ ْﻮم َﻣﻦ ﻳ‬
َ‫ﺐ َوﻻ‬ ‫ﻴ‬ ‫ﻐ‬
َ ‫ﻟ‬
ْ ‫ٱ‬ ‫ﻢ‬ ‫ﻠ‬
َ ‫َﻋ‬‫أ‬ ‫ﻻ‬
َ ‫و‬ ِ‫ٱﻪﻠﻟ‬
‫ﱠ‬ ‫ﻦ‬ ِ‫ﻨﺪى ﺧﺰآﺋ‬ ِ ‫ﻃَﺮدﺗـﱡﻬﻢ أَﻓَﻼَ ﺗَ َﺬ ﱠﻛﺮو َن۞وﻻَ أَﻗُﻮ ُل ﻟَ ُﻜﻢ ِﻋ‬
َ ُ ْ ْ َ ُ َ َ ْ َ ُ ُْ َ
‫ٱﻪﻠﻟُ أَ ْﻋﻠَ ُﻢ ِﲟَﺎ‬ ‫ﻳﻦ ﺗَـْﺰَد ِر ۤي أ َْﻋﻴُـﻨُ ُﻜ ْﻢ ﻟَﻦ ﻳـُ ْﺆﺗِﻴَـ ُﻬ ُﻢ ﱠ‬
‫ٱﻪﻠﻟُ َﺧ ْﲑاً ﱠ‬ ِ ِ ُ ُ‫ﻚ وﻻَ أَﻗ‬
َ ‫ﻮل ﻟﻠﱠﺬ‬
ِ ُ ُ‫أَﻗ‬
َ ٌ َ‫ﻮل إِّﱏ َﻣﻠ‬
ِِ ِ ۤ ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ِﰱ أَﻧْـ ُﻔﺴ ِﻬ ْﻢ إِِّﱐ إِذاً ﻟﱠﻤ َﻦ ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
170

Waya qawmi la as-alukum AAalayhi malan in ajriya illa AAala Allahi wama ana
bitaridi alladheena amanoo innahum mulaqoo rabbihim walakinnee arakum
qawman tajhaloona; Waya qawmi man yansurunee mina Allahi in taradtuhum
afala tadhakkaroona; Wala aqoolu lakum AAindee khaza-inu Allahi wala aAAlamu
alghayba wala aqoolu innee malakun wala aqoolu lilladheena tazdaree
aAAyunukum lan yu/tiyahumu Allahu khayran Allahu aAAlamu bima fee
anfusihim innee ithan lamina aldhdhalimeena; (Surat Hud 11:29-31)

Tafsir: Na akasema (Nabii Nuh) : Enyi watu wangu mimi sikuombeni malipo yeyote,
kwani malipo yangu yapo kwa Allah (Subhanah wa Ta’ala) na wala sitowafukuza wale
ambao wameniamini, kwani kwa hakika wanaenda kumlaki Mola wao, lakini naona
kua nyinyi ni watu ambao ni wajinga. Na enyi Watu wangu, Jee ni nani
atakaeninusuru mie na Allah, kama nikiwafukuza? Hivi jee hua mnafikiria lakini?
Na kamwe siwezi kusema kua mimi nnayo hazina kutoka kwa Allah na wala sijui juu
ya Ghaib (yasiyoonekana): ‘Na wala sisemi kua mimi ni Malaika, na sisemi juu ya
wale ambao mnawaangalia kwa dharau kua Allah hatowapa Khayr. Kwani Allah ndie
mwenye kujua mna nini ndani ya nafsi zao (Juu ya Imani yao) Kwani kama ni hivyo
basi hakika mimi nitakua ni miongoni mwa madhalimu.’

Nabii Nuh anawawekea wazi watu kua yeye hayuko kimaslahi ya kidunia na hivyo hana
haja ya mali kwani hayo yote ni mapambo ya mpito, kwa hivyo hata kama watu wake
hawatamkubali wote basi atabakia nao hao hao waliomkubali kuwaongoza na wala
hatowakataa au kuwafukuza, kwani yeye anafanya hivyo kwa ajili ya Mola wake, hivyo
jee atajifichia wapi kama ikiwa ameachana na Maamrisho ya Mola wake? Jee ni nani
atakaeweza kumnusuru na adhabu ya Mola wake?

Kwani Nabi Nuh ni mwenye kujua ukubwa na uwezo wa Mola wake, tofauti na watu
wake ambao walikua hawajui na wala hawataki kujua juu ya Mola wao, ambae ni mweye
kuwapenda na kuwahurumia na ndio maana akawatumia Mjumbe wake ili awaongoze.
Kisha aya inatuwekea wazi kua hata Mitume hua hawajui juu ya Ilm Al Ghayb isipokua
juu ya yale wanayofunuliwa na Mola wao tu, na hivyo basi si juu yake yeye kuwahukumu
watu wake hao, kwani yeye si mwenye uwezo wa kuona na kujua kile kilichomo ndani
ya Nafsi za viumbe wenzake hao kwa sababu mwenye uwezo huo ni muumba wa viumbe
peke yake ambae ni Allah Subhanah wa Ta’ala.

Hivyo Nabii Nuh anawaambia watu wake kua ingawa watu wake wanawaangalia wafuasi
wake kwa kuwadharau lakini hii haimanishi kua wafuasi wake hao wachache
wanaodharauliwa na watu wa jamii yao hawatokua na malipo mema mbele ya Mola wao,
kwani yeye Allah Subhanah wa Ta’ala ndie mwenye kujua juu yao na malipo yao yapo
kwa Mola wao na kama ikiwa Nabii Nuh atawahukumu watu hao basi bila ya shaka
171

atakua ni mwenye kufanya Dhulma sana dhidi yao, na yeye hataki kua miongoni mwa
watu Madhalim.

Na hii inatufunza sisi leo hii ambao tumekua na hali ya kua na urahisi kwetu kutokana na
ujinga wetu kua ni wa kuwahukumu viumbe wenzetu kutokana na yale wanayoyafanya
ambayo hua ni yenye kua tofauti na mitizamo yetu, na kutokana na kutojua kwetu
tumekua na wepesi wa kuwatuhumu Waislamu wenzetu kua ni Makafiri bila ya kujua
kua kufanya kwetu hivyo hua ni wenye kujidhulumu sisi na pia kuwadhulumu wenzetu
hao, na hivyo kua ni miongomi mwa Madhalim, kambo ambalo Nabii Nuh alilikataa na
kupingana nalo kwani yeye si Dhalim na hajui yaliyomo ndani ya nyoyo za Ibn Adam
ambao ni Viumbe wenzake.

Watu wa Nabi Nuh wakasema:

‫ﲔ۞ إِ ْن ُﻫ َﻮ إِﻻﱠ َر ُﺟ ٌﻞ‬ ِ ِ ‫ٱﻪﻠﻟَ ﻷَﻧﺰَل ﻣﻼَﺋِ َﻜﺔً ﱠﻣﺎ َِﲰﻌﻨَﺎ ِﻬﺑـٰ َﺬا ِ ۤﰲ‬
َ ‫آﺂﺑﺋﻨَﺎ ٱﻷَﱠوﻟ‬
َ َ ْ َ َ ُ‫﴿ َوﻟَْﻮ َﺷﺂءَ ﱠ‬
ٍ ‫ﺼﻮاْ ﺑِِﻪ َﺣ ﱠ ٰﱴ ِﺣ‬ ِِ
﴾‫ﲔ‬ ُ ‫ﺑِﻪ ﺟﻨﱠﺔٌ ﻓَـﺘَـَﺮﺑﱠ‬
Walaw shaa Allahu laanzala mala-ikatan ma samiAAna bihadha fee aba-ina al-
awwaleena; In huwa illa rajulun bihi jinnatun fatarabbasoo bihi hatta heenin (Surat
Al Muuminun 23:24-25)

Tafsir: (Wakasema watu hao) Kama Allah angetaka basi angetushushia Malaika,
hatujawahi kusikia sisi juu ya haya kutoka kwa wazee wetu waliotangulia; Hakika
huyu (Nabii Nuh) si yeyote isipokua ni Mwendawazimu msubirieni kwa mda kidogo.

Yaani katika kumuelezezea wazimu wake basi Watu hao wa Nabii Nuha walikua
wanamuona kua kama ni Bomu la Sekunde ambalo inabidi kujihadhari nalo kwa kukaa
nalo mbali kwani litaripuka wakati wowote na ndio maana wakatumia neno Hiinin
ambalo ni lenye kutokana na neno Hana lenye kumaanisha Kufikia Mda wake, Kuwasili
katika mda wake, Kupea kwa ajili ya kutoa matokeo husika. Kuwiva na kua tayari
Kuvunwa na pia humaanisha Kuvunwa.

Ambapo kwa upande mwengine basi anasema Sultan Al Balagha Imam Abu Qasim Al
Zamakhshari kuhusiana na aya hizi kua: ‘Angalia watu hawa walivyokua, yaani
walikua tayari kuyaamini Masanamu waliyoyachonga wenyewe lakini hapo hapo
walikua wanashindwa kumkubali Ibn Adam mwezao kua ni Mtume kutoka kwa
Mola wao, hivyo basi wakashauriana kua wacha wamsubiri Nabii Nuh kwa mda
kwani huenda labda atapona wenda wazimu wake, na vyenginevyo basi watamuua.’
172

Lakini walipoona kua bado Nabii Nuh anaendelea kujadiliana nao kuhusiana na
anayoyafanya kua anayafanya kwa kutekeleza amri za Mola wake tu basi watu hao
wakasema kumwambia Nabii Nuh kua kama isemavyo aya ifuatayo.

‫ﻨﺖ ِﻣ َﻦ‬ ِ ِِ ِ ‫﴿ﻗَﺎﻟُﻮاْ ٰﻳـﻨﻮح ﻗَ ْﺪ ﺟﺎدﻟْﺘـﻨﺎ ﻓَﺄَ ْﻛﺜـﺮ‬


َ ‫ت ﺟ َﺪاﻟَﻨَﺎ ﻓَﺄْﺗَﻨﺎ ﲟَﺎ ﺗَﻌ ُﺪ َ� إِن ُﻛ‬ َ َْ ََ َ َ ُ ُ
‫ﻳﻦ۞ َوﻻَ ﻳَﻨ َﻔﻌُ ُﻜ ْﻢ‬ ‫ﺰ‬ِ ‫ﺠ‬ِ ‫ٱﻪﻠﻟ إِن ﺷﺂء وﻣﺂ أَﻧﺘﻢ ِﲟﻌ‬ ‫ﱠ‬ ِِ‫ﺎل إِﱠﳕَﺎ �ْﺗِﻴ ُﻜﻢ ﺑ‬
‫ﻪ‬ َ ‫ﻗ‬
َ ۞ ‫ﲔ‬ ِ‫ﺼ ِﺎدﻗ‬
‫ٱﻟ ﱠ‬
َ ْ ُ ْ ُ َ َ َ َ ُ ْ َ َ
‫ﻳﺪ أَن ﻳـُ ْﻐ ِﻮﻳَ ُﻜ ْﻢ ُﻫ َﻮ َرﺑﱡ ُﻜ ْﻢ َوإِﻟَْﻴ ِﻪ‬ ‫َﻧﺼ َﺢ ﻟَ ُﻜ ْﻢ إِن َﻛﺎ َن ﱠ‬
ُ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻳُِﺮ‬ َ ‫ت أَ ْن أ‬ ‫ﺼ ِﺤ ۤﻲ إِ ْن أ ََرْد ﱡ‬ْ ُ‫ﻧ‬
﴾‫ﺗُـﺮ َﺟﻌُﻮ َن‬
ْ
Qaloo ya noohu qad jadaltana faaktharta jidalana fa/tina bima taAAiduna in kunta
mina alssadiqeena; Qala innama ya/teekum bihi Allahu in shaa wama antum
bimuAAjizeena; Wala yanfaAAukum nushee in aradtu an ansaha lakum in kana
Allahu yureedu an yughwiyakum huwa rabbukum wa-ilayhi turjaAAoona (Surat
Hud 11:32-34)

Tafsir: Wakasema (Watu hao):‘Ewe Nuh! Kwa hakika ushajadiliana nasi na kuzidisha
Mjadala dhidi yetu. Kwa hivyo tuoneshe unachotutishia (Kutoka kwa huyo Mungu
wako unaemtemegea) kama kweli wewe ni mkweli. Akasema (Nabii Nuh) Atakuleteeni
Allah juu yenu na nyinyi hamtoiepuka. Na hazitokufaeni nasaha zangu, kama Allah
anataka mpotoke kwani yeye ni Mola wenu na kwake yeye ndio marudio yenu.

Hapa tunaona kua aya hii imetumia neno Jadala ambalo kwa Kiswahili hua tunasema
kua linamaanisha Jadili, lakini kwa lugha ya Kiarabu hua halimaanishi Kujadili tu lakini
pia hua linamaanisha Kudhibiti kisawasawa kwa kutumia nguvu, Kugombana,
Kupurukushana, Kubishana, na pia Kuipeleka kesi katika Mahkama ili ihukumiwe.

Ambapo tunaona kua Al Malau yaani Mabwana wakubwa wa watu wa Nabii Nuh
washachoka kubishana na kujadiliana sana na Nabii Nuh kwani nae ametumia uwezo
wake wote katika kuwawekea wazi hoja zake tena kwa mda mrefu sana, huu unaonekana
kua ulikua ni madala mzito sana ambao hauna mwisho wake kwa watu wake, kwani
inaonekana kua Nabii Nuh hatosita katika jitihada zake hizo. Na imekua kama kwamba
Wamepelekwa Mahakamani na hukumu haitolewi.


173

KUGHARIKISHWA KWA WATU WA NABII NUH


Hivyo Watu hao wa Nabii Nuh wakaamua kumpa Nabii Nuh onyo la mwisho na kumpa
changamoto kua kama kweli wewe ni Mtume kutoka kwa Mola wako basi hebu tuoneshe
ukweli kwa uthibitisho wa vitendo kwani umekua ukisema kwa maneno tu lakini vitendo
hatuvioni, hivyo tuletee hio adhabu ambayo wewe na Mola wako mnaweza kutuletea.

Nabii Nuh akawaambia watu wake hao kua, bila ya shaka yeye hawezi kuwaepushia
Majaaliwa ya Allah Subhanah wa Ta’ala juu hata kama akiwanasihi vipi, kwani Adhabu
ya Allah Subhanah wa Ta’ala haitoepukika dhidi yao kwani wanajulikana kwa Ujinga
wao kiasi ya kua hata walipoingizwa kwenye Rehma za Mola wao kwa kutumiwa
Mjumbe kutokana na Miongoni mwao, ili waiepuke adhabu hio, lakini hawakutaka kwani
waliikimbia Rehma hio na kumdhalilisha Mtume wao ambae ndie aliekua kiongozi wa
kuwaingiza kwenye rehma hizo, ambapo Allah Subhanah wa Taála anatuwekea wazi juu
ya haya pale aliposema katika Qurán:

﴾‫ﻮح ﻓَ َﻜ ﱠﺬﺑُﻮاْ َﻋْﺒ َﺪ َ� وﻗَﺎﻟُﻮاْ َْﳎﻨُﻮ ٌن و ْٱزُد ِﺟﺮ‬ ْ َ‫﴿ َﻛ ﱠﺬﺑ‬


ٍ ُ‫ﺖ ﻗَـْﺒـﻠَ ُﻬ ْﻢ ﻗَـ ْﻮُم ﻧ‬
َ َ َ
Kadhdhabat qablahum qawmu noohin fakadhdhaboo AAabdana waqaloo
majnoonun waizdujira (Surat Al Qamar 54:9)

Tafsir: Walikadhibisha kabla yao watu wa Nabii Nuh, wakamkadhibisha Mja wetu, na
kusema: ‘Mwendawazimu’ na wakamdhalilisha na kumtishia.

Kutokana na changamoto za makarne ya miaka hadi kufikia watu hao kuweka wazi
matakwa yao kutoka kwa Nabii Nuh, basi bila ya kutaka Nabii Nuh akajikuta anaachana
na watu hao na kua ni mwenye kumuomba msaada Allah Subhnanah wa Ta’ala
amuingize katika nusra zake kama inavyotuelezea aya ifuatayo ambayo inasema kua:

ِ ‫ب ٱﻧﺼﺮِﱏ ِﲟَﺎ َﻛ ﱠﺬﺑ‬


﴾‫ﻮن‬ ِ َ َ‫﴿ﻗ‬
ُ ْ ُ ّ ‫ﺎل َر‬
Qala rabbi onsurnee bima kadhdhabooni (Surat Al Muuminun 23:26)
Tafsir: Akasema (Nuh) Ewe Mola wangu ninusuru kutokana na kukadhibishwa nao.
174

Na hivyo akaamua kumuachia Allah Subhanah wa Taála aingilie kati baina yake na watu
wake kwa kuomba msaada kutoka kwa Mola wake kama inavyosema aya:

ِ َ‫﴿ﻓَ َﺪﻋﺎ رﺑﱠﻪ أَِﱏ ﻣ ْﻐﻠُﻮب ﻓَﭑﻧﺘ‬


﴾‫ﺼْﺮ‬ ٌ َ ّ َُ َ
FadaAAa rabbahu annee maghloobun faintasir (Surat Al Qamar 54:10)
Tafsir: Kisha akamuomba Mola wake kwa kusema: Hakika mimi nimezidiwa hivyo
nisaidie!

Hii ni dua yenye sehemu mbili ya kwanza inawakilisha udhaifu wa Ibn Adam mbele ya
viumbe wenzake na pia mbele ya Mola wake, na pia inawakilisha kua na uwezo wa
Kujiamini, kua na Utulivu na kwa kumuomba Mola wake kutokana na kumtegemea Mola
wake. Hii ni dua ambayo muhimu sana pale mtu unapokua umedhulumiwa, unaweza
kuisoma FadaAAa rabbahu annee maghloobun faintasir mara 100 au mara 468 na
kisha unawasilisha kwa Mola wako juu ya jambo lako ulilodhulumiwa kwa kuanza na
maneno ya aya hio kuwa kusema: Rabbi Annee Maghloobun Faintasir.

Hivyo kwa kua Allah Subhanah wa Ta’ala ni mwenye kujua juu ya kila kiumbe wake na
hivyo kumteua Nabii Nuh ambae alikua na sifa bora ya Subra na Ustahamilivu wake wa
hali ya juu, na hivyo kujua kua kwa hali aliyofikia Nabii wake huyo basi itakua tayari
ameshafikia kikomo cha Ustahmilivu wake, kwani anasema Allah Subhanah wa Ta’ala
mwenyewe katika Surat Al Baqara kua:

ِ
﴾‫ﺖ‬ ْ َ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻧـَ ْﻔﺴﺎً إِﻻﱠ ُو ْﺳ َﻌ َﻬﺎ َﳍَﺎ َﻣﺎ َﻛ َﺴﺒ‬
ْ َ‫ﺖ َو َﻋﻠَْﻴـ َﻬﺎ َﻣﺎ ٱ ْﻛﺘَ َﺴﺒ‬ ‫ﻒ ﱠ‬ ُ ّ‫﴿ﻻَ ﻳُ َﻜﻠ‬
La yukallifu Allahu nafsan illa wusAAaha laha ma kasabat waAAalayha ma
iktasabat (Surat Al Baqara 1:286)

Tafsir: Haikalifishi Allah Nafsi (ya mtu) isipokua juu ya kile inachokiweza, analipwa
(mtu) kulingana na (jema) alilolichuma na anaadhibiwa kulingana na (maovu)
aliyochuma.

Ambapo ayah hii imetumia maneno mawili yanayotokana na asili ya neno moja ambalo
ni Kasaba. Neno Kasaba maana yake hua ni Kuchuma, Kupata, Kutafuta, Kukusanya,
Kufanya jambo au kitu.
175

Neno Kasaba ndio lililotoa neno Iktasaba ambalo maana yake hua ni Kufanya jambo
Ovu na kisha Kupata adhabu kali kutokana na Ovu hilo, wakati neno Kasabat hua
linamanisha Kufanya Jema au Ovu.

Ambapo aya hii inatuwekea wazi kua katika Uislam hakuna kitu kama Dhambi ya asili,
kwani kila Ibn Adam hua ni mwenye kuhesabiwa makosa yake anapotimia umri wa
miaka 15 ambao ndio umri unaojulikana kama umri wa Kubaleghe, yaani umri wa Kupea
na Kukua kiakili. Kwa Shariah za Kiislam Mtu anapofikia katika umri huu wa miaka 15
hua anaitwa Mukallaf yaani alie tayari Kubeba Majukumu ya Kumtii Mola wake na hivyo
anakua tayari kubeba dhambi za Makosa yake pale anapoachana na maamrisho ya Mola
wake na hii ni kulingana na namna atakavyoweza kuidhibiti Nafsi yake.

Kwani amesema Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Az Zukhruf al Din Imam Abu Hamid
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii kua: ‘Sijapata
kuona Mnyama Mkaidi kama Nafsi yangu kwani kila nikiivuta katika kufanya
Mema basi yeye hua ni mwenye kunivuta katika kufanya Maovu.’

Neno Mukallaf limetokana na sili ya neno Kalafa ambalo maana yake hua ni Kubeba
Mzigo, Kudhibitiwa na kitu kizito, kubeba Majukumu. Neno Kalafa ndio pia lililotoa
neno Mukallaf na pia lililotoa neno Yukallifu ambalo katika aya yetu tuliyoianggalia hapo
juu lietumiwa kwa kuwekewa kikanushi cha harfu ‘Lam’ na hivyo kua La Yukallifu
Allahu Nafsan illa wusAAaha yaani Haikalifishi au haibebeshi mzigo Allah Nafsi ya Mtu
isipokua juu ya ule uzito wa unachoweza kukibeba.

Hivyo baada ya Nabii Nuh kuomba Nusra kutoka kwa Mola wake, basi Allah Subhanahu
wa Ta’ala akajua kua kwa hakika Nabii wake anahitaji msaada wake basi akaikubali dua
ya Nabii Nuh lakini kwanza akamthibitishia kua:

ْ‫ﺲ ِﲟَﺎ َﻛﺎﻧُﻮا‬ ِ‫ﻚ إِﻻﱠ ﻣﻦ ﻗَ ْﺪ آﻣﻦ ﻓَﻼَ ﺗَـﺒـﺘَﺌ‬


َ ِ‫ﻮح أَﻧﱠﻪ ﻟَﻦ ﻳـ ْﺆِﻣﻦ ِﻣﻦ ﻗَـﻮ‬
‫ﻣ‬ ٍ ‫ﻧ‬
ُ ‫ﱃ‬
ٰ َ ِ ‫﴿وأ‬
ِ‫ُوﺣﻰ إ‬
ْ ْ َ َ َ ْ َ ُ ُ َ َ
﴾‫ﻳَـ ْﻔ َﻌﻠُﻮ َن‬
Waoohiya ila noohin annahu lan yu/mina min qawmika illa man qad amana fala
tabta-is bima kanoo yafAAaloona (Surah Hud 11:36)

Tafsir: Na tukamshushia Wahyi Nuh (kumwambia): Na hawatoamini miongoni mwa


watu wako isipokua wale waliokuamini tu. Hivyo Usiwe na huzuni juu ya yale
waliyokua wakiyafanya.
176

Hivyo Allah Subhanahu wa Ta’ala akamuwekea wazi Nabii Nuh kua bila ya shaka
amejitahid vya kutosha, na watu wake hao aliokua akiwapigania ili waokoke hawataooka
na hawatozidi idadi yao isipokua tu wale waliomkubali na hivyo basi itabidi Allah
Subhanah wa Ta’ala apitishe Hukmu yake kama walivyotaka wenyewe watu hao wa
Nabii Nuh kwa kuiomba adhabu hio juu yao kutokana na Kibri chao.


AL FULKA - SAFINA YA NABII NUH.


Hivyo kabla ya kupitisha hukmu yake baina ya Nabii Nuh na watu wake basi kwanza
akamuamrisha Nabii Nuh ajenge Safina kutokana na ujuzi atakaopewa na Allah
Subhanah wa Ta’ala kupitia katika usaidizi wa Malaika Jibril na kamwe hatakiwi tena
kuwazungumzia watu wake hao, kwa Allah Subhanah wa Ta’ala wala kuwausia watu
hao juu ya Allah Subhanah wa Taála.

﴾‫ﻳﻦ ﻇَﻠَ ُﻤ ۤﻮاْ إِﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ ﱡﻣ ْﻐَﺮﻗُﻮ َن‬ ِ‫ِ ِ ﱠ‬ ِ ِ ِ َ ‫﴿وٱﺻﻨَ ِﻊ ٱﻟْ ُﻔ ْﻠ‬
َ ‫ﻚ ﺄﺑ َْﻋﻴُﻨﻨَﺎ َوَو ْﺣﻴﻨَﺎ َوﻻَ ُﲣَﺎﻃْﺒ ِﲎ ﰱ ٱﻟﺬ‬ ْ َ
WaisnaAAi alfulka bi-aAAyunina wawahyina wala tukhatibnee fee
alladheena dhalamoo innahum mughraqoona (Surat Nuh 11:37)

Tafsir: Na jenga Safina chini ya uangalizi wetu na Wahyi wetu na wala usinihutubie
juu ya waliojidhulumu kwani kwa hakika watu hao ni miongoni mwa
watakaogharikishwa.

Aya hii ambayo imezungumzia Jahazi, Meli, yaani Safina na ingawa haikutumia neno
Safina lakini imetumia neno Al Fulka ambalo limetokana na asili ya neno Falaka ambalo
kwa Lugha ya Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Kua katika Umbo la Duara, Kua katika
Umbo la Meli au Jahazi na hivyo kua ni kitu chenye Kuelea juu juu. Neno Falaka ndio
lililotoa neno Falaki ambalo hua linamaanisha Nyota, Mwezi, Sayari, na kila kitu cha
Kimaumbile kilichoumbwa na Allah Subhanah wa Ta’ala kinachoelea Angani kama
zinavyoelea Nyota mwezi na Sayari. Hivyo basi Sayari na Safina vyote viwili vimeitwa
Al Fulki kwa sababu ya kauuvyote ni venye kuelea juu juu na tofauti yao ni kua Sayari
inaelea angani wakati Safina hua inaelea majini.
177

Neno Safina hua linamaanisha Kuchonga Umbo Zuri la kitu kwa Utaalamu, Kukata au
kupnguza kitu Mwishoni mwake na kukifanya kitu hicho kua kidogo zaid ya kilivyokua
hapo awali. Neno Safina ndio lililotoa neno Safinatun ambalo hua ni lenye kumaanisha
Jahazi, Boti, Gome la mti au Mbao ambayo ipo katika hali ya kuelea juu ya maji huku
ikiwa ni yenye kukata mawimbi na kuchana maji.

Na ingawa tunapozungumzia juu ya kisa cha Nabii Nuh hua tunataja sana Safina kuliko
Al Fulk, lakini ukweli ni kua Qur’an imetumia neno Safinatun kumaanisha Jahazi au
Safina mara tatu, ambapo mara moja tu ndio neno hili limetajwa kwenye kisa cha Nabii
Nuh na hii ni katika aya ya Surat Al Anqabut 29:15. Na mara mbili zilizobakia ni katika
Surat Al Kahf 18:71;79 pale ilipozungumzia kisa cha Nabii Musa na Al Khidhr kama
tutakavyoona hapo baadae katika kisa cha Nabii Musa. Hivyo basi mara nyengine zote
zilizobakia Qur’an imetumia neno Al Fulk katika kisa cha Nabii Nuh.

Hivyo tunarudi katika kisa chetu na kuona kua baada ya Nabii Nuh kuamrishwa kua
atengeneze Safina na Allah Subhanah wa Ta’ala basi nae akasema kama inavyoelezea
Qurán kwa kusema:

ِ ِ ِ ‫ب ﻻَ ﺗَ َﺬر ﻋﻠَﻰ ْاﻷَر‬


‫ﻚ إِن ﺗَ َﺬ ْرُﻫ ْﻢ‬
َ ‫ﻳﻦ َد ﱠ�راً ۞ إِﻧﱠ‬
َ ‫ض ﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻜﺎﻓ ِﺮ‬ ْ َ ْ ِّ ‫ﻮح ﱠر‬
ٌ ُ‫ﺎل ﻧ‬
َ َ‫﴿وﻗ‬
َ
ِ َ‫ﻀﻠﱡﻮاْ ِﻋﺒﺎد َك وﻻَ ﻳﻠِ ُﺪ ۤواْ إِﻻﱠ ﻓ‬
﴾ً‫ﺎﺟﺮاً َﻛ ﱠﻔﺎرا‬ ِ‫ﻳ‬
َ َ ََ ُ
Waqala noohun rabbi la tadhar AAala al-Ardhi mina alkafireena dayyaran; Innaka
in tadharhum yudhilloo AAibadaka wala yalidoo illa fajiran kaffaran (Surat Nuh
71:26-27)

Tafsir: Na akasema Nuh, Ya Rabb! Usimbakishe juu ya Ardhi hata kafiri mmoja katika
makazi yake. Kwani ikiwa utawabakisha basi watawapotosha waja wako na hawatozaa
isipokua wale waliokua hawakuamini.

Aya hii imetumia neno Dayyara ambalo ni lenye kutokana na neno Dara lenye
kumaanisha Kuzunguka au Kuzingira ambapo wingi wa neno Dara hua ni Diyyar na hua
linamaanisha Jengo linalotoa Hifadhi yaani Nyumba au Makazi. Hivyo neno Dayyara
hua ni lenye kumaanisha wenye kuishi kwenye Makazi yaani kila Ibn Adam wa kawaida,
hivyo basi Nabii Nuh alikua akiwaapiza Makafiri wote kwenye Makazi yao.

Ukweli ni kua Nabii Nuh alikua hajui hata Safina ndio nini hivyo akamuuliza Allah
Subhanah wa Taála: ‘Jee Safina ndio nini?’ Allah Subhanah wa Taála akamwambia
Nabii Nuh kua: ‘Safina ni nyumba ya mbao ambayo utakayokaa wewe na watu wako
itakayokua inaelea juu ya maji wakati pale nitakapo wagharikisha watu waovu’.
178

Nabii Nuh akashangaa na kuuliza: ‘Jee hayo maji yako wapi?’ Allah Subhanah wa
Taála akasema: ‘Hakika mimi nna uwezo wa kufanya kila kitu nikitakacho’. Nabii
Nuh akauliza tena: ‘Jee nitapata wapi mbao za kujengea nyumba hio itakayoelea?’
Allah Subhanah wa Taála akamwambia: ‘Panda miti’.

Nabii Nuh akapanda miti ya aina ya Mivule, ambayo ilichukua miaka 40 kukua na
kukomaa, huku Nabii Nuh akiwa ni mwenye kusita kuwausia watu wake kurudi kwa
Mola wao na huku Allah Subhanah wa Taála akionesha Miujiza yake kwa watu hao.
Kwani katika kipindi hiki cha miaka 40 basi hakuna mimba hata moja iliyotunga katika
matumbo ya uzazi ya Wanawake wa jamii ya watu hao, hivyo wote waliingia katika
kipindi kirefu cha Utasa yaani Wanaume walikua hawana nguvu ya kutosha katika idadi
ya wingi wa Manii yao kutoa watoto na Wanawake wakawa hawana mayai yatakatoweza
kubeba watoto.

Baada ya kupita miaka 40 basi Allah Subhanah wa Taála akamuamrisha Nabii Nuh
akaikate Mivule hio ambao iliyokua tayari ishapevuka, kisha aiwache ikauke ili apate
mbao za kutengenezea Nyumba inayotakiwa kutengenezwa.

Mivule hii ilikua mikubwa sana kiasi ya kua hakuna mtu alieweza kuinyanyua kutokana
pia na uzito wake, hivyo Nabii Nuh akamuomba Uj Ibn Anaq ambae alikuja na kumsaidia
kwa kuiburura miti hio na kuikusanya pamoja katia sehemu itakayotengenezewa Jahazi.
Uj Ibn Anaq hakua ni miongoni mwa watu waliokua wakiishi pamoja na Nabii Nuh,
kwani Uj Ibn Anaq hakua ni mwenye Dayyara kwani alikua ni mtu asieishi katika
Nyumba alikua akiishi katika moja kati ya kisiwa na alikua na mwili mkubwa sana kiasi
ya kua ilikua hakuna hata nyumba moja anayoweza kuingia ndani yake, na kwake yeye
kina kirefu cha bahari kilikua hakimfikii hata magotini.

Uj Ibn Anaq alikua ni mrefu kiasi ya kua alikua anapotaka maji ya kunywa basi alikua
akiyakamua Mawingu ya Mvua na anapotaka kula basi humchukua Samaki aina ya
Nyangumi na kumkausha na Jua kwa Mikono yake. Uj Ibn Unuq hakua ni mwenye
kuzama na kuangamia katika mafuriko kwa sababu yeye hakua ni miongoni mwa wenye
kuishi katika Dayyara. Na ingawa hakua ni mwenye kumuamini Nabii Nuh lakini alikua
ni mwenye kutekeleza maombi yake juu yake, ya kumkusanyia pamoja Mivule yote hio
iliyokatwa kwa ajili ya kutengeneza Safina.

Baada ya mbao kukauka Nabii Nuh akamuuliza Allah Subhanah wa Taála: ‘Jee niijenge
vipi hio nyumba?’ Allah Subhanah wa Taála akamwambia Nabii wake Nuh: ‘Ijenge
iwe kama umbo la Jogoo, lenye pande mbili sawia ambapo mbele iwe kama kichwa,
katikati kama tumbo na nyuma kama mkia kisha weka mlango ubavuni mwake.’
179

Allah Subhanah wa Taála akamtuma Malaika Jibril kumuongoza Nabii Nuh katika ujenzi
wa Safina hilo ambao mara tu ulipoanza basi watu wakaanza kumshangaa Nabii Nuh
kwani walikua hawajui anafanya nini. Hivyo wakamuuliza ndioa anatengeneza nini? Nae
akajibu Safina, hivyo wakaanza kumfuatilia na kumuona kua tayari ameshakua
mwendawazimu wakawa pia wanamdhihaki hali hii iliendelea hadi Nabii Nuh akaamua
kuwawekea wazi kwa kuwaambia kua wataona baadae ni nani atakaekuja kujuta baadae
kama vile asemavyo Allah Subhanah wa Ta’ala katika Surat Nuh:

‫ﺎل إِن ﺗَ ْﺴ َﺨُﺮواْ ِﻣﻨﱠﺎ‬َ َ‫ﻚ َوُﻛﻠﱠ َﻤﺎ َﻣﱠﺮ َﻋﻠَْﻴ ِﻪ َﻣﻠَـﺄٌ ِّﻣﻦ ﻗَـ ْﻮِﻣ ِﻪ َﺳ ِﺨُﺮواْ ِﻣْﻨﻪُ ﻗ‬ ْ َ‫﴿ َوﻳ‬
َ ‫ﺼﻨَ ُﻊ ٱﻟْ ُﻔ ْﻠ‬
‫اب ُﳜْ ِﺰ ِﻳﻪ َوَِﳛ ﱡﻞ‬ ِِ
ٌ ‫ف ﺗَـ ْﻌﻠَ ُﻤﻮ َن َﻣﻦ َ�ْﺗﻴﻪ َﻋ َﺬ‬ َ ‫ﻓَِﺈ ﱠ� ﻧَ ْﺴ َﺨُﺮ ِﻣﻨ ُﻜ ْﻢ َﻛ َﻤﺎ ﺗَ ْﺴ َﺨُﺮو َن۞ ﻓَ َﺴ ْﻮ‬
﴾‫اب ﱡﻣ ِﻘﻴﻢ‬ ِ
ٌ ٌ ‫َﻋﻠَْﻴﻪ َﻋ َﺬ‬
WayasnaAAu alfulka wakullama marra AAalayhi malaon min qawmihi sakhiroo
minhu qala in taskharoo minna fa-inna naskharu minkum kama taskharoona,
Fasawfa taAAlamoona man ya/teehi AAadhabun yukhzeehi wayahillu AAalayhi
AAadhabun muqeemun. (Surat Nuh 11:38-39)

Tafsir: Na wakati alipokua akitengeneza Safina, basi kila kiongozi miongoni mwa
viongozi wa watu wake alipokua akipita, alikua wakiwafanyia maskhara, ambapo nae
akasema: ‘Hakika nyinyi mnatufanyia sisi maskhara basi na sisi tutakufanyieni nyinyi
maskhara kama mnavyotufanyia sisi maskhara. Na kisha mtajua ni nani atakaepewa
adhabu itakayomfunika na adhiriko na ni nani atakaefikiwa na adhabu yenye
kudumu.’

Anasema Imam Abu Al Qasim Al Zamakhshari kuhusiana na aya hii kua: ‘Safina lilikua
ni kubwa na hivyo lilichukua mda mrefu kulitengeneza, kiasi ya kua baadhi ya
Viongozi wa Jamii ya Watu wa Nabii Nuh walipokua wakipita basi humfanyia
maskhara kwa kumwambia Nabii Nuh: ‘Ala! Sasa hivi umekua Seremala baada ya
kua Mtume?’ Na wengine walikua wakimfanyia maskhara pia kwa kumwambia:
‘Ala!! Unatengeneza Safina! Jee likishakua tayari litaelea na kusafiri juu ya nini?
Mchanga?’’

Allah Subhanah wa Taala akamshushia Wahyi Nabii wake Nuh na kumwambia kua
aharakishe katika utengenezaji wa Safina kwani kwa hakika dhihaka zao hawa watu
zinamzidishia hasira zake juu yao. Nabii Nuh akashirikiana na watoto wake Sham, Ham
na Yafith na wafuasi wake, anasema Dahhak Ibn Muzahim kua amesema Abd Allah Ibn
Abbas kua: ‘Nabii Nuh alitengeneza Safina lenye urefu wa dhiraa 660 kutoka
180

mwanzo hadi mwisho, Upana wa dhiraa 330 na urefu wa kutoka chini hadi juu kua
ni dhiraa 33.’ Ambalo aliliunganisha kwa misumari na vibanio vya chuma na kisha Allah
Subhanah wa Taála akajaalia kutokea kwa chem chem ya gundi nyeuse yenye kunata
kama mafuta karibu na eneo linapojengwa Safina hilo, na hivyo Nabii Nuh akachukua
gundi hio na kulipaka Safina zima ndani na nje na kuiacha ikaukie kua kama tabaka la
kuzuia maji yasiingie ndani ya Safina wala yasitoke nje ya Safina.

Tunapozunguumzia ukubwa wa Safina basi katika wakati wetu wa leo basi


tunazungumzia vyombo vya safari vya baharini ambavyo hadi hii leo inakua ni mfano
wa chombo cha kuigwa ambacho kimetengenezwa kwa kutumia ufundi wa hali ya juu,
kiasi ya kua haiwezekani kwa Safina hio kuzama hata bahari iwe na mawimbi makubwa
kiasi gani na pia hata bahari iwe imechafuka kiasi gani, kwani kwa vipimo vilivyotumika
basi ili Safina ipinduke au kuzama basi inabidi ilale kwa digiriz zaidi ya 90.

Kwani kwa vipimo vya leo basi tunaona kua Safina ilikua na urefu wa mita 160 kutoka
nyuma hadi mbele hii ni zaidi ya kiwanja kimoja na nusu cha mpira wa miguu, na upana
wake ni kiwanja kimoja kasorobo cha mpira wa miguu, yaani kama ingekua ndani ya
Safina hii wanajazwa Kondoo tu, basi wangeweza kuingia Kondoo 125,000.

Allah Subhanah wa Ta’ala anaelezea namna alivyomfahamisha Nabii Nuh hali


itakavyokua, kabla ya kutokea tokeo lilikousudiwa kutokea kwa ajili ya kuwaadhibu
Makafiri hao, na nini kitatokea baada ya kumalizika kwa Safina kwa kusema:

‫ﻮر‬ ِ ِ ِ ِ َ ‫﴿ﻓَﺄَوﺣﻴـﻨَﺂ إِﻟَﻴ ِﻪ أ َِن ٱﺻﻨَ ِﻊ ٱﻟْ ُﻔ ْﻠ‬


ُ ‫ﻚ ﺄﺑ َْﻋﻴُﻨﻨَﺎ َوَو ْﺣﻴﻨَﺎ ﻓَﺈ َذا َﺟﺂءَ أ َْﻣُﺮَ� َوﻓَ َﺎر ٱﻟﺘﱠـﻨﱡ‬ ْ ْ َْ ْ
َ‫ﻚ إِﻻﱠ َﻣﻦ َﺳﺒَ َﻖ َﻋﻠَْﻴ ِﻪ ٱﻟْ َﻘ ْﻮ ُل ِﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ َوﻻ‬ َ َ‫ﲔ َوأ َْﻫﻠ‬ ِ ْ ‫ﻚ ﻓِ َﻴﻬﺎ ِﻣﻦ ُﻛ ٍﻞ َزْو َﺟ‬
ِ ْ ‫ﲔ ٱﺛْـﻨَـ‬ ْ ُ‫ﭑﺳﻠ‬
ْ َ‫ﻓ‬
ّ
﴾‫ﺎﻃْﺒ ِﲎ ِﰱ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻇَﻠَﻤ ۤﻮاْ إِﻧـﱠ ُﻬﻢ ﱡﻣ ْﻐﺮﻗُﻮ َن‬ ِ َ‫ُﲣ‬
َ ْ ُ َ
Faawhayna ilayhi ani isnaAAi alfulka bi-aAAyunina wawahyina fa-idha jaa
amruna wafara alttannooru faosluk feeha min kullin zawjayni ithnayni waahlaka
illa man sabaqa AAalayhi alqawlu minhum wala tukhatibnee fee
alladheena dhalamoo innahum mughraqoona; (Surat Al Muminun 23:27)

Tafsir: Na kisha tukamshushia Wahyi juu yake ajenge Safina chini ya Uangalizi wetu,
na tukamshuhia Wahyi kumwambia itakapokuja amri yetu na Tanuri likafura
(likafoka) basi ingiza ndani yake (Safina) katika kila pea (ya Wanyama Dume na Jike)
na familia yako, isipokua wale ambao imewatangulia kauli miongoni mwao. Na
181

usinizungumzie mie juu ya wale waliofanya dhulma kwani kwa hakika wao
watagharikishwa.

Allah Subhanah wa Ta’ala katika ayah hii anatuwekea wazi kua alimuelekeza Nabii Nuh
kupitia kwa Malaika Jibril namna ya kujenga Safina, kwani lilikua linatakiwa liwe ni
lenye ukamilifu wa hali ya juu kwa sabau litachukua mda mrefu sana katika kuelea kwake
na hakutokua na sehemu ya Ardhi ya kushuka na kulitengeneza kama kama likiharibika.
Aya pia imetumia neno Tanuri ambalo hua linamaanisha Tanuri la udongo la moto wa
Kuokea Mikate, lakini sasa hapa tunaona kua Tanuri hili litakua nilenye kufoka maji
badala ya moto, hivyo basi kufoka kwa Tanuri hili ni moja kati ya Miujiza mikuu ya
Nabii Nuh badala ya lile la kutengeneza Safina na kisha kufuatia Gharika.

Kwa upande mwengine tunaona kua aya imetumia neno Aslaka ambalo hua ni lenye
kumaanisha Kufanya njia, Kupitia, Kuingia au Kupenya, hivyo basi hapa inatuonesha
Safina hili lilikua na Mlango wa Pembeni wa kuwaingizia kila aina ya Wanyama hao
ambao ni jike na dume, yaani wanyama hao hawakua ni wenye kubebwa na
kutumbukizwa ndani yake bali walikua ni wenye kuingizwa kwa kuongozwa na
kusukumwa.

Ama kuhusiana na pea za Wanyama hao basi kwa mtyizamo wa Mujaddid Ad Din Sultan
Al Mutakallimin Imam Al Ghazali Al Thani Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi yeye
anasema kua maana iliyokusudiwa hapa ni kua Wanyama hawa waliingizwa wawili
wawili kwa kila pea, yaani jike na dume na jike na dume kwa kila aina ya mnyama.

Vile vile aya pia imetumia neno Sabaqa ambalo humaanisha Kukimbilia, Kukipita kitu
au Kuwahi. Ambapo katika aya ifuatayo limetumika kama ifuatavyo:

‫ﱠت‬ ِ ِ ‫ﺂء وٱﻷَر‬ ِ ‫ض ٱﻟ ﱠﺴﻤ‬ِ ٍ ‫﴿ﺳﺎﺑُِﻘ ۤﻮاْ إِ َ ٰﱃ ﻣ ْﻐ ِﻔﺮةٍ ِﻣﻦ ﱠرﺑِ ُﻜﻢ وﺟﻨ‬
ْ ‫ض أُﻋﺪ‬ ْ َ َ ‫ﺮ‬ ‫ﻌ‬ ‫ﻛ‬َ ‫ﺎ‬‫ﻬ‬ ‫ﺿ‬
ُ ‫ﺮ‬ ‫ﻋ‬
َ
َْ َ ْ َ َ ْ ّ ّ َ َ ‫ﱠﺔ‬ َ
‫ﻀ ِﻞ‬ ‫ٱﻪﻠﻟِ ﻳـُ ْﺆﺗِ ِﻴﻪ َﻣﻦ ﻳَ َﺸﺂءُ َو ﱠ‬
ْ ‫ٱﻪﻠﻟُ ذُو ٱﻟْ َﻔ‬ ‫ﻀ ُﻞ ﱠ‬ ْ َ‫ﻚ ﻓ‬ ِ ِ ِ‫ﻟِﻠﱠ ِﺬﻳﻦ آﻣﻨﻮاْ ﺑِ ﱠ‬
َ ‫ﭑﻪﻠﻟ َوُر ُﺳﻠ ِﻪ ٰذﻟ‬ َُ َ
﴾‫ٱﻟْ َﻌ ِﻈﻴ ِﻢ‬
Sabiqoo ila maghfiratin min rabbikum wajannatin AAardhuha kaAAArdhi
alssama-i waal-ardi oAAiddat lilladheena amanoo biAllahi warusulihi dhalika
fadhlu Allahi yu/teehi man yashao waAllahu dhoo alfadhli alAAadheemi (Surat Al
Hadid 57:21)
182

Tafsir: Kimbilieni Msamaha kutoka kwa Mola wenu, na Pepo ambayo Upana wake
kama Mbingu na Ardhi, ambayo imetayarishwa kwa ajili ya wale waliomuamini Allah
na Mitume wake, hizo ndio Fadhila za Allah, humpa amtakae na Allah ni Mmiliki wa
Fadhila Kubwa sana.

Lakini hapa kwenye kisa cha Nabii Nuh limetumika Kwa Kusema: Illa man sabaqa
AAalayhi alqawlu minhum - Isipokua kwa Yule ambae Ametanguliwa na Kauli
miongoni mwao, yaani waingie wale waliomuamini Nabii Nuh tu na wale ambao Ujumbe
umewafika lakini hata hivyo haukukaa kwenye akili zao kwani ulikua kama ni wenye
kuwafikia na kisha kuwapita kwa kasi kupitia sikio moja na kutokea sikio jengine
kutokana na kutotaka kuutilia maanani ujumbe huo hivyo watu hao hawatoingia kwenye
Safina na bila ya shaka watakua ni wenye Kugharikishwa.

Safina lilipokua tayari basi Allah Subahnah wa Taála akamwambia Nabii Nuh: ‘Chukua
kila pea mbili dume na jike za kila aina za wanyama na kisha utakapoona Tanur
zitakapofoka kwa nguvu kutoka ardhini basi anza kuingia wewe na watu wako na
wanyama wako katika Safina.’ Kama zinavyosema aya zifuatazo:

ِ ْ ‫ٱﲪﻞ ﻓِ َﻴﻬﺎ ِﻣﻦ ُﻛ ٍﻞ َزْو َﺟ‬


ِ ْ ‫ﲔ ٱﺛْـﻨَـ‬ ِ ِ ﴿
‫ﻚ‬
َ َ‫ﲔ َوأ َْﻫﻠ‬ ّ ْ ْ ‫ﱡﻮر ﻗُـ ْﻠﻨَﺎ‬
ُ ‫َﺣ ﱠ ٰﱴ إذَا َﺟﺂءَ أ َْﻣُﺮَ� َوﻓَ َﺎر ٱﻟﺘﱠـﻨ‬
‫ﺎل ْٱرَﻛﺒُﻮاْ ﻓِ َﻴﻬﺎ‬ َ َ‫ﻴﻞ۞ َوﻗ‬ ِ ِ ِ
ٌ ‫إﻻﱠ َﻣﻦ َﺳﺒَ َﻖ َﻋﻠَْﻴﻪ ٱﻟْ َﻘ ْﻮ ُل َوَﻣ ْﻦ َآﻣ َﻦ َوَﻣﺂ َآﻣ َﻦ َﻣ َﻌﻪُ إﻻﱠ ﻗَﻠ‬
ِ
﴾‫ﻮر ﱠرِﺣﻴﻢ‬ ِ َ ‫ٱﻪﻠﻟِ َْﳎﺮ َاﻫﺎ وﻣﺮﺳ‬ ِ
ٌ ٌ ‫ﺎﻫﺎ إ ﱠن َرِّﰉ ﻟَﻐَ ُﻔ‬ َ ْ ُ َ َ ‫ﺑ ْﺴ ِﻢ ﱠ‬
Hatta idha jaa amruna wafara alttannooru qulna ihmil feeha min kullin zawjayni
ithnayni waahlaka illa man sabaqa AAalayhi alqawlu waman amana wama amana
maAAahu illa qaleelun, Waqala irkaboo feeha bismi Allahi majraha wamursaha
inna rabbee laghafoorun raheemun (Surat Hud 11:40-41)

Tafsir: Hadi pale ilipokuja amri yetu na Tanuri zikapofoka kwa nguvu. Nasi tukasema:
Ingia ndani yake na kila pea mbili (Dume na Jike) za Wanyama, na wewe na familia
yako, isipokua dhidi ya wale ambao wamefikiwa na ujumbe na walioamini. Na
hawakuamini isipokua kidogo tu. Na yeye (Nuh) akasema: Ingieni ndani yake, Kwa
Jina la Allah katika Kuelea kwake na katika Kutia Nanga kwake, kwani kwa hakika
Mola wangu ni mwingi wa Usamehevu na ni mwingi wa Rehma.

Nabii Nuh alisema kua: ‘Kwa jina la Allah katika kuelea kwake na katika kutia
nanga kwake yaani akimaanisha kua: ‘Kwa Jina la Allah Subhanah wa Ta’ala ambae
183

tunamtegemea yeye katika kila kitu, akitaka Safina lielee litaelea na kuelekea
atakako lielekee na akitaka lisimame basi litasimama.’’

Ama hapa kuna mitizamo tofauti juu ya maana ya neno Tannur ambalo ingawa kwa
lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Tanuri ambalo ni shimo la duara lenye kuwashiwa
moto ndani yake aidha kwa kuoka mikate, nyama, n.k, Chem Chem, Ardhi, Sehemu
ya juu kabisa ya Ardhi, Sehemu ambayo maji hua yanajikusanya pamoja katika
bonde.

Lakini kulingana na mtizamo wa Abd Allah Ibn Abbas basi yeye anasema kua: ‘Maji
yalitoka katika uso wa ardhi, na Waarabu huuita uso wa Ardhi kua ni Tannur.’

Ama kwa upande wa Qatadah Ibn Diama al Sudusi basi yeye anasema kua: ‘Tannur ni
sehemu Tukufu ya Ardhi na ni sehemu ambayo ipo juu.’

Ama kwa upande wa Hasan Al Basr basi yeye anasema kua: ‘Tannur lililotajwa hapa
basi ni Tanuri la kuokea mikate ambalo lilikua likitumiwa na Nabii Adam ambalo
lilikuwepo hadi katika kipindi cha Nabii Nuh, na ndio maana akaambiwa kua:
‘Utakapoona Tannur linafoka kwa nguvu, basi ingia wewe na watu wako katika
Safina’ hivyo maji yakafoka kutoka ndani ya Tanuri na alieona kufoka huko alikua
ni mke wake Nabii Nuh ambae nae akaenda kumtaarifu Nabii Nuh.’

Vile vile kuna kutofautiana juu ya sehemu ambayo lilikuwepo hilo Tannur. Kwani kwa
upande wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema kua: ‘Tannur
lilikua liko India, na lilifoka kwa nguvu na kumwagika na Nabii Nuh alipoona kua
hali imefikia hivyo basi akaanza kuchukua, kila aina ya mnyama dume na jike kama
alivyoamriwa na Allah Subhanah wa Taála’

Ama kwa upande wa Imam Mujahhid Ibn Jabr basi yeye anasema kua: ‘Tannur
lilikuwepo katika maeneno ya Kufah’ nchini Iraq. Ama kwa upande wa Imam Ismail
Abd Rahman Al Suddi basi yeye anasema kua: ‘Amir Al Shabi anaapa kua Tannur
halikufoka katika mji wowote isipokua katika maeneo ya mji wa Kufah kwani Nabii
Nuh alitengeneza Safina ndani ya Msikiti wa Kufah, na Tannur lilikuwepo katika
upande wa kulia wa Baab al Kindah (Mlango wa Kindah), kufoka kwake maji ilikua
ni dalili kwa Nabii Nuh dhidi ya kuangamizwa kwa watu wake.’

Na kwa upande wa Imam Muqatil Ibn Sulayman basi yeye anasema kua: ‘Tannur lilikua
ni Tanuri la Nabii Adam na lilikua lipo katika Ardhi ya Sham katika maeneo ya
Ayn al Ward.’
184

Ama kwa upande wa Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari basi yeye
anasema kua: ‘Lilikua ni Tanuri la mawe ambalo mwanzo lilikua likimilikiwa na
Nabii Adam na kufikia hadi katika kipindi cha Nabii Nuh. Allah Subhanah wa Taála
alijaalia kufoka kwa Tanuri hili kua ni sehemu ya Adhabu kwa ajili ya Watu wa
Nabii Nuh. Kama vile ambavyo alivyojaalia Moyo wa Rasul Alllah Salallahu Alayhi
wa Salam kuani wenye kufoka Nuru ya I’lm kwa Ummah wa Nabii Muhammad
Salallahu A’layhi wa Salam. Na pia kua ni Rehma kwa Ummah huu. Kwa Sababu
Allah Subhanah wa Taála ameupandisha darja Ummah huu kutokana na Utukufu
wa Nuru hiyo. Kwani Nuru ya Mitume wote imetokana na Nuru ya Rasul Allah
Salallahu Allahi wa Salam ambayo ndio Nuru ya Mbinguni, Nuru ya Ulimwenguni
na pia ndio Nuru ya Kesho Akhera. Na ndio maana akasema Allah Subhanah wa
Taála kua:

‫ﻮر‬ ‫ٱﻪﻠﻟُ َوﻳَـ ْﻐ ِﻔْﺮ ﻟَ ُﻜ ْﻢ ذُﻧُﻮﺑَ ُﻜ ْﻢ َو ﱠ‬


ٌ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻏ ُﻔ‬ ‫﴿ﻗُ ْﻞ إِن ُﻛﻨﺘُ ْﻢ ُِﲢﺒﱡﻮ َن ﱠ‬
‫ٱﻪﻠﻟَ ﻓَﭑﺗﱠﺒِﻌُ ِﻮﱏ ُْﳛﺒِْﺒ ُﻜ ُﻢ ﱠ‬
﴾‫ﱠرِﺣﻴﻢ‬
ٌ
Qul in kuntum tuhibboona Allaha faittabiAAoonee yuhbibkumu Allahu wayaghfir
lakum dhunoobakum waAllahu ghafoorun raheemun (Surat Al Imran 3:31)

Tafsir: Sema kama kweli mnampenda Allah basi nifuateni mimi na Allah
atakupendeni na kukusameheni madhambi yenu, kwani kwa hakika Allah ni mwingi
wa Usamehevu na ni mwingi wa Rehma.

Hivyo Allah Subhanah wa Taála ameyafanya mapenzi yetu kwake kua ni yenye
kujumuisha kumfuata Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam, na hivyo akayafanya
Malipo ya kumpenda yeye Allah Subhanah wa Taála kua ni kupata mapenzi yake
juu yetu, hii hua ni hali ya A’ala al Karamah yaani ya Kukirimiwa Heshima kubwa
sana.’

Na anasema Sultan Al Mutakkalimin Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua:
‘Haina haja ya kutafuta maana iliyofichika ya Tannur wakati maana halisi iko wazi,
yaani ni Tanuri la kuoka Mikate’

Hio ni miongoni mwa mitizamo ya Wanazuoni mbali mbali kuhusiana na Tanuri hivyo
tunarudi kwa Nabii Nuh ambae aliambiwa asubiri dalili ambayo ni kufoka kwa maji
katika sehemu ambayo haielekei kua itafoka maji, na yakishaanza kufoka maji hayo
kutoka kwenye Tanuri basi hapo itabidi yeye na wafuasi wake waingie ndani ya Safina.
185

Anasema Malik Ibn Sulayman Al Harawi kua: Nabii Nuh alikua na khofu ya
kuwaingiza Nyoka, Tandu na Nge ndani ya Jahazi kwa sababu ya kua huenda
watawadhuru watu waliomo ndani yake, lakini wadudu hao wakasema: ‘Kwa
hakika sisi hatutomdhuru yeyote yule atakae litaja jina lako’. Hivyo basi basi mtu
yeyote yule anaoogopa wadudu hao basi na asome aya ifuatayo:

�َ ‫ﲔ۞إِﻧﱠﻪُ ِﻣ ْﻦ ِﻋﺒَ ِﺎد‬ ِِ ِ ِ


َ ‫ﲔ۞إِ ﱠ� َﻛ ٰﺬﻟ‬
َ ‫ﻚ َْﳒ ِﺰى ٱﻟْ ُﻤ ْﺤﺴﻨ‬ َ ‫ﻮح ِﰱ ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬
ٍ ُ‫﴿ َﺳﻼٌَم َﻋﻠَ ٰﻰ ﻧ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ٱﻟْ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬
Salamun AAala noohin fee alAAalameena, Inna kadhalika najzee almuhsineena,
Innahu min AAibadina almu/mineena (Surat as Saffat 37:79-81)

Tafsir: Salam kutoka kwetu ziwe juu ya Nuh miongoni mwa Walimwengu, Kwa hakika
hivyo ndivo tunavyowazawadia Waja wenye kufanya mema, Hakika yeye alikua ni
miongoni mwa Waja wetu walioamini’

Baada ya Nabii Nuh kuingia ndani ya Safina basi wakafanya kama walivyoamriwa na
Allah Subhanah wa Ta’ala pale alipowaambia:

َ ‫ٱﳊَ ْﻤ ُﺪ ِﱠﻪﻠﻟِ ٱﻟﱠ ِﺬى ﳒَﱠ‬


‫ﺎ� ِﻣ َﻦ‬ ْ ‫ﻚ ﻓَـ ُﻘ ِﻞ‬ِ ‫ﻚ َﻋﻠَﻰ ٱﻟْ ُﻔ ْﻠ‬ َ ‫َﻧﺖ َوَﻣﻦ ﱠﻣ َﻌ‬
َ ‫ﺖأ‬ ْ ‫﴿ﻓَِﺈ َذا‬
َ ْ‫ٱﺳﺘَـ َﻮﻳ‬
ِ ِِ ِ
﴾‫ﲔ‬َ ‫َﻧﺖ َﺧْﻴـُﺮ ٱﻟْ ُﻤﻨ ِﺰﻟ‬
َ ‫ب أَﻧ ِﺰﻟْ ِﲎ ُﻣ َﻨﺰﻻً ﱡﻣﺒَ َﺎرﻛﺎً َوأ‬ِّ ‫ﲔ ۞ َوﻗُﻞ ﱠر‬َ ‫ٱﻟْ َﻘ ْﻮم ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
Fa-idha istawayta anta waman maAAaka AAala alfulki faquli alhamdu lillahi
alladhee najjana mina alqawmi aldhdhalimeena, Waqul rabbi anzilnee munzalan
mubarakan waanta khayru almunzileena (Surat Al Muuminun 23:28-29)

Tafsir: Na kisha mtakapopanda ndani ya Safina, wewe na wengineo watakaokua


pamoja nawe, basi semeni: ‘Alhamd Lillah Shukrani zote anastahiki Allah ambae
ametuokoa sisi kutokana na watu ambao ni Madhalimu’ na kisha sema: ‘Ewe Mola
wangu! Niteremshe katika sehemu yenye barka, kwani wewe ni m-bora wa
kuteremsha’

Ilikua ni miaka 2356 baada ya kufariki Nabii Adam, miaka 900 ya uhai wa Nabii Nuh
kupita na mwezi mosi Rajab ambapo Nabii Nuh na watu wake walipoanza kupanda
186

kwenye Safina hivyo walipokua ndani ya Safina basi Nabii Nuh akamuomba Allah
Subhanah wa Taala kwa kusema:

ِ َ‫ى وﻟِﻤﻦ دﺧﻞ ﺑـﻴ ِﱴ ﻣﺆِﻣﻨﺎً وﻟِْﻠﻤﺆِﻣﻨِﲔ وٱﻟْﻤﺆِﻣﻨ‬


‫ﺎت َوﻻَ ﺗَ ِﺰِد‬ ِِ ‫ب ٱ ْﻏ ِﻔْﺮ‬
ْ ُ َ َ ْ ُ َ ْ ُ َ َْ َ َ َ َ َ ‫ِﱃ َوﻟ َﻮﻟ َﺪ ﱠ‬ ِّ ‫﴿ ﱠر‬
﴾ً‫ﲔ إِﻻﱠ ﺗَـﺒَﺎرا‬ ِِ
َ ‫ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
Rabbi ighfir lee waliwalidayya waliman dakhala baytiya mu/minan
walilmu/mineena waalmu/minati wala tazidi aldhalimeena illa tabaran (Surat Nuh
71:28)

Tafsir: Ya Rabbi! nisamehe mimi na wazee wangu, na kila atakaeingia ndani ya


nyumba yangu kua alieamini, na walioamini wote Wanaume na Wanawake. Na
usiwazidishie Madhalimu isipokua maangamizo.

Neno Tabara maana yake hua ni Kuvunja na kutobakisha kitu. Kuangamiza kila kitu,
Kutekeza kila kitu, hivyo mbali ya kua Nabii Nuh aliwaombea watu wote waliomuasi
kua wasibakishwe hata mmoja yaani waangamizwe wote, lakini pia aliomba kua
wasibakishwe hata sehemu ya vipande vya mabaki yao, athari zao na dalili zao zote
zifutike juu ya uso wa ardhi. Na ndio maana basi Adhabu yao juu yao ilikua kubwa sana,
kwani ilikua tofauti na watu wa Mitume myengine waliofuatia baada yake ambao athari
zao zilibakia baada yao.

Anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Allah Subhanah wa Taála
aliteremsha mvua kwa siku 40 mfululizo usiku na mchana, wanyama wote Majike
na Madume walikuja na kujisalimisha wenyewe kwa Nabii Nuh. Miongoni mwa
Wanyama wa mwanzo ambao Nabii Nuh aliwaingiza kwenye Safina walikua ni
Ngómbe wa maziwa na kisha wakafuata Punda, walipoingia Punda basi Iblis
alinga’nga’nia kwenye mkia wa Punda hivyo Punda huyo ikabidi akawa hawezi
kiingia, Nabii Nuh akamuamrisha Punda aingie ndani lakini wapi, kila
akimuamrisha basi Punda hua ni mwenye kubakia pale pale mlangoni. Hadi
mwisho Nabii Nuh akasema bila ya kukusudia: ‘Ingia hata kama ikiwa Iblis yuko
pamoja nawe!’ Punda akaingia ndani, lakini Nabii Nuh akamuona Iblis na
kumzuia, Iblis akasema: ‘Kumbuka kua ulisema: ‘Ingia hata kama Iblis yuko
pamoja nawe hivyo inabidi nami niingie’ Nabii Nuh akasema: ‘Siwezi kukuruhusu!
Toka ewe Adui wa Allah! ’ Iblis akasema: ‘Mimi sitoki hivyo itakubidi unichukue
pamoja nawe.’ Hivyo Iblis akawa ni wenye kuigia na kua ni mwenye kukaa nje juu
ya Safina hilo.
187

Ama kwa upande wa Imam Wahb Ibn Munabih basi yeye anasema kua: ‘Baada ya Allah
Subhanah wa Taála kumwambia Nuh achukue pea ya Wanyama wa dume na jike
basi basi aliuliza: ‘Jee nitawafanya nini pale Ngombe atakapokua na Simba, na
Mbuzi atakapokua na Mbwa Mwitu?’’ Allah Subhanah wa Taála akamuuliza Nabii
Nuh: ‘Jee ni nani aliesababisha uadui baina yao?’ Nabii Nuh akajibu: ‘Ni wewe’
Hapo Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Basi usiwe na khofu kwani
nitawapatanisha baina yao’

Hivyo Nabii Nuh, Akawapakia Wanyama wa nyumbani na Wanyama wa Mwituni


katika sehemu moja ambayo ni sehemu ya chini ya Safina, na Allah Subhanah wa
Taála akawajaalia Simba kua ni wenye kuumwa hivyo wakawa hawawajali
wanyama wengine walio pamoja nao. Na yeye pamoja watu wengine wakakaa juu
pamoja na ndege akiwemo Kasuku. ’

Ama juu ya idadi ya watu hao ilikua ni watu wangapi basi kama tulivyosema hapo
mwanzo katika kurasa zilizotangulia kua kuna mitizamo tofauti, kwani Imam Qatadah
Ibn Diama Al Salusi basi yeye anasema: ‘Ndani ya Safina kulikua na Nabii Nuh,
Mkewe na watoto wake watatu Sham, Ham na Yafit na wake wao, hivyo wote
walikua ni watu wanane’

Imam Qatadah Ibn Diama Al Salusi anaendelea kusema kua: ‘Ham, akamuingilia
mkewe ndani ya Safina na Nabii Nuh akaomba Dua kwa Allah Subhanah wa Taála
hivyo Manii ya Ham yakabadilika na mkewe akapata watoto weusi.’

Ama kwa upande wa Imam Muhammad Ibn Saib Al Kalbi basi yeye anasema kua: ‘Nabii
Nuh hakuruhusu kuingiliana kimwili ndani ya Safina baina ya mke na mume’.

Ama kwa upande wa Imam Abu Muhammad Sulayman Ibn Mahran Al Asad Al Amash
basi yeye anasema kua: ‘Ndani ya Safina mlikua na watu 7, yaani Nabii Nuh, Watoto
wake watatu na Wake wa watoto wake’.

Ama kwa upande wa Muhammad Ibn Is-haq Ibn Yasr Ibn Khiyar basi yeye anasema kua:
‘Kulikua na watu 10 bila ya kuwahesabu wake zao. Walikua Nabii Nuh, Sham, Ham
na Yafith na wake 6 ambapo miongoni mwao watatu ni wake wa walioamini Nabii
Nuh na Waume zao’

Ama kwa upande wa Imam Muqatil Ibn Sulayman basi yeye anasema kua: ‘Walikua ni
watu 70 na zaidi, Nabii Nuh na Mke wake, Watoto wake na wake zao, wote kwa
pamoja walikua ni watu 78 nusu yao wakiwa ni Wanaume na nusu yao wakiwa ni
Wanawake’ na Abd Allah Ibn Abbas basi yeye anasema kua: ‘Walikua watu 80 na
188

Nabii Nuh aliuchukua mwili wa Nabii Adam akauweka kua ni mpaka baina ya
Wanaume na Wanawake’

Mara baada ya Nabii Nuh na watu wake na kila kilichohitajika kumaliza kupakiwa ndani
ya Safina, basi Maji yakaanza kufoka kwa nguvu zaidi na kumwagika kutoka mbinguni
kwa nguvu zaidi kama inavyoelezewa katika aya zifuatazo za Qurán.

‫ض ﻋُﻴُﻮ�ً ﻓَﺎﻟْﺘَـ َﻘﻰ ٱﳌﺂءُ َﻋﻠَ ٰﻰ‬ ‫َر‬


‫ﻷ‬ ‫ٱ‬ �
َ‫ﺮ‬‫ﺠ‬‫ﱠ‬ ‫ﻓ‬
َ‫و‬ ۞ ٍ
‫ﺮ‬ ِ ‫ﺂء ِﲟَ ٍﺎء ﱡﻣْﻨـﻬ‬
‫ﻤ‬ ِ ‫﴿ﻓَـ َﻔﺘﺤﻨﺂ أَﺑـﻮاب ٱﻟ ﱠﺴﻤ‬
َ َ ْ ْ َ َ َ َ َْ َْ َ
﴾‫أ َْﻣ ٍﺮ ﻗَ ْﺪ ﻗُ ِﺪر‬
َ
Fafatahna abwaba alssama-i bima-in munhamirin, Wafajjarna al-ardha
AAuyoonan failtaqa almao AAala amrin qad qudira, (Surat Al Qamar 54:11-12)

Tafsir: Na tukafungua milango ya mbiguni ya maji yaliyokua yakimwagika. Na


tukasababisha Ardhi kua ni yenye kufoka chemchem zenye nguvu, hivyo maji ya
mbinguni na ardhini yakakutana.

Kwani aya zinatuonesha Uwezo wa Allah Subhanah wa Ta'ala juu ya lile analolitaka kua
litokee na hivyo hapa zinatuonesha mfano wa Uzito na Ukubwa wa Adhabu zake kwa
kila wenye Kumuasi, na hizo ni adhabu za Duniani tu bado za Akhera.

Ya Allah Ya Karim Ya Ghafuru ya Rahim!

Tuingize kwenye Rehma zako na tuongoze katika njia iliyosahih kwani hakuna
muongozaji zaidi yako na utuepushe na adhabu zako kwani hakuna miongoni mwetu
anaeweza kustahmilia adhabu zako na hakuna atakaeweza kutuepusha nazo isipokua
wewe tu..Aamiin

Naam..tunapoziangalia aya hizo ambazo zinazungumzia Gharika ilivyokua basi ukweli


ni kua hakuna hata mmoja miongoni mwetu atakaeweza kuingiza akilini na kisha angalau
akakisia hali ilivyokua. Kwani hapa tunazungumzia Maji yaliyokua yakimwagika kutoka
Mbinguni ambayo wingi na mfululizo wake hauna kifani kwani ni zaidi ya maji
yanayomwagika kutoka kwenye Bwawa Kubwa linalofua umeme lililofunguliwa
Milango yake ya maji kisha maji hayo yakawa ni yenye kumwagika chini.

Na kwa upande wa ardhini basi maji yanavyofoka kwa wingi kutoka katika kila sehemu
ardhini kiasi ya kua wingi na ukubwa wa Mawimbi yake ni zaid ya Mawimbi ya Tsunami.
ambapo maji haya yalikua ni mithili ya sehemu ndogo tu ya silaha za Maangamizo ya
189

Allah, kiasi ya kua kwake yeye ni kuyaamrisha tu yaongezeke kwa ajili ya kugharikisha
na yanagharikisha.

Naam bila ya shaka kwa Allah Subhanah Allahu wa Ta’ala kila kitu kinawezekana kwani
yeye ndie Muumbaji na ni mmiliki wa majeshi ya Mbinguni na majeshi ya Ardhini na
juu ya kila kitu Ulimwenguni:

ِ‫ﻮب ٱﻟْﻤﺆِﻣﻨِﲔ ﻟِﻴـﺰداد ۤواْ إِﳝﺎ�ً ﱠﻣﻊ إِﳝﺎ�ِِﻢ وِﱠﻪﻠﻟ‬


ِ ُ‫َﻧﺰَل ٱﻟ ﱠﺴ ِﻜﻴﻨَﺔَ ِﰱ ﻗُـﻠ‬
‫أ‬ ۤ ‫﴿ﻫﻮ ٱﻟﱠ ِﺬ‬
‫ي‬
َْ َ َ َ ُ َ ْ َ َ ْ ُ َ َُ
﴾ً‫ٱﻪﻠﻟ َﻋﻠِﻴﻤﺎً َﺣﻜِﻴﻤﺎ‬ ِ ‫ﺟﻨُﻮد ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬
ِ ‫ات َوٱﻷ َْر‬
ُ‫ض َوَﻛﺎ َن ﱠ‬ ََ ُ ُ
Huwa alladhee anzala alssakeenata fee quloobi almu/mineena liyazdadoo eemanan
maAAa eemanihim walillahi junoodu alssamawati waal-Ardhi wakana Allahu
AAaleeman hakeeman (Surat Al Fatih 48:4)

Tafsir: Yeye ndie ambae anaeshusha utulivu ndani ya nyoyo za Waumini, ili wapate
kukua na Imani zao. Na kwa Allah ndiko kwenye umuliki wa Nguvu za Mbinguni na
Ardhini na daima Allah ni mwingi wa Ujuzi na Hikma.

Aya hii imetumia neno Junudu ambalo hua ni lenye utokana na neno Janada ambalo hua
ni lenye kumaanisha Jeshi, Usimamizi wa Majeshi, Nguvu za kivita au za kuadhibu
wanaomuasi mwenye mamlaka Juu yao. Na bila ya shaka hapa panazungumziwa
Muumba ambae ndie Mmiliki wa wa kila Kiumbe Ulimwenguni, Ardhini na Mbinguni.

Hivyo basi Allah Subhanah wa Ta’ala hua na uwezo wa kuwatumia Viumbe wake kua
kama Junudu wake kwa ajili ya kuwaadhibu wale wanaomkufuru na hivyo kua ni wenye
kupingana na Mitume wake, bila ya kujali ukubwa au udogo wa kiumbe anaetaka
kuadhibiwa au anaetaka kutumiwa kwa ajili ya kutoa adhabu husika kwa watu husika,
kuanzia Maji kwa watu wa Nabii Nuh, Mdudu Nzi kwa Namrudh Al Kabir, Vyura na
Chawa kwa Fir’awn na watu wake, n.k

Allah Subhanah wa Ta’ala anaendelea kutuwekea wazi yaliyofuata baada ya hapo pale
aliposema:
190

‫ات أَﻟْ َﻮ ٍاح َوُد ُﺳ ٍﺮ۞ َْﲡ ِﺮى ِﺄﺑ َْﻋﻴُﻨِﻨَﺎ َﺟَﺰآءً ﻟِّ َﻤﻦ َﻛﺎ َن ُﻛ ِﻔَﺮ۞ َوﻟََﻘ ْﺪ‬
ِ ‫﴿و َﲪ ْﻠﻨَﺎﻩ ﻋﻠَﻰ َذ‬
ٰ َ ُ َ َ
﴾‫ﻒ َﻛﺎ َن َﻋ َﺬ ِاﰉ وﻧُ ُﺬ ِر‬ ِ ِ
َ َ ‫ﺎﻫﺎ آﻳَﺔً ﻓَـ َﻬ ْﻞ ﻣﻦ ﱡﻣ ﱠﺪﻛ ٍﺮ۞ ﻓَ َﻜْﻴ‬ َ َ‫ﺗـَﱠﺮْﻛﻨ‬
Wahamalnahu AAala dhati alwahin wadusurin, Tajree bi-aAAyunina jazaan liman
kana kufira, Walaqad taraknaha ayatan fahal min muddakirin, Fakayfa kana
AAadhabee wanudhuri (Surat Al Qamar 54:13-15)

Tafsir: Na tukamchukua yeye ndani ya chombo cha mbao na misumari (Safina),


Akiwa anaelea chini ya uangalizi wa macho yetu, zawadi yake yeye aliekua
amekataliwa. Na kwa hakika, tumeiwacha kua kama ni kumbukumbu lakini ni nani
atakaekumbuka Na ni vipi (Ukubwa wake) Adhabu yangu na Muonyo wangu.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala aliyaruhusu Maji kumwagika kutoka mbinguni na


kukusanyika pamoja na yanayofoka kutoka ardhini bila ya kudidimia ndani ardhini,
kwani kila shimo na tundu la Ardhi lilitoa maji usiku na mchana kwa siku 40 kiasi ya kua
Safina na ukubwa wake wote basi likaanza kuelea juu juu kama vile lipo kati kati ya
Bahari.

Hapa aya pia imetumia neno Dusur ambalo hua ni lenye kutokana na neno Dasara
ambalo hua linamaanisha Kutengenezwa kwa Misumari, Kukishikamanisha kitu na
kukifanya kua kisichoweza kupitisha maji ndani, na pia hua ni lenye kumaanisha
Kupangua, Kutenganisha, Kupasua au Kuchana kitu kwa kutumia nguvu, kama vile
chombo cha baharini kinavyochana Maji.

Ambapo tunaona kua hii ilikua ni Safina ya mwanzo Kuundwa ulimwenguni, na ni ya


mwanzo kuweza kuelea bila ya kujaribiwa kabla yake, kwani majaribio yake ndio
matumizi yake, kiasi ya kua ilikua ni dalili au kumbukumbu na mfano kwa vyombo
vyengine vya safari vya baharini kuelea, na pia kua ni mfano kwa vizazi vyengine kuja
kuiona baadae, ambapo tuuaona kua Mujaddid Ad Din Al Hafidh Imam Shihab Ad Din
Ibn Hajar Al Asqalani basi yeye anasema kua: ‘Iliwahi kuonekana katika maeneo
baina ya Mto Tigris na Mto Euphrates katika Mlima Judy’

Na hivi ndivyo ilivyokua hali ya Safina la Nabii Nuh, kwani lilichana maji bila ya
kuathirika na Wingi wa maji, Ukubwa wa mawimbi, au Upepo uliopo juu yake, kwani
lilikua linaelea huku likiwa chini ya Uangalizi wa Muumba ambae ndie pia mwenye
kudhibiti jeshi la maangamizi la maji hayo kiasi ya kua waliomo ndani ya Safina
walijiona kua wapo kwenye salama, utulivu na amani kutokana na kumuamini Mola wao.
191

‫ﺐ‬ ‫ﻮح ٱﺑْـﻨَﻪُ َوَﻛﺎ َن ِﰱ َﻣ ْﻌ ِﺰٍل ٰﻳـﺒُـ َﱠ‬ ِ ِْ ‫﴿وِﻫﻰ َْﲡ ِﺮى ﻬﺑِِﻢ ِﰱ ﻣﻮ ٍج َﻛ‬
ْ ‫ﲎ ْٱرَﻛ‬ ٌ ُ‫ﭑﳉﺒَﺎل َو َ� َد ٰى ﻧ‬ َْ ْ َ َ
ِ ‫ﺼﻤ ِﲎ ِﻣﻦ ٱﻟْﻤ‬ ِ ِ ۤ ِ ِ‫ﱠﻣﻌﻨﺎ وﻻَ ﺗَ ُﻜﻦ ﱠﻣﻊ ٱﻟْ َﻜﺎﻓ‬
َ‫ﺎل ﻻ‬َ َ‫ﺂء ﻗ‬ َ َ ُ ‫ﺎل َﺳﺂ ِوي إ َ ٰﱃ َﺟﺒَ ٍﻞ ﻳَـ ْﻌ‬ َ َ‫ﻳﻦ۞ ﻗ‬
َ ‫ﺮ‬ َ َ ََ
َ ‫ٱﻪﻠﻟِ إِﻻﱠ َﻣﻦ ﱠرِﺣ َﻢ َو َﺣ‬
‫ﺎل ﺑـَْﻴـﻨَـ ُﻬ َﻤﺎ ٱﻟْ َﻤ ْﻮ ُج ﻓَ َﻜﺎ َن ِﻣ َﻦ‬ ‫ﺎﺻ َﻢ ٱﻟْﻴَـ ْﻮَم ِﻣ ْﻦ أ َْﻣ ِﺮ ﱠ‬
ِ ‫ﻋ‬
َ
﴾‫ﲔ‬ ِ
َ ‫ٱﻟْ ُﻤ ْﻐَﺮﻗ‬
Wahiya tajree bihim fee mawjin kaaljibali wanada noohunu ibnahu wakana fee
maAAzilin ya bunayya irkab maAAana wala takun maAAa alkafireena, Qala
saawee ila jabalin yaAAsimunee mina alma-i qala la AAasima alyawma min amri
Allahi illa man rahima wahala baynahuma almawju fakana mina almughraqeena
(Surat Hud 11:42-43)

Tafsir: Hivyo Safina ikaelea na kusafiri pamoja nao watu wake ikiwa kati kati ya
mawimbi makubwa kama Milima, na Nuh akamuita mtoto wake, ambae aliekua
amejitenga nae, (Kwa kumwambia) ‘Ewe Mtoto wangu njoo upande pamoja nasi na
usiwe miongoni mwa waliokufuru.’ Yule mtoto nae akajibu: ‘Nitaenda kupanda juu
ya Mlima utaniokoa dhidi ya Mafuriko ya maji haya.’ Nabii Nuh akasema: ‘Leo ni
siku ambayo hakuna usaidizi dhidi ya Majaaliwa ya Allah isipokua yule atakaeingizwa
ndani ya Rehma za Allah’. Na Wimbi likaja baina yao, na hivyo yeye (Mtoto wa Nabii
Nuh) akawa ni miongoni mwa waliogharikishwa.

Hivyo miongoni mwa waliogharikishwa basi alikuwemo pia Mtoto wa Kiume wa Nabii
Nuh anaeitwa Canaan ambae yeye alikua anajua kua mafuriko ya kawaida kamwe
hayawezi kufunika maeneno yaliyo juu ya Milimani, lakini haya hayakua ni mafuriko ya
kawaida bali yalikua ni mafuriko ya adhabu ya kugharikishwa, hivyo bila ya shaka
hakuna atakaeweza kuokoka isipokua yule ambae ameingizwa ndani ya rehma za Allah
Subhanah wa Taála.

Aya yetu imetumia neno Mauj ambalo ni lenye kutokana na neno Maja ambalo hua ni
lenye kumaanisha Tuna, Vimba, Kasirika, Yenye kutumia nguvu zake zote, Kutokua na
Utulivu, Kutopatana na hivyo kua ni yenye Kuchanganya kwa nguvu zaid. Hivyo Qur’an
hapa inayazungumzia maji ya bahari ambayo mawimbi yake kua ni sehemu ya gharika
hii waliyoangamiziwa watu wa Nabii Nuh kua na ukubwa kama Mlima.

Na tunapozungumzia maumbile ya ukubwa wa mawimbi ya bahari basi ukubwa zaidi


uliowahi kurikodiwa na wanasayasi ulikua ni urefu wa futi 121 ambayo ni sawa na mita
192

37 na tunapozungumzia ukubwa wa Wimbi la aina hio basi bila ya shaka hua tayari
tunazungumzia urefu wa mlima kwani urefu huo tayari ushavuka urefu wa nyumba yenye
Ghorofa 12, sasa hapa tunazungungumzia mawimbi ya maji ambayo tayari yameletewa
kama ni moja kati ya Junudu samawati wal Ardhi yaani nguvu za Jeshi la Mbiguni na
Ardhini ambalo limetayarishwa kwa ajili ya kutekeleza amri ya Muumba ambayo ni ya
kuwagharikisha waliokufuru tu. Sasa tafakkar kama ikiwa wimbi tu ni sawa na milima
jee utakuaje urefu wa kina cha maji yenyewe?

Ama kwa upande mwengine basi tunapoangalia juu ya namna Allah Subhanah wa Taála
anavyoielezea namna Gharika hiyo ilivyotokea katika Qurán kwa kuyaelezea Mawimbi
na ukubwa wake basi hapa inabidi tujue kua Kimaumbile Allah Subhanah wa Taála
ameyajaalia Mawimbi ya Maji kua na maumbile ya kua kila yanavyokua Makubwa basi
ndio yanavyokua na uwezo mkubwa zaidi wa kupandisha mvuke juu hewani na hivyo
kusababisha kunyesha mvua kubwa zaidi katika sehemu inayokusudiwa, yaani
inawezekana ikawa kuna sehemu fulani baharini ukatokezea upepo ambao nao
ukasabababisha mawimbi makubwa ambayo nayo yakasababisha mvuke mwingi sana
kupaa hewani, mvuke ambayo huchukuliwa na upepo na kupelekwa hadi katika sehemu
ambayo Allah Subhanah wa Taála anataka inyeshe mvua hio, iwe baharini au ardhini hii
hutegemeana na makadirio yake mwenyewe mwingi wa Hikma kwani kamwe mvua hio
haiwezi kunyesha katika sehemu ambayo haikukadiriwa inyeshe.

Subhana Allah! Kwani tunapozungumzia makadirio ya Allah Subhanah wa Taála juu ya


Gharika ya Maji yaliyokua yanamwagika katika mji wa Nabii Nuh, basi tunazungumzia
kwanza mvua iliyokua ikimwagika kutoka mbinguni, na maji yaliyomwagika kwa kufoka
kutoka ardhini ambayo nayo yakasababisha kutokea bahari yenye kina kirefu cha maji
yenye mawimbi makubwa, ambayo nayo pia yakasababisha mvua kutokana na wingi wa
maji yenyewe na ukubwa wa mawimbi yenyewe.

Hapo hapo kila mawimbi yanapokua makubwa, basi ndio hali inavyokua mbaya zaidi
kwa vyombo vya usafiri baharini kwani ukubwa wa mawimbi haupelekei tu kutotulia
kwa chombo husika kilichopo katika maji husika, lakini hupelekea pia husababisha
kutengenezeka kwa mvuke mwingi sana na hivyo kusababisha kukosekana kwa eneo
lenye hewa ya mvutano juu ya maji ambayo husababisha udhibiti wa chombo kwa
kukikandamiza juu ya maji na hivyo kukipa chombo husika utulivu wa kuelea bila ya
kuyumba juu ya maji.

Lakini kwa upande wa Safina ya Nabii Nuh, basi kila kitu kilikua kipo chini ya uangalizi
wa Allah Subhanah wa Taála, na hivyo Safina hio mbali ya kua imetengenezwa kwa
uangalizi wa Allah Subhanah wa Taála na hivyo ni kua ni yenye ukamilifu lakini hata
hivyo pia haikuathiriwa na mazingira ya eneo la usafiri wake ambayo nalo liko chini ya
193

amri ya Allah Subhanah wa Taála na hivyo ilisafiri kwa utulivu, usalama na Amani na
ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akasema.

﴾‫ات أَﻟْﻮ ٍاح وُد ُﺳ ٍﺮ۞ َْﲡ ِﺮى ِﺄﺑ َْﻋﻴُﻨِﻨَﺎ َﺟَﺰآء ﻟِّﻤﻦ َﻛﺎ َن ُﻛ ِﻔﺮ‬
ِ ﴿
َ َ ً َ َ ‫َو َﲪَْﻠﻨَﺎﻩُ َﻋﻠَ ٰﻰ َذ‬
Wahamalnahu AAala dhati alwahin wadusurin, Tajree bi-aAAyunina jazaan liman
kana kufira (Surat Al Qamar 54:13-14)

Tafsir: Na tukamchukua yeye ndani ya chombo cha mbao na misumari (Safina),


Akiwa anaelea chini ya uangalizi wa macho yetu, zawadi yake yeye aliekua
amekataliwa.

Anasema Umm ul Muuminina Aisha Radhi Allahu Anha kua: ‘Amesema Rasul Allahu
Salallahu Alayhi wa Salam kua: Kama Allah Subhanah wa Taála angekua ni
mwenye kumuonea huruma mtu yeyote yule miongoni mwa watu wa Nuh, basi
angemuonea huruma Mwanamke, ambae ni Mama wa Mtoto (Canaan) ambae
alikhofia kua maji yatamfikia mtoto huyo ambae alikua akimpenda sana hivyo
alienda nae hadi juu ya Mlima kileleni, na maji yalipomfikia mama huyu shingoni
basi mama huyu alimnyanyua mtoto wake juu ili asizame pamoja nae, lakini maji
yakawachukua wote wawili, hivyo kama Allah Angelikua ni mwenye kumuonea
huruma mtu yeyote yule katika watu wa Nabii Nuh, basi angemuonea huruma
mtoto huyu ’(Imam Muhammad Al Thalabi)

Mke huyu wa Nabii Nuh alikua akiitwa Wahila na alikua ni miongoni mwa watu ambao
walikua wanapingana na mumewe kisirisiri kwani alikua si mwenye kuamini juu ya
utume wa Nabii Nuh, hivyo akawa ni mwenye kuchukua siri za Nabii Nuh na kuzitoa nje
na yeye ndie alieanzisha kusema kua Nabii Nuh ni mwendawazimu hivyo nae akawa ni
miongoni mwa wale ambao hawakuingia ndani ya Safina wakati Nabii Nuh alipopanda
pamoja na watu waliomuamini, na ndio maana Allah Subhanah wa Taála akampigia
mfano Mwanamke huyu kwa kusema:

‫ﺖ َﻋْﺒ َﺪﻳْ ِﻦ ِﻣ ْﻦ‬ ٍ ِِ


َ ‫ﻮح َو ْٱﻣَﺮأََة ﻟُﻮط َﻛﺎﻧَـﺘَﺎ َْﲢ‬ َ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻣﺜَﻼً ﻟّﻠﱠﺬ‬
ٍ ُ‫ﻳﻦ َﻛ َﻔُﺮواْ ْٱﻣَﺮأََة ﻧ‬ ‫ب ﱠ‬ َ﴿
َ ‫ﺿَﺮ‬
‫ﱠﺎر َﻣ َﻊ‬ ‫ﻨ‬ ‫ٱﻟ‬ ‫ﻼ‬
َ ‫ﺧ‬ ‫ٱد‬ ‫ﻴﻞ‬ِ‫ٱﻪﻠﻟِ ﺷﻴﺌﺎً وﻗ‬
‫ﱠ‬ ‫ﻦ‬ ِ ‫ﺎﳘﺎ ﻓَـﻠَﻢ ﻳـ ْﻐﻨِﻴﻨَﺎ ﻋْﻨـﻬﻤﺎ‬
‫ﻣ‬ ُ ‫ﺘ‬ ‫ـ‬
َ ‫ﻧ‬ ‫ﺎ‬‫ﺨ‬ ‫ﻓ‬
َ ‫ﲔ‬ ِ ‫ِﻋﺒ ِﺎد َ� ﺻ‬
ِ َْ‫ﺎﳊ‬
َ ُ ْ َ َ ْ َ َ َ ُ َ ُ ْ َ َ َ َ َ
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ٱﻟﺪﱠاﺧﻠ‬
194

Dharaba Allahu mathalan lilladheena kafaroo imraata noohin waimraata lootin


kanata tahta AAabdayni min AAibadina salihayni fakhanatahuma falam yughniya
AAanhuma mina Allahi shay-an waqeela odkhula alnnara maAAa alddakhileena
(Surat At Tahrim 66:10)

Tafsir: Anakupigieni Allah mfano wa wale waliokufuru, Mke wa Nuh na Mke wa Lut
ambao walikua chini ya Waja wawili wema lakini waliwasaliti (Waume zao), hivyo
hawakuwanufaika na kitu chochote kutokana nao kutokana kwa Allah na
wakaambiwa: ‘Uingieni moto pamoja na wanaouingia’

Na Wahila hakua peke yake kutoka katika watu wa Nabii Nuh ambao walimpinga bali
pia miongoni mwao alikuwemo na huyu mtoto wake aitwae Canaan ambaye yeye alikua
yuko katika upande wa mama yake, jambo ambalo kinatuwekea wazi kua kila mtu ana
hiari ya kufuata upande autakao yaani wa upotovu na kujiangamiza au wa uongofu na
hivyo kua ni miongoni mwa walioamini na kupata usalama wa kidunia na kiakhera,
kwani vyenginevyo basi mtu huwezi kumlazimisha hata kama iwe tu huyo ni ndugu yako,
damu yako au mke wako.

Na ingawa Nabii Nuh alikua ni mwenye kujua kua yeye jukumu lake ni kutangazia tu
yale aliyoamrishwa kua atangazie na Mola wake, na yaliyobakia yote hayapo ndani ya
uwezo wake, bali yamo ndani ya uwezo wa Mola wake, hivyo japo kua alikua ni mwenye
kuwapenda watu wa familia yake na kujitahidi kuwaongoza katika njia iliyokua sahih,
hadi dakika za mwisho, lakini kwa bahati mbaya watu wawili wakawa si miongoni mwa
waliojaaliwa kuongoka kutokana na kujipotosha kwa khiari yao na kua ni miongoni mwa
waliojidhulumu Nafsi zao kama aya zinavyoendelea kutuelezea yaliyotokea baada ya
hapo kwa kusema:

ِ ُ‫﴿وﻗِﻴﻞ ٰ�َرض ٱﺑـﻠَﻌِﻰ ﻣﺂء ِك وﻳٰﺴﻤﺂء أَﻗْﻠِﻌِﻰ و ِﻏﻴﺾ ٱﻟْﻤﺂء وﻗ‬


‫ﻀ َﻰ ٱﻷ َْﻣُﺮ‬ َُ َ َ َ ُ ََ َ َ َ ْ ُ ْ َ َ
﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ ِ ِ ِ ‫ﻮد‬ِ ْ ‫وٱﺳﺘـﻮت ﻋﻠَﻰ‬
َ ‫ﻴﻞ ﺑـُ ْﻌﺪاً ﻟّْﻠ َﻘ ْﻮم ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
َ ‫ى َوﻗ‬
ّ ُ‫ٱﳉ‬ َ ْ ََْ َ
Waqeela ya ardhu iblaAAee maaki waya samao aqliAAee wagheedha almao
waqudhiya al-amru waistawat AAala aljoodiyyi waqeela buAAdan lilqawmi
aldhdhalimeena (Surat Hud 11:44)

Tafsir: Na ikasemwa: Ewe Ardhi yameze maji yako! na ewe Mbingu yazuie maji yako!
Na maji yakatoweka, na amri ya Allah ikawa ni yenye kukamilishwa (kwa
kugharikishwa kwa waliomuasi). Na (Safina) ikawa imesimama juu ya Mlima Juddi.
Na ikasemwa: Iwe ni yenye kuangamia kaumu ya wale walio madhalimu.
195

Hivyo, mafuriko yakaisha, mvua ikasita, na maji yote ardhini kayatoweka na Nabii Nuh
na watu wake na kila kilichomo ndani ya kwenye Safina wakajikuta wametuwama juu
ya Mlima Juddi, mlima ambao upo Mashariki ya Uturuki katika milima ya Ararat karibu
na nchi ya Armenia.

Ambapo wanafamilia wawili wa Nabii Nuh ambao ni Wahila na Canaan wakawa ni


miongoni mwa waliojidhulumu, jambo ambalo lilikua ni mtihani mkubwa zaid kwa Nabii
Nuh na kumtia uchungu zaidi na hivyo akamuomba Mola wake kutokana na huruma ya
mzazi kwa mtoto wake kama inavyosema aya inayofuatia:

‫َﺣ َﻜ ُﻢ‬
ْ ‫َﻧﺖ أ‬ ْ ‫ب إِ ﱠن ٱﺑُِﲎ ِﻣ ْﻦ أ َْﻫﻠِﻰ َوإِ ﱠن َو ْﻋ َﺪ َك‬
َ ‫ٱﳊَ ﱡﻖ َوأ‬ ِّ ‫ﺎل َر‬ ٌ ُ‫﴿ َو َ� َدى ﻧ‬
َ ‫ﻮح ﱠرﺑﱠﻪُ ﻓَـ َﻘ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ ْ
َ ‫ٱﳊَﺎﻛﻤ‬
Wanada noohun rabbahu faqala rabbi inna ibnee min ahlee wa-inna waAAdaka
alhaqqu waanta ahkamu alhakimeena

Tafsir: Na akanadi Nuh kwa Mola wake kwa kusema Ya Rabbi! Hakika Mtoto wangu
ni miongoni mwa familia yangu, na kwa hakika ahadi yako ni ya kweli, na wewe ni m-
bora wa kutoa hukmu (Surat Hud 11:45)

Kwa kua Nabii Nuh ni mwenye kujua basi bila ya shaka hakua ni mwenye kumuombea
mtoto wake moja kwa moja, bali alisema tu kua Allah Subhanah wa Taála aliahidi kua
atawaokoa watu wa familia yake, ambapo mtoto wake nae pia ni miongoni mwa watu wa
familia yake, na hivyo Nabii Nuh kamwe hakua ni mwenye kusahau maneno ya Allah
Subhanah wa Ta’ala pale alipomwambia hapo kabla kua:

﴾‫ﻳﻦ ﻇَﻠَ ُﻤ ۤﻮاْ إِﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ ﱡﻣ ْﻐَﺮﻗُﻮ َن‬ ِ‫ِ ِ ﱠ‬


َ ‫﴿ َوﻻَ ُﲣَﺎﻃْﺒ ِﲎ ﰱ ٱﻟﺬ‬
Wala tukhatibnee fee alladheena dhalamoo innahum mughraqoona (Surat Hud
11:37)

Tafsir: Na wala usinihutubie juu ya waliojidhulumu kwani kwa hakika watu hao ni
miongoni mwa watakaogharikishwa.

Hivyo Allah Subhanah wa Taála akaamua kumuwekea wazi Nabii Nuh hali halisi
ilivyokua kwa kumwambia:
196

ِ ِ ‫ﺎل ٰﻳـﻨﻮح إِﻧﱠﻪ ﻟَﻴﺲ ِﻣﻦ أَﻫﻠِﻚ إِﻧﱠﻪ ﻋﻤﻞ َﻏﻴـﺮ‬


‫ﻚ‬
َ َ‫ﺲ ﻟ‬ َ ُ ْ ٌ َ َ ُ َ ْ ْ َ ْ ُ ُ ُ َ َ‫﴿ﻗ‬
َ ‫ﺻﺎﻟ ٍﺢ ﻓَﻼَ ﺗَ ْﺴﺄَﻟْﻨـﻰ َﻣﺎ ﻟَْﻴ‬
ِ ِ ْ ‫َﻋﻈُﻚ أَن ﺗَ ُﻜﻮ َن ِﻣﻦ‬ ۤ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ٱﳉَﺎﻫﻠ‬ َ َ ِ ‫ﺑِِﻪ ِﻋ ْﻠ ٌﻢ إِِّﱐ أ‬
Qala ya noohu innahu laysa min ahlika innahu AAamalun ghayru salihin fala tas-
alni ma laysa laka bihi AAilmun innee aAAidhuka an takoona mina aljahileena
(Surah Hud 11:46)

Tafsir: Akasema: Ya Nuh ama kwa hakika yeye hakuwa miongoni mwa familia yako,
kwani amali zake hazikua njema, hivyo usiniulize mie juu ya kile usichokijua. Ama
kwa Hakika nakuusia ili usiwe miongoni mwa wajinga.

Yaani, udugu wa waja mbele yake yeye Allah Subhanah wa Taála hautegemeani
kutokana na damu inayotiririka ndani ya miili ya watu husika, au vinasaba vyao, au
kuzaliwa pamoja, kulelewa pamoja, n.k, bali hua unategemeana na Imani juu ya Allah
Subhanah wa Taála, na kwa kua watu hawa hawakua ni wenye kumuamini kikamilifu
bali walimuamini pale tu wanapokua mbele yake basi kamwe hawakuweza kua ni
miongoni watu wa familia yake, hivyo haina haja kwa Nabii Nuh kumtaka yeye
abadilishe majaaliwa ya watu ambayo yako nje ya uadilifu wa Allah Subhanah wa Taála.
Hapa sasa Nabii Nuh akaona uhalisi ulivyo na hivyo akasema:

‫ﺲ ِﱃ ﺑِِﻪ ِﻋ ْﻠ ٌﻢ َوإِﻻﱠ ﺗَـ ْﻐ ِﻔْﺮ ِﱃ َوﺗَـْﺮ َﲪِْ ۤﲏ‬ ‫ﻴ‬


َْ‫ﻟ‬ ‫ﺎ‬‫ﻣ‬ ‫ﻚ‬َ ‫ﻟ‬
ََ‫ﺄ‬ ‫َﺳ‬
ْ ‫أ‬ ‫ن‬
ْ َ
‫أ‬ ‫ﻚ‬
َ ِ‫ب إِِّ ۤﱐ أَﻋُﻮذُ ﺑ‬
ِّ ‫ﺎل َر‬
َ َ‫﴿ﻗ‬
َ َ
ِ ْ ‫أَ ُﻛﻦ ِﻣﻦ‬
﴾‫ﺎﺳ ِﺮﻳﻦ‬
َ َ‫ٱﳋ‬ َّ
Qala rabbi innee aAAoodhu bika an as-alaka ma laysa lee bihi AAilmun wa-illa
taghfir lee watarhamnee akun mina alkhasireena (Surat Hud 11:47)

Tafsir: Nuh akasema: Ya Rabbi! Naomba hifadhi yako kutokana na kukuuliza juu ya
kile nisichokua na I’lm nacho. Na kama hukunisamehe, na kua na Rehma name, basi
bila ya shaka nitakua ni miongoni mwa waliokula hasara.


197

UMMAH MPYA WA NABII NUH BAADA YA GHARIKA.



Na Wanasema wenye kujua kua Safina lilisafiri kwa kwanza kuelekea katika maeneo ya
Kusini Magharibi na lilipofika katika maeneo ya Mji wa Makkah kwenye eneo liliopo
sawia na Bayt Al Maamur mbinguni na Al Kaabah ardhini basi likazunguka mara 7, kisha
likaelekea upande wa Magharibi zaid kisha likarudi katika upande wa Mashariki na
baadae likapandisha upande wa Kaskazini.

Baada ya safari hio basi na mda mrefu wa miezi 6 kupita basi Nabii Nuh na watu wake
wakaamriwa kushuka kutoka katika Safina kama inavyoonesha aya inayofuatia ambayo
inasema:-

ِ ٍ ‫﴿ﻗِﻴﻞ ٰﻳـﻨُﻮح ٱﻫﺒِ ْﻂ ﺑِﺴﻼٍَم ِﻣﻨﱠﺎ وﺑﺮَﻛ‬


َ ‫ﻚ َو َﻋﻠَ ٰﻰ أ َُﻣ ٍﻢ ّﳑﱠﻦ ﱠﻣ َﻌ‬
‫ﻚ َوأ َُﻣ ٌﻢ‬ َ ‫ﺎت َﻋﻠَْﻴ‬ ََ ّ َ ْ ُ َ
﴾‫اب أَﻟِﻴﻢ‬ ِ ِ
ٌ ٌ ‫َﺳﻨُ َﻤﺘّﻌُ ُﻬ ْﻢ ﰒُﱠ َﳝَ ﱡﺴ ُﻬ ْﻢ ّﻣﻨﱠﺎ َﻋ َﺬ‬
Qeela ya noohu ihbit bisalamin minna wabarakatin AAalayka waAAala omamin
mimman maAAaka waomamun sanumattiAAuhum thumma yamassuhum minna
AAadhabun aleemun (Surat Hud 11:48)

Tafsir: Na ikasemwa: Ewe Nuh! Shuka huku ukiwa na salama na baraka juu yako
kutoka kwetu, pamoja na Umma wa walio pamoja nawe (na vizazi vyao), Watu ambao
tutawapa raha lakini baadae (watakuja watu wengine) wataonja adhabu kali kutoka
kwetu.

Tumeona kua kulingana na mtizamo wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua
watu waliokuwemo ndani ya Safina walikua ni 80, hivyo mnamo mwezi 10 Muharram
na ndio maana siku hio ya mwezi 10 Muharram ikaitwa siku ya Ashura na katika
kushuka kwao walikua pia ni watu 80 hivyo Nabii Nuh na watu wake hawa waliishi chini
ya Mlima Ararat na kuanzisha kijiji ambacho walikiita Thamanin kwa sababu kila mmoja
miongoni mwao alijengewa nyumba yake na hivyo Nyumba hizo zikawa ziko 80 na hadi
hii leo eneo hilo liliopo nchini Uturuki linaitwa Suk Themanin.

Watu hawa 80 ambao ni pamoja na Nabii Nuh walikaa kwenye Safina kwa miezi 6, kiasi
ya kua macho yao yaliathirika kutokana na kuangalia rangi ya buluu ya maji kwa mda
mrefu sana hivyo Nabii Nuh akawaambia watu wake wafunge katika siku hiyo ya Ashura
na pia wapake wanja machoni, utakaosaidia kusafisha macho yao. Na ndio maana
akasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu A’nhu kua amesema: ‘Rasul Allah
198

Salallahu A’layhi wa Salam kua: ‘Yeyote ule atakaepaka Wanja katika siku ya
Ashura basi hatoumwa na macho’’

Hali hii ya kuathirika kwa macho baada ya kuangalia rangi ya buluu kwa muda mrefu
ikiwemo mwangaza wa simu za mikononi, televisheni na michezo ya computer ambazo
nazo hutoa mawimbi ya mwangaza wa rangi ya buluu, pia imethibitishwa na wanasayansi
wa karne yetu wa Chuo kikuu cha Toledo nchini Marekani kwa kusema kua : ‘Kuangalia
sana mwangaza wa rangi ya buluu kwa mda mrefu kunaathiri macho yetu kwa
kuchangia katika kupunguza nguvu za macho kutokana na kudhurika kwa retina
(kiini cha macho) na hivyo jicho kukosa uwezo wa usambazaji wa madini muhimu
katika kioo cha jicho na kupunguza uwezo wa kuondoa seli na kemikali zisizotakiwa
baada ya kutumika kwake ndani ya jicho’

Ama upande mwengine basi hua tunaona kua watoto wengi wadogo siku hizi hua
ni wenye kuvaa miwani ya macho kwa sababu ya kua na matatizo ya macho,
kutokana na kua ni wenye kukaa sana ndani ya majumba na hivyo kukosa
muangaza wa jua ambako hupelekea kua na ugonjwa uitwao Myopia yaani
maradhi ya kutoona mbali. Na ndio maana Serikali za nchi nyingi za Mashariki ya
Mbali zimekua zikihimiza Wanafunzi wao wa Skuli za primary wawe ni wenye
kutumia mda maalum wa masomo yao wakiwa katika mazingira ya nje ya majengo
ya skuli zao, baada ya kuona kua wengi sana miongoni mwa Wanafunzi wao ni
wenye kuvaa miwani ya macho.

Baada ya kuteremka kutoka kwenye Safina hio basi Nabii Nuh akawaamrisha watu wake
wafunge kwa ajili ya kuonesha Shukran kwa Allah Subhanah wa Ta’ala, na siku hio
waliyofunga ilikua ni siku ya Mwezi 10 Muharram, na hivyo kua ndio asili ya funga ya
siku ya Ashura.

Nabii Nuh na watu wake wakaanza kuishi maisha mapya katika maeneo ya Suk
Themanin. Allah Subhanahu wa Ta’ala anasema katika Qurán kua:

ِ ‫﴿وﻟََﻘ ْﺪ َ� َد َا� ﻧُﻮح ﻓَـﻠَﻨِ ْﻌﻢ ٱﻟْﻤ ِﺠﻴﺒﻮ َن ۞ وﳒَﱠْﻴـﻨَـﻪُ وأ َْﻫﻠَﻪُ ِﻣﻦ ٱﻟْ َﻜﺮ‬
۞ ‫ب اﻟْ َﻌ ِﻈﻴ ِﻢ‬ ْ َ َ َ ُ ُ َ ٌ َ
ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫َو َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ذُِّرﻳـﱠﺘَﻪُ ُﻫ ُﻢ ٱﻟْﺒَﺎﻗ‬
Walaqad nadana Noohun falaniAAma almujeeboona; Wanajjaynahu waahlahu
mina alkarbi alAAadhimi; WajaAAalna dhurriyyatahu humu albaqeena (Surat As-
Saaffaat 37:75-77)
199

Tafsir: Na hakika Nuh alituomba; na sisi ni wabora katika kujibu maombi (dua); Na
tukamuokoa yeye na familia yake kutoka katika maangamizo makubwa; Na kizazi
chake, tukakifanya kuwa miongoni mwa waliobakia.

Naam aya hii ndio iliyomfanya Nabii Nuh kujulikana kwa Jina la Najjiyu Allah ambalo
ni jina linalotokana na neno Naja la Kiarabu ambalo maana yake hua ni Alieokolewa,
Aliefikishwa salama, Aliekimbizwa, Aliechiwa Huru, Anaepewa Siri au Msiri
ambae hua ni mwenye kujadiliana mambo ya siri baina yake na mwenye Siri. Hivyo
Nabii Nuh alipewa Jina hili kwa sababu alikua ni mwenye kujadiliana na Allah Subhanah
wa Taála na pia alikua ni aliokolewa na Allah Subhanah wa Taála.

Vile vile Allah Subhanah wa Taála anaendelea kutujuulisha juu ya kuiwacha Safina hio
kua kama kumbukumbu na uthibitisho kwa waja wake pale aliposema:

﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ِ ِ
َ ‫ـﺐ ٱﻟ ﱠﺴﻔﻴﻨَﺔ َو َﺟ َﻌ ْﻠﻨَ َـﻬﺂ ءَاﻳَﺔً ﻟّْﻠ َﻌـﻠَﻤ‬
َ ‫َﺻ َﺤ‬
ْ ‫﴿ﻓﺄ َْﳒَْﻴﻨـﻪُ وأ‬
Faanjaynahu waas-haba alssafeenati wajaAAalnaha ayatan lilAAalameena (Surat
An Qaboot 29:15)

Tafsir: Kisha tukamuokoa yeye na wale waliokuwemo pamoja nae ndani ya Safina na
tukaifanya Safina hiyo kua ni dalili kwa Ulimwengu.

Yaani uthibitisho kwa waja wake juu ya ukweli na mafunzo yaliyomo katika kisa cha
Nabii Nuh na pia kua kama dalili kwa Wasioamini juu ya yanayowafika wale
wanaomuasi Allah Subhanah wa Taála.

Na haya yanatiliwa mkazo umuhimu wake pale tunapoiangalia Surat Al Israa ambayo
ina aya zenye mchanganyiko uliopangika vizuri na wa kupendeza wa maelekezo,
maamrisho na dharuba kali zenye kuonya kwa wenye kuzingatia na kutafakkari. Kwani
mbali ya kua Sura hio iliteremshwa katika kipindi cha baada ya Safari ya Isra na Miraj
tukio ambalo lilitokea kabla ya Hijra ya Rasul Allah Salalahu Alayhi wa Salam kuelekea
Madina. Lakini pia Surat Al Israa ilikua ni yenye Kuamwaamrisha Waislam na kuwapa
Maelekezo juu ya Mambo mbali mbali na hapo hapo ni yenye Kuwaonya Makafiri wa
Makkah kua wajifunze kutokana na yaliyowakuta watu waliotangulia kabla yao.

Na ndio maana Sura hio kwanza inaanza na Utukufu wa Allah Subhanah wa Ta'ala, na
Uwezo wake juu ya Kila kuweka wazi Kua yeye ndie alimsafirisha Mtume wake
Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam kutoka Makka hadi Jerusalem na kisha
kumpandisha Mbinguni na Kumrudisha duniani baada ya kumfaradhishia Sala 5 kwa ajili
ya Ummat Muhammad na kisha kumrudisha Makka katika mda wa Mfupi sana. Kisha
200

aya 2 inayofuatia ya Sura hio inaelezea Maisha ya Nabii Musa na Watu watu wake wa
Bani Israil na namna alivyokua akiwausia, na kisha aya ya 3 ikamzungumzia Nabii Nuh
na namna alivyoingizwa kwenye Rehma za Mola wake yeye pamoja na Watu watu kama
zinavyoonesha aya zifuatazo:

﴾‫اﻪﻠﻟِ اﻟﱠﺮ ْﲪَـ ِﻦ اﻟﱠﺮِﺣﻴ ِﻢ‬


‫﴿ﺑِ ْﺴ ِﻢ ﱠ‬
ِِ ِ ْ ‫﴿ﺳْﺒﺤﺎ َن ٱﻟﱠ ِﺬى أَﺳﺮ ٰى ﺑِﻌْﺒ ِﺪﻩِ ﻟَْﻴﻼً ِﻣﻦ ٱﻟْﻤﺴ ِﺠ ِﺪ‬
‫ﺼﻰ‬َ ْ‫ٱﳊََﺮام إِ َ ٰﱃ ٱﻟْ َﻤ ْﺴﺠﺪ ٱﻷَﻗ‬ ْ َ َّ َ َْ َ ُ
ِ ِ ِ ِ ‫ٱﻟﱠ ِﺬى ﺎﺑرْﻛﻨَﺎ ﺣﻮﻟَﻪُ ﻟِﻨُ ِﺮﻳﻪُ ِﻣﻦ‬
‫ﻮﺳﻰ‬َ ‫ﻴﻊ ٱﻟﺒَﺼﲑُ۞ َوآﺗَـْﻴـﻨَﺂ ُﻣ‬ُ ‫آ�ﺗﻨَﺂ إﻧﱠﻪُ ُﻫ َﻮ ٱﻟ ﱠﺴﻤ‬
َ ْ َ َْ ََ
ِ ‫ٱﻟْ ِﻜﺘَﺎب وﺟﻌ ْﻠﻨَﺎﻩ ﻫ ًﺪى ﻟِّﺒ ِﲎ إِﺳﺮاﺋِﻴﻞ أَﻻﱠ ﺗَـﺘ‬
‫ﱠﺨ ُﺬواْ ِﻣﻦ ُد ِوﱏ َوﻛِﻴﻼً ۞ ذُِّرﻳﱠﺔَ َﻣ ْﻦ‬ َ َْ َ ُ ُ َ َ َ َ
﴾ً‫ﻮح إِﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن َﻋْﺒﺪاً َﺷ ُﻜﻮرا‬
ٍ ُ‫َﲪَْﻠﻨَﺎ َﻣ َﻊ ﻧ‬
Subhana alladhee asra biAAabdihi laylan mina almasjidi alharami ila almasjidi al-
aqsa alladhee barakna hawlahu linuriyahu min ayatina innahu huwa alssameeAAu
albaseeru; Waatayna moosa alkitaba wajaAAalnahu hudan libanee isra-eela alla
tattakhithoo min doonee wakeelan; Dhurriyyata man hamalna maAAa noohin
innahu kana AAabdan shakooran (Surat Al Israa 17:1-3)

Tafsir: Ametukuka yule ambae aliemsafirisha katika wakati wa Usiku Mja wake
kutoka katika Masjid Al Haram hadi masjid Al Aqsa ambao ni Mazingra yake ni yenye
kubarikiwa, kwa ajili ya kumuonesha dalili zetu, Hakika yeye (Allah Subhanah wa
Ta’ala) ni mwingi wa kusikia na ni mwenye kuona kila kitu. Na tukampa Musa Kitabu,
na kukifanya kua ni muongozo kwa watu wa Bani Israil (Tukisema): ‘Msimfanye
mwengine yeyote kua ni Msimamizi wenu’. Na Kizazi Cha Wale Tuliowabeba (Ndani
ya Safina) pamoja na Nuh, bila ya Shaka yeye alikua ni Mja mwenye Shukrani.

Hivyo aya hii inatuwekea wazi kua waliompinga Nabii Nuh walikua ni waliokufuru na
Waliomfuata Nabii Nuh walikua ni mfano wa kuigwa, hivyo hapa watu wanaonywa na
pia Kuusiwa kua Wafuate nyayo za Nabii Nuh kwani kwa hakika yeye Nabii Nuh alikua
ni Mja mwenye Shukurani mbele ya Mola wake.

Naam...aya hii inausia hivi kwa sababu ukweli ni kua Nabii Nuh alikua ni Muanzilishi
wa Ummah mpya uliotokana na kizazi kilichobakia ndani ya Safina lake kama ilivyosema
Surat Hud 11:48 yaani baada ya kile kilichoanzia kwa Nabii Adam hadi kwa Nabii Idris
201

kuteketea chote katika gharika ya mafuriko yaliyoifunika Ardhi yote ya Dunia nzima bila
ya kubakisha kitu chochote isipokua Safina na kila kilichomo ndani ya Safina yake.

Ama kuhusiana na mke wa Nabii Nuh ambae alieongoka na kua ni mwenye kumuamini
Allah Subhanah wa Ta'ala na hivyo kua ni mwenye kuingia ndani ya Safina pamoja na
Nabii Nuh basi kuna wasemao kua alikua akiitwa Amura na pia kuna wasemao kua alikua
akiitwa Haikal.

Ama kwa upande mwengine basi anasema Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi
Allahu Anhu kua: ‘Siku moja Ibilis aliamfuata Nabii Nuh na kumwambia kua: ‘Ya
Najiyu Allahi Nuh hakika mimi nina deni kubwa sana kwako wewe, kwani kwa
hakika wewe umenisaidia mimi sana na hivyo kua ni mwenye kunirahisishia kazi
yangu.’’

Nabii Nuh akamuuliza Iblis ‘Nimekurahisishia vipi mie wewe kazi yako?’

Ibilisi akajibu: ‘Hakika wewe umenirahisishia mimi kazi yangu ya kuwapotoa watu
wako, kwa sababu uliwalaani na hivyo nao wakaangamia moja kwa moja hadi
motoni, hivyo umenirahisishia mie kwa kunipunguzia Mashakil ya kuwashawishi
watu wako wapotoke ili waingie Motoni.’

Ibilisi akaendelea kusema: ‘Kwa hivyo ni wajibu wangu mimi kukulipa wewe
kutokana na kunisadia kwako huko kazi yangu. Hivyo nami nakusaidia kwa kuusia
juu ya sifa mbili zenye kuangamiza ambazo ewe Najjiyu Allah Inabidi ujitenge nazo
ambazo ni:-’

1- Choyo, Ewe Najjiyu Allah usimuonee Choyo au Wivu mwenzako kwa neema
aliyojaaliwa kua nayo kutokana na kupewa na Mola wake. Kwani kwa
hakika mimi nilikua m-bora sana lakini Wivu ndio ulioniponza na hivyo
kunisababishia kua na hali mbaya katika siku ya Malipo’
2- Ubakhili, Ewe Najiyyu Allah usiwe na ubakhili kwani Adam alifikwa na
aliyofikwa wakati alipokua Peponi kwa sababu ya kua na Ubakhili na hivyo
matokeo yake akashushwa Ulimwengu.

Hapa kama tunavyoona ni kua sifa ya mwanzo aliyoitaja Ibilisi ambayo tunatakiwa
kuachana nayo ni choyo au wivu na bila ya shaka kila kitu kiko wazi kwani Ibilis
alimuonea wivu Nabii Adam na hivyo alipoamrishwa yeye na kiumbe Malaika
wamsujudie basi Ibilisi akakataa kumsujudia kwani bainaya viumbe vitatu hivyo vyenye
hadhi alivyoviumba Allah Subhanah wa Ta’ala, yaani Malaika, Majini na Watu, basi wa
kwanza kuumbwa na Allah Subhanahu wa Ta’ala walikua ni Malaika ambao waliumbwa
202

katika siku ya Jumatano, na miaka baadae wakaumbwa Majini lakini katika siku ya Al
Khamis na pia miaka baadae akaumbwa Adam na pia katika siku ya Ijumaa, na kati ya
viumbe vyote, Adam alikua ni kiumbe bora mwenye hadhi ya juu zaid miongoni mwao,
hivyo ulipofika wakati wa kuumbwa kwake Allah Subhanahu wa Ta’ala aliwaambia
viumbe hao waliomtangulia katika kuumbwa kwa kusema kama inavyosema Qur’an:

‫َﲡ َﻌ ُﻞ ﻓِ َﻴﻬﺎ َﻣﻦ‬ ِ ِ ‫ﺎﻋﻞ ِﰱ ٱﻷَر‬


َْ ‫ض َﺧﻠﻴ َﻔﺔً ﻗَﺎﻟُﻮاْ أ‬ ْ
ِ ‫ﻚ ﻟِْﻠﻤﻠَـﺌِ َﻜ ِﺔ إِِﱐ ﺟ‬
ٌ َ ّ َ َ‫﴿وإِ ْذ ﻗ‬
َ َ ‫ﺎل َرﺑﱡ‬ َ
‫ﺎل إِِّ ۤﱐ أ َْﻋﻠَ ُﻢ َﻣﺎ‬
َ َ‫ﻚ ﻗ‬ َ َ‫س ﻟ‬
ِ ِ ِ ِ ِ ‫ﻳـ ْﻔ ِﺴ ُﺪ ﻓِﻴﻬﺎ وﻳﺴ ِﻔ‬
ُ ‫ﻚ ٱﻟ ّﺪ َﻣﺂءَ َوَْﳓ ُﻦ ﻧُ َﺴﺒّ ُﺢ ﲝَ ْﻤﺪ َك َوﻧـُ َﻘ ّﺪ‬
ُ ْ ََ َ ُ
﴾‫ﻻَ ﺗَـ ْﻌﻠَ ُﻤﻮ َن‬
Wa-idh qala rabbuka lilmala-ikati innee jaAAilun fee al-Ardhi khaleefatan qaloo
atajAAalu feeha man yufsidu feeha wayasfiku alddimaa wanahnu nusabbihu
bihamdika wanuqaddisu laka qala innee aAAlamu mala taAAlamoona (Surat Al
Baqara 2:30)

Tafsir: Na kumbuka wakati Mola wako aliposema kuwaambia Malaika: ‘Hakika mimi
nitajaalia Khalifah katika Ardhi kizazi baada ya kizazi’, nao wakasema ‘Utajaalia wale
ambao watafanya ufisadi na kumwaga damu ndani yake?, wakati sisi tunakusifu kwa
sifa zako, tunakushukuru na kukutukuza’ Allah akasema : ‘Mimi nnajua kile
msichokijua’

Anasema Imam Fakhr ad Din Al Razi kua: ‘Kauli ya Malaika ya kusema kua ‘Utajaalia
wale ambao watafanya ufisadi na kumwaga damu ndani yake?, wakati sisi tunakusifu
kwa sifa zako na kukushukuru na kukutuza’ ilikua ni kama maombi kutoka kwao
kua haina haja ya kuumbwa viumbe wengine kwani wao wanaweza kukaa pia
Duniani na kuendelea kumtukuza Allah Subhanah wa Ta’ala, lakini hata hivyo
Allah Subhanahu wa Ta’ala akawaambia, ‘Mimi nnajua kile msichokijua’,
akimaanisha kua Allah Subhanahu wa Ta’ala anajua vizuri zaidi ni lipi bora kwao
wao Malaika, baina ya kukaa Duniani ama Mbinguni.’

Kisha Allah Subhanahu wa Ta’ala akasema katika Qur’an:

‫ﺂء َﻫ ُـﺆﻻَِء‬ ِ ‫ﺎل أَﻧْﺒِﺌ ِﻮﱏ ِﺄﺑ َْﲰ‬


َ ُ َ ‫ﺿ ُﻬ ْﻢ َﻋﻠَﻰ اﻟْ َﻤﻠَـﺌِ َﻜ ِﺔ ﻓَـ َﻘ‬ ْ ‫﴿و َﻋﻠﱠ َﻢ ءَ َاد َم اﻷ‬
َ ‫َﲰَﺂءَ ُﻛﻠﱠ َﻬﺎ ﰒُﱠ َﻋَﺮ‬ َ
‫َﻧﺖ ٱﻟْ َﻌﻠِ ُﻴﻢ‬
َ ‫ﻚأ‬ َ ‫ﻚ ﻻَ ِﻋ ْﻠ َﻢ ﻟَﻨَﺂ إِﻻﱠ َﻣﺎ َﻋﻠﱠ ْﻤﺘَـﻨَﺂ إِﻧﱠ‬
َ َ‫ﲔ ۞ ﻗَﺎﻟُﻮاْ ُﺳْﺒ َﺤـﻨ‬
ِ ِ ‫إِن ُﻛﻨﺘﻢ‬
َ ‫ﺻـﺪﻗ‬َ ُْ
203

َ َ‫ﺎل ﻳَـﺎءَ َاد ُم أَﻧﺒِْﺌـ ُﻬﻢ ِﺄﺑ َْﲰَﺂﺋِ ِﻬ ْﻢ ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺂ أَﻧْـﺒَﺄ َُﻫ ْﻢ ِﺄﺑَ ْﲰَﺂﺋِ ِﻬﻢ ﻗ‬
‫ﺎل أَﻗُ ْﻞ ﻟﱠ ُﻜ ْﻢ إِِّﱐ‬ َ َ‫ٱﳊَ ِﻜ ُﻴﻢ ۞ ﻗ‬
ْ
﴾‫ض َوأ َْﻋﻠَ ُﻢ َﻣﺎ ﺗُـْﺒ ُﺪو َن َوَﻣﺎ ُﻛﻨﺘُ ْﻢ ﺗَ ْﻜﺘُ ُﻤﻮ َن‬ ِ ‫ات َوٱﻷ َْر‬ ِ ‫أَﻋﻠَﻢ َﻏﻴﺐ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬
ََ َْ ُْ
WaAAallama adama al-asmaa kullaha thumma AAaradahum AAala almala-ikati
faqala anbi-oonee bi-asma-i haola-i in kuntum sadiqeena; Qaloo subhanaka la
AAilma lana illa ma AAallamtana innaka anta alAAaleemu alhakeemu; Qala ya
adamu anbi/hum bi-asma-ihim falamma anbaahum bi-asma-ihim qala alam aqul
lakum innee aAAlamu ghayba alssamawati waal-Ardhi waaAAlamu ma tubdoona
wama kuntum taktumoona; (Surat Al Baqara 2:31-33)

Tafsir: Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, Kisha akavionesha vitu hivyo
kwa Malaika, na kuwaambia ‘Nitajieni majina ya vitu hivi ikiwa nyinyi ni wakweli’,
Wao (Malaika) wakasema: ‘Utukufu ni wako, Sisi hatuna I’lm isipokua ya kile
ulichotufundisha, hakika wewe ni mjuzi wa kila kitu na mwingi busara’. (Allah)
Akasema: ‘Ewe Adam watajie majina yake’, na alipowatajia majina ya vitu hivyo
(Allah akasema): ‘Jee sikukwambieni kua mimi najua mambo ya Ghayb
(yaliyofichika) mbinguni na ardhini, na nnajua kile mnachokiweka wazi na kile
mnachokificha’.

Hivyo Adam akafundiswa majina ya vitu vyote vilivyopo mbele yake yeye na viumbe
hivyo vyengine, kisha akaviuliza viumbe vyengine majina ya vitu hivyo, nao
wakashindwa kuvijua, Allah Subhanahu wa Ta’ala akamuuliza Adam ambae nae akataja
majina ya vitu hivyo, baada ya kutaja majina ya vitu hivyo Malaika wakajua kua Adam
yuko juu zaid yao ki I’lm na kiheshima, hivyo Allah Subhanahu wa Ta’ala akawaamrisha
kwa pamoja wote Malaika na Iblis waliopo mbele yake kumsujudia Adam.

‫َﰉ َوٱ ْﺳﺘَ ْﻜﺒَـَﺮ َوَﻛﺎ َن ِﻣ َﻦ‬


ٰ َ ‫ﻴﺲ أ‬ِ‫﴿وإِ ْذ ﻗُـ ْﻠﻨﺎ ﻟِْﻠﻤﻠَـﺌِ َﻜ ِﺔ ٱﺳﺠ ُﺪواْ ﻻًّدم ﻓَﺴﺠ ُﺪواْ إِﻻﱠ إِﺑﻠ‬
َ ْ َ َ ََ ُْ َ َ َ
﴾‫ﻳﻦ‬ ِ
‫ﺮ‬ ِ‫ٱﻟْ َﻜﺎﻓ‬
َ
Wa-idh qulna lilmala-ikati osjudoo li-adama fasajadoo illa ibleesa aba waistakbara
wakana mina alkafireena (Surat Al Baqara 2:34)

Tafsir: Na (Kumbuka) wakati tulipowaambia Malaika: ‘Msujudieni Adam’. Na


wakasjudu isipokua Iblis, akakataa na kua na kibri, na akawa ni miongoni mwa
waliokufuru.
204

Hikma iliyomo katika tokeo hili ni kuwaonesha Malaika na Iblis kua darja ya Adam iko
juu kuliko darja yao, kumuonesha Adam kua yeye ni kiumbe bora zaid kuliko viumbe
wawili hao, na pia kumuwekea wazi Adam kua Iblis ni Adui yake mkubwa ambae
aliekataa kua chini yake.

Ingawa Malaika na Iblis walipewa amri inayotakiwa kutekelezwa lakini Iblis alikataa
kuitii amri hiyo, si kutokana na kua yeye hakua Malaika, kwa sababu ingawa kweli
hakuwa miongoni mwa Malaika, lakini amri iliyotolewa ilikua ni ya jumla kwa wote
waliokuwepo sehemu hiyo, nae alijumuishwa katika amrisho hilo kutokana na kua nao
pamoja Malaika katika kujaribu kujipadisha darja yake, kujifananisha na kuwaiga
Malaika na kujumuika nao katika kila amali waifanyayo.

Lakini ukweli unarudi pale pale kua kwa sababu Iblis ni baba wa Majini, ambao ni
viumbe tofauti na Malaika, na moja kati ya sifa za Jini ni kua na hiari katika maamuzi
kama walivyo viumbe Bani Adam, basi hiari yake ikampa kibr na akajiona kua yeye ni
bora kuliko Adam na pia akawa ni mwenye kuona wivu, kwa nini yeye ameumbwa
mwanzo na ameshafanya ibada sana kisha Allah Subhnah wa Ta’ala ampe darja kiumbe
Ibn Adam ambae yeye anamjua ndani nje kwani alikua anamuona tangu wakati alipokua
akiumbwa.

Kwa upande mwengine basi Allah Subhanahu wa Ta’ala anaweka wazi darja aliyowapa
viumbe Bani Adam, kwa kuwapa uwezo wa kutumia kila kitu alichokiumba
Ulimwenguni, kuanzia Ardhi, Bahari, Hewa, Mbingu, Jua, Mwezi, Nyota n,k kwa ajili
ya manufaa yake, kama vile anavyosema katika Qur’an:

‫ﻀ ْﻠﻨَ ُـﻬ ْﻢ‬ ِ ‫﴿وﻟََﻘ ْﺪ َﻛﱠﺮﻣﻨَﺎ ﺑ ِﲎ ءادم و َﲪ ْﻠﻨَـﻬﻢ ِﰱ ٱﻟْﺒـ ِﺮ وٱﻟْﺒﺤ ِﺮ ورَزﻗْـﻨَـﻬﻢ ِﻣﻦ اﻟﻄﱠﻴِﺒ‬
‫ـﺖ َوﻓَ ﱠ‬َّ َ ْ ُ َ َ ْ َ َ ّ َ ْ ُ َ َ َ َ َ َ ْ َ
﴾ً‫ﻀﻴﻼ‬ ِ ‫ﻋﻠَﻰ َﻛﺜِ ٍﲑ ِّﳑﱠﻦ ﺧﻠَ ْﻘﻨَﺎ ﺗَـ ْﻔ‬
َ ْ َ
Walaqad karramna banee adama wahamalnahum fee albarri waalbahri
warazaqnahum mina alttayyibati wafadhalnahum AAala kathirin mimman
khalaqna tafdhilan (Surat Al Israa, 17:70)

Tafsir: Na kwa hakika tumemkirim Bani Adam, na tukawachukua na kuwaweka juu


ya Ardhi na juu ya bahari, na kuwajaalia kila kilicho kizuri na kilicho halali, na
tumewapendelea wao na kuwaweka juu kwa tofauti kubwa kulingana na viumbe wengi
tuliowaumba.

Na vile vile akasema tena:


205

ٍ �‫ﻚ ﻵ‬ِ ِ ِ ِ ِ ‫ات وﻣﺎ ِﰱ ْاﻷَر‬ ِ


‫ت‬ َ َ ‫ض َﲨﻴﻌﺎً ّﻣْﻨﻪُ إ ﱠن ِﰱ َذﻟ‬ ْ َ َ ‫﴿و َﺳ ﱠﺨَﺮ ﻟَ ُﻜ ْﻢ ﱠﻣﺎ ِﰱ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤ َﺎو‬
َ
﴾‫ﻟَِّﻘ ْﻮٍم ﻳَـﺘَـ َﻔ ﱠﻜُﺮو َن‬
Wasakhkhara lakum ma fee alssamawati wama fee al-Ardhi jameeAAan minhu
inna fee dhalika laayatin liqawmin yatafakkaroona (Surat Al Jathiyah, 45:13)

Tafsir: Na akaviweka chini yako kila kilichomo mbiguni na ardhini: Yote haya ni
kukupendeleeni kuotokana na ukarimu wake. Hakika katika haya kuna mafunzo
ndani yake kwa wale wenye kutafakkari.

Ama kuhusiana na Ubakhili, basi kwanza inabidi pia tukumbushane juu ya kilichoendelea
baada ya kuumbwa Nabii Adam ambapo tunaona kua anasema Allah Subhanah wa
Ta’ala:

َ‫ﺚ ِﺷْﺌـﺘُ َﻤﺎ َوﻻ‬


ُ ‫ﻚ ٱ ْﳉَﻨﱠﺔَ َوُﻛﻼَ ِﻣْﻨـ َﻬﺎ َر َﻏﺪاً َﺣْﻴ‬ َ ْ‫ٱﺳ ُﻜ ْﻦ أَﻧ‬
َ ‫ﺖ َوَزْو ُﺟ‬ ْ ‫آد ُم‬
َ �َ ‫﴿ َوﻗُـ ْﻠﻨَﺎ‬
ِِ ِ َ ‫ﺗَـ ْﻘﺮﺎﺑ ﻫـٰ ِﺬﻩِ ٱﻟﺸﱠﺠﺮَة ﻓَـﺘَ ُﻜ‬
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ﻮ� ﻣ َﻦ ٱﻟْﻈﱠﺎﻟﻤ‬ ََ َ ََ
Waqulna ya adamu oskun anta wazawjuka aljannata wakula minha raghadan
haythu shi/tuma wala taqraba hadhihi alshshajarata fatakoona mina
aldhdhalimeena. (Surat Al Baqara 2:35)

Tafsir: Na tukasema: ‘Ewe Adam, Kaa wewe na mke wako Peponi na kuleni kila kitu
kwa uhuru na raha mtakavyoridhika na vitu vilivyomo ndani yake popote pale
mtakapo, lakini msiukaribie mti huu kwani nyote mtakua ni miongoni mwa
waliojidhulumu.’

Tunapoyaangalia maumbile ya Nafsi ya Adam basi tunaona kua imeumbwa na kugawika


katika sehemu tatu, sehemu ya kwanza ni ile ijulikanayo kua ni Nafsi ya Matamanio
(Nafs-as-shahwaniyyah) ambayo huishawishi Nafsi kutamani kile inachokiona ni kizuri
kwake. Hali ya Nafsi ambayo ambayo iliwapelekea Adam na Hawa kua na hamu ya kula
tunda, tunda ambalo lenye ufunguo wa kusitisha hali waliyokua nayo viumbe Adam na
Hawa ya kutokua na uwezo wa kua na kifo.

Tunda hilo lilikua ni la kusitisha mfumo wa uhai wa maisha ya Peponi na kuanzisha


mfumo wa uhai wa maisha ya Duniani, kwani Adam na Hawa walikua tayari wanaishi
206

katika mfumo wa uhai wa Peponi ambao una kila kilicho bora, uhai ambao hauna
kuchoka wala kulala, hauna kuziona sehemu zao za siri na hivyo hauna kujisaidia,
kuingiliana na kuzaana wala hauna kifo na hivyo hawezi kua Khalifah wa Ardhini.

Lakini ni lazima kwanza tukumbuke kua Adam aliumbwa ili awe Khalifah Ardhini, na
hawezi kuutumikia wadhifa huo hadi pale atakapoitumia sehemu ya kwanza ambayo ni
ya Nafs-as-shahwaniyyah itakayo mpelekea kutoka Peponi na kushushwa Duniani
ambako atakua na uwezo wa kuzitumia sehemu mbili za Nafsi yake zilizobakia ambazo
ni (Nafs al Jinsiyyah) ambayo ni Nafsi ya matamanio ya kuingiliana kijinsia na kufanya
mapenzi na Hawa ili kujisikia raha na utulivu na pia kupata watoto na hivyo kuijaza
Dunia na kizazi cha Bani Adam ambao watakua tayari kuitumia sehemu ya tatu ya Nafsi
ijulikanayo kama (Nafs ash Shaitara) ambayo ni Nafsi ya kutamani kua Khalifah Ardhini.

Jukumu la kuwashawishi na hivyo kushindwa kujizuia na kuweza kuitumia Nafs-as-


shahwaniyyah lilikua ni la adui yao mkuu ambae alieapa kuwapotosha Bani Adam wote.
Yaani Iblis ambae nae alifanya kila juhudi hadi akafanikiwa kuwashawishi wote Adam
na Hawa kulitamani na kulila tunda hilo walilokatazwa hata kulikaribia na hivyo
wakamuasi Allah Subhanahu wa Ta’ala na kua ni miongoni mwa waliokula hasara.
Kwani baada ya kula tunda hilo tu Adam na Hawa wote kwa pamoja ikawa tayari
wameshaitumia sehemu ya kwanza ya hali ya Nafsi ya kusitisha iitwayo Nafs-as-
shahwaniyyah.

Hivyo ikabidi maumbile yao yasitishe hali ya mfumo wa kuishi maisha ya Peponi, na
kuhamia katika hali ya pili ambayo ni ya kuanzisha hali ya mfumo wa kuishi maisha ya
Duniani na hapo ndio wakaanza kuona vile walivyokua hawavioni na hawavijui kabla
yake. Kwani kabla yake walikua katika hali ya matamanio ya kula, kulala na kua Khalifah
wa viumbe vyote, lakini sasa hivi wakawa katika hali ya Bani Adam ambao ndani yake
kuna hali ya asili ya Adam, na Bani Adam hua hawezi kuiona hali yake halisi kwa
kutumia macho yake bali huweza kuiona pale atakapojiangalia kutokana na jicho la ndani
ya Nafsi yake. Hivyo Adam na Hawa ikawabidi wajijue kupitia katika hali ya Bani Adam
kwa ajili ya kuendelezea maisha yao wao na ya vizazi vyao ulimwenguni na pia
kutekeleza majukumu ya Amanah walioichukua.

Tunapoangalia katika Qur’an kuhusiana na tokeo hili basi tunaona kua, Qur’an kamwe
haikubagua baina ya Adam na Hawa kwa kusema ni nani alieanza kula tunda
lililokatazwa, na badala yake imewajumuisha Adam na Hawa wote kwa pamoja na kwa
wakati mmoja. Allah Subhanahu wa Ta’ala anatuelezea katika Surat Al A’raf pale
aliposema:
207

َ َ‫ي َﻋْﻨـ ُﻬ َﻤﺎ ِﻣﻦ َﺳ ْﻮءَاﻬﺗِِ َﻤﺎ َوﻗ‬


‫ﺎل َﻣﺎ‬ ِ
َ ‫ي َﳍَُﻤﺎ َﻣﺎ ُوور‬
ِ ِ
َ ‫س َﳍَُﻤﺎ ٱﻟﺸْﱠﻴﻄَﺎ ُن ﻟﻴُـْﺒﺪ‬
َ ‫﴿ﻓَـ َﻮ ْﺳ َﻮ‬
۞‫ﻳﻦ‬ ِ ِ‫ﻮ� ِﻣﻦ ٱ ْﳋﺎﻟ‬
‫ﺪ‬ َ ‫ﻜ‬
ُ ‫ﺗ‬
َ ‫َو‬‫أ‬ ِ
‫ﲔ‬ ‫ﻜ‬
َ ‫ﻠ‬
َ ‫ﻣ‬ �‫ﻮ‬
َ ‫ﻜ‬ُ ‫ﺗ‬
َ ‫َن‬‫أ‬ ‫ﻻ‬
َ ِ‫ﻧَـ َﻬـ ُﻜﻤﺎ رﺑﱡ ُﻜﻤﺎ َﻋﻦ َﻫ ِـﺬﻩِ ٱﻟﺸﱠﺠﺮةِ إ‬
َ َ َ ْ ْ َ ََ ْ َ َ َ
ِِ ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ﺎﲰَ ُﻬ َﻤﺂ إِِّﱐ ﻟَ ُﻜ َﻤﺎ ﻟَﻤ َﻦ ٱﻟﻨﱠﺎﺻﺤ‬ َ َ‫َوﻗ‬
Fawaswasa lahuma alshshaytanu liyubdiya lahuma ma wooriya AAanhuma min
saw-atihima waqala ma nahakuma rabbukuma AAan hadhihi alshshajarati illa an
takoona malakayni aw takoona mina alkhalideena; Waqasamahuma innee lakuma
lamina alnnasiheena; (Surat Al A’raf 7:20-21)

Tafsir: Kisha Shaytan akawatia wasi wasi juu yao wote wawili (kwa kuwashawishi
katika Nafsi zao) ili kufichua kile kilichofichwa hapo kabla kutoka kwao katika
sehemu zao za siri; akasema: ‘Mola wenu hakukukatazeni mti huu isipokua mtakua
Malaika au mtakaoishi milele (bila ya kifo); Na yeye (Shaytan) akawaapia wao wote
kwa Allah: ‘Hakika mimi ni mwenye kukunasihieni nyinyi mema’’

ِ ‫ﺼ َﻔ‬ ِ ْ‫ت َﳍﻤﺎ ﺳﻮءﺗُـﻬﻤﺎ وﻃَِﻔ َﻘﺎ َﳜ‬ ِ


‫ﺎن‬ َ َ ُ َ ْ َ َُ ْ ‫ﱠﺠَﺮَة ﺑَ َﺪ‬ َ ‫﴿ﻓَ َﺪﻟﱠ ُـﻬ َﻤﺎ ﺑﻐُُﺮوٍر ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ َذاﻗَﺎ ٱﻟﺸ‬
‫ﱠﺠَﺮةِ َوأَﻗُﻞ‬ ِ ِ ْ ‫ﻋﻠَﻴ ِﻬﻤﺎ ِﻣﻦ ورِق‬
َ ‫ٱﳉَﻨﱠﺔ َو َ� َد ُاﳘَﺎ َرﺑـﱡ ُﻬ َﻤﺂ أََﱂْ أَﻧْـ َﻬ ُﻜ َﻤﺎ َﻋﻦ ﺗ ْﻠ ُﻜ َﻤﺎ ٱﻟﺸ‬ ََ َ َْ
‫ﲔ ۞ ﻗَﺎﻻَ َرﺑـﱠﻨَﺎ ﻇَﻠَ ْﻤﻨَﺂ أَﻧ ُﻔ َﺴﻨَﺎ َوإِن ﱠﱂْ ﺗَـ ْﻐ ِﻔْﺮ ﻟَﻨَﺎ‬ ٌ ِ‫ﻟﱠ ُﻜ َﻤﺂ إِ ﱠن اﻟﺸْﱠﻴﻄَ َـﻦ ﻟَ ُﻜ َﻤﺎ َﻋ ُﺪ ﱞو ﱡﻣﺒ‬
ِ ْ ‫وﺗَـﺮ َﲪﻨَﺎ ﻟَﻨَ ُﻜﻮﻧَ ﱠﻦ ِﻣﻦ‬
﴾‫ﻳﻦ‬ َ ‫ٱﳋَﺎﺳ ِﺮ‬ َ ْ َْ
Fadallahuma bighuroorin falamma dhaqa alshshajarata badat lahuma saw-
atuhuma watafiqa yakhsifani AAalayhima min waraqi aljannati wanadahuma
rabbuhuma alam anhakuma AAan tilkuma alshshajarati waaqul lakuma inna
alshshaytana lakuma AAaduwwun mubeenun; Qala rabbana dhalamna anfusana
wa-in lam taghfir lana watarhamna lanakoonanna mina alkhasireena (Surat Al A’raf
7:22-23)

Tafsir: Hivyo akawapotosha wote kwa kuwalaghai. Na walipoonja yaliyokuwemo


katika mti huo, kile kilichofichika kwa kua ni aibu (uchi) kwao, kikawa ni chenye
kuonekana kwao wao na hivyo wakaanza kujificha kwa kutumia majani ya Peponi.
Na Mola wao akawaita (kwa kuwaambia): ‘Jee sikukukatazeni mimi mti huu?, na
kukuambieni: Hakika Shaytani ni adui alie dhahiri kwenu?’; Hivyo wao wakasema:
208

‘Ya Rabb! Hakika sisi tumejidhulumu Nafsi zetu. Na ikiwa hutotusamehe, na


kutuingiza katika Rehma zako, basi kwa hakika tutakua ni miongoni mwa wenye kula
hasara.’

Kisha aya zikaendelea kwa kusema:

ٍ ‫ض ُﻣﺴﺘَـ َﻘﱞﺮ وَﻣﺘَ ٌـﻊ إِ َ ٰﱃ ِﺣ‬


۞‫ﲔ‬ ِ ‫َر‬ ‫اﻷ‬ ‫ﰱ‬ ِ ‫ﺾ َﻋ ُﺪ ﱞو وﻟَ ُﻜﻢ‬ ٍ ‫ﻌ‬ ‫ـ‬‫ﺒ‬ِ‫ﺎل ٱﻫﺒِﻄُﻮاْ ﺑـﻌﻀ ُﻜﻢ ﻟ‬
َ ْ ْ ْ ْ َ ْ َ ْ ُ ْ َ ْ َ َ‫﴿ﻗ‬
﴾‫ﺎل ﻓِ َﻴﻬﺎ َْﲢﻴَـ ْﻮ َن َوﻓِ َﻴﻬﺎ َﲤُﻮﺗُﻮ َن َوِﻣْﻨـ َﻬﺎ ُﲣَْﺮ ُﺟﻮ َن‬َ َ‫ﻗ‬
Qala ihbitoo baAAdhukum libaAAdhin AAaduwwun walakum fee al-Ardhi
mustaqarrun wamataAAun ila heenin; Qala feeha tahyawna wafeeha tamootoona
waminha tukhrajoona (Surat Al A’raf 7:24-25)

Tafsir: Yeye (Allah) akasema: ‘Shukeni chini, baadhi miongoni mwenu ni adui wa
baadhi yenu (yaani baina ya Adam, Hawa na Shaytan). Ardhini itakua ni makazi yenu
na starehe kwa muda fulani; Akawaambia: ‘Ndani yake mtaishi na ndani yake
mtafariki, na kutokana nayo mtafufuliwa.’’

Hivyo basi kwa kua tumesema kua ubakhili kua ndio uliomtoa Nabii Adam na Hawa
Peponi basi inabidi tufaham kuhusiana na Ubakhili wa Nabi Adam na Hawa katika
maisha yao walipokua Peponi na inabidi kwanza tujue ni nini maana ya Ubakhili.

Ambapo tunaona kua Ubakhili hua ni Kuzuia na kutoitoa Neema uliyojaaliwa na Mola
wako ili uitumie kwa manufaa yako na kwa ajili ya manufaa ya Viumbe wenzako, lakini
sasa wewe ukawa hujatosheka na hivyo kua na khofu ya kua itaisha na hivyo kutaka
kujikusanyia nyengine zaidi bila ya kutoa ile uliyokua nayo

Na kwa upande wa Nabii Adam na Hawa walikua wana kila kitu, kwani W apo Peponi
na wanaishi katika Maumbile ya Kipeponi na walikua hawana haja ya kitu chochote
kwani Peponi kila kitu kipo. Hivyo wakajiuliza na wakaona kua wana kila kitu lakini
wameambiwa wasilile tunda la mti ulo karibu yao, Hivyo walipoambiwa na Ibilisi kua
sababu ya kukatazwa kwao kutolila tunda la mti huo basi si nyengine isipokua ni kua
litawapelekea kua ni wenye kuishi Milele, wakaona kumbe huenda ikawa hatutodumu
Milele humu Peponi na hivyo kuna uwezekano wa baadae kuja kuzikosa raha zilizomo
ndani yake, hivyo bora tutafute njia ya kuzuia kutokosa hizi raha za Peponi kwa kujaribu
kuongeza uwezo wa kuishi milele zitokanazo na tunda tulilokatazwa kulila.
209

Naam..huu ni Ubakhili ambao ni sawa na ule wa mtu Mwenye Neema aliyojaaliwa na


Mola wake akaibania bila kuitoa na kutotaka kuitumia kuwaneemesha wasiokua na
uwezo zaid yake na huku akijaribu Kutafuta Neema nyengine zaidi na kujilimbikizia kwa
kuona akitoa basi atafilisika hivyo bora abanie awe na Nyingi zaidi bila ya kutoa. Mtu
mwenye sifa ya Ubakhili hua ni mwenye kusahau kua Allah Subhanah wa Ta'ala
amesema Kwenye Qur'an baada ya Biismi Allahi Rahmani Rahim:

ِ‫ﲔ۞ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻳـُ ْﺆِﻣﻨُﻮ َن ﺑِﭑﻟْﻐَْﻴﺐ‬ ِ‫ ۤ ۤاﱂ۞ ٰذﻟِﻚ ٱﻟْ ِﻜﺘﺎب ﻻَ رﻳﺐ ﻓِ ِﻴﻪ ﻫ ًﺪى ﻟِّْﻠﻤﺘﱠﻘ‬١﴿
َ َ ُ ُ َ َْ ُ َ َ
﴾‫ﺎﻫﻢ ﻳـُْﻨ ِﻔ ُﻘﻮ َن‬ُ َ‫ﻨ‬ ‫ـ‬ْ‫ﻗ‬
‫ز‬َ‫ر‬ ‫ﱠﺎ‬
‫ﳑ‬ ‫و‬ ‫ة‬
َ ‫ﻼ‬ ‫ﺼ‬
‫ﱠ‬ ‫ٱﻟ‬ ‫ن‬
َ ‫ﻮ‬ ‫ﻴﻤ‬ ِ ‫وﻳ‬
‫ﻘ‬
ْ َ َ ُ َُ
Alif-lam-meem, Dhalika alkitabu la rayba feehi hudan lilmuttaqeena, Alladheena
yu/minoona bialghaybi wayuqeemoona alssalata wamimma razaqnahum yunfiqoona
(Surat Al Baqara 2:1-3)

Tafsir: Alif-lam-meem, Hiki ni Kitabu ambacho hakina shaka ndani yake chenye
muongozo kwa wale wenye kua na Taqwa. Wale ambao ni wenye kuamini Ulimwengu
wa Al Ghayb (Usioonekana), Wakasimamisha Sala, na Kutokana na Vile
tulivyowaruzuku wakawa ni wenye kuvitumia.

Subhanah Allah!

Wengi wanaifasiri aya hii kuhusiana na Mali tu. Lakini ukweli aya hii inajumuisha kila
mtu ulichofadhiliwa na kupandishwa darja kutokana nacho zaidi ya Ibn Adam wenzako.
Yaani ndani yake mnaingia Mali, Pesa, Uwezo, Nguvu, Afya, Madaraka, Ilmu n.k.
Kwani kila ulichofadhiliwa na Mola wako zaid ya wenzako basi hutakiwi ukitumie peke
yako, Kama una Mali na Pesa basi unatakiwa utumie kwa ajili yako, kwa ajili ya familia
yako, kwa ajili ya Mola wako, kwa ajili ya Waislam wenzako, Masikini. n.k

Kama umejaaliwa kua na Ilm basi unatakiwa uitumie Ilm yako kwa kuwanufaisha
wasiojua miongoni mwa Waislam Wenzako, kwani kutiko kwako Ilm yako hua ni
sehemu ya kuitolea Zakkah Ilm yako, Kama una Cheo basi usimamie haki za walio chini
yako n.k. nadhani hapa tumefahamiana kuhusiana na kutokua na Ubakhili.

Anasema Awn Ibn Abi Shadad kua: ‘Nabii Nuh aliishi kwa miaka 950 baada ya
Mafuriko, na kwa miaka 350 baada ya Mafuriko.’ Siku moja usiku Nabii Nuh
alietembelewa na Malaika Jibril na akamuuliza: ‘Ewe Mtume ambae ndie ulieishi
miaka mingi kuliko wote jee umeuonaje wakati wa uhai wako hapa ulimwenguni?’
Nabii Nuh akajibu: ‘Hakika nimeuona wakati wa uhai wangu kua ni sawa na mtu
210

alieingia katika chumba chenye milango miwili nae akaingia kupitia katika mlango
mmoja akatokea katika mlango wa pili’.

Naam hayo ni maneno ya Nabii ambae ameishi miaka zaidi ya 1000, jee itakuaje hali
yetu sisi mimi na wewe ambao tumepata kuishi miaka mingi ni 70 tukiulizwa tutasemaje?
Bila ya shaka tusema kama alivyosema Asif Barkhiya pale alipomwambia Nabii
Sulayman kuhusiana na kukileta kiti cha Malkia Balqis kua ni kama kupepesa macho
kwa kufumba na kufumbua tu, kwani anasema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qur’an
kua:

‫ِح َﻋ ِﻦ‬ ِ ِ ‫ﱠ‬ ‫ت َوإِﱠ‬ ِ ‫ﺲ َذآﺋَِﻘﺔُ ٱﻟْﻤﻮ‬ ٍ ‫﴿ ُﻛ ﱡﻞ ﻧَـ ْﻔ‬


َ ‫ﻮرُﻛ ْﻢ ﻳـَ ْﻮَم ٱﻟْﻘﻴَ َﺎﻣﺔ ﻓَ َﻤ ْﻦ ُز ْﺣﺰ‬
َ ‫ُﺟ‬
ُ ‫أ‬ ‫ن‬
َ ‫ﻮ‬ْ ‫ـ‬‫ﻓ‬‫ﻮ‬َ ‫ـ‬
ُ‫ﺗ‬ ‫ﺎ‬‫ﳕ‬
َ َْ
﴾‫ٱﳊَﻴَﺎةُ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ إِﻻﱠ َﻣﺘَﺎعُ ٱﻟْﻐُﺮوِر‬ ْ ‫ﻣﺎ‬ ‫و‬ ‫ﺎز‬َ‫ﻓ‬ ‫ﺪ‬ْ ‫ﻘ‬
َ ‫ـ‬
َ‫ﻓ‬ ‫ﺔ‬
َ ‫ﱠ‬
‫ﻨ‬ ‫ٱﳉ‬
ْ ‫ﻞ‬ ‫ﺧ‬ِ ‫ٱﻟﻨﱠﺎ ِر وأ ُْد‬
ُ َ َ َ َ َ
Kullu nafsin dha-iqatu almawti wa-innama tuwaffawna ojoorakum yawma
alqiyamati faman zuhziha AAani alnnari waodkhila aljannata faqad faza wama
alhayatu alddunya illa mataAAu alghuroori (Surat Al Imran 3:185)

Tafsir: Kila nafsi itayaonja mauti na kisha tutakulipeni malipo yenu katika siku ya
kiyama, na atakae okoka na Moto na kuingizwa Peponi basi atakua ni mwenye kufuzu,
na hayakua maisha ya Dunia ila ni starehe yenye kuhadaisha.

Na ndio maana wakati kifo kinamkaribia Nabii Nuh, basi alimwita mtoto wake mkubwa
aitwae Sham na kumteua kua ndie mrithi wake na kumwambia: ‘Ewe Mtoto wangu
hakika mimi nakuusia juu ya mambo mawili ambayo kamwe hutakiwi kuyafanya,
na mawili ambayo kamwe hutakiwi kuachana nayo, mambo hayo ni: ‘Achana na
kumshirikisha Allah Subhanah wa Taála na pia kamwe usiwe ni mwenye na Kibri,
kwani hatoingia Peponi yeyote yule ambae atakua na chembe ndogo ya Shirk na
chembe ndogo ya Kibri katika Moyo wake.

Ama juu ya mambo mawili ambayo ninayokuusia kushikamana nayo basi ni La


Ilaha Illa Allah na Subhaana Allah, ama kuhusiana na La Ilaha Illa Allah basi
hakika mimi nimewaona watu wakiunganishwa na kua ndugu kutokana na maneno
hayo mawili, na ni kutokana na maneno La Ilaha Illa Allah basi Safina hua ni lenye
kunaweza kusafiri, juu ya bahari zote zikichanganywa pamoja miaka na miaka bila
ya tatizo hadi kufika kwa Mola wake, na kama neno La Ilaha Illa Allah likiwekwa
juu ya mizani katika upande mmoja na katik akupande wa pil zikawekwa Mbigu
na Ardhi na kila kilichomo ndani yake basi uzito wa La Ilaha Illa Allah utapita uzito
wa Mbingu na Ardhi na kila kilichomo ndani yake. Na nakuusia kua mwenye
211

kupenda kusema Subhanah Allah kwa sababu hio ndio Dua inayowapatia viumbe
Riski zao.’’’


SIFA KUU ZA NABII NUH AMBAZO HAKUWAHI KUA NAZO IBN
ADAM MWENGINE


Nabii Nuh alikua na sifa zifuatazo:

1-Hakuna Mtume wala Nabii alieitwa kwa jina lake yaani ‘Nuh’ ambalo linatokana
na neno ‘Naha’ la Kiarabu ambalo maana yake hua ni Kujilaumu. Kwani Nabii
Nuh alikua anapenda kujilaumu laumu kutokana na matatizo ya watu wake.

2-Alikua ni Mtume na Nabii wa mwanzo kutumwa na Allah Subhanah wa Taála


kwa ajili ya kusimamia Shariah za Allah Subhanah wa Taála.

3-Alikua Mtume na Nabii wa mwanzo kupingana na Washirikina.

4-Alikua ni Mtume na Nabii wa mwanzo ambae watu wake waliangamizwa


kutokana na Dua yake.

5-Alikua ni Mtume na Nabii wa Mwanzo ambae alieambiwa: ‘Hakika mimi


nimewaumba Ibn Adam na kuwaamrisha wanitii mimi, lakini wao wakawa ni
wenye kufuata njia ya upotovu. Hivyo hasira zangu zikakua dhidi ya wale wasionitii
na hivyo nikawaadhibu hata wale wanaonitii, na nikawaadhibu viumbe wangu
kutokana na makosa ya Ibn Adam. Na kuanzia sasa hivi mimi naapa kwa jina langu
kua kamwe sitofanya hivyo tena katika hali kama hii, na kamwe sitosababisha
bahati za Ulimwengu huu zipishane miongoni mwa waja wangu, na hivyo
nitawalipa waja wangu katika siku ya Malipo’

6-Alikua ni Mtume na Nabii pekee ambae alieishi kwa miaka mingi, kiasi ya kua
anajulikana kua kama Mkuu miongoni mwa Mitume na Mkongwe miogoni mwa
Mitume.

7- Alikua na Muujiza wa kipekee ambao ni Umri wake mkubwa ambao aliuishi bila
ya kua kizee, bila ya kupungukiwa na nguvu wala kupungukiwa na jino hata moja.
212

8- Alikua ni Mtume na Nabii pekee ambae alieweza kuyafanya aliyoyafanya yeye,


kwani yeye mbali ya kua aliishi miaka yote hio lakini alikua pia akitekeleza wajibu
wake wa kuwausia watu kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala usiku na mchana,
kwa siri na kwa dhahir.

9-Alikua ni Mtume na Nabii pekee aliepatwa na madhila, karaha, matusi, majeraha,


n.k kutoka kwa watu wake tena kwa mda mrefu. Na ndio maana Allah Subhanah
wa Taála akasema kuhusiana na watu wake kua:

ِِ ِ ٍ ُ‫﴿وﻗَـﻮم ﻧ‬
َ ‫ﻮح ّﻣﻦ ﻗَـْﺒ ُﻞ إِﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻗَـ ْﻮﻣﺎً ﻓَﺎﺳﻘ‬
﴾‫ﲔ‬ َْ َ
Waqawma noohin min qablu innahum kanoo qawman fasiqeena (Surat Adh
Dhariyyat 51:46)

Tafsir: Na (ndivyo walivyokua waliokuja kabla yao) watu wa Nuh. Kwa hakika wao
Walikua ni Waasi waliopita mipaka ya uasi.

10-Ni Mtume na Nabii wa Pili kwa utukufu baada ya Nabii Muhammad Salallahu
A’layhi wa Salam, na ndio maana Allah Subhanah wa Taála akamtaja Nabii Nuh
kabla ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam pale aliposema kua:

‫ﲔ ِﻣﻦ ﺑَـ ْﻌ ِﺪﻩِ َوأ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إِ َ ٰﱃ إِﺑْـَﺮ ِاﻫ َﻴﻢ‬ ٍ ُ‫ﻚ َﻛ َﻤﺂ أ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إِ َ ٰﱃ ﻧ‬
َ ِّ‫ﻮح َوٱﻟﻨﱠﺒِﻴ‬ َ ‫﴿إِ ﱠ� أ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إِﻟَْﻴ‬
ِ ِ ‫ﺎق وﻳـﻌ ُﻘﻮب وٱﻷ‬ ِ ِ
‫ﺲ َوَﻫ ُﺎرو َن‬ َ ُ‫ﻮب َوﻳُﻮﻧ‬ َ ‫ﻴﺴ ٰﻰ َوأَﻳﱡ‬ َ ‫َﺳﺒَﺎط َوﻋ‬ ْ َ َ ْ َ َ َ ‫ﻴﻞ َوإْ ْﺳ َﺤ‬ َ ‫َوإ ْﲰَﺎﻋ‬
﴾ً‫ود َزﺑُﻮرا‬
َ ‫َو ُﺳﻠَْﻴ َﻤﺎ َن َوآﺗَـْﻴـﻨَﺎ َد ُاو‬
Inna awhayna ilayka kama awhayna ila noohin waalnnabiyyeena min baAAdihi
waawhayna ila ibraheema wa-ismaAAeela wa-ishaqa wayaAAqooba waal-asbati
waAAeesa waayyooba wayoonusa waharoona wasulaymana waatayna dawooda
zabooran (Surat An Nisaa 4:163)

Tafsir: Hakika sisi tumekushushia wewe (Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam)


Wahyi kama vile ambavyo tulivyomshushia Wahyi Nuh, na Manabii waliokuja baada
yake, Na tukamshushia Ibrahim na Ismail na Is-haq, na Yaqub na Al Asbat (Watoto
wa Nabii Yaqub), na Isa, na Ayub, na Yunus, na Haruna na Sulayman na tukampa
Daud Zabur.
213

Na pia pale Allah Subhanah wa Taála aliposema kua:

‫ﻴﺴﻰ ٱﺑْ ِﻦ‬ ِ‫ﻮح وإِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ وﻣﻮﺳﻰ وﻋ‬ ِ َ ‫﴿وإِ ْذ أَﺧ ْﺬ َ� ِﻣﻦ ٱﻟﻨﱠﺒِﻴِﲔ ِﻣﻴﺜَﺎﻗَـﻬﻢ وِﻣْﻨ‬
َ َ ٰ َ ُ َ َ َ ْ َ ٍ ‫ﻚ َوﻣﻦ ﻧﱡ‬ َ ُْ َ ّْ َ َ َ
﴾ً‫َﺧ ْﺬ َ� ِﻣْﻨـ ُﻬﻢ ِّﻣﻴﺜَﺎﻗﺎً َﻏﻠِﻴﻈﺎ‬
َ ‫َﻣْﺮَﱘَ َوأ‬
ْ
Wa-idh akhadhna mina alnnabiyyeena meethaqahum waminka wamin noohin wa-
ibraheema wamoosa waAAeesa ibni maryama waakhadhna minhum meethaqan
ghaleedhan (Surat Al Ahzab 33:7)

Tafsir: Na Tukachukua kutoka kwa Manabii Makubaliano, kutoka kwako (Ewe


Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam), kutok a kwa Nuh, kwa Ibrahim, kwa Musa,
kwa Isa ibn Maryam na tukachukua kutoka kwao Makubaliano yenye uzito mkubwa
sana.

11-Atakua ni Mtume wa pili, Nabii wa pili na mtu wa pili kutoka ndani ya Ardhi
katika siku ya kufufuliwa baada ya mtu wa kwanza ambae ni Rasul Allah Salallahu
aályhi wa Salam.

12- Alikua ni mtu wa mwanzo kutengeneza Safina na Allah Subhanah wa Taála


alimpa Safina ambalo alimuokolea kutokana na Gharika.

13- Alikua ni wa mwanzo kupewa jina la Mja mwema mwenye Shukrani pale Allah
Subhanah wa Taála aliposema:

﴾ً‫﴿إِﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن َﻋْﺒﺪاً َﺷ ُﻜﻮرا‬


Innahu kana AAabdan shakooran (Surat Al Isra 17:3)

Tafsir: Hakika yeye (Nuh) alikua ni Mja mwema mwenye Shukrani

14-Alikua ni Mtume na Nabii wa mwanzo aliejaaliwa kupewa Usalama na Baraka


pale Allah Subhanah wa Taála aliposema katika kua:
214

ِ ٍ ‫﴿ﻗِﻴﻞ ٰﻳـﻨُﻮح ٱﻫﺒِ ْﻂ ﺑِﺴﻼٍَم ِﻣﻨﱠﺎ وﺑﺮَﻛ‬


َ ‫ﻚ َو َﻋﻠَ ٰﻰ أ َُﻣ ٍﻢ ّﳑﱠﻦ ﱠﻣ َﻌ‬
‫ﻚ َوأ َُﻣ ٌﻢ‬ َ ‫ﺎت َﻋﻠَْﻴ‬ ََ ّ َ ْ ُ َ
﴾‫اب أَﻟِﻴﻢ‬ ِ ِ
ٌ ٌ ‫َﺳﻨُ َﻤﺘّﻌُ ُﻬ ْﻢ ﰒُﱠ َﳝَ ﱡﺴ ُﻬ ْﻢ ّﻣﻨﱠﺎ َﻋ َﺬ‬
Qeela ya noohu ihbit bisalamin minna wabarakatin AAalayka waAAala omamin
mimman maAAaka waomamun sanumattiAAuhum thumma yamassuhum minna
AAadhabun aleemun (Surat Hud 11:48)

Tafsir: Na ikasemwa: Ewe Nuh! Shuka huku ukiwa na salama na baraka juu yako
kutoka kwetu, pamoja na Umma wa walio pamoja nawe (na vizazi vyao), Watu ambao
tutawapa raha lakini baadae (watakuja watu wengine) wataonja adhabu kali kutoka
kwetu.

Na hivyo Watu wengine wote waliobakia na kua ni wenye Imani ya kumuamini Allah
Subhanah wa Ta’ala watakua katika hali hio ya kuingia katika salama na barka hadi siku
ya Kiama.

15-Alikua ni Mtume na Nabii ambae kizazi chake ndio chanzo cha Watu wote
waliofuatia baada yake. Kama vile ilivyosema katika Qurán

﴾‫ﲔ‬ ِ
َ ‫﴿ َو َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ذُِّرﻳـﱠﺘَﻪُ ُﻫ ُﻢ ٱﻟْﺒَﺎﻗ‬
WajaAAalna dhurriyyatahu humu albaqeena (Surat As Saffat 37:77)

Tafsir: Na Tukajaalia kizazi chake kua ndio kilichobakia.

Hivyo kila Bani Adam aliekua hai leo hii katika uso wa dunia basi ametokana na Nabii
Adam kupitia kwa watoto wa Nabii Nuh wakiwemo Saam ambae kizazi chake ndio
kilichotoa Waarabu, Haam ambae kizazi chake ndio watu wa Afrika, Yaafith ambae
kizazi chake ndio kilichotoa Wazungu n.k.

Kwani anasema Samura Ibn Jundub Al Fazari Radhi Allahu Anhu kua: Amesema Rasul
Allah A’layhi wa Salam kua Shaam ni baba wa Waarabu, Haam ni baba wa watu
wa Uhabeshi (Afrika Mashariki na Barbar wa Afrika Kaskazini) na Yafith ni Baba
wa Warumi.(Jamii Tirmidhi, Imam Ibn Jarir, Imam Abu Hatim Abd Rahman
Muhammad Ibn Idris Al Razi , Musnad Imam Ahmad Ibn Hanbal)
215

Ambapo Sham maana yake hua ni ‘Mwenye rangi ya Weupe kama ya Waarabu’ Ham
maana yake ni ‘Mwenye Rangi ya Kiza kama ya Waafrika’ na Yafith maana yake hua ni
‘Mwenye Rangi ya Weupe kama ya Wazungu.’

Watoto watano wa Sham ndio waliotoa vizazi vya watu wafuatao:


1. Elam (Waarabu)
2. Asshur (Assyria)
3. Lud (Waturuki)
4. Aram (Aramaic, Armenia, Iraq, Iran)
5. Arkhfshand (Wazee wa Nabii Ibrahim)

Watoto wanne wa Haam ndio waliotoa vizazi vya watu wafuatao:


1. Mizraim (Misri)
2. Cush (Sudan, Ethiopia)
3. Put (Lybia)
4. Canaan (Syria na upande wa Mashariki wa bahari ya Mediterranian)

Watoto 7 wa Yafith ndio waliotoa vizazi vya watu wafuatao:


1. Javan (Wazungu wanaopakana na Bahari ya Mediterranean)
2. Magog (Wenye asili ya Ulaya Mashariki, Bulgari, Slavian n.k)
3. Madai (Wahindi, Wakurdi, Waajemi na Watu wa Kusini mwa Bara la Asia)
4. Tubal (Jamii za watu wa Kusini mwa Bahari Nyeusi)
5. Tiras (Wajerumani na Waskandinavia)
6. Meshech (Warusi)
7. Gomer (Irish, Wales, Scotland, Uingereza)

Hivyo ndi vizazi vyengine vilivyofuatia baada yake kama anavyosema Allah Subhanahu
wa Ta’ala katika Qurán:

ِ ِ ‫﴿ﰒُﱠ أَﻧﺸﺄْ َ� ِﻣﻦ ﺑـﻌ ِﺪ‬


‫ٱﻪﻠﻟ‬
‫ٱﻋﺒُ ُﺪواْ َﱠ‬ ْ ‫ﻳﻦ ۞ ﻓَﺄ َْر َﺳ ْﻠﻨَﺎ ﻓﻴ ِﻬ ْﻢ َر ُﺳﻮﻻً ِّﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ أَ ِن‬ ِ
‫ﺮ‬ ‫اﺧ‬ ‫ء‬
َ َ ْ ْ َْ
َ �
ً ‫ﺮ‬‫ـ‬‫ﻗ‬
َ ‫ﻢ‬ ‫ﻫ‬ َ
ْ‫ﻳﻦ َﻛ َﻔُﺮواْ َوَﻛ ﱠﺬﺑُﻮا‬ ِ‫ِ ِِ ﱠ‬ َ َ‫َﻣﺎ ﻟَ ُﻜ ْﻢ ِّﻣ ْﻦ إِﻟَ ٍـﻪ َﻏْﻴـُﺮﻩُ أَﻓَﻼَ ﺗَـﺘﱠـ ُﻘﻮ َن۞ َوﻗ‬
َ ‫ﺎل ٱﻟْ َﻤﻸُ ﻣﻦ ﻗَـ ْﻮﻣﻪ ٱﻟﺬ‬
‫ٱﳊَﻴـﺎةِ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ َﻣﺎ َﻫـٰ َﺬا إِﻻﱠ ﺑَ َﺸٌﺮ ِّﻣﺜْـﻠُ ُﻜ ْﻢ َ�ْ ُﻛ ُﻞ ِﳑﱠﺎ‬ْ ‫ٱﻵﺧَﺮةِ َوأَﺗْـَﺮﻓْـﻨَ ُـﻬ ْﻢ ِﰱ‬ ِ ‫ﺂء‬ ِ ‫ﺑِﻠِ َﻘ‬
‫ب ِﳑﱠﺎ ﺗَ ْﺸَﺮﺑُﻮ َن ۞ َوﻟَﺌِ ْﻦ أَﻃَ ْﻌﺘُ ْﻢ ﺑَ َﺸﺮاً ِّﻣﺜْـﻠَ ُﻜ ْﻢ إِﻧﱠ ُﻜ ْﻢ إِذاً ﱠﳋَ ِـﺴُﺮو َن‬ ِ
ُ ‫َﺄﺗْ ُﻛﻠُﻮ َن ﻣْﻨﻪُ َوﻳَ ْﺸَﺮ‬
ِ ِ ِ
‫ﺎت‬
َ ‫ﺎت َﻫْﻴـ َﻬ‬ َ ‫۞ أَﻳَﻌ ُﺪ ُﻛ ْﻢ أَﻧﱠ ُﻜ ْﻢ إِ َذا ﻣﺘ ْﱞﻢ َوُﻛﻨﺘُ ْﻢ ﺗُـَﺮاﺎﺑً َوﻋﻈـﻤﺎً أَﻧﱠ ُﻜ ْﻢ ﱡﳐَْﺮ ُﺟﻮ َن ۞ َﻫْﻴـ َﻬ‬
216

‫ﲔ۞ إِ ْن ُﻫ َﻮ‬ ِ ِ ِ ِ
ُ ُ‫ﻮﻋ ُﺪو َن ۞ إِ ْن ﻫ َﻰ إِﻻﱠ َﺣﻴَﺎﺗُـﻨَﺎ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ َﳕ‬
َ ‫ﻮت َوَْﳓﻴَﺎ َوَﻣﺎ َْﳓ ُﻦ ﲟَْﺒـﻌُﻮﺛ‬ َ ُ‫ﻟ َﻤﺎ ﺗ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ ِ ِ‫إِﻻﱠ رﺟﻞ ٱﻓﺘـﺮ ٰى ﻋﻠَﻰ ﱠ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟ َﻛﺬﺎﺑً َوَﻣﺎ َْﳓ ُﻦ ﻟَﻪُ ﲟُْﺆﻣﻨ‬ ٰ َ ََ ٌ ُ َ
Thumma ansha/na min baAAdihim qarnan akhareena; Faarsalna feehim rasoolan
minhum ani oAAbudoo Allaha ma lakum min ilahin ghayruhu afala tattaqoona;
Waqala almalao min qawmihi alladhina kafaroo wakadhdhaboo biliqa-i al-akhirati
waatrafnahum fee alhayati alddunya ma hadha illa basharun mithlukum ya/kulu
mimma ta/kuloona minhu wayashrabu mimma tashraboona; Wala-in ataAAtum
basharan mithlakum innakum idhan lakhasiroona; AyaAAidukum annakum idha
mittum wakuntum turaban waAAidhaman annakum mukhrajoona; Hayhata
hayhata lima tooAAadoona; In hiya illa hayatuna alddunya namootu wanahya
wama nahnu bimabAAoothina; In huwa illa rajulun iftara AAala Allahi kadhiban
wama nahnu lahu bimu/mineena. (Surat Al Muuminuun 23:31-38)

Tafsri: Na kisha baada yao, tukaumba kizazi chengine; Tukawatumia Mtume kutoka
miongoni mwao aliekua akiwaambia: ‘Muabuduni Allah! Kwani hamna Mungu
mwengine isipokua yeye. Hamuwi na Taqwa?’; Na kiongozi wa watu wake ambae
hakuamini na kukanusha kuwepo kwa Akhera, na ambae tulimpa starehe na maridhio
ya dunia akasema: ‘Yeye ni mtu tu mithli yenu, anakula kile mnachokula nyinyi, na
kunywa kile mnachokunywa nyinyi.’; ‘Ikiwa mtawatii watu ambao wapo kama mlivyo
nyinyi wenyewe, basi kwa hakika mtakua ni miongoni mwa waliokula hasara’;
‘Anakuahidini kua mtakapokufa na mkawa mavumbi na mifupa, mtakua hai tena’;
‘Liko mbali (lisilowezekana), sana jambo hilo mliloahidiwa’; ‘Hakuna isipokua
maisha yetu haya ya hapa duniani! Tunakufa na tunaishi! Na kamwe
hatutofufuliwa!’; ‘Yeye ni mtu alievumbua uongo, dhidi ya Allah, na sisi
hatutomuamini’.

Aya hizo za Surat Al Muuminuun (23:31-38) zinazungumzia vizazi vilivyofuatia baada


ya kufariki Nabii Nuh kwani navyo pia baadae vilipotoka kama ilivyobashiri aya ya Surat
Hud 11:49, na hivyo ikabidi viletewe Mtume mwengine ambae alitoka katika kizazi cha
mtoto wa Nabii Nuh aliekua akiitwa Saam, ambae yeye aliamua kuishi katika mji wa
Damascus au Dimashq ambao upo katika eneo la Ardhi linalojulikana kama Sham
kutokana na jina la Sam Ibn Nuh lakini baadae kizazi hiki kilihamia kusini mwa Bara
Arabu, na ndio ukoo uliotoa Nabii Hud Ibn Shalikh Ibn Arfakhshand Ibn Sam, Ibn Nuh.

Watu wa Nabii Hud walikua wakiishi katika maeneo ya Hadhramawt, ambalo ni eneo la
Ardhi baina ya Yemen na Oman. Inasemekana kua Nabii Hud alikua akitokea katika ukoo
wa Aad Ibn Ud Ibn Sam Ibn Nuh. Baadhi ya Wanazuoni wanasema kua Nabii Hud alikua
217

ndie Nabii wa kwanza kuzungumza lugha ya Kiarabu, wengine wanasema alikua ni Nabii
Nuh na wengine pia wanasema kua alikua ni Nabii Adam.

‫ﻚ ِﻣﻦ‬ ِ ُ‫ﺐ ﻧ‬ ِ ‫﴿ﺗِْﻠﻚ ِﻣﻦ أَﻧْـﺒ‬


َ ‫َﻧﺖ َوﻻَ ﻗَـ ْﻮُﻣ‬
َ ‫ﻨﺖ ﺗَـ ْﻌﻠَ ُﻤ َﻬﺂ أ‬
َ ‫ﻚ َﻣﺎ ُﻛ‬ َ ‫ﻮﺣ َﻴﻬﺂ إِﻟَْﻴ‬ ِ ‫ﺂء ٱﻟْﻐَْﻴ‬َ ْ َ
ِ ِ ِ
﴾‫ﲔ‬َ ‫ﭑﺻِ ْﱪ إِ ﱠن ٱﻟْ َﻌﺎﻗﺒَﺔَ ﻟ ْﻠ ُﻤﺘﱠﻘ‬
ْ َ‫ﻗَـْﺒ ِﻞ َﻫـٰ َﺬا ﻓ‬
Tilka min anba-i alghaybi nooheeha ilayka ma kunta taAAlamuha anta wala
qawmuka min qabli hadha faisbir inna alAAaqibata lilmuttaqeena (Surat Hud
11:49)

Tafsir: Hizi ni habari za ghayb (zisizoonekana wala kujulikana) ambazo


tunakushushia wewe, hakuna anaezijua kabla yake si wewe wala si watu wako. Hivyo
Subiri kwani kwa hakika mwisho mwema ni kwa wenye Taqwa.

Miongoni mwa watoto wengine wa Sam walihamia katika mji wa Babylon ambako kizazi
chao ndio kilichomtoa Nabii mwengine ambae nae pia ni miongoni mwa Manabii
waliopata daraja ya kua Ulu ul Aa’zmin mina Rusul ambae ni Nabii Ibrahim ambapo
Allah Subhanah wa Taála anasema katika Qurán kua:

�َ ‫ﲔ ۞ إِﻧﱠﻪُ ِﻣ ْﻦ ِﻋﺒَ ِﺎد‬ ِِ ِ ِ


َ ‫ﻚ َْﳒ ِﺰى ٱﻟْ ُﻤ ْﺤﺴﻨ‬ َ ‫ﲔ ۞ إِ ﱠ� َﻛ ٰﺬﻟ‬َ ‫ﻮح ِﰱ ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬ٍ ُ‫﴿ َﺳﻼٌَم َﻋﻠَ ٰﻰ ﻧ‬
﴾‫ٱﻵﺧ ِﺮﻳﻦ ۞ وإِ ﱠن ِﻣﻦ ِﺷ َﻴﻌﺘِ ِﻪَ ِﻹﺑْـﺮ ِاﻫﻴﻢ‬َ ‫ﺎ‬‫ﻨ‬
َ ‫ـ‬ْ‫ﻗ‬
‫ﺮ‬ ‫ﻏ‬
ْ َ
‫أ‬ ‫ﰒ‬
‫ُﱠ‬ ۞‫ﲔ‬َ
ِ‫ٱﻟْﻤ ْﺆِﻣﻨ‬
َ َ َ َ َ ُ
Salamun AAala noohin fee alAAalameena, Inna kadhalika najzee almuhsineena,
Innahu min AAibadina almu/mineena, Thumma aghraqna al-akhareena Wa-inna
min sheeAAatihi la-ibraheema (Surat As Saffat 37:79-83)

Tafsir: Salam kutoka kwetu ziwe juu ya Nuh miongoni mwa Walimwengu, Kwa hakika
hivyo ndivo tunavyowazawadia Waja wenye kufanya mema, Hakika yeye alikua ni
miongoni mwa Waja wetu walioamini, na tukawagharikisha waliobakia, Na miongoni
mwa waliofuata njia zake (Nabii Nuh katika kumpwekesha Allah Subhanah wa Taála)
alikua ni Ibrahim.

Aya hii ya Surat As Saffat 37:83 imetumia neno ShiaAátihi ambalo limetokana na neno
Shayáh la Kiarabu ambalo hua ni lenye kumaanisha Kundi la Watu wenye kupenda
kusaidia au kufuata Mtizamo mmoja wa Mtu fulani au Kitu fulani. Ambapo kwa upande
218

Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye amesema kua neno hili hapa
limemaanisha Dini na kwa upande wa Imam Mujahid Ibn Sulayman basi yeye amesema
kua maana iliyokusudiwa hapa ni Njia na kwa upande wa Qatadah Ibn Diama Al Sadusi
basi anasema kua maana yake ni Dini au Ummah.

Hivyo basi kutokana na maana hizi tunaona kua aya hii inaenda sambamba kimaana na
ile aya isemayo:

ِ ‫ﭑﻋﺒ ُﺪ‬
﴾‫ون‬ ِ ِِ ِ
ُ ْ َ‫﴿إ ﱠن َﻫـٰﺬﻩ أُﱠﻣﺘُ ُﻜ ْﻢ أُﱠﻣﺔً َواﺣ َﺪ ًة َوأ ََ�ْ َرﺑﱡ ُﻜ ْﻢ ﻓ‬
Inna hadhihi ommatukum ommatan wahidatan waana rabbukum faoAAbudooni
(Surat Al Anbiyah 21:52)

Tafsir: Hakika Ummah huu ni Ummah mmoja na mimi ndie Mola wenu hivyo
niabuduni mimi pekee (msinishirikishe).

Yaani na aya zinatuwekea wazi kua Nabii Nuh alikua ni mwenye kufuata muongozo wa
mfumo wa maisha ambao ndio unaowapelekea viumbe kufuzu katika maisha ya hapa
Duniani na kesho Akhera muongozo wa mfumo ambao unatoka kwa Mola wa
Ulimwengu ambae ni Allah Subhanah wa Taála na muongozo wake huo ndio pia uliokua
ukifuatwa na Khalilu Allah Ibrahima.


KUVUKA MIPAKA KWA DHAMBI ZA WATU WA NABII NUH

Hivyo aya hii inatuwekea wazi kua hali ya mitihani ya Nabii Nuh na watu wake ilikua ni
ya kudumu kizazi baada ya kizazi watu wake walikua wakipingana nae na katika kipindi
hiki chote wapinzani wake walikua wakizidi kuongezeka na wafuasi wake wakizidi
kupungua. Allah Subhanah wa Taála anatujuulisha juu ya baadhi ya maasi waliyokua
wakiyafanya watu wa Nabii Nuh na namna alivyokua akikabiliana nao kwa kusema:

ِِ ِ ٍ ُ‫﴿وﻗَـﻮم ﻧ‬
َ ‫ﻮح ّﻣﻦ ﻗَـْﺒ ُﻞ إِﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻗَـ ْﻮﻣﺎً ﻓَﺎﺳﻘ‬
﴾‫ﲔ‬ َْ َ
219

Waqawma noohin min qablu innahum kanoo qawman fasiqeena (Surat Adh
Dhariyat 51:46)

Tafsir: Na watu wa Nuh kabla yao, kwa hakika walikua ni watu Mafasiq (Waasi
waliovuka Mipaka kwa uovu).

Na kisha aya zinatuwekea wazi kua Watu wa Nabii Nuh walikua wamevuka mipaka
kuliko wengine wote wale waliowahi kuwepo ulimwenguni kwa kusema:

﴾‫ﻮح ِّﻣﻦ ﻗَـْﺒﻞ إِﻧـﱠ ُﻬﻢ َﻛﺎﻧُﻮاْ ُﻫﻢ أَﻇْﻠَﻢ وأَﻃْﻐَ ٰﻰ‬
ٍ ُ‫﴿ َوﻗَـ ْﻮَم ﻧ‬
ََ ْ ْ ُ
Waqawma noohin min qablu innahum kanoo hum adhlama wa atgha (Surat An
Najm 53:52)

Tafsir: Na watu wa Nuh kabla yao, kwa hakika walikua ni waliozama katika dhulma
na kuvuka mipaka kusikokua na kifani.

Naam, aya hii ya Surat An Najm 53:52 imetumia neno Atgha ambalo ni asili ya neno
linalotokana na neno Tagha la kiarabu lenye maana ya kuvuka mipaka, kutoka katika
asili ya kimaumbile ya kitu ya kawaida, kua muasi, kutokua mtiifu, kua ni mwenye
kufanya dhulma, kutokua na hamu ya kujirekebisha kutokana na uovu au hali fulani.

Neno Tagha ndio lililotoa pia neno Taghut ambalo maana yake hua ni mtu mwenye
kufaya Maasi, mwenye kufanya dhulma, mwenye kuongoza watu katika Uasi, mwenye
kua na uwezo na nguvu za Kuasi, tunapoiangalia maana ya hili neno Taghut basi tunaona
kua liko katika hali ya Umoja ambao wingi wake katika hali hio hio.

Sasa neno hili Tagha pia limetoa ni Atgha lenye kumaanisha hali ya juu kabisa ya kuvuka
mipaka katika Uasi, na hivyo kutoka na kukaa mbali zaidi na hali ya maumbile ya kua na
utiifu

Tafakkar! Kwani hata Fir’awn ambae alijiita Mungu kama tutakapoona katika kurasa
zinazofuatia za kitabu hiki tutakapomzungumzia Nabii Musa, basi Qurán inamuelezea
Fir’awn kwa kutumia sifa ya kua ni mwenye Tagha kwa kusema Innahu Tagha kama
inavyosema aya ifuatayo ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala anamuamrisha Nabii wake
Musa kwa kumwambia:
220

﴾‫ﺐ إِ َ ٰﱃ ﻓِﺮ َﻋﻮ َن إِﻧﱠﻪُ ﻃَﻐَ ٰﻰ‬


ْ ‫﴿ٱ ْذ َﻫ‬
ْ ْ
Idhhab ila firAAawna innahu tagha (Surat Ta-Ha 20:24)

Tafsir: Nenda kwa Fir’awn, kwani kwa hakika, yeye ni mwenye kuvuka mipaka

Hivyo tunapozungumzia Atgha basi tunazungumzia hali ya sifa ya wingi wa kuvuka


mipaka maradufu yaani kufanya dhambi kiasi ya kua maasi hayo hua ni zaidi ya uasi wa
Tagha. Hivyo watu wa Nabii Nuh wameelezewa kwa kupewa sifa mbaya kabisa ya
Atgha! ya hali ya juu kabisa ya kuvuka mipaka yote ya ushirikina, uasi, kibri, n.k ambayo
haina mfano mbaya zaidi yake na kutokua na hamu katu katu ya kujirekebisha mbali ya
kuusiwa kwa mamia ya miaka.

Na aya zilizotangulia kabla ya ayah hii ya na aya zilizofuata baada ya aya hii Surat An
Najm 53:52 yaani aya za 53:50-53 basi ni aya zinazozungumzia juu ya watu wa A’ad na
Thamud na Qawm Lut ambao ni watu wa Nabii Saleh na Nabii Hud na Nabii Lut kua
walikua ni wenye kuvuka mipaka pia, lakini hata hivyo watu hao na kuvuka mipaka kwao
kote basi kamwe hawakuwahi kuwafikia watu wa Nabii Nuh kwa uasi wao na ndio maana
aya ikawainisha kwa kusema Kanu Adhlama wa Atgha waliokua ni waliozama katika
Dhulma ya hali ya juu kabisa na Uasi wa hali ya juu kabisa kupita wote.

Baada ya Allah Subhanah wa Taála kutuwekea wazi uasi wa hali ya watu wa Nabii Nuh
Alayhi Salaam, basi anatuainishia kua yeye si mwenye kudhulumu kwa kuwaadhibu watu
kabla ya kuwaonya, na hivyo akaamua kumtuma Nabii Nuh kwa watu hao ili kuwaonya
na kuwatanabahisha kua wasijisahau kwa kusema:

‫ﻮح أَﻻَ ﺗَـﺘﱠـ ُﻘﻮ َن ۞ إِِّﱏ ﻟَ ُﻜ ْﻢ‬ َ َ‫ﲔ ۞ إِ ْذ ﻗ‬ ِ


ٌ ُ‫ﻮﻫ ْﻢ ﻧ‬ ُ ‫ﺎل َﳍُْﻢ أ‬
ُ ‫َﺧ‬ َ ‫ﻮح ٱﻟْ ُﻤْﺮ َﺳﻠ‬ ْ َ‫﴿ َﻛ ﱠﺬﺑ‬
ٍ ُ‫ﺖ ﻗَـ ْﻮُم ﻧ‬
﴾‫ﻮن‬ِ ‫َﻃﻴﻌ‬ِ ‫ﻮل أ َِﻣﲔ ۞ ﻓَﭑﺗﱠـ ُﻘﻮاْ ﱠ‬
ُ ‫ٱﻪﻠﻟَ َوأ‬ ٌ ٌ ‫َر ُﺳ‬
Kadhdhabat qawmu noohin almursaleena, Idh qala lahum akhoohum noohun ala
tattaqoona, Innee lakum rasoolun ameenun, Faittaqoo Allaha waateeAAooni (Surat
Ash Shuara 26:105-109)

Tafsir: Walikadhibisha watu wa Nuh mitume yetu, waliambiwa na ndugu yao Nuh:
‘Jee hamumuogopi na Kumtii yeye? (Allah Subhanah wa Taála), Hakika mimi ni
Mtume wa kweli nilietumwa kwenu. Hivyo muogopeni Allah na mnitii mimi’
221

Naam, aya imesema kua Watu wa Nabii Nuh walikadhibisha Mitume yetu kwa sababu
ingawa alikua ni Mtume mmoja tu lakini kukataa kwao kumkubali Mtume mmoja huyo
basi kumekua ni sawa na kuwakadhibisha Mitume wengine wote. Na hii ni kwa sababu
Mitume wote hua ni wenye kuletwa kwa kutokana na Mungu mmoja ambae ni Allah
Subhanah wa Taála na hivyo Mitume wote kua na ujumbe unaousia juu ya jambo
kumpwekesha na kumtii Allah Subhanah wa Taála, hivyo hapa aya inatuwekea wazi kua
kumkataa hata Mtume mmoja miongoni mwa Mitume wa Allah na kuwakubali wengineo
basi hua ni sawa na kuwakataa Mitume wote. Kwa sababu Allah Subhanah wa Ta’ala
anasema katika Qurán:

‫ﻮل ِﲟَﺎ أُﻧ ِﺰَل إِﻟَْﻴ ِﻪ ِﻣﻦ ﱠرﺑِِّﻪ َواﻟْ ُﻤ ْﺆِﻣﻨُﻮ َن ُﻛﻞﱞ َآﻣ َﻦ ِﺎﺑ ّﻪﻠﻟِ َوَﻣﻶﺋِ َﻜﺘِ ِﻪ َوُﻛﺘُﺒِ ِﻪ‬
ُ ‫﴿ َآﻣ َﻦ اﻟﱠﺮ ُﺳ‬
ِ ٍ ‫ورﺳﻠِ ِﻪ ﻻَ ﻧـُ َﻔ ِﺮ ُق ﺑـﲔ أ‬
‫ﻚ‬ َ َ‫َﺣﺪ ِّﻣﻦ ﱡر ُﺳﻠ ِﻪ َوﻗَﺎﻟُﻮاْ َِﲰ ْﻌﻨَﺎ َوأَﻃَ ْﻌﻨَﺎ ﻏُ ْﻔَﺮاﻧ‬
َ ‫ﻚ َرﺑـﱠﻨَﺎ َوإِﻟَْﻴ‬ َ ََْ ّ ُ َُ
﴾‫ﺼﲑ‬ ِ
ُ ‫اﻟْ َﻤ‬
Amana alrrasoolu bima onzila ilayhi min rabbihi waalmu/minoona kullun amana
biAllahi wamala-ikatihi wakutubihi warusulihi la nufarriqu bayna ahadin min
rusulihi waqaloo samiAAna waataAAna ghufranaka rabbana wa-ilayka almaseeru
(Surat Al Baqara 2:285)

Tafsir: Ameamini Mtume (Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) juu ya kile


alichoshushiwa na Mola wake, na pia ndivyo wanavyoamini Waumini, Kila mmoja
anaamini juu ya Allah Subhanah wa Taála, Malaika wake, Vitabu vyake, Mitume
wake. Na wanasema: ‘Hatutofautishi baina ya Mitume yake’, na wa (Waumini)
husema: ‘Tunasikia na Kutii, tusamehe ewe Mola wetu, na kwako wewe ndio marejeo
ya wote’

Na akasema tena Allah Subhanah wa Taála katika Qurán juu ya ujumbe wa Nabii Nuh
kwa watu wake kwa kusema:

‫ٱﻪﻠﻟَ َﻣﺎ ﻟَ ُﻜ ْﻢ ِّﻣ ْﻦ إِﻟَـٍٰﻪ َﻏْﻴـُﺮﻩُ إِِّ ۤﱐ‬


‫ٱﻋﺒُ ُﺪواْ ﱠ‬ ِ َ ‫﴿ﻟََﻘ ْﺪ أَرﺳ ْﻠﻨﺎ ﻧُﻮﺣﺎً إِ َﱃ ﻗَـﻮِﻣ ِﻪ ﻓَـ َﻘ‬
ْ ‫ﺎل َ�ﻗَـ ْﻮم‬ ْ ٰ ََْ
﴾‫اب ﻳَـﻮٍم َﻋ ِﻈﻴ ٍﻢ‬
ْ َ ‫ﺎف َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ َﻋ َﺬ‬
ُ ‫َﺧ‬َ‫أ‬
222

Laqad arsalna noohan ila qawmihi faqala ya qawmi oAAbudoo Allaha ma lakum
min ilahin ghayruhu innee akhafu AAalaykum AAadhaba yawmin AAadheemin
(Surat Al Araf 7:59)

Tafsir: Ama kwa hakika tulimtuma Nuh kwa watu wake akasema: ‘Enyi watu wangu!
Muabuduni Allah ambae hamna Mola isipokua yeye, Bila ya shaka nnakukhofieni juu
ya Adhabu katika siku ya Kiama.’

Bila ya shaka Nabii Nuh alikua akiwaonea huruma sana watu wake kama inavyoonesha
aya, na hivyo alikua akiwakhofia kua huenda wakapata adhabu katika siku ya malipo na
alikua anawatakia mwisho mwema, kwani alikua hajui kua watu wake hao, hawana
mwisho mwema hapa duniani wala kesho akhera, kwani adhabu yao itaanza hapa hapo
duniani, na itakua haina mfano wake, na adhabu kama hio haikuwahi kutokea kabla yake
wala baada yake. Hivyo mbali ya kuwaonea huruma na kujitahid kwake lakini wenye
Mamlaka ya uongozi katika mji huo wakampinga na kumuona kua Nabii Nuh amepotoka
na anataka kuwapotoa watu wao kwa kusema:

ٍ ِ‫ﺿﻼٍَل ﱡﻣﺒ‬ ِِ ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ﺎل ٱﻟْ َﻤﻸُ ﻣﻦ ﻗَـ ْﻮﻣﻪ إِ ﱠ� ﻟَﻨَـَﺮ َاك ِﰱ‬
َ َ‫﴿ﻗ‬
Qala almalao min qawmihi inna lanaraka fee dhalalin mubeenin (Surat Al Araf 7:60)

Tafsir: Wakasema Viongozi kutoka katika Ummah wake: ‘Hakika sisi tunakuona
wewe kua ni miongoni mwa walio katika upotovu mkubwa sana.’

Aya imetumia neno Al Malau ambal ni lenye kutokana na neno Mala ambalo hua ni lenye
kumaanisha Kujaza, Kutosheleza, Kuridhisha, Kukamilia kua na sifa za kua Kiongozi
kiasi ya kua wenye kukukubali hua ni wenye kutosheka, kuvutiwa, kuridhika na
kuheshimika kutokana na muonekano wako na sifa stahiki juu ya watu hao. Hivyo hawa
wanaozungumziwa hapa walikua ni watu ambao ni wenye kukubalika katika jamii ya
watu wa Nabii Nuh kulingana na sifa zao stahiki.

Nabii Nuh akajitetea na kuwabembeleza watu wake hao kwa kusema:


223

‫ﲔ ۞ أُﺑَـﻠِّﻐُ ُﻜ ْﻢ‬ ِ ِ ِ ِ َ َ‫﴿ﻗ‬


َ ‫ب ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬ِّ ‫ﺿﻼَﻟَﺔٌ َوﻟـٰﻜ ِّﲎ َر ُﺳﻮٌل ّﻣﻦ ﱠر‬ َ ‫ﺲ ِﰉ‬ َ ‫ﺎل َ�ﻗَـ ْﻮم ﻟَْﻴ‬
‫ٱﻪﻠﻟِ َﻣﺎ ﻻَ ﺗَـ ْﻌﻠَ ُﻤﻮ َن۞ أ ََو َﻋ ِﺠْﺒـﺘُ ْﻢ أَن َﺟﺂءَ ُﻛ ْﻢ‬ ‫َﻧﺼ ُﺢ ﻟَ ُﻜ ْﻢ َوأ َْﻋﻠَ ُﻢ ِﻣ َﻦ ﱠ‬ ِ
َ ‫ِر َﺳﺎﻻَت َرِّﰉ َوأ‬
﴾‫ﻨﺬرُﻛﻢ وﻟِﺘَـﺘﱠـ ُﻘﻮاْ وﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜﻢ ﺗُـﺮ َﲪُﻮ َن‬
ِ ‫ِذ ْﻛﺮ ِﻣﻦ ﱠرﺑِ ُﻜﻢ ﻋﻠَﻰ رﺟ ٍﻞ ِﻣْﻨ ُﻜﻢ ﻟِﻴ‬
ْ ْ َ َ ْ َ ُ ْ ّ َُ ٰ َ ْ ّ ّ ٌ
Qala ya qawmi laysa bee dhalalatun walakinnee rasoolun min rabbi alAAalameena,
Oballighukum risalati rabbee waansahu lakum waaAAlamu mina Allahi ma la
taAAlamoona, Awa AAajibtum an jaakum dhikrun min rabbikum AAala rajulin
minkum liyundhirakum walitattaqoo walaAAallakum turhamoona. (Surat Al Araf
7:61-63)

Tafsir: Akasema (Nabii Nuh kuwaambia watu wake): Enyi watu wangu! Hakuna
upotovu kutoka kwangu, bali mimi ni Mtume kutoka kwa Mola wa Ulimwengu wote
na kila kilichomo ndani yake. Nakudhihirishieni ujumbe ulio wazi kutoka kwa Mola
wangu na kukuusieni na mimi nakijua kutoka kwa Allah kile ambacho nyinyi
hamkijui. Au mnastaajabu kua amekuja Mkumbushaji kutoka kwa Mola wenu kupitia
kwa mtu alie miongoni mwenu akuonyeni mpate kumtii na kumuogopa Allah ili muwe
miongoni mwa waliorehemewa.

Katika kulingania kwake huko basi Nabii Nuh alijaaliwa kupata wafuasi kidogo sana
miongoni mwa jamii yake ambao walikua ni Masikini na wasiokua na kitu. Ama juu ya
idadi ya wafuasi wake hao basi Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye
anasema kua walikua ni watu 80, na kwa upande wa Kabb Al Ahbar Radhi Allahu Anhu
basi yeye anasema kua walikua ni watu 72, na wakati huo huo kuna wanazuoni wasemao
kua idadi ya watu wake haikuwahi kufikia hata 20, idadi ambayo iliwapelekea Viongozi
wa mji wake kua ni wenye kumkejeli kama isemavyo Qurán:

ِ ِ‫ﱠ‬
َ ‫ﻳﻦ َﻛ َﻔُﺮواْ ِﻣﻦ ﻗ ْﻮِﻣ ِﻪ َﻣﺎ ﻧَـَﺮ َاك إِﻻﱠ ﺑَ َﺸﺮاً ِّﻣﺜْـﻠَﻨَﺎ َوَﻣﺎ ﻧَـَﺮ َاك ٱﺗﱠـﺒَـ َﻌ‬
‫ﻚ إِﻻﱠ‬ َ ‫ﺎل ٱﻟْ َﻤﻸُ ٱﻟﺬ‬ َ ‫﴿ﻓَـ َﻘ‬
‫ﻀ ٍﻞ ﺑَ ْﻞ ﻧَﻈُﻨﱡ ُﻜ ْﻢ‬ ْ َ‫ى ٱﻟﱠﺮأْى َوَﻣﺎ ﻧَـَﺮ ٰى ﻟَ ُﻜ ْﻢ َﻋﻠَْﻴـﻨَﺎ ِﻣﻦ ﻓ‬ ِ ‫ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻫﻢ أَر ِاذﻟُﻨَﺎ ﺎﺑ‬
‫د‬
َ َ َ ُْ َ
ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ِ‫َﻛﺎذﺑ‬
224

Faqala almalao alladheena kafaroo min qawmihi ma naraka illa basharan mithlana
wama naraka ittabaAAaka illa alladheena hum aradhiluna badiya alrra/yi wama
nara lakum AAalayna min fadhlin bal nadhunnukum kadhibeena (Surat Hud 11:27)

Tafsir: Wakasema Viongozi wa miongoni mwa waliokufuru kutoka katika watu wake:
‘Ama sisi tunakuona wewe kua ni mtu wa kawaida kama sisi, na hatuoni
wanaokufuata isipokua wale masikini wasiokua na ufahamu miongoni mwetu, na kwa
sababu wao wanakufuata bila ya kufikiria, na sisi tunakuona wewe kua huna faida
nasi, ukweli ni kua tunakuona kua ni muongo.’

Viongozi wa mji wake hawakusitia hapo tu katika kumkejeli na kumdhalilisha Nabii Nuh
kwa sababu hakufanikiwa kua ni mwenye kuweza kuwashawishi watu wa juu wenye
Mamlaka, wenye I’lm wenye umaarufu, Matajiri na wenye dini katika Ummah wake ili
wamfuate bali alifanikiwa kufuatwa na wale watu wa chini tena walio kidogo tu ambao
kwa mtizamo wa wenye kuendekeza mambo ya kidunia basi hua ni wenye kuwaona kua
ni watu wasioona mbali katika mitizamo na ufahamu wao, hivyo Viongozi wa mji huo
nao wakawa ni wenye kuwaonya watu hao walio chini yao kiufahamu na kimamlaka
ambao ndio wenye kumfuata Nabii Nuh kua wanaemfuata ni mtu asiekua na maana
kwani anafanya hivyo kwa ajili ya matamanio ya nafsi yake kwa ajili ya dunia yake na
hivyo si mwenye kufaa kufuatwa.

Kwani wao walikua wanamfananisha Nabii Nuh kua ni mtu kama wao, kwa sababu ni
mwenye Bashar Mithlahum yaani maumbile ya umbo la Ibn Adam kama wao. Neno la
kiarabu Bashar linatokana na mzizi wa neno ‘Ba-Shin-Ra’ ambalo si lenye kumaanisha
tu bashirio, furahio, habari muhimu yenye kubadilisha muonekano wa mtu aliepokea
habari hiyo aliyopewa na mgusano wa maingiliano lakini pia mzizi wa neno hilo ‘Ba-
Shin-Ra’ lina maana ya uwezo na uzuri wa muonekano wa umbo la nje la Bani Adam, na
hii ndio maana ambayo imetumika katika kulielezea ‘Umbo bora la kiumbe hai lenye kila
sifa bora na iliyokamilika kikamilifu’ la kiumbe Mtu katika aya ifuatayo:

ٍ ُ‫ﻚ ﻟِْﻠﻤﻶﺋِ َﻜ ِﺔ إِِﱏ ﺧـﻠِﻖ ﺑ َﺸﺮا ِﻣﻦ ﺻ ْﻠﺼ ٍـﻞ ِﻣﻦ َﲪٍﺈ ﱠﻣﺴﻨ‬
﴾‫ﻮن‬ َ َ‫﴿وإِ ْذ ﻗ‬
ْ َ ّْ َ َ ّ ً َ ٌ َ ّ َ َ ‫ﺎل َرﺑﱡ‬ َ
Wa-idh qala rabbuka lilmala-ikati innee khaliqun basharan min salsalin min hama-
in masnoonin (Surat Al Hijr 15:28).

Tafsir: Na (kumbuka) wakati Mola wako alipowaambia Malaika. Hakika mimi


nitamuumba Bashar kutokana na udongo wa mfinyanzi wenye asili ya weusi.
225

Kwa upande mwengine basi tunaona kua katika kumuelezea kiumbe Ibn Adam, aya pia
zimetumia neno ‘Insan’ linalotokanana mzizi wa neno ‘Alif-Nun-Siin’ lenye kumaanisha
sifa za kua na hisia mbali mbali za ufahamu, kua na sifa ya urafiki wa kuzungumza na
kusikiliza, kua na mazoea ya kuishi kijamii, sifa ya kua na ukaribu, kua na upendo,
ustahmilivu, huruma n.k.

Na ndio maana Allah Subhanahu wa Ta’ala akasema:

﴾‫َﺣ َﺴ ِﻦ ﺗَـ ْﻘ ِﻮ ٍﱘ‬ ۤ ِ


ْ ‫ﻧﺴﺎ َن ِﰲ أ‬
َ ‫﴿ﻟََﻘ ْﺪ َﺧﻠَ ْﻘﻨَﺎ ٱﻹ‬
Laqad khalaqna al-insana fee ahsani taqweemin (Surat Tinn 95:4)

Tafsir: Kwa hakika tumemuumba Insan katika Taqwim bora kabisa.

Tukiangalia tunaona kua aya hii mbali ya kutumia neno Insan lakini pia imetumia neno
Taqwim, na kusisitiza kua ni Taqwim bora kabisa, neno Taqwim linatokana na mzizi wa
neno Qa-Ma ambalo kwa kiarabu lina maana ya kua katika hali ya kusimama, kua thabiti,
madhubuti, kamilika, sawia bila kua na kasoro yeyote, kua na thamani, hali ya usimamizi,
hali ya ulinzi, hali ya mpangilio ulokamilika, hali ya mfumo kamili, hali ya umbo
lililokamilika n.k

Hivyo basi tunaweza kusema kua neno ‘Bashar’ linazungumzia mfumo uliokamilika wa
mwili au hali ya umbo bora la nje la Bani Adam na ufanyaji kazi wa viungo mbali mbali
vya mwili wake kama vile ngozi, kichwa, mdomo, masikio, macho, pua, mikono, kifua,
miguu n.k umbo ambalo pia viumbe wengine kama Malaika hulitumia, pale
wanapotumwa na Mola wao kuwaletea ujumbe Bani Adam walioteuliwa kupokea ujumbe
na Allah Subhanah wa Ta’ala.

Lakini neno ‘Insan’ hua linazungumzia mfumo wa umbo uliokamilika kiubora usiokua
na kasoro yeyote wa umbo la Bani Adam unaojumuisha pamoja mfumo wa ‘Bashar’ na
mfumo wa viungo vya ndani ya mwili wake unaogusia roho, Nafsi, moyo, ubongo, akili,
mfumo wa fahamu, mfumo wa damu, mfumo wa hisia n.k na pia ufanyaji kazi wa mifumo
hiyo na viungo hivyo vya ndani vikishirikiana na viungo vya nje kunakompelekea
kiumbe mtu kua na hisia mbali mbali za kimwili kama kuona, kusema, kusikia, kupenda,
kuchukia, kutamani, kutimiza mahitaji mbali mbali ya kinafsi, kiroho, kimwili, n.k.

Ubora, ukamilifu na uzuri wa Insan unaelezewa zaidi katika aya zinazofuatia:-


226

ٍ ‫ﺎن ِﻣﻦ ِﻃ‬ ِ ‫﴿ٱﻟﱠ ِﺬ ۤي أَﺣﺴﻦ ُﻛ ﱠﻞ َﺷﻲ ٍء ﺧﻠَ َﻘﻪ وﺑ َﺪأَ ﺧ ْﻠﻖ ٱ ِﻹﻧْﺴ‬
ُ‫ ﰒُﱠ َﺟ َﻌ َﻞ ﻧَ ْﺴﻠَﻪ‬- ‫ﲔ‬ َ َ َ ََ ُ َ ْ ََ ْ
ِ ‫ ﰒُﱠ ﺳ ﱠﻮاﻩ وﻧَـ َﻔﺦ ﻓِ ِﻴﻪ ِﻣﻦ ﱡر‬- ‫ﲔ‬
‫وﺣ ِﻪ َو َﺟ َﻌ َﻞ ﻟَ ُﻜ ُﻢ ٱﻟ ﱠﺴ ْﻤ َﻊ‬ ٍ ‫ِﻣﻦ ﺳﻼَﻟٍَﺔ ِﻣﻦ ﱠﻣ‬
ٍ ‫ﺂء ﱠﻣ ِﻬ‬
َ َُ َ ّ ُ
﴾‫ﺼ َﺎر َو ْاﻷَﻓْﺌِ َﺪةَ ﻗَﻠِﻴﻼً ﱠﻣﺎ ﺗَ ْﺸ ُﻜُﺮو َن‬
َ ْ‫َوٱﻷَﺑ‬
Alladhee ahsana kulla shay-in khalaqahu wabadaa khalqa al-insani min teenin,
Thumma jaAAala naslahu min sulalatin min ma-in maheenin; Thumma sawwahu
wanafakha feehi min roohihi wajaAAala lakumu alssamAAa waal-absara waal-af-
idata qaleelan ma tashkuroona (Surat As Sajda 32:7-9)

Tafsir: Ni yeye aliekifanya kizuri kila kitu alichokiumba, na akaanza kumuumba Insan
kutokana na udogo. Kisha akakijaalia kizazi chake kutokana mfano bora wa maji
yanayo dharaulika, kisha akamtengeneza katika hali iliyokamilika, na akampulizia
ndani yake sehemu ya roho yake, na akakupeni uwezo wa kusikia na kuona na kuhisi:
lakini mnashukuru kidogo tu!

Aya hizi zinamuelezea Insan alivyoumbwa na kukamilishwa kwake kwa kutumia kauli
isemayo ‘Kisha akampulizia ndani yake Ruhi yake’ ambayo inamaanisha kua Allah
Subhanahu wa Ta’ala alimpulizia Adam ndani yake Roho yake iliyoumbwa na Allah
Subhanah wa Ta’ala. Hivyo neno hili Ruh ambalo kwa Kiswahili tunasema ‘Roho’
ambayo Adam amepuliziwa hua halimaanishi kua ni kama sehemu ya Allah Subhanahu
wa Ta’ala ambayo imeingizwa ndani ya Adam. La hasha! kwani kusema, kufikiri au
kufahamu hivyo hupelekea kuinga katika Kufr.

Mujaddid ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din al Razi anasema katika
kufafanua maana kauli hiyo kua: ‘Kwa sababu Qur’an imeweka wazi kua Allah
Subhanah wa Ta’ala ni Ahad (mmoja), yaani umoja uzioweza kugawika katika
sehemu nyengine, na tafsiri inasema kua hii ‘Ruh’ imeumbwa moja, basi sifa ya
kujumuishwa kwake Ruh hii na Allah Subhanahu wa Ta’ala aliposema ‘Ruh’ yangu
hua ni kule kunakoelezeka kwa kiarabu kama Idhafat at Tashrif yaani ‘kupewa sifa
ya kutukuzwa’, inayoonesha kua Ruh au Roho iliyomo ndani ya mtu huyu wa
kwanza na kizazi chake chote kua ni ‘Tukufu, yenye Hadhi na Thamani kubwa
sana’’.

Hivyo kiuhalisia ni kua Nabii Nuh ni Nabii na hivyo ingawa ni mwenye Bashar kama
watu wengine lakini hua ni mwenye maumbile ya Al Ins yaliyotofauti na maumbile ya Al
Ins ya Ibn Adam wengine yaani Mitume na Manabii wao hua na hisia tofauti ndani ya
Miili yao, Nyoyo zao na Nafsi za na hivyo hua si wenye kumuasi Mola wao kutokana na
227

usafi wa Nyoyo zao na kutokana na kua na hali ya Utukufu wa juu wa darja zao, mbele
ya Mola wao na mbele ya viumbe wengine wote hapa Duniani na Akhera.

Na kutokana na kutojua na kutotaka kufaham kwao basi Viongozi hao wa watu wa Nabii
Nuh wakasema kama inavyotuwekea wazi aya ifuatayo:

‫ﱠﻞ‬ ُ ‫ﻳﻦ َﻛ َﻔُﺮواْ ِﻣﻦ ﻗَـ ْﻮِﻣ ِﻪ َﻣﺎ َﻫـٰ َﺬا إِﻻﱠ ﺑَ َﺸٌﺮ ِّﻣﺜْـﻠُ ُﻜ ْﻢ ﻳُِﺮ‬ ِ‫ﱠ‬
َ ‫ﻳﺪ أَن ﻳَـﺘَـ َﻔﻀ‬ َ ‫ﺎل ٱﻟْ َﻤﻸُ ٱﻟﺬ‬
َ ‫﴿ﻓَـ َﻘ‬
‫ﲔ۞ إِ ْن ُﻫ َﻮ إِﻻﱠ‬ ِ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻷَﻧﺰَل ﻣﻼَﺋِ َﻜﺔً ﱠﻣﺎ َِﲰﻌﻨَﺎ ِﻬﺑـٰ َﺬا ِ ۤﰲ‬
َ ‫آﺂﺑﺋﻨَﺎ ٱﻷَﱠوﻟ‬ َ َ ْ َ َ ُ‫َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ َوﻟَ ْﻮ َﺷﺂءَ ﱠ‬
ٍ ‫ﺼﻮاْ ﺑِِﻪ َﺣ ﱠ ٰﱴ ِﺣ‬ ِِ
﴾‫ﲔ‬
ُ ‫َر ُﺟ ٌﻞ ﺑِﻪ ﺟﻨﱠﺔٌ ﻓَـﺘَـَﺮﺑﱠ‬
Faqala almalao alladhheena kafaroo min qawmihi ma hadha illa basharun
mithlukum yureedu an yatafadhdhala AAalaykum walaw shaa Allahu laanzala
mala-ikatan ma samiAAna bihadha fee aba-ina al-awwaleena, In huwa illa rajulun
bihi jinnatun fatarabbasoo bihi hatta heenin (Surat Al Muuminun 23:24-25)

Tafsir: Wakasema Viongozi wa miongoni mwa watu wake waliokua hawakuamini:


‘Nani huyu? Isipokua ni mtu tu kama nyinyi ambae anataka kujipandisha darja zaidi
juu yenu, kwani kama Allah angependa basi angetuma Malaika, ama sisi kamwe
hatukuwahi kusikia mambo kama haya kutoka kwa mababa zetu waliotutangulia.
Huyu si yeyote isipokua ni mtu mwenye wazim, nyie subirini tu mtaona.’

Sultan al Balagha Imam Abu Qasim Mahmud Ibn Umar Al Zamakhshari anahoji juu ya
hoja za Watu wa Nabii Nuh kwa kusema: ‘Jee hali hii si ndio ile ambayo inaonekana
miongoni mwa wengi wanaojiita kua ni Waislam leo hii? Kua hua ni wenye
kumhukumu mtu na kumheshimu au kumdharau kulingana na vigezo vya kiasi
gani ya Mali mtu huyo anamiliki? Na hivyo hua ni wenye kusahau kua umiliki wa
Mali sio kigezo cha kumkaribisha mtu kwa Allah, kwani takriban mara zote Mali
hua ndio sababu ya kumpotosha mtu na kua mbali na Mola wake, watu wanasahau
kua Mitume hawaji kwa ajili ya kuitengeneza Dunia bali ni kinyume chake, hua
wanakuja kwa ajili ya kuwaamsha watu waachane na Dunia’

Hapa tunaona namna aya ilivyotumia neno Basharun Mithlukum kuweka wazi kua
Maumbile ya nje ya Muonekano wa Nabii Nuh ni sawia na wa Ibn Adam wengine lakini
Maumbile ya ndani ni tofauti, hivyo Nabii Nuh akaendelea kuwahoji na kuwawekea wazi
watu wake hao kua jambo analowausia ni lenye manufaa kwao kwani yeye ni mmoja kati
ya miongoni mwao hivyo anawatakia mema ila wao kwa mtizamo wao basi walikua
228

hawaioni hali hiyo, kwani walikua wanaichukia hali hio yenye manufaa nao ambayo
yasiyoonekana na macho yao, hivyo bila ya shaka hapa hali inakua kama ile hali ya mtu
ambae kamchukua Farasi hadi kwenye mto lakini kamwe hawezi kumlazimisha Farasi
huyo kunywa maji hayo, hivyo Nabii Nuh alikua ni mwenye kujua kua hakuna
kulazimishana katika dini hivyo akasema:
ِ ِِ ِ ِ ۤ ِ َ َ‫﴿ﻗ‬
َ ‫ﻨﺖ َﻋﻠَ ٰﻰ ﺑـَﻴِّﻨَ ٍﺔ ِّﻣﻦ ﱠرِّﰊ َو‬
ْ َ‫آﺎﺗِﱏ َر ْﲪَﺔً ّﻣ ْﻦ ﻋﻨﺪﻩ ﻓَـﻌُ ّﻤﻴ‬
‫ﺖ‬ ُ ‫ﺎل ٰﻳـ َﻘ ْﻮم أ ََرأَﻳْـﺘُ ْﻢ إِن ُﻛ‬
﴾‫ﻮﻫﺎ وأَﻧﺘُﻢ َﳍَﺎ َﻛﺎ ِرُﻫﻮ َن‬
ْ َ َ ‫َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ أَﻧـُْﻠ ِﺰُﻣ ُﻜ ُﻤ‬
Qala ya qawmi araaytum in kuntu AAala bayyinatin min rabbee waatanee
rahmatan min AAindihi faAAummiyat AAalaykum anulzimukumooha waantum
laha karihoona (Surat Hud 11:28)

Tafsir: Akasema Nuh: ‘Enyi watu wangu! Hebu niambieni, jee kama nikiwa na
vithitisho thabit kutoka kwa Mola wangu, na nimepewa Rehma kutoka kwake, lakini
imezibwa na mitizamo yenu, Jee nikulazimisheni kuikubali wakati mnaichukia sana
kiasi hicho?’

Nabii Nuh aliwaambia watu wake kua yeye anawausia kumuabudu Mungu mmoja ambae
ni Allah Subhanah wa Ta’ala si kwa sababu labda anataka Cheo na hivyo
kuwanyang’anya wenye Mamlaka nyadhifa zao, au Umaarufu wao au labda anataka Mali
awanyang’anye wenye Mali zao au labda apate Mali kutokana na yeye kudai malipo
kutoka kwa watu hao kwa kuwalingania kwake, la bali alikua anafanya hivyo kwa ajili
ya kutekeleza maamrisho ya Mola wake hivyo ni Mola wake pekee ndie atakaeweza
kumlipa kutokana na kuwalingania kwake kwa kusema.

ِ ِ ‫﴿وﻣﺂ أَﺳﺄَﻟُ ُﻜﻢ ﻋﻠَﻴ ِﻪ‬


‫ﲔ۞ ﻓَﭑﺗﱠـ ُﻘﻮاْ َﱠ‬
‫ٱﻪﻠﻟ‬ ِّ ‫ى إِﻻﱠ َﻋﻠَ ٰﻰ َر‬
َ ‫ب ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬ َ ‫ﺮ‬ِ ‫َﺟ‬
ْ ‫أ‬ ‫ن‬
ْ ِ‫َﺟ ٍﺮ إ‬
ْ ‫أ‬ ‫ﻦ‬
ْ ‫ﻣ‬ ْ َ ْ ْ ََ
﴾‫ﻮن‬ ِ ‫َﻃﻴﻌ‬ِ
ُ ‫َوأ‬
Wama as-alukum AAalayhi min ajrin in ajriya illa AAala rabbi alAAalameena,
Faittaqoo Allaha waateeAAooni (Surat Ash Shuara 26:109-110)

Tafsir: Mimi sikudaini kutoka kwenu ujira, kwani Malipo yangu yapo kwa Allah Mola
wa Ulimwengu. Mcheni Allah na mnitii.
229

Watu wa Nabii Nuh wakatoa hoja kua kweli hudai malipo wala ujira kutoka kwetu, lakini
jee mbona unafuatwa na watu dhalili kabisa, ambao hawajui lolote na wewe hujui lolote
juu yao? Nabii Nuh anajibu hoja kwa kuweka wazi kua hutakiwi kuangalia hali ya mtu,
darja ya mtu au uzuri wa mtu pale unapoamua kumlingania kwa ajili ya Mola wake,
unachotakiwa wewe ni kufikisha ujumbe tu, bila ya kujali muonekano wa nje wa mtu
husika au historia yake, kwani muonekano wa mtu si muhimu wala aliyokua akiyafanya
hapo kabla wakati alipokua hajui, si muhimu pia kwani jukumu la kutizama na kuona
ndani ya nyoyo za watu husika na kutoa hukumu juu yao ni la Allah Subhanah wa Ta’ala,
na jukumu lake yeye Nabii Nuh ni kuwaonesha njia sahih na kuwaonya, hivyo akawajibu
watu hao:

‫ﺎل َوَﻣﺎ ِﻋ ْﻠ ِﻤﻰ ِﲟَﺎ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳَـ ْﻌ َﻤﻠُﻮ َن ۞ إِ ْن‬ ۤ


َ َ‫ﻚ ٱﻷ َْرَذﻟُﻮ َن ۞ ﻗ‬ َ َ‫﴿ﻗَﺎﻟُﻮاْ أَﻧـُ ْﺆِﻣ ُﻦ ﻟ‬
َ ‫ﻚ َوٱﺗﱠـﺒَـ َﻌ‬
ِِ ِ ِ
‫ﲔ ۞ إِ ْن أ ََ� إِﻻﱠ‬ َ ‫ﺣ َﺴﺎﺑـُ ُﻬ ْﻢ إِﻻﱠ َﻋﻠَ ٰﻰ َرِّﰉ ﻟَ ْﻮ ﺗَ ْﺸﻌُُﺮو َن ۞ َوَﻣﺂ أ ََ�ْ ﺑِﻄَﺎ ِرد ٱﻟْ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬
ِ
﴾‫ﲔ‬ ٌ ِ‫ﻧَﺬ ٌﻳﺮ ﱡﻣﺒ‬
Qaloo anu/minu laka waittabaAAaka al-ardhaloona, Qala wama AAilmee bima
kanoo yaAAmaloona, In hisabuhum illa AAala rabbee law tashAAuroona, Wama
ana bitaridi almu/mineena, In ana illa nadheerun mubeenun (Surat Ash Shuara
26:111-115)

Tafsir: Watu hao wakasema: ‘Yaani wewe unataka sisi tukuamini wakati unafuatwa
na watu wa chini kabisa’, Nabii Nuh akasema: ‘Mimi nitajuaje kile ambacho wao (hao
mnaowaona hawana thamani) walikua wakikifanya? Hesabu yao ipo kwa Mola wao,
lau kama mngekua mnajua, na mimi siwafukuzi hawa walioniamini, kwani mimi ni
Muonyaji tu aliewazi’

Ama tunapozungumzia hesabu ya Dhambi basi hua kua dhambi za aina tatu, yaani kuna
dhambi ambazo kiumbe hua ni mwenye kuzifanya dhidi ya Mola wake, na kuna ambazo
hua anazifanya dhidi ya viumbe wenzake, na kuna dhambi ambazo kumbe hua anazifanya
dhidi ya Nafis yake na hivyo kua ni mwenye kujidhulumu mwenyewe Nafsi yake, na
hesabu ya Dhambi zote hizi mbali ya kua Allah Subhanah wa Taála anazijua na anaziona
kila zinapofanywa lakini pia hua ni zenye kuhudhurishwa mbele yake, hivyo bila ya
shaka yeye ndie mwenye hesabu za waja wake wote.

Hivyo Nabii Nuh akaendelea kuwaambia tena watu hao:


230

ِ ِ ِ ِ ِ ِ ‫﴿أ َِن ٱﻋﺒُ ُﺪواْ ﱠ‬


َ ‫ٱﻪﻠﻟَ َوٱﺗﱠـ ُﻘﻮﻩُ َوأَﻃﻴﻌُﻮن۞ ﻳَـ ْﻐﻔْﺮ ﻟَ ُﻜ ْﻢ ّﻣﻦ ذُﻧُﻮﺑِ ُﻜ ْﻢ َوﻳـُ َﺆ ّﺧْﺮُﻛ ْﻢ إ َ ٰﱃ أ‬
‫َﺟ ٍﻞ‬
﴾‫ٱﻪﻠﻟِ إِ َذا َﺟﺂء ﻻَ ﻳـُ َﺆ ﱠﺧﺮ ﻟَﻮ ُﻛﻨﺘُﻢ ﺗَـ ْﻌﻠَﻤﻮ َن‬ ‫َﺟ َﻞ ﱠ‬ ِ
َ ‫ﱡﻣ َﺴ ًّﻤﻰ إ ﱠن أ‬
ُ ْ ْ ُ َ
Ani oAAbudoo Allaha waittaqoohu waateeAAooni; Yaghfir lakum
min dhunoobikum wayu-akhkhirkum ila ajalin musamman inna ajala Allahi idha
jaa la yu-akhkharu law kuntum taAAlamoona (Surat Nuh 71:4-5)

Tafsir: Muabudini Allah na Muogopeni na Mnitii mimi. Allah atakusameheni madhambi


yenu na atakuakhirishieni majaaliwa yenu aliyokujaalieni. Kwani kwa hakika Majaaliwa
ya Allah yakija hua hayaepukiki lau kama mgelijua.

Hivyo Nabii Nuh anawawekea wazi watu wake njia za kupita ili kupata kuingizwa
kwenye Rehma za Mola wao na maneno yake katika aya hii yanatupa mazingatio ya kua
ni pale tutakapokua ni wenye kumtii Allah Subhanah wa Ta’ala basi ndipo tutakapokua
ni wenye kua na nafasi ya kuingia katika Rehma zake na hivyo kua ni wenye kusamehewa
dhambi zetu, kwani amesema Allah Subhanh wa Ta’ala katika Qur’an kua:

‫ٱﻪﻠﻟَ ﻳـَ ْﻐ ِﻔُﺮ‬


‫ٱﻪﻠﻟِ إِ ﱠن ﱠ‬
‫َﺳَﺮﻓُﻮاْ َﻋﻠَ ٰﻰ أَﻧ ُﻔ ِﺴ ِﻬ ْﻢ ﻻَ ﺗَـ ْﻘﻨَﻄُﻮاْ ِﻣﻦ ﱠر ْﲪَِﺔ ﱠ‬ ِ ‫﴿ﻗُﻞ ﻳٰﻌِﺒ ِﺎد ﱠ‬
ْ ‫ﻳﻦ أ‬
َ ‫ى ٱﻟﺬ‬
َ َ ْ
﴾‫ﲨﻴﻌﺎً إِﻧﱠﻪُ ُﻫﻮ ٱﻟْﻐَ ُﻔﻮر ٱﻟﱠﺮِﺣﻴﻢ‬ َِ ‫ٱﻟ ﱡﺬﻧُﻮب‬
َ
ُ ُ َ
Qul ya AAibadiya alladheena asrafoo AAala anfusihim la taqnatoo min rahmati
Allahi inna Allaha yaghfiru aldhdhunooba jameeAAan innahu huwa alghafooru
alrraheemu(Surat Az Zumar 39:53)

Tafsir: Sema: ‘Enyi Waja wangu waliovuka mipaka dhidi ya Nafsi zao (kwa kufanya
maovu) msivunjike moyo na Rehma za Allah, kwani kwa Hakika Allah anasamehe
dhambi zote, kwa hakika yeye ni mwingi wa Kusamehe na ni mwingi wa Rehma.’

Ambapo aya inatuthibitishia namna Allah Subhanah wa Ta’ala alivyokua na Ukarimu


na Huruma kwaViumbe wake kua tusivunjike Moyo kutokana na Usamehevu wake na
Rehma zae. Na hii ni kutokana na yeye Muumba kua ni wenye kuwajua viumbe wake na
Udhaifu wao ndani ya Nafsi zao, na ni mwenye kujua upinzani wao dhidi ya Nafsi zao
na Adui yao yaani Ibilis Laanatu Allah.
231

Na ingawa wengi miongoni mwa Wanazuoni wana mtizamo wa kua aya hii
inawazungumzia wasiokua Waislam kutokana na makosa waliyoyafanya katika
Ujahiliyyah wao kua watasamehewa madhambi yao yote bada ya kusilimu kwao na kua
ni wenye kufanya mema baada yake, ambapo mfano mzuri ni ule wa Khalid Ibn Walid
Radhi Allahu Anhu aliposilimu na kumuomba Rasul Allah Salallu Aalayhi wa Salam
mara tatu kua amuombee ili apate msamaha wa Allah Subhanah wa Ta’ala kutokana na
makosa yake aliyoyafanya katika zama za Ujahiliya ikiwemo kuwaua Waislam kadhaa
katika Vita vya Uhud na kusababisha madhara makubwa sana yaliyohatarisha Usalama
wa Uislam na Waislam kwa ujumla na hivyo Rasul Allah Salallu Aalayhi wa Salam
akamwambia Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu kua: ‘Hakika Madhambi yako yote
yaliyopita yamesamehewa mara tu baada ya Kusilimu kwako.’

Ambapo pia sababu ya kushushwa aya pia ni kua Kuna Mapagani ambao walikua
wamshafny makosa mengi sana, ikiwemo Zina na Kuua pia, hivyo walipofika mbele ya
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kutaka kusilimu kutokana na kuvutiwa na
ujumbe wa Uislam basi wakamwambia Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam kua:
‘Hakika juu ya kile unachowaitia Watu basi ni Kizuri sana, lakini jee unatumbiaje
kuhusiana na mambo yaliyofanywa na watu kama sisi?’ hivyo Allah Subhanah wa
Ta’ala akashusha aya mbili ambapo moja wapo ni ile inayosema:

‫ٱﻪﻠﻟُ إِﻻﱠ‬
‫ﺲ ٱﻟﱠِﱴ َﺣﱠﺮَم ﱠ‬ ‫ﻔ‬ْ ‫ـ‬‫ﱠ‬
‫ﻨ‬ ‫ٱﻟ‬ ‫ن‬
َ ‫ﻮ‬ُ‫ﻠ‬‫ـ‬‫ﺘ‬
ُ ‫ﻘ‬
ْ ‫ـ‬‫ﻳ‬ ‫ﻻ‬
َ ‫و‬ ‫ﺮ‬ ‫آﺧ‬
َ ‫ﺎ‬‫ﻬ‬َ ‫ـ‬
ٰ‫ﻟ‬
َِ‫ٱﻪﻠﻟِ إ‬
‫ﱠ‬ ‫ﻊ‬ ‫ﻣ‬ ‫ن‬َ ‫ﻮ‬ُ‫ﻋ‬‫ﺪ‬ْ ‫ﻳ‬ ‫ﻻ‬
َ ‫ﻳﻦ‬‫ﺬ‬ِ ‫﴿وٱﻟﱠ‬
َ َ َ َ َ َ َ َ َ
﴾ً‫ﻚ ﻳَـ ْﻠ َﻖ أَ َﺎﺛﻣﺎ‬ ِ ْ ِ‫ﺑ‬
َ ‫ﭑﳊَِّﻖ َوﻻَ ﻳَـْﺰﻧُﻮ َن َوَﻣﻦ ﻳَـ ْﻔ َﻌ ْﻞ ٰذﻟ‬
Waalladheena la yadAAoona maAAa Allahi ilahan akhara wala yaqtuloona
alnnafsa allatee harrama Allahu illa bialhaqqi wala yaznoona waman
yafAAal dhalika yalqa athaman(Surat Al Furqan 25:68)

Tafsir: Na wale ambao hawawaombi Miungu wengine pamoja na Allah, wala


hawakuua Nafsi aliyoiharamisha Allah isipokua kwa haki, na wala hawajazini, na kila
aliefanya hivyo basi atapata adhabu.

Na kisha akashusha aya hio ya Surat Az Zumar 39:53.

Lakini pia kwa upande mwengine basi kuna ile hadithi mashuhuri ya mtu alieua watu 99
ambayo anasem Imam Muslim kua; ‘Amesema Abu Said Al Khudhri Radhi Allahu Anhu
kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kulikua kuna mtu
miongoni mwa wliotangulia kabla yenu, ambae alikua ameua watu 99. Hivyo
akaulizia kuhusiana na mtu mwenye Ilm zaidi katika Ardhi, hivyo akaelekezwa
232

kwa Kuhani. Na hivyo mtu huyu akatoka hadi kwa Kuhani na kumuuliza kama
kuna Toba yake, na hivyo Kuhani huyo akasema : ‘Hakuna’ hivyo mtu huyo
akamuua Kuhani huyo na kutimiza idadi ya watu 100.

Kisha akauliza kuhusiana na mtu mwenye Ilm kubwa zaidi Ardhini, na


akaelekezwa kwa Mwanazuoni, ambae alimwambia kua yeye ameshaua watu 100.
Hivyo jee anayo nafasi ya Kutubu?’ Mwanazuoni huyo akamjibu kwa kumwambia:
‘Bila ya Shaka, kwani ni nani atakaeweza kukaa baina yake yeye na Toba yake?’
kisha akamuelekeza katika kijiji ambacho ndani yake wanakaa wacha Mungu. Na
kumwambia: ‘Na wewe pia nenda kakae nao ujitolee kwa ajili ya Allah na kamwe
usirudi katika mji ambao uliiku sio mji mzuri.’

Hivyo Mtu huyo akaondoa kuelekea katika Mji huo na alipofika katikati njiani
yakamkuta mauti, hivyo Malaika wa Rehma na Malaika wa Adhabu wakaanza
kugombaniana nae. Malaika wa Rehma akasema; ‘Huyu alikuja kutubu huku
Moyo wake ukiwa umemuelekea Allah.’ Na Malaika wa Adhabu akasema: ‘Huyu
hajawahi kufanya Jema hata moja katika Maisha yake.’ Hapo akatokea Malaika
akiwa katika maumbile ya Mtu ambae wakamteua kua mpatanishaji baina yao
akasema: ‘Pimeni masafa mawili ya Ardhi na kisha Mchukulieni kutokana na yale
ambayo yanaonesha kua anayakaribia’ na hivyo wakamkuta akiwa anakaribia
katika sehemu ya Ardhi ambayo anaielekea kwa kuzidi Nyanda moja. Hivyo
Malaika wa Rehma akaichukua Roho yake Mtu huyo’

Ambapo katika Hadithi nyengine basi tunaona kua inasema kua Mtu huyu alikua
anatambaa akielekea kwenye toba wakati kifo kilipomfikia, na hivyo Allah
Subhanah wa Ta’ala akaiamrisha Ardhi anayoielekea kujikunja, na akaiamrisha
Ardhi anayotokea Kujivuta.

Ambapo kwa upande wa Sahaba Mwanazuoni Abd allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu
na Wanazuoni wengine basi tunaona wanasema kua: ‘Maneno ya Aya hii yanawagusia
Waumini ambao mbali ya kua na Dhambi Kubwa na Ndogo basi wasivunjike Moyo
na Rehma za Allah Subhanah wa Ta’ala, kwani wanaweza wakasamehewa kama
ikiwa wataomba Msamaha’(Imam Ibn Jarir At Tabari.)

Ambapo anasema Imam Muhammad Ibn Is-haq kua ‘Umar Ibn Al hattab Radhi Allahu
Anhu alisema kua: ‘Hakika mimi nilikua nikijua katika nafsi yangu kua Allah
Subhanah wa Ta’ala hatokubali kitu chochote kua kama ni fidiya au toba kutoka
kwa walioamini, ambao kutokana na mitihani yao basi wakawa ni wenye kuangukia
kwenye kufuru, au hawakufanya Hijra lakini wakabakia katika mji wa Makkah,
hadi pale Allah Subhanah wa Ta’ala aliposhusha aya hii.’
233

Hivyo nami nikayandika na kuyatuma kwa Hisham Ibn Al As na kumwambia:


‘Wakati ziliponifikia basi nikaanza kupanda na kushuka katika Dhu Tuwa huku
nikiisoma kwa sauti kubwa, bila ya kuweza kufaham maana yake, na kisha
nikasema: ‘Ya Allah nipe maana ya maneno haya’ hivyo Allah akanijalia ndani ya
Moyo wangu kua ni mwenye kujua kua aya hii imekususdiwa kwa ajili yetu,
kutokana na namna tulivyokua tukijifikiria na hivyo kua inatuzungumzia sisi, hivyo
nikapanda Ngamia wangu na kuenda kuungana na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
Salam.’’(Imam Al Qurtubi)

Ambapo katika kutuonesha ukubwa wa Rehma zake Allah Subhanah wa Ta’ala juu yetu
basi amesema Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu kua: ‘Aya zenye Nguvu zaidi
katika aya za Qur’an kuhusiana na uthibitisho wa kiuaminifu basi ni zile aya
zisemazo:

‫۞وﻳَـْﺮُزﻗْﻪُ ِﻣ ْﻦ‬ ‫ﱠ‬ ِ ‫ﭑﻪﻠﻟِ وٱﻟْﻴـﻮِم‬


‫ٱﻵﺧ ِﺮ َوَﻣﻦ ﻳـَﺘ ِﱠﻖ ﱠ‬ ِ ِ ﴿
َ ً‫ٱﻪﻠﻟَ َْﳚ َﻌﻞ ﻟﻪُ ﳐََْﺮﺟﺎ‬ ْ َ َ ‫َﻣﻦ َﻛﺎ َن ﻳـُ ْﺆﻣ ُﻦ ﺑ ﱠ‬
‫ٱﻪﻠﻟَ َﺎﺑﻟِ ُﻎ أ َْﻣ ِﺮﻩِ ﻗَ ْﺪ َﺟ َﻌ َﻞ‬
‫ٱﻪﻠﻟِ ﻓَـ ُﻬ َﻮ َﺣ ْﺴﺒُﻪُ إِ ﱠن ﱠ‬
‫ﺐ َوَﻣﻦ ﻳَـﺘَـ َﻮﱠﻛ ْﻞ َﻋﻠَﻰ ﱠ‬ ِ َ‫ﺚ ﻻَ َﳛﺘ‬
ُ ْ ُ ‫َﺣْﻴ‬
‫ﺴ‬
﴾ً‫ٱﻪﻠﻟ ﻟِ ُﻜ ِﻞ َﺷﻲ ٍء ﻗَ ْﺪرا‬
ْ ّ ُ‫ﱠ‬
Man kana yu/minu biAllahi waalyawmi al-akhiri waman yattaqi Allaha yajAAal
lahu makhrajan; Wayarzuqhu min haythu la yahtasibu waman yatawakkal AAala
Allahi fahuwa hasbuhu inna Allaha balighu amrihi qad jaAAala Allahu likulli shay-
in qadran(Surat At Talaq 65:2-3)

Tafsir: Na yeyote yule atakaemuamini Allah na siku ya mwisho na akamcha Allah basi
atamjaalia njia ya kutoka na anatamruzuku kutokana na njia ambazo hakuzihesabu,
na atakamtegemea Allah basi atamtosheleza kwa ajili yake, kwani kwa hakika Allah
ni mwenye kumkamilishia mahitaji yake, kwa hakika Allah amejaalia kila kitu kwa
Makadirio maalum.

Ambapo anasema Imam Ahmad Ibn Hanbal kua: ‘Amesema Abu Dhar Radhi Allahu
Anhu kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alinisomea aya hii mwanzo mpaka
mwisho, na kisha akisoma na kuirudia tena na tena juu yangu mpaka nikaanza
kusinzia. halafu akasema: ‘Ya Abu Dhar! kama watu wataichukulia kiroho aya hii
basi itawatosheleza. ’

Kisha akaanza kuisoma tena mpaka nikaanza kusinzia, kisha akasema: ‘Ewe Abu
Dhar! Hivi jee kama ukifukuzwa kutoka katika Mji wa Madina utafanya nini?’
Nami nikajibu: ‘Nitaelekea katika maeneo makubwa na mapana na yenye usalama
234

mpaka niwe kama Njiwa mongoni mwa Njiwa wa Makkah.’ Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam akasema: ‘Hivyo jee utafanya nini kama ukifukuzwa kutoka
kwenye Mji wa Makkah?’ nami nikasema: ‘Nitaelekea katika maeneo makubwa na
mapana ya Syria na maeneo ya ardhi takatifu’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Hivi jee utafanyaje kama
ukifukuzw kutoka kwenye ardhi ya Syria?’ nami nikajibu: ‘Wa Allahi, kutokana
na jambo hilo basi mimi nitachukua Upanga’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
akasema: ‘Au utajafanya jambo jengine bora zaidi yake’ nami nikamjibu: ‘Au
nitafanya Jambo bora zaidi yake’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Kusikiliza na Kutii, hata kama
ikiwa ni kutoka kwa Mtumwa kutoka Abyssinia.’’

Na bila ya shaka maneno haya ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam yalikua
yanabashiria kile kitakachomtokea Abu Dhar Radhi Allahu Anhu hapo baadae katika
maisha yake, ambapo ilimbidi ahame kutoka katika Mji wa Madina kuelekea katika Mji
wa Makkah na kisha akahamia katika mji wa Damascus nchini Syria ambako nako
hakudumu kutokna na kua ni mwenye kuukosoa Utawala wa Muawwiyah Ibn Abu
Sufyan Radhi Allahu Anhu hivyo akaamriswa ahame kutoka kwenye ardhi ya Syria ili
akakae katik mji wa Rabdha ambao uko nje ya Mja wa Madina.

Ambapo anasema Abu Ayub Al Ansari Radhi Allahu Anhu ambae laikua anakaribia
katika sakarat ul mawt kua: ‘Hakika mimi kuna kitu nimekificha juu yenu ambacho
niliisikia kutoka kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambae aliniambia kua:
‘Hata kama ikiwa hamtofanya dhambi basi Allah Subhnah wa Ta’ala atawaleta
watu ambao watafanya Dhambi na kisha wataomba msamahaa wa Allah Subhanah
wa Ta’ala nae atawasamehe madhambi yao. ’’(Imam Ibn Hajar Al Haytami)

Naam, na kwa upande mwengine basi aya hii ya Surat Az Zumar 39:53 imezungumzia
juu ya Majaaliwa au Qadar ambapo tunapoingalia kwa kina zaidi basi tunaona kua Qadar
nazo pia zimegawika katika aina mbili: Aina ya kwanza hua ni Al Qadr Al Mubram
(isiyobadilika) na aina ya pili hua ni Al Qadr Al Muallaq (Inayobadilika kwa Masharti au
kwa Al Asbab). Na hii ni kwa sababu Allah Subhnah wa Ta'ala ameyaandika majaaliwa
juu ya kila kitu alichokiumba katika vitabu viwili tofauti ambavyo ni Lawh Al Ithbati na
Lawh Al Mahfoudh.

ِ َ‫ﻨﺪﻩُ أُﱡم ٱﻟْﻜِﺘ‬


﴾‫ﺎب‬ َ ‫ﺖ َو ِﻋ‬
ُ ِ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻣﺎ ﻳَ َﺸﺂءُ َوﻳـُﺜْﺒ‬
‫﴿ﳝَْ ُﺤﻮ ﱠ‬
235

Yamhoo Allahu ma yashao wayuthbitu waAAindahu ommu alkitabi (Surat Radd


13:39)

Tafsir: Allah Subhanah wa Ta'ala hufuta akitakacho na huthibitisha akitakacho. Na


kwake yeye ndio kwenye Kitabu Mama (Al Lawh Al Mahfudh)

Hivyo Allah Subhanah wa Ta'ala hua ni mwenye kufuta au kuakhirisha kile akitakacho
katika Majaaliwa yake juu ya mja wake kulingana na mazingira yanayotokana na Al
Asbab, majaaaliwa ambayo hua yameandikwa kwenye Al Lawh Al Ithbati na bila ya
shaka tunapozungumzia juu ya Al Qadar Al Muallaq basi hua ni ile Qadr ambayo
imeandikwa kwenye Al Lawh Al Ithbati yaani ni kitabu ambacho ndani yake mna
majaaliwa ya kila kiumbe ambayo inabidi yathibitishwe na kiumbe husika kulingana na
matumizi mazuri ya Neema za ufaham, akili na hiari aliyojaaliwa kiumbe huyo na Allah
Subhanah wa Ta'ala na hivyo Qadar ya mtu husika hua inaweza kubadilika kwa
kulingana na Masharti ya namna anavyoishi kiumbe husika hapa ulimwenguni.

Na tunapozungumzia juu ya Al Qadar Al Mubram basi hua ni ile Qadr ambayo


imeandikwa kwenye Al Lawh Al Mahfudh yaani ni kitabu ambacho ndani yake mna
majaaliwa ya kila kiumbe ambayo kamwe hayawezi kubadilishika katika kuishi kwake
kiumbe husika hapa ulimwenguni na kesho Akhera pia.

Ili kufahamu vizuri zaidi basi na tuchukulie mfano: Kama alivyosema Nabii Nuh katika
aya kua Yaghfir lakum min dhunoobikum wayu-akhkhirkum ila ajalin musamman
yaani Allah Subhanah wa Ta'ala atakusameheni madhambi yenu na
atakubadilishieni Majaaliwa yenu juu ya aliyokujaalieni.

Yaani hali inakua kama alivyothibitisha Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam kua katika
hadith kua: 'Qadr haibadilishiki isipokua kwa Dua, na hakuna kinachoongeza
maisha ya mtu isipokua Amali njema.'(Imam At Tirmidhi, Mustadrak Al Hakim) na hii
pia ndio maana ya ile aya isemayo kua:

﴾‫ﻳﺪﻧﱠ ُﻜﻢ وﻟَﺌِﻦ َﻛ َﻔﺮُْﰎ إِ ﱠن َﻋ َﺬ ِاﰉ ﻟَ َﺸ ِﺪﻳ ٌﺪ‬ِ ِ ِ﴿


ْ َ ْ َ ‫َوإ ْذ َﺄﺗَذﱠ َن َرﺑﱡ ُﻜ ْﻢ ﻟَﺌﻦ َﺷ َﻜْﺮُْﰎ َﻷَز‬
Wa-idh taadhdhana rabbukum la-in shakartum laazeedannakum wala-in kafartum
inna AAadhabee lashadeedun (Surat Ibrahim 14:7)

Tafsir: Na anatangazia Mola wenu kua: 'Kama mkinishukuru basi bila ya shaka
nitakuzidishieni na lakini kama mkinikufuru basi adhabu yangu ni kali sana'

Anasema Imam Abu Al Ḥasan Ali Ibn Uthmān Ibn ʿAli Al Ghaznawi Al Jullabi Al
Hujwiri kua: 'Hakika mimi niliwaona Masahaba wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
236

Salam walivyokua kuhusiana na Qadr kua ni kuamini kua kila kitu kimo ndani ya
udhibiti wa Allah Subhanah wa Ta'ala, huku watu wakiwa wanajichukulia kua
kama kwambo kila kitu chao kipo chini ya udhibiti wao' (Kashf Al Mahjub)

Kwa upande mwengine basi alisema pia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika
Hadith al Quds kua: 'Amesema Allah Subhanah wa Ta'ala kua mja huweka nadhiri
juu ya kile tu ambacho nimemjaalia kua kitokee kulingana na atakavyonadhiria na
kupitia katika nadhiri yake hio basi mimi hua ni mwenye kuchukua sehemu kutoka
kwa mtu alie bakhili'

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Shaykh ul Islami Al Hafidh Imam Ibn Hajar Al
Asqallani kua: 'Amesema Imam Al Baydawi kua hii ni kuhusiana na tabia ya watu
ambao huweka nadhiri kutokana na kupata neema na kukingwa na madhara, yaani
nadhiri ni kitu ambacho kimekatazwa kutokana na kua kitendo cha mtu mbakhili,
kwani mtu mkarimu anapokitaka kitu kizuri basi hujitahid mwenyewe mpaka
akakipata lakini mtu mbakhili hua hawezi kujitahid mpaka ajue kua atapata
malipo kutokana na kujitahid kwake huko.

Na hali hii hua haibadilishi hali ya majaaliwa kwani hua hakuna jambo jema
litakalopatikana kwa upande wa mtu huyo bakhili isipokua kile alichojaaliwa tu.
Na hivyo hua hakuna jambo ambalo litamsaidia yeye kumuepusha na madhara
yaliyojaaliwa kumfika, kiasi ya kua atafikwa na jambo lenye madhara ambalo
litampelekea kutoa kile ambacho asingetoa bila ya kufikwa na jambo hilo.'

Na akasema Shaykh Al Akbar Imam Abu Bakr Ibn Al Arabi kua: 'Hadithi hii hua ni
uthibitisho wa kua yule mtu ambae atakua ni mwenye kuweka nadhiri basi ni
lazima atomize nadhiri juu ya kile alichokinadhiria kutokana na kua hadith
imesema 'kuchukua kutoka kwa mtu mbakhili' kwani kama mtu huyo asinge
wajibishwa kutimiza kufanya juu ya kile alichokinadhiria, basi maelezo juu ya kua
na ubakhili yangekua hayahusiani na kuweka nadhiri. Kama mtu angekua huru na
kutotimiza nadhiri basi mtu huyo angebakia kua na ubakhili pia bila ya hata
kutimiza dhadhiri hio'

Kisha Shaykh Al Akbar Imam Abu Bakr Ibn Al Arabi anamalizia kwa kusema kua:
'Nadhiri hua ni sawa na Dua yaani hua haziepushi majaaliwa, bali hua ni sehemu
ya majaaliwa. Na kwa upande mmoja Nadhiri hua hazipendekezwi, lakini kwa
upande wa pili basi Dua hua zinapendekezwa. Na Dua hua zinapendekezwa kwa
sababu Dua hua ni sehemu ya Ibada ambayo inaweka udhaifu wa Kiumbe mbele
ya Mola wake. Wakati nadhiri hua hazipendekezwi kwa sababu hua ni zenye
kuchelewesha kitendo cha Ibada mpaka kwanza litekelezeke sharti fulani'

Tumalizie juu ya majaaliwa kwa kusema kua Allah Subhanah wa Ta'ala amepanga
237

majaaliwa yawe katika hali ya Al Qadr Al Mubram na Al Qadr Al Muallaq katika vitabu
viwili tofauti ambavyo ni Lawh Al Ithbati na Lawh Al Mahfoudh kwa ajili ya kuwatia ari
waja wake katika kufanya mema, kwani kwa kua Mja hua si mwenye kujua juu ya
majaaliwa ya Allah Subhanah wa Ta'ala juu a yake katika Lawh Mahfudh na hivyo basi
basi kwa kupitia katika katika Lawh Al Ithbati atakua ni mwenye kuthibitisha kufanya
mema na hivyo hua ni mwenye kujikinga na madhara na hapo hapo kua ni mwenye
kupata thawabu kutokana na kufanya mema yake hayo.

Vile vile Allah Subhanah wa Ta'ala amejaalia kua na Qadr mbili hizi na vitabu viwili
hivi kwa sababu ya kutaka waja wake wasiwe wavivu na hivyo wawe ni wenye kufanya
mambo yao kulingana na Hukum, Shariah, Asbab na Athari zinazotokana na Al Asbab
husika kwani Waja hao ni wenye kuishi katika Ulimwengu wenye Hikma, wa mfano mtu
anapoumwa hua ni mwenye kula dawa ilia apone kwa ajili ya kuendeleza maisha yake
na hivyo mtu huyo hua ni mwenye kuishi Ulimwenguni huku akiwa ni mwenye kujitahid
kufuata njia za kimaumbile kwa kutumia neema alizopewa na Mola wake akili, afya,
ufaham, ilm. Khiari n.k ambazo hua ni zenye kuenda sambamba na mazingira na sababu
za matukio na athari za matukio husika katika maisha yake yote hapa ulimwenguni.


238

‫ﺇﺑﺮﺍﻫﻴﻢ ﺧﻠﻴﻠﻮ ﺍﷲ‬



239

KHALILU ALLAH IBRAHIM AÁLAYHI SALATU WA SALAAM



﴾ً‫ﺎب إِﺑْـﺮ ِاﻫﻴﻢ إِﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن ِﺻ ِّﺪﻳﻘﺎً ﻧﱠﺒِﻴّﺎ‬
ِ َ‫﴿وٱذْ ُﻛﺮ ِﰱ ٱﻟْ ِﻜﺘ‬
َ َ ْ َ
Waodhkur fee alkitabi Ibraheema innahu kana Siddeeqan Nabiyyan (Surat Maryam
19:41)

Tafsir: Na ametajwa katika Kitabu Ibrahim. Hakika yeye alikua ni alieamini na ni


Nabii.


Neno Sadiq kwa kiarabu hua ni lenye kutokana na neno Sadaqa ambalo linamaanisha
Kua mkweli, Kweli, Kua na Ikhlas, Kuthibitisha ukweli uliosemwa na mtu mwengine.
Kusadiki, Kua na Imani, Kutimiza ahadi kama inavyostahiki, Kua na uhakika. Hivyo aya
tuliyoanza nayo inaweka wazi kua moja kati ya sifa za Nabii wa pili miongoni mwa
Manabii wenye sifa za Ulu ul Azmin Minna Rusul ambae ni Nabii Ibrahim Alayhi Salaam
ni kua alikua ni Sidiqan yaani mwenye Maumbile ya kupenda kuutafuta na kuujua ukweli
halisi ulivyo.

Jina Ibrahim hua linatokana na neno Ab Rahim ambalo kwa Kiarabu hua linamaanisha
Baba Mwenye sifa ya kua na Huruma Sana. Nabii Ibrahim hakua ni mtu mkweli tu lakini
alikua ni mtu wa ukweli na ni mwenye kudumu katika hali yake ya kuamini kiukweli na
ndio maana pia Allah Subhanah wa Taála akamjaalia kua na sifa nyengine ambayo
hakupewa Nabii wala Mtume mwengine yeyote yule ambayo ni ile sifa iliyotajwa katika
aya ifuatayo:

﴾ً‫اﻪﻠﻟُ إِﺑْـَﺮِﻫ َﻴﻢ َﺧﻠِﻴﻼ‬


‫﴿و ﱠاﲣَ َﺬ ﱠ‬
َ
Waittakhadha Allahu Ibraheema khaleelan (Surat An Nisaa 4:125)

Tafsir: Na Allâh akamchukulia Ibrâhim kua Khalil (Rafiki wa karibu sana).

Katika mpangilio wa Manabii na Mitume iliyotajwa katika Qurán, basi tunaona kua
Nabii Ibrahim alikua ni Nabii wa sita, na alikua ni Nabii ambae alie miongoni mwa
viumbe waliofikia darja ya karibu sana mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala darja
ambayo inajulikana kama ‘Khalilu Allah’ yaani ‘Rafiki wa kweli wa karibu sana
240

ambae mapenzi yake yote yaliyo ndani ya moyo wake yapo kwa yule ampendae,
kiasi ya kua hua hapuguzii hata chembe katika kutekelezea haki ya ampendae,
ambapo katika hali hii hapa basi tunazungumzia mapenzi baina ya Kiumbe ambae
ni Nabii Ibrahim kwa Muumba wake ni Allah Subhanah wa Ta’ala. Nabii Ibrahim
aliitwa pia Khalilu Allah kwa sababu hakuwahi kumkatalia mtu yeyote yule msaada
na yeye kwa upande wake kamwe hakuwahi kumuomba msaada yeyote yule
isipokua Allah Subhanah wa Taála.’

Anasema Imam Jaffar As Sadiq kua: ‘Nabii Ibrahim aliitwa Khalil Allah kwa sababu
alikua akipenda kumsujudia sana Allah Subhanah wa Taála’

Nabii Ibrahim alikua ni Nabii ambae alifuatia baada ya kupita kizazi cha watu wa Nabii
Saleh. Nabii Ibrahim ambae pia ana Sifa ya kua ni Baba wa Mitume, alizaliwa katika mji
wa Ur uliopo nchini Iraq. Hii ilikua takriban miaka 4000 kabla ya kuzaliwa Nabii Isa
Aálayhi Salam.

Ama kwa upande mwengine basi anasema Abu Ummamah Radhi Allahu Anhu kua:
‘Alisema Rasul allah Salallahu Alayhi wa Salam baada ya kuulizwa: ‘Jee kuna
kipindi gani baina ya Nabii Nuh na Nabii Ibrahim?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi
wa Salam akasema: ‘Karne 10’’(Mustadrak Al Hakim, Imam Al Tabarani katika Al
Mu’jam al-Kabir)

Wanahistoria wa Kiislam wanasema kua jina lake kamili alikua akiitwa Ibrahim Ibn
Tarikh Ibn Sharough Ibn Nahur Ibn Raghu Ibn Faligh Ibn Aher Ibn Shalih Ibn
Arfghshand Ibn Sam Ibn Nuh. Ukamili wa jina hili hua una mitizamo tofauti miongoni
mwa Wanazuoni kwani ingawa kuna mitizamo kua:

Wakati mzee Tarikh alipokua na umri wa miaka 75 alikua na watoto watatu ambao ni
Ibrahim, Haran na Nahur. Haran alikua na mtoto ambae alikua akiitwa Lut ambae baadae
nae akawa Nabii kama vile alivyokua binamu yake ambae ni Nabii Ibrahim.

Na baadhi ya wanahistoria wanasema kua baba yake Nabii Ibrahim alifariki kabla ya
kuzaliwa kwa Nabii Ibrahim, hivyo Nabii Ibrahim alikua akiishi na Ami yake ambae
alikua akimwita kwa jina la Baba kama vile ilivyo kawaida ya Waarabu kwani wao hua
ni wenye kuwaita Ami zao Baba, ambae jina lake halisi lilikua ni Azar, na kuna wasemao
kua Azar, lilikua ni jina la Sanamu maarufu kwa kuabudiwa. Na kwa upande mwengine
basi na neno Azar pia hua ni lenye kumaanisha Jina la Nyota ya Mirikh (Mars) kwa Lugha
ya Babylon.

Lakini hata hivyo tukiiangalia Qurán basi tunaona inasema kua baba yake Nabii Ibrahim
alikua akiitwa Azar.
241

ِ ِ ِ ِ َ َ‫﴿وإِ ْذ ﻗ‬
َ ‫ﻚ ِﰱ‬
‫ﺿﻠَ ٍـﻞ‬ ْ ‫ﺎل إِﺑْـَﺮﻫ ُﻴﻢ ﻻًّﺑِﻴﻪ ءَ َازَر أَﺗَـﺘﱠﺨ ُﺬ أ‬
َ ‫َﺻﻨَﺎﻣﺎً ءَاﳍَﺔً إِِّﱏ أ ََر َاك َوﻗَـ ْﻮَﻣ‬ َ
﴾‫ﲔ‬ ٍ ِ‫ﱡﻣﺒ‬
Wa-idh qala ibraheemu li-abeehi azara atattakhidhu asnaman alihatan innee araka
waqawmaka fee dhalalin mubeenin (Surat Al An’am 6:74)

Tafsir: Na (kumbuka) wakati Ibrâhim alipomwambia baba yake Azar: ‘Unawafanya


Masanamu kama Mungu? Hakika, nnakuona wewe na watu wako kua mko katika
dhulma kubwa’.

Hivyo Imam Fakhr Ad Din Al Razi anasema kuhusiana na aya hii kua: ‘Maana iliyowazi
ya aya hii ni kua Baba yake Nabii Ibrahim alikua akiitwa Azar, ijapokua baadhi ya
Wanazuoni wamesema kua jina lake lilikua ni Tarikh’ (Mafatih Al Ghayb)

Imam Jalal al Din Al Suyuti anasema kua: ‘Mtizamo huu wa kua Azar si baba yake
Ibrahim, umeripotiwa kutoka katika makundi ya Salaf (Watu wa vizazi vya
mwanzo vya Kiislam), ambapoImam Ibn Abi Hatim Abd Rahman Ibn Muhammad
Ibn Idris Al Razi amenukuu kupitia katika Sanad Dhaifu (Mnyororo au msururu
wa walionukuu hadith husika ulio dhaifu) iliofikia hadi kwa Abd Allah Ibn Abbas,
Hivyo jina la baba yake Nabii Ibrahim si Azar bali ni Tarikh’.

Imam Al Suyuti anaendelea kutuambia kua: ‘Imam Ibn Abi Shayba, Imam Ibn Al
Mundhiri, na Imam Abu Hatim Abd Rahman Muhammad Ibn Idris Al Razi wote
wamenukuu kupitia katika baadhi ya Sanad Sahih kutoka kwa Mujahid ambae
alisema kua: ‘Azar sio baba yake Nabii Ibrahim, kwani yeye jina lake ni Ibrahim
Ibn Tayrah Ibn Sharukh Ibn Nahur Ibn Faligh’’ Kwa upande mwengine basi
tunaona kua kuna mtu alimuuliza Imam Ismail Abd Rahman Al Suddi : ‘Jee Baba
yake Ibrahim alikua ni Azar?’ Imam Ismail Abd Rahman Al Suddi akajibu: ‘La!
Baba yake alikua akiitwa Tarakh’ (Imam Al Suyuti katika Masalikh Al Hunafa)

Anasema Imam Abu Jafar Ibn Muhammad Ibn Jarir Al Tabari kua: ‘Ametuambia sisi
Muhammad Ibn Hamid na Sufyan Ibn Waki kua Jarir ametuambia kua amesema
Imam Al Layth Ibn Saad kua amesema Mujahid kua: ‘Azar sio baba yake Nabii
Ibrahim.’

Katika kipindi alichozaliwa Nabii Ibrahim, eneo alilokua akiishi Nabii Ibrahim A’layhi
Salaam lilikua likitawaliwa na Mfalme anaejulikana kwa jina la Namrudh Al Kabir Ibn
Kanaan Ibn Kush Ibn Sham Ibn Nuh ambae yeye pamoja na watu wake anaowatawala
walikua wakiabudia masanamu. Al Namrudh Al Kabir alikua ni mfalme wa kwanza
242

kutawala Ulimwenguni na ni Mfalme wa kwanza kua ni mwenye kuvaa kofia ya Kifalme


huku akiwa na Ufalme mkubwa sana kiasi ya kua ukubwa wake ulienea kuanzia
Mashariki hadi Magharibi ya Ardhi, ambapo katika historia ya Dunia kuliwahi kua na
Wafalme wanne tu wa aina hio ambao ni: Namrudh Al Kabir na Nebucharneza wawili
ambao walikua ni washirikina na Dhul Qarnayn na Sulayman Ibn Daud ambao
wawili hawa walikua ni Manabii wa Allah Subhanah wa Ta’ala.

Mfalme Al Namrudh Al Kabir alikua na wapiga ramli wake ambao walikua


wakimtizamia kuhusiana na matukio yatakayotokea hapo baadae, safari moja wapiga
ramli hawa katika kuangalia kwao, basi wakaona kua kuna mtoto wa Kiume ambae
atazaliwa katika mwaka unaofuatia kwa ajili ya kuja kuleta mabadilio makubwa katika
jamii ya Mfalme Al Namrudh Al Kabir kiasi ya kua atahatarisha Mamlaka ya Mfalme
Namrudh Al Kabir, kwani atakua ni mwenye kupingana na njia za kuabudu Masanamu.
Hivyo wapiga ramli hawa wakamtaarifu Mfalme Namrudh Al Kabir juu ya habari hizi.

Anasema Imam Ismail Abd Rahman Al Suddi kua: ‘Namrudh Al Kabir alilala akaota
kua kuna Nyota yenye kung’ara sana ambayo imechomoza na hivyo mwangaza
wake, ukawa umeupita na kuuziba hata mwangaza wa Jua na Mwezi, hivyo
Namrudh Al Kabir akashtushwa sana na ndoto hii na hivyo akaamua kuwaita
wachawi, na wapiga ramli wake ili wambashirie juu ya ndoto hio. Wapiga ramli hao
wakamwambia Namrudh Al Kabir kua: ‘Kuna mtoto atakaezaliwa katika Ardhi
yake ndani ya mwaka huu, huyu atakua ni mtoto ambae atauangamiza utawala
wako na maangamio ya familia yako yatatokana na mikono yake.’’

Mara tu baada ya Al Namrudh Al Kabir kupata habari hizi basi akaamuru kua kuanzia
sasa kila mwanamke mja mzito afuatiliwe, kisha akamatwe na kufungiwa ndani hadi
atakapojifungua, na kama atajifungua mtoto wa kike basi anaachiwa huru pamoja na
mtoto wake, lakini kama atajifungua mtoto wa kiume basi bila ya shaka mtoto wake huyo
atauliwa na yeye mama mtu kuachiwa huru.

Hiki kilikua ni kipindi ambacho wanawake wajawazito wengi walikamatwa isipokua mke
wa Azar ambae ambae alikua akiitwa Tuta Bint Kirain nah ii ni kulingana na mtizamo
wa Imam Muhammad Ibn Jariri At Tabari, ambapo kwa Upande wa Thiqat ad-Din Imam
Ali Ibn Al Hasan Ibn 'Asakir Al Dimashq basi yeye amesema alikua akiitwa Anmatala
Bint Yakfur na kwa upande wa Imam Abū Isḥāq Ibrahīm Ibn Isḥāq Ibn Ibrāhīm Ibn Bishr
Al Ḥarbi basi yeye anasema kua alikua akiitwa Amila.

Ingawa Amila alikua ni mja mzito lakini mimba yake ilikua si yenye kuonesha kwani
ilikua ndio mimba yake ya mwanzo na vile vile alikua ni binti mdogo kiumri na mwenye
umbo dogo pia. Kipindi hiki Azar mwenyewe alikua amesafiri bila ya kujua kua mke
wake ni mja mzito pia.
243

Ulipofika mda wa kujifungua basi usiku Amila akakimbilia katika moja kati ya mapango
yaliyo nje ya mji huo na kujificha huko hadi akajifungua, na kweli alijifungua mtoto wa
kiume ambae aliamua bora kumuachia na kumhifadhi huko huko pangoni baada ya
kuuziba mlango wa Pango hilo kwa mawe, ikawa anaenda nyumbani na kurudi kila siku
kuangalia hali ya mtoto wake ambae alikua akikua katika hali ya maajabu mbali ya kua
hapati maziwa ya kutosha ya Amila na hivyo ni mwenye kutegemea chakula chake
kutokana na kunyonya kidole chake. Mtoto huyu aliitwa Ibrahim.

Anasem Imam Al Thalabi kua: Amesema Abu Zurayq kua: ‘Kila wakati ambao mama
yake Ibrahim alipokua akimtembelea Ibrahim basi alimkuta akiwa ni mwenye
kunyonya kidole, hivyo akaamua kuangalia vidole hivyo ambapo akaona kua kidole
kimoja kinatoa Maziwa, chengine kinatoa Asali, chengine kinatoa Maji na chengine
kinatoa Samli nyepesi.’

Ingawa Nabii Ibrahim alizaliwa katika mazingira hayo lakini alikua ni mwenye kukua
haraka sana kuliko mtoto wa kawaida kwani kukua kwake kwa siku moja kulikua ni
sawasawa na kukua kwa mwezi mmoja kwa mtoto wa kawaida, kiasi ya kua hakua ni
mwenye kukaa kwa siku nyingi sana kwenye pango hilo kwani alikaa kwa wiki mbili tu
na kisha akachukuliwa na kupelekwa kuishi pamoja na watu wa jamii yake.

Azar aliporudi safari yake alimuona mtoto mdogo wa kiume katika familia yake na
alipomuuliza Amila ni nani huyo basi aliambiwa kua ni mtoto wake na kuelezewa kisa
chake basi Azar alifurahi na kumpenda sana mtoto huyo hivyo wakaamua kua
wasimwambie Mfalme Namrudh Al Kabir kuhusiana na mtoto huyo, lakini furaha hio
haikudumu kwa mda mrefu kwani mtoto huyo alianza kuuliza juu ya Mola wake.

Siku moja Ibrahim alimuuliza Amila: ‘Jee Mama, ni nani Mlezi wangu mie?’ ambapo
mama yake akasema: ‘Mlezi wako wewe ni mimi hapa.’ Nabii Ibrahim akauliza tena:
‘Na jee ni nani Mlezi wako wewe?’ Amila akasema: ‘Mlezi wangu mie ni Namrudh
Al Kabir’. Nabii Ibrahim akamuuliza tena Amila: ‘Jee ni nani Mlezi wake Namrudh
Al Kabir?’.

Hapa sasa Amila akaona huyu mtoto anataka kuniletea balaa, kwani watu wakisikia haya
masuali anayoyauliza basi itakua hakuna usalama tena, na inawezekana kua huyu ndio
yule yule alietabiriwa na watu wa Namrudh Al Kabir, hivyo akamwambia Nabii Ibrahim:
‘Fumba mdomo wako!’. Nabii Ibrahim akanyamaza kimya hakumuuliza tena Amila
masuali hayo.

Baada ya muda akatokea Azar nyumbani hapo ambapo mara tu baada ya kuingia basi
Nabii Ibrahim akaanza kumhoji juu ya kile asichokijua lakini akiwa na hamu kubwa sana
ya kukijua, yaani ni nani Mola wake, au ni Mlezi wake halisi aliemlea tangu alipokua
ndani ya tumbo la Mama yake, na simlezi wake tu bali pia mlezi wa wazazi wake na
244

Mlezi wa kila kitu kilichopo ulimwenguni kwani Nabii Ibrahim alikua akijiuliza Man
huwa Rabbi? yaani Ni nani Mola wangu?

Ambapo neno Rabbi ambalo linatokana na neno Rabba la kiarabu ambalo hua haliwezi
kufafanulika kama inavyostahili katika lugha nyengine lakini hata hivyo kwa lugha ya
Kiswahili hua linamaanisha: Mlezi, Bwana, Msimamizi, Mmiliki, Mkuzaji,
Mnawirishaji, Muamuliaji, Mkamilishaji, Mtawala, Mfalme, Msimamiaji wa kitu tangu
mwanzo hadi mwisho kitu hicho kikakamilika, na ndio maana Waarabu hua ni wenye
kusema kua: Rabb al Qawm yaani Mtawala wa Jamii ya Watu au Rabb al Sabiyyah yaani
Alimlea mtoto hadi akakua, au Rabb al Amr yaani Msimamizi wa jambo tangu mwanzo
hadi mwisho, n.k.

Ama tunapozungumzia juu ya maana ya neno Rabbi kama vile alivyokua akitaka kujua
Nabii Ibrahim basi hua linamaanisha Sifa Tukufu na Jina tukufu la Allah Subhanah wa
Taála ambalo nalo pia maana yake hua hawezi kuelezeka ipasavyo pia kwa Lugha yeyote
ile lakini kwa kujaribu tu basi tunaweza kusema kua maana yake hua ni: Mola, Muumba,
Mtoaji Rizki, Mlezi kwa kila kitu kilichomo Ulimwenguni, Msimamizi wa Viumbe vyote
na kila kitu kilichomo Ulimwenguni kuanzia mwanzo wa kabla ya kuwepo vitu hivyo,
hadi kuwepo kwake hadi mwisho wake katika kukamilika kwake kikamilifu, Mwenye
kukamilisha vitu hatua kwa hatua kuanzia kutoka katika hali moja kuingia katika hali
nyengine iwe ya kiumbo, kimwili na kiroho, n.k

Na hii haimaanishi kua Mkamilishaji huyo yaani Allah Subhanah wa Taála hawezi
kukikamilisha kitu husika hadi kipitie katika hatua kwa hatua la, kwani Sifa hii Tukufu
ya Allah Subhanah wa Taála ni yenye kujumuisha uwezo wa kukikamilisha chochote
kwa ubora wa ukamilifu iwe kwa njia ya hatua kwa hatua tangu mwanzo wake hadi
mwisho wake kitu hicho na pia uwezo wa kukikamilisha kitu kwa muendelezo kamilifu
kwa njia ya Kun fa yakunu yaani kitu husika kikaamrishwa kiwe na kikawa hapo kwa
hapo kwa ukamilifu kama anayosema mwenyewe katika Qurán kua:

ُ ‫ﻀ ٰﻰ أ َْﻣﺮاً ﻓَِﺈﱠﳕَﺎ ﻳَـ ُﻘ‬ ِ ‫﴿ﺑ ِﺪﻳﻊ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬


﴾‫ﻮل ﻟَﻪُ ُﻛ ْﻦ ﻓَـﻴَ ُﻜﻮ ُن‬ َ َ‫ض َوإِ َذا ﻗ‬
ِ ‫ات َوٱﻷ َْر‬ ََ ُ َ
BadeeAAu alssamawati waal-Ardhi wa-idha qadha amran fa-innama yaqoolu lahu
kun fayakoonu (Surat Al Baqara 2:117)

Tafsir: Muumba wa Mbingu na Ardhi na anapotaka jambo lake basi hua ni mwenye
kuliamrisha jambo hilo kua na linakua.

Na hali hii haielezeki katika kuumba tu bali inaelezeka katika kila kitu chake akitakacho
ikiwemo kufufua kila kitu upya kama inavyoelezea aya inayofuatia:
245

ْ ِ‫ض ﺑ‬ ِ ِ
ُ ‫ﭑﳊَِّﻖ َوﻳَـ ْﻮَم ﻳَـ ُﻘ‬
ُ‫ﻮل ُﻛﻦ ﻓَـﻴَ ُﻜﻮ ُن ﻗَـ ْﻮﻟُﻪ‬ َ ‫﴿ َوُﻫ َﻮ ٱﻟﱠﺬى َﺧﻠَ َﻖ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤ َﺎوات َوٱﻷ َْر‬
‫ٱﳊَ ِﻜ ُﻴﻢ‬ْ ‫ﱠﻬ َﺎدةِ َوُﻫ َﻮ‬
َ ‫ﺐ َوٱﻟﺸ‬ ِ ‫ﺼﻮِر َﻋ ِﺎﱂُ ٱﻟْﻐَْﻴ‬
‫ﻚ ﻳَـ ْﻮَم ﻳُﻨ َﻔ ُﺦ ِﰱ ٱﻟ ﱡ‬
ُ ‫ٱﳊَ ﱡﻖ َوﻟَﻪُ ٱﻟْ ُﻤ ْﻠ‬
ْ
﴾‫ٱﳋَﺒِﲑ‬
ُ ْ
Wahuwa alladhee khalaqa alssamawati waal-ardha bialhaqqi wayawma yaqoolu
kun fayakoonu qawluhu alhaqqu walahu almulku yawma yunfakhu fee alssoori
AAalimu alghaybi waalshshahadati wahuwa alhakeemu alkhabeeru (Surat Al
AnAam 6:73)

Tafsir: Yeye ndie yule ambae alieumba mbigu na Ardhi kwa haki, na katika Siku hio
atasema Kua na Kitakua. Kauli yake ni ya hakina kwake yeye ndio kuna umiliki wa
siku ambayo litapulizwa baragumu. Ni mwenye kujua yaliyofichika na yaliyowazi nani
yeye ambae ni Mwingi wa Hikma na Mwenye Habari ju ya kila kitu.

Hivyo Nabii Ibrahim akamuuliza Azar juu ya Man Huwa Rabbi? ambapo Azar akajibu:
‘Ni Mama yako,’Nabii Ibrahim akauliza tena: ‘Na ni nani Mlezi wa Mama?’ ambapo
Azar akajibu: ‘Mlezi wake yeye ni mimi hapa.’ Nabii Ibrahim akauliza tena: ‘Na jee ni
nani Mlezi wako wewe?’ Azar akajibu: ‘Mlezi wangu mie ni Namrudh Al Kabir’.
Nabii Ibrahim akamuuliza tena Azar: ‘Jee ni nani Mlezi wake Namrudh Al Kabir?’.

Hapa sasa Azar akampiga kibao cha uso Nabii Ibrahim na kisha akamwambia: ‘Fumba
mdomo wako!.’ Na ndio maana Allah Subhanah wa Taála akasema juu yake Nabii
Ibrahim kua:

ِِ ِ ِ ِ
َ ‫﴿ َوﻟََﻘ ْﺪ آﺗَـْﻴـﻨَﺂ إِﺑْـَﺮاﻫ َﻴﻢ ُر ْﺷ َﺪﻩُ ﻣﻦ ﻗَـْﺒ ُﻞ َوُﻛﻨﱠﺎ ﺑِﻪ َﻋﺎﻟﻤ‬
﴾‫ﲔ‬
Walaqad atayna ibraheema rushdahu min qablu wakunna bihi AAalimeena (Surat
Al Anbiyah 21:51)

Tafsir: Na kwa Hakika tulimpa Ibrahim uongofu wake hapo kabla, kwani tulikua
tukijua juu yake.

Anasema Qatadah Ibn Diama Al Sadusi na Mujahid Ibn Jabar kua: ‘Maana ya Min Qabl
– yaani hapo kabla iliyotumika hapa basi inamaanisha kua ‘katika kipindi cha utoto
wake’.
246

Na maana hii inayoelezewa na Qatadah Ibn Diama na Mujahid Ibn Jabar inaonekana wazi
pale tunapoona namna Nabii Ibrahim alipokua katika kipindi hiki cha utotoni mwake
alikua ni mtoto ambae aliepea kiakili na mwenye Muelekeo Sahih kimaubile na ndio
maana tukaona kua aya haikutumia neno Hudahu yaani Muongozo wake linalotokana na
neno Huda ambalo lina maana mbili, maana ya kwanza ni Kua Yahudi, na maana ya pili
ni kua katika Muongozo au kurudi katika muongozo kwa utaratibu.

Lakini aya imetumia neno Rushdahu ambalo limetokana na neno Rashada ambalo kwa
Lugha ya Kiarabu hua linaamisha: Kufuata njia iliyokua Sahih, Kua katika njia au
muelekeo ulioongozwa ipasavyo. Hivyo neno Rashada ndio lililotoa neno Rushda
ambalo maana yake hua ni Njia Sahih, Muelekeo Sahih, Usahihi wa Mambo na
Vitendo, Kuenda au kuelekea moja kwa moja katika njia iliyonyooka, Kukua kwa
Mtoto, Kukua kiakili na kiufahamu na hivyo kua na uwezo wa kusimamia mambo
sahihi ipasavyo. Kua na uwezo mkubwa na umakini wa kujua uzito majukumu na
namna ya kuyasimamia ipasavyo.

Hivyo Nabii Ibrahim alikua akijua kusudio la kuumbwa kwake, kua lazima kuna Mola
aliemuumba na hivyo ni huyo ndie anaestahiki kuabudiwa. Yaani kama tunazungumzia
juu ya aina ya Nafsi kama tulivyozifafanua hapo awali basi naam Nabii Ibrahim
alijaaliwa tangu katika kuzaliwa kwake kua ni mwenye Nafs al Mutmainah iliyo katika
ya ubora ya darja ya An Nafsi Kamilah au An Nafsi Nurriyyah au An Nafsi Muhibah.

Siku ya pili Nabii Ibrahim akatoka nje na akawaona Wanyama wa nyumbani, Farasi,
Ngamia, Ng’ombe, Kondoo n.k. Hivyo akauliza hawa ndio nani? Akaambiwa hao ni
Wanyama wa Nyumbani Farasi, Ngamia, Ng’ombe, Kondoo, hapa Nabii Ibrahim
akajiambia mwenyewe katika Nafsi yake: ‘Bila ya shaka itakua kuna Muumba
aliewaumba Wanyama hawa.’

Nabii Ibrahim alikua ni mtu wa kutafakkar kutokana na kupewa Uongofu huo na Allah
Subhanah wa Ta’ala, hivyo katika kutembea kwake akaangalia Mbinguni na Ardhini
kisha akasema: ‘Bila ya shaka, Yule ambae alieniumba mie na kunilea, na kunipa
riski yangu, chakula changu na kinywaji changu, atakua ndie Mola wangu, hakika
mimi sina Mola isipokua yeye.’

Ulipofika usiku wake katika kutembea kwake basi Nabii Ibrahim akaona Nyota ya
Mushtara (Sayari ya Jupiter) imechomoza, na kuna baadhi wanasema kua ni Nyota ya
Zuhra (Sayari ya Venus) bila ya shaka huu ulikua ni usiku wa mwisho wa mwezi wa
Kiarabu na ndio maana akaziona Nyota hizo kwanza kabla ya kuchomoza kwa Mwezi
kwa sababu baadae pale alipouona Mwezi katika usiku huo huo basi akasema: ‘Hakika
yule ndie Mola wangu.’ kama anavyosema Allah Subhanah wa Taála katika aya
zifuatazo:
247

‫ﲔ‬ ِ‫ض وﻟِﻴ ُﻜﻮ َن ِﻣﻦ ٱﻟْﻤﻮﻗِﻨ‬ ِ ‫َر‬


‫ﻷ‬ ‫ٱ‬‫و‬ ‫ات‬ ِ ‫ﻚ ﻧُِﺮ ۤي إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ ﻣﻠَ ُﻜﻮت ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬ ِ
َ ‫﴿ َوَﻛ ٰﺬﻟ‬
َ ُ َ َ َ ْ َ َ َ َ َ َ َْ
ِ ۤ
‫ﺐ‬‫ﱡ‬ ‫ُﺣ‬ ‫أ‬ ‫ﻻ‬ ‫ﺎل‬ َ َ‫۞ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ َﺟ ﱠﻦ َﻋﻠَْﻴ ِﻪ ٱﻟْﻠﱠْﻴ ُﻞ َرأَى َﻛ ْﻮَﻛﺒﺎً ﻗ‬
َ َ‫ﺎل َﻫـٰ َﺬا َرِّﰉ ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺂ أَﻓَ َﻞ ﻗ‬
‫ﺎل ﻟَﺌِﻦ ﱠﱂْ ﻳـَ ْﻬ ِﺪِﱏ َرِّﰉ‬ َ َ‫ﲔ۞ ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺂ َرأَى ٱﻟْ َﻘ َﻤَﺮ َﺎﺑ ِزﻏﺎً ﻗ‬
َ َ‫ﺎل َﻫـٰ َﺬا َرِّﰉ ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺂ أَﻓَ َﻞ ﻗ‬ ِِ
َ ‫ٱﻵﻓﻠ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ِ
َ ّ‫ﻟَـﺄَ ُﻛﻮﻧَ ﱠﻦ ﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻘ ْﻮم ٱﻟﻀﱠﺎﻟ‬
Wakadhalika nuree ibraheema malakoota alssamawati waal-Ardhi waliyakoona
mina almooqineena, Falamma janna AAalayhi allaylu raa kawkaban qala hadha
rabbee falamma afala qala la ohibbu al-afileena, Falamma raa alqamara bazighan
qala hadha rabbee falamma afala qala la-in lam yahdinee rabbee laakoonanna mina
alqawmi aldhdhalleena (Surat Al AnAam 6:75-77)

Tafsir: Na Kadhalika tukamuonesha Ibrahim Ufalme wa Mbingu na Ardhi ili awe


miongoni mwa wenye Imani na Yaqini. Wakati ulipomjia Usiku, akafunikwa na kiza
na kuona Nyota basi akasema: ‘Huyu ndie Mola wangu’ lakini ilipozama basi
akasema: Hakika mimi sipendi wale wenye kuzama. Na alipoona Mwezi unachomoza
basi akasema: ‘huyu ndie Mola wangu’ lakini ulipozama, basi akasema: ‘Kama Mola
wangu hatoniongoza mimi basi kwa hakika nitakua ni miongoni mwa watu
waliopotea’.

Ama kuhusiana na maneno yasemayo ‘Wakadhalika nuree ibraheema malakoota


alssamawati waal-Ardhi waliyakoona mina almooqineena’ yaani ‘Na Kadhalika
tukamuonesha Ibrahim Ufalme wa Mbinguni na Ardhini ili awe miongoni mwa wenye
Imani na Yaqini.’ Basi anasema Mujaddid ad Din, Sultan al Mutakallimin Imam Fakhr
ad Din al Razi kua: ‘Juu ya neno Nuriy basi amesema Imam Abu Al Ma’ali Al
Juwayni Al Haramayn kua: I’lm ya Allah Subhanah wa Taála ni kubwa isiyokua na
mpaka. Na bila ya shaka I’lm yake juu ya kila kitu haina mwisho. Kwani kila
sehemu za viumbe wake hua zinaweza kuchukua maumbo yasiyokua na mwisho.

Hivyo I’lm ya Ufalme wake haina mwisho, na bila ya shaka kuipata I’lm hio kwa
yeyote yule miongoni mwa Viumbe wake hua haiwezekani, hivyo hubidi kupatikana
kidogo kidogo hatua kwa hatua. Na Vile vile tunaona kua hapa Allah Subhana wa
Taála hakutumia neno ‘Araynahu’ ambalo hua linamaanisha ‘Tulimuonesha’ yaani
katika hali ya kitendo kilichopita lakini ni chenye kumaanisha kuoneshwa kitu
chote kwa ghafla moja hapo kwa hapo, bali ametumia neno ‘Nuriy’ ambalo
linajumuisha hali iliyopo na hali inayokuja ambako ni kwenye kumaanisha kuwepo
248

kwa kitendo ambacho kinachoendelea na hivyo chenye kuambatana na muendelezo


unaoongezeka kidogo kidogo hatua kwa hatua’

Tunapoangalia kwa upande mmoja kauli hio ya Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi
tunaonaa kua amemnukuu Imam Abu Maali Al Juwayni Al Haramayn ambae ni mwalimu
wa Hujjat ul Islami Imam Abu hamid Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali ambae
mwanafunzi wake ndie mwalimu wa Imam Fakhr Ad Din Al Razi. Kwa upande wa pili
basi tunaona kua Imam Al Haramayn ametumia Ilm al Mantiq kufananua aya hii kwa
hoja na hii ndio inatuonesha umuhimu wa Il’m ul Mantiq.

Hivyo hapa Allah Subhanah wa Ta’ala anatuonesha umuhimu wa kutumia neema ya


Ufaham na Akili aliopewa kiumbe Ibn Adam kwa ajili ya kutafakkar. Kwani ukweli ni
kua Allah Subhanah wa Ta’ala alikua na uwezo wa kumuonesha Nabii wake Ibrahim
uhalisi wa kumjua Mola wake kwa ghafla moja, lakini aliamua kufanya hivyo kwa
kutumia Hikmaya kutufunza sisi waja wake umuhimu wa Kutafakkar.

Mujaddid ad Din, Sultan al Mutakallimin Imam Fakhr ad Din al Razi anamalizia


kutuelezea kuhusiana na neno Malakut lililotumika hapa kwa kusema kua: ‘Roho za Ibn
Adam hua haiwezi kukosa kuiona Nuru ya Allah Subhanah wa Taála, isipokua kuwa
sababu ya kuwepo kwa vizuizi. Na Jee ni vizuizi gani hivyo? Hivi ni vizuizi vya yale
mambo ambayo mtu hujishughulisha nayo ambayo hua hayahusiana na Muumba
na kumpelekea mtu kua mbali na Allah Subhanah wa Taála. Na bila ya shaka vizuizi
vikubwa hua ni Masanamu.

Kwani wakati Ibrahim alipoondoa kizuizi chake kwa kujitolea kwa ajili ya Allah
Subhanah wa Taála na akakataa kuwepo kwa chengine chochote kile zaidi yake
Allah Subhanah wa Taála basi alifanikiwa kupata ubainisho wa kuwepo kwa
Muumba. Aina hii ya Ubainisho wa kuwepo kwa Muumba hua hauonekani kwa
mtizamo wa jicho la kawaida, bali hua ni wenye kuonekana kwa mtizamo wa jicho
la ndani ya Moyo, na hili ndio jambo lililomuwezesha Nabii Ibrahim kujenga hoja
zake ambazo aliziwakilisha kwa watu wake kama inayoelezewa na aya
tunazoziangalia.

Ama kuhusiana na neno Yaqin basi ni hali ya kujihakikishia kwa Moyo ambayo
hupatikana pale wakati inapokua hakuna shaka yeyote ndani ya Moyo kutokana na
vithibitisho vinavyoonekana na Moyo husika.

Ama kwa upande wa Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari anasema
kuhusiana na aya hizi kua: ‘Bila ya shaka maana ya maneno ya Falamma janna
AAalayhi allaylu raa kawkaban qala hadha rabbee aya hii yenye kumaanisha Wakati
ulipomjia Usiku, akafunikwa na kiza na kuona Nyota basi akasema: ‘Huyu ndie Mola
wangu’ yametumika kama Ta’ridh (kuashiria kwa kutosema kitu kwa kauli ya wazi
249

moja kwa moja) kwa ajili ya manufaa ya watu wake, kwani watu hao walikua wako
katika hali ya kuchanganyikiwa akili zao. Bila ya shaka tunapoamuangalia Nabii
Ibrahim basi tunaona kua yeye alikua tayari ameshaongozwa hapo kabla na Mola
wake.’

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari anaendelea kwa kusema kua:
‘Maana ya maneno: ‘La-in lam yahdinee rabbee laakoonanna mina alqawmi
aldhdhalleena, yaani ‘Kama Mola wangu hatoniongoza mimi basi kwa hakika nitakua
ni miongoni mwa watu waliopotea’ yanaamnisha kua Dini ya Nabii Ibrahim, ilikua
ni yenye kujumuisha Sakhawa (Ukarimu), na hali ya Tabbari (kua na uhuru) ya
kutotegemea mtu yeyote au kitu chochote kile isipokua ni kumtegemea pekee Allah
Subhanah wa Taála tu.’

Aya zinaendelea kutuwekea wazi namna Nabii Ibrahim alivyokua akijaribu kutafakkar mpaka
akauona ukweli halisi kwa kusema:

‫ﺎل ٰﻳـ َﻘ ْﻮِم إِِّﱏ‬ َ َ‫ﺲ َﺎﺑ ِز َﻏﺔً ﻗ‬


ْ َ‫ﺎل َﻫـٰ َﺬا َرِّﰉ َﻫـٰ َﺬآ أَ ْﻛﺒَـُﺮ ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺂ أَﻓَـﻠ‬
َ َ‫ﺖ ﻗ‬ ْ ‫﴿ﻓَـﻠَﻤﺎﱠ َرأَى ٱﻟﺸ‬
َ ‫ﱠﻤ‬
﴾‫ﺑَِﺮ ۤيءٌ ِّﳑﱠﺎ ﺗُ ْﺸ ِﺮُﻛﻮ َن‬
Falamma raa alshshamsa bazighatan qala hadha rabbee hadha akbaru falamma
afalat qala ya qawmi innee baree-on mimma tushrikoona. (Surat Al AnAam 6:78)

Tafsir: Kisha alipoona Jua linachomoza, hivyo akasema: ‘Huyu ndie Mola wangu,
Hili ndio Kubwa.’ Lakini lilipotua basi akasema: ‘Enyi watu wangu Hakika mimi nipo
huru juu ya kile mnachokishirikisha.

Ama kuhusiana na walivyokua wakimshirikisha Watu hawa na Allah Subhana wa


Ta’ala basi walikua wakimshirikisha na Sayari kwani. Na ndio maana Nabii Ibrahim
akawa ni mwenye kuchunguza vile vitu ambavyo walikua wakiviabudu watu wa
jamii yake.

Ambapo kwa upande wa Imam Al Rabghuzi basi yeye anasema kua Allah Subhanah wa
Ta’ala alimfungulia Pazia Nabii Ibrahim na hivyo akawa ni mwenye kuona
visivyoonekana kuanzia chini ardhini hadi juu Mbinguni. Na kwa upande wa Allamah
Abu Abda Allah Muhammad Ahmad Al Tarafi basi yeye ansema kua Allah Subhanah
wa Ta’ala alimfungulia Pazia Nabii Ibrahim na hivyo akawa ni mwenye kuona katika
Mbingu saba zote na Ardhi saba zote na akatafakkari juu yake kisha akauona Utukufu
wa Mola wake na akaiona sehemu yake atakayaokua kesho Peponi
250

Kwani Imam Ismail lbn Kathir basi yeye anasema kua: ‘Watu wa Dimashq
(Damascus Syria) na wale waliokua karibu na maeneo hayo walikua ni wenye
kuabudu Sayari Saba na hivyo kila geti la kuingilia katika Mji wa Dimashq
ulikua na picha za Sayari hizo, na walikua wakitoa kafara kwa ajili ya Sayari
hizi na walikua na Sikukuu ambazo zilikua na Majina ya Sayari hizo. Ambazo
ni Mirikh, Mushtara, Atarid, Zuhra, Zohal, Shams na Qamar kwa hivyo
inawezekana kua Watu wa Nabii Ibrahim walikua pia katika maeneo hayo
katika wakati huo.’(Al Bidaya wa An Nihayah)

Allamah Abu Ala Mawdud anasema kua: Kutokana na hitimisho la Sir Leonard
Wooley ambae ni Mwanasayansi wa elimu mambo ya kale ni kua: Inakadiriwa kua
katika kipindi cha miaka ya 2100 Kabla ya kuzaliwa Nabii Isa ambacho ilikua ni
kipindi alichoishi Nabii Ibrahim, basi Mji wa Ur ulikua na watu takriban 500000,
basi mji huo ulikua ni mkubwa sana kwa upande wa kimaendeleo na kibiashara,
kiasi ya kua Wafanyabiashara walikua walilete bidhaa zao katika Mji wa Ur
kutokea katika miji ya Palmer na Niligiri kwa upande mmoja na kwa upande
mwengine ilikua hadi Anatolia. Eneo la mji wa Ur ulikua umeenea hadi katika
maeneno ya Iraq kaskazini kuelekea Magharibi. Watu wake wengi walikua ni
wafanya biashara.
Jamii ya watu hawa walikua wameweka mbele sana Dunia yao katika kutafuta pesa
kiasi ya kua katika mji wao ulikua na Miungu 5000, hivyo kila sehemu ilikua na
Mungu wake, ambapo Mungu wao Mkuu alikua akiitwa Nanar ambae alikua ni
Mungu wa mwezi na ndio maana baadae akaitwa Kamarina ambalo ndio jina
lililotoa jina la Qamar ambalo kwa Kiarabu hua linamaanisha Mwezi. Miji
myengine ilikua ikijulikana kama Larsar ambao baadae ndio uliochukua nafasi ya
Ur kama mji mkuu, na Mungu wake mkuu alikua akijulikana kama Shamas ambalo
ndio lililotoa neno Shams kwa Kiarabu ambalo hua linamaanisha Jua.

Chini ya Miungu hii kulikua kuna Miungu myengine midogo midogo mingi ambayo
ilikua imechukuliwa kutokana na nyota na sayari mbali mbali zinazoelea mbinguni
ambayo watu wa Miji hii walikua wakiitumia kwa ajiili ya kuomba mambo yao
tofauti. Mungu huyo Nannar alikua amewekwa kwenye Hekalu kubwa sana la
kifahari ambalo lilikua lipo juu mlimani. Pembeni yake kulikua na Hekalu la
kuabudia la Nin Gal ambae ndie mke wa Nannar. Ambapo kila siku usiku kulikua
na mfanya Ibada wa Kike anaingia katika chumba cha kulalia cha Hekalu hilo huku
akiwa amejipamba kama bi harusi. Wanawake wengi sana walikua wamejitolea
kwa ajii ya jambo hili na wao walikua na darja kubwa katika jamii kwani walikua
wakijulikana kama Waasharati wa kidini ambao hua wanajiolea kutolewa bikira
yao na Mtu asiejulikana katika Hekalu hilo kwa ajili ya Mungu na wasimamizi wa
Mahekalu hayo walikua ni Makuhani.
251

Nannar hakua tu ndio Mungu bali alikua pia ni Mkuu wa Wafanyabiashara, Mkuu
wa Utawala, Mkuu wa Viwanda, n.k. Miti mingi ilipandwa kwenye eneo la Hekalu
lake, hivyo ilikua kila siku watu wanaleta vitu vya kutoa kafara kama vile Maziwa,
Vyakula vya Nafaka, Madini ya Dhahabu, Vitambaa na kadhalika na Makuhani wa
Hekalu hilo ndio waliokua wakipokea Kafara hizo na pia ndio waliokua
wakisimamia baadhi ya Miradi mikubwa mikubwa ya Hekalu hilo kwa ajili ya
Mungu wao.

Ndani ya Hekalu hilo kuna uwanja mkubwa ambao hua unatumika kwa ajili ya
kutolea hukmu mbali mbali na Makuhani ambao hukmu zao ni zenye kutokana na
hukmu za Nannar. Familia yenye Mamlaka ya Ufalme wa Utawala wa mji huo
unatokana moja kwa moja kwa Nannar. Yaani Mtawala wa Ardhi hio ni Nannar
isipokua Mfalme hua ni mwenye kutawala kwa kumuwakilisha Nannar. Hivyo
kutokana na kua na uhusiano huo basi Mfalme nae pia alikua na hadhi ya Mungu
wa Mji huo na hivyo alikua ni mwenye kuabudiwa.

Allamah Abu Ala Mawdud anaendelea kusema kua: Kama ikiwa Mtizamo huu wa
sayansi ya mambo ya kale ni sahih basi bila ya shaka ni jambo lililowazi kua:
Ushirikina huu haukujumuisha mfumo wa Kidini tu, bali ulijumuisha mfumo
mzima wa maisha kuanzia kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii. Hivyo
jitihada za kueneza mfumo wenye kumpwekesha Allah Subhanah wa Taála
zilizokua zikifanywa na Nabii Ibrahim hazikua tu ni zenye kupingana na kuabudu
Masanamu, bali zilikua na uzito na ugumu mkubwa sana kwani zilikua ni zenye
kutishia athari za familia ya Kifalme ambayo ni yenye hadhi Kiutawala na pia
Kimungu. Na hapo hapo pia unaathiri mfumo mzima wa kijamii, kiuchumi, kisiasa
na kuwaathiri viongozi wote na Makuhani kiasi ya kua kukubaliana na mfumo
huowa Nabii Ibrahim basi kunapelekea kuufumua msingi mzima wa maisha tangu
chini na baada ya hapo ndio unyanyuliwe msingi mpya wa maisha wa Kumuamini
Mungu mmoja. Na ndio maana mara tu baada ya Nabii Ibrahim kuanzisha jitihada
zake hizo basi akawa ni mwenye kupigwa vita si tu Namrudh Al Kabir mwenyewe
pamoja na watu walio juu katika jamii lakini pia na watu waliochini katika jamii
hio.
Hivyo Nabiii Ibrahim akawa ni mwenye kuiwekea wazi Nafsi yake kwa kusema:

‫ض َﺣﻨِﻴﻔﺎً َوَﻣﺂ أ ََ�ْ ِﻣ َﻦ‬ ِ ِِ


ُ ‫﴿إِِّﱏ َو ﱠﺟ ْﻬ‬
َ ‫ﺖ َو ْﺟ ِﻬ َﻰ ﻟﻠﱠﺬى ﻓَﻄََﺮ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤ َﺎوات َوٱﻷ َْر‬
﴾‫ﲔ‬ ِ
َ ‫ٱﻟْ ُﻤ ْﺸ ِﺮﻛ‬
252

Innee wajjahtu wajhiya lilladhee fatara alssamawati waal-ardha haneefan wama


ana mina almushrikeena (Surat Al AnAam 6:79)

Tafsir: Kwani kwa Hakika mimi nimeugeuza uso wangu kwa yule ambae ndie
alieumba Mbinu na Ardhi na Nnamuabudu yeye na kamwe mimi si miongoni mwa
Washirikina’
Na kama tulivyoona kua jitihada za Nabii Ibrahim katika kupigana vita dhidi ya
Udhalimu huu ulianzia wakati bado akiwa mdogo. Kwani mbali ya mifano tuliyoaingalia
lakini pia kuna mifano mingi ya jitihada zake hizo na tunapoangalia kisa basi tunaona
kua Baba yake Nabii Ibrahim alikua ni mwenye kuchonga na kisha kuyauza Masanamu
anayoyachonga. Katika kipindi hiki Mzee huyu alikua akimpa Nabii Ibrahim Masanamu
hayo ambayo ni Miungu akaiuze, lakini njiani Nabii Ibrahim alikua akiyanadia
Masanamu hayo kwa sauti huku akisema: ‘Nauza chenye madhara na kisichokua na
maana. Nani anataka kile ambacho hakina maana na chenye kudhuru?’

Hivyo Nabii Ibrahim akawa anaranda nayo Masanamu hayo huku akinadia kuyakashifu
na hivyo kutonunuliwa na watu, na ikifika jioni huyarudisha kwa baba yake. Baadhi ya
wakati alikua akienda nayo katika mto na kuanza kuvizamisha vichwa vya Masanamu
hayo mtoni kwenye maji huku akiyaambia: ‘Mmekaa kutwa leo bila ya kula wala
kunywa kitu chochote bila ya shaka mtakua mnahisi njaa, hebu kunyweni maji hadi
mshibe na muishiwe na kiu yenu, kwani hamna maana yeyote ile.’ Watu wakawa
wanamuona namna Nabii Ibrahim anavyowafanyia Miungu yao, hivyo nao wakaanza
kugombana nae, na Nabii Ibrahim akawa ni mwenye kujaribu kuwafumbua macho watu
hao kwa kushindana nao kwa hoja kama inavyotuelezea Quran:

‫ﺎف َﻣﺎ ﺗُ ْﺸ ِﺮُﻛﻮ َن ﺑِِﻪ إِﻻﱠ‬ ِ ِ‫ٱﻪﻠﻟ‬ ِ ِ ۤ ‫ﺎل أ َُﲢﺎ ﱡﺟ‬


ُ ‫َﺧ‬ ‫أ‬ ‫ﻻ‬
َ
َ َ َ َ‫و‬ ‫اﱏ‬ ‫ﺪ‬
َ ‫ﻫ‬ ‫ﺪ‬
ْ ‫ﻗ‬
َ‫و‬ ‫ﱠ‬ ‫ﰱ‬ ‫ﱏ‬ّ َ َ َ‫﴿ َو َﺣﺂ ﱠﺟﻪُ ﻗَـ ْﻮُﻣﻪُ ﻗ‬
‫ﻮ‬
﴾‫ن‬ َ ‫أَن ﻳَ َﺸﺂءَ َرِّﰉ َﺷْﻴﺌﺎً َو ِﺳ َﻊ َرِّﰉ ُﻛ ﱠﻞ َﺷ ْﻲ ٍء ِﻋﻠْﻤﺎً أَﻓَﻼَ ﺗَـﺘَ َﺬ ﱠﻛُﺮو‬
Wahajjahu qawmuhu qala atuhajjoonnee fee Allahi waqad hadani wala akhafu ma
tushrikoona bihi illa an yashaa rabbee shay-an wasiAAa rabbee kulla shay-in
AAilman afala tatadhakkaroona;

Tafsir: Watu wake wakaanza kugombana nae. Ambapo nae akawambia:


‘Mnagombana na mimi kuhusiana na Allah? Wakati ni yeye alieniongoza mimi.
Hakika mimi siogopi kitu kutoka kwa wenye kumshirikisha yeye, isipokua kile
atakachonitakia Allah (kunifika basi kitanifika). Kwani Mola wangu ni mwenye kujua
juu ya kila kitu, Jee hamfikirii nyie? (Surat Al An Aam 6:80)
253

Aya inatuwekea wazi kua katika kugombana kwao basi watu hawa walimtisha Nabii
Ibrahim kwa kumwambia kua kama anataka adhurike na afikwe na maafa basi na
aendelee kuwadharau na kuwadhalilisha Miungu wao hao, kwani bila ya shaka kulingana
na mtizamo wao tunaona kua watu hawa walikua wakiwaamini sana Miungu wao hao,
na hivyo kuamini kua kama vile wanavyoweza kukutilia baraka katika mambo yao, basi
pia wanaweza kukusababishia madhara Miungu hao. Jambo ambalo Nabii Ibrahim alikua
hakubaliani nao na hivyo akawaambia:

‫ﭑﻪﻠﻟِ َﻣﺎ َﱂْ ﻳـُﻨَـِّﺰْل ﺑِِﻪ َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ‬


‫ﺎف َﻣﺂ أَ ْﺷَﺮْﻛﺘُ ْﻢ َوﻻَ َﲣَﺎﻓُﻮ َن أَﻧﱠ ُﻜ ْﻢ أَ ْﺷَﺮْﻛﺘُﻢ ﺑِ ﱠ‬ ُ ‫َﺧ‬ َ‫ﻒأ‬
َ ‫﴿ َوَﻛْﻴ‬
﴾‫ن‬ َ ‫َﺣ ﱡﻖ ﺑِﭑﻷ َْﻣ ِﻦ إِن ُﻛﻨﺘُ ْﻢ ﺗَـ ْﻌﻠَ ُﻤﻮ‬ َ‫ﲔأ‬ ِ ْ ‫ى ٱﻟْ َﻔ ِﺮﻳ َﻘ‬
‫ُﺳ ْﻠﻄَﺎ�ً ﻓَﺄَ ﱡ‬
Wakayfa akhafu ma ashraktum wala takhafoona annakum ashraktum biAllahi ma
lam yunazzil bihi AAalaykum sultanan faayyu alfareeqayni ahaqqu bial-amni in
kuntum taAAlamoona.(Surat Al An Aam 6:81)

Tafsir: Na itakuaje mimi niwakhofie wale ambao mnaowashirikisha na Allah, wakati


nyinyi hamna khofu kua mna mshirikisha Allah na vile vitu ambavyo havikushushwa
kua na Mamlaka juu yenu, Jee ni upande upi wenye haki ya kua na amani baina ya
mafarakano haya. Kama nyinyi kweli mnajua?.

Baada ya Nabii Ibrahim kuwawekea wazi watu wake kua hao kua kile
wanachogombaniana kwa hoja ni kile ambacho anachokihisi yeye ndani ya moyo wake,
kwani ni Mola wake ndie aliemuongoza hadi akahisi hicho anachokihisi na kukiamini na
hivyo kuwataka watu wake watafakar na kwa kua yeye anamjua Mola wake basi hakuna
kinachomtisha kwani Allah Subhanah wa Taála ni mwenye uwezo mkubwa sana hivyo
hakuna litakalomfika isipokua lile ambalo tayari limeshaandikwa na Allah Subhanah wa
Taála limfike na yeye tayari ameshajisalimisha kwa Mola wake.

Na kisha akawahoji kua kama kweli wana akili jee ni nani miongoni mwao ambae yuko
salama na kwenye haki? Yaani wao wenye kuamini Miungu ambayo wameitengeneza
kwa mikono yao, au yeye ambae ni mwenye kumuamini Mungu ambae ndie Muumba
wa kila kitu. Na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akasema kuhusiana na wale
wenye kumuamini yeye kua ni Muumba kua:
254

ۤ ِ‫﴿ ﱠ‬
َ ‫ﻚ َﳍُُﻢ ٱﻷ َْﻣ ُﻦ َوُﻫ ْﻢ ﱡﻣ ْﻬﺘَ ُﺪو َن۞ َوﺗِْﻠ‬
‫ﻚ‬ َ ِ‫ﻳﻦ َآﻣﻨُﻮاْ َوَﱂْ ﻳَـ ْﻠﺒِ ُﺴﻮاْ إِﳝَﺎﻧَـ ُﻬ ْﻢ ﺑِﻈُْﻠ ٍﻢ أ ُْوﻟَـٰﺌ‬
َ ‫ٱﻟ ﺬ‬
‫ﻚ َﺣ ِﻜ ٌﻴﻢ‬
َ ‫ﺎت ﱠﻣﻦ ﻧﱠ َﺸﺂءُ إِ ﱠن َرﺑﱠ‬ ٍ ‫ﺣ ﱠﺠﺘُـﻨَﺂ آﺗَـﻴـﻨَﺎﻫﺂ إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ ﻋﻠَﻰ ﻗَـﻮِﻣ ِﻪ ﻧَـﺮﻓَﻊ درﺟ‬
َ َ َ ُ ْ ْ ٰ َ َ َْ َ ْ ُ
﴾‫ﻋﻠِﻴﻢ‬
ٌ َ
Alladheena amanoo walam yalbisoo eemanahum bidhulmin ola-ika lahumu al-
amnu wahum muhtadoona; Watilka hujjatuna ataynaha ibraheema AAala
qawmihi narfaAAu darajatin man nashao inna rabbaka hakeemun AAaleemun
(Surat Al An Aam 6:82-83)

Tafsir: Ni wale wenye kuamini na wakawa hawakuifunika Imani yao na dhulma, basi
kwao wao ndio kuna Amani na ndio waliopewa muongozo. Na hivyo ndivyo
vithibitisho vyetu tulivyompa Ibrahim dhidi ya watu wake. Bila ya shaka sisi
humnyanyua darja tumtakae. Kwa hakika Mola wako ni mwingi wa Hikma ni mwenye
kujua kila kitu.’

Yaani zinathibitisha kua Allah Subhanah wa Taala huwapandisha darja wenye


kumuamni lakini tunaona kua aya pia imetumia neno Libas ambalo ni lenye kumaanisha
Kufunika, Kuhifadhi au Kukificha kitu na hivyo basi aya inatuwekea wazi kua ingawa
kua na Imani ya kuwepo kwa Muumba hua ni jambo la Maumbile kwa Viumbe
walioumbwa lakini pia Imani hio huweza kua ni yenye kufunikwa na kutu ambao ni
uchafu unaousababisha Moyo wa mtu husika usione wala kuhisi chochote juu ya uhalisia
wa Muumba wake.

Neno Libas pia halikutumika katika kuainisha umuhimu wa kuifunika Imani tu lakini pia
limetumika katika kuelezea kuendeleza kizazi na kupata utulivu basi Bani Adam hao
baada ya kuoana wanatakiwa wawe Lîbas baina yao, kwa kupendana, kuheshimiana,
kusitiriana, kuhifadhiana, kufarijiana, kusaidiana n.k na ndio maana Allah Subhanahu wa
Ta’ala akasema kuhusiana na uhusiano baina ya Mume na Mke kua:-

ِ ِ
ٌ َ‫ﺎس ﻟﱠ ُﻜ ْﻢ َوأَﻧﺘُ ْﻢ ﻟﺒ‬
﴾‫ﺎس ﱠﳍُ ﱠﻦ‬ ٌ َ‫﴿ﻫ ﱠﻦ ﻟﺒ‬
ُ
Hunna libasun lakum waantum libasun lahunna (Surat Al Baqara 2:187)

Tafsir: Wao (Wake zenu) ni Lîbas kwenu na nyie (Waume zao) ni Lîbas kwao.
255

Ingawa Allah Subhanahu wa Ta’ala amewajaalia Bani Adam, Lîbas kua kama stara na
pambo la miili yao, hifadhi ya utulivu wao, na Imani yao lakini pia amewajaalia Lîbas ya
Taqwa ambayo ni pambo la Nafsi ambayo ndio Lîbas bora zaid, kama anavyosema katika
Qur’an:

ِ ِ‫﴿ﻳـﺒ ِﲎ آدم ﻗَ ْﺪ أَﻧﺰﻟْﻨﺎ ﻋﻠَﻴ ُﻜﻢ ﻟِﺒﺎﺳﺎ ﻳـﻮا ِرى ﺳﻮءﺗِ ُﻜﻢ وِرﻳﺸﺎ وﻟ‬
َ ‫ﺎس ٱﻟﺘﱠـ ْﻘ َﻮ ٰى ٰذﻟ‬
‫ﻚ‬ ‫ﺒ‬
ُ َ ً َ ْ َ ْ َ َ ُ ً َ ْ ْ َ َ َ َ َ ََ
َ
﴾‫ٱﻪﻠﻟِ ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻬ ْﻢ ﻳَ ﱠﺬ ﱠﻛُﺮو َن‬
‫ـﺖ ﱠ‬ِ ‫ﻚ ِﻣﻦ آﻳ‬ِ
َ ْ َ ‫َﺧْﻴـٌﺮ ٰذﻟ‬
Ya banee adama qad anzalna AAalaykum libasan yuwaree saw-atikum wareeshan
walibasu alttaqwa dhalika khayrun dhalika min ayati Allahi laAAallahum
yadhdhakkaroona (Surat Al A’raf 7:26)

Tafsir: Enyi Bani Adam! Tumekushushieni Lîbas (Mavazi) juu yenu ili mjifunike na
pia kua kama Rish (Mapambo); na Lîbas (Mavazi) ya Taqwa, ni bora zaid. Hizo ni
miongoni mwa aya (Dalili, alama, ushahidi, nk) za Allah ili mpate kukumbuka.

Hivyo Libas ni muhimu sana katika maisha yetu kuanzia kwenye Ndoa, Mapenzi,
Huruma, Utulivu, Stara na kadhalika, lakini Libas Ya Taqwa ambayo ndio huihifadhi
Imani hua ni muhimu zaidi ili kuifanya kuzihifadhi Nyoyo zisifunikwe na Dhulma
ambayo itapelekea kukosekana kwa Amani na Uongofu katika maisha yetu ya hapa
Duniani na kesho Akhera.

Na aya pia inatuwekea wazi kua Nabii Ibrahim alifikia darja hio kutokana na
vithibitisho vya hoja kupitia katika ufahamu wake aliopewa na Mola wake na hivyo
kua na Imani juu ya Mola wake, na kua na Imani tu hakukutosheleza peke yake bali
ilimbidi kuamua kujitolea dhidi Washirikina kwa ajili ya Mola wake Allah Subhanah
wa Ta’ala, hivyo Allah Subhnah wa Ta’ala akampandisha darja Nabii Ibrahim kama
vile alivyowapandisha baadhi ya Mitume miongoni mwa Mitume kama anavyosema
mwenyewe katika aya ifuatayo:

‫ﻀ ُﻬ ْﻢ‬ ‫ﺾ ِّﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ ﱠﻣﻦ َﻛﻠﱠ َﻢ ﱠ‬


َ ‫ٱﻪﻠﻟُ َوَرﻓَ َﻊ ﺑَـ ْﻌ‬ ٍ ‫ﻀ ُﻬ ْﻢ َﻋﻠَ ٰﻰ ﺑَـ ْﻌ‬
َ ‫ﻀ ْﻠﻨَﺎ ﺑَـ ْﻌ‬ َ ‫﴿ﺗِْﻠ‬
‫ﻚ ٱﻟﱡﺮ ُﺳ ُﻞ ﻓَ ﱠ‬
‫وح ٱﻟْ ُﻘ ُﺪ ِس َوﻟَْﻮ َﺷﺂءَ ﱠ‬
‫ٱﻪﻠﻟُ َﻣﺎ‬ ِ َ‫ﺎت وآﺗَـﻴـﻨَﺎ ِﻋﻴﺴﻰ ٱﺑﻦ ﻣﺮَﱘ ٱﻟْﺒـﻴِﻨ‬
ِ ‫ﺎت َوأَﻳﱠ ْﺪ َ�ﻩُ ﺑُِﺮ‬ ٍ
َّ َ ْ َ َ ْ َ ْ َ ‫َد َر َﺟ‬
256

‫ٱﺧﺘَـﻠَ ُﻔﻮاْ ﻓَ ِﻤْﻨـ ُﻬ ْﻢ‬ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ‫ٱﻗْـﺘـﺘﻞ ٱﻟﱠ ِﺬ‬


ُ َ‫ﻳﻦ ﻣﻦ ﺑَـ ْﻌﺪﻫﻢ ّﻣﻦ ﺑَـ ْﻌﺪ َﻣﺎ َﺟﺂءَﺗْـ ُﻬ ُﻢ ٱﻟْﺒَـﻴِّﻨ‬
ْ ‫ﺎت َوﻟَـٰﻜ ِﻦ‬ َ َ ََ
﴾‫ﻳﺪ‬ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻣﺎ ٱﻗْـﺘَـﺘَـﻠُﻮاْ َوﻟَـٰ ِﻜ ﱠﻦ ﱠ‬
ُ ‫ٱﻪﻠﻟَ ﻳَـ ْﻔ َﻌ ُﻞ َﻣﺎ ﻳُِﺮ‬ ‫ﱠﻣ ْﻦ َآﻣ َﻦ َوِﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ ﱠﻣﻦ َﻛ َﻔَﺮ َوﻟَ ْﻮ َﺷﺂءَ ﱠ‬
Tilka alrrusulu faddalna baAAdhahum AAala baAAdhin minhum man kallama
Allahu warafaAAa baAAdhahum darajatin waatayna AAeesa ibna Maryama
albayyinati waayyadnahu biroohi alqudusi walaw shaa Allahu ma iqtatala
alladheena min baAAdhihim min baAAdhi ma jaat-humu albayyinatu walakini
ikhtalafoo faminhum man amana waminhum man kafara walaw shaa Allahu ma
iqtataloo walakinna Allaha yafAAalu ma yureedu (Surat Al Baqara 2:253)

Tafsir: Hao ni Mitume! Tumewafadhili baadhi juu ya baadhi yao miongoni mwao
wamo waliozungumza na Allah, Na tukawapandisha darja baadhi yao na tukampa Isa
Ibn Maryam ubainisho na tukamuongoza na Ruhi Al Qudus (Malaika Jibril). Na
kama angetaka Allah basi wasingeuana (kwa kupigana) wale ambao walifuata baada
yao baada ya kuletewa Ubainisho, lakini walitofautiana, na hivyo miongoni mwao
waliamini na wengine miogoni mwao walikufuru. Kama Allah angetaka basi
wasingeuana lakini Allah ni mwenye kufanya yale ayatakayo.

Hivyo Allah Subhanah wa Taála ambae ni mwingi wa Hikma na ni mwingi wa Kujua,


basi hua hampandishi darja mtu yeyote tu bali hua ni mwenye kumpandisha darja mtu
anaestahiki kupandishwa darja kulingana na Hikma zake na hivyo anajua ni nani mwenye
kustahiki kupandishwa darja husika. Anasema Mujaddid ad Din Imam Fakhr ad Din Al
Razi kua: Haya matokeo ya kumnyanyua darja Nabii Ibrahim yametokana na
vithibitisho na hoja alizojaaliwa kupewa Nabii Ibrahim na Allah Subhanah wa
Taála. Hii inamaanisha kua katika kipindi hiki cha utotoni mwake basi Nabii Ibrahim
alikua tayari keshakua Nabii na Mtume wa Allah Subhanah wa Taála tayari, hivyo hakua
ni mwenye kubahatisha na kua ni mwenye kutafakkari juu ya Mola wake na ndio maana
Allah Subhanah wa Taála akasema:

﴾‫ﺐ َﺳﻠِﻴ ٍﻢ‬


ٍ ‫﴿وإِ ﱠن ِﻣﻦ ِﺷ َﻴﻌﺘِ ِﻪَ ِﻹﺑْـﺮ ِاﻫﻴﻢ۞ إِ ْذ َﺟﺂء رﺑﱠﻪُ ﺑَِﻘ ْﻠ‬
ََ َ َ َ
Wa-inna min sheeAAatihi la-ibraheema; Idh jaa rabbahu biqalbin saleemin (Surat
As Saffat 37:83-84)

Tafsir: Na miongoni mwa waliofuata njia zake (Nabii Nuh katika kumpwekesha Allah
Subhanah wa Taála) alikua ni Ibrahim. Alipokuja kwa Mola wake akiwa na Moyo
msafi.
257

Hii ni aya ambayo inatuwekea wazi kua Nabii Ibrahim tangu wakati alipokua mdogo
alikua na sifa isiyokua na mfano wake, kwani alikua na moyo ambao ni msafi na usiokua
na shaka ndani yake. Moyo wake Ulikua ni Moyo uliovishwa Libas ya Taqwa. Anasema
Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi kuhusiana na aya
hii kua: ‘Nabii Ibrahim aliishi uhai wake wote hadi kufa huku akiwa ni mwenye
Moyo msafi ambao ulikua huru usiokua na uchafu wa dhambi za kumshirikisha
Mola wake, kua na shaka, kutoamini, kutodanganya, kua na chuki au kua na
husda’

Nabii Ibrahim alijaaliwa kua miongoni mwa wale waliokua na ufahamu wa kuona
upotovu huo na kujaribu kutafuta njia ya kumuongoa baba yake na watu waliomo katika
jamii yake na hivyo kupata upinzani mkubwa sana kutoka kwao kama inavyosema
Qurán:

‫ﺖ ِﱂَ ﺗَـ ْﻌﺒُ ُﺪ‬ َ َ َ‫ـﺐ إِﺑْـَﺮِﻫ َﻴﻢ إِﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن ِﺻ ِّﺪﻳﻘﺎً ﻧﱠﺒِﻴّﺎً ۞ إِ ْذ ﻗ‬
ِ ‫ﺎل ﻻًّﺑِ ِﻴﻪ �َﺑ‬ ِ َ‫﴿واذْ ُﻛﺮ ِﰱ اﻟْﻜِﺘ‬
ْ َ
‫ﺖ إِِّﱏ ﻗَ ْﺪ َﺟﺂءَِﱏ ِﻣ َﻦ اﻟْﻌِْﻠ ِﻢ‬ ِ ‫ﻨﻚ َﺷﻴﺌﺎً ۞ �َﺑ‬
َ
ِ
ْ َ ‫َﻣﺎ ﻻَ ﻳَ ْﺴ َﻤ ُﻊ َوﻻَ ﻳـَْﺒﺼُﺮ َوﻻَ ﻳـُ ْﻐ ِﲎ َﻋ‬
﴾ً�ّ‫ﻚ ﻓَﺎﺗﱠﺒِ ْﻌ ِﲎ أَ ْﻫ ِﺪ َك ِﺻَﺮاﻃﺎً َﺳ ِﻮ‬
َ ِ‫َﻣﺎ َﱂْ َ�ْﺗ‬

Waodhkur fee alkitabi ibraheema innahu kana siddeeqan Nabiyyan, Idh qala li-
abeehi ya abati lima taAAbudu ma la yasmaAAu wala yubsiru wala yughnee
AAanka shay-an. Ya abati innee qad jaanee mina alAAilmi ma lam ya/tika
faittabiAAnee ahdika siratan sawiyyan (Surat Maryam 19:41-43)

Tafsir: Na imehadithiwa katika kitabu Ibrahim, Kwa hakika alikua ni alieamini na


Nabii. Pale alipomwambia baba yake Ewe Baba yangu kipenzi kwa nini unakiabudu
kile kisichosikia, kisichoona na kisichokusaidia kitu? Ewe Baba yangu! Hakika
imenijia mimi I’lm ambayo haikukujia wewe. Hivyo nifuate nitakuongoza katika njia
iliyonyooka sawiya.

Aya zimetumia neno Siddiqan ambalo hua ni lenye kumaanisha Mtu aliesadiki, kwa
usadikisho wa hali ya juu kabisa na ni mkweli katika kupenda kwake kutaka kuujua
ukweli na kutaka kuwaongoza watu wake katika njia sahihi kwani Nabii Ibrahim alianza
kuuusia katika familia yake yaani wazee wake, kwa kumuita baba yake kwa kutumia
neno Abati ambalo ni neno linalotokana na neno Aba ambalo maana yake hua ni Baba,
Mzazi wa Kiume, au Mlezi wa Kiume, ambapo neno Abati hua linaashiria Cheo au Darja
au Jina la Mzazi analotumia Mtoto kuonesha namna mtoto huyo anavyomjali sana na
258

kumpenda sana Baba yake, Mzee wake wa Kiume au Mlezi wake kiasi ya kua hua hataki
Mzee wake huyo kumkera au awe ni mwenye Kujisikia vibaya kihisia kutokana na lile
analotaka kumwambia, kwani neno hilo hua linatoka kwene kina cha Hisia za upendo wa
Mwenye kuita.

Na ingawa Nabii Ibrahim ametumia njia hio hio ya kutumia neno hilo katik akufikisha
ujumbe wake, na kuonesha kua anafanya hivyo kutokana na mapenzi yake ya dhati kwa
wazee wake, lakini wapi watu wa familia yake hawakutaka kumfahamu wala kumsikiliza
na bado wakataka kumpa adhabu kama aliyotaka kupewa Najiyyu Allahi Nuh Alayhi
Salam, ambayo ni adhabu ya kumpiga mawe kama zinavyosema aya zifuatazo:

ۤ ِ ِ ِ ِ ِ
‫ﺎف‬
ُ ‫َﺧ‬ َ ‫﴿ ٰ�َﺑَﺖ ﻻَ ﺗَـ ْﻌﺒُﺪ ٱﻟﺸْﱠﻴﻄَﺎ َن إِ ﱠن ٱﻟﺸْﱠﻴﻄَﺎ َن َﻛﺎ َن ﻟﻠﱠﺮ ْﲪَـٰ ِﻦ َﻋﺼﻴّﺎً۞ ٰ�َﺑَﺖ إِِّﱐ أ‬
ِ َ َ‫ﺎن وﻟِﻴﺎً ۞ ﻗ‬ ِ ِ ِ ‫ﻚ ﻋ َﺬ‬
‫َﻧﺖ َﻋ ْﻦ‬ َ ‫ﺐأ‬ ٌ ‫ﺎل أ ََراﻏ‬ ّ َ َ‫اب ّﻣ َﻦ ٱﻟﱠﺮ ْﲪَـٰ ِﻦ ﻓَـﺘَ ُﻜﻮ َن ﻟﻠﺸْﱠﻴﻄ‬ ٌ َ َ ‫أَن َﳝَ ﱠﺴ‬
‫َﺳﺘَـ ْﻐ ِﻔُﺮ‬ َ َ‫ﱠﻚ َو ْٱﻫ ُﺠْﺮِﱏ َﻣﻠِﻴّﺎً۞ ﻗ‬ ِ ِ
ْ ‫ﻚ َﺳﺄ‬ َ ‫ﺎل َﺳﻼٌَم َﻋﻠَْﻴ‬ َ ‫آﳍَِﱴ ٰ�ِﺑْـَﺮاﻫ ُﻴﻢ ﻟَﺌِﻦ ﱠﱂْ ﺗَﻨﺘَ ِﻪ َﻷَْر ُﲨَﻨ‬
﴾ ً‫ﻚ رِّ ۤﰊ إِﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن ِﰉ َﺣ ِﻔﻴّﺎ‬
َ َ َ‫ﻟ‬
Ya abati la taAAbudi alshshaytana inna alshshaytana kana lilrrahmani AAasiyyan,
Ya abati innee akhafu an yamassaka AAadhabun mina alrrahmani fatakoona
lilshshyatani waliyyan, Qala araghibun anta AAan alihatee ya ibraheemu la-in lam
tantahi laarjumannaka waohjurnee maliyyan, Qala salamun AAalayka
saastaghfiru laka rabbee innahu kana bee hafiyyan.(Surat Maryam 19:44-47)

Tafsir: Ewe Baba yangu! Usimuabudu Shaytani, kwani kwa hakika Shaytani ni Muasi
kwa Mwingi wa Rehma (Allah Subhanah wa Taála). Ewe Baba yangu! Nakuhofia mie
itakufika adhabu ya Mwingi wa Rehma dhidi yako na kisha atakua Shaytani Rafiki
yako. Akajibu (Baba yake Nabii Ibrahim): Unawachukia Miungu wangu, Ewe
Ibrahim? Kama hujasita basi hakika mimi nitakupiga mawe, hivyo kwa sasa achana
na mie huku ukiwa katika hali nzuri (kabla sijakupiga mawe). Akasema (Nabii
Ibrahim) Salamu iwe juu yako (Ewe baba yangu). Mimi nitakuombea msamaha kwa
Mola wangu hakika yeye ni Mkarimu kwangu mie.

Tunapoziangalia aya hizi basi tunaona kua zimetaja mara kadhaa jina la sifa tukufu ya
Allah Subhanah wa Taála ambalo ni Rahman yaani Mwingi wa Rehma badala ya Allah,
na hii ni kwa sababu miongoni mwa alama za mwanzo alizoziona Nabii Ibrahim
zinazothibitisha kuwepo kwa Mola wake basi ni wingi wa Rehma zake, na juu ya hili
tutaona katika kurasa zinazofuatia tutakapoangalia aya za Surat Ash Shuara ambapo
259

Nabii Ibrahim anaainisha Rehma za Allah Subhanah wa Taa’ala juu yake kwa kutumia
vithibitisho vya hoja moja baada ya nyengine.

Na mbali ya kua Nabii Ibrahim anaanza kuweka wazi sifa za Mola wake kua ni Mwingi
wa Rehma lakini kwa upande mwengine basi tunaona kua Nabii Ibrahim anaweka wazi
pia kua: ‘Haina haja ya kua Muasi wa Mwingi wa Rehma wala kua na urafiki na
Adui wa mwingi wa Rehma, yaani Shaytan ambae ni muasi kwa Mola wake, na
kuweka wazi uadui wake Shaytan kwa Ibn Adam na matokeo ya kumfuata kwake
hua hakuna kisingizio cha kuokoka na adabu ya Allah Subhanah wa Taála, lakini
hapo hapo Nabii Ibrahim anaweka wazi kua Allah Subhanah wa Taála ni Mwenye
Uadilifu wa kutomdhulumu yeyote miongoni mwa viumbe wake na pia ni mwingi
wa Rehma kwa waja wake.’

Na ingawa Nabii Ibrahim alikua ni mdogo lakini kwa kua alikua ni mwenye hikma na
Busara basi alikua akijaribu kutumia Qawl Layyina katika kumnasihi baba yake
kuhusiana na mtihani uliopo mbele yake. Lakini hata hivyo baba yake huyo hakua ni
mwenye subra na hivyo hakua ni mwenye kutafakkari kile anachokifanya kabla ya
kukifanya na pia hakua ni mwenye kusikiliza kile anachoambiwa na mtoto wake hivyo
akamwambia Nabii Ibrahim kua: ‘Kumbe Unawachukia Miungu yangu. Hivyo basi
hebu achana na mie ewe Ibrahim wakati bado ukiwa katika hali nzuri kabla ya
kudhurika kutokana na nitakacho kufanya kama ukiendela kusema maneno yako
yasiyokua na maana.’

Hivyo mbali ya kua yeye Nabii Ibrahimi alitumia kauli laini katika kuwausia kwake,
lakini badala yake wakaamua kumuonya kwa ufedhuli kua kama anataka usalama wake,
basi aondoke mbele yao kabla ya kupigwa mawe na watu hao, lakini hata hivyo Nabii
Ibrahim kamwe hakua ni mwenye kuingiwa na hasira na hivyo akatumia Kalimatul Hilm
kauli ya Ustahmilivu dhidi ya Maadui zake, ya kuwatakia Usalama na Amani na pia
kuahidi kuwaombea Dua kwa Mola wake kwani kufanya hivyo hua ni miongoni mwa
sifa za Waumini pale wanaposhambuliwa kwa kauli sizo kama inavyoainisha aya
ifuatayo:

ِ
ُ ‫﴿ َوإِ َذا َﲰﻌُﻮاْ ٱﻟﻠﱠ ْﻐ َﻮ أ َْﻋَﺮ‬
‫ﺿﻮاْ َﻋْﻨﻪُ َوﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻟَﻨَﺂ أ َْﻋ َﻤﺎﻟُﻨَﺎ َوﻟَ ُﻜ ْﻢ أ َْﻋ َﻤﺎﻟُ ُﻜ ْﻢ َﺳﻼٌَم َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ْ ‫ﻻَ ﻧَـﺒـﺘﻐِﻰ‬
َ ‫ٱﳉَﺎﻫﻠ‬ َْ
Wa-idha samiAAoo allaghwa aAAradhoo AAanhu waqaloo lana aAAmaluna
walakum aAAmalukum salamun AAalaykum la nabtaghee aljahileena (Surat Al
Qasas 28:55)
260

Tafsir: Na wanaposikia kauli za kipuuzi hukaa mbali nazo na kusema: ‘Sisi tuna amali
zetu na nyinyi mna amali zenu, Amani iwe juu yenu. Hakika sisi hatuwatafuti wajinga’

Hivyo Nabii Ibrahim akaamua kuachana na familia yake lakini huku akiendelea
kutangazia wazi wazi juu ya kile anachokiamini kwa kuhoji huku akiainisha hoja zake
zilizowazi kwa kiufahamu, kiakili na kimantiq kama zinavyotuwekea wazi aya zifuatazo:

ِ ِ ِ َ َ‫﴿وٱﺗْﻞ ﻋﻠَﻴ ِﻬﻢ ﻧَـﺒﺄَ إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ ۞إِ ْذ ﻗ‬


ْ ‫ﺎلِ ﻷَﺑِﻴﻪ َوﻗَـ ْﻮﻣﻪ َﻣﺎ ﺗَـ ْﻌﺒُ ُﺪو َن۞ﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻧَـ ْﻌﺒُ ُﺪ أ‬
ً‫َﺻﻨَﺎﻣﺎ‬ َ َْ َ ْ ْ َ ُ َ
‫ﺎل َﻫ ْﻞ ﻳَ ْﺴ َﻤﻌُﻮﻧَ ُﻜ ْﻢ إِ ْذ ﺗَ ْﺪﻋُﻮ َن۞أ َْو ﻳَﻨ َﻔﻌُﻮﻧَ ُﻜ ْﻢ أ َْو‬ َ َ‫ﲔ۞ﻗ‬ ِِ
َ ‫ﻓَـﻨَﻈَ ﱡﻞ َﳍَﺎ َﻋﺎﻛﻔ‬
ِ
‫ﺎل أَﻓَـَﺮأَﻳْـﺘُ ْﻢ ﱠﻣﺎ ُﻛْﻨـﺘُ ْﻢ‬
َ َ‫ﻚ ﻳَـ ْﻔ َﻌﻠُﻮ َن۞ﻗ‬َ ‫آﺂﺑءَ َ� َﻛ ٰﺬﻟ‬َ �َ ‫ﻀﱡﺮو َن۞ﻗَﺎﻟُﻮاْ ﺑَ ْﻞ َو َﺟ ْﺪ‬ ُ َ‫ﻳ‬
‫ﲔ۞ٱﻟﱠ ِﺬى‬ ِ
َ ‫ب ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬ ‫آﺂﺑ ُؤُﻛ ُﻢ ٱﻷَﻗْ َﺪ ُﻣﻮ َن۞ﻓَِﺈﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ َﻋ ُﺪ ﱞو ِ ۤﱄ إِﻻﱠ َر ﱠ‬
َ ‫ﺗَـ ْﻌﺒُ ُﺪو َن۞أَﻧﺘُ ْﻢ َو‬
‫ﺖ ﻓَـ ُﻬ َﻮ‬ ُ‫ﺿ‬ ْ ‫ﲔ۞ َوإِ َذا َﻣ ِﺮ‬ ِ ‫َﺧﻠَ َﻘ ِﲎ ﻓَـ ُﻬﻮ ﻳـَ ْﻬ ِﺪﻳ ِﻦ۞وٱﻟﱠ ِﺬى ُﻫﻮ ﻳُﻄْﻌِﻤ ِﲎ وﻳَﺴ ِﻘ‬
ْ َ ُ َ َ َ
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ‫ﲔ۞وٱﻟﱠ ِﺬى ُﳝِﻴﺘُِﲎ ﰒُﱠ ُْﳛﻴ‬ ِِ
َ ‫ﻳَ ْﺸﻔ‬
Waotlu AAalayhim nabaa ibraheema; Idh qala li-abeehi waqawmihi ma
taAAbudoona; Qaloo naAAbudu asnaman fanadhallu laha AAakifeena; Qala hal
yasmaAAoonakum idh tadAAoona; Aw yanfaAAoonakum aw yadhurroona; Qaloo
bal wajadna abaana kadhalika yafAAaloona; Qala afaraaytum ma kuntum
taAAbudoona; Antum waabaokumu al-aqdamoona; Fa-innahum AAaduwwun lee
illa rabba alAAalameena; Alladhee khalaqanee fahuwa yahdeeni; Waalladhee
huwa yutAAimunee wayasqeeni; Wa-idha maridhtu fahuwa yashfeeni; Waalladhee
yumeetunee thumma yuhyeeni, Waalladhee atmaAAu an yaghfira lee khatee-atee
yawma alddeeni (Surat Ash Shuara 26:69-82)

Tafsir: Na wahadithie juu yao habari ya Ibrahim; Alipomwambia baba yake na watu
wake: ‘Ni nini mnachokiabudu?’; Nao wakajibu: ‘Tunaabudu Masanamu na
tumejitoolea kwa ajili yao’; Nae akahoji: ‘Jee wanakusikieni mnapowaomba maombi
yenu?; Au Wanakunufaisheni? Au Wanakudhuruni? ’, Nao wakajibu: ‘La! Bali
kadhalika hivi ndivyo walivyokua wakifanya Mababa zetu waliotangulia; Nae akahoji:
‘Jee mnakiangalia kile mnachokiabudu?; Nyie na Mababa zenu waliotangulia?; Ama
kwa hakika hao (Mnaowaabudu) ni Maadui kwangu mie! Isipokua Mola wa
Ulimwengu wote; (Kwani) Ni yeye ndie alieniumba na akaniongoza; Na ndie
261

anaenilisha na kuninywesha; Na ninapoumwa ndie anaenipa afya; Na ndie atakae


nisababishia Kufa na ndie atakaenifufua; Na ndie ambae nnamtegemea kunisamehe
makosa yangu katika siku ya kufufuliwa’

Hapa Nabii Ibrahim hakuwahoji watu wake juu ya kile wanachokiabudu kwa sababu ya
kutojua ni kitu gani wanachokiabudu kwani alikua akijua wanachokiabudu na anajua kua
watu wake hao hawatokanusha juu ya kile wanachokiabudu, hivyo aliwahoji kwa ajili ya
kuwaonesha dhahiri juu ya ujinga wao, ambapo nao watu wake hao kwa ujinga wao
walikua wakijivunia Miungu hio yao ya Masanamu ambayo waliyokua wakiiabudu
wakati wa Mchana na wakati wa usiku walikua wakiabudu Nyota na Mwezi kama hali
hio ya kuabudu mchana Masanamu inavyoainishwa wazi na neno Nadhalu lililotumika
katika aya.

Ambapo Nabii Ibrahim akawahoji tena kama jee wanasikia na kujibu wanapowaomba
dua zao? Na jee wana manufaa au madhara yeyote juu yao? Lakini watu hao wakasema
kua wao hawajali juu ya mambo hayo kwani wanafuata nyayo za wazee wao. Katika
kuielezea aya hii Qaloo bal wajadna abaana kadhalika yafAAaloona yaani ‘Wakasema
La! Bali kadhalika hivyi ndivyo walivyokua wakifanya Mababa zetu waliotutangulia’
basi anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Aya hii inatuonesha
mmoja kati ya misimamo thabiti ya Qurán dhidi ya Fasad – Ubaya – ya maumbile
ya kufanya Taqlid – Kufuata – mitizamo ya Dini kwa kurithi kwa kupitia katika
njia za watu wasiojua, ambao hawana Mamlaka ya Kiilm katika Dini.’

Hapa sasa inabidi tuwekeane wazi kua hii haimaanishi kua Mujaddid Ad Din Imam Fakhr
ad Din Al Razi anakataza Taqlid ya kufuata Maimamu wa Madhhab, na hivyo watu
wasifuate Madhhab, La! Kwani yeye mwenyewe ni mfuasi wa Skuli ya Fiqh ya Madhhab
ya Mujaddid ad Din Mujtahid Imam Muhammad Idris Al Shafii.

Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi anatuelezea kua: Nabii Ibrahim aliwahoji
kwa kusema: Afaraaytum ma kuntum taAAbudoona; Antum waabaokumu al-
aqdamoona yaani ‘Jee mnakiangalia na kukitafakari kile mnachokiabudu?; Nyie na
Mababa zenu waliotangulia?’ kwa kumaanisha kua Upotovu ni Upotovu, bila ya kujali
kua kama upotovu huo ni wa kuanzia leo au ni wenye urefu wa historia ya kuanzia kwake
au idadi ya wingi au udogo wa wapotovu wake.

Anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua Nabii Ibrahim
anawawekea wazi watu wake umuhimu wa Muumba ambae ni Allah Subhanah wa Taála
kwa kuwaambia kua Alladhee khalaqanee fahuwa yahdeeni; Waalladhee huwa
yutAAimunee wayasqeeni; Wa-idha maridhtu fahuwa yashfeeni; Waalladhee
yumeetunee thumma yuhyeeni, Waalladhee atmaAAu an yaghfira lee khatee-atee
yawma alddeeni: kua ‘Ni Allah Subhnah wa Ta’ala pekee ndie Muumba na ndie
262

anaemuongoza pale anapokosea na ndie anaemrudisha yeye katika njia iliyokua


Sahih. Ni Allah Subhnah wa Taála pekee ndie anaenisababishia mie kufa kwa
Ghalfa (kwa kuingia kwenye Mighafiliko) na kisha Hunifufua kwa njia ya Dhikr.
Na kisha Nabii Ibrahim anamuomba Allah Subhanah wa Taála amsamehe makosa
yake kwa kutumia kanuni za kumuommba Allah Subhanah wa Taála, kwa kuingia
katika hali ya kua na hisia za kua na Khofu na Matumaini huku akiwa ni mtu
ambae hana uhakika kua atasamehewa Dhambi zake.’

Kwa upande wa Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii kua: ‘Aya hii
‘Wa-idha maridhtu fahuwa yashfeeni - Na ninapoumwa ndie anaenipa afya’ Maana
halisi ya ayah hii huweza kufahamika kikamilifu na yule mtu mwenye Ilm ya
Utabibu tu. Na huu ni mfano unaotuwekea wazi kua Qur’an haizungumzii habari
ya I’lm ya dini tu pekee, bali pia inajumuisha fani za I’lm tofauti ndani yake,
ikiwemo I’lm ya Utabibu, I’lm ya Sayari, I’lm ya Mfumo wa Mwili wa Ibn Adam
n.k. Hivyo kamwe haiwezekani kuzifaham kikamilifu maana halisi ya aya za Allah
Subhanah wa Ta’ala bila ya kua na I’lm ya fani husika iliyozungumziwa ndani ya
aya husika.’

Ama kwa upande wa Mujahid na Ikrimah basi wao wanasema kuhusiana na maneno
yasemayo kua: ‘Waalladhee atmaAAu an yaghfira lee khatee-atee yawma alddeeni’
yaani ‘Na ndie ambae nnamtegemea kunisamehe makosa yangu katika siku ya
kufufuliwa’ hapa Nabii Ibrahim alikua akizungumzia makosa yake katika sehemu 3
ambazo ni pale aliposema kua: Kwanza pale aliposema kua anaumwa ili asiende
kwenye sherehe ya kina Namrudh Al Kabir kisha akayavunja Masanam. Pili pale
aliposema Mungu Mkuu ndie aliewavunja Miungu wenzake na Tatu pale
alipomwambia Mfalme wa Misri kua Sarah ni Dada Yake.

Kisha aya zinaendelea kutumbia kua Nabii Ibrahim aliendelea kumuombea Dua Azar
kutokana na kuahidi kua atamuombea ili aokoke kabla ya kufariki kwake, lakini mara tu
baada ya kufariki kwake akasita kumuombea kwa sababu ilikua tayari iko wazi kua Azar
hakua ni miongoni mwa walioamini, kama inavyosema aya ifuatayo:

ٍ ِ ِ ِ ِ ِ ‫﴿وﻣﺎ َﻛﺎ َن‬


َ ‫ٱﺳﺘ ْﻐ َﻔ ُﺎر إِﺑْـَﺮاﻫ َﻴﻢ ﻟـﺄَﺑِﻴﻪ إِﻻﱠ َﻋﻦ ﱠﻣ ْﻮﻋ َﺪة َو َﻋ َﺪ َﻫﺂ إِ ﱠ�ﻩُ ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ ﺗَـﺒَـ ﱠ‬
ُ‫ﲔ ﻟَﻪُ أَﻧﱠﻪ‬ ْ ََ
﴾‫َﻋ ُﺪ ﱞو ِّﱠﻪﻠﻟِ ﺗَـﺒَـﱠﺮأَ ِﻣْﻨﻪُ إِ ﱠن إِﺑْـﺮ ِاﻫﻴﻢ ﻟَـﺄَﱠواﻩٌ َﺣﻠِﻴﻢ‬
ٌ َ َ
263

Wama kana istighfaru ibraheema li-abeehi illa AAan mawAAidatin waAAadaha


iyyahu falamma tabayyana lahu annahu AAaduwwun lillahi tabarraa minhu inna
ibraheema laawwahun haleemun (Surat At Tawba 9:114)

Tafsir: Na hakua Ibrahim ni mwenye kumuombea maghfira baba yake isipokua, ni


kutokana na ahadi aliyomuahidi baba yake. Lakini ilipobainishwa juu yake kua baba
yake ni adui wa Mola wake basi akatengena nae. Hakika Ibrahim alikua ni mwenye
kumuomba Allah tena na tena kwa unyenyekevu na ni mstahmilivu.

Tunaona pia kua ayah hii imetuma neno Awwah ambalo hua ni lenye kumaanisha kua
Nabii Ibrahim alikua na sifa ya Moyo mlaini, mwenye huzuni, kulalamika na
unyenyekevu hadi kufikia kulia katika kuomba kwake. Ama kwa upande wa neno
Halimun basi linamaanisha kua Nabii Ibrahim alikua ni uwezo wa kujidhibiti hasira zake
na mstahmilivu pale anapofikwa na mitihani dhidi yake.

Hivyo aliendelea kuweka wazi kutokukubaliana nao upotovu wa watu wake kwani huo
ulikua ni Uadui dhidi yake, na hata huyo Mfalme Namrudh Al Kabir basi kamwe hawezi
kua ni Mungu wake, kwani Mola wake Nabii Ibrahim ni Mola wa Ulimwengu wote na
kila kilichomo ndani yake, ni Mola wa Kila kitu, kuanzia chenye maumbile ya
ulimwenguni hadi chenye maumbile ya Akhera kikubwa kinachohesabika na kidogo
kisichohesabika. Mola ambae ndie anaemtegemea kwa kila kitu na kumuomba muongozo
kwa kusema:

‫ٱﺟ َﻌﻞ ِّﱃ ﻟِ َﺴﺎ َن ِﺻ ْﺪ ٍق ِﰱ‬


ْ ‫ﲔ ۞ َو‬
ِِ ‫َﳊِْﻘ ِﲎ ﺑِﭑﻟ ﱠ‬
َ ‫ﺼﺎﳊ‬ ْ ‫ﺐ ِﱃ ُﺣ ْﻜﻤﺎً َوأ‬ ْ ‫ب َﻫ‬ ِّ ‫﴿ َر‬
ِ ِ ۤ ِ ِ ِ ِ ِ ِ
۞‫ﲔ‬َ ّ‫ٱﺟ َﻌ ْﻠ ِﲎ ﻣﻦ َوَرﺛَﺔ َﺟﻨﱠﺔ ٱﻟﻨﱠﻌﻴ ِﻢ۞ َوٱ ْﻏﻔْﺮِ ﻷَِﰊ إِﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن ﻣ َﻦ ٱﻟﻀﱠﺂﻟ‬ ْ ‫ﻳﻦ۞ َو‬ َ ‫ٱﻵﺧ ِﺮ‬
‫ﺐ‬ٍ ْ‫ٱﻪﻠﻟَ ﺑَِﻘﻠ‬
‫ﺎل َوﻻَ ﺑَـﻨُﻮ َن ۞ إِﻻﱠ َﻣ ْﻦ أَﺗَﻰ ﱠ‬
ٌ ‫َوﻻَ ُﲣِْﺰِﱏ ﻳَـ ْﻮَم ﻳـُْﺒـ َﻌﺜُﻮ َن۞ ﻳـَ ْﻮَم ﻻَ ﻳَﻨ َﻔ ُﻊ َﻣ‬
﴾‫َﺳﻠِﻴ ٍﻢ‬
Rabbi hab lee hukman waalhiqnee bialssaliheena; WaijAAal lee lisana sidqin fee al-
akhireena; WaijAAalnee min warathati jannati alnnaAAeemi; Waighfir li-abee
innahu kana mina aldhdhalleena; Wala tukhzinee yawma yubAAathoona; Yawma
la yanfaAAu malun wala banoona; Ill man atta Allah biqalbin Salimin.(Surat Ash
Shuara 26:83-89)
264

Tafsir: Ya Rabbi! Nipe Hikma juu yangu na unijumuishe na Waja wema; Na unijaalie
niwe ni mwenye kutajwa kwa sifa njema na vizazi vya watakaokuja; Na unijaalie kua
ni mrithi wa Neema za Peponi; Na umsamehe baba yangu kwani kwa hakika yeye ni
mwenye kupotoka; Na usinihuzunishe katika siku ya kufufuliwa, Katika siku ambayo
haitamfaa mtu Mali yake wala watoto wake, isipokua yule atakaemkabidhi Allah Moyo
ulio salama.

Hapa kuna baadhi wanaweza wakajiuliza mbona aya hii ya Surat Ash Shuara 26:86
inapingana na aya ya 114 ya Surat At Tawba?

Lakini ukweli ni kua hapa inabidi tujue kua Surat Ash Shuara ni Sura ilityoteremshwa
katika Mji wa Makkah katika kipindi cha katikati cha Uislam katika Mji huo, yaani kabla
ya Hijra. Ambapo Surat At Tawba iliteremshwa katika Mji wa Madina katika mwaka wa
9 Al Hijra, hivyo basi aya hio ya Surat Ash Shuaraa ilishushwa mwanzo na hivyo kuweka
wazi kua Nabii Ibrahim alikua ni mwenye kumuiombea dua baba yake kabla ya kujua
kua hakuna uwezekano wa kumuingiza katika Dini ya Allah Subhanah wa Ta’ala ambapo
aya ya Surat At Tawba ilikua inathibitisha kua baada ya Nabii Ibrahim kujua kua hakuna
uwezekano wa baba yake kumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala basi aliamua
kutomuombea Dua.

Anasema Abu Hurayra kua amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:
‘Katika siku ya malipo basi Nabii Ibrahim atakutana na Azar akiwa na uso mweusi
na wenye kujaa machozi na hivyo atamuonea huruma na kumuuliza: Ewe baba
yangu sikukwambia mie kua unifuate. Azar atasema: Ukinambia sasa hivi basi bila
ya shaka nitakufuata. Nabii Ibrahim atamwambia Allah Subhanah wa Ta’ala. Ya
Allah Hakika wewe uliniahidi kua hutonihuzunisha katika siku ya malipo, sasa jee
itakuaje hali yangu leo hii wakati baba yangu anataka kuangamia?’

‘Allah Subhanah wa Ta’ala atamwambia Nabii Ibrahima: Ewe Ibrahim hakika


Pepo yangu imeharamishiwa watu walionikufuru. Ewe Ibrahim angalia chini yako!
Nabii Ibrahim ataangalia chini yake katika sehemu ambayo alikua amesimama
Baba yake na ataona kuna Nge mkubwa sana, kisha Nge huyo atatumbukizwa
Ndani ya Moto.’(Sahih Bukhari) Nabii Ibrahim atajikisikia vibaya sana akimuona Nge
huyo na hivyo kua ni mwenye kuchukia na kukirihishwa nae na kuona bora alivyoingizwa
Motoni.

Nabii Ibrahim alikua akomba kua ajaaliwe Hikma pia kwa sababu Hikma hua
inajumuisha Ufaham na Ilm na pia huainajumuisha Ufahamu kamilifu wa Sifa Tukufu za
Allah Subhanah wa Ta’ala na pia hua ni zenye kumaanisha Utume.
265

Na vile vile baadhi tunaweza tukajiuliza, kwa nini Nabii Ibrahim anaendela kuomba Dua
kama hizi zinayoelezewa katika aya hizi inayojumuisha kuomba msamaha na kuomba
kutohuzunishwa au kutoadhirishwa katika siku ya Malipo, wakati yeye ni Nabii na ni
Mtume wa Allah Subhanah wa Ta’ala yaani ni mtu ambae ni mwenye Moyo ulio msafi
na salama ambao hauna shaka yeyote juu ya Mola wake ndani yake.

Jibu la suali hili ni kua: Anasema Abu Al Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Maumbile ya
kufanya Makosa katika Ulimwengu huu yanaweza yakawa hayaonekani hapa
Duniani, lakini hata hivyo matokeo yake yatakua wazi katika siku ya kuhesabiwa.’
Hivyo hii inaonesha kwa namna gani Nabii Ibrahim alivyokua na Ikhlas katika mambo
yake kiasi ya kua mbali ya kua ni alieamini lakini alikua bado alikua ana khofu asije
akamuasi Mola wake. Aya hii inatufundisha kua mbali ya kuoma maghfira na Pepo lakini
pia tusiwache na kuomba kua tusiadhirishwe katika siku ya Malipo.

Na Mujaddid ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi anasema kua: ‘Hapa inaonekana wazi
kua Nabii Ibrahim alianza na Dua kwa kumsifu na kumtukuza Mola wake. Na hii
ni kwa sababu Roho za Ibn Adam na Malaika zina maumbile sawia. Hivyo kila Ibn
Adam anavyojitahidi kumuomba Mola wake na kua na Utiifu kwa Mola wake basi
ndio anavyozidi kua na Ukaribu na Mola wake na kujulikana kidarja na Malaika
na hivyo kua na uwezo mkubwa zaidi wa Kiroho hapa Ulimwenguni. Na kwa
upande mwengine kila Ibn Adam anapozidi kuielekea Dunia yake basi ndivyo
anavyozidi kushuka chini darja yake na kuzidi kudidimia katika maumbile ya
Wanyama na kuzama katika kiza cha Dunia. Hivyo yeyote yule anaetaka
kumuomba Mola wake basi lazima kwanza amtukuze na kumsifu Mola wake ili
apate ukaribu kwa Mola wake na kukaribia au kufikia darja na uwezo wa Malaika’

Nabii Ibrahim pia aliomba ajaaliwe kua ni miongoni mwa Salihiin yaani Waja wema
wale ambayo Amali zao hua ni zenye kukubaliwa na Allah Subhanah wa Ta’ala, kwani
amali njema bila ya kua ni zenye kukubaliwa basi hua ni sawa na kujaza maji kwenye
pakacha yaani amali hizo hua hazina maana yayote ndani yake na katika kufanywa
kwake, hua ni sawa na kupoteza mda tu.

Kisha Nabii Ibrahim akaomba kua ajaaliwe kua ni mwenye kukumbukwa kwa sifa njema
na Vizazi vitakavyokuja baadae, na hii inatufunza sisi kua tujaribu kuacha athari njema
katika maisha yetu kiasi ya kua athari hizo ziwanufaishe vizazi vyetu na vizazi
vitakavyokuja baadae, lakini isiwe kwa njia ya kujionesha au kwa kujitakia umaarufu,
bali kujaribu kuwanufaisha wengine kutokana na zile Neema tulizopewa na Allah
Subhanah wa Ta’ala kwani hata Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua akiomba
dua kwa Allah Subhanah wa Ta’ala kua amjaalie aonekane mdogo mbele ya macho yake
mwenyewe lakini hapo hapo aonekane mkubwa mbele ya macho ya watu wake. Na hii
ni dua ambayo ni dawa ya kuondoa Kibr na Riya.
266

Na bila ya shaka tunaporudi kwa Nabii Ibrahim basi tunaona kua Allah Subhanah wa
Ta’ala alimkubalia dua yake na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akamuamrisha
Nabii Muhammad Sallahu Alayhi wa Salam kua awe nimwenye kufuata Milat Ibrahim,
na pia katika kumsalia kwake Rasul Allah Salallahu alayhi wa Salam ndani ya Sala zetu
basi Waislam tukaambiwa tumsalie kwa kusema: Allahuma Ssali aAla Muhammad wa
Aala alihi Muhammad kama ssalaita aAla Ibrahima wa aAla Alihi Ibrahima fi al
aAalamina innaka hamidun majid.

Aya pia zinatuwekea wazi umuhimu wa kuendelea kuomba kuingizwa Peponi mbali ya
kua ni wenye kufanya mambo mema. Na kisha inatuionesha umuhimu wa Amali njema
katika siku ya Malipo katika siku ambayo haitomfaa mtu mali yake wala Mali zake, bali
kitakachomfaa mtu ni Moyo uliojisalimisha mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala. Na pia
zinatuonesha umuhimu wa kutafakkar yatakayotokea katika Siku ya Malipo ambayo
haitomfaa mtu Mali yake wa Watoto wake kwani kila mmoja miongoni mwetu ataulizwa
juu ya alichokichuma iwe cha Halali au cha Haram.

Na namna alivyokitumia hicho alichokichuma jee ni kwa njia ya halali au ya haram, na


hivyo basi ni wale tu ambao waliochuma vichumo vyao kwa njia ya halali na kisha
wakakitumia kile walichokichuma kwa njia ya Halali basi ndio watakaokoka na kuvuna
Mavuno bora katika siku hio ya Malipo. Hivyo watoto wako na Mali zako zitakufaa kama
ikiwa umefika mbele ya Mola wako huku ukiwa na Moyo uliosalama.

Habari hizi za Nabii Ibrahim kupingana na mitizamo ya watu wake, na kutangazia uadui
na Mfame Namrudh Al Kabir na Miungu wenzake zikamfikia mwenyewe Mfalme
Namrudh Al Kabir. Hivyo basi akaamrisha Nabii Ibrahim akamatwe aletwe mbele yake.
Nabii Ibrahim akakamatwa na kufikishwa mbele ya Mfalme Namrudh Al Kabir na
kuulizwa: ‘Ewe Ibrahim nasikia kuna Mungu ambae unamtangazia kwa watu, na
unawataka watu wamuabudu Mungu huyo ambae wewe unasema kua ana uwezo
juu ya kila kitu na amekutuma wewe uwatumie watu ujumbe juu yake. Jee ndie
Mungu gani huyo?’

