Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 16

NADHARIA ZA TAFSIRI

Nadharia ni mfumo wa mawazo na maarifa yanayofasili taaluma mahususi. Pamoja na


kubainisha maana ya taaluma, nadharia hutumika wa kueleza mtazamo wa falsafa zake, data na
vifua vya uchambuzi, mbinu na taratibu za utafiti. Naza ni mambo yanayouiana.

Kwa kawaida nadharia ya taaluma moja hufuma kwa mitazamo mingi. Nadharia ya tafsirini
mfumo wa mitazamo mitatu ambazo huchangiana kwa kusafiri maana ya tafsiri, kubainisha
vikwazo na kutoa mwongozo wa utaratibu wa kutafsiri. Mitazamo mikuu iliyotambulika ni:

1. Isimu- linganisha katika jamii


2. Isimu-jamii katika jami
3. Mawasiliano katika jamii

Isimu- linganishi

Katika tafsiri isimu ni taaluma ya kisayansi inayozingatia lugha kama mfumo wa sauti, ambao
huwasilisha maana, huku ikitawaliwa na sharia za kisarufi.

Lazima maana wasilishwa pia kuhaliwe na wenyeji wa lugha.

Mwanzilishi wa nadharia hii ni catford(1965). Anahimili nadharia yake kwa hoja nne

a) Nadharia ya tafsiri huzingatia uhusiano Fulani baina ya lugha


b) Kazi ya tafsiri nikitendo cha kukutanisha lugha mbili
c) Tafsiri ni uwakilishi wa matini ya lugha moja kwa matini ya lugha nyingine.
d) Wajibu wa mtafsiri ni kutafta visawe vya kugha chasili katika lugha ya pokezi

Catford na wenzake wanasisitiza kuwa tunapotafsiri tunalinganisha sarufi za lugha mbili. Wana-
nadharia hawa, huwa hivyo wanazingatia tafsiri kwa mitazamo ya isimu-linganishi. Kulingana
na mtazamo huu, ufanisi wa tafsiri unategemea msomi aliyemiliki lugha mbili. Kimatamshi na
kimaandishi.

Kwa mujibu wa catford, daraj nne za umilisi wa lugha huhusika na ambazo ni nanga nne za
tafsiri:

i) Grafolojia
ii) Fonolojia
iii) Leksia
iv) Sarufi

Daraja hizi ni nanga nne tafsi

i) Grafolojia

Ni taaluma ya mwandiko, yaani uwakilishi wa maandishi na sifa za mifumo ya hati andishi.


Tafsiri grafolojia, kwa hivyo ni uwakilishi wa hati za mfumo tofauti.

Tumezoea kuandika nambari kwa hati za mifumo miwili: wa kiarabu na wa kirumi

Tutalingifiria mifumo hii za hati za nambari kwa tafsiri mbili miaka:

a) Kiarabu- kirubi
1950-mcml
b) 2021-mmxxi

Taaluma ya fonolojia inazingatia muundo, sifa na ruwaya za sauti zinavyotumika bayana na


lugha kwa jumla.

Taafsiri fonolojia huwakilisha sauti na ruwaza za sauti za lugha chasili kwa zile linganifu za
lugha pokezi. Matumizi ya tafsiri fonolojia hujitokeza katika utohozi wa mikono kama:

Kingereza------------kiswahili

a) radio redio
b) television televisheni

mageuko ya sauti hulenga kuridhisha kanuni husika huashiria tofauti za muundo wa leksia za
kingereza za Kiswahili

ii) leksia

ni mfumo wa maneno yenye maana ya kimsingi ya lugha moja. Mfumo wa maana za kimsingi
pamoja na kimaumbo ambazo huwakilisha maana hizo zote huitwa leksia. Tafsiria leksia ni
uwakilishi wa maana za kimsingi za lugha poleni. Zingatia uwakilishi wa kitaliki

 kiingereza
a course in translation is of great help to all language students
 Kiswahili
Kozi in tafsiri ni yenye manufaa mengi to wanafunzi lugha wote

Ni muhimu kutambua kuwa

Kiingereza na Kiswahili hutofautiana katika mipangilio ya maneno hufuata kanuni za sarufi

iii) Sarufi

Ni mfumo wa sharia unaotawala maumbo ya maneno na muundo wa sentesi. Hivi I vipengele


vya sarufi ambvyo hulingana na taaluma za mofolojia na sintaksia.

