Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 9

Mwalimu Joseph Leonard is on Facebook.

To connect with Mwalimu Joseph

Leonard, join Facebook today.

Join

or

Log In

Mwalimu Joseph Leonard

2 hrs ·

*SABABU TATU MHIMU ZINAZOSABABISHA MTU ASHINDWE KUOMBA*

Sehemu ya tatu.
*3.KIFUNGO*
Kifungo ni sababu nyingine inayomfanya mtu ashindwe kuomba.
Biblia inatambua uwepo wa nafsi iliyo kifungoni
* Zaburi 142:7 Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka,
Kwa kuwa Wewe unanikirimu.*
Pia Biblia inatambua uwepo wa watu walioibiwa na kutekwa
* Isaya 42:22 Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo,
wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala
hapana asemaye, Rudisha.*
Kiroho Kuna watu wameibiwa na kutekwa na mapepo, wamo katika magereza ya kipepo, ni watumwa
wa shetani.
Biblia inaamini pia uwepo wa wafungwa.
* Mathayo 4:18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari
njema. Amenituma KUWATANGAZIA WAFUNGWA KUFUNGULIWA KWAO, Na vipofu kupata kuona tena,
Kuwaacha huru waliosetwa,*
Kuna watu ni wafungwa, nafsi zao zimo katika magereza ya kipepo hawa wanatakiwa watangaziwe
Habari ya kufunguliwa kwao.
* Kazi moja wapo ya damu ya Yesu ni kuwatoa mateka wote walio vifungoni, waliobanwa na nguvu za
Giza na kuwaingiza katika ufalme wa Mungu*
Maana imeandikwa
* Wakolosai 1:13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa
Mwana wa pendo lake;*
Kwanini nimekupitisha katika hii mistari ni ili ujue yakwamba mtu anaweza akawa mfungwa katika
ulimwengu wa kiroho na kimwili akashindwa kuwa huru kuyafanya mapenzi ya Mungu.
* Sasa nisikilize vizuri mpendwa ni hivi mtu akiwa mfungwa wa shetani atakuwa mtumwa wa shetani
pia na kwasababu hiyo kwa jinsi ya nje hawezi kuwa na Uhuru wa kuyafanya mapenzi ya Mungu aliye hai*
Maana imeandikwa hivi
* Yohana 8:44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye
alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake.
Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.*
Ukiwa mfungwa wa shetani utafanya tamaa za shetani tu
Mwalimu
Pia biblia inasemaJoseph Leonard is on Facebook. To connect with
Mwalimu
* 2 Kor 6:14 Joseph
Msifungiwe niraLeonard,
pamoja najoin Facebook
wasioamini, kwatoday.
jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana
urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?*
Join
Hakuna shirika kati ya nuru na Giza hivyo kama umefungwa na mapepo * ustarajie kuwa na ushirika na
Mungu aliye hai si rahisi hata kidogo, ndiyoor matokeo yake unatamani kuomba na unajitahidi kutumia
nguvu zote ili uombe lakini wapi*
Log In
NI HIVI MTU ALIYEFUNGWA NAFSI YAKE NA MAPEPO
