Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 58

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

UCHAMBUZI WA MAJIBU YA WATAHINIWA


KATIKA MASWALI YA MTIHANI WA
KUMALIZA ELIMU YA MSINGI
MWAKA 2013

KISWAHILI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

UCHAMBUZI WA MAJIBU YA WATAHINIWA KATIKA

MASWALI YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA

MSINGI MWAKA 2013

KISWAHILI
Kimechapishwa na
Baraza la Mitihani la Tanzania,
S.L.P. 2624,
Dar es Salaam, Tanzania.

© Baraza la Mitihani la Tanzania, 2013

Haki zote zimehifadhiwa.

ii
YALIYOMO

DIBAJI ................................................................................................................. IV
1.0 UTANGULIZI ................................................................................................1
2.0 UCHAMBUZI WA MAJIBU YA WATAHINIWA .............................................1
2.1 SEHEMU A: SARUFI ......................................................................................1
2.2 SEHEMU B: LUGHA YA KIFASIHI ...................................................................19
2.3 SEHEMU C: UFAHAMU ................................................................................29
2.4 SEHEMU D: USHAIRI...................................................................................39
2.5 SEHEMU E: UTUNGAJI ................................................................................45
3.0 HITIMISHO .................................................................................................46
4.0 MAONI NA MAPENDEKEZO .....................................................................48
KIAMBATISHO A ................................................................................................49
 

iii
DIBAJI

Taarifa ya uchambuzi wa majibu ya maswali ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya


Msingi kwa somo la Kiswahili imeandaliwa kwa lengo la kutoa mrejesho kwa
wanafunzi, walimu, watunga sera, wakaguzi, watunga mitalaa na wadau
wengine wa elimu kuhusu namna wanafunzi walivyojibu maswali ya mtihani huo.
Majibu ya wanafunzi katika mtihani ni kiashiria kimojawapo kinachoonesha
mambo ambayo wanafunzi waliweza kujifunza kwa ufasaha na yale ambayo
hawakuweza kujifunza kwa ufasaha katika kipindi cha miaka saba ya elimu ya
msingi.

Katika taarifa hii, mambo mbalimbali ambayo yamechangia watahiniwa


kushindwa kujibu maswali kwa usahihi yameainishwa. Uchambuzi unaonesha
kuwa yafuatayo yamechangia kuwafanya wanafunzi kutoweza kujibu maswali
kwa usahihi: kushindwa kutambua matakwa ya swali, kuwa na uelewa mdogo
wa mada mbalimbali katika somo; kutofahamu kanuni za lugha na matumizi ya
misamiati; kutojibu kabisa baadhi ya maswali au kuchagua jibu zaidi ya moja
kinyume na maelekezo katika mtihani. Uchambuzi kwa kila swali umefanyika
ambapo dosari mbalimbali zilizojitokeza wakati watahiniwa walipokuwa wanajibu
maswali yao zimeainishwa kwa kuonesha idadi ya watahiniwa waliojibu maswali
kwa usahihi, walioshindwa kuchagua jibu sahihi, walioacha kujibu swali na
ambao waliandika jibu zaidi ya moja katika swali husika.

Baraza la Mitihani la Tanzania lina imani kuwa mrejesho uliotolewa


utawawezesha wadau mbalimbali wa elimu kuchukua hatua madhubuti ili
kuboresha ufundishaji na ujifunzaji kwa lengo la kupata ufumbuzi wa dosari
zilizoainishwa katika taarifa hii.

iv  
Aidha, Baraza la Mitihani la Tanzania lina imani kuwa endapo maoni
yaliyotolewa yatafanyiwa kazi ipasavyo, ujuzi na maarifa watakayopata
wanafunzi wanaohitimu elimu ya msingi vitaongezeka na hatimaye kiwango cha
ufaulu katika Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi kitaongezeka pia.

Mwisho Baraza la Mitihani linapenda kutoa shukrani za dhati kwa Maafisa


Mitihani, Makatibu Muhtasi na wengine wote waliohusika katika kuandaa taarifa
hii. Baraza litashukuru kupokea maoni na mapendekezo kutoka kwa walimu,
wanafunzi na wadau wengine wa elimu kwa ujumla ambayo yatasaidia katika
kuboresha taarifa ya uchambuzi wa maswali ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya
Msingi kwa siku zijazo.

Dkt. Charles E. Msonde


KAIMU KATIBU MTENDAJI

v
vi  
1.0 UTANGULIZI

Taarifa hii imeandaliwa kwa lengo la kutoa mrejesho kuhusu namna


ambavyo watahiniwa walijibu maswali katika mtihani wa somo la Kiswahili.
Mtihani wa Kiswahili ulikuwa na maswali 50 ya kuchagua jibu sahihi
ambayo yalikuwa yamegawanywa katika sehemu tano kama ifuatavyo:
Sehemu A: Sarufi; B: Lugha ya Kifasihi; C: Ufahamu; D: Ushairi; na E:
Utungaji. Jumla ya watahiniwa 867,983 walisajiliwa kufanya mtihani wa
PSLE 2013 ambapo miongoni mwao waliofanya mtihani wa somo la
Kiswahili walikuwa 844,719 na kati yao watahiniwa 583,348 sawa na
asilimia 69.06 walifaulu mtihani huo.

2.0 UCHAMBUZI WA MAJIBU YA WATAHINIWA

Uchambuzi wa majibu ya watahiniwa kwa kila swali umefanyika na


sehemu hii inaainisha maswali yaliyoulizwa na majibu ya kuchagua
waliyopewa. Idadi ya watahiniwa waliochagua kila jibu na asilimia yao
imeoneshwa. Aidha uchambuzi wa sababu zinazoweza kuwa zilichangia
kuwafanya wasichague jibu sahihi zimeainishwa.

2.1 Sehemu A: Sarufi

Swali la 1: Sweta langu limeshonwa na fundi mzoefu? “Mzoefu” ni aina


gani ya neno?
A. Kielezi
B. Kivumishi
C. Kiunganishi
D. Nomino
E. Kitenzi.

1  
Majibu ya watahiniwa

Chaguo A B* C D E Wasiojibu Mengine


Idadi ya
275,841 317,788 77,172 111,598 57,810 2,226 2,318
watahiniwa
Asilimia ya
32.65 37.62 9.14 13.21 6.84 0.26 0.27
watahiniwa

Swali lililenga kupima uwezo wa mtahiniwa wa kutambua aina za maneno.


Asilimia 37.62 ya watahiniwa walichagua jibu B “Kivumishi” ambalo ndilo jibu
sahihi. Asilimia 32.65 ya watahiniwa walichagua kipotoshi A ambacho ni
kielezi. Watahiniwa hao walipotoshwa na kitenzi “limeshonwa” ambacho
kilifuatwa na “fundi mzoefu,” hivyo kuona jibu sahihi ni kielezi na kusahau
kuwa neno fundi ni nomino. Hata hivyo, kwa kanuni ya lugha ya Kiswahili
nomino haiwezi kufuatwa na kielezi. Hali kadhalika kuwepo kwa asilimia
9.14 ya watahiniwa waliochagua kipotoshi C “Kiunganishi” inaonesha kuwa
watahiniwa hao walishindwa kujua kuwa neno “mzoefu” sio kiunganishi kwa
sababu kwa kuzingatia sintaksia ya lugha ya Kiswahili neno ambalo ni
kiunganishi haliwezi kukaa mwishoni mwa sentensi. Asilimia 13.21 ya
watahiniwa walichagua kipotoshi D “Nomino” ambacho ni jina
linalosimamiwa na neno “fundi” na wala sio kivumishi na asilimia 6.84
walichagua E “Kitenzi” ambacho nacho hakitoi taarifa yoyote kuhusu kazi ya
Nomino.

Swali la 2: “Ningejua ukweli wa mambo kabla __________ hapa bure saa


hizi.” Neno gani linakamilisha sentensi hiyo?
A. nisingalikuja
B. ningekuja
C. singelikuja
D. nisingelikuja
E. nisingekuja.
2  
Majibu ya watahiniwa

Chaguo A B C D E* Wasiojibu Mengine


Idadi ya
56,299 211,534 58,302 131,989 382,461 1,839 2,329
watahiniwa
Asilimia ya
6.66 25.04 6.9 15.62 45.27 0.22 0.28
watahiniwa

Swali lililenga kupima uwezo wa mtahiniwa kutumia maneno katika sentensi


zenye masharti. Watahiniwa walio wengi walikuwa na uelewa wa swali hili
kwani asilimia 45.27 walichagua jibu E ambalo ni sahihi. Uchaguzi wa
kipotoshi B “ningekuja” kwa watahiniwa 211,534 ambao ni sawa na asilimia
25.04 unaonesha kuwa watahiniwa hao waliathiriwa na umbo la “nge”
ambalo pia linajitokeza katika kitenzi “Ningekuja” bila kuzingatia taratibu
kuwa kauli hiyo ni ya kujilaumu yaani “ningejua” hivyo hukamilishwa na
ukanushi wa tendo yaani “nisingekuja.” Uchaguzi wa kipotoshi A, C na D
kwa asilimia 29.18 ya watahiniwa unaonesha kuwa watahiniwa waliathiriwa
na umbo la “singali,” “singeli” ambayo yote yanaonesha ukanushi lakini
wakashindwa kufuata masharti ya umbo la “nge” kufuatiwa na umbo la
“nge.”

Swali la 3: “UKIMWI unaua.” Mbunge alisema. Ipi ni kauli taarifa ya sentensi


hiyo kati ya hizi zifuatazo?
A. Mbunge aliwaambia UKIMWI unaua
B. Mbunge alisema UKIMWI unaua
C. UKIMWI unaua mbunge alisema
D. Mbunge alisema kwamba UKIMWI unaua
E. Mbunge alieleza UKIMWI unaua.

3  
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C D* E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
86,702 216,379 96,050 394,268 46,404 2,427 2,523
watahiniwa
Asilimia ya
10.26 25.61 11.37 46.67 5.49 0.29 0.3
watahiniwa

Swali lililenga kupima ujuzi wa watahiniwa katika kuelewa kauli za sentensi


na lilimtaka mtahiniwa kuonesha sentensi aliyopewa ipo katika kauli gani?
Aslimia 46.67 ya watahiniwa walichagua jibu D “Mbunge alisema kwamba
UKIMWI unaua” ambalo ni jibu sahihi. Uchaguzi huu unaonesha kuwa
watahiniwa walielewa kuwa kauli taarifa inaambatana na neno “kwamba”
katika kueleza kile kilichosemwa. Kuwepo kwa jumla ya asilimia 52.73 ya
waliochagua kati ya vipotoshi A, B, C na E kunaonesha wazi kuwa
watahiniwa walikosa ujuzi unaotawala muundo wa kauli katika sentensi.
Hivyo watahiniwa hao walishindwa kuelewa kuwa umbo la “kwamba” lilikuwa
kigezo muhimu katika kutoa kauli ya taarifa.