Tafsiri sarufi hata hivyo inarejelea maneno ambazo hutumika kwa kuunda sentesi bila yenyewe
kubeba maana za kimsingi. Hizi ni tafsiri kama

 Kiingereza
A course in translation is of great help to all language students
 Kiswahili
Course of translation is yenye great help kwa language students wote

Zingatia: maneno hujigawa majupo mawili mapana: ya kileksi

Ya kimuundo

Leksia ni kama nomino na kitenzi, neon muundo ni kama kiunganishi na kibainishi

Tafsiri hizi zina manufaa kwa mwanafunzi kwa kuzingatia viwango tofauti vya isimu, na hapo
kumulika vipengele vya lugha ambavyo havina budi kuchunguzwa kwingineko, utaratibu
mahususi unaweza kufaa taaluma za leskografia, pedolojia ya lugha na bila shaka isimu
linganishi yenyewe

Kitenzi neno-muundo ki kama kiunganishi na kibainishi

Tafsiri hizi zina manufaa kwa mwanafunzi kwa kuzingatia viwango tofauti vya isimu ,na hapo
kumulika vipengele vya lugha ambavyo havina budi kuchunguzwa kwingineko,utaratibu
mahususi unaweza kufaa taaluma za leskografia,pepedagojia ya lugha na bila shaka isimu-
linganishi yenyewe.
Utaratibu uliopemdekezwa ,hata hivyo,una matatizo kwa tafsiri.tunapotafsiri hatufuati hatua hizi
ila tunakabili matini kamilifu na kutafsiri maana yake sio yale maneno.

Tukitafsiri maneno yenyewe,kama vile nadharia inapendekeza kutokuwemo kwa matatizo kama
ukosefu wa visawe,utata wa maana upotovu wa maana na mahali katika tafsiri.wasomi
watambua umuhimun mkubwa wa nadharia ya isimu linganishi ,hususamchango wa catford
mwenyewe.nadharia hii inawakilisha jaribio la kwanza la kufafanua sayansi ya tafsiri,mtazamo
wake ,hata hivyo unamkuza sana mtafsiri kwa kumfunga na viwango vya muundo wa
lugha.inafaa nadharia impe mtafsiri uhuru Zaidi wa kutafsiri maana mtazamo uliojaribu kufanya
hivyo ni wa isimu jamii.

2.isimu jamii

Katika tafsiri isimu jamii ni taaluma inayofuma maarifa na haja za sosholojia kwa zile za
isimu.Kwa kawaida,taaluma hii hujaribu kufafanua uwiano wa mahusiano ja kijamii na
matumizi ya lugha .Isimu jamii katika tafsiri yazingatia sana umuhimu wa utamaduni kwa
utekelezi wa tafsiri.Miongoni mwa waasisi wake mashuhuri ni mtaaluma Eugene Nido(1974).

Nido na wenzake wamejenga nadhalia yao kufuatia matatizo ya tafsiri za biblia.Matatizo haya
yaletwa na vikwazo vya wingi wa lugha,tamaduni,waadishi na wasomaji.

Wingi wa lugha mahususi:chanzo cha mgongano wa miundo ya lugha.

Wingi wa tafsiri:chanzo cha migongano ya mitindo na mitazamo ya waaandishi.

Tofauti ya wasomaji:chanzo cha migongano ya tajiriba ya kijamii na kitamaduni.

Migongano hii inaashiria mikinzano mintarafu miundo na mitindo ya lugh a zenyewe,misingi ya


tamaduni,mitindoo ya waandishi,mtawalia,kulingana na mikinzani hii,nadhalia ya tafsiri yafaa
kuweza kujihimili kwa kuzingatia hoja nne za wamilifu wa lugha.

