Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 8

Jarida la kilimo endelevu Afrika Mashariki Toleo la 60, Septemba 2017

Mimea mbalimbali inaweza


kutumika kama dawa za asili


Ugonjwa wa Mbuzi 2
Usindikaji wa Ufuta 6

Picha: MkM

Picha: IN
Wadudu na madhara yake 8

Mpendwa mkulima
Katika kila eneo mtu alipo kuna fursa
ya kufanya kazi za uzalishaji mali na
hatimae kujiletea maendeleo. Jambo
kubwa linahitajika ni kufahamu kuwa
uchukue fursa ipi, na uitekeleze katika hali
Picha: MkM

Picha: IN
inayokubalika.
Kumekuwa na malalamiko mengi
kutoka kwa wakulima, wafugaji na wadau
wengine kuwa hakuna fursa kwa ajili
ya kuendeleza maisha ya kila siku, au
shughuli ambazo wameanzisha.
Shida iliyopo hapa si kweli kuwa
hakuna fursa, ila hujatambua kuwa ushike
lipi na uache lipi. Kwa lugha nyingine
uchukue fursa ipi na ni ipi uache. Na
Mara nyingi wakulima wamekuwa inayoweza kutumika kutengeneza hapa shida kubwa inayokabili wengi ni
wakiamini na kutumia madawa dawa, au kutumia kama ilivyo na kuleta kutaka kufanya kila jambo linalofanywa na
yaliyotengenezwa viwandani, bila ufanisi mkubwa katika kukabiliana na wengine. Abadan maisha hayawezi kuwa
kufahamu madhara yake kwa afya wadudu waharifu. na mafanikio kwa njia hiyo.
Jambo muhimu katika yote ni kufanya
zao, mazingira na hata wanyama Katika toleo hili utaweza kujifunza
kazi katika fursa ambayo itakupa ufanisi,
wanaowafuga. baadhi ya mimea na aina za wadudu kwanza ujitafakari mwenyewe kuwa ni
Hali hii imetokana na uelewa mdogo inayoweza kudhibiti. jambo lipi kati ya fursa zinazokuzunguka
walio nao kuhusiana na baadhi ya ambalo, linaugusa moyo wako mara kwa
mimea iliyopo kwenye mazingira yao Zaidi soma Uk 3 mara. Ni lipi ambalo linazunguka sana
kichwani mwako na kutamani kulifanya
Matunzo thabiti ni muhimu kwa mbuzi kila wakati.
Hivi sasa nchini Tanzania, Jambo hilo linaweza kuwa ni katika
Mbuzi ni moja ya wanyama ambao nyanja ya kilimo, ufugaji, usindikaji, au
wanajipatia umaarufu miongoni mwa aina nyingine yoyote ya kilimobiashara na
Picha: MkM

ufugaji. Halikadhalika, linaweza kuwa ni


wafungaji, kutokana na urahisi katika katika utunzaji wa mazingira na mambo
kuwafuga na malisho pia. mengine yanayofanana na hayo.
Mbali na hilo ni moja ya kitoweo Baada ya kujitambua kwa namna hiyo,
maarufu katika makabila mbalimbali basi shikilia lile unaloamini kuwa ndilo
hapa nchini, jambo linalofanya soko unalotamani kufanya. Baada ya hapo,
MkM kwenye mtandao unaweza kuanza kutafuta na kufuatilia
taarifa sahihi zinazohusiana na jambo
Njia ya mtandao yaani internet, hilo, bila kujali wengine katika eneo lako
inawasaidia wale wote ambao hawana wanafanya nini au kushawishiwa na mtu
namna ya kupata machapisho ya yoyote huondoka katika unachoamini.
Mfugaji Zadock Kitomari
Mkulima Mbunifu moja kwa moja, Ukishaamua ni fursa ipi unaichukua
kusoma kwenye mtandao na hata lake kuwa la uhakika na wafugaji na kuifanyia kazi baada ya kupata taarifa
kupakua nakala zao wao wenyewe. kuongeza pato kila uchwao. na elimu juu ya jambo hilo kwa kiwango
mkulimambunifu.org Pamoja na urahisi huo na faida unachoona kuwa utaweza kuanza, basi
http://issuu.com/mkulimambunifu kubwa mbuzi wasipotunzwa vizuri anza kufanyia kazi kwa bidii huku
http://www.facebook.com/mkulimam- na kupatiwa malazi na malisho sahihi ukisimamia malengo yako.
bunifu ni rahisi kushambuliwa na magonjwa Fursa zilizopo katika kilimo ni nyingi
kama vile magonjwa ya mapafu na sana na si lazima kufanya jambo hata
https://twitter.com/mkulimambunifu mengineyo. kama halileti faida kwa kuwa tu watu
+255 785 496 036 Zaidi soma Uk 2 wengine wanafanya jambo hilo.

