Professional Documents
Culture Documents
Sexually Transmitted Infections SWAHILI1
Sexually Transmitted Infections SWAHILI1
Magonjwa ya kuambukiza ya zinaa (STIs) ni magonjwa yanayosababishwa na vijidudu (vijidudu vidogo) vinavyoweza
kuambukia kutoka kwa mtu kufikia kwa mwengine kupitia kitendo cha zinaa, kulawiti na kulamba sehemu za siri.
KLAMIDIA *
• Ugonjwa wa kuambukiza (STI), unaosababishwa na bakteria.
• Mara nyingi hauna dalili.
• Unaweza kutokeza maumivu wakati wa kukojoa, usaa utoka kwenyi uume ama uke, ao maumivu kwenyi pande ya chini
ya tumbo ya mama.
• Unaweza kuwa hatari kwa maana unaweza kusababisha ugonjwa wa maumivu ya kiuno kwa wakinamama na uondoa
rutuba kwa wakinababa na wakinamama ikiwa kama hawakutibiwa.
• Uvumbuliwa haraka kupitia vipimo vya mkojo ao pamba.
• Unatibiwa na antibiotiki.
• Waliojamiana wanalazimika kutibiwa ili kuepukana na maambukizi ya magonjwa.
Kisonono *
• Husababishwa na bakteria.
• Inaweza kusababisha kuongezeka kwa usaa ndani ya uke ao maumivu makali ya chini ya tumbo kwa wakinamama na
kutoka kwa usaa kwenyi uume ao maumivu makali wakati wa kukojoa kwa wakinababa.
• Inaweza kutokuwa na dalili.
• Inatambuliwa haraka kupitia vipimo na hutibiwa na antibiotiki.
• Magumu yanaweza kujitokeza kama hakuna matibabu.
• Matibabu ya haraka dhidi ya mgonjwa na mwenzi wake ni ya muhimu kwa kuzuia maambukizo.
Kaswende *
• Husababishwa na bakteria.
• Matokeo ya mwanzo yanaweza kuleta kidonda kwenye sehemu za siri.
• Upele kwenye ngozi, kungoleka nyele sehemu mbalimbali kichwani, kusononeka kwa mwili ao kuotwa na majipu zenye
unyevu kandokando ya sehemu za siri na mkunduni zinaweza kujitokeza baadaye.
• Inatambuliwa kwa dalili na kupimwa damu.
• Hutibiwa na antibiotiki.
Homa ya manjano A
• Ugonjwa wa kuambukiza wa virusi unaoweza kuathiri maini.
• Utapanyika ukila kiwango kidogo cha mavi ya mtu alieathirika. (e.g. kulamba kandokando ya mkundu ao nafasi ingine ya
mwili ambao imeambatana na mkundu, kama vile vidole), pia utapanyika kupitia chakula na maji yalioathirika.
• Inatambuliwa kwa dalili na haraka kupimwa damu.
• Kuna chanjo ya kinga ya Homa ya manjano A
Homa ya manjano B *
• Ugonjwa wa kuambukiza wa virusi unaoweza kuathiri maini.
• Utapanyika kwa kupeana ugiligili wa mwili (damu, shahawa, uchafu utokao kwenye uke na kamasi za mkundu) wakati wa
kitendo cha zinaa kisicho na kinga kupitia uke, mkundu ao kulambula sehemu za siri na kuchangia shindano.
• Uvumbulikana haraka kupitia vipimo vya damu.
• Karibuni asili mbili juu ya mia ya Waustralia wana ugonjwa wa homa ya manjano B unaoweza kusababisha maini
kuathirika vikali.
• Kuna chanjo ya kinga ya Homa ya manjano B na matibabu yanapatikana.
Homa ya manjano C *
• Ugonjwa wa kuambukiza wa virusi unaoweza kuathiri maini na unaoweza kusababisha hasara kali.
• Haiainishi ya kwamba ni ugonjwa wa kuambukiza kwa maana hautapanyiki kwepesi kupitia zinaa. Unatapanyika kupitia damu,
hivyo kuchangia shindano, chale kwa kutumia shindano au kutoboa mwili kwa kutumia sindano / vifaa,, na hao wanaopewa damu
kuanzia 1990 wanaweza kuhatarika.
• Uvumbulikana kupitia vipimo vya damu.
• Musichangie shindano, wembe, miswaki ao vyombo vingine vinavyoweza kuambatana na damu.
• Mtu akiambukizwa home ya matumbo C inaweza kutibiwa. Kuwasiliana na homa ya matumbo C Baraza au kliniki ya 275 kwa
maelezo. Hakuna chanjo.
Sexually transmitted infections: Swahili Page 2 of 3
Last updated: June 2012
Kuzuia magonjwa ya kuambukiza
• Uwe tayari! Tumia mipira.
• Tenda kitendo cha zinaa kwa adhari. Ukamilishe ya kwamba shahawa, damu, ugiligili wa uke ao kutokea mkunduni
havimgusi patna mwengine.
• Jadiliana juu ya maambukizi yoyote ya zamani ya ngono na mpenzi wako.
• Kila mara tumia shindandano zilizo safi.
• Pakiwa vidonda, majipu ao vidonda kandokando ya kinywa ao kwenye sehemu ya siri, ao uchafu ukitoka usio wa
kawaida, epuka kuambatana na uke, mkundu na kulama sehemu ya siri ao kitendo chochote kinachoambatana na ngozi
ilioathirika.
Habari zaidi
Kwa habari nyingi zaidi kuhusu magonjwa ya kuambukiza uhusiane na Clinic 275:
Tel: 8222 5075
Wanaoita inchini: 1800 806 490
Address: 275 North Terrace, Adelaide
Website: www.stdservices.on.net
Website www.shinesa.org.au