Matumizi ya lugha huwiana na mifumo ya mawazo,mielekeo na falsafa za watu.Maana ya


maneno hutegemea tajriba na mifumo ya utamaduni.lugha ni guzo ya utamaduni sio chombo cha
mawasiliano tu.Hoja hizi kutetea kauli moja;kuwa kigezo imara Zaidi cha ufanuzi wa tafsiri ni
weledi wa mifumo ya utamaduni zina husika.kwa kutambua kuwa utamaduni ni dhana
changamano,nadharia imeitafsiri kwa kupambanua vipengele vitano:
Utamaduni ekolojia

Utamaduni mali

Utamaduni watu

Utamaduni dini

Utamaduni lugha

i. Utamaduni ekolojia

Ni ujuzi,mielekeo na falsafa zinazozaliwa na tajiriba ya mazingira za kiasilia,hususa hali ya


hewa kama vile majira ya angu,mandhari ya misitu,nyika,jangwa au bahari,ulalo wa nani kama
vile milima,mabonde au neni tambulale.

Tafsiri ya sentensi ifuatazo lahitaji ujuzi ya majira ya anga;mfano people living in the cold
climates experience four seasons in the year;spring ,summer,winter and autumn.

ii.utamaduni mali

ni jumla ya vitu vilivyoundwa na jamii buzana,kwa minajili ya urahisi wa kazi na maisha kwa
jumla.Hivi ni vitu kama vile mavazi vyakula,magari,majengo.utamaduni maliunajujenga
kutokana na utamaduni ekolojia na pia kudhihirisha maendeleo kiteknolojia.

Tafsiri sentensi hii inahitaji weledi wa mijengo;

Mfano –we had hoped to rent a bungalow to find a maisonete.

iii.utamaduni watu

hurejelea falsafa za kanuni za mahusiano ya kijamii,hususa yale ya muundo wa mfumo wa


familia,mwelekezo wa malezi,taasisi za serikali na utawala na taratibu za anasa na
starehe.Utahitaji kuelewa utamaduni wa mwafrika vizuri,ndio ufanikiwe kwa tafsiri ya kauli
kama ;I was rushing to meet my half-brother.

iv.utamaduni dini

unahusu mafunzo na desturi zinazofasiri Imani kuhusu mungu miungu au uungu wa


madhehebubayana.Hata hivyo mafunzo mengi ya kidini huimarishwa kwa kurejelea tajriba za
maisha ya kawaida na vipengele vingine vya utamaduni.kauli ifuatayo ilirejelea utamaduni wa
maakuli wa mayahudi na labda wazungu wengi

v.utamaduni lugha unabainika kwa matini amilifu na tanzu za fasihi andishi,fasihi simuliziz
pamoja na matumizi ya aina mbalimbali ya semi teule ya nadharia za fasihi huzingatia fasihi
kama kielelezo cha tajriba ya kijamii.Nafasi ya tajriba za jamii hujtokeza katika semi teule
kama vile methali lingaisha maudhui ya semi

a.kiingereza

one rotten apple spoils the whole barrel.

b.kiswahili

Nazi mbovu haraby ya nzima.

Pamoja na maudhui katika fasihi,mitazamo,asasi na mbinu za mawasiliano hutegemea


mahitaji,mwelekeo na matavajio ya hadhira.

Mawsiliano hayana budi kuamilisha leksia kwa njia mwafaka mtafsiri anapotafuta visawe
Zaidi,huanza kwa kufikiria maana za leksia.Leksia ni kimuli bora Zaidi cha utamaduni kuliko
vipengele vingine vya lugha.Mifumo ya leksia hukua kupitia ujenzi wa Nyanja mbalimbali za
utamanduni.kutokana na nafasi kubwa ya utamaduni katika matumizi ya lugha ,mtafsiri hana
budi kuzikabili tamaduni za lugha zote mbili,na kuvidhabiti vipengele vyote vya leksia ya kila
lugha inayohusika.

Nadharia hii inasisitiza kuwa maneno ni ishara za sifa Fulani za kitamaduni .Kwa hivyo maana
na matumizi ya maneno hutegemea tajriba mwelekeo na falsafa za wenye lugha.

Mtazamo wa isimu jamii katika tafsiri umefanikiwa kutoa uhuru Zaidi kwa mtafsiri.udhaifu
wake umo katika kule kulemewa kwa utamaduni.

Nadharia za tafsiri inahitaji kusonga mbele na kutoo uhuru Zaidi kufikiria mitindo na mikitadha
ya mawasiliano.Mitazamo uliofikiria jambo hili Zaidi ya mawasiliano.