Swali la 4: “Anna anatembea polepole __________twiga.” Kifungu kipi cha


maneno kinakamilisha sentensi hiyo?
A. mithili ya
B. mathalani ya
C. mahadhi ya
D. maridhawa ya
E. madhali ya.

4  
Majibu ya watahiniwa

Chaguo A* B C D E Wasiojibu Mengine


Idadi ya
422,895 117,383 80,359 126,784 89,662 4,730 2,940
watahiniwa
Asilimia ya
50.06 13.9 9.51 15.01 10.61 0.56 0.35
watahiniwa

Swali lililenga kupima matumizi ya msamiati wa Kiswahili ambapo ni asilimia


50.06 ya watahiniwa ndio waliochagua jibu A “mithili ya” ambalo ndilo jibu
sahihi. Asilimia 15.01 walichagua jibu D “maridhawa ya” ambalo si jibu
sahihi kwani neno hilo maana yake ni kuridhisha. Aidha, uchaguzi wa
kipotoshi B “mathalani ya” kwa asilimia 13.9 ambalo sio jibu sahihi
inaonesha kuwa watahiniwa walipotoshwa na neno “mathalani” ambalo lina
maana ya mfano lakini walishindwa kuelewa kuwa kisarufi mathalani
haiendani na “ya”. Uteuzi wa vipotoshi C “mahadhi ya” na E “madhali ya”
unaonesha kuwa watahiniwa hawakuwa na ujuzi wa maana mbalimbali za
maneno kwani kila kifungu cha maneno kilikuwa na maana tofauti kabisa na
kingine. Aidha mahadhi yanahusisha upandaji na ushukaji wa sauti katika
uimbaji na “madhali ya” ikiwa na maana ya “kwa sababu,” hivyo vifungu
vyote vina maana tofauti na “mithili ya.”

Swali la 5: Neno lipi halilandani na maneno yafuatayo?


A. Msonge
B. Tembe
C. Daraja
D. Kibanda
E. Ghorofa.

5  
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C* D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
117,640 182,789 399,380 51,234 87,293 3,507 2,910
watahiniwa
Asilimia ya
13.93 21.64 47.28 6.06 10.33 0.42 0.34
watahiniwa

Swali lililenga kupima uwezo wa mtahiniwa katika kutumia msamiati. Ni


asilimia 47.28 ya watahiniwa waliofanya mtihani waliweza kuchagua jibu
sahihi ambalo ni C “Daraja.” Asilimia 21.64 ya watahiniwa walichagua B
“Tembe” ambalo si jibu sahihi. Watahiniwa hawa walishindwa kuelewa
maana ya neno “Tembe” ambalo ni aina ya nyumba inayotumiwa na aina
mbalimbali ya makabila hapa nchini. Aidha, uchaguzi wa vipotoshi A, D na E
kwa asilimia 30.32 ambavyo vyote pia ni majina ya aina mbalimbali za
nyumba, unaonesha kuwa hawana maarifa ya kutosha ya misamiati ya
lugha ya Kiswahili. Hivyo watahiniwa hao walishindwa kuelewa kuwa
vipotoshi hivyo vinne ambavyo havikuwa majibu sahihi vyote vilikuwa na
maana moja ambayo ni aina za nyumba.

Swali la 6: Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo ni kauli ya kutendea?


A. Watoto wanacheza mpira
B. Mpira unachezwa na watoto
C. Watoto wanachezeana mpira
D. Watoto wanachezea mpira
E. Mpira unachezewa na watoto.

6  
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C D* E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
152,787 133,451 94,744 337,812 119,710 3,191 3,058
watahiniwa
Asilimia ya
18.09 15.8 11.22 39.99 14.17 0.38 0.36
watahiniwa

Swali lililenga kupima ujuzi wa kauli za vitenzi. Asilimia 39.99 ya watahiniwa


walichagua jibu sahihi D “Watoto wanachezea mpira.” Sababu iliyowafanya
watahiniwa kupata swali hili kwa usahihi ni uwezo wa kuhusisha umbo la
kisarufi -e- lililopo katika kauli ya kutendea na umbo -e- lililopo katika kitenzi
“wanachezea.” Watahiniwa waliochagua kati ya vipotoshi A, B na E ambao
ni asilimia 48.06 walishindwa kugundua upungufu uliokuwepo katika
vipotoshi hivyo ambapo umbo -e- halionekani likijipambanua. Aidha
waliochagua kipotoshi C ambao ni asilimia 11.22 walivutiwa na umbo la -
ean- bila kujua kuwa umbo hili lipo katika kauli ya kutendeana na wala sio
kutendea.

Swali la 7: “Tumejifunza__________ kujikinga na VVU na UKIMWI.” Kifungu


kipi cha maneno kati ya vifuatavyo kinakamilisha sentensi hiyo?
A. ibara ya
B. jinsi ya
C. jinsia ya
D. ilhali ya
E. aina ya
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B* C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
32,111 656,931 66,338 28,572 56,135 1,962 2,704
watahiniwa
Asilimia ya
3.8 77.77 7.85 3.38 6.65 0.23 0.32
watahiniwa

7  
Swali lililenga kupima uwezo wa watahiniwa kutumia sarufi ya lugha. Swali
hili ni miongoni mwa maswali yaliyojibiwa kwa usahihi na idadi kubwa ya
watahiniwa katika mtihani huu ambapo 77.77 ya watahiniwa ndio
waliochagua jibu sahihi yaani B “jinsi ya.” Uchaguzi wa kipotoshi C “jinsia
ya” unaonesha kuwa watahiniwa hawakuwa na ujuzi wa kuelewa tofauti
iliyopo kati ya “jinsi ya” ikiwa na maana “namna ya” na “jinsia ya” maana
yake ikiwa ni hali ya kuwa mume au mke. Aidha uchaguzi wa vipotoshi A
“ibara ya” D “ilhali ya” na E “aina ya” kwa asilimia 13.83 unaonesha kuwa
watahiniwa walishindwa kuelewa maana ya maneno hayo na jinsi
yasivyoweza kuikamilisha sentensi iliyotolewa.

Swali la 8: Sehemu ambayo ng’ombe huogeshwa ili kuwaepusha na


magonjwa huitwaje?
A. Mto
B. Bwawa
C. Ziwani
D. Josho
E. Joshi.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C D* E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
70,687 87,495 55,231 416,752 208,026 3,515 3,047
watahiniwa
Asilimia ya
8.37 10.36 6.54 49.33 24.63 0.42 0.36
watahiniwa

Swali lililenga kupima ujuzi wa mtahiniwa kuhusu matumizi ya msamiati


unaoonesha uhusiano wa sehemu mbalimbali ambapo huwepo maji au
chombo kinachohusika na maji. Asilimia 49.33 ya watahiniwa walichagua
jibu D “Josho” ambalo ni jibu sahihi. Uchaguzi wa vipotoshi A, B na C kwa

8  
asilimia 25.27 ulidhihirisha kuwa baadhi ya watahiniwa walikuwa hawajui
msamiati sahihi unaoelezea sehemu inayotumika kuwaogeshea ng’ombe ili
kuwaepusha na magonjwa kwani Mto, Bwawa na Ziwani ni sehemu zenye
maji na huenda ng’ombe wangeweza kuogeshewa lakini hazina dawa
maalum kwa ajili ya kuwaogesha na kuwaepusha na magonjwa. Uchaguzi
wa kipotoshi E “Joshi” ambacho sio jibu sahihi kikiwa na maana ya sehemu
ya mbele au tanga la mbele la chombo kinachosafiri ndani ya maji ulitokana
na kuvutiwa tu kwa watahiniwa kutokana na athari za kimatamshi.

Swali la 9: “Mboga haina chumvi ya kutosha.” Wingi wa sentensi hiyo ni


upi?
A. Mboga hazina chumvi ya kutosha
B. Mboga haina machumvi ya kutosha
C. Mamboga hayana chumvi ya kutosha
D. Mamboga hayana chumvi za kutosha
E. Mboga haina chumvi za kutosha.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A* B C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
571,409 54,177 55,294 50,746 107,616 2,653 2,858
watahiniwa
Asilimia ya
67.64 6.41 6.55 6.01 12.74 0.31 0.34
watahiniwa

Swali lililenga kupima uwezo wa mtahiniwa wa kutumia maneno katika


umoja na wingi. Watahiniwa wengi yaani asilimia 67.64 walikuwa na uelewa
wa swali hili kwani walichagua jibu A “Mboga hazina chumvi ya kutosha”
ambalo ni sahihi. Uchaguzi wa kipotoshi B, C na D kwa watahiniwa 160,217
ambao ni sawa na asilimia 18.97 unaonesha kuwa watahiniwa hao
waliathiriwa na tabia ya baadhi ya nomino ambazo zina uwezo wa kupokea
umbo la wingi kwa mfano boga (umoja) na maboga (wingi). Hivyo kwa athari

9  
hiyo wakaviona vipotoshi venye maneno “Mamboga” na “machumvi” kuwa
jibu sahihi wakati maneno hayo hayana umoja na wingi. Uteuzi wa kipotoshi
E unaonesha jinsi watahiniwa hao 107,616 sawa na asilimia 12.74
wasivyokuwa na ujuzi wa kutosha kuhusu wingi wa nomino “Chumvi” ambao
unabakia kuwa “chumvi” kwa umoja na wingi. Hali hii inadhihirisha kuwa
watahiniwa wengi hudhani kuwa ni lazima kila nomino kuwa na umbo
mahususi lioneshalo wingi.

Swali la 10: Nywele zinazoota kuanzia karibu na masikio mpaka kwenye


mashavu huitwaje?
A. Mvi
B. Sharafa
C. Ndevu
D. Sharubu
E. Kope.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B* C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
41,959 272,066 260,189 227,862 37,189 2,664 2,824
watahiniwa
Asilimia ya
4.97 32.21 30.8 26.97 4.4 0.32 0.33
watahiniwa

Swali lililenga kupima uwezo wa mtahiniwa katika kutumia msamiati. Ni


asilimia 32.21 tu ya watahiniwa waliofanya mtihani walioweza kuchagua jibu
sahihi ambalo ni B “Sharafa.” Asilimia 30.8 ya watahiniwa walichagua C
“ndevu” ambalo si jibu sahihi. Watahiniwa hawa walishindwa kuelewa
maana ya neno “ndevu” kuwa ni nywele zinazoota katika kidevu. Aidha,
inawezekana watahiniwa hawakuelewa kuwa nywele zinazoanzia kwenye
masikio zina jina tofauti ambalo ni sharafa. Kwa ujumla majibu yaliyotolewa
na watahiniwa yanaonesha wazi kuwa hawakuwa na ujuzi wa kutosha wa
10  
msamiati wa Kiswahili kwa vile vipotoshi A, D na E vina maana tofauti
kabisa na jibu sahihi ambalo ni “Sharafa” pamoja na kwamba zote ni nywele
lakini huota sehemu tofauti.

