Blasio - Duka La Spea Za Bajaj Na Pikipiki - Business - Plan 1 Draft

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 15

DUKA LA SPEA ZA PIKIPIKI -

Business Plan

BLASIO AUTO SPARE PARTS


MWANZA - TANZANIA

0scar Blasio
Mmiliki

Mkolani - MWZ

Phone: +255 719 530043


Fax:
Email: oscarblasio28@gmail.com

1
YALIYOMO

1 Muhtasari Mkuu ............................................................................... 3


1.1 MAELEZO YA KIFUPI KUHUSU MPANGO KAZI. ............................................................................ 3
1.2 TATIZO LILILOPO ........................................................................................................................... 3
1.3 SULUHISHO ................................................................................................................................... 3
1.4 VITU VYA KUFANYA ...................................................................................................................... 4

2 Our Team & Organization ................................................................. 4


2.1 Taarifa ya Misheni ........................................................................................................................ 4
2.2 Usimamizi & Timu Kazi ................................................................................................................. 4
2.3 MALENGO YA KAMPUNI .............................................................................................................. 5
2.3.1 Ukuaji wa Biashara ............................................................................................................... 5
2.3.2 Ufanisi wa Operesheni ......................................................................................................... 6
2.3.3 Kuboresha Muonekano Mzuri Katika Eneo La Biashara. .................................................... 6
2.3.4 Kujenga Jina La Biashara ...................................................................................................... 6
2.3.5 Kushiriki Huduma Za Kijamii ................................................................................................ 6

3 Bidhaa & Huduma. ............................................................................ 7


4 Uchambuzi wa soko .......................................................................... 9
4.1 Muhtasari wa Soko....................................................................................................................... 9
4.2 Wateja........................................................................................................................................... 9
4.3 Ushindani wa kibiashara .............................................................................................................. 9

5 Mkakati & Utekelezaji ........................................................................


6 Mpango wa fedha & Makadirio ..........................................................

2
1 Muhtasari Mkuu

1.1 MAELEZO YA KIFUPI KUHUSU MPANGO KAZI.


[DUKA LAVIPURI VYA PIKIPIKI, Mkolani - Mwanza]

Blasio Auto Spare Parts ni duka la Vipuri vya Pikipiki litakalofunguliwa ndani ya eneo la Mkolani -
Mwanza
Lengo la kufungua duka hili ni kutoa huduma bora ya uuzaji wa Vipuri vya Pikipiki aina zote katika
eneo hili, vile vile lengo jingine ni kuiingizia familia kipato zaidi.

Biashara:
Duka hili linamilikiwa na Bw.Oscar Blasio. Madhumuni makubwa ya kufungua duka hili ni kuboresha
zaidi kipato badala ya kutegemea shughuli alizokuwa nazo awali.

Bidhaa:
Atauza Vipuri mbalimbali za ‘tri-cycle Kama Bajaj TVS, na Pikipiki aina Boxer,Sanlg,
TVS,Fekon,Hajoue.Na ili kufanya muonekano wa duka upendeze na kuvutia makundi ya bidhaa hizi
yatapangwa kwa ustadi mkubwa.

Soko:
Soko la Vipuri vya Pikipiki nchini Tanzania hasa mijini ni kubwa na limekuwa na watu wengi wa
matabaka yote hasa la kati na juu ambao ndio wamiliki na watumiaji wa vyombo hivi vya moto.
Ingawa yapo maduka makubwa ya Vipuri vya Pikipiki Jumla na rejareja (Auto Spare Parts - Wholesale
mall) lakini bado idadi yake ni ndogo sana ukilinganisha na uhitaji uliopo.

Mikakati na Utekelezaji:
Upekee wa Blasio Auto Spare Parts ni eneo duka litakapokuwa, Mkolani eneo ambalo linafikika na
watu wengi kiurahisi hususani watumiaji wa vyombo hivi.Mkakati huu wa masoko utalenga zaidi
katika huduma nzuri kwa wateja pamoja na uwekaji bango kubwa juu ya duka litakalokuwa na
maandishi juu“Blasio Auto Spare Parts”.

