JosephLeonard MadharaYaDhambi 8

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 6

Mwalimu Joseph Leonard is on Facebook.

To connect with Mwalimu Joseph


Leonard, join Facebook today.

Join

or

Log In

Mwalimu Joseph Leonard


15 August at 09:00 ·

*DHAMBI NA MADHARA YAKE*


Sehemu ya nane.
*6.DHAMBI INAMPA MLANGO SHETANI WA KUMTAWALA MTU*
Biblia inasema hivi
* 1 Yohana 3:8 atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa
kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.*
Ni hivi kila anaye tenda dhambi anakuwa mali ya shetani na mawakala wake usije ukalisahau hili.
* Ukianza kutenda dhambi ni sawa na umemfungulia shetani na mapepo mlango wa kuingilia kwenye
maisha yako*
NASEMA HIVI DHAMBI NI MLANGO WA SHETANI NA MAWAKALA WAKE WA KUINGILIA JUU YA
MAISHA YA MTU.
* Mtu anayefanya dhambi hawezi kumkimbia shetani*
Ataanzisha biashara hata hivyo mawakala wa shetani wakiamua kuivuruga, wataivuruga tu.
Atatafuta Pesa chuma ulete wakiamua kuichukua, wataichukua kiulani tu.
Ndoa yake wachawi wakiamua kuivuruga, itavurugika tu.
Mapepo yakiamua kuingia ndani yako, yataingia tu.
Wachawi wakiamua kukuroga nasema hivi utarogeka tu
* Kwahiyo kama unafanya dhambi za aina yoyote tambua kwamba haupo salama kiroho*
MTU ANAYETENDA DHAMBI TAFSIRI YAKE NI KWAMBA AMEMKATAA YESU MTOA UZIMA NA
AMEMTAKA SHETANI MUUAJI.
* Matendo 3:14 Bali ninyi mlimkana yule Mtakatifu, yule Mwenye haki, mkataka mpewe mwuaji;*
Kwahiyo dhambi ni mlango wa shetani anao utumia kuingia ndani ya watu ili AIBE, ACHINJE na
KUHARIBU
* Yohana 10:10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha
wawe nao tele.*
Nasisitiza tena hauwezi kuukimbia ubaya wa shetani maishani mwako kama haujaikimbia dhambi.
* Ukiishinda dhambi ni rahisi kumshinda shetani na mawakala wake pia.*
KUMBUKA:
Mahusiano Yetu na Mungu aliye hai ndiyo yanayotupa uwezo wa kumshinda shetani kwahiyo
ukikorofisha kwa Bwana sahau kumshinda shetani.
*CHAKUFANYA ILI UISHINDE DHAMBI INAYOMPA NAFASI SHETANI KWENYE MAISHA YAKO*
Mwalimu
1.Mpe Yesu Joseph
maisha yako Leonard
ili awe is mwokozi
Bwana na on Facebook. To connect
wa maisha yako. with
Mwalimu Joseph Leonard, join Facebook today.
2.Funga na kuomba kwaajili ya kufanya toba iletayo ondoleo la dhambi.
MWISHO.
Join
* Warumi 8:37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye
aliyetupenda.* or

