Professional Documents
Culture Documents
User Guide Nokia 7 2 User Guide
User Guide Nokia 7 2 User Guide
User Guide Nokia 7 2 User Guide
2
Mwongozo wa mtumiaji
Toleo 2021-04-13 sw
Nokia 7.2 Mwongozo wa mtumiaji
Yaliyomo
2 Anza kutumia 6
Vitufe na sehemu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 6
3 Misingi 15
Arifa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15
Dhibiti sauti . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16
Redio ya FM . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17
Picha za skrini . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 19
Ufikiaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 19
Maisha ya betri . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 19
Simu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 21
Anwani . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 21
Tuma ujumbe . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 22
Barua . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 22
Tangamana na watu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 23
5 Kamera 24
Misingi ya kamera . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 24
Rekodi video . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 25
6 Intaneti na miunganisho 29
Amilisha Wi-Fi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 29
Vinjari wavuti . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 30
Bluetooth® . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 31
NFC . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 33
VPN . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 34
Tarehe na saa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 36
Saa ya kengele . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 36
Kalenda . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 37
8 Ramani 38
Hifadhi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 43
Misimbo ya ufikiaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 46
Simu za dharura . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 51
Uchakataji upya . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 53
Watoto wadogo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 55
Magari . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 56
Hakimiliki na ilani . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 58
Muhimu: Kwa maelezo muhimu kuhusu matumizi salama ya kifaa na betri yako, soma maelezo
ya ”Kwa usalama wako” na ”Usalama wa Bidhaa” katika mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji,
au kwenye www.nokia.com/support kabla utumie kifaa. Ili kujua jinsi ya kuanza kutumia kifaa
chako kipya, soma mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji.
2 Anza kutumia
Sasisha simu yako na ukubali visasisho vinavyopatikana vya programu ili upate vipengee vipya
na vilivyoboreshwa vya simu yako. Kusasisha programu kunaweza pia kuboresha utendakazi wa
simu yako.
VITUFE NA SEHEMU
Simu yako
Mwongozo huu wa mtumiaji unatumika kwa modeli zifuatazo: TA-1196, TA-1181, TA- 1178,
and TA-1193.
3. Maikrofoni
Baadhi ya vifaa vya ziada vilivyotajwa katika mwongozo huu wa mtumiaji, kama vile chaja, kifaa
cha kichwa, au kebo ya data, huenda vikauzwa kando.
Muhimu: Skrini ya kifaa na kifuniko cha nyuma imetengenezwa kwa glasi. Glasi hii inaweza
kuvunjika kifaa kikiangushwa mahali pagumu au kupokea mgongano mzito. Glasi ikivunjika,
usiguse sehemu za glasi za kifaa au ujaribu kuondoa glasi iliyovunjika kutoka kwa kifaa. Acha
kutumia kifaa hadi glasi ibadilishwe na mhudumu aliyeidhinishwa.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Sehemu nyingine za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke
kadi za mkopo au kadi nyingine zenye mkanda wa sumaku karibu na kifaa kwa kipindi cha muda
mrefu, kwa kuwa kadi hizo zinaweza kuharibika.
1 Kisaidizi cha Google hupatikana katika masoko na lugha zilizoteuliwa. Ambapo hakipatikani
Kisaidizi cha Google hubadilishwa kwa Utafutaji wa Google. Angalia upatikanaji katika
https://support.google.com/assistant.
1. Fungua trei ya SIM na kadi ya kumbukumbu: sukuma pini ya kufungua trei ndani ya shimo
la trei na uondoe trei. Tumia pini ya kufungua trei pekee iliyotolewa katika kifurushi cha
mauzo. Pini zingine za kufungua trei zinaweza kuharibu kifaa.
2. Weka nano-SIM kwenye kipenyo cha 1 kwenye trei na eneo la mguso likiangalia chini. Ikiwa
una simu yenye SIM mbili, telezesha SIM ya pili kwenye kipengo cha 2 kwenye trei eneo la
mguso likiangalia chini.
Muhimu: Usiondoe kadi ya kumbukumbu wakati programu inaitumia. Kufanya hivyo kunaweza
kuharibu kadi ya kumbukumbu na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Kidokezo: Tumia kadi ya kumbukumbu ya microSD yenye kasi, na ya hadi GB 512 kutoka kwa 1
mtengenezaji anayefahamika.
Tumia kadi halisi ya nano-SIM tu. Matumizi ya SIM kadi zisizotangamana huenda yakaharibu kadi au kifaa,
na huenda yakaharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Chaji betri
Simu yako inakubali kebo ya USB ya C. Pia unaweza kuchaji simu yako kutoka kwenye kompyuta
kwa kutumia kebo ya USB, lakini inaweza kuchukua muda mrefu zaidi.
Kama betri imeisha moto kabisa, huenda ikachukua dakika kadhaa kabla ya kiashiria chaji
kuonyeshwa.
Wakati unapowasha simu yako kwa mara ya kwanza, simu yako hukuelekeza usanidi
miunganisho ya mtandao na mipangilio ya simu yako.
1. Kuwasha simu yako, bonyeza na ushikilie kitufe cha nishati hadi simu iteteme.
2. Wakati simu imewashwa, chagua lugha na eneo lako.
3. Fuata maagizo yaliyoonyeshwa kwenye simu yako.
Huwezi kuhamisha data kutoka kwenye simu yako ya zamani hadi kwenye simu yako mpya kwa
kutumia akaunti ya Google
Ili kuhifadhi nakala ya data kwenye simu yako ya zamani kwenye akaunti yako ya Google, rejelea
mwongozo wa mtumiaji wa simu yako ya zamani.
Ikiwa simu yako ya awali ilikuwa ya Android, na uhifadhi nakala ya akaunti ya Google kwayo,
unaweza kurejesha mipangilio ya programu yako na manenosiri ya Wi-Fi.
1. Gusa Mipangilio > Mfumo > Mipangilio ya kina > Hifadhi nakala rudufu .
Ikiwa una toleo la SIM mbili, unaweza kuwa na SIM 2 kwenye simu yako, kwa mfano, moja ya kazi
yako na nyingine ya matumizi yako ya kibinafsi.
Kwa mfano, wakati unapiga simu, unaweza kuchagua ni SIM gani ya kutumia kwa kugusa kitufe
kinacholingana cha SIM 1 au SIM 2 baada ya kupiga nambari hiyo.
Simu yako huonyesha hali ya mtandao ya SIM zako kitofauti. SIM kadi zote zinapatikana kwa
wakati mmoja wakati kifaa hakitumiki, lakini wakai SIM kadi moja inatumika, kwa mfano, wakati
wa kupiga simu, ile nyingine inawezakosa kupatikana.
Hutaki kazi iingiliane na muda wako huru? Au una muunganisho wa bei nafuu wa data kwenye
SIM moja? Unaweza kuamua ni SIM gani unayotaka kutumia.
Kiwa unataka kuepuka kupiga simu kwa makosa wakati simu yako iko kwenye mfuko au begi
lako, unaweza kufunga vitufe na skrini yako.
Bonyeza kitufe cha nishati, na utelezeshe juu kwenye skrini. Ukiulizwa, toa hati tambulishi za
ziada.
Muhimu: Epuka kugwara skrini ya mguso. Usitumie kamwe kalamu, penseli halisi, au kitu
kingine chenye ncha kali kwenye skrini ya mguso.
Weka kidole chako kwenye kipengee kwa sekunde chache, na utelezeshe kidole chako kwenye
skrini.
Pitisha
Weka kidole chako kwenye skrini, na utelezeshe kidole chako kwenye mweleko unaotaka.
Telezesha kidole chako kwa haraka katika mwelekeo wa juu au chini kwenye skrini, na uinue
kidole chako. Ili kukomesha kutembeza, gusa skrini.
Weka vidole 2 kwenye kipengee, kama vile ramani, picha, au ukurasa wavuti, na utelezeshe
vidole vako vikiwa kando au pamoja.
Kufunga skrini katika hali ya wima, telezesha chini kutoka upande wa juu wa skrini, na uguse
Zungusha kiotomatiki .