1.2 TATIZO LILILOPO


[Upungufu Wa Utoaji Huduma Bora Katika Uuzaji Vipuri vya Pikipiki za aina zote zenye ubora na
zinazoendana na hali ya kipato cha Wateja Waliopo Katika mkoa wa MWANZA Hususani Eneo La
Mkolani]

1.3 SULUHISHO
[Suluhisho ni kuongeza na kuboresha huduma katika Maduka ya Biashara ya kuuza Vipuri vya Pikipiki
ilikuboresha upatikanaji wake na ili kuwarahishia watumiaji wa bidhaa hizi muhimu waliopo katika
eneo la Mkolani na viunga vyake.

3
1.4 VITU VYA KUFANYA
[Je! Ni hatua gani kuu ambazo nitahitaji kuchukua ili kufanikiwa?]

 Kuhakikisha mandhari ya duka kwa ujumla inakuwa ya kuvutia kwa kufanya usafi na kupanga
bidhaa katika mpangilio mzuri.
 Kubana matumizi kwa kukwepa gharama zisizo kuwa za lazima ikiwa ni pamoja na Mmiliki
wenyewe kutokujilipa mshahara kwa kipindi cha miezi 6 tangu kuanzishwa biashara ili faida
irudi kuukuza mtaji maradufu ndani ya muda mfupi.
 Kuhakikisha bidhaa zote za vipuri zinazotoka haraka haraka zinakuwepo dukani japo kila aina
kidogo kidogo hata kama jambo hili litalazimu kufanya manunuzi kila mara hasa kipindi
ambacho mtaji bado upo chini.

 Kutafiti mapungufu yaliyopo katika biashara hii hususani kupitia wafanyabiashara wanaouza
bidhaa hizi za vipuri vya Pikipiki kwa rejareja waliopo maeneo haya na maeneo jirani.
 Kupanga na kuzingatia muda maalumu wa kutoa huduma (muda wa kazi).
 Kuongeza bidhaa nyingine zinazoendana na soko la Spare Parts na ambazo zitahitajika na
wateja wa eneo hili.
 Kufanyia kazi maoni ya kila mteja wetu.
 Kutoa huduma bora ikiwemo lugha nzuri ya biashara.
 Kulipa wafanyakazi/vibarua kwa wakati.
 Kuweka nidhamu ya fedha katika mapato na matumizi.
 Kuwa na vibali ,leseni ya biashara kutoka mamlaka husika.

2 Our Team & Organization

2.1 TaarifayaMisheni
[Taarifa hii ya misheni inapaswa kuhusiana na timu ya kazi]
 Kwa kadiri biashara itakavyo ongezeka, nguvu kazi zaidi kwa maana ya wafanyakazi
watahitajika ambapo nitaweza kutoa ajira kwa mkataba wa muda maalum kwa malipo ya
mwezi (Mshahara).

 Ili kuboresha utaratibu huu wa ajira itaandaliwa mikataba wa ajira ya muda maalumu
(mikataba wa kazi) utakaosainiwa na mfanyakazi /wafanyakazi kabla ya kuanza kazi.

2.2 Usimamizi&TimuKazi
[Nani anayefanya kazi hii na mimi] [Nani ninayehitaji kumuajiri?]

 Wafanyakazi wenye ueledi na kauli nzuri.


 Wanaojituma na waaminifu
 Wanaojali muda
 Wabunifu
 Watakaofikia malengo yanayowekwa kiofisi.

4
[Una uzoefu wowote katika biashara hii?]
Kwa sasa bado ninaongeza ujuzi kupitia watu wanao fanya biashara kama hii na kupitia mwongozo
wa biashara hii ya Duka la Vipuri vya Pikipiki.

[Ni nini utafanya timu ya kazi ifanikiwe kufanya biashara yako kufaulu?

 Kuwapa siku moja ya mapumziko katika wiki.


 Kulipa wafanyakazi kwa wakati.
 Kutoa bonus pindi wanapovuka lengo la faida tuliojiwekea iwe ndani ya mwezi,miezi 3 ,6 au
mwaka.
 Kuwapa mafunzo na nyenzo zinazohitajika katika kazi.
 Kuwatengenezea mazingira mazuri ya kazi.

