Professional Documents
Culture Documents
Step Book 4
Step Book 4
Shukrani
Kitabu hiki kimeandaliwa na Sikika kwa lugha rahisi na kwa ufupi ili kuviwezesha vikundi vya kijamii au mashirika
ya hiyari katika ngazi ya msingi, kuendesha shughuli za Ufuatiliaji na Uwajibikaji wa Jamii (UUJ/SAM).
Ujuzi, uzoefu na umahiri wauongozi na wafanyakazi wa Sikika katika kuandaa na kuendesha mafunzo ya SAM
kwenye huduma za afya ndio uliofanikisha uandishi wa kitabu hiki. Shukrani za kipekee kwa timu za UUJ/SAM za
Iramba, Kondoa, Kiteto, Mpwapwa, Singida vijijini, Kibaha, Simanjiro na wilaya za mkoa wa Dar es Salaam kwani
bila ushiriki na kujitolea kwao, uzoefu wa SAM usingepatikana.
Uandaaji wa mafunzo ya SAM katika wilaya hizo pia usingefanikiwa bila ushiriki wa viongozi wa Halmashauri hizo
ambao walisaidia katika kutoa taarifa na nyaraka muhimu na pia kuandaa mazingira ya utekelezaji wa UUJ/SAM.
Irenei Kiria
Mkurugenzi Mtendaji
Hatimiliki © 2013
Shirika la Sikika
Tarehe ya kuchapishwa 2013
Kimeandaliwa na: Lilian R. Kallaghe, Idara ya Habari na Mawasiliano
Kimechapishwa na: Digitall Ltd.
i
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
Orodha ya Vifupisho
UUJ Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii
SAM Social Accountability Monitoring
BOQ Bill of Quantities (Makadirio ya Mzabuni)
CAG Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali
TAMISEMI Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
ii
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
Yaliyomo
1. Orodha ya Vifupisho ii
2. Utangulizi 1
3. Umuhimu wa kitabu hiki 2
4. Hatua kuu Muhimu kwa shughuli ya UUJ/SAM 3-16
5. Hitimisho 17
iii
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
Utangulizi
Sikika ilianza kutekeleza rasmi shughuli ya Ufuatiliaji na kuzingatia uzoefu, dhana na malengo ya Sikika ya kufanya
Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ), maarufu kama SAM - Social tathmini ya mifumo ya uwajibikaji katika ngazi zote za jamii
Accountability Monitoring) katika ngazi ya serikali ya mitaa/ na kisha kutetea, kwa lengo la kufikia upatikanaji wa huduma
vijiji mwanzoni mwa mwaka 2011. SAM/UUJ ni mchakato bora za afya kwa watanzania wote.
wa kuwawezesha wananchi kudai utawala bora na uwajibikaji
Tunatarajia kwamba kitabu hiki kitakuwa na manufaa kwenu;
katika utoaji wa huduma za jamii. Lengo ni kuwajengea
kitawawezesha wananchi kunufaika na kupata huduma bora
wananchi uwezo wa kutafuta taarifa na kuzichambua ili waweze
za kijamii hususani huduma za afya, ambazo ni haki yao
kufuatilia na kusimamia mipango, bajeti na utekelezaji wa
ya msingi na ya kikatiba. Ufuatiliaji utafanikiwa iwapo kila
miradi mbalimbali ya kijamii katika maeneo yao.
mdau, (mwananchi, diwani, kamati na bodi mbalimbali na
Kupitia SAM/UUJ, jamii husika inakuwa na uwezo wa watumishi wa umma) watatimiza wajibu wao kwa kushiriki
kuhoji uwajibikaji wa watendaji na watoa huduma, mathalan kikamilifu katika kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii.
huduma za afya katika sekta ya umma ili hatimaye waweze
kutoa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wananchi. Licha ya kulenga mifano ya sekta ya afya,
Matarajio ya UUJ/SAM ni kuona viongozi wanawajibika tunaamini kwamba, misingi na hatua za UUJ/
zaidi kwa wananchi wanaowatumikia na wananchi nao SAM zilizoainishwa katika kitabu hiki zinaweza
wanafahamu na kutekeleza wajibu wao kwa kufuatilia haki pia kutumika katika sekta nyingine za huduma
zao za msingi na kuwawajibisha watoa huduma wasiowajibika. zinazogusa maslahi ya wananchi.
