Professional Documents
Culture Documents
Young Investors Forum - Ripoti Ya Maonesho
Young Investors Forum - Ripoti Ya Maonesho
IMETOLEWA NA:-
MADA : -
WALENGWA: -
Washiriki wa maonesho
MAHALI ILIPOFANYIKA: -
Viwanja vya Kijitonyama, chuo kikuu cha Dar es salaam- ndaki ya technolojia za habari na
mawasilianao.
WAANDAJI: -
UNI TRADE FAIR.
TAREHE YA MAONESHO: -
06/02/2021
TAREHE YA RIPOTI: -
18/02/2021.
1
YALIYOMO
MADA UKURASA
2
1.0 UTANGULIZI
Ripoti hii inahusu elimu ya uwekezaji katika masoko ya mitaji Tanzania iliyotolewa na Young Investors
Forum kwa wanavyuo katika maonesho maalumu ya biashara ya wajasiliamali wanavyuo yaliyofanyika
tarehe 06/02/2021 katika viwanja vya Kijitonyama, Dar es salaam.
Tathmini iliyomo ndani ya ripoti hii ni kutoka kwa wakufunzi kwa siku Ishirini na Tano walizowezesha.
3
2.0 MAANDALIZI.
Maandalizi yalifanyika kwa muda wa wiki mbili kabla ya maonesho. Miongoni ya maandalizi hayo ni ;
Uandaaji wa tisheti za maonesho
Uandaaji wa nakala na vitabu
Uandaaji wa chakula kwa ajili ya watoa huduma
Uandaaji wa banda kiujumla, viti, meza na mwamvuli
Semina fupi kwaajili ya wahudumu wa siku ya maonesho.
Maonesho yalifanyika kwa muda wa siku moja, yalianza saa tatu kamili asubuhi na kumalizika saa kumi
na mbili jioni. Tuliweza kuwahudumia washiriki kwa namna ya kipekee, ikiwemo kutoa elimu ya jumla
juu ya masoko ya mitaji na fedha, kuruhusu washiriki kuuliza maswali na hatimae kuwagawia vitabu
vya uwekezaji vinavyochapishwa na Mamlaka ya Soko la Mitaji na Fedha Tanzania pamoja na Soko la
Hisa la Dar es salaam
4
4.0 MADA MBALIMBALI ZILIZOTOLEWA
Picha 2. Agness Kalinga akitoa maelezo kuhusu masoko ya mitaji kwa msihiriki wa maonesho
aliyetembelea meza ya YIF.
5
4.1.2 UWEKEZAJI KATIKA SOKO LA HISA LA DSE.
-Maana ya soko la hisa la DSE
-Historia ya soko la hisa la DSE
-Faida na changamoto za kuwekeza katika hisa
-Namna ya kutumia DSE Hisa Kiganjani.
-Namna ya kupata mitaji kupitia soko la hisa.
6
5.0 NAMNA MADA ZILIVYOTOLEWA
Mada zilitolewa kwa njia ya ushirikishi, washiriki waliweza pia kuchangia uelewa wao katika mada
zilizotolewa. Hii ilisaidia kujua mawazo mbalimbali na namna watu wengi wanavyolichukulia suala la
uwekezaji. Pia kila mshiriki aliyeweza kufika katika banda letu alipewa mtaalam mmoja hadi wawili
kuweza kumuelimisha mshiriki huyo katika mada zilizotajwa hapo juu. Mbali na hivyo washiriki
waliweza kupatiwa vitabu na nakala mbalimbali zinazoelezea uwekezaji katika masoko ya mitaji
kiundani zaidi. Ili kuboresha uhusiano wetu na washiriki wapya tuliweza kuchukua taarifa zao za
mawasiliano na kuwajumuisha katika makundi ya mtandao wa Whatsapp kuendelea kujifunza zaidi.
7
6.0 MATOKEO YA JUMLA YA MAONESHO
Washiriki wa maonesho haya waliweza kufahamu wahusika wakubwa katika masoko ya mitaji Tanzania
pamoja na kazi zao, bidhaa zilizopo na namna ambavyo wanaweza kushiriki kama wawekezaji katika
dhamana mbalimbali zilizopo sokoni.
Washiriki wa maonesho haya waliweza kufahamu kwa undani kuhusu historia ya soko la hisa la DSE,
fursa za uwekezaji zilizopo, namna ya kutumia DSE hisa kiganjani katika kununua , kuuza hisa na
kupata taarifa mbalimali za soko kwa urahisi. Baadhi walipakua DSE hisa kijanjani na kuanza kufanya
usajili. Wajasiliamali wanavyuo walioshirikiki maonesho haya walivutiwa sana na uwepo wa soko la
kukuza mitaji kwa wajasiliamali (Enterprise Growth Market) ambalo limewapa fursa za kukuza mitaji
ya biashara zao kupitia soko la hisa.
8
7.0 UJUMBE WA MGENI RASMI
Picha 4. Mgeni rasmi wa maonesho haya, Mr Suleman Malela kutoka Baraza la Taifa la uwezeshaji
kiuchumi akiwa katika meza ya Young Investors Forum
" Privatisatision
1 Issue
Tanzanian citizens have not been effectively involved in the privatisation
process.
2 Statement
The Government will design strategies to be used to assist Tanzanians to
own property or
purchase shares in state enterprises.
3 Strategies
The Government will take measures which will ensure that Tanzanians are
empowered and are
able to purchase shares in the state enterprises that are being privatised"
9
8.0 MAOMBI NA MAONI YA WASHIRIKI.
Washiriki wote walishukuru sana huduma zetu na walitoa maoni na mapendekezo mbalimbali ikiwemo:-
Maonesho na semina zinazotoa elimu ziwe zinafanyika mara kwa mara kusaidia kuongezeka
kwa washiriki katika masoko ya mitaji na fedha
Washiriki pia walipendekeza jukwaa la mtandaoni (online forum) iweze kukamilika kwa haraka
ili kutoa nafasi kwa watu wengine waliopo mbali ambao hawawezi kufikiwa moja kwa moja’
10
9.0 HITIMISHO
Hatuna budi kushukuru uongozi mzima wa UNI TRADE FAIR, uongozi wa chuo kikuu cha dar es
salaam ndaki ya technolojia za habari na mawasilianao.(CO-ICT) na washiriki wote walioweza
kujitokeza. Pia shukurani za kipekee kwa wafadhili wetu , Mamlaka ya masoko ya Mitaji na Dhamana
(CMSA). Uongozi wa Young Investor Forum unaahidi kuendelea kufanya majukumu yake kwa ufanisi
zaidi kuweza kuwafikia watu wengi zaidi.
“Learn|Practice|Invest”
11