Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 3

<- Layer8 version @version.

id@ -->

Mataifa na asili ya majina yake –


Botswana
September 3, 2020

Na Mwandishi Wetu

INAFAHAMIKA kwa jina la Jamhuri ya Bostwana, moja kati ya nchi zilizoko Kusini mwa Bara la Afrika
zilizowahi kutawaliwa na Waingereza.

Kama zilivyo nchi zingine, Bostwana nayo ina upekee wake. Mathalan, maji ni kitu kinachothaminiwa
zaidi na raia wa taifa hilo.

Kuonesha thamani, hata pesa yao wanaiita ‘Pula’, neno linalomaanisha mvua kwa lugha yao ya taifa,
Kisetswana. Pia, Botswana ndiyo nchi pekee Afrika yenye kiwango kidogo cha kesi za rushwa, ikiwa
kinara katika hilo tangu mwaka 1998.

Aidha,licha ya Kiingereza kuwa ndiyo lugha rasmi, Kiswetana ndiyo lugha yao pendwa, ikizingumzwa na
idadi kubwa ya watu, licha ya kwamba zipo zingine zaid ya 15.

Ikiwa na watu milioni mbili, kwa mujibu wa sensa ya mwaka juzi, hutakuwa umekosea kusema Botswana
ni ndogo mara mbili, ukilinganisha na Mkoa wa Dar es Salaam.

Pia, licha ya kuwa moja kati ya nchi ndogo katika uso wa dunia, bado Botswana ni kubwa na haiingii ‘top
10’ ya zile zenye idadi ndogo ya watu barani Afrika. Humo unaikuta Lesotho, Gabon, Guinea-Bissau,
Mauritius, Swaziland, Djibouti, Comoros, Cape Verde, Sao Tome & Principe, na Seychelles.
Tukiacha hayo, je, unaijua chimbuko la Botswana kufahamika kwa jina hilo? Safu hii ya ‘Nikujuze’ iko
hapa kukupa elimu hiyo. Tafadhali endelea na aya inayofuata.

Neno Botswana linatoka katika lugha ya kwao, likimaanisha ‘Ardhi ya Tswana’. Ni kama kusema ‘Ardhi ya
Wachaga’. Tswana ni jamii iliyokuwa ikiishi katika ardhi hiyo enzi hizo.

Ikiwa haina tofauti na jamii zingine, Watswana waliishi kwa kutegemea kilimo na ufugaji, hadi walipofika
wazungu. Hata wakoloni (Waingereza) waliendelea kulitumia jina hilo, Tswana, lakini wao wakimaanisha
‘watu wa Botswana’.

Ni kusema kwamba kwa kipindi chote cha ukoloni, eneo hilo liliendelea kuitwa Tswana, hadi neno
‘Botswana’ lilipoanza kutumika baada ya nchi hiyo kumkimbiza Mwingereza Septemba 30 mwaka 1966.

Mbaya kuhusu Botswana ni janga la Ukimwi, ikitajwa kuwa moja ya ‘kambi’ za ugonjwa huo, kama
unavyoweza pia kuizungumzia Afrika Kusini.

Licha ya uwepo wa programu za kudhibiti, zikienda sambamba na bajeti kubwa, bado kasi ya maambukizi
ya Ukimwi imekuwa ya kuogofya. Kwa miaka nane, kuanzia 2006 hadi 2013, kulikuwa na maambukizi
mapya 3000. Kufikia mwaka 2014, asilimia 20 ya milioni mbili wa Botswana walithibitika kuishi na virusi
vya Ukimwi.

Ikiwa na majirani Afrika Kusini, Namibia, Zimbabwe na Zambia, Botswana pia ina bahati mbaya, kwamba
asilimia 70 ya ardhi yake ndiyo Jangwa la Kalahari.

Awali, ilikuwa ikitajwa kwenye orodha ya nchi masikini duniani lakini kwa sasa inafahamika kuwa sehemu
ya zile zenye uchumi unaokuwa kwa kasi. Katika hilo, shukurani pekee kwa sekta ya madini, ufugaji na
utalii.

Ushirikiano wa Botswana na nchi zingine, kwa maana ya diplomasia ya kimataifa, uko vizuri kwani ni
mwanachama wa Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Zaidi ya hapo, taifa hilo ni mwanachama wa Jumuhiya ya Madola na Umoja wa Mataifa (UN).

Je, ungependa kumfahamu rais wake wa sasa? Ikitajwa kuwa ni moja kati ya nchi zinazoheshimu kwa
kiasi kikubwa misingi ya demokrasia, rais aliyeko madarakani anaitwa Ian Khama. Huyo ni motto wa
kiume wa rais wa kwanza wa Botswana, Seretse Khama.

Ndiye aliyepatikana katika ndoa ya Seretse na mwanamke mwenye asili ya Uingereza, Ruth Williams.
rai_posts
http://rai.co.tz

You might also like