Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

DAY 3: KUTENGENEZA HASIRA ZA USHINDI

Uamuzi wa kuacha punyeto na uraibu wote wa ngono ni HATUA KUBWA SANA KATIKA MAISHA YAKO na
ni ishara ya kukua.Katika kuutafuta uhuru lazima kujenga MSINGI IMARA AMBAO HATUA NYINGINE
ZITAFUATA.Lazima msukumo wa kutaka kuacha iwe kubwa kuliko msukumo wa kutaka kuangalia porn
ndipo ushindi unapatikana.Msingi imara unajengwa na KUTAMBUA MADHARA ULIYOYAPATA
KUTOKANA NA TABIA HII MBAYA NA PIA NINI AMBACO UNATAKA KUKUTIMIZA KATIKA MAISHA YAKO.

a)KUtambua madhara ya uraibu wa ngono:

Ili tushinde lazima tuwe na hasira na adui, na ili kupata hasira lazima TUKUMBUKE ADUI ALITUFANYA
NINI. Kama kwenye movies vile staring anavyokumbuka wazazi wake alivyouwawa ndipo huinuka kwa
hasira na kuanza kumpiga adui mateke mfululuzo.Hivyo kazi ya leo KUANDIKA MADHARA YOTE AMBAYO
UMEYAPATA KWA KUWA MRAIBU WA NGONO. Nasisitiza tena ANDIKA katika daftari lako la
mapambano

Maswali ya muongozo:

 Je uraibu huu umeleta matokeo gani katika maisha yangu katika siku zilizopita?
 Je ni matatizo gani ninayoyapitia sasa kutokana na tabia hii?
 Je ni matatizo gani naweza yapata baadaekutokana na tabia hii?
 Je tabia hii inawaathiri vipi watu wangu wa karibu hata kama hawajui tatizo langu?

b) Kutambua nini ni cha muhimu katika maisha yako unachotaka kukitimiza

Jambo lingine lazima tuandike nini unataka kutimiza katika maisha yako ambacho uraibu wa ngono
unakuzuia,labda unataka kufikia malengo ya elimu,kuwa mtumishi wa MUngu,kuwa mchezaji wa mpira
au kuwa mwaminifu kwa ndoa yako,Yote haya yanaweza kutupa hasira ya kutupilia mbali maisha ya
uraibu.Mimi mwenyewe nilikuwa natamani sana kumtumikia MUNGU,kusaidia watu na kuwa
mwaminifu kwa ndoa yangu,Mambo ambayo nisingeyatimiza kama ningeendelea kuwa mraibu wa
ngono.

HIvyo kazi nyingine ni kuandika nini lengo lako katika maisha linalozuiliwa na uraibu huu?nini unataka
kukitimiza kwa familia yako,jamii na vile unavotaka watu wengine wakuone.

Maswali ya muongozo:

 Ni malengo gani 3 ninayotaka kuyatimiza katika maisha yangu


 Ni mambo gani ni ya muhimu sana katika maisha yangu
 Je imani yangu ya dini inanifundisha nini kuhusu ngono?
 Nani ni mtumuhimu sana katika maisha yangu ambaye anaathiriwa au ataathiriwa na uraibu
wangu?

Mission katika maisha ina nguvu sana, pata muda wa kutafakari kujua nini unataka kufanya hapa duniani
kabla hujafa yaani lile jambo ambalo unaliwaza kila siku na kama huna huu ni wakati wa
kutafakari.Kumbuka niikuambia ukifuatilia program hii utakuwa mtu bora kuliko kama usingekuwa na
tatizo hili .Mtu asiyejua anapokwenda hawezi kupotea.UKIJUA LENGO AMBALO UNATAKA LITIMIZA
DUNIANI LITACHUKUA SEHEMU KUBWA YA MAISHA YAKO NA URAIBU UTAONDOKA

JIBU maswali hayo na unitumie ili kuendelea nahatua nyingine

You might also like