Ingawa nadharia imebadilika,kutofautisha vitengo vya utamanduni ni muhimu kutambua ya


kwamba utamaduni ni mfumo mmoja,kitengom kimojakinaathiri kinaathiri na kutegemea
kingine.
Mawasiliano katika tafsiri

Ni utaratibu wa kuhamisha ujumbe kutoka kwa mwasilishi hadi kwa mdokezi.indgawa kuna
mitazamo mingi ya nadharia ya mawasiliano tafsiri hurejelea mitazamo mingi ya naharia ya
mawasiliano,tafsiri mtazamo wa kitamaduni kulingana na mtazamo huu,utaratibu wa
mawasiliano hutuma vigezo vitano vya kimsingi.

Mwasilishi

Mdokezi

Ujumbe

Chombo

Vikwazo

a.mwasilishi

ni mwadishi/msomaji,msisitizo umo katika msimamo wake.

b.mpokezi

ni msomaji/msikilizaji;msisitizo huwekwa katika tajriba yake.

c.ujumbe

hisisitiza dhamira ya mwasilishi.

d.chombo

Ni lakabu ya lugha;ya maandishi,mazungumzo au ishara.

e.vikwazo

hurejerea matatizo mintarafu muktadha wa mawasiliano na utamaduni.

Mtazamo huu husisistia uwakilishi,upokezi,utathmini an ukuharifu wa ujumbe kwa hadhira ya


tafsiri.

Mahitaji ya utavatibu huu yashirikisha nguzo sita za mawasiliano.

a.kanuni za mitindo na matumizi ya lugha zote mbili.


b.mitindo ya sasili za matini

c.mifumo mahususi ya tamaduni za lugha zote mbili

d.dhamira ya matini au mwadishi

e.tajriba za kijamii na kitamaduni za mpokezi.

f.matarajio ya mpokezi.

Mawasiliano katika tafsiri ni mtazamo fasirivu Zaidi uliojaribu kukosoa mitazamo ya kiisimu.

Mtazamo huu,kwa hivyo haujisimamii ila umerejelea nadharia za kiisimu na kutoa mapendekezo
ya kuboresha tafsiri.mapendezo hayo hupewa hadhi ya nadharia.

Nadharia ya mawasiliano yatanguliza mapendekezo yake kwa kushambulia nadharia za kiisimu.

Lawama kubwa inayotolewa ni kule kutegemea muundo wa utamaduni wa lugha cha asili.

Lawama ya pili imo katika kule kusisitiza tafsiri za savufi na leksia.

Kuliingana na mtazamo wa mawasiliano,nadharia za kiisimu zafanana licha ya tofauti za


msisitizo.

Mfano huu wajitokeza viwango vitatu;

Mtafsiri ajifunzga Zaidi na miundo na mitindo ya lugha chasili.tena ajaribu kuwakilisha maana
kwa kuvejelea Zaidi mikitadha ya lugha chasili.

Tafsiri yajijenga katika utamaduni wa lugha chasili yaani,kiini cha uhalisia wa maana ni sura za
utamaduni wa lugha chasiri.

Tafsiri hutathmini Zaidi mitindo za mwandishi asilia kulika mahitaji ya hadhira.

Kwa jumla tafsiri mawasiliano yashuku kule kulemewa katika suva za muundo,mitindo na
utamaduni wa lugha chasili.

Kwa hivyo,hiki ndikyo chanzo cha upotovu wa maana kwa vile upotovu wa maana huletwa na
utamaduni..Nadharia za kiisimu kwa hivyo,hazina uwezo wa kufasiri maana.Badala yake
zzaonekana kama zamwelekeza mtafsiri kubadikisha maana ,ili tuweze kutafsiri maana,twahitaji
kubaini ujumbe ujumbena dhamiva ya mwandishi ,kishake tuwasilishe ujumbe huo katika tafsiri
kwa kurejelea tajiviba ya msomaji wa tafsiri.