Nabii Ibrahim akasema: ‘Mungu wangu ndio yule ambae ni mwenye uwezo wa
kuhuisha na kuua.’ Mfalme Namrudh Al Kabir akasema: ‘Hata mimi pia ninao uwezo
wa kuhuisha na kuua.’ Nabii Ibrahim akahoji: ‘Unawezaje kuhuisha na kuua?’
Namrudh Al Kabir akasema: ‘Nachukua watu wawili ambao wanastahiki kuuawa,
kisha nnamuua mmoja na kumsamehe mwengine hivyo nnakua nimemhuisha
mmoja na nimemuua mwengine’ Nabii Ibrahim akasema: ‘Mungu wangu mie ndie
yule ambae Asubuhi analitoa Jua upande wa Mashariki, na Jioni kulizamisha
katika upande wa Magharibi, hivyo wewe kama ni Mungu pia basi lichomozeshe
jua kutoka katika upande wa Magharibi na lifanye litue katika upande wa
Mashariki’. Hapa Mfalme Namrudh Al Kabir ikawa ameshindwa Hoja na hivyo akawa
267

amekaa kimya anatafakkari. Allah Subhanah wa Taala anaielezea habari hii katika aya
ifuatayo kwa kusema:

ِ ِ َ َ‫ٱﻪﻠﻟ ٱﻟْﻤ ْﻠﻚ إِ ْذ ﻗ‬ َ ‫﴿أََﱂْ ﺗَـَﺮ إِ َﱃ ٱﻟﱠ ِﺬى َﺣﺂ ﱠج إِﺑْـَﺮ ِاﻫ َﻴﻢ ِﰱ ِرﺑِِّﻪ أَ ْن‬
َِّ‫ﺎل إﺑْـَﺮاﻫ ُﻴﻢ َر‬
‫ﰉ‬ َ ُ ُ‫آﺎﺗﻩُ ﱠ‬
ِ ِ ‫ﺎل إِﺑْـﺮ ِاﻫﻴﻢ ﻓَِﺈ ﱠن ﱠ‬ ِ ِ ِ
‫ﺲ‬ِ ‫ﱠﻤ‬ْ ‫ٱﻪﻠﻟَ َ�ْﺗﻰ ﺑﭑﻟﺸ‬ ُ َ َ َ‫ﻴﺖ ﻗ‬ ُ ‫ُﺣﻴِـﻰ َوأُﻣ‬ ْ ‫ﺎل أ ََ� أ‬ ُ ‫ٱﻟﱠﺬى ُْﳛﻴِـﻰ َوُﳝ‬
َ َ‫ﻴﺖ ﻗ‬
ِ ْ‫ٱﻪﻠﻟ ﻻَ ﻳـﻬ ِﺪى ٱﻟْ َﻘﻮم ِﻣﻦ ٱﻟْﻤ ْﺸ ِﺮِق ﻓَﺄ‬ ِ ‫ب ﻓَـﺒ ِﻬ‬ ِ ِ
‫ت‬ َ َ َْ ْ َ ُ‫ﺖ ٱﻟﱠﺬى َﻛ َﻔَﺮ َو ﱠ‬ َ ُ ِ ‫ﻬﺑَﺎ ﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻤ ْﻐ ِﺮ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
Alam tara ila alladhee hajja ibraheema fee rabbihi an atahu Allahu almulka idh
qala ibraheemu rabbiya alladhee yuhyee wayumeetu qala ana ohyee waomeetu qala
ibraheemu fa-inna Allaha ya/tee bialshshamsi mina almashriqi fa/ti biha mina
almaghribi fabuhita alladhee kafara waAllahu la yahdee alqawma
aldhdhalimeena(Surat Al Baqara 2:258)

Tafsir: Jee umemuona yule ambae alihojiana na Ibrahim kuhusiana na Mola (Allah)
wake, kwa sababu Allah amempa Ufalme wakati Ibrahimu alipomwambia: ‘Mola
wangu ni yule ambae anaehuisha na kusababisha kifo’. Nae (Namrudh Al Kabir)
akasema: ‘Mimi nnahuisha na kuua’. Ibrahim akasema: ‘Kwa Hakika Allah!
Analichomozesha Jua kutoka katika upande wa Mashariki, na kulizamisha katika
upande wa Magharibi’. Hivyo wakashindwa Wasioamini. Na Allah hawaongozi watu
Madhalimu.

Watu hao wakamhoji zaid Nabii Ibrahim ambae nae akaendelea kwa kusema:

ِ ‫ب ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬ ِ ِ ‫ﭑﳊ ِﻖ أَم أ‬ ِ ۤ


‫ات‬ َ َ ‫ﺎل ﺑَﻞ ﱠرﺑﱡ ُﻜ ْﻢ َر ﱡ‬
َ َ‫ﲔ۞ ﻗ‬ َ ْ ّ َْ ِ‫﴿ﻗَﺎﻟُﻮاْ أَﺟْﺌـﺘَـﻨَﺎ ﺑ‬
َ ِ‫َﻧﺖ ﻣ َﻦ ٱﻟﻼﱠﻋﺒ‬
﴾‫ﱠﺎﻫ ِﺪﻳﻦ‬
ِ ‫ض ٱﻟﱠ ِﺬى ﻓﻄَﺮﻫ ﱠﻦ وأ ََ�ْ ﻋﻠَﻰ ٰذﻟِ ُﻜﻢ ِﻣﻦ ٱﻟﺸ‬
ِ ‫َوٱﻷ َْر‬
َ َ ّ ْ ٰ َ َ َُ
Qaloo aji/tana bialhaqqi am anta mina allaAAibeena; Qala bal rabbukum rabbu
alssamawati waal-Ardhi alldhee fatarahunna waana AAala dhalikum mina
alshshahideena (Surat Al Anbiyah 21:55-56)
268

Tafsir: Wakasema: ‘Jee umetuletea uthibitisho? Au wewe ni miongoni mwa wale


wenye kufanya mchezo?’ Akasema (Nabii Ibrahim): ‘La! (Mimi sifanyi mchezo) bali
Mola wenu ni Mola wa Mbingu na Ardhi, ambae ndie alieziumba na juu ya hilo basi
mimi ni mwenye kushuhudia’

Baada ya mahojiano hayo ambayo hayakuweza kuwadhibitishia watu hao basi Nabii
Ibrahim akataka kuwaonesha kwa vitendo watu wake udhaifu Miungu yao wanayoiabudu
na kutokua na uwezo wa kufanya kitu chochote kile kwa ajili yao au dhidi yao, hivyo
akawa ni mwenye kutafuta nafasi ya kuwadhihirishia juu ya jambo hilo katika moja kati
ya siku muhimu sana kwao yaani katika sikukuu yao ambapo watu wote hawa hutoka na
kujikusanya katika eneo moja kusheherekea kisha wanaporudi hua wanaipitia Miungu
yao na kuisujudia na kuishukuru.

Katika siku hio watu hawa wakamtaka Nabii Ibrahim afuatane nao pamoja katika sherehe
hizo, na kumwambia kua huenda akavutiwa na Miungu yao baada ya kuhudhuruia
sherehe hizo, hivyo nae akawahoji tena watu wake kwa kutoamini kile anachowausia bila
ya wao kutaka kumfahamu hivyo akasema.

َ ‫ﱡﺠ ِﻮم۞ ﻓَـ َﻘ‬


ْ‫ﺎل إِِّﱏ َﺳ ِﻘ ٌﻴﻢ ۞ ﻓَـﺘَـ َﻮﻟﱠْﻮا‬ ُ ‫ﲔ۞ ﻓَـﻨَﻈََﺮ ﻧَﻈَْﺮًة ِﰱ ٱﻟﻨ‬
ِ
ِّ ‫﴿ﻓَ َﻤﺎ ﻇَﻨﱡ ُﻜﻢ ﺑَِﺮ‬
َ ‫ب ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬
﴾‫َﻋْﻨﻪُ ُﻣ ْﺪﺑِ ِﺮﻳﻦ‬
َ
Fama dhannukum birabbi alAAalameena, Fanadhara nadhratan fee alnnujoomi;
Faqala innee saqeemun; Fatawallaw AAanhu mudbireena (Surat Saffat 37:87-89)

Tafsir: (Nabii Ibrahim) akawauliza watu Jee mnadhani vipi juu ya Mola wa
Ulimwengu wote? Kisha akaangalia, akiwa na mtizamo wa kuangalia Nyota. Kisha
akasema: Kwa hakika mimi sijisikii vizuri. Hivyo wakampa mgongo na kuondoka
kukimbilia mambo yao.

Aya imetumia neno Nujumi ambalo ni lenye kutokana na neno Najama ambalo ni lenye
kumaanisha Kuonekana, Kuchomoza, Kufuatana, Kukamilisha. Ambapo neno Nujum
hua ni lenye kumaanisha Nyota au Mkusanyiko wa Nyota na pia humaanisha Majani
yanayoota pamoja pamoja kwa kushikamana chini ardhini, na pia humaanisha Sehemu
za Qur’an kama zilivyoteremshwa katika wakati wa kipindi cha Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam.

Hivyo kuna Nujumi aina mbili ambapo baadhi ya Wafasiri wametafsiri kwa kutumia
maana ya kwanza ambayo ni Nyota za Mbinguni na maana ya pili ni kama alivyosema
269

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘Amesema Muhammad Ibn
Sawwar kua, amesema Amr Ibn Aala kua; ‘Maana ya ayah hii ni kua Nabii Ibrahim
aliangalia Nabat (Miti), kama vile alivyosema Allah Subhanah wa Ta’ala katika aya
ifuatayo ’

﴾‫ﱠﺠﺮ ﻳَﺴ ُﺠ َﺪ ِان‬ ْ ‫﴿ َوٱﻟﻨ‬


ْ ُ َ ‫ﱠﺠ ُﻢ َوٱﻟﺸ‬
Waalnnajmu waalshshajaru yasjudani (Surat Ar Rahman 55:6)

Tafsir: Na Najmu na Miti yote Iliyosjudu.

Ambapo wa upande wa Allama Yaqub Ibn Is-haq Ibn Al Kindi yeye lipoulizwa na mtoto
wa Khalfa Al Mutasim kuhusiana na ayah hii basi alisema: ‘Tukio la Kusjudu Kwa
Nyota kulikokusudiwa hapa kunamaanisha namna Nyota zinavyotuma mionzi
Ardhini na namna inayoathiri Dunia na viumbe vyake vyote.’

Lakini hata hivyo huo ni mtizamo wa Ilm Filasafa kwa hivyo tunaachana nao na kurudi
kwenye mtizamo wa kua Najmu ni Mimea inayotambaa isiyokua na Vigogo, na Shajaru
yaani Miti mikubwa mikubwa. Hivyo Nabii Ibrahim aliangalia Nyota huku kitafakkari
namna watu wake wanavyoziabudu na pia kwa upande mwengine basi aliziangalia
kuwaonesha watu wake kua anaziamini hivyo wasiwe na khofu nae.

Alfajir ya siku ya pili watu hao wakajitayarisha kwa ajili ya kuelekea kwenye
kuadhimisha sherehe yao, Hivyo wakati wanaondoka watu hawa basi walikua na kawaid
aya kuwacha vyakula vyao katika sehemu za kuabudia Miungu yao ndani ya Hekalu lao
ili Nanar ambae ni Mungu Mkuu na Miungu wengine iliyomo humo ndani ivijaze barka
vyakula hivyo, kabla ya wao kurudi katika sherehe zao na kuchukua vyakula hivyo na
kurudi navyo nyumbani kwa ajili ya kula baada ya kubarikiwa kwake, na Nabii Ibrahim
akasema kwa kichini chini.

﴾‫َﺻﻨَ َﺎﻣ ُﻜﻢ ﺑَـ ْﻌ َﺪ أَن ﺗُـﻮﻟﱡﻮاْ ُﻣ ْﺪﺑِ ِﺮﻳﻦ‬‫أ‬ ‫ﱠ‬


‫ن‬ ‫ﻴﺪ‬
َ ِ‫ﭑﻪﻠﻟِ َﻷَﻛ‬
‫﴿ َوﺗَ ﱠ‬
َ َ ْ ْ
WataAllahi laakeedanna asnamakum baAAda an tuwalloo mudbireena (Surat Al
Anbiya 21:57)

Tafsir: Na Wa Allahi nitayashughulikia ipasavyo Masanamu yenu baada ya nyinyi


kukimbilia mambo yenu.
270

Lakini mmoja kati ya watu wake alisikia kauli hio, hivyo baada ya kuondoka kwao basi
Nabii Ibrahim nae akaondoka kuelekea katika Hekalu lao, na akakuta vyakula
vimewekwa mbele ya Nanar na Miungu yao myengine hio ambapo akaiuliza Miungu hio
kwa kuifanyia dhihaka: ‘Ah! Mbona hamli? Wala hamzungumzi?’ Nanar na Miungu
hio ikawa wamebakia kimya kama ilivyokua kawaida ya Masanamu, kwani hua
hayasemi, hapa sasa Nabii Ibrahim, akaanza kuyashugulikia Masanamu hayo moja baada
ya jengine kama inavyopasa kushughulikiwa kulingana na alivyoamrishiwa na Allah
Subhanah wa Taála kupitia katika ufahamu wake Nabii Ibrahim, kwa sababu Mitume wa
Allah Subhanah wa Taála hua hawafanyi jambo wala hawasema jambo isipokua hua lina
hikma ndani yake, hivyo hapa hali ikawa kama inavyoelezewa na aya zifuatazo:

َ ‫غ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ‬
ً‫ﺿْﺮﺎﺑ‬ َ ‫ﻨﻄ ُﻘﻮ َن۞ ﻓَـَﺮا‬ ْ َ َ ‫غ إِ َ ٰﱃ ِآﳍَﺘِ ِﻬ ْﻢ ﻓَـ َﻘ‬
ِ َ‫ﺎل أَﻻَ َﺄﺗْ ُﻛﻠُﻮ َن۞ ﻣﺎ ﻟَ ُﻜﻢ ﻻَ ﺗ‬ َ ‫﴿ﻓَـَﺮا‬
﴾‫ﲔ‬ ِ ‫ﺑِﭑﻟْﻴَ ِﻤ‬
Faragha ila alihatihim faqala ala ta/kuloona, Ma lakum la tantiqoona Faragha
AAalayhim dharban bialyameeni; (Surat As Saffat 37:91-93)

Tafsir: Kisha akawageukia Miungu yao na kuwambia: ‘Jee Hamli?’; ‘Imekuaje


mbona hata hamzungumzi?’ Kisha akawageukia na kuwapiga kwa nguvu kwa mkono
wake wa kulia.

Kuishughulikia kwake Nabii Ibrahim Miungu hio hakukua katika kuyapiga tu Masanamu
hayo, kwani inavyopaswa kushughulikia ni kuyafanya kua hayafai tena kabisa kabisa
kwa kuyaangamiza yote isipokua lile lililo kubwa na lenye umuhimu sana kwao ambalo
ni Nanar lenyewe, akalibakisha ili liwe kama mfano kua hilo Nanar ndie aliewavyunja
vunja hao Miungu wengine na pia kua kama kithibitisho kua Miungu hio haiwezi hata
kujitetea wala kuteteana na inahitaji usimamizi wa watu hao badala ya watu hao kuhitaji
usimamizi wa Masanamu hayo na hivyo Masanamu hayo kamwe hayafai kuabudiwa, aya
zinatuelekea wazi yaliyotokea kwa kusema kua:

‫﴿ﻓَ َﺠ َﻌﻠَ ُﻬ ْﻢ ُﺟ َﺬاذاً إِﻻﱠ َﻛﺒِﲑاً ﱠﳍُْﻢ ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻬ ْﻢ إِﻟَْﻴ ِﻪ ﻳَـْﺮِﺟﻌُﻮ َن۞ ﻗَﺎﻟُﻮاْ َﻣﻦ ﻓَـ َﻌ َﻞ َﻫـٰ َﺬا ِﺂﺑ ِﳍَﺘِﻨَﺂ‬
‫ﺎل ﻟَﻪُ إِﺑْـَﺮ ِاﻫ ُﻴﻢ ۞ ﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻓَﺄْﺗُﻮاْ ﺑِِﻪ َﻋﻠَ ٰﻰ‬
ُ ‫ﲔ ﻗَﺎﻟُﻮاْ َِﲰ ْﻌﻨَﺎ ﻓَـ ًﱴ ﻳَ ْﺬ ُﻛُﺮُﻫ ْﻢ ﻳـُ َﻘ‬ ِِ ِ
َ ‫إِﻧﱠﻪُ ﻟَﻤ َﻦ ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
﴾‫ﱠﺎس ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻬﻢ ﻳَ ْﺸ َﻬ ُﺪو َن‬ِ ‫ﲔ ٱﻟﻨ‬ ِ ُ ‫أ َْﻋ‬
ْ
271

FajaAAalahum judhadhan illa kabeeran lahum laAAallahum ilayhi yarjiAAoona;


Qaloo man faAAala hadha bi-alihatina innahu lamina aldhdhalimeena; Qaloo
samiAAna fatan yadhkuruhum yuqalu lahu ibraheemu; Qaloo fa/too bihi AAala
aAAyuni alnnasi laAAallahum yashhadoona (Surat Al Anbiyah 21:58-61)

Tafsir: Hivyo akayajaalia kuyavunja vunja vipande vipande isipokua lile kubwa lao
(Nanar) ili warudi kwake. Nao wakasema: Jee ni nani aliewafanya hivi Miungu wetu?
Bila ya shaka atakua ni miongoni mwa waovu. Kisha wakasema: Tumemsikia mtu
akizungumzia dhidi yao anaeitwa Ibrahim. Nao wakasema: Mleteni hapa mbele ya
macho ya watu ili wapate kushuhudia.

Ama Imam Abu Jafar Muhammah Ibn Jarir Al Tabari basi yeye anasema kua: ‘Nabii
Ibrahim aliyavunja vunja Masanamu hao kwa shoka kisha shoka hilo akaliweka
juu ya bega la yule sanamu mkubwa aliembakisha’ ama juu ya kauli hii ya Ilayhi
yarjiAAoona yaani Wapate kurudi kwake basi inamaanisha kua Nabii Ibrahim
alikua akitegemea kua watu hawa watarudi kwake na kumkubali Mola wake ambae
ni Allah Subhanah wa Taála.

Ama kwa upande wa Imam Abu Al Qasim Al Zamakhshari basi yeye anasema kua: ‘Hii
Ilayhi yarjiAAoona yaani Wapate kurudi kwake basi inamaanisha kua Nabii Ibrahim
alikua akitegemea kua watu hawa watarudi kwa Nanar ili wapate kuuona ukweli
kua Sanamu hilo halina uwezo wowote.’

Baada ya kuona namna hali ilivyokua na watu hawa kuingia na huzuni kiasi ya kua baadhi
yao walikua wanakaribia kutokwa na machozi na wengine walikua wakilia kwa huzuni
ya kuangamizwa kwa Miungu yao hio wanayoitegemea, hivyo yule aliemsikia Nabii
Ibrahim akisema kua atawashughulikia Miungu hao pamoja na wenziwe aliewaambia juu
ya aliyoasikia basi wote kwa pamoja wakajithibitishia kua huyu aliefanya hivyo atakua
ni Nabii Ibrahim.

Na ingawa baadhi walikua hawana uhakika ni nani aliefanya kitendo hicho kibaya lakini
bila ya shaka wengi kati ya watu hawa walikua pia wanajua kua adui yao anaepingana
nao ni Nabii Ibrahim na ndie mtu pekee anaeweza kufanya hivyo kwani mara nyingi pia
kisha wadhalilisha Miungu yao hio hapo kabla, hivyo Mfalme Namrudh Al Kabir
akaamua kua Nabii Ibrahim akamatwe kwa haraka iwezekanavyo kisha aletwe mbele ya
hadhara kwa ajili ya kujibu tuhuma anazo shutumiwa ili watu wote wasione kua
ameonewa na yeye mwenyewe Nabii Ibrahim asije kusema kua ameonewa au
amesingiziwa juu ya jambo hilo, na ndio maana Quran ikasema:
272

﴾‫﴿ﻓَﺄَﻗْـﺒَـﻠُ ۤﻮاْ إِﻟَْﻴ ِﻪ ﻳَِﺰﻓﱡﻮ َن‬


Faaqbaloo ilayhi yaziffoona (Surat As Saffat 37:94)

Kisha (watu wake) wakakabiliana nae kwa haraka.

Hivyo Nabii Ibrahim akakamatwa kwa haraka sana ili kukabiliana na shutuma
anazotuhumiwa na kuanza mahojiano baina yake na watu hao kama isemavyo Qurán:

‫ﻮﻫ ْﻢ‬ُ‫ﻟ‬َ‫ﺄ‬‫ﺎﺳ‬‫ﻓ‬
َ ‫ا‬‫ﺬ‬َ ‫ـ‬
ٰ ‫ﻫ‬ ‫ﻢ‬ ‫ﻫ‬‫ﲑ‬ِ
‫ﺒ‬ ‫ﻛ‬
َ ‫ﻪ‬‫ﻠ‬
َ ‫ﻌ‬‫ـ‬َ‫ﻓ‬ ‫ﻞ‬‫ﺑ‬ ‫ﺎل‬
َ ‫ﻗ‬
َ ۞ ‫ﻴﻢ‬ ِ ‫﴿ﻗَﺎﻟُ ۤﻮاْ أَأَﻧْﺖ ﻓَـﻌ ْﻠﺖ ﻫـٰ َﺬا ِﺂﺑ ِﳍﺘِﻨﺎ ٰ�ِﺑـﺮ‬
‫اﻫ‬
ُ ْ َ ْ ُُ ُ َ ْ َ ُ َْ َ َ َ َ َ َ
﴾‫إِن َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳَـْﻨ ِﻄ ُﻘﻮ َن‬
Qaloo aanta faAAalta hadha bi-alihatina ya ibraheemu’; Qala bal faAAalahu
kabeeruhum hadha fais-aloohum in kanoo yantiqoona.(Surat Al Anbiyah 21:62-63)

Tafsir: Nao wakaasema: Jee ni wewe ndie amabe uliewafanyia hivi Miungu wetu ewe
Ibrahim? Nae (Nabii Ibrahim) akasema: La! Bali aliefanya hivyo ni huyu Mkubwa
wao, Waulizeni kama ni wenye kusema!

Nabii Ibrahim akawaambia watu hao, ni Nanar ndie aliewauawa Miungu wengine kwa
sababu alikua akiona wivu kua yeye ndie Mkubwa kuliko Miungu wengine wote hao
halafu yeye anaabudiwa sawasawa na Miungu hao wadogo, baada ya kutoa hoja hio basi
watu hao pamoja na Mfalme wao Namrudh Al Kabir wakaanza kusutana wao wenye kwa
wenyewe, lakini baada ya kutafakkar basi wakamwambia Nabii Ibrahim, kua lakini wewe
Ibrahim unajua kua hayo masanamu hayasemi.

Kama inavyosema Qurán:

ِ ‫﴿ﻓَـﺮﺟﻌ ۤﻮاْ إِ َ ٰﱃ أَﻧ ُﻔ ِﺴ ِﻬﻢ ﻓَـ َﻘﺎﻟُ ۤﻮاْ إِﻧﱠ ُﻜﻢ أَﻧﺘُﻢ ٱﻟﻈﱠﺎﻟِﻤﻮ َن ۞ ﰒُﱠ ﻧُ ِﻜﺴﻮاْ ﻋﻠَﻰ رء‬
‫وﺳ ِﻬ ْﻢ‬ُُ ٰ َ ُ ُ ُ ْ ْ ََُ
ۤ
ِ ‫ﻟََﻘ ْﺪ ﻋﻠِﻤﺖ ﻣﺎ ﻫـٰﺆﻻ ِء ﻳ‬
﴾‫ﻨﻄ ُﻘﻮ َن‬َ َُ َ َ ْ َ
273

FarajaAAoo ila anfusihim faqaloo innakum antumu aldhdhalimoona; Thumma


nukisoo AAala ruoosihim laqad AAalimta ma haola-i yantiqoona. (Surat Al Anbiyah
21:64-65)

Tafsir: Hivyo wakajisuta Nafsi zao na kusema: ‘Hakika nyie mnafanya Dhulma!’
Kisha wakamgeukia (Nabii Ibrahim) na kusema: ‘Kwa Hakika wewe (Ibrahim)
unajua kua haya (Masanam) hayasemi’

Nabii Ibrahim akaigeuza hoja hio na kuitumia dhidi yao kua ikiwa mnajua kua masanamu
hayo hayasemi, wala hayawezi kujitetetea wenyewe kwa sababu ni nyinyi ndio
mliyoyachonga jee kwa nini sasa mnayaabudu baada ya kumuabudu Mola wenu
aliekuumbeni nyie na kila kitu chenu kwa ajili yenu? Kwa kusema:

‫ﺎل أَﺗَـ ْﻌﺒُ ُﺪو َن َﻣﺎ ﺗَـْﻨ ِﺤﺘُﻮ َن۞ َو ﱠ‬


ً�‫ٱﻪﻠﻟُ َﺧﻠَ َﻘ ُﻜ ْﻢ َوَﻣﺎ ﺗَـ ْﻌ َﻤﻠُﻮ َن۞ﻗَﺎﻟُﻮاْ ٱﺑْـﻨُﻮاْ ﻟَﻪُ ﺑـُْﻨـﻴَﺎ‬ َ َ‫﴿ﻗ‬
﴾‫ﻓَﺄَﻟْ ُﻘﻮﻩُ ِﰱ ٱ ْﳉَ ِﺤﻴ ِﻢ‬
Qala ataAAbudoona ma tanhitoona; WaAllahu khalaqakum wama taAAmaloona,
Qaloo ibnoo lahu bunyanan faalqoohu fee aljaheemi (Surat As Saffat 37:95-97)

Tafsir: (Nabii Ibrahim) Akasema: Nyinyi mnayaabudu yale ambayo mmeyachonga


wenyewe, Wakati Allah amekuumbeni nyie na mnavyovitegeneza, Wakasema watu
hao: Mtengenezeeni jengo madhubuti (Tanuri maalum ambalo moto na joto lake lote
halitoki nje) na kisha mtumbukizeni Motoni.

Imam Muhammad Ibn Abdallah Al Kisai basi yeye anasema kua Miongoni mwa
waliomuamini Nabii Ibrahim ni Bibi Mtu mzima ambae Mfalme Namrudh Al Kabir
alimkata miguu yake na mikono yake yote. Na pia kuna kundi la watu wa Kuthan ambao
nao walikamatwa na kurushwa kwenye sehemu wanayofugiwa Simba, na pia kuna mtoto
mmoja mdogo wa Namrudh Al Kabir ambae nae alimkubali Nabii Ibrahim na hivyo
Mfalme Namrudh Al Kabir akamuua kwa kumtakata.

Allah Subhanah wa Ta’ala anayaelezea zaidi mahojiano haya yaliyotokea hapa katika
Surat Al Anbiyah kwa kuweka wazi kua watu hawa wa Nabii Ibrahim walipoona kua
wameshachoshwa na vitimbi vyake dhidi ya Miungu yao na hivyo wanashindwa kihoja,
hoja ambazo zinataka kuwafumbua watu macho ili waachane na upotovu wao na hivyo
kuwakosesha watu Maslahi yao.
274

Anasema Hasan Ibn Dinar kua amesema Layth Ibn Abi Sulayman kua amesemas
Mujahid kua: Hakika mie niliisoma aya hii mbele ya Abd Allah Ibn Umar aya
zisemazo:

‫ُف ﻟﱠ ُﻜ ْﻢ َوﻟِ َﻤﺎ‬


ٍّ ‫ﻀﱡﺮُﻛ ْﻢ ۞ أ‬ ِ‫ون ﱠ‬
ُ َ‫ٱﻪﻠﻟ َﻣﺎ ﻻَ ﻳَﻨ َﻔﻌُ ُﻜ ْﻢ َﺷْﻴﺌﺎً َوﻻَ ﻳ‬ ِ ‫ﺎل أَﻓَـﺘَـﻌﺒ ُﺪو َن ِﻣﻦ د‬
ُ ُ ْ َ َ‫﴿ﻗ‬
‫ٱﻧﺼُﺮ ۤواْ ِآﳍﺘَ ُﻜ ْﻢ إِن ُﻛﻨﺘُ ْﻢ‬ ِ ِ‫ون ﱠ‬
ُ ‫ٱﻪﻠﻟ أَﻓَﻼَ ﺗَـ ْﻌﻘﻠُﻮ َن ۞ ﻗَﺎﻟُﻮاْ َﺣِّﺮﻗُﻮﻩُ َو‬
ِ ‫ﺗَـﻌﺒ ُﺪو َن ِﻣﻦ د‬
ُ ُْ
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ﻓَﺎﻋﻠ‬
Qala afataAAbudoona min dooni Allahi ma la yanfaAAukum shay-an wala
yadhurrukum; Offin lakum walima taAAbudoona min dooni Allahi afala
taAAqiloona; Qaloo harriqoohu waonsuroo alihatakum in kuntum faAAileena
(Surat Al Anbiyah 21:66:68)

Tafsir: Nabii Ibrahim akasema: Ama nyinyi mnawaabudu wengine zaidi ya Allah,
(Miungu) ambao hawakunufaisheni kitu wala hawakudhuruni. Uff! Hamuoni aibu
nyinyi na Miungu yenu? jee mnatumia akili zenu lakini?(Namrudh Al Kabir na watu
wake) Wakasema: Mchomeni moto! Ili muwanusuru Miungu wenu kama ni watendaji
wa vitendo kweli.

Hivyo Abd Allah Ibn Umar akaniuliza kwa kusema: ‘Ya Mujahid Jee unamjua ni
nani aliewashauri watu hawa wamchome moto Ibrahim?’ name nikasema: ‘La
Simjui!’ Abd Allah Ibn Umar akasema: ‘Ni mmoja kati ya watu wa Mabedui wa
Uajemi’ Nami nikauliza: ‘Ya Abd Rahman! Jeekuna mabedui katika watu wa
Uajemi?’ nae akajibu: ‘Naam! Wakurd ndio Mabedui wa Uajemi, na ni miongoni
mwa mmoja wao ndio aliewashauri kua wamchome moto Ibrahim’

Hivyo Namrudh Al Kabir na watu wake wakaamua kufuata ushauri wa Mkurdi huyu na
kuona bora kuyaokoa Masanamu yao kisha wamuadhibu kwa kumuunguza Motoni Nabii
Ibrahim. Wanazuoni wa Ilm ya Tarikh wanasema kua: Mtu alietoa rai hii alikua akiitwa
Haynin, Haynin ni mtu ambae Allah Subhanah wa Taála alimsababishia Ardhi
kummeza na yuko katika hali ya adhabu ya geuzwa geuzwa ndani ya Ardhi hadi
katika siku ya kufufuliwa.

Baada ya watu hawa kukubaliana juu ya adhabu ya kumchoma moto Nabii Ibrahim kwa
kumtia kwenye Tanuri kubwa lililojengwa kwa umaalum wa umadhubuti na
uhifadhishaji wake joto la moto unaowashwa ndani yake, basi wakaamua kua kabla ya
275

kutimiza kusudio lao hilo kua kwanza wamkamate na kumfungia Nabii Ibrahim ndani ya
chumba ili asije akakimbia. Kisha wakajenga Tanuri hilo na wakaanza kazi ya kukusanya
kuni nyingi sana.Ambazo zinajumuisha kila aina ya mti ambao ni wenye kusifika kwa
uwakaji mkali moto na kutozimika kwake kirahisi kwa moto wake.

Watu hawa walikusanya kuni kwa muda wa mwezi mzima, kisha ulipofikia wingi wa
idadi yake waitakayo ya kuni hizo basi wakaanza kuziwasha moto kuni hizo, na
kuuwacha moto hadi ulipokolea ukali wake kiasi ya kua hata ndege walishindwa kuruka
katika eneo la anga liliopo juu ya moto huo na hata wao wenyewe walishindwa
kuukaribia moto huo kwa chini yake pale ulipokolea, hivyo Iblis akawapa mawazo ya
kutengeneza (Munjiniq) kifaa ambacho kitakaa kwa mbali ya moto huo, kisha
watamuweka Nabii Ibrahim juu yake na watakifyatua kifaa hicho ambacho kitamrusha
Nabii Ibrahim moja kwa moja hadi kati kati ndani ya tanuri hilo la moto huo.

Hapa sasa Mbingu na Ardhi, Malaika na Majini kwa pamoja wakaanza kumuomba Allah
Subhanah wa Taála, kumtaka amuokoe Nabii wake Ibrahim juu ya lile jambo linalotaka
kumfika kwani yeye ndie Mtu pekee anaemuabudu Allah Subhnaha wa Taála
Ulimwenguni hapa. Allah Subhanah wa Taála akasema: ‘Hakika mimi nakupeni nyie
uwezo wa kumuokoa na Moto huo kama atakuombeni na kuhitaji msaada wenu,
lakini kama hakukuombeni msaada wenu basi mwachieni mwenyewe, kwani bila
ya shaka ataniomba mimi msaada, kwani mimi ni mwenye kumjua Ibrahim, hakika
yeye ni Khalil wangu. Na mimi ni mwenye kujua ni nini nitakachokifanya kwa ajili
yake.’

Nabii Ibrahim akafungwa kamba na kuwekwa kwenye Munjiniq, na hapo hapo Malaika
wakamfuata Nabii Ibrahim, ambapo Malaika Mikail ambae ndie Malaika anaesimamia
Mvua akamfuata Nabii Ibrahim na kumwambia: ‘Kama unataka basi hakika mimi
nitauzima moto kwani hazina ya Maji na Mvua ipo chini ya usimamizi wangu’.
Huku Malaika wa Upepo akamwambia Nabii Ibrahim kwa kusema: ‘Hakika mimi nnao
uwezo wa kuupeperusha Moto wote huo juu angani’. Lakini hata hivyo Nabii Ibrahim
akawajibu Malaika hao kwa kusema: ‘Shukrani lakini sina haja na kitu chochote
kutoka kwenu’.

Kisha baada ya hapo Nabii Ibrahim akanyanyua yake mikono juu kwa kusema: ‘Ya Allah
hakika wewe ndie Mola pekee Mbinguni na Ardhini, unaestahiki kuabudiwa na
hakuna mtu yeyote yule hapa ardhini anaekuabudu isipokua mimi.’

Ama kwa upande wa Ubayy Ibn Kaáb Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema kua: ‘Baada
ya Nabii Ibrahim kufungwa kamba kwa ajili ya kurushwa ndani ya Moto basi
alisema: Hakuna Mola anaepaswa kuabudiwa isipokua wewe, utukufu ni wako
276

pekee, Mola wa Ulimwengu wote na ndie unaestahiki shukrani zote, Ufalme ni wako
na huna mshirika katika kuumba kwako’

Ghafla Munjiniq ikafyatuliwa na Nabii Ibrahim akajihisi kua ni mwenye kupaa na kuelea
angani kwa kasi kubwa sana, wakati akiwa bado yuko katika hali hio ya kuelea angani,
basi Malaika Jibril Alayhi Salam akamtokezea Nabii Ibrahim na kumwambia: ‘Ya
Ibrahim! Jee unahitaji kitu chochote?’ Nabii Ibrahim akamuuuliza Malaika Jibril:
‘Kutoka kwako wewe? La!’

Malaika Jibril akasema: ‘Basi Muombe Mola wako’. Bila ya shaka Nabii Ibrahim alikua
hana wasi wasi wowote kwani alikua na imani thabit kua Mola wake yuko pamoja nae
hivyo akasema: ‘Hakika mimi sihitaji kumuomba yeye kitu chochote, kwa sababu
yeye ni mwenye kujua kila kitu juu yangu na hivyo anajua majaaliwa yangu.
Hakika Allah anatitosheleza, na hakuna m-bora wa kumtegemea kuliko yeye.’

Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu A’nhu anasema kua Nabii Ibrahim Alayhi Salam
aliokolewa na Mola wake kutokana na moto huo kwa maneno yake hayo ya mwisho
aliyomwambia Jibril yaani:

﴾‫ﻴﻞ‬ِ ِ ‫﴿ﺣﺴﺒـﻨَﺎ ﱠ‬
ُ ‫اﻪﻠﻟُ َوﻧ ْﻌ َﻢ اﻟْ َﻮﻛ‬ ُْ َ
Hasbuna Allahu wa ni’ma al wakil (Surat Al Imran 3:173)

Tafsir: Hakika Allah anatutosheleza na hakuna m-bora wa kumtegemea kuliko yeye.

Tunapoiangalia ayah hii basi tunaona ingawa haya ni maneno yenye uzito mkubwa, lakini
kabla kuyatumia basi Muislam unatakiwa ufanye jitihada zako zote, na unaposhindwa
juu ya jambo husika basi ndio unaweza ukasema maneno haya kama inavyosema hadith
ifuatayo:

Kuna kesi baina ya watu wawili ililetwa mbele ya Rasul Allah Salallahu Aályhi wa
Salam, na baada ya kuhukumiwa kesi hio, basi yule ambae alieshtakiwa akaondoka
huku akisema:

﴾‫ﻴﻞ‬ِ ِ ‫﴿ﺣﺴﺒـﻨَﺎ ﱠ‬
ُ ‫اﻪﻠﻟُ َوﻧ ْﻌ َﻢ اﻟْ َﻮﻛ‬ ُْ َ
Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam aliposikia maneno haya, basi akamrisha
yule mtu aitwe, na alipofika mbele ya Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam basi
277

akamuuliza: Jee wakati ulipokua ukuiondoka hapa ulikua ukisema nini?’ yule mtu
akasema kua nilisema:

﴾‫ﻴﻞ‬ِ ِ ‫﴿ﺣﺴﺒـﻨَﺎ ﱠ‬
ُ ‫اﻪﻠﻟُ َوﻧ ْﻌ َﻢ اﻟْ َﻮﻛ‬ ُْ َ
Hapa Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema kumwambia yule mtu:

‫ﱯ‬ِ َ َ‫ ﻓَِﺈ َذا َﻏﻠَﺒ‬،‫ﺲ‬


َ ‫ َﺣ ْﺴ‬:‫ﻚ أ َْﻣٌﺮ ﻓَـ ُﻘ ْﻞ‬
ِ ‫ﻚ ِﺎﺑﻟْ َﻜْﻴ‬َ ‫ َوﻟَ ِﻜ ْﻦ َﻋﻠَْﻴ‬،‫ﻮم َﻋﻠَﻰ اﻟْ َﻌ ْﺠ ِﺰ‬ ‫إِ ﱠن ﱠ‬
ُ ُ‫اﻪﻠﻟَ ﻳَـﻠ‬
‫ﻴﻞ‬ ِ ِ ‫ﱠ‬
ُ ‫اﻪﻠﻟُ َوﻧ ْﻌ َﻢ اﻟْ َﻮﻛ‬
Hakika Allah analaumu juu ya udhaifu wako, lakini wewe unao ufaham wako
(utumie kwanza), na kama utashindwa katika jambo lako basi ndio unatakiwa
useme: Hasbuna Allahu wa ni’ma al wakil. (Imam An Nasai)

Hivyo Nabii Ibrahim ambae alikua bado yuko angani akahisi kuongezeka kwa kasi ya
kuelea kwake lakini kuelekea chini ardhini na ghafla akajihsi kua ni mwenye kutua chini
lakini si kwa hali ya kishindo wala ya kuhisi maumivu, ingawa hakutua katika sehemu
yeyote ile isipokua alitua moja kwa moja kati kati ndani ya Moto huo mkali uliokua
unawaka kwa wingi wa nguvu zote, lakini hata hivyo kutokana na ikhlasi iliyomo ndani
ya Moyo wake na katika maneno yake ya mwisho basi Allah Subhanah wa Ta’ala
akamuonesha Miujiza mikubwa Khalili wake Nabii Ibrahim pamoja na watu wa jamii
yake, kwani mbali ya wingi wa kuni na ukali wa moto huo lakini moto huo haukumgusa
Nabii Ibrahim hata unywele wake, ingawa uliziunguza kamba zote alizokua amefungwa
nazo. Kwani Allah Subhanah wa Ta’ala aliuamrisha moto huo uwe katika hali ambayo
ni kama anavyoielezea mwenyewe katika Qurán kua:

﴾‫﴿ﻗُـ ْﻠﻨَﺎ ﻳﻨَ ُﺎر ُﻛ ِﻮﱏ ﺑَـْﺮداً َو َﺳﻠَ َـﻤﺎ َﻋﻠَﻰ إِﺑْـَﺮِﻫ َﻴﻢ‬
Qulna ya naru koonee bardan wasalaman AAala ibraheema (Surat Al Anbiyah
21:69)

Tafsir: Na tukasema ewe moto kua baridi na salama kwa Ibrahim.

Ambapo wenye kujua wanasema kua maneno haya aliyasema Malaika Jibril kutokana na
Idhini aliyopewa na Allah Subhanah wa Taála na huo ni mtizamo wa Imam Ismail Abd
278

Rahman Al Suddi . Ama kwa upande mwengine basi anasema Abd Allah Ibn Abbas
Radhi Allahu Anhu kua: ‘Bila ya moto huo kuamrishwa kua na usalama, basi bila ya
shaka Ibrahim angefariki kutokana na hali ya ubaridi mtupu uliokua ndani ya moto
huo’.

Ama kwa upande wa Imam Qatadah Ibn Diama Al Sadusi basi yeye anasema kua: ‘Na
kutokana na amri hio basi hakuna moto hata mmoja uliokua unawaka ulimwenguni
katika wakati huo ilipotolewa amri hio isipokua moto huo ulikua katika hali hio ya
ubaridi.’ yaani katika siku hizi ambazo Nabii Ibrahim aliingizwa ndani ya moto basi
watu hawakua ni wenye kupika kwani hata maji yaliyotelekwa jikoni hayakua ni yenye
kupata Moto.

Anasema Mujtahid Imam Abu Bakr Muhammad Ibn Ibrahim Ibn Al Mundhir Al
Nishapuri Al Shafii kua: ‘Amesema Sulayman Ibn Sad Radhi Allahu Anhu kua:
‘Wakati Allah Subhanah wa Ta’ala aliposema: ‘Ya naru koonee bardan wasalaman
AAala Ibraheema’ basi Ami yake Nabii Ibrahim, akasema: ‘Ilikua ni kwa sababu
yangu mie ndio maana Moto ukawa haujamuunguza Ibrahim.’ Hivyo basi, Allah
Subhanah wa Ta’ala akajaalia kijinga cha Moto huo kuruka na kumuunguza
mguuni kwake Azar, na moto huo Ukamuunguza yeye’(Tafsir Imam Ibn Al Mundhir
Al Nishapuri)

Ama wanazuoni wamepingana juu ya Umri wa Nabii Ibrahim katika kipindi cha wakati
huu alipoingizwa Motoni na kutoka salama wa salimin, kwani kuna wasemao kua Nabi
Ibrahim alikua na umri wa miaka 16 lakini kwa upande wa Imam Abu Hasan Ali Ibn
Muhammad Ibn Habib Al Mawardi basi yeye anasema kua: ‘Nabii Ibrahim katika
kipindi alikua na umri wa miaka 26.’

Ama kwa upande wa Imam Abu Al Qasim Al Zamakhshari basi yeye anasema kuhusiana
na wale wenye kua na shaka kua inakuaje mtu anaingizwa katika moto wenye ukali wa
aina hii kisha mtu huyo anakua haungui hata unywele mmoja kua: ‘Allah Subhanah wa
Taala aliigeuza ngozi ya Nabii Ibrahim kua ni ngozi ambayo inastahmili moto na
hivyo kua na hali ya kutoungua kwa moto, kama vile ambavyo yalivyo maumbile
ya Malaika wa Motoni.’

Al Minhal Ibn Umar anasema kua Nabii Ibrahim mwenyewe alisema kua: ‘Katika uhai
wangu kamwe sikuwahi kua na wakati wa raha kama nilivyokua katika wakati
ambao nilikua nimeingizwa ndani ya Moto.’ Ama kwa upande wa Imam Ismail Abd
Rahman Al Suddi basi yeye anasema kua: ‘Malaika walimbeba Nabii Ibrahim kwenye
mikono yake wakamtoa kwenye moto na kumuweka chini, amapo Nabii Ibrahim
akajiona yuko kwenye Bustani yenye mito na iliojaa miwardi iliyochanua
mawArdhi ndani yake.’
279

Siku 7 zikapita, watu wakajua kua Nabii Ibrahim ameshateketea na kua kama jivu badala
ya mkaa. hivyo Moto ulipomalizika na kuzimika watu wakamuona Nabii Ibrahim akiwa
amekaa salama wa salimini ndani ya tanuri lile lililojaa majivu na yeye akiwa na mtu
mwengine ambae aliefanana nae alipotolewa na kuulizwa ni nani yule uliekua umekaa
nae, Nabii Ibrahim akajibu: Yule alikua ni Malaika wa vivuli Allah Subhanah wa
Ta’ala aliniletea ili nisiwe mpweke.

Allah Subhanah wa Taála anaweka wazi namna alivyoamua kumpandisha darja Nabii
Ibrahim kutokana na kua ni mwenye kufuzu mitihani mingi ikiwemo mtihani wa
kutumbukizwa Motoni ambao ulikua pia ni uthibitisho wa kuonesha uthabiti wa Imani
yake kwa Mola wake na pia kua ni mfano bora kwa walimwengu kutokana na kujitolea
kwa Mola wake, kama inavyoonesha aya ifuatayo:

ِ ‫ﻚ ﻟِﻠﻨ‬
َ َ‫ﱠﺎس إِ َﻣﺎﻣﺎً ﻗ‬
‫ﺎل‬ ِ ‫ﺎل إِِﱏ ﺟ‬
َ ُ‫ﺎﻋﻠ‬ ٍ ِ ِ ِ ِ ِِ
َ ّ َ َ‫﴿ َوإذ ٱﺑْـﺘَـﻠَ ٰﻰ إﺑْـَﺮاﻫ َﻴﻢ َرﺑﱡﻪُ ﺑ َﻜﻠ َﻤﺎت ﻓَﺄََﲤﱠُﻬ ﱠﻦ ﻗ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ ُ ‫ﺎل ﻻَ ﻳـﻨ‬
ََ َ َ‫َوِﻣﻦ ذُِّرﻳﱠِﱴ ﻗ‬
َ ‫ﺎل َﻋ ْﻬﺪى ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
Wa-idhi ibtala ibraheema rabbuhu bikalimatin faatammahunna qala innee
jaAAiluka lilnnasi imaman qala wamin dhurriyyatee qala la yanalu AAahdee
aldhdhalimeena (Surat Al Baqara 2:124)

Tafsir: Na kumbuka wakati Mola wake Ibrahim alipomjaribu kwa kumpa amri ambayo
nae aliitekeleza. Hivyo Allah Subhanah wa Taála akasema: Kwa hakika mimi
nitakufanya wewe kua kiongozi wa Watu. Ibrahim akasema: ‘Na watoto wangu
(Wafanye kua Viongozi)’. (Allah Subhanah wa Taála akasema) ‘Makubaliano yangu
hayawajumuishi Waliokua Madhalim’

Aya yetu hii imetumia neno Kalimaat ambalo hua ni lenye utokanana neno Kalama
ambalo kwa lugha ya Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Kusema, Kutoa Amri au
Kuelezea kwa Maneno. Hivyo neno Kalimatun hua ni lenye kumaanisha Maneno,
Maelezo, Mtizamo, Hoja, Ubashirio, Ujumbe, Utume, Maneno yanayotumiwa ili
kufafanua kitu au Mtizamo.

Katika kulifafanua maana ye neno Kalimat basi Imam Muhamad Ibn Muhammad
Murtada Al Zabidi anasema katika Taj Al Arusi kua: ‘Nabii Isa Ibn Maryam alikua
akiitwa pia Kalimat Allah kwa sababu kauli zake zilikua ni zenye uwaongza watu
kenye njia ya Allah Subhanah wa Ta’ala.’
280

Kwani anasema Imam Ibn Jariri Al Tabari kua: ‘Kaliman hizi alizopewa Nabii
Ibrahim zilikua zinajumuisha majukumu muhimu 30 yaliyotajwa kwenye aya
zifuatazo:

Aya ya 112 ya Surat At Tawba:

ِ ‫ﺎﺟ ُﺪو َن‬ ِ ‫ٱﳊ ِﺎﻣ ُﺪو َن ٱﻟ ﱠﺴﺎﺋِﺤﻮ َن ٱﻟﱠﺮاﻛِﻌﻮ َن ٱﻟ ﱠﺴ‬ ِ ِ


‫ٱﻵﻣُﺮو َن‬ ُ ُ َْ ‫﴿ٱﻟﺘﱠﺎﺋﺒُﻮ َن ٱﻟْ َﻌﺎﺑ ُﺪو َن‬
ِِ ِ ِ‫ود ﱠ‬ ِ ‫ٱﳊﺎﻓِﻈُﻮ َن ِﳊ ُﺪ‬ ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ٱﻪﻠﻟ َوﺑَ ّﺸ ِﺮ ٱﻟْ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬ ُ ُ ‫ﺑِﭑﻟْ َﻤ ْﻌُﺮوف َوٱﻟﻨ‬
َْ ‫ﱠﺎﻫﻮ َن َﻋ ِﻦ ٱﻟْ ُﻤﻨ َﻜ ِﺮ َو‬
Altta-iboona alAAabidoona alhamidoona alssa-ihoona alrrakiAAoona
alssajidoona al-amiroona bialmaAAroofi waalnnahoona AAani almunkari
waalhafidhoona lihudoodi Allahi wabashshiri almu/mineena (Surat At Tawba
9:112)

Tafsir: (Waumini ambao Allah Subhanah wa Ta’ala ameridhika na Maisha


yao ni) Wale ambao Wenye Kutubu, Wenye Kumuabudu, Wenye
Kumtukuza, Wenye Kufunga, Wenye Kurukuu na Kusujudu,Wenye
Kuamrishana Mema na Kukatazana Maovu, na Wenye Kujihifadhi ndani
ya mipaka aliyowekewa na Allah, na wabashirie mema Waumini.

Aya ya 35 ya Surat Al Ahzab:

ِ َ‫ﺎت وٱﻟْ َﻘﺎﻧِﺘِﲔ وٱﻟْ َﻘﺎﻧِﺘ‬ ِ ِ ِِ ِ ِ ِِ


‫ﺎت‬ َ َ َ َ‫ﲔ َوٱﻟْ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬ َ ‫ﲔ َوٱﻟْ ُﻤ ْﺴﻠ َﻤﺎت َوٱﻟْ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬َ ‫﴿إِ ﱠن ٱﻟْ ُﻤ ْﺴﻠﻤ‬
‫ﺎت‬ِ ‫ﺎﺷﻌ‬ ِ ْ ‫ﺎﺷﻌِﲔ و‬ ِ ْ ‫ات و‬ ِ ِ ‫ﺼﺎﺑِ ِﺮﻳﻦ وٱﻟ ﱠ‬ ِ ِ ‫ﺼ ِﺎدﻗِﲔ وٱﻟ ﱠ‬
َ َ‫ٱﳋ‬ َ َ َ‫ٱﳋ‬ َ ‫ﺼﺎﺑَﺮ‬ َ َ ‫ﺼﺎدﻗَﺎت َوٱﻟ ﱠ‬ َ َ ‫َوٱﻟ ﱠ‬
‫وﺟ ُﻬ ْﻢ‬ ِ ِ ْ ‫ﺎت و‬ ِ ‫ﺼﺎﺋِﻤ‬ ِ ِ ‫ﺎت وٱﻟ ﱠ‬ ِ َ‫وٱﻟْﻤﺘَﺼ ِّﺪﻗِﲔ وٱﻟْﻤﺘَﺼ ِّﺪﻗ‬
َ ‫ﲔ ﻓُـُﺮ‬ َ ‫ٱﳊَﺎﻓﻈ‬ َ َ ‫ﲔ وٱﻟ ﱠ‬ َ ‫ﺼﺎﺋﻤ‬ َ ُ َ َ َ ُ َ
﴾ً‫َﺟﺮاً َﻋ ِﻈﻴﻤﺎ‬ ِ ِ ِ ِ ‫ﺎت وٱﻟ ﱠﺬاﻛِـ ِﺮﻳﻦ ﱠ‬ ِ َ‫ٱﳊﺎﻓِـﻈ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟَ َﻛﺜﲑاً َوٱﻟ ﱠﺬاﻛَﺮات أ‬
‫َﻋ ﱠﺪ ﱠ‬
ْ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﳍُﻢ ﱠﻣ ْﻐﻔَﺮةً َوأ‬ َ َ َْ ‫َو‬
Inna almuslimeena waalmuslimati waalmu/mineena waalmu/minati
waalqaniteena waalqanitati waalssadiqeena waalssadiqati waalssabireena
waalssabirati waalkhashiAAeena waalkhashiAAati waalmutasaddiqeena
waalmutasaddiqati waalssa-imeena waalssa-imati waalhafidheena
281

furoojahum waalhafidhati waaldhdhakireena Allaha katheeran


waaldhdhakirati aAAadda Allahu lahum maghfiratan waajran
AAadheeman (Surat Al Hazab 33:35)’

Tafsir: Kwa hakika Waislam wa Kiume na Waislam wa Kike, Waumini wa


Kiume na Waumini wa Kike, Watiifu wa Kiume na Watiifu wa Kike kwa Allah,
Wakweli wa Kume na wakweli wa Kike, Wenye Subra wa Kume na Wenye
Subra wa Kike, Wanyenyekevu wa Kiume na Wanyenyekevu wa Kike, Wenye
kutoa Sadaqa wa iume na Wenye Kutoa Sadaqa wa Kike, Wenye Kufunga
Saum wa Kiume na Wenye Kufunga Saumu wa Kike, Wenye Kujihifadhi Tupu
zao Wa Kiume na Wenye Kujihifadhi Tupu zao Wa kike. Wenye Kumkumbuka
sana Allah miongoni mwa Wanaume na Wenye Kumkubuka Allah Miongoni
mwa Wanawake, Amewaandalia Allah Malipo Mazuri sana.

Aya ya 1 mpaka ya 10 za Surat Al Muuminun:

‫ﺻﻠﻮاَﻬﺗِِ ْﻢ‬َ ‫ﻳﻦ ُﻫ ْﻢ ِﰱ‬ َ


ِ ‫اﻪﻠﻟِ ٱﻟﱠﺮ ْﲪـٰ ِﻦ ٱﻟﱠﺮِﺣﻴ ِﻢ ۞ ﻗَ ْﺪ أَﻓْـﻠَﺢ ٱﻟْﻤﺆِﻣﻨﻮ َن ۞ ٱﻟﱠ‬
‫ﺬ‬ ُ ُْ َ ‫﴿ﺑِ ْﺴ ِﻢ ﱠ‬
۞ ‫ﺎﻋﻠُﻮ َن‬ ِ َ‫ﺎﺷﻌﻮ َن ۞ وٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻫﻢ ﻋ ِﻦ ٱﻟﻠﱠ ْﻐ ِﻮ ﱡﻣﻌ ِﺮﺿﻮ َن ۞ وٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻫﻢ ﻟِﻠﱠﺰَﻛﻮاةِ ﻓ‬ ِ
ُْ َ َ ُ ْ َ ُْ َ َ ُ ‫َﺧ‬
‫ﺖ أَْﳝَﺎﻧـُ ُﻬ ْﻢ ﻓَِﺈﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ‬ ِ ِ ِ ِ ِ‫ﱠ‬
ْ ‫ﻳﻦ ُﻫ ْﻢ ﻟ ُﻔُﺮوﺟ ِﻬ ْﻢ َﺣﺎﻓﻈُﻮ َن ۞ إِﻻﱠ َﻋﻠَ ٰﻰ أ َْزَواﺟ ِﻬ ْﻢ أ َْو َﻣﺎ َﻣﻠَ َﻜ‬َ ‫َوٱﻟﺬ‬
ِ‫۞ ﱠ‬ ِ
ِ‫ﻳﻦ ُﻫ ْﻢ‬ َ ‫ﺎدو َن َوٱﻟﺬ‬ ُ ‫ﻚ ُﻫ ُﻢ ٱﻟْ َﻌ‬ َ ِ‫ﻚ ﻓَﺄ ُْوﻟَـٰﺌ‬
َ ‫ﲔ ۞ ﻓَ َﻤ ِﻦ ٱﺑْـﺘَـﻐَ ٰﻰ َوَرآءَ ٰذﻟ‬ ِ
َ ‫َﻏْﻴـُﺮ َﻣﻠُﻮﻣ‬
ِ ِِ ِ‫۞ ﱠ‬ ِِ ِِ َ ‫ِ◌ﻷَﻣ‬
‫ﻚ ُﻫ ُﻢ‬ َ ِ‫ﺻﻠَ َﻮاﻬﺗ ْﻢ ُﳛَﺎﻓﻈُﻮ َن۞ أُْوﻟَـٰﺌ‬ َ ‫ﻳﻦ ُﻫ ْﻢ َﻋﻠَ ٰﻰ‬ َ ‫ﺎ�ﻬﺗ ْﻢ َو َﻋ ْﻬﺪﻫ ْﻢ َراﻋُﻮ َن َوٱﻟﺬ‬ َ
﴾‫ٱﻟْﻮا ِرﺛُﻮ َن‬
َ
Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Qad aflaha almu/minoona; Alladheena
hum fee salatihim khashiAAoona; Waalladheena hum AAani allaghwi
muAAridoona,Waalladheena hum lilzzakati faAAiloona; Waalladheena
hum lifuroojihim hafidhoona; Illa AAala azwajihim aw ma malakat
aymanuhum fa-innahum ghayru maloomeena; Famani ibtagha
waraa dhalika faola-ika humu alAAadoona; Waalladheena hum li-
amanatihim waAAahdihim raAAoona; Waalladheena hum AAala
282

salawatihim yuhafidhoona; Ola-ika humu alwarithoona (Surat Al Muuminun


23:1-10)

Tafsir: Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehma Mwingi wa Huruma; Kwa hakika
Wamefuzu Walioamini, Wale ambao ni wenye Unyenyekevu ndani ya Sala zao.
Na wale ambao ni wenyye kuyapamgongo maneno maovu, Na Wale wenye
kutoa Zakkah, Na wale wenye Kujihifadhi Tupu zao isipokua kwa wake zao na
wanaowamiliki mikononi mwao ambao hawawezi kulaumiwa juu yao, lakini
wale wanaotafuta zaidi ya hayo basi ndio waliovuka mipaka. Na wale wenye
kuweka amana zao na ahadi zao kuzitekeleza. Na wale ambao ni wenye
kuziifadhi Sala zao, Hakika wao ndio watakaorithishwa (Pepo).

Na aya ya 23 mpaka aya ya 32 za Surat Al Maarij.

‫ﻮم ۞ ﻟِّﻠ ﱠﺴﺂﺋِ ِﻞ‬ ِِ ۤ ‫﴿ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻫﻢ ﻋﻠَﻰ ﺻﻼَﻬﺗِِﻢ دآﺋِﻤﻮ َن ۞ وٱﻟﱠ ِﺬ‬
ٌ ُ‫ﻳﻦ ِﰲ أ َْﻣ َﻮاﳍ ْﻢ َﺣ ﱞﻖ ﱠﻣ ْﻌﻠ‬
َ َ ُ َ ْ َ ٰ َ ُْ َ
‫اب َرّﻬﺑِِﻢ ﱡﻣ ْﺸ ِﻔ ُﻘﻮ َن‬ ِ ‫وٱﻟْﻤ ْﺤﺮ ِوم ۞ وٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻳﺼ ِّﺪﻗُﻮ َن ﺑِﻴـﻮِم ٱﻟ ِّﺪﻳ ِﻦ ۞ وٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ُﻫﻢ ِﻣﻦ َﻋ َﺬ‬
ّْ َ َ َْ ََُ َ ُ َ َ
‫وﺟ ِﻬ ْﻢ َﺣﺎﻓِﻈُﻮ َن ۞ إِﻻﱠ َﻋﻠَ ٰﻰ‬ ِ ‫ﻮن ۞ وٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻫﻢ ﻟُِﻔﺮ‬
ُ ُْ َ َ
ٍ ‫۞ إِ ﱠن ﻋ َﺬاب رّﻬﺑِِﻢ َﻏﻴـﺮ ﻣﺄْﻣ‬
ُ َ ُْ ْ َ َ َ
ِ ِ ِ ِ
‫ﻚ‬ َ ‫ﲔ ۞ ﻓَ َﻤ ِﻦ ٱﺑْـﺘَـﻐَ ٰﻰ َوَرآءَ ٰذﻟ‬ َ ‫ﺖ أَْﳝَﺎﻧـُ ُﻬ ْﻢ ﻓَﺄﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ َﻏْﻴـُﺮ َﻣﻠُﻮﻣ‬ْ ‫أ َْزَواﺟ ِﻬ ْﻢ أ َْو َﻣﺎ َﻣﻠَ َﻜ‬
‫ﻳﻦ ُﻫ ْﻢ‬ ِ‫۞ ﱠ‬ ِِ ِِ َ ‫ﻓَﺄُوﻟَـٰﺌِﻚ ﻫﻢ ٱﻟْﻌﺎدو َن ۞ وٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻫﻢِ ﻷَﻣ‬
َ ‫ﺎ�ﻬﺗ ْﻢ َو َﻋ ْﻬﺪﻫ ْﻢ َراﻋُﻮ َن َواﻟﺬ‬ َ ُْ َ َ ُ َ ُُ َ ْ
ٍ ‫ﻚ ِﰱ ﺟﻨ‬ ِ ِِ ‫ﺑِﺸﻬﺎداﻬﺗِِﻢ ﻗَﺎﺋِﻤﻮ َن ۞ واﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻫﻢ ﻋﻠَﻰ‬
‫ﱠﺎت‬ َ َ ِ‫ﺻﻼَﻬﺗ ْﻢ ُﳛَﺎﻓﻈُﻮ َن ۞ أُْوﻟَـٰﺌ‬ َ ٰ َ ُْ َ َ ُ َ ََ
﴾‫ن‬ َ ‫ﱡﻣ ْﻜَﺮُﻣﻮ‬
Alladheena hum AAala salatihim da-imoona; Waalladheena fee amwalihim
haqqun maAAloomun; Lilssa-ili waalmahroomi; Waalladheena
yusaddiqoona biyawmi alddeeni; Waalladheena hum min AAadhabi
rabbihim mushfiqoona; Inna AAadhaba rabbihim ghayru ma/moonin;
Waalladheena hum lifuroojihim hafidhoona; Illa AAala azwajihim aw ma
malakat aymanuhum fa-innahum ghayru maloomeena; Famani ibtagha
waraa thalika faola-ika humu alAAadoona; Waalladheena hum li-
283

amanatihim waAAahdihim raAAoona; Waalldheena hum bishahadatihim


qa-imoona; Waalladheena hum AAala salatihim yuhafidhoona; Ola-ika fee
jannatin mukramoona(Surat Al Maarij 70:23-34)

Tafsir: Wale ambao niwenye kudumu na Sala Zao, Na wale ambao katika Mali
zao kuna haki Maalum kwa Masikini wenye Kuomba na Wasiokua na Kitu, na
Wale wenye Kuamini Siku ya Malipo. Na kwa Wale wenye kuogopa Adhabu za
Mola wao, Kwani kutokana na Adhabu ya Mola wao hawajisikii Salama nayo,
Na wale wenye Kujihifadhi Tupu zao isipokua kwa wake zao na wanaowamiliki
mikononi mwao ambao hawawezi kulaumiwa juu yao, lakini wale wanaotafuta
zaidi ya hayo basi ndio waliovuka mipaka. Na wale wenye kuweka amana zao
na ahadi zao kuzitekeleza. Na wale wanaosimama Imara kwenye Shahada zao,
Na wale wenye Kuzihifadhi Sala zao vizuri sana, hao ndio watakaoingia
Peponi.

Lakini hapo hapo kuna mtizamo wa Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu
ambao unasema kua: ‘Kalimat alizozitekeleza Nabii Ibrahim na zikampandisha Darja
ni mtihani aliyopewa na kisha akafuzu mitihani hiyo ambayo ni ya kutupwa ndani
ya Tanuri la Moto, Kupeleka kuuhama Mji wake na kuachana na Watu Wake,
Kusafiri Masafa Marefu kwa ajili ya Kuueneza Ujumbe wa Allah Subhanah wa
Ta’ala, Kumbdi kuwaacha Mke wake na Watoto wake peke yao katika eneo la
Jangwani lisilokua na Mtu, n.k ’

Hivyo hapa haimaanishi kua Allah Subhanah wa Ta’ala alimpa Mitihani Nabii Ibrahim
kwa ajili ya kumjaribu labda kwa sababu ya kua alikua hajui uthabiti wa Imani yake, La.
Kwani alikua anajua, bali alimpa mitihani kwa sababu ya kuja kutuuwekea wazi sisi mimi
na wewe ukubwa wa Imani yake na Ikhlas yake katika amali zake kwa ajili ya Mola
wake.

Ama kwa upande wa Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al
Razi basi yeye anasema kua: ‘Baada ya Allah Subhanah wa Ta’ala kuainisha neema
alizowaneemesha watu wa Bani Israil na namna walivyoonyesha dharau juu ya
neema hizo, basi anagusia kisa cha Nabii Ibrahim, na hii ni kwa sababu Nabii
Ibrahim alikua ni mwenye kukubalika na Watu tofauti wenye Imani na wasiokua
na Imani. Wakritso na Mayahudi, na hivyo kuweka wazi kua kukubalika kwa Nabii
Ibrahim na kupandishwa Darja kua ni Kiongozi wa Ummah basi hakutokani na
kitu chochote isipokua kunatokana na Jitihada zake na kujisalimi kikamilifu mbele
ya Allah Subhanah wa Ta’ala. Hivyo Mtu hawezi kupandishwa Darja moja kwa
moja bila ya kuonesha Jitihada zake na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala
akamuonya Nabii Ibrahim kua hawezi kua kiongozi wa wafanyao Maovu.’
284

Na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Nabii Ibrahim baada ya


kumuomba dua kua aviwapandishe darja na vizazi vyake, kua makubaliano hayo ya
kumpandisha yeye Nabii Ibrahim darja hayahusiani na watu waovu, Ambapo tunaona
kua kupandishwa huko kwake darja hakumaanishi kua na hata vizazi vyake vyote
vitapandishwa darja bila ya wao kufanya jitihada yeyote katika kujitolea kwa ajili ya
Mola wao. Hivyo Watu watakaomfuata yeye katika Imani basi ndio watakaoongoka na
watakaoachana nae na kumkana basi watakua ni waliopotoka na hivyo kua ni
waliojidhulumu Nafsi zao kutokana na ujinga wao na kujumuishwa katika miongoni mwa
wale wanaozungumziwa katika aya isemayo:

﴾ً‫﴿إِﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن ﻇَﻠُﻮﻣﺎً َﺟ ُﻬﻮﻻ‬


Innahu kana dhaluuman jahuulan (Surat Al Ahzab 33:72)

Tafsir Kwa hakika yeye (Ibn Adam) ni mwenye kujidhulumu na mjinga.

Kwani neno Dhaluma maana yake ni kua aliejidhulumu Nafsi yake na neno Jahula maana
yake hua ni Kutokujua matokeo yake.

Baada ya mtihani huo na Nabii Ibrahim kutolewa kutoka katika Tanuri la Moto basi
Namrudh Al Kabir akasema: ‘Hakika mimi nitatoa Kafara kwa ajili ya Mungu wako
aliekuokoa wewe na Moto huu, kwa sababu ya kua wewe umekataa kuabudu
Mungu yeyote isipokua yeye. Mimi nitachinja Ngo’mbe 4000’.

Nabii Ibrahim akasema kumwambia Namrudh Al Kabir: ‘Hakika Mungu wangu


hatopokea kitu chochote kutoka kwako wakati wewe ukiwa bado hujamuamini,
isipokua pale utakapo ihama Dini yako na kuifuata Dini yangu’

Namrudh Al Kabir akasema: ‘Ewe Ibrahim hakika mimi siwezi kuachana na Miungu
wangu, lakini bila ya shaka kuchinja nitachinja kwa ajili ya Mola wako’

Baada ya tukio hilo basi baadhi ya watu wakawa wanaanza kutafakkari juu ya Miujiza
iliyotokea baada ya Nabii Ibrahim kuingizwa Motoni na kutoka akiwa katika hali ya
uzima wa kutoungua hata chembe na badala yake zimeleta Manufaa kwa kudhihirisha
uwezo wa Mola wake Nabii Ibrahim hapa Namrudh Al Kabir akaona kua huenda Nabii
Ibrahim akapata Wafuasi ambao watamuunga mkono, hivyo kuendelea kutishia
Mamlaka yake na Miungu yake, hivyo akaamua kumpiga vita Nabii Ibrahim na Mola
wake, na kwa kua alikua ameshajua kua ni vigumu kumshinda Nabii Ibrahim peke yake
basi Namrudh Al Kabir akatayarisha jeshi lake.
285

Na kisha akamwambia Nabii Ibrahim kua anataka mapigano baina yake yeye na jeshi
lake la Miungu wake dhidi ya Nabii Ibrahim na jeshi la Mola wake. Hivyo Nabii Ibrahim
ingawa alikua peke yake, basi akakubaliana na mpango huo, na wakapanga siku na
sehemu ya uwanja wa mapambano. Kwani Namrudh Al Kabir alitumia Mda wake
kutayarisha jeshi lake shupavu na hapo hapo kuliandaa kimazoezi kwa ajili ya siku ya
Mapigano.

Ama kwa upande wa Nabii Ibrahim basi yeye alikua na Imani yake na Ikhlas mbele ya
Mola wake. Na ulipowadia siku ya siku, Nabii Ibrahim hakukimbia nchi wala hakigoma
kuenda kwenye uwanja wa Mapambano, hii ilikua ni siku kama hizi tulizonazo kwa
upande wa hali ya hewa, kwani jua lilikua kali sana na hakukua na hata mawingu. Nabii
Ibrahim Alipofika katika Uwanja wa Mapambano akakuta Jeshi kubwa sana la Namrudh
Al Kabir pamoja Namrudh Al Kabir mwenyewe na watu wake wakiwa na ari kubwa sana
ya Mapigano. Nabii Ibrahim akasogea katika eneo lake la kukabiliana na Namrudh Al
Kabir na jeshi lake kisha akamhakikishia Mola wake kua hakuna anaemtegemea isipokua
yeye. Subhana Allah w Allahu Akbar!

Kwani hapo hali ya hewa ilibadilka ghafla kutoka kwenye hali ya jua kali isiyokua na
mawingu na kuingia katika hali yenye Mawingu mazito sana yenye kutisha. Hivyo Mara
moja tu ghafla uwanja huo wa Mapigano ambao ulikua nje kabisa kwenye uwazi, basi
ukawa kama uwanja wa ulifungiwa ndani ya jengo kubwa fulani ambako juu yake kuna
paa jeusiii.

Ila sasa paa hilo halikua la bati wala la makuti wala la zege bali lilikua paa la jeshi la
Allah Subhanah wa Ta'ala ambalo lilikuja kumsaidia Khallilu Allah.

Na halikua paa la Wingu la Mawingu ya mvua bali lilikua paa la Wingu la Wadudu Mbu!
Na Mbu hao walikua balaa, kwani wingu zima la Mbu lilivamia jeshi la Namrudh Al
Kabir na watu wake! Na walikua na midomo yenye sindano kali sana ambayo
akikutafuna sehemu moja basi Maumivu yake makali sana unayahisi mwili mzima kiasi
ya kua kila mmoja miongoni mwa Wanajeshi wa Namrudh Al Kabir alitupa silaha na
kutafuta kwa kukimbilia, hivyo ingawa mdudu mbu ni mdudu mdogo sana lakini
madhara yake kimaumivu kwa jeshi hilo ilikua ni balaa.

Mpaka Namrudh Al Kabir mwenyewe alikimbia na katika kukimbia kwake ili kujihami
dhidi ya Mbu hao basi Allah Subhanah wa Ta'ala akajaalia mbu mmoja akaingia puani
mwake. Kwani kimaumbile basi Pua hua ni yenye kuunganika na Koo na Sehemu ya
Katikati ya ngoma ya Sikio, kupitia katika Mrija ambao unajulikana kama Eustachian.
Na hii ni kwa sababu ili mtu uwe ni mwenye kua na uwezo wa kusikia basi ngoma ya
sikio lazima iwe ni yenye kua na hewa ndani yake. Na ndio maana mtu unapokua
286

unaumwa na koo au tonsilis baadhi ya wakati basi basi hua ni mwenye kuhisi pia
maumivu kama ya kichomi cha sindano ndani ya sikio.
Naam, hivyo unaposikia kichomi cha sikio basi kumbuka adhabu aliyokua akiipata
Mfalme Al Namrudh Al Kabir baada ya kumkataa Mola wake, kisha nawe Mshukuru
Mola wako kwa kukujaalia kua na Utajiri Bora zaidi Duniani ambao ni Utajiri wa Kua
na Imani ya Dini ya Kiislam na kumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala na Mtume wake
Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam. Kwani kwa upande wa Namrudh Al Kabir
ambae yeye alimkufuru Mola wake basi alipatwa na maumivu makali mara 100 zaidi ya
unayoyahisi wewe wakati unapoumwa na sikio.

Maumivu yaliyotokana na mbu huyo yalimuadhibu sana kiasi ya kua ilimbidi Namrudh
Al Kabir kuwatafuta watu maalum wanne kwa ajili tu ya kumpiga Vibao vya nguvu vya
masikio kwa ajilli ya kupunguza maumivu ya hao ndani ya kichwa chake ili angalau
yapungue. Hali ambayo alidumu nayo kwa muda wa miaka 40 huku akiwa anapigwa
pigwa hadi kufariki kwake huku akiwa bado hajamkubali Mola wake na hivyo akawa ni
miongoni mwa waliojichagulia mahali maalum katika Moto wa Jahannam katika bonde
la Saqqar.

HIJRA YA NABII IBRAHIM KUTOKA KATIKA MJI WA UR
KUELEKEA FALESTINA

Hivyo baada ya tukio la mapigano baina ya Al Namrudh Al Kabir na jeshi la mdudu Mbu
huku Mfalme al Namrudh al Kabir akiwa ni mwenye kuendelea na adhabu ya kupigwa
vibao vya masikio basi Nabii Ibrahim akaamua kuchukua hatua ambayo ni ya kupenda
na kuchukia kwa ajili ya Allah Subhanah wa Taála na hivyo akawa ni mwenye kujitenga
na familia yake, na watu wake kwa ajili ya Mola wake hivyo akasema:

ِ ‫ٱﻪﻠﻟِ وأَدﻋﻮ رِﰉ ﻋﺴ ۤﻰ أَﻻﱠ أَ ُﻛﻮ َن ﺑِﺪﻋ‬


‫ﺂء َرِّﰉ‬ ِ ِ ِ ﴿
َُ َ َ ّ َ ُ ْ َ ‫َوأ َْﻋﺘَﺰﻟُ ُﻜ ْﻢ َوَﻣﺎ ﺗَ ْﺪﻋُﻮ َن ﻣﻦ ُدون ﱠ‬
﴾ً‫َﺷ ِﻘﻴّﺎ‬
WaaAAtazilukum wama tadAAoona min dooni Allahi waadAAoo rabbee AAasa
alla akoona biduAAa-i rabbee shaqiyyan (Surat Maryam 19:48)

Tafsir: Na mimi nitajitenga nanyi na kile mnachokiabudu zaid ya Allah. Na


nitamuomba Mola wangu. Na natumai kua huenda Mola wangu atanikubalia.
287

Aya inatuwekea wazi unyenyekevu wa Nabii Ibrahim ambae anajua kua ingawa yeye ni
Khalil Allah, na anaemuomba ana ukaribu nae lakini hata hivyo kujibu Maombi yake hua
si wajibu wa Mola wake kujibu kwani juu ya hilo basi Allah Subhanah wa Ta’ala hua ni
mwenye khiari juu yake. Kisha Nabii Ibrahim akaamua kuchukua hatua bora zaidi ya
kujitenga na watu hao ambayo ni kufanya Hijra kwa ajili ya Mola wake na akasema:

﴾‫ﺐ إِ َﱃ َرِّﰉ َﺳﻴَـ ْﻬ ِﺪﻳ ِﻦ‬ ِ ِ


ٌ ‫﴿إِّﱏ َذاﻫ‬
Innee dhahibun ila rabbee sayahdeeni; (Surat As Saffat 37:99)

Tafsir: ‘Hakika, mimi nnaenda kwa Mola wangu, na ataniongoza’

Ama kuhusiana na ayah hii basi Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr ad Din Al Razi basi
amesema kua: ‘Hapa Nabii Ibrahim alikua akimaanisha kua Hakika mimi nnahama
kwa ajili ya kutekeleza Amri ya Mola wangu.’

Kulingana na mtizamo wa Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Is-haq basi tunaona
kua: ‘Miongoni mwa waliomkubali Nabii Ibrahim katika watu wake ni pamoja na
Lut, ambae alikua ni Mtoto wa kaka yake Nabii Ibrahim na alikua akiitwa Lut Ibn
Harran Ibn Tara, Harran mdogo alikua ni kaka yake Nabii Ibrahim, na pia kulikua
na mtu mwengine aitwae Nahor Ibn Tara ambae nae pia alikua ni kaka yake Nabii
Ibrahim na alikua na mtoto aitwae Tanwil. Tanwil Ibn Nahur Ibn Tara alipooa basi
mkewe alizaa watoto wawili Laban na Rifkah, ambapo Rifkah ndio akawa mke wa
Nabii Is-haq Ibn Ibrahim ambao ndoa yao ndio iliyotoa mtoto ambae ni Nabii
Yaqub, Nabii Yaqub alikua na wake wawili ambao ni Liyah na Rahil, ambao nao
ni watoto wa Laban. Na pia alikuwemo Sarah ambae ni mtoto wa Harran mkubwa
ambae ni Ami yake Nabii Ibrahim’

Baada ya Ibrahim A’layhi Salaam kuamua kuhama yeye na mkewe Sarah ambae alikua
pia ni Binamu yake, kutoka katika mji huo na kumuomba Allah amjaalie kizazi chema
pamoja nae alikuwemo pia Lut aliekua ni mtoto wa binam yake Nabii Ibrahim. Ama
kuhusiana na jina la Lut basi hili ni jina linalotokana na neno Latta la Kiarabu ambalo
hua ni lenye kumaanisha Kua King’ang’anizi wa Mapenzi kiasi ya kua husikii wala
huoni, kua ni mwenye kumuweka akilini na mawazoni mtu umpendae.

Kwa hivyo ingawa Nabii Lut alikua ni mdogo kiumri lakini aliiamini Imani ya Nabii
Ibrahim na alikua ni mwenye kumpenda sana Nabii Ibrahim kiasi ya kua alikua akihisi
kua hawezi kukaa mbali na Nabii Ibrahim na hivyo popote atakapoenda itabidi aende nae
ili awe nae pamoja kiakili na kiimani pia hivyo akaamua kujitenga dhidi ya jamii ya watu
288

hao pamoja na Nabii Ibrahim na kutoka katika mji huo kama inavyosema Surat Al
Anqabuut:

ْ ‫ﺎﺟٌﺮ إِ َ ٰﱃ َرِّ ۤﰊ إِﻧﱠﻪُ ُﻫ َﻮ ٱﻟْ َﻌ ِﺰ ُﻳﺰ‬


﴾‫ٱﳊَ ِﻜ ُﻴﻢ‬ ِ ‫ﺎل إِِﱏ ﻣﻬ‬
َ ُ ّ َ َ‫ط َوﻗ‬
ٌ ‫ﺂﻣ َﻦ ﻟَﻪُ ﻟُﻮ‬
َ َ‫﴿ﻓ‬
Faamana lahu lootun waqala innee muhajirun ila rabbee innahu huwa alAAazeezu
alhakeemu (Surat Al Anqabuut 29:26)

Tafsir: Na hivyo Lut akamuamini. Nae (Ibrahim) akasema: ‘Hakika mimi Ninahama
kwa ajili ya Mola wangu, hakika yeye ni mwenye uwezo na ni mwingi wa busara’.

Hivyo Nabii Ibrahim Aálayhi Salam ambae ae alikua pia akimpenda sana Lut ambae nae
wakati huo alikua bado hajawa Nabii wakaamua kwa pamoja kuachana na watu hao, ili
wasiwe miongoni mwa watu hao wenye kufanya maovu, na kuamua kutoka katika mji
huo na kuelekea katika maeneo ya Harran au pia hujulikana kama Al Raha, (Maeneo
ambayo kwa wakati huu yapo Kaskazini mwa nchi ya Syria na pia kusini mwa nchi ya
Uturuki) na baada ya hapo wakahamia katika maeneo ya Kanaan (Maeneo ya Kanaan
kwa hivi sasa hujumuisha maeneo ya Kusini Magharibi ya nchi ya Syria, Lebanon,
Palestina na Israel) na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akasema katika Qurán
kua:

ِ ِ ِ ِ ‫﴿وﳒَﱠْﻴـﻨَـﻪُ َوﻟُﻮﻃﺎً إِ َﱃ اﻻﱞْر‬


َ ‫ض اﻟﱠِﱴ َﺎﺑ َرْﻛﻨَﺎ ﻓ َﻴﻬﺎ ﻟ ْﻠ َﻌـﻠَﻤ‬
﴾‫ﲔ‬ َ
Wanajjaynahu walootan ila al-Ardhi allatee barakna feeha lilAAalameena (Surat Al
Anbiyah 21:71)

Tafsir: Na tukamjaalia yeye na Lut (kwa kuwaongoza kuelekea) katika Ardhi


tulioibariki kwa Walimwengu.

Ingawa aya zinatuonesha kua waliohama pamoja kutoka katika Mji huo walikua ni Nabii
Ibrahim na Lut, lakini kuna baadhi ya Wanazuoni wanasema kua miongoni mwao
alikuwemo pia Sarah. Na kulingana na mtizamo wa Imam Ismail Abd Rahman Al Suddi
basi yeye anasema kua: Sarah alikua ni mtoto wa Mfalme wa Mji wa Harran (Harran
ni mji ambao upo katika Ardhi ya kusini ya nchi ya Uturuki ambayo imepakana na
Syria Kaskazini), hivyo Nabii Ibrahim alikutana na Sarah wakati alipokua akihama
kutoka katika mji wake kuelekea katika Ardhi ya nchini Syria, na alipofika katika
mji wa Harran basi ndio wakakutana na Sarah ambae nae alikua tayari
ameshagombana na watu wake, na Nabii Ibrahim alimuoa Sarah kwa sababu ya
kutaka kumuokoa kutokana na madhara ya Mfalme wa Ardhi hio.
289

Na ukweli ni kua mbali ya kua Sarah alikua ni Mwanamke Mcha Mungu na hivyo kua ni
kigezo tosha kwa Nabii Ibrahim kumpenda na kutaka kumuoa, lakini pia Allah Subhanah
wa Taála alimjaalia Sarah kua na uzuri wa kipee, kwani ulikua ni uzuri ambao kila
anaemuona na kumtizama basi kamwe hatoweza kustahmili kumtizama kwa mtizamo
mmoja, yaani lazima atarudisha macho yake kwa ajili ya kuiridhisha nafsi yake juu ya
kile kinachoonekana na macho yake. Na bila ya shaka, kutokana na Ucha Mungu wake
basi mara tu baada ya Sarah kuolewa na Nabii Ibrahim akawa ni mwanamke ambae
anaempenda na kumtii kikamilifu Mume wake.

Kutokana na ndoa yake hio na Nabii Ibrahim na uzuri wake wa kimaumbile, kitabia na
kujipamba kwa Libasi ya Taqwa basi Sarah akajaaliwa na Allah Subhanah wa Ta’ala kua
ni Mwanamke aliepanda Darja kwa kua ni mwanamke ambae alikua mke wa Khalil
Allah, Mama wa Mitume, Bibi wa Mitume, Bibi Mkuu wa Mitume na pia kua miongoni
mwa Wanawake waliotajwa kwenye Qur’an na kua ni mwanamke aliezugumza na
Malaika.

Hivyo baada ya mda wakaondoa katika mji wa Harran na kuelekea kusini hadi walipofika
katika maeneo ya Kanaan (Canaan ni eneo la Ardhi ya Sham ambalo linajumuisha Ardhi
ya nchi ya Syria, Jordan, Lebanon, na Palestina) walikaa na kuishi katika maeneo ya
Nablus, baadae Lut A’layhi Salaam yeye akahama na kuelekea Sadum ambayo ni sehemu
iliyopo kusini mwa Bahari iliokufa (Al Bahr al Mayyit au Dead Sea) na imepakana na
nchi ya Jordan kwa upande wa Mashariki, na kwa upande wa Magharibi imepakana na
Palestina na Israel. Nabii Ibrahim akaelekea Ramallah na kisha Jerusalem ambapo alikua
na ukaribu sana na mtawala wa Jerusalem aliekua akiitwa Malaki Sadek.

Baada ya Nabii Ibrahim kuoneshwa Ufalme wa Allah Subhanah wa Ta’ala basi siku moja
akawaona watu wanazini hivyo akawalaani na hapo hapo watu wale wakawa ni wenye
kufariki, akawaona watu wengine wanafanya liwati akawalaani pia, nao pia watu hao
wakafariki, akawaona watu wawili wengine pia wanazini akawalaani na hapo hapo
wakafariki. Nabii Ibrahim akawaona watu wengine wawili wanazini na akataka
kuwalaani tena, lakini kabla ya kuwalaani basi Allah Subhanah wa Taála akamwambia
Nabii Ibrahim:

‘Ya Ibrahim! Usiwalaani waja wangu, kwani kwa hakika mimi ni Mwingi wa
Usamehevu na mwingi wa Rehma. Na dhambi za waja wangu hazinidhuru mimi
kama vile ambavyo Ibada zao hazininufaishi na chochote. Na hivyo hua
siwafundishi wala siwadhibiti kwa kutumia adhabu zangu hapo kwa hapo. Hivyo
jizuie kutokana na kuwalaani waja wangu, kwani kwa hakika wewe umeteuliwa
kua ni muonyaji tu kuhusiana na adhabu zangu, wewe si mshirika wangu katika
Mamlaka yangu, na wala si mlinzi wala shuhuda juu ya viumbe wangu. Hakika
mimi nnawashughulikia waja wangu kwa kuangalia hali zifuatazo:
290

1: Wanatubu na mimi nakubali toba zao, wananiomba msamaha nami nawasamehe


dhambi zao na kuwahifadhia kasoro zao.

2: Nazuia adhabu zangu juu yao kwa kutokana na kujua kua wamebeba Roho za
waja wangu wema watakaoniamiani ndani ya viungo vyao vya uzazi. Hivyo
waumini wanapozaliwa kutokana nao na kutengana nao hapo ndio hua kuna
umuhimu wa kuwashughulikia waovu hao.

3: Ikiwa hawajabeba Waumini ndani ya viungo vyao vya Uzazi na hawakuwa ni


wenye kutubu, basi adhabu yangu niliyowatayarishia kesho Akhera ni nzito sana
kuliko unayowaombea wewe leo hapa Duniani. Kwa sababu adhabu zangu kwa
Waja wangu hua zinalingana na Mamlaka yangu na Ufalme wangu. Hivyo niwachie
Waja wangu kwa ajili yangu na usiingilie majaaliwa yao kwangu kwani mie ni
mwingi wa Rehma kwao wao na ni mwingi wa Uwezo na ni mwingi wa Hikma.
Hakika mimi nnajaalia kulingana na I’lm yangu juu yao na hivyo nawaachia
Majaaliwa yangu na uhuru wao wa kuamua mambo yao miongoni mwao.’

Ama kwa upande mwengine basi nasema Imam Jafar As Sadiq pia kua: ‘Mara baada ya
Nabii Ibrahim kuoneshwa Mamlaka ya Allah Subhanah wa Ta’ala na kisha kutokea
yaliyotokea kwa kuwaona wanaofanya Dhambi na kuwalaani na watu hao basi
Allah Subhanah wa Taála akamwambia Nabii Ibrahim: ‘Ya Ibrahim! Kwa hakika
Dua zako zimekubaliwa lakini, usiwalaani Waja wangu. Kwani kama ningetaka
basi nisingewaumba hapo kabla ya kufanya maasi. Waja wangu wako wa aina tatu:

Aina ya kwanza ni wanaoniabudu na wasionishirikisha na chochote, hawa


nawazawadia.

Aina ya pili ni wale wanaowaabudu wengine lakini hii haimaanishi kua Waja hao
hawako chini ya udhibiti wangu.

Aina ya tatu ni wale ambao ni Wananishirikisha lakini wamebeba Waja wema


watakaoniamini ndani ya viungo vyao vya uzazi. Hivyo baadae watatoa kizazi
kitakachokua ni chenye kuniamini na kuniabudu mimi’’

Naam tunapoangalia na kujaribu kuzingatia mafunzo yaliyomo ndani ya maneno hayo ya


Imam Jafar As Sadiq basi tunaona kua ndani yake mna mambo mengi sana amabyo
yanatugusa hususan sisi Waislam wa leo ambao hua ni wenye kukosa Subra na hivyo hua
ni wenye haraka ya kuhukumiana.

Katika kuishi kwake Nabii Ibrahim siku moja alipita pembeni ya mto na akakuta maiti
ya mnyama ambae nusu imo ndani ya Maji na Nusu ipo ufukweni. Hivyo samaki wadogo
291

wadogo wakawa wanakula sehemu ya mnyama huyo iliyomo ndani ya maji, Nabii
Ibrahim akatafakkari na kugundua kua kama kawaida samaki hao wadogo nao baadae
hua wanaliwa na samaki wakubwa na wadudu wengine wakubwa zaidi yao waliomo
ndani ya maji ya mto huo.

Wakati huo huo wadudu na wanyama wa ardhini wanakula sehemu ya mnyama huyo
iliyopo nchi kavu kisha nao pia baadae hua wanaliwa na wadudu na wanyama wakubwa
zaidi yao waliopo nchi kavu. Hivyo Nabii Ibrahim akaanza kustaajabu na kujiuliza hivi
inakuaje kua kiumbe huyu aliekufa analiwa na viumbe wengine na kisha viumbe hao nao
wanaliwa na viumbe wengine, nao wanaliwa na viumbe wengine halafu watafufuliwa
huku wakiwa na viungo vyao vyote kama walivyokua hapo kabla walipokua hai.

Hivyo akaona amuombe Allah Subhanah wa Taála ili apate kuona kwa mtizamo wa
Yaqin juu ya uwezo wa Allah Subhanah wa Taála katika uumbaji na namna anavyoweza
kufufua viumbe wake baada ya kufariki kwao, na hivyo akasema:

‫ﺎل ﺑَـﻠَ ٰﻰ َوﻟـٰﻜِﻦ ﻟِّﻴَﻄْ َﻤﺌِ ﱠﻦ ﻗَـ ْﻠِﱮ‬


َ َ‫ﺎل أ ََوَﱂْ ﺗُـ ْﺆِﻣﻦ ﻗ‬
َ َ‫ﻒ ُْﲢﻴِـﻰ ٱﻟْ َﻤ ْﻮﺗَ ٰﻰ ﻗ‬ َ ‫ب أَِرِﱏ َﻛْﻴ‬ ِّ ‫﴿ َر‬
‫ٱﺟ َﻌ ْﻞ َﻋﻠَ ٰﻰ ُﻛ ِّﻞ َﺟﺒَ ٍﻞ ِّﻣْﻨـ ُﻬ ﱠﻦ ُﺟْﺰءًا ﰒُﱠ‬
ْ ‫ﻚ ﰒُﱠ‬ َ ‫ﺼْﺮُﻫ ﱠﻦ إِﻟَْﻴ‬ ِ
ُ َ‫ﺎل ﻓَ ُﺨ ْﺬ أ َْرﺑَـ َﻌﺔً ّﻣ َﻦ ٱﻟﻄﱠِْﲑ ﻓ‬َ َ‫ﻗ‬
﴾‫ٱﻪﻠﻟ َﻋ ِﺰ ٌﻳﺰ َﺣ ِﻜﻴﻢ‬ َ َ‫ْٱدﻋُ ُﻬ ﱠﻦ َ�ْﺗِﻴﻨ‬
ٌ َ‫ٱﻋﻠَ ْﻢ أَ ﱠن ﱠ‬ ْ ‫ﻚ َﺳ ْﻌﻴﺎً َو‬
Rabbi arinee kayfa tuhyee almawta qala awa lam tu/min qala bala walakin liyatma-
inna qalbee qala fakhuth arbaAAatan mina alttayri fasurhunna ilayka thumma
ijAAal AAala kulli jabalin minhunna juz-an thumma odAAuhunna ya/teenaka
saAAyan waiAAlam anna Allaha AAazeezun hakeemun (Surat Al Baqara 2:260)

Tafsir: ‘Ewe Mola wangu! Nionyeshe vipi unavyohuisha maiti’ Akasema Allah
Subhanah wa Taála: ‘Jee huamini?’ Ibrahim akasema: ‘Naam! Naamini, Lakini
nataka niutulize Moyo wangu (niwe na Imani kubwa zaidi)’ Allah akasema: ‘Chukua
ndege wanne, wafuge, kisha (wachinje) uweke sehemu zao katika kila mlima. Kisha
waite, na watakuja kwako wewe kwa kasi kubwa, na utajua kua Allah ni mwenye
uwezo na ni mwingi wa Hikma.’

Aya inatuonesha kua Allah Subhanah wa Taála anamhoji Khalil wake kua; ‘Jee haamini
juu ya hayo?’ Ambapo Nabii Ibrahim nae akajibu: ‘Naam! Naamini.’ Hivyo hapa aya
inatuonesha kua kama Nabii Ibrahim hakua ni mwenye kuamini basi asingejibu Naam
Naamini. Na vile vile kwa upande mwengine basi Allah Subhanah wa Taála alikua pia
hana shaka juu ya Imani ya Khalil wake kwake, kwani kama angekua na shaka nae basi
292

kamwe asingemkubalia jambo hilo isipokua alimkubalia kwa kujua kua, kweli Khalil
wake ni mwenye kutaka kuutuliza Moyo wake kwa kuupa Yaqin zaidi.

Ama kwa upande wa Imam Abu Bakar Al Sizji basi yeye anasema juu ya ayah hii kua:
‘Nabii Ibrahim aliomba hivyo kwa sababu, ya kutaka kupata uthibitisho, pale
atakapoulizwa na maadai wa Allah Subhanah wa Taála, baada ya kusema kua Mola
wangu anaua na kuhuisha, akiulizwa jee una uthibitisho gani, basi ajibu hoja kwa
kutoa uthibitisho kutokana na kushuhudia hilo kwa macho yake.’

Ama kwa upande wa Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari basi yeye
anasema kua: ‘Nabii Ibrahim aliomba hivyo labda kwa sababu pia alikua anataka
kujitibitishia kua kweli yeye ni Khalil Allah. Na pia mtizamo mwengine ni
kumaanisha kua: ‘Hiki nnachokuomba mimi sina haki nacho, Hivyo ombi langu
hili ni kwa ajili ya kuridhisha Moyo wangu’ na hii ni kwa sababu ameitwa Khalil
Allah hata katika kipindi cha ujahiliya, na kama tulivyosema kua: ‘Alisema ili Moyo
wangu upate utulivu kwa kumaanisha kuujaza Yaqini Moyo wake juu ya darja yake
ya kua Khalil Allah. Na hii ni kwa sababu Nabii Ibrahim anajua kua Allah ni
mwenye kukhuisha na kufisha.’’

Ama kwa upande wa Mujaddid ad Din, Muhyyi ad Din Imam Abu Zakarriyah Yahya Ibn
Sharaf an Nawawi basi yeye anasema kua: ‘Amesema Imam Abu Ibrahim Al Muzani
Al Shafii, ambae ni mwanafunzi wa Imam Muhammad Idris Al Shafii kua: ‘Mtume
wetu hakumaanisha kua Nabii Ibrahim alikua ni mwenye Shaka pale aliposema
kua: ‘Inatubidi sisi kua na shaka zaidi kuliko Ibrahim’ Bali kile alichokikusudia
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ni kua: ‘Kama ingekua Mitume wa Allah
wanakua na shaka, basi na mimi ningekua na shaka pia. Lakini kwa kua mimi sina
shaka basi na Ibrahim pia hakua na shaka.’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam aliyasema haya kutokana na kua na


nyenyekevu kiasi ya kua alijiweka chini ya Nabii Ibrahim. Ama kuhusiana na
maneno: ‘Walakin liyatma-inna qalbee - Ili Moyo wangu upate utulivu’ basi hua ni
yenye kumaanisha: ‘Ili uthibitisho huo uweze, kunyanyua Imani yangu kutoka
katika darja moja ya chini hadi nyengine ya juu, yaani kutoka katika hali ya Ilm al
Yaqin kuingia katika hali ya Ayn al Yaqin ’’

Hivyo Nabii Ibrahim akachukua ndege wanne wa aina tofauti, akawafuga hadi
wakamzoea kwa kuwaita kwa majina yao, kiasi ya kua alikua akiita jina basi ndege husika
humfuata katika sehemu aliyomwita, kisha walipomzoea akawachinja kwa ajili ya Allah
Subhanah wa Taála. Baada ya kuwachinja, akawanyonyoa manyoya yao, na kisha nyama
zao akazitwanga twanga na kuzisaga kwa pamoja katika sehemu moja, kisha akachukua
mchanganyiko huo na kuuweka katika majabali kumi tofauti tofauti, akabakiwa na
midomo ya ndege hao kwenye mikono yake.
293

Kisha akakaa sehemu peke yake huku akiweka vyakula vya ndege hao chini yake, kisha
akaanza kuyaita majina ya ndege hao kwa Jina la Allah Subhanah wa Taála, mmoja baada
ya mmoja, na hapo akaona kwa macho yake namna ndege hao wanavyojiunga kiungo
kwa kiungo kutoka katika majabali hayo kumi tofauti, na kua ndege wanne tofauti
kwenye mikono ya Nabii Ibrahim, ambapo walipotimia basi akaiwacha midomo yao hio
na ndege hao wakatua chini na kuanza kula ardhini chini ya miguu yake. Subhanah Allah!

Hivyo basi Nabii Ibrahim alikua ni mwenye kuamiini pia kwa mtizamo wa Ain al Yaqin
yale ambayo yanawekwa wazi na aya ifuatayo kwa wale ambao wasioamini:

‫اب ﰒُﱠ ِﻣﻦ‬ ٍ ‫ﺚ ﻓَِﺈ ﱠ� َﺧﻠَ ْﻘﻨَﺎ ُﻛﻢ ِﻣﻦ ﺗُـﺮ‬


َ ّ ْ
ِ ‫ﺐ ِﻣﻦ ٱﻟْﺒـﻌ‬
ْ َ َ ّ ٍ ْ‫ﱠﺎس إِن ُﻛﻨﺘُ ْﻢ ِﰱ َرﻳ‬ ُ ‫ٰ�َﻳـﱡ َﻬﺎ ٱﻟﻨ‬
﴿
‫ﲔ ﻟَ ُﻜ ْﻢ َوﻧُِﻘﱡﺮ ِﰱ ٱﻷ َْر َﺣ ِﺎم‬ ٍِ ٍ ٍ ْ ‫ﻧﱡﻄْ َﻔ ٍﺔ ﰒُﱠ ِﻣﻦ ﻋﻠَ َﻘ ٍﺔ ﰒُﱠ ِﻣﻦ ﱡﻣ‬
َ ِّ‫ﻀﻐَﺔ ﱡﳐَﻠﱠ َﻘﺔ َو َﻏ ِْﲑ ُﳐَﻠﱠ َﻘﺔ ﻟّﻨُـﺒَـ‬ َ ْ
‫َﺷ ﱠﺪ ُﻛ ْﻢ َوِﻣﻨ ُﻜ ْﻢ ﱠﻣﻦ ﻳـُﺘَـ َﻮ ﱠٰﰱ‬ ۤ ِ
ُ ‫َﺟ ٍﻞ ﱡﻣ َﺴ ًّﻤﻰ ﰒُﱠ ُﳔْ ِﺮ ُﺟ ُﻜ ْﻢ ِﻃ ْﻔﻼً ﰒُﱠ ﻟﺘَـْﺒـﻠُﻐُﻮاْ أ‬ ِ
َ ‫َﻣﺎ ﻧَ َﺸﺂءُ إ َ ٰﱃ أ‬
ِ ِ ِ ِ ِ ِ
‫ض‬ َ ‫َوﻣﻨ ُﻜ ْﻢ ﱠﻣﻦ ﻳـَُﺮﱡد إِ َ ٰﱃ أ َْرَذل ٱﻟْﻌُ ُﻤ ِﺮ ﻟ َﻜْﻴﻼَ ﻳَـ ْﻌﻠَ َﻢ ﻣﻦ ﺑَـ ْﻌﺪ ﻋ ْﻠ ٍﻢ َﺷْﻴﺌﺎً َوﺗَـَﺮى ٱﻷَْر‬
﴾‫ﻴﺞ‬ ٍ ِ‫ﺖ ِﻣﻦ ُﻛ ِّﻞ َزْو ٍج َﻬﺑ‬ ْ َ‫ﺖ َوأَﻧﺒَـﺘ‬ ْ َ‫ت َوَرﺑ‬ ْ ‫َﻧﺰﻟْﻨَﺎ َﻋﻠَْﻴـ َﻬﺎ ٱﻟْ َﻤﺂءَ ْٱﻫﺘَـﱠﺰ‬
ِ
َ ‫َﻫﺎﻣ َﺪ ًة ﻓَِﺈ َذآ أ‬
Ya ayyuha alnnasu in kuntum fee raybin mina albaAAthi fa-inna khalaqnakum min
turabin thumma min nutfatin thumma min AAalaqatin thumma min mudghatin
mukhallaqatin waghayri mukhallaqatin linubayyina lakum wanuqirru fee al-
arhami ma nashao ila ajalin musamman thumma nukhrijukum tiflan thumma
litablughoo ashuddakum waminkum man yutawaffa waminkum man yuraddu ila
ardhali alAAumuri likayla yaAAlama min baAAdi AAilmin shay-an watara al-
ardha hamidatan fa-itha anzalna AAalayha almaa ihtazzat warabat waanbatat min
kulli zawjin baheejin(Surat Al Hajj 22:5)

Tafsir: Enye Ibn Adam! Kama ikiwa mna shaka na Kufufuliwa (Basi tafakkarini kua)
Kwa hakika tumekuumbeni kutokana na Udongo, kisha tukakutoeni kupitia ndani ya
tone (la manii ya Mwanamme na la Yai la Mwanamke), kisha tukakutoeni kupitia
ndani ya tone la damu iliyoganda, na kisha tukatuoeni kupitia ndani ya pande la
nyama ambalo sehemu yake moja imetengenezeka na sehemu nyengine
haijatengenezeka, ili tupate kukudhihirishieni (uwezo wetu kwenu). Na tuwajaalia
tuwatakao kua ni wenye kukaa ndani ya mifuko ya uzazi kwa mda maalum, kisha
tukawatoa nje kua Watoto, kisha tukakuleeni nyie ili mfikie mda wa kukukua
kikamilifu (Kimwili, Kufaham na Kiakili), na baadhi yenu wanakufa, na wengine
294

hurudishwa katika Ardhali Al Umuri (hali ya uzeeni wa kutojiweza), kiasi ya kua


hawajui kitu baada ya kua ni wenye kujua kila kitu. Na mnaona Ardhi inavyokua tupu
haina kitu lakini tunapoimwagia Mvua inatetemeka (kua hai)na kututumka na hivyo
huchomozesha kila aina ya vipando vinavyoota na kupendezesha jike na dume.

HIJRA YA NABII IBRAHIM KUTOKA JERUSALEM KUELEKEA


MISRI

Nabii Ibrahim alikaa Jerusalem kwa muda mrefu sana, lakini baadae akaondoka na
kuelekea katika Ardhi ya Misri kutokana na kuwepo kwa ukame katika Ardhi ya
Jerusalem na hivyo akaamua kuelekea Misri ambako ulikua na Wingi wa Chakula, na
mara tu alipowasilia katika Ardhi ya nchi hio basi habari zikafika kwa mfalme wa Misri
ambae alikua ni Mfalme Dhul Arsh Ibn Saruq Al Himyari kua kuna mgeni amekuja katika
Ardhi ya nchi hio akiwa na mwanamke mzuri asiekua na mfano wake. Hivyo Mfalme
Dhul Arsh akamualika Nabii Ibrahim katika kasri lake kwa ajili ya kutaka kumuona na
kumjua zaid mwanamke huyo aliesifiwa na watu wake mbele yake.

Nabii Ibrahim alipopata mualiko huo, basi akaupokea kwa mikono miwili na kuitikia
wito wa mualiko huo hivyo akaelekea kwa Mfalme kwa ajili ya kuonana nae. Alipofika
na kukutana nae basi Mfalme Dhul Arsh akamwambia Nabii Ibrahim kua alikua anataka
kumjua na kumuona mwanamke aliekuja nae katika mji huo, na alikua tayari kumpa
sehemu ya Nabii Ibrahim seemu ya Mamlaka yake kwa ajili tu ya kua na Mwanamke
huyo anaesifiwa uzuri wake. Hivyo Nabii Ibrahim akamwambia Mfalme Duhl Arsh kua
Dada yake huyo ni mkubwa na wala si mtoto mdogo hivyo basi kwanza kinachohitajika
ni ridhaa yake.

Mfalme Dhul Arsh akaamrisha Sarah akachukuliwe, apambwe kisha aletwe mbele yake
kisha aombwe ridhaa yake ya kua mke wake. Kwa kua Nabii Ibrahim alijua kua kutokana
na habari za Mfalme Dhul Arsh alizosikia hapo kabla ya hata kuonana nae, kua kama
akisema kua Sarah ni mke wake, basi bila ya shaka Mfalme Dhul Arsh atamuua Nabii
Ibrahim na kisha atamfanya Sarah kua ni mkewe tena kwa nguvu.

Hivyo kabla ya Nabii Ibrahim kumkabidhi Sarah kwa watumishi wa Mfalme Dhul Arsh
basi alimwita Sarah faragha na kumwambia: ‘Mfalme Dhul Arsh si mtu mzuri na ni
katili sana, hivyo ameniuliza mwanamke niliekuja nae ni nani kwangu nami
nikasema kua wewe ni ndugu yangu, hivyo usije ukanisaliti kwa kusema
vyenginevyo kwani huu niliousema ni ukweli kwa sababu wewe ni ndugu yangu wa
Kike katika Dini ya Allah Subhanah wa Taála na pia ni ndugu yangu pekee katika
295

Ardhi hii ambayo hakuna alieamuamini Allah Subhanah wa Taála isipokua mimi
na wewe.’

Kwani Allah Subhanah wa Ta’ala amesema katika Quran kua:

﴾ٌ‫﴿إِﱠﳕَﺎ ٱﻟْﻤ ْﺆِﻣﻨُﻮ َن إِ ْﺧﻮة‬


َ ُ
Innama almu/minoona ikhwatun (Surat Al Hujrat 49:10)

Tafsir: Hakika ya Wauimini ni Ndugu.

Baada ya kukubaliana juu ya hilo basi Sarah akatoka na watumishi wa Mfalme Dhul Arsh
hadi katika Kasri la Mfalme Duhl Arsh, huku akimuacha Nabii Ibrahim Nyumbani akiwa
katika hali ya kuwasiliana na Allah Subhanah wa Ta’ala kwa njia ya Sala na Dua. Hivyo
Sarah alipowasili mbele ya Mfalme Dhul Arsh basi Mfalme Dhul Arsh hakuamini kile
anachokiona mbele ya macho yake, kwani alikua mbele yake kulia kuna mwanamke
mzuri sana kupita kiasi zaidi ya hata vile alivyoelezewa na watu wake.

Kiasi ya kua akawa anajiuliza kama kweli kiumbe anaemuoa mbele ya macho yake ni
Malaika au ni Ibn Adam mwenye jinsia ya kike alietimia kwa uzuri wa maumbile na wa
Sura yake, hivyo akataka kujithibitishia kwa kutumia hisia za kugusa na kuhisi kwa
vidole vyake, na Moyo wake, ukauamuru ufahamu wake ambao nao ukaiamuru mikono
yake kunyooka ili kugusa na kuhisi uzuri wa kile kiumbe kinachooneka na macho yake.
Sarah akaomba dua kwa kusema: ‘Ya Allah! Muoneshe uwezo wako Dhalimu huyu.’

Naam..anaeyasema maneno hao ni Sara ambae ni Mwanamke mwenye Taqwa, Mtiifu


kwa Mumewe na pia ni Mke wa Nabii Ibrahim Khalilu Allah na anaombwa ombi hili ni
Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ndie mwenye uwezo wa kila kitu na ndio yeye ambae
aliesema Niombeni nitakujibuni katika aya ifuatayo:

‫ﻳﻦ ﻳَ ْﺴﺘَ ْﻜِﱪُو َن َﻋ ْﻦ ِﻋﺒَ َﺎدﺗِﻰ‬ ِ ‫ﻮﱐ أَﺳﺘ ِﺠﺐ ﻟَ ُﻜﻢ إِ ﱠن ٱﻟﱠ‬ۤ ِ ‫ﺎل رﺑﱡ ُﻜـﻢ ٱدﻋ‬
َ ‫ﺬ‬ ْ ْ َ ْ ُ ْ ْ َ َ َ‫﴿ َوﻗ‬
ِ
﴾‫اﺧ ِﺮﻳﻦ‬
َ ‫َﺳﻴَ ْﺪ ُﺧﻠُﻮ َن َﺟ َﻬﻨ َﱠﻢ َد‬
Waqala rabbukumu odAAoonee astajib lakum inna alladheena yastakbiroona
AAan AAibadatee sayadkhuloona jahannama dakhireena.(Surat Ghafir 40:60)

Tafsir: Na amesema Mola wako: ‘Niombeni Nitakujibuni, Hakika wale wanaofanya


Kibri kuhusiana kuabudiwa kwangu basi wataingia Jahanam huku wakinyanyasika.’
296

Na pia kama alivyosema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:

Amesema Allah Subhanah wa Ta’ala kua: ‘Hakika mimi natangazia Vita kwa yule
ambae anaonesha uadui kwa Walii wangu. Na jambo ninalolipenda zaidi ni lile
ambalo linalomkaribisha Mja wangu kwangu mimi lile ambalo nimelifanya kua ni
wajibu juu yake. Na mja wangu huanza kuupata Ukaribu kwangu kupitia katika
mambo ya Suna mpaka huanza kumpenda, hivyo nnaanza kua na hisia zake za
kusikia na ambazo anasikilizia’, na hisia zake za kuona ambazo anaonea, na mikono
yake ambayo anakamatia, na miguu yake ambayo anatembelea, na akiniomba basi
nitampa, na akiomba ulinzi wangu basi nitamlinda na kamwe sitosita kumfanyia
jambo lolote (kwa ajili yake) kama vile ambavyo hua nnavyosita kuchukua Roho ya
Muumini, kwani anachukia Kifo nami nachukia kumvunja Moyo.(Sahih Bukhari)

Hivyo basi hapo hapo ghafla Mfalme Dhul Arsh akapatwa na mshangao mwengine zaidi
kutoka katika mwili wake, kwani mkono uligoma kunyooka ili kuthibitisha kilichopo
mbele yake yaani imekua haifanyi kazi yake kutokana na amri yake kama vile mikono
hio imekua sio yake. Akajaribu tena mara ya pili, mara ya tatu lakini matokeo yake
yalikua ni yale yale. Hapa akajua kua huyu kiumbe mzuri alie mbele yake ni Mtakatifu
na mbali ya uzuri wake lakini ana Miujiza ya aina yake, hivyo akataharuki na kumwambia
Sarah: ‘Mbona imekua mambo ya Maajabu, kwani hivi wewe ni nani? Na kwanini
unaniletea Mitihani?’

Sarah akajibu: ‘Mitihani haitoki kwangu, bali inatoka kwa Mola wangu, na hii ni
kwa sababu umekua ukitumia nguvu’. Mfalme Dhul Arsh akasema: ‘La hakika mimi
sijatumia nguvu juu yako.’ Sarah akasema: ‘Naam ndio hukutumia nguvu dhi di
yangu lakini umetumia nguvu dhidi ya Nabii wa Allah Subhanah wa Ta’ala’ Mfalme
Dhul Arsh akauliza: ‘Nabii gani huyo?’ Sara akasema: ‘Umetumia nguvu dhidi ya
Nabii Ibrahim ambae ndie Allah Subhanah wa Ta’ala alimuangamizia Mfalme
Namrudh Al Kabir.’

Mfalme Dhul Arsh akasema: ‘Ama kwa hakika mimi sijamuona Nabii Ibrahim na
wala sijatumia nguvu dhidi yake.’ Sarah akasema: ‘Nabii Ibrahim ni Mume wangu,
na wewe unataka kunitenganisha mie na yeye’ Mfalme Dhul Arsh akasema: ‘Mtihani
umetukuta sote, kwa sababu mimi sikujua kua yeye ni Nabii Ibrahim, na sikujua
kua wewe ni mke wake kwani yeye alisema kua wewe ni dada yake. Na kama
angesema kua wewe ni mke wake basi mimi nisingefikia kufanya niliyokua nikitaka
kuyafanya.’

Sara akasema: ‘Wewe ni Mfalme Dhalim, hivyo kama angesema kua mie ni mke
wake basi hakika wewe ungemuua yeye na ungenichukua mie kwa nguvu.’ Mfalme
Dhul Arsh akasema: ‘Hakika mimi sijawahi kuchukua mali ya mtu bila ya ridhaa
yake.’ Baada ya maneno hayo akawaamrisha watu wake wakamchukue Nabii Ibrahim
297

kisha wamlete mbele yake. Nabii Ibrahim alipofikishwa mbele yake, basi Mfalme Dhul
Arsh basi akakimbilia na kupiga magoti chini yake huku akiwa ni mwenye kulia na
kusema: ‘Tafadhali nisamehe kwani kwa hakika mimi sikujua kua wewe ni Nabii
Ibrahim ambae Allah alimuangamiza Namrudh Al Kabir kupitia katika mikono
yako.’ Nabii Ibrahim akasema: ‘Naam! Hakika mimi ni Ibrahim Khalil Allah na bila
ya shaka nimekusamehe.’

Mfalme Dhul Arsh akasema: ‘Hebu nielezee kuhusiana na Mola wako’ Nabii Ibrahim
akasema: ‘Mola wangu ni Yule ambae ameumba Mbingu 7 na Ardhi 7. Ni Mola wa
Ulimwengu wote, Mamlaka yake yameenea kila mahali Ulimwenguni. Hana
mshirika wala hahitaji wa kushirikiana nae, hana mwanzo wala hana mwisho,
hakuzaa wala hakuzaliwa, hufanya atakavyo, humpa Mamlaka atakae na
humpokonya atakae, ni mwenye kuhuisha na ni mwenye kufisha, yeye ni mwenye
uhai wa milele.’

Mfalme Dhul Arsh akasema: ‘Hakika mimi kwa miaka 70 nimekua ni mwenye
kuiabudu Nyota ya Zuhura, miaka yote hi nimekua nikijiuliza, Jee ni nani alieweka
Mbingu juu bila ya kuwepo kwa Nguzo za kuzizuia zisianguke, Jee ni nani
anaesababisha Nyota Kuonekana na kutoweka na ni nani anaesababisha usiku na
mchana. Kumbe ni Mola wako. Na mikono yangu sasa hivi haifanyi kazi hivyo
niombee kwa Mola wako mikono yangu ipone’ Nabii Ibrahim akamuombea dua Dhul
Al Arsh na hapo hapo mkono wake ukapona. Dhul Arsh akasilimu na kua Muislam chini
ya Nabii Ibrahim.

Katika kasri ya Mfalme Dhul Arsh kulikua na mwanamke aliekua anaitwa Hajar ambae
nae alikua ni mzuri sana, Mwanamke huyu alikua ni Mkuu wa Wajakazi wote wa kike
wa Mfalme Dhul Arsh, ambae alipatikana baada ya utawala wa Mfalme Dhul Arsh
kuvamia Ardhi za jirani yake, na inasemekana kua alikua ni mwenye kutokana na kizazi
cha Nabii Saleh. Hivyo Dhul Arsh akamkabidhi Hajar kwa Sarah ili awe Mjakazi wake.

Baada ya mda Nabii Ibrahim akashushiwa Wahy na kuambiwa kua, inambidi arudi katika
Ardhi ya Palestina Hivyo Nabii Ibrahim A’layhi Salaam akarudi na familia yake tena
katika Ardhi ya Palestina na kuishi katika eneo la Beersheba ambapo alijenga nyumba
yake, Msikiti na Kisima kwa ajili yake na watu na wanyama wa eneo hilo, Kisima hicho
kilikua na Maji mengi sana. Nabii Ibrahim alikaa katika eneo la Beersheba kwa miaka
kadhaa hadi pale watu wa eneo hilo walipoanza kumpinga kutokana na kuwausia juu ya
Mola wao, hivyo akaamua kuhama na kuhamia katika eneo la Al Qaáh ambalo ni eneo
liliopo baina ya Ar Ramla na Jerusalem. Sarah akamwambia Nabii Ibrahim: ‘Mchukue
Hajar mfanye mke wako huenda Allah akakujaalia kupata Mtoto kupitia kwake’

Mara tu baada ya Nabii Ibrahim kuondoka katika mji wa Beersheba basi kile kisima
kikakauka maji yake hivyo watu wa mji huo wakatafakkar na kuambiana kua bila ya
298

shaka hali hi imetokana na kuhama kwa Nabii Ibrahim, hivyo wakatuma watu wao ili
wakamuombe Nabii Ibrahim arudi kwa watu hao, lakini hata hivyo Nabii Ibrahim
akakataa kurudi kwao lakini badala yake akawapa Mbuzi na kuwaambia kua wanatakiwa
waende na mbuzi hao katika Kisima hicho wakifika tu basi Maji ya Kisima hicho
yatapanda juu ambayo watayatumia watakavyo, lakini kwa sharti la kua wasimruhusu
mwanamke alie katika siku zake kuchota maji katika Kisiam hicho.

Na bila ya shaka walipofika katika eneo hilo la Kisima na kuwapeleka Mbuzi hao basi
maji yakajaa ndani ya Kisima, na hivyo watu hao wakafaidika na Maji hayo wa muda
mrefu hadi pale alipotokea Mwanamke mwenye hedhi na kuchota maji kutoka katika
kisima hicho, hivyo Maji hayo yakatoweka hapo hapo, na hayajatoka tena hadi hii leo.

Nabii Ibrahim akakaa katika mji wa Al Qaáh kwa mda mrefu huku Allah Subhanah wa
Taála akimjaalia kwa kumneemesha na mali na utajiri kiasi kikubwa kulingana na watu
wengine waliokua miongoni mwa watu wa Mji huo. Na pia Allah Subhanah wa Ta’ala
akamjaalia Nabii Ibrahim A’alyhi Salam na Hajar kupata mtoto wa kiume walieamua
kumuita Ismai’l. Nabii Ibrahim akawa ni mwenye kutoa sadaka na kuwakirimu kila
wenye matatizo kuanzia wagonjwa, wenye madeni, wasiokua na uwezo, wapita njia pia,
wasafiri n.k hivyo nyumbani kwake ilikua hakuna siku ambayo haitembelewi na wageni.
Lakini ghafla kikatokea kipindi cha ukame wa kutotembelewa na wageni nyumbani
kwake hapo kwa takriban wiki mbili. Jambo hili lilimhuzunisha sana Nabii Ibrahim lakini
hata hivyo akaendelea kua ni mwenye Subra, kwani bila ya shaka yeye ni mwenye
kumjua Mola wake kuliko kiumbe yeyote yule aliewahi kutokea kabla yake.

Hali hii ilibadilika ghafla pale siku moja wakati Allah Subhanah wa Taála alipoamua
kuonyesha Uwezo na Ghadhabu zake kwa wale wenye kumuasi na hapo hapo kuonesha
Rehma na Mapenzi yake kwa Waja wake wampendao, kwa kuwapa adhabu watu wa
binamu yake Nabii Ibrahim, yaani watu wa Nabii Lut au Qawm Lut na kumuingiza katika
Rehma zake Nabii Lut kwa kumuamrisha kuondoka katika mji huo kabla ya kushuka kwa
adhabu hio, na hapo hapo kuwapa habari zenye Neema, Rehma na Mapenzi ndani yake
waja wake ambao ni Nabii Ibrahim na familia yake inayojumuisha Sarah na Hajar.

Katika kipindi hiki cha tukio hili basi Nabii Ibrahim alikua na umri wa miaka 90 na Sarah
alikua na tayari nae anakaribia umri wa miaka 90. Anasema Amr Ash Shabi kua: ‘Nabii
Ibrahim alitumbukizwa Motoni wakati alipokua na umri wa miaka 16, Sarah
alijifungua mtoto Is-haq wakati akiwa na umri wa miaka 90.’

Katika siku hio Mji wa Al Qa’ah, ulitembelewa na wageni watatu. Nabii Ibrahim
alipowaona watu watatu hao namna walivyovyaa na utulivu waliokua nao basi alivutiwa
nao sana kiasi ya kua akaiambia nafsi yake kua, hakuna mtu yeyote anaestahiki
kuwakarimu watu hawa isipokua mimi. Hivyo akawapokea na kuwakaribisha nyumbani
kwake, na kuamua kuwatayarishia chakula kiitwacho Haniidh.
299

Hivyo akachagua Kondoo asiekua mdogo sana wala aliepea sana lakini akawa ni alienona
miongoni mwa Kondoo wake, akamchinja kisha Nyama yake akaitengeneza na kuioka
kwa kutumia mawe yaliyotiwa moto mkali sana hadi yakawa mekundu kwa moto, Nyama
ya Kondoo huyo ikawekwa juu ya chanja iliyo juu ya mawe hayo na hivyo nyama hio
kua katika hali ya kutoyagusa mawe hayo ya moto. Kisha Nyama na Moto huo
ukafunikwa pamoja ili kutoruhusu moto, harufu ya Nyama na mvuke wa moto huo kutoka
nje yake, na hivyo kuifanya Nyama hio baada ya mda kua ni yenye kuwiva na kua na
ladha yenye tamu na ulaini wa pekee.

Haniidh tunayokizungumzia hapa ni chakula ambacho ni nadra kupikwa na kuliwa katika


siku za kawaida isipokua katika siku za sherehe za Harusi au Sikukuu, hiki ndio chakula
ambacho Nabii Ibrahim aliwatayarishia wageni wake hao watukufu kutokana na
muonekano wao, bila ya yeye kujua kua hao ni wageni watukufu zaidi ya anavyofikiria
yeye.

Lakini jambo la kushangaza ni kua ingawa Nabii Ibrahim alihangaika kuwatayarishia


wageni wake hao chakula adhimu, na kisha akawawekea mbele yao lakini wageni hao
walisita kusogeza mikono yao ndani ya chombo walichowekewa chakula hicho. Hapa
kwa mtu wa kawaida baada ya kufanya jitihada zako zote kuwakirimu wageni wako kisha
likatokea tukio hili basi unaweza ukakosa subra na kujisikia vibaya kutokana na hali hio
iliyoneshwa na wageni hao kuonekana ni kua ya dharau. Lakini kwa upande wa Nabii
Ibrahim, badala ya kukasirika basi aliingiwa na Khofu kubwa sana, akawashukia na kua
na masuali mengi sana ya kujiuliza, kwani hili jambo halijawahi kutokea katika uhai
wake wote.

Ama kwa upande mwengine basi Nabii Ibrahim anajua kua Wageni wanapokuja katika
nyumba yako basi hua chini ya Ulinzi na Uangalifu wake, na hivyo nijukumu lako
kuwahudumia kwa ukarimu na wema, na wanapokataa ukarimu wako basi hua ni wenye
kujivua ugeni wao kwako na kutotaka ukarimu na wema wako. Nabii Ibrahim akahisi
kua hii ni ishara mbaya na hivyo huenda kuna jambo baya litatokea, lakini kumbe wageni
hawa walikua na habari njema kwake. Allah Subhanah wa Taála anatuelezea hali
ilivyokua kama anavyosema katika Qurán:

‫ﺚ أَن‬ َ َ‫ت ُر ُﺳﻠُﻨَﺂ إِﺑْـَﺮ ِاﻫ َﻴﻢ ﺑِﭑﻟْﺒُـ ْﺸَﺮ ٰى ﻗَﺎﻟُﻮاْ َﺳﻼَﻣﺎً ﻗ‬
َ ِ‫ﺎل َﺳﻼٌَم ﻓَ َﻤﺎ ﻟَﺒ‬ ْ َ‫﴿ َوﻟََﻘ ْﺪ َﺟﺂء‬
ً‫ﺲ ِﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ ِﺧﻴ َﻔﺔ‬ ‫ﺟ‬ ‫َو‬
‫أ‬‫و‬ ‫ﻢ‬ ‫ﻫ‬‫ﺮ‬‫ﻜ‬ِ َ‫ﺼﻞ إِﻟَﻴ ِﻪ ﻧ‬ ِ َ‫ﻴﺬ ۞ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ رأَى أَﻳ ِﺪﻳـﻬﻢ ﻻَ ﺗ‬ ٍ ِ‫ﺟﺂء ﺑِﻌِﺠ ٍﻞ ﺣﻨ‬
َ ََْ ْ َ ُ ْ ُ ْ َُ ْ َ َ ْ َ َ
﴾‫ﻮط‬ٍ ُ‫ﻒ إِ ﱠ� أُرِﺳﻠْﻨَﺎ إِ َ ٰﱃ ﻗَـﻮِم ﻟ‬
ْ ْ ْ َ‫ﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻻَ َﲣ‬
300

Walaqad jaat rusuluna ibraheema bialbushra qaloo salaman qala salamun fama
labitha an jaa biAAijlin haneedhin Falamma raa aydiyahum la tasilu ilayhi
nakirahum waawjasa minhum kheefatan qaloo la takhaf inna orsilna ila qawmi
lootin (Surat Hud 11:69-70)

Tafsir: Kwa hakika, walikuja Wajumbe wetu kwa Ibrahim wakiwa na habari njema.
Wakasema: ‘Salaam’ Nae akajibu: ‘Salaam’ Na hakuchelewa bali aliwatayarishia
Haniidhi. Kisha alipoona mikono yao haisogei kwenye chakula, akawa na wasiwasi
na kuingiwa na khofu juu yao. Nao wakasema: ‘Usiwe na khofu, hakika sisi
tumetumwa kwa watu wa Lut’

Aya zinatuonesha kua Wageni watukufu wa Nabii Ibrahim wamekuja kwa Nabii Ibrahim
lakini wakiwa pia ni wenye kuelekea kwa Nabii Lut, hivyo kwa upande mmoja tunaona
ni kua mbali ya kua Nabii ibrahim anataka kupewa habari njema lakini pia anaoneshwa
wazi kutekelezewa ahadi yake ambayo imo katika yale maneno yasemayo kua:

ِ ‫ﻚ ﻟِﻠﻨ‬
َ َ‫ﱠﺎس إِ َﻣﺎﻣﺎً ﻗ‬
‫ﺎل‬ ِ ‫ﺎل إِِﱏ ﺟ‬
َ ُ‫ﺎﻋﻠ‬ ٍ ِ ِ ِ ِ ِِ
َ ّ َ َ‫﴿ َوإذ ٱﺑْـﺘَـﻠَ ٰﻰ إﺑْـَﺮاﻫ َﻴﻢ َرﺑﱡﻪُ ﺑ َﻜﻠ َﻤﺎت ﻓَﺄََﲤﱠُﻬ ﱠﻦ ﻗ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ ُ ‫ﺎل ﻻَ ﻳـﻨ‬
ََ َ َ‫َوِﻣﻦ ذُِّرﻳﱠِﱴ ﻗ‬
َ ‫ﺎل َﻋ ْﻬﺪى ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
Wa-idhi ibtala ibraheema rabbuhu bikalimatin faatammahunna qala innee
jaAAiluka lilnnasi imaman qala wamin dhurriyyatee qala la yanalu AAahdee
aldhdhalimeena (Surat Al Baqara 2:124)

Tafsir: Na kumbuka wakati Mola wake Ibrahim alipomjaribu kwa kumpa amri ambayo
nae aliitekeleza. Hivyo Allah Subhanah wa Taála akasema: Kwa hakika mimi
nitakufanya wewe kua kiongozi wa Watu. Ibrahim akasema: ‘Na watoto wangu
(Wafanye kua Viongozi)’. (Allah Subhanah wa Taála akasema) ‘Makubaliano yangu
hayawajumuishi Waliokua Madhalim’

Na hivyo kuoneshwa kua tayari ameshakua kiongozi na si wa watu wake nyumbani tu


bali na watu wa motto wa Ami yake ambae ni Nabii Lut.

Habari hii inahadithiwa tena katika Surat Adh Dhariyat ambapo tunaona kua Allah
Subhanah wa Taála anaiaznia mwanzo kabisa kwa kuhoji kumhoji Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam kua Jee imekufikiea wewe Hadith ya wageni watukufu wa Ibrahim? Na
hivyo kua ni yenye kutuonesha kua mwanzo zilishuka aya za Surat Adh Dhariat na kisha
baadae ndio zikashuka aya za Surat Hud.
301

Ila sisi tulianza na Surat Hud kwa sababu ya kua tumeanza kukielezea chakula cha
Haniidh na Surat Hud ndio iliyotaja jina la Haniidh, hivyo katoka Surat Adh Dhariyat
basi tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala anasema:

ً‫ﲔ ۞ إِ ْذ َد َﺧﻠُﻮاْ َﻋﻠَْﻴ ِﻪ ﻓَـ َﻘﺎﻟُﻮاْ َﺳﻼَﻣﺎ‬ ِ ِ ِ ‫﴿ﻫﻞ أ ََﺎﺗ َك ﺣ ِﺪﻳﺚ ﺿﻴ‬
َ ‫ﻒ إِﺑْـَﺮاﻫ َﻴﻢ ٱﻟْ ُﻤ ْﻜَﺮﻣ‬ َْ ُ َ َْ
‫ﺎل‬ ٍ ‫غ إِ َ ٰﱃ أ َْﻫﻠِ ِﻪ ﻓَ َﺠﺂء ﺑِﻌِ ْﺠ ٍﻞ َِﲰ‬
َ َ‫ﲔ۞ ﻓَـ َﻘﱠﺮﺑَﻪُ إِﻟَْﻴ ِﻬ ْﻢ ﻗ‬ َ ‫ﺎل َﺳﻼٌَم ﻗَـ ْﻮٌم ﱡﻣﻨ َﻜُﺮو َن۞ ﻓَـَﺮا‬َ َ‫ﻗ‬
َ
﴾‫ﻒ وﺑَﺸﱠﺮوﻩُ ﺑِﻐُﻼٍَم َﻋﻠَﻴ ٍﻢ‬ ْ َ‫ﲣ‬َ ‫ﻻ‬
َ ‫ا‬
ْ‫ﻮ‬ ‫ﻟ‬
ُ ‫ﺎ‬‫ﻗ‬
َ ‫ﺔ‬
ً ‫ﻔ‬
َ ‫ﻴ‬ ِ ‫أَﻻَ َﺄﺗْ ُﻛﻠُﻮ َن۞ ﻓَﺄَوﺟﺲ ِﻣْﻨـﻬﻢ‬
‫ﺧ‬
ُ َ ُْ َ َ ْ
Hal ataka hadeethu ssayfi ibraheema almukrameena, Idh dakhaloo AAalayhi
faqaloo salaman qala salamun qawmun munkaroona, Faragha ila ahlihi fajaa
biAAijlin sameenin, Faqarrabahu ilayhim qala ala ta/kuloona, Faawjasa minhum
kheefatan qaloo la takhaf wabashsharoohu bighulamin AAaleemin (Surat Adh
Dhariyat 51:24-28)

Tafsir: Jee imekufikia wewe hadith ya watu watukufu wa Ibrahim? Walipowasili


kwake, kisha wakasema: ‘Salam!’ Nae akasema: ‘Salam! Enyi wageni Watukufu!’
Akakaa faragha na watu wa Nyumbani kwake, kisha akaleta Nyama iliyookwa. Na
akawasogezea karibu yao, huku akisema: ‘Jee Hamtokula?’. Kisha akawa na wasiwasi
na kuingiwa na khofu juu yao. Nao wakasema: ‘Usiwe na Khofu.’ Na tukambashiria
Mtoto mwenye ufahamu mpana.

Nabii Ibrahim akawauliza: ‘Vipi mbona hamtaki kula?’ Wale wageni wakasema: ‘Ya
Ibrahim! Hakika sisi tunakula chakula kwa Malipo’. Nabii Ibrahim akajibu: ‘Enyi
Wageni wangu! Hakika hiki nilicho kutayarishieni, hamtokila bure bure kwani
nacho pia kina malipo’. Wageni wakauliza: ‘Jee ni Malipo gani, Ya Ibrahim?’ Nabii
Ibrahim akasema: ‘Ni kuanza na Jina la Allah Subhanah wa Taála kabla ya kula na
kumshukuru Allah Subhanah wa Taála baada ya Kula.’

Malaika Jibril akamwangalia Malaika Mikail na kusema: ‘Bila ya shaka Ibrahim,


anastahiki kupewa sifa ya Khalilu Allah’ Kisha akamgeukia Nabii Ibrahim akamtuliza
na kumtoa Khofu kwa kumwambia: ‘Usiwe na khofu hakika sisi tumetumwa
kukuletea habari njema kutoka kwa Mola wako.’ Na hivyo wakampa Nabii Ibrahim
habari ya kupata Mtoto mwema wa kiume ambae nae atapata mtoto mwema pia wa
kiume. Mbele ya Sarah ambae kama zinavyoweka wazi Aya za Surat Hud pale
ziliposema:
302

۞‫ﻮب‬ َ ‫ﺎق َوِﻣﻦ َوَر ِآء إِ ْﺳ َﺤ‬


َ ‫ﺎق ﻳَـ ْﻌ ُﻘ‬ َ ‫ﺖ ﻓَـﺒَﺸْﱠﺮَ� َﻫﺎ ﺈﺑِِ ْﺳ َﺤ‬ ِ َ‫﴿وٱﻣﺮأَﺗُﻪ ﻗَﺂﺋِﻤﺔٌ ﻓ‬
ْ ‫ﻀﺤ َﻜ‬ َ َ ُ َْ َ
ْ‫ﻴﺐ۞ ﻗَﺎﻟُ ۤﻮا‬ ِ ِ ِ
ٌ ‫ﻮز َوَﻫـٰ َﺬا ﺑَـ ْﻌﻠﻰ َﺷْﻴﺨﺎً إ ﱠن َﻫـٰ َﺬا ﻟَ َﺸ ْﻲءٌ َﻋﺠ‬
ِ
ٌ ‫ﺖ ٰﻳـ َﻮﻳْـﻠَﺘَﺎ أَأَﻟ ُﺪ َوأ ََ�ْ َﻋ ُﺠ‬
ْ َ‫ﻗَﺎﻟ‬
﴾‫ﲪﻴ ٌﺪ ﱠِﳎﻴ ٌﺪ‬ َِ ‫ﺖ إِﻧﱠﻪ‬ِ ِ‫ٱﻪﻠﻟِ ر ْﲪﺔُ ﱠ‬ ِ ِ‫أَﺗَـﻌﺠﺒ‬
ُ ‫ٱﻪﻠﻟ َوﺑـََﺮَﻛﺎﺗُﻪُ َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ أ َْﻫ َﻞ ٱﻟْﺒَـْﻴ‬ َ َ ‫ﲔ ﻣ ْﻦ أ َْﻣ ِﺮ ﱠ‬ َ َْ
Waimraatuhu qa-imatun fadhahikat fabashsharnaha bi-ishaqa wamin wara-i
ishaqa yaAAqooba. Qalat ya waylata aalidu waana AAajoozun wahadha baAAlee
shaykhan inna hadha lashay-on AAajeebun, Qaloo ataAAjabeena min amri Allahi
rahmatu Allahi wabarakatuhu AAalaykum ahla albayti innahu hameedun
majeedun, (Surat Hud 11:70-73)

Tafsir: Na Mke wake aliekua amesimama akacheka, lakini tukambashiria habari


njema za Mtoto mwema Is-haqa na na baada ya Is-haqa yaquub. Akasema (kwa
kushangaa) ‘Ole wangu! Nitapata mtoto wakati mimi ni kikongwe, na huyu hapa
mume wangu ni kizee. Hakika hili ni jambo ajabu sana’. Nao (Malaika) wakasema:
‘Unaona ajabu juu ya yale aliyoyakadiria Allah? Rehma za Allah na Baraka zake ziwe
juu yenu, Enyi familia ya Ibrahim. Hakika yeye (Allah) Mwenye ni kustahiki sifa zote
na mwenye Kushinda.’

Aya yetu hii imetumia neno Fadhahiqat ambalo limetokana na neno Dhahiqa ambalo
kwa Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Kushangaa, Kustaajabu, Kufanya Dhihaka,
Kucheka, Kujawa na Hisia za ari ya kufanya jambo kutokana na kupendezewa na jambo
fulani. Neno Dhahiqa pia hua linamaanisha Kukenya, au kujawa na Nuru usoni kutokana
na kua na Furaha na pia hua ni lenye kumaanisha kuingia katika Hedhi yaani Mwanamke
anapoingia katika siku zake.

Wanazuoni wametofautiana juu ya sababu ya kucheka kwa Sarah, kwani Imam Ismail
Abd Rahman Al Suddi anasema kua: ‘Sarah aliona dhihaka kwa sababu Wageni
waligoma kula chakula Adhim walichokua wamewatayarishia. Hivyo kua na
mtizamo wa kua: ‘Ah! Hawa ni watu gani wasiokula chakula adhimu kama hiki
tulichowatayarishia?’’

Ama kwa upande mwengine basi tunaona pia kua hapa Sarah alicheka labda kwa sababu
ya kuona kua: ‘Hawa watu wamekataa ukarimu na wema wetu kisha wanataka
kutufanyia dhihaka zaidi ya kutuambia kua tutapata Mtoto wakati mimi nna umri
wa miaka 90 na mume wangu ana umri wa miaka 120, sote ni tayari tumeshakua
Vizee. Mda wetu wa kupata watoto umeshapita. Yatakuaje mambo haya?’
303

Ama kwa upande mwengine basi Mujahid Ibn Sulayman na Ikrimah Mawla Abd Allah
Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu wao wanasema kua Waarabu husema: ‘Yadhak al'Arnab
eindama yuhidh’ yaani ‘Sungura hua ni mwenye kucheka anapopata hedhi yake.’
Hivyo kutokana na mtizamo huo wa kilugha basi Sarah ambae alikua tayari keshaingia
katika kipindi cha kusitisha siku zake, basi alibadilika hali ya kimaumbile na akawa ni
mwenye kuingia katika siku zake.

Ni kawaida kwa Wanawake wa Kiarabu kujipiga piga vibao mashavuni au kwenye paji
la uso, wanapokua wamejawa na hisia za hasira au mshangao kwa kutoamini
wanayoyasikia au wanayoyaona kua yanatokea mbele ya macho yao. Hivyo Sarah
akajipiga piga vibao uso wake kutokana na kutoamini yatakayotokea na hali ikawa kama
isemavyo aya ifuatayo:

﴾‫ﻮز َﻋ ِﻘﻴﻢ‬ ْ ‫ﺼ ﱠﻜ‬


ِ
َ ‫﴿ﻓَﺄَﻗْـﺒَـﻠَﺖ ْٱﻣَﺮأَﺗُﻪُ ِﰱ‬
َ َ‫ﺻﱠﺮةٍ ﻓ‬
ٌ ٌ ‫ﺖ َﻋ ُﺠ‬ْ َ‫ﺖ َو ْﺟ َﻬ َﻬﺎ َوﻗَﺎﻟ‬
Faaqbalati imraatuhu fee sarratin fasakkat wajhaha waqalat AAajoozun
AAaqeemun (Surat Adh Dhariiyat 51:29)

Tafsir: Kisha akasogea Mke wake akiwa analia huku akiupiga vibao uso wake na
kusema kwa sauti: ‘Mimi ni Ajuza alie Tasa’

Bashirio hili la Malaika halikua ni lenye kumshangaza Sarah tu lakini pia lilimshangaza
pia Nabii Ibrahim, kwani yeye ni Mtu ambae ameridhika na Majaaliwa ya Mola wake
lakini hata hivyo akaendelea kuwahoji Malaika hao kama inavyosema aya ifuatayo:

ْ ِ‫ﲎ ٱﻟْ ِﻜﺒَـُﺮ ﻓَﺒِ َﻢ ﺗُـﺒَ ِّﺸُﺮو َن۞ ﻗَﺎﻟُﻮاْ ﺑَﺸْﱠﺮَ� َك ﺑ‬


َ‫ﭑﳊَِّﻖ ﻓَﻼ‬ ِ ِ َ َ‫﴿ﻗ‬
َ ‫ﺎل أَﺑَﺸْﱠﺮُﲤُﻮﱏ َﻋﻠَ ٰﻰ أَن ﱠﻣ ﱠﺴ‬
﴾‫ﻂ ِﻣﻦ ﱠر ْﲪَِﺔ رﺑِِّﻪ إِﻻﱠ ٱﻟﻀﱠﺂﻟﱡﻮ َن‬ ُ َ‫ﺎل َوَﻣﻦ ﻳَـ ْﻘﻨ‬ َ َ‫ﲔ۞ ﻗ‬ ِِ ِ
َ ‫ﺗَ ُﻜﻦ ّﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻘﺎﻧﻄ‬
َ
Qala abashshartumoonee AAala an massaniya alkibaru fabima tubashshirooni;
Qaloo bashsharnaka bialhaqqi fala takun mina alqaniteena; Qala waman yaqnatu
min rahmati rabbihi illa aldhdhalloona (Surat Al Hijr 15:53-56)

Tafsir: Nae (Ibrahim akasema): ‘Mnanibashiria mie Mtoto, wakati nikiwa katika umri
mkubwa? Jee ni nini ujumbe wenu’. Wao (Malaika) wakasema: ‘Hakika sisi tunakupa
ujumbe wa haki, hivyo usiwe ni miongoni mwa walikata tamaa.’ Nae (Ibrahim)
akasema: ‘Na jee nani atakaekata tamaa kutokana na Rehma za Mola wake isipokua
yule ambae amepotoka?’
304

Kwani aya zinatuonesha kua Ingawa Nabii Ibrahim alibashiriwa Mtoto mwema atakaetoa
Mtoto mwema na hivyo kuendeleza kizazi chema cha Manabii wataaoendeleza Imani ya
Kumuamini na kutomshirikisha Allah Subhanah wa Ta'ala. Lakini bado alikua ana
wasiwasi Juu ya kazi waliyokuja kufanya Malaika hao. Hivyo akauliza, hivi nyinyi
mmetumwa na Allah Subhanah wa Ta'ala kwa ajili ya kunitumia ujumbe huo tu?

Na hivyo akaambiwa kua asiwe ni mwenye kukata tamaa kutokana na rehma za Allah
Subhanah wa Ta'ala. Nae akamalizia kwa kutupa sisi mimi nawe pia ujumbe ambao ni
Wenye kufuata Milat Ibrahima kua: ‘Kamwe tusichoke kumuomba Allah Subhanah
wa Ta’ala na wala tusikate tamaa kutokana na Rehma zake, kwani wenye kukata
tamaa hua ni sawa na madhalimu wenye kujidhulumu.’

Hivyo ingawa Nabii Ibrahim aliamini ubashirio wa kua atapata Mtoto mwema na mjukuu
mwema na hivyo kumhakikishia kizazi kitakachotoa Mitume katika wakati wake na
baada ya kufariki kwake lakini bado akawa na wasiwasi kua haiwezekani hawa Malaika
waje kwa sababu ya kunibashiria mimi mtoto tu, bali lazima itakua kuna na kazi au jambo
jengine ambalo wamekuja maalum kulitekeleza. Nabii Ibrahim akajawa na shauku ya
kutaka kujua zaidi kusudio na lengo lao kuu hasa la safari yao hii ya kuja nyumbani
kwake. Hivyo akawauliza.

َ ‫ﲔ۞ إِﻻﱠ‬ ِ ٍ ِ
‫آل‬ َ ‫ﺎل ﻓَ َﻤﺎ َﺧﻄْﺒُ ُﻜ ْﻢ أَﻳـﱡ َﻬﺎ ٱﻟْ ُﻤْﺮ َﺳﻠُﻮ َن۞ ﻗَﺎﻟُﻮاْ إِ ﱠ� أ ُْرﺳ ْﻠﻨَﺂ إِ َ ٰﱃ ﻗَـ ْﻮم ﱡْﳎ ِﺮﻣ‬
َ َ‫﴿ﻗ‬
﴾‫ﲔ ۞ إِﻻﱠ ْٱﻣﺮأَﺗَﻪُ ﻗَﺪ ْﱠر َ� إِﻧـﱠ َﻬﺎ ﻟَ ِﻤﻦ ٱﻟْﻐَﺎﺑِ ِﺮﻳﻦ‬ ِ‫َﲨﻌ‬ْ ‫أ‬ ‫ﻢ‬ ‫ﻮﻫ‬ ‫ﺠ‬
‫ﱡ‬ ‫ﻨ‬
َ ‫ﻤ‬ َ‫ﻟ‬ ‫ﱠ‬
� ٍ ُ‫ﻟ‬
ِ‫ﻮط إ‬
َ َ َ َ َ ْ ُ ُ
Qala fama khatbukum ayyuha almursaloona; Qaloo inna orsilna ila qawmin
mujrimeena; Illa ala lootin inna lamunajjoohum ajmaAAeena;Illa imraatahu
qaddarna innaha lamina alghabireena, (Surat Al Hijr 15:57-60)

Tafsir: Akasema: ‘Jee ni nini ujumbe wenu enyi wajumbe?’ Nao wakasema: ‘Hakika
sisi tumetumwa kwa Mujrimun (Waliomkhalif Mola wao) Isipokua familia ya Lut,
hakika wao tutawaokoa, isipokua mke wake ambae tayari ameshakadiriwa kua atakua
ni miongoni mwa watakaobakia na kuangamia ’

Mara tu baada ya khofu kumuondoka Nabii Ibrahim juu ya wageni wake hao. Malaika
hao wakamuwekea wazi Nabii Ibrahim juu lengo kuu la kupita katika mji wake kua ni
kuelekea katika mji wa Nabii Lut ili kuwapa adhabu watu wa Nabii Lut, Nabii Ibrahim
akainwa na khfo na wasi wasi zaidi kwani katika mji huo yumo Lut ambae ni mtoto wa
ami yake hivyo anakua kaka yake, na pia kwa upande mwengine ndie mtu pekee
aliehhama nae kutoka katika mji wake walipofanya hijra kwa ajili ya kuachana na watu
wa Namrudh Al Kabir na hivyo Nabii Lut kua ni Mtu peke ambae alimkubali Nabii
305

Ibrahim pale wengine wote walipomkataa, hivyo Nabii Ibrahim akamuonea huruma
Nabii Lut na watu wake, na hivyo akaanza kumtetea Nabii Lut kama inavyosema aya
ifuatayo:

ٍ ُ‫﴿ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ َذﻫﺐ ﻋﻦ إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ ٱﻟﱠﺮوع وﺟﺂءﺗْﻪ ٱﻟْﺒ ْﺸﺮ ٰى ُﳚ ِﺎدﻟُﻨَﺎ ِﰱ ﻗَـﻮِم ﻟ‬
﴾‫ﻮط‬
ْ َ َ ُ ُ َ َ َ ُ ْ َ َْ ْ َ َ َ
Falamma dhahaba AAan ibraheema alrrawAAu wajaat-hu albushra yujadiluna fee
qawmi lootin (Surat Hud 11: 74)

Tafsir: Na baada ya kumuondoka Khofu Ibrahim na kumfikia habari (za Nabii Lut)
akaanza kujadiliana juu ya watu wa Nabii Lut.



KHALIL ALLAH IBRAHIM NA WATU WA NABII LUT.



Allah Subhanah wa Ta’ala anatufafanulia kuhusiana na hali ya upande wa Nabii Lut na
Watu wake katika mji wake pale aliposema katika aya ifuatavyo:

۞‫ﲔ‬ ِ ِ ‫ﺎل ﻟَِﻘﻮِﻣ ِﻪ أ ََﺄﺗْﺗُﻮ َن ٱﻟْ َﻔ‬


ِ ٍ ‫ﺎﺣ َﺸﺔَ ﻣﺎ ﺳﺒـ َﻘ ُﻜﻢ ِﻬﺑﺎ ِﻣﻦ أ‬ ِ ﴿
َ ‫َﺣﺪ ّﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬ َ ْ َ ْ ََ َ ْ َ َ‫َوﻟُﻮﻃﺎً إ ْذ ﻗ‬
ِ ِ ِ ِ
﴾‫ﺂء ﺑَﻞ أَﻧْـﺘُﻢ ﻗَـﻮٌم ﱡﻣﺴ ِﺮﻓُﻮ َن‬ ِ ‫إِﻧﱠ ُﻜ ْﻢ ﻟَﺘَﺄْﺗُﻮ َن‬
ْ ْ ْ ْ ‫ﺎل َﺷ ْﻬ َﻮًة ّﻣﻦ ُدون ٱﻟﻨّ َﺴ‬ َ ‫ٱﻟﺮ َﺟ‬
ّ
Walootan idh qala liqawmihi ata/toona alfahishata ma sabaqakum biha min ahadin
mina alAAalameena; Innakum lata/toona alrrijala shahwatan min dooni alnnisa-i
bal antum qawmun musrifoona. (Surat Al Araf 7:80-81)

Tafsir: Na Lut alisema kuwaambia watu wake: ‘Nyinyi mnafanya dhambi ambayo
haijawahi kufanywa na yeyote hapo kabla miongoni mwa Walimwengu. Kwani kwa
Hakika Mnawafanyia sivyo kwa kuwatamani Wanaume badala ya Wanawake, kwa
hakika nyinyi ni watu waliovuka Mipaka.’’

Ambapo katika Surat Al Anqabut tunaona kua aya zinafafanua zaid maneno ya Nabii Lut
kwa Watu wake kwa kusema:
306

‫ﻴﻞ َو َﺄﺗْﺗُﻮ َن ِﰱ َ� ِدﻳ ُﻜ ُﻢ ٱﻟْ ُﻤْﻨ َﻜَﺮ ﻓَ َﻤﺎ َﻛﺎ َن‬ ِ


َ ‫ﺎل َوﺗَـ ْﻘﻄَﻌُﻮ َن ٱﻟ ﱠﺴﺒ‬
ِ ‫﴿أَﺋِﻨﱠ ُﻜ ْﻢ ﻟَﺘَﺄْﺗُﻮ َن‬
َ ‫ٱﻟﺮ َﺟ‬
ّ
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ‫ٱﻪﻠﻟِ إِن ُﻛﻨﺖ ِﻣﻦ ٱﻟ ﱠ‬ ِ ‫ﺟﻮاب ﻗَـﻮِﻣ ِﻪ إِﻻﱠ أَن ﻗَﺎﻟُﻮاْ ٱﺋْﺘِﻨَﺎ ﺑِﻌ َﺬ‬
َ ‫ﺼﺎدﻗ‬ َ َ ‫اب ﱠ‬ َ ْ َ ََ
A-innakum lata/toona alrrijala wataqtaAAoona alssabeela wata/toona fee
nadeekumu almunkara fama kana jawaba qawmihi illa an qaloo i/tina biAAadhabi
Allahi in kunta mina alssadiqeena (Surat Al Anqabut 29:29)

Tafsir: Kwa Hakika Nyinyi Mnawafanyia sivyo Wanaume, na Mnakatisha Njia na


Kufanya Maovu katika Mikusanyiko yenu. Lakini watu hawa hawakujibu kitu
isipokua walisema: ‘Tuletee Adhabu ya Allah juu yetu kama wewe ni Msema kweli’

Naam, kama tunavyoona kua aya zetu zimetumia maneno mawili muhimu ambayo yote
hua ni yenye kufanana kimatamshi, maneno hayo ni La-Tta na Lata. Ambapo neno la
kwanza ndio lililotoa Jina la Nabii Lut, kwani alikua akiitwa Lut kwa sababu ya uasili ya

jina lake ni wenye kutokana na neno La-Tta ‫ﻵط‬ ambalo ni lenye kumaanisha Mtu
mwenye kumpenda sana Mtu mwengine, Kumuweka akilini na mawazoni mtu
umpendae, Kuchukua kitu kutoka katika sehemu yake, na pia humaanisha Kua na
Huruma sana na Kua na Uwezo wa Kufanya Kitu kwa Haraka sana.

Na neno la pili ni La-Ta ‫ﻟﺖ‬ ambalo ndio lililotoa neno Lata/Tuuna na ni lenye
kumaanisha Kujibu Suali ambalo halikukusudiwa au Suali ambalo Hukuulizwa, Kugeuza
Kitu au Kubadilisha kitu kutokana na maumbile yake.

Hivyo basi Nabii Lut alikua akiwalalamikia Watu wake kua walikua wakiwabadilisha
Maumbile Wanaume na kuwatamani kwa ajili ya kutimiza mahitaji yao ya kimatamanio
badala ya kutimiza matamanio hayo kwa Wanawake ambao kimaumbile ndio
walioumbwa maalum kwa ajili ya kuwapatia utulivu wa matamanio yao Wanaume.

Aya pia zimetumia maneno wataqtaAAoona alssabeela yaani Na mnakatisha njia,


ambapo kwa upande wa Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari basi yeye
anasema kuhusiana na maana ya maneno haya kua: Walikua wanakatisha njia za
Kimaumbile. Na kwa upande wa Imam Mujahid Ibn Sulayman basi yeye anasema
kuhusiana na maneno haya kua: ‘Watu hawa walikua wakiiingiliana na Wanaume
Njiani na katika kila sehemu wanayokusanyika kwa pamoja.’

Ama kwa upande mwengine basi anasema Ummu Hani Radhi Allahu Anha kua: ‘Hakika
mimi nilimuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam maana ya maneno
307

yasemayo wataqtaAAoona alssabeela basi yeye akasema kwa kunimabia kua: ‘Watu
hawa walikua wakiwarushia Mawe wapita njia kisha wanaanza kuwacheka.’’

Tunapoangalia Historia basi tunaona kua watu hawa wa Nabii Lut walikua wakiishi
katika Ardhi ya Mashariki ya nchi ya Jordan ambayo ilikua na miji mikubwa mitano
ambayo ni:

1-Admuta.
2-Ghamura au Gomorah.
3-Sabura.
4-Sadum Au Sodoma.
5-Saghura.

Miji hii ilikua ipo katikati ya njia kuu ya misafara kutoka Israil kupitia Syria hadi Misri
ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala ameelezea kama alivyosema katika aya ifuatayo:

﴾‫﴿وإِﻧـﱠ َﻬﺎ ﻟَﺒِﺴﺒِ ٍﻴﻞ ﱡﻣ ِﻘﻴ ٍﻢ‬


َ َ
Wa-innaha labisabeelin muqeemin. (Surat Al Hijr 15:76)

Tafsir: Na kwa Hakika (Miji hii) ilikua katika Njia Kuu.

Aya zinatuwekea wazi kua watu hawa miji yao ilikua ipo katika njia kuu ambayo
ilikuwepo katika wakati huo, na mpaka leo hii bado ipo na inajulikana kwa jina la Arava
Highway au Route nambari 90, barabara hii ambayo imepitia katika eneo la Ardhi la Miji
hii mitano ni barabara yenye urefu wa kilomita 480 na ni yenye kutumiwa na Wasafiri
kutokea katika Ardhi ya Misri, kupitia Jordan mpaka Palestina, Lebanon na Syria pia,
na ilikua inapita katika eneo hili ambalo limejaa rutba na barka kubwa sana kwani ilikua
kila kitu kinaota na kunawiri vizuri sana kama Bustani ya Peponi iliyopo Duniani.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala ameitaja Njia hii katika Qur’an Kwa kusema Wa-
innaha labisabeelin muqeemin ili kutuonesha umuhimu wa Miji hio kwa Wasafiri kwa
wakati huo kwani tunapozungumzia Safari za Masafa Marefu hata hii leo, kuna sehemu
ambazo Miji imekua mikubwa kwa sababu ya kua ipo njiani kwenye vituo vya
barabarani, na hivyo magari yanapofika katka maeneo hayo basi hua ni yenye kusimama
na kisha Wasafiri hua ni wenye kushuka kutoka katika magari na hivyo hua ni wenye
kujisaidia, kunyoosha miguu yao, kula, kupumuzika kidogo. n.k.

Na hii ni kulingana na hali yetu sisi ambao tunaishi katika wakati wa maendeleo ya kua
na Magari yanayotembea kwa kasi, sasa tunapozungumzia Misafara ya Wasafiri wa zama
308

hizo ambao walikua wakitembea kwa kutumia Ngamia, Farasi na Punda na wengine kwa
miguu, hua ni wenye kutembea kwa safari miezi na hivyo kupita katika maeneo ya
Majangwa, Milima, Michanga, Mawe na Mavumbi. Basi walikua wakifika katika
maeneo haya ya Miji ya watu wa Nabii Lut basi hua ni wenye kujisikia kua kama wako
Peponi, kwani hua ni wenye kuweza kupumzika ipasavyo na kujipatia mahitaji yao yote
ya safarini, kabla ya kumalizia safari yao.

Kiongozi wa Ardhi hizi alikua ni Mfalme pia ambae alikua akijulikana kwa jina la Sadum
Ibn Mushdim na Waziri wake Mkuu alikua akiitwa Gurmuz, ambapo watu wote wa Miji
hii walikua ni kama watu wa Mfalme Al Namrudh Al Kabir alieangamia kupitia kwenye
Mikono ya Nabii Ibrahim. Kwani Mfalme Sadum Ibn Mushdim na watu wake walikua
nao pia wanaabudu Masanam, lakini tofauti ni kua wakati ambapo wa Mfalme Al
Namrudh walikua wanaabudu Masanam zaidi ya 5000, basi watu wa Mfalme Sadum
walikua wakiabudu Masanam Manne tu ambayo ni:

1-Yabad.
2-Mashur.
3-Qub na
4-Qurt.

Kwani katika Ulimwengu Mzima kwa Wakati huo basi ilikua hakuna Masanam
yanayothaminiwa na kuonekana kua yana Barka na Manufaa zaid kwa Washirikina tangu
Kuanzia Kipindi cha Nabii Idrisa Alayhi Salam mpaka wakati huo, kama Masanam haya
manne. Kwani Ardhi ya Maeneo ya Miji Mitano hio ilikua kama Bustani ya Pepo ya
Duniani...yaani kila kitu kipo na kinapatikana ndani yake.

Kwani anasema Allah Subhanah wa Ta'ala katika Qur'an kua:

ِ ‫ﺲ وٱﻟﺜﱠﻤﺮ‬
‫ات‬ ِ ‫ﻔ‬
ُ ‫َﻧ‬
‫ﻷ‬ ‫ٱ‬‫و‬ ِ ‫ﺺ ِﻣﻦ ٱﻷَﻣﻮ‬
‫ال‬ ٍ ‫ﻘ‬ْ ‫ـ‬
َ ‫ﻧ‬‫و‬ ‫ﻮع‬
ِ ‫ٱﳉ‬
ْ ‫و‬ ‫ﻮف‬
ْ ‫ٱﳋ‬
ْ ‫ﻦ‬ ِ ‫﴿وﻟَﻨَـﺒـﻠُﻮﻧﱠ ُﻜﻢ ﺑِ َﺸﻲ ٍء‬
‫ﻣ‬
ََ َ َ َ َ َ ّ َ ُ َ َ َ ْ ْ َْ َ
ّ
﴾‫ﺼﻴﺒَﺔٌ ﻗَﺎﻟُﻮاْ إِ ﱠ� ﱠﻪﻠﻟِ وإِﻧﱠـﺂ إِﻟَْﻴ ِﻪ ر ِاﺟﻌﻮ َن‬
ِ ‫ﺼﺎﺑِ ِﺮﻳﻦ ۞ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ إِ َذآ أَﺻﺎﺑـْﺘـﻬﻢ ﱡﻣ‬ ِ
َ َ ََُ َ َ ‫َوﺑَ ّﺸ ِﺮ ٱﻟ ﱠ‬
Walanabluwannakum bishay-in mina alkhawfi waaljooAAi wanaqsin mina al-
amwali waal-anfusi waalththamarati wabashshiri alssabireena; Alladheena idha
asabat-hum museebatun qaloo inna lillahi wa-inna ilayhi rajiAAoona (Surat Al
Baqara 2:155-156)

Tafsir: Na kwa hakika tutakujaribuni kwa vitu vitokanavyo na Khofu, Njaa, Kupoteza
Mali, Nafsi na Mazao, Lakini wabashirie (Mema) wenye Subra. Ambao wanapofikwa
309

na Msiba hua ni wenye kusema: ‘Kwa Hakika Sisi ni wa Allah na Kwa hakika kwake
yeye tutarejea.’

Hivyo Watu wa Nabii Lut walipewa Mtihani na Allah Subhanah wa Ta'ala wa Kutiwa
Khofu ya Kukosa Mavuno kutoka katika Mabustani na Mashamba yao kuoneshwa kua
Miungu yao wanayoiamini kua sio na haina manufaa wala athari yeyote juu yao.

Kwani mwaka mmoja wa kipindi cha baridi basi Allah Subhanah wa Ta'ala alijaalia
kushuka Theluji nyingi sana kiasi ya kua mpaka Miji yao ikawafikia Theluji hio na hivyo
wakawa hawakupata kitu katika mazao yao. Na pia kama kawaida Allah Subhanah wa
Ta'ala akajaalia kua Mwaka huo wakaja watu wengi sana kwenye Miji yao kwa Sababu
walidhania kua Miji hio haikuathirika kwa Theluji.

Hivyo Watu wa Miji hio wakaanza kulalamika kua Kuna njaa na wakaaza kuwafukuza
watu waliokuja katika Miji yao lakini sasa watu hao wakawa hawafukuziki kwani
wakiondoka hawa basi wengine wapya wanakuja kwa sababu Miji yao ni Miji Maarufu
inajulikana na Kila mtu kua ni Miji yenye Rutba. Watu wa Miji hii wakashindwa kujizuia
hivyo wakamlalamikia Mfalme Sadum.

Mfalme Sadum akawaambia kua: "Nendeni Mkamsujudie Yule Mungu aitwae Zighal
kisha Mumueleze Shida zenu kwani kwa hakika yeye atawafukuza hawa Wageni na
pia atakutatulieni shida yenu ya Njaa"

Kwani Ibilisi akisikia habari hii hivyo akamteua Shaytan aitwae Khaskhas kwa ajili ya
Kuwapotosha Watu hao na hivyo akaingia ndani ya Mwili wa yule Mungu wao
walioambiwa wamuombe ambae ni Sanam liitwalo Zighal.

Hivyo walipomuomba basi Khaskhas akajibu maombi yao watu hao kwa kusema:
"Hakika kama mngekua mnanisikiliza tangu hapo kabla basi msingefikwa na
Matatizo yote haya. La hata hivyo hamna tatizo kwani bado hamjachelewa, hivyo
nendeni kwa hawa Wageni na kisha wakamateni na muwaingize kwenye Manumba
yenu kisha muwabake wote. Na bila ya shaka baada ya hapo Basi wataondoka wote
kwa Khiari yao na wengine wakisikia basi hawatokuja tena abadan"

Naam hapa sasa ndio mwanzoni mwa habari ya Watu wa Nabii Nuh kua ni wenye
kufanya waliyofanya ilipoanza, kwani walipewa mtihani ili warudi kwa Mola wao lakini
Wakazidi kujipoteza Njia na kua ni wenye kukufuru badala yake.

Na mara tu baada ya watu wa Nabii Lut kupewa ushauri waliopewa na Shaytan aitwae
Khaskhas basi wakatawanyika na kuanza kuwakamata wageni wote ndani ya Mji huo na
kuanza kuwafanyishia kile walichoambiwa wawafanyie.
310

Na baada ya hapo Khashkhas akawa anaingia katika maumbo ya Miili ya watu tofauti
ambao ni Wanaume, kisha anaingia katika Majumba na kuiba, na katika kila nyumba
anayoiba basi anafanya mpaka akamatwe kisha anapigwa na akisha pigwa siku ya pili
anaingia tena na kuiba, anapigwa tena na kisha akiachiwa anaingia siku ya tatu.

Katika kila mara ya tatu watu wa Nabii Lut wakawa wanaona ili wamkomeshe basi
Wafanye kama walivyoamriwa na Khaskhas kuhusiana na dawa ya kuwafukuza wageni
katika nchi yao yaani Wamuingilie kinyume cha Maumbile yake.

Hivyo nae akawa akipewa adhabu hio basi haibi tena katika nyumba hio, hadi watu wa
Nabii Lut wakaona kua hio ni rai nzuri sana kwani inaleta matokeo mazuri, hata wezi
hawaibi tena hivyo hadi wizi ulipoisha na wageni walipoisha basi watu hao wakawa
tayari washazoea kufanya jambo hilo na hivyo hawawezi kulikosa. Na hapa sasa ndio
wakawa wanakaa Njiani wanasubiri wageni wapita njia kiasi ya kua waliamua kujenga
minara kwa ajili tu ya Kuangalia kwa masafa marefu ili wajue kuna Msafara unakuja ama
la.
Na kama unakuja basi ndio wanakaa na Mawe yao njiani kisha Ukipita msafara kila
mmoja anarusha jiwe lake kwa mtu wake kwenye Msafara huo na hivyo Kujihalalishia
kua aliemchagua ni mtu wake na hivyo hua ni wenye kukatisha Njia ya Misafara hio

Yaani kwa upande mwengine basi watu hawa walikua wanafanya Ikrah ambalo ni neno
linalotokana na neno Karaha ambalo humaanisha Kukirihisha, Kutumia nguvu katika
kufanya jambo lenye kuudhi, linalochukiza na lisilofaa. Ambapo kwa upande wa Imam
Al Ad Din Al Kasani basi yeye anasema kua Ikrah hua ni Kutumia nguvu katika
Kumlazimisha Mtu bila ya kua na haki ya kufanya hivyo katika kumfanyia kitu mtu huyo
bila ya ridhaa yake.

Tunapoangalia kwa upande wa Fiqh basi tuaona kua hali waliyokua wakiifanya watu wa
Nabii Lut hua ni sawa na ile inayoitwa Hirabah ambayo hua inajumuisha Ikrah ndani
yake, ambapo neno Hirabah hua linamaanisha Kutumia Nguvu Katika Kufanya Kitu,
Dhulma au Karaha, Kufanya Ujambazi, Hali ya Mtu mmoja au Kundi la Watu wengi kua
ni wenye kusababisha Machafuko katika jamii kwa Mauaji, Unyang’anyi wa kutumia
nguvu ikiwemo kuwabaka au kuwaingilia Watu kimwili bila ya ridhaa yao iwe
Wanawake au Wanaume.

Hivyo kutokana na mazingira ya uzuri wake na barka ya Ardhi yake basi watu wengi
walikua wakipenda kupita katika njia hio, hivyo watu hawa wa Nabii Lut wakawa
wanatafuta njia ya kuwazuia wasafiri wasipite kwenye barabara yao hio ili wasije
wakanufaika na vilivyomo ndani yake katika Ardhi ya mji wao kwani walikua wanataka
kutumia neema hio kwa ajili yao peke yao kutokana na kuogopa kua isije ikamalizika
kutokana na kuwanufaisha wasafiri ambao sio miongoni mwa watu wao.
311

Hivyo Ibilisi akawahadaa na kuwafundisha njia ya kufanikisha malengo yao hayo, kua
wawakamate wasafiri wanaopita njia kisha wawaingilie hadharani ili wasafiri wasipite
tena katika mji wao, na ndio maana Nabii Lut akawaonya kwa kusema:

﴾‫ﺎل وﺗَـ ْﻘﻄَﻌُﻮ َن ٱﻟ ﱠﺴﺒِﻴﻞ و َﺄﺗْﺗُﻮ َن ِﰱ َ� ِدﻳ ُﻜﻢ ٱﻟْﻤْﻨ َﻜﺮ‬ ِ ‫﴿أَﺋِﻨﱠ ُﻜ ْﻢ ﻟَﺘَﺄْﺗُﻮ َن‬
َ ُ ُ ََ َ َ ‫ٱﻟﺮ َﺟ‬
ّ
A-innakum lata/toona alrrijala wataqtaAAoona alssabeela wata/toona fee
nadeekumu almunkara (Surat Al Anqabut 29:29)

Tafsir: Kwa Hakika Nyinyi Mnawafanyia sivyo Wanaume, na Mnakatisha Njia na


Kufanya Maovu katika Mikusanyiko yenu.

Ambapo kwa upande wa Imam Abu Is-haq Ahmad Ibn Muhammad Ibn Ibrahim Al
Thalabi Al Shafii basi yeye anasema kua: ‘Kua Watu hawa walikua wakiwarushia
Mawe wapita njia kuanishia kua ni uchaguzi wa kila mtu kumchagua mpita njia
wake kwa ajili ya kumuingilia halafu walikua wanachagua miongoni mwao hakimu
ambae atathibitisha umiliki wa mtu aliepigwa jiwe na mpigaji.’

Ambapo tunapozizngalia aya zote zinazozungumzia kisa hiki kwa ujumla basi tunaoana
kua zinatujumlishia kwa ujumla makosa ya watu wa Nabii Lut kua baada ya kua ni wenye
kuingiliana kinyume na Maumbile lakini pia walikua hawamuamini Allah Subhanah wa
Ta’ala, walikua wanaendekeza Matamanio ya kimwili yaliyozidi kiasi na kuvuka
mipaka, walikua ni wabaguzi wanaowabagua kijamii na kiuchumi watu wasiokua na asili
yao yaani wageni katika jamii yao, na kuwavunjisha watu safari au kuwakatiza watu
safari.

Hivyo bila ya shaka Allah Subhanah wa Ta'ala amelijata kosa la kukatisha njia au safari
kwa sababu miongoni mwa watu wanaotakiwa kuhurumiwa na kusaidiwa katika Dini ya
Kiislam hua ni Wasafiri na ndio maana ikawa kuna Upendeleo wa Kisharia kua Miongoni
mwa wenye Kustahiki Kupewa Zakkah, Sadaqa na kufanyiwa Ukarimu zaidi basi baada
ya Watu wako wa Karibu na Masikini hua ni Wasafiri wenye Matatizo ambapo ndani
yake wanaingia pia Wakimbizi wanaokimbia kwa ajili ya kuokoa Maisha yao, kwa mfano
sasa hivi nchini Syria, Libya, Yemen, Iraq, Afghanista, n.k.

Lakini inasikitisha kua leo wale wanaojiita kua ni Viongozi wa Nchi za Kiislam
wanawapiga vita Waislam wenzao kwa manufaa yao ya kidunia na kisha kusababisha
wimbi kubwa la Wakimbizi halafu hawawajali wala hawawasadii Wakimbizi hao. Na
hivyo kua ni wenye kusababishia Wakimbizi hao wa Kiislam Wanawake, Watoto na
Wazee kua na Hali mbaya yenye kusikitisha hadi kufikia Wanawake wa Kiislam
312

kuwabidi Kutoa Hongo ya Miili yao kwa ajili tu kupata mahitaji yao ya kila siku katika
kambi za Wakimbizi.

Ambapo kwa upande wa wale waliotanglia kabla yetu walikua wanaona bora wajitenge
na jamii zao wakae waishi maisha yao peke yao kuliko kushiriki katika kusababisha
Madhara baina ya Waislam kwa Waislam, tunyaoana haya pale tunapoangalia Maisha ya
Sahaba Saad Ibn AbI Waqqas Radhi Allahu Anhu ambae ni miongoni mwa Masahaba 10
waliobashiriwa Pepo, pia kwa Sahaba Abu Musa Al Ashari Radhi Allahu Anhu, n.k
ambao wao wote waliamua kutoshiriki katika mivutano na mapigano baina ya Waislam
ikiwemo fitna za mwanzo katika Uislam zilizosababisha vita vya Siffin na Vita vya
Ngamia.

Madhara ya Mitihani kama hii ya kupigana baina ya Waislam kwa Waislam ni Makubwa
sana ambao wengi wetu tuliokua hutupo katika maeneo hayo yenye mitihani hio na
hatufuatilii basi hua hatuoni ubaya wa athari zake, Ila kisa hiki cha Ibrahim na Nabii Lut
kinatufunza madhara ya hayo pale tunapingia katika hali ya kua ni miongoni mwa
Wasafiri hao kwa mfano ufuatao.

Tuchukulie kua mtu tayari umeshasafiri kwa miguu Juani bila ya kukutana na kivuli
Jangwani, Milimani na Maweni kwa Mwezi Mzima, halafu ukafika katika eneo
linalojulikana kama Bustani ya Peponi hapa Duniani kutokana na Uzuri wa Mazingira
yake kuna hali ya hewa mzuri, upepo na kivuli na bustani inayopendeza. Nawe ukawa
unasema Alhamd Lillah ingawa sijafika Nyumbani lakini nimefika katika Kituo cha
Mapumziko ya Safari kisha nitaendelea na safari baada ya kupumzika.

Sasa baada ya kufika tu katika Mji huo baada ya kupumzika basi watu wanakurushia
Kokoto kuashiria kua Umechaguliwa kua Mke wa Mtu utake usitake, uwe peke yako, na
Mkeo au na watoto wako na huenda nyote mkageuzwa kua ni wake za watu. Tena watu
wanakugombanieni na kuna Jaji maalum ambae anahalaisha kua Msafiri gani anastahiki
kua Mke wa nani kwa Wakati huo kwani yeye ndie aliemchagua Mwanzo, na hivi ndivyo
walivyokua wakifanyiwa Wasafiri na Watu wa Nabii Lut.

Na mithili ya hivo pia ndivyo wanavyofanyiwa Wanawake wa Kiislam katika kambi za


Wakimbizi zilizoko Syria, Yemen, Libya, Palestina, Lebanon, Bangladesh n.k kutokana
na matatizo ya kua Wajane, hawana kazi ya kujipatia riski zao na wana familia ambazo
hakuna wa kuziangalia isipoku wao, kwani Waume zao wamefariki kutokana na vita vya
Waislam kwa Waislam na hivyo Wanawake hawa wa Kiislam Masikini wamebakia na
ulezi wa Mayatima, Wazee, Wagonjwa, n.k.

Na hii ni kutokana na Ujinga wetu Waislam kubaguana na kisha wenyewe kwa wenyewe
Kuitana Makafiri, hivyo kila Muislam anaemuita Muislam mwenzake Kafiri, na pia
akawa ni mwenye kuunga mkono Waislam kwa Waislam kupingana na kupigana vita
313

kwa sababu ya tofauti tu ya itikadi za Madhhab yake. Basi hua na yeye amechangia katika
kila baya linalowakuta Wakimbizi wa Kiislam Ulimwenguni, kwani Uchafu wa Chuki
ndani ya Moyo wake kwa Waislam wenzake ndio asili ya Msiba huu, uliotukumba leo
hii katika jamii za Kiislam kutokana na kua hatujui au kutokana na kua tumesahau kua
Uislam si Kusali tu, kwani amesema Allah Subhanah wa Ta'ala katika Qur'an:

ِ‫ب وﻟَـٰ ِﻜ ﱠﻦ ٱﻟِْ ﱠﱪ ﻣﻦ آﻣﻦ ﺑِﭑ ﱠﻪﻠﻟ‬ ِ ِ ِ


ََ َْ َ ‫ﻮﻫ ُﻜ ْﻢ ﻗﺒَ َﻞ ٱﻟْ َﻤ ْﺸ ِﺮق َوٱﻟْ َﻤ ْﻐ ِﺮ‬ َ ‫ﺲ ٱﻟِْ ﱠﱪ أَن ﺗُـ َﻮﻟﱡﻮاْ ُو ُﺟ‬َ ‫﴿ﻟﱠْﻴ‬
‫ﺎل َﻋﻠَ ٰﻰ ُﺣﺒِّ ِﻪ َذ ِوى ٱﻟْ ُﻘْﺮَ ٰﰉ‬ َ ‫ﲔ َوآﺗَﻰ ٱﻟْ َﻤ‬ ِ
‫ﻴ‬ِ‫ﺒ‬‫ﱠ‬‫ﻨ‬ ‫ٱﻟ‬‫و‬ ِ
‫ﺎب‬ َِ ْ‫ٱﻵﺧ ِﺮ وٱﻟْﻤ ۤﻼﺋِ َﻜ ِﺔ وٱﻟ‬
‫ﺘ‬ ‫ﻜ‬ ِ ‫وٱﻟْﻴـﻮِم‬
َّ َ َ َ َ َْ َ
ِ َ‫ٱﻟﺮﻗ‬
ِ ‫ﲔ َوِﰱ‬ ِِ ِ
‫ﺼﻼةَ َوآﺗَﻰ‬ ‫ﺎب َوأَﻗَ َﺎم ٱﻟ ﱠ‬ ّ َ ‫ﲔ َوٱﺑْ َﻦ ٱﻟ ﱠﺴﺒِ ِﻴﻞ َوٱﻟ ﱠﺴﺂﺋﻠ‬ َ ‫َوٱﻟْﻴَـﺘَ َﺎﻣ ٰﻰ َوٱﻟْ َﻤ َﺴﺎﻛ‬
‫ﲔ ٱﻟْﺒَﺄْ ِس‬ ِ ِ ‫ﺂء وٱﻟ ﱠ‬ ِ ‫ﺼﺎﺑِ ِﺮﻳﻦ ِﰱ ٱﻟْﺒﺄْﺳ‬ ِ‫ٱﻟﱠﺰَﻛﺎ َة وٱﻟْﻤﻮﻓُﻮ َن ﺑِ َﻌ ْﻬ ِﺪ ِﻫﻢ إ‬
َ ‫ﻀﱠﺮاء َوﺣ‬ َ َ َ ‫ﱠ‬ ‫ٱﻟ‬ ‫و‬
َ ‫ا‬
ْ‫و‬ ‫ﺪ‬
ُ ‫ﺎﻫ‬
َ ‫ﻋ‬
َ ‫ا‬ ‫ذ‬
َ ْ ُ َ
ِ ‫أُوﻟَـٰﺌِ ﱠ‬
﴾‫ﻚ ُﻫ ُﻢ ٱﻟْ ُﻤﺘﱠـ ُﻘﻮ َن‬ َ ِ‫ﺻ َﺪﻗُﻮآ َوأُوﻟَـٰﺌ‬ َ ‫ﻳﻦ‬
َ ‫ﻚ ٱﻟ ﺬ‬ َ
Laysa albirra an tuwalloo wujoohakum qibala almashriqi waalmaghribi walakinna
albirra man amana biAllahi waalyawmi al-akhiri waalmala-ikati waalkitabi
waalnnabiyyeena waata almala AAala hubbihi thawee alqurba waalyatama
waalmasakeena waibna alssabeeli waalssa-ileena wafee alrriqabi waaqama
alssalata waata alzzakata waalmoofoona biAAahdihim idha AAahadoo
waalssabireena fee alba/sa-i waaldhdharra-i waheena alba/si ola-ika alladheena
sadaqoo waola-ika humu almuttaqoona(Surat Al Baqara 2:177).

Tafsir: Si Ucha Mungu Kua ni kelekeza Uso wenu Kibla cha Mashariki na Magharibi.
Lakini Ucha Mungu (Ni Sifa ya yule) Anaemuamini Allah na Siku ya Mwisho Na
Malaika Wake, Na Vitabu Vyake na Manabii wake. Na Kutoa Mali yake anayoipenda
juu yake. Kwa Watu Wake wa Karibu. Na kwa Mayatima na Masikini. Na Kwa
Wasafiri Na Kwa Wenye Kuomba (kwa Shida) na Kuwaachia Huru Watumwa (kwa
kuwalipia). Na Kusali na Kutoa Zaka na Kutekeleza Ahadi zao Wanapozitoa na Wenye
Subra katika Wakati wa Njaa na Katika Wakati Maradhi na Vita Hao Ndio Miongoni
mwa Waliosadiki na Hao Ndio wenye Taqwa.

Ambapo anasema Hujjat Ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Ibn Muhammad
Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali kuhusiana na aya hii kua: ‘Qur’an ina aya
zenye Hazina na zenye Lulu ndani yake. Hazina hua ni zile aya ambazo hua ni zenye
kuelezea Sifa na Majina Matukufu ya Allah Subhnaha wa Ta’ala na Uwezo wake
ambazo ziko aya 763. Na Lulu hua ni zile aya ambazo zenye kuainisha Njia
Iliyonyooka na aya zinazohimiza Kuifuata Njia hio na hizi zio aya 741.’
314

Hivyo Aya hii ya Surat Al Baqara 2:177 ni moja kati ya Aya 46 za Sura hio ambazo ni
zeney sifa ya kua ni Lulu Miongoni mwa Lulu za Qur’an, kwa upande mwegine basi ayah
hii inajulikana pia kama Minna Al Abwab Al Birr yaani Miongoni mwa zinazoainisha
Milango Ya Ucha Mungu, kwani inazungumzia sifa za Ucha Mungu kua si Kusali tu
bali ndani yake Ucha Mungu Mnajumuishwa Sifa za yule Anaemuamini Allah
Subhanah wa Ta’ala na Siku ya Mwisho Na Malaika Wake, Na Vitabu Vyake na
Manabii wake.

Na mwenye Kutoa Mali yake aliyokua na mapenzi makubwa sana juu yake kwa
kuwapa kwa kuwasaidia Watu wake wa karibu, Mayatima na Masikini. Na
kuwasaidia kwa kuwakirimu Wasafiri wenye shida na kuwasaidia wenye kuomba
msaada kutokana na ugumu wa shida walizokua nazo na kuwalipia fidia Wafungwa
na Watumwa ili wawe huru na Kusali na Kutoa Zaka na kutekeleza ahadi zao
wanapozitoa na Wenye Subra katika wakati wa njaa na katika wakati wa maradhi
na Vita. Hao ndio miongoni mwa waliosadiki na hao ndio wenye Taqwa.

Hivyo ndani yake ayah hii ndani yake mna sifa ambazo kila mmoja wetu anatakiwa
ajitathmini nazo na kuangalia juu yake kua kama anazo ama la, na kama hana basi inabidi
azipiganie ili awe nazo kwani aya inaweka wazi kua Uislam si Kusali tu, ambapo
kuhusiana na Masikini basi amesema Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu kua amesema:
‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: Masikini hua si yule ambae anapita
akiomba omba watu na kisha akapewa Tende mbili tatu, bali ni yule ambae
asiebainisha hali yake na ili watu wasimjue na kutaka kumsaidia’ (Bukhari na
Muslim).

Na amesema tena Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Mkono wenye Kutoa ni
bora kuliko Mkono wenye Kupokea, hivyo anzeni kuwapa wale wanaokutegemeeni.
Na Malengo ya Sadaqa ni kwa kile kinachotolewa na yule alienacho. Na yeyote yule
atakaejizua Kuomba basi Allah Subhanah wa Ta’ala atamruzuku na kumhifadhi
kutokana na Kuomba, na kumfanya yeye kua ni mwenye kujitosheleza.’ (Sahih
Muslim).

Ama kuhisiana na kujaribiwa kwa Maradhi basi amesema Imam Abu Abd Allah
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi kua amesema Abu
Hurayra Radhi Allahu Anhu kua amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:
‘Amesema Allah Subhanah wa Ta’ala kua: ‘Nnapomjaribu mmoja kati ya Waja
wangu kwa Maradhi na akawa si mwenye kulalamika basi hua nambadilishia
Nyama yake kwa Nyama bora zaidi, na Damu yake kwa damu bora zaidi. Hivyo
kama nikimjaalia Kifo basi hua ni mwenye kuingia kwenye Rehma zangu na kama
nikimjaalia kupona basi hua asiekua na Dhambi.’ Na Akaulizwa: ‘Jee ni katika hali
gani Nyama kuukuu inakua bora zaidi?’ Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Kwa
kumpa Nyama isiyokua na Dhambi.’ Na akaulizwa: ‘Jee ni katika hali gani Damu
315

inakua Mpya?’ Allah Subhanah wa Ta’ala akajibu: ‘Kwa kumpa Damu ambayo
haina Dhambi’’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta'ala aliamua kuwaadhibu watu wa Nabii Lut kwa makosa
yao ya kuingiliana kinyume na Maumbile tu, lakini pia ikiwemo Ushirikina na kutokata
kuwasaidia wenye shida na pia Kukatisha Njia kutokana na Ubaya wa Madhara yake

Kwani tunaona kua aya yetu imetumia neno Ibn Al Sabili yaani Mtoto wa Njiani, hii
haimaanishi Omba omba bali inamaanisha yaani Msafiri, Mtu Aliekwama Safarini au
Mtu aliesafarini kutoka sehemu moja kuelekea sehemu nyengine ambayo iko mbali na
Nyumbani Ambapo tunapoiangalia Qur’an basi tunaona kua Neno Ibn Al Sabiili
limetumika mara 9 katika Qur'an ambapo mara 8 kati yao zikiwa ni katika katika Kutilia
Mkazo Vitendo ambavyo vinahesabiwa kua ni kua na Ucha Mungu.

Hivyo basi kuwasaidia Wasafiri waliokua mbali na nyumbani kwao kutokana na


Matatizo ya Safari waliokua mbali na nyumbani kwao Kutokana na Matatizo ya Safari
basi hua ni sehemu ya Ucha Mungu na ni sehemu ya kua na Imani ya Ndani ya Dini ya
Kiislam.

Hata kama Msafiri huyo akiwa ni tajiri katika Mji wao basi kama ikiwa yuko safarini na
ana matatizo basi ni Wajibu wa Waislam Kumsaidia. Na ikiwa ni wajibu kwa Muislam
kumsaidia Msafiri basi hua ni wajibu kwake pia kutomsababishia Ibn Adam mwenzake
matatizo iwe anapokua katika safarini ama la. Na pia hua ni wajibu wa Muislam
kutomsababishia mwenzake kuingia katika hali ya kufikia kukimbia makazi yake na
kukimbilia sehemu nyengine.

Hivyo tunapozungumzia Watu wa Nabii Lut basi walikua pia ni wenye kufanya kila aina
ya Fahishatan ambapo neno Fahishatan limetokana na neno Fahusha ambalo kwa Lugha
ya Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Kuvuka Mipaka, Kuvuka hali ya kawaida katika
kufanya mambo Maovu yenye kutia Aibu, kufanya mambo ya Uasharati, Kufanya
mambo yasiyoingia akilini.

Neno Fahusha ndio lililotoa neno Fahishatan ambalo hua ni lenye kumaanisha
Kubainisha Tendo Ovu Wazi wazi, Kufanya Jambo la Aibu Lenye Kuonesha kua Mtu
Hana Heshima wala Adabu, Kutusi, Kuzini na pia humaanisha Kuingiliana Kinyume na
Maumbile.

Hivyo watu wa Nabii Lut wakawa ni wenye kuingiliana Wanaume kwa Wanaume,
Wenyeji kwa Wageni na pia kwa Wasafiri wapita njia wanaowateka. Hali hii iliendelea
mpaka Wanaume wakawa hawawataki Wake zao, hivyo Ibilisi nae akawavamia na
Wanawake nao kwa upande wao na akawafundisha namna ya kustareheshana wao kwa
wao.
316

Yaani Kifupi kila jambo ambalo linalojulikana kama Fahishatun ambalo linatokana na
Nafs Shahwaniyat - Nafsi ya Matamanio ya Kinyama yanayofanywa na Watu wa
Magharibi ambayo sasa hivi ndio wanasema kua ni haki za Kupendana Ibn Adam basi
asili yake ilikua ni kutoka kwa Watu wa Nabii Lut ambao nao walikua wakifanya wazi
wazi kama leo hii wanavyopigania Watu wa Magharibi kua mambo hayo yaruhusike na
kufanyika katika kila nchi katika wakati wetu.

Kwani kimaumbile kila kitu chenye Mwanzo basi hua na Mwisho wake pia, na kwa
viumbe basi hakuna kisichokua na Mwisho kwa sababu kila kitu kina mwanzo wake.

Ama tunapozungumzia kwa Upande wa Muumba basi bila ya shaka yeye Allah Subhanah
wa Ta'ala hana mwanzo na wala hana mwisho kwa sababu yeye ndie Muumba hivyo
hafanani na kitu chechote wala na yeyote.

Hivyo ikafika wakati ambao mwenyewe Muumba Allah Subhanah wa Ta'ala akaamua
kwa Makadirio na Huruma na Rehma zake kua imetosha kwa watu hao kufanya hayo
wafanyayo na kwa Hikma zake basi akaamua kuwatumia watu hao Mjumbe wake kwa
ajili ya Kuwaonya na kuwaongoza ili watote katika kiza hicho walichogubikwa na
Matamanio yao ya Nafsi yanayosimiwa na Ibilis mwenyewe.

Hiki kilikua ni kipindi ambacho Nabii Lut alikua akiishi na Nabii Ibrahim katika Maeneo
ya Al Quds Mjini Jerusalem nchini Falestina, katika kipindi hiki Nabii Lut alikua ni
Mkulima Hivyo siku moja wakati Nabii Lut alipokua Shambani akilima mara kwa mbali
akamuona kijana Mwanamme wa takriban miaka 20 ambae alikuja moja kwa moja
mpaka chini yake.

Kijana huyo akamsalimia Nabii Lut, ambae nae akitikia salama hio. Nabii akamuuliza
kwa kusema: ‘Ewe Kijana nikusaidie nini?’

Kijana huyo akasema: 'Ya Lut! Hakika mimi ni Malaika Jibril Al Amin.'

Kwani baada ya Nabii Lut kusikia maneno hayo basi aliwacha shughuli zake za
Shambani na kumuangalia vizuri Kijana huyo asemayo maneno hayo, kisha baada ya
kuridhika na kutafakkar basi akauliza: ‘Naam, Jee ni kitu gani kichokuleta kwangu
mimi ewe Jibril Al Amin!’

Malaika Jibril akasema: ‘Ya Lut! Hakika mimi nimekuja kukupa Salam kutoka kwa
Mola wako, ambae anasema Ewe Lut nenda katika Miji iliyopo kwenye Njia Kuu,
kisha wausie kua waache kufanya Fahishatan. Watangazie kua Hakuna Mola
anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokua Allah na wewe Lut ni Mjumbe wake
Kwao wao’
317

Hapa hali ya Muonekano wa Uso wa Nabii Lut ulibadilika na kusawijika ghafla moja
mara tu baada ya kusikia Maneno hayo kutoka kwa Malaika Jibril.

Kisha Nabii Lut akasema: ‘Kwa Hakika Hakuna Mola anaestahiki kuabudiwa
Isipokua Allah Subhanah wa Ta'ala, na bila ya shaka hakuma M-bora zaidi yake na
pia Hakuna Msaidizi bora kama yeye Allah Subhanah wa Ta'ala’

Kisha akaagana na Malaika Jibril, Nabii Lut akawacha shughuli yake ya Kulima na
akarudi hadi Nyumbani kwa Nabii Ibrahim, alipofika akampa habari hio kwa kusema:
"Ewe Ami yangu Hakika Mimi nimeshukiwa na Malaika Jibril na amenitangazia
kua mimi ni Nabii alietumwa kwa Watu Wabaya na Waovu kabisa kuliko wote"

Nabii Ibrahim akauliza: "Kwa Watu Gani hao?"

Nabii Lut akasema: "Watu wa Miji ya Barabara kuu"

Nabii Ibrahim akamwambia Nabii Lut: "Ya Lut! Sujudu Umshukuru Mola wako na
Kisha tekeleza Jukumu lako alilokupa Mola wako!"

Nabii Lut akasjudu akamshukuru Allah Subhanah wa Ta'ala na kisha baada ya hapo
akajitayarisha kwa ajili ya Safari ya kuelekea katika Ardhi ya Miji iliyopo katika
Barabara Kuu na katika kipindi hiki basi Nabii Lut alikua tayaris ameshaoa, na alikua na
wake wawili ambao ni : Waila na Wahila.

Na alikua na Watoto Watatu wa Kike ambao ni:

Zughula.
Arthama na
Baqna.

Na alikua na Ngamia Mmoja ambae alikua akimwita kwa jina la Ra'da na pia alikua na
Mbwa mmoja ambae alikua akimwita Dina.

Kabla ya Kuendelea basi nilikua nataka kuweka wazi kitu kimoja, ambacho ni kuhusiana
na Huyu Mke wa Nabii Lut anaeitwa Wahila, Kwani kama tunakumbuka basi
tulipozungumzia Kisa cha Nabii Nuh tulisema kua Mke wake alieangamia alikua akiitwa
pia Wahila.

Kwani Nabii Lut akafunga safari kutoka katika Mji wa Jerusalem na kuelekea katika Miji
iliyopo katika Barabara kuu, ambayo ni masafa ya kilomita 100 kutoka Jerusalem.
318

Na bila ya shaka Nabii Lut aliwachukua Wake zake hao wawili na Mabint zake watatu
na Ngamia wake na Mbwa wake huku akiwa ni mwenye kushindikizwa na Nabii Ibrahim
mpaka alipotoka katika Mipaka ya Jerusalem kisha Nabii Ibrahim akaomba dua kwa
Allah Subhanah wa Ta'ala kwa kusema: ‘Ya Allah! Hakika wewe unajua kua Lut ni
Utulivu Nafsi yangu na ni Faraja kwangu na pia ni msaidizi katika kutekeleza
Majukumu yangu. Nami nampenda sana kama vile anavyonipenda yeye. Hivyo Ya
Allah! Nakukabidhi Lut muweke ndani uangalizi wako, aende kama
ulivyomuamrisha nan a kuomba kua umrudishe salama baada ya ya kutimiza
majukumu yake uliyompa’

Kisha Baada ya Hapo Nabii Ibrahim akamkumbatia Nabii Lut na kisha akaagana na
familia ya Nabii Lut ambao nao wakaendelea na safari na Nabii Ibrahim akarudi
Nyumbani.

Nabii Lut na Familia yake walipokaribia karibu na Mipaka ya Mji wa Ghumura


(Gomorah) kabla ya kuingia ndani ya Mji huo basi Akashuka Malaika Jibril na
kumwambia Nabii Lut kua asiingie ndani ya Mji huo kwanza. Kwani kwake yeye ni Bora
kwanza kukaa nje ya Mji huo kabla ya Kuingia ndani yake.

Hivyo Nabii Lut na Familia yake wakapiga Kambi nje ya Mji huo, kwani haukuchukua
mda mrefu isipokua watu wa Mji wa Ghumura waliokaa juu minarani kupiga Doria
wakaliona Hema la Familia ya Nabii Lut. Hivyo wakaamua kutuma watu kuenda
kuangalia ni nani aliepiga kambi katika eneo hilo.

Na bila ya shaka walipomuona Nabii Lut na familia yake basi wakafurahi sana watu hao
kutokana na kuona kua tayari wameshapa vitu vipya. Hivyo wakarudisha habari katika
Mji wao na kuchaguana kwa ajili ya kuja kumkamata Nabii Lut na Familia yake.

Lakini walipojitayarisha na kuja kumteka Nabii Lut basi Nabii akawaamrisha Wanyama
wake yaani Mbwa wake na Ngamia wake ambao walikua ni pia ni walinzi wake
wawavamie watu hao, hivyo wakaanza fujo kubwa sana Wanyama hao kiasi ya kua Watu
hao wa Mji wa Ghumura wakakimbia na kushindwa kumteka nyara Nabii Lut na familia
yake.

Habari zikafika kwa Mfalme Sadum kuhusiana na ujio wa Mtu aliepiga Kambi nje ya
Mji na familia yake na ingawa mtu huyo ni Mzuri lakini hasogeleki hata kidogo, baada
ya kupata habari hio basi Mfalme Sadum akamtuma Gurmuz ambae ni Waziri wake
Mkuu na kumwambia aende akamuangalie Mtu Huyo ni Nani na anataka nini na kwanini
akakaa Nje ya Mji. Hivyo Gurmuz akachukua Jeshi kubwa sana na Kuelekea kwa Nabii
Lut.
319

Kama tunakumbuka basi tulipoangalia kisa cha Nabii Nuh basi tulisema kua Jina lake
hasa lilikua ni Tashakkaur na tukasema kua aliitwa Nuh kwa sababu Neno Nuh
linatokana na neno Naha ambalo kwa Lugha ya Kiarabu hua ni lenye kumaanisha
Kulalamika kwa huzuni na unyenyekevu kwa sauti ya chini sana. Kwani hio ndio iliyokua
sifa ya Tashshakur yaani Nabii Nuh alikua na na Unyenyekevu sana katika kumuomba
Mola wake huku akilalamika kwa sauti ya chini sana.

Na pia tulisema pia kua Nabii Lut ameitwa Lut kwa sababu jina hilo linatokana na neno
Latta Ambalo kwa Kiarabu hua ni lenye kumaanisha ya Mtu mwenye kumpenda sana
mtu mwengine kiasi ya kua anamuweka sana akilini na mawazoni na hivyo hawezi
kukosana nae mtu huyo ampendae na Nabii Lut alikua akimpenda sana Nabii Ibrahim
ambapo na Nabii Ibrahim alikua akimpenda sana pia Nabii Lut.

Kwa hivyo basi bila ya shaka Nabii Lut atakua nae pia alikua ana jina jengine, ila jee ni
jina gani hilo?

Hivyo tutapata jibu la suali hili baada ya kuangalia kile kilochotokea baada ya Nabii Lut
kuwasili kwenye mipaka ya mji wa Ghumura na kisha Mfalme Sadum kumtuma Gurmuz
ambae ni Waziri Mkuu aende akafuatilie jee mtu huyo ni nani na kwanini akapiga kambi
nje ya Mji. Hivyo Gurmuz akatoka na jeshi lake hadi kwa Nabii Lut, na alipofika kwa
Nabii Lut basi akaomba ruhusa ya kuzungumza nae.

Hivyo Gurmuz baada ya kumsalimia Nabii Lut basi akajitambulisha jina lake kua ni
Gurmuz na ni Waziri Mkuu wa Mfalme Sadum ambae ndie Mtawala wa eneo la Ardhi
hio ya Miji iliyopo barabara kuu, kisha baada ya hapo Gurmuz akamuuliza Nabii Lut:
‘Hivi wewe unaitwa nani?’

Na bila ya kusita basi Nabii Lut akajibu: ‘Mimi Naitwa Abd Allah.’

Gurmuz akasema: ‘Naam..Ewe Abd Allah! Hakika umekuja katika Miji yetu si kwa
ajili ya kututembelea na ndio maana ukakaa nje ya mipaka yake. Hivyo jee Ewe
Abd Allah! Umefuata nini kwenye Miji yetu?’

Nabii Lut akajibu: ‘Hakika mimi ni Mtume wa Allah Subhanah wa Ta’ala, hivyo
mwambie Mfalme wako kua nna ujumbe wake kutoka kwa Allah Subhanah wa
Ta’ala’

Hivyo Gurmuz akaondoka na Jeshi lake na kurudi kwa Mfalme Sadum. Lakini kabla
hajafika mbali basi Malaika Jibril akashuka na kumwambia Nabii Lut kua anasema Allah
Subhanah wa Ta’ala kua: ‘Ewe Lut nenda kwa Mfalme Sadum kakutane nae uso kwa
uso na kisha umpe ujumbe wangu kua asinishirikishe na kitu chochote na kua wewe
ni Mtume wangu kwao wao.’
320

Hivyo Nabii Lut akaondoka yeye na Mbwa wake na Ngamia na moja kwa moja akaelekea
kwa Mfalme Sadum huku Mbwa akiwa mbele yake na Ngamia wake akiwa Nyuma yake
kwa ajili ya kumpatia Ulinzi Nabii Lut na walipofika kwa Mfalme Sadum basi
akasalimiana nae na hapo Waziri Mkuu Gurmuz akamtambulisha Nabii Lut kwa Mfalme
Sadum kwa kumwambia kua huyu ndie yule Mtu aliepiga kambi nje ya Miji yao.

Mfalme Sadum akamuuliza Nabii Lut jina lake, ambapo Nabii Lut akajibu kwa kusema
kua ni Abd Allah.

Mfalme Sadum akauliza: 'Jee Jina lako lina maana gani?'

Nabii Lut akajibu: 'Maana yake ni Kua Mimi ni Mja wa Allah Subhanah wa Ta’ala'

Mfalme Sadum akauliza: 'Ewe Mja wa Allah Jee wewe ni Nani?'

Nabii Lut akajibu: ‘Mimi ni Nabii na Mtume wa Allah Subhanah wa Ta’ala’

Mfalme Sadum akauliza: ‘Nabii na Mtume wa Allah ndio maana yake nini?’

Nabii Lut akajibu: ‘Maana yake ni kua Mimi napokea Ujumbe kutoka kwa Allah
Subhanah wa Ta’ala na kisha Naufikisha kwa Nilioambiwa Niwafikishie Ujumbe
huo, kwa Mfano: Mimi Nimekuja kukupa Ujumbe wewe na watu wako kutoka Kwa
Allah Subhanah wa Ta'ala ambae ndie Muumba wa Kila Kitu, Anasema nikuambie
kua: Usimshirikishe kwani yeye hana Mshirika, Na Mimi ni Nabii na Mtume wake!’

Allah Subhanah wa Ta’ala anatuwekea wazi namna alivyokua na uwezo Mkubwa sana
juu ya viumbe wake na juu ya kila kitu na pia alivyokua na Wingi wa Huruma kwa
Viumbe wake na hivyo kila anapowaona kua wanapotoka basi na kumuasi basi anao
uwezo wa mkubwa sana kupita kiasi ya kuwaadhibu waasi hao tena kwa namna atakavyo,
lakini sasa Huruma zake Allah Subhnah wa Ta’ala hua ni zenye kupita ukubwa wa
Ghadhabu zake na ndio maana hua ni mwenye kuwapeleka Mitume viumbe wake ili
wawaongoze.

Lakini hata hivyo kama ilivyo kawaida ya Ibn Adam anaeumwa basi hua si kila anapewa
dawa basi hua ni mwenye kuzitumia dawa hizo ipasavyo na hivyo kunufaika nazo kwani
kuna baadhi hua ni wenye kuzipuuza na kuzitupa dawa hizo, na hii ndio hali waliyokua
nayo watu wa Nabii Lut, na wakazirembea badala yake kama zinavyoainisha aya kwa
kusema:
321

ِ ٍ ِ
َ َ‫ﲔ ۞ إِ ْذ ﻗ‬
‫ﺎل َﳍُْﻢ‬ َ ‫﴿ َوإِ ﱠن َرﺑﱠ‬
ْ َ‫ﻚ َﳍَُﻮ ٱﻟْ َﻌ ِﺰ ُﻳﺰ ٱﻟﱠﺮﺣ ُﻴﻢ ۞ َﻛ ﱠﺬﺑ‬
َ ‫ﺖ ﻗَـ ْﻮُم ﻟُﻮط ٱﻟْ ُﻤْﺮ َﺳﻠ‬
﴾‫ﻮن‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ وأَ ِﻃﻴﻌ‬ ِ ٌ ‫أَﺧﻮﻫﻢ ﻟُﻮ ٌط أَﻻ ﺗَـﺘﱠـ ُﻘﻮ َن ۞ إِِﱏ ﻟَ ُﻜﻢ رﺳ‬
ُ َ َ‫ﲔ ۞ ﻓَﭑﺗﱠـ ُﻘﻮاْ ﱠ‬ ٌ ‫ﻮل أَﻣ‬ َُ ْ ّ ُْ ُ
Wa-inna rabbaka lahuwa alAAazeezu alrraheemu, Kadhdhabat qawmu
lootin almursaleena, Idh qala lahum akhoohum lootun ala tattaqoona, Innee
lakum rasoolun ameenun, Faittaqoo Allaha waateeAAooni (Surat Ash Shuara
26:159-163)

Tafsir: Na kwa hakika Mola wako ni mwenye uwezo mkubwa sana na pia ni Mwingi
wa Huruma. Walikadhibisha watu wa Lut Mitume wetu. Wakati walipoambiwa na
Kaka yao Lut: ‘Jee hamumuogopi Allah na Kumtii’ Hakika mimi ni Mtume wa Kweli
juu yenu. Hivyo Muogopeni Allah na nitiini.

Mara baada ya kusikia Maneno hayo basi Mfalme Sadum akaona haya ya leo ni Mambo
mapya ambayo kamwe hakuwahi kuyasikia hapo kabla hivyo akamuuliza Nabii Lut kwa
kusema: ‘Haya unayoyasema ni Mapya na hakika mimi sijawahi kuyasikia, hivyo
labda nikuulize, Jee ni nani shahidi wako juu ya haya umayoyasema?’

Nabii Lut akasema: ‘Hakika mimi Mashahidi wangu ni hawa Wanyama wangu.’

Mfalme Sadum akashangaa na kuwaangalia watu wake ambao nao Walikua wanasikiliza
kwa Makini na kutoyaamini Masikio yao juu ya kile inayoyasikia.

Kisha Mfalme Sadum akauliza: ‘Hivi Tangu lini Wanyama Mbwa na Ngamia wakawa
ni wenye kutoa Ushahidi? Jee watatoaje Ushahidi wanyama hawa?’

Nabii Lut akatabasam kisha akajibu: ‘Wanyama hawa watatoa Ushahidi kwa
Kushuhudia kwao!’

Mfalme Sadum akaona naam tayari ameshapata hoja ya kumvunja nguvu Nabii Lut, kwa
kutumia silaha yake mwenyewe Nabii Lut hivyo akasema: 'Sawa Waambie Hao
Wanyama wako Washuhudie Mbele yetu nasi tuone!'

Nabii Lut akamgeukia Ngamia wake na kisha akasema: ‘Ewe Ra'da, Kwa Idhini ya
Allah kushuhudia juu ya nnayoyasema.’
322

Ra'da akasema: ‘Hakika Mimi nnashuhudia kua Hakuna Mungu anaestahiki


Kuabudiwa isipokua Allah Subhanah wa Ta'ala na wewe Nuh ni Nabii na Mtume
wake!’

Hapa Mfalme Sadum na Watu wote walio kwenye Baraza lake wakashangaa zaidi.

Na kisha Nabii Lut akamgeukia Mbwa wake na kusema: ‘Ewe Dina Kwa idhini ya
Allah juu ya haya nnayoyasema!’ Mbwa akasema: ‘Hakika mimi niko chini ya Amri
yako na nnashuhudia kua Hakuna Mungu anaestahiki kuabudiwa isipokua Allah
Subhanah wa Ta'ala na wewe Lut ni Nabii na Mtume wake!’

Subhanah Allah!

Kwani baada ya Miujiza hio, basi Mfalme Sadum akasimama na kisha akasema: ‘Hakika
Mimi sijawahi kuyaona haya hapo kabla labda kutoka kwa Wachawi! Au
mnayaonaje haya enyi Mawaziri wangu?’

Mawaziri wakasema: ‘Bila ya shaka Huyu Mtu ni miongoni mwa Wachawi!’

Hivyo mara baada ya Nabii Lut kumwambia Mfalme Sadum na Mawaziri wake
kuhusiana na Ujumbe wake, na kutoa vithibitisho vyake kupitia kwa Mashahidi wake
wawili ambao ni Ngamia na Mbwa walioshuhudia mbele ya watu hao kua hakuna Mola
anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokua Allah Subhanah wa Ta'ala

Basi Watu hao wakawa si wenye kumsikiliza na wakawa ni ni wenye kuanza kumfanyia
kejeli badala yake kama Allah Subhanah wa Ta’ala anavyotuelezea majibu ya watu hao
kwa kusema kua:

﴾‫ﻮﻫﻢ ِّﻣﻦ ﻗَـﺮﻳَﺘِ ُﻜﻢ إِﻧـﱠ ُﻬﻢ أ َُ�س ﻳَـﺘَﻄَ ﱠﻬﺮو َن‬ ‫ﺟ‬ ِ
‫ﺮ‬ ‫َﺧ‬‫أ‬ ‫ا‬
ْ‫ﻮ‬ۤ ُ‫﴿وﻣﺎ ﻛﺎن ﺟﻮاب ﻗـﻮِﻣ ِﻪ إِﻻﱠ أَن ﻗﺎﻟ‬
ُ ٌ ْ ْ ْ ْ ُ ُ ْ َ َْ َ ََ َ َ ََ
Wama kana jawaba qawmihi illa an qaloo akhrijoohum min qaryatikum innahum
onasun yatatahharoona (Surat Al Araf 7:82)

Tafsir: Na halikua jawabu la watu wake hao isipokua ni kusema kua: ‘Mfukuzeni
kutoka katika Miji yenu kwani wao ni watu wanaotaka kua Wasafi.’’

Mfalme Sadum akasema: ‘Ewe Abd Allah! Hakika wewe ni Mchawi, hivyo
usitufanyie mambo ya kichawi kisha ukatuambia kua tuachane na Miungu wetu
bora tuambie tu unataka nini ili tukupe kisha uachane nasi, kwani kama unataka
pesa basi tutakupa za kukutosha wewe na Ukoo wako wote.’
323

Na bila ya shaka hapa hatumzungumzii Mtu yeyote bali tunamzungumzia Nabiyyu Allahi
Lut ambae sifa zake ni kama walivyo Manabii na Mitume wengine, wanapopewa hoja
kama hizo, hua hawajibu vyovyote isipokua husema kama anavyosema Allah Subhanah
wa Ta'ala katika Qur'an:

ِ ِِ
﴾‫ﲔ‬ ِّ ‫ى إِﻻﱠ َﻋﻠَ ٰﻰ َر‬
َ ‫ب ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬ ْ ‫َﺟ ٍﺮ إِ ْن أ‬
َ ‫َﺟ ِﺮ‬ ْ ‫﴿ َوَﻣﺂ أ‬
ْ ‫َﺳﺄَﻟُ ُﻜ ْﻢ َﻋﻠَْﻴﻪ ﻣ ْﻦ أ‬
Wama as-alukum AAalayhi min ajrin in ajriya illa AAala rabbi alAAalameena
(Surat Ash Shuara 26:164)

Tafsir: Na mimi siombi kutoka kwenu nyie Ujira (Malipo), kwani kwa
hakika haupatikani Ujira wangu isipokua kutoka kwa Mola wa Ulimwengu Mzima.

Hapa kama tunavyoona aya zinatuwekea wazi kua Nabii Lut kwanza aliwausia watu
wake hao wa Miji mitano ya Admuta, Ghamura (Gomorrah), Sabura, Sadum (Sodom) na
Saghura kua Wawache kumshirikisha Mola wao, na wakati huo huo wamuamini yeye
kua ni Mtume alietumwa kwa ajili ya kuwaokoa wao kutokana na upotovu wao.

Na hii ni kabla ya kuwausia kuhusiana na Madhambi yao mengine na hivyo aya


zinatuonesha Uzito wa Dhambi ya Kufuru ya Kumshirikisha Allah Subhanah wa Ta'ala
kua haina Mfano wake katika Kutokukubalika kwake Abadan!

Ama kwa upande mwegine basi tunapoziangalia aya hizi za Surat Ash Shuara, ambapo
kwa mtizamo wa Bahr ul Ilm Sayyidna Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi
yeye anasema kua: ‘Surat Ash Shuara ni Sura ambao iliteremshwa katika kipindi cha
Kati kati cha Uislam wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipokua katika
mji wa Makkah. Kwani Surat Ash Shuara imeteremshwa baada ya kuteremshwa
Surat Ta-Ha kisha ikafuatia Surat Al Waqiah na kisha ndio ikafuatia Surat Ash
Shuara’

Kwani tunazungumzia kipindi ambacho hata Sayyidna Umar Ibn Al Khattab Radhi
Allahu Anhu alikua hajasilimu bado, kama tutakavyoona hapo tutakapoangalia kisa cha
Nabii Musa ambapo Sayyidna Umar Al Khattab ni Mtu wa 40 kuingia katika Uislam.
Hivyo hii inatuonesha kua Surat Ash Shuara ilishushwa katika kipindi cha mwanzoni
mwa Uislam kwani kipindi hicho ilikua Hawajafikia bado hata Waislam 40.

Tunapoiangalia Surat Ash Shuara basi tunaona kua ilishushwa kwa ajili ya kumtia nguvu
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na ndio maana ndani yake : Wamezungumziwa
Mitume wengi sana wakiwemo Nabii Nuh, Nabii Hud, Nabii Saleh Nabii Ibrahim, Nabii
324

Musa na Harun, Nabii Shuaib na Nabii Lut mwenyewe ambae ndie tunamzungumzia
katika kisa chetu tulichokua nacho sasa hivi.

Na bila ya shaka Surat Ash Shuara ni Miongoni mwa Sura ambazo zimekariri kwa
kurudia rudia baadhi ya aya ndani yake zenye ujumbe wa Mitume hao waliotangulia
kabla ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam pale walipokua hawakuaminiwa na
Wafuasi wao, na hali hii pia ilimkuta Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika
kipindi cha Mwanzoni cha Utume wake, hivyo watu wao hao kutokana na ujinga wao
walikua tayari kuwalipa Mitume hao wa Allah Subhanah wa Ta'ala kila kitu wakitakacho
ili tu wawachie Watu hao wandelee na Maovu yao na hivyo Mitume hao walikua ni
wenye kujibu:

ِ ِِ
﴾‫ﲔ‬ ِّ ‫ى إِﻻﱠ َﻋﻠَ ٰﻰ َر‬
َ ‫ب ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬ ْ ‫َﺟ ٍﺮ إِ ْن أ‬
َ ‫َﺟ ِﺮ‬ ْ ‫﴿ َوَﻣﺂ أ‬
ْ ‫َﺳﺄَﻟُ ُﻜ ْﻢ َﻋﻠَْﻴﻪ ﻣ ْﻦ أ‬
Wama as-alukum AAalayhi min ajrin in ajriya illa AAala rabbi alAAalameena
(Surat Ash Shuara 26:164)
Tafsir: Na mimi siombi kutoka kwenu nyie Ujira (Malipo), kwani kwa
hakika haupatikani Ujira wangu isipokua kutoka kwa Mola wa Ulimwengu Mzima.

Kwani maneno ya aya hio ambayo ni miongoni mwa aya zilizofanyiwa Takrir (kurudiwa
rudiwa) yana ujumbe mkubwa sana kwa kila mwenye kutafakkari hususan katika
Ulimwengu wa leo ambao kila mtu anafikiria Malipo ya Pesa kwanza katika kila kitu
afanyacho kabla ya kitu chochote kile basi kwanza ni Pesa.

Huu ni Mtihani mkubwa sana na unaosikitisha, kwani kwa Ujinga wa kupenda Malipo
ya pesa katika kila kitu hapa ulimwenguni basi mwishoni wa uhai wake mtu atajikuta
hana kitu ingawa alifanya Mema mengi sana. Na hivyo atakua ni miongoni mwa
Waliokula Hasara kesho Akhera. Allah atunusuru na kua ni Miongoni mwa waliokula
hasara...Aamiin ya Allah!

Kwa upande mwengine basi Surat Ash Shuara ilikua pia ikimuonesha Njia Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam wakati alipokua katika kipindi hiki kigumu cha kuwausia
watu wake wamuabudu Allah Subhanah wa Ta'ala na wamkubali yeye kua ni Mtume
wake juu yao, kwa kuwajenga Imani yao watu wa Makkah na kisha baada ya hapo ndio
yakafuatia Maamrisho na Makatazo ya Dini ya Allah Subhanah wa Ta'ala kupitia katika
Shariah zake Allah Subhanah wa Ta'ala na Sunnah zake Rasul Allah Salallahu Alayhi
wa Salam.

Yaani Allah Subhanah wa Ta'ala katika aya hizi za Surat Ash Shuara anamuwekea wazi
Rasul Allah Aalayhi wa Salam kua Walikuja Mitume waliotangulia kabla yako na
325

wakauwausia watu wao kua Wasimshirikishe Allah Subhanah wa Ta'ala na pia kuwataka
watu hao wawaamini Mitume hao. Na kisha baada ya hapo mbali ya kua ni wenye
Kupigwa vita lakini Mitume hao hawakusita bali waliendelea kua ni wenye
kuwabainishia Watu hao makosa yao Mengine zaidi ya kumshirikisha Allah Subhanah
wa Ta'ala.

Hivyo baada ya Nabii Lut kuwabainishia watu wake ujumbe wake huo na kisha
wakaukataa ujumbe wake wa kutomshirikisha Allah Subhanah wa Ta'ala. Hivyo nae
akaona bora amalizie na yale mengineyo maovu yasiyokubalika wayafanyayo watu hao
kwa kusema:

﴾‫ﺎل وﺗَـ ْﻘﻄَﻌُﻮ َن ٱﻟ ﱠﺴﺒِﻴﻞ و َﺄﺗْﺗُﻮ َن ِﰱ َ� ِدﻳ ُﻜﻢ ٱﻟْﻤْﻨ َﻜﺮ‬ ِ ‫﴿أَﺋِﻨﱠ ُﻜ ْﻢ ﻟَﺘَﺄْﺗُﻮ َن‬
َ ُ ُ ََ َ َ ‫ٱﻟﺮ َﺟ‬
ّ
A-innakum lata/toona alrrijala wataqtaAAoona alssabeela wata/toona fee
nadeekumu almunkara (Surat Al Anqabut 29:29)

Tafsir: Kwa Hakika Nyinyi Mnawafanyia sivyo Wanaume, na Mnakatisha Njia na


Kufanya Maovu katika Mikusanyiko yenu.

Haya ni maneno ya aya ambayo tumeshayaangalia hapo kabla, hivyo tuangalie na aya
nyengine ambayo yenye maneno yanaobainisha wazi yale ambayo Nabii Lut
aliowaambia watu hao wake kwa kusema:

‫ﲔ ۞ َوﺗَ َﺬ ُرو َن َﻣﺎ َﺧﻠَ َﻖ ﻟَ ُﻜ ْﻢ َرﺑﱡ ُﻜ ْﻢ ِّﻣ ْﻦ أ َْزَو ِاﺟ ُﻜ ْﻢ ﺑَ ْﻞ‬ ِ ِ


َ ‫﴿أ ََﺄﺗْﺗُﻮ َن ٱﻟ ﱡﺬ ْﻛَﺮا َن ﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬
﴾‫ﺎدو َن‬ُ ‫أَﻧﺘُ ْﻢ ﻗَـ ْﻮٌم َﻋ‬
Ata/toona aldhdhukrana mina alAAalameena, Watadharoona ma khalaqa lakum
rabbukum min azwajikum bal antum qawmun AAadoona (Surat Ash Shuara 26:165-
166)

Tafsir: Na Mnawaingilia wenye asili ya Kiume Miongoni mwa Walimwengu na


Mnawaacha aliekuumbieni Mola wenu. Kua miongoni mwa wake zenu. Hivyo Nyinyi
ni Watu wenye kuvuka Mipaka.

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Al Mushaqiqin Imam


Al Ghazali Al Thani Imam Fakhr Ad Din Al Razi Al Shafii kuhusiana na aya hizi kua:
‘Maana ya Maneno ya aya isemayo: Ata/toona aldhdhukrana mina alAAalameena
326

Na Mnawaingilia wenye asili ya Kiume Miongoni mwa Walimwengu yana maana


mbili zifuatazo:

1-Miongoni mwa Walimwengu basi nyinyi ndio peke yenu mfanyayo hayo.

2-Mmewachagua Walimwengu wa Kiume Kuwafanyia Dhambi hii.

Kisha Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi anaendelea kufafanua aya ya pili
inayofuatia baada ya hio ambayo inasema: ‘Watadharoona ma khalaqa lakum
rabbukum min azwajikum bal antum qawmun AAadoona yaani Na Mnawaacha
aliokuumbieni Mola wenu kua Miongoni mwa Wake zenu hivyo Nyinyi ni Watu
wenye kuvuka Mipaka. Kua yanamaanisha kua: ‘Watu wa Nabii Lut walikua pia
wanawaingilia Kinyume na Maumbile wake zao’’

Na huo pia ndio Mtizamo wa Jarrah Allah Imam Abu Qasim Mahmud Ibn Umar Ibn
Ahmad Al Zamakhshari, na pia ndio Mtizamo wa Imam Abu Jafar Muhammad Ibn Jariri
At Tabari Al Shafii, ambao wote hao wao wamenukuu mtizamo huo kutoka kwa Al
Mufassir Mujahid Ibn Sulayman.

Baada ya Nabii Lut kukamilisha kuainisha kwa kuwawekea wazi watu hao yale
aliyoamriwa Na Allah Subhanah wa Ta'ala kua awawekee wazi basi Mfalme Sadum na
Watu wake wakamjibu Nabii Lut kwa kusema:

﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ُ ‫﴿ﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻟَﺌِﻦ ﱠﱂْ ﺗَﻨﺘَ ِﻪ ٰﻳـﻠُﻮ‬


َ ‫ط ﻟَﺘَ ُﻜﻮﻧَ ﱠﻦ ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻤ ْﺨَﺮﺟ‬
Qaloo la-in lam tantahi ya lootu latakoonanna mina almukhrajeena (Surat Ash
Shuara 26:167)

Tafsir: Wakasema (watu hao) Na Kama Hujakoma Ewe Lut basi bila ya Shaka Utakua
ni Miongoni mwa Watakaofukuzwa

Na baada ya Nabii Lut kupewa Onyo kua kama hakukoma kuwausia basi atafukuzwa
kwenye Ardhi ya watu hao basi akanyanyua Mikono na Kumuuliza Mola wake Allah
Subhanah wa Ta'ala kwa kusema: ‘Ya Allah hakika watu hawa ni vigumu kwao
kunifaham mimi na kunisikiliza Wasia wangu juu yao, Jee nifanye Nini?’

Hapo akashuka Malaika Jibril na Wahyi usemao kua: ‘Ewe Lut! Anasema Allah
Subhanah wa Ta'ala kua Endelea kuwausia watu hawa kwa Muda wa Miaka 40,
Labda watakusikiliza na Kisha baada ya hapo kama hawajakusikiliza basi
tutapitisha kile inachobidi kiwapitie.’
327

Hivyo Nabii Lut akaondoka na kurudi kwenye familia yake, huku kila siku hua ni
mwenye kutoka kwenye Hema la familia yake na kuenda kuwausia watu wengine wa
Miji hio mmoja baada ya Mmoja kwa muda wa miaka 40. Kwani katika kipindi hicho
cha Miaka 40 basi hakuna hata mtu mmoja aliekubakia kufuata Wasia wa Nabii Lut juu
yake.

Na bila ya shaka Nabii Lut hakua ni Mwenye kuchoka katika kutaka kuwaokowa watu
wake hao kutokana Kiza cha Ujinga walichazama Ndani yake ambao nao ndio uliokua
ukipewalekea wao kuzama zaid kwenye Kufr, na ulipotimia mda wa miaka 39 basi Nabii
Lut akaamua kurudi tena kwa Mfalme Sadum mwenyewe ili kujaribu kumuusia kwa
mara ya mwisho, kwani huenda kusilim kwake kungepelekea kuepushwa kwa adhabu ya
watu hao.

Hivyo Nabii Lut akamwambia Mfalme Sadum: ‘Ewe Mfalme Sadum Muogope Mola
wako, ili uwe ni mwenye Kumuamini yeye tu na Kumuabudu, Nakuomba sema tu
Hakuna Mungu anaestahiki Kuabudiwa kwa Haki isipokua Allah Subhanah wa
Ta'ala na Lut ni Mtume wake.’

Ambapo Mfalme Sadum akakasirika na kumwambia Nabii Lut: ‘Hivi wewe Abd Allah
miaka yote hio Hujasahau tu kuhusiana na hii habari na wala hujachoka kuwausia
wati juu yake?’

Nabii Lut akajibu: ‘Ewe Mfalme Sadum hakika wewe hufaham kua Mimi Sikuja
hapa katika Miji yenu kwa ajili ya Matamanio ya Nafsi yangu au kwa Hiari yangu,
bali nimekuja kutokana na Maamrisho ya Mola wangu. Kwangu kama ingekua kwa
hiari yangu basi bila ya shaka mimi nisingefunga safari na Familia yangu kwa ajili
yenu abadan.’

Jibu hili la Nabii Lut lilimtia hasira zaidi Mfalme Sadum kwani linamaanisha kua wao ni
wenye kuendekeza Matamanio ya Nafsi zao, badala ya kufuata maamrisho ya Mola wao
Muumba. Hivyo Mfalme Sadum akamwambia Nabii Lut: ‘Ala! Kumbe unatekeleza
Amri ya Mola wako kwa sababu ya kumuogopa, haya tuoneshe basi hio adhabu ya
Mola wako ambayo wewe unaiogopa, tupate kuiona kama wewe ni Mkweli’

Allah Subhanah wa Ta'ala anatuelezea Majibu ya Mfalme Sadum na watu wake kwa
Nabii Lut pale aliposema katika aya ifuatayo:

﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ‫ٱﻪﻠﻟِ إِن ُﻛﻨﺖ ِﻣﻦ ٱﻟ ﱠ‬ ِ ‫﴿ﻓَﻤﺎ َﻛﺎ َن ﺟﻮاب ﻗَـﻮِﻣ ِﻪ إِﻻﱠ أَن ﻗَﺎﻟُﻮاْ ٱﺋْﺘِﻨَﺎ ﺑِﻌ َﺬ‬
َ ‫ﺼﺎدﻗ‬ َ َ ‫اب ﱠ‬ َ ْ َ ََ َ
328

Fama kana jawaba qawmihi illa an qaloo i/tina biAAadhabi Allahi in kunta mina
alssadiqeena (Surat Al Anqabuut 29:29)

Tafsir: Kisha Halikua jibu la Watu wake Isipokua walikua ni wenye kusema:
Tuletee Hio Adhabu Ya Allah (Huyo Mungu wako) kama wewe ni Mkweli

Hapa inabidi tufahamiane kua tunazungumzia hali ya Mtu ambae ameshawausia watu
kwa miaka 40, kila siku maneno hayo hayo lakini watu hao wamekua kama wanamuona
kua Nabii Lut ni mwenda wazimu, na kisha anawapa nafasi ya mwisho lakini watu hao
Wanamuonesha wazi Nabii Lut kua si chochote si lolote na hana uwezo wala nguvu
yeyote isipokua uchawi tu.

Hivyo hapa Nabii Lut akaona haina haja ya kuwausia na kuwaombea watu hawa, bora
wacha kiwafike lile nilichoamrishwa kuwaokoa nacho yaani Adhabu kali kutoka kwa
Mola wao. Hivyo basi Nabii Lut akanyanyua Mikono juu kisha akasema:

﴾‫ٱﻧﺼﺮِﱏ َﻋﻠَﻰ ٱﻟْ َﻘﻮِم ٱﻟْﻤ ْﻔ ِﺴ ِﺪﻳﻦ‬ ِّ ‫ﺎل َر‬


َ َ‫﴿ﻗ‬
َ ُ ْ ُْ ‫ب‬
Rabbi Unsurnii Aala Al Qawmin Al Mufsiddina.(Surat Al Anqabut 29:30).

Tafsir: Ewe Mola wangu Niokoe na Watu Mafisadi

Kwani tunaona kua aya hii yenye dua ya Nabii Lut dhidi ya watu wake inaonesha kua
anaomba kuokolewa dhidi ya Watu Mafisadi. Na ingawa wengi wetu tunatumia neno hili
lakini ni vizuri tulifafanue maana yake ili tupate kufaham maana ya aya tujue kwanini
Nabii Lut hakuomba kua anusuriwe na watu wafanyao Fahishatun bali ameomba
aokolewe na watu Mafisadi.

Ambapo neno Al Mufsidiina ni lenye kutokana na neno Fasada la Kiarabu ambalo hua
ni lenye kumaanisha Kua Muovu, Kuharibika, Kutofaa tena, Kutokua na Uwezo, Kua
Muovu, Kufanya Uovu au Machafuko Makubwa sana yaani kuondoa Kitu au Kuhamisha
Kitu kutoka katika hali yake ya kawaida na Kukitia kwenye hali ambayo kitu hicho
hakitofaa tena.

Na kwa upande wa Imam Muhammad Ibn Jarir At Tabari basi yeye anasema kuhusiana
na maana ya neno Fasada kua: ‘Kusababisha Machafuko ardhini kwa kutumia njia
yeyote ile ikiwemo vitisho, kutesa na nguvu katika kuvunja haki, sharia na heshima
za Ibn Adam.’
329

Hivyo Nabii Lut alikua akuomba dua aepukane na Watu ambao wamesababisha
Machafuko makubwa katika maisha ya watu wao na pia ya watu wengine kwa ujumla
kutokana na maovu yao na mara tu baada ya Nabii Lut Kuomba dua hio basi siku hio hio
usiku wake hivyo mara baada ya Nabii Lut Kuomba dua ya kutaka kuokolewa na
Mafisadi basi siku hio hio usiku wake Nabii Ibrahim alipolala akaona usingizini kua
Nabii Lut anajadiliana na Mtu mwengine lakini hajui alikua akijadiliana nae nini Mtu
huyo.

Nabii Ibrahim akashtuka sana na akaanza kuuulizia kuhusiana na Habari za Nabii Lut
kwa Wasafiri Lakini hakuweza kupata mtu wala jibu linaloridhisha kuhusiana nae. Hivyo
akaanza kuingiwa na khofu, na ingawa Nabii Ibrahim alikua anapenda wageni kutokana
na ukarimu wake lakini katika siku hio alikosa hamu ya kuwakirimu wageni.

Na Kukosa kwake wageni ikawa kama amekosa kutekeleza Jukumu lake la Kiimani
ambalo kwake yeye lilikua pia ni Wajib kwake. Hali hii hii ya Kukosa kualika Mgeni
katika eneo lake ikapelekea kukosekana Nyumbani kwake pia na kisha baada ya siku hio
basi akaendelea kukosa wageni nyumbani kwake kwa siku 10 mfululizo.

Ilipoingia siku ya 11 basi akaona la haiwezekani kustahamili kua Wageni sipati na na


hususan katika kipindi hiki ambacho nawahitaji sana ili niweze kupata habari za Lut.
Hivyo siku hio ya 11 Nabii Ibrahim akaamua kumuuliza Allah Subhanah wa Ta'ala:

"Ya Allah! Hivi mimi nimefanya kosa gani kwako na hivyo unaniadhibu kwa
kutonijaalia kutopata mgeni hata mmoja katika kipindi hiki?"

Ambapo Allah Subhanah wa Ta'ala akamjibu Nabii Ibrahim kupitia kwa Malaika Jibril
ambae alimhoji Nabii Ibrahim kwa kusema "Ya Ibrahim! Hakika Allah Subhanah wa
Ta'ala anakuuliza: Jee sie Mimi niliemlinda na kumhifadhi Lut hadi akawa pamoja
nawe?"

"Sasa ilikuaje wewe ukashindwa kuwakirimu Wageni katika siku ile Moja kwa ajili
ya Kua na Wasi wasi juu ya Lut?" Hivyo Nabii Ibrahim ikambidi aombe Msamaha
kwa Mola wake.

Na baada ya Kuomba Msamaha basi siku ya pili ambayo ni siku ya 12 basi Nabii Ibrahim
akapokea wageni ambao ndio wale Malaika tuliowazungumzia kwenye kisa Cha Nabii
Ibrahim walioleta habari ya kuzaliwa kwa Nabii Is'haq na kupitia kwake kuzaliwa Nabii
Yaqub.

Na kama tunakumbuka basi tulipozungumzia kisa cha Nabii Nuh nae pia alipewa
changamoto kama hio na alipoomba dua aokolewe basi akaambiwa apande Miti kwanza,
na kisha asubiri kwa mda wa miaka 40. Na kwa Nabii Ibrahim nae alipoomba dua ya
330

kuomba mtoto mwema basi alijibiwa baada ya miaka 80, na dua ya Mji wa Makkah kutoa
Mtume ilijibiwa baada ya Miaka zaidi ya 3000.

Na hapa kwa Nabii Lut tunaona kua anajibiwa Dua yake baada ya siku 11. Kwani kila
kitu anachokipanga Allah Subhanah wa Ta'ala hua anakipanga kwa Makadirio yaliyokua
bora kabisa kwa Manufaa bora ya Waja wake.

Hivyo baada ya kuomba Dua yake basi Malaika Jibril, Mikail na Israfil wakaja kwa ajili
ya Kutoa Majibu ya Dua ya Nabii Ibrahim aliyoiomba miaka 80 iliyopita ya kupata mtoto
mwema na pia Majibu ya Dua ya Nabii Lut ya ndani ya wiki 2. Hivyo baada ya Malaika
hao kumpa habari Nabii Ibrahim ya kupata mtoto basi akapewa pia habari ya Maangamizi
ya Watu wa Nabii Lut.

Na anasema Bahr Ul Ilm Abd Abdallah Ibn Abbas kua: Malaika hao Walimwambia Nabii
Ibrahim kua: ‘Hakika Sisi tutwaangamiza watu wa Miji hio’

Nabii Ibrahim akauliza: ‘Mtaangamiza vipi wakati Lut yumo ndani yake?’

Malaika wakasema: ‘Hakika Sisi tunajua nani na nani yumo ndani yake.’

Nabii Ibrahim akauliza: ‘Hivi jee mnaweza kuuangamiza mji ambao ndani yake mna
waumini 400?’

Malaika wakajibu: ‘La!’

Nabii Ibrahim akauliza: ‘Jee kama wangekuwemo Waumini 300?’

Malaika wakasema: ‘La!’

Nabii Ibrahim akauliza: ‘Jee kama wangekuwemo 200?’

Malaika wakajibu: ‘La!’

Nabii Ibrahima akauliza: ‘Kama wangekua Waumini 100?’

Malaika wakajibu: ‘La!’

Nabii Ibrahim akashuka na kuuliza mpaka ikafikia idadi ya Waumini 14.

Na Malaika wakajibu: ‘La!’


331

Kisha Malaika wakasema: ‘Ya Laiti kama Waumini wao wangefikia watano tu basi
bila ya shaka adhabu ingeondoloewa dhidi yao’.

Na kuna wanaosema kua Malaika hao walisema kua: ‘Ya laiti kama angeamini japo
mtu mmoja tu miongoni mwao basi adhabu hio ingeondolewa dhidi yao’

Na baada ya Nabii Ibrahim kupata habari hizi zilimhuzunisha sana na kuhoji kwa kuuliza
kua itakuaje, waangamizwe watu wa mji huo wakati ndani yake wamo watu
waliomuamini Allah Subhanah wa Taa’ala na ni wenye kumtii na kufanya Mema hivyo
Nabii Ibrahim akahoji huku akiwa na huzuni na khofu zaidi ya ile mara ya kwanza
alipowaona watu hao kua si wenye kula chakula chake kama inavyosema aya ifuatayo.

‫ﺖ ِﻣ َﻦ‬ ِ ِ ِ ِ َ َ‫﴿ﻗ‬
ْ َ‫ﺎل إِ ﱠن ﻓ َﻴﻬﺎ ﻟُﻮﻃﺎً ﻗَﺎﻟُﻮاْ َْﳓ ُﻦ أ َْﻋﻠَ ُﻢ ﲟَﻦ ﻓ َﻴﻬﺎ ﻟَﻨُـﻨَ ّﺠﻴَـﻨﱠﻪُ َوأ َْﻫﻠَﻪُ إِﻻﱠ ْٱﻣَﺮأَﺗَﻪُ َﻛﺎﻧ‬
﴾‫ٱﻟْﻐَﺎﺑِ ِﺮﻳﻦ‬
َ
Qala inna feeha lootan qaloo nahnu aAAlamu biman feeha lanunajjiyannahu
waahlahu illa imraatahu kanat mina alghabireena (Surat Al Anqabut 29:32)

Tafsir: Akasema (Ibrahim): ‘Lakini yumo Lut ndani yake (Mji huo)’. Nao wakasema:
‘Hakika sisi, tunajua zaidi ni nani aliemo ndani ya mji huo. Kwa hakika sisi
tutamuokoa yeye na familia yake. Isipokua Mke wake. Atakua ni miongoni mwa
watakaobakia na kuangamia’

Malaika wakajibu hoja za Nabii Ibrahim kwa kumuwekea wazi kua kutowaangamiza
watu wa Mji huo hua ni sawa na kuenda kinyume na maamrisho ya Allah Subhanah wa
Ta’ala na ndio maana Malaika wakasema kumwambia Nabi Ibrahim kua: ‘Hakika sisi
tunajua zaidi juu ya ni nani na nani waliomo ndani ya Mji huo’ yaani wakimaanisha
kua Allah Subhanah wa Ta’ala pamoja na wao waliotumwa kuifanya kazi hio wanajua
zaid yake Nabii Ibrahim, kwani tayari washaambiwa na Mola wao ni nini cha kufanya na
Allah Subhanah wa Taála alikua akijua kua Nabii Ibrahim kutokana na maumbile yake
basi atajaribu kuwaombea watu wa Nabii Lut hivyo akasema:

ِ ِ
‫اب ﻏَْﻴـُﺮ‬ َ ِّ‫ض َﻋ ْﻦ َﻫـٰ َﺬآ إِﻧﱠﻪُ ﻗَ ْﺪ َﺟﺂءَ أ َْﻣُﺮ َرﺑ‬
ٌ ‫ﻚ َوإِﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ آﺗﻴ ِﻬ ْﻢ َﻋ َﺬ‬ ْ ‫﴿ﻳٰـِﺈﺑْـَﺮاﻫ ُﻴﻢ أ َْﻋ ِﺮ‬
﴾‫ود‬ ٍ ‫ﻣﺮد‬
ُ َْ
332

Ya ibraheemu aAAridh AAan hadha innahu qad jaa amru rabbika wa-innahum
ateehim AAadhabun ghayru mardoodin (Surat Hud 11:76)

Tafsir: Ewe Ibrahim Achana nalo jambo hili, kwani kwa hakika inapita amri ya Mola
wako, kwa hakika itakuja adhabu juu yao ambayo haiwezekani kurudishwa

Hivyo Allah Subhanah wa Taála akaamua kumuwekea wazi Nabii Ibrahim kua mbali ya
kua yeye ni Khalili wake lakini juu ya majaaliwa ya watu wa Nabii Lut basi hakuna
kitakachoweza kuingilia kati na kupangua majaaliwa hayo, hivyo hali ikawa kama
tulivyoona katika kisa cha Nabii Nuh hapo awali pale Nabii Nuh alipomuombea Mtoto
wake, na akawekewa wazi kua huyo hakua ni miongoni mwa ndugu zake Kiimani.

Kisha baada ya hapo Malaika hao wakaanga na kutoka nyumbani kwa Nabii Ibrahim na
kuelekea katika kutekeleza Jukumu lao walilopewa na Mola wao kwa ajili ya Watu wa
Nabii Lut.

Ambapo anasema Imam Ismail Abd Rahman Al Suddi kua Malaika hao walipoondoka
kwa Nabii Ibrahim basi waliwasili kwa Nabii Lut katika kipindi cha wakati wa Mchana
na wakamkuta Bint wa Nabii Lut aitwae Zughula akiwa ni mwenye kuchota maji
kisimani kwa ajili ya familia yake. Ambapo Malaika hao Wakamsalimia Bint huyo na
kumuuliza kama katika maeneo hayo wanaweza kupata Nyumba ya kupumzikia wageni.

Zughula akajibu: ‘Naam ila inabidi msubiri kwanza niende nikaangalie, kisha
nitarudi na kukupeni jawabu linaloaminika zaidi.’

Kisha Zughula akaenda Kumwambia Nabii Lut kuhusiana na wageni hao kwani alikua
na Khofu kua wasije wakaonekana na watu wa Miji hio hivyo alipofika kwa baba yake
basi akasema: ‘Ewe Baba yangu kuna wageni wamekuja nimewaacha mbali kidogo
kwani naogopa watu wa Miji hii wasije wakawaona kisha wakakutia aibu kwa
sababu Wageni hao ni watu ambao uzuri wao sijawahi kuuona hapo kabla. Hivyo
bora nenda kawachukue haraka iwezekanavyo’

Na kulingana na Mtizamo wa Imam Ismail Abd Rahman Al Suddi basi yeye amesema
kua Malaika hawa kwanza walikutana na Bint Mkubwa wa Nabii Lut ambae nae
akampelekea Baba yake kuhusiana na wageni hao.

Lakini tunapoangalia kwa upande mwengine basi tunaona kua kulingana na Mtizamo wa
Qatadah Ibn Diama Al Sadusi kupitia kwa Hudhayfah Ibn Al Yaman Radhi Allahu Anhu
basi yeye anasema kua:
333

‘Allah Subhanah wa Ta'ala aliwaamrisha Malaika wake kwa kuwaambia kua:


Mtakapofika katika Mji wa Nabii Lut basi Msiwaangamize Watu wake hadi pale
Lut atakapothibitisha mara nne dhidi yao’

Hivyo Malaika hao walipofika katika Mji wa Nabii Lut wakakutana na Nabii Lut na
wakamwambia: ‘Hakika sisi tungependa kua Wageni wako katika usiku huu wa leo’

Hivyo Nabii Lut akaongozana nao Malaika hao kwa Mda wa saa moja kisha akawauliza:
‘Hivi nyinyi hamjawahi kusikia jambo lolote kuhusiana na Mji huu?’

Malaika wakauliza: ‘Kuhusiana na Nini?’

Nabii Lut akajibu: ‘Hakika mimi nnaapa kwa Mola wangu kua Watu wa Mji huu ni
Watu Waovu zaidi Ulimwenguni, kwani mimi sijawahi kuona Watu Waovu Kama
hawa kabla yao’

Na ukweli ni kua Nabii Lut: ‘Alirudia Kiapo hicho kinachothibitisha Maovu ya Watu
wake hao Mara nne’.

Na hivyo hii ndio ikawa Uthibitisho wa Nabii Lut wa mara Nne mfululizo walioambiwa
Malaika wasubiri uthibitisho wa mara nne kutoka kwa Nabii Lut.

Na hivyo walipowasili katika Nyumba yake Nabii Lut basi Nabii Lut akawakaribisha
huku akiwa ni mwenye kujua kua atakua na kazi kubwa na nzito sana ya kuwalinda Watu
hao kutokana na uzuri wa Sura zao na Maumbile yao dhidi ya watu wake.

Na pia atakua na kazi kubwa sana ya kugombana na Watu wake hao kwani watu walikua
ni wenye Kumzuia Nabii Lut asipokee Wageni kwa sababu ya Ucha Mungu wake na kwa
sababu ya kua ni mwenye kujitenga nao katika mambo yao maovu na kupingana nao.
Kwani Allah Subhanah wa Ta'ala anatuwekea wazi haya pale alipoelezea hali aliyokua
nayo Nabii Lut baada ya kuwapokea Malaika hao na kuwakaribisha Nyumbani kwake
kama zinavyosema aya:

﴾‫ﻴﺐ‬ ِ َ َ‫ﺎق ﻬﺑِِ ْﻢ ذَ ْرﻋﺎً َوﻗ‬ ِِ ۤ ِ


ٌ ‫ﺎل َﻫـٰ َﺬا ﻳَـ ْﻮٌم َﻋﺼ‬ َ‫ﺿ‬ ْ َ‫﴿ َوﻟَ ﱠﻤﺎ َﺟﺂء‬
َ ‫ت ُر ُﺳﻠُﻨَﺎ ﻟُﻮﻃﺎً ﺳﻲءَ ﻬﺑ ْﻢ َو‬
Walamma jaat rusuluna lootan see-a bihim wadhaqa bihim dharAAan waqala
hatha yawmun AAaseebun (Surat Hud 11:77)
334

Tafsir: Na walipokuja Wajumbe wetu kwa Lut akawa (Nabii Lut) ni mwenye Huzuni
na Wasiwasi juu ya Kudhuriwa kwao na akasema Hakika hii leo ni siku Nzito Sana
(Kimawazo)

Lakini hata hivyo Nabii Lut akawaambia Watoto wake hao wa kike.

‘Watayarishieni Chakula Wageni wapate Kula, Kwa sababu Watalala hapa na


kisha Itabidi Waongoke Alfajir kabla watu wa Mji Hawajaamka ili wasije
wakawaona na kisha wakaingia Matatizoni wageni hawa, na haitakiwi Watu wa
Miji hii kujua kuhusiana na Kuwasili kwa Ugeni huu katika Nyumba yetu.’

Na mpaka Nabii Lut anasema maneno haya na kutoa Onyo kua siri hio isitoke nje basi
alikua na hali kama aliyokua nayo Nabii Ibrahim baada ya kuwasili kwa wageni hao hapo
kwake yeye hapo kabla, yaani katika hali ya kutokujua kua Wageni hao si Ibn Adam bali
ni Malaika wa Allah Subhanah wa Ta'ala na ndio maana nae pia akaamrisha kua
waandiliwe Chakula.

Kwani mara baada ya Nabii Lut kuwataarifu watoto wake watayarishe chakula kwa ajili
ya wageni ambao watalala katika Nyumba yao na watakuja kuondoka alfajiri yake, na
kisha kuwaonya watu wa familia yake kua ugeni huo basi Wahila ambae ni mke wa Nabii
Lut aliekua Muasi kama alivyokua Wahila Mke wa Nabii Nuh kua ingawa alikua ni Mke
wa Mtume lakini alikua na sifa ya Upotovu, na kupingana na Mume wake kisiri siri na
hivyo akaangamia kwa unafiq wake.

Basi na Wahila wa Nabii Lut nae alitoka nje kimya kimya na kutangaza habari za kuwasili
kwa ugeni wa watu ambao uzuri wao hauna mfano wake ndani ya Nyumba ya Mume
wake yaani Nabii Lut.

Ama kuhusiana na namna alivyotangazia kuhusiana na Habari hii basi Wanazuoni


wametofautiana kwani kuna wanaosema kua alitoka nje na kutangaza kwa Majirani na
kuna wanaosema kua alikubalina nao Watu wanaopingana na Mumewe kua Wakija
wageni basi atawataarifu Watu hao kwa njia ya Kupanda Juu ya Ukuta wa Nyumba hio
katika sehemu ambayo ina kipaa cha Udongo na kisha kuwasha Moto, ambao huashiria
kua Kuna Wageni ndani ya Nyumba hio.

Na anasema Imam Abu Is-haq Ahmad Ibn Muhammad Ibn Ibrahim Al Thalabi kua:
‘Amesema Abu Hamza Al Thamali kua yeye amaeseikia kuhusiana na njia ambayo
Mke wa Nabii Lut alikua akitumia kuwapa habari ya kuja watu kwa Nabii Lut kua
kila wakija wageni kwake basj huwatuma Wafanyakazi wake na kuwaambia kua
waende kuwaambia watu hao yeye anahitaji Chumvi nyumbani kwake.’
335

Na hivyo kutokana na ujumbe huo basi Watu hao hua wanajua kua Wanaalikwa kwa ajili
ya kufanya maovu yanayopendwa na nafsi zao na hapa ndio unaona kwa nini vijana wa
siku hizi wakawa wanasema kua wanazamia chumvi hivyo kwa kila anaetumia maneno
hayo basi hua ni sawa na mwenye kufuata maneno ya Mke wa Nabii Lut alieangamia.

Ambapo anamalizia Imam Al Thalabi kutuambia kua Abu Hamza Al Thamali amesema
pia kua Mke huyu wa Nabii Lut yaani Wahila aligeuzwa kua Nguzo ya Chumvi kwa
sababu ya kuomba kwake Chumvi.

Ama kwa upande mwengine basi kuna wasemao kua Mke huyu wa Nabii Lut alikua ni
Mwenye kutoka nje na kisha kuwaambia Watu wa Nabii Lut wazi wazi kua: Kuna Ugeni
umekuja kwetu.

Na bila ya shaka mara tu baada ya Watu wa Nabii Lut kuona alama ya Moto kwenye
Nyumba ya Nabii Lut kutoka kwenye Minara yao ya kuangalia Mipaka ya Ardhi ya Nchi
yao ya Gumurah basi wakajua kua kwa Nabii Lut kuna Ugeni umewasili.

Kisha wakashuka na kusambaza habari juu ya ugeni huo yaani Watu hao walipopata
habari tu kua kwa Nabii Lut kuna Vijana wa Kiume Wazuri sana wamekuja basi kila mtu
aliacha kile alichokua akifanya na kukimbilia haraka sana kwa Nabii Lut kutokana na
kua na hamu ya kua yeye awe ndie Mtu wa Mwanzo kuwapata Vijana hao.

Hivyo ghafla Moja katika usiku huo kabla ya Chakula walichokua wanatayarishiwa
Malaika hao hakijawiva basi watu walikua washafika nje ya Nyumba ya Nabii Lut. Hapa
sasa Tafrani kubwa ikaanza, kwani yale aliyokua akiyakhofia Nabii Lut kua yatatokea
ndio yametokea, Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea haya pale aliposema:

ِ ‫﴿وﺟﺂءﻩ ﻗَـﻮﻣﻪ ﻳـﻬﺮﻋﻮ َن إِﻟَﻴ ِﻪ وِﻣﻦ ﻗَـﺒﻞ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳـﻌﻤﻠُﻮ َن ٱﻟ ﱠﺴﻴِﺌ‬


﴾‫ﺎت‬َّ َ َْ ُ ْ َ ْ ُ َ ْ ُ ُ ُ ْ َُ َ َ
Wajaahu qawmuhu yuhraAAoona ilayhi wamin qablu kanoo yaAAmaloona
alssayyi-ati(Surat Hud 11:78)

Tafsir: Na Wakaja Watu wake (Nabii Lut) Yuhra'Auna (wakiwa ni wenye kukimbilia)
kuelekea kwake na tangu Zamani walikua Wanafanya Madhambi (Hayo).

Hapa tuaona kua Aya yetu imetumia neno Yuhra'Auna ambalo ni lenye kutokana na neno
Hari'a ambalo kwa Lugha ya Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Kutembea kwa hatua za
Haraka Haraka, Kukimbilia, na pia humaanisha Kutiririka kwa Nguvu kubwa sana.
336

Ama kuhusiana na maana ya Neno Yuhra'una basi anasema Jarrah Allah Sultan Al
Balagha Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Neno Yuhra’auna Hua ni lenye
kumaanisha Kusukumwa na Nguvu fulani ili kukimbilia kitu fulani kutokana nan
a na hamu kubwa ya kitu hicho.’

Na kwa Upande wa Al Allamah Al Imam Muhammad Ibn Abd Allah Al Kisai basi yeye
anasema kua: ‘Neno Yuhra’una hua halitumiki katika kuelezea kitu chochote kile
isipokua katika hali ya kukimbilia kitu kutokana na kua na hamu kubwa ya
kukitamani kitu hicho.’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta'ala katika ayah anatuelezea hali ya hamu ya matamanio
waliyokua nayo watu wa Mji wa Nabii Lut baada ya kupata habari ya Ugeni uliowasili
Nyumbani kwa Nabii Lut, kiasi ya kua walimpelekea Nabii Lut kutoka nje ya Nyumba
yake ili kuwatuliza kabla hawajawa watu hao wengi Nyumbani kwake akashindwa
kuwatuliza na hivyo akatangazia kwa kusema:

ِ ‫ون ِﰱ ﺿﻴ‬
ِ ِ ِ ۤ ِ
‫ﺲ‬ ‫ﻴ‬َ‫ﻟ‬َ
َ ْ َْ‫أ‬ ‫ﻰ‬‫ﻔ‬ ‫ﺰ‬ ُ ًّ ْ ‫ﱠ‬ ‫ﻢ‬‫ﻜ‬ُ ‫ﻟ‬
َ ‫ﺮ‬‫ﻬ‬ْ‫ﻃ‬َ
ُْ َ َ َ ُ َ ْ ُ َ ‫ﺎل ٰﻳـ َﻘ ْﻮم َﻫـُٰﺆ ََ ُ ﱠ‬
‫ﲣ‬ ‫ﻻ‬‫و‬ ‫اﻪﻠﻟ‬ ‫ا‬‫ﻮ‬‫ﻘ‬ ‫ـ‬‫ﺗ‬ ‫ﺎ‬‫ﻓ‬ ‫أ‬ ‫ﻦ‬ ‫ﻫ‬ ‫ﻰ‬‫ﺎﺗ‬‫ﻨ‬ ‫ـ‬‫ﺑ‬ ‫ء‬ ‫ﻻ‬ َ َ‫﴿ﻗ‬
﴾‫ِﻣْﻨ ُﻜﻢ ر ُﺟﻞ ﱠرِﺷﻴ ٌﺪ‬
ٌ َْ
Qala ya qawmi haola-i banatee hunna atharu lakum faittaqoo Allaha wala
tukhzooni fee dhayfee alaysa minkum rajulun rasheedun (Surat Hud 11:78)

Tafsir: Akasema (Nabii Lut) Enyi Watu wangu, Hawa hapa Mabinti zangu Wako
Tohara kwa Ajili yenu (Kama mnataka Kuwaoa) Mcheni Allah na Wala
Msiniadhirishe mbele ya Wageni wangu Jee hakuna miongoni mwenu hata Mtu
alieongoka?

Kwani hapa tunaona kua Nabii Lut ametaja Mabinti wake, na hii haimaanishi kua yuko
Radhi kua Watoto wake wafanyiwe hivyo wanavyofanyiwa wengine la bali hapa Nabii
Lut alikua akimaanisha kuwaambia Watu wake kua Wanawake wa Ummah wake ni
Tohara kwao Wao watu hao, kwani amesema Allah Subhanah wa Ta’ala katika aya
ifuatayo katika kumuelezea Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:

ِ ِ ِ‫﴿ٱﻟﻨِﱠﱮ أَوَ ٰﱃ ﺑِﭑﻟْﻤ ْﺆِﻣﻨ‬


ْ ُ ‫ﲔ ﻣ ْﻦ أَﻧْـ ُﻔﺴ ِﻬ ْﻢ َوأ َْزَو‬
﴾ ‫اﺟﻪُ أُﱠﻣ َﻬﺎﺗُـ ُﻬﻢ‬ َ ُ ْ ‫ﱡ‬
Alnnabiyyu awla bialmu/mineena min anfusihim waazwajuhu
ommahatuhum (Surat Al Ahzab 33:6)
337

Tafsir: Nabii yuko karibu na Waumini wake kuliko Nafsi zao na wake zake (Mtume)
ni Mama zao (Waumini hao hivyo wawaheshimu na hawaruhusiki kuwaoa).

Kutokana na Mtizamo huo basi Nabii Nuh alikua akiwaambia watu wake kua Wanawake
wote wa Ummah wake ni Watoto wake. Hivyo basi Watu hao wakachukulia kauli hio
kama dhihaka kwani wanaona wanafanywa kama hawana akili na hawajulikani
wanachokitaka ni nini, hivyo nao wakajibu kua Hawana haja na Wanawake na kusema:

ِ
﴾‫ﻳﺪ‬ َ ‫ﻚ ِﻣ ْﻦ َﺣ ٍّﻖ َوإِﻧﱠ‬
ُ ‫ﻚ ﻟَﺘَـ ْﻌﻠَ ُﻢ َﻣﺎ ﻧُِﺮ‬ َ ِ‫ﺖ َﻣﺎ ﻟَﻨَﺎ ِﰱ ﺑـَﻨَﺎﺗ‬
َ ‫﴿ﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻟََﻘ ْﺪ َﻋﻠ ْﻤ‬
Qaloo laqad AAalimta ma lana fee banatika min haqqin wa-innaka lataAAlamu ma
nureedu (Surat Hud 11:79)

Tafsir: Kwa Hakika Unajua (Wewe Lut) Hatutaki kitu chochote kwa Mabinti zako na
Bila ya Shaka Wewe Unajua sisi tunataka nini (Surat Hud 11:79)

Ili kufaham vizuri Hali ilivyokua, basi jaribu kufikiria kua uko nyumbani kwako kisha
usiku huo wamefika wageni ambao watu wote wa maeneo unayoishi Wanawataka kwa
hamu kubwa sana Wageni wako hao Nawe umetoka nje kukabiliana na Watu hao wenye
Hali na Akili zilizoshuka chini kupita akili za Wanyama kutokana na Nguvu za Hisia za
Matamanio ya zao kwa Wageni wako, kwani ingawa Ibn Adam ameumbwa kwa umbo
lililo bora lililokamilika na kupewa Darja ya juu zaidi ya viumbe wote lakini hata hivyo
kutokana na ujinga wake wa kutoweza kudhibiti hisia zake za matamanio yake basi hua
ni mwenye kushuka katika darja ya chini zaidi ya walio chini kama zinavyosema aya:

﴾‫ﲔ‬ ِِ ۤ ِ ﴿
ْ ‫َﺣ َﺴ ِﻦ ﺗَـ ْﻘ ِﻮ ٍﱘ۞ﰒُﱠ َرَد ْد َ�ﻩُ أ‬
َ ‫َﺳ َﻔ َﻞ َﺳﺎﻓﻠ‬ ْ ‫ﻧﺴﺎ َن ِﰲ أ‬
َ ‫ﻟََﻘ ْﺪ َﺧﻠَ ْﻘﻨَﺎ ٱﻹ‬
Laqad khalaqna al-insana fee ahsani taqweemin; Thumma radadnahu asfala
safileena (Surat al Ala 95:4-5)

Tafsir: Kwa hakika tumemuumba Insan katika Taqwim bora kabisa. Na kisha
tukamshusha chini zaidi ya walio chini.

Na kama tulivyosema kua aya hii mbali ya kutumia neno Taqwim, na kusisitiza kua ni
Taqwim bora kabisa, neno Taqwim linatokana na mzizi wa neno Qa-Ma ambalo kwa
kiarabu lina maana ya kua katika hali ya Kusimama, Kua thabiti, Madhubuti, Kamilika,
sawia bila Kua na kasoro yeyote, kua na thamani, hali ya usimamizi, hali ya ulinzi, hali
338

ya mpangilio uliokamilika, hali ya mfumo kamili wa ufanyaji kazi wa umbo


lililokamilika n.k.

Na kisha aya zikatumia maneno mawili ambayo ni Asfala na Safilina ambayo ni yenye
kutokana na neno Safala ambalo kwa Lugha ya Kiarabu hua ni lenye kumaanisha
Kushuka chini, Kushuka Thamani, Kushuka Darja, Kutokua na Maana, Kutokua na
uwezo wa kutizamika kutokana na kua na hali ya udhalili mkubwa sana.

Hivyo aya zinatilia mkazo thamani ya Ibn Adam kimaumbile mbele ya Mola wake na pia
mbele ya Viumbe wengine ambao yeye Ibn Adam amepewa wadhifa wa kuwatawala na
kuwaweka chini yake pale anapokua anamkubali na kumtii Mola wake aliemuumba,
lakini hata hivyo hali ya ujinga wake ya kutotaka kumtii Mola wake basi hua ndio sababu
ya kushuka chini kwake.

Kwani Ahasan Taqwim alizojaaliwa Kiumbe Ibn Adam ameneemeshwa na Mola wake,
hivyo kama ataitumia ndivyo neema hizo basi Atakua Bora kama Mfalme na akitumia
sivyo basi atakua chini zaidi ya Mtumwa kama alivyosema Mujaddid Ad Din Hujjat ul
Islami Imam Al Shafii Al Thani, Az Zukhruf Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn
Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii kua: ‘Subra humfanya
Mtumwa hua Mfalme, na Matamanio ya Nafsi humfanya Malme kua Mtumwa’

Ambapo tunaona kua Watu wa Nabii Lut ingawa walikua na Ahsan Taqwim lakini
walishindwa kutumia neema ya Takwimi zao yaani kwa ajili ya kudhibiti Hisia za
Matamanio ya Nafsi zao na badala yake wakaziwachia na kua Watumwa wa hisia za
Matamanio ya Nafsi zao ambazo nazo zikawashusha Chini zaidi ya Walio chini na
kufanya Yasiyokua na maana waliyokua wakiyafanya.

Na matamanio hayo ya Nafsi zao yaliwapelekea kila mmoja miongoni mwao kua na
hamu ya kutaka kujishusha chini zaidi kwa kukimbilia kufanya dhambi. Na hamu hio
ndio iliyowapelekea kufika mbele ya Nyumba ya Nabii Lut na kuanza kumdai Nabii Lut
awatoe wageni waliowasili Nyumbani kwake.

Ya laiti watu hawa kama wangelijua na Nguvu za Mgeni Mmoja tu kati ya Wageni hao
Watatu ambao ni Malaika wa Allah Subhanah wa Ta'ala kwani tunapozungumzia
Viumbe Malaika basi bila ya shaka Malaika mmoja tu anaweza akaiangamiza Dunia
nzima ya wakati wetu kwa sekunde moja tu, ambayo ndio ina kila aina ya Silaha za Kisasa
ambazo hazijawahi kumuilikiwa na Vizazi vilivyotangulia hapo kabla katika historia ya
Dunia, sasa wacha mbali Dunia ya Wakati huo.

Hivyo madai ya watu hawa wa Nabii Lut kudai kwao kua wageni hao watolewe nje basi
ilikua ni kumuumiza kichwa zaidi Nabii Lut na hivyo Nabii Lut na kuzidishia uzito wa
339

Jukumu lake mbele ya Mola wake na hivyo akawa hana la kufanya isipokua kusema huku
akiwa ni mwenye huzuni na Majuto makubwa mbele ya watu hao katika kutomkubali
mitizamo yake kua:

ِ ِ ِ ِ َ َ‫﴿ﻗ‬
َ ‫ﺎل إِِّﱏ ﻟ َﻌ َﻤﻠ ُﻜ ْﻢ ّﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻘﺎﻟ‬
﴾‫ﲔ‬
Qala innee liAAamalikum mina alqaleena.(Surat Ash Shuara 26:168).

Tafsir: Akasema (Lut) Hakika juu ya mambo yenu basi mimi ninayapinga kwa chuki
kubwa sana.

Na kisha akaonesha wazi majuto yake na chuki juu ya mambo hayo na kutokua na uwezo
stahiki wa kukabiliana nayo, hivyo akamalizia kwa kusema:

ٍ ‫ﺎل ﻟَﻮ أَ ﱠن ِﱃ ﺑِ ُﻜﻢ ﻗُـ ﱠﻮةً أَو آ ِو ۤي إِ َ ٰﱃ رْﻛ ٍﻦ ﺷ ِﺪ‬


﴾‫ﻳﺪ‬ ﴿
َ ُ ْ ْ ْ َ َ‫ﻗ‬
Qala law anna lee bikum quwwatan aw awee ila ruknin shadeedin (Surat Hud 11:79)

Tafsir: Akasema Lau Kama ningekua na Nguvu Au ningekua na Msaidizi Mwenye


Nguvu kupingana nanyi

Nabii Lut aliyasema haya kuwatetea Wageni wake, bila ya kujua kua hao ndio Wasaidizi
wake na kasha akamalizia kwa kumgeukia mbora wa kumgeukia katika kuomba kila aina
ya msaada yaani Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kusema:

﴾‫ب ﱠِﳒِّﲎ وأ َْﻫﻠِﻰ ِﳑﱠﺎ ﻳَـ ْﻌﻤﻠُﻮ َن‬


ِّ ‫﴿ َر‬
َ َ
Rabbi najjinee waahlee mimma yaAAmaloona.(Surat Ash Shuara 26:169).

Tafsir: Ewe Mola wangu niokoe mimi na familia yangu kutokana na wanayoyafanya.

Ambapo alisema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua baada ya kusoma aya hizi
kua:

"Allah Muingize katika Rehma zake Kaka Yangu Lut ambae aliomba Msaada wa
Nguvu kutoka kwa Yule Mwenye Nguvu"
340

Wanasema Wanazuoni kulingana na aya hii kua, baada ya Nabii Lut basi Allah Subhanah
wa Ta'ala hakuwahi kutuma tena Mtume ispokua alimjaalia Mtume huyo kua na Nguvu
na Darja kwa ajilo ya Kukabiliana na Watu wake. Ambapo kwa Upande wa Bahr ul Ilm
Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye anatuelezea kile kilichofuatia baada
ya tukio hili kwa kusema:

‘Baada ya Hapo Lut aliufunga mlango wa Nyumba yake kwa nje huku Malaika
wakiwa ndani ili watu hao wasiingie ndani Malaika wakawa ni wenye kusikia
namna alivyokua na Hasira Nabii Lut na kuvunjika Moyo juu ya watu wake hao
wanaowataka kuwafanyia maovu wageni wake. Huku Watu hao nao wakiwa
wanaizunguka nyumba ya Nabii Lut kujaribu kutafuta sehemu yenye upenyo wa
kuingilia ndani.

Malaika hao wakamuonea huruma sana Nabii Lut na hivyo wakasema kumwambia Nabii
Lut: "Ewe Lut usiwe na Khofu wala huzuni kwani kwa hakika Usaidizi wako ni
wenye nguvu kubwa sana, na juu yao watu hao kuna adhabu kali ambayo
inawashukia na hawana njia ya kuiepuka" Kama zinavyosema aya kua:

ْ َ‫ﺎق ﻬﺑِِ ْﻢ َذ ْرﻋﺎً َوﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻻَ َﲣ‬


َ‫ﻒ َوﻻ‬ َ ‫ﺿ‬ ِِ ِ
َ ‫ت ُر ُﺳﻠُﻨَﺎ ﻟُﻮﻃﺎً ﺳﻲءَ ﻬﺑ ْﻢ َو‬ ْ َ‫﴿ َوﻟَ ﱠﻤﺂ أَن َﺟﺂء‬
﴾‫ﺖ ِﻣﻦ ٱﻟْﻐَﺎﺑِﺮﻳﻦ‬ َ َ‫ﻚ إِﻻﱠ ْٱﻣَﺮأَﺗ‬ َ ‫َْﲢَﺰ ْن إِ ﱠ� ُﻣﻨَ ﱡﺠ‬
َ َ ْ َ‫ﻚ َﻛﺎﻧ‬ َ َ‫ﻮك َوأ َْﻫﻠ‬
Walamma an jaat rusuluna lootan see-a bihim wadaqa bihim tharAAan waqaloo la
takhaf wala tahzan inna munajjooka waahlaka illa imraataka kanat mina
alghabireena (Surat Al Anqabut 29:33)

Tafsir: Na walipokuja Wajumbe wetu kwa Lut, akawa na huzuni na uzito kwa sababu
yao. Nao wakasema: ‘Usiwe na Khofu na wala usiwe na huzuni, kwani kwa hakika
sisi tutakuokoa wewe pamoja na familia yako, isipokua mke wako atakua ni miongoni
mwa watakaobakia.’

Hivyo Watu hawa wa Nabii Lut walikua hawawajui Watu waliokuwa wakiwataka, yaani
Malaika, na bila ya shaka hata kama wangetoka hao watu walio wataka watoke basi
wasingeweza kukabilian nao, na si wao tu bali hata sisi, kwani Nguvu na Uwezo wa
Viumbe Malaika ni Balaa Kubwa na Lenye kutisha sana.

Kwani mara baada ya Malaika kumpa ujumbe wake Nabii Lut basi wakamwambia Ingia
Ndani ewe Lut, na hapo Nabii Lut akaingia ndani ya Nyumba hio huku Watu nao wakiwa
341

nyuma yake kwa fujo. Hapo Malaika Jibril akasimama na kuomba ruhusa kwa Mola wake
awatie adabu watu hao, Allah Subhanah wa Ta'ala akampa ruhusa hio Malaika Jibril.

Basi hapo hapo ndani ya Nyumba hio kukabiliana na mlango wa nje kulitokea Mwangaza
mweupeeee! Mwangaza huo uliwapofua Macho watu wote ambao waliingia ndani ya
Nyumba ya Nabii Lut bila ya ruhusa na pia ukawapofua Macho wale waliokua nje na
kutaka kuingia ndani. Makelele ya Maumivu makali sana yaliyosikika hapo yalipelekea
hata wale waliokua na hamu ya Wageni wote kua ni wenye kutafuta njia ya Kukimbilia.

Ambapo Allah Subhanah wa Ta'ala anayaelezea haya katika Qur'an kwa kusema:

‫ﺿْﻴ ِﻔ ِﻪ ﻓَﻄَ َﻤ ْﺴﻨَﺂ أ َْﻋﻴُـﻨَـ ُﻬ ْﻢ‬


َ ‫۞وﻟََﻘ ْﺪ َر َاوُدوﻩُ َﻋﻦ‬ ِ ِ
َ ‫َوﻟََﻘ ْﺪ أَﻧ َﺬ َرُﻫ ْﻢ ﺑَﻄْ َﺸﺘَـﻨَﺎ ﻓَـﺘَ َﻤ َﺎرْواْ ﺑﭑﻟﻨﱡ ُﺬر‬
﴿
﴾‫اب ﱡﻣﺴﺘَ ِﻘﱞﺮ۞ﻓَ ُﺬوﻗُﻮاْ َﻋ َﺬ ِاﰉ وﻧُ ُﺬ ِر‬ ِ
َ ْ ٌ ‫ﺻﺒﱠ َﺤ ُﻬﻢ ﺑُ ْﻜَﺮًة َﻋ َﺬ‬ َ ‫۞وﻟََﻘ ْﺪ‬ َ ‫ﻓَ ُﺬوﻗُﻮاْ َﻋ َﺬ ِاﰉ َوﻧُ ُﺬر‬
Walaqad antharahum batshatana fatamaraw bialnnudhuri; Walaqad rawadoohu
AAan dhayfihi fatamasna aAAyunahum fadhooqoo AAadhabee wanudhuri;
Walaqad sabbahahum bukratan AAadhabun mustaqirrun; Fadhooqoo AAadhabee
wanudhuri(Surat Al Qamar 54:36-39)

Tafsir: Na Yeye (Lut) aliwaonya juu ya Adhabu yetu Lakini Walikua na shaka na Onyo
letu Na (hivyo watu hao) Wakataka Kumuadhirisha (Nabii Lut kwa kuwataka Wageni
wake) mbele ya Wageni wake Na tukayachukua Macho yao. (Tukawaambia) Onjeni
Adhabu Yangu Na Maonyo yangu. Na kwa hakika adhabu kali sana iliwavaa asubuhi
na mapema. Hivyo onjeni adhabu yangu na maonyo yangu.

Allahu Akbar! Ya Allah tuepushe na Adhabu zako kwani hakuna hata mmoja miongoni
mwetu anaeweza kuzistahamilia ukali na uzito wake...Aamiin.

Naam..inabidi tuombe dua kwa sababu hawa watu wa Nabii Lut wao mbali ya kua
walipofuliwa macho kwa wale walioenda Nyumbani kwake na wengine wakakimbia,
lakini hao waliokimbia unajua walifanya nini kwa ujinga wao?

Walirudi kwa Watu wao na kuwaambia kua Huyu Lut kumbe kaja na Wachawi Wakubwa
zaidi yake, lakini hata hivyo inabidi kesho asubuhi mapema tuwaamkie kwa ajili ya
kuwashughulikia Wachawi hao na Lut wao, ili watujue sie nani. Kwani kesho asubuhi
ndio wakati mzuri zaid wa kuwaonesha sie ni nani.
342

Ambapo kwa upande wa Nyumbani kwa Nabii Lut basi Malaika Jibril akamwambia
afunge kila kitu chake aondoke na familia yake na hakuna anaeruhusika kuangalia
Nyuma mara baada ya kutoka kwenye Nyumba yao hio.

Hivyo hapa hapakulika tena chakula kilichokua kinapikwa na Mabinti wa Nabii Lut kwa
ajili ya Wageni, kwani Nabii Lut aliamrisha kifungashwe kila kitu ili wapate kuondoka
haraka iwezekanavyo.

Na kisha Malaika hao wakamfafanulia Nabii Lut cha kufanya kwa kusema:

ۤ ِ ‫﴿ﻗﺎﻟُﻮاْ ٰﻳـﻠُﻮ ُط إِ ﱠ� رﺳﻞ رﺑِﻚ ﻟَﻦ ﻳ‬


َ‫ﻚ ﺑِِﻘﻄْ ٍﻊ ِّﻣ َﻦ ٱﻟْﻠﱠْﻴ ِﻞ َوﻻ‬ ِ
َ ‫َﺳ ِﺮ ِﺄﺑ َْﻫﻠ‬
ْ ‫ﻚ ﻓَﺄ‬َ ‫ﺼﻠُﻮاْ إِﻟَْﻴ‬ َ َ َّ ُ ُ ُ َ
‫َﺻﺎﺑَـ ُﻬ ْﻢ إِ ﱠن َﻣ ْﻮ ِﻋ َﺪ ُﻫ ُﻢ ٱﻟ ﱡ‬ ِ ِ ‫ﻳـ ْﻠﺘَ ِﻔ‬
‫ﺼْﺒ ُﺢ‬ َ ‫ﻚ إِﻧﱠﻪُ ُﻣﺼﻴﺒُـ َﻬﺎ َﻣﺂ أ‬َ َ‫َﺣ ٌﺪ إِﻻﱠ ْٱﻣَﺮأَﺗ‬
َ ‫ﺖ ﻣﻨ ُﻜ ْﻢ أ‬
ْ َ
﴾‫ﻳﺐ‬ٍ ‫ﺼْﺒﺢ ﺑَِﻘ ِﺮ‬
ُ ‫ﺲ ٱﻟ ﱡ‬ َ ‫أَﻟَْﻴ‬
Qaloo ya lootu inna rusulu rabbika lan yasiloo ilayka faasri bi-ahlika biqitAAin
mina allayli wala yaltafit minkum ahadun illa imraataka innahu museebuha ma
asabahum inna mawAAidahumu alssubhu alaysa alssubhu biqareebin (Surat Hud
11:81)

Tafsir: Wakasema (Malaika) Ewe Lut Hakika sisi ni Wajumbe Kutoka kwa Mola wako.
Hawatofika (kwa hata kukugusa) kwako. Hivyo Ondoka na Familia yako katikati ya
Usiku. Na Asiangalie Nyuma hata mmoja. Ila Mke wako Kwani Kwa hakika yatamsibu
yeye Yatakayowasibu wao (watu wako waovu). Kwa Hakika Mda waliopangiwa ni
Asubuhi na Asubuhi haiko mbali.

Ambapo anasema Mujjaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Al Ghazali Al Thani


Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Ama kuhusiana na maana ya maneno yasemayo:
‘Qita’am min al layl’ basi kulingana na mtizamo wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi
Allahu Anhu yanamaanisha: ‘Wakati wowote wa Usiku’ na kwa upande wa
Qatadah basi yeye anasema kua maana ya Qitah ni Usiku wa Manane na karibu na
Alfajir’

Ambapo anasema Said Ibn Musayyib kua: ‘Wakati Malaika waliposema kua
wamekuja kwa sababu kuna jambo litawasibu watu hao, hivyo Nabii Lut
akawaambia Malaika hao kua: ‘Waadhibuni sasa hivi’ Ndio maana Malaika
wakajibu: Wakati wao waliopangiwa ni Asubuhi’
343

Hivyo mara baada ya Malaika Jibril kumwambia Nabii Lut na familia yake wajitayarishe
kuondoka usiku huo huo kwani kuna jambo ambalo litawasibu watu hao basi kwa kua
Nabii Lut anawajua vizuri sana watu wake hao na matatizo yao basi akaomba kua bora
waadhibiwe wakati huo huo kabla ya kufika asubuhi, kwani asubuhi anaona kua iko
mbali sana, lakini Malaika Jibril akamwambia Nabii Lut kua kila kitu hua kinaenda na
Maqadiro yake Allah Subhnah wa Ta’ala, na Makadirio yake juu yao ni asubuhi na
asubuhi haiko mbali hivyo kama anavyoona Nabii Lut na kisha akambainishia Nabii Lut
kuhusiana na kitu gani kitakachowasibu watu hao kama zinavyosema aya:

ِ ‫﴿إِ ﱠ� ﻣﻨ ِﺰﻟُﻮ َن ﻋﻠَﻰ أَﻫ ِﻞ ﻫـٰ ِﺬﻩِ ٱﻟْ َﻘﺮﻳ ِﺔ ِرﺟﺰاً ِﻣﻦ ٱﻟ ﱠﺴﻤ‬
﴾‫ﺂء ِﲟَﺎ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳَـ ْﻔﺴ ُﻘﻮ َن‬
ُ َ َ ّ ْ َْ َ ْ ٰ َ ُ
Inna munziloona AAala ahli hadhihi alqaryati rijzan mina alssama-i bima kanoo
yafsuqoona (Surat Al Anqabut 29:34)

Tafsir: Kwa Hakika tutawashushia Watu hawa wa Miji hii Adhabu Kali kutoka
Mbinguni kutokana na kua ni wenye Kuasi (Mola wao)

Naam, baada ya kupata majibu hayo basi Nabii Lut akafunga funga vitu vyake na Familia
yake kisha wakaagana na Malaika na kutoka ndani Nyumba waliyokua wakikaa na
kuanza Safari ya kurudi Mjini Jerusalem kwa Nabii Ibrahim ambapo Allah Subhanah wa
Ta’ala anasema kwa kutuambia kua:

﴾‫ﲔ۞ إِﻻﱠ َﻋ ُﺠﻮزاً ِﰱ ٱﻟْﻐَﺎﺑِ ِﺮﻳﻦ‬ ِ ْ ‫﴿ﻓَـﻨَ ﱠﺠﻴـﻨَﺎﻩ وأَﻫﻠَﻪ أ‬


َ َ ‫َﲨَﻌ‬ ُ َُْ ْ
Fanajjaynahu waahlahu ajmaAAeena; Illa AAajoozan fee alghabireena. (Surat Ash
Shuara 26:170-171).

Tafsir: Na kisha tukamuokoa yeye na familia yake kwa pamoja, isipokua Bi Kizee
aliekua ni miongoni mwa waliobakia.

Ambapo Bi Kizee huyu si mwengine bali alikua ni Mke wake Nabii Lut aliekua akiitwa
Wahila ambae ndie yule alieelezewa kwenye aya ifuatayo:

﴾‫ﺖ ِﻣﻦ ٱﻟْﻐَﺎﺑِ ِﺮﻳﻦ‬ ِ ﴿


َ َ ْ َ‫ﻓَﺄَﳒَْﻴـﻨَﺎﻩُ َوأ َْﻫﻠَﻪُ إﻻﱠ ْٱﻣَﺮأَﺗَﻪُ َﻛﺎﻧ‬
Faanjaynahu waahlahu illa imraatahu kanat mina alghabireena.(Surat Al Araf:7:83)
344

Tafsir: Na kisha tukamuokoa yeye na watu wa nyumbani kwake isipokua Mke wake
ambae alikua ni miongoni mwa waliobakia.

Naam, hapa tunaona kua aya zimetumia neno Fanjayynahu wa ahlahu yaani Na Kisha
Tukawaokoa yeye na familia yake.

Na pia zimetumia neno Al Ghabiriina na kisha pia zikataja neno Imraatahu yaani Mke
wake na pia zikataja Aajuzan yaani Bikizee.

Hivyo tuanze na maana ya neno Al Ghabirina ambalo hu ni lenye kutokana na neno


Ghabara ambalo ni lenye kumaanisha Kubakia, au Kukaa au Kujaa Mavumbi kwa kitu
kinachokua kipo katika sehemu Moja kwa Mda Mrefu.

Kwani neno Ghabara Ndio lililotumika katika ile aya isemayo:

﴾ٌ‫﴿وو ُﺟﻮﻩٌ ﻳَـﻮَﻣﺌِ ٍﺬ َﻋﻠَْﻴـ َﻬﺎ َﻏﺒَـﺮة‬


َ ْ َُ
Wawujoohun yawma-idhin AAalayha ghabaratun. (Surat Abasa 80:40)

Tafsir: Na Nyuso (Nyengine) Siku hio zitakua zimejaa Vumbi.

Ama kwa upande mwengine Neno Ghabara pia hua linamaanisha Kubakia Nyuma na
pia hua linamaanisha Kuondoka baada ya Kubakia.

Kwani ingawa Neno hili hua linamaana zinazopingana kulingana na matumizi yake lakini
tunapoiangalia Qur'an basi tunaona mbali ya kua imetumia neno hili kumaanisha Kujaa
Vumbi kwa Nyuso katika Siku ya Malipo kama ilivyotumima kwenye Surat Abasa lakini
pia Qur'an imetumia neno Ghabara takriban Mara 7 katika kisa cha Nabii Lut
kumuelezea Mke wa Nabii Lut kua ni Miongoni mwa Mina Al Ghabirina yaani Miongoni
mwa Waliobakia.

Na kama tunakumbuka basi jana tulisema kua Kila Malaika Jibril alisema Watu wa Nabii
Lut hawawezi kuangamizwa Usiku huo kama alivyotaka Nabii Lut kwa wamepangiwa
kuangamizwa Asubuhi.

Hivyo basi anasema Allah Subhanah wa Ta'ala katika Surat Al Hijr 15:59-60 na katika
Surat An Naml 27:57 kua:
345

﴾‫﴿ﻓَﺄَﳒَْﻴـﻨَﺎﻩُ وأ َْﻫﻠَﻪُ إِﻻﱠ ْٱﻣﺮأَﺗَﻪُ ﻗَﺪ ْﱠرَ� َﻫﺎ ِﻣﻦ ٱﻟْﻐَﺎﺑِ ِﺮﻳﻦ‬
َ َ َ َ
Faanjaynahu waahlahu illa imraatahu qaddarnaha mina alghabireena (Surat An
Naml 27:57)

Tafsir: Na Kisha Tukamuokoa yeye (Lut) na Familia yake isipokua Mke wake
tuliemkadiria kua ni Miongoni mwa Waliobakia.

Hivyo basi Ajuza huyu alietajwa kwenye Surat Ash Shuara 26:171 si mwengine yeyote
isipokua ni Wahila yaani Mke wa Nabii Lut ambae aliekadiriwa kua aangamie kutokana
na sababu zilizoelezewa katika aya ifuatayo:

‫ﺖ َﻋْﺒ َﺪﻳْ ِﻦ ِﻣ ْﻦ‬ ٍ ِِ


َ ‫ﻮح َو ْٱﻣَﺮأَةَ ﻟُﻮط َﻛﺎﻧـَﺘَﺎ َْﲢ‬ َ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻣﺜَﻼً ﻟّﻠﱠﺬ‬
ٍ ُ‫ﻳﻦ َﻛ َﻔُﺮواْ ْٱﻣَﺮأَةَ ﻧ‬ ‫ب ﱠ‬ َ﴿
َ ‫ﺿَﺮ‬
ِ ِ‫ﺎﳘﺎ ﻓَـﻠَﻢ ﻳـ ْﻐﻨِﻴﻨﺎ ﻋْﻨـﻬﻤﺎ ِﻣﻦ ﱠ‬ ِ ِ َ �َ ‫ِﻋﺒَ ِﺎد‬
‫ﱠﺎر َﻣ َﻊ‬َ ‫ﻴﻞ ْٱد ُﺧﻼَ ٱﻟﻨ‬ َ ‫ٱﻪﻠﻟ َﺷْﻴﺌﺎً َوﻗ‬ َ َ ُ َ َ ُ ْ َُ َ‫ﺻﺎﳊَْﲔ ﻓَ َﺨﺎﻧَـﺘ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ٱﻟﺪﱠاﺧﻠ‬
Dharaba Allahu mathalan lilladheena kafaroo imraata noohin waimraata lootin
kanata tahta AAabdayni min AAibadina salihayni fakhanatahuma falam yughniya
AAanhuma mina Allahi shay-an waqeela odkhula alnnara maAAa alddakhileena
(Surat At Tahrim 66:10)

Tafsir: Anakupigieni Allah mfano wa wale waliokufuru, Mke wa Nuh na Mke wa Lut
ambao walikua chini ya Waja wawili wema lakini waliwasaliti (Waume zao), hivyo
hawakuwanufaika na kitu chochote kutokana nao kutokana kwa Allah na
wakaambiwa: ‘Uingieni moto pamoja na wanaouingia’

Hivyo ilipofika asubuhi hali ya hewa ya Miji hio ikabadilika ghafla na mara ikaanza
kunyesha mvua isiyokua ya kawaida.

ِ ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫﴿ َوأ َْﻣﻄَْﺮَ� َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ ﱠﻣﻄَﺮاً ﻓَﭑﻧْﻈُْﺮ َﻛْﻴ‬
َ ‫ﻒ َﻛﺎ َن َﻋﺎﻗﺒَﺔُ ٱﻟْ ُﻤ ْﺠ ِﺮﻣ‬
Waamtarna AAalayhim mataran faondhur kayfa kana AAaqibatu almujrimeena
(Surat Al Araf 7:83-84)
346

Tafsir: Na tukawanyeshea juu yao Mvua, hivyo angalieni walivyobakia wenye kufanya
maovu.

Hivyo aya zinatuwekea wazi kile kilichokuta watu wa Nabii Lut baada ya Nabii Lut na
familia yake kuondoka na ulipowadia mda wao waliopangiwa waadhibiwe yaani Asubuhi
ambapo Allah Subhanah wa Ta'ala anatuwekea wazi mda aliomuokoa Nabii Lut
kutokana na Adhabu dhidi ya watu hao ilikua kabla ya asubuhi kwa kusema:

﴾‫ﺎﻫﻢ ﺑِﺴ َﺤ ٍﺮ‬ ‫ﺎﺻﺒﺎً إِﻻﱠ َ ٍ ﱠ‬


ِ ‫﴿إِ ﱠ� أَرﺳ ْﻠﻨَﺎ ﻋﻠَﻴ ِﻬﻢ ﺣ‬
َ ُ َ‫آل ﻟُﻮط ﳒﱠْﻴـﻨ‬ َ ْ َْ َْ
Inna arsalna AAalayhim hasiban illa ala lootin najjaynahum bisaharin (Surat Al
Qamar 54:34)

Tafsir: Kwa Hakika tuliwatumia wao Hasiban Isipokua Lut ambae Tulimuokoa
Karibu na Asubuhi

Na tnaona kua aya imetumia neno Hasiban ambalo sikulitafsiri katika aya kwa sababu
nataka tupate taswira kamili ya hali ilivyokua, kama ilivyosema Aya.

Naam, neno Hasiban kwa Lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kurusha Kitu chenye
chenga chenga Kubwa kubwa na Ndogo ndogo kama Kokoto lakini sasa kitu hicho hua
kina asili ya Moto na hivyo kikingukia ndani ya Moto basi Hua ni chenye Kuzidishi Ukali
wa Moto Huo.

Kama vile vidonge vya Lami, Chuma, Dhahabu au Shaba iliyokua imoto na kua na rangi
nyekundu kutokana na umoto wake. Na ili kufaham Vizuri maana ya neno Hasiba basi
na tuangalie mfano wa Aya ifuatayo ambayo inasema:

‫ﺐ َﺟ َﻬﻨ َﱠﻢ أَﻧﺘُ ْﻢ َﳍَﺎ َوا ِرُدو َن۞ ﻟَ ْﻮ َﻛﺎ َن‬ ِ‫ون ﱠ‬ ِ ‫﴿إِﻧﱠ ُﻜﻢ وﻣﺎ ﺗَـﻌﺒ ُﺪو َن ِﻣﻦ د‬
ُ‫ﺼ‬َ ‫ٱﻪﻠﻟ َﺣ‬ ُ ُْ َ َ ْ
﴾‫وﻫﺎ وُﻛﻞﱞ ﻓِ َﻴﻬﺎ َﺧﺎﻟِ ُﺪو َن‬ ِ ِ ۤ
َ َ ‫َﻫـُٰﺆﻻء آﳍَﺔً ﱠﻣﺎ َوَرُد‬
Innakum wama taAAbudoona min dooni Allahi hasabu jahannama antum laha
waridoona; Law kana haola-i alihatan ma waradooha wakullun feeha khalidoona
(Surat Al Anbiyah 21:98-99)
347

Tafsir: Hakika nyinyi na mnavyoviabudu zaidi ya Allah si chochote bali ni Kuni za


Moto wa Jahanam ambao mtauingia ndani yake. Lau kama wangekua ni Miungu basi
wasingeingia Motoni, lakini wote ndani yake wataingia.

Naam tunarudi kwa huyu Wahila ambae ni Imraatan Lutan ambae ni Mke wake Nabii
Lut ambae aya zimesema kua yeye atakua ni miongoni mwa Mina Al Ghabiriina kama
inavyosema aya ifuatayo lakini hapo hapo Aya zimesema kua Nabii Lut aliondoka na
Familia yake sasa jee huyu Wahila ilikuaje akawa ni Miongoni mwa Mina Al Ghabiriina?

Hivyo aya zinatuainishia kile kilichotokea mpaka Wahila akawa ni aliebakia na watu
wake baada ya kua ni mwenye kutoka na famila yake inaonesha kua Wahila alikua ni
mwenye kubakia nyuma na hii ni kutokana na kutotaka kuondoka, lakini hali
ilivyobadilika basi akawa ni Mina Al Ghabiriina yaani Mwenye kuondoka baada ya
kubakia na hivyo kabla ya adhabu hio kuwakuta watu wake hao basi kwanza ilimkuta
yeye kabla hajakaribia familia yake na kisha ndio wakaadhibiwa watu wake, kwani aya
zinasema:

ِ
َ ‫ﻳﻦ ۞ إِ ﱠن ِﰱ ٰذﻟ‬
‫ﻚ‬ ِ ِ
َ ‫۞وأ َْﻣﻄَْﺮَ� َﻋﻠَْﻴﻬﻢ ﱠﻣﻄَﺮاً ﻓَ َﺴﺂءَ َﻣﻄَُﺮ ٱﻟْ ُﻤﻨ َﺬر‬ َ �َ‫﴿ﰒُﱠ َد ﱠﻣْﺮ‬
َ ‫ٱﻵﺧ ِﺮ‬
َ ‫ﻳﻦ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ﻵﻳَﺔً َوَﻣﺎ َﻛﺎ َن أَ ْﻛﺜَـُﺮُﻫﻢ ﱡﻣ ْﺆﻣﻨ‬
Thumma dammarna al-akhareena; Waamtarna AAalayhim mataran fasaa mataru
almundhareena; Inna fee Dhalika laayatan wama kana aktharuhum mu/mineena;
(Surat Ash Shuara 26:172-174)

Tafsir: Kisha tukawaangamiza wengine. Tukawanyeshea juu yao Mvua. Na (Bila ya


Shaka) ni Mbaya sana Mvua ya Watu Walioonywa. Kwa hakika katika haya kuna
mafunzo ndani yake lakini hata hivyo (watu) wengi wao si wenye kuamini.

Na tunapomuangalia Imam Ath Thalabi basi yeye anatuambia kwa kusema kua: ‘Kila
Mtu aliekua Miongoni mwa Watu hawa basi alipatwa na adhabu hio ya vijiwe vya
Moto hata kama alikua yuko nje ya Mji wake. Hivyo Mke wa Nabii Lut alitoka
pamoja na Familia yake na kisha watu wa Miji hio walipokua wakiadhibiwa
akasikia sauti kubwa hivyo akageuka nyuma kuangalia kinachotokea na kusema:
‘Masikini watu wangu’ Hivyo akapigwa jiwe na akafa hapo hapo na hivyo kua ni
miongoni mwa waliobakia na watu wake.’

Na baada ya hapo ikafuatia adhabu hio ambayo kamwe haijawahi kutokea hapo kabla,
kwani aya zinasema:
348

‫﴿ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ َﺟﺂءَ أ َْﻣُﺮَ� َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ َﻋﺎﻟِﻴَـ َﻬﺎ َﺳﺎﻓِﻠَ َﻬﺎ َوأ َْﻣﻄَْﺮَ� َﻋﻠَْﻴـ َﻬﺎ ِﺣ َﺠ َﺎرًة ِّﻣﻦ ِﺳ ِّﺠ ٍﻴﻞ‬
﴾‫ﻮد‬ٍ ‫ﱠﻣْﻨﻀ‬
ُ
Falamma jaa amruna jaAAalna AAaliyaha safilaha waamtarna AAalayha
hijaratan min sijjeelin mandhoodin (Surat Hud 11:82)

Tafsir: Na kisha lilipowadia jambo letu tukawajaalia juu yao kua chini. Na
tukawanyeshea juu yao mawe yaliyookwa moto yaliyokusanywa.

Ambapo hii ni moja kati ya aya zinazoelezea upekee wa tukio lilikadiriwa kuwakuta watu
wa Nabii Lut kutokana Maasi yao ambayo ni hali ya mchanganyiko wa adhabu tofauti
ikiwemo Mvua ya Mawe yenye Moto na sio moto uliokuwepo juu juu tu ya Mawe hayo
bali ni Mawe yenye kua na asili ya maumbile ya Moto. Na ukweli ni kua hali hii
inayoelezewa katika aya hizi sisi leo hatuwezi kufaham kama inavyotakiwa tufaham
matatizo yaliwakuta watu hawa kutokana na Mvua hio.

Lakini kwa upande mmoja tunaweza kuchukulia Mfano wa Mripuko wa Volcano Ambao
hua unakua ni Mripuko wa Magma yaani Uji uji wa Mawe yanayowaka moto, ukikugusa
uji wake huo basi unaondoka na Nyama yako katika sehemu ya mwili uliyokugusa.

Sasa uafadhali wa Volcano ni kua Unaweza kuikimbia lakini hii Mvua ya Adhabu
ambayo Mwenyewe alieishusha anaisifia Ubaya wake mvua hio hua haiepukiki kwa
Sababu Allah Subhanah wa Ta'ala anakua ameshakadiria kua tone fulani litue juu ya kitu
fulani, na tuchukulie Mfano kua katika Mvua hii basi Mfalme wao ambae ndie mkaidi
zaid yaani Mfalme Sudum basi yeye imnyeshee mtone 10 tu.

Hivyo kila tone linakuja na jina la mtu, kulingana na dhambi zake hivyo hata uwe chini
ya pango basi tone hilo linakufikia na Mvua hii ndio kama iliyomnyeshea Mfalme Abraha
ambae ni jeshi lake la Tembo yule Mfalme wa Uhabeshi alieamua kulivunja Al Kaabah
katika Mwaka wa Tembo alieelezewa katika Surat Al Fiil.

﴾‫﴿ﺗَـﺮِﻣﻴ ِﻬﻢ ِِﲝ َﺠﺎرةٍ ِّﻣﻦ ِﺳ ِّﺠ ٍﻴﻞ‬


َ ْ
Tarmeehim bihijaratin min sijjeelin (Surat Al Fiil 105:4)

Tafsir: Wakawapiga Mawe ya Motoni.


349

Ambapo Wanazuoni wanasema kua kila Kitone kimoja au Kijiwe kimoja kilichobebwa
na jeshi la Ndege wa Allah Subhanah wa Ta'ala. Kilikua na jina la Mtu, na kila mtu
akiangukiwa na kijiwe kimoja tu, kichwani basi kijiwe hicho humnyofoa mapande ya
nyama mtu huyo na kubakishia mfupa bila ya nyama ya mwili wa Mtu huyo alienyeshewa
na Mvua ya Mawe hayo.

Nafikiri kidogo tunapata kuona au kuhisi ukubwa wa Adhabu hio ya Mvua ya Watu
walioonywa na hivyo na kujua maana ya maneno ya aya yasemayo: Waamtarna Alayhim
Mataran - Na Tukawanyeshea juu yao Mvua. Fasaa Mataru Al Mundhiriina - Na (Bila
ya Shaka) ni Mbaya sana Mvua ya Watu walioonywa (Surat Ash Shuara 26: 173)

Kwani huo ni upande wa maumbile ya Mvua hio ambayo mpaka Wanasayansi


Wamedhibitisha kua hayo yamewakuta watu wa Nabii Lut. Hivyo tunarudi tena katika
aya tuliyoanza nayo ambayo sehemu yake bado haijathibitishwa na Wanasayansi, lakini
Qur'an imethibitisha kua imetokea.

Ama kwa upande mwengine basi Imam Muhammad Ibn Is-haq kua: ‘Baada ya Nabii
Lut kuondoka na familia yake, na watu wa Miji hio kuamka asubuhi yake basi
Malaika Jibril akatia Ubawa wake chini ya Ardhi ya Miji hio kasha akaichota na
kuinyanyua juu Mbinguni na kila kiu chake. Katika Miji hii kulikua na watu laki
nne pampja na wanyama wao, Ambapo walipandishwa juu mpaka wale wanyama
walioko kwenye Mbingu ya chini kabisa karibu na Dunia wakawa ni wene kusikia
sauti za vilio vya wanyama hao. Na kasha akaigeuza juu chini na kurudi nayo Ardhi
hio na kuibamiza ardhini sehemu hio katika sehemu aliyoichota hapo kabla’

Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua amesema Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu
Anhu kua Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Hakika mimi
niKISIKIA Milio ya Ngurumo za Radi basi hua nna khofu kua huenda yale Mawe
waliyotayarsihiwa watu wa Lut yatafanya kama yalivyofanya hapo kabla’

Ambapo anasema Imam Muqatil Ibn Sulayman kua: ‘Mimi nilimuuliza Mujahid Abu
Al Hajjaj: ‘Hivi jee Miongoni mwa watu wa Nabii Lut yupo mbae alie iepuka
Adhabu yake?’’

'Mujahid akajibu: ‘La Isipokua kuna Mtu mmoja tu ambae aliishi kwa siku 40
zaidi, na baada ya hapo watu wake kunyeshewa na mvua hio basi na yeye alikua
ndani ya Masjid Al Haram wakati jiwe lake liliposhuka, lakini sasa Malaika
wakalizuia Jiwe hilo na Kuliambia: ‘Rudi huko huo ulikotoka kwa sababu umekuja
ndani ya Eneo ambalo limefanywa kua ni Takatifu na Allah Subhanah wa Taa’la’

Hivyo Jiwe hilo likakaa nje ya Mji wa Makkah kwa mda wa siku 40 huku likwa
linaelea bain aya Mbingu na Ardhi likimsubiri Mtu wake atoke ndani ya Mji huo.
350

Hivyo Mtu huyo akafanya shughuli zake zilizomleta katika Mji huo kwa siku 40 na
kisha baada ya kumaliza shughuli hizo akatoka na kurudi alikotka na alipotoka nje
tu ya Mji wa Makkah basi jiwe hilo la Moto likamuangukia na kumuua.’'

Ama kwa hakika tuko ukingoni mwa kisa cha Nabii Lut ambapo anasema Imam
Muhammad Ibn Is-haq kua siku moja Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alisema
kumwambia Malaika Jibril: ‘Ewe Jibril, Hakika Allah amekupa wewe Majina na
amenielezea Majina hayo kwa kusema:

ٍ ‫ﻨﺪ ِذى ٱﻟْ َﻌﺮ ِش َﻣ ِﻜ‬


ٍ ‫ﲔ ۞ ﱡﻣﻄَ ٍﺎع ﰒَﱠ أ َِﻣ‬
﴾‫ﲔ‬ َ ‫﴿ ِذى ﻗُـ ﱠﻮةٍ ِﻋ‬
ْ
Dhee quwwatin AAinda dhee alAAarshi makeenin, MutaAAin thamma
ameenin(Surat At Takwir 81:20-21)

Tafsir: Mwenye Nguvu Na Mwenye Darja Kubwa kwa Mmiliki wa Arshi (Allah
Subhanah wa Ta'ala) Mwenye Kuitikiwa (Amri zake na Malaika) na Mwenye
Kuaminika

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamalizia kwa kumuuliza Malaika Jibril kwa
kusema: ‘Hivyo Ya Jibril, Hebu niambie kuhusiana na Uwezo wako?’

Ambapo Malaika Jibril akajibu: ‘Ewe Muhammad, Hakika mimi kwa Ubawa wangu
mmoja tu, niliichota Miji ya watu wa Lut na kuenda nayo Mbinguni hadi Viumbe
wanaoishi kwenye Mbingu ya chini kabisa wakawa ni wenye kusikia vilio vya
wanyama wao. Na kisha nikaigeuza Ardhi ya Miji hio Juu chini.’

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akauliza tena kwa kusema: ‘Ewe Jibril,
hebu nielezee ni kwa nini Allah akakuita wewe kua ni Mwenye Kutiiwa Amri zako?’

Malaika Jibril akasema: ‘Ewe Muhammad, hii ni kwa sababu mimi nikisema
kumwambia Ridhwan ambae ni Malaika Mlinzi wa Milango ya Pepo na Malik
ambae ni Malaika Mlinzi wa Milango ya Moto kua wafungue Milango ya Pepo na
Milango ya Moto basi bila ya shaka hua ni wenye kufungua Milango hio’

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akauliza tena kwa kusema: ‘Ewe Jibril
hebu niambie, kwanini akakuita kua wewe ni Muaminifu?’

Malaika Jibril akajibu: ‘Ewe Muhammad, hii ni kwa sababu Allah Subhanah wa
Ta’ala amewashushia Mitume wake vitabu Vitukufu Mia moja na nne na
hakumuuaminisha yeyote isipokua mie kuwaletea’
351

Naam..hii habari inayofuatia ndio nzito zaid kwani kulingana na mtizamo wa Imam Al
Mufassirin Muqatil Ibn Sulayman basi yeye anasema kua: ‘Miongoni mwa watu wa
Nabii Lut ambao walikua ni wenye kufanya Dhambi waliyoangamiziwa watu wa
Nabii Lut walikua si wote. Lakini Allah Subhanah wa Ta’ala aliwaangamiza wote
kwa sababu walikua hawakatazani, kama vile alivyotuamrisha Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam pale aliposema: ‘Ni lazima Muamrishane mema na
mkatazane Mabaya kwani la sivyo basi adhabu itakukumbeni nyote’’

Ama kwa upande mwengine tunaporudi katika aya inayoelezea kugeuzwa juu chini kwa
Miji ya Watu wa Nabii Lut ambayo inasema:

‫﴿ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ َﺟﺂءَ أ َْﻣُﺮَ� َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ َﻋﺎﻟِﻴَـ َﻬﺎ َﺳﺎﻓِﻠَ َﻬﺎ َوأ َْﻣﻄَْﺮَ� َﻋﻠَْﻴـ َﻬﺎ ِﺣ َﺠ َﺎرًة ِّﻣﻦ ِﺳ ِّﺠ ٍﻴﻞ‬
﴾‫ﻮد‬ٍ ‫ﱠﻣْﻨﻀ‬
ُ
Falamma jaa amruna jaAAalna AAaliyaha safilaha waamtarna AAalayha
hijaratan min sijjeelin mandhoodin (Surat Hud 11:82)

Tafsir: Na kisha lilipowadia jambo letu tukawajaalia juu yao kua chini. Na
tukawanyeshea juu yao mawe yaliyookwa moto yaliyokusanywa.

Basi tunaona kua Mwanasayansi wa Kijerumani wa mambo ya kale aitwae Werner Keller
anasema kuhusiana na kilichotokea katika eneo la Miji ya Watu wa Nabii Lut kwa
Mtizamo wa Kisayansi kua: ‘Mfululizo wa Miripuko, Mitetemeko ya Ardhi,
Ngurumo na Radi na kufoka kwa Gesi Kali yenye Kasi Kubwa sana kutoka ardhini
ulipelekea kua katia siku moja tu Miji ya watu hao kuzama ndani ya shimo kubwa
lisilokua na mwisho’

Yaani Werner Keller anaelezea kulingana na Vithibitisho vingi viliopo katika eneo la
Ardhi hio ambavyo vinaonekana mpaka leo hii. Kwani katika eneo hilo walilobamizwa
na kuzamishwa watu wa Miji hio kuna Bahari ya ndani ya eneo la Ardhi ya bara yaani
hua ni bahari ndogo na kubwa kuliko ziwa, bahari hii inaitwa Bahar Al Mayit, Dead Sea
au Bahari iliyokufa.

Na miongoni mwa vitibitisho vya maajabu ya eneo la bahari hio ni kua Bahari hio iko
katika eneo ambalo lina kina cha chini kabisa kuliko eneo lolote la Ardhi hapa Duniani.
Kwani lipo chini zaidi Duniani kwa mita 423. Na limeenda chini kwa mita 377 kutoka
katika usawa wa bahari katika baadhi ya maeneo yake limeenda chini kwa mita 100. Na
lina urefu wa kilomita 67 na upana wa kilomita 18.
352

Eneo la Ardhi ya Bahari hii imeitwa Bahari iliyokufa kwa sababu ndani yake bahari hio
hakuna aina yeyote ya samaki wanaoweza kuishi au viumbe wengine ambao wanaweza
kuishi kwenye Bahari za kawaida na hii ni kutokana na kua maji ya Bahari hii yana
chumvi nyingi sana ambayo wingi wake ni zaidi ya asilimia 30 ya chumvi iliyomo ndani
ya Maji ya Bahari ya kawaida. Na hivyo basi kuyafanya maji hayo kua ni na Uzito zaid
ya maji ya Bahari ya kawaida kiasi ya kua unaweza kulala juu yake na ukaelea bila ya
kuzama.

Kwani kama ukibahatika na kutembelea baadhi ya eneo la Bahari hio katika hali ya hewa
nzuri isiyokua na Mawingu basi unaweza pia kuona baadhi ya Maumbo ya Bustani nzuri
iliyokuwepo katika kipindi hicho ambayo hata hivyo leo hii ipo chini ya Maji na hivyo
kua ni Miti ya Chumvi kali sana. Tunamalizia kisa hiki kwa kauli ya Imam Abd Allah
Ibn Al Husayn Ibn Muhammad Al Thaqafi ambae anasema kua Abu Bakar Al Ayash
alimuuliza Abu Jaffar kwa kusema kua: ‘Hivi Jee Allah Subhanah wa Ta’ala
aliwaangamiza Wanawake wa Nabii Lut kwa makosa ya Waume zao tu au kwa
sababu gani?’

Abu Jafar akajibu kwa kusema: ‘La si hivyo, kwani miongoni mwa sifa za Allah
Subhanah wa Taala ni kua Hakuna Muadilifu zadi yake. Hivyo wanawake wa watu
wa Nabii Lut waliangamizwa kwa sababu wakati waume zao walipokua wakitimiza
Matamanio ya Miili yao kwa Wanaume wenzao, basin a Wanawake hao nao
wakawa wanatimiza matamanio ya miili yao kwa Wanawake wenzao. Hivyo
Adhabu ya Allah Subhanah wa Ta’ala ikawashukia wote kwa pamoja. ’

Hivyo Allah Subhanah wa Taála anamsifu Nabii Ibrahim na kumuwekea wazi


kutobadilika kwa majaaliwa yake dhidi ya Watu wa Nabii Lut kwa kusema:

ِ ِ ِ ِ ِ
ٌ ‫﴿إ ﱠن إﺑْـَﺮاﻫ َﻴﻢ َﳊَﻠ ٌﻴﻢ أَﱠواﻩٌ ﱡﻣﻨ‬
﴾‫ﻴﺐ‬
Inna ibraheema lahaleemun awwahun muneebun; (Surat Hud 11:75)

Tafsir: Hakika Ibrahim alikua ni mstahmilivu, mwenye kuomba na mwenye kurudi


kwa Mola wake.

Bila ya shaka aya Nabii Ibrahim alikua na sifa tatu bora ambazo nazo pia alikua nazo
Rasul Allahi Salallahu A’layhi wa Salam. Sifa hizo ni: Alikua ni mwenye kuadhibika
kwa muda mrefu kutokana na makosa ya watu wengine. Huruma zake na
ustahmilivu wake ulikua ni wa hali ya juu kabisa. Na kwa kila tatizo na mtihani
basi alikua ni mwenye kurudi kwa Mola wake.
353

Allah Subhanah wa Taala anamsifu tena Nabii Ibrahim A’layhi Salaam kwa kusema kua
alikua ni:

‫ﲔ۞ َﺷﺎﻛِﺮاً ِﻷَﻧْـﻌُ ِﻤ ِﻪ‬ ِ ِ ُ ‫﴿إِ ﱠن إِﺑـﺮِﻫﻴﻢ َﻛﺎ َن أُﱠﻣﺔً ﻗَـﻨِﺘًﺎ ِﱠﻪﻠﻟِ ﺣﻨِﻴ ًﻔﺎ وَﱂ ﻳ‬
َ ‫ﻚ ﻣ َﻦ اﻟْ ُﻤ ْﺸ ِﺮﻛ‬ ََْ َ َ َْ
ِ‫ٱﻵﺧﺮة‬ِ ِ ِ ِ ۞ٍِ ٍ ِ ِ
َ ‫ٱﺟﺘَـﺒَﺎﻩُ َوَﻫ َﺪاﻩُ إ َ ٰﱃ ﺻَﺮاط ﱡﻣ ْﺴﺘَﻘﻴﻢ َوآﺗَـْﻴـﻨَﺎﻩُ ﰱ ٱﻟْ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ َﺣ َﺴﻨَﺔً َوإﻧﱠﻪُ ﰱ‬ ْ
﴾‫ﲔ‬ ِِ ‫ﻟَ ِﻤﻦ ٱﻟ ﱠ‬
َ ‫ﺼﺎﳊ‬ َ
Inna Ibraheema kana ummatan qanitan lillahi haneefan walam yaku mina
almushrikeena. Shakiran li-anAAumihi ijtabahu wahadahu ila siratin
mustaqeemin; Waataynahu fee alddunya hasanatan wa-innahu fee al-akhirati
lamina alssaliheena (Surat An Nahl 16:120-123)

Tafsir: Hakika, Ibrâhim alikua ni Ummah (kiongozi mwenye sifa zote nzuri), mtiifu
kwa Allah, Hanifa (alieipa mgongo Dunia na kumjali Allâh tu pekee), na hakuwa
miongoni mwa Al-Mushrikûn (wenye kumshirikisha Allah). Alikua ni mwenye
kushukuru juu ya Neema zake, Na (Allah) alimchagua na kumuongoza katika njia
ilivyonyooka; Na tumempa yeye yaliyo mema Duniani na kesho Akhera atakua ni
miongoni mwa walio wema.

Naam..aya imempa Nabii Ibrahim darja ya kua ni Ummah ambapo mbali ya kua neno
hilo kwa kiarabu hua linamaanisha Jamii ya Watu fulani lakini pia neno hilo hua
linamaanisha Tabia, Njia ya Maisha, Vitendo vya Mtu, Dini, Imani, Kizazi, au mtu
mwenye sifa njema pekee na hivyo kua ni mfano wa Kuigwa.

Hivyo tunapozungumzia neno Ummatin hua lina maana nyingi na tofauti kama vile
yalivyo maneno mengi ya lugh ya Kiarabu ambayo ni lugha tajiri sana isiyokua na mfano
wake, kutokana na hali hio basi na tuangalie tofauti za kimatumizi ya neno hilo ambapo
tunaona kua limetumika mara kadhaa ikiwemo katika aya zifuatazo:

Pale lilipotumika kumaanisha ‘Kundi la watu’ katika aya inayomzungumzia Nabii Musa
Alayhi Salam pale iliposema:
354

‫ﱠﺎس ﻳَ ْﺴ ُﻘﻮ َن َوَو َﺟ َﺪ ِﻣﻦ ُدو�ِِ ُﻢ‬


ِ ‫﴿ َوﻟَ ﱠﻤﺎ َوَرَد َﻣﺂءَ َﻣ ْﺪﻳَ َﻦ َو َﺟ َﺪ َﻋﻠَْﻴ ِﻪ أُﱠﻣﺔً ِّﻣ َﻦ ٱﻟﻨ‬
‫ﻮ� َﺷْﻴ ٌﺦ‬ ِ ‫ﺼ ِﺪ َر‬
َ ُ‫ٱﻟﺮ َﻋﺂءُ َوأَﺑ‬ ْ ُ‫ﻳ‬ ‫ﱴ‬ٰ ‫ﱠ‬ ‫ﺣ‬
َ ‫ﻰ‬ ِ ‫ﺎل ﻣﺎ ﺧﻄْﺒ ُﻜﻤﺎ ﻗَﺎﻟَﺘﺎ ﻻَ ﻧَﺴ‬
‫ﻘ‬ ْ َ َ ُ َ َ َ َ‫ﻗ‬ ِ ‫ﲔ ﺗَ ُﺬود‬
‫ان‬ َ ِ َ‫ْٱﻣَﺮأَﺗ‬
ّ
﴾ٌ‫َﻛﺒِﲑ‬
Walamma warada maa madyana wajada AAalayhi ommatan mina alnnasi
yasqoona wawajada min doonihimu imraatayni tadhoodani qala ma khatbukuma
qalata la nasqee hatta yusdira alrriAAao waaboona shaykhun kabeerun (Surat Al
Qasas 28:23)

Tafsir: Na alipowasili kwenye eneo lenye maji (ya Kisima) la Maydan, akakuta Kundi
la watu wakinywesha maji mifugo yaona pembeni yao kukiwa na Wanawake wawili
wakizuia (mifugo yao). Akawaambia: ‘Nipeni Khabari yenu’ Nao wakasema:
‘Hatuwezi kuwapa Maji (mifugo yetu) mpaka wachungaji hawa waondoke na baba
yetu ni Mzee Sana’
Na kadhalika pale lilipotumika kumaanisha ‘Dini au Utaifa’ katika aya ifuatayo:

�َ ‫ﻮﻫﺂ إِ ﱠ� َو َﺟ ْﺪ‬ َ َ‫ﻚ ِﰱ ﻗَـْﺮﻳٍَﺔ ِّﻣﻦ ﻧﱠ ِﺬﻳ ٍﺮ إِﻻﱠ ﻗ‬


َ ُ‫ﺎل ُﻣْﺘـَﺮﻓ‬
ِ
َ ‫ﻚ َﻣﺂ أ َْر َﺳ ْﻠﻨَﺎ ِﻣﻦ ﻗَـْﺒﻠ‬
ِ
َ ‫﴿ َوَﻛ ٰﺬﻟ‬
﴾‫آﺂﺑء َ� َﻋﻠَ ٰﻰ أُﱠﻣ ٍﺔ وإِ ﱠ� َﻋﻠَ ٰﻰ آ َﺎﺛ ِرِﻫﻢ ﱡﻣ ْﻘﺘَ ُﺪو َن‬
َ ََ
Wakadhalika ma arsalna min qablika fee qaryatin min nadheerin illa qala
mutrafooha inna wajadna abaana AAala ommatin wa-inna AAala atharihim
muqtadoona (Surat az Zukhruf 43:23)
Tafsir: Na kadhalika hatukuwahi kutuma Mtume kabla yako (ewe Muhammad) katika
jamii ya watu kuwausia isipokua husema wenye neema miongoni mwao hua ni wenye
kusema: ‘Tumewakuta mababa zetu wakifuata Dini fulani, hivyo kwa hakika na sisi
tutafuata nyayo zao.’
Na pia pale aya zilipomzungumzia Mfungwa mwenzake Nabii Yusuf alieachiwa hapo
kabla na hivyo kumaanisha ‘Baada ya Mda fulani’ pale iliposema:

ِ ُ‫ﺎل ٱﻟﱠ ِﺬى َﳒَﺎ ِﻣْﻨـﻬﻤﺎ وٱ ﱠد َﻛﺮ ﺑـﻌ َﺪ أُﱠﻣ ٍﺔ أ ََ�ْ أُﻧَـﺒِﺌُ ُﻜﻢ ﺑِﺘَﺄْ ِوﻳﻠِ ِﻪ ﻓَﺄَرِﺳﻠ‬
﴾‫ﻮن‬ َ َ‫﴿ َوﻗ‬
ْ ْ ّ َْ َ َ َ ُ
355

Waqala alladhee naja minhuma waiddakara baAAda ommatin ana onabbi-okum


bita/weelihi faarsilooni (Surat Yusuf 12:45)

Tafsir: Na akasema yule ambae aliokolewa na kuachiwa (kutoka Jela) baada ya muda
mrefu kupita: ‘Nitakuambieni maana yake, nitumeni’

Naam hio ni mifano ya maana ya neno Ummatin kulingana na lilivyotumika katika


Qur’an hivyo tunarudi katika aya yetu ya Surat An Nahl 16:120 inayomzungumzia Nabii
Ibrahim na kuangalia mtizamo wa Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu ambae yeye
anasema kua: ‘Neno Ummah katika ayah hii linamaanisha kua ni mtu mwenye
kufanya Mema na Qanit maana yake hua ni mtu mwenye kumtii Allah Subhanah
wa Taála na Mtume wake Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam.’

Ama kulingana na mtizamo wa Shaykh Al Akbar Imam Ibn Arabi basi yeye anasema
kua: ‘Neno Ummah lililotumika hapa linamaanisha kua ni Mwenye Ilm kubwa
sana’. Ama kwa upande wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema
kua: ‘Kwa kua Nabii Ibrahim alikua ni Muislam peke yake basi ndio maana akawa
ni mwenye kuitwa kwa jina hilo la Ummah’ ama kwa upande wa Imam Fakhr Ad Din
Al Razi na Imam Al Zamakhshari basi wao wanasema kua: ‘Nabii Ibrahim alikua ni
mtu ambae amechanganya sifa zinazojumuisha Ummah Mzima’

Vile vile mbali ya kua aya imetumia neno Ummati na lakini aya yetu hii imetumiia neno
Hanifa ambalo nalo hua linamaanisha Kuegemea, Kuinamia, Kuelekea, Kuelemea,
Kufuata Dini Moja iliyosahih, Kua na Msimamo katika Dini iliyo sahih, Kuachana na
Dini ambayo siyo, au mitizamo ambayo siyo. Hivyo Nabii Ibrahim ameitwa Hanifa kwa
sababu alikua ni mwenye kuachana na kila kitu na kumgeukia Mola wake tu, au pia
tunaweza kusema kua neno hili linamaanisha Muadilifu.

Sifa hii ya Hanifa hua pia ni yenye kumaanisha mtu ambae ni mwenye kuyachukia kabisa
Masanamu na hivyo hua ni mwenye kuamini kuwepo kwa Mungu Mmoja tu.
Tunapoangalia historia basi tunaona kua Nabii Ibrahim alikua ni mtu wa mwanzo kua na
sifa hio, lakini hata hivyo baadae kwa watu Makkah na Madina waliokua wakifuata
vitabu vya Ahl Al Kitab wakaanza kutumia jina hilo kwa mfano Waraqah Ibn Nawfal Ibn
Asad Ibn Abd-al-Uzza Ibn Qusayy Al-Qurashi, ambae alikua ni Ibn Ami yake Bi Khadija
Bint Khuwaylid Radhi Allahu Anha mke wake Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa
Salam, Miongoni mwa waliokua na sifa ya Hanifa ni pamoja na Ubaid Allah Ibn Jahsh,
Uthman Ibn Khuwayris, Zaid Ibn Amir, Ummaya Ibn Abi Salt aliekua Chifu wa Mji wa
Madina n,k. wote hawa walikua ni wenye kuchukia kuyasujudia Masanam.

Aya zinamalizia kwa kuhakikisha kua Nabii Ibrahim alikua pia ni mwenye kumshukuru
Mola wake kutokana na neema alizopewa na Mola wake. Na hivyo kua ni Mtu alieongoka
356

na hivyo kurahisishiwa mambo yake kesho Akhera na kupewa Darja ya juu mbele ya
Allah Subhanah wa Taála na kupewa Heshima kubwa.

Imam Fakhr Ad Din Al Razi anasema kua Nabii Ibrahim alipewa yote haya kwa sababu
ya kuomba ile Dua isemayo:

‫ٱﺟ َﻌﻞ ِّﱃ ﻟِ َﺴﺎ َن ِﺻ ْﺪ ٍق ِﰱ‬


ْ ‫ﲔ ۞ َو‬
ِِ ‫َﳊِْﻘ ِﲎ ﺑِﭑﻟ ﱠ‬
َ ‫ﺼﺎﳊ‬ ْ ‫ﺐ ِﱃ ُﺣ ْﻜﻤﺎً َوأ‬ ِّ ‫﴿ َر‬
ْ ‫ب َﻫ‬
﴾‫ٱﺟ َﻌ ْﻠ ِﲎ ِﻣﻦ ورﺛَِﺔ َﺟﻨ ِﱠﺔ ٱﻟﻨﱠﻌِﻴ ِﻢ‬
ْ ‫و‬ ۞ ‫ﻳﻦ‬ ِ
‫ﺮ‬ ِ
‫ٱﻵﺧ‬
ََ َ َ
Rabbi hab lee hukman waalhiqnee bialssaliheena; WaijAAal lee lisana sidqin fee al-
akhireena; WaijAAalnee min warathati jannati alnnaAAeemi (Surat Ash Shuara
26:83-85)

Tafsir: Ya Rabbi! Nipe Hikma juu yangu na unijumuishe na Waja wema; Na unijaalie
niwe ni mwenye kutajwa kwa sifa njema na vizazi vya watakaokuja; Na unijaalie kua
ni mrithi wa Neema za Peponi.

Anasema Imam Al Zamakhshsari kuhusiana na aya hii kua: ‘Wakati Nabii Ibrahim
alipokua akiomba dua hii alikua akiomba muongozo wa kufanya mambo mema ili
awe na uhusiano mzuri na waja wema.’

Ama kwa upande mwengine basi tunaona kua Dua hii ilikua ikimaanisha kuomba kua ni
mfano bora hata kwa vizazi vijavyo kutokana na wema wake kiasi ya kua, nae anufaike
na malipo ya watakaofanya mema hayo yanayotokana na kufuata uongofu wake yeye
pamoja na kizazi chake ambacho ndicho kilichotoa Dhabihu Allah.


KHALIL ALLAH NA DHABIHU ALLAH

Neno Dhabaha kwa Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Kutawanya, Kukata, Kuchinja,
Kuchana, Kurarua, Kutoa Kafara, Kuua n.k Neno Dhabaha ndio lililotoa neno Adhbahu
yaani nnachinja na likatoa neno Dhabih yaani Anaechinjwa au Anaetolewa Kafara.

Tunapoiangalia Qurán basi tunaona kua pale ilipozungumzia kuhusiana na mtoto wa


Nabii Ibrahim aliekusudiwa kua ni Dhabih Allah yaani anaetolewa Kafara kwa Ajili ya
357

Allah basi haikuweka wazi alikua ni mtoto gani baina ya watoto wawili watukufu wa
Nabii Ibrahim ambao wote walikua ni Mitume na Manabii ambapo miongoni mwao basi
Is-haq ametajwa ndani ya Qurán mara 17 na Ismail ametajwa mara 12 na ingawa Ismail
ametajwa mara kidogo zaid ya Is-haq lakini yeye Ismail ametajwa katika matukio
muhimu zaid yaliyotokea katika Historia ya Kiislam katika kipindi cha uhai wao Mitume
hawa, kwa mfano katika hatua za ujengaji wa Bayt Allahi Al Haram katika mji wa
Makkah kama tutakavyoona hapo baadae katika kurasa zinazofuatia za Kitabu hiki.

Tunapoangalia historia ya kizazi cha Nabii Ibrahim basi tunaona kua Qurán imeanza
kukielezea kwa mara ya kwanza pale Nabii Ibrahim alipoomba dua na Allah Subhanah
wa Taála akamjibu dua hiyo katika aya zifuatazo:

﴾‫ﲔ۞ﻓَـﺒَﺸْﱠﺮَ�ﻩُ ﺑِﻐُﻼٍَم َﺣﻠِﻴ ٍﻢ‬


ِ ‫ﺼـﻠِ ِﺤ‬
‫ﺐ ِﱃ ِﻣ َﻦ اﻟ ﱠ‬ ِّ ‫﴿ َر‬
ْ ‫ب َﻫ‬
Rabbi hab lee mina alssaliheena: Fabashsharnahu bighulamin haleemin (Surat As
Saffat 37: 100-101)

Tafsir: Ya Rabbi nijaalie kua ni mwenye kizazi chema. Hivyo nasi tukambashiria juu
ya mtoto wa kiume mwenye ustahmilivu.

Aya hii inaonesha Dua ambayo Nabii Ibrahim aliiomba mara tu baada ya kuhama kutoka
katika Ardhi ya Iraq na kuhamia katika Ardhi ya Sham ambapo alipofika katika mji wa
Syria akamuomba Mola wake Allah Subhanah wa Taála kua amjaalie apate kizazi bora,
ambapo Allah Subhanah wa Taála akamkubalia Dua hiyo kwa kumwambia kua atampa
mtoto mwema wa kiume tena mwenye Subra na ustahmilivu.

Ingawa wengi miongoni mwa Wanazuoni wanasema kua mtoto huyu aliemaanishwa
katika ayah hii ya Surat Saffat 37:101 inayoonesha kukubaliwa kwa dua ya Nabii Ibrahim
kua ni Nabii Ismail ambae aliitwa Ismail kwa sababu neno Ismail limetokana na maneno
mawili ya lugha ya Kiyahudi ambayo ni ‘Sama’ na ‘Ail’ ambapo neno Sama maana yake
ni Kusikia, na neno Ail maana yake hua ni Mungu, hivyo basi Ismail maana yake
Nimekusikia, yaani Allah Subhanah wa Taála anamwambia Nabii Ismail kua amemsikia
kauli yake ya kujisalimisha kwake kwa Yaqini na Ikhlas.

Na hii inaonesha kua Nabii Ismail ndie aliekua mtoto wa mwanzo kuzaliwa na ndio
maana akawa anatajwa mwanzo kabla ya Nabii Is-haq katika aya ambazo zimewataja
Mitume hao wote wawili kwa pamoja kwa mfano kama zinavyoonesha aya mbili
zifuatazo:
358

ِ ‫ﭑﻪﻠﻟِ وﻣﺂ أُﻧْ ِﺰَل إِﻟَﻴـﻨَﺎ وﻣﺂ أُﻧ ِﺰَل إِ َ ٰﱃ إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ وإِ ْﲰ‬ ِ ۤ ُ‫﴿ﻗﻮﻟ‬
َ ‫ﻴﻞ َوإِ ْﺳ َﺤ‬
‫ﺎق‬ َ ‫ﺎﻋ‬ َ َ َ َْ ََ ْ ََ ‫ﱠ‬ ‫ﺑ‬ ‫ﱠﺎ‬
‫ﻨ‬ ‫آﻣ‬
َ ُ‫ا‬
ْ‫ﻮ‬
َ‫ﻴﺴ ٰﻰ َوَﻣﺎ أُوﺗِ َﻰ ٱﻟﻨﱠﺒِﻴﱡﻮ َن ِﻣﻦ ﱠرّﻬﺑِِ ْﻢ ﻻ‬
َ
ِ ‫ﺎط وﻣﺂ أُوﺗِﻰ ﻣﻮﺳﻰ و‬
‫ﻋ‬ َ ٰ َ ُ َ َ َ
ِ ‫وﻳـﻌ ُﻘﻮب وٱﻷَﺳﺒ‬
َْ َ َ ْ ََ
﴾‫َﺣ ٍﺪ ِّﻣْﻨـ ُﻬﻢ وَْﳓﻦ ﻟَﻪُ ُﻣﺴﻠِﻤﻮ َن‬ َ‫ﲔأ‬ َ ْ ‫ﻧـُ َﻔِّﺮ ُق ﺑَـ‬
ُ ْ ُ َْ
Qooloo amanna biAllahi wama onzila ilayna wama onzila ila ibraheema wa-
ismaAAeela wa-ishaqa wayaAAqooba waal-asbati wama ootiya moosa waAAeesa
wama ootiya alnnabiyyoona min rabbihim la nufarriqu bayna ahadin minhum
wanahnu lahu muslimoona (Surat Al Baqara 2:136)

Tafsir: Semeni (Enyi Waislam): ‘Tumeamuamini Allah na tulivyoteremshiwa, na


alivyoteremshiwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haq na Yaqub na Al Asbati (Watoto 12 wa
Nabii Yaqub) na kile alichoshushiwa Musa, na Isa na walivyoshushiwa Manabii
kutoka kwa Mola wao. Hakika sisi hatutofautishi baina yao na kwake yeye (Allah
Subhanah wa Taála) tumejisalimisha’.

Na katika aya ifuatayo:

‫ﲔ ِﻣﻦ ﺑَـ ْﻌ ِﺪﻩِ َوأ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إِ َ ٰﱃ إِﺑْـَﺮِﻫ َﻴﻢ‬ ٍ ُ‫ﻚ َﻛ َﻤﺂ أ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إِ َﱃ ﻧ‬
َ ِّ‫ﻮح َوٱﻟﻨﱠﺒِﻴ‬ َ ‫﴿إِ ﱠ� أ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إِﻟَْﻴ‬
‫ﺲ َوَﻫ ُـﺮو َن َو ُﺳﻠَْﻴ َﻤ َـﻦ‬ ُ‫ﻧ‬‫ﻮ‬ ‫ﻳ‬‫و‬ ‫ﻮب‬ ‫ﱡ‬‫ﻳ‬َ
‫أ‬‫و‬ ‫ﻰ‬ ‫ﻴﺴ‬ ِ ‫ﺎط و‬
‫ﻋ‬ ِ ‫وإِ ْﲰـﻌِﻴﻞ وإْﺳﺤـﻖ وﻳـﻌ ُﻘﻮب و ْاﻷَﺳﺒ‬
َ ُ َ َ َ ٰ َ َ َْ َ َ ْ ََ َ َ ْ َ َ َ َ
ِ َ ‫وءاﺗَـﻴـﻨَﺎ داوود زﺑﻮراً ۞ ورﺳﻼً ﻗَ ْﺪ ﻗَﺼﺼﻨَـﻬﻢ ﻋﻠَﻴ‬
‫ﺼ ُﻬ ْﻢ‬ْ‫ﺼ‬ ُ ‫ﻚ ﻣﻦ ﻗَـْﺒ ُﻞ َوُر ُﺳﻼً ﱠﱂْ ﻧَـ ْﻘ‬ ْ َ ُْ ْ َ ُ َُ َُ َ ُ َ ْ َ َ
ِ ‫ﻳﻦ ﻟِﺌَﻼﱠ ﻳَ ُﻜﻮ َن ﻟِﻠﻨ‬
‫ﱠﺎس‬ ِِ
َ ‫ﻳﻦ َوُﻣﻨﺬر‬
ِ ِ
َ ‫ﻮﺳﻰ ﺗَ ْﻜﻠﻴﻤﺎً ۞ ﱡر ُﺳﻼً ﱡﻣﺒَ ّﺸ ِﺮ‬ ‫ﻚ َوَﻛﻠﱠ َﻢ ﱠ‬
َ ‫اﻪﻠﻟُ ُﻣ‬ َ ‫َﻋﻠَْﻴ‬
﴾ً‫ٱﻪﻠﻟُ َﻋ ِﺰﻳﺰاً َﺣ ِﻜﻴﻤﺎ‬ ‫ٱﻪﻠﻟِ ُﺣ ﱠﺠﺔٌ ﺑَـ ْﻌ َﺪ اﻟﱡﺮ ُﺳ ِﻞ َوَﻛﺎ َن ﱠ‬ ‫َﻋﻠَﻰ ﱠ‬
Inna awhayna ilayka kama awhayna ila noohin waalnnabiyyeena min baAAdihi
waawhayna ila ibraheema wa-ismaAAeela wa-ishaqa wayaAAqooba waal-asbati
waAAeesa waayyooba wayoonusa waharoona wasulaymana waatayna dawooda
zabooran; Warusulan qad qasasnahum AAalayka min qablu warusulan lam
naqsus-hum AAalayka wakallama Allahu moosa takleeman; Rusulan
mubashshireena wamundhireena li-alla yakoona lilnnasi AAala Allahi hujjatun
baAAda alrrusuli wakana Allahu AAazeezan hakeeman (Surat An Nisaa 4:163-165)
359

Tafsir: Hakika tumekushushia Wahyi wewe kama vile tulivyomshushia Nuh na


Manabii waliofuata baada yake. Na pia tulimshushia Wahyi Ibrahim, Isma`il, Ishaq,
Ya`qub, na Al-Asbat (Watoto 12 wa Nabii Ya`qub ambao ni Simeon) `Isa, Ayyub,
Yunus, Harun, na Sulayman; na Daud tukampa Zabur. Na Mitume ambayo
tumekutajia wewe kabla, na Mitume ambayo hatukukutajia, na Musa aliezungumza
moja kwa moja na Allah. Mitume kama wabebaji ujumbe mwema na maonyo pia, ili
watu wawe hawana kisingizio baada ya (kutumiwa) Mitume. Hakika Allah ni mwenye
Uwezo na ni mwingi wa Hikma.

Lakini kuna kutofautiana kimtizamo juu ya kua Mtoto wa kwanza wa Nabii Ibrahim
alikua ni nani baina ya Ismail na Is-haq, yaani kuna wasemao kua alikua ni Ismail na
kuna wasemao kua alikua ni Is-haq, jambo ambalo limepelekea kutokea kwa mitizamo
tofauti pia juu ya kua ni mtoto gani aliyetakiwa awe Dhabihu Allah na hivyo akawa ni
mwenye kuzungumziwa katika aya ifuatayo:

ۤ ‫ﺎل ٰﻳـﺒـ‬
ِّ‫ﲎ إِِّﱐ أ ََر ٰى ِﰱ ٱﻟْ َﻤﻨَ ِﺎم أ‬
َ ُ‫َﱏ أَ ْذ َﲝ‬
‫ﻚ ﻓَﭑﻧﻈُْﺮ َﻣﺎ َذا‬ ‫﴿ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ ﺑَـﻠَ َﻎ َﻣ َﻌﻪُ ٱﻟ ﱠﺴ ْﻌ َﻰ ﻗَ َ ُ َﱠ‬
﴾‫ﺼﺎﺑِ ِﺮﻳﻦ‬ ِ ‫ﺖ ٱﻓْـﻌﻞ ﻣﺎ ﺗُـ ْﺆﻣﺮ ﺳﺘَ ِﺠ ُﺪِ ۤﱐ إِن َﺷﺂء ﱠ‬ ِ َ َ‫ﺗَـﺮ ٰى ﻗ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻣ َﻦ ٱﻟ ﱠ‬ َ َ ُ َ َ ْ َ َ‫ﺎل ٰ�َﺑ‬ َ
Falamma balagha maAAahu alssaAAya qala ya bunayya innee ara fee almanami
annee adhbahuka faondhur madha tara qala ya abati ifAAal ma tu/maru
satajidunee in shaa Allahu mina alssabireena (Surat Saffat 37:102)

Tafsir: Kisha Mtoto wake alipokua Mkubwa kiasi ya kua ni mwenye kutembea nae
(Ibrahim) Akasema: Ewe Mtoto Wangu Hakika mimi naona usingizini kua
nakuchinja, Hebu fikiria Jee unaonaje juu ya hili? Nae (Mtoto huyo) akajibu: Ewe
Baba yangu hakika fanya kama unavyoamrishwa, In-shaa-Allah mimi nitakua ni
miongoni mwa wenye kua na subra.

Kwani kuna wanaosema kua mtoto husika alikua ni Is-haq ambao huu ni mtizamo wa
Masahaba wakiwemo Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu, Ali Ibn Abi Talib Radhi
Allahu Anhu, Abda Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu, Abbas Ibn Abd al Mutallib
Radhi Allahu Anhu. Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu, Ikrimah Radhi Allahu Anhu na pia
miongoni mwa Tabiina waliofuatia baada yao ambapo tunaona kua wenye mtizamo huu
pia kua ni Qatadah, Kab Al Ahbar, Said Ibn Jubayr, Al Qasim Ibn Abui Birrah, Masruq
ibn Ajda, Abd Rahman Ibn Abi Thabit, Abu Al Huzayl, Imam Al Zuhri, Imam Ismail Ibn
Abd Rahmad Imam Ismail Abd Rahman Al Suddi, n.k.
360

Ambapo mtizamo wa Imam Ismail Abd Rahman Al Suddi ni ule usemao kua: Wakati
Nabii Ibrahim alipotembelewa na wajumbe wawili ambao waliotumwa kuelekea Al
Mutafikah, yaani miji ya Nabii Lut iliyoangamizwa, basi walimbashiria Nabii
Ibrahim habari njema ya kupata Mtoto kama isemavyo aya inayofuatia:

ِ ‫ﺎق وِﻣﻦ ور‬


َ َ َ ْ َ َ َ َ ‫﴿ ﻓَـﺒَﺸْﱠﺮَ� َﻫﺎ ﺈﺑِِ ْﺳ َﺤ‬
﴾‫ﻮب‬ ‫ﻘ‬
ُ ‫ﻌ‬
ْ ‫ـ‬ ‫ﻳ‬ ‫ﺎق‬
َ ‫ﺤ‬ ‫ﺳ‬ِ‫إ‬ ‫آء‬
Fabashsharnaha bi-ishaqa wamin wara-i ishaqa yaAAqooba (Surat Hud 11:71)

Tafsir: Kisha tukambashiria juu ya Is-haq na baada ya Is-haq Yaqub.

Ambapo Sarah akajipiga vibao usoni kwa kuona ni maskhara gani haya! kama
inavyosema aya inayofuatia:

﴾ ‫ﻮز َﻋ ِﻘ ٌﻴﻢ‬
ٌ ‫ﺖ َﻋ ُﺠ‬ ْ ‫ﺼ ﱠﻜ‬
ْ َ‫ﺖ َو ْﺟ َﻬ َﻬﺎ َوﻗَﺎﻟ‬ َ َ‫ﺻﱠﺮةٍ ﻓ‬
ِ
َ ‫﴿ ﻓَﺄَﻗْـﺒَـﻠَﺖ ْٱﻣَﺮأَﺗُﻪُ ِﰱ‬
Faaqbalati imraatuhu fee sarratin fasakkat wajhaha waqalat AAajoozun
AAaqeemun (Surat Adh Dhariyyat 51:21)

Tafsir: Akakabili Mke wake kwa sauti kubwa, huku akiupiga vibao uso wake na
kusema: Ajuza alie tasa!

Na pale aliposema Sara katika aya isemayo:

﴾‫ﻴﺐ‬ ِ ِ ِ ِ
ٌ ‫ﻮز َوَﻫـٰ َﺬا ﺑَـ ْﻌﻠﻰ َﺷْﻴﺨﺎً إ ﱠن َﻫـٰ َﺬا ﻟَ َﺸ ْﻲءٌ َﻋﺠ‬ ْ َ‫﴿ﻗَﺎﻟ‬
ٌ ‫ﺖ ٰﻳـ َﻮﻳْـﻠَﺘَﺎ أَأَﻟ ُﺪ َوأ ََ�ْ َﻋ ُﺠ‬
Qalat ya waylata aalidu waana AAajoozun wahadha baAAlee shaykhan inna hadha
lashay-on AAajeebun (Surat Hud 11:72)

Tafsir: Akasema: Ole wangu! Nitapata Mtoto wakati mie ni Ajuza na huyu Mume
wangu ni Mzee, hakika hili ni jambo la Maajabu.

Ambapo hapa Sarah akamwambia Jibril: ‘Jee kutakua na dalili gani?’. Jibril
akaokota kijiti kikavu kisha akakipinda katika vidole vyake na kikabenuka na
kugeuka kua ni kijiti kibichi chenye rangi ya kijani, hapa Nabii Ibrahim akasema:
‘Hii inamaanisha kua atakua ni Dhabihu Allah!’
361

Anasema Ibn Yassar kua: ‘Sarah alipata ujauzito wa Is-haq wakati Hajar akiwa
tayari ana uja uzito wa Ismail. Na watoto hawa walizaliwa katika kipindi kimoja
bila ya kupishana sana na hivyo watoto hawa walikua wakicheza na kukulia
pamoja. Siku moja walipokua wakishindana kutunga shabaha kwa kutumia Upinde
na Nabii Ibrahim akawa ni jaji wao, basi Ismail akashinda mashindano hayo.

Hivyo Nabii Ibrahim akampakata Ismail kumpongeza, kisha Is-haq akawa ni


mwenye kusimama pembeni yao. Akatokea Sarah na kuona tukio hili na hivyo
akamwambia Nabii Ibrahim: ‘Umemchukua mtoto wa mjakazi na kumpakata
wakati wangu mie umemwacha amesimama, huku ukiwa umeahidi kutonidhuru
mimi wala kunifanya nijisikie vibaya?’ Wivu ukamjaa Sarah na kuamua kua Hajar
atobolewe ndewe za Masikio yake ili kuonesha tofauti baina yao. Na huo ndio
mwanzo wa Wanawake kua ni wenye kutobolewa masikio kwa ajili ya kuvaa
herini.’

Ama kwa upande mwengine basi kuna wasemao kua Sarah alisema kua ‘Hakika mimi
nitamkata Hajar Pua, au nitamtoboa Masikio yake, lakini la! Bora nitamfanyia
Khitan.’ Hivyo Sarah akamtahiri Hajar na hio ikawa ndio asili ya Wanawake kua pia ni
wenye kufanyiwa Khitan yaani kua ni wenye kutahiriwa. Khitan hua ni sehemu ya
kujifanyia usafi wa mwili wa Ibn Adam, kama vile ilivyokua ni kawaida kwa Ibn Adam
kukata Kucha, Kunyoa nywele, Ndevu n.k.


KHITAN YA WANAWAKE KATIKA UISLAM.

Ama tunapozungumzia juu ya Khitan kwa upande wa wanawake, basi Wanazuoni
wametofautiana juu ya jambo hili. Kwani kwa upande wa Wafuasi wa Madhhab ya Imam
Abu Hanifa na Imam Malik basi wao wanasema kua Khitan ya Wanawake ni Sunna
inayotiliwa mkazo, ama kwa upande wa wafuasi wa Madhhab ya Imam Ahmad Ibn
Hanbal basi wao wanasema ni Sunna na kwa upande wa Madhhab ya Imam Al Shafii
basi wao wanasema kua ni Wajib. Lakini hata hivyo kwa kua siku hizi utaalamu huo wa
kufanya Khitan umekua adimu kiasi ya kua watu wanakeketa zaidi ya inavyotakiwa basi
jambo hili hua ni lisilokubalika.

Kwa sababu kukata zaidi ya ilivyoamrishwa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
hua ni kuenda kinyume na Maamrisho yake kwa kuzidisha na kuvuka mipaka, na hii ni
kulingana na mitizamo ya Mwanazuoni mkubwa wa karne yetu ambae ni wa Madhhab
ya Imam Al Shafii Mufti Ali Juma aliekua Mufti Mkuu Misri na pia Mufti wa Chuo
362

Kikuu cha Al Azhar cha Misri ambae anasema kua: ‘Khitan wanayofanyiwa
Wanawake siku hizi ni yenye kuwadhuru Wanawake kiakili na kimwili. Hivyo
Khitan hii inabidi isifanyike, ili kuunga mkono moja kati ya Malengo Makuu ya
Sharia za Dini ya Kiislam ambalo ni ‘Usidhuru wala Usijidhuru’ na hii ni kulingana
na kauli ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Usijdhuru wala
Usiwadhuru wenzako’ na hii pia hua ni kumvunjia mtu haki zake na hivyo hua ni
jambo la kuadhibiwa kwa anaelifanya.’

Kwani kulingana na mtizamo wa Imam Ibn Hazm na Imam Ibn Qudamah pia basi
wanasema kua: ‘Inapotokea Mwanamke akakatwa zaidi ya inavyotakiwa basi hua
kuna wajibu wa kulipwa fidia anayolipwa mtu ambae amedhulumiwa sehemu ya
kiungo cha mwili wake.’(Al Mahali Imam Ibn Hazm, na Al Mughni Imam Ibn
Qudamah.)

Na huo pia ndio mtizamo wa Wanazuoni Wakubwa wengine wa karne yetu akiwemo
Mufti Muhammad Said Al Tantawi, Mufti Ahmad Al Shaltut ambao wote walikua
Mamufti wakuu wa Misri na pia wa Chuo Kikuu cha Al Azhar, Shaykh Al Qaradawi,
Mufti Muhammad Lufti Al Sabagh n.k. na hukmu hii inatokana na mtizamo wa Hujjat ul
Islami Imam Abu Hamid Ibn Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali
ambae pia ni miongoni mwa waanzilishi wa I’lm ya Maqasid al Shariyyah (Makusudio
ya Sharia) pale aliposema: ‘Asilimia 90 ya Ufahamu wa Masuali ya Kifiqh hua
yanategemeana na Mwanafiqh kufaham maslahi ya jamii na uhalisi wa mazingira
waliyonayo. Hata kama utaalamu wa mtu katika maandiko (Qurán na Hadith) hua
ni wenye kuchukua asilimia 10 tu ya Fiqh.’

Ama juu ya vithibitisho vya mtizamo wa Madhhab ya Imam Al Shafii juu ya jambo hili
la Khitan kua ni Wajib basi tunaona kua anasema Imam Ibn Hazim katika Maratib al
Ijmaa kua: ‘Kuna makubaliano ya Ijmaa kua Khitan kwa wanawake ni jambo
lililoruhusika.’

Kwa upande mwengine basi Imam Shams Al Din Muhammad Ibn Ahmad Ibn Hamzah
Al Ramli Al Shafii maarufu kama Al Shafii Al Saghir anasema katika Nihayat Al Muhtaj
Sharh Al Muhtaj kua: ‘Mtizamo wa Mkuu wa Madhhab ya Al Imam Al Shafii juu ya
Khitan kua ni Wajib kwa Mwanamme na kwa Mwanamke, ama kwa Mwanamke
basi hua ni kuondoa sehemu kidogo tu iliyozidi inayofunika Kinembe au Kisimi.’

Na huo ndio pia mtizamo wa Al Faqih Imam Ibn Hajar Al Haytam katika kitabu chake
cha Tuhfah Al Muhtaj ambapo katika vitabu hivi basi tunaona kua vimetumia neno Bazr
ambalo maana yake hua ni sehemu ndogo iliyozidi katika sehemu inayofunika Kinembe.
Huu ndio Mtizamo unaojulikana kama Qawl Al Mutammad yaani mtizamo Unaokubalika
katika Madhhab ya Imam Al Shafii.
363

Hivyo Khitan ya Mwanamke haijumuishi kukatwa Kinembe au Kisimi au Mashavu yote


ya pembeni. Kwa sababu Kinembe, Kisimi na Mashavu ni sehemu ya viungo vya
Mwanamke ambayo vina kazi yake maalum ikiwemo kuhifadhi viungo vyengine vya uke
wa Mwanamke, kusaidia kuzalisha maji ya kimaumbile yanayohitajika kuwepo ili
kuharakisha hisia na kurahisisha kitendo cha kuingiliana kimapenzi baina ya Mume na
Mke kwa kuuroanisha Uke maji wakati wa Kuingiliana na wakati wa kujifungua,
kusaidia katika kuleta ukaribu wa kihisia baina ya Mke na Mume, kusaidia kuongeza
hisia za raha kwa Mwanamke katika wakati wa kuingiliana na pia kusaidia kuondoa
uchafu wa Uke na hivyo kua ni kiungo vinavyosaidia katika usafi wa uke kwa ujumla.

Na vile vile kwa upande mwengine basi kuna Mtizamo mwengine pia katika Madhhab
ya Imam Al Shafii ambao umetajwa na Imam An Nawawi katika Rawdat Talibin ambao
ni wenye kusema kua: ‘Khitan ni jambo linalopendekezwa’. Huu ni mtizamo wa Qawl
ul Mashhur yaani ni mtizamo Mashuhuri lakini hauna nguvu kwani sio mtizamo
unaokubalika katika Madhhab.

Imam Al Suyuti amezungumzia kuhusiana na kutahiriwa kwa Mitume na Manabii katika


ushairi kwa kuwataja miongoni mwao ni pamoja na Adam, Seth, Nuh, Sham, Idris, Musa,
Saleh, Lut, Yusuf, Shuaib, Yunus, Sulayman, Yahya na Isa Ibn Maryam Sala na Amani
ziwe juu yao. Na ushairi huo unamalizia na “Hatam Al Anbiyah (na Mtume wa
mwisho)” yaani Nabii Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam.

Tunapoangalia kitabu cha Muwatta cha Imam Malik basi tunaona kinasema kua:
‘Hakika mtu wa kwanza kuwakaribisha wageni nyumbani kwake, na alievaa
suruali ya ndani kwa mara ya kwanza na aliefanyiwa khitan kwa mara ya kwanza
alikua ni Nabii Ibrahim’. Na kisha baadae ndio Manabii wengine wakafanyiwa wengine
na watu wao. Na ingawa baadhi wanaweza kusema kua hio inayozungumziwa hapo ni
Khitan ya Wanaume lakini kwa upande mwengine basi tunaona kua kuna jamii za watu
ambao walikua walikua wakiwatahiri wanawake zao hata kabla ya kuja kwa Uislam
katika jamii hizo, kwa mfano: Takriban watu wote wa Uarabuni walikua na asili ya
kufanya hivyo kabla ya kuja Uislam, Watu wa Misri na hata watu wa Java
Indonesia pia.

Ama tunapoiangalia Khitan kisharia basi hua inaingia pia katika kanuni ya Fiqh isemayo
kua: ‘Kusababisha maumivu kwa Kiumbe hua inakubalika pale tu inapokua
matokeo ya kusabishwa kwa maumivu hayo yatakua ni kuleta manufaa baada
yake.’

Kwa upande wa manufaa ya kutahiriwa kwa Wanaume basi tunaona kua Wanasayansi
wamethibitisha kua: ‘Idadi ya waathirika wa maradhi ya fuko la uzazi kwa miongoni
mwa Wanawake wanaoishi katika jamii ambazo Wanaume wao wametahiriwa, iko
364

chini sana kuliko ile idadi ya waathirika wa maradhi hayo ambao ni wenye kuishi
katika jamii ya Wanaume waliokua hawajatahiriwa’

Kwa upande mwengine basi tunaona kua ingawa Khitan kwa baadhi ya Wanawake hua
ni yenye madhara pale inapofanywa sivyo kwa kukeketwa au kukatwa zaidi ya
inavyokubalika Kisharia lakini kwa upande mwengine basi hua ina faida hususan kwa
wale ambao ni wenye kua na mashavu makubwa kwani hua yanakera kwa kuingia ndani
ya uke wakati wa kuingiliana na Waume zao na hivyo kusababisha maumivu pia, na pia
hua ni yenye kuwasha yanapogusana na baadhi ya aina fulani za vitambaa vya nguo za
ndani, hususan katika wakati wa kutembea kwa miguu au wakati wa kuendesha kipando,
n.k’.

Ama tunapozungumzia Bazr yaani sehemu ndogo iliyozidi katika sehemu inayofunika
Kinembe au Kisimi inapofanyiwa Khitan inayokubalika kwa sharia za Kiislam basi hua
ni yenye kuongeza hisia za raha kwa Mwanamke pale anapoingiliana na Mume wake
kwa sababu Kinembe au Kisimi hua kiko karibu sana na nje na kinapoguswa au
kupapaswa basi hamu ya kuingiliana kwa upane wa mwanamke hua inaogezeka zaid, n.k.
na ndio maana Wanawake wengi wa nchi za Magharibi hua ni wenye kupenda kufanya
Khitan ya Bazr na ya Mashavu pia ambayo wao hua ni wenye kuiita Vaginoplasty au
Vagina Beautification (Marekebisho ya Uke, au Mapendezesho ya Uke), na kuna vituo
(clinic) maalum na vya bei ghali zenye wataalamu wenye kushughulikia Khitan
(Vaginoplasty au Vagina Beautification).

Tunarudi katika kisa chetu na kuona kua baada ya Hajar kufanyiwa Khitan basi maisha
yakaendelea kama kawaida hadi pale siku moja Ismail na Is-haq walipopigana katika
kucheza kwao kama ilivyo kawaida ya watoto wengine wote, hivyo Sarah akamwambia
Hajar kua: ‘Mimi nadhani wewe itakubidi uhame kutoka katika mji huu na uhamie
katika mji ulio mbali nami’. Sarah akamshauri Nabii Ibrahim kumhamisha Hajar na
Ismail katika mji mwengine. Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamshushia Wahy Nabii
Ibrahim kuihamishia familia yake hio katika mji wa Makkah ambao upo katika umbali
wa kilomita 1496 Kusini Mashariki ya Mji wa Jerusalem.

Ama kwa upande wa Mujaddid Ad Din Al Hafidh Imam Ibn Hajar Al Asqalani anasema
katika Fath Al Baar kua: ‘Inasemekana kua Sarah alikua ana Wivu mkubwa sana
hivyo Nabii Ibrahim akamhamisha Ismail na Mama yake na kuwapeleka katika Mji
wa Makkah.

Kwani amesema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Pale kilipotokea
kkilichotokea baina ya Wake wa Nabii Ibrahim basi Nabii Ibrahim akatoka na
Hajar na Ismail huku akiwa amebeba Siqaa - Mfuko wa Ngozi - Uliokua umejaa
Maji’’ hivyo maneno ya Ibn Abbas aliyosema kua: ‘Pale kilipotokea kilichotokea
365

baina ya Wake wa Nabii Ibrahim’ yanamaanisha: ‘Kuhusiana na Wivu wa Sarah


pale Hajar alipomzaa Ismail.’



GHIRA NA HASAD KATIKA UISLAM.



Amesema Allah Subhanah wa Ta’ala kuhusiana na Wivu katika Qur’an kua:

ً‫﴿إِن َْﲡﺘَﻨِﺒُﻮاْ َﻛﺒَﺂﺋَِﺮ َﻣﺎ ﺗـُْﻨـ َﻬ ْﻮ َن َﻋْﻨﻪُ ﻧُ َﻜ ِّﻔْﺮ َﻋْﻨ ُﻜ ْﻢ َﺳﻴِّﺌَﺎﺗِ ُﻜ ْﻢ َوﻧُ ْﺪ ِﺧ ْﻠ ُﻜ ْﻢ ﱡﻣ ْﺪ َﺧﻼً َﻛ ِﺮﳝﺎ‬
ْ‫ﻴﺐ ِّﳑﱠﺎ ٱ ْﻛﺘَ َﺴﺒُﻮا‬ ِ ِ ِ ٍ ‫ﻀ ُﻜﻢ ﻋﻠَﻰ ﺑـﻌ‬
ٌ ‫ﺾ ﻟّ ِّﻠﺮ َﺟﺎل ﻧَﺼ‬ ْ َ ٰ َ ْ َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﺑِﻪ ﺑَـ ْﻌ‬
ِ ‫۞وﻻَ ﺗَـﺘَﻤﻨـﱠﻮاْ ﻣﺎ ﻓَﻀﱠﻞ ﱠ‬
َ َ َْ َ
‫ٱﻪﻠﻟَ َﻛﺎ َن ﺑِ ُﻜ ِّﻞ َﺷ ْﻲ ٍء‬
‫ﻀﻠِ ِﻪ إِ ﱠن ﱠ‬ ِ ‫ﺼ‬ ِ ِ ِِ
ْ َ‫ٱﻪﻠﻟَ ِﻣﻦ ﻓ‬ ‫ٱﺳﺄَﻟُﻮاْ ﱠ‬ ْ ‫ﱭ َو‬ َ ْ ‫ﻴﺐ ّﳑﱠﺎ ٱ ْﻛﺘَ َﺴ‬ ٌ َ‫َوﻟﻠﻨّ َﺴﺂء ﻧ‬
﴾ً‫َﻋﻠِﻴﻤﺎ‬
Wala tatamannaw ma fadhdhala Allahu bihi baAAdhakum AAala baAAdhin
lilrrijali naseebun mimma iktasaboo walilnnisa-i naseebun mimma iktasabna wais-
aloo Allaha min fadhlihi inna Allaha kana bikulli shay-in AAaleeman (Surat An
Nisaa 4:32)

Tafsir: Na msitamani vile ambavyo Allah amewafadhilisha baadhi juu ya baadhi ya


wengine. Kwani kwa kila Mtu hua kuna malipo yake kutokana aliyoyachuma na kwa
Wanawake hua kuna malipo yake kutokana na aliyoyachuma, na muombeni Allah
fadhila zake, kwani kwa hakika Allah ni mwenye kujua juu ya kila kitu.

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala aliishusha ayah hii baada ya Umm ul Muuminina
Umm Salamah Radhi Allahu Anha alipotaka kujua kuhusiana na kwa nini Allah
Subhanah wa Ta’ala akaamrisha kua Wanaume wapate sehemu kubwa zaidi ya Urithi
tofauti na Mwanamke.

Hivyo ayah hii ilikua ni jibu la suali hilo ambalo kwa upande mmoja hua limetokana na
Wivu na pia kwa upande wa pili ni lenye kutokana na kutaka kujua sababu ya Hukmu
hio, ambapo tunapozungumzia kuhusiana na hisia za wivu basi Allah Subhanah wa
366

Ta’ala ametuwekea wazi kua ametuumba Ibn Adam na maumbile ya kua na hisia hizo
kwa manufaa yetu kama vile ilivyokua na manufaa ya Neema za hisia nyengine
zinazoukamilisha Mfumo Kamilifu wa Ufanyaji kazi wa Maumbile ya Mwili wa Ibn
Adam, kwani kutokana na hisia hizo kua ni mwenye kujali kuhusiana na usimamiaji na
uhifadhi wa kitu kilichomo ndani ya mamlaka yake au mamlaka ya mwenzake.

Na mbali ya kua kuna Wivu wa Kimaumbile wa Viumbe kwa Viumbe lakini pia hua kuna
Wivu wa Muumba kwa Viumbe wake:-

Wivu wa Muumba kwa Viumbe wake yaani Allah Subhanah wa Ta’ala kwa Viumbe
wake pale asiporidhika na kuchangia utiifu wa Maamrisho yake (kwa
Kumshirikisha) au kutokuwepo kwa utiifu wa Maamrisho yake kutoka kwa
Viumbe wake (kwa Kumuasi), Utiifu ambao anastahiki kufanyiwa yeye peke
yake.

Ambapo kuhusiana na aina hii ya Wivu basi amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
Salam kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala anakua na Wivu na Kiumbe pia anakua na
Wivu, kwani Allah Subhanah wa Ta’ala hua na wivu pale Mja wake anapofanya
Dhambi’ (Imam Bukhari)

Na kuna Wivu wa Viumbe juu ya Viumbe:-

Wivu wa Kiumbe kwa Kiumbe mwenzake juu ya kupenda kulinda au kuhifadhi


kile kilichomo ndani ya Mamlaka yake au ndani ya Mamlaka ya Kiumbe
mwenzake.

Ambapo ndani ya wivu wa aina hii hua kuna Wivu wa Kulinda na Kuhifadhi kile
kilichomo ndani ya Mamlaka yake Mtu ambao hua ni Wivu Mzuri na pia kuna
Wivu wa Mtu kutaka au kutamani kile ambacho hakimo ndani ya Mamlaka yake
bali kimo ndani ya Mamlaka ya Ibn Adam mwenzake na huu hua ni Wivu mbaya
usiokubalika katika Uislam.

Ama kuhusiana na Wivu Mzuri na unaokubalika katika Uislam ambao ni Wivu Mzuri
ambao hua unahimizwa kwa kila Muislam kua nao basi hua ni ule ambao kila Muislam
anatakiwa kua nao kwa ajili ya kulinda na kuhifadhi kile kilichomo ndani ya mamlaka
yake, na kuhusiana Wivu wa aina hii basi amesema Abd Allah Ibn Umar Radhi Allahu
Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam kua: ‘Aina tatu za
watu hawatoinga Peponi, na Allah Subhanah wa Ta’ala hatowaangalia watu hao
katika siku ya Malipo: Yule ambae Asiekua na Utiifu kwa Wazee wake, Yule
Mwanamke ambae anawaigiza Wanaume, na yule ambae ni Dayuuth.’’ (Musnad
Imam Ahmad)
367

Ambapo maana ya Dayuudh hua ni yule Mtu ambae hana Wivu wa Kulinda na Kuhifadhi
heshima ya Wanawake waliochini ya Mamlaka yake kwa mfano Mke, watoto wake wa
Kike, Dada zake n.k na hivyo hua anawaruhusu Wanawake hao kuchanganyika na
Wanaume kwa kukaa nao pamoja au kukaa nao mbali lakini kuwonesha miili yao mbele
ya Wanaume ambao hawastahiki kuonekana nao na hivyo hua ni wenye kuamsha hisia
za hamu na matamanio ya kimwli dhidi yao. Na hivyo Dayyuth hua ni sawa na
Mwanamme ambae anaruhusu Mke wake, Dada yake au Binti yake afanye mapenzi
mbele yake bila ya yeye kua ni mwenye kujali juu ya dhambi hio.

Ambapo kuna makubaliano ya Wanazuoni pia kua: ‘Hakuna jema juu ya yule
Mwanamme ambae hana Wivu wa kulinda na kuhifadhi wale Wanawake walio
chini ya Mamlaka yake.’