* Hawezi kuomba, hawezi kusoma Biblia, hawezi kupenda ibada wala hawezi kuwa mcha Mungu
maana ni mtumwa wa shetani*
DALILI ZA MTU ALIYEFUNGWA NA MAPEPO KIROHO.
Huenda zipo dalili nyingi lakini Mimi nitakupa hizi chache nilizojaariwa na Mungu.
*1.Ndoto mbaya*
Maana imeandikwa hivi
* Ayubu 4:13-15*
* 13 Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo
wanadamu.*
*14 Hofu iliniangukia na kutetema, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote.*
* 15 Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu; Na nywele za mwili wangu zilisimama.*
2.Woga uliopita kiasi tena usio na sababu yoyote au moyo kwenda mbio.
Imeandikwa hivi
* 2 Timotheo 1:7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa
kiasi.*
Kama Mungu hakutupa roho ya woga maana yake ni kwamba * roho ya woga yatoka kwa yule mwovu
shetani, kwahiyo woga inaweza kuwa dalili ya kifungo*
3.Kujihisi kuwa huenda una kifungo.
* Moja ya jambo linaloweza kulifanya jambo fulani liwepo ni pale mtu anapoanza kuwa na mashaka ya
uwepo wa hilo jambo*
Washwahili wanasema hivi * lisemwalo lipo na kama halipo laja*
Kwahiyo unaweza wewe mwenyewe kwa kujipima au ukijitazama kiwango cha maisha yako halafu
ukawa na mashaka yakwamba huenda una kifungo, please ukiona unajishuku usidharau huenda kweli
unacho umefungwa na mapepo.
Maana imeandikwa hivi.
* Mithali 23:7 Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini
moyo wake hauwi pamoja nawe.*
Kwahiyo vile unavyojiona unaweza ukawa ndivyo ulivyo, chukua hatua.
Pia biblia inasema hivi
* Ayubu 3:25 BHN Kile ninachokiogopa kimenipata, ninachokihofia ndicho kilichonikumba.*
Analolihofia mtu linaweza kuwa ndilo lililomukumba.
* Kwahiyo ukijiona una mashaka yakwamba huenda una kifungo usidharau chukua hatua ya kulipeleka
hilo jambo kwa Yesu ili lipanguliwe*
4.Uvivu usio wa kawaida, uchovu usio wa kawaida, miayo isiyo ya kawaida na usingizi usio wa kawaida
pindi unapotaka kuomba au kusoma Biblia.
* hii pia ni miongoni mwa dalili za kifungo*
5.Kujisikia mzito kama vile kuna kitu umebeba, hii pia inaweza kuwa dalili ya kifungo.
* CHAKUFANYA KAMA UNA DALILI HIZI*
*1.Kama haujaokoka mpe Yesu maisha yako ili akuokoe kutoka katika nguvu za Giza*
*2.Funga na ufanye toba ya kweli kisha tumia uwezo ulionao mdogo wa kuomba kwaajili ya kuzipangua
hila za shetani maishani mwako*
*3.Unaweza kumtafuta pia baba yako wa kiroho ili akusaidie kuomba*
KUMBUKA.
*Usipochukua hatua ya kuzibomoa kwa jina la Yesu hila hizi za shetani ni ngumu kwako kuyafanya
mapenzi ya Mungu, mbaya zaidi maisha yako yatayumba katika baazi ya maeneo.*
MWISHO.
* Yakobo 4:7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.*
Mungu awabariki sana
WhatsApp 0657117595
Mwl.Joseph Leonard