Msaada Wa Kitaalam Na Ushauri


Bodi ya wakurugenzi Oscar Blasio
Bodi ya Ushauri ya Usimamizi
Mwanasheria
Mhasibu
Wakala wa BIMA
BANK yako/Acc no.
Mshauri/Mtafiti wa biashara
Wakufunzi na Washauri wakuu

2.3 MALENGO YA BIASHARA

2.3.1 Ukuaji wa Biashara


 Katika kuikuza biashara hii ya Duka La Vipuri vya Pikipiki ni kufungua sehemu tatu zaidi za
biashara kama hii katika kipindi cha miaka(5)mitano kuanzia muda biashara hii ilipoanza.
Malengo haya yanaweza kujumuisha kukagua maeneo mengine ya kuwekeza ndani ya mji
huu na kuweka akiba asilimia 10% ya faida kila mwezi ili kufikia lengo hili.

 Kuanza kupata faida tangu mwezi wa kwanza na kuendelea.

 Kuanza usambazaji wa Vipuri vya Pikipiki kwa jumla na rejareja.

 Kuanzisha fursa nyingine za biashara.

5
2.3.2 Ufanisi wa Operesheni
Lengo lingine ni kuwa na muda maalumu kufanya matangazo ya biashara hii,ndani na nje ya eneo la
Mkolani

Na utoaji huduma endelevu kufungua mapema zaidi na kuchelewa kufunga na ikiwezekana kufanya
kazi hata siku za sikukuu ili kuwapa wateja uhakika zaidi wa kupata huduma zetu.

2.3.3 Kuboresha Muonekano Mzuri Katika Eneo La Biashara.


Kukarabati muonekano wa Ofisi/Eneo la biashara ili kulifanya liwe na mwonekano mzuri unaowavutia
wateja kila wa kati.

Kuweka mazingira rafiki kwa wateja wanaofika kuhudumiwa Dukani ikiwemo kuhakikisha pana
maegesho Parking) kwa ajili ya wateja wanaofika wakiwa na vyombo vyao vya usafiri.

2.3.4 Kujenga Jina La Biashara


Kupitia matangazo mbalimbali,mitandao ya kijamii, Redio,kuweka nembo ya biashara katika
vifungashio(mifuko) ya bidhaa,kuchapisha Majarida na Vipeperushi kutaisaidia biashara hii kukua
na kutambulika na watu wengi zaidi hususani walengwa.

2.3.5 Kushiriki Huduma Za Kijamii


Hii itafanyika pindi Biashara ikiwa inaendelea kupata faida na kukua,nitafanya kama shukrani kwa
jamii kwa kurudisha sehemu ya faida kwa kuchangia misaada wakati wa maafa,kuchangia vifaa vya
shule,huduma za afya n.k kwa jamii ya watu wa ndani na nje ya MWANZA

6
3 Bidhaa & Huduma.
Bidhaazitakazouzwa.
 Cam shafts GN
 Tyresza tri- Cycle (Bajaj)
 Tyres za Bodaboda
 Rim za boxer size 18,17
 Tubes size 16,17,18
 Rim
 Rim za Bajaj
 Piston
 Wiring
 Indicator
 Dashboard
 Sterling
 Taa ya mbele
 Site mirror
 Taa ya nyuma
 Switch ya funguo
 Switch ya taa yambele
 Switch ya indicator
 Clutch cable
 Clutch plate
 Clutch cent
 Battery N9, NS
 Accelator cable
 Bulb za indicator
 Bulb za taa ya nyuma
 Bulb ya taa ya mbele
 Bulb ya dashboard
 Oils series za shock up za boxer & TVS
 Oils series za gear level
 Oils series za spoket
 Bearings za mbele na nyuma
 Plugs
 Ring piston
 Piston ring
 Gasket overall
 Kick
 Kiti
 Shaft ya kick
 Shaft ya spoket
 Shaft ya gear level
 Engine coil

7
 Magnet coil
 Spoket full
 Spoket single
 Hub ya spoket ya nyuma
 Hub ya brake
 Brake pads
 Pushrods
 Stick brake
 Tank
 Mafuta ya brake
 Bearings kifua
 Stand kubwa
 Stand ndogo
 Spring break
 Spring ya stand kubwa
 Spring ya stand ndogo
 Maji ya battery
 Horn
 Timing chain & adjust
 Fuel pipes
 Bumper za battery
 Fuse box
 Fuse
 Uzi wa moto
 Cylinder head GN
 Mkasi GN
 Nali
 Bolt nuts
 End claft
 Master brake GN
 Koki ya mafuta
 Case ya nyuma GN
 Air cleaner
 Msumari tairi ya nyuma
 Msumari tairi ya mbele