MkM, S.L.P 14402, Arusha, Simu 0717 266 007, 0785 133 005 Barua pepe info@mkulimambunifu.org, www.mkulimambunifu.org
Toleo la 60, Septemba 2017
Fahamu ugonjwa wa homa ya mapafu kwa mbuzi
Mimi naitwa Eliudi Raymond, mbuzi
wangu wawili wamekufa mara tu

Picha: MkM
baada ya kuanza kutoka makamasi kwa
siku 2 mfululizo, je, unaweza kuwa
ni ugonjwa niliosikia kwa wenzangu
wakisema ni homa ya mapafu? Je, huu
ugonjwa ukoje na natibuje?
Patrick Jonathan
Ugonjwa wa homa ya mapafu ya
mbuzi (HMM) ni ugonjwa hatari wa
mbuzi unaosababishwa na bakteria
wajulikanao kama mycoplasma
capricolum subspecies capripneumoniae
(MCCP).
Dalili za ugonjwa huu
Ugonjwa huu unajidhihirisha kwa; Mbuzi mwenye homa ya mapafu huonekana mchovu na mwenye usingizi
• Kupumua kwa shida Wanyama wanaopata HMM kikohozi kuwa kizito), kupumua
• Homa kali (nyuzi 41-43 za Mbuzi ndio wanyama wa kwanza kwa shida ndani ya siku 2 hadi 3.
sentigredi). kupata ugonjwa huu na kondoo • Katika hatua za mwisho mbuzi
• Kukohoa. wanaweza kuupata pia hasa wakiwa hushindwa kutembea au
• Kutiririsha mafua. wanaishi na mbuzi. kusimama huku miguu yake
• Usambaaji wa haraka wa vifo Usambaaji wa HMM ya mbele akiwa amepanua na
vingi kwa mbuzi wa umri wowote, Ugonjwa huu huenea haraka sana shingo yake ikiwa imenyooka na
toka mnyama mmoja kwenda kwa kukakamaa.
pamoja na kutupa mimba kwa
mwingine kwa njia ya kugusana. • Mate yanaweza kuwa yanatoka
mbuzi wenye mimba.
Wadudu wa ugonjwa huu huwa kwa mfululizo mdomoni na mbuzi
Ugonjwa uligundulika lini? anaweza kuwa anakoroma au
kwenye maji maji ya mfumo wa
Ugonjwa huu ulithibitika kuwepo kulia kwa maumivu makali.
upumuaji/hewa.
nchini Tanzania mnamo mwaka 1998 • Mwisho mapovu puani na mate
Dalili za HMM huchukua muda gani
na tangu hapo umeonekana kusambaa mdomoni yanaweza kuonekana.
kudhihirika?
katika maeneo mbalimbali ya nchi, • Mbuzi mwenye mimba, inaweza
Ugonjwa huu huanza kuonesha
huku jitihada kidogo zikiwekwa kutoka.
dalili kuanzia siku 2 hadi ya 28 tangu
kuhusiana na kupambana na ugonjwa • Wanyama wenye ugonjwa
maambukizi yatokee na wastani ni siku
huu. hufikia asilimia 100 (wote huwa
10. Afya ya mbuzi huanza kudhoofu
Kwa Tanzania, ugonjwa huu wagonjwa) na vifo hufikia kati ya
na mwisho kusababisha kifo ndani ya
uliripotiwa kuwepo katika maeneo asilimia 60 hadi 100.
siku 7 tangu kuanza kwa ugonjwa huu.
ya Arusha, Morogoro, Dar es Salaam, • Mbuzi walioathirika sana
Matokeo wanaweza kufa ndani ya siku 7
Pwani, Tanga na Mtwara lakini pia
• Mbuzi walioathirika na HMM hadi 10 tangu waoneshe dalili.
kuna maeneo mengine mengi, ambayo wanaweza kufa ndani ya siku 1 hadi • Kuna baadhi ya mbuzi wanaoweza
dalili kwa mbuzi zimehisiwa kuwa ni 3 bila kuonesha dalili au wakiwa kuendelea kukohoa na kwa
za ugonjwa huu. na dalili chache sana zisizoweza muda mrefu huku wakitiririsha
Tatizo lililopo ni ugumu wa kuutambulisha ugonjwa. makamasi na kuendelea
kuthibitisha ugonjwa huu hasa kwa • Dalili za mwanzo ni homa kali kusambaza ugonjwa kwa muda
njia ya kuotesha wadudu lakini (nyuzi joto 41-43), kuchoka/ mrefu.
uwepo wa teknolojia mpya kama PCR kudhoofika, mwenye usingizi na
utawezesha kuutambua ugonjwa huu kukosa hamu ya kula, kukohoa
Inaendelea Uk. 7
kwa haraka zaidi. mara kwa mara (kwa nguvu na

