Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

MPANGO WA BIASHARA; KILIMO CHA PARACHICHI

MAHITAJI GHARAMA
1. SHAMBA (HEKARI 2) TAYARI LIPO
2. MICHE 200 (HEKARI 2) @5000X200= 1,000,000/-
3. VIBARUA {KWA AJILI YA KUCHIMBA MASHIMO} @2500X200= 500,000/-
4. SAMADI (MAKADIRIO} 350,000/-
5. MADAWA 500,000/-
6. PALIZI 4 @100,000 X HEKA 4 = 400,000/-
7. PAMPU KWA AJILI YA UMWAGILIAJI 300,000/-
8. DHARULA 400,000/-
9. Tenki la maji 450,000/=
JUMLA 3,900,000/-
1. UTANGULIZI
Parachichi ni zao linalooteshwa katika ukanda wa baridi na katika ardhi yenye rotuba na maji ya
kutosha. Njombe, Iringa, Mbeya, Moroogoro, Tanga na Kilimanjaro ni baadhi tu ya mikoa
inayolima Parachichi kwa wingi hapa Tanzania.
Mchanganuo ufuatao ni wa kilimo cha zao hili katika mkoa wa NJOMBE

2. MAHITAJI

3. SOKO
Kwa upande wa soko la parachichi hadi sasa lipo wazi na kuna uhitaji mkubwa wa parachichi na
hii inatokana na kuwepo kwa makampuni mbalimali ya ununuzi wa parachichi kutoka kwa
wakulima yanayofika hadi shambani kwa mkulima.
Kawaida Parachichi huuzwa kwa kupima kilogram. Kwa sasa bei ya parachichi Kg1 kwa soko la
Njombe ni tsh 1500-2000 na kilo moja hubeba wastani wa matunda matatu hadi manne.

4. MATARAJIO YA MAVUNO

Ekari moja yenye miche 100 ya parachichi ikihudumiwa vizur inatarajiwa kutoa matunda
kati ya 300 – 500 kwa msimu wa kwanza. Hapa ni wastani wa matunda 400.

Parachichi kawaida inauzwa kwa kupima kwa kilogram. Kwa sasa bei ya parachichi kg
1 kwa soko la njombe inakadiriwa kuwa 1500 – 2000/- na kg 1 inabeba wastani wa
matunda ya kawaida NNE (4) na kama matunda yamestawi vizuri Basi Tunda tatu
zinafikisha kg 1.

Hivyo Basi wastani wa matunda manne kujaza kg 1 ni sawa na kusema mche mmoja
wa matunda 400 unaweza kuzalisha kg 100 Na kwa kuwa bei ya zao hili inazidi
kupanda; ni dhahiri kwamba kg 1 ya parachichi haiwezi kushuka 1500/- kwa miaka
mitatu ijayo.
Kama bei itabaki kuwa 1500/- kwa kg maana yake kwa mche mmoja kuna tarajiwa
kuwa na kg 100 za parachichi.

1,500/- x 100 = 150,000 mara miche 100 = 15,000,000/- Jumla ya mauzo kwa ekari
moja.

Ili kupata faida kwa ekari moja: 15,000,000 – 8,600,000/- =6,400,000/-

Hivyo faida ya kwanza inatarajiwa kuwa milion sita na laki nne.


————————————————

Zao la Parachichi linaweza kuvunwa kwa takribani miaka 30 mfululizo. Ni miaka mitatu
tu ya mwanzo ndo kuna gharama kubwa za uendeshwaji. Kwa msimu wa pili na
kuendelea faida inatarajiwa kuongezeka kwa sababu mmea utakuwa na uwezo wa
kutoa matunda mengi zaidi ukilinganisha na msimu wa kwanza.

You might also like