Mifano ya kitabu hiki imejikita upande wa afya kwa
1
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
2
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
Hatua ya 1
Kupanga na Kuandaa Utekelezaji wa Uuj/SAM
Andaa malengo makuu na ainisha mwaka wa fedha Ni muhimu kufanya mawasiliano na madiwani
unaolenga kuufanyia tathmini. na watendaji wa kata mbalimbali za wilaya husika
Andaa barua za utambulisho yenye maelezo ya kina ili kuwajulisha nia ya kufanya zoezi la UUJ. Hii
juu ya lengo la kuunda timu ya UUJ. Katika barua itarahisisha uekelezaji, hususan wakati wa kutembelea
hiyo, unaweza kuainisha aina ya nyaraka zenye taarifa miradi mbalimbali iliyopo kwenye kata na itapunguza
mbalimbali ambazo utahitaji kupewa kutoka katika ofisi vipingamizi kutoka kwa viongozi/watendaji.
ya halmashauri ya Wilaya/Manispaa ikiwemo mipango Muhimu: Kabla ya kuanza zoezi hili,
ya shughuli za maendeleo, bajeti na taarifa za utekelezaji hakikisha una nyaraka zote zinazostahili.
ambazo timu yako ingependa kuzitumia kuendesha
zoezi la UUJ.
Peleka barua kwa viongozi husika: Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya na Mkuu wa Wilaya. Hawa
watawafahamisha viongozi wengine kama Katibu Tawala
wa Wilaya, Mganga Mkuu wa Wilaya, wakuu wa Idara
ama kiongozi mwingine wa wilaya au kata, kulingana na
sekta unayolenga kuifanyia kazi.
3
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
Hatua ya 2
Kuchagua Wajumbe wa Timu ya Uuj/Sam
Uchaguzi wa wajumbe wa UUJ ufanyike kupitia mikutano zinatumika kwa maslahi binafsi badala ya kunufaisha
ya hadhara ya vijiji/kata. Ili kuendesha zoezi la UUJ kwa wananchi,
mafanikio, ni muhimu kushirikiana na viongozi wa kijiji/ Elezea kwamba ni haki yao kudai uwajibikaji wa
kata ili kupata uhalali na msaada katika kuandaa mikutano watendaji na viongozi wao ikiwemo kuwataka
ya wananchi kwenye eneo husika. kurekebisha dosari za utekelezaji zinapojitokeza,
Katika mikutano hiyo, mambo yafuatayo ni muhimu
yafanyike:
4
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
5
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
Hatua ya 3
Kuandaa Mikutano ya Wadau Wakuu
Hatua hii ya tatu itakuwa na mikutano mikubwa miwili.
Mkutano wa kwanza ni wa Baraza la Madiwani ambao Muhimu: Mkutano wa Baraza la Madiwani
ndiyo wawakilishi rasmi wa wananchi. Hivyo basi, anza kwa ufanyike kabla ya Mkutano wa Wadau ili kupata
kuandaa mkutano na madiwani. Ni vyema kuandaa mkutano uhalali wa kuendelea na hatua zingine zote.
huo kabla au baada tu ya mkutano wa kisheria wa Baraza
la Madiwani ili kupata ushiriki mkubwa kwa wakati mmoja halmashauri ambao ni Mkurugenzi wa Halmashauri, wakuu
na pia kupunguza gharama. Katika mkutano wa idara za halmashauri pamoja na wawakilishi
huu, Madiwani waelezwe kuhusu: wa makundi muhimu yanayounda timu ya
SAM/UUJ. Makundi hayo ni;
Dhana ya UUJ na mchakato wake pamoja
na umuhimu wa madiwani kushiriki ili a. Wawakilishi wa wananchi ambao ni
kuleta ufanisi na kupata matokeo mazuri. watumia huduma,
Jinsi zoezi la UUJ litakavyo wasaidia b. Wawakilishi kutoka kamati za UKIMWI
katika kufuatilia na kusimamia utekelezaji na vituo vya afya,
wa miradi ya maendeleo iliyopangwa,
c. Uwakilishi wa wajumbe wa Bodi ya Afya
kwa manufaa ya wapiga kura wao.
ya Halmashauri,
Mkutano wa pili unahusu wadau wakuu wa d. Uwakilishi wa makundi ya watu wenye
sekta ambayo utaifanyia ufuatiliaji. Wadau mahitaji maalum; watu wenye ulemavu, watu
hawa ni pamoja na watendaji wa serikali/
6
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
wanaoishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU), kuelezea umuhimu wake katika kuimarisha uwajibikaji
e. Viongozi wa dini, wa wananchi na viongozi, lengo likiwa ni kuboresha
utoaji na upatikanaji wa huduma bora za jamii kwa
f. Wawakilishi wa wananchi ambao ni Madiwani, watanzania wote.
g. Mwakilishi mmoja Pili, kutoa fursa
kitoka mashirika ya kwa wadau kuchagua
hiyari, wawakilishi wao kujiunga
h. Mtu mashuhuri katika timu ya UUJ.
anayekubalika na Fursa hii ni kwa asasi
kuheshimika katika za kiraia, viongozi wa
dini, Maafisa Watendaji
jamii,
Kata na wawakilishi
i. Watendaji wa kata na wa Halmashauri.
j. Uwakilishi kutoka Kumbuka; katika
katika timu ya mkutano huu, wajumbe
uendeshaji ya kutoka ngazi ya jamii,
Madiwani na makundi
halmashauri, kwa Source: sambweti.blogspot.com
maalumu watakuwa
mfano, ya huduma za
wameshachaguliwa.
afya.