• Ili kuona programu zote za programu, • Ili kufunga programu, ipitishe juu.
telezesha juu kitufe cha nyumbani � na
kisha ukitelezeshe juu tena. • Ili kufunga programu zote zilizofunguliwa,
telezesha kulia kupitia programu zote, na
• IIi kwenda kwenye skrini ya mwanzo, gusa uguse FUTA ZOTE .
kitufe cha mwanzo. Programu uliyokuwa
ukitumia hubakia imefunguliwa chinichini. • Ili kurejesha kwenye skrini ya awali
uliyokuwa, gusa kitufe cha nyuma �. simu
• Ili kuona ni programu gani ulizofungua, yako hukumbuka programu na tovuti zote
pitisha juu kwenye kitufe cha mwanzo. ulizotembelea tangu wakati wa mwisho
• Ili kubadilisha kwa programu nyingine skrini yako ilipofungwa.
iliyofunguliwa, pitisha kulia.
Unatazama video, picha, kusoma vitabu za mtandaoni au kucheza michezo kwenye simu yako?
Kuona skrini vizuri, washa hali ya nguvu ili kurekebisha rangi, utofautishaji, na mwangaza
kulingana na matumizi yako.
Gusa Mipangilio > Onyesho > Mipangilio ya Kina > PureDisplay , na uwashe Hali ya nguvu .
Ili kuchagua programu ambazo zinatumia hali ya nguvu, gusa Mipangilio > Onyesho >
Mipangilio ya Kina > PureDisplay > Hali ya Nguvu . Chagua hali, kwa mfano, Picha na
uwezeshe programu kwenye orodha
Ikiwa unataka kuboresha ubora wa rangi kwenye skrini yako katika mazingira yenye
changamoto ya mwangaza, washa Usawazishaji weupe wa kiotomatiki .
Ikiwa unataka kuona maelezo zaidi kwenye skrini yako, washa SDR kuwa HDR (kiwango wastani
ya nguvu kuwa kiwango cha juu cha nguvu). Hii hubadilisha maudhui yako yote ya SDR kuwa
ubora wa HDR katika hali halisi.
3 Misingi
ARIFA
Unapopokea arifa mpya, kama vile ujumbe au simu zisizojibiwa, aikoni ya kiashiriaji huonekana
kwenye upau wa hali juu ya skrini. Ili kuona maelezo zaidi kuhusu arifa, kokota chini upau wa
hali. Ili kufunga mwonekano, pitisha juu kwenye skrini.
Ili kufungua paneli ya arifa, kokota upau wa hali chini. Ili kufunga paneli ya arifa, pitisha juu
kwenye skrini.
Ili kubadilisha mipangilio ya taarifa ya programu, gusa Mipangilio > Programu na arifa > na
uguse jina la programu ili ufungue mipangilio ya programu. Gusa Arifa . Unaweza kuzima au
kuwasha arifa kwa kila programu kivyake.
Kidokezo: Ili kuona nukta za arifa, gusa Mipangilio > Programu na arifa > Arifa na
ubadilishe Ruhusu nukta za arifa kwa washa. Nukta ndogo itaonekana kwenye ikoni ya
programu, ikiwa una arifa, lakini bado hatujaishughulikia. Gusa na ushikilie ikoni ili kuona
chaguo zinazopatikana, Unaweza kugusa arifa ili kuifungua, au telezesha ili kupuuza.
Kidokezo: Ili kuweka kitufe cha nishati/kufunga kumweka unapopokea arifa kutoka kwa
programu, gusa Mipangilio > Programu na arifa > Mipangilio ya kina > Taa ya arifa . Kitufe
cha nishati/kufunga kitamweka ikiwa una arifa, lakini bado hujaishughulikia.
Ili kuamilisha vipengele, gusa ikoni za mipangilio ya haraka kwenye paneli ya arifa. Ili kuona ikoni
zaidi, kokoa menyu chini.
Ili kupanga upya ikoni, gusa �, gusa na ushikilie ikoni, na uikokote kwenye eneo lingine.
DHIBITI SAUTI
Badilisha sauti
Ikiwa una tatizo la kusikia simu yako ikiita katika mazingira yenye kelele, au simu ina sauti ya
juu, unaweza kubadilisha sauti kama upendavyo kwa kutumia vitufe vya sauti upande wa simu
yako.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Bonyeza kitufe cha sauti upande wa simu yako ili uone upau wa hali ya sauti, gusa �, na
ukokote kitelezi kwenye upau wa sauti kwa midia na programu kushoto au kulia.
Ili kuweka simu kuwa kimya, bonyeza kitufe cha kupunguza zaidi, gusa � ili uweke simu yako
kutetema pekee na uguse � ili kuiweka kimya.
Dokezo: Hutaki kuweka simu yako katika hali kimya, lakini huwezi kujibu sasa hivi? Ili
kunyamazisha simu inayoingia, bonyeza kitufe cha kupunguza sauti. Pia unaweza kuweka simu
yako kunyamazisha mlio wakati unapochukua simu: gusa Mipangilio > Mfumo > Ishara >
Nyamazisha ikichukuliwa , na uwashe.
Ikiwa unataka kuweza kukataa simu inayoingia kwa kupindua simu, gusa Mipangilio > Mfumo
> Ishara > Pindua ili ukatae simu , na uwashe.
REDIO YA FM
Kusikiliza redio, unahitaji kuunganisha vifaa vinavyotangamana vya sauti kwenye simu. Vifaa vya
sauti hufanya kazi kama antena.
Sikiliza redio ya FM
Kidokezo cha utatuzi: Ikiwa redio haifanyi kazi, hakikisha kifaa cha kichwa kimeunganishwa
vizuri.
Jifunze jinsi ya kuandika maandishi kwa haraka na vizuri kwa kutumia usahihishaji matini wa
kibodi.
Simu yako hupendekeza maneno unapokuwa ukiandika, ili kukusaidia kuandika kwa haraka na
kwa usahihi zaidi. Mapendekezo ya maneno yanaweza kutopatikana katika lugha zote.
Wakati unapoanza kuandika neno, simu yako itapendekeza maneno yanayowezekana. Neno
unalotaka likionyeshwa kwenye upau wa mapendekezo, chagua neno. Ili kuona mapendekezo
zaidi, gusa na ushikilie pendekezo.
Dokezo: Ikiwa neno lililopendekezwa limewekwa alama ya koza, simu huitumia kiotomatiki
ili kubadilisha neno uliloandika. Ikiwa neno si sahihi, gusa na ushikilie ili kuona mapendekezo
mengine machache.
Ikiwa hutaki kibodi kupendekeza maneno unapokuwa ukicharaza, zima sahihisho za matini.
Gusa Mipangilio > Mfumo > Lugha na ingizo > Kibodi pepe . Teua kibodi unayotumia kwa
kawaida. Gusa Usahihishaji matini na uzime mbinu za kusahihisha matini ambayo hutaki
kutumia.
Sahihisha neno
Ukigundua ya kwamba umekosea tahajia ya neno, gusa ili kuona mapendekezo ya kusahihisha
neno.
Gusa Mipangilio > Mfumo > Lugha na ingizo > Mipangilio ya kina > Kikagua tahajia , na
uzime Tumia kikagua tahajia .
Kisaidizi cha Google hupatikana katika masoko na lugha zilizoteuliwa pekee. Ambapo
hakipatikani, Kisaidizi cha Google hubadilishwa kwa Utafutaji wa Google. Angalia upatikanaji
katika https://support.google.com/assistant. Kisaidizi cha Google kinaweza kukusaidia kwa
mfano, kutafuta maelezo mtandaoni, kutafsiri maneno na sentensi, kuandika vidokezo na
uteuzi wa kalenda. Unaweza kutumia Kisaidizi cha Google hata wakati simu yako imefungwa.
Hata hivyo, Kisaidizi cha Google hukuomba ufungue simu yako kabla ya kufikia data yako ya
kibinafsi.
Ili kufikia huduma za Kisaidizi cha Google, tumia kitufe cha Kisaidizi cha Google upande wa simu
yako:
Ikiwa nchi au eneo lako halikubali Kisaidizi cha Google, bado unaweza kutumia kitufe cha
Kisaidizi cha Google:
Kuzima Kisaidizi cha Google, gusa Mipangilio > Google > Tafuta, Usaidizi na Sauti >
Kisaidizi cha Google . Upande wa juu ya skrini, gusa Kisaidizi , chagua kifaa chako, na uzime
Kisaidizi cha Google .
PICHA ZA SKRINI
Ili kupiga picha ya skrini, fungua paneli ya arifa, na ukokote upau wa hali kuelekea chini. Gusa
Nasa skrini . Unaweza kutazama picha zilizonaswa katika Picha .
UFIKIAJI
Unaweza kubadilisha mipangilio mbalimbali ili kufanya kutumia simu yako kuwa rahisi.