Mkulima Mbunifu ni jarida huru kwa jamii ya wakulima zwa na Biovision (www.biovision.ch) kwa Mpangilio Ibrahim Isack, +255 676 293 261
Afrika Mashariki. Jarida ushirikiano na Sustainable Agriculture Tan- Zenith Media Ltd
Mhariri Msaidizi Flora Laanyuni
hili linaeneza habari za zania (SAT), (www.kilimo.org), Morogoro. Mhariri Ayubu S. Nnko
kilimo hai na kuruhusu Jarida hili linasambazwa kwa wakulima Mhariri Mkuu Venter Mwongera
majadiliano katika nyanja bila malipo. Anuani Mkulima Mbunifu
zote za kilimo endel- Mkulima Mbunifu linafadhiliwa na Biovision - www. Sakina, Majengo road, (Elerai Construction
biovision. block) S.L.P 14402, Arusha, Tanzania
evu. Jarida hili linatayar- Ujumbe Mfupi Pekee: 0785 496 036, 0766
Wachapishaji African Insect Science for Food and 841 366
ishwa kila mwezi na Mkulima Mbunifu,
Health (icipe), S.L.P 30772 - 00100 Nairobi, KENYA,
Arusha, ni moja wapo ya mradi wa Piga Simu 0717 266 007, 0785 133 005
Simu +254 20 863 2000, icipe@icipe.org, www.icipe.
mawasiliano ya wakulima unaotekele- Barua pepe info@mkulimambunifu.org,
org
www.mkulimambunifu.org
Toleo la 60, Septemba 2017
Mimea hii inaweza kutumika kama dawa za asili
Ni muhimu kwa wakulima kujifunza Wadudu wanaolengwa TAHADHARI: Kuwa makini na
aina mbalimbali za mimea inayoweza Mmea huu huweza kuwadhuru ujihadhari sana sumu hii isiingie
kutumika kutengeneza dawa za asili. na kuangamiza wadudu machoni kwani inaweza kusababisha
mafuta(kimamba), vithiripi, mbu, maumivu makali sana, hasa wakati
Ayubu Nnko viwavi, na wadudu wengineo kwa wa kutwanga, vumbi vumbi linaweza
ujumla. kuingia machoni.
Moja ya kanuni muhimu katika kilimo Mnanaa
Namna ya kutengeneza na kutumia
hai ni kutumia njia za asili ikiwemo Mnanaa hujulikana kitaalamu kama
mimea mbalimbali inayopatika katika • Twanga kiasi cha gramu 50-100
za majani ya utupa (hayo ni kama Datura stramonium. Mmea huu ni moja
mazingira yako, kukabiliana na ya mimea yenye sumu na hupatikana
wadudu waharibifu katika mazao. majani 50).
kwa wingi shambani, ambapo
Mashona nguo • Loweka kwenye lita moja ya maji husababisha wadudu kushindwa kula
safi. na ina viuadudu na pia ina asili ya viua
Mmea huu kitaalamu unajulikana
kama Bidens pilosa na wakulima wengi • Vundika kwa siku moja(acha ukungu.
huchukulia kama ni gugu. Mbegu zake kwenye maji usiku mmoja).
zinaweza kutumika kutayarisha dawa • Chuja kwa kichujio safi au pamba,

Picha: MkM
za kuulia wadudu waharibifu kwenye au nguo ya pamba tayari kwa
mazao. kunyunyiza.
Mmea huu una uwezo wa kuathiri TAHADHARI: Utupa ni sumu kwa
wadudu wa aina zote. Wadudu samaki, hivyo haishauriwi sana
huathiriwa wanapogusa kwa tumbo. kutumika nchini Tanzania. Pia mmea
huu usipotumika vizuri, unaweza
kuua wadudu rafiki katika mazingira.
Picha: MkM

Ni vyema ukatumika kwa tahadhari Mnanaa


kubwa, kwani unaweza kudhuru
binadamu pia. Namna ya kuandaa na kutumia
Unapotumika ni vyema ukasubiri •Twanga mbegu gramu 100.
kwa muda wa siku 10 zipite kwanza, •Loweka kwenye maji lita moja.
baada ya kunyunyiza kwenye mimea •Unaweza kukausha majani na
ndipo uweze kuvuna na kutumia ili kuyatwanga na kutumia kama vumbi
Mashona Nguo
kukwepa sumu iliyopo kwenye mmea vumbi kwenye mimea.
Namna ya kutumia isikudhuru.
Minyaa au Mwasa
• Jaza kikombe cha chai mbegu Topetope, Mstafeli
zilizokomaa na ongeza maji. Minyaa hujulikana kama Euphorbia
Huu ni mmea wa jamii inayojulikana tirucalli. Hii ni aina ya vichaka
• Chemsha kwa dakika 10 au loweka kama Annona spp. Mmea huu na jamii vinavyotumika kama uzio (mitarako)
kwa saa 24. nyingine ya topetope huathiri wadudu kwa ajili ya mifugo. Miti hii ni teketeke
• Ongeza lita moja ya maji ya sabuni endapo watameza au hushindwa na hupatikana sehemu kame.
na unyunyize shambani wakati kula Zaidi mimea na mara nyingine
huo huo. kutokana na harufu yake, wadudu
hukimbia au hawaisogelei kabisa

