Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 4

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

PRESIDENT’S OFFICE REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT

TANZANIA PRIVATE SCHOOLS’ TEACHERS UNION (TPTU)

Mobile: +255767664494 +255769756458

Email: tptutanzania@gmail.com Website: www.tptu.or.tz/en

Head Office: Nyabulogoya Street, Nyegezi - Mwanza.

MTIHANI WA KWANZA WA UPIMAJI DARASA LA SABA

KISWAHILI (K01)

MUDA: Saa 1: 40 ____ Machi, 2021

MAELEKEZO

1. Mtihani huu una kurasa nne zilizochapwa na zenye maswali 45 yaliyo katika sehemu A, B na C.

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu kama ilivyoelekezwa.

3. Weka kivuli kwenye herufi ya jibu lililo sahihi kwa swali la 1-40 kwenye fomu ya ORM uliyopewa

kama inavyoonesha. [A] [B] [C] [D] [E]

4. Ukitaka kubadilisha herufi ya jibu sahihi, futa kivuli ulichoweka kwa umakini kwa kutumia kifutio

safi kisha weka tena kivuli kwenye herufi ya jibu sahihi.

5. Kwa swali la 41-45 jaza taarifa sahihi sehemu ya ORM uliyopewa.

6. Andika Namba yako ya Mtihani kisha weka kivuli kwenye tarakimu za namba hiyo mahali husika

katika fomu yako ya OMR uliyopewa.

7. Tumia penseli ya HB kwa swali la 1-40 na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa swali la

41-45

1|Page
SEHEMU A.
Kwa swali 1-35 chagua jibu lililo sahihi na uweke kivuli kwenye herufi yake katika fomu ya
OMR uliyopewa.
1. Ili kufaulu mtihani .................... kujifunza kwa bidii.
(a) ni budi (b) hapana budi (c) kuna budi (d) basi budi (e) sina budi
2. “Nyumba imeharibiwa na mvua”. Sentensi hii ipo katika kauli ipi?
(a) kutenda (b) kutendeana (c) kutendwa (d) kutendewa (e) kutendeka
3. Neno linaloingizwa kwenye kamusi ili lipatiwe maana huitwaje?
(a) nomino (b) kidahizo (c) kitomeo (d) kitenzi (e) kiwakilishi
4. Nomino itokanayo na neno “kuwajibika” ni ............................
(a) uwajibikaji (b) wajibu (c) kuwajibisha (d) kuwajibishana (e) wajibisha

5. Wao ni walevi wa kupindukia. Neno liliotumika kama kiwakilishi katika sentensi hii ni lipi?
(a) walevi (b) kupindukia (c) wao (d) ni (e) wa
6. “Masalale!” Tumekwisha. Neno “Masalale” limetumika kama nini?
(a) kihisishi (b) kiwakilishi (c) kielezi (d) kitenzi (e) nomino
7. Kama ungaliniomba kitabu kile .............................
(a) ningalikupa (b) ningelikupa (c) ningekupa (d) nitakupa (e) nakupa
8. Neno lenye maana sawa na neno “thenashara” ni ...............................
(a) kumi na mbili (b) muongo mmoja (c) mia moja (d) ishirni na nne (e) karne
9. Neno “SAIDIANENI” lina jumla ya silabi ngapi? .................................
(a) nane (b) sita (c) saba (d) kumi (e) tano
10. Humo alimoingia mna giza totoro. Kiambishi –mo– kimeonesha nini katika sentensi hiyo?
(a) wakati (b) mahali (c) nafsi (d) jinsi (e) tamati
11. Kipi ni kiambishi cha nafsi katika neno “amehamia”? ...........................
(a) a- (b) -me- (c) -hamia- (d) –a (e) ame –
12. Samweli anaongea kimasai. Neno kimasai ni la aina gani? ......................
(a) nomino (b) kivumishi (c) kielezi (d) kihisishi (e) kihusishi
13. Kifaa kinachotumika kuhifadhi mishale kinaitwa ...........................
(a) upinde (b) sanduku la mishale (c) kasha la mishale (d) rubega (e) podo
14. “Watashindana lakini hawatashinda,” neno lakini ni aina gani ya neno?
(a) kiwakilishi (b) kivumishi (c) kiunganishi (d) kitenzi (e) kielezi
15. Rehema amepigiwa ngoma na Zena. Katika kauli hii ni nani mtenda? ............................
(a) Zena (b) amepigiwa (c) Rehema (d) ngoma (e) hakuna jibu
16. Shule yetu imeungua moto. Sentensi hii iko katika ngeli ya .........................
(a) ki – vi (b) u – i (c) i – zi (d) u – vi (e) a – wa
17. Wingi wa neno ungo ni ..............................
(a) vyungo (b) nyungo (c) maungo (d) ungo (e) viungo
2|Page
18. Kipi kishazi tegemezi katika sentensi hii? “Mjomba aliyesafiri juzi kwenda Tanga amepata ajali”
(a) amepata (b) aliyesafiri (c) mjomba aliyesafiri juzi (d) mjomba amepata (e) mjomba
19. Musa ana ukwasi. Maana yake Musa ana ................................
(a) Utajiri (b) afya njema (c) majivuno (d) tabia nzuri (e) kiburi
20. Sikusema wewe ni mwizi ....................
(a) sembuse (b) pengine (c) kweli (d) ndivyo (e) la hasha
21. Ngojangoja huumiza matumbo. Hii methali ni kinyume cha methali ipi?......................
(a) damu ni nzito kuliko (b) haraka haraka haina Baraka (c) kamba hukatikia pembamba
(d) akili ni nywele (e) bandubandu humaliza gogo.
22. Vitawe ni nini?............................
(a) maneno yenye sawa (b) maneno ya kebehi (c) maneno yanayotamkwa sawa
(d) maneno yanayoandikwa sawa (e) maneno yenye maana zaidi yamoja
23. Kupelekwa miyomboni. Maana ya nahau hii ni ................................
(a) kupelekwa mafichoni (b) kudanganywa (c) kupakaziwa
(d) kupekwa mahala salama (e) kupelekwa nyumbani
24. Kidimbwi kimezungukwa na majani. Nini maana ya kitendawili hiki?..................
(a) mdomo wa mwanaume (b) ulimi (c) kichwa (d) macho (e) kidevu
25. Yeye ................. kutupokea.
(a) ndiyo alikuja (b) ndiye aliyekuja (c) ndio aliokuja (d) ndiwo alikuja (e) ndie alikuja
26. Kuangusha uso. Maana ya nahau hii ni..............................
(a) kuona aibu (b) kuomba msamaha (c) kuinama (d) kulala chini (e) kuangalia chini
27. Tegua kitendawili hiki kwa kutumia jibu silabi mbili tu.”ajihami bila silaha”........................
(a) siafu (b) kinyonga (c) nyuki (d) upepo (e) sisimizi
28. Neno lisilohusiana na mengine kati ya haya ni ..........................
(a) maembe (b) mapera (c) maparachichi (d) mchungwa (e) ndizi
29. Hadi sasa hakuna mwanafunzi ...................... aliyeingia kidato cha kwanza.
(a) yoyote (b) wowote (c) yeyote (d) yote (e) yeote
30. Kumkalia mtu kitako ni ..............................
(a) kumkosoa (b) kumkashifu (c) kumsengenya (d) kumsifu (e) kumtukana