2. Gusa Ukubwa wa maandishi . Ili kuongeza au kupunguza ukubwa wa fonti, kokota kitelezi
cha kiwango cha ukubwa wa fonti.
2. Gusa Ukubwa wa skrini na urekebishe ukubwa wa mandishi, kokota kitelezi kiwango cha
ukubwa wa skrini.
MAISHA YA BETRI
Pata mengi kutoka kwa simu yako ukipata maisha ya betri unayotaka. Kuna hatua unazoweza
kuchukua kuokoa nishati kwenye simu yako.
Kuokoa nishati:
Hali ya ndege hufunga miunganisho kwenye mitandao ya simu za mkononi na huzima vipengele
pasiwaya vya kifaa chako.
SIMU
Piga simu
1. Gusa �.
3. Gusa �. Ikiwa umeingiza SIM ya pili, gusa aikoni inayolingana ili kupiga simu kutoka kwa SIM
maalum.
Jibu simu
Kataa simu
ANWANI
Ongeza jina
TUMA UJUMBE
Tuma ujumbe
Kidokezo: Ikiwa unataka kutuma picha katika ujumbe, gusa Picha , gusa picha unayotaka
kushiriki, na uguse �. Chagua Barua pepe .
BARUA
Unaweza kutuma barua kwa kutumai simu yako ukiwa mahali popote.
Wakati unatumia programu ya Gmail kwa mara ya kwanza, utaulizwa usanidi akaunti yako ya
barua pepe.
1. Gusa Gmail .
2. Unaweza kuchagua anwani iliyounganishwa na akaunti yako ya Google au gusa
Ongeza anwani ya barua pepe .
3. Baada ya kuongeza akaunti zote, gusa NIPELEKE KWA GMAIL .
Tuma barua
TANGAMANA NA WATU
Je, unataka kuunganika na kushiriki vitu na watu katika maisha yako? Ukiwa na programu ya
jamii, unaweza kupashwa ni nini kinachofanyikia marafiki wako.
Programu za jamii
Ili kuendelea kuwasiliana na marafiki na familia yako, ingia katika huduma zako za utumaji
ujumbe, kushiriki, na mitandao ya jamii. Chagua huduma unayotaka kutumia kutoka kwenye
skrini yako ya Mwanzo. Programu za jamii zinapatikana kwenye Duka la Google Play . Huduma
zinazopatikana huenda zikatofautiana.
5 Kamera
MISINGI YA KAMERA
Je, kwa nini ubebe kamera ya kando kama simu yako ina kila kitu unachohitaji ili kunasa
kumbukumbu? Kwa kutumia kamera ya simu yako, unaweza kupiga picha au kurekodi video kwa
urahisi.
Piga picha
Piga picha nzuri na maridadi – nasa nyakati bora katika albamu ya picha yako.
1. Gusa Kamera .
3. Gusa �.
Jipige picha
Unahitaji kujipiga picha nzuri? Tumia kamera ya mbele ya simu ili kupiga picha hiyo.
1. Gusa Kamera .
4. Gusa �.
Kwa kuongezea picha binafsi kamili, unaweza kupiga picha iliyogawanywa skrini kwa kutumia
kamera ya simu yako. Tumia kamera zote za mbele na nyuma kwa wakati mmoja.
Dokezo: Unapopiga picha ndani ya picha au kurekodi video ya picha ndani ya picha, na
unataka kusogeza picha ndogo, gusa na uishikilie na uikokote mahali unapotaka.
1. Gusa Kamera .
Kwa Lenzi ya Google, unaweza kutumia kitafuta lengo cha kamera yako kwa mfano kutambua
vitu, kunakili maandishi, kuchanganua misimbo, na kutafuta idhaa sawa.
1. Gusa Kamera .
2. Gusa � > �.
3. Elekeza kamera yako kwa kitu unachotaka kutambua, na ufuate maelezo kwenye skrini.
Dokezo: Unaweza tumia Lenzi ya Google kwa picha ambazo tayari umepiga. Gusa Picha , gusa
picha, na uguse �.
REKODI VIDEO
Rekodi video
Unaweza kurekodi video ya skrini iliyogawanywa kwa kutumia simu yako. Tumia kamera zote za
mbele na nyuma kwa wakati mmoja.
1. Gusa Kamera .
3. Gusa � Mbili kwa video iliyogawanywa skrini. Au, kurekodi video ya picha ndani ya picha,
gusa � P-I-P .
Tumia hali tofauti katika kamera yako ili kuboresha ubora wa picha zako.
Katika programu ya Kamera, gusa � ili kujifunza mengi kuhusu kila mpangilio.
Kama unataka kuweza kubadilisha eneo lengwa la picha yako baada ya kuipiga na kuweka
ukungu nyuma ya picha yako, tumia athari ya bokeh wakati unapiga picha. Hariri picha yako
kwa kutumia Kihariri cha Wima Kamili na ujaribu athari tofauti za kuweka ukungu katika
mandharinyuma. Unaweza kutumia athari za bokeh kupiga picha binafsi.
Hata baada ya usiku mrefu, unaweza bado kuonekana vizuri. Piga picha binafsi kwa kutumia
kichujio cha urembo.
3. Gusa �.
Ili kupiga picha zenye ubora wa juu usiku au katika hali ya mwangaza hafifu, washa hali ya Usiku.
Gusa Kamera > Usiku na ufuate maagizo kwenye simu yako.
Kupiga picha nzuri ya mazingira, washa hali ya mtazamo mpana, Gusa Kamera > �. Kurudi
kwenye hali ya kawaida, gusa > �.
Unataka kuwa na muda wa kuingia kwenye picha pia? Jaribu kutumia kipima saa.
1. Gusa Kamera .
2. Gusa �. Kitufe huonyesha mpangilio wa kipima saa. Ili kuibadilisha, iguse tena.
4. Gusa �.
1. Gusa Kamera > � > Mwonekano wa Picha > Picha kutoka kwa kamera ya mbele .
2. Chagua MP48 .
Ikiwa kuna kadi ya kumbukumbu kwenye simu yako, na kumbukumbu ya simu inajaa, hifadhi
picha na video ulizorekodi kwenye kadi ya kumbukumbu.
Dokezo: Kwa video ya ubora wa juu, rekodi video kwenye kumbukumbu ya simu yako.
1. Gusa Kamera .
Je, unataka kukumbuka nyakati hizo muhimu? Tazama picha na video kwenye simu yako.
Gusa Picha .
Cheza video
Ili kupelea video mbele au nyuma kwa haraka, kokota kitelezi chini ya skrini kulia au kushoto.
Ungependa kutazama picha na video zako kwenye skrini kubwa? Zisogeze kwenye kompyuta
yako.
Unaweza kutumia kidhibiti faili cha kompyuta yako kunakili au kusogeza picha na video zako
kwenye kompyuta.
Unganisha simu yako kwenye kompyuta na kebo ya USB inayotangamana. Ili kuweka aina ya
muunganisho wa USB, fungua paneli ya taarifa, na uguse taarifa ya USB.
Unaweza kushiriki picha na video zako kwa haraka na kwa urahisi ili marafiki na familia yako
wazione.
6 Intaneti na miunganisho
AMILISHA WI-FI
Kutumia muunganisho wa Wi-Fi kwa kawaida huwa haraka na bei nafuu kuliko kutumia
muunganisho wa data ya simu. Kama miunganisho yote ya Wi-Fi na data ya simu inapatikana,
simu hutumia muunganisho wa Wi-Fi.
Washa Wi-Fi
Muunganisho wako wa Wi-Fi unatumika wakati � imeonyeshwa kwenye upau wa hali juu ya
skrini.
Muhimu: Tumia usimbuaji ili kuongeza usalama wa muunganisho wako wa Wi-Fi. Kutumia
usimbuaji hupunguza hatari ya wengine kufikia data yako.
Dokezo: Ikiwa unataka kufuatilia maeneo wakati mawimbi ya setileti hayapatikani, kwa mfano 1
wakati uko ndani au kati ya majengo marefu, washa Wi-fi ili uboreshe usahihi wa mkao.
Kumbuka: Kutumia Wi-Fi huenda kumezuiwa katika nchi zingine. Kwa mfano, katika Ulaya, unaruhusiwa
tu kutumia 5150-5350 MHz Wi-Fi ukiwa ndani tu, na nchini Marekani na Kanada, unaruhusiwa kutumia
5.15-5.25 GHz Wi-Fi ukiwa ndani tu. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na utawala wa eneo lako.