8
4 Uchambuzi wa soko

4.1 Muhtasari wa Soko


Sekta ya Vipuri vya vyombo vya moto Hususani Pikipiki,Katika Soko la rejareja nchini Tanzania ni
sekta Inayokuwa Kila Siku kutokana na ukuaji wake ambapo kwa sasa soko la Vipuri limeteka zaidi na
kuwa kimbilio la watu wengi wanaomiliki vyombo hivi muhimu vya usafiri ikiwemo Pikipiki maarufu
Kama Bajaj na Bodaboda.
Soko nitakalolenga zaidi ni kundi la wenye kipato cha kati na juu na Kupitia wale wanaoishi mkoa wa
MWANZA katika eneo ambalo biashara hii ilipo.

4.2 Wateja
Walengwa wakuu ni wamiliki na madereva wa vyombo hivi vya Pikipiki waliopo Mwanza

4.3 Ushindani wa Kibiashara


[Ni washindani wangapi niko nao katika eneo la biashara yangu?]……………………………………………..

[Washindani wako ni nani na ni nini nguvu na udhaifu wao?


……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

[Je! Biashara yangu na suluhisho ninalotoa ni bora kuliko za washindani waliopo katika eneo
hili?]………………………………………………………………(Ndiyo/Hapana)
 Kwa kupokea taarifa kupitia wateja nitakao wahudumia nitaweza kubaini mahitaji yao na
kufanyia kazi mapungufu hayo ili kutoa huduma zilizo bora zaidi ya washindani kibiashara
waliopo .

9
JEDWALI: MLINGANYO WA UBORA WA HUDUMA KATIKA USHINDANI WA KIBIASHARA.

Sababu Mimi Ninaweza Siwezi Mshindani A Mshindani B Umuhimu Kwa Mteja

BIDHAA
BEI
UBORA
MACHAGUO
HUDUMA
KUAMINIKA
MAPUNGUFU
UTAALAMU
SIFA
MAHALI
MUONEKANO
NJIA ZA UUZAJI
SERA ZA MIKOPO
MATANGAZO
NEMBO

5 Mkakati & Utekelezaji

UPATAJI WA WATEJA/MBINU ZA MASOKO.


 Kuzingatia muda wa kufungua (mapema na kuchelewa kufunga) kutapelekea wateja
wanaohitaji huduma mapema au wale wanaochelewa kuzoea kuja kuhudumiwa kwangu.
 Kusambaza BIDHAA hadi mteja alipo kwa kuongeza gharama kidogo za usafiri kumfikia
mnunuzi husika.
 Kutoa zawadi ndogo ndogo kwa wateja .
 kujitolea au toa misaada ya kijamii yenye lengo la kujitangaza.
 Kutoa elimu au ushauri kuhusu Vipuri na bidhaa nyinginezo zinazouzwa na Blasio Auto Spare
Parts.
 Kujali wateja na kwa kuzingatia ubora wa bidhaa/huduma wanayohitaji.
 Vyombo vya habari, njia hii itahusisha, Televisheni, Redio, Magazeti n.k hizi ni njia ambazo
zimezoeleka zimekuwa zikitumika tangu zamani,ninaweza kuzitumia pia kutafuta soko la
bidhaa zetu.

10
[Gharama ipoje kupata hao wateja?]
 Kutumia mitandao ya kijamii gharama yake ni kutumia huduma ya internet lakini pia kufanya
malipo ya ‘sponsored ads’ pale inapohitajika ambapo gharama ya chinini usd 5 (tshs 12’000/-
) kwasiku 5.(kwa maelekezo zaidi Mshauri wa kibiashara – 0656325757)

 Kutengene za vipeperushi vinavyoelezea huduma /sehemu ulipo na pia anuani ya kurasa za


kijamii facebook /instagram ili kuzitangaza aina bidhaa na Huduma tunazotoa.
 Redioni– hutegemeana na gharama tajwa toka chombo cha habari husika.
 Misaadayakijamiiitategemeananahaliyakipato cha kampuni kwa wakati huo.

