Dua Mlango Wa Arafah, Umrah, Hijja

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 4

TAKBIRA YA HIJJA AU UMRAH

Vipi ataleta talbiyah aliyehirimia kwaajili ya hijjah au umrah

Labbayka-Allaahumma Labbayk. Labbayka laa shariyka Laka Labbayk. Innal-Hamda, wan-ni’-matah, Laka
wal-Mulk. Laa shariyka Lak.

MAANA YAKE;

Nimekuitika Ee Allaah nimekuitika. Nimekuitika Huna mshirika, nimekuitika. Hakika Himdi na Neema na
Ufalme ni Vyako. Huna mshirika.

KIARABU;

َ َ‫ك ل‬
‫ك‬ ُ ْ ‫مل‬
َ ‫ ال شَ رِي‬،‫ك‬ ُ ْ ‫ك وَال‬
َ َ ‫ل‬، ‫ة‬
َ ‫م‬
َ ْ‫ وَالنِّع‬،َ‫مد‬ َ ْ ‫ن ال‬
ْ ‫ح‬ َ ْ ‫ك لَبَّي‬
َّ ‫ إ‬،‫ك‬ َ َ‫ك ل‬ َ ْ ‫ لَبَّي‬،‫ك‬
َ ‫ك ال شَ رِي‬ َ ْ ‫م لَبَّي‬
َّ ُ‫ك اللَّه‬
َ ْ ‫لَبَّي‬

Takbira atakapofika katika hajar al-as'wad (katika alkaaba)

Rasuli wa Allaah (‫ )صلى هللا عليه وسلم‬alitufu kuzunguka Al-Ka’bah juu ya ngamia. Kila alipofika katika rukn
(Hajarul-Aswad) alikuwa anaashiria kwa kitu na kusema:

Allaahu Akbar

MAANA YAKE;

Allaah ni Mkubwa.

KIARABU;

‫هللاُ أ ْكبَر‬

Dua inayosomwa baina ya nguzo ya yemeni na hajar al-as'wad (katika alkaaba)

Alikuwa Rasuli wa Allaah ( ‫ )صلى هللا عليه وسلم‬akisema baina yake:

Rabb wetu Tupe katika dunia mazuri na katika Aakhirah (pia Tupe) mazuri na Tukinge na adhabu ya Moto

KIARABU;

َ ‫سنَةً َوقِنَا َع َذ‬


‫اب النَّا ِر‬ َ ‫سنَةً َوفِي اآْل ِخ َر ِة َح‬
َ ‫َربَّنَا آتِنَا ِفي ال ُّد ْنيَا َح‬

Dua ya kusomwa ukiwa umesimama katika mlima wa swafaa na mar'wah


Amesema Jaabir (‫ )رضي هللا عنه‬katika Hadiyth ndefu aliyoielezea Hijah ya Rasuli wa Allaah ( ‫صلى هللا عليه‬
‫ )وسلم‬kwamba alipokurubia Swafaa alisoma: Hakika Swafaa na Mar-wah ni katika alama za (Dini ya)
Allaah.

Abdau bimaa Badaa-Allaahu bih

MAANA YAKE;

Ninaanza kwa alichoanza Allaah

KIARABU;

‫َأ ْب َدُأ بِ َما بَ َدَأ هللاُ بِ ِه‬

Akaanza Swafaa akapanda mpaka akaiona Al-Ka’bah kisha akaielekea na kusema:

Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, Allaahu Akbar

MAANA YAKE;

Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa.

KIARABU;

‫ هللاُ أ ْكبَ ُر‬،‫ هللاُ أ ْكبَ ُر‬،‫هللاُ أ ْكبَ ُر‬

… kisha utasema yafuatayo mara tatu ukiomba du’aa (yoyote apendayo) baada ya kila mara:

Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahu mulku walahul Hamdu wa Huwa ’alaa kulli
shay-in Qadiyr. Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu, Anjaza wa’dahu, Wa naswara ’abdahu, wa hazzamal
ahzaaba Wahdah

MAANA YAKE;

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kuwa Peke Yake, wala hana mshirika. Ni wake ufalme na ni
Zake Himdi, Naye juu ya kila kitu ni Muweza, hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah hali ya kuwa Peke
Yake, Ametekeleza ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi Peke Yake.