Muhimu: Tumia usimbuaji ili kuongeza usalama wa muunganisho wako wa Wi-Fi. Kutumia usimbuaji
hupunguza hatari ya wengine kufikia data yako.
Telezesha chini kuanzia juu ya skrini, gusa Data ya simu na uwashe Data ya simu .
Telezesha chini kuanzia juu ya skrini, gusa � Data ya simu na uzime data ya simu .
Dokezo: Ili kufuata matumizi ya data yako, gusa Mipangilio > Mtandao na Intaneti >
Matumizi ya data .
Hali ya ndege hufunga miunganisho kwenye mitandao ya simu za mkononi na huzima vipengele
pasiwaya vya kifaa chako. Fuata maagizo na mahitaji ya usalama yanayotolewa na, kwa mfano,
ndege, na sheria na masharti yoyote husika. Inaporuhusiwa, unaweza kuunganisha kwenye
mtandao wa Wi-Fi ili, kwa mfano, vinjari intaneti au washa kushiriki Bluetooth kwenye hali ya
ndege.
1Kuunganisha kwenye intaneti wakati unatumia data ya nje ya mtandao wako wa kawaida, hasa ukiwa
ng’ambo, kunaweza kupandisha gharama ya data pakubwa.
VINJARI WAVUTI
Ni rahisi kutumia intaneti kwenye kompyuta yako ndogo mahali popote. Fanya simu yako
iwe mtandao-hewa wa Wi-Fi, na utumie muunganisho wako wa data ya simu ili ufikie intaneti
kwenye kompyuta yako ndogo au kifaa kingine.
2. Washa Sambaza intaneti ya Wi-Fi ili ushiriki muunganisho wako wa data ya simu
kwenye Wi-Fi, Shiriki intaneti kwa USB ili kutumia muunganisho wa USB, au
Shiriki intaneti kwa Bluetooth ili utumie Bluetooth.
Kifaa kile kingine hutumia data kutoka kwa mpango wako wa data, ambayo inaweza
kusababisha gharama ya matumizi ya data. Kwa maelezo kuhusu upatikanaji na gharama,
wasiliana na mtoa huduma wa mtandao wako.
Anza kuvinjari
Hakuna haja ya kompyuta – unaweza kuvinjari intaneti kwa urahisi kwenye simu yako.
Jifahamishe juu ya habari, na tembelea tovuti zako uzipendazo. Unaweza kutumia kivinjari
kwenye simu yako ili utazame kurasa za wavuti kwenye intaneti.
1. Gusa Chrome .
Dokezo: Kama mtoa huduma wako wa mtandao hakulipishi ada moja kwa uhamishaji data, ili
kuokoa gharama ya data, tumia mtandao wa Wi-Fi ili kuunganisha kwenye tovuti.
Tafuta wavuti
Chunguza wavuti na ulimwengu wa nje kwa kutumia Utafutaji wa Google. Unaweza kutumia
kibodi kuandika maneno yako ya utafutaji.
Katika Chrome,
3. Gusa �.
Ikiwa una wasiwasi kuhusu gharama ya matumizi yako ya data, simu yako itakusaidia kuzuia
baadhi ya programu dhidi ya kutuma au kupokea data wakati zinaendeshwa chinichini.
1. Gusa Mipangilio > Mtandao na Intaneti > � Matumizi ya data > Kiokoa data .
BLUETOOTH®
Unaweza kuuunganisha pasi waya kwenye vifaa vingine vinavyotangamana, kama vile simu,
kompyuta, vifaa vya sauti, na vifaa vya gari. Unaweza pia kutuma picha zako kwa simu
zinazotangamana au kwenye kompyuta yako.
Unaweza kuunganisha simu yako na vifaa vingi muhimu vya Bluetooth. Kwa mfano, na vifaa vya
sauti vya pasi waya (kinauzwa kando), unaweza kuongea na simu bila kutumia mikono - unaweza
kuendelea unachofanya, kama kufanya kazi kwenye kompyuta, wakati wa simu. Kuunganisha
simu kwenye kifaa cha Bluetooth huitwa kuoanisha.
Kwa kuwa vifaa vyenye teknolojia pasi waya ya Bluetooth huwasiliana kwa kutumia mawimbi ya
redio, havihitaji kuwa vinaangaliana. Hata hivyo, lazima vifaa vyako vya Bluetooth viwe mita 10
(futi 33) na kifaa kile kingine, ijapokuwa muunganisho unaweza kuathiriwa na vizuizi kama vile
kuta au kutoka vifaa vingine vya elektroniki.
vifaa vilivyolinganishwa vinaweza bado kuunganishwa kwenye simu yako wakati Bluetooth
imewashwa. Vifaa vingine vinaweza kugundua simu yako tu ikiwa mwonekano wa mipangilio ya
Bluetooth imefunguliwa.
Ikiwa unataka kushiriki picha zako au maudhui mengine na rafiki, zitume kwenye simu ya rafiki
yako kwa kutumia Bluetooth,
Unaweza kutumia zaidi ya muunganisho mmoja wa Bluetooth kwa wakati mmoja. Kwa mfano,
wakati unatumia vifaa vya sauti vya Bluetooth, unaweza bado kutuma vitu vingine kwenye simu
nyingine.
Ondoa uoanishaji
Ikiwa huna kifaa ulichooanisha na simu yako, unaweza kuondoa uoanishaji huo.
3. Gusa SAHAU .
NFC
Chunguza ulimwengu karibu na wewe. Ikiwa simu yako inakubali Mawasiliano ya Karibu na Eneo
(NFC), unaweza kugusa vifaa vya ziada ili kuviunganisha, na uguse lebo ili kumpigia mtu simu
au kufungua tovuti. Utendaji wa NFC unaweza kutumika na huduma na teknolojia fulani kama
gusa ili kulipa kwa kutumia kifaa chako. Huduma hizi zinaweza kukosa kupatikana katika eneo
wako. Kupata maelezo zaidi kuhusu upatikanaji wa huduma hizi, wasiliana na mtoa huduma wa
mtandao wako.
Washa vipengele vya NFC kwenye simu yako, na uanze kugusa ili kushiriki vitu au
kuunganisha kwenye vifaa. Ili kuona kama simu yako inakubali NFC, gusa Mipangilio >
Vifaa vilivyounganishwa > Mapendeleo ya Muunganisho .
• Unganisha kwenye vifaa vya ziada vinavyotangamana vya Bluetooth ambavyo vinakubali
NFC, kama vile vifaa vya sauti au kipasa sauti pasi waya.
• Gusa lebo ili upate maudhui zaidi ya simu yako, au kufikia huduma za mtandaoni.
• Lipa kwa kutumia simu yako, ikiwa inakubaliwa na mtoa huduma wa mtandao wako.
Eneo la NFC liko nyuma ya simu yako. Gusa simu, vifaa vya simu, lebo, au visomaji vingine na
eneo la NFC.
1. Gusa Mipangilio > Vifaa vilivyounganishwa > Mapendeleo ya muunganisho > NFC .
2. Washa NFC .
Lebo za NFC zinaweza kuwa na maelezo, kama vile anwani ya wavuti, nambari ya simu, au kadi
ya biashara. Maelezo unayotaka yako umbali wa mguso tu.
Unatumia mikono yako? Tumia vifaa vya sauti. Au kwa nini usisikilize muziki kwa kutumia vipasa
sauti pasi waya? Unahitaji tu kugusa kifaa cha ziada kinachotangaman na simu yako.
1. Gusa eneo la NFC na kifaa cha ziada na eneo la NFC ya simu yako.*
*Vifaa vya ziada vinauzwa kando. Upatikanaji wa vifaa vya ziada hutofautiana kimaeneo.
Ikiwa hutaki kuunganishwa tena kwenye kifaa cha ziada, unaweza kutenganisha kifaa hicho cha
ziada.
VPN
Huenda ukahitaji muunganisho wa mtandao pepe wa binafsi (VPN) ili kufikia rasilimali za
kampuni yako, kama vile intraneti au barua ya kampuni, au utumie huduma ya VPN kwa malengo
ya kibinafsi.
1. Gusa Mipangilio > Mtandao na Intaneti > Mipangilio ya kina > VPN .
TAREHE NA SAA
Fuatilia muda – jifunze jinsi ya kutumia simu yako kama saa, na hata pia saa ya kengele, na jinsi
ya kusasisha miadi, kazi, na ratiba zako.