Swali la 11: Sentensi ipi kati ya hizi ipo katika hali timilifu?
A. Mheshimiwa Rais anahutubia mkutano
B. Mheshimiwa Rais alihutubia mkutano
C. Mheshimiwa Rais atahutubia mkutano
D. Mheshimiwa Rais amehutubia mkutano
E. Mheshimiwa Rais alikuwa anahutubia mkutano.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C D* E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
299,649 88,311 66,092 241,306 142,887 3,293 3,215
watahiniwa
Asilimia ya
35.47 10.45 7.82 28.57 16.91 0.39 0.38
watahiniwa

Swali lililenga kupima uwezo wa mtahiniwa katika kutumia njeo ya wakati.


Asilimia 28.57 walichagua D “Mheshimiwa Rais amehutubia mkutano”
ambalo ni jibu sahihi kwa kuwa kitenzi “amehutubia” kina umbo “-me-”
ambalo ni umbo la hali timilifu. Asilimia 35.47 ya watahiniwa walichagua
kipotoshi A “anahutubia” ambacho sio jibu sahihi kwa sababu walishindwa
kutambua kuwa kitenzi hicho kina umbo “na” ambalo ni umbo la wakati
uliopo hali ya kuendelea na wala sio hali timilifu. Uteuzi wa vipotoshi B, C na
E kwa asilimia 35.18 unaonesha jinsi watahiniwa husika walivyoshindwa
kutambua maumbo yanayowakilisha dhana mbalimbali za njeo katika sarufi
ya Kiswahili.

11  
Swali la 12: Neno lipi ni tofauti na maneno mengine kati ya yafuatayo?
A. Maji
B. Maziwa
C. Soda
D. Juisi
E. Samli.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C D E* Wasiojibu Mengine
Idadi ya
88,955 78,139 38,787 28,707 604,472 2,327 3,366
watahiniwa
Asilimia ya
10.53 9.25 4.59 3.4 71.56 0.28 0.4
watahiniwa

Swali lililenga kupima ujuzi wa mtahiniwa kuhusu matumizi ya msamiati


unaoonesha uhusiano wa vitu vinavyotumiwa na jamii. Swali hili ni miongoni
mwa maswali yaliyojibiwa kwa usahihi na watahiniwa wengi kwani asilimia
71.56 ya watahiniwa walichagua jibu E “Samli” ambalo ni jibu sahihi.
Uchaguzi wa vipotoshi A, B, C na D kwa watahiniwa 234,588 sawa na
asilimia 27.77 ulidhihirisha kuwa watahiniwa hao walikuwa hawajui kuwa
vipotoshi hivyo vina mfanano kwa kuwa maji, maziwa, soda na juisi vyote ni
vinywaji lakini samli ni mafuta.

Swali la 13: “Kitabu chako ni kizuri, ukienda dukani nami uninunulie


_________.” Ni kifungu kipi cha maneno hukamilisha
sentensi hiyo.
A. kama hivyo
B. kama hiko
C. kama icho
D. mfano wa iko

12  
E. kama hicho.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C D E* Wasiojibu Mengine
Idadi ya
40,158 79,487 133,888 36,987 548,722 2,455 3,056
watahiniwa
Asilimia ya
4.75 9.41 15.85 4.38 64.96 0.29 0.36
watahiniwa

Swali lililenga kupima ujuzi wa mtahiniwa katika sarufi ya lugha. Asilimia


64.96 ya watahiniwa walichagua E “kama hicho” ambalo ni jibu sahihi.
Uchaguzi wa vipotoshi A, B, C na D kwa watahiniwa 290,520 ambao ni
sawa na asilimia 34.39 unadhihirisha kuwa watahiniwa hawakuwa na ujuzi
wa kutosha kuhusu muundo wa sentensi katika kuangalia upatanisho wa
kisarufi.

Swali la 14: “Tunda huachwa mpaka likauke.” Sentensi hiyo ikiwa katika hali
ya ukanushi itakuwa ipi kati ya zifuatazo?
A. Tunda haliachwi mpaka likauke
B. Tunda haliachi mpaka likauke
C. Tunda halikuachwa mpaka likauke
D. Tunda halitaachwa mpaka likauke
E. Tunda halijaachwa mpaka likauke.
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A* B C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
471,327 63,801 100,445 145,850 57,034 3,408 2,888
watahiniwa
Asilimia ya
55.79 7.55 11.89 17.27 6.75 0.4 0.34
watahiniwa

13  
Swali lililenga kupima uwezo wa mtahiniwa katika kutambua hali mbalimbali
zinazojitokeza katika sentensi. Asilimia 55.79 ya watahiniwa walichagua jibu
A “Tunda haliachwi mpaka likauke” ambalo ndilo jibu sahihi. Watahiniwa
145,850 sawa na asilimia 17.27 walichagua kipotoshi D “Tunda halitaachwa
mpaka likauke” ambacho si jibu sahihi na huenda walifanya hivyo kwa
sababu walidhani kuwa ili kuonesha hali ya ukanushi ni lazima iwe katika
wakati ujao jambo ambalo sio sahihi. Uteuzi wa vipotoshi B, C na E kwa
asilimia 26.19 inaonesha wazi kuwa watahiniwa husika hawakuwa na ujuzi
wa hali mbalimbali zinazojitokeza katika sentensi. Aidha, watahiniwa hao
hawakuweza kuona kuwa sentensi “Tunda huachwa mpaka likauke” ilikuwa
katika wakati wa mazoea hivyo hata jibu sahihi hupaswa kuwa katika wakati
huo huo wa mazoea.

Swali la 15: Mkutano haukufanyika kwa sababu mwenyekiti na katibu


hawakufika. Kifungu kipi cha maneno kati ya vifuatavyo
kinasadifu sentensi hiyo?
A. Mkutano uliairisha
B. Mkutano uliahirishwa
C. Mkutano ulihairishwa
D. Mkutano uliharishwa
E. Mkutano ulihairisha.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B* C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
111,847 370,963 258,799 52,724 44,562 3,126 2,732
watahiniwa
Asilimia ya
13.24 43.91 30.64 6.24 5.28 0.37 0.32
watahiniwa

14  
Swali lililenga kupima uwezo wa mtahiniwa katika utumizi wa lugha.
Watahiniwa 370,963 sawa na asilimia 43.91 walichagua B “Mkutano
uliahirishwa” ambalo ndilo jibu sahihi. Watahiniwa 311,523, sawa na asilimia
36.88 walichagua kati ya kipotoshi C “Mkutano ulihairishwa” na kipotoshi D
“Mkutano uliharishwa” ambavyo sio majibu sahihi jambo linaloonesha kuwa
walikosa maarifa ya semantiki ya Kiswahili. Watahiniwa hao walivutiwa na
neno “hairishwa” na “harishwa” bila kutambua kuwa kisarufi hayakuwa
maneno sahihi. Athari za kimatamshi zinaweza pia kuwa zilichangia kwa
watahiniwa waliochagua kipotoshi A “uliairishwa” na E “Ulihairisha” badala
ya “Uliahirishwa.”

Swali la 16: Mlinzi wa mlangoni huitwaje?


A. Boharia
B. Baharia
C. Bawaba
D. Banati
E. Bawabu.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C D E* Wasiojibu Mengine
Idadi ya
103,861 139,911 311,664 116,491 164,282 5,789 2,755
watahiniwa
Asilimia ya
12.29 16.56 36.89 13.79 19.45 0.69 0.33
watahiniwa

Swali lililenga kupima ujuzi wa mtahiniwa katika kutumia msamiati. Asilimia


19.45 tu ya watahiniwa waliofanya mtihani walichagua jibu E “Bawabu”
ambalo ndilo jibu sahihi. Watahiniwa 311,664 ambao ni sawa na asilimia
36.89 walichagua kipotoshi C “Bawaba” hali inayoonesha kuwa walikosa
maarifa ya kuelewa maana ya bawaba kwamba ni kipande cha chuma
15  
kinachopigiliwa kwenye mlango au dirisha ili kuwezesha kufunga na
kufungua. Watahiniwa hawa walichanganya bawaba na bawabu kwa vile ni
maneno yanayokaribiana kimatamshi ijapokuwa yana matumizi tofauti.
Uchaguzi wa vipotoshi A, B na D kwa watahiniwa 360,263 ambao ni sawa
na asilimia 42.64 unaonesha kuwa watahiniwa walishindwa kuelewa maana
ya maneno hayo kwa vile “Baharia” ni mfanyakazi wa chombo cha baharini,
“Boharia” ni mtunza vifaa katika ghala au bohari na “banati” ni mabinti au
wasichana. Hivyo hii inadhihirisha kuwa watahiniwa hawakuwa na ujuzi wa
kuelewa maana ya maneno hayo.

Swali la 17: Joshua yuko jikoni anapaa samaki. Neno “anapaa” kama
lilivyotumika katika sentensi hii lina maana ipi?
A. Kuwapaka samaki chumvi
B. Kuondoa magamba ya samaki
C. Kuondoa mifupa katika samaki
D. Kukausha samaki kwa moto
E. Kuwakata samaki vipande vipande.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B* C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
78,395 394,909 45,588 274,397 46,572 2,340 2,552
watahiniwa
Asilimia ya
9.28 46.75 5.4 32.48 5.51 0.28 0.3
watahiniwa

Swali lililenga kupima uelewa wa mtahiniwa katika matumizi ya msamiati.


Asilimia 46.75 walichagua jibu B “Kuondoa magamba ya samaki” ambalo
ndilo jibu sahihi. Watahiniwa 274,397 ambao ni sawa na asilimia 32.48
walichagua kipotoshi D “Kukausha samaki kwa moto” ambacho sio jibu
sahihi. Watahiniwa hao walichanganya maana ya neno ‘Kupaa’ ya kuchukua
16  
makaa mekoni kama vile kupalia mkaa, wakalifananisha na ‘kukausha’
ambalo sio jibu sahihi. Uteuzi wa vipotoshi A, C na E kwa asilimia 20.19
ambavyo vilikuwa sio majibu sahihi viliwashawishi watahiniwa kutokana na
zile hatua mbalimbali ambazo samaki huzipitia wakati wa kumtayarisha kwa
kupikwa.
Swali la 18: “Mtoto wa ng’ombe anaitwa ndama, watoto wa kuku, bata,
kanga wanaitwa vifaranga, kimatu ni mtoto wa nani?
A. Nzige
B. Nyuki
C. Inzi
D. Kipepeo
E. Buibui.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A* B C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
470,470 109,924 61,338 77,125 119,297 4,072 2,527
watahiniwa
Asilimia ya
55.69 13.01 7.26 9.13 14.12 0.48 0.3
watahiniwa

Swali lililenga katika kupima ujuzi wa mtahiniwa katika kutambua makundi


mbalimbali ya nomino. Asilimia 58.89 ya watahiniwa walichagua A “Nzige”
ambalo ndilo jibu sahihi. Uteuzi wa vipotoshi B, C, D na E kwa watahiniwa
367,684 sawa na asilimia 43.52 ulionesha kuwa watahiniwa hawakuwa na
maarifa kuhusu nomino za viumbe mbalimbali hivyo kushindwa kujua
“kimatu” ni mtoto wa nani. Aidha watahiniwa 4,072 hawakujibu swali hili.

Swali la 19: Kisawe cha neno “eupe” ni kipi?