Log In awabariki sana


Kwa leo niishie hapa na Mungu wa mbinguni
WhatsApp 0657117595
Mwl.Joseph Leonard

Recent post by Page

Mwalimu Joseph Leonard


23 mins ·

*DHAMBI NA MADHARA YAKE*


Sehemu ya Tisa.
*7.LENGO LA UJUMBE HUU*
Wakati tukiendelea kuona madhara ya dhambi ni vizuri pia tukaona lengo mhimu la Ujumbe huu.
Ujumbe una malengo yafuatayo.
*1.Kuwaandaa watu kwaajili ya unyakuo*
Tumaini kubwa tulilonalo kanisa ni ujio wa Yesu kutunyakua kwenda mbinguni.
Ni kanisa lipi litanyakuliwa ni hivi kanisa litakalonyakuliwa ni *kanisa safi* na *lisilo na dowa*,
*kanisa la watakatifu* ndiyo maana tunajifunza madhara ya dhambi ili watu waache dhambi kisha wawe
tayari kwaajili ya tukio kubwa la unyakuo ambalo kimsingi dalili zake zimeanza kuonekana.
Bibla inasema hivi.
* 1 Thesalonike 4:17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili
tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.*
Tunahubiriana, tunafundishana na tunaonyana kwa neno la Bwana yote haya ni kwasababu ya
kuwaandaa watu kwaajili ya unyakuo.
* Mtu mwenye dhambi hana sehemu katika unyakuo pindi parapanda ya Bwana itakapolia*
Mwenye sikio la kusikia na asikie
Lengo lingine la kukufundisha madhara ya dhambi ni hii.
*2.Kuyaandaa maisha yako yaliyo salama baada ya kufa*
Maana ya kifo.
* Kifo ni utengano kati ya mwili na roho.*
Yaani pale roho ya mtu inapotoka ndani ya mwili wake ni kifo
* Yakobo 2:26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo
imekufa.*
Kuna siku itafika Mimi Jose roho yangu itatoka ndani ya mwili Wangu hapo nitaitwa marehemu
* Hata wewe unayesoma Ujumbe huu kuna siku roho yako itatoka ndani ya mwili nawe utaitwa
marehemu *
Sote tuna imani yakuwa kuna siku itafika tutakufa lakini hata hivyo hatujui tutakapokufa tutakuwa katika
hali ipi?, hatujui tutakuwa katika hali ya mateso yasiyopimika au tutakuwa katika hali ya Amani
isiyopimika?, Hatujui tutakuwa katika hali ya kilio kisichopimika au tutakuwa katika hali ya furaha
isiyopimika? Anayejua haya yote ni Mungu pekee
* Lakini hata hivyo biblia imetupa ufahamu kwa kiasi juu ya ni kipi kinatokea pindi mtu anapokufa.*
Biblia inasema hivi.
* Waebrania 9:27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;*
Kwa mjibu wa haya maandiko utaona yakwamba mtu anapokufa * anapewa hukumu*
Nani mtoa hukumu
* 2 Timotheo 4:8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki,
atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.*
Kwenye haya maandiko Paulo mtume anamtaja Mungu kama *Bwana mhukumu mwenye haki* kwahiyo
atakaye mhukumu kila mmoja baada ya kufa ni Mungu.
* HUKUMU YA MUNGU NDIYO ITAKAYOAMUA UENDE MAHALI PEMA PEPONI AU UENDE MAHALI
PASIPO PEMA (motoni) KUTOKANA NA MAISHA YAKO YA HAPA DUNIANI*
Mwenye sikio la kusikia na asikie.
Sehemu nyingine biblia inasema hivi.
* Wagalatia 6:7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho
atakachovuna.*
Kama apandacho mtu ndicho atakachovuna maana yake ni kwamba kama ulipanda ubaya hapa duniani
baada ya kufa Mungu atakuhukumu ubaya pia, na kama ulipanda mema Mungu atakuhumu mema pia.
Mwenye sikio la kusikia na aendelee kutega sikio na asikie...
KWAHIYO WALE WALIOKWISHA KUFA HATA SASA KUNA WATU WAMESHALIPWA SAWA NA UBAYA
WAO NA KUNA WATU WAMESHALIPWA SAWA NA MEMA YAO WALIYOYAFANYA HAPA DUNIANI.
* Kuna watu Wapo kifuani mwa ibrahimu kama Razalo*
* Lakini pia kuna watu wapo kuzimu ya moto kama yule tajiri*
Fuatana nami katika maandiko haya
* Luka 16:19-25*
*19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula
sikuzote kwa anasa.*
*20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,*
*21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata
mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.*
*22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye
akafa, akazikwa.*
*23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na
Lazaro kifuani mwake.*
*24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini,
auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.*
*25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika
maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.*
Haya diyo matokeo ya hukumu kwa kila mtu pale anapokufa
* Kwahiyo lengo la Ujumbe huu ni kukuandaa pia kulala mahali pema peponi pindi umauti
utakapokupata*
Lengo la mwisho la Ujumbe huu ni hili lifuatalo.
*3.Ni ili utembee katika utimilifu wa baraka zako alizokukusudia Mungu ukiwa hapa duniani*
Mungu hambariki mwenye dhambi isipokuwa anawabariki watakatifu wake, wanaoishi kwa neno lake kila
iitwapo leo.
*WATAKATIFU WA MUNGU.*
Watamuita Mungu katika shida zao na Mungu atawaitikia na kuwajibu
* Zaburi 118:5 Katika shida yangu nalimwita Bwana; Bwana akanijibu akaniweka panapo nafasi.*
Watakatifu watamuita Mungu wao naye atawaitikia na kuwaonyesha mambo makubwa na mengine
wasiyoyajua
* Yerememia 33:3 Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu
usiyoyajua.*
Nasema hivi watakatifu wa Mungu watafuatwa na baraka za Mungu waingiapo na watokapo.
* Torati 28:6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.*
Kwahiyo ili baraka za Mungu ziwe juu yako nilazima uishi maisha mtakatifu ndiyo maana tunajifunza
madhara ya dhambi ni ili uikimbie dhambi kisha ukawe mrithi sawa sawa na ahadi za Bwana.
MWISHO.
* Warumi 8:28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale
wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.*
Kwa leo niishie hapa Mungu wa mbinguni awabariki sana
WhatsApp 0657117595
Mwl.Joseph Leonard

Mwalimu Joseph Leonard


15 August at 18:21 ·

LALA SALAMA WEWE NA FAMILIA YAKO YOTE KWA JINA LA YESU.

Mwalimu Joseph Leonard


15 August at 12:28 ·

MUNGU AMEAHIDI KUKUFANIKISHA IKIWA UTAKUBALI KUFUATA MASHARTI YAFUATAYO.


Kuangalia kuzitenda amri zake na Hukumu zake.
Kama umeomba kwa mda mrefu na haujajibiwa maombi yako si vibaya ukajitafakari kwa upya JE
UNAISHI KWA NENO LA MUNGU? AU MAISHA YAKO YAMEJAA USANII MWINGI? Ukijitafakari lazima
kuna maeneo haupo sawa sawa ndiyo maana mbingu zimekumyamanzia kimya.
MBIGU HAZIWEZI KUNYAMANZA KIMYA BILA SABABU, NASEMA HIVI JITAFUTE ULIPO, JITAFAKARI
HUENDA KUNA MAENEO KIROHO HAUPO SAWA SAWA.
Like, share na marafiki Ujumbe huu kuna watu Mungu anataka kusema nao.
WhatsApp 0657117595.

Related Pages
Michael J Moja
4K likes this
KARIBU UJIFUNZE NENO LA MUNGU UKUE KIROHO

Gospel Production
131K likes this
KARIBU KATIKA UKURASA HUU WA INJILI HAKIKA HAUTABAKI KAMA ULIVYO
ENDELEA KUSHARE POST ZETU NA...

Mch kalisti
11K likes this
Rev Kalisti

See More

You might also like