Unaweza kuweka simu yako kusasisha saa, tarehe, na ukanda wa saa kiotomatiki. Usasishaji
otomatiki ni huduma ya mtandao na huenda usipatikane kulingana na eneo lako au mtoa
huduma wa mtandao.
Gusa Mipangilio > Mfumo > Tarehe na Saa , na uwashe Tumia mpangilio wa saa 24 .
SAA YA KENGELE
Weka kengele
3. Ili kurekebisha kengele, iguse. Ili kuweka kengele kujirudia katika tarehe maalum, weka tiki
kwenye Rudia na uangazie siku za wiki.
Zima kengele
KALENDA
Dhibiti kalenda
Kalenda huongezwa kiotomatiki wakati unapoongeza akaunti kwenye simu yako. Ili kuongeza
akaunti mpya na kalenda, nenda kwenye menyu ya programu na uguse Mipangilio >
Watumiaji na akaunti > Ongeza akaunti .
Ongeza tukio
3. Ili kufanya tukio lijirudie siku fulani, gusa Chaguo zaidi > Isijirudie , na uchague ni mara
ngapi tukio linapaswa kujirudia.
4. Ili kuhariri muda wa ukumbusho, gusa muda unaosalia, na uchague muda unaotaka.
Futa miadi
1. Gusa tukio.
8 Ramani
Pata mahali
1. Gusa Ramani .
2. Andika maneno ya kutafuta, kama vile anwani ya mtaa au jina la mahali, katika upau wa
utafutaji.
Pata maelezo ya kutembea, kuendesha gari, au kutumia usafiri wa umma - tumia eneo lako la
sasa au eneo lingine kama mahali pa kuanzia.
2. Gusa Maelekezo . Ikoni iliyoangaziwa huonyesha hali ya usafiri, kwa mfano �. Ili kubadilisha
modi hii, chagua modi mpya chini ya upau wa utafutaji.
3. Kama hutaki mahali pa kuanza kuwa eneo lako la sasa, gusa Eneo lako , na utafute mahali
pengine pa kuanza.
Njia huonyeshwa kwenye ramani, pamoja na makadirio ya muda unaochukua kufika hapo. Ili
kuona maelekezo tondoti, pitisha juu kuanzia chini ya skrini.
Pakua ramani
Hifadhi ramani mpya kwenye simu yako kabla ya safari, ili uweze kuvinjari ramani bila
muunganisho wa intaneti wakati unasafiri.
1. Gusa Ramani > � > Ramani za nje ya mtandao > CHAGUA RAMANI YAKO MWENYEWE .
2. Chagua eneo kwenye ramani na uguse PAKUA .
Ikiwa ikoni � haipatikani, gusa ikoni ya akaunti ya mtumiaji ya Google au picha yako ya akaunti
ya mtumiaji ya Google.
Dokezo: Pia unaweza kuweka simu yako kusasisha ramani kiotomatiki. Gusa Ramani > � >
Ramani za nje ya mtandao > � na ubadilishe Sasisha ramani za nje ya mtandao kiotomatiki
na Pakua ramani za nje ya mtandao kiotomatiki kwa Washa .
Tumia Ramani ili kujua uko wapi, na ambatisha eneo lako kwenye picha unazopiga. Maelezo ya
eneo yanaweza kuambatishwa kwenye picha au video, kama eneo lako linaweza kubainishwa
kwa kutumia teknolojia ya mtandao. Ukishiriki picha au video ambayo ina maelezo ya eneo,
maelezo ya eneo yanaweza kuonyeshwa kwa wale wanaotazama picha au video. Baadhi ya
programu zinaweza kutumia maelezo yako ya maeneo ili kutoa huduma mbalimbali.
Picha yako huonyesha eneo lako kwenye ramani kwa kutumia mfumo wa mkao wa setileti, Wi-Fi,
au mkao wa mtandao (Cell ID).
Upatikanaji, usahihi na ukamilifu wa maelezo ya eneo hutegemea, kwa mfano, eneo lako,
maeneo ya karibu, na vyanzo vya mhusika mwingine, na huenda ukazuiwa. Huenda maelezo
ya eneo yasipatikane, kwa mfano, ndani ya majengo au chini ya ardhi. Kwa maelezo ya
sera yanayohusiana na mbinu za mkao, angalia HMD Global Privacy Policy, available at
http://www.nokia.com/phones/privacy.
Baadhi ya mifumo ya mkao wa setilaiti inaweza kuhitaji uhamishaji wa viwango vidogo vya
data kwenye mtandao wa simu. Kama unataka kuepuka gharama ya data, kwa mfano wakati
unasafiri, unaweza kuzima muunganisho wa data ya simu katika mipangilio ya simu yako.
Mkao wa Wi-Fi huboresha usahihi wa mkao wakati mawimbi ya setileti hayapatikani, hasa wakati
uko ndani au kati ya majengo marefu. Ukiwa uko katika mahali matumizi ya Wi-Fi yamekatazwa,
unaweza kuzima Wi-Fi katika mipangilio ya simu yako.
Simu yako ya Android inaweza kutumika kikamilifu kwa kutumia Google Play – programu,
muziki, filamu na vitabu vinapatikana zote uweze kuzifurahia.
1. Gusa Mipangilio > Akaunti > Ongeza akaunti > Google . Ukiulizwa, thibitisha mbinu ya
kufunga kifaa chako.
2. Andika hati tambulishi za akaunti yako ya Google na uguse Ifuatayo , au, kuunda akaunti
mpya, gusa Unda akaunti .
Pakua programu
Fungua uwezo wa simu yako – kuna maelfu ya programu zinazosubiri katika Duka la Google Play
ya kukusaidia na hii.1
2. Gusa upau wa utafutaji ili utafute programu, au chagua programu kutoka kwenye
mapendekezo yako.
Ili kuona programu zako, nenda kwenye skrini ya mwanzo na utelezeshe juu kutoka chini ya
skrini.
1Unahitaji kuongeza akaunti ya Google kwenye simu yako ili utumie huduma za Google Play. Mabadiliko
yanaweza kutumika kwa baadhi ya maudhui yanayopatikana kwenye Google Play. Ili kuongeza mbinu
ya malipo, gusa Play Store > Menyu > Akaunti > Mbinu za malipo . Hakikisha kila wakati una kibali
kutoka kwa mmiliki wa mbinu ya malipo wakati unanunua maudhui kutoka Google Play.
Kuwa katika hali sawa na mdundo - sasisha programu ya simu yako pasi waya ili upate vipengee
vipya na vilivyoboreshwa vya simu yako. Kusasisha programu kunaweza pia kuboresha
utendakazi wa simu yako.
Gusa Mipangilio > Mfumo > Mipangilio ya kina > Kisasisho cha mfumo > Kagua sasisho ili
kukagua kama visasisho vinapatikana.
Wakati simu yako inapokuarifu kwamba sasisho linapatikana, fuata maagizo yaliyoonyeshwa
kwenye simu yako. Ikiwa simu yako inaishiwa na kumbukumbu, huenda ukahitaji kusogeza
programu, picha, na vitu vyako vingine kwenye kadi ya kumbukumbu.
Onyo: ukisakinisha kisasisho cha programu, huwezi kutumia kifaa hicho, hata kupiga simu za
dharura, mpaka usasishaji ukamilike na kifaa kiwashwe upya.
Kabla ya kuanza kusasisha, unganisha chaja ua hakikisha betri ya kifaa ina nishati ya kutosha,
na unganishe kwenye Wi-Fi, kwa kuwa vifurushi vya kusasisha vinaweza kutumia data nyingi ya
simu.
Ili kuhakikisha data yako ni salama, tumia kipengele cha kuhifadhi nakala kwenye simu yako.
Data ya kifaa chako (kama vile manenosiri ya Wi-Fi na historia ya simu) na data ya simu (kama
mipangilio na faili zilizohifadhiwa na programu) zitahifadhiwa kwa umbali.
Gusa Mipangilio > Mfumo > Mipangilio ya kina > Hifadhi nakala rudufu , na uwashe hifadhi
nakala.
Ajali zinaweza kutokea - Ikiwa simu yako haifanyi kazi vizuri, unaweza kurejesha mipangilio
yake halisi. Au, ukinunua simu mpya, au uwe unataka kutupa au kuchakata upya simu yako, hivi
ndivyo unavyoweza kuondoa maelezo na maudhui yako ya kibinafsi. Kumbuka kwamba ni wajibu
wako kuondoa maudhui yote ya kibinafsi.