Tafsiri mwasiliano inahimili na kuimarika kwa kuzingatia hoja nne zifuatazo;

i.chochote ambacho hueleweka pia kina uwezo wa kutafsiriwa an basi kutafsiriwa.

ii.Hamna visawe vya kudumu maana ya maneno hudumu katika hali ya mabadiliko.

iii.tunatafsiriusemi wa lugha .usemi wa lugha inavyoyumiwa katika hali halisis ya


mawasiliano.maneno ni ishara na viwakilishi vya maana,sio maana yenywewe.

Tunatafsiri ili kumdhihirisha msomaji wa tafsiri.tunabadilika kujifunga na muundo,mitindo na


utamaduni wa lugha pokezi.

Licha ya kunagalia matumizi ya kanuni za savufi ya lugha bayana,pamoja na mahitaji ya


kitamaduni,mtafsiri ategema hali halisi ya usemi ili afasiri ujumbe kwa ufanikivu.hoja muhimu
ni kuwa unaweza kujua lugha lakini usielewe kile kichachozungumziwa.

Ni muhimu kuchunguza hali halisis ya mawasiliano ili kuepsusha hatari ya upotovu ya maana
ya kimiliki ufanikivuu wa tafsiri.

Tafsiri itakuwa imefanikiwa ikifikia kuwa kiwakilishi halisi cha ujumbe wa matini chasili.

Mtazamo,mchangowa mawasiliano umechangia nadharia ya tafsiri kwa kuleta maswala ya


sasili,muktadha na hali halisis ya mawasilinao pamoja na kusisitiza umuimu wa ujumbe
wenyewew na mpokezi wa ujumbe.

Upunguvu wake mkubwa Zaidi mnoumo kwa kule kupuuza umuhimu wa msingi ya sarufi na
utamaduni.ukweli in kuwa uhalisia wa ujumbe mara nyingi hutegema falsafa za lugha na
utamaduni.

Sawia mitazamo mingine kwa hivyo ,tafsiri mawasiliano in amchango wake pia na lawama
zake.Ili umnufaishe mtasiri unafaa kutumia pamoja na mitazamo ya kiisimu kwa kuzama katika
nadharia zote tunapatana na mbinu toshelevu Zaidi za kukabli vikwazo vya tafsiri.

Kw ajumla,kila kitu moja ya mitazamo mitatu ya nadharia ya tafsiri ina mihimili yake na pia
upungufu.Mwelekeo wenye busara utakuwa wa kutambua mchango wa kila mtazamo,kwa
madhumni ya kushirikisha katika tafsiri zetu.isitoshe kila mtazamo umemilikia mbinu za
kukabili maadhui ya vikwazo vya tafsiri.

Muhtasari

Somo hili limeangalia nadharia ya tafsiri kutambua mitazamo mitatu inayojijenga;

Isimu linganishi katika tafsiri

Isimu jamii katika tafsiri

Mawasiliano katika tafsiri

Kila mtazamo una mchango na pia udhaifu.mitazamo yote kwa hivyo inafaa kutumika kwa
kutavatibu tafsiri kulingana na aina ya matini.

Vikwazo vya tafsiri kitangulizi

Mitazamo tofauti ya nadharia ya tafsiri yaafiki uwa mtafsiri anakumbwa na vikwazo vingi.

Mtafsiri afaa kujihadhali na vikwazo hivi ili atafakari njia za kuvikumbali leo tujaribu vikwazo
vikuu vya tafsiri.

Malengo ya somo

Mnammo mwisho wa somo hili utamiliki ujuzi wa:

Kutafsiri dhana ya vkwazo vya tafsiri

Kubainisha vikwazo vikuu vya tafsiri

Kudhihirisha athari za kila kikwazo

Kupendekeza masuluhisho

Shabaha ya tafsiri ni kuhifadhi ,maan ana mguso wa matini chasiri.manna ni dhana nzito inazo-
jumuisha ujumbe,dhamiva na mtindoo wa mwandishi chasili.

Unahifadhi wa maana huvitwa kanuni ya mguso sawa.

Tafsiri ,hata hivyo mava nyingi hulaumiwa kwa upungufu wake kuliko kusifiwa kwa mafanikio
yake.lawama kubwa Zaidi ya tafsiri ni upotovu wa maana.
Upotovu wa maana huletwa na vikwazo vya tafsiri.kikwazo ni kigezo chochote ambacho
hutatiza ufanikivu wa kazi mahususi.