A. Chokaa
B. Angavu

17  
C. Theluji
D. Ukungu
E. Angaza
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B* C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
184,999 242,924 153,338 104,114 152,024 4,688 2,666
watahiniwa
Asilimia ya
21.9 28.76 18.15 12.32 18 0.55 0.32
watahiniwa

Swali lililenga kupima uelewa wa mtahiniwa kuhusu visawe vya maneno.


Asilimia 28.76 ya watahiniwa walichagua jibu B “Angavu” ambalo ndilo jibu
sahihi. Watahiniwa 184,999 sawa na asilimia 21.9 walichagua kipotoshi A
“Chokaa” ambalo sio sahihi kwani kila eupe sio unga mweupe ambao
hupatikana kwa kuchoma mawe, hali inayoashiria kuwa ama hawakuelewa
matakwa ya swali au hawakuwa na uelewa unaotakiwa wa visawe sahihi
vya maneno. Uchaguzi wa vipotoshi C, D na E ulidhihirisha pia kuwa baadhi
ya watahiniwa hawakuwa na ujuzi wa visawe sahihi vya maneno. Aidha
watahiniwa hao walishindwa kuelewa maana ya neno ‘eupe’ ili kuweza
kupata kisawe sahihi.

Swali la 20: Siku ya nne baada ya leo huitwaje?


A. Mtondo
B. Mtondo kutwa
C. Mtondogoo
D. Kesho kutwa
E. Mtondogoo kutwa.

18  
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C* D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
104,410 66,577 412,314 174,084 81,272 2,893 3,203
watahiniwa
Asilimia ya
12.36 7.88 48.81 20.61 9.62 0.34 0.38
watahiniwa

Swali lililenga kupima uwezo wa mtahiniwa katika kutambua majina ya


siku. Asilimia 48.81 ya watahiniwa waliofanya mtihani walichagua jibu C
“Mtondogoo” ambalo ndilo jibu sahihi. Watahiniwa 278,494 sawa na
asilimia 32.97 walichagua kipotoshi A “Mtondo” na D “Kesho kutwa,”
Watahiniwa hao walikosa uelewa kwamba “mtondo” ni siku ya tatu na
“kesho kutwa” ni siku ya pili baada ya leo. Uchaguzi wa vipotoshi B
“Mtondo kutwa” na E “Mtondogoo kutwa” kwa watahiniwa 147,849 ambao
ni sawa na asilimia 17.50 inaonesha kuwa watahiniwa hao walishindwa
kuelewa kuwa hakuna siku zenye kuitwa majina hayo.

2.2 Sehemu B: Lugha ya Kifasihi

Swali la 21: Tegua kitendawili kisemacho; “Mwenye kuitwa amefika


lakinimjumbe bado hajarudi.”
A. Nazi na mkwezi
B. Yai na kifaranga
C. Birika na chai
D. Nyama na ngozi
E. Chupa na mfuniko.

19  
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A* B C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
531,352 151,088 67,837 45,568 42,330 3,583 2,995
watahiniwa
Asilimia ya
62.9 17.89 8.03 5.39 5.01 0.42 0.35
watahiniwa

Swali lililenga kupima uelewa wa mtahiniwa kuhusu tanzu za semi na hasa


vitendawili. Asilimia 62.9 ya watahiniwa waliofanya mtihani walichagua jibu
A “Nazi na mkwezi” ambalo ndilo jibu sahihi. Asilimia 17.89 ya watahiniwa
walichagua kipotoshi B “Yai na kifaranga” ambalo sio jibu sahihi kwani
walishindwa kuelewa kuwa vyote viwili viko sehemu moja na hakuna safari
yoyote ioneshayo kuwa yupo mmoja wao anayetangulia. Uteuzi wa
vipotoshi C “Birika na Chai,” D “Nyama na ngozi” na E “Chupa na mfuniko”
vyote vinaonekana kuwepo pamoja na kutegemeana kwa vile kimoja
hakiwezi kuwepo na kingine kisiwepo kabisa. Hii inaonesha kuwa
watahiniwa hao hawakuwa na uelewa wa utegemezi huo.

Swali la 22: “Wakoloni walitunyanyasa lakini hatimaye unyanyasaji huo


ulifika ukingoni kwani _________________.” Ni methali ipi
kati ya zifuatazo inakamilisha sentensi hiyo?
A. hakuna marefu yasiyokuwa na ncha
B. mchumia juani hulia kivulini
C. ukiona vyaelea vimeundwa
D. umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
E. bandu bandu humaliza gogo.

20  
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A* B C D* E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
485,482 108,277 63,433 126,139 55,445 2,801 3,176
watahiniwa
Asilimia ya
57.47 12.82 7.51 14.93 6.56 0.33 0.38
watahiniwa

Swali lililenga kupima uelewa wa mtahiniwa kuhusu methali na hasa


ukamilishaji wake. Ni asilimia 57.47 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa
Kiswahili ndio waliochagua A “hakuna marefu yasiyokuwa na ncha”
ambalo ndilo jibu sahihi. Watahiniwa 108,277 sawa na asilimia 12.82
walichagua kipotoshi B “mchumia juani hulia kivulini” ambalo sio jibu
sahihi. Inawezekana watahiniwa hao walichagua jibu hilo kwa
kuhusianisha swali na dhana ya faraja aipatayo mtu baada ya mateso
makubwa. Aidha watahiniwa 245,017 ambao ni sawa na asilimia 29.00
walichagua vipotoshi C, “ukiona vyaelea vimeundwa” D “umoja ni nguvu
utengano ni udhaifu” na E “bandu bandu humaliza gogo” ambavyo vyote
havikuwa majibu sahihi kwa vile vinaelezea matokeo mazuri yanayotokana
na kazi ya pamoja na ushirikiano. Hivyo watahiniwa walishindwa kuelewa
kuwa methali waliyoulizwa ilikuwa inaonesha kuwa hakuna jambo
lisilokuwa na mwisho wake bila ya kutaka kujua huo mwisho ulikuwaje.

Swali la 23: “Kidagaa kimemwozea.” Msemo huu una maana gani?


A. Kukwepa kulipa deni
B. Kutowajibika kulipa
C. Kuelemewa na jambo
D. Kupoteza tumaini
E. Kulipa deni maradufu.

21  
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C* D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
192,645 91,149 368,544 99,386 84,901 5,040 3,088
watahiniwa
Asilimia ya
22.8 10.79 43.63 11.77 10.05 0.6 0.37
watahiniwa

Swali lililenga katika kupima uelewa wa mtahiniwa kuhusu matumizi ya


misemo mbalimbali ya Kiswahili. Asilimia 43.63 ya watahiniwa walichagua
jibu C “kuelemewa na jambo” ambalo ndilo jibu sahihi. Uchaguzi wa
vipotoshi A, B na E kwa watahiniwa 368,695 sawa na asilimia 43.64
unadhihirisha kuwa watahiniwa hao walishindwa kuelewa kuwa maneno
“kukwepa kulipa deni” ambalo lina maana sawa na “kutokuwajibika kulipa”
na “kulipa deni maradufu” ikiwa na maana kulipa zaidi ya ilivyotakiwa sio
majibu sahihi ambayo yangekuwa na maana ya “kidagaa kimemwozea.”
Aidha uteuzi wa kipotoshi D “Kupoteza tumaini” kwa watahiniwa 99,386
sawa na asilimia 11.77 ikiwa na maana kutokufanikiwa inaonesha wazi
kuwa haina maana iliyokusudiwa katika msemo huo. Hivyo uchambuzi
unaonesha kuwa watahiniwa hawakuweza kutambua kuwa maneno yote
hayo yaliyowekwa kwenye vipotoshi yana maana tofauti kabisa na ile ya
msemo “kidagaa kimemwozea” ambao maana yake ni kuelemewa na
jambo.

Swali la 24: “Kukubali kwa ulimi” ni msemo wenye maana ipi?


A. Kukubali kwa dhati
B. Kukubali kwa maneno
C. Kukubali bila kusema neno
D. Kukubali kimoyomoyo
E. Kukubali kwa moyo mmoja.

22  
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B* C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
79,597 410,027 102,204 114,055 132,241 3,448 3,181
watahiniwa
Asilimia ya
9.42 48.54 12.1 13.5 15.65 0.41 0.38
watahiniwa

Swali lililenga katika kupima uelewa wa mtahiniwa kuhusu matumizi ya


misemo mbalimbali ya Kiswahili. Asilimia 48.54 ya watahiniwa walichagua
jibu B “kukubali kwa maneno” ambalo ndilo jibu sahihi. Uchaguzi wa
vipotoshi A, C, D na E kwa watahiniwa 428,097 sawa na asilimia 50.67
unadhihirisha kuwa watahiniwa hao walishindwa kuelewa kuwa kukubali
kwa dhati ina maana sawa na kukubali kwa kusema neno na hata
kukubali kimoyomoyo. Uchambuzi unaonesha kuwa vipotoshi hivyo vinne
vina mfanano kimaana tofauti na matakwa ya swali ambayo yanahitaji
kukubali kwa ulimi tu ambayo maana yake ni kukubali tu lakini utekelezaji
wa jambo haufanyiki kabisa.

Swali la 25: Nahau isemayo, “amevimba kichwa” ina maana ipi?


A. Kupata mafanikio makubwa
B. Kukabidhiwa madaraka ya juu
C. Kuwa na hali ya hasira
D. Kuwa na hali ya huzuni
E. Kuwa na tabia ya majivuno.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C D E* Wasiojibu Mengine
Idadi ya
164,129 155,108 220,617 84,378 213,460 3,739 3,322
watahiniwa
Asilimia ya
19.43 18.36 26.12 9.99 25.27 0.44 0.39
watahiniwa

23  
Swali lililenga kupima uwezo wa watahiniwa kuhusu matumizi ya semi
katika lugha ya Kiswahili. Asilimia 25.27 ya watahiniwa walichagua jibu E
“kuwa na tabia ya majivuno” ambalo ni jibu sahihi. Uteuzi wa vipotoshi kati
ya A, B, C na D kwa asilimia 73.9 unaonesha ni kwa kwa kiasi gani
watahiniwa hawakuwa na ujuzi wa kutosha kuhusu semi mbalimbali za
Kiswahili. Kwa mfano “kupata mafanikio makubwa” msemo unaoendana
na hali hiyo ni “Kula uhondo kunataka matendo,” “Kukabidhiwa madaraka
makubwa” nao huweza kuendana na nahau isemayo “Kuua tembo kwa
ubua” yaani kufanikiwa jambo kwa urahisi bila ya kutarajia. Vipotoshi
vingine kama “Kuwa na hali ya hasira au hali ya huzuni” vina mfanano
uoneshao kuwa mtu hana raha, hivyo vyote hivyo visingefaa kuwa jibu
sahihi la nahau “amevimba kichwa” ambayo maana yake ni kuwa na
majivuno.

