Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 1

UTANGULIZI

Kila vita inayaofanikiwa huanza na mafunzo,ni kazi ya mwanafunzi kuzingatia mafunzo hayo.Uraibu wa
ngono ni tatizo la ubongo ambalo kama tutakavyoona hubadili kabisa mtazamo wa akili ya mtu,LAKINI
HABARI NJEMA NI KUWA AKILI INAWEZA KUBADILIKA NA KURUDI KATIKA HALI NZURI.

Unapofanya jambo Fulani na KULIRUDIA RUDIA akili hunasa, hivyo basi KAMA HUTA KATA TAMAA
KATIKA NJIA NITAKAZOKUELEZA hata kama umekuwa mraibu wa ngono kwa miaka mingi unaweza kuwa
na akili safi tena.Kupambana kupata uhuru SIO KITU RAHISI lakini KUNA FAIDA NA FURAHA KUBWA
KUWA HURU.Vita hii itageuza kabisa maisha yako na ukizingatia vizuri UTAZITUMIA KANUNI HIZI ZA
USHINDI hata katika sehemu nyingine za maisha ,wengi waliokuwa huru mbali na uraibu wa ngono
wamekuwa watu bora zaidi kuliko kama wasingekuwa na tatizo hili

Najua unaweza fikiri kuwa umejaribu mara nyingi bila mafanikio,pengine umeomba na kuombewa na
kufunga,kufanyiwa dua lakini bado hali iko palepale.Hapa tutajifunza kupambana kwa AKILI na si tu kwa
NGUVU.

Jambo la mwisho ambalo inabidi nikwambie wazi ni kuwa unaweza ukasema nikijifunza tu nikamaliza
course hii nitakuwa huru La! Training hii itakuandaa kuendeleza mapambano bila kukata tamaa,
MABADILIKO YA KWELI HAYATOKEI GHAFLA BALI HUCHUKUA MUDA.lakini bora kupambana kuliko kuwa
mateka wa huyu adui asiye na huruma.NAWEZA KUSHINDWA MAPAMBANO KADHAA LAKINI
TUKIZIFUATA HIZI KANUNI USHINDI WA VITA HII NI WETU

MAMBO YA KUJUA KUHUSU PROGRAMU HII

 KURECOVER KABISA KUTOKA KATIKA URAIBU WA NGONO HUCHUKUA MUDA HATA MWAKA
MZIMA (hukuingia katika shimo hili siku moja usitarajie kutoka siku moja),LAKINI KUENDELEA
KUTUNZA USHINDI NI JAMBO LA MAISHA YOTE
 LAZIMA UWE TAYARI KUFANYA KAZI NGUMU (HARD WORK) ILI KUPATA UHURU
 HUTAVUKA KWENDA HATUA NYINGINE KAMA HUJATIMIZA MAAGIZO YA SEHEMU ILIYOPITA
 HAPA UNAPEWA MBINU AMBAZO ZITAKUSAIDIA KATIKA KUJIPATIA UHURU

You might also like