Tatu, kutambulisha rasmi timu nzima ya wilaya na
Malengo ya mkutano wa pili wa wadau ni: kusomewa hadidu za rejea na Mkuu wa Wilaya au
Kwanza, kutambulisha zoezi la SAM/UUJ kwa wadau na mwakilishi wake.
7
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
Hatua ya 4
Mafunzo kwa Timu ya Uuj/SAM
Mafunzo ya UUJ/SAM ni muhimu ili kuwajengea uwezo na
kuipa timu uelewa mpana zaidi kuhusu hatua kuu tano za
mchakato, kuzifahamu nyaraka na taarifa husika zikiwemo za
mipango na ripoti za utekelezaji wa miradi ya umma.
8
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
9
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
Mafunzo ya UUJ/SAM yanachukua wastani wa wiki 2 hadi 3 yakijikita katika hatua kuu tano za mchakato wa kufikia
huduma bora za jamii:
10
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
1. Mipango na Mgawanyo wa Rasilimali: Ni kiasi gani 3. Usimamizi wa Utendaji/Ufanisi: Je, watoa huduma
cha fedha kilichopo? Nini kimepangwa kufanyika? wanatekeleza wajibu wao kwa ufanisi? Hatua hii pia
Watoa huduma wamepanga kuzitumia vipi? Mgawo inaangalia kama je, watumishi wa umma wanatoa huduma
wa fedha/rasilimali za umma hutolewa kulingana na bora za jamii? (Angalia: Ripoti ya Mkaguzi wa Ndani,
Mpango Mkakati ulioainisha shughuli zote kwa kina Muhtasari wa vikao vya Baraza la Madiwani, Ripoti ya
na kuidhinishwa, ili kusaidia vyombo vya usimamizi mwaka ya Utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Afya wa
kufuatilia. Uchambuzi ufanywe kwa kuangalia Mpango Halmashauri, Mpango Mkakati wa Halmashauri, BOQ).
Mkakati na vipaumbele vyake, kuona jinsi Mpango kazi 4. Usimamizi wa Uadilifu: Hii inaangalia mifumo iliyopo:
wa mwaka husika unavyoendana na vipaumbele vya Je, inawazuia watoa huduma za jamii kutotumia vibaya
Mpango Mkakati. Pia, kuangalia jinsi mgawanyo wa rasilimali za umma? Je, wanaotumia vibaya rasilimali
rasilimali unavyoendana na vipaumbele hivyo. za umma wanachukuliwa hatua gani? (Angalia: Ripoti
ya Mkaguzi wa Ndani, Muhtasari wa vikao vya Baraza
2. Usimamizi wa Matumizi: Je, ni jinsi gani fedha za la Madiwani, Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
umma zinatumika? Hatua hii inaangalia utaratibu wa Hesabu za Umma-CAG, taarifa za magazeti).
kusimamia matumizi na mapato kwa kipindi cha mwaka
5. Usimamizi wa Uwajibikaji: Je, maafisa na watumishi
wa fedha; kuhakikisha kuwa taarifa za matumizi ya
wa umma wanawajibishwa na Vyombo vya Usimamizi?
fedha zinatolewa kwa usahihi, zinaaminika, zinawezesha
(Bunge, Baraza la Madiwani, Taasisi za Ukaguzi: Ofisi
ufuatiliaji makini wa matumizi na kusaidia kufikia ya CAG). Moja ya shughuli zao kuu ni kuwasimamia
maamuzi sahihi. (Mfano wa nyaraka za uchambuzi watendaji wa serikali ili wafanye kazi kwa uwazi na
katika hatua hii ni MTEF , CCHP, Ripoti za utekelezaji ufanisi na kuwajibika kutokana na matumizi ya rasilimali
za kila robo/mwaka na Ripoti ya Mkaguzi wa Ndani, za umma. (Angalia: Muhtasari wa vikao vya Baraza la
BOQ) Madiwani, Ripoti za CAG.)