Picha: IN
• Unaweza kuponda mmea wote wa mimea.
shona nguo na kuufikicha kwenye
maji mpaka utoe juisi. Ongeza
Picha: MkM

sabuni kidogo na unyunyize


shambani.
Utupa
Mmea huu unajulikana kitaalamu
kama Tephrosia vogelii. Mmea huu
unafahamika sehemu nyingi duniani.
Mnyaa/Mwasa
Mmea huu una uwezo mkubwa wa
kupambana na aina mbalimbali za Namna ya kuandaa na kutumia
wadudu wanaoharibu mimea.
Sumu yake ambayo ipo kwenye
• Utupa humfanya mdudu ashindwe Topetope aina ya maziwa maziwa, matone 10
kula mimea. yachanganywe kwenye lita moja ya
Wadudu wanaolengwa
• Hufukuza wadudu kutokana na maji, nyunyiza kwenye mimea kukabili
harufu yake. • Wadudu mafuta(kimamba), jamii aina tofauti za wadudu shambani.
ya viwavi au vipepeo, mbu pamoja
na wadudu wengine. Ili kukabiliana na wadudu kama
sota(cutworm) na mchwa.
Picha: IN

• Namna ya kuandaa na kutumia


• Twanga tawi la minyaa kisha
• Twanga kiasi cha gramu 10 (au changanya na fukia kwenye
gramu 5-25) za mbegu au gramu udongo.
50-100 za majani ya topetope.
• Uwiano wa dawa na maji
• Loweka kwenye lita moja ya maji hutegemea eneo au kiasi cha
ya uvuguvugu. mimea shambani.
• Acha kwa saa ishirini na nne. TAHADHARI: Kuwa mwangalifu ili
Utupa • Chuja na unyunyize shambani. isiingie machoni.
Toleo la 60, Septemba 2017

Fahamu njia zinazoweza kutumika kul


Ni muhimu wafugaji wa kuku wa asili kwenye chumba cha pekee ili
kuacha kufuga kama mazoea tu na vifaranga visishambuliwe na kuku
kwa matumizi madogo madogo kama wengine, hali kadhalika kuwalinda
ya kitoweo na kujikimu kwa tatizo dhidi ya wanyama na ndege
liliopo kwa wakati huo, na badala yake wanaoshambulia vifaranga kama vile
uwe ni mradi rasmi. vicheche, mwewe na kunguru.
Amani Msuya Uleaji wa vifaranga mfumo wa
kubuni
Vifaranga ni hatua ya mwanzo Uleaji wa vifaranga kwa mfumo wa
ya ukuaji wa kuku, hivyo ni bora kubuni ulikuwa unatumika zaidi
kuchukua tahadhari ili kuhakikisha kwa ufugaji kuku wa kisasa ambao
ukuaji ulio bora wa vifaranga hao. hutotolewa kwa wingi.
Vifaranga vinahitaji malezi makini Katika mfumo huu vifaranga
kuepusha magonjwa yanayoweza huwekwa kwa pamoja kwenye
kusababisha vifo na hivyo kupunguza chumba maalum na kupatiwa joto
idadi ya kuku unaotarajia kuwa nao. maalum, chakula pamoja na maji.
Uhakika wa kuwa na kuku walio Utaratibu huu pia unaweza
bora na wengi utategemea matunzo kutumika kwa kuku wa Asili kwani
bora ya vifaranga utakayotoa tangu kitu muhimu ni joto la kutosheleza
siku ya kwanza vifaranga vitotolewe. ukuaji.
Vifo vingi vya vifaranga hutokea Kwa kutumia mfumo wa kubuni,
siku za mwanzoni vikishatotolewa. kuku wanaweza kunyang’anywa
Hivyo basi, ili mfugaji aweze vifaranga vyao mara tu baada ya
kupata tija na mafanikio kwa haraka kutotoa na kuviweka kwenye
kutokana na ufugaji wa kuku wa Bruda na hao kuku wakaachwa bila
Asili, ni vyema kuhakikisha vifaranga vifaranga.
vinalelewa katika mazingira mazuri Baada ya majuma mawili, kuku
toka siku ya kwanza. Vifaranga wakitunzwa vizuri ni dhahiri kuwa m
walionyang’anywa vifaranga hao
Uhitaji wa joto huanza tena kutaga na kuendelea na nishati, ambazo zimebuniwa hapa
Vifaranga huhitaji joto la ziada katika uhatamiaji hadi kutotoa tena. nchini na kufanyiwa utafiti wa kina na
kipindi cha mwanzo cha ukuaji Kwa mfumo huu kuku anaweza kuonekana kuwa na uwezo mkubwa
ambacho ni kati ya siku 1 hadi wiki kutotoa mara 5 hadi 6 badala ya mara wa kulea vifaranga.
ya nane. 2 hadi 3 kwa mwaka kama ilivyo sasa. Kutunza vifaranga kwa
Mara nyingi njia ya asili ya kutumia Kuna njia mbili za uleaji wa kutumia Mkombozi Bruda
kuku wazazi hutumika kutoa joto la vifaranga kwa mfumo wa Kifaa hiki kimeitwa Mkombozi kwa
ziada kwa vifaranga kwa kipindi cha kubuni: kuwa ni rahisi kukitengeneza na
wastani wa siku 90. Njia ya uleaji wa vifaranga kwa hata kukitumia na pia kimeonesha
Njia za uleaji wa vifaranga kutumia nishati mafanikio katika kulea vifaranga.
Kuna mifumo (2) miwili ya uleaji wa Njia hii inahusu kutunza vifaranga Namna Mkombozi Bruda
vifaranga ni: kwenye mzingo (mduara) ndani inavyofanya kazi
Uleaji wa vifaranga kwa ya chumba na kuvipatia joto kwa Huhifadhi joto la asili la vifaranga
mfumo wa asili kutumia taa ya kandiri (chemli), taa vyenyewe na kulifanya litumike tena
Uleaji wa vifaranga kwa mfumo ya umeme au jiko la mkaa. kuwapatia joto vifaranga hao. Kwani
wa asili ni ule uliozoeleka, ambapo Hata hivyo, njia hii ina gharama hakuna gharama ya kutafuta nishati
kuku mwenyewe baada ya kutotoa kubwa na wakati mwingine ili kuwapatia joto badala yake ni
hutembea na vifaranga vyake upatikanaji wake si wa uhakika. joto la vifaranga wenyewe ambalo
akivisaidia kutafuta chakula na Kwa njia hii unaweza kupima joto huwatunza na kuwapatia hifadhi
kuvikumbatia kila baada ya muda katika mzingo kama linatosha au la maalum inayohitajika. Kifaa hiki
fulani ili kuvipatia joto. kwa kuangalia hali ya usambaaji wa kinaweza kulea vifaranga 20 mpaka
Mfumo wa asili umekuwa vifaranga ndani ya mzingo. 70.
hauna tija kwa kusababisha ukuaji Njia ya uleaji wa vifaranga Vifaranga hulelewa kwa wiki 8 na
wa vifaranga kuwa duni na vingi isiyotumia nishati baada ya hapo huhamishiwa katika
kushambuliwa na wanyama na ndege Njia hii hutumika kulelea vifaranga banda la kuku wanaokua.
na vingine kufa. bila ya msaada wa nishati ya kuongeza
Picha: IN