Recent post by Page

Mwalimu Joseph Leonard

2 hrs ·

*SABABU TATU MHIMU ZINAZOSABABISHA MTU ASHINDWE KUOMBA*

Sehemu ya tatu.
*3.KIFUNGO*
Kifungo ni sababu nyingine inayomfanya mtu ashindwe kuomba.
Biblia inatambua uwepo wa nafsi iliyo kifungoni
* Zaburi 142:7 Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka,
Kwa kuwa Wewe unanikirimu.*
Pia Biblia inatambua uwepo wa watu walioibiwa na kutekwa
* Isaya 42:22 Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo,
wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala
hapana asemaye, Rudisha.*
Kiroho Kuna watu wameibiwa na kutekwa na mapepo, wamo katika magereza ya kipepo, ni watumwa
wa shetani.
Biblia inaamini pia uwepo wa wafungwa.
* Mathayo 4:18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari
njema. Amenituma KUWATANGAZIA WAFUNGWA KUFUNGULIWA KWAO, Na vipofu kupata kuona tena,
Kuwaacha huru waliosetwa,*
Kuna watu ni wafungwa, nafsi zao zimo katika magereza ya kipepo hawa wanatakiwa watangaziwe
Habari ya kufunguliwa kwao.
* Kazi moja wapo ya damu ya Yesu ni kuwatoa mateka wote walio vifungoni, waliobanwa na nguvu za
Giza na kuwaingiza katika ufalme wa Mungu*
Maana imeandikwa
* Wakolosai 1:13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa
Mwana wa pendo lake;*
Kwanini nimekupitisha katika hii mistari ni ili ujue yakwamba mtu anaweza akawa mfungwa katika
ulimwengu wa kiroho na kimwili akashindwa kuwa huru kuyafanya mapenzi ya Mungu.
* Sasa nisikilize vizuri mpendwa ni hivi mtu akiwa mfungwa wa shetani atakuwa mtumwa wa shetani
pia na kwasababu hiyo kwa jinsi ya nje hawezi kuwa na Uhuru wa kuyafanya mapenzi ya Mungu aliye hai*
Maana imeandikwa hivi
* Yohana 8:44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye
alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake.
Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.*
Ukiwa mfungwa wa shetani utafanya tamaa za shetani tu
Pia biblia inasema
* 2 Kor 6:14 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana
urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?*
Hakuna shirika kati ya nuru na Giza hivyo kama umefungwa na mapepo * ustarajie kuwa na ushirika na
Mungu aliye hai si rahisi hata kidogo, ndiyo matokeo yake unatamani kuomba na unajitahidi kutumia
nguvu zote ili uombe lakini wapi*
NI HIVI MTU ALIYEFUNGWA NAFSI YAKE NA MAPEPO
* Hawezi kuomba, hawezi kusoma Biblia, hawezi kupenda ibada wala hawezi kuwa mcha Mungu
maana ni mtumwa wa shetani*
DALILI ZA MTU ALIYEFUNGWA NA MAPEPO KIROHO.
Huenda zipo dalili nyingi lakini Mimi nitakupa hizi chache nilizojaariwa na Mungu.
*1.Ndoto mbaya*
Maana imeandikwa hivi
* Ayubu 4:13-15*
* 13 Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo
wanadamu.*
*14 Hofu iliniangukia na kutetema, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote.*
* 15 Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu; Na nywele za mwili wangu zilisimama.*
2.Woga uliopita kiasi tena usio na sababu yoyote au moyo kwenda mbio.
Imeandikwa hivi
* 2 Timotheo 1:7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa
kiasi.*
Kama Mungu hakutupa roho ya woga maana yake ni kwamba * roho ya woga yatoka kwa yule mwovu
shetani, kwahiyo woga inaweza kuwa dalili ya kifungo*
3.Kujihisi kuwa huenda una kifungo.
* Moja ya jambo linaloweza kulifanya jambo fulani liwepo ni pale mtu anapoanza kuwa na mashaka ya
uwepo wa hilo jambo*
Washwahili wanasema hivi * lisemwalo lipo na kama halipo laja*
Kwahiyo unaweza wewe mwenyewe kwa kujipima au ukijitazama kiwango cha maisha yako halafu
ukawa na mashaka yakwamba huenda una kifungo, please ukiona unajishuku usidharau huenda kweli
unacho umefungwa na mapepo.
Maana imeandikwa hivi.
* Mithali 23:7 Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini
moyo wake hauwi pamoja nawe.*
Kwahiyo vile unavyojiona unaweza ukawa ndivyo ulivyo, chukua hatua.
Pia biblia inasema hivi
* Ayubu 3:25 BHN Kile ninachokiogopa kimenipata, ninachokihofia ndicho kilichonikumba.*
Analolihofia mtu linaweza kuwa ndilo lililomukumba.
* Kwahiyo ukijiona una mashaka yakwamba huenda una kifungo usidharau chukua hatua ya kulipeleka
hilo jambo kwa Yesu ili lipanguliwe*
4.Uvivu usio wa kawaida, uchovu usio wa kawaida, miayo isiyo ya kawaida na usingizi usio wa kawaida
pindi unapotaka kuomba au kusoma Biblia.
* hii pia ni miongoni mwa dalili za kifungo*
5.Kujisikia mzito kama vile kuna kitu umebeba, hii pia inaweza kuwa dalili ya kifungo.
* CHAKUFANYA KAMA UNA DALILI HIZI*
*1.Kama haujaokoka mpe Yesu maisha yako ili akuokoe kutoka katika nguvu za Giza*
*2.Funga na ufanye toba ya kweli kisha tumia uwezo ulionao mdogo wa kuomba kwaajili ya kuzipangua
hila za shetani maishani mwako*
*3.Unaweza kumtafuta pia baba yako wa kiroho ili akusaidie kuomba*
KUMBUKA.
*Usipochukua hatua ya kuzibomoa kwa jina la Yesu hila hizi za shetani ni ngumu kwako kuyafanya
mapenzi ya Mungu, mbaya zaidi maisha yako yatayumba katika baazi ya maeneo.*
MWISHO.
* Yakobo 4:7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.*
Mungu awabariki sana
WhatsApp 0657117595
Mwl.Joseph Leonard