Vikwazo vine vikuu ni:

Tofauti za miundo ya lugha

Tofauti za mitindo ya lugha

Tofauti za tamaduni

Tofauti za mitazamo ya waadishi

1.tofauti za miundo ya lugha

Hapo awali tulitambua viwango vine vya muuundo wa lugha:leksia,sarufi,fonolojia na


grafolojia.Viwango muhimu Zaidi vya mjandala huu ni vya leksia na sarufi.Tafsiri nyingi
hutatizika katka mikutano ya mifumo ya leksia na kanuni za kisarufi.

Katika kuangalia mifump ya leksia tunazingatia mahusiano na matumizi ya maana msingi,kwa


kawaida lugha hutofautiana kwa nmana ambavyo zaamilisha maana msingi.Baadhi ya tofauti
kati ya Kiswahili na kiingereza zajitokeza katika matini hizi:

Kisw-nimevunjika mkono

Kiingereza-I have broken my arm/hand.

Matini hizi zaonyesha tofauti mbili,kwanza maana za kiingereza zimebainishwa Zaidi ya zile za
Kiswahili.pale ambapo kiingereza kina leksi mbili’arm’ na ‘hand’ au atumia arm kwa maana ya
mkono.pili kuna ukinzano wa mwelekeo wa dhana ya kuumia.kauli ya Kiswahili yyashiria kuwa
mtu kamili ameumia sio mkon tu,ilivyo katika usemi wa kiingereza.

Tofauti ya mwelekeo kuhusu maana inajitokez katikka falsafa ya ndoa.katika


Kiswahili,mwanaume huoa naye mwanamke anaolewa.kiingereza hukubalia wote wawili
kuoa.kwa matumizi haya maana hii imeranda uwanda mpana Zaidi-lakini maana za kiingereza
zimejitofautisha Zaidi kwa upande mwingine.mfano kiingereza

English-he married his sister


Kisw- alimwoa nduguye

She married her brother

Alimwoa nduguye.

Isipokuwa msemaji arejelea ndugu mkubwa,yaani dada au kaka,leksia ya Kiswahili haitoautishi


jinsia hata katika matumizi mengi ya lugha,Kiswahili hufafanua maana Zaidi kuliko
kiingereza .Haya ni matumiziz kama;

Kiingereza kiswahili

Africa barani afrika

In Kenya nchini Kenya

In nairobi mjini Nairobi

Matumizi ya kiusishi(ni) yaashiria tofauti nyingine muhimu kati ya sarufi za Kiswahili na


kiingereza.kiswahili hutuma mofu nyingi kwa neno moja ilhali maneno mengi ya kiingereza ni
mosimu mojamoja.Yaani lugha hizi hutofautiana kuegemea moflojia ambishi Zaidi au mofolojia
bainishi Zaidi imtawalia Zaidi ya hayo sintaksia za lugha hizi hukinzana katika kanuni za
upatano wa kisarufi,inavyojitokeza katika kauli;

Kiswa-vitabu vingi vilivyotafsiriwa ni za fasihi

Kiingereza-many translated books are literacy

Kulingana na mifano hizi,ni wazi kuwa upatano wa kisarufi hugusa viungo vingi vya sentensi za
Kiswahili lakini kitenzi pekee katika zile za kiingereza.pamoja na tofauti za kisarufi kila lugha
ina semi teule kama vile mafumbo,methali,vitendawili,nahau na tamathali za usemi.

Semi za lugha bayana hurejelea tajriba za kitamaduni.

Mfano kiswa- mzuri kama malaika

Kiingereza-as good as gold

Kufanana kama mapacha

As alike as two peas


Mifano hii inaonyesha wazi tofauti zilizomo za tofauti za matumizi za semi kati ya Kiswahili na
kingereza.kila matini linganifu inachukuliwa kuwa visawe lakini maneno yaliyotumika
hayarejellei maana za kawaida.mtafsiri anabidika kuelewa matumizi sahihi ya kila usemi kwa
kuzingatia ujumbe huo na muktadha mwafaka wa matumizi,mambo haya yasipozingatiwa
,tafsiri itapotosha maana.