Kwani amesema Al Mughirah kua amesema Sad Ibn Ubadah Radhi Allahu Anhu kua:
‘Ama mimi kama nikumuona Mwanamme akiwa na Mke wangu basi kwa hakika
nitampiga Upanga na wala si kwa Upaba wa Upanga huo. Ambapo Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam aliposikia maneno hayo basi akasema: ‘Jee mnasaajabu
kutokana na Wivu wa kulinda Heshima yake?’ Wallahi! Hakika mimi nina Wivu
wa Kulinda heshima yangu zaidi ya Wivu wake na Allah Subhanah wa Ta’ala ana
Wivu wa Kulinda Heshima yake zaidi yangu, kutokana na Wivu wake basi
amekataza madhambi ya siri na ya Dhahir, na hakuna mwenye Wivu wa Heshima
yake kama Allah’(Sahih Bukhari naMuslim)

Na anasema Imam Ibn Al Qayyim Al Jawziyah kua: ‘Wivu wa kulinda na kuhifadhi


kilicho chako hua ni sehemu ya Msingi wa Dini ya Kiislam, na yule ambae hana
Wivu wa aina hii hua ni sawa na asiekua na Dini, kwani Wivu huvihifadhi Moyo na
kuvihuisha viungo na kuhivihifadhi kutokana na maovu ya matamanio ya na kila
uovu, hivyo kukosa Wivu ndani ya Moyo hua ni sawa na kifo cha Moyo na viungo
kwa ujumla, kwani hua hakuna ulinzi hata wa madhambi madogo. Kwani mfano
wa Wivu wa kulinda na kuhifadhi katika Moyo hua ni sawa hua ni sawa na mfano
wa kinga ya Mwili inayoulinda mwli kutokana na Maradhi, hivyo nguvu ya ulinzi
huo ikikosekana basi basi hua hakuna kitu chengine chochote kitakachoweza
kuulinda mwili na madhara ya Maradhi’ (Ad DaAa Wad DaA waa’)

Ambapo Imam Mulla Ali Al Qari basi yeye anasema kua: ‘Al Dayyudh hua ni yule mtu
ambae ameridhika na maingiliano ya Kimwili ya Haramu ya Wanawake waliokua
chini yake kama vile Mkewe, Mtumwa wake au jamaa yake, au kua ni mwenye
kuridhika na kuchezeana baina yao na Wanaume wengine, na kufanya kila aina ya
dhambi kama kulewa, kudharau kujitoharisha n.k’(Mirqatul Mafatih)
368

Ama kuhusiana na Wivu wa Mtu kutaka au kutamani kile ambacho hakimo ndani ya
Mamlaka yake bali kimo ndani ya Mamlaka ya Ibn Adam mwenzake ambao hua ni Wivu
ambao unajulikana kama Ghirah au Hasad ambao hua ni Wivu mbaya na usiokubalika
katika Uislam ambapo amesema Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu kua : ‘Amesema Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: Haviunganiki kwa pamoja ndani ya Moyo wa
Muumini Wivu (Hasad) na Imani.’ (Sunan An Nasai)

Na Abda Allah Ibn Umar Radhi Allahu Anhu kua ‘Amesema Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam kuhusiana na wivu wa aina hiii kua: ‘Hairuhusiki kwa Muislam
kumuonea Wivu mwenzake isipokua juu ya:

1. Kua na Wivu juu ya Mtu ambae Allah Subhanah wa Ta’ala amemneemesha Mtu
huyo (Kitabu) Ilm na kisha akawa ni mwenye kuitumia Ilm hio usiku na mchana.
2. Kua na Wivu na Mtu ambae Allah Subhana wa Ta’ala amemneemesha Mtu huyo
Mali na Utajiri na kisha akawa ni mwenye Kuitumia Mali hio Usiku na
Mchana.’’ (Sahih Bukhari)

Ambapo kwa upande wa Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu
Bakr Al Ansari Al Qurtubi: ‘Hasad hua ni Wivu ambao Mtu mmoja hua anatamani
kua mwenzake akikose kile ambacho anakionea wivu kua nacho mwenzake huyo.
Ambapo kwa upande mwengine basi pale inapokua mtu anaona wivu lakini
hatamani kuona kua mwenzake huyo anaondokewa na kitu hicho, basi hii hua ni
hali inayojulikana kama Munafasah au Ghibt, ambapo Ghibt hua inaruhusika
kwani kwenye Hadithi ambayo inasema kua : ‘Watu wawili wanaruhusika kuonewa
wivu’ basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salaam ametumia neno Ghibt.’

Ambapo anasema Hujjat ul IslamiMujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn
Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali kua: ‘Mwenye kua na Ghira hua ni mtu
ambae hapendelei kuona kua Neema za Allah Subhanah wa Ta’ala ambazo
amemjaalia Mja wake, kwa mfano kama Ilm, Mali, Mapenzi ya Watu juu ya Mtu
husika, au jambo lolote Jema na hivyo Mtu mwenye Ghira hua ni mwenye kuona
bora mwenzake aondokewe na vitu hivyo’

Kwa upande wa Mujaddid Ad Din Imam Abu Abdullah Muhammad Idris Al Shafii basi
yeye anasem kua: ‘Ndani ya Moyo wa Mtu mwenye Ghira hua mna Moto ambao
unawaaka daima bila ya kuzima’ na Shaykh Ul Islami Imam Muhyi Ad Din Abu
Zakarriyah Yahya Ibn Sharaf An Nawawi amesema kua: ‘Ghira hua ni hali ya
Matamanio ya Mtu kutamani kua yule mwenye Neema imuondokee, iwe Neema ya
Kidini au ya Kidunia.’
369

Na Imam Muhammad Ibn Ahmad Al Safarrini Al Hanbali basi yeye alisema: ‘Mtu
mwenye Hasad hua ni mwenye kuchukia Neema ya Allah Subhanah wa Ta’ala hivyo
hua ni mwenye kuchukia kuona Neema hio ikiwa kwa Mja aliebarikiwa Neema hio.’
(Ghidha Al Albab)

Na akasema Imam Sufyan Ibn Uyaynah kua: ‘Wivu ndio Dhambi ya kwanza ambayo
Allah Subhanah wa Ta’ala aliyoasiwa Mbinguni pale Iblis alivyomuonea wivu
Adam, na ndio Dhambi ya kwanza ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala aliyo asiwa
Duniani pale Mtoto wa Adam alipomuua Kaka yake.’ (Al-Mujālasah wa Jawāhir
al-‘Ilm)

Na akasema Hasan Al Basr kua: ‘Wivu ndio uliomtoa Ibilisi Peponi.’

Ambapo Mujaddid Ad Din Al Hafidh Shihab Ad Din Abu Fadhl Imam Ibn Hajar
amesema katika Fat-h Al Barri kua: ‘Imani haikamiliki mpaka Muislam awe ni
mwenye kuachana na Hasad, Wivu, Ubinafsi, na Chuki.’

Wivu hua ni wenye kusababisha Dhambi nyingi sana na hiyvo hua ni wenye
kuangamiza Thawabu za mhusika kama alivyosema Rasul Allah Salallahu Alayhi
wa Salam katika Hadith kua: ‘Jihadharini na Wivu kwani hua ni wenye kula
mema ya mtu kama vile moto unavyokula kuni au majani makavu’

Amapo kwa upane wa wale ambao wataweza kuzidhibiti Nafsi zao kutokana na hisia
za Wivu basi hua ni wenye kupata Darja kubwa sana mbele ya Allah Subhanah wa
Taa’ala, na hii tunaliona wazo pale tunapoiangalia hadith ya Anas Ibn Malik Radhi
Allahu Anhu ambayo inasema kua: ‘Sisi tulikua tumekaa na Rasul Allah Salallahu
A’layhi wa Salam ambapo nae akasema: ‘Anaekuja mbele yenu ni miononi mwa
watu wa Peponi’ na akaja mtu miongoni mwa watu wa Ansari ambae ndevu
zake zilikua zimejaa maji ya udhu huku akiwa amekamata viatu vyake kwa
mkono wake wa kushoto.

Kisha baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kuondoka basi Abd
Allah Ibn Amr akamfuata Mtu huyo na kumwambia: ‘Hakika mimi
nimegombana na Baba yangu na nimeapa kua sitorudi nyumbani mpaka baada
ya siku 3, hivyo jee nnaweza kukaa kwako?’ yule mtu akasema : ‘Naam’’

‘Hivyo Abd Allah Ibn Amr akakaa kwa mtu huyo kwa siku 3 na kulala kwake
lakini kamwe hakuwahi kumuona mtu huyo akiamka usiku kusali Qiyamu Al
Layl. Lakini kila akipanda kitandani hua ni mwenye kumkumbuka Allah
Subhanah wa Taala na kisha hulala mpaka wakati wa Sala ya Alfajir. Abd Allah
370

Ibn Amr anasema kua kamwe hakuwahi kusikia jambo baya kutoka kwenye
ulimi wa Mtu huyo, hivyo baada ya siku 3 kumalizika, na kutoona kitu chochote
maalum kwa mtu huyo katika vitendo vyake basi akamuuliza kwa kusema:

‘Ewe Mja wa Allah, hakika mimi sikuwa ni mwenyekugombana na Baba yangu,


na wala sijavunja udugu nae. Ila nilimsikia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
Salam akisema mara 3 kua Mtu wa Peponi anakuja na kisha wewe ukaja. Hivyo
nami nikatamani kukaa nawe ili nione kile unachokifanya ili na mimi nikuige,
lakini sikuona kitu chochote maalum ambacho ulichokua ukikifanya. Hivyo
kwanini Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam amekupandisha Darja wewe?’

Yule Ansari akasema: ‘Mimi niko kama unavyoniona’. Hivyo wakati Abd Allah
Ibn Amr alipotaka kuondoka basi yule Ansari akasema: ‘Hakika mimi niko
kama ulivyoniona wewe. Isipokua hua sina kinyongo chochote ndani ya Nafsi
yangu juu ya Wislamu wenzangu, na hua simuonei wivu yeyote kutokana na
kila walichopewa na Allah Subhanah wa Ta’ala’

‘Abd Allah Ibn Amr akasema: ‘Basi hicho ndio ulichofanikiwa na ndio
ambacho sisi hatujakifikia bado’’(Musnad Imam Ahmad)

Hivyo anasema Hujjat Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn
Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali katika kutuelezea namna ya kujidhibiti na
kua madhambi ya Ghira na Hasad kua:

‘Ama kuhusiana na mambo yenye mema ndani yakebasi hua yanatakiwa


kuhukumiwa kutokana na wivu. Kwani kila chenye kusababisha wivu hua ni
chenye kuathiri maneno na vitendo, hivyo mtu huyo huwajibika kufanya
kinyume chake. Yaani kama wivu ukipelekea kumuonea wivu mtu basi mtu
huyo anaeona wivu anawajibika kuulazimisha Ulimi wake kua ni wenye
kumsifu na kumpendekeza kwa mema huyo anaemuonea wivu. Kama wivu
ukimfanya amfanyie mtu kibri, basi mtu huyo mwenye wivu uliompelekea kua
na Kibr hua na wajibu wa kuomba msamaha na kua na unyenyekevu. Haya
ndio matibabu ya Wivu na Hasad na ingawa ni machungu sana lakini hua ni
yenye manufaa makubwa sana’

Ambapo amesema Fudayl Ibn Iyad kua: ‘Kuvutiwa kwa kuhusudisha kwa mapenzi
hua ni sehemu ya Imani na kuhusudisha kwa hasad hua ni Unafiq. Muumini hua ni
mwenye kuwahusudisha Waumini wenzake kwa mapenzi na hua hawahasidi
wenzake. Na Mnafiq huwahasidi wenzake na hivyo hua hawahusudu kwa
kuwapenda wenzake. Muumini hua hayatilii maanani makosa ya mwenzake,
371

huwausia wenzake na kuwashauri katika mema, na Mnafiq huwaadhirisha


wenzake, na kuona makosa ya wenzake na huwasaliti wenzake.’(Hilyat Al Awliyaa)

Siku moja Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam aliulizwa na Masahabah zake:
‘Ya Rasul Allah Jee ni nani wabora miongoni mwa watu?’ Rasul Allah Salallahu
A’layhi wa Salam akasema: ‘Mtu bora ni yule ambae Mwenye Moyo uliokua
Msafi na Ulimi wenye kusema kweli.’ Masahaba wakasema: ‘Kwa hakika sisi
tunajua kuhusiana na Ulimi wenye kusema kweli, ila jee ndio upi Moyo uliokua
Msafi?’ Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Ni ule Moyo ambao
Msafi usiokua na uchafu wa Dhambi, Dhulma, Chuki na Hasad’(Sunan Ibn
Majah)

Hivyo Wivu na Hasad ni vitu vibaya sana kiasi ya kua Allah Subhanah wa Ta’ala
ameshusha Sura kamili ambayo ni kwa ajili ya kua ni kama kinga dhidi ya Hasad ya
mwenye kufanya uhasidi kama alivyosema katika Surat Al Falaq ambayo inamalizia
na aya ya kujikinga na Hasad isemayo:

﴾‫ﺎﺳ ٍﺪ إِذَا َﺣﺴ َﺪ‬


ِ ‫﴿وِﻣﻦ َﺷ ِﺮ ﺣ‬
َ ّ
َ َ
Wamin sharri hasidin idha hasada (Surat Al Falaq 113:3)

Tafsir: Na (Najikinga) kutokana na shari ya Hasidi Mwenye kufanya Uhasidi.

Ambapo kwa upande wa Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari basi yeye
anasema kua; ‘Maana ya maneno yasemayo Wamin sharri hasidin idha hasada basi
hua yanamaanisha kua kutokana na shari ya hasidi pale anapofanya vitendo vya
uhasidi’

Ambapo kwa upande wa Imam At Tirmidhi basi anasema kua: ‘Amesema Zubayr Ibn
Awwam Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
kua : ‘Kuna maradhi ya Ummah zilizotangulia yamekuja kwenye Ummah wenu, ni
Chuki na Wivu. Haya ni vinyozi, na sisemi kua yananyoa Nywele ila yananyoa
Imani’’(Jamii Tirmidhii)

Tunapo zungumzia wivu basi hua pia tunazungumzia hisia ambazo Ibn Adam mmoja
anapokua hawezi kukubali kua hali yake yeye iko tofauti na ya mwenzake kidarja yaani
imwenzake huyo kua yuko juu zaidi yake kwa njia moja au nyengine. Na hivyo hisia hizi
humfanya mtu kua kua na Kibri mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala, kawa sababu ni
Allah Subhaah wa Ta’ala pekee ndie aliemjaalia hali au sifa au darja aliyokua nayo
mwenzake huyo na ni Allah Subhanah wa Ta’ala ndie aliemnyima yeye sifa, hali au darja
372

hio, kwani Allah Subhanah wa Ta’ala hua ni mwenye kumjaalia kitu mtu amtakae kwa
hikma zake na humnyima amtakae kwa hikma zake, kwani kila mtu amepewa kile
ambacho ni chenye manufaa na kheri nae.

Hivyo inavyotakiwa kwa kila Muumini ni kua mwenye kuridhika na majaaliwa ya Mola
wake juu yake, na asiwe ni mwenye kuona wivu juu ya vile walivyopewa wenzake
kutokana na fadhila za Allah Subhanah wa Ta’ala juu yao kama zinavyokataza aya juu
ya Kuhusudisha huko kwa kuhoji pale ziliposema:

﴾‫ﻀﻠِ ِﻪ‬
ْ َ‫ٱﻪﻠﻟُ ِﻣﻦ ﻓ‬ ﴿
‫آﺎﺗ ُﻫ ُﻢ ﱠ‬ َ ‫أ َْم َْﳛ ُﺴ ُﺪو َن ٱﻟﻨ‬
َ ‫ﱠﺎس َﻋﻠَ ٰﻰ َﻣﺂ‬
Am yahsudoona alnnasa AAala ma atahumu Allahu min fadlihi (Surat An Nisaa
4:54)

Tafsir: Au Wanawahusudu watu kutokana na kile walichopewa na Allah kutokana na


fadhila zake?

Na pia katika kubainisha sababu ya Allah Subhnah wa Ta’ala kuwafadhilisha wengine


zaidi ya wengine kua ni kutokana na hikma zake kama zinavyosema aya:

‫ٱﳊَﻴَﺎةِ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ َوَرﻓَـ ْﻌﻨَﺎ‬


ْ ‫ﻴﺸﺘَـ ُﻬ ْﻢ ِﰱ‬ َ ِّ‫﴿أ َُﻫ ْﻢ ﻳَـ ْﻘ ِﺴ ُﻤﻮ َن َر ْﲪَﺔَ َرﺑ‬
َ ِ‫ﻚ َْﳓ ُﻦ ﻗَ َﺴ ْﻤﻨَﺎ ﺑـَْﻴـﻨَـ ُﻬ ْﻢ ﱠﻣﻌ‬
‫ﻚ َﺧْﻴـٌﺮ ِّﳑﱠﺎ‬ َ ِّ‫ﻀ ُﻬﻢ ﺑَـ ْﻌﻀﺎً ُﺳ ْﺨ ِﺮّ�ً َوَر ْﲪَﺔُ َرﺑ‬ ِ ِ ٍ
ُ ‫ﺾ َد َر َﺟﺎت ﻟّﻴَـﺘﱠﺨ َﺬ ﺑَـ ْﻌ‬ ٍ ‫ﻀ ُﻬ ْﻢ ﻓَـ ْﻮ َق ﺑَـ ْﻌ‬
َ ‫ﺑَـ ْﻌ‬
﴾‫َْﳚﻤﻌُﻮ َن‬
َ
Ahum yaqsimoona rahmata rabbika nahnu qasamna baynahum maAAeeshatahum
fee alhayati alddunya warafaAAna baAAdhahum fawqa baAAdhin darajatin
liyattakhidha baAAdhuhum baAAdhan sukhriyyan warahmatu rabbika khayrun
mimma yajmaAAoona(Surat Az Zukhruf 43:32)

Tafsir: Jee ni wao ndio wanaogawa Rehma za Mola wako? Ni sisi ndio tunaogawa
bayna yao katika maisha yao wanayoishi hapa Duniani, na tukawanyanyua daraja
baadhi kua juu ya baadhi yao, ili wawachukue baadhi yao kwa kuwaajiri katika kazi
zao. Na Rehma za Mola wako ni bora kuliko (Mali za Dunia) zikijumuishwa.

Ambapo kwa upande wa Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari basi yeye
anasema kua: ‘Ni Allah Subhanah wa Ta’ala ndie ambae anaegawa riziki baina ya
373

viumbe wake kutokana na kua yeye ndie Al Razzaq wa kila kiumbe Ulimwenguni,
hivyo kama inavyoonekana hakugawa Riziki kisawia miongoni mwa viumbe wake,
bali amegawa kwa kuwafanya baadhi kua na nguvu zaidi, baadhi kua dhaifu,
baadhi kua Matajiri, baadhi kua Masikini, baadhi kua Wamiliki wenye
kutegemewa na baadhi kua ni wenye kuwategemea wengine. Na hii ni kwa sbabu
watu wapate kutegemeana na kuingiliana kiuhusiano.

Kwani kama Allah Subhanah wa Ta’ala angewaachia watu wagawane wenyewe,


basi bila ya shaka ardhini ingekua hakuna uadilifu wala haki dhulma ingetawala
na maisha ya wengi yangeangamia’

Ama kuhusiana na hii basi linawekwa wazi na ile aya isemayo:

﴾ً‫ﻚ ﻓَِﺈذاً ﻻﱠ ﻳـُ ْﺆﺗُﻮ َن ٱﻟﻨﱠﺎس ﻧَِﻘﲑا‬


ِ ْ‫ﺼﻴﺐ ِﻣﻦ ٱﻟْﻤﻠ‬
ِ ﴿
َ ُ َ ّ ٌ َ‫أ َْم َﳍُْﻢ ﻧ‬
Am lahum naseebun mina almulki fa-ithan la yu/toona alnnasa naqeeran (Surat An
Nisaa 4:53)

Tafsir: Au wana Ujamaa katika Mamlaka (Ya Allah Subhanah wa Ta’ala) kwani kama
ni hivyo basi wasingewapa watu (riziki ya) hata ngozi laini ya kokwa ya Tende.

Naam bila ya shaka kama Allah Subhanah wa Ta’ala agejaalia kua riziki ya mtu mmoja
inatoka kwa mtu mwegine moja kwa moja basi ingekua hatari sana kwa sababu wivu na
husda ndio ingekua imetawala zaidi kwani Ibn Adam ni wenye maumbile ya kupenda
sana mapambo ya Dunia ambayo hata hivyo tumewekewa kwa ajili ya kua ni majaribio
tu juu yetu hapa Ulimwenguni kama zinavyosema aya:

ِ َ‫ات ِﻣﻦ ٱﻟﻨِّﺴ ِﺎء وٱﻟْﺒﻨِﲔ وٱﻟْ َﻘﻨ‬


‫ﺎﻃ ِﲑ ٱﻟْ ُﻤ َﻘْﻨﻄََﺮةِ ِﻣ َﻦ‬ ِ ‫ﺐ ٱﻟﺸ‬ ِ ‫﴿ ُزﻳِّ َﻦ ﻟِﻠﻨ‬
َ َ َ َ َ َ ‫ﱠﻬ َﻮ‬ َ ‫ﱠﺎس ُﺣ ﱡ‬
‫ٱﳊَﻴَﺎةِ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ َو ﱠ‬ ِ ِ ‫ٱﳊﺮ‬ ِ ِ ْ ‫ﺐ َوٱﻟْ ِﻔﻀ ِﱠﺔ َو‬ِ ‫ٱﻟ ﱠﺬ َﻫ‬
ُ‫ٱﻪﻠﻟ‬ ْ ُ‫ﻚ َﻣﺘَﺎع‬ َ ‫ث ٰذﻟ‬ َْْ ‫ٱﳋَْﻴ ِﻞ ٱﻟْ ُﻤ َﺴ ﱠﻮَﻣﺔ َوٱﻷَﻧْـ َﻌﺎم َو‬
﴾‫ﺂب‬ ِ ‫ِﻋْﻨ َﺪﻩُ ﺣﺴﻦ ٱﻟْﻤ‬
َ ُُْ
Zuyyina lilnnasi hubbu alshshahawati mina alnnisa-i waalbaneena waalqanateeri
almuqantarati mina aldhdhahabi waalfidhdhati waalkhayli almusawwamati waal-
anAAami waalharthi dhalika mataAAu alhayati alddunya waAllahu AAindahu
husnu almaabi (Surat Al Imran 3:14)
374

Tafsir: Vimependezeshwa kwa ajili ya Watu kupenda vyenye kutamanisha


vinavyotokana na Wanawake na Watoto na Wingi wa Marundo ya Dhahabu na Fedha
na Farasi (Vipando) Wazuri na Ng’ombe na Ardhi yenye Rutba, Hakika Haya ni
Mapambo ya Maisha ya Dunia na Kwa Allah ndiko kwenye Marudio Bora.

Ambapo hii ni miongoni mwa aya zilizoshuka baada ya vita vya Badr, na hivyo
kuzungumzia vita vya Badr lakini pia kwa upande mwengine basi aya hii pia inaweka
wazi kua vita, ugomvi na kufarikiana hua ni kunatokana na kugombaniana mapambo ya
Dunia kwa sababu nyingi sana ikiwemo wivu na hasad, na hivyo mapambo hayo kua ni
mtihani kwetu.
Na tunapoiangalia aya yetu hii katika kuainisha kwake mapambo hayo tunaona kua
jambo la mwanzo ililotaja miongoni mwa yaliyopendezeshwa kwa Ibn Adam kimaumbie
kupenda ni Wanawake, kisha ndio wanafuatia Watoto, na Mali kiasi ya kua hata
Mwanamme awe ni mcha Mungu kiasi gani basi kwake yeye inakua ni vigumu kujitenga
na kujidhibiti dhidi ya hisia za kimaumbile za kuwapenda Wanawake, ingawa kuna
Maimamu ambao walifanikiwa kujidhibiti na hivyo hawakua ni wenye kuoa kama Imam
Bishr Al Hafi, Al Jarir At Tabari, Imam An Nawawi, Imam Abu Is-haq Al Shirazi, Imam
Ibn Jamah, Imam Tahir Al Jazairi, Imam Abu Nasr Al Sizji n.k

Lakini hata hivyo tunaona katika Hadith ya Anas Ibn Malik Radhi Allahhu Anhu ambae
amesema kua: Siku moja Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua amekaa na
Masahaba zake, na akasema: Mambo matatu ya Dunia hii yamependezeshwa
kwangu mie: Mafuta mazuri, Wanawake na utulivu wa Salah katika macho yangu.

Ambapo Abu Bakr Radhi Allahu Anhu akasema: Hio ni Sahih! Na mimi napenda
vitu vitatu: Kuuangallia Uso wako (Ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam),
Kutumia Mali yangu kwa ajili yako na kwa ajili ya Bint yangu ambae ni Mke wako
ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.
Hapo akasema Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu: Hio ni Sahih! Na mambo
matatu nnayoyapenda mimi zaidi ni Kusimamia Haki, Kutakaza Maovu na Kuvaa
nguo za zamani.
Ambapo Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anhu akasema: Na mambo matatu
nnayoyapenda mimi zaidi ni Kuwalisha Masikini, kuwavisha Wasiokua na nguo na
Kusoma Qur’an.
Na akasema Ali Ibn Abi Talib Karam Allahu Wajh kua: Nami napenda mambo
matatu, Kuwakirimu wageni, Kufunga katika siku yenye Joto Sana na Kupigana
na maadui kwa upanga wangu.
Mara akatokea Malaika Jibril Alayhi Salam na akamwambia Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam kua: Allah Subhanah wa Ta’ala ameniambia nikuambieni kile
ninachokipenda mie kama ningekua nnakufa.?
375

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: Bila ya Shaka tuambie ewe Jibril.
Hapo Jibril akasema: Kama ningekua nyie basi ningependa mambo matatu:
Kuwaongoza watu waliopotoka, Kuwapenda wale wenye kufanya Ibada wakati
wakiwa na umasikini na napenda kumsaidia Masikini mwenye familia.
Ama kuhusiana na Allah Subhanah wa Ta’ala basi yeye anapenda sifa tatu za Mja
wake ambazo ni: Kujitahidi katika kumuelekea yeye, Kulia machozi wakati wa
kutubu na kua na Msimamo katika Wakati wa shida na Njaa.
Na kwa upande wa Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al
Ansari Al Qurtubi basi anaema kua; ‘Amesema Rasul Allah Salallahu A’layhi wa
Salam kua: ‘Wabora miongoni mwa watu wa Ummah wangu ni wale wenye wake
wengi.’(Sahih Bukhari)

Na pia kua amesema Aisha Radhi Allahu Anha kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu
A’layhi wa Salam kua: ‘Hakuna kitu anachokipenda zaidi Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam baada ya Wanawake, kama Farasi’’ ambapo hadithi kama hii ipo
tena kwenye Sunan An Nisai kutoka kwa Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu.

Na kwa upande mwengine anasema Abd Allah Ibn Amr kua: ‘Amesema Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Dunia ni Starehe na Starehe bora Duniani ni mke
alie Mwema’’(Sahih Muslim)

Hivyo tunapoziangalia Hadith hizi basi tunaona kua ingawa imezungumzia mambo
mengi lakini maneno ya Rasul Allah Salallah Alayhi wa Salam yanatufunza kua
tunatakiwa tuwe ni wenye msimamo wa kati ndani ya Nyoyo zetu pale tunapokua katika
hali ya kua ni wenye kupendana kwetu kimaumbile kwa Wanaume kupenda Wanawake
na pia kwa Wanawake kua ni wenye kupenda Wanaume, kwani kila kitu hapa
Ulimwenguni hua ni cha mpito. Na hivyo tujitahid kua ni wenye kutafuta utulivu wa
Nafsi zetu ndani ya Sala zetu, kwani ni kutokana na utulivu wa Nafsi ndani ya Sala ndio
kunakopatikana yale yenye thamani katika Akhera yetu.

Na kama tunavyona basi ni kua aya baada ya Wanawake basi ndio aya ikataja mambo
mengine wakiwemo watoto na mali Hivyo basi Waislam haina haja ya kuoneana wivu
na hasad kwa ajili ya umiliki mapambo ya kidunia, bali ni vizuri kuoneana wivu kwa ajili
ya Allah Subhnah wa Ta’ala kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
kua: ‘Pepo imefunikwa na mambo yasiyovutia wakati Moto umefunikwa na Mambo
yenye kutamanisha’(Sahih Muslim)

Na amesema Jalal Ad Din Al Rumi kua; ‘Uwachie Moyo Uogelee kweynye Bahari ya
Mapambo ya Dunia lakini Usiuwachie ukazama ndani yake.’ Kwani ukiuwachia Moyo
376

uzame ndani ya bahari ya Mapambo ya Dunia basi utaangamia kwa Wivu na Hasad na
Allah Subhanah wa Ta’ala amesema kuhusiana na Mapambo ya Dunia kua:

ِ ِ ِ‫ﻨﺪ رﺑ‬ ِ ‫ٱﳊﻴﺎةِ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴﺎ و‬ ِ


﴾‫ﲔ‬ َ َّ َ ‫ٱﻵﺧَﺮةُ ِﻋ‬
َ ‫ﻚ ﻟ ْﻠ ُﻤﺘﱠﻘ‬ َ َ َ ‫﴿ َوُز ْﺧُﺮﻓﺎً َوإِن ُﻛ ﱡﻞ ٰذﻟ‬
ََْ ُ‫ﻚ ﻟَ ﱠﻤﺎ َﻣﺘَﺎع‬
Wazukhrufan wa-in kullu dhalika lamma mataAAu alhayati alddunya waal-
akhiratu AAinda rabbika lilmuttaqeena (Surat Az Zukhruf 43:35)

Tafsir: Na mapambo ya Dhahabu, yote hayo hayakua isipokua ni starehe za Dunia hii.
Na Akhera iliyo kwa Mola wenu ni kwa ajili ya wenye Taqwa tu.

Na mapambo ya Dunia hii hua ni ya Kudunia si ya ki Akhera na ndio maana akasea Imam
At Tirmmidhi amesema kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:
‘Kama Dunia hii ingekua na Thaman ya Bawa la Mbu tu, basi asingempa mtu
aliemkufuru hata tone la maji ya kunywa.’’

Na anasema Imam Abu Hatim Muhammad Ibn Idris Ibn Al Mundhir Ibn Daud Ibn
Mahran Al Razi Al Hanzal Al Ghatafan kua: ‘Hasan Al Basr alisema kua: ‘Umar Ibn
Al Khattab aliandika Barua kwa Abu Musa Al Ashari na kumwambia: ‘Ridhika na
Riziki yako hapa Duniani, kwani Allah Subhanah wa Ta’ala amewafadhili zaidi
baadhi ya Waja wake zaidi ya wengine katika hali ya kua riziki hio kua ni kama
mtihani juu yao wote. Ambapo yule aliepewa zaidi akijaribiwa kama atamshukuru
Allah Subhanah wa Ta’ala na kutimiza wajibu wake ambao ni Wema wake na Mali
zake’’’

Kwani kutoridhika na alichokua nacho mtu ndiko kunako mpelekea mtu huyo kua ni
mwenye kumuonea Wivu na kumfanyia Hasad mwenzake. Hivyo kua na akili nyingi au
kufanya kazi kwa jitihada kubwa sana, hua sio sababu ya mtu kua ni mwenye kupata
riziki zaidi, kwani kua na zaidi hakutegemeani na akili, ufaham, wala jitihada katika
kutafuta riziki bali hua kunategemea na fadhila za Allah Subhanah wa Ta’ala juu ya mtu
husika na namna mtu husika anavyoonesha shukrani kwa Mola wake juu ya kile
alichofadhiliwa na Mola wake kama zinavyoendelea kubainisha aya:

‫آدى ِرْزﻗِ ِﻬ ْﻢ‬


ِ ِ‫ﱠ‬ ِ ِ ٍ ‫ﻀ ُﻜﻢ ﻋﻠَﻰ ﺑـﻌ‬
ِّ ُ‫ﻳﻦ ﻓ‬
ّ ‫ﻀﻠُﻮاْ ﺑَِﺮ‬ َ ‫ﺾ ﰱ ٱﻟِّْﺮْزق ﻓَ َﻤﺎ ٱﻟﺬ‬ ْ َ ٰ َ ْ َ ‫ﱠﻞ ﺑَـ ْﻌ‬ ‫﴿ َو ﱠ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻓَﻀ‬
﴾‫ٱﻪﻠﻟِ َْﳚ َﺤ ُﺪو َن‬
‫ﺖ أَْﳝَﺎﻧـُ ُﻬ ْﻢ ﻓَـ ُﻬ ْﻢ ﻓِ ِﻴﻪ َﺳ َﻮآءٌ أَﻓَﺒِﻨِ ْﻌ َﻤ ِﺔ ﱠ‬
ْ ‫َﻋﻠَ ٰﻰ َﻣﺎ َﻣﻠَ َﻜ‬
377

WaAllahu fadhdhala baAAdhakum AAala baAAdhin fee alrrizqi fama alladheena


fudhdhiloo biraddee rizqihim AAala ma malakat aymanuhum fahum feehi sawaon
afabiniAAmati Allahi yajhadoona (Surat An Nahl 16:71)

Tafsir: Na Allah amewafadhili baadhi yenu kwa baadhi ya wengine katika riziki, hivyo
jee wale waliofadhiliwa hawatorudisha riziki zao kwa wale wanaowamiliki, ili wawe
sawa ndani yake, hivyo jee watagombana kutokana na neema za Allah?

Ambapo aya inatuwekea umuhimu wa wale waliofadhiliwa zaidi kua ni wenye kuonesha
shukrani kwa Mola wao kwa kurudisha katika jamii kile walichofadhiliwa kwa
kuwasaidia wale waliochini yao, na hivyo hii hua ni yenye kuongeza mapenzi katika
jamii na hapo hapo kusaidia kupunguza napia kuondoa hisia za kuoneana wivu na husda
baina ya watu katika jamii.

Kama vile ilivyokua kwa Abd Allāh Ibn Al Muqaffa’ ambae alikua ni miongoni mwa
waja wema waiotangulia kabla yetu ambae yeye siku moja alikua amekaa nyumbani
kwake huku akiwa amefunikwa na kivuli cha Nyumba ya jirani yake. Halafu akasikia
kua jirani yake huyo anataka kuiuza nyumba yake hio kutokana na madeni aliyokua
anakabiliana nayo. Hivyo baada ya kusikia habari hio basi Ibn Al Muqaffa akaiambia
Nafsi yake kwa kusema: ‘Hakika mimi nitakua si mwenye kuheshimu utukufu wa
kivuli hiki kama ikiwa jirani yangu huyu ataiuza nyumba yake kwa ajili ya kulipia
madeni yake wakati mimi ninao uwezo wa kumlipia madeni yake.’ Hivyo Ibn Al
Muqaffah akampa jirani yakehuyo malipo ya bei aliyokua akiiuza nyumba yake na kisha
akamwambia: ‘Kalipe madeni yako, na baki nao nyumba yako.’

Ambapo katikakuhusiana na mtu kuridhika na ulichonacho basi kuna mfano mzuri wa


Ibn Al Muqaffah ambae siku moja alilalamikia kuwa kuna Panya nyumbani mwake.
Hivyo akaambiwa kua kama angekua na Paka nyumbani kwake basi ingekua afadhali
sana kwake. Hivyo Ibn Al Muqaffah akasema: ‘Hakika mimi nna khofu kua kama
nikiwa na Paka basi Panya watasikia sauti ya Paka, na kisha Paka hao watakimbilia
nyumbani kwa majirani zangu, na ivyo mimi kua ni mwenye kuwatamania majirani
zangu kilaambacho mimi sikitamani.’

Na ndio maana Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akatuusia kwa kusema kua:
‘Usiwaangalie wale walio juu yako kihali, bali waangalie wale waliochini yako na
hivyo hii itakusaidia wewe kukumbuka fadhila za Allah Subhanah wa Ta’ala juu
yako’(Sahih Muslim)

Kwa hivyo hisia za wivu tunatakiwa tujidhibiti nazo kwani ni za kimaumbile lakini
tumepewa kwa ajili ya kutunufaisha na wala zisiwe ni zenye kutuvukisha mipaka, kwani
Allah Subhanah wa Ta’ala ametupa waja wake neema nyingi sana zisizohisabika, ila ni
wachache sana wenye kuyaona haya kwani wengi wao hua hawayaoni kutokana na ujinga
378

wao wa kuangalia na kuona neema walizopewa wenzao tu na hivyo hua ni wenye


kukufuru na kujidhulumu kama alivyosema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qur’an:

‫ﻮﻫﺎ إِ ﱠن ٱﻹﻧْ َﺴﺎ َن‬ ِ‫آﺎﺗ ُﻛﻢ ِﻣﻦ ُﻛ ِﻞ ﻣﺎ ﺳﺄَﻟْﺘﻤﻮﻩ وإِن ﺗَـﻌ ﱡﺪواْ ﻧِﻌﻤﺔَ ﱠ‬ ﴿
َ‫ﺼ‬ ُ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻻَ ُْﲢ‬ َ ْ ُ َ ُ ُ ُ َ َ ّ ّ َ ‫َو‬
﴾‫ﻮم َﻛ ﱠﻔ ٌﺎر‬
ٌ ُ‫ﻟَﻈَﻠ‬
Waatakum min kulli ma saaltumoohu wa-in taAAuddoo niAAmata Allahi la
tuhsooha inna al-insana ladhaloomun kaffarun (Surat Ibrahim 14:34)

Tafsir: Na amekupeni nyinyi kila mlichotaka, na kama mkitaka kuzihesabu Neema za


Allah basi kamwe hamtoweza kuzihesabu. Kwa Hakika Mtu ni mwenye kujidhulumu
na mwenye kukufuru.

Na akasema Imam Abd Rahman Al Sulami kua: ‘Hasad ni kitu kibaya sana ambacho
mtu unatakiwa ukikimbie mbio kubwa sana kwani amesema Abu Qasim Ibrahim
Ibn Muhammad Al Nasrabadi kua amesema Abd Rahman Ibn Abu Hatam kua:
‘Hizi ni miongoni mwa wenye kutafuta njia za ufunguzi, hua hawana wivu wengine
kutokana na yale ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala amewajaalia juu yao, hua
hawaoni makosa ya wengine kwani hua wanakhofu na Allah Subhanah wa Ta’ala
kua asije akawajaali wao kua na dhambi kama za hao wengine. Na hivyo hua ni
wenye kuridhika na hikma za Allah Subhanah wa Ta’ala katika majaaliwa yake juu
yao, iwe kwa manufaa yao au dhidi yao’’

Ambapo miongoni mwa Madhara ya Wivu basi hua ni pale ambapo Ibn Adam anapokua
anaona kua hawezi kumpita yule Ibn Adam mwenzake ambae ndie mwenye wivu nae, na
hivyo hua ni mwenye kutamani kua mpinzani wake huyo aondokewe na neema hio
aliyojaaliwa na Allah Subhanah wa Ta’ala. Na hivyo matamanio hayo hua ni moja kati
ya hisia mbaya kabisa za matamanio kwa sababu hua ni zeye kusababisha madhara
makubwa zaidi kutokana nazo, kwani madhara mengi ya chuki, ubaguzi, vita na mauaji
hua ni yenye kutokana na hisia hizi za wivu baina ya viumbe Ulimwenguni.

Lakini tunapozungumzia kuhusiana na wivu wa Wanawake dhidi ya wake wenza wao


basi hua hili hua ni jambo la kimaumbile kwao wao. Hivyo Wanazuoni wanasema kua
Wanawake hawatohesabiwa katika Siku ya Malipo kuhusiana na Wivu huo isipokua pale
watakapokua wamevuka mipaka. Kama vile ambayo hawatohojiwa kuhusiana na
kutosali katika siku wanapokua katika siku zao.
379

Na tunapozungumzia kuhusiana na kuvuka mipaka ya wivu wa Wanawake wake wenza


basi hua tunazungumzia kuuvuka mipaka kwa kufanya kitu ambacho Allah Subhanah wa
Ta’ala na Mtume wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam wameweka wazi juu yake
kua ni makosa kufanya hivyo kwa mfano kwa kusengenya, kufitinisha, kuzulia, kudai
kua mke mwenza huyo aachwe n.k.

Kwani amesema Mujaddid Ad Din Al Hafidh Imam Ibn Hajar Al Asqalani kua:
‘Kimaumbile Wivu wa Wanawake hua si kitu ambacho baadhi hua wanauhisi na
baadhi hawauhisi. Lakini hhata hivyo kama Mwanamke akivuka mipaka basi hua
ni mwenye kubidi kulaumiwa juu yake, na hii ni kulingana na ile hadith isemayo
kua:

Amesema Jaabir Ibn Atiik Al Ansari Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kuna aina ya Wivu ambao Allah Subhanah
wa Ta’ala hua anaupenda, na huu ni ule wivu ambao hua kuna msingi wa kua na
shaka, na kuka wivu ambao Allah Subhanah wa Ta’ala hua anauchukia na huu ni
ule ambao hua upo bila ya kuwepo msingi wa kua na shaka’’

Hivyo Wivu hua ni sehemu ya Maumbile ya Mume na Mke ambayo hakuna


Mwanamke asiekua nayo, na hivyo hua haihesabiwi kua ni kosa hadi pale
Mwanamke huyo atakapovuka mipaka au kufanya kitu chochote kile ambacho
Allah Subhanah wa Ta’ala amekikataza. Hivi ndivyo inavyotakiwa kufahamika pale
tunapozungumzia kuhusiana na Wivu wa Wanawake kama walivyofaham
waliotangulia kabla yetu’(Fat-h Al Barr 9/326)

Ambapo Mujaddid Ad Din Al Hafidh Imam Ibn Hajar Al Asqalani anaendelea kutuambia
kwa upande mwengine kua: ‘Amesema Anas Ibn Malik kua: ‘Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam alikua na mmoja kati ya wake zake wakati, mmoja kati ya Umm
ul Muuminina Radhi Allahu Anha alipotuma sahahi ambayo ilikua imejaa chakula
kwa ajili yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam. Ambapo Mke wae huyo
ambae Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliku ayupo nyumbani kwake,
akaupiga mkono wa Mfanyakazi aliechukua chakula na sahani hio ikaanguka na
kuvunjika katika sehemu mbili.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaviokota vipande hivyo viwili kisha
akaviweka pamoja na kisha akaokota chakula kilichomwagika na kusema: ‘Mama
yako ana wivu.’ Kisha akamwambia mfanyakazi huyo asubiri mpaka alipopewa
sahani inayomilikiwa na Mke ambae yeye yuko ndani ya nyumba yake na kisha
akaichukua sahani hio na kuipeleka kwa Mke ambae sahani yake imevunjwa. Na
kuibakisha sahani iliyovunjwa ndani ya nyumba ya alievunja.’’
380

Ambapo katika hadith nyenginezo zilizozungumzia tukio hili zikiwemo zilizokuwemo


kwenye (Kitaab ‘Ishrat Al Nisaa’), zimetaja kua Mke alievunjiwa Sahani alikua ni
Umm Salamah Umm ul Muuminina Radhi Allahu Anha na alievunja sahani alikua ni
Aisha Umm ul Muuminina Radhi Allahu Anha.

Kutokana na hadith hizi basi Wanazuoni wanasema kua: ‘Hii inaonesha kua Wivu wa
Mwanamke hauhesabiwi kulingana na anayoyafanya kwa sababu akili yake hua
imegubikwa na kiza cha hasira iliyotokana na Wivu.’

Hivyo kwa wale wenye mtizamo wa kua mtoto alietaka kutolewa Dhabih alikua ni Is-
haq basi wanasema kua Is-haq alipokua mkubwa kiasi ya kua ni mwenye kutembea nae
Nabii Ibrahim, basi Nabii Ibrahim akaoteshwa usingizini na kuambiwa: ‘Tekeleza
uliloliahidi kua utamtoa kafara mtoto wako wa kiume kama Allah Akikupa mtoto
kupitia kwa Mkeo Sara’, Nabii Ibrahim alipoamka akamwambia Is-haq: ‘Twende
tukatoe kafara kwa Allah Subhanah wa Taála’ hivyo akachukua Kisu na Kamba,
na walipofika Milimani basi Is-haq akauliza: ‘Ewe baba yangu jee yuko wapi huyo
unaetaka kumtoa Dhabihu?’ ambapo Nabii Ibrahim akajibu:

﴾‫ﻚ ﻓَﭑﻧﻈُﺮ َﻣﺎ َذا ﺗَـﺮ ٰى‬ ‫ﲝ‬ َ ‫ذ‬


ْ َ
‫أ‬ ِ
‫َﱏ‬ ‫أ‬ ِ
‫ﺎم‬‫ﻨ‬ ‫ﻤ‬ ‫ﻟ‬
ْ ‫ٱ‬ ‫ﰱ‬ِ ‫ى‬
ٰ ‫َر‬
‫أ‬ ۤ ِِ‫﴿ ٰﻳـﺒـﲎ إ‬
‫ﱐ‬
َ ْ َ ُ ّ َ َ َ ّ ‫ُ َﱠ‬
Ya bunayya innee ara fee almanami annee adhbahuka faondhur madha tara (Surat
Saffat 37:102)

Tafsir: Ewe Mtoto Wangu Hakika mimi naona usingizini kua nakuchinja, Hebu
tafakkar Jee unaonaje juu ya hili?

Ambapo Nabii Is-haq nae akajibu:

﴾‫ﺼﺎﺑِ ِﺮﻳﻦ‬ ِ ‫ﺖ ٱﻓْـﻌﻞ ﻣﺎ ﺗـُ ْﺆﻣﺮ ﺳﺘَ ِﺠ ُﺪِ ۤﱐ إِن َﺷﺂء ﱠ‬


ِ
َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻣ َﻦ ٱﻟ ﱠ‬ َ َ ُ َ َ ْ َ َ‫﴿ ٰ�َﺑ‬
Ya abati ifAAal ma tu/maru satajidunee in shaa Allahu mina alssabireena (Surat
Saffat 37:102)

Tafsir: Ewe Baba yangu hakika fanya kama unavyoamrishwa, In shaa Allah mimi
nitakua ni miongoni mwa wenye kua na subra.

Ama kwa upande wa Amr Ash Shabi kua: ‘Nabii Ibrahim alitumbukizwa Motoni
wakati alipokua na umri wa miaka 16, Sarah alijifungua mtoto Is-haq wakati akiwa
na umri wa miaka 90. Wakati Is-haq alipotimia umri wa miaka 7 Is-haq alitaka
381

kutolewa Dhabihu, na sehemu ya Dhabihu yake ni Kilomita 2 kutoka Jerusalem.


Wakati Sarah alipopata habari hio ya kutaka kutolewa dhabihu Is-haq basi aliishi
kwa siku mbili na akafariki’

Ama kwa upande wa Zayd Ibn Aslam basi yeye anasema kua amesema Ubayd Allah Ibn
Ubayd Ibn Umayr kua amesema Babu yake kua Nabii Musa alimuuliza Allah Subhnaha
wa Taála: ‘Ya Allah Jee ni kwa nini watu wanasema Mungu wa Ibrahim na Is-haq
na Yaqub?’ ambapo Allah Subhanah wa Taála akasema: ‘Kwa sababu kwa Ibrahim
ilikua hakuna kilicho sawa na mie, isipokua alinichagua mie zaidi ya kitu chochote
kile, na Is-haq alijitolea bila ya kusita kua Dhabihu Allah kwa ajili yangu na hata
bila ya jambo hili basi angekua hakamatiki, ama kwa upande wa Yaqub basi alikua
kila nikimpa mtihani basi ndivyo anavyozidi kunipendelea mimi na kuonesha
fadhila zake kwangu.’

Ama kwa upande wa Abu Maysara basi yeye anasema kua Nabii Yusuf alimwambia
Mfalme wa Misri: ‘Jee utakula nami? kwani Wa Allahi mimi ni Yusuf Ibn Yaqub
Nabiyyu Allah mtoto wa Is-haq Dhabihu Allah, Mtoto wa Ibrahim Khalillu Allah’.
Hivyo wenye mtizamo wa kua alietakiwa awe Dhabih Allah ni Is-haq basi wanasema kua
tokeo hili lilitokea katika Ardhi ya Palestina.

Ama kwa upande mwengine basi kuna wanaosema kua mtoto husika alikua ni Ismail
ambao huu ni mtizamo wa Masahaba kama Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu,
Abd Allah Ibn Umar Radhi Allahu Anhu, Atta Ibn Abi Rabiah, na miongoni mwa Tabiina
wakiwemo kina Hasan Al Basr, Mujahid Ibn Sulayman, Muhammahad Ibn Al Hasan,
Muhammad Ibn Al Kaab Al Qurazi, Imam Abu Muhammad Sulayman Ibn Mahran Al
Asad Al Amash, Amir ul Muuminin Umar Ibn Abd al Aziz, Amr Ibn Ubayd, Imam
Muhammad Ibn Saib Al Kalbi, Imam Said Ibn Musayyib n.k

Ama kwa upande wa Muhammad Ibn Kab Al Qurazi basi yeye anasema kua: ‘Bila ya
Shaka Mtoto ambae aliekua anataka kutolewa Dhabihu kwa ajili ya Allah
Subhanah wa Taála alikua ni Ismail, kwani tunapoiangalia Qurán basi tunapata
ushahidi huo pale Allah Subhanah wa Taála aliposema katika Surat Saffat:

‫ﺎق َوِﻣﻦ‬
َ ‫ﲔ۞ َوَﺎﺑ َرْﻛﻨَﺎ َﻋﻠَْﻴ ِﻪ َو َﻋﻠَ ٰﻰ إِ ْﺳ َﺤ‬ ِِ ‫ﺎق ﻧَﺒِﻴﺎً ِﻣﻦ ٱﻟ ﱠ‬
َ ‫ﺼﺎﳊ‬ ِِ
َ ّ ّ َ ‫َوﺑَﺸْﱠﺮَ�ﻩُ ﺈﺑ ْﺳ َﺤ‬
﴿
ِِ ِ ِ ِ ِ
﴾‫ﲔ‬ ٌ ِ‫ذُِّرﻳﱠﺘ ِﻬ َﻤﺎ ُْﳏﺴ ٌﻦ َوﻇَﺎﱂٌ ﻟّﻨَـ ْﻔﺴﻪ ُﻣﺒ‬
382

Wabashsharnahu bi-is-haqa nabiyyan mina alssaliheena; Wabarakna AAalayhi


waAAala is-haqa wamin dhurriyyatihima muhsinun wadhalimun linafsihi
mubeenun (Surat Saffat 37:112-113)

Tafsir: Na tukambashiria juu ya Is-haq kua Nabii na miongoni mwa watu wema. Na
tukamjaalia yeye na Is-haq na kizazi chao kua ni chenye wenye kufanya mema
miongoni mwao na wenye kujidhulumu miongoni mwao wazi wazi.

Na baada ya hapo basi akasema tena Allah Subhanah wa Taala kua:

﴾‫ﻮب‬ َ ‫ﺎق َوِﻣﻦ َوَر ِآء إِ ْﺳ َﺤ‬


َ ‫ﺎق ﻳَـ ْﻌ ُﻘ‬ َ ‫ﺖ ﻓَـﺒَﺸْﱠﺮَ� َﻫﺎ ﺈﺑِِ ْﺳ َﺤ‬ ِ َ‫﴿وٱﻣﺮأَﺗُﻪ ﻗَﺂﺋِﻤﺔٌ ﻓ‬
ْ ‫ﻀﺤ َﻜ‬
َ َ ُ َْ َ
Waimraatuhu qa-imatun fadhahikat fabashsharnaha bi-ishaqa wamin wara-i
ishaqa yaAAqooba (Surat Hud 11:71)

Tafsir: Na Mkewe aliekua amesimama akacheka, lakini tukambashiria juu ya Is-haq


na baada ya Is-haq Yaqub.

Yaani hapa Allah Subhanah wa Taala anazungumzia kubashiriwa kwa Nabii


Ibrahim kupata mtoto na mjukuu, na kama ni hivyo, basi kamwe isingewezekana
kwake kuamrisha Is-haq awe Dhabihu Allah baada ya kua keshatoa ahadi ya kua
atampatia vizazi kupitia kwake Is-haq, hivyo aya hii inaonesha kua aliemrishwa
awe Dhabihu Allah ni Ismail.

Muhammad Ibn Kab Al Qurazi anaendelea kusema kua: ‘Niligusia juu ya jambo hili
kwa Amir ul Muuminina Umar Ibn Abdu al Aziz wakati tulipokua Syria ambapo
nae akasema: ‘Ama mimi kwa hakika sijaliangalia kwa kina jambo hili lakini
nadhani kua wewe upo sahih’, kisha Amir ul Muuminin akatuma aitwe mtu ambae
alikua pamoja na Amir ul Muuminina katika Ardhi ya Syria ambapo mtu huyo hapo
awali alikua ni Myahudi lakini baadae akasilimu na kua Muislam anaeaminika kua
na Imani nzuri sana, alipofika yule mtu basi Amir ul Muuminin akamuuliza yule
Yahudi: ‘Jee ni yupi baina ya watoto wawili wa Nabii Ibrahim alieamriwa
kuchinjwa?’’.

Yule Yahudi akasema: ‘Ni Ismail! Wallahi ya Amir ul Muuminin! Mayahudi


walikua wanaujua ukweli huu, lakini walikua wanakuoneeni choyo nyinyi
Waarabu, kua ni babu yenu Ismail ndie alieamriwa awe Dhabihu Allah, na hivyo
kua ni mwenye darja ya juu ya Subra na Ustahmilivu juu ya kile kilichoamrishwa
na Allah Subhanah wa Taála juu yake, lakini wao wanapinga na kukataa hili kwa
sababu Is-haq ni babu yao wao.’’
383

Ama kwa upande wa Mujaddid Din Sultan al Mutakallimin Imam Fakhr ad Din Al Razi
basi yeye hakuweka wazi katika Tafsir yake kua ni Is-haq au ni Ismail kutokana na kua
na mvutano baina ya mitizamo miwili hii ambayo yote ina vithibitisho vinavyotokana na
mitizamo ya Masahabah, Tabiina na Wanazuoni wanaokubalika kua ni wenye mitizamo
yenye nguvu baina yao, lakini hata hivyo Imam Fakhr ad Din Al Razi ameonesha
kuegemea katika upande wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu yaani kulingana
na uwazi wa juu juu wa aya kua mtoto alietakiwa awe Dhabihu Allah hapa alikua ni
Ismail.

Kwa upande mwengine basi tunoana Allah Subhana wa Ta’ala katika Surat Al Baqara
kua:
ِ ِ ِ ِ‫ﱠ‬ ِ ‫ﺖ َﻣﺜَﺎﺑَﺔً ﻟِّﻠﻨ‬
َ ‫ﱠﺎس َوأ َْﻣﻨﺎً َوٱﲣ ُﺬواْ ﻣﻦ ﱠﻣ َﻘﺎم إِﺑْـَﺮاﻫ َﻴﻢ ُﻣ‬
�َ ‫ﺼﻠًّﻰ َو َﻋ ِﻬ ْﺪ‬ َ ‫﴿ َوإِ ْذ َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ٱﻟْﺒَـْﻴ‬
﴾‫ﻮد‬ ِ ‫ﺎﻋﻴﻞ أَن ﻃَ ِﻬﺮا ﺑـﻴ ِﱴ ﻟِﻠﻄﱠﺎﺋِِﻔﲔ وٱﻟْﻌﺎﻛِ ِﻔﲔ وٱﻟﺮﱠﻛ ِﻊ ٱﻟ ﱡﺴﺠ‬
‫ََ َ ََﱡ‬ ِ ‫إِ َ ٰﱃ إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ وإِ ْﲰ‬
ُ َ ْ َ َ ّ َ َ َ َ َْ
Wa-idh jaAAalna albayta mathabatan lilnnasi waamnan waittakhidhoo min
maqami ibraheema musallan waAAahidna ila ibraheema wa-ismaAAeela an
tahhira baytiya liltta-ifeena waalAAakifeena waalrrukkaAAi alssujoodi (Surat Al
Baqara 2:125)

Tafsir: Na (Kumbuuka) wakati tulipoijaalia Nyumba (Al Kaabah) kua ni sehemu ya


kutembelea na kukusanyika mara kwa mara na ya amani kwa watu. Na ifanyeni
Maqam Ibrahima (Sehemu aliyosimamia Ibrahim) kua ni sehemu ya Kusalia. Na
tuliahidiana na (tulimuamrisha) Ibrahim na Ismail waisafishe Nyumba Yangu, kwa
ajili ya wale watakaoizuru na kuizunguka, watakaokaa (itiqaf) au watakao ruku na
kusujudu.

Ambapo ayah hii pia nayo pia ni uthibitisho wa kua Dhabihu Allah alikua ni Ismail kwani
hii ni aya inayothibitisha kua mtoto aliekua katika Mji wa Makkah ni Ismail na yeye ndie
aliehusika katika Ujenzi wa Al Kaabah na yeye pia ndie alienzisha kufanya ibada ya Hija
pamoja na Baba yake, na Dhabih ni Ibada inayoenda sambamba na Ibada ya Hija.

Ambapo anasema Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Al Asmai (Tabiina alieishi katika
karne ya 122-233 Al Hijra), alimuuliza Abu Amr Ibn Ala Al Basr, Jee mtoto aliekua
anataka kutolewa kafara alikua ni Is-haq au Ismail?’ ambapo Abu Amr Ibn Ala Al
Basr akasema: ‘Akili yako iko wapi? Jee ni lini Is-haq alikuwepo katika mji wa
Makkah? Ni Ismail ndie aliekuwepo katika mji wa Makkah na ni yeye ndie ambae
aliejenga Baytu Allah pamoja na baba yake, Hivyo sehemu ya Dhabih pia iko katika
mji wa Makkah.’
384

Abu Amr Ibn Al Ala Al Basri alikua ni Mwanazuoni wa Ilm Tafsir ya Quran na Lugha
ya Kiarabu aliefriki miaka minne baada ya kufariki Imam Abu Hanifa na miaka mine
baada ya kuzaliwa Mujaddid Ad Din Imam Abu Abdullah Muhammad Idris Al Shafii.
Abu Amr alikua ni miongoni mwa Wanasanad 7 wakuu wa wapokeaji wa mwanzo wa
Qur’an na pia alikua ni Mwalimu wake Imam Al Asmai.

Tunapoamuangalia Sultan Al Balagha Imam Abu Al Qasim Al Zamakhshari basi yeye


anasema kua: ‘Anasema Abd Allah As Sunabihi kua: Sisi tulikua pamoja na
Muawwiyah Ibn Abi Sufyan wakati watu walipobishana juu ya alietakiwa awe
Dhabihu Allah kua ni Ismail au Is-haq, ambapo Muawwiyah akasema: ‘Ama kwa
Hakika mmekutana na mtu sahih, kwani kwa hakika sisi tulikua tumekaa pamoja
na Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam, ambapo alikuja mtu na kusema: Hebu
ninufaishe na kile ambacho Allah Subhanah wa Ta’ala amekunufaisha nacho ya Ibn
Dhabihan (Ibn wa Dhabih mbili)’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaonesha
tabasam kubwa sana.’

As Sunaabihi anasema: ‘Sisi tukamuuliza Muawwiyah: ‘Ya Amir ul Muuminin. Jee


ndio nini tena maana ya hii Ibn Dhabihan’. Ambapo Muawwiyah akajibu: Wakati
Abd al Muttalib alipotakiwa achimbe kisima cha Zamzam, basi aliweka nadhiri kwa
Allah Subhanah wa Ta’ala kua kama atamfanyia wepesi katika jambo hilo basi basi
atamtoa kafara mmoja kati ya Watoto wake. Na bahati hio ya kutolewa kafara
ikamuangukia Abd Allah (Baba yake Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam),
baada ya kurahisishiwa jambo hili basi ikambidi atekeleze Nadhiri hio, lakini
Mjomba wake akamwambia Abd Muttalib, Usimchinje bali toa Ngamia 100 badala
yake, hivyo Abd Muttalib akachinja Ngamia 100, ambao ndio Dhabih ya kwanza,
na Dhabih ya pili ni Ismail.’

Hivyo kwa mtizamo wa wale ambao wanasema kua Dhabihu Allah alikua anataka
kutolewa Ismail basi wao wanasema kua tukio hili lilitokea katika Mji wa Makkah kwa
sababu huo ndio mji aliokua akiishi Nabii Ismail baada ya Nabii Ibrahim kuambiwa na
Sarah bora amhamishe Hajar na Ismail na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamshushia
Wahy Nabii Ibrahim kuihamishia familia yake hio katika eneo la bondeni ambalo lipo
katika umbali wa kilomita 1496 Kusini Mashariki ya Mji wa Jerusalem.


385

KHALIL ALLAH NA MJI WA MAKKAH AL MUKARRAMAH.



Mji Mtakatifu wa Makkah upo katika eneo hilo ambalo ni lenye bonde lililozungukwa
na Milima iliopo kwenye Jangwa tupu lililokua na majani yenye miba yaliyotawanyika
hapa na pale ambayo huota katika sehemu fulani za Jangwani kwa sababu ya kua na
uwezo wa kuweza kustahmili ukame. Eneo hili liko baina ya Mabara matatu ya Afrika,
Asia na Ulaya.

Na limezungukwa na Bahari ya Mediterrenean kwa upande wa Kaskazini Magharibi,


Bahari nyekundu kwa upande wa Magharibi, Bahari ya Uarabuni kwa upande wa Kusini
na Bahari ya Uajemi kwa upande wa Mashariki. Eneo hili limegawika katika sehemu
mbili ambazo ni Hijaz na Najd. Baina ya maeneo haya mawili kuna milima ya Sarat
iliyoenda sambamba na Bahari Nyekundu, ambayo inalitengenisha eneo la Mashariki la
Uarabuni ambalo ni la miinuko na hujulikana kama Najd, na eneo tambarare lililobakia
Magharibi mwa Uarabuni linalojulikana kama Hijaz. Eneo la Hijaz lina ukubwa wa
takriban kilomita 1400 kutoka katika mwambao wa Bahari Nyekundu.

Sehemu ya bonde aliyowasili Nabii Ibrahim A’layhi Salaam na familia yake, ambayo ni
kilomita 70 kutoka katika mwambao wa Mashariki wa Bahari Nyekundu ambayo imo
ndani ya eneo la Hijaz kuna bonde ambalo lilikua likijulikana kama Bakkah. Anasema
Imam Fakhr Ad Din Al Razi: ‘Herufi ya kwanza ya jina Bakkah baadae ilikuja
kubadilika na kua Makkah, kama vile ambavyo lilivyobadilika neno Lazib kua ni
Lazim.’ Nabii Ibrahim A’layhi Salaam aliwasili katika sehemu hii ambayo ni Tukufu ya
Bakkah kutokana na muongozo wa Allah Subhanahu wa Ta’ala kupitia kwa Malaika
Jibril, kwani Utukufu wa eneo hili unaelezewa na Allah Subhanah wa Taala pale
aliposema:

ِ ‫ﺖ ُو ِﺿ َﻊ ﻟِﻠﻨ‬
‫ﱠﺎس‬ ٍ ‫﴿ﻓَﭑﺗﱠﺒِﻌﻮاْ ِﻣﻠﱠﺔَ إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ ﺣﻨِﻴﻔﺎً وﻣﺎ َﻛﺎ َن ِﻣﻦ ٱﻟْﻤ ْﺸ ِﺮﻛِﲔ ۞إِ ﱠن أَﱠوَل ﺑـﻴ‬
َْ َ ُ َ َ َ َ َ َْ ُ
ِ ِ ِ ‫ﻟَﻠﱠ ِﺬى ﺑِﺒ ﱠﻜﺔَ ﻣﺒﺎرﻛﺎً وﻫ ًﺪى ﻟِّْﻠﻌﺎﻟَ ِﻤ‬
ُ‫ﺎت ﱠﻣ َﻘ ُﺎم إِﺑْـَﺮاﻫ َﻴﻢ َوَﻣ ْﻦ َد َﺧﻠَﻪ‬
ٌ َ‫ت ﺑَـﻴِّـﻨ‬
ٌ �‫آ‬
َ ‫ﲔ۞ ﻓﻴﻪ‬ َ َ ُ َ َ َُ َ
﴾ً‫َﻛﺎ َن ِآﻣﻨﺎ‬
FaittabiAAoo millata ibraheema haneefan wama kana mina almushrikeena;Inna
awwala baytin wudhiAAa lilnnasi lalladhee bibakkata mubarakan wahudan
lilAAalameena; Feehi ayatun bayyinatun maqamu ibraheema waman dakhalahu
kana aminan (Surat Al Maidah 3:95-97)
386

Tafsir: Fuateni mila ya Ibrahim kwani yeye alikua ni Hanifa (mwenye kumuabudu
Allah pekee), na wala hakua miongoni mwa wasihirikina. Kwa hakika! Nyumba ya
kwanza (ya kuabudia) iliyochaguliwa kwa ajili ya watu, ni ile ya Bakkah iliyojaa
Baraka, na uongofu kwa ajili Walimwengu. Ndani yake (Mila zake Nabii Ibrahim)
kuna dalili zilizowazi, na kila atakeingia katika Maqam Ibrahim (katika sehemu ya
Nabii Ibrahim) basi atakua ni mwenye kua katika Amani.

Ingawa kwa Lugha ya Kiarabu na Kiyahudi pia neno Bakkah kua ni lenye kumaanisha
Kulia Machozi na hivyo baadhi ya watu husema kua eneo lililotajwa katika aya hii
linamaanisha Ardhi ya Falestina katika eneo la bonde la Bayt ul Maqdis, kwa sababu
eneo hili ndio mara kadhaa limetajwa kua ndio sehemu iliyosifiwa kwa Barakah katika
aya nyingi ikiwemo tulizoziangalia katika kisa hiki pale Nabii Ibrahim, Nabii Lut na
Sarah walipohamia Falestina na pia katika mfano wa aya ifuatayo:

ِِ ِ ْ ‫﴿ﺳْﺒﺤﺎ َن ٱﻟﱠ ِﺬى أَﺳﺮ ٰى ﺑِﻌْﺒ ِﺪﻩِ ﻟَْﻴﻼً ِﻣﻦ ٱﻟْﻤﺴ ِﺠ ِﺪ‬
َ ْ‫ٱﳊََﺮام إِ َ ٰﱃ ٱﻟْ َﻤ ْﺴﺠﺪ ٱﻷَﻗ‬
‫ﺼﻰ‬ ْ َ َّ َ َْ َ ُ
﴾‫ﺼﲑ‬ ِ ‫ٱﻟﱠ ِﺬى ﺎﺑرْﻛﻨَﺎ ﺣﻮﻟَﻪ ﻟِﻨُ ِﺮﻳﻪ ِﻣﻦ آ�ﺗِﻨَﺂ إِﻧﱠﻪ ﻫﻮ ٱﻟ ﱠﺴ ِﻤﻴﻊ ٱﻟﺒ‬
ُ َ ُ َ ُ ُ َ ْ َُ ُ ْ َ َ َ
Subhana alladhee asra biAAabdihi laylan mina almasjidi alharami ila almasjidi al-
aqsa alladhee barakna hawlahu linuriyahu min ayatina innahu huwa alssameeAAu
albaseeru (Surat Al Isra 17:01)

Tafsir: Ametukuka yule ambae amempeleka Mja wake kutoka katika Masjid Al Haram
(Msikiti Mtakatifu) hadi katika Masjid al Aqsa (Msikiti wa Mbali) Baraqna Hawlahu
(ambao maeneo yake tumeyabariki) ili kumuakisia nuru yeye dalili zetu, hakika yeye
(Allah) ni mwingi wa kusikia na ni mwingi wa usamehevu.

Hivyo aya hii nyingi nyenginezo zimelitaja eneo la Bayt ul Maqdis kua ni Mubaraka,
huku aya hii hii ikiwa pia ni uthibisho kua tunapozungumzia Mji wa Makkah basi
umetajwa kwa kupewa sifa ya Masjid Al Haram (Surat Al Isra 17:01, Surat Al Baqara
2: 144, n.k), na Al Bayta (Surat Al Maidah 5:2), Bayt Al Atiq (Surat At Tur 52:4), Bayt
Al Maamur (Surat At Tur 52:4), Baytika Muharrami (Surat Ibrahim 14:37). Bayt Al
Haram (Surat Al Maidah 5:97).

Lakini vile vile kwa Lugha ya Kiarabu neno Bakkah hua ni lenye kutokana na neno
Tabbakah ambalo hua linamaanisha Mkusanyiko wa pamoja wa Watu na hivyo pia
tunapoangalia kwa Mtizamo huu basi hua tunaona kua Eneo la Al Kaábah pia ni eneo
lisilokosa mkusanyiko wa Watu tangu enzi na enzi hadi mwisho wa Dunia. Neno
Baakkah pia hua ni lenye kumaanisha Bonde lisilokua na Maji na hivyo hii hujumuisha
387

pia ni eneo la Bonde la Mji wa Makkah na ndio maana Imam Fakhr Ad Din Al Razi
akasema kua Bakkah ni Jina la Kábah ambayo ni nyumba ya mwanzo ya Kuamuabudia
Allah Subhanah wa Ta’ala.

Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi anaendelea kusema kua : ‘Uhalisi wa
sehemu kua ni iliyobarikiwa na hivyo kua ni tukufu hua unajumuisha mambo
mengi sana, ikiwemo kuzijaza barka ya Kiroho Nafsi za watu ambao wanaieleka
sehemu hio katika Ibada zao hususan wale ambao wapo karibu na eneo hilo kwa
kuishi au kwa kulitembelea.’

Na kama inavyojulikana kua Al Kaábah ni sehemu ambayo inaelekewa na Viumbe wa


aina tofauti katika nyakati zote kutoka katika maeneo ya Ardhi tofauti Duniani, na
Mbinguni pia na hivyo viumbe hao hua ni wenye kulizunguka eneo hilo. Ni jambo
lisilopingika pia kua wenye kulizunguka eneo hilo katika Ibada zao kutokana na
muongozo wa Qurán, Kitabu kilichoarikiwa hua nao ni wenye kubarikiwa na hivyo hua
ni waliojawa na Imani juu ya Mola wao katika Nafsi zao.

Hivyo Nabii Ibrahim alipowasili katika sehemu hii ya Bakkah ambayo tayari ilikua
ishajaaliwa kua ni kitovu cha Dini ya haki kwa Walimwengu wote ulimwenguni, alikuta
sehemu hio ikiwa haina kitu isipokua kama alama la mahame ya jengo moja la kale yaani
la zamani sana, sehemu hii ilikua na majani madogo madogo yenye miba yaliyoota kwa
kutawanyika hapa na pale kutokana na maumbile yake ya kua ni yenye kustahmili
sehemu zenye ukame. Nabii Ibrahim alipofika katika sehemu hio basi alimuuliza Malaika
Jibril: ‘Jee hii ndio sehemu ambayo natakiwa kuiwacha familia yangu?’ Malaika
Jibril akajibu: ‘Naam.’

Bila ya kujali kua hakuna kitu wala mtu katika sehemu hiyo lakini aliamua kutafuta miti
mikavu na majani makavu kwa ajili ya kutengeneza sehemu ya kijihifadhi familia yake
na kisha akaondoka na kuiacha familia yake hiyo na mfuko wa tende kama chakula chao
kwa muda fulani na kibuyu cha maji ya kunywa, akijua na kuamini kua Allah Subhanahu
wa Ta’ala atakua muangalizi wa familia hiyo na pia atakua ni muangalizi wa lile jambo
jema alilokua na nia ya kulifanya, jambo ambalo limetokana na ujumbe wa hisia kutoka
kwa Mola wake, hivyo Mola wake atamuangalizia kwani hakuna muangalizi bora
isipokua yeye.

Baada ya kuwaacha Nabii Ibrahim A’layhi Salaam aliwaaga na kuanza kurudi alikotoka,
Hajar alichanganyikiwa baada ya kuona kua anaachwa katika sehemu hiyo yeye peke
yake na mtoto wake Ismai’l, hivyo kabla hajafika mbali akamuuliza Nabii Ibrahim ‘Ya
Ibrahim, unatuwacha na nani katika sehemu hii tupu ya jangwa, isiokua na watu
wala chakula kwa ajili yetu?’,
388

Nabii Ibrahim akiwa na amejawa na uchungu na huruma kwa familia yake hio, hakujibu
bali aliendelea kuchukua hatua moja baada ya nyengine kuelekea Jerusalem, Hajar
alimkimbilia na kumuuliza tena swali hilo mara tatu bila ya kupata jibu, na hapo
akamuuliza, ‘Jee ni Allah Subhanah wa Ta’ala, ndie aliekuamrisha kufanya hivi?’,
na hapo Nabii Ibrahim A’layhi Salaam akajibu, ‘Naam!’. Hapo Hajar akasema,
‘Nimeridhia kwani nnajua kua kamwe Allah Subhanah wa Ta’ala hatotutupa’.

Mda baada ya kuondoka na kutembea kutoka alipoiwacha familia yake, na kua haioni
tena familia hio basi Nabii Ibrahim A’layhi Salaam, aligeuka upande aliotoka na
kunyanyua juu mikono yake na kisha akamuomba Mola wake kama inavyotuelezea aya
ifuatayo:

ِ ِ َ َ‫﴿وإِ ْذ ﻗ‬
۞‫َﺻﻨَ َﺎم‬ ْ ‫ﲎ أَن ﻧـﱠ ْﻌﺒُ َﺪ ٱﻷ‬ ‫ٱﺟﻨُـْﺒ ِﲎ َوﺑَِ ﱠ‬
ْ ‫ٱﺟ َﻌ ْﻞ َﻫـٰ َﺬا ٱﻟْﺒَـﻠَ َﺪ آﻣﻨﺎً َو‬
ْ ‫ب‬ ِّ ‫ﺎل إِﺑْـَﺮاﻫ ُﻴﻢ َر‬ َ
ِ ِ ‫َﺿﻠَْﻠ َﻦ َﻛﺜِﲑاً ِّﻣ َﻦ ٱﻟﻨ‬
‫ﻮر‬
ٌ ‫ﻚ َﻏ ُﻔ‬ َ ‫ﺼ ِﺎﱏ ﻓَِﺈﻧﱠ‬ َ ‫ﱠﺎس ﻓَ َﻤﻦ ﺗَﺒِ َﻌ ِﲎ ﻓَِﺈﻧﱠﻪُ ﻣ ِّﲎ َوَﻣ ْﻦ َﻋ‬ ْ ‫ب إِﻧـﱠ ُﻬ ﱠﻦ أ‬ ِّ ‫َر‬
‫ﻚ ٱﻟْ ُﻤ َﺤﱠﺮِم َرﺑـﱠﻨَﺎ‬ َ ‫ﻨﺖ ِﻣﻦ ذُِّرﻳﱠِﱴ ﺑَِﻮ ٍاد َﻏ ِْﲑ ِذى َزْرٍع ِﻋ‬
َ ِ‫ﻨﺪ ﺑَـْﻴﺘ‬ ُ ‫َﺳ َﻜ‬
ۤ
ْ ‫ﱠرﺣ ٌﻴﻢ ۞ ﱠرﺑـﱠﻨَﺂ إِ ﱠﱐ أ‬
ِ
‫ات‬ ِ ‫ﱠﺎس ﺗَـﻬ ِﻮ ۤي إِﻟَﻴ ِﻬﻢ وٱرزﻗْـﻬﻢ ِﻣﻦ ٱﻟﺜﱠﻤﺮ‬ ِ ‫ﻨ‬ ‫ٱﻟ‬ ‫ﻦ‬ ِ ‫ﺼﻼََة ﻓَﭑﺟﻌﻞ أَﻓْﺌِ َﺪ ًة‬
‫ﻣ‬ ‫ﱠ‬ ‫ٱﻟ‬ ‫ا‬
ْ‫ﻮ‬‫ﻴﻤ‬ ‫ﻘ‬ِ ‫ﻟِﻴ‬
ََ َ ّ ْ ُ ْ َ ْ ُ ْ ْ َّ َْ ْ ُ ُ
‫ٱﻪﻠﻟِ ِﻣﻦ‬ ‫ﻚ ﺗَـ ْﻌﻠَ ُﻢ َﻣﺎ ُﳔْ ِﻔﻰ َوَﻣﺎ ﻧـُ ْﻌﻠِ ُﻦ َوَﻣﺎ َﳜْ َﻔ ٰﻰ َﻋﻠَﻰ ﱠ‬ َ ‫ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻬ ْﻢ ﻳَ ْﺸ ُﻜُﺮو َن۞ َرﺑـﱠﻨَﺂ إِﻧﱠ‬
‫ﺐ ِﱃ َﻋﻠَﻰ ٱﻟْ ِﻜ َِﱪ‬ ِ ‫ﺂء ۞ ْ ِ ِ ﱠ‬ ِ ‫ض وﻻَ ِﰱ ٱﻟ ﱠﺴﻤ‬ ٍِ
َ ‫ٱﳊَ ْﻤ ُﺪ ﱠﻪﻠﻟ ٱﻟﺬى َوَﻫ‬ َ َ ِ ‫َﺷ ْﻲء ﰱ ٱﻷ َْر‬
‫ﺼﻼَةِ َوِﻣﻦ‬ ‫ٱﺟ َﻌ ْﻠ ِﲎ ُﻣ ِﻘ َﻴﻢ ٱﻟ ﱠ‬ ِ ‫ﺎق إِ ﱠن رِﰉ ﻟَﺴ ِﻤﻴﻊ ٱﻟﺪ‬ ِ ِ
ْ ‫ب‬ ِّ ‫ﱡﻋﺂء۞ َر‬ َ ُ َ ّ َ َ ‫ﻴﻞ َوإِ ْﺳ َﺤ‬ َ ‫إ ْﲰَﺎﻋ‬
ِ ِ ِ ‫ﺂء۞ رﺑـﱠﻨَﺎ ٱ ْﻏ ِﻔﺮ ِﱃ وﻟِﻮاﻟِ َﺪ ﱠ‬ ِ ِ
‫ﻮم‬
ُ ‫ﲔ ﻳَـ ْﻮَم ﻳَـ ُﻘ‬
َ ‫ى َوﻟ ْﻠ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬ ََ ْ َ ‫ذُّرﻳَِﱴ َرﺑـﱠﻨَﺎ َوﺗَـ َﻘﺒﱠ ْﻞ ُد َﻋ‬
﴾‫ﺎب‬ ِْ
ُ ‫ٱﳊ َﺴ‬
Wa-idh qala ibraheemu rabbi ijAAal hadha albalada aminan waojnubnee
wabaniyya an naAAbuda al-asnama; Rabbi innahunna adhlalna kathiiran mina
alnnasi faman tabiAAanee fa-innahu minnee waman AAasanee fa-innaka
ghafoorun raheemun;Rabbana innee askantu min dhurriyyatee biwadin ghayri dhi
zarAAin AAinda baytika almuharrami rabbana liyuqeemoo alssalata faijAAal af-
idatan mina alnnasi tahwee ilayhim waurzuqhum mina alththamarati laAAallahum
yashkuroona. Rabbana innaka taAAlamu ma nukhfee wama nuAAlinu wama
389

yakhfa AAala Allahi min shay-in fee al-Ardhi wala fee alssama/-I; Alhamdu lillahi
alladhee wahaba lee AAala alkibari ismaAAeela wa-ishaqa inna rabbee
lasameeAAu aldduAAa/-I; Rabbi ijAAalnee muqeema alssalati
wamin Dhurriyyatee rabbana wtaqabbal duAAa/-I; Rabbana ighfir lee
waliwalidayya walilmu/mineena yawma yaqoomu alhisabu (Surat Ibrahim 14:35-
41).

Tafsir: Na (kumbuka)wakati (Ibrahim)aliposema: Ewe Mola wangu ujaalie Mji huu


(wa Makkah) kua ni wenye Usalama na Amani, na nijaalie mimi na kizazi changu
kua mbali na wenye kuabudu Masanamu. Ewe Mola wangu, Kwa hakika
wamewapotosha watu wengi miongoni mwa Ibn Adam. Lakini yule utakaenifuata
mimi, basi ni hua ni miongoni mwangu na atakaeniasi basi hakika wewe ni mwingi
wa usamehemuu na mwingi wa Rehma. ‘Ya Rabbi! Nimewacha kizazi changu kiishi
katika bonde lisilokua na kitu, pembeni ya nyumba yako tukufu (Ka’bah), ili Ewe Mola
wetu, wapate kusimamisha Sala, hivyo zijaze mapenzi nyoyo za watu miongoni mwao
juu yao, na (Ya Allah) waruzuku matunda ili wapate kukushukuru; Ewe Mola wangu
hakika wewe ni mwenye kujua tuliyojificha kuyafanya na tuliyoyaweka wazi. Bila ya
shaka hakuna kinachofichikana kwa Allah ardhini na mbiguni; Shukrani zote
anastahiki Allah ambae ndie alienipendelea mie kwa kunipa uzeeni Ismail na Is-haq.
Hakika Mola wangu ni mwenye kusikia Maombi yote; Ya Rabbi nijaalie mie kua ni
mwenye kusimamisha Sala na kizazi change pia. Mola wetu nikubalie Dua yangu.
Mola wetu, Nisamehe mimi na wazazi wangu na Waislamu wote katika siku ya
Malipo’.

Anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kuhusiana na ayah hii kua: ‘Hii
inatufunza kua mara tu baada ya mtu anapokua huru na mashakil ya Dunia, basi
humbidi kujishughulisha na kumkumbuka na kumuomba Mola wake na kufanya
Ibada nyengine kwa ajili ya Mola wake.’

Anasema Abda Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kuhusiana na maneno yasemayo:
‘Rabbana liyuqeemoo alssalata faijAAal af-idatan mina alnnasi tahwee ilayhim’
yaani ‘Ewe Mola wetu, wapate kusimamisha Sala, hivyo zijaze mapenzi nyoyo za watu
miongoni mwao juu yao’ kua kuwepo kwa neno mina kabla ya Alnnasi
kunakomaanisha baadhi ya watu kunaonesha kua ni Waislamu tu ndio waliolengwa
hapa, kwani kama si hivyo basi ingekua wamelengwa watu wote basi Umati wa
Ulimwengu mzima wa watu ungelijazana katika Mji Mtukufu’

Jarah Allah Imam Abu Al Qasim Al Zamakhshari anasema kuhusiana na maneno


yasemayo: ‘Rabbana innaka taAAlamu ma nukhfee wama nuAAlinu wama yakhfa
AAala Allahi min shay-in fee al-Ardhi wala fee alssama/-I;’ yaani: ‘Ewe Mola wangu
hakika wewe ni mwenye kujua tuliyojificha kuyafanya na tuliyoyaweka wazi. Bila ya
shaka hakuna kinachofichikana kwa Allah ardhini na mbiguni.’ kua ‘Ingawa Allah
390

Subhnah wa Taála ni mwenye kujua, yaliyojifisha ndani ya nyoyo zetu, na hivyo hua
haina haja ya kumuwekea wazi kwa kumuomba, lakini hata hivyo inabidi kuonesha
unyenyekevu mbele yake yake Allah Subhana wa Ta’ala’ na maneno yasemayo:
‘Inna rabbee lasameeAAu aldduAAa/-I’ yaani : ‘Hakika Mola wangu ni mwenye
kusikia Maombi yote’ kunamaanisha kua: ‘Allah Subhanah wa Taála ni mwenye
kujibu Maombi yetu na hivyo kututekelezea yale tuliyomuomba katika dua zetu’

Hapa inabidi tukumbuke tena kua Nabii Ibrahim hakua ni mwenye kumuombea dua Ami
yake Azar, bali alikua ni mwenye kumuombea Dua Baba yake ambae ni Mzee Tarikh.

Amesema Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu kua amesema: ‘Tunda la Mwanzo la Msimu
wa Matunda ya Madina yalikua yakiwasilishwa mbele ya Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam ambae alikua akiomba dua kwa kusema: ‘Ya Allah Tuongozee
Barka katika Mazao yetu, Tuongezee Barka katika mji wetu, tuongezee Barka
katika Pishi Zetu na Vibaba vyetu. Ya Allah! Ibrahim alikua ni Khallil wako, Mja
wako na Mtume wako, na mimi pia ni Mja wako na Mtume wako! Ibrahim
aliuombea Mji wa Makkah hivyo na mimi nauombe Mji wa Madinah. Ujaalie
Mjiwa Madina kila kile ambacho Ibrahim alikiomba kwa ajili ya Mji wa Makkah
na ongezea Mara mbli yake zaidi.’ Na kisha baada ya hapo Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam alikua akimwita Mtoto mdogo kuliko wote na kumpa tunda
hilo.’(Sahih Muslim)

Ambapo kutokana na Dua za Nabii Ibrahim kuhusiana na Mji wa Makkah na pia Dua za
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kuhusiana na mji wa Madina basi ndio maana
mpaka leo Mji wa Madina hua ni wenye kua na wingi wa Matunda, vyakula na vitu
vyenginevyo maradufu zaidi ukilinganisha na mji wa Madina.

Kisha baada ya kuomba Dua hizo basi Nabii Ibrahim akaendelea na safari yake ya kurudi
Jerusalem. Kwa upande wa Hajar basi nae baada ya kupata jibu kua ni Allah Subhanah
wa Taála ndie aliemumrisha Nabii Ibrahim kuwaacha wao hapo basi khofu na wasiwasi
uliomuondoka na hapo nae akajua na akaamini kua hakuna muangalizi bora isipokua yule
ambae ameamrisha wao waachwe katika eneo hilo tu lisilokua na watu ambae Allah
Subhanahu wa Ta’ala hivyo atawasimamia tu.

Baada ya mda, tende waliyokua nayo ambayo ndio ilikua chakula chao na maji waliyokua
nayo yakamalizika na hapo Ismai’l akaanza kulia kwa kiu, Hajar akajaribu
kumnyamazisha lakini wapi, Ismai’l aliendelea kulia na kulia, hivyo Hajar akamuweka
chini na kuanza kuhangaika kutafuta tafuta labda huenda akapata maji, ili ampe mtoto
wake apate kunyamaza, akaanza kukimbia kuenda huku na kule na kurudi kumuangalia
mtoto wake lakini hakuweza kuyaona maji wala dalili ya maji.
391

Katika kuhangaika kwake huko, alikimbia baina ya vilima viwili vya Safa na Marwa
mara saba na aliporudi kwa mtoto wake akaona, chini ya nyayo za miguu ya mtoto wake
aliekua akilia kumeanza kububujika maji, akachota maji hayo na kumnywesha mtoto
wake Ismai’l, akajaza kibuyu chake na kisha akaona ayazungushie maji hayo kituta
kidogo cha mchanga ili yasije yakatawanyika na baadae yakatoweka na kuzama katika
mchanga mkavu mwingi uliokuwepo katika eneo la jangwa hilo.

Maji hayo yaliondoa kiu na njaa aliyokua nayo Ismai’l, tangu mara ya kwanza kuchotwa
maji hayo na Hajar takriban miaka 4000 iliopita, hadi hii leo maji hayo yamekua ni
ambayo hayajakauka na bado yanaendelea kububujika, bila ya kupungua wingi wake,
mbali ya kua yanachotwa na mamilioni ya watu na kuonjwa na karibu Waislamu wote
ulimwenguni kutokana na historia, Miujiza yake na pia upekee wa madini yalikuwemo
ndani yake. Maji hayo yanaitwa maji ya Zamzam ambapo awali yalikua yakitwa kama
Shabaa’Ah (Kitu chenye Kuridhisha)

Maji ya Zamzam, ambayo yana kina cha takriban mita nne ndani ya kisima chake
kilichojengewa yana asilimia kubwa sana ya madini ya Sodium na Potassium, wingi wa
madini ambayo haipatikani katika maji yeyote duniani, madini hayo huyafanya maji hayo
kua ni kisafisho cha sumu zote zilizomo ndani ya mwili na pia tiba ya maradhi mengi
sana na huharakisha kwa kiasi kikubwa uponaji wa maradhi ya kansa, sumu inayotokana
na chakula, kuungua, wingi wa kolesterol, ukurutu, kuchanganyikwa kiakili, kuondoa
uchovu, maradhi ya pressure na mengineyo.

Maji ya Zamzam hayana rangi wala harufu lakini yana ladha ya kipekee, yenye utofauti
na maji mengine yote yanayopatikana katika uso wa dunia. Wanasayansi wa chuo kikuu
cha Mfalme wa Saudi Arabia wanasema kua maji ya Zamzam yana Alkaline (kemikali
zinazokaa ndani ya maji na hivyo kuyafanya maji yasiwe na asidi) inayofanana na ya
maji ya bahari ambayo ni pH is 7.9 na pia kwa kila lita moja ya maji hayo ina madini ya
Sodium 133 mg/L, Calcium 96 mg/L, Magnesium 38.88 mg/L, Potassium 43.3 mg/,
Bicarbonate 195.4 mg/L, Chloride 163.3 mg/L, Fluoride 0.72 mg/L, Nitrate 124.8 mg/L,
Sulfate 124.0 mg/L.

Baada ya kumnywesha maji mtoto wake Isma’il, na kunywa yeye mwenyewe maji hayo,
alikaa na kumpakata na hapo Isma’il akalala, Hajar alimshukuru Allah Subhanahu wa
Ta’ala na akakaa na kupumzika, mara kwa mbali akaona ndege wanaruka na kuelea
hewani, wakaja hadi pale kwenye maji wakatua pembeni yake wakanywa na kuondoka,
kuja kwa ndege hao na kunywa maji katika sehemu huyo ilikua ni dalili nzuri kwani ni
jambo la kawaida kwa wasafiri wa misafara ya jangwani, wanapomalizikiwa na maji basi
huyatafuta kwa kuangalia juu angani, kwa kujaribu kutafuta ndege wanaoruka,
wakiwaona wanaruka ruka na kuzunguka katika sehemu fulani basi hujaribu kuelekea
392

katika maeneno hayo kwani sehemu ambazo kuna ndege huashiria uwezekano wa
kupatikana maji na chakula pia kwa ajili ya Ibn Adam.

Hajar alipoanza kunywa maji yale, akahisi kuondokwa pia na njaa yeye pamoja na mtoto
wake Ismai’l, na haukuchukua mda akatokea Malaika Jibril na kumwambia Hajar,
‘Usiogope kua peke yako. Kwani hapa itajengwa nyumba ya Allah na mtoto huyu
na baba yake. Hakika Allah hawatupi waja wake’.

Naam, Allah Subhanahu wa Ta’ala aliikubali dua ya Nabii Ibrahim, kwani ingawa
sehemu hiyo iliyokua ni jangwa lililokua halina kitu, lakini ilibadilika, kwani misafara
ya wasafiri wa jangwani waliona dalili za ndege waliokua wakiruka angani na kuonesha
kua sehemu hiyo kuna maji, hivyo eneo hilo lilianza kujulikana na wafanya biashara na
wasafiri na watu mbali mbali na hivyo kidogo kidogo likaanza kubadlika.

Watu wa kwanza kufika katika eneo hilo baada ya Hajar na Ismai’l kuanza kuishi hapo
walikua ni watu wa kabila la Banu Jurhum, ambao walikua wakitokea katka Ardhi ya Al
Yaman au Yemen wakielekea Kanaan au Sham. (Yemen, imeitwa Al Yaman kwa sababu
unapokua katika Ardhi ya Hijaz na ukaupa mgongo mwambao wa Bahari Nyekundu basi
eneo hilo hua lipo upande wa Al Yamin yaani upande wa kulia wa eneo la Ardhi ya
Makka, na eneo la Kanaan limeitwa Sham kwa sababu lipo upande wa Al Shimal au
kushoto na wegine wanasema pia kua eneo hilo limeitwa Sham kwa sababu ya kutokana
na mtu wa mwanzo kuishi hapo alikua ni Mtoto wa Nabii Nuh aitwae Sam)

Hivyo msafara huo wa watu wa Banu Jurhum uliokua ukitokea Al Yaman ulipiga kambi
katika sehemu ya Al Qada’, na baada ya muda walishangazwa na kuona kwa mbali kuna
ndege wakiruka ruka katika eneo walilokuwepo Hajar na Ismai’l, lakini bila ya kujua kua
sehemu hiyo kulikua na watu wawili hao, hivyo wakasema. ‘Ndege hupatikana katika
sehemu yenye maji, na sisi hatukuwahi kuona maji hata mara moja tulipokua
tukipita katika bonde hili’, hivyo wakatuma watu wao wakaangalie katika sehemu hiyo
wanaoruka ruka ndege hao kuna nini, watu hao walienda na waliporudi wakatoa taarifa
ya kuwepo maji na pia kua kuna mwanamke na mtoto wake, watu wa kabila hilo la Banu
Jurhum wakaamua kuenda kuzungumza na Hajar na kumuomba kama atawaruhusu
kupiga kambi katika sehemu hiyo pamoja nae, na wakamuuliza Hajar baada ya kuona
maji ya Zamzam: ‘Hiki Kisima kinamilikiwa na nani?’

Hajar akajibu: ‘Kinamilikiwa na huyu Mtoto.’ Ambapo watu hao wa Banu Jurhum
awalipomuangalia Ismail wakamuona kua ni mzuri na mwenye kuvutia sana, hivyo
wakauliza: ‘Jee huyu ni mtoto wa Nani?’ Hajar akajibu: ‘Ni Mtoto wa Ibrahim’ Watu
hao wakauliza: ‘Na jee Ibrahim ndio Nani?’ Hajar akajibu: ‘Ibrahim ndio Yule ambae
kupitia katika mikono yake ndio Mfalme Namrudh Al Kabir aliangamia’
393

Hapa watu hao wa Bau Jurhum wakakaa na kujadiliana kwa kusema kua ‘Ardhi ya nchi
yetu ni Kame na Watu wetu hawajatulia, hivyo wacha tuhamie hapa katika sehemu
hii’ na kisha wakasema kua: ‘Hakika wewe uko peke yako katika eneo hili, hivyo jee
unaonaje kama sisi tukihamia hapa na kisha tutakua tunakulipeni Kondoo
miongoni mwa mifugo yetu’

Hajar akawakubalia kwa sababu mbali ya kua kuna maji bali pia alikua yuko peke yake
hivyo akaona ni bora kukaa na watu wengine katika eneo hilo. Ambapo Kiongozi wao
watu hao alikua akiitwa Samaida Al Jurhum. Hivyo watu hao wakahama katika eneo hilo,
wakajenga Nyumba zao na Soko. Na hivyo wakawa ni wenye kumlipa Ismail asilimia
moja ya idadi ya mifugo yao. Sehemu hiyo ikawa ni mji unaojulikana kwa jina la Bakkah
(Makkah). Nabii Ibrahim A’layhi Salaam akawa anakuja kuitembelea familia yake kila
baada ya mda fulani katika mji huo wa Makkah lakini hua si mwenye kukaa saa katika
mji huo wa Makkah kwa sababu Sarah alikua hamruhusu kukaa katika mji huo kwa mda
mrefu na hivyo hua ni mwenye kuondoka na kurudi katika mji wa Jerusalem katika siku
hio hio.

Safari moja Nabii Ibrahim A’layhi Salaam aliitembelea familia yake, wakati Ismai’l
akiwa bado mdogo ahakua ni mwenyena hapo Allah Subhanahu wa Ta’ala akampa
mtihani wa kumuangalia, kwa kiasi gani anampenda mtoto wake huyo Ismai’l ambae ni
mtoto wake wa pekee, na vile vile ni kwa kiasi gani anavyompenda Mola wake, akaamua
kumpa mtihani uulizao jee ataitii amri ya Mola wake au atamuasi kwa kutotii amri hiyo
kutokana na kumpenda mtoto huyo? Mtihani huo haukua kwa Nabii Ibrahim peke yake
bali pia ulimjumuisha mtoto wake ambae nae alikua akiangaliwa kwa kiasi gani
anamuamini baba yake na kwa kiasi gani yuko tayari kutii amri ya Mola wake.

Hivyo, Nabii Ibrahim A’layhi Salaam alilala na kuota kua anamchinja mtoto wake
Ismai’l, na alipoamka akamwambia Ismai’l kuhusu jinsi alivyoona katika ndoto yake, na
hapo Ismai’l nae akamwambia baba yake kama hivyo ndivyo ulivyoamrishwa na Allah
Subhanahu wa Ta’ala basi In shaa Allah bila ya kusita naye atakuwa miongoni mwa
wenye subra na walio pamoja nae katika kutekeleza amri hiyo, hivyo likatokea tukio
lilioelezewa katika Surat Saffat 37:102 ambayyo inasema kua:

﴾‫﴿ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ ﺑَـﻠَ َﻎ َﻣ َﻌﻪُ ٱﻟ ﱠﺴ ْﻌﻰ‬


َ
Falamma balagha maAAahu alssaAAya.. (Surat Saffat 37:102)

Tafsir: Kisha Mtoto wake alipokua Mkubwa kiasi ya kua ni mwenye kutembea nae..
394

Yaani wakati Ismail alipokua na umri wa miaka 7 basi Nabii Ibrahim akamwambia Ismail
kua achukue kisu na kamba kisha watoke waende wakatafute kuni nje kidogo ya mji wa
Makkah, njiani Nabii Ibrahim akakutana na Iblis ambae alikua amejigeuza kuingia katika
umbo la Ibn Adam mzee, ambae alimuuliza Nabii Ibrahim: ‘Ewe Mzee! Jee unaelekea
wapi na unataka kufanya nini?’

Nabii Ibrahim akajibu: ‘Naenda bondeni kutafuta Kuni’

Iblis akasema: ‘Hakika wewe umenuia kuenda kumuua Ismail’

Nabii Ibrahima akasema: ‘Jee wewe ushawahi kuomuona baba akitaka kumuua
Mtoto wake?’

Iblis akasema: ‘Bila ya shaka! Ni wewe hapo ni wa Mwanzo!’

Nabii Ibrahim akauliza: ‘Na kwa nini mimi nimuuwe Mtoto wangu?’

Iblis akajibu: ‘Kwa sababu unafikiria kua Allah amekuamrisha kufanya hivyo.’

Nabii Ibrahim akajibu: ‘Kama ikiwa Allah ameniamrisha hivyo basi bila ya shaka
huo ni wajib wangu kuutekeleza’

Iblis akasema: ‘Bila ya shaka! Sie Allah aliekuamrisha kutekeleza amri hio bali ni
Iblis’

Nabii Ibrahim akajua kua huyu anaezungumza nae si Ibn Adam bali ni Iblis mwenyewe,
hivyo nae akasema: ‘Ewe Iblis laanat Allahi! Wallahi mimi nitatekeleza wajibu
wangu alioniamrisha Mola wangu bila ya kipingamizi chochote’.

Baada ya kuona kua mbinu zake zimegonga ukuta basi Iblis laanat Allahi akaachana na
Nabii Ibrahim na kumsogelea Ismail aliekua nyuma kidogo ya Nabii Ibrahim aliekua
anafuata hatua za baba yake na hivyo Iblis akawa ni mweye kusimama baina ya Nabii
Ibrahim na Ismail kisha akasema kumwambia Ismail: ‘Wa Allahi baba yako
anakuchukua ili akakuchinje huko mnakoelekea’
Ismail akauliza: ‘Jee ni kwa nini akanichinje mie? Jee ushawahi kuona baba akitaka
kumchinja Mwanawe?’

Iblis akasema: ‘Yule pale ndie baba mwenyewe’

Ismail akasema: ‘Lakini jee ni kwa nini Baba yangu atake kunichinja mie?’

Iblis akasema: ‘Ati anadhani kua Mola wake amemuamrisha yeye kufanya hivyo!’
395

Ismail akasema: ‘Ni wajibu wake kutekeleza jukumu la Mola wake juu yake, kwani
ni bora kwake kujisilimisha kwa Mola wake, na kwa hakika mimi pia
nitajisalimisha kwake na kukubaliana na lile alitakalo Mola wangu.’
Iblis baada ya kuona kua kamwe hatoweza kufanikiwa kuwalaghai watu wawili hawa ili
wasitekeleze wajibu wao kwa Mola wao na hivyo kua ni wenye kujisalimisha kwa Mola
wao, basi akaona kua hapa sasa inabidi atumie sila ya mwisho ambayo ni ya mama mzazi
wa Ismail, hivyo haraka sana akakimbilia hadi kwa Hajar. Alipofika kwa Hajar basi
akamwambia Hajar: ‘Ya Hajar! Jee unajua Ibrahim anampeleka wapi mtoto wako
Ismail?’

Hajar anasema: ‘Ameenda nae kuokota kuni kwa ajili ya kupikia.’

Iblis akasema: ‘Hakika wewe umekosea, kwani Ibrahim amemchukua Ismail kwa
ajili ya kuenda kumtoa Kafara’

Hajar akasema: ‘Inakuaje wewe unakua na Mtizamo kama huo? Kua Baba anaweza
kumchinja mtoto wake? Jee hujui kua Ibrahim ni mwenye kumpenda sana Ismail
na nimwenye huruma juu ya Mtoto wake huyo?’

Iblis akasema: ‘Naam! Ibrahim anadhani kua kufanya hivyo kunatokana na amrisho
la Mola wake.’

Hajar akasema: ‘Kama ikiwa ni Mola wake amemuamrisha hivyo, basi bila ya shaka
ni jukumu lake kujisalimisha na kutekeleza wajibu wake kwa Mola wake popote
pale atakapokuwepo.’

Hapa Iblis akajua kua, kamwe haitowezekana kuilaghai familia ya watu hawa, hivyo
akageuka na kurudi alikotoa huku akiwa amejawa na hasira za kushindwa kuwaingiza
watu hawa watatu muhimu katika kutimiza malengo yake ya kua pamoja nae katika
kumuasi Allah Subhanah wa Taála.

Nabii Ibrahim na Ismail walipofika katika maeneo ya bonde la Thabir basi Nabii Ibrahim
akamkaribia Ismail na kumwambia:

﴾‫ﻚ ﻓَﭑﻧﻈُﺮ َﻣﺎذَا ﺗَـﺮ ٰى‬ ‫ﲝ‬ ‫ذ‬ َ


‫أ‬ ِ
‫َﱏ‬ ‫أ‬ ِ َ‫ﲎ إِِّ ۤﱐ أَر ٰى ِﰱ ٱﻟْﻤﻨ‬
‫ﺎم‬ ﴿
َ ْ َ ُ َ ْ ّ َ َ ‫ٰﻳـﺒُـ َﱠ‬
Ya bunayya innee ara fee almanami annee adhbahuka faondhur madha tara (Surat
Saffat 37:102)
396

Tafsir: Ewe Mtoto Wangu Hakika mimi naona usingizini kua nakuchinja, Hebu
tafakkar Jee unaonaje juu ya hili?

Hili halikua ni suali la kushauriana bali lilikua ni suali la kutaarifiana hivyo hapa Nabii
Ibrahim alikua anamtaarifu Ismail juu ya jambo linalotaka kutokea ambapo na Ismail nae
bila ya kusita wala kufikiria mara mbili mbili basi akajibu kwa kusema:

﴾‫ﺼﺎﺑِ ِﺮﻳﻦ‬ ِ ‫ﺖ ٱﻓْـﻌﻞ ﻣﺎ ﺗـُ ْﺆﻣﺮ ﺳﺘَ ِﺠ ُﺪِ ۤﱐ إِن َﺷﺂء ﱠ‬


ِ
َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻣ َﻦ ٱﻟ ﱠ‬ َ َ ُ َ َ ْ َ َ‫﴿ ٰ�َﺑ‬
Ya abati ifAAal ma tu/maru satajidunee in shaa Allahu mina alssabireena (Surat
Saffat 37:102)

Tafsir: Ewe Baba yangu hakika fanya kama unavyoamrishwa, In shaa Allah mimi
nitakua ni miongoni mwa wenye kua na subra.

Ambapo tena Qur’an katika kuelezea kisa cha Nabii Ibrahim na tukio hili imetumia neno
Abati ambalo tumeliezea hapo kabla kua ni neno linalotokana na neno Aba ambalo maana
yake hua ni Baba, Mzazi wa Kiume, au Mlezi wa Kiume, ambapo neno Abati hua
linaashiria Cheo au Darja au Jina la Mzazi analotumia Mtoto kuonesha namna mtoto
huyo anavyomjali sana na kumpenda sana Baba yake, Mzee wake wa Kiume au Mlezi
wake kiasi ya kua hua hataki Mzee wake huyo kumkera au awe ni mwenye Kujisikia
vibaya kihisia kutokana na lile analotaka kumwambia, kwani neno hilo hua linatoka
kwene kina cha Hisia za upendo wa Mwenye kuita.

Ambapo hapo awali katika Surat Maryam 19:44 ilikua ni kwa Nabii Ibrahim kumuusia
Mzee wake ambae ni Azar wakati hapa katika aya yetu hii ya Surat Saffat 37:102 ni kwa
Nabii Ismail kumuusia baba yake yaani Nabii Ibrahim. Hivyo Ismail akamuuliza baba
yake, kwa kumwambia: ‘Ewe baba yangu Jee umemwambia mama juu ya habari
hii?’

Nabii Ibrahim akasema: ‘La Sijamwambia juu ya habari hii’

Ismail akasema: ‘Ni bora ilivyokua hukumwambia juu ya jambo hili. Kwa hivyo ewe
baba yangu, Utakapokua tayari kunichinja basi nifunge kamba hii vizuri, ili nisilete
purukushani nawe ukanionea huruma na ukakosa malipo kwa Allah juu ya jambo
hili, kwani kifo ni kitu kigumu. Na ikunje nguo yako ili damu yangu isirukie nguo
zako, ili mama yangu asiione akawa ni mwenye kuhuzunika kutokana nayo, kisha
kinoe kisu chako na ukipitishe kwa haraka shingoni mwangu ili kifo kiwe chepesi
kwangu. Utakaporudi kwa mama yangu, mpe salamu zangu na mrudishie shati
langu kama ikiwa utaona kua kufanya hivyo kutampatia yeye faraja.’
397

Nabii Ibrahim akasema: ‘Ma shaa Allah! ni msaidizi mzuri sana kwangu mtoto
wangu, hakika wewe unatekeleza kile ambacho Allah Subhanah wa Ta’ala
amekiamrisha kutekelezwa.’

Na kwa upande mwengine basi anasema Abu Al Tufayl kua: Amesema Abd Allah Ibn
Abbas Radhi Allahu Anhu kua: Wakati Nabii Ibrahim alipoamrishwa kumchinja
mtoto wake basi njiani akakutana na Iblis, ambae alijaribu kumtangulia kua mbele
yake, lakini hata hivyo Ibrahim akamtangulia yeye na kua mbele yake, kisha
akaelekea katika upande wa Jamara al Aqaba (wa Mashariki) ambapo Ibrahim
akampopoa mawe 7, na kisha Iblis akamtokezea kwa upande wa Jamara Al Wusta
(kati kati) yake ambapo Ibrahim akampopoa mawe 7 pia hadi akaondoka, na kisha
akamtokezea tena mara ya 3 katika Jamarat As Sughra na akampopoa mawe 7 na
kisha akaendelea katika kutekeleza amrisho lake aliloamriwa.’

Anasema Muhammad Ibn Abd Allah Al Azraqi ambae ni mwanazuoni wa Ilm ya Tarikh
kua: ‘Wakati Ibrahim alipoondoka Minna basi alipofika katika maeneo ya Al
Aqabah akatokezea Ibilisi pembeni ya Jamarat Al Aqaba (Chungu ya Changarawe
ya Mashariki), na Jibril akamwambia Nabii Ibrahim: ‘Mpige Mawe’ hivyo Ibrahim
akachukua mawe 7 na kuanza kumpopoa Ibilisi hivyo Ibilisi akatoweka. Kisha
alipofika mbele kwenye Jamarat Al Wusta (Chungu ya Changarawe ya Kati)
akatokea tena Ibilisi na Jibril akasema: ‘Mpige mawe’ Nabii Ibrahim akachukua
mawe 7 na kumpiga nayo tena hadi akatoweka. Na alipofika katika Jamarat Al
Sughra (Chungu ya Changarawe ndogo) Jibril akasema tena: ‘Mpige mawe’ na
Nabii Ibrahim akampiga mawe 7 hivyo Ibilisi akatoweka moja kwa moja.’

Hivyo walipofika Minna basi Nabii Ibrahim akachukua kamba akamfunga Ismail, kisha
akainama na kumbusu huku akilia na machozi yakimtiririka yeye na mtoto wake, huku
machozi ya Nabi Ibrahim yakikutana na machozi ya Nabii Ismail kwenye mashavu ya
Nabii Ismail, kisha akachukua kisu na kukinoa na kisha kukiweka juu ya shingo ya Ismail
na kuanza kukipitisha juu ya shingo ya Ismail, lakini mbali ya kua ni kisu hicho kilikua
ni kikali kilichonolewa ili kisisababishe machungu zaidi wakati wa kuchinja kwake lakini
kisu hicho kilipowekwa kwenye shingo ya Nabii Ibrahim kamwe hakikua ni chenye
kukata, yaani hali ilikua kama mtu kuchukua kisu na kuanza kukata kipande cha shaba,
Allah Subhanah wa Taála anayaeleza haya katika Qurán pale aliposema:

�‫ﺖ ٱﻟﱡﺮْؤ َ� إِ ﱠ‬
َ ْ‫ﺻ ﱠﺪﻗ‬
ِ
َ ‫ﲔ ۞ َو َ� َدﻳْـﻨَﺎﻩُ أَن ٰ�ِﺑْـَﺮاﻫ ُﻴﻢ ۞ ﻗَ ْﺪ‬ ِ ِ‫َﺳﻠَﻤﺎ وﺗَـﻠﱠﻪُ ﻟِﻠْ َﺠﺒ‬ ﴿
َ َ ْ ‫ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ أ‬
﴾‫ﲔ۞ وﻓَ َﺪﻳْـﻨَﺎﻩُ ﺑِ ِﺬﺑْ ٍﺢ َﻋ ِﻈﻴ ٍﻢ‬ِ ِ َ ِ‫ﻚ َْﳒ ِﺰى ٱﻟْﻤ ْﺤ ِﺴﻨ‬ ِ
َ ُ ‫ﲔ۞ إ ﱠن َﻫـٰ َﺬا َﳍَُﻮ ٱﻟْﺒَﻼَءُ ٱﻟْ ُﻤﺒ‬ ُ َ ‫َﻛ ٰﺬﻟ‬
398

Falamma aslama watallahu liljabeeni, Wanadaynahu an ya ibraheemu, Qad


saddaqta alrru/ya inna kadhalika najzee almuhsineena, Inna hadha lahuwa albalao
almubeenu, Wafadaynahu bidhibhin AAadheemin (Surat As Saffat 37:103-107)

Tafsir: Na kisha walipokua tayari washajisalimisha, na tayari ameshamlaza kichwa


chake chini, Nasi tukamnadia Ewe Ibrahim! Ama kwa Hakika, umesadikisha kile
ulichokiona (Ndoto) na kadhalika hivi ndivyo tunavyowalipa Muhsinin (wenye
kufanya mema) Bila ya shaka huo ulikua ni Mtihani ulio wazi. Na tukamkomboa kwa
kafara tukufu sana (Kondoo aliekwisha chinjwa).

Ama tunapoangalia aya hizi za Surat Saffat 37:103-107 ambazo ziko wazi kabisa juu ya
kilichotokea basi tunaona zinasema kua mara tu baada ya Nabii Ibrahim kutaka
kumchinja Ismail basi Allah Subhanah wa Ta’ala alimtuma Malaika Jibril amletee Nabii
Ibrahim Kondoo wa Peponi kua ni mbadala wa Dhabih inayotaka kutolewa, kondoo huyo
mwenye pembe alikua na rangi nyeupe na nyeusi.

Ambapo kwa upande wa Imam Al Tustari basi anasema kua: ‘Nabii Ibrahim alikua
akimpenda Mtoto wake kutokana na mapenzi ya kimaumbile, na hivyo fadhila za
Allah Subhanah wa Ta’ala na Ulinzi wake ulitumika kumrekebisha yeye juu ya hilo,
kiasi ya kua alimuamrisha kumtoa Kafara mtoto wake huyo ijapokua nia ya
amrisho hilo haikua ni kumtoa sadaka bali ilikua ni kumsafisha Moyo wake
kutokana na mapenzi juu ya wengine wote isipokua yeye kupitia katika njia ambayo
itamuathiri kwa undani zaidi. Na hivyo akawa ni mwenye kusafishwa Nafsi yake na
na kua si mwenye kufuata tabia ya maumbile yake. Na ndio maana Allah Subhanah
wa Ta’ala akasema:’

‫ﲔ۞ َوﻓَ َﺪﻳْـﻨَﺎﻩُ ﺑِ ِﺬﺑْ ٍﺢ‬ ِِ ِ


ُ ِ‫ﲔ۞ إِ ﱠن َﻫـٰ َﺬا َﳍَُﻮ ٱﻟْﺒَﻼَءُ ٱﻟْ ُﻤﺒ‬ َ ‫﴿إِ ﱠ� َﻛ ٰﺬﻟ‬
َ ‫ﻚ َْﳒ ِﺰى ٱﻟْ ُﻤ ْﺤﺴﻨ‬
﴾‫َﻋ ِﻈﻴ ٍﻢ‬
Inna kadhalika najzee almuhsineena, Inna hadha lahuwa albalao almubeenu (Surat
As Saffat 37:105-106)

Tafsir: Na kadhalika hivi ndivyo tunavyowalipa Muhsinin (wenye kufanya mema) Bila
ya shaka huo ulikua ni Mtihani ulio wazi.

Yaani Allah Subhanah wa Ta’ala anatuwekea wazi kua alimpa Nabii Ibrahim
mtihani ambae ni wenye Rehma ndani yake. Hivi jee hamkuona namna Allah
399

Subhanah wa Ta’ala alimtuma Nabii Ibrahim katika hali ya kua ni mwenye


Kuridhika nae.

Ambapo amesema Said Ibn Jubayr kua amesema Abd Allah Ibn Abbas kua: ‘Kondoo
alietolewa kafara kwa ajili ya Ismail ndie yule yule Kondoo ambae, Abil ambae ni
mtoto wa Nabii Adam alimtoa kafara na akakubaliwa kafara yake hio. Ibrahim
alimtuma mtoto wake akamchukue Kondoo huyo na kisha akaenda nae katika
maeneo ya Minna kwa ajili ya kumchinja. Naapa kwa yule ambae nafsi ya Abd
Allah Ibn Abbas imo mikononi mwake, kua ingawa hizi ni siku za awali za Uislam,
lakini hata hivyo bado kichwa cha Kondoo huyo bado kinaning’inia kwa pembe
zake mbili katika mikingo ya maji ya Al Kaabah na kimeshakauka.’

Allah Subhanah wa Taála anatuwekea wazi tena pia kua Al Dhabih Allah hapa alikua
Ismail alikua ni mwenye kusadiki na kutekeleza ahadi yake ya kua ni mwenye Subra pale
aliposema katika Qurán kua:

﴾ً‫ﺻ ِﺎد َق ٱﻟْﻮ ْﻋ ِﺪ وَﻛﺎ َن ر ُﺳﻮﻻً ﻧﱠﺒِﻴّﺎ‬


َ ‫ن‬
َ ‫ﺎ‬‫ﻛ‬َ ‫ﻪ‬
ُ ‫ﱠ‬
‫ﻧ‬ ِ‫ﺎﻋﻴﻞ إ‬َ ِ َ‫﴿وٱذْ ُﻛﺮ ِﰱ ٱﻟْ ِﻜﺘ‬
ِ ‫ﺎب إِ ْﲰ‬
َ َ َ َ ْ َ
Waodhkur fee alkitabi ismaAAeela innahu kana sadiqa alwaAAdi wakana rasoolan
nabiyyan (Surat Maryam 19:54)

Tafsir: Na ametajwa katika Kitabu Ismail, kwa hakika yeye alikua ni aliesadiki juu ya
kile alichokiahidi na hakua isipokua ni Mtume na Nabii.
Na akasema tena Allah Subhanah wa Taála juu ya Ismail.

﴾‫ﺼﺎﺑِ ِﺮﻳﻦ‬ ِ ِ ِ ‫﴿وإِ ْﲰ‬


ِ ‫ﺎﻋﻴﻞ وإِ ْد‬
َ ‫ﻳﺲ َوذَا ٱﻟْﻜ ْﻔ ِﻞ ُﻛﻞﱞ ّﻣ َﻦ ٱﻟ ﱠ‬
َ ‫ر‬ َ َ َ َ
Wa-ismaAAeela wa-idreesa wadha alkifli kullun mina alssabireena(Surat Al
Anbiyah 21:85)

Tafsir: Na Ismail, na Idris, na Dhul Kifl wote walikua ni miongoni mwa wenye Subra.

Tunaporudi katika Surat Saffat 37:108 basi tunaona kua Allah Subhanah wa Taála
anaendelea kutueleza kwa kusema:

ِ
﴾‫ٱﻵﺧ ِﺮﻳﻦ‬ ‫﴿ َوﺗَـَﺮْﻛﻨَﺎ َﻋﻠَْﻴ ِﻪ ِﰱ‬
َ
400

Watarakna AAalayhi fee al-akhireena (Surat Saafat 37:108)

Tafsir: Na tukamuachia yeye kua ukumbusho kwa Ummah utakaofuatia.

Naam, hapa kidogo tunaona kua aya zinajumuisha Wahusika wa Tukio hili wote wawili
kwa pamoja yaani Nabii Ibrahim na Ismail lakini hapo hapo zinasisitizia Mhusika Mkuu
wa tukio ambae ni Nabii Ibrahim.

Kwani tumeona kua Aya zimemtaja hali ya Mchinjaji, na kisha zikataja hali ya anaetaka
kuchinjwa, na kisha hapo hapo zikamtaja Nabii Ibrahim kuzuiwa Kuchinja, na zikataja
kua alietaka kuchinjwa amekombolewa kwa Dhabih Adhimu.

Kisha zikabainisha kua kuna Mtu miongoni mwa watu wawili hawa waliomo ndani ya
tukio kua Ameachwa kua ni kumbukumbu kutokana na tukuo hili kwa ajili ya
kukumbukwa na Vizazi vya baadae.

Lakini aya hazikutaja kama mtu huyo ni Mchinjaji au ni Alietaka kuchinjwa. Na kisha
baada ya hapo aya zinamtaja tena Nabii Ibrahim. Sasa tunapoangalia Mjumuisho huu wa
Aya basi bila ya shaka tunaweza tukasema kua alieachiwa hapa kua ni Kumbukumbu
kwa Vizazi Vijavyo kutokana na tukio hili, ni wote wawili yaani Nabii Ibrahim na Ismail.

Kwani wote ni wenye kukumbukwa kutokana na tukio hili. Na bila ya Shaka ametiliwa
Mkazo zaid Nabii Ibrahim kwa Sababu yeye ni Mhusika Mkuu. Na yeye ni Mhusika
Mkuu kwa Sababu Mtihani huu ni Mkubwa zaid kwake yeye kama Nabii na Kama Mzee
kwani Mara zote Mzee hua ni Mwenye kua tayari ajitolee Muhanga yeye kuliko kumtoa
Muhanga Mtoto wake.

Na bado Nabii Ibrahim alikua na Miaka zaidi ya 100 katika kipindi hiki, ambapo Ismail
hata miaka 10 hajafika, hivyo bila ya shaka Hapa Kama Nabii Ibrahim angeambiwa kua
Ajitoe yeye basi ingekua si mtihani mkubwa kwa sababu keshaishi sana, na Mtoto wake
huyu hana wasiwasi nae kuishi peke yaje na mama yake kwani anajua kua yuko chini ya
usimamizi wa Allah Subhanah wa Ta'ala.

Hivyo ndio maana Nabii Ibrahim akatiliwa Mkazo zaidi na kuwekwa zaidi katika tukio
hili ili kua ni Fundisho kwetu kuhisi na kuona Ukubwa wa Imani ya Nabii Ibrahim. Lakini
hapo hapo pia kuona Ukubwa wa Subra na Imani ya Ismail ambae alikua hajawa Matume
wala Nabii Bado.
401

ِِ ِ ِ ِ ِِ
۞‫ﲔ‬ َ ‫ﻳﻦ ۞ َﺳﻼٌَم َﻋﻠَ ٰﻰ إِﺑْـَﺮاﻫ َﻴﻢ۞ َﻛ ٰﺬﻟ‬
َ ‫ﻚ َْﳒ ِﺰى ٱﻟْ ُﻤ ْﺤﺴﻨ‬ َ ‫َوﺗَـَﺮْﻛﻨَﺎ َﻋﻠَْﻴﻪ ﰱ ٱﻵﺧ ِﺮ‬
﴿
﴾‫ﺎد� ٱﻟْﻤﺆِﻣﻨِﲔ‬ ِ ِ ِ
َ ْ ُ َ َ‫إِﻧﱠﻪُ ﻣ ْﻦ ﻋﺒ‬
Watarakna AAalayhi fee al-akhireena, Salamun AAala ibraheema, Kadhalika
najzee almuhsineena, Innahu min AAibadina almu/mineena (Surat Saafat 37:108-
111)

Halafu aya za Surat Saffat zinazofuatia baada ya hizo zinaanza na habari ya mtoto
mwengine wa Nabii Ibrahim ambae ni Is-haq kwa kusema:

‫ﺎق َوِﻣﻦ‬
َ ‫ﲔ ۞ َوَﺎﺑ َرْﻛﻨَﺎ َﻋﻠَْﻴ ِﻪ َو َﻋﻠَ ٰﻰ إِ ْﺳ َﺤ‬ ِِ ‫ﺎق ﻧَﺒِﻴﺎً ِﻣﻦ ٱﻟ ﱠ‬
َ ‫ﺼﺎﳊ‬ ِِ
َ ّ ّ َ ‫َوﺑَﺸْﱠﺮَ�ﻩُ ﺈﺑ ْﺳ َﺤ‬
﴿
ِِ ِ ِ ِ ِ
﴾‫ﲔ‬ ٌ ِ‫ذُِّرﻳﱠﺘ ِﻬ َﻤﺎ ُْﳏﺴ ٌﻦ َوﻇَﺎﱂٌ ﻟّﻨَـ ْﻔﺴﻪ ُﻣﺒ‬
Wabashsharnahu bi-ishaqa nabiyyan mina alssaliheena, Wabarakna AAalayhi
waAAala ishaqa wamin dhurriyyatihima muhsinun wadhalimun linafsihi
mubeenun (Surat Saffat 37:112-113)

Tafsir: Na tukambashiria kuhusiana na Is-haq, Nabii miongoni mwa waja wema. Na


Tukambariki yeye na Is-haqa na kizazi chao kua cha wenye kufanya mema na baadhi
ni wenye kujidhulumu nafsi zao wazi wazi.

Hivyo ayah mbili hizi ambazo pia zinambashiria Nabii Ibrahim kua Nabii Is-haq atakua
ni Nabii na mwenye kizazi cha wenye kufanya Mema. Hivyo kama Dhabihu Allah alikua
ni Is-haq basi kwa ni ayah hii ikawa ni yenye kupingana na ahadi ya kua Nabii Is-haq
atatoa kizazi chema? Bila ya shaka hapa kama Dhabihu Allah angekua ni Nabi Is-haq
basi Nabii Ibrahim angemuuliza Allah Subhanah wa Ta’ala imekuaje amuamrishe
kumchinja mtoto huyo ambae tayari ameshaahidi kutoa kizazi chema?

Hivyo bila ya shaka Dhabihu Allah hakua mwengine isipokua ni Nabii Ismail ambae ndie
aliepewa darja ya utukufu wa kua ni msaidizi katika ujenzi wa Baytu Allahi Al Haram.

Nabii Ismail na Hajar waliendelea kukaa na watu wa Banu Jurhum na wakaanza kua ni
wenye kuzungumza nao kwa lugha yao ambayo ilikua ni Lugha ya Kiarabu kwani ukweli
ni kua asili ya Waarabu imetokana na miongoni mwa makundi watu wa aina tatu ya
zifuatazo:-
402

1. Al Arab ul Baidah (‫ )اﻟﻌﺮب اﻟﺒﺎﺋﺪة‬Waarabu waliopotea: Hawa ni wale watu waliokua


miongoni mwa kizazi kilichotoweka cha watu wa ‘Ad, Thamûd, Tasam, Jadis na
Imlaq ambao walikua wakiishi katika maeneo ya Al Ahqaf yaliyopo baina ya
Hadramawt na Oman ambao Mtume wao alikua ni Nabii Hud A’layhi Salaam.
2. Al Arab ul Ariba (‫ )اﻟﻌﺮب اﻟﻌﺎرﺑﺔ‬Waarabu wenye Uarabu asilia: Hawa ni wale watu
waliokua ni miongoni mwa kizazi kilichotokana na Nabii Hud A’layhi Salaam
kupitia kwa Ya‘rub Ibn Yashjub Ibn Qahtan Ibn Hud ambao walikua wakijulikana
pia kama Waarabu wa Yarub wa Qahtan ambapo pia walikua wakitawala katika
maeneo ya Yemen.
3. Al Arab al Mustariba (‫ )اﻟﻌﺮب اﻟﻤﺴﺘﻌﺮﺑﺔ‬Waarabu waliopewa Uarabu kwa
kuchanganya vizazi: Hawa ni wale watu waliotokana na kizazi cha Nabii Ibrahim
A’layhi Salaam kupitia kwa Nabii Ismai’l A’layhi Salaam.

Baada ya Nabii Ibrahim kuchanganyika na watu wa Banu Jurhum basi alipokua mkubwa
akaoa mmoja kati ya wanawake wa watu hao. Ambapo mara baada ya ndoa hio basi Hajar
akafariki na kuzikwa ndani ya Hijr (Eneo liliopo Kaskazini Magharibi ya Al Kaabah
baina ya Ruqn al Iraq na Ruqn Al Sham ambapo kuna kikuta chenye umbo la Nusu Duara
chenye upana wa mita moja na nusu na urefu wa mita moja maarufu kama Hijr Ismail,
Hijr Al Kaaba au Hatira).

Hivyo Nabii Ismail akabaki peke yake pamoja na mke wake huyo aliekua akiitwa
Ammara na watu wa jamii ya mke wake, na haukuchukua mda basi Nabii Ibrahim
akamtembelea mtoto wake huyo Nabii Ismail na kumkuta Ammarah lakini Nabii Ismail
mweyewe hayupo Nyumbani kwake.

Hivyo akamuuliza Ammara baada ya kumsalimia kwa kumwambia kua: ‘Jee mwenye
Nyumba yuko wapi?’ Mke wa Nabii Ismail akajibu: ‘Ametoka ameenda kuwinda.’
Kwani ilikua ni kawaida ya Nabii Ismail kua ni mwenye kupenda kupanda Farasi,
kupigana mieleka na kutoka nje ya mji wa Makkah kwa ajili ya kuenda Wanyama wa
chakula wa aina mbali mbali kwa kutumia Upinde na pia kwa kutumia mitego, hivyo
Nabii Ismail alikua ni mtaalamu mkubwa wa Shabaha kwa kutumia Upinde.

Nabii Ibrahim akauliza: ‘Jee unaweza kunikanikaribisha chakula chochote kile au


kinywaji?’ Ammara akajibu: ‘Sina cha kukukaribishia, kwani hakuna watu
wanaokuja kututembelea’. Baada ya kujibiwa hivi basi Nabii Ibrahim akaaga na
kumwambia Ammara kua: ‘Basi akija mwenye Nyumba mpe Salam zangu na
mwambie kua abadilishe kizingiti cha mlango wake.’

Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kama Mke wa Ismail angekua
ni mwenye kumpa chakula Ibrahim katika Siku hio basi katika wakati huu Nafaka
zingekua rahisi kibei katika mji wa Makkah kutokana na Baraka za Ibrahim.’
403

Jioni Nabii Ismail aliporudi akasikia harufu ya Baba yake, hivyo akamuuliza Ammara:
‘Jee kuna mgeni yeyote yule alietembelea leo hii?’. Mke wake akasema: ‘Kuna Mzee
Mtu Mzima sana alikuja leo. Na anakusalimia’.

Nabii Ismail akajua lazima kutakua na Ujumbe muhimu kutoka kwa Baba yake hivyo
akauliza tena: ‘Jee amesemaje?’ Ammarah akajibu: ‘Amesema kua akija Mume wako
nisalimie na kisha mwambie kua abadilishe Kizingiti cha Mlango wake.’

Nabii Ismail akasema kumwambia Ammara kua: ‘Huyo alikua ni Baba yangu na
ujumbe huo unamaanisha kua mimi nikupe Talaka yako.’ Hivyo Nabii Ismail
akampa Talaka yake mwanamke huyo.

Hivyo Nabii Ismail akamuoa mwanamke mwengine wa Banu Jurhum aitwae Sayyida
Bint Mudad ambae ni mtoto wa Mudad Ibn Amr aliekua kiongozi wa ukoo wa Banu
Jurhum wenye asili ya Al Arab ul Ariba. Na mara nyengine tena Nabii Ibrahim
akatemelea na Mji wa Makkah na hakufanikiwa kumkuta tena Nabii Ismail lakini safari
hii akakutana mabadiliko ya kuonana na Sayyida Bint Mudad, akasema Alhamd Lillah
Ismail amefahamu maana iliyomo ndani ya ujumbe wangu niliomuachia, hivyo baada ya
kusalimia basi akauliza kwa kusema: ‘Jee Mwenye Nyumba Nimekuta?’.

Sayyida Bint Mudad akajibu: ‘Ametoka, ameenda kuwinda lakini hatochelewa


atarudi si mda mrefu Inshaa Allah. Ingia ndani ukaribie na Allah akuingize katika
rehma zake’

Nabii Ibrahim akauliza: ‘Jee unaweza kunikaribisha chakula chote kile au maji ya
kunywa?’. Sayyida Bint Mudad akajibu: ‘Naam, bila ya shaka.’ kisha akamtayarishia
Maziwa na Nyama na akaombea barka juu yake.

Kisha akamwambia Nabii Ibrahim: ‘Wacha nizikoshe na kuzichana Nywele zako’


Lakini Nabii Ibrahim akakataa kwa sababu hakuwa na mda mrefu wa kukaa katika
Nyumba hio hivyo Sayyida Bint Mudad akatoa jiwe la kukalia na kuliweka upande wa
kulia wa Nabii Ibrahim na kuanza kumkosha miguu yake, na alama ya nyayo yae
ikaganda kwenye jiwe hilo, baada ya hapo Nabii Ibrahim akala na kisha akaaga na
kumwambia Sayyyida Bint Mudad kua: ‘Akija Mume wako basi usisahau kumpa
salam zangu na mwambie kua: Kizingiti cha Mlango wake kiko Imara.’

Amesema Imam Abu Is-haq Ahmad Ibn Muhammad Ibn Ibrahim Al Thalabi Al
Shafii kuhusiana na Jiwe alilokoshewa Miguu yake Nabii Ibrahim na Sayyida bint
Muddad kua: Amesema Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu kua: ‘Hakika mimi
niliona alama ya Nyayo, Kisigino na Vidole vya miguu vya Ibrahim katika Jiwe
404

hilo. Lakini alama hizo zimefutika kutokana na kua watu walikua wakisugua
mikono yao katika jiwe hilo.’

Imam Ath Thalabi anaendelea kusema tena kua: Amesema Abd Allah Ibn Umar
Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:
‘Kona mbili za Maqam Ibrahim zilikua ni za jiwe la Zamaradi, kutoka katika
bustani ya Peponi, ambazo Allah alilizima Nuru yake Jiwe hilo, na hakika kama
ingekua Allah Subhanah wa Ta’ala hakuzizima Nuru za mawe hayo basi bila ya
shaka Nuru yake ingeifunika Dunia.’’

Baada ya mda Nabii Ismail akarudi kutoka mawindoni na kusikia tena harufu ya Baba
yake, hivyo akauliza kama alivyouliza siku ile kama kuna mtu yeyote alietembelea
ambapo Sayyida Bint Mudad akajibu: ‘Naam alitembelea Mtu Mzima Kizee mwenye
uso unaovutia na mwenye kunukia harufu nzuri sana, ambae aliniambia
nikusalimie na kusema kua Kizingiti cha Mlango wako kiko Imara, nami
nikamkosha miguu yake na hii hapa imeganda alama ya Nyayo yake.’ Nabii Ismail
akajibu: ‘Huyo ni Baba yangu Ibrahim, na wewe ndio hicho kizingiti, hivyo
amekuridhia na ameniusia nisiachane nawe’ na akajua kua ujumbe aliachiwa
unamaanisha ubora wa mke aliemuoa safari hii.

Hivyo ndoa baina ya Nabii Ismai’l Ibn Ibrahim A’layhi Salaam na Sayyida Bint Mudad
ndio iliyotoa kizazi kinachojulikana kama Al Arab al Mustariba ambao pia hujulikana
kama Waarabu wa Adnan Kizazi hiki cha watoto wa Nabii Ismai’l A’layhi Salaam
ambacho ndio asili halisi ya Al Arab al Mustariba kilikua na watoto waitwao ni Qidar,
Fidmah, Bana, Buth, ‘Awil, Taqis, Masma’, Taima, Jasham, Haidir, Duma, Yatur, na
Massa. Ambapo kizazi cha Taima baadae kilihamia katika maeneo ya Madinah al
Munawwara na kizazi cha Massa kilihamia katika maeneo ya Yemen ambapo mmoja
kati ya mtoto wake wa kike aitwae Sabiha aliolewa na ndugu yake Nabii Yaqub aitwae
Ays Ibn Is-haq Ibn Ibrahim.

Ambapo tunapozama katika Ilm ul Huruf na kuangalia majina ya Nabii Ismail na mke
wake wa mwanzo ambae ni Ammarah basi tunaona kua mbali ya kua Ammarah alikua ni
mwanamke asiekua na Akhlaq nzuri lakini pia Ammarah alikua haendani kijina na hivyo
kua si mwenye kuendana na Nabii Ismail kwa asilimia kubwa sana, hivyo hata kama
wangeendelea kubakia pamoja basi wasingedumu kwenye ndoa hio.

Ama kwa upande mwengine basi tunaona kua mbali ya kua na Ahklaq nzuri lakini
Sayyida Bint Maddad alikua pia ni mwenye kuendana kwa asilimia kubwa sana kijina na
kimaisha na Ismail kiasi ya kua walikua ndoa yao ilikua na mapenzi makubwa sana na
utshamilivu ndani yake.
405

Vile vile tunapoangalia kwa upande wa ndoa ya Nabii Ibrahim, Sarah na Hajar basi
tunaona kua Nabii Ibrahim alikua akimpenda sana Sarah, kwani walikua wakiendana
sana kimajina kiasi ya kua ilikua ni vigumu kwa Nabii Ibrahim kukaa mbali na Sarah.

Na pia Majina yanaonesha kua ingawa Nabii Ibrahim alikua anampenda sana Sarah lakini
hata hivyo kwa upande wa Hajar basi majina yao yalikua hayaendani sana kiasi ya kua
Nabii Ibrahim aliamua kumuoa Hajar kutokana na mapendekezo ya Sarah, kwani kwa
upande wake yeye Sarah basi alikua ni mwenye kuendana sana kijina na Hajar na hivyo
Sarah alikua ni mwenye kumpenda zaidi Hajar, lakini hata hivyo hisia za kimaumbile za
wivu zilimpelekea Sarah kuamua kumhamisha Hajar.

Na hivyo kutokana na kua jina la Nabii Ibrahim na Hajar si yenye kuendana sana basi
ndio maana ikawa rahisi kwa Nabii Ibrahim kumhamishia Hajar katika mji wa Makkah,
na hata Hajar nae hakuwa ni mwenye kulalamika sana kua mbali na Nabii Ibrahim, tofauti
na ilivyokua kwa Sarah ambapo tumeona kua Sarah alikua hamruhusu Nabii Ibrahim
kukaa mda mrefu katika mji wa Makkah.

Kwa hivyo ingekua vigumu zaidi kama Nabii Ibrahim kama angeambiwa amhamishie
Sarah katik amji wa Makkah na kisha yeye abakie na Hajar, kuliko kuamrishwa kwake
kua amhamishe Hajar, kutokana na kuendana kwao kimajina.


UJENZI WA BAYTU ALLAH AL HARAM


Safari ya Tatu wakati Nabi Ibrahim akiwa katika mji wa Jerusalem basi Allah Subhnah
wa Taála akamuamrisha Nabii Ibrahim kumjengea Nyumba Tukufu ambayo itakua ni
yenye kufanyiwa Ibada kwa ajili ya kumkumbuka Allah Subhanah wa Taála ila Nabii
Ibrahim akawa hajui aijenge wapi Nyumba hio, hivyo akauliza jee Nyumba hio inatakiwa
ijengwe wapi?

Ama juu ya jambo hili basi Wanazuoni wametofautiana pia kwani wapo wasemao kua
Allah Subhanah wa Taála alimtumia Sakina Nabii Ibrahim na hivyo kumuongoza hadi
Makkah katika eneo la Al Kaabah. Sakina inayozungumziwa hapa ilikua ni aina ya upepo
ambao Nabii Ibrahim aliufuata pale ulipoanza kuvuma na hivyo ukamuongoza hadi
katika sehemu inayotakiwa kujengwa Al Kaabah na ulipofika katika eneo hilo la Ardhi
ambalo kulikua na asili ya msingi wa Nyumba iliojengwa na Nabii Adam basi upepo huo
ulizunguka hapo hapo kwa dakika kadhaa na kukusanya kichuguu cha mchanga kuashiria
kua hio ndio sehemu inayotakiwa kujengwa Nyumba hio, Allah Subhanah wa Taála
406

akamtumia Nabii Ibrahim kiwingu ambacho kilitoa kivuli ambacho kilichomuainishia


ukubwa wa eneo na umbo la jengo la Al Kaabah.

Anasema Wahb Ibn Munabih kua: ‘Wakati Adam aliposhushwa Ulimwenguni na


kuona ukubwa wa Ulimwengu basi hukua akijua kua yuko peke yake yeye na Hawa
tu, hivyo akauliza kwa kusema: ‘Ya Allah. Jee katika Ardhi hii kuna viumbe
wengine wanaokutukuza zaidi yangu?’

Allah Subhanah wa Taála akamwambia Nabii Adam: ‘Usiwe na Khofu kwani kwa
hakika mimi nitajaliwa watu miongoni mwa kizazi chako ambao watakua
wananitukuza, na nitaweka ndani yake Nyumba ambazo zitanyanyuliwa kutokana
na kutukuzwa kwangu. Na kisha nitaichagua Nyumba moja miongoni mwa
Nyumba hizo ambayo nitaitukuza kutokana na Utukufu wangu na kisha nitaifanya
kua ni Nyumba iliyo salama kiasi ya kua usalama wake utawafanya awe salama kila
kiumbe atakaeingia ndani katika maeneo yake, iwe juu yake au chini yake.

Na yeyote yule atakaeutangazia Utukufu wa Nyumba hio kutokana na Utukufu


wake basi atakua chini ya Salama yangu na yeyote yule atakaekua anaitumia kwa
ajili ya kuwatia khofu watu basi bila ya shaka atakua ni mwenye kuvunja
maamrisho yangu na kujitoa ndani ya nusura yangu. Nitaifanya kua ndio Nyumba
ya kwanza kwa watu kutoka katika sehemu mbali mbali kuja huku wakiwa
wamechoka, na wamejaa mavumbi huku wakisema ‘Labayka Allahuma Labayk!’

Kwani hua ni mwenye kuja katika Nyumba yangu si kwa ajili ya chochote bali ni
kwa ajili yangu. Na kila atakaekuja atakua ni mgeni wangu na hivyo ni wajibu
wangu mimi Mwingi wa Rehma kwa watakaotembelea nyumba hio kuwaingiza
ndani ya Rehma zangu, ili awe ni mwenye kupata utulivu na msaada anaouhitaji.
Na wewe Adam utaijenga Nyumba hio, na wataijenga Mitume na Manabii wangu
watakaokuja vizazi baada ya vizazi kutoka katika Watoto wako.’’

Hivyo Nabii Adam akalijenga Al Kaabah ambalo likabakia katika eneo hilo hadi
katika kipindi cha Nabii Nuh wakati yalipotokea mafuriko na Allah Subhanah wa
Taála akalipandisha juu Al Kaabah katika Mbigu ya nne kwa uwezo wake. Na
kumtuma Malaika Jibril kulichukua Jiwe Jeusi na kulihifadhi katika Jabal Abu
Qubays ili lisije likaathirika kutokana na mafuriko ya wakati wa Nabii Nuh. Hivyo
eneo hilo la Al Kaabah likawa na kubakia na alama tu ya msingi wa Al Kaabah hadi
katika kipindi cha Nabii Ibrahim alipoamrishwa aunyanyue msingi huo.’

Ama kwa upande mwengine basi wapo wanaosema kua Allah Subhanah wa Taála
alituma kiwingu ambacho Nabii Ibrahim alikifuata kutoka alikotoka hadi katika Mji wa
Makkah na kilipofika katika eneo husika basi kikafanya kivuli cha umbo ambalo
407

linatakiwa lijengwe Al Kaabah. Na pia kuna wasemao kua aliemuongoza Nabii Ibrahim
alikua ni Malaika Jibril na hii ndio maana ya ile aya isemayo:

ِِ ِ ِ ‫ﺖ أَن ﻻﱠ ﺗُ ْﺸ ِﺮْك ِﰉ ﺷﻴﺌﺎً وﻃَ ِﻬﺮ ﺑـﻴ‬


ِ ‫﴿وإِ ْذ ﺑـ ﱠﻮأْ َ�ِ ِﻹﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ ﻣ َﻜﺎ َن ٱﻟْﺒـﻴ‬
َ ‫ﱴ ﻟﻠﻄﱠﺂﺋﻔ‬
‫ﲔ‬ َ ْ َ ْ ّ َ ْ َ َْ َ َ َْ َ َ
ِ ‫وٱﻟْ َﻘﺂﺋِ ِﻤﲔ وٱﻟﺮﱠﻛ ِﻊ ٱﻟ ﱡﺴﺠ‬
﴾‫ﻮد‬ ُ ‫ََﱡ‬ َ
Wa-idh bawwa/na li-ibraheema makana albayti an la tushrik bee shay-an watahhir
baytiya liltta-ifeena waalqa-imeena waalrrukkaAAi alssujoodi (Surat Al Hajj 22:26)
Tafsir: Na (Kumbuka) tulipomchagulia Ibrahim sehemu (Tukufu) ya Nyumba (Al
Kaabah) (Huku tukimwambia) Usishirikishe chochote nami, na isafishe Nyumba
yangu kwa ajili ya wale watakaoizunguka, na watakaosimama (kwa ajili ya Sala), na
watakao rukuu na watakao sujudu.

Hapa tunaona kua aya imetumia neno Bawwa/na ambapo ni neno la Kiarabu linalotokana
na neno Bawaá ambalo kwa kilugha hua ni lenye kumaanisha Kuchukua, Kuchagua,
Kuamua, Kuweka, Kutayarisha, Kutenga au Kuanzisha kitu au sehemu, hivyo hapa
kinachoainishwa na aya hii ni sehemu maalum ambayo ilikua tayari imeshachaguliwa na
Allah Subhanah wa Taála kwa ajili ya ujenzi wa hiyo Baytu Allah, kwani sehemu hii
ndio sehemu ambayo Malaika walilijega Al Kaabah miaka 2000 iliyopita kabla ya
kuumbwa Nabii Adam kutokana na amri ya Allah Subhanah wa Taála.

Neno Baytu ni neno linalotokana na neno Bata la Kiarabu ambalo maana yake hua ni:
Kuutumia Usiku kwa ajili ya kitu au jambo fulani, Kuvamia usiku, Kukesha. Neno Bata
ndio lililotoa neno Bayt ambalo maana yake hua ni Nyumba, Makazi, Chumba au Sehemu
ya Kuishi. Hivyo basi Jengo la Al Kaabah limeitwa Baytu Allahi kwa sababu Allah
Subhanah wa Taála ndie Muumba wa Ulimwengu na kila kitu kilichomo ndani yake,
hivyo Nyumba hii imejengwa kwa ajili ya Kumuabudu Allah Subhnah wa Taala tu ndani
yake, ambae yeye ndie alieinyanyua Darja ya Nyumba hii.

Hapa tunaona kua kama vile Allah Subhanah wa Taála aliwaamrisha Nabii Ibrahim na
Nabii Ismail kuisafisha na kuunyanyua upya msingi wa Nyumba yake kupitia katika
msingi ulioanzishwa na Nabii Adam basi nasi pia tunatakiwa kuyajenga na kuyanyanyua
maisha yetu upya kila baada ya mda, kwani maisha yetu ni maisha ambayo yenye
kubadilika badilika kila baada mda kwa makosa yetu ya kimaumbile hivyo hutubidi
kuyarudisha katika hali inayokubalika na kuridhisha mbele ya Allah Subhnah wa Taála.

Ama kuhusiana na kuelezea ni nani muasisi wa Masjid Al Aqsa, hakuna kukubaliana


miongoni mwa Wanazuoni kua ni nani muanzilishi halisi, kwani kuna mitizamo
408

inayotofautiana kuhusiana na muasisi wa msikiti huo. Mtizamo wa kwanza ni ule utokao


kwa Mujaddid Ad Din Shihab Ad Din Imam Ibn Hajar ambao wanasema kua Nabii Adam
A’layhi Salaam ndie mtu wa mwanzo kujenga Masjid Al Aqsa baada ya kulijenga Al
Kaabah, na ushahidi wao unatokana na Hadith ya Ibn Hisham katika kitabu chake cha Al
Tijan.

Imam Abu Bakr Ahmad Ibn Husayn Ibn Ali Ibn Musa Al Khosraji Al Bayhaqi anasema
katika kitabu chake Al Dalai’il kua Abdullah Ibn Umar Radhi Allahu Anhu amesema kua:

‘Allah Subhanahu wa Ta’ala alimtuma Jibril kwa Adam na akamuamrisha kujenga


nyumba ya Allah (Al Kaabah) halafu akamuamrisha aizunguke na kisha Adam
akaambiwa: Wewe ni mtu wa mwanzo na hii ni nyumba ya mwanzo kujengwa kwa
ajili ya Allah:’

Mtizamo huu pia unathibitishwa na katika Hadith nyengine ya Abu Dharr ambayo
inasema kua Abu Dharr alimuuliza Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam: ‘Ya
Rasul Allah! Jee ni upi msikiti uliojengwa mwanzo?’ naye akajibu ‘Al Masjid Al
Haram’, nami nikamuuliza tena: ‘Halafu ukafuatia upi?’ naye akajibu ‘Al Masjid
Al Aqsa’ nami nikamuuliza ‘Jee kuna mda gani wa kujengwa baina yao’, naye
akajibu ‘Miaka 40’ (Al-Bukhari).

Hivyo kutokana na ushahidi huu, ikiwa ni Nabii Adam ndie aliejenga Masjid Al Haram
na Masjid Al Aqsa umejengwa baada ya miaka 40 basi hii inamaanisha kua Nabii Adam
A’layhi Salaam ndie aliejenga Masjid Al Aqsa au alijenga mmoja kati ya watoto wake
kutokana na utofauti wa miaka baina yao.

Shaykh Ibn Taymiyah ni mmoja kati ya wale wenye mtizamo huo wa kua Masjid Al Aqsa
ulijuengwa na Nabii Ibrahim A’layhi Salaam pale aliposema kua ‘Mitume ilianza kusali
ndani ya Masjid Al Aqsa kuanzia wakati wa Nabii Ibrahim’ na pia kuna kauli ambayo
inasema Shaykh Ibn Taymiyah alisema kua: ‘Al Masjid Al Aqsa ulijengwa wakati wa
uhai wa Nabii Ibrahim’.

Ukiangalia baina ya mitizamo hii miwili ya kwanza na ya pili utaona kua kuna utofauti
wa kua, Wanazuoni wenye mtizamo wa kwanza wametofautiana na mtizamo wa pili kwa
sababu inasemekana kua Nabii Ibrahim A’layhi Salaam aliamrishwa aunyanyue msingi
wa Al Kaabah, na hivyo hakuujenga kuanzia kwenye msingi wake kwa kuchimba ardhini
bali alijenga kutokana na msingi wa jengo hilo ambao aliukuta tayari upo.

Mtizamo wa tatu ni ule usemao kua Nabii Yaqub ndie muanzilishi aliejenga Masjid Al
Aqsa, na miongoni mwa wanaounga mkono mtizamo huu ni pamoja na Imam Ibn Al
Qayim. Imam Ibn Al Qayim anasema katika kitabu chake Zad al-Ma‘ad kua: ‘Aliejenga
409

Masjid Al Aqsa ni Nabii Yaqub, na hii ilikua ni miaka 40 baada ya Nabii Ibrahim
kujenga Al Kaabah’

Kwa upande mwengine Imam Ibn Kathir pia ni miongoni mwa wanaounga mkono
mtizamo huo wa Imam Ibn Al Qayim kwani katika kitabu chake cha al Bidayah Wal
Nihayah. Anasema kua Nabii Yaqub alienda Jerusalem na akajenga jengo kama meza
ambayo ndiyo Al Masjid Al Aqsa na baadae Nabii Sulayman A’layhi Salaam akaufanyia
marekebisho.

Mtizamo wa nne ni ule mtizamo wenye shaka, mtazamo usemao kua mji wa Jerusalem
ulichaguliwa kutokana na amri ya Nabii Daud A’layhi Salaam ambae aliishi katika karne
ya 10 kabla ya kuja Nabii Isa A’layhi Salaam, kujenga sehemu ya kumuabudia Allah,
sehemu ambayo baadae ilifanyiwa marekebisho na Nabii Sulayman A’layhi Salaam
kutokana na Wahyi alioshushiwa na Allah Subhanahu wa Ta’ala, lakini mtizamo huu
unatokana na Agano la kale la biblia na pia hakuna ushahidi unaoounga mkono jambo
mtizamo huu katika vitabu vya Kiislam.

Hata hivyo, vyovyote vile itakavyokua, basi Masjid Al Aqsa ni sehemu muhimu na
takatifu kwa dini ya Kiislam, na ndio maana Allah Subhanahu wa Ta’ala akaichagua
kama sehemu pekee ambayo alimpeleka Nabii wake Muhammad Salallahu A’layhi wa
Salam ambae aliwasalisha Mitume wote katika msikiti huo na baadae akapanda juu
mbinguni katika safari ya Miraj.

Al Masjid Al Aqsa umetajwa katika Hadith nyingi za Nabii Muhammad Salallahu A’layhi
wa Salam ikiwemo Hadithi zifuatazo:

Anasema Abu Al-Darda Radhi Allahu Anhu kua Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa
Salam alisema: ‘Sala moja katika Masjid Al Haram (Makkah) ina thamani ya sala
100000, sala moja katika msikiti wangu (Masjid An Nabawi, Madina) in thamani ya
Sala 500 na Sala katika Al Aqsa (Jerusalem) ina thamani ya Sala 500 katika misikiti
myengine yote.’ (Al-Bukhari)

Ma’imunah Bint Sa‘d anasema kua Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam
aliulizwa kuhusiana na mtu ambae anataka lakini hawezi kusafiri na kuenda kusali katika
Al Masjid al-Aqsa, jee afanyeje? Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akasema:
‘Anaweza kutengeneza zawadi ya udi ambao aupeleke ukafukizwe msikitini humo,
na hii itakua ni sawa na yule aliesali ndani ya Msikiti huo’. (Imam Ahmad na Imam
Ibn Majah)
410

Ambapo Imam Jamal Al Din Al Qasimi Al Dimashq basi yeye nasema kua: ‘Maana ya
neno Aqsa hua linamaanisha ‘Wa Mbali’ na hivyo Masjid Al Aqsa umepewa jina
hilo kwa sababu ya kutokana na Umbali wake kutoka katika Mji wa Makkah.’

Na bila ya shaka Masjid Al Aqsa ni moja kati ya sehemu tukufu kwa dini ya Kiislam
kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Msifunge safari isipokua
kwa Miskiti mitatu: Msikiti huu – Masjid Nabawi, Madina - Masjid Al Haram
Makkah na Masjid Al Aqsa.’ (Muslim, Kitabul-Hajj, 15/415, 511, 512)

Ama kuhusiana na hadith hii basi inabidi tuifafanue kwani kuna baadhi hua wanaitumia
sivyo na hivyo kukataza watu kutembelea Miskiti ambapo anasema `Allamah Al Shaykh
Sulayman Ibn `Umar Ibn Mansur Al`Ujayli Al Misri Al Shafi'i Al Jamal kua: ‘Maana
ya maneno ‘Msifunge Safari’ hua inamaanisha kwa ajili ya Kusali Ndani yake.
Hivyo hii haijumuishi Kufunga safari kwa ajili ya jambo jengine zaidi ya Kusali
Ndani yake. Kwani Imam An Nawawi amesema kua: ‘Hakuna umuhimu wa
Kufunga safari kwa ajili tu ya Miskiti hii mitatu’ ambapo Al Hafidh Imam Zain Al
Din 'Abd Al-Rahim Al 'Iraqi amesema kua: ‘Miongoni mwa tafsiri bora ya Hadith
hii ni kua inahusiana na hukmu ya Miskiti, yaani msifunge safari kwa ajili kuenda
kusali katika Miskiti yeyote ile isipokua hii mitatu. Ama kuhusiana na kufunga
safari kwa ajili ya kuenda kwenye Msikiti kwa ajili ya kutafuta Ilm, Kutembelea
Waja wema na Wakuu wake mtu, kutembelea kwa ajili ya kufanya biashara, au
kwa ajili ya Kutalii na kadhalika basi haya hua hayahusiani na hadith hii.’’

Ambapo kwa upande mwengine basi kuna Hadith kama hii ambayo ni ya Abu Said al
Khudri Radhi Allahu Anhu ambayo inasema kua: ‘Amesema Rasul Allahi Salallahu
Alayhi wa Salam kua: ‘Mtu anaesali hatakiwi kufunga safari kwa ajili ya kusali
katika Msikiti wowote ule, isipokua katika Msikiti wa Makkah, Msikiti wa Al Aqsa
na katika Msikiti huu wangu’’ (Musnad Imam Ahmad, Musanaf Imam Ibn Abi Shayba)

Na anasema Shaykh ul Islami Imam Al Subki kua: ‘Hakuna sehemu hapa Duniani ambayo
inapendekezwa zaidi kuliko nyenginezo kwa mtu kusafiri kwa ajili ya sehemu husika
Ulimwenguni isipokua katika sehemu hizi tatu. Yaani hii ni kulingana na shariah
kusimamia manufaa yanayohusiana na msingi wa hukmu husika. Hivyo kuhusiana na
sehemu nyengine basi haitakiwi mtu kufunga safari kwa sababu ya sehemu husika, bali
inatakiwa mtu afunge safari kuenda katika sehemu kwa ajili ya kutembea, kutafuta
Ilm, na kufanya mambo ambayo yanaruhusika au yanapendekezwa.’

Na bila ya shaka kulingana na mitizamo hio ya Wanazuoni tuliyoaingalia kuhusiana na


Kutembelea Miskiti basi tunaona kua inaegemea katika aya tulizoziangalia hapo
mwanzoni mwa kitabu hiki ambazo ni aya zinazotilia mkazo na kuhimiza kutawanyika
na kusafiri katika Ardhi ambapo miongoni mwao ikiwemo ile isemayo:
411

ِ َ‫ﻨﺸﺊ ٱﻟﻨﱠ ْﺸﺄَة‬


‫ٱﻵﺧَﺮَة إِ ﱠن‬ ِ ‫ٱﳋ ْﻠﻖ ﰒُﱠ ﱠ‬ ِ ‫﴿ﻗُ ْﻞ ِﺳﲑُواْ ِﰱ ٱﻷ َْر‬
ُ ُ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻳ‬ َ َْ َ‫ﻒ ﺑَ َﺪأ‬َ ‫ض ﻓَﭑﻧﻈُُﺮواْ َﻛْﻴ‬
﴾‫ٱﻪﻠﻟ َﻋﻠَ ٰﻰ ُﻛ ِﻞ َﺷﻲ ٍء ﻗَ ِﺪﻳﺮ‬
ٌ ْ ّ َ‫ﱠ‬
Qul seeroo fee al-Ardhi faondhuroo kayfa badaa alkhalqa thumma Allahu yunshi-
o alnnash-ata al-akhirata inna Allaha AAala kulli shay-in qadeerun (Al-Ankabut
29:20)

Tafsir: Sema: Tembeeni katika Ardhi na mpate kuona (namna Allah) alivyoanzisha
Uumbaji wake, na kisha Allah atawafufua viumbe kesho Akhera. Kwa Hakika Allah
ni muweza juu ya kila kitu.

Hivyo basi hua inakubalika kufunga safari kuenda sehemu fulani kwa ajili ya kitu fulani
ambacho kimeruhusika au kimependekezwa kisharia na sio kufunga safari kuenda
sehemu fulani kwa ajili ya sehemu hio isipokua kwa sehemu tu hizo tatu tukufu
alizozitaja Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam ambapo Masjid Al Aqsa imetajwa
kwenye aya ifuatayo:

ِِ ِ ْ ‫﴿ﺳْﺒﺤﺎ َن ٱﻟﱠ ِﺬى أَﺳﺮ ٰى ﺑِﻌْﺒ ِﺪﻩِ ﻟَْﻴﻼً ِﻣﻦ ٱﻟْﻤﺴ ِﺠ ِﺪ‬
َ ْ‫ٱﳊََﺮام إِ َ ٰﱃ ٱﻟْ َﻤ ْﺴﺠﺪ ٱﻷَﻗ‬
‫ﺼﻰ‬ ْ َ َّ َ َْ َ ُ
﴾ُ‫ﺼﲑ‬ِ ‫ٱﻟﱠ ِﺬى ﺎﺑرْﻛﻨَﺎ ﺣﻮﻟَﻪ ﻟِﻨُ ِﺮﻳﻪ ِﻣﻦ آ�ﺗِﻨَﺂ إِﻧﱠﻪ ﻫﻮ ٱﻟ ﱠﺴ ِﻤﻴﻊ ٱﻟﺒ‬
َ ُ َ ُ ُ َ ْ َُ ُ ْ َ َ َ
Subhana alladhi asra biAAabdihi laylan mina almasjidi alharami ila almasjidi al-
aqsa alladhi barakna hawlahu linuriyahu min ayatina innahu huwa alssameeAAu
albaseeru (Surat Al Israa 17:1)

Tafsir: Ametukuka (Allah) ambae amemchukua mja wake katika safari ya usiku
kutoka Masjid Al Haram kuelekea Masjid Al Aqsa ambayo maeneo ya jirani yake
tumeyabariki ili kumuonesha yeye alama zetu, kwani yeye ni miongoni mwa wenye
kusikia na kuona (vitu vyote).

Anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Nabii Ibrahim alimwambia
Ismail kwa kusema: ‘Ewe Ismail, Hakika Allah Subhanah wa Ta’ala amenipa mimi
jukuu kubwa nilitekeleze’ Ismail akajibu: ‘Itabidi Ulitekeleze’ Nabii Ibrahim
akasema: ‘Jee utanisaidia?’ Ismail akajibu: ‘Bila ya Shaka.’ Nabii Ibrahim
akamuonesha Ismail muinuko mdogo wa Ardhi uliopo mbele yao na kusema: ‘Allah
Subhanah wa Ta’ala ameniamrisha mimi kujenga Nyumba yake katika sehemu hii’’
412

Kisha Nabii Ibrahim akaanza ujenzi wa Al Kaabah huku Nabii Ismail akiwa ni kibarua
mwenye kumpa Nabii Ibrahim jiwe moja baada ya jengine. Inasemekana kua Al Kaabah
lilijengwa kutokana na mawe ya aina tano tofauti ambayo ni kutokana na Jabal Al Sinai.
Jabal Al Zaytun, Jabal Lubnan, Jabal Al Juddi na Jabal al Hira.

Kwani amesema Allah Subhanah wa Taa’ala kua: ‘Yeyote yule atakaeskua ni mwenye
kusali Salal 5 huku akiwa ni mwenye kuelekea Mji wa Makka na kisha
akalizunguka Al Kaabah mara 5, basi nitamsamehe dhambi zake hata kama
ukubwa wake ikiwa ni sawa na Milima mitano.’

Walipokaribia kumaliza basi ikabakia sehemu ya jiwe moja ambalo Nabii Ismail
aliondoka na kuenda kulitafuta jiwe litakaloweza kukaa katika sehemu husika na
aliporudi akamkuta Nabii Ibrahim akiwa tayari ameshaliweka jiwe hilo katika sehemu
husika. Nabii Ismail akashangaa na kumuuliza Nabii Ibrahim: ‘Baba! Jee ni nani
aliekuletea hili Jiwe?’ Nabii Ibrahim akasema: ‘Kuna mtu aliniletea ambae alikua
hataki mimi nikutegemee wewe kuhusiana jiwe hili.’

Kisha Nabii Ibrahim akasema kumwambia Nabii Ismail: ‘Niletee jiwe zuri lenye
kupendeza, ili niliweke kwenye pembe ile liwe ni alama kwa ajili ya watu’. Lakini
kabla ya Nabii Ismail kuondoka kutafuta Jiwe hilo basi Jabal Abu Qubays likanadia: ‘Ya
Ibrahim! Hakika mimi ninalo jiwe hilo hivyo njoo ulichukue’ Hivyo Nabii Ibrahim
akaenda kwenye Jabal Abu Qubays na akalikuta Hajar Al Aswad (Jiwe Jeusi) na
kuliweka katika sehemu yake, na hivyo Jengo la Al Kaabah kua tayari katika hali ya kua
ni Nyumba itakayotembelewa mara kwa mara na watu mbali mbali wanaomuamini Allah
Subhanah wa Taála Ulimwenguni kama inavyosema aya:

ِ ِ ِ ِ‫ﱠ‬ ِ ‫ﺖ َﻣﺜَﺎﺑَﺔً ﻟِّﻠﻨ‬


َ ‫ﱠﺎس َوأ َْﻣﻨﺎً َوٱﲣ ُﺬواْ ﻣﻦ ﱠﻣ َﻘﺎم إِﺑْـَﺮاﻫ َﻴﻢ ُﻣ‬
�َ ‫ﺼﻠًّﻰ َو َﻋ ِﻬ ْﺪ‬ َ ‫﴿ َوإِ ْذ َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ٱﻟْﺒَـْﻴ‬
﴾‫ﻮد‬ ِ ‫ﺎﻋﻴﻞ أَن ﻃَ ِﻬﺮا ﺑـﻴ ِﱴ ﻟِﻠﻄﱠﺎﺋِِﻔﲔ وٱﻟْﻌﺎﻛِ ِﻔﲔ وٱﻟﺮﱠﻛ ِﻊ ٱﻟ ﱡﺴﺠ‬
‫ََ َ ََﱡ‬ ِ ‫إِ َ ٰﱃ إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ وإِ ْﲰ‬
ُ َ َ ْ َ ّ َ َ َ َ َْ
Wa-idh jaAAalna albayta mathabatan lilnnasi waamnan waittakhidhoo min
maqami ibraheema musallan waAAahidna ila ibraheema wa-ismaAAeela an
tahhira baytiya liltta-ifeena waalAAakifeena waalrrukkaAAi alssujoodi (Surat Al
Baqara 2:125)

Tafsir: Na (Kumbuuka) wakati tulipoijaalia Nyumba (Al Kaabah) kua ni sehemu ya


kutembelea na kukusanyika mara kwa mara na ya amani kwa watu. Na ifanyeni
Maqam Ibrahima (Sehemu aliyosimamia Ibrahim) kua ni sehemu ya Kusalia. Na
tuliahidiana na (tulimuamrisha) Ibrahim na Ismail waisafishe Nyumba Yangu, kwa
413

ajili ya wale watakaoizuru na kuizunguka, watakaokaa (itiqaf) au watakao ruku na


kusujudu.

Maqamat Ibrahima ni sehemu ambayo yenye jiwe ambalo Nabii Ibrahim alikua
amepanda na kusimama katika wakati wa kujenga Al Kaabah. Jiwe hilo lilikua kama
jukwaa kwa ajili ya Nabii Ibrahim kuweza kufikia juu zaidi katika kujenga ukuta wa Al
Kaabah, hivyo basi hili lilikua ni jiwe ambalo lina urefu wa centimeter 20 lilikua
linatembea pamoja nae bila ya yeye kujua kutoka sehemu moja hadi nyengine kuzunguka
ukuta wa Al Kaabah.

Kutokana na Miujiza ya Allah Subhanah wa Taála basi Jiwe hili lilibadilika hali yake ya
ugumu na kua ni katika hali ya ulaini kiasi ya kua Nabii Ibrahim hakua ni mwenye kuhisi
kuchoka katika kusimama kwake katika wakati wa ujenzi huo na hivyo miguu yake ilikua
kama iliyosimama juu kitu laini kama sponji sponji ambalo lilisababisha miguu hio
kuzama kwa sentimita 10 ndani ya Jiwe hilo, na hivyo kubakisha alama za nyayo zake
ambazo ziko hadi hii leo.

Walipokua katika harakati za kumalizia kazi ya ujenzi wa Nyumba hio tukufu ya Allah
Subhanah wa Ta’ala basi Nabii Ibrahim na Nabii Ismail basi wakamuomba Allah
Subhanah wa Ta’ala kama inavyosema aya ifuatayo:

‫َﻧﺖ‬ َ ‫ﻴﻞ َرﺑـﱠﻨَﺎ ﺗَـ َﻘﺒﱠ ْﻞ ِﻣﻨﱠﺂ إِﻧﱠ‬ ِ ‫ﺖ وإِ ْﲰ‬ ِ ‫﴿وإِ ْذ ﻳـﺮﻓَﻊ إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ ٱﻟْ َﻘﻮ‬
ِ ‫اﻋ َﺪ ِﻣﻦ ٱﻟْﺒـﻴ‬
َ ‫ﻚأ‬ ُ ‫ﺎﻋ‬ َ َ ْ َ َ َ ُ َ ْ ُ َْ َ
ِ ِ ْ ‫ٱﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ُﻣﺴﻠِﻤ‬ ِ ‫ٱﻟ ﱠﺴ ِﻤ‬
�َ‫ﻚ َوأَ ِر‬ َ ‫ﻚ َوِﻣﻦ ذُِّرﻳﱠﺘِﻨَﺂ أُﱠﻣﺔً ﱡﻣ ْﺴﻠ َﻤﺔً ﻟﱠ‬ َ َ‫ﲔ ﻟ‬ َْ ْ ‫ﻴﻊ ٱﻟْ َﻌﻠ ُﻴﻢ۞ َرﺑـﱠﻨَﺎ َو‬ ُ
‫ﺚ ﻓِﻴ ِﻬ ْﻢ َر ُﺳﻮﻻً ِّﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ‬ ْ ‫اب ٱﻟﱠﺮِﺣ ُﻴﻢ۞ َرﺑـﱠﻨَﺎ َوٱﺑْـ َﻌ‬ ُ ‫َﻧﺖ ٱﻟﺘﱠـ ﱠﻮ‬
َ ‫ﻚأ‬ َ ‫ﺐ َﻋﻠَْﻴـﻨَﺂ إِﻧﱠ‬
ْ ُ‫َﻣﻨَﺎﺳ َﻜﻨَﺎ َوﺗ‬
ِ
ِ
‫ٱﻟﻌ ِﺰ ُﻳﺰ‬
َ ‫َﻧﺖ‬ َ ‫ﻚأ‬ َ ‫ٱﳊِ ْﻜ َﻤﺔَ َوﻳـَُﺰّﻛِﻴ ِﻬ ْﻢ إِﻧﱠ‬
ْ ‫ﺎب َو‬ ِ
َ َ‫ﻚ َوﻳـُ َﻌﻠّ ُﻤ ُﻬ ُﻢ ٱﻟْﻜﺘ‬ َ ِ‫آ�ﺗ‬َ ‫ﻳَـْﺘـﻠُﻮاْ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ‬
﴾‫ٱﳊَ ِﻜﻴﻢ‬
ُ
Wa-idh yarfaAAu ibraheemu alqawaAAida mina albayti wa-ismaAAeelu rabbana
taqabbal minna innaka anta alssameeAAu alAAaleemu; Rabbana waijAAalna
muslimayni laka wamin dhurriyyatina ommatan muslimatan laka waarina
manasikana watub AAalayna innaka anta alttawwabu alrraheemu; Rabbana
waibAAath feehim rasoolan minhum yatloo AAalayhim ayatika
wayuAAallimuhumu alkitaba waalhikmata wayuzakkeehim innaka anta
alAAazeezu alhakeemu (Surat Al Baqara 2:127-129)
414

Tafsir: Na kumbuka wakati Ibrahim alipokua akinyanyua pamoja na Ismail msingi


wa Nyumba (Al Kaabah) (waliomba kwa kusema): ‘Ewe Mola wetu! Tukubalie jambo
letu hili. Kwani kwa hakika wewe ni mwingi wa Kusikia na ni mwenye kujua kila kitu.
Ewe Mola wetu! Tujaalie sisi tuwe ni wenye kujisalimisha kwako na vizazi vyetu na
Ummah wetu ujisalimishe kwako, na tuoneshe Manasika (njia au hatua zinazohitajika
kufanywa katika Hija na Umra) na utukubalie toba zetu. Kwani kwa hakika wewe ni
mwingi wa kusamehe na mwingi wa Rehma. Ewe Mola wetu! Watumie (Vizazi vyetu
hivyo) kutoka miongoni mwao Mtume. Ambae atawasomea aya zako na kuwaelimisha
juu ya Kitabu chako na Hikma na wape Utukufu. Kwani kwa hakika wewe ni mwenye
uwezo juu ya kila kitu na ni mwingi wa Hikma’

Aya zinatuonesha umuhimu wa kuonesha unyenyekevu katika kutekeleza Maamrisho ya


Allah Subhanah wa Taála na pia umuhimu wa kuomba kukubaliwa kwa amali zetu kila
baada ya kutekeleza amali hizo kwani si jukumu lake Allah Subhanah wa Taála kutulipa
kutokana na utekelezaji wa maamrisho yake, bali ni jukumu letu na kutulipa hua ni
khiyari yake kutokana na Rehma zake juu yetu. Na kwa kua Nabii Ibrahim na Nabii
Ismail walikua tayari ni wenye kujisalimisha kwa Allah Subhana wa Taála basi ni
jukumu lao pia kuomba kujaaliwa kua na msimamo katika maamrisho yake ya Mola wao
kama ilivyokua ni jukumu letu sisi mimi na wewe.

Aya hizi ni miongoni mwa aya ambazo zinatuthibitishia kua kuomba dua ya pamoja
baada ya kufanya Amali njema au Ibada yeyote kua ni sehemu ya kufuata Millat
Ibrahima, jambo ambalo ni tofauti na wale wapingao dua za pamoja baada ya Sala.

Ingawa Aya zinatuonesha kua wakati Nabii Ibrahim na Nabii Ismail walipokua
wakimalizia kujenga Jengo la Al Kaabah basi waliomba dua wakubaliwe Jambo lao hilo
la kujenga Nyumba hio ya Allah Subhanah wa Ta'ala, lakini kwetu sisi mimi na wewe
tunaweza tukaona ni Jambo la Kawaida, na hii ni kwa sababu wengi wetu hatuhisi uzito
wa Jambo hilo kwa sababu ya Udhaifu wa Imani katika Nyoyo zetu.

Na ndio maana kwa wale wanaojua na kutafakkar uzito wa ujumbe wa aya hizi basi hua
ni wenye kulia pale wanapozisoma aya hizi, kwa Mfano Imam Wuhayb Ibn Al Ward
ambae ni walimu wa Imam Sufyan Ibn Uyayna na pia Imam Abd Allah Ibn Mubarak
alikua ni mwenye kulia kila aisomapo hizi za Surat Al Baqara 2:127 Jee unajua kwa nini
Imam Wahb Ibn Al Wird alikua akilia?

Imam Wuhayb Ibn Al Ward alikua akilia kwa sababu alikua akitafakkar na huku alisema
kwa kumwambia Allah Subhanah wa Ta'ala: ‘Ya Allah! Ya Rahman Ya Rahim!
Hakika Khalil wako alikua anajenga Nyumba huku akiwa na khofu kua huenda
usimkubalie Jitihada zake hizo za kujenga Nyumba yako hio, wakati sisi leo hii
415

Tunaafanya hivi viamali vyetu vidogo vidogo visivyokua na thamani, halafu hua
tunafikiria kua vitakubaliwa.’

Hivyo ndivyo walivyokua waliotangulia kabla yetu, walikua wakitathamini mifano


ambayo Dharaba Allahu Mathalan - Ambayo Allah ameitoa kwa Kutupigia dharuba ili
tutafakkari na wao ndio walikua ni wenye kutafakkar tofauti mimi na wewe, tunasoma
Qur'an kama nyimbo hatutafakkar na hivyo hatuzingatii.

Kwani amesema Imam Abu Muhammad Al Husayn Ibn Mas'ud Ibn Muhammad Al Farra'
Al-Baghawi kua: ‘Amesema Mujahid kua Maana ya neno Kitabu na neno Hikma
yaliyotajwa kwenye aya ifuatayo:

َ‫ٱﳊِ ْﻜ َﻤﺔ‬ ِ ِ ِ ْ ‫﴿رﺑـﱠﻨﺎ وٱﺑـﻌ‬


ْ ‫ﺎب َو‬ َ ِ‫آ�ﺗ‬
َ َ‫ﻚ َوﻳـُ َﻌﻠّ ُﻤ ُﻬ ُﻢ ٱﻟْﻜﺘ‬
ِ
َ ‫ﺚ ﻓﻴ ِﻬ ْﻢ َر ُﺳﻮﻻً ّﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ ﻳـَْﺘـﻠُﻮاْ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ‬ َْ َ َ َ
﴾‫ٱﻟﻌ ِﺰ ُﻳﺰ ٱﳊَ ِﻜﻴﻢ‬
َ ‫َﻧﺖ‬ َ ‫ﻚأ‬ َ ‫َوﻳـَُﺰّﻛِﻴ ِﻬ ْﻢ إِﻧﱠ‬
ُ
Rabbana waibAAath feehim rasoolan minhum yatloo AAalayhim ayatika
wayuAAallimuhumu alkitaba waalhikmata wayuzakkeehim innaka anta
alAAazeezu alhakeemu (Surat Al Baqara 2:129)

Tafsir: Ewe Mola wetu! Watumie (Vizazi vyetu hivyo) kutoka miongoni mwao Mtume.
Ambae atawasomea aya zako na kuwaelimisha juu ya Kitabu chako na Hikma na wape
Utukufu. Kwani kwa hakika wewe ni mwenye uwezo juu ya kila kitu na ni mwingi wa
Hikma’

Yanamaanisha kua: ‘Kitabu ni Qur’an na Hikma hua inamaanisha Kuifaham


Qur’an’ ambapo wengine wamesema kua neno Hikma lililotumika hapa
linamaanisha Hukmu. Na wengine wamesema kua ni Ilm inayojumuisha na
kuifanyia kazi Ilm hio.’

Subhanah Allah! Tunapoangalia kisa cha Nabii Ibrahim basi tunaona kua miongoni mwa
Mitume ambao walijibiwa Dua zao lakini baada ya mda mrefu sana basi yeye na Nabii
Ismail ni miongoni mwao, kwani kama tulivyoona hapo awali kua alipokua na umri wa
miaka 16 alioomba apate kizazi chema pale aliposema:

ِ ‫ﺼـﻠِ ِﺤ‬
﴾‫ﲔ‬ ‫ﺐ ِﱃ ِﻣ َﻦ اﻟ ﱠ‬ ِّ ‫﴿ر‬
ْ ‫ب َﻫ‬ َ
Rabbi hab lee mina alssaliheena (Surat As Saffat 37: 100)
416

Tafsir: Ya Rabbi nijaalie kua ni mwenye kizazi chema.

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala akamjibu Dua hio na kumjaalia Ghulamun Haliimun
yaani mtoto wa Kiumwe mwenye ustamilivu baada ya kupita miaka 80 baadae pale
aliposema:

﴾‫﴿ﻓَـﺒَﺸْﱠﺮَ�ﻩُ ﺑِﻐُﻼٍَم َﺣﻠِﻴ ٍﻢ‬


Fabashsharnahu bighulamin haleemin (Surat As Saffat 37:101)

Tafsir: Hivyo nasi tukambashiria juu ya mtoto wa kiume mwenye ustahmilivu.

Na hivyo katika aya zetu za Surat Al Baqara basi tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala
alimkubalia Nabii Ibrahim na Nabii Ismail dua yao kwa pamoja pale walipoomba kwa
kusema:

َ‫ٱﳊِ ْﻜ َﻤﺔ‬ ِ ِ ِ ْ ‫﴿رﺑـﱠﻨﺎ وٱﺑـﻌ‬


ْ ‫ﺎب َو‬ َ ِ‫آ�ﺗ‬
َ َ‫ﻚ َوﻳـُ َﻌﻠّ ُﻤ ُﻬ ُﻢ ٱﻟْﻜﺘ‬
ِ
َ ‫ﺚ ﻓﻴ ِﻬ ْﻢ َر ُﺳﻮﻻً ّﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ ﻳـَْﺘـﻠُﻮاْ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ‬ َْ َ َ َ
﴾‫ٱﻟﻌ ِﺰ ُﻳﺰ ٱﳊَ ِﻜﻴﻢ‬
َ ‫َﻧﺖ‬ َ ‫ﻚأ‬ َ ‫َوﻳـَُﺰّﻛِﻴ ِﻬ ْﻢ إِﻧﱠ‬
ُ
Rabbana waibAAath feehim rasoolan minhum yatloo AAalayhim ayatika
wayuAAallimuhumu alkitaba waalhikmata wayuzakkeehim innaka anta
alAAazeezu alhakeemu (Surat Al Baqara 2:129)

Tafsir: Ewe Mola wetu! Watumie (Vizazi vyetu hivyo) kutoka miongoni mwao Mtume.
Ambae atawasomea aya zako na kuwaelimisha juu ya Kitabu chako na Hikma na wape
Utukufu. Kwani kwa hakika wewe ni mwenye uwezo juu ya kila kitu na ni mwingi wa
Hikma’

Hivyo Dua yao hio ilijibiwa zaidi ya miaka 3000 baadae pale Allah Subhanah wa Taala
aliposema katika Quran kuhusiana na Utukufu wa Waumini na Majukumu ya Rasul Allah
Sallahu Alayhi wa Salam juu yao kua:

‫آ�ﺗِِﻪ‬ ِ ِ ِ ‫ﺆﻣﻨِﲔ إِ ْذ ﺑـﻌ‬


َ َ َ َ ِ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻋﻠَﻰ ٱﻟْ ُﻤ‬
َ ‫ﺚ ﻓﻴ ِﻬ ْﻢ َر ُﺳﻮﻻً ّﻣ ْﻦ أَﻧْـ ُﻔﺴ ِﻬ ْﻢ ﻳَـْﺘـﻠُﻮاْ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ‬ ‫﴿ﻟََﻘ ْﺪ َﻣ ﱠﻦ ﱠ‬
ٍ ‫ﺿ‬ ِ ِ ِْ ‫وﻳـَﺰّﻛِﻴ ِﻬﻢ وﻳـﻌﻠِّﻤﻬﻢ ٱﻟْ ِﻜﺘَﺎب و‬
﴾‫ﲔ‬ ٍ ِ‫ﻼل ﱡﻣﺒ‬ َ ‫ٱﳊ ْﻜ َﻤﺔَ َوإِن َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻣ ْﻦ ﻗَـْﺒ ُﻞ ﻟَﻔﻰ‬ َ َ ُ ُ ُ ََُ ْ َُ
417

Laqad manna Allahu AAala almu/mineena idh baAAatha feehim rasoolan min
anfusihim yatloo AAalayhim ayatihi wayuzakkeehim wayuAAallimuhumu alkitaba
waalhikmata wa-in kanoo min qablu lafee dalalin mubeenin (Surat Al Imran 3:164)

Tafsir: Na kwa Hakika Allah amewafadhilisha Waumini kwa kuwashushia Mtume


ambae ni kutoka miongoni mwao. Ambae ni mwenye kuwasomea wao Aya zake, na
kuwatukuza (Kwa kuwasafisha Dhambi zao kutokana na kumfuata kwao) na
kuwafundisha (yaliyomo ndani ya) Kitabu na Hikma (za Sunna zake) wakati hapo
kabla walikua katika udhalili mkubwa ulio wazi.

Na pia pale aliposema katika aya isemayo:

‫آ�ﺗِِﻪ َوﻳـَُﺰّﻛِﻴ ِﻬ ْﻢ َوﻳـُ َﻌﻠِّ ُﻤ ُﻬ ُﻢ‬ ِ


َ ‫ﲔ َر ُﺳﻮﻻً ّﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ ﻳَـْﺘـﻠُﻮ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ‬
ِ
َ ِّ‫ﺚ ِﰱ ٱﻷ ُّﻣﻴ‬
ِ
َ ‫﴿ ُﻫ َﻮ ٱﻟﱠﺬى ﺑَـ َﻌ‬
ٍ ِ‫ﺿﻼٍَل ﱡﻣﺒ‬ ِ ِ ِْ ‫ٱﻟْ ِﻜﺘَﺎب و‬
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ٱﳊ ْﻜ َﻤﺔَ َوإِن َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻣﻦ ﻗَـْﺒ ُﻞ ﻟَﻔﻰ‬ َ َ
Huwa alladhee baAAatha fee al-ommiyyeena rasoolan minhum yatloo AAalayhim
ayatihi wayuzakkeehim wayuAAallimuhumu alkitaba waalhikmata wa-in kanoo
min qablu lafee dalalin mubeenin (Surat Al Jumuah 62:2)

Tafsir: Yeye (Allah Subhanah wa Ta’ala) ndie ambae amewaletea miongoni mwa
Wasiosoma Mtume kutoka miongoni mwao. Kuwasomea wao Aya zake, na
kuwatukuza (Kwa kuwasafisha Dhambi zao kutokana na kumfuata kwao) na
kuwafundisha (yaliyomo ndani ya) Kitabu na Hikma (za Sunna zake) wakati hapo
kabla walikua katika udhalili mkubwa ulio wazi.

Ambapo anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kuhusiana na
ayah hii kua: ‘Ummiyyina ni wale ambao wamemuamini Muhammad Salallahu
Alayhi wa Salam na hivyo kua ni wenye kujumuika nae kwa Ittiba (kumfuata) na
kwa Iqtidaa (kumuiga). Hivyo yeyote yule ambae hakumuiga basi huyo si miongoni
mwa watu wake.’

Ambapo neno Ummiyyina ambalo hua linamaanisha Wasiosoma hua pia linamaanisha
Umati ambao haujawahi kushushiwa kitabu chao hapo hapo kabla. Na hivyo basi hawana
hata ufahamu kuhusiana na vitabu vya Dini nyengine.
418

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anatuwekea wazi Upotovu na Utukufu wa baina ya


wale watakaomuasi na watakaomfuata Mtume huyo aliombewa Dua na Nabii Ismail na
Nabii Ismail yaani Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa kusema kua:

‫َﺿ ﱠﻞ أ َْﻋ َﻤﺎ َﳍُْﻢ‬ ِ‫اﻪﻠﻟِ ٱﻟﱠﺮ ْﲪـٰ ِﻦ ٱﻟﱠﺮِﺣﻴ ِﻢ ۞ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ َﻛ َﻔﺮواْ وﺻ ﱡﺪواْ ﻋﻦ ﺳﺒِ ِﻴﻞ ﱠ‬ ‫﴿ﺑِ ْﺴ ِﻢ ﱠ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟ أ‬ َ َ ََ ُ َ
‫ٱﳊَ ﱡﻖ ِﻣﻦ ﱠرّﻬﺑِِ ْﻢ‬ْ ‫ﺎت َو َآﻣﻨُﻮاْ ِﲟَﺎ ﻧـُِّﺰَل َﻋﻠَ ٰﻰ ُﳏَ ﱠﻤ ٍﺪ َوُﻫ َﻮ‬ ِ ‫۞وٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ آﻣﻨﻮاْ وﻋ ِﻤﻠُﻮاْ ٱﻟ ﱠ‬
ِ ‫ﺎﳊ‬
َ ‫ﺼ‬ َ َ َُ َ َ
﴾‫ﻛ ﱠﻔﺮ ﻋْﻨـﻬﻢ ﺳﻴِﺌﺎﻬﺗِِﻢ وأَﺻﻠَﺢ ﺎﺑ َﳍﻢ‬
ُْ َ َ ْ َ ْ َّ َ ْ ُ َ َ َ
Biismi Allahi AlRahmani AlRahiim; Alladheena kafaroo wasaddoo AAan sabeeli
Allahi adalla aAAmalahum; Waalladheena amanoo waAAamiloo alssalihati
waamanoo bima nuzzila AAala muhammadin wahuwa alhaqqu min rabbihim
kaffara AAanhum sayyi-atihim waaslaha balahum (Surat Muhammad 47:1-2)

Tafsir: Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehma Mwingi wa Huruma. Ama kwa wale
Waliokufuru (Kwa Kumkataa Allah Subhanah wa Ta’ala na Mtume wake Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam) na Kuwazuia (Watu) kutokana na kufuata njia ya Allah,
basi (Allah Subhanah wa Ta’ala) atazidhalilisha amali zake. Na kwa wale walioamini
na wakafanya mema, na wakaamini kile alichoshushiwa Muhammad (Salallahu
Alayhi wa Salam), ambacho ni cha haki kutoka kwa Mola wao, (Basi Mola wao)
atazikufuru Dhambi zao na kuwaingiza katika hali njema.

Naam..hizi ni miongoni mwa aya ambazo zinaainisha matumizi ya neno Kafara ambalo
humaanisha Kufuru katika hali tofauti kuelezea matokeo yanayotegemeana na aina ya
Kufuru baada ya Jambo fulani. Kwani neno Kafara maana yake hua ni Kufunika,
Kukataa, Kukufuru, Kuficha, Kutokua na Shukrani, Kusamehe, Kutotilia maanani, n.k.

Neno Kafara ndio lililotoa neno Kafir ambalo hua ni lenye kumaanisha Yule ambae
anaefukia Mbegu ardhini, Yule Anaeficha Neema aliyofadhiliwa na Mola wake na pia
humaanisha Ufuniko wa Wingu Jeusi au wa Kiza cha Usiku.

Hivyo neno Kafara hua ni kinyume na neno Iman, ambapo Iman hua ni Kukubali Ukweli
na Kafara hua ni Kuukataa Ukweli.

Maana hii pia inawekwa wazi na ile aya ya pili ambayo nayo pia imetumia neno Kafara
katika hali nzuri na hivyo kuainisha Matokeo Mazuri yatakayopatikana baada ya
Kupingana na Jambo lisilolokua sahih katika aya ifuatayo.
419

ِ ُ‫﴿ﻻَ إِ ْﻛﺮاﻩ ِﰱ ٱﻟ ِّﺪﻳ ِﻦ ﻗَﺪ ﺗﱠـﺒـ ﱠﲔ ٱﻟﱡﺮ ْﺷ ُﺪ ِﻣﻦ ٱﻟْﻐَ ِﻰ ﻓَﻤﻦ ﻳ ْﻜ ُﻔﺮ ﺑِﭑﻟﻄﱠﺎﻏ‬
‫ﻮت َوﻳْـ ْﺆِﻣﻦ‬ ْ َ َْ ّ َ ََ ََ
﴾‫ﻴﻊ َﻋﻠِ ٌﻴﻢ‬ ِ ‫ٱﻧﻔﺼﺎم َﳍﺎ و ﱠ‬
ٌ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﲰ‬ َ َ َ َ
ِ َ‫ﭑﻪﻠﻟِ ﻓَـ َﻘ ِﺪ ٱﺳﺘﻤﺴﻚ ﺑِﭑﻟْﻌﺮوةِ ٱﻟْﻮﺛْـ َﻘﻰ ﻻ‬
ٰ ُ َ ُْ َ َ ْ َ ْ ‫ﺑِ ﱠ‬
La ikraha fee alddeeni qad tabayyana alrrushdu mina alghayyi faman yakfur
bialttaghooti wayu/min biAllahi faqadi istamsaka bialAAurwati alwuthqa la
infisama laha waAllahu sameeAAun AAaleemun (Surat Al baqara 2:256)

Tafsir: Hamna kulazimishana katika dini. Kwa hakika njia ya uongofu imebainishwa
kutokana na ile isiyokua sahih. Hivyo atakaeikufuru Taghut (Miungu myengine na
maovu mengine) na akamuamini Allah basi atakua ni mwenye kuegemea egemeo
linaloaminika ambalo kamwe halitovunjika. Na Allah ni mwenye kusikia kila kitu na
ni mwenye kujua kila kitu.

Hivyo majibu ya Dua ya Nabii Ibrahim na Nabii Ismail waliyoomba katika Surat Al
Baqara 2:129 yamejibiwa na kuwekwa wazi katika aya tulizoziangalia hapo hapo juu,
Surat Muhammad 47:1-2, Surat Al Jumuah 62:2, katika aya ya Surat As Saff 61:6
inayozungumzia ubashirio wa Nabii Isa Ibn Maryam ambayo inaelezewa katika Hadith
inayofuatia na nyenginezo nyingi ambazo haina haja ya kuzianisha zote katika kitabu
chetu.

Ama tunapoangalia kwa upande wa hadith basi tunaona kua anasema Imam Ahmad Ibn
Hanbal katika Musnad Imam Ahmad kua: ‘Amesema Abu Umammah Radhi Allahu
Anhu kua nilimuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam: ‘Ya Rasul Allah
(Salallahu Alayhi wa Salam) hivi mara ya kwanza ulitajwa katika sehemu gani?’
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Hakika mimi nilikua ni Katika
Dua ya Baba yangu Ibrahim, Katika Ubashirio wa Isa Ibn Maryam na katika
Ubainisho wa Ndoto ya Mama yangu alipoona Nuru iliyotoka Mwilini mwake na
Kumurika Makasri ya Sham’’

Na baada ya kumalizika ujenzi wa Jengo hilo la Al Kaabah basi Jengo hilo lilikua liko
katika muonekano ambao ni la Nusu Duara. Ambapo ukuta wa Upande wa Kaskazini
ulikua na urefu wa futi 48 na nchi 6, Upande wa Magharibi ulikua na Urefu wa futi 46
na nchi 5, upande wa Hatim Sharif ulikua na urefu wa Futi 33 na upande wa Ruqn Al
Yaman na Ruqn Al Aswad ulikua na Urefu wa futi 30.

Ambapo tunapozungumzia umbo la Jengo la Al Kaabah basi hua tunazungumzia Jengo


ambalo linafanana kieneo na kivipimo na Jengo Tukufu ambalo pia lipo Mbinguni
linalojulikana kama Bayt Al Maamur. Kwani tumeona hapo kabla kama alivyosema Allah
Subhanah wa Ta’ala amesema kuhusiana na Al Kaabah Kua:
420

ِ
﴾ً‫ﱠﺎس وأ َْﻣﻨﺎ‬ َ ‫﴿ َوإِ ْذ َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ٱﻟْﺒَـْﻴ‬
َ ِ ‫ﺖ َﻣﺜَﺎﺑَﺔً ﻟّﻠﻨ‬
Wa-idh jaAAalna albayta mathabatan lilnnasi waamnan (Surat Al Baqara 2:125)

Tafsir: Na (Kumbuuka) wakati tulipoijaalia Nyumba (Al Kaabah) kua ni sehemu ya


kutembelea na kukusanyika mara kwa mara na ya amani kwa watu.

Ambapo ayah hii imetumia neno Mathabatan ambalo ni lenye kutokana na neno Thaba
ambalo kwa Lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kurudia, Kukusanyika, Kukusanya,
Kurudi, Kulipa, Kunadia Sala na pia humaanisha Kufidia.

Hivyo Mathabatan hua linamaanisha Sehemu ya Kutembelea na Kupumzika Kila baada


ya mda fulani, au Sehemu ya Kukutana na Kupongezana kila baada ya mda fulani.

Kwa Hivyo Jengo Tukufu la Al Kaabah limeitwa Mathabatan kwa sababu sehemu hio
ndio iliyoteuliwa na Muumba kua ndio sehemu ya mkusanyiko wa viumbe wa
ulimwenguni Walioamini ambao ni Watu na Majini kila baada ya mda kwa ajili ya Allah
Subhanah wa Ta’ala kama vile ambavyo wakutanavyo kila siku viumbe wa Mbinguni
yaani Malaika katika Jengo Tukufu la Mbinguni yaani Bayt ul Maamur ambalo amelitaja
Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qur’an pale aliposema kua

ِ ﴿
﴾‫ﺖ ٱﻟْﻤ ْﻌﻤﻮِر‬
ُ َ ‫َوٱﻟْﺒَـْﻴ‬
Waalbayti almaAAmoori (Surat At Tur 52:4)

Tafsir: Na kwa Nyumba inayotembelewa sana.

Neno A'mara kwa Lugha ya Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Kuishi, Kujenga, Kujaza
Kitu au Sehemu kwa watu au Viumbe wengine wa Allah Subhanah wa Ta’ala na pia
humaanisha Kutembelea.

Naam neno A'mara ndio lililotoa neno U'mrun yaani Umri na pia likatoa neno Umra
yaani Kutembelea Eneo Takatifu.

Kwani neno A'mara ndio lililotoa pia neno I'mran ambalo ni jina la Mtu, na pia likatoa
jina Muamara ambalo humaanisha Mtu Mwema. Na likatoa neno I'maratun yaani Imara.
Na si hivyo tu bali neno A'mara ndio lilitolotoa neno Ma'amur yaani Sehemu
Inayotembelewa sana na viumbe wengi iwe Watu, Majini au Malaika.
421

Yaani Nyumba ambayo inafanana na Al Kaabah ambayo ipo juu mbinguni na hivyo kua
ni yenye kutembelewa na Malaika 70,000 kwa kila siku ambao hua ni wenye kufanya
Tawaf.

Hawa ni Malaika ambao kamwe hawarudi tena kufanya Tawaf katika Bayt Al Maamur
kwani tangu iumbwe Bayt Maamur basi kila siku inazungukwa na Malaika 70000,
Wapya kama alivyosema Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam kuhusiana na alipoenda
katika safari ya Miraj kua:

‘Na kisha nikaoneshwa Al Bayt Al Maamur, nami nikamuuliza Malaika Jibril


Kuhusiana nayo, na akajibu: ‘Hii ndio Bayt al Maamur sehemu ambayo Malaika
70000 hua wasali kila siku na wanapoondoka basi hua hawarudi tena.’’(Sahih
Bukhari na Muslim)

Na amesema Qatadah Ibn Diama kua amesikia kua Bayt Al Maamur ni Msikiti ambao
upo katika Mbingu ya saba sawia na juu ya Al Kaabah kiasi ya kua kama kitu
kikianguka kutoka katika Bayt Al Maamur basi moja kwa moja kitaangukia kwenye
Al Kaabah. (Imam Ibn Jarir At Tabari)

Lakini baadae likawa na Umbo lenye kuenda sambamba kivipimo na pande nne za upepo
unaopepea katika eneo hilo, kwani Umbo la Al Kaaba haliko katika umbo la Al Murabbii
(Mraba au Pembe nne Kamilifu) bali lipo katika umbo la Mamduud (Umbo kama la
Kashata lakini si Kashata lenye pande sawia) kutokea Upande wa Kaskazini-Magharibi
na Upande wa Kusini-Mashariki. Kiasi ya kua linapingana na Upepo unaovuma na
kupepea katika eneo hilo kutoka pande tofauti unaojulikana kama Al Naqba ambao ulikua
unajumuisha aina nne za Upepo.

Upepo wa aina ya kwanza ni ule upepo wa Saba ambao ni wenye kutokea katika maeneo
ya Kusini Mashariki yaani maeneo ya Yemen, huu unapiga upande wa Kusini ambao ni
wa Ruqn al Yaman kuelekea Ruqn al Iraq kupitia ni wa Mashariki upande liliopo Ruqn
Hajar Al Aswad, Upepo wa aina ya pili ni Junub (Kusini) ambao unavuma kutokea
Kusini Ruqn al Yaman kuelekea Magharibi kuelekea Ruqn Al Shami, wa tatu ni Dabur
ambao unavuma kutokea Kaskazini Magharibi kutokea Ruqn Al Iraqi kuelekea Ruqn Al
Shami na Upepo wa aina ya nne ni Shimmal (Kaskazini) ambao unavuma kutokea
Kaskazini Mashariki Ruqn al Iraqi Kuelekea Ruqn Al Hajar Al Aswad.

Tunapougawa katikati ukuta wa Kaskazini-Magharibi na ukuta wa Kusini-Mashariki basi


tunaona kua katikati ya kuta mbili hizo kunagawika na kua sehemu hio ni yenye kuenda
sambamba na Mhimili wa Nyota ya Suhayl, ambayo ni Nyota inayong’ara sana na hua
ni yenye kuonekana katika upande wa Kusini wa Dunia na hivyo kua ni Nyota au Sayari
ambayo ipo Katikati ya Mfumo wa Sayari na Jua.
422

Nyota ya Suhayl ni Nyota ambayo ina ukubwa wa mara 70 zaidi ya ukubwa wa Jua na
hivyo ni Nyota iliyo mbali zaidi kwa kua katika umbali wa Kilomita 313 Milioni Kilomita
wakati Jua lenyewe liko katika umbali wa Kilomita Milioni 150 Milioni kutoka Duniani.
Nyota ya Suhayl ina nguvu za mvutano wa -37C ambapo nguvu hio kwa upande wa Jua
hua ni -27, vile vile hali joto ya Nyota ya Suhayl ni kali zaid kwa kua na Kilowatt 7,350
wakati Jua lina joto la Kilowat 5,778.

Nyota ya Suhayl ndio Nyota inayotumiwa na Wanasayansi kua ni alama ya kurekebishia


usawa wa kituo cha Utafiti wa Sayansi kilichopo Angani kiitwacho Mir (Kwa Lugha ya
Kirusi hua linamaanisha Salaam) ambacho ni cha nchi ya Urusi lakini ni chenye
kutumiwa na kutegemewa na nchi zote Ulimwenguni ikiwemo Marekani, na pia Nyota
hio ya Suhayl ndio inayotumiwa na Wanasayansi katika kuangalia Sehemu ya Kuingilia
na kutokea katika anga ya Dunia pale wanapoenda wao wenyewe juu Angani au
wanapotuma vifaa vyao angani.

Kwa upande mwengine basi tunaona kua Upande wa Ruqn Al Hajar hua ni wenye kuenda
sambamba na eneo linalochoomoza Jua katika wakati wa kipindi cha Masirat (Mwezi
Machi) na Sibtimbar (Mwezi Septemba) na kutua katika upande wa Ruqn Al Sham na
sehemu inayooneka mwezi Muandamo katika wakati wa kipindi hicho.

Vile vile Ukuta wa Kaskazini-Mashariki wa jengo hilo la Al-Kaaba, ni wenye kuenda


sambamba na upande unaochomoza Jua katika wakati wa Kipindi cha Joto ambacho hua
ni kipindi cha Haziran (Mwezi wa Juni) na kutua katika upande wa Kaskazini Magharibi
na pia pande unnaoonekana Muandamo wa Mwezi katika wakati wa kipindi hicho.

Na katika wakati wa Baridi ambapo hua ni wakati wa Kanuun (Mwezi wa Disemba) basi
Jua hua linachomozea katika upande Kusini Mashariki na Kuzama katika Upande wa
Kusini Magharibi na ndio pia upande unnaoonekana Muandamo wa mwezi katika kipindi
hicho.

Baada ya kuangalia Jengo la Al Kaabah tunarudi kwa katika kumalizika kwa ujenzi wa
Jengo hilo na tunaona kua: Nabii Ibrahim na Nabii Ismail walipoomba pia vizazi vyao
vijaaliwe kutoa Mtume atakae waelimisha juu ya Uislam na Hikma. Ambapo Hikma
iliyokusudiwa hapa ni Ilm ya Ufahamu ambayo humpelekea mtu kujua jema na kulifuata
na kulijua ovu ili kuachana nalo. Hivyo kwa mtizamo huo basi tunaona kua Mtume
alieombwa atokane na kizazi cha Nabii Ismail alikua na majukumu manne zifuatazo kwa
watu wake:

1- Kuwabainishia Uongofu, kupitia katika ujumbe uliomo ndan ya kitabu cha


Allah Subhanah wa Taála kama vile alivyoupokea ujumbe huo.
423

2- Kuwabainishia na kuutafsiri ujumbe huo atakaoamrishwa kuufikisha na


hivyo kua ni mwalimu wa Viumbe kutoka kwa Muumba.
3- Kuwabainishia wazi Hukmu za Sharia za Allah Subhanah wa Taála na
malengo, busara na hikma zilizomo ndani yake kwa kina.
4- Kuwabainishia wazi kwa vitendo ujumbe huo na kuufanyia kazi katika
mfumo wa Maisha yake ya kila siku.

Allah Subhanah wa Taála akaikubali dua yao hii, na hivyo akamtuma Malaika Jibril aje
kuwapa muongozo wa namna ya kufanya Ibada ya Hija. Ambapo Jibril akawaongoza
kwa kuenda nao Minna katika siku ya Tarwiyyah, na akawasalisha Sala ya Adhuhuri, Al
Asir, Maghrib na Isha na akakaa nao hadi Alfajir akawasalisha Sala ya Alfajir, kisha
wakaenda Arafah asubuhi na wakashinda huko, hadi jua lilipokaribia kuzama
akawachanganyia Sala za Adhuhuri na Al Asr kwa pamoja kisha akaenda nao katika
sehemu ya kusimama Arafah, na kiza kilipoingia akaenda nao Muzdalifah ambapo
akasali nao Maghrib na Isha kwa kuzichanganya pamoja. Akabakia nao hadi Alfajir
akasali nao na akabaki nao katika maeneo ya Quza kisha jua lilipochomoza akaoondoka
nao na kuelekea Mina.

Akawaonesha namna ya kurusha Mawe katika Jamara, kisha akawaamrisha kuchinja na


kunyoa. Kisha akawarudisha kutufu katika Al Kaabah. Na ndio maana Allah Subhanah
wa Taála akasema katika Surat Al Imran:

ِ ِ ِ ِ ِ
َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻓَﭑﺗﱠﺒِﻌُﻮاْ ﻣﻠﱠﺔَ إِﺑْـَﺮاﻫ َﻴﻢ َﺣﻨﻴﻔﺎً َوَﻣﺎ َﻛﺎ َن ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻤ ْﺸ ِﺮﻛ‬
﴾‫ﲔ‬ َ ‫﴿ﻗُ ْﻞ‬
‫ﺻ َﺪ َق ﱠ‬
Qul sadaqa Allahu faittabiAAoo millata ibraheema haneefan wama kana mina
almushrikeena (Surat Al Imran 3:95)

Tafsir: Sema: Allah amesema Ukweli fuateni Mila za Ibrahim Hanifa, na hakika yeye
hakua miongoni mwa Washirikina.


424

MILLAT IBRAHIMA

Neno Millat linatokana na neno Mala ambalo kwa Lugha ya Kiarabu hua ni lenye
kumaanisha Kuelezea, ambapo neno Millat hua linamaanisha Dini, Mila, Mfumo wa
Maisha wenye kufuata njia za Kiimani na pia humaanisha Hukmu, Kanuni au Sharia za
Dini husika.

Anasema Allah Subhanah wa Taála katika Surat Al Baqara:

ِ ِ ِ ِِ
ْ ‫ﺐ َﻋﻦ ّﻣﻠﱠﺔ إِﺑْـَﺮاﻫ َﻴﻢ إِﻻﱠ َﻣﻦ َﺳﻔﻪَ ﻧَـ ْﻔ َﺴﻪُ َوﻟََﻘﺪ‬
‫ٱﺻﻄََﻔْﻴـﻨَﺎﻩُ ِﰱ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ‬ ُ ‫َوَﻣﻦ ﻳَـْﺮ َﻏ‬
﴿
ِ ‫ﺎل أَﺳﻠَﻤ‬ ِ ‫ﺎل ﻟَﻪ رﺑﱡﻪ أ‬ ِِ ‫ٱﻵﺧﺮةِ ﻟَ ِﻤﻦ ٱﻟ ﱠ‬
ِ ِ ِ
‫ب‬ِّ ‫ﺖ ﻟَﺮ‬
ُ ْ ْ َ َ‫َﺳﻠ ْﻢ ﻗ‬ ْ ُ َ ُ َ َ‫ﲔ۞ إِ ْذ ﻗ‬ َ ‫ﺼﺎﳊ‬ َ َ ‫َوإﻧﱠﻪُ ﰱ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ
َ ‫ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬
Waman yarghabu AAan millati ibraheema illa man safiha nafsahu walaqadi
istafaynahu fee alddunya wa-innahu fee al-akhirati lamina alssaliheena, Idh qala
lahu rabbuhu aslim qala aslamtu lirabbi alAAalameena. (Surat Al Baqara 2:130-131)

Tafsir: Na jee ni nani atakaeipa mgongo Milat Ibrahima isipokua yule aliemjinga kwa
nafsi yake. Ama kwa kwa hakika tumemchagua yeye katika Dunia hii na bila ya shaka
kesho Akhera atakua ni miongoni mwa waja wema. Wakati Mola wake alipomwambia:
‘Jisalimishe’ nae akasema: ‘Hakika mimi nimejisalimisha kwa Mola wa Ulimwengu
wote’.

Tunapoangalia aya ya 130 basi tunaona kua imetumia neno Safiha ambalo ni lenye
kumaanisha Ujinga, kutokua na Ufaham, kua na Akili finyu, ambapo hapa limetumika
katika hali ya Safiha Nafsan na hivyo kua ni lenye kumaanisha kua Mtu husika kua ni
Mjinga na anaitia Ujinga Nafsi yake na Ufahamu wake na hivyo kujishusha hadhi yake.
Kwani neno Safiha Nafsan ndio msingi wa ile methali ya Kiarabu isemayo: ‘Man Arafah
Nafsah Arafah Rabbah’ yaani ‘Anaeijua Nafsi yake basi humjua Mola wake.’

Hivyo basi Allah Subhanah wa Taála anahoji kua Jee ni nani atakaeikataa Millat za Nabii
Ibrahim yaani Dini yake, Imani yake na Hukmu zake, isipokua yule anaeidanganya Nafsi
yake, anaeitia ujinga Nafsi yake na hivyo kua ni mtu mwenye kumkufuru Mola wale na
kuwakataa Mitume wake, na atakua ni mwenye kukataa kutomshirikisha Muumba wake
ambae ni Allah Subhanah wa Taála na hivyo mtu huyo kua asiekua na Akili, kama
inavyothibitishwa na aya ifuatayo:
425

ِ‫ٱﻹﳒﻴﻞ إِﻻﱠ ِﻣﻦ ﺑـﻌ ِﺪﻩ‬ ِْ ‫ﺖ ٱﻟﺘﱠﻮراةُ و‬ ِ َ‫ﺎب ِﱂ ُﲢﺂ ﱡﺟﻮ َن ِ ۤﰱ إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ وﻣﺂ أُﻧ ِﺰﻟ‬ ِ َ‫﴿ ٰ� َْﻫﻞ ٱﻟْ ِﻜﺘ‬
َْ ْ ُ َ َ َ َ َ َ ْ َ َ َ
ِ ۤ
ِ ‫أَﻓَﻼَ ﺗَـﻌ ِﻘﻠُﻮ َن۞ ٰﻫﺄَﻧْـﺘﻢ ﻫﺆﻻ ِء ﺣﺎﺟﺠﺘﻢ ﻓِﻴﻤﺎ ﻟَ ُﻜﻢ ﺑِِﻪ ِﻋ‬
‫ﺲ‬َ ‫ﻠﻢ ﻓَﻠ َﻢ ُﲢَﺂ ﱡﺟﻮ َن ﻓﻴ َﻤﺎ ﻟَْﻴ‬ ٌ َ ُْْ َ َ ُ َ ُْ ْ
ً‫ﺼَﺮاﻧِﻴّﺎ‬ ِ ِ ‫ﻟَ ُﻜ ْﻢ ﺑِِﻪ ِﻋﻠْ ٌﻢ َو ﱠ‬
ْ َ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻳَـ ْﻌﻠَ ُﻢ َوأَﻧْـﺘُ ْﻢ ﻻَ ﺗَـ ْﻌﻠَ ُﻤﻮ َن۞ َﻣﺎ َﻛﺎ َن إِﺑْـَﺮاﻫ ُﻴﻢ ﻳَـ ُﻬﻮد ّ�ً َوﻻَ ﻧ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ِ ِ ِ
َ ‫َوﻟـٰﻜ ْﻦ َﻛﺎ َن َﺣﻨﻴﻔﺎً ﱡﻣ ْﺴﻠﻤﺎً َوَﻣﺎ َﻛﺎ َن ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻤ ْﺸ ِﺮﻛ‬
Ya ahla alkitabi lima tuhajjoona fee ibraheema wama onzilati alttawratu waal-
injeelu illa min baAAdihi afala taAAqiloona; Ha antum haola-i hajajtum feema
lakum bihi AAilmun falima tuhajjoona feema laysa lakum bihi AAilmun waAllahu
yaAAlamu waantum la taAAlamoona; Ma kana ibraheemu yahoodiyyan wala
nasraniyyan walakin kana haneefan musliman wama kana mina almushrikeena.
(Surat Al Imran 3:65-67)

Tafsir: Enyi Watu wa Kitabu (Mayahudi na Wakritso)! Jee ni kwa nini mnapingana
juu ya Ibrahim wakati vilishushwa Tawrati na Injili baada ya kuja kwake, Jee hamna
akili? Kwa Hakika nyinyi ndio wale ambao Mnabishania Juu ya kile ambacho Hamna
Ilm Nacho Hivi Kwanini Mnabishana juu ya lile jambo ambalo Hamlijui? Ni Allah
ndie ajuae na nyinyi hamjui kitu kwa Hakika Hakua Ibrahim Yahudi wala Mkirist
Lakini alikua ni Hanifa (Ni mwenye kumuabudu Allah) Muislam na Hakua
Mshirikina

Ambapo ayah hii ilishushwa katika kipindi cha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
kulitokea mvutano baina ya watu wa Mji wa Najran ambao upo Kusini Magharibi mwa
Ardhi ya Saudia.

Ambapo anasema Imam Abu Bakr Ahmad Ibn Husayn Ibn Ali Ibn Musa Al Khosraji Al
Bayhaqi kua: ‘Amesema Abd Allah Ibn Abbas kua Wakristo wa Najran na
Mayahudi wlikua wakibishanna mbele ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
huku kila mmoja miongoni mwao alikua akisema kua Nabii Ibrahim alikua ni Mtu
aliekua akifuata Imani yao. Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akashusha aya
isemayo: Ya ahla alkitabi lima tuhajjoona fee ibraheema.’

Naam...aya hizi zina funzo Kubwa sana ndani yake ambalo ni lenye kusema kua:
426

Haina haja ya kubishana na Watu wasiojua Kitu. Na hili ndio Tatizo letu sisi leo hii Kua
Wale wasiojua kitu ndio wamekua balaa Wanapenda kubisha sanaa, kiasi ya kua Kama
hukushikamana na Mafunzo ya Aya hizo hapo juu basi Unaweza Ukaingia Wazimu.

Ama kwa Upande wa funzo la pili basi tunaona kua aya zinatuwekea wazi kua Nabii
Ibrahim hakua Myahudi na wala hakua Mkiristo kama tulivyosema hapo awali. Na bila
ya shaka Nabii Ibrahim hakua ni Muarabu.

Hivyo basi tunapoangalia Historia ya Nabii Ibrahim na vithibitisho vya aya basi tunaona
kua Nabii Ibrahim amekuja kututhibitishia pia kua mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala
hakuna kitu kilichokua bora isipokua Imani ya Kutomshirikisha Allah Subhanah wa
Ta'ala yaani Imani ya Dini ya Kiislam.

Hivyo haijaalishi umezaliwa Jerusalem, Saudia, Yemen, Iraq, Urusi, China, Marekani,
Zanzibar, Dar es Salam n.k au unaishi katika mji gani kwani kinachothaminiwa Mbele
ya Allah Subhanah wa Ta'ala ni Imani yako kwake yeye.

Na ndio maana tunaona kua Sahaba Salman Al Farsy Radhi Allahu Anhu alipokua akiishi
nchini Iraq alisema kumwambia Sahaba mwenzake Abu Dardaa Radhi Allahu Anhu pale
alipomuomba Salman Al Farsy Radhi Allahu Anhu kwa kusema: ‘Ya Salman! Njoo
uishi pamoja nasi katika Ardhi Tukufu’. Hivyo Salman Al Farsy Radhi Allahu Anhu
akasema: ‘Sio Ardhi ndio inayomfanya mtu awe Mtukufu bali ni matendo yake ndio
yanayomfanya mtu awe Mtukufu.’

Na Rasul Allah Salallalahu Alayhi wa Salam akasema kuwaambia Watu wake wa Kabila
la Quraysh kua: ‘Enyi Maquraysh, watu walio karibu na Ibrahim ni wale wenye
Taqwa. Hivyo Fuateni Milat Ibrahima ili isije ikatokea katika siku ya Malipo watu
wakaja na Amali njema kisha nyinyi mkaja kwangu huku miwa mmesheheni
mambo ya Kiduania kiasi ya kua mimi nikakugeuzieni Uso wangu kutoka kwenu
kuelekea upande mwengine’ (Imam Abu Hatim Abd Rahman Muhammad Ibn Idris Al
Razi )

Na hii ni kwa sababu Maquraysh walikua ni watu wenye asili ya Nabii Ibrahim kupitia
kwa Nabii Ismail kama tutakavyoona hapo baadae, ndani ya kitabu hiki ambapo pia kwaa
apande mwengine basi tuaona kua Mitume wote wakiwemo wa Mayahudi na Wakristo
walikua ni wenye kuusia ujumbe kutoka kwa Mola wa viumbe wote ambae ni Allah
Subhanah wa Taála na hivyo ni waliojisalimisha kwake yeye na moja kwa moja walikua
ni Waislam, hivyo hapa aya inaweka wazi tatizo la ujinga na kutotumia ufahamu na akili
zao Mayahudi na Wakristo ndiko kunakowapelekea wao kua ni wenye kukataa Millat
Ibrahim.
427

Hivyo Allah Subhanah wa Taála anawawekea wazi wale wote ambao hawatotumia akili
zao na hivyo kutoshikamana na Millat Ibrahim basi Mila zao hizo hazitokubaliwa na
hivyo watakua ni wenye kula hasara katika siku ya Malipo kwa kusema:

ِ ْ ‫ٱﻵﺧﺮةِ ِﻣﻦ‬
﴾‫ﺎﺳ ِﺮﻳﻦ‬ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ﴿
َ َ‫ٱﳋ‬ َ َ ‫َوَﻣﻦ ﻳَـْﺒـﺘَ ِﻎ َﻏْﻴـَﺮ ٱﻹ ْﺳﻼَم دﻳﻨﺎً ﻓَـﻠَ ْﻦ ﻳـُ ْﻘﺒَ َﻞ ﻣْﻨﻪُ َوُﻫ َﻮ ﰱ‬
Waman yabtaghi ghayra al-islami deenan falan yuqbala minhu wahuwa fee al-
akhirati mina alkhasireena (Surat Al Imran 3:85)

Tafsir: Na yeyote yule ambae atatafuta Dini nyengine (na kuifuata) zaidi ya Kiislam,
basi haitokubaliwa (Dini yake) kutoka kwake. Na Akhera atakua ni mingoni mwa
Waliokula hasara.

Imam Abu Al Qasim Al Zamakhshari anasema kuhusiana na ayah hii kua: ‘Katika ayah
hii Allah Subhanah wa Taála anathibitisha kua yeye pekee ndie mwenye Uwezo
Mkubwa Juu ya Kila kitu, na hana mpinzani yeyote. Na yeye ni Mwingi wa Hikma
na Uadilifu. Na dini peke mbele yake yeye ni Uislam, hivyo kuweka wazi kua Dini
ya Kiislam ni Din al Tawhid wal Al Adl. (Dini ya Kumpwekesha yeye Allah Subhanah
wa Taála na ya Uadilifu). Hivyo hakuna Mola anaepaswa Kuabudiwa kwa Haki
isipokua Allah Subhanah wa Taála, na eye peke yake ndie mmiliki wa Sifa za kua
na Wingi wa Uwezo na Wingi wa Hikma.’

Aya zinaendelea kuzungumzia juu ya Millati Ibrahima kwa kusema:

ِ ‫ﲎ إِ ﱠن ﱠ‬ ِِ ِ ِ ‫﴿وو ﱠ‬
‫ﻳﻦ ﻓَﻼَ َﲤُﻮﺗُ ﱠﻦ‬ َ ‫ٱﺻﻄََﻔ ٰﻰ ﻟَ ُﻜ ُﻢ ٱﻟ ّﺪ‬
ْ َ‫ٱﻪﻠﻟ‬ ُ ‫ﺻ ٰﻰ ﻬﺑَﺂ إِﺑْـَﺮاﻫ ُﻴﻢ ﺑَﻨﻴﻪ َوﻳَـ ْﻌ ُﻘ‬
‫ﻮب َ�ﺑَِ ﱠ‬ ََ
‫ﺎل ﻟِﺒَﻨِﻴ ِﻪ َﻣﺎ‬
َ َ‫ت إِ ْذ ﻗ‬ُ ‫ﻮب ٱﻟْ َﻤ ْﻮ‬ ‫ﻘ‬
ُ ‫ﻌ‬
ْ ‫ـ‬ ‫ﻳ‬
َ ََ َ َ َ ْ ‫ﺮ‬‫ﻀ‬َ ‫ﺣ‬ ‫ذ‬
ْ ِ‫إ‬ ‫آء‬ ‫ﺪ‬
َ ‫ﻬ‬ ‫ﺷ‬
ُ ‫ﻢ‬ ‫ﻨﺘ‬
ُ ‫ﻛ‬
ُ ‫َم‬
ْ ‫أ‬ ۞ ‫ن‬
َ ‫ﻮ‬ ‫ﻤ‬ ِ‫إَﻻﱠ وأَﻧْـﺘﻢ ﱡﻣﺴﻠ‬
ُ ْ ُ َ
َ ‫ﻴﻞ َوإِ ْﺳ َﺤ‬ ِ ِ ِ ِ َ ِ‫ﻚ وإِﻟَـٰﻪ آﺎﺑﺋ‬ ِ ِ ِ
‫ﺎق‬ َ ‫ﻚ إﺑْـَﺮاﻫ َﻴﻢ َوإ ْﲰَﺎﻋ‬ َ َ َ َ ‫ﺗَـ ْﻌﺒُ ُﺪو َن ﻣﻦ ﺑَـ ْﻌﺪى ﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻧَـ ْﻌﺒُ ُﺪ إﻟَـٰ َﻬ‬
ِ
‫ﺖ َوﻟَ ُﻜ ْﻢ ﱠﻣﺎ‬ ْ َ‫ﺖ َﳍَﺎ َﻣﺎ َﻛ َﺴﺒ‬ ْ َ‫ﻚ أُﱠﻣﺔٌ ﻗَ ْﺪ َﺧﻠ‬ َ ‫اﺣﺪاً َوَْﳓ ُﻦ ﻟَﻪُ ُﻣ ْﺴﻠ ُﻤﻮ َن ۞ ﺗِْﻠ‬ ِ ‫إِﻟَـٰﻬﺎً و‬
َ
ْ‫ﺼ َﺎر ٰى ﺗَـ ْﻬﺘَ ُﺪوا‬َ َ‫َﻛ َﺴْﺒـﺘُ ْﻢ َوﻻَ ﺗُ ْﺴﺄَﻟُﻮ َن َﻋ ﱠﻤﺎ َﻛﺎﻧُﻮا ﻳَـ ْﻌ َﻤﻠُﻮ َن ۞ َوﻗَﺎﻟُﻮاْ ُﻛﻮﻧُﻮاْ ُﻫﻮداً أ َْو ﻧ‬
ِ ِ ِ ِ ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ﻗُ ْﻞ ﺑَ ْﻞ ﻣﻠﱠﺔَ إِﺑْـَﺮاﻫ َﻴﻢ َﺣﻨﻴﻔﺎً َوَﻣﺎ َﻛﺎ َن ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻤ ْﺸ ِﺮﻛ‬
428

Wawassa biha ibraheemu baneehi wayaAAqoobu ya baniyya inna Allaha istafa


lakumu alddeena fala tamootunna illa waantum muslimoona, Am kuntum
shuhadaa idh hadara yaAAqooba almawtu idh qala libaneehi ma taAAbudoona
min baAAdee qaloo naAAbudu ilahaka wa-ilaha aba-ika ibraheema wa-
ismaAAeela wa-ishaqa ilahan wahidan wanahnu lahu muslimoona, Tilka ommatun
qad khalat laha ma kasabat walakum ma kasabtum wala tus-aloona AAamma kano
yaAAmaloona Waqaloo koonoo hoodan aw nasara tahtadoo qul bal millata
ibraheema haneefan wama kana mina almushrikeena (Surat Al Baqara 2:133-135)

Tafsir: Na wasia huu (wa Kujisalimisha kwa Allah) uliusiwa na Ibrahim kwa Watoto
wake na Yaqub (aliesema): Enyi watoto wangu! Hakika Allah amekuchagueni nyie
kwa ajili ya Dini ya kweli, hivyo msife isipokua mkiwa katika hali ya kua ni Waislam.
Au nyie mlikuwepo wakati kifo kilipomkaribia Yaqub ambae alisema kuwaambia
watoto wake: ‘Jee Mtaabudu nini baada yangu?’. Nao wakasema: ‘Tutamuabudu
Mola wako, na Mola wa Mababa zako Ibrahim, Ismail na Is-haq. Mungu mmoja na
kwake yeye sisi tumejisalimisha.’ Wao ni Ummah uliotangulia. Hakika wao watalipwa
kutokana na waliyoyachuma na nyie (Mtalipwa) kutokana na Mliyoyachuma. Na
kamwe hamtoulizwa juu ya ale ambayo wao walikua wakiyafanya. Na wao wakasema:
‘Kua Myahudi au Mkristo na utaongoka’. Waambie: ‘La! (hakika sisi tunafuata)
Milat Ibrahima Hanifa (Ya kutomshirikisha Allah Subhanah wa Taála) na kwa hakika
yeye hakua miongoni mwa Washirikina.’

Aya inazungumzia juu ya wasia wa Nabii Ibrahim kwa Watoto wake kuhusiana na
kushikamana na kujisalimisha kwa kufuata Millat Ibrahima hadi mwisho wa uhai wao
na namna ambavyo watoto wa Nabii Yaqub nao walivyousiwa na baba yao pia
kusimamia katika MIllat Ibrahima, ambapo nao wakaahidi kua watafuata Millat
walizofuata baba zake Nabii Yaqub ambao ni Nabii Is-haq, Nabii Ismail na Nabii
Ibrahim.

Ayah hii inatuwekea wazi pia kua ndugu wa Baba ni Baba na ndugu wa Mama ni Mama
na ndio maana Watoto wa Nabii Ibrahim wakasema kua Tutamuabudu Mungu wa
Mababa zako, Is-haq, Ismail na Ibrahim.

Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi yeye anafafanua zaidi kuhusiana
na wasia wa Nabii Ibrahim kupitia kwa Nabii Is-haq hadi kwa Nabii Yaqub pale
alipowauliza kuhusiana na nini watakachokiabudu baada ya kufariki kwake kua: ‘Nabii
Yaqub alikua ni mwenye kusisitiza umuhimu wa Kila Muislamu kujisalimisha kwa
Allah Subhanah wa Taála hadi mwisho wa Uhai wake mtu’.

Tunapoangalia tukio hili basi tunaona ujumbe mzito uliomo ndani ya ayah hizi ambao ni
wenye kutufunza juu ya kile ambacho Nabii Yaqub anawausia watoto wake katika wakati
429

wa mwishoni mwa uhai wake, kwani alikua hafikirii juu ya kifo chake, mali au umoja wa
watoto wake, bali alikua anafikiria kufuatwa kwa Millat Ibrahima na watoto wake katika
maisha yao wakati yeye atakapoua hayupo Ulimwenguni, hivyo wasia huo wa
kushikamana na Millati Ibrahima ni wasia wenye thamani na uzito mkubwa kuliko hazina
ya Mali za Ulimwenguni zote au kitu chochote chengine zaid yake ulimwenguni. Kwani
amesema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

َ ‫ﻴﻞ َوإِ ْﺳ َﺤ‬


‫ﺎق‬ ِ ‫ﭑﻪﻠﻟِ وﻣﺂ أُﻧْ ِﺰَل إِﻟَﻴـﻨَﺎ وﻣﺂ أُﻧ ِﺰَل إِ َ ٰﱃ إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ وإِ ْﲰ‬
‫ﺎﻋ‬ َ ْ ْ ‫ﱠ‬ ِ‫﴿ﻗُﻮﻟُ ۤﻮاْ آﻣﻨﱠﺎ ﺑ‬
َ َ َ َ َ َ َ َ َ
َ‫ﻴﺴ ٰﻰ َوَﻣﺎ أُوﺗِ َﻰ ٱﻟﻨﱠﺒِﻴﱡﻮ َن ِﻣﻦ ﱠرّﻬﺑِِ ْﻢ ﻻ‬ ِ
َ ‫ﻮﺳ ٰﻰ َوﻋ‬
ِ
َ ‫َﺳﺒَﺎط َوَﻣﺂ أُوﺗ َﻰ ُﻣ‬
ِ ‫وﻳـﻌ ُﻘﻮب وٱﻷ‬
ْ َ َ ْ ََ
‫َﺣ ٍﺪ ِّﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ َوَْﳓ ُﻦ ﻟَﻪُ ُﻣ ْﺴﻠِ ُﻤﻮ َن۞ ﻓَِﺈ ْن َآﻣﻨُﻮاْ ﲟِِﺜْ ِﻞ َﻣﺂ َآﻣْﻨـﺘُ ْﻢ ﺑِِﻪ ﻓَـ َﻘ ِﺪ‬
َ‫ﲔأ‬ َْ ‫ﻧـُ َﻔِّﺮ ُق ﺑَـ‬
﴾ ‫ﻴﻊ ٱﻟْ َﻌﻠِﻴﻢ‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ وﻫﻮ ٱﻟ ﱠﺴ‬
‫ﻤ‬ ُ ‫ﱠ‬ ‫ﻢ‬ ‫ﻬ‬
ُ ‫ﻜ‬
َ ‫ﻴ‬ ِ ‫ﺎق ﻓَﺴﻴ ْﻜ‬
‫ﻔ‬ ٍ ِ ِ ِ
َ َ ‫ْٱﻫﺘَ َﺪواْ ﱠوإن ﺗَـ َﻮﻟﱠْﻮاْ ﻓَﺈﱠﳕَﺎ ُﻫ ْﻢ ِﰱ ﺷ َﻘ‬
ُ ُ َ َُ ُ
Qooloo amanna biAllahi wama onzila ilayna wama onzila ila ibraheema wa-
ismaAAeela wa-ishaqa wayaAAqooba waal-asbati wama ootiya moosa waAAeesa
wama ootiya alnnabiyyoona min rabbihim la nufarriqu bayna ahadin minhum
wanahnu lahu muslimoona; Fa-in amanoo bimithli ma amantum bihi faqadi ihtadaw wa-
in tawallaw fa-innama hum fee shiqaqin fasayakfeekahumu Allahu wahuwa alssameeAAu
alAAaleemu (Surat Al Baqara 2:136-137)

Tafsir: Semeni (Enyi Waislam): ‘Tumeamuamini Allah na tulivyoteremshiwa, na


alivyoteremshiwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haq na Yaqub na Al Asbati(Watoto 12 wa
Nabii Yaqub) na kile alichoshushiwa Musa, na Isa na walivyoshushiwa Manabii
kutoka kwa Mola wao. Hakika sisi hatutofautishi baina yao na kwake yeye (Allah
Subhanah wa Taála) tumejisalimisha’ Na kama wakiamini kama mlivyoamini nyinyi
basi watakua wameongoka. Lakini wakipotoka, basi watakua ni wapingaji tu. Hivyo
Allah atawatosheleza kwani kwa hakika yeye ni mwenye kusika kila kitu na ni mwenye
kujua kila kitu.

Kwani kufuata Millati Ibrahima hua ni kufuata Sibghata Allah. Ambapo Allah Subhanah
wa Ta’ala anaweka wazi ubora wa wenye kufuata Sibghata Allah pale aliposema katika
aya iliyofuatia baada ya aya hizo kua:

﴾‫ٱﻪﻠﻟِ ِﺻْﺒـﻐَﺔً وَْﳓﻦ ﻟَﻪُ َﻋﺎﺑِﺪو َن‬ ‫ﻦ‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟِ وﻣﻦ أَﺣﺴﻦ‬ ِ﴿
ُ َ ‫ﱠ‬ َ ُ َ ْ ْ َ َ ‫ﺻْﺒـﻐَﺔَ ﱠ‬
‫ﻣ‬
430

Sibghata Allahi waman ahsanu mina Allahi sibghatan wanahnu lahu AAabidoona
(Surat Al Baqara 2:138).

Tafsir: Sibghata ya Allah, na jee na ipi ni bora zaidi ya Sibghata ya Allah, na kwa
hakika sisi ni wenye kumuabudu yeye.

Ambapo neno Sibghatan ni neno lilitokana na neno Sabagha ambalo humaanisha Kupaka
Rangi, Kutia Rangi, Kuzamisha Kitu, Kuchukua Sifa, Dini, Maumbile na pia baadhi
wamesema kua humaanisha Kubatiza.

Ambapo amaesema Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al


Razi ambae anasema kua: Amesema Abdallah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua:
‘Wakristo walikua wakiwakogesha Watoto wao katika siku ya 7 baada ya kuzaliwa
kwao kwa maji yenye rangi ya Zafarani, na kisha husema: ‘Sasa Hivi Mtoto amekua
Mkristo’’

Hivyo bila ya shaka tunapozungumzia ubatizo basi aya inapingana na wenye kufanya
mambo hayo ya kubatizana, kwani kwa kimaumbile kila Ibn Adam hua tayari
ameshabatizwa kua hakuna Mola anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokua Allah
Subhanah wa Ta’ala na hivyo hua ni mwenye kua na Sibghata Allah yaani hali ya Fitra.

Ama tunapozungumzia Sibghata Allah basi hua pia tunamaanisha kujua sifa tukufu za
Allah Subhanah wa Ta’ala na Hukmu na Sharia zake. Na tunapozungumzia kumaanisha
kupaka rangi basi hua tunamaanisha Kukipaka kitu rangi kiasi ya kua rangi hio ikakiathiri
kitu hicho, na hivyo basi kwa upande wa Sibghata Allah hua inamaanisha athari za Dini
ya Kiislam ndani ya Kiimani na Kimuonekano kuanzia ndani ya Moyo wa mtu mpaka
nje ya Mwili wake katika Vitendo na Maneno yake kua ni yenye kuenda sambamba na
maamrisho ya Mola wake.
Na hivyo aya zinatuonesha umuhimu wa kufuata Millat Ibrahima huku ukiwa katika
kusimamia Sibghata Allah.

Hapa tunaona kua mafunzo yanayopatikana katika kisa hiki cha Nabii Ibrahim ni mengi
sana na yenye thamani kubwa sana kama tutayazingatia, hususan katika wakati wetu huu
ambao kila siku zinavyoenda basi ndivyo nasi tunavyozidi kukaa mbali na Ilm za Kiroho
na Kinafsi na hivyo kua mbali na Mola wetu Subhanah wa Taála. Na ili kuturudisha sisi
kwa Mola wetu kinafsi na kiroho katika asili yetu ya Millat Ibrahima basi Allah
Subhanah wa Taála akaamua kumuamrisha Nabii Ibrahim aunyanyue msingi wa
Nyumba yake Tukufu na kisha baada ya hapo akamuamrisha Nabii Ibrahim awaite watu
waje kwake yaani katika Millat Ibrahima kwa kusema:
431

‫ﲔ ِﻣﻦ ُﻛ ِّﻞ ﻓَ ٍّﺞ‬ ِ ِ ‫ﻮك ِرﺟﺎﻻً وﻋﻠَﻰ ُﻛ ِﻞ‬


َ ‫ﺿﺎﻣ ٍﺮ َ�ْﺗ‬ َ ّ ٰ َ َ َ َ ُ‫ﭑﳊَ ِّﺞ َ�ْﺗ‬ ْ ِ‫ﱠﺎس ﺑ‬ِ ‫﴿ َوأَ ِذّن ِﰱ ٱﻟﻨ‬
ٍ ‫ٱﻪﻠﻟِ ِ ۤﰲ أ ﱠَ�ٍم ﱠﻣﻌﻠُﻮﻣ‬ ِ ِ
‫ﺎت َﻋﻠَ ٰﻰ َﻣﺎ َرَزﻗَـ ُﻬ ْﻢ‬ َ ْ ‫ٱﺳ َﻢ ﱠ‬ ْ ْ‫َﻋﻤﻴِ ٍﻖ۞ ﻟّﻴَ ْﺸ َﻬ ُﺪواْ َﻣﻨَﺎﻓ َﻊ َﳍُْﻢ َوﻳَ ْﺬ ُﻛُﺮوا‬
ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ‫ِﻣﻦ َﻬﺑ‬
ُ ‫ﺲ ٱﻟْ َﻔﻘ َﲑ۞ ﰒُﱠ ﻟْﻴَـ ْﻘ‬
‫ﻀﻮاْ ﺗَـ َﻔﺜَـ ُﻬ ْﻢ‬ َ ‫ﻴﻤﺔ ٱﻷَﻧْـ َﻌﺎم ﻓَ ُﻜﻠُﻮاْ ﻣْﻨـ َﻬﺎ َوأَﻃْﻌ ُﻤﻮاْ ٱﻟْﺒَﺂﺋ‬ َ ّ
﴾‫ﺖ ٱﻟْ َﻌﺘِ ِﻴﻖ‬
ِ ‫وﻟْﻴﻮﻓُﻮاْ ﻧُ ُﺬورﻫﻢ وﻟْﻴﻄﱠﱠﻮﻓُﻮاْ ﺑِﭑﻟْﺒـﻴ‬
َْ َ َ ْ َُ َُ
Waadhdhin fee alnnasi bialhajji ya/tooka rijalan waAAala kulli dhamirin ya/teena
min kulli fajjin AAameeqin, Liyashhadoo manafiAAa lahum wayadhkuroo isma
Allahi fee ayyamin maAAloomatin AAala ma razaqahum min baheemati al-
anAAami fakuloo minha waatAAimoo alba-isa alfaqeera, Thumma lyaqdoo
tafathahum walyoofoo nudhoorahum walyattawwafoo bialbayti alAAateeqi (Surat
Al Hajj 22:27-29)

Tafsir: Na waadhinie watu kwa ajili ya Hija, watakuja kwako kwa miguu na kwa kila
kipando (cha Mnyama aliechoka kwa kutoka mbali), watakuja kutoka katika kila
sehemu (Milimani, Mabondeni na vichochoroni kuliko fichikana). Ili waweze
kushuhudia yenye manufaa juu yao na walitaje Jina la Allah katika Ayyam al
Maalumat (siku maalum) zilizochaguliwa juu ya kile ambacho walichoruzukiwa
kutokana na Mnyama (Anaeliwa wa miguu minne kama Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo
n.k) Kisha kuleni kutokana nao na walisheni masikini wasiokua na uwezo. Kisha na
wamalize Manasik (Wajib wa Hija) juu yao. Na watimize nadhiri zao na wafanye
Tawafu yao katika Bayt al Atiq.

Ama tunapoiangalia aya hii ya Surat Al Hajj 22:27 basi tunaona kua Allah Subhanah wa
Ta'ala anamuamrisha Nabii Ibrahim kua awaadhinie watu. Na kisha akasema kua
Watakuja Kwako na Hakusema kua Watakuja tu, hivyo maana hii inaturudisha kwenye
Mada yetu ya Millat Ibrahima.

Yaani kila atakaekua ni mwenye kuenda Hija basi bila ya shaka atakua ni mwenye uwezo
wa kuhudhuria katika Ibada ya Hija na akaitikia wito wa Nabii Ibrahim na hivyo kua ni
Mwenye Kufutana Milat Ibrahim na bila ya shaka hua ni mwenye kuitikia wito wa kurudi
katika asili ya hali yake ya kimaumbile ya Sibghata Allah.

Ambapo anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘Hakika
Allah Subhanah wa Ta’ala anao waja wake ambao huenda Masjid Al Haram kwa
Sarir (Viti vya Kifalme), Kuna waendao kwa Vipando vya kawaida ambavyo hata
hivyo hua ni vyenye kuvutwa na Malaika’
432

Naam, bila ya Shaka na hapa ndio tunapata mfano wa Mujaddid Ad Din Imam Abd Allah
Alawi Al Haddad ambae ndie Muanzilishi wa Alawiyyah Tariqah. Kwani Imam Alawi
Al Haddad ingawa alikua ni Kipofu na ni mwenye kuishi katika Ardhi ya Nchini Yemen
katika maeneo ya Tarim Hadhramwat.

Lakini alikua kila siku anaonekana akiwa ni mwenye kufanya Tawaf yaani akizunguka
Al Kaabah nchini Saudi Arabia. Mpaka Ijumaa moja mmoja kati ya Wafagiaji wa Msikiti
wa Makkah ambae kila siku alikua akimuona Imam Al Hadad, akawa hakumuona. Yule
Mfagiaji akashangaa Imekuaje leo Imam Al Haddad amekosekana Kwenye kufanya
Tawaf.

Ukapita mda, yule Mfagiaji akakutana na Watu kutoka Yemen. Hivyo akamuulizia Imam
Al Haddad vipi mzima? na akaambiwa Imam Al Haddad amefariki mda mrefu na ilikua
ni siku ya Al Khamis baada ya Salat Al Asr. Yule Mfagiaji akasema: Ndio maana nikawa
sikumuona katika siku ya Ijumaa.

Kwani kwa upande mwengine Hata Imam Al Tustari Mwenyewe anasema Ahmad Ibn
Salim kua: ‘Siku moja nilienda kwa Imam Al Tustari na kwa hakika mlango wa
Nyumba yake ulikua mdogo sana. Lakini cha kushangaza ni kua nilipoingia ndani
ya nyumba yake basi niliona Farasi mkubwa sana. Hivyo nikashtuka, na hapo hapo
nikageuka na kutaka kukimbia, kwani sikuweza kufaham yule Farasi aliingiaje
ndani ya Nyumba ya Imam Al Tustari, lakini Imam Al Tustari akaniita na
nilipogeuka basi sikumuona yule Farasi kwani alikua ametoweka.’

Naam..hivyo Allah Subhanah wa Taala alimwambia Nabii Ibrahim kua Waite watu
watakuja Kwako kwa Miguu na kwa Vipando vya aina tofauti na kutoka katika sehemu
mbali mbali Milimani, Mabondeni, Kuvuka Majangwa, Misitu, Mito Maziwa na Bahari.
Watakuja!

Kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kila alieitikia wito wa
Ibrahim katika wakati aliponadia basi atahiji na kila aliekua hakuitikia basi
hatohiji’ na tunapozungumzia kuhiji basi hua kuna njia nyingi na hii ni kulingana na
namna mtu anavyosimamia katika Sibghata Allah. Ambapo mfano mmoja miongoni
mwao ni ule wa Imam Abdullah Ibn Mubarak, ambae alikua ni Imam

Ambapo anasema Imam Abu Bakr Ahmad Ibn 'Ali Ibn Thabit Ibn Ahmad Ibn Mahdi Al
Shafi'i kua Abdulla Ibn Mubarak alikua ni mwenye kujaaliwa kua na Ilm, Mali,
Mpiganaji Mahiri na Ucha Mungu mkubwa sana kiasi ya kua ilikua kila mwaka
unapowadia wakati wa Hija basi watu wa mji wake walikua ni wenye kumwambia
Abdullah Ibn Mubarak kua ni bora waende pamoja katika Ibada ya Hija. Ambapo nae
hua ni mwenye kuwaambia kua wamletee pesa za matumizi ya safari ya Hija kwa kila
anaetaka kuenda kwa mwaka huo.
433

Kisha Abdulla Ibn Mubarak huzichukua pesa hizo na kuzihifadhi kwenye kisanduku. Na
kisha huondoka nao watu hao na njiani hua ni mwenye kuwanunulia vyakula vizuri na
kila kitu wanachohitaji watu hao, kuanzia kwenye mji wa Baghdad mpaka katika mji wa
Madina. Na kisha kuwauliza watu wake: ‘Jee watoto wenu wametaka muwanunulie
nini na nini’ na baada ya kujibiwa basi hua ni mwenye kuwanunulia kila mmoja kile
alichoagiziwa.

Baada ya hapo huanza safari ya kuelekea katika mji wa Makkah. Na kuwasimamia watu
wake mpaka wakamaliza kufanya Ibada ya Hija. Na kisha huwauliza tena wameagiziwa
nini kwenye Mji wa Makkah. Na kisha humnunulia kila mmoja kama alivyoagiziwa. Na
kisha huanza safari ya kurudi Baghdad ambapo huwahudumia kwa mahitaji yao yote njia
nzima mpaka wafike majumbani mwao.

Na kisha baada ya kuwasili Majumbani mwao huwapambia nyumba zao na kuwafanyia


sherehe ya kufurahia kufanikiwa kwao kutekeleza Ibada ya Hija. Na kisha hukifungua
kisanduku cha zile pesa walizompa kabla ya kuondoka kwao, na kumrudishia pesa zake
kila mmoja wao. (Tarikh Baghdad)

Ambapo kwa upande mwengine basi anasema Imam Abu Al Fadl ‘Iyad Ibn Amr Ibn
Musa Ibn ‘Iyad Ibn Muhammad Ibn ‘Abdillah Ibn Musa Ibn ‘Iyad Al Yahsubi Al Sabt
kua safari moja Abdulla Ibn Al Mubarak alipokua safarini kuelekea katika Ibada ya
Hija basi hakufanikiwa kufika katika Mji wa Makkah, kwani alipofika katika Mji wa
Kufah tu nchini Iraq basi akakutana na Mwanamke ambae alikua ni mwenye
kumnyonyoa Bata ambae ni maiti.

Na kwa kua ni haram kula mnyama aliekufa basi Abdullah Ibn Mubarak akamuuliza
kama Bata huyo aliwahi kuchinjwa kabla ya kufa kwake, ambapo mwanamke huyo
akajibu kua hakuwahi kuchinjwa. Hivyo Abdullak Ibn Mubarak akauliza: ‘Kama
hakuwahi kuchinjwa jee ni kwa nini unamnyonyoa?’. Yule mwanamke akajibu: ‘Ili
familia yangu ipate chakula chake.’ Abdullah Ibn Mubarak akasema: ‘Hivi jee wewe
hujui kua ni haram kula mnyama ambae hakuchinjwa kwa jina la Allah Subhanah
wa Ta’ala?’

Yule mwanamke akasema kua anajua lakini ingawa nyama hio ni Haram kwake yeye
Abdullah Ibn Mubarak lakini ni kwa mda mrefu sasa imekua ni Halali kwake yeye na
familia yake, kwa sababu ya kutokana na kua na njaa iliyosababishwa na umasikini,
kwani baba yao alikua ni mtu tajiri sana lakini hata hivyo alidhulumiwa mali zake zote
na kisha akauliwa. Hivyo familia hio haina kitu na haina jambo la kufanya, hivyo ili
waweze kuishi kwa wakati huo basi inabidi wale bata huyo.
434

Baada ya kusikia hivyo basi Abdullah Ibn Mubarak akaulizia sehemu anayoishi
mwanamke huyo na kisha akaamua kuipelekea kila kitu chake ambacho alikusudia kua
atumie katika safari yake ya Hija tangu mwanzo mpaka mwisho wake. Na kisha
akabakisha sehemu kidogo tu ambayo itamsaidia yeye katika kipindi atakachokuwepo
katika mji wa Kufah, kwani Safari ya Hija haiewezekani tena kutekelezeka.

Hivyo akakodi chumba na kukaa kwa mda mpaka Mahujaj waliporudi kutoka katika
mji wa Makkah, na kisha yeye akafunga safari kurudi katika Mji wa Baghdad na
alipofika Baghdad akakutana na Mahujaj waliokua wakirudi kutoka Makkah. Mahujaji
hao walipomuona Abdullah Ibn Mubarak wakaanza kumpongeza kwa kutekeleza Ibada
ya Hija. Abdullah Ibn Mubarak akawaambia Mahujaji hao kua safari hio hakufanikiwa
kuenda katika safari ya Hija.

Lakni mmoja kati ya Mahujaji hao akasema: ‘Subhana Allah! Inakuaje hadi unasema
kua hukuenda wakati mimi nilikuachia mizigo yangu wakati tulipokua Minna
wakati tukielekea Arafah?’

Hapo na mwengine kati ya Mahujaji hao akasema: ‘Ya Ibn Mubarak! Jee sie wewe
yule ambae alininunulia mimi zawadi zangu?’ Abdullah Ibn Mubarak akajibu: ‘Ama
kwahakika mimi sijui nyinyi mnazungumzia nini. Kwa sababu mimi kweli mwaka
huu sikufanikiwa kuenda Hija.’ Kisha katika Usiku wa siku hio Abdullah Ibn
Mubarak alipolala basi akaota kua anasikia sauti inamuambia kua: ‘Mabruk ewe Ibn
Mubarak! Kwani kwa Hakika Allah Subhanah wa Ta’ala amekukubalia Sadaqa
yako, na hivyo amemtuma Malaika katika Maumbile yako ili afanye Hia kwa ajili
yako.’ (Tartib Al Madarik, cha Qadhi ‘Iyad, Al Bidayah w al Nihayah cha Ibn Kathir)

Ama kwa upande mwengine basi safari moja Abdullah Ibn Mubarak alilala pembeni na
Al Kaabah baada ya kumalizika Ibada ya Hija na akaota kua kua Malaika wawili ambao
walikua wanashuka kutoka juu Mbinguni kuja ardhini huku wakizungumza kwa
kuhojiana, ambapo mmoja wao alikua akimwambia mwanawe: ‘Hivi jee wewe unajua
watu wangapi mwaka huu wamefanya Ibada ya Hija?’

Yule Malaika mwenzake akajibu: ‘Wamekuja watu Laki Sita kufanya Ibada ya Hija’,
hapo yule wa mwanzo akasema: ‘Ila sijui kama hata mmoja miongoni mwao yumo
aliekubaliwa Hija zao’ ambapo yule wa pili akaujibu: ‘Kuna Mshona viatu wa
Dimashq ambae jina lake ni Ali Ibn Mufiq. Huyu bwana yeye hakuwahi kuja
kwenye Ibada ya Hija lakini, hata hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala amewakubalia
Mahujaj wote Hija zao kwa sababu ya nia yake ya kufanya Ibada ya Hija mwaka
huu.’
435

Hivyo baada ya Abdullah Ibn Mubarak kuona ndoto hio basi akaamka na kutaka kujua
ilikuaje mpaka mtu mmoja akawa ndio sababu ya Mahujaji wote kukubaliwa Hija zao.
Hivyo akahirisha safari ya kurudi katika nyumbani nchini Iraq na badala yake akafunga
safari kueleka nchini Syria katika maeneo ya Damascus kwa ajili ya kumtafuta Ali Ibn
Mufiq mshona Viatu. Na alipofika Damascus basi akaanza kumtafuta kwa kumuulizia
hadi akafanikiwa kumuona baada ya kuelekezwa ilipo nyumba yake.

Abdullah Ibn Mubarak alipofika mlangoni mwa nyumba hio aligona na kufunguliwa
mlango na Ali mwenyewe. Hivyo Abdulla Ibn Mubarak akajitambulisha, na hapo ghafla
muonekano wa uso wa Ali ukabadilika kwa mshangao na mshtuko, kwa sababu
alishangaa kuona kua Mwanazuoni Mkubwa na Mcha Mungu anaieshi nchini Iraq
amekuja nchini Syria kwa ajili ya kumtafuta yeye tu.

Kwani jina tu la Abdullah Ibn Mubarak ni jina kubwa sana kutokana na Ucha Mungu wa
Mwenye Jina hilo si katika kipindi hicho tu bali hadi katika wakati wetu na pia baada
yetu. Hivyo Ali akamkaribisha ndani Abdullah Ibn Mubarak kwa furaha na unyenyekevu
na kisha akamuuliza imekuaje mpaka ikawa anamtafuta kiasi ya kufuatwa kwa masafa
marefu kiasi hicho.

Abdulla Ibn Mubarak akasema: ‘Kwa hakika mimi nimekuja kwa ajili ya kukuuliza
suali moja tu ambalo ni kua: Hivi lini wewe utaenda kufanya Ibada ya Hija?’

Ali Ibn Mufiq akashangaa kutokana na suali hilo, lakini akajibu kwa kusema: ‘Hakika
mimi nimekua na nia na matumaini ya kuenda Hija kwa muda wa miaka 30 sasa
hivi, na mwaka huu nilifanikiwa kuchanga ilikua tayari niende Hija. Lakini sasa
Allah Subhanah wa Ta’ala hakunijaalia niende Hija, hivyo sikufanikiwa kua ni
mwenye kuenda Hija mwaka huu.’

Abdullah Ibn Mubarak akauliza: ‘Jee ni kwanini?’ Ali Ibn Mufiq akajibu: ‘Ni kwa
sababu ndivyo yalivyo majaalaiwa ya Allah Subhanah wa Ta’ala juu yangu.’
Abdullah Ibn Mubarak akaona hapa kwa mnyenyekevu huyu siwezi kujifunza kile
nilichokifuata ili nikijue, hivyo akatilia msisitizo ajue sababu iliyomzuia Ali Ibn Mufiq
mpaka akawa hajaenda kuhiji. Hivyo Ali ikambidi kuweka wazi kile kilichomsababishia
asiende kuhiji mwaka huo kwa kusema:

‘Siku moja nilienda kumtembelea jirani yangu ambae ni rafiki yangu mkubwa
sana, na nilipofika iliku ani wakati ambao familia yake ilikua inajitayarisha kwa
ajili ya chakula cha usiku ambacho tayari kimeshawekwa mezani kwa ajili ya
kuliwa. Na ingawa sikua ni mwenye kua na njaa, lakini nilidhani kua rafiki yangu
huyo, atanikaribisha nami nile pamoja nao kutokana na ukarimu wake. Lakini sasa
hali ilikua kinyume chake, kwani rafiki yangu huyo alionekana kama kwamba mtu
436

ambae hana raha wala hajisikii kua na uhuru kwa mimi kuwemo nyumbani mwake
na hivyo anaepuka kunikaribisha chakula hicho.

Baada ya mda kupita basi rafiki yangu akaniambia kua: ‘Samahami lakini mimi
siwezi kukualika wewe, kwa ajili ya chakula hiki tunachotaka kula, kwa sababu
sisi tumekaa bila ya kula kwa mda wa siku 3, hadi mimi mwenyewe nikashindwa
kujizuia kutokana na hali ya njaa ya watoto wangu. Hivyo leo nilipotoka
nikakutana na Maiti ya Punda, na kutokana na matatizo yangu basi nikakata
sehemu ya nyama yake na kuileta kwa mke wangu ili aipike angalau tuondoe njaa.
Hivyo nyama hiio ni halali kwetu sisi kuila kwa sababu ya njaa kubwa lakini kwa
hakika mimi siwezi kukupa wewe nyama hio.’

Ali Ibn Mufiq aliendelea kwa kusema: ‘Baada ya kusikia maneno hayo basi Moyo
wangu ulitoka damu kwa machozi, hivyo nikaaga na kisha nikatoka na kuelekea
nyumbani kwangu. Nilipofika nyumbani kwangu basi nikachukua Dinar 3000
ambazo nilizichanga kwa ajili ya kuendea Hija. Na kumpa Jirani yangu. Ingawa
mimi pia ilinibidi nikae na njaa katika kipindi hicho cha uchangaji wa pesa hizo,
lakini nilihisi kua kumsaidia jirani yangu wakati wa shida ni muhimu zaidi kwangu
kuliko kuenda Makkah kwa ajili ya Hija, na hata hivyo bado nna matumaini ya
kuenda Hija Inshaa Allah.’’

Abdullah bin Mubarak akafurahi sana kusikia habari hio na kisha akamuambia Ali Ibn
Mufiq kuhusiana na ndoto aliyoiona ambayo ndio iliyomfanya aakhirishe safari yake ya
kurudi Baghdad.

Visa hivi ni sehemu tu ya mafunzo yenye utonesha umuhimu wa kua ni wenye kufuata
Millati Ibrahima huku tukiwa ni wenye kusimamia kwenye Sibghata Allah.

Na hivyo kutuwekea wazi kua mtu unaweza ukawa ni mwenye kuitikia wito wa Nabii
Ibrahim wa kuenda Makkah kuhiji lakini hata hivyo Hija yako isiwe na uzito wowote
kutokana na kukosekana kwa Sibghata Allah katika matendo yako ambapo hali hua ni
tofauti na yule mtu mwenye kusimamia kwenye Sibgahat Allah ambae anaweza akawa
hakuenda Kuhiji lakini kawa ni mwenye kuhesabiwa na kulipwa na Allah Subhanah wa
Ta’ala sawasawa na alieenda au zaidi ya walioenda na kuhudhuria katika Ibada hio.

Hivyo tunarudi katika aya zetu za Surat Al Hajj 22:27-29 basi tunaona kua aya hizi ni
miongoni mwa aya zinazoelezea Manasiq ya Hija (Wajib wa Ibada ya Hija) ambayo
yametajwa ndani ya Qurán katika sehemu mbili tu. Ambapo mara ya kwanza ni katika
Surat Al Baqara 2: 196-203 ambazo zimezungumzia juu ya Kisimamo cha Arafat, Kulala
usiku Muzdalifat, Kukaa siku tatu katika mji wa Minna, kisha kuchinja na kunyoa na
ufanya Tawaf ya mwisho (Tawaf al Ifadah) na mara ya pili ndio katika aya hii ya Surat
Al Hajj 22:28.
437

Anasema Abd Allah Ibn Umar Radhi Allahu Anhu kua: ‘Ayyam Maa Lumat na Ayyam
al MaAdudat ni siku nne, ambapo siku ya Al Adhhab (ya Kuchinja) na siku mbili
zinazofuatia baada yake hua zinaitwa Ayyam al Malumat (Mwezi 10-12 Dhul Hija)
na siku tatu baada ya siku ya Al Adhha hua ni siku zinazoitwa Ayyam Al MaAdudat
(Mwezi 11-13 Dhul Hijja)’

Al Kaabah imeitwa Bayt Al Atiq kwa sababu neno Atiq linamaanisha kitu cha zamani
kizuri chenye thamani kubwa sana kupita kiasi na kilicho huru. Anasema Sufyan Ath
Thawri kua: ‘Imeitwa Bayt ul Atiq kwa sababu ndio Nyumba Aqdam (Kongwe)
kuliko zote, na ndio Ataqa (yenye Thamani) kuliko zote inayomilikiwa na Allah
Subhanah wa Taála. ’.

Ili tufaham kwa nini Imam Sufyan Ath Tawry akasema kuhusiana na Bayt ul Atiq
imeitwa hivyo kwa kutokana na thamani yake basi na tuangalie mfano wa kiumbe Ibn
Adam ambae ameumbwa na Muumba yaani Allah Subhanah wa Ta’ala kwa ajili ya kua
ni mwenye kumuabudu Mola wake kama zinavyosema aya:

ِ ‫ٱﳉِ ﱠﻦ وٱ ِﻹﻧﺲ إِﻻﱠ ﻟِﻴـﻌﺒ ُﺪ‬


﴾‫ون‬ ُْ َ َ َ ْ ‫ﺖ‬ ُ ‫﴿وَﻣﺎ َﺧﻠَ ْﻘ‬
َ
Wama khalaqtu aljinna waal-insa illa liyaAAbudooni. (Surat Adh Dhariyat 51:56).

Tafsri: Sikuwaumba Majini na Bani Adam isipokua waniabudu mimi.

Na kisha sababu ya pili ni kua ameumbwa kwa sababu ya kua ni Khalifa Ulimwenguni
kama alivyosema katika Qur’an:

﴾ً‫ض َﺧﻠِﻴ َﻔﺔ‬ ِ ‫ﻚ ﻟِْﻠﻤﻠَـﺌِ َﻜ ِﺔ إِِﱐ ﺟ‬


ِ ‫ﺎﻋ ٌﻞ ِﰱ ٱﻷ َْر‬ َ ّ َ َ‫﴿وإِ ْذ ﻗ‬
َ َ ‫ﺎل َرﺑﱡ‬ َ
Wa-idh qala rabbuka lilmala-ikati innee jaAAilun fee al-Ardhi khaleefatan (Surat
Al Baqara 2:30)

Tafsir: Na kumbuka wakati Mola wako aliposema kuwaambia Malaika: ‘Hakika mimi
nitajaalia Khalifah katika Ardhi kizazi baada ya kizazi’.

Sasa hapa inabidi tutafakkari thamani ya Ibn Adam na Darja yake hapa ulimwenguni
ambayo ni kua Khalifa yaani Mtawala, Mfalme au Kiongozi na kisha Allah Subhana wa
438

T’ala akateua eneo Maalum kwa ajili ya Nyumba ambayo itajengwa na Wabora zaid
miongoni mwa Makhalifa hao, na kisha Nyumba hio ndio itakayokua Muelekeo wa
Viumbe Wote Ulimwenguni katika wakati wa kufanya Ibada zao, kiasi ya kua hata
Khalifa huyo afanye Ibada vipi lakini kama hakuielekea Nyumba hio katika ibada zake
basi Ibada zake zote hizo zitakua batil. Nadhani kidoogo tumefahamiana kutokana na
mfano huo.

Ama kwa Upande wa Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari basi yeye
anasema kua: ‘Nyumba hii imeitwa Ataqa kwa sababu Nyumba hio kamwe haijawahi
kutekwa na watu Madhalimu wenye malengo Mabaya dhidi yake isipokua Allah
Subhanah wa Taála hua ni mwenye kumuangamiza Dhalim huyo na (Ataqa)
huiweka huru Nyumba hio dhidi ya Madhalim hao.

Ambapo amesema Al Hasan kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala ameiita Nyumba hio
kua ni Bayt ul Atiq kwa sababu ya kuipa heshima kubwa na thamani kama vile
ambavyo Waarabu wanapokua wanazungumzia na kumpa sifa Farasi mwenye
thamani kubwa kua ni Aatiq’

Na kuna wasemao kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala ameiita Aatiq kwa sababu
haijawahi kutokea kwa dhalim kua ni mwenye kutaka kuifanyia uharibifu isipokua
Allah Subhanah wa Ta’ala hua ni mwenye kumdhalilisha Dhalimu huyo na
kuiwachia huru nyumba yake, na baadhi wamesema pia kua, imeitwa Aatiq kwa
sababu ndio nyumba pekee ambayo imenusuriwa na Gharika ya Nabii Nuh baada
ya kunyanyuliwa juu angani.

Hivyo kama ilivyokua kwa Allah Subhanah wa Ta’ala kua ni mwenye kuinyanyua
Nyumba yake hio na kuinusuru basi ndivyo pia anavyoufanya Moyo wa Muumini
kutokana na kumshirikisha nae. Allah Subhanah wa Ta’ala ameiweka nyumba hio
kwenye Masjid Al Haram kua kama ni alama. Na ndivyo hivyo hivyo ambavyo
Moyo hua una Moyo mwengine Ndani yake ambao kupitia kwake ndio mja
anavyokua na uwezo wa kusimama mbele ya Mola wake bila ya kusita au
kushughulika na kitu chochote, isipokua hua katika hali ya utulivu juu ya Mola
wake (sākin ilayhi).’’

Hivyo baada ya Nabii Ibrahim kuamrishwa kuwatangazia watu kuhusiana na Hija basi
akamuuliza Allah Subhanah wa Taála: ‘Ya Rabb! Jee sauti yangu itatosha na kusikika
kwa umbali gani?’Allah Subhanah wa Taála akamwambia Nabii Ibrahim: ‘Adhini kwa
ajili ya kuniwakilisha kwangu, ni juu yake wewe Kuadhini na ni Juu yangu mie
Kufikisha’ Nabii Ibrahim akapanda juu ya Jabal Thabir na kisha akaadhini kuanzia
upande wa Kusini, kisha Mashariki, Kaskazini na Magharibi kwa kusema: ‘Enyi Wenye
Kumuabudu Allah! Mmeamrishwa kufanya Hija katika Bayt ul Atiiq. Hivyo njooni
mfanye Hija ili kuitikia wito wa Allah!’ Na hakuna Ibn Adam mweye kumuamini
439

kumuamini Allah Subhanah wa Taála ambae hakusikia tangu waliokua hai hadi waliokua
ndani ya kiza cha vizazi vya wazee wao katika vizazi vilivyofuatia baada ya Nabii
Ibrahim, hadi katika Kizazi chetu hadi katika vizazi vitakavyokuja.

Anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Baada ya Nabii Ibrahim
kuadhini juu ya Hija, basi sauti yake ilisikika ulimwenguni mzima. Kuanzia
Ardhini hadi Mbinguni, na hakuna kiumbe kilichosikia wito huo isipokua nacho
kiliitikia wito huo. Kuanzia kwa Ibn Adam mwenye kufuata Millat Ibrahima,
Majini, Milima, Miti na Wanyama wote waliitikia: ‘Labaika Allahhuma Labbaik!
Labaika la Sharika Laka Labaik!’’.

SIRI NA HIKMA YA IBADA YA HIJA KULINGANA NA MITIZAMO


YA WANAZUONI.


Naam ni Waislam wengi sana wanaolijua Al Kabah na wenye kujua juu ya umuhimu wa
Ibada ya Hija kama Aya na Hadith zinavyotuwekea wazi, lakini ni Waislam wachache
sana wenye kujitayarisha kuifanya Ibada hii kikamilifu na kua ni wenye kuitikia wito wa
Labaika Allahhuma Labbaik! Labaika la Sharika Laka Labaik! Na kua ni wenye
kufuata Millat Ibrahim ipasavyo. Miongoni mwa visa vinavyotufundisha namna ya
kunufaika na Ibada hii basi ni kile kisa cha Abu Said Ibn Abi Al Khayr aliekua akiishi
katika Mji wa Khurasan katika karne ya nne ya Uislam ambae aliulizwa: ‘Jee kwa nini
hutaki kuenda kuhihji katika mji wa Makkah kama vile wanavyofanya Waislam
wengine?’ basi Abu Said Al Khayr akasema: ‘Si Muhimu sana kufunga safari ya
miguu kwa umbali wa maelfu ya kilomita kwa ajili ya kulitembelea Jengo la Mawe.
Kwani Mja wa kweli wa Allah Subhanah wa Taála hua ni mwenye kubakia katika
sehemu yake alipo na Bayt al Ma’mur humfuata na kumzunguka yeye Usiku na
Mchana juu yake. Kwa mfano hebu niangalieni mie juu yangu.’ Watu wakatizama
juu ya kichwa chake na wakaiona Bayt Al Maamur juu yake.

Kwani anasema Shaykh ul Al Akbar Imam Abu Bakar Ibn Arabi kua: ‘Al Kaabah hua
inawakilisha Moyo wa Ibn Adam yaani Al Lubb (Ambayo kama tulivyooona katika
kurasa zilizotangulia zinazozungumzia Maumbile ya Moyo kua Al Lubb ndio
sehemu ambayo inaingia na kukaa Nuru ya Allah Subhanah wa Taála). Hivyo basi
kwa upande mmoja tunaweza kusema kua Al Kaabah na Moyo wa Ibn Adam si vitu
viwili tofauti, kwani Al Kaaba ya kweli hua ni sawa na Al Lubb iliyokamilia ambayo
ndio asili ya Ibada ya Sala, na hivyo mtu yeyote yule ambae atauchukua Moyo wake
na kuuweka katika hali yake ya Ukamilifu na akasali basi hua ni mwenye kusali
440

huku akiwa ndani ya Al Kaabah. Na hivyo Bayt al Maamur hua ni yenye


kumzunguka Ibn Adam huyo.’

Hivyo basi kutembelea Mji wa Makkah kwa ajili ya Ibada ya Hija hua hakuthibitishi
upatikanaji wa manufaa ya Kiroho yanayotakiwa kupatikana na Nafsi ya Mtu husika
kutokana na kua ni mwenye kufuata Millat Ibrahim na hivyo mtu huyo kua mwenye
kuihisi athari ya Ibada hio Kiroho, Kimoyo na Kinafsi kwani ni muhimu kwanza kujua
malengo na Siri iliyomo ndani ya Ibada ya Hija ambavyo ndivyo vinavyojumuisha moja
kati ya hatua muhimu zinazothibitisha kuafuata Milat Ibrahim.

Na ndio maana Wanazuoni wakatupa mifano ya kujifunza juu ya siri ya kua ni mwenye
kuitikia wito wa Nabii Ibrahim Alayhi Salam kwa kutuelezea mahojiano baina ya Imam
Zayn Al Abidin ambae alikua akimhoji Qutb Al Arifin Mujaddid Al Islam Imam Jafar
Abu Bakr Al Shibli baada ya kurudi kutoka katika safari ya Hijja, ambapo mfano wa
mahojiano hayo yameelezewa tena katika mtizamo mwengine unaotokana na Imam Abu
Abd Rahman Muhammad Ibn Al Husayn Ibn Muhammad Ibn Musa Ibn Khalid Ibn Salim
Ibn Zawwiyah Ibn Saif Ibn Qabisa Al Azdi Al Sulami Al Shafii Al Nishapuri alieishi
katika karne ya 4 Al Hijra ya Uislam na pia kutoka kwa Shaykh al Akbar Imam Abu Bakr
Ibn Arabi ambao Maimamu wote wawili hawa kwa pamoja wanasema kua kisa kilitokea
baina ya Qutb Al Arifin Mujaddid Al Islam Imam Jafar Abu Bakr Al Shibli na
Mwanafunzi wake ambae hata hivyo hawakumtaja jina, kua: ‘Imam Al Shibli
alimuuliza Mwanafunzi wake ambae alikua amerudi kutoka katika Ibada ya Hija
kwa kusema: ‘Jee ulipofika katika Miqaat ulivua mavazi ya kumuasi Mola wako na
kisha ukavaa mavazi ya Utiifu ya Ihram?’
Mwanafunzi huyo akajibu: ‘Naam!’
Al Shibli akamuuliza tena: ‘Jee katika Uvuaji huo, ulinuia kuvua pia Mavazi ya
Unafiq na kuvaa mavazi ya kuingia katika kufanya amali njema kwa Ikhlas?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akajibu kwa kusema: ‘Basi bila ya shaka wewe hukua ni mwenye
kuyavua mavazi yako yote kikamilifu katika Miqaat na wala hukuingia katika
Ihram’ Imam Al Shibli akaendelea kuuliza: ‘Jee Ulijitoharisha kikamilifu kwa
Udhu?’
Mwanafunzi akajibu: ‘Naam’.
Hivyo Imam Al Shibli akauliza: ‘Jee ulijitoharisha kutokana na dhambi zako zote na
kasoro zako zote?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akajibu: ‘Basi hujajitoharisha kikamilifu’ Imam Al Shibli akaendelea
kuuliza: ‘Jee Ulipojitoharisha ulinuia kujitoharisha kwa kutumia Nuru ya Tawbatan
Nasuhan mbele ya Allah Subhanah wa Taála?’
Mwanafunzi wake akajibu: ‘La’
Imam Al Shibli akauliza tena: ‘Jee ulipovaa Ihram ulikua ni mwenye nia ya kua
unajizuia na kila kitu ambacho kimekatazwa na Allah Subhanah wa Taála?’
441

Mwanafunzi akajibu: ‘La!’


Imam Al Shibli akasema: ‘Jee Ulipokua ukitimiza makubaliano ya Hija ulikua na nia
kua unafuta makubaliano ya wengineo wote isipokua na Allah Subhanah wa Taála?’
Imam Al Shibli akauliza: ‘Jee uliposema: Labaika Allahhumma Labbaik! Labaika la
Sharika Laka Labaik! Ulisikia Muitikio wa Mola wako juu yako ambao wewe ulikua
ukiitikia?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Basi bila ya shaka wewe hukua ni mwenye kujitoharisha,
wala hukuvaa Ihram na wala hukutekeleza makubalino ya Hijja’
Imam Al Shibli akauliza: ‘Jee ulipoingia katika Miqaat na kusali Rakaa 2 za Ihram
uliitikia Talbiya - Labaika Allahhumma Labbaik! Labaika la Sharika Lak Labaik!
Labaika Allahhumma Labbaik! Labaika la Sharika Lak Labaik!’
Mwanafunzi akajibu: ‘Naam!’
Imam Al Shibli akauliza: ‘Jee ulipoingia katika Miqaat ulitia nia ya kua unaingia
kimatembezi?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam A Shibli akauliza tena: ‘Jee Uliposali Rakaa 2 ulitia nia ya kua unajaribu kua
na ukaribu na Allah Subhanah wa Taála kwa kua ni mwenye kufanya Amali bora
na mambo mema kutokana na Ibada zako?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Jee ulipokua ukiitikia Talbiya - Labaika Allahhumma
Labbaik! Labaika la Sharika Lak Labaik! Labaika Allahhumma Labbaik! Labaika la
Sharika Lak Labaik! Ulikua na nia ya kua uko katika hali ya kua ni mwenye
kuzungumza na Allah Subhanah wa Taála ukiwa na Utiifu, kua ni mwenye kukaa
kimya kutokana na kuachana uasi.’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Basi kwa hakika wewe hukuingia katika Miqaat, hukusali
Sala yeyote na wala hukuitikia Talbiyyah’ Imam Al Shibli akendelea kuuliza: ‘Jee
uliingia katika Haraam na Uliliona Al Kaabah na Ulisali katika eneo hilo?’
Mwanafunzi akajibu: ‘Naam!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Jee ulipoingia katika Haraam ulikua na ni ya kua ni
mwenye kujiharamishia nafsi yako kila aina ya kusengenya kwa Waislam wote kwa
Ummah wa Kiislam?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Na jee Ulipofika katika Mji wa Makkah ulitia nia kwa
Moyo wako kua umefika katika eneo hilo kwa ajili ya Allah Subhanah wa Taála?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Kwa Hakika wewe hukuingia katika Haraam na Wala
Hujaliona Al Kaabah na wala hujasali.’ Imam Al Shibli akaendelea kuuliza: ‘Jee
ulitufu na uliigusa Ruqn na Ulifanya SaAi’
Mwanafunzi akasema: ‘Naam!’
442

Imam Al Shibli akauliza: ‘Na ulipofanya SaAi, ulinuia kua ulikua unaharakia
kumkimbilia Allah Subhanah wa Taála na Jee Allah Subhanahu wa Taála mwenye
kujua Siri zote anajua juu ya hilo’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Kwa Hakika wewe hukufanya Tawaf, hukuigusa Ruqn na
wala hukufaya SaAi’. Kisha Imam Al Shibli akaendela kwa kuuliza: ‘Jee Uliligusa
Hajar Al Aswad? Na jee Ulisimama katika Maqam Ibrahim na Ukasali Rakaa 2
ndani yake?’
Mwanafunzi akajibu: ‘Naam!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Ya Allah! Akh ya Akh! Yeyote yule ambae atakaeligusa
Hajar Al Aswad basi hua ni sawa na mwenye kugusana na Allah Subhanah wa Taála,
Hivyo Kua Jihadhari ewe Kijana ili usije ukayaangamiza malipo yako yote
yaliyotokana na kugusa kitu kitakatifu na kutukuzwa kisha wewe ukawa ni mwenye
kuharibu malipo yake kutokana na kuligusa kwako kwa kufanya maovu baadae
kwa mikono yako na kukamata mambo siyo kama walivyo wenye dhambi’
Imam Al Shibli akauliza: ‘Jee uliposimama katika Maqam Ibrahim ulitia nia kua
unasimama huku ukiwa ni mwenye kusimama kwa ajili ya kusimamia maamrisho
yote ya Allah Subhanah wa Taála na kua ni mwenye kusitisha maovu yote yaliyopita
kabla yake?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akauliza tena: ‘Jee wakati unasali rakaa mbili katika Maqam Ibrahim,
ulinuia kua unasali Sala kama alivyosali Nabii Ibrahim na hivyo kua ni mweye
kumuadhirisha Shaytan na Sala hizo?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akajibu: ‘Basi kwa Hakika wewe hukusimama na wala hukusiamam
katika Maqam Ibrahim.’ Imam Al Shibli akaendela kuuliza: ‘Jee uliangalia ndani ya
kisima cha Zamzam na ulikunywa Maji yake?’
Mwanafunzi akajibu: ‘Naam!’
Imam Al Shibli akauliza: ‘Jee wakati unaangalia ndani ya kisima cha Zamzam
uliangalia kama unaeangalia kwa utiifu mbele ya Allah Subhanah wa Taála? Na
hivyo kua ni mwenye kuamua kuyafunga macho yake na kutoangalia Maovu?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Basi kwa hakika wewe hukuangalia ndani ya kisima cha
Zamzam na wala hukunywa Maji yake’ Imam Al Shibli akauliza: ‘Jee ulikimbia Safa
na Marwa na ulitembelea kwa haraka huku na kule baina yake?’
Mwanafunzi akajibu: ‘Naam!’
Imam Al Shibli: ‘Jee katika kukimbia kwako huko ulikua katika hali ya matumaini
na khofu juu ya Mola wako?’
Mwanafunzi akasema: ‘La!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Basi kwa hakika wewe, hukua ni mwenye kukimbia Safa
na Marwa!’ Imam Al Shibli akamuuliza: ‘Jee ulienda Mina’
Mwanafunzi akajibu: ‘Naam.’
443

Imam Al Shibli akauliza: ‘Jee ulipofika ulinuia kua kila Muislm atakua huru
kutokana na madhara ya Ulimi wako na Moyo wako?’
Mwanafunzi akasema: ‘La!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Basi kwa hakika wewe hujaenda wewe Hujaenda Mina’
Imam Al Shibli akauliza: ‘Jee Ulikaa kwa mda mfupi katika Arafa na ukapanda Jabal
Al Rahman na ukaliona na kuifaham Wadi al Namira? Na jee uliomba Dua kwa
Allah Subhanah wa Taála karibu na Al Mil na Jamarat?’
Mwanafunzi akajibu: ‘Naam!’
Imam Al Shibli akauliza: ‘Jee katika kusimama kwako Arafa ulihisi katika Ufahamu
wako wa kiroho kuwepo kwa Allah Subhanah wa Taála na kujua juu ya Amali zako
njema, na kuingiza akilini kua kitabu chako cha amali njema kiko mikononi mwa
Allah Subhanah wa Taála? Ambae ndie mwenye kujua ya siri ya yaliyofichika ndani
ya Moyo wako?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akauliza tena: ‘Jee ulipopanda Jabal Al Rahma ulikua na nia ya
kumuomba Allah Subhanah wa Taála awaingize katika Rehma zake na awasaidie
katika matatizo yao Waumini wote wa Kiume na wa Kike?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akauliza tena: ‘Na jee ulipokua katiika Wadi Al Namira ulitia nia ya
kua utakua ni miongoni mwa wenye kukataza Mabaya na hivyo ni kua ni mwenye
kuachana nayo maovu wewe mwenyewe kwenye Nafsi yako? na hutokua ni mwenye
kuamrisha Mema hadi pale utakapokua wewe ni miongoni mwa wafanyao mema
katika Nafsi yako?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akauliza: ‘Na jee uliposimama katika maeneo ya Al Mil na Al
Jamaraat ulikua na nia ya kua maeneo hayo yanashuhudia matendo yako yote ya
Ibada yalikua yanakusimamia pamoja na Malaika wako wanaokusimamia
kutokana amri ya Allah Subhanah wa Ta’ala?’
Mwanafunzi akajib: ‘La!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Basi kwa hakika wewe hukua ni mwenye kusimama
Arafah, na wala hujaenda katika Jabal Al Rahma, na wala hukua ni mwenye kuiona
Wal Al Namirah na hukua ni mwenye kumuomba Mola wako.’ Imam Al Shibli
akaendelea kuuliza: ‘Jee ulipita baina ya Nguzo mbili na kusali Rakaa 2 kabla ya
kuvukana kuelekea Muzdalifa na kuchukua kokoto na kuvuka Masha’rul Haram?’
Mwanafunzi akajibu: ‘Naam!’
Imam Al Shibli akauliza: ‘Na jee uliposali Rakaa 2, ulikua na nia ya kua unasali kwa
ajili ya kumshukuru Mola wako ndani ya Masiku 10 ambayo hua ni yenye
kukuondoshea Mitihani na kukurahisishia kila jambo lakoo lililo gumu?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akauliza: ‘Jee katika kupita kwako baina ya Nguzo mbili bila ya
kuzidi kushoto wala kulia ulikua na nia ya kutovuka mipaka katika Dini ya Haki
444

kwa upande wa kulia au kutozidi katika upande wa kushoto kua na misimamo


yenye dharau ndani yake kwa Moyo wako, Ulimi wako na Viungo vyako?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Na jee ulipokua ukitembea katika maeneo ya Muzdalifat
na kuokota kokoto ulikua na nia ya kua ni mwenye kuvichuma vitendo vyako vyote
viovu na vya kijinga ulivyovifanya kutokana na kutokua na Ilm.’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Na jee ulipokua ukipita katika Masha’rul Haram ulikua
na nia ya kua umeuchimba Moyo wako na kuutia alama ya kua ni miongooni mwa
watu wenye Taqwa, na Khofu na Matumaini kwa Allah Subhanah wa Ta’ala?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Basi kwa hakika wewe hukupita baina ya nguzo 2 na
hukusali Rakaa 2 na walua hukuwasili katika maenoe ya Muzdalifat, hukuokota
kokoto na wala hukutembea katika Masha’rul Haram’ Imam Al Shibli akauliza: ‘Jee
ulitembelea Minna? Ukarusha kokoto katika Jamarat na ukanyoa nwele zako na
kuchinja na kusali katika Masjid al Kheef na kisha ukarudi Makkah na kufanya
Tawaf al Ifadha ya kurudi Makkah’
Mwanafunzi akajibu: ‘Naam!’
Imam al Shibli akauliza: ‘Jee ulipowasili katika maeneo ya Mina na kasha ukarusha
kokoto katika Jamarat ulikua na nia ya kua umefikia Malengo yako na Mola wako
ameshakutumizia mahitaji yako?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Na jee ulipokua ukirusha kokoto katika Jamarat ulikua
na nia ya kua unampiga adui yako Iblis na kwa kufanikiwa kufika kwako katka
Ibada ya Hija basi umefanikiwa kumuasi Iblis?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akasema: ‘Na jee ulipokua ukinyoa nywele zako ulikua na nia ya kua
unajisafisha na kujivua maovu yote na Dhulma za Ibn Adam na hivyo kua ni
mwenye kujisafisha na dhambi zako zote kama motto mchanga?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’
Imam Al Shibli akauliza: ‘Na jee katika wakati ukiwa unachinja Hadiya yako
ulikua na nia ya kua unachinja na kuukata mshipa wa uchoyo na ubakhili na
kushikamana na uhalisia wa Taqwa na kua ni mwenye kufuata Milat Ibrahim,
kama vile alivyokua akimtayarisha Mtoto wake, ambae alikua ni tunda la Moyo
wake ambae kupitia kwake basi alikua ni mwenye kuazisha Sunna ya
kupataukaribu kwa Allah Subhanah wa Ta’ala kwa wali waliokuja baada yake?’
Mwanafunzi akajibu: ‘La!’

Imam al Shibli akasema: ‘Na jee ulipokua ukirudi katika Mji wa Makkah, na kufanya
Tawaf al Ifadha ulikua na nia ya kua uarudi huku ukiwa ni miongoni mwa
walioingia katika Rehma za Allah Subhanah wa Ta’ala, katika utiifu wake na kua
445

umefanikiwa kuzipata ridhaa zake na umetekeleza majukumu yako kwake na kua


umepata ukaribu wake?’

Mwanafunzi akajibu: ‘La!’

Imam Al Shibli akasema: ‘Kutokana na hali hio basi kwa hakika wewe hukufika
katika maeneo ya Mina, hujarusha kokoto katika Jamarat, hukunyoa Nywele zako,
na wala hukuchinja Hadiya na hukusali Masjid al Kheef na wala hukurudi katika
mji wa Makka kufanya Tawaf Al Ifadha. Hivyo basi kwa hakika pia wewe hujaeda
katika Ibada ya Hija, hivyo rudi tena mwakani ukafanye tena Ibada hio upya!’

Mwanafunzi huyo akaanza kulia kutokana na yale aliyoyakosa baada ya kudhani kua ni
mwenye kufuata Millat Ibrahim kwa kuenda katika Ibada ya Hija wakati hakua ni
mwenye kujua Siri ya Ibada hio na malengo yanayotakiwa kufikiwa na manufaa
yanayotakiwa kupatikana ndani yake. Ndio maana ya maneno ya Shaykh ul Al Akbar
Imam Abu Bakr Ibn Al Arabi pale aliposea: ‘Wakati Allah Subhanah wa Ta’ala
alipouumba Mwili wa Ibn Adam basi aliweka Al Kaabah ndani yake, ambalo ni
Moyo. Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala amejaalia jengo hilo la Moyo kua ni kiungo
bora cha Muuumin. Na hivyo ametuambia kua Mbinguni ambako ndiko kwenye Al
Bayt Al Maamur na Ardhini ambako ndiko kwenye Al Kaabah, hakumzunguki yeye
bali yote hayo yako chini yake, isipokua Moyo wa Mja wake uliojaa Imani hua ni
wenye kumzunguka yeye, yaani kuzunguka kunako zungumziwa hapa
hakumaanishi chochote isipokua hua ni kwenye kumaanisha Ilm ya Moyo wa Mja
huyo katika Kumjua Allah Subhanah wa Ta’ala.’

Hivyo kwa hakika Allah Subhanahu wa Ta’ala alimkubalia dua zake Nabii Ibrahim
kutokana na yeye Nabii Ibrahim kua ni mwenye kumjua Mola wake, hivyo wito wake
huo wa kuwaita watu kuja kwa ajili ya Hija hivyo kizazi chake kikawa kinaongezeka na
kukua kidogo kidogo, hatua kwa hatua, watu kutoka katika miji mbali mbali wakaanza
kusikia kuhusiana na mji huo na nyumba hiyo na wakawa wanakuja kuutembelea na
kufanya Ibada katika mji huo na kizazi cha Nabii Ibrahim A’layhi Salaam na Nabii
Ismai’l A’layhi Salaam.

Ama kwa upande mmoja basi Hujjat Ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Ibn
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii basi yeye
anatuambia kua kuna aina tatu za watu wanaoenda kufanya Ibada ya Hija:

1- Wale wanaoenda kufanya Ibada ya Hija bila ya Matayarisho na hivyo hua ni


wenye kunufaika na baadhi ya mambo katika Ibada hio, lakini hua ni wenye
kukosa manufaa mengi sana ndani yake.
446

2- Wale wanaojitayarisha kimwili kwa ajili ya Ibada hio na matayarisho haya hua
ni muhimu.
3- Wale wanaojitayarisha kimwili, kiakili na kiufaham na hivyo hua wanajua
wanachokifanya na wanajua pia sababu ya kufaya hicho wanachokifanya, na
hivi ndivyo mtu unavyotakiwa kujitayarisha kwa Ibada ya Hija.

Hujjat Ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Ibn Muhammad Ibn Muhammad
Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii anaendelea kututaarifu kua ‘Miongoni
mwa Hikma za Ibada ya Hija ni mbili zifuatazo:

1-Ibada ya Hija ni kua mbadala wa kutembelea Nyumba za Kidini za watu


waliotangulia hapo kabla, kuna kauli ambayo inasema kua Allah Subhana wa
Ta’ala ameifanya Hija kua jambo la Kidini kwa Ummah wa Rasul Allah Salallahu
A’layhi wa Salam. Kwani Allah Subhanah wa Ta’ala, ameitukuza Bayt ul Atiq kwa
kujinasibisha nayo yeye mwenyewe kwa kuiita Baytu Allahi na hivyo kuifanya kua
ni nyumba ambayo wanaomuabudu lazima waielekee na waitembelee. Na
akalifanya eneo linaloizunguka Nyumba hio kua ni takatifu, na kuifanya Arafah
kua kama ni sehemu ya eneo lake takatifu. Kisha akatoa amri ya kutoua Mnyama
yeyote ndani yake na kutokata mti wowote ndani ya eneo hilo. Ni jambo lililowazi
kua Allah Subhanah wa Ta’ala, hahitaji sehemu wala makazi yeyote, kwani yeye ni
mwenye kukizunguka kila kitu na hakuna kitakacho mzunguka yeye.

Kutokana na Hikma zake Allah Subhanah wa Ta’ala, basi tunaona kua ndani ya
Ibada ya Hija mna Hikma ya kuwapa mtihani wa kuthibitisha namna ya
kumtumikia Allah Subhanah wa Ta’ala. Kwani Waja Watiifu watakuja kutoka
mbali na kwa wingi kwa ajili ya kuitikia wito wake, huku wakiwa katika hali ya kua
na nywele zilizokua timtim, na kua ni waliojaa mavumbi mwilini mwao, huku
wakiwa ni wenye kuonesha unyenyekevu kwa Mola wao, ambae ni Allah Subhanah
wa Ta’ala aliekua na Sifa ya Utukufu, jambo ambalo huenda sambamba na
kuonesha kua Utukufu wa sifa yake hauhusiani na kua na kuwepo katika sehemu
yeyote inayomzunguka yeye. Hivyo hii hua hali ya upekee ya kuonesha Utiifu juu
yake na kumtumikia yeye.

Kutokana na sababu hii basi, ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akataka
kuwepo kwa Ibada maalum ambazo hua ni zenye kuenda kiyume na maumbile na
ufahamu wa Ibn Adam. Ili vitendo hivyo kiibada viwe ni kwa ajili ya kujitolea na
kumtumikia Allah Subhanah wa Ta’ala pekee (kwa Ikhlas), na ndio maana Rasul
Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Ya Allah! Hakika sisi tumehudhuria
kwa ajili ya Hija, kwa ajili ya kukutumikia na kuonesha Utumwa wetu kwako’’
447

2- Safari ya kuenda Hija imefananishwa na Safari ya kuelekea Akhera, kwani mtu


anaejitayarisha kuenda Hija basi anatakiwa ajiandae na kila hatua anayoichukua
basi hua ni sambamba na hatua ya Akhera. Kwa mfano:

Mtu anapowaaga watu wake kwa ajili ya safari ya Hija basi pia anatakiwa afikirie
juu ya kuwaaga katika kipindi cha kifo chake, mtu anapoondoka na kutoka katika
nchi yake kuelekea Makkah basi afikirie juu ya wakati wa yeye kuondoka Duniani
na kuelekea Akhera. Unapobebwa ndani ya kipando basi unatakiwa ufikirie namna
utakavyobebwa ndani ya Jeneza. Wakati unapovaa Ihram basi kumbuka wakati
utakapovishwa Sanda. Unapovuka Majangwa na kuinga katika mipaka ya Mji
Mtakatifu, basi fikiria juu ya kuvuka mabonde ya ulimwengu huu kuelekea katika
ulimwengu wa Akhera (Kaburini). Wakati unapokua na khofu ya kuvamiwa na
wezi au maharamia basi kumbuka utakapokua na khofu katika kuhojiwa na
Munkar na Nakir, unapofikiria juu ya wanyama wenye kutisha njiani basi fikria
Nyoka na Ng’e watakao kuwepo Kaburini. Unapotengena na jamaa zako na familia
yako basi fikiria namna utaokavyokua peke yako Kaburini. Utakaposoma Talbiyah
basi kumbuka kuitikia wito wa Allah Subhanah wa Ta’ala katika siku ya Malipo.

Mtu unatakiwa ujikumbushe yote haya juu ya Akhera katika kila kitendo, kwani
katika kila kitendo unachokifanya basi kina Hikma yake na mafunzo yake na
ukumbusho kwa ajili ya Akhera, ambao kwa ila Mja kulingana na uwezo wake na
Ikhlas yake na malengo yake ya kutekeleza maamrisho ya Dini yake basi ataweza
kuyafaham wazi wazi.

Ni pale tu utakapokua ni mwenye kujua na kufaham Hikma zilizomo ndani ya Ibada ya


Hijja basi ndipo utakapopata athari yake ndani ya nyoyo na nafsi yako, na kua na
mabadiliko ndani ya maisha yako na hivyo utakua ni mwenye kunufaika na Ibada hio,
kwani anasema Hasan Al Basr baada ya kuulizwa: ‘Watu wanasema kua Mtu akirudi
katika Ibada ya Hijja basi hua ni mwenye kusamehewa dhambi zake zote kama
alivyozaliwa na Mama yake, Hivi jee? ni kweli’ Hasan Al Basr akajibu : ‘Naam, ni
kweli na uthibitisho wa jambo hilo ni kua Mtu huyo hua ni mwenye kuachana na
matendo maovu yote aliyokua akiyafanya hapo kabla.’

Ama kuhusiana na Umuhimu wa Ibada ya Hija na wanaohudhuria Ibada hio basi anasema
Shaykh ul Akbar Imam Abu Bakr Ibn Arabi kua: ‘Hakika mimi nilijiona nafanya
Tawaf katika Al Kaabah, na nikaona Majumba ya zamani sana ambayo inaonekana
kama yamejengwa zaidi ya miaka laki moja iliyopita. Na kisha nikaona kuna na
watu wengine wanafanya Tawaf pamoja nami, hivyo nikamuuliza mmoja wao: ‘Jee
unatoka nchi gani?’ yule mtu akanijibu: ‘Mie ni miongoni mwa waliotangulia kabla
yako.’ Namii nikamuuliza: ‘Jee ni miaka mingapi imepita tangu mmefariki?’ Yule
mtu akanijibu: ‘Zaidi ya miaka 40000’ Nami nikamuuliza: ‘Lakini mbona hio ni
448

zaidi ya miaka inayotutenganisha sisi na Adam?’. Yule Mtu akasema: ‘Jee


unamzungumzia Adam gani? Huyu Adam alie karibu nanyi au Adam mwengine?’’

Imam Ibn Al Arabi anaendelea kusema kua: ‘Hapa nikakumbuka Hadith ya Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: Kwa athari basi Allah Subhanah wa Ta’ala
alimuumba Adam, aliwaumba Adam 100,000 na baina ya kila Adam basi kuna
miaka 17000. Hivyo nikasema kuiambia Nafsi yangu. Inawezekana ikawa hawa
watu ambao wanasema kua ni Walionitangulia basi ndio hao wanaotokana na
Adam alietangulia.’

Naam..Mbali ya kua Allah Subhanah wa Taála anatuusia kua ni wenye kufuata Millat
Ibrahima lakini pia anatuwekea wazi mafunzo bora zaidi yaliyomo ndani ya kisa hiki cha
Nabii Ibrahim ni mfano wa kuigwa juu yetu pale alipobainisha hayo katika Surat Al
Muntahina ambayo ni Sura yenye malengo ya kusisitiza kusimamisha hali ya Sibghata
Allah ndani ya Nyoyo za Waumini kwa kusema baada ya:

ِ‫ٱﻟﱠﺮ‬
﴾‫ﺣﻴ ِﻢ‬ ‫اﻪﻠﻟِ ٱﻟﱠﺮ ْﲪـٰ ِﻦ‬
‫﴿ﺑِ ْﺴ ِﻢ ﱠ‬

‫ﱠﺨ ُﺬواْ َﻋ ُﺪ ِّوى َو َﻋ ُﺪ ﱠوُﻛ ْﻢ أ َْوﻟِﻴَﺂءَ ﺗُـ ْﻠ ُﻘﻮ َن إِﻟَْﻴ ِﻬ ْﻢ ﺑِﭑﻟْ َﻤ َﻮﱠدةِ َوﻗَ ْﺪ‬
ِ ‫﴿ ٰ�َﻳـﱡﻬﺎ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ آﻣﻨُﻮاْ ﻻَ ﺗَـﺘ‬
َ َ َ
‫ﭑﻪﻠﻟِ َرﺑِّ ُﻜ ْﻢ إِن ُﻛﻨﺘُ ْﻢ‬
‫ﻮل َوإِ ﱠ� ُﻛ ْﻢ أَن ﺗُـ ْﺆِﻣﻨُﻮاْ ﺑِ ﱠ‬ َ ‫َﻛ َﻔُﺮواْ ِﲟَﺎ َﺟﺂءَ ُﻛ ْﻢ ِّﻣ َﻦ ٱ ْﳊَِّﻖ ُﳜْ ِﺮ ُﺟﻮ َن ٱﻟﱠﺮ ُﺳ‬
‫ﺿﺎﺗِﻰ ﺗُ ِﺴﱡﺮو َن إِﻟَْﻴ ِﻬ ْﻢ ﺑِﭑﻟْ َﻤ َﻮﱠدةِ َوأ ََ�ْ أ َْﻋﻠَ ُﻢ ِﲟَﺂ‬ ِ ِ ِ
َ ‫َﺧَﺮ ْﺟﺘُ ْﻢ ﺟ َﻬﺎداً ِﰱ َﺳﺒِﻴﻠﻰ َوٱﺑْﺘﻐَﺂءَ َﻣْﺮ‬
‫ﺿ ﱠﻞ َﺳ َﻮآءَ ٱﻟ ﱠﺴﺒِ ِﻴﻞ۞ إِن ﻳَـﺜْـ َﻘ ُﻔﻮُﻛ ْﻢ‬ ِ
َ ‫َﺧ َﻔْﻴـﺘُ ْﻢ َوَﻣﺂ أ َْﻋﻠَﻨﺘُ ْﻢ َوَﻣﻦ ﻳَـ ْﻔ َﻌ ْﻠﻪُ ﻣﻨ ُﻜ ْﻢ ﻓَـ َﻘ ْﺪ‬
ْ‫أ‬
﴾‫ﻳَ ُﻜﻮﻧُﻮاْ ﻟَ ُﻜﻢ أ َْﻋ َﺪآء وﻳَـْﺒﺴﻄُ ۤﻮاْ إِﻟَْﻴ ُﻜﻢ أَﻳْ ِﺪﻳـَ ُﻬﻢ وأَﻟْ ِﺴﻨَـﺘَـ ُﻬﻢ ﺑِﭑﻟ ﱡﺴ ۤﻮِء ووﱡدواْ ﻟَﻮ ﺗَ ْﻜ ُﻔﺮو َن‬
ُ ْ ََ ْ َْ ْ ُ ًَ ْ
Ya ayyuha alladheena amanoo la tattakhidhoo AAaduwwee waAAaduwwakum
awliyaa tulqoona ilayhim bialmawaddati waqad kafaroo bima jaakum mina
alhaqqi yukhrijoona alrrasoola wa-iyyakum an tu/minoo biAllahi rabbikum in
kuntum kharajtum jihadan fee sabeelee waibtighaa mardhatee tusirroona ilayhim
bialmawaddati waana aAAlamu bima akhfaytum wama aAAlantum waman
yafAAalhu minkum faqad dhalla sawaa alssabeeli; In yathqafookum yakoonoo
lakam aAAdhaan wayabsutoo ilaykum aydiyahum waalsinatahum bialssoo-i
wawaddoo law takfuroona (Surat Al Mumtahina 60:1-2)
449

Tafsir: Enyi Mlioamini msiwafannye Maadui zangu na Maadui zenu kua ni Marafiki
zenu kwa kuwaonesha mapenzi wao wakati wakiwa ni wenye kukufuru juu ya kile
kilichokufikieni nyie ambacho ni cha Haki, na wakamfukuza Mtume na
wakakufukuzeni nyie mlioamuamini Allah ambae ni Mola wenu, hivyo kama ikiwa
mmejitolea kwa ajili yangu na mnatafuta ridhaa zangu. Mnaonesha urafiki nao
kisirisiri wakati mimi nnajua mnayoyaficha na mnayoyaweka wazi. Hivyo yeyote yule
miongoni mwenu atakaefanya hivyo basi kwa hakika atakua ni aliepotea katika njia
ilivyonyooka. Kwani kama wangekua wako juu zaidi yenu basi wangekuchukulieni
nyie kama maadui zao na wangetoa nje ndimi zao na kunyoosha mikono yao dhidi
yenu kwa maovu na wanatamani sana kua nyie muwe ni si wenye kukufuru.

Ambapo aya zinatuwekea wazi kua wale wenye kupingana na sifa za Allah Subhanah wa
Ta’ala basi hawataikiwi kufanywa kua ni marafiki wa Walioamini, yaani hii tunaona
kama vile alivyofanya Nabii Ibrahim pale alipoamua kutengana na Watu wake kutokana
na kutokukubaliana juu ya mtizamo wake wa uongofu wa Kutomshirikisha Allah
Subhanah wa Ta’ala na mtizamo wao wa upotovu wa Kumshirikisha Allah Subhanah wa
Ta’ala.

Hili ni jambao ambalo wengi wetu leo hii linatushinda kwani unakuta viongozi wa nchi
za Kiislam wanasaidiana na viongozi wa Kiyahudi na Manasara na ndio maana unakuta
Waislam wenyewe kwa wenyewe wanapingana na kupigana na kusababishiana madhara
mengi sana kwa Watoto, Wanawake na Wazee pia tunayaona haya katika nchi za Syria,
Yemen, Afghanistan n.k kwa sababu hio hio ya kutoenda sambamba kivitendo na aya hii,
na hivyo kua ni wenye kutofuata Millat Ibrahima na pia na Sunnah ya Rasul Allah
Salallahu A’layhi wa Salam kama alivyofanya katika vita vya Badr na Uhud pia ambapo
yeye alikataa kushirikiana na Makafiri kupigana vita dhidi ya Makafiri, kama
invyoonesha Hadith ifuatayo:

Anasema Ummu ul Muuminina Aisha Radhi Allahu Anha kua: ‘Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam alitoka kuelekea katika vita vya Badr. Hivyo kuna mtu miongoni
mwa Washirikina akamfuata na walipofika katika maeneo ya Harrat Al Wabra
akakutana nae na akasema: ‘Mimi nimekufuata kwani nataka kuungana nawe ili
nipate ngawira ya vita pamoja nawe.’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
akasema: ‘Jee wewe unaamini juu ya Allah na Mtume wake?’ Yule mtu akajibu:
‘La’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Basi Rudi kwani mimi siwezi
kupokea msaada kutoka kwa Kafiri’

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaendelea na safari yake mpaka
wakafika kwenye Mti. Yule mtu akatokea tena na wakazungumza kama
walivyozungumza hapo awali. Na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akajibu
tena: ‘La, Rudi kwani mimi siwezi kupokea Msaada kutoka kwa Kafiri’ lakini mtu
huyo akatokea tena katika maeneno ya Al Bayda, na wakahojiana tena kama hapo
450

kabla na yule Mtu akasema: ‘Naam’ hapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam :
‘Fa-ntaliq - Twende’’(Musnad Imam Ahmad)

Kwa upande mwengine basi anasema Imam Abū Ja'far Aḥmad Ibn Muḥammad
al-Ṭaḥawi kua Abu Humayd Al Said Radhi Allahu Anhu anasema kua: ‘Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam alitoka katika siku ya Vita vya Uhud mpaka akafika
katika maeneo ya bonde la Thaniyat Al Wada. Na mara likatokea kundi la jeshi
lilikua limetayarisha vizuri sana. Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akauliza:
‘Hawa Ndio nani?’ nao wakajibu: ‘Banu Qaynuda ambao ni watu wa Abd Allah
Ibn Salam. Na watu wa Abd Allah Ibn Ubay Ibn Al Salul.’ Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam akasema: ‘Basi silimuni’ ambapo nao wakakataa na Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Basi wache warudi, Kwani sisi hatutokubali
msaada wa Makafiri dhidi ya Makafiri’ ’ (Sharh Mushkil Al Athar)

Hivyo hadith zinatuonesha kua haikubaliki kushirikiana na Makafiri dhidi ya Makafiri,


lakini leo hii sisi tunashirikiana na Makafiri dhidi ya Waislam wenzetu. Ya Allah,
Mtihani mkubwa sana huu Wallahi.

Ama tunapoangalia mtizamo wa Mujaddid ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi yeye
anasema kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Mtu hua ni
mwenye kua na Dini ya Rafiki yake, hivyo angalieni ni nani mnafanya Urafiki
nao’’(Imam At Tirmidhii). Ambapo Imam At Tirmidhii mwenyewe amesema kua hii ni
Hadith Dhaif lakini hata hivyo amesema Imam Abu Zakariyah Sharaf An Nawawi
kuhusiana na hadithi hii kua ni Hadith inayoaminika.

Mujaddid ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi anaendelea kutuambia kua: ‘Amesema
Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam kua Mshikamano wenye Nguvu wa Iman
hua ni Kumfanya Mtu kua rafiki kwa ajili ya Allah, Kumfanya Mtu kua Adui kwa
ajili ya Allah na Kumpenda Mtu kwa ajili ya Allah’

Hivyo mtizamo wa Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi, Jarrah Allah Imam
Abu Al Qasim Al Zamakhshari na wengineo kuhusiana na aya hii kua: ‘Kama ikiwa
umejitolea katika njia ya Allah Subhanah wa Ta’ala na kutafuta fadhila zake basi
usiwafanye Makafiri kua ni Mrafiki zako’

Ambapo kuna kukubaliana kwa Wanazuoni kuhusiana na sababu ya kushushwa ayah hii
ni kua: Hatib Ibn Abi Baltah Radhi Allahu Anhu ambae alikua ni Muhajirina lakini asie
kua wa Quraysh aliepigana vita vya Badri, alikua na mali zake na familia yake katika Mji
wa Makkah alikua hana ulinzi wa Kabila lolote isipokua alikua ni mwenye ushirikiano
na Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anhu.
451

Hivyo wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipoamua kuvamia Mji wa
Makkah kwa sababu ya Watu wa Makkah kua ni wenye kuvunja Makubaliano ya
Hudaybiyah, basi alitangazia juu ya Matayarisho ya Safari lakini hakuweka wazi kua
watu wataelekea wapi bali alisema tu: ‘Ya Allah Ficha Habari zetu Juu yao’ na
kuwaambia Masahaba wajitayarishe. Hivyo Hatib Ibn Abi Baltah Radhi Allahu Anhu
alivyoona hali hio basi akaandika barua na kumpa mmoja kati ya Wanawake ili aipeleke
kwa Machifu wa Mji wa Makkah kuhusiana na dhamira ya Rasul Allah Salallahu Alayhi
wa Salam kwa nia ya kujipendekeza ili kama Waislam wakishindwa pale watakapovamia
basi familia yake na mali zake ziwe salama Mjini Makkah.

Anasema Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
Salam alinituma mie na Abu Marthad Radhi Allahu Anhu na Zubayr Ibn Awwam
Radhi Allahu Anhu na kutuambia: ‘Nendeni mpaka Khakh na mtamkuta
Mwanamke miongoni mwa Mapagani, ambae ana barua kutoka kwa Hatib Ibn
Baltah iliyotumwa kwa Makafiri wa Makkah.’ Nasi tukamkuta Mwanamke huyo
amepanda Ngamia katika sehemu hio ambayo aliyotuambia Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam kua tutamkuta, nasi tukamwambia: ‘Toa Barua’ nae akasema: ‘La
hatuna barua’ hivyo sisi tukamshusha kutoka kwenye Ngamia na kumsachi, lakini
hatukufanikiwa kuiona barua hio. Hivyo tukasema: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi
wa Salam hawezi kusema Uongo. Hivyo tupe barua au tutakuvua nguo zote’

Hivyo alivyoona kua hana khiari basi, akaitoa kutoka katika mkanda wake wa
kiuononi, kwani alikua amevaa nguo nyingi. Hivyo tukaichukua barua hiyo hadi
kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam. Na Umar Radhi Allahu Anhu akasema:
‘Ya Rasul Allah (Salallahu A’alayhi wa Salam)’ kwa hakika huyu amemsaliti Allah
na Mtume wake na Waumini pia, hivyo tumkate kichwa.’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kumuuliza Hatib Radhi Allahu
Anhu: ‘Jee ni kitu gni kilichokupelekea wewe kufanya hili jambo ulilolifanya?’
Hatib Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Wallahi, sijui nini kimenitokea, jee kuna kitu
ambacho kimenifanya mie nisimuamini Allah na Mtume wake (Salallahu A’alayhi
wa Salam), kwani nilikua nataka kuwathibitishia watu wangu ili wanilindie Watu
wangu na Mali zangu, kwani hakuna miongoni mwa Masahaba zako isipokua yeye anae
mtu wa kumuangalizia na kumlindia watu wake na mali zake.’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Amesema Ukweli na Hivyo


msimfikirie jambo lolote isipokua Jema.’

Umar Radhi Allahu Anhu akaendelea kusema: ‘Lakini Ya Rasul Allah, kwa hakika
huyu amemsaliti Allah na Mtume wake (Salallahu A’alayhi wa Salam)’ na Waumini
pia, hivyo tumkate kichwa.’
452

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Jee huyu sio yule ambae alipigana
pamoja nanyi katika vita vya Badr? Labda huenda Allah Subhanah wa Ta’ala na
kuwaambia: ‘Fanyeni Mnachotaka Peponi kwani hii ni Pepo yenu, au atasema:
‘Hakika mimi nimekusamehe’’

Macho ya Umar Radhi Allahu Anhu yakawa ni yenye kujaa machozi na kisha
akasema: ‘Hakika Allah na Mtume (Salallahu A’alayhi wa Salam) wake ni Wenye
Kujua zaidi’’

Ambapo kwa upande wa Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari basi yeye
anasema kua: ‘Huyu Mwanamke alikua anaitwa Sara na alikua ni Mtumwa wa Banu
Hashim ambae alikuja Madina Kutoka Makkah, na hivyo Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam alimuuliza kwa sababu gani akaja katika Mji wa Madina. Jee
amesilimu? Na mwanamke huyo akasema la hajasilimu ila watu wake wamefariki
katika vita vya Badr hivyo sasa hivi ana hali mbaya ya kimaisha, na alikua ni
muimbaji. Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayh wa Salam akamuuliza: ‘Vipi
kuhusiana na vijana wa Makkah hawakuhitaji tena?’ Mwanamke akajibu: ‘Baada
ya yaliyotokea katika Badr basi hawanitaki tena’’

Hivyo ukoo wa Abd ul Muttallib ukafanya mchango kwa ajili yake na kumfungia safari
ya kurudi Makkah ambapo Hatib Ibn Abi Baltah Radhi Allahu Anhu akakutana nae na
kumpa Dinar 10 kwa ajili ya kumbebea Barua yake. Ambapo Mwanamke huyu ni mmoja
kati ya watu wane ambao Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliamrisha kua wauliwe
katika Ukombozi wa Mji wa Makkah, lakini hata hivyo Mwanamke huyu alijificha na
baadae akaingia katika Uislam.

Hivyo aya zinaweka wazi kua mbali ya kua Waumini wanatakiwa kujiangalia dhidi ya
kusalitiana kutokana na ndugu na jamaa zao lakini vile vile wanatakiwa wawe makini
dhidi ya matamanio yao ili yasije yakawavutiwa na mipango ya siri ya Maadi zao ambayo
inaweza kuwapelekea Waumini hao kua ni wenye kutoka katika njia iliyonyooka na
kuingia kwenye njia za upotovu. Kwani kwa hakika katika siku ya Malipo basi Allah
Subhanah wa Ta’ala atawatengenisha waliofanya Wema na waliofanaya Maovu na hivyo
hakutokua na kufaana kwa ndugu, jamaa au marafiki kama zinavyoendelea kuweka wazi
aya ambazo ni zenye kutilia mkazo kuhusiana na Nabi Ibrahim kua ni Mfano bora wa
Kuigwa kwa kusema:

‫ٱﻪﻠﻟُ ِﲟَﺎ ﺗَـ ْﻌ َﻤﻠُﻮ َن‬ ِ ‫﴿ﻟَﻦ ﺗَﻨ َﻔﻌ ُﻜﻢ أَرﺣﺎﻣ ُﻜﻢ وﻻَ أَوﻻَ ُد ُﻛﻢ ﻳـﻮم ٱﻟْ ِﻘﻴﺎﻣ ِﺔ ﻳـ ْﻔ‬
‫ﺼ ُﻞ ﺑَـْﻴـﻨَ ُﻜ ْﻢ َو ﱠ‬ َ َ َ َ َْ ْ ْ َ ْ ُ َ ْ ْ َ
�‫ﻳﻦ َﻣ َﻌﻪُ إِ ْذ ﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻟَِﻘ ْﻮِﻣ ِﻬ ْﻢ إِ ﱠ‬ ِ ‫ﺼﲑ ۞ﻗَ ْﺪ َﻛﺎﻧَﺖ ﻟَ ُﻜﻢ أُﺳﻮةٌ ﺣﺴﻨﺔٌ ِ ۤﰲ إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ وٱﻟﱠ‬
‫ﺬ‬ ِ‫ﺑ‬
َ ََ َ ْ َ َ َ َْ ْ ْ ٌ َ
453

ُ‫ٱﻪﻠﻟِ َﻛ َﻔْﺮَ� ﺑِ ُﻜ ْﻢ َوﺑَ َﺪا ﺑَـْﻴـﻨَـﻨَﺎ َوﺑَـْﻴـﻨَ ُﻜ ُﻢ ٱﻟْ َﻌ َﺪ َاوة‬


‫ون ﱠ‬ ِ ‫ءآؤاْ ِﻣْﻨ ُﻜﻢ وِﳑﱠﺎ ﺗَـﻌﺒ ُﺪو َن ِﻣﻦ د‬
ُ ُ ْ َ ْ ّ ُ ‫ﺑـَُﺮ‬
ِ ‫ﭑﻪﻠﻟِ وﺣ َﺪﻩ إِﻻﱠ ﻗَـﻮَل إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢِ ﻷَﺑِ ِﻴﻪَ ﻷ‬ ِ ِ
‫ﻚ َوَﻣﺂ‬ َ َ‫َﺳﺘَـ ْﻐﻔَﺮ ﱠن ﻟ‬ ْ َ َ ْ ْ ُ ْ َ ‫ﻀﺂءُ أَﺑَﺪاً َﺣ ﱠ ٰﱴ ﺗُـ ْﺆﻣﻨُﻮاْ ﺑ ﱠ‬ َ ‫َوٱﻟْﺒَـ ْﻐ‬
ٍ ِ‫۞ أَﻣﻠِﻚ ﻟَﻚ ِﻣﻦ ﱠ‬
ِ َ ‫ﻚ أَﻧَـﺒـﻨَﺎ وإِﻟَﻴ‬
ُ‫ﻚ ٱﻟْ َﻤﺼﲑ‬ ْ َ ْ َ ‫ﻚ ﺗَـ َﻮﱠﻛ ْﻠﻨَﺎ َوإِﻟَْﻴ‬ َ ‫ٱﻪﻠﻟ ِﻣﻦ َﺷ ْﻲء ﱠرﺑـﱠﻨَﺎ َﻋﻠَْﻴ‬ َ َ ُ ْ
‫ٱﳊَﻜِ ُﻴﻢ۞ ﻟََﻘ ْﺪ‬ ِ ِِ ِ
ْ ‫َﻧﺖ ٱﻟْ َﻌ ِﺰ ُﻳﺰ‬ َ ‫ﻚأ‬ َ ‫ﻳﻦ َﻛ َﻔُﺮواْ َوٱ ْﻏﻔْﺮ ﻟَﻨَﺎ َرﺑـﱠﻨَﺂ إِﻧﱠ‬
َ ‫َرﺑـﱠﻨَﺎ ﻻَ َْﲡ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ﻓْﺘـﻨَﺔً ﻟّﻠﱠﺬ‬
‫ٱﻵﺧَﺮ َوَﻣﻦ ﻳَـﺘَـ َﻮﱠل ﻓَِﺈ ﱠن‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ وٱﻟْﻴـﻮم‬ ِ ِ
َ ْ َ َ َ‫ُﺳ َﻮةٌ َﺣ َﺴﻨَﺔٌ ﻟّ َﻤﻦ َﻛﺎ َن ﻳَـْﺮ ُﺟﻮ ﱠ‬ ْ ‫َﻛﺎ َن ﻟَ ُﻜ ْﻢ ﻓﻴ ِﻬ ْﻢ أ‬
﴾‫ﻴﺪ‬ ُ ‫ﲎ ٱ ْﳊَ ِﻤ‬ ‫ٱﻪﻠﻟَ ُﻫ َﻮ ٱﻟْﻐَِ ﱡ‬ ‫ﱠ‬
Lan tanfaAAakum arhamukum wala awladukum yawma alqiyamati yafsilu
baynakum waAllahu bima taAAmaloona baseerun; Qad kanat lakum oswatun
hasanatun fee ibraheema waalladheena maAAahu idh qaloo liqawmihim inna
buraao minkum wamimma taAAbudoona min dooni Allahi kafarna bikum wabada
baynana wabaynakumu alAAadawatu waalbaghdhao abadan hatta tu/minoo
biAllahi wahdahu illa qawla ibraheema li-abeehi laastaghfiranna laka wama amliku
laka mina Allahi min shay-in rabbana AAalayka tawakkalna wa-ilayka anabna wa-
ilayka almaseeru, Rabbana la tajAAalna fitnatan lilladheena kafaroo waighfir lana
rabbana innaka anta alAAazeezu alhakeemu. Laqad kana lakum feehim oswatun
hasanatun liman kana yarjoo Allaha waalyawma al-akhira waman yatawalla fa-
inna Allaha huwa alghanniyyu alhameedu (Surat Al Mumtahina 60:3-6)

Tafsir: Kwani hawatokufaeni jamaa zenu wala watoto wenu katika siku ya Kiyama,
Kwani yeye Allah Subhanah wa Ta’ala atakutofautisheni baina yenu na Allah ni
mwenye kuona kila mnachokifanya. Kwa hakika kumekua na mfano bora wa kuigwa
nanyi kwa Ibrahim na wale waliokua pamoja nae pale waliposema kuwaambia watu
wao: ‘Kwa hakika sisi tupo huru kutokana nanyi, na kile mnachokiabudu zaidi ya
Allah, tumekukataeni, na baina yetu na nyinyi kuna uadui na chuki ya Milele, hadi
pale mtakapomuamini Allah.’ Isipokua kauli yake (Ibrahim) kwa baba yake: ‘Kwa
hakika mimi nitakuombea msamaha kwwa ajili yako. Lakini hata hivyo sina uwezo
wowote mbele ya Allah.’ ‘Ewe Mola wetu! Sisi tunakutegemea wewe pekee na kwako
wewe tunarudi kwa kutubu, na kwako wewe ndio marejeo yetu.’ ‘Ewe Mola wetu!
Usitujaalie Fitna kwa Makafiri. Na Tusamehe madhambi yetu, Ewe Mola wetu kwa
hakika wewe ni Mwenye Uwezo juu ya kila kitu na ni Mwingi wa Hikma.’ Bila ya
Shaka! Ndani yao mna Mfano bora wa kufuatwa nanyi. Kwa wale ambao ni wenye
kutarajia kurudi kwa Mola wao na siku ya Mwisho. Na yeyote yule atakaeupa mgongo,
454

basi kwa hakika Allah ni Tajiri asiehitaji chochote kutoka kwa yeyote, Sifa zote njema
anastahiki yeye peke yake.’

Hivyo, aya zinatuwekea wazi kua kuna hali ya sifa ya upekee tunapomzungumzia Nabii
Ibrahim Alayhi Salam na hivyo kututaka tumfuate yeye na wale waliomkubali katika
wakati wa kipindi cha uhai wake wakiwemo Sarah, Nabii Lut, Hajar, Nabii Ismail, Nabii
Is-haq na pia waliofuatia baada yake na waliofuatia baada yake kama kina Nabii Yaqub,
Nabii Yusuf n.k Na ingawa Nabii Ibrahim anamuwekea wazi baba yake kua hatoweza
kumfanyia chochote mbele ya Allah Subhanah wa Taála hata kwa kumuombea Dua,
lakini hapo hapo aya inatuwekea wazi sisi pia kua hatutakiwi kuwaombea Dua Makafiri
wala kushirikiana nao.

Kwani Makafiri ni maadui wa Allah Subhanah wa Ta’ala na ni Maadui wa Waumini, na


kila tunavyoshirikiana nao basi ndio hua tunazidi kujiangamiza kama tunavyoona kwa
Ndugu zetu wa Syria na Yemen wanavyoangamia kutokana na Ushirikiano wa nchi za
Kiarabu Saudia, Imarati, Misri, Jordan n.k wanaposhirikiana na nchi za Magharibi
ikiwemo Marekani, Uingereza, Israil n.k kuzivamia na kufanya uharibifu katika Ardhi
hizo za Kiislam.

Ambapo madhara yake ndio yanapelekea Mamilioni ya Wakimbizi, Wanawake wa


Kiislam kua wajane wengi, watoto Mayatima kua wengi na kufikia hali ya kua wengi
miongoni mwa Wanawake wa Kiislam kuingia katika mitihani ya kutakiwa kimapenzi
na kufikia kutoa hongo ya ngono ili wapate mahitaji yao ya kila siku ikiwemo vyakula,
nguo na misaada myengine katika kambi za Wakimbizi. Huu ni mtihani mkubwa kuliko
tunavyofikiria sisi kwa kusoma, ambao ni wenye kutokana na madhara ya kutofuata
kwetu Milat Ibrahima na kuachana na Sibgahata Allah.

Ama kuhusiana na maneno Rabbana la tajAAalna fitnatan lilladheena kafaroo


waighfir lana - Ewe Mola wetu! Usitujaalie Fitna kwa Makafiri. Na Tusamehe
madhambi yetu basi anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu Imam Qatadah
Ibn Diama al Sadusi kua ni yenye kumaanisha kua: ‘Ya Allah! Usituadhirishe kwa
kutuadhibu sisi mbele yao, na wala usituadhibu sisi ndani ya mikono yako.’ Ili
Makafiri wasiseme kua: ‘Kama hawa Waislam Dini yao ingekua ni ya kweli basi
wasingeadhibiwa’’

Lakini hapo hapo Allah Subhnaha wa Ta’ala anamalizia kutubainishia katika Sura hio
kuhusiana na watu aliotukataza tusifanye urafiki nao kwa kusema:
455

‫ٱﻪﻠﻟُ ﻗَ ِﺪ ٌﻳﺮ َو ﱠ‬
ُ‫ٱﻪﻠﻟ‬ ‫ﻳﻦ َﻋ َﺎدﻳْـﺘُﻢ ِّﻣْﻨـ ُﻬﻢ ﱠﻣ َﻮﱠد ًة َو ﱠ‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ أَن َﳚﻌﻞ ﺑـﻴـﻨ ُﻜﻢ وﺑـ ﱠ‬
َ ‫ﲔ ٱﻟﺬ‬َْ َ َ ْ َ َْ َ َ ْ ُ‫﴿ َﻋ َﺴﻰ ﱠ‬
﴾‫ﺣﻴﻢ‬ ِ ‫َﻏ ُﻔ‬
ٌ ‫ﻮر ﱠر‬
ٌ
AAasa Allahu an yajAAala baynakum wabayna alladheena AAadaytum minhum
mawaddatan waAllahu qadeerun waAllahu ghafoorun raheemun (Surat Al
Mumtahina 60:7)

Na mfano wa tukio hili ni wa lile jambo lililofanyika baada ya kutekwa kwa Mji wa
Makkah ambapo tunaona kua Abu Sufyan Radhi Allahu Anhu mara tu baada ya kusilimu
na kua Muislam basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alimchagua kua awe Gavana
wa Yemen. Na alikaa huko hadi wakati wa kifo cha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
Salam, akaamua kurudi Mjini Madina ambapo njiani akakutana na Mtu ambae aliritadi
baada ya kusikia kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam amefariki. Na Abu Sufyan
Radhi Allahu Anhu akapigana nae hadi akamuua na hivyo kua ni Muislam wa Mwanzo
kupigana na walioritadi.

Hivyo Waislam tunatakiwa kua ni wenye kumuangalia na kumfuata Nabii Ibrahim si


katika Millatahu – Mila zake tu lakini pia katika namna alivyokua akiishi katika maisha
yake. Kwani Waumini wa tangu enzi hizo hadi wa wakati wetu na watakaofuatia baada
yetu basi nao pia ni wenye kukumbana na mitihani kama waliyokumbana nayo
waliotangulia kabla yetu.

Siku moja Khalill Allah Ibrahim wakati alipokua na mifugo yake ambao ilikua ni mingi
sana yenye mchanganyiko wa Kondoo, Mbuzi na Ngamia basi Malaika wakamuona
akiwa katika harakati zake hizo za kucungnga wanyama wake, hivyo wakamuuliza Allah
Subhanah wa Ta’ala: ‘Ya Allah Subhanah wa Taa’ala, hakika ewe ulisema kua
Ibrahim ni Khallil wako, kwani Moyo wake haufikirii chochote ndani yake isipokua
wewe. Hivi jee hata katika wakati wa sasa hivi akiwa na Mifugo yake hua pia
anakufikiria wewe?’ Allah Subhanah wa Ta’ala akawaambia Malaika hao:
‘Nakuruhusuni mumjaribu kwa kumpa mtihani.’

Hivyo Malaika Jibril akashuka ardhini akaingia katika umbo la Ibn Adam na kumsalimia
Khallilu Allah Ibrahim kwa kumwambia: ‘Salaam Alaykum, hivi jee mifugo yote hii
inamilikiwa na wewe?’ Khallilu Allah akajibu: ‘Wa Alaykum Salaam! Mifugo yote hii
inamilikiwa na Mola wangu. Hivyo kama ukimtukuza Mola wangu kwa neno Moja
tu litakalokua ni lenye kumtukuza basi kwa hakika mie nitakupa robo tatu ya
mifugo hii ili iwe yako.’ Hivyo Malaika Jibril akasema: ‘Sub-Hana Allah!’ na baada ya
hapo Khallilu Allah Ibrahim akampa Malaika Jibril robo tatu ya Mifugo yake. Kisha
Khallil Allah akamwambia Jibril kama ukimsabihi tena basi nitakupa nusu ya mifugo
456

yangu. Malaika Jibril akasema tena ‘Sub-Hana Allah’ Khallil Allah akampa Malaika
Jibril nusu ya Mifugo yake, kisha akamwambia Malaika Jibril: ‘Kama unataka basi
msabiih tena mara ya tatu na nitakupa mifugo yote iliyobakia.’

Malaika Jibril akasema: ‘Sub-Hana Allah!’ Khallil Allah akamwambia Malaika Jibril:
‘Haya kweheri Mifugo hii yote ni yako wewe’, na kisha akaondoka peke yake. Malaika
Jibril akamwita Khallilu Allah na kumwambia: ‘Ya Khallilu Allah! Mimi ni Malaika
Jibril, sina shida ya Mifugo yako nilikua nakujaribu tu’. Khallailu Allah akasema:
‘Mie hainihusu wewe ni nani, na wala siichukui Mifugo hio tena kwa sababu sio
yangu tena Nimeitoa kwa ajili ya Mola wangu’.

Hapa Allah Subhanah wa Ta’ala akawaambia Malaika wake: ‘Jee mnamuonaje


Ibrahim? Hafai kua Khallil wangu au Anafaa?’ Malaika wakajibu: ‘Ama kweli
Ibrahim ni Khallilu Allah!’ Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘hivyo nami
naikubali mifugo niliyopewa na Khallil wangu, wachukueni na wapelekeni katika
Jabal Qaf na waacheni huko kwa ajili yangu.’

Anasema Imam Al Thalabi kua: ‘Sarah alifariki katika Ardhi ya Sham katika mji
Hebron katika maeneo ya Jababirah akiwa na umri wa miaka 127. Hajar amezikwa
Makkah katika Hijr. Baada ya Sarah kufariki basi Nabii Ibrahim alioa mwanamke
wa Kanaan aitwae Katurah Bint Yaqtan na alizaa nae watoto watano wa kiume
ambao ni Jokshan, Zimran, Madan, Madd, Ashiq na Washuq. Na kisha pia akaoa
mke wa Kiarabu aitwae Hajun Bint Uhayb ambapo alipata nae watoto wanne wa
kiume ambao ni: Kaysan, Faruq, Lutan na Nafis, hivyo ukiwajumuisha watoto wote
wa Nabii Ibrahim pamoja na Is-haq na Ismail basi wanakua watoto 11. Na Ismail
ndie mtoto mkubwa wa mwanzo.

Akamuwacha Ismail katika Ardhi ya Hijaz, Is-haq katika Ardhi ya Sham na


wengine akawatawanya katika maeneo mengine ambapo watoto hao wakahoji kwa
kusema: ‘Ewe Baba! Kwanini umemfanya Ismail kua ni mwenye kuishi karibu
nawe na Is-haq kua pamoja nawe lakini ukatufanya sisi kua ni wenye kusihi mbali
nawe?’ ambapo Nabii Ibrahim akasema: ‘Hivyo ndivyo nilivyoamrishwa’ kisha
Nabii Ibrahim akawafudisha moja kati ya Majina Matukufu ya Allah Subhanah wa
Taála kwa ajili ya kuomba Mvua.’

Hivyo tunapoiangalia ile aya isemayo:

ِِ ِ ِ ِ ِ ِ َ ‫﴿وﺎﺑرْﻛﻨَﺎ ﻋﻠَﻴ ِﻪ وﻋﻠَﻰ إِﺳﺤ‬


ٌ ِ‫ﺎق َوﻣﻦ ذُِّرﻳﱠﺘ ِﻬ َﻤﺎ ُْﳏﺴ ٌﻦ َوﻇَﺎﱂٌ ﻟّﻨَـ ْﻔﺴﻪ ُﻣﺒ‬
﴾‫ﲔ‬ َ ْ ٰ َ َ ْ َ َ ََ
457

Wabarakna AAalayhi waAAala ishaqa wamin dhurriyyatihima muhsinun


wadhalimun linafsihi mubeenun (Surat Saffat 37:113)

Tafsir: Na Tukambariki yeye na Is-haqa na kizazi chao kua cha wenye kufanya mema
na baadhi ni wenye kujidhulumu nafsi zao wazi wazi.

Basi inatuwekea wazi kua waliozungumziwa hapa ambao ni wenye kujidhulumu


kutokana na kizazi cha Nabii Ibrahim basi si Nabii Ismail na wala si Nabii Is-haq bali ni
kutokana na hivi vizazi vyengine vilivyouliza suali la kwanini wao wakawa wamewekwa
mbali na Nabii Ibrahim.

Ama kwa upande wa Nabii Is-haq basi kizazi chake kilitokana na ndoa yake yeye na
mwanamke aitwae Ribika na wakapata watoto wawili mapacha ambao ni Yaqub na Aysa.
Katika wakati wa kuzaliwa kwao watoto hawa basi kwanza alizaliwa Aysa na kisha
akafuatia Yaqub, ambae alikua amekishika kisigino cha Aysa. Hivyo Nabii Yaqub
akaitwa Yaqub kwa sababu kisigino kwa Lugha ya Kiarabu hua kinaitwa Aqb, na ingawa
watoto hawa walikua mapacha lakini kitabia walikua ni watu wawili tofauti kwani Yaqub
alikua mtulivu na Mpole na Aysa alikua ni Matata sana, hivyo baadae waligombana
baada ya Nabii Yaqub kumuwahi Aysa katika kuombewa Dua na baba yao ambae ni
Nabii Is-haq.

Hivyo Aysa akatangaza kutaka kumuua Yaqub, hivyo Yaqub ikambidi akimbie kuokoa
maisha yake na kukimbilia kwa Mjomba yake, katika kukimbia huko basi alikua
akikimbia usiku usiku huku katika wakati wa mchana alikua akijificha ili asionekane,
kutokana na kutembea huko katika wakati wa Usiku basi Ndio Allah Subhanah wa Taála
akampa jina la Israil linaotokana na neno Saraa bi Layl yaani mwenye kutembea Usiku.
Hivyo kizazi cha Nabii Yaqub kikawa kinaitwa Bani Israil.

Nabii Yaqub alioa wanawake wawili ambao ni watoto wa Mjomba wake waitwao Liah
na Rashel, katika kipindi hiki ilikua inaruhusiwa kuoa mabinti wawili ndugu kwa pamoja,
kwani katazo la kuoa mabinti wawili kwa pamoja kwa mara ya kwanza lilishushwa katika
wakati wa Nabii Musa Aálayhi Salam kupitia katika Tawrat. Hivyo Nabii Yaqub
alipomuoa Liah alizaa watoto wanne wafuatao: Rubil, Yahud (alietoa kizazi cha
Mayahudi), Shamun na Lawi. Na Rashel akapata watoto wawili ambao ni Nabii
Yusuf na Shadad au Benyamin.

Nabii Yaqub pia alikua na Suria wawili ambapo mmoja alikua akiitwa Zulfa na
mwengine alikua akiitwa Bilha. Ambapo Zulfa akapata watoto watatu ambao ni
Dan, Naftali na Rubulan. Na Bilha akapata watoto watatu ambao ni Jad, Yashjar
na Ashar.
458

Watoto hawa wa Nabii Yaqub yaani Bani Israil wote kwa ujumla ni 12 na ndio waliokua
wakijulikana pia kama ni Asbat kwani kwa lugha ya Kiarabu neno Asbat linamaanisha
Matawi mengi ya Mti mmoja. Jina ambalo limetajwa mara 5 katika Qur’an ikiwemo
katika aya ifuatayo:

ِ ‫ﭑﻪﻠﻟِ وﻣﺂ أُﻧْ ِﺰَل إِﻟَﻴـﻨَﺎ وﻣﺂ أُﻧ ِﺰَل إِ َ ٰﱃ إِﺑـﺮ ِاﻫﻴﻢ وإِ ْﲰ‬ ِ ۤ ُ‫﴿ﻗﻮﻟ‬
َ ‫ﻴﻞ َوإِ ْﺳ َﺤ‬
‫ﺎق‬ ‫ﺎﻋ‬
َ َ َ َ َْ ََ ْ ََ ‫ﱠ‬ ‫ﺑ‬ ‫ﱠﺎ‬
‫ﻨ‬ ‫آﻣ‬
َ ُ‫ا‬
ْ‫ﻮ‬
َ‫ﻴﺴ ٰﻰ َوَﻣﺎ أُوﺗِ َﻰ ٱﻟﻨﱠﺒِﻴﱡﻮ َن ِﻣﻦ ﱠرّﻬﺑِِ ْﻢ ﻻ‬
َ َ
ِ ‫ﺎط وﻣﺂ أُوﺗِﻰ ﻣﻮﺳﻰ و‬
‫ﻋ‬ ٰ َ ُ َ َ
ِ ‫وﻳـﻌ ُﻘﻮب وٱﻷَﺳﺒ‬
َ َْ َ َ ْ ََ
﴾‫َﺣ ٍﺪ ِّﻣْﻨـ ُﻬﻢ وَْﳓﻦ ﻟَﻪُ ُﻣﺴﻠِﻤﻮ َن‬ َ‫ﲔأ‬ َ ْ ‫ﻧـُ َﻔِّﺮ ُق ﺑَـ‬
ُ ْ ُ َْ
Qooloo amanna biAllahi wama onzila ilayna wama onzila ila ibraheema wa-
ismaAAeela wa-ishaqa wayaAAqooba waal-asbati wama ootiya moosa waAAeesa
wama ootiya alnnabiyyoona min rabbihim la nufarriqu bayna ahadin minhum
wanahnu lahu muslimoona (Surat Al Baqara 2:136)

Tafsir: Sema (Enyi Mlioamini): ‘Hakika sisi Tunamuamini Allah, na kile


tulichoshushiwa na kile alichoshushiwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haq, na Yaqub, na
Asbaat (Watoto 12 wa Nabii Yaqub) na kile walichoshushiwa Musa na Isa, na kile
walichoshushiwa Mitume kutoka kwa Mola wao. Na hatutofautishi chochote baina
yao, na kwake yeye tumejisalimisha.’

Ama kuhusiana na kifo cha Nabii Ibrahim basi Imam Ismail Abd Rahman Al Suddi
anasema kua: ‘Allah Subhanah wa Taála alipotaka kumchukua Roho yake basi siku
moja alitokea mtu Mzee ambae alikuja kwa Nabii Ibrahim, Nabii Ibrahim
akamkaribisha chakula, na alipokua akila chakula hicho basi alikua anakosea mara
mkono unaenda Puani, mara Jichoni kutokana na kutetemeka kwa mikono hio.
Nabii Ibrahim akamuuliza Mzee yule kua ana tatizo gani? Ambapo yule Mzee
akajibu kua ana tatizo la Uzee. Nabii Ibrahim akamuuliza kwani una umri wa
miaka mingapi? Ambapo yule Mzee alipojibu basi Nabii Ibrahim akafanya
mahesabu na kugundua kua yeye ni mdogo kwa yule Mzee kwa umri wa miaka
miwili.

Nabii Ibrahim akauliza: ‘Jee na mimi nitakua na hali kama hio nikifikia umri
wako?’ Nabii Ibrahim akaomba kwa Mola wake kua asimjaalie kua ni mwenye
kufikia Umri kama huo.

Siku moja wakati Nabii Ibrahim alipokua anarudi nyumbani kwake basi akakutana
na kijana mmoja mzuri sana mwenye kuvutia. Nabii Ibrahim akamuuliza yule
459

kijana jina lake baada ya kumsalimia. Yule kijana akajibu kwa kusema kua:
‘Hakika mimi ni Malakat al Mawt’ Nabii Ibrahim akajibu: ‘Mashaa Allah! Bila ya
shaka hakuna mtu yeyote yule atakaekataa kuchukuliwa Roho yake na Malaika
Mzuri kama unavyoonekana wewe’. Hapo Malakat Al Mawt akasema: ‘Ya
Khalillahu Allah! Wakati Allah Anapomtakia wema Mja wake basi hunituma mimi
nikiwa katika hali ya kupendeza kama hii, na wakati ambao anataka kumuadhibu
Mja wake basi hunituma mimi katika hali ya muonekano mwengine unaotisha’

Tukio hili linatufundisha mimi nawe kua tujihadhari na kujichunga kwa ajili ya
kumridhisha Mola wetu kabla ya hata hatujakumbana na Malakat ul Mawt.

Kisha Malakat al Mawt akaichukua Roho ya Nabii Ibrahim. Kipindi hiki Nabii
Ibrahim alikua na umri wa miaka 200 na pia kuna wasemao kua alikua na umri wa
miaka 195. Nabii Ibrahim alizikwa pembeni ya Kaburi la Sarah katika Ardhi ya
Hebron.

Na kuna wanaosema kua: Nabii Ibrahim aliishi kwa mda wa miaka miwili tu baada
ya kufariki Sarah, na hii ilikua ni miaka 23 baada ya kuzaliwa Nabii Is-haq. Nabii
Ibrahi aliumwa kwa siku 25 na katika mwezi 5 Muharram katika wakati wa Sala
ya Adhuhuri alifariki huku akiwa ni mtu alieishi kwa umri wa miaka 129.

Na pia kuna wasemao kua: Nabii Ibrahim alimuomba Allah Subhanah wa Ta’ala kwa
kusema: ‘Ya Rabb nakuomba ukishakaribia mda wangu wa kuchukuliwa Roho
yangu basi nijuulishe kabla ili nijitayarishe kwa ajili ya kifo’. Hivyo Allah Subhanah
wa Ta’ala akamkubalia maombi hayo, na kisha baada ya mda wa kuchukuliwa Roho
yake ulipowadia na Malakat ul Mawt basi akatokea Malakat ul Mawt kwa Nabii Ibrahim
na kumwambia kua umewadia wakati wa kuchukua Roho yake.

Nabii Ibrahima akamuuliza Malakat ul Mawt: ‘Hakika mda wangu wa kuchukuliwa


Roho haujafika bado.’ Malakat ul Mawt akajibu: ‘Kama haujafika mda wako basi
kwa hakika mimi nisingepata amrisho la kukufuata na nisingekuja kwa ajili yako.’

Hapo Allah Subhanah wa Ta’ala akamuuliza Nabii Ibrahim: ‘Ya Ibrahim! Hivi hizi
nywele nyeupe zimeanza kuota lini kwenye kichwa chako?’ Nabii Ibrahim akajibu:
‘Mwaka mmoja uliopita’ Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Ya Ibrahim
hizo nywele nyeupe ndio kwenye kichwa na kidevu chako ndio mjumbe wenyewe
wa kukutayarisha na kifo’.

Nabii Ibrahim alipoambiwa hivyo basi akamwambia Malakat ul Mawt: ‘Ya Malakat al
Mawt! Hivi jee wewe ushawahi kusikia kua Rafiki Kipenzi akiichukua Roho ya
Rafiki yake kipenzi?’
460

Hapa sasa akashuka Malaika Jibril na kusema: ‘Ya Khallil Allah! Anauliza Allah
Subhanah wa Taa’ala Jee tangu lini Rafiki kipenzi akakataa kukutana na Rafiki
yake Kipenzi?’ hivyo hapa Nabii Ibrahim akasema: ‘Kama ni hivyo basi chukueni
Roho yangu ikakutane na Allah Subhanah wa Ta’ala.’

Hivyo Roho ya Nabii Ibrahim ikatolewa na kupandishwa juu Mbinguni, ilipofika basi
Roho za Mitume na Manabii wote zikaifuata Roho yake na kuiuliza: ‘Jee Kifo kinauma
Kiasi gani maumivu yake?’ Nabii Ibrahim akasema: ‘Ni kama Mtu achukue
Msumeno kisha akukate kiunoni mwako mara 1000 na kisha achemshe Maji
yamoto akumwamgie kuanzia kichwani mwako mara 1000, na kisha Upigwe
Mapanga mara 1000 hivyo ndivyo nilivyohisi mimi maumivu yake. Na kama ikiwa
hayo ni maumivu ya mtu alie Rafiki wa Karibu wa Allah Subhnah wa Ta’ala jee hali
itakuaje kwa yule ambae ni adui yake?’

Amesema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qur’an kua:

ْ ‫ﺼﻠﱠ ٰﻰ۞ ﺑَ ْﻞ ﺗُـ ْﺆﺛُِﺮو َن‬


۞‫ٱﳊَﻴَﺎ َة ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ‬ ِ
َ َ‫ٱﺳ َﻢ َرﺑِّﻪ ﻓ‬
ْ ‫﴿ﻗَ ْﺪ أَﻓْـﻠَ َﺢ َﻣﻦ ﺗَـَﺰﱠﻛ ٰﻰ۞ َوذَ َﻛَﺮ‬
‫ﻒ إِﺑْـَﺮ ِاﻫ َﻴﻢ‬
ِ ‫ُوﱃ۞ ﺻﺤ‬
ُ ُ ٰ َ ‫ﺼ ُﺤﻒ ٱﻷ‬
ِ ‫ٱﻵﺧﺮةُ َﺧﻴـﺮ وأَﺑـ َﻘ ٰﻰ۞ إِ ﱠن َﻫـٰ َﺬا ﻟَِﻔﻰ ٱﻟ ﱡ‬
ْ َ ٌ ْ َ ‫َو‬
ِ
﴾‫ﻮﺳ ٰﻰ‬َ ‫َوُﻣ‬
Qad aflaha man tazakka; Wadhakara isma rabbihi fasalla; Bal tu/thiroona
alhayata alddunya; Waal-akhiratu khayrun waabqa; Inna hadha lafee alssuhufi al-
oola; Suhufi ibraheema wamoosa(Surat Al Aála 87:14-19)

Tafsir: Ama kwa hakika amefuzu yule anaejitakasa, Na akalikumbuka jina la Mola
wake na kisha akasali. Lakini nyinyi mnakumbatia maisha ya Dunia. Ijapokua maisha
ya akhera ni bora na yenye kudumu zaidi. Hakika haya yametajwa katika Suhufi
zilizotangulia, Suhufi za Ibrahim na Musa.

Ambapo tunapozungumzia Suhufi Ibrahima basi tunaona kua Allah Subhanah wa Taála
alimpa Nabii Ibrahim Sahifa (vitabu) 20 ambazo ndani yake mlikua mna miongoni mwa
wasia na hikma zifuatazo:

1-Enyi Wenye Mamlaka mliosimamishwa kwa ajili ya kufanyiwa Mitihani, hakika


mimi sikukusimamisheni ili mtumie utajiri wa mali zenu, bali nimekusimamisheni
ili muwasaidie masikini wanaoniabudu, na bila ya shaka mimi sikatai maombi yao
isipokua kwa wanaonishirikisha.
461

2-Ni wajib wa kila mtu mwenye ufahamu isipokua anapokua na udhuru


kujisimamia katika mambo manne: Anapokua anamuomba Mola wake.
Anapojihesabu Nafsi yake, juu ya mema yake na maovu yake. Anapofikira Neema
za Mola wake Juu yake. Na anapojitelekezea matamanio ya Nafsi yake katika njia
ya Halali, bila ya shaka hili jambo la nne ni muhimu zaidi kwa sababu linasimamia
utulivu wa Moyo wake.

3-Ni wajibu wa mtu mwenye ufahamu kujua hali za watu katika jamii yake, ili
aweze kuiboresha hali ya Nafsi yake. Ni wajibu wake kuulinda ulimi wake, kwani
anaeulinda ulimi wake hua ni mchache katika kauli zake na huzungumza kile tu
chenye manufaa kwa Nafsi yake.

4-Mtu mwenye ufahamu hua ni mwenye kutamani mambo matatu: Maisha mazuri
Duniani, Maisha Mema kesho Akhera na Starehe zilizo halali kwake.



SIFA KUU ZA NABII IBRAHIM.



1- Nabii Ibrahim alijaaliwa kuona Mamlaka ya Allah Subhanah wa Taála ya
Mbinguni na Ardhini na hivyo kua ni mwenye Yaqin zaid.
2- Nabii Ibrahim alipewa Maarifah ya kujua kua Allah Subhanah wa Taála ndie wa
Mwanzo na wa Mwisho hakuna mwengine zaidi yake, hakuna mwenye Utukufu
zaidi yake na Usafi wake unatokana na kutokua na mithili yake. Nabii Ibrahim
alipoona Nyota na Mwezi aliziona kua zinabadilika na hivyo kila chenye
kubadilika hua lazima kina aliekiumba.
3- Nabii Ibrahim alijaaliwa Ushujaa ambao unaonekana wazi katika kuwahoji
watu wake wakiwemo wazee wake na wenye Mamlaka katika jamii yake, na hili
linaonekana wazi kutokana na kuwavunja vunja Masanamu ya watu wa jamii
yake na hivyo kukabiliana na watu wake yeye peke yake.
4- Nabii Ibrahim alikua na sifa ya Ustahmilivu na mwenye kujiheshimu kama
alivyosema Allah Subhanah wa Taála kua alikua ni mwenye kumuomba Allah
Subhanah wa Taála mara kwa mara na daima ni mwenye kumuomba Allah
msaada.
5- Nabii Ibrahim alikua ni mwenye kupenda kutoa Sadaka na Mkarimu.
462

6- Nabii Ibrahim alikua ni mwenye kupenda na kuchukia kwa ajili ya Allah


Subhanah wa Taála na hivyo alijitenga na familia yake kwa ajili ya Mola wake.
7- Nabii Ibrahim alikua nimwenye kukataza Maovu na kuamrisha mema.
8- Nabii Ibrahim alikua ni mwenye kupinga Maovu kwa njia ya Wema pale
alipoamua kumuombea Dua baba yake baada ya yeye kumkaripia Nabii
Ibrahim na kufikia kutaka kumpiga mawe.
9- Nabii Ibrahim alikua ni mwenye kumtegemea Allah Subhanah wa Taála kwa
kikamilifu.
10-Nabii Ibrahim alikua ni mwenye kutaka kua na watu wema tu, kiasi ya kua
aliomba dua juu ya jambo hilo.
11-Nabii Ibrahim alipewa Mtihani wa kuangamizwa pale alipoingizwa ndani ya
Moto.
12-Nabii Ibrahim alipewa Mtihani wa kumchinja mtoto wake.
13-Nabii Ibrahim alipewa Mtihani wa kujaribiwa Mke wake Sarah na Mfalme wa
Misri.
14-Nabii Ibrahim alikua na Subra kubwa kutokana na maneno ya Sarah.
15-Nabii Ibrahim alikua ni mwenye kujitolea Nafsi yake katika Kumtii Mola wake.
16-Nabii Ibrahim alisafishwa kutokana na kutokua si Myahudi wala si Mkristo.
17-Nabii Ibrahim alikua ni mwenye kukubaliwa dua yake ya kukhuisha waliokufa.
18-Nabii Ibrahim alikua ni Muongofu.
19-Nabii Ibrahim alikua ni Mweye kufuatwa na Mitume wote waliotangulia baada
yake.
20-Nabii Ibrahim alikua ni Mtu wa mwanzo Kutahiriwa baada ya kujitahiri
mwenyewe.
21-Nabii Ibrahim alikua ni Mtu wa mwanzo kuanza kutumia kauli ya Biismika
Allahuma.

Tumeona historia ya Nabii Nuh, tumemalizana na historia ya Nabii Ibrahim na sasa hivi
tunataka kuingia katika historia ya Nabii Musa ambapo tunaona kua Allah Subhanah wa
Taála anatuwekea wazi katika aya zifuatazo kua:
463

‫ﻳﻦ َﳜْ َﺸ ْﻮ َن‬ ِ ‫﴿وﻟََﻘ ْﺪ آﺗَـﻴـﻨﺎ ﻣﻮﺳﻰ وﻫﺎرو َن ٱﻟْ ُﻔﺮﻗَﺎ َن و ِﺿﻴﺂء وِذ ْﻛﺮاً ﻟﱠْﻠﻤﺘ ِﱠﻘ ۞ ﱠ‬
َ ‫ﲔ ٱﻟﺬ‬ َ ُ ًََ َ ْ ُ َ َ ٰ َ ُ َْ َ
ِ ِ ِ ‫ﺐ وﻫﻢ ِﻣﻦ ٱﻟ ﱠﺴ‬ ِ ِ
َ ‫ﺎﻋﺔ ُﻣ ْﺸﻔ ُﻘﻮ َن ۞ َوَﻫـٰ َﺬا ذ ْﻛٌﺮ ﱡﻣﺒَ َﺎرٌك أ‬
ُ‫َﻧﺰﻟْﻨَﺎﻩُ أَﻓَﺄَﻧْـﺘُ ْﻢ ﻟَﻪ‬ َ َ ّ ْ ُ َ ‫َرﺑـﱠ ُﻬ ْﻢ ﺑﭑﻟْﻐَْﻴ‬
ِِ ِ ِ ِ ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ُﻣﻨﻜُﺮو َن ۞ َوﻟََﻘ ْﺪ آﺗَـْﻴـﻨَﺂ إِﺑْـَﺮاﻫ َﻴﻢ ُر ْﺷ َﺪﻩُ ﻣﻦ ﻗَـْﺒ ُﻞ َوُﻛﻨﱠﺎ ﺑِﻪ َﻋﺎﻟﻤ‬
Walaqad atayna moosa waharoona alfurqana wadhiyaan wadhikran
lilmuttaqeena; Alladheena yakhshawna rabbahum bialghaybi wahum mina
alssaAAati mushfiqoona; Wahadha dhikrun mubarakun anzalnahu afaantum lahu
munkiroona; Walaqad atayna ibraheema rushdahu min qablu wakunna bihi
AAalimeena (Surat Al Anbiyah 21:48-51)

Tafsir: Na kwa Hakika tulimpa Musa na Harun (Furqan) Muongozo na mwangaza


ung’arao na ukumbusho kwa wenye Taqwa, Wale ambao wanaomuogopa Mola wao
bila ya hata kumuona huku wakiwa wanaogopa wakati wa Kiama utakapofika, Na bila
ya shaka huu ni Ukumbusho wenye barka tulio kushushieni, Jee mtadhubutu
kuukanusha? Na kwa hakika tulimpa Ibrahim uongofu wake hapo kabla, kwani
tulikua tukijua juu yake.

Anasema Allamah Sayyid Abu’l Ala Mawdudi juu ya aya hizi kua: Aya zinatuainishia
kua Mitume wote ni Ibn Adam, na wote wametumwa kwa Ibn Adam kwa lengo
Moja, na kua Allah Subhanah wa Taála amewachukulia Mtume wake katika
Upekee Maalum kutokana na Mitihani waliyokumbana nayo katika nyakati zao
tofauti za uhai wao, kwa kufikwa na mitihani yao wenyewe kwa wenyewe wao kama
Ibn Adam na pia kufikwa na mitihani iliyosababishwa na Ibn Adam wenzao yaani
maadui zao. Lakini hata hivyo Allah Subhanah wa Taála hakuwaacha mkono bali
alikua nao kwa kuwaingiza katika Rehma na Neema zake, kuwapa misaada yake
na kuwakubalia dua zao. Na bila ya shaka ingawa Mitume walisaidiwa na Allah
Subhanah wa Taála wakaingizwa kwenye Rehma zake na kufaidika na Neema zake
nyingi lakini Mitume hawa hawana sifa za kimungu kwani wao ni Ibn Adam, kama
walivyo Ibn Adam wengine.

Aya zimamalizia na maneno Walaqad atayna ibraheema rushdahu min qablu wakunna
bihi AAalimeena yaani Na kwa hakika tulimpa Ibrahim uongofu wake hapo kabla,
kwani tulikua tukijua juu yake. Maneno ambayo ingawa hapo awali tulisema kua
kulingana na mtizamo wa Qatadah na Mujahid juu ya maana ya Min Qabl – yaani Hapo
Kabla iliyotumika hapa katika aya hii ya Al Anbiyah 21:51 kua yanamaanisha ‘Hapo
kabla yaani katika kipindi cha utoto wake’.
464

Lakini kwa upande wa Mujaddid ud Din Sultan al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al
Razi basi yeye anasema juu ya kusudio la Min Qabl lililotumika hapa kua linamaanisha:
‘Tulimpa Ibrahim Uongofu kabla ya Nabii Musa’ na maana hii ndio inayotufungia
kisa cha Khalilu Allah Nabii Ibrahim na kutufungulia kisa cha Kallimu Allah Nabii Musa.


465

‫ﻣﻮﺳﻰ ﻛﺎﻟﻴﻤﻮ ﺍﷲ‬



466

KALLIMU ALLAH MUSA IBN AMRAN AÁLAYHI SALATU WA SALAAM




﴾ً‫ﻮﺳ ٰﻰ إِﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن ﳐُْﻠَﺼﺎً وَﻛﺎ َن ر ُﺳﻮﻻً ﻧﱠﺒِﻴّﺎ‬ ِ ِ ِ


َ َ َ ‫﴿ َوٱذْ ُﻛْﺮ ﰱ ٱﻟْﻜﺘَﺎب ُﻣ‬
Waodhkur fee alkitabi Musa innahu kana mukhlissan wa kana Rasulan Nabiyyan
(Surat Maryam 19:51)

Tafsir: Na ametajwa katika Kitabu Musa. Hakika yeye ni aliechaguliwa na akawa


Rasul na Nabii.

Tunapokiangalia kisa cha Nabii Musa basi tunaona kua kwa mara ya kwanza kimetajwa
ndani ya Qur’an katika Sura ya 20 ambayo ni Surat Ta-Ha. Hii ni Sura iliyoteremshwa
katika Mji wa Makkah katika kipindi cha mwanzo cha Uislam yaani kipidni cha Mitihani
kabla ya Waislam kufanya Hijra ya mwanzo kuelekea Uhabeshi au Ethiopia, hii ni Sura
ambayo inaenda sambamba na kuteremshwa kwa Surat Maryam, ambapo tunaona pia
kua Surat Ta-Ha iliteremshwa kabla ya kusilimu kwa Sayyidna Umar Ibn Al Khattab
Radhi Allahu Anhu.

Kwani Sayyidna Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu aliamka asubuhi na kuamua
kua imetosha kwa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kua ni mwenye
kusababisha mgawanyiko baina ya ndugu na ndugu wa Mji wa Makkah kwa kueneza
ujumbe aliokuja nao. Hivyo bora amalizane na fitna hio kwa kuukata mzizi mkuu wa
fitna ambao ni Nabii Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam. Hivyo akachukua Upanga
wake na kuelekea kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam. Alipokua njiani
akakutana na Nuaim Ibn Abd Allah ambae alimuuliza anaharakia wapi? Umar Ibn Al
Khattab Radhi Allahu Anhu alipomjibu basi Nuaim Ibn Abd Allah akasema: ‘Kama
unataka kufanya hivyo basi kwanza inabidi ujue kua Dada yako na Mume wake
tayari nao wameshaungana na Muhammad’

Hapa sasa Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu A’nhu akaingiwa na hasira zaidi na hivyo
akaakhirisha kuenda kwa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na kuamua kua
bora kwanza akamshughulikie Dada yake kisha ndio aende kwa Nabii Muhammad
Salallahu A’layhi wa Salam. Alipofika kwa Dada yake huyo ambae alikua anaitwa
Fatima Bint Al Khattab Radhi Allahu A’nha, basi akawasikia Fatima Bint Al Khattab
Radhi Allahu A’nha na mumewe ambae ni Said Ibn Zaid Radhi Allahu A’nhu wakiwa
wanasoma Maandiko aliyokuja nayo Khabbab Ibn Aratt Al Tamim Al Yamani Radhi
Allahu A’nhu. Mara baada ya kuingia basi Fatima Bint Al Khattab Radhi Allahu A’nha
467

akayaficha haraka sana Maandiko hayo na Khabbab Ibn Aratt Al Tamim Al Yamani
Radhi Allahu A’nhu akakimbilia kujificha haraka sana.

Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu akaanza kuwahoji juu ya kile walichokua
wakikisoma, lakini nao wakakaa kimya, hapo Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu A’nhu
akamkamata Said Ibn Zaid Radhi Allahu Anhu na kuanza kumkunja kwa nguvu, ambapo
Fatima Bint Al Khattab Radhi Allahu Anha nae akaingilia kati kumchomoa Mumewe
kutoka katika mikono ya Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu A’nhu na kutokana na
purukushani hizo basi Fatima Bint Al Khattab Radhi Allahu A’nha akaanguka chini na
kujeruhiwa. Baada ya kujeruhiwa huko basi Fatima Bint al Khattab Radhi Allahu A’nha
na Said Ibn Zaid Radhi Allahu A’nhu wakatoa kile walichokua wakikisoma na kusema:
‘Hakika sisi tumeingia katika Uislam hivyo fanya utakalofanya. Ewe Umar kwani
sisi hatutoachana na Imani yetu.’

Akiwa bado amejawa na hasira basi Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu A’nhu
akamuangalia usoni dada yake kutaka kufahamu ujasiri aliokua nao umetokea wapi,
lakini badala yake akaona kua damu inachumruzika usoni kutokana na jeraha alilolipata,
huruma ikamuingia Umar Ibn al Khattab Radhi Allahu A’nhu kutokana na kuona damu
hio kwenye uso wa Dada yake kipenzi. Hivyo akamwambia Dada yake huyo: ‘Tafadhali
nionesheni hicho mlichokua mkikisoma!’

Fatima Bint al Khattab Radhi Allahu A’nha akamwambia Umar Ibn Al Khattab Radhi
Allahu A’nhu: ‘Kula kiapo kwanza kua hutoichana pale tutakapokuonesha!’ baada
ya kuoneshwa basi Umar Ibn Al Khattab akataka kuigusa sehemu yaliyoandikiwa
maandiko hayo lakini hat ahivyo Fatima Bint Al Khattab akasema: ‘Hii huwzi kuigusa
mpaka uwe Tohara hivyo inabidi ukakogoe kwanza uwe msafi kisha ndio
tutakuruhusu kuyagusa maandiko hayo’

Hapa Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu A’nhu akaona haya masharti yameshakua
mengi, lakini kwa kua anataka kukiona kitu hicho chenye masharti mengi juu yake basi
akakubali kutii masharti hayo na moja kwa moja akaenda kukoga na kisha akarudi kwa
Dada yake.

Alipofika mbele ya Fatima Bint Al Khattab Radhi Allahu A’nha basi akapewa Maandiko
hayo na kuanza kuyasoma, na akaona kua yanaanza kwa kusema:

‫ﻚ ٱﻟْ ُﻘْﺮآ َن ﻟِﺘَ ْﺸ َﻘ ٰﻰ۞ إِﻻﱠ‬ ِ‫﴿ﺑِﺴ ِﻢ ﱠ‬


َ ‫اﻪﻠﻟ ٱﻟﱠﺮ ْﲪـٰ ِﻦ ٱﻟﱠﺮِﺣﻴ ِﻢ ۞ ﻃﻪ ۞ َﻣﺂ أَﻧَـَﺰﻟْﻨَﺎ َﻋﻠَْﻴ‬ ْ
‫ات ٱﻟْﻌُﻠَﻰ۞ ٱﻟﱠﺮ ْﲪَـٰ ُﻦ َﻋﻠَﻰ‬ ِ ‫ﺗَ ْﺬﻛِﺮًة ﻟِّﻤﻦ َﳜْ َﺸﻰ۞ ﺗَﻨ ِﺰﻳﻼً ِّﳑﱠﻦ ﺧﻠَﻖ ٱﻷَرض وٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬
ََ ََ ْ َ ْ ٰ َ َ
468

‫ﺖ‬ ِ ‫ٱﻟْﻌﺮ ِش ٱﺳﺘَـﻮ ٰى ۞ ﻟَﻪ ﻣﺎ ِﰱ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬


ِ ‫ات َوَﻣﺎ ِﰱ ٱﻷ َْر‬
َ ‫ض َوَﻣﺎ ﺑَـْﻴـﻨَـ ُﻬ َﻤﺎ َوَﻣﺎ َْﲢ‬ ََ َُ َ ْ َْ
ۤ ِ ‫ٱﻟﺜـﱠﺮ ٰى۞ وإِن َْﲡﻬﺮ ﺑِﭑﻟْ َﻘﻮِل ﻓَِﺈﻧﱠﻪ ﻳـﻌﻠَﻢ‬
ُ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻻ إِﻟَـٰﻪَ إِﻻﱠ ُﻫ َﻮ ﻟَﻪ‬
‫َﺧ َﻔﻰ۞ ﱠ‬ ْ ‫ٱﻟﺴﱠﺮ َوأ‬
ّ ُ َْ ُ ْ َْ َ َ
﴾‫ٱﳊُﺴ َ ٰﲎ‬
ْ ْ ُ‫َﲰَﺂء‬
ْ ‫ٱﻷ‬
Bismi Allahi alRrahmani alRraheemi; Ta-Ha; Ma anzalna AAalayka alqur-ana
litashqa; Illa tadhkiratan liman yakhsha; Tanzeelan mimman khalaqa al-ardha
waalssamawati alAAula; Alrrahmanu AAala alAAarshi istawa; Lahu ma fee
alssamawati wama fee al-Ardhi wama baynahuma wama tahta alththara; Wa-in
tajhar bialqawli fa-innahu yaAAlamu alssirra waakhfa; Allahu la ilaha illa huwa
lahu al-asmao alhusna (Surat Ta-Ha 20:1-8)

Tafsir: Kwa jina la Allah mwingi wa Rehma na mwingi wa Huruma; Ta-Ha, Kwa
Hatukuiteremsha hii Qur’an kwa ajili ya kukuingiza katika ugumu (wa mambo yako),
Ila huu ni ukumbusho kwa wenye kua na khofu. Imeteremshwa kutoka kwa Muumba
wa Ardhi na Mbingu zilizo juu. Mwingi wa Rehma kwenye Arshi yupo. Ni vyake
vilivyomo Mbinguni na Ardhini na baina yake na vilivyomo chini ya udongo wake. Na
hata kama wewe (Muhammad) utanyanyua sauti yako basi kwa hakika yeye, anajua
yaliyo ya siri na yale ambayo yamefichikana zaid. Hakuna Mungu isipokua yeye. Na
kwake yeye ndio kwenye umiliki wa Majina Bora.

Baada ya kusoma aya hizo za Surat Ta-Ha basi Moyo na Ufahamu wa Umar Ibn Al
Khattab Radhi Allahu A’anhu ulikua kama uliopigwa na dharuba moja kali sana ukapata
mshtuko na akajihisi kua ni mwenye kunyong’onyea na kuishiwa na nguvu, ujababari
wake wote ukatoweka,yaani alikua kama mtu amabe alikua kwenye kiza maisha yake
yote na kamwe hakuwahi kufikiria kua kuna rangi nyengine zaidi ya weusi wa kiza hicho,
lakini ghafla moja maneno haya ya Surat Ta-Ha yamemuwashia taa yenye Nuru kubwa
sana na hivyo akawa na ni mwenye kupigwa na bumbuwazi kama mnyama anaewindwa
usiku kizani halafu ghalfa akawashiwa taa kali sana za Spot Light za Kuwindia. Na hivyo
Umar Ibn Al Khattab akajisikia akisema: ‘Hakika Sijawahi kuona maneno Bora kama
haya!’.

