Professional Documents
Culture Documents
Lesson 03 - How To Use The Knight - Kiswahili
Lesson 03 - How To Use The Knight - Kiswahili
Karibu tena. Sasa tunaenda kujifunza jinsi ya kutumia jemedari. Imesemwa kwamba
jemedari anawakilisha kikosi au nguvu ya kijeshi ya mfalme. Hata njia ambayo
jemedari husonga ni sawia na jeshi la mfalme aliyepanda
farasi. Jemedari husonga kwa umbo la "L". Katika mfano
wetu, jemedari aliyewekwa kwenye mraba d5 hufanya hatua
mbili kwenda juu na kisha juu hatua moja zaidi. Kutoka kwa
mraba wa d5, jemedari anaweza kufikia miraba mingine
yoyote nane. Katika nyakati za zama za kati, jemedari
aliyekuwa amepanda farasi angesafiri moja kwa moja huku
akilenga shabaha halafu farasi angesonga kwa kasi kushoto
ili jemedari aweze kufyatua mshale wake kwa ufasaha bila
kichwa cha farasi kuwa njiani, kwa hivyo umbo la "L" katika
kusonga kwa jemedari kwenye mchezo wa sataranji. Kusonga kwao kunaweza kuwa
katika umbo la herufi "L" au hata kurudi nyuma na herufi "L". Kusonga kwa jemedari
kunaweza kuwa juu chini au upande upande, ili mradi kusonga kwao huunda aina
fulani ya "L". Lakini, jemedari lazima kila wakati asonge nafasi mbili na kisha ageuke.
Kwa mfano, ikiwa jemedari anataka kutoka katika mraba f1 kwenye daraja la kwanza
hadi hapa kwa hatua nne; anaweza kwenda juu mbili na kugeuka, juu mbili na
kugeuka, juu mbili na kugeuka, kisha kwa nafasi mbili za upande na ageuke kufikia
marudio anayotaka.
Hapo mwanzoni nilitaja ya kwamba vitunda kwa ujumla huanza mchezo. Na hiyo ni
kweli. Lakini, kipande kingine pekee ambacho kinaweza kuanza mchezo ni jemedari.
Kwa nini .... kwa sababu kinaweza kuruka juu ya kitunda