joto. Njia hii ni nzuri kwa wafugaji


Vile vile mizunguko ya utagaji wa
wadogo wadogo hasa waishio vijijini
kuku kwa mwaka huwa michache.
kwani hakuna gharama za kutafuta
Kwa kutumia mfumo huu vifaranga nishati ili kuwapatia joto badala yake
hulelewa kwa takribani miezi mitatu. joto la vifaranga wenyewe huwatunza
Kama utalea vifaranga kwa mfumo na kuwapatia hifadhi maalum
wa asili, basi ni vizuri kumtenga kuku inayohitajika.
Mkombozi Bruda
mwenye vifaranga na kumuweka Zipo aina mbili(2) za uleaji usiotumia
Toleo la 60, Septemba 2017

ea vifaranga wa kienyeji kwa manufaa


Wakati wa usiku, vifaranga
hufungiwa kwenye sehemu ya

Picha: MkM
kuhifadhi joto na hutenganishwa na
sehemu ya kuzungukia. Chakula na
maji safi huwekwa kwenye sehemu ya
kuzungukia wakati wote wa mchana.
Wiki ya kwanza vifaranga hutolewa
kwenye sehemu ya kuhifadhi
joto (wanapolala vifaranga) na
kuwekwa sehemu ya kuzungukia
(wanaposhinda vifaranga) kwa ajili
ya kupewa chakula
na maji.
Baada ya wiki ya kwanza milango
ya vifaranga ifunguliwe wakati wa
mchana na vifaranga waruhusiwe
kuzunguka sehemu ya kushindia.
Mkombozi ihamishwe mara kwa
mara kuruhusu vifaranga kupata
majani mabichi, wadudu na rasili
mali nyingine za vyakula.
Wiki ya kwanza Mkombozi huweza
kuhifadhi nyuzi joto kati ya 34C na
39C. Hata hivyo kiwango cha joto
hupunguzwa kwa nyuzi joto 3C kila
wiki kwa kupunguza majani makavu
mfugaji atapata faida na kufikia malengo katikati ya kiota na kuta za Mkombozi
kwenye mfuniko.
Namna ya kutengeneza Mkombozi Bruda
Muundo wa Mkombozi umejumuisha 30 na unene wa sentimita 3. Upana wa sehemu ya kuzungukia hutegemea
sehemu ya kuhifadhi joto na sehemu na urefu wa sehemu ya kuhifadhi idadi ya vifaranga wanaotarajiwa
ambayo huruhusu vifaranga joto hutegemea idadi ya vifaranga kulelewa.
kuzunguka. wanaotarajiwa kulelewa.
Sehemu ya kuhifadhi joto na ambapo Sehemu ya kuzunguka hutengenezwa
vifaranga hulala hutengenezwa kwa kwa vipande vinne vya mbao, vipande
vipande vinne vya mbao. hivyo vina upana wa sentimita 30 na
Vipande hivyo, vina upana wa sentimita unene wa sentimita 3. Upana na urefu

Vipimo vya utengenezaji wa Mkombozi Bruda Inaendelea Uk. 7

Vipimo sehemu ya kuhifadhi Joto (sm) Vipimo sehemu ya Kuzungukia (sm)