Hapo Khabbab Ibn Aratt Al Tamim Al Yamani Radhi Allahu A’nhu akajitokeza kutoka
katika sehemu aliyokua amejificha na kusema: ‘Wallahi! Kwa hakika mimi nilikua na
mategemeo makubwa zaidi Allah! atanufaika zaidi kutokana na jitihada zako
katika kueneza ujumbe wake. Kwani jana nilimsikia Muhammad Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam akiomba dua kwa kusema: ‘Ewe Mola wangu! Mjaalie
469

Abu Hakam Ibn Al Hisham (Abu Jahal) au Umar Ibn Al Khattab kua ni Muungaji
mkono wa Uislam’ Hivyo ya Umar! Muelekee Allah! Mueleke Allah!’

Maneno haya yalimuathiri sana Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu kiasi ya kua
hapo hapo akaongozana na Khabbab Ibn Aratt Al Tamim Al Yamani Radhi Allahu Anhu
hadi kwa Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam na kuigia katika Dini ya Kiislam.
Tukio hili la kusilimu kwa Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu lilitokea mara tu
baada ya Hijra ya kwanza ya Waislamu kuhamia Uhabeshi.

Tunapoziangalia aya hizo basi tunaona kua aya ya tano imetumia neno Istawa pale
iliposema: Alrrahmanu AAala alAAarshi Istawa; yaani Mwingi wa Rehma kwenye Arshi
Istawa. Ambapo neno Istawa ni lenye kutokana na neno Sawiya ambalo kwa lugha ya
Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Kua sawa, Kumaliza, Kukamilisha, Kuendana kama
inavyotakiwa, Kukifanya kitu au kukiweka kama inavyotakiwa kiwe. Hivyo neno Istawa
maana yake hua ni Kuanzisha kitu, Kua na Msimamo juu ya Kitu fulani, Kukielekea Kitu
au Kukaa juu yake.

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kuhusiana na Istawa
Ala Al Arsh kua: ‘Hapa haitakiwi kuchukuliwa kua yupo amekaa na hii ni kwa
sababu tatu zifuatazo: Kwanza Kulikua kuna wakati ambao hakukua na Arshi hadi
pale Allah Subhnah wa Ta’ala alipoiumba Arshi hio. Pili Dunia ni duara, hivyo kile
kilicho juu hua ni kiliopo chini kwa wengine, hivyo kutokana na maumbile hayo
basi Arshi inabidi iwe katika hali ya muelekeo fulani, lakini Allah Subhanah wa
Ta’ala hayuko katika Muelekeo wa yeyote yule. Tatu ni kua amesema Allah
Subhanah wa Ta’ala kua:

﴾ٌ‫ﻚ ﻓَـﻮﻗَـ ُﻬﻢ ﻳَـﻮَﻣﺌِ ٍﺬ َﲦَﺎﻧِﻴَﺔ‬ ِ‫ش رﺑ‬ ِ ‫ﻚ ﻋﻠَﻰ أَرﺟﺂﺋِﻬﺂ وَﳛ‬ ﴿
ْ ْ ْ َ ْ ُ ْ َ َ َ ْ ٰ َ ُ َ‫َوٱﻟْ َﻤﻠ‬
َ ّ َ ‫ﺮ‬‫ﻋ‬َ ‫ﻞ‬ ‫ﻤ‬
Waalmalaku AAala arja-iha wayahmilu AAarsha rabbika fawqahum yawma-ithin
thamaniyatun’ (Surat Al Haqqah 69:17)

Tafsir: Na Malaika watakua pembeni yake, na wataibeba Arshi ya Mola wako juu siku
hio ni wanane.

Hivyo Malaika wanane wataibeba Arshi katika siku hio na bila ya shaka alieumbwa
hawezi Kumbeba Muumbaji. Hivyo mtizamo wa kua juu ya Arshi inabidi uwekwe kando.


470

SURAT TA-HA, HARFU MUQATTAA’AT NA KISA CHA NABII MUSA.


Neno MuqattaA’at ni neno lililotokana na neno Qata’a ambalo kwa Lugha ya Kiarabu
hua linamaanisha Kukata, Kutengenisha, Kugawa, Kutofautisha. Hivyo Harfu
MuqattaA’at hua inamaanisha herufi za Lugha ya Kiarabu ambazo zinapoandikwa na
zinaposomwa hua zinasomwa kwa kutengenishwa kwa mfano neno Ta-Ha ambalo ndio
lililotoa jina la Sura ya 20 iliyomo ndani ya Qur’an, herufi hizi kwa baadhi pia hua
wanaziita kua ni Huruf al Mutafarriqa yaani Herufi zilizotenganika.

Ufafanuzi wa maana ya Neno Ta-Ha: Ingawa kuna Wanazuoni wasemao kua neno Ta-
Ha ni miongoni mwa yale maneno yanayojumuishwa katika Harfu MuqattaA’at (Harfu
zilizokatwa au zilizofupishwa) ambazo hua hakuna anaejua maana yake isipokua
mwenyewe Allah Subhanah wa Taála. Lakini kwa upande wa Mujaddid ad Din Sultan
Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi amesema kua: ‘Haiwezekani kua Allah
Subhanah wa Taála, aingize kitu ndani ya Kitabu chake Qur’an ambacho sisi
hatutokifaham maana yake. Na kwa sababu yeye Allah Subhanah wa Taála ndie
alietuamrisha sisi kukitafakkar kitabu chake kwa lengo la kutupa uongofu
kutokana nacho. Hivyo basi lengo hili la kuitafakkari Qur’an halitoweza kufikiwa
kama ikiwa hatutoifaham maana yake, kwani lengo hili huweza kufikiwa pale tu
baada ya kufaham maana yake. (Mafatih al Ghayb, Tafsir al Kabir)’

Baadhi ya wenye kujua wamesema kua Harfu hizo MuqaattaAt zinamaanisha:

Alif (‫)ا‬: Inayowakilisha neno Anā (‫أﻧﺎ‬, Mimi) au neno Allah ‫ﷲ‬.
Hā (‫)ه‬: Inayowakilisha neno Al-Hādī (‫اﻟﮭﺎدي‬, Muongozi) Inayowakilisha neno Huwa
(‫ھﻮ‬Yeye).
Ḥā (‫)ح‬: Inayowakilisha neno Al-Ḥamīd (‫اﻟﺤﻤﯿﺪ‬, Kushukuriwa).
Ṭā (‫)ط‬: Inayowakilisha neno (Ewe).
Yā (‫)ي‬: Inayowakilisha neno (Ewe) au Yaqin ‫ﯾﻘﯿﻦ‬
Kāf (‫)ك‬: Inayowakilisha neno Al-Kāfī (‫ﻛﺎﻓﻲ‬, Anaetosheleza).
Lām (‫)ل‬: Inayowakilisha neno Allāh (‫ﷲ‬, Herufi ya pili katika Neno Allah) au (Latif
‫)اﻟﺘﻒ‬
Mīm (‫)م‬: Inayowakilisha neno Al-ʿAlīm (‫اﻟﻌﻠﯿﻢ‬, Herufi ya mwisho ya neno Alim) au
inayowakilisha neno Al-Majīd (‫اﻟﻤﺠﯿﺪ‬, Mshindi).
Nūn (‫)ن‬: Inayowakilisha neno Al-Qalam (Inayowakilisha neno "Kalamu au Peni") au
(Nur‫) ﻧﺮ‬
Sīn (‫)س‬: Inayowakilisha neno As-Samī' (‫اﻟﺴﻤﯿﻊ‬, Mwenye Kusikia).
A’in (‫)ع‬: Inayowakilisha neno Al-ʿAlīm (‫اﻟﻌﻠﯿﻢ‬, Mwenye Kujua).
471

Ṣād (‫)ص‬: Inayowakilisha neno As-Ṣādiq (‫اﻟﺼﺎدق‬, Mkweli).


Qāf (‫)ق‬: Inayowakilisha neno Al-Qādir (‫اﻟﻘﺎدر‬, Mwenye Kukadiria).
Rā (‫)ر‬: Inayowakilisha neno Al Raa (Mwenye Kuona‫ ﺑﺼﯿﺮ‬/ ‫ ﯾﺮى‬/ ‫ رؤﯾﺎ‬/ ‫ رأى‬/ ‫)راﺋﻲ‬.

Qurán ina Surah 29 zilizoanzia na Huruf MuqattaA’at ambapo 3 kati yao zina herufi
1, 9 kati yao zina herufi 2, 13 kati yao ina herufi 3, 2 kati yao zina herufi 4 na 2 zina
herufi 5, Sura hizo ni:

Nambar Namba ya Surah Jina la Sura Huruf-a-MuqattaA’at


i 1 38 Surat Saad ‫ص‬ ٓ Saad
2 50 Surat Qaaf ٓ‫ ق‬Qaaf
3 68 Surat Al Qalam ٓ‫ ن‬Nun
4 40 Surat Al Ghafir ‫ ﺣ ٓﻢ‬Ha Mim
5 41 Surat Al Fusilaat ‫ ﺣ ٓﻢ‬Ha Mim
6 43 Surat Az Zukhruf ‫ ﺣ ٓﻢ‬Ha Mim
7 44 Surat Ad Dukhan ‫ ﺣ ٓﻢ‬Ha Mim
8 45 Surat Al Jathiyyah ‫ ﺣ ٓﻢ‬Ha Mim
9 46 Surat Al Ahqaaf ‫ ﺣ ٓﻢ‬Ha Mim
10 20 Surat Ta-Ha ‫ طﮫ‬Ta-Ha
11 27 Surat An Naml ‫طﺲ‬ ٓ Ta Sin
12 36 Sura Yasin ‫ﯾﺲ‬ ٓ Ya-Sin
13 10 Surat Yunus ‫ اﻟﺮ‬Alif Lam Ra
14 11 Surat Hud ‫ اﻟﺮ‬Alif Lam Ra
15 12 Surat Yusuf ‫ اﻟﺮ‬Alif Lam Ra
16 14 Surat Ibrahim ‫ اﻟﺮ‬Alif Lam Ra
17 15 Surat Al Hijr ‫ اﻟﺮ‬Alif Lam Ra
19 29 Surat Al Anqabut ‫ اﻟ ٓﻢ‬Alif Lam Mim
20 30 Surat Ar Rum ‫ اﻟ ٓﻢ‬Alif Lam Mim
21 31 Surat Luqman ‫ اﻟ ٓﻢ‬Alif Lam Mim
22 32 Surat As Sajda ‫ اﻟ ٓﻢ‬Alif Lam Mim
23 2 Surat Al Baqara ‫ اﻟﻢ‬Alif Lam Mim
24 3 Surat Al Imran ‫ اﻟﻢ‬Alif Lam Mim
18 26 Surat Ash Shuara ۤ‫طﺴﻢ‬ ۤ Taa Sin Mim
25 28 Surat Al Qasas ‫ ط ٓﺴ ٓﻢ‬Taa Sin Mim
26 7 Surat Al Araf ‫ﺺ‬ ٓ ‫ اﻟ ٓﻤ‬Alif Lam Mim
27 13 Surat Rad ‫ﺮ‬S‫اﻟ ٓﻤ‬d Alif Lam Mim
28 19 Surat Maryam ‫ﺺ‬ ٓ ‫ ٓﻛﮭﯿ ٓﻌ‬Kaf Ha Ya
29 42 Surat Ash Shuraa Aٓ‫ ٓﻢ ٓﻋ ٓﺴﻖ‬S‫ ﺣ‬Ha d Mim
A S K f
Tunapoangalia Harfu MuqattaAat kulingana na mitizamo ya Wanazuoni wenye Ilm ya
Tasawwuf katika Fani ya Ruhaniyya basi wao wanasema kua Harfu hizo ambazo ni zipo
mwanzo mwa sura 19 tulizoziangalia hapo juu kua zimezigawa harfu za lugha ya Kiarabu
nusu kwa nusu, kwani hizo zinaitwa Al Huruf Al Nuranniyah (Yaani Herufi zenye sifa
472

ya kua na Nuru) ambazo ziko 14. Na Herufi zilizobakia hua zinaitwa Al Huruf al
Dhalamiyyah ambazo nazo zimegawika sehemu mbili.

Sehemu ya kwanza ni yenye herufi 7 zenye sifa ya darja ya juu na sehemu ya pili ni zenye
darja ya chini. Herufi hizi hua zina athari yake kinguvu, ambapo katika Surat Al Fatiha
tunaona ina herufi zote hizo herufi 7 zenye darja ya chini ambazo hujulikana kama
Sawaqit al Fatihah.

Herufi hizo ni zenye kunasibishwa na Majina Matukufu ya Allah Subhanah wa Taála na


hivyo kua ni zenye kufanyiwa Dhikr kila moja katika siku yake kwa mpango ufuatao:

‫ ف‬Fa’- Al Fardan lenye kumaanisha Mwenye Upekee. Ambalo ni jina la Dhikr ya siku
ya Jumaatatu.
‫ ج‬Jim – Al Jabbar lenye kumaanisha Mwenye Nguvu na Ujabari wa kipekee ambalo ni
jina la Dhikr ya siku ya Jumanne.
‫ ش‬Shin – Al Shahid lenye kumaanisha Mwenye Kushuhudia kila kitu ambalo ni jina la
Dhikr ya siku ya Jumatano.
‫ ث‬Tha’- Al Thabit lenye kumaanisha Mwenye Uthabiti wa Kipekee ambalo ni jina la
Dhikr ya siku ya Alkhamis.
‫ ظ‬Dha – Al Dhahir lenye kumaanisha Mwenye Kuonekana dhahir kwa dalili zake
ambalo ni jina la Dhikr ya siku ya Ijumaa.
‫ خ‬Kha’ – Al Khabbir lenye kumaanisha Mwenye Habari juu ya Kila kitu ambalo ni jina
la Dhikr ya siku ya Jumamosi.
‫ ز‬Zay – Al Zakiy lenye kumaanisha Mwenye Utukufu wa Juu kabisa ambalo ni jina la
Dhikr ya siku ya Jumapili.

Ama kwa upande wa Dhu Nun Al Misri basi yeye anasema kua: ‘Majina Matukufu ya
Allah Subhanah wa Ta’ala, ni mharakisho wa dua ambayo ikiombwa kupitia katika
Majina hayo basi Dua hio hua ni yenye Kujibiwa Haraka. Na ndani yake mna
Herufi 7 na katika Ummu ul Kitaab yaani Surah Al Fatiha ambayo ni Sura yenye
Aya 7 basi herufi zote za Kiarabu zimo katika aya isipokua ‫ث‬Tha’ (500), ‫ ج‬Jim (3),
‫ خ‬Kha’ (600), ‫ ز‬Zal (7),‫ ش‬Shin (300), ‫ ظ‬Dha’ (900),‫ ف‬Fa’ (80) ’

Ama katika kitabu cha Manbah Usul Al Hikma basi Imam Al Sanusi mara kadhaa
amekua akitumia herufi hizo katika Dua zake kwa kuanzia na neno Wa Bi Haqqi ‫ث‬Tha’
(500), ‫ ج‬Jim (3), ‫ خ‬Kha’ (600), ‫ ز‬Zal (7),‫ ش‬Shin (300), ‫ ظ‬Dha’ (900),‫ ف‬Fa’ (80) .

Kwa upande wa Shaykh Al Akbar Imam Abu Bakr Ibn Al Arabi basi yeye anasema kua:
‘Inabidi Mjue Harfu Muqataa’at zote, zilizoanza mwanzoni mwa Sura za Qur’an ni
majina ya Malaika na nimezitaja katika baadhi ya matukio, ambapo kamwa
haijawahi kutokea kwangu kuzitumia bila ya kutokea Malaika ambae alinielezea
mie juu ya Jambo nisilolijua. Kwa kifupi hawa ni Walimu wangu. Hivyo nikiita
473

moja kati ya Harfu hizo basi hua ni sawa na kumuita mmoja kati ya Malaika ambae
nae hutokea na kunisaidia kama ninavyohitaji’

Ambapo:

Harfu Siku yake Msimamizi wake Jina Maalum


‫(خ‬600) Kha Jumapili Rawfa’il ‫ ﺧﺒﯿﺮ‬Khabir
‫(ش‬300) Shin Jumatatu Jibril ‫ ﺷﺎﻛﺮ‬Shakir
‫(ز‬7) Zal Jumanne Samsama’il ‫ زﻛﻲ‬Zakiy
‫(ظ‬900)Dhal Jumatano Mika’il ‫ ظﺎھﺮ‬Dhahir
‫(ث‬500) Tha Alkhamis Sirfaya’il ‫ ﺛﺎﺑﺖ‬Thabit
‫(ج‬3)Jim Ijumaa ‘Anya’il ‫ ﺟﺒﺎر‬Jabbar
‫(ف‬80) Fa Jumamosi ‘Azra’il ‫ ﻓﺎطﺮ‬Fatir

Shaykh Al Akbar Imam Abu Bakr Ibn Al Arabi anaendelea kutuambia katika Al-Durr al-
Maknūnfī 'Ilm al-Ḥurūf, kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala alimfundisha Nabii wake
Adam Jina tukufu kuliko yote. Kisha baada ya hapo Nabii Adam akamfundisha
mtoto wake Seth ambae nae akamfundisha Nabii Idrisa Alayhi Salaam. Nabii Idrisa
Alayhi Salaam alikua ni mwenye kupokea vitabu 30 kutoka kwa Allah Subhanah
wa Ta’ala na akapewa I’lm ya herufi, na siri za Hikma, Nambari na mambo
mengineyo, na yeye ndie aliyekua ni wa mwanzo kuandika kwa kutumia Kalamu.
Nabii Idrisa aliandika kitabu kiitwacho Kanz Al Asrar (Hazina ya Siri), ambacho
Thabit Ibn Qurta Al Harani ameandika kukielezea juu yake. Na mimi nilipokutana
nae Nabii Idrisa baada ya kupata ufunuo, basi nikamuuliza, ufunuo zaidi juu yake
ambapo nae akasema: ‘Ufunuo huu ni ile ambayo iliyohifadhiwa nje ya Kitabu
kwani myengine yote iliyobakia imefichika na imefungwa ndani yake. Kisha
akanifunulia baadhi ya Siri zisizojulikana ambazo hakuna mtu mwenye kuzijua juu
yake. Ilm hii ya Herufi baadae ikarithiwa na watu 40 tu wa Haramisa wa Misri’’

Kwani baadhi wanaweza kujiuliza kwa nini kila nikiandika herufi basi hua ninaandika
nambari mbele yake kwa mfano ‫ث‬Tha’ (500), ‫ ج‬Jim (3), ‫ خ‬Kha’ (600), ‫ ز‬Zal (7),‫ ش‬Shin
(300), ‫ ظ‬Dha’ (900),‫ ف‬Fa’ (80) n.k, kwani hii ni kulingana na mtizamo wa Ilm
Ruhaniyyah ambapo harfu hizi zimepewa thamani ya uzito wa kiidadi kama ifuatavyo.

80 ‫ ف‬70 ‫ ع‬60 ‫ س‬50 ‫ ن‬40 ‫ م‬30 ‫ ل‬20 ‫ ک‬10 ‫ ى‬9 ‫ ط‬8 ‫ ح‬7 ‫ ز‬6 ‫ و‬5 ‫ ه‬4 ‫ د‬3 ‫ ج‬2 ‫ ب‬1 ‫اﻟﻒ‬
.1000 ‫ غ‬900 ‫ ظ‬800 ‫ ض‬700 ‫ ف‬600 ‫ خ‬500 ‫ ث‬400 ‫ ت‬300 ‫ ش‬200 ‫ ر‬100 ‫ ق‬90 ‫ص‬

Na wenye Ilm Ruhaniyyah hua wanatumia uthibitisho wa kua kila kitu kina idadi yake
kinambari kutokana na ile aya ambayo inasema:
474

‫ﺼ ٰﻰ ُﻛ ﱠﻞ َﺷ ْﻲ ٍء‬
َ ‫َﺣ‬
ِ ‫ت رّﻬﺑِِﻢ وأ‬
ْ ‫َﺣﺎ َط ﲟَﺎ ﻟَ َﺪﻳْ ِﻬ ْﻢ َوأ‬
ِ ِ
َ َ ْ َ َ‫﴿ﻟّﻴَـ ْﻌﻠَ َﻢ أَن ﻗَ ْﺪ أَﺑْـﻠَﻐُﻮاْ ِر َﺳﺎﻻ‬
﴾ً‫َﻋ َﺪدا‬
LiyaAAlama an qad ablaghoo risalati rabbihim waahata bima ladayhim waahsa
kulla shay-in AAadadan (Surat Al Jinn 72:28)

Tafsir: Na huwalinda (Mitume) hadi ahakikishe kua wamefikisha ujumbe wa Mola


wao. Na yeye (Allah) amekizunguka na amekilinda kila kitu katika idadi.

‘Ambapo aya imetumia neno Ahata lenye kutokana na neno Ha-Ta linalomaanisha
Kuangalia, Kulinda, Kuzunguka, Kugubika, au Kujua kitu kwa Undani, na pia
ikatumia neno Ahsa ambalo linalotokana na neno Ha-Ssa ambalo hua ni lenye
kumaanisha Kupiga Changarawe au Kijiwe kimoja kimoja, Kuhesabu kwa
Umakini, Kutia Nambari, Kuhesabu Kiidadi, Kujua au Kufahamu Idadi ya Kitu’.

Ama kwa upande mwengine basi Imam Muhammad Ibn Is-haq amesema kua amesema
Imam Muhammad Ibn Saib Al Kalbi kua amesema Abu Salih, kua amesema Jabir Ibn
Abd Allah Ibn Riyab: Abu Yasir Ibn Akhtab, pamoja na baadhi ya Mayahudi
walipita mbele ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambae nae alikua akisoma
Surat Al Fatiha, kisha akasoma Alif Lam Miim, Dhalika Al Kitab La Rayba Fihi
Hudda lil Mutaqqin.

Hivyo (Abu Yasir Ibn Akhtab) akamfuata ndugu yake Huyayy Ibn Akhtab ambae
alikua amekaa na Mayahudi wenzake na kuwaambia: ‘Wallahi! Nimemsikia
Muhammad akisoma kile alichoteremshiwa, Alif Lam Miim, Dhalika Al Kitab La
Rayba Fihi Hudda lil Mutaqqin.’ Huyayy akamuuliza: ‘Umemsikia akisoma maneno
hayo?’ Abu Yasir akajibu; ‘Naam!’ Hivyo Mayahudi hao wakaondoka wote kwa
pamoja hadi kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kumuuliza: ‘Jee Jibril
amekuteremshia maneno yasemayo Alif Lam Miim, Dhalika Al Kitab La Rayba Fihi
Hudda lil Mutaqqin?’ Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Naam.’

Mayahudi wakasema: ‘Allah ameleta Mitume kabla yako, lakini sisi kamwe
hatujawahi kusikia miongoni mwao dambae ameataarifiwa juu ya mda wa
Mamlaka isipokua wewe. Na mda wa uhai watakaoishi watu wa Ummah wako
kwani, Alif ni 1, Lam ni 30, Mim ni 40, na hio jumla yake ni 71. Hivyo hio ni miaka
71, sasa jee tunataka kumfuata Mtume ambae Mamlaka yake mwisho wake ni
Miaka 71 na uhai wa Watu wake mwisho wao ni miaka 71?’
475

Kisha wakamuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam: ‘Ya Muhammad Jee
kuna jambo jengine uliloshushiwa zaidi linalofanana na hili?’ Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam akasema: ‘Naam.’ Mayahudi wakauliza: ‘Jee ni lipi?’ Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Alif Lam Mim Sad.’ Mayahudi wakasema:
‘Hio ni zaidi, kwani Alif ni 1, Lam ni 30, Mim ni 40, Sad ni 90 hivyo hapa
inamaanisha miaka 161.’

Mayahudi wakauliza: ‘Ya Muhammad jee kuna jengine zaid?’ Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Naam. Alif Lam Ra.’ Mayahudi wakasema:
‘Alif ni 1, Lam ni 30 na Ra ni 200. Hio hua ni miaka 231’.

Wakauliza tena: ‘Ya Muhammad jee kuna jengine zaid?’ Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam akasema: ‘Alif, Lam, Mim, Ra’. Mayahudi wakasema: ‘Alif ni 1,
Lam ni 30, Mim ni 40 na Ra ni 200. Hio ni miaka 271.’

Kisha Mayahudi hao wakaondoka na kusema: ‘Ya Muhammad hakika sisi


tumechanganyikiwa juu ya mambo yako haya, kwani hatujui juu ya mda wa
Mamlaka yaliopewa Ummah wako kama utakua ni mrefu ama la.’

Mayahudi hao wakaambiana: ‘Twende zetuni’ kisha wakaondoka kwa pamoja


huku Huyay akimwambia Abu Yasir pamoja na Rabbi wao kua: ‘Na ni nani
atakaeweza kujua kwani huenda miaka hio yote 71, 61,100, 231, na 271 hua ni 734
ni kwa ajili ya Ummah wa Muhammad, na bado kuna myengine ambayo
hayakuhesabiwa.’(Tarikh Imam Bukhari, Durr al Manthur na katika Al Itiqan Fi Ulumu
Ul Qur’an Imam Al Suyuti, Tafsir Imam Ibn Kathir Maktabah Qurtubah Al Qahira.)

Kwa upande wa Suhayli basi yeye anasema: ‘Inaonekana kua jumla ya idadi ya herufi
MuqataaAt zote zilizorudiwa ndio Urefu wa Mamlaka ya Ummah huu.’

Ama kwa upande wa Imam Abu Al Khayr Shams Al Din Muhammad Ibn Muhammad
Ibn Muhammad Ibn Ali Ibn Yusuf Al Jazari Al Shafii basi yeye anasema katika ushairi
wake wa Al I’lm Hukm Al Qiraat kua:

‫ﻣﻦ ﯾﺤﺴﻦ اﻟﺘﺠﻮﯾﺪ ﯾﻈﻔﺮ ﺑﺎﻟﺮﺷﺪ‬....‫واﻟﺒﯿﺖ ھﻮ أﺑﯿﺎﺗﮭﺎ ﻗﺎف وزاي ﻓﻲ اﻟﻌﺪد‬

7 = ‫ و زاي‬100 = ‫وﻗﺎف ﻓﻲ اﻟﻌﺪد‬

‫ ﺑﯿﺖ وﷲ أﻋﻠﻢ‬107 ‫آي ﻋﺪد اﻵﺑﯿﺎت‬


476

‘Na Nyumba yake ni Nyumba za Qaf na Zay katika Idadi..Na anaekiboresha kisomo
chake cha Tajwid kwa kutumia muongozo wa Jaffar,

Na Qaf kiidadi ni 100 na Zay 7 hivyo idadi ya nyumba yake ni 107.

Na Allah ni mwenye kujua zaid (Mandhumat Al Muqaddimat, Imam Ibn Al Jazari)

Vile vile tunapoangalia miongoni mwa Wanazuoni katika kuitafsiri Surat Ar Rum basi
anasema Imam Abu Shamah Shihab Ad Din Abd Rahman Ibn Ismail Ibn Ibrahim Ibn
Uthman Ibn Abi Baqr Ibn Ibrahim Ibn Muhammad Al Maqdisi kua: Alisema Imam Abu
Al Hakam Abd Salam Ibn Abd Al Rahman Ibn Mohammad Ibn Barrajan katika
kuitafsiri Surat Ar Rum:

﴾‫وم‬‫ﺮ‬‫ٱﻟ‬ ِ
‫ﺖ‬ ‫ﺒ‬ِ‫ﻠ‬ ‫ﻏ‬ ۞ ۤ ‫﴿ ۤاﻟ‬
‫ـﻢ‬
ُ ‫َُ ﱡ‬
Alif, Laam, Miim, Ghulibati Alrum (Surat 30:1-2)

Tafsir: Alif Laam Miim; Warumi wameshindwa.

Kua: ‘Jerusalem itakua chini ya Mamlaka ya Utawala wa Roman Empire hadi


katika mwaka 583 Al Hijr kwani katika mwaka huo ndio watakaposhindwa na
kupinduliwa. Na Jerusalem itakua chini ya Mikono ya Uislam hadi mwisho wa
Dunia. Na hii ni kulingana na idadi iliyomo ndani aya hii’. Na hivyo ndivyo
ilivyotokea. (Tarikh al-Khulafa, Imam Al Suyuti, Al Itiqan Fi Ulumu Ul Qur’an Imam Al
Suyuti)

Tafakkar! Kwani Imam Ibn Barrajani alichukua idadi ya neno Ghulibat yaani
watashindwa ambalo kiidadi ni 1432 na hivyo wenye kushindwa hua ni wenye kula
hasara hivyo akatoa neno Al Rum ambalo kiidadi ni 277, hivyo akapata jawabu ya 1155
kisha akajumlisha na nambari ya Sura ambayo ni 3 na kisha akajumlisha na nambari ya
aya ambayo ni 2 akapata jawabu ya mwaka 1187 Christian Era.

Ingawa hio ni mitizamo mbali mbali pale tunapozungumzia harfu Al MuqattaAat kupitia
katika Ilm ya Ruhaniyya lakini pia kuna mtizamo wa pili nao una ufafanuzi tofauti juu
yake, ufafanuzi huo unawekwa wazi na mfano ufuatao: Katika kipindi cha Utawala wa
Khalifa Al Mutawakkil ambae alikua ni mtawala wa Mamlaka ya Al Abbas, basi
aliandikwa barua na Mtawala wa Rum ambayo ilikua inseam: ‘Hakika mimi nimesikia
kua katika kitabu cha Dini yenu mna Sura ambayo ina herufi zote isipokua herufi
7 (Sawaqit al-Fatiha: ‫ ث‬Tha’ (500), ‫ ج‬Jim (3), ‫ خ‬Kha’ (600), ‫ ز‬Zal (7),‫ ش‬Shin (300),
‫ظ‬Dha’ (900),‫ ف‬Fa’ (80)) ndani yake. Na kama Surah hii ikisomwa basi humpatia
477

Pepo yule aisomae. Hivyo mimi nilikua nataka kujua ni Sura gani hio na kwa nini
herufi hizi hazimo ndani yake’

Suali la barua hii lilimchanganya sana Khalifa Abu Al-Faḍhl Jaʽfar ibn Muḥammad Al
Muʽtaṣim Billāh maarufu kama Al Mutawakkil, hivyo ikambidi kumtafuta Imam Ali An
Naqi ambae alikua akiishi katika Ardhi ya mjini Samara. Imam Ali An Naqi alipoulizwa
juu ya suali hilo basi akajibu: ‘Sura hio ni Surat Al Fatiha, na herufi hizo hazimo
ndani yake kwa sababu kila moja kati ya Sawaqit hizo zinawakilisha maneno yenye
maana maangamizo katika kauli ya Allah Subhanah wa Ta’ala.’

Khalifa al Mutawakkil akamuuliza Imam Ali An Naqi juu ya herufi 7 za Sawaqit, ambapo
Imam Ali An Naqi nae akajibu: ‘Herufi ya kwanza ni herufi ‫ ث‬Tha ambayo
inawakilisha maangamizo yaani Thubur, herufi ya pili ni ‫ ج‬Jim ambayo
inawakilisha Moto wa Jahannam yaani Jahim. Herufi ya tatu ni ‫ خ‬Kha ambayo
inawakilisha Ubaya yaani Khubth au Hasara yaani Khusr. Herufi ya nne ni ‫ ز‬Zal
ambayo inawakilisha Zaqqum ambao ni mti wa Motoni ambao Matunda yake ni
yenye sumu na machungu yasiyokua na mfano wake. Herufi ya tano ni ‫ ش‬Shin
ambayo inawakilisha Shaqawa. Herufi ya sita ni ‫ ظ‬Dhal ambayo inawakilisha
Dhulma na herufi ya saba ni ‫ ف‬Fe ambayo inawakilisha Afat yaani Mitihani na
maangamizo kwa ujumla.’

Kwa upande wa wataalamu wa Lugha wanasema kua kila herufi ya Kiarabu hua ina
maana pekee inayojitegemea kwa mfano: Herufi Alif inapokua peke yake inatumika
kuuliza Suali, herufi Mim inawakilisha kuuliza juu ya kitu au Mtu na pia humaanisha
wingi katika kiwakilishi, Herufi Lam huwakilisha Kukataa, n.k hivyo basi kulingana na
mtizamo huo hua tunaona kua Neno Alif Lam Mim hua linamaanisha hali ya Mahojiano,
Kupinga au Kuuliza masuali, yaani kupinga baadhi ya mambo na kuafikiana baina ya
mambo yanayopingana. Sultan Al Mutakallimi Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al
Razi anasema pia kua: ‘Waarabu walikua wakitumia herufi '‫ 'ع‬kumaanisha Pesa,
herufi '‫ 'غ‬kumaanisha Mawingu, herufi '‫ 'ن‬kumaanisha Samaki, n.k’

Katika kuunga mkono maana hizo basi tuangalie mifano ifuatayo ambapo tunapoangalia
moja kati ya mashairi ya Walid Ibn Uqba Ibn Abu Mua’yit basi tunaona kua anasema:

‫ﻗﻠﺖ ﻟﮭﺎ ﻗﻔﻲ ﻓﻘﺎﻟﺖ ﻗﺎف‬


Qultu Laha Qifiy faqalat Qaf.

Tafsir: ‘Nilimwambia yeye (Mwanamke): ‘Kaa Kidogo’, nae akajibu: ‘Qaf. Ambapo
herufi ya mwisho ambayo ni Qaf imetumika kuwakilisha neno: Waqaftu ‫ وﻗﻔﺖ‬ambalo
maana yake ni Kusimama. Mfano mwengine ni ule wa Imam Abu Abd Allah
478

Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi ambae anatoa mfano
kwa kusema kua Waarabu hua wanasema:

‫ﻛﻒ ﻟﻨﺎ اﻟﺴﯿﻒ ﺷﺎ‬


Qafa Lana al Sayf Shin yaani: ‘Unatutosha sisi Upanga kua Sha’ ambapo Herufi Shin
imetumika kumaanisha neno Shafii. Na wengine hua wanasema kua inamaanisha neno
Shahidan’

Kwa upande wa Imam Abu Talib Al Makki basi yeye anasema kua: ‘Sayyidna Ali Ibn
Abi Talib Karamah Allahu Wajh alikua akiomba dua kwa kwa maneno yasemayo:
‘Ya Kaf, Ha, Ayn, Sad, hakika mimi nakuomba kupitia kwako uninusuru na Dhambi
zenye kuangamiza, kuondokewa na Baraka, kuondokewa na mvua, au kuzidiwa na
Maadui zangu. Ya Allah! Tulinde dhidi ya Nafsi zetu.’’ Ambapo harfu Kaf
inawakilisha Jina la Allah Subhanah wa Ta’ala la Al Kafi, Ha ni Al Hadi, Ya ni Al Yaqin,
A’ayn ni Al A’lim na Sad ni Al Sadiq.

Ama tunapomuangalia Imam Tahir Ibn Ashur katika kuitafsiri Surat Yasin basi amesema
kua neno Ya Sin ambazo ni Harfu mbili za Ye na Sin hua linamaanisha Ya Sayyid yaani
Ewe Bwana (wa Mitume).

Ambapo Imam Hamid Al Din Abu Hasan Ahmad Ibn Abd Allah Al Kirmani basi yeye
anasema kuhusiana na Surat Ta-Ha kua: ‘Ta-Ha maana yake ni Mwezi Mweupe kwani
Harfu Ta ina uzito wa idadi ya 9 na harfu Ha ina thamani ina uzito wa idadi ya 5 na
ukijzijumlisha kwa pamoja unapata 14 kumaanisha mwezi 14 muandamo.’(Al
Gharaib)

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari ambae yeye anatuambia kua: ‘Kila
Kitabu ambacho Allah Subhanah wa Ta’ala alikishusha basi kina mfumo wa siri
ndani yake, na mfumo wa siri wa Qur’an umo katika herufi ambazo ndio ufunguzi
wa Sura husika, kwa sababu Herufi hizo ndizo ni Majina na Sifa zake. Kama
anavyosema Alif Lam Mim (2:1, 3:1, 29:1 na 31:1), au Sad (38:1) au Alif Lam Ra
(10:01, 11:1,) n,k. basi harfu hizi zinapojumuishwa pamoja, zinatoa jina Tukufu la
Allah Subhanah wa Ta’ala. Kwa mfano Alif, Lam, Ra, Ha, Mim na Nun basi hua
tunapata jina la Al Rahman. Ambapo kwa Abda Allah Ibn Abbas na Dahhaq Ibn
Muzahim basi wao wamesema kua Alif Lam Min hua inamaanisha: ‘Mimi ni Allah
na Nnajua’.

Ambapo kwa Upande wa Ali Ibn Abi Talib Karama Allahi Wajh basi yeye anasema kua:
‘Haya ni Majina ambayo, yapo katika hali ya herufi zilizotawanyika. Lakini kama
ikichukuliwa herufi moja kutoka katika kundi kila kwa mpangilio wa kua ni tofauti
479

na herufi iliyokaribu yake herufi hio, na zikakusanywa pamoja kiidadi basi hua ni
zenye kuunda jina la mwingi wa Rehma. Hivyo kama ikiwa jina hili litajulikana na
kisha likatumiwa katika maombi ya Dua basi litakua ni jina lenye Nguvu sana kiasi
ya kua Dua ya muombaji kwa kupita jina hilo itakua ni yenye kukubaliwa.’’

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari anaendelea kutufafanulia kwa
kutuambia kua: ‘Nimepokea Hadith kutoka kwa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu
Anhu ambae anasema kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala ameapa kua kitabu chake
hiki, alichomshushia Nabii Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam, ni kitabu
ambacho kipo chini ya uangalizi wake. Hivyo akasema: ‘Alif Lam Mim. Hiki ni
Kitabu..ambapo Alif hua inamanisha Allah, Lam inamaanisha Jibril na Mim hua
inamaanisha Muhammad, hivyo basi hapa inaonesha kua Allah Subhanah wa
Ta’ala, amekula kiapo kwa ajili yake yeye mwenyewe, na kwa ajili ya Malaika wake
Jibril, na kwa ajili ya Nabii wake Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam.’’’

Tumalizie kwa kuangalia upande wa Imam Jafar As Sadiq kupitia kwa Sufyan Ath
Thawry ambae anasema kua: ‘Mimi nilimuuliza Imam Jafar As Sadiq: ‘Ya Ibn Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam, jee ni nini maana maneno ya Allah Subhanah wa
Ta’ala katika kusema kwake Alif, Lam, Miim na Alif, Lam, Miim, Saad na Aliif, Lam,
Ra na Aliif, Lam, Miim, Ra na Kaf, Ha, Ya, ` Ayn, Saad na Ta, Ha na Ta, Siin na Ta,
Siin, Miim na Ya, Siin na Saad na Ha, Miim na Ha, Miim, `Ayn, Siin, Qaaf and Qaaf
na Niin’’

Imam Jafar As Saddiq akajibu: ‘Ama kuhusiana na Alif-Lam-Mim iliyo mwanzoni


mwa Surat Al Baqara basi hua inamaanisha Mimi ni Allah Mfalme na Alif-Lam-
Miim iliyo mwanzoni mwa Surat Al Imran basi hua yenye kumaanisha Mimi ni Allah
Mtukufu na Alif-Lam-Miim-Saad humaanisha Mimi ni Allah Muamuzi wa Kila kitu
na Mkweli. Alif-Lam-Ra hua inamaanisha Mimi ni Allah Mwenye Wingi wa
Usamahevu. Maana ya Alif-Lam-Miim-Ra hua inamanisha Mimi ni Allah Mwenye
Kuhuisha, Mwenye Kufisha, Mwenye Kutoa Rizki. Maana ya Kaf-Ha-Ya-Ayn-Sad
hua ni Mimi Mwenye Kutosheleza, Mwenye Kuongoza, Mwenye Kuhifadhi,
Mwenye Ilm, Mwenye katika Ahadi zake.

Ama kuhusiana na Ta-Ha basi hili ni jina miongoni mwa Majina ya Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam. Na hua linamaanisha Ewe Mwenye Kuutafuta ukweli
na Kuongoza katika njia ya Ukweli. Hatujakuteremshia Qur'an ili usifanikiwe
katika njia yako, bali tumekuteremshia kwa sababu ya kukuboreshea Hali yako.
Ama juu ya maana ya Ta-Sin basi maana yake hua ni Mimi ndie Mwenye Madai ya
Kutekelezewa na ndie Mwenye Kusikia Kila Kitu. Ama kuhusiana na Ta-Sin-Miim
basi hua inamaanisha Mimi Ndie mwenye Madai, mwenye Kuona Kila Kitu, ndio
wa Mwanzo na Ndie wa Mwisho.
480

Ama kuhusiana na Yasin basi nalo pia ni jina la Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
Salam na hua linamaanisha Ewe Mwenye Kusikiliza Uteremsho wetu na Qur'an
iliyojaa Hikma, Kwa Hakika wewe ni Mjumbe Wetu Katika Njia Iliyonyooka. Ama
kuhusiana na Saad basi ni Chemchem inayotiririka kutoka chini ya Arshi ya Allah
Subhanah wa Ta'ala na ndio kutokana na maji ya Chemchem hii basi ndio rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam alitilia Udhu wake pale alipopelekewa juu
Mbinguni katika Usiku wa Miraj. Na ndio Chemchem ambayo Malaika Jibril
huenda kujitumbukiza kila siku, kisha hutoka na kujikunuta Maji yote yaliyomo
kwenye mbawa zake. Na hakuna hata tone moja linalopukutika kutokana na maji
hayo kutoka kwenye mbawa zake isipokua Allah Subhanah wa Ta'ala hua ni
mwenye kuumba Malaika ambae hua ni mwenye kumtukuza na kumisfu Allah
Subhanah wa Ta'ala kwa mda wote mpaka siku ya Malipo.

Ama kuhusiana na Ha-Mim basi hua inamaanisha Mwenye Kustahiki Kusifiwa na


Kutukuzwa. na Ha-Miim-Ayn-Sin-Qaf basi hua linamaanisha Mstahmilivu,
Mwenye Kulipa Malipo Bora kwa Wanyao Mema, Mwenye Kujua Kila kitu,
Mwenye Kusikia Kila Kitu, Mwenye Uwezo wa Kila Kitu na mwenye Nguvu Juu ya
Kila kitu. Na Qaf hua inamaanisha Mlima ambao ni wenye Kuizunguka na
Kuifunika Dunia na kupitia katika Mlima huu ndio Allah Subhanah wa Ta'ala
akaitandaza Dunia kwa ajili ya Ibn Adam kuishi ndani yake. Ama Kuhusiana na
Nun basi huu ni Mto wa Peponi ambao Allah Subhanaha wa Ta'ala aliuambia
ujikusanye na uwe mgumu na akatoa Kalamu na Wino kutokana nao, kisha
akaiambia Kalamu hio: 'Andika!' nayo ikaandika kwenye Al Lawh Al Mahfudh kila
kitu kilichotokea na kitakachotokea hadi siku ya Malipo. Na Kalamu hio ni yenye
Nuru ya Allah Subhnaha wa Ta'ala na Lawh ni yenye Nuru ya Allah Subhanah wa
Ta'ala.'

Sufyan Ath Thawry akamwambia Imam Jafar As Sadiq: 'Ewe Ibn Rasul Allah! Hebu
Nielezee juu kikamilifu juu ya Amri ya Lawh na Kalamu na Wino wake na
nifundishe kile ambacho Allah Subhanah wa Ta'ala amekufundisha.' Imam Jafar
As Sadiq akasema: 'Ewe Ath Thawry, kwa hakika kama wewe usingekua mtu
anaestahiki kujibiwa basi mimi nisingekujibu. Hivyo fahamu kua Nun ni Malaika
anaeielekeza Kalamu, na Kalamu ni Malaika anaeielekeza Al Lawh, na Al Lawh ni
Malaika anaemuelekeza Malaika Israfil na Israfil anamuelekeza Mikail na Mikail
anamuelekeza Jibril na Jibril anawaelekeza Mitume wote Sala na Salamu ziwe Juu
yao' Sufyan Ath Thawry anasema kua, kisha Imam Jafar As Sadiq akaniambia:
'Haya nenda zako ewe Ath Thawry kwani hakuna kizingiti juu yako kutokana na
Ilm niliyokuachia kwako'’

Tunaporudi kwa Sultan Al Mutakallimi Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi
Al Shafii, na pia Imam Abu Jafar Muhammad Ibn Jarir at Tabari Al Shafii basi tunaona
kua wanasema pia kua: 'Harfu MuqataA'at zilikua pia ni zenye umuhimu wa kutaka
481

kuwaonesha Makafiri wa Mji wa Makkah utofauti na maajabu ya Qur'an na hivyo


iwavutie, kwani wao walikua ni wenye kuapa kua kamwe hawatosikiliza Qur'an.
Hivyo basi Maajabu ya Harfu hizi yaliwafanya wawe na hamu ya kutaka kujua
kuhusiana na Qur'an ambayo tayari walikua hawako tayari kuisikiliza.'

Na ndio maana pia akasema Sultan Al Balagha Imam Abu Al Qasim Al Zamakhshari na
Imam Nasir Ad Din Al Baydawi kua: 'Malengo ya Harfu MuqataA'at ni kuwawekea
wazi Makafiri kua Qur'an ina herufi ambazo na wao pia hua ni wenye kuzitumia
katika Lugha yao lakini hata hivyo wakawa ni wenye kushindwa kutoa mithili ya
sura moja tu ambayo itafananana na japo moja kati ya Sura 114 za zilizomo ndani
ya Qur'an'

Hivyo kwa njia moja au nyengine basi hua haishangazi kwanini wanazuoni wakawa wana
mitizamo tofuati juu ya herufi hizi kwa sababu Qur'an tukufu ina aya Mutashabihat
ambazo hua ni zenye maana nyingi ndani yake na hii hua ni yenye kuweka wazi Ukubwa
usiokua na mwisho wa I'lm ya alieteremsha Qur'an ambae ni Allah Subhanah wa Ta'ala.
Hivyo basi ni jambo la kawaida kwa Harfu Muqata'Aat kua ni zenye siri ndani yake na
pia kua na maana tofauti kulingana na mitizamo wa Wanazuoni tofauti juu yake.

Miongoni mwa Wanazuoni wa Tafsir waliotafsiri herufi hizi wametofautiana juu ya


maana halisi ya herufi mbili hizi za Ta-Ha zilizomo katika aya ya kwanza, ya Surat Ta-
ha kwani kuna wasemao kua neno Ta-Ha hua linamaanisha: ‘Ewe Ibn Adam’ na hii ni
kutokana na lugha ya watu wa Bani Aqik ambao wao hua wanatumia neno Ta-Ha kuitana
yaani badala ya kuitana Ya Rajul! basi hua wanaitana Ta-Ha! (Tafsir Abu Hayyan na
Tafsir Ibn Athir), kuna wasemao kua hua linamaanisha: ‘Ya Muhammad!’, Ya Habib na
hii ni kulingana na mtizamo wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu. Ama kwa
upande wa Imam Muhhib Ad Din Abu Al Faidh Al Murtada anasema katika Taj Al Arusi
kua neno hili hua linamaanisha ‘Kua na Utulivu’. Na Imam Ibn Al Hayyan basi yeye
anasema kua hili ni moja kati ya Majina ya Nabii Muhammad Salallahu Allahu wa Salam
ambalo ni lenye kummaanisha kua: ‘Ewe Nabii Bora’

Ukweli ni kua kuna mengi ya kuyazungumzia katika tafsir ya harfu hizi MuqataaAt kiasi
ya kua huenda kikahitajika kitabu chake kizima kinachojitegemea, hivyo tunasimamia
hapa na kisha tunarudi tena katika Surat Ta-Ha ambayo ndio Suran inayoanza na kisa
chetu cha Nabii Musa Alayhi Salatu wa Salam basi tunaingia katika Sura hii na kuona
kua Surat Ta-Ha inaanza kwa kuweka wazi kusudio la kuteremshiwa Qur’an kua si kwa
ajili ya kumuingiza katika mitihani Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam bali ni kwa
ajili ya kumpa muongozo ili kuuongoza Ulimwengu wote na kuurudhisha katika njia
iliyokua sahih na inayokubalika na muumba wa Ulimwengu na kisha baada ya hapo basi
Sura hio inaanza moja kwa moja kuhoji juu ya kuwahi kusikika kwa Kisa cha Nabii Musa
Alayhi Salaam kwa mtizamo ambao ni tofauti na mitizamo ya vitabu vyengine vya Ahl
al Kitab.
482

Na hii ni kwa sababu kwanza Maquraysh wa Makkah walikua wakimjua Nabii Musa kua
ni Mtume wa Allah Subhanah wa Taála kwa sababu walikua tayari wameshasikia habari
zake kutoka kwa Mayahudi wa Madina. Hivyo kwa upande wa pili basi Allah Subhanah
wa Taála alikua akimliwaza kipenzi chake Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa
Salam na Waislam kwa ujumla kua wasiwe na khofu juu ya kua na wafuasi kidogo na
hivyo kua ni wenye kunyanyaswa kutokana na idadi yao na kutokua na nguvu kwao,
kwani Nabii Musa Alayhi Salaam pia alikua peke yake dhidi ya Utawala wenye nguvu
wa Firáwn na Watu wake, na akawashinda na kwa upande mwengine basi ilikua
inawataka Waislam wawe na Subra na misimamo katika Imani yao kama vile ambavyo
walivyokua na Subra na Misimamo Wachawi wa Firáwn pale walipomkubali Nabii Musa
na kumgeuka Firáwn kama tutakavyoona hapo baadae katika kisa.

Hivyo kabla ya kungia katika aya 9 za mwanzo za Surat Ta-Ha basi na tuangalie maana
ya Biismi Allahi Al Rahmani Al Rahim:

﴾‫اﻪﻠﻟِ اﻟﱠﺮ ْﲪَـ ِﻦ اﻟﱠﺮِﺣﻴ ِﻢ‬


‫﴿ﺑِ ْﺴ ِﻢ ﱠ‬
Biismi Allahi AlRahmani AlRahiim.

Tafsir: Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehma Mwingi wa Huruma.

Hii ni aya ya mwanzo ya Qur’an na pia ni Utangulizi na Ufunguzi wa kila kitu


kinachofanywa na kila Mtu aliemuamini Allah Subhanah wa Ta’ala. Anasema Mujaddid
Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Al Mushakikin Shaykh ul Islami Imam Fakhr Ad
Din Al Razi kuhusiana na ayah hii kua: ‘Harfu Ba iliyopo mwanzoni mwa ayah hii hua
inamaanisha Ilsaq (kiunganishi) ‘Kwa’ ambacho kinaunganisha uanzaji wa kitendo
na jina la Allah Subhanah wa Ta’ala.’

Neno Allah kwa lugha ya Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Jina Tukufu ambalo ni la
Muumba wa Kila kitu, kilichomo kwenye Ulimwengu unaoonekana na usioonekana,
ambae ni Mmiliki wa kila kitu Mbinguni na Ardhini, ambae ndie mmiliki wa Sifa nzuri
zote na Majina Matukufu yote. Hivyo Majina yote Matukufu ya Allah Subhanah wa
Ta’ala na sifa zake Tukufu ambazo kwa ufahamu wa Ibn Adam hua haziwezi
kufafanulika kikamilifu na ipasavyo kama inavyobidi kuelezewa zilizotajwa ndani ya
Qur’an ni yenye kuweka wazi maana ya jina la Allah Subhanah wa Ta’ala kulingana na
Ufahamu wa Ibn Adam.

Anasema Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din, Zuhruf Ad Din Imam Al Shafii Al Thani
Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al
Shafii kua: 'Allah ni Jina la yule ambae yupo hai, ambae ni mwenye sifa za kua ni
483

Muumba na Mlezi juu ya kila kitu alichokiumba. Yeye ni mwenye upekee pale
tunapozungumzia usahihi wa kuwepo kwake, na bila ya shaka hakuka kitu
chengine chochote kile kilichokuwepo ambacho kinaweza kupewa kupewa sifa
stahiki ya kuwepo kwake kitu hicho kutokana na utukufu wa kuwepo kwake. Kwani
kile ambacho inabidi kiwepo kulingana na sifa ya kutoweka kwake, kwani kila
kinachokuwepo basi lazima kitoweke. ISIPOKUA kuwepo kwake Allah Subhanah
wa Ta'ala.'

Inabidi ujue kua Jina hili ‘Allah’ ni Jina Kubwa na Tukufu kuliko yote katika ya
Majina 99 ya Allah Subhanah wa Ta'ala, kwa sababu jina hili ndilo linalojumuisha
sifa zote za Allah Subhanah wa Ta'ala. Kwani kila jina lake moja hua na maana
moja, kama Alimu, Qawiyum, Qayyum n.k lakini jina hili la 'Allah' ni jina maalum
la Allah Subhanah wa Ta'ala. Hakuna mwenye kutumia jina la Allah isipokua Allah
mwenyewe. Iwe kwa njia ya moja kwa moja au kwa njia nyengine, wakati majina
mengine kama Al Qadir, Al Alim, ArRahman n,k yanaweza kutumika kwa njia
nyengine. Lakini jina la Allah halitumiki kwa yeyote yule isipokua yeye na ndio
maana likawa ndio jina Tukufu kuliko yote.'

Imam Jamal Islam Abu Qasim Abd Al Karim Ibn Hawazin Al Qushayri basi anasema
kua: 'Kilugha harfu Ba katika Neno Biismi Allahi hua kinawakilisha kiunganishi
yaani Bi-llah humaanisha Kupitia kwa Allah Subhanah wa Taa'la. Ambapo mambo
mapya hua ni yenye kubainishika na kupitia kwake yeye basi viumbe vilivyoumbwa
huwepo. Na hua kamwe hamna katika viumbe vipya vilivyoumbwa (hadith
makhluq) au mshikamano wa matukio yanayotokea sambamba (Hasl Mansuq), au
kutokana na kitu kinachoonekana au kinacho hisika kihisia kwa athari zake, n.k.
Au kitu chochote kutokana na jiwe au udongo au majani au miti au alama
zinazobakia ardhini (Rasm) au mabaki yaliyosimama (Talal) au hukmu yeyote au
sababu ambayo inayoonekana kuwepo kwake.

Ambapo hua haviwezi kuwepo isipokua kwa kuwepo mwenye Hakika ya kuwepo.
Na Hakika hio hua ni katika Mamlaka yake. Ambayo Mwanzo wake hua ni kutoka
kwake na Mwisho wake hua ni kurudi kwake. Kupitia kwake yeye basi yule
anaetangazia Tawhid Allah basi hua ni mwenye kupata na anaepinga hua ni
mwenye kukosa Iman. Kupitia kwake yeye basi yule anaekubali hua ni mwenye
kujua na kupitia kwake basi yule mwenye kuasi hua ni asiejua na kubakia nyuma.

Allah Subhanah wa Ta’ala amesema ‘Biismi Allahi’ hakusema ‘Bi Allahi’. Na


kulingana na mitizamo ya baadhi ya watu basi husema kua hii ni njia yakutafuta
Baraka kupitia katika kumtaja jina lake. Na kulingana na wengine basi basi hua ni
kutokana na tofauti ya maneno haya ‘Biismi Allahi’ na Kiapo ‘Bi Allahi’. Na
kulingana na baadhi ya Wanazuoni basi pia tunaona kua wanasema kua ni kwa
sababu ya ‘Ism’ jina basi ndio kitu hua ni chenye kinaitwa ‘Musamma’.
484

Ama kulingana na mtizamo wa wa watu wenye Ilm ya Ruhaniyyat ya Kiroho ya


‘Irfan’ basi ili kupata usafi wa Moyo kutokana na mshikamano na kuikomboa Nafsi
kutokana na vikwazo ili neno ‘Allah’ lipate kuingia ndani ya moyo uliokua msafi na
nafsi iliyosafika.

Baada ya kuitaja ayah hii, basi baadhi ya watu hua wanakumbushwa kutokana na
harfu ‘Ba’ ambayo ni yenye kutokana na Wema au Ukarimu (Birr) na Mawalii
wake na harfu ‘Sin’ ni kutokana na Siri ‘Sirr’ baina yake na wale aliowachagua na
kutokana na harfu ‘Mim’ kutokana na neno Rehma zake ‘Manna’ kwa waja wake
wenye Uwalii (Ahl Al Walaya). Ambao hua wanajua kua kutokana na Rehma zake
basi hua wenye kujua Siri zake, na kutokana na Rehma zake juu yao hua ni wenye
kutekeleza maamrisho yake, na kutokana nae Allah Subhanah wa Ta’ala basi hua
ni wenye kujua uwezo wake.

Na kwa upande mwengine basi kuna wasemao kua: kutokana na kusikia Biismi
Allahi hua ni wenye kukumbushwa kutokana na harfu ‘Ba’ inayotokana na neno
Wema au Ukarimu (Baraa) ya Allah Subhanah wa Ta’ala na harfu ‘Sin’ kutokana
na neno Salama na kutokua na kasoro na harfu ‘Mim’ inayotokana na neno
Utukufu wake Mkubwa (Majid) katika Utukufu wa kuelezewa kwake. Wengine hua
ni wenye kukumbushwa kutokana na harfu ‘Ba’ kutokana na Uzuri wake wenye
Upekee (Baha) na harfu ‘Sin’ kutokana na neno Kung’ara kwa Nuru yake (Sana),na
harfu ‘Mim’ kutokana na Mamlaka yake ‘Mulk’.

Ama kwa upande wa Imam Abd Razak Al Kashani basi yeye anasema kua: ‘Kupitia
katika kutojidhihirisha, basi yule alie na hali ya Al Wahid (Upekee) basi hujionesha
kupitia katika hali ya Al Wahidiyyah (Umoja). Hivyo hapa hali ya Al Ayan Al
Thabitah (Utibitisho) ambayo hua ni utambulisho kwa ulimwengu kujionesha
katika hali hii. Uthibitisho huu huendelea kujionesha katika sifa za kiumbaji.
Kutokana na kutokea na hali hio ya kujionesha basi, hali hio ya Al Tajalli Al
Shuhudiyy (kujidhihirisha wazi na kushuhudiwa) hupelekea kutokea maumbile ya
jina yaani Asmaiyyah.

Katika hali kama hii basi jina na sifa za Muumba hua ni zenye kuonekana wazi.
Hivyo basi jina hili la Allah hua ni jina ambalo huonesha sifa za Muumba, na jina
lake tukufu la Allah hua linaitwa Al Asm al Adhim. Kwa hivyo jina hili la Allah hua
ni jina la mwanzo katika majina yake yote, na hivyo hivyo ndivyo hali inavyokua
kwa sifa zake zote tukufu, kwani jina la Allah linajumuisha majina yake yote
Matukufu na sifa zake zote tukufu.

Jina la Allah hua linayaunganisha pamoja majina yake yote matukufu na sifa zake
zote tukufu, na hivyo Hadhrat Ilahiyyah (hudhihirisha sifa ya Uumbaji) hua inakua
inakaa juu ya Majina yake yote Matukufu
485

Ama kwa upande wa Shaykh Al Akbar Imam Ibn Arabi basi yeye anasema kua: ‘Jina la
Allah hua linawakilisha hali ya kuwepo kwake Muumbaji kupitia katika njia ya
Hikma na Busara, kwa mfano: Jina la Muumba (Al Asm Al Alam) hua linatokana
na vitu vilivyopewa majina. Kwa hivyo basi jina la Muumba hua linaashiria Tanzih
(Kutokuwepo Muingiliano) baina ya muumbaji na viumbe. Na jina la Muumba
hubainisha Ithbat (Uthibitisho) ya maumbile ya Sifa Tukufu. Hata hivyo hali ya yule
aliepo hua hairuhusu kugawanyika kiidadi kwa sababu Muumbaji ni Qiyam al Adad
(Alie mmoja Kiidadi). Majina ya muumbaji hua ni yenye cheo cha kuthibitisha sifa
tukufu, kwa mfano Al Alim (Mwenye kujua juu ya kila kitu), Al Qadir (Mwenye
uwezo wa kukadiria juu ya kila kitu) Al Murid (Mwenye uwezo wa Kutaka kila
kitu), Al Samiu (Mwenye Kusikia kila kitu) Al Basir (Mwenye Kuona Kila kitu),
n.k.’

Anasema Allaamah Abu Bishr Ibn Amr Ibn Uthman Ibn Qanbar Al Basr maarufu kama
Al Sibawayh anasema kua: ‘Herufi Alif na Lam yaani Al ambazo haziwezi
kutenganishwa peke yake mwanzoni mwa jina la Allah basi hua ni Muuganiko wa
Jina hilo na wala halitokani na Neno au Jina lolote. Kwani Jina Allah kamwe
haliwezi kua ni kifupi cha Al-Ilah kama wanavyodhani baadhi ya watu. Hivyo Jina
la Allah ni Jina kamili la Muumba na hivyo halina ushabihiano na Jina jengine
lolote la lugha yeyote. Hivyo basi Jina la Allah halitakiwi kutafsiriwa kwa lugha
yeyote bali linatakiwa kubakia katika hali yake ya asili kama lilivyo yaani Allah!’

Ama kwa upande wa Imam Nasir Ad Din Al Baydawi anasema kua: ‘Muongozo huu
wa kuanza na kila kitu na Biismi Allahi unamfunza Muumini kutafuta Baraka
kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala katika kila jambo lake katika maisha yake.’
Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Al Mushakiqin Shaykh ul Islami Imam
Al Ghazali Al Thani Imam Fakhr Ad Din Al Razi kuhusiana na ayah hii kua: ‘Biismi
Allahi hua inamfunza Muislam kuomba msaada kwa Allah Subhanah wa Ta’ala
kupitia katika Neema na Baraka zake katika kila kitu chake na hivyo hua ni yenye
kumfanya Muislam kuanza kila kitu chake na Dhikr Allah. Na ndio maana katika
kufanya kila kitu chako basi kuisoma ayah hii hua inapendekezwa na hua na hali
ya Mandub katika Sharia za Fiqh’

Katika kufafanua zaid maana aliyoinisha Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam
Al Muashakiqin Shaykh ul Islami Imam Al Ghazali Al Thani Imam Fakhr Ad Din Al Razi
katika kuielezea hali ya Biismi Allah kulingana na Sharia za Fiqh na matumizi yake basi
tunaona kua:

1) Biismi Allah hua ni Fardhi: kuitamka pale Muislam anapotaka kuchinja mnyama
kwa ajili ya kula au anaporusha Upinde, Mshale, Risasi wakati wa kuwinda au
anapomuachia Mnyama wa kuwindia katika wakati wa kuwinda.
486

Na pia ni FArdhi kwa Mtizamo wa Madhhab ya Imam Muhammad Idris Al Shafii


kuisoma katika Sala unaposoma Surat Al Fatiha au Mwanzoni mwa Sura nyengine
yeyote isipokua Surat At Tawba ile kwa sababu Biismi Allah hua ni Moja kati ya aya ya
mwanzo katika kila Sura isipokua Surat At Tawba. Na kuisoma kwa Biismi Allahi kwa
Sala za Kutoa Sauti hua ni Wajib kwa kila Sura isipokua Surat At Tawba au unapoanza
katikati ya Sura. Kusoma Biismi Allahi kwa Sauti hua kunaulainisha Moyo wa Msomaji.

Kwani anasema Imam Abu Zakariyyah Sharaf An Nawawi kua: ‘Mtu anaetaka kusoma
basi asome Biismi Allah Rahmani Rahim mwanzoni mwa kila Sura isipokua Surat
Baraa’ah (At Tawba), kwa sababu wengi miongoni mwa Wanazuoni wamesema kua
hii ni aya popote pale itakapoandikwa ndani ya Mus-haf. Na imeandikwa mwanzoni
mwa kila Sura isipokua katika Surat At Tawbah. Hivyo kama atasoma mwanzoni
mwa kila Sura isipokua Surat At Tawba basi hua na uhakika kua amesoma Qur’an
nzima au Sura nzima. Na kama atakua hakusoma Biismi Allah basi atakua
ameiacha sehemu ya Qur’an na hii ni kutokana na mtizamo wa wengi miongoni
mwa Wanazuoni’

2) Biismi Allah hua ni Sunnah kuitamka wakati wa kusoma Surat Al Fatiha katika Sala
kulingana na mtizamo wa Madhab ya Hanafi ambao ni mtizamo wa Imam Abu Hanifa,
Imam Ibn Al Hammam na Imam Al Halabi.

3) Biismi Allah hua si Mustahab wala si Sunnah na wala si Makruh kuitamka katika
wakati wa kusoma Surat Al Fatiha katika Sala kulingana na Mtizamo wa Imam Abu
Yusuf.
4) Biismi Allah hua ni Makruh kuitamka katika wakati kuisoma Surat At Tawba
ambayo haina Biismi Allahi mwanzoni mwake, ila kwa Mtizamo wa Imam Al Ramli basi
hua ni Sunnah kuitamka unapoanza kati kati ya Sura hio ama kwa upande wa Imam Ibn
Hajar Al Asqalani basi hua ni Sunnah kuisoma mwanzoni mwa Surat Tawbah na ni
Makruh kuisoma wakati unapoanza kati kati ya Surat At Tawba.

Na pia hua ni Makruh kuitamka katika wakati wa kufanya mambo ambayo yana shaka
ndani yake kwa mfano kama kuvuta sigara.

5) Biismi Allah hua ni Mubah kuitamka wakati wa kuanza kutembea, kukaa kitako au
kusimama.

6) Biismi Allah hua ni Haram Kuitamka katika wakati wa kufanya mambo ya Haram,
Kuitamka wakati unapokua na Janaba, Unapokua na Hedhi au Nifasi pale unapokua na
nia ya kuisoma aya za Qur’an isipokua haiwi haram pale inapokua unafanya hivyo kwa
sababu yua kutabarruk au kwa ajili ya kufanya Dhikr.
487

Ama kwa upande wa Shaykh Muhammad Al Amin Ash Shanqeeti basi yeye anasema
kua: ‘Wanazuoni wametofautiana juu juu ya Biismi Allahi kua ni aya mwanzoni
mwa kila Sura au ni aya mwanzoni wa Surat Al Fatiha tu au ni aya kamili
inayojitegemea kama aya nyengine ama la.
Ama kulingana na aya isemayo:

﴾‫ٱﻪﻠﻟِ ٱﻟﱠﺮ ْﲪَـٰ ِﻦ ٱﻟﱠﺮِﺣﻴ ِﻢ‬


‫﴿إِﻧﱠﻪُ ِﻣﻦ ُﺳﻠَْﻴ َﻤﺎ َن َوإِﻧﱠﻪُ ﺑِ ْﺴ ِﻢ ﱠ‬
Innahu min Sulaymana wa-innahu bismi Allahi alrrahmani alrraheemi

Tafsir: Hii ni kutoka kwa Sulayman na hakika inasema Biismi Allahi Rahmani Rahim
(Surat An Naml 27:30)

Basi bila ya shaka hii ni moja kati ya aya za Qur’an na hii ni kulingana na
makubaliano ya Ijmaa. Ama kuhusiana na Surat Baraat (At Tawbah) Basi Biismi
Allahi sio miongoni mwa aya za Sura hio, lakini kuna kutofautiana kuhusiana na
hayo mambo mengine, kwani baadhi ya Wanazuoni wa Usul wamesema kua Biismi
Allahi si miongoni mwa Aya za Qur’an na baadhi wamesema kua ni miongoni mwa
Aya ya Surat Al Fatiha tu. Na pia wako wanaosema kua Biismi Allahi ni Aya
Mwanzoni mwa kila Sura, na huu ni Mtizamo wa Imam Muhammad Idris Al Shafii.

Baada ya kuangalia mitizamo hio basi tunaona kua kuna umuhimu mkubwa sana kua
unapoanza kufanya kitu chako na kauli ya Biismi Allahi katika kila jambo lako jema na
linaloruhusika Kisharia hua pia ni mwenye kuonesha Shukrani kwa Mola wako kutokana
na kukujaalia Neema zake zisizohesabika kutoka kwake, katika uhai wako hapa
Ulimwenguni na hivyo hua ni mwenye kuukubali uwezo mkubwa wa Mola wako juu ya
kila kitu alichokujaalia, huku yeye akiwa si mhitaji wa kitu chochote kutoka kwako.

Kwa maana hiyo basi Muislam anapokua ni mwenye kuzoea kuanza kufanya jambo kila
jambo lake kwa Biismi Allahi basi hua ni mwenye kujichunga sana, katika mambo yake,
na hivyo hua si mwenye kutaka kuingiza mambo yasiyofaa ndani ya jambo hilo, au
mambo ya haram na hivo kumharibia jambo lake hilo, kwani kusema Biismi Allahi hua
kunamkumbusha Muislam kua anaanza kufanya jambo ambalo lake hilo ambalo litapita
katika njia za halali na hivyo kupata Baraka na Neema zaidi kutokana na kua limo ndani
ya Maamrisho ya Mola wake na pia kwa kua hua haliendani kinyume na maamrisho ya
Mola wake.
Na ndio maana akasema Al Ghawth Al Adham Al Qutb Muhyi Ad Din Shaykh Abd Al
Qadir Al Jilani kua:
488

‘Biismi Allah hua ni Hazina ya wale Ambao ni wenye kukumbuka.


Biismi Allah hua ni Muhimu sana na ni ulinzi wenye nguvu kwa walio dhaifu.
Biismi Allah hua ni Nuru kwa wenye kupenda na ni furaha kwa wenye kua na hamu.
Biismi Allah hua ni Liwazo kwa maumbile ya Nafsi zetu.
Biismi Allah hua ni Ukombozi wa Miili yetu.
Biismi Allah hua ni Nuru inayong’arisha vifua vyetu.
Biismi Allah hua ni Mfumo wa kanuni unaoendesha kila jambo katika maisha yetu.
Biismi Allah hua ni Taji la kila mwenye kujiamini.
Biismi Allah hua ni Taa ya wenye kufikia malengo yao.
Biismi Allah hua ni Maridhio ya mahitajio ya mwenye kuhitaji.
Biismi Allah hua ni Jina la yule ambae anaempandisha darja mja mmoja na
kumshusha darja Mja mwengine.
Biismi Allah hua ni Jina la yule ambae anaeuhifadhi Moto wa Jahannam kwa ajili
ya kuwachoma maadui zake kama malipo yao na anauhifadhi Uzuri wa Pepo kwa
ajili ya miadi ya Marafiki zake.
Biismi Allah hua ni Jina la Yule ambae yuko peke yake asiekua na Mshirika.
Biismi Allah hua ni Jina la Mwenye kuishai milele bila ya kua na Mwisho.
Biismi Allah hua ni Jina la yule ambae mwenye uwezo wa Upekee bila ya kuhitaji
usaidizi.
Biismi Allah hua ni Dua ambayo hua ni utangulizi wa kila Sura katika Qur’an.’

Naam, tunapoangalia kwa upande wa I’lm Ruhaniyyat basi wanasema Wanazuoni wenye
I’lm hio kua: ‘Kuna Majina 3000 ya Allah Subhanah wa Ta’ala. Ambapo kati ya hayo
basi Majina 1000 ni yenye kujulikana na Malaika pekee, Majina 1000 mengine
pekee yanajulikana na Manabii, Majina 300 yametajwa kwenye Tawrat, Majina
300 yametajwa kwenye Injeel, Majina 300 Yametajwa kwenye Zabur na Majina 99
yametajwa kwenye Qur’an Tukufu. Hivyo Majina yote hua ni 2999. Jina moja
lililobakia linajulikana na Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ambae amemjuulisha
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam juu ya Jina hilo na limo katika Biismi Allahi
Ar Rahmani Rahim. Hivyo mwenye kuisoma aya hio basi hua ni sawa na mwenye
kupata malipo ya aliesoma majina hayo 3000’

Baada ya kuangalia maana na matumizi ya Jina la Allah kwa kifupi kulingana na


mitizamo ya wanazuoni mbali mbali basin a tuangalie maana ya jina la pili lililoomo
katika Biismi Allahi Rahmani Rahim ambalo ni Rahman na Rahim, ambayo ni majina
yanayotokana na mzizi mmoja wa neno Rahima ambalo hua ni lenye kumaanisha
Kupenda, Kua na Upole, Kua na Huruma, Kua na Ukarimu, kua na Wema, Kua na
Rehema.

Na kama kawaida tunapozungumzia Sifa za Majina Matukufu ya Allah Subhanah wa


Taa’ala kimaana basi hua tunnajaribu tu kuelezea kulingana na mtizamo wa ufahamu wa
Ibn Adam, kwani ukweli ni kua kama anavyosema Mujaddid Ad Din Hujjat ul Islami
489

Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali kua kwa
vyovyote vile tutakavyojaribu kuelezea maana ya Majina Matukufu ya Allah Subhanah
wa Ta’ala basi kamwe hatutoweza kuelezea maana yake kikamilifu kama inavyostahiki,
yaani tuchukulie mfano wa hili neno Rahman ambalo limetumika kwenye aya ifuatayo:

﴾‫ٱﳊُﺴ َ ٰﲎ‬ ‫﴿ﻗُ ِﻞ ْٱدﻋُﻮاْ ﱠ‬


ْ ‫ٱﻪﻠﻟَ أَ ِو ْٱدﻋُﻮاْ ٱﻟﱠﺮ ْﲪَـٰ َﻦ أ َّ�ً ﱠﻣﺎ ﺗَ ْﺪﻋُﻮاْ ﻓَـﻠَﻪُ ٱﻷ‬
ْ ْ ُ‫َﲰَﺂء‬
Quli odAAoo Allaha awi odAAoo alrrahmana ayyan ma tadAAoo falahu al-asmao
alhusna (Surat Al Isra 17:110)
Tafsir: Sema (Ewe Muhammad): Muombe Allah au Muombe Mwingi wa Rehma,
vyovyote vile utakavyomuomba kwani kwake yeye ndiko kwenye Umiliki wa Majina
Matukufu.
Naam, ayah hii ya Surat Al Israa inaweka wazi umuhimu wa kumuomba Allah Subhanah
wa Ta’ala kwa kutumia Majina yake Matukufu ambapo Jina la Al Rahman linamaanisha
Yule ambae ni mwenye Rehma nyingi sana kupita kiasi na hivyo kutokua na mfano wake
katika Rehma zake, kwani yeye si mwenye kua na Rehma pekee tu bali pia hua ni
mwenye kusababisha Rehma zake kuwafikia wale awatakao miongoni mwa waja wake
waliomuamini kama inavyosema aya ifuatayo:

ِ ‫﴿ﻫﻮ ٱﻟﱠ ِﺬى ﻳﺼﻠِّﻰ ﻋﻠَﻴ ُﻜﻢ وﻣﻼَﺋِ َﻜﺘُﻪ ﻟِﻴﺨ ِﺮﺟ ُﻜﻢ ِﻣﻦ ٱﻟﻈﱡﻠُﻤ‬
‫ﺎت إِ َﱃ ٱﻟﻨﱡﻮِر َوَﻛﺎ َن‬ َ َّ ْ َ ْ ُ ُ ََ ْ ْ َ َ ُ َُ
﴾ً‫ﲔ رِﺣﻴﻤﺎ‬ ِِ ِ
َ َ ‫ﺑﭑﻟْ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬
Huwa alladhee yusallee AAalaykum wamala-ikatuhu liyukhrijakum mina
aldhdhulumati ila alnnoori wakana bialmu/mineena raheeman (Surat Al Ahzab
33:43)

Tafsir: Ni yeye ambae ndie mwenye kukusalia na Malaika wake, ili akutoe kutoka
katika kiza na kukuingiza katika Nuru. Na ni yeye ambae kwa Waumini ni Mwingi wa
Rehma.

Kulingana na aya hizi basi tunaona kua Ar Rahman maana yake ni mwenye sifa ya kua
na Rehma na Ar Rahim maana yake hua kutoa Rehma. Na kulingana na mtizamo wa
Shaykh Al Akbar Imam Muhyidiin Ibn Al Arabi basi yeye anasema kua kuna: ‘Neno Ar
Rahma lina athari mbili ambapo ya kwanza ni Athar bi al Dhat na Athar bi al Sual.
490

Na tunapozungumzia Athar bi al Dhat basi hua tunazungumzia athari inayotokana


na bainisho la Rehma za Allah Subhanah wa Ta’ala kupitia katika sifa za Rehma
hizo. Kwani kimaumbile basi viumbe vyote vilivyopo hua ni vyenye kuanisha sifa
ya kuwepo kwa Rehma zake. Ama kwa mtizamo mwengine basi tunapozungumzia
Athar bi al Sual basi hua tunazungumzia athari ya Rehma ilivyogaiwa kwa viumbe.
hususan kwa viumbe Ibn Adam ambao wao hua ni wenye kupewa Rehma kulingana
na jithada zao, kwa mfano pale wanapoomba kama inavyosema aya ifuatayo: ’

‫َﻧﺖ َﺧْﻴـُﺮ‬ ِ ِ ِ ِ ‫﴿إِﻧﱠﻪ َﻛﺎ َن ﻓَ ِﺮ‬


َ ‫ﻳﻖ ّﻣ ْﻦ ﻋﺒَﺎدى ﻳَـ ُﻘﻮﻟُﻮ َن َرﺑـﱠﻨَﺂ َآﻣﻨﱠﺎ ﻓَﭑ ْﻏﻔْﺮ ﻟَﻨَﺎ َو ْٱر َﲪْﻨَﺎ َوأ‬
ٌ ُ
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ٱﻟﱠﺮاﲪ‬
Innahu kana fareequn min AAibadee yaqooloona rabbana amanna faighfir lana
wairhamna waanta khayru alrrahimeena (Surat Al Muuminun 23:109)

Tafsir: ‘Bila ya shaka walikua ni miongoni mwa Makundi ya Waja wangu ambao
walikua wakisema: ‘Ewe Mola wetu! Hakika sisi tumekuamini, Hivyo tusamehe, na
utuingize katika Rehma zako, kwani kwa hakika wewe ni m-bora wa wenye kua na
Rehma.’

Yaani kutokana na jitihada hizo za kumuomba Mola wao basi Allah Subhanah wa Ta’ala
hua ni mweye kuwaingiza watu hao kwenye Rehma zake, kwani watu hao hua
wanajulikama kama Ahl al Hadhrah yaani watu ambao wameingia kwenye hadhara ya
Mola wao.

Sultan Al Mutakkalimin Mujaddid ad Din Imam Al Ghazali al Thani Imam Fakhr ad Din
Al Razi kua: ‘Katika Biismi Allahi’ kuna harfu 19, ambazo ni sawa na idadi ya
Malaika wa Jahannam ambao ni 19 hivyo kila unaposema Biismi Allahi basi unakua
na matumaini ya kuvuka kizuizi cha adhabu ya kila mmoja kati ya Malaika hao 19
wa Moto.’ (Na huo pia ndio mtizamo wa Mujaddid Ad Din Shaykh ul Islami Al Hafidh
Shaykh Ibn Hajar Al Asqalani katika kitabu chake Al Majmaa Al Muasisi na pia Imam
Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi katika
Ahkam Al Quran na Mujaddid Ad Din Imam Abd Rahman Al Suyuti katika Al Durr al
Mandhur)
Tunaingia katika maana ya Biismi Allahi Ar Rahmani Al Rahim ambapo tunaona kua
Hujjat Al Islami Mujaddid Ad Din Az Zuhruf ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn
Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali anasema kua: ‘Katika ayah hii basi tunaona
kua ndani yake mmejumuishwa Ilm yote inayohusiana na Sifa za Majina Matukufu
za Allah Subhanah wa Ta’ala, na Ilm ya Sifa za Ar Rahmani Ar Rahim
491

zimejumuishwa kwani hizi ni Sifa ambazo zimezipita Sifa zote Tukufu Kiuwezo na
Kiilm. Na Sifa mbili hizi hua ni zenye kuleta hali ya hisia nzuri na zinazovutia
tofauti na nyengine ambazo hua zinaamsha Ghadhabu au Khofu.’

Ama kulingana na mtizamo wa Shaykh Al Akbar Imam Ibn Arabi basi tunaona kua yeye
anasema kua: ‘Jina la Al Rahman hua ni Sifa yenye kujumuisha ukubwa kamilifu wa
Hikma zake kuhusiana na Ulimwengu mzima kulingana na mapokezi ya mwanzoni
mwa yule alie wa mwanzo. Al Rahim hua ni Sifa inayojumuisha ukubwa kamilifu
kimaana kwa ajili ya Ibn Adam kuhusiana na Mwishoni mwa yule alie wa mwisho.
Na hii ni kwa sababu wanasema wenye kujua kua: Ya Rahman hua ni kwa ajili ya
Dunia na Akhera na Ya Rahim hua ni kwa ajili ya Akhera. Hii inamaanisha
kuunyanyua Ukamilifu wa Ibn Adam na kuwakirimu kwa hali zote za ki ujumla na
kimahsusi kwa kila mmoja, na ni kudhihirisha Sifa ya Allah.’

Ama kwa upande wa Imam Nasir Ad Din Al Khayr Abd Allah Ibn Umar Al Baydawi
anasema kua: ‘Maneno haya mawili Al Rahmani Al Rahim hua yanathibtisha
thamani ya mubalagha (kutoa maana yenye uzito mkubwa wa kitu) kuhusiana na
Rehma. Kwani sifa ya Al Rahman hua ni yenye kujumuisha jumla ya Rehma za
Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kila kitu katika Ulimwengu huu, kwa Waumini na
wasiokua Waumini, kuhusiana na hali ya Maisha, Riziki, Afya, Akili, Ufahamu, n.k.
na Al Rahim hua inajumuisha Sifa za Allah Subhnah wa Ta’ala anaetoa fadhila zake
kwa Waumini, kwa kuwaongoza katika uongofu, Imani, Kufanya Mema na
kuachana na Maovu katika uhai wa Ulimwenguni, na hapo hapo kuwalipa furaha
ya Milele na mafanikio ya kweli kesho Akhera.’

Ama kwa upande wa Amir ul Muuminin Fi Al Hadith Imam Abdullah Ibn Mubarak basi
yeye anasema kua: ‘Al Rahman maana yake ni yule Mwenye Kujibu kama ikiwa
utamuuomba, na Al Rahim maana yake hua ni yule mwenye Hasira kali usipo
muomba’
Na pia kuna wasemao kua Al Rahman maana yake hua ni kutoa riski kwa Viumbe wake
na Al Rahim ni mwenye Kusamehe Dhambi za Walimuamini. Hivyo basi mtegemee
Allah Subhanah wa Ta’ala katika kutafuta riski yako, na mtegemee yeye katika
kusamehe kasoro zako. Kwani kimaumbile Ibn Adam hua ni mwenye hali tatu zifuatazo:

‘Kwanza ni hali ya kutokuwepo kwa kiumbe kinachohitaji kuwepo. Pili ni hali ya


kuishi kwa kiumbe anaetaka kuwepo Milele na Tatu ni hali ya mtu anaehitaji
Usamehevu katika uhai wa Akhera, hivyo mja hua ni mwenye kumhitaji Mola wake
na Sifa zake katika kutafakkari majina haya ambayo ni: Allah ambae ndie Mwenye
kumjaalia Mja huyo kuwepo kwake, Al Rahman ambae ndie anaetoa Riski kwa ajili
ya Mja wake kuendelea na Uhai wake na Al Rahim ambae ndie mwenye Kusamehe
Kasoro na makosa ya Mja katika siku ya Malipo’
492

Anasema Baddiuzzamman Said Nursi katika Risale Nuri kua: ‘Kauli ya Biismi Allahi
imejaa Baraka ya hazina kiasi ya kua kutokana na kukuunganisha na Allah
Subhanah wa Taa’ala basi hukubadilishia udhaifu wako na umasikini na kuuingiza
katika ukumbi wa Allah Subhanah wa Ta’ala. Hivyo mtu anaenza jambo lake na
Biismi Allahi basi hua ni mwenye kufanya jambo lake kwa jina la Mola wake na
hivyo hua ni sawa na anajiunga na Jeshi na kisha akawa ni mwenye kufanya mambo
hayo chini ya ngao ya jina la Taifa husika. Hua si mwenye kua na khofu na yeyote,
kwani hufanya kila jambo lake kwa jina la Shariah husika na hivyo kua na ngao
imara dhidi ya yeyote atakaepingana nae’

Baada ya ufafanuzi wa Biismi Allahi Al Rahmani Al Rahim basi tunaendelea na aya zetu
ambazo zinasema;

‫ﻚ ٱﻟْ ُﻘْﺮآ َن ﻟِﺘَ ْﺸ َﻘ ٰﻰ۞ إِﻻﱠ ﺗَ ْﺬﻛَِﺮًة ﻟِّ َﻤﻦ َﳜْ َﺸ ٰﻰ۞ ﺗَﻨ ِﺰﻳﻼً ِّﳑ ْﱠﻦ‬ َ ‫﴿ﻃﻪ ۞ َﻣﺂ أَﻧَـَﺰﻟْﻨَﺎ َﻋﻠَْﻴ‬
‫ٱﺳﺘَـ َﻮ ٰى ۞ ﻟَﻪُ َﻣﺎ ِﰱ‬ ِ
ْ ‫ض َوٱﻟ ﱠﺴ َﻤ َﺎوات ٱﻟْﻌُﻠَﻰ۞ ٱﻟﱠﺮ ْﲪَـٰ ُﻦ َﻋﻠَﻰ ٱﻟْ َﻌْﺮ ِش‬ َ ‫َﺧﻠَﻖ ٱﻷ َْر‬
ِ ِ ‫ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬
ُ‫ﺖ ٱﻟﺜـَﱠﺮ ٰى۞ َوإِن َْﲡ َﻬْﺮ ﺑِﭑﻟْ َﻘ ْﻮل ﻓَِﺈﻧﱠﻪ‬ َ ‫ض َوَﻣﺎ ﺑَـْﻴـﻨَـ ُﻬ َﻤﺎ َوَﻣﺎ َْﲢ‬ ِ ‫ات َوَﻣﺎ ِﰱ ٱﻷ َْر‬ ََ
ِ ۤ ِ
‫ﻳﺚ‬
ُ ‫ٱﳊُ ْﺴ َ ٰﲎ۞ َوَﻫ ْﻞ أ ََﺎﺗ َك َﺣﺪ‬ ْ ُ‫َﲰَﺂء‬ ْ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻻ إِﻟَـٰﻪَ إِﻻﱠ ُﻫ َﻮ ﻟَﻪُ ٱﻷ‬ ‫َﺧ َﻔﻰ۞ ﱠ‬ ْ ‫ٱﻟﺴﱠﺮ َوأ‬
ّ ‫ﻳَـ ْﻌﻠَ ُﻢ‬
﴾‫ﻮﺳ ٰﻰ‬َ ‫ُﻣ‬
Ta-Ha; Ma anzalna AAalayka alqur-ana litashqa; Illa tadhkiratan liman yakhsha;
Tanzeelan mimman khalaqa al-ardha waalssamawati alAAula; Alrrahmanu AAala
alAAarshi istawa; Lahu ma fee alssamawati wama fee al-Ardhi wama baynahuma
wama tahta alththara; Wa-in tajhar bialqawli fa-innahu yaAAlamu alssirra
waakhfa; Allahu la ilaha illa huwa lahu al-asmao alhusna, Wahal ataka hadeethu
Moosa (Surat Ta-Ha 20:1-9)

Tafsir: Ta-Ha, Kwa Hakika hatukuiteremsha hii Qur’an kwa ajili ya kukuingiza katika
Khofu, Ila huu ni ukumbusho kwa wenye kua na khofu. Imeteremshwa kutoka kwa
Muumba wa Ardhi na Mbingu alietukuka. Mwingi wa Rehma kwenye ya Arshi
amesimama. Ni vyake vilivyomo Mbinguni na Ardhini na baina yake na vilivyomo
chini ya udongo wake. Na hata kama wewe (Muhammad) utanyanyua sauti yako basi
kwa hakika yeye, anajua yaliyo ya siri na yale ambayo yamefichikana zaid. Hakuna
493

Mungu isipokua yeye. Na kwake yeye ndio kwenye umiliki wa Majina Bora. Na jee
imekufikia wewe Hadith ya Musa?

Tunapoangalia maana ya aya hizo hapo juu na mazingira, wakati na sababu za kushushwa
kwake, basi tunaona kua maana ya neno Ta-Ha ambalo ndio jina la Sura na pia ndio neno
la kwanza la Sura basi hua linaenda sambamba kimaana na namna lilivyofafanuliwa na
Imam Muhhib Ad Din Abu Al Faid Al Murtada katika Taj Al Arusi ambayo kama
tulivyoona kua hua ina maanisha: Kua na Utulivu, Tulia au Poa kwani kinachofuata
mbele yake ni hoja zinazoelezea yaliyowafika miongoni mwa Mitume waliotangulia na
kufikwa na mitihani mingi kabla ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam lakini
hata hivyo Mitume na Manabii hao wakawa na azma na Subra kubwa katika kutekeleza
majukumu yao waliyopewa na Mola wao katika maisha yao hapa Duniani, na hivyo
Surah hii kua ni yenye kumliwaza Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam, pale aya ya
9 ya Sura hii iliposema katika njia ya kuhoji na kuthibitisha:

﴾‫ﻮﺳ ٰﻰ‬ ِ
ُ ‫﴿ َوَﻫ ْﻞ أ ََﺎﺗ َك َﺣﺪ‬
َ ‫ﻳﺚ ُﻣ‬
Wahal ataka hadeethu Moosa (Surat Ta-Ha 20:9)

Tafsir: Na jee imekufikia wewe Hadith ya Musa?

Naam, kulingana na mitizamo wa Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi
yeye anasema kua: ‘Miongoni mwa Sura za Makka, basi inawezekana ikawa hii ni
aya ambayo inaonesha kua hii ni sehemu ambayo kwa mara ya kwanza Nabii Musa
anazungumziwa katika Qur’an na ndio maana ikawa ipo katika hali ya kuhoji kua
Jee imekufikia wewe hadith ya Musa?’

Ingawa aya ipo katika hali ya kuhoji lakini hapo hapo ipo katika hali ya kuthibitisha kua
anaeulizwa ambae ni Nabii Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam kua hajafikiwa na
Hadith hio na hivyo basi aya zinazofuatia baada ya hio zinaanza kwa kufafaunua kisa
chake Nabii Musa Alayhi Salam, ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anatuwekea wazi
kwa kusema kua:

﴾ً‫ﻮﺳ ٰﻰ إِﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن ﳐُْﻠَﺼﺎً وَﻛﺎ َن ر ُﺳﻮﻻً ﻧﱠﺒِﻴّﺎ‬ ِ ِ ِ


َ َ َ ‫﴿ َوٱذْ ُﻛْﺮ ﰱ ٱﻟْﻜﺘَﺎب ُﻣ‬
Waodhkur fee alkitabi Musa innahu kana mukhlissan wa kana Rasulan Nabiyyan
(Surat Maryam 19:51)
Tafsir: Na ametajwa katika Kitabu Musa. Hakika yeye alikua ni aliechaguliwa na
akawa Rasul na Nabii.
494

Ama kuhusiana na Nabii Musa basi jina lake ni Musa Ibn Imran Ibn Izhar Ibn Kuhath
Ibn Levi Ibn Yaqub Ibn Is-haq Ibn Khalilu Allahi Ibrahim Alayhi Salaam. Familia ya
Mzee Imran ambapo kwa lugha ya Kiyahudi hua anaitwa Amram (Maana ya neno
Amram kwa lugha ya Kiyahudi hua ni Rafiki wa Mungu Mtukufu) ilikua inajumuisha
mke wake mzee Imran ambae alikua akiitwa Najib Bint Shamwil Ibn Barakiyah Ibn
Yashan Ibn Khalilu Allahi Ibrahim Aálayhi Salam. Ambae ndie mama yake Nabii Musa,
Nabii Harun na dada yao anaeitwa Maryam. Kwa upande wa Mama yake Nabii Musa
basi kuna kutofautiana kimtizamo kwani kuna wasemao kua jina lake ni Yuhanz, kuna
wasemao kua ni Najiyah na pia kuna wasemao kua ni Yukhail.
W Allahu Aálam!

Lakini mimi kwa upande wangu basi nitakua ni mwenye kutumia jina la Yuhanz tangu
mwanzo wa kisa hiki hadi mwisho wake katika kila mara nitakapokua nikimzungumzia
Mama yake Nabii Musa. Naam..Allah Subhanah wa Ta’ala anaendelea kumwambia
Nabii wake Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam juu ya Nabii Musa kwa kusema:

ْ ِ‫ﻮﺳ ٰﻰ َوﻓِْﺮ َﻋ ْﻮ َن ﺑ‬ ِ ِ َ ‫ﲔ۞ ﻧَـْﺘـﻠُﻮاْ َﻋﻠَْﻴ‬ ِ َ‫ت ٱﻟْ ِﻜﺘ‬ ۤۤ


‫ﭑﳊَِّﻖ‬ َ ‫ﻚ ﻣﻦ ﻧـﱠﺒَﺈ ُﻣ‬ ِ ِ‫ﺎب ٱﻟْﻤﺒ‬
ُ ُ �‫آ‬َ ‫ﻚ‬ َ ‫﴿ﻃﺴﻢ۞ ﺗِْﻠ‬
ً‫ﻒ ﻃَﺂﺋَِﻔﺔ‬ ِ ْ َ‫ض وﺟﻌﻞ أَﻫﻠَﻬﺎ ِﺷﻴﻌﺎً ﻳﺴﺘ‬ ِ ِ ِ‫ﻟَِﻘﻮٍم ﻳـﺆِﻣﻨﻮ َن ۞ إِ ﱠن ﻓ‬
ُ ‫ﻀﻌ‬ َْ َ َ ْ َ
َ ََ ْ ‫َر‬ ‫ﻷ‬ ‫ٱ‬ ‫ﰱ‬ ‫ﻼ‬
َ ‫ﻋ‬
َ ‫ن‬َ ‫ﻮ‬ ‫ﻋ‬
َ
ْ ْ ‫ﺮ‬ ُ ُْ ْ
‫ﻳﺪ أَن ﱠﳕُ ﱠﻦ‬ ُ ‫ﻳﻦ ۞ َوﻧُِﺮ‬ ِِ ِ ِ ِ ِ ِ
َ ‫ّﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ ﻳُ َﺬﺑّ ُﺢ أَﺑْـﻨَﺂءَ ُﻫ ْﻢ َوﻳَ ْﺴﺘَ ْﺤِﲕ ﻧ َﺴﺎءَ ُﻫ ْﻢ إﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻤ ْﻔﺴﺪ‬
‫ﲔ ۞ َوُﳕَ ِّﻜ َﻦ َﳍُْﻢ‬ ِ ِ ِ ‫ﻀﻌِ ُﻔﻮاْ ِﰱ ٱﻷ َْر‬ ِ‫ﱠ‬
َ ‫ض َوَْﳒ َﻌﻠَ ُﻬ ْﻢ أَﺋ ﱠﻤﺔً َوَْﳒ َﻌﻠَ ُﻬ ُﻢ ٱﻟْ َﻮا ِرﺛ‬ ْ ُ‫ٱﺳﺘ‬
ْ ‫ﻳﻦ‬ َ ‫َﻋﻠَﻰ ٱﻟﺬ‬
﴾‫ﻮد ُﳘَﺎ ِﻣْﻨـ ُﻬﻢ ﱠﻣﺎ َﻛﺎﻧُﻮاْ َْﳛ َﺬرو َن‬ ِ ‫ض وﻧُِﺮ‬ ِ
ْ َ ُ‫ى ﻓْﺮ َﻋ ْﻮ َن َوَﻫ َﺎﻣﺎ َن َو ُﺟﻨ‬ َ َ ِ ‫ﰱ ٱﻷ َْر‬
Ta Sin-Mim; Tilka ayatu alkitabi almubeeni; Natloo AAalayka min naba-i Moosa
wafirAAawna bialhaqqi liqawmin yu/minoona; Inna firAAawna AAala fee al-
Ardhi wajaAAala ahlaha shiyaAAan yastadhAAifu ta-ifatan minhum yudhabbihu
abnaahum wayastahyee nisaahum innahu kana mina almufsideena; Wanureedu an
namunna AAala alladheena istudAAifoo fee al-Ardhi wanajAAalahum a-immatan
wanajAAalahumu alwaritheena; Wanumakkina lahum fee al-Ardhi wanuriya
firAAawna wahamana wajunoodahuma minhum ma kanoo yahdharoona(Surat Al
Qasas 28:1-6)

Tafsir: Ta-Sin-Mim Hizi ni aya za Kitabu kinachobainisha. Tunakusomea juu yako


kuhusiana na habari za Musa na Fir’awn kwa Ukweli, kwa watu wenye kuamini. Kwa
hakika Fir’awn alijipandisha darja katika ardhi, na akawafanya watu wake kua ni
waliogawanyika akawadhoofisha baadhi miongoni mwao, kwa kuwaua watoto wao wa
495

kiume na kuwaachia watoto wao a kike kua ni wenye kuishi. Kwa hakika yeye alikua
ni miongoni mwa mafisadi. Nasi tukataka kuwasaidia wale ambao walikua dhaifu
katika Ardhi (hio) na kuwafanyya kua ni Watawala na Warithi. Na kuwaanzilisha
katika Ardhi na tukamfanya Fir’awn na wenyeji wake kupata kile ambacho
wanakikhofia.

Ama kuhusiana na eneo la Ardhi iliyotajwa katika aya hizi basi nasema Sultan Al Balagha
Imam Abu Al Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Haya ni maeneo ya Ardhi za Misri na
Sham lakini bila ya kujumuisha maeneo ya Madyan.’

Kama tulivyoona katika kisa cha Nabii Ibrahim Aálayh Salam basi ni kua Ardhi ya nchi
ya Misri ilikua na utawala wa Kifalme tangu zamani sana, ambapo mmoja kati ya watu
wa Misri ni Hajar ambae ni mama yake Nabii Ismail Aálayhi Salam.

Na Nabii Musa alizaliwa katika Ardhi ya nchi ya Misri baada ya wazee wake
wanaotokana na Levi ambae ni mtoto wa na Nabii Yaqub Alayhi Salam kuhamia katika
Ardhi ya nchi hio kutokana na mualiko wa Nabii Yusuf Ibn Nabiyyu Allahi Yaqub Ibn
Nabiyu Allahi Is-haq Ibn Khallilu Allahu Nabiyyu Allahi Ibrahim Alayhim Salam. Hivyo
kutokana na mualiko huo basi kizazi cha Nabii Yaqub ambae ndie muanzilishi wa ukoo
wa Bani Israil kikawa ndio asili ya watu wa Bani Israil kua ni wenye kuishi katika Ardhi
ya Misri.

Baada ya kufariki Nabii Yusuf Alayhi Salaam, basi watu wa Bani Israil waliokua wakishi
katika Ardhi ya Miasri walikua ni watu 80, hawa walikua ni watu ambao waliambiwa na
Nabii Yusuf kua, wataishi salama wa salimina na watu Al Aqbat wa Misri, lakini baadae
watu hawa wa Bani Israil watakua ni wenye kujiona na kua na Kibri na hivo hawatokua
ni wenye kukatazana mabaya na hapo ndipo mambo yatakapobadilika na hivyo watu wa
Bani Israil watakua ni wenye kutawaliwa na kufanywa Watumwa na watu hao wa Misri.
Nabii Yusuf aliwaambia kua hali hii haitobadilika hadi pale atakapozaliwa mtoto aitwae
Amran ambae nae atapata mtoto aitwae Musa ambae atakua na mwili mkubwa wenye
nguvu, mrefu na mwenye ngozi yenye rangi kama ya Ngano, Musa huyu Ibn Imran
atakua ni Mtume wa Allah Subhanah wa Ta’ala na ndie atakaewaokoa Watu wa Bani
Israil kutokana na madhila ya watu wa Misri.

Hivyo baada ya kufariki Nabii Yusuf basi haukupita mda mrefu isipokua watu wa Bani
Israil wakaanza kuwaita watoto wao kwa jina la Imran, na mtoto huyo aitwae Imran
ikawa akipata mtoto wa kiume basi hua ni mwenye kumwita kwa jina la Musa, huku
wakitegemea kua Musa huyo ndio atakua ni Nabii Musa alietabiriwa na Nabii Yusuf.
Hali hii iliendelea mpaka Imran na Musa yakawa ni majina yaliyoenea Miongoni mwa
watu wa Bani Israil. Tofauti ya miaka baina ya Nabii Yusuf na Nabii Musa ni miaka 400.
496


ASILI YA FIR’AWN NA HAMMAN.


Neno Fir’awn ni lenye kutokana na neno Far’aa ambalo kwa Lugha ya Kiarabu hua
linamaanisha Kupanda juu zaid, Kushuka chini zaidi au Kupita zaidi ya. Neno Far’aa
ndio lilitoa neno Far’ia ambalo hua ni lenye kumaanisha Mtu mwenye Nywele Nyingi
sana kupita Kiasi. Na pia ndio lililotoa neno Far’un ambalo hua ni lenye kumaanisha Kitu
kilichochipua au kuchomoza, kama Nywele iliyochomoza, Tawi la mti au Majani. Kama
vile ilivyotumika katika aya ifuatayo ya Mithali:

ٍ ِ
ٌ ِ‫َﺻﻠُ َﻬﺎ َﺎﺛﺑ‬
‫ﺖ َوﻓَـْﺮﻋُ َﻬﺎ ِﰱ‬ ْ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻣﺜَﻼً َﻛﻠ َﻤﺔً ﻃَﻴِّﺒَﺔً َﻛ َﺸ َﺠﺮةٍ ﻃَﻴِّﺒَﺔ أ‬
‫ب ﱠ‬ َ ‫ﺿَﺮ‬ َ ‫﴿أََﱂْ ﺗَـَﺮ َﻛْﻴ‬
َ ‫ﻒ‬
﴾‫ﺂء‬ِ ‫ٱﻟ ﱠﺴﻤ‬
َ
Alam tara kayfa dharaba Allahu mathalan kalimatan tayyibatan kashajaratin
tayyibatin asluha thabitun wafarAAuha fee alssama/-I. (Surat Ibrahim 14:24)

Tafsir: Jee hujaona namna Allah anavyopiga mifano, kauli nzuri hua ni kama mti
ambao asili yake (mizizi yake) iko thabit (imekomaa ardhini) na umechipua kuelekea
juu angani.

Neno Far’aa ndio lililotoa neno Fir’awn ambalo hua ni lenye kumaanisha Darja ya Mtu
aliejuu zaidi katika Mamlaka ya Utawala wa Misri. Ama kwa upande wa Lugha ya Aqbat
jina la Fir’awn hua linatokana na neno Fer’aa ambalo hua linamaanisha Kasri au Jumba
Kubwa ambalo lilikua ndio makazi ya Utawala wa Mfalme wa Misri na baadae jina hilo
likahama kimatumizi na kua ni lenye kutumika kwa ajili ya mmiliki mwenye kuishi ndani
ya Jumba hilo ambae alikua ni Mfalme, hivyo akawa anaitwa Fer’aa.

Na tunapoiangalia Qur’an pale ilipokua ikizungumzia Watawala wa Misri basi haikuwahi


kutumia Jina la Fir’awn kwa Mtu yeyote isipokua kwa yule Mtawala alietajwa katika kisa
cha Nabii Musa Alayhi Salam kumaanisha Mfalme wa Misri wa wakati huo wa kipindi
cha Nabii Musa kwani hata ilipokua ikizungumzia kisa cha Nabii Yusuf Alayhi Salam
basi ilikua ikimtaja Mfalme Al Rayyan ambae alikua ndie Mfalme wa Misri basi haikua
ikimwita kwa jina la Fir’awn bali ilikua ikimwita kwa jina la Malik (Mfalme) kwa mfano
iliposema kwenye aya ifuatayo:
497

‫ﻚ ٱﻟْﻴَـ ْﻮَم ﻟَ َﺪﻳْـﻨَﺎ‬ َ َ‫ﺼﻪُ ﻟِﻨَـ ْﻔ ِﺴﻰ ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ َﻛﻠﱠ َﻤﻪُ ﻗ‬
َ ‫ﺎل إِﻧﱠ‬
ِ ‫ﺎل ٱﻟْﻤﻠِﻚ ٱﺋْـﺘ ِﻮﱏ ﺑِِﻪ أ‬
ْ ‫َﺳﺘَ ْﺨﻠ‬
ْ ُ ُ َ َ َ‫﴿ َوﻗ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ ‫ﻣ ِﻜ‬
ٌ ‫ﲔ أَﻣ‬ ٌ َ
Waqala almaliku i/toonee bihi astakhlishu linafsee falamma kallamahu qala innaka
alyawma ladayna makeenun ameenun (Surat Yusuf 12:54)

Tafsir: Na akasema Mfalme: Mleteni (Yusuf) Kwangu Nitamuachia huru kwa Ajili
yangu Na Kisha alipozungumza nae akasema. Kwa Hakika Leo hii Wewe uko pamoja
nasi katika darja ya Juu na mwenye Kuaminika

Ama kuhusiana na historia ya Fir’awn wa wakati wa kipindi cha Nabii Musa basi tunaona
kua kuna mitizamo tofauti juu ya asili yake Fir’awn huyo kwani kuna mtizamo usemao
kua:

Fir’awn wa wakati wa Nabii Musa hakua ni Mtu mwenye asili ya Misri bali alikua ni
mwenye asili ya Khurasan ambayo ni maeneo ya Asia ya kati baina ya maeneo ya kusini
mwa Ardhi ya Urusi katika nchi za Azerbaijan, Uzbekistan na Kazakhstan na kaskazini
mwa maeneo ya Ardhi ya Afghanistan, Pakistan, Iran. Mji aliotoka Fir’awn huyu ulikua
ukujilikana kama Balkh ambao upo nchini Afghanistan.

Mwaka mmoja katika kipindi cha Kiangazi, maeneo ya Ardhi ya Khurasan kulitokea
ukame na kukuwa na njaa kali sana, kiasi ya kua watu wakawa wanahaha kutafuta
chakula na hivyo wakawa wanahama kutoka katika maeneo ya Ardhi hio na kuhamia
katika maeneo mengine ambayo kulikua na uafadhali wa kupatikana chakula. Hivyo
miongoni mwa watu walioamua kuhama katika maeneo hayo ni Fir’awn ambae yeye
aliamua kuelekea katika maeno ya Ardhi ya Misri ambako kulikua hakuna shida ya njaa.
Katika safari yake hio akapitia katika Mji wa Bushanj na akakutana na Hamana ambae
yeye alikua ni mfanya biashara wa Mikate katika mji huo.

Fir’awn aliingia katika duka la mikate la Hamman na kutaka kununua mkate. Hivyo
Hamman akamuuliza Fir’awn: ‘Unaonekana kama ni mgeni katika mji huu, jee wewe
ni mtu wa wapi na unaelekea wapi?’ Fir’awn akasema kweli: ‘Naam kweli mimi si
mtu wa hapa, mimi ni mtu wa Balkh, na niko safarini kuelekea Misri.’

Na ingawa Hamman alikua ni muuza mikate lakini alikua ni mtu mwenye Ilm ya utabiri
na aliwahi kuona katika kuangalia kwake kupitia katika moja kati ya Ilm zake kua katika
Ardhi ya nchi Misri kutakua na Mfalme mpya, na yeye Hamman atakua Waziri wa fedha
498

wa Mfalme huyo, lakini akawa hajui itakuaje kwani yeye ni mtu wa Busanj, Khurasan,
ila ili awe na wadhifa wa Uwaziri huo basi kwanza inambidi afunge safari kuelekea Misri
ambayo si safari ndogo kwani kuna umbali wa maelfu ya kilomita mpaka afike huko.

Hivyo Hamman alipomuona Fir’awn na kumuuliza na kumwambia kua anaelekea Misri


basi Hamman akajua kua huyu ndie mtu anaefaa kuenda na mimi nchini Misr. Fir’awn
alikau si mtu ambae ni mwenye kujua kusoma, hivyo Hamman akamwambia Fir’awn:
‘Hata mimi pia nataka kuelekea huko huko Misri lakini kwanza inabidi kuna
mambo mawili matatu nataka kumalizana nayo, kama utaweza kunisubiri basi
tutaenda pamoja’.

Fir’awn akatafakari kIsha akamuuliza: ‘Kwani unataka kumalizana na nini?’


Hamman: akajibu: ‘Kabla ya kusafiri kwanza basi inanibidi niviuze vitu vyangu
vyote, kwani nikiondoka basi sitaki kurudi tena hapa.’ Fir’awn akamwambia
Hamman: ‘Kama una uhakika kua utaviuza na kisha utasafiri kuelekea Misri basi
hamna tatizo mie nitakusubiri, ili tusafiri pamoja.’

Hivyo Hamman akauza vitu vyake vyote, kisha wote wawili kwa pamoja wakafunga
safari kuelekea katika Ardhi ya Mji wa Misri, na walipofika huko basi wakanunua
shamba na wakawa wanalima Matikiti. Na baada mda Matikiti yalipopea, Hamman
akaenda nayo sokoni kuyauza, lakini watu wa Misri wakawa hawataki kununua na badala
yake wakawa wanayachukua bure. Hivyo kwa siku hio Hamman akarudi mikono mitupu
kwa Fir’awn, na akamueleza Fir’awn juu ya tabia za watu hao wa Misri alizoziona
alipofika sokoni ni kua watu hao hawataki kununua chakula, na badala yake wanachukua
bure lakini hata hivyo wanapenda kununua Mavazi tu.

Hivyo siku ya pili, Fir’awn akatoka nae Hamman pamoja hadi sokoni na walipofika,
watu wakaja kuchukua Matikiti, walipoanza kuchukua Fir’awn akamwambia Hamman:
‘Kuanzia sasa hivi kila mtu atakaechukua Tikiti basi na sisi tumpokonye Kilemba
au Kofia yake.’ Kuanzia siku hio ikawa Fir’awn na Hamman wakitoka asubuhi na
Matikiti basi jioni hua ni wenye kurudi na Vilemba na Kofia nyingi sana. Baada ya mda
Matikiti yao yakamalizika, na hivyo wakaanza kuuza Vilemba na Kofia. Hii ilikua ni
biashara nzuri sana na yenye faida sana kwao wao na maisha yao ghafla yakabadilika na
wakawa ni watu wenye fedha nyingi sana.

Hivyo Fir’awn an Hamman wakanunua Farasi na Silaha kisha katika ardhi ya shamba
lao wakaruhusu kua iwe ni sehemu ya kuzikia watu waliokufa, lakini kwa malipo ya
kipande kimoja cha Dhahabu kwa kila maiti, hali hii iliendelea kwa mda na wao wakawa
wanajikusanyia Dhahabu, hadi siku moja akafariki Mtoto wa Mfalme wa Misri. Watu
walipofika makaburini basi Fir’awn na Hamman wakamzuia Maiti huyo kua asizikwe,
hadi watakapolipwa vipande viwili vya dhahabu.
499

Mfalme akauliza: ‘Kwa nini mnatoza ushuru kwa ajili ya kuzikia?’ Fir’awn akahoji:
‘Na kwa nini tusitoze ushuru wakati hii sehemu ya Ardhi ni yetu?’. Hivyo Mfalme
akavutiwa sana na ubunifu wa Fir’awn, na hivyo akamlipa vipande viwili vya dhahabu
na kisha akawachagua Fir’awn na Hamman kua washauri katika Utawala wake.

Fir’awn akawa na ukaribu sana na Mfalme, na watu wakawa wanamsikiliza sana Fir’awn
kwani alikua ni Mwenye Misimamo yenye kuleta Maendeleo kwa walio chini yake na
akawa ni mwenye Mali nyingi sana. Siku moja af Fir’awn akaamua kumwambia Mfalme:
‘Ewe Mfalme Mtukufu! Jee unajua kua watu wako wanautajiri mkubwa sana na
wana uwezo mkubwa pia? Kwai kwa kila siku zinavyoenda basi na wao ndivyo
wanavyozidi kuendelea. Tuombe kua wasije kusababisha matatizo kwako baadae.’
Mfalme akashtuka.

Halafu baada ya hapo Fir’awn akawaambia watu walio chini yake kua: ‘Mfalme ana
mpango wa kuwanyang’anya mali zenu, na kuwaua viongozi wenu baada ya
kuwaalika kwenye ghafla ya chakula, kisha atawaua mmoja baada ya mmoja kwa
kuwaita ndani, hivyo akikualikeni basi chukueni silaha zenu pamoja nanyi na
akikuiteni ndani basi basi Muueni kabla hajakuueni’.

Kisha akamfuata Mfalme na kumwambia kua: ‘Matajiri wana mpango wa kukupidua


na kukuuua hivyo ni vigumu kuwakamata na kuwaua wote kwa pamoja, hivyo
inabidi uwaue mmoja baada ya mmoja, baada ya kuwaalika kuja kula chakula, na
kisha muite ndani kiongozi wao, akiingia ndani tu basi muue. Ukishamuua Kiongozi
wao basi waliobakia wataogopa na kua chini yako’

Hivyo Mfalme akawaalika Matajiri hao katika ghafla ya chakula, na kisha hali ikatokea
kama alivyotaka Fir’awn itokee, Mfalme akauawa, na watu wakamteua Fir’awn kua ni
Mtawala wao, nae akamteua Hamman kua Waziri wake wa Hazina.

Kwa upande wa pili basi tunaona kua kuna mtizamo wa wale wasemao kua Mtawala wa
Ardhi ya nchi Misri katika wakati wa kipidi cha Nabii Yusuf alikua ni mtu mwenye asili
ya Misr kwenyewe na alikua ni Fir’awn Al Rayyan Ibn Walid ambae ndie aliemchagua
Nabii Yusuf kua Waziri wa Hazina katika nchi yake. Ingawa Al Rayyan alisilimu na
hivyo kua ni mfuasi wa Dini ya Kiislam lakini alifariki kabla ya kufariki Nabii Yusuf.

Hivyo Mamlaka ya utawala yakarithiwa na Al Qabus Ibn Musab. Al Qabus alikua ni mtu
ambae aliekataa kusilimu na hivyo kuendelea kuishi katika maisha ya Kikafiri na
haikuchukua mda Nabii Yusuf nae akafariki dunia. Baada ya mda Al Qabus nae pia
akafariki na hivyo utawala ukarithiwa na Abu Al Abbas Ibn Al Walid Ibn Al Musab Ibn
Rayyan Ibn Irashah Ibn Tharwam Ibn Amr Ibn Faran Ibn Imlaq Ibn Lawudh Ibn Sham.
500

Mfalme Abu Al Abbas alikua ni Mfalme tajiri sana na mwenye kiburi kikubwa sana. Na
katika kipindi chake Basi watu wa Bani Israil walikua tayari washaenea kwa wingi sana
katika Ardhi ya nchini Misri. Hivyo Fir’awn Al Abbas akaamua kuwabagua na
kuwafanya kua ni watu wa daraja la chini na wenye kudharaulika kwa sababu ya kua si
watu wenye asili ya Misri kwani watu wa Misri asilia ni Al Aqbat. Baada ya mda Firáwn
akaamua kuwaingiza watu wa Bani Israil katika Utumwa kwa kuwachagua kua ni
wafanyakazi wa kazi ngumu zote za ndani ya Ardhi ya nchi hio, na kwa asieweza kufanya
kazi basi ilimbidi kulipa kodi kutokana na kutokua na uwezo wa kufanya kazi.

Ingawa alikua ni mwenye kuwafanya kua ni watumwa wake watu wote wa Bani Israil
lakini hata hivyo Fir’awn hakufanikiwa kuwashusha daraja watu wote hao wa Bani Israil.
Kwani mmoja miongoni mwa Bani Israil waliokua na darja mbele ya Firáwn alikua ni
mwanamke ambae Ma-shaa Allah mzuri sana, kupita kiasi. Mwanamke huyu alikua
akiitwa Asiya Bint Muzahim Ibn Ubayd Ibn Rayyan Ibn Ibn Walid. Hivyo Fir’awn
alipomuona kwa mara ya kwanza basi hapo hapo akampenda sana na akataka awe ni mke
wake hivyo akaamua kumuoa mwanamke huyu na kumhamishia katika kasri lake la
Kifalme.

Allah Subhanah wa Taála alimjaalia Firáwn maisha marefu yenye Mamlaka yenye
nguvu sana kiasi ya kua kila alivyokua akiishi zaidi ndivyo Mamlaka yake yalivyokua
yakizidi kuimarika na eneo lake kuongezeka, kwani jeshi lake lilikua lina nguvu sana
kiasi ya kua lilikua kila likivamia sehemu basi watu waliovamiwa hawawi na hali yeyote
ile isipokua hali ya kua chini ya Mamlaka yake Fir’awn. Mamlaka hayo yaliyokua
yakitanuka kila siku yalidumu kwa miaka na miaka huku watu wa Bani Israil wakiwa ni
wenye kuendelea kufanywa kua ni Watumwa wanaofanyishwa kazi ngumu kupita kiasi
bila ya kua na malipo wala khiyari wala maamuzi, katika kipindi hiki wakatokea Musa
Ibn Imran wengi sana kila mmoja akidai kua yeye ndie Musa alietabiriwa na Nabii Yusuf.

Kwani ilifikia hadi kua ni jambo la kawaida kwa Al Aqbat kupita njiani na kumuita mtu
yeyote yule wa Bani Israil na kisha kumtuma kumbebea mzigo wake au kumfanyia jambo
lolote lile atakalo yeye hata kama Mqibti huyo atataka kubebwa basi Mtu wa Bani Israil
husika humbidi kumbeba Mqibti huyo tena bure na bila ya kukataa amri hio. Baada ya
hali hii kudumu kwa mda mrefu bila ya Fir’awn kurudi kwa Mola wake basi Allah
Subhanah wa Taála akaamua kumzindua na kumuonya Fir’awn kwa kumjaalia kumletea
Mjumbe katika jamii yake kutoka kwa watu wa Bani Israil kwa ajili ya kumuongoza yeye
na kwa ajili ya kuwaokoa watu wa Bani Israil kutokana na udhalimu wake.

Na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akasema kuwaambia watu wa Bani Israil kua:
501

ِ ۤ ِ ‫﴿�ﺑ ِﲎ إِﺳﺮاﺋِﻴﻞ ٱذْ ُﻛﺮواْ ﻧِﻌﻤ‬


‫ﲔ‬َ ‫ﻀ ْﻠﺘُ ُﻜ ْﻢ َﻋﻠَﻰ ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬‫َﱏ ﻓَ ﱠ‬ ُ ‫ﱴ ٱﻟﱠِﱵ أَﻧْـ َﻌ ْﻤ‬
ِّ‫ﺖ َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ َوأ‬ َ َ ْ ُ َ َْ َ َ
‫ﺎﻋﺔٌ َوﻻَ ﻳـُ ْﺆ َﺧ ُﺬ‬ ِ ٍ ‫۞ َوٱﺗﱠـ ُﻘﻮاْ ﻳَـ ْﻮﻣﺎً ﻻﱠ َْﲡ ِﺰى ﻧـَ ْﻔﺲ َﻋﻦ ﻧـﱠ ْﻔ‬
َ ‫ﺲ َﺷْﻴﺌﺎً َوﻻَ ﻳـُ ْﻘﺒَ ُﻞ ﻣْﻨـ َﻬﺎ َﺷ َﻔ‬ ٌ
‫ﻮﻣﻮﻧَ ُﻜ ْﻢ ُﺳ ۤﻮَء‬ ِ ِ ِ ِ
ُ ‫ﺼُﺮو َن ۞ َوإ ْذ ﳒَﱠْﻴـﻨَﺎ ُﻛﻢ ّﻣ ْﻦ آل ﻓْﺮ َﻋ ْﻮ َن ﻳَ ُﺴ‬
ِ
َ ‫ﻣْﻨـ َﻬﺎ َﻋ ْﺪ ٌل َوﻻَ ُﻫ ْﻢ ﻳـُْﻨ‬
﴾‫اب ﻳُ َﺬِّﲝُﻮ َن أَﺑْـﻨَﺂء ُﻛﻢ وﻳَﺴﺘَ ْﺤﻴُﻮ َن ﻧِﺴﺂء ُﻛﻢ وِﰱ ٰذﻟِ ُﻜﻢ ﺑَ ۤﻼءٌ ِّﻣﻦ ﱠرﺑِّ ُﻜﻢ َﻋ ِﻈﻴﻢ‬ ِ ‫ٱﻟْﻌ َﺬ‬
َ
ٌ ْ ْ َْ َ َ ْ َْ َ
Ya banee isra-eela odhkuroo niAAmatiya allatee anAAamtu AAalaykum waannee
fadhdhaltukum AAala alAAalameena; Waittaqoo yawman la tajzee nafsun AAan
nafsin shay-an wala yuqbalu minha shafaAAatun wala yu/khadhu minha AAadlun
wala hum yunsaroona; Wa-idh najjaynakum min ali firAAawna yasoomoonakum
soo-a alAAadhabi yudhabbihoona abnaakum wayastahyoona nisaakum
wafee dhalikum balaon min rabbikum AAadheemun (Surat Al Baqara 2: 47- 49)

Tafsir: Enyi Bani Israil, kumbukeni Neema ambazo nimekuneemesheni juu yenu, na
kua nimekupendeleeni nyie juu ya Walimwengu wengine (Ibn Adam na Majini wa
kipindi chenu na waliotangulia kabla yenu). Na iogopeni siku ambayo Nafsi
haitaisaidia Nafsi nyengine kwa jambo lolote, na hautokubaliwa uombezi wala fidya
na wala hatosaidiwa mtu. Na kumbukeni tulipokuokoeni kutokana na watu wa
Fir’awn, ambao walikuingizeni nyie katika adhabu kali sana. Kwa kuwachinja watoto
wenu wa Kiume na kuwaachia hai watoto wa kike. Na katika hayo mlikua na mtihani
mkubwa kutoka kwa Mola wenu.

Naam aya zinazungumzia tukio la Fir’awn ambalo lilitokea baada ya watu wa Bani Israil
kupenda sana kutumia jina la Musa Ibn Imran, hivyo Fir’awn akaamua kufuatiliaa kwa
nini watu hawa hua wanalipenda jina la Musa Ibn Imran. Hadi akajua ukweli juu ya asili
na malengo ya jina hilo, hivyo akaanza kuwaua Musa Ibn Imran mmoja baada ya mmoja.


502

KUZALIWA KWA NABII MUSA.



Siku moja, Fir’awn alilala usiku na akaota, kua kuna moto mkubwa sana ambao ulikua
unatokea nchini Jerusalem ukawaka hadi katika maeneo ya Ardhi ya Misri, ambapo moto
huo ulipoingia Misri basi ukaunguza kila Nyumba ya Al Aqbat (Watu wa Misri) na
kubakisha nyumba za watu wa Bani Israil tu, ambazo zilikua hata kuguswa hazijaguswa
na moto huo. Firáwn akaamka huku jasho likimtoka kwani hadi nyumba yake nayo pia
ilikua aliona ndotoni kua inawaka moto, hivyo alipoamka akaanza kujiuliza juu ya Moto
huo wa Maajabu unaochagua Nyumba moja na kuiacha ya pili yake na ya tatu yake na
kisha kuivamia nyumba ya nne yake na kuiepuka ya tano yake, n.k.

Ulipowadia wakati wa asubuhi basi jambo la kwanza alilolifanya Firáwn ni kuitisha


Mkutano wa Mkuhani wake ambao ni wataalamu wa Ilm ya Sayari, Utabiri wa Ndoto na
Ilm ya Uchawi waliopo chini ya Mamlaka yake wote. Na walipokusanyika basi
akawaambia kuhusiana na ndoto yake hio aliyoiona usingizini. Baada ya Watabiri hao
kushauriana basi wakamwambia Fir’awn kua: ‘Ndoto hii, inamaanisha kua kuna
mtoto wa kiume ambae atazaliwa karibuni, na atakapokua mkubwa basi
atapapatuana na wewe katika Mamlaka yako, na atakapokushinda, basi
atawahamisha watu wa Bani Israil wote na kuwabadilisha baadhi ya watu wako
Imani yao.’

Ama kwa upande wa Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr
Al Ansari Al Qurtubi basi yeye anamnukuu Imam Abu Is-haq Muhammad Ibn Ibrahim
Ibn As Sirr Al Zajjaj na hivyo kua ni mwenye kutuambia kua: ‘Hapa tunaona mtizamo
wa Makafiri dhidi ya Waumini wa Dini ya Kiislam: Kupitia kwa Ujinga wa Fir’awn
ambae alitabiriwa na watabiri wake kua mmoja kati ya Mtoto wa Bani Israil atakua
na kuja uangusha Utawala wake, basi hapa inamaanisha kua kuna mambo mawili
yanayoweza kutokea ambayo ni: Kwanza, huenda watabiri hawa walikua ni
wakweli na hivyo basi tukio lingetokea kama walivyotabiri, ambapo kwa kua tukio
lishabashiriwa kua litatokea basi ilikua haina haja ya kuwaua watoto hao
watakaozaliwa, kwani tukio litatokea tu, halitoweza kuzuilika. Na Pili ni kua
huenda watabiri hawa walikua si wakweli ambapo pia hakuna sababu ya kuwaua
watoto hao watakaozaliwa, kwani utabiri wao si wa kweli.’

Mara baada ya kupata utabiri huo basi Firáwn, akaamrisha kua Wanawake waja wazito
wote waandikishwe kisha wakunga wote wakaamrishwa kua kila mtoto wa kiume wa
Bani Israil atakaezaliwa ni lazima achinjwe, na ikiwa ni mtoto wa kike basi aachiwe aishi.
Na kisha akateua watu maalum wa kuwasimamia wakunga hao katika kuhakikisha kua
kazi hio inafanyika ipasavyo.
503

Katika kipindi hiki Allah Subhanah wa Ta’ala akajaalia kua watu wazima wengi wa Bani
Israil wakawa ni wenye kufariki kwa wingi sana. Mtihani huu uliwapelekea watu wa Al
Aqbat kuingiwa na khofu na kuona kua kwa kua watoto wa kiume wa Bani Israil
wanachinjwa, na kubakishwa watoto wa Kike tu basi mwisho wake itakua hakuna
Mwanamme miongoni mwa watu wa Bani Israil na hivyo itakua hakuna Watumwa wa
kufanya kazi Ngumu. Kwa hivyo wakamfuata Fir’wan na kumshauri kua bora abadilishe
maamuzi kwa kusema kua mwaka mmoja watoto hao wa kiume wachinjwe na mwaka
mmoja wasichinjwe. Fir’awn akakubaliana na ushauri huo na hivyo akapitisha amri hio.

Hivyo katika mwaka ambao watoto wa kiume walikua wakiachiwa basi Allah Subhanah
wa Ta’ala akajaalia kua ndio mwaka aliozaliwa kaka yake Nabii Musa ambae ni Nabii
Harun Ibn Imran. Na katika mwaka uliofuatia baada yake ambao ndio mwaka wa
kuchinjwa watoto basi Yuhanz akawa na ujauzito wa Kallimu Allah Musa Ibn Imran
anasema Allah Subhanah wa Ta’ala pale alipomwambia Nabii Muhammad Salallahu
A’layhi wa Salam katika Quran:

ِ َ ‫﴿ورﺳﻼً ﻗَ ْﺪ ﻗَﺼﺼﻨَـﻬﻢ ﻋﻠَﻴ‬


‫ﻚ َوَﻛﻠﱠ َﻢ ﱠ‬
ُ‫اﻪﻠﻟ‬ َ ‫ﺼ ُﻬ ْﻢ َﻋﻠَْﻴ‬
ْ‫ﺼ‬ُ ‫ﻚ ﻣﻦ ﻗَـْﺒ ُﻞ َوُر ُﺳﻼً ﱠﱂْ ﻧـَ ْﻘ‬ ْ َ ُْ ْ َ ُ َُ
﴾ً‫ﻮﺳﻰ ﺗَ ْﻜﻠِﻴﻤﺎ‬ َ ‫ُﻣ‬
Warusulan qad qasasnahum AAalayka min qablu warusulan lam naqsus-hum
AAalayka wakallama Allahu moosa takleeman (Surat An Nisaa 4:164)

Tafsir: Na Mitume ambayo tumekutajia wewe kabla, na Mitume ambayo


hatukukutajia, na Musa aliezungumza moja kwa moja na Allah.

Katika mwaka huu mzee Imran akafariki dunia na hivyo akabakia Yuhanz peke yake na
watoto wake wawili huku akiwa bado ni mja mzito, wakati wa kujifungua ulipowadia
basi Yuhanz akawa na khofu kubwa sana kwani alikua akijua kua mtoto wake huyo kama
akiwa ni wa kiume basi bila ya shaka atakua ni mwenye kuchinjwa. Siku ya kujifungua
ilipowadia Yuhanz akajifungua katika wakati wa Sala ya Isha, hivyo baada ya kujifungua
salama akagundua kua aliezaliwa ni mtoto wa Kiume, hivyo akampa mtoto wake huyo
jina la Musa.

Yuhanz akamchukua mtoto huyo na kumhifadhi kwenye guo ili asipate baridi huku binti
yake Maryam akiwa ni mwenye kutayarisha chakula cha usiku ambacho kilikua ni mikate
iliyokua ikiokwa kwenye Tanuri. Mara ghafla mlango wao ukagongwa na Yuhanz
akajawa na khofu kua huenda wakawa ni askari wa Fir’awn washapata habari kutoka
kwa wapelelezi wa Al Aqbat na hivyo wamekuja kumuangalia mtoto huyo kama ni wa
kiume basi wamchukue wakamchinje. Hivyo akamchukua Musa ambae alikua bado
504

amezongwa kwenye guo lake na taratibu akamtia kwenye tanuri la mikate, kwani aliona
bora amchome moto mtoto wake kuliko kumuachia Fir’awn akamuua kwa mikono yake.

Maryam alipofungua mlango uliokua ukigongwa basi akajikuta kua ni mwenye


kukabiliana uso kwa uso na askari wa Fir’awn ambao nao bila ya shaka walikua ni
waliokuja kwa kususdio la kumuangalia mtoto aliezaliwa, lakini walipoingia ndani
kutafuta basi hawakukuta mtoto wala mwanamke ambae aliekua akionesha kua ndio
kwanza leo hii amejifungua au labda ni mwenye uja uzito hivyo wakatoka bila hata ya
kufunga mlango kutokana na hasira walizokua nazo baada ya kupata habari ambayo
ilikua inaonesha kua sio sahih.

Baada ya askari hao kuondoka Yuhanz akafungua mlango wa Tanuri na kumuangalia


mtoto wake kujua kama alikwisha kufa kwa joto au yuko hai, kwani hakua ni mwenye
kusikia sauti ya kulia kwa maumivu ya kuungua wala ya kusikia joto kutoka kwa mtoto
huyo, hivyo kimya chake hicho kilikua ni kizito na chenye kutisha sana. Lakini cha
kustaajabisha ni kua alipomtoa mtoto huyo basi alimkuta akiwa mzima na wala guo lake
alilomzungushia halikuungua.

Yuhanz akamshukuru Mola wake huku akimuangalia mtoto wake ambae alikua ni mzuri
na mwenye kuvutia katika macho yake. Furaha ikajaa ndani ya Moyo wake, lakini hata
hivyo ghafla akakumbuka kua uzuri wa mtoto huyo na uhai wake huyo si wa kudumu
kwa mda mrefu kiasi ya kua huenda akawa si mwenye kufanikiwa kua mkubwa mbele
ya macho yake, kwani yuko hatarini kupoteza maisha yake hivyo hisia za huzuni zikajaa
katika Moyo wake, na kuanza kutafakkar nini afanye ili aweze kuokoa maisha ya mtoto
wake huyo. Katika kutafakkar kwake huko basi ikatokea ile hali ambayo Allah Subhanah
wa Ta’ala anaielezea katika aya ifuatayo:

‫ﺖ َﻋﻠَْﻴ ِﻪ ﻓَﺄَﻟْ ِﻘ ِﻴﻪ ِﰱ ٱﻟﻴَِّﻢ َوﻻَ َﲣَ ِﺎﰱ‬


ِ ‫﴿وأَوﺣﻴـﻨَﺂ إِ َ ٰﱃ أُِم ﻣﻮﺳﻰ أَ ْن أَر ِﺿﻌِ ِﻴﻪ ﻓَِﺈ َذا ِﺧ ْﻔ‬
ْ َٰ ُّ َْ ْ َ
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ِ ِ ‫وﻻَ َْﲢﺰِ ۤﱐ إِ ﱠ� رآ ﱡدوﻩ إِﻟَﻴ‬
َ ‫ﻚ َو َﺟﺎﻋﻠُﻮﻩُ ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻤْﺮ َﺳﻠ‬ ْ ُ َ َ َ
Waawhayna ila ommi moosa an ardhiAAeehi fa-idha khifti AAalayhi faalqeehi fee
alyammi wala takhafee wala tahzanee inna raddoohu ilayki wajaAAiloohu mina
almursaleena (Surat Al Qasas 28:7)

Tafsir: Na tukamshushia Wahyi mama yake Musa (kumwambia): ‘Mnyonyeshe


(Musa), lakini kama ikiwa utakhofia juu yake, basi mtie mtoni na wala usiwe na khofu
yeyote wala huzuni. Kwani kwa hakika sisi tutamrudisha kwako wewe na tutamfanya
kua ni miongoni mwa Mitume wetu’.
505

Anasema Imam Abu 'Abd Allah Muhammad Ibn Ahmad Ibn Abu Bakr Al
Ansari Al Qurtubi kua: ‘Aya hii ina Maamrisho mawili ndani yake, ina Makatazo
mawili ndani yake na ina Ahadi mbili ndani yake ambazo ni:

Maamrisho Mawili ni ‘ArdhiAAeehi’ na ‘Faalqeehi fee Alyammi’ yaani


‘Mnyonyeshe’ na ‘Mtie katika Mto’.

Makatatazo Mawili ni ‘Wala Takhafee wala Tahzanee’ yaani ‘Usiwe na khofu wala
Usiwe na Huzuni’.

Ahadi Mbili ni ‘Inna Raddoohu ilayki wajaAAiloohu Mina al Mursaleena’ yaani


‘Kwa hakika sisi Tutamrudisha kwako na Tutamfanya kua ni Miongoni mwa
Mitume yetu’.’

Ama kuhusiana na neno wa Awhayna ila Ummi Musa yaani na Tukamshushia Wahyi
Mama yake Musa basi tushazungumzia juu ya maana yake pale tulipozungumzia juu ya
Mitume na Manabii katika Sura ya kwanza ya kitabu hiki. Ambapo tumeona kua kuna
kutofautiana kwa mitizamo juu ya kua Mwanamke anaweza kua Nabii au la, na hivyo
wenye kusema kua anaweza basi wametumia ayah hii kama uthibitisho.

‫ﻮت ﻓَﭑﻗْ ِﺬﻓِ ِﻴﻪ ِﰱ ٱﻟْﻴَِّﻢ ﻓَـﻠْﻴُـ ْﻠ ِﻘ ِﻪ‬


ِ ‫ﻚ ﻣﺎ ﻳﻮﺣﻰ۞أ َِن ٱﻗْ ِﺬﻓِ ِﻴﻪ ِﰱ ٱﻟﺘﱠﺎﺑ‬
ُ
ِ
ٰ َ ُ َ َ ‫﴿إِ ْذ أ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إِ َ ٰﱃ أ ُّﻣ‬
ِ ِ ِ
‫ﺼﻨَ َﻊ َﻋﻠَ ٰﻰ‬ ْ ُ‫ﻚ َﳏَﺒﱠﺔً ّﻣ ِّﲎ َوﻟﺘ‬ ُ ‫ٱﻟْﻴَ ﱡﻢ ﺑِﭑﻟ ﱠﺴﺎﺣ ِﻞ َ�ْ ُﺧ ْﺬﻩُ َﻋ ُﺪ ﱞو ِّﱃ َو َﻋ ُﺪ ﱞو ﻟﱠﻪُ َوأَﻟْ َﻘْﻴ‬
َ ‫ﺖ َﻋﻠَْﻴ‬
﴾‫َﻋْﻴ ِ ۤﲏ‬
Idh awhayna ila ommika ma yooha, Ani iqdhifeehi fee alttabooti faiqdhifeehi fee
alyammi falyulqihi alyammu bialssahili ya/khudhhu AAaduwwun lee
waAAaduwwun lahu waalqaytu AAalayka mahabbatan minnee walitusnaAAa
AAala AAaynee (Surat Al Ta-Ha 20:38-39)

Tafsir: Tulipomshushia Wahyi Mama yako juu yako juu ya tuliyomshushia,


tukamwambia Mtie ndani ya Tabut na kisha kitie ndani ya Mto, kisha Mto
utakichukua mpaka ukingoni, na atachukuliwa na adui yangu na adui yake. Na
nitakupamba kwa mapenzi kutoka kwangu, ili uwe ni mwenye kulelewa kutoka chini
ya uangalizi wangu.

Siku moja Ibilisi aliulizwa: ‘Hivi jee uliwahi kumpenda mtu yeyote yule hapo kabla?’
Iblis akajibu: ‘La isipokua Musa Ibn Imran’ akaulizwa tena Iblis: ‘Kwanini?’ Iblisi
506

akasema: ‘Kwa sababu Allah Subhanah wa Ta’ala amesema: Waalqaytu AAalayka


mahabbatan minnee - Na nitakupamba kwa mapenzi kutoka kwangu, Hivyo sikiweza
kujizuia kumpenda’

Hivyo baada ya Yuhanz kupata Wahyi unaomshauri hivyo basi akatoka nyumbani kwake
hadi kwa fundi Seremala mmoja ambae alikua ni miongoni mwa watu wa Misri aitwae
Hirbila na pia wengine wanasema kua alikua Seremala huyu alikua akiitwa Hizqil, na
akamuomba amtengenezee kisanduku ambacho kitakua na tundu lakini hakitoweza
kuingia maji ndani yake.

Anasema Mufasir Imam Muqatil Ibn Sulayman kua: ‘Mtu alietengeneza kisanduku
alikua ni Hizqil, yeye alikua ni Mtu aliemuamini Allah miongoni mwa watu wa
Fir’awn. Kisanduku hiki kilitengenezwa kwa kutumia mti wa aina ya miti ambayo
mbao zake hua ni zenye kutengenezewa kartasi. Mama yake Nabii Musa
akakichukua na kukitia pamba kwa ndani pembeni yake na kisha akamchukua
Nabii Musa akamtia ndani yake, akakifunika na kukitumbukiza katika Mto Nile
akawa ni mwenye kukiangalia hadi kikapotea katika upeo wa macho yake. Iblis
akaingia katika akili yake na hivyo akawa ni mwenye kusema: Nimefanya nini mie
kwa mtoto wangu? Kwani kama angebakia namie na kisha akauliwa basi ingekua
bora kwani ningemvisha sanda, kisha nikamzika. Kuliko kumtumbukiza Mtoni na
kisha baadae akakutana na Mamba.’

Kwa upande mwengine basi anasema Al Dahhaq Ibn Muzahim kua amesema Abd Allah
Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Wakati mama yake Nabii Musa alipoona juu ya
misimamo ya Fir’awn kwa watoto wa kiume wa Bani Israil basi akaingiwa na khofu
juu ya mtoto wake, hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamshushia Wahy na
kumwambia kua amtie kwenye kisanduku na kisha amtumbukize kwenye maji.
Hivyo Yuhanz akaenda kwa Seremala wa Kimisri, na akanunua kisanduku kidogo,
lakini Seremala akamuuliza: ‘Kama cha kutilia nini?’ kwa sababu Yuhanz alikua
ni Mtu ambae asiependa kusema Uongo basi akajibu: ‘Kwa ajili ya kumtilia mtoto’.

Hivyo fundi Seremala huyu akatoka na kupeleka habari kwa Fir’awn, lakini
alipofika getini kabla ya kuingia ndani basi walinzi wakamuuliza anachokitaka, na
ikawa hawezi kusema hivyo akaanza kupiga makele huku akionesha kwa ishara za
kutumia mikono, na ikawa hakuna kufahamiana baina yao, hivyo, wakamfukuza
lakini akagoma kuondoka, hivyo wakampiga bakora na kumfukuza. Seremala
akaondoka, lakini aliporudi nyumbani akawa anaweza kusema kama kawaida.

Hivyo akaamua kurudi tena kwa Fir’awn, lakini alipofika getini hali ikawa ndio ile
ile, ya kua hawezi kuzungumza wala kuona, akaanza kupiga kelele tena walinzi
wakampiga bakora tena, na kumfukuza, Seremala akaondoka na kukimbilia
507

jangwani, akaanza kulia na kumuomba Allah Subhnah wa Ta’ala amsamehe na


kuahidi kua kamwe hatomueleza mtu yeyote kuhusiana na mtoto wa Yuhanz.
Seremala huyu akawa ni mwenye kuona tena na kuweza kusema, hivyo akasjudu
na kumshukuru Mola wake, na akajua kua maajabu haya ni kutoka kwa Mola
wake. Hivyo akawa ni mwenye kumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala. Akarudi
nyumbani akatengeneza kisanduku na kisha akampelekea Yuhanz.’

Hivyo Yuhanz akamtia Nabii Musa ndani ya Kisanduku na kisha akakitumbukiza


Kisanduku hicho ndani ya Mto Nile. Hiki kilikua ni kipindi ambacho Fir’awn alikua Mke
Mkubwa ambae alipata nae mtoto wake mdogo wa kike aliekua akimpenda sana. Lakini
sasa Allah Subhnah wa Ta’ala akamjaali mtoto huyu kua ni mwenye maradhi ya Ukoma,
hivyo matabibu wakamwambia Fir’awn kua Bint yake anaweza kupona maradhi yake,
kutokana na dawa itakayopatikana kutoka ndani ya Mto Nile katika siku ya Jumatatu
asubuhi katika kipindi cha kuchomoza jua, na kikishapatikana kitu hicho basi maji maji
yake inatakiwa kujipaka katika sehemu ya mwili iliyoathirika ngozi.


KULELEWA NABII MUSA NA ASIYAH BINT MUZAHIM NA
FIR’AWN.


Ilipoingia siku ya Jumatatu katika wakati wa Alfajir basi kama kawaida yake Asiyah Bint
Muzahim, akiwa na bint wa Fir’awn walitoka na kuelekea katika bustani yao iliyopo
katika upande wa mwambao wa mto Nile, katika kutembea tembea kwao huko mara kwa
mbali pembeni ya mikoko wakaona kisanduku kinaelea elea juu ya Maji ya Mto Nile
huku kikiwa kama kimekwama baada ya kuzuiwa na magugu maji yanayoelea kwenye
mto huo. Hivyo Asiyah Bint Muzahim akawaamrisha wafanyakazi wake kwa kusema:
‘Hakika mimi naona kama kile ni kisanduku, hivyo kakichukueni mkilete
tukiangalie mna nini ndani yake, kwani huenda ikawa ndani yake mna dawa ya
maradhi inayotakiwa.’

Wafanyakazi wa Fir’awn wakakikimbilia kisanduku hicho na kisha wakakibeba na


kukileta mbele yake. Walipoamrishwa waifungue wakashindwa kukifungua. Wakataka
kukivunja lakini wapi, hapo Asiyah Bint Muzahim akasogea karibu ya kisanduku hicho
na kuchungulia ndani yake. Alipochungulia basi ikatoka Nuru ndani ya kisanduku hicho
na kuingia ndani hadi katika Moyo wake kupitia katika macho yake. Na hii ndio ikawa
sababu ya Asiyah kua ni mwenye kuongoka na kupewa darja na Mola wake. Hapo Asiyah
508

Bint Muzahim akajaribu kukifungua kisanduku ambacho kiliwashinda wafanyakazi wa


Fir’awn na kisanduku kikafunguka kwa wepesi na urahisi kama kwamba kilikua
kinasubiri ufunguo unaotokana na mtizamo wa macho yake.

Sub-hana Allah! Asiyah Bint Muzahim hakuamini macho yake pale alipokifungua
kisanduku hicho na macho yake kukutana na mtoto mzuri mchanga mwenye kutabasam
mbele yake. Tabasam hili la mtoto huyu lilikua ni la aina yake, kwani athari yake iligusa
moja kwa moja katika kina cha Nafsi na Moyo wa Asiyah bint Muzahim, ambao Moyo
huo nao bila ya kutaka ukausababisha uso wa Asiyah Bint Muzahim kua ni wenye kujaa
tabasama zuri na la kupendeza, tabasam ambalo kwa mda mrefu hakuwahi kuoneshwa
hata Fir’awn mwenyewe.

Asiyah Bint Muzahim akashindwa kujizuia akaingiza mikono yake ndani ya kisanduku
hicho na kumchukua mtoto huyo kutoka ndani ya kisanduku hicho, na alipomtoa ndani
yake basi mazingira waliyokuwepo yakabadilika na kujaa Nuru ya Amani Salama na
Upendo kiasi ya kua hata bint wa Fir’awn mwenyewe akamfurahia mtoto aliemuona
kutoka sandukuni humo kutokana na uzuri wake, alipomkaribia akampangusa mate ya
mtoto huyo yaliyo kwenye pembeni mwa midomo yake na moja kwa moja akajaribu
kujipaka katika sehemu iliyoathirika ya ngozi, ambapo hapo hapo bila ya kuchukua mda
basi ngozi ya bint huyo ilipoa na ikarudi katika hali yake ya kawaida ya maumbile yake
kama kwamba kamwe hakua ni mwenye kuumwa kwa sekunde moja kabla yake.

Asiyah Bint Muzahim akamkumbatia mtoto huyo kutokana na maajabu ya mtoto huyo,
mapenzi na furaha ilionekana wazi kutoka katika moyo wake na macho yake, wote kwa
pamoja wakakatisha mda wao wa kukaa bustanini na kuamua kurudi ndani ya kasri lao
la Kifalme pamoja na mtoto wao huyo waliemuokota. Kwa ajili ya kumtayarishia makazi
ya kumhifadhi pamoja nao, kama inavyosema aya ifuatayo:

ِ ِ ِ ُ ‫﴿ﻓَﭑﻟْﺘـ َﻘﻄَﻪ‬
َ ُ‫آل ﻓْﺮ َﻋ ْﻮ َن ﻟﻴَ ُﻜﻮ َن َﳍُْﻢ َﻋ ُﺪ ّواً َو َﺣَﺰ�ً إِ ﱠن ﻓْﺮ َﻋ ْﻮ َن َوَﻫ َﺎﻣﺎ َن َو ُﺟﻨ‬
ْ‫ﻮد ُﳘَﺎ َﻛﺎﻧُﻮا‬ ُ َ
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫َﺧﺎﻃﺌ‬
Failtaqatahu alu firAAawna liyakoona lahum AAaduwwan wahazanan inna
firAAawna wahamana wajunoodahuma kanoo khati-eena (Surat Al Qasas 28:8)

Tafsir: Kisha wakamuokota watu wa Nyumba ya Fir’awn, ili awe adui yao na sababu
ya huzuni yao. Kwa hakika Fir’awn na Hamana na Jeshi lao walikua ni watu wenye
makosa hatia kubwa sana.
509

Naam hapa tunaona kua aya imewajumuisha Fir’awn na Hamman kua ni wenye Hatia
kubwa sana. Kwa kuwaainisha kwa kutumia neno Khati-iina ambalo kimaana hua
linamaanisha kufanya dhambi kwa kukusudia na pia humaanisha kufanya dhambi bila ya
kukusudia. Kwani anasema Mujaddid Ad Din Imam Al Mushaqiqin, Sultan Al
Mutakallimin Imam Al Ghazali Al Thani, Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: Kuna tofauti
baina ya Mukhtiyy na Khattiy ambapo neno Mukhtiyy hua ni lenye kumaanisha mtu
anaefanya dhambi bila ya kujua wala kukusudia, na neno Khattiy hua ni lenye
kumaanisha Mtu mwenye kufanya dhambi kwa kujua na pia kwa kukusudia.

Anasema Sultan Al Balagha Imam Abu Al Qasim Al Zamakhshari kuhusiana na ayah hii
kua: ‘Aya inawataja kina Fir’awn na Hamana kua ni wenye kufanya makosa katika
kila jambo walifanyalo.’

Ingawa Asiyah Bint Muzahim na Bint Fir’awn walikua ni wenye furaha kutokana na
tukio hilo la mtoto huyo, lakini hali hio ya furaha ilikatishwa ghafla pale walipoingia
ndani ya Kasri lao na kukutana na washauri wa karibu wa Fir’awn walipopata habari ya
kuokotwa kwa kisanduku hicho chenye mtoto ndani yake na hivyo kuharibu furaha hio
baada ya kumfuata Fir’awn na kumwambia: ‘Ewe Fir’awn! Jee una habari kuhusiana
na mtoto alieokotwa Bustanini mtoni? Hakika sisi tunadhani kua huyu Mtoto
alieokotwa ni mtoto miongoni mwa watoto wa Bani Israil, ambae tayari umeshaona
matokeo yake ndani ya ndoto yako uliyoiota nasi tukakuonya juu yake. Hivyo
tunakushauri mrudishe kwa kumtupa kwenye mto au muue badala yake.’

Habari hii ilimshtua sana Fir’awn na hivyo alipopata ushauri huu basi ulimuingia ndani
ya ufahamu wa moyo na akili yake, hivyo akatoka na kuelekea kwa Asiyah Bint Muzahim
na kutaka kujua kumetokea nini, hapo Asiyah Bint Muzahim akaelezea yaliyotokea hadi
kupatikana kwa dawa ya binti yake Fir’awn na kumalizia kwa kusema huku akiwa
amejawa na tabasamu lenye kupendeza kua: ‘Kwa hakika ndoto yetu ya kupata mtoto
wa kiume imetimia, haya ni majaaliwa mema kwetu sisi kupata mtoto mzuri sana
kama huyu’.

Kauli hii ilimkera sana Fir’awn kwani ingawa ilikua inatoka kinywani mwa kipenzi cha
roho yake ambae kamwe hataki kumkera hata mara moja katika maisha yake, lakini
ushauri huo ulikua unatishia usalama wa mamlaka yake kiasi ya kua hisia za mapenzi
yake kwa mke wake zilizidiwa na hisia za kibri zilizojaa ndani ya moyo wake ambacho
kilimpelekea kua ni mwenye kusahau, uzuri wa tabasamu la furaha linaloonekana
kwenye uso wa mkewe kipenzi Asiyah bint Muzahim, na pia furaha ya kupatikana kwa
dawa iliyoponesha maradhi ya bint yake.

Hivyo akasema: ‘Huyu mtoto anaweza kua ndio sababu ya kuyaangamiza mamlaka
yangu, hivyo bora tusimuachie kuishi pamoja nasi, bora tumuue kabla kuja
510

kusababisha madhara baadae.’ Asiyah Bint Muzahim akasema: ‘Hivi jee kweli
kupitia kwa Mtoto huyu mmoja tu basi watu wa Bani Israil wataweza kutatuliwa
matatizo yao na yeye?’

Ambapo Qur’an inatuambia kua Asiyah Bint Muzahim akasema kua:

ِ ٍ ْ ‫ﺖ ْٱﻣﺮأَةُ ﻓِﺮ َﻋﻮ َن ﻗُـﱠﺮةُ َﻋ‬


َ َ‫ﲔ ِّﱃ َوﻟ‬
ُ‫ﻚ ﻻَ ﺗَـ ْﻘﺘُـﻠُﻮﻩُ َﻋ َﺴ ٰﻰ أَن ﻳَـْﻨـ َﻔ َﻌﻨَﺎ أ َْو ﻧَـﺘﱠﺨ َﺬﻩ‬
ِ ﴿
ْ ْ َ َ‫َوﻗَﺎﻟ‬
﴾‫وﻟَﺪاً وُﻫﻢ ﻻَ ﻳَ ْﺸﻌُﺮو َن‬
ُ ْ َ َ
Waqalati imraatu firAAawna qurratu AAaynin lee walaka la taqtuloohu AAasa an
yanfaAAana aw nattakhidhahu waladan wahum la yashAAuroona (Surat Al Qasas
28:9)

Tafsir: Na akasema mke wa Fir’awn ‘Utulivu wa Macho yangu na yako! Usimuue,


kwani huenda akatufaa na tutamfanya kua ni mtoto wetu’ lakini hawakua ni wenye
kujua.

Anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kuhusiana na kauli ya ayah hii basi
ni kua: ‘Wakati Asiyah Bint Muzahim aliposema kua: ‘Huenda akatufaa’ basi
Fir’awn akajibu kwa kutopendezwa na kauli hio kwa kusema: ‘Labda atakufaa
wewe lakini sio mimi.’’ Ambapo kama tutakavyoona hapo baadae kua maneno yake
haya yalikua ni ya kweli, kua Nabii Musa atamfaa Asiyah Bint Muzahim na hatomfaa
Fir’awn.

Kwa upande mmoja basi ayah hii inatutilia mkazo umuhimu wa kuangalia na kuona kheri
katika kila tukio linalotokea katika maisha yetu na hivyo kua na mtizamo wa kua kila
kitu kina kheri ndani yake katika katika maisha yetu.

Ama kwa upande mwengine basi tunaona kua aya imetumia neno Qurrat AAaynin
ambalo ni lenye kujumuisha maneno mawili, moja Qurrat ambalo maana yake hua ni
Utulivu, Ubaridi, Ukimya, Burudisho, Toshelezo, Ridhio n.k. na neno la pili ni Aayni
ambalo kwa Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Jicho, Kuangalia, Kitundu cha
kuchungulia, Kuchunguza na pia humaanisha Chem chem ya Maji, hivyo basi Jicho
limeitwa Aayn kwa sababu ni lenye kuona na wakati huo huo hua ni lenye kujisafisha
kwa maji yake ya kimaumbile na lenye kutiririka Machozi.

Hivyo basi tunapozungumzia Qurrat AAaynin hua tunazungumzia hali ya hisia ya


Utulivu, raha na burudani inayopatikana ndani ya Nafsi na Moyo wa Mtu kutokana na
511

Mtizamo wa Jicho baada ya kuona au kuangalia, na hivyo kuona kwa jicho huko
huupelekea Moyo kua na Utulivu, na mfano hai ni pale unapotafakari na kuona
kimaumbile kua mtu huwezi kulala na kuupumzisha mwili wako bila ya kuyapa utulivu
macho yako kwa kuyafumba macho hayo, na kupata usingizi. Na kila macho yako
yanavyokua katika hali ya utulivu basi ndivyo unavyozidi kupata usingizi mwanana na
hivyo kua ni mwenye kuupumzisha mwili wako na kuzihuisha seli za mwili na hivyo
kuiboresha kinga ya mwili wako na pia kuusababishia ufahamu wako kua na uwezo wa
kuhifadhi mambo mengi zaid.

Na ndio maana unapomuangalia mtu anaeota na kuona jinamizi usingizini basi macho
yake hua hayana utulivu kwani hua yanageuka huku na kule kwa kasi na hivyo
kuupelekea Moyo kukosa utulivu na mapigo yake ya Moyo hua ni yenye kuongezeka
kupita kiasi na Ibn Adam hujikuta kua ni mwenye kutokwa na majasho na mwenye
kushtuka shtuka kwa nguvu mwili wake.

Ambapo hali ya tukio hili wa upande mwengine pia hua ni lenye kushabihiana na tukio
la Nabii Yusuf pale Allah Subhanah wa Ta'ala anielezea hali ilivyokua baada ya Nabii
Yusuf kunadiwa na kisha kununuliwa kwa kusema katika Qur'an:

ِ ِ ِِ ِ ‫ﺎل ٱﻟﱠ ِﺬى ٱ ْﺷﺘَـﺮاﻩ ِﻣﻦ ِﻣ‬ َ َ‫﴿ َوﻗ‬


ُ‫ﺼَﺮ ﻟ ْـﺎﻣَﺮأَﺗﻪ أَ ْﻛ ِﺮﻣﻰ َﻣﺜْـ َﻮاﻩُ َﻋ َﺴ ٰﻰ أَن ﻳَﻨ َﻔ َﻌﻨَﺂ أَْو ﻧَـﺘﱠﺨ َﺬﻩ‬
ْ ّ َُ
ِ ‫ﻒ ِﰱ ٱﻷ َْر‬ ِ ِ
﴾‫ض‬ ُ ُ‫ﻚ َﻣ ﱠﻜﻨﱠﺎ ﻟﻴ‬
َ ‫ﻮﺳ‬ َ ‫َوﻟَﺪاً َوَﻛ ٰﺬﻟ‬
Waqala alladhee ishtarahu min misra liimraatihi akrimee mathwahu AAasa an
yanfaAAana aw nattakhidhahu waladan wakadhalika makkanna liyoosufa fee al-
Ardhi (Surat Yusuf 12:21)

Tafsir: Na akasema yule (Qitfir) ambae aliemnunua (Nabii Yusuf) nchini Misri
kumwambia Mke wake: Mkirimu ajisikie yupo Nyumbani huenda akatufaa au
tutamfanya kua ni Mtoto wetu. Hivyo ndivyo tulivyosimamisha makazi Yusuf katika
Ardhi ya Misri.

Yaani hali iliyomtokezea Nabii Yusuf baada ya kuingia ndani ya Ardhi ya Mji wa Misri
na kulelewa na Mfalme wa Misri na kua mbali na Mzee wake yaani Nabii Yaqub Alayhi
Salam, na hivyo kua ndio sababu ya Bani Israil kuhamia nchini Misri basi ndio hali
ambayo ilimtokezea Nabii Musa Alayhi Salam kulelewa na Mfalme wa Misri na hivyo
kua mbali na Wazee wake na pia kua ndio sababu watu wa Bani Israil kuhama kutoka
katika mji wa Misri.
512

Ambapo tunaporudi kwa upande wa Nabii Musa basi kwa upande mmoja wa tunaona
kua familia moja imejawa na furaha na tukio hili la kutupwa na kuokotwa kwa Mtoto
huyu, ambayo ni familia ya Fir’awn na Asiyah Bint Muzahim lakini kwa upande
mwengine familia nyengine ilikua na khofu na wasi wasi juu ya tukio hili, kwani baada
ya Allah Subhanah wa Ta’ala kutuelezea juu ya furaha ya Asiyah Bint Muzahim basi
anatuelezea hali aliyokua nayo Yuhanz pale aliposema:

ۤ
‫ت ﻟَﺘُـْﺒ ِﺪى ﺑِِﻪ ﻟَ ْﻮﻻ أَن ﱠرﺑَﻄْﻨَﺎ َﻋﻠَ ٰﻰ ﻗَـ ْﻠﺒِ َﻬﺎ‬
ْ ‫ﻮﺳ ٰﻰ ﻓَﺎ ِرﻏﺎً إِن َﻛ َﺎد‬ ِ ْ ‫﴿ َوأ‬
َ ‫َﺻﺒَ َﺢ ﻓُـ َﺆ ُاد أ ُّم ُﻣ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ ِ
َ ‫ﻟﺘَ ُﻜﻮ َن ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬
Waasbaha fu-adu ommi moosa farighan in kadat latubdee bihi lawla an rabatna
AAala qalbiha litakoona mina almu/mineena (Surat Al Qasas 28:10)

Tafsir: Na kikajaa kifua cha Mama yake Musa kikawa kitupu (hakifikirii kitu
chochoote ndani yake isipokua Musa). Alikua anakaribia kufichua juu yake, kama
tusingeupa nguvu Moyo wake na hivyo akawa ni miongoni mwa Walioamini.

Anasema Mujtahid Imam Abu Baqr Muhammad Ibn Ibrahim Ibn Al Mundhir Al
Nishapuri Al Shafii juu ya aya hii kua: ‘Moyo wa Yuhanz ulikua hauna kitu chochote
kile ndani yake isipokua kumkumbuka Musa tu. Hakuweza kufikiria wala
kuzungumza juu ya chochote kile isipokua Musa. Aya imetumia kiwakilishi Bihi
kumuwakilisha Nabii Musa katika moyo wa Yuhanz kiasi ya kua ilikua inaogopewa
kua huenda katika kukaa kwake na hali hio basi atafichua siri ya kumpoteza mtoto
wake kwa maadui zake.’

Anasema Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Ahmad Ibn Abu Baqr Al Ansari Al
Qurtubi Al Maliki kua: ‘Na hivyo akawa ni miongoni mwa walioamini kwa
kumaanisha kua ni Muumini alieamini Ahadi ya Allah Subhanah wa Ta’ala wakati
alipoahidi kua atamrudishia mtoto wake huyo.’

Hivyo mara tu baada ya kumtumbukiza Mtoni mtoto wake basi Yuhanz akamwambia
binti yake Maryam kua amfuatilie ili ajue mwisho wake itakuaje, kama inavyosema aya
ifuatayo.

ِِ ‫ﺼ ِﻴﻪ ﻓَـﺒﺼﺮ‬ ِ ِ ‫﴿وﻗَﺎﻟَﺖِ ﻷ‬


﴾‫ﺐ وُﻫﻢ ﻻَ ﻳَ ْﺸﻌُﺮو َن‬
ُ
ٍ ْ َ ُ َ ِّ ُ‫ُﺧﺘﻪ ﻗ‬
ْ َ ُ‫ت ﺑﻪ َﻋﻦ ُﺟﻨ‬ ْ ْ َ
513

Waqalat li-okhtihi qusseehi fabasurat bihi AAan junubin wahum la yashAAuroona


(Surat Al Qasas 28:11)

Tafsir: Na hivyo akasema (Yuhanz) kumwambia dada yake (Musa): ‘Mfuate’. Hivyo
akamfuatilia kwa mbali, huku wao (kina Asiyah Bint Muzahim na watu wa Fir’awn)
wakiwa si wenye kuona (juu ya jambo hilo).

Hivyo Maryam akawa ni mwenye kumfuatilia kwa mbali ndugu yake huyo aliemo ndani
ya kisanduku hicho, huku akijificha ficha kwa mbali kuangalia utakuaje mwisho wa
ndugu yake, ambae hata hivyo ndugu huyo alikua chini ya uangalizi bora wa yule ambae
ni m-bora wa kupanga na kusimamia, huku Fir’awn na watu wake wakiwa hawajui ni
nini kilichokwisha panga na kukadiriwa kua kitatokea, hivyo Maryam akifuatilia
kisanduku hadi pale alipoona kua kimeokotwa na Wafanyakazi wa Fir’awn.

ٍ ِ ِ ِ
ُ‫ﺖ َﻫ ْﻞ أ َُدﻟﱡ ُﻜ ْﻢ َﻋﻠَ ٰﻰ أ َْﻫ ِﻞ ﺑَـْﻴﺖ ﻳَ ْﻜ ُﻔﻠُﻮﻧَﻪ‬ ْ َ‫﴿ َو َﺣﱠﺮْﻣﻨَﺎ َﻋﻠَْﻴﻪ ٱﻟْ َﻤَﺮاﺿ َﻊ ﻣﻦ ﻗَـْﺒ ُﻞ ﻓَـ َﻘﺎﻟ‬
‫ﻟَ ُﻜ ْﻢ َوُﻫ ْﻢ ﻟَﻪُ َ� ِﺻ ُﺤﻮ َن۞ﻓَـَﺮَد ْد َ�ﻩُ إِ َ ٰﱃ أ ُِّﻣ ِﻪ َﻛ ْﻰ ﺗَـ َﻘﱠﺮ َﻋْﻴـﻨُـ َﻬﺎ َوﻻَ َْﲢَﺰ َن َوﻟِﺘَـ ْﻌﻠَ َﻢ أَ ﱠن‬
﴾‫ٱﻪﻠﻟِ َﺣ ﱞﻖ وﻟَـٰ ِﻜ ﱠﻦ أَ ْﻛﺜَـﺮُﻫﻢ ﻻَ ﻳَـ ْﻌﻠَﻤﻮ َن‬ ‫َو ْﻋ َﺪ ﱠ‬
ُ ْ َ َ
Waharramna AAalayhi almaradhiAAa min qablu faqalat hal adullukum AAala
ahli baytin yakfuloonahu lakum wahum lahu nasihoona; Faradadnahu ila ommihi
kay taqarra AAaynuha wala tahzana walitaAAlama anna waAAda Allahi haqqun
walakinna aktharahum la yaAAlamoona (Surat Al Qasas 28:12-13)

Tafsir: Na tulikua tushamharamishia juu yake kunyonya (kwa wanyonyeshaji wengine


wote) hapo kabla. Hivyo (Maryam dada yake Nabii Musa) akawashauri kwa
kuwaambia: ‘Jee nikuelekezeni katika nyumba ya watu ambayo watamlea kwa ajili
yenu huku wakiwa ni wenye kumnasihi?’ Hivyo tukamrudisha kwa mama yake ili
afurahi na asiwe ni mwenye huzuni na apate kujua kua Ahadi ya Allah ni ya kweli,
lakini wengi wao si wenye kujua juu ya hilo.

Aya inatuwekea wazi umuhimu wa Maziwa ya Mama kwa Mtoto na hii ni kwa sababu
ili mtoto akue kimaumbile na kua na afya nzuri basi hu ni mwenye kuhitaji lishe bora
tangu anapokua tumboni mwa mama yake hadi anapozaliwa na pia baada ya kuzaliwa
kwake, na bila ya shaka hakuna lishe iliyo bora kwake zaidi ya maziwa ya Mama. Kwani
hua ni lishe ambayo inajumuisha virutubisho vyote muhimu kwa ajili ya ukuaji wa mwili
wake na ulinzi wa afya yake, kwani ndani ya maziwa ya Mama hua mna Madini na
514

Vitamin muhimu kama ya Mafuta, Protini, Calcium Citrate, Phospahate, Sodium,


Potassium, Maji, Sukari ya aina ya Lactose, Chumvi n.k
Kimaumbile maziwa ya mama huanza kujaa kwenye Maziwa ya Mama mara tu baada ya
kuzaliwa kwa mtoto ambapo hali yake na wingi wake huongezeka kwa kadri ya siku
zinavyoendelea baada ya kuzaliwa Mtoto na hii ni kutokana na maumbile ya mtoto
anaezaliwa pia kwani hua ni mwenye kuhitaji aina ya aina tofauti baina ya siku 6 za
mwanzo baada ya kuzaliwa ambayo hua ni mepesi zaidi ukilinganisha na yale yanayotoka
wiki moja baadae na kuendelea hadi mwaka wa pili baada ya kuzaliwa na. Na ndio maana
kuna Makubaliano ya Wanazuoni kua Kinamama wawanyonyeshe watoto wao katika
kipindi hiki cha mara baada ya kuzaliwa kiasi ya kua hata kama wakiwa wanataka
walipwe kwa kunyoyesha huko basi inabidi walipwe.
Kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Hakuna Maziwa Bora
kwa Mtoto mchanga kama Maziwa ya Mama.’
Kama anavyosema Mujaddid ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi
katika kuifafanua aya ifuatayo ya kunyonyesha ambayo inasema:

ِ ِ ِ َ‫ﲔ َﻛ ِﺎﻣﻠ‬ ِ ِ
‫ﺎﻋﺔَ َوﻋﻠَﻰ‬ َ‫ﺿ‬ َ ‫ﲔ ﻟ َﻤ ْﻦ أ ََر َاد أَن ﻳُﺘ ﱠﻢ ٱﻟﱠﺮ‬ ْ ِ ْ َ‫ات ﻳـُْﺮﺿ ْﻌ َﻦ أ َْوﻻَ َد ُﻫ ﱠﻦ َﺣ ْﻮﻟ‬ ُ ‫﴿ َوٱﻟْ َﻮاﻟ َﺪ‬
ِ ‫ﻮد ﻟَﻪ ِرْزﻗُـﻬ ﱠﻦ وﻛِﺴﻮﺗـُﻬ ﱠﻦ ﺑِﭑﻟْﻤﻌﺮ‬ ِ ُ‫ٱﻟْﻤﻮﻟ‬
‫ﻀﺂ ﱠر‬ َ ُ‫ﺲ إِﻻﱠ ُو ْﺳ َﻌ َﻬﺎ ﻻَ ﺗ‬ ٌ ‫ﻔ‬ْ ‫ـ‬
َ‫ﻧ‬ ‫ﻒ‬ُ ‫وف ﻻَ ﺗُ َﻜﻠﱠ‬
ُ ْ َ ُ ْ
َ َ ُ ُ َْ
ِ ِ ِ ‫واﻟِ َﺪةٌ ﺑِﻮﻟَ ِﺪﻫﺎ وﻻَ ﻣﻮﻟُﻮد ﻟﱠﻪ ﺑِﻮﻟَ ِﺪﻩِ وﻋﻠَﻰ ٱﻟْﻮا ِر‬
‫ﺼﺎﻻً َﻋﻦ‬ َ ‫ﻚ ﻓَِﺈ ْن أََر َادا ﻓ‬ َ ‫ث ِﻣﺜْ ُﻞ ٰذﻟ‬ َ َ َ َ ُ ٌ َْ َ َ َ َ
ۤ ِ ٍ ‫ﺗَـﺮ‬
َ‫دﰎ أَن ﺗَ ْﺴﺘَـْﺮ ِﺿﻌُﻮاْ أ َْوﻻَ َد ُﻛ ْﻢ ﻓَﻼ‬ ْ‫ﺎح َﻋﻠَْﻴ ِﻬ َﻤﺎ َوإِ ْن أ ََر ﱡ‬َ َ‫اض ّﻣْﻨـ ُﻬ َﻤﺎ َوﺗَ َﺸ ُﺎوٍر ﻓَﻼَ ُﺟﻨ‬ َ
‫ٱﻪﻠﻟَ ِﲟَﺎ‬ ۤ
‫ٱﻋﻠَ ُﻤﻮاْ أَ ﱠن ﱠ‬ ‫وف َوٱﺗﱠـ ُﻘﻮاْ ﱠ‬ ِ ‫ﺟﻨَﺎح ﻋﻠَﻴ ُﻜﻢ إِ َذا ﺳﻠﱠﻤﺘﻢ ﱠﻣﺂ آﺗَـﻴـﺘﻢ ﺑِﭑﻟْﻤﻌﺮ‬
ْ ‫ٱﻪﻠﻟَ َو‬ ُْ َ ُ ْ ُْ َ ْ ْ َ َ ُ
﴾ٌ‫ﺼﲑ‬ ِ ‫ﺗَـﻌﻤﻠُﻮ َن ﺑ‬
َ َْ
Waalwalidatu yurdiAAna awladahunna hawlayni kamilayni liman arada an
yutimma alrradaAAata waAAala almawloodi lahu rizquhunna wakiswatuhunna
bialmaAAroofi la tukallafu nafsun illa wusAAaha la tudarra walidatun biwaladiha
wala mawloodun lahu biwaladihi waAAala alwarithi mithlu dhalika fa-in arada
fisalan AAan taradin minhuma watashawurin fala junaha AAalayhima wa-in
aradtum an tastardiAAoo awladakum fala junaha AAalaykum itha sallamtum ma
ataytum bialmaAAroofi waittaqoo Allaha waiAAlamoo anna Allaha bima
taAAmaloona baseerun.(Surat Al Baqara 2:233)
515

Tafsir: Na Kina Mama wawanyonyeshe Watoto wao kwa miaka miwili kamili. Kwa
wale wanaotaka kukamilisha mda wa kunyonya, lakini na Baba wa Mtoto ni juu yake
kuwatafutia Riski yao na kuwavisha kwa wema, na hakuna kuikalifisha Nafsi isipokua
kulingana na uwezo wake. Na Mama asidhuriwe kuhusiana na Mtoto wake, na wala
Baba kuhusiana na Mtoto wake. Na ni mithili yake kuhusiana na urithi. Lakini kama
wakiamua kukubaliana juu ya unyonyeshaji basi hua hakuna makosa juu yao. Na
kama ukiamua juu ya mnyonyeshaji kwa watoto wenu, basi hakuna makosa juu yako,
pale inapokua unamlipa (Mama) kiwa wema. Na mcheni Allah huku mkijua kua kwa
hakika yeye ni mwenye kuona juu ya kila mnachokifanya.
Kua: ‘Inakubalika kumpeleka mtoto kwa Mnyonyeshaji katika hali zifuatazo:
Kama ikiwa Mke ameolewa na Mume mwengine na anatimiza majukumu yake ya
kuingiliana na huyo Mume mwengine kwa ajili ya kupata Watoto na hivyo
majukumu hayo hua yanaingilia na kumzuia Mke kunyonyesha. Na kama Mke
ameachwa na Mumewe na hivyo akakataa kumnyonyesha Mtoto kwa sababu ya
kua na khofu kua atachuja uzuri wake, na hivyo atakosa Mtu mwengine wa
kumuoa. Kama akikataa kwa kusudio la kumlipizia kisasi Mume alieachana nae
kutokana na kutalikiana nae. Kama Mke akiwa mgonjwa na hivyo kua si mwenye
kukaukwa na Maziwa yake, au kua na Mimba nyengine wakati akiwa
ananyonyesha, n.k basi hua inaruhusika kumtafuta mnyonyeshaji hadi mtoto apate
wa kumnyonyesha. Vyenginevyo basi hua ni Wajibu wa Mama kumnyonyesha
Mtoto wake.’
Na katika kutilia mkazo umuhimu wa mtoto kunyonya maziwa basi ndio maana
Wanazuoni wakasema kua: ‘Inapotokea mtu akawa na Mtumwa wake akawa ni
mwenye kumnyonyesha Mtoto wa Muislam ambae hana uwezo wa kunyonyesha
basi, baada ya Mtumwa huyo kumaliza kipindi cha kumnyonyesha Mtoto huyo, basi
hua ni wajibu kwa mmiliki huyo kumuachia huru Mtumwa huyo na hivyo hua ni
mwenye kuhesabika kua kama hakua ni Mtumwa.’
Anasema Allamah Abu Ali Al Husein Ibn Abd Allah Ibn Sina katika kitabu chake cha Al
Qanun fi At Tibb kua: ‘Mwanamke mnyonyeshaji anatakiwa awe na sifa za kua na
umri unaoanzia miaka 25 hadi 35 kwa sababu Wanawake wenye umri wa baina ya
miaka hii hua na afya nzuri na ni watulivu, kwani Wanawake wanapokua chini ya
baina ya Umri huu au zaidi ya baina ya Umri huu basi hua ni wasiokua na utulivu
wa kihisia jambo ambalo husababisa upungufu wa uzalishwaji wa maziwa katika
matiti yao.’
Kwa upande mwengine basi wanasayansi wanasema kua kitendo cha unyonyaji wa Mtoto
kwenye Titi la Mama hua kunasaidia ongezeko la uzalishwaji wa Prolactin na Oxytocin
na hivyo kua ni wenye kupelekea kuleta Mapenzi, Utulivu na Ukaribu baina ya Mama na
Mtoto na kumpelekea Mtoto kua na Mapenzi zaidi na Mama yake na pia kua ni mwenye
516

Afya njema na mwili wenye kinga imara kuliko mtoto ambae hakua ni mwenye kunyonya
maziwa ya Mama.

Hio ndio Hikma na mafunzo yanayopatikana katika aya hizo za unyenyoshaji wa Mtoto
kama zinavyoelezewa ndani ya Qur’an hususan katika kisa chetu cha Nabii Musa ambae
yeye kwa upande wake basi Allah Subhanah wa Ta’ala ametuwekea wazi kua alikua
tayari ameshamharamishia kunyonya kutoka kwa Mwanamke mwengine yeyote yule
isipokua mama yake yaani Yuhanz. Kwani Asiyah alitangazia kua anatafuta Mwanamke
wa kumnyonyesha Mtoto huyo lakini kila Mwanamke anaekuja basi Musa hakutaka
kunyonya ziwa lake, hivyo Asiyah bint Muzahim akaamua kutangazia kua yeyote yule
atakae mnyonyesha Maziwa mtoto wake huyo, basi atamlipa malipo yeyote anayoyataka
yeye na atamtajirisha na atakua na ukaribu nae kwa kumsaidia kwake.

Ingawa kulikua kuna uwezekano wa Nabii Musa kunyonya kwa Mwanamke mwengine
lakini pia hivyo Nabii Musa hakutaka kunyonya ziwa la Mwanamke yeyote isipokua la
Yuhanz. Hivyo aya inatuwekea wazi Miujiza yake Muumba katika kumzuia Nabii Musa
asinyonye kwa Mwanamke mwengine ili arudi ndani ya mikono ya Mama yake na hivyo
kua ni mwenye kulelewa nae, na hapo hapo kwa upande wa Yuhanz kua ni mwenye
kutimiziwa ahadi aliyopewa na Mola wake ya kua atarudishiwa mtoto wake kwani kwa
hakika Allah Subhanah wa Ta’ala si mwenye kuvunja ahadi yake, kama ilivyosema aya
yetu na aya nyengine ikiwemo:

﴾‫ﻒ ٱﻟْ ِﻤ َﻴﻌ َﺎد‬ ِ ‫﴿إِ ﱠن ﱠ‬


ُ ‫ٱﻪﻠﻟَ ﻻَ ُﳜْﻠ‬
Inna Allaha la yukhlifu almeeAAada (Surat Ar Rad 13:31)

Tafsir: Kwa hakika Allah si Mwenye kutotimiza ahadi zake.

Tukio hili la Allah Subhanah wa Ta’ala kumnusuru Nabii Musa kutochinjwa na Fir’awn
na kurudishwa mikononi mwa Yuhanz ambae ni mama yake mzazi na kamwe
haikuwaingia akilini watu wa Fir’awn kua Yuhanz ndie mama yake mzazi kutokana na
kua na mtoto mdogo ambae ni Harun aliekua akimnyonyesha linatuonesha wazi kudra
kamilifu ya Allah Subhnah wa Ta’ala kwa kupitisha Nusra yake na Rehma zake kwani
yeye ni mwenye uwezo juu ya kila kitu na hivyo humnusuru na kumuingiza katika Rehma
zake amtakae kama isemavyo inayofuatia na aya nyengine za ahadi za Allah:
517

ِ ِ‫ٱﻪﻠﻟِ ﻳﻨﺼﺮ ﻣﻦ ﻳﺸﺂء وﻫﻮ ٱﻟْﻌ ِﺰﻳﺰ ٱﻟﱠﺮِﺣﻴﻢ ۞ وﻋ َﺪ ﱠ‬


ُ‫ٱﻪﻠﻟُ َو ْﻋ َﺪﻩ‬
‫ﻒ ﱠ‬ ُ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻻَ ُﳜْﻠ‬ َْ ُ ْ َ‫﴿ﺑِﻨ‬
ُ َ َ ُ َ ُ َ َ َ ُ ُ َ ‫ﺼ ِﺮ ﱠ‬
ِ ‫َوﻟَـٰ ِﻜ ﱠﻦ أَ ْﻛﺜَـَﺮ ٱﻟﻨ‬
﴾‫ﱠﺎس ﻻَ ﻳَـ ْﻌﻠَﻤﻮ َن‬
ُ
Binasri Allahi yansuru man yashao wahuwa alAAazeezu alrraheemu; WaAAda
Allahi la yukhlifu Allahu waAAdahu walakinna akthara alnnasi la yaAAlamoona
(Surat Rum 30:6)

Tafsir: Kutokana na Nusra za Allah, Humnusuru amtakae, na yeye ni mwingi wa


Utukufu na ni mwingi wa Rehma. Na hio ni Ahadi ya Allah, havunji Allah ahadi yake,
lakini watu wengi hawajui juu ya hilo.

Hivyo Maryam alipopata habari hio ya kutafutwa mnyonyeshaji akamwambia Asiyah


Bint Muzahim kua: ‘Jee nikufahamisheni nyumba ya mwanamke ambae ataweza
kumnyonyesha na kumlea kwa heshima Mtoto wenu?’ Asiyah Bint Muzahim akajibu:
‘Naam! Tufahamishe’, hivyo Maryam akawafahamisha na kisha akatoka nao watu wa
Fir’awn hadi kwa Yuhanz, na walipofika wakamkuta akiwa na Harun. Hivyo Yuhanz
akapewa taarifa kutoka kwa Asiyah Bint Muzahim kisha akachukuliwa hadi katika
Jumba kifalme la Fir’awn na alipofika basi akaombwa na Asiyah Bint Muzahim kua
ajaribu kumsaidia kumnyonyeshea mtoto wake kwani tayari ameshajaribu kwa
Wanawake wengi sana bila ya mafanikio hivyo Yuhanz nae akakubali juu ya ombi hilo.

Asiyah Bint Muzahim akamleta Nabii Musa mbele ya Yuhanz na kumkabidhi kwenye
mikono yake, hapa moyo wa Yuhanz ukajawa na furaha na akamkumbatia mtoto huyo
huku macho yake akiwa ni yaliyojaa machozi kutokana na kutaka kulia kwa furaha,
jambo hili lilimshangaza sana Asiyah Bint Muzahim na Fir’awn pia ambao wote kwa
pamoja walikua mbele yake, walipomuuliza mbona imekua hivyo basi akasema ni
kutokana na uzuri na utukufu wa mtoto aliepewa amnyonyeshe.

Jibu hili halikumstaajabisha Asiyah Bint Muzahim na wala hakuweza kujua kua huyu
mtoto alikua ni mtoto wa Yuhanz, kwani Allah Subhnahah wa Taa’ala alimjaalia Nabi
Musa kua na muonekano tofauti na Yuhanz, na wala hakua ni mwenye kufanana na
Maryam na wala si mwenye kufanana na Harun, kwani yeye alikua na muonekano wa
rangi ya kiza kidogo tofauti na watu wa familia yake ambao wao walikua ni wenye rangi
ya weupe.

Yuhanz akamchukua Nabii Musa na kujaribu kumnyonyesha kutokana na maziwa yake,


na hapo hapo bila ya hata kufundishwa basi Nabii Musa akalitia mdomoni ziwa la Yuhanz
na kuanza kunyonya maziwa yaliyomo ndani yake. Tukio hili lilimfurahisha sana Asiyah
518

Bint Muzahim kiasi ya kua akamshikilia Yuhanz kuhamia katika jumba la Fir’awn kwa
kumwambia kua: ‘Kaa pamoja name ili kumlea Mtoto wangu huyu kwani mimi
kamwe sijawahi kupenda kitu kama namna nnavyompenda mtoto huyu’.

Lakini Yuhanz akapingana na maamuzi hayo na akakataa shauri hilo la kuishi pamoja
nao ndani ya Jumba hilo, kwani hii ilikua inambidi kumchuka na Harun pia ndani ya
Jumba hilo na familia yake yote, hivyo akaomba badala yake aruhusiwe kutoishi nao
pamoja ndani ya jumba hilo na badala yake bora aruhusiwe kumchukua mtoto huyo
nyumbani kwake, na vyenginevyo basi hatoweza kumnyonyesha mtoto huyo. Sharti hili
lilimpelekea Asiyah Bint Muzahim kukubaliana na ombi hilo la Yuhanz kwani hakuna
njia nyengine kufanya ili kupata maziwa ya Mtoto huyo.

Hivyo Asiyah Bint Muzahim akampa Yuhanz mtoto huyo aondoke nae hadi nyumbani
kwake. Na bila ya shaka Yuhanz alimlea mtoto huyo kwa malezi yaliyo bora na upendo
huku akiwa ni mwenye kutimiziwa mahitaji yake yote na familia ya Fir’awn kwa muda
wa miaka miwili kamili hadi Nabii Musa alipowacha mwenyewe kunyonya.

Baada ya kupita miaka miwili basi Nabii Musa akarudishwa katika kasri la Fir’awn kwa
Asiyah Bint Muzahim na Fir’awn mwenyewe. Hivyo katika kipindi hiki ambacho Nabii
Musa alipokua na umri wa miaka miwili basi siku moja Fir’awn alimchukua na kumbeba
mikono mwake. Basi Nabii Musa alizikamata ndevu za Fir’awn na kuanza kuzivuta kwa
nguvu zake zote. Kiasi ya kua Fir’awn alihisi maumivu kwenye kidevu and shingo yake
yote hivi akajiuliza: ‘Iisje kua huyu ndio yule mtoto aliebashiriwa kua ataniua?’
ambapo Asiyah bint Muzahim akasikia maneno hayo hivyo akasema:

‘Haya si maneno mazuri ya kumzungumia Mtoto Mdogo kama huyu, kwani


hajafikisha hata miaka mitatu, hana akili hivyo. Lakini kama unadhani
vyenginevyo basi mjaribu.’

Hivyo vikaletwa vibakuli viwili ambapo kimoja ndani yake yakatiwa makaa mekundu ya
moto na kibakuli chengine zikawekwa Peremende Nyekundu na kuwekwa mbele yake
Nabii Musa. Nabii Musa akanyoosha mkono kuelekea kwenye Peremende Nyekundu
lakini hapo hapo akatokea Malaika Jibril na kumvuta mkono wake Nabii Musa hadi
kwenye Kibakuli cha Makaa mekundu ya Moto.

Nabii Musa akachukua kaa la Moto ambalo hata hivyo halijamuungaza mkono wake na
alipolikaribisha Mdomoni mwake basi alitoa ulimi wake kuonja ladha yake na Kaa hilo
likamuunguza Ulimi wake na hapo hapo akalitupa chini kaa hilo. Hapo Asiyah Bint
Muzahim akasem kumwambia Fir’awn: ‘Si umeona? Kama angekua na akili hizo basi
asingechagua kaa la moto, bali angelichagua Peremende badala yake.’
519

Na kuna wasemao kua Nabii Musa katika siku hio alikua akicheza na Fimbo na alipofika
mbele ya Fir’awan basi akampiga nayo kichwani kwa nguvu zake zote. Na Fir’awn
alipokasirika basi Asiyah bint Muzahim akamtetea Nabii Musa kwa kumletea kibakuli
cha Mkaa wa Mawe ya Moto na cha pili kilikua na Lakti ya Zamaradi nyekundu, na Nabii
Musa alipoekewa mbele yake basi akachagua Kaa la Moto, hivyo Fir’awn akajua kua
Nabii Musa alimpiga kwa sababu ya mambo ya mchezo wa kitoto.

Anasema Ka’ab al Ahbar kua: ‘Nabiyyu Allahi Harun Ibn Imran alikua ni mtu
mwenye ufasaha wa Lugha, na maneno yaliyo wazi. Na alipokua akizuungumza
alikua akaizungumza kwa makusudio na ufaham mkubwa sana. Alikua ni mrefu
zaidi ya Nabii Musa na alikua na alama ya kidoto Usoni mwake na pia kwenye Ulimi
wake. Ambapo Nabii Musa alikua na ngozi ya rangi yenye weupe wa kiza uliofifia,
mwenye nywele zilizosongamana na alikua mrefu kama vile mmoja kati ya watu wa
kabila la Azd Shanuah. Nabii Musa alikua ni mzito wa kusema katika maneno yake,
na alikua na mwenye kusema haraka haraka. Na alikua ni mwenye kidoto cheusi
pia kwenye Ulimi wake.’

Nabii Musa akaendelea kulelewa na kuishi ndani ya Jumba la Fir’awn mpaka akafikia
umri mkubwa wa kubalegh kama inavyosema aya:

ِِ ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ٱﺳﺘَـ َﻮ ٰى آﺗَـْﻴـﻨَﺎﻩُ ُﺣ ْﻜﻤﺎً َو ِﻋ ْﻠﻤﺎً َوَﻛ ٰﺬﻟ‬
َ ‫ﻚ َْﳒ ِﺰى ٱﻟْ ُﻤ ْﺤﺴﻨ‬ ُ ‫﴿ َوﻟَ ﱠﻤﺎ ﺑـَﻠَ َﻎ أ‬
ْ ‫َﺷﺪﱠﻩُ َو‬
Walamma balagha ashuddahu waistawa ataynahu hukman waAAilman
wakadhalika najzee almuhsineena (Surat Al Qasas 28:14)

Tafsir: Na alipobaleghe akawa na nguvu na kukamilia, tukampa hikma na Ilmu na


kadhalika hivyo ndivyo tunavyowalipa wenye kufanya mema.

Anasema Sultan Al Balagha Imam Abu Al Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Neno Istawa
lililotumika hapa hua linamaanisha kukua kwa mwili hadi kufikia kilele kiasi ya
kua hakuna uwezekano wa kukua zaid.’

Aya imetumia neno Balagha ambalo kwa lugha ya Kiswahili hua tunasema Baleghe basi
hua linamaanisha Kufikia, Kukua, Kupea, Kukua Kiufaham, Kilugha, kua na ubora wa
hali ya juu. Na pia imesema kua Nabii Musa alijaaliwa Hikma, yaani Ilm, Akili, Ufaham
na Busara.

Katika kipindi chote hiki ambacho Nabii Musa alikua akikaa kwa Fir’awn alikua
akipendwa sana na Fir’awn kiasi ya kua ilikua kila anapoenda Fir’awn basi na Nabii
520

Musa lazima awepo, Nabii Musa akawa anaitwa Musa Ibn Fir’awn. Anapanda Farasi
kama anaepanda Fir’awn, na alikua anapanda katika gari moja la Farasi na Fir’awn,
anavaa nguo sawia kama anavyovaa Fir’awn. Na hii ni kutokana na Hikma zake Allah
Subhanah wa Ta’ala kwa ajili ya kumuandaa Nabii Musa awe karibu na adui yake yaani
Fir’awn asimuogope na ili awe ni mwenye kumjua ndani nje adui yake.


HIJRA YA KWANZA YA NABII MUSA KUTOKA MISRI KUELEKEA
MADYAN.


Hivyo katika kipindi hiki ambacho Nabii Musa alikua na umri wa miaka 30 tayari basi
watu wa Bani Israil wakawa wanapata afueni kutokana na kua Nabii Musa ni mwenye
asili ya watu wa Bani Israil. Siku moja mchana Nabii Musa alikua amelala, kwani ilikua
ni kawaida ya watu wa Misri kulala wakati wa Mchana mpaka Alaasiri. Nabii Musa
alipomka akaambiwa kua Fir’awn ameshatoka na Farasi wake na Walinzi wake
wakielekea katika moja ya mitaa ya mji wa Ibn Haj ambao upo katika umbali wa kilomita
20 kwa upande wa kusini kutoka katika mji wa Al Qahira - Cairo, hivyo nae akapanda
Farasi wake na kuelekea alikoelekea Fir’awn, alipofika katika maeneo ya soko la Al Menf
(Memphis) akakuta kua eneo hilo halina hata Mtu mmoja kwani wote walikua
wamefunga maduka na wamelala bado hawajaamka.

Na ndio likatokea lile tukio ambao Allah Subhanah wa Ta’ala analiezea katika Qur’an
kwa kusema kua:

‫ﲔ ﻳَـ ْﻘﺘَﺘِﻼَ ِن َﻫـٰ َﺬا ِﻣﻦ‬ ِ ْ َ‫ﲔ َﻏ ْﻔﻠَ ٍﺔ ِّﻣ ْﻦ أ َْﻫﻠِ َﻬﺎ ﻓَـﻮ َﺟ َﺪ ﻓِ َﻴﻬﺎ ر ُﺟﻠ‬
ِ ‫﴿وَد َﺧﻞ ٱﻟْﻤ ِﺪﻳﻨَﺔَ َﻋﻠَ ٰﻰ ِﺣ‬
َ َ َ َ َ
ِ ِ ِ ِِ ِ ِ ِ ِ ِ ِِ ِ
ُ‫ﭑﺳﺘَـﻐَﺎﺛَﻪُ ٱﻟﱠﺬى ﻣﻦ ﺷ َﻴﻌﺘﻪ َﻋﻠَﻰ ٱﻟﱠﺬى ﻣ ْﻦ َﻋ ُﺪ ِّوﻩ ﻓَـ َﻮَﻛَﺰﻩ‬ ْ َ‫ﺷ َﻴﻌﺘﻪ َوَﻫـٰ َﺬا ﻣ ْﻦ َﻋ ُﺪ ِّوﻩ ﻓ‬
ِ ‫ﺎن إِﻧﱠﻪ ﻋ ُﺪ ﱞو ﱡﻣ‬ ِ ِ َ َ‫ﻀ ٰﻰ َﻋﻠَْﻴ ِﻪ ﻗ‬
﴾‫ﲔ‬ ٌ ِ‫ﻀﻞﱞ ﱡﻣﺒ‬ َ ُ َ‫ﺎل َﻫـٰ َﺬا ﻣ ْﻦ َﻋ َﻤ ِﻞ ٱﻟﺸْﱠﻴﻄ‬ َ ‫ﻮﺳ ٰﻰ ﻓَـ َﻘ‬
َ ‫ُﻣ‬
Wadakhala almadeenata AAala heeni ghaflatin min ahliha fawajada feeha
rajulayni yaqtatilani hadha min sheeAAatihi wahadha min AAaduwwihi
faistaghadhahu alladhee min sheeAAatihi AAala alladhee min AAaduwwihi
521

fawakazahu moosa faqadha AAalayhi qala hadha min AAamali alshshaytani


innahu AAaduwwun mudhillun mubeenun (Surat Al Qasas 28:15)

Tafsir: Na akaingia katika Mji wakati ambao wate wake walikua wameghafilika. Na
akakuta watu wawili wanapigana. Mmoja ni mtu wa upande wake (wa Bani Israil) na
mwengine ni wa upande wa adui yake (Mtu wa Fir’awn), akaomba msaada mtu wa
upande wake dhidi ya adui yake. Hivyo Musa akampiga Ngumi na akammaliza. Na
kisha akasema hii ni amali ya Shaytan, hakika yeye ni adui mpotovu aliewazi.

Hivyo Nabii Musa akakutana na watu wawili wanaopigana mmoja wao akiwa ni mtu wa
Bani Israil aliekua akiitwa Samirii na mwengine akiwa ni mtu wa Misri yaani wa Aqbat
aliekua akiitwa Fatun ambae alikua ni mpishi wa Fir’awn ambae alikua ana mzigo wa
kuni ameuweka chini na hivyo amemwita Samirii ambebee kuni hizo na Samirii
alipokataa ikabidi amlazimishe hadi kufikia kua wakaingiana maungoni. Katika
mapigano yao basi Samirii akawa ni mwenye kuzidiwa nguvu na Fatun, hivyo Samirii
alipomuona Nabii Musa anakuja basi akaomba kumwambia Nabii Musa kua amsaidie
kwani Fatun anamuonea.

Nabii Musa akamwambia Fatun amuache Samirii asiendelee kumpiga ambapo Fatun
akasema: ‘Hakika mimi siwezi kumuacha huyu kwa sababu hataki kunifanyia kazi
ya baba yako Fir’awn’. Nabii Musa akapandwa na hasira na kisha akashuka kutoka
kwenye Farasi wake na akamtoa Samirii ndani ya mikono ya Fatun, lakini Fatun nae
ikawa hataki kuachana na Samirii kwa sababu kwa wakati huo ndie msaidizi wake pekee
anaeweza kumsaidia katika kazi yake, na hivyo akamvamia Nabii Musa.

Na alipomvamia basi Nabii Musa akakunja mkono wake ngumi na akampiga ngumi moja
Fatun, na ndio maana aya ikasema ‘Fawakazahu Musa’ ambapo anasema Sultan al
Balagha Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kua neno: ‘Wakaza Wakz maana yake hua
ni kukunja Vidole vya mkono na Kushambulia kwa Ngumi.’

Aya vile vile inayaelezea hali ya matokeo ya tukio hili la shambulio la ngumi ya Nabii
Musa dhidi ya Fatun kwa kutumia maneno yasemayo faqadha AAalayhi ambapo neno
Faqadha linatokana na neno Qadha lenye kumaanisha Kukamilisha, Kumaliza, Kufikisha
Mwisho wake, Kuridhisha, Kutekeleza, Kutoa hukumu, Kubainisha na pia humaanisha
Kujaalia, Kuumba, Kuamua kama lilivyotumika katika aya ifuatayo;

ُ ‫ﻀ ٰﻰ أ َْﻣﺮاً ﻓَِﺈﱠﳕَﺎ ﻳَـ ُﻘ‬ ِ ‫﴿ﺑ ِﺪﻳﻊ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬


﴾‫ﻮل ﻟَﻪُ ُﻛ ْﻦ ﻓَـﻴَ ُﻜﻮ ُن‬ َ َ‫ض َوإِ َذا ﻗ‬
ِ ‫ات َوٱﻷ َْر‬ ََ ُ َ
BadeeAAu alssamawati waal-ardi wa-idha qadha amran fa-innama yaqoolu lahu
kun fayakoonu (Surat Al Baqara 2:117)
522

Tafsir: Mwanzilishi wa Mbingu na Ardhi na anapotaka kuamua Jambo liwe basi kwa
hakika hua ni mwenye kusema Kua na (Jambo hilo)linakua.

Hivyo Neno Qadha lililotumika hapa katika ayah hii ya Surat Al Baqara 2:117
limetumika kumaanisha Kuamua, Kujaalia au Kuumba, ambapo kwa upande wa kisa cha
Nabii Musa na Fatun limetumika kumaanisha Kufikishwa Mwisho wake Fatun kwani
kwani aya imesema faqadha AAalayhi na hivyo kutuwekea wazi kua baada Fatun
kuguswa na ngumi hio moja tu ya Nabii Musa basi hapo hapo akaanguka chini na kutulia
tulii kwani ilimfikisha mwishoni wa Uhai wake.

Hivyo Nabii Musa akaainama na kumuangalia Fatun kwa ukaribu na kugundua kua tayari
ameshafariki. Subhanah Allah, hapa Nabii Musa akaanza kujuta kua kwanini akawa ni
mwenye kushindwa kujizuia? Kwanini hakumsukuma tu na badala yake akampiga
ngumi? akajiona kua ni mtu ambae amekosa Subra. Hivyo Nabii Musa akasema: ‘Hakika
hii ni Amali ya Shaytani, ambae ni Mpotovu alie wazi’ kisha akarudi kwa Mola wake
na kusema:

﴾‫ﺖ ﻧـَ ْﻔ ِﺴﻰ ﻓَﭑ ْﻏ ِﻔﺮ ِﱃ ﻓَـﻐَ َﻔﺮ ﻟَﻪُ إِﻧﱠﻪُ ُﻫﻮ ٱﻟْﻐَ ُﻔﻮر ٱﻟﱠﺮِﺣﻴﻢ‬ ِّ ‫ﺎل َر‬
ُ ‫ب إِِّﱏ ﻇَﻠَ ْﻤ‬ َ َ‫﴿ﻗ‬
ُ ُ َ َ ْ
Qala rabbi innee dhalamtu nafsee faighfir lee faghafara lahu innahu huwa
alghafooru alrraheemu (Surat Al Qasas 28:16)

Tafsir: Aakasema: Ewe Mola wangu hakika mimi nimeshaidhulumu Nafsi, hivyo
nisamehe, nae akamsamehe kwani kwa hakika yeye (Allah Subhanah wa Ta’ala) ni
mwingi wa kusamehe na ni mwingi wa Rehma.

Aya zinatuonesha kua Nabii Musa alipomuomba Mola wake msamaha kwa kosa
alilolifanya bila ya kukusudia basi Allah Subhanah wa Ta’ala alimsamehe makosa yake.
Ambapo anasema Wahb Ibn Munabih kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala alimwambia
Nabii Musa kua kama uliemuua angeua ni kiumbe ambae alieniamini mimi japo
kwa mara moja basi Hakika mimi ningekuadhibu ewe Musa lakini kwa kua huyu
hakuwahi kuniamini mimi hata mara moja basi nimekusamehe’.

Na kutokana na mfano huo basi inatakiwa tujue kua haikubaliki kumdhulumu Nafsi yake
Mtu asiemuamini Allah Subhanah wa Ta’ala au kumdhulumu mali yake, na kwa
anaedhulumu nafsi ya mtu kama huyu asiekua Muislam kwa Makusudi basi kulingana na
mtizamo wa Madhhab ya Imam Malik, Imam Al Shafii na Imam Ahmad Ibn Hanbal basi
hua inabidi kulipa Fidya, ama kwa Mtizamo wa Madhhab ya Imam Abu Hanifa basi
anaedhulumu Nafsi Adhabu yake hua ni kifo bila ya kujali kama aliedhulumiwa ni
Muislam ama la.
523

Ambapo anasema Al Hafidh Mujaddid Ad Din Imam Shihab Ad Din Ibn Hajar al
Asqalani kua: ‘Inapokua kuna ukweli kua Waislam na wasiokua Waislam wanaishi
pamoja kwa Usalama basi Ukweli huu hua unaharamisha mali zao na uhai wao
kuchukuliwa na Waislam’

Hivyo ya Nabii Musa kuneemeshwa neema ya kusamehewa kosa lake basi akasema kama
inavyosema aya:

ِ ِ ِ ِ ‫ﺎل ر‬
َ ‫ﺖ َﻋﻠَ ﱠﻰ ﻓَـﻠَ ْﻦ أَ ُﻛﻮ َن ﻇَ ِﻬﲑاً ﻟّْﻠ ُﻤ ْﺠ ِﺮﻣ‬
﴾‫ﲔ‬ ّ َ َ َ‫﴿ﻗ‬
َ ‫ب ﲟَﺂ أَﻧْـ َﻌ ْﻤ‬
Qala rabbi bima anAAamta AAalayya falan akoona dhaheeran lilmujrimeena
(Surat Al Qasas 28:17)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa) Ewe Mola wangu kutokana na kile ulichonineemesha,
basi sitokua ni msaidizi wa Wenye Kuasi.

Ambapo kutokana na ayah hii basi amesema Ata Ibn Abi Rabbah kua: ‘Haikubaliki,
kwa mtu yeyote yule kua ni msaidizi wa Mtu mwenye kufanya dhulma, iwe kua ni
mwandishi wake au rafiki yake’

Na kwa upande mwengine anasema Sultan Al Balagha Imam Abu Qasim Al


Zamakhshari kua: ‘Ad Dahhaq aliombwa na Mfalme wake aitwae Sulayman Ibn
Muslim kua akagawe Sadaka kwa watu wa Mji wa Bukhara na akakataa,
akaombwa mara kadhaa na akakataa hivyo hivyo na alipoulizwa kwa nini hataki
basi alisema kua: ‘Hakika mimi sitaki kua ni miongoni mwa wasaidizi wa
wanaowafanyia watu dhulma’.

Na Ataa Ibn Abi Rabbah aliulizwa kwa kuambiwa kua: ‘Hakika mimi ninae ndugu
yangu ambae anajipaia kichumo chake kutokana na kalamu yake. Hua anaandika
mahesabu yanayoinga na kutoka n ,k. na ana familia na watoto na akiachana na
kazi hio basi atakua ni mwenye kuishi katika hali ya kua na madeni’ Ataa Ibn Abi
Rabbah akauiliza: ‘Jee anafanya kazi kwa nani?’ na akajibwa kua ni kwa Khalid
Ibn Abd Allah Al Kasra(Ambae ni mmoja kati ya Watu wa Utawala wa Banu
Ummayad). Hivyo Ataa Ibn Abi Rabbah akauliza: ‘Hivi nyinyi hamkusikia kua
mmoja kati ya watu wema ambae alisema: ‘Rabbi bima anAAamta AAalayya falan
akoona dhaheeran lilmujrimeena - Ewe Mola wangu kutokana na kile
ulichonineemesha, basi sitokua ni msaidizi wa Wenye Kuasi.’’’

Na kwa upande wa Shaykh ul Islami Sultan Ulamaa Abu Muhammad Izz al-Din Abd Al
Aziz Ibn Abd Salaam Al Sulami pia amesema kua: ‘Haikubaliki kwa Khatib wa Sala
524

ya Ijumaa Kuwaombea Dua Viongozi ambao ni wenye kudhulumu’ ambapo yeye


mwenyewe pia alikua akimuomba Allah Subhanah wa Ta’ala katika Khutba ya Sala ya
Ijumaa awahilikishe Maaadui wa Uislam (Ambao walikua ni Crusaders) na kila
anaesaidiana na Maadui hao akiwemo mfalme wa nchi yake katika wakati huo aliekua
akiitwa Mfalme Salih Ismail wa Syria.

Baada ya tukio hilo basi Nabii Musa akawa ni mtu mwenye wasi wasi kua isije kua
aliawahi kunekana na mtu mwengie zaidi ya Samirii, kwani kama ikiwa ameonekana basi
kuna hatari ya kukamatwa kwake ambako nako kutapelekea kuuliwa. Kwani Maiti ya
Fatun ilipoonekana na hivyo habari ikamfikia Fir’awn kua Fatun amefariki na
inasadikiwa kua alimuua ni mmoja kati ya watu wa Bani Israil. Hivyo Fir’awn
akaamrisha kua muuaji wa Fatun atafutwe na akishapatikana basi apelekwe kwa Fir’awn
na atamhukumu adhabu ya kifo hata kama akiwa ni mtoto wake.

Siku ya pili asubuhi wakati Nabii Musa anatembea tembea katika harakati zake katika
Mji huo mara akamuona tena Samirii anapigana na mtu mwengine wa Bani Israil na
akamomba tena msaada Nabii Musa kama zinavyosema aya:

ِ ‫ﺼَﺮﻩُ ﺑِﭑﻷ َْﻣ‬ ِ ِ ِ ِ ِ


ُ‫ﺼ ِﺮ ُﺧﻪ‬
ْ َ‫ﺲ ﻳَ ْﺴﺘ‬ ْ ‫ﺐ ﻓَِﺈذَا ٱﻟﱠﺬى‬
َ ‫ٱﺳﺘَـْﻨ‬ ْ ‫﴿ﻓَﺄ‬
ُ ‫َﺻﺒَ َﺢ ﰱ ٱﻟْ َﻤﺪﻳﻨَﺔ َﺧﺂﺋﻔﺎً ﻳَـﺘَـَﺮﻗﱠ‬
﴾‫ﲔ‬ٌ ِ‫ي ﱡﻣﺒ‬ َ ‫ﻮﺳ ٰﻰ إِﻧﱠ‬
‫ﻚ ﻟَﻐَ ِﻮ ﱞ‬ َ ‫ﺎل ﻟَﻪُ ُﻣ‬ َ َ‫ﻗ‬
Faasbaha fee almadeenati kha-ifan yataraqqabu fa-idha alladhee istansarahu bial-
amsi yastasrikhuhu qala lahu moosa innaka laghawiyyun mubeenun (Surat Al Qasas
28:18)

Tafsir: Akaendelea na mambo yake kwenye Mji huku akiwa na khofu, na mara
akakutana na yule ambae alieomba msaada wake Jana. Musa akamwambia Hakika
wewe ni Mpotovu wa dhahiri.

Baada ya kumwambia maneno hayo Nabii Musa akawa ni mwenye kumsogelea Samirii
na Mmisri anaepigana nae huku akiwa ni mwenye kujuta kwanini jana akamsaidia
Samirii, hivyo akamzuia yule Mmisri na kisha akamkamata Samirii na kusema: ‘Hakika
wewe ni mtu Mpotovu sana’, na baada ya kusikia maneno hayo basi Samirii akaona kua
leo ni zamu yake atauliwa na Nabii Musa hivyo akaponyoka kutoka kwenye mikono ya
Nabii Musa na kukimbia huku akisema: ‘Ewe Musa unataka kuniua kama ulivyomuua
yule Mtu wa jana? Hakika wewe unataka kua mwenye kufanya dhulma na wala si
mwenye kutaka kupatanisha.’

Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea hali ilivyokua kwa kusema:


525

ُ ‫ﻮﺳ ٰﻰ أَﺗُِﺮ‬
‫ﻳﺪ أَن ﺗَـ ْﻘﺘُـﻠَِﲎ‬ َ َ‫ﺶ ﺑِﭑﻟﱠ ِﺬى ُﻫ َﻮ َﻋ ُﺪ ﱞو ﱠﳍَُﻤﺎ ﻗ‬
َ ُ‫ﺎل ٰﳝ‬
ِ
َ ‫﴿ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺂ أَ ْن أ ََر َاد أَن ﻳَـْﺒﻄ‬
ُ ‫ض َوَﻣﺎ ﺗُِﺮ‬
‫ﻳﺪ أَن‬ ِ ‫ﻳﺪ إِﻻﱠ أَن ﺗَ ُﻜﻮ َن َﺟﺒﱠﺎراً ِﰱ ٱﻷ َْر‬ ُ ‫ﺲ إِن ﺗُِﺮ‬ِ ‫ﺖ ﻧَـ ْﻔﺴﺎً ﺑِﭑﻷ َْﻣ‬ َ ‫َﻛ َﻤﺎ ﻗَـﺘَـ ْﻠ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ‫ﺗَ ُﻜﻮ َن ِﻣﻦ ٱﻟْﻤ‬
َ ‫ﺼﻠﺤ‬ ْ ُ َ
Falamma an arada an yabtisha bialladhee huwa AAaduwwun lahuma qala ya
moosa atureedu an taqtulanee kama qatalta nafsan bial-amsi in tureedu illa an
takoona jabbaran fee al-Ardhi wama tureedu an takoona mina almusliheena(Surat
Al Qasas 28:19)

Tafsir: Na kisha alipotaka kumkamata yule ambae ni adui yao wote (Mmisri) basi
akasema yule mtu (Samirii): ‘Ewe Musa Jee unataka kuniua mie kama ulivyomuua
yule mtu Jana? Hakika wewe unataka kua ni mwenye kufanya Ujabari kwenye Ardhi
na wala hutaki kua ni mwenye kufanya Mema.’

Baada ya kusikia maneno hayo basi yule Mmisri akaondoka haraka na kuelekea kwa
Fir’awn na kutoa habari kua aliemuua Fatun jana alikua ni Nabii Musa na kisha akaelezea
yaliyotokea leo baina yake na Nabii Musa na Samirii. Fir’awn aliposikia hayo akaamrisha
kua haraka sana Nabii Musa atafutwe na kisha akamatwe aletwe mbele yake na kisha
auliwe.

Inasemekana kua Fir’awn alikua anasifa tatu ambazo ni nzuri: Kwanza alikua ni Mkarimu
wa Kutoa. Pili alikua ni Mwenye kuhakikisha kua Barabara na njia zote ziko salama na
hazisababishai usumbufu kwa Wasafiri. Tatu alikua ni mwenye Kuhukumu kwa Uadilifu
hata kama yeye atakua ni mwenye kudhurika kwa upande wake kutokana na Uadilifu
huo.

Miongoni mwa waliosikia habari hii alikuwepo Mtu mmoja ambae alikua akiitwa Hizqil
ambae yeye alikua ni mwenye kufuata Millati Ibrahim, hivyo akatoka haraka sana ili
ampe habari Nabii Musa kabla watu wa Fir’awn hawajawahi kumkamata na kisha
kumpeleka kwa Fir’an ili akaadhibiwe adhabu ya kifo kama zinavyosema aya:

َ ِ‫ﻮﺳ ٰﻰ إِ ﱠن ٱﻟْ َﻤ َﻸَ َ�َْﲤُِﺮو َن ﺑ‬


‫ﻚ‬ َ َ‫ﺼﻰ ٱﻟْ َﻤ ِﺪﻳﻨَ ِﺔ ﻳَ ْﺴ َﻌ ٰﻰ ﻗ‬
َ ُ‫ﺎل ٰﳝ‬
ِ
َ ْ‫﴿ َو َﺟﺂءَ َر ُﺟ ٌﻞ ّﻣ ْﻦ أَﻗ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ َ َ‫ﻮك ﻓَﭑﺧﺮج إِِﱏ ﻟ‬ ِ
َ ‫ﻚ ﻣ َﻦ ٱﻟﻨﱠﺎﺻﺤ‬ ّ ْ ُ ْ َ ُ‫ﻟﻴَـ ْﻘﺘُـﻠ‬
526

Wajaa rajulun min aqsa almadeenati yasAAa qala ya moosa inna almalaa
ya/tamiroona bika liyaqtulooka faokhruj innee laka mina alnnasiheena (Surat Al
Qasas 28:20)

Tafsir: Na akaja Mtu kutoka sehemu ya mbali ya Mji akikimbia, akasema: ‘Ewe Musa
hakika Machifu wanajadiliana juu yako ili wakuue, hivyo Kimbia kwani kwa hakika
mimi kwako ni mwenye kukunasihi’

Nabii Musa akashtuka na kuchanganyikiwa kwani alikua hajui hata akimbilie wapi, kwa
sababu Mamlaka ya Utawala wa Fir’awn unatawala Ardhi kubwa sana, ilikua imeanzia
Misri mpaka kwenye Jangwa la Sina lote, hivyo ilikua inamibidi lazima awe ni mwenye
kua nje kabisa ya Mamlaka ya Ardhi ya Utawala huo, ambapo tukio hili pia
linashabihiana na lile tukio lililotokea upande wa Nabii Yusuf kwani kwa upande wake
yeye ilimbidi akimbilie ndani ya Mamlaka na wala si nje ya Mamlaka ili kupata hifadhi
zaidi na akasema:

‘Ya Allah! Kabla kuja Wanawake hawa basi nilikua na mtihani wa kishawishi cha
Mwanamke mmoja tu, lakini sasa hivi wamekua wengi sana nao wote kwa pamoja
wanashirikiana pamoja na Zulaykha dhidi yangu, jee nifanye nini mie? Hivyo mimi
naona kua kuenda Jela ni bora kuliko kubakia nje kisha nikatekeleza
wanayoyataka wanawake hawa.’

Kwani Aya zinasema kua:

‫ﺐ‬ ‫َﺻ‬‫أ‬ ‫ﻦ‬ ‫ﻫ‬ ‫ﺪ‬ ‫ﻴ‬ ‫ﻛ‬ ‫ﲎ‬ِ ‫ﻋ‬ ‫ف‬ ِ
‫ﺮ‬ ‫ﺼ‬ ‫ﺗ‬ ‫ﱠ‬
‫ﻻ‬ ِ‫ﱃ ِﳑﱠﺎ ﻳ ْﺪﻋُﻮﻧَِ ۤﲏ إِﻟَْﻴ ِﻪ وإ‬ ِ ِ ‫ﺎل ر‬
ِ ‫ٱﻟﺴ ْﺠﻦ أَﺣ ﱡ‬ ّ َ َ َ‫﴿ﻗ‬
ُ ْ ‫ﱠ‬ ُ َ ْ َ ّ َ ْ ْ َ َ َ ‫ﺐ إ َﱠ‬ َ ُ ّ ‫ب‬
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ْ ‫إِﻟَﻴ ِﻬ ﱠﻦ وأَ ُﻛﻦ ِﻣﻦ‬
َ ‫ٱﳉَﺎﻫﻠ‬ َّ َ ْ
Qala rabbi alssijnu ahabbu ilayya mimma yadAAoonanee ilayhi wa-illa tasrif
AAannee kaydahunna asbu ilayhinna waakun mina aljahileena (Surat Yusuf 12:33).

Tafsir: Akasema (Nabii Yusuf) Ewe Mola wangu! Kifungo ni bora Kwangu Kuliko kile
ambacho wanachonitia Wao. Na kama hukuzigeuza Mbinu zao kutoka kwangu. Na
nikawa ni miongoni mwa Wajinga (Kutokana na kufanya Dhambi huku wakijua juu
ya dhambi hio)

Hivyo baada ya tukio hili Nabii Musa akakimbilia nje ya Misri huku nae akimuomba
msaada Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kusema:
527

﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ ِ ِ ِ ‫ﺎل ر‬ ِ ِ ﴿
َ ‫ب َﳒِّﲎ ﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻘ ْﻮم ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬ ُ ‫ﻓَ َﺨَﺮ َج ﻣْﻨـ َﻬﺎ َﺧﺂﺋﻔﺎً ﻳَـﺘَـَﺮﻗﱠ‬
ّ َ َ َ‫ﺐ ﻗ‬
Fakharaja minha kha-ifan yataraqqabu qala rabbi najjinee mina alqawmi
aldhdhalimeena (Surat Al Qasas 28:21)

Tafsir: Akakimbia kutokana ndani yake (Katika Ardhi ya Misri) hukua akiwa katika
hali ya khofu akasema: ‘Ewe Mola wangu niokoke na kutokana na Watu waovu.’

Hivyo Allah Subhnah wa Ta’ala akamshushia muongozo wa kumuonesha njia ya


kukimbilia na ambayo ni ya kukimbilia upande wa Kusini Mashariki ya eneo la Ardhi ya
Misri baada ya kuvuka eneo la Jangwa la Sinai katika eneo la Mji wa Madiyan ambalo
lipo Kaskazini Magharibi ya Ardhi ya nchi ya Saudi Arabia na Mashariki ya Ghuba ya
Aqaba kama zinavyosema aya:

﴾‫ﺎل َﻋﺴ ٰﻰ رِّ ۤﰊ أَن ﻳـَ ْﻬ ِﺪﻳَِﲎ َﺳﻮآء ٱﻟ ﱠﺴﺒِ ِﻴﻞ‬ ِ ﴿


ََ َ َ َ َ‫َوﻟَ ﱠﻤﺎ ﺗَـ َﻮ ﱠﺟﻪَ ﺗ ْﻠ َﻘﺂءَ َﻣ ْﺪﻳَ َﻦ ﻗ‬
Walamma tawajjaha tilqaa madyana qala AAasa rabbee an yahdiyanee sawaa
alssabeeli (Surat Al Qasas 28:22)

Tafsir: Na akaelekea katika Mji wa Madyan huku akisema: ‘Huenda Mola wangu
ataiongoza katika njia iliyokua ni sawia’

Hii ilikua ni safari ndefu ya takriban wiki nzima usiku na mchana huku Nabii Musa akiwa
hana chakula chochote isipokua alikua akila Majani tu njiani, na alipowasili katika Ardhi
na Midyan basi alikua taabani sanakwa sababu hakua ni mwenye kupita katika njia
ambayo anaweza kuonekana na watu alikua akipita katika sehemu ambazo hazipitiki na
mtu yeyote. Lakini hata hivyo alikua ameridhika kua ametoka kwenye mikono ya Watu
madhalim na anaelekea kwenye Ardhi ambayo ni ya watu ambao ni tofauti alioachana
nao kwani alioachana nao walikua ni watu wa Misri wenye asili ya Al Aqbat na
anakoelekea ni kwa watu wenye asili ya Kiarabu hivyo labda safari hio ya kuhama na
kukimbilia anakokimbilia itakua ni ya kheri na salama kwake kutokana na mipango ya
Mola wake.

Alipowasili katika maeneo hayo ya Ardhi ya Madyan basi alipumzika kwenye kigogo
cha Mti ulokua na kivuli kizuri sana ukampitia usingizi na akapumzika na kulala, na
baada ya kumpumzika kwa mda basi mara akashtuka baada ya kusikia sauti kama za
Wafugaji na wanyama wao, hivyo akachunguza na kunyatia katika sehemu zinakotokea
sauti hizo na mara akaona kisima cha Maji ambacho kulikua kimezungukwa na Wafugaji
528

wa kiume huku wakinyweshea maji wanyama wao na pembeni kuna Wanawake wawili
ambao wamekaa kwa kujitenga peke yao wakiwazuia na kondoo wao,

Taratibu Nabii Musa akaelekea katika upande ambao waliokau wamekaa Wanawake hao
peke yako na wanyama wao na kuanza kuwauliza imekuaje wakawa wamejitenga peke
yao hivyo? Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea tukio hili kwa kusema:

ِ َ‫ﱠﺎس ﻳَﺴ ُﻘﻮ َن وو َﺟ َﺪ ِﻣﻦ ُدو�ِِﻢ ْٱﻣﺮأَﺗ‬ ِ ِ ﴿


‫ﲔ‬ َ ُ َ َ ْ ِ ‫َوﻟَ ﱠﻤﺎ َوَرَد َﻣﺂءَ َﻣ ْﺪﻳَ َﻦ َو َﺟ َﺪ َﻋﻠَْﻴﻪ أُﱠﻣﺔً ّﻣ َﻦ ٱﻟﻨ‬
﴾ٌ‫ﻮ� َﺷْﻴ ٌﺦ َﻛﺒِﲑ‬ ِ ‫ﺼ ِﺪ َر‬
َ ُ‫ٱﻟﺮ َﻋﺂءُ َوأَﺑ‬ ِ َ َ‫ود ِان ﻗ‬
ّ ْ ُ‫ﺎل َﻣﺎ َﺧﻄْﺒُ ُﻜ َﻤﺎ ﻗَﺎﻟَﺘَﺎ ﻻَ ﻧَ ْﺴﻘﻰ َﺣ ﱠ ٰﱴ ﻳ‬ َ ‫ﺗَ ُﺬ‬
Walamma warada maa madyana wajada AAalayhi ommatan mina alnnasi
yasqoona wawajada min doonihimu imraatayni tadhoodani qala ma khatbukuma
qalata la nasqee hatta yusdira alrriAAao waaboona shaykhun kabeerun (Surat Al
Qasas 28:23)

Tafsir: Na alipowasili kwenye sehemu inayonyweshewa Maji ya Madyan, akaona


kundi la Wanaume wakinyweshea (Maji wanyama wao). Na pembeni yao akaona
Wanawake wawili wakiwazuia wanyama wao, akasema (Nabii Musa): ‘Mnataka
kufanya nini?’Nao wakasema: ‘Hatuwezi kuwanywesha Wanyama wetu mpaka
Wafugaji waondoe Wanyama wao na Baba yetu ni Mzee sana’

Hapa tunaona kua aya imetumia asili ya neno Khataba pale Nabii Musa alipowauliza
Wanawake wawili hao kwa kusema: ‘Ma khatbukuma’ ambalo ni lenye hali ya kuuliza
suali juu ya kitu kilichotokea kwani neno Khatbukum linatokana na neno Khutba ambalo
ni linamaanisha Kukhutubia, Kusoma Khutba, Kutoa Maneno au Ujumbe. Na pia hua ni
lenye kumaanisha Kuposa pale linapotumika neno Khitbatan. Neno Khataba limetoa
neno Khatbun ambalo hua linamaanisha Jambo, Kusababisha Jambo litokee, Jambo
ambalo Mtu hua anatamani au analitaka litokee.

Hivyo Nabii Musa akashangaa kuona kua Wafugaji wa kiume wanawanywesha Maji
Wanyama wao huku hawa Wanawake wawili wakiwa Wamejitenga peke yao na kujaribu
kuwazuia Wanyama wao ili wasichanganike na Wanyama wengine wa Wafugaji hao na
hapo hapo kuwazuia Wanyama wao wasinywe Maji katika wakati huo. Huku pembeni
yao kukiwa na Kisima chengine ambacho kimewekewa Jiwe kubwa juu yake, na hakuna
anaekitumia Kisma hicho.

Na ndio maana akawauliza: Ma khatbukuma – Jee Kitu gani kimekutokeeni? Au


kimekifikeni? Ambapo Wanawake hao wawili wakajibu kua, hawawezi kuwanywesha
Maji Wanyama wao wakati wapo Wachungaji hao wa Kiume kwa sababu wao ni
529

Wanawake dhaifu kinguvu na kimwili na baba yao ni Mtu Mzima sana hivyo hawezi
yeye kua ni mwenye kuchunga Wanyama hao badala yao, Hivyo basi jukumu hilo ni lao
wao, Nabii Musa akawaonea huruma Wanawake hao.

Hii pia inatonesha namna Nabii Musa alivyokua na msimamo katika kupigania haki za
wanyonge, Wanawake na Wageni kiasi ya kua hata kama hawajui basi alikua tayari ni
Mtu mwenye kua tayari kuwapigania haki zao, ambapo mara ya kwanza alipigana na
kuua Mtu kutokana na kupigania haki ya mtu asiemjua, na hii haishangazi sana kwani
hata Tawrat yenyewe basi imetaja zaidi ya mara 30 umuhimu wa kupigania haki za
wageni, wanawake na wanyonge.

Tunaporudi kwa Wanawake hawa wawili aliokutana nao Nabii Musa Kisimani basi
mmoja ambae ni mdogo kiumri alikua akiitwa Liya na mwengine ambae ni mkubwa
kiumri alikua akitwa Zafura, hivyo Nabii Musa akaangalia huku na kule ili ajue la
kufanya katika kuwasaidi wanawake hao, na katika upande wa pili wao akaona Kisima
kisichotumika ambacho kimefunikwa na jiwe kubwa sana ambalo kulinyanyua tu
inahitaji zaidi ya watu watano. Hivyo Nabii Musa akasogea kwenye Kisima hicho
kisichotumika na kisha peke yake akaliondoa Jiwe hilo Kisimani hapo na kuwasaidia
Wanawake hao kuwanyweshea Maji Wanyama wao, na kisha Wanawake hao
wakaondoka na Wanyama wao kabla hata ya Wafugaji wa Kiume walio kuwepo hapo
kuondoka.

Ama kwa upande wa Jarrah Allah Imam Abu Al Qasim Al Zamakhshari basi anasema
kua: ‘Wafugaji hao walikifunika jiwe kisima ambalo ilikua inahitaji watu 7
kulinyanyua, na wengine wanasema kua ni watu kumi na wengine wanasema watu
40 na wengine wanasema 100, lakini Nabii Musa aliliondoa peke yake.’

Ambapo kwa Upande wa Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu basi yeye amesema
kua jiwe hilo alilolinyanyua Nabii Musa liliku alikinyanyuliwa na watu 10 kutokana na
Uzito wake.

Na ingawa baadhi ya Wanazuoni wanasema kua baba yao Mabinti hao alikua ni Nabii
Ayoub na hivyo Nabii Musa alikaa na Nabii Ayoub kwa miaka 12 katika mji huo wa
Madyan na kisha Nabii Ayoub akafariki Dunia. Na Mabinti hawa hawakusema kua Baba
yao ni Mtume wa Allah Subhanah wa Ta’ala bali walisema kua Baba yao ni Shaykh Al
Kabir yaani Mtu Mzima Mzee Sana kwa sababu walikua hawajui Nabii Musa ni mtu
mwenye kufuata Dini gani, hivyo huenda Mtume huyo ikawa asikubalike na
asiheshimike kutokana na mtizamo wa Dini ya Nabii Musa, lakini tunapozungumzia Mtu
Mzima Mzee sana basi Dini zote hua zinakubaliana juu ya kuwaheshimu, kuwaonea
huruma na kuwasaidia watu wazima.
530

Ambapo kwa upande wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi tunaoana kua
yeye amesema kua: ‘Jina la baba wa Mke wa Nabii Musa alikua akiitwa Thabrun,
na huyu ndie aliemuajiri Nabii Musa. Kwani yeye alikua ni Chifu wa Midyan na
alikua ni Mtoto wa Kaka yake Nabii Shuayb, majina ya Mabinti hao ni Liya na
mwengine anaitwa Zafura ambae ndie aliekua mke wa Nabii Musa. Hivyo
Wanawake hao walipomwambia Nabii Musa habari yao, basi Nabii Musa
akawaonea huruma, kwani juu ya Kisima hicho kulikua na Jiwe kubwa sana
ambalo kuliondoa linahitaji watu wengi.’

Na huo pia ndio mtizamo wa Abd Allah Ibn Masoud Radhi Allahu Anhu na Abu Ubaydah
Ibn Jarrah Radhi Allahu Anhu, ambapo kwa upande wa Hasan Al Basr basi yeye alisema
kua: ‘Kuna watu ambao walisema kua huyu alikua ni Shuayb, Lakini (laysa huwa
Shuʿayb). huyo hakua Shuayb bali alikua ni Mmiliki wa Kisima katika Wakati huo’

Ama kwa upande wa Abu Said Ibn Abd Malik Ibn Abi Uthman basi yeye anasema kua:
‘Hakika mimi nimetembelea eneo hilo na kukiona Kisima hicho, na Kisima
kinachozungumziwa hapa ambacho chenye jiwe juu yake basi sio kile ambacho
walikua wakinyweshea Maji Wafugaji wa Kiume. Hivyo Musa akaliondoa Jiwe hilo
na kisha akachukua ndoo yao na kusema: ‘Haya leteni Wanyama wenu’ na kisha
akawasaidia Wanawake hao kuwanyweshea Maji Wanyama wao mpaka kiu ya
Wanyama wao yote ikamalizika’

Hikma za Allah Subhanah wa Taála ndani ya Qurán katika kuielezea sehemu hii ya kisa
hiki kwa ajili yetu ni pamoja na kutufunza umuhimu wa kitu ambacho katika Ulimwengu
wetu kimekua ni kitu adimu sana, kitu hiki kinajulikana kama Haya:

Neno Hayya ambalo kwa Kiswahili hua tunasema Haya basi kwa Kiarabu hua
linamaanisha Kuishi, Kukesha Usiku, Kua Hai, Kuitilia Ardhi mbolea, Kumuachia Mtu
hai, Kuondoa Heshima, Kua na Aibu, Kuadhirisha na pia humaanisha Kuomba Msamaha.

Hisia za Haya na Iman ni mambo mawili ambayo yanaendana sambamba, hivyo


moja wapo likikosekana basi na jengine pia hua ni lenye kutoweka (Mustadrak Al
Hakim)

Amesema tena Rasul Allah Salallahu Aálayhi wa Salam kua: ‘Haya ni Sehemu ya
Iman’ na pia ‘Haya haizalishi chochote isipokua uzuri ndani yake’ (Sahih Bukhari,
Sahih Muslim)

Tunapozungumzia Haya katika Uislam basi hua tunazugumzia hali zifatazo za aibu.

Haya mbele ya Allah Subhanah wa Taála – Muislam anatakiwa kua ni mwenye aibu
na haya kutokana na kua Allah Subhnaha wa Taála anamuona na kumjua hadi ndani ya
531

Moyo wake na hivyo anajua kila anachokifanya, anachokifikiria na ila kitu kuhusiana na
dhambi zake, iwe mtu huyo yuko peke yake au yuko pamoja na watu wengine.

Haya mbele ya Malaika – Kwani Malaika ni Viumbe watukufu na wenye uwezo wa


kumuona Ibn Adam ingawa yeye hamuoni na hivyo hua ni wenye kuona kila ovu
alifanyalo Ibn Adam husika.

Haya mbele ya Ibn Adam wengine – Kwani hali hii huzuia kudhuriana baina ya Ibn
Adam iwe kwa kuadhirishana, kuvujiana heshima, kujeruhiana kwa maneno au kwa
vitendo na hivyo huzuia ufanyaji wazi wazi wa matendo maovu.

Haya ya Mtu mwenyewe kwa mwenyewe – Kwani hii ni hali ya mtu kuhisi vibaya
kufanya vitedo viovu, na ni pale mtu anapoona aibu na kujisikia vibaya kufanya mambo
maovu basi ndio hua anazidi kuupata ukaribu kwa Mola wake kwa kumuogopa, na kumtii
na kuachana na makatazo yake.

Kwani tunapoangalia namna Wanawake hawa wawili ambao walivyokua wakijaribu


kuwazuia wanyama wao wasichanganyike na wanyama wa wafugaji wengine ambao ni
Wanaume, kiasi ya kua walikua wako tayari kusubiri hadi wachungaji hao wamalize
kuwanywesha maji wanyama wao, ili wapate kuwanywesha Wanyama wao bila ya
purukushani na kwa utulivu bila ya kuwepo Wachungaji Wanaume na kuanza kupigana
nao vikumbo jambo ambalo limetoweka katika jamii zetu kwani Wanawake wamekua
hawana haya jee ni Wanawake wangapi leo hii wanachanganyika na kupigana vikumbo
na Wanaume masokoni, Madukani n, k.

Vile vile aya inatuonesha umuhimu wa Wanawake kuzungumza kwa kujiamini pale
anapostahiki kuomba kwa ajili ya kupata msaada anapokua na matatizo, anapodai haki
yake n.k hivyo Mwanamke pia anatakiwa kua ni mwenye kujiheshimu na kujua namna
ya kuzungumza kwa kujiamini inapohitajika kufanya hivyo.

Baada ya kumaliza kuwasaidia kuwanyeshea Maji wanyama wao hao basi Nabii Musa
akarudi kivulini na kuendelea kupumzika bia ya kudai malipo wala fadhila kutokana na
jambo alilolifanya, huku Wanawake hao nao wakiwa ni wenye kuondoka na Wanyama
wao, bila ya kutaka kuendelea kukaa na kujuana zaidi na Mtu aliewasaidia kazi yao katika
siku hio, hii ni tofauti na hali ilivyo katika jamii yetu leo hii kwani bila ya shaka kama
ingekua katika kipindi chetu basi tayari ingekua kimeshapatikana kisingizio cha kujuana
majina na kuombana nambari za simu tayari, na kisha baada ya hapo ndio balaa linaanza.

Hivyo aya pia zinatuonesha uzuri wa matumizi ndio ya hali ya kua na hisia za Haya
kubwa sana miongoni wa watu watatu hawa yaani Nabii Musa, Zafura na Liya, kwani
kila mmoja wao alikua anajaribu kupunguza uhusiano wa ukaribu baina yao. Ambapo
532

Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea katika Qur’an kilichofuatia baada ya Nabii Musa
kuwaona kuwauliza kilichowafika Wanawake hao na kujibiwa kwa kusema:

﴾ٌ‫ﱃ ِﻣ ْﻦ َﺧ ٍْﲑ ﻓَِﻘﲑ‬


‫ﺖ إِ َﱠ‬ ِ ِ ‫ﺎل ر‬
َ ‫ب إِِّﱏ ﻟ َﻤﺂ أ‬
َ ْ‫َﻧﺰﻟ‬
ِ
ّ َ َ ‫﴿ﻓَ َﺴ َﻘ ٰﻰ َﳍَُﻤﺎ ﰒُﱠ ﺗَـ َﻮﱠ ٰﱃ إِ َﱃ ٱﻟﻈّ ِّﻞ ﻓَـ َﻘ‬
Fasaqa lahuma thumma tawalla ila aldhdhilli faqala rabbi innee lima anzalta ilayya
min khayrin faqeerun (Surat Al Qasas 28:24)

Tafsir: Hivyo akawanyweshea Maji Wanyama wao na kisha akarudi kivulini na


akasema: ‘Ewe Mola wangu, Hakika mimi ni mwenye kuhitaji kheri yeyote ile
utakayonipa’

Aya inatuonesha kua Nabii Musa ameomba kitu kinachojulikana kama Khayr ambapo
neno Khayr hua ni linamaanisha Kheri, Utajiri au Mali nyingi zilizopatikana kutokana na
njia ya halali, Faida, Mambo mema na pia humaanisha Farasi kama lilivyotumika katika
aya zifuatazo:

﴾‫ٱﳋَِْﲑ ﻟَ َﺸ ِﺪﻳ ٌﺪ‬ ِ ِ ِ﴿


ْ ‫ﺐ‬ّ ُ‫َوإﻧﱠﻪُ ﳊ‬
Wa-innahu lihubbi alkhayri lashadeedun (Surat Al A’adiyati 100:8)

Tafsir: Na kwa hakika yeye ni mwenye kupenda Utajiri kwa Moyo wake wote

Na pale lilipotumika katika aya ambayo ni yenye kusema:

ِ ‫ﭑﳊِﺠ‬ ِ ْ ‫ٱﳋَِْﲑ َﻋﻦ ِذ ْﻛ ِﺮ رِّﰉ ﺣ ﱠ ٰﱴ ﺗَـﻮار‬ ۤ َ ‫﴿ﻓَـﻘ‬


﴾‫ﺎب‬ َ ْ ‫تﺑ‬ ََ َ َ ْ ‫ﺐ‬‫ﺖ ُﺣ ﱠ‬ ْ ‫ﺎل إِِّﱐ أ‬
ُ ‫َﺣﺒَـْﺒ‬ َ
Faqala innee ahbabtu hubba alkhayri AAan dhikri rabbee hatta tawarat
bialhijabi (Surat Sad 38:32)

Tafsir: Kisha (Nabii Sulayman) akasema: ‘Dah, hakika mimi nilijawa na mapenzi ya
kupenda Farasi kuliko kumkumbuka Mola wangu mpaka mda umepita na (Jua)
limeshajificha’

Hivyo kuna wasemao kua hapa Nabii Musa alipoomba Khayr basi alikua akimaanisha
kuomba rizki ya kheri atakayojaaliwa yaani chakula, ambapo anasema Bahr Ul Ilm Abd
533

Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Nabii Musa aliyasema maneno haya
kutokana na kua na njaa kwani kama mtu angeona ndani ya tumbo lake basi
angeona kua hamna kitu isipokua rangi ya kijani inayotokana na kua ni mwenye
kula Majani kwa mda wote huo. Hivyo Nabii Musa hakumuomba Allah Subhanah
wa Ta’ala kitu chochote hapa isipokua Chakula.’

Dua hii aliyoiomba Nabii Musa inatuonesha umuhimu wa kutochoka kumuomba Allah
Subahah wa Ta’ala hata kwa jambo dogo kama hili aliloliomba Nabii Musa. Anasema
Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu kua: ‘Hakika mimi nilipanda Ngamia wangu
kwa mda wa siku mbili mpaka nikafika katika Mji wa Madyan, na nikaulizia
kuhusiana na Mti ambao Musa alikaa na kupumzika chini yake. Nikauona kua ni
ulionawiri huku ukiwa na majani ya rangi ya kijani. Ngamia wangu aliekua na njaa
alikimbilia na akaanza kula Majani ya Mti huo, kwa mda wa saa moja na kisha
akatapika, name nikamuombea dua Nabii Musa kisha nikaondoka.’

Na hivyo kuna wanaosema kua kama Nabii Musa ingekua hakuomba chakula basi Allah
Subhanah wa Ta’ala asingemfanya kua ni wenye kumtegemea Mzee Thabrun hapo
baadae katika kipindi atakachokua anaishi katika mji huu alipofika wa Madyan.

Ambapo kwa upande wa Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari basi yeye
anasema kua: ‘Nabii Musa alisema:

﴾ٌ‫ﱃ ِﻣ ْﻦ َﺧ ٍْﲑ ﻓَِﻘﲑ‬


‫ﺖ إِ َﱠ‬ ِ ِ ‫﴿ر‬
َ ‫ب إِِّﱏ ﻟ َﻤﺂ أ‬
َ ْ‫َﻧﺰﻟ‬ َّ
Rabbi innee lima anzalta ilayya min khayrin faqeerun (Surat Al Qasas 28:24)

Tafsir: ‘Ewe Mola wangu, Hakika mimi ni mwenye kuhitaji kheri yeyote ile
utakayonipa’

Kwa kumaanisha kua: ‘Hakika mimi nnahitaji kitu chochote cha hapa Duniani
utakachonitumia na cha Akhera kua kama ulinzi kutokana na maadui zangu ambao
ni Watu Madhalimu’’

Na kutokana na mtizamo huo basi tunaona pia kama ilivyokua kwa Nabii Yusuf kua
alitoka kwenye usimamizi na uangalizi wa Nabii Yaqub na kujisalimisha kwenye
Usimamizi wa Mola wake na kua ni mwenye kutegemea msaada wa Allah Subhanah wa
Ta’ala tu, wakati kwa upande wa Nabii Musa basi yeye alikua ni mwenye kutoka kwenye
Uangalizi wa Fir’awn na kuingia kwenye uangalizi wa Mola wake na kua ni mwenye
kutegemea msaada wa Allah Subhanah wa Ta’ala tu.
534


MAISHA YA NABII MUSA KATIKA MJI WA MADYAN.

Mara baada ya Zafura na Liya kusaidiwa kunyweshewa maji wanyama wao basi
waliondoka na moja kwa moja wakarudi Nyumbani kwao, ambapo Mzee Thabrun
alipowaona akashangaa kua imekuaje leo hii wamewahi kurudi kabla ya mda wakati siku
nyengine zote hua wanachelewa nao wakasema: ‘Kuna mtu Mkarimu sana alituona
tunavyosubiri na Wanyama wetu kuwanyweshea maji, na akatusaidia kuwachotea
Maji na kutunyweshea maji wanyama wetu.’

Mzee Thabrun akasema: ‘Nendeni kamwiteni huyo Mtu aje kwangu ili nipate
kumshukuru.’ Hivyo akatoka Zafura na kuelekea kwa Nabii Musa kama zinavyosema
aya:

ٍ ‫﴿ﻓَﺠﺂءﺗْﻪ إِﺣﺪ ُاﳘﺎ ﲤَْ ِﺸﻰ ﻋﻠَﻰ ٱﺳﺘِﺤﻴ‬


ِ َ ‫ﺂء ﻗَﺎﻟَﺖ إِ ﱠن أَِﰉ ﻳ ْﺪﻋ‬
‫َﺟَﺮ َﻣﺎ‬ْ‫ﻚأ‬ َ َ‫ﻮك ﻟﻴَ ْﺠ ِﺰﻳ‬ ُ َ ْ َْ ْ َ َ َْ َُ َ
‫ت ِﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻘ ْﻮِم‬ َ ‫ﻒ َﳒَ ْﻮ‬
ْ َ‫ﺎل ﻻَ َﲣ‬
َ َ‫ﺺ ﻗ‬َ ‫ﺼ‬
ِ ‫ﺳ َﻘﻴﺖ ﻟَﻨَﺎ ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ ﺟﺂءﻩ وﻗَ ﱠ‬
َ ‫ﺺ َﻋﻠَْﻴﻪ ٱﻟْ َﻘ‬ َ َُ َ ََْ
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
Fajaat-hu ihdahuma tamshee AAala istihya-in qalat inna abee yadAAooka
liyajziyaka ajra ma saqayta lana falamma jaahu waqassa AAalayhi alqasasa qala
la takhaf najawta mina alqawmi aldhdhalimeena (Surat Al Qasas 28:25)

Tafsir: Na kisha akaja mmoja kati yao (Wanawake hao)huku akitembea kwa mwendo
wa kua na haya. Na akasema: ‘Hakika baba yangu anakuita ili akulipe ujira wako
kutokana na kutusaidia’ na hivyo alipofika na kumuelezea kisa chake basi akasema:
‘Usiwe na Khofu kwani kwa hakika umeokoka kutokana na watu Madhalim’

Aya imetumia neno Tamshii Aala Istihaya ambalo ni lenye kuainisha namna alivyokua
akitembea binti huyo aitwae Zafura kua ni mwenye kutembea kwa taratibu bila ya haraka
na huku akiwa akiangalia chini na amejiziba uso wake kwa kiganja chake na nguo yake
aliyojitanda kutokana na kujaribu kuzitafuta hisia za kutomuangalia anaekabiliana nae
kutokana na haya hizo kwani mbele yake kuna Mwanamme shababi ambae amejikuta
535

kua yuko nae peke yake katika maeneo ambayo ni mbali na nyumbani na hivyo kua pia
si salama kwake kua peke yake na Mwanamme huyo asiemjua.

Kama anavyosema Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mwanamke huyu
alienda kwa Musa huku akiwa amejiziba uso kwa kutumia mkono wa nguo yake,
akiwa anaona haya tofauti na Wanawake wa sasa hivi ambao hua hawaoni haya, na
hivyo hua ni wenye kutafuta visingizio vya kutoka majumbani mwao.’

Anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Shida huyafanya mambo
yasiyoruhusika kua ni yenye kuruhusika’ kwa sababu hairuhusiki kwa Mwanamke
kutoka peke yake kuenda kwa Mwanamme asiemjua wakawa peke yao, lakini hapa ilikua
hakuna la kufanya kwani katika familia yao ilikua hakuna wa kutumwa isipokua mmoja
kati ya Wanawake hawa. Na pia ndio maana ikabidi Wanawake hawa wawe ndio
wanaochunga Wanyama katika familia yao na pia baba yao alikua ni mwenye kuwaamini
sana kutokana na namna alivyowalea mabinti zake wawili hawa.

Hivyo alipofika mbele ya Nabii Musa basi akampa ujumbe wa wito wake kutoka kwa
baba yake na Nabii Musa akakubaliana na wito huo jambo ambalo kwa upande mwengine
linatuonesha kua inakubalika kupokea Malipo ambayo hayakukusudiwa kulipwa au
hayakutegemewa kua ni malipo baada ya kufaya jambo jema na hivyo malipo hayo hua
hayafuti amali njema iliyofanywa na mtu husika. Na bila ya shaka Nabii Musa alikubali
wito huo kwa sababu pia aliona kua Dua yake aliyomuomba Mola wake ilikua
imekubaliwa, hivyo huenda akapata njia ya kutokea kwenye matatizo yake kwa ujumla,
na bila ya shaka hivyo ndivyo ilivyokua.

Kuna baadhi wanaweza wakajiuliza inakuaje mpaka Mwanamke huyu anamfuata Nabii
Musa na kumpa mwaliko kutoka kwa Baba yake huku wakiwa hawajuani na Nabii Musa
anakubaliana na Mualiko huo? Ambapo Mujaddid ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi
anatuambia kuhusiana na hili kua: ‘Inaruhusika kwa Mwanamme kukubaliana na
wito wa Mwanamke asiemjua na kufuatana nae kama Mwanamme huyo atakua na
Taqwa na tahadhari’

Hivyo Nabii Musa akanyanyuka kutoka katika kigogo alichokua amekaaa, na kuitikia
wito huo, huku Zafura akiwa ni mwenye kugeuka na kuanza kuongoza njia, mara ghafla
ukatokea upepo kutoka nyuma yao na upepo huo ukaikandamiza nguo aliyovaa
Mwanamke huyo kwenye Mwili wake kwa nyuma na hivyo kua ni wenye kuanisha
maumbile ya viungo vya mwili wake kwa sehemu ya nyuma ambavyo hapo awali ilikua
havionekani.

Nabii Musa aliona kwa jicho la Mtizamo mmoja tu, na kisha akasema kumwambia
Zefura, ambae nae alihisi namna upepo ulivyokua unakandamiza kwenye mwili wake
kua: ‘Bora kaa nyuma yangu nami nitembee mbele yako niongoze njia, na kama
536

nikikosea njia basi rusha kijiwe upande ambao natakiwa nielekee kwa sababu sisi
Watoto wa Yaqub hua hatuangalii Nyuma ya Miili ya Wanawake.’

Hivyo wakaongoza kwa namna hio, yaani Nabii Musa mbele na Zafura akiwa nyuma
yake hadi wakafika nyumbani kwa Mzee Thabrun ambae alikua ni mzee sana, Nabii
Musa akakaribishwa chakula, lakini akasema kua hahitaji malipo, na Mzee Thabrun
akamwambia kwa kusema kua: ‘Hakika haya si Malipo bali ni ukarimu wetu juu
yako.’, kasha wakala chakula na katika kuzungumza kwao basi Nabii Musa akawaelezea
habari yake juu ya yaliyomkuta nchini Misri na kwanini akajikuta yupo Kisimani
alipowaona Mabinti wa Mzee Thabrun.

Kisa cha Nabii Musa kwa familia ya Mzee Thabrun kiliwavutia sana watu wa familia
hiyo na hivyo kutokana na matukio yaliyomo ndani yake na namna Nabii Musa alivyokua
akionesha maumbile ya tabia nzuri zilizojaa uaminifu na Ucha Mungu mbele Mabinti
wawili hao na Mzee mwenyewe basi wanafamilia hao wakaona kua hakuna mtu mzuri
ambae na mwenye sifa zinazofaa kujumuika katika familia yao kama zaidi ya Nabii
Musa, hivyo wanafamilia hao wakamwambia Nabii Musa: ‘Jee ni nani ambae
anaependa kuishi pamoja na miongoni mwa watu Madhalimu? Ni bora
ulivyokimbia kutoka katika Ardhi ya nchi hio’ Mzee Thabrun akamwambia Nabii
Musa: ‘Usiwe na Khofu kwani hapa uko salama na Mamlaka ya madhalimu wa
Misri hayafiki katika katika Ardhi ya Madyan.’

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea juu ya yaliyotokea baada ya Nabii Musa
kukaribishwa ndani ya Familia hio kama zinavyosema aya:

ِ ‫ﺖ ٱﺳﺘَﺄْ ِﺟﺮﻩ إِ ﱠن ﺧﻴـﺮ ﻣ ِﻦ ٱﺳﺘَﺄْﺟﺮت ٱﻟْ َﻘ ِﻮ ﱡ‬


ِ
﴾‫ﲔ‬
ُ ‫ى ٱﻷَﻣ‬ َ ْ َ ْ َ َ ْ َ ُ ْ ْ َ‫ﺖ إِ ْﺣ َﺪ ُاﳘَﺎ ٰ�َﺑ‬
ْ َ‫﴿ﻗَﺎﻟ‬
Qalat ihdahuma ya abati ista/jirhu inna khayra mani ista/jarta alqawiyyu alameenu
(Surat Al Qasas 28:26)

Tafsir: Akasema mmoja wao (Zafura): ‘Ewe Baba Muajiri kwani kwa hakika m-bora
wa kuajiriwa ni yule mwenye nguvu na mwenye kuaminika’

Ambapo anasema Sultan Al Balagha Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari
kua: ‘Maneno haya aliyoyasema Zafura hua hayaongozeki ubora wake kwani yako
wazi kua unapotaka kumuajiri mtu basi sifa bora ni kua na Nguvu au uwezo wa
kufanya kazi husika na Uaminifu. Na unapohakikisha kuwepo kwa sifa hizo basi
unaweza ukamuachia akufanyie kazi kisha yako nawe bila ya wasi wasi wowote
ukasahau kuhusiana na ufanywaji wa kazi hio.’
537

Anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Baba wa watoto hawa
alimuuliza Zafura: ‘Jee ni kitu gani kilichokufanya wewe ujue kua huyu ni mtu
ambae ni Mwenye Nguvu na ni Muaminifu?’’ ambapo Zafura akajibu: ‘Kutokana
na namna alivyolinyanyua jiwe ambalo kulinyanyua linahitaji watu wengi na
alivyokua akichota maji kutoka kisimani, na uaminifu wake ni kutokana na kua
kamwe hakua ni mwenye kutuangalia kwa mtizamo wa jicho la mara ya pili, na
nilipokuja nae hapa nyumbani alikataa kutembea nyuma yangu’

Ambapo amesema Rasul Allahi Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Wanawake wawili
walikua wako sahih zaid ya Wanawake wengine, na Wanawake wote hao walisema
walipokua wakimuangalia Musa na wakatoa Hukmu Muwafaka mmoja kati yao
alikua ni Mke wa Fir’awn (Asiyah Bint Muzahim) pale aliposema:

ِ ‫ﻚ ﻻَ ﺗَـ ْﻘﺘُـﻠُﻮﻩ ﻋﺴﻰ أَن ﻳـْﻨـ َﻔﻌﻨَﺎ أَو ﻧَـﺘ‬


َ‫ﱠﺨ َﺬﻩُ َوﻟَﺪاً َوُﻫ ْﻢ ﻻ‬ َ َ‫ﲔ ِّﱃ َوﻟ‬
ٍ ْ ‫﴿ ﻗُـﱠﺮةُ َﻋ‬
ْ َ َ ََٰ ُ
﴾‫ﻳَ ْﺸﻌُﺮو َن‬
ُ
Qurratu AAaynin lee walaka la taqtuloohu AAasa an yanfaAAana aw
nattakhidhahu waladan wahum la yashAAuroona (Surat Al Qasas 28:9)

Tafsir: ‘Utulivu wa Macho yangu na yako! Usimuue, kwani huenda akatufaa na


tutamfanya kua ni mtoto wetu’ lakini hawakua ni wenye kujua.

Na wa pili ni Bint wa Shuayb (Zafura) pale aliposema:

﴾‫ﲔ‬ ِ ‫ﺖ ٱﺳﺘَﺄْ ِﺟﺮﻩ إِ ﱠن ﺧﻴـﺮ ﻣ ِﻦ ٱﺳﺘَﺄْﺟﺮت ٱﻟْ َﻘ ِﻮ ﱡ‬


ِ
ُ ‫ى ٱﻷَﻣ‬ َ ْ َ ْ َ َ ْ َ ُ ْ ْ َ‫﴿ ٰ�َﺑ‬
Ya Abati Ista/jirhu inna khayra mani ista/jarta alqawiyyu alameenu (Surat Al Qasas
28:26)

Tafsir: ‘Ewe Baba Muajiri kwani kwa hakika m-bora wa kuajiriwa ni yule mwenye
nguvu na mwenye kuaminika’’

Kulingana na hadith hio na ujumbe uliomo ndani ya matukio haya ya kisa hiki cha Nabii
Musa alipofika katika Ardhi ya Mji wa Madyan basi tunaona kua, kuna baadhi yetu
miongoni mwetu hua ni wenye kuifaham sivyo na hivyo kua ni wenye kuitumia sivyo
pia ile aya ya Qawwam ambayo ni wenye kusema:
538

‫ﺾ َوِﲟَﺂ أَﻧْـ َﻔ ُﻘﻮاْ ِﻣ ْﻦ‬


ٍ ‫ﻀ ُﻬ ْﻢ َﻋﻠَ ٰﻰ ﺑَـ ْﻌ‬ ِ ‫ﺎل ﻗَـ ﱠﻮاﻣﻮ َن ﻋﻠَﻰ ٱﻟﻨِﺴ‬
ِ ‫ﺂء‬ ِ ﴿
َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﺑَـ ْﻌ‬
‫ﱠﻞ ﱠ‬ َ ‫ﻀ‬ َ‫ﻓ‬ ‫ﺎ‬‫ﲟ‬
َ َ ّ َ ُ ُ ‫ٱﻟﺮ َﺟ‬ ّ
﴾‫أ َْﻣ َﻮاﳍِِ ْﻢ‬
Alrrijalu qawwamoona AAala alnnisa-i bima fadhdhala Allahu baAAdhahum
AAala baAAdhin wabima anfaqoo min amwalihim (Surat An Nisaa 4:34)

Tafsir: Wanaume ni Qawwamoona (wasimamizi) juu ya Wanawake kutokana na kua


Allah amewafadhili baadhi yao (Wanaume) juu ya baadhi yao (Wanawake) kutokana
na kile wanachokichuma na kukitumia juu yao.

Na hivyo watu hao wasiojua hua ni wenye kutotaka hata kuwasomesha elimu za juu
watoto wao wa kike, kutotaka kusikiliza ushauri wao, kuwadharau. Kuwapinga mitizamo
yao n.k halafu hapo hapo watu hao hua nio wa kwanza wanapoenda mahospitalini kutaka
kua Wake zao na Watoto wao wa Kike wahudumiwe na Madaktari wa Kike, hivyo
hawataki Wake zao wahudumiwe na Madaktari wa Kiume, halafu hapo hapo hawataki
Wanawake wapate Elimu ya juu, sasa hizi sijui ni akili gani? ila bila ya shaka ni akili
zinazotokana na kuifaham sivyo Qur’an hususan ayah hii ya Qawwam.

Kwani maana ya neno Qawwam kwa kilugha hua linamaanisha kusimamia au kuhudumia
kitu kwa muda mrefu, hivyo tunapozungumzia kifamilia basi neno hili hua linajumuisha
jukumu la kusimamia kimwili, kimahitaji, kiheshima na kimajukumu kwa upande wa
kidunia na kiakhera.

Hivyo maana ya neno Qawwam hua kamwe haimaanishi kama vile wanavyofikiria watu
wengi kua maana yake ni kudhibiti, kuweka chini yake au chini ya mamlaka yake, kuzuia
sauti zao na mitizamo yao, n.k kwani tu akifikiria hivyo basi hua ni mwenye kufikiria
kama walivyokua wakifikiria watu wa jamii Kijahiliyyah.

Kwani katika kuielezea maana ya aya hii, basi anasema Imam Fakhr al Din Al Razi
kuhusiana na aya hii ya Surat An Nisaa 4:34 kua: ‘Alrrijalu qawwamoona AAala
alnnisa-i (Wanaume ni wasimamizi wa Wanawake) ina uhusiano na aya nyengine
kabla yake isemayo:

ِ ‫﴿وﻻَ ﺗَـﺘَﻤﻨـﱠﻮاْ ﻣﺎ ﻓَﻀﱠﻞ ﱠ‬


﴾‫ﺾ‬ َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﺑِﻪ ﺑَـ ْﻌ‬
ٍ ‫ﻀ ُﻜ ْﻢ َﻋﻠَ ٰﻰ ﺑَـ ْﻌ‬
َ َ َْ َ
Wala tatamannaw ma fadhala Allahu bihi baAAdhakum AAala baAAdhin’(Surat
An Nisaa 4:32)
539

Tafsir: Na wala msitamani kile ambacho Allah amewafadhili baadhi yenu kuliko
wengine.

Imam Fakhr Ad Din Al Razi anaendelea kwa kusema: Aya ambayo tulisema kua
ilishushwa kwa sababu baadhi ya Wanawake walitoa kauli kuhusiana na Allah
kuwapendelea katika Urithi Wanaume. Hivyo Allah ameweka wazi katika ayah hii
kua amewafadhili tu Wanaume juu ya Wanwake kwa sababu Wanaume ni
Wasimamizi wa Wanawake.

Kwani ingawa wote Mke na Mume wanafaidika na matunda na haki zinazotokana


na kua pamoja, basi Allah amemuamrisha Mwanamme kumlipa Mwanamke
sehemu ya ndoa yao, na kumhudumia katika mahitaji ya kila siku, hivyo ongezeko
la upande mmoja hukabiliana sambamba na ongezeko la upande wa pili – na hivyo
hua kama vile hamna pendeleo baina yao. Jambo hili linaweka wazi mpangilio wa
namna zilivyopangika aya.’

Kutokana na Mtizamo huo basi tunaona kua Mwanamke ni Ibn Adam kama Mwanamme
hivyo hua pia ni mtu ambae anatakiwa apewe nafasi na asisikilizwe anapotaka kutoa
mchango na ushauri katika maisha na mambo mbali mbali waliyokua na ujuzi nayo juu
yake, na pia asomeshwe ili aweze kupata elimu ya juu na hapo ndipo itakapowezekana
kwa Wanawake wa Kiislam kua ni wenye kuhudumiwa na nyanja tofauti na Wanawake
wenzao wa Kiislam ikiwemo Madaktari na Wahudumu wa Kike wa Kiislam katika
Mahospitali.

Tunaporudi katika mfano wa kisa basi tunaona kua mbali ya kua Zafura alikua ni
Mwanamke mwenye kuona Haya na hii ni kutokana na Imani yake na Maumbile yake
lakini pia kutokana na maumbile yake hayo basi alikua ni mtu mwenye upeo mpana
kiufaham na ni mwenye kuona mbali.

Na ndio maana kutokana na kuona mbali kwake Zafura na kumpa ujumbe huo na
vithibitisho baba yake basi Thabrun akawa ni mwenye kuju thamani ya Mtu aliekuwepo
mbele yake, kiasi ya kua vithibitisho hivyo havikupelekea tu kutaka kumuajiri Nabii
Musa bali vilipelekea kumthibitishia yeye kua haiwezekani kumkosa na kumpoteza mtu
kama huyo, hivyo bora wamvute na wamuingize kwenye familia yao kabisa, kwani pia
ni hasara kubwa sana kumpoteza mtu ambae umuhimu wake unahitajika sana katika
familia, hivyo Thabrun akachukua maamuzi kwa kusema kama zinavyothibitisa aya:
540

‫ﲔ َﻋﻠَ ٰﻰ أَن َﺄﺗْ ُﺟَﺮِﱏ َﲦَ ِﺎﱏَ ِﺣ َﺠ ٍﺞ‬ ۤ َ َ‫﴿ﻗ‬


‫ﻚ إِ ْﺣ َﺪى ٱﺑْـﻨَـ َﱠ‬
ِ ْ ‫ﱴ َﻫﺎﺗَـ‬ َ ‫ﻳﺪ أَ ْن أُﻧﻜِ َﺤ‬
ُ ‫ﺎل إِِّﱐ أُِر‬
‫ﻚ َﺳﺘَ ِﺠ ُﺪِﱏ إِن َﺷﺎءَ ﱠ‬
ُ‫اﻪﻠﻟ‬ َ ‫َﺷ ﱠﻖ َﻋﻠَْﻴ‬ ُ ‫ﻳﺪ أَ ْن أ‬ ُ ‫ﻨﺪ َك َوَﻣﺂ أُِر‬ ِ ِ‫ﻓَِﺈ ْن أَْﲤَﻤﺖ ﻋ ْﺸﺮاً ﻓَ ِﻤﻦ ﻋ‬
ْ َ َ ْ
ِ ْ َ‫َﺟﻠ‬ ِ َ َ‫ﺼﺎﳊِِﲔ۞ﻗ‬ ِ
‫ﺖ ﻓَﻼَ ﻋُ ْﺪ َوا َن َﻋﻠَ ﱠﻰ‬
ُ ‫ﻀْﻴ‬
َ َ‫ﲔ ﻗ‬ َ ‫ﻚ أَﱠﳝَﺎ ٱﻷ‬ َ َ‫ﻚ ﺑَـْﻴ ِﲎ َوﺑَـْﻴـﻨ‬َ ‫ﺎل ٰذﻟ‬ َ ‫ﻣ َﻦ اﻟ ﱠ‬
﴾‫ﻮل وﻛِﻴﻞ‬
ٌ َ ُ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻋﻠَ ٰﻰ َﻣﺎ ﻧَـ ُﻘ‬ ‫َو ﱠ‬
Qala innee oreedu an onkihaka ihda ibnatayya hatayni AAala an ta/juranee
thamaniya hijajin fa-in atmamta AAashran famin AAindika wama oreedu an
ashuqqa AAalayka satajidunee in shaa Allahu mina alssaliheena Qala dhalika
baynee wabaynaka ayyama al-ajalayni qadaytu fala AAudwana AAalayya
waAllahu AAala ma naqoolu wakeelun (Surat Al Qasas 28:27-28)

Tafsir: Akasema (Thabrun): ‘Hakika mimi nataka nikuozeshe mmoja kati ya binti
yangu kwa sharti la kua unifanyie kazi kwa miaka minane, lakini kama utakamilisha
miaka kumi basi itakua umenisaidi, lakini hata hivyo sitaki kukutia kwenye ugumu,
hivyo Allah In-shaa Allah nitakua ni miongoni mwa waja wema’ Nae (Musa)
akasema: ‘Juu ya hilo tumekubaliana baina ya mimi na wewe, na vyovyote vile
nitakavyotumikia baina ya vipindi hivyo basi hukuna kudhulumiwa juu yangu na
Allah ni wakili juu ya nnacho kisema.’

Aya zintatuonesha unyenyekevu wa Nabii Musa na Ucha Mungu wake kwani ametoka
kwenye maisha ya Mtoto wa Mfalme na moja kwa moja kuangukia kwenye hali kua ni
mchungaji wa Kondoo tena kwa miaka kadhaa, na ingawa aliombwa kutoa mtizamo
wake juu ya jambo hilo lakini nae hakua ni mwenye kusikitika wala kukataa, na badala
yake alisema: ‘Hamna ugumu wowote, hilo na wala hutokua wewe ni mwenye
kunidhulumu mimi kutokana na kunipa kazi kama hio na kwa hakika Allah ni
wakili wangu juu ya hilo.’

Hali hii inanikumbusha kisa cha Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu ambae alikua ni
Jenerali Mkuu wa Majeshi ya Kiislam katika kipindi cha uhai wa Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam na pia katika kipindi cha Utawala wa Sayyidna Abu Bakr Radhi Allahu
Anhu, na alipoingia madarakani Sayyidna Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu basi
Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu akashushwa cheo na kua Mpiganaji wa Kawaida
na Jukumu la Genereli Mkuu akapewa Abu Ubaydah Ibn Jarrah Radhi Allahu Anhu.

Na ingawa wapiganaji wote wa Jeshi la Kiislam walihoji na kutaka kugomea mabadiliko


hayo, lakini Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu mwenyewe akasema kwa ridhaa na
541

bila ya kinyongo kua: ‘Hamna tatizo, wakati Umar ni Amir ul Muuminina, basi sisi
wajibu wetu ni Kusikiliza na Kutii’ na hivyo ndivyo wanavyokua watu wenye Imani
na namna wanavyokubaliana na Majaaliwa na Makadirio ya Mola wao juu yao bila ya
kusikitika.

Ambapo aliulizwa Rasul Allah Salallahu Alayhi was Salam: ‘Jee Musa alitumika kwa
kipindi gani baina ya vipindi hivyo viwili?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
akasema kua: ‘Alitimiza kipindi kamilifu na kile kilichokubalika na Macho yake.’

Kwani anasema Imam Abu Bakr Ahmad Ibn Husayn Ibn Ali Ibn Musa Al Khosraji Al
Bayhaqi kua amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kama akiwa mtu
ni mwenye sifa nzuri za Kidini akaja kuposa kwa mmoja wenu, basi muozesheni
kwa binti yenu kwani vyengievyo itakua kuna ufisadi mkubwa sana kwenye Ardhi

Ambapo kwa upande mwengine basi tuaona kua aya inatonesha kua ni jambo la kawaida
kwa Baba kumtafutia Mume mzuri anaefaa kwa ajili ya Binti yake, kama katika mfano
wa Sayyidna Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu alipokua akimtafutia Mume binti
yake atwae Hafsa ambae mumewe alifariki katika vita vya Badr na hivyo Umar Ibn Al
Khattab akawa ana hamu kubwa kua Bint yake aolewe na Masahaba wenzake yaani Abu
Bakr As Siddiq Radhi Allahu Anhu au Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anhu na
alipowambia juu ya ombi lake hilo basi wakawa wamekaa kimya na hivyo Hafsa
akajaaliwa kupata Mume Bora zaidi ambae ni Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Na pia pale inapotokea hali ambayo Binti mwenyewe kua ni Mwenye kutafuta Mume
kwa nia ya mapenzi na kutaka kuheshimika na kupata taadhima kwa mfano kama
ilivyokua kwa Umm ul Muuminina Khadija Bint Khuwaylid Radhi Allahu Anha pale
alipotaka kuolewa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam akakubaliana na ndoa hio na wakaona na hivyo ndoa hio kua ni ndoa
ya kwanza ya Rasul Allah Salallahu A’alayhi wa Salam.

Na pia kama vile ilivyokua katika ndoa yake ya mwisho ya Rasul Allah Salallahu
A’alayhi wa Salam katika mwaka wa 7 Al Hijra pale Maymuna Bint Harith Al Hilaliyah
ambae ni Mama yake mdogo Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu na pia ni Mama yake
mkubwa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu alipomuomba Rasul Allah Salallahu
A’alayhi wa Salam kua amuoe.

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Imam Ibn Hajar Al Asaqalani katika Al Isaba kua
amesema Aisha Ummu ul Muuminina kua: ‘Maymuna Bint Harith Radhi Allahu Anha
alikua ni Mke Mwenye Taqwa zaidi miongoni mwa wake Rasul Allah Salallahu
A’alayhi wa Salam na pia ni mwenye kujitolea zaidi kwa ajili ya watu wake.’
542

Hivyo tunapozungumzia suali hili la Baba kumtafutia Mume Binti yake au Mwanamke
kumfuata Mwanamme anaempenda ili amuoe kwa ajili yake basi kwa kisharia Mahari
hua ni jambo la lazima kwa Mwanamme kutoa, kwa ajili ya kumlipia Mwanamke huyo
Mahari yake, kulingana na namna watakavyokubaliana, kama ilivyokua katika ndoa ya
hii ya Nabii Musa na Zafora na kama namna walivyokubaliana na kama ilivyokua kwa
ndoa ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Umm ul Muuuminina Khadija Bint
Khuwaylid Al Kubra kwa namna walivyokubaliana.

Ambapo kwa upande mwengine basi pia kuna hali ambayo inajulikana kama Hibbah
ambalo ni neno la Kiarabu linalomaanisha Zawadi yaani Kitu Mtu hua ambacho anatoa
bila ya kutegemea Malipo badala yake. Na Kisharia hua linamaanisha Kummilikisha mtu
kitu kwa hiari yake mwenyewe Mmiliki wa kitu husika kua kitu hicho anammilikisha
mtu mwengine amtakae bila ya Kutegemea Malipo au Fadhila kutoka kwake na
Humilikishwa kwa Ridhaa ya mmilikishaji.

Na ingawa hali hii ipo katika Mali tu lakini tunapozungumzia kuhusiana na Hibbah ya
ndoa basi hua tunamaanisha hali ambayo Mwanamke hua ni mwenye kutaka
kujimilikisha mwenyewe kwa Mwanamme ili aolewe nae kama vile ilivyoruhusiwa kwa
upande wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliruhusiwa na Allah Subhanah wa
Ta’ala, kuoa Mwanamke ambae ametaka kuolewa na yeye Rasul Allahi Salallahu
A’alayhi wa Salam akamridhia Mwanamke huyo basi aliruhusika kumuoa bila ya yeye
Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam kulipa Mahari yeyote, na hii iliruhusika kwa
upande wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam tu.

Hivyo Hibbah haikuruhusika kwa Mtu mwengine yeyote badala yake isipokua kwa Rasul
Allah Salallahu A’lahi wa Salam kama ilivyosema aya ifuatayo:

ۤ ِ‫﴿ ٰ�َﻳـﱡﻬﺎ ٱﻟﻨِﱠﱮ إِ ﱠ� أَﺣﻠَﻠْﻨﺎ ﻟَﻚ أَزواﺟﻚ ٱﻟﻼﱠ‬


‫ﻚ‬َ ُ‫ﺖ َﳝِﻴﻨ‬ ْ ‫ﻮرُﻫ ﱠﻦ َوَﻣﺎ َﻣﻠَ َﻜ‬ َُ‫ُﺟ‬ ‫أ‬ ‫ﺖ‬َ ‫ﻴ‬
ْ ‫ـ‬
َ ‫ﺗ‬‫آ‬ ‫ﰐ‬ َ َ َْ َ َ ْ ‫َ ﱡ‬
‫ﺎت‬ ِ َ‫ﻚ وﺑـﻨ‬ ِ ِ
َ َ َ ‫ﻚ َوﺑَـﻨَﺎت َﺧﺎﻟ‬ َ ِ‫ﺎت َﻋ ﱠﻤﺎﺗ‬ ِ َ‫ﻚ وﺑـﻨ‬ ِ ِ
َ َ َ ‫ﻚ َوﺑَـﻨَﺎت َﻋ ّﻤ‬ ‫ِﳑﱠﺂ أَﻓَﺂءَ ﱠ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻋﻠَْﻴ‬
ِ ِ‫ﺖ ﻧَـ ْﻔ َﺴ َﻬﺎ ﻟِﻠﻨ‬
‫ﱠﱮ إِ ْن أ ََر َاد‬ ِ
ْ َ‫ﻚ َو ْٱﻣَﺮأًَة ﱡﻣ ْﺆﻣﻨَﺔً إِن َوَﻫﺒ‬
ِ َ ِ‫ﺧﺎﻻَﺗ‬
َ ‫ﻚ ٱﻟﻼﱠﺗﻰ َﻫ‬
َ ‫ﺎﺟْﺮ َن َﻣ َﻌ‬ َ
ّ
‫ﺿﻨَﺎ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ‬ ِ ِ ِ ِ ِ َ ‫ٱﻟﻨِﱠﱮ أَن ﻳﺴﺘَﻨﻜِﺤﻬﺎ ﺧﺎﻟِﺼﺔً ﻟﱠ‬
ْ ‫ﲔ ﻗَ ْﺪ َﻋﻠ ْﻤﻨَﺎ َﻣﺎ ﻓَـَﺮ‬ َ ‫ﻚ ﻣﻦ ُدون ٱﻟْ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬ َ َ ََ ْ َ ‫ﱡ‬
ِ ِ ۤ
ً‫ٱﻪﻠﻟُ َﻏ ُﻔﻮرا‬‫ﻚ َﺣَﺮ ٌج َوَﻛﺎ َن ﱠ‬ َ ‫ﺖ أَْﳝَﺎﻧـُ ُﻬ ْﻢ ﻟ َﻜْﻴﻼَ ﻳَ ُﻜﻮ َن َﻋﻠَْﻴ‬ْ ‫ِﰲ أ َْزَواﺟ ِﻬ ْـﻢ َوَﻣﺎ َﻣﻠَ َﻜ‬
﴾ً‫ﱠرِﺣﻴﻤﺎ‬
543

Ya ayyuha alnnabiyyu inna ahlalna laka azwajaka allatee atayta ojoorahunna


wama malakat yameenuka mimma afaa Allahu AAalayka wabanati AAammika
wabanati AAammatika wabanati khalika wabanati khalatika allatee hajarna
maAAaka waimraatan mu/minatan in wahabat nafsaha lilnnabiyyi in arada
alnnabiyyu an yastankihaha khalisatan laka min dooni almu/mineena qad
AAalimna ma faradna AAalayhim fee azwajihim wama malakat aymanuhum
likayla yakoona AAalayka harajun wakana Allahu ghafooran raheeman (Surat Al
Ahzab 33:50)

Tafsir: Ewe Nabii (Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam)! Kwa Hakika


tumekuhalalishia wake zako, ambao umewalipia mahari yao, na ambao mkono wako
wa kulia unawamiliki (wanawake waliotekwa vitani na watumwa) ambao Allah
amekupa, na binti wa Ami zako, bint wa Ammah (shangazi) zako, binti wa Khal
(wajomba) zako, binti wa Khalah (mama wadogo) ambao walihama (kutoka Makkah)
pamoja nawe, na mwanawake alieamini ikiwa atajipeleka (kutaka kuolewa) kwa
Mtume, na Mtume akataka kumuoa; Haki ambayo ni yako tu (kwa Nabii Muhammad
peke yake), lakini si kwa Waumini wengine. Hakika tunajua ni kipi tulichowaamrisha
kuhusiana na wake zao na wale wanaomilikiwa na mikono yao ya kulia - Ili kusiwe na
uzito kwako wewe. Na Allah ni mwingi wa Kusamehe na mwingi wa Rehma.

Ambapo anasema Shaykh Wahbah Al Zuhaily, kuhusiana na amrisho la ayah hii ni kua:
‘Hili ni Amrisho linaloelezea aina za Wanawake ambao wanaweza kuolewa na
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambao ni Wanawake walioamini na
kujipeleka wenyewe kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ili waolewe, na
ikawa kuna uhakika kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anataka kumuoa
Mwanamke huyo, basi hii hua Hibbah, yaani Ndoa bila Mahari wala Walii wala
Shahidi, ambayo ni Ndoa iliyo makhsusi kwake yeye Rasul Allah Salallahu Alayhi
wa Salam tu’

Hivyo Nabii Musa akakubaliana na mtizamo wa Thabrun baada ya majadiliano yao kua
mahari yawe kama alivyotaka Mzee Thabrun, na hivyo Nabii Musa akawa ni mwenye
kuajiriwa na familia ya Mzee Thabrun na kuishi Nyumba moja na familia ya Mzee
Thabrun kwa moyo safi bila ya kipingamizi wala kujisikia vibaya ndani ya nafsi yake.

Tunapoangalia kwa upande wa Hikma na Busara ya Nabii Musa kua ni mwenye


kujaaliwa kufuga Wanyama kama hawa yaani Mbuzi na Kondoo basi tunaona kua hii ni
sawa na Hikma ya matayarisho ya kiakili, kiufaham na kiujuzi kwa takriban Mitume
wote ambao walikua ni wenye kufanya kazi hio, kwani Wanyama hua viumbe dhaifu
wasiokua na akili wanaohitaji kuhudumiwa na kusimamiwa katika kila kitu, hivyo hua
inahitajika Subira kubwa sana na Usatahamilivu katika kuwahudumia kwa ukarimu na
upole bila ya kutumia nguvu au kuwaonea kwa kuwapiga Wanyama hao kutokana na
544

udaifu wa ufaham wao, jambo ambalo hua pia inahitajika kwa Watu wanaopelekewa
Mitume katika Jamii zao.

Na pia ni kama inavyowekwa wazi a hadith ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
kama anavyosema Utba Ibn Nadar Radhi Aallahu Anhu kua: ‘Masahaba walikuja kwa
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na wakawa ni wenye kusoma Surat Al Qasas,
na walipofika katika kisa cha Nabii Musa basi akasema Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam kua: ‘Musa Alayhi Salam aliajiri kwa miaka minane mpaka kumi
kufanya kazi kwa ajili ya Kujilinda Nafsi yake na Kujaza Tumbo lake.’’


FIMBO YA NABII MUSA


Baada ya makubaliano hayo basi, Nabii Musa akawa ni mwenye kuchunga Kondoo wa
Mzee Thabrun, na hivyo Mzee huyo akaamua kumpa Nabii Musa Fimbo ya kuchungia
Kondoo hao na akamtuma Zafura akachukue moja kati ya Fimbo zilizomo kwenye
chumba cha kuhifadhia vitu mbali mbali ndani yake, na alipomletea Fimbo hio basi
Thabrun akamrudisha na Fimbo hio na kumuambia kua akachukua Fimbo nyengine,
lakini kila akienda na kiweka kisha akachukua Fimbo nyengine basi Fimbo aliyoichukua
hua ni ile ile ambayo alirudishwa nayo.

Hivyo Mzee Thabrun akaamua kumpa Nabii Musa Fimbo hio hio, lakini baadae akajuta
kwa sababu Fimbo hio alipewa na Nabii Ayoub aiweke mpaka atakapokuja Mtu
anaestahiki kua ni Mmiliki wa Fimbo hio. Hivyo Mzee Thabrun akamwita Nabii Musa
akamwambia amrudishie Fimbo hio, lakini na Nabii Musa nae akawa ni mtu ambae
aliipenda sana Fimbo hio na hivyo akawa mzito kuirudisha Fimbo hio.

Nabii Musa akawa anajitetea namna alivyoipenda na namna atakavyoitumia na kuitunza


Fimbo hio kiasi ya kua ikawa kuna mabishano baina yao kuhusiana na nani atakaeweza
kuitunza vizuri zaidi Fimbo hio. Kwani Mzee Thabrun amekaa nayo kw amda mrefu sana
na aliweza kuitunza bila ya tatizo lolote, na Nabii Musa ndio kwanza ameanza kukaa
nayo na kuitumia, hivyo katika kubishana kwao basi Allah Subhanah wa Ta’ala
akamuamrisha Malaika aingie katika Maumbile ya Ibn Adam kisha aende akatatue
mabishano hayo, na mara akatokea mtu mzima aliekua anapita karibu ya Nabii Musa na
Mzee Thabrun na alipouliza wanabishana nini na kuambiwa basi akashauri kua Fimbo
545

hio iwekwe chini, kisha atakaeweza kuinyanyua baada ya kuwekwa kwake chini basi
atakua ndie anaestahili kua mmiliki wa Fimbo hio.

Fimbo ikawekwa chini, kisha Mzee Thabrun akawa ndie wa mwanzo kujaribu
kuinyanyua Fimbo hio, lakini kila akiinyanyua basi Fimbo hio ilikua imeganda pale pale
chini kama iliyoota mizizi mirefu sana na hivyo haing’oki kutoka ardhini. Akajaribu mara
kadhaa, lakini matokeo yake yakawa ni yale yale. Baada ya majaribio kadhaa basi ikafika
zamu ya Nabii Musa ambae nae alipoinyanyua Fimbo hio, basi ilinyanyuka na mikono
yake kama vile kitu ambacho kimeanguka na kisha kikaokotwa hapo hapo, kwa ulaini na
wepesi kabisa bila ya kutumia nguvu za aina yeyote.

Ambapo kwa upande wa Muqatil Ibn Sulayman basi yeye anasema kua: ‘Fimbo ya Nabii
Musa alipewa na Malaika Jibril katika siku ambayo alihama kutoka Misri kuelekea
Madyan’

Na kwa upande wa Kaab Al Ahbar basi yeye anasema kua: ‘Hakika alipokuja Abd
Allah Ibn Amr Ibn Al Aas Radhi Allahu Anhu katika Mji wa Makkah, basi mimi
nilisema kua: ‘Muulizeni kuhusiana na mambo matatu, na kama akijua majibu
yake basi bila ya shaka atakua ni Mtu mwenye Il’m kweli. Muulizeni kuhusiana na
kitu cha Peponi ambacho Allah Subhanah wa Ta’ala amekiweka Duniani kwa ajili
ya Ibn Adam, Muulizeni kuhusiana na Kitu cha Mwanzo kuwekwa Ardhini,
Muulizeni kuhusiana na Mti wa Mwanzo uliopandwa Ardhini.’’

Baada ya Abd Allah Ibn Amr Ibn Al Aas Radhi Allahu Anhu kuulizwa masuali hayo basi
akajibu: ‘Ama kuhusiana na kitu cha mwanzo cha Peponi ambacho Allah Subhanah
wa Ta’ala amekiweka Duniani kwa ajili ya watu ni Hajar Al Aswad. Kitu cha
Mwanzo umewekwa ardhini ni Kisima cha Barhut kilichopo katika Ardhi ya
Yemen ambacho Roho za Makafiri husafiri kupitia hapo, ama kuhusiana na Mti wa
mwanzo kuwekwa ardhini ni Mti ambao Musa amekata kutokana nao Fimbo yake.’

Na baada ya Kaab kuambiwa majibu hayo aliyoyatoa Abd Allah Ibn Amr Al As Radhi
Allahu Anhu basi akasema: ‘Naam, bila ya shaka amesema kweli na anaenda
sambamba na mafunzo kwani kwa hakika huo ndio Mti aliokata Musa Fimbo yake,
na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akatia Miujiza yake ndani yake.’

Ama kwa upande Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye amesema kua:
‘Mtawala wa Bazantiyun alimuandikia barua Muawwiyah na kumwambia kua
amwambie kuhusiana na viumbe wanne ambao hawakuwahi kucheza ndani ya
Tumbo la Uzazi. Hivyo Muawwiyah alipoisoma Barua hio akasema: ‘Ya Allah
Muadhirishe Mtawala huyu, hivi mimi nitajuaje kuhusiana na Viumbe hivyo?’
Ambapo mmoja kati ya watu wake akasema: ‘Mwandikie Abd Allah Ibn Abbas
546

umuulize anaweza akawa anajua’ Hivyo akaniandikia mie barua nami nikamjibu:
‘Ama kuhusiana na Viumbe Vitano ambavyo havikucheza ndani ya tumbo la Uzazi
la Mama ni Adam, Hawa, Kondoo alieshushiwa Nabii Ibrahim kwa ajili ya
kumuokoa Nabii Ismail na Fimbo ya Musa ambayo alipokua akiitupa chini hugeuka
Nyoka.’’

Na kuhusiana na jina la Fimbo hio basi Wanazuoni nao pia wametofautiana juu yake
kwani kuna wasema kua ilikua ikiitwa Masa na huu ni mtizamo wa Said Ibn Jubayr
ambapo kwa mtizamo wa Muqatil Ibn Sulayman basi yeye anasema kua ilikua ikiitwa
Naf’ah yaani yenye Kufaa, na Imam Ibn Habban yeye amesema kua ilikua ikiitwa
Ghiyath yaani Msaidizi.


HIJRA YA PILI YA NABII MUSA KUTOKA MADYAN KUELEKEA
MISRI.


Baada ya Nabii Musa kutimiza miaka 10 katika mji wa Madyan huku akiwa ni Mfugaji
wa wanyama wa Mzee Thabrun hukua akiwa na Kondoo kadhaa kama alivyoahidiwa na
Mzee Thabrun na hapo hapo akiwa na Mke wake ambae ni binti wa Mzee Thabrun ambae
ni Zafora, huku Kondoo hao wakiwa na Baraka sana katika Kuzaa kwao, kwani walikua
wanazaa maradufu zaidi ya hapo awali kabla ya kuwasili Nabii Musa katika mji huo wa
Madyan.

Siku moja baada ya kutumiza mda wake basi Nabii Musa alitoka na familia yake na
Mifugo yake kutoka katika Mji huo huku akiwa na nia ya kumtafuta kaka yake Nabii
Harun ambae alikua akimfikria kwa mda wote aliokua amekaa katika Mji wa Madyan
hivyo akaamua atafute njia ya kumtoa kutoka katika Ardhi ya Misri kaka yake huyo ili
aje nae katika Ardhi ya Madyan, ambayo hii ilikua ni miongoni mwa sababu ya kua Nabii
Musa atoke kutoka katika Mji wa Madyan, ambako alikwenda kutayarishwa kimaumbile
na kiufaham kwa ajili ya kubeba jukumu kubwa na zito kutoka kwa Muumba wake ambae
ni Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo Nabii Musa akajikuta yupo katika upande wa
kulia wa Mlima wa Tur katika jangwa la Sinai.

Alipofika katika upande huo wa Magharibi wa Jangwa la Sina, kaika mda wa wakati wa
Jioni hali ya hewa ikaanza kubadilika ghafla, Nabii Musa na familia yake wakaamua kua
watafute eneo zuri ili wapige kambi, kwani hawawezi kuendelea tena na safari yao. Na
547

kila mda unavyozidi kuenda basi ndivyo hali ilivyozidi kua mbaya kwani Upepo
haukutulia na hivyo ukayasukuma Mawingu katia eneo la Jangwani hapo na
yakakusanyika na kaanza kutanda kwa uzito na wingi juu angani, kiza kikaanza kaingia
na kuashiria mvua kubwa inayotaka kuanza kunyesha katika maeneo hayo, huku radi
kavu na ngurumo zikatawala Jangwani na giza likazidi kugubika na mvua ndogo ndogo
ikaanza kunyesha Jangwani.

Hali hii ilidumu kwa masaa kadhaa, halafu mvua ikakata kabisa lakini kiza kilikua
kimezidi kutanda kutokana na wingu lililobakia juu angani, kiasi ya kua haiwezekani
kuona hata Nyota moja angani na hivyo hakuna uwezo wa kujua upande gani ni
Mashariki na upande gani ni Magharibi wala Kusini wala Kaskazini, hivyo ilikua vigumu
kwa Nabii Musa ambae ni mzoefu wa kungalia muelekeo wa Nyota Angani kwani mda
wa miaka 10 amekua akitumia Muongozo wa Nyota wakati unapoingia Usiku anapokua
Malishoni.

Lakini katika siku ya leo, na katika wakati huu, yaliyotokea yalikua ni maajabu makubwa
sana kwake yeye, kwani hakuweza kujua kua wanatakiwa waelekee upande gani, wakati
mda usiku unazidi unaenda basi na baridi nayo inazidi kuongezeka kwani hivyo ndivyo
ilivyo hali ya mazingira ya Jangwani. Wakati wa Mchana kunakua na Jua kali na Joto
sana na wakati wa Usiku hua kunakua na Baridi kali sana nah ii ni kwa sababu mchanga
una maumbile ya kutohifadhi Joto Ndani yake, hivyo wakati wa mchana linapopiga Jua
juu ya Mchanga basi mchanga huo hulirudisha nje yake Joto la jua hilo, na katika wakati
wa usiku Mchanga huo hua unaachia Joto lake kwa kasi kubwa sana na hivyo hua
kunatokea baridi kali na ya haraka sana kutokana na kupoa kwa mchanga huo hususan
inapokua katika wakati wa hali ya hewa ya Baridi.

Hivyo Nabii Musa na familia yake kidogo kidogo wakaanza kuhisi baridi kutokana na
mazingira ya hali ya hewa hio, wakataka kuwasha Moto ili wapate kuoka Moto, lakini
ikawa hakuna cha kuwashia, kwani kila kitu kimeroa chapa chapa, wakawa hawajui la
kufanya wala wapi kwa kuelekea ilikuomba msaada. Nabii Musa akakaa kimya na
kuanza kutumia hisia zake za kimaumbile kwani labda huenda akaweza kusikia sauti
zinazoashiria kuwepo kwa viumbe wengine karibu na eneo walilopiga kambi Jangwani
hapo, lakini hakuweza kusikia kitu, akajaribu kuangaza macho yake huku na kule ili
labda ataona kitu kitakachoweza kumsaidia, lakini wapi, kwani Jangwani baada ya mvua
hio kupita basi hapo kulikua kumetanda kimyaa kizito sana kinachotisha na kumetulia
sana kiasi ya kua hakuna hata sauti ya mdudu inayosikilikana.

Nabii Musa akashangaa na kujiuliza masuali mengi sana, imekuaje hali hii leo hii, kwani
si ya kawaida hivyo katika kuendelea kuchunguza kwake basi mara ghafla kwa mbali
katika maeneo ya Mlimani akaona mwangaza kama wa Moto unaomurika, Allah
Subhanah wa Ta’ala anazungumzia hali aliyokua nayo Nabii Musa pale alisema katika
aya isemayo:
548

‫ﺎلِ ﻷ َْﻫﻠِ ِﻪ‬ َ َ‫ﺐ ٱﻟﻄﱡﻮِر َ�راً ﻗ‬ ِ ِ‫َﺟﻞ و َﺳﺎر ِﺄﺑ َْﻫﻠِ ِﻪ آﻧَﺲ ِﻣﻦ َﺟﺎﻧ‬
َ َ َ َ َ ‫ﻮﺳﻰ ٱﻷ‬ َ ‫ﻀ ٰﻰ ُﻣ‬ َ َ‫﴿ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ ﻗ‬
‫ﺖ َ�راً ﻟﱠ َﻌﻠِّ ۤﻲ آﺗِﻴ ُﻜ ْﻢ ِّﻣْﻨـ َﻬﺎ ِﲞٍََﱪ أ َْو َﺟ ْﺬ َوةٍ ِّﻣ َﻦ ٱﻟﻨﱠﺎ ِر ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜ ْﻢ‬ ۤ ۤ
ُ ‫ْٱﻣ ُﻜﺜُـﻮاْ إِِّﱐ آﻧَ ْﺴ‬
﴾‫ﺼﻄَﻠُﻮ َن‬ ْ َ‫ﺗ‬
Falamma qadha moosa al-ajala wasara bi-ahlihi anasa min janibi alttoori naran
qala li-ahlihi omkuthoo innee anastu naran laAAallee ateekum minha bikhabarin
aw jadhwatin mina alnnari laAAallakum tastaloona (Surat Al Qasas 28:29)

Tafsir: Hivyo alipotimiza Musa mda wake waliokubaliana na akawa anatembea na


Watu wa Familia yake. Akaona Moto katika Mlima Tur, akasema kuwaambia watu
wake: ‘Subirini nimeona Moto. Na hivyo labda nnaweza nikakuleteeni habari au
kijinga ili mpate kuoka Moto.’

Nuru ya muangaza huu ilikua ni Nuru ya matumaini kwake yeye Nabii Musa na familia
yae kiasi ya kua akapata nguvu ya ghafla na mwili wake kuhisi hali ya joto kutokana na
matumaini ya kuona Moto huo, kwani alikua anajua kua atapata msaada unaohitajika,
ambao ni aidha Moto wa kuwawashia familia yake ili wapate kupata joto na kuondokana
na baridi waliyokua nayo au atapata kuulizia njia na hivyo kupata habari zozote
kuhusiana na njia na muongozo wa anaouhitaji katika safari yake, kwani huenda moto
huo ukawa umewasha na wachungaji kama yeye au wasafiri waliokwama njiani kama
yeye, kama zinavyofafanua pia aya zifuatazo:

ٍ َ‫ﺖ َ�راً ﻟﱠ َﻌﻠِّ ۤﻲ آﺗِﻴ ُﻜ ْﻢ ِّﻣْﻨـ َﻬﺎ ﺑَِﻘﺒ‬ ۤ ۤ ِ ِ َ ‫﴿إِ ْذ رأَى َ�راً ﻓَـ َﻘ‬
‫ﺲ أ َْو‬ ُ ‫ﺎل ﻷ َْﻫﻠﻪ ْٱﻣ ُﻜﺜُـﻮاْ إِِّﱐ آﻧَ ْﺴ‬ َ
﴾‫أ َِﺟ ُﺪ َﻋﻠَﻰ ٱﻟﻨﱠﺎ ِر ُﻫ ًﺪى‬
Idh raa naran faqala li-ahlihi omkuthoo innee anastu naran laAAallee ateekum
minha biqabasin aw ajidu AAala alnnari hudan (Surat Ta-Ha 20:10)

Tafsir: Alipoona Moto na akasema kuiambia familia yake: Subirini kwani kwa hakika
mimi nimeona Moto, hivyo labda nnaweza kukuleteeni kijinga kutokana nao au
nnaweza nikapata muongozo kutokana nao.

Hivyo Nabii Musa akaiwacha familia yake katika sehemu waliyopiga kambi hio huku
yeye taratibu akiwa ni mwenye kuelekea mlimani katika upande aliouona Moto huo,
549

ingawa ilikua mbali lakini kwa mtizamo wake na shida aliyokua nayo basi masafa yake
yalikua ni ya karibu na alipofika katika sehemu aliyouona moto huo, basi akajikuta kua
yupo kwenye sehemu ya arkupidhi ambayo na kama kibonde hivi na huku kukiwa na
mwangaza mkubwa ambao ulikua umezagaa kutoka kwenye upeo wa Macho yake na
moja kwa moja kushikamana na Mti mmoja mkubwa ulionawiri sana uliopo mbele yake,
na hivyo moto huo kua ni wenye kuwaka kuanzia ndani ya Mti huo huku ukiwa hautoi
moshi wa aina yeyote, na kila unavyozidi kuwaka basi ndivyo Mti huo unavyozidi
kunawiri na kupendeza na kuvutia kwa mng’aro wa kua na rangi ya kijani zaidi katika
majani yake.

Ambapo Imam Abu Muhammad Al Husayn Ibn Mas'ud Ibn Muhammad Al Farra' Al-
Baghawi kua katika kukielezea kile alichokiona Nabii Musa katika eneo hili basi anasema
kua: ‘Nabii Musa hakuweza kujua kua Nuru ya Allah Subhanah wa Ta’ala aliyokua
akiiona ambayo ni yenye kuwaka haikua ni Moto’

Hali hii ilimshangaza na kumshtua sana Nabii Musa, kwani hajawahi kuona Moto wa
ajabu kama huo ambao ni wenye kuwaka kwenye Mti ulionawiri, huku mti huo ukizidi
kunawiri na wingi wa majani yake kuongezeka kutokana na kuongezeka kwa Moto huo.

Kwani anasema Abu Musa Al Ashari Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Pazia la Allah Subhanah wa Ta’ala ni Nuru ambayo
mwangaza wake ni wenye kung’arisha kitu chochote kile ambacho macho yanaweza
kukiona kama Nuru hio itaachiwa Duniani. ’’

Nabii Musa akabaki kasimama huku akiangalia na kutulia kimyaa kutokana na kupigwa
na bumbuwazi lililompelekea kutokujua afanye nini, kwani amejikuta yuko peke yake
hakuna dalili ya kuwepo kiumbe mwengine karibu yake, lakini hapo hapo akakumbuka
familia yake na kusudio alilolifuata katika eneo hilo hivyo akataka aelekee kwenye Mti
huo ili ajaribu kutumia fimbo yake kuchukua Moto huo. Lakini alipokaribia Mti huo basi
mara akasikia sauti inamwita kwa jina lake kutoka katika Mti huo wenye kuwaka Moto
huo. Kama zinavyotuambia aya zifuatazo:

ِ ‫ﻚ ﺑِﭑﻟْ َﻮ ِاد ٱﻟْ ُﻤ َﻘﺪ‬ ۤ ِ


‫ﱠس‬ َ ‫ﻚ إِﻧﱠ‬
َ ‫ﭑﺧﻠَ ْﻊ ﻧَـ ْﻌﻠَْﻴ‬ َ ‫ﻮﺳ ٰﻰ۞ إِِّﱐ أ ََ�ْ َرﺑﱡ‬
ْ َ‫ﻚ ﻓ‬ َ ُ‫ى ٰﳝ‬َ ‫ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺂ أ ََﺎﺗ َﻫﺎ ﻧُﻮد‬
﴿
﴾‫ﻮﺣ ۤﻰ‬ ِ ِ َ‫ﻃُﻮى ۞ وأ ََ� ٱﺧﺘـﺮﺗُﻚ ﻓ‬
َ ُ‫ﭑﺳﺘَﻤ ْﻊ ﻟ َﻤﺎ ﻳ‬ ْ َ َْ ْ َ ً
Falamma ataha noodiya ya moosa, Innee ana rabbuka faikhlaAA naAAlayka
innaka bialwadi almuqaddasi tuwan, Waana ikhtartuka faistamiAA lima yooha
(Surat Ta-Ha 20:10-13)
550

Tafsir: Na alipoukaribia, aliitwa: Ewe Musa. Hakika mimi ni Mola wako, hivyo vua
viatu vyako kwani upo katika Bonde Takatifu la Tuwa, Na mimi nimekuchagua wewe
hivyo sikiliza nayokushushia.

Anasema Imam Ibn Jariri At Tabari kuhusiana na ayah hii kua: Nabii Musa aliambiwa
avue viatu hapa katika sehemu hii kwa sababu ya kutakiwa Nyayo zake zikanyage
mchanga wa Ardhi hio Takatifu na hivyo kua ni zenye kupata Baraka kutokana
nayo Ardhi hio.

Ambapo kwa upande wa Hujjat ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad
Ibn Muhammad Al Ghazali basi yeye anasema kua: ‘Nabii Musa aliambiwa avue viatu
kwa kumaanishiwa kua achane na Ulimwengu wa Dunia hii kwani anaingia katika
Ulimwengu wa Akhera kwa kumuelekea Allah Subhanah wa Ta’ala pekee’

Na kwa upande wa Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al
Ansari Al Qurtubi basi yeye anasema kua Aliambiwa afanye hivyo kutokana na
kutakiwa kua ni mwenye Unyenyekevu kwani tayari anaingia kwenye hali ya kua
ni mwenye kufanya Ibada. Watu waliotangulia kabla yetu ambao ni miongoni mwa
Vizazi vitatu vya mwanzo vya Uislam walikua wakitufu huku wakiwa miguu chini.

Aya zinatuonesha kua Allah Subhanah wa Ta’ala anamwambia Nabii Musa kua
amemteua na hivyo asikilize kwa makini anayotaka kuambiwa, na anasema Imam Sufyan
Ibn Uyaynah kua: ‘Hatua ya mwanzo ya kutafuta Ilm hua ni Kusikiliza kwa makini,
kisha kuhifadhi uliyoyasikia, kisha kuyafanyia kazi uliyoyasikia na kisha ndio
kuyatawanya kwa kuyafundisha kwa wengine.’

Na kwa upande mwengine basi tuaona kua katika kipindi cha kabla ya kuja Uislam
Waarabu walikua wakifanya Tawaf huku wakiwa uchi, na hua hawali kitu chochote
chenye mafuta ndani yake, na hujitahid kula chakula kidogo sana, hivyo Allah Subhana
wa Ta’ala akaishusha aya ya 31 ya Surat al Araf ambapo kwa upande wa Imam
Muhammad Ibn Saib Al Kalbi basi yeye anasema kua isemayo kua Waislam walikua
wakizunguka Al Kaabah huku wakiwa na Nguo zao, hivyo Makafiri wakawa ni wenye
kulalamikia juu ya jambo hili hivyo Allah Subhana wa Ta’ala akaishusha aya ya 31 ya
Surat al Araf isemayo:

ۤ
‫آد َم ُﺧ ُﺬواْ ِزﻳﻨَـﺘَ ُﻜ ْﻢ ِﻋﻨ َﺪ ُﻛ ِّﻞ َﻣ ْﺴ ِﺠ ٍﺪ وُﻛﻠُﻮاْ َوٱ ْﺷَﺮﺑُﻮاْ َوﻻَ ﺗُ ْﺴ ِﺮﻓُـﻮاْ إِﻧﱠﻪُ ﻻَ ُِﳛ ﱡ‬
‫ﺐ‬ ۤ
َ ‫﴿ َ�ﺑَِﲏ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ
َ ‫ٱﻟْ ُﻤ ْﺴ ِﺮﻓ‬
551

Ya banee adama khudhoo zeenatakum AAinda kulli masjidin wakuloo waishraboo


wala tusrifoo innahu la yuhibbu almusrifeena (Surat Al Araf 7:31)

Tafsir: Enyi Ibn Adam, Chukueni Mapambano yenu katika kila Sala na kuleni na
mnywe lakini msivuke mipaka, kwani kwa Hakika Yeye Allah hapendi wanaofanya
Israfu.

Na kwa upande mwengine basi tunaona kua Ayah hii ni uthibitisho wa Sunna ya Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua unapotaka Kufanya Ibada ya Sala basi ni vizuri
Kuvaa nguo Nzuri, Kutumia Miswak na Kujitia mafuta Mazuri hususan katika siku ya
Ijumaa na Siku za Iddi, na ndio maana Hasan Al Basr alikua akipendeza sana kuliko mtu
yeyote katika Siku ya Ijumaa na katika Siku ya Idd na pia Tamim Al Dari alinunua Joho
la Dirham 1000 ambalo lilikua zuri sana kwa ajili ya Sala ya Ijumaa tu.

Na hapa ndio panaingia kuhusiana na hili suali la Watu kua ni wenye kusali huku wakiwa
wamevaa viatu kutokana na ushahidi wa Aya hii na Hadith za Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam ikiwemo ile ambayo inasema kua:

Amesema Abu Said Al Khudri kua: Wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
alipokua anasalisha, alivivua viatu vyake na akaviweka kushotoni mwake. Hivyo
watu walipoona hivyo basi nao wakavua viatu vyao na kuviweka kushotoni mwao.
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipomaliza kusali akawauliza Masahaba
zake: ‘Kwanini, mkavivua viatu vyenu?’ Masahaba wakasema: ‘Tumekuona wewe
umevua hivyo nasi tukavua pia.’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema:
‘Jibril alishuka akaniambia kua kuna uchafu kwenye viatu vyangu, hivyo kama
ikiwa mmoja wenu amekuja Msikitini na akaona Uchafu kwenye viatu vyake basi
na aupanguse na kisha asali navyo’ (Sunan Abu Daud)

Ambapo amesema Imam Nawawi kuhusiana na Hadith hii kua: ‘Katika Hadithi hii
kuna ruhusa ya kusali huku mtu akiwa amevaa Viatu na Soksi za Ngozi pale mtu
huyo anapokua na uhakika kua havina uchafu. Ama kuhusiana na Viatu na Soksi
za Ngozi zinapokua na uchafu na kisha alievaa akaupangusa ardhini, kama Sala
yake hua ni Sahih ama la, basi kuna mitizamo miwili katika upande wa Madhhab
ya Imam Al Shafii Rahimahumu Allah. Na Mtizamo unaokubalika ni kua SALA
HIO HUA NI BATIL.’ (Sharh Sahih Muslim)

Ambapo kwa Upande wa Mujaddid Ad Din Al Hafidh Imam Shihab Ad Din Ibn Hajar Al
Asqalani basi yeye anasema kua: ‘Amesema Imam Ibn Battal Kusali huku Mtu ukiwa
umevaa Viatu huku ukijua kua havina uchafu basi hua ni jambo lililoruhusika,
kama alivyosema Imam Muhammad Ibn Ali Ibn Wahab Ibn Muti Al Qushayr Ibn
Al Fatah Ibn Daqiq Al Id kua hili si jambo lililoendekezwa (La Minna Al
Mustahabbat) kwani kusali huku ukiwa umevaa viatu vyako hua hakuhusiani na
552

hali ambayo ni yenye kutakiwa wakati ukiwa katika Sala. Ijapokua Viatu ni sehemu
ya Mvazi yaliyotajwa kwenye aya isemayo:

﴾‫آد َم ُﺧ ُﺬواْ ِزﻳﻨَـﺘَ ُﻜﻢ ِﻋﻨ َﺪ ُﻛ ِﻞ َﻣﺴ ِﺠ ٍﺪ‬


َ
ۤ ِ ‫﴿�ﺑ‬
‫ﲏ‬ ََ
ْ ّ ْ
Ya banee adama khuthoo zeenatakum AAinda kulli masjidin (Surat Al Araf 7:31)

Tafsir: Enyi Ibn Adam, Chukueni Mapambano yenu katika kila sehemu za Sala.

Lakini hata hivyo tunapoangalia hua tunaona ukweli kua viatu hua vinagusana na
uchafu na kutokana na hilo basi viatu hivyo hua ni visivyokua na vigezo stahiki vya
sifa ya Darja hio (ya kua ni Mapambo) na hivyo hua ni vyenye kupingana na kuenda
kinyume na maana ya kujipamba wakati ikionekana kua unatoa Uchafu kwenye
viatu hivyo, na hivyo hali hii hua inatiliwa maanani kwa sababu Kuachana na yaliyo
maovu hua ni bora kabla ya kufuatilia yale yaliyo Mema.

Mujaddid Ad Din Al Hafidh Imam Sihab Ad Din Ibn Hajar Al Asqallani anaendelea kwa
kusema kua: Imam Abu Daud na Al Hakim wameelezea Hadith iliyosimuliwa na
Shaddad Ibn Aws Radhi Allahu Anhu kua amesema Rasul Allah Salallahu Alyhi wa
Salam kua: ‘Jitofautisheni na Mayahudi, kwani wao hawasali na Viatu wala Soksi
za Ngozi.’ Hivyo bas Kusali ukiwa umevaa Viatu hua inakubalika kama ni kwa ajili
ya kujitofautisha huko.’

Ambapo kwa upande wa Mujaddid ad Din Imam Muhammad Zahid Al Kawthar


basi yeye anasema kua: ‘Sala ya kusali wakati ukiwa umevaa viatu hua inakubalika
pale inapokua visafi na havimzuii mtu kutokana na kuweka vichwa vya vidole vya
miguu juu ya Ardhi kama vile inavyohitaji Sujudu, na hii ni kulingana na Mtizamo
wa Imam Al Khattabi na wengineo.

Kwani Msikiti wa Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam, ulikua umeshonewa kwa
Kokoto na Vyumba vya wake zake vilikua vimeshikamana na Msikiti, Hivyo ilikua
hamna uwezekano wa kua uchafu unaweza kuganda kwenye viatu vyake wakati
akitembea. Na pia Mji wa Madina Munawwarat ulikua hauna uchafu wa kinyesi cha
Wanyama kwani ulikua unasafishwa na Masahaba baada ya Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam ambae alikua amewaamrisha kua wasimamie usafi wa ndani ya
nyumba zao na barazani mwao. Na haina haja ya kuitaja Nyumba ya Allah
Subhanah wa Ta’ala. Kwa hivyo watu walikua wanaweza kujilinda dhidi ya
Uchafu, na pia Ardhi yao ilikua ni ya mchanga mlaini hivyo inakua rahisi kujitenga
na Ucha uliotawanyika, na walipokua wanataka kumwaga maji walikua wanaenda
553

sehemu za mbali na majimba yao na walikua wanatafuta sehemu ambayo maji


hajatotuwama’

Na kila wakati ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipokua anataka
kuenda kumwaga maji basi alikua akienda katika sehemu ambayo hatoonekana na
watu, na alikua alikataza sehemu za kulaani ambazo miongoni mwao ni Kujisaidia
vichochoroni, Katika sehemu za Vivulini ambazo watu hua wanapumzikia, kama
iliyotajwa kwenye hadith na Imam Abu Daud.

Hali hii ni tofauti na hali tuliyokua nayo leo mitaani na vyooni mwetu ambapo hua
haiwezekani kujilinda kutokana na kusambaa na kutawanyika kwa uchafu kwani
vyoo vyetu vina sakafu ngumu la juu kiasi ya kua Uchafu lazima utarudi nyuma na
kuruka ruka hususan kama mtu akiwa amejisaidia huku akiwa amesimama.

Na bila ya shaka imethibitishwa kwenye hadith sahih kua Rasul Allah Salallahu
Alyhi wa Salam alivua viatu wakati alipokua akisali katika kipindi cha kuiteka
Makkah, hivyo huu hua unakua ni uthibitisho wa Mwisho unaobatilisha baina ya
hali mbili hizi kama vile alipovivua viatu baada ya kuambiwa na Jibril kua vina
uchafu, hivyo ilikua ni hali inayoruhusika kusali baada ya kusafisha viatu jambo
ambalo limekua ni uthibitisho kwa Wanazuoni. Na inapendekezwa kwa wale
ambao wanaona kua kufanya hivyo hua ni kujitofautisha na Mayahudi pale
inapokua kuna uthibitisho wa usafi wa viatu hivyo kua alifanya hivyo kwa ajili ya
kujitofatisha na Mayahudi.

Lakini hata hivyo Watu wa Ahl Al Kitab leo hii hua wanaingia na Vitu katika
sehemu za Ibada na wanasali na viatu vyao, hivyo ili sisi kuweza kujitofatisha nao
basi inabidi tusali bila ya kuvaa viatu na sio tunasali tukiwa tunasali tukiwa
tumevaa viatu kama wafanayavyo wao.

Ama kuhusiana na kauli ya Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu kua Naam Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam alisali na Viatu, basi inabidi tujue kua hii alifanya
si kutokana na kua ndio kawaida yake. Na hili limewekwa wazi na Imam An
Nawawi katika Sharh al Muslim pale aipozunguzia Sala za Qiyam Al Layl.

Hivyo ingawa kulingana na Hadith za Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi
tunaona kua aliwahi kusali na Viatu Msikitini na Masahaba pia waliwahi kusali na Viatu,
na kua iliruhusiwa pale inapokua kuna vigezo vinavyokubalika. Lakini hata hivyo hali
ya sasa hivi ya kimazingira na kimaisha ni tofauti na zama hizo za Masahaba, kwani
mbali ya kua sasa hivi Wakristo na Mayahudi wanasali na Viatu lakini pia katika zama
hizo Miskiti ilikua haina Mazulia wala sakafu ya Saruji, hivyo kwa kipindi kama hiki
basi kama ikiwa kila mtu ataruhusiwa kusali na Viatu Mskitini basi hali hii itapelekea
kuchafuka na kufujika kwa Mazulia, Mabusati n.k na pia kutahijaka Wafanyakazi wengi
554

wa kusafisha Msikiti kwa kila baada ya kipindi cha Sala, kwani vyenginevyo hali itakua
ni ya watu wenye kusali kwenye Mazulia yaliyojaa mavumbi na michanga.

Hivyo basi wanaokubalika kusali na viatu hua ni wale tu watu ambao hawana budi yaani
kwa mfano kuna watu ambao ni Walemavu wa Miguu na hivyo hua haiwezekani kwao
kua bila ya viatu au haiwezekani kusimama labda au kuvua na kuvaa viatu mara kwa
mara, na hata hivyo kuruhusika kwao hua inabidi pia lazima watimize sharti la kua viatu
hivyo ni visafi visivyokua na uchafu wowote ndani wala nje yake na hivyo hua si wenye
kuwaudhi Waumuni wengine wanaosali pamoja nao, na hivyo kutosababisha Karaha,
Kinyaa, Chuki na Mvutano baina ya Waumini.
Tunapoendelea kuangalia mtizamo mwengine wa kwa nini Nabii Musa akaambiwa avuae
viatu basi anasema Imam Ahmad Ibn Muhammad Al Thalabi kua: ‘Amesema Sad Ibn
Jubayr kua: ‘Nabii Musa aliambiwa kua tembea juu ya sehemu ya Ardhi hii huku
ukiwa miguu chini kama vile unataka kuingia kwenyye Al Kaabah. Ili upate Baraka
ya Ardhi hii’ ama wale wanaofaham kuhusiana na maana ya vitu basi wamesema
kua Viatu hua vinamaanisha Mwanamke, na hivyo ndivyo inavyotafsiriwa kwenye
Ndoto, kwa hivyo hapa Nabii Musa alikua ameambiwa kua uachie huru Moyo wako
kutokana na kua ya Mawazo ya Mke wako.’
Yaani hapa tayari Nabii Musa anajuulishwa kuhusiana na umakini anaotakiwa kua nao
wakati yupo kwenye Ardhi hio Takatifu huku akiwa mbele ya Mola wake aliekua
akimtegemea na kumuomba msaada mara kadhaa.
Na pia Aya yetu inatuonesha kua Nabii Musa aliitwa kwenye Bonde la Muqaddas la
Tuwa, hivyo hii inaonesha kua eneo hili limetukuzwa na kutiwa Baraka kwani Neno
Muqaddas ni lenye kutokana na neno Qadus ambalo hua ni lenye kumaanisha Kua na
Usafi Usiokua na Doa, Kua na Utukufu na kutokua na Makosa. Na pia neno Qadus
ambalo ndio lililotoa neno Muqaddas hua pia linamaanisha Kuzungumza na Allah
Subhanah wa Ta’ala katika njia inayostahiki, na kuondoa kutoka katika sifa za Allah
Subhanah Ta’ala kila lililokua silo.
Hivyo neno Tuwa lililotumika hapa hua linaaanisha kua ni Jina la Bonde ambalo lipo
katika Ardhi ya Jangwa la Sinai nchini Misri, na Bonde hili limekua Takatifu kwa sababu
ni katika eneo hili ndio lililochaguliwa na Allah Subhanah wa Ta’ala kuzungumza na
Nabii Musa na hivyo akawa ni wenye kusikia maneno ya Allah Subhanah wa Ta’ala na
ndio maana pia Nabii Musa akawa ni mwenye kuitwa Kalimu Allah yaani Nabii Musa
ndie Mtu pekee aliezungumza na Allah Subhanah wa Ta’ala hapa Duniani.
Ambapo kwa upande wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam pia nae alizungumza
nae lakini si hapa Duniani bali Mbinguni pale alipoenda kwenye safari ya Isra na Miraj,
hivyo aya zinaendelea kutubainshia mtizamo mwengine juu ya yaliyotokea kwa kusema
kua:
555

ِ‫ﱠﺠﺮة‬ ِِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ
ِ ‫ﻮد‬ ﴿
َ َ ‫ى ﻣﻦ َﺷﺎﻃﻰء ٱﻟْ َﻮادى ٱﻷَْﳝَ ِﻦ ﰱ ٱﻟْﺒُـ ْﻘ َﻌﺔ ٱﻟْ ُﻤﺒَ َﺎرَﻛﺔ ﻣ َﻦ ٱﻟﺸ‬ َ ُ‫ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺂ أ ََﺎﺗ َﻫﺎ ﻧ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ
َ ‫ب ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬ ‫ﻮﺳ ٰﻰ إِِّ ۤﱐ أ ََ� ﱠ‬
‫ٱﻪﻠﻟُ َر ﱡ‬ َ ُ‫أَن ٰﳝ‬
Falamma ataha noodiya min shati-i alwadi al-aymani fee albuqAAati almubarakati
mina alshshajarati an ya moosa innee ana Allahu rabbu alAAalameena (Surat Al
Qasas 28:30)

Tafsir: Na alipoufikia (Moto huo) akaitwa kwa upande wa Kulia wa Bonde


lililobarikiwa (akaitwa) kutoka katika Mti: Ewe Musa Hakika mimi ni Allah Mola wa
Ulimwengu wote.

Ambapo kwa upande wa Imam Abd al Azizi Al Mahdawi ambae ni Mwalimu wake
Shaykh ul Al Akbar Imam Abu Bakr Ibn Arabi kua: ‘Allah Subhanah Allah
alizungumza na Nabii Musa kutoka kwenye Arshi na hivyo akamjaalia Nabii Musa
kua ni mwenye kusikia sauti hio kupitia kwenye Mti huo. Kwani Allah Subhanah
wa Ta’ala hawezi kufananishwa kisifa na Viumbe wake.’

Na kwa upande wa Imam Abu Abdullah Muhammad Ibn Ahmad Ibn Abu Bakr Al Ansar
Al Qurtubi basi yeye anasema kua Imam Abu Is-haq kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala
aliumba njia au mfumo ambao ulikua umo ndani ya Ufaham wa Nabii Musa na
hivyo mfumo huo ndio ikawa sababu ya kumsaidia yeye kuweza kusikia Maneno ya
Allah Subhanah wa Ta’ala alipokua akizungumza nae. Hivyo sauti hio ilikua ni
maalum kwa ajili ya Maumbile ya Nabii Musa’

Na Mujaddid Ad Did Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad
Ibn Muhammad Al Ghazali na Wanazuoni wanaofuata mtizamo wa akida ya Ashari basi
wao wanasema kua: ‘Nabii Musa alisikia kauli ya Milele ya Allah Subhnah wa Ta’ala
ambayo haina maneno ndani yake wala sauti’ Kwani amesema Allah Subhnah wa
Ta’ala kua:

﴾ً‫ﻮﺳ ٰﻰ ﺗَ ْﻜﻠِﻴﻤﺎ‬ ‫﴿ َوَﻛﻠﱠ َﻢ ﱠ‬


َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ُﻣ‬
Wakallama Allahu moosa takleeman (Surat An Nisaa 4:164)

Tafsir: Na akazungumza Allah na Musa moja kwa Moja.


556

Ambapo kuhusiana na namna Allah Subhanah wa Ta’ala alipojitambulisha kwa Nabii


Musa basi anasema Imam Abu Abd Allah Sahl Al Tustari anasema kua Allah Subhanah
wa Ta’ala alichukua sehemu ya jina lake Tukufu la Allah na kutoa maneno yasemayo:

﴾‫ﲔ‬ ِ ‫﴿أ ََ� ﱠ‬


َ ‫ب ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬
‫ٱﻪﻠﻟُ َر ﱡ‬
Ana Allahu rabbu alAAalameena (Surat Al Qasas 28:30)

Tafsir: Mimi ni Allah Mola wa Ulimwengu wote.

Baada ya kujitambulisha basi Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Nabii Musa


kuhusiana na Utukufu wake na Utukufu wa Nabii Musa kutokana na Hikma zake kwa
kusema kua:
ِ‫ﻮدى أَن ﺑﻮِرَك ﻣﻦ ِﰱ ٱﻟﻨﱠﺎ ِر وﻣﻦ ﺣﻮَﳍﺎ وﺳﺒﺤﺎ َن ﱠ‬ ِ
ِّ ‫ٱﻪﻠﻟ َر‬
‫ب‬ َ ُْ َ َ ْ َ ْ َ َ َ ُ َ ُ‫﴿ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ َﺟﺂءَ َﻫﺎ ﻧ‬
﴾‫ٱﳊَ ِﻜﻴﻢ‬
ْ ‫ﻳﺰ‬
ُ ِ ‫ٱﻪﻠﻟُ ٱﻟْ َﻌ‬
‫ﺰ‬ ‫ﱠ‬ �َ
َ ‫أ‬ ‫ﻪ‬
ُ ‫ﱠ‬
‫ﻧ‬ ِ‫ﲔ ۞ ٰﳝُﻮﺳ ٰﻰ إ‬
َ َ
ِ َ‫ٱﻟْﻌﺎﻟ‬
‫ﻤ‬ َ
ُ
Falamma jaaha noodiya an boorika man fee alnnari waman hawlaha wa subhana
Allahi rabbi alAAalameena, Ya Musa innahu ana Allahu alAAazeezu alhakeemu,
(Surat An Naml 27:8-10)

Tafsir: Lakini alipoukaribia akaambiwa: Amebarikiwa yule ambae yumo ndani ya


Moto na alie karibu nao na utukufu ni wa Allah pekee Mola wa Ulimwengu wote. Ewe
Musa Hakika mimi ni Allah Mwenye Uwezo wa Kila Kitu na Mwenye Hikma.

Subhanah Allah! Aya zinatuonesha kua mpaka hapa Nabii Musa hajaambiwa kua yeye
ni Mtume bali alikua ni mwenye kuambiwa tu kua asikilize anayoambiwa kupitika katika
njia ya Wahyi anaoshushiwa kwa njia ya Maneno na hivyo kuwekewa wazi kua tayari
ameshakua ni Nabii na hivyo upekee wa hili tukio tukufu la kuzungumza na Allah
Subhanah wa Ta’ala na kupandishwa darja ya kua ni mwenye utukufu wa kuzungumza
na Allah Subhanah wa Ta’ala basi moja kwa moja ni lenye kutuwekea wazi sisi na Nabii
Musa mwenyewe kua tayari ameshakua ni Mtume na Nabii ila suali la kujiuliza ni kua
jee kwa watu gani?

Ambapo kabla ya Nabii Musa kujibiwa suali hilo basi kwanza alipewa maamrisho
yanayomhusu yeye Binafsi na pamoja nasi, na hii ni kulingana na aya zisemazo:
557

﴾‫ﺼ ٰﻠﻮَة ﻟِ ِﺬ ْﻛ ِﺮ ۤي‬ ِ ِۤ ِۤ


‫ﱠ‬ ‫ٱﻟ‬ ِ
‫ﻢ‬ ‫َﻗ‬‫أ‬
‫و‬ ‫ﱏ‬ِ ‫ﺪ‬‫ﺒ‬‫ﭑﻋ‬ ‫ﻓ‬ �َ
‫أ‬ ‫ﻻ‬ ‫﴿إِﻧﱠِ ۤﲏ أ ََ� ﱠ‬
َ ْ ُ ْ َ َْ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻻ إﻟَـٰﻪَ إ‬
Innanee ana Allahu la ilaha illa ana faoAAbudnee waaqimi alssalata lidhikree (Surat
Ta-Ha 20:14)

Tafsir: Hakika mimi ni Allah, Hakuna Mungu isipokua mie, hivyo niabudu na
usimamishe Sala kwa ajili ya kunimbuka.

Ambapo kulingana na mtizamo wa Imam Ibn Jarrir At Tabari basi yeye anasema
kuhusiana na ayah hii kua: ‘Sali katika kila wakati utakaonikumbuka’ na hii ni
kutokana na ile hadith isemayo kua: Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
Salam kua ‘Pale mmoja wenu anapokua amelala na kupitiliza katika Sala zake au
akasahau, basi mwache asali atakapoamka au pale atakapokumbuka, kwani Allah
Subhanah wa Ta’ala amesema kua: Waaqimi alssalata lidhikree’ (Sahih Bukhari na
Muslim)

Kwa upande wa Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al
Ansari Al Qurtubi basi yeye anasema kulingana na aya hii na hadithi hii: ‘Wanazuoni
wanakubaliana kua: ‘Kama mtu hakusali kwa makusudi basi anaweza kusali kama
ikiwa atatubu baada yake, na hali hii hua pia kuhusiana na Ibada ya Funga kwa
yule ambae atakua hakufunga, ambapo kwa wale baadhi waliopingana na hukmu
hii basi hua ni kutokana na kutaka kutilia mkazo umuhimu wa Sala, na kutowapa
nguvu ya kuwaunga mkono wale ambao wasiotaka kusali kabisa kwa makusudi,
hata kwa hio baadae.’

Hivyo kisha baada ya hapo Allah Subhanah wa Ta’ala akaendelea kumwambia Nabii
Musa kwa kusema:

َ ‫ﺼ ﱠﺪﻧﱠ‬
‫ﻚ‬ ِ ٍ ‫﴿إِ ﱠن ٱﻟ ﱠﺴﺎﻋﺔَ آﺗِﻴﺔٌ أَ َﻛﺎد أُﺧ ِﻔﻴﻬﺎ ﻟِﺘُﺠﺰ ٰى ُﻛ ﱡﻞ ﻧَـ ْﻔ‬
ُ َ‫ﺲ ﲟَﺎ ﺗَ ْﺴ َﻌ ٰﻰ۞ ﻓَﻼَ ﻳ‬ َْ َ ْ ُ َ َ
﴾‫َﻋْﻨـ َﻬﺎ َﻣﻦ ﻻﱠ ﻳـُ ْﺆِﻣﻦ ِﻬﺑَﺎ وٱﺗـﱠﺒَ َﻊ َﻫﻮاﻩُ ﻓَـﺘَـﺮَد ٰى‬
ْ َ َ ُ
Inna alssaAAata atiyatun akadu okhfeeha litujza kullu nafsin bima tasAAa; Fala
yasuddannaka AAanha man la yu/minu biha waittabaAAa hawahu fatarda (Surat
Ta-Ha 20:14-16)
558

Tafsir: Kwa Hakika Saa inakaribia na nia yangu ni kuificha ili kila Nafsi ilipwe juu
ya kile ilichojitahidi: Hivyo mwache yule ambae asioamini juu yake (Saa ya Kiama)
afuate matamanio ya Nafsi zao.

Ambapo anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu na Qatadah Al Sadusi kua:
‘Neno Akadu lililotumika hapa linamaanisha Takriban au Karibu yake’ na kuna
wasemao kua Akadu maana yake hua ni Hali ya kutaka (kuificha siku hio) kutokana na
kujuliknaa na viumbe

Na pia kuna wanaosema kua maana ya ayah hii ni kua: ‘Hakika mimi bado kidogo
niifiche ili iwe ni siku ya jambo ambalo litatokea ghafla moja’

Hapa tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala anaanza kumbainishia maamrisho yake
Nabii Musa ambayo anatakiwa ayatekeleze kwa kwenye Nafsi yake kwanza, kabla ya
kuyafikisha kwa watu wengine, na kwa wasiotaka kuamini juu ya hayo basi hamna tatizo,
kwani siku ya Malipo ipo karibu sana na hapo ndio watu watajua ukweli kuhusiana na
njia waliyoifuata kama ilikua ni ya Uongofu au ya upotovu. Maneno haya na Maamrisho
yake yalimfanya Nabii Musa kutulia tulii.

Na hii ni kutokana na Maumbile ya Kiumbe Ibn Adam ambapo Mtu yeyote yule
anaetokewa na Jambo la kushtua au kushangaza na kupigwa na bumbuwazi basi hua
katika hali ya kutojiamini na kutojua ni nini cha kufanya hadi akili ya mtu huyu itulie
kwanza na kutafakkari na kuona wazi kile kinachotokea mbele yake, na hapo hua ni
mwenye kujua kama anaota ama la.

Na kwa kua Allah Subhhanah wa Ta’ala ni mjuzi juu ya kila kitu a yeye ndie Muumba
wa Kila kitu basi pia ni mwenye kujua hali aliyokua nayo Nabi Musa katika wakati huu
ambao tukio hili inatokea mbele yake, na hivyo akaamua kumtoa Nabii wake huyo
aliemchagua kutoka katika hali hio ya kimaumbile ya kupigwa na bumbuwazi na
kumuingiza katika hali ya uhalisi wa hali ya mazingira na kila kitu kinachoendelea mbele
ya macho yake kua si ndoto bali ni tukio la kweli kama lilivyokua mbele yake, hivyo
Allah Subhanah wa Ta’ala akamuuliza Nabii Musa.

﴾‫ﻮﺳ ٰﻰ‬ َ ِ‫ﻚ ﺑِﻴَ ِﻤﻴﻨ‬


َ ُ‫ﻚ ٰﳝ‬ َ ‫﴿ َوَﻣﺎ ﺗِْﻠ‬
Wama tilka biyameenika ya Moosa?’ (Surat Ta-Ha 20:17)

Tafsir: ‘Na jee nini hicho mkononi mwako ewe Musa?’


559

Na pia hapo hapo Allah Subhanah wa Ta’ala alikua anataka kumuonesha Nabii Musa
thamani, Matumizi na Miujiza ya fimbo aliyokua nayo Nabii Musa zaidi ya anavyojua
yeye Nabii Musa, ambae alijibu kwa kusema:

﴾‫ُﺧﺮ ٰى‬ ِ ِ‫ﺶ ِﻬﺑﺎ ﻋﻠَﻰ َﻏﻨ ِﻤﻰ و‬ ِ﴿


ُ ‫ﱃ ﻓ َﻴﻬﺎ َﻣﺂ ِر‬
َْ ‫ب أ‬ ََ َ ٰ َ َ ‫ﱡ‬ ‫َﻫ‬
ُ ‫أ‬
‫و‬ َ ‫ﺎ‬‫ﻬ‬َ ‫ـ‬‫ﻴ‬ْ ‫ﻠ‬
َ ‫ﻋ‬
َ ُ
‫ﺄ‬ ‫ﱠ‬
‫ﻛ‬‫ﻮ‬ ‫ـ‬
َ‫ﺗ‬
َ ََ‫أ‬ ‫ﺎى‬‫ﺼ‬َ ‫ﻋ‬
َ ‫ﻰ‬
َ ‫ﻫ‬
Hiya AAasaya atawakkao AAalayha waahushshu biha AAala ghanamie waliya
feeha maaribu okhra (Surat Ta-Ha 20:18)

Tafsir: Hii ni fimbo yangu. Ambayo naiegemea, na kuitumia kupukutishia Majani kwa
ajili ya wanyama wangu na naitumia kwa matumizi mengineyo.

Tukio hili linanikumbusha kauli ya Imam Abu Hasan Al Shadhili alipopata ufunuo
wakati alipoenda Jerusalem na akamuona Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
alipokua akizungumza na Nabii Musa Alayhi Salaam na Nabii Isa Ibn Maryam Alayhi
Salam ambapo Nabii Musa alimuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa
kusema:

‘Ya Rasul Allah! Hakika wewe umesema kua Wanazuoni wa Ummah wako ni sawa
na Mitume ya Ummah wa Bani Israil hivi ni kweli?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Naam, bila ya shaka. Jee mnataka
nikuonesheni mfano?’ Nabii Musa Alayhi Salam akasema: ‘Naam tuoeneshe’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaamrisha kwa kuita katika watu wa Ummah
wake: ‘Ingia kwenye hadhara, Ya Al Ghazali’

Mara Hujjat Ul Islami Zukhruf Ad Din Mujadid ad Din Mujtahid Imam Abu Hamid
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii akanyanyuka
kutoka katika Umma wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kuingia katika mbele
ya hadhara ya Mitume hao, na kisha akasema: ‘Niko mbele yako ya Rasul Allah!’

Hujjat Ul Islami Zukhruf Ad Din Mujadid ad Din Mujtahid Imam Abu Hamid
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii alipofika
mbele yao, basi Nabii Musa akamuangalia kisha akamuliza: ‘Kijana unaitwa Nani?’

Hujjat Ul Islami Zukhruf Ad Din Mujadid ad Din Mujtahid Imam Abu Hamid
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii akajibu:
‘Naitwa Abu Hamid Ibn Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhamamd Al Ghazali
Al Tusi Al Shafii’
560

Nabii Musa akamwangalia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, kisha akamgeukia
Hujjat Ul Islami Zukhruf Ad Din Mujadid ad Din Mujtahid Imam Abu Hamid
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii na
kumwambia: ‘Ndio Akhlaq gani hio unatuonesha, hakika mimi nimekuuliza jina lako
tu, sikutaka kujua nasaba yako.’

Hujjat Ul Islami Zukhruf Ad Din Mujadid ad Din Mujtahid Imam Abu Hamid
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii akamgeukia
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kisha akamuuliza: ‘Ya Rasul Allah! Jee nimjibu
Kallimu Allah Musa au nikae kimya?’

Rasul Salallahu Alayhi wa Salam akajibu: ‘Jisikie Huru kumjibu ya Al Ghazali.’

Hujjat Ul Islami Zukhruf Ad Din Mujadid ad Din Mujtahid Imam Abu Hamid
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii akamgeukia
Nabii Musa na kumwambia: ‘Kumbuka ya Kallimu Allah pale Allah Subhanah wa
Ta’ala alipokuuliza.

﴾‫ﻮﺳ ٰﻰ‬ َ ِ‫ﻚ ﺑِﻴَ ِﻤﻴﻨ‬


َ ُ‫ﻚ ٰﳝ‬ َ ‫﴿ َوَﻣﺎ ﺗِْﻠ‬
Wama tilka biyameenika ya Moosa?’ (Surat Ta-Ha 20:17)

Tafsir: ‘Na jee nini hicho mkononi mwako ewe Musa?’

Hujjat Ul Islami Zukhruf Ad Din Mujadid ad Din Mujtahid Imam Abu Hamid
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii akaendela
kumwambia Nabi Musa Alayhi Salam, basi hakika wewe Kallimu Allah Musa ulijibu:

﴾‫ُﺧﺮ ٰى‬ ِ ِ‫ﺶ ِﻬﺑﺎ ﻋﻠَﻰ َﻏﻨ ِﻤﻰ و‬ ِ﴿


ُ ‫ﱃ ﻓ َﻴﻬﺎ َﻣﺂ ِر‬
َْ ‫ب أ‬ َ َ َ ٰ َ َ ‫ﱡ‬ ‫َﻫ‬
ُ ‫أ‬
‫و‬ َ ‫ﺎ‬‫ﻬ‬َ ‫ـ‬‫ﻴ‬ْ ‫ﻠ‬
َ ‫ﻋ‬
َ ُ
‫ﺄ‬ ‫ﱠ‬
‫ﻛ‬‫ﻮ‬َ ‫ـ‬
َ‫ﺗ‬َ‫أ‬ ‫ﺎى‬
َ ‫ﺼ‬َ ‫ﻋ‬
َ ‫ﻰ‬
َ ‫ﻫ‬
Hiya AAasaya atawakkao AAalayha waahushshu biha AAala ghanamie waliya
feeha maaribu okhra (Surat Ta-Ha 20:18)

Tafsir: Hii ni fimbo yangu. Ambayo naiegemea, na kuitumia kupukutishia Majani kwa
ajili ya wanyama wangu na naitumia kwa matumizi mengineyo.

Hujjat Ul Islami Zukhruf Ad Din Mujadid ad Din Mujtahid Imam Abu Hamid
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii akaendela
561

kumwambia Nabii Musa: ‘Hivyo hapa Allah Subhanah wa Ta’ala alikuuliza tu, ni nini
hicho mikononi mwako ewe Musa? Hakutaka kujua unafanyia nini na nini, hicho
ulichokua nacho mikononi mwako, lakini wewe ulijibu yote na kuelezea kwa
pamoja.’

Hapo Nabii Musa akatabasamu na kisha akamgeukia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
Salam na kumwambia: ‘Hakika umesema kweli Ya Rasul Allah! Kwani Wanazuoni
wako ni sawa na Mitume wa Bani Israil’

Rasul Allah Salalahu Alayhi wa Salam akatabasam na kuwageukia Nabii Musa na Nabii
Isa na kisha akawauliza: ‘Jee Katika Ummah wenu mnae mtu Mwenye I’lm kama
huyu?’ ambapo Nabii Musa na Nabii Isa Ibn Maryam wakajibu: ‘La Hakuna!’

Ambapo ni kawaida ya Mitume kua ni wenye kama alivyojibu Nabii Musa Alayhi Salam
kwani hata Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam aliku ani mwenye kujibu hivyo kwa
kufafanua pale alipoulizwa kuhusiana na Maji ya Bahari kama hua yako Tohara ama la
ambapo nae akajibu: ‘Maji yake ni Tohara na Maiti wake ni Haram kuliwa.’

Ama kuhusiana na Mtu kua ni mwenye kuchukua Fimbo anapotembea basi alisema
Hasan Al Basr kua: ‘Kuna mambo Sita katika kutembea na Fimbo ambayo ni:
Sunnah ya Mitume na Manabii, Pambo la Wenye Taqwa, Silaha dhidi ya Maadui,
Egemeo kwa ajili ya walio dhaifu, Chukio kwa Wanafiq na Huongeza Utiifu juu ya
Mtu’

Na ukweli ni kua hata Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam alikua ni mwenye
kutembea na Fimbo na alikua akiitumia kwa mambo kadhaa ikiwemo kuiegemea
anapotoa Khutba, kama inavyosema hadith ya Hakam Ibn Hazan Radhi Allahu Anhu
ambae anasema kua: ‘Tulishuhudia Sala ya Ijumaa na Rasul Allah Salallahu Alayhi
wa Salam huku akiwa amesimama, akiegemea Fimbo au Upinde ’(Sunan Abu Daud)

Na hivyo kutokana na uthibitisho wa Hadith hii basi tunaona kua Kusoma Khutba ya Sala ya
Ijumaa huku Khatib akiwa ameshika Fimbo hua ni kunakopendekezwa sana kwani ni Sunnah
ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Na wakati mwengine alikua ni mwenye kuiweka mbele yake kama kizuizi au Sutra
anapokua anasali. Kuliashiria Hajar Al Aswad alipokua akifanya Tawaf, kama
anavyosema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allah Anhu katika Hadith ifuatayo: ‘Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam alilizunguka Al Kaabah katika Hija ya kuaga huku
akiwa yuko juu ya Ngamia na alikua akiligusa Hajar Al Aswad kwa kutumia Mihjan
(yaani Mkongojo)’ (Imam Muslim)
562

Na Imam At Tirmidhii anasema kua: ‘Amesema Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu kua:
‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliupita mti wenye Majani makavu, hivyo
akaugonga kwa Fimbo yake na kusababisha Majani yake yaanguke kisha akasema:
‘Ama kwa Hakika kusema Alhamd Lillah, Subhana Allah na Lailaha Illa Allah
husababisha dhambi kuanguka kutoka kwenye Mwenye kufanya Ibada kama vile
ambavyo yanavyoanguka Majani haya.’’’

Ambapo Imam Ahmad Ibn Hanbal anasema katika Musnad Imam Ahmad kua:
‘Amesema Az Zuhri kua amesema Abd Allah Ibn Unays kua: Baada ya
kuamrishwa na Rasul Allah Salallau Alayhi wa Salam kumuua Khalid Ibn Sufyan
Ibn Nabih ambae aalikua anatayarisha jeshi kwa ajili ya kumuua Rasul Allah
Salallahu Aalayhi wa Salam. Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
alifuatana na mimi na kisha akaingia ndani ya Nyumba yake na kunipa mimi Fimbo
yake na kusema: ‘Kaa nayo hii ewe Abdullah Ibn Unays’, hivyo nami nikawa nayo
Fimbo hio na watu wakawa wananiuliza ni Fimbo ya nini? Na nilipojibu kua
amenipa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi wakaniambia kua niulize ni ya
nini?’

‘Hivyo nikarudi kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kumuuliza: ‘Jee hii
Fimbo umenipa kwa ajili ya nini?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema:
‘Kwa ajili ya kua ni kama Aya baina yangu na yako katika siku ya Malipo, kwani
ni wachache sana watakaokua na Fimbo katika siku hio.’’

Imam Ahmad Ibn Hanbal anaendelea kutuambia kua: ‘Abdallah Ibn Unays
aliifungamanisha Fimbo hio na Upanga wake na kamwe hakuachana nayo hadi
alipofariki ambapo aliusia kua akifariki basi azikwe nayo na akazikwa nayo.’

Ambapo kwa upande wa Shaykh ul Islami Al Muhaqqiq Al Faqih Imam Ibn Hajar Al
Haytami basi yeye anasema kutokana na Hadith hii kua Katika Siku ya Kiama ni watu
wachache sana wakiwemo Mitume na Manabii ambao katika siku hio watakua ni wenye
Kua na Fimbo (Kitab Al Ba`th). Na huo pia ndio mtizamo wa Mujadid ad Din Imam Ibn
Hajar Al Asqalani.

Na kwa upande wa Imam Abu Abdullah Sahl Al Tustari kua: ‘Hapa Nabii Musa alikua
anaambiwa kuhusiana na umuhimu wa fimbo yake na Mtaumizi yake ambayo yeye
mwenyewe hayajui na hivyo kuwekewa wazi kua Fimbo hio ina matumizi mengi
sana hivyo mbali ya kua ni mwenye kupewa Darja mbele ya Mola wake lakini hata
hivyo Ilm ya viumbe mbele ya Ilm ya Muumba ni ndogo sana.’ Na bila ya shaka
matumizi yake Fimbo hio zaidi tutayaona kama yatakavyoonesha matumizi yake hapo
baadae.
563

Ambapo kwa Upande wa Mujaddid Ad Din Imam Abu Abdullah Muhammad Idris Al
Shafii basi yeye alikua pia ni mwenye kutembea na Fimbo na alipoulizwa kwanini hua
anatembea na Fimbo basi alijibu kwa kusema kua: ‘Ni kwa ajili ya Kujikumbusha kua
Hapa Duniani mimi ni Msafiri, na nnapita tu.’

Na Mujaddid Ad Din, Sultan Al Mutakalimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi yeye
anasema kua: ‘Jee Hivi wewe Musa Unajua kuhusiana na hio Fimbo iliyomo
mikononi mwako? Ambayo haikunufaishi wala haikudhuru lakini ambayo ni yenye
kugeuga Nyoka Mkubwa Sana?’

Hivyo hapo Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Nabii Musa kwanini akawa ni
mwenye kujaaliwa darja hio ya Utukufu mbele ya Mola wake, lakini kwanza kwa
kubainishiwa Thamani ya Fimbo yake hio kwa kuambiwa:

﴾‫ﻮﺳ ٰﻰ‬ ِ َ َ‫﴿ﻗ‬


َ ُ‫ﺎل أَﻟْﻘ َﻬﺎ ٰﳝ‬
Qala alqiha ya moosa (Surat Ta-Ha 20:19)

Tafsir: Akasema (Allah) Itupe ewe Musa.

Hivyo Nabii Musa akaitupa chini Fimbo yake hio na mara ghafla fimbo hio ilipogusa
Ardhi tu, basi upande mmoja ukageua na kua ni kihwa chenye kutoa ndimi mbili na
upande mmoja ukawa ni mkia na hivyo kuanza kujikunjakuja na kujipinda kama Nyoka
ambae ni mwepesi na ni mwenye kasi katika kutambaa kwake kama zinavyosema aya
zilizoelezea tukio hili katika hali tatu tofauti:-

﴾‫ﺎﻫﺎ ﻓَِﺈذَا ِﻫﻰ َﺣﻴﱠﺔٌ ﺗَﺴ َﻌ ٰﻰ‬


َ ‫﴿ﻓَﺄَﻟْ َﻘ‬
ْ َ
Faalqaha fa-idha hiya hayyatun tasAAa,(Surat Ta-Ha 20:20)

Tafsir: Akaitupa na ghafla ikawa Nyoka aliehai atembeae kwa kasi.

Ambapo tukio hili linaelezewa tena katika aya isemayo:


564

ِ ِ
َ‫ﻮﺳ ٰﻰ ﻻ‬ َ ُ‫ﺐ ٰﳝ‬ ْ ‫آﻫﺎ ﺗَـ ْﻬﺘَـﱡﺰ َﻛﺄَﻧـﱠ َﻬﺎ َﺟﺂ ﱞن َوﱠ ٰﱃ ُﻣ ْﺪﺑﺮاً َوَﱂْ ﻳـُ َﻌ ّﻘ‬
َ ‫ﺎك ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ َر‬
َ‫ﺼ‬ َ ‫﴿ َوأَﻟْ ِﻖ َﻋ‬
‫ﱠل ُﺣ ْﺴﻨﺎً ﺑَـ ْﻌ َﺪ ُﺳ ۤﻮٍء ﻓَِﺈِّﱏ‬ َ ‫ى ٱﻟْ ُﻤْﺮ َﺳﻠُﻮ َن۞ إِﻻﱠ َﻣﻦ ﻇَﻠَ َﻢ ﰒُﱠ ﺑَﺪ‬ ‫ﺎف ﻟَ َﺪ ﱠ‬ ُ َ‫ﻒ إِِّﱏ ﻻَ َﳜ‬ ْ َ‫َﲣ‬
﴾‫ﻮر ﱠرِﺣﻴﻢ‬
ٌ ٌ ‫َﻏ ُﻔ‬
Waalqi AAasaka falamma raaha tahtazzu kaannaha jannun walla mudbiran walam
yuAAaqqib ya moosa la takhaf innee la yakhafu ladayya almursaloona, Illa
man dhalama thumma baddala husnan baAAda soo-in fa-innee ghafoorun
raheemun (Surat An Naml 27: 10-11)

Tafsir: Na Tupa fimbo yako ewe Musa na alipoiona inateleza kama Nyoka, akakimbia
bila ya kuangalia nyuma (akaambiwa) Ewe Musa usiwe na Khofu. Kwani Mitume
hawawi na Khofu wanapokua mbele yangu. Ispokua yule ambae amefanya ovu na
kisha baadae akabadilisha ovu kwa jema. Kwa hakika mimi ni mwingi wa kusamehe
na mwingi wa Rehma.
Na pia pale Allah Subhanah wa Ta’ala aliposema katika Surat Al Qasas:

ِ ِ
‫ﻮﺳ ٰﻰ‬ ْ ‫آﻫﺎ ﺗَـ ْﻬﺘَـﱡﺰ َﻛﺄَﻧـﱠ َﻬﺎ َﺟﺂ ﱞن َوﱠ ٰﱃ ُﻣ ْﺪﺑﺮاً َوَﱂْ ﻳـُ َﻌ ّﻘ‬
َ ُ‫ﺐ ٰﳝ‬ َ ‫ﺎك ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ َر‬
َ‫ﺼ‬ َ ‫﴿ َوأَ ْن أَﻟْ ِﻖ َﻋ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ِ َ ‫ﻒ إِﻧﱠ‬ ْ َ‫أَﻗْﺒِ ْﻞ َوﻻَ َﲣ‬
َ ‫ﻚ ﻣ َﻦ ٱﻵﻣﻨ‬
Waan alqi AAasaka falamma raaha tahtazzu kaannaha jannun walla mudbiran
walam yuAAaqqib ya moosa aqbil wala takhaf innaka mina al-amineena (Surat Al
Qasas 28:31)

Tafsir: Na itupe Fimbo yako. Na mara ilipoanza kutembea kama Nyoka akageuka na
kukimbia, na Akaambiwa Ewe Musa. Kabiliana nae na wala usiwe na Khofu kwani
kwa hakika upo mbele ya Waliokua na Amani.

Tunapoziangalia aya zinazozungumzia tukio hili basi tunaona kua zimetumia maneno
matatu katika kuelezea Miujiza ya Fimbo ya Nabii katika namna inavyogeka kua Nyoka.
Ambapo imetumiea neno Hayya, yaani Nyoka wa Kawaida, ikatumia neno Jan yaani
Nyoka Mwembamba Mdogo ambae ni mwenye uwezo wa kuteleza haraka kutokana na
maumbile ya Mwili wake na ikatumia neno Thuban kumaanisha Chatu Mkubwa Sana.
565

Na hii ni kutokana na mazingira yanayohitajika katika kubadilika kwake Fimbo hio kua
Nyoka, kwa mfano hapa tumeona kua aya hizi za Surat Ta-ha 20:20, Sural An Naml
27:10 na Surat Al Qasas 28:31 zimetumia neno Hayya na Jan wakati Fimbo hio
ilipoheuka mbele ya Nabii Musa mwenyewe wakati akiwa peke yake, na kisha Surat Al
Aaraf 7:107, Surat Ash Shuara 26:32 zimetumia neno Thuban katika kuelezea Ukubwa
wa Nyoka huyo kulinganisha na Nyoka wengine waliopo karibu yake kama tutakavyoona
hapo baadae katika kisa.

Ambapo tunapoangalia Historia ya Misri basi mpaka Fir’awn katika Kofia yake ya
Ufalme alikua ni mwenye nembo ya Nyoka, hii inaonesha namna Nyoka alivyokua
anaogopewa na kufanywa kama Mungu miongoni mwa jamii za watu wa Misri, na
bila ya shaka Nyoka ni Mnyama ambae kimaumbile hua anaogopewa zaidi na Ibn
Adam Ulimwenguni.

Na hii ni kutokana na uwezo wake wa kuteleza kwa kasi kubwa sana ardhini, kwenye
miti majani, kwenye ukuta na hata kwenye maji bila ya kua na miguu ambao si kua
tu unawachanganya Viumbe Ibn Adam bali pia unawachanganya wanyama wengine
kwani hua ni mwendo wa kushtusha, na kujaaliwa kwake kua na uwezo mkubwa wa
kusababisha madhara makubwa yanayopelekea kuhatarisha maisha ya kiumbe
mwengine kutokana na Sumu yake. Hivyo ni maumbile ya kiumbe Ibn Adam kua na
khofu ya kiumbe Nyoka kutokana na maumbile yake mdudu huyo yanayompelekea
kua hatarini anapokua mbele ya mdudu huyo anaetishia uhai wake.

Kwani miongoni mwa sifa ambazo zinaufanya Mwili wa Ibn Adam kua ni wenye
Ukamilifu basi ni ufanyajia kazi wa mifumo tofauti iliyomo ndani yake, ambapo
katika tukio kama hili basi mara tu baada ya macho kuona kitu husika na kisha
kupeleka habari katika Ubongo ambao hua ni wenye kutafsiri na kutathmini kile
kinachoonekana mbele ya macho ya Mtu husika kua ni kitu kizuri ama si kizuri na
hivyo nini kinatakiwa kufanywa.

Hivyo baada ya Ubongo kutathmini na kugundua kua kitu kinachoonekana mbele ya


Macho ya Ibn Adam husika ni cha Hatari basi Ubongo huo haraka sana hutuma
ujumbe kwenye sehemu ya Ubongo ambayo huunganisha hutuma taarifa kwenye
kiungo kinachofanya kazi ya kuzalisha kemikali zinazojulikana kama Adrenalin
ndani ya mwili wa Ibn Adam.

Kemikali za Adrenalin hua na kazi ya kuuandaa mwili wa Ibn Adam na kuutarifu


kua zinatakiwa zichukuliwe hatua za maamuzi ya haraka sana ili kujihami na hatari
iliyopo mbele yake, aidha kwa kukabiliana na hatari hio kama kuna uwezo wa
kukabiliana nayo na kuulinda mwili na madhara yanayotaka kusababishiwa mwili
huo au kuukimbiza mwili huo wa mtu husika na hivyo kua mbali zaidi na hatari hio.
566

Hivyo basi kemikali hizo za Adrenalin zinapozalishwa basi moja kwa moja hua ni
zenye kuudhibiti mfumo wa Mzima wa mapigo ya Moyo unaosimamia Mfumo wa
wa Damu ya Ibn Adam ndani ya mwili wake na hivyo Moyo wa mtu husika hua ni
wenye kufanya kazi kwa kasi zaidi kwa kupunguza mzunguko wa matumizi ya Damu
katika sehemu zisizokua muhimu kwa sana kufanya kazi ndani ya mwili wa Ibn
Adam kwa wakati huo ili kuongeza matumizi ya mzunguko wa Damu kwenye
sehemu tofauti za viungo vya mwili vinavyohitajika zaidi kwa huo ikiwemo kwenye
Ubongo ili Mtu awe na Umakini zaidi katika kutathmini hatari hio kabla ya
kukabiliana nayo au kuiepuka kwa kuikimbia, na kuharakisha Damu kwenye Misuli
ya Mwili kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki za kupigana au kukimmbia, na hapo
hapo kupunguza hisia za maumivu kama ikibidi mwili wa mtu husika ukabiliane na
hatari hio kwa uwezo wake wote.

Mapigo ya Moyo anapoongezeka basi na Mapafu nayo hutanuka zaidi ili kuongezea
hewa ya Oxygen ndani ya mwili kwa ajili ya kusambaza Damu zaidi na kuongeza
sukari aina ya Glucose ndani ya damu ili sehemu tofauti za mwili zinazotakiwa
kufanya kazi kwa umakini na kwa nguvu zaidi ziweze kufanya kazi kutokana na
tukio husika.

Ama kwa upande mwengine basi inapotokea tukio kubwa ambalo ni la kushtua sana
kiasi ya kua haliwezi kuingia ndani ya ufaham wa Ibn Adam na kuweza kutafsirika
ipasavyo kimaumbile kutokana na kua hali hio hua haijawahi kutokea au kuonekana
au kufikirika hapo kabla basi ndio tunaona kua mwili wa Ibn Adam hua unashindwa
kustahamili na hiyo Mtu husika hua ni mwenye kuishiwa na nguvu na ghafla hua ni
mwenye kuanguka na kupoteza faham kutokana na kua Mfumo wake wa
kimaumbile kushindwa kupeleka Damu inayotosheleza kwenye Ubongo kutafsiri
kinachotokea, na kwenye Misuli ya Miguu na Mikono na viungo vyengine stahiki
kuweza kuchukua hatau stahiki.

Na hii ni kutokana na Hikma zake Allah Subhanah wa Ta’ala kujaribu kutuonesha


mbali ya kua ametuumba katika umbo lililo bora lakini hata hivyo sisi ni viumbe
dhaifu kama alivyosema katika aya:

﴾ً‫ﺿﻌِﻴﻔﺎ‬
َ ‫ﻧﺴﺎ ُن‬ ِ ‫﴿و ُﺧﻠِ َﻖ ٱ‬
‫ﻹ‬
َ َ
Wakhuliqa al insanu dhaAAeefan (Surat An Nisaa 4: 28)

Tafsir: Na tumemuumba Mtu kua ni Dhaif.


567

Ambapo kutokana na ayah hii basi tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala ametuuumba
kua ni dhaifu ambapo kwa wenye kutafakkari basi hua ni wenye kujua kua hawatakiwi
kua na Kibri mbele ya Mola wao na mbele ya Viumbe wenzao na badala yake wanatakiwa
kua na Unyenyekevu mbele yake yeye Muumba wetu na pia mbele ya viumbe wenzetu.

Kwa hivyo kutokana na hali ya Maumbile ya Miili ya Ibn Adam ilivyo basi haishangazi
kuona kua Nabii Musa aliingiwa na Khofu ya Kimaumbile na kutaka kukimbia pale
Fimbo yake hio ilipogeuka kua na Maumbile ya Nyoka mwenye Kutambaa kwa kasi
sana, na kutokana na hikma zake basi Allah Subhanah wa Ta’ala aliijaalia Fimbo hii
kuingia katika hali hio ya kiumbe anaetisha yaani Nyoka kwa ajili ya kumtayarisha Nabii
Musa kiakili na kiufaham ili awe tayari mwenye kua ana uwezo wa kukabiliana na
Maadui zake ambao wao kwa upande wao wamewatukuza na kuwaogopa Wadudu hao
waitwao Nyoka, ambao hata hivyo hua wanao uwezo wa kuwadhibiti kwa kutumia njia
tofauti ikiwemo uchawi wanaotumia sana katika maisha yako ya kila siku ya kijamii.

Hivyo baada ya kutokea tukio hilo la Fimbo kugeuka Nyoka, na Nabii Musa kuingiwa
na khofu ya kimumbile na kutaka kukimbia basi Allah Subhanah wa Ta’ala akamtuliza
na kumtoa khofu hio Nabii Musa kwa kumbaianishia kua hio ni sawa na Fimbo yake na
asiwe na khofu nayo kwani akiikamata basi itarudi katika hali yake ya awali ya kawaida
kama zinavyosema aya:

ٰ َ ‫ﻴﺪ َﻫﺎ ِﺳ َﲑﺗَـ َﻬﺎ ٱﻷ‬


﴾‫ُوﱃ‬ ُ ِ‫ﻒ َﺳﻨُﻌ‬ َ َ‫﴿ﻗ‬
ْ َ‫ﺎل ُﺧ ْﺬ َﻫﺎ َوﻻَ َﲣ‬
Qala khudhha wala takhaf sanuAAeeduha seerataha al-oola (Surat Ta-Ha 20: 21)

Tafsir: Akaambiwa: Ichukue na tutairudisha katika hali yake ya awali.

Ambapo katika Surat Al Qasas basi tunaona kua Nabii Musa anaamrishwa kwa
kuambiwa kua amkabili Nyoka huyo, kwa kumkamata na wala asiwe na khofu yeyote na
wala hatomsababishia madhara yeyote, kwani kwa hakika yeye na kila kitu chake kipo
ndani ya usimamizi wa Allah Subhanah wa Ta’ala ambao ndani yake ni kwenye Amani
isiyokua na mfano wake:

﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ِ َ ‫ﻒ إِﻧﱠ‬
ْ َ‫ﻮﺳ ٰﻰ أَﻗْﺒِ ْﻞ َوﻻَ َﲣ‬
َ ‫ﻚ ﻣ َﻦ ٱﻵﻣﻨ‬ َ ُ‫﴿ ٰﳝ‬
Ya Moosa aqbil wala takhaf innaka mina al-amineena (Surat Al Qasas 28:31)
568

Tafsir: Ewe Musa. Kabiliana nae na wala usiwe na Khofu kwani kwa hakika upo mbele
ya wenye kua na Amani.

Hapa tumeona kua Nabii Musa amepewa silaha ya kwanza ambayo ni Muujiza wa Fimbo
yake ambao atauhitaji kuutumia katika harakati zake anazotaka kupewa, na kisha baada
silaha hio basi anapewa silaha ya pili ambayo ni ya Miujiza wa kubadilisha muonekano
wa Mkono wake kutoka katika hali ya kawaida na kua katika hali ya weupe wa upekee
unaong’ara kama vile ambavyo ulivyokua uking’ara Mti uliopo mbele yake, kwa
kuambiwa kua:

‫ﻚ ِﻣ َﻦ‬ ٍۤ
َ ‫ﺎﺣ‬
َ َ‫ﻚ َﺟﻨ‬ ْ ‫ﻀﺂءَ ِﻣ ْﻦ َﻏ ِْﲑ ُﺳﻮء َو‬
َ ‫ٱﺿ ُﻤ ْﻢ إِﻟَْﻴ‬ َ ِ‫ﻚ ﻳَ َﺪ َك ِﰱ َﺟْﻴﺒ‬
َ ‫ﻚ َﲣُْﺮ ْج ﺑَـْﻴ‬ ْ ﴿
ْ ُ‫ٱﺳﻠ‬
ِِ ِِ ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ِّ‫ﺎ� ِن ِﻣﻦ ﱠرﺑ‬
َ ‫ﻚ إِ َ ٰﱃ ﻓْﺮ َﻋ ْﻮ َن َوَﻣﻠَﺌﻪ إِﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻗَـ ْﻮﻣﺎً ﻓَﺎﺳﻘ‬ َ ِ‫ﺐ ﻓَ َﺬاﻧ‬
َ ‫ﻚ ﺑـُْﺮَﻫ‬ ِ ‫ٱﻟﱠﺮْﻫ‬
Osluk yadaka fee jaybika takhruj baydhaa min ghayri soo-in waodhmum ilayka
janahaka mina alrrahbi fadhanika burhanani min rabbika ila firAAawna wamala-
ihi innahum kanoo qawman fasiqeena; (Surat Al Qasas 28:32)

Tafsir: Na uingize Mkono wako ndani ya kifua (cha nguo yako na kisha utakapoutoa)
utatoka huku ukiwa mweupe bila ya madoa yeyote na kisha usogeze mkono wako
pembeni yako utakapokua na khofu. Na hivyo ni Vithibitisho viwili kutoka kwa Mola
wako kwenda kwa Fir’awn na Machifu wake kwani kwa hakika wao ni watu waovu.

Nabii Musa akauangalia mkono wake huo namna ulivyokua umebadilika rangi yake,
huku macho yake yakishindwa kuamini na pia kuendelea kuangalia zaidi mng’aro wa
mkono huo, kwani ulikua ni mkubwa sana kiasi ya kua alihisi kua kama akiendelea
kuangalia zaiidi basi macho yake yangekua ni yenye kuumia, hivyo akauweka mkono
huo pembeni yake na hivyo ukawa ni wenye kurudi katika hali yake ya kimaumbile ya
kawaida.

Ambapo katika sehemu nyengine basi tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala
ameijumuisha Miujiza yote tisa katika tukio hili, kumaanisha kua mbali ya kua
amembainishia Nabii Musa Miujiza hii miwili mikuu hapa katika Bonde hili Tukufu la
Tuwa, lakini kuna miujiza myengine ambayo atamjaalia kua nayo hapo atakapokua
anakabiliana na Fir’awn na watu wake kama tutakavyoona hapo baadae katika kisa na
kama zinavyosema aya:
569

ٍ �‫ﻚ َﲣْﺮج ﺑـﻴﻀﺂء ِﻣﻦ َﻏ ِﲑ ﺳ ۤﻮٍء ِﰱ ﺗِﺴ ِﻊ آ‬


‫ت إِ َ ٰﱃ ﻓِْﺮ َﻋ ْﻮ َن‬ ِ ِ
َ ْ ُ ْ ْ َ َ َْ ْ ُ َ ِ‫﴿ َوأ َْدﺧ ْﻞ ﻳَ َﺪ َك ﰱ َﺟْﻴﺒ‬
ِِ ِِ
﴾‫ﲔ‬َ ‫َوﻗَـ ْﻮﻣﻪ إِﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻗَـ ْﻮﻣﺎً ﻓَﺎﺳﻘ‬
Waadkhil yadaka fee jaybika takhruj baydaa min ghayri soo-in fee tisAAi ayatin
ila firAAawna waqawmihi innahum kanoo qawman fasiqeena (Surat An Naml 27:12)

Tafsir: Na uingize Mkono wako ndani ya kifua (cha nguo yako na kisha utakapoutoa)
utatoka huku ukiwa mweupe bila ya tatizo lolote, hii ni miongoni mwa Miujiza tisa
utakayoenda nayo kwa Fir’awn na watu wake kwani kwa hakika wao ni watu Waovu.

