Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 7

BIBLIA NI JIBU LAKO

UNATAMBULIKAJE KATIKA ULIMWENGU WA ROHO?


Hosea P. Gambo Jnr. 3 years ago

Advertisements

Merito Tagalile

~0657 048393
~0625 610925
Marko 1:23-26

23 Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu;


akapaza sauti,
24 akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza?
25 Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba
kinywa, umtoke.
26 Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka.

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu,


Kama unavyoweza kupima kiwango cha ufahamu wa mtu ndivyo nguvu za rohon
zinaweza kupimwa kwako, na hizo zinapimwa kwa jinsi ya rohon.

Katika vita yoyote ya rohon adui huwa anakuona wewe unaweza usimuone na
usimfahamu lakin yeye anakuona vizuri na anakufahamu vizuri,

Na mfano ukiwa unalindwa na moto wewe unaweza usijue labla yule adui yako
iwe mchawi mganga aseme kwa watu aah huyu ndugu ni hatari haingiliki au
ukiingia utakuta moto au bahari na akishasimulia ndipo wewe uje kuambiwa na
watu, au waweza muombea mtu kisha mapepo yakalipuka na kusema huyu mtu
tulimtafuta sana, hiyo ipo

Sasa hiyo huwa haitokei ukiwa huna ratiba special yamaombi na kusoma Neno+
kufunga ili uongeze viwango, ili rohon uonekane moto nilazima uwe na ratiba
special, hakika nakuhakikishia utayasikia, watu watakusimulia na utayapata tu,

Nakwambia haya ili uongeze bidii ya ukaribu na Mungu katika Maombi, Neno na
kufunga, ukiweka bidii kutaka Mungu adhihilike kwako Mungu atadhihilika tu,

Hata kama unafunga sana na kuomba na hujaona matokeo, badilika anza upya,
tubu na mwambie Bwana aonekane kwako acha wokovu wa mazoea usio na
udhihilisho wowote wa nguvu za Mungu kwako na katika jamii yako, ukidhamilia
kumtafuta Mungu kweli maisha yako yatabadilika, familia yako itabadilika na jamii
yako itabadilika sababu ya Maombi yako na kujituma kwako,

Hata kama unajiona una nguvu za Mungu kidogo USIRIDHIKE, ongeza bidii ili
Mungu aonekane kwa viwango vikubwa kwako, mwana wa Mungu Mungu wetu
hana ubaguzi ukimtafuta kwa bidii atadhihilika tu katika maisha yako.

Sikia Yesu alitambulika namapepo, alitambulika kama mtakatifu wa Mungu, rohon


alionekana nguvu kuu alizonazo,

Mwana wa Mungu kuwa na tamaa ya kutafuta udhihilisho wa Ki-Mungu ndani


yako, weka kiu, omba kiu ya kumcha Mungu na kuzitafuta nguvu za Mungu,
Mathayo 5:6

Wewe sio wakawaida usijione mnyonge, chochote kinachokusumbua na


kinachokuzuia kupata mpenyo unauwezo wa Kukisambaratisha, damu ya Yesu ipo,
moto wa Yesu upo jina la Yesu lipo,

Omba mamlaka ya Ki-Mungu ijae ndani yako na nguvu za Ki-Mungu zijae ndani
yako ili Mungu adhihilike zaburi 105:4

Ili uwe moto rohon weka ratiba ya mifungo iwe kila wiki, kila mwezi itegemee vile
ndani yako unasukumwaje, unapokua unafunga unaupa nguvu utu wako wa ndani
kutawala na kuweza kusikia Mungu anasema nini na utaweza kusikia maelekezo
toka wa Mungu sababu ya kufunga, Neno, na Maombi, ukiweka ratiba hiyo
nakuhakikishia muda si mrefu, utakua mtu wa tofauti na WA kipekee kiroho.

Tafuta na taman kutambulika rohon, taman kuwa mbabe rohon ili usichezewe
wala kushambuliwa na chochote.

Barikiwa na Bwana Yesu

Kama umebarikiwa na ujumbe huu share kwa ndugu jamaa na rafiki zako popote
pale facebook, whatsup na kwenye magroup ya Whatsup hutaachwa hivyo hivyo
bali utabarikiwa kwa kuitangaza injili kwa kushare.

Ukipenda kutumiwa masomo ya Neno la Mungu kila siku kwa Whatsup tuma
majina yako mawili inbox, whatsup kwa namba ya Tigo 0657 048393 kuomba
kuunganishwa kupewa masomo kila siku na utatumiwa, pia kwa ushauri na
maombi piga namba zilizopo hapo chini, na Mungu wambinguni akubariki sana.
https://biblianijibulako.wordpress.com
Advertisements

Share with:

Related

USHAURI KWA MSINGI USHAURI KWA MSINGI


WA NENO: WA NENO:
July 16, 2020 July 16, 2020

MAMBO YA MSINGI
KATIKA MAOMBI:
August 12, 2020
With 2 comments

Categories: Uncategorized

Leave a Comment

BIBLIA NI JIBU LAKO


Back to top
Advertisements

You might also like