KIARABU;

ُ‫ص َر َع ْب َده‬َ َ‫ َون‬،ُ‫ ال ِإلَهَ إال هللاُ َو ْح َدهُ َأ ْن َجزَ َو ْع َده‬،‫الح ْم ُد و ُه َو عَلى ُك ِّل شَي ٍء قَدي ٌر‬
َ ُ‫ لَهُ ال ُم ْل ُك َولَه‬،ُ‫ش ِري َك لَه‬
َ ‫ال ِإلهَ إالَّ هللاُ َو ْح َدهُ ال‬
ُ‫اب َو ْح َده‬ َ َ‫َو َه َز َم اَأل ْحز‬

DUA SIKU YA ARAFAH

Rasuli wa Allaah (‫ )صلى هللا عليه وسلم‬amesema: Du’aa bora kabisa ni du’aa ya siku ya ’Arafah. Na bora ya
niliyoyasema mimi na Manabii kabla yangu ni

Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahul Mulku walahul Hamdu wa Huwa ’alaa kulli shay-in
Qadiyr.

MAANA YAKE;

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah hali ya kuwa Peke Yake hana mshirika. Ni Wake Ufalme na ni Zake
Himdi, Naye juu ya kila kitu ni Muweza.

KIARABU;

‫الح ْم ُد و ُه َو َعلَى ُك ِّل ش َْي ٍء قَدي ٌر‬


َ ُ‫ لَهُ ال ُم ْل ُك ولَه‬،ُ‫ال ِإلَهَ إالَّ هللاُ َو ْح َدهُ ال شَري َك لَه‬.

Utajo katika mash-arul haram (muzdalifa)

Hadiyth ya Jaabir (‫ )رضي هللا عنه‬kwamba: ”Rasuli wa Allaah (‫ )صلى هللا عليه وسلم‬alimpanda Al-Qaswa (jina
la ngamia wake) mpaka alipofika Mash’arul Haraam (Muzdalifah), kisha akaelekea Qiblah akamuomba
Du’aa kwa Allaah, akaleta takbiyr (akamtukuza - Allaahu Akbar), akaleta Tahliyl (akampwekesha – laa
ilaaha illa Allaah) akamkanusha kuweko mwabudiwa mwengine na akampwekesha. Hakuacha kusimama
mpaka kulipopambazuka ndipo alipoondoka kabla ya kutoka jua”

Faida: Sehemu hiyo ya Muzdalifah Haajj anapaswa kumdhukuru Allaah ( ‫ )ع ّز وج ّل‬kwa kila aina ya
Adhkaar, kuswali Jamaa’ah, na kuomba Du’aa, kuomba maghfirah, kumshukuru na kumsifu Allaah ( ‫ع ّز‬
‫ )وج ّل‬na kadhaalika.

Takbira anaporusha kila jiwe katika jamarah (nguzo)

Allaahu Akbar

MAANA YAKE;

Allaah ni Mkubwa

KIARABU;

‫َأهّلل ُ َأ ْكبَ ُر‬

”Rasuli wa Allaah (‫ )صلى هللا عليه وسلم‬Alikuwa kila aliporusha kijiwe katika Jamarah (nguzo) tatu alisema: "
Allaahu Akbar" ...kisha akisogea na kusimama akielekea Qiblah akiomba du’aa huku akiinua mikono yake.
Akifanya hivyo aliporusha vijiwe katika Jamarah ya kwanza na ya pili. Ama Jamarah ya tatu (Al-’Aqabah)
alirusha na akamtukuza Allaah (Allaahu Akbar) kwa kila kijiwe kisha alikuwa hasimami bali akimaliza
anaondoka”

You might also like