Hivyo baada ya Allah Subahanh wa Ta’ala kumpa Silaha hizo mbili Nabii Musa na
kumhifadhia nyengine saba kwa ajili ya matumizi ya uthibitisho wa baadae basi
anambainishia kua zitatumika kua kama ni vithibitisho dhidi ya Fir’awn, kwani umefika
wakati wa kuonywa ili arudi kwa Mola wake, na muonyaji hawezi kua mtu yeyote
isipokua yule aliechaguliwa na Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ni Nabii Musa, na
hivyo kua tayari ni mwenye kubainishiwa kua yeye tayari ameshakua ni Mtume wa Allah
Subhanah wa Ta’ala na kua ni mwenye kupokea amri ya kwanza ambayo anatakiwa
aifikishe kwa mhusika ambayo ni yenye kusema:

ِ ِ
َ ِّ‫ﻚ إِ َ ٰﱃ َرﺑ‬
‫ﻚ‬ َ َ‫ﻚ إِ َ ٰﱃ أَن ﺗَـَﺰﱠﻛ ٰﻰ۞ َوأ َْﻫﺪﻳ‬
َ ‫ﺐ إِ َ ٰﱃ ﻓْﺮ َﻋ ْﻮ َن إِﻧﱠﻪُ ﻃَﻐَ ٰﻰ۞ ﻓَـ ُﻘ ْﻞ َﻫﻞ ﻟﱠ‬
ْ ‫﴿ٱ ْذ َﻫ‬
﴾‫ﻓَـﺘَ ْﺨ َﺸ ٰﻰ‬
Idhhab ila firAAawna innahu tagha; Faqul hal laka ila an tazakka; Waahdiyaka ila
rabbika fatakhsha (Surat An Naziat 79:17)

Tafsir: Nenda kwa Fir’awn kwani kwa hakika amevuka Mipaka, Na Mwambie: ‘Jee
utajisafisha?’Na Kisha nitakuongoza kwa Mola wako na Kumuogopa.

Yaani Nabii Musa anatakiwa akamshauri Fir’awn na kumuusia kuhusiana na maarifa ya


Allah Subhanah wa Ta’ala ili apate kumjua, kwani ni kutokana na kumjua Allah
Subhanah wa Ta’ala basi ndio Nyoyo zinakua na khofu juu yake kama anavyosema
mwenyewe katika Surat Fatir:
570

ِ‫ٱﻪﻠﻟ ِﻣﻦ ِﻋﺒ ِﺎدﻩ‬ ِ َ ِ‫ﻒ أَﻟْﻮاﻧُﻪُ َﻛ ٰﺬﻟ‬ ِ ِ


ِّ ‫ﱠو‬ ِ ‫﴿ َوِﻣ َﻦ ٱﻟﻨ‬
َ ْ َ‫ﻚ إﱠﳕَﺎ َﳜْ َﺸﻰ ﱠ‬ َ ٌ ‫آب َوٱﻷَﻧْـ َﻌﺎم ﳐُْﺘَﻠ‬ َ ‫ﱠﺎس َوٱﻟﺪ‬
ٌ َ ‫ٱﻪﻠﻟَ َﻋ ِﺰ ٌﻳﺰ‬
﴾‫ﻏ ُﻔﻮر‬ ‫ٱﻟْﻌُﻠَ َﻤﺎءُ إِ ﱠن ﱠ‬
Wamina alnnasi waalddawabbi waal-anAAami mukhtalifun alwanuhu kadhalika
innama yakhsha Allaha min AAibadihi alAAulamao inna Allaha AAazeezun
ghafoorun (Surat Fatir 35:28)

Tafsir: Na miongoni mwa Watu na Ddawabbi (Viumbe Hai wote na Wanyama) na


Ng’ombe kuna Waliotafautiana rangi zao, Kadhalika (hivyo ndivyo vilivyo viumbe vya
Allah Subhanah wa Ta’ala) Kwa hakika wanaomuogopa Allah ni miongoni mwa Waja
wake Wenye I’lm, kwa hakika Allah ni mwingi wa Utukufu na ni mwingi wa
Usamehevu.

Hii ni miongoni mwa aya ambazo zinabainisha Utukufu na uwezo wa Hali ya juu kabisa
wa Allah Subhanah wa Ta’ala katika kuumba kwake uwezo ambao unaweza kuonekana
kwake kwa kutumia neema ya Nuru, na bila ya shaka Nuru kuu katika Nuru zote
tunazozijua na tusizozijua basi ni Nuru ya Allah Subhanah wa Ta’ala, kwani ndio yenye
kubainisha kila kitu kinachoonekana na kisichonekana na macho yetu. Na
tunapozungumzia visivyoonekana kwa mtizamo wa macho yetu basi hua vinaonekana
kwa mtizamo wa Jicho la Moyo, ambalo ni linaloona kwa kutumia Nuru ya Moyo.

Na katika aya yetu hii basi Allah Subhanah wa Ta’ala hakutumia mfano wa
vinavyoonekana kwa Mtizamo wa Nuru ya Moyo, na hii ni kwa sababu si kila mtu hua
ni mwenye uwezo wa kuweza kuona kwa kutumia mtizamo wa Moyo, na ndio maana
akatumia mifano ya sifa za rangi za Viumbe vinavyoonekana na mtizamo wa Macho ili
mtizamo huo wa macho uweze kuuthibitishia Mtizamo wa Moyo kwa watakaoafakkari
juu ya kile kinachoelezewa ndani ya mfano wa rangi tofauti za Vitu na Viumbe mbali
mbali wa Allah Subhanah wa Ta’ala.

Ambapo kama tunapoona ni kua aya yetu katika kuainisha sifa ya Viumbe na Vitu hivyo
basi imetumia neno Alwanuhu ambalo kwa Lugha ya Kiarabu hua ni lenye kutokana na
neno Launun ambalo maana yake hua ni Rangi, Muonekano wa Nje wa Kitu. Umbo la
nje la kitu, Aina ya Kitu au Hali ya Kitu. Hivyo neno Alwanuhu lililotumika hapa hua ni
lenye kumaanisha Rangi zake Nyingi au Rangi zake mbali mbali.

Hivyo kutokana na Hikma za Allah Subhanah wa Ta’ala ndio maana akatumia mfano wa
vinavyoonekana kwa kutumia Nuru ya miongoni mwa alivyoviumba, ambayo ni Nuru ya
Jua, kwani mbali ya kua Nuru ya jua ndio chanzo cha uhai wa kila kiumbe kilichomo
Ulimwenguni, kwani bila kuwepo kwa Nuru ya Jua basi hua ni vigumu kwa viumbe
571

kuweza kujipatia chakula chao hapa Ulimwenguni kwa sababu Nuru ya Jua ndio yenye
kusababisha Mimea kua ni yenye kutoa Maua, Majani, Mizizi na Matunda yenye ladha
na rangi mbali mbali kua ni yenye kuota ardhini na kua ni chanzo cha chakula kwa ajili
ya kila viumbe hai wa aina mbali mbali.

Na kwa upande mwengine basi Nuru hio ya jua hua ni yenye kusababisha sisi kua ni
wenye kuona kwa kwa kutumia Macho yetu baada ya Nuru hio kuingia kwenye kioo cha
Jicho la Ibn Adam ambacho kinajumuisha nukta Milioni 120 ambazo hutumika kuangaza
unapokua kwenye Kiza na Nukta Milioni 7 ambazo hutumika kuangaza unapokua
kwenye Nuru na hivyo kusafirisha taswira ya kile kilichoonekana mtizamo wa jicho hilo
na kukiwakilisha kwenye ufaham wa Ibn Adam na kutafsiriwa na Ufaham ambao
humuwezesha Ibn Adam husika kuona uzuri wa Viumbe na vitu vyengine vya Maumbile
Ulimwenguni vyenye maumbo na rangi tofauti na hapo hapo kuweza kutofautisha
utofauti baina ya maumbile yao hayo na rangi zao hizo na uzuri wao na ubaya wao
ukubwa wao udogo wao na umbali wa kitu hicho kinachoangaliwa na sehemu aliopo
mwenye jicho linaloangalia.

Subhanah wa Allah! Kwani ingawa macho ya Ibn Adam yana uwezo mkubwa kiasi
hicho, lakini hata hivyo mbali ya kua na uwezo huo basi kamwe Macho hayo hayawezi
kufikia ule uwezo wa Ndege aina ya Eagle ambae ni mwenye Uwezo wa kuona kwa
Umakini zaidi na kwa masafa ya mbali zaidi ya mara kumi ikilinganiswa na Uwezo wa
Ibn Adam.

Kwa upande wa Qur’an basi tunaona kua imetaja rangi aina kadhaa ikiwemo Abyadh
yaani Nyeupe katika (Surat Al Baqara 2:187, Surat Al Araf 7:108, Surat Ta-Ha 20:22
n.k), Aswad yaani Nyeusi (Surat Al Imran 3:106), Ahmar yaani Nyekundu (Surat
Fatir 35:27), Ahdhar yaani Rangi ya kiza ya Kijani, Wardat yaani Rangi ya Wardi (Surat
Rahman 55:37), Arzaq yaani Buluu (Surat Ta-Ha 20:102) na Asfar yaani Rangi ya
Manjano (Surat Al Baqara 2:96) na hii ni kutokana na Rangi kuu zilizokua zikitumika
katika Lugha ya Asili ya Kiarabu kwa wakati huo kuanisha rangi zenye kiza na zenye
mwangaza, ambapo baadae ndio yakaja kuongezeka majina ya rangi yenginezo katika
Lugha hio kutokana na athari za kimaendeleo na miingiliano ya kiutamaduni
Ulimwenguni, kama ilivyokua kwa Lugha nyengine zote.

Kwani rangi kuu za asili ziko tatu tu yaani Nyekundu, Kijani na Buluu ambapo inapokua
hakuna rangi basi hali ya kitu hua ni yenye kuonekana kua ni Nyeusi na inapokua kuna
rangi zote kwa pamoja basi hali ya kitu hicho hua inaonekena kua ni chenye Rangi
Nyeupe. Yaani tunapokiona kitu kina rangi Nyeusi basi hii inamaanisha kua kitu hicho
kimenyonya au kimepitisha rangi zote ndani yake na hivyo hazikutokea nje yake, na kitu
kinapoonekana kua kina rangi nyeupe basi hua inamaanisha kua kitu hicho hakijapitisha
rangi yeyote ndani yake na rangi zote kwa pamoja zimeakisiwa na zimebakia nje juu ya
kitu hicho.
572

Hivyo kuhusiana na kutofautiana kwa muonekano wa rangi husika hua kunategemea na


ukubwa wa mawimbi ya Miozi ya Nuru ya Rangi husika, kwani Ibn Adam hua ni wenye
uwezo wa kuona Mionzi ya mawimbi ya umeme wa mvutano wa sumaku yenye ukubwa
wa kuanzia Nanomita 380 mpaka 700, Ambapo kila Nanomita moja basi hua ni sawa na
nukta moja katika Nukta Bilioni moja zilizomo kwenye eneo lenye kubwa wa mita moja.

Na mionzi ya Nuru inapopiga kwenye kitu husika kisha macho yetu yakakiona kitu hicho
kua ni cheupe basi hii hua inamaanisha kua kitu hicho hakiwezi kunyonya Nuru ya rangi
ya aina yeyote ndani yake, na macho yetu yakikiona kua ni cheusi basi humaanisha kua
kitu kimenyonya Nuru za aina ya rangi zote ndani yake, ili kufaham vizuri zaidi basi na
tuchukulie mfano wa maji ya baharini ambayo ni kama kawaida ya maji mengine yeyote
yale Ulimwenguni hua ni yenye sifa ya kutokua na rangi yeyote.

Lakini sasa ni kawaida ya maji yanapokua mengi hua ni yenye uwezo mkubwa zaidi wa
kunyonya ndani yake Mionzi ya Nuru za Rangi zote ikiwemo Infra red, Ultra violet, n.k
isipokua Mionzi ya rangi ya Buluu, na hii ni kwa sababu Mionzi ya rangi ya Buluu hua
ni yenye Maumbile ya kua na Mawimbi mafupi ya Sumaku tofauti na Mawimbi ya rangi
nyengine na hivyo hua ni kubakishwa na kuakisiwa na Maji hayo na hivyo kua ni yenye
kuyaonesha Maji ya Bahari kua na rangi ya Buluu ya Bahari na hii pia hua ni kulingana
na hali ya hewa pale inapokua hakuna mawingu na pia kulingana na hali ya mchanga
ulipo chini ya Bahari husika.

Hali ya Rangi ya maji pia huweza kuchukua rangi nyengine kutokana na athari za vitu
vyengine vyenye rangi, kwa mfano maji ya Bahari Nyekundu ambayo imeitwa bahari
nyekundu kwa sababu ya kua ni sehemu yenye bakteria wengi waitwao cynobakteria
ambao wengi wao wanapokufa hua na rangi nyekudu na hivyo rangi yao hio kuyaathiri
maji ya Bahari hio.

Mfano mwengine ni wa hali ya Mbingu ambazo kwa mtizamo wa Macho wetu hua ni
zenye kuonekana na rangi ya Buluu au Samawati na hivyo hii haimaanishi kua Mbingu
zina rangi ya Buluu, bali inamaanisha kua tabaka la juu ya Dunia yetu na Sayari nyengine
kimaumbile hua ni lenye wezo wa kutawanya Miozi ya rangi ya Buluu kwa haraka zaidi,
hivyo mionzi ya Nuru za rangi mbali mbali zinazotoka kwenye Jua zinapoingia kwenye
tabaka hilo hua ni zenye kutawanya kwa pamoja lakini kwa kua mawimbi ya Nuru ya
Rangi ya Buluu ni mafupi basi hutawanyika haraka zaidi na kuonekana kwa wingi zaidi
na macho yetu.

Aya hii ya sifa ya maumbile ya Rangi pia tunaweza kuifafanua kwa kutumia mfano
mwengine ambao ni muhimu zaidi uliotajwa na Allah Subhanah wa Ta’ala pale
aliposema:
573

ْ‫ﲔ ۞ َﻛﻼﱠ ﺑَ ْﻞ َرا َن َﻋﻠَ ٰﻰ ﻗُـﻠُﻮﻬﺑِِ ْﻢ ﱠﻣﺎ َﻛﺎﻧُﻮا‬ ِ ِ ‫ﺎل أ‬ ِ ِ


َ ‫َﺳﺎﻃﲑُ ٱﻷَﱠوﻟ‬ َ ‫﴿إ َذا ﺗُـْﺘـﻠَ ٰﻰ َﻋﻠَْﻴﻪ‬
َ َ َ‫آ�ﺗُـﻨَﺎ ﻗ‬
﴾‫ﻳَ ْﻜ ِﺴﺒُﻮ َن‬
Idha tutla AAalayhi ayatuna qala asateeru al-awwaleena, Kalla bal rana AAala
quloobihim ma kanoo yaksiboona (Surat Al Mutaffifin 83:13-14)

Tafsir: Anapopewa Aya zetu, husema : ‘Ni Hikaya za Kale’. Haikua! Isipokua kwenye
Nyoyo zao kuna Rana kutokana na waliyokua wakiyafanya.

Mfano huu unatuonesha namna Allah Subhanah wa Ta’ala alivyotumia neno Rana katika
ayah hii kuelezea hali za Nyoyo za baadhi ya Ibn Adam ambao ni wenye kupingana na
ujumbe wa Qur’an na hivyo wanaposomewa aya hizo basi hua ni wenye kusema kua Hizi
hazikua chochote isipokua ni Hikaya za Watu waliotangulia. Ambapo neno Rana hua
linamaanisha Kua na Kutu, Kua na Uchafu, Hali ya Kitu kua ni yenye sehemu
iliyofunikwa na kitu chengine tofauti ambacha na hivyo hua ni yenye kuichafua hali ya
asili ya kimaumbile ya kitu hicho, Kua na Hali isiokua nzuri au kuchafuka au Kua na
Dhambi.

Hivyo basi hii haimaanishi kua Nyoyo hizo zinakua na kutu labda kwa sababu
zimenyeshewa na Mvua, au zimetoboka, bali aya inazungumzia Hali ya Maumbile ya
Moyo wa kila Ibn Adam ambao hua ni wenye kua na Maumbile ya Nuru ya Fitra, yaani
hali ya kumjua Mola wake aliemuumba. Na hivyo mtu anapokua anafanya Dhambi basi
Dhambi hizo hua ni zenye kuiathiri Nuru ya asili ya Moyo huo.

Na kwa kua Nuru hio ni ya Maumbile basi athari ya Dhambi hizo hua haiwezi kupenya
moja kwa Moja ndani ya Moyo na hivyo badala yake hua ni yenye kubakia na kuakisiwa
nje juu ya Moyo wa Mtu husika, na hivyo athari hio kidogokidogo hua ni yenye kuzuia
kuenea Nuru ya Kimaumbile ya Imani ya Moyo husika.

Kwani hua kuna tofauti kubwa baina ya Moyo wenye Kutu na Moyo usiokua na Kutu,
kwani Moyo wenye kua na Kutu hua ni sawa na Moyo ambao Usiokua na mwenyewe
kwani hausimamiwi wala haushughulikiwi na hivyo hua haupanguswi na hivyo hua ni
wenye kupoteza mng’aro wa Nuru yake ya asili ambapo Moyo usiokua na Kutu hua ni
Moyo ambao mbali ya kua ni wenye Nuru ya Kimaumbile ya Fitra ya Kumjua Muumbaji
wake lakini pia hua ni kama wenye kusuguliwa na kupanguswa na pamba ya Ikhlas na
King’arisho cha Istighfar na hivyo Moyo huo hua hauwezi kua ni wenye kubakia na
Rana, yaani Kutu kwani kila wakati hua ni wenye kusimamiwa na kushughulikiwa na
kubakia kua ni wenye Kung’ara na hivyo hua ni wenye kupendeza na kuvutia.
574

Hivyo tuaporudi katika aya ya Surat Fatir 35:28 na kuitizama kwa mtizamo mwengine
basi tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea kua kama ilivyokua kwa viumbe
kua na hali za rangi tofauti baina yao na hivyo baadhi yao kua ni wenye kupendeza na
kuvutia zaidi kutokana na uzuri wa rangi zao, na wengine kua ni wa kawaida katika
maumbile ya rangi zao hizo basi ndivyo ilivyo kwa Imani ya waja wake wenye Ilm ya
Kumjua Allah Subhanah wa Ta’ala kwani kuna wenye na kuna wasiokua na Imani kabisa
na kwa kila mwenye Ilm zaidi juu ya Mola wake basi hua ni mwenye Moyo wenye Nuru
zaidi na hivyo kua na Imani zaid kutokana na kumjua zaidi Mola wake na hivyo hua ni
mwenye kumuogopa zaidi Mola wake.

Na ndio maana wakasema Wananzuoni kuhusiana na maneno ya ayah hii yasemayo kua
ni Wenye Ilm tu ndio wenye Kumuogopa Allah Subhanah wa Ta’ala kua: Ni Wenye Ilm
pekee ndio wenye kujua Majina na Sifa Tukufu za Allah Subhanah wa Ta’ala na
hivyo hua ni wenye kumuogopa Allah Subhanah wa Ta’ala kama inavyotakiwa
aogopewe.

Ambapo amesema Abdallah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu kua: ‘Ilm hua si sawa na
Wingi wa Kunukuu bali hua ni katika wingi wa Kumuogopa Allah Subhanah wa
Ta’ala’

Na akasema Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mtu mwenye Ilm ya kumjua
Allah Subhanah wa Ta’ala kweli hua ni yule ambae hawavunji Moyo watu juu ya
Rehma za Allah Subhanah wa Ta’ala, na yule ambae hawafanyii Watu urahisi wa
kumuasi Allah Subhana wa Ta’ala. Na yule ambae hawafanyi Watu wakawa ni
wenye kujihisi kua wako salama kutokana na Adhabu za Allah Subhanah wa Ta’ala
juu yao, na pia ni yule ambae asieachana na Qur’an, kwani kwa hakika hakuna
manufaa katika Ucha Mungu pale inapokua Mtu husika hana Ufaham wala
Mazingatio katika kisomo chake cha Qur’an.’

Ambapo anasema Imam Ibn Abi Hayyan Al Taymi kua: ‘Miongoni mwa Wanazuoni
basi kuna wa aina tatu:

1-Wenye Ilm ambao ni wenye Kumjua Allah Subhana wa Ta’ala na wakawa pia ni
wenye kujua Maamrisho yake.

2-Wenye Ilm ambao ni wenye kumjua Allah Subhana wa Ta’ala lakini hawayajui
maamrisho yake.

3-Wenye Ilm ambao ni wenye kuyajua maamrisho ya Allah Subhana wa Ta’ala


lakini si wenye kumjua Allah Subhana wa Ta’ala.
575

Hivyo miongoni mwa Wenye Ilm basi ni wale waliomo kwenye Kundi la Kwanza tu
ndio ambao ni wenye kumuogopa Allah Subhana wa Ta’ala’

Kwani hao ndio ambao ni wenye kumjua Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo kua ni
wenye kuyajua maamrisho yake kuhusiana na ni lipi la kulikimbilia na ni lipi la
kulikimbia.

Na bila ya shaka kwa upande wa Imam Abu Muhammad Abd Al Haqq Ibn Ghalib Ibn
Atiya Al Andalus basi yeye anasema kua: ‘Aya hii haimaanishi kua hakuna
asiemuogopa Allah Subhanah wa Ta’ala isipokua wenye Ilm, bali ni yenye kutilia
mkazo kwa kutumia neno Innama kusisitiza sifa kuu za Wanazuoni kua ni wale
ambao wanaomuogopa Allah Subhana wa Ta’ala. Hivyo basi haimaanishi kua
wasiokua Wanazuoni hawawezi kua na sifa ya kua ni wenye kumuogopa Allah
Subhana wa Ta’ala.’

Hivyo baada ya Nabii Musa kupewa amri hio ya kua aende kumuusia Fir’awn kuhusiana
na Mola wake labda atakua ni mwenye kumkumbuka au ni mwenye kumuogopa Mola
wake kwani kwa hakika amevuka mipaka kwa kukufuru kama zinavyosema Allah
Subhanah wa Ta’ala kua:

﴾‫ﺐ إِ َ ٰﱃ ﻓِﺮ َﻋﻮ َن إِﻧﱠﻪُ ﻃَﻐَ ٰﻰ‬


ْ ‫﴿ٱ ْذ َﻫ‬
ْ ْ
Idhhab ila firAAawna innahu tagha (Surat Ta-Ha 20:24)

Tafsir: Nenda kwa Fir’awn, kwani kwa hakika, yeye ni mwenye kuvuka mipaka

Hivyo Nabii Musa akaanza kuona na kuhisi uzito wa jukumu analotaka kupewa na Mola
wake, na ingawa amepewa vithibitisho hivyo viwili lakini hata hivyo alikua akijua kua
kazi yake sio ndogo hivyo kutokana na mtizamo wa watu wa Misri dhidi yake na hivyo
anakhofu kua kama wamsakama kwa shutma zao basi huenda akashindwa kua na Subra
kutokana na joto litakalojaa ndani ya Kifua chake kkutokana na maneno yao, hivyo
akadhihirisha hayo kama zinavyosema aya:

‫ﺻ ْﺪ ِرى َوﻻَ ﻳَﻨﻄَﻠِ ُﻖ ﻟِ َﺴ ِﺎﱏ ﻓَﺄ َْرِﺳ ْﻞ‬ ِ ‫ﻮن ۞ وﻳ‬ ِ ‫ﺎف أَن ﻳ َﻜ ِّﺬﺑ‬ ۤ ِِ‫ب إ‬
َ ‫ﻴﻖ‬
ُ ‫ﻀ‬ ََ ُ ُ ُ ‫َﺧ‬
َ ‫أ‬ ‫ﱐ‬ّ ِّ ‫ﺎل َر‬
َ َ‫﴿ﻗ‬
﴾‫إِ َ ٰﱃ َﻫﺎرو َن‬
ُ
576

Qala rabbi innee akhafu an yukadhdhibooni; Wayadheequ sadree wala yantaliqu


lisanee faarsil ila haroona(Surat Ash Shuara 26:12-13)

Tafsir: Akasema Ewe Mola wangu! Hakika mimi nna khofu kua Watanikadhibisha,
Na Kifua changu Kimebana, na Ulimi wangu hautokua huru (Kiufasaha), Mtume
Harun (pamoja nami).

Na hali hii ya kifua kua ni chenye kubana hua ni kutokana na hisia za kimaumbile za
kibinadam yaani kama vile alivyosema Allah Subhanah wa Ta’ala kumthibitishia hali
aliyokua nayo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam pale aliposema kwa katika aya za
mwishoni za Surat Al Hijr kwa kumwambia kua:

ِ ‫ﺎك ٱﻟْﻤﺴﺘـﻬ ِﺰﺋِ ﱠ‬ ِ ِ


‫ﻳﻦ‬
َ ‫ﲔ۞ٱﻟﺬ‬ َ ْ َ ْ ُ َ َ‫ﲔ۞إِ ﱠ� َﻛ َﻔْﻴـﻨ‬ َ ‫ض َﻋ ِﻦ ٱﻟْ ُﻤ ْﺸ ِﺮﻛ‬ ْ َ‫﴿ﻓ‬
ْ ‫ﭑﺻ َﺪ ْع ﲟَﺎ ﺗُـ ْﺆَﻣُﺮ َوأ َْﻋ ِﺮ‬
‫ﺻ ْﺪ ُرَك ِﲟَﺎ‬
َ ‫ﻴﻖ‬
ِ َ ‫ف ﻳـﻌﻠَﻤﻮ َن۞ وﻟََﻘ ْﺪ ﻧَـﻌﻠَﻢ أَﻧﱠ‬
ُ ‫ﻚ ﻳَﻀ‬ ْ ْ َ ‫ﻮ‬ ‫ﺴ‬ ‫ﻓ‬
َ ‫ﺮ‬ ‫آﺧ‬
َ ً‫ﺎ‬‫ﻬ‬ ٰ‫ـ‬ ‫ﻟ‬ِ‫ٱﻪﻠﻟِ إ‬
‫َْﳚ َﻌﻠُﻮ َن َﻣ َﻊ ﱠ‬
ُ َ ُ َ ْ َ َ
ِ ‫ﺎﺟ‬
ِ ‫ﻳـ ُﻘﻮﻟُﻮ َن۞ ﻓَﺴﺒِﺢ ِﲝﻤ ِﺪ رﺑِﻚ وُﻛﻦ ِﻣﻦ ٱﻟ ﱠﺴ‬
‫ﻚ‬َ َ‫ﻚ َﺣ ﱠ ٰﱴ َ�ْﺗِﻴ‬ ْ ‫ﻳﻦ ۞ َو‬
َ ‫ٱﻋﺒُ ْﺪ َرﺑﱠ‬ َ ‫ﺪ‬ َ ّ ْ َ َ َّ ْ َ ْ ّ َ َ
﴾‫ﲔ‬ ِ
ُ ‫ٱﻟْﻴَﻘ‬
FaisdaAA bima tu/maru waaAAridh AAani almushrikeena, Inna kafaynaka
almustahzi-eena, Alladheena yajAAaloona maAAa Allahi ilahan akhara fasawfa
yaAAlamoona, Walaqad naAAlamu annaka yadheequ sadruka bima yaqooloona,
Fasabbih bihamdi rabbika wakun mina alssajideena, WaoAAbud rabbaka hatta
ya/tiyaka alyaqeenu(Surat Al Hijr 15:94-99)

Tafsir: Hivyo tangazia juu ya kile ulichoamriwa na wape mgongo washirikina. Kwani
kwa hakika sisi tutakutosheleza dhidi ya wanaokufanyia mzaha. Wale ambao
waliofanyia Allah Mungu mwengine zaidi yake, na kisha watakuja kujua. Kwa Hakika
sisi tunajua kua Kilivyobana Kifua chako kutokana na wanayoyasema. Hivyo Mtukuze
kwa kuonesha shukrani kwa Mola wako na kua miongoni mwa wenye kusujudu. Na
Muabudu Mola wako mpaka itakapokujia yakini.

Sasa hapa Allah Subhanah wa Ta’ala anatuonesha namna hali ilivyokua kwa kipenzi
chake yaani Imami Al Anbiyah Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam ambae hapo kabla
alimtanua kifua chake kama alivyosema katika Surat Al Inshirah baada ya Biismi Allahi
Al Rahmani Al Rahiim:
577

ِ‫﴿ﺑِﺴ ِﻢ ﱠ‬
۞‫ﻨﻚ ِوْزَرَك‬ َ ‫ﺻ ْﺪ َرَك ۞ َوَو‬
َ ‫ﺿ ْﻌﻨَﺎ َﻋ‬ َ ‫ﻚ‬َ َ‫اﻪﻠﻟ ٱﻟﱠﺮ ْﲪـٰ ِﻦ ٱﻟﱠﺮِﺣﻴ ِﻢ۞ أََﱂْ ﻧَ ْﺸَﺮ ْح ﻟ‬ ْ
﴾‫ﻚ ِذ ْﻛﺮَك‬ ۤ ِ
َ َ َ‫۞وَرﻓَـ ْﻌﻨَﺎ ﻟ‬
َ ‫ﺾ ﻇَ ْﻬَﺮَك‬ َ ‫ٱﻟﱠﺬي أَﻧ َﻘ‬
Alam nashrah laka sadraka, WawadhaAAna AAanka wizraka, Alladhee
anqada dhahraka, WarafaAAna laka dhikraka. (Surat Al Inshirah 94:1-3)

Tafsir: Jee Hatukukufunua kifua chako (Ewe Muhammad)? Na kuondoa kutoka


kwako Uzito? Ambao ulikua ukididimiza chini? Na kisha tukaupandisha ukumbusho
wako?

Yaani Allah Subhanah wa Ta’ala anamliwaza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
kutokana na mitihani anayokumbana nayo kutokana kwa watu wake wa Mji wa Makkah
ambao ni wenye kutokaa katika kabila moja nae yaani ndugu zake, kaka zake, baba zake,
mama zake n.k ambao hapo kabla walikua wakimpenda na kumuamini sasa lakina ghafla
mara baada ya kua ni mwenye kuwausia watu hao kuhusiana na kumpwekesha Allah
Subhanah wa Ta’ala basi wamegeuka na kua maadui zake wakuu wenye chuki kubwa
dhidi yake.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anasema kumuwekea wazi Nabii Muhammad


Salallahu Alayhi wa Salam kua amempendelea kwa mambo matatu makuu, ambapo
jambo la kwanza ni Sharh as Sudur kutanuliwa au kufunuliwa kwa Kifua, la pili ni
kuondolewa Uzito aliokua nao hapo kabla ya kushushiwa Wahyi, na la tatu ni
kupandiswa darja ya juu kabisa kuliko viumbe wote.

Hivyo bila ya shaka Nabii Musa alikua anajua mtihani aliokua nao mbele yake, kwani
yeye anaenda kukabilana na mmoja kati ya Wafalme wenye nguvu kubwa sana ya
kimamlaka, kiuchumi na kijeshi Ulimwenguni, tena peke yake, lakini hata hivyo aliamua
kukabiliana nao mtihani huo mzito kama alivyoamrisha Mola wake na ndio maana
akaamua kumuomba Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kusema:

ْ‫ٱﺣﻠُ ْﻞ ﻋُ ْﻘ َﺪةً ِّﻣﻦ ﻟِّ َﺴ ِﺎﱐ۞ﻳـَ ْﻔ َﻘ ُﻬﻮا‬ ۤ ِ ‫ب ٱﺷﺮح ِﱃ ﺻﺪ ِري۞وﻳ ِﺴﺮ‬


ْ َ ْ ْ ّ َ َ ْ َ ْ َ ْ ِّ ‫ﺎل َر‬
‫ي۞و‬ ِ
‫ﺮ‬ ‫َﻣ‬‫أ‬ ‫ﱄ‬ َ َ‫﴿ﻗ‬
‫َﺧﻲ۞ٱ ْﺷ ُﺪ ْد ﺑِِﻪ أ َْزِري۞ َوأَ ْﺷ ِﺮْﻛﻪُ ِ ۤﰲ‬ِ ‫ﻗَـﻮِﱄ۞وٱﺟﻌﻞ ِّﱃ وِزﻳﺮاً ِﻣﻦ أَﻫﻠِﻲ۞ﻫﺎرو َن أ‬
ُ َ ْ ّْ َ َْ َ ْ
﴾ً‫ﺼﲑا‬ ِ ‫ﻚ ُﻛﻨﺖ ﺑِﻨَﺎ ﺑ‬ ِ ِ ِ‫ﻚ َﻛﺜ‬
َ ‫أ َْﻣ ِﺮي۞ َﻛ ْﻰ ﻧُ َﺴﺒِّ َﺤ‬
َ َ َ ‫۞وﻧَ ْﺬ ُﻛَﺮَك َﻛﺜﲑاً۞إﻧﱠ‬ َ ‫ا‬
ً‫ﲑ‬
578

Qala rabbi ishrah lee sadree; Wayassir lee amree; Waohlul AAuqdatan min lisanee;
Yafqahoo qawlee; WaijAAal lee wazeeran min ahlee; Haroona akhee; Oshdud bihi
azree; Waashrik-hu fee amree; Kay nusabbihaka katheeran; Wanadhkuraka
katheeran; Innaka kunta bina baseeran(Surat Ta-Ha 20:25-35)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa) Ewe Mola wangu nitanulie Kifua changu. Na
unirahisishie Jambo langu, Na niondoshee Fundo katika Ulimi wangu, Wapate
kunifaham kauli yangu, Na nijaalie Waziri kutokana na Watu wangu. Kaka yangu
Haruna, Niongezee Nguvu pamoja nae, Nae mshirikishe katika jambo langu hili, ili
tupate kukutuza kwa wingi, na kukukumbuka kwa wingi. Kwani kwa hakika wewe juu
yetu ni mwenye kutuona.

Katika aya hizi Allah Subhanah wa Ta’ala anatuonesha namna Nabii Musa
alivyokubaliana na kujitayarisha kubeba Jukumu hilo zito sana hivyo anaainisha vitu
vyengine pia muhimu vinavyohitajika katika utekelezaji wa Jukumu hilo, hivyo basi
kuweka wazi kua ingawa yuko tayari kubeba jukumu lakini hata hivyo anahitaji kua na
mambo muhimu mengine ya kimaumbile yatakayomuewezesha kutekeleza jukumu hilo
kikamilifu kama inavyostahiki na kwa urahisi zaid.

Na ndio maana Nabii Musa akaomba kua apewe Sharh as Sudur kwa kutumia neno
Ishrah ambalo ni lenye kumaanisha Kufungua, Kutanua, Kukuza, Kutawanya, Kuweka
wazi, Kuzidisha Imani na hii ni kutokana na yale maneno aliyoyasema kuhusiana na
Kifua chake katika aya tuliyoiangalia hapo kabla ambayo ni aya ya Surat Ash Shuara
26:13.

Kisha baada ya hapo katika Dua yake akaomba kua apewe Umadhubuti wa Mshikamano
baina yake na msaidizi wake kwa kutumia neno Ushdud bihi Azri ambapo neno Ushdud
ni lenye kutokana na neno Shadda ambalo hua ni lenye kumaanisha Kubana Vizuri Sana,
Kudhibiti, Kufanya kua Madhubuti, Kua na Ugumu, Kua na Nguvu, Kua na Uwezo wa
Nguvu za Mwili na za Kiakili, Kua na Uwezo wa Hali ya Juu.

Na neno Azri ni linalotokana na neno Azara ambalo maana yake hua ni Kuongeza Nguvu,
Kuunga Mkono, Kusaidia kinguvu, Kukuza Kiukubwa na Kinguvu.

Neno Azara ndio ndio lilitumika kutoa jina la Baba yake Mlezi Nabii Ibrahim na pia
likatoa neno Azrun ambalo hua ni lenye kumaanisha Nguvu. Mgongo au Sehemu ya
Katikati ya Mwili wa Ibn Adam ambayo ndio hua inayoupa nguvu mwili mzima wa Ibn
Adam katika ufanyaji kazi wake Kwa kutumia Nguvu za Mwili.

Hivyo basi, tunapoangalia maombi ya Nabii Musa kwa ujumla katika aya hizi basi
tunaona kua maombi yake yanajumuisha mambo manane yanayohitajika kwa ajili ya
kuweza kutekeleza ipasavyo majukumu yake hayo mbele ya Uangalizi wa Mola wake
579

ambae anaona wazi kila kitu na ni mwenye kujua kama Nabii Musa anahitaji Msaidizi
ama la, maombi hayo ni kua:

1-Afuguliwe Kifua
2-Arahishiwe uzito wa Jukumu lake hilo.
3-Alainishiwe Ulimi wake ili awe na hoja zinazokubalika.
4-Ajaaliwe msaidizi miogoni mwa Ndugu zake.
5-Ambapo Msaidizi huyo asiwe mtu mwengine yeyote isipokua Harun ambae ni
kaka yake.
6-Ambae nae awe na Uwezo wa Kumuongezea Nguvu juu ya Jukumu lake hilo.
7-Harun awe ni Mshirika wake katika kila kitu kuhusiana na Jambo hilo.
8-Ili wote kwa pamoja wapate kua ni wenye kuwamtukuza Allah Subhanah wa
Ta’ala.

Ambapo anasema Ka'b al Ahbar kua: ‘Nabii Harun Alayh Salam alikua ni mtu
aliekua na uwezo mkubwa sana wa kuzungumza kwa ufasaha, na alipokua
akizungumza basi alikua akizungumza kwa malengo na makusudio ya kutumia
Ilm aliyokua nayo katika kujua kwake Lugha, na alikua ni mrefu zaidi ya Nabii
Musa na ni mwenye ndugu yaani kidoto cheusi kwenye ncha ya ulimi wake.
Ambapo Nabii Musa alikua si mtu mwenye rangi ya ngozi yenye Weupe bali
yenye kiza, nywele zilizojikunja na alikua mrefu na alikua na ulimi uliokua
mzito wa lafdhi katika kusema kwake na alikua na kidoto pia kwenye ncha ya
ulimi wake’

Na bila ya shaka Nabii Musa alikua ana khofu kwa sababu alikua anajua kua
kutokana na yeye kua ni mwenye kosa la kuua mmoja kati ya watu wa Misri basi
huenda watu wa Misri wakimuona tu watamkamata na hapo hapo kumchukulia
hatua ya kumpa adhabu ya kifo na kumuua kabla ya hata yeye kufanikisha jukumu
la kufikisha ujumbe aliopewa na Mola wake kwa watu hao, hivyo akasema:

ِ ‫ﻮن۞ وأ‬ ِ ُ‫ﺎف أَن ﻳـ ْﻘﺘُـﻠ‬ ِ ‫ب إِِﱏ ﻗَـﺘَـ ْﻠﺖ‬


‫َﺧﻰ َﻫ ُﺎرو ُن ُﻫ َﻮ‬ َ َ ُ ‫َﺧ‬
َ ‫ﺄ‬َ‫ﻓ‬ ‫ﺎ‬
ً ‫ﺴ‬ ‫ﻔ‬
ْ ‫ـ‬
َ ‫ﻧ‬ ‫ﻢ‬ ‫ﻬ‬
ْ ُ
ُ ‫ـ‬ ‫ﻨ‬
ْ ‫ﻣ‬ ّ ِّ ‫ﺎل َر‬
َ َ‫﴿ﻗ‬
ِ ‫ﺎف أَن ﻳ َﻜ ِّﺬﺑ‬ ۤ ِ ‫أَﻓْﺼﺢ ِﻣ ِﲎ ﻟِﺴﺎ�ً ﻓَﺄَرِﺳ ْﻠﻪ ﻣﻌِﻰ ِردءاً ﻳ‬
َ َ‫ﻮن۞ ﻗ‬
‫ﺎل‬ ُ ُ ُ ‫َﺧ‬ َ ‫ﺼ ّﺪﻗُِﲎ إِِّﱐ أ‬ َُ ْ َ َُ ْ َ ّ َُ
‫ﺼﻠُﻮ َن إِﻟَْﻴ ُﻜ َﻤﺎ ِﺂﺑ َ�ﺗِﻨَﺂ أَﻧﺘُ َﻤﺎ‬
ِ ‫ﻴﻚ وَْﳒﻌﻞ ﻟَ ُﻜﻤﺎ ﺳ ْﻠﻄَﺎ�ً ﻓَﻼَ ﻳ‬
َ ُ َ ُ َ َ َ ‫ﻀ َﺪ َك ِﺄﺑَﺧ‬
ِ
ُ ‫َﺳﻨَ ُﺸ ﱡﺪ َﻋ‬
﴾‫وَﻣ ِﻦ ٱﺗﱠـﺒَـ َﻌ ُﻜﻤﺎ ٱﻟْﻐَﺎﻟِﺒُﻮ َن‬
َ َ
580

Qala rabbi innee qataltu minhum nafsan faakhafu an yaqtulooni; Waakhee


haroonu huwa afsahu minnee lisanan faarsilhu maAAiya rid-an yusaddiqunee
innee akhafu an yukadhdhibooni; Qala sanashuddu AAadudaka bi-akheeka
wanajAAalu lakuma sultanan fala yasiloona ilaykuma bi-ayatina antuma wamani
ittabaAAakuma alghaliboona (Surat Al Qasas 28:33-35)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa) Ewe Mola wangu Hakika mimi nimeua Mtu miongoni
mwao, na nna khofu kua huenda wakaniua. Na kaka yangu Harun kwa hakika yeye
ni mwenye ufasaha zaidi yangu kiulimi hivyo Mtume pamoja nami kuniunga mkono
kwani kwa hakika na khofu kua watanikanusha. Allah Subhanah wa Ta’ala akasema:
Tutakuunga mkono kupitia kwa kaka yako, na tutakupeni nyote uwezo na hivyo
hawatokua na uwezo wa kukudhuruni kutokana na vithibitisho vyetu. Hivyo nyinyi
wawili pamoja na watakaokufuateni mtakua ni washindi.

Hivyo baada ya Nabii Musa kuanisha mahitaji yake yatakayorahisha utekelezaji wa


majukumu yake basi Allah Subhanah wa Taala akamkubalia Nabii Musa na kisha
akaanza kumuainishia namna alivyomsimamia hapo kabla tangu alipotaka kuzaliwa
mpaka hapo alipofikia katika hali aliyokua nayo? Na hivyo basi kumthibitishia kua bila
ya shaka yuko pamoja nae kila wakati na katika kila kitu kwa kumwambia kua:

‫ُﺧَﺮ ٰى۞ إِ ْذ أ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إِ َ ٰﱃ‬ ِ َ َ‫﴿ﻗ‬


ْ ‫ﻚ َﻣﱠﺮةً أ‬ َ ‫ﻮﺳ ٰﻰ۞ َوﻟََﻘ ْﺪ َﻣﻨَـﻨﱠﺎ َﻋﻠَْﻴ‬ َ ُ‫ﻚ ٰﳝ‬
َ َ‫ﻴﺖ ُﺳ ْﺆﻟ‬ َ ‫ﺎل ﻗَ ْﺪ أُوﺗ‬
‫ت ﻓَﭑﻗْ ِﺬﻓِ ِﻴﻪ‬ ِ ‫ﻚ ﻣﺎ ﻳﻮﺣﻰ۞أ َِن ٱﻗْ ِﺬﻓِ ِﻴﻪ ِﰱ ٱﻟﺘﱠﺎﺑﻮ‬
ُ
ِ
ٰ َ ُ َ َ ‫ﻮﺣ ٰﻰ۞إِ ْذ أ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إِ َ ٰﱃ أ ُّﻣ‬
َ ُ‫ﻚ َﻣﺎ ﻳ‬ َ ‫أ ُِّﻣ‬
‫ﻚ َﳏَﺒﱠﺔً ِّﻣ ِّﲎ‬ ِ ِِ
ُ ‫ِﰱ ٱﻟْﻴَِّﻢ ﻓَـ ْﻠﻴُـ ْﻠﻘﻪ ٱﻟْﻴَ ﱡﻢ ﺑِﭑﻟ ﱠﺴﺎﺣ ِﻞ َ�ْ ُﺧ ْﺬﻩُ َﻋ ُﺪ ﱞو ِّﱃ َو َﻋ ُﺪ ﱞو ﻟﱠﻪُ َوأَﻟْ َﻘْﻴ‬
َ ‫ﺖ َﻋﻠَْﻴ‬
﴾‫ﺼﻨَ َﻊ َﻋﻠَ ٰﻰ َﻋْﻴ ِ ۤﲏ‬ ِ
ْ ُ‫َوﻟﺘ‬
Qala qad ooteeta su/laka ya Moosa, Walaqad mananna AAalayka marratan
okhra, Idh awhayna ila ommika ma yooha, Ani iqdhifeehi fee alttabooti faiqdhifeehi
fee alyammi falyulqihi alyammu bialssahili ya/khuthhu AAaduwwun lee
waAAaduwwun lahu waalqaytu AAalayka mahabbatan minnee walitusnaAAa
AAala AAaynee (Surat Al Ta-Ha 20:36-39)

Tafsir: Tukasema: ‘Kwa Hakika Umepewa Uliyoomba ewe Musa’, Na kwa Kwa hakika
tunakupendelea tena kwa mara ya pili, Tulipomshushia Wahyi Mama yako juu yako
juu ya tuliyomshushia, tukamwambia Mtie ndani ya Tabut na kisha kitie ndani ya Mto,
kisha Mto utakichukua mpaka ukingoni, na kuna adui yangu na adui yake. Na
581

nitakupamba kwa mapenzi kutoka kwangu, ili uwe ni mwenye kulelewa kutoka chini
ya uangalizi wangu.

Ama kuhusiana na maneno ya aya hizi basi Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakalimin
Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Hivi kwa nini Allah Subhanah wa Ta’ala akasema
hapa kuhusiana na kumfadhilisha tena Nabii Musa, yaani kwanini akukumbusha
juu ya hilo? Jibu lake ni kua Kwanza kuhusiana na Neema za Allah Suhbahanh wa
Ta’ala kwa waja wake, ili zisiwe ni zenye kuchukuliwa kua hazina thamani juu
yake. Pili ni kua Nabii Musa anawekewa wazi kua hakua ni mwenye kufanya jambo
lolote lile mpaka akawa ni mwenye kulipwa fadhila hizo, bali zinatokana na kua ni
Rehma kutoka kwa Mola wake. ’

Ambapo anasema Imam Abu Muhammad Sahl Abdallah Al Tustari kua: ‘Allah
Subhanah wa Ta’ala amemuwekea wazi Nabii Musa kuhusiana na namna
anavyomjua Nabii Musa kabla ya kumpa kwake majukumu yeyote. Amemjaalia
juu yake Mapenzi yake ndani ya moyo wa mja wake huyo, hivyo hizi ni miongoni
mwa Nyoyo ambazo tayari zimeshatunukiwa zawadi kabla ya kufanya jambo lolote,
na kuadhibiwa kabla ya kua na rai ya tukio husika, kama vile mtu ambavyo hua ni
mwenye kuhisi furaha ndani ya Moyo wake bila ya kujua sababu ya furaha hio, au
kuhisi huzuni ndani ya nyeoyo yake bila ya kujua sababu ya huzuni hio’

‘Kwani dalili ya mapenzi hua ni kumbatio la utiifu na la kufuta hisia za hitajio la


kua na yeyote yule isipokua Allah Subhanah wa Ta’ala, kwani Allah Subhanah wa
Ta’ala alimuuliza Nabii Musa: ‘Hivi jee unajua kwa nini mie nnakumwagia mapenzi
yangu juu yako’Nabii Musa akajibu kwa kusema: ‘La’. Allah Subhanah wa Ta’ala
akajibu: ‘Kwa sababu ulitafuta ridhaa yangu. Hivyo ewe Musa daima niweke
kwenye akili yako, na kamwe usinisahau katika hali yeyote, kua na hima katika
kunikumbuka kwako, kwani kwa hakika mimi nitakujaalia njia ya muongozo
wako’’

Na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akawambia Nabii Musa kwa kusema:

ۤ ِ
َ ‫ﺎك إِ َ ٰﱃ أ ُِّﻣ‬
‫ﻚ َﻛ ْﻰ‬ َ َ‫ﻮل َﻫ ْﻞ أ َُدﻟﱡ ُﻜ ْﻢ َﻋﻠَ ٰﻰ َﻣﻦ ﻳَ ْﻜ ُﻔﻠُﻪُ ﻓَـَﺮ َﺟ ْﻌﻨ‬
ُ ‫ﻚ ﻓَـﺘَـ ُﻘ‬َ ُ‫ُﺧﺘ‬ ْ ‫﴿إِ ْذ ﲤَْﺸﻲ أ‬
‫ﲔ‬ ِ ِ ْ‫ﱠﺎك ﻓُـﺘُﻮ�ً ﻓَـﻠَﺒِﺜ‬ َ ‫ﺎك ِﻣ َﻦ ٱﻟْﻐَِّﻢ َوﻓَـﺘَـﻨ‬
َ ‫ﺖ ﺳﻨ‬ َ َ َ‫ﺖ ﻧَـ ْﻔﺴﺎً ﻓَـﻨَ ﱠﺠْﻴـﻨ‬
َ ْ‫ﺗَـ َﻘﱠﺮ َﻋْﻴـﻨُﻬﺎ َوﻻَ َْﲢَﺰ َن َوﻗَـﺘَـﻠ‬
582

‫َﻧﺖ‬
‫أ‬ ‫ﺐ‬‫ﻫ‬‫ذ‬ْ ‫ٱ‬ ۞ ‫ﻲ‬ ‫ﺴ‬ِ ‫ﻚ ﻟِﻨَـ ْﻔ‬ ‫ﺘ‬ ‫ﻌ‬ ‫ـ‬ ‫ﻨ‬َ‫ﻄ‬ ‫ٱﺻ‬ ‫و‬ ۞‫ﻰ‬ ‫ﻮﺳ‬ ‫ﳝ‬ٰ ٍ
‫ر‬ ‫ﺪ‬
َ ‫ﻗ‬
َ ‫ﻰ‬ ‫ﻠ‬
َ ‫ﻋ‬ ‫ﺖ‬‫ﺌ‬
ْ ِ ‫ِ ۤﰲ أَﻫ ِﻞ ﻣ ْﺪﻳﻦ ﰒُﱠ‬
‫ﺟ‬
َ ْ َ َ ُ َ
ْ ْ َ َ ٰ ُ ٰ َ َ ََ َ ْ
﴾‫ﻮك ِﺂﺑ َ�ﺗِﻰ وﻻَ ﺗَﻨِﻴَﺎ ِﰱ ِذ ْﻛ ِﺮي ۞ ٱ ْذ َﻫﺒَﺂ إِ َ ٰﱃ ﻓِﺮ َﻋﻮ َن إِﻧﱠﻪُ ﻃَﻐَ ٰﻰ‬
َ ‫َﺧ‬
ُ ‫َوأ‬
ْ ْ َ
Idh tamshee okhtuka fataqoolu hal adullukum AAala man yakfuluhu
farajaAAnaka ila ommika kay taqarra AAaynuha wala tahzana waqatalta nafsan
fanajjaynaka mina alghammi wafatannaka futoonan falabithta sineena fee ahli
madyana thumma ji/ta AAala qadarin ya moosa, WaistanaAAtuka linafsee, Idhhab
anta waakhooka bi-ayatee wala taniya fee dhikree, Idhhaba ila firAAawna innahu
tagha(Surat Al Ta-Ha 20:40-43)

Tafsir: Wakati Dada yako alipoenda na kusema: ‘Hivi jee nikuonesheni atakaeweza
kumnyonyesha?’ hivyo tukakurudisha kwa Mama yako, ili apate utulivu wa macho
yake na asiwe na huzuni, na kisha ukamuua Mtu. Lakini tukakuokoa wewe kutokana
na tatizo hilo kubwa na tukakupa mtihani mkubwa. Kisha ukakaa kwa miaka kadhaa
pamoja na watu wa mji wa Madyan. Na kisha ukaja hapa kulingana na mda
niliokukadiria, Ewe Musa. Na nimekuchagua kwa ajili yangu. Hivyo nenda wewe na
kaka yako mkiwa na aya zangu na wala msiwe na uregevu katika kunikumbuka.
Nendeni kwa Firawn kwani kwa hakika amevuka mipaka.

Yaani Allah Subhanah wa Ta’ala anamuelezea hata kwa hatu maisha aliyoyapitia Nabii
Musa na kumuwekea wazi kua, alikua akimsimamia na kumchunga na alikua akimpa
mitihani Nabii Musa ili awe ni mwenye kumkumbuka Mola wake, ili ajihisi ajue kua ni
vigumu kua ni mwenye kujitegemea peke yake bila ya kua ni mwenye kumtegemea Mola
wake, na hivyo ndivyo hali ilivyokua kwa waliotangulia kabla yetu na kwetu sisi na kwa
watakaokuja baada yetu pia, ili tunapewa Mitihani na Mola wetu ili tuwe wanyenyekevu
juu ya Muumba wetu ambae si mwengine isipokua ni Allah Subhanah wa Ta’ala.

Hapa tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala amemwambia Nabii Musa kua
amemchagua kwa ajili yake, na hivyo kumuewekea wazi kua na yeye ni Jukumu lake
kujitolea si kwa ajili ya chochote kile au si kwa ajili ya yeyote yule isipokua kwa ajili ya
Mola wake, na kisha akatilia mkazo kwa kumwambia Nabii Musa kua: ‘Na kamwe
msiwe na uregevu au dharau katika kunikumbuka’ yaani wasiwe ni wenye
kumkumbuka Allah Subhanah wa Ta’ala kwa mda mchache bali wawe
wanamkummbuka kila wakati na wala wasiwe ni wenye kumkumbuka kwa ulimi wao tu,
huku wakiwa hawamkumbuki ndani ya Nyoyo zao, kwani watakapomkumbuka mara
kwa mara kwa Nyoyo zao na Ndimi zao basi ndivyo watakapokumbuka jukumu lao juu
yake, na ujumbe wake.
583

Hii pia ni kutokana na Hikma ya kutilia mkazo pia ujumbe wanaopewa na namna
wanavyotakiwa kuufikisha ujumbe huo, kwani baada ya aya hio basi Allah Subhanah wa
Ta’ala anamuusia Nabii Musa kuhusiana na namna ya kumfikishia Fir’awn ujumbe wake
kwa kumfundisha moja katika adabu za njia za mawasiliano kama tulivyoelezea hapo
kabla katika aina za Kauli kwa kumwambia:

﴾‫﴿ﻓَـ ُﻘﻮﻻَ ﻟَﻪُ ﻗَـﻮﻻً ﻟﱠﻴِّﻨﺎً ﻟﱠ َﻌﻠﱠﻪُ ﻳَـﺘَ َﺬ ﱠﻛﺮ أ َْو َﳜْ َﺸ ٰﻰ‬
ُ ْ
Faqoola lahu qawlan layyinan laAAallahu yatadhakkaru aw yakhsha (Surat Al Ta-
Ha 20:44)

Tafsir: Na zungumzeni nae kwa kauli Laini kwani huenda akakumbuka au akawa na
khofu.

Na kutokana na kua Allah Subhanah wa Ta’ala ni mwenye kujua kila kitu na kumjua
kwa kina kila kiumbe aliemuumba basi alikua anajua kua Fir’awn kamwe hatoweza kua
ni mwenye kuamini kutokana na kibri chake na kuvuka mipaka kwake na ndio maana
katika kumuusia Nabii Musa namna ya kuwasiliana na Fir’awn, akamwambia kua
zungumza nae kwa kauli laini, zenye kulainisha Nyoyo ambazo labda huenda
zikampelekea Fir’awn kuwa ni mwenye kumkumbuka Mola wake na hivyo kua na khofu
nae, na ndio maana hapa Allah Subhanah wa Ta’ala ikawa hakusema kua huenda Fir’awn
ataamini, kwani hatoamini hata iwe vipi.

Ambapo ayah hii pia inatuwekea wazi umuhimu wa wenye kufikisha ujumbe wa Allah
Subhanah wa Ta’ala kua ni wenye kutakiwa kutumia njia zenye busara kwa kutumia
kauli ambazo ni zenye ulaini ndani yake, ili kurahisisha upokewaji wa ujumbe huo na pia
kurahisisha kukubalika kwa ujumbe huo kwa walengwa, na pia kuzungumza kwa Ulaini
na Wazee wetu na pia kwa wale ambao ni watu waliotulea na kutusimamia tangu udogoni
mwetu, kwani kama tulivyoona hapo awali kua Nabii Musa alilelewa na Fir’awn.

Ambapo Imam Abu Muhammad Sahl Abd Allah Al Tustari basi yeye anasema kuhusiana
na ayah ii kua: ‘Allah Sbhanah wa Ta’ala anamwita Nabii Musa kwa kumvisha Joho
ambalo linajulikana kama Joho la Mutaaddibun yaani wenye Adabu na kisha
kumuondolea hali ya Mutahajjimun yaani wenye kua na pupa na haraka, kwa
kumpa fadhila na uwezo alioupata kutoka kwake Allah Subhanah wa Ta’ala’

Ambapo siku moja Imam Al Junaid alikua akiisoma ayah hii isemayo:
584

﴾‫﴿ﻓَـ ُﻘﻮﻻَ ﻟَﻪُ ﻗَـﻮﻻً ﻟﱠﻴِّﻨﺎً ﻟﱠ َﻌﻠﱠﻪُ ﻳَـﺘَ َﺬ ﱠﻛﺮ أ َْو َﳜْ َﺸ ٰﻰ‬
ُ ْ
Faqoola lahu qawlan layyinan laAAallahu yatadhakkaru aw yakhsha (Surat Al Ta-
Ha 20:44)

Tafsir: Na zungumzeni nae kwa kauli Laini kwani huenda akakumbuka au akawa na
khofu.

Na kisha akasema: ‘Ewe Mola wangu! Huu ndio ukarimu wako kwa mtu ambae
ndie aliesema:

﴾‫َﻋﻠَ ٰﻰ‬
ْ ‫﴿ أ ََ�ْ َرﺑﱡ ُﻜ ُﻢ ٱﻷ‬
Ana Rabbukumu al-aAAla (Surat An Naziat 79: 24)

Tafsir: ‘Mimi ndie Mola wenu Mkuu’’

Hivi Jee utakuaje Ukarimu wako juu ya yule Mtu amabe ndie aliesema: ‘Ana
Aa’abduk wa anta Rabbi - Mimi ni Mja wako na Wewe ndie Mola wangu’. Huu ndio
Ukarimu wako kwa yule ambae ndie aliekua akijitukuza na kujipandisha Darja na
kusema: ‘Ana Rabbukumu al-aAAla’ Jee hali utakuaje Ukarimu wako kwa yule
ambae ni mwenye kusema ‘Subhana Rabbi al aAa'la – Ametukuka Mola wangu
Mtukufu’’

Hivyo hapa Allah Subhanah wa Ta’ala anampelekea Ujumbe Fir’awn ambao utamfikia
kwa si kwa njia ya vitisho bali kwa njia ya ulani na wepesi kufahamika ili baadae asije
akapata kisingizio cha kua hakufikiwa na Ujumbe kutoka kwa Mola wake na wala asije
akasema kua hakuonywa hapo kabla ya kuhusiana na kupotea kwake kabla ya
kuangamizwa kwake, kwani tayari alishamtumia Mtume kwa ajili ya kumuonya na si
mmoja bali Mitume wawili sambamba kama zinavyosema Aya:

﴾ً‫َﺧﺎﻩُ َﻫﺎرو َن وِزﻳﺮا‬ ِ


َ ُ َ ‫ﺎب َو َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ َﻣ َﻌﻪُ أ‬ َ ‫﴿ َوﻟََﻘ ْﺪ آﺗَـْﻴـﻨَﺎ ُﻣ‬
َ َ‫ﻮﺳﻰ ٱﻟْﻜﺘ‬
Walaqad atayna moosa alkitaba wajaAAalna maAAahu akhahu haroona
wazeeran(Surat Al Qasas 28:33-35)
585

Tafsir: Na kwa hakika tumempa Musa Kitabu na tukamjaalia pamoja nae Kaka yake
Harun kua Msaidizi wake.

Na huu ni upekee ambao hajawahi kupendelewa Mtu mwengine yeyeote asiekua ni


miongoni mwa Watu wa Bani Israil, kwani Fir’awn ndie mtu pekee ambae alitumiwa
Mitume wawili sambamba, tukiondoa Watu wa Bani Israil ambao wao walipata nafasi
kama hii kwa kupewa Mitume miwili hawa sambamba na Fir’awn na wakapewa Mitume
zaidi ya wawili pale walipotumiwa Nabii Zakarriya, Nabii Yayha na Nabii Isa Ibn
Maryam sambamba kama tutakavyoona katika kisa cha Nabii Isa baada ya kumaliza kisa
hiki cha Nabii Musa.

Hivyo baada ya kupokea ujumbe huo kutoka kwa Mola wake basi Nabii Musa alirudi
katika familia yake, na kumuelezea Mke wake na watoto wake wawili waliokua wakiitwa
Gershom na Eliezer, na kisha akawaambia wao warudi katika Mji wa Madyan wakiwa
wamefuatana na mmoja kati ya misafara iliyokua ikielekea huko ili yeye aendelee na
safari yake kwa ajili ya kutekeleza jukumu alilopewa na Mola wake, familia yake hii
ilikaa katika mji wa Madyan hadi pale ulipowadiwa wakati wa kuelekea katika mji wa
Jerusalem ulipowadia baada ya kugharikishwa Fir’awn na jeshi lake.

Nabii Musa akaondoka kuelekea Misri huku akiwa hajui anaelekea wapi, akiwa hana
chochote yaani kama alivyokua katika safari yake ya kwanza kutoka mji wa Misri
kuelekea katika Mji wa Madyan alipokua akimkimbia Fir’awn isipokua safari hii alikua
akirudi kwa kumkimbilia Fir’awn ili kumuonya kutokana na kuvuka mipaka kwake, huku
Nabii Musa akiwa na silaha yenye upekee ambayo ni fimbo yake mkononi mwake, na
muongozo wa Mola wake.

Huku Allah Subhanah wa Ta’ala akimshushia Wahy Nabii Harun kumjuulisha kuhusiana
na kuteuliwa kwake kua ni Nabii na Mtume Waziri wa Nabii Musa, hivyo anatakiwa
kukutana na Nabii Musa katika mwezi Mosi Dhul Hijja katika mwambao wa Mto Nile.
Hii ilikua ni siku ya Jumatatu.

Walipokutana katika usiku wa kuamkia Mwezi Mosi Dhul Hijja basi kwanza
hawakuweza kujuana isipokua Nabii Musa alikua ni mwenye kuhisi tu kua huyu ndie
Harun. Kwani Nabii Musa alikua amevaa nguo za kuchungia wanyama, na hivyo alidhani
kua ni miongoni wa wachungaji wanyama, Hivyo Nabii Harun akamsalimia Mchungaji
huyo na kisha akamuuliza : ‘Jee wewe ni nani?’ Nabii Musa akajibu: ‘Mimi ni Mtumwa
naelekea kwa Mola wangu.’ Nabii Harun akauliza: ‘Bwana wako ndio Nani?’ Nabii
Musa akajibu: ‘Mola alieumba Ulimwengu wote na kila kitu kilichomo ndani yake’

Nabii Harun akauliza: ‘Jee anaitwa Nani?’ Nabii Musa akajibu: ‘Anaitwa Allah
Subhanan wa Ta’ala’, baada ya kusikia jibu hilo basi Nabii Harun akaanguka na
kuzimia, kwani hakutegemea kua huyo aliemuona atakua ni ndugu yake aliepoteana nae
586

miaka 10 iliyopita. Ambapo kwa upande wa Nabii Musa nae akashtuka alipomuona
Harun ameanguka na kuzimia kwani alidhani kua kaka yake hamuamini Mungu wake.
Lakini Nabii Harun alipoamka basi akauliza: ‘Hebu nielezee kuhusiana na Mungu
wako’ Nabii Musa akasema: ‘Mola wangu ni yule ambae Hakuna Mola isipokua
yeye. ’ Nabii Harun akajua kua huyu anaezugumza nae si mwengine isipokua ni Ndugu
yake, yaani Nabii Musa.

Hivyo wakajuana na kukumbatiana kutokana na kutoonana kwa mda mrefu sana, kisha
wakaanza kujadiliana kuhusiana na jukumu liliopo mbele yao, huku Nabii Harun akiwa
na wasi wasi kutokana uzito wa jukumu lao hilo na nguvu na uwezo wa wanaetakiwa
kukabiliana nae yaani Fir’awn na Jeshi lake, na hii pia ni kwa sababu Fir’awan alikua na
sifa ya kua ni Mtu mwenye sifa ya kuitwa kua ni Mzee wa Al Awtad ambalo ni neno
linalomaanisha maana tofauti. Kwani aya zinavyosema kua:

﴾‫﴿وﻓِﺮ َﻋﻮ َن ِذى ٱﻷ َْو َﺎﺗ ِد‬


ْ َْ
WafirAAawna dhee al-awtadi (Surat Al Fajr 89:10)

Tafsir: Na Fir’awn mwenye kupigilia Vigingi.

Ambapo neno Al Awtad maana yake hua ni Kupigilia kitu kwa kutumia nguvu hadi kitu
hicho kizame ndani ya kitu chengine, Kupigilia Kijiti, Nguzo au Kigingi ndani ya Ardhi,
Kuweka kitu au kukisimamisha ndani ya Kitu kiasi ya kua kitu hicho hua ni vigumu
kutoka tena nje ya kitu hicho, Kuwekea nguzo Kitu ili kitu hicho kisimame kwa
umadhubuti kama vile linavyopigiliwa hema, au majiti ya kufungia kamba ya kuanikia
nguo au kama vile Ardhi ilivyosimamisha na kudidimiziwa Milima ndani yake na Allah
Subhanah wa Ta’ala kwa ajili ya kuifanya iwe madhubuti na yenye kutulia kama
inavyosema Qur’an:

َ َ‫ٱﳉِﺒ‬
﴾ ً‫ﺎل أ َْو َﺎﺗدا‬ ْ ‫ض ِﻣ َﻬﺎداً ۞ َو‬
َ ‫﴿أََﱂْ َْﳒ َﻌ ِﻞ ٱﻷ َْر‬
Alam najAAali al-arda mihadan; Waaljibala awtadan (Surat An Nabaa 78:6-7)

Tafsir: Na tukajaalia Ardhi kua ni iliyotandikwa. Na Milima kua ni Awatadan (ndio


mihimili yake, au nguzo zake)

Kwani tunapoiangalia Milima basi tunaona kua kina cha urefu wake kuelekea chini ya
Ardhi hua ni mara mbili ya urefu wake kuelekea juu ardhini, na hii ni kwa sababu ya
kuifanya Ardhi iwe ni yenye kutulia kutokana na kupigiliwa na mashina ya Milima ndani
yake.
587

Ama kwa upande mwengine basi neno Awtad hua pia ni lenye kumaanisha Ukubwa wa
Kijeshi na Kisilaha kwani ukubwa wa Jeshi na Silaha hua ni wenye uwezo wa kulazimisha
chochote kile kitakiwacho hata kama itakua si kitu cha halali, yaani ambapo kwa mtizamo
huu basi tuaona kua Fir’awn alikua ni mwenye Jeshi kubwa sana kiasi ya kua amekua ni
mwenye kutumia vibaya Mamlaka yake hayo dhidi ya watu wa Bani Israil.

Ambapo tuaporudi kwenye upande wa mwanzo yaani upande wa kua neno Awtad
linamaanisha kua ni Vigingi basi tunaona kua Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al
Razi anasema kua amesema Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu kua: ‘Fir’awn
alikua akiwafunga watu kwenye vigingi vinne (vigingi viwili kwenye mikono miwili
na vigingi viwili kwenye miguu miwili) kwa ajili ya kuwaadhibu na kisha huwawekea
Jiwe juu yao mpaka kufa kwao’

Na Imam Thabit Al Bunani basi yeye anasema kua: ‘Firawn aliitwa hivi kwa sababu
aliifunga mikono na miguu ya Mke wake aliemuamini Allah Subhanah wa Ta’ala
kwenye vigingi ardhini na kumuwekea Jiwe zito juu yake mpaka akafariki’

Ambapo kwa upande wa Jarrah Allah Imam Al Zamakhshari basi yeye anasema kua:
‘Fir’awn alipewa Jina hili kwa sababu alimtesa Mke wake na Mtoto wake wa kike
aitwae Nashita.’

Na pia kwa upande wa Said Ibn Jubayr na Mujahid Ibn Sulayman basi wao wanasema
kua: ‘Awtad hizi zilikua ni zile ambazo Fir’awn alikua akizipigilia chini ardhini
anapopiga kambi kwa ajili ya kuangalia michezo na mashindano mbali mbali.’

Hivyo basi Nabii Musa na Nabii Harun wakasema:

ُ َ‫﴿ﻗَﺎﻻَ َرﺑـﱠﻨَﺂ إِﻧـﱠﻨَﺎ َﳔ‬


﴾‫ﺎف أَن ﻳَـ ْﻔﺮ َط َﻋﻠَْﻴـﻨَﺂ أ َْو أَن ﻳَﻄْﻐَﻰ‬
ُ
Qala rabbana innana nakhafu an yafruta AAalayna aw an yatgha(Surat Ta-Ha
20:45)

Tafsir: Wakasema: ‘Ewe Mola wetu! kwa hakika sisi tunakhofu kua huenda
akaharakisha kutuadhibu au atavuka mipaka dhidi yetu’.

Yaani kama tulivyosema hapo kabla kua wanaogopa kua huenda Fir’awn akazidi Kibri
chake mara tu baada ya kuwaona pamoja na Nabii Musa akawachukulia hatua hata kabla
ya kuwasikiliza, hivyo ikabidi Allah Subhanah wa Ta’ala awatulize Mitume wake wawili
hawa kwa kuwabainishia kua hakika yeye yuko karibu nao tena sana kwani anawaona na
anawasikia pia.
588

UKARIBU WA ALLAH SUBHANAH WA TA’ALA KWA NABII MUSA


NABII HARUN NA VIUMBE WAKE KWA UJUMLA.


Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akawaambia na kuwathibitishia kuwatoa khofu
Manabii wake hao wawili kwa kusema kua:

﴾‫َﲰَ ُﻊ وأَر ٰى‬ ِ َ َ‫﴿ ﻗ‬


َ َ ْ ‫ﺎل ﻻَ َﲣَﺎﻓَﺂ إﻧﱠِﲎ َﻣ َﻌ ُﻜ َﻤﺂ أ‬
Qala la takhafa innanee maAAakuma asmaAAu waara, (Surat Ta-Ha 20:46)

Tafsir: Yeye (Allah Subhanah wa Ta’ala) akasema Msiwe na khofu kwani kwa hakika
mimi niko pamoja nanyi nakusikieni na nakuoneni.

Yaani Allah Subhanah wa Ta’ala yuko pamoja nao katika kila hatua wanayoichukua
katika maisha yao na katika jambo lao hili alilowaamrisha kulifanya na yeye analijua
uizto wake vizuri zaid kwani yeye Allah Subhanah wa Ta’ala yupo karibu sana na kila
alichokiumba kama anavyothibitisha hivyo pale aliposema kuhusiana na Kiumbe Ibn
Adam ambae ndie Khalifa wake hapa ulimwenguni, Kiumbe mwenye ubora zaidi kuliko
Viumbe wote, Kiumbe mwenye akili kuliko viumbe wote kua:

‫ب إِﻟَْﻴ ِﻪ ِﻣ ْﻦ َﺣْﺒ ِﻞ‬ ِ ‫﴿وﻟََﻘ ْﺪ ﺧﻠَ ْﻘﻨَﺎ ٱ ِﻹﻧﺴﺎ َن وﻧَـﻌﻠَﻢ ﻣﺎ ﺗُـﻮﺳ ِﻮ‬
ُ ‫س ﺑِﻪ ﻧَـ ْﻔ ُﺴﻪُ َوَْﳓ ُﻦ أَﻗْـَﺮ‬
ُ َْ َُ ْ َ َ َ َ
ِ ‫ٱﻟْﻮِر‬
﴾‫ﻳﺪ‬
َ
Walaqad khalaqna al-insana wanaAAlamu ma tuwaswisu bihi nafsuhu wanahnu
aqrabu ilayhi min habli alwareedi (Surat Qaf 50:16)

Tafsir: Na kwa hakika sisi tumemuumba Mtu, na tunajua kile kinachomnong’oneza


kwenye nafsi yake. Nasi tupo karibu nae kuliko Mshipa wake mkuu wa damu.

Aya hii imetumia neno Habli ambalo hua ni lenye kutokana na neno Habala ambalo hua
ni lenye kumaanisha Kufunga, Kukamata, Kutega Mtego. Ambapo neno Habli hua
linamanisha Kufunga kwa makubaliano, Kamba, Kusitisha kwa Ghafla, Kuunganisha,
Na pia humaanisha Mishipa Miwili Mikuu ya Damu iliyopita ndani ya Shingo ya Ibn
Adam kutokea Moyoni.
589

Na pia ikatumia neno Wariid ambalo ni lenye kutokana na neno Warada lenye
kumaanisha Kuwasili, Kukaribia, Kufikia, Kuingia Ndani Yake, Kua ndani yake na pia
humaanisha Kuchota Maji.

Hili ni neno ambalo limetumika mara 7 tu katika Qur’an ambapo mmoja kati ya mfano
wa matumizi yake ni pale aliposema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qur’an:

ِ ‫ﻚ ﺣْﺘﻤﺎً ﱠﻣ ْﻘ‬
﴾ً‫ﻀﻴّﺎ‬ ِ ِ ِ ِ
َ َ ّ‫﴿ َوإن ّﻣﻨ ُﻜ ْﻢ إﻻﱠ َوا ِرُد َﻫﺎ َﻛﺎ َن َﻋﻠَ ٰﻰ َرﺑ‬
Wa-in minkum illa wariduha kana AAala rabbika hatman maqdhiyyan (Surat
Maryam 19:71)

Tafsir: Na Hakuna hata mmoja miongoni mwenu ila ataukaribia (Moto wa Jahanama)
kwani hili kwa Mola wako ni hatma ambayo ni lazima itimizwe.

Na ingawa hii ni aya ambayo inasema kua kila mmoja miogoni mwetu atauingia iwe
Muumini au Kafiri, kua Ataufikia, Atawasili, au Ataukaribia Moto wa Jahannam kwani
hili jambo ambalo tayari limeshahitimishwa kua litutokee mbele ya Allah Subhanah wa
Ta’ala katika siku ya Malipo na hivyo kua ni jambo la kushangaza sana kwa baadhi ya
watu miongoni mwetu kwani wanajua kua Allah Subhanah wa Ta’ala ameahidi mara
kadhaa kua Watakaofuzu miongoni mwa waja wake basi malipo yao yatakua ni Pepo,
halafu ayah inasema kua hakuna hata mmoja miongoni mwetu isipokua ataungia Moto
wa Jahanam. Hivyo basi imekuaje?

Hivyo basi anasema Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu kua: ‘Neno hili Wariduha
halimaanishi kua ni kungia Motoni, bali hua linamaanisha kupita, kwa kuvuka juu
yake kwa kutumia Sirat, ambapo Sirat hua ni Daraja lililopita juu ya Moto wa
Jahannam. Hili ni daraja ambalo Walioamini Allah Subhanah wa Ta’ala pekee ndio
watakaopita juu yake, na hivyo kuna baadhi wataweza kupita juu yake na kua ni
waliiokolewa na Moto huo, na kuna wengine watashindwa na hivyo watakua ni
wenye kuanguka ndani ya Moto wa Jahannam.

Ama kuhusiana na Wasiomuamini Allah Subhanah wa Ta’aa basi hawatopita


kwenye Sirat kwani wao watakua ni moja kwa moja ni wenye kuuingia Moto huo
na hivyo kua ni kuni za Moto huo.’

Ambapo tunapozungumzia kuhusiana na Sirat basi Waarabu wanamaanisha kua ni njia


yenye vigezo vifuatavyo:

1- Njia iliyonyooka Sawia.


590

2- Njia inayoelekea katika sehemu maalumu iliyokusudiwa kuelekea


3- Njia hii hua si ndefu bali hua ni fupi.
4- Njia iliyokua pana kwa ajili ya wapiti njia husika.
5- Nji iliyokua iko wazi kiasi ya kua mpita njia husika hua anaona kilichopo
mwisho wa njia hio.

Na amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Sirat hua ni daraja ambalo
ni lenye kutleza na kua na miba pembeni yake, ambapo baadhi ya Waumini
watapita juu ayake kwa kasi kubwa sana kama kufumba na kufumbua. Wengine
watapita kwa kasi kama Radi, wengine kama kwa kasi ya Upepo, wengine kama
kwa kasi ya Mpanda Farasi, wengine watakua salama na hawatodhurika hata
kidogo na wengine watachunika, na kuna wengine wataangukia ndani ya Moto wa
Jahannam. Mtu wa mwisho atavuka daraja kwa kuburuzwa’(Sahih Imam Bukhari)

Aya hii pia inafafanuliwa na aya inayofuata baada yake ambapo aya zote mbili kwa
pamoja zimekaa katika mpangilio ufuatao:

ْ‫ﻳﻦ ٱﺗﱠـ َﻘﻮا‬ ِ ‫ﻀﻴﺎً۞ ﰒُﱠ ﻧـُﻨ ِﺠﻰ ٱﻟﱠ‬


‫ﺬ‬ ِ ‫ﻚ ﺣْﺘﻤﺎً ﱠﻣ ْﻘ‬ ِ‫﴿وإِن ِّﻣﻨ ُﻜﻢ إِﻻﱠ وا ِرُد َﻫﺎ َﻛﺎ َن َﻋﻠَ ٰﻰ رﺑ‬
َ ّ َ ّ َ َ ّ َ َ ْ َ
﴾ً‫ﲔ ﻓِ َﻴﻬﺎ ِﺟﺜِﻴّﺎ‬ ِِ
َ ‫ﱠوﻧَ َﺬ ُر ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
Wa-in minkum illa wariduha kana AAala rabbika hatman maqdhiyyan; Thumma
nunajjee alladheena ittaqaw wanadharu aldhdhalimeena feeha jithiyyan (Surat
Maryam 19:71-72)

Tafsir: Na Hakuna hata mmoja miongoni mwenu ila ataukaribia (Moto wa Jahanama)
kwani hili kwa Mola wako ni hatma ambayo ni lazima itimizwe. Kisha tutawaokoa
wale ambao ni wenye Taqwa na tutawaacha Madhalimu ndani yake wakiwa ni wenye
kupiga magoti.

Tumalizie mfano wa upitaji wa kwenye Sirat ili tupate kufaham zaidi maana ya neno
Warada, kwa kuangalia mfano wa Imam Ali Al Daqqaq ambae yeye alipofariki basi
mwanafunzi wake alilala na kumuona kwenye ndoto Imam Al Daqqaq ambae alikua
akivuka Daraja la Sirat ambalo lilikua pana sana, hivyo mwanafunzi huyo akamuuliza
Imam Al Daqqaq: ‘Imekuaje? Mbona sisi tunajua kua Sirat ni Daraja ambalo ni
jembamba sana kama unywele na ncha yake kama ya upanga’

Imam Al Daqqaq akajibu: ‘Hakika nyinyi hamjakosea katika kujua kwenu hivyo.
Kwani Sirat hua linategemea na mpitaji juu yake. Yaani kama mtu alikua makini
591

katika kutekeleza maamrisho ya Allah Subhanah wa Ta’ala basi Sirat hua pana kwa
ajili yake, na kama alikua mchovu na hana umakini katika kutekeleza maamrisho
ya Allah Subhanah wa Ta’ala basi Sirat itakua nyembamba sana kwa ajili yake ’

Ambapo kwa Upande wa Muhaqqiq Al Faqih Imam Shihab Ad Din Abu Al Abbas
Ahmad Ibn Muhammad Ibn Ali Ibn Hajar Al Haytami Al Shafii Al Makki basi yeye
amesema kuhusiana na ayah hii kua: ‘Amesema Ibn Sumayyah kua amesema Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: Katika siku ya Malipo kutakua na Mlango
wa kuingilia ambao hakuna mtu yeyote yule Alieamaini au Asieamini ambae
hatopita katika mlango huo na kuingia Motoni, Lakini Moto huo utakua baridi na
Salama kwa walioamini kama vile ambavyo ulivyokua baridi na salama moto wa
Ibrahim.’ Na huo pia ndio mtizamo wa Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Ahmad
Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi.

Na kwa upande mwengine basi pia majibu ya suali hilo linalotokana na ayah hii ya Surat
Maryam 19:71 yanatafafanulika kwa vizuri zaidi kwa kutumia ile aya isemayo:

ِ ‫﴿ِ ﱠ‬
َ ِ‫ٱﳊُ ْﺴ َ ٰﲎ أ ُْوﻟَـٰﺌ‬
﴾‫ﻚ َﻋْﻨـ َﻬﺎ ُﻣْﺒـ َﻌ ُﺪو َن‬ ْ ‫ﺖ َﳍُْﻢ ِّﻣﻨﱠﺎ‬ َ ‫إ ﱠن ٱﻟﺬ‬
ْ ‫ﻳﻦ َﺳﺒَـ َﻘ‬
Inna alladheena sabaqat lahum minna alhusna ola-ika AAanha mubAAadoona
(Surat Al Anbiyah 21:101)

Tafsir: Hakika kwa wale ambao wametanguliwa na Mema kutoka kwetu, basi
watewekwa mbali nao (Moto wa Jahannam).

Yaani ingawa hakuna hata mmoja miongoni mwetu isipokua atakua Wariduha yaani
atauingia ndani yake au ataukaribia Moto wa Jahannam lakini kwa wale ambao
wamejaaliwa kua wasiiuingie moto huo kutokana na Mema yao basi hawatouingia na
hivyo watawekwa mbali na Moto huo.

Hivyo asili ya neno Warada lililotumika katika aya Surat Qaf 50:16 linatuwekea wazi
kua Allah Subhanah wa Ta’ala yupo karibu sana na Viumbe wake kuliko hata namna
viumbe hao walivyokua na ukaribu na miili yao na nafsi zao, Na hii ni bila ya shaka kwa
sababu yote haya yanawekwa wazi na ile aya tukufu kuliko aya zote ambayo ni yenye
kujulikana kama Ayat al Kursiy.


592

UTUKUFU WA AYAT AL KURSIY


Neno Kursiy ni lenye kutokana na neno Karasa ambalo kwa Luha ya Kiarabu hua ni
lenye kumaanisha Kuanzisha Jengo, Kukusanya, Kua na Msingi Imara, Kuegemea,
Kuingia na Kuhifadhi kitu ndani yake, Kua Mkali, Kua na Uwezo, Mamlaka na pia Arshi
au Kiti cha Kifalme. Na hii ndio kama ile maana ambayo imetumiwa na ile aya
inayoelezea kisa cha Nabii Sulayman Ibn Daud Alayhi Salam ambayo inasema:

ِِ
َ �ََ ‫﴿ َوﻟََﻘ ْﺪ ﻓَـﺘَـﻨﱠﺎ ُﺳﻠَْﻴ َﻤﺎ َن َوأَﻟْ َﻘْﻴـﻨَﺎ َﻋﻠَ ٰﻰ ُﻛْﺮﺳﻴِّﻪ َﺟ َﺴﺪاً ﰒُﱠ أ‬
﴾‫ب‬
Walaqad fatanna Sulaymana waalqayna AAala kursiyyihi jasadan thumma anaba
(Surat Sad 38:34).

Tafsir: Na kwa hakika tulimfitinisha Sulayman, na tukaweka kwenye Kiti chake


Kiwiliwili na kisha nae akarudi kwa kutubia (kwa Mola wake).

Neno Karasa ndio lililotoa neno Kursiy ambalo pia hua linamaanisha Ilm na Ufaham na
ndio maana wenye Lugha yao walikua wakimuelezea Mtu aliesoma na kua na Ilm basi
hua ni wenye kusema: Huwa min Ahl Al Kursiy yaani Yeye ni miongoni mwa Watu
ambao walikaa kwenye kiti na kuitafuta na kisha wakawa ni wenye kuipata elimu.

Hivyo amesema Ubay Ibn Ka’ab Radhi Allahu Anhu kua: Aliniuliza Rasul Alah
Salallahu Aalyhi wa Salam: Ewe Abu Mundhir! Jee unajua ni Ipi Aya Adhimu
kuliko zote katika Kitabu cha Allah?’ name nikasema: ‘Allah na Mtume wake ni
wenye kujua zaidi’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema tena: ‘Jee
kulingana na mtizamo wako, unajua ni ipi Aya Adhimu kuliko aya zote za Qur’an?’
nami nikajibu: ‘Ni Allahu la ilaha illa huwa alhayyu alqayyoomu’. Hapo Rasul Allah
Salallahu Aalayhi wa Salam akanipigapiga begani na kusema: ‘Furahia Ilm yako
ewe Abu Mundhir! Kwani mimi nnaapa kwa yule ambae Roho yangu imo ndani ya
mikono yake, kua ina Ulimi na Midomo miwili na inamsabih Allah Subhanah wa
Ta’ala chini ya Arshi yake’(Sahih Muslim).

Ayat ul Kursi imeitwa jina la Ayat al Kursi kwa sababu ndio aya pekee ambayo ndani
yake imetumia neno Kursiy kumaanisha kama Kursiy na pia Kursiy kumaanisha Arshi ya
Allah Subhanah wa Ta’ala na hii ni kulingana na mtizamo wa baadhi ya Wanazuoni ni
kua Kursiy ya Allah Subhanah wa Ta’ala hua pia inamaanisha Arshi ya Allah Subhanah
wa Ta’ala.
593

Kwani neno Arshi ni neno linalotokana na neno Arasha ambalo kwa Lugha ya Kiarabu
hua pia linamaanisha Kiti cha Kifalme, Kujenga, Kusimamisha na pia humaanisha
Mamlaka, kama vile lilivyotumika tena katika Surat An Naml ilipozungumzia tena kisa
cha Nabii Sulayman Ibn Daud pale alipopokea habari kutoka kwa Hud Hud kuhusiana
na Malkia Bilqis kwa kusema:

﴾‫ش َﻋ ِﻈﻴﻢ‬ ٍ ِ ‫ﺪت ٱﻣﺮأًَة ﲤَْﻠِ ُﻜﻬﻢ وأُوﺗِﻴ‬ ِِ﴿


ٌ ٌ ‫ﺖ ﻣﻦ ُﻛ ِّﻞ َﺷ ْﻲء َوَﳍَﺎ َﻋْﺮ‬
ْ َ َ ُْ َ ْ ‫إ ّﱏ َو َﺟ ﱡ‬
Innee wajadtu imraatan tamlikuhum waootiyat min kulli shay-in walaha AAarshun
AAadheemun (Surat An Naml 27:23).

Tafsir: Kwa hakika mimi nimekuta Mwanamke anawatala na amepewa kila kitu
(anachostahki kua nacho Mtawala Mkubwa mwengue Nguvu Ulimwenguni) na Arshi
Tukufu Kubwa sana.

Hapa tunaona kua Imam Abu Al Hasan Ali Ibn Muhammad Ibn Habib Al Mawardi Al
Shafii basi yeye anasema kuhusiana na Kursiy kua: ‘Kuhusiana na Kursiy basi kuna
mitizamo miwili juuu yake ambapo mtizamo wa kwanza ni ule usemao kua, ni kitu
kilichoumbwa na Allah Subhanah wa Ta’ala, na mtizamo wa pili ni miongoni mwa
sifa za Allah Subhhanah wa Ta’ala ambapo kwa wale wasemao kua Kursiy ni
miongoni mwa sifa za Allah Subhanah wa Ta’ala basi wao wametaitafsiri katika hali
zifuatazo:’

1-Kua ni Ilm ya Allah Subhanah wa Ta’ala.


2-Kua ni Uwezo wa Allah Subhanah wa Ta’ala.
3-Kua ni Mamlaka ya Allah Subhanah wa Ta’ala.
4-Kua ni Makadirio ya Allah Subhanah wa Ta’ala.

Ambapo kwa wale wanaosema kua Kursiy ni kitu kilichoumbwa na Allah Subhanah wa
Ta’ala basi hua inamaanisha mambo matatu yafuatayo:

1-Kua ni Arshi yenyewe.


2-Ni Kiti cha Chini na wala si Arshi yenyewe.
3-Ni Kiti ambacho chini yake kuna Maji.

Na hivyo basi kwa upande wa Imam Ad Dahhaq Ibn Muzahim yeye akawa ni mwenye
kusema kua: ‘Hakika sisi tunajua kuhusiana na Kursiy na Arshi za Duniani ziko vipi,
na zinatumiwa kwa matumizi gani. Lakini tunapozungumzia Arshi na Kursiy ya
Allah Subhanah wa Ta’ala basi ni yeye peke yake ndie mwenye kujua maana yake.’
594

Ama kwa upande wa Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al
Razi basi yeye anasimamia kwenye msimamo wa Mujahid Mujtahid Imam Abu Bakr
Muhammad Ibn Ali Ibn Isma’il Al Qaffal Ash Shashi Al Khurasan Al Shafii ambae yeye
amesema kua: ‘Maneno haya yametumika kuelezea Ukubwa wa Allah Subhanah wa
Ta’ala kupitia katika njia ya Taswira, yaani Allah Subhanah wa Ta’ala anawasilisha
kwa viumbe wake ujumbe wake kupitia katika njia ambayo ni yenye kuwawekea
wazi kupitia vile vitu ambavyo wanavijua kupitia kwa Wafalme wao ili waweze
kufaham Sifa zake na Utukufu wake. Kiasi ya kua amelifanya Al Kaabah kua ni
nyumba kwa ajili yake na ili watu walizunguke kama vile wafanyavyo kwenye
Majumba ya Wafalme wao… Hivyo basi pia amemithilisha kwa mfano kuhusiana
na Kursiy yake.’

Na amesema Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam kua: ‘Kulinganisha na Kursiy basi
Mbingu saba hazina ukubwa wowote isipokua kama ni Pete tu iliyotupwa Jangwani
na kulinganisha na Arshi basi Kursiy hua ni sawa na Pete tu iliyotupwa
Jangwani’(Sahih Ibn Hibban)

Ayat Al Qursy ambayo ilishuka katika mji wa Madina mbali ya kua Ayat al Kursiy kua
inajulikana kama Ayat Al Arshi lakini hua pia inajulikana kwa majina yafuatayo:

1-Sayyidat Ayi Al Qur’an.


2-Al Ruqqyat.
3-Ayyati Al Haris.
4-Wa Al Muhsanati.
5-Wa Al Junnati.
6-Wa Al Waqqiyati.
7-Wa Al Kafiyyati.
8-Wa Al Sharifati.
9-Wa Al Aadhimati.
10-Wa Ashraf Ayati.
11-Wa Aadham Ayati.
12-WatudaAai fii al Tawrati Ayyati Allah.

Hivyo tunapozungumzia Ayat Al Kursiy basi hua tunazungumzia kuhusiana na maneno


Matukufu ya Allah Subhanah wa Ta’ala yaliyomo katika aya tukufu kuliko zote ambayo
ni yenye kusema kua:
595

ِ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻻَ إِﻟَـٰﻪ إِﻻﱠ ﻫﻮ ٱ ْﳊﻰ ٱﻟْ َﻘﻴﱡﻮم ﻻَ َﺄﺗْﺧ ُﺬﻩ ِﺳﻨَﺔٌ وﻻَ ﻧـَﻮم ﻟﱠﻪ ﻣﺎ ِﰱ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬
‫ات‬ ََ َ ُ ٌْ َ ُ ُ ُ ‫﴿ ﱠُ َ ُ َ َ ﱡ‬
‫ﲔ أَﻳْ ِﺪﻳ ِﻬ ْﻢ َوَﻣﺎ‬ ِِ ِ ِ
َْ ‫ض َﻣﻦ ذَا ٱﻟﱠﺬى ﻳَ ْﺸ َﻔ ُﻊ ﻋْﻨ َﺪﻩُ إِﻻﱠ ﺈﺑِِ ْذﻧﻪ ﻳَـ ْﻌﻠَ ُﻢ َﻣﺎ ﺑَـ‬ ِ ‫َوَﻣﺎ ِﰱ ٱﻷ َْر‬
ِ ‫ﺧ ْﻠ َﻔﻬﻢ وﻻَ ُِﳛﻴﻄُﻮ َن ﺑِ َﺸﻲ ٍء ِﻣﻦ ِﻋ ْﻠ ِﻤ ِﻪ إِﻻﱠ ِﲟَﺎ َﺷﺂء و ِﺳﻊ ُﻛﺮِﺳﻴﱡﻪ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬
‫ات‬ ََ ُ ْ َ ََ ّْ ْ َ ُْ َ
﴾‫ودﻩُ ِﺣ ْﻔﻈُ ُﻬﻤﺎ وُﻫﻮ ٱﻟْ َﻌﻠِ ﱡﻰ ٱﻟْ َﻌ ِﻈﻴﻢ‬ ُ ‫ض َوﻻَ ﻳـَ ُﺆ‬
َ ‫َوٱﻷ َْر‬
ُ َ َ َ
Allahu la ilaha illa huwa alhayyu alqayyoomu la ta/khudhuhu sinatun wala
nawmun lahu ma fee alssamawati wama fee al-Ardhi man dha alladhee yashfaAAu
AAindahu illa bi-idhnihi yaAAlamu ma bayna aydeehim wama khalfahum wala
yuheetoona bishay-in min AAilmihi illa bima shaa wasiAAa kursiyyuhu
alssamawati waal-ardha wala yaooduhu hifdhuhuma wahuwa alAAaliyyu
alAAadheemu (Surat Al Baqara 2:255)

Tafsir: Allah! La ilaha illa Huwa (Hakuna Mungu anaestahiki kuabudiwa isipokua
yeye), Mwenye kuishi Milele, Mwenye kusimamia na kukipa Ulinzi kila kitu,
Asiepitiwa na kusinzia na wala asiepitiwa na Usingizi. Kwake yeye ndiko kwenye
umiliki wa kila kitu kilichopo Mbinguni na kilichopo Ardhini. Ni nani ambae
anaeweza kumuingilia katika maamuzi yake isipokua kutokana na idhini yake. Kwani
yeye ni mwenye kujua kila kinachotokea kabla yake (kwa viumbe wake hapa
Ulimwenguni) na baada yake (Kesho Akhera kwa viumbe wake). Na hakuna anaejua
chochote katika Ilm yake isipokua kwa atakalo. Kursiy yake imeenea kuanzia
Mbinguni mpaka Ardhini na si mwenye kuchoka katika kusimamia kwake na
kuhifadhi kwake. Na ni yeye ndie mwenye Darja ya Juu kabisa na ni yeye ndie mwenye
Utukufu Zaidi.

Ambapo kulingana na ayah na hadithi basi tunaona kua ingawa Kursiy imeenea kuanzia
Mbinguni mpaka Ardhini lakini hii haimaanishi kua iko katika sehemu fulani au labda
kua ina umbo fulani bali hua inmaanisha kua ni alama ya Uwezo, Mamlaka, Nguvu, Ilm
ya Kujua na kumiliki na kudhibiti kila kitu.

Ama kwa upande wangu mimi basi napenda zaidi kuifafanua ayah hii kulingana na
mtizamo wa Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Zukhruf Ad Din Imam Al Shafii Al Thani
Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali al Shafii
ambae yeye anahoji kuhusiana na ayah hii yaani Ayat ul Qursy kwa kusema kua: ‘Hivi
Jee unao uwezo wa kufikiria kwa nini Ayah hii ya Kursiy ikaitwa kua ni Aya Kuu
kati ya aya za Qur’an?.
596

Hivyo kama huna uwezo wa kujua hilo kutokana na ufahamu wako, basi faham
kua: Ayah hii imeitwa kua ni aya Kuu kwa sababu ni aya ambayo inajumuisha
ndani yake Sifa zake, Hali yake ya Kimungu na Majukumu yake Allah Subhanah
wa Ta’ala, Ambapo:

Allahu - linamaanisha Hali yake ya Kimungu,

La ilaha illa huwa – Hakuna Mungu anaestahiki Kuabudiwa isipokua yeye, hua
yanamaanisha Umoja wa Upekee wa Hali yake ya Kimungu.

Al Hayyu al Qayyoomu - Mwenye kuishi Milele, Mwenye kusimamia na kukipa


Ulinzi kila kitu hua yanamaanisha Sifa ya Hali yake na Utukufu wake yaani
Mwenye kuwepo na Mwenye Kujisimamia Mwenyewe na kila kitu ni chenye
Kumtegemea yeye kutokana na Usimamizi wake na hivyo kila kitu hua ni chenye
kutokana na chanzo cha kwake yeye yaani hii ni hali ambayo ya utukufu wa juu
kabisa na ukubwa usiokua na kifani ndani yake.

La ta/khudhuhu sinatun wala nawmun – Asiepitiwa na kusinzia na wala asiepitiwa


na Usingizi humaanisha kua yeye ni alie huru kutokana na Sifa zenye kuelezea
Matukio ambayo hayawezekani kumtokea katika hali yake. Ambapo kua kwake
Huru na yasiyoweza kumtokea hua hakumaanishi kua mambo hayo yamefichikana
na hayapo ndani ya sehemu ya I’lm yake bali kunamaanisha kua yako wazi kwake
kuliko vyengine vyote.

Lahu ma fee alssamawati wama fee al-Ardhi - Kwake yeye ndiko kwenye umiliki wa
kila kitu kilichopo Mbinguni na kilichopo Ardhini, kunamaanisha kua kila kitu
kinatokana nae na kila kitu kitarejea kwake.’

Man dha alladhee yashfaAAu AAindahu illa bi-idhnihi – Ni nani ambae anaeweza
kumuingilia katika maamuzi yake isipokua kutokana na idhini yake kunamaanisha
kua Hali yake ni ya kua ni mwenye Mamlaka na Maamrisho juu ya kila kitu na
yeyote yule atakaekua na haki ya kuingilia kati ya maamrisho yake basi hua ni
mwenye kufanya hivyo kutokana na Idhini yake, kwani ni yeye pekee ndie mwenye
uwezo na mamlaka wa kuruhusu kitu kinachotakwa kitokee kua kitokee, na hivyo
mamlaka haya hua ni yenye kupingana kua yeye ni mwenye mshirika katika
maamuzi yake na mamlaka yake

YaAAlamu ma bayna aydeehim wama khalfahum wala yuheetoona bishay-in min


AAilmihi illa bima shaa - Kwani yeye ni mwenye kujua kila kinachotokea kabla yake
(kwa viumbe wake hapa Ulimwenguni) na baada yake (Kesho Akhera kwa viumbe
wake). Na hakuna anaejua chochote katika Ilm yake isipokua kwa atakalo,
humaanisha kuweka wazi sifa ya I’lm yake juu ya kila kitu kinachojulikana na
597

kisichojulikana, na hali yake ya upekee wake katika kua na I’lm hio na kua hakuna
mwengine mwenye kujua zaidi yake, na yeyote yule mwenye kujua baadhi ya
mambo hua ni kutokana na Idhini yake yeye na majaaliwa yake na makadirio yake
Allah Subhanah wa Ta’ala kwa huyo anaejua juu ya hayo anayoyajua.

WasiAAa kursiyyuhu alssamawati waal-ardha - Kursy yake imeenea kuanzia


Mbinguni mpaka Ardhini, hua kunamaanisha Ukubwa wa Mmalaka yake na
Ukamilifu wake kiuwezo, ambapo katika hili kuna Siri ambayo haiwezekani
kuwekwa wazi kulingana na hali yaukubwa wake, kwani Ilm ya Kursy ya Allah
Subhanah wa Ta’ala na sifa zake na upana na ukubwa wa Mbingu na Ardhi hua ni
Ilm yenye Hikma na Busara ndani yake ambayo inajumuisha kwa pamoja aina
nyengine za Ilm.

Wala yaooduhu hifdhuhuma - Na si mwenye kuchoka katika kusimamia kwake na


kuhifadhi kwake, humaanisha Sifa yake Kiuwezo na Ukamilifu wake na kutokua na
Udhaifu na kutokua na Kasoro kwake.

Wahuwa alAAaliyyu alAAadheemu - Na ni yeye ndie mwenye Darja ya Juu kabisa na


ni yeye ndie mwenye Utukufu zaidi, humaanisha Sifa mbili kuu ambazo zitachukua
mda kutafsiri’

Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Al Shafi Al Thani Imam Abu Hamid
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhamad Al Ghazali al Shafii anaendelea kutuambia
kuhusiana na Ayat Al Kursiy kua: ‘Hivyo unapoitafakari maana ya inayopatikana
ndani ya Ayat al Kursiy na kisha ukazisoma aya nyengine zote za Qur’an basi kamwe
hutoweza kuona maana zote hizi ambazo zinajumusiha Upekee wa Allah Subhanah
wa Ta’ala, Utukufu wake na Maelezo ya Sifa zake kwa hali ya juu Kabisa zikiwa
zimekusanywa pamoja, katika aya Moja.

Na hii ndio sababu ya kwa nini Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawa ni
mwenye kusema kua: ‘Ayat Al Kursiy ndio Chifu wa Aya za Qur’an’ (Imam At
Tirmidhii).

Kwani mwanzoni mwa aya isemayo:

‫ٱﻪﻠﻟُ أَﻧﱠﻪُ ﻻَ إِﻟَـٰﻪَ إِﻻﱠ ُﻫ َﻮ َوٱﻟْ َﻤﻼَﺋِ َﻜﺔُ َوأ ُْوﻟُﻮاْ ٱﻟْﻌِْﻠ ِﻢ ﻗَﺂﺋِ َﻤﺎً ﺑِﭑﻟْ ِﻘ ْﺴ ِﻂ ﻻَ إِﻟَـٰﻪَ إِﻻﱠ‬
‫﴿ َﺷ ِﻬ َﺪ ﱠ‬
﴾‫ٱﳊَ ِﻜﻴﻢ‬ ِ
ُ ْ ‫ُﻫ َﻮ ٱﻟْ َﻌﺰ ُﻳﺰ‬
598

Shahida Allahu annahu la ilaha illa huwa waalmala-ikatu waoloo alAAilmi qa-iman
bialqisti la ilaha illa huwa alAAazeezu alhakeemu (Surat Al Imran 3:18)

Tafsir: Allah anashuhudia kua kwa hakika hakuna Mungu anaestahiki kuabudiwa
kwa haki isipokua yeye, na Malaika wake na wenye Ilm kua yeye ni mwenye
kusimamia kwa Uadilifu. Hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokua yeye mwenye
wingi wa Uwezo na mwenye wingi wa Hikma.

Ndani yake ayah hii mna Utukufu wa Allah Subhanah wa Ta’ala na Upekee wake.
Ambapo katika aya zisemazo:

‫ﻚ ِﳑﱠ ْﻦ ﺗَ َﺸﺂءُ َوﺗُﻌِﱡﺰ‬ َ ْ‫ﻚ َﻣﻦ ﺗَ َﺸﺂءُ َوﺗَﻨ ِﺰعُ ٱﻟْ ُﻤﻠ‬ َ ‫ﻚ ﺗُـ ْﺆﺗِﻰ ٱﻟْ ُﻤ ْﻠ‬
ِ ْ‫ﻚ ٱﻟْﻤﻠ‬
ُ َ
ِ‫﴿ﻗُ ِﻞ ٱﻟﻠﱠﻬ ﱠﻢ ﻣﺎﻟ‬
َ ُ
‫ﻚ َﻋﻠَ ٰﻰ ُﻛ ِّﻞ َﺷ ْﻲ ٍء ﻗَ ِﺪ ٌﻳﺮ۞ ﺗُﻮﻟِ ُﺞ ٱﻟﻠﱠْﻴ َﻞ‬ ِ ِ
َ ‫َﻣﻦ ﺗَ َﺸﺂءُ َوﺗُﺬ ﱡل َﻣﻦ ﺗَ َﺸﺂءُ ﺑِﻴَﺪ َك ٱ ْﳋَْﻴـُﺮ إِﻧﱠ‬
‫ﺖ ِﻣ َﻦ‬ ِ ِ ِ ْ ‫ِﰱ ٱﻟْﻨـﱠﻬﺎ ِر وﺗُﻮﻟِﺞ ٱﻟﻨـﱠﻬﺎر ِﰱ ٱﻟْﻠﱠﻴ ِﻞ وُﲣْﺮِج‬
َ ِّ‫ِج ٱﻟَ َﻤﻴ‬
ُ ‫ٱﳊَ ﱠﻰ ﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻤﻴّﺖ َوُﲣْﺮ‬ ُ َ ْ ََ ُ َ َ
﴾‫ﺎب‬ ٍ ‫ٱﳊ ِﻰ وﺗَـﺮُز ُق ﻣﻦ ﺗَ َﺸﺂء ﺑِﻐَ ِْﲑ ِﺣﺴ‬
َ ُ َ ْ َ ّ َْ
Quli allahumma malika almulki tu/tee almulka man tashao watanziAAu almulka
mimman tashao watuAAizzu man tashao watudhillu man tashao biyadika alkhayru
innaka AAala kulli shay-in qadeerun; Tooliju allayla fee alnnahari watooliju
alnnahara fee allayli watukhriju alhayya mina almayyiti watukhriju almayyita
mina alhayyi watarzuqu man tashao bighayri hisabin (Surat Al Imran 3:26-27)

Tafsir: Sema Ewe Allah mmiliki wa Ufalme, unampa Ufalme umtakae na


unampokonya Umtakae, na unampandisha darja umtakae na unamshusha darja
umtakae, ndani ya umiliki wako mna kheri na kwa hakika wewe ni mwenye uwezo wa
kufanya kila kitu. Unaufanya Usiku kuingia ndani ya Mchana, na unaufanya Mchana
kuingia ndani ya Usiku, unatoa Uhai kutoka ndani ya vilivyokufa na unatoa
vilivyokufa ndani ya vilivyo hai, na unamruzuku umtakae bila ya hesabu.

Ndani yake mmetajwa Majukumu yake Allah Subhanah wa Ta’ala na uwezo wake
kinguvu na katika Surat Al Fatiha kumegusiwa juu ya sifa hizi bila ya kua ni zenye
kuelezewa ndani yake, na hivyo basi kua ni zilizoelezewa ndani ya Ayat al Kursiy.

Ambapo aya zinazoikaribia Ayat al Kursiy kwa yote haya kimaana hua ni zile aya
za mwishoni mwa Surat Hashr zisemazo:
599

‫ﱠﻬ َﺎدةِ ُﻫ َﻮ ٱﻟﱠﺮ ْﲪَـٰ ُﻦ ٱﻟﱠﺮِﺣ ُﻴﻢ ۞ ُﻫ َﻮ‬ َ ‫ﺐ َوٱﻟﺸ‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟُ ٱﻟﱠ ِﺬى ﻻَ إِﻟَـٰﻪَ إِﻻﱠ ُﻫﻮ َﻋ ِﺎﱂُ ٱﻟْﻐَْﻴ‬
‫﴿ ُﻫ َﻮ ﱠ‬
َ
ْ ‫ﱡوس ٱﻟ ﱠﺴﻼَ ُم ٱﻟْ ُﻤ ْﺆِﻣ ُﻦ ٱﻟْ ُﻤ َﻬْﻴ ِﻤ ُﻦ ٱﻟْ َﻌ ِﺰ ُﻳﺰ‬
‫ٱﳉَﺒﱠ ُﺎر‬ ‫ﺪ‬ ‫ﻘ‬ ‫ﻟ‬
ْ ‫ٱ‬ ‫ﻚ‬ ِ‫ٱﻪﻠﻟ ٱﻟﱠ ِﺬى ﻻَ إِﻟَـٰﻪ إِﻻﱠ ﻫﻮ ٱﻟْﻤﻠ‬
ُ ُ ُ َ َُ َ ُ‫ﱠ‬
ُ‫َﲰَﺂء‬ ْ ‫ﺼ ِّﻮُر ﻟَﻪُ ٱﻷ‬َ ‫ئ ٱﻟْ ُﻤ‬ ُ ‫ٱﳋَﺎﻟِ ُﻖ ٱﻟْﺒَﺎ ِر‬ ‫ٱﻪﻠﻟِ َﻋ ﱠﻤﺎ ﻳُ ْﺸ ِﺮُﻛﻮ َن۞ ُﻫ َﻮ ﱠ‬
ْ ُ‫ٱﻪﻠﻟ‬ ‫ٱﻟْ ُﻤﺘَ َﻜِّﱪُ ُﺳْﺒ َﺤﺎ َن ﱠ‬
﴾‫ٱﳊَ ِﻜﻴﻢ‬ ِ ِ ‫ات َوٱﻷ َْر‬ِ ‫ٱﳊﺴﲎ ﻳﺴﺒِﺢ ﻟَﻪ ﻣﺎ ِﰱ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬
ُ ْ ‫ض َوُﻫ َﻮ ٱﻟْ َﻌﺰ ُﻳﺰ‬ ََ َ ُ ُ ّ َ ُ ٰ َ ْ ُْ
Huwa Allahu alladhee la ilaha illa huwa AAalimu alghaybi waalshshahadati huwa
alrrahmanu alrraheemu, Huwa Allahu alladhee la ilaha illa huwa almaliku
alquddoosu alssalamu almu/minu almuhayminu alAAazeezu aljabbaru
almutakabbiru subhana Allahi AAamma yushrikoona; Huwa Allahu alkhaliqu
albari-o almusawwiru lahu al-asmao alhusna yusabbihu lahu ma fee alssamawati
waal-Ardhi wahuwa alAAazeezu alhakeemu(Surat Hashr 59:26-27)

Tafsir: Yeye ndie Allah ambae hakuna Mungu anaestahiki kuabudiwa isipokua yeye,
Mwenye kujua juu ya Ulimwengu wa yaliyofichikana na ya Ulimwengu wa yaliyowazi,
ndie yeye Mwingi wa Rehma na mwingi wa Huruma. Yeye ndie Allah ambae ni
mwenye Ufalme, asiekua na kasoro, Mwenye Kutoa Usalama (kwa Viumbe wake na
kila kitu) mwenye kusimamia viumbe wake. Mwenye Uwezo, Mwenye Ujabari, Mwenye
Ukubwa, Utukufu ni wake Allah Subhanah wa Ta’ala, yuko mbali na
wanavyomshirikisha navyo. Yeye ni Allah Muumba wa Kila kitu, Muanzilishi wa Kila
Kitu, Mwenye kuumba Maumbo Mazuri, kwake yeye ndiko kwenye Umiliki wa Majina
bora. Kinamtukuza kila kilichomo Mbinguni na kila kilichomo Ardhini na ndie
mwenye uwezo wa kila kitu na mwenye hikma.’

Na pia tukijumuisha zile aya za mwanzoni za Surat Al Hadid zisemazo:

‫ض َوُﻫ َﻮ ٱﻟْ َﻌ ِﺰ ُﻳﺰ‬


ِ ‫ات َوٱﻷ َْر‬ ِ ‫اﻪﻠﻟِ ٱﻟﱠﺮ ْﲪـٰ ِﻦ ٱﻟﱠﺮِﺣﻴ ِﻢ۞ ﺳﺒﱠﺢ ِﱠﻪﻠﻟِ ﻣﺎ ِﰱ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬
‫﴿ﺑِ ْﺴ ِﻢ ﱠ‬
ََ َ َ َ
‫ﻴﺖ َوُﻫ َﻮ َﻋﻠَ ٰﻰ ُﻛ ِّﻞ َﺷ ْﻲ ٍء ﻗَ ِﺪ ٌﻳﺮ‬ ِ
ُ ‫ض ُْﳛﻴِـﻰ َوُﳝ‬
ِ ‫ﻚ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬
ِ ‫ات َوٱﻷ َْر‬ ۞ ِْ
َ َ ُ ‫ٱﳊَﻜ ُﻴﻢ ﻟَﻪُ ُﻣ ْﻠ‬
‫ﺎﻃ ُﻦ َوُﻫ َﻮ ﺑِ ُﻜ ِّﻞ َﺷ ْﻲ ٍء َﻋﻠِ ٌﻴﻢ ۞ ُﻫ َﻮ ٱﻟﱠ ِﺬى َﺧﻠَ َﻖ‬ ِ ‫ﺎﻫﺮ وٱﻟْﺒ‬ِ ِ
َ َ ُ ‫۞ ُﻫ َﻮ ٱﻷَﱠو ُل َوٱﻵﺧُﺮ َوٱﻟﻈﱠ‬
‫ٱﺳﺘَـ َﻮ ٰى َﻋﻠَﻰ ٱﻟْ َﻌْﺮ ِش ﻳَـ ْﻌﻠَ ُﻢ َﻣﺎ ﻳَﻠِ ُﺞ ِﰱ‬ ٍ ِ ِ َ ‫ات وٱﻷَر‬
ْ ‫ض ِﰱ ﺳﺘﱠﺔ أ ﱠَ�م ﰒُﱠ‬
ِ
ْ َ ‫ٱﻟ ﱠﺴ َﻤ َﺎو‬
600

ِ ‫ض وﻣﺎ َﳜﺮج ِﻣْﻨـﻬﺎ وﻣﺎ ﻳﻨ ِﺰُل ِﻣﻦ ٱﻟ ﱠﺴﻤ‬


‫ﺂء َوَﻣﺎ ﻳَـ ْﻌُﺮ ُج ﻓِ َﻴﻬﺎ َوُﻫ َﻮ َﻣ َﻌ ُﻜ ْﻢ أَﻳْ َﻦ َﻣﺎ‬ َ َ َ َ َ َ ُ ُْ َ َ ِ ‫ٱﻷ َْر‬
‫ٱﻪﻠﻟِ ﺗُـْﺮ َﺟ ُﻊ‬
‫ض َوإِ َﱃ ﱠ‬ ِ ‫ات َوٱﻷ َْر‬ ِ ‫ﻚ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬ ‫ِ ﱠ‬ ِ ‫ُﻛﻨﺘُﻢ و ﱠ‬
َ َ ُ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﲟَﺎ ﺗَـ ْﻌ َﻤﻠُﻮ َن ﺑَﺼﲑٌ۞ ﻟﻪُ ُﻣ ْﻠ‬ َْ
ِ ‫ٱﻷُﻣﻮر ۞ ﻳﻮﻟِﺞ ٱﻟْﻠﱠﻴﻞ ِﰱ ٱﻟﻨـﱠﻬﺎ ِر وﻳﻮﻟِﺞ ٱﻟﻨـﱠﻬﺎر ِﰱ ٱﻟْﻠﱠﻴ ِﻞ وﻫﻮ ﻋﻠِﻴﻢ ﺑِ َﺬ‬
‫ات‬ ٌ َ ََُ ْ َ َ ُ َُ َ َْ ُ ُ ُ ُ
﴾‫ﺼ ُﺪوِر‬
‫ٱﻟ ﱡ‬
Biismi Allahi AlRahmani AlRahiim, Sabbaha lillahi ma fee alssamawati waal-Ardhi
wahuwa alAAazeezu alhakeemu, Lahu mulku alssamawati waal-Ardhi yuhyee
wayumeetu wahuwa AAala kulli shay-in qadeerun, Huwa al-awwalu waal-akhiru
waaldhdhahiru waalbatinu wahuwa bikulli shay-in AAaleemun; Huwa alladhee
khalaqa alssamawati waal-ardhah fee sittati ayyamin thumma istawa AAala
alAAarshi yaAAlamu ma yaliju fee al-Ardhi wama yakhruju minha wama yanzilu
mina alssama-i wama yaAAruju feeha wahuwa maAAakum ayna ma kuntum
waAllahu bima taAAmaloona baseerun; Lahu mulku alssamawati waal-Ardhi wa-
ila Allahi turjaAAu al-omooru; Yooliju allayla fee alnnahari wayooliju alnnahara
fee allayi wahuwa AAaleemun bidhati alssudoori (Surat Al Hadid 57:1-6)

Tafsir: Kwa jina la Allah Mwingi wa Rehma mwingi wa Huruma. Kinamtukuza Allah
kila kilichomo Mbinguni na Ardhini na ni yeye ndie mwenye uwezo juu ya kila kitu na
ni mwingi wa Hikma. Kwake yeye ndiko kwenye Ufalme wa Mbinguni na wa Ardhini
ndie mwenye kusababisha uhai na ndie mwenye kusababisha mauti na ni mwenye
uwezo juu wa kila kitu. Yeye ndie wa mwanzo na wa mwisho ndie alie Juu kabisa na
ndie alie Karibu kabisa, na ndie mwenye kujua kila kitu. Yeye ndie alieumba Mbingu
na Ardhi kwa siku sita na kisha akawa kwenye Arshi (kwa namna anavyojua yeye
mwenyewe) anajua kila kinachoingia ndani ya Ardhi na kila kinachotoka ndani ya
ardhi, na hua pamoja nawe popote pale utakapokua na Allah ni mwenye kuona kila
unachokifanya. Uko kwake Ufalme wa Mbinguni na Ardhini na kila kitu kitarejea
kwake. Huutoa Usiku kutoka katika Mchana na Huutoa mchana Kutoka katika Usiku,
na ni yeye mwenye kujua kile kilichomo ndani ya Kifua (Siri ya kila Kiumbe wake).

Kwani Aya hizi zinajumuisha Sifa na majina mengi matukufu ya Allah Subhanah
wa Ta’ala. Lakini hata hivyo aya hizi idadi yake ni zaidi ya aya Moja, wakati Ayat
Al Kursiy ni Aya Moja Tu!

Hivyo unapolinganisha Ayat Al Kursiy na moja kati ya aya hizi basi unaona kua
Ayat Al Kursiy Imefungamanisha na Kujumuisha zaidi malengo ya Qur’an na
kutokana na sababu hio basi ndio maana ayah hii ikawa ni yenye kuitwa Mkuu wa
601

aya zote za Qur’an, na hivyo ndivyo alivyosema Rasul Allah Salallahhu Alayhi wa
Salam.

Na itakuaje isiwe hivyo wakati ndani yake kuna maneno yasemayo: ‘Huwa alhayyu
alqayyoomu’ ambalo ni Jina Kubwa zaidi lenye Siri kubwa sana ndani yake. Na hii
inathibitishwa na hadith isemayo kua Jina tukufu Kubwa zaidi limo katika aya ya
mwanzoni ya Surat Al Imran mbayo inasema:

ُ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻻَ إِﻟَـٰﻪَ إِﻻﱠ ُﻫ َﻮ ٱ ْﳊَ ﱡﻰ ٱﻟْ َﻘﻴﱡ‬


﴾‫ﻮم‬ ‫﴿ﱠ‬
Allahu la ilaha illa huwa alhayyu alqayyoomu (Surat Al Imran 3:2)

Tafsir: Allah! La ilaha illa Huwa (Hakuna Mungu anaestahiki kuabudiwa isipokua
yeye), Mwenye kuishi Milele, Mwenye kusimamia na kukipa Ulinzi kila kitu.

Na pia katika aya ya Surat Ta-Ha pale Allah Subhanah wa Ta’ala aliposema:

﴾ً‫ﺎب َﻣ ْﻦ َﲪَﻞ ﻇُْﻠﻤﺎ‬‫ﺧ‬ ‫ﺪ‬


ْ ‫ﻗ‬
َ‫و‬ ِ ‫ﺖ ٱﻟْﻮﺟﻮﻩ ﻟِﻠْﺤ ِﻰ ٱﻟْ َﻘﻴﱡ‬
‫ﻮم‬ ِ َ‫﴿وﻋﻨ‬
َ َ َ َ ّ َ ُ ُ ُ ََ
WaAAanati alwujoohu lilhayyi alqayyoomi waqad khaba man hamala dhulman
(Surat Ta-Ha 20:111)

Tafsir: Na Nyuso zote zitanyenyekea kwa Mwenye kuishi Milele na Mwenye


kusimamia na kukipa Ulinzi kila kitu, na kwa hakika atafeli atakaebeba Dhulma.

Huo ni Mtizamo wa Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Al
Ghazali katika kuielezea maana ya Ayat Al Kursiy na hivyo kutuwekea wazi uwezo wa
Allah Subhanah wa Ta’ala juu ya viumbe wake na kila kitu.

Ambapo kwa upande wa Al Aaliyyu Al Aaadhiim hua ni Sifa zinazomaanisha Utukufu


wake na Uwezo wa hali ya Juu Kabisa wa Allah Subhanah wa Ta’ala ambapo ndani yake
mnajumuishika maana ya kua yeye ndie aliejuu kabisa kwa Kiutukufu na Kiuwezo kwa
usiokua na mipaka kwa Viumbe wake na kwa kila kitu, na ndie aliejuu kabisa kwa
ukamilifu, na hivyo amekikadiria kila kitu kwa ukamilifu kuanzia mwanzo wake mpaka
mwisho wake kitu hicho na hakuna atakaeweza kupangua makadirio hayo kwa sababu
yeye ndie Muumba alieumba kila kitu.
602

Na anasema Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Al Mushakkikin Imam Al


Ghazali Al Thani Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Maneno Alhayyu Alqayyoomu
yanafafanulika katika hali mbili:

Kwanza ni katika Kauli ya Ubay Ibn Qa’ab Radhi Allahu Anhu alipomwambia
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam amfundishe kuhusiana na Ism Adhim
ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kua limo katika maneno
yasemayo:

ُ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻻَ إِﻟَـٰﻪَ إِﻻﱠ ُﻫ َﻮ ٱ ْﳊَ ﱡﻰ ٱﻟْ َﻘﻴﱡ‬


﴾‫ﻮم‬ ‫﴿ﱠ‬
Allahu la ilaha illa huwa alhayyu alqayyoomu (Surat Al Imran 3:2)

Tafsir: Allah! La ilaha illa Huwa (Hakuna Mungu anaestahiki kuabudiwa isipokua
yeye), Mwenye kuishi Milele, Mwenye kusimamia na kukipa Ulinzi kila kitu.

Pili: Ambapo katika Alhayyu humaanisha kua yuko hai kwa Ulimwengu wake hivyo
hua anasikia kila linalosemwa na anaona kila linalofanywa na Viumbe wake.

Na katika Alqayyoomu humaanisha kua ni mwenye kumsimamia Ulimwengu wake


na viumbe wake bila kuhitaji msimamizi mwengine zaidi yake.’

Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Al Mushakkikin Imam Fakhr Ad Din Al


Razi kua: ‘Kwa Hali zote basi hakuna tofauti kimtizamo miongoni mwa Wanazuoni
kua Allah Subhanah wa Ta’ala Hayuko katika sehemu Yeyote, Hayuko katika kila
sehemu na wala hayuko katika Upande Maalum. Hivyo basi ayah hii inatakiwa
ichukuliwe maana yake kwa kumithilisha kulingana na hisia za Ibn Adam, na
inapokubalika hukmu hio basi hua inawezekana kutumika ipasavyo pale
inapostahiki. Ambapo hua inatubidi kutumia maana ya kumithilisha kwa sababu
kuu mbili zinazotokana na kupingana kwa kauli mbili ambazo ni Thumma istawa
AAala alAAarshi yaani Na kisha akawa kwenye Arshi na kauli ya Wahuwa
maAAakum ayna ma kuntum yaani Na yuko pamoja nawe popote pale utakapokua’
zilizomo katika aya isemayo:
603

ٍ ِ ِ َ ‫ات وٱﻷَر‬ ِ ِ
ْ ‫ض ِﰱ ﺳﺘﱠﺔ أَﱠ�م ﰒُﱠ‬
‫ٱﺳﺘَـ َﻮ ٰى َﻋﻠَﻰ ٱﻟْ َﻌْﺮ ِش ﻳَـ ْﻌﻠَ ُﻢ‬ ْ َ ‫﴿ ُﻫ َﻮ ٱﻟﱠﺬى َﺧﻠَ َﻖ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤ َﺎو‬
ِ ‫ض وﻣﺎ َﳜﺮج ِﻣْﻨـﻬﺎ وﻣﺎ ﻳﻨ ِﺰُل ِﻣﻦ ٱﻟ ﱠﺴﻤ‬
‫ﺂء َوَﻣﺎ ﻳَـ ْﻌُﺮ ُج ﻓِ َﻴﻬﺎ َوُﻫ َﻮ‬ ِ ِ
َ َ َ َ َ َ ُ ُْ َ َ ِ ‫َﻣﺎ ﻳَﻠ ُﺞ ﰱ ٱﻷ َْر‬
﴾ٌ‫ﺼﲑ‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ ِﲟَﺎ ﺗَـﻌﻤﻠُﻮ َن ﺑ‬
َ َ ْ ُ‫َﻣ َﻌ ُﻜ ْﻢ أَﻳْ َﻦ َﻣﺎ ُﻛﻨﺘُ ْﻢ َو ﱠ‬
Huwa alladhee khalaqa alssamawati waal-ardhah fee sittati ayyamin thumma
istawa AAala alAAarshi yaAAlamu ma yaliju fee al-Ardhi wama yakhruju minha
wama yanzilu mina alssama-i wama yaAAruju feeha wahuwa maAAakum ayna ma
kuntum waAllahu bima taAAmaloona baseerun(Surat Al Hadid 57:4)

Tafsir: Yeye ndie alieumba Mbingu na Ardhi kwa siku sita na kisha akawa kwenye
Arshi (kwa namna anavyojua yeye mwenyewe) anajua kila kinachoingia ndani ya
Ardhi na kila kinachotoka ndani ya ardhi, na hua pamoja nawe popote pale
utakapokua na Allah ni mwenye kuona kila unachokifanya.

Kauli ya Na kisha akawa kwenye Arshi na kauli ya Yuko pamoja nawe popote pale
utakapokua (ambazo hatutakiwi kuzipatanisha). Huku tukijaribu kukumbuka
maneno ya Imam Abu Al Ma’ali Al Haramain pale aliposema kua: ‘Muhammad
Salallahu Alayhi wa Salam alikua Karibu na Allah Subhanah wa Ta’ala katika
Safari yake ya Isra na Miraj, kuliko hata namna Nabii Yunus Ibn Matta alivyokua
wakati akiwa ndani ya tumbo la Chewa’’

Ambapo kwa upande wa Imam Abu Muhamamd Abdallah Sahl Al Tustari basi yeye
anasema kua: ‘Maana ya Al Hayyu Al Qayyoomu ni Sifa yake Allah Subhanah wa
Ta’ala ambae ndie yule anaesimamia kila kitu kuhusiana na Viumbe wake, Maisha
yao, Uhai wao, Matendo yao na Riziki Zao. Kwani yeye ndie yule ambae mwenye
kulipa wema kwa wema na mwenye kulipa maovu kwa usamehevu, lakini hua ni
mwenye kulipa Unafiq, Kufuru na Uzushi kwa Adhabu. Hivyo Mtu yeyote yule
anaesema: ‘Hakuna Mola anaestahiki kuabudiwa isipokua Allah Subhanah wa
Ta’ala,’ hua amefunga Mkataba na Allah Subhanah wa Ta’ala, hivyo hua ni haramu
kwake Mtu huyo baada ya kufunga Mkataba na Allah Subhanah wa Ta’ala kua ni
mwenye kumuasi Allah Subhanah wa Ta’ala katika maamrisho yake, au makatazo
yake katika hali ya faragha au hadharani, au kumuunga mkono Adui yake Allah
Subhanah wa Ta’ala au kuonesha Uadui dhidi ya Rafiki yake Allah Subhanah wa
Ta’ala.’
604

Kwa upande wa Bahr al Il’m Sahaba Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu, Imam
Sufyan Ath Thawry, Imam Al Bayhaqi na Imam Al Tabari basi wao wanasema kua
Kursiy inamaanisha Ilm yake kama inavyobainisha aya ifuatayo:

ْ‫ض ِﻣﺜْـﻠَ ُﻬ ﱠﻦ ﻳَـﺘَـﻨَـﱠﺰُل ٱﻷ َْﻣُﺮ ﺑَـْﻴـﻨَـ ُﻬ ﱠﻦ ﻟِّﺘَـ ْﻌﻠَ ُﻤ ۤﻮا‬


ِ ‫ات َوِﻣ َﻦ ٱﻷ َْر‬ ٍ ‫ٱﻪﻠﻟ ٱﻟﱠ ِﺬى ﺧﻠَﻖ ﺳﺒﻊ َﲰﺎو‬
َ َ َ َْ َ َ ُ‫ﱠ‬
﴿
﴾‫َﺣﺎ َط ﺑِ ُﻜ ِﻞ َﺷﻲ ٍء ِﻋ ْﻠﻤﺎ‬ ‫ٱﻪﻠﻟَ َﻋﻠَ ٰﻰ ُﻛ ِّﻞ َﺷ ْﻲ ٍء ﻗَ ِﺪ ٌﻳﺮ َوأَ ﱠن ﱠ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟَ ﻗَ ْﺪ أ‬ ‫أَ ﱠن ﱠ‬
َ ْ ّ
Allahu alladhee khalaqa sabAAa samawatin wamina al-Ardhi mithlahunna
yatanazzalu al-amru baynahunna litaAAlamoo anna Allaha AAala kulli shay-in
qadeerun waanna Allaha qad ahata bikulli shay-in AAilman(Surat At Talaq 65:12)

Tafsir: Ni Allah Ndie ambae alieumba Mbingu Saba na Ardhi Mithili yake, amri yake
hushuka baina yake ili mpate kujua kua kwa hakika Allah ni mwenye uwezo wa
kukadiria kila kitu, na kwa hakika yeye amekigubika kila kitu kwa Ilm yake.

Kwani Ibn Adam hua ni mwenye kuipata Ilm yake kutokana na kua ni yenye kupitia
kwenye Moyo wake. Hivyo basi Kursiy hua ni kitu chenye jukumu la kukusanya aina
zote za I’lm kupitia kwenye Moyo wa Ibn Adam ili aweze kupata I’lm kupitia katika
Moyo wake, na Arshi ina jukumu la Kukusanya I’lm ya Moyo wa Ibn Adam
inayohusiana na kumjua Mola wake. Hivyo basi Kursiy kusudio lake hua ni kuwaruhusu
Viumbe wa Allah Subhanah wa Ta’ala kupata I’lm juu yake kuhusiana na Ulimwengu
wake.

Ayat al Kursiy ni moja kati ya aya ndefu miongoni mwa aya za Qur’an ambapo aya iliyo
refu zaidi ni Ayat dayn yaani aya ya deni ambayo ni aya ya Surat Al Baqara 2:282, ama
kuhusiana na Ayat Al Kursiy basi ndani yake mna herufi 170 zilizounda maneno 50
yaliyobebwa na sentensi 10 zenye Majina Matukufu Matano ya Allah Subhanah wa
Ta’ala na viwakilishi vya Majina na Sifa zake zaidi ya 13 ambazo ndani yake mna
ujumbe wenye uzito mkubwa sana, kwani zimeainisha vithibitisho zaidi ya 10 vya sifa
ya Umoja wa pekee wa Allah Subhanah wa Ta’ala.

Ambapo Jarrah Allah Imam Abu Al Abbas Al Zamakhshari anasema kuhusiana na ayah
hii kua: ‘Kwa hakika hii ndio Aya Tukufu kuliko zote katika aya za Qur’an na hii
ni kwa sababu inazungumzia Upekee wa Allah Subhanah wa Ta’ala, jambo ambalo
linatupelekea kuhitimisha juu ya Upekee wake huo kua ni Jambo Tukufu kuliko
yote miongoni mwa matawi ya I’lm.’
605

Na kwa upande Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Ahmad Ibn Abu Bakr Al Ansari
Al Qurtubi, basi yeye anasema kuhusiana na ayah hii kua: ‘Bila ya shaka hii ni aya
Tukufu kuliko zote na hii ni kwa sababu ya kua ndani yake mna majina ya Allah
Subhanah wa Ta’ala ambayo yametajwa mara 18 aidha kwa njia ya jina moja kwa
moja au kwa njia ya kiwakilishi cha Jina.’ Ambapo kwa njia ya jina moja kwa moja
basi imeteja Majina Matukufu matano ambayo ni Allahu, Al Hayyu, Al Qayyum, Al
Aaliyyu na Al Aadhiimu na na kwa njia ya kiwakilishi cha jina basi imetaja mara 13.

FADHILA ZA AYAT AL KURSIY


Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Ahmad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi
anaendelea kutuambia kua: ‘Na Sahaba Abd Rahman Ibn Awf Radhi Allahu Anhu
alikua ni mwenye kuisoma ayah hii katika pembe nne za nyumba yake kila
anapoingia ndani yake.’

Ambapo amesema Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Katika Surat Al Baqara kuna Aya ambayo ni Aya
bora zaidi ya Aya zote za Qur’an, kwani haisomwi ndani ya Nyumba isipokua
Shaytani hua ni mwenye kukimbia kutoka ndani ya Nyumba hio’’

Na amesema Imam Mulla Ali Al Qari kua amesema Imam Bayhaqi kua: ‘Allah
Subhanah wa Ta’ala huipa ulinzi Nyumba ya Mtu anaesoma Ayat Al Kursiy
anapoingia kitandani mwake anapolala usiku na pia huzipa ulinzi Nyumba za
majirani zake’

Na akasema Abu Umammah kua amesema: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
kua: ‘Yeyote yule atakaesoma Ayat al Kursiy mara tu baada ya kusali Sala yake ya
FArdhi basi hua hakuna kitu kitakachosimama baina yake yeye na kuingia kwake
Peponi isipokua kifo’’(Imam An Nasai)

Amesema Hafiz Imam Muhammad Ibn Mahmud Ibn al Najjar Al Baghdadi maarufu
kama Imam Ibn Al Najjar katika kitabu chake cha Ta’rikh Baghdad kua amesema Abd
Allah Ibn `Abbas kua amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Yeyote
yule atakaesoma Ayat Al Kursiy kila baada ya Sala ya FArdhi basi Allah Subhanah
wa Ta’ala atamjaalia mtu huyo Moyo wenye shukrani ndani yake, na amali za
Siddiqun na malipo ya Mitume, na kua ni mwenye kuingizwa ndani ya Rehma zake
na hatomzuia kuingia Peponi isipokua kwa kifo chake na kisha baada yake ataingia
Peponi’ (Durr Al Mandhur, Majmaa Al Zawaid, al Awasat)
606

Yeyote yule atakae isoma Ayat Al Kursiy kwa mara 18 kila siku basi basi Allah
Subhanah wa Ta’ala atamzidishia Imani, na atamfungulia kifua chake kwa kumjaza
Hikma ndani yake, kumrahisishia Riziki, na Kumuongezea Heshima mbele ya watu
wake, na atakua ni mwenye kukingwa na majanga mbali mbali.

Na yeyote yule atakaeisoma Ayat Al Kursiy huku akiwa na msimamo kila baada ya
Sala ya fardhi asubuhi na jioni, na katika kila mlango anaouingia iwe nyumbani au
sokoni na kila anapopanda kitandani basi In-Shaa Allah atakua ni mwenye
kuhifadhika na vishawishi vya Shaytan na udhalimu wa kila alie dhalimu na kila
anaedhuru. Na Nyumba yake na familia yake zitahifadhika kutokana na madhara
mbali mbali.

Na akasema Imam Sharaf Al Din, Shihab Al Din Ahmad Ibn Ali Ibn Yusuf Al Buni Al
Maliki Al Ifriqi Kua: ‘Yeyote yule atakaesoma Ayat Al Kursiy mara 50, na kisha
akapulizia ndani ya maji ya Mvua na kisha akanywa Maji hayo, basi In-Shaa Allah
Subhanah wa Ta’ala atamjaalia kua na Ufaham mzuri sana na kumrahisishia
masomo yake’

Na yeyote yule atakaesoma Ayat al Kursiy baada ya kila Sala ya Fardhi, In-shaa
Allah, Allah Subhana wa Ta’ala atamsamee dhambi zake, na atakaesoma wakati
anapoenda kulala basi atakua huru na Shaytan, na wale watakaoisoma wakati
wakiwa na Hasira au Mashakil ya Moyo basi watapata utulivu ndani nyoyo zao.

Yeyote yule atakaeisoma Ayat Al Kursiy kwa mara ya idadi ya herufi zake yaani
mara 170, basi Inshaa Allah Allah Subhanah wa Ta’ala atamsaidia katika uzito wa
jambo lake, atamzidishia Ufaham, na kumuongezea Riziki na kulipwa anachodai.

Yeyote yule aliekua na khofu na maadui zake basi na achore kinga ya Duara kwa
kutumia Pumzi zake huku akiwa anasoma Ayat Al Kursiy mara 50 au mara 170, In-
shaa Allah Allah Subhanah wa Ta’ala atamlinda dhidi ya Maadui hao kwani
hawatoweza kumdhuru huku nao hawatoiona ukuta wa kinga hio.

Na akasema Shaykh Al Akbar Imam Muhyi Ad Din Abu Bakr Ibn Arabi kua: ‘Yeyote
yule atakaeisoma Ayat al Kursiy mara 1000 katika mda wa siku 40 basi kwa ajili ya
Allah Subhanah wa Ta’ala, kwa ajili ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, na
kwa ajili ya Qur’an basi Allah Subhanah wa Ta’ala atamnawirishia muonekano
wake wa Kiroho, atamuondolea matatizo na kumuondolea kua na utegemezi na
watu.’

Yeyote yule atakaeisoma Ayat Al Kursiy mara tu baada ya kutoka nyumbani kwake
basi Allahu Subhanah wa Ta’ala humjaalia Malaika 70,000 kama ulinzi dhidi yake
na ambao hua ni wenye kumuombea Maghfira kwa ajili yake tangu wakati
607

alipotoka nje ya nyumba yake akaelekea katika safari yake ya halali mpaka
atakaporudi nyumbani kwake.

Na inapendekezwa kusoma Ayat ul Kursiy kabla ya kulala kwa sababu ndani yake
imejumuisha Kalimat at Tawhid - Allahu alladhee la ilaha illa huwa - hivyo mtu
ukiisoma kisha ukalala na hayo ndio yakawa ndio maneno yako ya mwisho basi hua
mna bashirio jema ndani yake.

Wanasema wenye kujua kua yeyote yule atakaesoma Ayat Al Kursiy mara 7 wakati
anapokua safarini basi ataenda na kufika salama na kurudi salama safari yake.

Na yeyote yule atakaechukua mchanga na kisha akausomea Ayat Al Kursiy mara 7


kisha akaumwagia Makaburini hapo basi watapa Rehma za Allah Subhanah wa
Ta’ala watu waliomo ndani ya Makaburi hayo.

Na kama Mji, Nyumba au sehemu imezingirwa na Maadui na hivyo kua ni wenye


kuwatishia waliomo ndani yake, basi waliomo ndani yake kama watasoma Ayat Al
Kursiy mara 1100 kwa kila siku usiku basi baada ya siku tatu In-shaa Allah Maadui
hao wataondoka na kuwaachia na kutokua nao haja tena watu hao waliowazingira.

Kama ikiwa kuna ndugu yako, mume wako au mke wako hakupendi au
amefitinishwa nawe basi chukua kinywaji au chakula kisha kisomee Ayat Al Kursiy
mara 41 na umpe ndugu yako huyo ale au anywe basi In-shaa Allah atakua ni
mwenye kukupenda kama ilivyokua akikupenda hapo awali.

Yeyote yule atakeisoma Ayat Al Kursy mara 170 saa moja asubuhi katika siku ya
Jumapili basi atajaaliwa kua na Darja kubwa katika jamii. In-shaa Allah

Yeyote yule atakeisoma Ayat Al Kursy mara 170 saa moja asubuhi katika siku ya
Jumatatu basi atakua na Ufunguzi wa mambo yake na Urahisi katika kujipatia
Riziki zake na mahitaji yake ya Kidunia. In-shaa Allah.

Yeyote yule atakeisoma Ayat Al Kursy mara 170 saa moja asubuhi katika siku ya
Jumanne basi atakua na Ulinzi na Ushindi dhidi ya Kila kitakachotaka Kumdhuru
na kutokubalika katika jamii In-shaa Allah.

Yeyote yule atakeisoma Ayat Al Kursy mara 170 saa moja asubuhi katika siku ya
Jumatano basi atawashinda Maadui zake na atakua na mahusiano mazuri na watu
wake katika Jamii yake In-shaa Allah.
608

Yeyote yule atakeisoma Ayat Al Kursy mara 170 saa moja asubuhi katika siku ya
Alkhamis basi atakua na Ufaham Mpana, I’lm kubwa na ataondokewa na matatizo
ya Akili Ufaham na wa Mawazo In-shaa Allah.

Yeyote yule atakeisoma Ayat Al Kursy mara 170 saa moja asubuhi katika siku ya
Ijumaa basi atakua ni mwenye kupendwa katika jamii na pia na Viumbe wote wa
Allah Subhanah wa Ta’ala na mambo yake yatanyooka In-shaa Allah.

Yeyote yule atakeisoma Ayat Al Kursy mara 170 saa moja asubuhi katika siku ya
Jumamosi basi atakua na uwezo na heshima kubwa sana katika jamii In-shaa Allah.

Hayo yote hupatikana kutokana na Idhini ya Allah Subhana wa Ta’ala na unaweza


kusoma mara 170 au mara 313 au zaidi kwa kadiri ya uwezo wako.

Hivyo Ayat Al Kursiy ina faida nyingi sana ndani yake na Wanazuoni wenye Ilm
Ruhaniyyat wamezizungumzia sana akiwemo Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali na Dua zake, kiasi ya kua siwezi
kuziainisha zote humu kwa sababu inabidi utayarishe kitabu chake kamili na ukweli ni
kua kama ukijizoesha kudumu nayo, basi hua ni kinga kubwa sana dhidi ya Mitihani
mingi ya Kiduni ikiwemo Uchawi, Husda, Kijicho, Majini na Mashaytan, madhara ya
Ibn Adam na Viumbe wengineo, n.k

Na hali hii ya miujiza ya Ayat Al Kursiy ni yenye kuthibitisha Utukufu wa Aya hio na pia
kuthibitisha kua Allah Subhanah Ta’ala amekizunguka kila kitu miongoni mwa Viumbe
wake, ana habari juu ya kila kitu anaona kila kila kitu, anajua kila kitu na ni mwenye
uwezo juu ya kila kitu.

Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Yeyote yule atakaefanya
mambo matatu basi atakua ni mwenye kuonja utamu wa Imani: Atakaemuabudu
Allah Subhanah wa Ta’ala anaestahiki kuabudiwa peke yake. Anaeisafisha Mali
yake kwa Moyo safi kwa kutoa kutokana nayo kila mwaka, kwa kutotoa Ng’ombe
wazee, au wasiokua na Thamani, Wasiokua na Maradhi, Wasiotoa Maziwa bali
walio katikati na kati miongoni mwao. Na atakaejisafisha Nafsi yake’ Masahaba
wakauliza: ‘Na Jee ndio vipi hivyo kujisafisha Nafsi?’ Rasul Allah Salallahu A’layhi
wa Salam akasema: ‘Ni Kujua kua Allah Subhanah wa Ta’ala yuko katika kila
sehemu anayokuwepo yeye’(Imam Al Bayhaqi)

Na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akawaambia Nabii Musa na Nabii Harun kua:
‘Hakika mimi nipo pamoja nanyi kwani nnakuoneni na nnakushuhudieni katika
kila hatua ya maisha yenu na nakuungeni mkono kupitia katika uwezo wangu
(quwwa), hivyo basi msiwe na khofu yeyote wala wasi wasi wowote, nendeni kwa
609

Fir’awn mkatakeleze majukumu yenu niliyokuamrisheni. Mwambieni kua mna


ujumbe kutoka kwa Mola wa Ulimwengu wote’ kama inavyosema Aya:

ۤ
﴾‫ﲔ‬ ِ َ‫ب ٱﻟْﻌﺎﻟ‬
‫ﻤ‬
َ َ ّ َ َُ ِ ‫ر‬ ‫ﻮل‬
ُ ‫ﺳ‬‫ر‬ ‫ﱠ‬
� ِ
‫إ‬ ‫ﻮﻻ‬ ‫﴿ﻓَﺄْﺗِﻴَﺎ ﻓِْﺮ َﻋ ْﻮ َن ﻓَـ ُﻘ‬
Fa/tiya firAAawna faqoola inna rasoolu rabbi alAAalameena (Surat Ash Shuaraa
26:16)

Tafsir: Na mtakapofika mbele ya Fir’awn mwambieni: ‘Hakika sisi ni Mitume kutoka


kwa Mola wa Ulimwengu wote na kila kilichomo ndani yake’


NABII MUSA NA NABII HARUN WAKABILIANA NA FIR’AWN.


Hivyo anasema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:
ِ ِ ِ ۤ ِ ۤ
‫ﺎك‬‫ﻨ‬ ‫ـ‬‫ﺌ‬‫ﺟ‬ ‫ﺪ‬ ‫ﻗ‬ ‫ﻢ‬‫ﻬ‬ ‫ـ‬‫ﺑ‬ ‫ﺬ‬
ّ ‫ﻌ‬‫ـ‬‫ﺗ‬ ‫ﻻ‬ ‫و‬ ‫ﻴﻞ‬ ‫اﺋ‬‫ﺮ‬ ‫ﺳ‬ ِ
‫إ‬ ‫ﲏ‬ ِ ‫ﺑ‬
َ َ ْ ْ َ ْ ُ ْ َ ُ َ َ َ َ ْ َ ََ َ ْ ْ َ َ َّ َ ُ َ‫ﺎ‬‫ﻨ‬ ‫ﻌ‬‫ﻣ‬ ‫ﻞ‬ ‫ﺳ‬ ‫َر‬
‫ﺄ‬ ‫ﻓ‬ ‫ﻚ‬ ِ
‫ﺑ‬‫ر‬ ‫ﻻ‬‫ﻮ‬ ‫ﺳ‬‫ر‬ �‫ﱠ‬ ِ
‫إ‬ ‫ﻮﻻ‬ ‫﴿ﻓَﺄْﺗِﻴَﺎﻩُ ﻓَـ ُﻘ‬
﴾‫ﻚ وٱﻟ ﱠﺴﻼَ ُم َﻋﻠَ ٰﻰ َﻣ ِﻦ ٱﺗـﱠﺒَ َﻊ ٱ ْﳍَُﺪ ٰى‬ ِ ٍِِ
َ َ ّ‫ﺂﺑﻳَﺔ ّﻣﻦ ﱠرﺑ‬
Fa/tiyahu faqoola inna rasoola rabbika faarsil maAAana banee isra-eela wala
tuAAadhdhibhum qad ji/naka bi-ayatin min rabbika waalssalamu AAala mani
ittabaAAa alhuda;(Surat Ta-Ha 20:47)

Tafsir: Hivyo nyote nendeni kwake na mwambieni: ‘Hakika sisi ni Mitume wa Mola
wako, hivyo waachie huru watu wa Bani Israil waondoke pamoja nasi, na usiwatese
kwani kwa hakika tumekuja na Dalili kutoka kwa Mola wako. Na Usalama utakua juu
ya yule mwenye kufuata Uongofu wake.’ ’

Ambapo aya inatuwekea wazi kua walipotumwa Nabii Musa na Nabii Harun kufikisha
ujumbe kwa Fir’awn, basi mbali ya kua waliambiwa kua wazungumze nae kwa kauli
laini, lakini pia waliamrishwa kua watumie hikma na hoja na vithibitisho kwani amesema
610

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam: ‘Nyoyo zimeumbwa kua na Maumbile ya


kupenda wenye ukarimu juu yao, na kuchukia wenye kutokua na ukarimu juu yao’

Kama vile ambavyo Nabii Sulayman alivyofikisha ujumbe kwa Malkia Bilqis ambae nae
alipoupokea alisema:
ِ‫ٱﻪﻠﻟ‬
‫ﺎب َﻛ ِﺮﱘٌ ۞إِﻧﱠﻪُ ِﻣﻦ ُﺳﻠَْﻴ َﻤﺎ َن َوإِﻧﱠﻪُ ﺑِ ْﺴ ِﻢ ﱠ‬ ِ ‫﴿ﻗَﺎﻟَﺖ ٰ�َﻳـﱡﻬﺎ ٱﻟْﻤ َﻸُ إِِ ۤﱐ أُﻟْ ِﻘﻰ إِ َﱠ‬
ٌ َ‫ﱃ ﻛﺘ‬ َ ّ َ َ ْ
﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ
َ ‫ٱﻟﱠﺮ ْﲪَـٰ ِﻦ ٱﻟﱠﺮﺣﻴ ِﻢ۞أَﻻﱠ ﺗَـ ْﻌﻠُﻮاْ َﻋﻠَ ﱠﻰ َوأْﺗُ ِﻮﱏ ُﻣ ْﺴﻠﻤ‬
Qalat ya ayyuha almalao innee olqiya ilayya kitabun kareemun, Innahu min
sulaymana wa-innahu bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Alla taAAloo AAalayya
wa/toonee muslimeena (Surat An Naml 27:29-31)

Tafsir: Akasema (Malkia Bilqis): ‘Enyi Machifu wangu hakika mimi nimepewa Barua
yenye Ukarimu, (Ambayo inasema) Kwa Hakika hii ni kutoka kwa Sulaymani, na kwa
Hakika (imeanza na) Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehma Mwingi wa Upole. (na
inausia kua) Msiwe ni wenye kujitukuza dhidi yangu, bali njooni kwangu mkiwa ni
wenye hali ya Kujisalimisha.’

Ambapo hapa tunaona kua Barua hii ya Nabii Sulayman kwa Malkia Bilqis ni fupi na
yenye kujumuisha Qawlan Layyina, Qawlan Sadida na Qawlan Baligha ndani yake,
kwani Nabii Sulayman amejitambulisha kua yeye ni Sulayman alietumwa na Muumba
kufikisha ujumbe kwa walengwa wa Ujumbe huo kua wajisalimishe kwa Mola wao bila
ya matatizo yeyote.

Na hivyo ndivyo wanavyofikisha ujumbe wao Mitume wa Allah Subhanah wa Ta’ala


kama walivyoambiwa Nabii Musa na Nabii Harun wamwambie Fir’awn kua: ‘Qad
ji/naka bi-ayatin min rabbika waalssalamu AAala mani ittabaAAa alhuda’ yaani
Kwani kwa hakika tumekuja na Dalili kutoka kwa Mola wako. Na Usalamaa utakua
juu ya yule mwenye kufuata Uongofu wake Mola wako.

Hivyo Nabii Musa na Nabii Harun kwa pamoja wakafunga safari hadi kwa Fir’awn,
ambapo kuna wanaosema kua hawakuenda kuonana nae moja kwa moja kwanza bali
walikaa kwenye geti la kuingilia kwenye Kasri lake kwa mda ambapo kuna kuna walinzi
kadhaa, hadi pale Askari hao walipohoji, kama vile ilivyo leo hii huwezi kuonana na
wenye Mamlaka mpaka uwe na miadi nao, hivyo ukisimama kwenye Mageti ya watu
kwa mda basi lazima uulizwe kwanini ukasimama hapo.
611

Na Nabii Musa na Nabii Harun walipoulizwa kwa nini wakasimama hapo hapo kwa mda
mrefu basi nao wakahoji ni kwani hairuhusiwi kusimama hapo wakati Ardhi yote ni ya
Muumba wa Ulimwengu wote ambae ni Allah Subhanah wa Ta’ala?

Haya yalikua ni maneno ambayo ni yenye kuenda kinyume na mitizamo ya watu wa


Misri kwani kwao wao Mungu ni mmoja tu ambae ni Fir’awn, hakuna mwengine zaidi
yake, na kuamini vyeginevyo hua ni kosa kubwa la Jinai ambalo linahukumiwa na
hakimu Mkuu wa Misri ambae ni Fir’awn mwenyewe. Hivyo habari ya kesi hii
akapelekewa Fir’awn, ambae alikua kwenye kiako cha Baraza lake na Mawaziri wake,
haraka sana akataka awaone hao wenye mtizamo huo ni kina nani, hivyo akaamrisha
waletwe mbele yake.

Nabii Musa na Nabii Harun wakakamatwa na kufikishwa mbele ya Mahkama yenye


Wazee wa Baraza wa Watu wa Misri inayoongozwa na hakimu Mkuu Fir’awn kwa kosa
la Jinai la kumkanusha Mungu wa Watu wa Misri ambae ni Fir’awn mwenyewe. Firawn
alipomuona Nabii Musa na Nabii Harun wanaingizwa ndani kwenye eneo la baraza yao
wanayokaa na kujadiliana na kutoa hukumu ya mambo mbali mbali ya Mamlaka yao basi
akashangaa sana kua imekuaje leo hii watu wawili hao yaani Musa aliemlea mwenyewe
na Harun ambae ni mmoja kati ya watu wa Bani Israil wakawa ni wenye kumkanusha
yeye na hivyo kua ni wenye kutangazia kuwepo kwa Mamlaka ya Ufalme wa Mungu
mwengine katika Ardhi yake hio.

Anasema Hasan Al Basr kua: ‘Nabii Musa alipoingia ndani kwenye kasri la Fir’awn,
basi Nabii Musa alikua ni mwenye kusema ndani ya Moyo wake kua; ‘Hakuna Mola
anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokua Allah Subhanah wa Taa’ala, ambae ndie
mwingi wa Subra mwingi wa Hikma. Shukrani zote anastahiki yeye ambae ndie
Muumba wa Mbingu Saba na Ardhi Saba na kila kitu kilichomo ndani yake. Yeye
ndie Mola wa Arshi Tukufu. Salama na Amani ziwe juu ya Mitume, na utukufu ni
wako pekee ewe Mola wa Ulimwengu wote. Kutokana nawe Mola wangu tunajilinda
na Mauaji yake na Madhara yake na tunaomba Ulinzi wako kwa kila namna
utakavyoweza kutulinda.’’.

Baada ya maneno hayo basi Moyo wake Nabii Musa ukawa umetulia na ni wenye
kujiamini sana na vya kutosha kwani ameuwakilisha kwa m-bora wa wenye kutegemewa
kwa kila kitu na katika kila sehemu. Na walipowasili mbele yake basi Fir’awn
akamuuliza kwa kejeli kama kwamba hawajui watu hao na ambao hawana darja yeyote
mbele yake: ‘Ah! Nyinyi ndio kina nani?’ Nabii Musa ajaibu: ‘Sisi ni Mitume wa Allah
Subhanah wa Ta’ala, Mola wa Ulimwengu wote, na kila kilichomo ndani yake’

Fir’awn akatabasam huku akijiuliza Mas-khara gani haya unayotuletea ewe Musa, hivyo
akamhoji Nabii Musa kwa kusema kua ‘Hivi ni nani mwengine aliekulea wewe Musa
tangu ulipokua mtoto mdogo wakati hata mnyonyeshaji ulikua huna na
612

ukatafutiwa, ukakua hadi kuanza kusema wakati ulikua hujui, ukavishwa vizuri na
kulishwa tangu mdogo mpaka ukawa mkubwa kwa miaka na miaka, kisha ukaasi
na kukimbia Misri kama sio mimi? Ama kweli wewe umekua ni mwenye kupingana
nami wazi wazi’ kama zinavyosema aya:

ِِ ِ ِ ْ‫ﻚ ﻓِﻴﻨَﺎ وﻟِﻴﺪاً وﻟَﺒِﺜ‬


‫ﻚ ٱﻟﱠِﱴ‬ َ ‫ﲔ ۞ َوﻓَـ َﻌ ْﻠ‬
َ َ‫ﺖ ﻓَـ ْﻌﻠَﺘ‬ َ َ َ َ ِّ‫ﺎل أََﱂْ ﻧـَُﺮﺑ‬
َ ‫ﺖ ﻓﻴﻨَﺎ ﻣ ْﻦ ﻋُ ُﻤ ِﺮَك ﺳﻨ‬ َ َ‫﴿ﻗ‬
﴾‫َﻧﺖ ِﻣﻦ ٱﻟْ َﻜﺎﻓِ ِﺮﻳﻦ‬
َ َ َ ‫ﺖ َوأ‬ َ ‫ﻓَـ َﻌ ْﻠ‬
Qala alam nurabbika feena waleedan walabithta feena min AAumurika sineena;
WafaAAalta faAAlataka allatee faAAalta waanta mina alkafireena; Qala
faAAaltuha idhan waana mina aldhdhalleena (Surat Ash Shuara 26:18-22)

Tafsir: Akasema (Fir’awn kumuuliza Nabii Musa): Hivi sio sisi tuliokulea wewe
pamoja nasi wakati ulipokua mtoto? na ukaishi kwa miaka mingi uliyoishi pamoja
nasi? Na ukafanya mambo yako uliyoyafanya? Na kwa hakika wewe ni miongoni mwa
wenye kukufuru’

Fir’awn akaendelea kumhoji Nabii Musa kwa kusema: ‘Na mbali ya kukulea na
kukufanyia kila kitu, na kusihi kama nianavyoisihi mimi na kufanya kila kitu
nikifanyacho, lakini hukuwa na shukrani na badala yake ukayafanya mauaji
uliyoyafanya, kwa kutuulia mmoja kati ya Watu wetu, na kisha unarudi kupingana
na Imani yetu.’

Nabii Musa akajibu hoja hizo mbele ya Fir’awn kwa kusema:

‫ﺪت ﺑَِﲎ‬
‫ﱡﻬﺎ َﻋﻠَ ﱠﻰ أَ ْن َﻋﺒﱠ ﱠ‬ ِ َ ‫ﺎل ﻓَـﻌ ْﻠﺘُـﻬﺂ إِذاً وأ ََ�ْ ِﻣﻦ ٱﻟﻀﱠﺎﻟِّﲔ۞ وﺗِْﻠ‬ ﴿
َ ‫ﻚ ﻧ ْﻌ َﻤﺔٌ َﲤُﻨـ‬ َ َ َ َ َ َ َ َ‫ﻗ‬
﴾‫إِ ْﺳﺮاﺋِﻴﻞ‬
َ َ
Qala faAAaltuha idhan waana mina aldhdhalleena; Fafarartu minkum lamma
khiftukum fawahaba lee rabbee hukman wajaAAalanee mina almursaleena;
Watilka niAAmatun tamunnuha AAalayya an AAabbadta banee isra-eela (Surat
Ash Shuara 26:18-22)

Tafsir: Nabii Musa akasema: ‘Nilifanya hayo wakati nilipokua miongoni mwa
waliopotea, hivyo nikakimbia kutoka kwenu kutokana na kukuogopeni. Lakini Mola
613

wangu. Amenijaalia Hikma na amenijaalia kua miongoni mwa Mitume wake. Na hio
neema yako uliyonifadhilisha mie (imekua ndio sababu) kuwazuia watu wa Bani
Israil?’

Yaani Nabii Musa anamwambia Fir’awn kua hakika mimi nilifanya hivyo kwa sababu
nilikua ni sawa na wewe yaani miongoni mwa waliopotea na wasiokua na uongofu, na
nikakimbia kwa kuogopa kulipiziwa kisasi cha kufanya kosa ambalo sikulikusudia, kua
nimpige ngumi moja ili nimuue, na ndio maana nimerudi sasa hivi mbele yako nikiwa ni
mwenye kupata uongofu kutoka kwa Mola wangu na kujaaliwa kupewa Utume kutokana
na Ukarimu wake juu yangu ambapo ni tofauti nawe ambae ulitaka kunipa adhabu ya
Kifo kutokana na ukatili wako.

Nabii Musa akamhoji Fir’awn hivi inakuaje kua unasema umenifadhili wakati ni mfumo
wako wa kuwatesa na kuwaua watoto wa kiume wa Bani Israil ndio uliopelekea mimi
kuingia kwenye njia ya maisha ya kutumbukizwa mtoni na kisha kua ni mwenye
kulelewa nawe, ndani ya jumba lako?

Kisha Nabii Musa akaendelea kusema kwa kutumia kauli laini yenye onyo ndani yake
ambalo ni la kutomlenga Fir’awn na watu wake moja kwa moja kua kama Fir’awn na
watu wake wakipingana na ujumbe wao kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala basi
watafikwa na adhabu kali sana, lakini badala yake akasema kua:

﴾‫ب وﺗَـﻮﱠ ٰﱃ‬ ‫ﱠ‬


‫ﺬ‬ ‫ﻛ‬
َ ‫ﻦ‬‫ﻣ‬ ‫ﻰ‬ ‫ﻠ‬
َ ‫ﻋ‬ ‫اب‬ ‫ﺬ‬
َ ‫ﻌ‬ ‫ﻟ‬
ْ ‫ٱ‬ ‫ﱠ‬
‫ن‬ َ
‫أ‬ ‫ﺂ‬َ‫ﻨ‬‫ـ‬ ‫ﻴ‬َ‫ﻟ‬ ِ ‫﴿إِ ﱠ� ﻗَ ْﺪ أ‬
ِ‫ُوﺣﻰ إ‬
ََ َ َ ٰ َ َ َ ْ َ
Inna qad oohiya ilayna anna alAAadhaba AAala man kadhdhaba watawalla (Surat
Ta-Ha 20:48)

Tafsir: Kwa hakika tumeshushiwa sisi kua Adhabu kali itakua juu ya yule atakaepinga
na kugeukia upande wa pili.’ ’

Fir’awn akaona kua Nabii Musa anamletea maneno ya maajabu kabisa ambayo hayana
mfano wake huku akiwa ni mwenye kutaka kumshinda kwa hoja. Na Nabii Musa na
Nabii Harun imewahusu nini kutaka kuingilia Mamlaka yake Fir’awn hivyo moja kwa
moja akaamua kuulizia kuhusiana na namna walivyojitambulisha Nabii Musa na Nabii
Harun kua ni Mitume wa Mola wa Ulimwengu:

﴾‫ﻮﺳ ٰﻰ‬ َ َ‫﴿ﻗ‬


َ ُ‫ﺎل ﻓَ َﻤﻦ ﱠرﺑﱡ ُﻜ َﻤﺎ ٰﳝ‬
614

Qala faman rabbukuma ya moosa (Surat Ta-Ha 20:49)

Tafsir: Akasema (Fir’awn) Na Jee ni Nani Huyo Mungu wenu Ewe Musa?

Ambapo Nabii Musa akajibu:

ٍ ‫ﺎل رﺑـﱡﻨﺎ ٱﻟﱠ ِﺬ ۤي أَﻋﻄَﻰ ُﻛﻞ ﺷ‬


﴾‫ﻲء َﺧ ْﻠ َﻘﻪُ ﰒُﱠ َﻫ َﺪ ٰى‬ َ ‫ْ ٰ ﱠ‬ َ َ َ َ‫﴿ﻗ‬
Qala rabbuna alladhee aAAta kulla shay-in khalqahu thumma hada (Surat Ta-Ha
20:50)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa) Mola wetu ni yule ambae amekipa kila kitu Maumbile
yake na kisha akakiongoza.

Yaani Nabii Musa anamuwekea wazi Fir’awn na watu wake kua Allah Subhanah wa
Ta’ala ndie ambae ameumba kila kitu katika maumbile tofauti na yanayopendeza na
kasha akajaalia mahitaji yote yanayohitajika na vitu hivyo na kuvionesha njia ya kupata
mahitajio yao bila ya shida wala matataizo yeyote, kwa mfano alivyojaalia mimea kua ni
yenye kupata mahitajio yake ya maji na madini mbali mbali ardhini na angani kupitia
mionzi ya jua kwa ajili ya kutengeneza chakula chake, alivyojaalia wadudu kua ni wenye
kula kutokanana vinavyoota ardhini, ambao nao huliwa na ndege ambao aliowajaalia kua
ni wenye kuruka angani kwa kutumia hewa iliyomo angani ndani yake, kama vile
alivyojaalia maji kua na uzito ili Meli ziweze kuelea juu yake, na kua na wepesi
unaowawezesha samaki kua ni wenye kuelea na kuzama kwa namna watakavyo kutokana
na kua ni wenye kuhitaji kuishi ndani yake na wakawa ni wenye kula na kuchuja hewa
ndani ya Maji.

Allah Subhanah wa Taa’ala amejaalia Wanyama kua ni wenye kutegemea Mimea


inayoota ardhini kwa ajili ya chakula chao, na akawajaalia wanyama wengine kuwahitaji
wanyama hao wanaokula majani kwa ajili ya chakula chao, kama vile alivyojaalia Tai,
Simba na Chui kua ni wenye kula wanyama wenzao kama Sungura, Paa, Punda, Nyati
n.k na pia alivyojaalia Ibn Adam kua ni mwenye kula vitokanavyo na Mimea na wanyama
walao mimea hio kama Kuku, Sungura, Paa, Mbuzi, Ngombe, Ngamia, n.k na akaajalia
wengineo kua ni kwa ajili ya kuwarahisishia kazi zao Ibn Adam, kama Punda, Farasi,
Ngamia, n.k.

Na ingawa katika maneno ya ayah hii basi Nabii Musa tayari ameshazungumzia kila kitu
kilichoumbwa na Allah Subhanah wa Taa’la na kutaja sifa yake ya usimamizi wake juu
ya vitu hivyo lakini Fir’awn bado alikua ni mwenye kutaka kumkwamisha kwa hoja
Nabii Musa akaendelea kuuliza:
615

﴾‫ﲔ‬ ِ ‫ﺎل ﻓِْﺮ َﻋ ْﻮ ُن َوَﻣﺎ َر ﱡ‬


َ ‫ب ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬ َ َ‫﴿ﻗ‬
Qala firAAawnu wama rabbu alAAalameena(Surat Ash Shuara 26:22)

Tafsir: Akasema Fir’awn na ni nani huyo Mola wa Ulimwengu wote?

Hivyo Nabii Musa akajibu kwa kutumia njia ya Kumelezea Allah Subhanah wa Ta’ala
kupitia katika Sifa zake tukufu na Mamlaka yake yaliyoenea katika kila sehemu
Ulimwenguni.

ِِ ِ ‫ب ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬
َ ‫ض َوَﻣﺎ ﺑَـْﻴـﻨَـ ُﻬ َﻤﺂ إِن ُﻛﻨﺘُ ْﻢ ﱡﻣﻮﻗﻨ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ ‫ات َوٱﻷ َْر‬ َ َ‫﴿ﻗ‬
َ َ ‫ﺎل َر ﱡ‬
Qala rabbu alssamawati waal-Ardhi wama baynahuma in kuntum mooqineena
(Surat Ash Shuara 26:23)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa) Mola wa Mbingu na Ardhi na kila kilichomo baina yake
kama ikiwa nyinyi ni wenye kutaka kujithibitishia kwa uhakika.

Huku Nabii Musa akibainisha kua anaemlenga kwa ujumbe huo kua si Fir’awn peke
yake, bali yeye na Baraza zima la Mawaziri wake kwa kutilia mkazo kua watafakari uzito
wa ujumbe wake anaowafikishia na kuwabainishia uhalisi wa maumbile ya Ulimwengu
na Muumba wake ulivyo katika maneno yasemayo in kuntum mooqineena yaani Kama
ikiwa nyinyi ni wenye kutaka kujithibitishia kwa uhakika.

Fir’awn akatabasam kwa kuona kua sasa huyu Kijana aliemlea mwenyewe, aliempenda
na kumtunza kama alivyokua akijitunza yeye mwenyewe kua anaonesha dharau na hivyo
anataka kufanya mzaha mbele yake na baraza lake la Mawaziri, hivyo Fir’awn
akawageukia Mawaziri wake huku akiwauliza ili wathibitishe kua aliyoyasema Nabii
Musa mbele yao wameyasikia au ameyasikia yeye kwa masikio yake peke yake tu. Hivyo
akauliza huku akicheka:

﴾‫ﺎل ﻟِﻤ ْﻦ َﺣﻮﻟَﻪُ أَﻻَ ﺗَﺴﺘَ ِﻤﻌُﻮ َن‬ ﴿


ْ ْ َ َ َ‫ﻗ‬
Qala liman hawlahu ala tastamiAAoona (Surat Ash Shuara 26:25)

Tafsir: Akasema (Fir’awn) kuwaambia wale waliomzunguka: ‘Jee Hamkumsikia?


(alichokisema)’
616

Mawaziri hao nao wakacheka sana kuthibitisha kua wamesikia maneno asemayo Nabii
Musa lakini hawayatilii maanani na hawakubaliani nayo kwa sababu hawajawahi kusikia
kuhusiana na Mungu huyo abadan na Mungu wao wanaomjua wao ni Fir’awn. Hivyo
wanasubiri kauli kutoka kwa Fir’awn ambae akaendelea kumhoji Nabii Musa na Nabii
Harun.

﴾‫ُوﱃ‬ ِ ‫ﺎل ﻓَﻤﺎ ﺎﺑ ُل ٱﻟْ ُﻘﺮ‬


ٰ َ ‫ون ٱﻷ‬ ﴿
ُ َ َ َ َ‫ﻗ‬
Qala fama balu alqurooni al-oola (Surat Ta-Ha 20:51)

Tafsir: Akasema (Firáwn): ‘Jee ni ni hali yao wale waliotangulia kabla yetu?’

Yaani Fir’awn anamhoji Nabii Musa kua kama kweli kuna Mungu, alieumba kila kitu na
kukipa muongozo, kwa nini watu waliotangulia kabla yao basi hawakumuabudu Mola
wao? Ufahamu wao na akili zao ilikuaje ukawakoseshea uongofu? Jee walikua hawana
Akili na Ufahamu? Ina maana wameangamia au vipi?

Ambapo Nabii Musa akaona kua kwa kua Watu hao bado hawajawa ni wenye kutafakari
na kutaka kujithibitishia ujumbe wake kwa vithibitisho vilivyowazi basi yeye inambidi
haraka sana afafanue kwa kutoa hoja zaidi kabla ya hata Fir’awn kutoa hoja nyengine,
hivyo Nabii Musa kwanza akaweka wazi kumwambia Fir’awn na watu wake kua Mola
wao wanaomzungumzia wao ambae ndie aliewatuma kwa Fir’awn na watu wake si Mola
mwengine yeyote isipokua ndio huyo huyo Mola wa hao mababa zao watu waliotangulia
hapo kabla yao, kwa kusema:

﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ‫ب‬ َ َ‫﴿ﻗ‬


َ ‫آﺂﺑﺋ ُﻜ ُﻢ ٱﻷَﱠوﻟ‬
َ ‫ﺎل َرﺑﱡ ُﻜ ْﻢ َوَر ﱡ‬
Qala rabbukum warabbu aba-ikumu al-awwaleena (Surat Ash Shuara 26:26)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa) Mola wenu na ni Mola wa Mababa zenu waliotangulia
kabla yenu.

Na kutokana na kua Allah Subhanah wa Ta’ala ndie Mola wa Ulimwengu na kila kitu
kilichomo ndani yake basi ni mwenye kujua juu ya kila kitu na juu ya hao Mababa zao
pia, na miongoni mwa sifa zake tukufu ni kua kwa hakika yeye si mwenye kusahau wala
si mwenye kughafilika juu ya kitu chochote kile, na hivyo basi hakuna anaejua kuhusiana
na hatma ya watu hao isipokua ni kua hatma yao iko kwake yeye Muumba aliewaumba,
na hivyo yeye ndie mwenye kujua hali yao iko vipi huko waliko na pia itakua vipi hapo
baadae, hivyo Nabii Musa akabainisha haya kwa kusema:
617

ِ
﴾‫ﻀ ﱡﻞ رِّﰉ وﻻَ ﻳَﻨﺴﻰ‬ ٍ ِ ِ َ ‫ﺎل ﻋِ ْﻠﻤﻬﺎ ِﻋ‬
َ َ َ َ‫ﻨﺪ َرِّﰉ ﰱ ﻛﺘَﺎب ﻻﱠ ﻳ‬ َ ُ َ َ‫﴿ﻗ‬
Qala AAilmuha AAinda rabbee fee kitabin la yadhillu rabbee wala yansa. (Surat Ta-
Ha 20:52)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa) Ilm kuhusiana nao (Watu jao waliotangulia kabla yao)
ipo kwa Mola wangu, imehifadhiwa kitabuni, kwani hakosei Mola wangu na wala
hasahau.

Hivyo Fir’awn alihoji kuhusiana na watu waliotangulia kabla yao ili kuchochea hisia za
hasira za watu dhidi ya Nabii Musa na Nabii Harun kutokana na kua watu hao walikua
ni wenye kuwatukuza watu waliotangulia kabla yao ambao ni wazee wao, lakini hata
hivyo Nabii Musa kutokana na Hikma zake alizopewa na Mola wake basi alijibu
inavyotakiwa na hivyo kuwarudisha watu kutoka kwenye hisia za hasira na kuwaingiza
kwenye hisia za kubainishiwa juu ya Uwezo wa Mola wao juu yao.

Na kasha baada ya mahojiano hayo na vithibitisho vyake Nabii Musa basi


akawabainishaa malengo yake makuu juu ya Fir’awn na watu wake hao kwa njia ya
kuwashauri kwa huruma na upole kwa kusema:

ِ ‫﴿ﻫﻞ ﻟﱠﻚ إِ َ ٰﱃ أَن ﺗَـَﺰﱠﻛﻰ‬


َ ِّ‫ﻚ إِ َ ٰﱃ َرﺑ‬
﴾‫ﻚ ﻓَـﺘَ ْﺨ َﺸ ٰﻰ‬ َ َ‫۞وأ َْﻫﺪﻳ‬
َ ٰ َ َ
Hal laka ila an tazakka; Waahdiyaka ila rabbika fatakhsha; (Surat An Naziat 79:18-
19)

Tafsir: ‘Jee utajitakasa Nafsi yako (Kutokana na Kufr)? Nami nitakuongoza kwa Mola
wako ili umuogope na kumtii?

Ambapo Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi anasema kuhusiana na maneno
ya ayah ii kua: ‘Yule mwenye kuoa na khofu basi hua ni mwenye kusafiri usiku
kucha, na yule anaesafiri usiku kucha basi bila ya shaka atafikia sehemu anayotaka
kwenda.’

Naam, bila ya shaka, lakini hata hivyo kwa upande wa Fir’awn yeye hana khofu, na wala
hataki kusafiri kwa kuihamisha Nafsi yake kutokana katika kufru na kuiingiza katika
Nuru anayooneshwa na Nabii Musa na Nabii Harun hivyo akasema kuwaambia Mawaziri
wake kua:
618

﴾‫ﺎل إِ ﱠن ر ُﺳﻮﻟَ ُﻜﻢ ٱﻟﱠ ِﺬ ۤي أ ُْرِﺳﻞ إِﻟَْﻴ ُﻜﻢ ﻟَﻤ ْﺠﻨُﻮ ٌن‬ ﴿
َ ْ َ ُ َ َ َ‫ﻗ‬
Qala inna rasoolakumu alladhee orsila ilaykum lamajnoonun (Surat Ash Shuara
26:27)

Tafsir: Akasema (Fir’awn): ‘Kwa hakika Mtume wenu mliotumiwa juu yenu ni
alietokwa na Akili.’

Aya imetumia neno Majnun ambalo ni lenye kutokana na neno Janna la Kiarabu ambalo
hua ni lenye kumaanisha Kua na Kiza, Kufichika, Kutoonekana, Kufurahia kitu sana
mpaka Mtu akachanganyikiwa, Kuondokewa na Akili kutokana na Furaha Kubwa sana
au Kutokana na Huzuni kubwa sana.

Subhanah wa Allah! Hali hii ya kua ni Majnun kutokana na kitu Fulani ndio aliyoisema
Hasan Al Basr kuwaambia watu Tabii Tabiina, yaani wale walioishi huku wakiwa
hawajawahi kuwaona Masahaba kua: ‘Hakika mimi nimewaona Masahaba
waliopigana vita vya Badr walivyokua wakiishi, na nakuoneni mnavyoishi nyie, na
leo hii kama Masahaba hao watafufuka basi nyinyi mtawaona wao kua ni
Waliochanganyikiwa kwa namna wanavyoishi na wanavyomuamini na kumuogopa
Allah Subhanah wa Ta’ala na wao watakuoneni nyinyi kua hamkumuamini Allah
Subhanah wa Ta’ala kutokana na mnavyoishi.’

Hivyo Fir’awn tayari ameweka wazi kua Mitume hao waliotumwa katika Ardhi ya nchi
ya Misri, hawakutumwa kwa ajili yake kwani haendani nao kimtizamo na hivyo labda
wametumwa kwa Mawaziri wake na kwa watu wengine waliochini yake tu hivyo yeye
hahusiki nao abadan kwani yeye ni ndio Mungu na hivyo mwenye akili zaidi, na Mitume
hao waliopo mbele yao ni waliochanganyikiwa na kutokwa na akili kutokana na kuamini
jambo lao hilo la kua na sifa ya Utume kiasi ya kua hawaoni wala hawasikii chochote
badala yake.

Kusikia maneno hayo basi Nabii Musa akaona kua inabidi afafanue zaid kuhusiana na
Mola wake, na huenda labda watu hao pamoja na Fir’awn watamfaham vizuri zaidi na
kubadilisha mtizamo wao, na kama watatafakari basi wataona wazi kua yeye si
mwendawazimu bali ni mwenye hikma na busara kubwa na jambo analowausia si kamwe
si kwa ajili ya maslahi ya Nafsi yake bali ni kwa ajili ya maslahi na manufaa ya Nafsi
zao, hivyo akawaambia kwa kusema:

﴾‫ب وَﻣﺎ ﺑَـْﻴـﻨَـ ُﻬﻤﺂ إِن ُﻛﻨﺘُﻢ ﺗَـ ْﻌ ِﻘﻠُﻮ َن‬


ِ ِ َ َ‫﴿ﻗ‬
ْ َ َ ‫ب ٱﻟْ َﻤ ْﺸ ِﺮق َوٱﻟْ َﻤ ْﻐ ِﺮ‬
‫ﺎل َر ﱡ‬
619

Qala rabbu almashriqi waalmaghribi wama baynahuma in kuntum taAAqiloona


(Surat As Shuara 26:28)

Tafsir: Akasema: (Mola Wangu nnaekuusieni juu yake ni) Mola wa Mashariki na
Magharibi na kila kilichomo ndani yake baina yake, kama mtatumia akili zenu (basi
mtafaham).

Yaani hapa katika kuelezea Mamlaka na Ukubwa wake Allah Subhanah wa Ta’ala basi
Nabii Musa anajaribu kuwaelimisha watu hao kua kama wao wanajihesabu kua ndio
watawala wa eneo la Ardhi ya Misri, na kiongozi wao ndio Mungu wao, basi Mungu
anaewausia yeye Nabii Musa si tu ndie Mola wa eneo hilo la Misri lakini ni Mola wa
eneo lote la Ulimwengu mzima kuanzia Mashariki mpaka Magharibi na ndie mmiliki wa
kila kitu kilichomo ndani yake, hivyo kama wakitumia akili zao basi watajua kua hakuna
anaestahiki kuabudiwa isipokua Mola huyo ambae ni Allah Subhanah wa Ta’ala mwenye
Uwezo juu ya Kila kitu na mwenye Ukubwa zaidi ya kila kitu, kwani yeye ndie alieumba
kila kitu.

Ambapo kauli hii ilimkera sana Fir’awn, kwani ilikua ni yenye kumtuhumu yeye na
Mawaziri wake kua wao ni wenda wazimu na si watu wenye kutumia akili zao. Na anajua
kua kama wakitumia akili zao basi watauona wazi ukweli halisi ulivyo, na huenda
wakafumbuka macho na kuamua kuachana na kumuamini Fira’wn kua ni Mungu ambapo
jambo hili litatishia Nguvu na uwezo mkubwa wa Mamlaka yake,

Kwani Mamlaka ya Fir’awn yalikua makubwa kutokana na kua watu wake walikua
wakiamini pia kua Fir’awn ndio chanzo cha nguvu ya kijeshi na ya kiuchumi mzuri na
baraka waliyokua nayo watu wa Misri, na raha wanayoipata kutokana na kua ni wenye
kufanyiwa kila kitu na watu wa Bani Israil na ndio maana wakawa wanamtukuza Fir’awn
na kua wanafanya kama anavyowaamrisha Fir’awn katika kila kitu ikiwemo
kuwatumikisha watu wa Bani Israil kwa ajili ya kazi zao mbali mbali, Hivyo basi
akasema Fir’awn kuwatishia Mawaziri wake kua atawafanya kua Wafungwa na
watafanya kazi kamam Watumwa kama walivyokua watu wa Bani Israil kama watakua
ni wenye kupingana na Umungu wake na hivyo kua ni wenye kupingana pia na Mamlaka
yake kwa kuwaambia Mawaziri wake kua:

﴾‫ﲔ‬ ِ ِ َ ‫ﺎل ﻟَﺌِ ِﻦ ﱠٱﲣَ ْﺬت إِﻟَـٰﻬﺎً َﻏ ِﲑى ◌ﻷَﺟﻌﻠَﻨ‬


َ َ‫﴿ ﻗ‬
َ ‫ﱠﻚ ﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻤ ْﺴ ُﺠﻮﻧ‬ َْ َ ْ َ
Qala la-ini ittakhadhta ilahan ghayree laajAAalannaka mina almasjooneena (Surat
As Shuara 26:29)
620

Tafsir: Akasema (Firawn): ‘Kama mtachukua Mola zaidi yangu basi nitakujaalieni
kua ni wenye kufungwa Jela’

Khofu ikawajaa Mawaziri hao, kwani wakaanza kuona hatari ya kua Wafungwa na
Watumwa kama watu wa Bani Israil, kwani wanajua adhabu wanayoipata watu hao kua
haistahamiliki, hususan kwa mtu mwenye kuzoea raha ya kua na Madaraka. Hali hii ya
khofu hua haishangazi kwani ni hali ambayo ni ya kimaumbile na ndio mtihani wa wengi
sana miongoni mwetu leo hii yaani wale wenye kuendekeza matamanio ya kidunia hua
wanashindwa kuidhibiti aina hii ya hisia ya khofu, na hivyo kua ni watumwa wa watu
wenye Mamlaka zaidi yao na pia watumwa wa wenye Mali zaid yao.

Nabii Musa akaona kua sasa mambo yashaanza kua hayadhibitiki, kwani mahojiano
yamekua makali sana kama alivyotegemea yatakavyokua mbali ya kua amekua ni
mwenye kutumia kauli laini, zisizokua na munkar wala jazba ndani yake kwani
amejitahid kua ni mwenye kutumia neema ya Hikma, Busara na Ushauri aliopewa na
Mola wake yaani Allah Subhanah wa Ta’ala.

Nabii Musa akaona kua anatakiwa ajipange upya hivyo akatafakari achukue hatua gani
zaid, ili afanikishe malengo yake na hivyo kua ni mwenye kurasahisisha uzito wa jukumu
alilopewa na Mola wake ambae katika wakati huo yuko pamoja nae na ni mweny ekusikia
kila kitu na ni mwenye kuona kila kitu, na hapo hapo Allah Subhanah wa Taa’ala
akamjaalia Nabii Musa kukumbuka kua amepewa silaha mbili zenye uzito na maajabu
ya kipee ambazo bado hajazitumia, hivyo akaona kua kwa kua mambo yanataka kutoka
nje ya udhibiti wake basi akaona kua umefika wakati wa kutumia hizo silaha mbili
ambazo ni muhimu sana kwake, na hivyo Nabii Musa akasema:

ٍ ‫ﺎل أَوﻟَﻮ ِﺟﺌـﺘﻚ ﺑِﺸ‬


ٍ ِ‫ﻲء ﱡﻣﺒ‬
﴾‫ﲔ‬ َ َ ُ ْ ْ َ َ َ‫﴿ﻗ‬
Qala awa law ji/tuka bishay-in mubeenin (Surat As Shuara 26:30)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa): Jee hata kama nikikutoleeni kitu kitakacho
kubainishieni?

Maneno haya yalimtuliza kidogo Fir’awn kwani aliona kua sasa hivi Nabii Musa
amejiingiza mwenyewe ndani ya mtego alioutega mwenyewe, kwani ikiwa ameshidnwa
kuwathibitishia Mawaziri hao mbele yake basi ana nini zaidi kitakachoweza
kuwathibitishia wasadiki ujumbe wake, hivyo akamwangalia Nabii Musa na kisha
akamwambia kwa kusema:
621

﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ‫ت ﺑِِﻪ إِن ُﻛﻨﺖ ِﻣﻦ ٱﻟ ﱠ‬


ِ ْ‫ﺎل ﻓَﺄ‬
َ َ‫﴿ﻗ‬
َ ‫ﺼﺎدﻗ‬ َ َ
Qala fa/ti bihi in kunta mina alssadiqeena (Surat As Shuara 26:31)

Tafsir: Akasema (Fir’awn) utoe uthibitisho wako kama wewe ni kusema Kweli.

Nabii Musa akamshukuru Mola wake kwa kumpa silaha mbili hizo na kua ni mwenye
kujaaliwa kua na uwezo wa kuzitumia kwa kutoa vithibitisho hivyo na kwa kua ni
mwenye kupewa Nafasi ya kutoa vithibitisho hivyo mbele ya Fir’awn, na kua na uwezo
wa kufikisha ujumbe huo peke yake kwa utulivu bila ya wasi wasi wowote huku Waziri
wake yaani Nabii Harun akiwa amesimama pembeni yake akisubiri, kusaidia kutoa au
kujibu hoja kama ikihitajika msaada wake. Kwa sababu baadhi ya wakati hoja
zinapotolewa na kuungwa mkono na watu wawili basi hua zina nguvu zaidi kuliko zikiwa
ni za mtu mmoja.

Hivyo Nabii Musa akaamua kutumia silaha zake mbili hizo alizopewa na Mola wake kua
ni kama vithibitisho vyake kama zinavyobainisha aya:

ِ ِ ‫﴿ﻓَﺄَﻟْ َﻘﻰ ﻋﺼﺎﻩ ﻓَِﺈ َذا ِﻫﻰ ﺛـُﻌﺒﺎ ٌن ﱡﻣﺒِﲔ۞ وﻧَـﺰع ﻳ َﺪﻩ ﻓَِﺈ َذا ِﻫﻰ ﺑـﻴ‬
﴾‫ﱠﺎﻇ ِﺮﻳﻦ‬
َ ‫ﻀﺂءُ ﻟﻠﻨ‬
َ َْ َ ُ َ ََ َ ٌ َْ َ ََُ ٰ
Faalqa AAasahu fa-idha hiya thuAAbanun mubeenun; WanazaAAa yadahu fa-
idha hiya baydhao lilnnadhireena (Surat As Shuara 26:32-33)

Tafsir: Hivyo (Nabii Musa) akaitupa Fimbo yake, kisha ikawa Joka kubwa lenye
kubainika, na kisha akautoa mkono wake ukawa ni mweupe kwa wenye kutizama na
kuona

Hivyo Nabii Musa akaitupa chini fimbo yake, na hapo hapo fimbo hio ikageuka kua Joka
kubwa sana, kiasi ya kua ikawa tafrani kubwa sana kwenye ukumbi wa baraza la
mahojiano hayo na ingawa lilikua ni kubwa sana lakini lilikua halitoshi ukubwa wake,
kwani kila mtu aliekuwepo hapo basi alitaka kua mbali zaidi nan je kabisa ya Ukumbi
huo.

Na hata Fir’awn mwenyewe alishtuka na kujawa na khofu kubwa sana kiasi ya kua
aliruka na kutoka kwenye kiti chake cha enzi cha Umungu na Ufalme wake, kwani Joka
hilo lilikua likielekea katika upande wake, hivyo alipoona ukubwa wa hatari
anayokabiliana nayo katika wakati huu na yuko hatarini kupoteza maisha yake, basi
622

akamwambia Nabii Musa: ‘Ewe Musa nakuomba kwa Utukufu wa Mola wako, lizuie
Joka lako, nami nitawaachia watu wako’

Nabii Musa akasogea mbele kisha akainama na kuiokota Fimbo yake, ambayo baada ya
kuguswa tu na mikono yake ilibadilika kutoka katika maumbile ya Joka lenye kutisha na
kuingia kwenye Maumbile ya Fimbo ya Nabii Musa ya kuchungia wanyama wake.

Baada ya dakika kadhaa, tafrani kupungua na watu kurudi katika hali yao ya utulivu wa
kawaida, basi Nabii Musa akaunyanyua juu mkono wake wa Kulia kisha akauliza: ‘Jee
Mnauona mkono wangu huu?’. Fir’awn akasema: ‘Huo ni mkono wako kama
ilivyokua mikono ya kila mtu. Hivi jee unataka kutuoneshaa kitu gani cha maajabu
kutokana na Mkono wako huo?’

Nabii Musa akaingiza mkono wake ndani ya shingo ya Kanzu yake kuupelekea kushotoni
mwa kifua chake na alipoutoa nje yake basi mkono huo ukawa mweupe wenye Nuru
inayong’ara sana zaidi ya kioo kinachoangazwa na mionzi ya jua kali la saa sita mchana,
mng’aro ambao kila mtu aliekuwepo hapo na aliekuwepo nje ya Ukumbi huo uliona na
kuuhisi hata kama mtu akiwa amefumba macho yake kutokana na kua ni wenye kuumiza
macho kwa weupe wake unapoutulizia mtizamo wa macho yako.

Watu waliokuwepo hapo, walishangazwa na mabadiliko ya Miujiza ya Mkono wake


Nabii Musa, na wakaanza kuyafinya macho yao na kuyafumba ili kuyazuia yasiathirike
na ukali wa Nuru ya muangaza wa Mkono wake. Kisha baada ya hapo Nabii Musa
akauingiza tena mkono wake ndani ya shingo ya Kanzu yake na akautoa huku ukiwa uko
katika hali ya kawaida kama ulivyokua hapo awali wakati alipokua akiingia kwenye
ukumbi wa Baraza hilo. Watu wote waliokuwepo hapo walishangazwa na kupigwa na
butwaa kutokana na maajabu ya Miujiza hio, ambapo wa kwanza uliwakimbiza kutokana
katika sehemu zao na huu wa pili uliwazuia na kuwagandisha kwenye sehemu zao.

Anasema Imam hmad Ibn Muhammad Ath Thalabi kua: ‘Kutokana na Miujiza hio,
basi Fir’awn alikua anakaribia kukubaliana na Uthibitisho wa Miujiza hio. Lakini
Hamman akasema kumwambia Firawn ‘Wewe ni Mungu unaeabudiwa, inakuaje
unataka kufuata Mtizamo wa Mtumwa’’

Kwani amesema Allah Subhanah wa Ta’ala kuhusiana na Hamman ambae tayari


trumeshamungalia historia yake hapo kabla katika kurasa zilizopita na Qarun ambae
tutamuelezea zaidi katika kurasa zinazofuatia, kwani hawa walikua ndio washauri wake
wakuu kuliko wote kua:
623

ْ‫ﲔ ۞ إِ َ ٰﱃ ﻓِْﺮ َﻋ ْﻮ َن َوَﻫ َﺎﻣﺎ َن َوﻗَ ُﺎرو َن ﻓَـ َﻘﺎﻟُﻮا‬


ٍ ِ‫ﺎن ﱡﻣﺒ‬ٍ َ‫﴿وﻟََﻘ ْﺪ أَرﺳ ْﻠﻨَﺎ ﻣﻮﺳ ٰﻰ ِﺂﺑ�ﺗِﻨَﺎ وﺳ ْﻠﻄ‬
َُ َ َ ُ َْ َ
﴾‫اب‬ ِ
ٌ ‫َﺳﺎﺣٌﺮ َﻛـ ﱠﺬ‬
Walaqad arsalna moosa bi-ayatina wasultanin mubeenin; Ila firAAawna
wahamana waqaroona faqaloo sahirun kadhdhabun (Surat Al Ghafir 40:24-25)

Tafsir: Na kwa Hakika tulimtuma Musa na aya zetu na vithibitisho vilivyowazi, kwa
Fir’awn na Hammana na Qaruun wakasema: ‘Mchawi! Muongo Mkubwa’

Hivyo maneno hayo yalimpa nguvu Fir’awn na kumuamsha kutokana na hisia za Utulivu
uliotawala ukumbini hapo. Na utulivu huu uliotokana na vithibitisho vya wazi vya Nabii
Musa na Nabii Harun kwa watu wake, ulimtia khofu Fir’awn na akaona kua huenda watu
wake hao wameshaanza kuvutiwa na vithibitisho walivyooneshwa, hivyo akakasirika na
kuingiwa na khofu ya kupoteza Mamlaka yake ya Kimungu na Kiutawala, akaamua
kuonesha dharau kutokana na kibri chake na kukebehi baadala ya kutumia subra na hikma
hivyo akasema kumwambia Nabii Musa kama zinavyobainisha aya:

ٍ َ‫﴿ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ ﺟﺂءﻫﻢ ﱡﻣﻮﺳﻰ ِﺂﺑ�ﺗِﻨَﺎ ﺑـﻴِﻨ‬


‫ﺎت ﻗَﺎﻟُﻮاْ َﻣﺎ َﻫـٰ َﺬآ إِﻻﱠ ِﺳ ْﺤٌﺮ ﱡﻣ ْﻔﺘَـًﺮى َوَﻣﺎ َِﲰ ْﻌﻨَﺎ‬ َّ َ ٰ َ ُ َ َ
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ‫ِﻬﺑـٰ َﺬا ِ ۤﰲ‬
َ ‫آﺂﺑﺋﻨَﺎ ٱﻷَﱠوﻟ‬ َ َ
Falamma jaahum moosa bi-ayatina bayyinatin qaloo ma hadha illa sihrun
muftaran wama samiAAna bihadha fee aba-ina al-awwaleena; (Surat Al Qasas
28:36)

Tafsir: Na kisha baada ya kuja Musa na aya zetu zenye kubainisha,(basi Fir’awn)
akasema: Nini Hiki isipokua ni Uchawi uliovumbuliwa, na hatukuwahi kusikia sisi
juu ya hili kutoka kwa Mababa zetu waliotangulia.

Ambapo hali ilikua ni tofauti na ni kinyume chake kwa upande wa Nabii Musa, na hii
inaweka wazi tofauti baina ya Nafsi iliyotawaliwa na Matamanio ya Kidunia kama ya
Fir’awn ambayo hua ni iliyojaa kiza cha Kufr na hivyo kua na Kibr na dharau na Nafsi
iliyotawaliwa na Matamanio ya Kiakhera, ambayo hua ni iliyojaa Nuru ya Imani kama
ya Nabii Musa ambae mbali ya kua ni mwenye kupea kiufaham na kihikma lakini pia ni
mwenye Imani kubwa kwa Mola wake basi akajibu hoja hio kwa kurudi tena kwa Mola
wake kwa kusema:
624

ِ ‫ﺎل ﻣﻮﺳﻰ رِ ۤﰊ أَﻋﻠَﻢ ِﲟﻦ ﺟﺂء ﺑِﭑ ْﳍ َﺪ ٰى ِﻣﻦ ِﻋ‬


‫ﻨﺪﻩِ َوَﻣﻦ ﺗَ ُﻜﻮ ُن ﻟَﻪُ َﻋﺎﻗِﺒَﺔُ ٱﻟﺪﱠا ِر‬ ْ ُ َ َ َ ُ ْ ّ َ ٰ َ ُ َ َ‫﴿ َوﻗ‬
﴾‫إِﻧﱠﻪُ ﻻَ ﻳـُ ْﻔﻠِﺢ ٱﻟﻈﱠﺎﻟِﻤﻮ َن‬
ُ ُ
Waqala moosa rabbee aAAlamu biman jaa bialhuda min AAindihi waman takoonu
lahu AAaqibatu alddari innahu la yuflihu aldhdhalimoona (Surat Al Qasas 28:37)

Tafsir: Na akasema Musa: ‘Mola wangu ni mwenye kujua juu ya yule ambae umemjia
Uongofu kutoka kwake, na ni nani atakae kua na mwisho wenye furaha. Kwani kwa
hakika hawatofuzu wale wenye kufanya dhulma’

Kwa upande mwengine basi Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea kwa kufafanua zaidi
hali ya matokeo ya mahojiano hayo makali yenye hoja nzito na vithibitisho baina
vilivyowazi ambapo mahojiano kama haya ndani ya Qur’an tunayaona kwenye kisa cha
Nabii Ibrahim tu, ambapo matokeo ya Mahojiano haya baina ya Nabii Musa hayana
mfano wake kwani hata kwa upande wa Nabii Ibrahim basi hakua ni mwenye kupata
matokeo yanayosikitisha na kutisha yanayotokana na ujinga kama matokeo aliyoyapata
Nabii Musa kutoka kwa Fir’awn kama inavyobainishwa na Allah Subhanah wa Ta’ala
pale aliposema katika Surat An Naziat kua:

۞‫ﺼ ٰﻰ۞ﰒُﱠ أ َْدﺑَـَﺮ ﻳَ ْﺴ َﻌ ٰﻰ۞ ﻓَ َﺤ َﺸَﺮ ﻓَـﻨَ َﺎد ٰى‬ َ ‫ب َو َﻋ‬ َ ‫﴿ﻓَﺄ ََراﻩُ ٱﻵﻳَﺔَ ٱﻟْ ُﻜْﺒـَﺮ ٰى۞ ﻓَ َﻜ ﱠﺬ‬
﴾‫َﻋﻠَ ٰﻰ‬ ْ ‫ﺎل أ ََ�ْ َرﺑﱡ ُﻜ ُﻢ ٱﻷ‬
َ ‫ﻓَـ َﻘ‬
Faarahu al-ayata alkubra; Fakadhdhaba waAAasa; Thumma adbara yasAAa;
Fahashara fanada; Faqala ana rabbukumu al-aAAla (Surat An Naziat 79:20-24)

Tafsir: Kisha (Musa) akamuonesha yeye (Fir’awn) Miujiza mikubwa. Lakini (Firawn)
akakadhibisha kisha akageuka (na kuupa mgongo Wasia huo alioletewa na Mola
wake kupitia kwa Nabii Musa) na kuasi. Na kisha akawakusanya watu wake na
kuwanadia: ‘Mimi ndie Mola wenu Mkuu’’

Na anasema Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakkalimin Imam Al Ghazali Al Thani Imam


Fakhr Ad Din Al Razi kuhusiana na kauli hio ya Fir’awn kua: ‘Wakati Fir’awn
aliposema kua Ana rabbukumu al-aAAla yaani Mimi ndie Mungu wenu Mkuu, basi
hakumaanisha kua yeye ndie Muumbaji wa Ulimwengu na Kusimamia kila
625

kilichomo ndani yake, kwa sababu alikua ni Mtu asieamini kuwepo kwa Muumba.
Na hivyo alikua akimaanisha kua anakanusha kuwepo kwa Allah Subhanah wa
Ta’ala ambae ndie Muumba wa Ulimwengu na kila kilichomo ndani yake ambae
ndie msimamizi wa kila kitu alichokiumba ambae ndie atakaesimamia kila kitu
katika siku ya Malipo, hivyo kwa mtizamo wake basi alikua naweka wazi kua
hakuna Muumbaji kama huyo na mwenye uwezo huo, hivyo yeye anajihesabu na
kujitangazia kua ndio Mungu Mkuu ambae ndie mwenye kutunga Sheria zote
katika Mamlaka yake, Sheria ambazo kila mtu ndani ya Mamlaka yake anatakiwa
azifuate atake, asitake’

Kutokana na kauli hio basi ndio maana siku moja Fir’awn alikua yuko chooni anakoga
mara ghafla akamtokezea Ibilisi katika umbo la mtu asiemjua hivyo Fir’awn akamuuliza:
‘Wewe ni nani na umetokea wapi?’ yule mtu akasema: ‘Ole wako unauliza mimi
nani?’ Fir’awn akasema: ‘Naam sikujui’Ibilisi akasema: ‘Inakuaje kua hunijui wakati
wewe ndie ulieniumba na ukasema:

﴾‫﴿أ ََ�ْ رﺑﱡ ُﻜﻢ ٱﻷ َْﻋﻠَ ٰﻰ‬


ُ َ
Ana Rabbukumu al-aAAla (Surat An Naziat 79: 24)

Tafsir: ‘Mimi ndie Mola wenu Mkuu’ ’’

Na pia kwa upande mwengine basi wanasema Imam Ibn Jariri At Tabari, Imam Ahmad
Ibn Muhammad Ath Thalabi, nk kua: ‘Malaika Jibril alimwambia Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Katika viumbe wote basi hakuna viumbe niliokua
nikiwachukia kama nilivyokua nikiwachukia viumbe wawili. Wa kwanza ni Jini
aitwae Ibilisi pale alipokataa kumsujudia Adam. Na mwengine ni Ibn Adam aitwae
Fir’awn pale aliposema Mimi ndie Mola wenu Mkuu’ yalaiti kama ungeniona ewe
Muhammad namna nilivyochukua Matope na kumsokomezea mdomoni mwake ili
asije akatamka wakati anazama, na kisha Allah Subhnaha wa Ta’ala akamuonea
Huruma.’(Imam At Tirimidhii)

Hivyo baada ya Firawn kukubaliana na washauri wake wakuu ambao ni Hamman na


Qarun na kutangazia kua yeye ndio Mungu Mkuu basi akawaambia Machifu wake
waliobakia kwa kusema kua:
626

‫ﻳﺪ أَن ُﳜْ ِﺮ َﺟ ُﻜ ْﻢ ِّﻣ ْﻦ أ َْر ِﺿ ُﻜ ْﻢ‬ ِ ‫ﺎل ﻟِْﻠﻤ َِﻺ ﺣﻮﻟَﻪ إِ ﱠن ﻫـٰ َﺬا ﻟَﺴ‬
ُ ‫ﺎﺣٌﺮ َﻋﻠِ ٌﻴﻢ ۞ ﻳُِﺮ‬ ﴿
َ َ ُ ْ َ َ َ َ‫ﻗ‬
۞ ‫ﺎﺷ ِﺮﻳﻦ‬ ِ ِ ِ ْ ‫َﺧﺎﻩُ وٱﺑْـ َﻌ‬ ِ ۤ ۞ ِ ِِ
َ ‫ﺚ ﰱ ٱﻟْ َﻤ َﺪآﺋ ِﻦ َﺣ‬ َ َ ‫ﺑﺴ ْﺤ ِﺮﻩ ﻓَ َﻤﺎ َذا َﺄﺗْ ُﻣُﺮو َن ﻗَﺎﻟُﻮاْ أ َْرﺟ ْﻪ َوأ‬
﴾‫ﻮك ﺑِ ُﻜ ِﻞ َﺳ ﱠﺤﺎ ٍر َﻋﻠِﻴ ٍﻢ‬
ّ َ ُ‫َ�ْﺗ‬
Qala lilmala-i hawlahu inna hadha lasahirun AAaleemun; Yureedu an
yukhrijakum min ardhikum bisihrihi famadha ta/muroona; Qaloo arjih waakhahu
waibAAath fee almada-ini hashireena; Ya/tooka bikulli sahharin AAaleemin (Surat
Ash Shuara 26:34-37)

Tafsir: Akasema (Fir’awn) kuwaambia Machifu wake: ‘Hakika huyu ni Mchawi


mwenye kujua. Anataka kukuhamisheni kutoka katika Ardhi yenu kwa Uchawi wake
jee mnasemaje?’. Hivyo wakasema (Machifu hao) Muondoe yeye na Kaka yake kisha
watume wanadiaji katika Miji. Kukuletea kwako wewe Wachawi wenye kujua sana.

Na baada ya kushauriana na watu wake hao, na kupata mtizamo wao ambao pia
unaendana na mtizamo wake basi akamgeukia Nabii Musa kuanza kumshambulia Nabii
Musa kwa shutma za kua ni mchawi anaetaka kuwafukuza Watu wa Misri kutoka katika
Ardhi yao, na ingawa hajawahi kushambuliwa kwa mashambulizi ya aina yeyote yale
yaliyokua yanatishia uimara wa Mamlaka yake bila ya yeye kutokua mshindi, lakini hata
hivyo kwa mara ya kwanza mashambulizi haya ya hoja na vithibitisho vya Nabii Musa
yalikua yanatishia uimara wa Mamlaka yake, kama ilivyobashiriwa kwenye ndoto
aliyoiota miaka 40 iliyopita.

Hivyo Firawn akaamua kua bora amalizane nao Manabii hao wawili kwa kuwaua kabisa,
lakini watu wake wakapinga na wakashauri kua bora wauliwe watoto wa kiume wa
watakao wafuata Nabii Musa na Nabii Harun, kwani kufanya hivyo kutawatia khofu watu
ili wasiwafuate na hivyo kua ni wenye kukosa wafuasi, na watakua wamepunguza sana
nguvu za Mitume hao wanaotishia Mamlaka yao waliokuwepo mbele yao kama
zinavyosema aya:
627

ِ ‫ﻨﺪ َ� ﻗَﺎﻟُﻮاْ ٱﻗْـﺘـﻠُ ۤﻮاْ أَﺑـﻨﺂء ٱﻟﱠ‬


ِ ِ‫ﭑﳊ ِﻖ ِﻣﻦ ﻋ‬ ِ
ْ‫ٱﺳﺘَ ْﺤﻴُﻮا‬ ‫و‬ ‫ﻪ‬ ‫ﻌ‬‫ﻣ‬ ‫ا‬
ْ‫ﻮ‬ ‫ﻨ‬ ‫آﻣ‬
ْ َ ُ َ َ َ َ َ َْ ُ
ُ ‫ﻳﻦ‬ ‫ﺬ‬ ْ ّ َْ ‫﴿ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ َﺟﺂءَ ُﻫ ْﻢ ﺑ‬
ِ َ َ‫ﻧِﺴﺂءﻫﻢ وﻣﺎ َﻛـﻴ ُﺪ ٱﻟْ َﻜﺎﻓِ ِﺮﻳﻦ إِﻻﱠ ِﰱ ﺿﻼٍَل۞ وﻗ‬
ُ‫ﻮﺳﻰ َوﻟْﻴَ ْﺪع‬َ ‫ﺎل ﻓْﺮ َﻋ ْﻮ ُن ذَ ُر ِوﱐ أَﻗْـﺘُ ْﻞ ُﻣ‬ َ َ َ ْ ََ ْ َُ َ
ِ ‫ﺎف أَن ﻳـﺒ ِّﺪ َل‬
﴾‫ض اﻟْ َﻔﺴ َﺎد‬
َ ِ ‫َر‬
ْ ‫اﻷ‬
ْ ‫ﰲ‬ِ ‫ﺮ‬ ‫ﻬ‬ِ ‫ﻈ‬
ْ
َ ُ ْ ْ ‫ﻳ‬ ‫َن‬ ‫أ‬ ‫َو‬
‫أ‬ ‫ﻢ‬ ‫ﻜ‬
ُ ‫ﻳﻨ‬
َ ‫د‬ َُ ُ ‫َﺧ‬ َ ‫َرﺑﱠﻪُ إِِّﱐ أ‬
Falamma jaahum bialhaqqi min AAindina qaloo oqtuloo abnaa alladheena amanoo
maAAahu waistahyoo nisaahum wama kaydu alkafireena illa fee dhalalin; Waqala
firAAawnu dharoonee aqtul moosa walyadAAu rabbahu innee akhafu an yubaddila
deenakum aw an yudhhira fee al-Ardhi alfasada. (Surat Al Ghafir 40:25-27)

Tafsir: Na kisha walipofikishiwa ukweli kutoka kwetu, wakasema: ‘Wauwe watoto wa


kiume wa wote wale watakaomuamini na wacha watoto wao wa kike wabakie kuishi’
Lakini mbinu za Makafiri hua si chochote ila ni zenye kudhalilika. Fir’awn akasema:
Wacha mie nimuue Musa, na wacha amuite Mola wake (anizuie hapo nitakapomuua),
kwani nna khofu kua atakubadilishieni Dini yenu au anaweza akasababisha
Machafuko katika Ardhi (ya Misri).

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kuhusiana na aya hizi
kua: ‘Inawezekana kua watu wa Fir’awn hawakutaka Nabii Musa auliwe kwa
sababu alikua akimpa changamoto Fir’awn na hivyo kumfanya kutokua na utulivu
wa Nafsi yake kwani anafikiria sana madhara ya Nabii Musa na Nabii Harun dhidi
ya Utawala wake, jambo ambalo hua litawapa utulivu washirika wake hao ambao
walikua hawana utulivu kutokana na Kibr cha Fir’awn dhidi yao.’

Naam hata katika kipindi chetu Wanasiasa Ulimwenguni mara nyingi hua wanafanya
hivyo pale wanapopata changamoto nzito zinazowachafulia majina yao, sifa zao, n.k
baada ya kufanya ufisadi, basi huanzisha tukio la kuwatia khofu watu wao, na kisha tukio
hilo hulihusisha na maadui zao wa ndani au wa nje ya nchi zao na hivyo kuzihamisha
akili za watu kutoka katika kufikiria kasoro na makosa ya Wanasiasa hao na kuhamia
katika uvumi huo au tukio hilo jipya lililoanzishwa na Wanasiasa hao na hivyo
kuwachanganya akili watu wao kwani watu hao hua ni wenye kufikiria na kuzungumzia
uvumi huo au tukio hilo la khofu lililotokea na hivyo huacha kufikiria ufisadi uliofanywa
mda mfupi tu uliopita na viongozi wao wa kisiasa.

Hivyo wakati Fir’awn anashauriana na watu wake kuhusiana na namna ya kupingana na


madai hayo na kuzima nguvu za Nabii Musa dhidi ya Mamlaka yake, basi Nabii Musa
akahisi kua wanapanga namna ya kuwadhuru hivyo nae akasema kuwaambia watu hao:
628

ِ ‫اﳊِﺴ‬
﴾‫ﺎب‬ ِ ِ ِ ‫ٍِ ﱠ‬ ِ ِ ِ ‫ﺎل ﻣﻮﺳﻰ إِِﱐ ﻋ ْﺬ‬
ُ ُ ّ َ ُ َ َ‫﴿ َوﻗ‬
َ ْ ‫ت ﺑَﺮِّﰊ َوَرﺑّ ُﻜﻢ ّﻣﻦ ُﻛ ِّﻞ ُﻣﺘَ َﻜ ّﱪ ﻻ ﻳـُ ْﺆﻣ ُﻦ ﺑﻴَـ ْﻮم‬
Waqala moosa innee AAudhtu birabbee warabbikum min kulli mutakabbirin la
yu/minu biyawmi alhisabi. (Surat Al Ghafir 40:27)

Tafsir: Akasema Musa: ‘Hakika Mimi Naomba Ulinzi wa Mola wangu na kwa Mola
wenu juu ya kila mwenye Kibri asieamini siku ya Malipo’.

Ambapo anasema Al Muhaqqiq Imam Shihab Ad Din Ibn Hajar Al Haytami kua:
Amesema Abu Burdah kua: Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipokua na
khofu kutoka kwa watu basi alikua akiomba dua kwa kusema: ‘Ya Allah! Hakika
sisi tunakuweka wewe mbele ya Vifua vyao. Na kuomba Ulinzi wako dhidi ya
madhara yao’

Hivyo baada ya Nabii Musa kuomba Dua hio iliyomo ndani ya aya ya Surat Ghafir 40:27
basi hapo hapo Allah Subhanah wa Ta’ala akajaalia kua Nabii Musa kua ni mwenye
kupata muungaji mkono kutoka ndani ya Watu wa Fir’awn waliokuwepo hapo barazani
ambapo aya zinasema kuhusiana nae kua:

ُ‫ٱﻪﻠﻟ‬
‫ﰉ ﱠ‬ َ ‫ﺎل َر ُﺟ ٌﻞ ﱡﻣ ْﺆِﻣ ٌﻦ ِّﻣ ْﻦ ِآل ﻓِْﺮ َﻋ ْﻮ َن ﻳَ ْﻜﺘُ ُﻢ إِﳝَﺎﻧَﻪُ أَﺗَـ ْﻘﺘُـﻠُﻮ َن َر ُﺟﻼً أَن ﻳَـ ُﻘ‬
َِّ‫ﻮل َر‬ َ َ‫﴿ َوﻗ‬
ً‫ﺻ ِﺎدﻗﺎ‬ ِ ِ ِ َ‫وﻗَ ْﺪ ﺟﺂء ُﻛﻢ ﺑِﭑﻟْﺒـﻴِﻨ‬
َ ‫ﻚ‬ ُ َ‫ﻚ َﻛﺎذﺎﺑً ﻓَـ َﻌﻠَْﻴ ِﻪ َﻛﺬﺑُﻪُ َوإِن ﻳ‬ ُ َ‫ﺎت ِﻣﻦ ﱠرﺑِّ ُﻜ ْﻢ َوإِن ﻳ‬ َّ ْ َ َ َ
﴾‫اب‬ ٌ ‫ف َﻛ ﱠﺬ‬ٌ ‫ٱﻪﻠﻟَ ﻻَ ﻳَـ ْﻬ ِﺪى َﻣ ْﻦ ُﻫ َﻮ ُﻣ ْﺴ ِﺮ‬ ‫ﺾ ٱﻟﱠ ِﺬى ﻳَﻌِ ُﺪ ُﻛ ْﻢ إِ ﱠن ﱠ‬ ِ
ُ ‫ﻳُﺼْﺒ ُﻜ ْﻢ ﺑَـ ْﻌ‬
Waqala rajulun mu/minun min ali firAAawna yaktumu eemanahu ataqtuloona
rajulan an yaqoola rabbiyya Allahu waqad jaakum bialbayyinati min rabbikum
wa-in yaku kadhiban faAAalayhi kadhibuhu wa-in yaku sadiqan yusibkum
baAAdhu alladhee yaAAidukum inna Allaha la yahdee man huwa musrifun
kadhdhabun (Surat Al Ghafir 40:28)

Tafsir: Akasema mtu alieamini (Miujiza ya Nabii Musa) miongoni mwa watu wa
Fir’awn: ‘Jee mnataka kumuua mtu ambae amesema kua Mola wangu ni Allah, na
amekuja akiwa na vithibitisho vilivyowazi kutoka kwa Mola wenu? Na kama akiwa
Muongo basi ni juu yake (Dhambi ya) Uongo huo. Lakini kama akiwa anasema ukweli
basi maangamizo anayotishia yatakufikieni’ kwani kwa hakika Allah hawaongozi
wenye kufanya Machafuko na Kusema Uongo.
629

Aya inatuonesha usahihi wa ile hadith ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambae
aliulizwa na Masahaba zake: ‘Ya Rasul Allah! Hivi jee ni ipi Jihadi Bora kuliko zote?’
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Kusema Ukweli mbele ya
Kiongozi katili’ (Imam An Nasai)

Anasema Mujtahid Imam Imam Abu Bakr Muhammad Ibn Ibrahim Ibn Al Mundhiri Al
Nishapuri Al Shafii kua kulingana na Mtizamo wa Sahaba Abd Allah Ibn Abbas Radhi
Allahu Anhu basi ni kua Katika kipindi hiki katika Ardhi ya Misri kulikua na watu
watatu tu waliokua wakimuamini Nabii Musa na Nabii Harun ambao ni Asiyah
Bint Muzahim, na Huyu alietajwa katika ayah hii na yule Hizqil yule aliemuonya
Nabii Musa kua akimbie katika aya isemayo:

َ ِ‫ﻮﺳ ٰﻰ إِ ﱠن ٱﻟْ َﻤ َﻸَ َ�َْﲤُِﺮو َن ﺑ‬


‫ﻚ‬ َ َ‫ﺼﻰ ٱﻟْ َﻤ ِﺪﻳﻨَ ِﺔ ﻳَ ْﺴ َﻌ ٰﻰ ﻗ‬
َ ُ‫ﺎل ٰﳝ‬
ِ
َ ْ‫﴿ َو َﺟﺂءَ َر ُﺟ ٌﻞ ّﻣ ْﻦ أَﻗ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ َ َ‫ﻮك ﻓَﭑﺧﺮج إِِﱏ ﻟ‬ ِ
َ ‫ﻚ ﻣ َﻦ ٱﻟﻨﱠﺎﺻﺤ‬ ّ ْ ُ ْ َ ُ‫ﻟﻴَـ ْﻘﺘُـﻠ‬
Wajaa rajulun min aqsa almadeenati yasAAa qala ya moosa inna almalaa
ya/tamiroona bika liyaqtulooka faokhruj innee laka mina alnnasiheena (Surat Al
Qasas 28:20)

Tafsir: Na akaja Mtu kutoka sehemu ya mbali ya Mji akikimbia, akasema: ‘Ewe Musa
hakika Machifu wanajadiliana juu yako ili wakuue, hivyo Kimbia kwani kwa hakika
mimi kwako wewe ni mwenye kukunasihi’

Ambapo kwa mtizamo mwengine basi inawezekana kua huyu aliesema maneno haya ya
aya ya 28 ya Surat Ghafir anaweza akawa ndio huyo huyo mtu mmoja yaani Hizqil, kwa
sababu huyu alietajwa kwenye Surat Al Qasas alimuonya Nabii Musa baada ya kua ni
mwenye kusikia namna walivyokua wakijadiliana Firawn na watu kuhusiana na kumuua
Nabii Musa hapo kabla, hivyo itakua nae ni miongoni mwa wazee wa Baraza la Fir’awn
na ndio maana na hata hapa katika baraza hili pia alikuwepo, lakini Allahu A’alam.

Anasema Imam Al Qurtubi kua amesema Imam Abu Nu`aym katika Fadha’il al Sahabah
kua Muhammad Ibn `Aqil kua: ‘Siku moja Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu
alituuliza sisi kwenye Khutba kwa kusema kua: Enyi Watu hebu tuambieni jee ni
nani Mtu ambae aliekua naujasiri kuliko wote?’

Nasi tukasema: ‘Ni wewe!’


630

Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Ama kuhusiana namie basi bila ya
shaka sikuwahi kukutana na mtu katika mapigano isipokua hua ni mwenye kufanya
uadilifu, lakini nambieni jee ni nani ambae ni shujaa zaidi miongoni mwa watu
wote?’

Watu wakasema: ‘Kama ni hivyo basi sisi tutakua hatumjui’

Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Ni Abu Bakr! Radhi Allahu Anhu
kwani katika siku ya Vita vya Badr, tulijenga kibanda kwa ajili ya Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam, kasha tukajiuliza lakioni jee ni nani atakaebakia na
Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam ili kumlinda dhini ya Makafiri? Wa Allahi
hakuna aliemkaribia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam isipokua Abu Bakr
alirusha Upanga wake juu ya Kichwa cha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam,
hakuna hata mmoja miongoni mwa Makafiri isipokua alikumbana na Abu Bakr’

Hakika Abu Bakr ni Mtu Jasiri sana kwani mimi nilimuona Rasul Allah Salallahu
Alyahi wa Salam wakati alipokua amekamatwa na Makafiri katika Mji wa Makkah.
Wakati huyu anamvuta huku na yule anamvuta kule, na yeye akiwa anavutana na
mwengine. Huku wakiwa wanasema: ‘Hivi wewe ndie yule mtu ambae amemfanya
Mungu kua mmoja?’

Wa Allahi! Hakuna hata mmoja aliewakaribia Makafiri hao isipokua Abu Bakr
aliwavamia na kumsukuma mmoja kule na kumvuta mwengine huku akisema:
‘Hivi nyinyi mtamuua Mtu ambae anasema kua Allah ndie Mungu wagu?’

Hapa Ali Radhi Allahu Anhu akalivuta Joho lake na kujifunika Kichwa chake huku
akilia mpaka Ndevu zake zikaroa. Kisha akauliza: ‘Hebu Niapieni kwa jina la
Allah, Jee ni Nani bora? Ni Muumini miongoni mwa Watu wa Fir’awn au ni Abu
Bakr?’

Watu wakabakia kimyaa. Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Jee
Mtanijibu?’ kasha akaendelea kusema: ‘Wa Allahi! Abu Bakr ni Bora! Kuliko
Muumini aliekua miongoni mwa Watu wa Fira’wn, kwani Muumini huyo aliificha
Imani yake wakati Abu Bakr alikua ni mwenye kuweka wazi Imani yake.’

Ambapo kwa upande mwengine basi amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
kua: ‘Watu watatu ni wa mwanzo miongoni mwa Ummah ambao hawakusita
kumkubali Allah Subhanah wa Ta’ala hata kidogo: Habib kijana Seremala
alieamini miongoni mwa watu wa Yasin, Hizqil, Muumini miongoni mwa watu wa
Fir’awn na Ali Muumini katika Familia ya Muhammad (Salallahu A’alayhi wa
Salam) na yeye ndie mwenye upekee kuliko wote.’
631

Hivyo kauli hio ya Muumini huyu ambae ni miongoni mwa watu wa Fir’awn yaani Hizqil
yenye hoja nzito aliyoitoa wakati akiwa ni miongoni mwa waliokua wakimuamini Nabii
Musa ndani ya Baraza la wazee la Fir’awn basi ilimpekea Fir’awn kua ni mwenye kusema
kua:

�َ َ‫ٱﻪﻠﻟِ إِن َﺟﺂء‬


‫ﻨﺼُﺮَ� ِﻣﻦ َﺄﺑْ ِس ﱠ‬ ‫ﻳ‬ ‫ﻦ‬‫ﻤ‬ َ‫ﻓ‬ ‫ض‬ِ ‫َر‬‫ﻷ‬ ‫ٱ‬ ‫ﰱ‬ِ ‫ﻳﻦ‬ ِ
‫ﺮ‬ ِ َ‫﴿ ٰﻳـ َﻘ ِﻮم ﻟَ ُﻜﻢ ٱﻟْﻤ ْﻠﻚ ٱﻟْﻴـﻮم ﻇ‬
‫ﺎﻫ‬
ُ َ َ ْ َ ََْ ُ ُ ُ
﴾‫ﺎل ﻓِﺮ َﻋﻮ ُن َﻣﺂ أُِرﻳ ُﻜﻢ إِﻻﱠ َﻣﺂ أَر ٰى وَﻣﺂ أ َْﻫ ِﺪﻳ ُﻜﻢ إِﻻﱠ َﺳﺒِﻴﻞ ٱﻟﱠﺮ َﺷ ِﺎد‬
َ ْ َ َ ْ ْ ْ َ َ‫ﻗ‬
Ya qawmi lakumu almulku alyawma dhahireena fee al-Ardhi faman yansuruna min
ba/si Allahi in jaana qala firAAawnu ma oreekum illa ma ara wama ahdeekum illa
sabeela alrrashadi (Surat Ghafir 40:29)

Tafsir: (Akasema Fir’awn) Enyi Watu wangu! Mamlaka yenu yamejidhidhirisha leo
hii kwenye Ardhi, lakini jee ni nani atakaetunusuru na Adhabu ya Allah kama
ikitushukia? Fir’awan (Akaendela) kusema: Na mimi sikuonesheni Nyie isipokua kile
ninachokiona (kua ni sahih) na sikuongozeni nyinyi isipokua kwenye njia ya uongofu
ulio sahih.

Hapa Fir’awn anatuwekea wazi kua kulingana na Mtizamo wake basi maneno haya ni
yenye kuenda kinyume na namna anavyoamini na namna anavyotaka iwe, hivyo alikua
akisema uongo, ili kuonesha kua Utawala wake na Mamlaka yake una nguvu na uko
katika njia ya haki na iliyo sahih kiuongofu tofauti na njia anayotaka kuwapitisha watu
Nabii Musa.

Ambapo Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi Wa Salam kua: ‘Hakuna Kiongozi
atakaekabidhiwa Madaraka yakuwaongoza Waislam, kasha akawadanganya
Waislam hao isipokua Allah Subhanah wa Ta’ala humharamishia Pepo Kiongozi
huyo’(Sahih Bukhari, Sahih Muslim)

Hivyo baada ya maneno hayo basi akaamua kusimama na kukabiliana kwa nguvu zake
zote dhidi ya mashambulizi hayo yanayotishia Mamlaka yake na akamwambia Nabii
Musa kwa kusema kua:

‫ﱠﻚ ﺑِ ِﺴ ْﺤ ٍﺮ ِّﻣﺜْﻠِ ِﻪ‬


َ ‫ﻮﺳ ٰﻰ۞ ﻓَـﻠَﻨَﺄْﺗِﻴَـﻨ‬
َ ‫ﳝ‬
ُ ٰ ‫ك‬
َ ِ
‫ﺮ‬ ‫ﺤ‬ْ
ِ ِ‫ﺎل أ َِﺟْﺌـﺘَـﻨَﺎ ﻟِﺘُﺨ ِﺮﺟﻨَﺎ ِﻣﻦ أَر ِﺿﻨَﺎ ﺑ‬
‫ﺴ‬ ْ ْ َ ْ َ َ‫﴿ﻗ‬
﴾‫َﻧﺖ َﻣ َﻜﺎ�ً ُﺳﻮى‬ ِ ِ َ َ‫ﻓَﭑﺟﻌﻞ ﺑـﻴـﻨَـﻨَﺎ وﺑـﻴـﻨ‬
ً َ ‫ﻚ َﻣ ْﻮﻋﺪاً ﻻﱠ ُﳔْﻠ ُﻔﻪُ َْﳓ ُﻦ َوﻻَ أ‬ َْ َ َْ ْ َ ْ
632

Qala aji/tana litukhrijana min ardhina bisihrika ya moosa; Falana/tiyannaka


bisihrin mithlihi faijAAal baynana wabaynaka mawAAidan la nukhlifuhu nahnu
wala anta makanan suwan (Surat Ta-Ha 20:57-58)

Tafsir: Akasema (Fir’awn kumwambia Nabii Musa): ‘Hivi umekuja kwa ajili ya
kutufukuza kutoka ndani ya Ardhi yetu kwa kutumia Uchawi wako ewe Musa?’ Hivyo
bila ya shaka nasi tutakuonesha uchawi mithli yake, hivyo chagua baina yetu na baina
yako miadi ambayo hatutoweza kuivunja sisi wala wewe katika sehemu iliyowazi.

Ambapo anasema Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kuhusiana na aya hii
kua: ‘Suali hili alilouliza Hapa Fir’awn linaonesha kua Fir’awn amejithibitishia kua
Ujumbe aliokuja nao Musa ni ujumbe ambao si wa kawaida yaani umepita uwezo
wa kimaumbile, na hivyo kama Fir’awn hatojipanga na kujihami ipasavyo basi
atakua ni mwenye kupoteza kila kitu alichokua nacho kutokana na Musa. Na kama
angejua japo kidogo tu kua Musa ni mchawi basi tangu mwanzo asingemjali hata
kidogo.’

Ambapo tunaona kua aya imetumia neno MawaAAidan ambalo ni neno linalotokana na
na neno Wa’aada lenye kumaanisha Ahadi au Miadi ya kutekeleza kitu ambayo hua iko
katika hali ya kuahidi au hali ya kutishia. Hivyo neno Mawa’Aidatun hua linamanisha
Mda maalum au Sehemu Maalum ya utekelezaji au utokeaji wa Jambo fulani.

Na pia ikatumia neno Makanan suwan ambalo ni lenye kumaanisha sehemu ya uwanja
ambayo iko wazi kwa kila upande sawia, ambalo kile kitakachofanyika kitakua
kinaonekana na kila mtu kiasi ya kua hakuna hata mtu mmoja atakae kua na kisingizio
labda kua mwenzake amependelewa.

Hivyo basi Fir’awn alikua anajiamini na ana uhakika kua atashinda na hivyo kua ni
mwenye kuwaadhirisha Nabii Musa na Nabii Harun mbele ya watu wote, na ndio maana
akamwambia Nabii Musa kua achague yeye sehemu na wakati autakao yeye mwenyewe
kwa ajili ya kuoneshana, nani mkali zaidi yaani Wachawi wa Fir’awn au Nabii Musa.

Ambapo na kwa upande wa Nabii Musa nae, akakubaliana na shauri hilo na kulipokea
kwa mikono miwili, na ingawa ameambiwa achague siku yeyote, lakini yeye akaamua
kuchagu siku Maalum ambayo ni siku muhimu kuliko sote kwa jamii ya watu wa Misri,
siku ambayo hata watu wa shamba na vijijini hua ni wenye kuja mjini kutokana na
umuhimu wa siku hio, na hivyo Mji Mkuu wa Misri hufurikwa pia na maelfu ya watu
ambao hua ni wenye kufanya Maandamano ya Sherehe kutoka Katika maeneo ya Kasri
la Mfalme kuelekea kwenye maeneo ya Makaburi ya Wafalme ya Umm al Qaab.

Hii ni siku ya sikukuu ya watu wa Misri inayoadhimishwa kila mwaka kwa ajili ya
Mungu aitwae Osiris ambae kwa mtizamo wao hua ni Mungu wa chini ya Ardhi na hivyo
633

hua ni mwenye kuwapokea vizuri na kuwakaribisha watu wanaokufa na kuzikwa ardhini


na ndie mwenye kusimamia kufurika kwa Mto Nile, mafuriko ambayo ni yenye
kusababisha Ardhi ya Misri kujaa maji na kua na rutba na kuwezesha kuotesha mimea ya
mazao na bustani zinazonawiri sana.

Hivyo Nabii Musa akauchagua wakati wa asubuhi mapema wa siku hii na kusema:

ِ ِ ‫ﺎل ﻣﻮﻋِ ُﺪ ُﻛﻢ ﻳـﻮم‬


﴾‫ﺿ ًﺤﻰ‬ ّ ُ ْ َ ْ ْ َ َ َ‫﴿ﻗ‬
ُ ‫ٱﻟﺰﻳﻨَﺔ َوأَن ُْﳛ َﺸَﺮ ٱﻟﻨ‬
ُ ‫ﱠﺎس‬
Qala mawAAidukum yawmu alzzeenati waan yuhshara alnnasu dhuhan (Surat Ta-
Ha 20:59)

Tafsir: Musa akasema: ‘Mda wenu ni siku ya sikukuu na wacha watu wakutane baada
ya Jua Kuchomoza’

Baada ya Nabii Musa kukubaliana na Miadi hio, basi Fir’awn akageuka kujitayarisha
kuondoka kwenye hadhara hio, ili aweze kujipanga upya kwa kutafuta wachawi wake
wenye mbinu kubwa na nzuri zaidi kwa ajili ya kurudi tena kukabiliana na mashambulizi
makali ya Nabii Musa na Nabii Harun, kama inavyosema aya ifuatayo:

﴾‫﴿ﻓَـﺘَـ َﻮﱠ ٰﱃ ﻓِْﺮ َﻋ ْﻮ ُن ﻓَ َﺠ َﻤ َﻊ َﻛْﻴ َﺪﻩُ ﰒُﱠ أَﺗَ ٰﻰ‬


Fatawalla firAAawnu fajamaAAa kaydahu thumma ata (Surat Ta-Ha 20:60)

Tafsir: Hivyo akageuka Fir’awn, kisha akakusanya mbinu zake kisha akarudi.

Tunapoiangalia Lugha ya Kiarabu basi tunaona kua ina maneno mafupi mafupi yenye
maana pana sana kwa mfano maneno yanayoainisha Kitendo cha mwendo wa kutoka
katika hatua moja na kurudia katika hatua ya awali kama vile pale Allah Subhanah wa
wa Ta’ala ilipotumia ndani ya Qur’an neno Aba ambalo humaanisha Kurudi kutoka
sehemu Moja au Kurudia Kitu ambapo mara nyingi imetumia neno hili kwa ajili ya wale
watu ambao ni wenye kurudi mara kwa mara kwa Mola wao baada ya kufanya Dhambi.

Na pia akatumia neno Ala ambalo pia humaanisha Kurudi kua katika hali ya awali na pia
humaanisha Kuwahi. Na pia akatumia neno Ata ambalo ndio lililotumika katika aya yetu
hii ya Surat Ta-Ha 20:60 kumaanisha Kurudi kwa Kiurahisi, Kuleta, Kukifikia kitu kwa
hiari na Utiifu iwe kwa Maneno, kwa Vitendo au kwa Maamrisho.
634

Hivyo neno Ata lililotumika katika aya ya Surat Ta-Ha 20:60 limetumika kubainisha
namna Fir’awn alivyojizatiti kwa hiari yake kurudi tena katika Uwanja wa Mapambano
dhidi ya Mpinzani wake ambae ni Nabii Musa tena neno Ata linaweka wazi namna
Fir’awn alivyojitayarisha kurudi bila ya kuona uzito wowote juu ya Marudiano hayo huku
akiwa amejitayarisha Kikamilifu, Kiutiifu, Kiushirikiano na Kiheshima kwa kuzingatia
vigezo vyote na Masharti.

Kwani alikua anajua kua baada ya matayarisho ya mbinu zake atakazo tayarisha basi bila
ya shaka ushindi hautakua ni wa upande wowote ule isipokua ni wa upande wake yeye
na washirika wake na ndio maana hata alipotoa shauri hilo la marudiano basi alimpa
Nabii Musa uhuru wa kuchagua siku na sehemu aitakayo yeye ya marudiano.

Hivyo Nabii Musa akatoa Onyo kwa kuwaambia Fir’awn na watu wake:

ٍ ِ ِ ِ‫ﺎل َﳍﻢ ﱡﻣﻮﺳﻰ وﻳـﻠَ ُﻜﻢ ﻻَ ﺗَـ ْﻔﺘـﺮواْ ﻋﻠَﻰ ﱠ‬


َ ‫ٱﻪﻠﻟ َﻛﺬﺎﺑً ﻓَـﻴُ ْﺴﺤﺘَ ُﻜﻢ ﺑِ َﻌ َﺬاب َوﻗَ ْﺪ َﺧ‬
‫ﺎب‬ َ َُ ْ ْ َ ٰ َ ُْ َ َ‫ﻗ‬
﴿
﴾‫َﻣ ِﻦ ٱﻓْـﺘَـﺮ ٰى‬
َ
Qala lahum moosa waylakum la taftaroo AAala Allahi kadhiban fayus-hitakum
biAAadhabin waqad khaba mani iftara (Surat Ta-Ha 20:61)

Tafsir: Akasema Musa kuwaambia wao (Kina Fir’awn) Ole wenu! Msije mkamsingizia
Allah Uongo, kwani atakuangamizeni vibaya sana kwa adhabu, na bila ya shaka
anaesingizia (juu ya Allah Subhanah wa Ta’ala) atashindwa vibaya sana.

Hili ni onyo ambalo lilikua linawatishia kina Fir’awn kua wasije wakawa ni wenye
kushindwa na mbinu zao zote, kisha wakamsingizia Allah Subhanah wa Ta’ala, kwani
bila ya shaka watashindwa vibaya sana hata kama watatumia mbinu gani na hivyo basi
hapa Nabii Musa alikua ni mwenye kuthibitisha kwa mara nyengine tena kua
anayoyazungumza hayatokani na matamanio yake ya kinafsi, bali ni yenye kutoka kwa
Allah Subhanah wa Ta’ala amabae ni mwenye uwezo juu ya kila kitu, hivyo kutokana
na kauli hio basi Fir’rawn na washauri wake wakafanya kama zisemavyo aya kua:

﴾‫ﱠﺠﻮ ٰى‬ ۤ
َ ‫﴿ﻓَـﺘَـﻨَ َﺎزﻋُﻮاْ أ َْﻣَﺮُﻫ ْﻢ ﺑَـْﻴـﻨَـ ُﻬ ْﻢ َوأ‬
َ ْ ‫َﺳﱡﺮواْ ٱﻟﻨ‬
FatanazaAAoo amrahum baynahum waasarroo alnnajwa (Surat Ta-Ha 20:62)
635

Tafsir: Wakajadiliana nini wafanye juu ya jambo lao baina yao na wakayafanya kua
siri mazungumzo yao.

Fir’awn na washauri wake wawili yaani Hamman na Qarun wakajadiliana kwa siri
kuhusiana na nini cha kufanya ili wawe ni wenye kupata ushindi mkubwa sana na
kuwaadhirisha Nabii Musa na Nabii Harun mbele ya watu wao, na pia ni kipi cha kufanya
kama mambo yakiharibika na hivyo wakawa ni walioshindwa na kuadhirishwa mbele ya
watu wao.

Ama kuhusiana na ni kipi cha kufanya ili washinde, na ni kipi cha kufanya ili
wasiadhirike, basi majibu juu ya suali hili litafichuka itakapowasili siku ya Makabiliano
baina ya Nabii Musa, Nabii Harun na Wachawi hao wa Fir’awn.

MAKABILIANO BAINA YA NABII MUSA NA NABII HARUN DHIDI


YA WACHAWI WA FIR’AWN.

Baada ya mahojiano hayo basi Nabii Musa na Nabii Harun wakatoka ndani ya Kasri la
Fir’awn huku ikiwa ni wakati wa Magharibu na kuna mvua kali sana iliyokua ikinyesha
hivyo wakakimbilia katika moja kati ya nyumba za watu wa Bani Israil ambayo ilikua
inamilikiwa na rafiki wa kike wa Mama yao, na hivyo wakajitambulisha kua wao ni
Mitume wa Allah Subhanah wa Ta’ala na kuomba kama kuna sehemu ambayo wanaweza
kujificha mvua mpaka asubuhi yake. Na ingawa walijitambulisha hivyo lakini mwenye
nyumba hio hakua ni mwenye kuwaamini kutokana na waliyokua wakiyasema kua wao
ni Mitume wa Allah Subhanah wa Ta’ala lakini aliwaruhusu kulala katika nyumba hio.

Na anasema Imam Ahmad Ibn Muhammad Ath Thalabi kua katika usiku huo Fir’awn
aliwatuma watu wawafuatilie kina Nabii Musa na Nabii Harun kisha wawatie adabu.
Hivyo watu hao wa Misri wakawafuatilia kina Nabii Musa na wakajua walipofikia, na
wakaamua kua usiku wawavamie, na walipovamia wakati Nabii Musa na Nabii Harun
wakiwa wamelala basi mwenye nyumba alikua hajalala, hivyo mara akawaona watu
wamevamia, na marfa ghafla akaona Fimbo ya Nabii Musa inapigana na watu hao, na
ilipigana nao na kuwashinda mpaka wakakimbia wote. Hivyo huyu mtu wa Bani Israil
ambae ni mwanamke akawa ni miongoni mwa watu wa mwanzo kuwakubali Nabii Musa
na Nabii Harun kutokana na Miujiza ya Fimbo ya Nabii Musa.

Hivyo tukioa hili lilizidi kuwathibitishai watu wa Misri kuhusiana na Imani yao ya kua
Nabii Musa na Nabii Harun walikau wakitumia kweli uchawi, hivyo kabla ya siku husika
ya marudiano ambayo ni siku ya Sikukuu basi Fir’awn akatangazia kua na mashindano
ya kutafutwa kwa Wachawi ndani ya Ardhi ya Misri, hivyo kila mtu anaejua Uchawi
636

akajiandikisha na kufanyiwa majaribio uwezo wake wa Kichawi na kisha


wakashindanishwa na kufanyiwa mchujo mkali mpaka wakapatikana Wachawi bora
zaidi miongoni mwa Wachawi waliopo katika Ardhi yake na kisha wakawatayarishiwa
na kuhudumiwa juu ya kila kitu wakitakacho ili wawe na utulivu na umakini kwa ajili ya
siku hio maalum.

ِ ‫ﺎت ﻳَـ ْﻮٍم ﱠﻣ ْﻌﻠُ ٍﻮم ۞ َوﻗِﻴﻞ ﻟِﻠﻨ‬


‫ﱠﺎس َﻫ ْﻞ أَﻧﺘُ ْﻢ ﱡْﳎﺘَ ِﻤﻌُﻮ َن ۞ ﻟَ َﻌﻠﱠﻨَﺎ‬ ِ ‫﴿ﻓَﺠ ِﻤﻊ ٱﻟ ﱠﺴﺤﺮةُ ﻟِ ِﻤﻴ َﻘ‬
ََ َ ُ
َ
ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ِ‫ﻧَـﺘﱠﺒِ ُﻊ ٱﻟ ﱠﺴ َﺤَﺮَة إِن َﻛﺎﻧُﻮاْ ُﻫ ُﻢ ٱﻟْﻐَﺎﻟﺒ‬
FajumiAAa alssaharatu limeeqati yawmin maAAloomin; Waqeela lilnnasi hal
antum mujtamiAAoona; LaAAallana nattabiAAu alssaharata in kanoo humu
alghalibeena. (Surat Ash Shuara 26:38-40)

Tafsir: Hivyo wakakusanywa Wachawi katika mda na siku hio maalum. Na


wakaambiwa watu: ‘Jee na nyie Mtajumuika pamoja?’ Ili tuweze kuwafuata Wachawi
(Wa Fir’awn) kama wakishinda?

Tukio hili la Siku hii ilitangaziwa kwa kila mtu kutakiwa kua ni mwenye kuhudhuria
kwenye mashindano hayo maalum baina ya Nabii Musa, Nabii Harun na Wachawi bora
wa Ardhi ya Misri, mara tu baada ya kumalizika maandamo na shamra shamra za asubuhi
za siku hio ya Sikukuu, ili wachawi wa Fir’awn na watu wake wakishinda basi wawe ni
wenye kufuatwa na hivyo kua ni wenye kusaidia kuimarisha zaidi nguvu za mamlaka ya
Utawala wa Fir’awn.

Na ilipowadia siku hio basi watu wakakusanyika asubuhi mapema mara tu baada ya
shamra shamra za matayarisho ya sikukuu, kwani mbali ya kua ni sikukuu lakini ukweli
ni kua siku hio ilikua na umaalum wa pekee, na hivyo kila mtu alikua anataka kuona
mashindano hayo waliyotaarifiwa kuhudhuria, Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea
hali ya siku hio ilivyokua, kwa kusema kwenye Qur’an:

ِ ِِ
‫ﺎل ﻧَـ َﻌ ْﻢ‬ َ ِ‫َﺟﺮاً إِن ُﻛﻨﱠﺎ َْﳓ ُﻦ ٱﻟْﻐَﺎﻟﺒ‬
َ َ‫ﲔ۞ﻗ‬ ْ ‫﴿ ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ َﺟﺂءَ ٱﻟ ﱠﺴ َﺤَﺮةُ ﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻟﻔْﺮ َﻋ ْﻮ َن أَإِ ﱠن ﻟَﻨَﺎَ ﻷ‬
ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ِ‫َوإِﻧﱠ ُﻜ ْﻢ إِذاً ﻟﱠﻤ َﻦ ٱﻟْ ُﻤ َﻘﱠﺮﺑ‬
637

Falamma jaa alssaharatu qaloo lifirAAawna a-inna lana laajran in kunna nahnu
alghalibeena; Qala naAAam wa-innakum idhan lamina almuqarrabeena (Surat Ash
Shuara 26:40-42)

Tafsir: Na kisha wakaja Wachawi ambao wakasema kumwambia Fir’awn: ‘Jee


tutapata Malipo kama tukiwa sisi ndio Washindi?’ (Fir’awn) akasema: ‘Naam, na kwa
hakika nyinyi mtakua ni miongoni mwa waliokua karibu nami’

Aya inatubainishia sehemu ya manong’onezo yasiri waliyokubaliana Fir’awn na


Hamman na Qarun ambayo ni kua kama wachawi wao watashinda, kua watawazawadia
zawadi ambayo hakuna hata mmoja miongoni mwao ambae hataki kua ni mwenye
kuikosa zawadi hio adhimu, tuchukulie mfano wa leo sisi katika maisha yetu, ambapo
wengi sana miongoni mwetu hua ni wenye kupenda kuikumbatia Dunia na hivyo mtu
hujipendekeza na hufanya kila mbinu ili awe karibu na wenye Mamlaka, yaani kila mtu
akiwa na ukaribu na mtu mwenye madaraka ya kidunia hua ni mwenye kujiona kua
hakuna kama yeye, kwani kila kitu chake kinachohusiana na dunia yake hua ni chenye
kufanyika kiurahisi.

Ambapo waliotangulia kabla yetu walikua wanawakimbia watu wenye Mamlaka


kutokana na ucha Mungu wao. Kwa mfano Tabii Tabiina Abu Abd Rahman Abd Allah
Ibn Abd Al Aziz Ibn Abd Allah Al Amir aliefariki katika mwaka 184 Al Hijra ambae
kutokana na ucha Mungu wake basi hata Khalifa Harun Rashid wa Baghdad alikua
akifunga safari kuelekea Madina kwa ajili tu ya kumfuata Abd Allah Al Amiri na
kumuomba ushauri wake.

Abd Allah Al Amir aliamua kuhamia Makaburini pale Kaka yake alipochaguliwa kua ni
Gavana wa Mji wa Madina kwa sababu ya kutopenda kua na Ukaribu na watu wenye
Mamlaka. Na alipoulizwa kwanini akahamia Makaburini basi Abd Allah Al Amir
akasema kua: ‘Hakuna kinachowaidhisha zaidi kama Maakaburi, Hakuna
kinachofarijisha kama kusoma na hakuna Ulinzi Bora kama kua peke yako huku
ukiwa na Mola wako tu.’

Hivyo ndivyo walivyokua wacha Mungu wenye kujua madhara ya kua na ukaribu na
wenye Mamlaka, tofauti na sisi leo hii tusiojua, hivyo ikiwa sisi leo hii mtu unafanya kila
uwezavyo ili upate madaraka au uwe na ukaribu na wenye madaraka ya Mawaziri,
Ubunge, Uwakilishi n,k basi hali itakuaje kwa Wachawi wa Fir’awn ambao wao
waliahidiwa kua wakishinda watakua na ukaribu na Fir’awn ambae ndie Mungu wa Ardhi
ya Misri, kwani furaha yao iliwapelekea kusahau kuuliza jee hali itakuaje kama
wakishindwa? Ambapo sisi tutapata jibu lake mara baada ya kupata matokeo ya
Makabiliano haya.
638

Lakini hapo hapo pia Fir’awn na washauri wake wakawajaza sumu Wachawi wao hao
ambao ni watu wa Misri ili wazidi kuwachukia Nabii Musa na Nabii Harun na wala
wasiwe na khofu dhidi yao, ingawa njia wanazotumia Manabii hao zinaonesha kua si
Wachawi, lakini Manabii hao hawana mpya yeyote kwani ni wachawi tu kama walivyo
wachawi wengine na hivyo wao Wachawi wa Misri wanatakiwa kuonesha umahiri wao
zaidi katika mbinu zao kiuchawi, kama anavyosema Allah Subhanah wa Ta’ala katika
aya zifuatazo:

‫ﻳﺪ ِان أَن ُﳜْ ِﺮ َﺟﺎ ُﻛ ْﻢ ِّﻣ ْﻦ أ َْر ِﺿ ُﻜ ْﻢ ﺑِ ِﺴ ْﺤ ِﺮِﳘَﺎ َوﻳَ ْﺬ َﻫﺒَﺎ‬ َ ‫ﺎﺣَﺮ ِان ﻳُِﺮ‬ِ ‫﴿ﻗَﺎﻟُ ۤﻮاْ إِ ْن ﻫـٰ َﺬ ِان ﻟَﺴ‬
َ َ
﴾‫ٱﺳﺘَـ ْﻌﻠَ ٰﻰ‬ ِْ ‫ﺑِﻄَ ِﺮﻳ َﻘﺘِ ُﻜﻢ ٱﻟْﻤﺜْـﻠَﻰ۞ ﻓَﺄ‬
ْ ‫ﺻ ّﻔﺎً َوﻗَ ْﺪ أَﻓْـﻠَ َﺢ ٱﻟْﻴَـ ْﻮَم َﻣ ِﻦ‬
َ ْ‫َﲨﻌُﻮاْ َﻛْﻴ َﺪ ُﻛ ْﻢ ﰒُﱠ ٱﺋْـﺘُﻮا‬ ٰ ُ ُ
Qaloo in hadhani lasahirani yureedani an yukhrijakum min ardhikum bisihrihima
wayadhhaba bitareeqatikumu almuthla; FaajmiAAoo kaydakum thumma i/too
saffan waqad aflaha alyawma mani istaAAla (Surat Ta-Ha 20:63-64)

Tafsir: Wakasema (Firawn na Washauri wake) Kwa Hakika hawa (Nabii Musa na
Nabii Harun) si chochote isipokua ni wachawi wawili ambao wanataka kukufukuzeni
nyinyi kutoka katika Ardhi yenu na kukuondoleeni njia yenu ya Maisha ya Mfano
wake wa kipekee. Hivyo kusanyeni pamoja mbinu zenu na mjipange kwenye Safu, na
kwa hakika atafanikiwa sana leo hii mwenye kushinda.

Aya zinatuonesha mbinu nyengine za siri walizotumia kina Fir’awn ili washinde
mashambulizi yao hayo, ambazo ni za kisaikolojia, kwa kuwatia khofu wachawi wao kua
Nabii Musa na Nabii Harun ni maadui zao ambao ni Wachawi wanaotaka kuwahatarishia
kuvinjika kwa njia yao ya Maisha walizoishi Wazee wao, wanazoishi wao wenyewe
ndani yake na watakayoishi vizazi vyao vya baadae, njia ya mfumo wa maisha ambayo
hauna mfano wake, ambayo ndani yake unajumuisha Imani yao, tamaduni zao, uchumi
wao, mazingira yao wanayoishi ya kua darja ya juu kwani ni mabwana dhidi ya watu wa
Bani Israil ambao ni watumwa wao kwa vizazi na vizazi, n,k.

Ambapo kwa upande mwengine basi anasema Imam Ahmad Ibn Muhammad Ath Thalabi
kua: ‘Amesema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Baada ya Fir’awn
kuona maajabu ya Nabii Musa basi akajua kua haiwezakani kumshinda Nabii
Musa isipokua kwa kutumia mtu mwenye kutumia njia kama anazotumia yeye.
Hivyo akawachagua vijana miongoni mwa vijana wa watu wa Bani Israil na kisha
akawaweka kwenye mji wa Al Gharqa kwa ajili ya kusomeshwa Uchawi kama
wanavyosomeshwa katika skuli mambo mengine. Na kisha Fir’awn akamwambia
639

Nabii Musa achague siku na sehemu kwa ajili ya kukutana na vijana hao na
Mwalimu wao.

Na kisha akamwambia Mwalimu wao: ‘Jee umewasomesha vizuri?’ Mwalimu huyo


akajibu: ‘Kwa hakika nimewasomesha kila kitu kilicho bora kuhusiana na Uchawi
ambao hakuna mtu katika Ulimwengu huu atakaeweza kuudhibiti uchawi huo,
isipokua labda kitu hicho kiwe ni chenye kutokana na hali ya Mbinguni kwani
hakuna atakaeweza kua na uwezo juu ya mambo hayo.’’’

Hivyo Fir’awn, Hamman na Qarun na wazee wa Baraza wakawaahidi Wachawi wao hao,
kua kama wakishinda katika mashindano ya leo hii basi watakua ni watu waliofanikiwa
sana, kwa malipo na kwa heshima ya kusimamia na kulinda njia ya mfumo wao bora wa
Kimaisha. Kisha wachawi hao wakaamrishwa kujipanga safu kwani walikua wengi sana,
ambapo kuna tyofauti ya Idadi yao kulingana na Mtizamo wa Wanazuoni ambapo kuna
wasema kua walikua Wachawi 900, waliojitayarisha kuoneshana uwezo wao na Nabii
Musa na Nabii Harun.

Ambapo kwa upande wa Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye
anasema kua: ‘Walikua Wachawi 70’ Ambapo kwa upande wa Muqatil Ibn Sulayman
basi yeye anasema kua walikua ni Wachawi 72 na Mwalimu wao alikua ajiitwa Shamun.
Kwa upande wa Al Qalbi basi yeye anasema kua walikua ni Wachawi 70, bila ya
kuwahesabu wale ambao walikua ni Walimu wa wachawi hao. Kaab amesema kua
walikua 12000, wakati Al Suddi alisema kua walikua 30000.

Bila ya shaka hii sehemu waliyokusanyika Fir’awn, Haman, Qarun na Wachawi wao na
na watu wengine wa Misri na Nabii Musa na Nabii Harun ilikua ni sehemu ambayo
kubwa sana na yenye uwazi na kujengewa jukwaa kubwa maalum la aina yake ili kila
mtu awe ni mwenye kukaa na kuona kinachoendelea mbele ya macho yake. Kisha watu
hao wakakaa katika sehemu zao juu ya jukwaa hilo kuwazunguka Nabii Musa na
Wapinzani wao wanaotaka kuonesha utaalamu wa Uchawi wao, ambapo Wachawi hao
walikua wamepanga safu katika upande mmoja huku wakiwa wanajiamini kua mbali ya
wingi wao na Uzoefu wao lakini pia kutokana na Uwezo na Nguvu ya Mungu wao
Fir’awn ambae yuko upande wao basi watashinda tu.

Huku Nabii Musa na Nabii Harun wakasimama katika upande wa pili, huku nao wakiwa
hawana wasi wasi wowote kwani wanajua kua wako katika njia sahihi, na batil haiwezi
kusimama mbele ya haki, ambayo wanaisimamia wao kutokana na maamrisho ya Mola
wao, Mola wa Ulimwengu wote ambae ni Allah Subahanh wa Ta’ala ambae mwenye
anatuelezea yaliyofuatia baada ya hapo kama zinavyosema aya zifuatazo:
640

﴾‫ﻮﺳ ٰﻰ إِ ﱠﻣﺂ أَن ﺗُـ ْﻠ ِﻘﻰ وإِ ﱠﻣﺂ أَن ﻧﱠ ُﻜﻮ َن أَﱠوَل َﻣ ْﻦ أَﻟْ َﻘ ٰﻰ‬
َ ُ‫﴿ﻗَﺎﻟُﻮاْ ٰﳝ‬
ََ
Qaloo ya moosa imma an tulqiya wa-imma an nakoona awwala man alqa (Surat Ta-
Ha 20:65)

Tafsir: Wakasema (Wachawi wa Fir’awn) ‘Ewe Musa Jee utarusha au sisi tuwe ndio
wa mwanzo kurusha?’

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Imam Al Mushakkikin Imam Fakhr Ad Din Al Razi
kua: ‘Maneno ya aya yanatuonesha kua Wachawi hawa walikua ni wenye kuwapa
Heshima zao kina Nabii Musa na Nabii Harun, na kutokana na kufanya jambo hilo
basi Allah Subhanah wa Ta’ala akawazawadia Wachawi hawa malipo ya
kuwaonesha njia ya uongofu baada ya tukio hili’

Hivyo basi ingawa wachawi hawa walikua ni wenye kuamini nguvu na uwezo wa
Fir’awn kimungu hapa ardhini, lakini pia walikua wanajua kua kuna mambo ambayo
Mungu wao huyo hawezi kuyafanya kwani yamo nje ya mipaka ya uwezo wake, hivyo
mbali ya kua wanamuamini Fir’awn lakini walikua wanaonesha kua wako tayari
kukubaliana na matokeo, kwani hakuna mchawi zaidi yao katika Ardhi hio, na bila ya
shaka wao ni wenye kujua na kua uwezo wa kujua kama atakaoufanya Nabii Musa ni
uchawi ama ni Miujiza.

Hivyo Nabii Musa akawaruhusu kuanza wao kwanza ili wapate kuonesha uwezo wao,
kwani Nabii Musa alikua akijua kua bila ya shaka uwezo wa Mola wake hauna mfano
wake, hivyo basi ushindi ni wake, lakini ili kuwabainishia ukweli watu waliopo hapo
mbele yake basi kwanza na waanze hao wenye kusimamia kwenye Batil ili yeye apate
kuonesha ilipo haki. Hivyo Wachawi hao wakaanza kwa kutumia utukufu wa jina la yule
wanaemuamini na kumtukuza yaani Fir’awn, kama Allah Subhanah wa Ta’ala
anavyotuelezea katika aya ifuatayo:

﴾‫ﺼﻴﱠـ ُﻬﻢ وﻗَﺎﻟُﻮاْ ﺑِﻌِﱠﺰةِ ﻓِﺮ َﻋﻮ َن إِ ﱠ� ﻟَﻨَ ْﺤﻦ ٱﻟْﻐَﺎﻟِﺒُﻮ َن‬
ِِ ِ ﴿
ُ ْ َ ْ ‫ﻓَﺄَﻟْ َﻘ ْﻮاْ ﺣﺒَﺎ َﳍُْﻢ َوﻋ‬
Faalqaw hibalahum waAAisiyyahum waqaloo biAAizzati firAAawna inna lanahnu
alghaliboona (Surat Ash Shuara 26:44)

Tafsir: Hivyo wakarusha kamba zao na fimbo zao na wakasema: ‘Kutokana na


Utukufu wa Fir’awn kwa hakini sisi tutakua ni washindi’
641

Katika kurusha kwao kamba na fimbo zao, wachawi hao basi kama kawaida ya wachawi
wote basi wakawa ni wenye kufanya kiini macho mbele ya watu waliokuwepo hapo, na
hivyo watu wakaanza kuona vitu hivyo vilivyotupwa vimekua Nyoka, kadhaa
wanatambaa mbele yao, na watu waliokua wakiangalia wakaanza kuingiwa na khofu ya
ghafla kutokana na kutokea kwa nyoka hao wengi wakubwa na wa aina tofauti kwa ghafla
moja kutokana na uwezo mkubwa wa wachawi hao, watu wakataharuki kila mmoja
akataka kukimbilia upande wake kama anavyosema Allah Subhanah wa Ta’ala
kuhusiana na tukio hili kua:

﴾‫ﻮﻫﻢ و َﺟﺂءوا ﺑِ ِﺴ ْﺤ ٍﺮ َﻋ ِﻈﻴ ٍﻢ‬ ‫ﺒ‬ ‫ﻫ‬‫ﺮ‬ ‫ـ‬ ‫ﺘ‬ ‫ٱﺳ‬‫و‬ ِ


‫ﱠﺎس‬
‫ﻨ‬ ‫ٱﻟ‬ ‫ﲔ‬ ‫َﻋ‬‫أ‬ ‫ا‬‫و‬ۤ ‫ﺎل أَﻟْﻘﻮا ﻓـﻠَﻤﺂ أَﻟْﻘﻮا ﺳﺤﺮ‬ ﴿
ُ َ ْ ُ ُ َ ْ َ ْ َ َُ ْ ْ ُ َ َ ْ ْ َ ‫ﻗَ َ ُ ْ ْ َ ﱠ‬
Qala alqoo falamma alqaw saharoo aAAyuna alnnasi waistarhaboohum wajaoo
bisihrin AAadheemin (Surat Al Araf 7:116)

Tafsir: Akasema: Rusheni, na kisha baada ya kurusha wakawafanyia kiini macho


watu na kuwajaza watu khofu na walikuja na uchawi mkubwa sana.

Ambapo aya yetu hii imetumia neno Istarhabuuhum linalotokana na neno Rahiba ambalo
kwa Lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kuingiwa na khofu kutokana na kitu ambacho
hakikutegemewa kua kitatokea kutokana na maajabu yake. Hivyo hii hua ni Khofu
ambayo imejaa mshangao mkubwa ndani yake.

Ambapo kiini macho cha wachawi hao hakikua ni chenye kuathiri mtizamo wa macho
wa watizamaji hao peke yao tu akiwemo Fir’awn na Mawaziri wake, bali pia kiliathiri
mitizamo ya macho ya Nabii Musa na Nabii Harun kwa pamoja kama zinavyobainisha
aya:

﴾‫ﺼﻴﱡـ ُﻬﻢ ُﳜَﻴﱠﻞ إِﻟَْﻴ ِﻪ ِﻣﻦ ِﺳ ْﺤ ِﺮِﻫﻢ أَﻧـﱠ َﻬﺎ ﺗَﺴ َﻌ ٰﻰ‬
ِ ‫ﺎل ﺑﻞ أَﻟْ ُﻘﻮاْ ﻓَِﺈذَا ِﺣﺒﺎ ُﳍﻢ و ِﻋ‬ ﴿
ْ ْ ُ ْ َ ُْ َ ْ َ َ َ‫ﻗ‬
Qala bal alqoo fa-idha hibaluhum waAAisiyyuhum yukhayyalu ilayhi min sihrihim
annaha tasAAa (Surat Ta-Ha 20:65-66)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa) ‘Rusheni nyie.’ Kisha Kamba zao na Fimbo zao
zikaonekana kwake yeye (Nabii Musa) kutokana na uchawi wao kua ni zenye
kutembea kwa wepesi na kwa kasi.

Aya zinaendelea kutuelezea hali ilivyokua kwa upande wa Nabii Musa kwani kutokana
na macho yake kua ni yenye kuona Nyoka wengi hao wa aina tofauti na taharuki ya watu
642

wote waliokuwepo hapo basi nae aliingiwa na khofu ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala
ameielezea khofu hio kwa kutumia neno Awjasa kama zinavyosema aya:

﴾‫ﻮﺳﻰ‬ ِ ِ ِ ِ ‫﴿ﻓَﺄَوﺟ‬
َ ‫ﺲ ﰱ ﻧَـ ْﻔﺴﻪ ﺧﻴ َﻔﺔً ﱡﻣ‬
َ َْ
Faawjasa fee nafsihi kheefatan Moosa; (Surat Ta-Ha 20:67-69)

Tafsir: Hivyo akaingiwa na hali ya Khofu kwenye nafsi yake Musa.

Utajiri wa Lugha ya Kiarabu ni mkubwa sana kwani tumeona namna Allah Subhanah wa
Ta’ala alivyotumia maneno tofauti kuelezea aina tofauti za khofu kwa mfano hii Khofu
ya Wajasa ambayo ndio iliyomkumba Nabii Musa baada ya kuona wingi wa Nyoka
waliopo mbele yake wakati yeye ana fimbo moja tu, hivyo aya zinaelezea aina hii ya
khofu kwa kusema kua Faawjasa fee nafsihi kheefatan moosa yaani Hivyo akaingiwa na
mtizamo wa hali ya Khofu kwenye nafsi yake Musa ambapo khofu hii hua ni ile hisia ya
khofu anayoihisi mtu ambae anajua kuogelea kisha akawa ni mwenye kusafiri katika
chombo cha baharani anachosafiria na kisha ghafla moja kikaanza kikazama baharini bila
ya kutarajia, huku akiwa na uhakika kua bahari hio ni bahari yenye Samaki Papa hatari
sana wanaokula watu, yaani hua anajiambia kua mimi najua kuogelea lakini jee kitafuatia
nini baada ya kuogelea kwangu wakati bahari hii ina kina kirefu na kuna Papa wala watu,
jee nitaweza mimi kuwaepuka na kuwakimbia Papa hao na utaalamu wangu wa
kuogelea?

Hivyo neno Wajasa linamaanisha kua Nabii Musa aliingiwa na mawazo ya khofu juu ya
kile kitakachofuatia baada ya kutokea Nyoka hao tofauti, kwani yeye alikua anajua kua
Fimbo yake itageuka Nyoka pia, lakini jee ikishageuka kua Nyoka kitafuatia nini baada
yake? Nyoka hao watafukuzana, watacheza pamoja, watapigana ama vipi? Na kama
watapigana Jee Nyoka wangu mie mmoja ataweza kupigana na Nyoka wa aina zote
hawa? Na jee watu waliokuwepo hapa mbele yetu watamuamini nani zaidi mimi au hawa
wachawi?

Kabla ya kuendela basi na tuangalie mifano mwengine wa aina ya khofu iliyotajwa ndani
ya Qur’an ambayo ni ile iliyozungumziwa katika ya zifuatazo:

﴾ٌ‫ﻮب ﻳَـﻮَﻣﺌِ ٍﺬ و ِاﺟ َﻔﺔ‬ ۞ ِ ۞ ِ ُ ‫﴿ﻳَـﻮَم ﺗَـﺮ ُﺟ‬


َ ْ ٌ ُ‫ﻒ ٱﻟﱠﺮاﺟ َﻔﺔُ ﺗَـْﺘـﺒَـﻌُ َﻬﺎ ٱﻟﱠﺮادﻓَﺔُ ﻗُـﻠ‬ ْ ْ
Yawma tarjufu alrrajifatu; TatbaAAuha alrradifatu, Quloobun yawma-idhin
wajifatun (Surat An Naziat 79:6-8)
643

Tafsir: Katika Siku hio (ya Kiama litakapopulizwa Baragumu la Kwanza) Ardhi
itatikisika kwa nguvu sana (Na kila Mtu atakufa), Kisha litapulizwa Baragumu la
pili(na kila Mtu atafufuliwa) (Baadhi ya) Nyoyo siku hio zitatetemeka kwa Wasiwasi
na Khofu.

Ambapo aya hizi zinazungumzia tukio la Kupulizwa Baragumu la kwanza la kufa


kutolewa Roho kwa Viumbe wote na kisha kupulizwa kwa baragumu la pili ambapo aya
ya 8 inaelezea hali ya baadhi ya Watu itakavyokua kutokana na kua na hisia za Khofu
lakini kwa kusema Quloobun yawma-idhin wajifatun yaani (Baadhi ya) Nyoyo siku hio
zitatetemeka kwa Wasiwasi na Khofu. Hivyo hii ni aina ya Khofu ya inayoelezewa
kutoakana na neno Wajafa ambalo hua linamaanisha Kua Katika hali ya kushutuka na
hivyo kuufanya Moyo kua ni wenye kupiga kwa kasi sana na kwa nguvu nyingi kutokana
na Woga Mkubwa sana kiasi ya kua Woga huo hua unazipelekea Nyoyo hizo kua ni
zenye kupiga kama vile ambavyo zinavyopiga ardhini kwato za Farasi anaeenda kwa kasi
sana mpaka vishindo vya Kwato zake zikawa ni zenye kusikika.

Ambapo mfano mwengine wa aina ya khofu iliyotajwa kwenye Qur’an hua ni ule
ulitoajwa katika ile aya inayosema:

ِ ِ ‫﴿إِﱠﳕَﺎ ٱﻟْﻤﺆِﻣﻨﻮ َن ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ إِذَا ذُﻛِﺮ ﱠ‬


ُ‫آ�ﺗُﻪ‬ ْ َ‫ﺖ ﻗُـﻠُﻮﺑـُ ُﻬ ْﻢ َوإِ َذا ﺗُﻠﻴ‬
َ ‫ﺖ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ‬ ْ َ‫ٱﻪﻠﻟُ َوﺟﻠ‬ َ َ ُ ُْ
﴾‫َز َادﺗْـ ُﻬ ْﻢ إِﳝَﺎ�ً َو َﻋﻠَ ٰﻰ َرّﻬﺑِِ ْﻢ ﻳَـﺘَـ َﻮﱠﻛﻠُﻮ َن‬
Innama almu/minoona alladheena idha dhukira Allahu wajilat quloobuhum wa-
idha tuliyat AAalayhim ayatuhu zadat-hum eemanan waAAala rabbihim
yatawakkaloona (Surat Al Anfal 8:2)

Tafsir: Hakika ya Waumini hua ni wale ambao anapotajwa Allah mbele yao huhisi
khofu kwenye nyoyo zao na hizi aya (za Qur’an) wanaposomewa, hua ni wenye kuzidi
Imani yao, na hivyo hua ni wenye kumtegemea Mola wao katika kila kitu chao.

Naam hii ni aya ambayo wengi wetu tunaijua na kuinukuu sana, ambapo tunapoiangalia
ayah ii basi tunaona kua imetumia neno Wajilat pale iliposema Innama almu/minoona
alladheena idha dhukira Allahu wajilat quloobuhum yaani Hakika ya Waumini hua ni
wale ambao anapotajwa Allah mbele yao huhisi khofu kwenye nyoyo zao.

Ambapo neno Wajilat limetumika kuainisha aina ya Khofu inayotokana na neno Wajala
ambalo hua linamaanisha Kua na hisia za Khofu ambazo hua ni zenye kutokana na woga
wenye Majuto ndani yake kutokana na kua na Makosa yaliyofanyika hapo kabla.
644

Ambapo Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi analielezea neno hili kwa
kusema kua: ‘Wajl hua ni aina mbili za khofu ambazo hua ni zenye hali tofauti lakini
zenye kuendana sambamba ambapo hali ya kwanza hua ni Khofu ya Kuogopa
adhabu ya Allah Subhanah wa Ta’ala na hali ya pili hua ni inayotokana na Mtu
kujua Ukubwa, Uwezo wake Allah Subhanah wa Ta’ala juu ya Viumbe wake na
Utukufu wake. Mtu mwenye Dhambi hua ni mwenye kuhisi hali hii ya kwanza.

Ambapo hali ya pili hua ni ile ambayo haiepukiki kwa yeyote yule asiekua na
dhambi yaani awe Mtume au Malaika kwani hii hua ni Khofu ambayo wanayo wote
kulingana na darja moja au nyengine ya Kiumbe husika, hivyo khofu
inayozungumziwa na aya hii hua basi hua ni hali ya Khofu ya aina ya kwanza.’

Na kuhusiana na Wajl basi amesema Shahar Bint Hawshab kua amesema Abu Dardaa
Radhi Allahu Anhu kua: ‘Wajl maana yake hua ni mtetemeko wa Nyoyo wenye hali
kama ya kua na Moto yaani kama vile linavyochomwa jani la Mtende, hivi jee
Shahar unajua wewe hali hio?’ na Shahar akasema: ‘Naam.’ Abu Dardaa Radhi Allahu
Anhu akasema: ‘Basi Omba Dua katika wakati huo kwani huo ni wakati ambao
huenda Dua zako zikakubaliwa.’

Na akasema Thabit Ibn Bunani amesema pia kua: ‘Hakika mimi hua nnajua wakati
Dua zangu zinapokubaliwa.’ Hivyo akaulizwa: ‘Hua unajuaje?’ Thabit Al Bunani
akasema: ‘Wakati Ngozi yangu inapokua inatetemeka, Moyo wangu unapokua
unapiga kwa kasi na Macho yangu yanapokua yamejaa Machozi’

Hivyo tunarudi katika hali aliyokua nayo Nabii Musa kama ilivyowekwa wazi na Allah
Subhanah wa Ta’ala aliposema Faawjasa fee nafsihi kheefatan Moosa yaani Hivyo
akaingiwa na hali ya Khofu kwenye Nafsi yake Musa.

Na hapa sasa Muumba wa kila kitu ambae ndie aliemtuma Nabii Musa kwa Fir’awn yaani
Allah Subhanah wa Ta’ala ikambidi amtulize Mtume wake huyo ambae tayari kutokana
na maumbile yake basi amekua na khofu, na kwa vile alimwambia kwa kumuahidi kua
yuko pamoja nae na ni mwenye kuona kila kitu na kusikia kila kitu, basi akatimiza ahadi
yake kwa Mtume wake huyo kwa kumtuliza kwa maneno kama zinavyosema aya:

‫ﺻﻨَـﻌُ ۤﻮاْ إِﱠﳕَﺎ‬


َ ‫ﻒ َﻣﺎ‬ َ ِ‫َﻋﻠَ ٰﻰ۞ َوأَﻟْ ِﻖ َﻣﺎ ِﰱ َﳝِﻴﻨ‬
ْ ‫ﻚ ﺗَـ ْﻠ َﻘ‬ ْ ‫َﻧﺖ ٱﻷ‬
َ ‫ﻚأ‬َ ‫ﻒ إِﻧﱠ‬ْ َ‫﴿ﻗُـ ْﻠﻨَﺎ ﻻَ َﲣ‬
﴾‫ﺚ أَﺗَ ٰﻰ‬ ُ ‫ﺎﺣُﺮ َﺣْﻴ‬ِ ‫ﺎﺣ ٍﺮ وﻻَ ﻳـ ْﻔﻠِﺢ ٱﻟ ﱠﺴ‬
ِ
ُ ُ َ ‫ﺻﻨَـﻌُﻮاْ َﻛْﻴ ُﺪ َﺳ‬ َ
645

Qulna la takhaf innaka anta al-aAAla; Waalqi ma fee yameenika talqaf ma


sanaAAoo innama sanaAAoo kaydu sahirin wala yuflihu alssahiru haythu
ata (Surat Ta-Ha 20:67-69)

Tafsir: Hivyo akaingiwa na hali ya Khofu kwenye nafsi yake Musa. Nasi tukamwambia
Usiwe na Khofu kwani wewe utakua Juu. Na tupa hicho ulichokua nacho kwenye
mkono wako wa kulia, itavimeza kwa haraka sana vyote vilivyofanyiwa usanii kwani
kwa hakika hui ni mbinu ya usanii wa Wachawi na hawawezi kufuzu Wachawi hata
wawe na mbinu za aina gani.

Naam, baada ya Nabii Musa kupewa ubainisho huo na Allah Subhanah wa Ta’ala basi
khofu yote ikamtoka kwani tayari alikua anajua kua, ni nini kitakachotokea baada yake
na hivyo atakua ni mshindi kutokana na vithibitisho yake na hivyo atakubalika na watu
waliopo mbele yao lakini kuhusiana na kutokana na njia gani basi alikua bado hajui
itakuaje, ambapo tukio linalofuatia baada ya hapo linaelezewa na aya yenye mtizamo wa
upande mwengine wa tukio hilo ambayo imesema:

ْ ‫ﻒ َﻣﺎ َ�ْﻓِ ُﻜﻮ َن ۞ ﻓَـ َﻮﻗَ َﻊ‬


‫ٱﳊَ ﱡﻖ‬ ِ
ُ ‫ﺎك ﻓَِﺈذَا ﻫ َﻰ ﺗَـ ْﻠ َﻘ‬ َ‫ﺼ‬ ِ
َ ‫﴿ َوأ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إ َ ٰﱃ ُﻣ‬
َ ‫ﻮﺳ ٰﻰ أَ ْن أَﻟْ ِﻖ َﻋ‬
ِ ‫ﻚ وٱﻧ َﻘﻠَﺒﻮاْ ﺻ‬
﴾‫ﺎﻏ ِﺮﻳﻦ‬ ِ‫وﺑﻄَﻞ ﻣﺎ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳـﻌﻤﻠُﻮ َن۞ ﻓَـﻐُﻠِﺒﻮاْ ﻫﻨﺎﻟ‬
َ َ ُ َ َُ ُ
َ َ َْ َ َ ََ
Waawhayna ila moosa an alqi AAasaka fa-idha hiya talqafu ma ya/fikoona; (Surat
Al Araf 7:117)

Tafsir: Na tukamshushia wahy Musa (kumwambia) ‘Tupa fimbo yako’ na kisha


ikavimeza haraka sana vyote hivyo walivyovionesha.

Hivyo Nabii Musa akatabasam kisha akanyanyua mikono yake na akataja jina la Mola
wake kuashiria kua anatupa Fimbo hio kwa ajili ya Jina la Mola wake. Biismi Allahi Ar
Rahmani Ar Rahim na kisha akaitupa chini Fimbo yake.

Tafakkar! Kwani mara tu baada ya Fimbo hio ya Nabii Musa kugusa Ardhi basi iligeuka
ikawa ni Joka kubwa sana ambalo halijawahi kuonekana hapo kabla na Nabii Musa
mwenyewe, na Nabii Harun wala Fir’awn na Baraza lake na Wachawi wake na wala watu
waliokuwepo hapo kwa ajili ya kuangalia, ambapo mbali ya kua Joka hili lilikua kubwa
lakini pia lilikua na kasi isiyokua ya kawaida hususan katika kuwavamvia na kuwameza
Nyoka wa maadui zake Nabii Musa. Yaani hapa hali ilikua kama Nyangumi
anavyofungua kidogo mdomo wake na kisha akameza kundi zima la Samaki
mchanganyiko, Wakubwa, Wadogo na Dagaa.
646

Kiasi ya kua kufumba na kufumbua Nyoka wote waliokuwepo ardhini hapo walitoweka
kwa kuingia mdomoni mwa Joka la Nabii Musa, kwani hakuna hata Nyoka mmoja wa
wachawi hao isipokua alimezwa kiajabu na Joka la Nabii Musa, ambapo ingawa tukio
hili lilichukua sekunde kadhaa lakini kwa waliohudhuria ilikua kama tukio lisilotaka
kumalizika haraka, kwani ilikua kama ndoto ya kutisha ambayo mtu unaota halafu
unaomba imalizike kwa kuzindukana, lakini haimaliziki kwa kuzindukana kama
unavyotaka, kwani hii ilikua si ndoto bali ilikua ni hali halisi ya tukio hilo lilivyokua la
sekunde chache zilizoonekana kua kama dakika kadhaa.

Hivyo uwanja ukawa hautoshi watu waliokimbia wakakimbia, kwani kila mtu aliona kua
baada ya Joka hilo kumalizana na Nyoka hao basi huenda likataka kuongezea na baadhi
ya watu miongoni mwao, na waliobakia wakabakia huku wakiwa hawaamini
walichokiona kwa macho yao, kwani kweli Wachawi wa Fir’awn walikua wanatisha na
Uchawi wa Nyoka wao, lakini aliyoyafanya Nabii Musa yalikua hayana mfano wake,
kwani yalikua yanatisha mara 100 zaidi yake kwani wake yeye ulikua si Uchawi bali
ilikua ni Miujiza kutoka kwa Muumba wa kila kitu ambae ni Allah Subhanah wa Ta’ala.

MAANA NA TOFAUTI BAINA YA MUUJIZA, UCHAWI NA KARAMA.



Hivyo kabla ya kuendelea kuelezea kilichotokea baada ya hapo basi na tuangalie maana
na tofauti baina ya Miujiza, Uchawi na Karamah ili tupate kujua kilichotokea baina ya
Nabii Musa, Nabii Harun na Wachawi wa Fir’awn. Ambapo hapo kabla tuliona
kuhusiana na mtizamo wa Allamah Muhammad Sarfaraz Khan Safdar juu ya maana ya
Miujiza katika kurasa zilizotangulia.

Hivyo basi na tuangalie mtizamo wa Imam Saad Ad Din Masud Ibn Abd Allah Ibn Umar
Al Taftazani ambae yeye pia anasema kua: ‘Neno Muujiza hua ni lenye kutokana na
neno Ajz ambalo kwa lugh aya Kiarabu hua linamaanisha kinyume na Uwezo, Kitu
kisichoweza kuzuilika, kutokana upekee wake na Maajabu yake. Hivyo Muujiza
hua ni tukio ambalo hua ni lenye kuenda Kinyume na Maumbile ya Ulimwengu
ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala huyaumba kupitia kwa Mitume wake ili
kuwaunga mkono madai yao ya Utume dhidi ya Wanaopingana nao na hivyo hua
ni wenye kuthibitisha Utume wao ambao hua hauwezi kutekelezwa na
wengine.’(Imam Taftazani, Sharhul Aqaid An-Nasafiyya).

Ambapo neno Sihr hua ni lenye kutokana na neno Sahara la Kiarabu ambalo hua ni lenye
kumaanisha Kuroga, Kufanya Kiini Macho, Kunyima Ufaham wa Jambo au Kitu,
Kudanganya, Kuchanganya Muonekano wa Kitu kutokana na Mtizamo wa Jicho na
kukifanya kitu hicho kionekane vyengine, Kuficha Kitu ili kisionekane, Usanii wa
647

Kuonesha Uongo kupitia katika njia ya Ukweli, Kukigeuza kitu kutoka katika hali yake
ya kawaida na kukifanya kionekane kua kiko katika hali nyengine tofauti na maumbile
yake.

Hivyo Sihr hua ni uwezo wa kutumia njia au mbinu ambazo inaaminika kua zina uwezo
wa kuathiri hali ya kimaumbile ya kitu na kukifany akitu hicho kionekane kua
kinamuonekano mwengine tofauti na muonekano wa maumbile yake.

Ambapo anasema Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al
Ansari Al Qurtubi kua: ‘Sihr maana yake hua ni Kukificha Kitu kwa kutumia mbinu
maalum, hivyo Wachawi hufanya Mbinu kukionesha kitu kionekane kua kipo
katika muonekano mwengine, yaani Sihr hua si chochote bali hua kama vile
ambavyo mtu anaetembea Jangwani katika wakati wa Jua kali kisha kwa mbali
mbele yake akaona kua kama kuna Maji, na akifika karibu yke katik aeneo hilo
aliloona kua kuna maji basi hua haoni kitu isipokua mchanga mkavu badala yake.’

Ama kwa upande wa Karama basi ni neno linalotokana na neno la Kiarabu ambalo ni
hilo hilo Karama lenye kumaanisha Kua na Uwezo wa Kuzalisha Kitu, Kua na Thamani,
Kua na uwezo wa Kutoa Kitu, Kua Karimu, Kua na Utukufu, Kua ni mwenye
kuheshimika.

Hivyo Karama hua ni Uwezo ambao anaopewa Mtu kutokana na kua na Taqwa na
Ukaribu wa Hali ya Juu mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo kua ni mwenye
darja ya Uwalii mbele Allah Subhanah wa Ta’ala. Hivyo tunaposema Waliyu Allah basi
hua tunamaanisha Walii wa Allah Subhanah wa Ta’ala ambae hua ni Mja wa Allah
Ambae hua alie karibu na Allah Subhanah wa Ta’al kwa Kiroho na Kivitendo na kwa
kila kitu, kama inavyosema Hadith Al Quds ifuatayo:

Anasema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: Amesema Allah Subhanah wa
Ta’ala kua: ‘Hakika mimi natangazia Vita kwa yule ambae anaonesha uadui kwa
Walii wangu. Na jambo ninalolipenda zaidi ni lile ambalo linalomkaribisha Mja
wangu kwangu mimi lile ambalo nimelifanya kua ni wajibu juu yake. Na mja wangu
huanza kuupata Ukaribu kwangu kupitia katika mambo ya Sunna mpaka huanza
kumpenda, hivyo nnaanza kua ni hisia zake za kusikia na ambazo anasikilizia’, na
hisia zake za kuona ambazo anaonea, na mikono yake ambayo anakamatia, na
miguu yake ambayo anatembelea, na akiniomba basi nitampa, na akiomba ulinzi
wangu basi nitamlinda na kamwe sitosita kumfanyia jambo lolote (kwa ajili yake)
kama vile ambavyo hua nnavyosita kuchukua Roho ya Muumini, kwani anachukia
Kifo name nachukia kumvunja Moyo.(Sahih Bukhari)

Anasema Imam Jamal Islam Abu Qasim Abd Al Karim Ibn Hawazin Al Qushayri kua:
Neno Walii lina maana mbili, maana ya kwanza ni ile inayomaanisha kua: ‘Mtu
648

ambae Mambo yake yanatawaliwa na kuongozwa na Allah Subhanah wa Ta’ala.


Kama inavyosema Qur’an:

﴾‫ﲔ‬ ِِ ‫ٱﻪﻠﻟ ٱﻟﱠ ِﺬى ﻧَـﱠﺰَل ٱﻟْ ِﻜﺘَﺎب وﻫﻮ ﻳـﺘَـﻮﱠﱃ ٱﻟ ﱠ‬ ِ ِ‫﴿إِ ﱠن وﻟ‬
َ ‫ﺼﺎﳊ‬ َََ َ َ ُ ‫ﱠ‬
ُ ََّ‫ـﻰ‬ ‫ﻴ‬
Inna waliyyiya Allahu alladhee nazzala alkitaba wahuwa yatawalla alssaliheena
(Surat Al Araf 7:196)

Tafsir: Kwa hakika Walii wangu ni Allah ni yule ambae ameshusha kitabu na
kuwasimamia wanaofanya mema.

Maana ya pili hua ni yenye kumaanisha Jitihada kubwa sana ya vitendo vyake yule
ambae anaesimamiwa Mambo yake. Yaani Walii ni yule ambae amezama kila
wakati katika kumtii na kumuabudu Allah Subhana wa Ta’ala hadi kufikia hali ya
kua mambo yake mema hua yanafuatana moja baada ya jengine bila ya kukatishwa
na hata uasi mdogo mbele ya Mola wake.

Hivyo ili Walii wa Allah Subhanah wa Ta’ala awe Walii kweli basi maana zote mbili
lazima zijumuike pamoja, kwa yeye kua ni mwenye kkutekeleza Majukumu ya
Allah Subhanah wa Ta’ala kwa Yaqini na uangalifu bila ya kuchoka na hivyo Allah
Subhanah wa Ta’ala hua ni mwenye Kumlinda Walii wake huyo kutokana na
madhambi katika wakati wa raha na katika wakati wa mitihani. Kwani moja kati
ya manufaa ya kua Walii wa Allah Subhanah wa Ta’ala basi hua ni kufaidika na
Ulinzi wake yaani kua Mahfudh. Yaani hua ni sawa kama vile ambavyo kwa
Mitume basi lazima wawe ni Masum yaani wasiokua na makosa.

Hivyo Karamah hutokea kwa ajili ya Kuthibitisha Imani na Msimamo wa Mja kwa Mola
wake, Kuthibitisha Hoja dhidi ya maadui wa Allah Subhanah wa Ta’ala kwa mfano kama
vile Jenerali Bora wa Kivita katika Historia ya Dunia ambae kamwe hajawahi kushindwa
kwenye mapigano yeyote katika uhai wake na huyu si mwengine bali ni Saif Allah Khalid
Ibn Walid Radhi Allahu Anhu ambae alitakiwa anywe bilauri ya Sumu kali sana ili
athibitishe kua kweli Allah Subhanah wa Ta’ala ndio Mola wa Ulimwengu wote, na
kama akipona baada ya kunywa Sumu hio basi maadui zake hao wote watasilimu na kua
Waislam, na kutokana na Ombi hilo basi Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu akaonesha
Makarama yake kwa kunywa Sumu hio kibakuli kizima bila ya Kudhurika na Ngome hio
ya Maadui ikajisalimisha kwa Allah Subhanah wa Ta’ala kupitia kwake yeye Saifu Allah
Mas’ul Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu.

Hivyo maumbile ya Miujiza na Karamah hua yanafanana kwani hua ni yenye kutokea
kutokana na uwezo wa Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo mambo mawili haya hua ni
649

yenye kutofautiana na Sihr kwa sababu za uasili wake na utokeaji wake, ambapo
miongoni mwa tofauti hizo ni pamoja na:

1-Muujiza hua ni kitu ambacho hua kinatokea na kupingana na hali ya maumbile


ya kitu kutokana na uwezo na idhini ya Muumba yaani Allah Subhanah wa Ta’ala
juu ya kitu hicho na matokeo yake. Ambapo Sihr hua ni kitu kinachotokea
kulingana na mbinu za alizojifunza kiumbe yaani Mchawi husika.

2-Muujiza hua hausababishi kitu chochote isipokua hua ni wenye kusababisha


Kheri ndani yake, wakati Sihr hua ni yenye kusababisha madhara ndani yake.

3-Muujiza hua hauwezi kubatilishwa kwa sababu unatokana na matakwa ya


Muumba Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo hakuna atakaeweza kubatilisha
Muujiza huo au kuusitisha athari yake isipokua mwenye Muumba, lakini kwa
upande wa Sihr basi hua inaweza ikabatilishwa na Muumba mwenyewe au na
viumbe wengine kwa sababu unatokana na matakwa ya Viumbe. N.k

Hivyo bila ya shaka, Miujiza na Karamah hua ni matukio ambayo yanastaajabisha


kutokana na kuvunja sharia na kanuni za Kimaumbile kwani hutokea kuthibitisha
kuwepo kwa Muumba ambae ndie mwenye uwezo wa kufanya atakavyo juu ya viumbe
wake, na kwa kua ni matukio yenye kutoka moja kwa moja kwa Allah Subhanah wa
Ta’ala basi hua ni yaliyo juu kiuwezo na kinguvu na hivyo mbinu za matukio ya kiini
macho zifanywazo na Viumbe dhidi ya mipango yake basi hua si chochote si lolote mbele
ya maamuzi yake.

Na ndio maana, baada ya kutokea Miujiza ya Nabii Musa na Fimbo yake kuwameza
Nyoka wote wa Wachawi wa Fir’awn basi hapo hapo Wachawi hao wakajua kua, kwa
tukio hilo lililotokea basi kamwe haiwezekani kua kilichofanyika kimetokana na athari
za uchawi, kwani kweli kua wao wamewadanganya watu kwa kuwafanyia kiini macho,
lakini Nabii Musa hakua ni mwenye kufanya hivyo na ndio maana yakatokea
yaliyotokea, na kama alioufanya Nabii Musa ulikua ni uchawi, basi vimeenda wapi
Vyuma, Fimbo na Kamba zao walizozitupa na kugeuka Nyoka?

Hivyo ukabainika ukweli na waliokua wanaopingana nao ukweli huo ambao ni Fiarwn
na Wachawi wake wakawa ni waliozidiwa nguvu, na kua walioadhirika na kua wadogo
badala ya kua kama walivyokua hapo kabla, wenye nguvu na wenye kujigamba kama
walivyokua hapo kabla kama alisema Allah Subhanah wa Ta’ala alipojibu hoja hio pale
aliposema:

ِ ْ‫ﻚ وٱﻧ َﻘﻠَﺒﻮا‬


﴾‫ﺎﻏ ِﺮﻳﻦ‬ ِ ِ ْ ‫﴿ﻓَـ َﻮﻗَ َﻊ‬
َ ‫ﺻ‬ َ ُ َ َ ‫ٱﳊَ ﱡﻖ َوﺑَﻄَ َﻞ َﻣﺎ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳَـ ْﻌ َﻤﻠُﻮ َن۞ ﻓَـﻐُﻠﺒُﻮاْ ُﻫﻨَﺎﻟ‬
650

FawaqaAAa alhaqqu wabatala ma kanoo yaAAmaloona, Faghuliboo hunalika


wainqalaboo saghireena (Surat Al Araf 7:118-119)

Tafsir: Ukajulikana Ukweli na yakawa batili (yakawa hayana athari yeyote) yote
waliyoyafanya, hivyo wakawa wameshindwa na kua ni waliorudishwa huku wakiwa
wadogo (wameadhirika).

Ambapo kuhusiana na aya hizi basi anasema Imam Abu Hatim Abd Rahman Muhammad
Ibn Idris Al Razi Abd Rahman Muhammad Ibn Idris Al Razi kua: ‘Amesema Abu
Sulaym kua: ‘Tumepokea kutoka katika vizazi vilivyotangulia kabla yetu kua:
Kusoma aya mbili za Surat Yunus 10:81-82, Aya tano za Surat Al Araf 7:118-122 na
aya ya 29 ya Surat Ta-Ha hua ni tiba ya Sihri kwa Idhini ya Allah Subhanah wa
Ta’ala pale inaposomewa kwenye Bakuli la maji kisha maji hayo amwagiwe
kichwani Mgonja huyo. ’’

Hivyo Nabii Musa akaichukua tena Fimbo yake hiyo na kuikamata mkononi na hapo
hapo Wachawi wote wa Fir’awn wakajikuta kua ni wenye kuenda chini bila ya
kutegemea na kua ni wenye kusujudu kutokana na kuzidiwa na nguvu za maajabu ya
Miujiza hio, na wakajisalimisha kwa Allah Subhanah wa Ta’ala kama zinavyosema aya:

﴾‫وﻣﻮﺳﻰ‬ ‫ن‬ ‫و‬‫ﺎر‬‫ﻫ‬ ِ


‫ب‬ ‫ﺮ‬ِ
‫ﺑ‬ ‫ﱠﺎ‬
‫ﻨ‬ ‫آﻣ‬ ‫ا‬
ْ‫ﻮ‬ۤ ُ‫﴿ﻓﺄُﻟْ ِﻘﻰ ٱﻟﺴﺤﺮة ﺳ ﱠﺠﺪا ﻗﺎﻟ‬
ٰ َ ُ َ ُ َ ّ َ َ َ ً ُ َُ َ ‫َ َ ﱠ‬
َ
Faolqiya alssaharatu sujjadan qaloo amanna birabbi haroona wamoosa; (Surat Ta-
Ha 20:70)

Tafsir: Kisha wakaanguka Wachawi hao huku wakiwa katika kusujudu, wakasema:
‘Tumeamini Mola wa Harun na Musa’.

Ambapo tunaona kua aya hio imebainisha kuamini kwa Wachawi hao ambao wamesema
kua wamemuamini Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ni Mola wa Mitume hao wawili
waliopo mbele yao, na Wachawi hawa wakabainisha kua Mitume hao ni Nabii Harun na
Nabii Musa ambapo kwa aya hii kuanza kumtaja Nabii Harun basi inakua ni yenye
kuweka wazi heshima ya ukubwa wa Nabii Harun kiumri zaidi ya Nabii Musa, na kwa
upande mwengine basi hii pia ni kulingana na mpangalio wa Qur’an katika kuainisha
mpangilio mzuri wa kilugha na kimtiririko wa aya zake, na hivyo kumrahisishia msomaji
katika usomaji wake, uhifadhi wake, uvutiaji wake, n.k

Ambapo kwa upande mwengine basi aya zinalielezea tukio hilo kwa kusema:
651

﴾‫ﻮﺳ ٰﻰ وَﻫﺎرو َن‬ ِّ ‫ﲔ۞ ر‬ ِ َ‫ب ٱﻟْﻌﺎﻟ‬


ِ ِ ۤ ُ‫ﺎﺟ ِﺪﻳﻦ۞ﻗﺎﻟ‬
ِ ِ ﴿
ُ َ َ ُ َ َ َ ّ َ َ َ َ ‫َوأُﻟْﻘ َﻰ ٱﻟ ﱠﺴ َﺤَﺮةُ َﺳ‬
‫ﻣ‬ ‫ب‬ ‫ﻤ‬ ‫ﺮ‬‫ﺑ‬ ‫ﱠﺎ‬
‫ﻨ‬ ‫آﻣ‬ ‫ا‬
ْ‫ﻮ‬
Waolqiya alssaharatu sajideena; Qaloo amanna birabbi alAAalameena; Rabbi
moosa waharoona (Surat Al Araf 7:120-122)

Tafsir: Na wakaanguka Wachawi hao huku wakiwa katika kusujudu, Wakasema


(Wachawi hao) Tumeamini juu ya Mola wa Ulimwengu wote, Mola wa Musa na
Harun.

Ambapo aya hizi nazo pia zinaelezea mtizamo huo huo lakini kwa upande mwengine,
kwa kuanza na Nabii Musa kisha zikamtaja Nabii Harun na hii haimaanishi kua aya
zinagongana wala kua zinapingana kwa sababu kusema Haruna na Musa na kusema Musa
na Harun kote hua kuna maana moja, isipokua ni kama tulivyosema kua aya za Surat Ta-
Ha zimeanza na Nabii Harun kwa kuainisha heshima ya ukubwa kiumri ambapo aya hizi
za Surat Al Araf zimeanza na Nabii Musa na kisha Nabii Harun kuanisha heshima ya
Ukubwa kwa kidarja baina ya Manabii wawili hawa na pia kuainisha mpangilio mzuri
Lugha na uzuri wa mtiririko wa aya katika Sura.

Ambapo tunaona kua Surah hii ya 7 katika mpangilio wa Sura za Qur’an basi ni Sura
ambayo ina aya 206 ambazo ndani yake imezungumzia mambo tofauti ikiwa na lengo
kuu kuwausia na kuwaita Makafiri katika Dini ya Allah Subhanah wa Ta’al, na hivyo
kuelezea visa vya Manabii mbali mbali ndani yake akiwemo Nabii Adam, Nabii Salih,
Nabii Nuh, Nabii Hud, Nabii Lut, Nabii Shuayb, na Nabii Musa, huku aya zote hizo 206
zikiwa ni zenye kumalizia na herufi Nun mwishoni mwa aya zake kama zinavyoonesha
aya zetu hizi tatu zisemazo:

﴾‫ﻮﺳ ٰﻰ وَﻫﺎرو َن‬ ِّ ‫ﲔ۞ ر‬ ِ َ‫ب ٱﻟْﻌﺎﻟ‬


ِ ِ ۤ ُ‫ﺎﺟ ِﺪﻳﻦ۞ﻗﺎﻟ‬
ِ ِ ﴿
ُ َ َ ُ َ َ َ ّ َ َ َ َ ‫َوأُﻟْﻘ َﻰ ٱﻟ ﱠﺴ َﺤَﺮةُ َﺳ‬
‫ﻣ‬ ‫ب‬ ‫ﻤ‬ ‫ﺮ‬‫ﺑ‬ ‫ﱠﺎ‬
‫ﻨ‬ ‫آﻣ‬ ‫ا‬
ْ‫ﻮ‬
Waolqiya Alssaharatu Sajidiina; Qaluu Amanna birabbi alAAalamiina; Rabii Muusa
wa Haruna.(Surat Al Araf 7:120-122)

Mpangilio huu wa vina kati aya za Qur’an ni moja kati ya Miujiza ya Qur’an kwani
ingawa Qur’ana haikushuka yote kwa pamoja, na imeshushwa kwa mda wa miaka 23
lakini ina mpangilio ambao ni wa kipekee, kwa sababu kila Aya imeshuka kwa wakati
wake na pia kulingana na tukio lake maalum, tena bila ya mpangilio, lakini
unapoziangalia Aya basi tunaona kua zimepangika kama kwamba aya zote zimeshuka
kwa wakati mmoja, na hii ni kwa sababu Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua
652

akiambiwa na Malaika Jibril baada ya kushushiwa aya husika kua ayah hii utaiweka
kwenye Sura fulani baada ya aya fulani kabla ya aya fulani.

Kama anavyosema Imam Ahmad Ibn Hanbal katika Musnad Imam Hanbal katika hadith
ya Uthman Ibn Al Aas Radhi Allahu Anhu amabe anasema: ‘Mimi nilikua nimekaa na
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na mara akawa ni mwenye kukaza macho
katika kukiangalia kitu fulani, kisha akainamisha macho yake mpaka akawa kama
anaiangalia ardhi, na kisha akaangalia kitu chengine na akasema: ‘Amekuja Jibril
na akaniambia kuiweka ayah hii katika sehemu hii ya Surah hii.’’

‫ﺂء ِذى ٱﻟْ ُﻘْﺮَ ٰﰉ َوﻳـَْﻨـ َﻬ ٰﻰ َﻋ ِﻦ ٱﻟْ َﻔ ْﺤ َﺸ ِﺎء‬


ِ ‫ﺎن وإِﻳﺘ‬
َ َ ِ ‫ٱﻹﺣ َﺴ‬ ِ
ْ ‫ٱﻪﻠﻟَ َ�ْ ُﻣُﺮ ﺑِﭑﻟْ َﻌ ْﺪل َو‬
‫﴿إِ ﱠن ﱠ‬
﴾‫َوٱﻟْ ُﻤْﻨ َﻜ ِﺮ َوٱﻟْﺒَـ ْﻐ ِﻰ ﻳَﻌِﻈُ ُﻜ ْﻢ ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜ ْﻢ ﺗَ َﺬ ﱠﻛُﺮو َن‬
Inna Allaha ya’muru bialAAadli waal-ihsani wa-eeta-i dhi alqurba wayanha AAani
alfahsha-i waalmunkari waalbaghyi yaAAidhukum laAAallakum tadhakkaroona
(Surat An-Nahl, 16:90)

Tafsir: Hakika Allah anaamrisha uadilifu na ihsan, na kuwasaidia ndugu na jamaa,


na amekataza al Fahshaa (Madhambi), uovu na udhalim wa aina zote, Anakuonyeni
ili muwe wenye kukumbuka.

Tunarudi katika kisa chetu cha Nabii Musa katika aya zetu za Surat Al Araf 7:120-122
zisemazo kua: Waolqiya Alssaharatu Sajidiina; Qaluu Amanna birabbi alAAalamiina;
Rabii Muusa wa Haruna. Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Sultan al Mutakkalimin
Imam Fakhr Ad Din Al Razi kuhusiana na aya hizi kua: ‘Wakati Wachawi hao
waliposema kua Tumemuamini Mungu wa Ulimwengu, basi Fir’awn akawauliza
kwa kusema kua: ‘Yaani Mnamaanisha mimi si ndio?’ Wachawi hao nao
wakasema: ‘Mungu wa Musa Na Harun’’

Hivyo baada ya Wachawi hao kusema hivyo basi Fir’awn akathibitisha kwa kuweka wazi
ile siri aliyokua akinongo’onezana na Hamman na Qarun pale mara ya kwanza
walipokabiliana na Nabii Musa na Nabii Harun kwenye baraza la Fir’awn katika tukio la
aya ya Surat Ta-Ha 20:62 yasemayo: FatanazaAAuu Amrahum Baynahum Waasaruu
AlNajwa yaani Na wakajadilana nini wafanye juu ya jambo lao baina yao na waafanya
kua siri mazungumzo yao yaani kuhusiana na nini watakachofanya kama ikiwa
wataadhirika, hivyo walichokubaliana kukifanya kama ikiwa Wachawi wao watashindwa
basi kinawekwa wazi na aya zinazosema:
653

‫ٱﻟﺴ ْﺤَﺮ ﻓَ َﻸُﻗَ ِﻄّ َﻌ ﱠﻦ‬


ِ ‫ِ ِ ﱠِ ﱠ‬ َ َ‫﴿ ﻗ‬
ّ ‫ﺎل َآﻣﻨﺘُ ْﻢ ﻟَﻪُ ﻗَـْﺒ َﻞ أَ ْن ءَاذَ َن ﻟَ ُﻜ ْﻢ إﻧﱠﻪُ ﻟَ َﻜﺒﲑُُﻛ ُﻢ ٱﻟﺬى َﻋﻠ َﻤ ُﻜ ُﻢ‬
َ ‫ﱠﺨ ِﻞ َوﻟَﺘَـ ْﻌﻠَ ُﻤ ﱠﻦ أَﻳـﱡﻨَﺂ أ‬
‫َﺷ ﱡﺪ‬ ِ ‫ﺻﻠِّﺒَـﻨﱠ ُﻜ ْﻢ ِﰱ ُﺟ ُﺬ‬
ْ ‫وع ٱﻟﻨ‬
ٍ ِ ِ ِ
َ ُ‫أَﻳْﺪﻳَ ُﻜ ْﻢ َوأ َْر ُﺟﻠَ ُﻜ ْﻢ ّﻣ ْﻦ ﺧﻼَف َوَﻷ‬
﴾‫ﻋ َﺬاﺎﺑً وأَﺑـ َﻘﻰ‬
ٰ َْ َ
Qala amantum lahu qabla an adhana lakum innahu lakabeerukumu alladhee
AAallamakumu alssihra falaoqattiAAanna aydiyakum waarjulakum min khilafin
walaosallibannakum fee judhooAAi alnnakhli walataAAlamunna ayyuna ashaddu
AAadhaban waabqa (Surat Ta-Ha 20:71)

Tafsir: Akasema (Fir’awn): ‘Mmemuamini hata kabla ya mimi kukuamrisheni? Ama


kwa hakika yeye ni Mkubwa wenu ambae ndie aliekufundisheni Uchawi, hivyo
nitakukateni mikono yenu na miguu yenu ya pande tofauti na bila ya shaka
nitakusulubuni kwenye vigogo vya Mitende na kisha mtajua ni nani (miongoni mwetu
mimi na Mola wenu) mwenye kutoa adhabu kubwa na yenye kudumu’

Hivyo Fir’awn akawajia juu Wachawi wake hao ambao alikua akijisifa kua nao, ambao
aliwatunza na kuwaamini kwa kila kitu na kuamini ubora wao kua hakuna mchawi
mwenye uwezo mkubwa zaid yao, lakini badala yake wamekua wadogo mbele ya Nabii
Musa na Nabii Harun, na kisha pia wakawaamini Manabii hao mbele ya halaiki ya watu
wote was Misri. Na hivyo kua ni dhalilisho kubwa sana kupita kiasi mbele ya Utawala
wa Fir’awn kwani kukubali kwao huko kunahatarisha kuanguka kwa Mamlaka hayo
yaliyodumu kwakarne na karne, halafu yanataka kuangushwa na watu wawili tu, ambao
hata upanga hawajanyanyua katika jaribio lao hilo linaloonekana kua ni lenye kua na
mafanikio makubwa sana na kuto athari kubwa sana kwa Jamii.

Ambapo kwa upande wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu na Abd Allah Ibn
Masud Radhi Allahu Anhu basi wao wanasema kua: ‘Nabii Musa alimuita Mkuu wa
wachawi hao kabla ya Makabiliano yao na kumwambia kua: ‘Jee kama utaukubali
ukweli kama ukiwa ni miongoni mwa walioshindwa?’ Mchawi huyo akajibu huku
akijinata kwa kausema kua: ‘Hakika mimi nnaapa kua kesho nitaonesha Uchawi
ambao haujawahi kuoneka hapo kabla, na hakuna atakaeweza kuushindana nao.
Hivyo kama ukinishinda basi nitakuamini’ ’Na Fir’awn alikuwepo wakati Mkuu huyo
wa Wachawi alipokua akiahidi hivyo.
654

Na ndio maana baada ya kushindwa kwao basi Fir’awn akawa ni mwenye kuwashutumua
Wachawi hao kua wameshirikiana na Manabii Wawili hao na hivyo huenda wakawa ni
wakubwa wao katika fani hio ya Ilm ya Uchawi. akaamua kutoa adhabu kali ya kitaifa
ambayo kila mmoja miongoni mwa Wachawi hao atakumbana nayo kama hakua ni
mwenye kumkanusha Mola wa Nabii Musa na Nabii Harun, kwa kuonesha mfano ni nani
mwenye kutoa adhabu kali baina yake na Mola wa Nabii Musa na Nabii Harun, ambapo
ukali wa adhabu hio utaonekana na kila mmoja miongoni mwa watu Ardhi ya Misri, ili
kuwatia khofu watu wasije wakafuata mtizamo wa Nabii Musa na Nabii Harun na
Wachawi hao.

Na pia Fir’awn akaweka wazi kua ukali wa adhabu hio ni wenye kutokana pia na
kisingizio kua kuamini kwao Wachawi hao kutapelekea kuwafanya watu wa Bani Israil
na kila atakaeamini Mtizamo huo kua ni mwenye kuihama Ardhi ya nchi hio, na hivyo
pia kua ni wenye kupunguza nguvu ya Mamlaka ya Utawala wake katika Ardhi hio kwa
kusema:

‫ﺎل ﻓِْﺮ َﻋ ْﻮ ُن َآﻣﻨﺘُ ْﻢ ﺑِِﻪ ﻗَـْﺒ َﻞ أَن آذَ َن ﻟَ ُﻜ ْﻢ إِ ﱠن َﻫـٰ َﺬا ﻟَ َﻤ ْﻜٌﺮ ﱠﻣ َﻜْﺮُﲤُﻮﻩُ ِﰱ ٱﻟْ َﻤ ِﺪﻳﻨَ ِﺔ‬
َ َ‫﴿ﻗ‬
ٍ َ‫ف ﺗَـﻌﻠَﻤﻮ َن۞ﻟَـﺄُﻗَ ِﻄّﻌ ﱠﻦ أَﻳ ِﺪﻳ ُﻜﻢ وأَرﺟﻠَ ُﻜﻢ ِﻣﻦ ِﺧﻼ‬ ِ ِ
‫ف ﰒُﱠ‬ ّْ ْ َُْ ْ َ ْ َ ُ ْ َ ‫ﻟﺘُ ْﺨ ِﺮ ُﺟﻮاْ ﻣْﻨـ َﻬﺂ أ َْﻫﻠَ َﻬﺎ ﻓَ َﺴ ْﻮ‬
﴾‫َﲨَﻌِﲔ‬ ْ ‫ُﺻﻠِّﺒَـﻨﱠ ُﻜ ْﻢ أ‬
َ ‫ﻟَـﺄ‬
Qala firAAawnu amantum bihi qabla an adhana lakum inna hadha lamakrun
makartumoohu fee almadeenati litukhrijoo minha ahlaha fasawfa taAAlamoona;
LaoqatiAAanna aydiyakum waarjulakum min khilafin thumma laosallibannakum
ajmaAAeena (Surat Al Araf 7:123-124)

Tafsir: Fir’awn akasema: ‘Mmemuamini hata kabla ya mimi kukuamrisheni’ Hakika


huu ni mpango mlioupanga katika mji ili kuwahamisha kutoka ndani yake watu wake.
Lakini Mtujua (kitakachofuatia); Kwani nitakukateni mikono yenu na miguu yenu
pande tofauti na kisha nitakusulubuni nyote kwa pamoja.

Ambapo kwa mtizamo wa Imam Ahmad Ibn Muhammad Ath Thalabi basi yeye anasema
kua viongozi wa Wachawi hao walikua ni watano ambao ni Sabur, Ghadur, Hafaz,
Musifa na Khitat. Na hawa ndio waliokua ni wenye kumuamini Allah Subhanah wa
Ta’ala baada ya Kuona Miujiza ya Nabii Musa.

Aya yetu hii imetumia neno Salaba ambalo wengi hua wanalitafsiri kama Kusulubu,
lakini neno hili pia hua linamanisha Kuua mtu kwa kutumia njia Maarufu inayojulikana
na wengi, Kukata Kiungo cha Mwili na Kisha Kutoa Nyama ya ndani ya Mfupa. Hivyo
655

adhabu hio inakua ni kukatwa Mikono na Miguu kwa Upanga na kasha kutolewa Nyama
ya Ndani ya Mfupa uliokatwa na kishwa kutundikwa juu ya Mti mpaka Ufe.

Hivyo ingawa Adhabu hio ilikua kali sana lakini Wakuu wa Wachawi hao hawakua na
Woga hivyo wakasema:

ِ �‫﴿ﻗَﺎﻟُ ۤﻮاْ إِ ﱠ� إِ َ ٰﱃ رﺑِﻨَﺎ ﻣﻨ َﻘﻠِﺒﻮ َن۞ وﻣﺎ ﺗَ ِﻨﻘﻢ ِﻣﻨﱠﺂ إِﻻﱠ أَ ْن آﻣﻨﱠﺎ ِﺂﺑ‬
‫ت َرﺑِّﻨَﺎ ﻟَ ﱠﻤﺎ َﺟﺂءَﺗْـﻨَﺎ‬ َ َ ُ َ َ ُ ُ َّ
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ﺻ ْﱪاً َوﺗَـ َﻮﻓﱠـﻨَﺎ ُﻣ ْﺴﻠﻤ‬
َ ‫َرﺑـﱠﻨَﺂ أَﻓْ ِﺮ ْغ َﻋﻠَْﻴـﻨَﺎ‬
Qaloo inna ila rabbina munqaliboona; Wama tanqimu minna illa an amanna bi-
ayati rabbina lamma jaatna rabbana afrigh AAalayna sabran watawaffana
muslimeena(Surat Al Araf 7:125-126)

Tafsir: Wakasema (Wachawi hao): ‘Hakika sisi kwa Mola wetu tunarudi; Na wewe
unatufanyia kisasi sisi kwa sababu tu ya kua tumeamini vithibitisho vyake
vilipotufikia. Ewe Mola wetu tumwagie Subira na utujaalie sisi kua ni wenye kufariki
hali ya kua ni Waislam’.

Naam bila ya shaka hapa tunaona mfano wa watu wenye Imani ya kweli, ambao sio tu
wameamini lakini pia mbali ya kuahidiwa kua wataadhibiwa adhabu kali yenye upekee
katika mfano wake lakini hapo hapo wakaamua kua ni wenye kusema ukweli mbele ya
Mtawala ambae ni Mkatili, asiejali watu wake, bali ni mwenye kujali Maslahi yake.
Hivyo mbali ya kua watu hawa wameamini lakini pia ni wenye kupigania Imani yao
mbele ya Adui yao tena bila ya kua na woga wala wasiwasi.

Ambapo baada ya majibishano hayo basi Wachawi hao wakakamatwa na Fir’awn na


kukatwa mikono ya kulia na miguu ya kushoto, wakatolewa nyama ya ndani ya mifupa
ya miguu na mikono waliyokatwa na kisha wakatundikwa kwenye vigogo vya Mitende
mpaka wakafa.

Ambapo unapoangalia hali ya Wachawi hawa katika siku hio, basi unaona kua waliamka
asubuhi wakia ni Makafiri lakini waliimalizia siku hio huku wakiwa ni Waumini wa
Kweli tena waliokufa Jihadi na hivyo katika siku hio hio moja walijiepusha na Moto wa
Jahannam ambao waliamka wakiwa wanauelekea lakini baada ya tukio hilo wakawa ni
wenye kuukimbia kwa kasi kubwa sana na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akawajaalia
kua ni wenye kuingia Peponi.
656

Nabii Musa akaondoka na Nabii Harun na Fimbo yake hadi katika maeneo wanayokaa
watu wa Bani Israil na kujumuika pamoja na watu wake hao, na kisha akawa ni mwenye
kuwausia watu hao wa Bani Israil kuhusiana na Mola wao ambae ni Allah Subhanah wa
Ta’ala na kuhusianai na jukumku lake juu yao huku akiwa ni mwenye kusubiri amrisho
litakalofuatia kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala.

Ambapo kwa upande wa Watu wa Misri basi baada ya Miujiza ya Fimbo ya Nabii Musa,
na kusulubiwa kwa wachawi wake Fir’awn, basi watu wakashangazwa na ukubwa na
uthabiti wa Imani ya watu hao waliokua ni wenye kumuamini Nabii Musa ambao
hawakua ni watu wa Bani Israil bali walikua ni watu wa Misri, hivyo Firawn na watu
wake wakawa na khofu kua hueanda Nabii Musa akapata watu wengi na wafuasi wake
wataongezeka kutokana na kukubalika na hata wakubwa wa Wachawi hao na
kumuadhirisha Fir’awn mbele ya halaiki ya watu. Hivyo watu hao wakasema
kumwambia Fir’awn kama zinavyosema aya.

ِ ‫ﻮﺳ ٰﻰ َوﻗَـ ْﻮَﻣﻪُ ﻟِﻴُـ ْﻔ ِﺴ ُﺪواْ ِﰱ ٱﻷ َْر‬ ِ ِ ِ َ َ‫﴿ َوﻗ‬


‫ض َوﻳَ َﺬ َرَك‬ َ ‫ﺎل ٱﻟْ َﻤﻸُ ﻣﻦ ﻗَـ ْﻮم ﻓْﺮ َﻋﻮ َن أَﺗَ َﺬ ُر ُﻣ‬
﴾‫ﺎﻫﺮو َن‬ ِ َ‫ﺎل ﺳﻨـ َﻘﺘِﻞ أَﺑـﻨﺂءﻫﻢ وﻧَﺴﺘﺤﻴِـﻰ ﻧِﺴﺂءﻫﻢ وإِ ﱠ� ﻓَـﻮﻗَـﻬﻢ ﻗ‬ َ ‫ﻗ‬
َ ‫ﻚ‬ ‫ﺘ‬ ِ‫و‬
‫آﳍ‬
ُ
ُ ْ ْ َْ َ َ ُ ْ َ ُ
ْ َْ َ ُ َ َ ْ ّ ُ َ َ َ
Waqala almalao min qawmi firAAawna atadharu moosa waqawmahu liyufsidoo fee
al-Ardhi wayadharaka waalihataka qala sanuqattilu abnaahum wanastahyee
nisaahum wa-inna fawqahum qahiroona (Surat Al Araf 7:127)

Tafsir: Wakasema Machifu miongoni mwa watu wa Fir’awn (kumuuliza Fir’awn):


‘Utamuachia Musa na watu wake wafanye israf katika Ardhi na hivyo kuachana nawe
na kuachana na Miungu yako?’ Nae (Fir’awn) akasema: ‘Tutawaua Watoto wao na
kisha tutawaachia hai Wanawake zao na bila ya shaka sisi tuna uwezo usiopingika
dhidi yao’’

Ambapo ingawa aya imetumia neno, ‘Aalihatak’ kumaanisha Miungu wako lakini kwa
kisomo chengine pia hua linasomeka kama ‘Ilahatak’ kumaanisha ‘Uungu wako’ na hii
ni kulingana na mtizamo wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu na hivyo
kumaanisha kua watu hao walikua wakijadili kuhusiana na hatari ya kuachwa kuabudiwa
kwa Fir’awn, lakini Wanazuoni wengine wanasema kuhususiana na ayah hii kua: ‘Aya
inabidi isomeke kama ilivyo kwa kutumia neno Aalihatak kwa sababu Firawn
alikua na Miungu yake ambao alikua akiiabudu mbali ya ile ambayo aliwataka
watu wake wanaiabudu na ndio maana akawa ni mwenye kusema kua yeye ndie
Mungu Mkuu kwani Miungu hio myengine ilikua inaabudiwa kutokana na
maamrisho yake’
657

Allah Subhanah wa Ta’ala anatuwekea wazi kuhusiana na hali ilivyokua baada ya hapo
kua mbali ya watu hao kuonyeshwa Miujiza hio mikubwa na Nabii Musa na Nabii Harun,
iliyowapelekea kuamini kwa Wachawi wa Fir’awn, lakini adhabu waliyopewa Wachawi
hao iliwapelekea watu kua na khofu kubwa kutokana na kua kila atakaekua anafuata
Imani ya Nabii Musa na Nabii Harun basi atakua ni miongoni mwa watakaokua ni mifano
hai ya kukatwa mikono na miguu na kisha kutolewa nyama za ndani za mifupa hio na
kutundikwa mpaka kifo, kama vile walivyotolewa mifano Wachawi wa Fir’awn, na
kutokana na khofu hio basi ikawa ni watu wachache sana miongoni mwa Watu wa
Fir’awn waliokua wakimfuata, na hata hivyo nao walikua wakimfuata kwa kificho
kutokana na woga huo kama zinavyosema aya:

‫ف ِّﻣﻦ ﻓِْﺮ َﻋ ْﻮ َن َوَﻣﻠَﺌِ ِﻬ ْﻢ أَن‬ٍ ‫﴿ ﻓَﻤﺂ آﻣﻦ ﻟِﻤﻮﺳﻰ إِﻻﱠ ذُ ِرﻳﱠﺔٌ ِﻣﻦ ﻗَـﻮِﻣ ِﻪ ﻋﻠَﻰ ﺧﻮ‬
َْ ٰ َ ْ ّ ّ ٰ َ ُ ََ َ
ِ ِ ِ ‫ﻳَـ ْﻔﺘِﻨَـ ُﻬ ْﻢ َوإِ ﱠن ﻓِْﺮ َﻋ ْﻮ َن ﻟَ َﻌ ٍﺎل ِﰱ ٱﻷ َْر‬
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ض َوإِﻧﱠﻪُ ﻟَﻤ َﻦ ٱﻟْ ُﻤ ْﺴ ِﺮﻓ‬
Fama amana limoosa illa dhurriyyatun min qawmihi AAala khawfin min
firAAawna wamala-ihim an yaftinahum wa-inna firAAawna laAAalin fee al-Ardhi
wa-innahu lamina almusrifeena (Surat Yunus 10:83-86)

Tafsir: Lakini hakuna aliemuamini Musa isipokua waliomo katika Kizazi cha watu
wake (Watu wa Bani Israil) kutokana na khofu ya Fir’awn na Machifu wake kua
watawachukulia hatua, na kwa hakika Fir’awn alikua mwenye kibri kwenye Ardhi na
ni mwenye kufanya Israfu.

Ingawa aya hii imetumia neno Dhurriyatun ambalo maana yake hua ni Kizazi, lakini
Wazuoni wametofautina kuhusiana na neno hili katika ayah hii kwani kwa upande wa
Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu na Imam Ad Dahaq Ibn Muzahim basi wao
wamesema kua: ‘Neno hili hapa linamaanisha Idadi ndogo ya Wafuasi’, ambapo kwa
upande wa Imam Mujahid Ibn Sulayman na Iman Abu Muhammad Sulaiman Ibn
Mihran Al Kahili Al Asad Al Amash basi wao wanasema kua : ‘Kwa kua Watu wa
Bani Israil aliozaliwa nao Nabii Musa wengi wao walikua wameuliwa na hivyo
waliobakia walikua ni wa kizazi kilichofuata baada yake, basi ndio maana aya
ikatumia neno Dhurriyat kumaanisha Kizazi kilichozaliwa baada yao’

Na pia kuna wasemao kua neno hili limemaanisha: ‘Kua ni watu wachache wa miongoni
mwa watu Misri waliomuamini Nabii Musa’ na pia kuna wasemao kua Dhurriyat:
‘Walikua ni watoto waliochanganya baina ya Wanaume wa Misri na Wanawake wa
658

Bani Israil waliozaliwa baada ya kipindi cha kuuuliwa Watoto wa kiume wa Bani
Israil’

Hivyo Nabii Musa akawausia watu wake hao waliokua wakimuamini kuwatoa khofu kwa
kuwaambia kua kama kweli wanamuamini Allah Subhanah wa Ta’ala basi na
wajisalimishe kwake kikamilifu kwa kumtegemea kwa kila kitu:

ْ‫ﲔ ۞ ﻓَـ َﻘﺎﻟُﻮا‬ ِ ِ‫ﭑﻪﻠﻟِ ﻓَـﻌﻠَﻴ ِﻪ ﺗَـﻮﱠﻛﻠُ ۤﻮاْ إِن ُﻛﻨﺘُﻢ ﱡﻣﺴﻠ‬
‫ﻤ‬ ِ ِِ َ َ‫﴿ َوﻗ‬
َ ْ َ ْ َ ‫ﻮﺳ ٰﻰ ٰﻳـ َﻘ ْﻮم إن ُﻛﻨﺘُ ْﻢ َآﻣﻨﺘُ ْﻢ ﺑ ﱠ‬ َ ‫ﺎل ُﻣ‬
‫ﻚ ِﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻘ ْﻮِم‬
َ ِ‫ﲔ۞ َوَِﳒّﻨَﺎ ﺑَِﺮ ْﲪَﺘ‬ ِِ ِ ِ ِ ِ‫ﻋﻠَﻰ ﱠ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟ ﺗَـ َﻮﱠﻛ ْﻠﻨَﺎ َرﺑـﱠﻨَﺎ ﻻَ َْﲡ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ﻓْﺘـﻨَﺔً ﻟّْﻠ َﻘ ْﻮم ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬ ٰ َ
﴾‫ٱﻟْ َﻜﺎﻓِ ِﺮﻳﻦ‬
َ
Waqala moosa ya qawmi in kuntum amantum biAllahi faAAalayhi tawakkaloo in
kuntum muslimeena; Faqaloo AAala Allahi tawakkalna rabbana la tajAAalna
fitnatan lilqawmi aldhdhalimeena; Wanajjina birahmatika mina alqawmi
alkafireena (Surat Yunus 10:84-86)

Tafsir: Na akasema Musa (Kuwaambia watu wake): ‘Enyi watu wangu kama ikiwa
mmemuemini Allah basi mtegemeeni yeye katika kila kitu kama ikiwa Mmejisalimisha
kwa Allah’ Nao wakasema: ‘Kwake yeye Allah sisi tunategemea, ewe Mola wetu
usitujaalie kua ni mtihani dhidi ya Watu Madhalimu. Na utuokoe kwa Rehma zako
kutokana na watu waliokufuru.’

Na bila ya shaka watu hao walithibitisha hilo, na kisha wakamuomba Allah Subhanah wa
Ta’ala kwa kusema: Rabbana la tajAAalna fitnatan lilqawmi aldhdhalimeena;
Wanajjina birahmatika mina alqawmi alkafireena yaani ‘Ewe Mola wetu usitujaalie
kua ni mtihani dhidi ya Watu Madhalimu. Na utuokoe kwa Rehma zako kutokana na
watu waliokufuru’ kumaanisha kua Wanamuomba Allah Subhanah wa Ta’ala
asiwajaalie wakawa ni wenye kua juu zaidi kiuzuri wa maisha zaidi ya watu wa Fir’awn
kwani hali ikiwa hivyo kimaisha basi itakua ni mtihani mkubwa sana dhaidi yao.

Hiki kilikua ni kipindi kigumu sana kwa Nabii Musa, Nabii Harun na wafuasi wao
wakiwemo watu wa Bani Israil na baadhi ya watu wa Misri waliokua wakimkubali Nabii
Musa, kwani Fir’awn na watu wake walifanya kila jitihada kuhakikisha kua Wafuasi hao
wanapata adhabu kali kila pale wanapojidhirisha kua wanakubaliana na Imani ya Nabii
Musa na hivyo kua ni wenye kupingana na Imani ya Fir’awn na watu wake, hivyo Nabii
Musa akawausia na kuwatuliza watu wake kwa kusema:
659

‫ض ِﱠﻪﻠﻟِ ﻳُﻮِرﺛـُ َﻬﺎ َﻣﻦ ﻳَ َﺸﺂءُ ِﻣ ْﻦ‬ ‫َر‬‫ﻷ‬ ‫ٱ‬ ‫ﱠ‬


‫ن‬ ِ
‫إ‬ ‫ا‬‫و‬ۤ ‫ﭑﻪﻠﻟِ وٱﺻِﱪ‬ ِ ِ ْ ‫ﺎل ﻣﻮﺳ ٰﻰ ﻟَِﻘﻮِﻣ ِﻪ‬ ﴿
َ ْ ْ ُ ْ َ ‫ٱﺳﺘَﻌﻴﻨُﻮا ﺑ ﱠ‬ ْ َ ُ َ َ‫ﻗ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ِ ِِ ِ
َ ‫ﻋﺒَﺎدﻩ َوٱﻟْ َﻌﺎﻗﺒَﺔُ ﻟ ْﻠ ُﻤﺘﱠﻘ‬
Qala moosa liqawmihi istaAAeenoo biAllahi waisbiroo inna al-ardha lillahi
yoorithuha man yashao min AAibadihi waalAAaqibatu lilmuttaqeena (Surat Al Araf
7:128)

Tafsir: Akasema Musa kuwaambia watu wake ‘Ombeni Msaada kwa Allah na Kuweni
na Subra kwani kwa hakika Ardhi ni ya Allah hivyo humrithisha amtakae miongoni
mwa waja wake na mwisho mwema uko kwa wenye Taqwa’.

Allah Subhanah wa Ta’ala akamshushia Wahyi Nabii Musa kama anavyosema:

ً‫ٱﺟ َﻌﻠُﻮاْ ﺑـُﻴُﻮﺗَ ُﻜ ْﻢ ﻗِْﺒـﻠَﺔ‬


ْ ‫ﺼَﺮ ﺑـُﻴُﻮﺎﺗً َو‬
ِِ ِ ِ ِِ
ْ ‫ﻮﺳ ٰﻰ َوأَﺧﻴﻪ أَن ﺗَـﺒَـ ﱠﻮءَا ﻟ َﻘ ْﻮﻣ ُﻜ َﻤﺎ ﲟ‬ ِ
َ ‫﴿ َوأ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إ َ ٰﱃ ُﻣ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ ِ
َ ‫ﺼﻼَةَ َوﺑَ ّﺸ ِﺮ ٱﻟْ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬
‫ﻴﻤﻮاْ ٱﻟ ﱠ‬ ُ ‫َوأَﻗ‬
Waawhayna ila moosa waakheehi an tabawwaa liqawmikuma bimisra buyootan
waijAAaloo buyootakum qiblatan waaqeemoo alssalata wabashshiri almu/mineena
(Surat Yunus 10:87)

Tafsir: Na tukamshushia Wahy Musa na Kaka yake (Kuwaambia): ‘Chukueni Makazi


ya Watu wenu Nchini Misiri na mzifanye (baadhi ya) Nyumba kua ni sehemu za Ibada
zenu, na msimamishe Sala na Wabashirieni Walioamini ’

Aya inatubainishia kua Allah Subhanah wa Ta’ala kutokana na Rehma zake basi
akawaamrisha Nabii Musa na Nabii Harun kuwaambia wafuasi wao kua: Wafanye siri
Ibada zao ndani ya Majumba yao, kwa sababu haiwezekani kwao wao kufanya Ibada
wazi wazi katika majumba ya Ibada kutokana na hali ya mazingira ilivyo, kwani Fir’awn
akiwaona basi adhabu yake juu yao ni isiyokua na mfano wake.

Ambapo tunapoangalia historia ya Dunia hususan katika kipindi cha karne yetu mnamo
mwaka 1902 baada ya kuundwa kwa Shikiriko la Kikoministi la Kisovieti la Urusi na
hivyo kufutwa Imani za Dini za aina zote zinzofuatwa na wananchi wa Ardhi ya
Shirikisho hilo ambapo ndani yake mlikua mna nchi zenye wafuasi wa Dini ya Kiislam
kama Kazakhstan, Uzbekistan, Turkmenistan, Azerbaijan, Chechniya n.k basi amrisho la
660

ayah hii lilitumika tena kwa Waislam wa maeneo ya nchi hizo kwani walipigwa
marufuku kufanya Ibada zao hadharani na katika Majumba ya Ibada kiasi ya kua ilikua
hakuna sauti ya Adhana wala kisomo cha Qur’an kilichokua kikisikika katika maeneo ya
Ardhi hizo.

Lakini hata hivyo katazo hilo la kupiga marufuku Imani zote za Dini halikuwarudisha
nyuma Waislam wa Ardhi za nchi hizo wala hawakuvunjika moyo, kwani waliendela
kufanya Ibada zao kimya kimya na kuhifadhi, kufundishana na kuendelea kusimamia
maamrisho ya Imani yao kwa mda wa takriban miaka 90, kwani hali hii ilidumu hadi pale
liliposambaratika Shirikisho hilo la Kikoministi la Urusi mnamo mwaka 1990, na hivyo
nchi hizo kua huru, na kurudi katika hali ya kawaida ya watu kufanya Ibada zao kwa
uhuru na usalama bila ya vipingamizi vyovyote.

Tukirudi kwa upande wa watu waliokua katika Ardhi ya Fir’awn iliwabidi kujificha
jificha na kwa waliobainika basi yaliwakuta kama yale yaliyowakuta miongoni mwa
Wafuasi wa Siri wa Nabii Musa ambao ni pamoja na Msusi wa Mtoto wa Kike wa
Fir’awn na familia yake na Asiyah Bint Muzahim ambae ndie aliemuokota Nabii Musa
alipokua Mtoto na kumlea kama tulivyoona hapo kabla.

VIFO VYA MSUSI WA BINTI FIR’AWN NA ASIYAH BINT MUZAHIM.



Miongoni mwa waliokua wakimuamini Nabii Musa na Nabii Harun alikuwemo Hizqil
na familia yake, ambapo mke wake Hizqil aliekua akiitwa Mashita alikua ni Msusi wa
Mtoto wa kike wa Fir’awn, alikua ni mja wa Allah Subhanah wa Ta’ala mwenye Taqwa
lakini alikua akimsimamia Mtoto wa kike wa Fir’awn. Na anasema Said Ibn Jubayr kua
amesema AbdAllah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua amesema Rasul Allahu Alayhi wa
Salam kua: ‘Wakati nilipokua katika Safari ya Miraji, nilipita katika sehemu
amabyo ilikua ikinukia vizuri sana. Nami nikamuuliza Malaika Jibril: ‘Hivi Jee hii
harufu ni ya nini?’’

‘Malaika Jibril akasema: ‘Hio ni harufu ya Msusi wa Binti wa Fir’awn na Familia


yake. Siku moja alikua akimsuka Mtoto wa Kike wa Fir’awn na mara
kikamuanguka Kitana chake alichokua akimsukia Nywele Binti wa Fir’awn. Na
hivyo Msusi huyo akasema: ‘Biismi Allah!’ na Bint huyo aliposikia maneno hayo
basi akasema: ‘Mungu Baba yangu?’ Msusi huyo akasema: ‘La! Bali ni Mungu
wangu mie na Mungu wa Baba yako.’ Hivyo Binti huyo akasema: ‘Nitamwambia
Baba kuhusiana na hili’’
661

Hivyo Fir’awn alipopata habari hio, basi akamwita Msusi huyo, na akamuuliza:
‘Jee ni nani Mola wako?’ Msusi huyo akajibu: ‘Mola wangu mie na Mola wako
wewe ni Allah!’ Hivyo Fir’awn aliposikia Jibu hilo basi akaamrisha kua uwashwe
moto ndani ya Tanuri la Shaba na kisha Msusi huyo na watoto wake waingizwe
ndani ya Tanuri hilo la Shaba.’

Msusi aliposikia hivyo basi akasema: ‘Hamna tatizo isipokua nilikua nina ombi
moja’. Fir’awn akamuuliza Msusi huyo: ‘Jee ni ombi gani hilo?’ Msusi akajibu:
‘Kwa sharti la kua mara baada ya kuungua kwetu basi ikusanye mifupa yetu yote
yangu mie na ya watoto wangu kisha uizike ardhini.’ Fir’awn akasema: ‘Bila ya
shaka tutakufanyia hivyo kwani hilo ni Jukumu letu.’

Hivyo ukawashwa Moto na wakaanza kutiwa watoto wa Msusi huyo mmoja baada
ya mmoj ambele ya Msusi huyo hadi akabakia Mtoto mmoja mdogo wa mwisho
ambae alikua ni wa kunyonyesha ambae alisema kumwambia Mama yake: ‘Mama
usisite, kua na msimamo kwani uko katika njia ya haki.’ Na hivyo wakaingiza wote
kwa pamoja ndani ya Tanuri hilo la Moto.’

Na mwengine miongoni mwao basi alikuwemo pia Mama yake mlezi Nabii Musa yaani
mke wa Fir’awn ambae ametajwa katika ile aya isemayo:

‫ب ٱﺑْ ِﻦ ِﱃ ِﻋﻨ َﺪ َك ﺑَـْﻴﺘﺎً ِﰱ‬ ِ ِِ


ِّ ‫ﺖ َر‬ ْ َ‫ﻳﻦ َآﻣﻨُﻮاْ ْٱﻣَﺮأََة ﻓْﺮ َﻋ ْﻮ َن إِ ْذ ﻗَﺎﻟ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻣﺜَﻼً ﻟّﻠﱠﺬ‬
‫ب ﱠ‬ َ ‫ﺿَﺮ‬
َ ‫﴿ َو‬
ِِ ِ ِ ِ ِِ ِ ِ ِ ِْ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ٱﳉَﻨﱠﺔ َوَﳒِّﲎ ﻣﻦ ﻓْﺮ َﻋ ْﻮ َن َو َﻋ َﻤﻠﻪ َوَﳒِّﲎ ﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻘ ْﻮم ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
Wadharaba Allahu mathalan lilladheena amanoo imraata firAAawna idh qalat
rabbi ibni lee AAindaka baytan fee aljannati wanajjinee min firAAawna
waAAamalihi wanajjinee mina alqawmi aldhdhalimeena. (Surat At Tahrim 66:11)

Tafsir: Na Allah anatoa mfano kwa wale walioamini: Mke wa Fir’awn, pale
aliposema: ‘Ewe Mola wangu! Nijengee mimi nyumba kwako wewe Peponi, na
uniokoe kutokana na Fir’awn na amali zake, niokoe kutokana na watu madhalimu’

Ambapo ayah hii inamzungumzia Asiyah Bint Muzahim ambae ingawa alikua ni Mke
wa Fir’awn lakini alikua ni Mja wa Allah Subhanah wa Ta’ala mwenye Taqwa na
mwenye kumuabudu Allah Subhanah wa Ta’ala kwa siri kutokana na khofu yake dhidi
ya Fir’awn ambayo alidumu nayo mpaka katika siku hio alipokua amekaa dirishani huku
akiangalia mandhari nzuri inayovutia ya nje na mara akaona makabiliano baina ya Msusi
na Fir’awn a,bayo yalivutiwa zaidi na macho yake na kufuatilia kwa makini kutaka kujua
662

kitachofuatia baada yake, hadi alipoona tukio la Fir’awn alipokua akiiangamiza familia
ya Hizqil yaani ya Msusi wa Bint yake Fir’awn kupitia kwa Mke mwengine.

Ambapo baada ya tukio hili Asiyah Bint Muzahim aliona namna Roho za Waumini hao
zilipokua zikitolewa na kupandishwa juu na Malaika, hivyo nae akapata ari zaid, hivyo
Fir’awn aliporudi ndani basi akamuelezea yaliyowafika watu wa Familia ya Msusi huyo,
hivyo Asiyah akasema: ‘Ole wako Ewe Fir’awn, hivi ni kitu gani hasa kilichokufanya
wewe ujipandishe darja ya kutaka kumfikia Mola wako?’ Fir’awn akasema: ‘Hakika
ewe Kipenzi changu mimi naona kua Ufahamu wako umeingiwa na wazimu kama
waliokua nao watu wa familia ya Msusi huyo.’

Asiyah Bint Muzahim akajibu: ‘Bila ya shaka mimi sijaingiwa na Wazimu na wala
sijachanganyikiwa, isipokua mimi naamini juu ya kuwepo Mungu ambae ni
Muumba wa kila kitu, ambae ndie Mungu wa Musa, Mungu wangu mie na Mungu
wako wewe pia. ’

Fir’awn kusikia maneno hayo basi akatoka hadi kwa mama yake Asiyah Bint Muzahim
na kumwambia kua azungumze na Binti yake kwani anaonekana kama kachanganyikiwa
kutokana na kutokuukubali Uungu wa Fir’awn. Mama huyo akatika mpaka kwa Binti
yake na kumshawishi abadili mtizamo wa Imani yake.

Lakini hata hivyo Asiyah Bint Muzahim alikataa katu katu kubadilisha mtizamo huo, na
hivyo ikabidi Fir’awn apitishe hukumu yake dhidi ya wasaliti wanaousaliti Uungu wake,
na kwa upande wa Asiyah basi alifungwa mikono yake na miguu yake kwenye vipingili
vine na kisha akaanza kuvutwa viongo vyake hivyo kutoka katika pande nne tofauti.

Kama vile ambavyo alivyofungwa Sumaiyah Bint Khayyat Radhi Allahu Anha ambae ni
mke wa Yassir Ibn Amir Radhi Allahu Anhu ambao ndio wazee wa Amar Ibn Yasir Radhi
Allahu Anhu Sumayyah ndie Muislam wa mwanzo kua shahidi katika Mji wa Makkah,
kwa kufungwa kamba kila mkono na mguu wake na kisha kupigwa Mkuki wa Tumbo
mara kadhaa na Abu Jahal mpaka akafariki kutokana na majeraha ya Mkuki huo.

Ambapo anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kuhusiana na tukio hili kua:
‘Fir’awn alimchukua Asiyah Bint Muzahim Mke wake na kuanza kumuadhibu ili
aingie kwenye Imani yake, ambapo wakati alipokua akiadhibiwa basi Nabii Musa
alipita akaliona tukio hilo hivyo Asiyah akamlalamikia Nabii Musa maumivu yake
kwa kutumia ishara ya vidole vyake, hivyo Nabii Musa akamuombe kwa Allah
Subhanah wa Ta’ala ampunguzie maumivu yake hadi kufariki kwake, na hivyo
akawa hahisi tena mamumivu yake na ndio akasema:’
663

‫ٱﳉَﻨ ِﱠﺔ َوَِﳒِّﲎ ِﻣﻦ ﻓِْﺮ َﻋ ْﻮ َن َو َﻋ َﻤﻠِ ِﻪ َوَِﳒِّﲎ ِﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻘ ْﻮِم‬ َ ‫ب ٱﺑْ ِﻦ ِﱃ ِﻋ‬
ْ ‫ﻨﺪ َك ﺑَـْﻴﺘﺎً ِﰱ‬ ِّ ‫﴿ َر‬
ِِ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
Rabbi ibni lee AAindaka baytan fee aljannati wanajjinee min firAAawna
waAAamalihi wanajjinee mina alqawmi aldhdhalimeena. (Surat At Tahrim 66:11)

Tafsir: ‘Ewe Mola wangu! Nijengee mimi nyumba kwako wewe Peponi, na uniokoe
kutokana na Fir’awn na amali zake, niokoe kutokana na watu madhalimu’

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia: ‘Angalia juu’ na Asiyah Bint


Muzahim alipoangalia juu akatabasam kwa alikua amelioona Jumba lake la Lulu, Almasi
na Dhahabu likiwa Peponi. Fir’awn alipomuona anatabasam basi akasema: ‘Angalia
wendawazimu wake anafurahia namna anavyoadhibiwa’

Baada ya tukio hili basi Fir’awn akatafakari na kujiuliza kwanini Asiyah alikua ni
mwenye kuangalia juu huku akitabasam wakati anaadhibiwa, kwani haiwezekani
kutokana na adhabu anazowaadhibu wasaliti wake ziwe ni zenye kuwastarehesha badala
yake wasaliti hao, hivyo akatafuta kisingizio cha kua nae anataka kumjua Mungu wa
Nabii Musa kama kweli yuko huko juu wanakokuangalia wafuasi wa Nabii Musa.

KISINGIZIO CHA FIR’AWN CHA KUMTAFUTA MUUMBA.



Ni kawaida kwa Viumbe Ibn Adam kua ni wenye kutafuta visingizio pale wanapokua
hawakubaliana na mtizamo fulani ijapokua wanajua kua mtizamo huo ndio sahih, na ndio
maana akasema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qur’an kua:

﴾ُ‫ﺼﲑةٌ ۞ وﻟَﻮ أَﻟْ َﻘ ٰﻰ َﻣ َﻌ ِﺎذﻳﺮﻩ‬


ِ ِِ ِ ﴿
َ َ ‫ﺑَ ِﻞ ٱﻹ‬
ْ َ َ َ‫ﻧﺴﺎ ُن َﻋﻠَ ٰﻰ ﻧَـ ْﻔﺴﻪ ﺑ‬
Bali al-insanu AAala nafsihi baseeratun; Walaw alqa maAAadheerahu (Surat
75:14-15)

Tafsir: Lakini Mtu juu ya Nafsi yake ni Mwenye kujishuhudia, Ingawa hua ni mwenye
kutoa visingizio.
664

Na mbali ya kua ni wenye sifa ya kutokosa kua na visingizio lakini pia kimaumbile Ibn
Adam pia hua na sifa ya kupenda Kujadili jadili mambo, kama alivyosema Allah
Saubhanah wa Ta’ala katika Qur’an:

‫ﱠﺎس ِﻣﻦ ُﻛ ِّﻞ َﻣﺜَ ٍﻞ َوَﻛﺎ َن ٱ ِﻹﻧْ َﺴﺎ ُن أَ ْﻛﺜَـَﺮ َﺷ ْﻲ ٍء‬


ِ ‫آن ﻟِﻠﻨ‬
ِ ‫﴿ وﻟََﻘ ْﺪ ﺻﱠﺮﻓْـﻨَﺎ ِﰱ ﻫـٰ َﺬا ٱﻟْ ُﻘﺮ‬
ْ َ َ َ
﴾ً‫َﺟ َﺪﻻ‬
Walaqad sarrafna fee hadha alqur-ani lilnnasi min kulli mathalin wakana
al-insanu akthara shay-in jadalan (Surat Al Ahqaf 18:54)

Tafsir: Kwa hakika tumeweka wazi ndani ya hii Qur’an kwa ajili ya watu kila
aina ya Mifano, lakini hakua Mtu isipokua hua ni mwenye kupenda Kujadili
jadili sana.

Ambapo katika kipindi cha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam pale usiku wa siku
moja Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam alimtembelea mtoto wake Fatima Bint
Rasul Radhi Allahu Anha aliekua pamoja na Mumewe Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu
Anhu nyumbani kwao, na alikaribishwa ndani basi akawauliza watoto wake hao: ‘Hivi
Jee Mtasali Tahajjud leo Usiku?’ Aali Ibn Abi Talib akasema: ‘Ya Rasul Allah. Hakika
sisi ni Viumbe wa Allah Subhanah wa Ta’ala na Roho zetu zimo ndani ya Mikono
yake, Hivyo akitujaalia kusali basi atatuamsha tusali.’

Kiosha baada ya hapo basi Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu anasema kua: ‘Rasul
Allah Salallahu Aalyhi wa Salam alipigwa na butwaa na jibu langu hilo na hivyo
hakusema chochote, kisha akapiga kofi paja lake na kusema:’

﴾ً‫﴿ وَﻛﺎ َن ٱ ِﻹﻧْﺴﺎ ُن أَ ْﻛﺜَـﺮ َﺷﻲ ٍء َﺟ َﺪﻻ‬


ْ َ َ َ
Wakana al-insanu akthara shay-in jadalan (Surat Al Ahqaf 18:54)

Tafsir: Lakini hakua Mtu isipokua hua ni mwenye kupenda Kujadili jadili sana.

Hivyo bila ya shaka ya kutokana na kua Ibn Adam ni mwenye kupenda Kujadili basi
haishangazni ia kuona kua wale wasioamini kuwepo kwa Muumba basi hua ni wenye
kukimbilia kutafuta juu Mbinguni ili wapate hoja za Majadiliano kuhusiana na kama
yupo huko juu anaonekana ama la, wakati vithibitisho vya kuwepo kwake viko ndani ya
665

miili yao na vimewazunguka kila mahali. Hivyo Fir’awn akaamua kuonesha dhihaka
dhidi ya Nabii Musa na watu wake kwa kumwambia Mshauri wake:

‫ﺖ ﻟَ ُﻜ ْﻢ ِّﻣ ْﻦ إِﻟَـٍٰﻪ َﻏ ِْﲑى ﻓَﺄ َْوﻗِ ْﺪ ِﱃ ٰﻳـ َﻬ َﺎﻣﺎ ُن َﻋﻠَﻰ‬ ِ ِ َ َ‫﴿وﻗ‬


ُ ‫ﺎل ﻓْﺮ َﻋ ْﻮ ُن ٰ�َﻳـﱡ َﻬﺎ ٱﻟْ َﻤ َﻸُ َﻣﺎ َﻋﻠ ْﻤ‬ َ
ِ ِ ِٰ‫ﲔ ﻓَﭑﺟﻌﻞ ِّﱃ ﺻﺮﺣﺎً ﻟﱠﻌﻠِّ ۤﻲ أَﻃﱠﻠِﻊ إِ َ ٰﱃ إِﻟَـ‬ ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ِ‫ﻮﺳ ٰﻰ َوإِِّﱐَ ﻷَﻇُﻨﱡﻪُ ﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻜﺎذﺑ‬ َ ُ ‫ﻣ‬ ‫ﻪ‬ ُ َ َْ َ ْ ِ ّ‫ٱﻟﻄ‬
Waqala firAAawnu ya ayyuha almalao ma AAalimtu lakum min ilahin ghayree
faawqid lee ya hamanu AAala altteeni faijAAal lee sarhan laAAallee attaliAAu ila
ilahi moosa wa-innee laadhunnuhu mina alkadhibeena (Surat Al Qasas 28:38)

Tafsir: Na akasema Fir’awn: ‘Enyi Machifu wangu, sijui mimi kua nyinyi mnae
Mungu zaidi yangu. Niwashie Moto Ewe Haman! Oka Moto (Matofali ya) Udongo, na
unijengee mimi Mnara ili niweze kumuangalia Mungu wa Musa. Kwani kwa Hakika,
nadhani kua Musa ni miongoni mwa wenye kusema Uongo.’

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Hakuna njia ya
kuthibitisha kama mnara huo ulijengwa ama la, ambapo kiufaham basi tunaona
kua haukujengwa. Ama kuhusiana na hadith zinazozungumzia kujengwa kwake
basi hua si chochote isipokua ni zenye kufungua njia ya kupiga vita maneno ya
Qur’an’

Hivyo Fir’awn alikua akitafuta kisingizio kua kweli anataka kumjua Mungu wa Nabii
Musa na hivyo kama kweli Muumba yupo basi hakuna njia wala uwezekano mwengine
wa kumuona isipokua kwa kumtafuta juu Mbinguni, na kutokana na kua na mtizamo
wake huo basi Allah Subhanah wa Ta’ala akamzibia njia ya kuuona ukweli halisi kama
zinavyosema aya kwa mtizamo mwengine kuhusiana na tukio hilo:

ِ ‫ﺎل ﻓِﺮﻋﻮ ُن ٰﻳـﻬﺎﻣﺎ ُن ٱﺑ ِﻦ ِﱃ ﺻﺮﺣﺎً ﻟﱠﻌـﻠِّ ۤﻲ أَﺑـﻠُ ُﻎ ٱﻷَﺳﺒﺎب ۞أَﺳﺒﺎب ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬


‫ات‬ َ َ َ َْ َ َْ ْ َ َْ ْ َ َ ْ َ ْ َ َ‫﴿ َوﻗ‬
ِ ِ‫ﻚ زﻳِﻦ ﻟِِﻔﺮﻋﻮ َن ﺳ ۤﻮء ﻋﻤﻠ‬ ِ ِ ِِ ِ ِ
ُ َ َ َ ُ ُ ْ َ ْ َ ُّ َ ‫ﻮﺳ ٰﻰ َوإِِّﱏ ﻷَﻇُﻨﱡﻪُ َﻛﺎذﺎﺑً َوَﻛ ٰـﺬﻟ‬
‫ﺻ ﱠﺪ‬ ‫و‬ ‫ﻪ‬ َ ‫ﻓَﺄَﻃﱠﻠ َﻊ إ َ ٰﱃ إﻟَـٰﻪ ُﻣ‬
﴾‫ﺎب‬ ٍ ‫َﻋ ِﻦ ٱﻟ ﱠﺴﺒِ ِﻴﻞ وﻣﺎ َﻛ ْـﻴ ُﺪ ﻓِﺮ َﻋﻮ َن إِﻻﱠ ِﰱ ﺗَـﺒ‬
َ ْ ْ ََ
Waqala firAAawnu ya hamanu ibni lee sarhan laAAallee ablughu al-asbaba;
Asbaba alssamawati faattaliAAa ila ilahi moosa wa-innee laadhunnuhu kadhiban
666

wakadhalika zuyyina lifirAAawna soo-o AAamalihi wasudda AAani alssabeeli


wama kaydu firAAawna illa fee tababin (Surat Ghafir 40:35-36)

Tafsir: Na akasema Fir’awn: ‘Ewe Haman nijengee Mnara ili nizifikie sababu
(Njia), Sababu za Mbingu ili nipate kumuangalia Mungu wa Musa kwani kwa
hakika mimi nadhani kua anasema Uongo. Hivyo limepambwa kwa (mtizamo wa
macho ya) Fir’awn jambo lake ovu na hivyo akawa ni mwenye kufunikiwa njia (ya
haki) na mbinu za Fir’awn hazikumuelekeza kokote isipokua katika maangamizo.

Hivyo mbinu zake Fir’awn hazikumsaidia kitu, kwani vithibitisho viko vingi sana, lakini
kutokana na Kibri chake basi vithibitisho hivyo vikawa havionekani na macho yake hata
kama angeoneshwa vipi, tofauti na vile ilivyowezekana kuonekana kwa miongoni mwa
vithibitisho kwa waliooneshwa kwa kutumia mifano ya kawaida tu kama vile kwakupitia
mfano aliotoa Imam Jafar As Sadiq katika kuthibitisha kuwepo kwa Muumba wa
Ulimwengu yaani Allah Subhanah wa Ta’ala baada ya mmoja kati ya watu wanaopinga
kuwepo kwa Muumba kuanzisha Mjadala mbele yake basi Imam Jafar As Sadiq
alimuuliza Mtu huyo kwa kusema: ‘Hivi wewe umeshawahi kuona Bahari na namna
ilivyo kwa ukubwa wake na maajabu yake?’

Na mtu huyo akajibu: ‘Naam, kwa hakika mimi nimesafiri Baharini, na ikawahi
kutokea gharika na Jahazi likazama na Mabaharia pia wakazama. Mimi
nikakamata pande moja la mbao ambalo nalo likatawanyika na kuelea mbali nami.
Lakini nikasukumwa na mawimbi mpaka nikafika ufukweni.’

Imam Jafar As Sadiq akasema: ‘Hivyo wewe ulikua unategemea Jahazi, Mbao na
Mabaharia wa Jahazi hilo, lakini hata hivyo vyote hivyo vilipoachana nawe basi
bado uliendelea kua na matumaini kua utakua salama’
Yule mtu akajibu kwa kusema: ‘Naam.’

Imam Jafar As Sadiq akasema: ‘Hivyo katika kua na matumaini kwako huko ulikua
ukimtegemea nani?’

Yule mtu akapigwa na bumbuwazi, kwani alikua hana la kusema na akabakia ameinama
chini.

Imam Jafar akasema: ‘Bila ya shaka, ulikua ukimtegemea Muumba, kwani ndie
pekee ambae wewe ulikua na matumaini nae na yeye ndie aliekuokoa wewe usizame
kama walivyozama wengine’. Hivyo hapo hapo mjadala ukamalizika kwani yule mtu
alikua hana kisingizio na akaingia katika dini ya Kiislam.
667

Na mfano wa pili kama huo ni mfano wa Imam Nu’man Ibn Thabit ambae ni maarufu
kama Imam Abu Hanifa ambae alifariki katika mwaka aliozaliwa Imam Muhammad Idris
Al Shafii.

Ambapo safari moja Imam Abu Hanifa alivamiwa na watu ambao walikua wanataka
kumuua kutokana na kutofautiana kwao kimtizamo wa kua wao wanaamini kua hakuna
Muumba, hivyo bila ya kua na khofu basi Imam Abu Hanifa akawaambia watu hao kua:
‘Nijibuni suali moja kisha mtanifanya mnavyotaka’

Watu hao wakasema: ‘Haya tunakupa suali moja tu, uliza.’

Imam Abu Hanifa akasema: ‘Jee mtasemaje kama nikikuambieni kua, hakika mimi
nimeona Jahazi ambalo halina Nahodha huku likiwa limejaa shehena ya mizigo
katikati ya Bahari iliyochafuka kutokana na gharika, lakini Jahazi hilo likiwa
linaendelea na safari bila ya kuzama. Jee mtasema kua jambo hilo linawezekana
ama ala?’

Watu hao wakasema: ‘Kwa hakika hayo unayoyasema ni maneno ambayo hayaingii
akilini.’

Imam Abu Hanifa akasema: ‘Subhanah Allah wa Allahu Akbar! Hivi kama ikiwa akili
haiwezi kukubali kua Jahazi haliwezi kuelea na kuendelea na safari bila ya
Nahodha basi jee itakuaje akili iweze kukubali kuhusiana na Ulimwengu na kila
kitu chake na mabadiliko yake yote yanayotokea ndani na nje yake kisha utulie
kama ulivyotulia kimpangilio bila ya kuwepo Muumba wake?’

Baada ya hoja hio, basi watu hao wakatafakkari na wakakosa jibu la suali hilo, hivyo
wakajisalimisha kwa Allah Subhanah wa Ta’ala na kuingia katika Dini ya Uislam kutika
mikono ya Imam Abu Hanifa kutokana na hoja na vithibitisho vyake Imam Abu Hanifa
juu ya kuwepo kwa Mola wake.
Tukiachana na mtizamo wa kiufaham wa kawaida basi na tuangalie kwa upande wa
mtizamo wa Kii’lm kwa kumuangalia Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu
Hamid Muhamamd Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali katika Al Risalah al
Qudsiyyah ambae yeye anatuthibtishia kuwepo kwa Muumba kwa kutumia Ayat Al
Kawniyah.

668

AYAT KAWNIYAH NA UTHIBITISHO WA KUWEPO KWA MUUMBA.



Tunapoiangalia Qur-an basi tunaona kua ndani yake mna aya ambazo hua zinajulikana
kama Ayat Kawniyah yaani aya zinazozungumzia Maumbile ya Kiulimwengu. Neno
Kawniyah linatokana na neno Kawan lenye kumaanisha Maumbile, hivyo aya hizi
zimeitwa Ayat Kawniyah kwa sababu ni aya ambazo zinazungumzia Maumbile ya vitu
vilivyoumbwa na Muumba yaani Allah Subhanah wa Ta’ala kwa ajili ya Ulimwengu
wake.

Ayat Kawniyah ni aya ambazo zinamhimiza Muumini kua ni mwenye kumkumbuka


Mola wake, kuona Hikma zake na Uwezo wake katika kila kitu, kutafakkari na
kuchunguza na kujifunza kuhusiana na maumbile yake anayoishi, namna yalivyoumbwa,
namna yanavyomsaidia kwa manufaa yake, namna ya kuyahifadhi na kutoyafanyia
ufisadi.n.k

Hivyo Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Muhamamd Ibn Muhammad
Ibn Muhammad Al Ghazali katika Al Risalah al Qudsiyyah basi ametumia aya kadhaa
kuthibitisha kuwepo kwa Muumba Ayat Kawniyah hizi ni aya ambazo kwa kila mtu
mwenye kuzisoma na akazifaham hata yule mwenye ufaham mdogo basi hua ni zenye
kumtosheleza kumthibitishia kua kuna Muumba, na bila ya shaka sitoweza kuziangalia
aya zote za Ayat Kawniyah alizozitumia kama vithibitisho bali tutaangalia baadhi tu ya
aya hizo, ili angalau tupate kufaham, na miongoni mwa aya hizo ni pamoja na ile aya
iliyoshushwa baada ya aya ifuatayo:

ِ ‫﴿وإِﻟَـٰﻬ ُﻜﻢ إِﻟَـٰﻪ و‬


﴾‫اﺣ ٌﺪ ﻻﱠ إِﻟَـٰﻪَ إِﻻﱠ ُﻫﻮ ٱﻟﱠﺮ ْﲪَـٰﻦ ٱﻟﱠﺮِﺣﻴﻢ‬
ُ ُ َ ٌَ ْ ُ َ
Wa-ilahukum ilahun wahidun la ilaha illa huwa alrrahmanu alrraheemu (Surat Al
Baqara 2:163)

Tafsir: Na Mungu wenu ni Mungu Mmoja, Hakuna Mungu anaestahiki kuabudiwa


isipokua yeye Mwingi wa Rehma Mwingi wa Huruma.

Ambapo mara tu baada ya kushushwa aya hii basi Makafiri wa Makkah waliokua na
Miungu 360 ndani ya Al Kaabah wakamwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
kua: ‘Itakuaje Mungu mmoja atosheleze juu ya kila kitu katika Ulimwengu huu?’

Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi anasema


kuhusiana na aya hii kua: ‘Aya hii maana yake ni kua Allah Subhanah wa Ta’ala ni
Mmoja katika Mitizamo mitatu tofauti.
669

1-Mtizamo wa Mwanzo ni kutokana na namna alivyo katika hali yake ambayo ni


ya Umoja na hana hali nyengine na wala hashirikiki na hali nyengine hivyo hawezi
kugawika.

2-Mtizamo wa Pili ni kuhusiana na Sifa Zake kua hakuna hata mmoja mwenye
kujumuishwa nae katika Sifa zake kutokana na Upekee wake hivyo hakuna
mwengine zaidi mwenye sifa kama zake.

3-Mtizamo wa Tatu ni katika Mambo yake yaani hakuna hata mmoja anaeweza
kuiga Mambo yake ayafanyayo.’