[Thamani ya Maisha ya Wateja wako itakuwa nini?]


 Wateja wote wa hususani wamiliki na maderava wa pikipiki,wataweza kupata elimu na
ushauri mzuri wakati wa manunuzi ya vipuri utakaowasaidia kuchagua bidhaa orijino
zitakazoendana na viwango ubora na kuokoa fedha kwa kuepuka gharama za kununua vipuri
kila mara.

 Pia watakao tumia bidhaa zetu wataokoa muda wao kwa sababu Blasio Auto Spare Parts,
Tutaweza kumfikia mteja alipo kwa haraka mara tu anapohitaji huduma na bidhaa zetu ndani
ya eneo la Sido.

UPATIKANAJI WA BIDHAA KWA JUMLA.


 Manunuzi Jumla ya BIDHAA yataweza kufanyika ndani ya Tanzania kupitia wauzaji wa jumla
waliopo Dar es Salaam K/KOO mtaa wa msimbazi,likoma au pia nje ya TANZANIA kwa kuagiza
mzigo kupitia makampuni au wafanyabiashara binafsi watakaokubalika kufanya Biashara na
Blasio Auto Spare Parts.

11
6 Mpango wa fedha & Makadirio
6.1 Gharama za Kuanzisha na Ufadhili
Gharama zote za kuanza biashara hii zitatokana na vyanzo vyangu BINAFSI VYA MAPATO.

JEDWALI LA KADIRIO LA GHARAMA

BIDHAA MANUNUZI MAUZO FAIDA


(JUMLA)
STERING GN,TVS,BM 6000
TAA YA NYUMA GN 8500
TAA YA NYUMA TVS 8000
TAA YA NYUMA BM 7500
TAA YA MBELE GN KUBWA 12000
TAA YA MBELE GN NDOGO 10000
TAA YA MBELE BM 12000
TAA YA MBELE TVS 13000
SIDE MIRROR BM 7000
SIDE MIRROR TVS 7000
SWITCH YA FUNGUO GN 3500
SWITCH YA FUNGUO TVS 7500
SWITCH YA FUNGUO BM 7000
CLUTCH CABLE 1100
CLUTCH PLATE 2500
GN CLUTCH CENTRE TUNDU 4 7000
CLUTCH CENTRE TUNDU 5 7500
CLUTCH CENTRE TUNDU 6 7500
BATTERY N9 22000
ACCELERATOR CABLE 1100
CAM SHAFT GN 8000
CAM SHAFT TVS 9000
CAM SHAFT BM 8000
BAJAJ TYRE 55000
RIM BODABODA GN MBELE 55000
RIM BODABODA GN NYUMA 50000

12
RIM 17’ TVS & BM MBELE 40000
RIM 17’ TVS & BM NYUMA 45000
TYRE GN NYUMA 45000
TYRE GN MBELE 40000
RIM TVS MBELE 65000
RIM TVS NYUMA 60000
RIM BM MBELE 60000
RIM BM NYUMA 55000
TUBE SIZE 16 MBELE 40000
TUBE SIZE 16 NYUMA 45000
RIM BAJAJI 70000
PISTON GN 150 5500
PISTON GN 125 5000
PISTON BM 9500
PISTON TVS 10000
WIRING GN 8000
WIRING BM 10000
WIRING TVS 15000
DASH BOARD GN 12000
DASH BOARD TVS 18000
DASH BOARD BM 18000

13
14
Gharamazakuanzia
Gharamazalazima
LESENI/SHERIA NA VIBALI
MANUNUZI YA AWALI YA BIDHAA ZOTE JUMLA
MANUNUZI MENGINEYO
BANGO LENYE JINA LA BIASHARA
MSHAHARA WA MFANYAKAZI
CHAGA ZA KUPANGIA BIDHAA
SHOWCASE DISPLAY CABINET
KODI YA FRAME @MWEZI_________ XMIEZI _____
MAREKEBISHO YA FRAME
MENGINEYO

Jumlayagharamazalazima

Kadirio la gharamazamwezi
kodi
Vyakutumia
Mishahara / Posho
Gharamayawastaniyakilamwezi
x Idadiyamiezi:
GharamaJumlayaMwezi
GharamazaKuanzishajumla

15

You might also like