1. Gusa Mipangilio > Mfumo > Mipangilio ya kina > Weka upya chaguo >
Futa data yote (rejesha data ya mwanzo) .
HIFADHI
Ili kukagua kiwango cha kumbukumbu kinachopatikana, gusa Mipangilio > Hifadhi .
• Programu
Unaweza pia kusogeza maudhui, kama vile picha na video, kwenye kadi yako ya kumbukumbu.
Ili kukagua kiasi cha kumbukumbu unacho na jinsi inavyotumika, gusa Mipangilio > Hifadhi .
Gusa Play Store > � > Programu na michezo yangu , chagua programu unayotaka kuondoa,
na uguse SANIDUA .
Unaweza kunakili picha, video, na maudhui mengine yaliyoundwa na wewe kati ya simu na
kompyuta yako ili kuonyesha au kuzihifadhi.
2. Kwenye kompyuta yako, fungua kisimamia faili, na uvinjari kwenye simu yako.
3. Kokota na udondoshe vipengee kutoka kwenye simu hadi kompyuta yako, au kutoka kwenye
kompyuta hadi simu yako.
Hakikisha umeweka faili katika folda sahihi kwenye simu yako, au huenda usiweze kuziona.
Unaweza kufungua simu yako kwa kugusa na kidole chako. Sanidi ID ya alama yako ya kidole
kwa usalama wa ziada.
1. Gusa Mipangilio > Usalama na Eneo > Alama ya kidole . Kama hujasanidi kufuli ya skrini
kwenye simu yako, gusa Sanidi funga skrini .
2. Chagua ni mbinu gani ya hifadhi nakala ya kufungua unayotaka kutumia kwenye skrini ya
kufunga na ufuate maagizo yaliyoonyeshwa kwenye simu yako.
Ikiwa kuna hitilafu ya sensa ya alama ya kidole, na huwezi kutumia mbinu mbadala za kuingia
ili kurejesha au kuweka upya simu kwa njia yoyote ile, simu yako itahitaji huduma kutoka kwa
mtu aliyeidhinishwa. Huenda gharama ya ziada ikatumika, na data yote ya kibinafsi kwenye
simu huenda ikafutwa. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na care point iliyo karibu ya simu yako, au
muuzaji wa simu yako.
1. Gusa Mipangilio > Usalama na Eneo > Kufungua kwa uso . Kama hujasanidi kufuli ya skrini
kwenye simu yako, gusa Sanidi funga skrini .
2. Chagua ni mbinu gani ya hifadhi nakala ya kufungua unayotaka kutumia kwenye skrini ya
kufunga na ufuate maagizo yaliyoonyeshwa kwenye simu yako.
Fungua macho yako na uhakikishe uso wako unaonekana kikamilifu na hujafunikwa na kitu
chochote, kama vile kofia au miwani.
Kumbuka: Kutumia uso wako kufungua simu yako si salama kama kutumia alama ya kidole,
ruwaza au nenosiri. Huenda simu yako imefunguliwa na mtu au kitu chenye mwonekano huo
mmoja. Huenda kufungua kwa uso kusifanye kazi vizuri katika mazingira yenye mwangaza wa
nyuma au wenye giza au mkali.
Ikiwa kuna hitilafu ya kutambua uso, na huwezi kutumia mbinu mbadala za kuingia ili kurejesha
au kuweka upya simu kwa njia yoyote ile, simu yako itahitaji huduma. Huenda gharama ya ziada
ikatumika, na data yote ya kibinafsi kwenye simu huenda ikafutwa. Kwa maelezo zaidi, wasiliana
na kituo cha huduma kilichoidhinishwa kilicho karibu cha simu yako, au muuzaji wa simu yako.
Ikiwa SIM kadi yako ilikuja na msimbo msingi wa PIN ya SIM, unaweza kuibadilisha ili kuwa
salama zaidi. Sio watoa huduma wote wa mtandao wanakubali hii.
Unaweza kuchagua ni dijiti gani za kutumiza kwa PIN ya SIM. Msimbo wa PIN ya SIM unaweza
kuwa wa dijiti 4-8.
1. Gusa Mipangilio > Usalama na Eneo > Mipangilio ya kina > Kufunga SIM kadi .
2. Chini ya kadi iliyoteuliwa ya SIM, gusa Badilisha nenosiri la kuzuia .
Dokezo: Kama hutaki kulinda SIM yako kwa msimbo wa PIN, badilisha Funga SIM kadi kwa
Zima , na ucharaze PIN yako ya sasa.
MISIMBO YA UFIKIAJI
Msimbo wa kufunga
Msimbo wa IMEI
Msimbo wa IMEI hutumiwa kutambua simu katika mtandao. Huenda pia ukahitaji kupeana
nambari kwa kituo chako kilichoidhinishwa cha huduma au muuzaji wa simu.
Msimbo wa IMEI wa simu yako umechapishwa pia kwenye simu yako au kwenye trei ya SIM
kulingana na modeli ya simu yako. Ikiwa simu yako ina kifuniko kinachoweza kuondolewa cha
nyuma, unaweza kupata msimbo wa IMEI chini ya kifuniko.
Ukipoteza simu yako, unaweza kuitafuta, kuifunga, au kuifuta kwa mbali ikiwa umeingia kwenye
Akaunti ya Google. Tafuta Kifaa Changu huwashwa kimsingi kwa simu zinazohusishwa na
Akaunti ya Google.
Wakati Tafuta Kifaa Changu kinapounganishwa na simu yako, utaona eneo la simu, na simu
itapata arifa.
2. Ikiwa una zaidi ya simu moja, bofya simu iliyopotea juu ya skrini.
3. Kwenye ramani, angalia kuhusu mahali simu iko. Eneo huwa ukadiriaji na huenda lisiwe
sahihi.
Iwapo kifaa chako hakiwezi kupatikana, Tafuta Kifaa Changu itaonyesha eneo la mwisho
linalojulikana, ikiwa ipo. Ili kufunga au kufuta simu yako, fuata maagizo kwenye tovuti.
Soma maelekezo haya rahisi. Kutoyafuata kunaweza kuwa hatari au kinyume cha sheria na
masharti. Kwa maelezo zaidi, soma mwongozo kamili wa mtumiaji.
Zima kifaa wakati matumizi ya simu za mkononi yamekatazwa au wakati yanaweza kusababisha
mwingiliano au hatari, kwa mfano, ndani ya ndege au hospitalini, au karibu na vifaa vya
matibabu, mafuta, kemikali, au maeneo yenye mlipuko. Tii maagizo yote katika maeneo
yaliyozuiwa.
Tii sheria zote za mahali ulipo. Daima iache mikono yako iwe huru wakati unaendesha gari. Kitu
cha kuzingatia kwanza unapoendesha gari unapaswa kuwa usalama barabarani.
MWINGILIANO
Vifaa vyote visivyotumia waya vina uwezekano wa kupata mwingiliano, ambao unaweza kuathiri
utendaji kazi wake.
HUDUMA ILIYOIDHINISHWA
Tumia betri, chaja, na vifaa vya ziada ambavyo vimeidhinishwa na HMD Global Oy kwa ajili ya
matumizi na kifaa hiki tu. Usiunganishe bidhaa ambazo haziendani pamoja.
Ikiwa kifaa chako kinaweza kuzuia maji, tafadhali rejelea ukadiriaji wake wa IP kwa mwongozo
zaidi wa kina.
SEHEMU ZA GLASI
Kifaa na/au skrini yake imetengenezwa kwa glasi. Glasi hii inaweza kuvunjika kifaa kikiangushwa
mahali pagumu au kupokea mgongano mzito. Glasi ikivunjika, usiguse sehemu za glasi za kifaa
au ujaribu kuondoa glasi iliyovunjika kutoka kwa kifaa. Acha kutumia kifaa hadi glasi ibadilishwe
na mhudumu aliyeidhinishwa.
Kuzuia madhara yanayowezekana ya kusikia, usisikilize katika viwango vya juu vya sauti kwa
muda mrefu. Kuwa mwangalifu wakati unashikilia kifaa chako karibu na sikio wakati kipaza sauti
kinatumika.