Swali la 26: “Kitanda usichokilalia hujui kunguni wake.” Methali ipi kati ya
zifuatazo ina maana sawa na hiyo?
A. Pema usipopema ukipema si pema tena
B. Kizuri hakikosi ila
C. Mtu siri kusema na moyo wake
D. Nyumba usiyoilala ndani hujui ila yake
E. Pilipili usiyoila yakuwashia nini.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C D* E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
96,096 80,122 73,449 375,725 212,474 3,701 3,186
watahiniwa
Asilimia ya
11.38 9.48 8.69 44.48 25.15 0.44 0.38
watahiniwa

24  
Swali lililenga kupima uelewa wa mtahiniwa kuhusu kutambua maana ya
methali aliyopewa. Asilimia 44.48 ya watahiniwa walichagua D “Nyumba
usiyoilala ndani hujui ila yake,” ambalo ndilo jibu sahihi. Watahiniwa
212,474 sawa na asilimia 25.15 waliochagua E “Pilipili usiyoila
yakuwashia nini” hawakuwa na uelewa wa methali hiyo na walishindwa
kutambua kuwa maneno “ya kuwashia nini” yakiwa na maana “usiyaingilie
mambo yasiyokuhusu” katika ukamilishaji wa methali hiyo hayana maana
sawa na maneno ya methali iliyoulizwa “hujui kunguni wake.” yakiwa na
maana kwamba huwezi kukisia uzito wa jambo ambalo halijakufika.

Aidha, watahiniwa 249,667 sawa na asilimia 29.55 walichagua kati ya


vipotoshi A “Pema usipopema, ukipema si pema tena” ikiwa na maana
pahali pazuri ni pale ambapo hujapafika, B “Kizuri hakikosi ila” ikiwa na
maana hakuna kizuri kilichokamilika bila kuwa na kasoro hata kidogo na
C “Mtu siri kusema na moyo wake” ikiwa na maana siri huwekwa moyoni
kwani ikisemwa sio siri tena. Uchambuzi unaonesha kwamba watahiniwa
hao wanaonekana kutokusoma kwa umakini na kuelewa kuwa methali
zote hizo zina maana tofauti kabisa na methali iliyoulizwa. Hali hiyo
inadhihirisha kuwa watahiniwa hawakuwa na uelewa wa matakwa ya
swali. Swali hilo lilitarajiwa kuwa miongoni mwa maswali ambayo
watahiniwa wangeweza kuyajibu kwa usahihi kwa kuwa methali hiyo
hutumika mara kwa mara katika jamii.

Swali la 27: “Nina mwanangu mweupe nikimtia maji hufa.” Kitendawili


hicho kina maana ipi?
A. Maziwa
B. Tui la nazi
C. Majivu
D. Barafu
25  
E. Karatasi.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C D E* Wasiojibu Mengine
Idadi ya
109,407 107,793 159,392 133,366 327,579 3,878 3,338
watahiniwa
Asilimia ya
12.95 12.76 18.87 15.79 38.78 0.46 0.4
watahiniwa

Swali lililenga katika kupima uelewa wa mtahiniwa kuhusu matumizi ya


misemo mbalimbali ya Kiswahili na hasa vitendawili. Asilimia 38.78 ya
watahiniwa walichagua jibu E “Karatasi” ambalo ndilo jibu sahihi.
Uchaguzi wa vipotoshi A “Maziwa” na D “Barafu” kwa asilimia 12.95 na
asilimia 15.79 ambavyo sio majibu sahihi unadhihirisha kuwa watahiniwa
hao walishindwa kuelewa kuwa matumizi ya maziwa na barafu hayawezi
kuathirika kwa sababu hata kama yangetiwa maji yangeweza kuendelea
kutumika. Uteuzi wa kipotoshi C “Majivu” kwa watahiniwa 159,392 sawa
na asilimia 18.87 unaonesha kuwa watahiniwa hao hawakuwa na uelewa
kuhusu utambuzi wa rangi ya kijivu ambayo sio nyeupe. Aidha uchaguzi
wa kipotoshi B “Tui la nazi” kwa watahiniwa 107,793 sawa na asilimia
12.76 ambacho sio jibu sahihi unaonesha kuwa watahiniwa
walishawishiwa na ile dhana ya kuwa na tui la nazi zito yaani lile la
mwanzo lakini wakasahau kuwa lipo tui la nazi jepesi ambalo hupatikana
kwa kuongeza maji na linatumika tu bila madhara yoyote. Hivyo karatasi
ndio jibu sahihi kwa sababu ikiwa bado ina maji haiwezi kutumika na
ikilowa zaidi huvurugika kabisa.

Swali la 28: “Bwana mkubwa amelala ndani lakini ndevu zipo nje
zapepea.” Jibu sahihi la kitendawili hiki ni lipi?
A. Ulezi
B. Mpunga
26  
C. Ngano
D. Mahindi
E. Mtama.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C D* E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
32,459 40,138 33,954 706,152 26,903 2,429 2,718
watahiniwa
Asilimia ya
3.84 4.75 4.02 83.59 3.18 0.29 0.32
watahiniwa

Swali lililenga kupima uelewa wa watahiniwa kuhusu semi na hasa


vitendawili. Hili ni miongoni mwa maswali yaliyojibiwa vizuri sana kwani
asilimia 83.59 ya watahiniwa waliofanya mtihani walichagua D “Mahindi”
ambalo ndilo jibu sahihi. Swali hili lilijibiwa vizuri na watahiniwa wengi kwa
sababu linaonesha kuwa walikuwa na uelewa wa kitendawili hicho
ambacho hutumika mara kwa mara. Asilimia 15.79 ya watahiniwa
walichagua kati ya vipotoshi A, B, C na E kwa kuwa hawakuwa na uelewa
wa kutosha kuhusu vitendawili na hususan kitendawili walichoulizwa
katika swali hili.

Swali la 29: “Kazi mbaya si mchezo mwema.” Methali inayofanana na


methali hiyo ni ipi?
A. Hewala haigombi
B. Mchezea tope humrukia
C. Heri kuwa mbichi kuliko kuungua
D. Hucheka kovu asiyekuwa na jeraha
E. Hukunyima tonge, hakunyimi neno.

27  
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C* D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
64,692 273,929 196,878 179,499 120,354 6,505 2,896
watahiniwa
Asilimia ya
7.66 32.43 23.31 21.25 14.25 0.77 0.34
watahiniwa

Swali lilikuwa linapima uwezo wa watahiniwa kutambua methali iliyo sawa


na “Kazi mbaya si mchezo mwema.” Asilimia 23.31 walichagua jibu sahihi
C “Heri kuwa mbichi kuliko kuungua” kuwa methali inayofanana na
isemayo “Kazi mbaya si mchezo mwema” ambayo ina maana kwamba ni
heri ukaifanya kazi hata kama matokeo yake yakiwa mabaya kuliko kukaa
bure na kucheza kwani hakuna mchezo ulio mwema. Asilimia 32.43 ya
watahiniwa walichagua kipotoshi B “Mchezea tope humrukia” yenye
maana ya aanzishaye ubaya humrudia/huathirika mwenyewe. Uteuzi wa
vipotoshi A, D na E unaonesha kwamba watahiniwa husika walikosa ujuzi
wa kutambua maana sahihi ya methali hizo hivyo kushindwa kujua ni
methali ipi inafanana na ile waliyopewa katika swali.

Swali la 30: Msemo usemao, “kushikwa sikio” una maana ipi?


A. Kusemwa
B. Kunong’onezwa
C. Kuelezwa
D. Kusengenywa
E. Kuonywa

28  
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C D E* Wasiojibu Mengine
Idadi ya
72,095 484,582 79,651 85,162 115,799 4,412 3,052
watahiniwa
Asilimia ya
8.53 57.36 9.43 10.08 13.71 0.52 0.36
watahiniwa

Swali lilikuwa linapima uwezo wa mtahiniwa wa kuchambua misemo


mbalimbali na matumizi yake katika mazingira au muktadha. Asilimia
13.71 ya watahiniwa walijibu swali kwa usahihi kwa kuonesha maana
halisi ya msemo “kushikwa sikio” ambayo ni chaguzi E “Kuonywa.”
Asilimia 57.36 walichagua kipotoshi B “Kunong’onezwa” jibu ambalo
halikuwa sahihi ambalo linaendana na nahau isemayo “kuumwa
sikio/kung’atwa sikio.” Waliochagua vipotoshi A, C na D ni asilimia 28.04,
watahiniwa hao walishindwa kufafanua maana ya msemo huo kutokana
na vipotoshi hivyo vyote kuhusisha taarifa ambayo hutolewa kwa mtu
akiwepo au asipokuwepo. Kilichohitajika ili kuweza kujibu swali kwa
usahihi ni uelewa wa nahau hiyo.

2.3 Sehemu C: Ufahamu


Katika sehemu hii watahiniwa walitakiwa kusoma kifungu cha habari na
kujibu maswali yaliyotokana na kifungu hicho. Kifungu walichopewa
kilisomeka kama ifuatavyo:

Maji ni moja kati ya vitu vitatu muhimu sana vinavyotuwezesha kuishi.


Vitu vingine ni hewa na chakula. Hewa ndiyo yenye umuhimu wa kwanza,
ikifuatiwa na chakula. Kusingelikuwa na maji maisha ya binadamu na ya
viumbe wengine yasingeliwezekana. Kila mtu anaelewa umuhimu wa maji
katika maisha. Maji yanatawala maisha kwa kiasi kikubwa sana. Baadhi
ya viumbe kama vile samaki, mamba, kasa, konokono, nyangumi na
29  
wengineo maskani yao ni majini, hivyo maji yakikosekana viumbe hao
huweza kuaga dunia.

Binadamu anatumia maji kwa shughuli mbalimbali. Shughuli hizo ni


pamoja na kupikia, kufulia, kusafishia vyombo, kuoga na kunywa. Katika
sehemu nyingi za nchi yetu watu hutumia maji kwa kumwagilia bustani za
mboga, maua na miti. Katika maeneo yenye mito mikubwa na maziwa,
maji yake hutumika kwa kumwagilia mashamba kama yale ya mpunga na
mahindi. Kilimo cha umwagiliaji kinafaa kwa sababu mkulima anakuwa na
uhakika wa kuvuna.

Maji ya mvua huwawezesha watu kulima na kupanda mazao ya chakula


na ya biashara. Hivyo zipo sehemu ambazo wakulima hulima kilimo cha
umwagiliaji lakini sehemu kubwa ya wakulima hutegemea kilimo cha
mvua.

Kwa ujumla maji yawe ya mvua au yanayotokana na mito au maziwa


yana umuhimu mkubwa mno kwa binadamu kama walivyosema wahenga
maji ni uhai, hivyo inashauriwa kwamba ni muhimu kwa kila mtu kunywa
maji safi na salama ili kulinda siha zetu.

Swali la 31: Vitu vitatu muhimu vinavyomwezesha binadamu kuishi ni


vipi?

