Ukaguzi Ujenzi

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

1. Utangulizi.

Shule ilianza kujengwa kupitia michango mbalimbali ya wadau kwa kuchangia


ujenzi huo. Michanngo hiyo kutoka kwa wadau mbalimbali ilijumuisha rasilimali
fedha pamoja na vifaa vya ujenzi.
2. Lengo la ukaguzi .
Ukaguzi ulilenga kujua mapato na matumizi yaliyotumika hadi hakufikia hatua hii
ya ujenzi wa chumba kimoja cha darasa.
3. Eneo lililofanyiwa ukaguzi.
Ukaguzi umefanyika katika eneo la mapato(michango) kutoka kwa wadau pia eneo
la matumizi ya michango hiyo inayojumuisha fedha pamoja na vifaa vifaa vya
ujenzi kutoka kwa wadau.
4. Njia zilizotumika kwenye ukaguzi.
Wakati wa ukaguzi njia mbalimbali zilitumika kufanya ukaguzi ikiwemo kupitia
taarifa za benki ,kupitia kitabu cha stakabadhi kilichotumika kukusanyia michango
na ahadi mbalimbali kutoka kwa wadau mbalimbali pamoja na mihutasari
iliyotumika kufanya malipo ya ujenzi.

5. Matokeo ya ukaguzi.
Matumizi kutoka katika michango ya fedha na vifaa vya ujenzi.
Baaada ya kukagua mapato ya ya michango mbalimbali ya wadau pamoja na vifaa
vya ujenzi tulikagua matumizimi ya michango hiyo ili kujilidhisha na yafuatayo:
 Kama kiasi kilichopokelewa kama michango ya wadau ilitumika katika
shughuli za ujenzi husika
 Fedha zilizoingizwa kwenye akaunti zilitumika kwa kazi iliyokusudiwa
.
Tulibaini mapungufu yafuatayo wakati wa matumizi ya fedha kwa ujenzi
unaoendelea:-
 Michango kukusanywa na kuanza kutumika bila kupitia benki hivyo kuwepo
na mashaka kama fedha hizi zinatumika kwenye kazi zilizokusudiwa
 Malipo kufanyika bila kuwepo mihutasari ya vikao vinavyokubaliana
manunuzi husika.
 Hakuna kamati ya mapokezi ya vifaa vinavyonunuliwa hii inatokana na
kutokuwepo kwa taarifa ya mapokezi ya vifaa vilivyonunuliwa wakati ujenzi
unaendelea.
 Hakuna taarifa ya ukaguzi wa kazi zilizofanyika ilikujiridhisha na ubora wa
kazi iliyofanyika
 Hakuna reja ya stoo inayoonsha mwenendo wa upokeaji wa vifaa na utoaji
wa vifaa wakati wa utekelezaji shughuli za ujenzi kitu ambacho kinaweza
kusababisha upoteaji wa vifaa vya ujenzi na pia kutokujulikana kwa
takwimu sahihi za za gharama ya ujenzi unaoendelea.
6. Ushauri na maoni .
 Michango yote inayokusanywa inapashwa kuwekwa benki ilikujua kiasi cha
fedha kilichokusanywa
 Matumizi yote ya fedha yanapashwa kutoka baada ya kamati kufanya kikao
na kukubaliana malipo yanayoenda kufanyika.
 Reja ya stoo ni muhimu saana ilikujua idadi ya vifaa vilivyonunuliwa na
kutumika.
 Kuwepo na kamati ya mapokezi ya vifaa na kuandika taarifa ya vifaa
vilivyopokelewa kwa ajili ya ujenzi.
 Kamati ya ujenzi inapashwa kufanya kazi yake na sio kazi ifanyike kwa
watu wawili pekee.

7. Shukrani
Napenda kutoa shukrani za dhati kwa timu yangu iliyofanya kazi kwa ufanisi , pia
kwa wadu wote wa maendeleo waliochangia katika kuhakikisha kazi hii
inakamilika kwa ufanisi na haraka.

You might also like