SAR
Kifaa hiki kinatimiza matakwa ya maelekezo ya ujiwekaji wazi kwa frikwensi za redio wakati
kikitumika ama kwenye mkao wa kawaida kwenye sikio au wakati kikiwekwa angalau sentimita
1.5 (inchi 5/8) kutoka kwenye mwili. Thamani maalum za juu za SAR zinaweza kupatikana
katika sehemu ya Maelezo ya Cheti ya (SAR) ya mwongozo huu wa mtumiaji. Kwa maelezo zaidi,
angalia sehemu ya Maelezo ya Cheti (SAR) ya mwongozu huu wa mtumiaji au nenda kwenye
www.sar-tick.com.
SIMU ZA DHARURA
Muhimu: Miunganisho katika hali zote haiwezi kuhakikishwa. Kamwe usitegemee tu simu
pasiwaya kwa mawasiliano muhimu kama vile tiba za dharura.
• Washa simu.
1. Charaza namba rasmi ya dharura ya eneo lako la sasa. Nambari za simu ya dharura
hutofautiana kimaeneo.
2. Gusa �.
3. Toa maelezo yanayofaa kwa usahihi kama iwezekanavyo. Usikate simu hadi upewe ruhusa ya
kufanya hivyo.
• Weka SIM kadi ndani ya simu. Ikiwa huna SIM kadi, kwenye skrini ya kufunga, gusa Dharura .
• Zima vizuizi vya simu katika simu yako, kama vile uzuiaji simu, upigaji uliopangwa, au kikundi
maalum cha watumiaji.
• Ikiwa mtandao wa simu haupatikani, unaweza pia kujaribu kupiga simu ya intaneti, ikiwa
unaweza kufikia intaneti.
Shughulikia kifaa chako, betri, chaja na vifaa vya ziada kwa uangalifu. Mapendekezo yafuatayo
yatakusaidia kufanya kifaa chako kifanye kazi.
Wakati wa utendajikazi kwa muda mrefu, kifaa kinaweza kuwa na joto. Katika hali nyingi, hii
ni kawaida. Kuepuka kupata joto sana, huenda kifaa kikapunguza kasi kiotomatiki, kikafunga
programu, kikazima kuchaji, na ikiwezekana, kikajizima. Kama kifaa hakifanyi kazi sawasawa,
kipeleke kwenye kitengo cha mtengenezaji aliyeidhinishwa kilicho karibu.
UCHAKATAJI UPYA
Daima rudisha bidhaa zako za elektroniki, betri na nyezo za kifurushi zilizotumiwa kwa maeneo
maalum ya ukusanyaji. Kwa njia hii utasaidia kuzuia utupaji taka usiodhibitiwa na kukuza
uchakataji upya wa nyenzo. Bidhaa za umeme na elektroniki huwa na nyenzo nyingi za thamani,
ikiwa ni pamoja na madini (kama vile shaba, aluminiamu, chuma, na magnesiamu) na madini ya
thamani (kama vile dhahabu, fedha, na paladiamu) Nyenzo zote za kifaa zinaweza kufufuliwa
kama nyenzo na nishati.
Alama ya pipa iliyo na mkato kwenye bidhaa, betri, maandishi, au kifurushi chako
hukukumbusha kwamba bidhaa zote za elektroniki na betri lazima zipelekwe kwenye
mkusanyiko tofauti wakati bidhaa inapokwisha. Usitupe bidhaa hizi kama takataka
zisizochambuliwa za manispaa: zipeleke zichakatwe. Kwa maelezo juu ya eneo la uchakataji lililo
karibu na wewe, wasiliana na mamlaka ya taka ya eneo lako.
Ili ukague ikiwa simu yako ina betri inayoweza kuondolewa au isiyoweza kuondolewa, angalia
Mwongozo wa kuanza kutumia.
Vifaa vilivyo na beti inayoweza kuondolewa Tumia kifaa chako na betri halisi tu inayoweza
kuchajiwa upya. Betri inaweza kuchajiwa na kuondolewa chaji hata mara mia, lakini hatimaye
itachoka. Wakati muda wa kuongea na muda wa kusubiri unaonekana wazi kuwa mfupi kuliko
kawaida, badilisha betri.
Vifaa vilivyo na betri isiyoweza kuondolewa Usijaribu kuitoa betri, kwa sababu unaweza
kuharibu kifaa. Betri inaweza kuchajiwa na kuondolewa chaji hata mara mia, lakini hatimaye
itachoka. Wakati muda wa kuongea na muda wa kusubiri unaonekana wazi kuwa mfupi kuliko
kawaida, kubadilisha betri, peleka kifaa hicho kwenye kitengo cha mtengenezaji aliyeidhinishwa
kilicho karibu.
Chaji kifaa chako na chapa inayotangamana. Aina ya plagi ya chaja huenda ikatofautiana. Muda
wa kuchaji unaweza kutofautiana kulingana na uwezo wa kifaa.
Kifaa chako kikikamiliza kuchajiwa, chomoa chaja kutoka kwenye kifaa na soketi ya umeme.
Tafadhali kumbuka kwamba kuchaji kwa mfululizo hakupaswi kuzidi saa 12. Ikiachwa bila
kutumika, betri iliyokuwa imejaa chaji itapoteza chaji yake kadri muda unavyopita.
Halijoto ya juu sana hupunguza uwezo na maisha ya betri. Daima jaribu kuweka betri kwenye
halijoto kati ya 15°C na 25°C (59°F na 77°F) kwa utendakazi bora. Kifaa chenye betri moto au
baridi kinaweza kisifanye kazi kwa muda. Kumbuka kwamba huenda betri ikaisha haraka katika
halijoto baridi na kupoteza nishati ya kutosha na kuzima simu katika dakika chache. Ukiwa nje
katika halijoto baridi, weka simu yako ikiwa na joto kiasi.
Tii sheria za eneo lako. Peleka ichakatwe upya ikiwezekana. Usitupe kama takataka za kawaida
za nyumbani.
Usiweke betri kwenye shinikizo la chini sana la hewa au kuiwacha kwenye halijoto ya juu sana,
kwa mfano kuitupa kwenye moto, kwa kuwa hiyo inaweza kusababisha betri kulipuka au kuvuja
kiowevu au gesi inayoweza kuwaka moto.
Usifungue, kukata, kuvunja, kukunja, kutoa, au kuharibu betri kwa njia yoyote ile. Kama betri
itavuja, usiruhusu umaji uguse ngozi au macho. Hii ikifanyika, osha maeneo yaliyoathirika mara
moja na maji, au tafuta msaada wa kitabibu. Usirekebishe, kujaribu kuingiza vitu vigeni kwenye
betri, au kuizamisha au kuiweka kwenye maji au aina nyingine ya umaji. Betri zinaweza kulipuka
kama zimeharibika.
Tumia betri na chaja kwa matumizi yaliyokusudiwa tu. Matumizi mabaya, au matumizi
yasiyoidhinishwa au yasiyotangamana na betri au chaja huenda yakaleta hatari ya moto,
mlipuko au hatari nyingine, na huenda ikabatilisha uhalali wowote ulioidhinishwa au waranti.
Kama unaamini betri au chaja imeharibika, ipeleke kwa kituo cha huduma au muuza simu
yako kabla ya kuendelea kuitumia. Kamwe usitumie betri au chaja yoyote iliyoharibika.
Tumia chaja ndani ya nyumba tu. Usichaji kifaa chako wakati wa dhoruba ya radi. Wakati
chaja haijajumuishwa katika furushi la mauzo, chaji kifaa chako kwa kutumia kebo ya data
(iliyojumuishwa) na adapta ya nishati ya USB (inaweza kuuzwa kando). Unaweza kuchaji kifaa
chako na kebo za wahusika wengine na adapta za nishati ambazo zinatangamana na USB 2.0
au baadaye na kanuni husika za nchi na viwango vya usalama vya kimataifa na mkoa. Huenda
adapta nyingine zisitimize viwango husika vya usalama, na kuchaji kwa kutumia adapta hizo
kunaweza kusababisha hatari ya kupoteza mali au majeraha ya kibinafsi.
Ili kuchopoa chaja au kifaa chochote cha ziada, kamata na uvute plagi na siyo waya.
Kwa kuongezea, zifuatazo hutumika ikiwa kifaa chako kina betri inayoweza kuondolewa:
WATOTO WADOGO
Kifaa chako na viboreshaji vyake sio sesere. Vinaweza kuwa na sehemu ndogo ndogo. Viweke
mbali na watoto wadogo.