A. Hewa, chakula na nyumba


B. Hewa, maji na chakula
C. Maji, ushauri na hewa
D. Maji, hewa na mvua
E. Chakula, mvua na hewa.

30  
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B* C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
56,401 678,082 38,598 34,293 32,064 2,568 2,747
watahiniwa
Asilimia ya
6.68 80.27 4.57 4.06 3.8 0.3 0.33
watahiniwa

Swali lilikuwa linapima ufahamu wa mtahiniwa baada ya kusoma kifungu


cha habari. Swali hili ni miongoni mwa maswali ya ufahamu yaliyojibiwa
vizuri kwani asilimia 80.27 ya watahiniwa waliweza kujibu swali kwa
usahihi kwa kuchagua vitu vitatu muhimu ambavyo ni B “Hewa, maji na
chakula” kutokana na usomaji wa makini, uelewa na uwezo wa
kuyatambua mawazo makuu katika habari waliyosoma. Asilimia 6.68
walichagua kipotoshi A “Hewa, chakula na nyumba” kwa vile hawakuwa
na uelewa kuwa maji yalikuwa na umuhimu kuliko nyumba. Uchaguzi wa
vipotoshi C “Maji, ushauri na hewa”, D “Maji, hewa na mvua” na E
“Chakula, mvua na hewa” uliofanywa na watahiniwa 104,955 sawa na
asilimia 12.43 unaonesha kuwa watahiniwa hao walishindwa kuelewa
kuwa ushauri na mvua haviwezi kuwa na umuhimu zaidi ya maji na
chakula kama ilivyoelezwa kwenye habari yenyewe. Kwa hiyo uchaguzi
wa vipotoshi A, C, D na E ulifanywa na watahiniwa ambao walishindwa
kutambua kuwa vipotoshi hivyo havitoi muhtasari wa mambo matatu
muhimu ya habari waliyopewa.

Swali la 32: Wakulima wengi kama ilivyoelezwa katika habari hii hulima
kilimo kinachotegemea nini?
A. Mito
B. Umwagiliaji
C. Mvua
D. Mabwawa

31  
E. Maziwa.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C* D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
61,052 247,974 467,394 31,721 30,503 3,345 2,764
watahiniwa
Asilimia ya
7.23 29.35 55.33 3.76 3.61 0.4 0.33
watahiniwa

Swali hili lilikuwa linapima ufahamu wa mambo muhimu yaliyoelezwa


katika habari. Asilimia 55.33 ya watahiniwa walijibu swali kwa usahihi
kwani walichagua jibu C “Mvua” ambalo ndilo jibu sahihi. Asilimia 29.35
walichagua kipotoshi B, “umwagiliaji” kwa kuwa hawakusoma habari kwa
makini. Aidha asilimia 14.57 walichagua vipotoshi kati ya A, D na E kwa
kuwa walikosa kutambua kuwa “mito,” “mabwawa” na “maziwa” haviwezi
kutegemewa katika kilimo kwa sababu kuna maeneo mengi nchini
ambayo hayana vyanzo hivyo vya maji.

Swali la 33: Kiumbe yupi kati ya wafuatao halandani na wenzie?


A. Kima
B. Mamba
C. Nyangumi
D. Kasa
E. Samaki.

Majibu ya watahiniwa

Chaguo A* B C D E Wasiojibu Mengine


Idadi ya
557,008 58,929 69,940 71,257 80,800 3,723 3,096
watahiniwa
Asilimia ya
65.94 6.98 8.28 8.44 9.56 0.44 0.37
watahiniwa

32  
Swali lilikuwa linapima ufahamu wa kusoma kwa makini kifungu cha
habari na kutambua mambo muhimu yaliyoelezwa. Asilimia 65.94 ya
watahiniwa waliofanya mtihani waliweza kujibu swali hili kwa usahihi kwa
kuchagua jibu A “Kima” kwa sababu aya ya kwanza ilikuwa inajitosheleza
kueleza wanyama wote wanaoishi majini. Watahiniwa waliochagua
vipotoshi B, “Mamba” C, “Nyangumi,” D “Kasa” na E, “Samaki” walikuwa
asilimia 33.26, watahiniwa hao walikosa ujuzi wa kusoma kwa makini na
kupata ufahamu kutoka katika kifungu walichopewa. Aidha watahiniwa
hao walishindwa kutambua kuwa katika orodha hiyo ya viumbe ina sifa
moja inayofanana ambayo ni kuishi majini isipokuwa Kima ambaye ni
jamii ya nyani na tumbili na huishi nchi kavu.

Swali la 34: Kilimo cha umwagiliaji kina sifa gani kubwa?


A. Uvunaji upo dhahiri
B. Kinatumia maji ya maziwa makubwa
C. Kinatumia maji yaliyohifadhiwa
D. Mazao hayapati magonjwa
E. Kinalimika majira yoyote.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A* B C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
269,117 124,299 81,753 75,141 286,743 4,823 2,877
watahiniwa
Asilimia ya
31.86 14.71 9.68 8.9 33.94 0.57 0.34
watahiniwa

Swali lilikuwa linapima tathmini ya uelewa wa watahiniwa kuhusu habari


waliyoisoma. Asilimia 31.86 walijibu swali kwa kuchagua jibu A “Uvunaji
upo dhahiri” ambalo ni sahihi. Watahiniwa hao waliweza kuisoma habari
na kuelewa kuwa maana ya neno sifa ni uzuri au ubaya wa kitu, hivyo sifa

33  
kubwa ya kilimo cha umwagiliaji ni uvunaji ulio wa uhakika. Asilimia 33.94
ya watahiniwa walichagua kipotoshi E “Kinalimika majira yoyote”
ambacho sio jibu sahihi kwa sababu habari hiyo haikueleza kuhusu kilimo
kinacholimika majira yote. Uteuzi wa vipotoshi B na C unaonesha kuwa
watahiniwa walipotoshwa na dhana ya uhitaji wa maji mengi katika kilimo
cha umwagiliaji. Aidha uteuzi wa kipotoshi D unaonesha uelewa mdogo
wa usomaji wa habari kwa vile suala la mazao kupata magonjwa
halikuelezwa kabisa katika habari waliyopewa.

Swali la 35: Neno “siha” kama lilivyotumika katika kifungu hiki cha habari
lina maana gani?
A. Afya njema
B. Sifa njema
C. Maisha mema
D. Tabia njema
E. Kinywa safi.
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A* B C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
522,011 96,416 102,676 58,783 60,369 2,027 2,471
watahiniwa
Asilimia ya
61.79 11.41 12.15 6.96 7.15 0.24 0.29
watahiniwa

Swali lilikuwa linapima maarifa ya watahiniwa kuhusu maana ya misamiati


kama ilivyotumika katika kifungu cha habari. Asilimia 61.79 ya watahiniwa
walijibu swali kwa usahihi kutokana na maarifa waliyokuwa nayo na hivyo
walichagua jibu A “Afya njema” ambalo ndilo maana sahihi ya neno ‘siha.’
Jumla ya watahiniwa 96,416 sawa na asilimia 11.41 walichagua B “sifa
njema” ambalo si jibu sahihi. Inawezekana watahiniwa hao walivutiwa na
kipotoshi hicho kwa kuwa kinahusisha uzuri wa kitu na wakahusisha na

34  
neno “siha” ambalo linahusu afya. Aidha, uteuzi wa vipotoshi C “Maisha
mema,” D “Tabia njema” na E “Kinywa safi” unaonesha kuwa watahiniwa
walikosa maarifa ya kuwawezesha kufahamu maana za misamiati na
hasa ikizingatiwa kuwa maneno hayo yanahusiana ingawa yana maana
tofauti.

Swali la 36: “Kuaga dunia” ni msemo wenye maana gani?


A. Kuzirai
B. Kuzimu
C. Kulala fofofo
D. Kufariki
E. Kufia mbali.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C D* E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
32,740 42,344 60,330 677,250 27,632 2,289 2,168
watahiniwa
Asilimia ya
3.88 5.01 7.14 80.17 3.27 0.27 0.26
watahiniwa

Swali lilikuwa linapima matumizi ya semi za Kiswahili. Swali hili ni


miongoni mwa maswali yaliyojibiwa vizuri sana yanayohusiana na maana
ya misemo. Asilimia 80.17 walijibu swali kwa usahihi kwa kuchagua jibu D
“Kufariki” ambalo ndilo jibu sahihi. Watahiniwa hao walikuwa wanajua
matumizi sahihi ya nahau hiyo. Watahiniwa 163,046 ambao ni sawa na
asilimia 19.30 walichagua kati ya vipotoshi A, B, C, na E ambayo si
majibu sahihi kwa kuwa walikosa maarifa kuhusu maana inayowakilishwa
na semi za Kiswahili hasa nahau.

35  
Swali la 37: Ni kwanini mtunzi wa habari hii anashauri watu kunywa maji
safi na salama?
A. Ili kuondokana na kiu
B. Ili kulinda vinywa vyetu
C. Ili kuburudisha mwili
D. Ili kuondokana na kichocho
E. Ili kulinda afya zetu.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C D E* Wasiojibu Mengine
Idadi ya
48,792 54,616 49,117 72,858 612,145 4,027 3,198
watahiniwa
Asilimia ya
5.78 6.47 5.81 8.62 72.46 0.48 0.38
watahiniwa

Swali lilikuwa linapima tathmini ya uelewa wa watahiniwa kuhusu


mafunzo yatokanayo na habari waliyosoma. Asilimia 72.46 ya watahiniwa
walielewa habari na kuweza kulinganisha ushauri utokanao na habari hiyo
kuwa ni E “Ili kulinda afya zetu.” Aidha, kipotoshi A “Ili kuondokana na kiu”
kilichochaguliwa na watahiniwa 48,792 sawa na asilimia 5.78 kilionekana
kuwashawishi watahiniwa hao wachache kwa sababu watahiniwa hao
wameifikiria kiu ya maji zaidi badala ya matokeo yatokanayo na kunywa
maji safi na salama. Uteuzi wa vipotoshi B “Ili kulinda vinywa vyetu”, C “Ili
kuburudisha mwili” na D “Ili kuondokana na kichocho” ambavyo sio majibu
sahihi unaonesha kuwa watahiniwa 176,591 sawa na asilimia 20.9
walikosa uelewa wa maana ya ushauri ambao maana yake ni maelekezo
yanayotolewa kwa mtu ili yamsaidie kupata suluhisho fulani. Hivyo
vipotoshi hivyo havikuwa ushauri wa kupata suluhisho la kudumu kama
lile la kulinda afya zetu.

36  
Swali la 38: Neno “maskani” kama lilivyotumika katika kifungu cha habari
lina maana gani?
A. Nyumba
B. Makao
C. Maisha
D. Mahitaji
E. Shughuli.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B* C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya 141,329
193,176 381,999 60,204 61,284 3,745 3,016
watahiniwa
Asilimia ya
22.87 45.22 16.73 7.13 7.25 0.44 0.36
watahiniwa

Swali lilikuwa linapima uwezo wa mtahiniwa wa kueleza maana ya


msamiati “maskani” kama ulivyotumika katika kifungu cha habari. Asilimia
45.22 walijibu swali kwa usahihi kwa kuchagua jibu B “Makao.” Kipotoshi
A “nyumba” kilichaguliwa kwa asilimia 22.87 ambayo ni kubwa zaidi kuliko
vipotoshi vingine vyote kwa sababu kina mfanano mkubwa na dhana ya
neno maskani kwa vile maskani kwa maana nyingine ni mahali anapoishi
mtu ambapo huweza kuwa nyumba lakini katika kifungu hiki
kinachozungumziwa ni wanyama ambao hawaishi kwenye nyumba ila
makao yao ni majini. Uteuzi wa vipotoshi C “Maisha” D “Mahitaji” na E
“Shughuli” ambavyo havikuwa majibu sahihi ulifanywa na watahiniwa
262,817 sawa na asilimia 31.11 kutokana na uelewa mdogo wa
watahiniwa kuhusu maana ya neno “maskani.”