(Wanapolala vifaranga) (Wanaposhinda vifaranga)

Kina Urefu Upana Kina Urefu Upana

30 26 26 30 56 56

30 30 37 37 30 80 80

40 30 45 45 30 98 98

50 30 52 52 30 113 113

60 30 63 63 30 139 139

70 30 68 68 30 150 150
Toleo la 60, Septemba 2017
Okoa upotevu wa ufuta kwa kusindika ili kupata mafuta
Ufuta husindikwa ili kupata bidhaa
ya mafuta ambayo hutumika katika

Picha: IN
mapishi mbalimbali. Mafuta ya ufuta
hukamuliiwa kwa kutumia njia za asili
au kwa kutumia mashine.
Flora Laanyuni

Njia za asili za kukamua ufuta zina


ufanisi mdogo ukilinganisha na zile
za kukamua kwa kutumia mashine
hivyo ni vyema kutumia mashine.
Kuna mashine za aina mbili
zinazotumika kukamua mafuta,
mashine za mkono na zile Mbegu za ufuta zikikamuliwa zinatoa mafuta yaliyosafi na salama kwa afya
zinazoendeshwa na injini au umeme. vyenye upana wa sentimita 20 na safi na vifungashio safi.
Mashine za mkono zinazotumika urefu wa sentimita 30.
Jinsi ya kukamu mafuta kwa
zaidi hapa nchini ni za aina ya daraja Malighafi Ram
(bridge press) na Ram. Malighafi zinazohitajika ni mbegu • Anika mbegu za ufuta juani kwa
Kukamua ufuta kwa kutumia safi za ufuta na maji safi na salama. kuzitandaza kwenye mabati ili
mashine ya daraja zipate joto la kutosha.
Jinsi ya kukamua ufuta
Mashine ya daraja ni moja ya • Jaza mbegu za ufuta kwenye
• Nyunyizia maji kidogo kwenye
mashine za kisasa zinazoweza mpare wa kulishia kisha funga
ufuta ili kuongeza unyevu kufikia
kukamua mafuta ya ufuta. Mashine wenzo ili kuzuia mbegu za ufuta
asilimia 11 hadi 13 kwani mafuta
zisitoke.
hizi huendeshwa kwa mikono na hutoka vizuri zaidi kwenye
• Nyanyua wenzozuia mpaka juu
zina uwezo wa kukamua mafuta kwa kiwango hicho cha unyevu.
ili kuruhusu piston kusukuma
asilimia 68 hadi 72. Inawezekana • Jaza ufuta kwenye vifuko vya
mbegu za ufuta ziingie ndani ya
nguo au viroba kisha panga
eneo la shindilio.
vifuko hivyo kwenye silinda na
Picha: MkM

• Nyanyua tena wenzozuia mpaka


kuanza kuzungusha mhimili
juu na kushusha na wakati
hadi mafuta yaanze kutoka
huohuo ukiendelea kujaza
kupitia matundu ya silinda.
mbegu za ufuta kwenye mpare
• Acha kwa muda mafuta
wa kulishia.
yaendelee kutoka kisha endelea
• Wenzozuia ikiwa nzito ni dalili
kuzungusha muhimili hadi
kuwa msukumo wa kutosha
mafuta yaishe.
umejengeka na msukumo huo
• Muhimili ukiacha kuzunguka ni
utasababisha mafuta kuanza
Mashine ya kukamua Ufuta
dalili kuwa mafuta yamekwisha.
kutoka.
• Kusanya mafuta, chuja na
kukamua kilo 25 za ufuta kwa saa. • Mafuta yanapoanza kutoka
fungasha kwenye chupa safi
Ili kupata ufanisi mzuri wa mashine legeza wenzozuia ili kuruhusu
zilizochemshwa.
hii, ni muhimu ufuta uwe na unyevu mashudu kutoka.
• Hakikisha chupa ni kavu na zina
wa kati ya asilimia 11 hadi 13. Iwapo • Chuja na hifadhi mafuta kwenye
mifuniko.
vyombo safi vyenye mifuniko
unyevu utakuwa chini ya kiwango • Weka lebo na lakiri kisha hifadhi
vilivyochemshwa.
hicho, inashauriwa kunyunyiza mahali pasafi, pakavu na pasipo
maji kidogo kwenye ufuta kabla ya na mwanga mkali. Matumizi
kukamua ili kupata kiwango kidogo Kukamua mbegu za ufuta kwa Mafuta ya ufuta hutumika katika
cha unyevu. kutumia mashine ya Ram mapishi mbalimbali ili kuongeza
Vifaa Mashine ya Ram ina uwezo wa ladha na pia husaidia kuleta nguvu
Vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya kusindika kilo 7 za mbegu za ufuta na joto mwilini.
kukamua mafuta ya ufuta ni pamoja kwa ufanisi wa asilimia 57. Aina ya Mbegu za ufuta huchanganywa na
Ram (BP-30) ina uwezo wa kukamua vyakula mbalimbali kama vile mikate,
na mashune ya daraja, sufuria,
lita 20 za mafuta kwa siku. keki, na mboga.
vifungashio, chombo cha kukinga
mafuta, chujio safi, lebo na lakiri. Vifaa Kwa maelezo zaidi unaweza
Aidha, kunahitajika pia kuwepo na Vifaa vya kutumia ni pamoja na ndoo, kuwasiliana na Lucy Mvungi Kwa
mifuko midogo ya nguo au viroba mashine ya Ram, chujio au kitambaa namba 0755 565 621
Toleo la 60, Septemba 2017
Inaendelea kutoka Uk. 2 Ugonjwa wa homa ya mapafu kwa mbuzi
Viuvimbe vidogo vya rangi ya Maabara kuotesha wadudu na • Unapoona dalili za ugonjwa huu
njano huonekana kwenye mapafu na kutambua kwa njia za kikemikali muarifu mtaalamu wa mifugo
matezi yaliyo karibu na mapafu huwa (ELISA na PCR). mapema iwezekanavyo ili tatizo
yamevimba. lipatiwe ufumbuzi.
Kwa mbuzi wanaokaa kwa