Mwalimu Joseph Leonard

Mwalimu Joseph Leonard
Yesterday at 04:50 ·

*SABABU TATU MHIMU ZINAZOSABABISHA MTU ASHINDWE KUOMBA*

Sehemu ya pili.
*2.HUKUMU YA MOYO*
Sababu nyingine inayosababisha mtu ashindwe kuomba ni *hukumu ya moyo*
* Moyo unapomhukumu mtu husababisha huyo mtu kukosa ujasiri wa kusogea mbele za Mungu
kwaajili ya kupeleka mahitaji yake*
Biblia inasema hivi
* 1 Yohana 3:21 Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu;*
Kama biblia inasema mioyo yetu isipotuhukumu tuna ujasiri kwa Mungu kinyume chake nikuwa *
MIOYO YETU IKITUHUKUMU HATUWEZI KUWA NA UJASIRI KWA MUNGU*
Nasema hivi hauwezi ukawa na ujasiri wa kumuomba Mungu wakati moyo wako unakuhumu.
Huenda bado haujanielewa namaanisha nini ngoja niongeze volume kidogo.
* UNAPOSIKIA HATIA MOYONI MAANA YAKE NI KUWA ROHO MTAKATIFU ANAKUJULISHA
YAKWAMBA KUNA DHAMBI UMEIFANYA UWE UNAJUA AU HAUJUI*
Maana kazi moja wapo ya Roho mtakatifu ni kumthibitishia mtu kwamba amekosea kuhusu dhambi.
* Yohana 16:8 BHN Naye atakapokuja atawathibitishia walimwengu kwamba wamekosea kuhusu
dhambi, uadilifu na hukumu ya Mungu.*
Matokeo yake ni kwamba kama wewe ni mzinzi, muasherati, muongo, mwizi, mgomvi, mtukanaji,
mchawi, mshirikina n.k unashindwa kuwa na ujasiri wa kumuomba Mungu maana moyoni mwako
unaisikia hatia inayokuhumu
NARUDIA TENA HAUWEZI UKAWA NA UJASIRI WA KUOMBA WAKATI MOYO WAKO MWENYEWE
UNAKUZOMEA NA KUKUONA MNAFIKI KWASABABU YA TABIA ZAKO MBAYA ZA SIRINI.
* MOYO WAKO UKIKUHUMU SHUGHURI ZOTE ZA KIROHO HAUWEZI UKAWA NA UJASIRI WA
KUZIFANYA, HATA UKIZIFANYA HAUWEZI KUZIFANYA KATIKA UBORA UNAOTAKIWA*
Kama kuna hatia ndani ya moyo utajitahidi kuhubiri, kuimba, kufundisha neno au kuomba lakini
utashindwa tu, na hata ukiweza hautafanya katika ubora unaotakiwa.
* Haya yote ni matokeo ya uovu kukuhumu moyoni*
JAMBO LA KUFANYA ILI UWE NA UJASIRI WA KUSIMAMA MBELE ZA MUNGU.
* Ni kufanya Toba ya kweli ikibidi kwa kufunga na kuomba*
Mwakasege aliwahi kusema hivi *"Kazi mojawapo ya Toba ni kukuingiza katika msimu mpya wa
kuburudishwa*
Maana imeandikwa hivi
* Matendo 3:19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa
kuwako kwake Bwana;*
Kwahiyo ili moto wa kuomba uingie ndani yako unahitaji kufanya Toba ya kweli ili hatia iondoke, kisha
moyoni mwako ibakie shwari kuu.
* Narudia tena kama unasikia hatia moyoni mwako pindi unapotaka kuomba bila kujali unajua makosa
yako au haujui wewe Fanya Toba utashangaa ghafla unalipuka moto wa maombi moyoni mwako*
MWISHO.
* Waebrania 4:16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya
kutusaidia wakati wa mahitaji.*
Kwa leo niishie hapa hadi kipindi kijacho, Mungu awabariki sana
WhatsApp 0657117595
Mwl.Joseph Leonard