Hivyo baada ya aya hio na Makafiri kutoa hoja zao kuhusiana na Mungu mmoja
anawezaje kutosheleza kila kitu basi Allah Subhanah wa Ta’ala akashusha aya ambayo
ni miongoni mwa aya zinazothibitisha kuwepo kwa Allah Subhanah wa Ta’ala kwa
kubainisha kua:

ِ ‫ف ٱﻟﻠﱠﻴ ِﻞ وٱﻟﻨـﱠﻬﺎ ِر وٱﻟْ ُﻔ ْﻠ‬ ِ َ‫ض وٱﺧﺘِﻼ‬ ِ


‫ﻚ ٱﻟﱠِﱴ َْﲡ ِﺮى‬ َ َ َ ْ ْ َ ِ ‫﴿إِ ﱠن ِﰱ َﺧ ْﻠ ِﻖ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤ َﺎوات َوٱﻷ َْر‬
ِ ‫ﺂء ﻓَﺄ‬ ٍ ِِ ِ ‫ِﰱ ٱﻟْﺒﺤ ِﺮ ِﲟَﺎ ﻳﻨ َﻔﻊ ٱﻟﻨﱠﺎس وﻣﺂ أَﻧﺰَل ﱠ‬
َ ‫َﺣﻴَﺎ ﺑِﻪ ٱﻷ َْر‬
‫ض‬ ْ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻣ َﻦ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤﺂء ﻣﻦ ﱠﻣ‬ َ ََ َ ُ َ ْ َ
ِ ‫ٱﻟﺮ� ِح وٱﻟ ﱠﺴﺤ‬ ِ ‫ﺼ ِﺮ‬ ٍ‫ﺚ ﻓِﻴﻬﺎ ِﻣﻦ ُﻛ ِﻞ دآﺑﱠ‬ ِ‫ﺑـﻌ َﺪ ﻣﻮ‬
َْ ‫ﺎب ٱﻟْ ُﻤ َﺴ ﱠﺨ ِﺮ ﺑَـ‬
‫ﲔ‬ َ َ َّ ِ ‫ﻳﻒ‬ ْ ‫ﺗ‬
َ‫و‬َ ‫ﺔ‬ َ ّ َ ‫ﱠ‬ ‫ﺑ‬‫و‬ ‫ﺎ‬‫ﻬﺗ‬
َ
ََ ْ َ ْ َ
﴾‫ت ﻟَِّﻘﻮٍم ﻳَـ ْﻌ ِﻘﻠُﻮ َن‬ٍ ‫ض‬ ِ
َ ِ ‫ٱﻟ ﱠﺴ َﻤﺂء َوٱﻷ َْر‬
ْ �‫ﻵ‬
Inna fee khalqi alssamawati waal-Ardhi waikhtilafi allayli waalnnahari waalfulki
allatee tajree fee albahri bima yanfaAAu alnnasa wama anzala Allahu mina
alssama-i min ma-in faahya bihi al-ardha baAAda mawtiha wabaththa feeha min
kulli dabbatin watasreefi alrriyahi waalssahabi almusakhkhari bayna alssama-i
waal-Ardhi laayatin liqawmin yaAAqiloona (Surat Al Baqara 2:164)

Tafsir: Hakika Mumbile ya Mbingu na Ardhi, na kutofautiana baina ya Mchana na


Usiku, katika kusafiri kwa Vyombo Baharini kwa ajili ya manufaa ya watu, katika
Mvua ambayo Allah anaishusha kutoka Mbinguni na uhai anaoihuishia Ardhi baada
ya kufa kwake; Na Wanyama wa aina tofauti waliotawanyika ardhini, katika
mabadiliko ya Upepo na Mawingu yanayofuatana nayo baina ya Ardhi na Mbingu.
Mna uthibitisho ndani yake kwa watu wenye kutumia akili.
670

Naam hii ni miongoni mwa aya za Qur’an ambazo zinajulikana kama Ayat Kawniyah.
Ambapo tunapoiangalia aya hii basi tunaona kua imeainisha ndani yake vithibitisho sita
vya kimaumbie vinavyothibitisha kuwepo kwa Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ndie
Muumba wa kila kitu na vitu 6 hivyo ni: Uumbwaji wa Mbingu na Ardhi, Kutofautiana
baina ya Usiku na Mchana, Kuelea kwa Vyombo vya Usafiri Baharini, Kunyesha Mvua,
Kuenea kwa Wanyama wa Ardhini na kuwepo kwa Hewa na kuvuma kwa Upepo.

1-DALILI KATIKA KUUMBWA MBINGU NA ARDHI


Katika kuumbwa kwa Mbingu na Ardhi basi ni kama alivyosema Allah Subhanah wa
Ta’ala kua watu wanajua kua kuna Muumba ambae ndie alieumba kia kitu ambae ni
Allah Subhanah w Ta’ala lakini wanamshirikisha kutokana na upotovu wao wa kutotaka
kumfuata na kumuabudu na hivyo hua ni wenye kumshirikisha badaa yake kwa makusudi
kama inavyosema aya ifuatayo:

ِ ِ
‫ٱﻪﻠﻟُ ﻗُ ْﻞ أَﻓَـَﺮأَﻳْـﺘُﻢ ﱠﻣﺎ ﺗَ ْﺪﻋُﻮ َن‬
‫ض ﻟَﻴَـ ُﻘﻮﻟُ ﱠﻦ ﱠ‬َ ‫﴿ َوﻟَﺌﻦ َﺳﺄَﻟْﺘَـ ُﻬ ْﻢ ﱠﻣ ْﻦ َﺧﻠَ َﻖ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤ َﺎوات َوٱﻷ َْر‬
‫ﺿِّﺮﻩِ أ َْو أ ََر َادِﱏ ﺑَِﺮ ْﲪٍَﺔ َﻫ ْﻞ‬ ِ
ُ ‫ﻀٍّﺮ َﻫ ْﻞ ُﻫ ﱠﻦ َﻛﺎﺷ َﻔ‬
ُ ‫ﺎت‬ ُ ِ‫ٱﻪﻠﻟُ ﺑ‬‫ٱﻪﻠﻟِ إِ ْن أ ََر َادِﱏَ ﱠ‬
‫ون ﱠ‬ ِ ‫ِﻣﻦ د‬
ُ
﴾‫ٱﻪﻠﻟ َﻋﻠَْﻴ ِﻪ ﻳَـﺘَـﻮﱠﻛـﻞ ٱﻟْﻤﺘَـﻮّﻛِﻠُﻮ َن‬ ‫ﱠ‬ ‫ﱮ‬ِ ‫ﺴ‬‫ﺣ‬ ‫ﻞ‬ ُ‫ﻗ‬ ‫ﻪ‬ِ ِ‫ﻫ ﱠﻦ ﳑُْ ِﺴ َﻜﺎت ر ْﲪﺘ‬
َُ ُ َ ُ َْ ْ ََُ َ ُ
Wala-in saaltahum man khalaqa alssamawati waal-ardha layaqoolunna Allahu qul
afaraaytum ma tadAAoona min dooni Allahi in aradaniya Allahu bidhurrin hal
hunna kashifatu dhurrihi aw aradanee birahmatin hal hunna mumsikatu rahmatihi
qul hasbiya Allahu AAalayhi yatawakkalu almutawakkiloona (Surat Az Zumar
39:38)

Tafsir: Na kama ukiwauliza: ‘Ni Nani alieumba Mbingu na Ardhi’ basi hua ni
watasema ‘Ni Allah’. Hivyo waambie: ‘Jee mnaona hivyo vitu mnavyoviabudu zaidi
ya Allah, kua kama Allah akitaka kunidhuru, vitaniepusha na madhara yake? Au
kama Allah akitaka kuniingiza kwenye Rehma zake, jee vitanizuia na Rehma zake?’
Sema: ‘Ananitosheleza mimi Allah, kwani juu yake yeye wenye kumuamini hua ni
wenye kuamini’
671

Kwani Allah Subhanahu wa Ta’ala ndie alieanzisha Ulimwengu unaojumuisha Mbingu


na Ardhi, kama Surat Fatir inavyosema:

ِ ‫ات َوٱﻷ َْر‬


﴾‫ض‬ ِ َ‫ٱﳊﻤ ُﺪ ِﱠﻪﻠﻟِ ﻓ‬
ِ ‫ﺎﻃ ِﺮ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬
ََ ْ َْ ﴿
Alhamdu lillahi fatiri alssamawati waal-Ardhi (Surat Fatir 35:1)

Tafsir: Sifa zote na Shukrani anastahiki Allah, alieanzisha kwa kuumba (bila ya
kutokana na kitu chochote) Mbingu na ardhi.

Ambapo katika kuanzishwa kwake huko basi vyote viwili hivi vilikua ni kitu kimoja
kama anavyoelezea mwenyewe Muumba kwa kusema:

‫ﺎﳘَﺎ َو َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ِﻣ َﻦ‬


ُ َ‫ض َﻛﺎﻧـَﺘَﺎ َرﺗْﻘﺎً ﻓَـ َﻔﺘَـ ْﻘﻨ‬ ‫َر‬‫ﻷ‬ ‫ٱ‬‫و‬ ِ ‫﴿أَوَﱂ ﻳـﺮ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ َﻛ َﻔﺮ ۤواْ أَ ﱠن ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬
‫ات‬
َ ْ َ ََ ُ َ ََ ْ َ
‫ض َرَو ِاﺳ َﻰ أَن َﲤِﻴ َﺪ ﻬﺑِِ ْﻢ‬ ِ ‫ َو َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ِﰱ ْاﻷ َْر‬- ‫ﺂء ُﻛ ﱠﻞ َﺷﻲ ٍء َﺣ ٍﻲ أَﻓَﻼَ ﻳـُ ْﺆِﻣﻨُﻮ َن‬ ِ ‫ٱﻟْﻤ‬
َ
ّ ْ
‫ َو َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ اﻟ ﱠﺴ َﻤﺂءَ َﺳ ْﻘﻔﺎً ﱠْﳏ ُﻔﻮﻇﺎً َوُﻫ ْﻢ‬- ‫َو َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ﻓِ َﻴﻬﺎ ﻓِ َﺠﺎﺟﺎً ُﺳﺒُﻼً ﻟﱠ َﻌﻠﱠ ُﻬ ْﻢ ﻳـَ ْﻬﺘَ ُﺪو َن‬
‫ﺲ َواﻟْ َﻘ َﻤَﺮ ُﻛﻞﱞ ِﰱ‬ ‫ﱠﻤ‬
ْ ‫ﺸ‬ ‫اﻟ‬
‫و‬ ‫ـﺮ‬‫ﱠﻬ‬
َ ‫ـ‬‫ﻨ‬ ‫اﻟ‬
‫و‬ ‫ﻞ‬ ‫ﻴ‬
ْ‫ وُﻫﻮ ٱﻟﱠ ِﺬى َﺧﻠَ َﻖ اﻟﱠ‬- ‫ﺿﻮ َن‬ ُ ِ ‫َﻋ ْﻦ ءَاﻳَـﺘِ َﻬﺎ ُﻣ ْﻌ‬
‫ﺮ‬
َ َ َ َ َ َ َ
﴾‫ﻚ ﻳَ ْﺴﺒَ ُﺤﻮ َن‬ٍ َ‫ﻓَـﻠ‬
Awa lam yara alladhina kafaroo anna alssamawati waal-ardha kanata ratqan
fafataqnahuma wajaAAalna mina alma-i kulla shay-in hayyin afala yu/minoona;
WajaAAalna fee al-Ardhi rawasiya an tameeda bihim wajaAAalna feeha fijajan
subulan laAAallahum yahtadoona; WajaAAalna alssamaa saqfan mahfoodhan
wahum AAan ayatiha muAAridhoona; Wahuwa alladhi khalaqa allayla
waalnnahara waalshshamsa waalqamara kullun fee falakin yasbahoona (Surat Al
Anbiya 21:30-33)

Tafsir: Jee wale wasioamini hawajui kua Mbingu na Ardhi vilikua ni kitu kimoja, na
baadae tukavibagua, na tukaumba kila kitu kutokana na Maji? Jee hawaamini?; Na
tukaweka katika Dunia, Milima iliyoimarika ili isitikisike pamoja nayo, na tukaweka
ndani yake njia kwa ajili yao ili wapite bila kupotea. Na tukaifanya Mbingu kua paa
lililo salama na lenye kudhibitiwa vizuri sana. Lakini hata hivyo wanageukia upande
672

wa pili wa dalili zetu; Na ni yeye alieumba usiku na mchana, jua na mwezi, na kila
kimoja kinaelea katika njia yake.

Aya hiyo inaweka wazi kua katika kuumbwa kwa ulimwengu unaonekana, basi kwanza
Mbingu na Ardhi vilikua ni kitu kimoja kilichoungana lakini baadae vikatenganishwa na
kila moja kikawa mbali na mwenzake, zikawekwa Ardhi saba na Mbingu saba, kisha
ikawekwa hewa baina ya Ardhi ya mwisho ya juu na Mbingu ya mwisho ya chini na
ikasababiswha mvua kunyesha kutoka mbinguni na baada ya hapo miti ikaota ardhini.

Qur’an imethibitisha mara mbili kua baina ya vitu viwili hivi, yaani Mbingu na ardhi,
kua Ardhi iliumbwa mwanzo kuliko Mbingu, katika aya zifuatazo:

ِ ‫ﲨﻴﻌﺎً ﰒُﱠ اﺳﺘـﻮى إِ َﱃ اﻟ ﱠﺴﻤ‬


‫ﺂء ﻓَ َﺴ ﱠﻮ ُاﻫ ﱠﻦ َﺳْﺒ َﻊ‬ َِ ‫ض‬ ِ ‫﴿ﻫ َﻮ اﻟﱠ ِﺬى َﺧﻠَ َﻖ ﻟَ ُﻜﻢ ﱠﻣﺎ ِﰱ ْاﻷ َْر‬
َ َ َْ ُ
﴾‫ات َوُﻫ َﻮ ﺑِ ُﻜ ِّﻞ َﺷ ْﻰ ٍء َﻋﻠِ ٌﻴﻢ‬ٍ ‫َﲰـﻮ‬
ََ
Huwa alladhii khalaqa lakum ma fee al-Ardhi jamiAAan thumma istawa ila
alssama-i fasawwahunna sabAAa samawatin wahuwa bikulli shay-in Aaaleemun
(Surat Al Baqarah 2:29)

Tafsir: Ni yeye alieumba kila kitu kwa ajili yenu ardhini, na kisha akasimama na
kuzielekea mbigu na akaziweka sawa Mbingu saba, yeye ni mjuzi wa kila kitu.

Na vile vile katika aya ya pili inayosema:

ِ َ ‫ﲔ وَﲡﻌﻠُﻮ َن ﻟَﻪ أ‬ ِ ِ
َ ‫َﻧﺪاداً ٰذﻟ‬
‫ﻚ‬ ُ َ ْ َ ِ ْ ‫ض ِﰱ ﻳَـ ْﻮَﻣ‬ َ ‫﴿ﻗُ ْﻞ أَءﻧﱠ ُﻜ ْﻢ ﻟَﺘَ ْﻜ ُﻔُﺮو َن ﺑِﭑﻟﱠﺬى َﺧﻠَ َﻖ ْاﻷ َْر‬
‫ﱠر ﻓِ َﻴﻬﺂ أَﻗْـ َﻮﺗَـ َﻬﺎ ِ ۤﰲ‬ ‫ﺪ‬َ
َ َ‫ﻗ‬‫و‬ ‫ﺎ‬ ‫ﻴﻬ‬
َ
ِ‫ وﺟﻌﻞ ﻓِﻴﻬﺎ رو ِاﺳﻰ ِﻣﻦ ﻓَـﻮﻗِﻬﺎ وﺑـﺮَك ﻓ‬- ‫ب ٱﻟْﻌﺎﻟَ ِﻤﲔ‬
ََ َ َ ْ َ َ َ َ َ َ َ َ َ َ ‫َر ﱡ‬
‫ﺎل َﳍَﺎ‬ َ ‫ﺂء َوِﻫ َﻰ ُد َﺧﺎ ٌن ﻓَـ َﻘ‬ِ ‫ ﰒُﱠ ٱﺳﺘـﻮ ٰى إِ َﱃ ٱﻟ ﱠﺴﻤ‬- ‫أَرﺑـﻌ ِﺔ أ ﱠَ�ٍم ﺳﻮآء ﻟِّﻠ ﱠﺴﺂﺋِﻠِﲔ‬
َ ََْ َ ً ََ َ َْ
‫ات ِﰱ‬ ٍ ‫ ﻓَـ َﻘﻀﺎﻫ ﱠﻦ ﺳﺒﻊ َﲰﺎو‬- ‫ض ٱﺋْﺘِﻴﺎ ﻃَﻮﻋﺎً أَو َﻛﺮﻫﺎً ﻗَﺎﻟَﺘَﺂ أَﺗَـﻴـﻨَﺎ ﻃَﺂﺋِﻌِﲔ‬ ِ ‫َر‬ ‫ﻸ‬ ِ‫وﻟ‬
َ َ َ ْ َ ُ َ َ ْ ْ ْ ْ َ ْ َ
ِ ٍ
‫ﻚ‬َ ‫ﻴﺢ َو ِﺣ ْﻔﻈﺎً ٰذﻟ‬ ِ َ َ‫ﺂء أ َْﻣﺮَﻫﺎ وَزﻳـﱠﻨﱠﺎ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺂء اﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ ِﲟ‬
َ ‫ﺼـﺒ‬ َ َ
ِ
َ َ َ‫ﻳَـ ْﻮَﻣ ْﲔ َوأ َْو َﺣﻰ ﰱ ُﻛ ِّﻞ َﲰ‬
ِ
﴾‫ﺗَـ ْﻘ ِﺪ ُﻳﺮ ٱﻟْ َﻌ ِﺰﻳ ِﺰ ٱﻟْ َﻌﻠِﻴ ِﻢ‬
673

Qul a-innakum latakfuroona bialladhii khalaqa al-ardha fee yawmayni


watajAAaloona lahu andadan dhalika rabbu alAAalameena; WajaAAala feeha
rawasiya min fawqiha wabaraka feeha waqaddara feeha aqwataha fee arbaAAati
ayyamin sawaan lilssa-ileena; Thumma istawa ila alssama-i wahiya dukhanun
faqala laha walil-Ardhi i/tiya tawAAan aw karhan qalata atayna ta-iAAeena
Faqadahunna sabAAa samawatin fee yawmayni waawha fee kulli sama-in amraha
wazayyanna alssamaa alddunya bimasabeeha wahifdhan dhalika taqdeeru
alAAazeezi alAAaleemi (Surat Fusilat 41:9-12)

Tafsir: Sema (Ewe Muhammad) Hakika nyinyi mnamkufuru yule ambae ameiumba
Ardhi kwa siku mbili na mmetengeneza washirika wengine (kumshirikisha) pamoja
nae? Yeye ndie ambae, ni Mola wa kila kitu kilichopo. Ameweka (ardhini) milima
imara juu yake na akaibariki, na akakadiria ndani yake rizki (kwa watakaoishi ndani
yake) kwa siku nne sawia, kwa wote wale wanaouliza (kuhusiana na uumbwaji wake).
Kisha akasimama kuielekea Mbingu wakati ikiwa katika hali ya moshi, na akaiambia
(hiyo mbingu) na ardhi: ‘Njooni nyote wawili iwe kwa hiari au bila hiari.’ Vyote
vikasema: ‘Tunakuja kwa hiari’. Kisha akazimalizia kua Mbingu saba katika siku
mbili, na akaipangia kila Mbingu yake jambo lake. Na tukaipamba Mbingu ya karibu
(ya chini) kwa taa ili ziwe pambo na pia kama ulinzi (kutokana na Shaytan). Hayo
ndio makadirio ya mwenye uwezo na mwenye kujua.

Tafakkar kwani aya hii kamwe haipingani na zile aya za Surah Al-Nazi’at zisemazo:

ِ
َ َ‫ َوأَ ْﻏﻄ‬- ‫ َرﻓَ َﻊ َﲰْ َﻜ َﻬﺎ ﻓَ َﺴ ﱠﻮ َاﻫﺎ‬- ‫َﺷ ﱡﺪ َﺧ ْﻠﻘﺎً أَم ٱﻟ ﱠﺴ َﻤﺂءُ ﺑَـﻨَ َـﻬﺎ‬
‫ﺶ ﻟَْﻴـﻠَ َﻬﺎ‬ َ ‫﴿أَءَﻧﺘُ ْﻢ أ‬
- ‫َﺧَﺮ َج ِﻣْﻨـ َﻬﺎ َﻣﺂءَ َﻫﺎ َوَﻣْﺮ َﻋ َـﻬﺎ‬ ِ
ْ ‫ أ‬- ‫ﻚ َد َﺣ َـﻬﺎ‬ َ ‫ض ﺑَـ ْﻌ َﺪ ٰذﻟ‬
َ ‫ َو ْاﻷ َْر‬- ‫ﺿ َﺤ َـﻬﺎ‬ُ ‫َﺧَﺮ َج‬ ْ ‫َوأ‬
﴾‫ َﻣﺘَـﻌﺎً ﻟﱠ ُﻜ ْﻢ َوِﻷَﻧْـ َﻌ ِﺎﻣ ُﻜ ْﻢ‬- ‫ﺎل أ َْر َﺳ َـﻬﺎ‬
َ َ‫ٱﳉِﺒ‬
ْ ‫َو‬
Aantum ashaddu khalqan ami alssamao banaha; RafaAAa samkaha fasawwaha;
Waaghtasha laylaha waakhraja dhuhaha; Waal-ardha baAAda dhalika dahaha;
Akhraja minha maaha wamarAAaha; Waaljibala arsaha; MataAAan lakum wali-
anAAamikum (Surah Al Nazi’at 79:27-33)

Tafsir: Jee nyinyi ni wagumu zaidi kuwaumba, au ni Mbingu alizoziumba?


Aliinyanyulia urefu wake, akaiamrisha ikakaa sawa sawa, akaufunika kwa kiza usiku
wake, na huuleta kwa muangaza mchana wake. Na baada ya hapo akaitandaza ardhi,
na akatoa ndani yake maji yake na malisho yake. Na majabali akaimarishia, (ili kua)
malisho na manufaa kwenu na wanyama wenu.
674

Kwani kutokana na aya hizo tatu tulizoziangalia tunaona kua Mbingu na Ardhi vilikua ni
kitu kimoja, halafu vikatenganishwa kila kimoja peke yake, kwa kwanza kuumbwa kwa
Ardhi lakini bila ya kutandazwa kisha ndio ikaumbwa Mbingu na kupambwa na
kujaaliwa usiku na mchana na kila kitu chake.

Na baada ya hapo ndio Ardhi ikatandazwa na kuwekewa Majabali (Milima) ambayo


uimara na urefu wake kwenda chini ya Ardhi ni mara mbili zaid ya vile inavyoonekana
milima kutokana na muonekano wake wa juu ya Ardhi namna ulivyoelekea juu hewani,
na hii ni kwa sababu ya kuiimarisha Ardhi itulie bila ya kuyumba. Baada ya kuimarishwa
huko, Ardhi ikakadiriwa matumizi ya viumbe vyote vitakavyokuja kuishi juu yake na
kisha ikatoa maji yake ambayo ni pamoja na mito na maziwa na pia ikatoa malisho yake
ambayo ni pamoja na majani na miti yenye kutoa vivuli, vyakula, matunda n.k.

Kisha baada ya hapo Allah Subhanah wa Ta’ala anawafafanulia wale ambao


hawatafakkar na hawaoni na hivyo watajiuliza kwa kusema kwani kuna nini katika
kuumbwa kwa Mbingu na Ardhi kwa kusema katika aya ifuatayo:

﴾‫ﺿﻮ َن‬ ِ ‫﴿وﺟﻌ ْﻠﻨﺎ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺂء ﺳ ْﻘﻔﺎً ﱠﳏ ُﻔﻮﻇﺎً وﻫﻢ ﻋﻦ‬


ُ ‫آ�ﻬﺗَﺎ ُﻣ ْﻌ ِﺮ‬
َ ْ َ ْ َُ ْ َ َ َ َ ََ َ
WajaAAalna alssamaa saqfan mahfoodhan wahum AAan ayatiha muAAridhoona;
(Surat Al Anbiyah 21:32)

Tafsir: Na tukazifanya Mbingu kua ni sakafu ya juu iliyohifadhiwa vizuri lakini bado
wanaipa mgongo dalili zake.

Ni kawaida kwa Ibn Adam anapojenga nyumba yake hua ni mwenye kujisifu kwa
kuweka sakafu ya vigae vya marumaru kutoka Hispania katika Nyumba yake, na hata
Nabii Sulaiman alipojenga Jumba lake na kisha akamkaribisha Malkia Bilqis basi
alijenga Nyumba yake kwa matofali ya Dhahabu, na sakafu ya kioo, ambapo sakafu zote
hizo ni za chini na hata kama ikwa ni ya juu kama dari au varanda basi hawezekani na
Ibn Adam kujengwa hata kwa Madini gani, bila ya kua na nguzo au kitegemezi.

Ambapo tunapoziangalia Mbingu basi tunaona kua zimetanda kama Sakafu ya Dari
madhubuti yenye maumbile ya ukubwa na uzuri wa kipekee na unaostaajabisha na bila
ya kua na nguzo wala egemeo, na bila ya shaka ukiangalia na kutafakkari basi ufaham
wako huondokewa na kila kitu ndani yake na badala yake hua ni wenye kujaa ukubwa
wa kutokua na mwanzo wala mwisho wa Muumba, Uhai wa Milele usiokua na Kifo wa
Muumba, Uwezo mkubwa sana na wingi wa Rehma zake Muumba. n,k kwani amesema
Allah Subhnah wa Ta’ala kua:
675

ِ ‫﴿وٱﻟ ﱠﺴﻤﺂء ﺑـﻨَـﻴـﻨَﺎﻫﺎ ِﺄﺑَﻳ ٍﺪ وإِ ﱠ� ﻟَﻤ‬


﴾‫ﻮﺳﻌُﻮ َن‬
ُ َ ْ َ ََْ َ َ
Waalssamaa banaynaha bi-aydin wa-inna lamoosiAAoona (Surat Adh Dhariyat
51:47)

Tafsir: Na Mbingu tumezijenga kwa Uwezo Mkubwa na kwa hakika sisi tunauongeza
upana na ukubwa wake.

Ambapo aya imetumia neno Banaynaha linalotokana na neno Bana lenye kumaanisha
Kujenga, Kusimamisha. Neno Bana ndio lililtoa neno Banaha ambalo linamaanisha
Jengo maalum la upekee ambalo ni madhubuti sana lililojengwa kwa ajili ya Hifadhi au
Ulinzi na Usalama na ingawa ni lenye kujumuisha sehemu tofauti lakini halina kasoro
yeyote.

Na pia ikatumia neno Aydin ambalo linatokana na neno Yada linalomaanisha Kugusa,
Kutosheleza, Kufanya Jema, Kuonesha Ukubwa, Nguvu, Uwezo na Mamlaka. Na pia
Wenye lugha yao husema ‘Aa’a Yadin – Kwa hiari ya Mikono yangu’ wanapompa mtu
msaada kumaanisha kua ni mwenye kutoa kwa hiari yao kutokana na ukarimu wao na
kua na uwezo juu ya wanacho kitoa.

Hivyo aya hii inatuonesha Uwezo wa Allah Subhanah wa Taala katika kuumba kwake
Mbingu zenye upekee katika kila kitu kwa ajili ya kutupa hifadhi bora Viumbe wake kua
ni sehemu ya Kuonesha Nguvu, Uwezo na Mamlaka yake Muumba, na Rehma zake na
Ukarimu wake juu yetu hivyo tunatakiwa kua ni wenye kumshukuru kwani mfano wa
maumbile ya Mbingu tu hua ni kithibitisho tosha juu ya Uwezo wake katika kila kitu.

Hivi jee tunapozungumzia Ukubwa wa Maumbile ya Mbingu hua tunazungumzia nini?


Bila ya shaka ni kua kwa wengi tunapozungumzia Mbingu basi hua wanadhani kua
tunazungumzia kitu ambacho ukiangalia kwa macho basi unaweza kudhani kua ni kama
sehemu nusu ya ganda la Chungwa au Mwamvuli wenye rangi ya samawati ambao uko
juu na kuifunika Dunia huku Nyota na Mwezi zikiwa zinaning’nia chini yake. Lakini
ukweli ni kua Maumbile ya Mbingu ni makubwa sana kwani yana ukubwa na upana wa
zaidi ya miaka Milioni 6.5 ya Nuru.

Na miaka ya Nuru hua mda ambao unapimwa kwa kutumia masafa ambayo Nuru husafiri
kutoka sehemu moja kuelekea katika sehemu nyengine kwa kasi ya kilomita 300 kwa
sekunde moja yaani kwa saa moja hua ni masafa ya kilomita Bilioni moja, hivyo
tukihesabia kwa mwaka hua na masafa ya kilomita Trilioni tisa na nusu yaani
9500,000,000,000 km. Huo ni mwaka mmoja, na Maumbile ya Mbingu ni zaidi ya Miaka
Milioni 6.5, na hayo ni makisio tu, na bado Ulimwengu unatanuka kama Allah Subhanah
676

wa Ta’ala amesema katika aya yetu hii kua ‘Wa-inna lamoosiAAoona – Na


tunauongeza Upana na Ukubwa wake.’

Kwani hapa bado hatujazungumzia kuhusiana na Black Holes (Mashimo Jeusi) ambayo
hua ni maeneo yaliopo Angani ambayo yanakadiriwa kua wingi wake unafikia Bilioni
kiidadi, ambapo kila shimo Jeusi Moja lenye nguvu kubwa sana za mvuto kasi kubwa
sana ndani yake na hivyo lina uwezo wa kumeza ndani yake kila kitu kinachokaribia
karibu yake na kutoweka milele kinapoingia ndani yake.

Kwa mfano tarehe 12-10-2020 Wanasayansi waliona namna Black Hole ilivyoivuta moja
kati ya Nyota zilizokaribu nayo na kuinyonya baada ya kuiyeysuha kwa nguvu za Joto
lake kama vile namna mtu anavyoinyonya na kuivuta tambi kutoka kwenye sahani hadi
ikatowekea ndani ya Mdomo wake.

Hivyo basi tunapoangalia na kuchunguza Maumbile ya Mbingu basi hua tunaona kua
katika kuumba kwake Mbingu Allah Subhanah wa Ta’ala hua hakujumuishi kubainisha
Uwezo wake, Nguvu zake, Mamlaka yake n.k tu lakini pia kunajumuisha kuonesha
Rehma zake juu yetu kama alivyosema katika aya ifuatayo:

ِ ‫﴿ﻫﻮ ٱﻟﱠ ِﺬى ﻳ ِﺮﻳ ُﻜﻢ آ�ﺗِِﻪ وﻳـﻨـ ِﺰُل ﻟَ ُﻜﻢ ِﻣﻦ ٱﻟ ﱠﺴﻤ‬
‫ﺂء ِرْزﻗﺎً َوَﻣﺎ ﻳَـﺘَ َﺬ ﱠﻛُﺮ إِﻻﱠ َﻣﻦ‬ َ َّ ّ َُ َ َ ْ ُ َُ
﴾‫ﻳُﻨِﻴﺐ‬
ُ
Huwa alladhee yureekum ayatihi wayunazzilu lakum mina alssama-i rizqan wama
yatadhakkaru illa man yuneebu (Surat Ghafir 40:13)

Tafsir: Yeye ndie ambae anaekuonesheni Dalili zake, na kukushushieni kutoka


Mbinguni Riziki, na hawatokumbuka isipokua wale warudio kwa Mola wao

Yaani Allah Subhanah wa Ta’ala ni mweye kuwaonesha viumbe wake dalili zake na
huwatumia riziki zao kutoka Mbinguni lakini hakuna anaethamini Rehma zake na Neema
zake isipokua wale waliuomuamini tu.

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kuhusiana na ayah ii
kua: ‘Udhihirisho wa Dalili zake hua ni wenye kuhuisha Nyoyo kama vile
kushushwa kwa Riziki kunavyohuisha Mwili’’

Ambapo kwa upande mwengine basi pia hua tunaweza kusema kua mbali ya kua Riziki
iliyotajwa hapa hua inamaanisha kukuza Imani ya Kiroho katika kumuamini Allah
677

Subhanah wa Ta’ala lakini pia maana ya Riziki iliyokusudiwa hapa basi hua ni ya
Mahitajio ya Viumbe vilivyomo Duniani kwa sababu kila kitu kilichopo Duniani hua
kinategemea Mahitajio yake ya Kimaisha kutokana na Mwangaza wa Jua ambalo liko
juu Mbinguni. Na hii ni kwa sababu Mwangaza wa Jua ndio Msingi wa matayarisho ya
chakula cha kila kitu hapa Duniani, kwani kutokana na Jua basi ndio mimea hua ni yenye
kukua ambayo nayo na mazao yake hua ni chakula cha Wanyama, Ndege Na Wadudu
mbali mbali ambao nao hua ni chakula cha wanyama wengine wakiwemo pia Ibn Adam.

Na mbali ya kua Ibn Adam anategemea Mimea kwa ajili ya chakula chake, ambacho hua
ni baadhi aya mizizi ya mimea hio, vigogo, majani, maua, matunda ya mimea hio lakini
pia Ibn Adam anategemea mimea katika mahitajio yake mengi sana ikiwemo hifadhi ya
mavazi, na makazi, zana mbali mbali za kufanyia kazi zake za kimaisha ambazo zote hizo
hua zinategemea kuwepo kwa mimea ambayo nayo kuota kwake hua inategemea Jua.
Lakini Wama yatadhakkaru illa man yuneebu.

Hivyo bila ya kuwepo kwa Muangaza wa Jua na Joto lake basi isingewezekana kuishi
hapa Duniani, na hii inaonekana wazi pale tunapoangalia Sayari ya mbali kabisa
inayojulikana kama Eris ambayo iko mbali sana na Jua hua haiwezekani kuishi ndaniyake
kwa sababu ya Baridi kali hivyo kila kitu chake hua ni chenye kuganda kwa Baridi, na
bila ya shaka joto la jua likiwa kubwa kama vile lilivyokua katika Sayari ya Mirih (Mars)
ilivyo karibu na Jua basi kila kitu Duniani kingeyayuka na kua Mvuke badala yake.

Rehma na Neema zake pia kutoka Mbinguni na manufaa yake juu yetu ni kua Mbingu
zina matabaka yenye uzito wa hewa tofauti kwa ajili ya kutunufaisha na athari nzuri za
baadhi ya Sayari kutokana na mionzi yake ya Nuru n.k na hapo hapo kutukinga na
madhara kwa kuchuja wingi wa nguvu za mionzi ya Sayari tofauti ikiwemo pia
Jua,Mwezi, Nyota nk ambazo zote ziko katika hali ya fii falakin yasbahuuna na
kupelekea kupatikana kwa usiku na mchana kama inavyosema aya inayofuatia baada ya
tuliyoanza nayo inayozungumzia Mbingu kua ni Sakafu (Surat Al Anbiyah 21:32) kwani
aya hio inasema:

ٍ َ‫﴿ وﻫﻮ ٱﻟﱠ ِﺬى ﺧﻠَﻖ ٱﻟْﻠﱠﻴﻞ وٱﻟﻨـﱠﻬﺎر وٱﻟﺸﱠﻤﺲ وٱﻟْ َﻘﻤﺮ ُﻛﻞﱞ ِﰱ ﻓَـﻠ‬
﴾‫ﻚ ﻳَﺴﺒَ ُﺤﻮ َن‬
ْ ََ َ َ ْ َ َ َ َ َ ْ َ َ ََُ
Wahuwa alladhee khalaqa allayla waalnnahara waalshshamsa waalqamara kullun
fee falakin yasbahoona (Surat Al Anbiyah 21:33)

Tafsir: Na yeye ndie ambae alieumba Usiku na Mchana na Jua na Mwezi, Kila kimoja
kinaelea katika njia yake.
678

Aya zinaendelea kuthibitisha Ukubwa wa Allah Subhanah wa Ta’ala Kiuwezo kwa


kuvielezea vithibitisho vilivyomo Mbinguni ambavyo viko katika hali ya fii falakin
yasbahuuna, ambapo neno Falaka hua linamaanisha Kua na Umbo la Duara, Kua ni
Yenye Kuelea katika Maumbile yake au Mzunguko wake, au Mhimili wake.

Kisha ikatumia neno Yasbahuuna linatokana na neno Sabaha ambalo hua linamaanisha
Kusifia, Kukuza, Kutukuza au Kusheherekea pale linapotumika na kua nyuma ya jina
tukufu la Allah kama tunavyosema Subhanah Allah au mbele ya yake tunaposema Allah
Subhanah wa Ta’ala.

Neno Sabaha ndio lililotoa neno Sabihat ambalo humaanisha Watu ambao wanateleza
kwa urahisi katika kufanikisha malengo yao, Watu wenye uwezo mkubwa wa
kuzungumza na pia watu ambao hua hawategemei watu wengine katika kufanya mambo
yao.

Neno Sabaha humaanisha Kuogelea, Kuelea, Kuteleza, Kurudia kufanya jambo hilo hilo
la kila siku, Kuenda kwa kubiruka biruka kama Mpira na pia humaanisha Mwendo wa
taratibu wa Farasi.

Kwa mtizamo wa kileo wa kisayansi basi aya hii iko wazi kimaana, hivyo basi aya hii ni
vizuri kwetu kuiangalia katika mtizamo wa Wanazuoni waliotangulia ili tupate kujua
mtizamo wao ulikuaje miaka 1300 iliyopita kabla ya maendeleo ya Kisayansi ambapo
kwa upande wa Imam Ad Dahaq Ibn Muzahim na Mujahid Ibn Sulayman basi wao
wanasema kua Neno Falak lililotumika hapa linamaanisha Muhimili kama ule
Muhimili wa jiwe la kusagia nafaka hivyo kila kimoja miongoni mwa vitu hivyo
vilivyopo Mbinguni vinazunguka kwenye muhimili wake.

Ambapo kwa upande wa Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din
Al Razi basi yeye amesema kua: ‘Maana iliyokusudiwa hapa inaweza ikawa moja
katia ya tatu zifuatazo: Kwanza: Anga haitembei wala haizunguki, isipokua
vilivyomo ndani yake ndio vinazunguka. Pili: Anga inazunguka lakini Vilivyomo
ndani ya havizunguki. Tatu: Vyote viwili, Anga na vilivyomo ndani yake
vinazunguka ila kwa mielekeo tofauti.’

Ambapo mpaka sasa hivi basi kuna uthibitisho kua Anga iko katika mzunguko wake na
inazunguka taratibu sana na vilivyomo ndani yake pia viko katika mzunguko wake, ila
hakuna uthibitisho kua Ulimwengu mzima unazunguka na unapoviangalia vyote hivyo
basi unaona kua vinazunguka kwa kujitegemea tena bila ya kuwepo hata nguzo ndani
yake, nje yake au baina yake.

Kisha baada ya hapo Allah Subhanah wa Ta’ala anatuwekea wazi kuhusiana na


maumbile ya Ardhi kwa kusema:
679

ٍ ‫﴿وٱﻷَرض ﻣ َﺪ ْد َ�ﻫﺎ وأَﻟْ َﻘﻴـﻨَﺎ ﻓِﻴﻬﺎ رو ِاﺳﻰ وأَﻧْـﺒـْﺘـﻨَﺎ ﻓِﻴﻬﺎ ِﻣﻦ ُﻛ ِﻞ َﺷﻲ ٍء ﱠﻣﻮُز‬
‫ون‬ ْ ْ ّ َ َ َ َ ََ َ ْ َ َ َ َ ْ َ
ٍ ِ ِ
َ ‫۞وإِن ِّﻣﻦ َﺷ ْﻲء إِﻻﱠ ِﻋ‬
�َ ‫ﻨﺪ‬ َ ‫ﲔ‬ َ ‫ﺶ َوَﻣﻦ ﻟﱠ ْﺴﺘُ ْﻢ ﻟَﻪُ ﺑَِﺮا ِزﻗ‬ ِ
َ ‫۞ َو َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ﻟَ ُﻜ ْﻢ ﻓ َﻴﻬﺎ َﻣ َﻌﺎﻳ‬
﴾‫َﺧَﺰاﺋِﻨُﻪُ وَﻣﺎ ﻧـُﻨَـِّﺰﻟُﻪُ إِﻻﱠ ﺑَِﻘ َﺪ ٍر ﱠﻣ ْﻌﻠُ ٍﻮم‬
َ
Waal-ardha madadnaha waalqayna feeha rawasiya waanbatna feeha min kulli
shay-in mawzoonin; WajaAAalna lakum feeha maAAayisha waman lastum lahu
biraziqeena; Wa-in min shay-in illa AAindana khaza-inuhu wama nunazziluhu illa
biqadarin maAAloomin (Surat Al Hijr 15:19-21)

Tafsir: Na Ardhi tumeitandaza na kuweka ndani yake Milima madhubuti na tukajaalia


ndani yake kuchipua (kuota) kila kitu kwa mpangilio. Na tukakujaalieni ndani yake
njia ya kutafutia maisha kwa ajili yenu na kwa ajili ya wale ambao hamuwaruzuku
nyinyi. Na hakuna kitu chochote isipokua kipo kwenye akiba yetu, na hatukishushi
isipokua kwa makadirio yetu maalum.

Aya inabainisha kua Milima imejaaliwa kua ni nguzo ambazo zipo kwa ajili ya kuipa
Ardhi umadhubuti, na ndani yake imepewa uwezo wa kuotesha mimea ya aina mbali
mbali kwa mpangilio uliopangika kwa ajili ya viumbe wanaoishi Duniani kwa mpangilio
wa kua Mimea fulani iote katika Ardhi ya aina fulani iote katika maeneo ya Ardhi fulani,
na iwe inatoa maua aina gani kuwa ajili ya kuipamba Ardhi husika na pia iwe inazaa
mazao gani kwa ajili ya watu husika na kwa kiasi gani. Na hivyo kwa maeneo tofauti
Ardhini kuweza kua ni yenye kuzalisha mazao tofauti. Hii yote ni kwa ajili yetu na kwa
ajili ya wengineo ambao watu wanadhani kua wanawaruzuku wao kumbe wanarazukiwa
na Allah Subhanah wa Ta’ala, ikiwemo familia zetu, wanyama wa kufuga na viumbe
wengine na kila kitu kilichomo ndani yake ardhini kinatolewa kwa makadirio yake
Muumba na kwa ajili ya manufaa yao viumbe na kwa ajili ya kuwajaribu viumbe, kama
zinavyosema aya:

ِ‫ض ِزﻳﻨﺔً ﱠﳍﺎ ﻟ‬


﴾ً‫ﻋﻤﻼ‬
َ ‫ﻦ‬
َ َُ‫ﺴ‬‫َﺣ‬
ْ ‫أ‬ ‫ﻢ‬‫ﻬ‬ُ ْ َ َ َ ِ ‫﴿إِ ﱠ� َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ َﻣﺎ َﻋﻠَﻰ ٱﻷ َْر‬
‫ـ‬
‫ﱡ‬‫ﻳ‬َ‫أ‬ ‫ﻢ‬‫ﻫ‬ُ ‫ﻮ‬ُ‫ﻠ‬‫ـ‬‫ﺒ‬ْ ‫ـ‬‫ﻨ‬
َ
Inna jaAAalna ma AAala al-Ardhi zeenatan laha linabluwahum ayyuhum ahsanu
AAamalan (Surat Al Kahf 18:07)

Tafsir: Kwa Hakika tumejaalia kwenye Ardhi vizuri kwa ajili yake, ili tuwajaribu
(Watu) kuwaona ni wepi miongoni mwao ni wabora katika kufanya mema.
680

Hivyo kupitia katika mzunguko wa makadirio maalum ya Muumba kuanzia kwenye


Madini tofauti yaliyomo ardhini, kwa ajili ya matumizi ya mapambo mbali mbali na zana
za kurahisishia kufanyia kazi tofauti, Madini pia na wadudu tofauti waliomo ndani yake,
maji yaliyomo ndani yake, udongo uliopo juu yake, hewa inayoingia ndani yake na iliyo
juu yake ambavyo vyote hivyo vipo kwa ajili ya kuwezesha mimea tofauti kuota kwa
manufaa ya Watu na viumbe wengine waliopo juu ardhini kutokana na kuwepo kwa
mionzi ya Jua ambayo hupatikana katika kila siku katika wakati wa Mchana.

2-DALILI KATIKA KUUMBWA USIKU NA MCHANA


Katika Uumbwaji wa Dunia na kutofautiana baina ya Mchana na Usiku na kubadilika
kwa ukubwa wake wa nyakati hizo kulingana na misimu tofauti ya Mwaka kutokana na
Maumbile ya Duara ya Dunia basi anasema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

ِ ِ
‫ﺲ َوٱﻟْ َﻘ َﻤَﺮ ُﻛﻞﱞ‬ ْ ‫ﱠﻬ َﺎر ِﰱ ٱﻟْﻠﱠْﻴ ِﻞ َو َﺳ ﱠﺨَﺮ ٱﻟﺸ‬
َ ‫ﱠﻤ‬ َ ‫﴿ﻳُﻮﻟ ُﺞ ٱﻟْﻠﱠْﻴ َﻞ ِﰱ ٱﻟﻨـ‬
َ ‫ﱠﻬﺎ ِر َوﻳُﻮﻟ ُﺞ ٱﻟﻨـ‬
‫ﻳﻦ ﺗَ ْﺪﻋُﻮ َن ِﻣﻦ ُدوﻧِِﻪ َﻣﺎ‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ رﺑﱡ ُﻜﻢ ﻟَﻪ ٱﻟْﻤ ْﻠ ﱠ‬ ِ
َ ‫ﻚ َوٱﻟﺬ‬ُ ُ ُ ْ َ ُ‫َﺟ ٍﻞ ﱡﻣ َﺴ ًّﻤﻰ ٰذﻟ ُﻜ ُﻢ ﱠ‬ َ ‫َْﳚ ِﺮى ﻷ‬
﴾‫ﳝَْﻠِ ُﻜﻮ َن ِﻣﻦ ﻗِﻄْ ِﻤ ٍﲑ‬
Yooliju allayla fee alnnahari wayooliju alnnahara fee allayli wasakhkhara
alshshamsa waalqamara kullun yajree li-ajalin musamman dhalikumu Allahu
rabbukum lahu almulku waalladheena tadAAoona min doonihi ma yamlikoona min
qitmeerin (Surat Fatir 35:13)

Tafsir: Anauingiza Usiku kwenye Mchana, na anauingiza Mchana kwenye Usiku na


akavifanya Jua na Mwezi kua kila kimoja ni chenye kupita katika njia yake
iliyojaaliwa. Huyo ndio Allah Mola wenu, yeye ndie Mwenye Mamlaka, na wale ambao
mnao waomba zaidi yake hawamiliki chochote hata Qitmir (Ngozi Laini ya Kokwa ya
Tende)

Ambapo aya hii imetumia neno Yuliiju ambalo ni lenye kutokana na neno Walaja lenye
kumaanisha Kuingia, Kupenya, Kulinda, Kukaribiana sana na Kutegemeana japo kua ni
Tofauti Kimaumbile, hivyo basi japo kua Usiku na Mchana ni vitu vyenye maumbile
681

tofauti kwani kimoja kina Kiza na chengine kina Nuru lakini vitu viwili hivi ni vyenye
Kuingiliana na Kulindana kiasi ya kua Kimoja hakiwezi kuwepo kinapokosekana
chengine.

Na bila ya shaka Allah Subhnah wa Ta’ala ameanza na kuutaja Usiku kabla ya Mchana
kwa sababu kwa upande wa Kiislam na Kalenda ya Kiislam basi Siku hua inaanza na
wakati wa Usiku yaani Magharibi baada ya kuzama Jua na hivyo hua ni yenye
kumalizikia katika wakati wa Mchana yaani linapozama Jua, ambapo hali ni tofauti kwa
upande wa Siku za Kalenda za Magharibi ambapo siku hua inaanza saa sita Usiku na
hivyo kua ni yenye kuanza Asubuhi na kumalizikia Jioni yaani wakati wa Usiku.

Katika aya hii tunaona pia Allah Subhanah wa Ta’ala aelezea Ukubwa wake na Mamlaka
yake katika kuumba kwake na kumiliki kwake na kisha ametumia neno Qitmir katika
kuelezea kutokua na maana Msaada wala Mamlaka juu ya kitu chochote wale ambao ni
wenye kushirikishwa nae na wale wasiomuamini. Ambapo neno Qitmir hua linamaanisha
Ngozi laini na nyepesi sana inayokaa baina ya Kokwa ya Tende na Nyama ya Tende, hii
ni ngozi ambayo wengi miongoni mwetu hua hawaioni kutokana na kua ni wenye kuitupa
Kokwa ya Tende baada ya Kula Nyama ya Tende ambayo ndio Tende yenyewe na ndio
yenye Manufaa kwa Mwili na yenye Ladha ya Utamu wenyewe.

Neno Qitmir pia hua ni sawa na neno Fatila ambalo nalo pia hua ni lenye kumaanisha
Ngozi laini na nyepesi sana inayokaa baina ya Kokwa ya Tende na Nyama ya Tende,
pale Qur’an iliposema kuhusiana na siku ya Malipo kua:

‫ﻚ ﻳَـ ْﻘَﺮُؤو َن ﻛِﺘَﺎﺑَـ ُﻬ ْﻢ‬


َ ِ‫﴿ ﻳَـ ْﻮَم ﻧَ ْﺪﻋُﻮاْ ُﻛ ﱠﻞ أ َُ� ٍس ﺈﺑِِ َﻣ ِﺎﻣ ِﻬ ْﻢ ﻓَ َﻤ ْﻦ أُوﺗِ َﻰ ﻛِﺘَﺎﺑَﻪُ ﺑِﻴَ ِﻤﻴﻨِ ِﻪ ﻓَﺄ ُْوﻟَـٰﺌ‬
﴾ً‫وﻻَ ﻳُﻈْﻠَﻤﻮ َن ﻓَﺘِﻴﻼ‬
ُ َ
Yawma nadAAoo kulla onasin bi-imamihim faman ootiya kitabahu biyameenihi
faola-ika yaqraoona kitabahum wala yudhlamoona fateelan (Surat Al Israa17:71)

Tafsir: Katika siku watakayonadiwa watu wote na Imam wake, na kisha atakaepewa
kitabu chake kwa mkono wa kulia basi huyo atasoma kitabu chake, na
hatodhulumiwa hata kwa ule udogo wa ngozi laini sana ya kokwa ya tende.

Ambapo si katika Qur’an wala si katika Sunnah kua kuna uthibitisho wa kua kama watu
watapewa vitabu vyao hivyo na Malaika ama watapewaje, isipokua maneno ya mwanzo
ya vitabu hivyo yatakua:
682

﴾ً‫ﻚ َﺣ ِﺴﻴﺒﺎ‬ َ ‫ﻚ َﻛ َﻔ ٰﻰ ﺑِﻨَـ ْﻔ ِﺴ‬


َ ‫ﻚ ٱﻟْﻴَـ ْﻮَم َﻋﻠَْﻴ‬ َ َ‫﴿ٱﻗْـَﺮأْ َﻛﺘَﺎﺑ‬
Iqra/ kitabaka kafa binafsika alyawma AAalayka haseeban (Surat Al Isra 17:14)

Tafsir: Soma Kitabu chako Nafsi yake mwenyewe inatosheleza leo hii kua ni hesabu
juu yako.

Hivyo hali ya maumbile ya Usiku na Mchana kutokana na makadirio yake katika kuumba
kwake ni kwa ajili ya manufaa ya Viumbe vilivyomo ndani yake Ulimwenguni na ndio
maana athari yake tukawa tunaihisi mpaka ndani ya miili yetu ambayo ni yenye
maumbile bora na ukamilifu wa kipekee kama anavyosema Allah Subhanah wa Ta’ala
katika Qur’an kua:

﴾‫َﺣ َﺴ ِﻦ ﺗَـ ْﻘ ِﻮ ٍﱘ‬‫أ‬ ۤ ِ ‫﴿ﻟَﻘﺪ ﺧﻠَﻘﻨﺎ ٱ ِﻹﻧﺴﺎن‬


‫ﰲ‬
ْ َ َ َْ َ ْ َ
Laqad khalaqna al-insana fee ahsani taqweemin (Surat Tinn 95:4)

Tafsir: Kwa hakika tumemuumba Mtu katika Taqwim bora kabisa.

Ambapo aya imetumia neno Taqwim, ambalo ni lenye kutokana na mzizi wa neno Qa-
Ma ambalo kwa Lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kua katika hali ya Kusimama
Sawia, Kua Thabiti, Madhubuti, Kamilifu, Kua bila ya kasoro yeyote, Kua na Thamani,
hali ya Usimamizi, Hali ya ulinzi, Hali ya mpangilio uliokamilika, hali ya Mfumo kamili,
hali ya Umbo lililokamilika n.k

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala amesifia hali ya kua Taqwim lakini hii si Taqwim ya
kawaida bali ni Ahsani Taqwim yaani Taqwim Bora. Hivyo basi Taqwim
inayozungunziwa katika ayah hii ambayo ni Taqwim bora humaanisha hali ya maumbile
inayojumuisha Mfumo Kamilifu wa Mwili mzima wa Ibn Adam na ufanyaji kazi wake
kuanzia ndani ya mwili wake ambamo mna Mifumo kamilifu tofauti ndani yake ikiwemo
Mfumo wa Damu, Mfumo wa Chakula, Mfumo wa Ubongo, Mfumo wa Viungo, Mfumo
wa Ufaham, Mfumo wa Hisia n.k ambayo hua ni yenye kuenda sambamba kiufanyaji
kazi na Maumbile ya mfumo wa Viungo vya nje ya mwili na kukamilisha Muonekano
mzuri wa Maumbile ya mwili wa Ibn Adam.

Miongoni mwa sifa bora za Ukamilifu huo ni kua na mfumo unaozalisha Kemikali
ambazo hua ni zenye kua na kazi tofauti ndani ya Miili yetu, ambapo moja miongoni
mwao kemikali hizo ni ile inayojulikana kwa jina la Seratonin ambayo huzalishwa na
683

Mfumo Kamilifu wa Ubongo. Seratonin hua ni Kemikali inayohusiana na Uhifadhi wa


Kumbukumbu, Ufaham, Hisia za Furaha, Mapenzi, Uchangamfu n.k

Kemikali ya Seratonin pia hua ni yenye kufanya kazi ya kumsababishia mtu kua na hali
ya kuhisi Usingizi kutokana kua ni yenye kusaidia uzalishwaji wa Kemikali nyengine
iitwayo Melatonin ambayo nayo huzalishwa katika Mfumo wa Ubongo na kisha
kuingizwa ndani ya Mfumo wa Damu.

Melatonin hua ni kemikali ambayo ni yenye kusimamia Mfumo wa saa ya ndani ya Mwili
wa Ibn Adam ambao ndio unaoutaarifu Mwili kua sasa hivi ni usiku na umefika mda wa
Kulala ili mwili na ufaham upate kupumzika kwa ajili ya majukumu ya siku inayofuata
na Seratonin hua ni yenye kusimamia Mtu kuchangamka na kua macho pale
linapochomoza Jua kwa kuutayarisha mwili na ufaham baada ya kupumzika kwake na
kumtaarifu mtu kua umefika wakati wa kuamka na kuushughulisha mwili, akili na
ufaham kwa ajili ya majukumu ya siku mpya.

Hivyo basi kama ilivyokua kua kuna mategemeano baina ya uingiaji wa Usiku na
Mchana kiulimwengu basi ndio hivyo ilivyokua kuna mategemeano baina ya Kemikali
za Seratonin na Melatonin katika ufanyaji kazi wao kwa Seratonin kubainisha kua
umefika wakati wa Mchana na kiza kinapoingia Melatonin kuubainishia mwili kua
umefika wakati wa Usiku na hivyo mwili inabidi upumzike.

Katika kuthibitisha hili basi mbali ya kua katika wakati wa usiku mtu hua unahisi
Usingizi zaidi kuliko wakati wa Mchana. Kiasi ya kua hata wale wanaofanya kazi za
kukesha Usiku basi Mchana hua hawezi kulala na kupata usingizi ambao ni sawa kama
vile ambavyo wanaoupata kama wangelala wakati wa usiku.

Aukama mtu atasafiri kutoka upande mmoja wa Duani kwa mfano kutoka Afrika kueleka
Canada, au kutoka Afrika kuelekea Australia, basi kwa kua kuna utofauti wa mda wa
kuingia Usiku na Mchana baina ya sehemu aliyotoka basi akifika sehemu aliyoelekea
basi hatoweza kulala na kupata usingizi hata kama ikiwa ni usiku na hii ni kwa sababu
uzalishwaji wa Melatonin katika mwili wake hua haujazoea mazingira mapya ya nyakati
za kuzama na kuchomoza kwa Jua katika sehemu aliyowasili na hua bado unaendana na
hali ya mazingira ya sehemu aliyokuwepo hapo kabla.

Hivyo mwanzoni mtu kama huyu hua ni mwenye kupata shida ya kulala na kupata
usingizi kwa siku mbili tatu hadi pale atakapozoea mazingira hayo mapya na hivyo
uzalishwaji huo wa kemikali za Seratonin na Melatonin ndani ya mwili wake ukae sawa
na kua ni wenye kuendana sambamba na hali ya mazingira ya kuchomoza na kuzama
kwa jua katika Ardhi ya ugenini aliyokuwepo.
684

Mfano mwengine ni ule ambao wengi wetu tunaujua sana kutokana na kuumwa baadhi
ya Maradhi tofauti katika uhai wetu, hivyo tuchukulie mfano wa mtu anaeumwa na
Homa, Kifua, Jino, n.k basi hua tunajua kua mgonjwa hua ni mwenye kuzidiwa zaidi hali
ya maradhi yake katika wakati wa usiku kuliko katika wakati wa mchana, kiasi ya kua
mtu hujiuliza inakuaje mpaka maradhi hayo hua yanajua kua umeingia usiku?

Hivyo Mfumo wa uzalishwaji wa Seratonin na Melatonin ndio unaoutaarifu mwili


kuhusiana na mabadiliko ya nyakati za Usiku na Mchana katika maisha yetu
Ulimwenguni na hii si kwetu sisi tu bali hata kwa Ndege, Wanyama wa ardhini na Samaki
pia hua ni wenye miili yenye kujua mabadiliko hayo ya nyakati za kila siku, kwani pia
kama wanyama wengine wangekua hawana ufaham huo ndani ya miili yao na hivyo
kukosa hisia ya kuupumzisha mwili kwa kulala basi ingekua hatari sana.

Mabadiliko haya hua Usiku na Mchana hua ni kwa ajili ya manufaa ya yetu na kwa ajili
ya Viumbe vilivyomo Ulimwenguni kama anavyosema mwenyewe Muumba katika aya
zinazofuata:

﴾ً‫ﱠﻬﺎر َﻣ َﻌﺎﺷﺎ‬ ۞ ِ ۞ ﴿
َ َ ‫َو َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ﻧَـ ْﻮَﻣ ُﻜ ْﻢ ُﺳﺒَﺎﺎﺗً َو َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ٱﻟﻠﱠْﻴ َﻞ ﻟﺒَﺎﺳﺎً َو َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ٱﻟﻨـ‬
WajaAAalna nawmakum subatan WajaAAalna allayla libasan; WajaAAalna
alnnahara maAAashan; (Surat An Nabaa 78:9-11)

Tafsir: Na tukajaalia Usingizi kua ni Pumziko, Na tukaujaalia Usiku kua ni Libas


(Vazi), Na Tukajaalia Mchana kua ni wa Maisha (kutafutia)

Hivyo katika aya hizi Allah Subhanah wa Ta’ala anatubainishia Umuhimu na Manufaa
yanayopatikana kutokana na kuwepo kwa Maumbile ya Usingizi, Usiku na Mchana kwa
ajili ya Viumbe wake ambapo tunaona kua aya zimetumia neno Subata ambalo hua
linamaanisha Kupumzika, Kutulia, Kujinyoosha, Kukatisha, Kusitisha, Kulala, Kusinzia
Kunakotokana na Machofu.

Na hali za hatua za hisia ya Usingizi imetajwa mara kadhaa ndani ya Qur’an kwa
kuainisha hali na hatua zake tofauti kimaumbile kama vile walivyoelezea Wansayansi
wetu leo hii, na hii hali ya Subatan hua ni hali ya hatua ya mwisho ya Usingizi ambayo
hua ni hali ya kulala kwa Usingizi mzito wa kutosha kuupumzisha mwili na ambao ndio
unaompelekea mtu kua ni mwenye kuota ndani yake, ambapo hali ya kwanza ya hisia ya
Usingizi hua ni ile ya Sinatun ambayo imetajwa katika sehemu ya mwanzoni ya Ayat Al
Kursiy ambayo imetumia neno Sinatun kwa kusema:
685

﴾‫ﻮم ﻻَ َﺄﺗْ ُﺧ ُﺬﻩُ ِﺳﻨَﺔٌ وﻻَ ﻧـَﻮٌم‬


ُ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻻَ إِﻟَـٰﻪَ إِﻻﱠ ُﻫ َﻮ ٱ ْﳊَ ﱡﻰ ٱﻟْ َﻘﻴﱡ‬
‫﴿ﱠ‬
ْ َ
Allahu la ilaha illa huwa alhayyu alqayyoomu la ta/khudhuhu sinatun wala
nawmun (Surat Al Baqara 2:255)

Tafsir: Allah! La ilaha illa Huwa (Hakuna Mungu anaestahiki kuabudiwa isipokua
yeye), Mwenye kuishi Milele, Mwenye kusimamia na kukipa Ulinzi kila kitu,
Asiepitiwa na kusinzia na wala asiepitiwa na Usingizi.

Ambapo neno Sinatun hua linatokana na neno Wasana ambalo hua linamaanisha Kua na
hisia ya kutaka Kulala au Kusinzia ambayo hua ni hatua ya kwanza ya hisia ya Usingizi,
na hivyo kumaanisha udhaifu wa Ibn Adam wa kua ni mwenye kuhitaji mapumziko ya
mwili wake kutokana na maumbile yake, lakini maana iliyotumika katika ayah hii
haimzungumzii Kiumbe bali inamzungumzia Muumbaji, na hivyo kumuelezea kua ni
asie kua na sifa za kiumbe, kwani yeye yuko mbali na sifa za viumbe wake hahitaji
kupumzika kwa sababu hana sifa ya kuchoka na hivyo hasinzii na wala halali.

Hivyo Sinatun hua ni sehemu ya hatua ya kwanza ya hisia ya Usingizi ambapo hatua ya
pili hua ni NaaAsa. Ambalo ni neno linalomaanisha Kupumzika, Kua na Udhaifu wa
Mwili kutokana na Machovu au Kuingia Ndani ya hatua ya Usingizi yaani Kulala kwa
dakika kadhaa.

Ambapo tunaona katika Qur’an kua Allah Subhanah wa Ta’ala amelitumia neno NaaAsa
mara mbili ambazo ni mara zinazoelezea hali ya kulala kwa dakika kadhaa, kwani aya
zilizotumiwa ndani yake ni zile aya ambazo zinazozungumzia hali ya Usingizi wa Watu
ambao wako vitani, hivyo hua ni tofauti na Usingizi wa Nyumbani kwani hua ni usingizi
wa kupunguza machovu kwa kiasi ya dakika kadhaa, ili angalau ukiamka uwe na umakini
kidogo na nguvu mpya, Ambapo miongoni mwa aya hizo ni ile inayozungumzia tukio la
vita vya Badr kama ilivyosema aya:

ِ ِِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ
َ ‫ﺎس أ ََﻣﻨَﺔً ّﻣْﻨﻪُ َوﻳـُﻨَـِّﺰُل َﻋﻠَْﻴ ُﻜﻢ ّﻣ َﻦ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤﺂء َﻣﺂءً ﻟّﻴُﻄَ ّﻬَﺮُﻛ ْﻢ ﺑﻪ َوﻳُ ْﺬﻫ‬
‫ﺐ‬ َ ‫﴿إِ ْذ ﻳـُﻐَ ّﺸﻴ ُﻜ ُﻢ ٱﻟﻨـ‬
َ ‫ﱡﻌ‬
﴾‫ﺖ ﺑِِﻪ ٱﻷَﻗْ َﺪ َام‬ َ ِ‫ﺎن َوﻟِﻴَـْﺮﺑ‬
َ ِّ‫ﻂ َﻋﻠَ ٰﻰ ﻗُـﻠُﻮﺑِ ُﻜ ْﻢ َوﻳـُﺜَـﺒ‬
ِ َ‫ﻋﻨ ُﻜﻢ ِرﺟﺰ ٱﻟﺸﱠﻴﻄ‬
ْ َْ ْ َ
Idh yughashsheekumu alnnuAAasa amanatan minhu wayunazzilu AAalaykum
mina alssama-i maan liyutahhirakum bihi wayudhhiba AAankum rijza
686

alshshaytani waliyarbita AAala quloobikum wayuthabbita bihi al-aqdama (Surat


Al Anfal 8:11)

Tafsir: Na (kumbukeni) alipokufunikeni nyie na NuaAsa kama Amani kutoka kwake


na akakutumieni Maji kutoka Mbinguni ili akutoharisheni na kukutoeni wasiwasi
kutoka kwa Shaytani na kuzitia nguvu Nyoyo zenu na kuiimarisha miguu yenu.

Ambapo aya inafafanulika vizuri sana pale tunapoangalia ufafanuzi wa Mujaddid Ad Din
Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi ambae anasema kua: ‘Kutokana na
kua kimaumbile ni vigumu kwa Mtu mwenye Khofu kupata usingizi na kulala, basi
Allah Subhanah wa Ta’ala amesema kua: ‘Na (kumbukeni) alipokufunikeni nyie na
NuaAsa’ ambayo ni miongoni mwa Miujiza yake ya kupitia na usingizi wa muda
mfupi katika wakati huo, kwani kama wangelala moja kwa moja basi bila ya shaka
Maadui zao wangewashambulia ’

Na anasema Imam Muhammad Ibn Is-haq kua: ‘Amesema Ali Ibn Abi Talib Radhi
Allahu Anhu kua: ‘Tulikua hatuna mpanda Farasi katika vita hivyo isipokua Miqdad
Al Aswad. Nami sikuona yeyote yule miongoni mwetu isipokua alikua ni mwenye
kulala, ila Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambae alikua chini ya mti akilia
na kuomba dua mpaka asubuhi’’

Na mara ya pili ni neno NuaAsa limetumika katika ile aya inayozungumzia tukio
lililotokea baada ya Vita vya Uhud pale Waislam waliposhindwa baada ya Khalid Ibn
Walid kuwaongoza Makafiri na kupata Ushindi kisha Abu Sufyan na Khalid Ibn Walid
kurushiana maneno na Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam kuhusiana na ushindi wao
huo na kisha wakaondoka, na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akasema kuhusiana na
wapiganaji wa Upande wa Waislam na watu wa Mji wa Madina kua:

‫َﻧﺰَل َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ ِّﻣ ْﻦ ﺑَـ ْﻌ ِﺪ ٱﻟْﻐَِّﻢ أ ََﻣﻨَﺔً ﻧـﱡ َﻌﺎﺳﺎً ﻳَـ ْﻐ َﺸ ٰﻰ ﻃَﺂﺋَِﻔﺔً ِّﻣْﻨ ُﻜ ْﻢ َوﻃَﺂﺋَِﻔﺔٌ ﻗَ ْﺪ‬
َ ‫﴿ﰒُﱠ أ‬
‫ﺎﻫﻠِﻴﱠِﺔ ﻳَـ ُﻘﻮﻟُﻮ َن َﻫ ْﻞ ﻟﱠﻨَﺎ ِﻣ َﻦ ٱﻷ َْﻣ ِﺮ‬
ِ ‫ٱﳉ‬
َْ ‫ﭑﻪﻠﻟ َﻏْﻴـَﺮ ٱ ْﳊَِّﻖ ﻇَ ﱠﻦ‬
ِ‫أ ََﳘﱠْﺘـﻬﻢ أَﻧْـ ُﻔﺴﻬﻢ ﻳﻈُﻨﱡﻮ َن ﺑِ ﱠ‬
َ ُُْ ُْ
ۤ ِِ ٍ
َ َ‫ِﻣ ْﻦ َﺷ ْﻲء ﻗُ ْﻞ إِ ﱠن ٱﻷ َْﻣَﺮ ُﻛﻠﱠﻪُ ﱠﻪﻠﻟ ُﳜْ ُﻔﻮ َن ِﰱ أَﻧْـ ُﻔ ِﺴ ِﻬﻢ ﱠﻣﺎ ﻻَ ﻳـُْﺒ ُﺪو َن ﻟ‬
‫ﻚ ﻳَـ ُﻘﻮﻟُﻮ َن ﻟَ ْﻮ‬
ِ‫ﱠ‬ ِ ِ ‫ﱠ‬ ِ ِ
‫ﻳﻦ‬
َ ‫ﺎﻫﻨَﺎ ﻗُ ْﻞ ﻟ ْﻮ ُﻛْﻨـﺘُ ْﻢ ﰱ ﺑـُﻴُﻮﺗ ُﻜ ْﻢ ﻟَﺒَـَﺮَز ٱﻟﺬ‬ُ ‫َﻛﺎ َن ﻟَﻨَﺎ ﻣ َﻦ ٱﻷ َْﻣ ِﺮ َﺷ ْﻲءٌ ﱠﻣﺎ ﻗُﺘ ْﻠﻨَﺎ َﻫ‬
687

‫ﺺ َﻣﺎ ِﰱ‬ ِ ِ ‫ﺎﺟﻌِ ِﻬ ْﻢ َوﻟِﻴَـْﺒـﺘَﻠِﻰ ﱠ‬


ِ ‫ُﻛﺘِﺐ ﻋﻠَﻴ ِﻬﻢ ٱﻟْ َﻘْﺘﻞ إِ َ ٰﱃ ﻣﻀ‬
ُ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻣﺎ ِﰱ‬
َ ‫ﺻ ُﺪوِرُﻛ ْﻢ َوﻟﻴُ َﻤ ّﺤ‬ َ َ ُ ُ َْ َ
﴾‫ﺼ ُﺪوِر‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻋﻠِﻴﻢ ﺑِ َﺬ‬
‫ات ٱﻟ ﱡ‬ ٌ َ ُ‫ﻗُـﻠُﻮﺑِ ُﻜ ْﻢ َو ﱠ‬
Thumma anzala AAalaykum min baAAdi alghammi amanatan nuAAasan
yaghsha ta-ifatan minkum wata-ifatun qad ahammat-hum anfusuhum
yadhunnoona biAllahi ghayra alhaqqi dhanna aljahiliyyati yaqooloona hal lana
mina al-amri min shay-in qul inna al-amra kullahu lillahi yukhfoona fee anfusihim
ma la yubdoona laka yaqooloona law kana lana mina al-amri shay-on ma qutilna
hahuna qul law kuntum fee buyootikum labaraza alladheena kutiba AAalayhimu
alqatlu ila madhajiAAihim waliyabtaliya Allahu ma fee sudoorikum waliyumahhisa
ma fee quloobikum waAllahu AAaleemun bidhati alssudoori (Surat Al Imraan
3:154)
Tafsir: Na kisha akakushushieni juu yenu baada ya kutokua na utulivu (wa kiakili),
Amani ya NuaAsa iliyokufunikeni watu miongoni mwenu lakini watu wengine
walikuwa wakifikiria nafsi zao (namna ya kujikoa) wakimdhania sivyo Allah, dhana
za kijahiliya wakasema: ‘Hivi imetuhusu nini sisi jambo hili?’. Waambie (Ewe
Muhammad) Jambo hili linamhusu Allah pekee. Walikua wanaficha kwenye Nafsi zao
kile ambacho hawataki kukuambia kwa kusema kua: ‘Kama ingekua sisi tuna kauli
juu ya jambo hili basi tusingeuliwa’ Waambie kua: ‘Kama mngebakia katika majumba
yenu basi wale ambao waliokua wameandikiwa kifo wangefika kwenye sehemu
waliyoandikiwa Kifo’ Ili awajaribu kuhusiana na kilichomo ndani ya vifua vyenu na
kuyatoa yaliyomo ndani ya Nyoyo zenu. Na kwa hakika Allah ni mwenye kujua
yaliyomo ndani ya Vifua.
Ambapo kwa upande wa Abd Allah Ibn Abbas anasema kua: ‘Baada ya Vita vya Uhud
na Abu Sufyan kuondoka basi Rasul Allah Salallahu A’alayhi wa Salam akatuma
mtu akawaangalie jee Wameelekea wapi Makafiri hao, katika Mji wa Makkah au
Madina kushambulia, lakini ikaonekana kua Makafiri hao wamerudi Makkah
hivyo Waislam wakapata afueni na Utulivu hivyo NuaAsa ikawakumba Waislam
hao’
Ambapo kwa Upande wa Al Suddi basi yeye nasema kua: ‘Wanafiq hawakuweza kujua
kama Makafiri wameshinda ama wameshindwa, na hawakuamini ni kwanini
Makafiri wa Makkah hawakuuvamia Mji wa Madina hivyo wakawa wanahaha, na
ndio maana aya ikasema kua lakini watu wengine waliokua wakifikiria nafsi zao’
Na akasema Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu kua: ‘NuaAsa katika wakati wa
Vita hua ni kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala, lakini katika wakati wa Sala
hua ni kutoka kwa Shaytan.’
688

Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi yeye
anasemakua: ‘NuaAsa katika Vita hua ni kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala kwa
sababu usingizi huo humjia mtu katika wakati wa vita pale anapokua ni mwenye
kumtegemea Allah Subhanah wa Ta’ala pekee wakati NuaAsa katika Sala hua ni
wenye kutokana na Shaytan kwa sababu ya kua mbali na Allah Subhanah wa
Ta’ala’
Hivyo NuaAsa hua ni wenye kumaanisha usingizi wa mapumziko ya mda mfupi baada
ya kuchoka kutokanana kua katika mazingira ya hatari na yenye kuchosha iwe Mchana
au Usiku. Kisha baada ya hatua hio ya NuAas basi inafuatia hatu ya hali ya usingizi wa
Hujuu ambao ni wenye kutokana na neno Hajaa ambalo ndio lililotumika katika aya
ifuatayo:

﴾‫َﺳ َﺤﺎ ِر ُﻫﻢ ﻳَﺴﺘَـ ْﻐ ِﻔﺮو َن‬ ِ ِ ﴿


ُ ْ ْ َ ‫َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻗَﻠﻴﻼً ّﻣﻦ ٱﻟﻠﱠْﻴ ِﻞ َﻣﺎ ﻳَـ ْﻬ َﺠﻌُﻮ َن‬
ْ ‫۞وﺑِﭑﻷ‬
Kanoo qaleelan mina allayli ma yahjaAAoona; Wabial-ashari hum yastaghfiroona
(Surat Adh Dhariyat 51:17-18)
Tafsi: ‘Walikua kidoogo tu katika wakati wa Usiku yahjaAAoona, na katika mda wa
kabla ya Alfajir walikua wakifanya Istighfar’
Ambapo ayah hii inayowazungumzia Waislam wenye sifa ya Muhsinun yaani wenye
kufanya mema kua ni wenye kulala kidogo tu usiku na kisha kuamka na kusali kutokana
na Taqwa na Matumaini yao kwa Mola wao, hivyo ayah hii imetumia neno YahjaAAoona
linalotokana na neno Hajaa ambalo hua ni lenye kumaanisha: Kusinzia na Kulala kwa
kwa mda mfupi pia kunakotokana na kua katika sehemu yenye ukimya na utulivu wa
wakati wa Usiku.
Na baada ya Hajaa, ndio inafuatia hali ya usingizi ya Subatan ambao tulioanza nao katika
kuzungumzia neema ya Usingizi katika aya isemayo WajaAAalna nawmakum subatan
(Surat An Nabaa 78:9) kisha inafuatia hali ya usingizi wa Ruquud ambalo ni neno
linalotokana na neno Raqada ambalo ni lenye kumaanisha Kulala kwa Mda mrefu au
Kupumzika kwa mda mrefu, Kua Mchovu sana kiasi ya kua hakuna kinachotakikana
katika hali hio isipokua Kulala tu. Ambapo neno Raqada ndio lililotoa neno Marqad
ambalo maana yake hua ni Kitanda, Sehemu ya Kulalia, na pia humaanisha Kaburi.
Neno hili limetumika katika Surat Al Qahf katika kuelezea hali ya kulala ya watu ambao
wanajulikana kama As-hab Al Qahf ambao ni Maksalmina, Tamlikha, Martunas,
Baynunas, Saarnunas, Zunwanas, Kashfitatnunas na Mbwa wao ambae ni
mwenye kuitwa Qitmiir, ambapo Allah Subhanaha wa Ta’ala anatuelezea hali yao hio
ya Kulala ilivyokua kwa kusema:
689

ِ
ِّ ‫ات‬
‫ٱﻟﺸ َﻤ ِﺎل َوَﻛ ْﻠﺒُـ ُﻬ ْﻢ‬ َ ‫ﲔ َو َذ‬ ِ ‫ات ٱﻟﻴَ ِﻤ‬ ٌ ُ‫﴿ َوَْﲢ َﺴﺒُـ ُﻬ ْﻢ أَﻳْـ َﻘﺎﻇﺎً َوُﻫ ْﻢ ُرﻗ‬
َ َ‫ﻮد َوﻧـُ َﻘﻠّﺒُـ ُﻬ ْﻢ ذ‬
‫ﺖ ِﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ‬ ِ ِ ِ ‫ﻴﺪ ﻟَ ِﻮ ٱﻃﱠﻠَﻌﺖ ﻋﻠَﻴ ِﻬﻢ ﻟَﻮﻟﱠﻴ‬ ِ ‫ﻂ ِذراﻋﻴ ِﻪ ﺑِﭑﻟﻮ ِﺻ‬ ِ ‫ﺎﺑ‬
َ ‫ﺖ ﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ ﻓَﺮاراً َوﻟَ ُﻤﻠْﺌ‬َ َْ ْ َْ َ ْ َ ْ َ َ ٌ ‫ﺳ‬ َ
﴾ً‫ر ْﻋﺒﺎ‬
ُ
Watahsabuhum ayqadhan wahum ruqoodun wanuqallibuhum dhata alyameeni
wadhata alshshimali wakalbuhum basitun dhiraAAayhi bialwaseedi lawi
ittalaAAta AAalayhim lawallayta minhum firaran walamuli/ta minhum ruAAban
(Surat Qahf 18:18)
Tafsir: Na kama ungewaona basi ungedhani kua wako macho, huku wakiwa katika
Ruquudun. Na tuliwageuza kuliani mwao na kushotoni mwao na Mbwa wao akiwa
amenyoosha miguu yake kwenye Mlango wa kuingilia (Pangoni) Kama ungewaona
basi ungerudi nyuma na kuwakimbia kutokana kupigwa na mshangao mkubwa sana.

﴾ً‫ﲔ و ْٱزَد ُادواْ ﺗِﺴﻌﺎ‬ ِ ِ ٍ ِ َ َ‫﴿وﻟَﺒِﺜُﻮاْ ِﰱ َﻛﻬ ِﻔ ِﻬﻢ ﺛ‬


ْ َ َ ‫ﻼث ﻣﺌَﺔ ﺳﻨ‬ ْ ْ َ
Walabithoo fee kahfihim thalatha mi-atin sineena waizdadoo tisAAan (Surat Al Qahf
18:25)
Tafsir: ‘Na walikaa kwenye Pango lao kwa miaka mia tatu na uongeze (miaka) tisa’
Ambapo tunaona kua aya inasema kua Watu hawa walilala kwa miaka 309 huku macho
yao yakiwa wazi. Aya vile vile zinatuwekea wazi pia umuhimu wa kugeuka wakati wa
Kulala, kwani ingawa tumesema kua Misuli ya Mwili hua inapumzika kufanya kazi na
kuregea katika wakati wa kulala lakini kuna hisia ambazo hua zinafanya kazi kwa
asilimia ndogo sana, kama hisia ya Maumivu na kusikia, na ndio maana mtu unapolala
basi ukichoka upande mmoja hua unageuza mwili wako bila ya kujijua na kulalia upande
mwengine wa mwili wako, na hivyo hua unafanya si kwa amri yako bali ni kutokana na
amri ya Mola wako ambae ndie anaekugeuza upande mwengine kulingana na makadirio
yake aliyokukadiria kutokana na ukamilifu wa maumbile yako.
Hivyo ni baadhi ya vithibitisho vinavyothibitisha aina za usingizi, muhimu wake na
manufaa yake juu yetu kwa kulingana na mtizamo wa Qur’an na kisayansi, ambapo
tunapoangalia kwa upande wa Sunna za Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi
tunaona kua zimetajwa aina tatu za usingizi wa mchana pale aliposema: ‘Kulala asubuhi
mapema hua ni kuusaliti ujahilia, kulala mchana hua ni sahih na kulala jioni hua
ujinga’ (Imam Ibn Hajar Al Asqalani katika Fat-h Al Bar)
690

Aina hizo za Usingizi ni Ghaylula ambao ni usingizi wa baada ya Sala ya Alfajir ambao
ni makruh na haupendekezwi kwani husababishia kupungua kwa riziki kutokana na kua
huo na wakati wa kujishughulisha kwa matayarisho ya kutafuta riziki. Na kuna Usingizi
uitwao Qaylula ambao ni Usingizi aliokua akiutumia Rasul Allah Salallahu Alayhi Salam
kwa ajili ya kumuwezesha kuamka usiku kusali Salat Tahajjud.
Huu hua ni usingizi wa saa moja baada ya Salat Al Dhuhur hua si wa muda mrefu, kwani
humalizika kabla ya kuingia Salat Al Asr usingizi huu huzidisha umakini wa Mwili na
Ufaham wa mtu. Halafu kuna Faylula ambao ni usingizi wa baada ya Salat Al Asr mpaka
Maghrib ambao huifanya siku kua fupi na hivyo ni siku hio hua ni siku isiyokua na faida
kwa kutowezekana kuzalisha chochote ndani yake
Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anatubainishia umuhimu wa Usingizi kua tumejaaliwa
kua nao kwa sababu ya kua ni wenye kuipumzisha Miili ya viumbe ili iwe na nguvu na
uwezo zaid kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake hapa Ulimwenguni kwa manufaa
ya kiakhera kwa kusema na tukaujaalia Usiku kua ni Libas.

MAANA YA LIBAS KATIKA USIKU, KATIKA NDOA NA KATIKA


TAQWA


Amesema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qur’an kua:

﴾ً‫﴿و َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ﻧَـﻮَﻣ ُﻜﻢ ُﺳﺒَﺎﺎﺗً ۞ و َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ٱﻟﻠﱠْﻴﻞ ﻟِﺒَﺎﺳﺎ‬


َ َ ْ ْ َ
WajaAAalna nawmakum subatan WajaAAalna allayla libasan; (Surat An Nabaa
78:9-10)

Tafsir: Na tukajaalia Usingizi kua ni Pumziko, Na tukaujaalia Usiku kua ni Libas


(Vazi).

Ambapo tunapoangalia neno Libas basi tunaona kua ni neno lililotumika pia katika aya
nyingi ikiwemo katika aya zisemayo:

ِ ِ
ٌ َ‫ﺎس ﻟﱠ ُﻜ ْﻢ َوأَﻧﺘُ ْﻢ ﻟﺒ‬
﴾‫ﺎس ﱠﳍُ ﱠﻦ‬ ٌ َ‫﴿ﻫ ﱠﻦ ﻟﺒ‬
ُ
691

Hunna libasun lakum waantum libasun lahunna (Surat Al Baqara 2:187)

Tafsir: Wao (Wake zenu) ni Lîbas kwenu na nyie (Waume zao) ni Lîbas kwao.

Neno Lîbas kwa kiarabu lina maana ya Kuficha, Kufanya kitu kisionekane, Kukifanya
Kitu kua ni chenye kuwachanganya wengine kutokana na utofauti wa muoekano wake
wa asili, Stara, Hifadhi, Nguo au Vazi.

Na kama inavyojulikana kazi ya Vazi ni kuvaliwa ili Kuulinda na Kuuhifadhi mwili wa


Bani Adam na athari za nje kama vile Jua, Mvua, Joto, Baridi, n.k, kusitiri sehemu za siri
ambazo ni aibu kuzionesha, Kuupendezesha mwili, basi ndio hivyo hivyo ilivyo ndoa
kwa Mume na Mke

Na kama ilivyokua haifai kuvaa nguo inayokubana kwa sababu itakuwekea wazi siri zako
na pia iko siku itakuchanikia na kukuadhirisha kwa kukuweka uchi mbele za watu, ndio
hivyo ndivyo ilivyo Libasi ya Ndoa yaani lazima kuwe na kuheshimiana baina ya Mume
na Mke, kwani nguo haitakiwi iwe ni yenye kubana sana, kwani iko siku itakuvunjia
heshima mbele za watu, na haitakiwi iwe ni yenye kupwaya, kwani ukivaa nguo
inayopwaya basi utakua na kazi ya kila wakati kipandisha juu isiburure chini au isikuvuke
n,k basi ndio vile vile inavyotakiwa kua hali ya mahusiano ya Ndoa iwe katika hali ya
kati na kati, isiwe Mume na Mke wanaogopana sana na wala isiwe Mke na Mume wako
huru sana na hivyo kuvuka miaka ya sharia na hukmu za ndoa.

Na kama inavyositiri Libasi kwa Mwili, na kumridhisha mvaaji na upata utulivu wa Nafsi
yake kutokna na kua hana wasiwasi kwani amevaa na kupendeza na hayuko uchi mbele
za watu, basi ndivyo wanavyositiriana, wanavyoridhishana, wanavyopeana utulivu na
kulindana Mume na Mke kutokana na vishawishi na matamanio ya nje yaliyokatazwa,
na hivyo kuwapelekea kusaidiana si kutokana na athari za nje tu bali na katika kumcha
Mola wao pale wanapotimiza matamanio hayo katika njia inayoruhusika kisharia.

Ingawa Allah Subhanahu wa Ta’ala amewajaalia Bani Adam, Lîbas kua kama Stara na
pambo la Miili yao, lakini pia amewajaalia Lîbas ya Taqwa ambayo ni pambo la Nafsi na
hua ni Lîbas bora zaid kwani hua ni yenye kuupa Moyo na Nafsi stara na utulivu zaid
kama zinavyosema aya zinazokataza Tabarruj ambazo zimo katika Surat Al Araf, Surat
An Nur na Surat Al Ahzab.

Ambapo neno Tabarruj linatokana na neno Baraja ambalo humaanisha Kua na Hali ya
Juu, Kua na Hali Nzuri ya Mafanikio na pia humaanisha Kuonekana Vizuri kwa Juu.
Ambapo neno Baraja ndio lililotoa neno Burujun ambalo hua ni lenye kumaanisha Kasri
lililoenda juu, Mzunguko wa Nyota na pia humaanisha Nyota.
692

Hivyo neno Tabarruj hua linamaanisha hali ya Kuonesha, Kuweka wazi na Kubainisha
Vilivyo juu kwa Uzuri au Mafanikio, ama kwa Kiislam hua linamaanisha Kuonesha au
Kuweka wazi Mapambo ya Mwili au Sehemu za Maumbile ya Mwili zinazovutia,
ambapo ndani yake pia mnaingia pia Utembeaji wa Mwanamke katika hali ya
kutamanisha Wanaume uzuri wa Mapambo yake ya Kimaumbile na wa Kujipamba kwa
mapambo ya Kuvaa. Kama inavyosema aya ifuatayo pale Allah Subhanah wa Ta’ala
alipowaambia Wake wa Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam kua:

‫ﲔ‬ ِ ‫ُوﱃ َوأَﻗِ ْﻤ َﻦ ٱﻟ ﱠ‬


َ ‫ﺼﻠﻮاََة َوآﺗ‬ ٰ َ ‫ﺎﻫﻠِﻴﱠ ِﺔ ٱﻷ‬
ِ ‫ٱﳉ‬ ِ
َْ ‫﴿ َوﻗَـْﺮ َن ِﰱ ﺑـُﻴُﻮﺗ ُﻜ ﱠﻦ َوﻻَ ﺗَـﺒَـﱠﺮ ْﺟ َﻦ ﺗَـﺒَـﱡﺮ َج‬
ِ ‫ٱﻟﺮﺟﺲ أَﻫﻞ ٱﻟْﺒـﻴ‬ ِ ِ ‫ﻳﺪ ﱠ‬ ُ ‫ٱﻪﻠﻟَ َوَر ُﺳﻮﻟَﻪُ إِﱠﳕَﺎ ﻳُِﺮ‬ ِ ‫ٱﻟﱠﺰَﻛﻮا َة وأ‬
‫ﺖ‬ ْ َ َ ْ َ ْ ِّ ‫ﺐ َﻋﻨ ُﻜ ُـﻢ‬ َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻟﻴُ ْﺬﻫ‬ ‫َﻃ ْﻌ َﻦ ﱠ‬ َ
﴾ً‫وﻳُﻄَ ِّﻬﺮُﻛﻢ ﺗَﻄْ ِﻬﻴ ـﺮا‬
َْ َ
Waqarna fee buyootikunna wala tabarrajna tabarruja aljahiliyyati al-oola
waaqimna alssalata waateena alzzakata waatiAAna Allaha warasoolahu innama
yureedu Allahu liyudhhiba AAankumu alrrijsa ahla albayti wayutahhirakum tat-
heeran (Surat Al Ahzab 33:33)

Tafsir: Na kaeni katika Majumba yenu na wala Msijioneshe kama Muonesho wa


katika kipindi cha Ujahiliya cha awali, na simamishen Sala, na toeni Zakkah na Mtiini
Allah na Mtume wake, kwani kwa hakika anataka Allah kukuondoleeni dhambi, Enyi
watu wa Nyumbani (kwa Mushammad Salallahu Alayhi wa Salam) na akutoharisheni
kwa tohara kamilifu.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anabainisha aina tofauti muhimu za Libas na hapo hapo
anakataza Tabarruj kwa kusema:

ِ ِ‫﴿ﻳـﺒ ِﲎ آدم ﻗَ ْﺪ أَﻧﺰﻟْﻨﺎ ﻋﻠَﻴ ُﻜﻢ ﻟِﺒﺎﺳﺎ ﻳـﻮا ِرى ﺳﻮءﺗِ ُﻜﻢ وِرﻳﺸﺎ وﻟ‬
َ ‫ﺎس ٱﻟﺘﱠـ ْﻘ َﻮ ٰى ٰذﻟ‬
‫ﻚ‬ ‫ﺒ‬
ُ َ ً َ ْ َ ْ َ َ ُ ً َ ْ ْ َ َ َ َ َ ََ
َ
﴾‫ٱﻪﻠﻟِ ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻬ ْﻢ ﻳَ ﱠﺬ ﱠﻛُﺮو َن‬
‫ـﺖ ﱠ‬ِ ‫ﻚ ِﻣﻦ آﻳ‬ِ
َ ْ َ ‫َﺧْﻴـٌﺮ ٰذﻟ‬
Ya banee adama qad anzalna AAalaykum libasan yuwaree saw-atikum wareeshan
walibasu alttaqwa dhalika khayrun dhalika min ayati Allahi laAAallahum
yadhdhakkaroona (Surat Al A’raf 7:26)
693

Tafsir: Enyi Bani Adam! Tumekushushieni Lîbas (Mavazi) juu yenu ili mjisitiri
sehemu zenu za siri na pia kua kama Rish (Mapambo); na Lîbas (Mavazi) ya Taqwa,
ni bora zaid. Hizo ni miongoni mwa aya (Dalili, alama, ushahidi, nk) za Allah ili mpate
kukumbuka.

Hivyo ingawa hii ni miongoni mwa aya zinazozungumzia Neema za Allah Subhana wa
Ta’ala ya kutujaalia Libas yaani Mavazi kua ni sehemu ya mapambo na stara kwa miili
yetu lakini pia aya hii inatuainishia umuhimu wa neema ya Ufaham na akili ambayo Ibn
Adam tumepewa na Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo kua ni wenye kuweza kushona
na kufuma mavazi yetu kwa kutumia neema ya mimea mbali mbali inayoota ardhini.

Ambapo aya pia imetumia neno Sawah ambao hua linamaanisha sehemu za katikati za
mwili yaani sehemu za siri au Awrah yaani Uchi. Ambapo neno Awrah hua linamaanisha
Sehemu ya Siri, Sehemu iliyofichikana, Sehemu ambayo ikionekana basi hua
inamsababishia Mtu kua ni mwenye Kujisikia vibaya kwa kuona haya na aibu.

Imam Shams Ad Din Muhammad Ibn Ahmad Khatib Al Shibrini Al Shafii basi anasema
kua: ‘Neno Awrah hua linamaanisha sehemu ya Mwili ambayo imekatazwa
kuoneshwa kwa Mwanamme au kwa Mwanamke, na hua inamaanisha sehemu ya
Mwili ambayo ni wajibu kuihifadhi’ (Al Mughni Al Muhtaj)

Ama kwa upande wa Mwanamme sehemu hizo hua ni baina ya juu ya Kitovu hadi chini
ya Magoti. Na kwa upande wa Mwanamke basi hua ni mwili mzima isipokua Uso,
Mikono na Miguu. Na tunapozugumzia awrah kwa upande wa Mwanamke basi kuna hali
mbili za kujistiri awrah ambapo hali ya kwanza hua ni Ndani ya Sala na ya pili hua ni
Nje ya Sala.

Na tunapozungumzia ndani ya Sala basi hua ni kutokana na uthibitisho unaowajumuisha


Wanawake na Wanaume pamoja kama ilivyosema aya ifuatayo:

ۤ
‫آد َم ُﺧ ُﺬواْ ِزﻳﻨَـﺘَ ُﻜ ْﻢ ِﻋﻨ َﺪ ُﻛ ِّﻞ َﻣ ْﺴ ِﺠ ٍﺪ وُﻛﻠُﻮاْ َوٱ ْﺷَﺮﺑُﻮاْ َوﻻَ ﺗُ ْﺴ ِﺮﻓُـﻮاْ إِﻧﱠﻪُ ﻻَ ُِﳛ ﱡ‬
‫ﺐ‬ ۤ
َ ‫﴿ َ�ﺑَِﲏ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ
َ ‫ٱﻟْ ُﻤ ْﺴ ِﺮﻓ‬
Ya banee adama khudhoo zeenatakum AAinda kulli masjidin wakuloo waishraboo
wala tusrifoo innahu la yuhibbu almusrifeena (Surat Al Araf 7:31)
694

Tafsir: Enyi Ibn Adam, Chukueni Mapambano yenu katika kila Sala na kuleni na
mnywe lakini msivuke mipaka, kwani kwa Hakika Yeye Allah hapendi wanaofanya
Israfu.

Hivyo katika Sala Mwanamke anatakiwa ajistiri Mwili mzima isipokua Uso, Viganja vya
Mikono na Miguu bila ya kujali kama anasali nje au ndani, peke yake au na Wanawake
wenzake, ambapo kwa baadhi ya Wanazuoni basi wanasema kua mpaka miguu pia
isionekane na pia kwa mtizamo wa baadhi ya Wanazuoni basi ni kua tunapozugumzia
Uso basi ndani yake hua haijumuishiki sehemu ya chini ya Kidevu kwa sababu sio
sehemu ya uso, hivyo kama inawezekana basi vizuri sehemu hio nayo kufunikwa.

Ama kuhusiana kuvaa Libas na stara nje ya Sala basi hua ni kama ilivyoelezewa ndani
ya aya zifuatazo za Tabbarruj:

‫ﲔ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ﱠﻦ ِﻣﻦ‬ ِ ِ‫ﺂء ٱﻟْﻤ ْﺆِﻣﻨ‬ ِ ِ ِ‫﴿ ٰ�َﻳـﱡﻬﺎ ٱﻟﻨِﱠﱮ ﻗُﻞِ ﻷَزو ِاﺟﻚ وﺑـﻨﺎﺗ‬
َ ‫ﲔ ﻳُ ْﺪﻧ‬َ ُ ‫ﻚ َوﻧ َﺴ‬ َ ََ َ َ َ ْ ‫َ ﱡ‬
﴾ً‫ٱﻪﻠﻟ َﻏ ُﻔﻮراً ﱠرِﺣﻴﻤﺎ‬ ِ
ُ‫ﱏ أَن ﻳـُ ْﻌَﺮﻓْ َﻦ ﻓَﻼَ ﻳـُ ْﺆ َذﻳْ َﻦ َوَﻛﺎ َن ﱠ‬ َ ‫َﺟﻼَﺑِﻴﺒِ ِﻬ ﱠﻦ ٰذﻟ‬
َٰ ‫ﻚ أ َْد‬
Ya ayyuha alnnabiyyu qul li-azwajika wabanatika wanisa-i almu/mineena
yudneena AAalayhinna min jalabeebihinna dhalika adna an yuAArafna fala
yu/dhayna wakana Allahu ghafooran raheeman (Surat Al Ahzab 33:59)

Tafsir: Ewe Nabii, waambie Wake zako, na Watoto wako, na Wanawake Walioamini
kua washushie nguo zao za nje, kufanya hivyo kutawatofautisha watajulikana (kwa
kuheshimika) na hawatobughudhiwa na hakua Allah isipokua ni mwingi wa Rehma
na Usamehevu.

Aya imezunguzia kuhusiana na vazi la Jilbab ambalo ni neno linalotokana na neno


Jalaba ambalo humaanisha Kukusanya, au Kuchukua kitu kutoka katika sehemu moja
kukipeleka katika sehemu nyengine, hivyo kwa upande mmoja basi tunaweza kusema
kua Jilbab hua ni vazi ambalo wanavaa wanawake kwa kujifunika na kuzikutanisha
pande tofauti za vazi hilo katika sehemu moja.

Na kwa upande mwengine basi Jilbab hua ni Buibui ambalo hua linaufunika mwili wote
wa mwanamke kuanzia mabegani mpaka miguuni bila ya kumbana na hua linajumuisha
na Hijab au Mtandio juu yake ambao hua ni wenye kufunika Kichwa, Shingo Mabega na
Kifua.
695

Ambapo aya hii inazungumzia hali ilipokua hapo kabla katika zama za Ujahiliyya kulikua
na dasturi ya Wanawake kutoka katika wakati wa jioni kwa ajili ya kuenda kujisaidia
kwani ilikua hakuna vyoo ndani ya nyumba zao. Hivyo ilikua ni kawaida ya Wanaume
nao walikua wakikaa vibarazani na kuanza kuwafanyia uhuni na kuwabughudhi kwa
macho na maneno ya matamanio Wanawake hao, hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala
aashusha aya hii ili Wanawake wa Kiislam wajihifadhi na hivyo wakitoka watakua
hawaonekani na hawajulikani na kuheshimika zaidi kutokana na macho ya Wanaue hao.

Na pia Libas na Stara nje ya Sala katika aya ifuatayo:

ِ ِ ‫ﻀﻦ ِﻣﻦ أَﺑ‬ ِ ِ ِ


‫ﻳﻦ ِزﻳﻨَـﺘَـ ُﻬ ﱠﻦ‬
َ ‫وﺟ ُﻬ ﱠﻦ َوﻻَ ﻳـُْﺒﺪ‬ َ ‫ﺼﺎ ِرﻫ ﱠﻦ َوَْﳛ َﻔﻈْ َﻦ ﻓُـُﺮ‬ َ ْ ْ َْ ‫ﻀ‬ ُ ‫﴿ َوﻗُﻞ ﻟّْﻠ ُﻤ ْﺆﻣﻨَﺎت ﻳَـ ْﻐ‬
‫ﻳﻦ ِزﻳﻨَـﺘَـ ُﻬ ﱠﻦ إِﻻﱠ‬ ِ ِِ ِ ِ ْ ‫إِﻻﱠ ﻣﺎ ﻇَﻬﺮ ِﻣْﻨـﻬﺎ وﻟْﻴ‬
َ ‫ﻀ ِﺮﺑْ َﻦ ﲞُ ُﻤ ِﺮﻫ ﱠﻦ َﻋﻠَ ٰﻰ ُﺟﻴُﻮﻬﺑ ﱠﻦ َوﻻَ ﻳـُْﺒﺪ‬ َ َ َ ََ َ
ِ ‫ﻟِﺒـﻌﻮﻟَﺘِ ِﻬ ﱠﻦ أَو آﺂﺑﺋِ ِﻬ ﱠﻦ أَو آﺂﺑ ِء ﺑـﻌﻮﻟَﺘِ ِﻬ ﱠﻦ أَو أَﺑـﻨﺂﺋِ ِﻬ ﱠﻦ أَو أَﺑـﻨ‬
‫ﺂء ﺑـُﻌُﻮﻟَﺘِ ِﻬ ﱠﻦ أ َْو إِ ْﺧ َﻮا�ِِ ﱠﻦ‬ َْ ْ َْ ْ ُُ َ ْ َ ْ ُُ
ِ ِ ِ ِِ ‫أَو ﺑ ِ ۤﲏ إِﺧﻮا�ِِ ﱠﻦ أَو ﺑ ِﲎ أ‬
َ ‫ﺖ أَْﳝَﺎﻧـُ ُﻬ ﱠﻦ أَ ِو ٱﻟﺘﱠﺎﺑِﻌ‬
‫ﲔ‬ ْ ‫َﺧ َﻮاﻬﺗ ﱠﻦ أَْو ﻧ َﺴﺂﺋ ِﻬ ﱠﻦ أ َْو َﻣﺎ َﻣﻠَ َﻜ‬َ َ ْ َْ َ ْ
ِ ‫ات ٱﻟﻨِﺴ‬ ِ ِ‫ِ ﱠ‬ ِ ِ ‫َﻏ ِْﲑ أُوِﱃ ٱ ِﻹرﺑ ِﺔ ِﻣﻦ‬
َ‫ﺂء َوﻻ‬ َ ّ ‫ﻳﻦ َﱂْ ﻳَﻈْ َﻬُﺮواْ َﻋﻠَ ٰﻰ َﻋ ْﻮَر‬ َ ‫ٱﻟﺮ َﺟﺎل أَ ِو ٱﻟﻄّْﻔ ِﻞ ٱﻟﺬ‬ ّ َ َْ ْ
‫ﲨﻴﻌﺎً أَﻳـﱡ َﻬﺎ ٱﻟْ ُﻤ ْﺆِﻣﻨُﻮ َن‬ ‫ﲔ ِﻣﻦ ِزﻳﻨَﺘِ ِﻬ ﱠﻦ َوﺗُﻮﺑـُ ۤﻮاْ إِ َﱃ ﱠ‬
َِ ِ‫ٱﻪﻠﻟ‬ ِ ِ ِ
َ ‫ﻀ ِﺮﺑْ َﻦ ِﺄﺑ َْر ُﺟﻠ ِﻬ ﱠﻦ ﻟﻴُـ ْﻌﻠَ َﻢ َﻣﺎ ُﳜْﻔ‬
ْ َ‫ﻳ‬
﴾‫ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜﻢ ﺗُـ ْﻔﻠِ ُﺤﻮ َن‬
ْ
Waqul lilmu/minati yaghdudna min absarihinna wayahfadhna furoojahunna wala
yubdeena zeenatahunna illa ma dhahara minha walyadribna bikhumurihinna
AAala juyoobihinna wala yubdeena zeenatahunna illa libuAAoolatihinna aw aba-
ihinna aw aba-i buAAoolatihinna aw abna-ihinna aw abna-i buAAoolatihinna aw
ikhwanihinna aw banee ikhwanihinna aw banee akhawatihinna aw nisa-ihinna aw
ma malakat aymanuhunna awi alttabiAAeena ghayri olee al-irbati mina alrrijali
awi alttifli alladheena lam yadhharoo AAala AAawrati alnnisa-i wala yadhribna bi-
arjulihinna liyuAAlama ma yukhfeena min zeenatihinna watooboo ila Allahi
jameeAAan ayyuha almu/minoona laAAallakum tuflihoona (Surat An Nur 24:31)

Tafsir: Na waambie Wanawake walioamini wainamishe mitizamo (ya macho) yao, na


wazihifadhi sehem zao za siri, na wasioneshe mapambo yao isipokua yale yaliuyokua
ni dhahiri, na washushe mitandio yao kote kifuani mwao, na wasioneshe mapambo
696

yao ia kwa Waume zao, au Mababa zao au Mababa wa Waume zao au kwa Watoto
wao, au kwa Watoto wa Waume zao, au kwa Ndugu zao wa Kiume au Watoto wa ndugu
zao, au Wanawake wao (waliokua Waislam wenzao) au Wanaomilikiwa na mikono
yao ya kulia (Watumwa wao) au Wasaidizi wa Ndani wazee wasiokua na Hamu, au
watoto wasiojua kuhusiana na Uchi wa Mwanamke na wala wasipige pige miguu yao
kuonesha waliyoficha katika mapambo yao. Na tubuni kwa Allah nyote kwa pamoja
enyi mlioamini ilimpate kua mliofuzu.

Hivyo hii ni aya ambayo inaainisha aina ya watu ambao Mwanamke anaruhusika kukaa
mbele yao bila ya kua na khofu ya kuficha mapambo ya maumbile ya mwili wake na pia
mapambo ya kujipamba kama herini, mkufu bangili, kikuba n.k, na hawa ni wale watu
ambao hawezi kuoana nao na pia aya ikazungumzia kuhusiana na Wanawake wao, yaani
Wanawake wenzake wa Kiislam tu. Ambapo kwa upande wa Imam Ibn Jarir At Tabari
basi yeye ansema kua: ‘Aya hii inamaanisha kua Mwanamke anatakiwa ajistiri
anapokua mbele za watu, na anaruhusika kuachia wazi Uso na Mikono yake, hivyo
anaruhusika pia kuonesha Mikono na Uso wake na mapambo ambayo yanaonekana
katika sehemu hizo kambayo hua ni zinaat dhahira. ’ ambapo huu pia ni mtizamo wa
Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu na Maimamu kama Ata Ibn Rabah, Said Ibn
Jubayr, Ad Dahak ana Al Awzai, ambapo kwa Wanazuoni wa baadae basi wao wanasema
kua kama Mwanamke akijipamba kwenye sehemu hizo basi itambidi azistiri pia sehemu
hizo.

Na kwa upande wa Mujadid Ad Din Imam Fakhr al-Din al-Razi basi yeye
nasema katka kuitafsiri aya hii kua: ‘Ama kuhusiana na Kauli ya Allah
Subhanah wa Ta’ala isemayo aw nisa-ihinna yaani Wanawake zao basi kuna
mitizamo miwili juu yake ambapo wa kwanza ni ule usemao hawa hua ni wale
Wanawake ambao wako pamoja nao kiimani katika dini moja yaani Waislam.
Ambapo anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kuhusiana nao kua:
‘Hairuhusiwi kwa Mwanamke wa Kiislam kutojistiri anapokua mbele ya
Wanawake ambao si Waislam, na hivyo hua anaruhusiwa kuonesha mbele yao kile
ambacho inaruhusika kwa Mwanamme ambae anaruhusika kumuoa.’’

‘Ambapo Amir ul Muuminin Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu


alimuandikia Barua Abu Ubaidah Ibn Jarrah Radhi Allahu Anhu
isemayo kua: ‘Nimesikia kua Wanawake wa Kiislam wanaingia katika
Mahammam ya Kukogea pamoja na Wanawake wa Ahl al Kitab, hivyo
Wazuie kuhusiana na kufanya hivyo kwani watazoea’

Na mtizamo wa pili ni ule usemao kua: ‘Inaruhusika kwa Mwanamke


kutojistiri mbele ya Wanawake wote na huu ni mtizamo ambao una
msingi wa Istihbab yaani mtizamo wa juu.’
697

Ambapo kwa upande wa Shaykh Ul Islami Imam Zayn Ad Din Abu Yahya
Ahmad Ibn Muhamamd Zakariyyah Al Ansari basi yeye anasema kua: ‘Awra
ya Mwanamke wa Kiislam mbele ya Mwanamke asiekua Muislam hua ni
ile inayoruhusika kuonekana wakati akiwa anafanya kazi kwa mfano
Uso wake, Kichwa, Mikono mpaka kwenye visugudi na miguu mpaka
kwenye magoti.’ (Asna al-Matalib, 14/280)

Na kwa upande wa Al Faqih Al Muhaqiq Imam Shihab Ad Din Abu Abbas


Ahmad Ibn Muhammad Ibn Ali Ibn Hajar Al Haytami basi yeye ansema kua:
‘Mtizamo unaokubalika kuhusiana na jambo hili ni kua hairuhusiki kwa
Mwanamke asiekua Muislam awe dhimmi au Kafir harbi kumuangalia
Mwanamke wa Kiislam isipokua kwa kile ambacho kitaweza kuonekana
wakati Mwanamke wa Kiislam atakapokua akifanya kazi’ (Tuhfah al-
Muhtaj,7/200)

Na hii ni kutokana na hadith ya Anas Ibn Malik Radhi Allah Anhu ambae alisema:
‘Katika vita vya Uhud watu waliondoka ma kumuacha Rasul Allah Salallahu Alayhi
wa Salam huku Abu Talha Radhi Allahu Anhu akiwa mbele ya Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam, ambae ni mahiri sana kwa kutumia upinde, na alivunja pinde
mbile au tatu katia siku hio, ambapo ilikua mtu akipita mbele huku akiwa mkoba
wa mipinde basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam husema: ‘Mwachie Abu
Talha’ na kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hunyanyua kichwa chake
kuwaangalia maaduai, ambapo Abu Talha Radhi Allahu Anhu husema: ‘Wacha
Baba yangu ana Mama yangu watolewe Kafara kwa ajili yako! Usinyanye kichwa
chako usije ukapigwa upinde bora nipigwe shingo yangu kuliko kupigwa wewe.’
Nami nikaona Aisha bint Abu Bakar Radhi Allahu Anha na Ummu Salama Radhi
Allahu Anha wakiwa wamekunja kanzu zao hivyo ikawa nnaona bangili zao za
miguuni huku wakiwa wanabeba vibuyu vya maji migongoni mwao na kuyamwaga
kwenye midomo ya Majeruhi, walikua wakirudi kuvijaza na kuwamwagia tena
midomoni mwao majeruhi, Upanga ulianguka kutoka mikononi mwa Abu Talha
mara mbili tatu katika siku hii’(Sahih Bukhari)

Ambapo kwa upande wa Amin Al Fatawa Allamah Imam Muhammad Ibn


Amin Ibn Abidin Al Shami Al Hanafi Al Maturidi basi amesema kua:
‘Hairuhusiki kwa Mwanamke wa Kiislam, kutojistiri mbele ya
Mwanamke wa Kiyahudi au Mkristo au asieamini Mungu, isipokua kama
mwanamke huyo atakua ni Mtumwa wake, na hairuhusiki kwa
Mwanamke Fasiqa kuona Mwili wa Mwanamke wa Kiislam kwa sababu
anaweza akayaelezea Maumbile ya Mwanamke huyo kwa Wanaume
hivyo Mwanamke wa Kiislam hatakiwi kuvua nguo zake za nje kama
buibui au hijab mbele yake’
698

Hivyo basi Libas kwa Mwanamke wa Kiislam kujistiri mbele ya mwanamke


asiekua Muislam ni muhimu kutokana na kuwepo kwa uwezekano wa
kuelezewa Maumbile ya mwili wake kwa Wanaume wengine, na hivyo
kuepuka mitihani myengine ya matamanio ya nafsi isiyokua isiyotakikana,
kwani kujiepusha na sababu zinazoelekaea kutokea kwa mitihani hio pia hua
ni sawa na kuvaa Libas ya Taqwa.

Ambapo tunapozungumzia Libas At Taqwa basi hua tunazungumza hali


ambayo ni ya Kujistiri na Kujihifadhi Kiroho na Kinafsi na kuonesha
Shukrani kwa Allah Subhanah wa Taala na hivyo kua ni mwenye Kutii
maamrisho yake na kuachana na Makatazo yake hii ni kutokana na kujua
wingi wa Neema za Remha zake juu yetu, kama alivyosema katika Qur’an:

﴾‫ﻮر ﱠرِﺣﻴﻢ‬ ‫ﻮﻫﺂ إِ ﱠن ﱠ‬ ِ‫﴿وإِن ﺗَـﻌ ﱡﺪواْ ﻧِﻌﻤﺔَ ﱠ‬


ٌ ٌ ‫ٱﻪﻠﻟَ ﻟَﻐَ ُﻔ‬ َ‫ﺼ‬ ُ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻻَ ُْﲢ‬ َْ ُ َ
Wa-in taAAuddoo niAAmata Allahi la tuhsooha inna Allaha laghafoorun raheemun
(Surat An Nahl 16:18)

Tafsir: Na kama mtazihesabu Neema za Allah (Juu yenu) bsi hamtoweza kuzihesabu
kwaini kwa Hakika Allah ni mwingi wa Kusamehe na ni mwingi wa Rehma.

Ambapo alisema Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anhu kua: ‘Enyi watu
Muogopeni Allah mnapokua faragha kwani nimemsikia Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam akisema kua: ‘Naapa kwa yule ambae Mikono yake
imeushikilia Uhai wangu kua, hakuna hata mtu mmoja atakaefanya jambo la siri
isipokua Allah Subhanah wa Ta’ala atamvalisha nguo itakayomuonesha kwa kila
mtu, kama ikiwa jambo jema basi ni jema na ikiwa baya basi ni baya.’’

Na mfano mwengine wa Libasi ya Taqwa ni ule usemao: ‘Siku moja Rasul


Allah Salallahu Alayhi wa Salam Aliwauliza Mashaba zake: ‘Hivi Jee yuko miongoni
mwenu ambae anaweza akawa kama Abu DamDam?’

‘Masahaba wakauliza: ‘Abu Damdam ndio nani?’. Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
Salam akaijibu Abu Damdam ni mmoja kati ya watu wa kabila fulani ambae alikua
akiishi kabla ya kipindi chenu. Na alikua akisema: ‘Hakika mimi nimemsamehe
kila mtu ambae amenitukana na kunisengenya’’ (Imam Abu Daud)

Hivyo kama ilivyokua namna Nguo zinavyo tustiri na kutulinda Miili yetu basi ndio
hivyo hivyo inavyotupelekea Libas ya Taqwa kua ni wenye kujipendezesha kwa kufanya
mema na kujistiri kutokana na kufanya maovu, na hivyo kukukaribisha kua karibu na
Muumba ambae ni AllAh Subhanah wa Ta’ala. Ambapo amesema Abd Rahman Ibn Zaid
kuhusiana na Libas ya Taqwa kua: ‘Wakati mtu anapokua na Libas ya Taqwa basi
699

Allah Subhanah wa Ta’ala humfunikia makosa yake na hivyo hii ndio hua Libas ya
Taqwa’

Baada ya kuangalia mifano ya Libasi katika Mwili na Taqwa na tuangalie kwa upande
wa Usiku kua ni Libas kama isemavyo aya:

﴾ً‫﴿و َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ٱﻟﻠﱠْﻴﻞ ﻟِﺒَﺎﺳﺎ‬


َ َ
WajaAAalna allayla libasan; (Surat An Nabaa 78:9)

Tafsir: Na tukaujaalia Usiku kua ni Libas

Na tunaona kua aya inamaanisha kua Usiku mbali ya kua umejaaliwa kua ni Vazi na
Pambo la Dunia ambalo linawatofautishia Viumbe wanaoishi Ulimwenguni ili maumbile
yao yaweze kujua kuhusiana na mda wanaoishi ndani yake na mabadiliko ya nyakati na
mambo yao mbali mbali yanayotokea katika maisha yao, lakini pia Usiku umekua ni
Libasi pia kwa kumaanisha kua ni sehemu ya Kuituliza na Kuipumzisha Miili ya viumbe
wanaoishi Ulimwenguni na Kupata Stara na Hifadhi ya Miili yao na Ufaham wao ndani
ya Makazi yao.

Kwani unapoingia Usiku, Melatonin zinazalishwa na mtu unahisi usingizi na kuanza


kulala basi mara tu unapoingia kwenye usingizi Mwili wako wote hua ni wenye
kupunguza kasi ya ufanyaji kazi wa viungo vyake na kuvipumzisha, kwa mfano
unapolala basi Ufaham wako hufuta kila kitu ambacho hakina maana wala umuhimu
ndani yake, na kubakisha yale yenye maana na umuhimu tu ndani yake ambayo nayo
huyahifadhi kwa ajili ya kuja kuyakumbuka baadae, na ndio maana wakati muhimu wa
kuhifadhi kitu akilini hususan kwa wanafunzi wafanyao Mitihani basi hua si kabla ya
kulala bali hua baada ya kuamka mapema kabla ya Alfajir.

Unapolala pia Misuli husitisha ufanyaji kazi wake na kupumzika, Ubongo huongeza
uzalishwaji wa Kemikali ndani ya mwili ikiwemo zile zenye asili ya Protein za Cytokines
ambazo ni zenye kuimarisha Libas ya ndani ya mwili wako kwa kusimamia Ulinzi wa
kupigana na maradhi mbali mbali na uponeshaji wa ndani na nje ya mwili wako, kwani
bila ya kuzalishwa kwake basi kinga ya mwili wako hua dhaifu na katika kipindi hiki
ambacho umelala ndio pia mwili wako unakua kimaumbile kwani ndani ya mwili wako
mnazalishwa kemikali za kuukuza mwili kimaumbile kutokana na Pituitary Gland, na
hapo hapo huachiwa Kemikali za kuzuia hisia za kutaka kujisaidia na hivyo kukupelekea
kutotaka kuenda chooni mara kwa mara, kwa ajili ya kujisaidia wakati wa Usiku. n.k
700

Ukweli ni kua kimaumbile Usingizi una faida nyingi sana na ndio maana ukawa
unahesabika kua ni miongoni mwa haki za mwili wa Ibd Adam kama alivyosema Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam kumwambia Abd Allah Ibn Amr Radhi Allahu Anhu
ambae alikua anapenda kusali usiku kucha kua: ‘Sali na pia Lala, kwani mwili wako
una haki yake juu yako’ (Sahih Bukhari) na akasema tena kua: ‘Yeyote yule atakaehisi
usingizi wakati anasali, basi na akalale mpaka umtoke usingizi wake, kwani kusali
huku akiwa na usingizi mtu hua hajui kama anaomba msamaha au anaiombea
mabaya Nafsi yake’(Sahih Bukhari)

Hivyo Usingizi ni Silaha yako ya Kimaumbile kwa ajili ya Manufaa ya Mwili wako na
Ufaham wako, na inakubidi kuitumia ipasavyo. Kwani usipoituima ipasavyo basi hua
umeuvunjia haki yake Mwili wako na Ufaham wao, na hivyo hua ni sawa Upanga
usiokua na Makali, yaani hua ni mwenye kukosa Afya na Umakini wa Mwili wako
kutokana na kuchoka na kutokua na mapumziko ya kutosha ya kiufaham na kimwili.

Na tunapozungumzia kuhusiana na kuutumia ipasavyo Usingizi wako kwa ajili ya


Manufaa yako basi hua ni kama alivyosema Mujaddid Ad Din Hujjat Ul Islami Imam
Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammahd Al Ghazali ambae amesema:
‘Faham kua Usiku na Mchana unajumuisha masaa 24: Hivyo usilale zaidi ya masaa
manane, kwani hayo hua yanatosheleza kwa ajili yako. Na hii ni kwa mfano kama
ulikua umeandikiwa uishi miaka 60 basi utakua umetumia miaka 20 ambayo ni
robo tatu ya uhai wako.’

Hivyo ukilala zaidi ya masaa hayo bila ya kua na kisingizio basi utakua ni mwenye
kuzifanyia Israfu Rehma za Allah Subhanah wa Ta’ala badala ya kua ni mwenye
kumshukuru kama zinavyothibitisha aya kuhusiana na Rehma za Usiku na Mchana kua:

‫ﻀﻠِ ِﻪ َوﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜ ْﻢ‬ ِ


ْ َ‫ﱠﻬ َﺎر ﻟِﺘَ ْﺴ ُﻜﻨُﻮاْ ﻓِ ِﻴﻪ َوﻟﺘَﺒﺘَـﻐُﻮاْ ِﻣﻦ ﻓ‬ ِِ ِ
َ ‫﴿ َوﻣﻦ ﱠر ْﲪَﺘﻪ َﺟ َﻌ َﻞ ﻟَ ُﻜ ُﻢ ٱﻟْﻠﱠْﻴ َﻞ َوٱﻟﻨـ‬
﴾‫ﺗَ ْﺸ ُﻜﺮو َن‬
ُ
Wamin rahmatihi jaAAala lakumu allayla waalnnahara litaskunoo feehi
walitabtaghoo min fadhlihi walaAAallakum tashkuroona (Surat Al Qasas 28:)

Tafsir: Na katika Rehma zake ni kukujaalieni Usiku na Mchana ili mpate


utulivu ndani yake, na kujitafutia fadhila zake na ili muwe ni wenye
Kushukuru.
701

Hio ni kuhusiana na umuhimu wa neema ya Usingizi na Usiku kwa Viumbe ambayo


tumejaaliwa na Muumba kama ilivyosema mwenyewe ndani ya Qur’an, na hivyo
kututhibitishia kua yuko Muumba wa Kila Kitu ambae ni Allah Subhanah wa Ta’ala,
hivyo tumalizie kuhusiana na Mchana kama ilivyolezewa na Aya ya 11 ya Surat An
Nabaa ambayo inasema:

﴾ً‫ﱠﻬﺎر َﻣ َﻌﺎﺷﺎ‬ ﴿
َ َ ‫َو َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ٱﻟﻨـ‬
WajaAAalna alnnahara maAAashan; (Surat An Nabaa 78:11)

Tafsir: Na Tukajaalia Mchana kua ni wa Maisha (kutafutia)

Kama tulivyoona kua aya mbili zilizofuata kabla ya hii zilikua zinazungumzia Usingizi
na Usiku zimetumia maneno Subata na Libasa kumaanisha kua Nyakati hizo ni maalum
kwa ajili ya Stara, Hifadhi, Utulivu na Mapumziko, ambapo aya hii inazungumzia
Mchana imetumia neno MaaAshan.

Neno MaaAshan linatokana na neno Aasha ambalo hua ni lenye kumaanisha Kuishi,
Kuishi maisha kwa kutumaia njia fulani, Kutumia mda wa maisha kwa kupitia njia au
mfumo fulani, ambapo neno MaaAshan hua linamaanisha Maisha, Kuhangaikia
mahitaji ya Maisha au wakati wa kutafutia riziki.

Ama kwa upande wa ImamAbu Abd Allah Muhamad Sahl Al Tustari basi yeye anasema
kuhusiana na MaaAshan kua: ‘Hii inamanisha kua ni Nuru ya Nyoyo kupitia katika
Kumkumbuka kwake Allah Subhanah wa Ta’ala ambayo ndio mahitaji ya Roho na
Nafsi na Akili, Kama ilivyokua kwa mahitaji ya Malaika kwani wao Maisha yao ni
katika Dhikr kiasi ya kua kama wakizuiwa kufanya Dhikr basi wataangamia, lakini
tunapozungumzia aina nyengine ya maisha basi hua ni kama wanavyoishi watu
wengine wa kawaida kama kula kunywa, kujistiri n,k na hii ni kulingana na
maumbile ya Viumbe.’

Kwani Amr Ibn Al Qays alikua akisema kila inapoingia Asubuhi kua: ‘Ya Rabbi!
Hakika watu wameshatawanyika kwa ajili ya kujitafutia mahitaji yao, lakini mimi
hitajio langu ni Moja tu: Ambalo ni kua Nataka Unisamehe Dhambi zangu.’
Hivyo MaaAshan hua ndani yake pia mnajumuishika kila kile kilichohalalishwa na
kilichoharamishwa, kilichohalalishwa hua ni kile ambacho Allah Subhnaah wa Ta’ala
ameturuzuku na kisha akaturuhusu kukitumia kama alivyosema katika Qur’an:
702

‫ٱﻟﺮْز َق ﻟِ َﻤﻦ ﻳَ َﺸﺂءُ ِﻣ ْﻦ ِﻋﺒَ ِﺎدﻩِ َوﻳَـ ْﻘ ِﺪ ُر ﻟَﻪُ َوَﻣﺂ أَﻧ َﻔ ْﻘﺘُ ْﻢ ِّﻣﻦ َﺷ ْﻲ ٍء‬
ِ ‫ﻂ‬ ِ ﴿
ّ ُ ‫ﻗُ ْﻞ إ ﱠن َرِّﰉ ﻳَـْﺒ ُﺴ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ
َ ‫ﻓَـ ُﻬ َﻮ ُﳜْﻠ ُﻔﻪُ َوُﻫ َﻮ َﺧْﻴـُﺮ ٱﻟﱠﺮا ِزﻗ‬
Qul inna rabbee yabsutu alrrizqa liman yashao min AAibadihi wayaqdiru lahu
wama anfaqtum min shay-in fahuwa yukhlifuhu wahuwa khayru alrraziqeena
(Surat Saba 34:39)

Tafsir: Sema: Mola wangu humpa riziki amtakae miongoni mwa waja wake na
humzuilia na chochotete mtakachotumia (kwa ajili ya Allah Subhanah wa Taa’ala)
basi atakirudisha kwani kwa hakika yeye ni m-bora wa kutoa riziki.

Ama kuhusiana na kilichoharamishwa basi hicho hua ni sehemu ya Moto wa Jahannam,


na bila ya shaka hakuna kitu kigumu kama kuzuia madhara ya kuwadhuru wengine na
kushikamana na kile kilichohalalishwa.

Na mbali ya kua Usiku na Mchana vimejaaliwa kua ni kwa ajili ya kupumzikia na


kutafutia maisha lakini pia vitu viwili hivi vimejaaliwa kua ni sehemu ya Mazingira yetu
tunayoishi ndani yake ili tupate kujua kuhusiana na mahesabu ya mda wa masaa, masiku,
wiki, miezi na miaka kama zinavyosema aya:

ْ‫ﺼَﺮةً ﻟِﺘَـْﺒـﺘَـﻐُﻮا‬ِ ‫ﲔ ﻓَﻤﺤﻮ َ� آﻳﺔَ ٱﻟْﻠﱠﻴ ِﻞ وﺟﻌ ْﻠﻨَﺂ آﻳﺔَ ٱﻟﻨـﱠﻬﺎ ِر ﻣﺒ‬
ْ ُ َ َ َ َ َ ْ َ ْ َ َ ِ ْ ‫ﱠﻬ َﺎر آﻳَـﺘَـ‬ َ ‫﴿ َو َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ٱﻟْﻠﱠْﻴ َﻞ َوٱﻟﻨـ‬
﴾ً‫ﺼﻴﻼ‬ ِ ‫ﺼﻠْﻨَﺎﻩ ﺗَـ ْﻔ‬ ٍ ِْ ‫ٱﻟﺴﻨِﲔ و‬ ِ ‫ﻀﻼً ِﻣﻦ ﱠرﺑِ ُﻜﻢ وﻟِﺘَـﻌﻠَﻤﻮاْ ﻋ َﺪد‬
ُ ‫ﺎب َوُﻛ ﱠﻞ َﺷ ْﻲء ﻓَ ﱠ‬ َ ‫ٱﳊ َﺴ‬ َ ّ َ َ ُ ْ َ ْ ّ ّ ْ َ‫ﻓ‬
َ
WajaAAalna allayla waalnnahara ayatayni famahawna ayata allayli wajaAAalna
ayata alnnahari mubsiratan litabtaghoo fadhlan min rabbikum walitaAAlamoo
AAadada alssineena waalhisaba wakulla shay-in fassalnahu tafseelan (Surat Al Isra
17:12)

Tafsir: Na tumejaalia Usiku na Mchana kua ni vithibitisho viwili, kisha tukaitia kiza
dalili ya usiku na tukaijaalia dalili ya Mchana kua ni yenye kung’ara ili mpate
kutafuta fadhila ndani yake kutoka kwa Mola wenu, na mate kujua Idadi ya miaka na
mahesabu, na kila kitu tumekifafanua kwa ufafanuzi.
703

Tunapoiangalia aya yetu basi tunaona kua imetumia neno Famahawna linalotokana na
neno Maha ambalo ni lenye kumaanisha Kutia kiza, Kufanya kitu kiwe kimefifia, Kutia
Doa, Kuficha, Kuondoa au Kufuta.

Ambapo kwa upande wa Amir al Muuminin Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu basi
anasema kuhusiana na kutiwa kiza kwa Usiku kunamaanisha ‘Muonekano wa Mwezi
Usiku hua una madoa madoa meusi.’ Ama kwa upande wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi
Allahu Anhu basi yeye anasema kua: ‘Mwanzoni wa Maumbile yake Mwezi ulikua
unang’ara kama Jua, lakini baadae Allah Subhanah wa Ta’ala akaiondoa Nuru
yake hio’

Ambapo tunapouangalia mtizamo wa Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allau Anhu
basi tunaona si wa kawaida na hivyo kudhihirisha ile Dua aliyoombewa na Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam alipokua mdogo baada ya pale alipoamrishwa na Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam atie udhu kisha asali nae pembeni yake, lakini hata hivyo Abd
Allah Ibn Abass Radhi Allahu Anhu hakutii amri hio ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
Salam.

Hivyo baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kumaliza kusali basi akamuuliza
Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu: ‘Ya Ibn Abbas hivi kwanini hukusali
pamoja nami wakati nilipokuambia kua sali pamoja nami pembeni yangu?’. Abd
Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu ambae wakati huo alikua na umri wa miaka 6
akasema: ‘Ya Rasul Allah! Hakika wewe Darja yako ni kubwa sana ndani ya macho
yangu, kwangu mimi kusimama pamoja nawe pembeni yako katika Sala.’

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akatabasamu kisha akampigapiga


begani kumpongeza na kisha akanyanyua mikono juu na kusema:

ِ ِ ِّ ‫اﻟﻠﱠﻬ ﱠﻢ ﻓَِّﻘﻬﻪ ِﰲ‬


َ ‫اﻟﺪﻳ ِﻦ َو َﻋﻠّ ْﻤﻪُ اﻟﺘﱠﺄْو‬
‫ﻳﻞ‬ ُْ ُ
Allahuma Faqihhu fii alDiini wa aAaalimhu alTa-wiila.

‘Ya Allah, Mjaalie kua ni mwenye Ufaham wa Dini, na Mjaalie awe ni mwenye Ilm
ya Dini na mwenye kujua maana na Tafsiri yake.’

Hivyo tumesema kua mtizamo wake Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allau Anhu
si wa kawaida kwa sababu ingawa maneno hayo aliyasema miaka 1441 iliyopita lakini
leo hii Wanasayansi wamethibitisha kua ingawa hawajui ni nini asili ya Maumbile ya
Mwezi lakini hata hivyo wamesema kua vithibitisho vinaonesha kua hapo awali
maumbile ya Mwezi yalikua ni ya gesi nzito kama uji wa Moto wa Volcano ambayo ni
704

maumbile kama ya Jua lakini baadae Maumbile hayo ya Mwezi yakapoa na kua kama
Jiwe lililotokana na mripuko wa Volkano na kisha likapoa ambalo lenye unene wa kina
cha kilomita 1330.

Kisha aya iya ikamalizia kuhusiana na umuhimu wa Usiku na Mchana ni kuhusiana na


mahesabu ya Nyakati kuhusiana na Saa, Siku, Wiki, Mwezi, Mwaka n.k na hii ni
kutokana na sababu nyingi ikiwemo kua na mpangilio katika kutekeleza Majukumu yetu
kwa Viumbe wenzetu hapa ulimweguni na pia kwa Mola wetu. Kwani bila ya kua na
uwezo wa kujua kutokana na kutokuwepo kwa Usiku na Mchana basi bila ya shaka
ingekua hakuna mpangilio wa jambo lolote katika maisha yetu, yaani ingawa tungekua
tuna akili lakini bado hali yetu ingekua hamna tofauti na Wanyama.

Hivyo kuwepo kwa Usikua na Mchana tu peke yake ua ni kithibitisho tosha


kinachobainisha kuwepo kwa Muumba wa Kila kitu amae ndie aliekikadiria kila kitu
katika makadirio yake na hivyo kila kitu kua katika mpanilo wake. Baada ya kubainisha
hayo basi aya inamalizia kwa kuweka wazi kua Qur’an imefafanua kila kitu kuhusiana
na Upekee wa Allah Subhanah wa Ta’ala, Umoja wake, Ukubwa wake, Uwezo wake,
Mamlaka yake, Malengo ya Kuumbwa kwetu sisi Ibn Adam na Mazingira yetu na nini
tunachotakiwa kukifanya sisi viumbe wake, n.k

Hivyo kutokana na mtizamo huo basi tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala amejaalia
Mchana kua ni sehemu ya kujitafutia mahitaji ya maisha yetu hapa duniani, ambapo ndani
yake mahitaji hayo kuna mahitaji ya kiroho ambayo ni kwa ajili ya Akhera yetu na
mahitaji ya kimwili ambayo ni kwa ajili ya kuturahisishia uwezo wa upatikanaji wa
mahitaji ya maisha yetu hapa Duniani kwa Ardhini na Baharini.

3-DALILI KATIKA UUMBWAJI WA BAHARI.


Uumbwaji wa Bahari na manufaa yake kwa Viumbe vilivyomo Ulimwenguni, kwani
moja bahari ni eneo ambalo limechukua asilimia 97% ya Maji yaliyomo Ulimwenguni
na pia Bahari ni yenye kuchukua eneo la asilimia 70% la Dunia. Hivyo haishangazi kwa
nini Allah Subhanah wa Ta’ala akajaalia Bahari kua na eno kubwa zaidi ya ardhi, kwa
sababu moja kati ya manufaa ya Bahari tukiachana na manufaa ya Usafiri, basi ni lile la
kua na kazi ya kudhibiti na kuhifadhi mvuke wa Joto linalotokana na Jua na kisha
kuusafirisha mvuke huo kutoka katika maeneo ya katikati ya Dunia na kuupeleka katika
maeneo ya ncha za Dunia za Kusini na Kaskazini na hivyo kurekebisha usawa wa hali ya
hewa katika maeneo hayo kwa kuipandishia hali ya Joto, na hivyo watu kuweza kuishi
705

kutokana na kuwepo kwa ujoto huo katika maeneno hayo, keani vyenginevyo basi
ingekua ni vigumu kuwezekana kuishi kwenye sehemu hizo.

Bahari pia hua ni yenye kunyonya hewa ya Carbondioxide, ambayo inatolewa na viumbe
baada ya kuvuta hewa ya Oxygen, na pia hunyonya hewa ya carbon inayotolewa na
mashine na vyombo mbalimbali vya usafiri Duniani mbali mbali zinazotumiwa na Ibn
Adam Uliwenguni, na hivyo hua kama Chujio ya kuchuja hewa Ulimwenguni kwa ajili
ya kuweka mazingira safi na mazuri kwa ajili ya Viumbe bora waishio ndani yake, yaani
Ibn Adam, ambao nao kutokana na ujinga wao na dharau zao zinazotokana na
kuendekeza Matamanio ya Kidunia basi wamekua ni wenye kuifanyia Israfu neema hio
muhimu sana katika maisha yao hapa Ulimwenguni ambayo ni neema ya Maji ya Bahari.

Na matokeo yake ndio kama tunavyoona mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababisha


kuparaganyika kwa mpangilio wa Misimu ya mwaka ya kimaumbile, na kuyeyuka kwa
barafu katika maeneo ya Kusini na Kaskazini ya Dunia na hivyo kusababisha Joto kua ni
lenye kuongezeka, na hivyo kuongezeka kwa ukame, kuzuka kwa moto katika baadhi ya
maeneo, kuogezeka kwa eneo la Jangwa Ulimwenguni n.k.

Ama kuhusiana na manufaa na umuhimu wa Bahari hua ni yenye kutokana na Maumbile


ya Maji ambayo huwezesha Ueleaji wa Vyombo vya Usafiri Baharini, ambapo Allah
Subhanah wa Ta’ala amejaalia Maji kua na Uzito wa kubeba Vitu na pia Maji na Hewa
kua na maumbile ya kutawanyika hivyo kuviwezesha vyombo tofauti kua na uwezo wa
kuelea na kusafiri juu yake bila ya kipingamizi kwa ajili ya Manufaa ya Ibn Adam na
hivyo kutokana na ukubwa wake basi vyombo hivyo huonekana kua kama Mlima
unaotembea kama inavyosema aya:

ْ ‫آ�ﺗِِﻪ ٱ ْﳉََﻮا ِر ِﰱ ٱﻟْﺒَ ْﺤ ِﺮ َﻛﭑﻷ‬


﴾‫َﻋﻼَِم‬ ِ
َ ‫﴿ َوﻣ ْﻦ‬
Wamin ayatihi aljawari fee albahri kaal-aAAlami (Surat Ash-shura 42:32)

Tafsir: Na miongoni mwa Dalili zake ni Meli Baharini kua kama Milima.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta'ala anatubainishia katika aya hii kua Vyombo vya
Baharini vinapokua vinaelea hua vinakua kama Milima, na hii si kutokana na Namna
vinavyotengenezwa Vyombo hivyo kutokana na Ujuzi aliofundishwa Nabii Nuh na Allah
Subhanah wa Ta'ala kupitia kwa Malaika Jibril, lakini pia ni kutokana na Maumbile ya
Maji kwa namna yalivyojaaliwa na alieyaumba Maji hayo

Kwani Allah Subhanah wa Ta'ala ameyajaalia Maji kua Mepesi kwa Viumbe wanaoishi
ndani yake na hapo hapo kua ni mazito kwa Vile Vitakavyokaa Juu yake na hivyo kua na
706

Uwezo wa kubeba Vyombo vya Usafiri wa Baharini tena kwa Manufaa yetu sisi Viumbe
wake wapendwa ambao ni Ibn Adam na Vyombo vya Baharini hua kama Milima
vinapokua juu ya Maji ya Bahari kutokana na Umbo la vyombo hivyo kua Nusu ni vyenye
kuzama Ndani ya Maji kama vile inavyozama Milima ardhini, na Nusu huchomoza na
kuelea Juu ya Maji na hivyo hua ni sawa na namna Milima inavyochomoza juu Ardhini.

Hivyo hapa Allah Subhanah wa Ta'ala anatuwekea wazi Dalili zake kwa mifano iliyohai
na iliyokua rahisi kabisa kuifaham. Na hii pia inaweka wazi Miujiza ya Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam kupitia katika Kitabu chake kitukufu alichokuja nacho kwa
ajili ya Kuwaongoza Walimwengu.

Kwa Sababu ingawa huu ni Mfano rahisi kwetu sisi kiakili kuufaham, lakini ukweli ni
kua ili utoe mfano huu basi inabidi uwe ni Mtu ambae aenaishi karibu na Bahari, Ziwa
au Mto, ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua akiishi Jangwani, hivyo
kwake yeye hua ni vigumu kuyajua na kuyasema haya kwa utaalam kama wa
mtengenezaji wa vyombo vya Baharaini, hivo bila ya shaka hakuna alieyasema haya
isipokua ni Muumba mwenyewe katika kuthibitisha kuwepo kwake kwa wale
watakaotafakkari, na bila ya shaka hakuna pia anaesababisa vyombo hivyo kua ni vyenye
kuelea Baharini isipokua ni Allah Subhanah wa Ta’ala peke yake kama inavyosema aya
ifuatayo:

‫ﻀﻠِ ِﻪ إِﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن ﺑِ ُﻜ ْﻢ‬


ْ َ‫ﻚ ِﰱ ٱﻟْﺒَ ْﺤ ِﺮ ﻟِﺘَـْﺒـﺘَـﻐُﻮاْ ِﻣﻦ ﻓ‬ ِ ِ
َ ‫﴿ ﱠرﺑﱡ ُﻜ ُﻢ ٱﻟﱠﺬى ﻳـُْﺰﺟﻰ ﻟَ ُﻜ ُﻢ ٱﻟْ ُﻔ ْﻠ‬
﴾ً‫رِﺣﻴﻤﺎ‬
َ
Rabbukumu alladhee yuzjee lakumu alfulka fee albahri litabtaghoo min fadlihi
innahu kana bikum raheeman(Surat Al sraa 17:66)

Tafsir: Mola wako ndio yule ambae anae viendesha kwa ajili yenu Vyombo vya
baharini, ili muweze kutafuta fadhila zake, hakika yeye kwenu nyie ni mwingi wa
Rehma.

Mbali ya kua ayah hii inazungumzia baadhi ya Vyombo ambavyo vinatumia Upepo
katika kusafiri Baharini na hivyo baadhi ya watu wanaweza wakasema kua ayah hii
haivihusu vyombo vyenye kutumia Mashine lakini hapo hapo kama tulivyosema kuelea
kwake tu chombo baharini hutokana na Rehma za Allah Subhanah wa Ta’ala na pia hizo
mashine zimetokana na Neema ya Ufaham ambao viumbe Ibn Adam wamepewa na Mola
wao na hivyo wakawa na uwezo wa kuidhibiti Bahari kwa kua na uwezo wa kutengeneza
707

Mashine hizo kwa ajili ya kurahisisha maisha yao katika kutafuta na mahitaji yao mbali
mbali kwa njia ya Bahari kama inavyosema aya ifuatayo:

ً‫﴿ َوُﻫ َﻮ ٱﻟﱠ ِﺬى َﺳ ﱠﺨَﺮ ٱﻟْﺒَ ْﺤَﺮ ﻟِﺘَﺄْ ُﻛﻠُﻮاْ ِﻣْﻨﻪُ َﳊْﻤﺎً ﻃَ ِﺮّ�ً َوﺗَ ْﺴﺘَ ْﺨ ِﺮ ُﺟﻮاْ ِﻣْﻨﻪُ ِﺣ ْﻠﻴَﺔ‬
﴾‫ﻀﻠِ ِﻪ وﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜﻢ ﺗَ ْﺸ ُﻜﺮو َن‬ ‫ﻓ‬ ‫ﻦ‬ ‫ﻣ‬ِ ْ‫اﺧﺮ ﻓِ ِﻴﻪ وﻟِﺘَـﺒـﺘَـﻐُﻮا‬
ِ َ ‫ﺗَـ ْﻠﺒﺴﻮﻧَـﻬﺎ وﺗَـﺮى ٱﻟْ ُﻔ ْﻠ‬
ُ ْ َ ْ َ ْ َ َ ‫ﻚ َﻣ َﻮ‬ ََ َ َُ
Wahuwa alladhee sakhkhara albahra lita/kuloo minhu lahman tariyyan
watastakhrijoo minhu hilyatan talbasoonaha watara alfulka mawakhira feehi
walitabtaghoo min fadhlihi walaAAallakum tashkuroona (Surat An Nahl 16:14)

Tafsir: Na ni yeye ndie alieweka bahari ndani ya udhibiti wenu, ili mpate kula
kutokana nayo Nyama laini (ya Samaki wake) na mpate kutoa kutoka ndani yake
mapambo (ya Lulu, Marijani n.k) ya kuvaa, na mnaona Vyombo vya Baharini
vinavyopasua ndani yake, ili mpate kutafuta fadhila zake na mpate kua ni wenye
kushukuru.

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Kwa hakika
Kama Allah Subhanah wa Ta’ala hakuumba Miti,Chuma na zana tofauti za
kutengenezea Meli, na kama ahukuwawezesha Ibn Adam kua na uwezo wa
Kutumia vitu hivyo, na kama hakuyajaalia Maji kua ni yenye maumbile ya
kutembea na kuwezesha Meli kua ni zenye kuelea juu yake, na kama hakuumba
Upepo na wingi wa nguvu yake, na kama hakuumba Mito na kuifanya kua Mipana
na yenye vina virefu vya maji ili kuruhusu Vyombo vya baharini kutembea ndani
yake. Basi ingekua hakuna manufaa yeyote yanayopatikana kutokana na Vyombo
hivyo vinavyoelea Baharini. Kwa hakika yeye Allah Subhanah wa Ta’ala ndie
Msimamizi na Mwenye Udhibiti wa vitu hivi vyote.’

Ama kwa upande wa aya yetu basi tunaona kua ya imetumia neno Mawakhir ambalo hua
ni lenye kutokana na neno Makhr ambalo maana yake hua ni Kuchana kitu, Kupasua kitu
au Kutawanya Mawimbi na kutoa sauti ya mtawanyo huo kama vile vyombo vya baharini
vinavyopasua na kutawanya Maji na Hewa katika kuenda kwake.

Hivyo ayah hii inazungumzia kila kitu ambacho kinatumika baharini kwa njia ya
kutawanya Maji ikiwemo Meli, Visima vya Mafuta na Gesi vya Baharini, Madaraja ya
juu juu baharini ambayo nguzo zake zinachukua sehemu ya Maji ya Bahari kwa
kuyatawanya na pia Madaraja yenye umbo la Duara ndani kwa ndani chini Baharini.
708

Miongoni mwa maeneo ambayo hayajafanyiwa uchunguzi wa kutosha Ulimwenguni


kutokana na kutokua na uwezo stahiki katika kuichunguza kwake basi ni Bahari, kwani
ndani ya Bahari mna aina za Viumbe zaidi ya laki tatu 300,000 wakiwemo Samaki
ambao nyama yao ni laini na yenye faida kubwa sana kwa Ibn Adam lakini ni viumbe
wachache sana wanaoishi Baharini ni wanaojulikana na Ibn Adam, kwa upande
mwengine basi pia Baharini mna Madini ya Thamani ikiwemo ya Mapambo ndani yake
ikiwemo Lulu na Marijani, n.k

Na tunapozungumzia Bahari basi hua tunazungumzia eneo ambalo ni lenye Maumbile


makubwa sana kwa kina na pia kwa upana kama zinavyosema aya:

ِِ ِ ِِ ِ ِ ٍ
ٌ ‫﴿أ َْو َﻛﻈُﻠُ َﻤﺎت ِﰱ َْﲝ ٍﺮ ﱡﳉّ ٍّﻲ ﻳَـ ْﻐ َﺸﺎﻩُ َﻣ ْﻮ ٌج ّﻣﻦ ﻓَـ ْﻮﻗﻪ َﻣ ْﻮ ٌج ّﻣﻦ ﻓَـ ْﻮﻗﻪ َﺳ َﺤ‬
‫ﺎب‬
ُ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻟَﻪ‬ ْ ‫ﺾ إِ َذآ أ‬
‫َﺧَﺮ َج ﻳَ َﺪﻩُ َﱂْ ﻳَ َﻜ ْﺪ ﻳَـَﺮ َاﻫﺎ َوَﻣﻦ ﱠﱂْ َْﳚ َﻌ ِﻞ ﱠ‬ ٍ ‫ﻀ َﻬﺎ ﻓَـ ْﻮ َق ﺑَـ ْﻌ‬
ُ ‫ﺎت ﺑَـ ْﻌ‬
ٌ ‫ﻇُﻠُ َﻤ‬
﴾‫ﻧُﻮراً ﻓَﻤﺎ ﻟَﻪُ ِﻣﻦ ﻧُﻮٍر‬
َ
Aw kadhulumatin fee bahrin lujjiyyin yaghshahu mawjun min fawqihi mawjun min
fawqihi sahabun dhulumatun baAAduha fawqa baAAdin idha akhraja yadahu lam
yakad yaraha waman lam yajAAali Allahu lahu nooran fama lahu min noorin(Surat
An Nur 24:40)

Tafsir: Au (hali ya asieamini Allah ) hua ni kama kiza ndani ya kina kirefu cha bahari.
Ambacho kimezidiwa na Mawimbi makubwa na mawimbi mengine makubwa juu yake,
na kufunikwa na mawingu meusi, kiza kimoja juu ya chengine, hata kama mtu
akinyoosha mkono wake itakua vigumu kuuona. Na kwa yule ambae Allah hajampa
Nuru basi kwake yeye hua hakuna Nuru.

Aya hii inazungumzia kuhusiana na aina ya kiza cha wale waliokufuru na kutomuamini
Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo Watu hao hua katika kiza cha kutokua na Imani, na
hivyo kumithilisha na kiza kilichomo ndani ya kina cha maji ya Baharini. Na hii ni kwa
sababu kina cha Bahari ni kirefu sana kwani katika Bahari ya Pacific kuna sehemu ina
urefu wa kina cha kuenda chini kwa umbali wa masafa ya kilomita 11.

Na unapozama na kufikia katika urefu wa mita 200 tu basi tayari inakua hamna nuru
ndani yake na huwezi kuona hata mkono wako kama ilivyosema aya. Na ukizama zaidi
basi unakutana na Mawimbi ya ndani kwa ndani ambayo nayo ni makubwa kuliko
Mawimbi yanayopatikana juu ya bahari na hii ni kwa sababu Maji yaliyokua kwenye
kina hicho yana uzito zaidi ya maji ya juu Baharini, Mawimbi haya juu ya Mawimbi hua
709

yanatofautiana kulingana na kina cha Bahari, kwani kila unavyozidi kuzama basi hua
unaona kuna aina tofauti ya tabaka za Mawimbi na pia maji yake hua na mabadiliko ya
chumvi tofuti.

Na Ibn Adam hua hawezi kuzama zaidi ya mita 200 ndani ya Bahari bila ya kua na kifaa
maalum cha usaidizi wa uhai wake na ni wenye kujua kuhusiana na hatari ya maisha yake
anapokua Baharini na hua ni wenye kumtegemea Allah Subhanah wa Ta’ala anapokua
Safarini ndani ya Bahari kama inavyosema aya ifuatayo:

‫ﺎﻫ ْﻢ إِ َﱃ ٱﻟْﺒَـِّﺮ إِذَا ُﻫ ْﻢ‬ ِّ ‫ﺼﲔ ﻟَﻪ ٱﻟ‬ ِ ِ‫ٱﻪﻠﻟ ﳐُْﻠ‬ ِ ‫﴿ﻓَِﺈذَا رﻛِﺒﻮاْ ِﰱ ٱﻟْ ُﻔ ْﻠ‬
ُ ‫ﻳﻦ ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ ﳒَﱠ‬
َ ‫ﺪ‬ ُ َ َ ‫ﱠ‬ ‫ا‬
ْ‫ﻮ‬ُ ‫ﻋ‬
َ ‫د‬
َ ‫ﻚ‬ َُ
﴾‫ﻳُ ْﺸ ِﺮُﻛﻮ َن‬
Fa-idha rakiboo fee alfulki daAAawoo Allaha mukhliseena lahu alddeena falamma
najjahum ila albarri idha hum yushrikoona (Surat Al Anqabut 29:65)

Tafsir: Na kisha wanapopanda Meli humuomba Allah kwa Ikhlasi na Imani, na kisha
wakishaokoka baharini basi hua washirikina.

Na hivyo kutokana na imani hio hua ni wenye kuamini kua kuokoka kwao Baharini hua
ni kwenye kutokana na ustadi na ujuzi wa Nahodha wa chombo husika, badala ya
kumshukuru Allah Subhnah wa Ta’ala ambae ndie anaewaokoa viumbe wake na kila
aina ya kiza, we cha Baharini, cha Kiimani, cha Mitihani na Matatizo, n.k kama
inavyosema aya ifuatayo:

َ َ‫ﻀﱡﺮﻋﺎً َو ُﺧ ْﻔﻴَﺔً ﻟﱠﺌِ ْﻦ أَﳒ‬ ِ ِ ِ


�‫ﺎ‬ َ َ‫﴿ﻗُ ْﻞ َﻣﻦ ﻳـُﻨَ ّﺠﻴ ُﻜ ْﻢ ّﻣﻦ ﻇُﻠُ َﻤﺎت ٱﻟْﺒَـِّﺮ َوٱﻟْﺒَ ْﺤ ِﺮ ﺗَ ْﺪﻋُﻮﻧَﻪُ ﺗ‬
ٍ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻳـﻨَ ِﺠﻴ ُﻜﻢ ِﻣْﻨـﻬﺎ وِﻣﻦ ُﻛ ِﻞ َﻛﺮ‬
‫ب ﰒُﱠ أَﻧﺘُ ْﻢ‬ ‫ﱠ‬ ‫ﻞ‬ِ ُ‫ﻗ‬ ۞ ‫ﻳﻦ‬ِ
‫ﺮ‬ ِ‫ِﻣﻦ ﻫـٰ ِﺬﻩِ ﻟَﻨَ ُﻜﻮﻧَ ﱠﻦ ِﻣﻦ ٱﻟﺸﱠﺎﻛ‬
َ ْ
ْ ّ َ َ ّ ْ ّ ُ ُ َ َ
﴾‫ﺗُ ْﺸ ِﺮُﻛﻮ َن‬
Qul man yunajjeekum min dhulumati albarri waalbahri tadAAoonahu
tadarruAAan wakhufyatan la-in anjana min hadhihi lanakoonanna mina
alshshakireena; Quli Allahu yunajjeekum minha wamin kulli karbin thumma
antum tushrikoona (Surat Al AnAam 6:63-64)
710

Tafsir: Sema (Ewe Muhamamd) Jee ni nani anae kuokoeni nyie kutokana na kiza
cha Ardhini na cha Baharini? Na mnapomuita kwa unyenyekevu kwa siri mkisema:
‘Kama Allah akituokoa kutokana na hatari hii basi tutakua na shukrani’ Sema
(Ewe Muhammad): ‘Allah ndie anaekuokoeni nyinyi kutokana na matatizo yote na
kisha mnamshirikisha.’

Lakini uhalisi hua ni vyenginevyo, ili kufaham haya basi na tuangalie mfano wa Imam
Ibrahim Ibn Adham Ibn Mnasur Al Taymi Al Balkhi ambae ni Tabiina aliefariki mnamo
mwaka 161 Al Hijra.

Ambapo siku moja katika kipindi cha Uhai wake alikua akisafiri Baharini ndani ya Jahazi
pamoja na watu wengine, na mara Usingizi mwanana ukampitia na akalala. Wakati akiwa
amelala huku safari ikiendelea na mara ghafla hali ya hewa ikabadilika ikaanza kunyesha
Mvua kubwa, Upepo ukawa mkali na Bahari ikaanza kuchafuka. Mawimbi yakawa
makubwa, na watu wakaingiwa na khfu na wengine wakaanza kulia kumuomba Allah
Subhanah wa Ta’ala awasaidie, lakini hali haikutulia.

Watu hao wakakumbuka kua ndani ya Jahazi miogoni mwa Wasafiri pia yumo Mcha
Mungu ambae ni Imam Ibrahim Ibn Adham. Hivyo wakamkimbilia na wakamkuta kalala
fofofo hana hata habari, hivyo wakamuamsha na kumuelezea hali ilivyochafuka Baharini
na hatari watakayokabiliana nayo kama Bahari haijatulia, yaani ya watazama. Imam
Ibrahim Ibn Adham akaamka akasimama kisha akasema: ‘Ya Allah! Hakika
umetuonesha Nguvu na Uwezo wako, hivyo tunakuomba utuoneshe Rehma na
Maghfira yako’ basi ingawa haya yalikua ni maneno machache lakini hapo hapo Bahari
ikatulia na kua shwari kama Bakuli lililojaa mafuta ya kupikia yaani juu hua kama kioo
kinavyotulia na kuonesha kivuli cha Sura yako unapokiangalia na ikawa hakuna tena
Upepo wala Mvua.

4-DALILI KATIKA UNYESHAJI WA MVUA.


Katika Unyeshaji wa Mvua ambayo maji yake ndio chanzo cha kurutubisha kila kitu
Duniani Kuanzia Mito, Maziwa. Bahari na Viumbe waliomo ndani yake, Mimea,
Wanyama mpaka Ibn Adam na hua inashushwa kwa makadirio maalum, ili mvua hio
isinufaishe isipokua kwa waliokusudiwa kunufaika nayo, na ili isidhuru isipokua kwa
waliokusudiwa kudhurik nayo na hii ni kutokana na kusababishwa na Ujinga wetu,
Dharau zetu, Dhulma zetu, na kukosa shukrani kwetu juu ya Mola wetu.

Allah Subhanah wa Ta’ala anasema kuhusiana na Makadirio hayo kua:


711

‫ﺎب ﺑِِﻪ‬
ٍ ‫ض وإِ ﱠ� َﻋﻠَ ٰﻰ َذ َﻫ‬ ِ ْ ‫ﺂء َﻣﺂء ﺑَِﻘ َﺪ ٍر ﻓَﺄ‬ ِ ِ ‫﴿وأ‬
َ ِ ‫َﺳ َﻜﻨﱠﺎﻩُ ﰱ ٱﻷ َْر‬ ً ‫َﻧﺰﻟْﻨَﺎ ﻣ َﻦ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤ‬ ََ
‫ﺎب ﻟﱠ ُﻜ ْﻢ ﻓِ َﻴﻬﺎ ﻓَـ َﻮاﻛِﻪُ َﻛﺜِ َﲑةٌ َوِﻣْﻨـ َﻬﺎ‬
ٍ َ‫ﱠﺎت ِﻣﻦ ﱠِﳔ ٍﻴﻞ وأ َْﻋﻨ‬
َ ّ
ٍ ‫َﻧﺸﺄْ َ� ﻟَ ُﻜﻢ ﺑِِﻪ ﺟﻨ‬
َ ْ َ ‫ﺄ‬ ‫ﻓ‬
َ ۞‫ن‬َ ‫و‬‫ر‬
ُ
ِ ‫ﻟََﻘ‬
‫ﺎد‬
﴾‫َﺄﺗْ ُﻛﻠُﻮ َن‬
Waanzalna mina alssama-i maan biqadarin faaskannahu fee al-Ardhi wa-inna
AAala dhahabin bihi laqadiroona; Faansha/na lakum bihi jannatin min nakheelin
waaAAnabin lakum feeha fawakihu katheeratun waminha ta/kuloona (Surat Al
Muuminun 23:18-19)

Tafsir: Na tunashusha kutoka Mbinguni Maji kwa makadirio na kisha tunayahifadhi


Ardhini na kwa hakika ni kwa urahisi tunaweza kuiondoa kwa makadirio. Na kisha
kutokana nayo tunakupeni bustani za Mitende na Mizabibu ambayo ina matunda
mengi na kutokana nayo mnakula.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anathibitisha kua yeye ndie anaeikadiria Mvua inyeshe
kwa sehemu gani na kwa kiasi gani, na vile vile nirahisi kwake kuisitisha Mvua hio
isishuke na pia kuyasitisha Maji yasikae ardhini.

Ambapo kutokana na Aya hii basi alisema Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Ahmad
Ibn Abu Baqr Al Ansari Al Qurtubi kua: ‘Harfu Lam iliyotumika hapa katika neno
Laqadiruuna hua ni Lam ya Ta-qiid ambayo hua ni Lam ya Kutilia mkazo Uhakika
wa kufanyika jambo husika kwa Urahisi sana’, yaani Allah Subhanah wa Ta’ala
anatuwekea wazi kua yeye anaweza kuyaondoa Maji yasihifadhike mwenye Mawingu,
na hivyo kuyasababishia Mawingu hayo kua ni yasiyomwaga Mvua kutoka Mbinguni na
pia anaweza akayafanya Maji yasihifadhike Ardhini, tena kwa mara moja na kwa urahisi
sana tu kwa Kun fayakunu.

Ama kwa upande wa Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Mvuke wa
Maji kutoka Baharini hupaa angani na kuchujwa hadi kua msafi na kuwacha
uchafu wake wote, na baada ya hapo mvuke huo hua mzito na unapozidi uzito wake
basi huanguka Ardhini kama Mvua.’

Na miongoni mwa faida zake Mvua hio basi hua ni kuotesha mimea tofauti kama
tulivyoona hapo kabla, ila hapa aya imetaja Mitende na Mizabibu kwa sababu mimea hio
ndio maarufu kwa Waarabu katika wakati huo, kwani kama ingetajwa Embe au Nazi basi
712

ingekua ni vigumu kwa Masahaba kufahama na hivyo Mimea hii hua pia inawakilisha
Mimea myengine yote iliyobakia.

Katika kutaka kutufafanulia zaidi basi Allah Subhanah wa Ta’ala anaelezea namna
inavyoanza kutayarishwa Mvua hatua kwa hatua kwa kusema katika aya ifuatayo kua:

‫ﻒ ﺑـَْﻴـﻨَﻪُ ﰒُﱠ َْﳚ َﻌﻠُﻪُ ُرَﻛﺎﻣﺎً ﻓَـﺘَـَﺮى ٱﻟْ َﻮْد َق َﳜُْﺮ ُج‬ ِ ِ ‫﴿أََﱂ ﺗَـﺮ أَ ﱠن ﱠ‬
ُ ّ‫ٱﻪﻠﻟَ ﻳـُْﺰﺟﻰ َﺳ َﺤﺎﺎﺑً ﰒُﱠ ﻳـُ َﺆﻟ‬ َ ْ
‫ﺂء‬ ‫ﺸ‬ ‫ﻳ‬ ‫ﻦ‬ ‫ﻣ‬ ِِ‫ﺼﻴﺐ ﺑ‬
‫ﻪ‬ ِ ‫ﺂء ِﻣﻦ ِﺟﺒ ٍﺎل ﻓِﻴﻬﺎ ِﻣﻦ ﺑـﺮٍد ﻓَـﻴ‬ ِ ‫ِﻣﻦ ِﺧﻼَﻟِِﻪ وﻳـﻨـ ِﺰُل ِﻣﻦ ٱﻟ ﱠﺴﻤ‬
ُ َ َ َ ُ ُ َ َ َ َ َ َ ّ َُ َ ْ
ِ ِ‫وﻳﺼ ِﺮﻓُﻪ ﻋﻦ ﱠﻣﻦ ﻳ َﺸﺂء ﻳ َﻜﺎد ﺳﻨَﺎ ﺑـﺮﻗ‬
﴾‫ﺼﺎ ِر‬َ ْ‫ﺐ ﺑِﭑﻷَﺑ‬ ‫ﻫ‬ ‫ﺬ‬ْ ‫ﻳ‬ ‫ﻪ‬
ُ َ َْ َ ُ َ ُ َ
َ َ ُ ْ ََ
Alam tara anna Allaha yuzjee sahaban thumma yu-allifu baynahu thumma
yajAAaluhu rukaman fatara alwadqa yakhruju min khilalihi wayunazzilu mina
alssama-i min jibalin feeha min baradin fayuseebu bihi man yashao wayasrifuhu
AAan man yashao yakadu sana barqihi yadhhabu bial-absari(Surat Nur 24:43)

Tafsir: Jee umeona namna Allah anavyoyasukuma Mawingu kwa taratibu, na kisha
huyakusanya pamoja na huyajaalia kua chungu ya Matabaka, na mnaona Mvua
inakuja kutoka ndani yake, na hushusha kutoka katika Mbingu Mlima ambao ndani
yake mna vipande vya barafu na humpiga amtakae na humuepusha amtakae, mwanga
wa Radi ya kukaribia kupofua macho.

Aya imetumia neno Yujzi ambalo linatokana na neno Zaja linalomaanisha Kusukuma,
Kutia ari bila ya kua na papara, Kuendesha. Na kisha ikatumia neno Sahaban ambalo
maana yake hua ni Kuburura, na pia humaanisha Mawingu yaliyokusanywa

Hivyo Aya inatubainishia namna Mawingu yanavyokusanywa kwa kutumia Upepo


taratibu, kulingana na makadirio yake Allah Subhanah wa Ta’ala juu ya eneo husika, na
wakati husika na hali ya hewa husika kiasi ya kua hua ni vigumu kwa Ibn Adam kuainisha
Mvua hio itanyesha katika eneo gani hasa la Ardhi kwa uhakika, na ndio maana watabiri
ya hali ya hewa hua hawezi kusema kua Mvua itanyesha katika Mtaa fulani mpaka mtaa
fulani bali hua wanajumuisha eneo kubwa husika kwa ujumla.

Ambapo katika wakati ambao Mawingu yanapokua yanakusanywa taratibu na Upepo


basi Mawingu hayo hua katika hali ambayo wataalamu wanaiita hali ya Mawingu ya
Stratus na baada ya kukusanywa pamoja basi hua ni Mawingu ambayo hua yanajulikana
kama Culumus. Na ndio maana aya ikasema kua Wayunazzilu mina alssama-i min
713

jibalin feeha min baradin yaani Na hushusha kutoka katika Mbingu Mlima ambao
ndani yake mna vipande vya barafu.

Hii ni kwa sababu mkusanyiko wa Mawingu ya Culumus hua na urefu mkubwa sana
kuelekea juu Mbinguni na hua na muonekano kama Mlima ambao huweza kufikia urefu
wa 20 Km kwenda juu. Mawingu hayo yanapokua tayari yameshapevuka hua yanakua
na hali inayojulikana kama Mawingu ya Nimbus na hua tayari kwa ajili ya kumwaga Maji
iliyoyabeba aidha kuyamwaga kwa njia ya Mvua au Theluji au Barafu kwani hali ya
Mvua, Theluji (barafu laini) au Barafu ngumu kama jiwe hua inategemeana pia na hali
ya hewa ya eneo husika ambapo katika baadhi ya maeneo ya sehemu za Baridi mawingu
hayo husababisha kunyesha kwa Barafu ya mawe ambayo hufikia ukubwa wa Chungwa.

Ambapo kuhusiana na Utabiri basi amesema Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn
Ahmad Ibn Abu Baqr Al Ansari Al Qurtubi kua amesema Rasul Allah Slallahu Alayhi
wa Salam kua: ‘Miongoni mwa watu kuna wale ambao wanao Ufunguo wa Mema na
Kufuli za Maovu. Na pia kuna wengine ambao wana Ufunguo wa Maovu na Kufuli
za Mema. Hivyo kuna bashirio Jema kwa yule ambae amepewa Ufunguo wa Mema
katika mikono yake na Allah Subhanah wa Ta’ala na Ole wake yule ambae katika
mikono yake amepewa Ufunguo wa Maovu.’(Sahih Ibn Majah, Sahih Imam Abu Hatim
Abd Rahman Muhammad Ibn Idris Al Razi )

Haya yote yametajwa ndani ya Qur’an na Muumba kupitia kwa Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam ambae alikua akiishi Jangwani miaka 1441 iliyopita na hivyo hakuwahi
kuona wala kujua kuhusiana na namna mvua inavyotegenezwa na ukubwa wa Mawingu
yanavyokua kama lima kuelekea juu na kisha si kuelezea namna inavyonyesha Mvua ya
Maji tu bali Mvua ya Mawe ya Barafu na theluji pia. Huu ni miogoni mwa Miujiza ya
Qur’an na pia ni uthibitisho kua Rasul Allahi Salallahu Alayhi wa Salam hakuambiwa
haya na mwengine yeyote isipokua na Muumba wa Ulimwengu na kilakitu kilichomo
ndaniyake ambae ni Allah Subhanah wa Ta’ala.

Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Ahmad Ibn Abu Baqr Al Ansari Al Qurtubi
anaendelea kutuambia kua: ‘Ama kuhusiana na Kutabiri Mvua kutokana na dalili za
kimaumbile basi hua inaruhusika. Ambapo pia Daktari hua si mwenye kupata
dhambi kama atatabiri kutokana na kuona kua ziwa la kulia la mama mja mzito
limefifia rangi yake au limekua kubwa kidogo na hivyo itakua ni mtoto wa kiume
na kama ikiwa ziwa la kushoto liko hivyo basi atakua ni mtoto wa kike, au kama
mama mja mzito akiona kua tumbo lake kwa upande wa kulia ni zito zaidi basi
atakua ni mtoto wa kike.

Na pia kama mtu atatabiri tarehe ya kupatwa kwa Jua au kwa Mwezi na akapatia
basi hua hana kosa kwani Allah Subhanah wa Ta’ala amesema katika Quran:’
714

﴾‫ﻮن ٱﻟْ َﻘ ِﺪ ِﱘ‬


ِ ‫﴿وٱﻟْ َﻘﻤﺮ ﻗَﺪﱠرَ�ﻩ ﻣﻨَﺎ ِزَل ﺣ ﱠ ٰﱴ ﻋﺎد َﻛﭑﻟﻌﺮﺟ‬
ُ ُْ َ َ َ َ ُ ْ ََ َ
Waalqamara qaddarnahu manazila hatta AAada kaalAAurjooni alqadeemi (Surat
Yasin 36:39)

Tafsir: Na Mwezi tumeukadiria vituo vyake mpaka hurudia ukawa kama Jani la
Mtende lililokauka.

Lakini hata hivyo Watabiri wanaotabiri kupatwa kwa mwezi wanatakiwa


kudhibitiwa, kwa sababu kutokana na kutangazia kwao basi hua ni wenye
kuwahatarishia watu Imani zao, (kwani watu wa Ujahiliyah walikua wakiamini kua
mtu anaetabiri Kupatwa kwa Jua au mwezi hua ana Nguvu maalum) hivyo
wanatakiwa kutobainisha Ilm yao bali wanatakiwa wakae nayo Ilm yao katika Nafsi
zao na wasizitangazie tangazie’

Allah Subhanah wa Ta’ala anatuwekea wazi kinachofuatia pale baada ya Mvua, au


Theluji hio kuanguka katika eneo husika, kwa kututolea mfano wa Ardhi kame isiyokua
na miti ambayo hufufuka na kisha kutumia kithibitisho hicho kuweka wazi uwezo wake
katika kuhuisha na kufufua kwa kusema:

ِ َ ‫آ�ﺗِِﻪ أَﻧﱠ‬ ِ
‫ﺖ‬
ْ َ‫ت َوَرﺑ‬ َ ‫ض َﺧﺎﺷ َﻌﺔً ﻓَِﺈ َذآ أ‬
ْ ‫َﻧﺰﻟْﻨَﺎ َﻋﻠَْﻴـ َﻬﺎ ٱﻟْ َﻤﺂءَ ْٱﻫﺘَـﱠﺰ‬ َ ‫ﻚ ﺗَـَﺮى ٱﻷ َْر‬ َ ‫﴿ َوﻣ ْﻦ‬
﴾‫ﺎﻫﺎ ﻟَﻤ ْﺤ ِﻰ ٱﻟْﻤﻮﺗَ ٰﻰ إِﻧﱠﻪُ َﻋﻠَ ٰﻰ ُﻛ ِﻞ َﺷﻲ ٍء ﻗَ ِﺪﻳﺮ‬ ‫ﻴ‬ ‫َﺣ‬‫أ‬ ۤ ‫إِ ﱠن ٱﻟﱠ ِﺬ‬
‫ي‬
ٌ ْ ّ َْ ُ َ َ ْ
Wamin ayatihi annaka tara al-ardha khashiAAatan fa-idha anzalna AAalayha
almaa ihtazzat warabat inna alladhee ahyaha lamuhyee almawta innahu AAala
kulli shay-in qadeerun (Surat Ha-Mim Sajda/Fussilat 41:39)

Tafsir: Na miongoni mwa dalili zake ni kua mnaona kua Ardhi imekauka, na
tunapoimwagia juu yake Maji, hutetemeka na kututumka, bila ya shaka yule
anaeihuisha, ni mwenye kuweza kuwahuisha waliokufa, kwani kwa hakika yeye ni
mwenye kuweza kukadiria juu ya kila kitu.

Hivyo manufaa ya Mvua kua ni kuihuisha Ardhi baada ya kufa kwake na hivyo
kuinawirisha na kua ni yenye kupendeza, kwa kuotesha mimea juu yake na kutoa
matunda mbali mbali lakini hapo hapo anamithilisha manufaa ya mvua juu ya Ardhi na
namna inavyofufuka kua ni sawa na namna inavyowezekana kufufuliwa kwa kila kitu
kilichokufa.
715

Anasema Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu kua: ‘Hakuna hata sehemu moja
ya Ardhi ambayo hua ni yenye kupata mvua zaidi ya sehemu nyengine, bali Allah
Subhana wa Ta’ala hua ni mwenye kuishusha kwa makadirio yake’

Na amesema Imam Abu Abd Allah Sahl Al Tustari kua amesema ‘Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam kua Hivi jee Qur’an haifanani na Maua ya Nyoyo? Hivi jee Imani
haioteshi Utajiri ndani ya Nyoyo? Hivyo jee Mvua haisababishi Maua kuota? Na
jee Tamaa haisababisha Unafiq kuota ndani ya Nyoyo kama vile ambavyo Umande
unavyosababisha Majani kuota?’

Ambapo tunapoiangalia aya basi tunaona kua imetumie neno Ihtazzat ambalo ni lenye
kutokana na neno Hazza ambalo hua linamaanisha Kutikisika, Kutuna, Kututumka,
Kupwita. Hivyo neno Ihtazzat hua linamaanisha Kusisimka.

Na pia aya ikatumia neno Khashiatan ambalo ni lenye kutokana na neno KhashaA
ambalo wengi wetu hua tunalifahamu kua linamaanisha Unyenyekevu. Lakini neno
KhashaA ambalo mbali ya kua linamaanisha Kua na Unyenyekevu, Kujishusha Darja au
Hadhi, Kuinamisha Macho Chini, Kujilinda kwa ajili ya Allah Subhanah wa Taala lakini
pia hua linamaanisha Kavu, Jangwa, Tasa au Kitu au Eneo Lisiloweza kutoa Mazao.

Na bila ya shaka tunapoangalia Mvua inaponyesha kwenye Ardhi ambayo haikupata


Mvua kwa Muda Mrefu basi hua unaona namna sehemu ya juu ya Ardhi hio namna
inavyosisimka na kutetemeka, na hii hua inaonekana kwa macho mara tu Mvua
inapoanza kunyesha, lakini kwa upande mwengine basi hali hii huendelea wakati Mvua
inapokua inanyesha na mara baada ya kumalizika kunyesha, kwa sababu mvuke wa Mvua
unaponyanyuliwa kutoka Baharini na kupandishwa juu basi hua unanyanyuka na sehemu
ya tabaka fulani la mabaki ya chembe chembe ndogo ndogo sana za Madini yanayotokana
na baadhi ya Mimea ya Baharini na Viumbe hai wa Baharini ambazo hua zinaelea juu ya
maji na hua haziwezi kuonekana kabisa na Macho ya Ibn Adam.

Tabaka hili hua linajumuisha ndani yake Madini mbali mbali yanayopatikana Baharini
kama Chumvi, Magnesium, Potassium, Phospohrous, Shaba, Zink, Cobalt, n.k ambalo
hua linapopanda juu Angani pamoja mvuke wa Mvua kwa ajili ya kukusanya Mvua, na
kisha inaponeysha Mvua, kemikali hizi huangushwa Ardhini na kuingia ndani ya Ardhi
kutokana na Mtetemeko wa mwanzo wa tone la Maji, Theluji au Barafu linapotua juu ya
ardhi, na hivyo kuchangia kuendeleza muongezeko wa virutubisho vya Ardhi ambavyo
hua vinahitajika sana katika ukuaji wa mimea mbali mbali ardhini na hivyo hua ni barka
kwa Ardhi husika na pia hunufaisha viumbe waishio juu yake, kama zinavyosema aya.
716

ِ‫ﺼ‬
﴾‫ﻴﺪ‬ ِ ‫ﺐ ٱ ْﳊ‬ ٍ ِِ ِ ِ
َ ‫﴿ َوﻧَـﱠﺰﻟْﻨَﺎ ﻣ َﻦ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤﺂء َﻣﺂءً ﱡﻣﺒَ َﺎرﻛﺎً ﻓَﺄَﻧﺒَـْﺘـﻨَﺎ ﺑﻪ َﺟﻨﱠﺎت َو َﺣ ﱠ‬
Wanazzalna mina alssama-i maan mubarakan faanbatna bihi jannatin wahabba
alhaseedi (Surat Qaf 50:9)

Tafsir : Na tunashusha kutoka Mbinguni Maji yenye Baraka na kufanya juu yake
(Ardhi) kuota Bustani na Punje za Kuvuna.

Ambapo Wanasayansi wanasema kua Ardhi hua inamwagiwa takriban tani Milioni 150
za Madini hayo yanayopatikana Baharini kutokana na Mvua kwa kila mwaka, hivyo hii
hua ni mbolea ya Kimaumbile ambayo inapatikana kutokana na Rehma zake Allah
Subhanah wa Ta’ala kwa ajili ya kuwanufaisha Viumbe wake mbali mbali hapa Duniani,
hivyo bila ya shaka, bila ya kuwepo Mvua basi Ardhi ingekua haikaliki, na ingawa haya
tunayazungumzia leo na kuthibitisha kulingana na kuwepo Uwezo wa Kisayansi, lakini
haya pia yalisemwa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam miaka 1441 iliyopita,
kupitia katika Qur’an ambacho na kitabu cha Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo
kuthibitisha kuwepo kwake yeye Muumba.

Ambapo aya imetumia mfano wa Vyakula vya Punje Punje au Nafaka, ambayo ni kitu
kidogo sana kiasi ya kuaama ukikiona kimeanguka chini ardhini basi utakidharau, tofauti
na chakula chengine kama Matikiti kwa mfano ambayo pia yanaota Uarabuni, lakini sasa
Punje punje hizo hizo ndogo hua na thamani kubwa zinapokua kwenye shuke lake kwa
mfano Ngano au Shairi, ambazo mbali na udogo wake lakini hakuna yeyote anaeweza
kuziumba isipokua mwenyewe Muumba wa kila kitu ambae ni Allah Subhanah wa
Ta’ala na hapo hapo kwa sababu pia ya kua vyakula hivyo ndivyo vyakula vilivyokua
vikitumika sana katika maeneo ya Urabuni kwa kufanyia mikate.

Hivyo Allah Subhana wa Ta’ala amejaalia haya kwa Viumbe wake ili tupate kua ni enye
kumshukuru, Lakini Jeetunaonesha shukurani zetu kwa Mola wetu? Mbali ya namna
tunavyopenda kula kwetu? Hebu na tuangalie mfano anaotupa Hujjat Ul Islami Imam
Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali angalau tupate kujua tofauti ya
Kiimani baina ya hali zetuna waliotangulia kabla yetu, amapo Hujjat ul Islami Imam Al
Ghazali anatuambia kua;

‘Usiku Mmoja katika Mji wa Ray basi watu 20 waliokua na njaa walipata Slesi 2 za
Mkate. Lakini kwa kua walikua wengi basi wakaamua kuziweka juu ya sahani
kisha kuzima taa ili kuweka kiza na hivyo waliojaaliwa kupata riziki yao wapate
riziki yao, na wasiojaaliwa basi iwe sio riziki yao. Hivyo wakakaa kiza kwa dakika
kadhaa, kisha wakawasha taa na walipoangalia juu ya Sahani basi Silesi zilikua ziko
vile vile, kwani kila mmoja alikua anapendelea kua kwanza apate mwenzake riziki
yake kabla ya kupata yeye kwa nafsi yake.’
717

Ambapo tunapoangalia mfano huu basi tuaona kua kwa upande wetu sisi leo hii basi hali
ingekua vyenginevyo, kwani isingebakia hata kipande cha slesi kwenye sahani baada ya
kuwashwa taa, kwani kila mmoja angependa kua slesi hio iwe yake, kutokana na kupenda
Kula, Kufanya Israfu katika Chakula na hivyo kupungukiwa na Imani, tofauti na
waliotangulia kabla yetu.

Kisha baada ya kuelezea namna Mvua inavyoihuisha Ardhi basi Allah Subhanah wa
Ta’ala anatuwekea wazi namna Mvua inavyosababisha kukua kwa mimea na Matunda
tofauti kutokana na Mvua kwa kusema:

ِ ٍ ِ ِ ِ ‫﴿وﻫﻮ ٱﻟﱠ ِﺬ ۤي أ‬
ُ‫َﺧَﺮ ْﺟﻨَﺎ ﻣْﻨﻪ‬ ْ ‫ﺎت ُﻛ ِّﻞ َﺷ ْﻲء ﻓَﺄ‬ َ َ‫َﺧَﺮ ْﺟﻨَﺎ ﺑِﻪ ﻧـَﺒ‬ ْ ‫َﻧﺰَل ﻣ َﻦ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤﺂء َﻣﺂءً ﻓَﺄ‬ َ ََُ
ٍ ‫ﻀﺮاً ﱡﳔْﺮِج ِﻣْﻨﻪ ﺣﺒﺎً ﱡﻣﺘَـﺮاﻛِﺒﺎً وِﻣﻦ ٱﻟﻨﱠﺨ ِﻞ ِﻣﻦ ﻃَْﻠﻌِﻬﺎ ﻗِْﻨـﻮا ٌن داﻧِﻴﺔٌ وﺟﻨ‬
‫ﱠﺎت ِّﻣ ْﻦ‬ ِ‫ﺧ‬
ََ َ َ َ َ ْ َ َ َ َّ ُ ُ َ
‫ﺎب َوٱﻟﱠﺰﻳْـﺘُﻮ َن َوٱﻟﱡﺮﱠﻣﺎ َن ُﻣ ْﺸﺘَﺒِﻬﺎً َو َﻏْﻴـَﺮ ُﻣﺘَ َﺸﺎﺑٍِﻪ ٱﻧْﻈُُﺮ ۤواْ إِِ ٰﱃ َﲦَِﺮﻩِ إِ َذآ أَْﲦََﺮ َوﻳَـْﻨﻌِ ِﻪ إِ ﱠن‬
ٍ َ‫أ َْﻋﻨ‬
﴾‫ت ﻟَِّﻘﻮٍم ﻳـُ ْﺆِﻣﻨُﻮ َن‬ ٍ ‫ِﰱ ٰذﻟِ ُﻜﻢ‬
ْ �‫ﻵ‬ َ ْ
Wahuwa alladhee anzala mina alssama-i maan faakhrajna bihi nabata kulli shay-
in faakhrajna minhu khadiran nukhriju minhu habban mutarakiban wamina
alnnakhli min talAAiha qinwanun daniyatun wajannatin min aAAnabin
waalzzaytoona waalrrummana mushtabihan waghayra mutashabihin undhuroo ila
thamarihi idha athmara wayanAAihi inna fee dhalikum laayatin liqawmin
yu/minoona (Surat Al AnAaam 6:99)

Tafsir: Ni yeye ndie anaeshusha Mvua kutoka Mbinguni, Na ni sisi tunaotoa kutokana
nayo vitu vyote, ni sisi tunaotoa kutokana nayo Mimea ambayo tunatoa nafaka
zilizopangika kwa matabaka. Na kutokana na Mitende tunatoa Matunda ambayo
mashada yake yananing’inia karibu na chini, na tunatoa bustani za Mizabibu na
Mizaituni na Mikomamanga, yaliyofanana lakini ni yenye kutofautiana. Angalia kila
Tunda linapozaliwa na linapopea. Kwa hakika katika haya kuna mafunzo kwa wenye
kuamini.

Anasema Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakkalimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi


kuhusiana na aya hii kua: ‘Kuanzia mwanzoni mwa kuchomoza kwake Tunda mpaka
kupea kwake, basi tund ahusika hua na hali tofauti za kimaumbile na sifa tofauti,
kuanzia kitu kichungua mwanzoni hadi kufikia kua kitamu mwishoni, kuanzia
rangi ya Kijani na kumalizia katika rangi nyekundu, zambarau, manjano n.k na
katika hali yake ya mwisho huanzia kua ni lenye kutia Joto Mwilini na lenye
718

kuupoza Miwli au kinyume chake, kuanzia kilichokua sumu mwanzoni na


kumalizikia katika hali ya kua kitamu, hakika hizi zote ni dalili zinazojibainisha
wazi hatua kwa hatua.’

Ambapo katika Surat Yasin basi Allah Subhnaha wa Ta’ala anasema kuhusiana na
Unyeshaji Mvua katika Ardhi iliyokufa hadi kufufuka kwa na kua ni yenye kutoa
Matunda kwa kusema:

ِ ِ
َ ‫َﺧَﺮ ْﺟﻨَﺎ ﻣْﻨـ َﻬﺎ َﺣﺒّﺎً ﻓَﻤْﻨﻪُ َ�ْ ُﻛﻠُﻮ َن‬
‫۞و َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ‬ ْ ‫ﺎﻫﺎ َوأ‬
َ َ‫َﺣﻴَـْﻴـﻨ‬
ْ ‫ض ٱﻟْ َﻤْﻴـﺘَﺔُ أ‬ُ ‫﴿ َوآﻳَﺔٌ ﱠﳍُُﻢ ٱﻷ َْر‬
‫ﻮن۞ﻟِﻴَﺄْ ُﻛﻠُﻮاْ ِﻣﻦ َﲦَِﺮﻩِ َوَﻣﺎ‬ِ ‫ﺎب وﻓَ ﱠﺠﺮَ� ﻓِﻴﻬﺎ ِﻣﻦ ٱﻟْﻌﻴ‬ ٍ ِ‫ٍ ِ ﱠ‬ ِ
ُُ َ َ ْ َ َ‫ﻓ َﻴﻬﺎ َﺟﻨﱠﺎت ّﻣﻦ ﳔ ٍﻴﻞ َوأ َْﻋﻨ‬
﴾‫َﻋ ِﻤﻠَْﺘﻪُ أَﻳْ ِﺪﻳ ِﻬﻢ أَﻓَﻼَ ﻳَ ْﺸ ُﻜﺮو َن‬
ُ ْ
Waayatun lahumu al-ardhu almaytatu ahyaynaha waakhrajna minha habban
faminhu ya/kuloona; WajaAAalna feeha jannatin min nakheelin waaAAnabin
wafajjarna feeha mina alAAuyooni; Liya/kuloo min thamarihi wama AAamilat-hu
aydeehim afala yashkuroona (Surat Yasin 36:33-35)

Tafsir: Na katika dalili zake kwao ni Ardhi iliyokufa tunaifufua na tunaotesha


kutokana nayo Nafaka ambazo mnakula, na tunatoa kutokana nayo Mabustani ya
Mitende na Mizabibu, Na tunasababisha Chemchem za maji kutoka ndani yake, ili
waweze kula mazao yake. Na sio mikono yao ndio inayofanya hivyo. Hivyo jee
hawashukuru.

Ambapo tunapoiangalia aya basi tunaona kua imetumia neno Habban ambalo kwa Lugha
ya Kiarabu hua linamaanisha Punje au Nafaka, na hua halina Wingi wala Umoja na halina
pia Jinsia.

Na pia ikatumia harfu Mim kabla katika maneno yasemayo ‘wama AAamilat-hu
aydeehim’, hivyo kama tukiichukulia Mim hii kua ni ya Kukanusha basi hapa maneno
haya hua na maana isemayo: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala ameyaumba Matunda ili
tupate kula’, hivyo Matunda haya yameumbwa na Allah Subhanah wa Ta’ala na
hayakuumbwa na Ibn Adam. Na kama Mim hii ikichukuliwa ni Kiwakilishi cha Jina basi
basi aya hii hua inamaanisha: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala ameyaumba Matunda ili
tule huku yakiwa bado Mazuri na pia tuyakamue na kuyafanya Juice, au tuyale
kwa kuyakata vipande vipande n.k’ ambapo maana zote mbili hizi hua ni sahih.
719

Amesema Imam Al Tustari kua: ‘Kua Karibu na Wenye Hikma kwani Allah
Subhanah wa Taala, huzihuisha Nyoyo zilizokufa kama vile anavyoihuisha Ardhi
kwa kuimwagia Mvua.’

Na katika kuhuishwa kwake Ardhi basi hujumuisha pia kuhusiwa kwa Mfumo wa
chakula cha Wanyama mbali mbali Ulimwenguni.

5-DALILI KATIKA UUMBWAJI WA WANYAMA MBALI MBALI.


Katika Uumbwaji wa Wanyama mbali mbali waliotawanyika Ulimwenguni, ambapo
katika sehemu hii aya imetumia neno Daaba ambalo ni lenye Wanyama wanaotembea
ardhini na ingawa linamaanisha Wanyama wadogo wadogo lakini Wanyama hawa wote
ni viumbe wa Allah Subhanah wa Ta’ala.

‫ﺎﺣْﻴ ِﻪ إِﻻﱠ أ َُﻣ ٌﻢ أ َْﻣﺜَﺎﻟُ ُﻜ ْﻢ ﱠﻣﺎ ﻓَـﱠﺮﻃْﻨَﺎ ِﰱ‬ ِ ِ ِ ِ ‫﴿ َوَﻣﺎ ِﻣﻦ َدآﺑﱠٍﺔ ِﰱ ٱﻷ َْر‬
َ َ‫ض َوﻻَ ﻃَﺎﺋ ٍﺮ ﻳَﻄﲑُ ﲜَﻨ‬
﴾‫ﺎب ِﻣﻦ َﺷﻲ ٍء ﰒُﱠ إِ َ ٰﱃ رّﻬﺑِِﻢ ُْﳛ َﺸﺮو َن‬ ِ
ِ َ‫ٱﻟﻜﺘ‬
ُ ْ َ ْ
Wama min dabbatin fee al-Ardhi wala ta-irin yateeru bijanahayhi illa omamun
amthalukum ma farratna fee alkitabi min shay-in thumma ila rabbihim
yuhsharoona (Surat Al Anaam 6:38)

Tafsir: Na hakuna mnyama anaetembea ardhini wala Ndege anaeruka angani kwa
mbawa zake mbili isipokua wa wako kijamii kama nyinyi: Hatukudharau chochote
ndani ya kitabu, kisha mbele ya Mola wao watakusanywa pamoja.

Hii ni miongoni mwa aya zinazozungumzia maumbile ya Wanyama wanaotembea


Ardhini na Ndege wanaoruka angani. Hivyo aya sio kua haikuzungumzia Kuku, Bata n.k
au haizungumzii kuhusiana na Samaki wanaoishi ndani ya Maji la! Bali aya hii
imejumuisha Wanyama wote kwa ujumla kua maisha yao wanaishi kijamii. Na ndio
maana hata Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi
alipoulizwa kuhusiana na kwanini hapa hawakutajwa na Wanyama wanaoishi Baharini
basi alisema: ‘Wanyama wanaoishi Baharini hua wanajumuishwa na wanaoishi
Ardhini kwa sababu wanatambaa ndani ya Maji na pia wanaweza wakawa
wanajumuishwa na Ndege wanaoruka Angani kwa kuelea hewani kwani nao ni
wenye kuelea ndani ya Maji’
720

Ambapo wanyama wote hawa wameumbwa kwa ajili ya Manufaa ya Ibn Adam kwa njia
moja au nyengine, ambapo tunaona katika manufaa ya mfano wa Mnyama wa kufuga
nyumbani kama Ng’ombe kupitia katika aya ifuatayo:

ِ ْ ‫﴿وإِ ﱠن ﻟَ ُﻜﻢ ِﰱ ٱﻷَﻧْـ َﻌ ِﺎم ﻟَﻌِْﺒـﺮًة ﻧﱡﺴ ِﻘﻴ ُﻜﻢ ِّﳑﱠﺎ ِﰱ ﺑُﻄُﻮﻧِِﻪ ِﻣﻦ ﺑَـ‬
ٍ ‫ﲔ ﻓَـﺮ‬
ً‫ث َوَدٍم ﻟﱠﺒَﻨﺎ‬ ْ ْ ْ َ ْ َ
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ِ
َ ِ‫َﺧﺎﻟﺼﺎً َﺳﺂﺋﻐﺎً ﻟﻠﺸﱠﺎ ِرﺑ‬
Wa-inna lakum fee al-anAAami laAAibratan nusqeekum mimma fee butoonihi min
bayni farthin wadamin labanan khalisan sa-ighan lilshsharibeena (Surat An Nahl
16:66)

Tafsir: Na kwa hakika Katika Ng’ombe kuna mafunzo kwa ajili yenu. Kwani
tunakupeni kile ambacho ni cha kukinywa kutoka Matumboni mwao, baina ya Choo
na Damu mnapata Maziwa Safi yenye ladha nzuri kwa Wanywaji.

Ambapo tunapowachunguza Wanyama mbali mbali namna wanavyoishi katika Jamii zao
basi tunaona kua wanaishi kijamii na hii inadhihirishwa na aya inayoainisha mfano wa
mdudu mdogo aitwae Sisimizi:

‫۞ﺣ ﱠ ٰﱴ إِذَآ أَﺗَـ ْﻮا‬ ِ ْ‫ﻮدﻩُ ِﻣ َﻦ ٱ ْﳉِ ِّﻦ َوٱ ِﻹﻧ‬ ِ ِ


َ ‫ﻮزﻋُﻮ َن‬ َ ُ‫ﺲ َوٱﻟﻄﱠِْﲑ ﻓَـ ُﻬ ْﻢ ﻳ‬ ُ ُ‫﴿ َو ُﺣﺸَﺮ ﻟ ُﺴﻠَْﻴ َﻤﺎ َن ُﺟﻨ‬
‫ﺖ ﳕَْﻠَﺔٌ ٰ�َﻳـﱡ َﻬﺎ ٱﻟﻨ ْﱠﻤ ُﻞ ْٱد ُﺧﻠُﻮاْ َﻣ َﺴﺎﻛِﻨَ ُﻜ ْﻢ ﻻَ َْﳛ ِﻄ َﻤﻨﱠ ُﻜ ْﻢ‬ ِ
ْ َ‫َﻋﻠَ ٰﻰ َوادى ٱﻟﻨ ْﱠﻤ ِﻞ ﻗَﺎﻟ‬
﴾‫ﻮدﻩُ وُﻫﻢ ﻻَ ﻳَ ْﺸﻌُﺮو َن‬
ُ ْ َ ُ ُ‫ُﺳﻠَْﻴ َﻤﺎ ُن َو ُﺟﻨ‬
Wahushira lisulaymana junooduhu mina aljinni waal-insi waalttayri fahum
yoozaAAoona; Hatta idha ataw AAala wadi alnnamli qalat namlatun ya ayyuha
alnnamlu odkhuloo masakinakum la yahtimannakum sulaymanu wajunooduhu
wahum la yashAAuroona (Surat An Naml 27:17-18)

Tafsir: Na akakusanya Sulayman jeshi lake miongoni mwa Majini na Watu na Ndege
hukua wakiwa katika Mwendo wa Maandamo. Mpaka walipofika katika Bonde la
Sisimizi na mmoja katia ya Sisimizi akasema: ‘Enyi Sisimizi Ingieni katika Majumba
yenu ili asije Sulayman na Jeshi lake akakuvunjeni wakati wakiwa hawana habari
nanyi’
721

Ambapo kulingana na Mtizamo wa Imam Ibn Maymunah basi Sisimizi huyu alikua
akiitwa Takhiya na kwa upande wa Imam Ad Dahhaq Ibn Muhazim basi anasema
kua Sisimizi huyu alikua akiitwa Khurma. Na tunapokiangalia kisa hiki bila ya
kutafakkari basi tunaona kua hakina uzito wowote ndani yake, lakini ukweli ni kua hii ni
aya inayothibitisha kua Hata wadudu nao pia wako kama Ibn Adam yaani wanaishi
kijamii.

Kwani Wadudu Sisimizi hua ni wenye kushirikiana katika majukumu yao kiasi ya kua
wakipata chakula basi hukihifadhi na wanapokua hua wanakula kwa pamoja na hua
wanakitafuta kwa pamoja. Na Sisimizi anapotoka kutafuta chakula basi hua anamwaga
aina fulani ya kemikali ambayo hua ni njia inayomuongoza ili asipotee akirudi.

Na huendelea na safari yake mpaka akute chakula, na akishakikuta basi huacha Kemikali
ambayo inaonesha sehemu aliyopata chakula husika, kisha anarudi kwenye Nyumba yao
huku njia nzima akiwa ameacha chemikali hio ili kuwaelekeza wenzake wapi kinpatikana
chakula hicho alichokuja nacho na kua chakula chengine kimebakia huko alikokitoa. Na
Sisimizi wa mwisho ambao ataondoka na kumalizia chakula cha mwisho kilichoonekana
basi nae huacha kemikali ya kutaarifu kua upande huo hakuna tena chakula ili wenzake
wasihangaike tena kutafuta chakula katika upande huo.

Ama uthibitisho mwengine ni ule unaoonekana pale tunapoangalia kuhusiana na namna


Wanyama wanavyohama kutoka katika sehemu Moja kuelekea katika sehemu nyengine
katika Nyakati tofauti kulingana na Mabadiliko ya hali ya Misimu ya Mwaka, ikiwemo
miongoni mwa Samaki, Ndege, Wanyama wa Mwituni n.k kwani hua hawahami mmoja
mmoja bali hua wanahama kwa pamoja kundi zima.

Na hili linathibitisha kua Wanyama katika kuumbwa kwao basi sio kua hawakujaaliwa
kua na Ufaham, kwani ufaham wanao, na hivyo hua ni wenye kuhama kwa ajili ya
kutafuta chakula chao, kwa mfano baadhi ya ndege hua wanahama pale hali ya hewa
inapokua baridi kali au joto kali na hivyo Ardhi hua ngumu na kutokana na kushindwa
kuweza kutoa wadudu ndani ya ardh, wadudu ambao nao huhama kutoka juu ya Ardhi
na kuhamia chini zaidi kutokanana mazingira ya juu juu ya Ardhi kua magumu kwao
kujitafutia chakula na hivyo kutokana na kuhama kwa wadudu hao basi Ndege nao
huamua kuhamia kwenye sehemu yenye ulaini wa ardhi.

Kwa mfano kuna ndege ambao wanaishi New Zealand ambao huamua kufanya Hijra ya
kuhamia Alaska ambao ni umbali wa kilomita 10000. Ndege hawa wanapohama hua ni
wenye kutumia ufaham ambao wamejaaliwa na Allah Subhanah wa Ta’ala wa kua na
uwezo wa kujua Muelekeo wa wanakoelekea au wanakorudi katika wakati wa Usiku kwa
kutumia Nyota na Mchana hua kwa kutumia Jua kutokana na nguvu za kimaumbile za
mvutano wa Sumaku zinazalishwa na Nuru ya Jua.
722

Na hata katika kuelea kwao hua ni kutokana na Maumbile yao waliyopewa na Muumba
wao, na Maumbile ya Hewa kuwa na uwezo wa Kuwabeba na hivyo wakawa ni wenye
kuelea juu juu angani kama zinavyoelea Meli juu ya maji na ni kutokana na Mamubile
hayo basi ndio Ibn Adam akajifunza na kua na uwezo wa kutengeneza Ndege. Allah
Subhanah wa Ta’ala anazungumzia Maumbile ya Ndege kwa kusema kama zinavyosema
aya:

ِ ِ ‫ات ِﰱ ﺟ ِﻮ ٱﻟ ﱠﺴﻤ‬
‫ﺂء َﻣﺎ ﳝُْ ِﺴ ُﻜ ُﻬ ﱠﻦ إِﻻﱠ ﱠ‬ ٍ ‫﴿أََﱂ ﻳـﺮواْ إِ َ ٰﱃ ٱﻟﻄﱠ ِﲑ ﻣﺴ ﱠﺨﺮ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟُ إِ ﱠن ِﰱ ٰذﻟ‬
‫ﻚ‬ َ َّ َ َُ ْ ْ ََ ْ
﴾‫ت ﻟَِّﻘﻮٍم ﻳـُ ْﺆِﻣﻨُﻮ َن‬
ٍ
ْ �َ ‫َﻵ‬
Alam yaraw ila alttayri musakhkharatin fee jawwi alssama-i ma yumsikuhunna illa
Allahu inna fee dhalika laayatin liqawmin yu/minoona (Surat An Nahl 16:79)

Tafsir: Hivi Jee hawaoni namna Ndege anavyoruka katikati angani? Hakuna
anaemzuia (ili aelee) isipokua Allah. Hakika katika haya kuna Dalili kwa Watu wenye
kuamini.

Ambapo anasem Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakkalimin Imam Fakhr Ad Di Al Razi


kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala amewaumba Ndege katika maumbile ambayo,
yanawarushusu kuelea Angani, na akaijaalia Anga kua ni sehemu ambayo
inawezekana Kuelea Juu yake. Ama kwa Ndege basi amewapa Mbawa ambazo
zinakunjika na kunyooka, na akijaalia Anga ni yenye kupenyeka kutokana na
maumbile yake. Hivyo basi vyote viwili hivyo Ndege na Anga vimejaaliwa
Maumbile ambayo yanaruhusu kitendo cha kuelea kua ni chenye kutokea kwake. ’

‘Hivyo kimaumbile hapa hua kuna Udhibiti na Mwenye kudhibitiwa, ambapo


mwenye kudhibitiwa hua ni hana njia nyengine isipokua kutii kikamilifu matakwa
ya Allah Subhanah wa Ta’ala na kukubaliana na majaaliwa yake juu yake, na hivyo
kua ni yenye kuendana na malengo ya kudhibitiwa kwake. Na hivyo kutokua hali
nyengine yoyote ile isipokua ile ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala ameijaalia kua
nayo na kujisalimisha chini ya Uwezo wa Allah Subhanah wa Ta’ala. Na kutokana
na kujaaliwa kwake kitu hicho kua na maumbile yake hayo basi hua ni chenye
kufikia Malengo ambayo yenye manufaa nacho kitu husika na hivyo hua ni chenye
kuendana katika utaratibu mzuri wa kimaumbile na hivyo kua ni chenye kuonesha
Hikma na Rehma za Allah Subhanah wa Ta’ala. ’

Ama kwa upande wa Samaki basi hua ni wenye kufuata mabadiliko ya ladha ya Maji ya
Bahari na pia hutumia muonekano wa sakafu ya Mchanga wa chini baharini na hivyo hua
723

ni wenye kujau kua wanaelekea upande fulani, na baadhi ya samaki hutumia hisia ya
harufu kurudi katika sehemu waliyotaga mayai yao mei kadhaa hapo kabla kama vile
wanavyotumia harufu Wanyama wa Msituni ambao wao hua ni wenye kutumia hisia ya
harufu ya Mvua katika kuhama kwao.

Amesema Imam Sufyan Ibn Uyaynah kua: ‘Hakuna Miongoni mwa Jamii ya Watu
isipokua kuna kufanana na miongoni mwa Wanyama. Kwani kuna Mtu miongoni
mwao ambae hua na Tabia kama za Chui katika kuvamia kwake, kuna anaekimbia
kama Mbwa mwitu na kuna anaebweka kama anavyobweka Mbwa, kuna
anaecheza kama anavyocheza Tausi na pia kuna mwenye tabia za Nguruwe:
hujulikana kutokana na kua ukimuwekea chakula kizuri mbele yake hatokila lakini
ukimuwekea matapisha ya mtu basi atakula. Na kuna miongoni mwenu ambae
atasikia maneno hamsini ya Hikma na hatohifadhi hata moja lakini akisikia neno
moja tu ovu basi huhifadhi. Hivyo enyi ndugu zangu fahamuni kua kila unapokaa
hua kuna mnyama pembeni yako kwa hivyo kua makini.’

Hivyo katika kuumbwa Wanyama mna dalili nyingi sana, na kila kitu kilichomo
Ulimwenguni kinajulikana na Muumba kwani yeye andie aliekiumba na hivyo hua ni
mwenye kukiandikia Riziki yake nani mwenye kujua kila kitu juu yake kama inavyosema
aya ifuatayo:

‫ٱﻪﻠﻟِ ِرْزﻗُـ َﻬﺎ َوﻳَـ ْﻌﻠَ ُﻢ ُﻣ ْﺴﺘَـ َﻘﱠﺮَﻫﺎ َوُﻣ ْﺴﺘَـ ْﻮَد َﻋ َﻬﺎ ُﻛﻞﱞ‬ ِ ‫﴿ َوَﻣﺎ ِﻣﻦ َدآﺑﱠٍﺔ ِﰱ ٱﻷ َْر‬
‫ض إِﻻﱠ َﻋﻠَﻰ ﱠ‬
﴾‫ﲔ‬ٍ ِ‫ﺎب ﱡﻣﺒ‬ ٍ َ‫ِﰱ ﻛِﺘ‬
Wama min dabbatin fee al-Ardhi illa AAala Allahi rizquha wayaAAlamu
mustaqarraha wamustawdaAAaha kullun fee kitabin mubeenin (Surat Hud 11:6)

Tasfir: Na hakuna katika Mnyama ambae anatembea ardhini isipokua riziki yake hua
ni kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala, na yeye ni mwenye kujua sehemu anayoishi
(Mnyama huyo) na sehemu atakayofia (Mnyama huyo) kwani kila kitu kimo kwenye
kitabu chenye kubainisha.

Ambapo kulingana na mtizamo wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi tunaona
yeye anasema kua: ‘Neno Mustaqarr hua linamaanisha sehemu wanayorudia wakati
wa jioni kwa ajili ya kulala, na neno Mustawda hua linaamisha sehemu ambayo
Watakayokufa na kumalizia Uhai wao hapa Duniani.’
724

Na kwa upande wa Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema kua:
‘Neno Mustaqarr hua linamaanisha tumboa la Uzazi alilozaliwa, na neno Mustawda
hua linaamisha sehemu ambayo Watakayokufa na kumalizia Uhai wao hapa
Duniani’

6-DALILI KATIKA MAUMBILE YA HALI YA UPEPO WA ALRIYYAH


Katika Mumbile ya Kuvuma kwa Hewa yaani Upepo na kukusanywa kwa Mawingu,
ambapo tukio hili limetajwa kwa mara ya kwanza na Qur’an katika aya ie aya isemayo:

ِ ِِ ِ ِِ ٍ ِ ِ ‫آ�ﺗِِﻪ أَن ﻳـُْﺮِﺳﻞ‬ ِ


‫ﻚ‬ َ ‫ٱﻟﺮَ� َح ُﻣﺒَ ّﺸَﺮات َوﻟﻴُﺬﻳ َﻘ ُﻜ ْﻢ ّﻣﻦ ﱠر ْﲪَﺘﻪ َوﻟﺘَ ْﺠ ِﺮ‬
ُ ‫ى ٱﻟْ ُﻔ ْﻠ‬ ّ َ َ ‫﴿ َوﻣ ْﻦ‬
﴾‫ﻀﻠِ ِﻪ وﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜﻢ ﺗَ ْﺸ ُﻜﺮو َن‬ ِ ِ ِ ِ
ُ ْ َ ْ َ‫ﺄﺑ َْﻣ ِﺮﻩ َوﻟﺘَـْﺒـﺘَـﻐُﻮاْ ﻣﻦ ﻓ‬
Wamin ayatihi an yursila alrriyaha mubashshiratin waliyudheeqakum min
rahmatihi walitajriya alfulku bi-amrihi walitabtaghoo min fadhlihi
walaAAallakum tashkuroona (Surat Ar Rum 30:46)

Tafsir: Na miongoni mwa alama zake ni kua anakutumieni Upepo kama bashirio jema
kukuonjesheni nyinyi Rehma zake, na Vyombo vya baharini visafiri kwa amri yake,
na nyinyi mpate kutafuta fadhila zake ili mpate kua ni wenye kushukuru.

Aya yetu hii imetumia neno AlRriyaha ambalo ni lenye kutokana na neno Raha. Neno
Raha ni neno Lenye kumaanisha Kufanya Kitu fulani katika wakati wa Jioni au Kuenda
sehemu fulani katika wakati wa Jioni.

Neno Raha ndio lililotoa neno Rihun ambao humaanisha Upepo, Nguvu, Uwezo,
Udhibiti, Utawala, Ushindi, Kitu kizuri na Kisafi kabisa na pia humaanisha Msaada dhidi
ya Maadui yaani Adhabu na pia humaanisha Rehma na Huruma kutoka kwa Allah
Subhanah wa Ta’ala kama lilivyofafanuliwa na aya ifuatayo:
725

‫ﲔ ﻳَ َﺪ ْى‬ ِ ‫﴿أَﱠﻣﻦ ﻳـﻬ ِﺪﻳ ُﻜﻢ ِﰱ ﻇُﻠُﻤ‬


ِ ‫ﺎت ٱﻟْﺒَـ ِﺮ َوٱﻟْﺒَ ْﺤ ِﺮ َوَﻣﻦ ﻳـُْﺮِﺳﻞ‬
َْ ‫ٱﻟﺮَ� َح ﺑُ ْﺸًﺮى ﺑَـ‬
ّ ُ ّ َ ْ َْ
﴾‫ٱﻪﻠﻟ َﻋ ﱠﻤﺎ ﻳُ ْﺸ ِﺮُﻛﻮ َن‬
ُ‫ﺎﱃ ﱠ‬َ ‫ٱﻪﻠﻟِ ﺗَـ َﻌ‬
‫َر ْﲪَﺘِ ِﻪ أَإِﻟَـٰﻪٌ ﱠﻣ َﻊ ﱠ‬
Amman yahdeekum fee dhulumati albarri waalbahri waman yursilu alrriyaha
bushran bayna yaday rahmatihi a-ilahun maAAa Allahi taAAala Allahu AAamma
yushrikoona (Surat An Naml 27:63)

Tafsir: Ama (jee sio bora yule ambae) anaekuongozeni katika kiza cha Ardhini na
Baharini na akakutumieni Upepo kua bashirio jema linalobainisha msaada wa
Rehma zake, Jee kuna Mungu pamoja na Allah alietukuka? Yuko mbali na
wanavyomshirikisha navyo.

Tunapoangalia kwa upande wa neno Raha linapotumika katika hali ya wingi na hivyo
kutamkika kama Al Riyyaha kama katika mfano wa aya hizi basi hua linamaanisha
Rehma au Neema ya Allah Subhanah wa Ta’ala kwa Viumbe wake kama pia lilivotumika
katika aya ifuatayo:

﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ِ ِ ‫ٱﻟﺮ�ح ﻟَﻮاﻗِﺢ ﻓَﺄ‬


َ ‫َﺳ َﻘْﻴـﻨَﺎ ُﻛ ُﻤﻮﻩُ َوَﻣﺂ أَﻧْـﺘُ ْﻢ ﻟَﻪُ ﲞَﺎ ِزﻧ‬ َ َ َ َ َِّ ‫﴿ َوأ َْر َﺳ ْﻠﻨَﺎ‬
ْ ‫َﻧﺰﻟْﻨَﺎ ﻣ َﻦ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤﺂء َﻣﺎءً ﻓَﺄ‬
Waarsalna alrriyaha lawaqiha faanzalna mina alssama-i maan faasqaynakumoohu
wama antum lahu bikhazineena (Surat Al Hijr 15:22)

Tafsir: Na tunatuma Upepo Mwingi wenye kupandikiza, Na kisha tunateremsha


kutoka Mbinguni Maji na kukupeni nyinyi mkanywa, na sio nyinyi ambao ndio wenye
hazina yake.

Ambapo Aya imetumia neno Lawaqiha ambalo ni leye kutokana na neno Laqaha lenye
kumaanisha Kutia Mimba, Kupandikiza, Kurutubisha, Kusababishia Kuzaa, Kutoa
Matunda kutokana na kilichopandikizwa, Kusababisha Mawingu kutoa Mvua na pia
huaanisha Kutia Chanjo.

Hivyo maneno Alrriyaha lawaqiha hua yanamaanisha Aina ya Upepo mwingi ambao ni
wenye kunyanyua na kuyakusanya Mawingu ambayo ni yenye kuzalisha Mvua, Upepo
ambao ni wenye kubeba Mvuke wa Maji kutoka Baharini kuelekea Juu ardhini kisha
ukasababisha Mawingu ya Mvua, na pia yanamaanisha Upepo ambao hua ni wenye
Kubeba Unga (Pollen) laini wa Mbegu za Uzazi za Maua Jike na Dume na Kuzipandikiza
katika Maua.
726

Ambapo kwa upane wa Imam Abu Al Thana Shihab Ad Din Sayyid Mahmud Ibn Abd
Allah Al Husayni Al Alusi Al Baghdad anasema kuhusiana na Upepo huu kua: ‘Huu hua
ni Mzunguko wa Upepo ambao hua unasambaa katika sehemu tofauti kwa sababu
kama Upepo unakusanywa pamoja na kuelekezwa katika sehemu moja au
muelekeo mmoja basi Upepo huo hua na Nguvu kubwa sana ya Maangamizo ya
kuangamiza kila kitu katika njia yake. Kwa hivyo basi Upepo huu unachukuliwa
kua ni Upepo Mwingi unaosambaa na kupepea sehemu tofauti na kutawanyika
katika pande tofauti na muhimu kuliko yote ni kua aina hii ya wingi wa Upepo hua
unasaidia kuchanganya Mawingu, na kusafisha hali ya hewa na kupandikiza
Mawingu.’

Ambapo kwa Mtizamo wa Shaykh ul Islami Imam Muhammad Tahir Ibn Ashur basi yeye
anasema kua: ‘Upepo hua ni wenye kusafirisha Unga wa uzazi wa Maua kutoka
katika Mti wa Kike kuupeleka katika Mti wa Kiume na hapo hapo Mti wa kike hua
tayari uliokwisha pandikizwa na utazaa na matokeo yake hua ni kupatikana kwa
mazao.’

Ambapo Imam Ibn Ashur anaendelea kutuambia kua: ‘Upepo unaobashiria Bashirio
Jema la Mvua hua ni Upepo Mlaini, Mwepesi na wenye Rehma ndani yake’ kama
alivyosema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

ً‫ﺖ َﺳ َﺤﺎﺎﺑً ﺛَِﻘﺎﻻ‬ ِِ


ْ ‫ﲔ ﻳَ َﺪ ْى َر ْﲪَﺘﻪ َﺣ ﱠ ٰﱴ إِذَآ أَﻗَـﻠﱠ‬َْ ‫ﺮى ﺑَـ‬ ِ ‫﴿ َوُﻫﻮ ٱﻟﱠ ِﺬى ﻳـُْﺮِﺳﻞ‬
ً ‫ٱﻟﺮَ� َح ﺑُ ْﺸ‬
ّ ُ َ
ِ ِ ‫ﺖ ﻓَﺄَﻧْـﺰﻟْﻨﺎ ﺑِِﻪ ٱﻟْﻤﺂء ﻓَﺄَﺧﺮﺟﻨﺎ ﺑِِﻪ ِﻣﻦ ُﻛ ِﻞ ٱﻟﺜﱠﻤﺮ‬ ٍ ِ
‫ِج‬
ُ ‫ﻚ ُﳔْﺮ‬ َ ‫ات َﻛ ٰﺬﻟ‬ ََ ّ َْ َْ َ َ َ َ ٍ ِّ‫ُﺳ ْﻘﻨَﺎﻩُ ﻟﺒَـﻠَﺪ ﱠﻣﻴ‬
﴾‫ٱﻟْﻤﻮﺗَ ٰﻰ ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜﻢ ﺗَ َﺬ ﱠﻛﺮو َن‬
ُ ْ ْ
Wahuwa alladhee yursilu alrriyaha bushran bayna yaday rahmatihi hatta idha
aqallat sahaban thiqalan suqnahu libaladin mayyitin faanzalna bihi almaa
faakhrajna bihi min kulli alththamarati kadhalika nukhriju almawta laAAallakum
tadhakkaroona (Surat Al Araf 7:57)

Tafsir: Yeye ndie ambae anaeshusha Upepo Mwingi kua bashirio jema linalobainisha
msaada wa Rehma zake, mpaka unapobeba Mawingu yaliyojaa na kisha
tunayasukuma katika Ardhi iliyokufa na kisha tunashusha Maji juu yake na kisha
hutoa kutokana nayo kila aina ya Matunda, na mithili yake tutakavyowafufua
waliokufa ili mpate kukumbuka.
727

DALILI KATIKA MAUMBILE YA HALI YA UPEPO WA RIHAN


Neno Raha linapotumika katika hali ya Umoja ambapo hutamkwa kama Al Rihi au Rihan
basi hua linamaanisha Adhabu Kali Sana ya aina fulani ya Upepo wenye Kuangamiza
kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala na hii hua kama vile lilivyotumika neno Rihu
katika aya ifuatayo:

ِ ِ ِ‫﴿ﺣﻨـ َﻔﺂء ﱠﻪﻠﻟِ َﻏﻴـﺮ ﻣ ْﺸ ِﺮﻛِﲔ ﺑِِﻪ وﻣﻦ ﻳ ْﺸ ِﺮْك ﺑِ ﱠ‬


ُ‫ﭑﻪﻠﻟ ﻓَ َﻜﺄَﱠﳕَﺎ َﺧﱠﺮ ﻣ َﻦ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤﺂء ﻓَـﺘَ ْﺨﻄَُﻔﻪ‬ ُ َ َ َ ُ َ ْ َ َُ
﴾‫ﺎن َﺳ ِﺤ ٍﻴﻖ‬ ٍ ‫ٱﻟﺮﻳﺢ ِﰱ ﻣ َﻜ‬ ِِ
َ ُ ِّ ‫ٱﻟﻄﱠْﻴـُﺮ أ َْو ﺗَـ ْﻬ ِﻮى ﺑﻪ‬
Hunafaa lillahi ghayra mushrikeena bihi waman yushrik biAllahi fakaannama
kharra mina alssama-i fatakhtafuhu alttayru aw tahwee bihi alrreehu fee makanin
saheeqin (Surat Al Hajj 22:31)

Tafsir: Kutomuabudu yeyote yule isipokua Allah, Kutomshirikisha, Na Kwa yeyote


Yule Mwenye kumshirisha Allah, hua kama ni yule ambae ameanguka kutoka
Mbinguni na kisha Ndege wakamnyakua kwa nguvu (wakamteka Nyara), au Upepo
ukampeperusha yeye katika sehemu ya mbali kabisa.

Ambapo aya katika kufafanua kwake imetumia neno Khatafa ambalo humaanisha
Kukwapua, Kunyakua, Kuiba, Kuteka Nyara kwa nguvu na kisha kukimbia kwa kasi
kubwa sana.

Hivyo inatuwekea wazi kua Kumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala kunampandisha mtu
Darjaya Juu kabisa na Kumshirikisha hua ni kumporomosha mtu huyo kutoka Mbinguni
ambapo ingawa kwa Maumil ya Dunia basi kila kinachoanguka kutoka juu hua ni chenye
kukimbilia chini, na ndio maana Waswahili wakasema kua alie juu mngoje chini yaani
kwa vyovyote vile atashuka chini, lakini aya hii inasema vyenginenvyo, kwani Allah
Subhanah wa Ta’ala ananasibisha kitendo cha kufanya Kufuru hua ni sawa na Mtu
anaeanguka lakini hata hivyo kabla ya kufika chini, basi juu kwa juu akanyakuliwa na
Ndege aina ya Eagle au Upepo Mkali sana na hivyo kwa Mtu huyo hua hakuna salama
kwani hua haijulikani mwisho wake utakua vipi, atapatikana ama la, atakua salama ama
la, na bila ya shaka mtu kama huyu hua ni aliepotea na hivyo hua hana usalama. Hivyo
angalau huyo alieanguka na akafika chini na akaonekana, kuliko yule ambae alieanguka
na kabla ya kufika chini akatoweka.
728

Na kwa Upande wa Jarrah Allah Sultan Al Balagha Imam Abu Qasim Al Zamakhshari
basi anasema kuhusiana na aya hii kua: ‘Kumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala hua
ni sawa na Mbingu na Urefu wake, ambapo kumshirikisha na chochote kile hua ni
sawa na kuanguka kutoka juu Mbinguni, ambapo mawazo maovu hua ni sawa na
Ndege ambao humnyakua mtu na Shaytan anaelezewa kua ni sawa na Upepo Mkali
sana ambao humpeperusha mbali sana Mtu mwenye kufanya Kufr ’

Ili kupata kufaham zaidi maana ya Rihan ambayo ni hali ya umoja ya Upepo ambao
humaanisha Maangamizi basi na tuangalie kama vile ilivyotumika katika aya zifuatazo:

‫۞ﺳ ﱠﺨَﺮَﻫﺎ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ َﺳْﺒ َﻊ ﻟَﻴَ ٍﺎل َوَﲦَﺎﻧِﻴَﺔَ أ ﱠَ�ٍم‬ ٍ ‫ﻳﺢ ﺻﺮﺻ ٍﺮ ﻋﺎﺗِﻴ‬
‫ﺔ‬ َ َ َ ٍ ِ
‫ﺮ‬ ِ‫ﺎد ﻓَﺄ ُْﻫﻠِ ُﻜﻮاْ ﺑ‬
ٌ ‫﴿ َوأ ََﻣﺎ َﻋ‬
َ َ ْ
‫ﺻْﺮ َﻋ ٰﻰ َﻛﺄَﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ أ َْﻋ َﺠ ُﺎز َﳔْ ٍﻞ َﺧﺎ ِوﻳٍَﺔ۞ﻓَـ َﻬ ْﻞ ﺗَـَﺮ ٰى َﳍُﻢ ِّﻣﻦ‬ ِ
َ ‫ُﺣ ُﺴﻮﻣﺎً ﻓَـﺘَـَﺮى ٱﻟْ َﻘ ْﻮَم ﻓ َﻴﻬﺎ‬
﴾‫َﺎﺑﻗِﻴَ ٍﺔ‬
Waamma AAadun faohlikoo bireehin sarsarin AAatiyatin; Sakhkharaha
AAalayhim sabAAa layalin wathamaniyata ayyamin husooman fatara alqawma
feeha sarAAa kaannahum aAAjazu nakhlin khawiyatun; Fahal tara lahum min
baqiyatin (Surat Al Haaqa 69:6-8)

Tafsir: Na ama Aad wameangamizwa kwa Upepo Mkali sana. Alioulazimisha Allah
Juu yao kwa usiku saba na michana minane mfululizo, kiasi ya kua ungeweza kuona
watu wa jamii yao wameangushwa, kama kwamba ni mabua ya magogo ya Mitende.
Jee mnaona mabaki yao?

Subhana Allah! Aya inawazungumzia watu wa Al Ahqaf ambayo ni maeneo yenye


udongo mgumu mwekundu unaoambatana na chungu nyingi sana za mkusanyiko wa
Mchanga wa Jangwani zilizopinda pinda na kuchora maumbo ya nusu mwezi ya chungu
za nyingi mchanga.

Ambapo haya hayakua ni maeneo yeyote isipokua maeneo ya Watu wa Kabila la Aad,
ambao ni watu wa Nabii Hud ambapo kama tulivyosema kua Kabila au Jamii ya watu wa
Aad walikua ni wenye kuishi katika maeneo ya Al Ahqaf ya upande wa Kusini yaani kwa
maana hio, basi watu hawa walikua ni waishio katika eneo la Ardhi ya baina ya
Hadhramawt nchini Yemen na Oman, ambapo pia kuna baadhi ya wasemao kua eneo hili
pia limeingia mpaka katika sehemu ya Kusini ya Ardhi ya Saudia.
729

Ambao Allah Subahanh wa Ta’ala aliwatumia Mtume wao ambae ni Nabii Hud
aliewausia lakini wakamkanusha kwa sababu ya neema waliyojaaliwa na Mola wao kama
alivyowakumbusha Nabii wao huyo kwa kusema:

‫ﻨﺬ َرُﻛ ْﻢ َوٱذ ُﻛُﺮ ۤواْ إِ ْذ‬


ِ ‫﴿أَو ﻋ ِﺠﺒـﺘﻢ أَن ﺟﺂء ُﻛﻢ ِذ ْﻛﺮ ِﻣﻦ ﱠرﺑِ ُﻜﻢ ﻋﻠَﻰ رﺟ ٍﻞ ِﻣﻨ ُﻜﻢ ﻟِﻴ‬
ُ ْ ّ ُ َ ٰ َ ْ ّ ّ ٌ ْ َ َ ُْْ َ َ
‫ٱﳋَْﻠ ِﻖ ﺑَ ْﺴﻄَﺔً ﻓَﭑذْ ُﻛُﺮ ۤواْ آﻵءَ ﱠ‬
ِ‫ٱﻪﻠﻟ‬ ٍ ُ‫َﺟ َﻌﻠَ ُﻜ ْﻢ ُﺧﻠَ َﻔﺂءَ ِﻣﻦ ﺑَـ ْﻌ ِﺪ ﻗَـ ْﻮِم ﻧ‬
ْ ‫ﻮح َوَزا َد ُﻛ ْﻢ ِﰱ‬
﴾‫ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜﻢ ﺗـُ ْﻔﻠِ ُﺤﻮ َن‬
ْ
Awa AAajibtum an jaakum dhikrun min rabbikum AAala rajulin minkum
liyunthirakum waodhkuroo idh jaAAalakum khulafaa min baAAdi qawmi noohin
wazadakum fee alkhalqi bastatan faodhkuroo alaa Allahi laAAallakum
tuflihoona(Surat Al Araf 7:69)

Tafsir: Hivi jee mnastaajabu kua umekuja ukumbusho kutoka kwa Mola wenu kupitia
kwa Mtu ambae ni kutoka miongoni mwenu, na Kumbukeni kua amekujaalieni kua
Makhalifa baada ya Watu wa Nabii Nuh, na Kakuzidishieni Maumbile makubwa
miongoni mwa Viumbe hivyo Kumbukeni Neema za Allah ili muwe ni wenye kufuzu

Ambapo watu hawa wanasifiwa kua walikua na sifa ya watu wenye Maumbile ambayo
hawakuwahi kupewa watu wengine na kuiainisha sifa hio kwa kuumia neno Bastatan
ambalo ni lenye kutokana na neno Basata ambalo hua linamaanisha Kukuza, Kuongeza
Ukubwa, Kuvuta kama mpira mpaka mwisho wa uvutwaji wake, Kutanua, Kutosheleza
Ukubwa wake, Kupata Kitu kwa wingi zaidi ya Kutosha.

Hivyo basi aya inatuwekea wazi kua Miili ya Watu hawa ilikua haina Mfano wake
Kiukubwa, Kinguvu, Kiafya, Kiurefu na Kiupana ambapo anasema Bahr ul Ilm Abd
Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Urefu wa kila mmoja kati ya Watu hawa
ulikua ni Dhiraa 80’ Na Dhiraa Moja na Robo hua na ukubwa wa Futi 2, sasa hapa
tunazungumzia Urefu wa mtu mwenye urefu wa Futi 120.

Watu hawa pia walikua na Mali nyingi sana kiasi ya kua walikua wakifanya Israfu kwa
kujenga Majumba ya Dhahabu kwa ajili ya kujionesha tu, bila ya kua ni wenye kukaa
ndani yake, na pia kutokana na Ukubwa wao basi walikua wakivamia Mji wa watu
wengine basi walikua wakiteketea kila kitu kwa kutumia nguvu kubwa sana.
730

‫۞وإِ َذا ﺑَﻄَ ْﺸﺘُ ْﻢ‬ ِ ‫ﱠﺨ ُﺬو َن ﻣ‬


ِ ‫﴿أَﺗَـﺒـﻨُﻮ َن ﺑِ ُﻜ ِﻞ ِرﻳ ٍﻊ آﻳﺔً ﺗَـﻌﺒـﺜُﻮ َن۞وﺗَـﺘ‬
َ ‫ﺼﺎﻧ َﻊ ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜ ْﻢ َﲣْﻠُ ُﺪو َن‬
َ َ َ َْ َ ّ ْ
﴾‫ﻮن‬ِ ‫َﻃﻴﻌ‬ ِ ‫ﺑﻄَ ْﺸﺘُﻢ ﺟﺒﱠﺎ ِرﻳﻦ۞ﻓَﭑﺗﱠـ ُﻘﻮاْ ﱠ‬
ُ ‫ٱﻪﻠﻟَ َوأ‬ َ َ ْ َ
Atabnoona bikulli reeAAin ayatan taAAbathoona; Watattakhidhoona masaniAAa
laAAallakum takhludoona; Wa-idha batashtum batashtum jabbareena; Faittaqoo
Allaha waateeAAooni(Surat Ash Shuara 26:128-131)

Tafsir: Mnajenga katika Kile sehemu iliyo juu Makasri Makubwa, wakati hamuishi
ndani yake? Na Mnajichukulia Makasri Mazuri kama kwamba Mtaishi Ndani yake
Milele. Na Mkivamia Mnavima Kama Majabari. Mcheni Allah na nitiini mimi.

Tunapoiangalia aya ya 128 inasema kua Atabnuuna bikulli riiaAain ayatin taAabathuuna
yaani Nabii Hud anawaambia watu wake kua wanajenga katika kila sehemu iliyo juu
Makasri Makubwa ambayo hawaishi ndani yake.

Halafu aya hii imetumia neno RiiAAin ambalo ni lenye kutokana na neno Ra'Aa ambalo
kwa Lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kuona, Kutizama, Kufikiria, Kua na Mtizamo
au Kuhukumu baada ya kuona. Neno RaA'a ndio lililotoa neno Ri'ya ambalo ni lenye
kuonesha Sifa isiyotakiwa katika Uislam ambayo ni sifa mbaya ya Kujiona, Kujionesha,
au Kujivuna.

Hivyo Basi Nabii Hud alikua akiwalaumu watu wake kutokana na Sifa hio mbaya ya
Kujionesha na Kujivuna kwa kujenga Majumba ambayo hawayahijati na wala
hawayatumii kwa jambo lolote isipokua Kuonesha Uwezo wao.

Na tunapoiangalia aya ya 129 basi tunaona kua katika kuyaelezea Majumba hayo
imetumia neno MasaniA'aa ambalo linamaanisha kitu kinachotokana na Usanii mkubwa
sana wa Kiumbe anapofanya kitu kwa kutumia akili, nguvu, wakati na jitihada kubwa
sana mpaka kitu kipendeze sana, yaani watu hawa walikua hawajali mda wanaotumia, na
uwezo gani wala mali gani, kwani kwao wao mda si muhimu kwa sababu wanaona kua
wanao wa kutosha kwani wataishi milele, hivyo kila kitu chao walikua wanakitumia kwa
ajili ya Mapambo ya Dunia kwa kuona kua wataishi Milele, na hivyo kua ni wenye
kupingana na maumbile ya viumbe ambavyo vina maumbile ya kua ni vyenye
kukikimbilia Kifo. Hivyo aya hii inatuwekea wazi umuhimu wa kutotumia Mda mwingi
kwa ajili ya Dunia.

Ambapo aya ya 130 nayo imetumia maneno yenye kuainisha sifa zinazotokana na neno
Batashta na neno Jabar.
731

Ambapo neno Batashta hua linamaanisha Kukamata kwa nguvu, Kuzidi nguvu,
Kudhuumu au Kuua kwa Kutumia Nguvu, ambapo hili ni neno lililotumika mara 10 tu
ndani ya Qur'an na mara mbili miongoni mwao ni katika aya hii katika kuelezea Uovu
wa watu hawa wa Al Ahqaf.

Kisha aya ikatumia neno Jabbar ambalo tunapo lizungumzia kwa Viumbe basi hua ni
sifa ya Mtu asiekua na Huruma juu ya wale ambao waliokua chini yake na hivyo kua ni
wenye kusababisha madhara na dhulma kubwa kwa wale wasiokua na nguvu dhidi yake
kutokana na Nguvu zake.

Naam aya tatu hizi zinabainisha miongoni mwa makosa waliyokua wakiyafanya watu
hawa wa Nabii Hud. Lakini mbali ya Ukubwa wao basi hawakuweza kujilinda na adhabu
kutoka kwa Mola wao, kwani baada ya kumuasi Mola wao na kuadhibiwa kwa Upepo
kama inavyosema Surat Al Haaqa 69:6-8 Ambapo katika Aya yetu hii Allah Subhanah
wa Ta'ala anatuainishia namna hali halisi ilivyokua kwa kututolea Mfano hai wa Magogo
ya Miti ya Mitende.

Kwa kua sisi kwetu Mitende sio Mingi basi na tuchukulie Mfano wa Magogo ya Mnazi
namna Mti wake Ulivyojishona kwa umadhubuti wa nyuzi zake ndani yake. Hivyo
chukua mfano huo wa gogo la Mti wa Mnazi kisha ingiza akilini inakua kuaje mpaka
linakua Bua. Ambapo tunapozungumzia Bua basi hua tunazungumzia kitu ambacho
chepesi hakina kitu ndani yake na hivyo kinapeperushwa kwa urahisi na Upepo wa
kawaida tu.

Hivyo baada ya kupata picha hio, basi rudisha akili yako kwa Miili ya Watu hawa wa
Nabii Hud, wenye Urefu wa Futi 100 kisha na ukubwa wao wote huo, basi hawakuweza
kufanya chochote ilipowadia adhabu ya Mola wao na badala yake wakawa wamebakia
kama Mabua mepesi yanayo peperushwa na Upepo.

Na katika kuthibitisha wepesi wao huo wa kua kama mabua na mbali ya kua na Miili
mikubwa kuliko watu wengine wote Ulimwenguni waliowahi kuumbwa, Basi Allah
Subhanah wa Ta'ala anahoji:

﴾‫﴿ ﻓَـ َﻬﻞ ﺗَـﺮ ٰى َﳍُﻢ ِّﻣﻦ َﺎﺑﻗِﻴَ ٍﺔ‬


َ ْ
Fahal tara lahum min baqiyatin (Surat Al Haaqa 69:6-8)

Tafsir: Hivi Jee mnaona mabaki yao?


732

Hivyo basi Upepo wenye hali ya Umoja hua ni Adhabu kutoka kwa Allah Subhanah wa
Ta’ala kama ilivyosema aya yetu hii:

﴾‫ﺻ ٍﺮ َﻋﺎﺗِﻴَ ٍﺔ‬


َ ‫ﺻْﺮ‬ ٍ ‫ﺎد ﻓَﺄ ُْﻫﻠِ ُﻜﻮاْ ﺑِ ِﺮ‬
َ ‫ﻳﺢ‬ ٌ ‫﴿ َوأ ََﻣﺎ َﻋ‬
Waamma AAadun faohlikoo bireehin sarsarin AAatiyatin(Surat Al Haaqa 69:6-8)

Tafsir: Na ama Aad wameangamizwa kwa Upepo Mkali sana.

Ambapo Upepo huo umeainishwa sifa yake kwa kutumia neno Sarsarin linatokana na
Neno Sarra lenye kumaanisha Kulia au Kuvuma kwa Sauti kubwa sana. Hivyo neno
Sarsarin linamaanisha Upepo Mkali wenye ngumu sana na unapovuma hua unatoa sauti
kubwa sana. Na pia neno Sarsarin hua linamaanisha Upepo Mkali sana wenye Baridi kali
sana.

Na Anasem Imam Is-haq Ibn Bishr kua: ‘Allah Subhanah wa Ta'ala aliuamrisha
Upepo uwapulize watu wa Nabii Hud, hivyo Upepo huo ulijikusanya kisha
ukapuliza bila ya kua na mipaka yake wala mwisho wake, yaani kama Mvuke
ambao unaotoka kwenye tundu za Pua za Fahali (Ng'ombe Dume mwenye Hasira
kubwa sana) mpaka Ardhi ikatetemeka na Malaika wakasema: Ya Allah! Kwa hali
hii Viumbe hawa hawatoweza kuustahamilia Upepo huu, kwani Utaangamiza kila
kitu kilichomo katika Ardhi yao kuanzia Juu ya Ardhi mpaka nchini yake.’

Upepo Huu ulikua Mkali Sana kiasi ya kua ukikupuliza basi unachana ngozi yako na
kukitoa kila kitu ndani ya mwili wako na kutokea upande wa pili wa mwili wako Upepo
huo ulikua ni wenye kuvuma na kutoa Sauti Kali sana mara 1000 zaidi ya sauti Upepo
wa kawaida unapovuma.

Upepo huo haukua ni wenye kuvuma labda kwa mda wa saa moja au mawili, bali ulivuma
kwa wiki nzima usiku na mchana bila ya kupungua kasi wala nguvu yake katika
kuangamiza kwake! Kwani wiki nzima hii ilikua hakuna kwa kukimbilia wala kwa
kujifichia isipokua kwa Nabii Hud aliekua ndani ya Rehma za Allah.

Kwa wale ambao wameshawahi kuishia katika nchi zenye Theluji na Baridi Kali basi hua
kuna Upepo fulani hivi katika kipindi cha Baridi ukikupiga kama hujavaa Gloves
mikononi mwako basi hata ukiingiza Mkono wako kwenye mfuko wa Jeans iliyobana
basi mkono wako huo kwa upande wa nje yake hua unauhisi Kama unajichinja kwa
maumivu, kutokana na kupigwa na Upepo wa Baridi. Au Unakua unahisi kama unaungua
maji ya Moto mkono wako huo kutokana na Baridi hio, na ndio maana basi baadhi ya
Wanazuoni wakasema kua Upepo huo ulikua ni wa Moto kutokana na ukali wake.
733

Ila hapa mimi nimetumia mfano wa Upepo ulio katika hali ya wingi yaa Al Riyyah wa
Baridi kali, sasa usiseme kuhusiana na Upepo huo wa Rihun walioletewa watu wa Nabii
Hud, tena ukiwa na Kusudio Maalum la Kuadhibu na kuangamiza, kama unatafakkari na
kuzingatia basi utaona uzito wa hoja hii iliyobainishwa hapa na aya hii.

Ambapo anasema Imam Al Suddi kua kua: Watu hawa wa Hud walipopelekewa Upepo
huo kwanza waliona ukali wake kwa kupeperushwa Ngamia wao na wakajikuta na
wao pia wamekua miongoni mwao, kwani kila aliekimbilia Ndani Nyumbani kwake
basi Upepo ulimfuata huko huko na kumtoa nje kwa kumpeperusha mpaka
wakaaangamia wote na baada ya kuangamizwa kwao huko basi Allah Subhanah wa
Ta'ala akatuma Ndege kwa ajili ya kuyabeba mabua ya Miili yao na kuitupa
baharini

Na kwa upande mwengine basi neno Raha pia ndio ililotoa neno Ruh ambalo hua ni lenye
kumaanisha Rehma na linapotumika kama jina hua linamaanisha Pumzi ya Uhai na pia
kwa upande mwengine hua linatumika kama Rahat na hivyo kuwakilisha Kua Huru
kutokana na Huzuni na Maumivu na Kua na Uhai wenye Utulivu kutokana na kua na
Rehma ndani yake.

Ambapo kuhusiana na aya hii ya Kawniyah ya Surat Al Baqara 2:164 basi Mujaddid Ad
Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi katika Tafsir yake basi
amefafanua kwa kina sana kuthibitisha kuhusiana na Maumbile ya Ulimwengu na
kuwepo kwa Muumba wake na kuweka wazi kua Maumbile ya Dunia ni ya Duara na
hivyo sehemu moja inapokua Mchana basi sehemu nyengine inakua Usiku, na kisha
kuweka wazi pia kua kutokana na Maumbile ya kila mtu kua ni yenye kutofautiana na
mtu mwengine basi hii inaweka wazi kua kila mtu hua na utofauti wake huo tangu wakati
akiwa ndani ya Manii.

Baada ya aya hio basi Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid
Muhamamd Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali akatumia pia aya 16
zifuatazo ambazo zina hoja nzito ndani yake kwa kusema:

‫ﺼ ِّﺪﻗُﻮ َن۞أَﻓَـَﺮأَﻳْـﺘُ ْﻢ ﱠﻣﺎ ﲤُْﻨُﻮ َن ۞ أَأَﻧﺘُ ْﻢ َﲣْﻠُ ُﻘﻮﻧَﻪُ أَم َْﳓ ُﻦ‬
َ ُ‫﴿ َْﳓ ُﻦ َﺧﻠَ ْﻘﻨَﺎ ُﻛ ْﻢ ﻓَـﻠَ ْﻮﻻَ ﺗ‬
‫ﲔ ۞ َﻋﻠَ ٰﻰ أَن ﻧـﱡﺒَ ِّﺪ َل‬ ِ ِ
َ ‫ت َوَﻣﺎ َْﳓ ُﻦ ﲟَ ْﺴﺒُﻮﻗ‬
ِْ
َ ‫ٱﳋَﺎﻟ ُﻘﻮ َن ۞ َْﳓ ُﻦ ﻗَﺪ ْﱠرَ� ﺑَـْﻴـﻨَ ُﻜ ُﻢ ٱﻟْ َﻤ ْﻮ‬
ٰ َ ‫ﻨﺸﺌَ ُﻜ ْﻢ ِﰱ َﻣﺎ ﻻَ ﺗَـ ْﻌﻠَ ُﻤﻮ َن ۞ َوﻟََﻘ ْﺪ َﻋﻠِ ْﻤﺘُ ُﻢ ٱﻟﻨﱠ ْﺸﺄَةَ ٱﻷ‬
‫ُوﱃ ﻓَـﻠَ ْﻮﻻَ ﺗَ َﺬ ﱠﻛُﺮو َن‬ ِ ُ‫أَﻣﺜَﺎﻟَ ُﻜﻢ وﻧ‬
َْ ْ
734

ُ‫۞ أَﻓَـَﺮأَﻳْـﺘُﻢ ﱠﻣﺎ َْﲢُﺮﺛُﻮ َن ۞ أَأَﻧﺘُ ْﻢ ﺗَـْﺰَرﻋُﻮﻧَﻪُ أ َْم َْﳓ ُﻦ ٱﻟﱠﺰا ِرﻋُﻮ َن ۞ ﻟَ ْﻮ ﻧَ َﺸﺂءُ َﳉََﻌ ْﻠﻨَﺎﻩ‬
۞ ُ ‫ُﺣﻄَﺎﻣﺎً ﻓَﻈَْﻠﺘُﻢ ﺗَـ َﻔ ﱠﻜ ُﻬﻮ َن ۞ إِ ﱠ� ﻟَﻤ ْﻐﺮُﻣﻮ َن ۞ ﺑَﻞ َْﳓﻦ َْﳏﺮ‬
َ‫وﻣﻮ َن أَﻓَـَﺮأَﻳْـﺘُ ُﻢ ٱﻟْ َﻤﺂء‬ ُ ُ ْ َُ ْ
ِ ِ ِ
ُ‫ٱﻟﱠﺬى ﺗَ ْﺸَﺮﺑُﻮ َن ۞ أَأَﻧﺘُ ْﻢ أَﻧْـَﺰﻟْﺘُ ُﻤﻮﻩُ ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻤْﺰن أ َْم َْﳓ ُﻦ ٱﻟْ ُﻤْﻨ ِﺰﻟُﻮ َن ۞ ﻟَ ْﻮ ﻧَ َﺸﺂءُ َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎﻩ‬
‫ﻧﺸﺄْ ُْﰎ َﺷ َﺠَﺮﺗَـ َﻬﺂ أ َْم‬َ َ‫ﻮرو َن ۞ أَأَﻧﺘُ ْﻢ أ‬ ‫أُ َﺟﺎﺟﺎً ﻓَـﻠَ ْﻮﻻَ ﺗَ ْﺸ ُﻜﺮو َن ۞ أَﻓَـﺮأَﻳْـﺘُﻢ ٱﻟﻨ ﱠ‬
ُ ُ‫ﱠﺎر ٱﻟ ِﱴ ﺗ‬َ ُ َ ُ
ِ ِ ِ
‫ﻚ‬َ ِّ‫ﭑﺳ ِﻢ َرﺑ‬ ْ ِ‫ﻳﻦ ۞ ﻓَ َﺴﺒِّ ْﺢ ﺑ‬ َ َ‫َْﳓ ُﻦ ٱﻟْ ُﻤﻨﺸﺌُﻮ َن ۞ َْﳓ ُﻦ َﺟ َﻌ ْﻠﻨ‬
َ ‫ﺎﻫﺎ ﺗَ ْﺬﻛَﺮًة َوَﻣﺘَﺎﻋﺎً ﻟّْﻠ ُﻤ ْﻘ ِﻮ‬
﴾‫ٱﻟْ َﻌ ِﻈﻴ ِﻢ‬
Nahnu khalaqnakum falawla tusaddiqoona; Afaraaytum ma tumnoona; Aantum
takhluqoonahu am nahnu alkhaliqoona; Nahnu qaddarna baynakumu almawta
wama nahnu bimasbooqeena; AAala an nubaddila amthalakum wanunshi-akum
fee ma la taAAlamoona; Walaqad AAalimtumu alnnash-ata al-oola falawla
tadhakkaroona; Afaraaytum ma tahruthoona; Aantum tazraAAoonahu am nahnu
alzzariAAoona; Law nashao lajaAAalnahu hutaman fadhaltum tafakkahoona ;
Inna lamughramoona; Bal nahnu mahroomoona; Afaraaytumu almaa alladhee
tashraboona; Aantum anzaltumoohu mina almuzni am nahnu almunziloona; Law
nashao jaAAalnahu ojajan falawla tashkuroona; Afaraaytumu alnnara allatee
tooroona; Aantum ansha/tum shajarataha am nahnu almunshi-oona ; Nahnu
jaAAalnaha tadhkiratan wamataAAan lilmuqweena; Fasabbih biismi rabbika
alAAadheemi (Surat Al Waqiah 56: 57-74).

Tafsir: Sisi ndio tuliokuumbeni, Hivyo kwanini Hamuamini? Hebu niambieni


kuhusiana na Manii mnayoyatoa; Jee ni nyinyi mnayoyaumba au ni sisi ndio
waumbaji? Sisi tumekukadirieni nyinyi nyote baina yenu Mauti na sio kama hatuwezi;
kukugeuzeni nyinyi na kukuumbeni katika maumbo ambayo hamyajui; Na bila ya
shaka mshajua kuhusiana na Maumbile ya kwanza (ya Nabii Adam), hivi kwa nini
hamkumbuki? Niambieni kuhusiana na Mbegu mnazopanda ardhini; Ni nyinyi ndio
mnaoziotesha au sisi ndio waoteshaji? Kama tungetaka basi tungejaalia kua
zilizovurugika kwa kuzikausha nanyi mngekua ni wenye kujuta (baada yake);
Mkisema: ‘Hakika sisi tumeangamia, La! Bali tumeshazuiliwa!(Neema na Baraka ya
kua na Ardhi yenye rutba na kutoa mazao)’; Niambieni kuhusaiana na Maji
mnayokunywa; Jee ni nyinyi ndio mnayosashusha kutoka Mawinguni au sisi ndio
washushaji? Kama tungetaka basi tungeyafanya kua ni ya Chumvi (yasiyonyweka),
735

Hivi Haamshukuru nyinyi? Niambieni kuhusiana na Moto mnaowasha; Jee ni nyinyi


mnaoufanya Mti wake kukua au sisi ndio wakuzaji? Na tumeufanya kua ni
kumbukumbu na mafikio ya wanaosafiri. Litukuze jina la Mola wako mtukufu.

Aya hizi pia zinatuainishia aina ya Munasaba ambao ni Upekee wa Mpangilio wa Qur’an
kwa upande wa Kilugha kwani zinainisha mfano wa namna Allah Subhanah wa Ta’ala
alipotumia harfu ya mwisho ya neno la aya kumaanisha mwanzo mwa Mada katika Sura
husika, kujumuisha Umoja wa Mada na kisha kubadilisha harfu kuanisha Mwisho wa
mada husika katika Sura kwani aya hizi zote zimemalizikia na harfu Nun yenye Fatiha
juu yake ambapo aya ya kabla ya Mada hii imamlizikia na harfu Nun yenye Kisra chini
yake na mada ikafungwa kwa aya iliyomalizikia na harfu Mim.

Ambapo anasema Shaykh ul Islami Imam Abū Abd Allah Badr Ad Dīn Mohammed Ibn
Abd Allah Ibn Bahādir Al Zarkashi Al Shafii kua: ‘Munasabah ndani ya Qur’an hua
ni mfanano au ukaribu baina ya Aya tofauti, Sura na maneno ambayo hupelekea
kuwepo kwa uhusiano baina yao. Uhusianao huu hua ni wenye kutoa muunganisho
wa kimaana.’

Ambapo mpangilio huu hua unajulikana kama Munasaba yaani Mnasaba, Muingiliano
au Uhusiano wa baina ya sehemu zilizomo ndani ya Qura’an. Kwani kulingana na
maumbile yake basi Qur’an ina aina zifuatazo za Munasaba ndani yake:

1. Munasaba baina ya Mwisho wa Surah na mwanzo wa Sura inayofuatia baada yake.


2. Munasaba baina ya Jina la Sura na Mada ya Sura au Malengo ya Sura.
3. Munasaba baina ya Aya ya Mwanzo ya Ufunguzi wa Sura na yaliyomo ndani ya Sura.
4. Munasaba baina ya Aya ya mwanzo na Aya ya mwisho ya Sura.
5. Munasaba baina ya Aya moja na Aya nyengine ndani ya Sura.
6. Munasaba baina ya Neno moja na Maneno mengine katika Sura.
7. Munasaba baina ya Kundi la Aya na yaliyomo ndani ya aya.
8. Munasaba baina ya Mwisho wa Sura na Mwanzo wa Sura inayofuatia.
9. Munasaba baina ya Yaliyomo ndani ya Sura na Sura iliyo kabla yake au baada yake.

Ambapo aya ya 71-72 zinaelezea kuhusiana na mimea na namna inavyotunufaisha


kutokana na kua na uwezo wa kuwaka moto na kuturahisishia mambo mengi sana katika
maisha yetu, na hivyo aya inatuwekea wazi umuhimu wa madini ya chlorophyl ambayo
ndio inayosafirisha na kuibadilisha nguvu ya mionzi ya jua kwa ajili ya kutengenezea
chakula cha mimea na pia kwa ajili ya kuiwezesha mimea hio kua ni yenye kuwaka na
kutoa moto pale inapochomwa kutokana na kua mimea ndani yake hua na gesi ya Carbon,
Haydrogen na Oxygen ambazo ni zenye kuungua zinapopata joto kali sana.

Tukio hili tutalifahamu vizuri zaidi pale tunapojiuliza inakua kuaje mpaka kitu fulani
kinakua kinawaka moto. Ambapo kwanza inabidi tufahamu kua ili kitu fulani kiwake
736

basi lazima kuwe kuna aina ya nguvu ambayo hua inasafirishika kutoka katika hali moja
ya ubaridi kuingia kwenye hali nyengine ya joto, aina hii ya nguvu hua katika maumbile
ya sehemu ndogo ya kitu yaani Atom iwe kitu hicho kina hali ya uyabisi, maji maji au
hewa.

Nguvu hio yenye kusafirishika kutoka katika hali ya ubaridi kuingia kwenye hali ya joto
inapoanza kusafiri hua na uwezo wa kukipa joto na kikausha kitu kilicho karibu yake na
hivyo hua na uwezo wa kusafirisha na kulisambaza joto hilo mbele zaidi, kutokana na
kua kila kitu husika kinapopata joto basi kimaumbile atom zake hua zinatawanyika na
kuachana achana badala ya kushikamana na hivyo kusababisha kuzalishwa kwa gesi
yenye ujoto ambayo nayo inapokutana na gesi ya Oxygen iliyomo kwenye hewa basi
husababisha kutokea kwa cheche za moto ambazo nazo husababisha mripuko wa Moto.

Na inapokua kuna mchanganyiko wa gesi ya kutosha na hewa ya Oxygen ya kutosha basi


moto utakaowaka utakua ni wenye rangi ya Buluu na usiokua na moshi, na inapokua
hakuna hakuna mchanganyiko wa kutosha basi moto utakaowaka utakua ni wenye rangi
ya manjano, au mwekundu na hivyo kua ni wenye kutoa moshi na kusababisha
kuzalishwa kwa hewa chafu ya Carbon na Carbonmonoxide.

Hivyo basi bila ya shaka

Hivyo bila ya shaka katika vithibitisho vyote hivi tulivyoviangalia katika aya basi hua ni
vyenye kudhihirisha kuwepo kwa Muumba wa Ulimwengu ambae ni Allah Subhana wa
Ta’ala ambae ndie alieumba kila kitu na kudhibiti kila kitu na kusimamia kila kitu
kilichopo Ulimwenguni.

Tunaporudi kwa Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn
Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali basi nae anaendelea kutuambia kuhusiana na
kutokuwepo kwa Umilele wa Ulimwengu kwa kusema: ‘Kila kilichoanza kuwepo, basi
kina Muanzilishi wa kuwepo kwake. Na kwa kua Ulimwengu Ulianza kuwepo, basi
bila ya shaka kuna Muanzilishi wa kuwepo kwake, na Muanzilishi huyo ni Allah
Subhanah wa Ta’ala.’

Ambapo kwa upande wa Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Al Ghazali Al


Thani Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi yeye anasema kua: ‘Kuna njia nne za
kuthibitisha kuwepo kwa Muumba ambazo ni:

1-Kuwepo kwa kitu ambacho kuwepo kwake hua kunategemea na ulazima wa


kuwepo kitu hicho ama la. Kama kuna ulazima wa kuwepo kitu hicho basi hua
hamna tatizo, lakini kama hamna ulazima kuwepo kitu hicho, basi lazima kuwe na
kitu ambacho kitasababisha kuwepo kwake kitu hicho. Na kama lazima kuwepo
737

kwa msababishaji wa kuwepo kwa kitu hicho, basi pia hua hamna tatizo. Lakini
hata hivyo haya yote hayawezekani kua hivyo.’

2-Inajulikana kua kila kitu chenye kuchukua nafasi mwanzo wake hua ni kipya, na
kila kitu kipya hua kimeanzishwa na mwengine. Hivyo haiwezekani kwa
muanzishaji mpya kua ni mwenye kutokana na kitu kipya bila ya Muanzishaji kua
mpya pia.

3-Kama ikiwa kuna kitu ambacho kinajulikana kwa sifa ya kua ni Dunia, na kuna
kitu chengine kinajulikana kwa sifa ya kua ni Nyota. Basi bila ya shaka lazima
kutakua kuna kitu ambacho kimeamua kua kitu kipi kiwe na sifa ya Dunia na kipi
kiwe na sifa ya Nyota.

4-Inawezekana kuonekana na kuthibitishika kutokana na maumbile ya Nafsi


yenyewe ya Ibn Adam. Kwa mfano: Tunapoangalia Manii ambayo hua yako katika
hali ya mchanganyiko wa majimaji.

Yaani kama maumbile hua hayana Muumbaji na hua yanatokea yenyewe tu


kimaumbile, basi hua ni rahisi kukubalika kiufaham kua Manii hayo yatatoa
Kiumbe mwenye umbo la Maumbile fulani. Lakini hata hivyo ukweli ni kua kuna
utofauti wa Maumbile ya kila aina ya kiumbe, hata kwa Ibn Adam wenyewe. Hivyo
basi si maumbile ndio yanayoamua kiumbe gani azaliwe au aumbwe, bali kuna
Muumba ambae ndie anaeamua hivyo.

Tumalizie na mtizamo wa Shaykh Hamza Yusuf amabe anasema kua: ‘Jambo


linaostaajabisha kuhusiana na watu wasioamini kuwepo kwa Muumba ni kua,
baadhi yao hua wanakanusha kuwepo kwa Muumba kwa sababu ya mtizamo wao
juu ya Muumba ni wa kumkuza sana, na hivyo husema: ‘Itakuaje mimi niamini
kuwepo kwa Mungu ambae ataruhusu kua Ulimwengu uwe na hali kama hii.?’

Wakati suali la kujiuliza hasa hua sio hilo bali hua ni lile lisemalo: ‘Jee kuna tatizo
gani kwa Ibn Adam, ambao Allah Subhanah wa Ta’ala amewajaaalia kua na Hiari,
kwanini wao wanaruhusu mambo yanayotokea yatokee? Kwa sababu Allah
Subhanah wa Ta’ala ana kila haki ya kuuuliza kwanini mkaruhusu haya yatokee?

Hivi kwanini wewe Mtu mzima ukambaka mtoto mdogo? Jee sikukupa mimi akili
wewe? Sikukupa uwezo? Sikukupa Ilm? Sikukupa hiari? Sikukupa uwezo wa
kudhibiti matamanio yako? Kisha unafanya haya?’

Hilo ndio suali la kujiuliza. Hivyo haitakiwi kujiuliza Mungu yuko wapi, bali
inatakiwa ujiulize, hivi jee uko wapi wema wa watu ambao Mungu amewaumba?
738

Ambapo watu wanasema kua Mungu hatusikilizi. Lakini ni sisi ndio hatumsikilizi
Mungu, kwani ametuma Vitabu, na kutuambia kua: ‘Msifanye ufisadi katika ardhi,
hakika mimi nimekupeni nyinyi Mizan kamilifu ili msivuke mipaka. Na sasa hivi
ndio tunajua kuhusiana na mahusiano ya viumbe yaliyokadiriwa kwenye usawa.
Kwani kama ukiwaua Buibui basi Nzi watatawala.’’

USAWIA WA MIZANI KATIKA MAUMBILE YA VILIVYOMO


ULIMWENGUNI.


Neno Mizani limetokana na neno Wazana ambalo hua ni lenye kumaanisha Mizani,
Kupima kwa ukamilifu, Kugawa sawia au Kuhukumu kwa uadilifu,

Ambapo amesema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

‫ﻴﻤﻮاْ ٱﻟْ َﻮْز َن ﺑِﭑﻟْ ِﻘ ْﺴ ِﻂ‬ِ ‫﴿وٱﻟ ﱠﺴﻤﺂء رﻓَـﻌﻬﺎ ووﺿﻊ ٱﻟْ ِﻤﻴﺰا َن۞أَﻻﱠ ﺗَﻄْﻐَﻮاْ ِﰱ ٱﻟْ ِﻤﻴﺰ ِان‬
ُ ‫۞وأَﻗ‬
َ َ ْ َ َ َ ََ َ َ َ َ َ َ
﴾‫وﻻَ ُﲣْ ِﺴﺮواْ ٱﻟْ ِﻤ َﻴﺰا َن‬
ُ َ
Waalssamaa rafaAAaha wawadhaAAa almeezana; Alla tatghaw fee almeezani;
Waaqeemoo alwazna bialqisti wala tukhsiroo almeezana (Surat Ar Rahman 55:7-9)

Tafsir: Na Mbingu alizozinyanyua Juu na akaweka na Mizani. Ili msivuke mipaka ya


Mizani; Na Simamieni Uzani kwa Uadilifu na wala msipunguze Uzani.

Ambapo katika aya hizi, basi mbali ya kua Allah Subhnah wa Ta’ala amezunguzia
maumbile ya Mbingu na hivyo ukitafakkari basi unaona pia kua ameweka wazi kua ni
yeye Allah Subhanah wa Ta’ala ndie anaenyanyua na kukipandisha juu kila kitu, iwe
kimaumbile au kidarja, lakini pia akazungumzia kuhusiana na kuwekwa kwa Mizani ya
makadirio yake ambayo ndio iliyopima na kuweka usawia wa hali ya Maumbile ya Juu
Mbinguni, Angani pamoja na Duniani na hivyo matokeo yake usawia huo basi
unapelekea Ulimwengu wote kwa Ujumla na vilivyomo ndani yake kua ni vilivyotulia
kutokana na kuwepo kwa usawia wa kila kitu kuanzia kwenye Mpangilio wa Mbingu na
Ardhi, Nyota na Sayari, Ardhi ya Nchi kavu na Bahari, Mimea na Wanyama, Nguvu za
Mvutano na Msukumano wa Mawimbia ya Sumaku, Nguvu za Graviti n.k.
739

Hivyo Usawia huo umekamilia kimizani Kiasi ya kua hata mpangilio wa Jua, Mwezi,
Sayari na Nyota mbali mbali na athari zake kwa kila kilichomo ndani yake Ulimwenguni
na namna zinavyotegemeana, basi ikiondolewa moja tu kati ya vitu hivyo kutoka katika
sehemu yake ya kimaumile iliyopangiwa kuwepo na Mola wake, basi utasababisha
Maangamizo ya kila kitu.

Na pia kwa upande wa kila kitu kilichomo Duniani kua vyote viko katika mpangilio
uliokamilia uliopimwa kwa Mizani, kuanzia Mimea, Ardhi, Hewa, Bahari, Wanyama,
Wadudu n.k na usawia huo wa Mizani uko kwa manufaa ya Ibn Adam ambae ndie
Khalifa au Mtawala aliewekwa na Mola wake hapa Ulimwenguni kwa sharti la kua
asifanye Ufisadi, kiasi ya kua akifanya Israfu au Ufisadi kwa kimoja tu kati ya hiyo basi
ataathirika mwenyewe na kujiharibia Maisha yake na Uzuri wa Mazingira yake anayoishi
aliyojaaliwa na Mola wake kutokana na Rehma zake juu yake, na hivyo basi Israfu hio
itampelekea Ibn Adam kujiondolea urahisi wa Kujipatia Mahitaji yake Muhimu katika
Maisha yake, na hapo hapo atakua ni mwenye kua na dhima mbele ya Mola wake, kwa
sababu ya kupingana na maamrisho ya Mola wake.

Na kwa upande mwengine basi aya zinazungumzia pia Mizani ya Uadilifu wa Kuachana
na makatazo ya Muumba ambae ni Allah Subhanah wa Ta’ala na kushikamana na
Maamrisho yake, na kisha zikazunguzia Mizani ya Uadilifu wa Vipimo baina yetu Ibn
Adam. Hivyo basi aya hizi zinazungumzia Mizani aina tatu:

-Mizani ya Utiifu na Uadilifu kwake yeye Muumba wetu.

-Mizani ya Usawia wa Maumbile ya Dunia na Ulimwengu, Mazingira yake na


Viumbe wengine na kila kilichomo Ndani yake.

-Mizani ya Uadilifu Baina yetu Ibn Adam.

Ambapo anasema Imam Abu Abd Allah Sahl Al Tustari kua: ‘Allah Subhanah wa
Ta'ala amemfundisha Ibn Adam Lugha ya Kuwasiliana kutokana na Nafsi ya Mtu
husika. Akampa Ufaham Ibn Adam kwa kupitia Akili zake kisha akampa Ibn Adam
Mtihani wa Nafsi yake, Akampa Matamanio ya Kimaumbile, na Akampa Ufaham
wa Maumbile ya Nafsi yake, Kisha Allah Subhanah wa Ta'ala akampa Ibn Adam
I'lm na kisha akamfafanulia juu ya Ilm hio Kisha akamuwekea Mizani ya
Maamrisho na Makatazo yake kupitia katika Kiwiliwili chake Ibn Adam huyo’

Na amesema Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Al Ghazali kua: ‘Amesema
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Hakika Ibn Adam mna Mola wenu
ambae ana haki yake juu yenu katika Kutekeleza Majukumu aliyo kupeni na
atakuadhibuni kwa Kuyadharau Majukumu hayo na pia atakulipeni kwa
740

kuyatekeleza Majukumu hayo na amenitumia Kama Mtume wake juu yenu ili
kukuwekeeni wazi juu ya hili’

Kwani Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad
Al Ghazal anaendelea kutuambia kua; ‘Kwa Hivyo Jukumu la kwanza juu yetu ni
kujua kua: Jee sisi tunae Muumba ama la? Na Kama Kuna Muumba, Jee anao
uwezo wa Kutuamrisha Kufanya Mema na kutukataza Mabaya? Na kisha
akatutumia Mitume pia kama anao uwezo huo, Jee anao uwezo wa Kutuadhibu
kama Tukimkosea na hivyo pia Kutupa Zawadi kama tukimtii? Na Kama Jee anao
Uwezo huo, Basi Jee huyu Mtu aliemtuma kwa ajili yetu ambae amesema kua yeye
ni Mtume ni Mkweli ama la?’

Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al
Ghazali anaendelea kutuambia kua: ‘Hivyo Baada ya Masuali yote haya Kua yako
Wazi kwetu sisi, basi bilaya shaka, kama tutakua na akili timamu, basi ni jukumu
letu kutekeleza majukumu tuliyopewa na Mola wetu. Ni jukumu letu kua
waangalifu katika kuziangalia na kuzichunga nafsi zetu, na ukawa wenye kujua
kua maisha ya hapa Duniani ni ya Mpito ambayo kamwe hayafanani na maisha ya
Milele ya Kesho akhera.’

Kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Zipambeni Tabia
Zenu’ Na hii ni kwa sababu tabia njema hua zinadhibiti matamanio ya Nafsi na
Hasira. Na bila ya shaka inawezekana kuboresha Tabia Zetu na hii ni kwa sababu
kama ikiwa wanyama wa Mwituni kama Tai, Mbwa na Farasi mwitu wanaweza
kubdilika na kufugika na kutiwa hatamu basi itakuaje Ibn Adam ashindwe
kubadilisha tabia yake?

Kufanya Mema Hufungua Milango ya Nyoyo kuelekea katika Pepo na Kupelekea


kwenye Ukaribu na Allah Subhanah wa Ta'ala na Kufanya Mabaya hua ni kua na
Maradhi ya Moyo na kujawa na Sumu ya Nafsi

Maradhi ambayo hukuharibia Maisha yako ya Milele ya Akhera na pia Maisha


yako ya Mpito hapa Duniani na bila ya shaka kila mtu anajua kua Mwenye Maradhi
hua ni mwenye Kumtafuta Daktari wa kumtibu Maradhi hayo hapa Duniani

Sasa kama ikiwa Mtu unatafuta Tiba ili ajitibu Mwili wake hapa hapa Duniani basi
wajibu wa kila Ibn Adam kutafuta Tiba ya Nafsi yake hapa hapa Duniani, kwani
maisha ya Akhera ni yenye thamani kubwa sana mwenye kumuamini Allah
Subhanah wa Ta’ala.

Katika Nafsi ya Kila Ibn Adam hua kuna Vitu Vitatu ambao ndivyo vinavyohusika
na Usimamizi na Udhibiti wa Nafsi ambavyo ni:
741

1-Matamanio - Ambayo Humpotosha Mtu na hivyo Kumuingiza kwenye Maradhi


na Vitendo Viovu

2-Hasira - Ambayo Humpelekea Mtu kusababisha Madhara na kufikia hata Kuua.

3-Ubinafsi - Ambao humpelekea Mtu kutokua Na Uaminifu, Kutotosheka na


Kufanya Ufisadi.

Ambapo kwa Upande wa Ibn Adam basi wao wako wa aina Mbili

1- Wale Ibn Adam ambao ni wenye uwezo wa Kuvidhibiti vitu vitatu hivyo na
kuviweka chini ya Udhibiti wao, Watu hawa hua na Darja ya Wafalme na Maamiri
hata kama wakiwa ni wenye kuonekana kua ni wenye Kuvaa Nguo zilizochoka

2-Ibn Adam ambao Hawawezi Lolote Isipokua kujisalimisha chini ya Vitu vitatu
Hivyo na Kutii Matakwa ya Vitu hivyo

Hawa Hua Ni wajinga wasiokua na akili ambao ni Watumwa wa Matamanio Ya


Nafsi zao, Hata Kama Wakiwa ni Wafalme, Maamiri au Mawaziri.

Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al
Ghazali anaendelea kutuambia kuhusiana na Ibn Adam wasioweza kuzidhibiti Nafsi zao
kua: ‘Hawa wanao Uwezo Mkubwa sana wa Kukupotosha kiasi ya Kua wanaweza
kukuonesha Kiza na wakakuambia kua Ni Nuru kwani Wao hua ni Wasioamini
kuhusiana na Mpito wa Dunia hii na hivyo hua hawajui kua Maumbile ya
Ulimwengu yako aina 2 ambayo nia Maumbile ya Ulimwengu Unaoonekana Ambao
Hua unabadilika Kulingana na Mazingira.

Na Ulimwengu Usioonekana Ambao ni wa Kiroho Ulimwengu wa Kiroho ndio


Ulimwengu Pekee ambao hauna Mabadiliko Ndani yake kwani Kila kitu chake ni
cha Hakika na ni chenye Kudumu hivyo Mtu Mwenye Imani ya Kweli hua ni
mwenye kuona Ulimwengu kwa Kutumia Roho yake na wala si kwa Nafsi yake.

Na Ulimwengu huu wa Kiroho Huonekana wazi Mara ya Unapotaka Kukata Roho


na Hapo Mtu hua Unauona Ulimwengu wa Dunia ya Mpito Unaoonekana kua Upo
Juu Chini na Kila kitu Chake alichokua nacho Hutoweka, na hapo ndio Mtu
anapoambiwa.

﴾‫ﺼﺮَك ٱﻟْﻴَـﻮَم َﺣ ِﺪﻳ ٌﺪ‬ ِ َ ‫﴿ﻟﱠَﻘ ْﺪ ُﻛﻨﺖ ِﰱ َﻏ ْﻔﻠَ ٍﺔ ِﻣﻦ ﻫـٰ َﺬا ﻓَ َﻜ َﺸ ْﻔﻨَﺎ ﻋ‬
ْ ُ َ َ‫ﻨﻚ ﻏﻄَﺂءَ َك ﻓَـﺒ‬ َ َ ّْ َ
742

Laqad kunta fee ghaflatin min hadha fakashafna AAanka ghitaaka fabasaruka
alyawma hadeedun(Surat Qaf 50:22)

Tafsir: Hakika wewe Ulikua Umeghafilika na Hili Na Sasa Hivi Tumekuondolea Pazia
lako Mtazamo wako Leo Hio ni Mkali Sana (Wenye Kuona Kila kitu)

Hivyo basi hivyo ni baadhi ya vithibitisho vinavyothibitisha kuwepo kwa Allah


Subhanah wa Ta’ala na na mizano alizotuwekea viumbe wake, kwa asieviona basi hua
ni mwenye kuambiwa kama ilivyosema aya hio ya Surat Qaf 50:22, na kwa upande wa
Fir’awn alikua anaviona lakini alikua ni mwenye kuvifumbia Macho na kutotaka kurudi
kwa Mola wake kwani Allah Subhanah wa Ta’ala anasema:

ٍ ِ‫ﺼﺮةً وِذ ْﻛﺮ ٰى ﻟِ ُﻜ ِﻞ َﻋْﺒ ٍﺪ ﱡﻣﻨ‬


﴾‫ﻴﺐ‬ ِ ‫﴿ﺗَـﺒ‬
ّ َ َ ْ َ
Tabsiratan wadhikra likulli AAabdin muneebin.(Surat Qaf 50:8)

Tafsir: Ni Ushahidi na Ukumbusho kwa kila Mja mwenye (kutaka) kurudi


kwa Allah.

Ingawa Fir’awn na watu wake walikua hawataki kurudi kwa Mola wao na
kutubia lakini Allah Subhanah w Ta’ala aliendelea kuwaonesha wazi dalili
zake watu hao kwa kuwafanyia Miujiza ya aina yake.

MIUJIZA TISA YA NABII MUSA KWA FIR’AWN NA WATU WAKE.


Anasema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Surat Al Isra kua:

َ ‫ﻴﻞ إِ ْذ َﺟﺂءَ ُﻫ ْﻢ ﻓَـ َﻘ‬ِ ِ ٍ ٍ ‫﴿وﻟََﻘ ْﺪ آﺗَـﻴـﻨَﺎ ﻣﻮﺳﻰ ﺗِﺴﻊ‬


ُ‫ﺎل ﻟَﻪ‬ ْ َ‫آ�ت ﺑـَﻴِّﻨَﺎت ﻓ‬
َ ‫ﭑﺳﺄ َْل ﺑَِﲎ إ ْﺳَﺮاﺋ‬ َ َْ َٰ ُ ْ َ
ِ
﴾ً‫ﻮﺳ ٰﻰ َﻣﺴ ُﺤﻮرا‬
ْ َ ُ‫ﱡﻚ ٰﳝ‬ َ ‫ﻓْﺮ َﻋﻮ ُن إِِّﱏ َﻷَﻇُﻨ‬
Walaqad atayna moosa tisAAa ayatin bayyinatin fais-al banee isra-eela idh jaahum
faqala lahu firAAawnu innee laadhunnuka ya moosa mas-hooran (Surat Al Isra
17:101)
743

Tafsir: Na kwa hakika tulimpa Musa Aya Tisa zilizo wazi, waulize Bani Israil,
alipowajia (Nabii Musa) Fir’awn akasema: ‘Hakika mimi nnadhani kua wewe Musa
umerogwa ’

Ambapo kuhusiana na aya hii basi Wanazuoni wametofautiana kuhusiana na hili neno
Aya limemaanisha kua ni Miujiza tisa au ni Aya tisa zilizomo kwenye kitabu alichopewa
Nabii Musa yaani Tawrat, ambapo anasema Imam At Tirmidhii kua amesema Safwan
Ibn Assal Radhi Allahu Anhu kua: ‘Kulikua na Mayahudi wawili ambapo mmoja
alimwambia mwenzake kua kua: ‘Twende kwa huyu Mtume tukamuulize’. Na
mwenzake akajibu: ‘Usimwambie kitu chochote Mtume huyu kwani ukimwambia
basi atakua na macho manne.’

Hivyo wakatoka mpaka kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na walipofika
wakamuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ni nini maana ya maneno
yasemayo: Walaqad atayna moosa tisAAa ayatin bayyinatin? Na kwa hakika tulimpa
Musa Aya Tisa zilizo wazi.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akajibu: ‘Ni kua: Msimshirikishe Allah,
Msichukue Maisha ambayo Allah ameyaharamisha isipokua kwa Haki. Msizini,
Usiibe,Usimsababishie Mtu asiekua na kosa kuuliwa na Mtawala, Msile Riba,
Msimsingizie Mwanamke mwema, Msikimibie uwanja wa Vita na maalum kwenu
nyinyi enyi Mayahudi msiinajis Tawrat’ Mayahudi hao wakaubusu mkono wa Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam nakisha waksema: ‘Kwa hakika wewe ni Mtume
wa Kweli.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Kwa hivyo ni kitu gani
kinachokuzuieni kuingia katika Uislam?’ Mayahudi hao wakasema: ‘Daud aliomba
Dua kwa Mola wake kua Utume ubakie kwenye Kizazi chake, na pia tukijiunga
nawe basi Mayahudi watatuua’’’(Imam At Tirmidhii, Imam An Nasai)

Ambapo kwa upande wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu, Matr al Waraq. Ata,
Mujahid na Amr Ash Shabi basi wao wanasema kua: ‘Miujiza hio ilikua ni Kung’ara
kwa Mkono wake, Fimbo yake, Tufan, Nzige, Chawa, Vyura, Damu, Miaka ya
Ukame na Kuteketea kwa mazao’’

Hivyo baada ya Fir’awn kumwambia Nabii Musa kua yeye anadhani kua Nabii Musa
amerogwa, basi Nabii Musa akamuwekea wazi Fir’awn hapo hapo uso kwa uso mbele ya
watu wote kwa kumwambia:
744

ِ ‫ب ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬ ِ ۤ ِ
‫ﺼﺂﺋَِﺮ َوإِِّﱏ‬ ‫ﺑ‬ ِ
‫ض‬ ‫َر‬
‫ﻷ‬ ‫ٱ‬‫و‬
ََ ْ َ ََ ‫َﱡ‬‫ات‬ ‫ر‬ ‫ﱠ‬
‫ﻻ‬ ِ
‫إ‬ ‫ء‬ ‫ﻻ‬ ‫َﻧﺰَل َﻫـُٰﺆ‬
َ ‫ﺖ َﻣﺂ أ‬ َ َ‫﴿ﻗ‬
َ ‫ﺎل ﻟََﻘ ْﺪ َﻋﻠ ْﻤ‬
﴾ً‫ﱡﻚ ٰﻳ ِﻔﺮ َﻋﻮ ُن َﻣﺜْـﺒُﻮرا‬
ْ َ ‫َﻷَﻇُﻨ‬
Qala laqad AAalimta ma anzala haola-i illa rabbu alssamawati waal-ardi basa-ira
wa-innee laadhunnuka ya firAAawnu mathbooran (Surat Al Isra 17:102)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa) Kwa hakika unajua wewe kua hakuna alieshusha
(Miujiza hii) isipokua Mola wa Mbingu na Ardhi kua kama vithibitisho (vya kuwepo
kwake peke yake) na mimi nnadhani ewe Fir’awn kua Umeshaangamia.

Aya inatuonesha Ujasiri na namna alivyokua akijiamini Nabii Musa mbele ya Fir’awn
kwani anamwambia kua: ‘Mimi nnafikiri kua wewe ndio una wazimu, hivyo wacha
nikuambie nini nnachodhania kuhusiana nawe. Mimi nnadhani kua kwa hakika
wewe Umelaaniwa na umeshaingia kwenye Maangamizi’

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea hali waliyokua nayo Watu wa Bani Israil
kwani baada ya tukio hilo basi wote waliokua wakimfuata Nabii Musa walikua chini ya
vikwazo na mateso makubwa sana kiasi ya kua watu wa Bani Israil walikua
wakifanyishwa kazi bila ya kulipwa wala kupewa chakula au kuhudumiwa kwa njia
yeyote ile, na walikua wanaishi katika hali duni ambayo ni zaidi ya Wanyama kwani hata
hao wanyama wa kufuga walikua wakihudumiwa tofauti na ilivyokua kwa upande wao.

Hivyo watu wa Bani Israil wakaanza kumsikitikia Nabii Musa kuhusiana na mitihani yao
na ugumu wa maisha yao ambapo nae akawausia kua na Subra katika kipindi hicho, kwa
kusema:

ِ ِ ‫﴿ﻗَﺎﻟُ ۤﻮاْ أ‬
َ َ‫ُوذﻳﻨَﺎ ِﻣﻦ ﻗَـْﺒ ِﻞ أَن َﺄﺗْﺗِﻴَـﻨَﺎ َوِﻣﻦ ﺑَـ ْﻌ ِﺪ َﻣﺎ ِﺟْﺌـﺘَـﻨَﺎ ﻗ‬
َ ‫ﺎل َﻋ َﺴ ٰﻰ َرﺑﱡ ُﻜ ْﻢ أَن ﻳـُ ْﻬﻠ‬
‫ﻚ‬
﴾‫ﻒ ﺗَـ ْﻌﻤﻠُﻮ َن‬
َ َ ‫ض ﻓَـﻴَﻨﻈُْﺮ َﻛْﻴ‬ ِ ‫َﻋ ُﺪ ﱠوُﻛ ْﻢ َوﻳَ ْﺴﺘَ ْﺨﻠِ َﻔ ُﻜ ْﻢ ِﰱ ٱﻷ َْر‬

Qaloo oodheena min qabli an ta/tiyana wamin baAAdi ma ji/tana qala AAasa
rabbukum an yuhlika AAaduwwakum wayastakhlifakum fee al-Ardhi fayandhura
kayfa taAAmaloona (Surat Al Araf 7:129)
745

Tafsir: Wakasema (Watu wa Bani Israil): ‘Hakika sisi tumeudhiwa sana kabla ya kuja
kwako na baada ya kuja kwako’ Nabii Musa akasema: ‘Inawezekana ikawa Mola
wenu anataka kumuangamiza Adui yenu na kukufanyeni nyie kua Makhalifa hapa
ardhini kisha akuoneni ni nini mtakachokifanya.’

Ingawa kuna tofauti ya mitizamo kuhusiana na asili ya maneno hayo kwani kuna wasema
kua watu wa Bani Israil waliyasema hayo kabla ya kuanza safari ya kuhama nchini Misri
na kuvuka bahari, lakini kwa upande wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu na
Mujahid Ibn Sulayman basi wao wanasema kuhusiana na aya hii kua: ‘Aya hii
inatupeleka mpaka mwisho wa sehemu inayo wazungumzia Watu wa Fira’wn na
watu wa Nabii Musa walipowasili katika mwambao wa Bahari ambapo baina yao
mbele yao kuna Jeshi la Fir’awn. Hivyo wakasema watu wa Bani Israil
kumlalamikia Nabii Musa kua: ‘Hakika sisi tumekua tukiteswa kabla ya kuja
kwako na baada ya kuja kwako.’’

Nabii Musa akawahakikishia Watu wake hao kua Allah Subhnah wa Ta’ala atawatatulia
hali waliyokua nayo, na atawaangamiza Fir’awn na watu wake na kisha atawarithisha
watu wa Banii Israil Ardhi ambayo wataishi kwa usalama na amani ndani yake, na
atawaangalia vipi watakavyoishi ndani yake yaani kwa kuonesha shukran kwake ama la.

Kwani Muumini anapokua amefikwa na Mitihani basi hua anatakiwa awe ni mwenye
kuichukulia Mitihani hio kutoka kwa Mola wake kwa kua na hali zifuatazo:

-Anatakiwa awe na Ustahmilivu kutokana na Mitihani hio, asilalamike juu ya


mitihani hio, na badala yake anatakiwa kua ni mwenye kumshukuru Mola wake
kwani Mtihani huo hua ni bora kwake katika wakati huo. Na hivyo kama Allah
Subhanah wa Ta’ala akiamua kumuachia katika hali yake hio hua ni kwa sababu
anastahili kua katika hali hio, na kama akimuondolea Mitihani hio basi hua ni
kutokana na Rehma zake juu ya mja wake huyo.

-Anatakiwa kua ni mwenye kumshukuru na kumkumbuka Mola wake zaidi kuliko


kua katika hali ya kuomba dua na kama akiwa ni mwenye kuomba dua basi aombe
zaidi kuhusiana na kuzidishiwa Imani ya dini yake.

-Anatakiwa aendelee na kufanya mema kwa ikhlas hata baada ya kuondolewa


Mitihani hio na Mola wake.

-Anatakiwa awe ni mwenye kumfikiria Mola wake tu hata baada ya kutoka katika
Mitihani huo, hivyo asiwe ni mwenye kufikiria Mitihani yake. Kwani Allah
Subhanah wa Ta’ala humpandisha Darja mtu aliempa Neema au Mtihani pale
inapokua mtu huyo hafikirii kuhusiana na Neema hio au Mtihani huo bali
anapokua anafikiria kuhusiana na yule aliempa Neema hio au Mtihani huo.
746

Ambapo kwa upande wa Fir’awn pia basi hakua ni mwenye kumfikiria wala
kumkumbuka Mola wake aliempa neema aliyokua nayo bali alikua akifikiria neema
aliyokua nayo tu, na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akajaribu kuwapa mitihani Fir’awn
na watu wake ili warudi kwa Mola wao kama zinavyoweka wazi aya.

ِ ‫ﺺ ِﻣﻦ ٱﻟﺜﱠﻤﺮ‬
﴾‫ات ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻬﻢ ﻳَ ﱠﺬ ﱠﻛﺮو َن‬ ِ ِ ِ‫آل ﻓِﺮﻋﻮ َن ﺑ‬
ُ ْ َ َ ّ ٍ ‫ﲔ َوﻧَـ ْﻘ‬
َ ‫ﭑﻟﺴﻨ‬
ّ َ ‫﴿ َوﻟََﻘ ْﺪ أ‬
َ ْ َ �َ ‫َﺧ ْﺬ‬
Walaqad akhadhna ala firAAawna bialssineena wanaqsin mina alththamarati
laAAallahum yadhdhakkaroona (Surat Al Araf 7:130)

Tafsir: Na kwa hakika tuliwapa watu wa Fir’awn adhabu ya Ukame wa miaka na


upungufu wa mazao ili wapate kua ni wenye kukumbuka (kuhusiana na Mola wao).

Ingawa Ardhi ya nchi ya Misri ni yenye kunufaika sana na maji ya Mto Nile, na hivyo
kua ni wenye kuongoza kwa kuzalisha mazao ya kilimo kutokana na rutba ya Ardhi yao
iliyo ukingoni wa Mto Nile na hivyo pia hurahisisha kazi ya umwaligiliaji maji
mashambani, lakini Allah Subhanah wa Ta’ala aliwaonesha Miujiza yake kua hakuna
kitu kinachoota ardhini isipokua kutokana na majaaliwa yake. Na kuwajaalia hali ya
Ukame wa Miaka kadhaa ili warudi kwake Allah Subhanah wa Ta’ala.

Lakini hata hivyo, Mtihani hio kamwe haikua ni yenye kuwafanya kua ni wenye
kumkumbuka Mola wao bali hali ilikua kinyume chake, kwani walikua wakimtupia Nabii
Musa katika ila msiba na mtihani unaowakuta kutokana na kuona kua yeye Nabii Musa
ndie aliekua akiwatia Nuksi na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akasema:

ِ ِ ِ ِِ ْ ‫﴿ﻓَِﺈ َذا َﺟﺂءَﺗْـ ُﻬ ُﻢ‬


َ ُ‫ٱﳊَ َﺴﻨَﺔُ ﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻟَﻨَﺎ َﻫـٰﺬﻩ َوإن ﺗُﺼْﺒـ ُﻬ ْﻢ َﺳﻴِّﺌَﺔٌ ﻳَﻄﱠﻴﱠـُﺮواْ ﲟ‬
ُ‫ﻮﺳ ٰﻰ َوَﻣﻦ ﱠﻣ َﻌﻪ‬
﴾‫ٱﻪﻠﻟِ وﻟَـٰ ِﻜ ﱠﻦ أَ ْﻛﺜَـﺮُﻫﻢ ﻻَ ﻳَـ ْﻌﻠَﻤﻮ َن‬ ِ ِ ‫ﱠ‬ ِ ۤ
ُ ْ َ ‫ﱠ‬
َ َ ْ ُُ‫ﻨﺪ‬ ‫ﻋ‬ ‫ﻢ‬ ‫ﻫ‬ ‫ﺮ‬ ‫ﺎﺋ‬َ‫ﻃ‬ ‫ﺎ‬‫ﳕ‬
َ ‫إ‬ ‫َﻻ‬‫أ‬
Fa-idha jaat-humu alhasanatu qaloo lana hadhihi wa-in tusibhum sayyi-atun
yattayyaroo bimoosa waman maAAahu ala innama ta-iruhum AAinda Allahi
walakinna aktharahum la yaAAlamoona (Surat Al Araf 7:131)

Tafsir: Kisha linapowajia kila jema hua wanasema kua: ‘Hili ni letu’ na linapowajia
Ovu basi humtupia Musa na walio pamoja nae. Ama kwa hakika Uovu wao ni kutoka
kwa Allah lakini wengi wao hawajui.
747

Ambapo aya imetumia maneno yasemayo Yattayyaroo bi Muusa ambapo neno


Yattayyaroo linatokana na neno Tara ambalo hua ni lenye kumaanisha Kuruka, Kupaa
Angani, Kurukia Jambo, Kuharakia kufanya Jambo. Neno Tara ndio lililotoa neno Tairun
ambalo humaanisha Nuksi, Jambo Ovu, Bahati mbaya na pia humaanisha Mtu anaepaa
juu katika kuisimamia Nafsi yake kwa ajili ya Imani ya Dini huku akiwa ameachana
kabisa na Mambo ya Kidunia.

Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakkalimin Imam Fakhr Ad Din Al Raz anayafafanua


maneno haya kwa kusema kua: ‘Ilikua ni kawaida kwa Utamaduni wa Waarabu
kuagua jambo jema na jambo baya kwa njia ya kuangalia ndege, yaani kua kama
ameruka kutoka katika kitu fulani kwa hiari yake mwenyewe au si kwa hiari yake,
aidha kama amerukia upande wa kulia au wa kushoto, au kwa kuelekea juu moja
kwa moja, na kisha hunasibisha mruko wa ndege husika na tukio husika kama
litakua jema au ovu, hivyo basi neno hilo ndio ikawa linatumika kumaanisha
matokeo ya jambo husika kama jema au ovu ’

Hivyo watu wa Misri wakamwambia Nabii Musa kua:

﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ِ َ َ‫﴿وﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻣﻬﻤﺎ َﺄﺗْﺗِﻨَﺎ ﺑِِﻪ ِﻣﻦ آﻳ ٍﺔ ﻟِّﺘَﺴﺤﺮَ� ِﻬﺑﺎ ﻓَﻤﺎ َْﳓﻦ ﻟ‬
َ ‫ﻚ ﲟُْﺆﻣﻨ‬ ُ َ َ ََ ْ َ َ َْ َ
Waqaloo mahma ta/tina bihi min ayatin litasharana biha fama nahnu laka
bimu/mineena (Surat Al Araf 7:132)

Tafsir: Na wakasema (kumwambia Nabii Musa): ‘Hata utupe Aya gani zitakazo
onesha uchawi wako kwetu, hatutoweza kukuamini.’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akaamua kuwashushia Mtihani mmoja baada ya


mwengine kama anavyobainisha katika aya ifuatayo:

ٍ َ‫ﺼﻼ‬
‫ت‬ ٍ �‫ﻀ َﻔ ِﺎدع وٱﻟﺪﱠم آ‬
‫ت ّﻣ َﻔ ﱠ‬ ْ ‫﴿ﻓَﺄ َْر َﺳ ْﻠﻨَﺎ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ُﻢ ٱﻟﻄﱡﻮﻓَﺎ َن َو‬
َ َ َ َ ‫ٱﳉََﺮ َاد َوٱﻟْ ُﻘ ﱠﻤ َﻞ َوٱﻟ ﱠ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ
َ ‫ﭑﺳﺘَ ْﻜﺒَـُﺮواْ َوَﻛﺎﻧُﻮاْ ﻗَـ ْﻮﻣﺎً ﱡْﳎ ِﺮﻣ‬
ْ َ‫ﻓ‬
Faarsalna AAalayhimu alttoofana waaljarada waalqummala waaldhdhafadiAAa
waalddama ayatin mufassalatin faistakbaroo wakanoo qawman mujrimeena (Surat
Al Araf 7:133)
748

Tafsir: Hivyo tukawatumia Tufani, na Nzige, na Chawa, na Vyura na Damu. Aya zetu
zilizowazi lakini hata hivyo wakaendelea kua na Kibri na kua watu wahalifu wenye
makosa.

Ambapo anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Adhabu ya Mwanzo
ilikua ni Tufani, ambayo ilikua ni Maji yaliyoshushwa kutoka Mbinguni’, na kwa
upande wa Wahb Ibn Munabih basi yeye anasema kua: ‘Ilikua ni Maradhi ya
Maambukizo ambayo yaliwakumba watoto wa mwanzo wote wa watu wa Misri
mpaka wakatekea wote.’

Ambapo wa upande wa Said Ibn Jubayr basi yeye anasema kua: ‘Tufan ilikua ni
Wadudu ambao walitokana na Ngano’ ambapo kwa Upande wa Mujahid basi yeye
anasema kua walikua ni Nzige.

Na kwa Upande wa Imam Ahmad Ibn Muhammad Ath Thalabi basi yeye anasema ku:
‘Tufani hii ilika ni mvua kubwa sana kiasi ya kua kila kitu kiliangamia isipokua
nyumba za Watu wa Bani Israil, ingawa nyumba hio zilikua karibu karibu lakini
nyumba zilizoathirika ilikua ni za watu wa Misri tu, kiasi ya kua watu walikua
hawawei kukaa ndani ya nyumba zao kwa mda wa wiki nzima, tangu Jumamosi
mpaka Jumamosi, na ilipofikia mda huo basi, Fir’awn na Watu wake wakamuomba
Nabii Musa awaombee kwa Mola wake ili awaondolee Miihani huo na kisha
watamuamini Nabii Musa na pia watawaachia huru watu wa Bani Israil. Hivyo
Nabii Musa akawaombea na Allah Subhanah wa Ta’ala akawaondolea Mafuriko
hayo, lakini hata hivyo watu hao hawakua ni wenye kutekeleza ahadi yao bali ndio
walizidi kuwatesa watu wa Bani Israil.’

Kama zinavyoelezea aya kwa kusema:

ِ َ ِ‫ﻚ ِﲟَﺎ ﻋ ِﻬ َﺪ ﻋ‬ ِ ‫﴿ َوﻟَ ﱠﻤﺎ َوﻗَ َﻊ َﻋﻠَْﻴ ِﻬﻢ‬


‫ﺖ‬
َ ‫ﻨﺪ َك ﻟَﺌﻦ َﻛ َﺸ ْﻔ‬ َ َ ‫ﻮﺳ ٰﻰ ْٱدعُ ﻟَﻨَﺎ َرﺑﱠ‬ َ ُ‫ٱﻟﺮ ْﺟُﺰ ﻗَﺎﻟُﻮاْ ٰﳝ‬
ّ ُ
ِ ‫ﻚ ﺑَِ ۤﲏ إِ ْﺳﺮآﺋِﻴﻞ۞ ﻓَـﻠَﻤﺎﱠ َﻛ َﺸ ْﻔﻨَﺎ َﻋْﻨـ ُﻬﻢ‬
‫ٱﻟﺮ ْﺟَﺰ‬ َ ‫ﻌ‬
َ ‫ﻣ‬
َ ‫ﻦ‬
‫ﱠ‬ َ‫ﻠ‬ ِ‫ﻚ وﻟَﻨُـﺮ‬
‫ﺳ‬ ْ َ َ ‫ﻟ‬
َ ‫ﻦ‬
‫ﱠ‬ ‫ﻨ‬
َ ِ‫ٱﻟﺮﺟﺰ ﻟَﻨُـ ْﺆ‬
‫ﻣ‬ َ ْ ِّ ‫َﻋﻨﱠﺎ‬
ّ ُ َ َ
﴾‫َﺟ ٍﻞ ُﻫﻢ َﺎﺑﻟِﻐُﻮﻩُ إِذَا ُﻫﻢ ﻳَﻨ ُﻜﺜُﻮ َن‬ ِ
َ ‫إ َ ٰﱃ أ‬
ْ
Walamma waqaAAa AAalayhimu alrrijzu qaloo ya moosa odAAu lana rabbaka
bima AAahida AAindaka la-in kashafta AAanna alrrijza lanu/minanna laka
walanursilanna maAAaka banee isra-eela; Falamma kashafna AAanhumu alrrijza
ila ajalin hum balighoohu idha hum yankuthoona (Surat Al Araf 7:134-135)
749

Tafsir: Na mara inapowafikia juu yao adhabu basi husema: Ewe Musa mwambie Mola
wako kutokana na ahadi yake juu yako, kua kama utatuondolea adhabu basi
tutakuamini na tutawaachia watu wa Bani Israil uondoke nao. Lakini
tunapowaondolea adhabu kulingana na masharti watakayotekeleza, basi huyavunja
masharti hayo.

Kwani baada ya watu wa Misri kutoa ahadi hio basi Nabii Musa akawaombea kwa Allah
Subhanah wa Ta’ala na Dua hio ikajibiwa kwa kuiondoa Tufani hio, na kisha Allah
Subhanah wa Ta’ala akajaalia kujaa rutba Ardhi ya nchi ya Misri tena upya na kila kitu
kikaota na kunawiri vizuri sana juu yake. Na kutokana na ukame uliokuwepo hapo awali
na kisha kufuatia mafuriko na kufuatia mazao kunawiri basi watu hao wa Misri wakaona
kua, kumbe hii haikua ni adhabu bali ilikua ni hali ya maumbile tu. Hivyo wakasema:
Lana hadhihi yaani hili ni letu.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akawashushia mtihani wa Al Jarada yaani Nzige


ambao walikuja kama Wingu kubwa sana kiasi ya kua mchana ulibadilika na usiku kwani
jua lilikua halionekani kutokana na wingi wao, na walikua kila kitu kilichoota na kustawi
ardhini baada ya Mvua hio, na si hivyo tu bali baada ya kumaliza viotavyo ardhini basi
wakaingia Majumbani, na kuanza kula akiba ya chakula chote na baada ya kamaliza basi
waliendelea kula kila kitu chenye asili ya Mbao ndani yake, Meza, Viti, Vitanda,
Makabati, Madirisha na Milango pia nakisha wakahamia kwenye Mapaa ya Makuti, hadi
ikafika hali ya kua Nyumba za Watu wa Misri hazikaliki ndani yake kwani hakuna
Usalama wala Hifadhi ndani yake, huku nyumba za Watu wa Bani Israil zikiwa
hazijaathirika na kitu chochote.

Hivyo walipoona kua hali imefikia hivyo basi Watu wa Misri wakawammabia Nabii
Musa awaombee tena, na watatimiza masharti ya Allah Subhanah wa Ta’ala kama
walivyotakiwa hapo kabla. Hivyo Nabii Musa akaomba kwa Allah Subhanah wa Ta’ala
na akashushiwa Wahyi kua aende kwenye sehemu yenye Miti mingi kisha aelekee
Upande wa Mashariki huku akiioneshea upande huo Fimbo yake, na alipofanya hivyo
basi Nzige wote walitoa katika Ardhi ya Misri na kutowekea katika upande wa Mashariki
alioelekezea Nabii Musa Fimbo yake.

Baada ya hapo hali ya maisha ya watu wa Misri ikarudi na kua ya kawaida, watu
wakajenga nyumba zao upya na kuendelea kuishi kama kawaida lakini wakagoma
kutekeleza ahadi waliyoiahidi hapo hapo kabla, kwani Nabii Musa alipowakumbusha
kuhusiana na ahadi ya kumuamini na kuwaachia huru watu wa Bani Israil basi watu hao
wa Misri wakiogozwa na Fir’awn wakasema kua sharti hilo haliwezekani kutekelezeka.

Nabii Musa akamuomba Allah Subhanah wa Ta’ala awaoneshe uwezo wa jeshi lake
hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Nabii Musa aende katika maeneno ya
Ardhi ya Ayn Shams ambayo kuna mlima wenye udongo mwekundu, kisha akishafika
750

aupige fimbo yanke Mlima huo, hivyo Nabii Musa akaelekea kwenye Mlima huo kisha
akaupiga fimbo yake, na wakatokezea Qummal yaani wadudu Chawa. Subhanah Allah!

Hili jeshi la Chawa lilikua hatari zaidi kwani Wadudu hao walikua kila kitu na kuingia
ndani yake, kiasi ya kua mpaka ndani ya mikate ikipikwa na kuwiva basi ikitiwa mdomo
tu hua wanamiminika Chawa kutoka ndani yake. Chawa hawa walikula nywele zote za
miili ya Watu wa Fir’awn, hivyo wote wakawa vipara, hawana Nyusi wala kope wala
ndevu wala sharafa, na katika kila sehemu inayoliwa na Chawa hao basi huacha vipele
badala yake hivyo watu wa Misri walikua weupee wenye vidonda vidonda mwili mzima
ikawa hata usiku kulala haiwezekani. Na ingawa hali hii ilikua kwa mda wa siku saba tu,
lakini ukubwa adhabu yake ilikua kama miaka saba.

Hivyo Fir’awn na watu wake wakamtafuta Nabii Musa na kumuomba kua awaombee
waondokewe na wadudu hao huku wakiapaa kua watatekeleza masharti waliyokubaliana
nae hapo kabla, Nabii Musa akaomba kwa Mola wake na akaambiwa akakipige tena kile
kilima kilichopo Ayn Shams, na alipokipiga basi Chawa wote wakatoweka kwenye Ardhi
ya Misri.

Baada ya kutoweka kwa Chawa hao basi Watu wa Misri wakasema kua kweli Nabi Musa
ni Mchawi, na ndio maana anawafinyia hivyo anavyowafanyia, na bila ya shaka
wameshayaonja mengi kwa hivyo hana adhabu mpya zaidi cha kuwaadhibia, hivyo
kamwe hawatowaachia huru watu wa Bani Israil, kwani ni watumwa wao na hawana
wengine wa kuwafanyia kazi zao isipikua wao. Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala
akawaachia watu hawa kwa mda wa siku 40. Kisha akaamua kuwaonesha Muujiza
mwengine kwa kumwamrisha Nabii Musa aende kwenye mwambao wa Mto Nile kisha
akaichomeke Fimbo yake kwenye maji ya Mto huo, na kisha aitoe hukua akiielekezea
upande wa Kusini, Mashariki, Kaskazini na Magharib ya maji ya Mto huo.

Bada ya Nabii Musa kufanya kama alivyoamrishwa na Mola wake basi ghafla moja
kulisikia vilio vya DhdhafadiaA’a yaani Vyura, ambao walitoka katika kila upande wa
Mto Nile na kuelekea kwenye Ardhi ya Misri. Vyura hawa wingi wake ilikua kama vile
Ardhi yote ya Misri imetandikwa Majani, kwani ilikua hamna sehemu ya kuweka mguu,
isipokua utakanyaga vyura kila sehemu mpaka majumbani. Watu wa Misri waliwaua
Vyura mpaka wakachoka wenyewe kwani ilikua kila ukiwaua nido wanazidi
kuongezeka.

Ilikua unaweza kufungua sanduku la nguo ukitoa nguo basi wanatoka na vyura ndani
yake, vyuira mpaka kitandani hakulaliki wala hakusimamiki na wala hakunyweki maji
kwani ukinywa maji basi wanatoka vyura ndani ya chombo cha maji na kuingia
mdomoni, na mpaka ukipika basi ukifunua mkungu wa sufuria badala ya kua mna
chakula basi unakutana na Vyura ndani yake, kawaida wadudu Vyura hua wanakaa
kwenye maji ya baridi lakini Miujiza ya Vyura hawa ilikua mpaka kwenye maji
751

yanayochemka wanatoka vyura. Na la sauti zao kali zisizosita wala kupungua kasi wala
ukubwa wa sauti yake ndio mtihani kubwa zaidi.

Siku chache baada ya kutokea Vyura basi watu wakamkabili Fir’awn tena na kumsikitikia
matatizo yao, hivyo ikabidi atafutwe tena Nabii Musa kwa ajili ya kuwaondoa Vyura hao
baaada ya mara nyengine tena kutoa ahadi kwao. Nabii Musa akawaonea huruma na
akawaombea kwa Allah Subhanah wa Ta’ala kuondolewa kwa Adhabu ya Vyura hao.
Ilipotimia siku ya saba basi Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Nabii musa aende
tena kwenye mto Nile kisha akaizamishe tena fimbo yake kwenye maji ya Mto huo na
Vyura hao wote watarudi kwenye maji, Nabii Musa akatekeleza amri ya Mola wake na a
Vyura wakarudi kwenye Mto Nile, kisha Allah Subhanah wa Ta’ala akajaalia Upepo
ambao ukavuma na kuwapeperusha Vyura wote waliokufa kwa kukanywagwa na watu
wa Misri.

Nabii Musa akawakumbusha watu wa Fir’awn kuhusiana na ahadi yao lakini nao
wakazidisha Kibri dhidi yake na kumwambia kua afanye atakachofanya lakni kamwe
hawatomuamini wala hawatowaachia huru watu wa Bani Israil, Nabii Musa akamshtakia
Mola wake juu ya jitihada zake hizo na kutokukubali watu wa Fir’awn kutimiza ahadi
yao, hivyo baada ya siku kadhaa Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Nabii Musa
kua aende tena kwenye Mto Nile akaichomeke Fimbo yake kwenye maji yake. Nabii
Musa akafanya tena kama alivyoelekezwa na Mola wake.

Baada ya tukio hilo basi kilichofutaia ni Muujiza wa Dam yaani Damu kutiririka kwenye
Maji ya Ardhi ya nchi ya Misri. Kwani baada ya Nabi Musa kuitoa fimbo yake kwenye
Maji ya Mto Nile basi Maji hayo yote yakawa na rangi nyekundu na kua na harufu ya
Damu. Na si maji yam to huo tu basi mpaka mjai ya visima vyote, na pia maji
yaliyohifadhiwa kwenye mahodhi na vyombo vyote vya kuhifadhia Maji nchini humo.
Lakini maajabu ya maji hayo yalikua na upekee kwani maji ya watu wa Bani Israil
hayakuathirika, nata hata walipokua wakichota maji kutoka katika kisima kimoja basi
akichota Mmisri maji hua ni Damu, akichota Bani Israil hua ni Maji.

Watu wa Misri walipata tabu sana kwa kiu na kutoweza kupika, ikafikia hali kua wakawa
wanajua kua watu wa Bani Israil wanatumia maji kama kawaida kwani kwao wao
hayabadilikia, basi ikawa wanawaomba watu wa Bani Israil Maji kwa kwanza kuyatia
mdomoni mwao watu hao ili yasibadilike kua ni damu ili na wao wapate kunywa. Lakini
njia haikusaidia kitu kwani hata hao watu wa Bani Israil walipo fanya hivyo basi akiyatia
mdomoni hua ni maji ya kawaida akitaka kummiminia mtu wa Misri basi
kinachomiminika hakika chengine isipokua ni Damu.

Watu wa Misri wakamlalamikia tena Fir’awn na Fir’awn akamwita Nabii Musa na


kuahidi tena upya, hivyo Nabii Musa akaomba tena kwa Allah Subhanah wa Ta’ala na
akaamabiwa akaichomeke tena Fimbo yake kwenye mto Nile na bila ya shaka Maji ya
752

Mto huo yakawa ni Maji meupa kama kawaida na hapo hapo maji mengine yote
yaliyobakia kwenye Ardhi ya Misri yakageuka na kua Meupa ya kawaida na yenye ladha
kama maji ya kawaida, kupata kwao tena maji upya kwa watu wa Misri ilikua ni kama
sikukuuu, lakini bila ya shaka hawawezi kusheherekea bila ya kua na wafanyakazi, kama
vile ambavyo hawawezi kuishi bila ya kua na wafanyakazi wa kuwafanyia kazi zao
ngumu ambao ni watu wa Bani Israil.

Ambapo anasema Imam Ahmad Ibn Muhammad Ath Thalabi kua: ‘Amesema Said
Nawf Al Bakkali ambae ni mtoto wa mke wa Kaab Al Akhbar kua: ‘Baada ya Nabii
Musa kuwashinda wachawi wa Fir’awn, basi Nabii Musa alikaa na watu hao wa
Fir’awnkwa miaka 20 hukua akiwa ni mwenye kuwaonesha Dalili za Mafuriko,
Nzige, Chawa, Vyura na Damu’’

Baada ya kutimia miaka 20 kwa Nabii Musa kukaa na watu wake wa Bani Israil na
pamoja na watu wa Fir’awn na kutoona matunda yeyote kutokana na jitihada zake za
kuwausia watu hao basi akaamua kumuomba Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kusema:

ْ ‫ﺖ ﻓِْﺮ َﻋ ْﻮ َن َوَﻣﻸَﻩُ ِزﻳﻨَﺔً َوأ َْﻣ َﻮاﻻً ِﰱ‬


‫ٱﳊَﻴَﺎةِ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ َرﺑـﱠﻨَﺎ‬ َ ‫ﻮﺳ ٰﻰ َرﺑـﱠﻨَﺂ إِﻧﱠ‬
َ ‫ﻚ آﺗَـْﻴ‬ َ َ‫﴿ َوﻗ‬
َ ‫ﺎل ُﻣ‬
ْ‫ﺲ َﻋﻠَ ٰﻰ أ َْﻣ َﻮاﳍِِ ْﻢ َوٱ ْﺷ ُﺪ ْد َﻋﻠَ ٰﻰ ﻗُـﻠُﻮﻬﺑِِ ْﻢ ﻓَﻼَ ﻳـُ ْﺆِﻣﻨُﻮا‬
ْ
ِ ْ‫ﻚ رﺑـﱠﻨَﺎ ٱﻃ‬
‫ﻤ‬ َ َ
ِ‫ﻀﻠﱡﻮاْ ﻋﻦ ﺳﺒِﻴﻠ‬
َ َ
ِ ‫ﻟِﻴ‬
ُ
﴾‫ﺣ ﱠﱴ ﻳـﺮواْ ٱﻟْﻌ َﺬاب ٱﻷَﻟِﻴﻢ‬
َ َ َ ُ ََ ٰ َ
Waqala moosa rabbana innaka atayta firAAawna wamalaahu zeenatan
waamwalan fee alhayati alddunya rabbana liyudhilloo AAan sabeelika rabbana
itmis AAala amwalihim waoshdud AAala quloobihim fala yu/minoo hatta yarawoo
alAAadhaba al-aleema(Surat Yunus 10:88)

Tafsir: Na akasema Musa: ‘Ewe Mola wangu! Hakika wewe umempa Fir’awn na
Watu wake Mapambo na Mali katika maisha ya Kidunia Ewe Mola wangu!
(Wanazitumia)ili kupotoa (Watu)kutoka katika muelekeo wako, Ewe Mola wangu
uteketeze Utajiri wao na watilie Ugumu katika Nyoyo zao, ili wasiamini mpaka
watakapopata Adhabu Kali sana.’

Ambapo baada ya Dua hio basi Nabii Harun akaitikia Aamin. Na hivyo Allah Subhanah
wa Ta’ala akasema:

﴾‫ﭑﺳﺘَ ِﻘﻴﻤﺎ وﻻَ ﺗَـﺘﱠﺒِ َﻌﺂ ِّن َﺳﺒِﻴﻞ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻻَ ﻳَـ ْﻌﻠَﻤﻮ َن‬ ِ َ َ‫﴿ﻗ‬
ُ َ َ َ َ ْ َ‫ﺖ ﱠد ْﻋ َﻮﺗُ ُﻜ َﻤﺎ ﻓ‬
ْ َ‫ﺎل ﻗَ ْﺪ أُﺟﻴﺒ‬
753

Qala qad ojeebat daAAwatukuma faistaqeema wala tattabiAAanni sabeela


alladheena la yaAAlamoona(Surat Yunus 10:89)

Tafsir: Akasema (Allah Subhanah wa Ta’ala) Hakika Mmejibiwa Dua yenu, hivyo
kueni katika mstari ulionyoka na wala msifuate njia ya wale ambao wasiojua.

Allah Subahanh wa Ta’ala anawambia Nabii Musa na Nabii Harun kua msiwe kama wale
wasiojua ambao hua ni wenye kuchanganyikiwa pale yanapochelewa kujibiwa maombi
yao waliyomuomba Allah Subhanah wa Ta’ala kutokana na kutojua kuhusiana na ahadi
za Allah Subhanah wa Ta’ala ambae amesema; Niombeni nitakujibuni. Kama
inavyosema aya:

‫ﻳﻦ ﻳَ ْﺴﺘَ ْﻜِﱪُو َن َﻋ ْﻦ ِﻋﺒَ َﺎدﺗِﻰ‬ ِ ‫ﻮﱐ أَﺳﺘ ِﺠﺐ ﻟَ ُﻜﻢ إِ ﱠن ٱﻟﱠ‬ۤ ِ ‫ﺎل رﺑﱡ ُﻜـﻢ ٱدﻋ‬
َ ‫ﺬ‬ ْ ْ َ ْ ُ ْ ْ َ َ َ‫﴿ َوﻗ‬
﴾‫اﺧ ِﺮﻳﻦ‬ِ
َ ‫َﺳﻴَ ْﺪ ُﺧﻠُﻮ َن َﺟ َﻬﻨ َﱠﻢ َد‬
Waqala rabbukumu odAAoonee astajib lakum inna alladheena yastakbiroona
AAan AAibadatee sayadkhuloona jahannama dakhireena (Surat Ghafir 40:60)

Tafsir: Na anasema Mola wenu: ‘Niombeni Nitakujibu, Hakika ya wale ambao


wanakufanyia Kibri kuabudiwa kwangu (na hawaniamini) bila ya shaka wataingia
Motoni wakiwa katika hali ya kuadhirika’

Anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kuhusiana na dua hio kua: ‘Dua hio
ya Nabii Musa Nabii Harun ilijibiwa na Allah Subhanah wa Ta’ala baada ya Miaka
40.’ Yaani baada ya Nabii Musa, Nabii Harun na watu wa Bani Israil kuvuka Bahari na
kisha Firawn na Jeshi lake kuangamizwa.

Hii pia inatuonesha umuhimu wa kutovunjika Moyo kutokana na kumuomba Dua Allah
Subhanah wa Ta’ala kwani kama tulivyoona hapo kabla katika kisa cha Nabii Ibrahim
kua dua yake ya mwanzo ya kutaka kizazi chema ilijibiwa baada ya miaka 80, na dua ya
kuombea Ardhi ya Mji wa Makkah ilijibiwa karne na Karne baadae yaani baada ya Kuja
Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam kwa sababu Allah Subhanah wa Ta’ala hua anajibu
Dua anazoombwa kulingana na Hali na Mazingira ya Muombaji na katika hali na
mazingira ambayo anaona kua yanafaa kutokana na wingi wa Hikma zake, kwa sababu
unaweza ukaomba Dua katika wakati ambao hata ukijibiwa basi Dua hio ikawa haina
manufaa nawe kama zinavyosema aya:
754

ُ َ‫ﺐ َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ُﻢ ٱﻟْ ِﻘﺘ‬


‫ﺎل َوُﻫ َﻮ ُﻛْﺮﻩٌ ﻟﱠ ُﻜ ْﻢ َو َﻋ َﺴ ٰﻰ أَن ﺗَ ْﻜَﺮُﻫﻮاْ َﺷْﻴﺌﺎً َوُﻫ َﻮ َﺧْﻴـٌﺮ ﻟﱠ ُﻜ ْﻢ‬ ِ ﴿
َ ‫ُﻛﺘ‬
﴾‫ٱﻪﻠﻟ ﻳَـ ْﻌﻠَﻢ وأَﻧْـﺘُﻢ ﻻَ ﺗَـ ْﻌﻠَﻤﻮ َن‬ ‫ﱠ‬ ِ
ُ ْ َ ُ ُ‫َو َﻋ َﺴ ٰﻰ أَن ُﲢﺒﱡﻮاْ َﺷْﻴﺌﺎً َوُﻫ َﻮ َﺷﱞﺮ ﻟ ُﻜ ْﻢ َو ﱠ‬
Kutiba AAalaykumu alqitalu wahuwa kurhun lakum waAAasa an takrahoo shay-
an wahuwa khayrun lakum waAAasa an tuhibboo shay-an wahuwa sharrun lakum
waAllahu yaAAlamu waantum la taAAlamoona(Surat Al Baqara 2:216)

Tafsir: Imeamrishwa kwenu Mapigano (kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala)


ingawa Mnaichukia na inawezekana ikawa mnakichukia kitu ambacho ni bora kwenu,
na inawezekana mkawa mnakipenda kitu ambacho kina shari nanyi, Na Allah ndie
mwenye kujua na Nyinyi hamjui.

Ambapo aya hii wengi hua wanaitafsiri sivyo, hivyo inabidi tujue kua Kusudio la
Amrisho linalohalalisha kupigana Jihad au kupigana vita kwa ajili ya Allah
Subhanah wa Ta’ala hujumisha mambo yafuatayo:

1- Kwa ajili ya kujilinda na kurudisha mashambulizi ya maadui.

2- Kuondoa dhulma ya kidini na kusimamisha uhuru wa kuabudu ili watu wapate uhuru
wa kuabudu na na nafasi ya kufanya Ibada zao kwa uhuru bila ya madhara.

Na masharti ya mapigano hayo huhusisha mambo yafuatayo:

1- Kusudio lake kuu lisiwe ni lenye kutokana na mapendekezo ya kibinafsi au kutafuta


faida kwa mtu fulani katika mapigano hayo.

2- Mapigano yawe ni lazima dhidi ya wale wapiganaji husika na wala sio wananchi
wasiokua na hatia ambao hawapo katika maeneo ya uwanja wa vita au wale ambao
hawahusiki kwa kutokua na silaha ama si miongoni mwa wapiganaji wa maadui.

3- Kuua wanawake na watoto hakuruhusiki kabisa. Katika Sahih Muslim kuna Hadith ya
Abd Allah Ibn Umar Radhi Allahu Anhu isemayo kua Nabii Muhammad Salallahu A’layi
wa Salam aliwaona watoto na wanawake wameuliwa katika vita na hapo akalaani kuwaua
Wanawake, Watoto na Wazee wasiokua na hatia na katika Hadith nyengine akasema kua
‘Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam ameharamisha kuu wanawake na
watoto’. Anasema Imam An Nawawi kuhusiana na Hadithi hizi kua : ‘Kuna Ijma’a ya
Wanazuoni kuhusiana na Hadith hizi kua hukmu yake inatumika katika vita pale
itakapokua Wanawake na Watoto hawapigani na Waislam. Lakini ikiwa
wanapigana basi Wanazuoni wengi wanasema inaruhusika kuwaua’ (Sharh Sahih
Muslim).
755

4- Kuyalinda Maisha ya mateka wa vita na kutovunjiwa haki zao za kibinaadamu.

5- Kuyalinda mazingira ambako kunajumuisha, makatazo ya kuua wanyama, kukata miti,


kuteketeza mazao mashambani, kuharibu mali, kuvunja majumba, kutia sumu na
kuchafua vyanzo vya maji iwe mto,visima, n.k

6- Kuulinda uhuru wa kuabudu kwa waumini wanaoamini dini nyengine wengine iwe
majumbani mwao, makanisani, mahekalu,n.k.

7- Kuvamia maadui kwa kuwashtukizia kumeharamishwa kabisa. Kwani amesema Nabii


Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kua : ‘Mu’umini hawaui wenzake. Imani
huondoka kwa kuua’. Imam Ibn Athir anasema kuhusiana na Hadithi hii kua ‘Mauaji
yaliyokusudiwa hapa ni kwa kuwashtukizia wengine bila ya kuwapa onyo, wakati
wakiwa hawajajitayarisha’ (Al-Nihaya fi Gharib al-Hadith wa al-Athar 3/775)

Imam Abu al-Hassan Ali Ibn Muhammad Ibn Muhammad ash Shaybani 'Izz Al Din Ibn
Al Athir Al Jazari anasema kuhusiana na Hadithi hii kua ‘Mauaji yaliyokusudiwa hapa
ni kwa kuwashtukizia wengine bila ya kuwapa onyo, wakati wakiwa
hawajajitayarisha’ (Al-Nihaya fi Gharib al-Hadith wa al-Athar 3/775)

8- Ruhusa ya kuingia katika nchi hua inahesabika kama makubaliano ya kiusalama ya


ukimya kua hairuhusiki kufanya ufisadi katika nchi ya maadui. Imam Abu l Qasim
Al Khiraqi 'Umar Ibn Al Husain Al Baghdadi Al Dimashqi anasema katika Mukhtasr
wake: ‘Yeyote yule anaeingia katika nchi ya maadui zake haruhusiwi kuwalaghai
na kuwapora Mali zao’, katika kuielezea kauli hii Imam Ibn Qudamah Al Maqdīsī
Muwaffaq Al Dīn Abū Muḥammad ʿAbd Allāh Ibn Aḥmad Ibn Muḥammad, anasema
katika Al Mughni, ‘Hairuhusiki kuwasaliti wao [Wasiokua Waislamu katika nchi
isiyokua si ya Waislam], kwa sababu kuna makubaliano ya kimya ya mtu kuingia
katika mji kwa usalama kutokana na sharti la kua mtu huyo anaeomba ruhusa ya
kuingia katika mji wa kigeni hatowadhuru au hatowasaliti watu wa mji huo. Hivyo
mtu yeyote yule atakaeingia katika mji wetu kwa usalama na kisha akatusaliti hua
anavunja makubaliano hayo. Hivyo hili hua ni katazo kwa sababu kua kufanya
hivyo hua kunasababisha hadaa ambayo imeharamishwa katika dini yetu.’ (Al-
Mughn̄i 9/237).

9- Adui ni lazima awe ni miongoni mwa wale ambao Muislam ameruhusika kupigana
nao, kwani ikiwa adui ni yule ambae kuna makubalianao ya kusitisha makubaliano na
Waislam, basi hua hairuhusiki kumvamia adui wakati wa usiku kwa sababu kufanya
hivyo hua ni kuvunja makubaliano ya usalama baina yao katika mambo yanayohusu
uhai, mali na heshima.

10- Hairuhusiki kuwatumia watu kama ngao ili kujilinda isipokua katika wakati wa vita
na katika hali maalum, ambavyo ni kama ilivyoelezewa na Wanazuoni.
756

Na anasema Imam Mansur Ibn Yunus Al Bahutī katika Sharh Muntahā Al Iradāt kua:
‘Hairuhusiki kuanzisha mapigano bila ya kupata amri ya Kiongozi, kwa sababu
yeye ndio mwenye mamlaka ya kufanya maamuzi kwa kutangazia vita, na hii ni
kwa sababu yeye ndie ambae hua na maelezo yote kuhusiana na maadui zake.
Ruhusa yake hua ni Wajibu, isipokua pale inapotekezea kua Waislam wamevamiwa
na wasiokua Waislam kwa ghafla bila ya kujua, na wanakhofia usalama wao, hapo
wataruhusika kupigana bila ya kusubiri ruhusa ya kiongozi wao kwa ajili ya
manufaa yao wote’

Hivyo Mapigano ya Vita vya Jihad yana Masharti yake na sababu zake, na ndio maana
pia tunapoangalia mfano wa kisa cha Nabii Musa basi tunaona kua kwa upande wao Nabii
Musa na Nabii Harun hawakuamrishwa kua wapigane na watu wa Misri bali walipewa
amri nyengine ambayo ni ya kufanya Hijra ya kuwahamisha watu wa Bani Israil kutoka
katika Ardhi ya nchini Misri, kuelekea katika Ardhi Takatifu ya Jerusalem.

HIJRA YA TATU YA NABII MUSA – MUUJIZA WA KUPASUKA KWA


BAHARI NA KUANGAMIA KWA FIR’AWN NA JESHI LAKE.


Hivyo baada ya Fir’awn na Watu wa Misri kukataa kutekeleza makubaliano yao na Nabii
Musa na kugoma kumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala mbali ya kuoneshwa Miujiza
kadhaa basi Allah Subhanah wa Ta’ala akaamua kuchukua hatua dhidi ya watu hao,
kwani hali ya watu hao imekua haina tofauti na ile hali ya watu wote waliotangulia kabla
yao na waliofuata baada yao ambao ni wasiomuamini Allah Subhanah wa Ta’ala yaani
pale wanapopewa Mitihani basi hua ni wenye kumuamini na kukubaliana na masharti
yake lakini wanapoondolewa Mitihani hio basi hugeuka na kua kama sio wao walioahidi
hapo kabla kama zinavyosema aya zifuatazo:

‫ﱠﺎس إِﱠﳕَﺎ ﺑَـ ْﻐﻴُ ُﻜ ْﻢ َﻋﻠَ ٰﻰ‬ ِ ْ ‫ض ﺑِﻐَ ِْﲑ‬ ِ ‫ﺎﻫ ْﻢ إِ َذا ُﻫ ْﻢ ﻳَـْﺒـﻐُﻮ َن ِﰱ ٱﻷ َْر‬
ُ ‫ٱﳊَ ّﻖ ٰ�َﻳـﱡ َﻬﺎ ٱﻟﻨ‬ ُ َ‫﴿ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺂ أَﳒ‬
‫ٱﳊَﻴَﺎةِ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ ﰒُﱠ إِﻟَﻴﻨَﺎ َﻣْﺮِﺟﻌُ ُﻜ ْﻢ ﻓَـﻨُـﻨَـﺒِّﺌُ ُﻜ ْﻢ ِﲟَﺎ ُﻛﻨﺘُ ْﻢ ﺗَـ ْﻌ َﻤﻠُﻮ َن۞إِﱠﳕَﺎ َﻣﺜَ ُﻞ‬
ْ ‫ﺎع‬ ِ
َ َ‫أَﻧ ُﻔﺴ ُﻜ ْﻢ ﱠﻣﺘ‬
‫ض ِﳑﱠﺎ َ�ْ ُﻛ ُﻞ‬ ُ َ‫ﻂ ﺑِﻪ ﻧَـﺒ‬
ِ ‫ﺎت ٱﻷ َْر‬ ِ َ َ‫ﺂء ﻓَﭑﺧﺘَـﻠ‬ ِ ِ ‫ﺂء أ‬
ْ ‫َﻧﺰﻟْﻨَﺎﻩُ ﻣ َﻦ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤ‬
ٍ ِ ْ
َ ‫ٱﳊَﻴَﺎة ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ َﻛ َﻤ‬
‫ﺖ َوﻇَ ﱠﻦ أ َْﻫﻠُ َﻬﺂ أَﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ‬ ِ ‫ٱﻟﻨﱠﺎس وٱﻷَﻧْـﻌﺎم ﺣ ﱠﱴ إِ َذآ أ‬
ْ َ‫ض ُز ْﺧُﺮﻓَـ َﻬﺎ َوٱ ﱠزﻳـﱠﻨ‬ ُ ‫َﺧ َﺬت ٱﻷ َْر‬ َ ٰ َ َُ َُ
757

ِ ‫ﺼﻴﺪاً َﻛﺄَن ﱠﱂْ ﺗَـ ْﻐ َﻦ ﺑِﭑﻷ َْﻣ‬


‫ﺲ‬ ِ ‫ﻗَ ِﺎدرو َن ﻋﻠَﻴـﻬﺂ أ ََﺎﺗﻫﺂ أَﻣﺮَ� ﻟَﻴﻼً أَو ﻧَـﻬﺎراً ﻓَﺠﻌ ْﻠﻨَﺎﻫﺎ ﺣ‬
َ َ َ َ َ ْ ْ ُْ َ َ ْ َ ُ
‫ٱﻪﻠﻟُ ﻳَ ْﺪﻋُ ۤﻮ إِ َ ٰﱃ َدا ِر ٱﻟ ﱠﺴﻼَِم َوﻳَـ ْﻬ ِﺪى‬
‫ت ﻟَِﻘ ْﻮٍم ﻳَـﺘَـ َﻔ ﱠﻜُﺮو َن۞ َو ﱠ‬
ِ �‫ﺼﻞ ٱﻵ‬
َ ُ
ِ ‫ﻚ ﻧـُ َﻔ‬
ّ َ
ِ‫َﻛ ٰﺬﻟ‬
﴾‫اط ﱡﻣﺴﺘَ ِﻘﻴ ٍﻢ‬ ٍ ِ ِ
ْ ‫َﻣﻦ ﻳَ َﺸﺂءُ إ َ ٰﱃ ﺻَﺮ‬
Idha hum yabghoona fee al-ardi bighayri alhaqqi ya ayyuha alnnasu innama
baghyukum AAala anfusikum mataAAa alhayati alddunya thumma ilayna
marjiAAukum fanunabbi-okum bima kuntum taAAmaloona, Innama mathalu
alhayati alddunya kama-in anzalnahu mina alssama-i faikhtalata bihi nabatu al-
Ardhi mimma ya/kulu alnnasu waal-anAAamu hatta idha akhadhati al-ardhu
zukhrufaha waizzayyanat wadhanna ahluha annahum qadiroona AAalayha ataha
amruna laylan aw naharan fajaAAalnaha haseedan kaan lam taghna bial-amsi
kadhalika nufassilu al-ayati liqawmin yatafakkaroona; WaAllahu yadAAoo ila dari
alssalami wayahdee man yashao ila siratin mustaqeemin (Surat Yunus 10:23-25)

Tafsir: Kisha baada ya (Allah Subhanah wa Ta’ala) kuwaokoa basi hua Wanamuasi
(Allah Subhanah wa Ta’ala) juu ya Ardhi kwa kutofanya haki. Enyi Watu! Uasi wenu
(dhidi ya Allah Subhanah wa Ta’ala)hua ni kwa ajili ya Nafsi zenu wenyewe, kwani
huo ni ufupi wa starehe za maisha ya Dunia hii, na kisha kwetu sisi ndio Marudio
yenu, na kisha tutakuelezeeni mliyokua mkiyafanya; Kwani kwa hakika Mithali ya
maisha ya Dunia hii, hua ni kama Mvua tunayoishusha kutoka Mbinguni, ambayo
kutokana nayo huotesha Mimea mbali mbali ardhini ambayo Watu na Ng’ombe
wanakula mpaka Ardhi ikawa imejaa mapambo yake na kupendeza na watu wakajihisi
kua wanauwezo nayo juu ya kila kitu. Ambapo amri yetu huifikia Usiku au Mchana
na kuifanya (Ardhi) hio kua kama ilivyovunwa kwa kufyekwa yote, kama kwamba
haikunawiri jana yake. Hivyo ndivyo tunavyoweka wazi aya zetu kwa kina kwa watu
wenye kutafakkari. Na Allah huwaita katika Makazi ya Usalama (Peponi), na
huwaongoza awatakao katika Njia iliyonyooka.

Hivyo huu ni kama mfano wa watu wa Fir’awn ambao waliokolewa mara kadhaa baada
ya kujaribiwa kwa mitihani na kisha walipookolewa wakarudi katika Uasi dhidi ya Nafsi
zao, na wakajiona kua wako juu wanaweza kufanya wanalotaka kwani wanaishi kwenye
Ardhi iliyonawiri sana kutokana na neema walizojaaliwa na Mola wao ambae hata hivyo
hawataki kumkubali, hivyo Allah Subhana wa Ta’ala akaamua kupitisha amri yake
kulingana na makadirio yake.

Lakini kwanza Allah Subhanah wa Ta’ala inabidi kumuongoza Nabii Musa, Nabii Harun
na Watu wao wa Bani Israil katika njia iliyonyooka kwa kufanya Hijra ya kuihama Ardhi
758

ya Misri na kuhamia katika Ardhi takatifu ya Jerusalem. Hivyo ulipowadia mda wa


kufanyika kwa Hijra hio basi Allah Subhanah wa Ta’ala akamshushia Nabii Musa Wahy
kumwambia:

﴾‫َﺳ ِﺮ ﺑِﻌِﺒَ ِﺎد ۤي إِﻧﱠ ُﻜﻢ ﱡﻣﺘﱠﺒِﻌُﻮ َن‬


ْ ‫ﻮﺳ ٰﻰ أَ ْن أ‬ ِ
َ ‫﴿وأ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إ َ ٰﱃ ُﻣ‬
َ
Waawhayna ila moosa an asri biAAibadee innakum muttabaAAoona (Surat Ash-
Shuara 26:52)

Tafsir: Na tukamshushia Wahy Musa (kumwambia kua) ‘Wahamishe waja wangu


wakati wa Usiku, kwani kwa hakika mtafukuziwa’

Hii inaonesha kukubaliwa Dua ya Nabii Musa na Nabii Harun basi tunaona baada ya
kuomba Dua yao na kukubaliwa basi ingawa watu wa Misri walikua na Mali nyingi
ambazo walizirithi kutokana na Hazina waliyoachiwa na Nabii Yusuf, lakini Allah
Subhanah wa Ta’ala alijaalia Mali yao yote hio ya watu wa Misri kuingia ndani ya
mikono ya watu wa Bani Israil baada ya kuwaamrisha kua wafanye sherehe ya sikukuu
kwa ajili ya kumtukuza Allah Subhanah wa Taa’la na kumshukuru kutokana na
kuwaondoshea Mitihani katika Ardhi ya Misri, na kisha wawaombe Watu wa Misri
wawaazime Mapambo yao kwa ajili ya sherehe hio, huku Allah Subhanah wa Ta’ala
akiahidi kua Watu wa Misri watatoa Mali zao na Mapambo yao kwa ajili ya Sherehe hio.

Kwani mapambo hayo yatakua hayawafai watu wa Misri kutokana na kua na khofu ya
maradhi watakayokua nayo kila mwenye kua na Mapambo hayo ya thamani nyumbani
kwake, yanayojumuisha Dhahabu, Almasi, Lulu n.k yatageuka kua mawe watakapobakia
nayo watu wa Misri, hivyo kia mtu ataona bora kwa wakati huo yawe salama mbali nae,
huku bila ya kujua kua hio ilikua ni sehemu ya kutoa kwao fidya kwa ajili ya kuwalipa
Watu wa Bani Israil kutokana na walivyowafanyia.

Anasema Imam Abu Abd Allah Ahmad Ibn Muhammad Ibn Ibrahim Al Thalabi kua:
‘Allah Subhanah wa Ta’ala aliwaambia Nabii Musa na Nabii Harun kua:
Zikusanyeni familia nne za watu wa Bani Israil katika Nyumba Moja, Kisha
wachinje Kondoo mmoja wapake Damu yake kwenye boriti ya Mlango, kwani
natuma Adhabu kwa watu wa Misri, Watakuja Malaika ambao hawatoingia katika
nyumba yeye mlango wenye Damu, na watawachinja watoto wa Mwanzo wote wa
Watu wa Misri pamoja na wanyama wao wa kwanza kisha wataangamia wote ila
nyinyi mtaokoka. Na okeni Mikate, kisha Ondokeni na Waja wangu Usiku mpaka
Baharini. Mkishafika itashuka amri yangu.’
759

Hivyo watu wa Bani Israil wakafanya kama walivyomariswha na Allah Subhanah wa


Ta’ala na watu wa Misri wakawa wanashangaa ni kwa nini wanafanya hivyo,
walipowauliza kwanini wanafanya hivyo basi wakasema kua wameamrishwa na Mola
wa Nabii Musa kua wafanye hivyo, hivyo watu wa Misri wakadharau na kuona kua Nabii
Musa na Nabii Harun watu wao wamechanganyikiwa. Kisha Usiku huo Watu wa Bani
Israil wakajitayarisha na safari ya kuelekea katika bahari nyekundu, na mda ulipowadia
basi wakatoka kimya kimya mmoja baada ya mwengine huku wakiwa na mapambo ya
thamani waliyoazimwa na watu wa Misri hapo kabla.

Na ilipofika alfajiri ya siku ya pili basi watu wa Misri wakawa ndio waliochanganyikiwa,
kwani katika kila nyumba yao kulisikikana kilio kikali sana cha huzuni na majonzi,
kinachotokana na kufariki kwa kila mmoja kati ya watoto wa mwanzo wa familia ya watu
wa Misri na pia mmoja kati ya wanyama wao wa mwanzo.

Hivyo basi hawakua hata na habari kua Nabii Musa, Nabii Harun na watu wao tayari
wameshaondoka mda mrefu sana, kwani hamkani waliokua nayo iliwatosheleza
kuwaghafilisha kila kitu kuhusiana na watu wa Bani Israil na hadi walipotahamaki basi
ilikua tayari Nabii Musa na watu wake, washafika mbali sana kuelekea katika Bahari
Nyekundu. Msafara huo uliokua ukiongozwa na Nabii Harun ambae alikua mbele na
Nabii Musa alikua ndie mtu wa mwisho kabisa katika msafara huo ambao mbali ya kua
na Wazee, Watoto na Wanawake na Wanaume lakini pia ulijumuisha Vijana wapiganaji
600,000 wa Bani Israil.

Baada ya watu wa Msri kumaliza kuzika maiti wao ndio wakataharuki na kugundua kua
watu wa Bani Israil tayari wameshaondoka wote, na Fir’awn alipopata habari ya
kuondoka kwa Nabii Musa na Watu wake basi akasema: ‘Bila ya shaka mauaji haya
yatakua yamefanywa na watu wa Bani Israil, na ndio maana wakakimbia tena na
mali zetu zote, hivyo inabidi tuwakimbilie ili tuwakamate na kuwarudisha kabla
hawajawahi kufika mbali, hivyo tayarisheni Jeshi kubwa sana tukawakamate.’

Allah Subhanah wa Ta’ala anayaelezea haya kwa kusema:

‫۞وإِﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ ﻟَﻨَﺎ‬ ِ‫ﺎﺷ ِﺮﻳﻦ۞إِ ﱠن ﻫـٰﺆ ۤﻻ ِء ﻟَ ِﺸﺮِذﻣﺔٌ ﻗَﻠ‬ ِ ِ ِ ِ ﴿


َ ‫ن‬َ ‫ﻮ‬ُ‫ﻠ‬ ‫ﻴ‬ َْ َُ َ ‫ﻓَﺄ َْر َﺳ َﻞ ﻓْﺮ َﻋﻮ ُن ﰱ ٱﻟْ َﻤ َﺪآﺋ ِﻦ َﺣ‬
﴾‫ﻴﻊ َﺣ ِﺎذرو َن‬ ٌ ‫ﻤ‬ِ ‫ﻟَﻐَﺂﺋِﻈُﻮ َن۞وإِ ﱠ� َﳉ‬
َ َ
ُ
Faarsala firAAawnu fee almada-ini hashireena; Inna haola-i lashirdhimatun
qaleeloona; Wa-innahum lana lagha-idhoona; Wa-inna lajameeAAun hadhiroona
(Surat Ash Shuara 26:53-56)
760

Tafsir: Kisha akatuma Fir’awn katika Miji wanadiaji. (wenye kusema) Hakika hawa
ni kikundi kidogo sana, Na kwa hakika wametughadhibisha sana, na sisi tuko wengi
na tumejitayarisha kwa lolote.

Ambapo tunaona kua aya zimetumia neno Shirdhimat ambalo linatokana na neno
Sharadha ambalo hua linamaanisha Kundi Dogo la Watu waliotawanyika tawanyika
wenye kustahiki kuchukiwa, na kisha ikaongezea neno Qaliil kuainisha namna Fir’awn
na watu wake wa Misri walivyomdharau Nabii Musa na Nabii Harun na watu wa Bani
Israil.

Na hapo hapo zikatumi neno Ghaidhuuna linalotokana na neno Gadha ambalo hua
linamaanisha Kukera kusiko sameheka, Kughadhibisha sana, Kutia hasira kubwa sana,
Kukereketa na pia Kuchokoza. Na hivyo kuainisha hali waliyokua nayo watu wa Misri
dhidi ya watu wa Bani Israil kutokana na mitihani yote iliyowakuta hapo kabla ambapo
kwa mtizamo wao basi ni kua ilisababishwa na Nabii Musa, na kisha hili tukio la kuuawa
kwa Watoto wao, Wayama wao wa mwanzo wote na kutoweka kwa Mali zao.

Watu hao wa Bani Israil wakajisifu kwa kutumia hali inayoainishwa na neno Hadhiruuna
ambalo ni lenye kutokana na neno Hadhara ambalo hua linamaanisha Kua katika hali ya
Umakini wa kua tayari kwa Jambo lolote litakalotokea. Hivyo aya zinabainisha kua watu
hawa wa Fir’awn wanaweka wazi kua wako tayari hata kuwaangamiza watu hao wa Bani
Israil kama ikiwa itashindikana kuwarudisha katika Ardhi ya Misri.

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anaendelea kutuelezea kwa kusema:

‫ﺎﻫﺎ ﺑَِ ۤﲏ‬ ِ ٍ ٍ ِ َ‫﴿ﻓَﺄَﺧﺮﺟﻨ‬


َ ‫۞وُﻛﻨُﻮٍز َوَﻣ َﻘ ٍﺎم َﻛ ِﺮٍﱘ۞ َﻛ ٰﺬﻟ‬
َ َ‫ﻚ َوأ َْوَرﺛْـﻨ‬ َ ‫ﺎﻫ ْﻢ ّﻣﻦ َﺟﻨﱠﺎت َوﻋُﻴُﻮن‬
ُ ْ َْ
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ِ
َ ‫ﻮﻫﻢ ﱡﻣ ْﺸ ِﺮﻗ‬ ُ ُ‫ﻴﻞ۞ﻓَﺄَﺗْـﺒَـﻌ‬
َ ‫إ ْﺳَﺮاﺋ‬
Faakhrajnahum min jannatin waAAuyoonin; Wakunoozin wamaqamin kareemin;
Kadhalika waawrathnaha banee isra-eela; FaatbaAAoohum mushriqeena (Surat
Ash Shuara 26:57-60)

Tafsir: Na kisha tukawatoa kwenye Mabustani yao na Chemchem, na Mali na Makazi


mazuri ya heshima. Kadhalika ndivyo tulivyowarithisha watu wa Bani Israil (Mali za
Watu wa Misri); Hivyo (Watu wa Misri) wakawakimbilia Alfajir (Watu wa Bani Israil).

Allah Subhanaha wa Ta’ala anatuelezea Neema waliyokua nayo watu wa Misri katika
Ardhi yao kua ilikua imenawiri sana Ardhi yao na hivyo walikua na Mabustani
761

yaliyopendeza kutokana na Mto Nile ambapo hali yake ilikua inategemea na kujaa na
kupungua kwa Maji yake na hivyo kunasibishwa na chemchem za Maji.

Ambapo kuhusiana na maana ya aya hii basi tunaona kua wakati Waislam walipoiteka
Ardhi ya nchi ya Misri katika kipindi cha Utawala wa Amir ul Muuminin Umar Ibn Al
Khattab Radhi Allahu Anhu ambae alimkabidhi Amr Ibn Al Aas Radhi Allahu Anhu kua
Gavana wa Ardhi hio, basi alikuta Maji ya Mto Nile yakiwa yako chini kabisa, na hivyo
watu wa Misri wakamlalamikia Amr Ibn Al Aas Radhi Allahu Anhu na kumwambia kua
wao katika wakati wao walikua wakitoa kafara ya Mwanamke mwari kila inavyotokea
hivyo.

Hivyo Amr Ibn Al Aas Radhi Allahu Anhu akapingana na shauri hilo kwani Uislam
haukubaliani na mitizamo ya Imani kama hizo. Hivyo watu wa maeneo hayo wakaamua
kua watahama maeneo hayo, kwani haiwezekani tena kuishi katika maeneno hayo.
Hivyo Amr Ibn Al Aas Radhi Allahu Anhu akaamua kumuandikia barua Amir ul
Muuminin Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu kuhusiana na tatizo hilo.

Hivyo Amir ul Muuminin Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu akasema kua
anaandika barua ambayo itabidi itupwe ndani ya Mto Nile na kisha akaandika Barua
isemayo: ‘Biismi Allahi ArRahmani ArRahiim, Kutoka kwa Mja wa Allah Subhanah
wa Ta’ala, Amir ul Muuminin Umar Ibn Al Khattab kuelekea kwa Mto Nile wa
Misri, Alhamd Lillahi Rabbi Al Aaalamiin, kama ikiwa unafuata Amri yako katika
kutiririka kwako basi unaweza kubakia kama ulivyo, lakini kama unafuata Amri
ya Allah Subhanah wa Ta’ala katika kutiririka kwako, basi sisi tunamuomba Allah
Subhanah wa Ta’ala akijaalie kua ni wenye kutiririsha kwa wingi Maji yako’.

Na bia ya shaka Barua hio ilipowasili nchini Misri na kutumbuzwa ndani ya Mto Nile
basi mto huo ukafurika Maji yake katika siku ya pili yake. Ambapo anasema Imam Abu
Abd Allah Muhammad Ibn Ahmad Ibn Abu Baqr Al Ansari Al Qurtubi kua: ‘Amesema
Imam Muslim kua: ‘Sayhaan, Jayhaan, Niil na Furat kua yote ni Mito ya Peponi,
kwani katika Hadith ya Isra na Miraj Rasul Allah Salallahu Allahu Alayhi wa Salam
aliona Mito mine ambayo ndani yake imetoka Mito Miwili inayoonekana wazi na
miwili isiyoonekana wazi, hivyo akamuuliza Jibril kuhusiana nayo nae Jibril
akajibu kua Mito miwili ambayo haionekani wazi ni Mito ya Peponi na Mito miwili
inayonekana wazi ni Mito ya Niil na Furat (Nile na Euphrate)’’
Tunarudi kwa Nabi Musa na kuona kua baada ya yeye kuondoka na watu wake basi
akakumbuka kua Nabii Yusuf alisema kua Maiti yake itabakia katika Ardhi ya nchini
Misri mpaka pale atakapokuja Musa na kisha atakapohama basi atahama nayo Mauiti hio
na kurudi nayo katika Ardhi Takatifu ya Jerusalem, hivyo akataka kutekeleza jukumu
lake hilo kwa ajili ya Nabii Yusuf lakini akawa hajui Nabii Yusuf amezikwa wapi.
762

Hivyo akawauliza watu wake na mmoja kati ya watu hao alikuwemo Bibi mmoja mtu
mzima sana ambae alisema kua: ‘Hakika mimi nnapajua alipozikwa, ila siwezi
kukupeleka mpaka unipe ahadi juu ya jambo moja.’ Nabii Musa akamuuliza: ‘Ahadi
juu ya nini?’ Yule bibi akasema: ‘Uniahidi kua mimi nitakua pamoja nawe Peponi’
hivyo Nabii Musa akamuomba Allah Subhanah wa Ta’ala juu ya kutekelezwa kwa ahadi
hio na Allah Subhanah wa Ta’ala akamkubalia maombi yake hayo.

Ambapo kwa upande wa Imam Abu Hatim Abd Rahman Muhammad Ibn Idris Al Razi
kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, alikutana na Bedui mmoja ambae
alikua ni mtu mzuri katika ukaribishaji wake wageni, hivyo Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam akakubaliana kuingia nae katika makubaliano baina yao. Hivyo
yule Bedui akaja kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambapo nae
akamuuliza: ‘Jee ulikua unataka nini?’ yule Bedui akasema : ‘Nataka Ngamia na
kila kitu chake na pia nataka Mbuzi kadhaa wa Maziwa kwa ajili ya Mke wangu.’’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Hivi wewe ni Dhaifu kiasi hicho
kiasi ya kua unataka kua kama Bibi Kizee wa Bani Israil?’ Masahaba wakauliza: ‘Ya
Rasul Allah! Hivi ni kisa gani hicho cha huyo bibi kizee wa Bani Israil?’ Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Wakati Musa alipoondoka na watu wa Bani
Israil basi walipotea njia hivyo akawauliza Wanazuoni wa Bani Israil, imekuaje?
Wanazuoni hao wakasema: ‘Inabidi tukuambie kua Yusuf alipokua anakaribia
kufariki basi alichukua ahadi kutoka kwetu kua hatutohama katika Ardhi ya Misri
bila ya kuhama na Jeneza lake’ hivyo Nabii Musa akauliza: ‘Jee nani anaejua liko
wapi Kaburi la Yusuf?’ Watu wa Bani Israil wakasema: ‘Hakuna anaelijua liko wapi
isipokua Bibi Kizee wa Bani Israil.’

Hivyo Musa akataka aitiwe bibi huyo na alipofika mbele yake basi akamuomba
awaelekeze kwenye Kaburi la Yusuf, Bibi Kizee huyo akasema: ‘Hakika mimi
sitokuelekeza mpaka utakaponiahidi kitu’ Musa akauliza: ‘Kitu gani?’ Yule Bibi
Kizee akasema: ‘Nataka uniahidi kua mimi nitakua pamoja nawe Peponi’ hivyo
ombi hili lilikua gumu kwa Nabi Musa, na akawa anasita, lakini watu wa Bani Israil
wakamwambia Musa: ‘Muahidi anachokitaka!’ Hivyo Musa akamkubalia ahadi
hio, kisha Bibi Kizee huyo akawaongoza kwenye eneo lenye bonde dogo la maji
lililojaa majani, kisha akawaambia watu wa Bani Israil wayatoe Maji hayo, kisha
akawaambia wachimbe na walipochimba wakaliona Jeneza alilozikiwa Yusuf. Na
mara tu baada ya kulichukua basi wakaiona njia yao kama kwamba ilikua ni wakati
wa mchana.’

Ambapo anasema Imam Ahmad Ibn Muhammad Ath Thalabi kua: ‘Urwa Ibn Zubayr
kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala alimuamrisha Musa kutoka katika Ardhi ya Misri
katika wakati wa Alfajir, hivyi Musa akamuomba Allah Subhanah wa Ta’ala
amkawilishie kuchomoza kwa Alfajir hilo mpaka atakapomalizana na jambo la
763

Nabii Yusuf. Nae akamkawilishia, na ndio toka kuanzia siku hio basi Mayahudi hua
lazima wahamishie maiti zao kokote kule zitakazokuwepo kuzipeleka katika Ardhi
Takatifu. ’

Hivyo baada ya kuuchukua mwili wa Nabii Yusuf pamoja nao basi wakaanza safari yao
ambayo ilikua ni nzito kwani ndani yake hamkua na Wanajeshi vijana bali mlikua na
Wazee, Wanawake, Watoto na Wagonjwa pia. Hivyo safari yao hio iliwachukua mda wa
siku tatu mpaka kufika katika mwambao Baharini.

Ambapo kwa upande wake Fir’awn nae basi akatayarisha jeshi la watu 300,000
waliopanda Farasi, ambalo ndani yake mna kikosi cha wapiganaji mahiri maalum cha
wapanda Farasi Dume 100,000 wenye rangi Nyeusi tupu ambao mbele yake walikua
wakiongozwa na Hamman, huu ni mfano wa wengi miongoni mwa viongozi wa leo
wenye misafara ya kua na magari meusi matupu. Hivyo haikuchukua mda isipokua
Msafara huo wa Fir’awn na watu wake ulikua ni wenye kuukaribia msafara wa Nabii
Musa na watu wa Bani Israil.

Hivyo baada ya watu wa Bani Israil kuona hali ilivyokua yaani, vumbi kubwa sana
linatimka kwa mbali kutoka nyuma yao na hivyo kumaanisha kua Fir’awn na watu wake
wanawakaribia na wao mbele yao hakuna kwa kukimbilia isipokua Baharini na hawajui
kuogoelea wala hawa na chombo cha kuvukia basi watu hao wakasema kumwambia
Nabii Musa kama zinavyoelezea aya:

‫ﺎل َﻛﻼﱠ إِ ﱠن َﻣﻌِ َﻰ‬


َ َ‫ﻮﺳ ٰﻰ إِ ﱠ� ﻟَ ُﻤ ْﺪ َرُﻛﻮ َن۞ﻗ‬
َ ‫ﺎب ُﻣ‬ ُ ‫َﺻ َﺤ‬ْ ‫ﺎل أ‬
ِ ‫ٱﳉﻤﻌ‬
َ َ‫ﺎن ﻗ‬ َ ْ َْ ‫﴿ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ ﺗَـَﺮاءَى‬
﴾‫رِّﰉ َﺳﻴَـ ْﻬ ِﺪﻳ ِﻦ‬
َ
Falamma taraa aljamAAani qala as-habu moosa inna lamudrakoon; Qala kalla
inna maAAiya rabbee sayahdeeni(Surat Ash Shuara 26: 61-62)

Tafsir: Na kisha walipoona kua wanakabiliana basi wakasema watu wa Nabii Musa:
‘Hakika sisi tutakamatwa’ Akasema (Nabii Musa)La! Kwa hakika mimi niko pamoja
na Mola wangu hivyo ataniongoza.

Hivyo aya inatuwekea wazi hali waliyokua nayo watu wa Bani Israil, na kuonesha kua
tayari walikua wameshavunjika Moyo na Rehma za Allah Subhanah wa Ta’ala juu yao
na hivyo kutokua kuhusiana na Ukubwa wa Uwezo wake na hali hii inawekwa wazi na
maneno waliyosema yaani Inna Lamudrakuun ambapo neno Mudrakuun ni lenye
kutokana na neno Daraka ambalo hua ni lenye kumaanisha Kupitwa, Kukutwa,
764

Kufikiwa, Kukamatwa baada ya kupitwa au baada ya kufikia uwezo wa mwisho wa kitu


husika. Neno Daraka ndio lililotoa neno Darakun ambalo hua linamaanisha Chini kabisa
ya kitu kama Shimo, Ukingo wa sehemu iliyoenda chini kwenye kina kirefu kiasi ya kua
ukisogeza mguu kidogo tu basi bila ya shaka na kwa hakika utaangamia.

Hivyo hii ndio hali walijiona kua nayo watu wa Bani Israil na ndio maana Nabii Musa
akasema kuwaambia watu wake hao kua: ‘Inna maAAiya Rabbee sayahdeeni – Kwa
hakika mimi ninae Mola wangu ataniongoza’ yaani kama nyinyi hamumuamini Mola
wangu basi mimi nnamuamini na najua kua kamwe hatoniacha Mkono atanionesha njia
tu ya kutokea kwenye Mtihani huu. Kisha Nabii Musa akawarudisha watu hao kwa Mola
wao na kuwabainishia uwezo wake juu ya kila kitu kwa kusema:

‫ﻒ‬ ِ ‫ﻚ َﻋ ُﺪ ﱠوُﻛ ْﻢ َوﻳَ ْﺴﺘَ ْﺨﻠِ َﻔ ُﻜ ْﻢ ِﰱ ٱﻷ َْر‬


َ ‫ض ﻓَـﻴَﻨﻈُْﺮ َﻛْﻴ‬
ِ َ َ‫﴿ﻗ‬
َ ‫ﺎل َﻋ َﺴ ٰﻰ َرﺑﱡ ُﻜ ْﻢ أَن ﻳـُ ْﻬﻠ‬
﴾‫ﺗَـ ْﻌﻤﻠُﻮ َن‬
َ
Qala AAasa rabbukum an yuhlika AAaduwwakum wayastakhlifakum fee al-Ardhi
fayandhura kayfa taAAmaloona (Surat Al Araf 7:129)

Tafsir: (Nabii Musa) Akasema: ‘Inawezekana ikawa Mola wenu anataka


kumuangamiza Adui yenu na kukufanyeni nyie kua Makhalifa hapa ardhini kisha
akuoneni ni nini mtakachokifanya.’

Lakini hata hivyo watu wa Bani Israil wakawa hawana subra kwani baadhi yao wakaanza
kuingia baharini, lakini badala yake wakajikuta wanazama, akiwemo Hizqil na Farasi
wake, baada ya kuona hali hio basi watu hao wa Bani Israil wakajawa na khofu zaidi,
lakini Nabii Musa akakaa huku akisubiri wamalizike kukaribia watu wake, ili afanye
kama alivyoambiwa na Mola wake kama zinavyosema aya:

‫ب َﳍُْﻢ ﻃَ ِﺮﻳﻘﺎً ِﰱ ٱﻟْﺒَ ْﺤ ِﺮ ﻳـَﺒَﺴﺎً ﻻﱠ‬ ْ َ‫َﺳ ِﺮ ﺑِﻌِﺒَ ِﺎدى ﻓ‬


ْ ‫ﭑﺿ ِﺮ‬ ِ
َ ‫﴿ َوﻟََﻘ ْﺪ أ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إ َ ٰﱃ ُﻣ‬
ْ ‫ﻮﺳ ٰﻰ أَ ْن أ‬
﴾‫ﺎف َدرﻛﺎً وﻻَ َﲣْ َﺸ ٰﻰ‬
َ َ ُ َ‫َﲣ‬
Walaqad awhayna ila moosa an asri biAAibadee faidhrib lahum tareeqan fee
albahri yabasan la takhafu darakan wala takhsha; (Surat Ta-Ha 20:77)
765

Tafsir: Na kwa hakika tulimshushia Musa Wahyi kumwambia: ‘Safiri na waja wangu
katika wakati wa Usiku, na Ipige (Ipasue) kwa ajili yao njia kavu kwenye Bahari na
wala usiwe na khofu ya kupitwa wala usiogope (kuzama Baharini) ’

Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea kwa mtizamo mwengine wa kina zaidi tukio juu
ya hilo baada ya kumshushia Wahyi Nabii Musa na kumwambia kua atumie Fimbo yake
kwa ajili ya kuipiga Bahari iliyo mbele yake, kama zinavyosema aya:

‫ﺎك ٱﻟْﺒَ ْﺤَﺮ ﻓَﭑﻧ َﻔﻠَ َﻖ ﻓَ َﻜﺎ َن ُﻛ ﱡﻞ ﻓِْﺮٍق َﻛﭑﻟﻄﱠْﻮِد‬ َ‫ﺼ‬ َ ‫ٱﺿ ِﺮب ﺑَِّﻌ‬ْ ‫ﻮﺳ ٰﻰ أ َِن‬ ِ
َ ‫﴿ﻓَﺄ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إ َ ٰﱃ ُﻣ‬
‫ﲔ۞ﰒُﱠ أَ ْﻏَﺮﻗْـﻨَﺎ‬ ِ ْ ‫ٱﻟْﻌ ِﻈﻴ ِﻢ۞وأ َْزﻟَْﻔﻨَﺎ ﰒَﱠ ٱﻵﺧ ِﺮﻳﻦ۞وأَﳒﻴـﻨَﺎ ﻣﻮﺳﻰ وﻣﻦ ﱠﻣﻌﻪ أ‬
َ ‫َﲨَﻌ‬ ُ َ َ َ ٰ َ ُ َْ َ َ َ َ َ
ِِ ِ
‫ﻚ َﳍَُﻮ ٱﻟْ َﻌ ِﺰ ُﻳﺰ‬َ ‫۞وإِ ﱠن َرﺑﱠ‬
َ ‫ﲔ‬ َ ‫ﻳﻦ۞إِ ﱠن ِﰱ ٰذﻟ‬
َ ‫ﻚَ ﻵﻳَﺔً َوَﻣﺎ َﻛﺎ َن أَ ْﻛﺜَـُﺮُﻫﻢ ﱡﻣ ْﺆﻣﻨ‬ َ ‫ٱﻵﺧ ِﺮ‬
َ
﴾‫ٱﻟﱠﺮِﺣﻴﻢ‬
ُ
Faawhayna ila moosa ani idrib biAAasaka albahra fainfalaqa fakana kullu firqin
kaalttawdi alAAadheemi; Waazlafna thamma al-akhareena; Waanjayna Moosa
waman maAAahu ajmaAAeena; Thumma aghraqna al-akhareena, Inna fee dhalika
laayatan wama kana aktharuhum mu/mineena; Wa-inna rabbaka lahuwa
alAAazeezu alrraheemu (Surat Ash Shuara 26:63-68)

Tafsir: Na kisha tukamshushia Wahy Musa (kumwambia): ‘Ipige kwa Fimbo yako
Bahari’ na ikaachia na kila upande ikawa kama Jabali kubwa sana. Kisha tukalileta
karibu kundi lililobakia (la Fir’awn), na tukamuokoa Musa na kila aliekua nae kwa
pamoja. Na kisha tukawagharikisha waliobakia. Na katika hayo mna dalili zetu lakini
wengi wao hawaamini. Na kwa hakika Mola wako ni mwenye Uwezo mkubwa na
Mwingi wa Rehma.

Anasema Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Allah Subhanah wa
Ta’ala ni mwenye uwezo mkubwa sana katika kuwashughulikia Wasioamini na ni
Mwenye Rehma Nyingi sana katika kuwashughulikia Waliomuamini.’

Hivyo Nabii Musa akaipiga Fimbo Bahari hio na mara hapo hapo Bahari ikapasuka mbele
ya Macho yake, Iman Abu Muhammad Sulaiman Ibn Mihran Al Kahili Al Asad Al
Amash basi anasema kua: ‘Amesema Shaqiq kua amesema Abd Allah Radhi Allahu
Anhu kua amesema Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam kua: ‘Jee nikufudisheni
maneno aliyoyasema Musa wakati alipowavusha watu wa Bani Israil Baharini?’
Nasi tukasema : ‘Naam’ Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Alisema:
766

‘Ya Allah! Shukrani zote Unastahiki wewe peke yako. Na kwako wewe wanarudi
wale wenye matatizo, Wewe ndie unaetegemewa kwa kuombwa Msaada, na kwako
wewe pekee ndio tunakokutegemea, hakuna uwezo wala nguvu isipokua kwa Allah,
aliejuu na alie na nguvu juu ya kila kitu.’ Abd Allah Radhi Allahu Anhu anasema
kua: ‘Kamwe sikuwahi kuachana na Maneno hayo tangu nilipomsikia Rasul Allah
Sallhu Alayhi wa Salam akiyatamka.’’’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anaelezea namna alivyowashughulikia Fir’awn na


watu wake katika aya ifuatayo:

ِ ُ‫﴿ﻓَﺄَﺗْـﺒـﻌﻬﻢ ﻓِﺮﻋﻮ ُن ِﲜﻨ‬


﴾‫ﻮدﻩِ ﻓَـﻐَ ِﺸﻴَـ ُﻬﻢ ِّﻣﻦ ٱﻟْﻴَِﻢ َﻣﺎ َﻏ ِﺸﻴَـ ُﻬﻢ‬
ْ ّ َ ْ ُ َْ ْ ْ ُ َ َ
FaatbaAAahum firAAawnu bijunoodihi faghashiyahum mina alyammi ma
ghashiyahum (Surat Ta-Ha 20: 77-78)

Tafsir: Na kisha wakamfuata Firawn na jeshi lake lakini wakafunikwa gubi gubi na
Mafuriko yenye kuwafunika gubi gubi.

Ambapo aya imetumia neno Ghasha lenye kumaanisha Kufunika Gubi Gubi, Kuficha,
Kukaa juu yake na ikatumia neno Al Yammi linalotokana na neno Yamm ambalo hua ni
lenya kumaanisha Kutoswa ndani ya Maji au Kurushwa Ndani ya Maji. Neno Yamm ndio
lililotoa neno Tayammam yaani Kufanya Tayammam kwa kutia Udhu kwa kutumia
Mchanga ulio tohara, kwa kupiga mikono juu ya Mchanga huo na kisha kujipangusia
mikononi mpaka kwenye visugudi na Uso kama kwamba unakosha viungo hivyo kwa
Maji. Neno Yamm pia hua linamaanisha sehemu yenye maji mengi sana kama Bahari,
Mto, Ziwa au Mafuriko.

Hivyo hapa Allah Subhanah wa Ta’ala anaielezea hali ilivyokua kwa muonekano wa kua
haiwezekani hata mmoja miongoni mwao aliekua ni mwenye uwezo wa Kutoka ndani ya
Mafuriko hayo yanayofunika gubi gubi, na hivyo kuonesha kua hii hali ya kufunikwa
haikua ni ya kutokana na upande mmoja tu wa Mafuriko kama vile Maji ya Tsunami bali
ni kutoka pande zaidi ya moja yaani mafuriko kama ya Bahasha inavyofunga kwa
kukusanya pande zake tofauti katikati ya Bahasha hio na kugubika kila kitu kilichomo
ndani yake na hivyo kuweka wazi kua hii ilikua ni pande mbili za Bahari zilizokua
zimekaa kama Ukuta wa Maji na kati kati yake Ardhi kavu kabisa na kisha zikagubuka.

Ambapo anasema Imam Ahmad Muhammad Ath Thalabi kua: ‘Baada ya Nabii Musa
kuipiga Bahari na kupasuka basi wale waliozama walioonekana wakiwa
wamesimama wakiwa wazima akiwemo Hizqil na Farasi wake.’
767

Baada ya Bahari hio Kupasuka basi Nabii Musa akawaongoza watu kuvuka ndani yake
na watu wa Bani Israil wakavuka huku wakiwa wanakanyaga mchanga mkavu kabisa
bila ya kuamini macho yao huku kuliani na kushotoni mwao kukiwa na milima miwili
mikubwa sana ya Maji iliyopakana pembeni ya ya Ardhi wanayoikanyaga kwa miguu
yao, hii ilikua ni sikua ya mwezi 10 Muharram.

