Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

James January Kayunguya,

S.L.P – 555,
KIGOMA.

05/04/2021
Kumb. Na: KDC/H6/PF. 120/35

Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,


S.L.P – 332,
KIGOMA.

K.K Mganga Mkuu,


Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma,
S.L.P – 555,
KIGOMA.

YAH: MAELEZO YA KWANINI NISICHUKULIWE HATUA ZA KINIDHAMU


KUTOKANA NA KUTOTEKELEZA MAAMUZI YA KIKAO CHA TAREHE
04/01/2021 CHA CHMT YA HALMASHAURI YA WILAYA KIGOMA.

Husika na mada tajwa hapo juu,

Nikirejea barua yangu ya tarehe 21/01/2021 yenye Kumb.Na.KDC/H6/PF.


120/30, niliomba ombi la kusitishiwa uamuzi wa kunihamisha kutoka kituo cha
afya Mwamgongo kwenda zahanati ya Bugamba, uliotokana na kikao cha
CHMT ya halmashauri ya wilaya Kigoma, cha tarehe 04/01/2021.

Katika barua hiyo niliainisha sababu tatu zilizonipelekea kuomba kusitishwa


kwa uamuzi huo juu yangu.Lakini licha ya kuanisha sababu hizo kuu tatu za
msingi, katika barua hii ya maelezo ni ngependa kugusia zaidi sababu yangu ya
tatu katika barua hiyo, ambapo nilieleza ni kwa jinsi gani CHMT ya halmashauri
ya wilaya kigoma ilishindwa kuzingatia usawa katika mchakato mzima wa
kuhamisha watumishi katika kikao walichokaa tarehe hiyo 04/01/2021.

Kulingana na uhalisia wa ugumu wa mazingira ya kazi kwa upande wa


watumishi tunao hudumu katika vituo vya mwambao wa ziwa. Pia, kama
ajenda kuu ya kikao cha CHMT cha tarehe 04/01/2021 ililenga kuboresha
huduma za Afya katika vituo. Basi ni dhahiri kwamba CHMT, kama wasimamizi
wetu katika kazi, walipaswa kuzingatia changamoto hiyo na kuipa kipaumbele,
kwenye mchakato mzima wa uhamishaji wa watumishi ndani ya halmashauri.
Ikiwa ni fursa pekee ya msimamizi au mwajiri kutoa motisha kwa mwajiriwa, ili
kuchochea ubora,ufanisi na uadilifu katika utoaji huduma vituoni.
Binafsi nime hudumu kwa zaidi ya miaka mitatu katika kituo cha Afya
Mwamgongo ambacho ni miongoni mwa vituo vilivyopo katika mwambao wa
ziwa. Huduma hiyo nimekuwa nikiitoa kwa ubora, uadilifu na ufanisi mkubwa
tangu nimeajiriwa, licha ya changamoto zote za mazingira ambazo nimekuwa
niki zikabili tangu siku ya kwanza ya ajira yangu.Hivyo mategemeo yangu kwa
muajiri wangu yalikuwa ni kunipa unafuu katika kuni badilishia mazingira yangu
ya kazi, kwa uvumilivu na uadilifu nilio uonesha, na si kuniongezea ukubwa wa
changamoto.

Ukweli ni kwamba licha ya uvumilivu na uadilifu niliouonesha kwa zaidi ya


miaka mitatu ya utumishi wangu katika kituo changu. Bado haipotezi ukweli wa
kuwa nimekuwa nikihudumu kwenye mazingira magumu, hususani katika
ustawi wa maisha binafsi ya mtumishi, ambalo ndio lengo na tegemeo kuu la
kila mtumishi katika ajira yake.

Hivyo kwa mujibu wa maamuzi ya kikao hicho. Ni dhahiri kuwa CHMT


ilishindwa kuzingatia na kuitumia vizuri haki yangu ya msingi ya kunibadilisha
mazingira ya kazi kama kisemavyo kifungu cha 8(3)(h) cha Sheria ya Utumishi
wa Umma, Sura 298.Na hiyo ndio moja ya sababu kuu zilizonipelekea kukata
shauri na kuomba kusitishwa kwa uhamisho wangu.

Mwisho, nami kupitia haki yangu ya msingi ya kusikilizwa kabla ya kuchukuliwa


hatua za kinidhamu (kama kisemavyo kifungu cha 23 (2) (b)cha Sheria ya
Utumishi wa Umma, Sura 298 na Kanuni ya 44 na 45 za Kanuni za Utumishi
wa Umma (2003), naleta kwako ombi la kupitia tena kwa undani mchakato
mzima wa uamisho uliofanyika kwa watumishi wa afya ndani ya halmashauri,
kutokana na kikao cha tarehe 04/01/2021, na kujiridhisha kama haki ilitendeka
katika mchakato huo. Sababu usahihi wa maamuzi ndio utakaoleta matokeo
chanya katika kufikia lengo la kuu la kikao ambalo ni kuboresha huduma za
afya katika vituo na halmashauri ya wilaya ya kigoma kwa ujumla.

Natumaini maelezo yangu yataeleweka na kuzingatiwa.

Wako mtiifu katika ujenzi wa taifa,


`

James J. Kayunguya
AFISA TABIBU II
KITUO CHA AFYA MWAMGONGO

Nakala: AfisaUtumishi H/W Kigoma - KwaTaarifa

You might also like