Swali la 39: Kichwa cha habari kinachofaa kwa kifungu hiki ni kipi?
A. Hewa ni muhimu
B. Maji ni uhai

37  
C. Maji salama
D. Hewa na chakula
E. Siha bora.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B* C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
88,750 459,468 83,227 104,644 102,109 3,573 2,982
watahiniwa
Asilimia ya
10.51 54.39 9.85 12.39 12.09 0.42 0.35
watahiniwa

Swali lilikuwa linawapima watahiniwa kuhusu uelewa wa maudhui ya


habari kwa ujumla. Asilimia 54.39 walijibu swali kwa usahihi kwa kubaini
kichwa cha habari kuwa ni B “Maji ni uhai.” Watahiniwa 378,730 sawa na
asilimia 44.84 waliochagua vipotoshi A, C, D na E walikosa uelewa
utokanao na usomaji wa habari kwa makini.

Swali la 40: Methali ipi inaendana na habari hii kati ya zifuatazo?


A. Mpanda ovyo ndiye mla ovyo
B. Ahangaikae hupata
C. Maji hufuata mkondo
D. Maji yakimwagika hayazoleki
E. Alisifuye jua limemwangaza.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C D E* Wasiojibu Mengine
Idadi ya
177,815 144,645 204,834 205,294 103,698 5,178 3,289
watahiniwa
Asilimia ya
21.05 17.12 24.25 24.3 12.28 0.61 0.39
watahiniwa

38  
Swali lilikuwa linampima mtahiniwa kuhusu uelewa wa maudhui au
ujumbe wa habari kwa ujumla. Asilimia 12.28 walijibu swali kwa usahihi
kwa kubaini methali inayoendana na habari waliyoisoma ambayo ni E
“Alisifuye jua limemwangaza.” Methali hii ina maana kuwa anayetoa
maelezo ya kina kuhusu jambo fulani ni yule anayejua faida za kitu fulani
au jambo hilo. Mwandishi wa habari hii anasifu umuhimu wa maji kwa
kuwa anajua faida mbalimbali za maji. Asilimia 21.05 ya watahiniwa
walichagua kipotoshi A, “Mpanda ovyo ndiye mla ovyo” yenye maana
kuwa usipokuwa makini katika kufanya jambo hutopata mafanikio.
Uchaguzi huo unaonesha kuwa watahiniwa hao hawakuelewa maudhui
ya habari waliyoisoma kwani methali hiyo haihusiani kabisa na umuhimu
wa maji. Asilimia 17.12 ya watahiniwa walichagua kipotoshi B,
“Ahangaikaye hupata” methali yenye maana kuwa mtu anayepata taabu
wakati wa kufanya jambo fulani mwishowe hupata mafanikio, maana hii ni
tofauti na maudhui ya kifungu cha habari hii. Aidha, asilimia 24.25
walichagua kipotoshi C “Maji hufuata mkondo” ambayo ni methali yenye
maana kuwa kila jambo hufuata taratibu na kanuni zake. Hali kadhalika,
asilimia 24.3 walichagua kipotoshi D “Maji yakimwagika hayazoleki”
methali yenye maana ya kuwa jambo likiharibika halirekebishiki. Kwa
ujumla uchambuzi wa swali hili unaonesha wazi kuwa watahiniwa hawana
maarifa ya kutosha kuhusu maana za methali kwani methali walizochagua
kuwa ni jibu hazihusiani kabisa na kifungu cha habari walichopewa.

2.4 Sehemu D: Ushairi

Katika sehemu hii watahiniwa walitakiwa kusoma shairi lililotolewa na kujibu


maswali yanayotokana na shairi hilo.

Nyumbani kwako kuzuri, japokuwa ni pangoni,


Nyumba yako ni johari, ya mwenzako sitamani,
Hata pawe pa tajiri, hapafai maishani,
39  
Nyumbani kwako johari, kwingine usitamani.

Kwingine usitamani, nyumbani kwako johari,


Unaishi kwa amani, na pia kwa ujasiri,
Hiyo kweli abadani, nyumbani kunasetiri,
Nyumbani kwako johari, kwingine usitamani.

Uipende nyumba yako, utaona raha yake,


Kisha penda ndugu yako, kwako apaone kwake,
Dunia mahangaiko, usipende pekepeke,
Nyumbani kwako johari, kwingine usitamani.

Usichague jirani, bali chagua rafiki,


Usitenge asilani, shauri pia afiki,
Palipo na burudani, kaa nao marafiki,
Nyumbani kwako johari, kwingine usitamani

Swali la 41: Kichwa cha shairi kinachofaa ni kipi?


A. Johari ni nyumba
B. Nyumbani si pangoni
C. Tuthamini kwetu
D. Tupende majirani
E. Tupende marafiki.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C* D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
153,483 194,805 352,715 67,492 68,949 4,275 3,034
watahiniwa
Asilimia ya
18.17 23.06 41.75 7.99 8.16 0.51 0.36
watahiniwa

Swali lilikuwa linawapima watahiniwa kuhusu uelewa wa maudhui au


ujumbe wa shairi kwa ujumla. Asilimia 41.75 walijibu swali kwa usahihi
kwa kubaini kichwa cha shairi kuwa ni C “Tuthamini kwetu.” Watahiniwa
484,729 sawa na asilimia 57.38 waliochagua vipotoshi kati ya A, B, D na
E walikosa uelewa utokanao na usomaji wa shairi kwa makini.
40  
Swali la 42: Kituo katika shairi hili ni kipi?
A. Nyumbani kwako johari, kwingine usitamani
B. Usichague jirani, bali chagua rafiki
C. Kwingine usitamani, nyumbani kwako johari
D. Nyumbani kwako kuzuri, japokuwa ni pangoni
E. Uipende nyumba yako, utaona raha yake.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A* B C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
581,933 67,427 66,862 62,999 58,749 3,312 3,471
watahiniwa
Asilimia ya
68.89 7.98 7.91 7.46 6.95 0.39 0.41
watahiniwa

Swali lilikuwa linapima maarifa ya mtahiniwa kuhusu kanuni za utunzi wa


shairi. Asilimia 68.89 ya watahiniwa walijibu swali kwa usahihi kwa
kuchagua jibu A “Nyumbani kwako johari, kwingine usitamani” kwa kuwa
walikuwa na maarifa ya kutosha kuhusu utunzi wa mashairi hasa dhana
ya kituo. Watahiniwa 256,037 sawa na asilimia 30.3 ya watahiniwa
walichagua vipotoshi kati ya B, C, D na E kwa kuwa walikosa ujuzi wa
dhana ya kituo ambacho ni mstari wa mwisho unaojirudia katika kila ubeti.

Swali la 43: Neno “johari” kama lilivyotumiwa na mtunzi lina maana gani?
A. Kitu kilicho dhahiri
B. Kitu chenye dhamana
C. Kitu cha thamani
D. Kitu cha matamanio
E. Kitu cha kujivunia.

41  
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C* D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
92,800 101,570 344,881 123,087 174,594 4,619 3,202
watahiniwa
Asilimia ya
10.99 12.02 40.83 14.57 20.67 0.55 0.38
watahiniwa

Swali lilikuwa linapima matumizi ya msamiati kama ulivyotumika katika


shairi. Asilimia 40.83 ya watahiniwa walijibu kwa usahihi kwa kuchagua
jibu C “Kitu cha thamani” ambalo ndilo lilikuwa na maana sawa na neno
“johari.” Aidha watahiniwa 492,051 sawa na asilimia 58.25 walichagua
vipotoshi kati ya A, B, D na E, ambavyo sio majibu sahihi. Watahiniwa
hao walishindwa kutofautisha maana ya neno johari na maneno kama vile
“dhahiri” ambalo ni sawa na bayana au waziwazi, “dhamana” lenye
maana ya ahadi inayotolewa ili kumdhamini mtu anayetaka kukopa au
anayekabiliwa na mashitaka mahakamani, pia “matamanio” lenye maana
ya jambo ambalo mtu anatamani angekuwa nalo. Aidha, neno “kujivunia”
lenye maana ya kuringia au hali ya kuona fahari kwa mafanikio
yaliyopatikana. Kwa ujumla maneno yaliyomo katika vipotoshi A, B, D na
E yana maana ambayo haihusiani kabisa na neno johari.

Swali la 44: Neno “pekepeke” kama lilivyotumiwa na mshairi lina maana


gani?
A. Ukatili
B. Ufitini
C. Uonevu
D. Uchoyo
E. Uwongo.

42  
Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B* C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
150,364 193,315 106,530 281,195 105,134 4,977 3,238
watahiniwa
Asilimia ya
17.8 22.88 12.61 33.29 12.45 0.59 0.38
watahiniwa

Swali lilikuwa linapima matumizi ya misamiati kama ilivyotumika katika


habari. Asilimia 22.88 ya watahiniwa walijibu kwa usahihi kwa kuchagua
jibu B “Ufitini” ambalo ndilo lilikuwa na maana sawa na neno “pekepeke.”
Aidha watahiniwa 643,223 sawa na asilimia 76.15 walichagua vipotoshi
kati ya A, C, D na E, kwa kuwa walishindwa kutofautisha hali ya kutokuwa
na huruma na udhalimu (ukatili) kumfanyia mtu dhuluma, mateso au
unyanyasaji (uonevu), hali ya kutokupenda kutoa kitu (uchoyo) na tabia
ya kuwadanganya wengine (uwongo). Hivyo kushindwa kwa watahiniwa
hao ni kutokana na kutokuelewa maana mbalimbali za maneno.

Swali la 45: Vina vya kati na vya mwisho katika ubeti wa tatu ni vipi?
A. Ko na Ke
B. U na Ke
C. Du na Ke
D. Ri na Ni
E. Ki na Ke.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A* B C D E Wasiojibu Mengine
Idadi ya
489,035 103,262 87,583 107,893 49,382 4,373 3,225
watahiniwa
Asilimia ya
57.89 12.22 10.37 12.77 5.85 0.52 0.38
watahiniwa

43  
Swali lilikuwa linapima maarifa ya mtahiniwa kuhusu kanuni za utunzi wa
shairi. Asilimia 57.89 ya watahiniwa walijibu swali kwa usahihi kwa
kuchagua jibu A ‘ko’ na ‘ke’ kwa kuwa walikuwa na maarifa ya kutosha
kuhusu mbinu za utunzi wa mashairi kama vina vya kati na vya mwisho.
Asilimia 41.21 ya watahiniwa waliochagua vipotoshi kati ya B, C, D na E
walikosa ujuzi wa kuvijua vina vya kati na vya mwisho katika ubeti wa tatu
wa shairi hili kwa kuwa hawana ujuzi wa kutosha kuhusu kanuni za utunzi
wa mashairi.