Watu hawa wakavuka kwa salama na amani kabla ya hata kukutwa na watu wa Fir’awn
aliekua nyuma yao, kama zinavyosema aya:

﴾‫آل ﻓِﺮ َﻋﻮ َن وأَﻧْـﺘُﻢ ﺗَﻨﻈُﺮو َن‬ ِ ِ﴿


ُ ْ َ ْ ْ َ ‫َوإ ْذ ﻓَـَﺮﻗْـﻨَﺎ ﺑ ُﻜ ُﻢ ٱﻟْﺒَ ْﺤَﺮ ﻓَﺄَﳒَْﻴـﻨَﺎ ُﻛ ْﻢ َوأَ ْﻏَﺮﻗْـﻨَﺎ‬
Wa-ith faraqna bikumu albahra faanjaynakum waaghraqna ala firAAawna
waantum tandhuroona (Surat Al Baqara 2:50)

Tafsir: Na (Kumbukeni) tulipo kupasulieni kwa ajili yenu Bahari na tukakuokoeni na


kuwaangamiza Watu wa Fir’awn huku mkiwa mnaona.

Kwani mara tu baada ya Nabii Musa na watu wa mwanzoni wa Bani Israil kufika upande
wa pili wa Bahari na huku nusu yao wakiwa bado wapo katikati ya bahari wakiendelea
kuvuka basi Nabii Musa alisimama na kuwaangalia watu wake hao, wakimalizia kuvuka,
kisha baada ya hapo Firawn na Jeshi lake wakawasili kwenye upande wa pili wa
Mwambao wa Bahari hio huku wakishangaa kilichotokea na kua ni chenye kuonekana
mbele ya Macho yao, kwani wao wamewahi kupita sehemu hio mara kadhaa katika
kampeni zao za kivita na hakuna hata mara moja waliyoona kua sehemu hio imekauka
maji.

Na si kukauka Maji tu bali imekatika. Hivyo basi kabla yakuingia sehemu hio ya Bahari
iliyopasuka wakasita na kumsubiri Fir’awn awasili ili wajadiliane nini cha kufanya
kwaini ingwa wanawaona watu wa Bani Israil wakiwa wanavuka lakini hii hali
wanayoina mbele yao si ya kawaida kwani huenda ukawa ni mtego dhidi yao na hivyo
wakiingia huenda Bahari ikafunika.

Lakini hata hivyo Fir’awn na Jeshi lake la Farasi Weusi watupu alipowasili, basi hakua
ni mwenye kushangaa, bali alikua ni mwenye kuingiwa na ari na hivyo akasema
kuwaambia watu wake: ‘Mnaona Bahari imepasuka kwa ajili yangu, ili tupate
kuwakamata maadui zetu, mnasubiri nini? Wafuateni kabla hawajafika upande wa
pili’

Hivyo ingawa watu hao wa Misri walisita kuingia lakini Farasi weusi wa Kikosi Maalum
ambao wote walikua ni Farasi Dume wakakimbilia ndani ya mpasuko huo wa Bahari na
768

kuanza kuwafukuzia watu wa Bani Israil, na hii ni kwa sababu kama anavyosema Imam
Ahmad Ibn Muhammad Ath Thalabi kua: ‘Jeshi la Fir’awn lilikua halina Farasi Jike
kwani wote ni Farasi Dume, hivyo akatokea Malaika Jibri akiwa na Farasi Jike
mwenye shurufu (harufu ya Mnyama Jike aliekua tayari kupandwa na Mnyama
Dume), na hivyo mara tu baada ya Farasi Dume hao wa Jeshi la Fir’awn kusikia
harufu ya shurufu kali sana ya Farasi Jike huyo anakimbia kuwakimbilia watu wa
Bani Israil, basi Farasi Dume wote hao wakaanza kumkimbilia Farasi Jike huyo,
huku Jeshi la Fir’awn likifikiria kua mpanda Farasi huyo ni miongoni mwa
Mwanajeshi wao, nao wakamfuata mpaka wote wakaingia kwenye mpasuko huo
wa Bahari. ’

Wakati tukio hili linatokea basi Nabii Musa alikua amekaa anaangaia na kutafakkari nini
cha kufanya mara tu baada ya Watu wa Bani Israil kumalizika kuvuka hadi upande wa
pili na kabla ya Fir’awn na watu wake kuwafikia wao katika upande huo wa pili uliopo.
Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Nabii Musa usifanye chochote wewe kaa
angalia tu iwache bahari kama ilivyo, kwani itatimiza kile ambacho imekadiriwa
kukitimiza. Kama inavyosema aya ifuatayo:

﴾‫﴿وٱﺗْـﺮِك ٱﻟْﺒَ ْﺤﺮ رْﻫﻮاً إِﻧـﱠ ُﻬﻢ ُﺟﻨ ٌﺪ ﱡﻣ ْﻐﺮﻗُﻮ َن‬


َ ْ ََ ُ َ
Waotruki albahra rahwan innahum jundun mughraqoona (Surat Ad Dukhan 44:24)

Tafsir: Na iwache Bahari itulie kwani kwa hakika wao ni Jeshi litakaloangamia.

Aya imetumia neno Rahwan linaotokana na neno Raha ambalo ni tofauti na lile
tulilofafanua kimaana tulipozungumzia Upepo kwani lile lina harfu alif baina ya harfu
Ra na Ha na hili lina harfu Alfu baada ya Ha na hivyo hua linamaanisha Utulivu, Kutulia
Tulii, Kua Kimya bila sauti Kutembea taratibu, Bahari iliyotulia na pia humaanisha
Sehemu ya Ardhi iliyokauka na Kua Kavu kabisa.

Hivyo Nabii Musa akaiwacha Bahari kama alivyoamrishwa na Mola wake huku Fir’awn
na Jeshi lake likaingia kwenye Mtego wa mpasuko huo wa Bahari Kavu na hadi
walipoingia wote na kufika katikati basi Bahari hio ikatekeleza amrisho la Mola wake
kwa kujiunga mpasuko wake huo na kuwaghaikisha Fir’awn na Watu wake kama
zisemavyo aya:
769

ِ ِ ِۤ ِ
ُ‫ﻮدﻩُ ﺑَـ ْﻐﻴﺎً َو َﻋ ْﺪواً َﺣ ﱠ ٰﱴ إِ َذآ أ َْد َرَﻛﻪ‬ َ ‫َو َﺟ َﺎوْزَ� ﺑﺒَِﲏ إ ْﺳَﺮاﺋ‬
ُ ُ‫ﻴﻞ ٱﻟْﺒَ ْﺤَﺮ ﻓَﺄَﺗْـﺒَـ َﻌ ُﻬ ْﻢ ﻓْﺮ َﻋ ْﻮ ُن َو ُﺟﻨ‬ ﴿
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ‫ﺎل آﻣﻨﺖ أَﻧﱠﻪ ۤﻻ إِﻟِـٰﻪ إِﻻﱠ ٱﻟﱠ ِﺬى آﻣﻨَﺖ ﺑِِﻪ ﺑ ۤﻨﻮاْ إِﺳﺮاﺋِﻴﻞ وأ ََ�ْ ِﻣﻦ ٱﻟْﻤﺴﻠ‬
‫ﻤ‬
َ ْ ُ َ َ َ َْ َ ْ َ َ ُ ُ َ َ َ‫ٱﻟْﻐََﺮ ُق ﻗ‬
Wajawazna bibanee isra-eela albahra faatbaAAahum firAAawnu wajunooduhu
baghyan waAAadwan hatta idha adrakahu algharaqu qala amantu annahu la ilaha
illa alladhee amanat bihi banoo isra-eela waana mina almuslimeena.(Surat Yunus
10:90)

Tafsir: Na tukawavusha Bahari watu wa Bani Israil, kisha Firawn na Jeshi lake
wakawafuata kwa (ajili ya) ukandamizaji na uadui, mpaka alipokua anaangamia kwa
kugharikishwa (ndio) akasema: ‘Nimeamini kua kwa hakika Hakuna Mungu
Isipokua Yeye (Anaestahiki Kuabudiwa), ambae anaaminiwa na Bani Israil na mimi
ni miongoni mwa Waliojisalimisha (Kwake Allah Subhanah wa Ta’ala)’

Na anasema Imam Ibn Jariri At Tabari, Imam Ahmad Ibn Muhammad Ath Thalabi, nk
kua: ‘Malaika Jibril alimwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:
‘Katika viumbe wote basi hakuna viumbe niliokua nikiwachukia kama nilivyokua
nikiwachukia viumbe wawili. Wa kwanza ni Jini aitwae Ibilisi pale alipokataa
kumsujudia Adam. Na mwengine ni Ibn Adam aitwae Fir’awn pale aliposema Mimi
ndie Mola wenu Mkuu’ yalaiti kama ungeniona ewe Muhammad namna
nilivyochukua Matope na kumsokomezea mdomoni mwake ili asije akatamka
wakati anazama, na kisha Allah Subhnaha wa Ta’ala akamuonea Huruma.’(Imam
At Tirimidhii)

Ambapo kwa upande wa Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi na Jarrah Allah
Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kuhusiana na hadith hio kua: ‘Imani ya Kafiri
aliekua katika Sakarat Al Mawt hua kaikubaliki, Imani ya Mtu hua imo ndani ya
Moyo hivyo si lazima kutamka kama vile inavyokua kwa mtu ambae ni Bubu.
Yeyote yule anaemuombea Mtu afe katika hali ya kua Kafiri basi na yeye hua ni
Kafiri.’

Kwani Allah Subhanah wa Ta’ala anasema kua:

ِ ِ ‫ﺖ ٱﻟﺘـﱠﻮﺑﺔُ ﻟِﻠﱠ‬
ِ ‫﴿وﻟَﻴﺴ‬
‫ﺎل‬
َ َ‫ت ﻗ‬
ُ ‫َﺣ َﺪ ُﻫ ُﻢ ٱﻟْ َﻤ ْﻮ‬ َ ‫ﻳﻦ ﻳـَ ْﻌ َﻤﻠُﻮ َن ٱﻟ ﱠﺴﻴِّﺌَﺎت َﺣ ﱠ ٰﱴ إِذَا َﺣ‬
َ ‫ﻀَﺮ أ‬ َ ‫ﺬ‬ َ ْ ََْ
﴾ً‫ﻚ أ َْﻋﺘَ ْﺪ َ� َﳍُﻢ َﻋ َﺬاﺎﺑً أَﻟِﻴﻤﺎ‬
َ ِ‫إِِﱏ ﺗُـﺒﺖ ٱﻵ َن وﻻَ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ َﳝُﻮﺗُﻮ َن وﻫﻢ ُﻛ ﱠﻔﺎر أُوﻟَـٰﺌ‬
ْ ْ ٌ َُْ َ َ ُْ ّ
770

Walaysati alttawbatu lilladheena yaAAmaloona alssayyi-ati hatta idha hadhara


ahadahumu almawtu qala innee tubtu al-ana wala alladheena yamootoona wahum
kuffarun ola-ika aAAtadna lahum AAadhaban aleeman (Surat An Nisaa 4:18)

Tafsir: Na wala haikubaliki Toba ya wale ambao aanaendelea kufanya Maasi mpaka
yanapomfikia mmoja wao Mauti ndio akasema: ‘Hakika Mimi Nimetubu’ na pia wale
ambao wanakufa huku wakiwa ni Makafiri, kwani hao tumewatayarishia Adhabu kali
sana.

Ambapo aya hii inawalenga pia wale ambao Walioamini lakini wakawa wanadumu
katika kufanya dhambi bila ya kufanya Istighfar wa makosa ya dhambi zao.

Hivyo Kwa Upande wa Imam Mubarakpuri basi yeye anasema kua : ‘Kitendo
alichofanya Malaika Jibril kinakubalika mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala ambae
alikua akijua kua Fir’awn hawezi kuamini mpaka afikie katika hali hio, ambayo ni
hali ambayo Imani ya Asieamini hua haina manufaa yeyote.

Na ukweli ni kua katika hali kama hio ya mtu kuingia kwenye Sakarat Al Mawt hua
unaondolewa pazia na hivyo yasiyoonekana katika Ulimwengu wa Al Ghayb hua ni
yenye kuonekana, kwa alie katika Sakarat Al Mawt basi bila ya shaka kutamka Shahada
hua hakusaidii kitu kwa asieamini, na Wanazuoni wanasema pia kua hata kwa mwenye
kuamini basi kama akisema Maneno siyo katika wakati huu basi maneno hayo hua
hayahesabiwi kwani hua katika Sakarat Al Mawt.

Kwani neno Sakarat hua linamaanisha Kufunga, Kuzima, Kukatisha, Kuchanganyikiwa


akili na Ufahamu kutokana na Mshtuko wa tukio Kubwa Sana, Khofu au Maumivu
Makali sana, au Raha inayotokana na Starehe ya Hisia Kubwa Sana za Mapenzi na pia
humaanisha Kulewa, au Kutokwa na Akili…w Allahu A’Alam!

Hivyo Fir’awn akaambiwa:

﴾‫ﻨﺖ ِﻣﻦ ٱﻟْﻤ ْﻔ ِﺴ ِﺪﻳﻦ‬ َ ‫﴿آﻵ َن َوﻗَ ْﺪ َﻋ‬


َ ُ َ َ ‫ﺖ ﻗَـْﺒ ُﻞ َوُﻛ‬
َ ‫ﺼْﻴ‬
Al-ana waqad AAasayta qablu wakunta mina almufsideena (Surat Yunus 10:91)

Tafsir: Sasa hivi tena! Wakati ulikua ni mwenye kuasi hapo kabla na kua ni miongoni
mwa wenye kufanya Ufisadi.

Wakati tukio hili la kufunga Bahari na kugharikishwa Fir’awn linatokea basi Watu wa
Bani Israil wakasikia Sauti kubwa sana ya Ukuta wa Mawimbi ya Bahari kutokana na
Ukubwa wa nguvu zake katika kuanguka kwake na namna yanavyofunika na kuangamiza
771

kila kinachotakiwa kuangamizwa, basi Watu hao wakamuuliza Nabii Musa kwa
mshangao kubwa: ‘He! Nini kimetokea mbona Sauti ya Dharuba ni Kubwa sana? ’
Nabii Musa akawaambia : ‘Huo ni Mshindo wa Adhabu inayomuangamiza Fir’awn
na Jeshi Lake’

Watu wa Bani Israil wakasema: ‘Haiwezekani kua Fir’awn aangamie, hivi


hujamuona wewe namna alivyokua akiishi na kudumu madarakani na kufanya
mambo ambao hayawezekani kufanywa na watu wengine?’ hivyo Allah Subhanah
wa Ta’ala akiamrisha Bahari hio kuuopoa Mwili wake juu ya Maji na kuutupa ufukweni,
ili watu wa Bani Israil waweze kuamini kua kweli Fir’awn ameshaangamia na pia kua ni
uthibitisho kwa watakaokuja baada yake kama zinavyosema aya:

‫آ�ﺗِﻨَﺎ‬ ِ ‫ﻚ آﻳَﺔً َوإِ ﱠن َﻛﺜِﲑاً ِّﻣ َﻦ ٱﻟﻨ‬ ِ ِ ِ‫﴿ﻓَﭑﻟْﻴـﻮم ﻧـُﻨ ِﺠﻴﻚ ﺑِﺒ َﺪﻧ‬
َ ‫ﱠﺎس َﻋ ْﻦ‬ َ ‫ﻚ ﻟﺘَ ُﻜﻮ َن ﻟ َﻤ ْﻦ َﺧ ْﻠ َﻔ‬
َ َ َ ّ َ ََْ
﴾‫ﻟَﻐَﺎﻓِﻠُﻮ َن‬
Faalyawma nunajjeeka bibadanika litakoona liman khalfaka ayatan wa-inna
katheeran mina alnnasi AAan ayatina laghafiloona. (Surat Yunus 10:92)

Tafsir: Hivyo leo tutauokoa Mwili wako ili upate kua ni uthibitisho kwa watakaokuja
baada yako, na kwa hakika wengi miongoni mwa watu kuhusiana na vithibitisho vyetu
hua ni wenye kughafilika navyo.

Ambapo aya zimetumia neno Badan lenye kumaanisha Kukua, Kua na Kiwiliwili bila ya
Roho. Ambapo neno Badan hua ni sawa kimaana na neno Jism isipokua Badan hua
linatumika kuelezea muonekano wa Kiumri na neno Jism hua linatumika kuelezea hali
ya Muonekano wa Rangi ya Nje ya Mwili. Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala alikua
akiweka wazi kua atauopoa Mwili wa Firawn utakaodumu kwa mda mrefu Kiumri, kwa
ajili ya kua ni kithibitisho kwa ajili ya watakaokuja baadae.

Ambapo kwa upande wa Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari basi yeye
anasema kua: ‘Maneno bibadanika yanamaanisha Mwiili Mtupu yaani usiokua na
Roho ndani yake wala Nguo juu yake.’

Ambapo kuna uthibitisho wa ahadi hii ya Allah Subhanah wa Ta’ala iliyoelezewa


kwenye aya hii juu ya Fir’awn kuwekwa kua ni Uthibitisho ni kutokana kupatikana kwa
Mwili huo wa Fir’awn mnamo mwaka 1898 katika mji wa Al Aqsur ambapo upo katika
umbali wa kilomita 800 kutoka katika Bahari ya Mediterrenean na hivyo kua karibu na
Mto Nile, ambapo Mwili huo ulikua umehifadhiwa kwa miaka 3000 katika chumba cha
chini ya ardhi kwenye moja kati ya Pyramids ambayo yalikua yakitumika kaa sehemu ya
772

hifadhi Miili ya Fir’awn Watawala wa Misri, ambapo baada ya kufanyiwa uchunguzi


mnamo mwaka 1975 basi vipimo vilionesha kua Mwili wa mtu huyo ulifikwa na Mauti
baada ya kunywa Maji mengi sana ya chumvi kulikotokea sambamba na kishindo
kikubwa sana kilichofuatia baada ya kunywa Maji hayo na kabla ya kufariki kwake,
Mwili huo umehifadhiwa katika Makumbusho ya Historia ya Misri.

Baada ya tukio la kuangamia wa Fir’awn basi Allah Subhanah wa Ta’ala anatuwekea


wazi uthibitisho wa kutimiziwa ahadi ya Nabii Musa aliyowaahidi watu wa Bani Israil
kupitia kwa Allah Subhanah wa Ta’ala pale aliposema:

ِ ِ َ‫﴿وﻟََﻘ ْﺪ ﺑـ ﱠﻮأْ َ� ﺑ ِ ۤﲏ إِﺳﺮاﺋِﻴﻞ ﻣﺒـ ﱠﻮأَ ِﺻ ْﺪ ٍق ورزﻗْـﻨ‬


ْ ‫ﺎﻫ ْﻢ ّﻣ َﻦ ٱﻟﻄﱠﻴِّﺒَﺎت ﻓَ َﻤﺎ‬
‫ٱﺧﺘَـﻠَ ُﻔﻮاْ َﺣ ﱠ ٰﱴ‬ ُ َََ َُ َ َ ْ َ َ َ
﴾‫ﻀﻰ ﺑَـْﻴـﻨَـ ُﻬﻢ ﻳَـﻮَم ٱﻟْ ِﻘﻴَ َﺎﻣ ِﺔ ﻓِﻴﻤﺎ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻓِ ِﻴﻪ َﳜْﺘَﻠِ ُﻔﻮ َن‬
ِ ‫ﻚ ﻳـ ْﻘ‬
َ َ ‫ﺑ‬
‫ﱠ‬‫ر‬ ‫ﱠ‬
‫ن‬ ِ‫ﺟﺂء ُﻫﻢ ٱﻟْﻌِْﻠﻢ إ‬
َ ْ ْ َ ُ ُ َ َ
Walaqad bawwa/na banee isra-eela mubawwaa sidqin warazaqnahum mina
alttayyibati fama ikhtalafoo hatta jaahumu alAAilmu inna rabbaka yaqdee
baynahum yawma alqiyamati feema kanoo feehi yakhtalifoona (Surat Yunus 10: 93)

Tafsir: Na kwa hakika tuliwaweka Bani Israil katika makazi yaliyo bora (Sham na
Misri), na tukawaruzuku miongoni mwa vitu vizuri, na hawakutofautiana mpaka pale
walipopata Ilm, Hakika Allah atahukumu baina yao katika siku ya Kiama juu ya kile
walichokua wakitofautiana.

Ambapo aya imetumia neno Mubawwaa Sidqin ambapo neno Sidqin ni lenye kutokana
na neno Sadaqa lenye kumaanisha Kua kweli, Kua na Ikhlas, Kusadiki, Kuthibitisha
Ukweli, Kutimiza Miadi, Ahadi au Makubaliano, Bora zaidi kuliko vyengine,
Kukubalika zaidi, n.k. hivyo hapa aya inamaanisha kua Watu wa Bani Israil waliwekwa
kwenye sehemu ya Makazi y a Ardhi ambayo ndio waliyoahidiwa ambayo ni bora.

Hivyo kutokana na maana hio basi Wanazuoni wanasema kua ardhi iliyokusudiwa hapa
ni Sham na Misri na huo ni mtizamo wa Imam Ad Dahhaq Ibn Muzahim na Imam
Qatadah Al Saddusi, na hii ni kutokana na kua Utawala wa Fir’awn ulikua umeanzia
Misri na kuenea hadi katika eneo zima la Magharibi la Jangwa la Sinai mpaka katika
maeneo ya Kusini ya Palestina ya Ghaza na Asqalan.

Ambapo anasema Abdullah Ibn Khawla al Azadi Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mimi
nilimwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa kusema kua: ‘Ya Rasul
Allah (Salallahu Alayhi wa Salam) nichagulie mimi sehemu ya ambayo ya kufanyia
Hijra.’ Nae akasema: ‘Unaweza kuelekea Sham, kwani Allah Subhanah wa Ta’ala
773

ameichagua seehemu ya ardhi hio kua ni vutio kwa ajili ya wale walio bora
miongoni mwa watu’’(Imam Ahmad)

Na kwa upande wa Imam At Trimidhi basi yeye anasema kua: ‘Amesema Wathilah Ibn Al
Asqa Radhi Allahu Anhu kua amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua
Ifanyeni Ardhi ya Sham kua ndio Mahali penu pa kufikia kwani ndio sehemu bora
miongoni mwa sehemu ambazo Waja wake bora wameishi’na hivyo Wathilah Ibn Al
Asqa Radhi Allahu Anhu alihamia nchini Syria na akafariki huko huko.

Hivyo kutokana na kua aya imetaja maneno yasemayo Mubawwaa Sidqin basi
Wanazuoni wametofautiana kuhusiana Makazi hayo, kwani wapo wasemao kua ni Ardhi
waliyoahidiwa yaani Ardhi ya Sham na kuna wasemao kua wa ilikua ni ardhi ya Misri
na hii ni kutokana na aya zisemazo:

‫ﺎﻫﺎ ﺑَِ ۤﲏ‬ ِ ٍ ٍ ِ َ‫﴿ﻓَﺄَﺧﺮﺟﻨ‬


َ ‫۞وُﻛﻨُﻮٍز َوَﻣ َﻘ ٍﺎم َﻛ ِﺮٍﱘ۞ َﻛ ٰﺬﻟ‬
َ َ‫ﻚ َوأ َْوَرﺛْـﻨ‬ َ ‫ﺎﻫ ْﻢ ّﻣﻦ َﺟﻨﱠﺎت َوﻋُﻴُﻮن‬
ُ ْ َْ
﴾‫إِ ْﺳﺮاﺋِﻴﻞ‬
َ َ
Faakhrajnahum min jannatin waAAuyoonin; Wakunoozin wamaqamin kareemin;
Kadhalika waawrathnaha banee isra-eela; (Surat Ash Shuara 26:57-60)

Tafsir: Na kisha tukawatoa kwenye Mabustani yao na Chemchem, na Mali na Makazi


mazuri ya heshima. Kadhalika ndivyo tulivyowarithisha watu wa Bani Israil (Mali za
Watu wa Misri).

Ambapo wenye mtizamo huo basi wanasema kua baada ya kugharikishwa kwa Fir’awn
na jeshi lake basi Allah Subhanah wa Ta’ala aliwarithisha watu wa Bani Israil Mashamba
ya Watu wa Misri, Makazi yao na Mali zao kwa ujumla kama inavyosema Aya ifuatayo:

‫ض َوَﻣﻐَﺎ ِرﺑَـ َﻬﺎ ٱﻟﱠِﱴ َﺎﺑ َرْﻛﻨَﺎ‬


ِ ‫ﻀ َﻌ ُﻔﻮ َن َﻣ َﺸﺎ ِر َق ٱﻷ َْر‬ْ َ‫ﻳﻦ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳُ ْﺴﺘ‬ ِ‫ﱠ‬ ﴿
َ ‫َوأ َْوَرﺛْـﻨَﺎ ٱﻟْ َﻘ ْﻮَم ٱﻟﺬ‬
‫ﺼﻨَ ُﻊ‬ْ َ‫ﺻﺒَـُﺮواْ َوَد ﱠﻣْﺮَ� َﻣﺎ َﻛﺎ َن ﻳ‬
َ ‫ﻴﻞ ﲟَﺎ‬
ِ ِ‫ٱﳊﺴﲎ ﻋﻠَﻰ ﺑ ِ ۤﲏ إِﺳﺮآﺋ‬
ْ ٰ َ ٰ َ ْ ‫ﻚ‬َ ِ‫ﺖ َﻛﻠِﻤﺔُ رﺑ‬
ّ ْ ‫ﱠ‬‫ﲤ‬
َ‫و‬ ‫ﺎ‬‫ﻴﻬ‬
َ
ِ‫ﻓ‬
َ َ َ ْ ُ َ َ َ
﴾‫ﻓِﺮ َﻋﻮ ُن وﻗَـﻮُﻣﻪُ وَﻣﺎ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳـَ ْﻌ ِﺮ ُﺷﻮ َن‬
َ َْ ْ ْ
774

Waawrathna alqawma alladheena kanoo yustaduAAafoona mashariqa al-ardhi


wamagharibaha allatee barakna feeha watammat kalimatu rabbika alhusna AAala
banee isra-eela bima sabaroo wadammarna ma kana yasnaAAu firAAawnu
waqawmuhu wama kanoo yaAArishoona (Surat Al Araf 7:137)

Tafsir: Na tukawarithisha Watu wale ambao waliokua ni dhaif ardhi za Mashariki na


Magharibi ambazo tumezibariki ndani yake na ikakamilika kauli tukufu ya Mola wako
kwa Watu wa Bani Israil kutokana na Subira yao na tukayaangamiza Makazi yote
yaliyosaniiwa vizuri na kujengwa Fir’awn na watu wake

Ambapo kuhusiana na aya hii basi anasema Imam Abu Hasan Ali Ibn Muhammad Ibn
Habib Al Mawardi Al Shafii kua : ‘Watu wa Bani Israil walirudi katika ardhi ya
nchini Misri baada ya Kuangamia kwa Fir’awn.’ Na mtizamo huu pia unathibitishwa
na aya zifuatazo:

ٍ ٍ ِ ِ ِ ﴿
‫وع‬ َ ‫َوٱﺗْـُﺮك ٱﻟْﺒَ ْﺤَﺮ َرْﻫﻮاً إﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ ُﺟﻨ ٌﺪ ﱡﻣ ْﻐَﺮﻗُﻮ َن۞ َﻛ ْﻢ ﺗَـَﺮُﻛﻮاْ ﻣﻦ َﺟﻨﱠﺎت َوﻋُﻴُﻮن‬
ٍ ‫۞وُزُر‬
ِ ِ ِ ٍ
َ ‫آﺧ ِﺮ‬
‫ﻳﻦ۞ﻓَ َﻤﺎ‬ َ ً‫ﺎﻫﺎ ﻗَـ ْﻮﻣﺎ‬
َ َ‫ﻚ َوأ َْوَرﺛْـﻨ‬ َ ‫َوَﻣ َﻘ ٍﺎم َﻛ ِﺮٍﱘ۞ َوﻧَـ ْﻌ َﻤﺔ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻓ َﻴﻬﺎ ﻓَﺎﻛ ِﻬ‬
َ ‫ﲔ۞ َﻛ ٰﺬﻟ‬
﴾‫ض وَﻣﺎ َﻛﺎﻧُﻮاْ ُﻣﻨﻈَ ِﺮﻳﻦ‬ ِ ْ ‫ﺑَ َﻜ‬
َ َ ُ ‫ﺖ َﻋﻠَْﻴﻬ ُﻢ ٱﻟ ﱠﺴ َﻤﺂءُ َوٱﻷ َْر‬
Waotruki albahra rahwan innahum jundun mughraqoona;Kam tarakoo min
jannatin waAAuyoonin; WazurooAAin wamaqamin kareemin; WanaAAmatin
kanoo feeha fakiheena; Kadhalika waawrathnaha qawman akhareena; Fama bakat
AAalayhimu alssamao waal-arddu wama kanoo mundhareena (Surat Ad Dukhan
44:24-29)

Tafsir: Na iwache Bahari itulie kwani kwa hakika wao ni Jeshi litakaloangamia. ‘Jee
(Fir’awn na watu wake) waliacha Mabustani na Chemchem ngapi?; Na Mashamba
Yaliyonawiri na akazi Mazuri sana; Na Neema za Kimaisha ambazo walikua
wakijifaharishia; Na kadhalika tulivyowarithisha baada yao; Na Mbingu
hazikuwalilia na wala hawakuongezewa (Mda wao wa kuishi).’

Subhanah Allah! Aya inatuwekea wazi sisi, waliotangulia kabla yetu na watakaokuja
baada yetu kua, tusihadaike na vizuri vya Ulimwengu kwani vina mwisho wake, iwe
Mamlaka, Mali, Uzuri, Afya n.k kwani zote hizo ni neema za Allah Subhanah wa Ta’ala
juu yetu hivyo tunatakiwa kua ni wenye kushukuru na kumkumbuka Mola wetu alietupa
Neema hizo tunazojifaharishia kua nazo, kwani tutaondoka na tutaziwacha Ulimwenguni
775

utakapofika mda wetu na wala hatutaongezewa hata sekunde ya Kuishi ndani yake
Ulimwenguni.

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea hali waliyokua nayo Fir’awn na Jeshi
lake katika wakati huo na baada ya wakati huo, mpaka hii leo hadi kesho katka siku ya
Kiama:

ُ‫ﻒ َﻛﺎ َن َﻋﺎﻗِﺒَﺔ‬


َ ‫ﻮدﻩُ ﻓَـﻨَـﺒَ ْﺬ َ� ُﻫ ْﻢ ِﰱ ٱﻟْﻴَِّﻢ ﻓَﭑﻧﻈُْﺮ َﻛْﻴ‬ َ ‫﴿ﻓَﺄ‬
َ ُ‫َﺧ ْﺬ َ�ﻩُ َو ُﺟﻨ‬
ِ ‫ٱﻟﻈﱠﺎﻟِ ِﻤﲔ۞وﺟﻌ ْﻠﻨَﺎﻫﻢ أَﺋِ ﱠﻤﺔً ﻳ ْﺪﻋﻮ َن إِ َﱃ ٱﻟﻨﱠﺎ ِر وﻳـﻮم ٱﻟْ ِﻘ‬
ُ َ‫ﻨﺼُﺮو َن۞ َوأَﺗْـﺒَـ ْﻌﻨ‬
‫ﺎﻫﻢ‬ َ ُ‫ﻴﺎﻣﺔ ﻻَ ﻳ‬ َ َ ََْ ُ َ ُْ ََ َ َ
ِ ِ ِ ِ ِِ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ِﰱ َﻫﺬﻩ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ ﻟَ ْﻌﻨَﺔً َوﻳَـ ْﻮَم اﻟﻘﻴَ َﺎﻣﺔ ُﻫ ْﻢ ّﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻤ ْﻘﺒُﻮﺣ‬
Faakhadhnahu wajunoodahu fanabadhnahum fee alyammi faondhur kayfa kana
AAaqibatu aldhdhalimeena; WajaAAalnahum a-immatan yadAAoona ila alnnari
wayawma alqiyamati la yunsaroona; WaatbaAAnahum fee hadhihi alddunya
laAAnatan wayawma alqiyamati hum mina almaqbooheena (Surat Al Qasas 28:40-
42)

Tafsir: Hivyo tukamkamata yeye na Jeshi lake, kisha tukawarusha (tukawazamisha)


kwenye Maji (Baharini), hivyo angalia unavyokua mwisho wao wale wanaofanya
Udhalimu. Natumewafanya wao kua viongozi wanaoita (watu) kwenye Moto, katika
siku ya Kiama hawata nusurika. Na tumeifanya laana kua ni yenye kuwafuata wao
katika Dunia hii, na katika siku ya Malipo watakua ni miongoni mwa watakaokosa
Rehma za Mola wao.

Ambapo tunaona kua aya zimetumia neno Nabadhnahu lenye kutokana na neno Nabadha
ambalo hua ni lenye kumaanisha Kurembea mbali,Kurusha, Kutupa au Kudharau kitu
ambapo anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi na pia Jarrah Allah
Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kua : ‘Allah Subhanah wa Ta’ala ametumia neno
hili hapa katika aya hii kumaanisha namna walivyokua hawana thamani mbele
yake watu hao kwani walirembewa kama mtu unavyorembea Mdudu Mjusi
aliekufa.’

Hivyo anasema Imam Ahmad Muhammad Ath Thalabi kua: ‘Baada ya Fir’awn na Jeshi
lake kugharikishwa basi Nabii Musa aliteua Watu 24,000 miongoni mwa Jeshi la
Vijana la watu wa Bani Israil na kuwagawa katika sehemu mbili, ambapo sehemu
moja iliongozwa na Joshua Ibn Nun na sehemu ya pili lililongozwa na Kaleb Ibn
Jefuneh na kisha Watu hao 24,000 wakaenda katika ardhi ya Misri na kuhodhi kila
776

kitu walichoweza kuhodhi katika ardhi ya Misri kwani ilikua hakuna Mtawala wala
wapiganaji wao kwani walikua wote wameangamia na Fir’awn. Kisha Joshua
akachagua Kiongozi miongoni mwa Watu wa Misri ili awaongoze watu hao na yeye
akarudikwa Nabii Musa’

Kutokana na aya hizi basi tunaona kuna baadhi ya Wanazuoni wasemao kua baadhi ya
watu wa Bani Israil walibakia na Nabii Musa na kuelekea Sham na baadhi yao waliamua
kurudi nchini Misri na ndio maana mpaka leo kwa baadhi ya watu wa Bani Israil basi
wanaichukulia Ardhi ya nchini Misri kua ni ardhi ya pili kwa utukufu baada ya ardhi ya
Jerusalem, na hii ni kwa sababu katika kipindi cha Jeremiah watu wa Bani Israil walikua
wakiishi pia nchini katika ardhi za Misri na Libya na Ethiopia.

Hivyo basi watu wa Misri waliokua karibu na Utawala waliwaambia watu hao wa Misri
kua Fir’awn hakufariki bali ameenda nchini Abisiniyya kwa ajili ya kuongeza nguvu Jeshi
lake, na hivyo atarudi kwa ajili ya kupigana tena na watu wa Bani Israil, na hivyo Watu
wa Bani Israil walikaa nchini Misri kwa miaka 13 baada ya kuangamia kwa Fir’awn wa
Nabii Musa, kisha wakafukuzwa baada ya kutokea Fir’awn mpya aliekua amemrithi
Fir’awn wa Nabii Musa.

Tunarudi katika kipindi cha mara baada ya tukio la kugharikishwa kwa Fir’awn ambapo
tunasema kua hata maji ya Bahari waliyoivuka hayajakauka miguuni mwao Watu wa
Bani Israil wakati wakiwa na Nabii Musa wakiendelea na safari yao, basi njiani wakakuta
jamii ya watu ambao ni wenye kushikamana na kuabudu Masanamu na hivyo hali ikawa
kama zisemavyo aya:

ْ‫َﺻﻨَ ٍﺎم ﱠﳍُْﻢ ﻗَﺎﻟُﻮا‬ ٍ ِ ِۤ ِ ﴿


َ ‫َو َﺟ َﺎوْزَ� ﺑﺒَِﲏ إ ْﺳَﺮآﺋ‬
ْ ‫ﻴﻞ ٱﻟْﺒَ ْﺤَﺮ ﻓَﺄَﺗَـ ْﻮاْ َﻋﻠَ ٰﻰ ﻗَـ ْﻮم ﻳَـ ْﻌ ُﻜ ُﻔﻮ َن َﻋﻠَ ٰﻰ أ‬
﴾‫ﺎل إِﻧﱠ ُﻜﻢ ﻗَـﻮٌم َْﲡ َﻬﻠُﻮ َن‬ ِ ِ
ْ ْ َ َ‫ٱﺟ َﻌ ْﻞ ﻟﱠﻨَﺂ إﻟَـٰﻬﺎً َﻛ َﻤﺎ َﳍُْﻢ آﳍَﺔٌ ﻗ‬ ْ ‫ﻮﺳ ٰﻰ‬َ ُ‫ٰﳝ‬
Wajawazna bibanee isra-eela albahra faataw AAala qawmin yaAAkufoona AAala
asnamin lahum qaloo ya moosa ijAAal lana ilahan kama lahum alihatun qala
innakum qawmun tajhaloona (Surat Al Arafa 7:138)

Tafsir: Na tukawavusha Bani Israil kwenye Bahari, na wakakutana na watu waliokua


wameshikamana na Masanam yao, Hivyo wakasema: ‘Ewe Musa tujaalie na sisi
Mungu kama walivyokua na Mungu wao’ Akasema (Nabii Musa): ‘Hakika Nyini ni
watu Wajinga’

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi
kua: ‘Hapa watu wa Bani Israil walikua wakimaanisha kua Nabii Musa bora
777

awatengenezee Miungu myengine midogo midogo ambayo wataitumia kupitia kwao


kwa ajili ya kumuomba Allah Subhanah wa Ta’ala kuliko kutokua na Miungu hio’

Imam Abu Muhammad Al Husayn Ibn Mas'ud Ibn Muhammad Al Farra' Al-Baghawi
yeye anasema kua: ‘Kuomba kwao Masanamu watu hawa wa Bani Israil, hakukua
ni kwa sababu ya kua labda wanashaka juu ya kuhusiana na kumpwekeshaa Allah
Subhanah wa Ta’ala, bali walikua na malengo ya kumtafuta Mungu mmoja kupitia
katika njia ya kua na kitu ambacho kitawapelekea kuhisi kwa hisia za kuona na
kugusa kitu hicho ambako hakutowapelekea kua na madhara katika imani yao hio,
na ndio maana Nabii Musa akasema kua: ‘Innakum qawmun tajhaloona - Hakika
nyinyi ni watu wajinga’ ’

Ambapo Abu Waqid Al Laythi Radhi Allahu Anhu kua: ‘Safari moja tulikua safarini
na Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam na tukakutana na Mti mkubwa sana
ulionawiri, nasi tukasema: ‘Ya Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam Upe Mti huu
alama ya heshima, kama vie ambavyo walivyokua wakifanya Mapagani kwenye
Miti mikubwa kwa ajili ya kuning’iniza silaha zao na kukaa chini yake’ Rasul Allah
Salallahu Aalayhi wa Salam akasema: ‘Allahu Akbar! Hii itakua ni sawa na watu wa
Bani Israil waliposema kumwamba Nabii wao: ‘Ewe Musa! Tuwekee na sisi Mungu
kama walivyokua nao wao Mungu’ bila ya shaka mtawafuata wale waliotangulia
kabla yenu katika kila kitu’’(Imam At Tabarani, Imam Al Qurtubi)

Ambapo anasema Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Ahmad Ibn Abu Baqr Al Ansari
Al Qurtubi kua: ‘Mapagani wa Kiarabu walikua wakiipa heshima Miti mikubwa
kwa kuiita Dhat Anawat (sehemu ambayo inaning’inizwa silaha) na hivyo hua
wakifika katika Mti huo basi hua ni wenye kuomba kupata baraka kwa kutundika
silaha zao na kisha huchutaa chini yake kwa mda kabla ya kuondoka.’

Na aya hii inatukumbusha ile tokeo lililotokea baada ya vita vya Ngamia katika kipindi
cha Utawala wa Amir ul Muuminin Ali Ibn Talib Radhi Allahu Anhu ambalo Imam
Ahmad Muhammad Ath Thalabi anatuelezea kwa kusema kua: ‘Amesema Muhammad
Ibn Qays kua: ‘Kuna Yahudi alikuja kwa Amir ul Muuminin Ali Ibn Talib Radhi
Allahu Anhu na kumwambia: ‘Tayari Mshachinjana! yaani hamkuweza kujidhibiti
hata kwa miaka 25 baada ya kufariki Mtume wenu ’’ Amir ul Muuminin Ali Ibn
Talib Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Naam, lakini angalau kwetu sisi kwani katika
kipindi hicho kumekua na Subra na Kheri nyingi ndani yake, lakini nyinyi hata
miguu yenu haikuwahi kukauka maji ya Baharini basi mkasema: ‘Ya Moosa ijAAal
lana ilahan kama lahum alihatun - Ewe Musa tujaalie na sisi Mungu kama
walivyokua na Mungu wao’’’

Hivyo Nabii Musa akawaambia watu wa Bani Israil kua haina haja ya kua na ujinga huo,
kwani Allah Subhanaha wa Ta’ala ameahidi kua atawapa Muongozo wa nini cha kufanya
778

na nini cha kutofanya kupitia katika kitabu chake atakachowashushia kupitia kwake,
ambacho ni Tawrat.

MUNAJAT NABI MUSA KATIKA KUKABIDHIWA TAWRAT.


Neno Munajat maana yake hua ni mnong’onezo baina ya Allah Subhaah wa Ta’ala na
Mja wake ambao hua ni wa kubadilishana maneno au kauli nzuri na laini ambazo
kutokana nazo basi Moyo wa mja husika hua ni wenye kupata utulivu ndani yake.

Miongoni mwa Viumbe waliojaaliwa kua na Munajat na Mola wao, basi ni Nabii Musa
na hii ni kwa sababu Nabii Musa alikua ni mwenye Ikhlasi kwa Mola wake na ni mwenye
Ikhlasi kwa Dini yake kama alivyosema mwenyewe Allah Subhanah wa Ta'ala katika
Qur’an:

﴾ً‫ﻮﺳ ٰﻰ إِﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن ﳐُْﻠَﺼﺎً وَﻛﺎ َن ر ُﺳﻮﻻً ﻧﱠﺒِﻴّﺎ‬ ِ ِ ِ


َ َ َ ‫﴿ َوٱذْ ُﻛْﺮ ﰱ ٱﻟْﻜﺘَﺎب ُﻣ‬
Waodhkur fee alkitabi moosa innahu kana mukhlasan wakana rasoolan nabiyyan
(Surat Maryam 19:51)

Tafsir: Na ametajwa kwenye Kitabu Musa, kwa hakika yeye alikua ni mwenye Ikhlasi
na alikua ni Mtume na Nabii.

Hivyo baada ya Nabii Musa kuwaahidi watu wa Bani Israil kuhusiana na maamrisho ya
mfumo wa Maisha wanayotakiwa kuishi basi Nabii Musa akaomba kwa Mola wake ili
aweze kuwatimizia watu wake wa Bani Israil juu ya ahadi hio. Na hivyo Allah Subhanah
wa Ta’ala akamwambia Nabii Musa kua aelekee katika Jangwa la Sinai ambapo ndipo
atakapozungumza na Mola wake na kupewa Maamrisho yake kupitia kwenye kitabu
chake, lakini akifika huko basi kabla ya kuzungumza na Mola wake inambidi kwanza
afunge kwa siku 30, kisha akoge na kujitoharisha kwa ajili ya kuzungumza na Mola wake.

Hivyo Nabii Musa akamuachia Nabii Harun wadhifa wa usimamizi juu ya watu wake na
akaanza safari ya kuelekea katika Jangwa la Sinai alipofika basi akafunga kwa siku 30,
kisha na kisha akajitoharisha lakini kwa kua katika kufunga kwake alikua si mwenye
kuipenda harufu ya Mdomo wake inayotokana na kufunga kwake, basi akawa anapiga
Msuwaki ili kukaa harufu hio, hivyo Malaika wakasema kua walikua wanaipenda harufu
ya Mtu aliefunga aliyokua nayo Nabii Musa kutoka Mdomoni mwake, lakini harufu hio
779

inakatika kutokana na kupiga Msuwaki kwake, hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala


akamuongezea siku 10 zaidi za kufunga ili asiwe ni mwenye kupiga msuwaki ndani ya
Funga yake

Kwa upande mwengine basi kuna wasemao kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala
alimchagulia Nabii Musa Siku 30 za Mwezi wa Dhul Qaidah na siku 10 za mwanzoni
za mwezi wa Dhul Hijja na hivyo siku hizo zikawa ni 40’. Ambapo miongoni mwa
wenye mtizamo huo ni pamoja Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu na
pia Mujtahid Imam Abu Bakr Muhammad Ibn Ibrahim Ibn Al Mundhiri Al Nishapuri Al
Shafii, na mitizamo hii yote ni kutokana na walivyofahamu Wanazuoni kulingana na
maneno ya Allah Subhnah wa Ta’ala kama inavyosema Qur’an kuhusiana na siku hizo
katika aya ifuatayo:

ِ ِ ِ ِ
‫ﺎل‬
َ َ‫ﲔ ﻟَْﻴـﻠَﺔً َوﻗ‬َ ‫ﺎت َرﺑِّﻪ أَْرﺑَﻌ‬
ُ ‫ﺎﻫﺎ ﺑِ َﻌ ْﺸ ٍﺮ ﻓَـﺘَ ﱠﻢ ﻣﻴ َﻘ‬
َ َ‫ﲔ ﻟَْﻴـﻠَﺔً َوأَْﲤَ ْﻤﻨ‬
َ ‫ﻮﺳ ٰﻰ ﺛَﻼَﺛ‬ َ ‫﴿ َوَو‬
َ ‫اﻋ ْﺪ َ� ُﻣ‬
﴾‫َﺻﻠِ ْﺢ وﻻَ ﺗَـﺘﱠﺒِ ْﻊ َﺳﺒِﻴﻞ ٱﻟْﻤ ْﻔ ِﺴ ِﺪﻳﻦ‬ ِ ِ ِِِ
َ ُ َ َ ْ ‫ٱﺧﻠُْﻔ ِﲎ ﰱ ﻗَـ ْﻮﻣﻰ َوأ‬ ْ ‫ﻮﺳ ٰﻰ ﻟـﺄَﺧﻴﻪ َﻫ ُﺎرو َن‬
َ ‫ُﻣ‬
WawaAAadna moosa thalatheena laylatan waatmamnaha biAAashrin fatamma
meeqatu rabbihi arbaAAeena laylatan waqala moosa li-akheehi haroona okhlufnee
fee qawmee waaslih wala tattabiAA sabeela almufsideena(Surat Al Araf 7:142)

Tafsir: Na tukamchagulia Musa Usiku thalathini na tukakamilisha kwa Kumi zaidi,


akakamilisha kipindi cha Mola wake Usiku Arubaini, akasema Musa kumwambia
Kaka yake Haruna: ‘Chukua Nafasi yangu katika Jamii yangu, na kua katika njia
sahih na wala usifuate njia ya Mafisadi’

Ambapo aya yetu imetuma neno WaA’ad ambalo hua linamaanisha Kuahidi, Kutoa
Ahadi kwa Kuadhibu au kwa Kulipa Mema, neno WaA’ad ndio lililotoa neno MiaAd
yaani Miadi au Sehemu ya Kukutana kutokana na Kuahidiana au Wakati wa Kukutana
kutokana na Kuahidiana.

Hivyo basi ili kuwe na Miadi basi ni lazima kuwe na pande mbili zinazoahidiana, ambapo
katika aya yetu hii basi tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala anatuambia kua
Waliahidiana na Nabii Musa kulingana na kipimo cha wakati ambacho ni Usiku 40
ambazo Nabii Musa atakua ni mwenye kufanya Ibada katika Mlima wa Jangwa la Sinai
kwenye Mlima wa Tur, na baada ya hapo basi ndio Allah Subhanah wa Ta’ala
atamkabidhi Nabii Musa kitabu cha Tawrat.

Na katika kuainisha kipimo hicho cha wakati basi Allah Subhanah wa Ta’ala ametumia
neno Laylatan ambalo maana yake hua ni Usiku. Na anasema Imam Ahmad Al Marzuqi
780

Al Maliki Al Makki kua: ‘Neno Laylatan na Neno Laylun yote hua yana maana moja
isipokua, Neno Laylatan hua linatumika kua ni kinyume cha neno Yawm yaani Siku
na neno Laylun hua linatumika kua ni kinyume cha neno Nahar yaani Mchana. Na
hivyo neno Laylatan hua linatumika kumaanisha maana pana zaid Laylun kama vile
ambavyo lilivyokua na maana pana zaidi neno Yawm kuliko Nahar’

Ambapo kwa upande wa Shaykh Al Akbar Imam Abu Bakr Ibn Arabi basi yeye amesema
kua: ‘Hesabu ya mambo ya Kidunia hua inahesabiwa kwa kutumia Jua na hesabu
ya Mambo ya Kiakhera hua inahesabiwa kwa kutumia Mwezi.’

Imam Jamal Islam Abu Qasim Abd Al Karim Ibn Hawazin Al Qushayri kua: ‘Allah
Subhanah wa Ta’ala kua makubaliano ya miadi ya Mlima Tur yalikua ni kwa
sababu ya kua katika mara ya kwanza wakati Nabii Musa alipozungumza na Allah
Subhanah wa Ta’ala ilikua ni katika hali ya kushtukiza, ambapo katika miadi hii
ilikua ni kukutana kwa ajili ya mazungumzo yanayotegemewa kutokea hivyo ni
Mautano yaliyo katika hali yenye kujaa furaha na raha ya Kiroho’

Aya pia imetumia neno Miqat ambalo ni lenye kutokana na neno Waqata ambalo hua
linamaanisha Wakati, Chagulia Kipindi cha Wakati wa kufanya jambo au Kitu, Kuamua
wakati wa Kitu fulani. Hivyo Neno Waqata ndiolililotoa neno Waqt ambalo hua hali ya
Umoja ya Wakati na likatoa neno Miqat ambalo hua ni hali ya wingi wa wakati au
Nyakati. Ambapo mbali ya kua neno Miqat linamaanisha hali ya wingi wa wakati yaani
Nyakati lakini pia neno hilo hua linamaanisha Wakati Maalum uliopangwa kwa ajili ya
kufanya Kitu maalum, au Sehemu maalum iliyopangwa kwa ajili ya kufanya kitu
Maalum.

Ambapo tunapoiangalia aya yetu hii basi tuaona kua Nabii Musa anamuomba kaka yake
ambae ni Nabii Harun kua amsaidie kubeba jukumu lake katika jamii yake kwani alikua
akijuakua kutokana na hali yao basi waliyokua nayo watu wake hao wa Bani Israil huenda
wakawa ni wenye kutaka kumuasi Mola wao kama walivyotaka kufanya hapo kabla
baada ya kuvuka bahari na kuoneshwa Miujiza kadhaa mbele ya macho yao, kwa kutaka
kua wafanyiwe Miungu myengine kama waliyokua nayo watu wengine wanaoabudu
masanam.

Na ndio maana Nabii Musa akasema: Ukhlufnee fee qawmee waaslih wala tattabiAA
sabeela almufsideena - Chukua Nafasi ya Ukhalifa wangu katika Jamii yangu, na
kua katika njia sahih na wala usifuate njia ya Mafisadi’

Hivyo baada ya kutimia wakati huo maalum basi Nabii Musa akajikuta kua akiwa tayari
kuigia katika kutimziwa miadi ya mazungumzo baina yake na Mola wake katika sehemu
waliyokubaliana kama zinavyosema aya:
781

﴾ً‫ﺐ ٱﻟﻄﱡﻮِر ٱﻷَْﳝَ ِﻦ وﻗَـﱠﺮﺑْـﻨَﺎﻩُ َِﳒﻴّﺎ‬


ِ ِ‫﴿و َ� َدﻳْـﻨَﺎﻩُ ِﻣﻦ َﺟﺎﻧ‬
َ َ
Wanadaynahu min janibi alttoori al-aymani waqarrabnahu najiyyan (Surat
Maryam 19:52)

Tafsir: Na tukamwita kutoka katika Upande wa Kulia wa (Mlima)Tur na


tukakaribiana nae kwa Kimazunguzo ya faragha.

Ambapo alifika katika sehemu husika ambayo ni kulia ya Mlima Tur au wengine kama
Al Hafidh Imam Abu Jafar Muhammad Ibn Jarir At Tabari basi anasema kua ni kuliani
kwake wakati alipokua amesimama akiutizama Mlima Tur basi basi akawa yuko katika
hali sana na Mola wake, yaani katika hali ambayo Allah Subhah wa Ta’ala anaielezea
kua kama ni Qarrabna Najiyyan

Ambapo neno Qarrabna linatokana na neno Qariba ambalo ni lenye kumanisha


Kusogelea Karibu, Kukaribia Kimasafa, Kicheo au Kidarja. Neno Qariba ndio lililotoa
pia neno Muqarrabuna ambalo hua linamaanisha Aliepewa Ruhusa au Nafasi ya
Kukaribia.

Na neno Najiyyan lililotumika hapa basi mbali ya kua limetokna na neno Naja lenye
kumaanisha Kuachiwa Huru, Kuokolewa au pia Uokozi kama tulivyozungumzia kwenye
kisa cha Nabii Nuh ambae ndie mwenye sifa ya Najiyyu Allah, na pia katika kisa cha
Nabii Ibrahim na Nabii Lut.

Lakini neno Naja ndio lililotoa neno Najwan ambalo hua pia linamaanisha Mnong’onezo,
Maneno ya Siri au ya Faragha ambayo hata yakizungumzwa mbele ya watu wengi basi
watakaosikia hua ni waliokusudiwa tu.

Hivyo basi Neno Najiyyan lililotumika hapa hua linamaanisha Mazungumzo ya


Kujadiliana kwa Faragha, na hivyo ukaribu huu aliokua nao Nabii Musa alipofika mbele
ya sehemu aliyokubaliana na Allah Subhanah wa Ta’ala umeelezewa kua ni Qarabna
Najiyyan kwa sababu ulikua ni Mkaribio uliotokana na Makubaliano ya miadi baina ya
Nabii Musa na Mola wake yaani wa Kiumbe alieruhusiwa Kukaribia Mbele ya Mola
wake kiasi ya kua anasema Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu na
Imam Mujahid Ibn Sulayman, Imam Abu Aliyyah Rafiah Ibn Mahran, Mujaddid Ad Din
Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala
alimkaribisha Nabii Musa karibu yake kiasi ya kua Nabii Musa alikua akisikia
Milio ya sauti za Kalamu ambazo Malaika walikua wakizitumia katika kuandika
kwao Tawrat.’
782

Hivyo baada ya Nabii Musa kuingia katika Munajat na Mola wake ambayo ni katika hali
ya Qarrabna Najiyyan ambapo baadhi mongoni mwetu wanawea wakajiuliza hii hali ya
mazungumzo baina ya Kiumbe na Mola wake inakua kuaje yaani mpaka Nabii Musa
akawa ni mwenye kuisikia Sauti ya Allah Subhanah wa Ta’ala?.

Ambapo jibu la suali hili linajibiwa na Hujjat Ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu
Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali ambae anasema kua:
‘Nabii Musa alisikia sauti ambao ni moja kati ya Sifa za Milele za Allah Subhanah
wa Ta’ala ambayo imo katika hali ya Uungu wake (na mamlaka yake) na Nabii
Musa hakuisikia sauti hio kwa hali ya Sauti wala ya Maandishi.’

‘Ambapo ingawa kusikia hua ni kwenye kuwezekana kutokana na hisia za kusikia


laini hii ni hali ambayo haiwezekani kuielezea kihisia, kwa sababu kuuliza suali la
kua alisikia vipi, hua ni sawa na Mtu ambae hana nguvu za kiume kua ni mweye
kuuliza Raha ya Hisia inayopatikana katika kuigiliana kimwili na Mwanamke.
Kwani itakua vigumu kumuelezea mtu kama huyu raha inayopatikana kwenye
kuigiliana kimwili na Mwanamke wakati yeye hajawahi kufanya hata mara moja,
yaani itakua hakuna njia isipokua kumuelezea mtu huyu kuigiliana kimwili na
Mwanamke kwa kumfananishia na Raha ya kula Chakula kitamu sana. Ambapo
kufananisha huko nako kamwe hakutokua sawia.’

‘Hivyo haiwezekani kwa mtu kufaham Nabii Musa alisikia vipi Sauti hio ya Allah
Subhnaha wa Ta’ala, kwa sababu hali hio ya hisia za kusikia sauti hio alijaaliwa
kupewa Nabii Musa, hivyo inabidi kufaham kua Allah Subhanah wa Ta’ala
alimuwezesha Nabii Musa kua ni mwenye hisia za kuisikia Sauti yake hio. Na
haiwezekani kwa mtu kumfananishia sauti hio kwa sababu hakuna kinachofanana
na Sauti hio ya Allah Subhanah wa Ta’ala.

Kwani kama tunavyoona kuwepo kwake kupitia katika sifa zake Tukufu Allah
Subhana wa Ta’ala bila ya kumuona yeye mwenyewe ambavyo ni tofauti na
tunavyoiona miili yetu na matukio mengine basi ndio hivyo hivyo pia ilivyokua ni
tofauti katika kusikikana sauti yake ambayo hua ni tofauti na hakufananani na
kusikia sauti au herufi’

Ambapo wanasema Imam Muhammad Ibn Is-haq, Wahb Ibn Munabih kua: ‘Kulikua
kuna Mapazia 70 baina ya Nabii Musa na Allah Subhanah wa Ta’ala, na kisha Allah
Subhanah wa Ta’ala akayanyayua yote isipokua moja tu, hivyo Nabii Musa
akaingia moja kwa moja na kuzama katika mazungumzo na Mola wake, hisia ya
raha aliyoipata ikampelekea kuomba kuonana na Mola wake, hivyo Nabii Musa
akasema.: ‘Rabbi arinee andhur ilayka - Ewe Mola wangu Nioneshe nipate Nikuone’’

Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea hali ilivyokua katika Munajat hio kwa kusema:
783

ۤ ِ ‫ﺎل ر‬ ِ ِ ِ ‫﴿وﻟَ ﱠﻤﺎ ﺟﺂء ﻣ‬


‫ﺎل ﻟَﻦ ﺗَـَﺮ ِاﱏ‬ َ َ‫ﻚ ﻗ‬ َ ‫ب أَِرِﱐ أَﻧﻈُْﺮ إِﻟَْﻴ‬ّ َ َ َ‫ﻮﺳ ٰﻰ ﻟﻤﻴ َﻘﺎﺗﻨَﺎ َوَﻛﻠﱠ َﻤﻪُ َرﺑﱡﻪُ ﻗ‬َ َُ َ َ
‫ف ﺗَـَﺮ ِاﱏ ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ َﲡَﻠﱠ ٰﻰ َرﺑﱡﻪُ ﻟِﻠْ َﺠﺒَ ِﻞ‬ ِ ْ ‫َوﻟَـٰ ِﻜ ِﻦ اﻧْﻈُْﺮ إِ َﱃ‬
ْ ‫اﳉَﺒَ ِﻞ ﻓَِﺈن‬
َ ‫اﺳﺘَـ َﻘﱠﺮ َﻣ َﻜﺎﻧَﻪُ ﻓَ َﺴ ْﻮ‬
‫ﻚ َوأ ََ�ْ أَﱠو ُل‬ َ ‫ﺖ إِﻟَْﻴ‬
ُ ‫ﻚ ﺗُـْﺒ‬ َ َ‫ﺎل ُﺳْﺒ َﺤﺎﻧ‬َ َ‫ﺎق ﻗ‬ َ َ‫ﺻﻌِﻘﺎً ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺂ أَﻓ‬
َ ‫ﻣﻮﺳ ٰﻰ‬
َ ‫َﺟ َﻌﻠَﻪُ َد ّﻛﺎً َو َﺧﱠﺮ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ٱﻟْ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬
Walamma jaa moosa limeeqatina wakallamahu rabbuhu qala rabbi arinee andhur
ilayka qala lan taranee walakini ondhur ila aljabali fa-ini istaqarra makanahu
fasawfa taranee falamma tajalla rabbuhu liljabali jaAAalahu dakkan wakharra
moosa saAAiqan falamma afaqa qala subhanaka tubtu ilayka waana awwalu
almu/mineena (Surat Al Araf 7:143)

Tafsir: Na kisha akaja Musa katika eneo na mda maalum tuliompangia na


akazugungumza na Mola wake, (Nabii Musa)akasema : ‘Ewe Mola wangu Nioneshe
nipate Nikuone’ Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Huwezi kuniona, lakini
angalia Mlima, kama utabakia katika sehemu yake. Basi nawe utaweza utaniona’
Kisha alipouonesha Utukufu wake Mola wake kwa Mlima, akaujaalia kua ni wenye
kupukutika na kua vumbi. Na akaanguka nakupoteza faham Musa. Kisha
alipozindukana akasema: ‘Utukufu ni wako, Mimi Natubu kwako na hakika mimi ni
wa awali miongoni mwa Walioamini.’

Ambapo wanasema wanazuni kuhusiana na aya hii kua inawezekana kuonekana sehemu
ya Uzuri wa Allah Subhanah wa Ta’ala kwani kama ingekua haiwezekani basi Nabii
Musa asingeomba Kumuona Mola wake. Isipokua haiwezekani kuonekana sehemu ya
Uzuri huo hapa Duniani na hii ni kutokana na Maumbile ya Mazingira ya Duniani, lakini
Ufaham unasema kua inawezekana na ndio maana Nabii Musa akaomba kutokea kwa
jambo hilo.

Hivyo Allah Subhnah wa Ta’ala aliposema kua: Lan taranee walakini ondhur ila
aljabali fa-ini istaqarra makanahu fasawfa taranee - Huwezi kuniona, lakini angalia
Mlima, kama utabakia katika sehemu yake. Basi nawe utaweza utaniona’ basi Allah
Subhanah wa Ta’ala alikua akimaanisha kua Kiwiliwili chake Nabii Musa hakiwezi
Kustahamili kuuona Uzuri huo ila Roho yake inaweza kustahamili kwa sababu
Kiungo hicho ni Chenye Nguvu na uwezo wa Kustahmili kuliko Mlima kama
alivyosema katika aya ifuatayo:
784

ِ‫ﺎﺷﻌﺎً ﱡﻣﺘﺼ ِّﺪﻋﺎً ِﻣﻦ ﺧ ْﺸﻴ ِﺔ ﱠ‬


َ ‫ٱﻪﻠﻟ َوﺗِْﻠ‬
‫ﻚ‬ َ َ ّْ َ َ
ِ ‫﴿ﻟَﻮ أَﻧﺰﻟْﻨَﺎ ﻫـٰ َﺬا ٱﻟْ ُﻘﺮآ َن ﻋﻠَﻰ ﺟﺒ ٍﻞ ﻟﱠﺮأَﻳـﺘَﻪ ﺧ‬
َ ُ ْ َ ََ ٰ َ ْ َ َ ْ
ُ ْ ِ ‫ﻀ ِﺮﺑـُ َﻬﺎ ﻟِﻠﻨ‬
﴾‫ﱠﺎس ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻬﻢ ﻳَـﺘَـ َﻔ ﱠﻜﺮو َن‬ ْ َ‫ﺎل ﻧ‬
ُ َ‫ٱﻷ َْﻣﺜ‬
Law anzalna hadha alqur-ana AAala jabalin laraaytahu khashiAAan
mutasaddiAAan min khashyati Allahi watilka al-amthalu nadhribuha lilnnasi
laAAallahum yatafakkaroona; (Surat Hashir 59:21)

Tafsir: Lau kama tungeishusha hii Qur’an kwenye Mlima, basi Mlima huo
ungebubujika kwa khofu kutokana na Khofu ya kumuogopa Allah. Na hii ndio mifano
tunayowapigia watu ili wapate kutafakkari.

Ambapo anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kuhusiana na
aya hio kua: ‘Hakika Allah Subhanah wa Ta’ala anasema kua nimeishusha hii
Qur’an ndani ya Nyoyo zao Ibn Adam ili waihifadhi na juu yao iwe maamrisho
yake. Hamtodhurika kwa kihifadhi kwake ndani ya Nyoyo zenu kwa sababu ya
Ulinzi wangu na Rehma zangu na Uangalizi wangu juu yenu’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala alikua akimwambia Nabii Musa kua Roho inaweza
Kustahmili kutokana na Rehma zake Allah Subhanah wa Ta’ala juu yake lakini Mwili
hautaweza kustahamili, Lakini hata hivyo kama Nabii Musa anadhani kua ataweza
kustahmili basi hebu auangalie Mlima, kama utaweza kubakia katika sehemu yake basi
na yeye ataweza kumuona.

Ambapo kwa upande mwengine basi tunona pia kua aya hii imetumia neno: Lan kabla
ya neno Taranee na hivyo kua ni yenye kusimamia Msisitizo wa kutoweza kutokea
kwa tukio la kuonekana kwa sehemu ya uzuri wake Allah Subhnah wa Ta’ala hapa
Ulimwenguni.

Ama kuhusiana na sehemu ya uzuri huo wa Allah Subhanah wa Ta’ala iliyooneshwa kwa
Mlima huo ambao nao ukapukutika basi Wanazuoni pia wametofautiana juu yake, kwani
kwa upande wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema kua: ‘Ilikua
ni sehemu ya Nuru ya Allah Subhanah wa Ta’ala ndio iliyooneshwa Mlima.’ Na kwa
upande wa Imam Ad Dahaq Ibn Muzahim basi yeye anasema kua: ‘Ilikua ni Nuru ya
sehemu ya moja kati ya Mapazia ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala aliionesha kwa
ukubwa wa kama Pua ya Ng’ombe.’ Ambapo kwa upande wa Imam Al Hasan anasema
kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala hakujionesha bali aliuuliza tu Mlima kua jee
utaweza kunistahmilia? Na Mlima ukapukutika huku Nabii Musa akiwa
anauangalia.’
785

Ambapo anasema Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam baada ya kuisoma aya hii (Surat Al Araf 7:143) basi alionesha
sehemu ya ncha ya kidole chake kidogo cha mwisho kuonesha sehemu ambayo Allah
Subhanah wa Ta’ala aliionesha kwa Mlima huo ambao nao ukapukutika’(Imam At
Tirmidhii)

Tukio hili la kuanguka chini kwa Mlima lilikua ni tukio ambalo halikutegemewa kua
linawezekana kutokea mbele ya macho ya Nabii Musa na wala halikua ni lenye kufikirika
hata ndani ya ufaham wake kua linaweza likatokea, hivyo tukio hilo lilimsababishia
Mshtuko mkubwa sana Nabii Musa, kiasi ya kua Mwili wake ulishindwa kustahamili na
viungo vyake vya ndani ya Mwili wake, ikiwemo Moyo ambavyo ndio
vilivyomsababishia kua na uwezo wa kukmbia pale kwa mara ya kwanza alipozungumza
na Mola wake na kisha akaambiwa aitupe fimbo yake ambayo nayo ikageuka Nyoka.

Hivyo mshtuko wa ghfla wa mara hii ambao ulikua ni mkubwa zaidi ulisababisha viungo
vyamwaili wake kugoma kufanya kazi kama inayotakiwa vifanye kimaumbile, kwani
ghafla Moyo wake ulipungua kasi ya mapigo yake na hivyo hewa ikawa haiigii vya
kutosha ndani ya Mwili wake a usambazaji wa Damu ukapungua ndani ya mwili wake,
na hivyo viungo vyote vya mwili vikashindwa kufanya kazi zake kikamilifu mwili
ukaishiwa na nguvu kiasi ya kua Nabii Musa alishindwa hata kujizuia kutokanana
udhaifu wa Mwili wake, na moja kwa moja mwili wake huo ukaanguka mpaka chini juu
ya Ardhi na hapo hapo Ufaham wake ukatoweka.

Ambapo wakati tunapozungumzia tukio hili basi tukumbuke tukio jengine kama hili
ambalo liliwahi kumtokea Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam pale alipomuomba
Malaika Jibril ajioneshe mbele yake huku akiwa katika Maumbile aliyoumbwa na Mola
wake.

Kama anavyosema Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam alimuambia Malaika Jibril kua ajioneshe mbele
yake katka Umbo lake la Kimaumbile. Ambapo Malaika Jibril akasema: ‘Muombe
Mola wako’. Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuomba Allah Subhnaha
wa Ta’ala na mara likatokea Umbo la Malaika Jibril katika upande wa Mshariki,
ambalo lilikua likikua na kutanuka, mpaka Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
akaangukachini na kupoteza faham. Malaika Jibril akaja karibu ya Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam kumnyanyua na kumfuta Udenda uliokuwepo kwenye
mashavu yake’(Musnad Imam Ahmad)

Hivyo tukio la kuanguka na kuzimia baada ya kupata mshtuko kubwa wa ghafla ambao
haukuweza kutegemewa kwa Nabii Musa na pia kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
Salam ni tukio la kawaida kwa Maumbile ya Ibn Adam na wala si kasoro au labda ni
maradhi, na kutokea kwa matukio haya na kisha kua ni yenye kuelezewa ndani ya Qur’an
786

na Hadith ni moja kati ya Hikma zake Allah Subahanh wa Ta’ala katika kutuonesha
Udhaifu wetu sisi viumbe Ibn Adam mbele ya Viumbe wake Malaika na pia mbele yake
yeye Mwenyewe Muumba, na hivyo tupate kujua kua sisi si chochote si lolote kwani
kama ikiwa hali hii imewatokezea Mitume wake ambao ndio viumbe wake vipenzi, jee
hali itakuaje kwetu sisi mimi na wewe.

Hivyo tunatakiwa tuwe watiifu na turudi kwa Mola wetu kwa unyenyekevu. Ambapo
anasema Imam Abu Talib Al Makki katika Qut Al Qulub Fii Muamalat Al Mahbuub kua:
‘Nabii Musa alimuuliza Allah Subhaah wa Ta’ala kwa kusema: ‘Ya! Allah! Jee wapi
nnaweza nikakupata?’ Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Kwa wale ambao
wenye nyoyo zilizovunjika na kulainika.’’

Hivyo baada ya Nabii Musa kupata faham zake na kuomba msamaha kwa Mola wake
basi Allah Subhnah wa Ta’ala akawambia Nabii Musa kua:

َ ُ‫ﱠﺎس ﺑِ ِﺮ َﺳﺎﻻَﺗِﻰ َوﺑِ َﻜﻼَِﻣﻰ ﻓَ ُﺨ ْﺬ َﻣﺂ آﺗَـْﻴـﺘ‬


‫ﻚ‬ ِ ‫ﻚ َﻋﻠَﻰ ٱﻟﻨ‬ ْ ‫ﻮﺳ ٰﻰ إِِّﱏ‬
َ ُ‫ٱﺻﻄََﻔْﻴـﺘ‬ َ َ‫﴿ﻗ‬
َ ُ‫ﺎل ٰﳝ‬
﴾‫وُﻛ ْﻦ ِّﻣﻦ ٱﻟﺸﱠﺎﻛِ ِﺮﻳﻦ‬
َ َ َ
Qala ya moosa innee istafaytuka AAala alnnasi birisalatee wabikalamee fakhudh
ma ataytuka wakun mina alshshakireena (Surat Al Araf 7:144)

Tafsir: Akasema (Allah Subhanah wa Ta’ala): ‘Ewe Musa! Hakika mimi


nimekuchagua wewe juu ya watu wengine kwa Ujumbe wangu na kwa Kauli yangu,
hivyo chukua nitakachokupa na kua ni miongoni mwa wenye kushukuru’.

Anasema Imam Muhammad Ibn Saib Al Kalbi kua; ‘Nabii Musa alipoteza faham
katika siku ya Alkhamis ambayo ilikua ni siku ya Arafah na akapewa Tawrat katika
siku ya Ijumaa ambayo ni siku ya kuchinja.’

Na anasema Imam Ahmad Ibn Muhammad Ath Thalabi kua: ‘Kabla ya Allah Subhanah
wa Ta’ala kujitokeza mbele ya Mlima basi Mlima huo likua Umesimama sawia
Mgumu na wenye Mawe na ulionyooka, lakini Allah Subhanah wa Ta’ala
alipojitokeza kwenye Mlima huo basi Mlima huo ukaanguka na kua Ardhi iliyo
tambarare huku Milima myengine yote iliyokua karibu yake ikawa ni yeye kua na
mapango ndani yake.

Kisha baada ya hapo Allah Subhanah wa Ta’ala akamtuma Malaika Jibril aende
Peponi akakate Mti ambao kutokana nao akatoa vipande 9 vya mbao vyenye urefu
787

na upana wake ni dhiraa 10 kama ilivyokua urefu wa mikono ya Nabii Musa. Na


kisha akamumarisha Malaika Jibril amletee Maatawi 9 yenye Majani kutoka
katika Mti wa Peponi kisha akayakusanya pamoja na ya kawa ni Miangaza ya Nuru
ambayo ikawa kalamu yeye urefu kutoka Mbinguni mpaka Duniani. Na kisha Allah
Subhanah wa Ta’ala akamuandikia Nabii Musa Tawrat kiasi ya kua Nabii Musa
kwa ni mwenye kusikia sauti ya Muandiko wa Kalamu hio kwenye Mbao hizo. Hii
ilikua ni siku ya Ijumaa.’

Allah Subhanah wa Ta’ala analielezea tukio hili katika Qur’an pale aliposema:

ٍ‫ﺼﻴﻼً ﻟِّ ُﻜ ِﻞ َﺷﻲ ٍء ﻓَﺨ ْﺬﻫﺎ ﺑُِﻘ ﱠﻮة‬ِ ‫﴿وَﻛﺘَـﺒـﻨَﺎ ﻟَﻪ ِﰱ ٱﻷَﻟْﻮ ِاح ِﻣﻦ ُﻛ ِﻞ َﺷﻲ ٍء ﱠﻣﻮﻋِﻈَﺔً وﺗَـ ْﻔ‬
َ ُ ْ ّ َ ْ ْ ّ َ ُ ْ َ
﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ ‫ﻚ �ْﺧ ُﺬواْ ِﺄﺑ‬
َ ‫َﺣ َﺴﻨ َﻬﺎ َﺳﺄ ُْوِرﻳ ُﻜ ْﻢ َد َار ٱﻟْ َﻔﺎﺳﻘ‬
ْ ُ َ َ ‫َوأْ ُﻣْﺮ ﻗَـ ْﻮَﻣ‬
Wakatabna lahu fee al-alwahi min kulli shay-in mawAAidhatan watafseelan likulli
shay-in fakhudhha biquwwatin wa/mur qawmaka ya/khudhoo bi-ahsaniha
saoreekum dara alfasiqeena(Surat Al Araf 7:145)

Tafsir: Na tukamuandikia kwa ajili yake kwenye Ubao na kuelezea kila kitu na
tukamwambia: Shikamana nazo na waamrishe watu wako wachukue katika mema
yaliyomo ndani yake, nami nitakuonesha makazi ya Waovu.

Baada ya Allah Subhanah wa Ta’ala kumuandikia Nabii Musa Tawrat basi akamwambia
Malaika Jibril ashuke nayo ili akamkabidhi Nabii Musa maandiko hayo na kisha
amuambie Nabii Musa kua ashikamane nayo yeye na Watu wake, lakini Malaika Jibril
alipojaribu kuyabeba maandiko hayo basi alishindwa kuyanyanyua maandiko hayo
kutokana na uzito wa yaliyomo ndani yake, Malaika Jibril akasema : ‘Ya Allah ni nani
atakaeweza kuyabeba maandiko haya kutokana na Nuru yake na uzito wa kimaana
wa maneno yake?’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akawapa kazi Malaika wake kila mmoja abebe herufi
moja ya maandiko hayo wampelekee Nabii Musa. Malaika hao wakabeba Maandiko hayo
na walipofika mbele ya Nabii Musa wakamuonesha Nabii Musa maandiko hayo, ambapo
pembeni yake kulikua na Mlima ambao Ulitetemeka na kupasuka baada ya kuyaona
maandiko hayo, na kusema : ‘Ya Allah ni nani atakaeweza kustahmili uzito wa
kimaana wa maneno yake?’ na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akasema pia
kuhusiana na Qur’an kua:
788

ِ‫ﺎﺷﻌﺎً ﱡﻣﺘﺼ ِّﺪﻋﺎً ِﻣﻦ ﺧ ْﺸﻴ ِﺔ ﱠ‬


َ ‫ٱﻪﻠﻟ َوﺗِْﻠ‬
‫ﻚ‬ َ َ ّْ َ َ
ِ ‫﴿ﻟَﻮ أَﻧﺰﻟْﻨَﺎ ﻫـٰ َﺬا ٱﻟْ ُﻘﺮآ َن ﻋﻠَﻰ ﺟﺒ ٍﻞ ﻟﱠﺮأَﻳـﺘَﻪ ﺧ‬
َ ُ ْ َ ََ ٰ َ ْ َ َ ْ
ُ ْ ِ ‫ﻀ ِﺮﺑـُ َﻬﺎ ﻟِﻠﻨ‬
﴾‫ﱠﺎس ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻬﻢ ﻳَـﺘَـ َﻔ ﱠﻜﺮو َن‬ ْ َ‫ﺎل ﻧ‬
ُ َ‫ٱﻷ َْﻣﺜ‬
Law anzalna hadha alqur-ana AAala jabalin laraaytahu khashiAAan
mutasaddiAAan min khashyati Allahi watilka al-amthalu nadhribuha lilnnasi
laAAallahum yatafakkaroona; (Surat Hashir 59:21)

Tafsir: Lau kama tungeishusha hii Qur’an kwenye Mlima, basi Mlima huo
ungebubujika kwa khofu kutokana na Khofu ya kumuogopa Allah. Na hii ndio mifano
tunayowapigia watu ili wapate kutafakkari.

MUNAJAT NABI MUSA: MITHILI YA TAWRAT NDANI YA QUR’AN.


Hivyo Nabii Musa akakabidhiwa maandiko hayo na kuambiwa kua ashikamane nayo
yeye na watu wake, lakini kila alipojaribu kubeba andiko moja tu kati ya maandiko hayo
basi alishindwa kuyabeba kutokana na uzito wake. Hivyo Nabii Musa akamuomba Allah
Subhanah wa Ta’ala amrahisishie Uzito wa maandiko hayo na kujaribu tena kuyabeba
lakini akashindwa pia, hivyo akamuomba tena Mola wake na kumuomba tena mpaka
akafanikwa kua ni mwenye kuweza kuyabeba maandiko hayo.

Ambapo wanasema Wanazuoni kua mithili ya maandiko yaliyomo ndani ya Tawrat basi
ni kama vile alivyoambiwa Rasul Allahu Salallahu A’layhi wa Salam kwenye Qur’an
katika aya zifuatazo:

َ‫﴿ﻗُ ْﻞ ﺗَـ َﻌﺎﻟَ ْﻮاْ أَﺗْ ُﻞ َﻣﺎ َﺣﱠﺮَم َرﺑﱡ ُﻜ ْﻢ َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ أَﻻﱠ ﺗُ ْﺸ ِﺮُﻛﻮاْ ﺑِِﻪ َﺷْﻴﺌﺎً َوﺑِﭑﻟْ َﻮاﻟِ َﺪﻳْ ِﻦ إِ ْﺣ َﺴﺎ�ً َوﻻ‬
‫ﺶ َﻣﺎ ﻇَ َﻬَﺮ ِﻣْﻨـ َﻬﺎ‬ ِ ‫ٍ ﱠ‬ ِ ۤ
َ ‫ﺗَـ ْﻘﺘُـﻠُﻮاْ أ َْوﻻَ َد ُﻛ ْﻢ ّﻣ ْﻦ ْإﻣﻼَق ْﳓ ُﻦ ﻧَـْﺮُزﻗُ ُﻜ ْﻢ َوإِ ﱠ� ُﻫ ْﻢ َوﻻَ ﺗَـ ْﻘَﺮﺑُﻮاْ ٱﻟْ َﻔ َﻮاﺣ‬
‫ﺻﺎ ُﻛ ْﻢ ﺑِِﻪ ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜ ْﻢ‬ ‫ﭑﳊَِّﻖ ٰذﻟِ ُﻜ ْﻢ َو ﱠ‬ ْ ِ‫ٱﻪﻠﻟُ إِﻻﱠ ﺑ‬
‫ﺲ ٱﻟﱠِﱴ َﺣﱠﺮَم ﱠ‬ َ ‫َوَﻣﺎ ﺑَﻄَ َﻦ َوﻻَ ﺗَـ ْﻘﺘُـﻠُﻮاْ ٱﻟﻨﱠـ ْﻔ‬
ِ ِ َ ‫ﺗَـﻌ ِﻘﻠُﻮ َن۞وﻻَ ﺗَـ ْﻘﺮﺑﻮاْ ﻣ‬
‫َﺷ ﱠﺪﻩُ َوأ َْوﻓُﻮاْ ٱﻟْ َﻜْﻴ َﻞ‬ ْ ‫ﺎل ٱﻟْﻴَﺘﻴ ِﻢ إِﻻﱠ ﺑِﭑﻟﱠِﱴ ﻫ َﻰ أ‬
ُ ‫َﺣ َﺴ ُﻦ َﺣ ﱠ ٰﱴ ﻳـَْﺒـﻠُ َﻎ أ‬ َ َُ َ ْ
789

‫ﭑﻋ ِﺪﻟُﻮاْ َوﻟَْﻮ َﻛﺎ َن ذَا ﻗُـْﺮَ ٰﰉ‬


ْ َ‫ﻒ ﻧَـ ْﻔﺴﺎً إِﻻﱠ ُو ْﺳ َﻌ َﻬﺎ َوإِ َذا ﻗُـ ْﻠﺘُ ْﻢ ﻓ‬
ِ ِ ِ ِ
ُ ّ‫َوٱﻟْﻤ َﻴﺰا َن ﺑِﭑﻟْﻘ ْﺴﻂ ﻻَ ﻧُ َﻜﻠ‬
ً‫اﻃﻰ ُﻣ ْﺴﺘَ ِﻘﻴﻤﺎ‬ ِ ‫ﺻﺎ ُﻛﻢ ﺑِِﻪ ﻟَﻌﻠﱠ ُﻜﻢ ﺗَ َﺬ ﱠﻛﺮو َن۞وأَ ﱠن ﻫـٰ َﺬا ِﺻﺮ‬
َ َ َ ُ ْ َ ْ َ ْ ‫ﱠ‬ ‫و‬ ‫ﻢ‬ ‫ﻜ‬ُ ِ‫ٱﻪﻠﻟِ أَوﻓُﻮاْ ٰذﻟ‬
ْ ‫ﱠ‬ ِ ‫وﺑِﻌﻬ‬
‫ﺪ‬ َْ َ
﴾‫ﺻﺎ ُﻛﻢ ﺑِِﻪ ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜﻢ ﺗَـﺘﱠـ ُﻘﻮ َن‬ ِ ِِ ِ ِ ِ ِ
ْ ْ ‫ﻓَﭑﺗﱠﺒﻌُﻮﻩُ َوﻻَ ﺗَـﺘﱠﺒﻌُﻮاْ ٱﻟ ﱡﺴﺒُ َﻞ ﻓَـﺘَـ َﻔﱠﺮ َق ﺑ ُﻜ ْﻢ َﻋﻦ َﺳﺒﻴﻠﻪ ٰذﻟ ُﻜ ْﻢ َو ﱠ‬
Qul taAAalaw atlu ma harrama rabbukum AAalaykum alla tushrikoo bihi shay-an
wabialwalidayni ihsanan wala taqtuloo awladakum min imlaqin nahnu
narzuqukum wa-iyyahum wala taqraboo alfawahisha ma dhahara minha wama
batana wala taqtuloo alnnafsa allatee harrama Allahu illa bialhaqqi dhalikum
wassakum bihi laAAallakum taAAqiloona;Wala taqraboo mala alyateemi illa
biallatee hiya ahsanu hatta yablugha ashuddahu waawfoo alkayla waalmeezana
bialqisti la nukallifu nafsan illa wusAAaha wa-idha qultum faiAAdiloo walaw
kana dha qurba wabiAAahdi Allahi awfoo dhalikum wassakum bihi laAAallakum
tadhakkaroona; Waanna hadha siratee mustaqeeman faittabiAAoohu wala
tattabiAAoo alssubula fatafarraqa bikum AAan sabeelihi dhalikum wassakum bihi
laAAallakum tattaqoona. (Surat Al Anaam 6:151-153)

Tafsir: Sema (Ewe Muhammad): ‘Njooni nitakusomeeni alichokiharamisha juu yenu


Mola wenu, Msimshirikishe nae na kitu chochote, Wafanyieni wema na kuwatii Wazee
wenu, Msiwaue watoto wenu kwa kuogopa kuangukia kwenye Umasikini, Kwani sisi
tunakuruzukuni nyinyi na wao. Na msiyakaribie Madhambi iwe kwa dhahiri au kwa
siri na Msiue Nafsi yeyote ile aliyoiharamisha Allah isipokua kwa haki (kutokana na
Sharia za Kiislam). Haya mmeamrishwa ili mpate kufahamu; Na wala msiikarbie mali
ya yatima isipokua kwa wema. Mpaka atakapofikia umri wa baleghe, na timizeni
Mizani kwa Uadilifu. Hatuikalifishi Nafsi isipokua juu ya kile inachokiweza. Na
Mtakaposema kuweni na Uadilifu (Katika kuahidi kwenu na katika kutoa Hukmu)
hata kama kwa (anaehusika) ni jamaa wa karibu. Na timizeni Miadi ya Allah (katika
kumtii kwake). Hayo ni maamrisho yake ili mpate kukumbuka. Na kwa hakika hii ndio
njia yangu iliyonyooka, hivyo ifuateni na msifuate njia nyengine, kwani
zitakupotosheni kutokana na njia yake. Haya amekuamrisheni ili mpate kua ni wenye
Taqwa.’

Hivyo hizi ni miongoni mwa ya aya zilizomo ndani ya kitabu cha Nabii Musa yaani
Tawrat ambazo pia maamrisho yake yametiliwa mkazo ndani ya Qur’an na bila ya shaka
tunapoiangalia Qur’an basi tunaona kua miongoni mwa Aya zinazungumzia uzito wa
haki za wazee wetu juu yetu kiasi ya kua tunaona kua mara kadha Allah Subhanah wa
Ta’ala anapozungumzia kuhusiana na Haki zake basi hua ni mwenye kuzidai sambamba
na Haki za Wazee wetu na hii ni kwa sababu Wazee wetu ndio sababu ya kuzaliwa
790

kwetu na ni kutokana na jitihada zao juu yetu katika kutulea basi ndio kunapatikana
ukuaji wa maumbile ya miili yetu.

Ndani ya aya hizi Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea pia umuhimu wa kutokua na
khofu ya maisha na upatikanaji wa riziki yake kwani yeye ndio mtoaji wa riziki ya kila
kiumbe wake na hivyo ikatumia neno Imlaq ambalo limetokana na neno Malaqa lenye
kumaanisha Kufuta, Kusafisha, Kuanguka Chini, Kuingia kwenye Umasikini au
Kufilisika.

Ambapo aliulizwa Rasul Allah Salllahu Alayhi wa Salam: ‘Jee ni dhambi ipi kubwa
kuliko zote?’ ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Ni
kumshirikisha Allah Subhana wa Ta’ala wakati yeye ndie ambae aliekuumba’
kishaakaulizwa tena Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam: ‘Kisha baada ya hio?’
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Kumuua Mtoto wako kwa khofu
ya kua atachukua sehemu ya riziki yako.’ Akaulizwa tena : ‘Kisha baada ya hio?’
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam : ‘Kuzini na Mke wa Jirani yako.’(Sahih
Muslim)

Ndani yake aya hizi pia zimezungumzia kuhusiana na kuzidhibiti Nafsi na matamanio
yake kwa kutoyakaribia mambo yanayosababisha kupeleka kufanya maasi ambapo
amesema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu, Imam Ad Dahhaq Ibn Muzahim
wanasema kuhusiana na aya hii kua: ‘Ilikua ni kawaida ya Mapagani kua walikua
wakifanya Zina kwa siri, huku wakiwa na mtizamo wa kua Kuzini kuliko katazwa
ni kuzini hadharani’

Na akasema Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu kua amesema Rasul Allah Salllahu
Alayhi wa Salam kua: ‘Hakuna mwenye hisia kubwa za heshima kuliko Allah
Subhanah wa Ta’ala, kwa hivyo amekataza aina zote za kuvunjiana heshima iwe
hadharani au kwa faragha’

Ambapo kuhusiana na damu isiyoruhusika kumwagwa kisharia basi ni kama alivyosema:


Rasul Allah Salllahu Alayhi wa Salam kua: ‘Damu ya Muislam aliethibtisha kua
hakuna Mola anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokua Allah Subhnaha wa Ta’ala
na kua mimi ni Mtume wake hua ni haram kuimwaga isipokua katika mambo
matatu: ‘Uhai kwa Uhai, Mzinifu alieoa na Alietoka katika Uislam’

Ambapo kwa upande mwengine basi Maamrisho hayo aliyopewa Nabii Musa
yamefafanuliwa kwa kina zaidi pia katika aya zifuatazo:
791

ٍ ‫ﻶﺧﺮةُ أَ ْﻛﺒـﺮ درﺟ‬ ِ


‫ﺎت َوأَ ْﻛﺒَـُﺮ‬ َ َ َ ُ َ َ َ‫ﺾ َوﻟ‬ ٍ ‫ﻀ ُﻬ ْﻢ َﻋﻠَ ٰﻰ ﺑَـ ْﻌ‬ َ ‫ﻀ ْﻠﻨَﺎ ﺑَـ ْﻌ‬
‫ﻒ ﻓَ ﱠ‬ َ ‫﴿ٱﻧﻈُْﺮ َﻛْﻴ‬
ِ‫ﻀﻴﻼً۞ﻻﱠ َﲡﻌﻞ ﻣﻊ ﱠ‬ ِ ‫ﺗَـ ْﻔ‬
‫ﻚ أَﻻﱠ‬ َ ‫ﻀ ٰﻰ َرﺑﱡ‬ َ َ‫آﺧَﺮ ﻓَـﺘَـ ْﻘﻌُ َﺪ َﻣ ْﺬ ُﻣﻮﻣﺎً ﱠﳐْ ُﺬوﻻً۞ َوﻗ‬َ ً‫ٱﻪﻠﻟ إِﻟَـٰﻬﺎ‬ َ َ َْ
ۤ
َ ‫ﺗَـ ْﻌﺒُ ُﺪواْ إِﻻﱠ إِ ﱠ�ﻩُ َوﺑِﭑﻟْ َﻮاﻟِ َﺪﻳْ ِﻦ إِ ْﺣ َﺴﺎ�ً إِ ﱠﻣﺎ ﻳَـْﺒـﻠُﻐَ ﱠﻦ ِﻋ‬
‫ﻨﺪ َك ٱﻟْ ِﻜﺒَـَﺮ أَ َﺣ ُﺪ ُﳘَﺎ أ َْو ﻛِﻼَ ُﳘَﺎ‬
‫ﺎح ٱﻟ ﱡﺬ ِّل‬ ِ ‫ُف وﻻَ ﺗَـْﻨـﻬﺮُﳘﺎ وﻗُﻞ ﱠﳍﻤﺎ ﻗَـﻮﻻً َﻛ ِﺮﳝﺎً۞و‬ ٍ
َ َ‫ﺾ َﳍَُﻤﺎ َﺟﻨ‬ ْ ‫ٱﺧﻔ‬ ْ َ ْ َُ َ َ ْ َ َ ّ ‫ﻓَﻼَ ﺗَـ ُﻘﻞ ﱠﳍَُﻤﺂ أ‬
‫ﻮﺳ ُﻜ ْﻢ إِن‬ ِ ‫ب ٱر َﲪﻬﻤﺎ َﻛﻤﺎ رﺑـﱠﻴ ِﺎﱏ ﺻﻐِﲑاً۞ ﱠرﺑﱡ ُﻜﻢ أَ ْﻋﻠَﻢ ِﲟَﺎ ِﰱ ﻧـُ ُﻔ‬ ِ ِ ِ
ُ ْ َ َ َ َ َ ُ ْ ْ ّ ‫ﻣ َﻦ ٱﻟﱠﺮ ْﲪَﺔ َوﻗُﻞ ﱠر‬
ِ ِِ ْ‫ﺗَ ُﻜﻮﻧُﻮا‬
﴾ً‫ﲔ َﻏ ُﻔﻮرا‬ َ ِ‫ﲔ ﻓَِﺈﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن ﻟﻸَﱠواﺑ‬ َ ‫ﺻﺎﳊ‬ َ
Ondhur kayfa fadhdhalna baAAdhahum AAala baAAdhin walal-akhiratu akbaru
darajatin waakbaru tafdheelan; La tajAAal maAAa Allahi ilahan akhara
fataqAAuda madhmooman makhdhoolan; Waqada rabbuka alla taAAbudoo illa
iyyahu wabialwalidayni ihsanan imma yablughanna AAindaka alkibara
ahaduhuma aw kilahuma fala taqul lahuma offin wala tanharhuma waqul lahuma
qawlan kareeman; Waikhfidh lahuma janaha aldhdhulli mina alrrahmati waqul
rabbi irhamhuma kama rabbayanee sagheeran; Rabbukum aAAlamu bima fee
nufoosikum in takoonoo saliheena fa-innahu kana lil-awwabeena ghafooran; (Surat
Al Isra 17:21-25)

Tafsir: Angalia namna tulivyowafadhili baadhi yao juu ya baadhi ya wengine na kwa
hakika Akhera kuna darja kubwa zaid na kuna fadhila kubwa zaidi. Na usijaalie
pamoja na Allah Mungu mwengine au utajikuta ukiwa umekaa chini huku
ukikosolewa na ukiwa umeachwa peke yako. Na Mola wako anataka Usimuabudu
Mungu yeyote isipokua yeye, na uwafayie wema wazazi wako, na ikiwa mmoja wao
atafikia umri wa Uzee katika uhai wako basi usiwaambie hata Uff! Na usiwakaripie
bali zungumza nao kwa heshima. Na washushie kwa ajili yao Mbawa ya Unyenyekevu
wenye Rehma na sema : ‘Mola wangu Waingize katika Rehema zako kama
walivyonilea mimi nilipokua Mdogo.’ Mola wako anajua zaidi juu ya kile kilichomo
ndani ya Nafsi yako. Hivyo kama utakua ni Mtu mwema basi kwa hakika yeye ni
mwingi wa Usamehevu kwa wale wenye kurudi kwake.

Kama tulivyoona katika aya zilizotangulia basi hapa katika aya hizi pia Allah Subhanah
wa Ta’ala anatilia tena mkazo umuhimu wa kuwapa haki zao wazee. Kuwahurumia na
kutowakemea hata kwa kuwaambia akh! Na katika kutilia mkazo hilo basi aya zimesema:
Waikhfidh lahuma janaha aldhdhulli mina alrrahmati waqul rabbi irhamhuma kama
792

rabbayanee sagheeran yaani Na washushie kwa ajili yao Mbawa ya Unyenyekevu


wenye Rehma na sema: ‘Mola wangu Waingize katika Rehema zako kama
walivyonilea mimi nilipokua Mdogo.’

Ambapo ayah hii imetumia maneno Waikhfidh lahuma janaha ambao ni msemo
unaomaanisha Kumuinamishia Mtu bega, au Ubawa kama wa Ndege kwa yaani kwa
kumpa kumjali na kumpa mtu msaada huku ukiwa na Huruma, Mapenzi na
Unyenyekevu, kama vile ambavyo Ndege anavyowatandazia mabawa yake vifaranga
vyake kwa ajili ya kuwahudumia kwa kuwahifadhi wasidhurike kwa sababu ya kua
hawana uwezo wa kujihudumia wao wenyewe.

Na ili tufaham kwa vizuri zaidi basi na tuangalie mfano wa aya zifuatazo ambazo Allah
Subhanah wa Ta’ala alikua anamuusia na kumfundisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
Salam anavyotakiwa awe kwa wale watakao Muamini yeye na Allah Subhanah wa Ta’ala
kama alivyosema:

‫ﺾ‬ ِ ‫﴿ﻻَ َﲤُﱠﺪ ﱠن ﻋﻴـﻨـﻴﻚ إِ َ ٰﱃ ﻣﺎ ﻣﺘـﱠﻌﻨﺎ ﺑِِﻪ أَزواﺟﺎً ِﻣْﻨـﻬﻢ وﻻَ َﲢﺰ ْن ﻋﻠَﻴ ِﻬﻢ و‬
ْ ‫ٱﺧﻔ‬
ْ َ ْ ْ َ َْ َ ْ ُ ّ َ ْ َ ْ َ َ َ ْ َ َْ
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ِ َ ‫ﺟﻨَﺎﺣ‬
َ ‫ﻚ ﻟ ْﻠ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬ َ َ
La tamuddanna AAaynayka ila ma mattaAAna bihi azwajan minhum wala tahzan
AAalayhim waikhfidh janahaka lilmu/mineena(Surat Al Hijr 15:88)

Tafsir: Usidumishe Macho yake katika kila ambacho wamepewa baadhi ya watu
miongoni mwao wala usihuzunike juu yao, na yainamishe mabawa yako kwa ajili ya
Waumini.

Yaani Rasul Allah Salallahu Allahu Alayhi wa Salam anaambiwa kua asijali Mali na
Utajiri waliopewa Makafiri kwani alichopewa yeye ambacho ni Qur’an ni bora zaidi,
hivyo anachohitajiwa yeye kukifanya si chochote isipokua kua na Huruma na
Wanaomuamini. Kwani waliyopewa watu hao ni mapambo ya kidunia wakati
wanayoyakimbilia wanaomuamini Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hua ni kwa
ajili ya Mola wao na Akhera yao.

Na akasema tena Allah Subhanah wa Ta’ala katika aya ifuatayo kua:

﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ َ ‫ﻚ ﻟِﻤ ِﻦ ٱﺗﱠـﺒـﻌ‬ ِ ‫﴿و‬


َ ‫ﻚ ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬ َ َ َ َ ‫ﺎﺣ‬ َ َ‫ﺾ َﺟﻨ‬
ْ ‫ٱﺧﻔ‬
ْ َ
793

Waikhfidh janahaka limani ittabaAAaka mina almu/mineena(Surat Ash Shuara


26:215)

Tafsir: Na wainamishie Mabawa yako wanaokufuata miongoni mwa Waumini.

Kisha baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua ni mwenye sifa hio ya Kua
ni mwenye Kuwashushia Bega lake Waumini basi Allah Subhanah wa Ta’ala ndio
anatubainishia na kutufafanulia maana ya sifa hio ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
Salam juu yetu kwa kusema:

ِِ ِ ِ ِ ِ ٌ ‫﴿ﻟََﻘ ْﺪ ﺟﺂء ُﻛﻢ رﺳ‬


َ ‫ﻳﺺ َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ ﺑِﭑﻟْ ُﻤ ْﺆﻣﻨ‬
‫ﲔ‬ ٌ ‫ﻮل ّﻣ ْﻦ أَﻧ ُﻔﺴ ُﻜ ْﻢ َﻋ ِﺰ ٌﻳﺰ َﻋﻠَْﻴﻪ َﻣﺎ َﻋﻨﺘ ْﱡﻢ َﺣ ِﺮ‬ َُ ْ َ َ
﴾‫وف ﱠرِﺣﻴﻢ‬
ٌ ٌ ُ‫َرء‬
Laqad jaakum rasoolun min anfusikum AAazeezun AAalayhi ma AAanittum
hareesun AAalaykum bialmu/mineena raoofun raheemun (Surat At Tawba 9:128)

Tafsir: Kwa hakika amekuja Mtume kutokana nanyi ambae inamuuma na


kumhuzunisha juu yake kutokana na kitakachozidishieni Uzito, na yeye ana ari juu
yenu (katika kukusimamieni ili mpate uongofu, msamehewe makosa yenu mpate
kuingia Peponi na mpate kuoka na adhabu ya Moto) kwani (yeye Muhammad
Salallahu Alyahi wa Salam) kwa Waumini ni mwingi wa Huruma na Rehma.

Ambapo anasema Al Hafidh Imam Abu Jafar Muhammad Ibn Jarir At Tabari kuhusiana
na ayah hii na hadhith hii kua: ‘Umar Radhi Allahu Anhu alikua hakubalia kua aya
ya Qur’an iandikwe ndani ya msahafu bila ya kuwepo kwa mashahidi wawili
kuhusiana na aya hio. Lakini kuhusiana na ayah hii basi hakuhitaji shahidi yeyote
kwani Rasul Aallah Salallahu Alayhi wa Salam alikua ni kama alivyoelezewa
kwenye ayah ii.’

Anasema Bahr Ul Ilm Abd Alah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Kuna watu wawili
walikuja Usingizini katika ndoto ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambapo
mmoja alisimama katika upande wa miguu yake na mwengine akasimama kwenye
upande wa Kichwa chake, kisha yule aliesimama miguuni akasema: ‘Mfano wa yule
ambae yeye na wafuasi wake hua ni kama watu ambao wamesafiri na kukaribia
kufika katika malengo yao, lakini wakawa hana mahitaji ya kutosha kumalizia
safari yo iliyobakia, na hivyo wakawa pia hawawezi kurudi walipotokea. Watu hao
walikaa katika hali hio mpaka pale alipotokea mtu aliekua amevaa Joho la Hariri
na kusema: ‘Jee mtanifuata mie kama nikikupelekeni kwenye Bustani iliyonawiri
794

na yenye Chemchem za Maji ndani yake’ nao watu hao wakasema: ‘Naam’ hivyo
mtu huyo akawachukua watu hao na kuwapeleka kwenye Bustani hio, kiasi ya kua
walipofika wakala mpaka wakashiba na kunenepa.’

Kisha akaja tena mtu huyo na kuwaambia watu hao: ‘Jee ni kweli kua mimi
sikukuteni nyie katika hali ile kisha mkaniahidi kua mtanifuata nami nikakuleteni
hapa kwenye Bustani iliyonawiri na mito ndani yake?’ watu hao wakasema: ‘Naam
ni kweli’ Hivyo Mtu huyo akasema: ‘Basi kuna Bustani Nyengine nzuri zaidi ya hiii
hivyo nifutaeni’ hivyo baadhi ya watu katika kundi hilo wakasema kua: ‘Hakika
huyu amesema Ukweli hivyo kwa ajili ya Allah basi sisi tutamfuata’ na baadhi
wakasema: ‘Hakika sisi tumeridhika na tulichokipata na hivyo tutabakia hapa
hapa.’’

Ama kuhusiana na umuhimu wa kua na kuwafanyia wema, kua na ustahmilivu, ukarimu


na upendo kwa Wazazi wawili basi anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahi Anhu
kua: ‘Mimi nilimuuliza Rasul Allah Salallahu Alyahi wa Salam, Ya Rasu Allah! Jee
ni lipi jambo bora Zaidi mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala?’ Rasul Allah Salallahu
Alyahi wa Salam akasema kua: ‘Kusali katika Nyakati zake’ Nami nikamuuliza
tena: ‘Kisha baada ya Hilo?’ nae akajibu: ‘Kuwafanyia wema Wazazi wawili’ nami
nikauliza tena: ‘Kisha baada ya hilo?’ nae akajibu: ‘Kupigana kwa ajili ya Allah
Subhanah wa Ta’ala.’

Hivyo basi kuwafanyia wema Wazazi wawili kumeamrishwa ndani ya Tawrat na pia
nadni ya Quran, yaani hata kama wazazi hao watakua si Waislam, na hii pia ni kutokana
na amrisho liliomo katika aya ifuatayo;

‫ﻳﻦ َﱂْ ﻳـُ َﻘﺎﺗِﻠُﻮُﻛ ْﻢ ِﰱ ٱﻟ ِّﺪﻳ ِﻦ َوَﱂْ ُﳜْ ِﺮ ُﺟﻮُﻛ ْﻢ ِّﻣﻦ ِد َ� ِرُﻛ ْﻢ أَن‬ ِ‫ﱠ‬ ‫﴿ﻻﱠ ﻳَـْﻨـ َﻬﺎ ُﻛ ُﻢ ﱠ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻋ ِﻦ ٱﻟﺬ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ ‫ﺐ ٱﻟْﻤ ْﻘ ِﺴ‬
‫ﻄ‬ ‫ﳛ‬ُِ ‫ٱﻪﻠﻟ‬
‫ﱠ‬ ‫ﱠ‬
‫ن‬ ِ‫إ‬ ‫ﻢ‬ ِ
‫ﻬ‬ ‫ﻴ‬َ‫ﻟ‬ ِ‫إ‬ ‫ا‬
ْ ‫ﻮ‬ۤ ُ‫ﺗـﺒـﺮوﻫﻢ وﺗـﻘ ِﺴﻄ‬
َ ُ ‫ﱡ‬ َ ْ ْ ْ ُ َ ْ ُ ‫ََ ﱡ‬
La yanhakumu Allahu AAani alladheena lam yuqatilookum fee alddeeni walam
yukhrijookum min diyarikum an tabarroohum watuqsitoo ilayhim inna Allaha
yuhibbu almuqsiteena (Surat Al Muntahina 60:8)

Tafsir: Allah hakukatazeni nyie juu ya wale ambao hawakukupigeni vita katika Dini
yenu wala hawakukufukuzeni kutoka katika majumba, yenu kuwafanyia Uadilifu
kwani kwa hakika Allah anawapenda wenye kufanya Uadilifu.

Ambapo miongoni mwa mifano ya kuwashushia bawa la huruma wazee wawili ni ule
unaopatikana katika hadith ya Hudhayfah Radhi Allahu Anhu ambae aliomba ruhusa kwa
795

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ya kupigana na baba yake vitani ili amuue lakini
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salama akamwambia Hudhayfah Radhi Allahu Anhu
kua: ‘Wacha mtu mwengine amuue badala yako.’

Na mfano mwengine ni ule wa Imam Abu Yusuf Al Hanafi ambae ni mwanafunzi wa


Imam Abu Hanifa ambae anasema kua: ‘Kama ikiwa Muislam ana Baba yake ambae
si Muislam, kisha baba huyo akamuomba Mtoto wake huyo amuwashie Moto ili
apike Nyama ya Nguruwe, basi Mtoto huyo humbidi kumuwashia Moto huo baba
yake huyo.’

Ama tunapozungumzia kuhusiana na Utiifu wa kuwashushia bawa la huruma Baba na


Mama basi anasema Al Muhaqiq Imam Ahmad Ibn Muhammad Ibn Hajar Al Makki Al
Haytam kua: ‘Kama ikiwa wazee wataudhika na jambo Fulani, basi ni wajibu wa
Mtoto kua ni mwenye kuachana na jambo hilo. Lakini hata hivyo kama
tunazungumzia kuhusiana na mmoja kati ya wazee kua ni mwenye, atamkataza
Mtoto wake Jambo au Kitu kutokana na kutokua na akili kwa mzee huyo, au
kutokua na uwezo wa kutofautisha baina ya Jema na Ovu, na kama jambo hilo
halitoonekana kua ni kutokua na utiifu kwa wazee katika utamaduni wa jamii, basi
Mtoto hawajibiki kutekelezea amri za Wazee wake na hatoweza kuhesabika kua ni
mwenye kufanya Dhambi.’

‘Kwa mfano: Kama ikiwa mtu anampenda Mke wake au Mume wake na hataki
kuachana nae lakini hapo hapo ikawa mmoja kati ya wazee wake anataka kua
mtoto huyo aachane na Mke au Mume huyo. Basi Mke au Mume halazimiki
kuanachana na mwenzake hata kama ikiwa kutakiwa kuachana kwao huko
kunatokana na mmoja kati yao kua na kasoro katika mambo ya dini’

Ama maamrisho mengine na makatazo ya Wazee hua pia na hali kama hio, yaani
kama ikiwa makatazo yao yanatokana na kutokua na akili timamu au kutokua ni
wenye kufaham jambo husika basi Mtoto hua hawajibiki kuwatii pale inapokua
mazingira ya jambo husika kua halihesabiki ni sehemu ya kuwadhalilisha Wazee
au kuwaumiza Wazee kulingana na mtizamo wa watu katika Jamii’(Al Zawjir al
Iqtarif Al Kabir.)

Kisha aya zenye maamrisho yaliyomo ndani ya Tawrat na Qur’an pia zinaendelea kwa
kusema:

ِِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ
َ ‫﴿ َوآت َذا ٱﻟْ ُﻘْﺮَ ٰﰉ َﺣ ﱠﻘﻪُ َوٱﻟْﻤ ْﺴﻜ‬
َ ‫ﲔ َوٱﺑْ َﻦ ٱﻟ ﱠﺴﺒ ِﻴﻞ َوﻻَ ﺗُـﺒَ ّﺬ ْر ﺗَـْﺒﺬﻳﺮاً۞إ ﱠن ٱﻟْ ُﻤﺒَ ّﺬر‬
‫ﻳﻦ‬
‫ﺂء‬ ‫ﻐ‬
َ ِ‫ﲔ وَﻛﺎ َن ٱﻟﺸﱠﻴﻄَﺎ ُن ﻟِﺮﺑِِﻪ َﻛ ُﻔﻮراً۞وإِ ﱠﻣﺎ ﺗُـﻌ ِﺮﺿ ﱠﻦ ﻋْﻨـﻬﻢ ٱﺑﺘ‬ ِ ‫ﺎﻃ‬ِ ‫َﻛﺎﻧـُ ۤﻮاْ إِﺧﻮا َن ٱﻟﺸﱠﻴ‬
َ ُ ْ ُ َ َ ْ َ ّ َ ْ َ َ َْ
796

ِ
َ ‫ﻮﻫﺎ ﻓَـ ُﻘﻞ ﱠﳍُْﻢ ﻗَـ ْﻮﻻً ﱠﻣْﻴ ُﺴﻮراً۞ َوﻻَ َْﲡ َﻌ ْﻞ ﻳَ َﺪ َك َﻣ ْﻐﻠُﻮﻟَﺔً إِ َ ٰﱃ ﻋُﻨُﻘ‬
‫ﻚ‬ َ ‫ﻚ ﺗَـْﺮ ُﺟ‬ َ ِّ‫َر ْﲪٍَﺔ ِّﻣﻦ ﱠرﺑ‬
ِ‫ٱﻟﺮز َق ﻟ‬
ُ َ َ ِّْ ‫ﻂ‬
‫ﺂء‬ ‫ﺸ‬
َ ‫ﻳ‬ ‫ﻦ‬‫ﻤ‬ ُ ‫ﻚ ﻳَـْﺒ ُﺴ‬َ ‫َوﻻَ ﺗَـْﺒ ُﺴﻄْ َﻬﺎ ُﻛ ﱠﻞ ٱﻟْﺒَ ْﺴ ِﻂ ﻓَـﺘَـ ْﻘﻌُ َﺪ َﻣﻠُﻮﻣﺎً ﱠْﳏ ُﺴﻮراً۞إِ ﱠن َرﺑﱠ‬
ٍ ‫ﺼﲑاً۞وﻻَ ﺗَـ ْﻘﺘُـﻠُ ۤﻮاْ أَوﻻ َد ُﻛﻢ ﺧ ْﺸﻴﺔَ إِﻣ‬
‫ﻼق ﱠْﳓ ُﻦ‬ ِ ‫وﻳـ ْﻘ ِﺪر إِﻧﱠﻪ َﻛﺎ َن ﺑِﻌِﺒ ِﺎدﻩِ ﺧﺒِﲑاً ﺑ‬
ْ َ َ ْ ْ َ َ َ َ ُ ُ ََ
﴾ً‫ﻧَـﺮُزﻗُـ ُﻬﻢ وإِ ﱠ� ُﻛﻢ إ ﱠن ﻗَـْﺘـﻠَ ُﻬﻢ َﻛﺎ َن ِﺧﻄْﺌﺎً َﻛﺒِﲑا‬
ْ َْ ْ
Waati dha alqurba haqqahu waalmiskeena waibna alssabeeli wala tubadhdhir
tabdheeran; Inna almubadhdhireena kanoo ikhwana alshshayateeni wakana
alshshaytanu lirabbihi kafooran; Wa-imma tuAAridhanna AAanhumu ibtighaa
rahmatin min rabbika tarjooha faqul lahum qawlan maysooran; Wala tajAAal
yadaka maghloolatan ila AAunuqika wala tabsutha kulla albasti fataqAAuda
malooman mahsooran; Inna rabbaka yabsutu alrrizqa liman yashao wayaqdiru
innahu kana biAAibadihi khabeeran baseeran; Wala taqtuloo awladakum
khashyata imlaqin nahnu narzuquhum wa-iyyakum inna qatlahum kana khit-an
kabeeran; (Surat Al Isra 17:26-31)

Tafsir: Na mpe (mtu) wa karibu yako haki yake na Masikini na Wasafiri. Na wala
usitumie ovyo (Mali yako) katika matumizi yako. Kwani wanaotumia ovyo ni ndugu
wa Shetani, na kwa hakika Shetani kwa Mola wake ni Muasi. Na kama ukiwapa
mgongo (kutokana na kua huna cha kuwapa)huku ukiwa ni mwenye kutegemea
Rehma za Mola wako basi zungumza nao kwa ulaini. Na wala usiufanye mkono wako
ukawa ni wenye kufungwa kwenye shingo yako, na wala usiunyooshe sana na hivyo
ukawa ni mwenye kulaumiwa na mwenye ufukara. Kwa hakika Allah humtanulia
riziki amtakae na hum-bania amtakae, kwani kwa hakika yeye ni mwenye habari juu
ya kila kitu na ni mwenye kuona juu ya kila kitu. Na Msiwaue watoto wenu kwa
kuogopa ufukara, kwani sisi ndio tunao kuruzukuni nyie na wao, kwa Hakika kuwaua
wao ni dhambi kubwa sana.

Hapa tunaona kua Maamrisho ya aya hizi yanahusiana na namna ya kutumia Mali bila ya
kufanya Israfu, au kutumia Mali au neema ya Allah Subhanah wa Ta’ala kwa ajili ya
wakati sio na kwa ajili ya kitu sicho yaani kufanyia mambo siyo au kufanya sivyo,
ambapo ndani yake mnaingia mpaka namna ya kutia udhu kwani anasema Jarrah Allah
Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Amesema Abd Allah Ibn Umar kua, siku
moja Rasul Allahi Salallahu Alayhi wa Salam alipita akamuona Saad akiwa anatia
Udhu, hivyo Rasul Allah Salallahu Aalayhi w Salam akasema: ‘Kwanini Unafanya
Israfu ya Saad?’ ambapo Saad akauliza: ‘Kwani Jee kuna Israf mpaka kwenye
797

kutia Udhu?’’ Rasul Allahi Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Naam, hata kama
ikiwa unatia Udhu kwenye maji ya chemchem inayotiririka’

Ambapo kuhusianana na Watu wako wa karibu na masikini na wasafiri ambao ni watu


wanaostahiki kutumia kwa ajili yao basi anasema Asma Bint Abu Baqr Radhi Allahu Anhu
kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Tumia kwa njia hii na
ile, na usibakishe Allah Subhanah wa Ta’ala atabakisha kwa ajili yako pia, na wala
usihesabu au Allah Subhanah wa Ta’ala atahesabu kwa ajili yako’’(Sahih Muslim)

Na akasema tena Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Mfano wa Mtu Bakihili
na Mtu Mkarimu hua ni sawa na watu wawili tofauti ambao wamevaa nguo ya ngao
ya chuma inayomzuia kifuani mpaka shingoni, ambapo yule mwenye Ukarimu hua
hatumii chochote kile isipokua Nguo yake hio hua ni yenye kuongezeka kwenye
mwili wake mpaka ikafunika mwili wote na kuanza kuburura nyuma yake, ambapo
mfano wa Mtu Bakhili basi hua hana nia ya kutumia na hivyo nguo yake hhio
huanza kumbana huku kila akiivuta kuitanua basi haitanuki.’(Bukhari)

Hivyo inapotokea kua na uwezo wa kuwasaidia Ibn Adam wengine wanaostahiki basi hu
anatakiwa amshukuru Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kumjaalia uwezo huo wa kua
nacho cha kusaidia kwa kumsaidia mtu mwenye kustahiki kusaidiwa, bila ya kumsema
vibaya wala kumdai shukrani au malipo haop baadae kutokana na kumsaidia huko katika
wakati huo aliokua na shida.

Aya zimezungumzia tena kuhusiana na riziki na kutowaua watoto kwa kuuogopa umasikini
kwani yeye ndie mwenye kutoa riziki ambapo pia amesema Rasul Allah Salallahu A’layhi
wa Salam kua: ‘Amesema Allah Subhanah wa Ta’ala kua: ‘Kuna miongoni mwa Waja
wangu ambao hakuna kinachomfaa isipokua Umasikini, hivyo kama ikiwa nitataka
kumpa riziki basi itamuangamiza. Na kuna Miongoni mwa waja wangu hakuna
kinachomfaa isipokua kua na Uwezo, hivyo kama nikitaka kumtia Umasikini basi
utampelekea kuharibika kwa Dini yake.’’

Hivyo basi Allah Subhanah wa Ta’ala ni mwenye kutoa kwa Hikma zake. Aya hizo zenye
maamrisho yaliyomo ndani ya Tawrat na Qur’an pia zikamalizia kwa kusema:

‫ﺲ ٱﻟﱠِﱴ َﺣﱠﺮَم ﱠ‬ ِ ِ ِ َٰ ‫ٱﻟﺰ‬


ِّ ْ‫﴿ َوﻻَ ﺗَـ ْﻘﺮﺑُﻮا‬
ُ‫ٱﻪﻠﻟ‬ َ ً‫ﱏ إﻧﱠﻪُ َﻛﺎ َن ﻓَﺎﺣ َﺸﺔً َو َﺳﺂءَ َﺳﺒﻴﻼ‬
َ ‫۞وﻻَ ﺗَـ ْﻘﺘُـﻠُﻮاْ ٱﻟﻨﱠـ ْﻔ‬ َ
ِِِ ِ
ُ‫إِﻻﱠ ﺑِﭑﳊَِّﻖ َوَﻣﻦ ﻗُﺘ َﻞ َﻣﻈْﻠُﻮﻣﺎً ﻓَـ َﻘ ْﺪ َﺟ َﻌ ْﻠﻨَﺎ ﻟ َﻮﻟﻴِّﻪ ُﺳ ْﻠﻄَﺎ�ً ﻓَﻼَ ﻳُ ْﺴ ِﺮف ِﰱ ٱﻟْ َﻘْﺘ ِﻞ إِﻧﱠﻪ‬
ِ ِ َ ‫َﻛﺎ َن ﻣْﻨﺼﻮراً۞وﻻَ ﺗَـ ْﻘﺮﺑﻮاْ ﻣ‬
ْ‫َﺷﺪﱠﻩُ َوأ َْوﻓُﻮا‬ ُ ‫َﺣ َﺴ ُﻦ َﺣ ﱠ ٰﱴ ﻳَـْﺒـﻠُ َﻎ أ‬ ْ ‫ﺎل ٱﻟْﻴَﺘﻴ ِﻢ إِﻻﱠ ﺑِﭑﻟﱠِﱴ ﻫ َﻰ أ‬ َ َُ َ ُ َ
798

ِ َ‫ﭑﻟﻘ ْﺴﻄ‬
‫ﺎس‬ ِ ِ‫ِﺎﺑﻟْﻌﻬ ِﺪ إِ ﱠن ٱﻟْﻌﻬ َﺪ َﻛﺎ َن ﻣﺴﺆوﻻً۞وأَوﻓُﻮا ٱﻟْ َﻜﻴﻞ إِذا ﻛِ ْﻠﺘﻢ وِزﻧُﻮاْ ﺑ‬
َ ُْ َْ ْ َ ُْ َ َْ َْ
‫ﻚ ﺑِِﻪ ِﻋ ْﻠ ٌﻢ إِ ﱠن ٱﻟ ﱠﺴ ْﻤ َﻊ‬ ِ ْ ِ‫ٱﻟْﻤﺴﺘ ِﻘﻴ ِﻢ ٰذﻟ‬
َ َ‫ﺲ ﻟ‬َ َ ‫ﻴ‬
َْ‫ﻟ‬ ‫ﺎ‬‫ﻣ‬ ‫ﻒ‬ُ ‫ﻘ‬ْ ‫ـ‬
َ‫ﺗ‬ ‫ﻻ‬
َ ‫و‬
َ ۞ ‫ﻼ‬
ً ‫ﻳ‬‫و‬ ‫ﺄﺗ‬َ ‫ﻦ‬ ‫ﺴ‬
َُ َ ٌ‫َﺣ‬
ْ ‫أ‬
‫و‬ ‫ﺮ‬ ‫ـ‬‫ﻴ‬ْ ‫ﺧ‬
َ ‫ﻚ‬َ َْ ُ
‫ﻚ‬َ ‫ض َﻣَﺮﺣﺎً إِﻧﱠ‬ ِ ‫ﺶ ِﰱ ٱﻷ َْر‬ ِ َْ‫ﻚ َﻛﺎ َن َﻋْﻨﻪُ َﻣ ْﺴ ُﺆوﻻً۞ َوﻻَ ﲤ‬ َ ِ‫ﺼَﺮ َوٱﻟْ ُﻔ َﺆ َاد ُﻛ ﱡﻞ أُوﻟـٰﺌ‬َ َ‫َوٱﻟْﺒ‬
ِ
‫ﻚ‬َ ِّ‫ﻚ َﻛﺎ َن َﺳﻴِّﺌُﻪُ ِﻋْﻨ َﺪ َرﺑ‬َ ‫ﺎل ﻃُﻮﻻً۞ ُﻛ ﱡﻞ ٰذﻟ‬ َ َ‫ٱﳉِﺒ‬
ْ ‫ض َوﻟَﻦ ﺗَـْﺒـﻠُ َﻎ‬ َ ‫ﻟَﻦ َﲣْ ِﺮ َق ٱﻷ َْر‬
ِ‫ٱﳊِ ْﻜﻤ ِﺔ وﻻَ َﲡﻌﻞ ﻣﻊ ﱠ‬ ِ َ ‫ﻚ رﺑﱡ‬ ِ ِ‫ﻣ ْﻜﺮوﻫﺎً۞ ٰذﻟ‬
َ ً‫ٱﻪﻠﻟ إِﻟَـٰﻬﺎ‬
‫آﺧَﺮ‬ َ َ ْ َ ْ َ َ ْ ‫ﻚ ﻣ َﻦ‬
ِ
َ َ ‫ﻚ ﳑﱠﺂ أ َْو َﺣ ٰﻰ إﻟَْﻴ‬ َ ُ َ
﴾ً‫ﻓَـﺘُـ ْﻠ َﻘ ٰﻰ ِﰱ َﺟ َﻬﻨﱠﻢ َﻣﻠُﻮﻣﺎً ﱠﻣ ْﺪ ُﺣﻮرا‬
َ
Wala taqraboo alzzina innahu kana fahishatan wasaa sabeelan; Wala taqtuloo
alnnafsa allatee harrama Allahu illa bialhaqqi waman qutila madhlooman faqad
jaAAalna liwaliyyihi sultanan fala yusrif fee alqatli innahu kana mansooran; Wala
taqraboo mala alyateemi illa biallatee hiya ahsanu hatta yablugha ashuddahu
waawfoo bialAAahdi inna alAAahda kana mas-oolan; Waawfoo alkayla idha
kiltum wazinoo bialqistasi almustaqeemi dhalika khayrun waahsanu ta/weelan;
Wala taqfu ma laysa laka bihi AAilmun inna alssamAAa waalbasara waalfu-ada
kullu ola-ika kana AAanhu mas-oolan; Wala tamshi fee al-ardhi marahan innaka
lan takhriqa al-ardha walan tablugha aljibala toolan; Kullu dhalika kana sayyi-ohu
AAinda rabbika makroohan; Dhalika mimma awha ilayka rabbuka mina alhikmati
wala tajAAal maAAa Allahi ilahan akhara fatulqa fee jahannama malooman
madhooran (Surat Al Isra 17:32-39)

Tafsir: Na wala usiikaribie Zina kwani kwa hakika huo ni Uchafu na njia ya
Maovu.Na wala usiiwe Nafsi ambayo Allah ameiharamisha isipokua kwa haki, na kwa
alieuliwa basi amedhulumiwa na tumetoa mamlaka ya kudai kulipiza kisasi kwa walii
wake, lakini asivuke mipaka katika kuua kwake, kwani kwa hakika atakua
amenusuriwa. Na wala usiikaribie Mali ya Yatima isipkua kwa njia ya kuiboresha
mpaka (Yatima huyo) atakapo baleghe. Na tekelezeni Ahadi kwani kwa hakika juu ya
Ahadi Mtaulizwa. Na timizeni Vipimo mnapopima na pimeni kwa Uadilifu, kwani hio
ndio njia iliyonyooka. Na hio ndio kheri na ndio kwenye mwisho mwema. Na usifuate
kile ambacho huna Elimu navho . kwani kwa hakika juu ya Masikio, juu ya kuona
na juu ya Moyo, kila kimoja juu yake mtaulizwa. Na msitembee juu ya Ardhi kwa
madaha, kwani kwa hakika kamwe hamtoweza kudidimia ndani ya ardhi, na wala
hamtoufikia urefu wa milima. Kadhalika yote hayo yote ni Maovu na mbele ya Mola
wako ni yenye kukirihisha. Hii ni sehemu ya hikma umeshushiwa kutoka kwa Mola
799

wako. Na usimshirikishe Allah ili usije ukavurumishwa kwenye Moto huku ukiwa ni
mwenye kulaumiwa na mwenye kukataliwa.

Hizo ni aya 18 za Surat Al Isra zinazofafanua mithili ya yaliyomo ndani ya kitabu


alichopewa Nabii Musa yaani Tawrat kwa ajili ya watu wa Bani Israil kama anavyosema
Allah Subhanah wa Tala katika Qur’an

ِ ‫﴿ﰒُﱠ آﺗَـﻴـﻨَﺎ ﻣﻮﺳﻰ ٱﻟْ ِﻜﺘَﺎب َﲤَﺎﻣﺎً ﻋﻠَﻰ ٱﻟﱠ ِﺬ ۤي أَﺣﺴﻦ وﺗَـ ْﻔ‬
‫ﺼﻴﻼً ﻟِّ ُﻜ ِّﻞ َﺷ ْﻲ ٍء َوُﻫ ًﺪى‬ َ ََ ْ َ َ َ ُ ْ
ِ ِِ ‫ﱠ‬
﴾‫ﺂء رّﻬﺑِِﻢ ﻳـُ ْﺆِﻣﻨُﻮ َن‬
ْ َ ‫َوَر ْﲪَﺔً ﻟ َﻌﻠﱠ ُﻬ ْﻢ ﺑﻠ َﻘ‬
Thumma atayna moosa alkitaba tamaman AAala alladhee ahsana watafseelan
likulli shay-in wahudan warahmatan laAAallahum biliqa-i rabbihim yu/minoona
(Surat Al Anaam 6: 154)

Tafsir: Na kisha tukampa Musa kitabu kilichokamilia kwa wale wenye kufanya Mema.
Na tukaelezea kila kitu ndani yake na Muongozo na Rehma ili wapate kuamini
kuhusianana na kukutana na Mola wao.

Kisha Allah Subhnah wa Ta’ala anabainisha yaliyomo ndani yake Tawrat kwa kifupi
kwa kusema

ِ ‫ﺼﺂﺋَِﺮ ﻟِﻠﻨ‬
‫ﱠﺎس‬ ٰ َ ‫ﺎب ِﻣﻦ ﺑَـ ْﻌ ِﺪ َﻣﺂ أ َْﻫﻠَ ْﻜﻨَﺎ ٱﻟْ ُﻘُﺮو َن ٱﻷ‬
َ َ‫ُوﱃ ﺑ‬
ِ
َ ‫﴿ َوﻟََﻘ ْﺪ آﺗَـْﻴـﻨَﺎ ُﻣ‬
َ َ‫ﻮﺳﻰ ٱﻟْﻜﺘ‬
﴾‫وُﻫ ًﺪى ور ْﲪَﺔً ﻟﱠ َﻌﻠﱠ ُﻬﻢ ﻳَـﺘَ َﺬ ﱠﻛﺮو َن‬
ُ ْ ََ َ
Walaqad atayna moosa alkitaba min baAAdi ma ahlakna alquroona al-oola basa-
ira lilnnasi wahudan warahmatan laAAallahum yatadhakkaroona; (Surat Al Qasas
28:43)

Tafsir: Na kwa hakika tulimpa Musa kitabu baada ya kuwaangamiza waliotangulia,


kua ni Nuru kwa Watu na Muongozo na Rehma ili wapate kukumbuka.

Anasema Said Ibn Malik Ibn Sinan Al Khazraji Al Khudri Radhi Allahu Anhu maarufu
kama Abu Said Al Khudri kuhusiana na aya hizi kua: ‘Baada ya Allah Subhanah wa
Ta’ala kuishusha Tawrat basi hakuwahi kuuangamiza Ummah wowote kupitia kwa
njia ya Adhabu ya kutokea Mbinguni, isipokua kwa kuwabadilisha watu katika
Kima na Nguruwe na hii ni ktokana na maneno yasemayo kua: Walaqad atayna
800

moosa alkitaba min baAAdi ma ahlakna alquroona al-oola - Na kwa hakika tulimpa
Musa kitabu baada ya kuwaangamiza waliotangulia.’

Ambao baadhi ya Wanazuoni wanasema kua: ‘Kutokana na kusishwa huko kwa


adhabu za Magamizo basi ndio maana baadae Allah Subhanah wa Ta’ala
akaamrisha kupiganwa kwa vita vya Jihadi badala yake.’

Ambapo anasema Imam Yahya Ibn Sallam kua: ‘Tawrat ndio kitabu cha Mwanzo
kilichoshushwa kilichokua na maamrisho kuhusiana na yaliyohalalishwa na
yaliyoharamishwa ndani yake.’

Ambapo kwa upande wa Imam Abu Hayyan basi yeye anasema kua: ‘Kwa utukufu basi
Kitabu cha Tawrat ndio Kitabu cha Kwanza kushushwa kikiwa na Maamrisho ya
Mungu na hivyo Tawrat kua ni kitabu ambacho kilichoanzisha Ukurasa mpya
katika Historia ya Dini Ulimwenguni.’

Anasema Imam Ahmd Muhammad Ath Thalabi kua amesema Abd Allah Ibn Abbas
Radhi Allau Anhu kua: ‘Baada ya Nabii Musa kupewa Tawrat basi akasema: ‘Ya
Allah Hakika umenipa mimi heshima ambayo hukuwahi kumpa Mtu yeyote.’ Allah
Subhanah wa Ta’ala akamwambia kua: ‘Bila ya shaka, na pia utakufa huku ukiwa
umepata radhi na Mapenzi ya Muhammad’ Nabii Musa akauliza: ‘Muhammad
Ndio nani?’

Allah Subhanah wa Ta’ala akasema kua: ‘Ahmad ambae Jina lake nimelikadiria
miaka 2000 kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi, kwani yeye ni Mtume wangu na ni
Rafiki yangu, ambae nimemhagua mongoni mwa Waja wangu. Hakika yeye ni
mwenye ukaribu sana nami kuliko viumbe vyengine vyote, na Malaika wote’

Nabii Musa akasema: ‘Ya Allah! Kama Muhammad ni bora kuliko viumbe wako
wote, hivi jee hii inamaanisha kua umeumba watu ambao ni bora zaidi kuliko
Ummah wangu?’

Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Ubora wa Umati wa Muhammad ni ba uliko


viumbe wote’ Nabii Musa akasema; ‘Ya Allah,hakika mimi natamani kua
ningekutana na nae na kukutana na watu wake pia. ’ Allah Subhanah wa Ta’ala
akasema: ‘Ewe Musa huwezi kukutana nao, lakini unaweza kusikia maneno yao.’
Kisha Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Enyi Umati wa Muhammad!’ kisha nasi
watu Umati wa Muhammad sote tukaitikia kutoka ndani ya Mapazia ya sehemu za
siri za Wazee wetu kwa kusema: ‘Ya Allah! Sisi Hapa, hakika wewe ndie Mola wetu,
shukrani zote unastahiki wewe peke yako Utukufu ni wako, na Ufalm ni wako. Na
wala huna mshirika.
801

Hapo Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Enyi Umati wa Muhammad! Kwa


hakika Rehma zangu zimezizidi Ghadhabu zangu, na Usamehevu wangu umezizidi
Adhabu zangu, hakika mimi nimekujiuni kabla ya kuniomba, nimeusameheni
kabla ya hata kufanya makosa yenu. Na katika siku ya Malipo yeyote yule
atakaesema La ilaha illa Allah, Muhammad Rasul Allah ataingia Peponi hata kama
dhambi zake zitakua kama mapovu ya Bahari.’

Na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akasema:

﴾‫ﱠﺎﻫ ِﺪﻳﻦ‬
ِ ِ ِ ِ‫ﻨﺖ ِﲜَﺎﻧ‬
ِ َ َ‫ﺐ ٱﻟْﻐَﺮِِﰉ إِ ْذ ﻗ‬ َ ‫﴿ َوَﻣﺎ ُﻛ‬
َ ‫ﻛﻨﺖ ﻣ َﻦ ٱﻟﺸ‬
َ ‫ﻮﺳﻰ ٱﻷ َْﻣَﺮ َوَﻣﺎ‬
َ ‫ﻀْﻴـﻨَﺂ إ َ ٰﱃ ُﻣ‬ ّ ْ
Wama kunta bijanibi algharbiyyi idh qadhayna ila Moosa al-amra wama kunta
mina alshshahideena (Surat Al Qasas 28:44)

Tafsir: Na wewe (Muhammad) hukuwepo katika upande wa Magharibi wakati


tulipompa Musa amri zetu na hukuwa miongoni mwa Mashahidi.

Baada ya hapo basi Allah Subhanah wa Ta’ala akamwamibia Nabii Musa : ‘Ewe Musa
hivi jee unajua kua wakati wewe umekuja huku katika siku hizi 40 basi watu wako
wamevutwa na kushawishika, na kua ni wenye kuniasi?’ Nabii Musa akashtuka na
kuuliza: ‘Ya Allah itakuaje wawe ni wenye kukuasi wakati wewe ndie uliowaokoa
kutokana na Fir’awn? Na kuwavusha bahari na kuwaneemesha?’ Allah Subhanah
wa Ta’ala akasema: ‘Wametengeza Ndama ambae ni mwenye kutoa sauti na
kumfanya kua ndio Mungu wao.’ Nabii Musa akauliza: ‘Wamewezaje kufanya
hivyo?’ Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Ewe Musa! Ewe Baba wa Sharia!
Hakika mimi nimewarahisishia juu ya hilo kwani nimewaona wao katika Nyoyo
zao, kua wanalitaka sana jambo hilo’.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anahoji kuhusiana na Ufaham wa Bani Israil baada ya
kumtengeneza Ndama huyo na kuanza kumuabudia kwa kusema kwenye ya ifuatayo:

َ‫ﻮﺳ ٰﻰ ِﻣﻦ ﺑَـ ْﻌ ِﺪﻩِ ِﻣ ْﻦ ُﺣﻠِﻴِّ ِﻬ ْﻢ ِﻋ ْﺠﻼً َﺟ َﺴﺪاً ﻟﱠﻪُ ُﺧ َﻮ ٌار أََﱂْ ﻳـََﺮْواْ أَﻧﱠﻪُ ﻻ‬ ‫ﱠ‬
َ ‫﴿ َوٱﲣَ َﺬ ﻗَـ ْﻮُم ُﻣ‬
ِِ ِ ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫ﻳُ َﻜﻠّ ُﻤ ُﻬ ْﻢ َوﻻَ ﻳَـ ْﻬﺪﻳ ِﻬ ْﻢ َﺳﺒِﻴﻼً ﱠٱﲣَ ُﺬوﻩُ َوَﻛﺎﻧُﻮاْ ﻇَﺎﻟﻤ‬
Waittakhadha qawmu moosa min baAAdihi min huliyyihim AAijlan jasadan lahu
khuwarun alam yaraw annahu la yukallimuhum wala yahdeehim sabeelan
ittakhadhoohu wakanoo dhalimeena (Surat Al Araf 7:148)
802

Tafsir: Na wakachukua watu wa Musa baada ya kuondoka kwake, kutokana na


mapambo yao wakajaalia Umbo la Ndama. Aliekua akilia. Hivi hawakuona kua alikua
hasemi nao wala hawawaongozi njia? Walimchukulia kua ni kwa ajili na kumuabudu
na wakawa waliopotea.

Hivyo Nabii Musa ikambidi achukue Maandiko yake aliyopewa na Mola wake ya Tawrat
na kisha haraka arudi kuwakimbilia Watu wake, kwa ajili ya kuwawahi kabla
hawajaangamia kwenye kufuru zaidi kutokana na kua ni wenye Kumuabudia Ng’ombe
walietengenezewa na Samirii.

SAMIRII, ATHARI RASULI NA NDAMA WA DHAHABU WA BANI


ISRAIL


Jina Samirii linatokana na neno inatokana na neno Samara ambalo kwa lugha ya kiarabu
hua linamaanisha Usiku wa Mwezi Mpevu abao watuhua wanakaa Barazani wakati wa
Uskua na Kuzungumza, na hivyo pia hua linamaanisha Kukesha Usiku kwa ajili ya
Kuzungumza maneno yasiyokua na maana, Kuzungumza Maneno ya Kipuuzi katika
wakati wa Usiku, Kuuhuisha Usiku kwa Kuhadithiana hadithi za Kipuuzi au Mambo ya
Kipuuzi.

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anasema katika Qur’an kuhusiana na Makafiri wa


kabila la Quraysh kua:

﴾‫﴿ ُﻣﺴﺘَ ْﻜِ ِﱪﻳﻦ ﺑِِﻪ َﺳ ِﺎﻣﺮاً ﺗَـ ْﻬ ُﺠﺮو َن‬


ُ َ ْ
Mustakbireena bihi samiran tahjuroona (Surat Al Muuminuun 23:67)

Tafsir: Wakiwa na Kiburi wakizungumza mambo ya Kipuuzi wakati wa Usiku.

Ambapo katika aya hii basi Allah Subhanah wa Ta’ala mbali ya kua ametumia neno
Samiran pale aliposema samiran tahjuroona lakini pia akatumia neno Tahjuruuna
ambalo linamaanisha Kuukataa au Kuudharau Ukweli na hivyo pia kutokana na maana
hio basi hua ni lenye humaanisha Kuzungumza Upuuzi.

Ambapo neno Bihi liilotumia hapa hua linamaanisha kua kinachozugumzwa hapa ni Al
Kaabah na hii ni kutokana ana kukaa kwao Makafiri hao katika eneo hlo katika wakati
803

wa Usiku na kuzungumza maneno yasiyokua na maana, na pia inaweza ikawa


anaezungumziwa hapa ni Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwani Makafiri hao
walikua pia wakizungumza maneno ya kipuuzi dhidi yake katika wakati wa Usiku
kutokana na kutomkubali kua ni yeye ni Rasul Allah.

Ama kutokana na aya hii basi ndio maana Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu
A’nhu akasema kua: ‘Haipendezi kua katika wakati wa Usiku watu wanauhuisha
kwa kuzungumza maneno ya Kipuuzi badala ya kuhuisha kwa kufanya mema.’

Hivyo ingawa tunapozungumzia neno Samirii kwa upande wa Lugha ya Kimisri basi hua
kuna neno Shemiir ambalo hua linamaanisha Mgeni au mtu asieishi katika Ardhi ya Nchi
husika, na hii inaweza ikawa sahih kua Samirii anatokana na watu wa Misri kwa sababu
ni miongoni mwa watu wa Msri ndio walikua wakiabudia Masanamu ya Ng’ombe.

Lakini hapo hapo pia tunapoangalia asili ya neno Samara kama tulivyoiona hapo kabla
basi unaona kua huenda Samirii ameitwa Samirii kwa sababu kua ni Mtu mwenye
kuzungumza maneno ya kipuuzi yaliyo wapotosha watu wa Bani Israil kutokana na
kutomuamini kwake Nabii Musa.

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea alivyokua akimtaarifu Nabii Musa hapo
kabla kuhusiana na aliyoyafanya Samirii baada ya Nabii Musa kwa kumhoji huku
akisema:

ِ ِ ‫ﺎل ﻫﻢ أُو ۤﻻ ِء ﻋﻠَﻰ أَﺛَِﺮى وﻋ‬ ِ َ‫ﻚ ﻋﻦ ﻗ‬


‫ﻚ‬ ‫ﻴ‬‫ﻟ‬
َ ‫إ‬ ‫ﺖ‬
َ ْ ُ ََ ‫ﻠ‬
ْ ‫ﺠ‬ ٰ َ ْ ْ ُ َ َ‫ﻮﺳ ٰﻰ۞ﻗ‬ َ ُ‫ﻚ ٰﳝ‬ َ ‫ﻮﻣ‬ َ َ َ‫﴿ َوَﻣﺂ أ َْﻋ َﺠﻠ‬
﴾‫ي‬ ‫َﺿﻠﱠ ُﻬ ُﻢ ٱﻟ ﱠﺴ ِﺎﻣ ِﺮ ﱡ‬ ِ ِ ‫ﺎل ﻓَِﺈ ﱠ� ﻗَ ْﺪ ﻓَـﺘـﻨﱠﺎ ﻗَـﻮﻣ‬ ِ ِ‫ر‬
َ ‫ﻚ ﻣﻦ ﺑَـ ْﻌﺪ َك َوأ‬
َ َْ َ َ َ‫ﺿ ٰﻰ۞ﻗ‬
َ ‫ب ﻟﺘَـْﺮ‬َّ
Wama aAAjalaka AAan qawmika ya moosa; Qala hum ola-i AAala atharee
waAAajiltu ilayka rabbi litardha; Qala fa-inna qad fatanna qawmaka min
baAAdika waadhallahumu alssamiriyyu (Surat Ta-Ha 20:83-85)

Tafsir: Akasema (Allah Subhanah wa Ta’ala) Na jee ni kitu gani kilichokufanya


uharakishe kutoka kwa watu wako ewe Musa? Akasema (Nabii Musa) ‘Wao wapo
kwenye Athari zangu, Na nimekimbilia kwako Mola wangu ili Uniridhie.’ Akasema
(Allah Subhanah wa Ta’ala): ‘Kwa Hakika tumewapa Mtihani watu wako, wakati
ulipokua hupo, na ameshawapotosha Samirii’

Ambapo kuhusiana na maneno ya Nabii Musa pale alipojibu kwa kusema: ‘Hum ola-i
AAala Atharee’ yaani ‘Wao wapo kwenye Athari zangu’ basi miongoni mwa wafasiri
basi wamefasiri kauli hii kwa kusema kua: Hii inaamanisha kua Nabii Musa alikua
804

anamaanisha kua: ‘Wao wako nyuma yangu’ ambapo neno Hum ola-i yaani Wao
linawakilisha watu 70 wa Bani Israil ambao walikua wamebakia chini ya Mlima
wakimsubri Nabii Musa.

Kwani watu hao 70 wa Bani Israil walikuja pamoja na Nabii Musa kwa ajili ya
kushuhudia namna Nabi Musa anavyoshushiwa maamrisho yake na makatazo yake Allah
Subhanah wa Ta’ala katika Kitabu cha Tawrat ambapo aliwawacha nyuma na kisha yeye
peke yake akaharakisha kukimbilia kuzungumza na Mola wake.

Ambapo kwa upande wa Imam Hasan Al Basr basi yeye anasema kuhusana na maneno
ya Nabii Musa yamaliziyo aya hio yasema kua: ‘WaAAajiltu ilayka rabbi litardha yaani
Na nimekimbilia kwako Mola wangu ili Uniridhie basi yaamaanisha kua :
‘Nimekimbilia kwako Mola wangu kwa sababu Watu wa Bani Israil wanafuata
Nyayo zangu wa ajili ya muongozo.’ Na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala
akasema kumhakikishia Nabii Musa kua anavyofikiria basi sivyo ilivyo kiuhalisia
kwani: ‘Qala fa-inna qad fatanna qawmaka min baAAdika waadhallahumu
alssamiriyyu yaani Akasema (Allah Subhanah wa Ta’ala): ‘Kwa Hakika tumewapa
Mtihani watu wako, wakati ulipokua hupo, na ameshawapotosha Samirii’

Ambapo wa upande wa Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Ahmad Ibn Abu Baqr Al
Ansari Al Qurtubi basi yeye anasema kua: ‘Aya hii inaonesha kua kutokana na hamu
aliyokua nayo Nabii Musa katika kuzungumza na Mola wake Nabii Musa basi
aliona kua watu wake hawana mwendo wa kutembea kwao kwani walikua
wanatembea kidogo kidogo na hivyo yeye akawawacha nyuma na kutangulia kwa
haraka haraka na na hivyo alipoulizwa kwa nini akaharakisha basi ndio akajibu
kua wanafuata nyayo zake yaani wako nyuma yake’

Ambapo hapa tunaona kua aya imetumia neno Athari ambalo linaokana na neno Athara
Ambalo hua linamaanisha Athiri, Ushahidi, Uthibitisho, Alama za Nyao au Hatua,
Vutiwa, Nukuu, Mafunzo, Sehemu ya Ilmu inayotoka kwa Msomeshaji na kumfikia
Msomeshwaji, na pia humaanisha kua ni Alama inayoachwa kwa ajili ya Kumbukumbu.

Na kwa upande mwengine basi anasema Imam Qatadah Al Saddusi kua: ‘Samirii alikua
ni mmoja kati ya watu wa Misri ambae alikua akitokana katika kabila la Al
Samirah, ambae alikua ni Adui wa Allah Subhanah wa Ta’ala aliejificha ndani ya
watu wa Nabii Musa. ’

Na akasema Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua ‘Samirii alikua
akiitwa Musa Zafir na alikua ni mvunjaji umoja wa Dini ya Allah Subhnah wa
Ta’ala. Kwani alitokana na watu waliokua wakiabudu Ng’ombe na alikua
akiwapenda sana Ng’ombe.’
805

Kwa upande wa Imam Ismail Abd Rahman Al Suddi basi yeye anasema kua; ‘Samiri
alikua ni miongoni mwa watu wa Bani Israil wa Nabii Musa ambae alikua na
miongoni mwa watoto waliozaliwa katika kipindi cha kuchinjwa Watoto wa Kiume,
katika kipindi hiki Wanawake wa Bani Israil walikua wakikimbilia kwenye
Mapango kwa ajili ya kujifungua na kuwaacha watoto wao mapangoni ili
wasichinjwe na Fir’awn. Allah Subhanah wa Ta’ala aliwapa hifadhi kwa
kuwapelekea watoto hao Malaika kwa ajili ya kuwasimamia, na hivyo Samirii
alikua akisimamiwa na Malaika Jibril ambae alikua akimpa kidole chake chenye
kutoka Maziwa na Asali anyonye kama chakula chake.

Hivyo Samirii alikua ni mtu pekee miongoni mwa watu wa Bani Israil wenye
kumjua Malaika Jibril. Na katika kipindi cha Kuvuka Bahari basi Samirii
alichukua athari ya kwato ya Farasi wa Malaika Jibril iliyoachwa kwenye mchanga
uliokanyagwa na Farasi huyo.’

Hivyo Nabii Musa alipoaga na kuondoka kwa ajili ya kuelekea Milimani kuzungumza na
Mola wake basi alisema kua atakaa huko kwa siku 30, lakini sasa Allah Subhanah wa
Ta’ala kwa hikma zake akamuongezea Nabii Musa siku 10 zaidi na hivyo ikawa ni siku
40, kwa ajili ya kuwapa Mtihani watu wa Bani Israil, baada ya kukosa Subra pale mara
baada ya kuvuka Bahari na kutaka kua watengenezewe Mungu wa sanamu.

Ilipofika siku ya 30, na kisha Nabii Musa akawa haonekani basi watu wa Bani Israil
wakaanza kusema kaua: ‘Hakika Musa haaminiki kwani amevunja miadi, alisema
kua atarudi baada ya siku 30 lakini hajarudi’, na hapa Ibilis akaanza kusimamia kazi
yake kwa moja kwa moja kina ndani ya ufaham wa rafiki yake ambae ni Samirii na
kuanza kumshawishi kua awatengenezee wau wa Bani Israil sanam kwa ajili ya
kuliabudia.

Ambapo kwa upande wa Nabii Harun basi nae akajua kua watu wake hao alioachiwa
awasimamie watampa mtihani kubwa sana, hususan baada ya kupita hio siku ya30, kwani
watataka kutengeneza Sanamu kwa kutumia Dhahabu walizochukua kutoka kwa watu
wa Misri. Hivyo akawamrisha watu hao wa Bani Israil kua wachimbe shimo kisha wazitie
Dhahabu zao zote walizozirithi kutoka kwa watu wa Misri kwenye shimo hilo, kwani
kisharia tayari zimeshakua si halali yao, kutokana na kutomuamini Mtume wao, hivyo
inabidi zikae ndani ya shimo hilo mpaka atakaporudi Nabii Musa ili atote hukumu yake
juu yake dhahabu hizo.

Watu hao wa Bani Israil wakakubaliana na shauri hilo, na katika kufanya kwao hivyo
huko bsi Samirii akauchukua mchanga aliouchota kutokana na athari za kwato za Farasi
wa Malaika Jibril na akaumwagia juu ya Dhahabu hizo zilizomo ndani ya shimo hilo. Na
hapo hapo ndani ya Shimo hilo likatokea Umbo la Ng’ombe ambae hapo hapo nae
akaanza kutoa sauti ya Mlio wa Ng’ombe. Na hapo Samirii akawaambia watu wa Bani
806

Israil kua: ‘Kwa hakika huyu ndio Mungu wenu na ndie pia Mungu wa Musa, ila
sasa Musa ameenda kumtafuta Mungu wake, wakati ameuacha huku na ndio
maana ikawa hajarudi kwa sababu hajamuona bado.’ Kama zinavyosema aya;

﴾‫ﻮﺳ ٰﻰ ﻓَـﻨَ ِﺴﻲ‬ ِ ِ ِ


ْ ‫﴿ﻓَﺄ‬
َ ‫َﺧَﺮ َج َﳍُْﻢ ﻋ ْﺠﻼً َﺟ َﺴﺪاً ﻟﱠﻪُ ُﺧ َﻮ ٌار ﻓَـ َﻘﺎﻟُﻮاْ َﻫـٰ َﺬآ إﻟَـٰ ُﻬ ُﻜ ْﻢ َوإﻟَـٰﻪُ ُﻣ‬
َ
Faakhraja lahum AAijlan jasadan lahu khuwarun faqaloo hadha ilahukum wa-
ilahu moosa fanasiya(Surat Taha 20:88)

Tafsir: Na kisha (Samirii) akawatolea haraka Umbo la Ndama lenye kutoa sauti.
Wakasema (watu wa Bani Israil): ‘Huyu ndio Mungu wenu na Mungu wa Musa,
lakini (Musa) amemsahau’

Aya imetuma neno Aaijlan ambalo ni lenye kutokana na neno Aajil lenye kumaanisha
Kufaharakisha, Kua na Haraka kubwa sana, Kuzidisha kasi au haraka.

Ambapo anasema Amir Ul Muuminin Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu kua :
‘Ng’ombe huyu alikua akiitwa Al Ijl na hii ni kwa sababu (ta’aajjaluhu) alijaaliwa
kua kwa haraka sana kabla ya kurudi Nabii Musa.’ Na kwa upande wa Hasan Al Basr
basi yeye anasema kua: ‘Ng’ombe huyu alikua akiitwa Bahamut’

Aya pia imetuia neno Khuwarun ambalo ni lenye kumaanisha Kutoa sauti kama Ng’ombe
au kama Upinde unaovutwa na kisha ukaachiwa. Na hivyo kumaanisha kua Ngo’mbe
huyo alikua akitoa sauti kama ya Ndama au kama ya kitu kinachovutwa na kuachiwa na
kutoa sauti ya Mvumo kama unavyovuma Upinde baada ya kuachiwa kwake.

Na ikatumia pia neno Fanasiya ambalo kulingana na Mtizamo wa Sultan Al Mutakallimin


Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi anasema kua: ‘Amesema Abd Allah Ibn Abbas Radhi
Allahu Anhu, Mujahhid Ibn Sulayman na Qatadah Al Sadusi kua: ‘Neno Fanasiyah
linamaanisha kua ni kauli iliyomtoka Samirii ambae alikua aimaaisha kua: ‘Musa
amesahau sehemu ambayo alikua akitakiwa amtafute Ng’ombe huyo ambae ndie
Mungu wenu mnaetakiwa Mumuabudu.’’’

Baada ya tukio hilo basi Nabii Harun akaingilia kati na kujaribu kuwafumbua macho wa
hao wa Bani Israil lakini jitihada zake hazikufua dafu mbele ya matamanio ya Watu wa
Bani Israil na jitihada za Samirii ya usimamizi wa Ibilisi. Allah Subhanah wa Ta’ala
anaielezea hali ilivyokua kwa kusema kama zisemavyo aya:
807

ِ ِ
‫ﺎل َﳍُْﻢ‬ َ َ‫۞وﻟََﻘ ْﺪ ﻗ‬
َ ً‫ﺿّﺮاً َوﻻَ ﻧَـ ْﻔﻌﺎ‬َ ‫ﻚ َﳍُْﻢ‬ ُ ‫﴿أَﻓَﻼَ ﻳَـَﺮْو َن أَﻻﱠ ﻳَـْﺮﺟ ُﻊ إِﻟَْﻴ ِﻬ ْﻢ ﻗَـ ْﻮﻻً َوﻻَ ﳝَْﻠ‬
ْ‫َﻃﻴﻌُ ۤﻮا‬
ِ ‫ﻫﺎرو ُن ِﻣﻦ ﻗَـﺒﻞ ٰﻳـ َﻘﻮِم إِﱠﳕَﺎ ﻓُﺘِﻨﺘُﻢ ﺑِِﻪ وإِ ﱠن رﺑﱠ ُﻜﻢ ٱﻟﱠﺮ ْﲪـٰﻦ ﻓَﭑﺗﱠﺒِﻌ ِﻮﱏ وأ‬
َ ُ َُ ُ َ َ ْ ْ ُْ َُ
﴾‫ﻮﺳ ٰﻰ‬ ‫ﻣ‬ ‫ﺎ‬‫ﻨ‬ ‫ـ‬‫ﻴ‬ َ‫ﻟ‬ِ‫ﲔ ﺣ ﱠ ٰﱴ ﻳـﺮِﺟﻊ إ‬ ِ ِ‫أَﻣ ِﺮي۞ﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻟَﻦ ﻧـﱠﺒـﺮح ﻋﻠَﻴ ِﻪ ﻋﺎﻛ‬
‫ﻔ‬
َ ُ َ ْ َ َْ َ َ َ ْ َ َ َْ ْ
Afala yarawna alla yarjiAAu ilayhim qawlan wala yamliku lahum ddarran wala
nafAAan; Walaqad qala lahum haroonu min qablu ya qawmi innama futintum bihi
wa-inna rabbakumu alrrahmanu faittabiAAoonee waateeAAoo amree; Qaloo lan
nabraha AAalayhi AAakifeena hatta yarjiAAa ilayna moosa (Surat Taha 20:89-91)

Tafsir: Hivi hawakuona kua hawarudishii kauli na wala hana uwezo wa uwanufaisha
wala wa kuwadhuru?; Na Harun kwa hakika aliwaambia hapo kabla: ‘Enyi watu
wangu, Hakika nyinyi mmefitinishwa, kwani kwa hakika Mola wenu ni Mwingi wa
Rehma, hivyo nifuteni na fuateni maamrisho yangu.’ Wao wakasema: ‘Kamwe
Hatutoachana kushikamana nae mpaka atakaporudi kwetu Musa.’

Hivyo aya zinatuwekea wazi kua Nabii Harun aliwabainishia watu wa Bani Israil mambo
matatu: Ambayo ni kua kwanza wanatakiwa wajue kua wamefikwa na Mtihani
mkubwa sana, ambao unawapotosha na kisha jambo la pili ni kuhusianana ni nini
wanachotakiwa kufanya kutokana na Mtihani huo, kwa kuwapa ufumbuzi wa
Mtihani huo kua: ‘Warudi kwa Mola wao ambae ni Mwingi wa Rehma, hivyo
anaweza kuwasamehe baada ya kufikwa na mitihani hio kama watarudi kwa Mola
wao. Na jambo la tatu ni kuhusiana na la kufanya baada ya kurudi kwa Mola wao,
ambalo ni kua ni wenye kumfuata yeye Nabii Harun katika kila atakacho
waelekeza.

Lakini watu hao wa Bani Israil wakasema kumwambia Nabii Harun: ‘Hakika sisi
tutashikamana na Sanam letu hili hadi hapo atakaporudi Musa kisha tuone
atasemaje, kwani huenda nae baada ya kujua kilichotokea basi huenda akawa ni
mwenye kufuata Mungu tunaemfuata sisi.’

Kwani aya imetumia neno AAakifeena ambalo ni lenye kutokana na neno Aakafa ambalo
ni lenye kumaanisha Kupanga Mpangilio, Kushikamana, Kuzuia, Kusimamia Mpangilio
Fulani, Kubakia katika hali ya awali, n.k. Neno Aakafa ndio lililotoa neno Itiqaf ambalo
hua ni lenye kumaanisha Kubakia na Kukaa ndani ya Msikiti katika masiku 10 ya mwisho
ya ndani ya Mwezi wa Ramadhani.
808

Hivyo Watu hawa wa Bani Israil walikua wanatilia Mkazo kua hawatoachana na
kuliabudu Sanam la Ndama huyo hata iwe vipi, na wataendelea kufanya hivyo mpaka
atakaporudi Nabii Musa. Na hali hii pia inatiliwa kazo katika kauli yao ambayo imetumia
neno Lan Nabraha.

Ambapo neno Nabraha hua ni lenye utokana na neno Baraha ambalo humaanisha
Kuondoka, Kuachana na Kitu, Kukomesha kufanya kitu. Lakini hapa sasa ipo katika hali
ya Kukanusha kwa kutumia neno Lan a hivyo kua Lan nabraha AAalayhi AAakifeena
kumaanisha kua Kamwe Hatutoachana juu yake kushikamana nae.

Hivyo katika kundi la watu wote hao wa Bani Israil ambao ni zaidi ya watu 600,000 basi
watu wachache tu yaani watu 12,000 ndio ambao walikubaliana na Nabii Harun ni hivyo
kua ni wafuasi wake, na waliobakia wote wakawa ni wafuasi wa Samirii na Ibilisi na
hivyo kua ni wenye kumuabudu Ng’ombe walietengenezewa na Samirii na wakawa
tayari kwa lolote lile dhidi ya yule atakawakataza kuliabudia Sanam hilo.

Allah Subhana wa Ta’ala anayaelezea yaliyotokea baada ya Nabii Musa kuondoka kwa
watu wake na kumwachia mamlaka yake kwa Nabii Harun na watu wa Bani Israil kua
ni wenye uasi katika Aya zifutazo kwa kusema :

﴾‫ﲔ ﻟَْﻴـﻠَﺔً ﰒُﱠ ﱠٱﲣَ ْﺬ ُﰎُ ٱﻟْﻌِ ْﺠﻞ ِﻣﻦ ﺑَـ ْﻌ ِﺪﻩِ وأَﻧْـﺘُﻢ ﻇَﺎﻟِﻤﻮ َن‬
َ
ِ‫﴿وإِ ْذ واﻋ ْﺪ َ� ﻣﻮﺳﻰ أَرﺑﻌ‬
َْ ٰ َ ُ َ َ َ
ُ ْ َ َ
Wa-idh waAAadna moosa arbaAAeena laylatan thumma ittakdhtumu alAAijla
min baAAdihi waantum dhalimoona(Surat Al Baqara 2:51)

Tafsir: Na Kumbuka tulipomchagulia Musa Usiku arubaini, kisha (alipokua hayupo)


Mkachukua Ndama baada yake, na mkawa wenye kufanya udhalimu.

Hivyo Nabii Musa akarudi na Maandiko yake kwa watu wake na alipokua anakaribia basi
akasikia suti za shamra shamra za ngoma na nyimbo walizokua wakiimba watu wa Bani
Israil, na kwa mbali akawaona watu wake hao wakiwa wanapiga ngoma na kucheza huku
wakiwa ni wenye kumzunguka Ndama wao huyo walietengenezea na Samirii huku
wanacheza, ambapo anasema Allah Subhanah wa Ta’ala kuhusiana na hali ilivyokua kwa
kusema katika aya ifuatayo:

‫ﺎل ﺑِْﺌ َﺴ َﻤﺎ َﺧﻠَ ْﻔﺘُ ُﻤ ِﻮﱏ ِﻣﻦ ﺑَـ ْﻌ ِﺪ ۤي‬ َ َ‫ﻀﺒَﺎ َن أ َِﺳﻔﺎً ﻗ‬
ْ ‫ﻮﺳ ٰﻰ إِ َ ٰﱃ ﻗَـ ْﻮِﻣ ِﻪ َﻏ‬
َ ‫﴿ َوﻟَ ﱠﻤﺎ َر َﺟ َﻊ ُﻣ‬
ِ ‫أَﻋ ِﺠ ْﻠﺘُﻢ أَﻣﺮ رﺑِ ُﻜﻢ وأَﻟْ َﻘﻰ ٱﻷَﻟْﻮاح وأَﺧ َﺬ ﺑِﺮأْ ِس أ‬
َ َ‫َﺧ ِﻴﻪ َﳚُﱡﺮﻩُ إِﻟَْﻴ ِﻪ ﻗ‬
‫ﺎل ٱﺑْ َﻦ أُﱠم إِ ﱠن‬ َ َ َََ َ ْ َّ َ ْ ْ َ
809

‫َﻋ َﺪآءَ َوﻻَ َْﲡ َﻌ ْﻠ ِﲎ َﻣ َﻊ ٱﻟْ َﻘ ْﻮِم‬ َِ ‫ﺖ‬


ْ ‫ﰉ ٱﻷ‬ ِ
ُ ‫ﻀ َﻌ ُﻔ ِﻮﱏ َوَﻛ‬
ْ ‫ﺎدواْ ﻳَـ ْﻘﺘُـﻠُﻮﻧَِﲎ ﻓَﻼَ ﺗُ ْﺸﻤ‬ ْ َ‫ٱﺳﺘ‬
ْ ‫ٱﻟْ َﻘ ْﻮَم‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ
ََ ‫ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
Walamma rajaAAa moosa ila qawmihi ghadhbana asifan qala bi/sama
khalaftumoonee min baAAdee aAAajiltum amra rabbikum waalqa al-alwaha
waakhadha bira/si akheehi yajurruhu ilayhi qala ibna omma inna alqawma
istadhAAafoonee wakadoo yaqtuloonanee fala tushmit biya al-aAAdaa wala
tajAAalnee maAAa alqawmi aldhdhalimeena (SuratAl Araf 7:150)

Tafsir: Na kisha aliporejea Musa kwa Watu wake na Hasira na huzuni akasema: ‘Ni
jambo baya sana mlilofanya baada yangu, Hivi (siamini mie kua) ndio mmekimbilia
jambo (la kumtengeneza na kumuabudu) Mungu wenu?’ Na akayaweka (chini)
Maandiko na akamkamata kaka yake kwa (Nywele za) kichwa chake na kumvuta
katika upande wake. (Harun) akasema: ‘Ewe Mtoto wa Mama yangu. Kwa hakika
watu walinichukulia mimi kua ni dhaifu na walikua wanataka kuniua, hivyo
usiwafanye Maadui wafurahike dhidi yangu, na wala usinijumuishe na watu
Madhalimu.’

Hivyo Nabii Musa alipofika kwa watu wake alikua ni mtu ambae amejawa na hasira
ambayo iliamabatana na huzuni, kwani ingawa alikua ameshaambiwa na Mola wake hapo
kabla kuhusiana na yaliyotokea kwa watu wake na alikua ni mweye kuamini maneno
aliyoambiwa na Mola wake, lakini sasa alikua hajaona uhalisi wa jambo hilo kwa macho
yake, na kama tunavyojua kua kusikia si kuona, kwani ni baada ya kuona kwa macho
yake basi ndio akathibitisha aliyoambiwa huku akiwa hayaamini macho yake juu ya kile
inayoyathibitisha.

Na hivyo hapo hapo akayaweka chini maandiko aliyopewa na Mola wake, ambayo ni
kwa ajili ya watu wake ambao hata hivyo kwa wakati huo walikua tayari washaanza
kumkana kua si watu wake, ambapo katika kuelezea tukio hili basi Allah Subhanah wa
Ta’ala amtumia neno Alqa ambalo ambalo linatokana na neno Laqiya lenye kumaanisha
Kulaki yaani Kupokea Kitu au Mtu, Kukutana na Mtu au Kitu, Kukipitia Kitu,
Kukitegemea, Kukumbana na Kitu, Kuegemea Kitu, Kuelekea katika Muelekeo
Unaoelekea Kitu au Unaokabiliana na Kitu n.k.

Ambapo neno Alqa hua linamaanisha Kutupa, Kuangusha, Kuweka chini, Kutoa kitu au
Ushauri, Kuweka Kitu Chini au kwenye sehemu fulani. Ambapo neno Alqa ndio pia
lililotumika katika aya isemayo:
810

‫ﺖ َﻋﻠَْﻴ ِﻪ ﻓَﺄَﻟْ ِﻘ ِﻴﻪ ِﰱ ٱﻟﻴَِّﻢ َوﻻَ َﲣَ ِﺎﰱ‬


ِ ‫﴿وأَوﺣﻴـﻨَﺂ إِ َ ٰﱃ أُِم ﻣﻮﺳﻰ أَ ْن أَر ِﺿﻌِ ِﻴﻪ ﻓَِﺈ َذا ِﺧ ْﻔ‬
ْ َٰ ُّ َْ ْ َ
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ِ ِ ‫وﻻَ َْﲢﺰِ ۤﱐ إِ ﱠ� رآ ﱡدوﻩ إِﻟَﻴ‬
َ ‫ﻚ َو َﺟﺎﻋﻠُﻮﻩُ ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻤْﺮ َﺳﻠ‬ ْ ُ َ َ َ
Waawhayna ila ommi moosa an ardhiAAeehi fa-idha khifti AAalayhi faalqeehi fee
alyammi wala takhafee wala tahzanee inna raddoohu ilayki wajaAAiloohu mina
almursaleena (Surat Al Qasas 28:7)

Tafsir: Na tukamshushia Wahyi mama yake Musa (kumwambia): ‘Mnyonyeshe


(Musa), lakini kama ikiwa utakhofia juu yake, basi mtie mtoni na wala usiwe na khofu
yeyote wala huzuni. Kwani kwa hakika sisi tutamrudisha kwako wewe na tutamfanya
kua ni miongoni mwa Mitume wetu’.

Ndio pia lililotumika katika aya ifuatayo ambayo inasema:

﴾‫ﻮﺳ ٰﻰ‬ ِ َ َ‫﴿ﻗ‬


َ ُ‫ﺎل أَﻟْﻘ َﻬﺎ ٰﳝ‬
Qala alqiha ya moosa (Surat Ta-Ha 20:19)

Tafsir: Akasema (Allah) Itupe (Fimbo yako hio) ewe Musa.

Hivyo hapa inawezekana ikawa aliyatupa maandiko hayo kwa hasira, lakini pia
inawezekana kua aliyaweka chini kutokana na kujua utukufu wa Maandiko hayo, ambapo
mtizamo wa kua aliweka chini ndio unaoingia akilini zaidi na hii ni kutokana utukufu wa
Mandiko hayo, Utukufu wa Nabii Musa na Ikhlas aliyokua nayo kwa Mola wake. Wa
Allahu Aalam.

Na kisha baada ya hapo basi Nabii Musa akamkamata na kumshugulikia yule ambae
alimkabidhi Madaraka yake kua ndie msimamizi wa watu wake pale atakapokua hayupo
yaani Nabii Harun, kwani inabidi ajibu masuali yanayostahiki kujibiwa mbele yake Nabii
Musa.

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala analielezea tena tukio hilo kwa mtizamo wa upande
mwengine kwa kusema:
811

‫ﺎل ٰﻳﭑﺑْـﻨَﺄُِّم‬ ِ ۤ ‫ﺎل ٰﻳـﻬﺮون ﻣﺎ ﻣﻨـﻌﻚ إِ ْذ رأَﻳـﺘـﻬﻢ ﺿﻠﱡ‬


َ َ‫ﺖ أ َْﻣ ِﺮي۞ﻗ‬ ‫ﻴ‬ ‫ﺼ‬
َ َْ َ َ‫ﻌ‬‫ـ‬َ‫ﻓ‬َ‫أ‬ ِ
‫ﻦ‬ ‫ﻌ‬‫ﺒ‬‫ﱠ‬‫ﺘ‬ ‫ـ‬
َ ‫ﺗ‬ ‫ﱠ‬
‫ﻻ‬ َ
‫أ‬ ۞ ْ‫ا‬
‫ﻮ‬ َ ْ ُ َْ َ َ َ َ َ َ ُ ُ َ َ َ‫﴿ﻗ‬
ِ‫ﻮل ﻓَـﱠﺮﻗْﺖ ﺑـﲔ ﺑ ِ ۤﲏ إِﺳﺮآﺋ‬ ِ ‫ﻻَ َﺄﺗْﺧ ْﺬ ﺑِﻠِﺤﻴ ِﱴ وﻻَ ﺑِﺮأْ ِﺳﻰ إِِﱏ ﺧ‬
ْ‫ﻴﻞ َوَﱂ‬
َ َ ْ َ َ ْ َ َ َ ‫ﻘ‬
ُ ‫ـ‬
َ‫ﺗ‬ ‫َن‬‫أ‬ ‫ﻴﺖ‬
ُ ‫ﺸ‬ َ ّ َ َ َْ ُ
﴾‫ﺐ ﻗَـﻮِﱄ‬
ْ ْ ُ‫ﺗَـْﺮﻗ‬
Qala ya haroonu ma manaAAaka idh raaytahum dhalloo; Alla tattabiAAani
afaAAasayta amree; Qala yabnaomma la ta/khudh bilihyatee wala bira/see innee
khasheetu an taqoola farraqta bayna banee isra-eela walam tarqub qawlee(Surat
Taha 20:92-94)

Tafsir: ‘Akasema (Nabii Musa baada ya kukamata Nabii Harun): ‘Ewe Harun
unamaana gani ulipowaona wanapotoka (nawe ukawaachia)?’(Kwanini)
Hukunifuata mimi? Umeasi Maamrisho yangu?’ Akasema (Nabii Harun): ‘Ewe
Mtoto wa Mama yangu, usinikamate Ndevu zangu wala Kichwa changu, kwani kwa
Hakika mimi ilikua nna khofu ya kua utaniambia kua: ‘Umefarakanisha baina ya
watu wa Bani Israil, na hivyo hukuheshimu kauli yangu’’

Ambapo anasema Imam Muhammad Ibn Jarir At Tabari kua: ‘Nabii Harun ametumia
neno ‘Ibn Ummi’ yaani ‘Mtoto wa Mama yangu’ badala ya ‘Ibn Abi’ yaani ‘Mtoto
wa Baba yangu’ kwa sababu ya Kumlainisha Nabii Musa apunguze hasira zake
kwake, ambapo hii hua ni sawa na Waarabu wanapokua wanabishana hua ni wenye
kuambiana ‘Ya Ibn Al Halal’ yaani ‘Ewe Mtoto wa Halali’ ili kupunguzana hasira.’

Na kwa upande mwengine basi Nabii Harun ametumia kauli hii kwa sababu ya umuhimu
wa kua Udugu wao si wa Kiimani tu lakini pia Udugu wao unatoka kwa Mama ambae
ndie aliewazaa na hivyo wote wawili kwa pamoja mmoja baada ya mwenzake kua ni
waliolala kwenye Mfuko mmoja wa Uzazi wa Mama yao.

Na hapa pia aya zinatuonesha umuhimu wa kutosababisha Ufa katika jamii, kwani
kusababisha huko huenda kukapelekea kibuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe
katika jamii usika kama vile ilivyokua katika ardhi nyingi za jamii za Kiislam leo hii,
kwa mfano nchini Syria, Yemen, Libya, Afghanistan,n.k ambapo madhara yake hua ni
makubwa zaidi kma tunavyoona wanavyodhalilika na kudhurika Waislam wengi leo hii,
wakiwemo Wanawake na Watoto ambapo Wanawake Wajane wa Kiislam wa maeneo
hayo wanafikia Kuuza Miili yao, kwa ajili ya kutokana na kukosa Watu wa kuwasaidia
katika kujipatia mahitaji yao ya kila siku ya Familia zao.
812

Na Wanawake na Watoto ndio wenye kufikwa na mitihani mikubwa zaidi baada ya


kutokea nyufa katika Jamii zinazosababisha mapigano ya Waislam wenyewe kwa
wenyewe. Na nio maana Nabii Harun akasema kumwambia Nabii Musa kua: ‘Innee
khasheetu an taqoola farraqta bayna banee isra-eela’ yaani ‘Hakika mimi ilikua nna
khofu ya kua utaniambia kua: ‘Umefarakanisha baina ya watu wa Bani Israil’

Na kwa upande mwengie tunaona kua Nabii Harun anamwambia Nabii Musa kua alikua
akijaribu kuokoa Maisha yake na kusimamia Umoja wa watu wake kwa vyenginevyo
basi miongoni mwa watu hao wenye misimamo mikali wangemuua kama angejaribu
kuwazuia wasiabudie Ndama wao basi ingekua balaa zaidi, kwani zuio lake hilo
lisingepelekea yeye kupoteza maisha yake tu, lakini pia vingetokea vita vikubwa baina
ya watu wanaomuunga mkono yeye na Nabii Musa na watu wa Samirii, ambao walikua
ni mara kumi zaidi yao kiidadi.

Na ndio maana akasema: ‘Ibna omma inna alqawma istadhAAafoonee wakadoo


yaqtuloonanee fala tushmit biya al-aAAdaa wala tajAAalnee maAAa alqawmi
aldhdhalimeena yaani ‘Ewe Mtoto wa Mama yangu. Kwa hakika watu walinichukulia
mimi kua ni dhaifu na walikua wanataka kuniua, hivyo usiwafanye Maadui
wafurahike dhidi yangu, na wala usinijumuishe na watu Madhalimu.’

Baada ya Nabii Harun kujitetea kwa kutoa hoja nzito, basi moja kwa moja Nabii Musa
akamgeukia mhusika mkuu ambae ndie muanzilishi wa mpasuko baina ya watu wa Bani
Israil ambae ni Samirii mwenyewe, na kumuuliza:

‫ﻚ ٰﻳ َﺴ ِﺎﻣ ِﺮ ﱡ‬
﴾‫ي‬ َ َ‫﴿ﻗ‬
َ ُ‫ﺎل ﻓَ َﻤﺎ َﺧﻄْﺒ‬
Qala fama khatbuka ya samiriyyu; (Surat Taha 20:95)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa) ‘Jee ni nini Khutba yako Ewe Samirii’

Aya imetumia Neno Khutba ambalo ingawa hua tunaitafsiri kama Khutuba lakini
kwaupande mwengine hua pia linamaanisha Kuzungumza, Kutoa Nasaha,Usia wa
Maneno, Kutia Mori kwa maneno, Kufunga Ndoa, Kuanzisha Jambo, Kitu, Mpango au
Biashara, Jambo au Kitu au Makusudio au Malengo ambayo mtu hua ana hamu nayo
kuyafanya au kuyafikia.

Hivyo kwa kua Nabii Musa alikua hajui ilikua kuaje mpaka Samirii akafikia kuwapotosha
wenzake kwa kuwatengenezea Sanam hilo, hivyo akamuuliza Samirii: ‘Jee ni nini
Malengo yako uliyokususdia kufanya Ewe Samirii mpaka ukaamua Kutengeneza
sanamu hili la Ndama huyu, na hivyo kuwapotosha wenzako wote?’
813

Ambapo Samirii akamwambia Nabii Musa kua: ‘Hakika mimi nimeona lile ambalo
wengine hawakuweza kuliona, kutokana na kua Mpandaji Farasi alikua ni Malaika
Jibril, basi nikachukua athari ya kwato ya Farasi huyo na kisha nikafanya kile
ambacho Nafsi yangu imenielekeza nifanye kutokana na Matamanio yake na hivyo
nikanyunyizia mchanga wenye athari hio kwenye Moto uliochomewa dhahabu na
Matokeo yake akatokea Ndama huyo, na kadhalika Nafsi yangu ikaniambia kua
huyu Ndio Mungu wangu.’

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea juu ya haya kwa kusema:

ِ ِ ‫ﻀﺔً ِﻣﻦ أَﺛَِﺮ ٱﻟﱠﺮﺳ‬ ْ َ‫ﺼُﺮواْ ﺑِِﻪ ﻓَـ َﻘﺒ‬ ِ ‫ﺎل ﺑﺼﺮ‬
َ ‫ﻮل ﻓَـﻨَـﺒَ ْﺬﺗـُ َﻬﺎ َوَﻛ ٰﺬﻟ‬
‫ﻚ‬ ُ ْ ّ َ ‫ﺖ ﻗَـْﺒ‬ُ‫ﻀ‬ ُ ْ ُ َ َ َ‫﴿ﻗ‬
ُ ‫ت ﲟَﺎ َﱂْ ﻳـَْﺒ‬
﴾‫ﺖ ِﱃ ﻧَـ ْﻔ ِﺴﻲ‬ْ َ‫َﺳ ﱠﻮﻟ‬
Qala basurtu bima lam yabsuroo bihi faqabadhtu qabdhatan min athari alrrasooli
fanabadhtuha wakadhalika sawwalat lee nafsee; (Surat Taha 20:96)

Tafsir: Akasema : Samirii ‘Hakika mimi nimeona kile ambacho hawajakiona wengine,
na kisha nikachukua vinavyochukuliwa kutokana na athari ya (kwato ya Farasi wa)
Mjumbe (Jibril) Nikarushia (Ndani ya Moto uliokua na Dhahabu za watu wa Misri)
Kadhalika hivyo ndivyo ilivyoniamrisha Nafsi yangu’

Ama tunapoangalia kuhusiana na hali aliyoielezea Samiri ya kua alimuona Mtume yaani
Malaika Jibril na akachukua athari za kwato za Farasi wake, basi mbali ya kua jambo hili
linawezekana ikawa kama walivyosema Maimamu kama Imam Ismail Abd Rahman Al
Suddi, Imam Ahmad Ibn Muhammad Ath Thalabi na wengineo kua Samiri alilelewa na
Malaika Jibril na ndio maana akamjua, lakini kwa upande mwengine pia kutokana na
Hikma zake Allah Subhanah wa Ta’ala hua anawajaalia waja wake kua na uwezo huo
wa kuwaona viumbe wa Ulimwengu usiooekana na mtu kawaida kama Malaika, kwa
Mfano Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Al Ghazali, Imam Abdul Qadir
Al Jaylani, Imam Abu Hasan Al Shadhili, Shaykh Al Akbar Imam Ibn Arabi, na
wengineo.

Ambapo kwa baadhi yao, tukio hili hua ni Neema na kwa baadhi yao hua ni laana,
ambapo mfano wa kua ni laana hua ni kama huu wa Samirii, na miongoni mwa mfano
wa Neema na Rehma hua kama ule wa Shaybah Ibn Uthman Radhi Allahu Anhu ambae
alikua ndio kwanza amesilimu na hivyo katika vita vya Hunayn aliingiwa na ushawishi
814

wa kulipiza kisasi cha Kuuliwa baba yake na kaka yake, kwa kumuua Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam.

Na hivyo alipopata nafasi hio ya kua peke yake na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
bsi akamua kuitumia, lakini alipomkaribia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi
akaona mwangaza kama wa radi baina yake na baina ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
Salam, hivyo akarudi nyuma na kuziba macho yake kutokana na ukali wa Mwangaza
huo.

Na hapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akageuka na akamuona Shaybah Ibn
Uthman Radhi Allahu Anhu na akajiuliza mbona Shayba haendi kwenye uwanja wa
Mapambano, hivyo akadhani kua Shaytan amemshawishi Shaybah Ibn Uthman Radhi
Allahu Anhu Radhi Allahu Anhu kukimbia mapigano hivyo akasema: ‘Ya Allah,
Muondolee Shaytan!’ na kisha akamwambia Shaybah Radhi Allahu Anhu: ‘Shayba!
Nenda kakabiliane na Makafiri’.

Shaybah Ibn Uthman Radhi Allahu Anhu alipogeuka na kutaka kuelekea kwenye
mapambano basi ghafla akasita tena na kusema; ‘Ya Rasul Allah hakika mimi naona
Farasi mzuri sana mbele yangu’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema:
‘Ewe Shaybah hakuna anaewaona hao isipokua yule aliekua hakuniamini’ kisha
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akauweka mkono wake kwenye kifua cha
Shaybah Ibn Uthman Radhi Allahu Anhu na kusema mara tatu: ‘Ya Allah! Muongoze
Shaybah.’

Ambapo tunapokiangalia kisa hiki cha Shaybah Ibn Uthman Radhi Allahu Anhu basi
tunaona kua mara ya kwanza alipotaka kumuua Rasul Allah Salallahu A’lyhi wa Salam
basi aliona yasiyoonekana na watu wengine yaani hio Nuru ambayo lilikua ni Ngao
inayomkinga Rasul Allah Salam dhidi ya madui zake na inaweza ikawa inatokana na
Ulinzi mkali wa Malaika wanaomlinda adhihurike na hali kama hi pia iliwahi kumtokea
Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu kabla ya kuslimu kwake pale katika Vita vya
Khandak ambapo alihadithia kwa kusema kua: ‘Hakika mimi nilimuona Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam ambae alikua akisalisha na nilikua nna uhakika kua
naweza kuingia katika kambi ya Maadui na kumuua na kisha nikakimbia bila ya
Madhara yeyote, lakini sasa kila nikitaka kuchukua hatua hio, basi nilikua nahisi
kua kuna nguvu za aina fulani ambazo ni nzito sana zinanizuia kufanya jambo hilo,
mpaka nilipoamua kuachana nalo wazo hilo.’

Ambapo tukio la pili la Shaybah Ibn Uthman Radhi Allahu Anhu la kumuona Farasi
Mzuri mbele yake na hivyo kua ni mwenye kumzuia asiende kupigana na Makafiri basi
alikua akimuona Shaytan ambae ndie aliekua akimzuia asitekeleze maamrisho ya Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam.
815

Na kwa upande wa Mujaddid Ad Din Sultan Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi
basi yeye anatuelezea pia mtizamo mwengine na hivyo kua ni mwenye kusema kua:
‘Neno Athar linamaanisha hua linamaanisha pia athari ya kauli au kivitendo au
mafunzo ya mtu fulani kwa ujumla, hivyo maneno yasemayo: ‘Faqabadhtu
qabdhatan min athari alrrasooli fanabadhtuha’ hua pia inaweza kumaanisha kua:
‘Kisha nikachukua miongoni mwa mafunzo ya Mtume na kutumia’ hivyo
inawezekana kua Mtume aliekusudiwa hapa ambae zimetumiwa athari yake hakua
mwengine isipokua ni Nabii Musa mwenyewe. Hivyo basi Samirii alikua
akimaanisha kua yeye hakufanya jambo lolote isipokua amefanya kile ambacho
alikua akifanya Nabii Musa’

Ambapo tunaona kua Mujaddid Ad Din Sultan Mutakallimin Imam FakhrAd Din Al Razi
amefafanua hivyo kwa mtizamo mwengine, kwa sababu ya maana ya neno Athari ambalo
pia tulilifafanua hapo kabla maana yake pale lilipotumika katika aya ifuatayo:

﴾‫ﺿﻰ‬ ِ‫ب ﻟ‬
ِ ِ ِ ‫ﺎل ﻫﻢ أُو ۤﻻ ِء ﻋﻠَﻰ أَﺛَِﺮى وﻋ‬
‫ﺮ‬‫ـ‬ ‫ﺘ‬ ‫ر‬ ‫ﻚ‬‫ﻴ‬َ‫ﻟ‬
َ َْ ّ َ َ ْ ُ َ َ‫إ‬ ‫ﺖ‬‫ﻠ‬ْ ‫ﺠ‬ ٰ َ ْ ْ ُ َ َ‫﴿ﻗ‬
Qala hum ola-i AAala atharee waAAajiltu ilayka rabbi litardha(Surat Ta-Ha 20:84)

Tafsir: Wao wanafuata Athari zangu, hivyo nikakimbilia kwa ajili yako Mola wangu
ili Uniridhie.’

Hivyo hapa kwa mtizamo wa Mujaddid Ad Din Sultan Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din
Al Razi basi tunaweza kusema pia kua Samirii alikua si mwenye kumuamini Nabii Musa
na si mwenye kumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo basi alikua akimuona
Nabii Musa kua si mwenye kufanya Miujiza bali ni mweye kufanya Uchawi hivyo na
yeye kwa mtizamo wake huo basi akaona kua anafanya kama alivyokua akifanya Nabii
Musa, kwani hivyo ndivyo ilivyo muamrisha Nafsi yake ingawa alikua hayuko sahih
kutokana na mtizamo wake huo.

Na hivyo baada ya Nabii Musa kuliona hilo la kua Samirii hakuwa ni mwenye kumuamini
yeye wala hakumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala basi akasema kama zinavyosema
aya:
816

‫ﻚ َﻣ ْﻮﻋِﺪاً ﻟﱠﻦ‬ َ َ‫ﺎس َوإِ ﱠن ﻟ‬ ِ َ ‫ٱﳊﻴﺎةِ أَن ﺗَـ ُﻘ‬ َ َ‫ﺐ ﻓَِﺈ ﱠن ﻟ‬
َ ‫ﻮل ﻻَ ﻣ َﺴ‬ ََْ ‫ﻚ ِﰱ‬ ْ ‫ﺎل ﻓَﭑ ْذ َﻫ‬َ َ‫﴿ ﻗ‬
ِ َ‫ﻚ ٱﻟﱠ ِﺬى ﻇَْﻠﺖ ﻋﻠَﻴ ِﻪ ﻋﺎﻛِﻔﺎً ﻟﱠﻨُﺤ ِﺮﻗَـﻨﱠﻪ ﰒُﱠ ﻟَﻨ‬
‫ﻨﺴ َﻔﻨﱠﻪُ ِﰱ ٱﻟْﻴَِّﻢ‬ َ ‫ُﲣْﻠَ َﻔﻪُ َوٱﻧﻈُْﺮ إِ َ ٰﱃ إِﻟَـٰ ِﻬ‬
ُ َّ َ َْ َ
﴾ً‫ﻧَﺴﻔﺎ‬
ْ
Qala faidhhab fa-inna laka fee alhayati an taqoola la misasa wa-inna laka
mawAAidan lan tukhlafahu waondhur ila ilahika alladhee dhalta AAalayhi
AAakifan lanuharriqannahu thumma lanansifannahu fee alyammi nasfan (Surat
Ta-Ha 20:97)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa kumwambia Samirii): ‘Ondoka. Kwani kwa hakika
(Adhabu yako) katika Maisha haya utakua unasema; ‘Usiniguse’ na (kwa adhabu
yako ya baadae) ni kua kuna ahadi ambayo haitowezekana kutokua na Muangalie
Mungu wako ambae umejidhalilisha kumuabudia juu yake, kwani tutamchoma
Moto kisha tutayatawanya mabaki yake kwenye bahari’

Hiyo Nabii Musa akamfukuza Samirii kutoka katika jamii ya Watu wa Bani Israil na
kutokana na laana aliyolaaniwa na Nabii Musa basi Samirii akawa ni mwenye kujitenga
nao watu hao, na watu wa Bani Israil Walijitenga nae kwani hali yake ilikua mbaya kiasi
ya kua kila mtu anaegusana nae basi mtu huyo hua ni mwenye kuugua Maradhi yenye
maumivu makali sana yasiyojulikana, na yeye pia alikua kila akigusana na watu basi hua
na maumivu makali zaidi, hivyo akawa ni wenye kuwaambia watu kua wasimguse., na
Sanam lake likachomwa Moto lote na jivu lake likaingizwa ndani ya Mto.

Baada ya kumalizika kwa Hukmu hio basi watu wa Bani Israil waliokua wakifuata
mtizamo wa Samirii na kupotoshwa wakaanza kujuta kutokana na waliyoyafanya kama
zinavyobainisha aya:

‫ﺿﻠﱡﻮاْ ﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻟَﺌِﻦ ﱠﱂْ ﻳَـْﺮ َﲪْﻨَﺎ َرﺑـﱡﻨَﺎ َوﻳَـ ْﻐ ِﻔْﺮ ﻟَﻨَﺎ‬ ِ ۤ ِ
َ ‫﴿ َوﻟَ ﱠﻤﺎ ُﺳﻘ َﻂ َﰲ أَﻳْﺪﻳ ِﻬ ْﻢ َوَرأ َْواْ أَﻧـﱠ ُﻬ ْﻢ ﻗَ ْﺪ‬
﴾‫ﺎﺳ ِﺮﻳﻦ‬ ِ ْ ‫ﻟَﻨَ ُﻜﻮﻧَ ﱠﻦ ِﻣﻦ‬
َ َ‫ٱﳋ‬ َ
Walamma suqita fee aydeehim waraaw annahum qad dhalloo qaloo la-in lam
yarhamna rabbuna wayaghfir lana lanakoonanna mina alkhasireena (Surat Al Araf
7:149)
817

Tafsir: Na kisha (Watu wa Bani Israil) wakajuta kutokana na waliyoyafanya kwa


mikono yao na kuona kua wamepotea basi wakasema: ‘Kama hajatuingiza kwenye
Rehma zake Mola wetu na akatusamehe basi kwa hakika tutakua miongoni mwa
waliokula hasara.’

Hapa tunaona pia kua aya inawazunumzia wau wa Bani Isail kwa kusema kua Walamma
Suqita fii Aydiihim ambapo neno Suqita hua linamaanisha Kuanguka, Kuanguka Chini,
Kusababishia Kuanguka, Kuvunjika kwa kitu kilichokua kimesimama na kisha kuanguka
chini kutokana na mvunjiko huo.

Hivyo Suqita fii Aydiihim hua kunamaanisha Kuvunjika na kuanguka kwa jambo
kutokana na uzito wake ndani ya mikono ya wabebaji, yaani Kuchukua kitu
kilichodhaniwa kua kina thamani kubwa na kisha kuachiwa kianguke kutokana na
kuonekana kua kume kitu hicho hakina thamani yeyote bali kina madhara mkubwa sana
ndani yake, na hivyo wabebaji hao waliobeba kitu hicho hua hawabakiwi na kitu
chengine chochote isipokua hubakiwa na Majuto makubwa sana, juu ya kwanini
wakakibeba kitu hicho, na kwanini hawakuachana nacho tangu hapo awali.

Hivyo kutokana na kua na hali hio basi watu wa Bani Israil ndio wakasema: La-in lam
yarhamna rabbuna wayaghfir lana lanakoonanna mina alkhasireena yaani Kama
hajatuingizwa kwenye Rehma zake Mola wetu na akatusamehe basi kwa hakika
tutakua miongoni mwa waliokula hasara.

Ambapo baada ya kuchunguza chanzo cha matatizo na kutoa hukmu yake basi Nabii
Musa akarudi kwa Mola wake na kumuomba msamaha kwa ajili yake na kwa ajili ya
ndugu yake kutokana na makosa yao waliyoyafanya kwa kusema:

﴾‫ﲔ‬ ِِ ِ ‫ب ٱ ْﻏ ِﻔﺮ ِﱃ وِﻷ‬


َ ِ‫َﺧﻰ َوأ َْد ِﺧ ْﻠﻨَﺎ ِﰱ َر ْﲪَﺘ‬ ِ َ َ‫﴿ﻗ‬
َ ‫َﻧﺖ أ َْر َﺣ ُﻢ ٱﻟﱠﺮاﲪ‬
َ ‫ﻚ َوأ‬ َ ْ ّ ‫ﺎل َر‬
Qala rabbi ighfir lee wali-akhee waadkhilna fee rahmatika waanta arhamu
alrrahimeena (Surat Al Araf 7:151)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa): Ewe Mola wangu nisamehe mimi na Kaka yangu,
na utuingize kwenye Rehma zako, kwani kwa hakika wewe ni mwingi wa Rehma
miongoni mwa wenye Rehma.

Allah Subhanah wa Ta’ala akamsamehene Nabii Musa na Nabii Harun kwa makosa yao
waliomba wamasehewe kisha baada ya hapo Allah Subhanah wa Ta’ala akasema
kumwambia Nabii Musa kua:
818

‫ٱﳊَﻴﺎةِ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ‬
ْ ‫ﺐ ِّﻣﻦ ﱠرّﻬﺑِِ ْﻢ َوِذﻟﱠﺔٌ ِﰱ‬ ِ ِ ‫﴿ِ ﱠ‬
ٌ‫ﻀ‬ َ ‫ﻳﻦ ﱠٱﲣَ ُﺬواْ ٱﻟْﻌ ْﺠ َﻞ َﺳﻴَـﻨَﺎ ُﳍُْﻢ َﻏ‬
َ ‫إ ﱠن ٱﻟﺬ‬
﴾‫ﻚ َْﳒ ِﺰى ٱﻟْﻤ ْﻔ َِﱰﻳﻦ‬ ِ
َ ُ َ ‫َوَﻛ ٰﺬﻟ‬
Inna alladheena ittakhadhoo alAAijla sayanaluhum ghadabun min rabbihim
wadhillatun fee alhayati alddunya wakadhalika najzee almuftareena; (Surat Al Araf
7:152)

Tafsir: Kwa hakika wale ambao walimchukua Ndama (kwa ajili ya kumuabudia) basi
karibuni watafikwa na ghadhabu kutoka kwa Mola wao na watadhalilika katika
maisha haya ya Dunia na hivyo ndivyo tunavyowalipa waanzishaji wa uovu.

Ambapo aya inatuonesha kua Allah Subhanah wa Ta’ala hakuwasamehe watu hao wa
Bani Israil, mpaka ipitishwe hukmu yake dhid iyao kutokana na Uovu wao wa
Kumshirikisha na Hivyo Nabii Musa akawaambia watu wake hao ni kitu gani cha
kufanya ili wapate kusamehewa, kama zinavyosema aya:

‫ﻮﺳ ٰﻰ ﻟَِﻘ ْﻮِﻣ ِﻪ‬


َ ‫ﺎل ُﻣ‬ َ َ‫۞وإِ ْذ ﻗ‬ َ ‫ن‬
َ ‫و‬ ‫ﺪ‬
ُ ‫ﺘ‬
َ ‫ﻬ‬
ْ ‫ـ‬
َ ‫ﺗ‬ ‫ﻢ‬
ْ ‫ﻜ‬
ُ ‫ﱠ‬
‫ﻠ‬ ‫ﻌ‬
َ ‫ﻟ‬
َ ‫ن‬
َ ‫ﺎ‬َ‫ﻗ‬
‫ﺮ‬ ‫ﻔ‬
ُ
ْ َ ‫ﻟ‬
ْ ‫ٱ‬
‫و‬ ‫ﺎب‬
َ َ‫ﺘ‬ ِ‫﴿وإِ ْذ آﺗَـﻴـﻨَﺎ ﻣﻮﺳﻰ ٱﻟْﻜ‬
َ ُ ْ َ
‫ﭑﲣَ ِﺎذ ُﻛ ُﻢ ٱﻟْﻌِ ْﺠ َﻞ ﻓَـﺘُﻮﺑـُ ۤﻮاْ إِ َ ٰﱃ َﺎﺑ ِرﺋِ ُﻜ ْﻢ ﻓَﭑﻗْـﺘُـﻠُ ۤﻮاْ أَﻧ ُﻔ َﺴ ُﻜ ْﻢ‬ِّ ِ‫َ�ﻗَـ ْﻮِم إِﻧﱠ ُﻜ ْﻢ ﻇَﻠَ ْﻤﺘُ ْﻢ أَﻧْـ ُﻔ َﺴ ُﻜ ْﻢ ﺑ‬
﴾‫اب ٱﻟﱠﺮِﺣﻴﻢ‬ ِ ِ ِ
ُ ُ ‫ﺎب َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ إِﻧﱠﻪُ ُﻫ َﻮ ٱﻟﺘﱠـ ﱠﻮ‬ َ َ‫ٰذﻟ ُﻜ ْﻢ َﺧْﻴـٌﺮ ﻟﱠ ُﻜ ْﻢ ﻋْﻨ َﺪ َﺎﺑ ِرﺋ ُﻜ ْﻢ ﻓَـﺘ‬
Wa-idh atayna moosa alkitaba waalfurqana laAAallakum tahtadoona;Wa-idth
qala moosa liqawmihi ya qawmi innakum dhalamtum anfusakum biittikhadhikumu
alAAijla fatooboo ila bari-ikum faoqtuloo anfusakum dhalikum khayrun lakum
AAinda bari-ikum fataba AAalaykum innahu huwa alttawwabu alrraheemu (Surat
Al Baqara 2:53-54)

Tafsir: Na kumbuka tulipompa Musa Kitabu na muongozo ili mpate kuongoka. Na


akasema Musa kuwaambia watu wake: ‘Enyi watu wangu kwa hakika mmejidhulumu
Nafsi zenu kwa kumchukulia (kumuabudu) Ndama, hivyo tubuni kwa Mola wenu kwa
kujiua wenyewe, kwani hivyo ni bora kwenu kwa Mola wenu.’ Na kisha akakubali
Toba yenu kwani kwa hakika yeye ni mwenye kupokea Toba na ni mwingi wa Rehma.

Watu wa Bani Israil wakamwambia Nabii Musa kua: ‘Itawezekanaje kuuna wenyewe
kwa wenyewe, hilo ni jambo gumu sana kwani mongoni mwetu mna wazee wetu,
819

ndugu zetu,watoto wetu na majirani zetu.’ Nabii Musa akawambia kua: ‘Hio ndio
njia pekee ya kujisafisha kutokana na makosa mliyoyafanya, na mtaweza kwa
sababu Damu yenu tayari imeshakua halali kumwagwa, hivyo atakaekataa kuawa
basi toba yake haitokubaliwa.’

Kisha baada ya hapo Allah Subhaah wa Ta’ala akashusha kiwingu kikubwa sana
ambacho ukungu wake ulikua mkubwa sana kiasi ya kua Watu wa Bani Israil
hawakuweza kuonana, na hivyo wakaanza kushambuliana na kuuana wenyewe kwa
wenyewe.

Mapigano hayo yaliendelea kwa masaa kadha, kisha Nabii Musa na Nabii Harun
wakaomba dua, kwa Allah Subhnaha wa Ta’ala kua damu iliyomwagika imetosha, hivyo
Allah Subhnah wa Ta’ala akakiondoa Kiwingu na ukungu wake huo, na hapo watu wa
Bani Israil wakasitisha mapigano hayo, Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Nabii
Musa kua:

‫ﻮر‬ ِ ِ ‫ﺎت ﰒُﱠ َﺎﺗﺑﻮاْ ِﻣﻦ ﺑـﻌ ِﺪﻫﺎ وآﻣﻨـ ۤﻮاْ إِ ﱠن رﺑﱠ‬
ِ ‫﴿وٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻋ ِﻤﻠُﻮاْ ٱﻟ ﱠﺴﻴِﺌ‬
ٌ ‫ﻚ ﻣﻦ ﺑَـ ْﻌﺪ َﻫﺎ ﻟَﻐَ ُﻔ‬
َ َ َُ َ َ ْ َ ُ َّ َ َ َ
﴾‫ﱠرِﺣﻴﻢ‬
ٌ
Waalladheena AAamiloo alssayyi-ati thumma taboo min baAAdiha waamanoo inna
rabbaka min baAAdiha laghafoorun raheemun (Surat Al Araf 7: 153)

Tafsir: Na wale ambao wamefanya Madhambi kisha akatubu baada yake, na akaamini
basi kwa hakika Mola wako ni Mwingi wa Usamehevu na ni mwingi wa Rehma.

Ambapo anasema Imam Ibn Abi Hatim Abd Rahman Ibn Muhammad Ibn Idris Ibn Al
Mundhir Al Hanzali Al Razi Al Shafii kua: ‘Aliulizwa Abd Allah Ibn Masud Radhi
Allahu Anhu kua: ‘Jee kuna Hukmu gani kwa Mtu aliezini na Mwanamke na kisha
akamuoa?’ hivyo Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu akanukuu aya hii,
ambapo watu hao waliomuuliza walimuuliza kama mara kumi lakini nae jibu lake
likawa hilo hilo.’

Imam Abu Hasan Ali Ibn Umar Ibn Ahmad Ibn Mahdi Al Daraqutni anasema husiana na
Mwanamme kumuoa Mwanamke aliezini nae kua amesema Abd Allah Ibn Abbas Radhi
Allahu Anhu kua: ‘Sehemu ya mwanzo ya mahusiano hayo hua ni Al Sifah (Zina) na
ehemu ya pili ya mahusiano hua ni Al Nikaah (Ndoa ya Sharia ya Kiislam)’(Sunan
Ad Daraqutni)
820

Na Imam Abd Razzaq Ibn Hammam Ibn Nafii Al Sana’ni kua: ‘Amesema Abd Allah
Ibn Abbas Radhi Allau Anhu kuhusia na Mwanamme aliezini na Mwanamke na
kisha akamuoa, basi kua: ‘Ndoa ni bora zaidi’ na kwa upande wa Abu Bakr As
Siddiq Radhi Allahu Anhu basi amesema kua: ‘Hakuna Toba bora kama kumuoa,
kwani wote hua wametoka kwenye Zina na kuingia kwenye Nikaah ya
Kiislam.’’(Musannaf Ibn Abd Razzaq)

Tunrudi kwa Nabii Musa na Watu wa Bani Israil na kuona kua baada ya tukio hilo la
kuuana basi Allah Subhaah wa Ta’ala anatuelezea kilichofuatia kwa Nabii Musa kwa
kusema kua:

ٌ‫اح َوِﰱ ﻧُ ْﺴ َﺨﺘِ َﻬﺎ ُﻫ ًﺪى َوَر ْﲪَﺔ‬


َ ‫َﺧ َﺬ ٱﻷَﻟْ َﻮ‬
َ‫ﺐأ‬ ُ‫ﻀ‬ َ َ‫ﻮﺳﻰ ٱﻟْﻐ‬ َ ‫﴿ َوﻟَﻤﺎﱠ َﺳ َﻜ‬
َ ‫ﺖ َﻋﻦ ﱡﻣ‬
﴾‫ﻟِّﻠﱠ ِﺬﻳﻦ ُﻫﻢ ﻟِﺮّﻬﺑِِﻢ ﻳَـﺮَﻫﺒُﻮ َن‬
ْ ْ َ ْ َ
Walamma sakata AAan moosa alghadhabu akhadha al-alwaha wafee nuskhatiha
hudan warahmatun lilladheena hum lirabbihim yarhaboona (Surat Al Araf 7:154)

Tafsir: ‘Na kisha baada ya kua na hali ya Utulivu Musa kutokana na ghadhabu zake
akayachukua maandiko na katika maandiko yake mna Muongozo na Rehma kwa wale
ambao ni wenye kumuogopa Mola wao.’

Nabii Musa akawa ni mwenye kuendelea kukaa na watu wake wa Bani Israil kwa masiku
kadhaa akiwawafindisha makatazo na maamrisho yaliyomo ndani ya Tawrat, lakini
baada ya kupita mda basi watu hao wakaanza kulalamika kua makatazo hayo ni magumu
kwao, hivyo hawawezi kushikamana na maamrisho hayo na makatazo yake mpaka waone
namna Nabii Musa anavyoshushiwa maamrisho hayo, hivyo Nabii Musa akafikisha
ujumbe huo wa watu wake kwa Mola wake, na Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia
Nabii Musa kua achague watu 70 kutoka katika makabila tofauti ya watu wa Bani Israil
na kisha akamwambia kua aende nao watu hao katika Mlima wa Tur,

Hivyo mda ulipowadia basi Nabii Musa akaelekea na watu wake mpaka kwenye Mlima
wa Tur, na walipofika basi Nabii Musa akawawacha watu wake hao chini ya Mlima kisha
yeye akaelekea juu katika eneo alilokubaliana na Mola wake, na mara hapo hapo Allah
Subhanah wa Ta’ala akashusha kiwingu ambacho kiliwafunika watu hao wa Banii Israil
na hivyo wakawa hawawezi kumuona Nabii Musa na wala wao wenyewe hawaonani.

Wakabakia katika hali hio kwa dakika kadhaa kisha wakasikia sauti ambayo walikua
hawaifaham ni ya kitu gani, na kisha hapo hapo likatokea tetemeko kubwa sana la Ardhi
821

hivyo wakaingiwa na khofu kubwa sana na tafrani, hali ambayo walibakia nayo mpaka
aliporudi Nabii Musa kama zinavyosema aya:

ِ ِِ ِ
‫ب ﻟَ ْﻮ‬ ِّ ‫ﺎل َر‬َ َ‫َﺧ َﺬﺗْـ ُﻬ ُﻢ ٱﻟﱠﺮ ْﺟ َﻔﺔُ ﻗ‬
َ ‫ﲔ َر ُﺟﻼً ﻟّﻤﻴ َﻘﺎﺗﻨَﺎ ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ أ‬ َ ‫ﻮﺳ ٰﻰ ﻗَـ ْﻮَﻣﻪُ َﺳْﺒﻌ‬ ْ ‫﴿ َو‬
َ ‫ٱﺧﺘَ َﺎر ُﻣ‬
‫ى أَﺗُـ ْﻬﻠِ ُﻜﻨَﺎ ِﲟَﺎ ﻓَـ َﻌ َﻞ ٱﻟ ﱡﺴ َﻔ َﻬﺂءُ ِﻣﻨﱠﺂ إِ ْن ِﻫﻰ إِﻻﱠ‬َ �‫ﱠ‬ ِ‫ﺖ أ َْﻫﻠَ ْﻜﺘَـ ُﻬﻢ ِّﻣﻦ ﻗَـْﺒﻞ وإ‬
َ ُ ْ َ ‫ﺌ‬
ْ ِ
‫ﺷ‬
َ
‫َﻧﺖ‬ ِ ِ ‫ﻀﻞ ِﻬﺑﺎ ﻣﻦ ﺗَﺸﺂء وﺗَـﻬ ِﺪى ﻣﻦ ﺗَﺸﺂء أ‬ ِ َ ُ‫ﻓِْﺘـﻨَـﺘ‬
َ ‫َﻧﺖ َوﻟﻴﱡـﻨَﺎ ﻓَﭑ ْﻏﻔْﺮ ﻟَﻨَﺎ َو ْٱر َﲪْﻨَﺎ َوأ‬ َ ُ َ َ ْ َ ُ َ َ َ ‫ﻚ ﺗُ ﱡ‬
‫ﻚ‬ ِ ‫ﺧﻴـﺮ ٱﻟْﻐَﺎﻓِ ِﺮﻳﻦ۞وٱ ْﻛﺘُﺐ ﻟَﻨَﺎ ِﰱ ﻫـٰ ِﺬﻩِ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴﺎ ﺣﺴﻨَﺔً وِﰱ‬
َ ‫ٱﻵﺧَﺮةِ إِ ﱠ� ُﻫ ْﺪﻧَـﺂ إِﻟَْﻴ‬ َ ََ َ َ ْ َ َ َُْ
ِِ ٍ ِ َ ‫ﻴﺐ ﺑِِﻪ َﻣ ْﻦ أ‬ ِ ۤ
َ ‫ﺖ ُﻛ ﱠﻞ َﺷ ْﻲء ﻓَ َﺴﺄَ ْﻛﺘُـﺒُـ َﻬﺎ ﻟﻠﱠﺬ‬
‫ﻳﻦ‬ ْ ‫َﺷﺂءُ َوَر ْﲪَِﱴ َوﺳ َﻌ‬ ُ ‫ﺎل َﻋ َﺬ ِاﰊ أُﺻ‬ َ َ‫ﻗ‬
﴾‫ﻳَـﺘﱠـ ُﻘﻮ َن وﻳـُ ْﺆﺗُﻮ َن ٱﻟﱠﺰَﻛ ٰﻮَة وٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ُﻫﻢ ِﺂﺑ َ�ﺗِﻨَﺎ ﻳـُ ْﺆِﻣﻨُﻮ َن‬
َ َ َ
Waikhtara moosa qawmahu sabAAeena rajulan limeeqatina falamma akhadhat-
humu alrrajfatu qala rabbi law shi/ta ahlaktahum min qablu wa-iyyaya atuhlikuna
bima faAAala alssufahao minna in hiya illa fitnatuka tudhillu biha man tashao
watahdee man tashao anta waliyyuna faighfir lana wairhamna waanta khayru
alghafireena; Waoktub lana fee hadhihi alddunya hasanatan wafee al-akhirati inna
hudna ilayka qala AAadhabee oseebu bihi man ashao warahmatee wasiAAat kulla
shay-in fasaaktubuha lilladheena yattaqoona wayu/toona alzzakata waalladheena
hum bi-ayatina yu/minoona (Surat Al Araf 7:155-156)

Tafsir: Na Musa akachagua watu sabini kutoka katika kaumu yake, kwa ajili ya mda
na sehemu ya miadi yetu. na walipofikwa na tetemeko kubwa la ardhi Nabii Musa
akasema: ‘Ewe, Mola wangu kama ungekua unataka basi ungewaangamiza wao na
mimi hapo kabla, hivyo jee utatuangamiza kwa makosa ya baadhi ya wajinga miongoni
mwetu? ni kutokana na mitihani yako ndio humpotosha umtakae, na humuongoza
umtakae. Kwani kwa hakika wewe ni Msimamizi juu yetu, hivyo tusamehe na kua na
Rehma juu yetu. Kwani wewe ni mbora wa kusamehe. Na tuandikie mema katika
Dunia hii na kesho Akhera, kwani kwa hakika sisi tumekugeukia wewe’ . Akasema
(Allah Subhanah wa Ta’ala): ‘Adhabu yangu inamsibu nimtakae, na Rehma zangu
zinafunukika kila kitu. Hivyo nitawaandikia (Rehma) wale wenye Taqwa, na wale
ambao ni wenye kuamini dalili zetu’

Aya zinatuonesha kua wakati Nabii Musa akiwa anazungumza na Mola wake basi alihisi
tetemeko hilo la Ardhi na hivyo akajua kua watu wake hao wa Bani Israil wanataka
822

kuangamizwa hivyo akawa ni mwenye kuwaombea watu wake hao kwa Mola wake.
Lakini hapo hapo Allah Subhanah wa Ta’ala, kwa kua anawajua viumbe wake hao wa
Bani Israil na ubishi wao basi akamwambia Nabii Musa kua bila ya shaka yeye ni mweye
kujua kila kitu na ni mwenye Hikma nyingi sana, ivyo anajua ni nani anaestahiki Rehma
zake na ni nani anaestahiki adhabu zake, hivyo watakaokoka na kuingizwa ndani ya
Rehma zake miongoni mwa watu wake hao basi ni wale watakaomuamini yeye tu.

Hivyo Nabii Musa akarudi kwa watu wake, huku akiwa amebadilika muonekano wake,
kwani amejaa Nuru, na mbali ya kua na mabadiliko hayo lakini watu wake hao
wakalalamika juu ya yaliyotokea, na Nabii Musa akawaambia juu ya aliyoambiwa na
Mola wake, lakini watu hawa 70 wa Bani Israil wakasema kua hawaamini
wanachokisikia kutoka kwa Nabii Musa kama vile ambavyo hawakuamini kuhusiana na
yaliyotokea yote na waliyoyasikia hivyo wakasema: ‘Hakika sisi hatutoamini Mpaka
tumuone wazi wazi Mola wako’

Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea haya kwa kusema:

ِ‫ﺼ‬ َ َ‫ﻮﺳ ٰﻰ ﻟَﻦ ﻧـﱡ ْﺆِﻣ َﻦ ﻟ‬ ِ


ُ‫ﺎﻋ َﻘﺔ‬ ‫َﺧ َﺬﺗْ ُﻜ ُﻢ ٱﻟ ﱠ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟَ َﺟ ْﻬَﺮًة ﻓَﺄ‬
‫ﻚ َﺣ ﱠ ٰﱴ ﻧَـَﺮى ﱠ‬ َ ‫﴿ َوإ ْذ ﻗُـ ْﻠﺘُ ْﻢ َ� ُﻣ‬
﴾‫وأَﻧْـﺘُﻢ ﺗَﻨﻈُﺮو َن۞ﰒُﱠ ﺑَـ َﻌﺜْـﻨَﺎ ُﻛﻢ ِّﻣﻦ ﺑَـ ْﻌ ِﺪ َﻣﻮﺗِ ُﻜﻢ ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜﻢ ﺗَ ْﺸ ُﻜﺮو َن‬
ُ ْ ْ ْ ُ ْ َ
Wa-idh qultum ya moosa lan nu/mina laka hatta nara Allaha jahratan
faakhadhatkumu alssaAAiqatu waantum tandhuroona; Thumma baAAathnakum
min baAAdi mawtikum laAAallakum tashkuroona (Surat Al Baqara 2:55-56)

Tafsir:Na kumbuka waliposema kumwambia Musa : ‘Hakika sisi hatutokuamini


wewe mpaka tumuone Allah waziwazi. Lakini mkapigwa na Radi wakati
mkiangalia’. Na kisha tukakufufueni kutokana na mauti yenu ili muwe ni wenye
kushukuru.

Ambapo baada ya kusema ya Watu wa Bani Israil kusema maneno hayo basi Allah
Subhanaha wa Ta’ala akawashushia Radi ambayo iliwaua watu hao wote, isipokua Nabii
Musa, hivyo Nabii Musa alipoona hali hio basi akashtuka na kisha akamlalamikia Mola
wake kua jee watu wa Bani Israil watamchukulia vipi kama ikiwa hajarudi na watu hao
70 alioondoka nao kisha awaambie kua wamekufa wote kutokana na ubishi wao?

Bila ya shaka ni maumbile ya Ibn Adam kua na khofu kutokana na tukio kama hilo
linapokutokea mbeleya macho yako, hususan mtu unapokua umechukua dhamana juu ya
823

watu hao halafu watu hao wakafa wote mikononi mwako, hivyo kimaumbile basi Nabii
Musa alikua alikua yuko sahih kulalamikia kuhusiana na tukio hilo, na hii nikwa sababu
hakua nimwenyekujua mnahikma gani ndani yake tokeo hilo ambapo Allah Subhanah
wa Ta’ala alikua anataka kuwaonesha uwezo wake juu yao watu hao kua anaweza
kuwaua na kisha kuwafufua na hivyo labda watakua na uwezo wa kutafakkari na hivyo
kua ni wenye kumuamini Muumba wao na kumshukuru baada ya kuwafufua kwao
mmoja mmoja mbele ya Nabii Musa.

Na kisa baada ya kufufuliwa watu hapo basi Allah Subhanah wa Ta’ala akawaonesha
Muujiza mmoja mkubwa ambao ni wa kuunyanyua Mlima wa Tur uliopo mbele yao na
kuuweka ukiwa unaelea angani kidogo juu yao, kisha Allah Subhanah wa Ta’ala
akamwambia Nabii Musa awaaambie watu hao kua wanatakiwa wazingatie na pia
washikamane na maarisho yake kama zinayosema aya:

‫ﻮر ُﺧ ُﺬواْ َﻣﺂ آﺗَـْﻴـﻨَﺎ ُﻛﻢ ﺑُِﻘ ﱠﻮةٍ َوٱذْ ُﻛُﺮواْ َﻣﺎ‬ ِ
َ ‫﴿ َوإِ ْذ أ‬
َ ‫َﺧ ْﺬ َ� ﻣﻴﺜَﺎﻗَ ُﻜ ْﻢ َوَرﻓَـ ْﻌﻨَﺎ ﻓَـ ْﻮﻗَ ُﻜ ُﻢ ٱﻟﻄﱡ‬
﴾‫ﻓِ ِﻴﻪ ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜﻢ ﺗَـﺘﱠـ ُﻘﻮ َن‬
ْ
Wa-idh akhadhna meethaqakum warafaAAna fawqakumu alttoora khudhoo ma
ataynakum biquwwatin waodhkuroo ma feehi laAAallakum tattaqoona (Surat Al
Baqara 2:63)

Tafsir: Na (Kumbukeni) tulipochukua ahadi nzito kutoka kwenu na tukaunyanyua Tur


(Mlima) juu yenu tukisema: ‘Shikamaneni na tulichokupeni na zingatieni yaliyomo
ndani yake ili mpate kua wenye Taqwa.’

Ambapo kikawaida basi tunajua kua Allah Subhanah wa Ta’ala anasema katika Qur’an
kua;

ِ ‫﴿ﻻَ إِ ْﻛﺮاﻩ ِﰱ ٱﻟ ِّﺪﻳ ِﻦ ﻗَﺪ ﺗﱠـﺒـ ﱠﲔ ٱﻟﱡﺮ ْﺷ ُﺪ ِﻣﻦ ٱﻟْﻐَ ِﻰ ﻓَﻤﻦ ﻳ ْﻜ ُﻔﺮ ﺑِﭑﻟﻄﱠﺎﻏُﻮ‬
‫ت َوﻳْـ ْﺆِﻣﻦ‬ ْ َ َْ ّ َ ََ ََ
﴾‫ﻴﻊ َﻋﻠِ ٌﻴﻢ‬ ِ ‫ٱﻧﻔﺼﺎم َﳍﺎ و ﱠ‬ ِ ِ ِ ‫ﭑﻪﻠﻟِ ﻓَـ َﻘ ِﺪ ٱﺳﺘﻤﺴ‬ ‫ﺑِ ﱠ‬
ٌ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﲰ‬ َ َ َ َ َ‫ﻚ ﺑﭑﻟْﻌُْﺮَوة ٱﻟْ ُﻮﺛْـ َﻘ ٰﻰ ﻻ‬ َ َ ْ َْ
La ikraha fee alddeeni qad tabayyana alrrushdu mina alghayyi faman yakfur
bialttaghooti wayu/min biAllahi faqadi istamsaka bialAAurwati alwuthqa la
infisama laha waAllahu sameeAAun AAaleemun (Surat Al baqara 2:256)
824

Tafsir: Hamna kulazimishana katika dini. Kwa hakika njia ya uongofu imebainishwa
kutokana na ile isiyokua sahih. Hivyo atakaeikufuru Taghut (Miungu myengine na
maovu mengine) na akamuamini Allah basi atakua ni mwenye kuegemea egemeo
linaloaminika ambalo kamwe halitovunjika. Na Allah ni mwenye kusikia kila kitu na
ni mwenye kujua kila kitu.

Lakini sasa kwa upande wa watu wa Bani Israil ilibidi wawe ni weye kulazamishwa. Kwa
sababu wao ndio waliokua wakiomba kua waletewe uongofu kupitia kwa Nabii Musa,
halafu badala yake wanaukataa na kupingana nao mbali ya kuoneshwa vihibitisho kadhaa
vikubwa vikubwa, hivyo watu hawa 70 wakawa ni miongoni mwa watu waliokua
wakishikamana na maamrisho ya Allah Subahanah wa Ta’ala katika watu wa Nabii Musa
na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala anaendelea kutuambia kua:

﴾‫ﭑﳊَِّﻖ وﺑِِﻪ ﻳَـ ْﻌ ِﺪﻟُﻮ َن‬ِ ِ ِ


َ ‫﴿ َوﻣﻦ ﻗَـ ْﻮم ُﻣ‬
َ ْ ‫ﻮﺳ ٰﻰ أُﱠﻣﺔٌ ﻳـَ ْﻬ ُﺪو َن ﺑ‬
Wamin qawmi moosa ommatun yahdoona bialhaqqi wabihi yaAAdiloona (Surat Al
Aaraf 7:159)

Tafsir: Na katika watu wa Musa mna Ummah ulioongoka katika haki na ni wenye
Uadilifu.

Ambapo anasema Imam Ahmad Ibn Muhammad Ath Thalabi kua: ‘Ameniambia mimi
Al Hasan kua amesema Anas kua amesema Rasul Allah Salallahu Alyahi wa Salam
kua: ‘Wakati watu sabini wanapoondoka kwa ajili ya mkusanyiko basi hua ni sawa
na wawakilishi 70 wa Musa mbele ya Mola wao na ni bora zadi.’’

QARUN, MALI ZAKE NA KIBRI CHAKE.


Neno Qarun kwa Lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kukusanya au Kuunganisha vitu
viwili kwa pamoja.

Tuapozungumzia Qarun ndani ya Qur’an katika kisa cha Nabii Musa basi hua
tunamzungumzia yule mtu ambae alikua akijulikana kama Qarun Ibn Izhar Ibn Kuhath
Ibn Levi Ibn Yaqub yaani Mtoto wa Ami yake Nabii Musa ambae Allah Subhanah wa
Taala kwa jina ndani ya Qur’an mara tatu ambazo ni pale aliposema kuhusiana nae kua:
825

ٍ َ‫﴿وﻟََﻘ ْﺪ أَرﺳ ْﻠﻨَﺎ ﻣﻮﺳ ٰﻰ ِﺂﺑ�ﺗِﻨَﺎ وﺳ ْﻠﻄ‬


ٍ ِ‫ﺎن ﱡﻣﺒ‬
﴾‫ﲔ‬ َُ َ َ ُ َْ َ
Walaqad arsalna moosa bi-ayatina wasultanin mubeenin; Ila firAAawna
wahamana waqaroona faqaloo sahirun kadhdhabun (Surat Mu/minuun 40:23-24)

Tafsir: Na kwa hakika tulimtuma Musa na aya zetu na Vithibitisho vyenye nguvu kwa
Fir’awn na Hamana na Qarun, lakini wakamuita kua: ‘Mchawi, Muongo Mkubwa’

Na akamtaja tena katika aya yake peke kwa kusema kua:

ِ ِ ِ ِ
ُ‫ﻮﺳ ٰﻰ ﻓَـﺒَـﻐَ ٰﻰ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ َوآﺗَـْﻴـﻨَﺎﻩُ ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻜﻨُﻮِز َﻣﺂ إِ ﱠن َﻣ َﻔﺎﲢَﻪ‬
َ ‫﴿إ ﱠن ﻗَ ُﺎرو َن َﻛﺎ َن ﻣﻦ ﻗَـ ْﻮم ُﻣ‬
ِ
﴾‫ﲔ‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻻَ ُِﳛ ﱡ‬
َ ‫ﺐ ٱﻟْ َﻔ ِﺮﺣ‬ ِ
َ‫ﺎل ﻟَﻪُ ﻗَـ ْﻮُﻣﻪُ ﻻَ ﺗَـ ْﻔَﺮ ْح إ ﱠن ﱠ‬ َ َ‫ﺼﺒَ ِﺔ أ ُْوِﱃ ٱﻟْ ُﻘ ﱠﻮةِ إِ ْذ ﻗ‬
ْ ُ‫ﻟَﺘَـﻨُﻮءُ ﺑِﭑﻟْﻌ‬
Inna qaroona kana min qawmi moosa fabagha AAalayhim waataynahu mina
alkunoozi ma inna mafatihahu latanoo-o bialAAusbati olee alquwwati idh qala lahu
qawmuhu la tafrah inna Allaha la yuhibbu alfariheena (Surat Al Qasas 28:76)

Tafsir: ‘Kwa hakika Qarun alikua ni miongoni mwa watu wa Musa lakini alikua na
Kiburi na Dharau juu yao (Bani Israil), na tukampa hazina ambazo Funguo zake
ingekua ni mzigo mkubwa kwa watu wetu wengi wenye nguvu. Wakati watu wake
walipomwambia: Usijifaharishie kwani Allah hawapendi wenye kujifaharisha’

Aya imetumia neno Bagha ambao hua linamaanisha Kuvuka mipaka, Kusema Uongo,
Kufanya Uovu, Kufanya dhulma, Nyanyasa mtu, Chukia, Dharau na pia humaanisha
Kutamani. Ambapo hapa neno Bagha limeongezewa kihusishi A’alayhi na hivyo
kumaaanisha Kufanya Ukandamizaji, kua na Kibri na Dharau juu ya watu fulani .

Hivyo mbali ya kua Qarun alikua na Mali nyingi lakini ilikua kaika maisa yake kuna itu
ambacho kimekosekana, ambacho ni wafuasi wengi kwa ajili yake., ambapo hali ilikua
ni tofauti kwa upande wa Nabii Musa na Nabii Harun ambao wao walikua ni Wafuasi
wengi sana, hivyo Qarun akawa pia ni mwenye kua na Wivu na Nabii Musa na Nabii
Harun na hapo hapo akawa ni mwenye kuwachukia watu wa Bani Israil wenzake kwa
sababu hawamfuati isipokua wachache.

Ambapo katika kuelezea Neema ya Mali aliyojaaliwa kua nayo Qarun na wingi wake
basi Allah Subhanah wa Ta’ala anatueleza kwa kutubainishia uzito wa funguo zake tu za
maghala ya hazina ya Mali anazomiliki yeye Qarun kwa kutumia neno Latanauu ambalo
826

ni lenye kutokana na neno Na’a ambalo hua linamaanisha Kudidimiza kitu chini
kutokana na Uzito wa kitu, Kunyanyuka kwa kutumia nguvu nyingi sana kutokana na
kubebeshwa uzito, Kunyanyuka kwa Maumivu, Nung’unika kutokana na kuzidiwa na
Uzito wa kitu.

Hivyo Qarun alikua ni mtu Tajiri sana mingoni wa watu wa Bani Israil na wa Misri kwa
pamoja kiasi ya kua wanazuoni wenyewe wametofautiana na kuhusiana na Uzito wa
funguo zake na wingi wa wachukuzi wa funguo hizo, kwani kwa upande wa Imam Ad
Dahhak Ibn Muzahim basi yeye anasema kua: ‘Funguo zake zilikua zinabebwa na
watu kuanzia watatu mpaka kumi kutokana na wingi wake.’

Na kwa upande wa Imam Mujahid Ibn Sulayman basi yeye anasema kua: ‘Wingi wa
funguo zake ulikua unabebwa na watu 10 mpaka 15’

Hivyo aya zinatuonesha kua Qarun alikua ni miongoni mwa watu wa Bani Israil lakini
yeye alikua ni mwenye kujaliwa kua na Mali nyingi sana na hivyo ingawa alikua si Mtu
wa Misri lakini kutokana na Utajiri aliokua nao basi alikua na hadhi kubwa sana mbele
ya Utawala wa Misri na hivyo kua na ukaribu na Fir’awn na Hamman ambako nako
kulimpelekea kua ni mwenye kuwadharau na kuwanyanyasa watu wa Bani Israil na hali
hio ya chuki hio ilizidi mara pale Nabii Musa alipokua akianza kumtaka atoe Zakkah
kutoka katika sehemu ya Mali yake ambapo Qarun akagoma kutoa sehemu ya Mali hio
kwa ajili ya Mola wake, Allah Subhanah wa Ta’ala anamuelezea Qarun na namna
alivyokua akiusiwa na miongoni mwa watu wa Bani Israil wenye Il’m kwa kusema katika
aya zifuatazo:

‫َﺣ ِﺴﻦ َﻛ َﻤﺂ‬ ِ َ ‫ﺼﻴﺒ‬


ِ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ ٱﻟﺪﱠار‬ ِ‫﴿وٱﺑـﺘ ِﻎ ﻓ‬
ْ ‫ﻚ ﻣ َﻦ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ َوأ‬ َ َ‫ﻨﺲ ﻧ‬ َ ‫ﺗ‬
َ ‫ﻻ‬
َ ‫و‬
َ ‫ة‬
َ‫ﺮ‬َ ‫ٱﻵﺧ‬ َ ُ ‫ﱠ‬ ‫ك‬ َ ‫آﺎﺗ‬
َ ‫ﺂ‬ ‫ﻴﻤ‬
َ َْ َ
﴾‫ﺐ ٱﻟْﻤ ْﻔ ِﺴ ِﺪﻳﻦ‬ ِ ‫ض إِ ﱠن ﱠ‬ ِ ‫ﻚ َوﻻَ ﺗَـْﺒ ِﻎ ٱﻟْ َﻔ َﺴ َﺎد ِﰱ ٱﻷ َْر‬ َ ‫ٱﻪﻠﻟُ إِﻟَْﻴ‬
َ ُ ‫ٱﻪﻠﻟَ ﻻَ ُﳛ ﱡ‬ ‫َﺣ َﺴ َﻦ ﱠ‬ْ‫أ‬
Waibtaghi feema ataka Allahu alddara al-akhirata wala tansa naseebaka mina
alddunya waahsin kama ahsana Allahu ilayka wala tabghi alfasada fee al-ardhi inna
Allaha la yuhibbu almufsideena; (Surat Al Qasas 28:77)

Tafsir: (Akaambiwa)‘Lakini tafutia kwa kutumia kile ambacho Allah amekupa,


makazi ya Akhera, na wala usisahau sehemu ya Dunia yako na fanya mema kama
alivyokufanyia mema Allah na wala usifanye Ufisadi katika Ardhi. Kwani kwa hakika
Allah Hawapendi wenye kufanya Ufisadi.’
827

Ambapo maana ya maneno ya mwanzo ya aya hii yasemayo Waibtaghi feema ataka
Allahu alddara al-akhirata yaani (Akaambiwa)‘Lakini tafutia kwa kutumia kile ambacho
Allah amekupa, makazi ya Akhera, yanafafanuliwa na ile aya isemayo:

‫ٱﻪﻠﻟِ ُﻫ َﻮ‬
‫ﻨﺪ ﱠ‬َ ‫ٱﻪﻠﻟَ ﻗَـْﺮﺿﺎً َﺣ َﺴﻨﺎً َوَﻣﺎ ﺗُـ َﻘ ِّﺪ ُﻣﻮاْ ﻷَﻧ ُﻔ ِﺴ ُﻜ ْﻢ ِّﻣ ْﻦ َﺧ ٍْﲑ َِﲡ ُﺪوﻩُ ِﻋ‬ ُ ‫﴿ َوأَﻗْ ِﺮ‬
‫ﺿﻮاُ ﱠ‬
﴾ً‫َﺟﺮا‬ْ ‫َﺧ ْﲑاً َوأ َْﻋﻈَ َﻢ أ‬
Waaqridhoo Allaha qardhan hasanan wama tuqaddimoo li-anfusikum min khayrin
tajidoohu AAinda Allahi huwa khayran waaAAdhama ajran (Surat Al Muzammil
73:20)

Tafsir: Na Mtengeeni Allah mtengeo wa mambo mema na kila chema mnacho


kitanguliza hua ni kwa ajili ya Nafsi zenu mtakikuta mbele ya Allah kwani yeye ni
m-bora wa kulipa Malipo bora.

Ambapo neno Qaradhan hua linamaanisha Kukata, Kuweka pembeni, Kutenga,


Kugeuka, Kuachana na jambo au kitu, Kufanya Mema na pia humaanisha Kutenga kitu
kwa ajili ya Allah Subhana wa Ta’ala.

Hivyo aya hii inafafanuliwa na ile hadith ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
ambae aliuliza kwa kusema kua ‘Hivi jee ni nani miongoni mwenu ambae Mali ya
Mrithi wake ni bora zaidi ya mali yake?’ Masahabah wakasema: ‘Ya Rasul Allah!
Hakuna miongoni mwetu isipokua Mali yake hua anaipenda zaidi’ Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salama akasema: ‘Mali yke mtu hua ni ie aiyoitanguliza kwa
Mola wake.’

Ambapo anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Hii inamaanisha kua
Kamwe usiache kufanya mema kwa ajili ya kumridhisha Allah Subhanah wa Ta’ala
katika Dunia hii’ ambapo kwa upande mwengine hii pia inamaanisha kua : ‘Usisahau
kuchukua sehemu yako ya Dunia ambayo ni haki yako katika mambo mbali mbali
ya halali ikiwemo kujitafutia mahitaji yako Muhimu kiafya kimwili,
kujipendezesha, kimvazi, kimakazi n.k kwani Mola wako ana haki juu yako, mwili
wako wako una haki yake juu yako, familia yako, mke wako, watoto wako n.k vyote
vina haki juu yako’

Mbali ya kua Qarun aliusiwa na watu wa Banii Israil kuhusiana na kutosahau sehemu
yake ya Dunia na kuitumia kwa ajili ya Mola wake lakini hata hivyo nae hakuyatilia
maanani maneno hayo na hivyo akawa ni mwenye kujibu
828

‫ﻚ ِﻣﻦ ﻗَـْﺒﻠِ ِﻪ ِﻣ َﻦ‬ ‫ﻨﺪ ۤي أ ََوَﱂْ ﻳَـ ْﻌﻠَ ْﻢ أَ ﱠن ﱠ‬


َ َ‫ٱﻪﻠﻟَ ﻗَ ْﺪ أ َْﻫﻠ‬
ِ ‫ﺎل إِﱠﳕَﺂ أُوﺗِﻴﺘﻪ ﻋﻠَﻰ ﻋِ ْﻠ ٍﻢ ِﻋ‬
ٰ َ ُُ َ َ‫﴿ﻗ‬
‫َﺷ ﱡﺪ ِﻣْﻨﻪُ ﻗُـ ﱠﻮةً َوأَ ْﻛﺜَـُﺮ َﲨْﻌﺎً َوﻻَ ﻳُ ْﺴﺄ َُل َﻋﻦ ذُﻧُﻮﻬﺑِِ ُﻢ‬ ِ ‫ٱﻟْ ُﻘﺮ‬
َ ‫ون َﻣ ْﻦ ُﻫ َﻮ أ‬ُ
ُ ‫ﻳﻦ ﻳُِﺮ‬ ِ ‫ٱﻟْﻤﺠ ِﺮﻣﻮ َن۞ﻓَﺨﺮج ﻋﻠَﻰ ﻗَـﻮِﻣ ِﻪ ِﰱ ِزﻳﻨﺘِ ِﻪ ﻗَ َ ﱠ‬
‫ﺖ ﻟَﻨَﺎ‬ َ ‫ﻳﺪو َن ٱ ْﳊَﻴَﺎ َة ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ ٰﻳـﻠَْﻴ‬ َ ‫ﺎل ٱﻟﺬ‬ َ ْ ٰ َ َ ََ ُُْ
﴾‫ﻆ َﻋ ِﻈﻴ ٍﻢ‬ ٍّ ‫ِﻣﺜْ َﻞ َﻣﺂ أُوﺗِ َﻰ ﻗَ ُﺎرو ُن إِﻧﱠﻪُ ﻟَ ُﺬو َﺣ‬
Qala innama ooteetuhu AAala AAilmin AAindee awa lam yaAAlam anna Allaha
qad ahlaka min qablihi mina alqurooni man huwa ashaddu minhu quwwatan
waaktharu jamAAan wala yus-alu AAan dhunoobihimu almujrimoona; Fakharaja
AAala qawmihi fee zeenatihi qala alladheena yureedoona alhayata alddunya ya
layta lana mithla ma ootiya qaroonu innahu ladhoo hadhdhin AAadheemin (Surat
Al Qasas 28:78-79)

Tafsir: Akasema (Qarun): ‘Hivi nimepewa mimi kwa sababu ya Ilm niliyokua nayo’.
Hakua ni mwenye kujua kua Allah Aliwaangamiza kabla yake vizazi vya watu ambao
walikua na nguvu kuliko yeye, na walikua na Mali nyingi walizokusanya kuliko yeye.
Lakini kwa wafanyao maovu hawatohojiwa kuhusiana na makosa yao (Kwa sababu
Allah Subhanah wa Ta’ala anawajua sana, hivyo atawaadhibu bila ya kuwahesabia).
Hivyo akatoka kwa watu wake huku akiwa anajidai na mapambo yake, Wakasema
wale ambao waliokua wakiyatamania maisha ya Dunia: ‘Ya laiti tungekua na
(mali)kama aliyopewa Qarun. Kwani kwa hakika yeye ni mwenye bahati kubwa sana’.

Ambapo wanasema wanazuoni kua mbali ya kula Qarun alikua ni mwenye kupewa Mali
na tajiri lakini pia alikua ni mtu wa tatu kwa Ilm baada ya Nabii Musa na Nabii Harun,
ila alikua akiitumia sivyo Ilm yake na ndio maana akasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi
Allahu Anhu kua: ‘Qarun alikua na Il’m ya kubadilisha hali ya asilia ya kitu na
kukiingiza katika hali nyengine, kwa kubadilisha Vitu kua Dhahabu’

Ambapo kwa upande wa Sayyib Ibn Al Musayyib basi yeye anasema kua: ‘Nabii Musa
alikua akijua Ilm ya Kubadilisha hali asilia ya vitu na kuviingiza katika hali
nyengine, na akamsomesha Joshua Ibn Nun sehemu tatu ya Ilm hio na
akamfundisha Qarun pia sehemu hio hio ya robo tatu, lakini Qarun akaachana nao
Nabii Musa na Joshua na hivyo akawa ni mwenye kufanya namna afanyavyo na
hivyo akawa na Utajiri huo.’
829

Na anasema Imam Ibn Jarir At Tabari kua: ‘Qarun alikua akifikiria kua kama Allah
Subhanah wa Ta’ala hakuridhika nae, na hajui kuhusiana Utukufu wake, basi
asingempa hizo mali alizompa’

Ambapo kwa upande wa Imam Abu Sulayman Al Darani basi yeye anasema kua ‘Qarun
alikua akijitolea kufanya Ibada kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala peke yake
mimani kwa mda wa siku 40. Kiasiliya kua akafikia darja ya juu kabisa miongoni
mwa watu wa Banii Israil. Ambapo Ibilisi akajaribu kumtumia Mashaytani wadogo
wadogo ili wakampotoshe lakini wakashindwa. Hivyo Ibilisi akaamua kuingia
mwenyewe kazini.

Hivyo Ibilisi akahamia kwa Qarun na kisha kuanza Urafiki nae kwa kumuonesha
namna anavyofanya Ibada zaidi yake, kiasi ya kua Qarun akavutiwa sana na Ucha
mungu wa Ibilisi bla ya kumuakua ni Ibilisi. Hivyo wakawa pamoja kisha baada ya
md basi Ibilisi akamwambia Qarun, kua yeye anadhani kua inabidi wapunguze
kufaya Ibada kwani kwa kiwango walichofikia basi imetosha hivyo haina haja ya
kutembelea wagonjwa wa Bani Israil wala kuwasaidia.

Kidogo kigdogo Ibilisi akaanza kumpotosha Qarun na kumwambia inabidi siku ya


Ijuma tusifanye Ibada bali tuwe ni wenye kutafuta Mali badala yake, hivyo Qarun
akamkubalia na kisha baada ya hapo, Ibilisi akamwambia Qarun kua wawe
wanafanya Ibada siku moja kisha siku nyengine wanatafuta Mali. Ambapo baada
ya tukio hio basi Ibilisi akamkimbia Qarun na kumwachia akiwa anaendelea
mwenyewe na hapo Milango ya Mali ikamfungukia Qarun.’

Na kwa upande wa Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari basi yeye
anasema kua: ‘Hakuna mtu yeyote yule ambae anaejihesabu kua kila kitu
kimetokana na jitihada zake basi hatofuzu. Mtu mwenye bahati hua ni yule ambae
anayazuia macho yake kutokana na kutizama hadhi yake na matendo yake kwani
huyu hua ni mwenye kufadhiliwa na Mola wake na hivyo hua ni mwenye rehma
kwa wenzake, huku akiwa anaangalia fadhila za Mola wake katika kufanya mema
yake.’

‘Kwa uane mwengine basi Mtu aliepotoka ua ni yule ambae anajiwekea darja yake
na ya watu wake na matendo yake kua ni mazuri sana mbele ya maco yake. Iasi ya
kua anafikia hali ya kua ni mwenye kua na Kibri na hujihesabia kua vyote hivyo
vimetokana na jitihada zake. Na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala
akamzugumzia Qarun kutokana na maneno yake pale aliposema: Qala innama
ooteetuhu AAala AAilmin yaani Akasema (Qarun): ‘Hivi nimepewa mimi kwa sababu
ya Ilm niliyokua nayo’.’
830

‘Na hii ni kwa sababu Qarun alikua ni miongoni mwa Wabora wa waliosoma katika
watu wa Bani Israil, alijidai kua kila alichonacho ni kutokana na Nafsi yake
mwenyewe, hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akaijaalia Ardhi kummeza. Na hii ni
maana ya juu juu ya Aya.’

‘Ambapo jee ni watu wangapi leo hii wameshazama katika matatizo kutokana na
kutokujua wanachokifanya? Kwani kuzama kwa mtu katika matatizo hua
kunatokana na kukoseshwa Ulinzi wa Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo
kuingizwa kwenye usimamizi wake mwenyewe mtu huyo ambapo hua ni mweye kua
na Ulimi ulioregea na huanza kusema mambo yasiyokua na maana, hii pia hua
inamaanisha kua mtu huyu hua ni mwemye upofu wa kutoona fadhila za Allah
Subhanah wa Ta’ala juu yake, na hushindwa kuonesha shukran kutokana na
alichoneemeshwa n a hivyo hua ni mwenye kuangamia.’

Ambapo anasema Muqatil Ibn Sulayman kua: ‘Qarun alikua akitoka na Farasi wake
Mweupe mwenye Soji la Dhahabu na lililonakshiwa kwa rangi ya Zambarau, alikua
akifuatana na Askari wake laki moja na Wanawake 600 ambao walikua wamevaa
nguo nyekundu na mapambao yao waliyojipambia vizuri sana na kupanda Farasi
weupe.’

Allah Subhanah wa Ta’ala anaendelea kusema kua: Awa lam yaAAlam anna Allaha qad
ahlaka min qablihi mina alqurooni man huwa ashaddu minhu quwwatan waaktharu
jamAAan wala yus-alu AAan dhunoobihimu almujrimoona – Yaani - (Qarun) Hakua ni
mwenye kujua kua Allah Aliwaangamiza kabla yake vizazi vya watu ambao walikua na
nguvu kuliko yeye, na walikua na Mali nyingi walizokusanya kuliko yeye. Lakini kwa
wafanyao maovu hawatohojiwa kuhusiana na makosa yao (Kwa sababu Allah Subhanah
wa Ta’ala anawajua sana, hivyo atawaadhibu bila ya kuwahesabia).

Yaani kama ikiwa Utajiri na Mali hua ni sehemu ya kukubalika mbele ya Allah Subhanah
wa Ta’ala basi kwanini Vizazi vya watu waliotangulia ambao walikua na Nguvu na Mali
nyingi sana kuliko yeye viliangamizwa? Na kisha hapo hapo Allah Subhanah wa Ta’ala
anasema kua wote hao waliotangulia hapo kabla ambao waliangamizwa kwa dhambi
zao, haikua na haja kwake yeye kuwahoji au kuwahesabia makosa yao, kwani yeye ni
mwenye kua na habari juu ya makosa yao waliyokua wakiyafanya.

Na kutokana na kutokujua kwao basi baadhi ya watu wa Bani Israil wakaona kua Qarun
amefaidi kutokana na kua ni mwenye Mali nyingi sana kiasi hicho hivyo wakasema:
‘Hakika Qarun ana Bahati kweli’ hivyo wakasema wale ambao ni wenye Ilm miongoni
mwa watu wa Bani Israil kua:
831

ِ ‫ٱﻪﻠﻟِ ﺧﻴـﺮ ﻟِّﻤﻦ آﻣﻦ وﻋ ِﻤﻞ ﺻ‬ ِ ِ ‫﴿وﻗَ َ ﱠ‬


َ‫ﺎﳊﺎً َوﻻ‬ َ َ َ َ َ َ ْ َ ٌ ْ َ ‫اب ﱠ‬ ُ ‫ﻳﻦ أُوﺗُﻮاْ ٱﻟْﻌ ْﻠ َﻢ َوﻳْـﻠَ ُﻜ ْﻢ ﺛَـ َﻮ‬
َ ‫ﺎل ٱﻟﺬ‬ َ
﴾‫ﺼﺎﺑِﺮو َن‬ ِ َ ‫ﻳـﻠَ ﱠﻘ‬
ُ ‫ﺎﻫﺂ إﻻﱠ ٱﻟ ﱠ‬ ُ
Waqala alladheena ootoo alAAilma waylakum thawabu Allahi khayrun liman
amana waAAamila salihan wala yulaqqaha illa alssabiroona; (Surat Al Qasas 28:80)

Tafsir: Lakini Wakasema wale waliopewa Ilm ya Dini: ‘Ole wenu! Kwani malipo ya
Allah (akhera) ni bora kwa wale wenye kuamini na wakafanya mema, na hayapatikani
isipokua wenye Subra’.

Kwani wenye Subra ndio wale ambao Allah Subhanah wa Ta’ala amewataja kwa
kusema:

َ‫ٱﺳﺘَـ َﻘ ُﺎﻣﻮاْ ﺗَـﺘَـﻨَـﱠﺰُل َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ُﻢ ٱﻟْ َﻤﻼَﺋِ َﻜﺔُ أَﻻﱠ َﲣَﺎﻓُﻮاْ َوﻻ‬ ِ ‫﴿إِ ﱠن ٱﻟﱠ‬
ْ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﰒُﱠ‬
‫ﻳﻦ ﻗَﺎﻟُﻮاْ َرﺑـﱡﻨَﺎ ﱠ‬
َ ‫ﺬ‬
‫ﻮﻋ ُﺪو َن۞ َْﳓ ُﻦ أ َْوﻟِﻴَﺂ ُؤُﻛ ْﻢ ِﰱ ٱ ْﳊَﻴَﺎةِ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ َوِﰱ‬ ِ ْ ِ‫َْﲢﺰﻧُﻮاْ وأَﺑ ِﺸﺮواْ ﺑ‬
َ ُ‫ﭑﳉَﻨﱠﺔ ٱﻟﱠِﱴ ُﻛﻨﺘُ ْﻢ ﺗ‬ ُ َْ َ
‫ٱﻵﺧَﺮةِ َوﻟَ ُﻜ ْﻢ ﻓِ َﻴﻬﺎ َﻣﺎ ﺗَ ْﺸﺘَ ِﻬ ۤﻲ أَﻧ ُﻔ ُﺴ ُﻜ ْﻢ َوﻟَ ُﻜ ْﻢ ﻓِ َﻴﻬﺎ َﻣﺎ ﺗَﺪﱠﻋُﻮ َن۞ﻧـُُﺰﻻً ِّﻣ ْﻦ َﻏ ُﻔﻮٍر‬
ِ
﴾‫ﱠرِﺣﻴ ٍﻢ‬
Inna alladheena qaloo rabbuna Allahu thumma istaqamoo tatanazzalu
AAalayhimu almala-ikatu alla takhafoo wala tahzanoo waabshiroo bialjannati
allatee kuntum tooAAadoona; Nahnu awliyaokum fee alhayati alddunya wafee al-
akhirati walakum feeha ma tashtahee anfusukum walakum feeha ma
taddaAAoona; Nuzulan min ghafoorin raheemin (Surat Fussilat 41:30-32)

Tafsir: Kwa hakika wale wasemao Mola wetu ni Allah (pekee), na kisha wakawa na
msimamo, basi watashuka juu yao Malaika huku wakisema: ‘Msiwe na Khofu wala
Huzuni, na tunakubashirieni Pepo ambayo Mliahidiwa. Hakika sisi ni Wasimamizi
wenu katika Maisha haya Dunia na ya Akhera’ kwa ajili yenu ndani yake mna kila
kitu kinachokitamaniwa na Nafsi zenu na mna kila mtakachokitaka. Mmetayarishiwa
na mwingi wa Kusamehe na mwingi wa Rehma.
832

Ambapo kwa upande wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema
kua: ‘Istiqamah maana yake hua ni Kumtii Allah Subhanah wa Ta’ala katika kila
jambo ambalo ni la Wajib bila ya kuyakwepa mambo hayo.’

Ambapo kwa upande mwengine basi safari moja Rasul Allahi Salallahu Alayhi wa Salam
alifuatwa na Thaqafi ambae alimuuliza: ‘Ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
niambie mimi kuhusiana na jambo ambalo natakiwa nishikamane nalo.’ Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Sema kua Mola wangu ni Allah Subhanah wa
Ta’ala na kisha kua na Msimamo’ Thaqafi akauliza: ‘Ya Rasul Allah Salallahu Alayhi
wa Salam, jee kuna kitu gani kibaya zaidi ambacho unakiogopa kuhusiana nami?’
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaukamata Ulimi wake kisha akasema: ‘Ni
Hiki’(Sahih Muslim)

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Tukio hii la
kuambiwa maneno haya hua linatokea katika sehemu tatu ambazo ni: Katika
wakati wa Kutolewa Roho, Ndani ya Kaburi na Katika siku a Kufufuliwa.’

Ama kuhusiana na tukio hili basi Muhaqiq Al Faqih Imam Shihab Ad Din Abu Abbas
Ahmad Ibn Muhammad Ibn Ali Ibn Hajar Al Haytami Al Makki Al Shafii basi yeye
ameihakiki kua ni sahih ile hadithi isemayo kua: ‘Amesema Bara Ibn Azib Radhi
Allahu Anhu amesema kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
kua:Wakati Muumini anapoondoka hapa Ulimwenguni kuelekea Akhera basi
Malaika wenye Sura nyeupe zinazong’ara hua ni wenye kumshukia huku wakiwa
na Nuru kama ya Jua kwenye Nyuso zao, hua na Sanda za Peponi na Harufu ya
Peponi. Hua ni wenye kukaa mbali nae kwenyeUpeo wa Macho. Kisha Malaika wa
Mauti, humjia kichwani mwake na kusema: ‘Ewe Roho Safi, Toka nje uingie
kwenye Msamaha na Ridhaa ya Allah’

Na katikawakati ambao Kafiri anaondoka hapa Ulimwenguni kuelekea Akhera basi


Malaika wenye Nyuso nyeusi humshukia huku wakiwa na Kitambaa kigumu
(Kama Msasa) kisha wanakaa mbali nae kwa upeo wa macho. Kisha Malaika wa
Mauti anakaa kwenye kichwa chake na kusema: ‘Ewe Roho chafu Toka nje kwenye
Ghadhabu na Adhabu za Allah’’(Musnad Imam Ahmad)

Ambapo tunapozungumzia kuhusiana na maneno La takhaf wala Tahzan basi anasema


Imam Ismail Abd Rahman Al Suddi kua: ‘Hii inamaanisha Usiwe n Khofu kuhusiana
na Yajayo na wala Usiwe na Huzuni kutokana na Yaliyopita’

Na hii ni kwa sababu Khofu na Huzuni hua ni mambo mawili ambayo ndio chanzo cha
Matatizo ya takriban watu wote Uimweguni, kwani kil mtu hua ana khofu juu ya kile
asichokijua ambacho kitakachoktokea hapo baadae, wakati Huzuni hua ni kuhuzunikia
mambo yaliyokwisha tokea, ambapo hofu ya yatayokutokea hua ni kubwa kuliko huzuni
833

ya yaliyopita, na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala mara zote ndani ya Qur’an hua
anaitaja Khofu mwanzo kisha ndio huitaja Huzuni.

Ambapo kwa upande mwengine basi wanasema Wanazuoni kua Allah Subhanah wa
Ta’ala amezigawa tabia njema miongoni mwa Waja wake kama vile ambavyo
alivyozigawa Mali, kwani kwa Hakika Allah Subhanah wa Ta’ala humpa Utajiri yule
ampendae na yule asiempenda miongoni mwa Waja Wake, ila hampi neema ya Imani
Mja wake isipokua kwa yule ambae ni mwenye kumpenda, na ndio maana akasema Allah
Subhanah wa Ta’ala kua:

ِِ ِ ِ ‫ٱﻪﻠﻟِ وﻋ ِﻤﻞ ﺻ‬ ِ
َ‫۞وﻻ‬ َ ‫ﲔ‬ َ ‫ﺎل إِﻧﱠِﲎ ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻤ ْﺴﻠﻤ‬ َ َ‫ﺎﳊﺎً َوﻗ‬ َ َ َ َ ‫َﺣ َﺴ ُﻦ ﻗَـ ْﻮﻻً ّﳑﱠﻦ َد َﻋﺂ إِ َﱃ ﱠ‬ ْ ‫﴿ َوَﻣ ْﻦ أ‬
ِ ِ
َ َ‫َﺣ َﺴ ُﻦ ﻓَِﺈ َذا ٱﻟﱠﺬى ﺑَـْﻴـﻨ‬
ٌ‫ﻚ َوﺑَـْﻴـﻨَﻪُ َﻋ َﺪ َاوة‬ ْ ‫ٱﳊَ َﺴﻨَﺔُ َوﻻَ ٱﻟ ﱠﺴﻴِّﺌَﺔُ ْٱدﻓَ ْﻊ ﺑِﭑﻟﱠِﱴ ﻫ َﻰ أ‬
ْ ‫ﺗَ ْﺴﺘَ ِﻮى‬
﴾‫ﻆ َﻋ ِﻈﻴ ٍﻢ‬ ٍّ ‫ﺎﻫﺂ إِﻻﱠ ذُو َﺣ‬ ِ ‫ﲪﻴﻢ۞وﻣﺎ ﻳـﻠَ ﱠﻘ ِ ﱠ‬ ِ
َ ‫ﺻﺒَـُﺮواْ َوَﻣﺎ ﻳـُﻠَ ﱠﻘ‬ َ ‫ﺎﻫﺎ إﻻﱠ ٱﻟﺬ‬
َ ‫ﻳﻦ‬ َ ُ َ َ ٌ َ ‫َﻛﺄَﻧﱠﻪُ َوِﱄﱞ‬
Waman ahsanu qawlan mimman daAAa ila Allahi waAAamila salihan waqala
innanee mina almuslimeena; Wala tastawee alhasanatu wala alssayyi-atu idfaAA
biallatee hiya ahsanu fa-idha alladhee baynaka wabaynahu AAadawatun kaannahu
waliyyun hameemun; Wama yulaqqaha illa alladheena sabaroo wama yulaqqaha
illa thoo hadhdhin AAadheemin (Surat Fussilat 41:33-35)

Tafsir:Na ni nani mwenye kauli njema kuliko yule ambae ni mwenye kuwaita watu
kwa Allah, akafanya Mema na akasema ‘Hakika mimi miongoni mwa Waislam’ Na
wala haiwi sawa mambo mema na mambo maovu, yabadilisheni (maovu) kwa yaliyo
bora, kwani kwa hakika yeye alie baina yenu na baina yao ni adui yenu kama rafiki
wa karibu. Lakini hakuna anaepewa (sifa hizo za kua ni Muumini) isipokua miongoni
mwa wenye Subra na wala hapewi isipokua yule mwenye hadhi tukufu.

Hivyo wenye Ilm miongoni mwa watu wa Bani Israil wakawausia watu wao
wanaomuona Qarun kua kafaidi kutokana na kua na Mali nyingi sana, kua na Imani ni
bora kuliko Mali kwani kua na Imani hua ni kuingizwa ndani ya Rehma za Allah
Subhanah wa Ta’ala na kupewa Mali bila ya Iman hua ni mtihani mkubwa sana badala
yake na hua hakuna wa kukunusuru kutokana na mtihani wake isipokua Mola wako, na
hili linathibitishwa na Allah Subhanah wa Ta’ala kama anavyotuhadithia juu ya yale
yaliyomtokea Qarun kwa kusema:
834

‫ٱﻪﻠﻟِ َوَﻣﺎ َﻛﺎ َن‬


‫ون ﱠ‬ِ ‫﴿ﻓَﺨﺴ ْﻔﻨَﺎ ﺑِِﻪ وﺑِ َﺪا ِرﻩِ ٱﻷَرض ﻓَﻤﺎ َﻛﺎ َن ﻟَﻪ ِﻣﻦ ﻓِﺌَ ٍﺔ ﻳﻨﺼﺮوﻧَﻪ ِﻣﻦ د‬
ُ ُ ُُ َ ُ َ َ ْ َ ََ
﴾‫ﺼ ِﺮﻳﻦ‬ ِ ِ
َ َ‫ﻣ َﻦ ٱﻟْ ُﻤﻨﺘ‬
Fakhasafna bihi wabidarihi al-ardha fama kana lahu min fi-atin yansuroonahu min
dooni Allahi wama kana mina almuntasireena (Surat Al Qasas 28:81)

Tafsir: Hivyo tukajaalia Ardhi kummeza yeye na Makazi yake. Na hakua na kundi
wala wasaidizi wa kumsaidia dhidi ya Allah na hakua ni miongoni mwa wenye kuweza
kujinusuru wenyewe.

Tunapolifuatilia tukio hili basi tunaona kua Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi
Allahu Anhu anasema kua: ‘Qarun alijenga nyumba kubwa sana yenye Milango na
Uwa wa Dhahabu, atu wa Bani Israil wakawa wanatembeea Nyumba yake na
wanapokuja ua anawasaidia kwa shida zao tofati, hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala
akamuamrisha Nabii Musa kukusanya pesa za Zakkah, na hivyo Qarun baada ya
kuambiwa kuusiana na kutoa Zakkah basi akakubaliana na Ibada hio na akawa
anatoa sehemu moja katika kila sehemu 1,000 ya mali yake, laini sasa baada ya Mad
Qarun akaona kua Mali yake inapungua, hivyo akawa ni mwenye kukataa kutoa
zaid.

Hivyo akaamua kutumia njia ambayo itamfanya yeye na watu wengine kua ni
wasiotoa Zakkah, kwa kuwaambia watu wa Bani Israil kua: ‘Hivi Jee mnajua
nyinyi kua kutokana na kua kila kitu anachokumbieni Musa hua mnafanya, basi
Musa ameamua kukupokonyeni Mali zenukwa kukuamrisheni kua mtoe Zakkah’
Watu wa Bani Israil wakasema: ‘Kwa hakika wewe hua unatusaidia sana sisi katika
mambo mbali mbali yetu hivyo tunakusikiliza jee unasemaje?’

Qarun akasema: ‘Nileteeni Mwanamke mzinifu ili nizungumze nae, kisha tutampa
hongo iliakubaliane na kumzulia Musa kua aizini nae, ukishafanya hivyo basi bila
ya shaka watu wote wa Bani Isarial watampa mgongo Musa. Nasi tutafanikiwa
katika Jambo letu tunalolitaka’

Hivyo watu wa Bani Israil wakamleta Mzinifu huyo kwa Qarun ambae nae
akazungumza nae juu ya anayoyataka yatokee na kuahidi kua atampa mali nyingi
kama akaifanikisha kufanya hivyo. Hivyo Mwanamke huyo akakubaliana na jambo
hilo, ilipofika siku ya pili basi Basi Nabii Musa akawa anawausia watu wa Bani
Israil kwa kuwaambia kua: ‘Enyi watu wa Banii Israil nakutangazieni kua Sharia
za Allah zinasema kua Mtu yeyote atakaeiba basi adhabu yake akatwe Mkono,
835

Mzinifu asieoa adhabu yake apigwe fimbo 100 na Mzinifu alieoa basi adhabu yake
ni kupigwa mawe mpaka kufa.’

Qarun ambae nae alikuwepo hapo akasema: ‘Jee Musa Hata wewe?’ Nabii Musa
akasema: ‘Naam…hata mimi!’ Qarun akasema: ‘Kama ni hivyo basi mbona watu wa
Bani Israil wanasema kua nawe umezini na fulani?’ Nabii Musa akashangaa na
kuuliza: ‘Musa mimi au?’ Qarun akasema: ‘Naam wewe!’ Nabii Musa akasema;
‘Mwiteni huyo nnaesingiziwa kua nimezini nae, na kama akikubali basi itakua
kweli.’

Watu wakamwita mwanamke huyo na alipofika akaulizwa, basi mwanamke huyo


akashindwa kujibu na akasema badala yake kua: ‘La! Hakika hawa watu wanasema
Uongo, kwani Qarun ametaka kunihonga mie ili nimzulie Musa.’ Baada ya kusemwa
maneno hayo basi Qarun alifadhaika na kuona haya kutokana na kuadhirishwa mbele za
watu wote hao. Ambapo kwa upande wa Nabii Musa nae akapiga magoti chini na
kumlalamikia Mola wake kwa kusema; ‘Ya Allah hakika Mja wako huyu
amenisababishia madhara makubwa sana, hivyo kama mimini Mtume wao ya Allah
basi nipe Mamlaka ya kumuadhibu Mtu huyu. ’ ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala
akajibu maombi hayo kwa kusema kua: ‘Usiwe na huzuni kwani nitakunyanyua Uso
wako kwa kuiweka Ardhi kwenye Mamalaka yako, hivyo nawe utafanya
Unavyotaka kwa amri yako.’

Nabii Musa akanyanyuka kutoka katika sehemu aliyopiga magoti na kisha akasema
kuwaambia watu wa Bani Israil kua: ‘Enyi watu wa Bani Israil, hakika mimi
nimetumwa kwa Qarun kama vile ilivyotumwa kwa Fir’awn , hivyo kila aliekua
katika Upande wa Qarun basi na akae katika upande wake na kila asiekua nae basi
na akae upande wangu’

Baada ya Nabii Musa kusema maneno hayo, basi haraka sana watu wakaitega na Qarun,
isipkuawatu wawili ambao walibakia nae, hapo Nabii Musa akasema: ‘Ardhi Wakamate
watu hao’ na miguu ya watu hao ikazama ndani ya Ardhi, Nabii Musa akasema: ‘Ardhi
wakamate!’ watu hao wakazama mpaka magotini huku wakipiga kelele kuomba
samahani kwa Nabii Musa, lakini Nabii Musa akasema tena: ‘Ardhi wakamate’ na watu
hao wakazama mpaka shingoni uhku wakiwa wanalia na kuomba Msamaha, Nabii Musa
akaamrisha tena na hivyo wakazama wote.

Allah Subhanah wa Ta’ala akasema kumwambia Nabii Musa: ‘Ewe Musa ulikua mkali
sana dhidi yao, kwani wamekuomba msamaha mara 70, lakini hukua na huruma
nao, ya laiti kama wangeniomba mimi basi wangenikutani mwenye kuyapokea
maombi yao’
836

Baada yakuzama Qarun na Watu wake basi Watu wa Bani Israil wakawa wanaulizana
kuhusiana na Mali za Qarun na Nyumba yake, hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala
akamwambia Nabii Musa kua aizamishe na Mali na Nyumba ya Qarun, kisha baada ya
Nabii Musa kufanya hivyo basi akamwambia Nabii Musa: ‘Ewe Musa hakika wewe ni
mtu wa mwisho kwangu mimi kumpa mamlaka ya kuidhibiti ardhi.’

Allah Subhanah wa Ta’ala anaelezea mwisho wa wale waliokua wakimpinga kutokana


na kua na Mali nyingi na Mamalaka makubwa waliyokua nayo, na hivyo kua ni
waliokosa shukrani mbele ya Mola wao mbali ya kua wameoneshwa vithibitisho vya
wazi na Nabii Musa kwa kusema katika aya ya mwisho miongoni mwa tatu zilizomtaja
Qarun kua hawakuweza kukimbia Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kusema:

ِ ِ‫﴿وﻗَﺎرو َن وﻓ‬
‫ض‬ ْ َ‫ﻮﺳ ٰﻰ ﺑِﭑﻟْﺒَـﻴِّﻨَﺎت ﻓ‬
ِ ‫ﭑﺳﺘَ ْﻜﺒَـُﺮواْ ِﰱ ٱﻷ َْر‬ ‫ﻣ‬
‫ﱡ‬
َ ْ َ ‫ﻢ‬ ‫ﻫ‬
ُ ‫ﺂء‬ ‫ﺟ‬
َ ‫ﺪ‬ْ ‫ﻘ‬
َ ‫ﻟ‬
َ‫و‬َ ‫ن‬
َ ‫ﺎ‬‫ﺎﻣ‬
َ ‫ﻫ‬
َ ‫و‬ ‫ن‬
َ ‫ﻮ‬ ‫ﻋ‬
َ ‫ﺮ‬
َ ْ َْ ُ َ
ِ
﴾‫ﲔ‬ َ ‫َوَﻣﺎ َﻛﺎﻧُﻮاْ َﺳﺎﺑِﻘ‬
Waqaroona wafirAAawna wahamana walaqad jaahum moosa bialbayyinati
faistakbaroo fee al-ardhi wama kanoo sabiqeena (Surat Al Anqbut 29:39)

Tafsir: Na Qarun, Na Firawn, na Haman kwa hakika walijiwa na Musa na vithibitisho


vilivyo wazi, lakini wakafanya Kibri katika Ardhi na hata hivyo hawakuweza
kututangulia (kwa kutukimbia) sisi.

Na tunapoiangalia aya hii basi tunaona kua inatuonesha kua ingawa watu hawa watatu
wametajwa pamoja lakini kulingana na mpangilio wake basi tunaweza kusema kua Qarun
aliangamia kabla ya Firawn na Hamman, na hivyo ndivyo ulivyokua mwisho wa Qarun,
ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anaendelea kutuambia kuhusiana na wale waliokua
wakitamani kua na neema kama aliyokua nayo Qarun kua:

‫ٱﻟﺮْز َق ﻟِ َﻤﻦ‬ِ ‫ﻂ‬


ّ ُ ََُ ‫ﺴ‬ ‫ﺒ‬
ْ ‫ـ‬‫ﻳ‬ ‫ٱﻪﻠﻟ‬
‫ﱠ‬ ‫ﱠ‬
‫ن‬ َ
‫ﺄ‬ ‫ﻜ‬
َ ‫ﻳ‬
ْ‫و‬َ ‫ن‬
َ ‫ﻮ‬ ‫ﻟ‬
ُ‫ﻮ‬ ‫ﻘ‬
ُ ‫ـ‬
َ‫ﻳ‬ ِ
‫ﺲ‬ ‫َﻣ‬
ْ ‫ﻷ‬ ‫ﭑ‬ِ‫َﺻﺒﺢ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ َﲤَﻨـﱠﻮاْ ﻣ َﻜﺎﻧَﻪُ ﺑ‬
َ ْ َ َ َ ْ ‫﴿ َوأ‬
ۤ ِ ِِ ِ ِ
‫ﻒ ﺑِﻨَﺎ َوﻳْ َﻜﺄَﻧﱠﻪُ ﻻَ ﻳـُ ْﻔﻠِ ُﺢ‬ َ َ ََ َ ََْ ُ‫ﻳَ َﺸﺂءُ ﻣ ْﻦ ﻋﺒَﺎدﻩ َوﻳَـ ْﻘﺪ ُر ﻟَْﻮ ﱠ ﱠ ﱠ‬
‫ﺴ‬ ‫ﳋ‬ ‫ﺎ‬‫ﻨ‬ ‫ـ‬ ‫ﻴ‬ ‫ﻠ‬ ‫ﻋ‬ ‫ٱﻪﻠﻟ‬ ‫ﻦ‬ ‫ﻣ‬ ‫َن‬
‫أ‬ ‫ﻻ‬
َ‫ض َوﻻ‬ ِ ‫ﻳﺪو َن ﻋُﻠُّﻮاً ِﰱ ٱﻷ َْر‬ ُ ‫ﻳﻦ ﻻَ ﻳُِﺮ‬ ِ ‫ٱﻵﺧﺮةُ َﳒﻌﻠُﻬﺎ ﻟِﻠﱠ‬
‫ﺬ‬ ِ ‫ﻚ ٱﻟﺪﱠار‬ ‫ﻠ‬
ِْ‫ٱﻟْ َﻜﺎﻓِﺮو َن۞ﺗ‬
َ َ َ ْ َ ُ َ ُ
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ِ
َ ‫ﻓَ َﺴﺎداً َوٱﻟْ َﻌﺎﻗﺒَﺔُ ﻟ ْﻠ ُﻤﺘﱠﻘ‬
837

Waasbaha alladheena tamannaw makanahu bial-amsi yaqooloona waykaanna


Allaha yabsutu alrrizqa liman yashao min AAibadihi wayaqdiru lawla an manna
Allahu AAalayna lakhasafa bina waykaannahu la yuflihu alkafiroona; Tilka
alddaru al-akhiratu najAAaluha lillatheena la yureedoona AAuluwwan fee al-ardhi
wala fasadan waalAAaqibatu lilmuttaqeena (Surat Al Qasas 28:82-83)

Tafsir: Na wale waliokua wakitamani nafasi yake hapo kabla wakaanza kusema:
‘Huwezi kujua kua ni Allah ndie ambae anaewazidishia au kumpunguzia riziki
amtakae katika waja wake, ya laiti kama Allah angekua si mkarimu kwetu basi
angetujaaalia na sisi pia kumezwa na Ardhi hamjui kua Makafiri kamwe hawatokua
ni wenye kufuzu.’

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala ametueleza kisa cha Fir’awn na Qarun ndani ya kisa
cha Nabii Musa kwa sababu ya mafunzo yake ambayo yanaelezewa na aya zifuatazo:

﴾‫ﭑﳊَِّﻖ ﻟَِﻘﻮٍم ﻳـُ ْﺆِﻣﻨُﻮ َن‬ِ ِ ِ ِ َ ‫﴿ﻧَـْﺘـﻠُﻮاْ َﻋﻠَْﻴ‬


َ ‫ﻚ ﻣﻦ ﻧـﱠﺒَﺈ ُﻣ‬
ْ ْ ‫ﻮﺳ ٰﻰ َوﻓْﺮ َﻋ ْﻮ َن ﺑ‬
Natloo AAalayka min naba-i moosa wafirAAawna bialhaqqi liqawmin
yu/minoona(Surat Al Qasas 28:3)

Tafsir: Sisi tunakuhadithia wewe kuhusiana na Habari za Musa na Fir’awn kwa


ukweli kwa watu wenye kuamini.

Na kisha kumalizia sababu kuu kwa kusema:

‫ٱﻪﻠﻟِ َﺧْﻴـٌﺮ َوأَﺑْـ َﻘ ٰﻰ‬


‫ﻨﺪ ﱠ‬ ْ ُ‫﴿ َوَﻣﺂ أُوﺗِﻴﺘُﻢ ِّﻣﻦ َﺷ ْﻲ ٍء ﻓَ َﻤﺘَﺎع‬
َ ‫ٱﳊَﻴَﺎةِ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ َوِزﻳﻨَـﺘُـ َﻬﺎ َوَﻣﺎ ِﻋ‬
﴾‫أَﻓَﻼَ ﺗَـ ْﻌ ِﻘﻠُﻮ َن‬
Wama ooteetum min shay-in famataAAu alhayati alddunya wazeenatuha wama
AAinda Allahi khayrun waabqa afala taAAqiloona (Surat Al Qasas 28:60)

Tafsir: Na chochote kile ulichopewa basi hua ni starehe na mapambo ya Dunia, na


kile kilichopo mbele ya Allah hua ni bora zaidi. Hivi nyinyi hamna akili?

Ambapo amesema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Allah Subhanah wa
Ta’ala amejaalia ndani ya Ulimwengu wa Dunia hii kua na watu wa aina tatu ambao
ni Waumini, Wanafiq na Wasioamini. Ambapo Waumuni hua ni wenye kujiandaa
838

na Akhera yao, Wanafiq hua ni wenye kukimbilia Mapambo ya Dunia na


Wasioamini hukimbilia Starehe za Dunia’

Na miongoni mwa watu waliopendelwa kwa kufadhiliwa na kupewa kila walichokua


wakikitaka na kukihitaji na Mola wao hapa Ulimwenguni basi walikua ni watu wa Bani
Israil.

WATU WA BANII ISRAIL NA FADHILA WALIZOPEWA NA MOLA


WAO


Anasema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qur’an kua:

﴾‫ﲔ‬ ِ ۤ ِ ‫﴿�ﺑ ِﲎ إِﺳﺮاﺋِﻴﻞ ٱذْ ُﻛﺮواْ ﻧِﻌﻤ‬


َ ‫ﻀ ْﻠﺘُ ُﻜ ْﻢ َﻋﻠَﻰ ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬
‫َﱏ ﻓَ ﱠ‬ ُ ‫ﱴ ٱﻟﱠِﱵ أَﻧْـ َﻌ ْﻤ‬
ِّ‫ﺖ َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ َوأ‬ َ َ ْ ُ َ َْ َ َ
Ya banee isra-eela udhkuroo niAAmatiya allatee anAAamtu AAalaykum waannee
fadhdhaltukum AAala alAAalameena(Surat Al Baqara 2:47)

Tafsir: Enyi Bani Israil! Kumbukeni, neema zangu nilizo kuneemesheni juu yenu na
kukupendeleeni zaidi ya Viumbe wengine (wa wakati wenu)

Hii ni aya ambayo yenye kuanzisha mfululizo wa aya zenye kuainisha Neeema na fadhila
walizopewa watu wa Bani Israil na Allah Subhanah wa Ta’ala na namna walivyozipokea
neema hizo bila ya kuonesha shukurani kwa Mola wao, na bado walikua wakichukulia
Ubora wao kutokana na kufadhiliwa huko kua wao ndio pekee watakaoingia Peponi kama
vile ambavyo walivyokua wakichukulia Wakristo kua wao ndio pekee watakaoingia
Peponi kama zinavyosema aya.

ْ‫ﻚ أ ََﻣﺎﻧِﻴﱡـ ُﻬ ْﻢ ﻗُ ْﻞ َﻫﺎﺗُﻮا‬


َ ‫ﺼ َﺎر ٰى ﺗِْﻠ‬َ َ‫ٱﳉَﻨﱠﺔَ إِﻻﱠ َﻣﻦ َﻛﺎ َن ُﻫﻮداً أ َْو ﻧ‬
ْ ‫﴿ َوﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻟَﻦ ﻳَ ْﺪ ُﺧ َﻞ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ‫ﺑـﺮﻫﺎﻧَ ُﻜﻢ إِن ُﻛْﻨـﺘﻢ‬
َ ‫ﺻﺎدﻗ‬ َ ُْ ْ َ ُْ
Waqaloo lan yadkhula aljannata illa man kana hoodan aw nasara tilka
amaniyyuhum qul hatoo burhanakum in kuntum sadiqeena (Surat Al Baqara 2:111)
839

Tafsir: Na Wanasema: ‘Hatoingia Peponi isipokua yule atakaekua ni Myahudi


(Kutokana na Mtizamo wao) au Mkristo (Kutokana na Mtizmo wao)’Haya ni
Matamanio yao (Hivyo Ewe Muhammad) Waambie kua: ‘Leteni Vithibiisho vyenu
kama ikiwa kweli nyinyi ni wakweli’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anatuambia kua hio ni kutokana na Matamanio yao na
ndio maana katika aya nyengine Allah Subhanah wa Ta’ala akawa ni mwenye kuwaonya
kutokana na kujigamba kwao watu hao wa Bani Israil kwa kusema:

‫ﺎﻋﺔٌ َوﻻَ ﻳـُ ْﺆ َﺧ ُﺬ‬ ِ ٍ ‫﴿ َوٱﺗﱠـ ُﻘﻮاْ ﻳـَ ْﻮﻣﺎً ﻻﱠ َْﲡ ِﺰى ﻧـَ ْﻔﺲ َﻋﻦ ﻧـﱠ ْﻔ‬
َ ‫ﺲ َﺷْﻴﺌﺎً َوﻻَ ﻳـُ ْﻘﺒَ ُﻞ ﻣْﻨـ َﻬﺎ َﺷ َﻔ‬ ٌ
﴾‫ﺼﺮو َن‬ ِ
ُ َ ‫ﻣْﻨـ َﻬﺎ َﻋ ْﺪ ٌل َوﻻَ ُﻫ ْﻢ ﻳـُْﻨ‬
Waittaqoo yawman la tajzee nafsun AAan nafsin shay-an wala yuqbalu minha
shafaAAatun wala yu/khadhu minha AAadlun wala hum yunsaroona (Surat Al
Baqara 2:48)

Tafsir: Na iogopeni siku ambayo hakuna Nafsi itakayoisaidia Nafsi nyengine, na wala
hautakubaliwa Uombezi wa Mtu yeyote wala fidiya na wala hawatonusuriwa.

Hapa inabidi tujue kua aya hii inawazungumzia watu wa Bani Israil, Wakristo na kila
asiemuamini Allah Subhnah wa Ta’ala, ambapo kwa wale wenye kumuamini Allah
Subhanah wa Ta’ala basi wao hua haiwahusu kwani kwa upande wao basi kutakua na
hali ya kuombewa mbele ya Mola wao kupitia kwa Mitume, Manabii, Mawalii, Wacha
Mungu na Waja wema wenye kupata Ridhaa za Allah Subhanah wa Ta’ala na kwa kila
yule ambae Allah Subhanah wa Ta’ala kwa rehma zake atampa nafasi ya kufanya hivyo
Muumini atakaemjaalia kuwaombea Waumini wengine.

Kwa pande mwengine basi amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:
‘Wacha yule ambae aliemkosa ndugu yake, iwe kwa heshima au kwa kitu chengine
chochote kile basi na amalizane nae kabisa kabla ya kufika siku ambayo mtu
hatakua na Dinar wala Dirham katika umiliki wake, na kama akiwa na amali njema
katika malipo yake basi ndio zitakazo chukuliwa na kua ndio fidya kwa wale
aliowakosea. Na kama ikiwa hana amali njema basi basi itachukuliwa sehemu ya
dhambi za aliedhulumiwa na kupewa aliedhulumu kwenye kitabu chake.’

Ambapo Nabii Musa pia aliwaambia watu wake hao wa Bani Israil hapo kabla kua:
840

ِ ِ ِ ِ‫ﺎل ﻣﻮﺳﻰ ﻟَِﻘﻮِﻣ ِﻪ �ﻗَـﻮِم ٱذْ ُﻛﺮواْ ﻧِﻌﻤﺔَ ﱠ‬ ِ﴿


َ‫ٱﻪﻠﻟ َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ إ ْذ َﺟ َﻌ َﻞ ﻓﻴ ُﻜ ْﻢ أَﻧْﺒﻴَﺂء‬ َ ْ ُ ْ َ ْ ٰ َ ُ َ َ‫َوإ ْذ ﻗ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ‫تأ‬ ِ
َ ‫َﺣﺪاً ّﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬ َ ‫آﺎﺗ ُﻛ ْﻢ ﱠﻣﺎ َﱂْ ﻳـُ ْﺆ‬
َ ‫َو َﺟ َﻌﻠَ ُﻜ ْﻢ ﱡﻣﻠُﻮﻛﺎً َو‬
Wa-ith qala moosa liqawmihi ya qawmi odhkuroo niAAmata Allahi AAalaykum
idh jaAAala feekum anbiyaa wajaAAalakum mulookan waatakum ma lam yu/ti
ahadan mina alAAalameena (Surat Al Maidah 5:20)

Tafsir: Na (Kumbukeni) aliposema Musa kuwaambia watu wake: ‘Kumbukeni Neema


za Allah juu yenu, alipokujaalieni kutokana nanyi Manabii na akakujaalieni Wafalme
na akakupeni kile ambacho hakumpa hata mmoja miongoni mwa Walimwengu.’

Hivyo Nabii Musa anawakumbusha watu wa Bani Israil kua wanatakiwa wasiwe ni
wenye kujivunia Neema na fadhila za Allah Subhanah wa Ta’ala juu yao na bali
wanatakiwa wawe na Shukran kwa Mola wao kutokana na fadhila alizowafadhili na
alizowajaalia.

Ambapo ingawa nimetafsiri neno Mulukan kua ni Wafalme lakini pia hapa wanaingia
ndani yake watu wenye Mamlaka makubwa, Vyeo vikubwa, Wenye Uwezo na pia Watu
Walio huru, kwani kutokana na kua Watu wa Bani Israila walikua watumwa kwa karne
za miaka basi walipokombolewa na Nabii Musa basi hali yao ikawa wamekua kama
Wafalme kutokana na kua huru na hii ni kulingana na mtizamo wa Mujaddid Ad Din
Imam Fahr Ad Din Al Razi na pia Sultan Al Balagha Imam Abu Qasim Al Zamakhshari
ambao wao wanamalizia kwa kusema kua Watu wa Bani Israila walikua kama Wafalme
wenye kusimamia mambo yao wenyewe baada ya kukombolewa na Nabii Musa kutoka
katika Mateso ya Fir’awn na watu wake.

Ambapo anasema Imam Ibn Jarir At Tabari kua: ‘Abd Allah Ibn Amr kua: ‘Siku moja
aliulizwa Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn `Abbas Radhi Allahu Anhu basi siku moja
aliulizwa; ‘Hivi Jee sisi sio wale ambao wametajwa kwenye ile aya isemayo’’

ِ‫ٱﻪﻠﻟ‬ ِ ِ﴿
ْ َ‫ُﺧ ِﺮ ُﺟﻮاْ ِﻣﻦ ِد َ� ِرِﻫ ْﻢ َوأ َْﻣ َﻮاﳍِِ ْﻢ ﻳَـْﺒـﺘَـﻐُﻮ َن ﻓ‬
‫ﻀﻼً ِّﻣ َﻦ ﱠ‬ ْ ‫ﻳﻦ أ‬
ِ ‫ﺎﺟ ِﺮ ﱠ‬
َ ‫ﻳﻦ اﻟﺬ‬
ِ
َ ‫ﻟ ْﻠ ُﻔ َﻘَﺮآء اﻟْ ُﻤ َﻬ‬
﴾‫ﺼ ِﺎدﻗُﻮ َن‬ ‫ﻚ ُﻫ ُﻢ ٱﻟ ﱠ‬ َ ِ‫ٱﻪﻠﻟَ َوَر ُﺳﻮﻟَﻪُ أ ُْوﻟَـٰﺌ‬
‫ﻨﺼُﺮو َن ﱠ‬ ْ ‫َوِر‬
ُ َ‫ﺿ َﻮا�ً َوﻳ‬
841

Lilfuqara-i almuhajireena alladheena okhrijoo min diyarihim waamwalihim


yabtaghoona fadlan mina Allahi waridhwanan wayansuroona Allaha warasoolahu
ola-ika humu alssadiqoona (Surat Al Hashr 59:8)

Tafsir: (Ngawira) Ni kwa Mafukara waliohama ambao walifukuzwa kutoka katika


Majumba yao na (kupokonywa) Mali zao, kwa ajili ya kutafuta fadhila za Allah na
Ridhaa yake, na katika kumnusuru Allah na Mume wake, hao ndio ndio walio wa
kweli.

Hivyo Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn `Abbas Radhi Allahu Anhu akamuuliza mtu huyo: ‘Jee
unae Mke ambae anaekupa utulivu?’ Mtu huyo akajibu: ‘Ninae’ Bahr Ul Ilm Abd
Allah Ibn `Abbas Radhi Allahu Anhu akauliza : ‘Jee unao Nyumba?’ Mtu huyo akajibu:
‘Ninayo’, Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn `Abbas Radhi Allahu Anhu: ‘Basi wewe ni Tajiri’
Mtu huyo akasema : ‘Na ninae Mfanyakazi pia’ Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn `Abbas
Radhi Allahu Anhu : ‘Basi wewe ni Mfalme!’

Na Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Ahmad Ibn Abu Baqr Al Ansari Al Qurtubi
basi yeye anasema: ‘Amesema Rasul Allah Salallau Alayhi wa Salam kua: ‘Yeyote
yule atakaeamka asubuhi akiwa na utulivu na Nafsi yake na Moyo wake na akawa
na Riziki inayomtosheleza kwa siku hio basi hua kama aliepewa Dunia Nzima’’

Na miongoni mwa mambo waliyopendelewa watu wa Bani Israil ambavyo hawakuwahi


kufadhiliwa viumbe wengine wowote na Mola wao basi mbali ya kuokolewa na madhila
ya Watu wa Misri lakini pia wamefadhiliwa katika mambo mengi sana ikiwemo kama
vile Allah Subhanah wa Ta’ala alivyoainisha kwa kusema katika aya zifuatazo:

ِ‫﴿ﰒُﱠ ﺑـﻌﺜْـﻨَﺎ ُﻛﻢ ِﻣﻦ ﺑـﻌ ِﺪ ﻣﻮﺗ‬


َ ‫۞وﻇَﻠﱠْﻠﻨَﺎ َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ُﻢ ٱﻟْﻐَ َﻤ َﺎم َوأ‬
‫َﻧﺰﻟْﻨَﺎ‬ َ ُ ‫ن‬َ ‫و‬ ‫ﺮ‬‫ﻜ‬ُ ‫ﺸ‬
ْ ‫ﺗ‬
َ ‫ﻢ‬
ْ ‫ﻜ‬
ُ ‫ﱠ‬
‫ﻠ‬ ‫ﻌ‬
َ ‫ﻟ‬
َ ‫ﻢ‬ ‫ﻜ‬
ُ
ْ َْ َْ ّ ََ
ْ‫ﻮ� َوﻟَـٰ ِﻜﻦ َﻛﺎﻧـُ ۤﻮا‬ ِ ‫ﻋﻠَﻴ ُﻜﻢ ٱﻟْﻤ ﱠﻦ وٱﻟ ﱠﺴ ْﻠﻮ ٰى ُﻛﻠُﻮاْ ِﻣﻦ ﻃَﻴِﺒ‬
َ ‫ﺎت َﻣﺎ َرَزﻗْـﻨَﺎ ُﻛ ْﻢ َوَﻣﺎ ﻇَﻠَ ُﻤ‬ َّ َ َ َ ُ َْ
﴾‫أَﻧْـ ُﻔﺴ ُﻬﻢ ﻳَﻈْﻠِﻤﻮ َن‬
ُ ْ َ
Thumma baAAathnakum min baAAdi mawtikum laAAallakum
tashkuroona; Wadhallalna AAalaykumu alghamama waanzalna AAalaykumu
almanna waalssalwa kuloo min tayyibati ma razaqnakum wama dhalamoona
walakin kanoo anfusahum yadhlimoona (Surat Al Baqara 2:56-57)

Tafsir: Na kisha tukakufufueni baada ya kufa kwenu ili mpate kua ni wenye
kushukuru. Na tukakudhalalishieni juu yenu Mawingu na tukakushushieni Manna
842

na Salwa (tukikwambieni): ‘Kuleni miongoni mwa vizuri na vya halali tulivyo


kuruzukuni, na hawakudhulumiwa isipokua wao ndio waliojidhulumu Nafsi zao’

Ambapo aya inatukumbusha tukio la Watu wa Bani Israil namna walivyofadhiliwa hapo
kabla na Allah Subhanah wa Ta’ala baada ya kuuliwa na kisha kufufuliwa watu wao
mbele ya Nabii Musa na hivyo kua ni wenye kuoneshwa Uwezo wa Allah Subhanah wa
Ta’ala ili wapate kuonesha shukrani kwa Mola wao.

Na kisha baada ya hapo, inatubainishia hali ya Watu wa Bani Israil walipokua pamoja
Jangwani wakamwambia Nabii Musa kua: ‘Hakika ewe Musa, umetutoa kenye ardhi
nzuri tuliyokua tunaishi na kukaa kivulini ndani ya Majumba yetu, kisha ukatuleta
kwenye Jangwa ambapo hamna hata kivuli’.

Hivyo Allah Subhnah wa Ta’ala anawakumbusha namna alivyo wadhalalishia Mawingu


meupe ambayo kawaida hua hana joto tofauti na mawingu meusi ambayo hua yana joto
na kimambuile mawingu hua yanakaa na kuelea juu angani, lakini kwa ajili ya Watu wa
Bani Israil basi akayadhalilisha kwa ajili yao yaani akayashusha chini kwa ajili yao ili
yapate kua ni Mwamvuli utakaowafunika na kuwahifadhi na madhara ya Jua kali la
Jangwani na hivyo Mawingu hayo kua ni yenye kuwafuata katika kila sehemu
wanayokuwepo kutokana na kua ni yenye kuambatana na Upepo mzuri maridhawa
unaoyasukuma Mawingu hayo kwa ajili ya kuwafuata wao na kuwapuliza wao tu.

Na kisha baada ya tukio hilo basi watu hao wakaaanza kulalamika na kusema: ‘Ewe
Musa kwelimeusaidiakwakutondeshea ukali wajua na hivyo kutupunguzia
madhara ya kiu, lakini jee vipi kuhusiana na chakula mbona hatuoni chakukila?’

Hivyo Nabii Musa akamuomba Allah Subhanah wa Ta’ala awajaalie kua na chakula watu
wake hao, na hivyo wakawa ni wenye kushushiwa aina ya chakula kinachojulikana
Manna na Salwa kutoka Mbinguni.

Neno Manna hua ni lenye kumaanisha Kuchosha, Kugombeza au kukaripia, Kua na


Rehma au huruma, Kuokoa Kutokana na jambo au kitu fulani, na pia hua linamaanisha
Kukatisha kitu fulani.

Hivyo basi neno Manna hua pia linamaanisha Kumkatia Mtu shida yake kwa kumsaidia
itu kitakachomalizia shidayake hio, na hivyo basi kwa upande mmoja maana iliyotumika
haa hua inamaanisha kua Walijaaliwa neema au Rehema ambayo ilipelekea kukatisha
shida yao ya njaa.

Ama kwa upande wa Imam Mujahid Ibn Sulayman basiyeye anasema kua: ‘Manna
ilikua kama Utomvu ambao uliota kwenye Miti kwa ajili ya watu wa Bani Israil, na
ilikua n ladha ya Utamu kama Asali.’ Na kwa upande wa Imam Ad Dahhak Ibn
843

Muzahim basi yeye anasema kua : ‘Manna ilikua ni kama Mkate wa ngano uliookwa’
na kwa Upande wa Imam Ismail Abd Rahman Al Suddi basi anasema kua; ‘Manna ilikua
kama Asali ambayo ilikua ikianguka Usika kutoka katika miti na hivyo Asubuhi
huikinga na kuila’

Na kuna wasemo kua Manna ilikua kama theluji ambayo ilikua inaanguka na kuganda
kwenye Miti katika wakati wa Usiku hivyo wakati wa asubuhi watu wa Bani Israil
walikua wakiiparua au kuukata kwa kuuchuma na kisha kuipasha Moto na kuila. Na ndio
maana Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kua: ‘Uyoga umetokana na
Manna hivyo kilichomo ndani yake hua ni dawa ya jicho’(Imam Ibn Majah)

Hivyo baada ya kua ni wenye kushiwa Manna basi watu wa Bani Israil wakaanza
kulalamika kwa Nabii Musa na kumwambia kua; ‘Ewe Musa hakika hii Manna kwa
namna ilivyokua Tamu basi hua inakinaisha na tukila sana inaweza ikatuua’

Ambapo Neno Salwa hua linamaanisha Kudharau kitu au Kutojali kitu fulani, Kupata
kitu bila ya kufanya Bidii au Jitihada, na pia humaanisha aina ya Asali na pia humaanisha
Jina la ndege aina ya Kware.

Ambapo kwa upande wa ImamAbu Is-haq Ibn Ibrahim Ibn Muhammad Ibn Al Sari Al
Zajjaj basi yeye anasema kua: ‘Salwa inajumuisha kila kitu ambacho Allah Subhanah
wa Ta’ala aliwaruzuku kwa kuwazawadia watu wa Bani Israil wakati walipokua
Jangwani bila ya watu hao wa Bani Israil kufanya jitihada yeyote.’

Na kwa upande wa Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye
anasema kua: ‘Salwa ni Ndege ambae hua ni mwenye kufanana na Kware.’ Ambapo
kwa upande wa Imam Abu Aliyah basi yeye anasema kua: ‘Salwa ni Ndege mwenye
rangi nyekundu ambae Allah Subhanah wa Ta’ala aliwashushia watu wa Banii Israil
kama Mvua iliyokua ikitiririsha maji yake mfululizo kwa masafa ya urefu wa
Mshare kutoka juu ambao ulikua ni wa ndege waliojipanga mmoja juu ya
mwenzake.’

Na kuna wasemao kua Salwa walikua ni aina ya Ndege wadogo wadogo kama njiwa
ambao walikua ni watamu sana, na walikua wakishushwa huku wakiwa
washanyonyolewa manyoya yao.

Hivyo Allah Subhanh wa Ta’ala aliwashushia watu hao wa Bani Israil Manna na Salwa
ambao walikua wakwatosheleza kila mmoja kati ya watu wa Bani Israil kwa chakula cha
siku moja usiku na mchana na kila inapofika siku ya Ijumaa basi walikua wanasushiwa
chakula cha siku mbili, huku wakionywa kua wasifanye Israfu, ambapo Allah Subhanah
wa Ta’ala anatuelezea katika Qur’an kwa kusema:
844

‫ﺐ ٱﻟﻄﱡﻮِر ٱﻷَْﳝَ َﻦ َوﻧَـﱠﺰﻟْﻨَﺎ‬ ِ ِ ِ ِ ﴿


َ ‫اﻋ ْﺪ َ� ُﻛ ْﻢ َﺟﺎﻧ‬ َ ‫ﻴﻞ ﻗَ ْﺪ أَﳒَْﻴـﻨَﺎ ُﻛ ْﻢ ّﻣ ْﻦ َﻋ ُﺪ ِّوُﻛ ْﻢ َوَو‬
َ ‫ﻳٰـﺒَِﲎ إ ْﺳَﺮاﺋ‬
‫ﺎت َﻣﺎ َرَزﻗْـﻨَﺎ ُﻛ ْﻢ َوﻻَ ﺗَﻄْﻐَ ْﻮاْ ﻓِ ِﻴﻪ ﻓَـﻴَ ِﺤ ﱠﻞ‬ِ ‫ﻋﻠَﻴ ُﻜﻢ ٱﻟْﻤ ﱠﻦ وٱﻟ ﱠﺴ ْﻠﻮ ٰى۞ ُﻛﻠُﻮاْ ِﻣﻦ ﻃَﻴِﺒ‬
َّ َ َ َ ُ َْ
ِ ِ ِ
‫ب َو َآﻣ َﻦ‬ َ ‫ﻀِﱮ ﻓَـ َﻘ ْﺪ َﻫ َﻮ ٰى۞ َوإِِّﱏ ﻟَﻐَ ﱠﻔ ٌﺎر ﻟّ َﻤﻦ َﺎﺗ‬ َ ‫ﻀِﱮ َوَﻣﻦ َْﳛﻠ ْﻞ َﻋﻠَْﻴﻪ َﻏ‬ َ ‫َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ْﻢ َﻏ‬
﴾‫ﺎﳊَﺎً ﰒُﱠ ْٱﻫﺘَ َﺪ ٰى‬ ِ ‫وﻋ ِﻤﻞ ﺻ‬
َ َ ََ
Ya banee isra-eela qad anjaynakum min AAaduwwikum wawaAAadnakum janiba
alttoori al-aymana wanazzalna AAalaykumu almanna waalssalwa; Kuloo min
tayyibati ma razaqnakum wala tatghaw feehi fayahilla AAalaykum ghadhabee
waman yahlil AAalayhi ghadhabee faqad hawa Wa-innee laghaffarun liman taba
waamana waAAamila salihan thumma ihtada (Surat Ta-Ha 20:80-82)

Tafsir: Enyi Bani Israil hakika sisi tumekuokoeni kutokana na adui yenu na
tukaahidiana na nyie katika Upande wa Kulia wa Mlima Turi na tukakushushieni
Manna na Salwa. (Tukwambieni) Kuleni miongoni mwa Vizuri na Halali ambavyo
tulivyo kuruzukuni na msifanye maovu ndani yake, ili hasira zangu zisije
zikakushukieni na kwa yule anaeshukiwa na hasira zangu basi kwa hakika hua ni
alieangamia. Na kwa hakika mimi ni mwingi wa usamehevu kwa wenye kutubu, na
mwenye kuamini na kisha akaongoka na akadumu katika kufanya mema.

Hivyo watu wa Bani Israil walishushiwa Manna na Salwa kisha wakaambiwa Uhalali
wake na manufaaa yake kwa miili yao, kisha wakaambiwa kua wasifanye Israfu wala
wasiwe na tamaa, au kua na khofu kua labda kesho yake watakula nini. Lakini hata hivyo
watu hawa wa Bani Israil wakaanza kulalalamika kua hawana maji na kunywa, na wana
kiu kubwa sana, hivyo Allah Subhnah wa Ta’ala kawapendelea kwa kuwafadhili kama
zisemavyo aya;

‫ٱﺳﺘَ ْﺴ َﻘﺎﻩُ ﻗَـ ْﻮُﻣﻪُ أ َِن‬ ِ


ْ ‫ﻮﺳ ٰﻰ إِذ‬ ِ
َ ‫َﺳﺒَﺎﻃﺎً أ َُﳑﺎً َوأ َْو َﺣْﻴـﻨَﺂ إ َ ٰﱃ ُﻣ‬ ُ َ‫﴿ َوﻗَﻄﱠ ْﻌﻨ‬
ْ ‫ﺎﻫ ُﻢ ٱﺛْـﻨَـ َ ْﱴ َﻋ ْﺸَﺮَة أ‬
‫ﺖ ِﻣْﻨﻪُ ٱﺛْـﻨَـﺘَﺎ َﻋ ْﺸَﺮةَ َﻋْﻴﻨﺎً ﻗَ ْﺪ َﻋﻠِ َﻢ ُﻛ ﱡﻞ أ َُ� ٍس‬ ْ ‫ٱﳊَ َﺠَﺮ ﻓَﭑﻧﺒَ َﺠ َﺴ‬ْ ‫ﺎك‬ َ‫ﺼ‬ َ ‫ٱﺿ ِﺮب ﺑَِّﻌ‬ ْ
‫ﺎت َﻣﺎ‬ ِ ‫ﱠﻣ ْﺸﺮﺑـﻬﻢ وﻇَﻠﱠْﻠﻨَﺎ ﻋﻠَﻴ ِﻬﻢ ٱﻟْﻐَﻤﺎم وأَﻧْـﺰﻟْﻨَﺎ ﻋﻠَﻴ ِﻬﻢ ٱﻟْﻤ ﱠﻦ وٱﻟ ﱠﺴ ْﻠﻮ ٰى ُﻛﻠُﻮاْ ِﻣﻦ ﻃَﻴِﺒ‬
َّ َ َ َ ُ َْ َ َ َ َ ُ َْ َ ْ ُ ََ
﴾‫ﻮ� وﻟَـٰﻜِﻦ َﻛﺎﻧـُ ۤﻮاْ أَﻧْـ ُﻔﺴ ُﻬﻢ ﻳَﻈْﻠِﻤﻮ َن‬
ُ ْ َ َ َ ‫َرَزﻗْـﻨَﺎ ُﻛ ْﻢ َوَﻣﺎ ﻇَﻠَ ُﻤ‬
845

WaqattaAAnahumu ithnatay AAashrata asbatan omaman waawhayna ila moosa


idhi istasqahu qawmuhu ani idrib biAAasaka alhajara fainbajasat minhu ithnata
AAashrata AAaynan qad AAalima kullu onasin mashrabahum wadhallalna
AAalayhimu alghamama waanzalna AAalayhimu almanna waalssalwa kuloo min
tayyibati ma razaqnakum wama dhalamoona walakin kanoo anfusahum
yadhlimoona(Surat Al Aaraf 7:160)

Tafsir: Na tukawagawanya katika Matawi kumi na mbili na kumshushia Wahyi Musa


kumuongoza wakati watu wake walipotaka Maji, kwa kumwambia kua: ‘Lipige Jiwe
kwa Fimbo yako’ na yakatoka kutokana nalo chemchem kumi na mbili, hivyo kila
kundi miongoni mwao wakawa na sehemu ya Kunywea maji. Na tukayadhalilisha
Mawingu kwa ajili yao na tukawashushia Manna na Salwa (tukawaambia): ‘Kuleni
katika vilivyo bora na halali katika tunavyokuruzukuni, na hatukuwadhulumu, lakini
wao ndio waliojidhulumu nafsi zao.’

Ama kuhusiana na Jiwe hilo na chemchem yake basi Wanazuoni wametofautiana juu
yake kwanikwa upande wa Imam Wahb Ibn Munabih basi yeye anasema kua : ‘Katika
Safari yao watu Bani Israil basi ilikua kila wakiona kiu basi Nabii Musa alikua
akipiga fimbo jiwe lolote liliopo karibu yao, na jiwe hilo hua ni lenye kumwagika
chemchem kumi na mbili’ hivyo watu wa Bani Israil wakasema: ‘Kama Musa
akiipoteza Fimbo yake basi bila ya shaka sisi tutakufa kutokana na kiu’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamshushia Wahyi Nabii Musa kumwambia kua:
‘Kuanzia sasa hivi, usilipige jiwe kwa fimbo yako, bali liamrishe tu jiwe basi nalo
litatatoa maji.’ Na kisha baada ya hapo wau hao wakasema: ‘Hivi jee hali itakuaje
kama tukifika katika sehemu ambayo haina Mawe?’ Hivyo Allah Subhanah wa
Ta’ala akamshushia Wahyi Nabii Musa kumwambia kua: ‘Kuanzia sasa hivi, hilo jiwe
itabidi uwe unatembea nalo, wakitaka maji basi unaweka chini kisha unaliamrisha
nalitatoa maji’

Ambapo kwa upande mwengine basi kuna wasemao kua: ‘Tangu mwanzo hili lilikua
ni Jiwe maalum lenye kutoa chemchem hizo na hii ni kutokana na neno Jiwe yaani
Hajara kua limeandikwa kwa kutumia kivumishi cha Al mwanzoni mwake na hivyo
kua ‘AlHajara’’

Na kwa upande wa Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye
anasema kua: ‘Lilikua ni Jiwe ambalo ni Jepesi na lenye ukubwa kama kichwa cha
mtu, na Nabii Musa aliamrishwa kulibeba na akawa analiweka kwenye mkoba
uliobebwa na Mnyama wake, hivyo watu wa Bani Israil walipokua wakihitaji Maji
basi Nabii Musa alikua akilitoa Jiwe hilo na kulipiga kwa fimbo yake na kisha Jiwe
hilo hutoa maji’
846

Ambapo kwa upande wa Imam Abu Muhammad Said Ibn Jubayr basi yeye amesema
kua: ‘Hili lilikua ni jwe ambalo Nabii Musa alikua akitembea nalo, na ndio jiwe
ambalo alikua akilitumia kuzuilia nguo zake wakati alipokua akikoga na kisha Jiwe
hilo likakimbia na nguo hizo, hivyo jiwe liliposimama basi Malaika Jibril akashuka
a Kumwabia Nabii Musa kua: ‘Allah Subhanaha wa Ta’ala anasema kua: Ewe
Musa lichukue Jiwe hili kwani mimi nina uwezo juu yake na wewe ua miujiza
kutokana nalo‘’’

Na tunapozungumzia kuhusiana na habari hii anayoizungumza Imam Abu Muhammad


Said Ibn Jubayr basi hua tunazungumzia ile habari ya kero, adha na maudhi ya watu wa
Bani Israil juu ya Nabii Musa ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala aliyagusia katika aya
ifuatayo:

ِ ‫﴿ ٰ�َﻳـﱡﻬﺎ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ آﻣﻨﻮاْ ﻻَ ﺗ ُﻜﻮﻧﻮاْ َﻛﭑﻟﱠ ِﺬﻳﻦ آذَواْ ﻣﻮﺳﻰ ﻓَ ﱠﱪأَﻩ ﱠ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﳑﱠﺎ ﻗَﺎﻟُﻮاْ َوَﻛﺎ َن ِﻋ‬
‫ﻨﺪ‬ ُ َٰ ُ ْ َ ُ َ َُ َ َ
﴾ً‫ٱﻪﻠﻟِ وِﺟﻴﻬﺎ‬
َ ‫ﱠ‬
Ya ayyuha alladheena amanoo la takoonoo kaalladheena adhaw moosa fabarraahu
Allahu mimma qaloo wakana AAinda Allahi wajeehan(Surat Al Ahzab 33:69)

Tafsir: Enyi Mlioamini msiwe kama waliomfanyia adha Musa, ambapo Allah
akamsafisha kutokana na kile walichomzulia na akawa mbele ya Allah ni mwenye
kupanda darja.

Kwani watu wa Bani Israil walikua kila wakienda kukoga basi hua ni wenye kupenda
kukoga wengi kwa pamoja kisha huvua nguo zote na hivyo hua ni wenye kuonana na
kuangaliana sehemu zao za siri. Hivyo Nabii Musa kwa uande wake alikua hapendi
kufnya hivyo, na hapa sasa ndio yakaja haya maudhi ya watu wa Bani Israil dhidi yake.

Adha na Maudhi hayo ya watu wa Bani Israil yanafafanuliwa na Bahr ul Ilm Abd Allah
Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu ambae anasema kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam kua: ‘Nabii Musa likua ni mtu mwenye haya sana, na hivyo alikua
akichukua tahadhari kubwa sana katika kujihifadhi kwake kiasi ya kua alikua
kamwe haiwachi wazi sehemu yeyote ya mwili wake kutokana na kuona haya. Hvyo
baadh ya watu wa Bani Israil wakawa wanasema kua: ‘Nabii Musa ana kasoro ya
maradhi mwilini mwake na ndio maana akawa anajihifadhi kila wakati.’

‘Hivyo Allah Subanah wa Ta’ala akataka kumsafisha kutokana na zulio hilo


analozuliwa na siku moja baada ya kuhakikisha kua yukopeke yake, bsi akavua
nguo zake na kuanza kukoga, na nguo zake akaziweka juu ya Jiwe. Hivyo baada ya
847

kumaliza kukoga bsi akawa anataka kuchukua nguo zake iliavae lakini sasa jiwe
hilo likaanza kubiringita pamoja na nguo zake, Nabii Musa akalikimbilia Jiwe hilo
huu akisema: ‘Ewe Jiwe, Nguo zangu!’ na hapo wakatokea watu wa Bani Israil na
kumkuta Nabii Musa akiwa katika hali hio ya maumbile yake bora miongoni mwa
viumbe wa Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo wakajithibitishia kua hakuwa na
kasoro yeyote. Jiwe likasimama na Nabii Musa akavaa nguo zake.’

Ama kuhusiana na kujidhulumu Nafsi zao watu wa Bani Israil katika wakati wa tukio
linaloelezewa katika aya hizi za Manna na Salwa basi kulitokana na kufanya Israf ambao
dhidi ya neema hio ya Manna na Salwa na kutoamini uwezo wa Mola wao kutokana na
kuona kua huenda kesho ikawa hakuna chakula kitakachoshuka, hivyo wakawa
wakishushiwa ua wanachukua zaidi kwa ajili ya kuweka akiba na wakawa wanavificha
baadhi ya vyakula hivyo kwa ajili ya kesho yake hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala
akajaalia kua ikifika kesho yake basi Chakula hicho hua kimeharibika na kujaa mafunza,
lakini hawakusita kubakisha kwa ajili ya kesho yake hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala
akasita kuwashushia Manna na Salwa hio ambayo walikua hawatumii jitihada yeyote
katika kuipata kwake.

Na kutokana na kutokua na shukurani kwao juu ya Mola wao basi Mayahudi


wakamwambia Nabii Musa kua wameshachoka na chakula hicho kimoja tu kila siku
kama zinavyosema aya:

ِ ٍ ِ ‫﴿وإِ ْذ ﻗُـ ْﻠﺘﻢ �ﻣﻮﺳﻰ ﻟَﻦ ﻧﱠﺼِﱪ ﻋﻠَﻰ ﻃَﻌ ٍﺎم و‬


ُ ِ‫ﻚ ُﳜْﺮ ِْج ﻟَﻨَﺎ ﳑﱠﺎ ﺗُـْﻨﺒ‬
‫ﺖ‬ َ ‫اﺣﺪ ﻓَ ْﭑدعُ ﻟَﻨَﺎ َرﺑﱠ‬ َ َ ٰ َ َْ ٰ َ ُ َ ُْ َ
‫ﺎل أَﺗَ ْﺴﺘَـْﺒ ِﺪﻟُﻮ َن ٱﻟﱠ ِﺬى ُﻫ َﻮ‬ َ َ‫ﺼﻠِ َﻬﺎ ﻗ‬ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ‫ٱﻷَر‬
َ َ‫ض ﻣﻦ ﺑَـ ْﻘﻠ َﻬﺎ َوﻗﺜﱠﺂﺋ َﻬﺎ َوﻓُﻮﻣ َﻬﺎ َو َﻋ َﺪﺳ َﻬﺎ َوﺑ‬
ُ ْ
ُ‫ﺖ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ُﻢ ٱﻟ ِّﺬﻟﱠﺔ‬
ْ َ‫ﺿ ِﺮﺑ‬
ِ ِ ٰ ‫أَد‬
ْ ‫ﱏ ﺑِﭑﻟﱠﺬى ُﻫ َﻮ َﺧْﻴـٌﺮ ْٱﻫﺒِﻄُﻮاْ ﻣ‬
ُ ‫ﺼﺮاً ﻓَِﺈ ﱠن ﻟَ ُﻜ ْﻢ ﱠﻣﺎ َﺳﺄَﻟْﺘُ ْﻢ َو‬ َْ
ِ‫ٱﻪﻠﻟ‬
‫ت ﱠ‬ ِ �‫ﻚ ِﺄﺑَﻧـﱠﻬﻢ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳ ْﻜ ُﻔﺮو َن ِﺂﺑ‬ ِ‫ٱﻪﻠﻟِ ٰذﻟ‬ ‫ﻦ‬ ِ‫ﺐ‬ ٍ َ َ‫وٱﻟْﻤﺴ َﻜﻨَﺔُ و َﺂﺑءوا ﺑِﻐ‬
َ ُ َ ْ ُ َ ‫ﱠ‬ َ ‫ﻀ‬
‫ﻣ‬
ّ ُ َ َْ َ
﴾‫ﺼﻮاْ ﱠوَﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳَـ ْﻌﺘَ ُﺪو َن‬ ِ َ ِ‫وﻳـ ْﻘﺘُـﻠُﻮ َن ٱﻟﻨﱠﺒِﻴِﲔ ﺑِﻐَ ِﲑ ٱ ْﳊ ِﻖ ٰذﻟ‬
َ ‫ﻚ ﲟَﺎ َﻋ‬ َّ ْ َ ّ ََ
Wa-idh qultum ya moosa lan nasbira AAala taAAamin wahidin faodAAu lana
rabbaka yukhrij lana mimma tunbitu al-ardhu min baqliha waqiththa-iha
wafoomiha waAAadasiha wabasaliha qala atastabdiloona alladhee huwa adna
bialladhee huwa khayrun ihbitoo misran fa-inna lakum ma saaltum wadhuribat
AAalayhimu aldhdhillatu waalmaskanatu wabaoo bighadhabin mina
Allahi dhalika bi-annahum kanoo yakfuroona bi-ayati Allahi wayaqtuloona
848

alnnabiyyeena bighayri alhaqqi dhalika bima AAasaw wakanoo yaAAtadoona


(Surat Al Baqara 2:61)

Tafsir: Na (kumbukeni enyi Mayahudi) mliposema: ‘Ewe Musa hatuwezi sisi


kuvumilia chakula hiki cha aina moja. Hivyo muombe Mola wako kwa ajili yetu
atuletee kile ambacho kinaota ardhini miongoni mwa Majani, Matango, Vitunguu
Thoum, Dengu, Vitunguu Maji’ Akasema Nabii Musa: ‘Yaani Mnataka kubadilishiwa
kile ambacho ni bora kwenu kwa ajili ya kisichokua bora? (basi bora) Nendeni katika
Mji wowote ule ambao mtapata hicho mnachokiomba.’ Na tukawapa dharuba juu yao
ya Udhalilisho na Umasikini, na wakajisababishia Ghadhabu za Allah Juu yao,
kutokana na kua ni wenye kukanusha Aya za Allah na kuwaua Mitume wake bila ya
kua na haki (ya kufanya hivyo) na hii ni kwa sababu walimuasi Allah na kuvuka
mipaka.

Aya hii inaonesha namna watu wa Bani Israil au Mayahudi walivyokua wako mbali
kabisa na Mola wao, kiasi ya kua ilikua kila wakimuomba Nabii Musa basi walikua
wakisema Mwambie Mola wako, yaani Allah Subhanah wa Ta’ala katika kuwasaidia
kote kutokana na Madhila na mashakil yao na kuwapendelea kwa kuwafadhili kwake
kote basi bado wao hawajamuamini na kumuona kua si Mola wao mbali ya kuoneshwa
vithibitisho vingi sana tena vya wazi wazi na Manabii wao.

Lakini hapo hapo hii haimaanishi kua Mayahudi wote walikua wako hivyo, kwani baada
ya aya hii basi aya inayofuatia baada yake yaani aya ya 62 ya Surat Al Baqara, ambayo
ilishushwa kutoa ufafanuzi kuhusiana na hali Mayahudi waliomuamini Nabii Musa baada
ya Sahaba Salman Al Farisi Radhi Allahu Anhu alipomuuliza Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam kwa kusema: ‘Ya Rasul Allah! Jee ni ipi hali yao baada ya Kifo wale
watu ambao mimi nilitumia mda wangu kua nao kabla ya kuja kwako, katika
maeneo ya Uajemi Iraq n.k kwani hawa walikua wanafunga, wanamtumikia Allah,
na walikua wanasubiri kuwasili kwa Mtume wa mwisho.’

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kua: ‘Watu hao wataenda
Motoni’

Na baada ya kusema kua wataenda Motoni basi Allah Subhanah wa Ta'ala akashusha
aya ifuatayo:

‫ﭑﻪﻠﻟِ َوٱﻟْﻴَـ ْﻮِم‬


‫ﲔ َﻣ ْﻦ َآﻣ َﻦ ﺑِ ﱠ‬ ِ ‫﴿إِ ﱠن ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ آﻣﻨُﻮاْ وٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻫﺎدواْ وٱﻟﻨﱠﺼﺎر ٰى وٱﻟ ﱠ‬
َ ‫ﺼﺎﺑِﺌ‬ َ ََ َ َُ َ َ َ َ
﴾‫ف َﻋﻠَْﻴ ِﻬﻢ وﻻَ ُﻫﻢ َْﳛَﺰﻧُﻮ َن‬ ٌ ‫ﻨﺪ َرّﻬﺑِِ ْﻢ َوﻻَ َﺧ ْﻮ‬
َ ‫َﺟُﺮُﻫ ْﻢ ِﻋ‬ ِ ‫ٱﻵﺧ ِﺮ وﻋ ِﻤﻞ‬
ِ
ْ َْ ْ ‫ﺻﺎﳊﺎً ﻓَـﻠَ ُﻬ ْﻢ أ‬
َ َ ََ
849

Inna alladheena amanoo waalladheena hadoo waalnnasara waalssabi-eena man


amana biAllahi waalyawmi al-akhiri waAAamila salihan falahum ajruhum AAinda
rabbihim wala khawfun AAalayhim wala hum yahzanoona (SuratAl Baaqra 2:62)

Tafsir: Hakika ya Wale Walioamini na wale ambao ni Mayahudi, na Manasara na


Masabian na Waliomuamini Allah na Siku ya Malipo na Wakafanya Mema basi
Malipo yao Yapo kwa Mola wao Wala Hakuna Khofu juu yao wala hawatokua na
Huzuni.

Hivyo baada ya kushuka aya hio basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamalizia
kwa kusema: ‘Yeyote yule ambae aliekua ni Mnasara anaemfuata Allah Subhanah
wa Ta'ala ipasavyo na akafa kabla ya kuja kwangu, basi bila ya shaka ataokoka,
Lakini kama alisikia kuhusiana nami na kisha akawa hakuniamini basi bila ya
shaka hatookoka.’(Imam Ibn Abi Hatim)

Ambapo hii ni miongoni mwa aya za Mwanzo kuzungumzia Mayahudi kama sehemu ya
Jamii ya Wafuasi wa Imani ya Kiyahudi Aya hii pia imewataja Manasara yaani Wakristo
wa Asili, ambapo kuna wasemao kua wameitwa Manasara kwa Sababu ya asili yao kua
ni Maeneo ya Nazareti ambayo Nabii Isa aliishi mwanzoni mwa Maisha yake.

Na kuna wasemao kua wameitwa Manasara kutokana na neno Nusra ambalo ni lenye
kumaanisha Msaada, kutokana na kua Wafuasi wa Nabii Isa walikua wanasema kua wao
ni Ansaru Allah. Na pia kuna wasemao kua wameitwa Manasara kwa sababu asili yao ya
mwanzo ni katika maeneo ya Nasrani.

Na aya hii pia imewataja watu wa Sabaa ambao ni mchanganyiko wa watu waliokua si
Mayahudi wala si Wakristo bali walikua wakiabudu Miungu yao tofauti Moto, Jua,
Malaika n.k

Hivyo aya hii inatilia mkazo kua Malipo ya kua na Imani ya Kumuamini Allah Subhanah
wa Ta'ala hua hayategemei Mtu alikua na Dini gani hapo kabla, kwani Muhimu ni kua
Mtu huyo anafuata Maamrisho ya ujumbe wa Allah Subhanah wa Ta’ala baada ya Mtu
huyo kumfikia ujumbe huo.

Tunapokiangalia kisa cha Nabii Musa basi tunaona kua mbali ya kua Allah Subhanah wa
Ta’ala amakihadithia kisa cha Mayahudi, Fir’awn na Qarun ndani yake kutokana na
umuhimu wa mafunzo yake lakini pia ndani yake amehadithia kisa Qisa Al Mustaqilla
yaani Kisa kinachojitegemea chenye Mafunzo yanayobainisha Umuhimu wa kua na
Subra na Imani katika Dini ya Kiislam ambacho ni cha Nabii Musa na Al Khidhr.
850

UHAI NA MAISHA YA AL KHIDHR.


Siku moja Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu alikua amekaa na watu wa Ahl al
Kitab. Mmoja miongoni mwao akasema: Ya Ibn Abbas! Nawf mtoto wa mke wa Kaab
anadai kua Musa aliekua akitafuta I'lm alikua ni Musa Ibn Manaseh!

Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Nawf amesema Uongo! Kwani
Ubay Ibn Kab ameniambia mimi kua amesema Rasul Allah Salallahu A'layhi wa
Salam kua Musa ambae ni Nabii wa Bani Israil alimuuliza Mola wake: Ya Rabb!
Kama ikiwa kuna yeyote miongoni mwa Waja wako ambae ana I'lm zaidi yangu
basi nielekeze alipo nimfuate’

Allah Subhanah wa Ta'ala akamjibu: ‘Naam yupo mtu mwenye I'lm zaidi yako’.

Kisha akamfahamisha alipo mtu huyo na kumfahamisha Nabii Musa sehemu


atakayoweza kuonana nae. Ambapo anasema Imam Abu Abd Rahman Muhammad Ibn
Al Husayn Ibn Muhammad Ibn Musa Ibn Khalid Ibn Salim Ibn Zawwiyah Ibn Saif Ibn
Qabisa Al Azdi Al Sulami Al Shafii Al Nishapuri kua:

‘Kuna Watu kutokana na kutokua na Ilm, basi katika kusoma kwao Qur'an kwa
mfano katika kisa cha Nabii Musa na Al Khidhr hua Wanaona kua Al Khidhr yuko
Juu zaid ya Nabii Musa Na hii ni kwa Sababu hua hawajui kua Allah Subhanah wa
Ta'ala humjaalia kila Kiumbe wake uwezo wake, kulingana na Majaaliwa yake juu
ya Kiumbe husika hususan pale inapoonekana kua Nabii Musa aliambiwa aende
akajifunze kwa Al Khidhr’

‘Allah Subhanah wa Ta'ala hua anawatofautisha baadhi ya Waja wake kulingana


na Mda na Wakati husika. Kwa Mfano Mitume hua Wanajaaliwa kua na Uwezo
wa Kufanya Miujiza wakati Waja wengine hua hawajaaliwi kua na Sifa hio.
Ambapo kwa upande mwengine kuna Waja ambao hua Wanajaaliwa vile ambavyo
hawakujaaliwa kua navyo Mitume.’

‘Kwa Mfano Maryam Bint Imran alijaaliwa kupokea chakula alichokua akiletewa
Chumbani mwake, Lakini hakuna Mtume hata mmoja ambae alifanyiwa Mijuiza
hio. Au Asif Ibn Barhiya alikileta Kiti cha Malkia wa Sheba Bilqis mbele ya Nabii
Sulayman Lakini hapo hapo Asif Ibn Barkhiya mwenyewe hakua ni Mtume wala
Nabii na wala hili halithibitishi kua Asif Ibn Barkhiya alikua ni bora kuliko Nabii
Sulayman.nk’
851

‘Hivyo Al Khidhr alijaaliwa kua na Ilm zaidi ya Nabii lakini hakuwa yuko juu zaidi
ya Nabii Musa, kwa Sababu kama Al Khidhr angeona sehemu ndogo tu ya yale
aliyoyaona Nabii Musa kuhusiana na Mola wake basi bila ya shaka Al Khidhr
asingeweza Kustahmili kutokana na Maumbile ya mwili wake na hivyo
angeangamia moja kwa moja kiasi ya kua kisingebakia hata kitu kimoja cha
sehemu ya Mwili wake’

Anasema Harun Ibn Atrah kua amemsikia baba yake kua amesema Abd Allah Ibn Abbas
Radhi Allahu Anhu kua: ‘Nabii Musa alimuuliza Mola wake: ‘Ya Rabbi Jee ni yupi
miongoni mwa waja wako ni kipenzi zaidi kwako?’

Allah Subhanah wa Ta'ala akajibu: ‘Ni yule ambae anaenikimbuka kila mara na hivyo
kamwe hanisahau’.

Nabii Musa akauliza tena: ‘Jee ni yupi miongoni mwa waja wako ambae ni Muadilifu
zaidi?’

Allah Subhanah wa Ta'ala akasema: ‘Ni yule ambae anaetoa Hukmu kwa Uadilifu na
akawa si mwenye kufuata Matamanio yake’.

Nabii Musa akauliza: ‘Jee ni yupi miongoni mwa waja wako ni Mwenye I'lm zaidi?’

Allah Subhanah wa Ta'ala Akajibu: ‘Mwenye ilmu zaidi miongoni mwa waja wangu
ni yule ambae anaejifunza kile ambacho watu Wanaojifunza hukifanyia jitihada
wakijue ili wawe bora zaidi. Labda huenda atakipata katika maneno ambayo
yatamuongoza katika njia iliyonyooka au kitamuokoa na uovu.’

Nabii Musa akauliza: ‘Jee katika Ulimwengu huu mwenye I'lm zaid yangu?’

Allah Subhanah wa Ta'ala Aakajibu: ‘Naam’

Nabii Musa akauliza: ‘Jee nitampata wapi?’

Allah Subhanah wa Ta'ala Akajibu: ‘Katika mwambao wa bahari, juu ya jiwe


ambapo huwaachia huru samaki’, kisha Allah Subhanah wa Ta'ala akamfanya samaki
kua ni alama na muongozo kwa Musa kwa kusema: ‘Funga safari na chukua samaki
wa kukausha, na samaki huyo atakapokua hai basi ndio utakua umempata mtu
wako.’

Na kw aupande mwengine kuna wasemao kua Nabii Musa alimshukuru Allah Subhanah
wa Ta’ala baada ya kumpa Tawrat kisha akauliza: ‘Ewe Mola wangu Jee hii Ilm
uliyonipa mie, kuna mtu yeyeote yule ambae umemjaalia kua nayo zaidi yangu?’
852

Nabii Musa akaambiwa kua: ‘Ewe Musa Kuna mtu ambae anaishi kisiwani, huyu ana
ilm kubwa sana kwani Ilm yako kwake yeye hua ni sawa na tone la Bahari ambapo
Ilim yake yeye ndio Bahari yenyewe.’

Nabii Musa akasema: ‘Ewe Mola wangu nijaalie mie kua ni mwenye heshima ya
kukutana nae mtu huyo.’ Allah Subhanah wa Ta’ala akasema kumwambia Nabii Musa:
‘Ewe Musa chukua samaki kisha nenda katika sehemu ambayo bahari ya Aqabah
na Bahari ya Suez zimekutana na utamkuta amekaa hapo, alama yako itakua ni
Samaki wako atakapokua hai’

Nabii Musa akauliza kwa kusema: ‘Ewe Mola wangu, Jee mtu huyo huyo ni
miongoni mwa Manabii au ni miongoni mwa Mitume?’’ Allah Subhanah wa Ta’ala
akasema kumwambia Nabii Musa: ‘Hakika yeye ni miongoni mwa Manabii ambapo
wewe ni miongoni mwa Mitume.’

Hivyo Nabii Musa akaamua kufunga safari hio yeye pamoja na Mwanafunzi wake aitwae
Joshua kwa ajili ya kumtafuta Mtu huyo mwenye zaidi ili apate kuongeza mafunzo
kwenye ufaham wake.

Hivyo ndani ya kisa hiki tutakachokiangalia katika kurasa zinazofuatia basi ndani yake
mna mafunzo mengi ambapo kwa hapa mwanzoni tu basi tayari tumeshapata mafunzo
yafuatayo:

1-Kweli Nabii Musa alikua na Hikma kwani hata Allah Subhanah wa Ta'ala
mwenyewe alimsifia kua alimpa I'lm na Hikma..lakini hata hivyo inabidi mtu
kufahamu kua I'lm Na Hikma za kila kitu hua haiwezekani kujumuishwa
kikamilifu ndani ya ufaham wa Ibn Adam mmoja tu pekee.

2-Ni jambo la Muhimu kuendelea kutafuta na kukuza I'lm katika ufahamu wetu na
ndio maana Nabii Musa akasema hatositisha safari yake hadi aonane na aliemzidi
ki'Ilm hata kama atatumia miaka na miaka.

Hivyo Ibn Adam haifai kusema au kuona kua: Unajua sana au Umesoma sana, n.k kwani
I'lm na Hikma zetu ni Tone katika Maji ya Bahari! Kwani kama ikiwa Nabii Musa
aliondolewa Hikma kwa kujiona ana Hikma, Jee itakuaje kwangu mie na wewe?

Na wenye kujua hua kamwe hawajioni kua wana Il’m na ndio maana akasema Hujjat Ul
Islam Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad A Ghazali Al
Tusi Al Shafii ambae mpaka sasa hakuna aliekua na sifa ya Hujjat ul Islami yaani
uthibitisho wa Uislam isipokua yeye kutokana na wingi na Ukubwa wa Ilm yake, na
hivyo anasema Sultan Al Mutakallimin Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi
kua: ‘Uwezo na I’lm ya Imam Abu Hamid Al Ghazali ilikua kama vile Allah
853

Subhanahu wa Ta’ala amezikusanya I’lm zote kwa pamoja, halafu akamuonesha


Imam Al Ghazal’.

Na Imam Al Haramayn Abu Al Ma'ali Al Juwayni ambae alimsomesha Imam Abu Hamid
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali kwa muda wa miaka 5 alisema
kua: ‘Al Ghazali ni Bahari inayokata kiu ya I’lm’.

Na pia Imam Muhammad Ibn Yahya ambae alikua ni mwanafunzi wa Hujjat Ul Islam
Mujaddidi Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al
Shafii alisema kua: ‘Imam Al Ghazal alikua ni Imam Al Shafi’i wa pili’.

Hivyo basi mbali ya kusifiwa kote huko lakini Hujjat Ul Islam Mujaddidi Ad Din Imam
Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad A Ghazali Al Tusi Al Shafii yeye mwenyewe
anasema kua: ‘Hakika mimi kila nikizidi kusoma basi ndio hua najiona kua kumbe
mimi sijui kitu chochote’

Na ndio maana akasema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

﴾‫ﺎت ﱠﻣﻦ ﻧﱠ َﺸﺂء وﻓَـﻮ َق ُﻛ ِﻞ ِذى ِﻋ ْﻠ ٍﻢ َﻋﻠِﻴﻢ‬


ٍ ‫﴿ﻧَـﺮﻓَﻊ درﺟ‬
َ ََ ُ ْ
ٌ ّ ْ َُ
NarfaAAu darajatin man nashao wafawqa kulli dhiAAilmin AAaleemun (Surat
Yusuf 12:76)

Tafsir: Hakika sisi humpandisha darja tumtakae Na Kwa kila alie juu kwa Ilm, basi
kuna ajuae zaid.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anaanza kutuelezea kisa cha Al Khidhr na Nabii Musa
kwa kusema:

ِ ۤ ِ
﴾ً‫ﺣ ُﻘﺒﺎ‬ َ ِ َ َ
ُ ‫ﻮﺳ ٰﻰ ﻟ َﻔﺘَﺎﻩُ ﻻ أﺑْـَﺮ ُح َﺣ ﱠ ٰﱴ أﺑْـﻠُ َﻎ َْﳎ َﻤ َﻊ ٱﻟْﺒَ ْﺤَﺮﻳْﻦ أ ْو أ َْﻣﻀ َﻰ‬ َ َ‫﴿ َوإِ ْذ ﻗ‬
َ ‫ﺎل ُﻣ‬
Wa-idh qala moosa lifatahu la abrahu hatta ablugha majmaAAa albahrayni aw
amdiya huquban; (Surat Al Kahf 18:60-61)

Tafsir: ‘Na (Kumbuka) wakati Musa aliposema kumwambia Mwanafunzi wake;


‘Sitosita kusafiri mpaka nifike kwenye sehemu iliyoungana Bahari mbili au mpaka
nitumize miaka na miaka katika kusafiri kwangu’.
854

Hapa tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala katika kumuelezea mtu aliekua amefuatana
na Nabii Musa katika safari yake hio kwa kutumia neno Fatahu ambalo linatokana neno
Fatiya ambalo hua linamaanisha Kua Kijana, Kua alie baleghe, Kua Jasiri, Kua Mkarimu
au kua na sifa za Mwanamme aliekamilia.

Neno Fatiya hua pia linamaanisha Msaidizi anaekua nae mtu katika mambo yake ambae
hua ni Kijana Shababi wa Kiume, Mfanyakazi.

Ambapo tunaona kua amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua; ‘Kama
mmoja wenu akimwita mfanyakazi wake basi na amwite Fata (kama ni
mwanamme) au Fatat (Kama ni Mwanamke) na asimwite Mtumwa’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala aliposema kua Nabii Musa alisema kumwambia Li
Fatahu basi alikua akimaanisha kua Nabii Musa alimwambia Msaidizi wake ambae
kiumri alikua ni mdogo kuliko yeye kwani huyu alikua ni kijana ambae amekamilia
kimwili na kiujasiri. Huyu Fatahu hakua mtu mwengine yeyote yule isipokua alikua ni
Joshua Ibn Nun, ambae ndie yule aliekua wa Mwanzo kuingia kwenye Bahari pale watu
wa Bani Israil walipokua wanafukuziwa na Fir’awn na jeshi lake, kabla ya kugharikishwa
kwao.

Hivyo kutokana na Ujasiri wake na namna alivyokua akimuamini Nabii Musa na pia
akimuamini Allah Subhanah wa Ta’ala basi Joshua alikua ndio mtu wa mwanzo kuingia
Baharini na Farasi wake na kisha akazama lakini akawa yuko hai ndani yake, na Allah
Subhanah wa Ta’ala akamuonesha Muujiza kupitia kwake, kwani ingawa alizama lakini
akaja juu na wala hakufariki bali alikua hai ndani ya Maji yeye na Farasi wake, na mbali
ya hivyo, lakini Joshua pia alikua ni Mrithi wa Uongozi wa Nabii Musa juu ya watu wa
Bani Israil.

Ambapo anasema Sultan Al Balagha Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakshari kua:
‘Majmaaa Al Bahrain yaani Munganisho wa Bahari Mbili inamaanisha pia kua ni
Al Bahrain Al I’lm yaani Bahari Mbili za Ilm’ Hivyo kutokana na Mtizamo huo basi
tunaona kua hapa zinazungumziwa Bahari mbili za Ilm ya Nabii Musa na ya huyu Mja
ambae aliambiwa akakutane nae, kwani kila mmoja wao miongn mwao amejaaliwa kuna
na Bahari y Ilm ambayo hakujaaliwa kua nayo mwenzake.

Aya pia katika kuelezea jitihada na wakati ambao Nabii Musa atautumia katika kutafuta
kwake Ilm hio aliyopewa Mja huyo basi imetumia neno Huquba ambalo hua
linamaanisha Mwaka usiokua na Mvua, Kipindi kisichokua na Matunda yeyote ndani
yake na pia humaanisha Jambo au Kitu ambacho kitachukua mda mrefu yaani miaka na
miaka ambapo kuna wasemao kua hua linamaanisha kipindi cha miaka kuazia mwaka
Mmoja mpaka miaka Thamanini, lakini pia kuna waliolitafsiri kama vile lilivyotumika
katika aya ifuatayo:
855

﴾ً‫أَﺣ َﻘﺎﺎﺑ‬ ِ ِ‫﴿ﻻﱠﺑِﺜ‬


ْ ‫ﲔ ﻓ َﻴﻬﺂ‬
َ
Labitheena feeha ahqaban(Surat An Nabaa 78:23)

Tafsir: Na watakaa ndani yake kwa miaka.

Ambapo kwa upande wa Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allah Anhu, Imam
Qatadah Ibn Diama na Imam Ibn Zayd basiyeye anasema kua: ‘Neno Huquban hua
linatumika kwa kuainisha kipindi kirefu cha Miaka ambacho hua kinaweza
kikafikia urefu wa Milele’

Na hivyo basi Aya hii hua inatuonesha umuhimu wa kua na jitihada za Kutafuta Ilm, kiasi
ya kua mtu unatakiwa usiachane nazo juhudi hizo za kutafuta Ilm hata kama itakuchukua
miaka na miaka mpaka kuipata, kwani Ilm ni hazina yenye thamani kubwa sana, kwa
sababu kidarja basi baada ya Imani ya kumjua Allah Subhanah wa Ta’ala a, ambacho
ndio kitu chenye thamani kubwa zaidi basi kinachofuatia ni Ilm kama alivyosema Allah
Subahanh wa Ta’ala katika Qur’an:

ُ‫ٱﻪﻠﻟ‬
‫ﺲ ﻓَﭑﻓْ َﺴ ُﺤﻮاْ ﻳَـ ْﻔ َﺴ ِﺢ ﱠ‬ ِ ِ‫ﻳﻦ َآﻣﻨُﻮاْ إِذَا ﻗِﻴﻞ ﻟَ ُﻜ ْﻢ ﺗَـ َﻔ ﱠﺴ ُﺤﻮاْ ِﰱ ٱﻟْ َﻤ َﺠﺎﻟ‬
َ
ِ ‫﴿ ٰ�َﻳـﱡﻬﺎ ٱﻟﱠ‬
‫ﺬ‬ َ
َ
‫ﻳﻦ أُوﺗُﻮاْ ٱﻟْﻌِْﻠ َﻢ‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ آﻣﻨﻮاْ ِﻣﻨ ُﻜﻢ وٱﻟﱠ‬
‫ﺬ‬ ‫ﱠ‬ ‫ﻊ‬ ِ ‫ﻓ‬
َ‫ﺮ‬ ‫ـ‬‫ﻳ‬ ‫ا‬
ْ‫و‬‫ﺰ‬ ‫ﺎﻧﺸ‬‫ﻓ‬
َ ‫ا‬
ْ‫و‬ ‫ﺰ‬ ‫ٱﻧﺸ‬ ‫ﻴﻞ‬ِ‫ﻟَ ُﻜﻢ وإِ َذا ﻗ‬
َ َْ ُ َ َ ُ َْ ُ ُ ُ ُ َ َْ
﴾‫ن ﺧﺒِﲑ‬ ِ ‫ﺎت و ﱠ‬ ٍ
ٌ َ َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﲟَﺎ ﺗَـ ْﻌ َﻤﻠُﻮ‬ َ ‫َد َر َﺟ‬
Ya ayyuha alladheena amanoo idha qeela lakum tafassahoo fee almajalisi faifsahoo
yafsahi Allahu lakum wa-idha qeela onshuzoo faonshuzoo yarfaAAi Allahu
alladheena amanoo minkum waalladheena ootoo alAAilma darajatin waAllahu
bima taAAmaloona khabeerun (Surat Al Mujaddila 58:11)

Tafsir: Enyi Mlioamini kama mkiambiwa wekeni nafasi kwenye sehemu mnazokaa na
kujadiliana mambo tofauti basi wekeni nafasi, kwani Allah atakuwekeeni nafasi
(Katika Rehma zake), na mkiambiwa nyanyukeni (mkafanye mema kwa ajili ya
Allah)basi nyanyukeni, kwani Allah huwanyanyua darja wale walioamini miongoni
mwenu na wale waliopewa I’lm, na Allah ni mwenye habari juu ya kila
mnachokifanya.

Hivyo basi bila ya shaka Ilm ni kitu chenye thamani kubwa sana, na hivyo inabidi
uutumie wakati wako ambao nao pia una thamani kwa ajili ya kutafuta Ilm, kwani
856

amesema Imam Abu Abd Rahman Muhammad Ibn Al Husayn Ibn Muhammad Ibn Musa
Ibn Khalid Ibn Salim Ibn Zawwiyah Ibn Saif Ibn Qabisa Al Azdi Al Sulami Al Shafii Al
Nishapuri kua: ‘Amesema Imam Al Tustari kua: Fahamu kua Wakati ni kitu chenye
thamani kubwa sana, hivyo usiutumie wakati wako isipokua kwa kitu chenye
thamani zaidi mbele yako na mbele ya Mola wako’

Ambapo kwa upande mwengine basi kwa kutumia maana ya Huquban yenye kumaanisha
Ukame au kutokua na Mvua basi pia inaingia maana yake kua Nabii Musa aliamua
kutafuta Ilm kwa vyovyote vile itakavyokua kupitia kwa mtu huyo alieahidiwa kua
amepewa Ilm Ladduni kua atampatia Ilm.

Na tunapozungumzia kutafuta Ilm basi hua hakuna wakati kwani kama tunavyoona kua
hapa tayari Nabii Musa alikua ameshapewa Utume na ameshafanya Miujiza mingi na
ameshapewa Tawrat hivyo inamaana kua alikua keshapita zaidi ya Umri wa miaka 50.

Ambapo kwa Upande mwengine pia kuna mfano mzuri sana wa miongoni mwa
Maimamu walioishi katika karne ya 3 Al Hijra ambae ni mwanazuoni mkubwa sana wa
Madhhab ya Imam Al Shafii aitwae Al Faqih Imam Abu Bakr Abd Allah Ibn Ahmad Ibn
Abd Allah Al Qaffal Al Marwazi Al Shashi Al Khurasan Al Shafii, ambae ni maarufu
kama Imam Al Qaffal au Imam Al Marwazi au pia Imam Al Shashi.

Imam Al Qaffal alikua ni Muislam wa kawaida tu, kama walivyo Waislam wengine
ambao ni Maamuma, na alikua ni fundi wa Kufuli na ndio maana akaitwa Al Qaffal kwa
sababu neno Kufuli limetokana na neno Qaffal ambalo ni la Kiarabu. Hivyo mpaka Imam
Al Qaffal anafikia Umri wa miaka 40 basi alikua hana Ilm ya aina yeyote, isipokua
kuchonga funguo na kutengeneza Kufuli.

Siku moja akasikia kua kuna Al Qaffal ambae mwengine ambae alitengeneza Kufuli
ndogo sana yenye uzito wa nusu gramu, na hivyo watu wakamsifu sana Al Qaffal huyo
kwa ujuzi wake, kutokana na kusifiwa kwa Al Qaffal huyo basi Imam Al Qaffal akataka
avuje rikodi ya Al Qaffal huyo anaesifiwa na hivyo nae akatengeneza Kufuli ambayo ni
ndogo kwa mara tatu zaidi. Na kisha akaifanyia maonesho kufuli hio kwa watu lakini
hata hivyo hakuna hata mtu mmoja alievutiwa na kumpa Imam Al Qaffal hongera stahiki.

Tukio hili ilimvunja moyo sana, na wakati analalamika basi mmoja katia ya marafiki
zake akamwambia kua: ‘Heshima ya Mtu hua haipandi Darja kwa kutokana na
kutengeza kufuli, bali hupanda darja kutokana na kua na I’lm’ ambapo na Imam Al
Qaffal nae akasema: ‘Hakika mimi nitakua ni mwenye kutafuta Ilm na nitakua ni
mwenye Ilm’

Na bila ya shaka Imam Al Qaffal wakati huo akiwa na miaka 40, basi akajitahid hadi
akafikia malengo yake ya kutafuta Ilm kwa kumchagua mmoja kati ya Wanazuoni
857

wakubwa kua ni mwalimu wake ambae siku ya kwanza tu alimfundisha maneno


yafuatayo yaliyomo mwanzoni mwa kitabu cha Mukhtasar Al Muzani cha Imam Al
Muzani, ambae ni mwanafunzi wa Imam Al Shafii, ambapo maneno hayo yanaema:
‘Hadha Kitab Ikhtasarat’ Imam Al Qaffal aliporudi nyumbani akayakariri maneno haya
usiku wote, hadi akapata usingizi.

Lakini alipoamka asubuhi ikawa ameyasahau maneno hayo, akaona hii sasa ishakua kazi
kubwa sana, kwani maneno matatu tu yameshinda kuyahifadhi jee atafika? Hivyo
akatoka nje na akakutana na Jirani yake ambae ni mwanamke na kuumuuliza Imam Al
Qaffal: ‘Ya Al Qaffal! Ni kitabu gani hicho ambacho jana sisi hatukulala kwa
sababu ya wewe kua ni mwenye kurdia rudia kwa sauti Hadha Kitab Ikhtasarat?’

Hapo Imam Al Qaffal akasema: ‘Naam..Al Hamdlillah Hadha Kitab Al Ikhtasarat’


kisha akaelekea kwa Mwalimu wake na kumuelezea alivyovunjika Moyo kutokana na
kisa chake, ambapo mwalimu wake huyo akamwambia: ‘Usijaribu kuifanya kasoro hio
kua ni kipingamizi kwako wewe na kutokua na hamu ya kutoendelea kutafuta Ilm,
kwani ukiendelea kuhifadhi kidogo kidogo basi mwisho wake ufahamu wako
utakua ni wenye kuzoea na kua na maumbile ya kuhifadhi unayoyasoma.’

Huu ulikua ni ushauri ambao ulimfanya Imam Al Qaffal kua kama anavyosema Imam Al
Samaani kuhusiana nae kua: ‘Imam Al Qaffal Al Marwazi Al Shashi alikua mpole na
mkarimu miongoni mwa Maimamu wa Madhhab ya Imam Al Shafii na alikua
akihesabiwa kua ni miongoni mwa Maimamu wenye nguvu kubwa sana ya Ufaham
wa juu wa Ilm kuliko Imam yeyote yule katika wakati wake.’

Imam Al Samaani anaendeea kusema kua: ‘Imam Al Qaffal Al Marwazi Al Shashi


alikua na upekee katika wakati kwa Ilm ya Fiqh, Kwa kuhifadhi kwa Ucha Mungu
na kua na Taqwa, na hii ni kwa sababu Imam Al Qaffal Al Marwazi alikua
amesoma vitabu ambavyo ilikua hakuna alievisoma na wala hakuna aliekua navyo
vitabu hivyo.’

Na kwa upande wa Al Faqih Imam Nasir Ibn Umar basi anasema kua: ‘Katika wakati
wake ilikua hakuna mtu mwenye Ilm kama Abu Bakr Al Qaffal, na hakutokua na
mtu mwengine mithili yake kwani sisi tulikua tukisema: ‘Abu Bakr Al Qaffal ni
Malaika mwenye Umbo la Ibn Adam ambae kazi yake ni kuhadithia na
kuzungumza Ilm ili watu waandike. Imam Al Qaffal al Marwazi alikua ni kiongozi
wa Fiqh na alikua ni mfano wa watu walioachana na dunia hii’.

Katika kipindi cha Uhai wake na kutokana na Ilm yake basi Imam Al Qafal alifanikiwa
kuibadilisha Fiqh ya Utawala wa ardhi yake ambayo ilikua ikifuata Fiqh ya Madhhab ya
Imam Abu Hanifa na kuufanya Utawala wa Sultan Mahmoud wa ardhi ya Marwaz kua
ni yenye kufuata Fiqh ya Madhhab ya Imam Al Shafii kutokana na nguvu ya hoja zake
858

na wingi wa Ilm yake, kwani Imam Al Qaffal Al Shashi Al Marwazi Al Shafii alifanikiwa
kua ndio nguzo ya Fiqh ya Madhhab ya Imam Al Shafii kwa upande wa Tariqah ya
Khurasan.

Na tunasema kua ni Tariqah ya Khurasan kwa sababu hapo kabla ya kuja Hujjat ul Islami
Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al
Ghazali katika karne ya 5 Al Hijra basi Wafuasi wa Skuli ya Fiqh ya Madhhab ya Imam
Al Shafii walikua wamegawika katika matawi mawili, yenye Fiqh zinazofanana lakini
zenye kutofautiana kidoogo kimitizamo na kulikua na Tariqah ya Baghdad na Tariqah
ya Khurasan, na alikua ni Hujjat ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad
Ibn Muhammad Al Ghazali ambae ndie alieziunganisha Tariqah mbili hizi. Na kuzifanya
kua Tariqah Moja.

Hivyo huo ni mfano miongoni mwa mifano bora ya mtu kutotakiwa kujiona kua
umepitwa na wakati wa kusoma kutokana na kua na umri mkubwa kwani wakati ni kitu
chenye thamani kubwa sana hivyo utumie kwa ajili ya kutafuta Ilm itakayo kunufaisha
na akhera yako.

Kwani Imam Al Qaffal kaanza kusoma wakati akiwa na umri wa miaka 40, na katika kisa
chetu basi tunaona kua Nabii Musa akiwa anakaribia miaka 50 basi ameamua kutafuta
Ilm kutoka kwa Al Khidhr ambae ni mtu alieambiwa amtafute kwani ala Ilm zaid yake
na katika kuonesha azma yake hio basi akamwambia Joshua ambae ni Msaidizi wake
kua, atamtafuta mwenye Ilm huyo hadi amuone hata kama itachukua miaka mingapi.

Ambapo amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kama Mtu atakua ni
mwenye kupenda kutafuta Ilm, bsi milango ya Pepo itafunguka kwa ajili yake,
Allah Subhanah wa Ta’ala ataridhika na mja wake huyo, na hivyo mwili wake
hautoliwa na fnza Kaburini na Peponi atakua ni rafiki yake Al Khidhr’

Hivyo baada ya kuweka ahadi hio basi Nabii Musa na Joshua wakajitayarisha kwa safari
na walipokamilisha matayarisho wakaanza safari yao huku wakiwa na chakula chao
ambacho ndani yake mna mikate na samaki wa kubanika ambae walifahamishwa na Allah
Subhanah wa Ta’ala wapi watampata watampata Samaki huyo. Safari ilikua ndefu na
ilichukua mda mrefu, lakini hata hivyo kutokana na ari yao basi hawakua ni wenye
kusikia uchovu sana na walifanikiwa kuwasili katika maeneo ambayo kwa mbali
waliyoana kua yanafaa kupiga kambi kutokana na uzuri wa muonekano wa mandhari
yake kutoka kwa mbali, na hivyo walipoyakaribia basi ilikua tayari kiza cha usiku
kimeshaingia.

Hivyo wakapiga kambi katika eneo hilo ambalo lilikua na jiwe kubwa sana na chemchem
ya maji, hivyo wakafanya Ibada zao kisha wakala na wakapumzika hadi Alfajir mapema
859

ambapo waliamka na kisha wakasali na kufunga funga mizigo yao na kuanza kuendelea
na safari yao, ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anailezea hali hio kwa kusema:

﴾ً‫ﺳﺮﺎﺑ‬ ِ ِ ِ ‫ﱠ‬ ِ ِِ
َ َ ‫ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ ﺑَـﻠَﻐَﺎ َْﳎ َﻤ َﻊ ﺑَـْﻴﻨﻬ َﻤﺎ ﻧَﺴﻴَﺎ ُﺣﻮﺗَـ ُﻬ َﻤﺎ ﻓَﭑﲣَ َﺬ َﺳﺒﻴﻠَﻪُ ﰱ ٱﻟْﺒَ ْﺤﺮ‬
﴿

Falamma balagha majmaAAa baynihima nasiya hootahuma faittakhadha


sabeelahu fee albahri saraban (Surat Al Kahf 18: 61)

Tafsir: Lakini walipofika katika maungano ya bahari mbili, (wakaona kua)


wamesahau Samaki wao. Na akatelezea kwenye maji kama kwenye njia’

Katika kumuelezea samaki huyu basi Allah Subhanah wa Ta’ala ametumia neno Hutta
ambalo hua linamaanisha Kurukaruka, Kutembea tembea katika sehemu tofauti kwa ajili
ya kutafuta chakula na pia hua linamaanisha Samaki.

Aya pia imetumia neno Saraba ambalo hua ni lenye kumaanisha Kuenda kwa Uhuru,
Kuelea, Kukimbia, Kuenda kwa dhahiri, Kuteleza au Kutiririka. Neno Saraba hua pia
linamaanisha Chungu ya Mchanga ambao haujashikamana. Ambapo Abd Allah Ibn
Abbas Radhi Allahu Anhu anasema kua neno Saraba hua linamaanisha kua Samaki huyu
alipotoka kwenye Mfuko na kisha kuangukia ardhini kuelekea Baharini basi alikua ni
mwenye kuacha alama katika kutiririka kwake kwenye mchanga uliopo hapo kuelekea
kwenye maji.

Hivyo inamaanisha kua baada ya kuondoka kwao kutoka kwenye sehemu waliyopiga
kambi wakagundua kua Samaki hayumo kwenye sehemu waliyomuweka hapo kabla na
hii ni kutokana na hali ya kua Nabii Musa alisahau kuulizia kuhusiana na yule Samaki
wakati walipokua wanakula na Joshua nae pia alisahau kukumbusha kuhusiana na
Samaki huyo wakati wa kula.

Ambapo anasema Abd Rahman Ibn Zayd kua: ‘Maajabu yalioje kwa samaki ambae
alikua tayari aliwe lakini akabadilika na kua mzima na kutelezea Baharini, kwani
ilikua ni kipande cha Samaki.’

Na waligundua juu ya tukio hili la kutoweka samaki wao pale mara baada ya Nabii Musa
kua ni mwenye kuhisi njaa, hivyo akamwambia Joshua kama zinavyobainisha aya kwa
kusema:
860

ِ ِ ِ ِ َ َ‫﴿ﻓَـﻠَ ﱠﻤﺎ ﺟﺎوزا ﻗ‬


‫ﺎل‬
َ َ‫ﺼﺒﺎً۞ ﻗ‬ َ َ‫ﺎل ﻟ َﻔﺘَﺎﻩُ آﺗﻨَﺎ َﻏ َﺪآءَ َ� ﻟََﻘ ْﺪ ﻟَﻘﻴﻨَﺎ ﻣﻦ َﺳ َﻔ ِﺮَ� َﻫـٰ َﺬا ﻧ‬ ََ َ
‫ﻮت َوَﻣﺂ أَﻧْ َﺴﺎﻧِﻴﻪُ إِﻻﱠ ٱﻟﺸْﱠﻴﻄَﺎ ُن أَ ْن‬
َ ُ‫ٱﳊ‬ ْ ‫ﻴﺖ‬ ِ
ُ ‫ﺼ ْﺨَﺮةِ ﻓَِﺈِّﱏ ﻧَﺴ‬ ‫ﺖ إِ ْذ أ ََوﻳْـﻨَﺂ إِ َﱃ ٱﻟ ﱠ‬
َ ْ‫أ ََرأَﻳ‬
﴾ً‫أَذْ ُﻛﺮﻩُ و ﱠٱﲣَ َﺬ َﺳﺒِﻴﻠَﻪُ ِﰱ ٱﻟْﺒَ ْﺤ ِﺮ َﻋ َﺠﺒﺎ‬
َ َ
Falamma jawaza qala lifatahu atina ghadaana laqad laqeena min safarina hadha
nasaban; Qala araayta idh awayna ila alssakhrati fa-innee naseetu alhoota wama
ansaneehu illa alshshaytanu an adhkurahu waittakhadha sabeelahu fee albahri
AAajaban (Surat Al Kahf 18:62-63)

Tafsir: Na Kisha walipopita (katika sehemu waliyokubaliana) akasema (Musa)


kumwambia Msaidizi wake: ‘Tutolee chakula chetu cha asubuhi kwani kwa hakika
tumekutana na uchovu katika safari yetu hii.’ Akasema (Joshua) Hivi jee
unakumbuka tulipopumzika kwenye jiwe? kwa hakika mimi nimemsahau (samaki
katika sehemu hio) na hakuna isipokua shaytan ndie alienifanya nisahau
kumkumbuka, na akafuata njia yake Baharini kimaajabu.

Aya zinatuonesha kua baada ya safari ndefu Nabii Musa akawa anahisi kuchoka hivyo
akaona kua umefika wakati wa kula ili kuipa miili nguvu kwa ajili ya kuendelea na safari,
hivyo Nabii Musa akamwamia Joshua kua atayarishe chakula kwani washatembea kwa
mda mrefu, ambapo baada ya kuamriwa hivyo basi Joshua nae akakumbuka kua yule
samaki ametoka kwenye mkoba na kuelekea Baharini.

Na hii inaonesha kua Joshua aidha aliona namna samaki alivyotoka na kukimbilia
baharini kwa urahisi na kushindwa kumzuia kutokana na maajabu ya Miujiza aliyoiona
ya samaki aliebanikwa, ambae ni kipande kugeuka kua mzima na mwenye kuishi na
kukimbilia Bahari. Au pia inamaanisha kua Joshua hakumuona samaki huyo wakati
anatoka kwenye mkoba na kukimbilia Baharini, lakini aliona alama ya njia aliyoiachwa
Samaki huyo wakati akikimbilia kwa kuteleza kuelekea Baharani kwa urahisi sana.

Hivyo mbali ya kua aliona moja kati ya matukio hayo ya Maajabu lakini hapo hapo aya
zinaonesha kua Joshua alisahau kabisa kumwambia Nabii Musa kuhusiana na tukio hilo,
ambapo kuna baadhi wanaweza wakajiuliza ilikuje mpaka Joshua akasahau kuhusiana na
tukio la ajabu kama hili?

Hivyo anasema Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Inabidi tufahamu
kua Joshua hapa alikua na Mmoja kati ya Watu watukufu mbele ya Allah Subhanah
wa Ta’ala, hivyo alikua akiona mambo mengi yanayotokea ya kimiujiza’. Hivyo
861

haiwezekani kua kwake yeye kila anachokiona cha Miujiza amuelezee au amuulize Nabii
Musa.

Ambapo anasema Imam Muhammad Ibn Saib Al Kalbi kua: ‘Joshua alikoga kwenye
chemchem ya maji iliyokua ikitiririka katika sehemu hio na maji yake yakaingia
kwenye mkoba ambao ndani yake alikuwemo samaki wao, na samaki huyo akawa
hai na kuruka ruka kutokana na maji hayo na kutumbukia kwenye maji’.

Hivyo Nabii Musa baada ya kusikia kuhusiana na habari hio ya samaki wao aliekua
sarraba basi hali ikawa kama zinavyosema aya:

ِ‫ﺎل ٰذﻟِﻚ ﻣﺎ ﻛﻨﱠﺎ ﻧـﺒ ِﻎ ﻓﭑرﺗﺪﱠا ﻋﻠَﻰ آﺎﺛ ِر‬


﴾ً‫ﻗَﺼﺼﺎ‬
َ َ َ ٰ َ َْ َ َْ ُ َ َ َ َ‫﴿ﻗ‬
‫ﺎ‬‫ﳘ‬
Qala dhalika ma kunna nabghi fairtadda AAala atharihima qasasan(Surat Al Kahf
18:64)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa) : ‘Hicho ndicho tulichokua tukikitafuta’ kisha


wakarudi kupitia katika athari zao (nyayo zao) kuzifuata.

Allah Subhana wa Ta’ala anatuonesha utajiri wa Lugha ya Kiarabu na uzuri wa


mpangilio wake ndani ya Quran na hivyo kuturahishia kutiririka nazo aya zake, kwani
aya zote za kisa hiki zimemalizia na fat-ha ambapo tunapoiangalia aya hii basi tunaona
kua imemalizia na maneno Atharihima Qasasan ambapo Athari maana yake hua ni Athari
Au Hatua au Nyayo na neno Qasasan linamaanisha Kuweka au kupiga Muhuri, Kurudia
kitu, Kufuata kitu na pia humaanisha kuhadithia Kisa au kuhadithia Hadith au Kutaja
kitu.

Hivyo basi baada ya kugundua kua wanachokifuata na kukitafuta wamekiacha nyuma na


wameshakipita basi Nabii Musa na Joshua waligeuka na kuanza kufuata hatua za nyayo
zao walizopita hapo kabla ili wafike kwa urahisi pale katika sehemu ambayo walipopiga
kambi jana yake. Na hii inatufunza pia umuhimu wa kutovunjika Moyo katika kutafuta
Ilm kwani Nabii Musa ilimibidi akirudie kile ambacho ameshakipita hapo kabla.

Nao wakarudi moja kwa moja huku njaa yote na machovu yakiwa yamekata, kwani
habari hizi zilimtia ari kubwa sana Nabii Musa na Joshua na hivyo haraka sana
wakakimbilia walipotoka, na walipofika..Subhnah Allah anaelezea Allah Subhanah wa
Ta’ala kwa kusema:

ِ
﴾ً‫ﻋ ْﻠﻤﺎ‬ ِ ِ‫﴿ﻓَـﻮﺟ َﺪا ﻋﺒﺪاً ِﻣﻦ ِﻋﺒ ِﺎد َ� آﺗَـﻴـﻨﺎﻩ ر ْﲪﺔً ِﻣﻦ ﻋ‬
�‫ﻨﺪ َ� َو َﻋﻠﱠ ْﻤﻨَﺎﻩُ ِﻣﻦ ﻟﱠ ُﺪ ﱠ‬ ْ ّ َ َ ُ َْ َ ْ ّ َْ َ َ
862

Fawajada AAabdan min AAibadina ataynahu rahmatan min AAindina


waAAallamnahu min ladunna AAilman(Surat Al Kahf 18:65)

Tafsir: Kisha wakampata mja miongoni mwa waja wetu ambae tumempa Rehma na
tukamfundisha kutoka kwetu I’lmu.

Anasema Sultan Al Balagha Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Mtu
huyo alikua ni Al Khidhr neno lenye kumaanisha mwenye Rangi ya Kijani, na
walimkuta akiwa amelala huku akiwa amejifunika shuka kuanzia kichwani mpaka
miguuni, alikua ni mtu ambae amepewa Ilm iliyofichika na isiyojulikana.’

Ambapo kuhusiana na ni kwa nini akawa anaitwa Al Khidhr yaani mwenye rangi ya
Kijani basi Wanazuoni wametofautiana juu yake, kwani wapo wanaosema kua ameitwa
wa Kijani kwa sababu Hikma na Busara zake ni zenye kunawirisha Ufaham, ambapo kwa
upande mwengine basi anasema Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua Al Khidhr ameitwa hiyo kwa sababu alikaa
kwenye ardhi ambayo ni kame yenye majani makavu na ardhi hio ikawa na rangi
ya Kijani kutokana na kuguswa nae.’

Kwani neno Al Khidhr linatokana na neno Khadhira ambalo hua linamaanisha Kua na
Rangi ya Kijani, Kua na Majani ya rangi ya kijani kilichopea na Kunawiri.