Utendakazi wa kifaa cha kupitisha mawimbi ya redio, pamoja na simu pasiwaya, huenda
zikaingiliana na utendakazi wa vifaa vya matibabu ambavyo havijakingwa vizuri. Wasiliana na
daktari au mtengenezaji wa kifaa cha matibabu ili ubainishe kama kimekingwa vizuri dhidi ya
nguvu ya nje ya redio.
Ikiwa una maswali yoyote kuhusu kutumia kifaa chako pasiwaya na kifaa cha matibabu
kilichopachikwa, wasiliana na mtoa huduma wako wa afya.
Kifaa chako kinaweza kupata virusi na vitu vingine vyenye madhara. Chukua tahadhari
zifuatazo:
MAGARI
Zima kifaa chako katika eneo lolote lenya mazingira yanayoweza kulipika, kama vile karibu na
pampu za mafuta katika vituo vya mafuta. Cheche zinaweza kusababisha mlipuko au moto
unaoweza kuleta majeraha au kifo. Kumbuka vikwazo katika maeneo yenye mafuta; viwanda
vya kemikali; au mahali ambapo shughuli za ulipuaji zinaendelea kufanyika. Maeneo yenye
mazingira yenye uwezekano wa milipuko yanaweza kuwa na alama zisizo dhahiri. Haya kwa
kawaida ni maeneo ambapo unaweza kushauriwa kuzima injini yako, chini ya sitaha kwenye boti,
uhamishaji kemikali au suhula za kuhifadhi, na ambapo hewa ina kemikali au chembechembe
kama vile nafaka, vumbi au poda ya chuma. Wasiliana na watengeneza magari yanayotumia
mafuta aina ya gesi oevu ya petroli iliyoyeyushwa (kama vile propeni au buteni) ikiwa kifaa hiki
kinaweza kutumiwa vizuri katika maeneo yao.
Kifaa hiki cha mkononi kinatimiza maelekezo yanayohusu ujiwekaji wazi kwa mawimbi ya
redio.
Kifaa chako cha mkononi ni transmita na kipokezi cha redio. Kimeundwa kisizidishe viwango
vya ufichuzi vya mawimbi ya redio (maeneo ya mawimbi ya redio ya sumaku ya umeme),
vinavyopendekezwa na miongozo ya kimataifa kutoka kwa shirika huru la kisayansi ICNIRP.
Maelekezo haya yanajumuisha viwango vya usalama vilivyoundwa kuhakikisha usalama wa
watu wote, Haijalishi umri na afya. Maelekezo ya ufichuzi yanategemea Kiwango Maalum cha
Ufyonzaji (SAR), ambacho ni onyesho la nguvu ya kiwango cha masafa ya redio (RF) ambayo
inawekwa kichwani au mwilini wakati kifaa kinatumika. Kiwango cha SAR cha ICNIRP cha vifaa
vya simu ni 2.0 W/kg kwa wastani wa gramu kumi za tishu.
Vipimo vya SAR vinatekelezwa kwa kifaa katika mikao ya kawaida ya uendeshaji, wakati kifaa
kinapitisha katika kiwango chake cha juu zaidi kilichoidhinishwa cha nishati, katika bendi zote
zilizopimwa za masafa.
Kifaa hiki kinatimiza matakwa ya maelekezo ya ujiwekaji wazi kichwani au wakati kimewekwa
angalau inchi 5/8 (sentimita 1.5) kutoka kwenye mwili. Wakati kikasha cha kubebea, kishikiza
kwenye mkanda au aina nyingi ya kishikizi kikitumika kwa matumizi ya kuvaliwa mwilini,
kinatakiwa kisiwe na chuma na kinatakiwa kuweka angalia umbali uliotajwa hapo juu kutoka
kwenye mwili.
Wakati wa matumizi ya kawaida, thamani za SAR kwa kawaida huwa chini ya thamani zilizotajwa
hapa juu. Hii ni kwa sababu, kwa malengo ya ubora wa mfumo na kupunguza mwingiliano
kwenye mtandao, nguvu ya kufanya kazi ya kifaa chako cha mkononi hupunguzwa kiotomati
wakati nguvu kamili haihitajiki kwa simu. Nguvu towe inavyoendelea kuwa chini, ndivyo thamani
ya SAR inavyokuwa chini.
Huenda modeli za vifaa zikawa na matoleo tofauti na zaidi ya thamani moja. Mabadiliko ya
vijenzi na muundo yanaweza kufanyika baada ya muda na baadhi ya mabadiliko yanaweza
kuathiri thamani za SAR.
Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye www.sar-tick.com. Kumbuka kwamba vifaa vya mkononi
huenda vikapitisha hata kama hupigi simu.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kwamba maelezo ya sasa ya kisayansi hayaashirii
hitaji la tahadhari zozote maalum wakati wa kutumia vifaa vya mkononi. Ikiwa unavutiwa
na kupunguza ufichuzi wako, wanapendekeza upunguze matumizi yako au utumie
kifaa kisichotumia mikono ili kuweka kifaa mbali na kichwa na mwili wako. Kwa maelezo
zaidi na ufafanuzi na majadiliano kuhusu ufichuzi wa RF, nenda kwenye tovuti ya WHO
www.who.int/peh-emf/en.
Unapokuwa ukitumia kifaa hiki, tii sheria zote na heshimu utamaduni wa wenyeji, uhuru binafsi
wa mtu na haki halali za wengine, ikiwemo hakimiliki. Kinga za hakimiliki zinaweza kukuzuia dhidi
ya kunakili, kurekebisha au kuhamisha picha, muziki na vitu vingine.
HAKIMILIKI NA ILANI
Yaliyomo katika waraka huu yametolewa ”kama yalivyo”. Isipokuwa kama inatakiwa hivyo na
sheria husika, hakuna dhamana za aina yoyote, ama za moja kwa moja au zisizo bayana, pamoja
na, lakini isiyokomea hapo, dhamana zisizo bayana za uuzikaji wa kibiashara na ufaaji kwa
matumizi fulani, zinazotolewa kuhusiana na usahihi, uaminikaji au yaliyomo ndani ya waraka
huu. HMD Global ina haki ya kupitia na kusahihisha waraka huu au kuuondoa wakati wowote bila
kutoa taarifa kwanza.
Kwa kadiri inayohusiwa na sheria husika, hakuna wakati wowote ule HMD Global au wenye leseni
wake watawajibika kwa upotevu wowote wa data au mapato au uharibifu wowote ule, uwe
maalum, wa ajali, unatokana na, au usiokuwa wa moja kwa moja uliosababishwa.
Ni marufuku kutoa upya, kuhamisha au kusambaza sehemu ya yaliyomo au yote katika waraka
huu katika hali yoyote ile bila ya kupewa kwanza idhini ya kuandikwa kutoka kwa HMD Global.
HMD Global inaendesha sera ya kuendelea kubuni. HMD Global ina haki ya kufanya mabadiliko
na kuboresha bidhaa yake yoyote iliyoelezwa katika waraka huu bila kutoa taarifa kwanza.
HMD Global haitoi wakilishi wowote, waranti au kuwajibika kwa utendaji kazi, maudhui, au
usaidizi wa mtumiaji wa programu za mhusika wa tatu zilizotolewa na kifaa chako. Kwa kutumia
programu, unakubali kwamba programu imetolewa kama ilivyo.
Upakuaji wa ramani, michezo, muziki na video na upakiaji taswira na video huenda ukajumuisha
upitishaji wa viwango vikubwa vya data. Huenda mtoa huduma wako akatoza kwa upitishaji
data. Upatikanaji wa bidhaa, huduma na vipengele fulani unaweza zikatofautiana kimaeneo.
Tafadhali wasiliana na muuzaji wa eneo lako kwa maelezo zaidi na upatikanaji wa chaguo za
lugha.
Ainisho, vipengele na maelezo mengine yote ya bidhaa yaliyotolewa yanaweza kubadilika bila
ilani.
HMD Global Oy ndio ina leseni ya kipekee ya chapa ya Nokia ya simu na kompyuta kibao. Nokia
ni alama ya biashara iliyosajiliwa ya Nokia Corporation.
ZEISS na nembo ya ZEISS ni alama zilizosajiliwa za biashara za Carl Zeiss AG zinazotumika chini
ya leseni ya Carl Zeiss Vision GmbH.
Android, Google na alama na nembo zingine husika ni alama za biashara za Google LLC.
Alama ya neno na nembo za Bluetooth zinamilikiwa na Bluetooth SIG, Inc. na matumizi yoyote
ya alama hizo na HMD Global yako chini ya leseni.
OZO
Qualcomm aptX