Picha: IN
Matibabu
muda mrefu, mapafu yao huwa
Kwa kutumia dawa za antibayotiki
yameshikamana na kuta za mbavu
pamoja na uvimbe kwenye mapafu aina ya tylosin (kwa kuchoma 10mg/
(majipu) wenye kapsuli imara. kg kwa siku tatu mfululizo), imekuwa
ikitumika na inaonekana kufaa katika
Magonjwa yanayofanana na HMM
Sotoka ya mbuzi: (Peste des petits Pafu lililo athiriwa na ugonjwa wa HMM hatua za mwanzo wa ugonjwa.
ruminants, PPR) Ugonjwa huu kondoo Kukinga na kupambana na HMM Ukichelewa mbuzi huonekana
pia hupata sawa na mbuzi kwa usawa. • Kuepuka kuingiza mbuzi wenye kama wamepona lakini huendelea
Pasteurellosis: Ugonjwa huu ugonjwa au toka nchi zenye kusambaza ugonjwa kwa mbuzi
hushambulia mapafu yote wakati ugonjwa. wengine.
HMM hushambulia upande mmoja tu. • Chanjo pia ikitumika kwa Aidha, Oxytetracycline (OTC) katika
MAKEPS: (Mastitis, Arthritis, utaratibu mzuri kuchanja mbuzi dozi ya 15mg kwa kila kg 1 ya uzito
Keratitis, Pneumonia na Septicaemia wote itasaidia kuondoa ugonjwa, wa mbuzi (15mg/kg), Erythromycin
syndrome) huathiri viungo vingine nje baadhi ya nchi zimefanikiwa.
na Streptomycin zinaweza kutumika
ya mapafu. • Kama kuna mlipuko, mbuzi
mapema ugonjwa unapogunduliwa.
Utambuzi wa HMM wazuiwe kutembea hovyo na
kuchangamana na wale wenye Kwa maelezo zaidi, unaweza
Kwa mfugaji, dalili zilizotajwa
hapo juu zitautambulisha ugonjwa wa ugonjwa, kuchinja mbuzi wote kuwasiliana na mtaalamu wa
pamoja na matokeo baada ya kumchinja walio athirika na kumwagia dawa mifugo kutoka SUA Augustino
na jinsi ugonjwa unavyosambaa kwa (Sodium Hypochlorite) sehemu Chengula kwa namba +255 767 605
mbuzi wengine. waliyokuwa wanalala. 098

Inaendelea kutoka Uk. 5 Utunzaji wa vifaranga wa kienyeji


Kutengeneza sehemu ya kuhifadhi • Paa au mfuniko huzungushwa Tabia chache mbaya zinazoweza
joto kwa gunia lenye mkunjo mmoja au kujitokeza kwa kuku wa asili.
• Unganisha vipande hivyo vya miwili na kuweka majani makavu Tabia mbaya au kwa kiingereza
mbao ili kupata umbo la mraba. au maranda kwa madhumuni ya ‘vices’ miongoni mwa kuku wa Asili
• Toboa matundu 4 kila upande wa kuhifadhi joto. mara nyingi siyo jambo linalotokea
juu wa umbo la mraba matundu • Juu ya sehemu ya kuzungukia mara kwa mara. Hata hivyo, kuna
yatakuwa 16. ambamo vifaranga hushinda
baadhi ya tabia mbaya ambazo kuku
• Toboa mlango upande mmoja huweza kufunikwa na wavu au
wa Asili anaweza kuwa nazo. Tabia
ambao vipimo vyake vitategemea vifaa vingine vyovyote vilivyo
rahisi kupatikana, kama vile fito hizi ni pamoja na ulaji wa mayai na
ukubwa wa Bruda. kudonoana. Tatizo kubwa kati ya haya
za mianzi au miti ili mradi viweze
• Tengeneza sehemu ya sakafu
kuwalinda vifaranga dhidi ya matatizo mawili ni ulaji wa mayai.
kwa kutumia mbao nyepesi ili
maadui.
kupunguza gharama.
• Unaweza kutumia wavu (Coffee
Picha: MkM