Hivyo Al Khidhr alikua ni Mja wa Allah Subhanah wa Ta’ala ambae amepewa Ilm
maalum kupitia kwa njia ya Wahy kwa njia ya Ilham ambayo hua wanapewa Mitume na
Manabii na Waja wema.

Ambapo wanazuoni wanasema kua Al Khidhr alikua akiitwa Balya Ibn Malkan Ibn Flakh
Ibn Anmbar Ibn Salakh Ibn Arfakhszyad Ibn Sam Ibn Nuh Ibn Lamek Ibn Mutawasiliykh
Ibn Idris Ibn Yard Ibn Mahalail Ibn Qayanyn Ibn Yanasy Ibn Seith Ibn Adam.

Ambapo kwa upande wa Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali basi anatuambia kuhusiana na
Ilm aliyokua nayo Al Khidhr kwa kuaianishia aina za Ilm pale aliposema: ‘Ama
kuhusiana na I’lm basi hua kuna aina mbili. Ambapo ya kwanza hua ni Ilm ambayo
hua ni Taa’lim Al Insan yaani inayotokana kwa njia ya kufudishwa na Mtu ambayo
imegawika katika sehemu mbili:

Ya kwanza hua ni Kusoma kwa kupitia njia ya kufudishwa na wengine na ya pili


hua ni kwa kupitia njia ya Mtu kusoma kwa kujifunza mwenyewe kwa kwa kutumia
Ufaham wake.
863

Aina ya pili ya Ilm hua ni Ilm ambayo hua ni Taa’alim Al Rabbana ambayo hii
hupatikana kwa kupitia kwa njia ya Allah Subhanah waTa’ala, hii nayo pia
imegawika katika sehemu mbili ambazo ni:

Ya kwanza hua ni Ilm kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala kuwashushia Manabii
wake ambayo hua inaitwa Al Ilm Al Anbiyah.

Ya pili hua ni Ilm kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala moja kwa moja kwa moja
kwa waja wake aliowachagua hii huainaitwa Al Ilm Al Laduni’

Ambapo kuhusiana na Al Khidhr kua ni Nabii ama La basi anasema Sultan Al


Mutakallimin Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Al Khidhr alikua ni
Mja aliechaguliwa Na Allah Subhanah wa Ta’ala kupata Unabii kwa njia ya Rehma
na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akasema kuhusiana nae kua ‘Ataynahu
Rahmah’ yaani Tumempa Rehma . Hii hua ni alama ya Unabii kwani kila ‘Nubuwah’
yaani Unabii hua ni Rehma lakini si kila Rehma hua Unabii, na kisha Allah
Subhanah wa Ta’ala akasema kua ‘WaAAallamnahu min ladunna Aailman yaani Na
tukamfundisha kutoka kwetu I’lmu.’ Ambapo hii inamaanisha kua mja huyu wa
Allah Subhanah wa Ta’ala hakufundishwa na Mtu wala na Mwalimu bali
alifundishwa moja kwa moja na Allah Subhanah wa Ta’ala.

Ambapo kwa upande wa Shaykh Al Akbar Imam Muhyi Ad Din Abu Bakr Ibn Arabi basi
yeye anasem kua: ‘Mawalii hua wana I’lm ambazo hua hazipatikani kwa Mitume,
kwani I’lm aliyokua nayo Al Khidhr ambayo Nabii Musa hakua nayo ilikua ni Ilm
Ladduni ambayo ni I’lm iliyofichikana. Hii hua ni Ilm ambayo ipo kwenye harfu
Waw ambayo hua ni harfu iliyofichikana baina ya harfu Kaf na harfu Nun katika
neno la Allah Subhanah wa Ta’ala ambalo ni KuN yaani Kua.

Kwani unapolitamka neno KuN basi hua lina harfu tatu ambapo ya kwanza ni harfu
iliyowazi na ya mwisho ni harfu Nun ambayo pia iko wazi na katikati yake kuna
harfu Waw ambayo imefichikana, na hivyo neno hili hua linajumuisha yaliyowazi
na yaliyofichikana. Na hivyo kumaanisha kua Allah Subhanah wa Ta’ala ambae
ndie Mungu wa Haki na ndie mwenye sifa zinazobainisha yaliyowazi na
yaliyofichikana.

Na pia hua linamaanisha Insan Al Kamil yaani Mtu aliekamilia ambae ndie Khalifa
wake hapa ardhini na mpangilio wake ambao Allah Subhanh wa Ta’ala
anaudhihirisha katika maneno yake ambayo anasema:

َ ‫﴿إِﱠﳕَﺎ ﻗَـ ْﻮﻟُﻨَﺎ ﻟِ َﺸ ْﻰ ٍء إِ َذآ أ ََرْد َ�ﻩُ أَن ﻧـﱠ ُﻘ‬


﴾‫ﻮل ﻟَﻪُ ُﻛ ْﻦ ﻓَـﻴَ ُﻜﻮ ُن‬
864

Innama qawluna lishay-in idha aradnahu an naqoola lahu kun fayakoonu (Surat An
Nahl 16:40)

Tafsir: Kwa hakika! Kauli yetu juu kitu tunachokikusudia, ni kukiambia Kua na
kinakua

Hivyo ametoa Herufi tatu, mbili zilizo wazi na moja iliyofichikana, ambapo katika
hali hii basi Insan Al Kamil yani Mtu aliekamilia hua ni mwenye kua na Mamlaka
ya Ukhalifa wa haki kama ilivyo baina ya herufi ya kabla yake na baada yake katika
neno Kun.’

Kwa upande mwengine basi kuna wasemao kua Ilm Ladunni hua pia ndio ile
inayojulikana kama Ilm Al Batin (yaani Ilm Iliyofichikana na hivyo hua inajulikana na
watu waliojaaliwa tu na Allah Subhanah wa Ta’ala) ambayo hua ni tofauti na Ilm Adh
Dhahir ambayo hua ni Ilm iliyo wazi, kwani Ilm Adh Dhahir hua inapatikana kutokana
na kusomeshwa na kusoma vitabu ambapo Ilm Batin hutokana na mtu husika kua ni
mwenye kufanyia kazi yale anayoyajua yanayotokana na Ilm Adh Dhahir na hivyo hua
na uzoefu ambao humpelekea kua na uwezo wa kufungua Milango ya kua na Ilm Batin.

Hii inakua kama vile ambavyo amesema Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu katika hadith
iliyomo kwenye Sahih Bukhari ambayo anasema kua yeye amesomeshwa na Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam Ilm za aina mbili yaani Ilm Adh Dhahir ambayo ni I’lm ya
Hadith na Ilm Al Batin ambayo ni siri yake, hadithi hio inasema kua; ‘Hakika mimi
nimepata Ilm za aina mbili kutoka kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, ya
kwanza tayari nimeshaisambaza ama hii ya pili kama nikiinukuu basi nitakatwa
Shingo.’

Ama kuhusiana na maisha yake anayoishi na uhai wake Al Khidhr basi kuna kutofautiana
kimtizamo kwani kuna mitizamo mingi sana kuhusiana nae kwani kuna wasemao kua
alianzia kuishi uhai wake duniani katika kipindi cha Nabii Adam na ndie aliemzika Nabii
Adam na kuna wasemao kua aliishi pia katika wakati wa Nabii Nuh, na pia alikuwa
akiishi katika kipindi cha Nabii Ibrahim, na katika kisa cha Dhul Qarnayn na katika hiki
kisa cha Nabii Musa na pia yumo katika kisa cha Nabii Sulayman na hata katika kisa cha
Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam pia yumo, hivyo kama nikimuelezea kwa kina
kuhusiana na Maisha yake na Uhai wake basi bila ya shaka itabidi niandike kitabu kizima
peke yake.

Kwa hivyo tutamzungumzia kwa juu juu kuhusiana na uhai wake ili tupate kufaham
kuhusiana nae japo kidogo katika kisa hiki cha Nabii Musa. Ambapo inabidi tufaham kua
Wanazuoni wanasema kua kimaumbile Uhai umegawika katika Darja tano tofauti
ambazo ni:
865

1- Darja ya Kwanza ambayo ni ya Uhai wa Maisha tunaoishi sisi viumbe Ibn Adam
wa kawaida ambao hua ni wenye mipaka ya mahitajio ya Kimaumbile ambayo
yanahitajikana kila kumbe Ibn Adam.

2- Darja ya Pili ambayo ni ya Uhai wanaoishi Viumbe kama Al Khidr na Nabii Ilyas
ambao hua una mipaka lakini haifikii mipaka iliyomo katika darja ya Uhai wa
aina ya kwanza, kwani darja hii kimaumbile hua inawaruhusu viumbe wake kua
katika sehemu tofauti katika wakati mmoja, na hivyo hua wanaweza kula na
kunywa kama sisi lakini hapo hapo huwa hawafanya hivyo kwa sababu ya
Ulazima kama ilivyo kwetu sisi ambao ili tuishi basi kula hua ni lazima lakini
kwao wao hua si lazima kufanya hivyo, kwani wanaweza kuishi bila ya kula kwa
mda mrefu zaidi na bila ya kudhurika kiafya na hivyo basi hata maumbile ya
miili yao hua si yenye kuathirika na athari ya wakati kwa mfano kuzeeka,
kutoweka katika sehemu moja na kutokea katika sehemu nyengine kwa haraka
sana. n.k

3- Darja ya Tatu ambayo n ya Uhai wa maisha ya Viumbe kama Nabii Idris na


Nabii Isa. Ambao wao maumbile yao yapo katika hali ambayo haihitaji mahitajio
ya Kibinadam kwani maumbile yao hua yapo kama maumbile ya Kimalaika
ambao wanaishi Mbinguni lakini wakiwa na miili ya Kibinadam.

4- Darja ya Nne ambayo ni ya Uhai wa Maisha ya Waumini waliofanikiwa kupata


Ushahidi baada ya kufariki kutokana na kujitolea muhanga kwa Ajili ya Allah
Subhanah wa Ta’ala. Hivyo hua wamejaaliwa wapo katka mazingira ya Kua ni
wenye kuishi kama wlivyokua wakiishi Ulimwenguni lakini wakiwa na raha ya
kila aina ndani yake, na hivyo hua hawajioni kua wamekufa kama vile ambavyo
wanavyojiona Ibn Adam wengine walioko Makaburini baada ya kufariki kwao.
Yaani ili kuelewa vizuri hali hii basi kwa kifupi tuchukulie mfano wa hali ya mtu
ambae amelala na kisha akaota yuko Peponi na hivyo hua ni mwenye kuomba
asizindukane katika ndoto yake kutokana na uzuri wa ndoto hio.

5- Darja ya Tano ambayo ni ya Uhai wa Maisha ya Kiroho baada ya kufariki na


kuingia Kaburini, ambayo kwa upande mwengine hua pia ni ya Mtu aliekufa na
akajijua kua amekufa na hivyo hua anaishi maisha ya kiroho ambayo mfano
wake pia hua ni kama wa mtu alielala na kisha akaanza kuota ndani ya usingizi
866

wake huo, ambapo hali yake katika mazingira hayo ya kaburini hua
yanategemea na namna alivyokua akiishi Duniani kabla ya kuingia Kaburini.

Yaani kama alikua ni Mtiifu kwa Mola wake basi atakua katika hali nzuri ambayo
inafanana na ya Mashahidi na hivyo atakua katika hali kama ya mtu ambae anaota
na kisha kutokana na raha na uzuri wa Ndoto hio kua yuko Peponi basi ataomba
ndoto hio iendelee milele.

Lakini kama alikua si mwenye kua na Utiifu kwa Mola wake na hivyo kua ni muasi
basi ali ya mtu huyu mfano wake hua ni kama mtu alielala na kisha akaota ndoto
ya jinamizi na yenye kutisha kwani anapata adhabu sawia na za watu wa Mtoni na
hivyo hua anataka kuzindukana lakini sasa haiwezekani, kwa sababu
anaezindukana kutoka ndotoni hua ni alie hai tu.

Hivyo basi kulingana na mitizamo ya Wanazuoni tunaona kua Al Khidhr yupo hai katika
hali ya maumbile ya Uhai wa darja ya pili ambayo ni hali aliyokua nayo Nabii Ilyas pia.

Na ndio maana Wanazuoni wa Tafsir wamekua wakisema kua: ‘Kuna Manabii wanne
ambao wapo hai, ambapo wawili kati yao wanaishi Duniani na wawili wanaishi
Mbinguni. Wanaoishi Duniani ni Al Khidhr na Ilyas na wanaishi Mbinguni ni Idris
na Isa.’

akasema Imam Sufyan Ibn Uyaynah kua amesema Amr Ibn Dinar kua; ‘Al Khidhr na
Ilyas watakua hai wanaoishi hapa Duniani hadi pale itakapokua hakuna Qur’an
Duniani’

Ambapo amesema Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu kua: ‘Al Khidhr anaishi
Baharini na Ilyas anaishi Ardhini ambapo wawili hawa hua nin wenye kukutana
kilasikuusiku katika Ukuta wa Dhul Qarnayn baina ya Watu na Juj wa Majuj, na
pia hua wanafanya Ibada ya Hija pamoja kila mwaka na wanakunywa maji ya
Zamzam ambayo huwatosheleza kwa mwaka mzima.’

Akasema Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu tena pia kua: ‘Katika Maziko ya Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikuja mtu ambae ana ndevu za rangi nyekundu,
ambae alipita huku akiwa analia na kisha akawageukia Masahaba na akasema:
‘Kwa Allah Subhanah wa Ta’ala ndiko kwenye Uliwazo wa kila Mtihani na fidia ya
kila kilichopotea hivyo mgeukieni Allah kwa kuomba Msamaha na kwa kia
mnachokitamani.’ Hivyo Masahaba wakaulizana kama wanamjua mu huyo,
ambapo Abu Bakr Radhi Allahu Anhu na Ali Ibn Abi Talib Radhih Allahu Anhu
867

wakasema: ‘Naam yule ni ndugu yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, Al
Khidhr Alayhi Salam.’

Na akasema tena Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mimi nilitoka siku moja na
Rasul Alla Salallahu Alayhi wa Salam ambapo mar ghafla tukasiia sauti kutoka kwa
baadhi ya watu, ambpo nae akasema: ‘Anas hebu kaangalie kuna nini tena?’ Hivyo
mimi nikaenda na nilipofika nikakuta kuna mtu anaomba Dua kwa kusema kua:
‘Ya Allah! Nijaalie mimi kua ni miongoni mwa watu wa Ummah wa Muhammad
ambao umeujaalia kua ni wenye kuingizwa kwenye rehma zako na kusamehewa,
na maombi yao kua ni yenye kukubaliwa, na toba zao kukubaliwa’

Hivyo mimi nikarudi kwa Rasul Allah Salallau A’layhi wa Salam na kumwambia
kuhusiana na niliyoyaona na kuniambia kua: ‘Nenda kamwambie kua: ‘Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam anakuuliza: ‘Wewe ni Nani?’ Nami nikarudi kwa mu
huyo na na kumpa ujumbe wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam nae akasema:
‘Mwambie kua mimi ni Ndugu yake, yaani Al Khidr na mwambie kua aniombee
kwa Allah Subhanah wa Ta’ala kua anijaalie niwe miongoni mwa watu wa Ummah
wa Muhammad ambao umeujaalia kua ni wenye kuingizwa kwenye rehma zako na
kusamehewa, na maombi yao kua ni yenye kukubaliwa, na toba zao kukubaliwa’’’

Ama kwa upande wa Shaykh al Islami Muhyi Ad Din Imam Abu Zakarriyah Yahya Ibn
Sharaf An Nawawi basi anasema kuhusiana na Al Khidhr kua: ‘Ama kuhusiana na
yaliyotufikia sisi kuhusiana na Al Khidhr kutoka kwa Wanafiqh wanaokubalika ni
kua: ‘Kuhusiana na kisa cha Al Khidhr kumtembelea Rasul Allah Salallahu Alayhi
wa salam baada ya kufariki kwake basi ni kua imenukuliwa na Imam Al Shafii
katika kitabu chake cha Al Umm kupitia katika sanad ambayo ni dhaifu ya nukuu
hio. Ambamo hata hivyo (Imam Al Shafii) hakutaja jina la Al Khidhr bali alisema
tu kua: ‘Masahaba walisikia kua kuna mtu aliesema kadha wa kadha.’Jina la Al
Khidhr halikutajwa na Imam Al Shafii isipokua baadhi ya Wanafiqh wetu ambao
ni wenye uthibitisho wao wenyewe ndio wakaandika jina la Al Khidhr. Hivyo
Mtizamo sahih ni kua Al Khidhr yuko hai na anaishi na hii ni kulingana na wengi
miongoni mwa wanazuoni.’’

Na kwa upande wa Shaykh al Islami Imam Shams Ad Din Al Ramli Al Shafii basi yeye
anasema kuhusiana na Al Khidhr na Nabii Ilyas kua: ‘Al Khidhr ni Nabii na wala si
Walii na hii ni kulingana na Mtizamo wa wengi miongoni mwa Wanazuoni, kama
vile ambavyo alivyosema Al Khidhr ndani ya Qur’an kua: ‘Sikufanya haya kwa
hiari yangu’ na kama alivyosema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qur’an kua:
‘Tumempa Rehma kutoka kwetu’ ambayo hua inamaanisha kua ni Wahy na
Unabii’
868

‘Na hivyo Kauli hii ya kua amejaaliwa Rehma ambayo inamaanisha Wahy na
Unabii hua haimaanishi kua ni Uwalii. Na huo ndio uhalisi ulivyo hata kama baadhi
ya Wanazuoni wanasema kua si Nabii. Na mtizamo sahih ni kua bado yuko hai
kama alivyosema Imam Ibn Salah, kua: ‘Wengi miongoni mwa Wanazuoni
wamekubaliana kua yuko hai kwani hata watu wa kawaida wanaamini juu ya hili’
na Imam An Nawawi amesem kua: ‘Wengi miongoni mwa Wanazuoni wanasema
kua Al Khidhr anaishi miongoni mwetu, na juu ya hili pia wanakubaliana Watu
wenye Ilm ya Tasawwuf na watu Wacha Mungu, ambao wamethibitisha kua
wamemuona kwa kupitia njia ya kupata ufunuo, na wakakutana nae katika hali ya
kawaida, na kupata Ilm kutoka kwake, baada ya kumuuliza masuali na kupata
majibu ya masuali hayo kutoka kwake na pia kutokana na kuonekana kwake katika
sehemu takatifu mara nyingi sana. Hivyo basi Al Khidhr ni Ibn Adam na wala si
Malaika na sehemu ya makazi yake yapo kama yalipo makazi ya Ilyas ambapo ni
katika ardhi ya Uarabuni.’’

Ambapo anasema Imam Abd Raḥmān Ibn Alī Ibn. Muḥammad Abu Al Farash Ibn Al Jawzy
kua: ‘Bilal Al Khawas alikutana na Al Khidhr na kumuuliza: ‘Jee unasemaje
kuhusiana na Imam Al Shafii’ Al Khidhr akasema: ‘Hakika yeye Al Shafii ni Nguzo
ya Mawalii’ Bilal Al Khawas akauliza: ‘Na Ahma Ibn Hnabal?’ Al Khiudhr
akasema: ‘Yeye ni Siddiq’’

Na kwa upande wa Imam Shams Ad Din Muhammad Ibn Abd Rahman Al Sakhawi basi
anasema kua: ‘Ni jambo lialojulikana sana ua An Nawawi alikua akikutana na na Al
Khidhr na kuzungumza nae kuhusiana na mengi katika Ufunuo wake’ ambapo
Imam An Nawawi alikua kumwita Al Khidhr kwa jina la Abu Al Abbas.

Naam, hio ni kwa ufupi kuhusiana na Uhai na Maisha ya Al Khidhr, hivyo tunarudi kwa
Nabii Musa katika sehemu aliyokutana na Al Khidhr.

QISA AL MUSTAQILLA - NABII MUSA NA AL KHIDHR


Nabii Musa na Joshua wakamkuta Al Khidhr akiwa anasali katika Msala wa rangi ya
Kijani ambao unaelea juu ya maji, wakamsubiri mpaka alipomaliza kisha wakamsalimia
na Al Khidhr kwa kusema: ‘Asalaam Alaykum’. Na Al Khidhr akaitikia salam hio kwa
kusema: ‘Wa Alaykum Salaam ewe Mtume wa Bani Israil’ Nabii Musa akashangaa na
kumuuliza Al Khidhr: ‘Umejuaje kua mimi ni Mtume wa Bani Israil?’
869

Al Khidhr akasema: ‘Aliekutuma kwangu ndie alieniambia kua nani anakuja


kwangu’ na kisha Al Khidhr akamwambia Nabii Musa: ‘Ewe Musa kama umekuja
kuuliza suali basi uliza, na usikilize jibu lake, kisha uendelee na majukumu yako,
nami niendelee na majukumu yangu, ili usinipelekee mimi kua ni mwenye
kusimamisha majukumu yangu mbele ya Mola wangu, na pia usijipelekee wewe
ambae ni Mtume mwenye majukumu makubwa zaidi mbele ya Mola wako,kua ni
mwenye kusimamisha majukumu yako mbele ya Mola wako, nami sitaki kua ni
mwenye kukosea katika kutekeleza majukumu yangu.’

Nabii Musa akasema; ‘La, Hakuna suali, ila Mola wangu amenituma nije kwako ili
nipate kujifunza miongoni mwa Hikma alizokuajaalia wewe kua nazo.’

Wakati wanazungumza mara akatokea ndege ambae akanywa maji na kisha akaondoka,
Al Khidhr akasema: ‘Ewe Musa! Kua muangalifu kwani wewe ni mwenye Ilm zaidi
miongoni mwa watu wa Bani Israil na miongoni mwa watu wa Ulimwenguni katika
wakati huu, lakini Ilm yako na yangu na ya waliotangulia kabla yetu na ya
watakaokuja baada yetu basi hua si zaidi ya maji aliyochukua ndege kwenye
mdomo wake kutoka kwenye Bahari, ukilinganisha na Ilm ya Allah Subhanah wa
Ta’ala.’

Nabii Musa akasema kama inavyosema aya ifuatayo:

﴾ً‫ﺖ ر ْﺷﺪا‬ ِ‫ﺎل ﻟَﻪ ﻣﻮﺳﻰ ﻫﻞ أَﺗﱠﺒِﻌﻚ ﻋﻠَﻰ أَن ﺗُـﻌﻠِّﻤ ِﻦ ِﳑﱠﺎ ﻋﻠ‬
ُ ُْ
َ ‫ﻤ‬ّ ََ ٰ َ َ ُ ْ َ ٰ َ ُ ُ َ َ‫﴿ﻗ‬
Qala lahu moosa hal attabiAAuka AAala an tuAAallimani mimma AAullimta
rushdan (Surat Al Kahf 18:65)

Tafsir: Akasema Musa (kumwambia Al Khidhr): ‘Jee nikufate ili upate kunifundisha
sehemu ya kile ulichofundishwa kwa uongofu?’

Ambapo aya inatufahamisha namna inavyotakiwa mtu mwenye kutafuta Ilm awe na hali
gani mbele ya yule anaetaka kupata Ilm kutoka kwake, yaani kama alivyosema Mujaddid
Ad Dini Imam Fakhr Ad Din Al Razi kuhusiana na aya hii kua : ‘Aya inatuonesha kua
Mwanafunzi anatakiwa awe na unyenyekevu mbele ya Mwalimu wake’ kwani aya
inatuonesha namna Nabii Musa anavyokubaliana na hali ya kua ingawa yeye ni Mtume
wa Allah Subhanah wa Ta’ala lakini hapo hapo kuna mambo yeye bado ana ujinga nayo
yaani hayajui. Hivyo basi anakubali kua mjinga na hivyo kua ni mwenye kuomba ruhusa
ili apate kufundishwa hayo asiyoyajua.
870

Na kutokana na Nabii Musa kua na hali hio basi Al Khidhr akamuwekewa wazi Nabii
Musa kwa kumwabia kua:

ِ ِ ِ ‫ﻚ ﻟَﻦ ﺗَﺴﺘَ ِﻄ‬


ْ ُ ‫ﺼِﱪُ َﻋﻠَ ٰﻰ َﻣﺎ َﱂْ ُﲢ ْﻂ ﺑِﻪ‬
﴾ً‫ﺧﱪا‬
َ ‫ﺻ ْﱪاً ۞ َوَﻛْﻴ‬
ْ َ‫ﻒ ﺗ‬ َ ‫ﻴﻊ َﻣﻌ َﻰ‬
َ ْ َ ‫ﺎل إِﻧﱠ‬
َ َ‫﴿ﻗ‬
Qala innaka lan tastateeAAa maAAiya sabran; Wakayfa tasbiru AAala ma lam
tuhit bihi khubran(Surat Al Kahf 18:67-68)

Tafsir: Akasema (Al Khidhr) ‘Kwa Hakika wewe hutoweza kua na subira nami; Na
vipi utasubira juu ya kile ambacho hujapewa habari yake?’

Hivyo Al Khidhr anamwabia Nabii Musa kua Ilm aliyokua nayo yeye ni tofauti na namna
yanavyoonekana maisha kwani yeye ni mwenye kua na habari juu ya yale ambayo
wengine hawana habari nayo, na hivyo basi kwake yeye Al Khidhr kutokana na kua na
habari ya yasiyojulikana habari yake hua ni mwenye kuweza kuona kuhusiana na kile
kinachoonekana kua ni faida kwa wengine kua kwake yeye hua ni hasara, na hasara kua
ni faida, na ukatili hua unaweza ukawa ni huruma na kulipa wema kutokana na uovu
huweza kua ni Uadilifu, hii yote ni kutokana na Hikma zake Allah Subhanah wa Ta’ala.

Hivyo kwa Nabii Musa inaweza ikawa mtihani kwake na hivyo kushindwa kua na Subra
juu ya mambo ambayo hana habari nayo wala matokeo yake, lakini Al Khidhr ana habari
ya matokeo ya mambo hayo kwani yeye Al Khidhr amepewa Ilm ambayo Nabii Musa
hakupewa na hapo hapo Nabii Musa amepewa Ilm zaidi ya Al Khidhr. Hivyo Nabii Musa
akasema:

ِ ‫ٱﻪﻠﻟ ﺻﺎﺑِﺮاً وﻻَ أ َْﻋ‬ ِ ۤ ِ َ َ‫﴿ﻗ‬


َ َ ُ‫ﺎل َﺳﺘَﺠ ُﺪِﱐ إن َﺷﺂءَ ﱠ‬
﴾ً‫أﻣﺮا‬
ْ ‫ﻚ‬
َ َ‫ﺼﻰ ﻟ‬
Qala satajidunee in shaa Allahu sabiran wala aAAsee laka amran(Surat Al Kahf
18:69)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa) ‘In shaa Allah utanikuta mimi kua ni mwenye kua na
Subra na wala sitoasi amri yako’.

Hapa Nabii Musa anaweka wazi kwa kuahidi kua hatomuasi Mwalimu wake huyo
kutokana na namna alivyokua na hamu na ari ya kutaka kujifunza kutoka kwake, na hivyo
atakua na Subra juu ya kila kitu kitakachotokea, In-shaa Allah, yaani kama Allah
Subhanah wa Ta’ala akimjaalia kumuwezesha kua na Subra juu ya jambo husika, kwani
ingawa Nabii Musa anahesabika kua ni miongoni mwa Manabii wenye Subra na azma
871

kubwa yaani Ulu ul Azmin minna Rusul lakini hata hivyo hajui hali itakuaje hapo baadae
kwani katika mambo ambayo mtu anaweza akaahidi lakini akashindwa kutimiza ahadi
yake hapo baadae kutokana na hali ya mazingira basi ni Subra, yaani mtu unaweza
ukaahidi kua utakua mstahmilivu lakini ukweli ni kua kimaumbile basi kila mtu anakua
na mipaka yake ya kua na Subra.

Na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akatufundisha ndani ya Qur’an kuomba dua
iliyomo ndani ya aya ifuatayo:

ِ
َ‫ﺖ َرﺑـﱠﻨَﺎ ﻻ‬
ْ َ‫ﺖ َو َﻋﻠَْﻴـ َﻬﺎ َﻣﺎ ٱ ْﻛﺘَ َﺴﺒ‬ْ َ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻧَـ ْﻔﺴﺎً إِﻻﱠ ُو ْﺳ َﻌ َﻬﺎ َﳍَﺎ َﻣﺎ َﻛ َﺴﺒ‬ ‫ﻒ ﱠ‬ ُ ّ‫﴿ﻻَ ﻳُ َﻜﻠ‬
ِ‫ﱠ‬ ِ ِ ِ
‫ﻳﻦ‬
َ ‫ﺻﺮاً َﻛ َﻤﺎ َﲪَْﻠﺘَﻪُ َﻋﻠَﻰ ٱﻟﺬ‬ ْ ِ‫َﺧﻄَﺄْ َ� َرﺑـﱠﻨَﺎ َوﻻَ َْﲢﻤ ْﻞ َﻋﻠَْﻴـﻨَﺂ إ‬ ْ ‫ﺗُـ َﺆاﺧ ْﺬ َ� إِن ﻧﱠﺴﻴﻨَﺂ أ َْو أ‬
ِ ِ
‫ﺖ‬َ ‫ﻒ َﻋﻨﱠﺎ َوٱ ْﻏﻔْﺮ ﻟَﻨَﺎ َو ْٱر َﲪْﻨَﺂ أَﻧ‬ ُ ‫ٱﻋ‬ ْ ‫ِﻣﻦ ﻗَـْﺒﻠﻨَﺎ َرﺑـﱠﻨَﺎ َوﻻَ ُﲢَ ِّﻤ ْﻠﻨَﺎ َﻣﺎ ﻻَ ﻃَﺎﻗَﺔَ ﻟَﻨَﺎ ﺑِِﻪ َو‬
﴾‫ﺼﺮَ� َﻋﻠَﻰ ٱﻟْ َﻘﻮِم ٱﻟْ َﻜﺎﻓِ ِﺮﻳﻦ‬
َ ْ ْ ُ ْ‫َﻣ ْﻮﻻَ َ� ﻓَﭑﻧ‬
La yukallifu Allahu nafsan illa wusAAaha laha ma kasabat waAAalayha ma
iktasabat rabbana la tu-akhidhna in naseena aw akhta/na rabbana wala tahmil
AAalayna isran kama hamaltahu AAala alladheena min qablina rabbana wala
tuhammilna ma la taqata lana bihi waoAAfu AAanna waighfir lana wairhamna
anta mawlana faonsurna AAala alqawmi alkafireena (Surat Al Baqara 2:286)

Tafsir: Haikalifishi Allah Nafsi (ya mtu yeyote)isipokua juu ya kile inachokiweza,
inalipwa (Nafsi ya Mtu) kutokana na (mema) iliyoyachuma na itaadhibiwa kutokana
na (dhambi) ilizozichuma. ‘Ewe Mola wetu Usituadhibu kutokana na tulichokisahau
au tulichokikosea. Ewe Mola wetu usitubebeshe mizigo kama ulivyowabebesha
waliotangulia kabla yetu. Ewe Mola wetu Usitubebeshe mizigo zaidi ya uwezo wetu,
Tusamehe na utuingize kweye Msamaha wako na utuingize kwenye Rehma zako kwani
wewe ndie Msimamizi wetu na tunusuru dhidi ya watu wenye kukufuru’

Ambapo katika kutilia mkazo umuhimu wa Dua iliyomo ndani ya aya hii basi Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam amesema kuhusiana na aya hii pamoja na ile kabla ya aya hii
yaani aya ya 287 ya Surat Al Baqara kua: ‘Hakika mimi nimepewa aya mbili ambazo
zilikuwemo kwenye hazina iliyomo chini ya Arshi, ambazo hakuwahi kupewa
Mtume yeyote yule hapo kabla.’

Hivyo Al Khidhr akakubaliana na ahadi hio ya Nabii Musa kua atakua na Subra, na
kukubali kua atafuatana nae lakini kwa sharti la kumpa tahadhari Nabii Musa kwa
872

kumwambia kua yeye anajua kua inawezekana kua na Subra kutokana na Vitendo vyangu
lakini itakua vigumu kutofanya lolote dhidi ya vitendo vyangu hivyo utashindwa kujizuia
na utataka kuniuliza masuali, hivyo basi usiniulize chochote mpaka pale mimi
mwenyewe nitakapoona kua tayari umefika mda wa kukufafanulia, kama zilivyosema
aya:

ٍ
ْ ‫ِذ‬
﴾ً‫ﻛﺮا‬
ُ‫ﻚ ﻣْﻨﻪ‬ َ ‫ُﺣ ِﺪ‬
ِ َ َ‫ث ﻟ‬ ِ َ َ‫﴿ﻗ‬
ْ ‫ﺎل ﻓَِﺈن ٱﺗـﱠﺒَـ ْﻌﺘَِﲎ ﻓَﻼَ ﺗَ ْﺴﺄَﻟْﲎ َﻋﻦ َﺷﻲء َﺣ ﱠ ٰﱴ أ‬
Qala fa-ini ittabaAAtanee fala tas-alnee AAan shay-in hatta ohditha laka
minhu dhikran(Surat Al Kahf 18:70)

Tafsir: Akasema (Al Khidhr) ‘Hivyo kama utanifuata basi usiniulize chochote hadi
pale nitakapo kuhadithia mimi kutokana nalo ukumbusho wake’

Hivyo Al Khidhr akamalizia Ibada zake na kisha akaondoka yeye na Nabii Musa na
Joshua ambao walikua wanamfuata nyuma yake, wakatembea kwa takriban masafa ya
Parasang 2 yaani Kilomita 12, hivyo kwa kua Nabii Musa na Joshua hawakuwahi kula
pale walipokumbuka kuhusiana na Samaki wao na walipomuona kua katoweka basi njaa
yao yote ilitoweka, na hawakuihisi tena baada ya kukutana na Al Khidhr mpaka baada
ya masafa hayo ya kilomita 12, hivyo Nabii Musa akasema: ‘Hakika mimi nimechoka
na siwezi kuendelea zaidi na safari, mpaka baada ya kula’ hivyo wakakaa kitako na
Allah Subhanah wa Ta’ala akajaalia wakaona mbele yao Malaika ambae amekuja na
sahani za vyakula, ambapo sahani moja miongoni mwao ilikua imeshapikwa na mbili
zikawa bado hazijapikwa, kisha wakaambiwa kua iliyopikwa ni ya Al Khidhr a ambazo
hazijapikwa ni za Musa na Joshua.

Nabii Musa akanyanyuka na kutafuta kuni yeye na Joshua kwa ajili ya kuoika chakula
chao, huku Al Khidhr alikaa na kuwasubiri mpaka kilipokuatayari chkula chao na
wakakaa na kuanza kula pamoja huku Al Khidhr akiwa ni mwenye kusema:
‘Namshukuru Allah Subhanah wa Ta’ala kwa Rehma zake na hikma zake, kwani
amemtumia Mja wake mwenye Subra chakula kilichokua kimeshapikwa ili ale bila
ya kutumia jitihada yeyote , na akamtumiia mja wake asiekua na Subra chakula
ambacho hakijapikwa ili apate kula baada ya kufanya jitihada.’

Ambapo anasema Ubayy Ibn Kaab Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Al Khidhr na Nabii Musa waliendelea na safari
yao, pembeni ya mwambao wa Bahari, mara wakaliona Jahazi linapita na
wakaomba wachukuliwe na Jahazi hilo, wakachukuliwa bila ya Malipo yeyote, na
walipofika bali baharini basi Al Khidhr akachukua shoka na kulitoboa Jahazi hilo,
ili maji yapate kuingia ndani yake. Hivyo Musa akachukua nguo yake na kuiziba
873

sehemu hio. Nabii Musa akasema: ‘Jee umelitoboa ili uwazamishe watu wake?
Hakika watu hawa wametuchukua na kutufanyia ukarimu halafu wewe umetoboa
tundu kwenye Jahazi lao.’’’

Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea hali hio katika aya ifuatayo ambayo inasema:

ِ ِ َ َ‫﴿ﻓَﭑﻧْﻄَﻠَ َﻘﺎ َﺣ ﱠ ٰﱴ إِ َذا َرﻛِﺒَﺎ ِﰱ ٱﻟ ﱠﺴ ِﻔﻴﻨَ ِﺔ َﺧَﺮﻗَـ َﻬﺎ ﻗ‬


َ ‫َﺧَﺮﻗْـﺘَـ َﻬﺎ ﻟﺘُـ ْﻐ ِﺮ َق أ َْﻫﻠَ َﻬﺎ ﻟََﻘ ْﺪ ﺟْﺌ‬
‫ﺖ‬ َ ‫ﺎل أ‬
﴾ً‫ﺷﻴﺌﺎً إِﻣﺮا‬
ْ َْ
Faintalaqa hatta idha rakiba fee alssafeenati kharaqaha qala akharaqtaha
litughriqa ahlaha laqad ji/ta shay-an imran(Surat Al Kahf 18:71)

Tafsir: Hivyo wakaondoka na kufuatana pamoja mpaka wakapanda kwenye Jahazi.


(Al Khidhr) Akalitoboa, akasema (Nabii Musa); ‘Umelitoboa ili uwagharikishe watu
wake, kwa hakika umefanya jambo kubwa sana (kutokana na Ubaya wake)’

Aya imetumia neno Intalaqa ambalo ni lenye kutokana na neno Talaqa hua linamaanisha
Talaka, Kuacha, Kua huru kutokana na Ushirika wa kitu, Kukataa kukubaliana juu ya
Usimamizi wa kitu. Ambapo neno Intalaqa hua linamaanisha Kuanza kufanya Jambo au
kitu, Kuanza kuondoka au kua Huru.

Tunapoiangalia aya basi imetumia neno Imran ambao limetokana na neno Amara ambalo
hua ni leneye kumaanisha Amri, Amuru au Jambo ambalo hua ni lenye kusababisha
Matokeo fulani baada ya kufanywa kwake. Ambapo tunapozungumzia Amri kwa upande
wa Allah Subhanah wa Ta’ala basi jambo hilo hua halina matokeo yeyote isipokua
mazuri na yenye manufaa ndani yake kutokana na hikma zake. Lakini tunapozungumzia
Amri kutoka kwa upande wa Kiumbe basi hua kuna yenye kusababsisha Matokeo mazuri
na pia hua kuna yenye kusababisha matokeo mabaya.

Hivyo hapa Nabii Musa alikua akimwambia Al Khidhr kua kwa hakika wewe umefanya
Jambo lenye Amrisho ambalo ni lenye matokeo makubwa sana kutokana na ubaya wake,
kwani litaiamrisha Jahazi hio kuzama na kuwagharikisha watu wote waliomo ndani ya
Jahazi hilo ambao waliwasaidia wao hapo kabla.

Na anasema Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua; ‘Nabii Musa
akasema ndani ya Nafsi yake, Hivi nnafanya nini mie na Mtu huyu, wakati kama
ningekua na watu wa Bani Israil basi ningekua nawasomea Tawrat sasa hivi na
kuwaamrisha kufanya mema na wangekua wananitii.’
874

Ambapo Al Khidhr akamwambia Nabii Musa: ‘Jee nikuambie ulikua unasema nini
ndani ya Nafsi yako?’ Nabii Musa akasema: ‘Naam, niambie’ Al Khidhr akasema:
‘Ulikua unasema kua : ‘Hivi nnafanya nini mie na Mtu huyu, wakati kama ningekua
na watu wa Bani Israil basi ningekua nawasomea Tawrat sasa hivi na kuwaamrisha
kufanya mema na wangekua wananitii’’ Nabii Musa akakaa kimya.

Wanazuoni wanasema kua kutokana na aya hii ya Al Khidhr kuonesha kua ni mwenye
kulitoboa Jahazi basi ndani yake ndio tunapata Uthibitisho wa Hukmu ndani yake ya
kua Msimamizi wa Kitu au Mali ya Yatima Mali ya Mtu wa karibu yake au alie
chini ya Mamlaka yake basi hua anaruhusika kuipunguza au kuizuia kutompa pale
anapoona kua kufanya hivyo katika wakati huo kutakua na manufaa juu ya
mwenye mali hio, labda kwa mfano kwa kuogopa kua akimkabidhi Mtu huyo basi
labda ataifanyia Israfu na ataituma katika hali isiyokubalika kisharia na kupelekea
kujiangamiza au kusababisha maasi kwa Mola wake.

Hivyo Nabii Musa alipomuona Al Khidhr anatoboa Jahazi basi akashtuka sana na kuona
huyu Al Khidhr sasa anataka kusababisha maafa makubwa sana, kwani anataka
kuwazamisha watu wote waliomo ndani ya Jahazi na hii ni kwa sababu Nabii Musa alikua
amesahau kua sio kila kinachotiwa kwenye Maji kikawa na kisha kikatobolewa basi hua
ni chenye kuzama, kwani hata Yuhanz ambae ni mama yake Nabii Musa basi aliamrishwa
na Mola wake kua amtie kwenye kisanduku Nabii Musa kisha amtie Mtoni huku akiwa
ameachia kitundu kama sehemu ya kupitia hewa ndani ya kisanduku hicho, na ada ya
kisanduku hicho kutiwa mtoni basi Nabii Musa hakua ni mwenye kuzama bali alikua
ndani ya Rehma baada yake na matokeo yake akapata mafanikio kwa kuokotwa na
kulelewa ndani ya Kasri la Kifalme, kama zilivyosema aya:

ِ ‫ﻮت ﻓَﭑﻗْ ِﺬﻓِ ِﻴﻪ ِﰱ ٱﻟْﻴ ِﻢ ﻓَـ ْﻠﻴـ ْﻠ ِﻘ ِﻪ ٱﻟْﻴ ﱡﻢ ﺑِﭑﻟ ﱠﺴ‬
‫ﺎﺣ ِﻞ َ�ْ ُﺧ ْﺬﻩُ َﻋ ُﺪ ﱞو ِّﱃ‬ ِ ‫﴿أ َِن ٱﻗْ ِﺬﻓِ ِﻴﻪ ِﰱ ٱﻟﺘﱠﺎﺑ‬
َ ُ َّ ُ
﴾‫ﺼﻨَ َﻊ َﻋﻠَ ٰﻰ َﻋْﻴ ِ ۤﲏ‬ ِ ِ
ْ ُ‫ﻚ َﳏَﺒﱠﺔً ّﻣ ِّﲎ َوﻟﺘ‬ َ ‫ﺖ َﻋﻠَْﻴ‬ ُ ‫َو َﻋ ُﺪ ﱞو ﻟﱠﻪُ َوأَﻟْ َﻘْﻴ‬
Ani iqdhifeehi fee alttabooti faiqdhifeehi fee alyammi falyulqihi alyammu bialssahili
ya/khudhhu AAaduwwun lee waAAaduwwun lahu waalqaytu AAalayka
mahabbatan minnee walitusnaAAa AAala AAaynee (Surat Al Ta-Ha 20:39)

Tafsir: (Tukamwambia Yuhanz) Mtie ndani ya Tabut na kisha kitie ndani ya Mto,
kisha Mto utakichukua mpaka ukingoni, na atachukuliwa na adui yangu na adui yake.
Na nitakupamba kwa mapenzi kutoka kwangu, ili uwe ni mwenye kulelewa kutoka
chini ya uangalizi wangu.
875

Hivyo baada ya Al Khidhr kumwambia Nabii Musa juu yake anachokifiria basi akasema
kwa kumuuliza Nabii Musa:

﴾ً‫ﺻﱪا‬ ِ ‫ﻚ ﻟَﻦ ﺗَﺴﺘَ ِﻄ‬


َ ‫ﺎل أََﱂْ أَﻗُ ْﻞ إِﻧﱠ‬
َ َ‫﴿ﻗ‬
ْ َ ‫ﻴﻊ َﻣﻌ َﻰ‬
َ ْ
Qala alam aqul innaka lan tastateeAAa maAAiya sabran (Surat Al Kahf 18:72)

Tafsir: Akasema (Al Khidhr): ‘Hivi jee sikukuambia mimi kua kwa hakika wewe
hutoweza kua na Subra nami?’

Yaani hapa Al Khidhr anamuwekea wazi Nabii Musa kua hili jambo alilolifanya basi
amelifanya kwa makusudi, kwani kwa hakika yeye anajua anachokifanya, kutokana na
kua na habari juu ya tukio litakalofuata baada yake, ambapo Nabii Musa hana habari juu
ya matokeo ya tukio hilo. Hivyo jee kwanini Nabii Musa anakua hana Subra?

Hivyo Nabii Musa akajitetea kwa unyenyekevu mbele ya Mwalimu wake huyo
alietumwa akasome kwake, kwani anaona kua Mwalimu huyu tayari anayajua mengi
nisiyoyajua mimi, hivyo kama sikujitetea basi nitakosa faida nyingi kutoka kwake hivyo
akasema:

ِ ِ ِ ِ ِ
﴾ً‫ﻋﺴﺮا‬
ُ ‫ﺎل ﻻَ ﺗـُ َﺆاﺧ ْﺬِﱏ ﲟَﺎ ﻧَﺴ‬
ْ ُ ‫ﻴﺖ َوﻻَ ﺗُـْﺮﻫ ْﻘ ِﲎ ﻣ ْﻦ أ َْﻣ ِﺮى‬ َ َ‫﴿ﻗ‬
Qala la tu-akhidhnee bima naseetu wala turhiqnee min amree AAusran(Surat Al
Kahf 18:73)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa): ‘Usinichukulie (Vibaya) kutokana na nilicho kisahau


na wala usiniadhibu kwa kunifanyia uzito juu ya jambo langu hili zito’

Ambapo tunaona kua katika kujitetea kwake basi Nabii Musa ametumia maneno mawili
mazito kwenye kauli yake, ambapo neno la kwanza ni pale aliposema La Tu-akhidhnii
ambalo ni neno Akhadha lenye kikanushi cha harfu Lam kabla yake. Ambapo neno
Akhadha hua linamaanisha Kuchukua, Kupokea, Kukubali, Kunyang’anya, Kuadhibu,
Kukamata, Kutia mikononi, Kuzuia na pia humaanisha Kushikamanisha.

Hivyo basi Nabii Musa alitumia kauli ambayo ni yenye hoja nzito ndani yake kwa
kusema kua Usinichukulie Vibaya, au usinilaumu kutokana na kile ambacho ni kitu
kinachotokana na maumbile ya kila Ibn Adam ambacho ni kughafilika na kusahau
kutokana na tukio husika na uzito wake, kwani kitendo kinachofanywa kutokana na hisia
za kimaumbile za kusahau hua hakiwezi kuhesabiwa na kisha kushikamanishwa na
876

Adhabu, na hapo hapo kauli hii inaonesha kuomba msamaha ndani yake kwani kosa
lililofanyika halikufanywa kwa kukusudiwa.

Nabii Musa pia akatoa hoja ya pili kwa kutumia neno Wala Turhiqnee ambalo ni neno
Rahaqa lenye kikanushi cha harfu Lam pia kabla yake. Ambapo neno Rahaqa hua
linamaanisha Kufuatilia kwa Karibu, Kufunika, Kua na Ujinga, Kutokua na Adabu,
Kuharakisha, Kufikia, Kuchukulia, Kunyanyasa, Kudhulumu, Kukandamiza na pia
Kuwekea Vikwazo, au Kuwekea Ugumu.

Hivyo Nabii Musa anamwambia Al Khidhr kwa kumtaka asimlaumu kwa kosa ambalo
hakulikusudia na wala asimuwekee vikwazo katika jambo lake hilo gumu na zito la
kutafuta Ilm kutoka kwake na hivyo kumpelekea kuishiwa na subra zaidi, hivyo
amstahmilie ili anufaike zaidi. Na hapo Al Khidhr akamstahmilia Nabii Musa na
kumruhusu kufuatana nae huku wakiendelea katika safari yao hio mpaka wakafika
katika sehemu nyengine ya nchi kavu na kushuka kwenye Jahazi hilo katika miunaoitwa
Ayla Mji wa Aylah ambao kwa kiyahudi hua unaitwa mji wa Eilat, upo kusini mwa nchi
ya Falestina Ambayo leo imekua Israel, mji huu wa Eilat upo katika mwambao wa Bahari
nyekundu katika Ghuba ya Aqaba, Ghuba ambayo inapakanisha mipaka ya nchi 4 za
Kiarabu ambazo ni: Misri, Falestina, Jordan na Saudia.

Hivyo Nabii Musa na Al Khidr walipofika katika mji wa Aylah, wakawa wanatembea
kwa miguu kama zinavyosema aya:

ٍ ‫ﺖ ﻧـَ ْﻔﺴﺎً َزﻛِﻴﱠﺔً ﺑِﻐَ ِْﲑ ﻧَـ ْﻔ‬


‫ﺲ ﻟﱠَﻘ ْﺪ‬ َ َ‫﴿ﻓَﭑﻧْﻄَﻠَ َﻘﺎ َﺣ ﱠ ٰﱴ إِ َذا ﻟَِﻘﻴَﺎ ﻏُﻼَﻣﺎً ﻓَـ َﻘﺘَـﻠَﻪُ ﻗ‬
َ ‫ﺎل أَﻗَـﺘَـ ْﻠ‬
﴾ً‫ﺖ َﺷْﻴﺌﺎً ﻧﱡ ْﻜﺮا‬ ِ
َ ‫ﺟْﺌ‬
Faintalaqa hatta idha laqiya ghulaman faqatalahu qala aqatalta nafsan zakiyyatan
bighayri nafsin laqad ji/ta shay-an nukran(Surat Al Kahf 18:74)

Tafsir: Hivyo wakaendelea (na safari yao) mpaka wakakuta Mtoto, kisha (Al Khidhr)
akamuua. Akasema (Nabii Musa ) : ‘Umeiua Nafsi isiyokua na kosa ambayo haikuua
Nafsi nyengine, kwa hakika wewe Umefanya jambo baya sana.’

Katika kutembea kwao basi wakakutana na watoto 10 ambao walikua wanacheza, na


mmoja miongoni mwao alikua ni mzuri sana na mwenye uso wenye kung’ara na kuvutia.
Ambapo wanazuoni wametofutiana juu ya jina lake, kwani kuna wasemao kua alikua
akiitwa Hasanud, na kuna wasemao kua alikua akiitwa Simiuin na kuna wesemao kua ni
Hison na wengine wanasema kua ni Hussayn na Baba yake alikua anaitwa Malas na
Mama yake alikua kiitwa Rahmah ambapo huu ni mtizamo wa Imam Wahb Ibn Munabih.
877

Hivyo Al Khidhr akamvizia na kumkamata mtoto huyo bila ya kuoenakana na yeyote


isipokua na Allah Subhanah wa Ta’ala na wale aliofuatana nao na kisha akamuua, ama
kuhusiana na alivyomuua basi kuna wasema kua Al Khidhr alimpiga Jiwe mtoto huyo,
na kuna wasemao kua alimkata kichwa, na pia kuna wasemao kua alimpiga kichwa chake
na ukuta wa kisima kilichopo katika eneo hilo, ambapo baada ya Al Khidhr kumuua
mtoto huyo basi Nabii Musa akasema: ‘Umeiua Nafsi isiyokua na kosa ambayo haikuua
Nafsi nyengine, kwa hakika wewe Umefanya jambo baya sana.’

Ambapo Nafsi Zakkiyah hua inamaanisha Nafsi ambayo ni safi haina kosa aidha kwa
kutokana na kua mwenye Nafsi hio kua ni mtu ambae hajafikia Umri wa kua ni Mukallaf
yaani hajafikia Umri wa kubaleghe na hivyo hawezi kuhesabiwa kua ana dhambi kwani
haandikia dhambi. Na pia Nafsi Zakkiyah hua inamaanisha kua nafsi ya Mtu ambae
alifanya Dhambi lakini baadae akawa ni mwenye kutubu kwa Mola wake.

Naam, katika kumkosoa Al Khidr katika Jahazi, basi Nabii Musa alitumia neno Shay-an
Imran! Ambalo maana yake ni Jambo litakalokua na matokeo mabaya yaani Dhambi
kubwa, na kwa vile Jahazi halikuzama basi ile dhambi haikua kubwa sana.

Lakini katika tukio hili la kuua basi tunaona kua Nabii Musa anakosoa kwa kutumia neno
Shay-an Nukran!!

Ambapo neno Nukran maana yake hua ni Dhambi Kubwa ambayo Uzito na Kuchukiza
kwake ni Kukubwa, kiasi ya kua huweza kumpelekea Mtu kuachana na mtu aliefanya
kosa hilo na kumchukia sana kwani anastahiki kuadhibiwa kwa kosa hilo la kumuua mtu
asiekua na hatia hata Adhabu yake pia hua ni kubwa sana...Kwani Hukm ya jambo
alilolifanya Al Khidr mbele ya Nabii Musa hua ni Kifo!

Hivyo akasema Al Khidhr kumwambia Nabii Musa kua:

﴾ً‫ﺻ ْﱪا‬ ِ ‫ﻚ ﻟَﻦ ﺗَﺴﺘَ ِﻄ‬


َ ‫ﻚ إِﻧﱠ‬
َ ‫ﺎل أََﱂْ أَﻗُ ْﻞ ﻟﱠ‬
َ َ‫﴿ﻗ‬
َ ‫ﻴﻊ َﻣﻌ َﻰ‬
َ ْ
Qala alam aqul laka innaka lan tastateeAAa maAAiya sabran (Surat Al Kahf 18:74)

Tafsir: Akasema (Al Khidhr); ‘Jee sikukuambia mie Wewe kua kwa hakika hutoweza
wewe kua na Subra nami?’

Ambapo anasema Jarrah Allah Sultan Al Balagha Imam Abu Qasim Al Zamakhshari
kua: ‘Al Khidhr hapa amerudia maneno yake yale yale ya mwanzo, lakini safari hii
akaongezea na neno Laka yaani ‘Wewe’ kumtilia mkazo Musa kuhusiana na
uhakika wa manenoyake aliyoyasema hapo kabla.’
878

Hivyo Nabii Musa akasema:

﴾ً‫ﺖ ِﻣﻦ ﻟﱠ ُﺪِّﱏ ﻋُ ْﺬرا‬ ِ ُ‫ﻚ ﻋﻦ َﺷﻲ ٍء ﺑـﻌ َﺪﻫﺎ ﻓَﻼَ ﺗ‬


َ ‫ﺼﺎﺣْﺒ ِﲎ ﻗَ ْﺪ ﺑَـﻠَ ْﻐ‬
َ َ ْ َ ْ َ َ ُ‫ﺎل إِن َﺳﺄَﻟْﺘ‬
َ َ‫﴿ﻗ‬
Qala in saaltuka AAan shay-in baAAdaha fala tusahibnee qad balaghta min
ladunnee AAudhran(Surat Al Kahf 18:76)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa): ‘Kama nikikuuliza juu ya kitu chengine chochote kile
baada yake basi usiwe na urafiki nami kwani kwa hakika utakua umepata kutoka
kwangu Udhuru.’

Ambapo neno Balaghta linatokana na neno Balagha ambalo hua inamaanisha Kuwasili,
Kufikia mwisho, Kufikia Malengo, Kupata kinachotakiwa, Kupea, Kukaribia na pia
humaanisha Kubaleghe.

Hivyo Nabii Musa aliendelea kumuomba msamaha Al Khidhr kutokana na kile ambacho
alichokikosea na kukirudia tena kwa mara ya pili mbali ya kua alikua tayari ameshapewa
Onyo kua hatoweza kua na subra juu ya yale asiyokua na habari nayo, kutokana na ukweli
huo basi akaamua kumuwekea wazi Al Khidhr kua kama Nabii Musa akirudia tena kosa
hilo basi na aachane nae kwani itakua tayari ameshapata udhuru wa kuachana na Nabii
Musa kutokana na kutokua na Subra.

Ambapo anasema Ubbay Ibn Ka’ab Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam aliisoma aya hii na kisha akamsalia Musa na kisha akasema: ‘Musa
alikua akiona haya mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala kutokana na kurudia
kuuliza kwake’’

Hapa tunaona kua Nabii Musa alikua pia amesahau kuhuisiana na aliyoyafanya yeye pale
alipompigia ngumi Fatun ambae ndio yule mtu wa Misri aliekua akipigana na Samirii,
ambapoNabii Musa akamuua Mtu huyo bila ya kukusudia kutokana na ngumi hio, kama
zilivyosema aya:
879

ِ ْ َ‫ﲔ َﻏ ْﻔﻠَ ٍﺔ ِّﻣ ْﻦ أ َْﻫﻠِ َﻬﺎ ﻓَـﻮ َﺟ َﺪ ﻓِ َﻴﻬﺎ ر ُﺟﻠ‬


‫ﲔ ﻳَـ ْﻘﺘَﺘِﻼَ ِن َﻫـٰ َﺬا‬ ِ ‫﴿وَد َﺧﻞ ٱﻟْﻤ ِﺪﻳﻨَﺔَ َﻋﻠَ ٰﻰ ِﺣ‬
َ َ َ َ َ
ِ‫ِﻣﻦ ِﺷﻴﻌﺘِ ِﻪ وﻫـٰ َﺬا ِﻣﻦ ﻋ ُﺪ ِوﻩِ ﻓَﭑﺳﺘـﻐَﺎﺛَﻪ ٱﻟﱠ ِﺬى ِﻣﻦ ِﺷﻴﻌﺘِ ِﻪ ﻋﻠَﻰ ٱﻟﱠ ِﺬى ِﻣﻦ ﻋ ُﺪ ِوﻩ‬
ّ َ ْ َ َ ُ َْ ّ َ ْ َ َ َ
ِ ‫ﺎن إِﻧﱠﻪ ﻋ ُﺪ ﱞو ﱡﻣ‬ ِ ِ َ َ‫ﻀ ٰﻰ َﻋﻠَْﻴ ِﻪ ﻗ‬
﴾‫ﲔ‬ ٌ ِ‫ﻀﻞﱞ ﱡﻣﺒ‬ َ ُ َ‫ﺎل َﻫـٰ َﺬا ﻣ ْﻦ َﻋ َﻤ ِﻞ ٱﻟﺸْﱠﻴﻄ‬ َ ‫ﻮﺳ ٰﻰ ﻓَـ َﻘ‬
َ ‫ﻓَـ َﻮَﻛَﺰﻩُ ُﻣ‬
Wadakhala almadeenata AAala heeni ghaflatin min ahliha fawajada feeha
rajulayni yaqtatilani hadha min sheeAAatihi wahadha min AAaduwwihi
faistaghadhahu alladhee min sheeAAatihi AAala alladhee min AAaduwwihi
fawakazahu moosa faqadha AAalayhi qala hadha min AAamali alshshaytani
innahu AAaduwwun mudhillun mubeenun (Surat Al Qasas 28:15)

Tafsir: Na akaingia katika Mji wakati ambao wate wake walikua wameghafilika. Na
akakuta watu wawili wanapigana. Mmoja ni mtu wa upande wake (wa Bani Israil) na
mwengine ni wa upande wa adui yake (Mtu wa Fir’awn), akaomba msaada mtu wa
upande wake dhidi ya adui yake. Hivyo Musa akampiga Ngumi na akammaliza. Na
kisha akasema hii ni amali ya Shaytan, hakika yeye ni adui mpotovu aliewazi.

Na hivyo tukio hili la Al Khidr la kuua kwa kukusudia ambalo ni tofauti na lile tukio la
Nabii Musa la kuua bila ya kukusudia yote kwa pamoja yanatuonesha kua tukio la kitu
au jambo lolote lile hua haliko kama linavyoonekana kwa nje au kwa juu juu tu, bali
inabidi uwe na Ilm ya ndani ya kina ndio utaweza kujua matokeo yake, kwani kwa upande
wa Nabii Musa hapa alijaaliwa kutokewa na tukio hili kua ni kama sababu ya kumfanya
yeye awe ni mwenye kuikimbia ardhi ya nchi ya Misri, kwa ajili ya kutayarishwa kupewa
Majukumu mazito ya Utume na Mola wake.

Hivyo ingawa tukio lilikua ni baya lakini lilikua na malengo mema yatakayosababisha
baadae matokeo mazuri zaidi ndani yake, ambapo hali hii pia ipo kwa tukio la Al Khidhr
alipomuua Mtoto huyu kama tutakavyoona hapo baadae kulingana na namna
zilivyofafanua aya.

Hivyo Al Khidhr akamsamehe Nabii Musa na kwa pamoja wakaendelea na safari yao
kama zinavyosema aya:

ٍ
ُ ‫ﻀﻴِّ ُﻔ‬
‫ﻮﳘَﺎ ﻓَـ َﻮ َﺟ َﺪا‬ ْ ‫﴿ﻓَﭑﻧﻄَﻠَ َﻘﺎ َﺣ ﱠ ٰﱴ إِ َذآ أَﺗَـﻴَﺂ أ َْﻫ َﻞ ﻗَـْﺮﻳَﺔ‬
َ ُ‫ٱﺳﺘَﻄْ َﻌ َﻤﺂ أ َْﻫﻠَ َﻬﺎ ﻓَﺄَﺑـَ ْﻮاْ أَن ﻳ‬
﴾ً‫َﺟﺮا‬ ِ
ْ ‫ت َﻋﻠَْﻴﻪ أ‬ َ ‫ﺖ ﻻَ ﱠﲣَ ْﺬ‬
ِ َ َ‫ﺾ ﻓَﺄَﻗَﺎﻣﻪ ﻗ‬
َ ‫ﺎل ﻟَ ْﻮ ﺷْﺌ‬ ُ َ ‫ﻳﺪ أَن ﻳَﻨ َﻘ ﱠ‬ ُ ‫ﻓِ َﻴﻬﺎ ِﺟ َﺪاراً ﻳُِﺮ‬
880

Faintalaqa hatta idha ataya ahla qaryatin istatAAama ahlaha faabaw an


yudhayyifoohuma fawajada feeha jidaran yureedu an yanqadhdha faaqamahu qala
law shi/ta laittakhadhta AAalayhi ajran(Surat Al Kahf 18:77)

Tafsir: Hivyo wakaendelea na safari yao mpaka wakakuta watu wa Mji, wakawaomba
watu wa Mji huo chakula, lakini wakakataa kuwakaribisha, n wakakuta ndani yake
(Mji huo) Ukuta unaotaka kuanguka nae (Al Khidhr) akaunyanyua, akasema (Musa):
‘Kama ungetaka basi bila ya shaka ungechukua Ujira kutoka kwao’

Ambapo Wanazuoni wametofautiana kuhusina na jina la mji huo, kwani kuna


wanaosema kua ni Antakiya ambao upo Uturuki na kuna wasemao kua ni mji wa Nazareti
na Al Khidhr, Nabii Musa na Joshua waliwasili katika Mji huo katika wakati wa Usiku.
Ambapo anasema Qatadah Ibn Diamah Al Sadusi kua: ‘Watu wa Mji huo walikua ni
Wabakhili sana na walikua hawawapi wasafiri haki zao.’

Hivyo katika Usiku huo hawakua na chakula wala maji na ingawa ilikua baridi lakini
hawakupata sehemu ya kupumzikia wala kujihifadhi isipokua walijipumzisha pembeni
ya ukuta wa Nyumba moja iliyokua njiani katika mji huo. Hivyo asubuhi yake walipokua
wanataka kutoka kwenye mji huo kuendelea na safari yao,wakauona Ukuta wa nyumba
ambayo walilala pembeni yake kua ulikua ni ukuta ambao unataka kuanguka kutokana
na kutokua na hali nzuri kutokana na ukongwe wake.

Hivyo Al Khidhr akaubomoa ukuta huo na kisha akaujenga tena upya. Ambapo wa
upande wa Said Ibn Jubar basi anasema kua: ‘Al Khidhr aliunyoosha ukuta huo kwa
kutumia mikono yake’ na baada ya kumaliza kuuinua Ukuta huo basi Nabii Musa
akamwambia Al Khidhr kua: ‘Kama ungetaka basi bila ya shaka, usinge ujenga ukuta
huo hadi pale watu wa mji huu kukulipa ujira wako au kwa kutupatia chakula’

Ambapo hapa Nabii Musa alikua amesahau kua haya aliyoyafanya Al Khidhr pia kua ni
sawa na yale aliyoyafanya yeye hapo kabla alipowasili katika mji wa Madyan, baada ya
kuwasaidia Imraatayn wakati alipowakuta wakiwa ni wenye kusubiri kuwanywesha maji
wanyama wao katika mji wa Madyan pale ziliposema aya:

‫ﱠﺎس ﻳَ ْﺴ ُﻘﻮ َن َوَو َﺟ َﺪ ِﻣﻦ ُدو�ِِ ُﻢ‬


ِ ‫﴿ َوﻟَ ﱠﻤﺎ َوَرَد َﻣﺂءَ َﻣ ْﺪﻳَ َﻦ َو َﺟ َﺪ َﻋﻠَْﻴ ِﻪ أُﱠﻣﺔً ِّﻣ َﻦ ٱﻟﻨ‬
‫ﻮ� َﺷْﻴ ٌﺦ‬ ِ ‫ﺼ ِﺪ َر‬ ِ َ َ‫ود ِان ﻗ‬ ِ َ‫ْٱﻣﺮأَﺗ‬
ّ ْ ُ‫ﺎل َﻣﺎ َﺧﻄْﺒُ ُﻜ َﻤﺎ ﻗَﺎﻟَﺘَﺎ ﻻَ ﻧَ ْﺴﻘﻰ َﺣ ﱠ ٰﱴ ﻳ‬
َ ُ‫ٱﻟﺮ َﻋﺂءُ َوأَﺑ‬ َ ‫ﲔ ﺗَ ُﺬ‬ َ
881

‫ﱃ ِﻣ ْﻦ َﺧ ٍْﲑ‬
‫ﺖ إِ َﱠ‬ ِ ِ ‫ﺎل ر‬ ِ
َ ‫ب إِِّﱏ ﻟ َﻤﺂ أ‬
َ ْ‫َﻧﺰﻟ‬ ّ َ َ ‫َﻛﺒِﲑٌ۞ ﻓَ َﺴ َﻘ ٰﻰ َﳍَُﻤﺎ ﰒُﱠ ﺗَـ َﻮﱠ ٰﱃ إِ َﱃ ٱﻟﻈّ ِّﻞ ﻓَـ َﻘ‬
﴾ٌ‫ﻓَِﻘﲑ‬
Walamma warada maa madyana wajada AAalayhi ommatan mina alnnasi
yasqoona wawajada min doonihimu imraatayni tadhoodani qala ma khatbukuma
qalata la nasqee hatta yusdira alrriAAao waaboona shaykhun kabeerun; Fasaqa
lahuma thumma tawalla ila aldhdhilli faqala rabbi innee lima anzalta ilayya min
khayrin faqeerun (Surat Al Qasas 28:23-24)

Tafsir: Na alipowasili kwenye sehemu inayonyweshewa Maji ya Madyan, akaona


kundi la Wanaume wakinyweshea (Maji wanyama wao). Na pembeni yao akaona
Wanawake wawili wakiwazuia wanyama wao, akasema (Nabii Musa): ‘Mnataka
kufanya nini?’Nao wakasema: ‘Hatuwezi kuwanywesha Wanyama wetu mpaka
Wafugaji waondoe Wanyama wao na Baba yetu ni Mzee sana; Hivyo akawanyweshea
Maji Wanyama wao na kisha akarudi kivulini na akasema: ‘Ewe Mola wangu, Hakika
mimi ni mwenye kuhitaji kheri yeyote ile utakayonipa’

Hivyo baada ya Nabii Musa kushauri juu ya lile ambalo hakuombwa ushauri juu yake,
wakati na yeye pia alifanya kama alivyofanya mwenzake kwa kuwasidia Imraatayn bila
ya kudai malipo kutoka kwao katika wakati huo, basi Al Khidr akamwambia Nabii Musa
kua umefika muda wa kuachana baina yao kama zinavyosema aya:

ِ ِ
َ ‫ﻚ ﺑِﺘَﺄْ ِو ِﻳﻞ َﻣﺎ َﱂْ ﺗَ ْﺴﺘَﻄﻊ ﻋﱠﻠَْﻴﻪ‬
﴾ً‫ﺻ ْﱪا‬ َ ُ‫ﻚ َﺳﺄُﻧَـﺒِّﺌ‬ ُ ‫ﺎل َﻫـٰ َﺬا ﻓَِﺮ‬
َ ِ‫اق ﺑَـْﻴ ِﲎ َوﺑَـْﻴﻨ‬ َ َ‫﴿ﻗ‬
Qala hadha firaqu baynee wabaynika saonabbi-oka bita/weeli ma lam tastatiAA
AAalayhi sabran (SuratAl Kahf 18:78)

Tafsir: Akasema (Al Khidhr kumwambia Nabii Musa) : ‘Hapa ndio muachano wetu
baina yako na baina yangu, hivyo nitakupa habari ya tafsiri ya yale ambayo
umeshindwa kua na Subra nayo’

Ambapo Al Khidhr akatilia mkazo na kuthibitisha kuachana baina yake yeye Al Khidhr
na baina ya Nabii Musa kunakotokana na kuvunjika kwa makubaliano baina yao baina
ya Nabii Musa na yeye Al Khidhr, kwani Nabii Musa tayari ameshavunja masharti mara
tatu ambayo hapo awali alikubaliana nae kua ataweza kua na subra na yale asiyokua na
habari nayo hivyo Nabii Musa alifeli katika hali zifuatazo.
882

Alifeli mtihani wa kwanza kwenye Jahazi kutokana na kusahau Masharti ya


Mtihani wake.

Akafeli mtihani wa pili kwenye Mauaji ya yule kijana kutokana na Mazingira ya


Mtihani huo yaliyompelekea kudai maelezo kuhusiana na tukio hilo ambayo
hakutakiwa ayadai.

Na pia akafeli Mtihani wa tatu na wa Mwisho kutokana na kukusudia kufeli


mtihani huo ili awachane na Al Khidhr kwa kutoa ushauri ambao hakutakiwa
autoe!

Lakini sasa kabla ya kuachana huko baina yao basi kwanza inabidi Al Khidhr amfafanulie
Nabii Musa yale ambayo alishindwa kua na ustahmilivu nayo juu yake, hivyo akaanza
kufafanua maana ya yale mambo matatu aliyoyafanya hapo kabla mbele ya Nabii Musa
kwa kusema:

ِ ‫دت أَ ْن أ‬
‫َﻋﻴﺒَـ َﻬﺎ َوَﻛﺎ َن‬ ‫ﲔ ﻳَـ ْﻌ َﻤﻠُﻮ َن ِﰱ ٱﻟْﺒَ ْﺤ ِﺮ ﻓَﺄ ََر ﱡ‬ ِ ِ َ‫﴿أَﱠﻣﺎ ٱﻟ ﱠﺴ ِﻔﻴﻨَﺔُ ﻓَ َﻜﺎﻧ‬
َ ‫ﺖ ﻟ َﻤ َﺴﺎﻛ‬ ْ
﴾ً‫ﺼﺒﺎ‬ ٍ ِ ٌ ِ‫َوَرآءَ ُﻫﻢ ﱠﻣﻠ‬
ْ ‫ﻚ َ�ْ ُﺧ ُﺬ ُﻛ ﱠﻞ َﺳﻔﻴﻨَﺔ َﻏ‬
Amma alssafeenatu fakanat limasakeena yaAAmaloona fee albahri faaradtu an
aAAeebaha wakana waraahum malikun ya/khudhu kulla safeenatin ghasban
(SuratAl Kahf 18:79)

Tafsir: (Akasema Al Khidhr kumwambia Nabii Musa)‘Ama Kuhusiana na Jahazi, basi


lilikua ni la Masikini waliokua wakifanyia kazi baharini, hivyo nilitaka kulitia kasoro,
kwa sababu kabla yao kulikua kuna Mfalme ambae alikua akiliteka kila Jahazi kwa
nguvu’

Ambapo anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Ama kuhusiana na
Safina basi lilikua linamilikiwa na Masikini, ingawa lilikua lina thamani ya Dinar
1000, kwani Msafiri ni masikini hata kama akiwa na Dirham 1000’

Ambapo anasema Imam Ka’ab Al Ahbar kua: ‘Jahazi hili lilikua linamilikiwa na
ndugu 10 ambao walilirithi kutoka kwa baba yao.’

Ambapo kutokana na aya hii basi anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi
kua: ‘Imam Muhammad Idris Al Shafii alihitimisha kutokana na aya hii kua:
‘Fukara hua na hali mbaya zaidi kuliko Masikini, kwani ingawa watu hawa walikua
wanamiliki Jahazi lakini Allah Subhanah wa Ta’ala aliwaita kua ni Maskini’
883

Ambapo neno Fuqara hua ni lenye kutokana na neno Faqura ambalo hua linaaamansha
Mtu Aliekua Maskini, Mtu Mwenye Shida Kubwa na Nyingi sana. Hivyo neno Fuqara
hua linatumika kumaanisha Mtu ambae anawategemea watu wengine kwa ajili ya
mahitajio yake ya kimaisha kutokana na sababu mbali mbali za kimaumbile ikiwemo
Uzee, Ulemavu au kutokana na mitihani mbali mbali ya kimaisha, na ndio maana neno
Faqira hua pia linamaanisha Kuzidiwa na Mithani ambayo huweza kumpelekea Mtu
kuhisi uzito wa maumivu ya Mtihani huo ndani ya Uti wa Mgongo, na neno Faqiratun
hua linamaanisha Mtihani wa Kuvunjika Mgongo.

Ambapo kwa upande wa neno Masakin hua linatokana na neno Sakana ambalo hua
linamaanisha Kutulia, Kukaa Kimya, Kusimama tulii. Hivyo neno Masakin hua
linamaanisha Mnyenyekevu, Mtulivu, Masikini, Mtu anaestahiki kusaidiwa kutokana na
Udhaifu au Unyenyekevu wake.

Neno Sakana ndio pia lililotoa neno Sikin yaani Kisu ambacho Kimeitwa hivyo kwa
sababu Kisu ndio chanzo cha Kukifanya Kiumbe Kitulie baada ya Kuchinjwa kwake.

Ambapo kwa upande wa Imam Muhyi Ad Din Imam Abu Zakarriyah Sharaf An Nawawi
basi yeye anasema kua: ‘Maneno haya mawili Fukara na Masakin hua yana maana
moja yanapokua yametumika katika sehemu tofauti, lakini yanapotumika katika
sehemu moja hua yana maana tofauti.’

Miongoni mwa mifano ya matumizi ya maneno haya mawili katika sehemu moja basi
hua ni katika ile aya ya hukumu ya miongoni mwa wanaostahiki kupewa Zakkah ambayo
inasema:

‫ﲔ َﻋﻠَْﻴـ َﻬﺎ َوٱﻟْ ُﻤ َﺆﻟﱠَﻔ ِﺔ ﻗُـﻠُﻮﺑـُ ُﻬ ْﻢ َوِﰱ‬ ِِ ِ ِ‫ﺎت ﻟِْﻠ ُﻔ َﻘﺮ ِآء وٱﻟْﻤﺴﺎﻛ‬
َ ‫ﲔ َوٱﻟْ َﻌﺎﻣﻠ‬ ‫﴿إِﱠﳕَﺎ ٱﻟ ﱠ‬
َ َ َ َ ُ َ‫ﺼ َﺪﻗ‬
﴾‫ٱﻪﻠﻟ َﻋﻠِﻴﻢ َﺣ ِﻜﻴﻢ‬ ِ‫ٱﻪﻠﻟِ وٱﺑ ِﻦ ٱﻟ ﱠﺴﺒِ ِﻴﻞ ﻓَ ِﺮﻳﻀﺔً ِﻣﻦ ﱠ‬
ْ َ ‫ﲔ َوِﰱ َﺳﺒِ ِﻴﻞ ﱠ‬
ِ ِ َ‫ٱﻟﺮﻗ‬
َ ‫ﺎب َوٱﻟْﻐَﺎ ِرﻣ‬ ِ
ٌ ٌ ُ‫ٱﻪﻠﻟ َو ﱠ‬ َّ َ ّ
Innama alssadaqatu lilfuqara-i waalmasakeeni waalAAamileena AAalayha
waalmu-allafati quloobuhum wafee alrriqabi waalgharimeena wafee sabeeli Allahi
waibni alssabeeli fareedatan mina Allahi waAllahu AAaleemun hakeemun (Surat At
Tawba 9:60)

Tafsir: Kwa hakika Sadaka (Zakkah) ni kwa ajili ya Mafukara na Masikini na


wanaoisimamia (Katika kuikusanya na Kugawa) na kwa ambao Nyoyo zao zimeinamia
katika Uislam, na kuwaachia huru waliokamatwa, na wenye madeni, na kwa ajili ya
884

njia ya Allah, na wasafiri hua ni Wajibu kutoka kwa Allah, na Allah ni Mwingi wa
kujua na ni Mwingi wa Hikma.

Na Wanazuoni wametofautiana katika maana ya maneno haya mawili kutokana na


yalivyotumika hapa kwani kwa upande wa Wanazuoni wa Madhhab ya Imam
Muhammad Idris Al Shafii na wafuasi wa Maddhhab ya Imam Ahmad Ibn Hanbal basi
wao wanasema kua: ‘Fukara hua ni tu mwenye shida zaidi fuliko Masikini na hii ni
kutokana na mpangilio wa maneno haya yaliyotajwa kwenye aya hii, kwani
mwanzo ametajwa Fukara na kisha baadae ndio akatajwa Masikini.’

Na kwa upande wa Wanazuoni wa Madhhab ya Imam Abu Hanjfa na Maddhhab ya Imam


Malik Ibn Anas basi waao wanasem kua: ‘Maskini ndie mwenye shida zaidi kuliko
Fukara.’

Kwa kumalizia basi kuhusiana na Fukra na Masikini basi tunaona kua:

Wanazuoni wa Madhhab ya Imam Abu Hanifa basi wao wanafafanua maana mbili hizi
kwa kusema: ‘Masikini hua ni mtu ambae hana kitu kabisa. Fukara hua ni mtu
ambae anacho kitu kidogo ambacho hata hivyo hakimtoshi kwa mahitaji yake ya
kila siku’

Wanazuoni wa Madhhab ya Imam Malik Ibn Anas basi wao wanafafanua maana mbili
hizi kwa kusema: ‘Masikini hua ni mtu ambae hana kitu kabisa na hivyo hua
anaomba watu msaada. Fukara hua hana kitu hata kidogo lakini hata hivyo haombi
kwa watu.’

Wanazuoni wa Madhhab ya Imam Muhammad Idris Al Shafii basi wao wanafafanua


maana mbili hizi kwa kusema: ‘Fukara hua ni mtu ambae hana kitu kabisa. Maskini
hua ni mtu ambae anacho kitu kidogo ambacho hata hivyo hakimtoshi kwa mahitaji
yake ya kila siku’

Wanazuoni wa Madhhab ya Imam Ahmad Ibn Hanbal basi wao wanafafanua maana mbili
hizi kwa kusema: ‘Fukara hua ni mtu ambae hana hata kitu kitachomtosheleza hata
nusu ya mahitaji yake. Maskini hua ni mtu ambae anacho kitu kidogo ambacho ni
zaidi ya nusu ya mahitaji yake na hivyo hua hakimtoshi kwa mahitaji yake ya kila
siku’

Ambapo anasema Imam Abu Jafar Muhammad Ibn Jarir At Tabari kua : ‘Amesema Abu
Hurayra Radhi Allahu Anhu kua : ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
kua: ‘Masikini wa kweli hua si yule ambae anaenda na kuwaomba watu kwa ajili
ya Tende moja mbili, au kwa kula chakula mdomo mmoja au miwili, bali ni yule
885

ambae anaeona haya kuomba, soma kama unataka: ‘La yas-aloona alnnasa
ilhafan’’

Ambapo maneno yasemayo La yas-aloona alnnasa ilhafan ni yale yaliyomo katika aya
isemayo:

‫ض َْﳛ َﺴﺒُـ ُﻬ ُﻢ‬ ِ ‫ﺿْﺮﺎﺑً ِﰱ ٱﻷ َْر‬ ِ ِ‫ُﺣﺼﺮواْ ِﰱ ﺳﺒِ ِﻴﻞ ﱠ‬ ِ ِ‫﴿ ِ ِ ﱠ‬


َ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻻَ ﻳَ ْﺴﺘَﻄﻴﻌُﻮ َن‬ َ ُ ‫ﻳﻦ أ‬ َ ‫ﻟ ْﻠ ُﻔ َﻘَﺮآء ٱﻟﺬ‬
‫ﱠﺎس إِ ْﳊَﺎﻓﺎً َوَﻣﺎ‬
‫ﻨ‬ ‫ٱﻟ‬ ‫ن‬ ‫ﻮ‬ ‫ﻟ‬َ‫ﺄ‬ ‫ﺴ‬ ‫ﻳ‬ ‫ﻻ‬ ‫ﻢ‬ ‫ﺎﻫ‬ ‫ﻴﻤ‬ ‫ﺴ‬ِ ِ‫ﻒ ﺗَـﻌ ِﺮﻓُـﻬﻢ ﺑ‬ ِ ‫ٱﳉ‬
ِ ‫ﺎﻫﻞ أَ ْﻏﻨِﻴﺂء ِﻣﻦ ٱﻟﺘـﱠﻌ ﱡﻔ‬
َ َ ُ ْ َ َ ْ ُ َ ُ ْ َ َ َ َ ُ َْ
﴾‫ٱﻪﻠﻟ ﺑِِﻪ َﻋﻠِﻴﻢ‬
‫ﱠ‬ ‫ن‬‫ﱠ‬ َِ‫ﺗُ ِﻨﻔ ُﻘﻮاْ ِﻣﻦ َﺧ ٍْﲑ ﻓ‬
‫ﺈ‬ ْ
ٌ َ
Lilfuqara-i alladheena ohsiroo fee sabeeli Allahi la yastateeAAoona darban fee al-
ardhi yahsabuhumu aljahilu aghniyaa mina alttaAAaffufi taAArifuhum
biseemahum la yas-aloona alnnasa ilhafan wama tunfiqoo min khayrin fa-inna
Allaha bihi AAaleemun (Surat Al Baqara 2:173)

Tafsir: (Sadaka hua ni) Kwa Mafukara ambao wamezuilika kujitolea kwa ajili ya
Allah, na hawawezi kutembea Ardhini (kwa ajili ya kufanya kazi au biashara), na wale
wasiowajua huwadhania kua ni matajiri kutokana na kujiheshimu kwao. Unaweza
kuwajua kutokana na alama yao, hua hawawaombi watu kwa kukera, na chochote kile
mtakachotumia kwa ajili ya kheri basi Allah anajua juu yake.

Hivyo katika hadithi hii tunaona kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ametumia
neno Masikini na kuifafanua hali yao katika aya inayozungumzia Fukara, na hii ni
kutokana na kuingiliana kimaana na kimatumizi kwa maneno hayo. Hivyo basi kuna watu
wa aina mbili wasiokua na uwezo, kuna wale ambao hua ni wenye kuomba na wale
wasioomba.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakua ni mwenye kutofautisha baina ya
hali za watu wawili hawa, na kutokana na aya hii basi tunaweza kusema kua Faqir hua ni
yule ambae si mwenye kuomba na Masikini hua ni mwenye kuomba.

Na kuhusiana na neno Wara’a lililotumika katika aya hii basi kwa upande wa Imam Abu
Hasan Ali Ibn Muhammad Ibn Habib Al Mawardi Al Shafii basi yeye anasema kua:
‘Waarabu hua ni walio tofautiana katika matumizi ya neno Waraa katika hali tatu
tofauti ambapo hua ni kua linaweza likatumika katika kila hali na katika kila
sehemu na katika hali ya mkabala’
886

Ambapo neno Waraa limetumika tena katika zile aya zinazosema:

﴾‫ﻳﺪ‬ ٍ ِ
ٍ ‫ﺂء ﺻ ِﺪ‬ ِِ ِ
َ ‫﴿ ّﻣﻦ َوَرآﺋﻪ َﺟ َﻬﻨ ُﱠﻢ َوﻳُ ْﺴ َﻘ ٰﻰ ﻣﻦ ﱠﻣ‬
Min wara-ihi jahannamu wayusqa min ma-in sadeedin (Surat Ibrahim 14:16)

Tafsir:(Wara-ihi)Mbele yake (Kila Kiongozi aliekua Dhalimu) kuna Jahannam na


atanyweshwa maji yenye kuchemka sana.

Na katika ile aya isemayo:

‫ﺖ َﻛﻼﱠ إِﻧـﱠ َﻬﺎ َﻛﻠِ َﻤﺔٌ ُﻫ َﻮ ﻗَﺂﺋِﻠُ َﻬﺎ َوِﻣﻦ َوَرآﺋِ ِﻬ ْﻢ ﺑـَْﺮَز ٌخ‬ ُ ‫ﻴﻤﺎ ﺗَـَﺮْﻛ‬
ِ ِ ‫﴿ﻟَﻌﻠِّ ۤﻲ أَﻋﻤﻞ‬
َ ‫ﺻﺎﳊﺎً ﻓ‬
َ ُ َْ َ
﴾‫إِ َ ٰﱃ ﻳَـﻮِم ﻳـُْﺒـ َﻌﺜُﻮ َن‬
ْ
LaAAallee aAAmalu salihan feema taraktu kalla innaha kalimatun huwa qa-iluha
wamin wara-ihim barzakhun ila yawmi yubAAathoona (Surat Al Muuminuun
23:100)

Tafsr: Ili nipate kufanya mema kutokana na kile nilichokiwacha nyuma, la, bali hayo
ni maneno tu anayozungumza na nyuma (wara-ihim) yao kuna Barzakh (pazia) mpaka
katika siku watakayofufuliwa.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala alimbainishia Al Khidhr kuhusiana na Mfalme


aliekuwepo kabla yao ambae alikua analiteka nyara kila Jahazi ambalo lisilokua na
kasoro na kisha hulitaifisha na kulifanya kua ni lake, hivyo Al Khidhr akalitoboa Jahazi
hilo ili lisitaifishwe kwani kutokana na hali yake hio basi litakua tayari lina kasoro na
hivyo ingawa Nabii Musa aliona kua Al Khidhr amefanya makosa makubwa lakini
kumbe amefanya wema badala yake.

Ambapo Wanazuoni wametofautiana juu ya jina la Mfalme huyu kwani kuna wasemao
kua alikua akiitwa Jolanda, ambapo Imam Muhammad Ibn Is-haq basi yeye anasema kua
alikua anaitwa Marwan Ibn Julandi Al Urdun, na pia kuna wasemao kua alikua akiitwa
Hadad Ibn Badad.

Kisha Al Khidhr akasema kumwambia Nabii Musa kua:


887

‫ﲔ ﻓَ َﺨ ِﺸﻴﻨَﺂ أَن ﻳـُْﺮِﻫ َﻘ ُﻬ َﻤﺎ ﻃُ ْﻐﻴَﺎ�ً َوُﻛ ْﻔﺮاً۞ﻓَﺄ ََرْد َ� أَن‬ ِ ْ ‫﴿وأَﱠﻣﺎ ٱﻟْﻐُﻼَ ُم ﻓَ َﻜﺎ َن أَﺑـَﻮاﻩُ ُﻣ ْﺆِﻣﻨَـ‬
َ َ
﴾ً‫ب ر ْﲪﺎ‬ ِ ِ
ُ َ ‫ﻳـُْﺒﺪ َﳍَُﻤﺎ َرﺑـﱡ ُﻬ َﻤﺎ َﺧ ْﲑاً ّﻣْﻨﻪُ َزَﻛ ٰـﻮةً َوأَﻗْـَﺮ‬
Waamma alghulamu fakana abawahu mu/minayni fakhasheena an yurhiqahuma
tughyanan wakufran, Faaradna an yubdilahuma rabbuhuma khayran minhu
zakatan waaqraba ruhman (SuratAl Kahf 18:80)

Tafsir: Ama kuhusiana na yule kijana, basi walikua wazazi wake ni Waumini wawili
hivyo tulikua na khofu kua atawaangamiza kwa Uasi na Dhulma. Hivyo tukataka
awabadilishie Mola wao kwa yule alie bora zaidi katika usafi na kuwakaribia
kihuruma na kimapenzi.

Ambapo amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Mtoto wa Kiume
ambae Al Khidhr alimuua basi alimuuwa akiwa ni Mshirikina, hivyo kama
angefikia umri wa kubaleghe basi angepingana na wazee wake kwa uasi na
Ushirikina’(Imam Abu Daud)

Kwa upande mwengine basi siku moja Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu
aliulizwa kuhusiana na mateka ambao ni vijana wadogo waliotekwa vitani kama wauliwe
ama la?: Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu akamwambia aliemuuliza suali hilo
kwa kusema: ‘Kama wewe ni Al Khidhr na hivyo unao uwezo wa kutofautisha baina
ya Muumini na Mshirikina, basi unaweza kuwaua, lakini wewe si Al Khidhr hivyo
waachie huru’

Aya imetumia neno Badala ambao ni lenye kumaanisha Kubadilisha, Kuchukua kitu
kimoja kutoka katika sehemu yake na kukiweka kitu chengine kwenye sehemu ya kitu
hicho kilichoondolewa, Kupata kitu chengine badala ya kile kilichokuwepo hapo awali.

Ambapo tunaona kua aya imemalizia na neno Ruhman ambalo ni lenye kutokana na neno
Rahma ambalo ni lenye kumaaisha Rahma, Rehma, Kupenda, Kua na Huruma,
Kufadhilia au Kusaidia na pia neno Rahma hua linamaanisha Uhusiano wa Jamaa na pia
humaanisha Fuko la Uzazi ambalo hua anakaa mtoto ndani yake anapokua ndani ya
tumbo la mama.

Kutokana na maana hio basi Wanazuoni wanasema kua hapa Al Khidhr aliposema kua
Faaradna an yubdilahuma rabbuhuma khayran minhu zakatan waaqraba ruhman
yaani Hivyo tukataka awabadilishie Mola wao kwa yule alie bora zaidi katika usafi na
kuwakaribia kihuruma na kimapenzi. Basi alikua akimaanisha hivyo, na pia kuna
wanaosema kua alikua akimaanisha kua Hivyo tukataka awabadilishie Mola wao kwa
888

yule alie bora zaidi katika usafi na kua ni mwenye ukaribu zaidi na fuko la uzazi la
Mama yake kwa kutoa watoto bora na wenye Imam juu ya Allah Subhanah wa Ta’ala,
na ndio maana tunapoangalia mtizamo wa Imam Jafar Ibn Muhammad basi akawa
anasema kua Familia hii ilipata mtoto wa Kike baada yake ambae kutokana nae
walizaliwa Manabii 70.

Ambapo kwa upande wa Imam Muhammad Ibn Saib Al Kalbi basi yeye anasema kua:
‘Allah Subhanah wa Ta’ala aliwabadilishia hawa wazazi badala yake mtoto wa kike
ambae aliolewa na Nabii na akazaa watoto ambao ni Manabii pia.’

Kisha Al Khidhr akaendelea kumuelezea Nabii Musa kwa kusema kua:

ُ ُ‫ﲔ ِﰱ ٱﻟْ َﻤ ِﺪﻳﻨَ ِﺔ َوَﻛﺎ َن َْﲢﺘَﻪُ َﻛ ٌﻨﺰ ﱠﳍَُﻤﺎ َوَﻛﺎ َن أَﺑ‬


‫ﻮﳘَﺎ‬ ِ ِ
ِ ْ ‫ﲔ ﻳَﺘِﻴﻤ‬
َ ْ ‫ٱﳉ َﺪ ُار ﻓَ َﻜﺎ َن ﻟﻐُﻼََﻣ‬
ِْ ‫﴿وأَﱠﻣﺎ‬
َ
ِ
َ ِّ‫ﱠﳘَﺎ َوﻳَ ْﺴﺘَ ْﺨ ِﺮ َﺟﺎ َﻛ َﻨﺰُﳘَﺎ َر ْﲪَﺔً ِّﻣﻦ ﱠرﺑ‬
ُ‫ﻚ َوَﻣﺎ ﻓَـ َﻌ ْﻠﺘُﻪ‬ ُ ‫َﺷﺪ‬ُ ‫ﻚ أَن ﻳَـْﺒـﻠُﻐَﺂ أ‬
َ ‫ﺻﺎﳊﺎً ﻓَﺄ ََر َاد َرﺑﱡ‬
َ
﴾ً‫ﺻ ْﱪا‬ ِ ِ ِ َ ِ‫َﻋ ْﻦ أ َْﻣ ِﺮى ٰذﻟ‬
َ ‫ﻳﻞ َﻣﺎ َﱂْ ﺗَ ْﺴﻄـﻊ ﻋﱠﻠَْﻴﻪ‬ ُ ‫ﻚ َﺄﺗْو‬
Waamma aljidaru fakana lighulamayni yateemayni fee almadeenati wakana
tahtahu kanzun lahuma wakana aboohuma salihan faarada rabbuka an yablugha
ashuddahuma wayastakhrija kanzahuma rahmatan min rabbika wama
faAAaltuhu AAan amree dhalika ta/weelu ma lam tastiAA AAalayhi sabran (Surat
Al Kahf 18:82)

Tafsir: Ama kuhusiana na Ukuta basi ulikua ni wa Watoto wawili wa kiume Mayatima
katika Mji na chini yake kulikua na hazina kwa ajili yao na baba yao alikua ni Mtu
mwema. Hivyo alitaka Mola wako kua wabaleghe na kisha waichukue hazina yao
kama Rehma kutoka kwa Mola wako, nami sikutekeleza hivyo kwa amri yangu tu. Hio
ndio maana ya yale uliyoshindwa kua na Subra nayo.

Ambapo Wanazuoni wanasema kua Ukuta huo ulikua ni wa Mayatima wawili ambao
walikua wakiitwa Asra na Sarim. Ambao walikua ni watoto wa Mja wa Allah Subhanah
wa Ta’ala ambae alikua ni Mcha Mungu sana na alikua akijulikana kwa jina la
Mukannas. Na pia kuna wasemao kua Mcha Mungu huyu hakua ni watoto wake
mayatima hawa, bali walikua ni wenye kutokana na kizazi chake, hivyo kutokana na
Ucha Mungu wake basi Allah Subhanah wa Ta’ala akawa ni mwenye kumhifadhia kizazi
chake hicho kilichotokana nae.
889

Hivyo Al Khidhr alipewa habari ya kua ukuta huo umehifadhi hazina chini yake ambapo
alipouangalia basi akauona kua ukuta huo unataka kuanguka na akaamrishwa aujenge na
hii ni kutokana na kua watu waliokua wanaishi kwenye mji huo hawakua ni watu wenye
sifa nzuri basi bila ya shaka kama ukuta utaanguka na watu hao wakaiona hazina hio basi
takua rahisi kwao kuihodhi na kuwadhulumu mayatima hao haki yao.

Na amesema Imam Ibn Mardawiyah kua: ‘Amesema Jabir kua amesema Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala huhifadhi mema ya Mja
wake Mwema kwa ajili ya Mtoto wake, na Mtoto wa Mtoto wake na jamaa zake’’

Na akasema Imam Ibn Abi Hatim Abd Rahman Ibn Muhammad Ibn Idris Ibn Al Mundhir
Al Hanzali Al Razi Al Shafii kua : ‘Amesema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu
Anhu kua Allah Subhanah wa Ta’ala hupatanisha Mja na mema wake na mema ya
mtoto wa mja wake huyo na humlinda na kumhifadhi yeye na wanaomzunguka kwa
wema’

Imam Ahmad Ibn Muhammad Ath Thalabi anaendelea kutuambia kua; ‘Siku Moja kuna
mtu mmoja aliingia katika makazi ya Khalifa Harun Rashid kwa ajili ya kutaka
kumuua Khalifa Harun Rashid. Lakini alipoingia ndani hakuweza kumfanya
chochote Khalifa Harun Rashid na hivyo akamwachia Khalifa Harun Rashid:
‘Hivyo Khalifa Harun Rashid alipoulizwa alifanya nini mpaka akawa ni mwenye
kuokoka kutokana na kuuliwa na mtu huyo basi akasema: ‘Nilisema: ‘Ewe yule
ambae uliwahifadhi watoto wawili kutokana na Ucha Mungu wa Baba yao, basi
nihifadhi mimi kutokana na Ucha Mungu wa Mababa zangu waliotangulia kabla
yangu’’’’

Ambapo kwa upande wa Imam Sayyib Ibn Mussayib basi nae pia alikua akimuona Mtoto
wake basi alikua ni mwenye kusema: ‘Ewe Mtoto wangu Mdogo wa Kiume,
nitaongeza Dua zangu juu yako, na hivyo huenda nikapata hifadhi kupitia kwako’
na kisha huisoma aya hii ya Surat Al Kahf 18:82 isemayo:

ُ ُ‫ﲔ ِﰱ ٱﻟْ َﻤ ِﺪﻳﻨَ ِﺔ َوَﻛﺎ َن َْﲢﺘَﻪُ َﻛ ٌﻨﺰ ﱠﳍَُﻤﺎ َوَﻛﺎ َن أَﺑ‬


‫ﻮﳘَﺎ‬ ِ ِ
ِ ْ ‫ﲔ ﻳَﺘِﻴﻤ‬
َ ْ ‫ٱﳉ َﺪ ُار ﻓَ َﻜﺎ َن ﻟﻐُﻼََﻣ‬
ِْ ‫﴿وأَﱠﻣﺎ‬
َ
ِ
َ ِّ‫ﱠﳘَﺎ َوﻳَ ْﺴﺘَ ْﺨ ِﺮ َﺟﺎ َﻛ َﻨﺰُﳘَﺎ َر ْﲪَﺔً ِّﻣﻦ ﱠرﺑ‬
ُ‫ﻚ َوَﻣﺎ ﻓَـ َﻌ ْﻠﺘُﻪ‬ ُ ‫َﺷﺪ‬ُ ‫ﻚ أَن ﻳَـْﺒـﻠُﻐَﺂ أ‬
َ ‫ﺻﺎﳊﺎً ﻓَﺄ ََر َاد َرﺑﱡ‬
َ
﴾ً‫ﺻ ْﱪا‬ ِ ِ ِ َ ِ‫َﻋ ْﻦ أ َْﻣ ِﺮى ٰذﻟ‬
َ ‫ﻳﻞ َﻣﺎ َﱂْ ﺗَ ْﺴﻄـﻊ ﻋﱠﻠَْﻴﻪ‬ ُ ‫ﻚ َﺄﺗْو‬
Waamma aljidaru fakana lighulamayni yateemayni fee almadeenati wakana
tahtahu kanzun lahuma wakana aboohuma salihan faarada rabbuka an yablugha
890

ashuddahuma wayastakhrija kanzahuma rahmatan min rabbika wama


faAAaltuhu AAan amree dhalika ta/weelu ma lam tastiAA AAalayhi sabran (Surat
Al Kahf 18:82)

Tafsir: Ama kuhusiana na Ukuta basi ulikua ni wa Watoto wawili wa kiume Mayatima
katika Mji na chini yake kulikua na hazina kwa ajili yao na baba yao alikua ni Mtu
mwema. Hivyo alitaka Mola wako kua wabaleghe na kisha waichukue hazina yao
kama Rehma kutoka kw a Mola wako, nami sikutekeleza hivyo kwa amri yangu tu.
Hio ndio maana ya yale uliyoshindwa kua na Subra nayo.

Na pia kuhusiana na aya hii basi kwa upande wa Imam Ahmad Ibn Muhammad Ath
Thalabi basi yeye anasema kua: ‘Abu Darda Radhi Allahu Anhu anasema kua:
‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Maana ya maneno
yasemamayo: Wakana tahtahu kanzun lahuma’ yaani ‘na chini yake kulikua na
hazina kwa ajili yao’ basi yalikua yanamaanisha kua hazina hio ilikua ni Dhahabu
na Fedha, na baba yao ambae alikua akiitwa Kashish alikua Mcha Mungu aliekua
kwenye Msitari ulionyooka. Walihifadhiwa kwa sababu ya Baba yao, ingawa
haukuzungumziwa ucha Mungu wao. Lakini baina yao na Baba yao ambae
walihifadhiwa kutokana nae basi kuna Mababa 7’’

Hivyo kwa upande wa hazina hio basi Wanazuoni wametofautiana pia kwani kuna
wasemo kua: Hazina hio ilikua ni Kartasi zilizoandikwa Ilm Kubwa ndani yake, na huu
ni mtizamo wa Said Ibn Jubayr, ambapo kwa upande wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi
Allahu Anhu basi yeye anasema kua: Ni pande la Dhahabu na kwa upande wa Ikrimah
basi amesema kua ni Hazina hio ni Mali pia kuna wasemo kua ilikua ni hazina ya mali
na dhahabu.

Tunapoziangalia aya tatu hizi alizotumia Al Khidhr katika kumfafanulia kwake Nabii
Musa juu ya yale aliyoshindwa kua na ustahamilivu nayo kutokana na kutokua na Ilm
nayo, na hivyo yeye Al Khidhr kuyabainisha kwa sababu ya kua na Ilm nayo basi alitumia
maneno matatu tofauti katika kila tukio kulingana na mazingira yake ambapo maneno
matatu hayo yote yametokana na neno Rada.

Neno Rada hua ni lenye kumaanisha Kutafuta, Kuomba kitu kwa upole, Kutaka,
Kutembea tembea kwa taratibu. Neno Rada ndio lililotoa neno Iradatun ambalo
humaanisha Khiari, Kua na Uhuru wa Kutaka kufanya kitu au jambo. Neno Rada ndio
lililotoa maneno Faaradtu, Faaradna, Faarada ambayo Al Khidhr aliyatumia
kuwakilisha namna ya utekelezaji wa Majukumu hayo ulikua unatokana na matakwa ya
nani.

Ambapo Al Khidhr alipoelezea tukio la kwenye Jahazi katika Surat Al Qasas 18:79 basi
alisema:
891

ِ ‫دت أَ ْن أ‬
﴾‫َﻋﻴﺒَـ َﻬﺎ‬ ‫﴿ﻓَﺄ ََر ﱡ‬
‘Faaradtu an aAAeebaha’ yaani ‘Hivyo nilitaka mimi Aibu (Kulitia kasoro)’

Na hivyo alitumia neno Faaradtu kuwakilisha hoja yake kua Jambo hilo halikutokana na
Amri ya Allah Subhana wa Ta’ala, kwani yeye Al Khidhr alifanya hivyo kutokana na
kupewa Habari na Allah Subhanaha wa Ta’ala kuhusiana na hali ya maisha ya wenye
Jahazi na hali ya Jahazi lenyewe na namna wanavyolitegemea, na pia kupewa habari
kuhusiana na namna Mfalme huyo anavyotaifisha Majahazi.

Hivyo kutokana na kupewa habari hizo basi akajua kua jukumu lake yeye ni kulitia aibu
au kulitia kasoro jahazi hilo, kutokana na Ufahamu wake aliojaaliwa na Mola wake yaani
hii inakua na kama alivyonasibisha Nabii Ibrahim pale aliposema.

ْ ‫۞وإِذَا َﻣ ِﺮ‬ ِِ ِ ِ ‫﴿ٱﻟﱠ ِﺬى ﺧﻠَ َﻘ ِﲎ ﻓَـﻬﻮ ﻳـﻬ ِﺪﻳ ِﻦ ﱠ‬


‫ﺖ ﻓَـ ُﻬ َﻮ‬
ُ‫ﺿ‬ َ ‫۞وٱﻟﺬى ُﻫ َﻮ ﻳُﻄْﻌ ُﻤ ِﲎ َوﻳَ ْﺴﻘﲔ‬ َ َْ َُ َ
﴾‫ﲔ‬ ِ ‫ﻳَ ْﺸ ِﻔ‬
Alladhee khalaqanee fahuwa yahdeeni; Waalladhee huwa yutAAimunee
wayasqeeni; Wa-idha maridhtu fahuwa yashfeeni (Surat Ash Shuara 26:78-81)

Tafsir: (Kwani) Ni yeye ndie alieniumba na akaniongoza; Na ndie anaenilisha na


kuninywesha; Na ninapoumwa ndie anaenipa afya’

Ambapo hapa Nabii Ibrahim amenasibisha kuumwa kwake kua hua ni kutokana na yeye
mwenyewe na hali ya afya yake na kupona kwake hua kunatokana na Mola wake.

Na kisha Al Khidhr alipoelezea tukio la Kumuua yule mtoto katika aya ya Surat Al Qasas
18:81 basi alisema:

﴾‫﴿ﻓَﺄَرْد َ� أَن ﻳـُْﺒ ِﺪ َﳍُﻤﺎ رﺑـﱡ ُﻬﻤﺎ‬


َ َ َ َ
‘Faaradna an yubdilahuma rabbuhuma’ yaani ‘Hivyo Tulitaka awabadilishie Mola
wao’ na hivyo alitumia neno Faaradna kuwakilisha hoja yake katika hali ya kua jambo
hilo lilitokana na Amri ya Allah Subhnah wa Ta’ala na pia lilitokana na Khiari yake yeye
Mtekelezaji, yaani yeye aliamrishwa afanye hivyo na akatekeleza pia kutokana na yeye
mwenyewe kua ni mwenye kutaka kufanya hivyo baada ya kupewa habari hio juu yake.
892

Na kisha Al Khidhr alipoelezea tukio la Kuujenga Ukuta wa Nyumba uliokua unataka


kuanguka katika aya ya Surat Al Qasas 18:82 basi alisema:

﴾‫ﻚ‬
َ ‫﴿ﻓَﺄ ََر َاد َرﺑﱡ‬
‘Faarada rabbuka’ yaani ‘Hivyo Alitaka Mola wako’

Na hivyo alitumia neno Faarada kuwakilisha hoja yake katika hali ya kua jambo hilo
lilitokana na Amri ya Allah Subhnah wa Ta’ala bila ya yeye kutaka na hii ni kwa sababu
yeye hakua ni mwenye kujua matokeo yake yatakuaje hapo baadae, isipokua Allah
Subhanah wa Ta’ala ndie mwenye kujua, na hivyo kututhibitishia kua, hakuna anaejua
kuhusiana na Ghayb isipokua Allah Subhnah wa Ta’ala na hivyo kutokana na Hikma
zake Allah Subhanah wa Ta’ala basi humfunulia habari hizo amtakae juu ya yale
ayatakayo kua Kiumbe wake husika aliemchagua kujua ayajue, kama alivyosema katika
Qur’an:

ٍ ‫ﻀ ٰﻰ ِﻣﻦ ﱠرﺳ‬
‫ﻮل ﻓَِﺈﻧﱠ ُﻪ‬ ‫ﺗ‬
‫ٱر‬ ِ
‫ﻦ‬ ‫ﻣ‬ ‫ﱠ‬
‫ﻻ‬ ِ‫ﺐ ﻓَﻼَ ﻳﻈْ ِﻬﺮ َﻋﻠَ ٰﻰ َﻏْﻴﺒِ ِﻪ أَﺣﺪاً ۞ إ‬ ِ ‫ﻴ‬ ‫ﻐ‬‫ﻟ‬
ْ ‫ٱ‬ ِ ‫﴿ﻋ‬
‫ﺎﱂ‬
ُ َ َ ْ َ َ ُ ُ َ
ْ َُ
ِ َ‫ﲔ ﻳ َﺪﻳ ِﻪ وِﻣﻦ ﺧ ْﻠ ِﻔ ِﻪ رﺻﺪاً ۞ ﻟِّﻴـﻌﻠَﻢ أَن ﻗَ ْﺪ أَﺑـﻠَﻐُﻮاْ ِرﺳﺎﻻ‬
‫ت َرّﻬﺑِِ ْﻢ‬ ِ ُ ُ‫ﻳﺴﻠ‬
َ ْ َ َْ َ َ َ ْ َ ْ َ ِ ْ َ‫ﻚ ﻣﻦ ﺑـ‬ َْ
﴾ً‫ﺼ ٰﻰ ُﻛ ﱠﻞ َﺷﻲ ٍء َﻋ َﺪدا‬ َ ‫َﺣ‬
ْ ‫أ‬
‫و‬ ‫ﻢ‬ ِ ْ‫َﺣﺎ َط ِﲟَﺎ ﻟَ َﺪﻳ‬
‫ﻬ‬ َ ‫َوأ‬
ْ َ ْ
AAalimu alghaybi fala yudhhiru AAala ghaybihi ahadan, Illa mani irtadha min
rasoolin fa-innahu yasluku min bayni yadayhi wamin khalfihi rasadan,
LiyaAAlama an qad ablaghoo risalati rabbihim waahata bima ladayhim waahsa
kulla shay-in AAadadan (Surat Al Jin 72:26-28)

Tafsir: Ni yeye (pekee) ndie anaejua kuhusiana na Ghayb, na hivyo hamdhihirishii


yeyote yule kuhusiana na Ghayb. Isipokua Mtume wake aliemchangua na hivyo
humuwekea waangalizi mbele yake na nyuma yake. Ili wapate kujua kua wameleta na
kuufikisha Ujumbe wa Mola wao, na ni yeye aliekizunguka kila walichonacho na
huchukua hesabu juu ya kila kitu.

Hivyo basi Al Khidhr kutokana na kua ni miongoni mwa wale ambao waliochaguliwa na
Allah Subhanah wa Ta’ala kua ni wenye kufunuliwa habari za Ghayb kutoka kwa Mola
wao basi anaweka wazi kua hakuujenga ukuta huo isipokua aliujenga kutokana na amri
893

ya Mola wake Nabii Musa ambae pia ndie Mola wa Al Khidhr na ndie Mola wa
Ulimwengu wote, kama zinavyobainisha aya pale ziliposema:

ُ ُ‫ﲔ ِﰱ ٱﻟْ َﻤ ِﺪﻳﻨَ ِﺔ َوَﻛﺎ َن َْﲢﺘَﻪُ َﻛ ٌﻨﺰ ﱠﳍَُﻤﺎ َوَﻛﺎ َن أَﺑ‬


‫ﻮﳘَﺎ‬ َ
ِ ْ ‫ٱﳉِ َﺪار ﻓَ َﻜﺎ َن ﻟِﻐُﻼََﻣ‬
ِ ْ ‫ﲔ ﻳَﺘِﻴﻤ‬
ُ ْ ‫َوأَﱠﻣﺎ‬
﴿
ِ
َ ِّ‫ﱠﳘَﺎ َوﻳَ ْﺴﺘَ ْﺨ ِﺮ َﺟﺎ َﻛ َﻨﺰُﳘَﺎ َر ْﲪَﺔً ِّﻣﻦ ﱠرﺑ‬
ُ‫ﻚ َوَﻣﺎ ﻓَـ َﻌ ْﻠﺘُﻪ‬ ُ ‫َﺷﺪ‬ُ ‫ﻚ أَن ﻳَـْﺒـﻠُﻐَﺂ أ‬َ ‫ﺻﺎﳊﺎً ﻓَﺄ ََر َاد َرﺑﱡ‬
َ
﴾‫َﻋ ْﻦ أ َْﻣ ِﺮى‬
Waamma aljidaru fakana lighulamayni yateemayni fee almadeenati wakana
tahtahu kanzun lahuma wakana aboohuma salihan faarada rabbuka an yablugha
ashuddahuma wayastakhrija kanzahuma rahmatan min rabbika wama
faAAaltuhu AAan amree (Surat Al Kahf 18:82)

Tafsir: Ama kuhusiana na Ukuta basi ulikua ni wa Watoto wawili wa kiume Mayatima
katika Mji na chini yake kulikua na hazina na baba yao alikua ni Mtu mwema. Hivyo
alitaka Mola wako kua wabaleghe na kisha waichukue hazina yao kama Rehma
kutoka kwa Mola wako, nami sikutekeleza hivyo kwa amri yangu tu.

Hivyo Al Khidhr akamwambia Nabii Musa baada ya kumfafanulia malengo na


madhumuni yaliyompelekea ufanya kama alivyofanya kwa kusema: ‘Ewe Musa
ulinilaumu mimi kwa kulitoboa Jahazi, Kumuua Mtoto na Kuusimamisha Ukuta
kwa ajili ya kukimbilia malipo mbele ya Mola wangu kesho Akhera.

Hakika wewe ulinilaumu kwa kutoboa Jahazi kwa kukhofia kua watu wake
watazama ndani yake na hivyo kua ni mwenye kusahau kua wakati Mama yako
alipokutia kwenye Maji ya Mto Nile, wewe ulikua mtoto mchanga, dhaifu na bado
Allah Subhanah wa Ta’ala alikulinda na kukuhifadhi.’

Na ulinilaumu mimi kwa kumuua Mtoto ambae ni Kafiri bila ya sababu yeyote, na
hivyo ukawa ni mwenye kusahau kua wewe mwenyewe ulimuua Mmisri bila ya
sababu yeyote.

Na ulinilaumu mimi kwa kutotaka malipo nilipounyanyua Ukuta na hivyo kua ni


mwenye kusahau kua hata wewe ulichota maji na kuwapa wanyama wa Shuayb
kwa ajii ya Malipo ya kesho Akhera kwa ajili ya Mfalme wa siku ya Malipo.
894

Kisha baada ya hapo, basi Nabii Musa na Joshua wakaachana na Al Khidhr na kurudi
Jangwani kwa ajili ya kukutana na watu wa Bani Israil. Ambapo katika kisa hiki ndani yake
pia tunajifunza mambo yafuatayo:

1-Ni jambo muhimu sana kwa kila mwenye kutafuta Ilm kujihisi kua ana upungufu
katika Ilm yake na hivyo awe tayari kutafuta njia ya kujiongezea Ilm.

2-Mwenye kutafuta Ilm anatakiwa awe mnyenyekevu kwa mwalimu wake pale
inapokua Mwalimu huyo hayuko katika njia za kumuasi Mola Allah Subhanah wa
Ta’ala.

3-Mwanafunzi anatakiwa awe na Heshima, Adabu, Ukarimu, na Upole kwa


Mwalimu wake.

4-Inakubalika kwa mtu kufanya Dhambi ndogo kwa ajili ya kuepusha Dhambi
kubwa.

5-Wazazi wema hata kama wameshatangulia Akhera basi hua na uwezo wa


kunufaisha vizazi vyao kutokana na mema yao waliyoyafanya hapo kabla kama vile
ambavyo watoto wema hua na uwezo wa kuwanufaisha wazazi wao waliokwisha
tangulia Akhera kutokana na mema wanayoyafanya watoto wao katika wakati wa
uhai wao.

6-Umuhimu wa kua na ukarimu na kufanya mema hata kwa wale waliokufanyia


maovu, yaani ingawa inakubalika kulipiza kisasi kwa maovu bila ya kuvuka mipaka
ya kisasi, lakini kusamehe na kua na ukarimu ni bora zaid.

Tumalizie kisa cha Al Khidhr na kauli ya Imam Ahmad Ibn Muhammad Ath Thalabi
ambae anaendelea kutuambia kua: ‘Amesema Abu Ummamah Al Bahili Radhi Allahu
Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliuliza kwa kusema : ‘Jee
nikupeni nyie habari ya Al Khidhr?’ Masahaba wakaitikia kwa kusema: ‘Bila ya
Shaka Ya Rasul Allah!’

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Wakati Al Khidhr alipokua
anatembea katika moja kati ya masoko ya Bani Israil, basi akakutana na miongoni
mwa masikini wa Bani Israil ambae alimwambia Al Khidhr kwa kusema kua:
‘Allah akubariki, naomba Sadaka yako!’

Al Khidhr akajibu: ‘Hakika mimi Namuamini Allah Subhanah wa Ta’ala, na hivyo


alitakalo Allah Subhanah wa Ta’ala kua basi litakua. Na sina cha kukupa.’ Hivyo
Mtu wa Bani Israil akarudia kwa kusema: ‘Allah akubariki, naomba Sadaka yako!
895

Hakika mimi naona uso wako umejaa Huruma na hivyo nataka Huruma iliyomo
ndani ya Moyo wako.’’

Al Khidhr akajibu: ‘Hakika mimi Namuamini Allah Subhanah wa Ta’ala, na hivyo


alitakalo Allah Subhanah wa Ta’ala kua basi litakua. Na sina cha kukupa. Lakini
kamata mkono wangu ili uniuze humu ndani sokoni’ Yule mtu wa Bani Israil
akasema: ‘Itakua kama unavyotaka iwe?’ Al Khidhr akajibu: ‘Mimi ninasema
ukweli, na wewe umetaka jambo kubwa sana kwani umeniulizia kuhusiana na
Allah Subhanah wa Ta’ala nami nimekujibu kua chukua mkono wangu ili uniuze
ndani ya soko hili.’

‘Hivyo Mtu huyo wa Bani Israil akamkamata mkono Al Khidhr akapita nae sokoni
kumuuza na akafanikiwa kumuuza kwa Dirham 400. Hivyo Al Khidhr akakaa na
Mmiliki wake huyo kwa siku kadhaa, lakini hata hivyo Mmiliki huyo hakuona
manufaa yeyote kutokana nae. Hivyo Al Khidhr akasema kumwambia Mmiliki
wake huyo kua: ‘Niajiri’.

Mmiliki huyo akasema kumwambia Al Khidhr: ‘Hakika wewe ni mtu mzima sana,
nami sipendi kukuzidishia Uzito wa majukumu’ Al Khdhr akasema:
‘Hutonizidishia uzito wa Majukumu’ hivyo Mmiliki huyo akasema: ‘Basi Nyanyuka
unisaidie kulisogeza hili jiwe kutoka hapa hadi pale.’ Hilo Jiwe lilikua ni jiwe kubwa
ambalo haliwezi kuondolewa isipokua na watu 6 kwa mda wa siku nzima. Lakini
kwa upande wa Al Khidhr alilihamisha jiwe hilo kwa mda wa saa moja, kwani Allah
Subhanah wa Ta’ala alimtumia Malaika akawa ni mwenye kumsaidia Al Khidhr’

Hivyo mmiliki huyo wa Al Khidhr akafurahi sana na akasema kumwambia Al


Khidhr: ‘Hongera sana’ kisha Mmiliki huyo akawa anataka kusafiri hivyo
akamwambia Al Khidhr: ‘Kwa hakika mimi nakuona wewe kua ni Mja mwema
mcha Mungu na Muaminifu na mwenye wasia mzuri hivyo chukua nafasi yangu
katika Jamii yangu’

Al Khidhr akasema: ‘In-shaa Allah, lakini bora nitumie mie kwa jambo jengine’
Mmiliki akasema kumwambia Al Khidhr: ‘Hakika mimi sipendi kukubebesha
Mzigo’ Al Khidhr akasema: ‘Hutokua ni mwenye kunibebesha Mzigo Mkubwa’
hivyo yule Mmiliki akasema: ‘Sawa, basi nifanye matofali kwani nataka kujenga
kasri nitakaporudi’ kisha akasafiri.

Na aliporudi kutoka safarini akakuta Al Khidhr tayari ameshajenga Kasri kama


alivyotaka liwe Mmiliki wake huyo, hivyo akashangaa sana na kumuuuliza Al
Khidhr: ‘Hebu niambie hivi wewe ni nani?’ Al Khidhr akajibu: ‘Mimi ni Mtumwa
wako ulie ninuanua’ yule mmiliki akasema: ‘Nakuomba kwa jila la Allah ni ambie
wewe ni nani.’
896

Al Khidhr akasema: ‘Hiki ni kiapo ambacho kimenifanya mimi niwe mtiifu. Ama
kuhusiana na mimi basi mimi ni Al Khidhr, Omba omba aliniomba mimi sadaka
kwa ajili ya Mola wangu kumpa yeye, lakini mimi nikawa sina cha kumpa. Hivyo
name nikamkubalia aniuze. Kwani imenifikia mimi kua yeyote yule, atakaeombwa
na Mola wake na mtu huyo akawa na uwezo lakini akawa hakumtimizia haja yake
yule alieomba basi atasimama katika siku ya Malipo mbele ya Mola wake huku Uso
wake ukiwa hauna ngozi wala nyama bali una mifupa mitupu inayogongana’

Hivyo Mmiliki huyo wa Al Khidhr aliposikia maneno hayo akaanza kulia huku akiinama
na kumbusu Al Khidhr na huku akisema: ‘Naapa kwa Mama yangu na Baba yangu,
kwa hakika mimi nimekufanyisha kazi wewe zaidi ya uwezo wako, lakini kwa
sababu sikukujua hivyo nihukumu kwa Mali zangui na watu wangu, na kama
utataka nikuachie huru basi nitakuachia huru’ Al Khidhr akasema: ‘Ndio lakini
mimi ningependa Mtu atakaeniwachia huru ndio awe ni mwenye kumuamini Allah
Subhanah wa Ta’ala’

Na mtu huyo alikua si mwenye kumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala, hivyo akasilimu
na kua Muislam, kisha akampa Al Khidhr Dinar 400 na kumuachia huru. Hivyo Allah
Subhanah wa Ta’ala akamshushia Wahy Al Khidhr na kumwambia: ‘Nilikuokoa wewe
kutoka Utumwani, na Kafiri akawa Muumini na nikakupa Dinar moja kwa kila
Dirham ili upate kujifunza kua hakuna atakaedhurika na wala kula hasara
kutokana na kunitumikia mimi’

Hivyo baada ya Nabii Musa kuachana na Al Khidhr na kurudi kwa watu wake basi
akakumbana na mkasa w kisa kinchojulikana kama kisa cha Ngo’mbe wa Bani Israil.

NABII MUSA NA BAQARATUN SAFRAU - KISA CHA NG’OMBE WA


BANI ISRAIL.


Neno Baqarah kwa Lugha ya kiarabu hua linamanisha Ngombe, yaani bila ya kujali kama
ni Ngombe Jike au Ngombe Dume. Ambapo tunapokiangalia kisa hiki basi tunaona kua
aliezungumziwa ndani yake ni Ngo’mbe Dume. Kwani miongoni mwa masharti ya
Ngo’mbe aliezungumziwa ndani yake kisa hiki basi ni yenye kuonesha kua ni mwenye
sifa za kua ni Ng’ombe Dume, kama tutakavyoona hapo baadae katika kisa hiki.

Ambapo kisa kilianza kutokea mara tu baada ya watu wa Bani Israil kuokota maiti ya
mtu ambae alitupwa mbele ya mlango wa Nyumba moja ya mtu wa Bani Israil ambae
nae alipoulizwa kuhusiana nayo basi akakanusha kua anahusika na kifo cha Maiti huyo.
897

Na wanazuoni wametofautiana kuhusiana na tukio hilo kwani kuna wasemao kua kulikua
na mtu mmoja wa Bani Israil ambae alikua na mjomba wake ambae alikua ni tajiri sana
na alikua hana mtoto wala ndugu yae mwengine yeyote isipokua kijana huyo wa Bani
Israil, hivyo kijana huyo akaamua kumuua Mjomba wake huyo ili apate kurithi Mali hio,
na kisha akautupa mwili wa maiti hiyo mtaani na kuanza kudai haki yake ya kisasi dhidi
ya muuaji wa Maiti hio.

Na kuna wasemao kua katika jamii ya watu wa Bani Israil kulikua na Mwanamke ambae
alikua mzuri sana, mwenye kuheshimika na mwenye Ilm, hivyo watu kadhaa wakataka
kumuoa Mwanamke huyo. Ambapo mjomba wa mwanamke huyo alikua na watoto
watatu wa kiume, na mmoja kati yao alikua ni mcha Mungu sana na hivyo Mwanamke
huyo akakubalia kuolewa na mtoto huyo wa kiume wa mjomba wake.

Lakini ndugu zake wawili hao wakaona wivu juu ya ndoa hio, hivyo wakamwita usiku
mmoja na kisha wakamuua na kuutupa mwili wake mtaani. Ilipoingia asubuhi ya siku
hio basi watu wawili hao wakaenda kwa Nabii Musa na kuanza kulalamika na kulia
kuhusiana na kifo cha ndugu yao huyo na kutaka akamatwe aliemuua ndugu yao huyo
kisha ahukumiwe.

Nabii Musa akawaita watu wa Bani Israil na kuwauliza na kuwahoji kuhusiana na mauaji
hayo, lakini hakuna hata mmoja aliekubali kua anahusika au anamjua muuaji wa mtu
huyo alieuliwa. Hivyo Nabii Musa akawaambia watu wa Bani Israil kua itawabidi walipe
fidia kuhusiana na mauaji hayo, na watu wa Bani Israil wakamwambia Nabii Musa:
‘Itakuaje tulipe fidiya wakati kila mtu ameapa na iko wazi kua hakuna miongoni
mwetu alieua?’

Nabii Musa akaema: ‘Manufaa yaiyokuwemo kwenye hili ni katika kutii maamrisho
ya Allah Subhanah wa Ta’ala’ watu wa Bani Israil wakasema: ‘Ewe Musa hayo
usemayo ni sawa lakini, lakini adhabu ya dhambi hii ni kubwa sana, hivyo Muombe
Mola wako atubainishie wazi tubate kumjua muuaji ili tumpe adhabu stahiki na
hivyo hatutokua ni wenye kulipa fidia.’Nabii Musa akasema: ‘Ya Allah, hakika wewe
ni mwenye kujua kila kitu, kilichowzi na kilichofichikana hivyo nibainishie ni nani
Muuaji’

Allah Subhanah wa Ta’ala akamshushia Wahy Nabii Musa kwa kusema: ‘Allah
Subhanah wa Ta’ala atakubainishieni muuaji kama ikiwa mtachinja Ng’ombe na
kisha mumpige maiti wenu huyo na sehemu ya kiungo cha Ng’ombe huyo. Kisha
Allah Subhanah wa Ta’ala atamfufua maiti huyo. Hili itatokea kama mkitiii
mmrisho ya Allah Subhanah wa Ta’ala, na venginenvyo basi itabidi mlipe fidia’ watu
wa Banii Israil wakasema: ‘Jee unatufanyia Mzaha? Itakuaje kiungo cha Ngombe
aliechinjwa na kufariki kiwe na uwezo wa kumfufua mtu aiekufa hapo kabla?’
898

Ambapo kwa upande wa Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Ahmad Ibn Abu Baqr
Al Ansari Al Qurtubi basi yeye anasema kua; ‘Kuna mitizamo miwili kuhusiana na
sababu ya kuuliwa kwa Mtu huyo. Na mmoja kati ya mitizamo hio ni kua kulikua
kuna mtu ambae alikua anataka kumuoazesha binti yake ambae alikua mzuri sana
kwa mtoto wa kiume wa Mjomba wake, lakini Mjomba wake huyo akakataa ndoa
hio, hivyo mtu huyo akamuua Mjomba wake huyo na kisha akautupa mwili wa
Maiti hio baina ya Vijiji viwili.

Na mtizamo wa pili ni ule usemao kua, kuna mtu ambae alimuua mwenzake kwa
ajili ya matamanio ya kurithi mali itakayotokana na kifo cha mwenzake huyo. Na
kisha akajidai kua kuna watu wa kabila fulani ambao ndio waliomuua. Na hivyo
watu wakaanza kugombana na kutaka kupigana kwa sababu ya kuhutumiana
huko, na hivyo wakelekea kwa Nabii Musa ambae nae akawaambia kua wachinje
Ng’ombe.’

Ambapo kwa upande wa Sharia ya Kiislam basi hua hairuhusiki kwa muuaji kurithi kwa
aliemuua, na hii ni kulingana na Hadith ya Rasul Allah Salallahu Alayi wa Salam ambayo
inasema:

ُ ‫ْاﻟﻘَﺎﺗِ ُﻞ ﻻَ َﯾ ِﺮ‬
‫ث‬

Al Qatilu la Yarith - Muuaji hatorithi. (Jami’ al-Tirmidhi)

Ambapo huo ni mtizamo wa wengi miongoni mwa wanazuoni yaani kuna makubaliano
juu ya hilo, bila ya kujali kama Muuaji aliua kwa kukusudia au aliua bila ya kukusudia.
Na katika hadith nyengine basi amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:

َ ‫ْﺲ ِﻟ ْﻠﻘَﺎﺗِ ِﻞ‬


‫ﺷ ْﻰ ٌء‬ َ ‫ﻟَﯿ‬

Laysa Li Qatili Shay-un – Hakuna Kitu kwa Alieua. (Sunan Abu Daud)

Ambapo anasema Imam Muhammad Al Zuhayly katika: ‘Kama mrithi akimuua


Mwenye Mali basi mrithi huyo hua hana cha Kurithi, iwe ameua kwa makusudi au
kwa bahati mbaya, kwa njia ya moja kwa moja au kwa kupitia njia nyengine
itakayo sababisha mauaji hayo. Kama vile ambavyo ilivyokua Hukmu ya Muuaji,
au ya Shahidi ambae atapelekea mtu alieandika wasia kuhukumiwa adhabu ya kifo,
iwe kwa nguvu ya msukumo au kwa hiari, iwe Mukallaf (Mtu aliefikia umri wa
kufanya Taqlif yaani umri wa kubaleghe na kua na akili timamu hivyo kufikia umri
wa kua ni mwenye ulazima wa kutekeleza majukumu yake mbele ya Mola wake na
viumbe wenzake) au la. Na hii ni kulingana na hadith inayojielezea hapo juu.’ (Al-
Mu’tamad Fil-Fiqh ul Shafi’i)
899

Na miongoni mwa sababu na hikma ya kuzuiwa kwa Urithi kwa alieua hua kunatokana
na kua mauaji hua yanaweza kusababisha kuvunjika kwa uhusiano ambao unapelekea
kua watu wanarithiana. Na kwa upande mwengine basi katika Ilm ya Fiqh kuna kanuni
isemayo kua:

َ ‫ﺷ ْﯿﺌًﺎ ﻗَ ْﺒ َﻞ أ َ َوا ِﻧ ِﮫ ﻋ ُْﻮ ِﻗ‬


‫ﺐ َﺑ ُﺤ ْﺮ َﻣﺎ ِﻧ ِﮫ‬ َ ‫َﻣ ْﻦ ﺗ َ َﻌ ﱠﺠ َﻞ‬

Man taAajjala shay-an kabla awa-nihi Aa’Uuwqiba bahurma-nihi – Anaeharakisha


jambo kabla ya wakati wake, huadhibiwa kwa kuzuiliwa kutokana na kukipata kitu
hicho.

Ambapo kanuni hii inatuwekea wazi kua muuaji alikua anakimbilia kupata mirathi yake
kwa kupitia njia ya mauaji, na hivyo hua ni mwenye kuzuiliwa kuipata mirathi hio. Na
busara iliyomo ndani ya kuzuiliwa kurithi kwa muuaji ni kwa sababu Mauaji hua
yanaweza kusababisha kuvunjika kwa uhusiano ambao ndio sababu au chanzo cha
Muislam kua ni mwenye kuweza kumrithi Muislam mwenzake.

Na kwa upande mwengine basi, Mrithi (ambae ndie alieuliwa) anaweza akamrithi
muuaji. Kwa mfano mrithi anapomjeruhi mrithiwa au alieandika wasia juu yake, na kisha
mrithi huyo akafariki kabla ya kufariki aliejeruhiwa, kisha jeraha alilomsababishia
alieandika wasia hapo kabla likasababisha kifo cha mrithiwa, hivyo katika hali kama hii
basi yule mrithiwa aliejeruhiwa hua na uwezo wa kurithi mali ya aliemjeruhi yeye (na
kisha baada ya hapo atakapokufa yule aliejeruhiwa kutokana na kujeruhiwa kwake huko
basi ndio itaheshbika kua ni mauaji). Na hii ni kwa sababu hua hakuna kipingamizi
kitakachomzuia yule aliejeruhiwa kua asimrithi aliejeruhi baada ya kufa kwake wakati
yeye aliejeruhiwa akiwa yuko hai kutokana na kua ni wenye uhusiano wa kurithiana.

Ama kuhusiana na maelezo juu ya aina ya mauaji na kuruhisika au kutoruhusika kurithi


kulingana na Madhhab tofauti basi kuna kutofautiana mitizamo ifutayo:

1- Madhhab ya Imam Abu Hanifa – Humzuia Muuaji kutokana na Kurithi


isipokua katika hali zifuatazo: Kuua kunakokubalika Kisharia, Kuua kwa
Kujihami, Kuua kwa Mtoto au Mwendawazimu, Kuua kwa kupitia njia ya
mzunguko yaani si kwa njia ya moja kwa moja.
2- Madhhab ya Imam Malik – Humzuia Muuaji kutokana na Kurithi ikiwemo
Mtoto mdogo na asiekua na akili pia isipokua katika hali zifutazo: Kuua
kunaokubalika Kisharia, Kuua kwa Kujihami, Kuua kwa kulipa Kisasi Kuua
bila ya kukusudia.
3- Madhhab ya Imam Al Shafii – Humzuia Muuaji kutokana na Kurithi katika
kila bila ya kujali kama Mtu ni mwendawazimu au ni mtoto mdogo.
900

4- Madhhab ya Imam Ahmad Ibn Hanbal – Humzuia Muuaji kutokana Kurithi


isipokua katika hali zifuatazo: Mauaji yaliyokubalika Kisharia, Mauaji ya
Kujihami au katika Vita, Mauaji ya Kulipiza Kisasi.

Na vile vile hairuhusiki pia kwa Muislam kumrtihi asiekua Muislam na kwa asiekua
Muislam kumrithi Muislam, kama alivyosema Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam
kua: ‘Muislam kumrtihi asiekua Muislam na pia asiekua Muislam haruhusiki
kumrithi Muislam’ (Imam Bukhari, Imam Muslim,Muwatta Imam Malik, Imam At
Tirmidhi, Imam Abu Dawud na Imam Ibn Majah) na pia Wanazuoni wanakubaliana kua
Mmiliki wa Mtumwa hamrithi Mtumwa wake wala Mtumwa hawezi kurithi kutoka kwa
Bwana wake.

Hivyo tunapoiangalia Qur’an basi tunaona kua kisa hiki cha Nabii Musa na Ngo’mbe wa
Bani Israil kinaanza na ile aya isemayo:

ِ ‫ٱﻪﻠﻟ �ْﻣﺮُﻛﻢ أَ ْن ﺗَ ْﺬ َﲝﻮاْ ﺑـ َﻘﺮًة ﻗَﺎﻟُ ۤﻮاْ أَﺗَـﺘ‬ ِ ِ ِ ِ ‫ﺎل ﻣ‬ ِ


‫ﺎل‬
َ َ‫ﱠﺨ ُﺬ َ� ُﻫُﺰواً ﻗ‬ ََ ُ َ ُ َ َ‫﴿ َوإ ْذ ﻗ‬
ْ ُ ُ َ َ‫ﻮﺳ ٰﻰ ﻟ َﻘ ْﻮﻣﻪ إ ﱠن ﱠ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ ِ ْ ‫ﭑﻪﻠﻟِ أَ ْن أَ ُﻛﻮ َن ِﻣﻦ‬ ‫أَﻋُﻮذُ ﺑِ ﱠ‬
َ ‫ٱﳉَﺎﻫﻠ‬ َ
Wa-idh qala moosa liqawmihi inna Allaha ya/murukum an tadhbahoo baqaratan
qaloo atattakhidhuna huzuwan qala aAAodhu biAllahi an akoona mina
aljahileena(Surat Al Baqara 2:67)

Tafsir: Na kumbuka aliposema Musa Kuwaambia Watu wake: ‘Hakika Allah


anakuamrisheni nyinyi mchinje Ng’ombe.’ Wakasema: ‘Hivi Jee Unatufanyia
Mzaha?’ Akasema (Nabii Musa): ‘Najilinda kwa Allah kutokana na kua miongoni
mwa Wajinga’

Kisa cha Nabii Musa na Ng’ombe wa watu wa Bani Israil ni kisa ambacho
kinatudhihirishia Maumbile ya tabia za watu wa Bani Israil ambao walikua ni watu
wenye kuwasikiliza Mitume wao lakini hata hivyo hapo hapo walikua kua si wenye
kuyatilia maanani yale wanayoambiwa na Mitume wao kwani walikua hawajui thamani
yao mbee ya Mola wao, wala hawajui thamani ya Mtume wao mbele yao na hivyo
walikua ni wenye kufuata sharia lakini bila ya kutaka wala kuridhia yaani kama
wanalazimishwa hivyo hua ni wenye kumtii Mola wao lakini si katika njia ya Kiroho,
bali katika njia au hali ya kua ni wenye kufanya maskhara, ambapo Ibn Adam anapokua
katika hali kama hii ya kukataa kile chenye manufaa nae basi hua ni mwenye sifa ya kua
na Ujinga.
901

Yaani hapa hali inakua kama alivyosema Hujjat Ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu
Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali kua: ‘Hakuna Mtu
atakaemiliki Theluji, isipokua itakua rahisi kwake kuibadilisha na Kito cha
Thamani cha Almasi. Hali kadhalika Dunia hii hua ni sawa na Theluji inayoyeyuka
kwa Jua, na hivyo mwisho wake itamalizika. Wakati Uhalisi wa Akhera yako hua
ni sawa na kito cha thamani cha Almasi, ambayo hua ni yenye kudumu Milele’

Hivyo watu wa Bani Israil walikua ni wenye kupenda kuikumbatia Dunia yao na hivyo
kua ni sawa na wenye kupenda kumiliki Theluji kutokana na ubaridi baridi wake ambao
hata hivyo si yenye kudumu, hivyo wakawa hawako tayari kuibadilisha kwa Kito cha
Thamani cha Almasi ambacho ni kitu chenye kudumu zaidi na chenye thamani zaidi na
manufaa zaidi yaani Akhera yao.

Ambapo tunapoiangalia aya yetu hii basi tunaona kua Nabii Musa alipowashauri watu
wake hao wa Bani Israil kuhusiana na maamrisho ya Mola wake juu yao, basi nao
wakadhani kua kama ilivyokua kawaida yao wao kua ni wenye kufanya Maskhara
kutokana na ujinga wao, basi na Nabii wao pia ni mwenye tabia kama zao na hivyo
wakamwambia kuhusiana na amrisho hilo la Mola wao juu yao kua: ‘Atattakhidhuna
huzuwan? - Hivi (wewe Musa) Unatutania, Unatufanyia Mzaha, Unatufanyia
Maskhara au?’

Na ndio maana Nabii Musa akawaambia watu hao: ‘aAAodhu biAllahi an akoona mina
aljahileena - Najilinda kwa Allah kutokana na kua miongoni mwa Wajinga’ yaani
kwa hakika yeye si mwenye kufanya Mzaha mbele ya maamrisho ya Mola wake kwani
kufanya mzaha katika Ibada au maamrisho ya Allah Subhanah wa Ta’ala basi hua ni sifa
mbaya sana ya Ujinga mkubwa sana usiokua na Manufaa yeyote ndani yake.

Hivyo pia inapotokea kwa baadhi ya maadui wa Uislam wanapokua ni wenye


kuwachokoza na kuwafanyia mzaha Waislam kutokana na mambo mbali mbali ikiwemo
Mavazi ya Wanawake wa Kiislam, Ibada za Kiislam, Maisha tunayoishi Waislam n.k
basi Qur’an inatufundisha kua tunatakiwa kua ni wenye subra na kutojibu mashambulizi
yao ya maneno kwani wao hua ni wenye kufanya hivyo kutokana na Ujinga wao, nasi
tunachotakiwa kukifanya ni kukaa kunyamaza au kusema: ‘aAAodhu biAllahi an
akoona mina aljahileena - Najilinda kwa Allah kutokana na kua miongoni mwa
Wajinga’’ kwani tukiwajibu mashambulizi hayo basi nasi hua hatuna tofauti na wao.

Kwani neno Huzuwan linatokana na neno Hazaa ambalo hua linamaanisha Kudhalilisha,
Kufanyia Mzaha, Kudharau, Kuchokoza, Kufanyia mtu kuoekana kua hana maana, au
anachekesha kutokana na ujinga au jambo lisiloingia akilini na pia humaanisha Kulipa
kwa kuadhibu kutokana na kufanyiwa Mzaha kama inavyomaanisha sehemu ya kwanza
ya aya ifuatayo:
902

‫ٱﻪﻠﻟِ إِﻧﱠﻪُ ﻻَ ُِﳛ ﱡ‬


‫ﺐ‬ ‫َﺟُﺮﻩُ َﻋﻠَﻰ ﱠ‬ ِ ٍ
ْ ‫﴿ َو َﺟَﺰآءُ َﺳﻴِّﺌَﺔ َﺳﻴِّﺌَﺔٌ ّﻣﺜْـﻠُ َﻬﺎ ﻓَ َﻤ ْﻦ َﻋ َﻔﺎ َوأ‬
ْ ‫َﺻﻠَ َﺢ ﻓَﺄ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ٱﻟﻈﱠﺎﻟﻤ‬
Wajazao sayyi-atin sayyi-atun mithluha faman AAafa waaslaha faajruhu AAala
Allahi innahu la yuhibbu aldhdhalimeena(Surat Ash Shura 42:40)

Tafsir: Na malipo ya Ubaya hua ni Ubaya mithili yake. Lakini yeyote atakae samehe
na kufanya suluhu basi Malipo yake yapo kwa Allah, kwani kwa hakika Allah
hawapendi Madhalimu.

Ambapo sehemu ya kwanza ya aya inazungumzia malipo ya mwenye Ubaya ni


kufanyiwa Ubaya mithili yake, lakini na sehemu ya pili ya aya inazungumzia ubora wa
kusamehe na kudharau Ubaya uliofanyiwa ambapo katika hali kama hii basi tunakutana
na mfano mzuri wa Saifu Allah Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu Generali bora zaidi
wa Jeshi la Kiislam na katika Historia ya Dunia pia kwani kamwe hakuwahi kushindwa
mapigano yeyote aliyopigana katika Uhai wake na ndie mtu alieweka historia ya Dunia
ambayo haijavunjwa mpaka leo hii, pale alipotukanwa na mmoja kati ya Madui zake, na
badala yake Saifu Allah Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu ingawa alikua na uwezo
wa kulipa kisasi lakini hakufanya hivyo na badala yake akajibu: ‘Unalolijaza ni daftari
la Madhambi yako, hivyo lijaze kwa kila ukitacho na kwa kadiri uwezavyo’

Mfano mwengine ni pale Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu ambae wakati
alipokua akipigana katika vita vya Khandaq, adui yake aliekua akipigana nae ambae
ilikua bado sekunde tu auliwe na adui huyo, lakini akafanikiwa kumuangusha adui yake
huyo na adui huyo akautemea mate uso wake Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu
Anhuwenye busara, lakini Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu hakumfanya
kitu na akamuachia.

Baadae alipoulizwa sababu ya kumuachia adui yule wakati Allah Subhanah wa Ta’ala
alikua amempa nguvu ya kua na uwezo wa kumuua, Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Radhi
Allahu Anhu alijibu: ‘Nilikua napigana kwa ajili ya Allah, na aliponitemea mate
niliogopa kua kama ningemuua basi ingekua nimemuua kwa sababu ya kulipiza
kisasi cha kutemewa mate’, Kitendo hiki cha Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu
Anhu hakikua cha kijinga bali kilikua ni kitendo kinachoashiria ujasiri na busara kwa
upande wa Uiislam.

Mfano mwengine ni wa Ahnaf Ibn Qays Radhi Allahu Anhu ambae alikua pia ni
miongoni mwa Jenerali wa Jeshi la Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na katika
wakati alipokua akiishi katia ardhi ya Iraq, basi siku moja alifuatwa nyuma na mtu ambae
903

alikua akimtukana, lakini hata hivyo Ahnaf Ibn Qays Radhi Allahu Anhu kutokana na
kujua kua mtu huyo anafanya hivyo kutokana na ujinga wake basi akamuachia mpaka
alipokua anakaribia karibu na nyumbani kwake na kisha akasimama na kumwambia mtu
huyo: ‘Ewe Kijana kama una la zaidi la kusema basi sema kabisa, kwani naingia
kwenye maeneo ya himaya yangu hivyo wasije wakakusikia watu kisha
wakakusababishia madhara.’

Na Imam Abu Hasan Ali Ibn Muhammad Ibn Habib Al Mawardi Al Shafii amesem kua:
‘Umar Ibn Abd Al Aziz Radhi Allahu Anhu amesema kua: ‘Jihadharini na Kufanya
Mzaha kwani unaweza kua ni Ujuinga utakaosababisha kuwepo kwa Kinyongo’ Na
miongoni mwa Watu wenye Hikma alisema kua: ‘Kwa Hakika Mzaha ni aina ya
Udhalilisho isipokua pale unapomfurahisha yule anaefanyiwa Mzaha.’ Na pia
ikasemwa kua: Mzaha umeitwa kua mzaha kwa sababu unampotosha mtu
kutokana na ukweli’

Hio ni badhi ya mifano ambayo ya watu wenye Subra na Hikma za kupigiwa mifano,
katika kukataa kwao kua ni miongoni mwa watu wajinga kama vile ambayo Nabii Musa
alivyokataa kua Mjinga mbele ya watu wa Bani Israil, na hivyo baada ya Nabii Musa
kuwabainishia watu wake hao kua anachokisema si mzaha kwa kuwaambia:

‘Najilinda mimi kwa Allah Subhnah wa Ta’ala kutokana na kua ni mwenye


kufanya Mzaha, kwa kusema kitu ambacho hakukisema Allah Subhanah wa Ta’ala,
au kutokana na kua ni mwenye kukataa maamrisho ya Moa wangu na
kuyachukulia kua ni upuuzi mtupu, kutokana na kutokua na ukamilifu wa ilmu na
ufahamu, kama vile ambavyo nyinyi mnavyokataa.’

‘Hivi jee amjuia nyinyi kua ingawa Manii ya Mwanamme na Mayai ya Mwanamke
hayana uhai lakini, hata hivyo Manii hayo na Mayai hayo yanapokutana ndani ya
Mfuko wa uzazi wa Mwanamke, Basi Allah Subhanah wa Ta’ala huumba kutokana
nayo Mtu alie hai? Hivi jee hamjawahi nyie kupanda Mbegu zilizokufa ndani ya
Ardhi iliyokufa na kutokana navyo basi Allah Subhanah wa Taala huotesha Majani
na Mimea tofauti?’

Lakini hata hivyo watu hao wa Bani Israil wakaendelea na mzaha wao kwa kumwambia
Nabii Musa kwa kusema:

‫ض َوﻻَ ﺑِ ْﻜٌﺮ‬
ٌ ‫ﻮل إِﻧـﱠ َﻬﺎ ﺑَـ َﻘَﺮةٌ ﻻﱠ ﻓَﺎ ِر‬ َ َ‫ﲔ ﻟﱠﻨَﺎ َﻣﺎ ِﻫ َﻰ ﻗ‬
ُ ‫ﺎل إِﻧﱠﻪُ ﻳَـ ُﻘ‬ َ ِّ‫ﻚ ﻳـُﺒَـ‬
َ ‫﴿ﻗَﺎﻟُﻮاْ ْٱدعُ ﻟَﻨَﺎ َرﺑﱠ‬
﴾‫ﻚ ﻓَﭑﻓْـ َﻌﻠُﻮاْ َﻣﺎ ﺗُـ ْﺆَﻣﺮو َن‬ ِ ‫ﻋﻮا ٌن ﺑـ‬
َ ‫ﲔ ٰذﻟ‬َ َْ ََ
904

Qaloo odAAu lana rabbaka yubayyin lana ma hiya qala innahu yaqoolu innaha
baqaratun la faridhun wala bikrun AAawanun bayna dhalika faifAAaloo ma
tu/maroona(Surat Al Baqara 2:68)

Tafsir: Wakasema (Watu wa Bani Israil): ‘Muulize Mola wako kwa ajili yetu kua
atubainishie Ng’ombe gani huyo’ Nabii Musa akasema kua: ‘Anasema (Allah
Subhanah wa Ta’ala kua) Ng’ombe huyo asiwe Mzee wala Mdogo, bali awe baina
yake, hivyo fanyeni kile mnachomrishwa.’

Ambapo ingawa watu hawa wa Bani Israil walikua ni wenye kufanya mzaha na maskhara
juu ya amrisho hili, na hivyo kua ni wenye kutafuta visingizio tofauti, lakini hapo hapo
Allah Subhanah wa Ta’ala kwa Hikma zake na Busara zake, akajaalia kuwa ni mwenye
kuwapeleka kule kule wanakotaka kuelekea ambako walikokukimbia hapo kabla yaani
kwenye kulipa fidia ambayo waliikataa kulipa, na hivyo basi matokeo yake ikawabidi
walipe fidia kubwa zaidi wasiyo itegemea katika kumtafuta Ng’ombe mwenye masharti
waliyojiwekea wao wenyewe kutokana na kutokubali kirahisi kutii maamrisho ya Mola
wao kupitia kwa Mtume wao.

Na kuhusiana na asili ya Ngo’mbe huyu basi kuna kutofautiana kimtizamo pia kwani
anasema Imam Ismail Abd Rahman Al Suddi kua: ‘Kulikua na kijana miongoni mwa
watu wa Bani Israil ambae alikua anamjali sana Baba yake kiasi ya kua, siku moja
aliletewa Lulu ambayo alikubali kuinunua kwa bei ya 50000 na hivyo kua ni
mwenye kupata faida kubwa sana kutokana na urahisi wa bei yake. Lakini ikawa
hawezi kuilipia kwa wakati huohuo Lulu hio kwa sababu ufunguo wa sanduku la
pesa ulikua umo ndani ya kisanduku ambacho Baba yake alikua amekifanyia kama
mto kwa kuweka kichwa chake katika wakati huo alipokua amelala usingizi mzito.’

Hivyo muuzaji huyo alipodai mlipo yake basi kijana huyo akakataa kulipa na
kuomba apewe mda mpaka atapoamka baba yake, ambae amelala na yeye anaona
shida kumuamsha. Hivyo mwenye Lulu akasema: ‘Mwamshe Baba yako unipe pesa
zangu nami nitakupunguzia 10000, kwa kufanya hivyo’’

Laini kijana huyo akasema: ‘Kwa hakika mimi siwezi kumwamsha Baba yangu
wakati akiwa amelala, hivyo nitakuongezea 10000 kwa kusubiri mpaka
atakapomka Baba yangu ili nikulipe’ lakini Muuzaji huyo akakataa na kuendelea
kudai malipo yake, hivyo kijana huyo akasema: ‘Basi nitakuongeza 20000 badala
ya 10000 kama ukisubiri nikulipe atakapoamka Baba yangu.’ Hivyo muuzaji huyo
akakubaliana na sharti hilo na kusubiri malipo yake ya 70000 ambayo atayapata
baada ya kuamka Baba wa Kijana huyo.’

‘Na alipoamka Baba yake akamuelezea yaliyotokea na hivo muuzaji Lulu


akalipwaa n kisha Baba huyo kamuombea Dua Mtoto wake. N kish akamwambia:
905

‘Kwa hakika wewe umefanya Jambo sahih, hivyo na yule Ngo’mbe wetu mmoja
aliebakia nakukabidhi wewe awe chini ya Mamlaka yako’ ’

Ambapo kwa Upande wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema
kua: ‘Miongoni mwa watu wa Bani Israil kulikua na Mcha Mungu mmoja ambae
alikua na Mtoto mmoja na Ndama mmoja. Hivyo siku moja akamchukua Ndama
huyo na Kumpeleka hadi kichakani na kusema: ‘Ya Allah Hakika mimi nakuachia
chini ya usimamizi wako Ndama huyu hadi atakapokua mkubwa’. Na baada ya mda
Mzee huyo akafariki na Ndama huyo kabakia kichakani huko, na ikawa kila
akiwaona watu basi hua ni mwenye kukimbia na kujificha.’

Baada ya mtoto huyo aliebakia na mama yake kua mkubwa basi nae akawa mcha
Mungu sana kiasi ya kua alikua ni mwenye kuugawa usiku wake katika sehemu
tatu. Ambapo sehemu ya kwanza alikua akiutumia kwa ajili ya Kufanya Ibada,
sehemu ya pili alikua akiitumia kwa ajili ya Kulala na sehemu iliyobaki alikua
akiitumia kwa ajili ya kukaa na Mama yake katika upande wa kichwani mwake
kabla ya kuamka kwake.

Siku moja Mama yake akamwambia mtoto huyo: ‘Ewe Mtoto wangu Baba yako
amekuachia Urithi wa Ng’ombe ambae yuko kwenye kichaka fulani chini ya
uangalizi wa Allah Subhanah wa Ta’ala. Hivyo nenda kamuite kwa jina Mungu wa
Ibrahim na Ismail na Is-haq, kua Ng’ombe huyo aje kwako. Ngo’mbe huyu ana
alama ya upekee kwani ukimuona basi ngozi yake ina rangi yenye kung’ara kama
mionzi inayotoka kwenye Jua, na anaitwa (Baqaratun Safrao) Ngo’mbe Mwenye
Rangi ya Njano ya Dhahabu inayong’ara.’

Hivyo mtoto huyo Akaenda hadi kwenye kichaka hicho na akamuona Ngo’mbe
huyo na kumuita kwa kusema: ‘Hakika mimi nakuita kwa jina la Mungu wa
Ibrahim, na Ismail na Is-haq Kua uje kwangu kwa idhini yake.’ Ngo’mbe huyo hapo
hapo akamsogelea Mtoto huyo taratibu hadi akamfikia na kisha Mtoto huyo
akamshika Ngo’mbe huyo kwenye kichwa na kuongozana nae, Allah Subhanah wa
Ta’ala akamjaalia Ngo’mbe huyo kua ni mwenye kusema kumwambia Mtoto huyo
kua: ‘Ewe Kijana nipandie bora Mgongoni, kwani hivyo itakua ni rahisi kwako
kunidhibiti na kuniongoza.’

Kijana huyo kasema ‘La, siwezi kufanya hivyo kwa sababu Mama yangu
ameniambia nifanye hivi nilivyofanya.’ Yule Ngo’ombe akasema: ‘Kwa jina la
Mungu wa Bani Israil, kwa hakika kama ungenipandia mgongoni basi ndio
usingeweza kunidhibiti. Hivyo twende kwani kama ungeuamrisha Mlima ung’oke
basi ungeng’oka kwa ajili yako. Kutokana na utiifu na kujitolea kwa Mama yako.’
906

Hivyo Kijana huyu na Ngo’ombe wake wakaendelea na safari yao kuelekea kwa
Mama yake , walipokua njiani wakakutana na Ibilisi ambae alijieguza katika Umbo
la Ibn Adam mzee sana na kumwambia Kijana huyo: ‘Ewe Kijana hakika mimi, ni
mfugaji wa Ngo’mbe, na ambae miongoni mwa Ngo’mbe wangu mmoja ni Fahali
ambae nilimbebesha vitu vyangu na nilipokua najisaidia basi Ngo’mbe huyo
akanikimbia, na kila kitu changu, na niko taabani hivyo nilikua naomba unipandise
juu ya Ngo’ombe wako huyo hadi hapo mbele hivyo nitakupa ujira wa Ngo’mbe
wawili.’

Lakini hata hivyo kijana huyo hakua ni mwenye kutilia maanani maneno hayo ya
Ibilisi na hivyo akasema kumwambia mzee huyo kua: ‘Nenda tu, huku ukiwa ni
mwenye kumtegemea Mola wako kwani kwa hakika Allah Subhanah wa Ta’ala ni
mwenye kujua kila kitu kuhusiana nawe na anajua ni kwa namna gani atakufikisha
unakoenda kutokana na Majaaliwa yake juu yako.’

Hivyo Ibilisi kamwambia Kijana huyo kua: ‘Kama utapenda basi niuzie mie huyu
Ngo’ombe nami nitakulipa kwa thamni ya Ngo’mbe 10 zaidi yake.’ Kijana
akasema: ‘Kwa hakika mimi Mama yangu hakuniamrisha kufanya Jambo hilo’.
Kisha baada ya hapo, mara ghafla akatokea Ndege ambae alikuja mbele ya
Ngo’mbe huyo na Ngombe huyo akakimbia kukimbilia uwarani, na hapo hapo
Mzee huyo nae akatoweka mbele ya macho ya kijana huyo.

Kijana akamwita tena Ngo’mbe huyo wa kusema: ‘Ewe Ngo’mbe hakika nakuita
kwa jina la Mungu wa Ibrahim, na Ismail na Is-haq kua uje kwangu kwa idhini
yake.’ Hivyo Ngo’mbe akaja mbele ya Kijana na huyo na kusema: ‘Ewe ulie mtiifu
kwa mama yake! Hivyi hujamuona Ibilisi, laanat Allahi ambae alikua akitaka
kuniiba mimi? Kwa akika kama agenipandia mimi mgongoni basi usingeweza
kufanya jambo lolote juu yangu. Lakini ulipoomba kwa jina la Mungu wa Ibrahim
basi akatokea Malaika na kunichomoa kutoka kwenye mikono ya Ibilisi, na
kunirudisha mimi kwako wewe kutokana na utiifu wako kwa Mama yako.’

Hivyo Kijana huyo akamchukua Ngo’mbe huyo hadi kwa Mama yake ambae nae
alisema kumwambia Mtoto wake huyo kua: ‘Masikini Mtoto wangu, huna kitu
chochote unachomiliki isipokua Ngo’ombe huyu. Hivyo nenda nae Sokoni
ukamuuze, kwa Dinar 3 lakini kabla hujamuuza basi nitaarifu kuhusiana n
mnunuzi wke’. Hivyo kijana huyo akatoka nae Ngo’mbe huyo na kuelekea Sokoni.

Ambapo Allah Subhanah wa Taa’ala akamtumia Mtihani wa Malaika mwenye


kutaka kumnunua Ngo’mbe huyo ili kuwaonesha Malaika wake utiifu wa Mja wake
huyo kwa Mama yake. Malaika huyo akamuuliza Kijana huyo: ‘Jee bei gani
unamuuza Ngo’mbe wako?’ Kijana akajibu: ‘Dinari 3, lakini kwanza inabidi
ipatikane ridhaa ya Mama yangu juu ya atakae mnunua’
907

Hivyo Malaika akasema: ‘Nitakulipa Dinar 6 lakini uniuzie bila ya kutafuta ushauri
wa Mama yako juu yangu.’ Hivyo kijana huyo akajibu: ‘Hata kama ukinipa kigunia
cha Dhahabu basi kwa hakika mimi sitoweza kukuuzia Ngo’mbe huyo hadi
nitakapopata ridhaa ya Mama yangu juu yako’ kisha akarudi kwa Mama yake na
kumwambia yaliyotokea, hivyo Mama akamwambia mtoto wake huyo: ‘Vizuri,
nenda kamuuze kwa Dinar 6’

Kijana akarudi tena Sokoni na akakutana na Malaika huyo ambae akamuuliza


Kijana huyo: ‘Jee Mama yako amekubali kua umuuze kwa Dinar 6 bila ya kutafuta
ushari wake?’ Kijana akajibu: Amekubali kua nimuuze kwa Dinari 6, lakini
kwanza inabidi ipatikane ridhaa yake’

Hivyo Malaika akasema: ‘Nitakulipa Dinar 12 lakini uniuzie bila ya kutafuta


ushauri wa Mama yako juu yangu.’ Hivyo kijana huyo akajibu: ‘Kwa hakika mimi
sitoweza kukuuzia Ngo’mbe huyo hadi nitakapopata ridhaa ya Mama yangu juu
yako’ kisha akarudi kwa Mama yake na kumwambia yaliyotokea, hivyo Mama
akamwambia mtoto wake huyo: ‘Vizuri, kwani huyo aliekuulizia hakua Ibn Adam
bali alikua ni Malaika kukujaribu. Hivyo rudi na ukimuona tena basi Muulize jee
anataka kumnunua Ngo’mbe ama la?’

Hivyo Kijana akarudi Sokoni na akautana na Malaika huyo tena na kumpa ujumbe
aliopewa na Mama yake, Malaika akasema kumwambia kijana huyo kua: ‘Nenda
kwa Mama yako, kisha Mwambie kua, mnataiwa mkae nae Ngo’mbe huyu, kwani
Musa Ibn Imran atamnunua kutoka kwenu, kwa ajili ya Mtu alieuliwa miongoni
mwa watu wa Bani Israil, na akija Musa na kutaka kumnunua basi msimuuze
isipokua kwa ujazo wa Dinar zitakazojaa ndani ya Ngozi yake.’

Hivyo kijana huyu akarudi na Ngo’mbe wake huyo hadi kwa Mama yake na
kumwambia yaliyotokea na walivyoamrishwa kufanya juu yake.

Ambapo tunarudi kwa watu wa Bani Israil na kuona kua mbali ya kua waliambiwa na
Nabii Musa kua: ‘FaifAAaloo ma tu/maroona’ yaani ‘Hivyo fanyeni kile
mnachomrishwa.’ Na hivyo haina haja ya kuuliza masuali mengi ambayo yatapelekea
kuainisha uzito wa masharti ndani ya amrisho walilopewa, kwani Allah Subhnah wa
Ta’ala si mwenye kutaka kuwapa uzito waja wake wanaomtii katika maamrisho yake
kutokana na kujua udhaifu wao wa kimaumbile na ndio maana akasema kwenye Qur’an:

ِ
﴾‫ﺖ‬ ْ َ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻧَـ ْﻔﺴﺎً إِﻻﱠ ُو ْﺳ َﻌ َﻬﺎ َﳍَﺎ َﻣﺎ َﻛ َﺴﺒ‬
ْ َ‫ﺖ َو َﻋﻠَْﻴـ َﻬﺎ َﻣﺎ ٱ ْﻛﺘَ َﺴﺒ‬ ‫ﻒ ﱠ‬ ُ ّ‫﴿ﻻَ ﻳُ َﻜﻠ‬
908

La yukallifu Allahu nafsan illa wusAAaha laha ma kasabat waAAalayha ma


iktasabat (Surat Al Baqara 2:286)

Tafsir: Haikalifishi Allah Nafsi (ya mtu yeyote)isipokua juu ya kile inachokiweza,
inalipwa (Nafsi ya Mtu) kutokana na (mema) iliyoyachuma na itaadhibiwa kutokana
na (dhambi) ilizozichuma.’

Ambapo aya hii imetumia neno Was ambalo kuhusiana nalo basi anasema Sultan Al
Balagha Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Neno Was hua
linatumika katika Lugha ya Kiarabu kumaanisha Kitendo ambacho mtu anaweza
kukifanya kwa kutumia ugumu au uzito mkubwa sana, kwa mfano: ‘Kuna
uwezekano wa Ibn Adam kua ni mwenye kusali zaidi ya mara 5 kwa siku, Kufunga
zaidi ya siku 30 kwa Mwaka, kufanya Ibada ya Hija zaidi ya mara 1 katika uhai
wake, Lakini Allah Subhanah wa Ta’ala, ameamrisha kutokana na Rehma zake juu
ya kile ambacho kinawezekana wa urahisi juu yake ’’

Lakini hata hivyo kwa upane wa watu wa Bani Israil kutokana na ujinga wao na kutokua
na Imani na Mtume wao basi wakaona kua bora waulize masuali zaidi kuhusiana na
umaalum wa Ngombe huyo, ili wampe Ugumu Nabii Musa wa kupatikana kwa Ngo’mbe
huyo na hivyo kuwe na kushindikana kwa utekelezwaji wa amrisho hilo, bila ya kujua
kua alietoa amrisho hilo ni Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ni mwenye Sifa bora
zisiszokua na mfano juu ya kila kitu ikiwemo kua ni Al Aalim yaani Mwingi wa kujua
kila kitu, Al Khabiru yaani Mwenye Habari juu ya kila kitu, Al Qadir yaani ni m-bora wa
kukakadiria kila kitu na hivyo alitakalo kua basi bila ya shaka litakua na hivyo wakasema
watu hao wa Bani Israil kumwambia Nabii Musa kama zinavyosema aya kua:

‫ﺻ ْﻔَﺮآءُ ﻓَﺎﻗِ ٌـﻊ‬


َ ٌ‫ﻮل إِﻧـﱠ َﻬﺎ ﺑَـ َﻘَﺮة‬
ُ ‫ﺎل إِﻧﱠﻪُ ﻳَـ ُﻘ‬َ َ‫ﻚ ﻳـُﺒَـِّﲔ ﻟﱠﻨَﺎ َﻣﺎ ﻟَ ْﻮﻧـُ َﻬﺎ ﻗ‬
َ ‫﴿ﻗَﺎﻟُﻮاْ ْٱدعُ ﻟَﻨَﺎ َرﺑﱠ‬
﴾‫ﱠﺎﻇ ِﺮﻳﻦ‬ ِ ‫ﱠ‬
َ ‫ﻟ ْﻮﻧـُ َﻬﺎ ﺗَ ُﺴﱡﺮ ٱﻟﻨ‬
Qaloo odAAu lana rabbaka yubayyin lana ma lawnuha qala innahu yaqoolu innaha
baqaratun safrao faqiAAun lawnuha tasurru alnnadhireena;(Surat Al Baqara 2:69)

Tafsir: Wakasema (Watu wa Bani Israil): ‘Muulize Mola wako kwa ajili yetu kua
atubainishie rangi gani (Ng’ombe)huyo’ Akasema (Nabii Musa): ‘Anasema (Allah
Subhanah wa Ta’ala) Huyo awe ni Ngombe wa Njano inayong’ara rangi yake, iwe ni
yenye kuwafurahisha wenye kuitizama.’

Lakini watu hao wa Bani Israil hawakua ni wenye kutosheka na mabainisho hayo juu ya
Ngo’mbe huyo hivyo wakaendelea kuuliza kwa kusema:
909

‫ﻚ ﻳـُﺒَـِّﲔ ﻟﱠﻨَﺎ َﻣﺎ ِﻫ َﻰ إِ ﱠن ٱﻟﺒَـ َﻘَﺮ ﺗَ َﺸﺎﺑَﻪَ َﻋﻠَْﻴـﻨَﺎ َوإِ ﱠ� إِن َﺷﺂءَ ﱠ‬
ُ‫ٱﻪﻠﻟ‬ َ ‫﴿ﻗَﺎﻟُﻮاْ ْٱدعُ ﻟَﻨَﺎ َرﺑﱠ‬
﴾‫ﻟَﻤ ْﻬﺘَ ُﺪو َن‬
ُ
Qaloo odAAu lana rabbaka yubayyin lana ma hiya inna albaqara tashabaha
AAalayna wa-inna in shaa Allahu lamuhtadoona; (Surat Al Baqara 2:70)

Tafsir: Wakasema (Watu wa Bani Israil): ‘Muulize Mola wako kwa ajili yetu kua ndio
(Ng’ombe) yupi huyo?, kwani kwetu sisi Ngo’ombe wote wanashabihiana na kwa
hakika kama Allah akitaka basi tutakua tuliongoka’

Na amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Wallahi! Kama


hawakutofautisha hivyo (kwa kusema In-shaa Allah) basi wasingekubaliwa mpaka
mwisho wa Dunia’

Hivyo Nabii Musa akawaambia watu hao wa Bani Israil kua:

‫ث ُﻣ َﺴﻠﱠ َﻤﺔٌ ﻻﱠ‬ ْ ‫ض َوﻻَ ﺗَ ْﺴ ِﻘﻰ‬


َ ‫ٱﳊَْﺮ‬ ِ ٌ ُ‫ﻮل إِﻧـﱠﻬﺎ ﺑـ َﻘﺮةٌ ﻻﱠ َذﻟ‬
َ ‫ﻮل ﺗُﺜﲑُ ٱﻷ َْر‬ َ َ َ ُ ‫ﺎل إﻧﱠﻪُ ﻳَـ ُﻘ‬
ِ َ َ‫﴿ ﻗ‬
﴾‫ﺎدواْ ﻳَـ ْﻔ َﻌﻠُﻮ َن‬ ْ ِ‫ﺖ ﺑ‬ ِ ِ ِ
َ ُ‫ﭑﳊَِّﻖ ﻓَ َﺬ َﲝ‬
ُ ‫ﻮﻫﺎ َوَﻣﺎ َﻛ‬ َ ‫ﺷﻴَﺔَ ﻓ َﻴﻬﺎ ﻗَﺎﻟُﻮاْ ٱﻵ َن ﺟْﺌ‬
Qala innahu yaqoolu innaha baqaratun la dhaloolun tutheeru al-ardha wala tasqee
alhartha musallamatun la shiyata feeha qaloo al-ana ji/ta bialhaqqi fadhabahooha
wama kadoo yafAAaloona; (Surat Al Baqara 2:71)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa): ‘Anasema kua Ngombe huyo asiwe alietumiwa kwa
kuigeuza ardhi wala kumwagilia maji, awe salama na wala asiwe na baka.’
Wakasema:’ ‘Sasa hivi umetuletea Ukweli’ hivyo wakamchinja ingawa walikua karibu
wasifanye hivyo.

Ambapo aya zinatuonesha kua Allah Subhanah wa Ta’ala katika kumuelezea kwake
Ngo’mbe huyu basi amesema kua asiwe mdogo sana na wala asiwe mzee na asiwe ni
yule ambae aliedhalilishwa kwa kugeuza ardhi yaani anaefanyishwa kazi ya kutibua ardhi
kwa Jembe la kuvuta la Ngombe, na wala asiwe ni mwenye kufanyishwa kazi ya
kumwagilia maji ardhini, ambapo tunapotafakari basi tunaona kua masharti ya Ngombe
huyu kua anaonekana ni Ngombe Dume kwa sababu ni Ngo’mbe dume tu ndie pekee
anaefanyishwa kazi za Kulima, Kuvuta gari, kumwagilia Maji n.k
910

Na kisha Ngombe huyo asiwe na kasoro katika mwili wake awe ni yule ambae yuko
salama yaani aliekamilika kwa kila kitu kiasi ya kua hata hio rangi yake ya Manjano ya
Dhahabu yenye kung’ara isiwe ni yenye kupauka, wala yenye kiza wala yenye baka au
doa juu yake, na hivyo Ngo’mbe huyu kua ni mwenye kuenda sambamba na namna
yalivyo maumbile ya Ngo’mbe wa yule kijana wetu wa Bani Israil ambae alieambiwa na
Malaika kua asimuuze ngombe wake huyo, kwani Nabii Musa atamhitaji Ngo’mbe huyo.

Hivyo Watu wa Bani Israil wkasema; ‘Ama sasa hivi Umesema Ukweli ewe Musa,
kwani umemuelezea namna alivyotakiwa aelezewe’ hivyo wakamtafuta Ngo’ombe
huyo na hawakufanikiwa kumpata katika sehemu nyengine yeyote ile isipokua kwa yule
kijana mwenye utiifu mkubwa kwa Mama yake. Na walipomuona Ngo’ombe huyo kwa
kijana huyo basi ilikua bado kidogo wasimnunue kutokana na ughali wa thamani yake.

Kwani waliambiwa bei yake ni mara 10 zaidi. Ambapo kuna wasemao kua walimnunua
kwa Kigunia cha Dhahabu, na kuna wasemao kua walimnunua kwa kupima uzito wa
Ngo’mbe huyo na kisha kuzidisha mara 10 ya uzito wa Dhahabu waliyokua wanatakiwa
kulipa, na kuna wasemao kua waliambiwa kua bei ya Ngo’mbe huyo ni kuijaza Ngozi
yake kwa Dhahabu, watu wa Bani Israil wakakataa kufanya hivyo na kurudi kwa Nabii
Musa na kusema kua Ngo’mbe huyo ni ghali sana, na Nabii Musa akawaambia kua kama
hio ndio bei yake basi inabidi walipe, hivyo watu wa Bani Israil wakakubaliana na bei
hio.

Kutokana na kutotaka kwao kufuata maamrisho ya Mola wao juu ya jambo hilo basi
baada ya kulipa basi Allah Subahanah wa Ta’ala akawa ni mwenye kubainisha na
kuweka wazi kile ambacho walichokua wakikificha ama zinavyosema aya:

﴾‫ِج ﱠﻣﺎ ُﻛْﻨـﺘُﻢ ﺗَ ْﻜﺘُﻤﻮ َن‬


ُ ْ ‫﴿ َوإِ ْذ ﻗَـﺘَـ ْﻠﺘُ ْﻢ ﻧَـ ْﻔﺴﺎً ﻓَﭑ ﱠد َارأُْْﰎ ﻓِ َﻴﻬﺎ َو ﱠ‬
ٌ ‫ٱﻪﻠﻟُ ﳐُْﺮ‬
Wa-idh qataltum nafsan faiddara/tum feeha waAllahu mukhrijun ma kuntum
taktumoona; (Surat Al Baqara 2:72)

Tafsir: Na (kumbukeni) baada ya kuiua Nafsi na kuanza kugombana juu yake. Lakini
Allah akakitoa nje kile mlichokua mkikificha.

Ambapo kwa upande mwengine basi kile kilichofichikana na hivyo kubainishwa na Allah
Subhanah wa Ta’ala pia inaingia ile hali ya kutoamini kwao watu wa Bani Israil ndani
ya Nafsi zao na Nyoyo zao kua kama kweli inawezekana kwa maiti huyo kufufuka baada
ya kupigwa na sehemu ya nyama ya Ngo’mbe huyo ambae ameshachinjwa na kua
ameshakufa tayari na hivyo wakabainishiwa kua wafikiriacho kua hakiwezekani mbele
yao basi hua kinawezekana mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala tena kwa urahisi sana.
911

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Nabii Musa baada ya kuchinjwa


Ngo’mbe huyo kua:

﴾‫آ�ﺗِِﻪ ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜﻢ ﺗَـ ْﻌ ِﻘﻠُﻮ َن‬ ِ ِ ‫ٱﺿ ِﺮﺑﻮﻩ ﺑِﺒـﻌ‬


ْ َ ‫ٱﻪﻠﻟُ ٱﻟْ َﻤ ْﻮﺗَ ٰﻰ َوﻳُِﺮﻳ ُﻜ ْﻢ‬ َ ‫ﻀ َﻬﺎ َﻛ ٰﺬﻟ‬
‫ﻚ ُْﳛِﲕ ﱠ‬ ْ َ ُ ُ ْ ‫﴿ﻓَـ ُﻘ ْﻠﻨَﺎ‬
Faqulna idriboohu bibaAAdiha kadhalika yuhyee Allahu almawta wayureekum
ayatihi laAAallakum taAAqiloona; (Surat Al Baqara 2:68:73)

Tafsir: Tukasema (Kumwmbia Musa): ‘Mpige (Maiti) kwa baadhi yake (ya Nyama ya
Ngo’mbe)’ Kadhalika Hivyo Ndivyo anavyofufua Allah maiti na kukuonesheni nyinyi
dalili zake ili mpate kufahamu.

Ambapo Wanazuoni wametofautiana kuhusiana na sehemu gani ya Ngo’mbe aliyopigwa


nayo maiti huyo kwani kwa upande wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allau Anhu basi yeye
anasema kua: ‘Walimpiga kwa mfupa laini unaounganisha pingili za mifupa.’
Ambapo kwa upande wa Imam Ad Dahhak Ibn Muzahim anasema kua: ‘Walimpiga kwa
Ulimi wa Ngo’mbe huyo’. Kwa sababu alikua anatakiwa apigwe ili aseme na Ulimi ndio
sehemu ya Mwili inayozungumza.

Na kwa upande wa Imam Mujahid Ibn Sulaymn na Imam Said Ibn Jubayr wao wanasema
kua: ‘Walimpiga kwa mkia wa Ngo’mbe huyo.’ Na hii ni kwa sababu hiki kipingili cha
Mkia cha Kiuno ndio sehemu ambayo haiozi nda ndio itakayotumika kufufuliwa kwa
viumbe wote katika siku ya Kiama.

Kama alivyosema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Hakuna sehemu ya
Mwili ya Ibn Adam isiyooza isipokua mfupa mmoja, ambao ni mfupa wa mwisho
wa Uti wa Mgongo ambao Ibn Adam atafufuliwa kutokana nao katika siku ya
malipo’(Imam Bukhari, Imam An Nasai, Imam Ibn Majah, Imam Abu Daud)

Hivyo baada ya kuipiga Maiti hio na sehemu hiyo ya Ngo’mbe huyo basi Maiti hiyo
ikafufuka na kusimama na kusema alieniua ni fulani ibn fulani na kisha baada ya hapo
mtu huyo akaanguka chini na kua mfu.

Ambapo anasema Jarrah Allaah, Sultan Al Balagha Imam Abu Qasim Al Zamakshari
kua: ‘Kuna watu wanaweza wakahoji, hivi jee kwanini Allah Subhnaha wa Ta’ala
hakuharakisha kumfufua Mtu bila ya kuhusisha amrisho la kuchinjwa Ng’ombe?’

Hivyo jibu la suali hili ni kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala amefanya hivyo kwa
sababu ya kuweka sababu ya kutokea kwa jambo hilo kupitia kati hali na masharti
ambayo ndani yake mna manufaa, ambayo ni kupatikana Ukaribu wa Allah
912

Subhanah wa Ta’ala kutokana na kuchinjwa kwa Ngo’mbe huyo kunakotokana na


amrisho lake.

Pili, ni kufundisha kua Kiumbe anapoamrishwa na Muumba wake kufanya jambo,


basi jambo hilo hua linatakiwa kufanywa kwa vizuri na kwa kikamilifu.

Tatu, ni kumuwekea wazi Kiumbe kua anapoamrishwa kufanya jambo na Mola


wake, basi anatakiwa aharakishe kutekeleza amrisho hilo na asitafute visingizio
vitakavyopelekea jambo hilo kua gumu kwake kulitekeleza.

Nne, Kumsaidia Yatima

Tano, Kwa Wajinga hawatakiwi kuyachukulia maneno ya watu wenye Hikma kua
ni Mzaha au ujinga.

Sita, Kwa Mtu anetafuta ukaribu na Mola wake kwa utoa kwa ajii yake basi hua ni
wajibu wake katika kutoa kwake uchagua kilicho bora zaidi.

Saba, kuweka wazi kua anaethibitisha matokeo ya Jambo husika ndio muhimu
kuliko matokeo ya jambo husika.’

Tunapokiangalia kisa hiki basi tunaona kua mbali ya kua watu wa Bani Israil walikua
wakaidi, wajinga na wasiokubali kutaka kuwafuata Mitume yao mbali ya vithibitisho
walivyowekewa wazi, lakini pia watu hao walikua ni Mabakhili na kutokana na Ubakhili
wao basi Allah Subhanah wa Ta’ala akaamua kuwasababishia kutoa zaidi ya ie
wanachokizuia kutokana na Ubakhili wao.

MADHARA YA UBAKHILI NA FAIDA YA KUTOKUA NA UBAKHILI


KATIKA JAMII.


Neno Bakhila kwa lugha ya Kiarabu hua linamaanisha hua linamaanisha Bakhili, Kuzuia
kitu na kukiweka bila ya kukitumia, Kua na ugumu wa Kutoa. Hii ni moja kati ya sifa
mbaya sana ambayo huwapelekea watu kua mbali na Mola wao ambae ndie aliewajaaliwa
Viumbe wake kila kitu kutokana na Rehma zake juu yao.

Wakati Allah Subhanah wa Ta’ala anawahimiza watu kutoa sadaka, zakkah, misaada n.k
na hivyo kua ni wenye kuachana na Ubakhili kwa kusema katika Qur’an kua:
913

‫َﺿ َﻌﺎﻓﺎً َﻛﺜِ َﲑًة َو ﱠ‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻗَـﺮﺿﺎً ﺣﺴﻨﺎً ﻓَـﻴﻀ‬ ِ


ُ ِ‫ٱﻪﻠﻟُ ﻳَـ ْﻘﺒ‬
‫ﺾ‬ ْ ‫ﺎﻋ َﻔﻪُ ﻟَﻪُ أ‬ َ ُ َ َ ْ َ‫ض ﱠ‬ ُ ‫﴿ ﱠﻣﻦ َذا ٱﻟﱠﺬى ﻳـُ ْﻘ ِﺮ‬
﴾‫ﻂ وإِﻟَْﻴ ِﻪ ﺗُـﺮ َﺟﻌُﻮ َن‬
ْ َ ُ ‫َوﻳَـْﺒ ُﺴ‬
Man dha alladhee yuqridhu Allaha qardhan hasanan fayudhaAAifahu lahu
adhAAafan katheeratan waAllahu yaqbidhu wayabsutu wa-ilayhi
turjaAAoona(Surat A Baqara 2:245)

Tafsir: Jee ni nani atakaemuazima Allah muazimo mwema ili apate kumzidishia mara
nyingi zaidi? Na Allah ndie mwenye kupunguza na ndie mwenye kuongeza. Na kwake
yeye ndio kwenye marudio yenu.

Aya imetumia neno Qardhan ambalo hua linamaanisha Kukata, Kugeuka, Kuzuia na pia
kufanya Jambo jema.

Ambapo anasema Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Ahmad Ibn Abu Baqr Al Ansari
Al Qurtubi kua amesema Zayd Ibn Aslam Radhi Allahu Anhu kua: ‘Wakati aya hii
iliposhushwa, basi Abu Darda alimwambia Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam
kua: ‘Ya Rasul Allah! Baba yangu na Mama yangu wawe ni kafara kwa ajili yako!
Hivi Jee Allah Subhanah wa Ta’ala anatuomba mkopo wakati yeye hahitaji
Mkopo?’ Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema ‘Naam, kwani anataka
kukuingizeni Peponi kutokana nao’

Abu Darda akasema kumwambia Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam: ‘Hivi Jee
kama nikimkopesha ataniahidi Pepo mimi na Mtoto wangu Darda?’ Rasul Allah
Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Naam.’ Abu Darda akasema kumwambia
Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam: ‘Ya Rasul Allah, Nipe Mkono wako!’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam, akampa mkono Abu Darda, na Abu Darda
akasema: ‘Mimi nina Bustani Mbili, Moja kwenye maeneo ya Safila na moja
kwenye maeneo ya Aliyah. Wa Allahi hivyo ndio vitu nnavyomiliki. Na hivyo
nimemkopesha Allah Subhanah wa Ta’ala.’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘La fanya moja kwa ajili yake na
jengine kwa ajili ya kujipatia riski yako wewe na wanaokutegemea.’ Abu Darda
akasema: ‘Ya Rasul Allah! Hakika mimi ninashuhudia kua nimeyatumia vizuri
mashamba hayo kwa ajili ya kumkopesha Allah Subhanah wa Ta’ala’’ Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Allah atakulipa wewe kwa Pepo badala yake’
914

Naam.. Bustani moja ya Abu Darda Radhi Allahu Anhu ilikua na Mitende 600, hivyo
Abu Darda Radhi Allahu Anhu akaenda hadi kwa Ummu Darda Radhi Allahu Anha na
kumkuta akiwa kwenye Bustani hizo na watoto wakicheza ndani yake, Abu Darda Radhi
Allahu Anhu akasema kumwambia Ummu Darda Radhi Allahu Anha kua:

‘Mola wangu ameniongoza katika njia iliyoongoka, njia ya mema na usahih, hivyo
ondokeni kwenye Bustani ya Al Widad, kwani nimeikopesha mpaka katika siku ya
Malipo, kwa Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kumtegemea na kwa khiari yangu bila
ya kutafuta msaada wake wala Malipo kutoka kwake, isipokua kwa kutumainia
zaidi kesho Akhera. Hivyo tokeni wewe na watoto. Kwani bila ya shaka Taqwa ndio
zawadi bora kwa mtu kuitanguliza Akhera.’

Ummu Darda Radhi Allahu Anha akasema: ‘Ni mkopo bora Allah akubarikie
kutokana na ulichomkopesha. Kwani kwa hakika Allah amekupa habari njema na
zenye kufurahisha, mtu kama wewe huridhika na alichokikopesha huku akiwa na
Imani kubwa sana. Kwani kwa hakika Allah ameshawaruzuku wanaonitegemea na
kunipa Tende za Ajwa na Maua yanayong’aria. Bila shaka Mtumwa amepata kile
alichojitahidi kupanda na ameshachuma.’

Kisha Ummu Darda Radhi Allahu Anha akawatoa watoto waliokua wanacheza kwenye
Bustani hio huku akiwahimiza kutema tende zilizomo midomoni mwao na pia
kuziangusha zilizomo mikononi mwao. Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema:
‘Jee ni Mitende mingapi. Na makoja mangapi ya Tende na Nyumba Ngapi Abu
Darda atapata badala yake.’

Ambapo amesema Shaykh ul Akbar Muhyi Ad Din Imam Abu Bakr Ibn Al Arabi
kuhusiana na aya hii kua: ‘Kutokana na Hukmu, Busara na Uwezo Makadirio na
Majaaliwa ya Muumba, basi watu waliposikia aya hii basi waligawika katika
makundi matatu tofauti. Kundi la mwanzo ni la wale waliochini ambao walisema:

‘Mola wa Muhammad ni Masikini na hivyo anatuhitaji na sisi ni Matajiri na tuko


huru.’ Huu ni ujinga wa wazi, kwani hawa wanibiw na ile aya isemayo:

﴾‫ٱﻪﻠﻟ ﻓَِﻘﲑٌ وَْﳓﻦ أَ ْﻏﻨِﻴَﺂء‬ ِ‫ٱﻪﻠﻟ ﻗَـﻮَل ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻗَﺎﻟُ ۤﻮاْ إ‬ ِ ﴿
ُ ُ َ َ ‫ﱠ‬ ‫ﱠ‬
‫ن‬ َ ْ ُ‫ﻟﱠَﻘ ْﺪ َﲰ َﻊ ﱠ‬
Laqad samiAAa Allahu qawla alladheena qaloo inna Allaha faqeerun wanahnu
aghniyaon (Surat Al Imran 3:181)

Tafsir: ‘Kwa hakika amezisikia Allah, kauli za wale wanaosema: ‘Hakika Allah ni
masikini na sisi ni Matajiri.’
915

Kundi la pili ni wale wanaopendelea Ubakhili na kua na tamaa ya Mali na hivyo


hua hawaitumii mali hio kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala, au huwawalipia
watu fidya, au kuwanunua Watumwa na kuwaacha huru, na hivyo hua ni wavivu
sana kwani wao hua ni wenye kuitii na kuitegemea Dunia hii tu.

Na kundi la tatu hua ni wenye kujipanga na kuchukua maamuzi juu ya kile


walichokisikia kwa kukikimbilia kukitekeleza kwa kasi kubwa sana kama Abu
Darda na wengineo, ambapo aya hapa imetumia neno Qardh ambalo hua
linamaanisha kila kitu ambacho ambacho kina malipo baada yake.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala hua si mwenye kuhitaji mkopo wala si mwenye kuhitaji
kitu chochote bali kila kitu hua kinamhitaji yeye, lakini Allah Subhanah wa Ta’ala ni
mwenye kupenda wale wenye kumuamini kua ni wenye kutokua na ubakhili na hivyo
kua ni wenye kutoa kwa ajili ya malipo ya kesho Akhera. Na malipo ya kutoa na
kukopesha kwa ajili yake Allah Subhanah wa Ta’ala hua ni makubwa sana kama
tulivyoona katika hadithi ya Abu Dardaa Radhi Allahu Anhu na pia kwenye hadithi
ifuatayo ambayo inasema:

‘Amesema Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu A’layhi
wa Salam amesema kua: ‘Katika Usiku wa Safari ya Miraj niliona kwenye Mlango
kumeandikwa ‘Sadaqah hulipwa mara 10 zaidi na Mkopo hulipwa mara 18 zaidi’
Hivyo nikamuuliza Jibril: ‘Hivi kwanini Mkopo hua ni bora kuliko Sadaqah?’ Jibril
akajibu: ‘Kwa sababu Muombaji hua anaweza kuomba wakati ana kitu japo
kidogo, lakini mkopaji hua hakopi isipokua pale anapokua hana kitu kabisa’’’

Hivyo wale wenye kua na ubakhili na kujizuia kutoa kwao hua ni sawa na wenye
kutoamini na kutokubali kwao kua kuna kufufuliwa na pia kua kila kitu kilichomo
Ardhini na Mbinguni kiko chini ya Umiliki wake Allah Subhanah wa Ta’ala kama
anavyosema katika Surat Al Maidah kua:

‫ﻀﻠِ ِﻪ ُﻫ َﻮ َﺧ ْﲑاً ﱠﳍُْﻢ ﺑَ ْﻞ ُﻫ َﻮ َﺷﱞﺮ‬


ْ َ‫ٱﻪﻠﻟُ ِﻣ ْﻦ ﻓ‬ َ ‫ﻳﻦ ﻳَـْﺒ َﺨﻠُﻮ َن ِﲟَﺂ‬
‫آﺎﺗ ُﻫ ُﻢ ﱠ‬ ِ ‫ﱭ ٱﻟﱠ‬
َ ‫َوﻻَ َْﳛ َﺴ َ ﱠ‬
‫ﺬ‬ ﴿
‫ٱﻪﻠﻟُ ِﲟَﺎ‬ ِ ‫اث ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬ ِ ِِ ِ ِ ِِ ِ
ِ ‫ات َوٱﻷ َْر‬
‫ض َو ﱠ‬ َ َ ُ ‫ﱠﳍُْﻢ َﺳﻴُﻄَﱠﻮﻗُﻮ َن َﻣﺎ َﲞﻠُﻮاْ ﺑﻪ ﻳَـ ْﻮَم ٱﻟْﻘﻴَ َﺎﻣﺔ َو ﱠﻪﻠﻟ ﻣ َﲑ‬
﴾ٌ‫ﺗَـ ْﻌﻤﻠُﻮ َن َﺧﺒِﲑ‬
َ
Wala yahsabanna alladheena yabkhaloona bima atahummu Allahu min fadhlihi
huwa khayran lahum bal huwa sharrun lahum sayutawwaqoona ma bakhiloo bihi
916

yawma alqiyamati walillahi meerathu alssamawati waal-ardhi waAllahu bima


taAAmaloona khabeerun; (Surat Al Imran 3:180)

Tafsir: Na wala usiwahesabu wale ambao Mabakhili wa kile ambacho wamepewa na


Allah kutokana na fadhila zake kua ni kheri kwao, bali hua ni shari kwao. Kwani
watafungwa navyo shingoni mwao wanavyovionea ubakhili katika siku ya Kiama na
kwa Allah ndiko kuliko na mirathi ya Mbinguni na Ardhini, na Allah ni mwenye
habari juu ya kila mnachokifanya.

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kuhusiana na aya hii
kua: ‘Hakuna kutofutiana kwa mtizamo baina ya Wanazuoni kua Ubakhili hua
unajumuisha kuzuia kila kitu ambacho unapokua nacho basi hua ni wajibu
kukitumia, hivyo kukizuia kitu ambacho huna wajibu wa kukitumia hua
hakuhesabiki kua ni Ubakhili.’

Maumbile haya ya Watu wa Bani Israil yanaonekana pia katika wakati wa Rasul Allah
Salallahu A’layhi wa Salam kama ilivyothibitishwa na Allah Subhanah wa Ta’ala katika
Qur’an katika tukio lililotokea na kusababisha kushushwa kwa aya ifuatayo:

ِ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻗَـﻮَل ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻗَﺎﻟُ ۤﻮاْ إِ ﱠن ﱠ‬ ِ ﴿


ُ ُ‫ٱﻪﻠﻟَ ﻓَﻘﲑٌ َوَْﳓ ُﻦ أَ ْﻏﻨﻴَﺂءُ َﺳﻨَ ْﻜﺘ‬
ْ‫ﺐ َﻣﺎ ﻗَﺎﻟُﻮا‬ َ ْ ُ‫ﻟﱠَﻘ ْﺪ َﲰ َﻊ ﱠ‬
﴾‫اب ٱ ْﳊَِﺮ ِﻳﻖ‬
َ ‫ﻮل ذُوﻗُﻮاْ َﻋ َﺬ‬ ُ ‫َوﻗَـْﺘـﻠَ ُﻬ ُﻢ ٱﻷَﻧﺒِﻴَﺎءَ ﺑِﻐَ ِْﲑ َﺣ ٍّﻖ َوﻧَـ ُﻘ‬
Laqad samiAAa Allahu qawla alladheena qaloo inna Allaha faqeerun wanahnu
aghniyaon sanaktubu ma qaloo waqatlahumu al-anbiyaa bighayri haqqin
wanaqoolu dhooqoo AAadhaba alhareeqi, (Surat Al Imran 3:181)

Tafsir: Hakika Allah amesikia kauli ya wale ambao wamesema: ‘Kwa Hakika Allah ni
Fakiri na sisi ni Matajiri’ Hivyo tunaandika waliyoyasema na kuwaua kwao Manabii
bila ya kua na Haki (ya kufanya hivyo) na tutawaambia; ‘Onjeni Adhabu (ya Moto)
yenye kuunguza.’

Ambapo Imam Muhammad Ibn Is-haq yeye anasema kuhusiana na sababu ya kushushwa
aya hii kua: ‘Abu Bakr Radhi Allahu Anhu aliwatembelea Mayahudi ambao walikua
wakisoma kutoka kwa Rabbi wao anaeitwa Finhas. Hivyo Abu Bakr akawaambia
Mayahudi hao kua wamuogope Allah Subhanaah wa Ta’ala kwa kuingia kwenye
Uislam, kwani yeye anajua kwa dhati kua Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam
ni Mtume wa Allah Subhanah wa Ta’ala. Finhas kasema huku akiwa amejawa na
Kiburi kua: ‘Allah anaonekana kua anawahitaji watu wa Bani Israil, lakini sisi
watu wa Bani Israil hatumhitaji Allah. Kwani kama Allah angekua Tajiri basi
917

asingekua ni mwenye kutafuta Mikopo, na amewaharamishia Waislam kutokula


Riba lakini amewaruhusu Mayahudi kula Riba, hivyo hili ni jambo ambalo
linaloonyesha kua Allah anawahitaji zaidi Mayahudi kuliko Mayahudi
wanavyomhitaji Allah.’’ Hivyo Abu Bakr akakasirika na kisha akampiga Finhas kibao
cha uso.

Hivyo Finhas akamshtakia Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam kuhusiana na


kupigwa na Finhas. Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuuliza Abu
Bakr Radhi Allahu Anhu sababu ya kumpiga kibao Finhas, na baada ya Abu Bakr Radhi
Allahu Anhu kuelezea kilichotokea basi Finhas akakanusha juu ya hilo, hivyo Allah
Subhanah wa Ta’ala akashusha aya hio ya Surat Al Imran 3:181.

Ambapo kuhusiana na Watu wa Bani Israil kuwaua Mitume wao basi tutaliona hili katika
juzuu ya pili ya kitabu hii pale tutakapomzungumzia Nabii Isa Ibn Maryam ambamo
ndani yake inabidi tuzungumzie kisa cha Nabii Zakariyah na Nabii Yahya. Na bila ya
shaka tunaangalia haya si kwa sababu ya kua yanawahusu watu wa Bani Israil tu bali ni
kwa sababu ya kua pia yana mafunzo mengi ndani yake na hivyo tusipojifunza kutokana
na makosa yao ikiwemo kua na ubakhili wati tumewekewa wazi madhara yake hapa
Duniani na kesho Akhera basi nasi tutakuwa hatuna tofauti nao watu hao.

Kwani Allah Subhanah wa Ta’ala anaendelea kuwaambia watu wa Bani Israil kutokana
na Ubakhili wao na kila yule atakaekua na sifa ya Ubakhili kua watatiwa Motoni na kisha
wataambiwa kua:

ِ ِ‫ٱﻪﻠﻟ ﻟَﻴﺲ ﺑِﻈَﻼﱠٍم ﻟِّﻠْﻌﺒ‬


﴾‫ﻴﺪ‬ ‫ﱠ‬ ‫ﱠ‬
‫ن‬ َ
‫أ‬‫و‬ ‫ﻢ‬ ‫ﻜ‬
ُ ‫ﻳ‬ ِ ‫﴿ ٰذﻟِﻚ ِﲟﺎ ﻗَﺪﱠﻣﺖ أَﻳ‬
‫ﺪ‬
َ َ َ َْ ْ ْ َ َ َ
ْ
Dhalika bima qaddamat aydeekum waanna Allaha laysa bidhallamin lilAAabeedi,
(Surat Al Imran 3:182)

Tafsir: Haya ni kwa sababu ya yale mliyoyafanya kwa mikono yenu na kamwe Allah
hakua ni mwenye kuwadhulumu Waja wake.

Ambapo maneno Dhalika bima qaddamat aydeekum yaani haya ni kutokana na yale
mliyokua mkiyafanya kwa mikono yenu basi ni yenye kutilia mkazo nia zao na misimamo
yao katika kusimamia na kutekeleza hayo makosa yao waliyokua wakiyafanya hapa
Ulimwenguni. Na kisha Allah Subhana wa Ta’ala anaweka wazi kua hatodhulumiwa mtu
kutokana na makosa yake, kwani kila Mtu atalipwa kulingana na makosa yake bila
kuzidishiwa wala kupunguziwa.
918

Kwani kama ikiwa wale waliowafanyia mzaha Mitume wao, Waliowachinja Mitume
wao, Waliosema kua Allah Subhanah wa Ta’ala ni Masikini na hivyo kujiona kua wao
ni Matajiri, waliofanya Israfu na Ufisadi, n.k wakiingizwa Peponi pamoja na wenye
Taqwa na wenye kufanya Mema, na wenye kumuamini Mola wao na Mitume wake, na
kutoa kile walichokua nacho kwa ajili ya Mola wao n,k basi itakua hakuna uadilifu kwake
yeye Muumba na hivyo hali hii kua ni yenye kupingana na Sifa tukufu ya Allah Subhanah
wa Ta’ala ya Al Adl yaani mwenye Uadilifu wa hali ya juu kabisa usiokua na mfano, na
hivyo kwake yeye Muumba kutokua na Uadilifu hua ni jambo ambalo kamwe
haliwezekani, kwani yeye yuko mbali sana kabisa kabisa na wenye kudhulumu.

Na ndio maana akasema Shaykh ul Islami Imam Abu Abdullah Badr Ad Din Muhammad
Ibn Abda Allah Ibn Bahadir Al Zarkashi kua: ‘Maana ya neno Dhalam ambalo liko
katika hali ya juu kabisa ya kudhulumu, na hivyo kumaanisha maana nyingi
ikiwemo ile yenye kutilia mkazo mara tatu kua Allah Subhanah wa Ta’ala si
Mwenye kudhulumu, Si Mwenye Kudhulumu, si mwe nye ku dhu lu mu!’

Isipokua labda kwa kumsingizia kunakotokana na wale wasiomuamini na wasiomjua na


hivyo kua ni wenye kumkadhibisha kutokana na ujinga wao, na ndio maana Allah
Subhanah wa Ta’ala akawahoji wale wenye kumkadhibisha kwa kusema kua:

ِ ‫ﻳﻦ ِﰱ ٱﻷ َْر‬ ِِ ِ ِ ‫﴿أَم َْﳒﻌﻞ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ آﻣﻨُﻮاْ وﻋ ِﻤﻠُﻮاْ ٱﻟ ﱠ‬


‫ض أ َْم َْﳒ َﻌ ُﻞ‬ َ ‫ﺼﺎﳊَﺎت َﻛﭑﻟْ ُﻤ ْﻔﺴﺪ‬ ََ َ َ َُ ْ
﴾‫ﲔ َﻛﭑﻟْ ُﻔ ﱠﺠﺎ ِر‬ ِ
َ ‫ٱﻟْ ُﻤﺘﱠﻘ‬
Am najAAalu alladheena amanoo waAAamiloo alssalihati kaalmufsideena fee al-
ardhi am najAAalu almuttaqeena kaalfujjari (Surat Sad 38:28)

Tafsir: Au (mnataka) tuwajaalie wale ambao walioamini na wakafanya Mema wawe


kama waliokua wakifanya ufisadi Ardhini? Au tuwajaalie wenye Taqwa kua kama
wenye kuvuka mipaka ya maovu?

Kisha Aya zinaendelea kutuwekea wazi makosa mengine ya watu wa Bani Israil
waliyoyafanya pale walipomwambia Nabii Musa kua:
919

‫ﱠﺎر‬‫ﻨ‬ ‫ٱﻟ‬ ‫ﻪ‬‫ﻠ‬


ُ ‫ﻛ‬ ْ
‫ﺄﺗ‬ ‫ن‬ٍ ‫ﻮل ﺣ ﱠ ٰﱴ �ْﺗِﻴـﻨَﺎ ﺑُِﻘﺮﺎﺑ‬ ٍ ‫ٱﻪﻠﻟ َﻋ ِﻬ َﺪ إِﻟَﻴـﻨَﺎ أَﻻﱠ ﻧـُ ْﺆِﻣﻦ ﻟِﺮﺳ‬
‫ﱠ‬ ‫ن‬‫ﱠ‬ ِ
‫إ‬ ْ‫ا‬
‫ﻮ‬ ۤ ُ‫﴿ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻗﺎﻟ‬
ُ ُ ُ َ َْ َ َ َ ُ َ َ ْ َ ََ
ِ ِ ِ ِ ِ
ُ ‫ﻗُ ْﻞ ﻗَ ْﺪ َﺟﺂءَ ُﻛ ْﻢ ُر ُﺳ ٌﻞ ّﻣ ْﻦ ﻗَـْﺒﻠﻰ ﺑِﭑﻟْﺒَـﻴِّﻨَﺎت َوﺑِﭑﻟﱠﺬى ﻗـُ ْﻠﺘُ ْﻢ ﻓَﻠ َﻢ ﻗَـﺘَـ ْﻠﺘُ ُﻤ‬
‫ﻮﻫ ْﻢ إِن ُﻛﻨﺘُ ْﻢ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ﺻﺎدﻗ‬ َ
Alladheena qaloo inna Allaha AAahida ilayna alla nu/mina lirasoolin hatta
ya/tiyana biqurbanin ta/kuluhu alnnaru qul qad jaakum rusulun min qablee
bialbayyinati wabialladhee qultum falima qataltumoohum in
kutum sadiqeena(Surat Al Imran 3:183)

Tafsir: Wale ambao walisema: ‘Hakika Allah ametuahidi kua tusimumini Mtume
yeyote hadi pale atakapotuletea Kafara ambayo italiwa na Moto (Kutoka Mbinguni).
Sema; ‘Walikuja Mitume kabla yangu, wakiwa na vithibitisho vilivyowazi n hata hivyo
manvyovingumzia. Hivyo kwanini mkawaua kama nyinyi ni wakweli?’’

Imam Muhammad Ibn Saib Al Kalbi anasema kuhusiana na sababu ya kushushwa kwa
aya hii kua: ‘Kundi la Mayahudi wakiwemo Kab Ibn Al Ashraf, Mali Ibn Sayf,
Wahb Ibn Yahudha na Finhas walikuja kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam
na kumwambia kua: ‘Hivyo wewe unadai kua, Allah amekutuma wewe kuja kwetu,
wakati yeye mwenyewe ametutumia sisi kitabu ambacho ndani yake amefunga
makubaliano nasi, kua tusimfuate Mtume yeyote mpaka awe ni mwenye kutuletea
Kafara ambayo itachukuliwa na moto, hivyo ukitufanyia hivyo basi sisi
tutakuamini.’ Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akashusha aya hii.’

Ambapo Wanazuoni wanasema kua hali hii yaa kutoa Kafara na kisha baada ya Kafara
hio huombwa Dua na hivyo hutokea Moto ambao huiunguza Kafara hio na kutoweka
nayo angani ilikuwepo katika wakati wa Manabii waliotangulia na katika wakati wa
Nabii Musa pia lakini hata hivyo ilibatilishwa katika wakati wa Nabii Isa.

Ambapo anasema Imam Ahmad Ibn Muhammad Ath Thalabi kua: ‘Amesema Wahb
Ibn Munabih kua, Allah Subhanah wa Ta’ala alimshushia Nabii Musa Wahy kua
achague sehemu ya kufanya Ibada kwa ajili ya Watu wake, ambayo itakua ni
sehemu tukufu kwa ajili ya kuweka Taurat na Jengo maalum kwa ajili ya kutolea
Kafara, ambapo sehemu hio ya kufanyia Ibada inatakiwa iwe ni ya Mahema
ambayo yatafunikwa nje na ndani yake na ngozi ya Kondoo hao waliotolewa
Kafara, na kamba zake ziwe ni zenye kutokana na Manyoya ya Kondoo hao, na
hakutakiwa Mtu Mwanamke mwenye siku zake kua ni miongoni mwa watakao
920

fuma kamba hizo wala Mwanamme asiekua tohara kukausha Ngozi hizo na kati
kati yake Mahema hayo kuwe na Jengo la kutolea Kafara hio.’

Kisha baada ya kujengwa Mahema hayo, basi Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia
Nabii Musa kua: ‘Hakika mimi nitatuma Moto kutoka Mbinguni ambao hauna
Moshi, na ambao hautounguza kitu chochote na wala hautokua ni wenye kuzimika
na hivyo utakua ni wenye kuimaliza Kafara hio, ambako itakua kukubaliwa
kwake.’ Kisha Nabii Musa akamwambia Nabii Harun: ‘Hakika Allah Subhanah wa
Ta’ala amenichagua mimi, kuhusiana na Moto ambao utashuka kutoka Mbinguni
kwa ajili ya kuichukua Kafara na hivyo kua ni alama ya kukubaliwa kwake, na
hivyo nami nakukabidhi jukumu hio juu yako.’

Hivyo basi bia ya shaka Watu wa Bani Israil walikua ni wenye kutoa Kafara kwa ajili ya
Allah Subhnah wa Ta’ala kama vile ambavyo walivyokua wakifanya watu wengine
waliotangulia kabla yao, ambapo wakati yote haya yanatokea basi watu hao walikua bado
hawajafika katika ardhi takatifu waliyoahidiwa na Nabii Musa kua wametayarishiwa na
Mola wao, bali walikua wapo karibu na eneo la ardhi hio, na hii ilikua ni kwa sababu
ilikua haujafika mda wao wa kuwasili na kuingia kwenye ardhi ya Mji huo walioahidiwa.

Ambao hata hivyo Mji huyo haukua mtupu kwani ulikua unakaliwa na watu wengine
ambao, iliwabidi watu wa Bani Israil wapigane nao watu hao ili wawatoe kwenye ardhi
hio kisha ndio wahamie wao.

AMRISHO LA KWANZA LA BANII ISRAIL KUINGIA KWENYE ARDHI


TAKATIFU.


Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea haya kwa kusema kua:

‫ﺂء‬ َِ‫ٱﻪﻠﻟِ َﻋﻠَْﻴ ُﻜﻢ إِ ْذ َﺟ َﻌﻞ ﻓِﻴ ُﻜﻢ أَﻧْﺒ‬


‫ﻴ‬ ‫ﺔ‬ ‫ﻤ‬ ِ‫ﺎل ﻣﻮﺳﻰ ﻟَِﻘﻮِﻣ ِﻪ �ﻗَـﻮِم ٱذْ ُﻛﺮواْ ﻧ‬ ِ﴿
َ ْ َ ْ ‫ﱠ‬ َ َ ُ ْ َ ْ ٰ َ ُ َ َ‫َوإ ْذ ﻗ‬
‫ﻌ‬
ْ
‫ض‬ ِ ِ ِ ‫تأ‬ ِ
َ ‫ﲔ۞ َ�ﻗَـ ْﻮم ْاد ُﺧﻠُﻮا اﻷ َْر‬ َ ‫َﺣﺪاً ّﻣ َﻦ ٱﻟْ َﻌﺎﻟَﻤ‬ َ ‫آﺎﺗ ُﻛ ْﻢ ﱠﻣﺎ َﱂْ ﻳـُ ْﺆ‬ َ ‫َو َﺟ َﻌﻠَ ُﻜ ْﻢ ﱡﻣﻠُﻮﻛﺎً َو‬
﴾‫ﺎﺳ ِﺮﻳﻦ‬ ِ ‫اﻪﻠﻟ ﻟَ ُﻜﻢ وﻻَ ﺗَـﺮﺗَ ﱡﺪوا ﻋﻠَﻰ أ َْدﺎﺑ ِرُﻛﻢ ﻓَـﺘَـْﻨـ َﻘﻠِﺒﻮا ﺧ‬ ‫اﳌ َﻘﺪ َ ﱠ‬
َ َ ُ ْ َ ٰ َ ْ َ ْ ُ‫ﺐ ﱠ‬ َ َ‫ﱠﺳﺔَ اﻟ ِﱴ َﻛﺘ‬ ُ
Wa-idh qala moosa liqawmihi ya qawmi odhkuroo niAAmata Allahi AAalaykum
idh jaAAala feekum anbiyaa wajaAAalakum mulookan waatakum ma lam yu/ti
921

ahadan mina alAAalameena; Ya qawmi odkhuloo al-ardha almuqaddasata allatee


kataba Allahu lakum wala tartaddoo AAala adbarikum fatanqaliboo khasireena;
(Surat Al Maidah 5:20)

Tafsir: Na (Kumbukeni) aliposema Musa kuwaambia watu wake: ‘Kumbukeni Neema


za Allah juu yenu, alipokujaalieni kutokana nanyi Manabii na akakujaalieni Wafalme
na akakupeni kile ambacho hakumpa hata mmoja miongoni mwa Walimwengu.’
(Akaendelea Kusema Nabii Musa): ‘Enyi watu wangu, ingieni katika Ardhi takatifu
ambayo amekuandikieni Allah juu yenu. Na wala msigeuke kwani (mkigeuka) mtarudi
huku mkiwa mmekula hasara’

Hivyo kama tulipoona hapo kabla kua Nabii Musa anawakumbusha watu wa Bani Israil
kua wanatakiwa wasiwe ni wenye kujivunia Neema na fadhila za Allah Subhanah wa
Ta’ala juu yao, bali wanatakiwa wawe na Shukran kwa Mola wao kutokana na fadhila
alizowafadhili na alizowajaalia. Na kisha Nabii Musa akawaamrisha watu wake hao wa
Bani Israil kwa kuwaambia kua waingie katika ardhi waliyoahidiwa na Allah Subhanah
wa Ta’ala lakini kwa sharti la kua wasirudi nyuma kwani wakirudi nyuma basi watakua
ni miongoni mwa waliokula hasara.

Ambapo watu hao wa Bani Israil walipoikaribia ardhi hio basi wakaiona kua ni ardhi
ambayo imenawiri kutokana na rutba ya Ardhi yake, kwani hii ilikua ni ardhi ya Canaan
ambayo ndio iliyokua ardhi ya mababu zao waliohama kwenye ardhi hio na kuelekea
katika ardhi ya Misri baada ya Nabii Yusuf kuihamishia familia yake kutoka katika ardhi
ya Canaan na kuhamia katika ardhi ya Misri.

Hivyo kabla ya kuingia katika Ardhi hio basi watu waa Bani Israil wakaamua bora
kutuma wapelelezi kwa ajili ya kuenda kuchunguza na kuangalia mazingira yake kwa
ujumla na watu wake wanaotakiwa kupigana nao yako vipi. Hivyo wakatuma watu 12
yaani mmoja kutoka katika kila kabila lao watu wa Banii Israil, watu hao wakafanikiwa
kuingia ndani ya Ardhi hio kwa kilomita kadhaa na kuukaribia mji wa Jesrualem.

Na kisha wakarudi na kuleta habari juu ya yale waliyoyaona katika ardhi hio, na
kuhadithia kua wameona ardhi iliyonawiri na kua na rutba n wakaleta vitibitish vya
baadhi ya matunda yanayoota kwenye ardhi hio ikiwemo Machungwa, Makomamanga,
Zabibu, Tini, Zaituni n.k ambayo yote kutokana na ukubwa wao basi hayabebeki kwa
mikono ya mtu mmoja, lakini pia wakasema kua mbali ya kua ardhi hio ina rutba lakini
watu wake pia wana rutba kwani ni watu wenye miili mikubwa sana na afya nzuri sana
kiasi ya kua watu hao wa Bani Israil wakajawa na khofu kwani walikua wana uhakika
kua kutokana na udogo wa Maumbile yao, basi kamwe haiwezekani kwao wao kuingia
na kupigana na watu wenye maumbile makubwa kimwili maradufu zaidi yao kama
yalivyo maumbile ya watu wa Ardhi hio dhidi yao.
922

Ama Wanazuoni wametofautiana kuhusiana na sehemu ya ardhi husika waliyoahidiwa,


kwani tunpozungumzia ardhi ya Canaan basi hua tunazungumzia eneo la ardhi ya
Falestina, Jordan, Lebanon na ardhi yote ya Syria kwa ujumla. Ambapo kwa upande wa
Abd Allah Ibn Umar Radhi Allahu Anhu basi yeye ansema kua: ‘Eneo la Ardhi Takatifu
limeitwa kua ni Ardhi Takatifu kwa sababu ya Utukufu wake kuanzia Ardhini
kulekea juu mpaka Mbinguni. Na Jerusalem ni ardhi Takatifu kwa sababu ya
Utukufu wake kutoka Ardhini mpaka Mbinguni.’

Na kwa upande wa Imam Muqatil Ibn Sulayman basi yeye anasema kua: ‘Ni maeneo ya
Mlima Sinai na ardi iliyouzunguka Mlima huo’ Ambapo kwa upande wa Imam Ismail
Abd Rahman Al Suddi basi yeye anasema kua: ‘Ni eneo la Ardhi ya Arihaan (Jericho)’
na kwa upande wa Imam Ad Dahhaq Ibn Muzahim basi anasema kua: ‘Ni eneo la ardhi
ya Ramallah na Jordan’ na Imam Qatadah Al Sadusi basi yeye anasema kua : ‘Eneo
lote la Sham’

Imam Muhammad Ibn Saib Al Kalbi yeye amesema kua ni: ‘Eneo la Dimashq
(Damascus) na Falestina’ Imam Muhammad Ibn Saib Al Kalbi anendela kusem kua:
‘Nabii Ibrahim alisimama kwenye Mlima wa Lebnan na akaambiwa na Allah
Subhanah wa Ta’ala kua: ‘Angalia, kila unachokiona mpaka kwenye Upeo wa
Macho yako kimefanywa kua kitukufu wa ajili yako na kwa ajili aya Kizazi chako
na ndio maana Allah Subahanh wa Ta’ala akawaambia watu wa Bani Israil:

﴾‫اﻪﻠﻟ ﻟَ ُﻜﻢ‬
‫ﱠ‬ ‫ﺐ‬‫ﺘ‬ ‫ﻛ‬
َ ‫ﱴ‬ِ‫ﱠ‬‫ﻟ‬‫ا‬ ‫ﺔ‬ ‫ﱠﺳ‬‫ﺪ‬ ‫ﻘ‬
َ ‫اﳌ‬ ‫ض‬ ‫َر‬‫ﻷ‬‫ا‬ ‫ا‬
‫ﻮ‬ ‫ﻠ‬
ُ ‫ﺧ‬ ‫اد‬ ِ‫﴿�ﻗَـﻮ‬
‫م‬
ْ ُ َ َ َ َ َ ْ ُ ْ ْ َ
ُ
Ya qawmi odkhuloo al-ardha almuqaddasata allatee kataba Allahu lakum.(Surat Al
Maidah 5:21)

Tafsir: (Akaendelea Kusema Nabii Musa): ‘Enyi watu wangu, ingieni katika Ardhi
takatifu ambayo amekuandikieni Allah juu yenu.’

Ambapo aya hii imetumia neno Kataba ambalo ni lenye kumaanisha kua ni Amrisho
ambalo walilopewa watu wa Bani Israil na Allah Subhanah wa Taala kua Ili kuingia
ndani ya ardhi hio basi inawabidi watu hao wa bani Israil wapigane na watu hao
waliowauta kwenye Mji huo, kwani neno hilo ndio lile lililotumika kwenye ile aya yenye
amrisho la kufunga mwezi wa Ramadhani pale aliposema Allah Subhanah wa Ta’ala
katika aya ifuatayo:
923

‫ﻳﻦ ِﻣﻦ ﻗَـْﺒﻠِ ُﻜ ْﻢ‬ ِ‫ﱠ‬


َ ‫ﺐ َﻋﻠَﻰ ٱﻟﺬ‬
ِ
َ ‫ٱﻟﺼﻴَ ُﺎم َﻛ َﻤﺎ ُﻛﺘ‬
ِ
ّ ‫ﺐ َﻋﻠَْﻴ ُﻜ ُﻢ‬
ِ ِ‫ﱠ‬
َ ‫ٰ�َﻳـﱡ َﻬﺎ ٱﻟﺬ‬
َ ‫ﻳﻦ َآﻣﻨُﻮاْ ُﻛﺘ‬
﴿
﴾‫ن‬ َ ‫ﻟَ َﻌﻠﱠ ُﻜ ْﻢ ﺗَـﺘﱠـ ُﻘﻮ‬
Ya ayyuha alladheena amanoo kutiba AAalaykumu alssiyamu kama kutiba AAala
alladheena min qablikum laAAallakum tattaqoona (Surat Al Baqara 2:183)

Tafsir: Enyi Mlioamini Mmeamrishwa juu yenu kufunga kama vile walivyoamrishwa
juu yao wale waliotangulia kabla yenu ili mpate kua Wacha Mungu.

Na hivyo baada ya Watu wa Bani Israil kuambiwa kuhusiana na amrisho hilo na


kuelezewa maumbile ya watu wanaoishi kwenye ardhi hio basi kama kawaida yao,
wakaanza kulalamika na kusema: ‘Hakika ya bora kwetu sisi basi tungebakia kwenye
ardhi ya Misri, au tungebakia huku huku Jangwani kuliko kuingia kwenye Ardhi
hio tunayoambiwa kua ni Tukufu lakini tuipigani kwa kupigana na watu hao kwani
Wanawake wetu, Watoto wetu na Mali zetu zote zitakua ngawira zao. Hivyo
hatuwezi kuingia ndani ya ardhi hio mpka watu hao watoke’ kama anavyosema Allah
Subhanah wa Ta’ala:

‫ﻳﻦ َوإِ ﱠ� ﻟَﻦ ﻧﱠ ْﺪ ُﺧﻠَ َﻬﺎ َﺣ ﱠ ٰﱴ َﳜُْﺮ ُﺟﻮاْ ِﻣْﻨـ َﻬﺎ ﻓَِﺈن‬ِ ِ ِ ‫﴿ ﻗَﺎﻟُﻮا �ﻣ‬
َ ‫ﻮﺳ ٰﻰ إ ﱠن ﻓ َﻴﻬﺎ ﻗَـ ْﻮﻣﺎً َﺟﺒﱠﺎر‬
َ َُ
﴾‫اﺧﻠُﻮ َن‬ ِ ‫َﳜْﺮﺟﻮاْ ِﻣْﻨـﻬﺎ ﻓَِﺈ ﱠ� د‬
َ َ ُُ
Qaloo ya moosa inna feeha qawman jabbareena wa-inna lan nadkhulaha hatta
yakhrujoo minha fa-in yakhrujoo minha fa-inna dakhiloona(Surat Al Maidah 5:22)

Tafsir: Wakasema (Watu wa Bani Israil): ‘Ewe Musa hakika ndani yake (Ardhi hio)
kuna watu Majabari na hivyo hatutoingia sisi ndani yake mpaka watakapoondoka
kutoka ndani yake, kisha nasi tutaingia’

Nabii Musa akajaribu kuwausia watu wa Bani Israil kua kama watafanya jitihada katika
kutekeleza amri hio kutokana na kua na Imani na Mola wao basi bila ya shaka Allah
Subhanah wa Ta’ala atawasaidia na kuwapa ushindi dhidi ya watu hao, kwani mbali ya
ukubwa wa maumbile yao lakini hata hivyo watu hao hawana Imani ndani ya Nyoyo zao
na hivyo watashinda na kupewa ushindi kama walivyopewa hapo awali dhidi ya Jeshi la
Fir’awn na hivyo kua ni wenye kuvuka salama Baharini.
924

Lakini watu hao wakakataa na kusema kama wangejua basi bora hata Misri wasingetoka,
yaani bora wangebakia kwenye ardhi hio hio ya Misri na kuendelea kua Watumwa au
hata bora wangerudi katika Ardhi ya Misri. Hivyo Joshua na mwenzake aliekua akiitwa
Kalib Ibn Yuqana wao wakajaribu kuwashawishi watu hao kwa kuwaambia kama
zinavyosema Aya:

‫ﺎب ﻓَِﺈ َذا‬ ِ‫ِ ِ ﱠ‬


َ َ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ َﻤﺎ ْٱد ُﺧﻠُﻮاْ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ُﻢ ٱﻟْﺒ‬
‫ﻳﻦ َﳜَﺎﻓُﻮ َن أَﻧْـ َﻌ َﻢ ﱠ‬ َ َ‫﴿ﻗ‬
َ ‫ﺎل َر ُﺟﻼَن ﻣ َﻦ ٱﻟﺬ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ‫ٱﻪﻠﻟِ ﻓَـﺘَـﻮﱠﻛﻠُ ۤﻮاْ إِن ُﻛﻨﺘُﻢ ﱡﻣ ْﺆِﻣﻨ‬ ِ ِ
َ َ ‫َد َﺧ ْﻠﺘُ ُﻤﻮﻩُ ﻓَﺈﻧﱠ ُﻜ ْﻢ َﻏﺎﻟﺒُﻮ َن َو َﻋﻠَﻰ ﱠ‬
Qala rajulani mina alladheena yakhafoona anAAama Allahu AAalayhima
odkhuloo AAalayhimu albaba fa-idha dakhaltumoohu fa-innakum ghaliboona
waAAala Allahi fatawakkaloo in kuntum mu/mineena; (Surat Al Maidah 5:23)

Tafsir: Wakasema watu wawili miongoni mwa waliokua wakimuogopa Allah ambao
(Allah) aliwaneemesha (kwa) juu yao : ‘Washambulieni kwenye Geti na mkisha ingia
ndani basi mtakua ni wenye kuwashinda, na kwa Allah tegemeeni kama kweli nyinyi
ni Mmeamini.’

Hivyo Joshua na Kalib wakawashawishi watu wa Bani Israil, kua wafanye kama
wanavyoamrishwa na Mola wao kwa kuwavamia watu wa Mji huo kupitia kwenye Geti
kuu la mji huo, huku wakiwa ni wenye kumuamini na kumtegema Allah Subhanah wa
Ta’ala kua atawasaidia pale watakapojisaidia nafsi zao na kuonesha jitihada katika
mapigano yao dhidi ya watu hao ambao tayari wamesha halalishiwa kupigana nao, hivyo
wakifanikiwa kuingia ndani ya geti lao basi bila shaka watauteka mji huo kirahisi
kutokana na radhi na msaada wa Allah Subhanah wa Ta’ala juu yao.

Lakini hata hivyo jitihada zao hazikufua dafu kwani na badala yae watu hao wa Bani
Israil wakaahidi kuwapiga mawe Joshua na Kalib kama ikiwaa wataendelea
kuwashawishi kuhusiana na jambo hilo, kisha watu wa Bani Israil wakamgeukia Nabii
Musa na kumwambia:

ۤ ِ‫﴿ﻗَﺎﻟُﻮاْ �ﻣﻮﺳ ۤﻰ إِ ﱠ� ﻟَﻦ ﻧﱠ ْﺪﺧﻠَﻬﺂ أَﺑﺪاً ﱠﻣﺎ داﻣﻮاْ ﻓ‬


‫ﻚ ﻓَـ َﻘﺎﺗِﻼ‬
َ ‫َﻧﺖ َوَرﺑﱡ‬
َ ‫ﺐأ‬ْ ‫ﻫ‬
َ ‫ذ‬
ْ ‫ﭑ‬َ‫ﻓ‬ ‫ﺎ‬‫ﻴﻬ‬
َ َُ َ َُ ْ َ َُ
ِ َ‫إِ ﱠ� ﻫﺎﻫﻨَﺎ ﻗ‬
﴾‫ﺎﻋ ُﺪو َن‬ َُ
925

Qaloo ya moosa inna lan nadkhulaha abadan ma damoo feeha fa-idhhab anta
warabbuka faqatila inna hahuna qaAAidoona; (Surat Al Maidah 5:24)

Tafsir: Wakasema: ‘Ewe Musa hatutoingia sisi wakati wao wanadumu ndani yake.
Hivyo nenda wewe na Mola wako mkapigane nao, sisi tunakaa hapa (kukusubirini)’

Hii ndio hali waliyokua nayo watu wa Bani Israil na namna walivyokua wakimchukulia
Nabii wao, kwani walikua wakionesha dhahiri kua ni wenye Ubinafsi wa hali ya juu na
hivyo kua ni wenye kumvunja Moyo, ambapo tunapoangalia kwa upande wa Uislam basi
tunaona kua Masahaba walikua na mtizamo na misimamo tofauti kwani mnamo mwaka
wa pili Al Hijra, Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alitoka na Masahaba wake katika
Mji wa Madina kwa ajili ya kuenda kuuvamia na kuutaifisha msafara wa Abu Sufyan
uliokua ukitoka Syria, kwa ajili ya kulipiza kisasi Mali za Waislam zilizotaifishwa na
Makafiri katika Mji wa Makkah.

Lakini sasa walipofika katika maeneo ya Badr basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
Salam akapata habari kua Makafiri wamepata habari juu yao na hivyo wametayarisha
Jeshi kubwa sana kwa ajili ya kupigana nao Waislam, ambapo wao Waislam walikua
hawajajitayarisha kwa ajili ya Vita lakini kwa hali inavyokwenda basi itabid wapigane
Vita. Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaomba Ushauri kwa kuwauliza
Waislam; ‘Jee tufanye nini?’

Hivyo wakati Waislam wamekaa kimya na kufikiria cha kufanya, basi akasimama
Miqdad Ibn Aswad Al Kindi Radhi Allahu Anhu kisha akasema: ‘Ya Rasul Allah
(Salallahu Alayhi wa Salam) Tekeleza plani ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala,
kwani kwa hakika sisi hatutosema kama walivyosema Mayahudi kumwambia Nabii
wao Musa kua:

ِ َ‫ﻚ ﻓَـ َﻘﺎﺗِ ۤﻼ إِ ﱠ� ﻫﺎﻫﻨَﺎ ﻗ‬


﴾‫ﺎﻋ ُﺪو َن‬ َُ َ ‫َﻧﺖ َوَرﺑﱡ‬
َ ‫ﺐأ‬ْ ‫﴿ﻓَﭑ ْذ َﻫ‬
Fa-idhhab anta warabbuka faqatila inna hahuna qaAAidoona; (Surat Al Maidah
5:24)

Tafsir: Hivyo nenda wewe na Mola wako mkapigane nao, sisi tunakaa hapa
(kukusubirini)’

Badala yake sisi tunasema: ‘Nenda wewe na Mola wako mkapigane na sisi tuko
pamoja nanyi na tutapigana. Wa Allahi! Nnaapa kwa yule ambae amekutuma wewe
kwa Haki, kua hata kama ukituongoza kwenye Birkul Ghimad (Maeneo ya
Ethiopia) basi sis tutapigana pamoja nawe dhidi ya wale watakaopingana na haki
926

na hata kama ikiwa kuna makundi na makundi ya Makabila baina ya Madina na


Birkul Ghimad basi tutapigana mpaka tufike huko, na bila ya shaka tutapigana kwa
upande wa Kulia kwako, Kushoto kwako, Mbele yako na Nyuma yako mpaka Allah
Subhanah wa Ta’ala atupe Ushindi.’

Hapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akafurahi na kutabasam kisha akawageukia
watu wa Madina na kuwauliza: ‘Jee mnasemaje? Tufanye nini?’

Ambapo kwa upande wa watu wa Madina akasimama Saad Ibn Muadh Radhi Allahu
Anhu na kasema: ‘Ya Rasul Allah (Salallahu Alayhi wa Salam) Hakika sisi
tumekuamini wewe, Tumekuamini wewe, na tumekubali kauukisemacho ni cha
kweli. Hivyo tumeahidi kua ni wenye kukusikiliza na kukutii. Hivyo Ya Rasul Allah
(Salallahu Alayhi wa Salam) Fanya unavyotaka kufanya kwani hata ukituambia
tuvuke Bahari Nyekudu basi Tutavuka.’’

Hivyo baada ya Nabii Musa kuambiwa na Mayahudi kua aende yeye pamoja na Mungu
wake akapigane na watu wa Mji huo, basi hapo hapo akarudisha majibu kwa Mola wake
kuhusiana na kuvunjika Moyo kwake juu ya watu wake kama zinavyothibitisha aya pale
ziliposema kua:

ِ ‫َﺧﻰ ﻓَﭑﻓْـﺮ ْق ﺑـﻴـﻨَـﻨَﺎ وﺑـﲔ ٱﻟْ َﻘﻮِم ٱﻟْ َﻔ‬


ِ ‫ﺎﺳ‬ ِ ‫ﻚ إِﻻﱠ ﻧَـ ْﻔ ِﺴﻰ وأ‬ ِ‫ب إِِﱏ ۤﻻ أَﻣﻠ‬
﴾‫ﲔ‬
َ ‫ﻘ‬ ْ َ ْ َ َ َْ ُ َ ُ ْ ّ ِّ ‫ﺎل َر‬ َ َ‫﴿ﻗ‬

Qala rabbi innee la amliku illa nafsee waakhee faofruq baynana wabayna alqawmi
alfasiqeena; (Surat Al Maidah 5:25)

Tafsir: Akasema(Musa): ‘Ewe Mola wangu sina Mamlaka isipokua juu ya Nafi yangu
na Kaka yangu, hivyo tutenganishe baina yetu na baina ya Watu wenye kufanya
Maasi.’

Allah Subhanah wa Ta’ala akamjibu Nabii Musa kwa kusema: ‘Ewe Musa hakika
mimi, nimewafadhili nilivyowafadhili kwa sababu yako wewe ua uko pamoja nao,
lakini kwa kua umeshachoka nao kutokana na ukaidi wao na hivyo kua ni mwenye
kuwalani na kuwaita kua ni watu wenye kufanya Maasi na unataka kutengana nao,
basi mimi nnaapa kwa Utukufu wangu, kua nitawaharamishia kuingia ndani ya
Ardhi takatifu isipokua kwa Mja wangu Joshua na Kalib.

Na hivyo nitawaongoza kwa kuwahangaisha watu wa Bani Israil walioasi katika


Jangwa Kwa muda wa miaka 40, kiasi ya kua vifo vyao vitawakumba ndani ya
Jangwa hili, isipokua Watoto wao ambao ndio hawakua ni wenye kuniasi ndio
watakaoingia kwenye Ardhi Takatifu.’
927

Haya yanawekwa wazi ndani ya Qur’an pale iliposema:

‫س َﻋﻠَﻰ ٱﻟْ َﻘ ْﻮِم‬ ِ ‫ﲔ َﺳﻨَﺔً ﻳَﺘِ ُﻴﻬﻮ َن ِﰱ ٱﻷ َْر‬


َ ْ‫ض ﻓَﻼَ َﺄﺗ‬
ِ
َ ‫ﺎل ﻓَِﺈﻧـﱠ َﻬﺎ ُﳏَﱠﺮَﻣﺔٌ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ أ َْرﺑَﻌ‬
َ َ‫﴿ﻗ‬
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ٱﻟْ َﻔﺎﺳﻘ‬
Qala fa-innaha muharramatun AAalayhim arbaAAeena sanatan yateehoona fee al-
ardhi fala ta/sa AAala alqawmi alfasiqeena (Surat Al Maidah 5:26)

Tafsir: Akasema (Allah Subhanah wa Ta’ala): ‘Kwa hivyo (Ardhi hio Takatifu)
imehramishwa kwao kwa miaka arubaini watahangaika kwenye Ardhi, hivyo
usiwahuzunikie watu waasi.’

Hivyo watu wa Bani Israil walihangaika kwenye Jangwa kwa Muda wa miaka 40, kila
wakienda wanakotaka kuenda basi wakiamka asubuhi hujikuta wako pale pale
walipoondoka jana, hali hii iliendelea mpaka wazee wote waliokubaliana juu ya kumuasi
Allah Subhaana wa Ta’ala na kukataa kupigana kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala
wakafariki wote na kubakia Joshua na Kalib tu na kizazi kipya cha watu wa Bani Israil,
na hawaa ndio ambao waliofanikiwa kuingia kwenye Ardhi Takatifu baada ya kupigana
kutokana na kuongozwa na Joshua na Kalib.

Ambapo katika kipindi hiki cha ndani ya Miaka 40 basi Allah Subhanah wa Ta’ala
kuwatenganisha Nabii Musa na Naabii Harun kwa kuwachukua na kuwaingiza katika
Mamlaka yake ya Mbinguni baada ya kuwaonjesha mauti.

MAUTI YA NABII HARUN NA NABII MUSA


Anasema Imam Ismail Abd Rahmn Al Suddi kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala
alimsushia Wahyi Nabii Musa kumwambia kua Umefika wakati wa kumchukua
Harun, hivyo nenda nae katika Mlima Murran.’ kipindi hii Nabii Harun alikua ana
umri wa miaka 120. Hivyo Nabii Musa na Nabii Harun wakatoka pamoja hadi kwenye
Mlima Murran, na walipofika hapo wakakuta mti ambao hawakuwahi kuuona hapo
kabla, kwani mti huo ulikua ni mzuri sana halafu chini yake ilikua kuna Nyumba ambayo
ndani yake mnatoka harufu nzuri sana inayotoka kwenye chumba kimoja chenye Kitanda
kilichotandikwa vizuri sana kiasi ya kua kilikua kinavutia na kunukia vizuri sana.
928

Hivyo Nabii Musa na Nabii Harun wakagonga na kutaka kuingia ndani yake lakini ikawa
hamna mtu ndani yake hivyo wakaingia ndani, na Nabii Harun alipokiona Kitanda hicho
basi akatamani kulala juu yake. Hivyo akamwambia Nabii Musa: ‘Ewe Ndugu yangu
hakika mimi natamani kulala juu ya Kitanda hiki lakini naogopa kua nitamkera
mwenye Nyumba hii.’ Nabii Musa akamwambia Nabii Harun: ‘Ewe Kaka yangu
hamna tatizo usiwe na khofu Lala tu kwani mimi nitazungumza na mmiliki wa
Nyumba hii na atatufaham’

Hivyo Nabii Harun akapanda juu yake Kitanda hicho na Kulala na hapo hapo
akachukuliwa Roho yake, kisha Nyumba hio, na Kitanda hicho na Mwili wa Nabii Harun
vikatoweka mbele ya macho ya Nabii Musa na kupaa angani badala yake.

Nabii Musa aliporudi kwa Watu wa Bani Israil huku akiwa peke yake basi watu hao
wakaanza kumshutumu Nabii Musa kua amemuua Kaka yake. Hivyo Nabii Musa
akawawekea wazi Watu hao kua, kwa hakika yeye hawezi kua ni mwenye kumuua Kaka
yake ambae anampenda kuliko anavyoipenda Nafsi yake na isha kuwaelezea yaliyotokea
badala yake. Lakini watu hao hawakumuamini Nabii Musa hivyo ikabidi Nabii Musa
aombe Dua kwa Allah Subhnah wa Ta’ala na dua hio ilijibiwa kwa Allah Subhanah waa
Ta’ala kukishusha chini Kitanda kilichomchukua Nabii Harun ili watu wa Bani Israil
waone yaliyotokea baada yake.

Na kuna wesemao kua Nabii Musa na Nabii Harun walitoka wakaenda kwenye pango
ambalo lipo kwenye Mlima wa Murran karibu na Mlima wa Sinai na walipofika ndani
yake basi Nabii Haruna akafariki ndani yake, hivyo Nabii Musa akamzika ndani ya pango
hilo na kisha akarudi kwa watu wa Bani Israil ambao nao walipomuona karudi peke yake
basi wakamshutumu kua amemmuua Kaka yake. Hivyo Nabii Musa akawaelezea
yaliyotoea lakini watu hao wakashindwa kumuamini Nabii Musa.

Hivyo Allah Subhnah wa Ta’ala akamshushia Wahyi Nabii Musa kua awapeleke watu
hao wa Bani Israil kwenye Kaburi la Nabii Harun kisha amuite Nabii Hraun athibitishe
ukweli halisi ulivyo, Nabii Musa akatoka nao watu hao hadi kwenye pango hilo na
alipofika kwenye eneo la kaburi la Nabii Harun basi Nabii Musa akaomba dua kua Nabii
Harun afufuke kwa Idhini yake Muumba, na Nabii Haruna alipofufuka basi Nabii Musa
akamuuliza kama jee ameuliwa au amekufa kifo cha kimaumbie? Nabii Harun akajibu:
‘La nimekufa kifo cha Kimaumbie.’

Ama kwa upande wa kifo Nabii Musa basi anasema Imam Ismail Abd Rahamn Al Suddi
kua: ‘Abu Malik, Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu, Abd Allah Ibn Masud
Radhi Allahu Anhu na wengineo wamesema kua ‘Wakati Nabii Musa alipokua
akitembea na Joshua Ibn Nun basi kikaja Kiwingu cheusi sana, hivyo Joshu
lipokiona Kiwingu hicho akadhani kua Kiama kimewadia hivyo akasema: ‘Enyi
watu wa Bani Israil nadhani kua Kiama kimewadia.’ Na kisha hapo hapo Nabii
929

Musa akatoweka huku Joshua akiwa ni mwenye kuona kutoweka kwake huko na
akajaribu kuwahi kumzuia Nabii Musa kwa kuikamata kanzu ya Nabii Musa na
hivyo akabakiwa na kanzu hio tupu mikononi mwake.’

‘Hivyo watu wa Bani Israil wakamuona Joshua akiwa na kanzu ya Nabii Musa
hivyo wakamkamata Joshua na kumwambia kua: ‘Joshua hakika wewe umemuua
Musa’ Joshua akasema: ‘Wallahi mimi sikumuua Nabii Musa isipokua
ameniponyoka’

Lakini watu wa Bani Israil wakataka kumuua Joshua, hivyo Joshua akawaambia
Watu wa Bani Israil, kua Nipeni siku tatu nitakuthibitishieni kilichotokea. Hivyo
Joshua akasali na kuomba Dua na kisha usiku huo akaja mtu ndani ya ndoto za
watu wa Bani Israil ambae akawaambia watu hao kua: ‘Joshua hakumuua Musa’
hivyo watu hao wakamuachia huru Joshua.’

Ambapo kwa Upande wa Imam Wahb Ibn Munabih basi yeye anasema kua: ‘Nabii Musa
alitoka kuenda kujitfutia mahitaji yake na njiani akakutana na kundi la Malaika,
nae akawajua kua ni Malaika na alipowakaribia akaona kua wanachimba Kaburi
ambalo lilikua zuri sana, na uzuri wake ulikua haujawahi kuoenakana. Hivyo Nabii
Musa akashangaa na kuwauliza Malaika hao: ‘Enyi Malaika wa Allah, hivi jee
Mnalichimba Kaburi hili kwa ajili ya nani? Mbona zuri sana?’

Malaika wakjibu: ‘Hili ni Kaburi la Mja mwema wa Allah Subhanah wa Ta’ala


ambae ni Mja alieridhiwa na Mola wake’ Nabii Musa akasema: ‘Ama kwa hakika,
mja huyu atakua na darja kubwa sana mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala, kwani
hata hio sehemu ya kulalia mwili wake mimi sijawahi kuiona uzuri wake.’ Malaika
hao wakasema: ‘Ya Kalimu Allah hivi jee wewe ungependa kua katika nafasi ya
Mtu huyo?’ Nabii Musa akasema: ‘Naam, bila ya shaka.’

Malaika wakasema: ‘Basi ingia na ulale ndani yake huku ukiwa ni mwenye
kumuelekea Mola wako na utahisi wepesi zaidi wa kuvuta na kutoa pumzi kifuani
mwako.’ Nabii Musa akaingia Kaburini humo akalala na kumuelekea Mola wake,
akavuta na uto pumzi ndni ya kifua chake na Mola wake akaichukua Roho yake,
kisha Malaika Wakamfukia’

Ambapo kw upande mwengine basi amesema Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu kua
amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Malaika wa mauti alitumwa
kuchukua Roho ya Nabii Musa, na alipofika, Nabii Musa akampiga kibao na
kumpofua jicho moja. hivyo Izrail akarudi kwa Allah Subhanah wa Ta’ala na
kumwambia: ‘Ya Allah! Umenituma kwa kwa mja wako ambae hataki Kufa.’
Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamrudishia jicho lake.’(Sahih Muslim)
930

Ambapo kuna bdhi wanweza wakajiuliza kuhusiana na hadithi hii, kua kwanini Nabii
Musa akampiga kibao Malaika Izrail, hivyo hapa inaonekana kua Allah Subhanah wa
Ta’ala alitaka kumjaribu Nabii Musa, kama vile ambavyo anavyowajaribu Waja wake
wema kwa kuwatumia Malaika katika maumbile ya Ibn Adam katika matukio
mbalimbali, ambapo baadhi ya wakati watu hao hua ni wenye kuwaona na kuwajua kua
kiumbe huyu ni Malaika na baadhi ya wakati hua hawawajui na hii hua inategemea na
namna anavyotaka mwenyewe Allah Subhanah wa Ta’ala kulingana na Hikma zake
katika tukio husika.

Hivyo katika tukio hili basi Nabii Musa hakua ni mwenye kujua kua mtu huyo alikua ni
Malaika, na hivyo alimpiga kibao kwa sababu ya namna alivyomvamia Nabii Musa,
yaani hii inakua kama vile ambayo tulivyoona katika kisa cha Nabii Ibrahim pale
alipowapokea wageni na kuwapikia na kisha akawawekea chakula, bila ya kujua kua ni
Malaika, hivyo kama ilivyokua kwa Nabii Ibrahim kua angejua kua watu hao walikua ni
Malaika basi asingewatayarishia chakula watu hao, basi na Nabii Musa kama angejua
kua Mtu huyo ni Malaika asingempiga kibao kiumbe huyo.

AMRISHO LA PILI LA BANII ISRAIL KUINGIA KWENYE ARDHI


TAKATIFU NA NAMNA WALIVYOBADILISHA AMRISHO.


Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea kuhusiana na kilichotokea baada ya kufariki
Nabii Harun na Nabii Musa baada ya kupita miaka 40 kuhusiana na amrisho la pili kupitia
kwa Joshua Ibn Nun kwa kusema:

‫ﺎب‬ ِ ُ ‫﴿وإِ ْذ ﻗُـ ْﻠﻨَﺎ ْٱدﺧﻠُﻮاْ ﻫـٰ ِﺬﻩِ ٱﻟْ َﻘﺮﻳﺔَ ﻓَ ُﻜﻠُﻮاْ ِﻣْﻨـﻬﺎ ﺣﻴ‬
َ َ‫ﺚ ﺷْﺌـﺘُ ْﻢ َرﻏَﺪاً َو ْٱد ُﺧﻠُﻮاْ ٱﻟْﺒ‬ َْ َ َْ َ ُ َ
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ﻳﺪ ٱﻟْ ُﻤ ْﺤﺴﻨ‬ ُ ‫ُﺳ ﱠﺠﺪاً َوﻗُﻮﻟُﻮاْ ِﺣﻄﱠﺔٌ ﻧـﱠ ْﻐ ِﻔْﺮ ﻟَ ُﻜ ْﻢ َﺧﻄَ َﺎ� ُﻛ ْﻢ َو َﺳﻨَ ِﺰ‬
Wa-idh qulna odkhuloo hadhihi alqaryata fakuloo minha haythu shi/tum raghadan
waodkhuloo albaba sujjadan waqooloo hittatun naghfir lakum khatayakum
wasanazeedu almuhsineena(Surat Al Baqara 2:58)

Tafsir: Na (kumbuka) tulipowaambia (Watu wa Bani Israil): ‘Ingieni Ndani ya Mji


huu na kisha kuleni ndani yake kila Mkitakacho kwa Uhuru na Raha na Starehe, na
931

ingieni katika Mlango wake Mkiwa mmeinama huku mkisema ‘Hittatun’’ Na nasi
tutakusameheni nyinyi madhambi yenu na tutakuzididshieni mema’.

Na kisha akasema tena Allah Subhanah wa Ta’ala katika Aya ifuatayo

ِ ِ‫﴿وإِ ْذ ﻗ‬
ْ‫ﺚ ِﺷْﺌـﺘُ ْﻢ َوﻗُﻮﻟُﻮاْ ِﺣﻄﱠﺔٌ َو ْٱد ُﺧﻠُﻮا‬ ُ ‫ٱﺳ ُﻜﻨُﻮاْ َﻫـٰﺬﻩِ ٱﻟْ َﻘْﺮﻳَﺔَ َوُﻛﻠُﻮاْ ِﻣْﻨـ َﻬﺎ َﺣْﻴ‬
ْ ‫ﻴﻞ َﳍُُﻢ‬
َ َ
ۤ
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ﻳﺪ ٱﻟْ ُﻤ ْﺤﺴﻨ‬ ُ ‫ﺎب ُﺳ ﱠﺠﺪاً ﻧـﱠ ْﻐ ِﻔْﺮ ﻟَ ُﻜ ْﻢ َﺧ ِﻄﻴـﺌَﺎﺗِ ُﻜ ْﻢ َﺳﻨَ ِﺰ‬َ َ‫ٱﻟْﺒ‬
Wa-idh qeela lahumu oskunoo hadhihi alqaryata wakuloo minha haythu shi/tum
waqooloo hittatun waodkhuloo albaba sujjadan naghfir lakum khatee-atikum
sanazeedu almuhsineena(Surat Al Araf 7:161)

Tafsir: Na (Kumbuka) Walipoambiwa: ‘Kaeni ndani ya Mji huu na kuleni ndani yake
kila mkitakacho na semeni ‘Hittatun’, na ingieni katika Mlango wake huku mkiinama,
nasi tutakusameheni dhambi zenu na kukuzidishieni mema.’

Tunapoziangalia Aya hizi basi tunaona kua zinamaamrisho yanayofanana sana kimaneno
na kimaana isipokua zinatofautiana katika maana ya matukio yaliyolezewa ndani yake
kwani:

Wakati aya ya 58 ya Surat Al Baqara inasema:

﴾َ‫﴿وإِ ْذ ﻗُـ ْﻠﻨَﺎ ْٱد ُﺧﻠُﻮاْ َﻫـٰ ِﺬﻩِ ٱﻟْ َﻘﺮﻳَﺔ‬


ْ َ
‘Wa-idh qulna odkhuloo hadhihi alqaryata’ yaani ‘Na (kumbuka) tulipowaambia
(Watu wa Bani Israil): ‘Ingieni Ndani ya Mji huu’ na hivyo kumanisha kua amrisho
hili lilikua kabla ya watu hawa kuingia ndani ya Mji husika.

Lakini aya ya 161 ya Surat Al Araf ikasema;

﴾َ‫ٱﺳ ُﻜﻨُﻮاْ َﻫـٰ ِﺬﻩِ ٱﻟْ َﻘﺮﻳَﺔ‬ ِ ِ﴿


ْ ْ ‫ﻴﻞ َﳍُُﻢ‬
َ ‫َوإ ْذ ﻗ‬
‘Wa-idh qeela lahumu oskunoo hadhihi alqaryata’ yaani ‘Na (Kumbuka)
Walipoambiwa: ‘Kaeni ndani ya Mji huu’. Na hivyo kumaanisha kua amrisho hili
lilikuja baada ya watu hawa Kuingia ndani ya Mji husika.
932

Kisha aya ya 58 ya Surat Al Baqara ikasema;

﴾ً‫ﺚ ِﺷْﺌـﺘُﻢ ر َﻏﺪا‬ ِ ﴿


َ ْ ُ ‫ﻓَ ُﻜﻠُﻮاْ ﻣْﻨـ َﻬﺎ َﺣْﻴ‬
Fakuloo minha haythu shi/tum raghadan yaani Kisha kuleni ndani yake kila
Mkitakacho kwa Uhuru na Raha na Starehe. Na aya kua ni yenye kutumia neno
Raghada Ambalo halikutumiwa na aya ya 161 ya Surat Al Araf. Ambapo neno Raghada
hua ni lenye kutokana na neno Raghida lenye kumaanisha kujaaliwa kua na Neema ya
Vitu vingi, Kula Vitu bila ya maudhi yaani kwa Uhuru Raha na Starehe na pia
humaanisha Kuishi kwa uhuru na raha.

Hivyo hili ni amrisho ambalo ndani yake lina ahadi yenye manufaa kwa watu hawa wa
Bani Israil kwani watakapotii amrisho hilo basi Allah Subhanah wa Ta’ala anawahidi
kua watakula kwa kadri wawezavyo na kwa kadri watakavyo na watakua na hali ya raha
kuridhisha ambayo tofauti na hali ya Jangwani waliyonayo kabla ya kuingia kwenye
Ardhi hio walioahidiwa.

Lakini aya ya 161 ya Surat Al Araf ikasema;

﴾‫ﺚ ِﺷْﺌـﺘُﻢ‬ ِ ﴿
ْ ُ ‫َوُﻛﻠُﻮاْ ﻣْﻨـ َﻬﺎ َﺣْﻴ‬
Wakuloo minha haythu shi/tum yaani Na kuleni ndani yake kila mkitakacho.

Hizi Aya pia ni aya ambazo zimetuma neno Hitattun ambalo limetokana na neno Hatta
ambalo ni lenye kumaanisha Kuweka Kitu chini, Kuachana na Kitu, Kushusha, Kutua,
Kusamehe, Kufuta Dhambi na pia humaanishaa Kuomba Dua ya Kutubu na Kufutiwa
Madhambi na vile vile hua linamaanisha Kusema Ukweli.

Hivyo aya ya 58 ya Surat Al Baqara imesema;

﴾ٌ‫ﺎب ُﺳ ﱠﺠﺪاً وﻗُﻮﻟُﻮاْ ِﺣﻄﱠﺔ‬


َ َ‫﴿ َو ْٱد ُﺧﻠُﻮاْ ٱﻟْﺒ‬
َ
Waodkhuloo albaba sujjadan waqooloo hittatun yaani Na ingieni katika Mlango wake
Mkiwa mmeinama huku mkisema ‘Hittatun’’

Lakini aya ya 161 ya Surat Al Araf ikasema;


933

﴾ً‫ﺎب ُﺳ ﱠﺠﺪا‬ ِ
َ َ‫﴿ َوﻗُﻮﻟُﻮاْ ﺣﻄﱠﺔٌ َو ْٱد ُﺧﻠُﻮاْ ٱﻟْﺒ‬
Waqooloo hittatun waodkhuloo albaba sujjadan yaani Na semeni ‘Hittatun’, na
ingieni katika Mlango wake huku mkiinama.

Hivyo basi Imam Abu Al Hussein Ahmed Ibn Faris Ibn Zakaria Al Qazwini Al Razi kua:
‘Neno Hitattun ambalo waliamrishwa waliseme ili wasamehewe Dhambi zao.’

Hivyo Wanazuoni wametofautiana kuhusiana na maana iliyotumika katika amrisho hili


waliloambiwa Watu wa Bani Israil walitekeleze, ambapo kwa upande wa Bahr ul Ilm
Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema kua: ‘Hii inamaanisha kua
Waliambiwa wasema kua: ‘Hakuna Mungu Isipokua Allah Subhanah wa Ta’ala.’’

Na kuna wasemao kua waliambiwa waseme Hitattun ambalo ni neno Lenye kumaanisha
Usamehevu, na kuna wasemao kua waliambiwa waseme hivyo na kisha watasamehewa
madhambi yao.

Lakini hata hivyo watu hawa wa Bani Israil walishindwa hata kufanya hivyo mbali ya
kua hawakua ni wale wale waliokua pamoja na Nabii Musa na Nabii Harun, bali walikua
ni watu wa kizazi kipya kilichotokea baada ya miaka 40 ya kuhangaika Jangwani
ambacho chenye kuongozwa na Joshua Ibn Nun na Calib na kua ni wenye kutii amri ya
kupigana na watu waliokata kupigana nao wazee wao hapo kabla na hivyo kizazi hicho
kufanikiwa kuingia katika Mji walioahidiwa mababa na mababu zao.

Kisha aya zikatumia neno Khatayakum na neno Khatiatikum ambayo ni yenye kutokana
na neno Khatia ambalo ni lenye kumaanisha Hatia, Kosa, Dhambi, Kufanya Makosa.
Ambapo neno Khatia ndio lililotoa neno Khitun ambalo humaanisha Kufanya Makosa au
Madhambi kwa Kukusudia na na pia neno hilo Khatia likatoa neno Khataya ambalo
wingi wake hua ni Khatiatun na hivyo hua linamaanisha Kufanya Makosa au Madhambi
kwa Kukusudia kutokana na Kua kua hili ni kosa na kufanya kwa Kutokusudia kutokana
na kutokuju kua hili ni kosa.

Kwa upande mwengine basi katika kufafanua mzizi wa neno Khatia basi Mujaddid Ad
Din, Sultan AlMutakallimin, Imam Al Mushaqiqin Shaykh Ul Islami, Imam Fakhr Ad Din
Al Razi akasema kua: ‘Kuna tofauti baina ya neno Mukhtiyy na neno Khattiy. Kwani
neno Mukhtiyy maana yake hua ni Mtu mwenye kufanya Dhambi bila ya kujua na
neno Khatiyy maana yake hua ni mwenye kufanya Dhambi kwa kujua na kwa
makusudi.’
934

Kutokana na maana hio basi maneno Khatayakum na neno Khatiatikum yote mawili ni
yenye kumanisha wingi wa neno Khatia, kwani mfumo wa Nahau wa lugha ya Kiarabu
hua ni wenye kuruhusu kutumia hali ya wingi wa kawaida na hali ya wingi ya mvunjo
wa maneno yaani Jamii Taksir ambao hua ni wenye kulivunja neno husika kutokana na
wingi wake wa kawaida na kupachika katikati yake neno hilo herufi ambayo hubadilisha
wingi wa neno kimaandiko na kimatamshi tu, bila ya kupoteza maana sahihi ya wingi wa
neno hilo.

Ambapo mara kadhaa mfumo huu hua ni wenye kuruhusu kupachika herufi uuna na iina
kwa neno lenye asili ya Kiume na hupachika herufi aatun na aatin pale inapokua neno ni
lenye asili ya Kike kama tulivyoona kwenye mfano wa matumizi ya maneno yaliyomo
katika aya tunazoziangalia yaani neno Khatayakum na neno Khatiatikum na hivyo bsi
kutuonesha kua neno Khatiatikum ni neno liliopo katika hali ya Jamii Taksir (Wingi
uliovunjwa kinahau)

Ili kufaham vizuri zaidi basi na tuangalie mfano mwengine ambao ni wenye kutokana na
neno Sunbulatun ambalo maana yake hua Shuke la Ngano ambalo neno hili wingi wake
wa kawaida hua ni Sunbulat na wingi wake wa mvunjo au wa Jamii Taksir basi hua ni
Sanabil.

Ambapo Mfumo huu wa wingi wa Jamii Taksir wa neno Sunbulatun umetumika katika
aya mbili tofauti za Surat Al Baqara 2:261 na aya ya Surat Yusuf 12:43 ambazo zinasema:

‫ﺖ َﺳْﺒ َﻊ َﺳﻨَﺎﺑِ َﻞ ِﰱ‬ ٍ ِ‫﴿ ﱠﻣﺜﻞ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻳـْﻨ ِﻔ ُﻘﻮ َن أَﻣﻮا َﳍﻢ ِﰱ ﺳﺒِ ِﻴﻞ ﱠ‬
ْ َ‫ٱﻪﻠﻟ َﻛ َﻤﺜَ ِﻞ َﺣﺒﱠﺔ أَﻧﺒَـﺘ‬ َ ُْ َ ْ ُ َ َُ
﴾‫ٱﻪﻠﻟ و ِاﺳ ٌﻊ َﻋﻠِﻴﻢ‬ ِ ‫ﺎﻋ‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻳ‬ ٍ ٍِ
َ ُ ُ‫ُﻛ ِّﻞ ُﺳﻨﺒُـﻠَﺔ ّﻣﺌَﺔُ َﺣﺒﱠﺔ َو ﱠ‬
ٌ َ ُ‫ﻒ ﻟ َﻤﻦ ﻳَ َﺸﺂءُ َو ﱠ‬ ُ ‫ﻀ‬
Mathalu alladheena yunfiqoona amwalahum fee sabeeli Allahi kamathali habbatin
anbatat sabAAa sanabila fee kulli sunbulatin mi-atu habbatin waAllahu
yudhaAAifu liman yashao waAllahu wasiAAun AAaleemun(Surat Al Baqara 2:261)

Tafsir:Mithili ya wale ambao ni wenye kutumia Mali zao kwa njia ya Allah hua ni sawa
na mfano wa Punje; Zinazoota na kutoa Sanabila Saba (Mashuke saba) na kila
Sunbulati (Mashuke) kua na Punje Mia. Na Allah humuongezea zaidi yule amtakae.
Na Allah ni Mwenye kuwatosheleza kwa kila Viumbe wake. Na ni mwenye kujua juu
ya kila kitu.

Ambapo katika aya hii basi Allah Subhnah wa Ta’ala anafananisha matumizi ya
Muumini kwa ajili yake kua ni sawa na Sanabila Saba na Malipo yake yeye Allah
935

Subhnah wa Ta’ala kwa juu ya Mja wake huyo kua ni sawa na Sunbulatin kwa sababu
ya kuweka wazi wingi wake na ukubwa wa malipo yake Allah Subhanah wa Ta’ala
kulingana na kile kingi alichokitoa Mja wake kulingana na Mtizamo wa Mja huyo.

Kama inavyoainisha hadithi ya Abu Masud Al Ansari Radhi Allahu Anhu ambae
amesema kua: ‘Kuna Mtu alikuja na Ngamia akiwa na hatamu yake na kisha
akasema: ‘Huyu ni kwa ajili ya Allah’’ Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam
akasema: ‘Kwa ajili yako, katika siku ya Malipo kutakua na Ngamia 700 ambao ni
wenye hatamu zao’(Sahih Muslim)

Ambapo Imam Ahmad Ibn Musa Al Marduwayh anasema kuhusiana na aya hii ya Surat
Al Baqara 2:261 kua: ‘Wakati aya hii iliposhushwa basi Rasul Allah Salallahu Alayhi
wa Salam alikua akiomba dua kwa kusema: ‘Uzidishie Ummah wangu ya Rabbi!’
hivyo ndio Allah Subhanah wa Ta’ala akaishusha aya hii. Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salam akasema tena: ‘Uzidishie Ummah wangu ya Rabbi!’ na hapo Allah
Subhanah wa Ta’ala akashusha aya isemayo’

ِِ ِِ ِ‫﴿ ِ ِ ﱠ‬
ُ ‫َﺣ َﺴﻨُﻮاْ ِﰱ َﻫـٰﺬﻩ ٱﻟ ﱡﺪﻧْـﻴَﺎ َﺣ َﺴﻨَﺔٌ َوأ َْر‬
‫ض‬ َ ‫ﻳﻦ َآﻣﻨُﻮاْ ٱﺗﱠـ ُﻘﻮاْ َرﺑﱠ ُﻜ ْﻢ ﻟﻠﱠﺬ‬
ْ ‫ﻳﻦ أ‬ َ ‫ﻗُ ْﻞ ٰﻳﻌﺒَﺎد ٱﻟﺬ‬
﴾‫ﺎب‬ ٍ ‫َﺟﺮُﻫﻢ ﺑِﻐَ ِْﲑ ِﺣﺴ‬ ‫أ‬ ‫ن‬ ‫و‬‫ﺮ‬ِ‫ﺼﺎﺑ‬ ‫ٱﻟ‬ ‫ﰱ‬‫ﱠ‬ ‫ﻮ‬ ‫ـ‬‫ﻳ‬ ‫ﺎ‬‫ﳕ‬ ‫ﱠ‬ ِ‫ٱﻪﻠﻟِ و ِاﺳ َﻌﺔٌ إ‬
َ ْ َ ْ َ ُ ‫ﱠ‬ َ ُ َ َ ‫ﱠ‬
Qul ya AAibadi alladheena amanoo ittaqoo rabbakum lilladheena ahsanoo fee
hadhihi alddunya hasanatun waardhuu Allahi wasiAAatun innama yuwaffa
alssabiroona ajrahum bighayri hisabin(Surah al-Zumar 39:10)

Tafsir: Sema (Ewe Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam): ‘Enyi waja wangu
mlioamini, Muogopeni Mola wenu na timizeni wajibu waenu juu yake. Kwani kwa
wale wafanyao Mema katika Dunia hii malipo yao ni Mema. Na Ardhi ya Allah ni
kubwa (hivyo kama hamuwezi kufanya Ibada katika sehemu moja basi nendeni katika
sehemu nyengine), kwani ni wale wenye subira tu ndio watakaopata malipo yao
kikamilifu bila ya hesabu’

Hivyo kwa wenye kujua maana ya maneno ya aya hizi na ujumbe wa Haditi hizo za Rasul
Allah Slallahu Alayhi wa Salam basi hua ni wenye kukimbilia kufanya mema kwa ajili
ya Allah Subhanah wa Ta’ala, kama alivyokua Abu Ubaydah Ibn Jarrah Radi Allahu
Anhu pale alipokua anaumwa, ambapo Waislam walipomtembelea kumtizama
anaendeleaje baada ya kumkuta akiwa amelala huku akiwa ameeleka ukutani, hivyo
wakamuuliza Mke wake aliekua amekaa kitako kitandani pembeni yake huku akiwa
amejitanda nguo zake kwa kusema: ‘Vipi amelalaje Usiku?’
936

Ambapo mke wake akajibu: ‘Amelala huku akijikusanyia Thawabu’’

Abu Ubaydah Ibn Jarrah Radi Allahu Anhu akasema: ‘La si kwa ajili ya kujikusanyia
Thawabu’ na kisha akageuka na kuwaangalia Masahaba wenzake na kuwaambia: ‘Hivi
Jee hamtaki nyinyi kujua kwanini mimi nikasema hivyo?’

Masahaba wakajibu: ‘Hakika sisi Jibu lako hatujalipenda kiasi ya kua hatuwezi
kukuuliza suali hilo.’

Abu Ubaydah Ibn Jarrah Radi Allahu Anhu akasema: ‘Kwa sababu mimi nimemsikia
Rasula Allah Salallahu A’layhi wa Salam akisema: ‘Yeyote yule atakaetumia kwa
ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala basi malipo yake hua ni mara 100, na yeyote yule
atakaetumia kwa ajili ya Nafsi yake, kwa ajili ya Familia yake, au atakaetembelea
Mgonjwa basi malipo yake hua ni mara 10 zaidi. Na Funga ni hua ngao pale
inapokua mtu husika hajaivunja ngao hio. Na yeyote yule atakaejaribiwa kwa
kasoro ya Kimwili basi atakua ni mwenye kufutiwa dhambi zake.’(Imam Ibn Kathir)

Tumalizie mfano wa Jamii Taksir wa neno Sunbulatun uliotumika katika aya ya pili
ambayo ni tofauti na aya ya Surat Al Baqara 2:261 tuliyoiangalia, ambapo hii ni ile aya
ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala ameiweka katika Surat Yusuf pale alipozungumzia
Ndoto aliyoota Mfalme wa Misri kwa kusema:

ٍ ‫ات ِﲰ‬
ٌ ‫ﺎن َ�ْ ُﻛﻠُ ُﻬ ﱠﻦ َﺳْﺒ ٌﻊ ﻋِ َﺠ‬ ٍ ۤ ِ َ َ‫﴿وﻗ‬
‫ﺎف َو َﺳْﺒ َﻊ‬ َ ‫ﻚ إِِّﱐ أ ََر ٰى َﺳْﺒ َﻊ ﺑَـ َﻘَﺮ‬
ُ ‫ﺎل ٱﻟْ َﻤﻠ‬ َ
�َ‫ى إِن ُﻛﻨﺘُ ْﻢ ﻟِﻠﱡﺮْؤ‬ ِ ِ ٍ ِ ‫ﻀ ٍﺮ وأ‬
َ �َ‫ُﺧَﺮ َ�ﺑ َﺴﺎت ٰ�َﻳـﱡ َﻬﺎ ٱﻟْ َﻤﻠَـﺄُ أَﻓْـﺘُﻮﱏ ﰱ ُرْؤ‬
ٍ
َ َ ْ ‫ُﺳْﻨـﺒُﻼَت ُﺧ‬
﴾‫ﺗَـ ْﻌﺒُـﺮو َن‬
ُ
Waqala almaliku innee ara sabAAa baqaratin simanin ya/kuluhunna sabAAun
AAijafun wasabAAa sunbulatin khudrin waokhara yabisatin ya ayyuha almalao
aftoonee fee ru/yaya in kuntum lilrru/ya taAAburoona (Surat Yusuf 12:43)

Tafsir: Na akasema Mfalme Hakika mimi nimeona Ng'ombe Saba Walionona


waliokua wakiliwa na (Ng'ombe) Saba Waliokonda na Saba Sunbulatin yaliyonawiri
(Ya Ngano) na Mengineo (Mashuke Saba) Ambayo ni Makavu. Enyi Machifu
nitafsirieni Ndoto hii kama ikiwa Nyinyi kuhusiana na Ndoto Mnatafsiri.
937

Ambapo katika aya hii tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala ametumia neno Sunbulati
na kuainisha wingi wa Mashuke kihesabu kua ni 7 kwa kusema wasabAAa sunbulatin,
wakati katika aya iliyotangulia ya Surat Al Baqara ametaja pia Mashuke 7 lakini kwa
kutumia maneno sabAAa sanabila, ambapo kama tulivyosema kua Sanabila hua ni wingi
wa Mvunjo wa Sunbulatun.

Hivyo badhi wanaweza wakajiuliza kwanini kote kote isitumie wingi wa Sanabila tu
ambao ni katika hali ya Jamii Taksir au wingi wa Sunbulatin? Ambayo ni katika hali ya
kawaida.

Jibu la suali hili linapatikana pale tunapoangalia na kuona kua mara nyingi Qur’an
imekua ni yenye kuonesha upekee wa matumizi ya Lugha yake katika sehemu tofauti na
hii ni kwa ajili ya kupendezesha aya katika usomaji na kurahisisha kufahamika na
kuhifadhika, na ndio maana tunapoiangalia aya ya 261 ya Surat Al Baqara katika sehemu
iliyozungumzia Mashuke 7 na Mashuke 100 basi ikasema: ‘kamathali habbatin
anbatat sabAAa sanabila fee kulli sunbulatin mi-atu habbatin’ yaani : ‘Hua ni sawa
na mfano wa Punje; Zinazoota na kutoa Sanabila Saba (Mashuke saba) na kila
Sunbulati (Mashuke) kua na Punje Mia.’

Hivyo kama ingekua imetajwa sabaa Sanabila kisha ikafuatia miaat Sanabila au kama
ingetajwa kwanza sabaa Sunbulatin na kisha ikafuatia tena Miaat Sunbulatin basi
ingekua haivutii kilugha, kimatamshi na kiusomaji n.k na ndio kama alivyosema Sultan
al Balagha Imam Abu Qasim Mahmud Ibn Umar Al Zamakhshari kua: ‘Kama ukihoji
jee ni kwa nini aya kwanza imetumia neno Sanah na kisha ikatumia neno Aám?
Basi jibu litakua ni kua kutumia neno moja katika kauli moja kunatakiwa
kuepukwe kutokana na manufaa ya ufasaha wa lugha, isipokua pale inapokua
kufanya hivyo hua ni kwa makusudi kwa ajili ya kutilia mkazo jambo
husika.’(Tafsir Al Kashshaf)

Lakini si hivyo tu kwani kwa upande mwengine basi aya imetumia maneno haya katika
hali hizi kama tulivyosema hapo kabla kua ni utokana na kua aya inamzungumzia Allah
Subhanah wa Ta’ala ambae ndie mlipaji na namna anavyolipa basi ikatumia hali hizi
mbili za wingi kwa ajili ya kuonesha namna Allah Subhanah wa Ta’ala anavyolipa wingi
wa wema wake kwa waja wake, kiasi ya kua wingi wake huo hua hauhesabiki wala
hauingii akilini mwa viumbe wake, na hii ni kutokana na Rehma zake Allah Subhanah
wa Ta’ala, ukarimu wake na utajiri wake ambao hauna mwisho.

Kama vile ilivyoelezewa kwenye ile hadith isemayo kua ‘Amesema Rasul Allah
Salallau Alayhi wa Salam kua: ‘Kila Jambo jema ambalo Ibn Adam analifanya basi
huzidishwa kuanzia mara 10 mpaka mara 700. Na Allah Amesema isipokua Funga
kwani inafanywa kwa ajili yangu hivyo nami nitailipa kwa malipo zaidi, kwani Mtu
938

hua ni mwenye kuachana na matamanio yake, kula na kunywa kwa ajili


yangu.’’(Bukhari na Muslim)

Hivyo tunaporudi na kuziangalia aya zetu mbili hizi zinazozungumzia amrisho la pili la
kuingia kwenye Mji Mtakatifu walilopewa watu wa Bani Israil ambazo zinasema;

‫ﺎب‬ ِ ُ ‫﴿وإِ ْذ ﻗُـ ْﻠﻨَﺎ ْٱدﺧﻠُﻮاْ ﻫـٰ ِﺬﻩِ ٱﻟْ َﻘﺮﻳﺔَ ﻓَ ُﻜﻠُﻮاْ ِﻣْﻨـﻬﺎ ﺣﻴ‬
َ َ‫ﺚ ﺷْﺌـﺘُ ْﻢ َرﻏَﺪاً َو ْٱد ُﺧﻠُﻮاْ ٱﻟْﺒ‬ َْ َ َْ َ ُ َ
﴾‫ﲔ‬ ِِ
َ ‫ﻳﺪ ٱﻟْ ُﻤ ْﺤﺴﻨ‬ ُ ‫ُﺳ ﱠﺠﺪاً َوﻗُﻮﻟُﻮاْ ِﺣﻄﱠﺔٌ ﻧـﱠ ْﻐ ِﻔْﺮ ﻟَ ُﻜ ْﻢ َﺧﻄَ َﺎ� ُﻛ ْﻢ َو َﺳﻨَ ِﺰ‬
Wa-idh qulna odkhuloo hadhihi alqaryata fakuloo minha haythu shi/tum raghadan
waodkhuloo albaba sujjadan waqooloo hittatun naghfir lakum khatayakum
wasanazeedu almuhsineena(Surat Al Baqara 2:58)

Tafsir: Na (kumbuka) tulipowaambia (Watu wa Bani Israil): ‘Ingieni Ndani ya Mji


huu na kisha kuleni ndani yake kila Mkitakacho kwa Uhuru na Raha na Starehe, na
ingieni katika Mlango wake Mkiwa mmeinama huku mkisema ‘Hittatun’’ Na nasi
tutakusameheni nyinyi madhambi yenu na tutakuzididshieni mema’.

Na ile aya isemayo:

ِ ِ ِ﴿
ْ‫ﺚ ِﺷْﺌـﺘُ ْﻢ َوﻗُﻮﻟُﻮاْ ِﺣﻄﱠﺔٌ َو ْٱد ُﺧﻠُﻮا‬ ُ ‫ٱﺳ ُﻜﻨُﻮاْ َﻫـٰﺬﻩِ ٱﻟْ َﻘْﺮﻳَﺔَ َوُﻛﻠُﻮاْ ِﻣْﻨـ َﻬﺎ َﺣْﻴ‬
ْ ‫ﻴﻞ َﳍُُﻢ‬
َ ‫َوإ ْذ ﻗ‬
﴾‫ﲔ‬ ِ‫ﻳﺪ ٱﻟْﻤﺤ ِﺴﻨ‬ ُ ِ
‫ﺰ‬ ‫ﻨ‬
َ ‫ﺳ‬ ‫ﻢ‬ ‫ﻜ‬
ُ ِ‫ٱﻟْﺒﺎب ﺳ ﱠﺠﺪاً ﻧـﱠ ْﻐ ِﻔﺮ ﻟَ ُﻜﻢ ﺧ ِﻄ ۤﻴـﺌَﺎﺗ‬
َ ُْ َ ْ َ ْ ْ ُ َ َ
Wa-idh qeela lahumu oskunoo hadhihi alqaryata wakuloo minha haythu shi/tum
waqooloo hittatun waodkhuloo albaba sujjadan naghfir lakum khatee-atikum
sanazeedu almuhsineena(Surat Al Araf 7:161)

Tafsir: Na (Kumbuka) Walipoambiwa: ‘Kaeni ndani ya Mji huu na kuleni ndani yake
kila mkitakacho na semeni ‘Hittatun’, na ingieni katika Mlango wake huku mkiinama,
nasi tutakusameheni dhambi zenu na kukuzidishieni mema.’

Basi tunaona kua kutokana na kua aya Mutashabihat yaani Zimeshabihiana au


Zimefanana lakini zinautofauti wa matukio yake, ambapo moja inaonesha kua amrisho
lilishuka kabla ya kuingia ndani ya Mji na nyengine inaonesha kua amrisho lilishuka
939

baada ya kuingia ndani ya mji huo, na hivyo Wanazuoni wametofautiana juu ya wakati
yaliposhuka maamrisho hayo, kwani kuna wasemao kua amrisho la kwanza la aya ya 58
ya Surat Al Baqara la kuingia ndani ya Mji Mtakatifu lilishuka pamoja na lile amrisho la
kuingia katika Mji huo wakati Nabii Musa na Nabii Harun wakiwa hai na hivyo Amrisho
la pili la Surat Al Aaraf 7:161 lilishuka miaka 40 baada ya Kufariki Nabii Musa na Nabii
Harun, hivyo basi amrisho hili lilishuka kama Wahya kupitia kwa Joshua Ibn Nun ambae
nae alikua Nabii mrithi wa Nabii Musa baada ya kufariki Nabii Musa.

Ambapo kwa upande mwengine basi kuna Wanazuoni wanaosema kua maamrisho haya
yote mawili yalishuka kupitia kwa Joshua yaani miaka 40 baada ya kufariki Nabii Musa
na Nabii Harun.

Hivyo basi kwa upande wetu sisi mimi na wewe hatutakiwi kua ni wenye kuchanganywa
au kujichanganya juu ya mitizamo hii inayotofautiana juu ya suali hili kwani suali hili
halina umuhimu wowote, hivyo hata kama tukijua basi halitotunufaisha na kitu chochote,
na hii ni kwa sababu Allah Subhanah wa Ta’ala anapohadithia hadithi ndani ya Qur’an
basi hua hatuhadithii kwa sababu ya kutufurahisha au kufanya mzaha, bali hua anafanya
hivyo kwa ajili ya kutupa mafunzo yaliyomo ndani yake kua kama ikiwa Ibn Adam
watatii amri zake basi watanufaika na manufaa mengi sana ndani yake ikiwemo kwa
upande wa maslahi yao kimwili, kinafsi na kiroho na pia kusamehewa madhambi yao.

Kwani makusudio ya maamrisho ya Allah Subhanah wa Ta’ala juu ya viumbe hua ni


kwa ajili ya kusimamia Maslahi ya viumbe wake. Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Az
Zukhruf Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al
Ghazali kua, ‘Maslahi ya Bani Adam hua yanatakiwa yaende sambamba na
Maqasid ash Sharia’h, kwa sababu msingi mkuu wa kuwekwa kwa Sharia’h na
Allah Subhanahu wa Ta’ala ni kuyalinda maslahi ya Bani Adam dhidi ya madhara’.

Neno Maqasid ambalo liko katika hali ya wingi wa neno Maqsid, ambalo maana yake
hua ni Makusudio, Malengo au Matumizi ya kitu. Lakini tunapolizungumzia katika
mtizamo kwa Sharia’h basi neno hili hutoa maana ya ‘Manufaa au Maslahi’.

Imam Abu Ishaq al Shatibi, anasema kua ‘Maqasid hua ni sehemu ya ‘Ilm al Yaqin,
ambayo hua ni moja kati ya vyanzo vitatu ya I’lm (ambapo vyanzo vyenginezo ni
pamoja na Haqq al Yaqin, ambayo hua ni I’lm ya uhakika inayotokana na kitabu
kitukufu na ‘Ain al Yaqin, ambayo hua ni I’lm ambayo hutokana na kuona kwa
macho vithibitisho vya ulimwengu unaoonekana. Hivyo tunaweza pia kuihesabu
Maqasid al Sharia’h kua ni moyo wa sehemu ya I’lm inayojulikana kua ni ‘Ilm al
‘Adl (I’lm ya Uadilifu).’

Tukiiangalia Ilm al ‘Adl au I’lm ya Uadilifu kwa ndani kidogo tunaona kua nayo vile
vile hujumuisha majukumu ya Bani Adam kiroho na kijamii. Kwa upande wa kiroho hua
940

inajumuisha haki nne zifuatazo:-

1) Haqq al Din, Haki ya kua huru na katika kubeba jukumu la kumuabudu Allah
Subhanahu wa Ta’ala na kuutafuta ukweli na uadilifu.

2) Haqq al Nafs, Haki ya kuyaheshimu na kuyahifadhi maisha ya Bani Adam ambayo


vile vile hua inajulikana kama haqq al haya.

3) Haqq al Mahid, (kutokana na neno wahada au umoja), Jukumu la kuheshimu


mshikamano wa Tawhid (umoja) ya viumbe vyote na kuhifadhi mazingira
yanaowazunguka viumbe hao.

4) Haqq al Nasl, Jukumu la kuheshimu kizazi cha watu kutokana na utukufu wa kila
kiumbe kilichomo ndani yake kwa pamoja.

Na vile vile hua inajumuisha haki nne zifuatazo kwa upande wa kijamii:

1) Haqq al Mal, Haki ya kuheshimu mali ya mtu binafsi, kuheshimu jumuiya


zinazohusiana na mambo ya mali, mikopo na kodi kwa ajili ya manufaa ya jamii katika
kumuwezesha Bani Adam kua na uwezo wa kujikomboa kutoka katika kutumwa na
umasikini.

2) Haqq al Hurriyah, Kuheshimu uhuru wa kiuamuzi wa watu na jamii kwa ujumla


kuhusiana na uhalali wa mambo ya uongozi miongoni mwa jamii husika.

3) Haqq al ‘Ilm, Kuheshimu jukumu la uhuru wa kutafuta I’lm na pia uhuru wa


kimawazo kupitia katika njia mbali mbali.

4) Haqq al Karama, Kuheshimu heshima ya utu katika jamii, kama vile kutovunja haki
za wanawake, watoto, wazee, wafanyakazi n.k.

Hivyo Maqasid ash Sharia’h (Makusudio ya Sharia’h) hua ni makusudio, malengo,


matumizi au manufaa ambayo Sharia’h inayatarajia kwa ajili ya kuilinda na kuihifadhi
jamii ya Kiislam, ambapo manufaa hayo yaliyokuwemo ndani ya Sharia’h ya Kiislam
yamegawika katika sehemu tatu:-

Al Maslaha Mu'tabarah: Manufaa ya Mambo yaliyoidhinishwa: Haya hua ni manufaa


yote ya yale yanayopatikana katika mambo ambayo tayari yameidhinishwa na
kudhibitiwa na Allah Subhanahu wa Ta’ala katika hali ya kua mamlaka yake yanaweza
kuthibitishwa kutoka katika Sharia’h za Allah Subhanah wa Ta’ala kutokana na
maandiko.
941

Al Maslaha Mulghaah: Manufaa ya Mambo yaliyobatilishwa au kutenguliwa: Haya


hua ni manufaa yote ya yale yanayopatikana katika mambo ambayo Sharia’h
imeyabatilisha au kuyatengua kwa sababu hua hayatoi matokeo mazuri baadae na hivyo
kupelekea katika madhara, mfano wa mambo hayo ni kama vile Riba, Kamari, Wizi,
Ufisadi n.k.

Al Maslah al Maskut’anha: Manufaa ya Mambo ambayo hayajaidhinishwa: Haya


hua ni manufaa yote ya yale yanayopatikana kutoka katika mambo ambayo
hayajaidhinishwa na Allah Subhanah wa Ta’ala, kwa sababu ya kua manufaa ya watu na
jamii yanawezekana ni mengi sana hivyo Sharia’h haikuidhinisha baadhi ya manufaa
hayo na hivyo hua hakuna ushahidi wa kimaandiko kuhusiana na mambo hayo. Kutokana
na kanuni za Fiqh manufaa ya mambo kama haya hua yanajulikana kua ni miongoni mwa
manufaa ya mambo ambayo hayakuidhinishwa na hivyo hua ni jukumu la Wanazuoni au
wanafiqh kuyafanyia kazi ili kupata na kisha kutoa idhinisho lake. Manufaa haya pia hua
yanajulikana kama Al Maslaha Al Mursalah au Al Munasib Al Mursal.

Wanazuoni wanaoongoza katika utaalamu wa I’lm ya Maqasid ambao ni pamoja na


Imam Abu Hamid Ibn Muhammad Al Ghazal, Imam Fakhr Din Ar Razi, Imam Ash
Shatibi, Imam Ibn Ashur, Imam Abu Zahra, A’lamah ‘Abd Al Rahman Ibn Khaldun,
Shah Waliyu Allah, n.k, wanasema kua Maqāsid ash Sharia’h na Hukmu ul Taklif
(hukmu za Taklifi) hua ni kwa ajili ya kusimamia Maslahi ya Jamii, kama
inavyothibitishwa na ushahidi uliomo ndani ya Qur’an na Sunna za Nabii Muhammad
Salallahu A’layhi wa Salam.

Kwani Allah Subhanahu wa Ta’ala anasema katika Qur’an:

ِ ِ
َ ‫ـﻚ إِﻻﱠ َر ْﲪَﺔً ﻟّْﻠ َﻌـﻠَﻤ‬
﴾‫ﲔ‬ َ َ‫﴿وَﻣﺂ أ َْر َﺳ ْﻠﻨ‬
َ
Wama arsalnaka illa rahmatan lilAAalameena (Surat Al Anbiyah 21:107)

Tafsir: Hatukukutuma wewe (Muhammad) isipokua ni kua Rehma kwa A’lamin.

Ambapo neno Rahmatan linamaanisha Rehma, Neema, Manufaa, Maslahi n.k na neno
A’lamin linamanisha viumbe vyote vilivyomo Ulimwenguni wakiwemo Bani Adam,
hapa tunaona kua Qur’an imeweka wazi kua Rehma ndio kusudio muhimu zaid katika
Utume wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, na hivyo Rehma ndio kusudio
pekee la Sharia’h, ambayo imeshushwa kwa ajili ya Maslahi ya Bani Adam.
942

Tukiangalia mfano mmoja wa Hadith inayotoka kwa Amr Ibn Yahya Al-Mazini ambae
amemsikia baba yake akisema kua amesema Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa
Salam kua: ‘Hakuna kujidhuru wala kudhuru’, Hadith hii inafahamika sana na
kutumika sana katika kusimamisha moja kati ya hukmu za Sharia’h za Kiislam, ambayo
ni miongoni mwa misingi wa Maslahi ya Maqasid al Sharia’h.

Mujaddid Ad Din Az Zukhruf Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn
Muhammad Al Ghazali anayaelezea maslahi ya Maqasid al Sharia’h katika Al Mustasfa
min usul ul Fiqh, kwa kusema kua Maslahi ya Maqasid al Sharia’h yamegawika katika
darja tatu ambazo ni:

1. Al Maslah Al Dharuriyat - Maslahi ya Dharura au ya Lazima.


2. Al Maslah Al Hajiyaat - Maslahi ya Ziada.
3. Al Maslah Al Tahsiniyaat - Maslahi ya Kupendezesha.

Mujaddid Ad Din Az Zukhruf Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn
Muhammad Al Ghazali anaendelea kwa kusema kua, ‘Maslahi ya Lazima ni yale
ambayo yanapokosekana basi hutokea machafuko katika jamii, Maslahi ya Ziada
ni yale ambayo yanasaidia kurahisisha maisha ya Bani Adam na Maslahi ya
Kupendezesha ni yale yanayohusiana na Maadili, Tabia, Makazi, Mavazi ya Bani
Adam, n.k.’

Maslahi hayo matatu yanawakilisha muongozo unaoonesha maendeleo ya jamii


kulingana na mtizamo wa Maqasid Ash Shariyyah. Darja ya kwanza ambayo ni
Dharuriyat hua ni darja ya Lazima inayowakilisha kiwango cha chini kabisa cha
maendeleo ambacho kila mtu, kila jumuyia na kila jamii inatakiwa ikifikie na kua nacho.
Darja hii inajumuisha Al Dharuriyat al Khams (Maslahi matano muhimu) Ulimwenguni.
Darja ya pili (Hajiyaat) inatoa muelekeo wa uendelezaji wa maslahi matano hayo na
darja ya tatu (Tahsiniyaat) inawakilisha mapendekezo ya kuboreaha na kudumisha
maslahi matano hayo yaliyo muhimu.

1. Al Dharuriyat al Khams - Maslahi Matano ya Lazima: Darja hii inajumuisha yale


mambo ambayo yanategemewa katika maisha ya Duniani na Akhera. Na hivyo kuachana
na mambo hayo hua kunapelekea ugumu usio stahamilika katika maisha ya Dunia au
adhabu katika maisha ya Akhera. Maslahi hayo ni Al-Din (Dini), Al-Nafs (Nafsi au Uhai),
Al Aql (Akili au Ufahamu), Al Nasl (Kizazi) na Al Maal (Mali), na hivyo kila
kinachopingana au kukosesha maslahi hayo hua kinajulikana kama Mufsada (Kifanyacho
Ufisadi).

Kwani msingi wa kuwepo kwa maslahi haya hua si kwa ajili ya kulinda maslahi hayo na
kuzuia madhara tu bali pia hua ni kuenda sambamba na Maqasid Ash Sharia’h. Kwani
Maqasid Ash Sharia’h humsaidia Bani Adam katika kumhakikishia hifadhi, usimamizi
943

wa haki ya maslahi yake ya Al Dharuriyat al Khams kibinafsi na kijamii katika maisha


ya Duniani na Akhera. Umuhimu wa maslahi yaliyomo ndani ya darja ya Al Dharurriyah
Al Khams hufafanulika zaidi kama ifuatavyo:-

a) Hifdh al Din – Umuhimu wa kuihifadhi Dini: Kuhakikisha kusimamishwa kwa


Dini, kwani Allah Subhanahu wa Ta’ala ameifanya Imani na Ibada kua ni jambo la
wajib. Kuhakikisha kuhifadhiwa na kuendelezwa kwa Dini kupitia njia mbali mbali
za ikiwemo Aqidah, kiroho, kimwili, Akhlaq (kitabia na kimaadili), kufanya Ibada na
kutekeleza maamrisho yake kuanzia kwa mtu mmoja mmoja, kwa jamii na Ummah
kwa ujumla.

b) Hifdh al Nafs - Umuhimu wa kuyahifadhi Maisha: Kuhakikisha ulinzi wa maisha


ya Bani Adam, kwa sababu Allah Subhanahu wa Ta’ala, amehalalilisha ndoa, kula
vyakula vyenye afya na kuishi maisha yenye afya na amekataza kuyaondoa maisha
hayo, kuyadhuru au kuyahatarisha maisha hayo kutokana na Bani Adam au viumbe
wengine wa hatari na kuweka adhabu za wale watakaofanya hivyo.

c) Hifdh al Aql - Umuhimu wa kuuhifadhi Ufahamu: kwa sababu Allah Subhanahu


wa Ta’ala amesisitiza kuendeleza ufahamu wenye akili, na akakataza yale mambo
ambayo yanadhoofisha ufahamu wa akili kama vile ulevi, madawa ya kulevya,
uchawi n.k. Na hivyo akaweka adhabu dhidi ya yale aliyoyakataza ili Bani Adam
wajitenge nayo, kwa sababu ufahamu ni msingi wa majukumu ya kiakili ambayo
amepewa Bani Adam.

d) Hifdh al Nasl - Umuhimu wa kukihifadhi Kizazi: Ndoa imehalalishwa kwa ajili


ya kuihifadhi familia (kimwili, kiroho na kihisia), kuifurahisha Nafsi na kuzuia
uasharati na kuchanganya kizazi ambako hupelekea kutojua nani mtoto wa nani na
nani ni baba wa nani. Hukmu na adhabu zimewekwa ili kuhakikisha kua kizazi
kinaendelezwa kisharia ili kuendeleza maisha ya Bani Adam.

e) Hifdh al Maal - Umuhimu wa kuihifadhi Mali: Kwa sababu Allah Subhanahu wa


Ta’ala ameweka wazi kua wajib kwa kila Bani Adam kuihudumia Nafsi yake
mwenyewe na vile vile kuwahudumia wale walio chini yake kwa kutumia mali, na
pia akaweka hukmu za kuuza na kununua baina ya Bani Adam, kuzilinda mali kupitia
katika njia za kiuchumi na kufundisha usimamizi na uongozi mzuri ili kuhakikisha
uadilifu katika kubadilishana na kuzuia dhulma, ufisadi na migogoro.

2. Hajiyaat (Maslahi ya Ziada): Darja hii inajumuisha yale maslahi ambayo huhesabiwa
kua ni ya ziada ambayo ikiwa yatadharauliwa basi yatasababisha ugumu wa maisha ya
mtu mmoja biNafsi au jamii kwa ujumla lakini bila ya kukatisha au kubadilisha
muonekano wa maisha ya kawaida. Maslahi ya Ziada hua yanahitajika ili kuendesha
maisha ya kawaida yanayoongozwa na Sharia’h.
944

Na vile vile inaimarisha na kutoa muelekeo wa uendelezaji wa maslahi matano muhimu


au Al Dharurriyah Al Khams. Mfano wa mifano ya maslahi yaliyokuwemo ndani ya darja
hii ni kupata urahisi katika kufanya Ibada za Sala na Funga katika nyakati za safari na
maradhi, kutoa da’wa na kupata I’lm ili kuulinda ufahamu, vile vile uhifadhi wa
mazingira tunayoishi pia huingia katika darja hii kwani hua ni kuzuia madhara kwa vizazi
vyetu na pia vizazi vijavyo, n.k.

3. Tahsiniyaat (Maslahi ya Kupendezesha). Darja hii inajumuisha uboreshaji na


upendezeshaji wa maslahi matano muhimu au Al Dharurriyah Al Khams, kitabia,
kimaadili na kimahitaji katika njia za kupendezesha kimavazi, kimakazi, kupendezesha
maisha kibinafsi na kijamii, kwani haya ni mambo ambayo Uislam unayaunga mkono
lakini kwa kusisitiza kua ni mahitaji ya mwisho katika maisha.

Hivyo basi amrisho walilopewa watu wa Bani Israil na Allah Subhana wa Ta’ala lilikua
ni amrisho lenye kusimamia Maslahi yao kwa ujumla, ambapo amesema Abu Hurayrah
Radhi Allahu Anhu kua ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:
‘Waliambiwa watu wa Bani Israil ingieni katika Mji huu huku mkisema Hitta
(Tuondolee mzigo wa Madhambi yetu) ambapo tutakusameheni madhambi yenu.
Lakini nao wakageuza maneno na wakaingia kwenye mij huku wakiwa
wanajiburura matako yao huku wakisema: ‘Hintatun Shairatun’’(Sahih Muslim)

Lakini hata hivyo watu hao wa Bani Israil badala yake, watu hao wa Bani Israil wakawa
ni wenye kuendelea kufanya mzaha na wakabadilisha maneno waliyoambiwa hivyo
baada ya kusema Hitta – ‘Tusamehe Madhambi yetu’ basi wakasema Hintatun
Shairatun maneno ambayo maana yake hua ni ‘Punje ya Ngano kwenye sikio’

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala analieleza tukio hili kwa kusema:

‫ﻴﻞ َﳍُْﻢ ﻓَﺄ َْر َﺳ ْﻠﻨَﺎ َﻋﻠَْﻴ ِﻬ ْﻢ ِر ْﺟﺰاً ِّﻣ َﻦ‬ ِ ِ‫ﱠ‬ ِ ِ ‫﴿ﻓَـﺒﺪ َ ﱠ‬
َ ‫ﻳﻦ ﻇَﻠَ ُﻤﻮاْ ﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ ﻗَـ ْﻮﻻً َﻏْﻴـَﺮ ٱﻟﺬى ﻗ‬
َ ‫ﱠل ٱﻟﺬ‬ َ
ِ ‫ٱﻟ ﱠﺴﻤ‬
﴾‫ﺂء ِﲟَﺎ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳَﻈْﻠِﻤﻮ‬
ُ َ
Fabaddala alladheena dhalamoo minhum qawlan ghayra alladhee qeela lahum
faarsalna AAalayhim rijzan mina alssama-i bima kanoo yadhlimoona (Surat Al Araf
7:162)

Tafsir: Lakini wakabadilisha wale ambao waliofanya maovu miongoni mwao, kauli
tofauti na waliyoambiwa, hivyo tukawatumia Adhabu kutoka Mbinguni kutokana na
yale maovu waliyokua wakiyafanya.
945

Na akalizungumzia tena hili katika Surat Al Araf pale aliposema:

ً‫ﻳﻦ ﻇَﻠَ ُﻤﻮاْ ِر ْﺟﺰا‬ ِ‫ﱠ‬ ِ‫ﱠل ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻇَﻠَﻤﻮاْ ﻗَـﻮﻻً َﻏﻴـﺮ ٱﻟﱠ ِﺬى ﻗ‬ ﴿
َ ‫ﻴﻞ َﳍُْﻢ ﻓَﺄ‬
َ ‫َﻧﺰﻟْﻨَﺎ َﻋﻠَﻰ ٱﻟﺬ‬ َ َ ْ ْ ُ َ َ ‫ﻓَـﺒَﺪ‬
ِ ‫ِﻣﻦ ٱﻟ ﱠﺴﻤ‬
﴾‫ﺂء ِﲟَﺎ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳَـ ْﻔﺴ ُﻘﻮ َن‬
ُ َ َّ
Fabaddala alladheena dhalamoo qawlan ghayra alladhee qeela lahum faanzalna
AAala alladheena dhalamoo rijzan mina alssama-i bima kanoo yafsuqoona (Surat
Al Baqara 2:59)

Tafsir: Lakini wakabadilisha wale waliofanya maovu kauli tofauti na waliyoambiwa,


hivyo tukawashushia walifanya makosa, Rijzan (Adhabu) kutoka Mbinguni kutokana
na Uasi wao.

Aya yetu imetumia neno Rijzan ambalo limetokana na neno Rujz ambao maana yake hua
ni Kunguruma, Kuchafua. Kuangamiza, Kufanya Uovu, Kuadhibu, Maradhi ya
Maambukizo, Jambo ambalo linastahiki Adhabu.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akawashushia Rijzan watu hawa ambayo ilikua ni
adhabu ya Maradhi ya maambukizo yaliyoua watu 70000 miongoni mwao watu wa Bani
Israil na kuna baadhi wanasema kua walifariki watu 120000.

Kwani hua hairuhusiki kubadilisha maneno ya Allah Subhanah wa Ta’ala, na pia hua
haikubaliki kubadilisha maneno ya Mitume, Na ndio maana tunapoangalia kwa upande
wa Uislam basi hua tunaona si kua tu haikubaliki kubadilisha maneno ya Qura’an,
maneno ya Hadith za Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam lakini pia kamwe
hairuhusiki kubadilisha maana ya ujumbe wa Aya za Qur’an au Hadithi au maamrisho
ya Allah Subhanah wa Ta’ala au maamrisho ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Ambapo tunapozungumzia maneno ya aya za Qur’an ambayo ni Matukufu sana kutokana


na kua ni yenye kutoka kwa mwenyewe Muumba wa kila kitu yaani Allah Subhanah wa
Ta’ala ambae anathibitisha Utukufu na ubora wa Qur’an yake hio kwa kusema:

‫ﺼ ُﺪوِر َوُﻫ ًﺪى‬‫ﱠﺎس ﻗَ ْﺪ َﺟﺂءَﺗْ ُﻜ ْﻢ ﱠﻣ ْﻮ ِﻋﻈَﺔٌ ِّﻣﻦ ﱠرﺑِّ ُﻜ ْﻢ َو ِﺷ َﻔﺂءٌ ﻟِّ َﻤﺎ ِﰱ ٱﻟ ﱡ‬
ُ ‫ٰ�َﻳـﱡ َﻬﺎ ٱﻟﻨ‬
﴿
﴾‫ﻚ ﻓَـ ْﻠﻴَـ ْﻔﺮ ُﺣﻮاْ ُﻫﻮ َﺧْﻴـﺮ ِّﳑﱠﺎ َْﳚﻤﻌُﻮ َن‬
َ
ِ‫ٱﻪﻠﻟِ وﺑِﺮ ْﲪﺘِ ِﻪ ﻓَﺒِ ٰﺬﻟ‬
‫ﱠ‬ ِ
‫ﻞ‬ ‫ﻀ‬
ْ ‫ﻔ‬َ ِ‫ﲔ۞ﻗُﻞ ﺑ‬ ِ‫ور ْﲪﺔٌ ﻟِّْﻠﻤ ْﺆِﻣﻨ‬
َ ٌ َ َ َ ََ ْ َ ُ َ ََ
946

Ya ayyuha alnnasu qad jaatkum mawAAithatun min rabbikum washifaon lima fee
alssudoori wahudan warahmatun lilmu/mineena; Qul bifadli Allahi wabirahmatihi
fabidhalika falyafrahoo huwa khayrun mimma yajmaAAoona (Surat Yunus 10:57-
58)

Tafsir: ‘Enyi Watu kwa hakika yamekuja kwenu Mawaidh kutokaa kwa Mola
wenu, na Ponyo kwa yale yiomo ndani ya Vifua yenu. Na Muongozo na Rehma kwa
Watakaomini. Hivyo sema: Kwa Fadila za Allah na Rehma zake, kutokana nazo
Wafurahie, kwani hizo ni bora kuliko (Mali) wanazojikusanyia.’

Na anavyothibitisha Nabii wake Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam kama


alivyosema Abu Dhar Al Ghifari Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah
Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Hakuna kitu kinachosaidia kupata ukaribu kwa
Allah kama kile ambacho kimetoka moja kwa moja kutoka kwake yaani
Qur’an.’’(Imam At Tirmidhii)

Na akasema Jabir Ibn Abd Allah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Nabii Salallahu
Alayhi wa Salam kua: ‘Qur’ani ni Muombeaji na ni Mdai ambae madai yake
yanakubaliwa. Hivyo atakeiweka mbele yake Qur’an basi itampeleka Peponi, na
atakaeiweka Nyuma yaake basi itampeleka Motoni.’’(Imam Ibn Hibban)

Basi tunaona kua kutokana na utukufu huo, na darja yake na hivyo kama ilivyosemwa
katika aya hizi na nyenginezo na hadithi hizi na nyenginezo kua kama ikisoma sivyo basi
hua aikubalii kisharia na hua haina manufaa yeyote ndani yake, bali hua na madhara
ambayo ni kama yaliyowafika watu wa Bani Israil ama mabaya zaidi, kwani Qur’an si
kitu chengine chochote isipokua ni maneno matukufu ya Allah Subhnah wa Ta’ala
ambayo ameyashusa kama yalivyo kupitia kwa Malaika Jibril kufikia kwa Mtume wake
Muhammad Salallahu Alyhi wa Salam, hivyo ikiwa na maneno mengine ndani yake zaidi
ya yale yaliyoshushwa nayo hapo hapo kabla, basi hio hua si Qur’an.

Na pia hairuhusiki kubadilisha maneno ya Aya au Hadithi hata kama maneno hayo
hayatobadilisha maana ya Aya au Hadithi kwani anasema Al Musannif Imam Badr Ad
Din Abu Abdullah Muhammd Ibn Abdullah Bahadir Al Zarkashi katika kufafanua tofauti
baina ya Tafsir na Tarjuma ambapo neno Tarjuma hua linamanisha Kubuni au Kuagua
maana, kua: ‘Inaruhusika Kutafsiri Qur’an kutoka katika Lugha Moja kuingia
kwenye Lugha nyengine, Kwa sababu Tafsir inajumuisha kile ambacho kinakua
katika hali ya maumbile ya kimaana ambacho hua ni kitu kinachohitajika na kua
ni kitu cha wajib.

Tarjuma hua ni kubadilisha neno kwa kuweka neno jengine katika kile
kinachofahamika kimaana kwa msikilizaji, hivyo wakati Tarjuma inabadilisha
947

maana katika ufahamu wa mwenye kusikiliza, basi Tafsir hua inamtaarifu


msikilizaji kile ambacho mwenye kutafsiri amekifaham.’

Hivyo Tafsir hua inamtaarifu msikilizaji juu kile ambacho mwenye kutafsiri amekifaham
na Tarjuma hua yenye kubadilisha maneno, na bila ya shaka kuna tofauti baina ya
mabadilisho ya maneno na ufafanuzi wa maneno.

Ambapo kwa upande wa Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Ahmad Ibn Abu Baqr
Al Ansari Al Qurtubi basi yeye anasema kua: ‘Katika baadhi ya Maneno na baadhi ya
Maandiko maneno hua ni sehemu ya kusudio linaloenda sambamba na hitajiko la
kufikisha ujumbe husika, hivyo basi kutokana na hali hii hua hairuhusiki
kubadilisha maneno.’

Yaani kwa mfano tukichukulia maneno ya Hadith ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa
Salam katika maneno ya Adhana, Iqama na Ibada ya Sala basi hairuhusiki kuongezwa
kitu chengine ndani yake mambo hayo isipokua yale ambayo ameyasema na kuyaruhusu
mwenyewe Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika hadithi zinazoelezea mambo
hayo.

Na amesema Muhammad Ibn Jubyr Ibn Mutim Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Baba
yake kua : ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alisimama katika Khaif katika
maeneo ya Mina na kisha akasema kua: ‘Allah amjaalie kua ni mwenye Uso wenye
Nuru, yule mtu anaesikia ninachokisema na kisha akakifikisha (kwa wengine kama
alivyosikia). Kuna wale ambo ni wenye I‘lm lakini hawan Ufahaam na hivyo
inaezekana ikawa kuna wanaofikisha Ilm kwa wale ambao ni wenye Ufaham zaidi
kuliko wao’’(Sunnah Ibn Majah)

Na kwa upande mwengine basi tunapozungumzia Kauli nyengine za Rasul Allah


Salallahu Alayhi wa Salam ambazo ndani yae hua ni maana ya maaneno ndio
inayohitajika kutokana na umuhimu wake basi Mujaddid Ad Din Imam Muhammad Idris
Al Shafii, amesema kua: ‘Inaruhusika kutoa hadithi kwa kutumia maana yake peke
yake pale inapokua anaenukuu hadihi hio kua ni mwenye sifa ya kua na Ilm
kamilifu ya Lugha ya Kiarabu na pia inapokua mtu huyo anajua mazingira ya tukio
lililosababisha kutamkwa kwa maneno ya Hadith hio, hivyo kutokua ni mwenye
kupoteza maana na kusudio la kauli ya hadithi hio’

Hivyo kutokana na mtizamo huo basi tunaona kua ni bora kuihadithia Hadithi ya Rasul
Allah Salallahu Alayhi wa Salam kama ilivyotamkwa na Rasul Allah Salallahu Alayhi
wa Salam, lakini hapo hapo hua inaruhusika pia kuhadithia maana ya ujumbe wa Hadithi
kama mtu atakua ameyasahau maneno ya hadith hio, lakini hairuhusiki kuongea maneno
au kubadilisha ndani yake, kwani kufanya hivyo basi hua ni sawa na kufanya
walivyofanya Mayahudi na Manasara.
948

NAMNA MAYAHUDI NA MANASARA WALIVYOBADILISHA


MANENO NDANI YA VITABU VYAO ASILIA.


Allah Subhnah wa Ta’ala anatuelezea namna Mayahudi na Manasara walivyofanya ndani
ya vitabu vyao walivyoshushiwa na Mola wao kwa kuweka mitizamo yao kama
zinavyobainisha aya zenye kuwaonya waliofanya hivyo pale ziliposema:

‫ٱﻪﻠﻟِ ﻟِﻴَ ْﺸﺘَـُﺮواْ ﺑِِﻪ‬


‫ﺎب ِﺄﺑَﻳْ ِﺪﻳ ِﻬ ْﻢ ﰒُﱠ ﻳَـ ُﻘﻮﻟُﻮ َن َﻫـٰ َﺬا ِﻣ ْﻦ ِﻋْﻨ ِﺪ ﱠ‬ ِ
َ َ‫ﻳﻦ ﻳَ ْﻜﺘُـﺒُﻮ َن ٱﻟْﻜﺘ‬
ِِ ﴿
َ ‫ﻓَـ َﻮﻳْ ٌﻞ ﻟّﻠﱠﺬ‬
﴾‫ﺖ أَﻳْ ِﺪﻳ ِﻬﻢ ووﻳْﻞ ﱠﳍُﻢ ِّﳑﱠﺎ ﻳَ ْﻜ ِﺴﺒُﻮ َن‬ ِ ِ
ْ َ‫َﲦَﻨﺎً ﻗَﻠﻴﻼً ﻓَـ َﻮﻳْ ٌﻞ ﱠﳍُْﻢ ّﳑﱠﺎ َﻛﺘَـﺒ‬
ْ ٌ ََ ْ
Fawaylun lilladheena yaktuboona alkitaba bi-aydeehim thumma yaqooloona hadha
min AAindi Allahi liyashtaroo bihi thamanan qaleelan fawaylun lahum mimma
katabat aydeehim wawaylun lahum mimma yaksiboona(Surat Al Bqara 2:79)

Tafsir: Hivyo Ole wao wale ambao wameandika vitabu kwa mikono yao na kisha
wakasema kua: ‘Hiki kinatoka kwa Allah’ ili kukibadilisha (kwa kukiuza na
kukinunua) kwa thamani ndogo, na Ole wao juu ya kile kilichoandikwa kwa mikono
yao na Ole wao juu ya kile wanachokichuma kutokana nacho.

Na kisha watu hao hua ni wenye kusema:

ِ ِ‫ﻨﺪ ﱠ‬ َ ‫ودةً ﻗُ ْﻞ أ ﱠَﲣَ ْﺬ ُْﰎ ِﻋ‬


‫ﻒ‬
َ ‫ٱﻪﻠﻟ َﻋ ْﻬﺪاً ﻓَـﻠَ ْﻦ ُﳜْﻠ‬ َ ‫ﱠﺎر إِﻻﱠ أ ﱠَ�ﻣﺎً ﱠﻣ ْﻌ ُﺪ‬
ُ ‫َوﻗَﺎﻟُﻮاْ ﻟَﻦ َﲤَ ﱠﺴﻨَﺎ ٱﻟﻨ‬
﴿
﴾‫ٱﻪﻠﻟِ َﻣﺎ ﻻَ ﺗَـ ْﻌﻠَﻤﻮن‬ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻋ ْﻬ َﺪﻩُ أ َْم ﺗَـ ُﻘﻮﻟُﻮ َن َﻋﻠَﻰ ﱠ‬
‫ﱠ‬
ُ
Waqaloo lan tamassana alnnaru illa ayyaman maAAdoodatan qul attakhathtum
AAinda Allahi AAahdan falan yukhlifa Allahu AAahdahu am taqooloona AAala
Allahi ma la taAAlamoona(Surat Al Bqara 2:80)

Tafsir: Na wao(Mayahudi) husema: ‘Na hautotugusa sisi Moto isipokua wa masiku


machache. Waambie(Ewe Muhammad) Jee mmewekeana ahadi na Allah? Hivyo
Allah hatovunja ahadi yake juu yenu? Au mnasema juu ya Allah kuhusiana na kile
msichokijua?’
949

Kisha Allah Subhnah wa Ta’ala anamalizia kitakachowakuta watu hao kwa kusema:

‫ﺎب ٱﻟﻨﱠﺎ ِر ُﻫ ْﻢ ﻓِ َﻴﻬﺎ‬ ۤ ۤ


ُ ‫َﺻ َﺤ‬ َ ِ‫ﺖ ﺑِِﻪ َﺧ ِﻄﻴـﺌَـﺘُﻪُ ﻓَﺄ ُْوﻟَـﺌ‬
ْ ‫ﻚأ‬ َ ‫ﺐ َﺳﻴِّﺌَﺔً َوأ‬
ْ َ‫َﺣﺎﻃ‬ َ ‫ﺑَـﻠَ ٰﻰ َﻣﻦ َﻛ َﺴ‬
﴿
﴾‫َﺧﺎﻟِ ُﺪو َن‬
Bala man kasaba sayyi-atan waahatat bihi khatee-atuhu faola-ika as-habu alnnari
hum feeha khalidoona(Surat Al Baqara 2:81)

Tafsir: Naam! Atakaefanya Dhambi na kisha akazungukwa na makosa yake. Basi


watakua ni watu wa Motoni. Watakaa ndani yae Milele.

Ambapo katika aya hizo basi tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala amewazungumzia
Mayahudi, lakini hii haimaanishi kua ni Mayahudi peke yao waliofanya kubadilisha
maneno kwenye vitabu vyao walivyoshushiwa, kwani Qur’ani pia ikawazungumzia tena
watu wengine waliofanya kama hivyo kwa kusema katika aya zifuatazo kua:

‫ﺎﺳﻴَﺔً ُﳛَِّﺮﻓُﻮ َن ٱﻟْ َﻜﻠِ َﻢ َﻋﻦ‬ ِ َ‫ﻀ ِﻬﻢ ِﻣﻴﺜَﺎﻗَـﻬﻢ ﻟَﻌﻨﱠﺎﻫﻢ وﺟﻌ ْﻠﻨَﺎ ﻗُـﻠُﻮﺑـﻬﻢ ﻗ‬
ْ َُ ََ َ ُْ ُْ ّ
ِ ‫﴿ﻓَﺒِﻤﺎ ﻧَـ ْﻘ‬
َ
ِ
ً‫اﺿﻌِ ِﻪ َوﻧَ ُﺴﻮاْ َﺣﻈًّﺎ ّﳑﱠﺎ ذُ ّﻛُِﺮواْ ﺑِِﻪ َوﻻَ ﺗَـَﺰ ُال ﺗَﻄﱠﻠِ ُﻊ َﻋﻠَ ٰﻰ َﺧﺂﺋِﻨَ ٍﺔ ِّﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ إِﻻﱠ ﻗَﻠِﻴﻼ‬ ِ ‫ﱠﻣﻮ‬
َ
�‫ﻳﻦ ﻗَﺎﻟُﻮاْ إِ ﱠ‬ ِ ‫ﺐ ٱﻟْﻤﺤ ِﺴﻨِ ِ ﱠ‬ ِ ‫ﭑﻋﻒ ﻋْﻨـﻬﻢ وٱﺻ َﻔﺢ إِ ﱠن ﱠ‬ ِ
َ ‫ﲔ۞ َوﻣ َﻦ ٱﻟﺬ‬ َ ْ ُ ‫ٱﻪﻠﻟَ ُﳛ ﱡ‬ ْ ْ َ ْ ُ َ ُ ْ َ‫ّﻣْﻨـ ُﻬ ُﻢ ﻓ‬
َ‫َﺧ ْﺬ َ� ِﻣﻴﺜَﺎﻗَـ ُﻬ ْﻢ ﻓَـﻨَ ُﺴﻮاْ َﺣﻈّﺎً ِّﳑﱠﺎ ذُ ّﻛُِﺮواْ ﺑِِﻪ ﻓَﺄَ ْﻏَﺮﻳْـﻨَﺎ ﺑَـْﻴـﻨَـ ُﻬ ُﻢ ٱﻟْ َﻌ َﺪ َاوة‬
َ ‫ﺼ َﺎر ٰى أ‬َ َ‫ﻧ‬
﴾‫ﺼﻨَـﻌُﻮ َن‬ ِ ‫ف ﻳـﻨَـﺒِﺌُـﻬﻢ ﱠ‬ ِ ‫وٱﻟْﺒـ ْﻐﻀﺂء إِ َ ٰﱃ ﻳـﻮِم ٱﻟْ ِﻘﻴﺎﻣ‬
ْ َ‫ٱﻪﻠﻟُ ﲟَﺎ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳ‬ َ ‫ﻮ‬ ‫ﺳ‬‫و‬ ‫ﺔ‬
ُ ُ ّ ُ ْ َ َ َ َ َْ َ َ َ َ
Fabima naqdhihim meethaqahum laAAannahum wajaAAalna quloobahum
qasiyatan yuharrifoona alkalima AAan mawadhiAAihi wanasoo hadhdhan
mimma dhukkiroo bihi wala tazalu tattaliAAu AAala kha-inatin minhum illa
qaleelan minhum faoAAfu AAanhum waisfah inna Allaha yuhibbu almuhsineena;
Wamina alladheena qaloo inna nasara akhadhna meethaqahum fanasoo hadhdhan
mimma dhukkiroo bihi faaghrayna baynahumu alAAadawata waalbaghdaa ila
yawmi alqiyamati wasawfa yunabbi-ohumu Allahu bima kanoo
yasnaAAoona(Surat Al Maidah 5:13-14)
950

Tafsir: Hivyo kutokana na kuvunja Makubaliano yao, basi sisi tumewalaani na


kuzifanya ngumu Nyoyo zao. Wamebadilisha maneno kutoka katika Mawaidha yake
na kusahau sehemu nzuri ya Ukumbusho waliotumiwa. Na hutoacha kugundua
uhalifu kutoka kwao isipokua kwa wachache miongoni mwao. Lakini wasamehe na
dharau(makosa yao kama watasilimu). Kwani Allah anawapenda wenye kufanya
mema. Na wale ambao ni wenye kusema: ‘Hakika sisi Manasara’ basi tumechukua
ahadi kutoka kwao, lakini wamesahau sehemu ya mazuri tuliyowakumbusha. Hivyo
tumewapandikizia baina yao uadui mpaka siku ya Kiama na kisha atawabainishia
Allah juu ya kile walichokua wakikifanya

Hivyo kutokana na maana hio basi tunaona kua aya tulizoanza nazo za Surat Al Baqara
2:27-81 zinawazungumzia Mayahudi na aya hizi za Surat Al Maidah 5:13-14
zinawazungumzia Wakristo.

Ambapo Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kuhusiana na aya hizi za Surat
Al Maidah 5:13 ambayo imetumia neno Qasiyah kua: ‘Neno Qasiya limetokana na neno
Qaswa ambalo ni lenye kumanisha Ugumu. Na ndio maana watu husema kuhusiana
na Dirham ya kughushi kua ni Dirham Qasiy, kwa sababu Dhahabu halisi na Fedha
halisi hua ni nyepesi lakini zinapoghushiwa na kuchanganywa na kitu chengine hua
Ngumu.’

Yaani nyoyo zao zimekua ngumu kiasi ya kua walibadilisha maneno ya Mola wao, na
kuyaandika kulingana na matamanio yao ya Kidunia na kuwapotosha watu wao kutokana
na ujumbe halisi na kuwaingiza kwenye Kufru wafuasi wao kwani kwenye vitabu vyao
hua ni wenye kusema kua Nabii Isa Ibn Maryam ni Mungu, kama ilivyoelezewa kwenye
aya zifuatazo:

ً‫ٱﻪﻠﻟِ َﺷْﻴﺌﺎ‬
‫ﻚ ِﻣ َﻦ ﱠ‬ ِ
ُ ‫ﻴﺢ ٱﺑْ ُﻦ َﻣْﺮَﱘَ ﻗُ ْﻞ ﻓَ َﻤﻦ ﳝَْﻠ‬ ِ ‫ٱﻪﻠﻟ ﻫﻮ ٱﻟْﻤ‬
‫ﺴ‬ ُ ‫ﱠ‬ ‫ﱠ‬
‫ن‬ ِ‫﴿ﻟﱠَﻘ ْﺪ َﻛ َﻔﺮ ٱﻟﱠ ِﺬﻳﻦ ﻗَﺂﻟُ ۤﻮاْ إ‬
ُ َ َ َ َ َ
ِ ِ َِ ‫ض‬ ِ ‫ﻴﺢ ٱﺑْ َﻦ َﻣْﺮَﱘَ َوأُﱠﻣﻪُ َوَﻣﻦ ِﰱ ٱﻷ َْر‬ ِ َ ِ‫إِ ْن أَراد أَن ﻳـﻬﻠ‬
‫ﻚ‬ُ ‫ﲨﻴﻌﺎً َو ﱠﻪﻠﻟ ُﻣ ْﻠ‬ َ ‫ﻚ ٱﻟْ َﻤﺴ‬ ُْ َ َ
﴾‫ٱﻪﻠﻟ َﻋﻠَ ٰﻰ ُﻛ ِﻞ َﺷﻲ ٍء ﻗَ ِﺪﻳﺮ‬ ِ ‫ات َوٱﻷ َْر‬ ِ ‫ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬
ٌ ْ ّ ُ‫ض َوَﻣﺎ ﺑَـْﻴـﻨَـ ُﻬ َﻤﺎ َﳜْﻠُ ُﻖ َﻣﺎ ﻳَ َﺸﺂءُ َو ﱠ‬ ََ
Laqad kafara alladheena qaloo inna Allaha huwa almaseehu ibnu maryama qul
faman yamliku mina Allahi shay-an in aradha an yuhlika almaseeha ibna maryama
waommahu waman fee al-ardhi jameeAAan walillahi mulku alssamawati waal-
ardhi wama baynahuma yakhluqu ma yashao waAllahu AAala kulli shay-in
qadeerun.(Surat Al Maidah 5:17)
951

Tafsir: Kwa hakika wamekufuru wale ambao ni wenye kusema kua: ‘Mungu ni Masih
Ibn Maryam’ Waambie (Ewe Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam kua) Jee ni nani
anaeweza kushindana na Allah kama atataka kumuangamiza Masih Ibn Maryam na
Mama yake na kila kilichomo Ardhini? Na kwa hakika upo kwa Allah Umiliki wa
Mbingu na Ardhi na kila kilichomo baina yake, hukiumba akitakacho, na Allah ni
mwenye uwezo juu ya kila kitu.

Hapa tunaona kua aya imemchanganya na Maryam bint Imran ndani yake na hii ni kwa
sababu ya kua kama anavyosema Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamahshari kua:
‘Hii ni kwa ajili ya kuweka wazi kua Wote wawili yaani Nabii Isa na Mama yake ni
Viumbe walioumbwa na Allah Subhanah wa Ta’ala hivyo hwawezi kua ni Miungu.’

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakkalimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi
kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala ni mwenye kuumba kwa kadiri atakavyo, kwani
badhiya wakati hua anaumba bila ya uwepo kwa Baba wala Mama, kama kwa
mfano atika maumbile ya Nabii Adam, na kwa baadhi ya wakati anaumba bila ya
kuwepo Mama, kama kwa mfano katika maumbile ya Mama yetu Hawa, na baadhi
ya wakati hua anaumba bila ya kuwepo Baba kwa mfano katika maumbile ya Nabii
Isa. Hivyo Wakristo hawatakiwi kua ni wenye kushangzwa na Miujiza ya kuzaliwa
kwa Nabii Isa bila ya kuwepo baba yake na hivyo kua ni wenye kumpa sifaa ya
Umungu.’

Kisha Allah Subhanah wa Ta’ala akawajumuisha Mayahudi na Wakristo kulingana na


aina za Kufuru zao za pamoja zinazolingana kutokana na ujinga wao kama ilivyoainisha
katika aya ifuatayo:

ِ ِ‫ﺖ ٱﻟﻨﱠﺼﺎرى ٱﻟْﻤ ِﺴﻴﺢ ٱﺑﻦ ﱠ‬ ِ َ‫ٱﻪﻠﻟِ وﻗَﺎﻟ‬ ِ


َ ‫ٱﻪﻠﻟ ٰذﻟ‬
‫ﻚ ﻗَـ ْﻮُﳍُﻢ‬ ُْ ُ َ َ َ ُ ‫﴿ َوﻗَﺎﻟَﺖ ٱﻟْﻴَـ ُﻬ‬
َ ‫ﻮد ﻋَُﺰﻳْـٌﺮ ٱﺑْ ُﻦ ﱠ‬
﴾‫َﱏ ﻳـُ ْﺆﻓَ ُﻜﻮ َن‬ ‫ﻳﻦ َﻛ َﻔُﺮواْ ِﻣﻦ ﻗَـْﺒ ُﻞ ﻗَﺎﺗَـﻠَ ُﻬ ُﻢ ﱠ‬
ٰ‫ٱﻪﻠﻟُ أ ﱠ‬ ِ‫ﱠ‬ ِ ‫ِﺄﺑَﻓْـﻮ ِاﻫ ِﻬﻢ ﻳ‬
َ ‫ﻀﺎﻫﺌُﻮ َن ﻗَـ ْﻮَل ٱﻟﺬ‬
َُْ َ
Waqalati alyahoodu AAuzayrun ibnu Allahi waqalati alnnasara almaseehu ibnu
Allahi dhalika qawluhum bi-afwahihim yudahi-oona qawla alladheena kafaroo min
qablu qatalahumu Allahu anna yu/fakoona (Surat At Tawbah 9:30)

Tafsir: Na wanasema Mayahudi kua Uzayr ni Mtoto wa Allah, na wanaema Wakristo


kua Masih ni Mtoto wa Allah, hayo ni maneno kutoka midomoni mwao, wanaiga
maneno ya wale ambao waliokufuru hapo zamani. Allah awaangamize, kwani
wamepotoka sana.
952

Ambapo amesema Mujaddid Ad Din, Sultan Al Mutakkalimin Imam Fakhr Ad Din Al


Razi kua: ‘Amesema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu uhusiana na Uzayr
kuitwa hivyo na Mayahudi kua: ‘Kuna kipindi Watu wa Bani Israil walimuasi sana
Allah Subhanah wa Ta’ala hivyo Allah Subhnah wa Ta’ala akawaondolea Taurat
ndani ya Vifua vyao na wakapoteza kopi yao waliyokua nayo pamoja na Tabut
(Sanduku alilorithi Nabii Musa kutoka kwa Nabii Ibrahim kupitia kwa Nabii hadi
Nabii mpaka kwa Nabii Musa) ambalo lilitekwa na maadui zao katika vita.

Ambapo Uzayr ambae alikuwepo katika wakati huo na hivyo alikua amejihifadhi
Milimani, hivyo akaomba Dua na kisha Taurat ikashuswa kwake kwa njia ya
Wahyi.

Lakini hata hivyo Watu wa Bani Israil walipomuona kua anaisoma Taurat basi
wakawa wanashaka nayo, hadi pae walipolipata Tabut na kuanza kuilinganisha
Taurat ya Uzayr na ya Nabii Musa iliyomo kwenye Tabut na kuona kua iko sawia,
basi wakashangaa sana na kisha wakasema kua bila ya shaka Uzayr atakua ni Mtoto
wa Allah’ Astagh fir Allah!

Na pia kutokana na waliyokua wakiyasema Mayahudi na Wakristo kuhusiana na yale


yaliyoandikwa kwenye Vitabu vyao kama isemavyo aya:

‫َﺣﺒﱠ ُﺎؤﻩُ ﻗُ ْﻞ ﻓَﻠِ َﻢ ﻳـُ َﻌ ِّﺬﺑُ ُﻜﻢ ﺑِ ُﺬﻧُﻮﺑِ ُﻜﻢ ﺑَ ْﻞ‬


ِ ‫ٱﻪﻠﻟِ وأ‬
َ ‫ﱠﺼ َﺎر ٰى َْﳓ ُﻦ أَﺑْـﻨَﺎءُ ﱠ‬َ ‫ﻮد َوٱﻟﻨ‬
ِ
ُ ‫﴿ َوﻗَﺎﻟَﺖ ٱﻟْﻴَـ ُﻬ‬
ِ ‫ﻚ ٱﻟ ﱠﺴﻤﺎو‬
‫ات‬ ِِ ِ ِ ِ ِ
َ َ ُ ‫ب َﻣﻦ ﻳَ َﺸﺂءُ َو ﱠﻪﻠﻟ ُﻣ ْﻠ‬ ُ ‫أَﻧﺘُ ْﻢ ﺑَ َﺸٌﺮ ﳑ ْﱠﻦ َﺧﻠَ َﻖ ﻳَـ ْﻐﻔُﺮ ﻟ َﻤﻦ ﻳَ َﺸﺂءُ َوﻳـُ َﻌ ّﺬ‬
﴾‫ﺼﲑ‬ ِ ِِ ِ ‫َوٱﻷ َْر‬
ُ ‫ض َوَﻣﺎ ﺑـَْﻴـﻨَـ ُﻬ َﻤﺎ َوإﻟَْﻴﻪ ٱﻟْ َﻤ‬
Waqalati alyahoodu waalnnasara nahnu abnao Allahi waahibbaohu qul falima
yuAAadhdhibukum bidhunoobikum bal antum basharun mimman khalaqa
yaghfiru liman yashao wayuAAadhdhibu man yashao walillahi mulku alssamawati
waal-ardi wama baynahuma wa-ilayhi almaseeru(Surat Al Maidah 5:18)

Tafsir: Na wanasema Mayahudi na Maanasara kua : ‘Sisi ni Watoto wa Mungu na


wapenzi wake’ Waambie (Ewe Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam kua) :
‘Kwanini basi akuadhibuni nyinyi kutokana na Dhambi zenu?’ La, hamkua nyinyi
isipokua ni watu wanaotokana na (watu) aliowaumba, (Allah) huwasamehe awatakao
na huwaadhibu awatako na kwa Allah ndiko kwenye umiliki wa Mbingu na Ardhi na
kila kilichomo baina yake na kwake yeye ndio marejeo yenu.
953

Ambapo aliulizwa Mwanafiqh na Mwanatasawwuf: ‘Jee imeandikwa wapi katika


Qur’an kua anaependwa hatoadhibiwa na anaependa?’ Mwanafiqh akashindwa
kujibu, hivyo Mwanatasawwuf akainukuu aya hii ya Surat Al Maidah 5:18

Na kuusiana na hali hii basi anasema Imam Ahmd Ibn Hanbal kua: ‘Siku moja Msafara
wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ulikua unapita katika sehemu ambayo
mtoto alikua akikatisha mbele yake, hivyo Mama wa Mtoto huyo akamkimbilia
Mtoto wake huku akipiga kelele kwa kusema: ‘Mtoto wangu! Mtoto wangu!’ kisha
akamnyakua haraka sana na kumuweka pembeni.’

Baada ya kutokea tukio hili basi Masahaba wakamuuliza Rasul Allah Salallahu
Alayhi wa Salama kwa kusema ‘Ya Rasul Allah! Haitegemewi kuonekana kua Mama
huyu anaweza kumtia Motoni Mtoto wake’. Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salama
akasema: ‘Wallahi Allah pia hatomtia yule ampendae ndani ya Moto.’

‫ﻀ ُﻬ ْﻢ‬ ‫ﺾ ِّﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ ﱠﻣﻦ َﻛﻠﱠ َﻢ ﱠ‬


َ ‫ٱﻪﻠﻟُ َوَرﻓَ َﻊ ﺑَـ ْﻌ‬ ٍ ‫ﻀ ُﻬ ْﻢ َﻋﻠَ ٰﻰ ﺑَـ ْﻌ‬
َ ‫ﻀ ْﻠﻨَﺎ ﺑَـ ْﻌ‬ َ ‫﴿ﺗِْﻠ‬
‫ﻚ ٱﻟﱡﺮ ُﺳ ُﻞ ﻓَ ﱠ‬
‫ٱﻪﻠﻟُ َﻣﺎ‬‫وح ٱﻟْ ُﻘ ُﺪ ِس َوﻟَْﻮ َﺷﺂءَ ﱠ‬ ِ ‫ﺎت َوأَﻳﱠ ْﺪ َ�ﻩُ ﺑُِﺮ‬ ِ َ‫ﺎت وآﺗَـﻴـﻨَﺎ ِﻋﻴﺴﻰ ٱﺑﻦ ﻣﺮَﱘ ٱﻟْﺒـﻴِﻨ‬ ٍ
َّ َ ْ َ َ ْ َ ْ َ ‫َد َر َﺟ‬
‫ٱﺧﺘَـﻠَ ُﻔﻮاْ ﻓَ ِﻤْﻨـ ُﻬ ْﻢ‬ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ‫ٱﻗْـﺘـﺘﻞ ٱﻟﱠ ِﺬ‬
ُ َ‫ﻳﻦ ﻣﻦ ﺑَـ ْﻌﺪﻫﻢ ّﻣﻦ ﺑَـ ْﻌﺪ َﻣﺎ َﺟﺂءَﺗْـ ُﻬ ُﻢ ٱﻟْﺒَـﻴِّﻨ‬
ْ ‫ﺎت َوﻟَـٰﻜ ِﻦ‬ َ َ ََ
﴾‫ﻳﺪ‬ ‫ٱﻪﻠﻟُ َﻣﺎ ٱﻗْـﺘَـﺘَـﻠُﻮاْ َوﻟَـٰ ِﻜ ﱠﻦ ﱠ‬
ُ ‫ٱﻪﻠﻟَ ﻳَـ ْﻔ َﻌ ُﻞ َﻣﺎ ﻳُِﺮ‬ ‫ﱠﻣ ْﻦ َآﻣ َﻦ َوِﻣْﻨـ ُﻬ ْﻢ ﱠﻣﻦ َﻛ َﻔَﺮ َوﻟَ ْﻮ َﺷﺂءَ ﱠ‬
Tilka alrrusulu fadhdhalna baAAdhahum AAala baAAdhin minhum man kallama
Allahu warafaAAa baAAdahum darajatin waatayna AAeesa ibna maryama
albayyinati waayyadnahu biroohi alqudusi walaw shaa Allahu ma iqtatala
alladheena min baAAdihim min baAAdi ma jaat-humu albayyinatu walakini
ikhtalafoo faminhum man amana waminhum man kafara walaw shaa Allahu ma
iqtataloo walakinna Allaha yafAAalu ma yureedu(Surat Baqara 2:253)

Tafsir: Hao ni Mitume! Tumewafadhili baadhi yao juu ya baadhi miongoni mwao
wamo waliozungumza na Allah, Na tukawapandisha darja baadhi yao na tukampa Isa
Ibn Maryam ubainisho na tukamuongoza na Ruhi Al Qudus (Malaika Jibril). Na
kama angetaka Allah basi wasingeuana (kwa kupigana) wale ambao walifuata baada
yao baada ya kuletewa Ubainisho, lakini walitofautianna, na hivyo miongoni mwao
waiamini na wengine miogoni mwao walikufuru. Kama Allah angetaka basi
wasingeuana lakini Allah ni mwenye kufanya yale ayatakayo.
954

KAULI, WASIA NA MAFUNZO YALIYOMO NDANI YA KISA CHA


NABII MUSA.


Amesema Al Hafidh Imam Shams Ad Din Abu Abdillah Muhammad Ibn Ahmad Ibn
Uthman Ibn Qaymaz Ibn Abdillah Al Turkmani Al Fariqi Ad Dimashq Adh Dhahabi
kua : ‘Siku moja kuna Mwanamke alienda kwa Nabii Musa na kumwambia: ‘Ya
Nabbiyu Allah kwa hakika mimi nimefanya makosa makubwa sana, hivyo niombee
kwa Allah ili anisamehe’

Nabii Musa akauliza: ‘Jee umefanya kosa gani?’

Yule Mwanamke akasema: ‘Kwa Hakika mimi nimezini na kisha nikajifungua Mtoto
kisha nikamuua.’

Nabii Musa akamwambia Mwanamke huyo: ‘Haya ondoka haraka ewe Mwanamke
muovu, kabla ya Moto hujatuangamiza sisi sote pamoja kwa sababu ya Dhambi
zako.’

Baada ya kuambiwa maneno hayo basi yule Mwanamke akaondoka huku akiwa ni
mwenye kuvunjika Moyo sana. Ambapo mara Malaika Jibril akashuka kwa Nabii Musa
na kumuuliza: ‘Ewe Musa hivi kwanini wewe umemfukuza Mwanamke aliekua
anataka kutubu? hivi hujawahi wewe kuona mtu ambae ni muovu zaidi yake?’

Nabi Musa akasema: ‘La, ni nani muovu zaidi yake?’

Malaika Jibril akasema; ‘Ni yule mtu ambae ni wenye kudumu katika kuacha Sala
kwa mda mrefu na kwa Makusudi’’(Al Kabair)


Anasema Shaykh Ul Akbar Imam Ibn Arabi kua aliwahi kuoneshwa katika ufunuo kua
anazunngumza na Nabii Musa, hivyo akamuuliza Nabii Musa: ‘Hivi ilikuaje ewe
Kallimu Allah ilikuaje ukaomba kumuona Allah Subhanah wa Ta’ala wakati Rasul
Allah Salallah Alayhi wa Salam alisema kua: ‘Hakuna atakaeweza kumuona Allah
Subhanah wa Ta’ala mpaka baada ya kufariki Mtu huyo?’. Hivyo Nabii Musa
akasema: ‘Na ilikua kama hivyo, kwani nilipoomba kumuona kwake, akanijibu
955

hivyo nami nikaanguka chini, na nikamuona katika hali yangu niliyokua nayo ya
kutokua na kuchanganyikiwa’’


Allah Subhanah wa Ta’ala alimuuliza Nabii Musa: ‘Ewe Musa, hivi jee umefanya
jambo lolote kwa ajili yangu?’

Nabii Musa akasema: ‘Naam, Ewe Mola wangu, hakika mimi nimesali, nimefunga
na kuta sadaka kwa ajili yako’

Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Ewe Musa hivi jee hujui wewe kua yote haayo
uliyoyafanya ni kwa ajili yako? Hivyo jee umempenda mtu kwa ajili yangu na
umewahi kumchukia mtu kwa ajili yangu?’

Hivyo Nabii Musa akajua kua Kumpenda Mtu na kumchukia Mtu kwa ajii ya Allah
Subhanah wa Ta’ala ni miongoni mwa Ibada kubwa sana.


Katika wakati wa uhai wake, Nabii Musa alikumbwa na wakati mgumu pamoja na watu
wake, kwani ilikua hakuna Mvua kwa mda mrefu, hivyo Nabii Musa akatoka na watu
wake kwa ajili ya kuenda kusali Sala ya Mvua na hivyo akasali kwa siku tatu mfululizo
lakini hata hivyo mvua haikunyesha, na ivyo Nabii Musa akamuuliza Allah Subhanah wa
Ta’ala mbona ameshamuomba kwa siku tatu na Mvua haijanyesha? Jee amefanya kosa
gani?

Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Nabii Musa: ‘Ewe Musa! Kwa hakika kuna
msengenyaji ndani ya watu wako, nami hua sipokei Maombi ya Wasengenyaji.’

Hivyo Nabii Musa akamwambia Allah Subhanah wa Ta’ala: ‘Ya Allah nitajie jina la
Mengenyaji huyo.’

Allah Subhanah wa Ta’ala: ‘Ewe Musa umesahahu kua mimi nimekataza


kusengenya?’

Hivyo Nabii Musa akawaambia watu wake kua Waombe msamaha kutokana na
usengenyaji. Na walipofanya hivyo basi Mvua ikanyesha baada yake.
956


Siku Moja Nabii Musa alimuuliza Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kusema: ‘Ya Allah
Jee ni nani nani umpendae zaidi miongoni mwa waja wako?’

Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Ewe Musa, Hakika ya Mtu nnaempenda mie
miongoni mwa Waja wangu basi ni yule anaejihisi kua kama amejichoma mwiba
mguuni pale Muumini mwenzake anapojichoma na Mwiba.’


Nabii Musa alikuta maiti ya mtu ambae anamjua na amekufa huku akiwa amechanwa
chanwa tumbo lake na wanyama wa mwituni. Hivyo Nabii Musa akasimama na
kumuangalia mtu huyo na kisha akamuuliza Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kusema: ‘
Ya Allah, huyu ni Mja mtiifu kwako, hivi imekuaje mpaka akawa katika hali kama
hii? Jee kuna Hikma gani ndai yake tukio hili?’

Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Ewe Musa, Mja wangu huyu ameniomba mimi
Darja ya juu ambayo kamwe hawezi kuifikia kwa amai zake, hivyo nami nikampa
mtihani huo ili afikie Darja aitakayo.’


Allah Subhanah wa Ta’ala alimshushia Wahyi Nabii Musa kumwambia: ‘Ewe Musa
Hakika mimi ninamkasirikia Mja wangu kutona na kukataa mambo manne
yafuatayo: Kwanza, Ingawa hua nnawaneemesha sana Waja wangu kwa neema
nyingi sana lakini ninapowataka wanikopeshe, hua Wanakataa kunikopesha. Pili,
ninapowaamrisha wakae mbli na Shaytani bsi hu Wanakataa, Tatu, Ingawa
inawakaribisha Peponi, Lakini wanakataa Kuja na Nne ni kua Ingawa nimewaonya
kuhusiana na Jahannam lakini wao bado wanafanya mambo yatakayowaingiza
Motoni.’


Amesema Abda Alla Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala
alimshushia Wahy Nabii Musa kwa kumwambia ‘Ewe Musa hakika mimi hua
nnamchukia zaid miongoni mwa waja wangu yule ambae ni mwenye Kujiona ndani
ya Moyo wake, mwenye kibri kwenye Ulimi wake, Ubakhili kwenye mikono yake
na mwenye kusababisha madhara katika maumbile yake. ’’
957


Imam Abu Hasan Ali Ibn Muhammad Ibn Habib Al Mawardi Al Shafii anasema kua:
‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alisemaa kua: ‘Sahifa za Nabii Musa zina
mafunzo mengi sana n amifo mingi sana, kwa mfano: ‘Inakuaje Mtu mwenye
kuamini Jahanam anaweza kua ni mwenye Kucheka, Inakuaje Mtu anaeona
mabadilio ya Dunia kua ni mwenye kuitegemea Dunia, Inakuaj Mtu mwenye
Kuamini juu ya Kifo kua ni mwenye Kufanya mambo siyo? Inakuaje Mtu mwenye
kuamini juu ya Siku ya Malipo kua ni Mvivu katika kufanya Mema?’’’


Siku Moja Nabii Musa alikua amekaa na kundi la watu, mara akatokea Ibilisi na
kumsalimia Nabii Musa, hivyo Nabii Musa kamuuliza: ‘Hivi wewe ni Nani?’

Ibilisi akasema: ‘Mimi ni Ibilisi’

Nabii Musa kauliza: ‘Unataka nini ewe Ibilisi?’

Ibilisi akasema: ‘Hakika Mimi naijua Daraja yako mbele ya Mola wako, hivyo
nimekuja kukusalimia.’

Nabii Musa akasema; ‘Niambie ewe Ibilisi, hebu niambie jee ni dhambi gani ambayo
mtu anapoifanya basi wewe hua unamzidi nguvu?’

Ibilisi akasema: ‘Wakati mtu anapojiona ndani ya Nafsi yake, na hivyo kua ni
mwenye kuhisi kua ameshafanya Ibada nyingi sana, na hivyo hua ni mwenye
kusahau dhambi zake, hapo ndio ninapomdhibiti’


Nabii Musa alisema kumwambia Allah Subhnah wa Ta’ala kua: ‘Ya Allah Hakika
kukushukuru kwangu ni Neema inayotoka kwako ambayo nayo inahitaji shukrani
yake.’

Allah Subhnah wa Ta’ala akasema: ‘Utakapojua juu ya kua Neema zote zinatoka
kwangu basi ndio nitakapoikubali Ilm yako ya kujua hivyo kua ni shukurani juu
yangu.’


958

Kaab Al Akhbar anasema kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala alimwambia Nabii Musa
kua: ‘Ewe Musa unapouona Umasikini unakujia wewe basi usalimie kwa kusema:
‘Karibu ewe dalili ya Waja wema.’’’


Imam Ata Al Khurasani amesema kua: ‘Nabii Musa, alienda ufukweni Baharini, na
akaona kuna mtu anavua samaki. Mtu huyo akasema: ‘Bismillahi’ na kisha
akarusha mshipi wake kwenye maji, lakini hakuvua samaki hata mmoja. Na kisha
akamuona mtu mwengine aliekua mbali na mtu huyo ambae alichukua mshipi wake
na kuema ‘Bismishaytani’ na aliporusha mshipi basi akavua samaki wengi tu. Nabii
Musa akashangaa sana juu ya tukio hili, na kusema: ‘Ya Allah! Inakuaje yanatokea
haya mbali ya kuwepo na uwezo wako?’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akasema kuwaambia Malaika: ‘Muonesheni


Mtume wangu huyu tofauti ya darja ya watu hawa kwenye macho yake.’ Kisha
Nabii Musa alipooneshwa arja ya mtu ambae hakuvua samaki basi akasema: ‘Ya
Allah, mfano huu umetosha, nami nimeridhika na yaliyotokea.’’


Imam Abu Hasan Ali Ibn Muhammad Ibn Habib Al Mawardi Al Shafii kua Nabii Musa
aliomba dua dhidi ya watu wake, ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Nabii
Musa kua ameijibu Dua yake hio kwa kuwajaalia watu hao wa Bani Israil kua ni wenye
kutawaliwa na Wajinga.

Nabii Musa akasema: ‘Ya Allah! Hakika mimi nakuomba kua bora uwaadhibu watu
hawa kwa haraka sana.’

Allah Subhanah wa Ta’ala akahoji: ‘Ewe Musa, Hivi jee Kuna Adhabu Gani Kali na
ya Haraka kuliko Hii ya Watu Kutawaliwa na Wajinga?’


Nabii Musa alikutana na mtu ambae ana matatizo mengi sana, hivyo akamuomba Allah
Subhanah wa Ta’ala kw kusema: ‘Ya Allah Muingize kwenye Rehma zako Mja wako
huyu.’

Allah Subhanah wa Ta’ala akamjibu Nabii Musa kwa kumwambia: ‘Hivi Jee
innawezekana kuwepo na Rehma kubwa zaidi ya hii juu ya Mja huyu?’ ambapo hii
959

inamaanisha kua Muumini napokua na Mitihani basi hua na Malipo makubwa zaidi,
kama atamshukuru Mola wake na kua na ustahamilivu wa kutolalamikia juu ya Mitihani
hio, na kama angejua umuhimu wa Mitihani hio kua ni kumkaribishia zaidi kwa Mola
wake basi asingelalalamiki juu yake.


Allah Subhnah wa Ta’ala alimwambia Nabii Musa: ‘Mtu wa mwisho kuingia Peponi
ni yule ambae anaetubu na kuachana na kusengenya. Na mtu wa mwanzo kuingia
Motoni ni yule anaedumu katika usengenyaji’


Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Nabii Musa alimuuliza Allah
Subhanah wa Ta’ala, Ya Allah, Hivi jee ni nani mtu mwenye thamani kubwa zaidi
mbele ya Mcho yako?’

‘Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Yule Mtu ambae anaemsamehe mwenzake


wakati anao uwezo wa kulipiza kisasi.’’


Nabii Musa alioneshwa na Allah Subhanah wa Ta’ala mtu mmoja ambae alikua
amekaa chini ya kivuli cha Arshi ya Allah Subhanah wa Ta’ala hivyo akataka kujua
ilikuaje mpaka mtu huyo akapata nafasi kama hio?

Allah Subanah wa Ta’ala akamwambia Nabii Musa: ‘Mtu huyu amefikia daraja hii
kutokana na Mambo matatu ambayo ni: Hakua na Wivu juu ya Mtu yeyote, Hakua
na usengenyaji, na hakua ni mwenye kutowatii wazazi wake.’


Allah Subhanah wa Ta’ala alimwambia Nabii Musa: ‘Ewe Musa, Usiikumbatie Dunia
na wala usiuwachie Moyo wako ukishikamana nayo kwa sababu haiwezekani kuja
kwangu mbele yangu huku ukiwa na Dhambi zaidi ya Kuikumbatia Dunia na
Kuushikamanisha Moyo wako na Dunia’


960

Nabii Musa alimuuliza Allah Subhanah wa Ta’ala: ‘Hivi Jee ni yupi kati ya Waja wako
ambae ni tajiri zaidi?’ Allah Subhanah wa Ta’ala akajibu: ‘Ni yule ambae
alieridhika na kile nilichompa.’


Nabii Musa alimuomba Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kusema: ‘Ewe Mola wangu,
nioneshe darja ya Muhammad (Salallahu Alayhi wa Salam) na baadhi ya Watu wa
Umma wake’

Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Ewe Musa hakika wewe huwezi kuona wala
kujua darja yote hio, hivyo nitakuonesha sehemu tu ya Darja hio, ambayo ndio
niliyomfanyia Muhammad (Salallahu Alayi wa Salam) kua awe na Darja ya juu
kuliko viumbe wengine wote’

Kisha baada ya hapo Ukafunguka Mlango, na Nabii Musa akaona Ulimwengu wa Kiroho,
na kisha akaoneshwa Nuru ya darja ya Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam tu na
ukaribu aliokua nao karibu ya Allah Subhnah wa Ta’ala , bila ya uangalia kwa umakini
basii hapo hapo mwili wa Nabii Musa ulipoteza nguvu na kutaka kuanguka na kuzimia,
lakini hakuzimia.

Na badala yake Nabii Musa akauliza kwa kusema: ‘Ya Allah! Umemyanyua katika
Darja kubwa namna hio kwa sababu gani?’

Allah Subhnah wa Ta’ala akasema: ‘Kutokana na sifa na Tabia nilizompa.’

Nabii Musa akauliza kwa kusema: ‘Hivi Jee ni Sifa na Tabia Gani hio?’

Allah Subhnah wa Ta’ala akasema: ‘Iithar! (yaani kutokua na Ubinafsi na hivyo kua
ni mwenye kuwajali watu wengine kuliko mtu unavyojijali wewe mwenyewe). Hivyo
Mtu yeyote yule atakaekuja kwangu akiwa na sifa hio basi kwa hakika mimi hua
nnaona haya kumuhesabia Mtu huyo na hivyo nitamlipa kwa kumuweka popote
pale anapotaka Peponi.’


Anasema Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al
Qurtubi kua: ‘Al Mughira Ibn Shuba amesema kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu
A’layhi wa Salam kua : ‘Nabii Musa alimuuza Allah Subhanah wa Ta’ala, Ya Allah,
hivi jee ni wepi kati ya Watu wa Peponi ambao watakua katika darja ya chini kabisa
ya Pepo?’
961

Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Miongoni mwa wale wanaostahiki Kuingia


Peponi, basi watakuwemo wale ambao wataambiwa: ‘Ingia Peponi,’ ambapo mtu
atasema: ‘Ewew Moa wetu Jee nitaingiaje Peponi wakati kila mtu tayari
ameshvachukua Nafasi yake ndani yake?’’

Hivyo watu hao wataambiwa: ‘Hivi Jee haikuridhisha wewe kuambiwa kua ndani
yake kuna Mamlaka yako ambayo ukubwa wake kama Mamlaka ya Ufalme wa
Mfalme wa Dunia?’ Mtu huyo atasema: ‘Itaniridhisha sana tu.’

Hivyo watu hao wataambiwa: ‘Hivyo kwa ajili yako wewe kuna kama hivyo na
kama hivyo na kama hivyo na kama hivyo’ ikifika mara ya tano basi mtu huyo
atasema: ‘Imeniridhisha Sana tu ewe Mola wangu.’

Hivyo mtu huyo ataambiwa na Allah Subhanah wa Ta’ala: ‘Hio ni kwa ajili yako,
mara kumi zaidi na kwa ajili yako pia mna kila kitu unachokitamani na
kinachovutiwa na macho yako.’ mtu huyo atasema: ‘Imeniridhisha Sana tu ewe
Mola wangu.’

Nabii Musa akauliza: ‘Hivyo ya Allah, Jee itakuaje hali ya Darja yao ya walio juu
kabisa?’ Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Hao ni Miongoni mwa
waliochaguliwa, nitawapa heshima yao kwa mikono yangu na kuwapigia mihuri juu
yake, Watakua na neema ambazo hazikuwahi kuonekana kwa Macho yake,
hazikuwahi kusikia kwa Masikio, na hazikuwahi kufikirika kwenye Ufahamu.’’

Hii inabainishwa na ile aya isemayo:’

ٍ ُ ‫ُﺧ ِﻔﻰ َﳍُﻢ ِّﻣﻦ ﻗُـﱠﺮةِ أ َْﻋ‬


﴾‫ﲔ َﺟَﺰآء ِﲟَﺎ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳَـ ْﻌﻤﻠُﻮ َن‬ ْ ‫ﺲ ﱠﻣﺂ أ‬ ﴿
َ ً ٌ ‫ﻓَﻼَ ﺗَـ ْﻌﻠَ ُﻢ ﻧَـ ْﻔ‬
Fala taAAlamu nafsun ma okhfiya lahum min qurrati aAAyunin jazaan bima
kanoo yaAAmaloona(Surat Al Sajda 32:17)

Tafsir: Hakuna Nafsi inayojua kile ambacho kimefichwa kutokana na mtizamo


unaotulizisha na kufurahisha macho. Malipo kutokana na kile walichokua
wakikifanya.

Ambapo aya imetumia neno Ukhfiya lenye kutokana na neno Khafiya ambalo hua ni
lenye kumaanisha Kufichika, Kutoonekana, Kufunikwa. Hili pia ni miongoni mwa
maneno ya Lugha ya Kiarabu ambayo hua yana maana mbili tofauti zinazopingana na
kuvutana yaani kama kwa mfano kama katika kitendo cha mtu kumuangalia mtu
mwengine kwa mtizamo wa jicho la wizi yaani unaangalia lakini huangalii kitendo
962

ambacho Waarabu hua wanasema ‘Tarfin Khafiyyin’ kwani neno hili Khafiya hua pia
linamaanisha Kufunua, Kuweka wazi na Kubainisha.

Ambapo anasema Abdallah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu kua: ‘Imeandikwa kwenye
Taurat kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala amewatayarishia wale ambao ni wenye
kukaa mbali na Vtandaa vyao katika wakati wa usiku, vile ambavyo havijawahi
kuonekana na macho, havijasikikana na masikio wala na Malaika na havijafikirika
na ufaham.’’

Na anasema Imam Ahmd Ibn Hanbal kua ‘Amesema Muadh Ibn Jabal Radhi Allahu
Anhu kua: ‘Mimi nilikua na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika moja
kati ya safari zake, wakati mmoja nilikaribia karibu yake huku tukiwa tumepanda
vipando na niamuuliza kwa kusema: ‘Ya Rasul Allah (Salallahu Alayhi wa Salam)
Jee utaniambia mie kuusiana na amali ambayo nikiifanya basi itaniongoza Peponi
na kuniepusha na Moto?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Hakika wewe umeniuliza mimi
kitu ambacho ni kikubwa sana, lakini ni kitu ambacho hua rahisi kwa mtu ambae
Allah Subhanah wa Ta’ala amemrahisishia kukitelekeza. Muabudu Allah bila ya
kumshirikisha na chochote, Simamisha Sala, Toa Zakkah, Funga Ramadhani na
Fanya Hija,’’

Na kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaniuliza: ‘Jee nikuongoze


kwenye mlango wa Mema yote? Funga, ni ngao, Sadaka, ni ufutio wa dhambi, na
Qiyaam Al Layl.’ Kisha akasoma aya zifuatazo:

ِ ِ ‫ﺎﰱ ﺟﻨﻮﺑـﻬﻢ ﻋ ِﻦ ٱﻟْﻤ‬


‫ﺎﻫ ْﻢ‬ َ َ َ ْ ُ ُ ُ ُ َٰ ‫﴿ﺗَـﺘَ َﺠ‬
ُ َ‫ﻀﺎﺟ ِﻊ ﻳَ ْﺪﻋُﻮ َن َرﺑـﱠ ُﻬ ْﻢ َﺧ ْﻮﻓﺎً َوﻃَ َﻤﻌﺎً َوﳑﱠﺎ َرَزﻗْـﻨ‬
﴾‫ﲔ َﺟَﺰآء ِﲟَﺎ َﻛﺎﻧُﻮاْ ﻳَـ ْﻌﻤﻠُﻮ َن‬ ٍ ُ ‫ُﺧ ِﻔﻰ َﳍُﻢ ِّﻣﻦ ﻗُـﱠﺮةِ أ َْﻋ‬
ْ ‫أ‬ ‫ﺂ‬ ‫ﻣ‬
‫ﱠ‬ ‫ﺲ‬‫ﻔ‬ْ ‫ـ‬
َ‫ﻧ‬ ‫ﻢ‬َ‫ﻠ‬ ‫ﻌ‬
ْ ‫ـ‬
َ‫ﺗ‬ ‫ﻼ‬
َ ‫ﻓ‬
َ ۞ ‫ﻳُ ِﻨﻔ ُﻘﻮ َن‬
َ ً ٌ ُ
Tatajafa junoobuhum AAani almadajiAAi yadAAoona rabbahum khawfan
watamaAAan wamimma razaqnahum yunfiqoona ; Fala taAAlamu nafsun ma
okhfiya lahum min qurrati aAAyunin jazaan bima kanoo yaAAmaloona (Surat Al
Sajda 32:16-17)

Tafsir: Zimeachana Mbavu zao (kutoka) kwenye vitanda vyao wakimuomba Mola wao
kwa Khofu na Matumainio na wanatoa(Sadaka na Zakkah) kutokana na
tulivyowaruzuku. Hakuna Nafsi inayojua kile ambacho kimefichwa kutokana na
mtizamo unaotulizisha na kufurahisha macho. Malipo kutokana na kile walichokua
wakikifanya
963

Na kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaniuliza: ‘Jee nikuambie


kuhusiana na Ncha, Nguzo na Mhimili? Ni Jihad.’ Na kisha akaongezea: ‘Jee
nikuambie kuhusiana na kile ambacho kinachoumiza kila kitu?’ Nami nikasema:
‘Niambie ewe Na kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam’

Lakini mmoja kati ya wapanda Farasi akatukaribia, nami nikawa nakhofia kua
atamsababishia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kutojali juu ya suali hilo,
hivyo nami nikamuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam: ‘Ya Rasul Allah
(Salallahu Alayhi wa Salam) uliniambia kua: Jee nikuambie kuhusiana na kile
ambacho kinachoumiza kila kitu?’

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akautoa nje Ulimi wake na
kuugusaa na kusema: ‘Uweke huu chini ya Uthibiti’ nami nikauliza: ‘Jee tutaulizwa
juu yake?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Mama yako awe ni
mwenye kukupoteza wewe! Hivi jee unadhani kua watu wataingizwa Motoni kwa
sababu ya Nyuso zao? Au kwa sababu ya Pua zao? bali wataingizwa kutokana na
walichokichuma kwa ndimi zao’(Imam At Tirmidhii)



HITIMISHO LA JUZUU YA KWANZA.



Na hapa ndio tunafikia mwisho wa Juzuu ya kwanza ya Kitabu hiki cha Ulu ul Aazimin
Minna al Rusul ambayo ndani yake nimewazungumzia Mitume watatu kati ya Watano
wenye sifa hio ya kua na Azma Thabit Miongoni mwa Mitume ambao ni Nabii Nuh,
Nabii Ibrahim na Nabii Musa kama tulivyoona ambapo Manabii wawili waliobakia yaani
Nabii Isa Ibn Maryam na Nabii Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam basi In-shaa
Allah tutawazungumzia kwenye kitabu kitachofutia ambacho ni cha Juzuu ya Pili ya Ulu
ul Azmin Mina Rusul.

‫وﺎﺑﻪﻠﻟ اﻟﺘﻮﻓﻴﻖ واﳍﺪاﻳﺔ‬


Wa Billahi Tawfiq wa Al Hidaya!

MARUDIO YA VITABU VILIVYOTUMIKA KATIKA KITABU HIKI:



964

AL BURHANI FII ULUM UL QUR’AN – Shaykh Islami Imam Abu Abd Allah Badr
Ad Din Muhammad Ibn Abd Allah Ibn Bahadir Al Zarkashi Al Shafii.
AL DIWAN AL IMAM AL SHAFII – Mujaddid Ad Din Imam Abu Abd Allah
Muhammad Idris Al Shafii.
AL ITQAN FII ULUM UL QUR’AN – Mujaddid ud Din ImamAbu Fadhl Abd Rahman
Ibn Kamal Al Din Abi Baqr Ibn Muhammad Ibn Sabiq Al Din Jalal Ad Din Al Misri Al
Suyuti Al Shafii.
AL MUTAMMAD FI FIQH UL SHAFII – Imam Muhammad Al Zuhayly Ad Dimashq
Al Shafii.
AL RISALAT AL QUDSIYYAH FII QAWAID AL AQAID – Hujjat ul Islami Mujaddid
ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al
Shafii.
AR RUH AL MAÁNI FI TAFSIR AL QURAN AL ADHIM WA SABAA AL
MATHANI - Imam Abu Al Thana Shihab Din Sayyid Mahmud Ibn Abd Allah Al Husayn
Al Alusi Al Baghdadi Al Hanafi
ARAIS FI MAJALIS FI QASAS AL ANBIYAH – Imam Abu Is-haq Ahmad Ibn
Muhammad Ibn Ibrahim Al Thalabi Al Shafii.
BAYAN AL FARQ BAYN AL SADR WA AL QALB WA AL FUAD WA AL LUBB -
Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Ali Ibn Hasan Ibn Bashir Al Hakim Al Tirmidhi
Al Shafii.
FUSUS AL HIKAM – Shaykh Al Akbar Muhyi ad Din Imam Abu Bakar Ibn Arabi Al
Andalus Al Maliki.
HUJJAT UL BALIGHA - Mujaddid ud Din Qutb Ad Din Ahmad Shah Wali Allah Ibn
Abd Rahman Ibn Umar Ad Dahlawi
JAMI’I LI AHKAM AL QUR’AN- TAFSIR AL QURTUBI - Imam Abu Abd Allah
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi.
KITAB AL ARBAIN FI USUL AD DIN - Hujjat ul Islami Mujaddid ad Din Imam Abu
Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Shafii.
KITAB JAWAHIR AL QUR’AN - Hujjat ul Islami Mujaddid ad Din Imam Abu Hamid
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Shafii.
MAKHTUWATTI AL SIRR AL QUDUSIY FII TAFSIR AYATI AL KURSIY – Imam
Zayn Ad Din Mansur Ibn Abi Nasr Al Tablawi Al Azhari Al Shafii.
MASNAWI NURIYA - Baddiuzzamman Said Nursi Al Turkiy Al Hanafi.
MUFRADAT FI GHARIB AL QURAN - Allamah Abu Qasim Ibn Husein Ibn Mufadhal
Ibn Muhammad Raghib Al Isfahani.
QISAS AL ANBIYAAH- Allamah Nasiruddin Burhan Ad Din Al Rabghuzi.
TAFHIM AL QURAN – Allamah Sayyid Abu Ala Mawdudi Al Hanafi.
TAFSIR AL KABIR – MAFATIH AL GHAYB – Sultan al Mutakallimin Mujaddid ud
Din Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Umar Ibn Al Husayn Al Taymi Al Bakri Al
Tabaristan Fakhr Ad Din Al Razi Al Shafii.
965

TAFSIR AL KASHSHAF AN TAHQIQ AL TANZIL - Sultan Al Balagha Jarrah Allah


Imam Abu Al Qasim Mahmud Ibn Umar Ibn Ahmad Al Zamakhshari Al Hanafi Al
Mutazila.
TAFSIR AL MAWARDI AN NUQAT WA AL UYUN - Imam Abu Hasan Ali Ibn
Muhammad Ibn Habib Al Mawardi Al Shafii
TAFSIR AL QURÁN AL ADHIM – Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abdallah Al
Tustari Al Shafii
TARIKH AL RUSUL W AL MULUK– Imam Abu Jafar Muhammad Ibn Jarir at Tabari
Al Shafii
TAFSIR AL QASIMI AL MUSSAMA MAHASIN AL TA’WIL- Imam Jamal Al Din
Muhammad Al Qasimi Al Dimashq
TANBIH UL GHAFILIIN – Imam Abu Layth Nasir Ibn Muhammad Samarqandi
TARIKH AL KHULAFA – Mujaddid ud Din Imam Abu Fadhl Abd Rahman Ibn Kamal
Al Din Abi Baqr Ibn Muhammad Ibn Sabiq Al Din Jalal Ad Din Al Misri Al Suyuti Al
Shafii
THE HEART CODE BOOK: TAPING THE WISDOM AND POWER OF OUR
HEART ENERGY – Paul Pearsall, PhD



MARUDIO YA MTANDAO VILIVYOTUMIKA KATIKA KITABU HIKI


www.aliftaa.jo
www.dar-alifta.org
www.livingislam.com
www.muftiwp.gov.my
www.seekersguidance.com
www.sunnahmuakada.wordpress.com
www.questionsonislam.com

You might also like