Katiba Ya Kikundi Cha Wazalendodocx

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 6

KATIBA YA KIKUNDI CHA WAZALENDO GROUP

(WAGRO) KINONDONI TAREHE 21/10/2020

KATIBA YA CHAMA
Jina la Kikundi ni Wazalendo Group (WAGRO)
Kikundi cha Wajasiriamali wadogo wadogo

1.0. UANACHAMA
Maana ya uanachama:- Mwanachama ni yule mtu aliye jiunga kwenye kikundi kwa hiari yake kwa
kukubaliana na taratibu pamoja na masharti ya kikundi. Idadi ya Wanachama ni (10)

2.0. MADHUMUNI/ MALENGO YA KIKUNDI


1. Kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii
2. Kusaidiana katika shida na raha
3. Kujishughulisha na shughuli za kiuchumi

3.0. WAJIBU WA WANAKIKUNDI WA WAZALENDO GROUP (WAGRO)


1. Mwanachama awe mwenyeji wa kinondoni
2. Mwanachama awe mtu wa kuchangia mawazo chanya ili kuleta maendeleo ya kikundi
3. Anapaswa kutunza nidhamu ya Chama chetu na ajiheshimu na kuwaheshimu wanachama wenzake
4. Atimize wajibu wake kulingana na katiba.

4.0 UONGOZI
Kikundi kitakuwa na viongozi wafuatao:-
1. Mwenyekiti
2. Katibu
3. Mweka hazina.

5.0 SIFA ZA KIONGOZI


1. Awe mwaminifu
2. Awe na uwezo wa kuogoza.
3. Awe na msimamo thabiti
6.0 KAZI ZA KIONGOZI
 Mwenyekiti: - Ndiye msimamizi mkuu wa shughuli zote za kikundi.
 Katibu: - Kusaidiana na Mwenyekiti kuitisha vikao, kuandaa na kutunza kumbukumbu za
vikao, kutoa taarifa halisi za kikundi , ndiye mtendaji mkuu wa shughuli zote za kikundi.
 Mwekahazina:- Kukusanya na kutunza fedha za kikundi, kutoa taarifa ya mapato na
matumizi ya kila mwezi, kutoa taarifa ya fedha ya mwaka.
 Mjumbe mmoja (1):- Anasaidiana na viongozi wa kikundi kama kuna kazi za ziada au
kutoa mawazo kwa viongozi.

7.0 MUDA WA UONGOZI


 Uongozi utadumu Kwa muda wa miaka miwili.
 Akiongoza vizuri ataendelea tena kuongoza
 Kujiudhuru uanachama
 Kifo
 wanachama kutokua na imani naye

KUBADILI KWA KATIBA


Katiba hii inaweza kubadilishwa au kufanyiwa marekebisho Kwa utaratibu ufuatao.
(1) Kwenye mkutano mkuu wa chama

(2) Mkutano wa dharula

AGENDA
1. Kufungua
2. Kusoma muhtasari wa kikao kilichopita 18/10/2021
3. Kupitisha katiba
4. Mengineyo
5. Kuchangua viongozi
6. Kusajili kikundi ngazi ya Wilaya
7. Ufunguzi wa akaunti.
8. Kufunga kikao
AGENDA NA. 01/2021 KUFUNGUA KIKAO
Mwenyekiti amefunga kikao mnamo Saa2:30 Asubuhi akiwaomba wajumbe wachangie mawazo
mbalimbali katika kikao.

AGENDA NA. 02/2021: KUSOMA MUHTASARI WA KIKAO KILICHOPITA CHA


TAREHE 18/10/2021.
Katibu alisoma muhtasari wa kikao kilichopita. Wajumbe walikubaliana na muhtasari uliosomwa.

AGENDA NA. 03/2021: KUPITISHA KATIBA


Katibu amesoma katiba yote kama ilivyoandikwa na wajumbe kukubaliana nayo.

AGENDA NA. 04/2021: MENGINEYO


Wajumbe waliongelea umuhimu wa kuchangia mchango wa kila mwisho wa mwezi ili kuongeza
ukuaji wa mfuko wa kikundi.

AGENDA NA. 05/ 2021: KUCHAGUA VIONGOZI


Baada ya majadiliano mafupi wajumbe wamependekeza viongozi watakaochaguliwa kwenye
kikundi chetu waongoze muda wa miaka miwili kama Katiba inavyoelekeza.

Viongozi wenyewe ni:-


1. Ndugu Shikome R Nyanda M/kiti
2. Ndugu Emmanuel Mallya Katibu
3. Ndugu Denis Avit M/Hazina

AGENDA NA. 06/2021: KUSAJILI KIKUNDI NGAZI YA (W)


Tuliweza kuonana na afisa maendeleo ya jamii wa kata ya kayanga na akatushauri ili kikundi chetu
kusajili lazima tuwe na katiba ya kikundi yenye mambo ya msingi li kudumisha kikundi chetu
na kuambatanisha vitu muhimu kama:-
1. Barua ya M/kiti wa Kitongoji
2. Barua kikundi kupitia (k.k)Mtendaji wa Kata
3. Muhtasari wa kikundi na mahudhurio yenye sahihi halisi.

AGENDA NA. 07/2021: UFUNGUZI WA AKAUNTI


Wajumbe tumekubaliana baada ya kumaliza kusajili rasmi kikundi ngazi ya halmashauri
tujipange kwa ajili ya kufungua akaunti ya kikundi.
AGENDA NA. 08/2021: KUFUNGA
Mwenyekiti amefunga kikao mnamo Saa 1030 Jioni kwa kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao
mzuri wa mawazo na kuwatakia kila la kheri wanaporudi nyumbani.

………………………
Shikome Nyanda
M/KITI
KIKUNDI CHA WAZALENDO,
(WAGRO),
KITONGOJI KINONDONI,
KATA-KINONDONI,
KINONDONI.
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA,
S.L.P …..,
KINDONDONI.

K.K,
AFISA MTENDAJI,
KATA KINONDONI,
S.L.P ……,
KINONDONI.

YAH: OMBI LA USAJILI WA KIKUNDI CHA WAZALENDO


(WAGRO)
Husika na kichwa cha habari hapo juu,
Sisi ni Wanakikundi cha Wazalendo kinachojishughulisha na ujasiriamali mdomdogo Kinondoni mjini.
Kwa kutambua utaratibu wa Kikundi uliopo katika Wilaya yetu tunaomba usajili wa Kikundi chetu ili
tuweze kutambuliwa rasmi ndani na nje ya Wilaya yetu.
Tumeambatanisha muhtasari wa Kikundi na Katiba.
Tunatumaini ombi letu utalipokea.

Wako katika ujenzi wa Taifa.

……………………….. ……………….……..
EMMANUEL MALLYA SHIKOME NYANDA
KATIBU M/KITI
MUHTASARI WA KIKUNDI CHA KARAGWE TUINUANE
KIUCHUMI (KIKATUKI) KITONGOJI KAGURURU,
KATA KAYANGA, TAREHE 21/10/2021

WALIOHUDHURIA:-
NA. JINA KAMILI CHEO SAHIHI
1. SHIKOME NYANDA M/KITI
2. EMMANUEL MALLYA KATIBU
3. DENIS AVIT M/HAZINA
4. MATOKE MATOKE MJUMBE
5. EMMANUEL CONSTANTINE MJUMBE
6. MANINGU CHARLES MJUMBE
7. MJUMBE
8. MJUMBE
9. MJUMBE
10. MJUMBE

You might also like