Mwalimu Joseph Leonard

20 August at 09:58 ·

*SABABU TATU MHIMU ZINAZOSABABISHA MTU ASHINDWE KUOMBA*

Watu wengi sana wanatamani wawe waombaji lakini tatizo linakuja pale wanapotaka kuchukua hatua
hapo ndipo wengi wanaposhindwa kuomba.
* Watu wengi inapofika wakati wanataka kuomba ghafla hujikuta wanapata uvivu usio wa kawaida,
uchovu usio wa kawaida, usingizi usio wa kawaida au miayo isiyo ya kawaida jambo ambalo linawafanya
wabakie kuliona suala la kuomba kama ndoto kwao*
Nini sababu zinazopelekea mtu ashindwe kuomba
* Kwanini iwe rahisi kwa mtu kuimba bongo fleva kwa masaa hata mawili, au aangalie TV kwa masaa
hata matano lakini ashindwe kuomba walau hata nusu saa shida nini hapa lazima kuna tatizo kubwa
hasa kiroho*
Huenda zipo sababu nyingi zinazosababisha mtu ashindwe kuomba lakini Mimi nitakupa hizi tatu MHIMU
nilizojaariwa na Roho wa Mungu.
*1.Mwili*
Sababu ya kwanza inayosababisha mtu asiombe ni mwili.
* Mwili huwa haupendi mtu ayafanye mapenzi ya Mungu*
Biblia inasema hivi
* Warumi 8:7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala
haiwezi kuitii.*
Nachotaka uone hapa ni neno * NIA YA MWILI NI UADUI JUU YA MUNGU*
Kwahiyo nia iliyopo ndani ya mwili wa mtu huwa haitaki kuyafanya mapenzi ya Mungu ndiyo sababu
unajikuta unataka kuomba lakini nia ya mwili inakugomea.
Sehemu nyingine imeandikwa hivi.
* Wagalatia 5:17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa
maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.*
Kwa maana nyingine tunaweza kusema hivi
* Nia ya mwili ni kuipendeza dunia lakini nia ya Roho ni kumpendeza Mungu kwahiyo nia ya mwili na
Roho zinapingana kiasi cha kwamba mtu hawezi kufanya anachotaka*
Matokeo yake nikwamba unajikuta unataka kuomba lakini nia ya mwili inakugomea, inakataa kata,
kata wewe usiombe.
MWILI UKIKATAA UNAJIKUTA UNAKUWA MTUMWA WA MWILI BADALA YA KUWA MTUMWA WA
MUNGU, UNAJIKUTA UNAFANYA LILE USILOLIPENDA LAKINI ULIPENDALO HAULITENDI.
* Warumi 7:14-15 & 24*
*14 Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini
ya dhambi.*
*15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.*
* 24 Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?*
Kwahiyo usishangae unapenda kusoma biblia lakini hausomi, unapenda kuomba lakini hauombi hii ni
kwasababu nia ya mwili inakugomea.
Pia Biblia inasema hivi.
* Mathayo 26:41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.*
Mwili ni mdhaifu siku zote wala hautaki kumpendeza Mungu kwahiyo ili uyafanye mapenzi ya Mungu
nilazima utafute kuushughurikia mwili, vinginevyo hauwezi kuyafanya mapenzi ya Mungu.
*JINSI YA KUISHUGHUKIA NIA YA MWILI ILI UWEZE KUOMBA.*
Njia ni moja tu ni kuenenda kwa msaada wa Roho mtakatifu.
* Wagalatia 5:16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.*
Jinsi ya kuenenda kwa Roho.
* Ni kuruhusu ujazo wa nguvu za Roho mtakatifu ndani yako*
Usipojazwa nguvu za Roho mtakatifu si rahisi kuishinda nia ya mwili.
Maana imeandikwa hivi.
* Wafilipi 4:13 BHN Naweza kuikabili kila hali kwani Kristo hunipa nguvu.*
Kama hauna nguvu za Roho mtakatifu ndani yako tafuta kujazwa ili uweze kuishinda nia ya mwili.
*MWISHO.*
*“Nakuombea Mungu akujaze kwa nguvu zake kuanzia sasa na yale yaliyokushinda ukapewe kuyaweza
kwa jina la Yesu”*
Kwa leo niishie hapa na Mungu awabariki sana .
WhatsApp 0657117595
Mwl.Joseph Leonard

Related Pages

Michael J Moja
4.3K likes this
KARIBU UJIFUNZE NENO LA MUNGU UKUE KIROHO

Thobias & Navoneiwa Kiwalu-Mamre Ministry

1.8K likes this
Utainua misingi ya vizazi vingi"(Isaya 58:12)

Mch kalisti
11K likes this
Rev Kalisti

See More

You might also like