Swali la 46: Funzo linalopatikana katika shairi hilo linawakilishwa na


methali ipi kati ya zifuatazo?
A. Raha haiji ila baada ya tabu
B. Mkataa pema pabaya panamwita
C. Ukikosa shukuru kupata kuna mungu
D. Fimbo ya mbali haiui nyoka
E. Usiache mbachao kwa msala upitao.

Majibu ya watahiniwa
Chaguo A B C D E* Wasiojibu Mengine
Idadi ya
193,078 218,657 142,832 95,286 185,862 5,178 3,860
watahiniwa
Asilimia ya
22.86 25.88 16.91 11.28 22 0.61 0.46
watahiniwa

Swali lilikuwa linapima uwezo wa mtahiniwa kuhusu tathmini ya shairi


alilolisoma. Asilimia 22 tu walikuwa na uelewa wa funzo linalopatikana
katika shairi, hivyo waliweza kuchagua jibu sahihi ambalo lilikuwa E
“Usiache mbachao kwa msala upitao” methali yenye maana ya usidharau
kilicho chako unachodhani kuwa ni kibaya kwa kutegemea kinachopita
unachodhani kuwa ni kizuri, shairi hili linahimiza mtu kuthamini kilicho

44  
chake. Watahiniwa waliochagua kipotoshi A “Raha haiji ila baada ya tabu”
ni asilimia 22.86, watahiniwa hawa walishindwa kuelewa kuwa maana ya
methali hiyo ni kuwa huwezi kupata raha mpaka usumbuke au utaabike
sana, kipotoshi B “Mkataa pema pabaya panamwita” kilichaguliwa na
asilimia 25.88, watahiniwa hawa walishindwa kuelewa maana ya methali
hiyo ambayo ni anayekataa jambo zuri baya linamngoja. Aidha, kipotoshi
C “Ukikosa shukuru kupata kuna mungu” kilichaguliwa na asilimia 16.91,
ambayo ni methali yenye maana ya kuwa ukosapo kitu mshukuru mungu
kwani ndiye mwenye uwezo wa kutoa, hivyo usiwe na tabia ya
kulalamika. Asilimia 11.28 walichagua kipotoshi D, “Fimbo ya mbali haiui
nyoka” ambayo ni methali yenye maana kuwa huwezi kufanikisha jambo
kwa kutegemea kitu kilicho mbali nawe. Vipotoshi A–D vina maana
ambayo ni tofauti na maudhui ya shairi.

2.5 Sehemu E: Utungaji


Katika sehemu hii, watahiniwa walipewa habari yenye sentensi nne (4)
zilizoandikwa bila mtiririko sahihi na walitakiwa wazipange sentensi hizo ili
ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C na D.

Swali la 47: Vilevile matunda huongeza damu mwilini.


Swali la 48: Hivyo matunda yana umuhimu mkubwa katika miili yetu.
Swali la 49: Lakini watu wasiokula matunda hupata maradhi kama vile
ugonjwa wa fizi, macho na ngozi.
Swali la 50: Kula matunda kunasaidia kuponyesha magonjwa na
vidonda haraka, pia husaidia macho kuona vizuri katika
mwanga hafifu.

45  
Majibu ya watahiniwa
Swali Jibu sahihi Idadi ya Asimilia ya % wasiojibu % mengine % Jibu E
watahiniwa watahiniwa
47 B 347,166 41.1 0.41 0.37 3.52
48 D 300,283 35.55 0.35 0.4 3.39
49 C 295,995 35.04 0.34 0.35 3.78
50 A 513,711 60.81 0.26 0.32 3.8

Swali hili lililenga kupima uwezo wa watahiniwa katika upangaji wa


mawazo katika mtiririko wenye mantiki. Zaidi ya nusu ya watahiniwa
ambao ni asilimia 60.81 waliweza kuandika sentensi ya kwanza kwa
usahihi kama ilivyotakiwa. Hata hivyo asilimia ilipungua katika upangaji
wa sentensi ya pili kwani ni asilimia 41.1 tu ndiyo walioandika sentensi
hiyo kwa usahihi. Katika kukamilisha sentensi mbili za mwisho asilimia ya
watahiniwa ilipungua zaidi hadi kufikia asilimia 35.04 kwa sentensi ya tatu
na 35.55 kwa sentensi ya nne. Asilimia 3.8 hadi 3.78 walijibu maswali
haya kama yale ya kuchagua kwa kujaza kipengele E ambacho
hakikuwepo katika sehemu hii ya mtihani. Watahiniwa hawa
hawakuelewa maelekezo ya swali na pia inaelekea kuwa walikuwa
wanachagua majibu bila kusoma kilichoandikwa kwani wangekuwa
wanasoma wangebaini kuwa herufi E haikuwa miongoni mwa herufi
walizopaswa kuziandika katika swali hilo.

3.0 HITIMISHO

Uchambuzi wa namna watahiniwa walivyojibu maswali unaonesha


changamoto mbalimbali ambazo watahiniwa walikumbana nazo
walipokuwa wakifanya mtihani. Kwa ujumla kiwango cha ufaulu kwa kila
mada kimekuwa ni cha wastani. Uchambuzi unaonesha kuwa katika kila
mada kuna maswali yaliyojibiwa vibaya na idadi kubwa ya watahiniwa

46  
lakini pia yapo yaliyojibiwa vizuri na Idadi kubwa ya watahiniwa. Kwa
upande wa maswali yaliyojibiwa vibaya ni kama vile, swali la 16 kutoka
mada ya Sarufi ambapo ni asilimia 19.45 tu ya watahiniwa ndio walioweza
kuchagua jibu sahihi. Pia swali la 30 kutoka mada ya Lugha ya Kifasihi
lilijibiwa kwa usahihi na asilimia ndogo (13.71). Vile vile ufaulu mdogo
ulijitokeza katika swali la 40 lililotoka katika mada ya Ufahamu, idadi ya
watahiniwa waliojibu swali hilo kwa usahihi ni asilima 12.28 tu. Aidha, kwa
upande wa maswali yaliyojibiwa vizuri na watahiniwa ni swali la 28 kutoka
katika mada ya Lugha ya Kifasihi, ambapo asilimia 83.59 waliweza
kuchagua jibu sahihi. Maswali mawili kutoka katika mada ya Ufahamu pia
yalijibiwa vizuri yaani swali la 31 ambalo lilijibiwa vizuri na asilimia 80.27
na swali la 36 lililojibiwa vizuri na asilimia 80.17. Uchambuzi wa ufaulu
wa watahiniwa kwa kila mada katika somo la Kiswahili umewasilishwa
katika Kiambatisho A.

Kutokana na uchambuzi huu, inaonesha wazi kuwa suala la ujifunzaji na


ufundishaji wa somo la Kiswahili kwa shule za msingi linatakiwa lifanyike
kwa ukamilifu ili kuwawezesha wanafunzi kutumia Kiswahili fasaha. Kwa
kupitia wadau mbalimbali wa lugha ya Kiswahili, somo hili linatakiwa
kupewa kipaumbele kwa kuwawezesha wanafunzi kupata maarifa ya
kutosha kuhusu somo la Kiswahili ili waweze kukabiliana na changamoto
mbalimbali za kitaaluma na za kimaisha kuhusiana na lugha ya Kiswahili.

Itambulike wazi kuwa Kiswahili ni lugha ya Taifa, ni sehemu ya utamaduni


wa Mtanzania na ni lugha inayotegemewa katika kuziunganisha nchi za
Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na pia hutumika kimataifa. Hivyo, ni vema
juhudi endelevu za kuinua lugha hii zifanyike kuanzia shule za msingi hadi
elimu ya juu. Kwa kufanya hivi, lugha hii ya Kiswahili itakuwa imetendewa
haki na kupewa hadhi inayostahili katika taifa hili.

47  
4.0 MAONI NA MAPENDEKEZO

Ili kuwawezesha watahiniwa kupata maarifa na ujuzi wa kutosha na pia


katika kuboresha matokeo yao katika mtihani wa Kiswahili mambo
yafuatayo hayana budi kuzingatiwa:
(a) Mamlaka husika zihakikishe kuwa shule zote za msingi zinakuwa
na vitabu vya kiada na vya ziada vya kutosha kwa ajili ya somo la
Kiswahili.

(b) Walimu wanaofundisha somo la Kiswahili katika shule za msingi


wanatakiwa kufundisha mada zote kwa ukamilifu kama
ilivyoelekezwa katika muhtasari.

(c) Ili kupata ujifunzaji na ufundishaji wenye mafanikio, walimu


wanatakiwa kutoa mazoezi ya kutosha kwa wanafunzi kuhusiana na
mada mbalimbali wanazofundisha, ikiwa ni pamoja na kuwapa
wanafunzi mrejeo wa matokeo ya mazoezi hayo kila mara.

(d) Wanafunzi wajengwe kifikra kuhusiana na umuhimu wa somo la


Kiswahili katika maisha yao ili waweze kuondoa dhana iliyojengeka
kwa wengi ya kuliona somo la Kiswahili kama somo lisilo na tija
kwao kwa maisha ya baadaye.

(e) Wanafunzi wahamasishwe katika kutumia Kiswahili sanifu katika


mazungumzo na maandishi yao ya kila siku ili kuboresha misamiati
na sarufi ya lugha ya Kiswahili kwa ujumla.

48  
KIAMBATISHO A

UCHAMBUZI WA UFAULU WA WATAHINIWA KWA KILA MADA KATIKA


SOMO LA KISWAHILI

NA MADA NAMBA ASILIMIA YA WASTANI MAONI


YA SWALI UFAULU WA
UFAULU
(%)
1. Sarufi 1 37.62
2 45.27
3 46.67
4 50.06
5 47.28
6 39.99
7 77.77
8 49.33 47.91 Wastani
9 67.64
10 32.21
11 28.57
12 71.56
13 64.96
14 55.79
15 43.91
16 19.45
17 46.75
18 55.69
19 28.76
20 48.81
2. Lugha ya 21 62.9
Kifasihi 22 57.47
23 43.63
24 48.54
25 25.27
26 44.48 44.17 Wastani
27 38.78
28 83.59
29 23.31
30 13.71
3. Ufahamu 31 80.27
32 55.33 55.97 Wastani
49  
NA MADA NAMBA ASILIMIA YA WASTANI MAONI
YA SWALI UFAULU WA
UFAULU
(%)
33 65.94
34 31.86
35 61.79
36 80.17
37 72.46
38 45.22
39 54.39
40 12.28
4. Ushairi 41 41.75
42 68.89
43 40.83
44 22.88 42.37 Wastani
45 57.89
46 22
5. Utungaji 47 41.1
48 35.55 43.13 Wastani
49 35.04
50 60.81

50  

You might also like