Professional Documents
Culture Documents
Kuitwa Kwenye Usaili 2022 Konstebo 470
Kuitwa Kwenye Usaili 2022 Konstebo 470
Kwa wale waliotuma maombi yao kupitia Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar wanatakiwa
kufika Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) siku ya Jumapili ya tarehe 06
Februari, 2022 saa 2:00 asubuhi.
Waombaji wote wanatakiwa kufika na Cheti cha Kuzaliwa, Kitambulisho cha Taifa au
Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA), Vyeti halisi vya taaluma, Cheti cha kuhitimu
Mafunzo ya Awali ya Kijeshi kutoka JKT/JKU, Kalamu ya wino ya buluu, Vyeti vingine vya
Uhitimu wa mafunzo katika fani mbalimbali.
Kwa waombaji ambao muundo wa fani zao unatakiwa kusajiliwa na Bodi za Taaluma,
wanatakiwa kufika na Vyeti halisi vya Usajili pamoja na leseni za kufanyia kazi kwa fani
husika.
Aidha, wasailiwa wote wanatakiwa kujigharamia chakula, usafiri na malazi wakati wote wa
zoezi husika.
Tahadhari:
Mwombaji yeyote atakayebainika kuwasilisha nyaraka za kughushi
atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa Mahakamani.
Limetolewa na;
SI Paul Msele
Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji
28 Januari, 2022.