Semi za lugha hujumuika katika uwanja wa maana ambatano.Maana ambatano hutumika pale
ambapo matini hufasiriwa mzimamzima bila kuchanganua maana zinazojumuika matumizi ya
maana ambatano ni kaida ya mizungumzo ya kawaida.lugha ianpo angaliwa hivi pia huitwa
mtindo ya lugha.

Swali

Bainisha viwango vya ukinzano wa sarufi kwa kulinganisha matumizi ya lugha mbili.

Tofauti za mitindo ya lugha

Pia huitwa sasiliza lugha.dhana ya sasili hunusika iwapo matumizi ya mitindo ya lugha
hulingana na mahitaji ya taaluma bayana,kama vile isimu fasihi,sharia,matibabu na uhadisi.sajili
vilevile hueleza sura bainifu za muktadha pana wa mawasiliano na mfungano wa kijamii.Baadhi
ya mikitadha pana ani mazungumzo ya biashara na mafuma ya dini.

Sasili hubainika kupitia mbinu tatu kuu za matumizi ya lugha.mbinu hiziz ni

i.uteuzi wa msamiati

ii.muundo wa maumbo ya sentensi

iii.na muwala wa matini

muundo wa sentensi unahusu sharia za usarifu na ukabalifu nayo maumbo hueleza mahusiano ya
vishanzi vya tungo moja.

Mtiriko wa matini nao hufuma manna na ujumbe kupitia ukinzani wa mitindo ya


lugha,ytunabansiha vikwazo vya tafsiri

a.isitilanii
b.majina ya kudumu na unukuzi

c.mafumbo na semi zalugha

d. ruwaza za maumbo

a)istilahi ni maneno ya kiufundi yaani maneno zenye maana maalum mintarafu somo au taaluma
bayana.huenda pia maneno haya yakawakilisha maana dhamia kulingana na sasili yake.Tatizo la
istilahi hutokea pale ambapo mojawapo ya lugha mbili in sajili nyingi Zaidi kutegemea
maendeleo ya elimu na teknolojia.Huenda pia sajili moja,hasa za sayansi imestawi kadri kubwa
Zaidi katika lugha chasili tofauiti na lugha pelezi.Hiki ni kusema kuwa maana zake
zimebainishwa kiwango kikubwa.

Hali kadhalika ,istilahi huwa nyingi kuliko zile za lugha isiyofikia kiwango sawa.

Mtafsiri wa Kiswahili anatatizwa na baadhi ya istilahi.Anabidika kueleza maana hizi au kutohoa


istilahi za kiingereza.neno lililotoka lugha nyingine na kutoholewa ,kama vile fonetiki huitwa
neno-mkapo.

Lexical –leksia

Langue-sarufi mingi

Parole –sarufi milifu

Grammatical system-mfumo wa kisarufi

Zingatia kuwa neno sarufi tayari ni mkopo kutoka kiarabu,ishara ya kuwa maelezo ya Kiswahili
yanatumia istilahi kutoka lugha tofauti.hali hii inazua shida Zaidi kwa matni yenye mtazamo
wakihistoria.Pamoja na tatizo la istilahi sasili za sayansi sawa na ile za sharia hubeba tatizo la
maumbo ya sentensi.

Matini za kiufundi na kisayansi huwa zimeshidiliwo maumbo ya sentensi changamano.inakuwa


vingumu kuwa mtafsiri kudhabiti mifumo ya mawazo katika matini za sajili hizi na vigumu Zaidi
kutafsiri kwa ufanikivu.

Isitoshe matini nyingi za kisheria zilizoandikwa kwa kiingeraza, hutumia mkopo sisisi kutoka
kifaransa. Fikiria makini kama:
Kenya is born a defacto and a multiparty state.

Ugumu wa mattini hii umo katika dhana mbili: defacto na dejure.

- Labda dhana hizi zitafisiriwe kuwakilisha maons za kikweli na kisheria , au kihalisia na


kihalali mtawalia? Ili ujarikiwe kutafsiri matini kama hii vizuri inakubidi uelezwe vizuri
mada yenyewe na hat somo kamilifu linalohusika.
- Pengine utumie kamusi ya kitaalamu, kamusi maalum za sheria.