Sikiliza kwa makini kifungu cha maneno kitakachosomwa kisha jibu maswali yafuatayo kwa
usahihi
MASWALI.
31. Neno uzalendo limetumika kama ............................
(a) kitenzi (b) kielezi (c) kivumishi (d) kiwakilishi (e) kiunganishi
32. Mwalimu Julius Nyerere ni mzalendo namba moja kwa sababu .......................
(a) ni baba wa taifa (b) ni rais wa kwanza wa Tanzania (c) alipigania uhuru wetu
(d) alizilinda rasilimali za taifa (d) tunamuenzi
3|Page
33. Rasilimali za taifa zilizotajwa katika kifungu cha maneno ni ...........................
(a) shule, hospitali, viwanda na barabara
(b) madini, misitu, mbuga za wanayama, bahari, maziwa na mito
(c) mikoa, wilaya, vijiji na vitongoji
(d) Mwalimu Julius Nyerere, Jakaya Kikwete na John Magufuli
(e) kujitoa mhanga kulinda rasilimali na kutetea taifa
34. Wingi wa neno uzalendo ni .............................
(a) wazalendo (b) mazalendo (c) mzalendo (d) uzalendo (e) mizalendo
35. Kutokana na kifungu cha maneno, ni njia ipi bora ya kumuenzi Mwalimu Julius Nyerere?
(a) kusharehekea siku yake ya kuzaliwa (b) kusherehekea siku yake ya kufa
(c) kuzilinda rasilimali za taifa (d) kutembelea kaburi lake (e) kusoma kwa bidii

SEHEMU B
Panga sentensi zifuatazo ili zilete mtiririko sahihi kwa kuzipa herufi A, B, D na E
36. Pia ana nundu kubwa inayohifadhi mafuta ambayo ni akiba wakati wa shida .......................
37. Kwa hali hiyo ngamia anaweza kuishi kwa muda mrefu bila chakula au maji ........................
38. Ngamia ana miguu yenye utando wa ngozi kwenye kwato zake ..........................................
39. Tumbo lake liweza kuhifadhi kiasi kikubwa cha maji ...........................................................
40. Utando huu humuwezesha kutembea kwenye mchangani bila kunasa ..................................

SEHEMU: C
Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yafuatayo
Ni njaa kuondolewa, ukawa huna mshiko
Watuo ukafiwa, ukasalia na yako
Siku ukijatolewa, msiwe na mwenzi wako
Hapo utaona mwako, utakuliza ukiwa

Utakuliza ukiwa, likupatalo sumbuko


Wakati umelemewa, sipo kitandani mwako
Huna unayemjuwa, mbali na kwenu uliko
Hapo utaona mwako, utauliza ukiwa

Maswali
41. Shairi ulilosoma lina beti ngapi?
42. Onesha vina vya kati na vya mwisho katika shairi hili
43. Taja jina la mstari wa mwisho katika kila ubeti wa shairi hili.
44. Shairi hili lina mishororo mingapi?
45. Ni nini kazi ya mshororo wa mwisho katika kila ubeti wa shairi hili?

4|Page

You might also like