Wire) ili kuruhusu hewa ya


kutosha kwenye Bruda. Kama
utatumia wavu, inashauriwa
ufunike na karatasi ya nailoni hasa
wakati wa msimu wa mvua.
• Tengeneza sehemu ya kiota kwa
wavu au kwa karatasi ngumu
(Hard Board).
• Unapotumia wavu, zungusha
sehemu ya ndani ya kiota na
kuacha sehemu ya mlango tu.
• Weka majani makavu au maranda
baina ya kuta za mbao na wavu Mchoro unaoonesha banda ambalo mfugaji anaweza kutengeneza kwa ajili ya ufugaji wa
bila kushindilia. kuku wa asili.
Toleo la 60, Septemba 2017

Fahamu wadudu hawa na madhara Mrejesho wa


yake ya kiuchumi kwa mazao wasomaji wa MkM
Hawa ni baadhi ya wadudu ambao Namna ya kumtambua: Ana rangi
huathiri mazao na kusababisha hasara. mbili ambazo ni nyekundu na nyeusi.
Katika Makala hii tutaeleza kwa kudokeza
tu, kisha utaweza kufuatilia kwa undani
zaidi kupitia wataalamu wa kilimo.
Ayubu Nnko
Funza wa vitumba (American
Bollworm)
Uharibifu: Wadudu hawa
hushambulia vitumba na Hutembea haraka haraka, wawili
matunda machanga. Mdudu huyu wawili.
anaposhambulia hutoboa tundu la Kalidea (Blue Bug, Calidea) Gothelf Z. Pallangyo Nashukuru
mviringo.
Uharibifu: Mdudu huyu hushambulia Sana kwa elimu tuliyopata kutokana
matunda kwa kufyonza utomvu, na gezeti la MkM
hivyo kusababisha tunda kunyauka 1. Limewapa wakulima mwanga
na kuharibika kabisa. sana wakawa na kilimo cha
kibiashara na ufugaji bora.
2. Wanakikundi wamesajili
kikundi brela na kujiunga
Namna ya kumtambua: Ana rangi
na asasi, za kifedha ili
nyeusi, kijani au kahawia, na ana
kukopesheka waweze
mstari mweupe pande zote za tumbo.
kuitendea elimu waliyoipata
Funza mwenye Nywele (Spiny kupitia MkM kazi.
Bollworm)
3. Tunaomba elimu hii izidi
Uharibifu: Mdudu huyu hushambulia kuwepo kwani tumepanua
majani na matunda machanga. Hali Namna ya kumtambua: Ni mdudu wigo na tunao wanakikundi
hii hudumaza mmea na kusababisha mkubwa mwenye rangi ya bluu na wengine walioko Kikatiti
hasara kwa kukosa mavuno. nyeusi inayovutia. ambao tumeanza kuwapa
Vidukari-Wadudu Mafuta elimu ya MkM.
(Cotton Aphids) 4. Mpaka sasa tunao wanakikundi
Uharibifu: Hufyonza majani na shina walioanza kufuga kuku,
na husababisha unato (asali) kwenye sungura, ng’ombe na mbuzi ila
majani au shina pamoja na nyuzi za bado ni midogo ikitengemaa
pamba. tutawajulisha mtutembelee.
MWISHO: Tunatoa shukrani zetu
Namna ya kumtambua: Ana nywele
za dhati kwa timu nzima ya MkM,
ndefu (spines) za rangi ya kahawia
Na wote wanaohusika Asanteni.
kwenye mgongo.
gothelfpallangyo@gmail.com
Viwavi wa majani (Spodoptera)
Dominic Nganyagwa kutoka
Uharibifu: Mdudu huyu hushambulia nyanda za juu kusini mkazi wa
majani. Mbeya. Nimekuwa msomaji mzuri
wa majarida yenu yameniniongezea
upana na maarifa juu ya kilimo
Chawa jani (Cotton Jassids) cha kisasa,ufugaji wenye tija na
Uharibifu: Wadudu hawa hufyonza kupambana na magonjwa katika
utomvu sehemu ya chini ya majani mimea. isyesye@hotmail.com
hivyo kusababisha majani kuharibika.
Jinsi ya kumtambua: Ana madoa Jinsi ya kutambua: Ana rangi ya
Timothy Wambura Nimekutana
na gazeti lenu, nimebarikiwa sana
mawili meusi ya pembe tatu, sehemu kijani na hutembea kiubavu juu ya
kwa kazi nzuri mnayofanya.
ya mbele ya mgongo. jani.
Natamani kuwa nalipata.Asanteni
Kangambili (Cotton Stainers) sana. timothywambura@gmail.com
Uharibifu: Mdudu huyu hufyonza
utomvu kwenye matunda na Unaweza kututumia maoni yako na
mbegu ambazo hazijakomaa, hivyo kutupa mrejesho kwa kupitia njia ya
kusababisha rangi kwenye nyuzi za Barua pepe, Ujumbe mfupi wa simu,
pamba. kwa kupiga simu au njia ya posta.

You might also like