Kwa jumla hii ni kanuni ya tafsiri za matini, taalamu, n ahata taarifa za habari ni majina
maalaum.

b. majina maalum ni majiina ya kudumu kama yale yanayoita watu, wanyama, mahali,
mandahari za nchi, mito, milima. Majina hayo hutofautishwa kisarufi na yale ya kawaida. Jina la
kawaida linafuata sharia za kisarufi, hasa zile za maumbo na mageuzi ya maneno. Jina maalum
halibaniwi na vikwazo vya muundo wa sarufi. Badala yake, usemi huzingatia misumo ya maana.

Kinadharia kwa hivyo , majina maalum yamo nje ya sharia za sarufi. Nogana maelezo ya kisimu
kama yale ya kunkuni za umoja- wingi kwa hivyo ni mahali kutafsiri majina haya. Kuna tafsiri
ambazo tayari hutumiwa. Ishara ya kuwa tafsiri kama hizo tayari zimekubaliwa na jamii ya lugha
dokezi. Tafsiri hizi ni kama: Jesus-Yesu

Joseph-yusufu

Lucy- lucia

Mary- maria

Ingawa majina ya kudumu yamo nje za kanuni za sarufi yenywe, utohozi wa majina haya
umefuata sharia Fulani za mfumo wa sauti. Kila sauti ya J(j), kwa mfano hugeuka kuwa (y).huku
kunaitwa kudhoofu kwa sauti . la muhimu Zaidi ni kuwa kila jina la Kiswahili linafungwa kwa
sauti ya vokali, na muundo wa maneno umefululiza sauti za konsonanti vokali(kv). Hii ni kanuni
muhimu ya masomo ya mfumo wa sauti za Kiswahili.

Zingatia- vokali mbili zilizofululiza nithili ya tamati mwa maria na lucia, hutambuliwa kuwa
sauti mseto: hutamkwa kwa muda sawa na ule wa vokali moja sahili.
Hata kama jina limetoholewa huna ruhusa ya kulitafsiri iwapo mwenyeji huitwa kwa ile za
kigeni. Mhusika akiwa lucy, kwa mfano atabaki lucy na sio lucia.

Kuandamana na majina ya kudumu kwa majina za masharika haya kwa kawaida huwa mkururo
wa maneno yanayofasili asili au jukumu la shirika . mtafsiri hana mbinu nyingine ya kuwakilisha
majina haya ila kuwa tafsiri sisisi.

Mara mingi tafsiri hiyo huambatanishwa akionimu ya lugha chasili ili maana itambulike kwa
urahisi.

Miambatanisho kama hii ina lengo la kurahisisha mawasiliano lakini kwa kufanya hivyo,
inapuza kipengele kimoja cha muundo na womilifu huu wa sarufi ya Kiswahili. Wamilifu huu
wahusu kielezi kihusishi kinavyorejelea mahali.

Lugha ya kingereza inasalia mahitaji kama haya kwa rowaza za shahada katika kiingereza ina
ubanifu wa kilekea, kionetiki na kipragramatiki. Swala la kipragramatiki linahusika kwa wingi
katika lugha ya mafumbu.

c. mafumbo na semi za lugha mara nyingi hutumiwa kwa makusudi ya kushadidi ujumbe Fulani.
Hivi ni kusema kuwa msomaji ana hiari za kutumia lugha nyepesi za kawaida lakini akihiari
kuamilisha ile nzito. Tulivyoona hapo awali lugha ya mafumbo ni msemo kutoka lugha mbili
hata kutoka lugha moja, inazuu ukinzano. Nahau hizi zina ukinzano, ingawa zote hurejelea maan
aya kufa:

kila moja ya semi hizi inadhamiria lengo fulanni. Lengo hilo laweza kuwa arifa halisi, kuonyesha
huzuni n ahata mzana. Lengo bayana huenda na mguso wake. Mtafsiri anahitaji kubaini mguso
wa kauli mahususi ili aepushe upotovu wa maana.

Waandishi wengi wamezungumzia matumizi ya methali kila lugha ina methali ambazo hunakidi
tajiribu ya kitamaduni au kijamii ya wenyeji. Kwa vile tasiriba ya binadamu ina ulinganifu wa
kiwango Fulani, baadhi ya maana za methali hulingana licha ya misemo hioy kutumia maneno
tofauti.

You might also like