11
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
Hatua ya 5
Kutembelea Miradi/Maeneo ya Utekelezaji
Katika hatua hii, kazi kubwa ya timu ya UUJ/SAM itakuwa Andaa ratiba.
ni kulinganisha taarifa za utekelezaji zilizofanyiwa uchambuzi Andaa ripoti ya awali ambayo itaainisha maswala
na hali halisi: Je, kilichoandikwa ndicho kilichofanyika? yanayohitaji kuhakikiwa na kufuatiliwa wakati wa
Shughuli zilizopangwa zimetekelezwa au la? Kwa kiwango kutembelea maeneo, miradi ama sehemu shughuli hizo
gani? Je, utekelezaji unaendana na thamani ya fedha zilipotekelezwa.
zilizotengwa na kutumika? Je, miradi iliyoandikwa kwenye
Andaa ratiba ya usafiri.
taarifa ni halisi na inaendana na mipango na bajeti au fedha
Wasiliana na viongozi (diwani, wenyeviti wa mitaa/vijiji na
zilizotengwa?
watendaji wa mitaa/kata) ili kupata wananchi kwa ajili ya
kupata maelezo, ufafanuzi na uzoefu wao.
Gawa majukumu kwa wajumbe wote wa timu ya SAM/
UUJ.
Tumia nyenzo za kukusanya kumbukumbu kama vile
kamera za picha mnato na ikibidi kamera ya video.
Baada ya kuona hali halisi ya utekelezaji wa miradi katika maeneo
mbalimbali, timu ya UUJ/SAM iandike ripoti ya matokeo.
Ripoti hii italinganisha hali halisi kutoka katika vitongoji/vijiji/
kata, ikilinganishwa na bajeti na mipango iliyoandikwa kwenye
taarifa za Halmashauri zilizochambuliwa awali.
12
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
Hatua ya 6
Kuwasilisha Matokeo ya Awali kwa halmashauri/Sekta husika
Baada ya kukamilisha mafunzo na kufanya uchambuzi, taarifa ya awali iandaliwe kuonesha mambo yaliyobainika. Timu ikae
upya kulinganisha taarifa za Halmashauri au Idara husika na hali halisi ya utekelezaji kwenye maeneo yaliyotembelewa.
Taarifa ipelekwe kwenye mkutano wa ndani (watendaji wa Halmashauri) ili kutoa fursa kwa Idara husika kutoa ufafanuzi.
xvi
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
Hatua ya 7
Mkutano wa Pili wa Wadau
Hii ni hatua muhimu inayolenga kutoa mrejesho wa kazi Timu ya UUJ/SAM isome taarifa ya matokeo
zilizofanyika kuanzia mafunzo hadi ziara ya maeneo husika ya ufuatiliaji. Ni muhimu kutoa uthibitisho wa
ili kupata ufafanuzi, hali halisi kwa kutumia
uthibitisho na uhalalisho vielelezo vya picha.
kutoka kwa watendaji wa
Watendaji watoe
serikali (watumishi wa
Ufafanuzi, Uthibitisho
umma). Katika hatua
na Uhalalisho kutokana
hii, wadau wote walioitwa
na maamuzi waliyofanya.
awali huitwa tena kwa
mara ya pili ili washiriki Kufikia
kupokea mrejesho. Ni makubaliano na kupanga
vyema mkutano huu tarehe ya kutoa mrejesho
ukaandaliwa, kusimamiwa katika mkutano wa
na kuendeshwa na wajumbe wa timu ya UUJ/SAM na hadhara.
Mkuu wa Wilaya awe Mwenyekiti wa Mkutano.
14
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
Hatua ya 8
Kuwasilisha Matokeo kwa Walipa Kodi-Wananchi
Wananchi ndio walipa kodi, watumiaji wa huduma za jamii
na wenye mamlaka na haki ya kufahamu jinsi rasilimali
zao zinavyotumika. Hivyo, ni muhimu wapewe mrejesho
wa shughuli nzima ya UUJ/SAM. Mrejesho huu ufanyike
kupitia mikutano ya jamii, machapisho na ripoti. Hii itawapa
mwangaza na ari wananchi wengine ambao hawakushiriki
kwenye shughuli hiyo:
Kufuatilia masuala yanayowahusu ikiwemo kudai
taarifa mbalimbali za mapato na matumizi.
Kutoa malalamiko na maoni yao kwa wahusika ili
yashughulikiwe.
Kushiriki katika mikutano ya jami, kuhoji na kujadili
miradi/shughuli za maendeleo yanayowahusu.
Muhimu: Upatikanaji wa taarifa unahamasisha uwazi
na kukuza ushiriki wa jamii hivyo kutimiza haki na
wajibu wa kuwawajibisha watendaji wasiotekeleza
majukumu yao.
15
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
Hatua ya 9
Kuandaa Mpango wa Ufuatiliaji
16
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
Hitimisho
Shughuli za UUJ/SAM ni endelevu na zinamhusu kila mmoja wetu;
iwe mwananchi, mtendaji, diwani, mbunge au kiongozi yeyote!
Boresha Huduma
Wajibika Shiriki
za Jamii
17
Hatua 9 za Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii – UUJ/ SAM
xxii