Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 20

Jifunzegari

Gari limetengenezwa kwa njia ya mifumo. Mifumo hii


hufanya kazi pamoja kuhakikisha mtumiaji anakidhi mahitaji
yake ya usafiri na pia anakua salama.
Mifumo hii ndo inaliwezesha gari kutembea bila shida na ka-
ma kuna shida kwenye sehemu ya mfumo gari halifanyi kazi
inavyotakiwa na hivyo humtaarufu mtumiaji kupitia sign za
dashboard na mtumiaji akipuuza inawezapelekea kuharibika
kwa mfumo mzima, kisha mfumo mwingine na mwisho wa
siku gari zima. Ndo maana ni muhimu kila mtumiaji kujua ma-
ra tu tatizo linapotokea kuepusha haya.
Kwenye kitabu hiki tutaongelea mfumommoja mmoja na na
utunzaji wake. Tumejitahidi kuiweka katika lugha rahisi am-
bayo kila mtu ataelewa. Lengo la kitabu hiki sio kukufundisha
ufundi bali ni kukusaidia kujua nini kifanyike gari lako lidumu
muda mrefu/milele na ni muda gani uende kwa fundi.

Gari imegawanyika katika sehemu kuu tatu.


1. ENGINE
Hii ni sehemu ya gari inayobadili nguvu ya kikemikali
(mafuta) kuwa nguvu ya kimitambo. ENGINE ndo inalifan
ya gari kwenda mbele au kurudi nyuma. Sehemu hii imeg
awanyika mara tatu ambazo ni Crank case, Cylinder block
na Cylinder head.
2. BODY
Hii ni sehemu ya gari inayotukika kubebea watu au mizigo.
Sehemu hii pia hutengeneza umbo la gari na aina yake.
3. CHASSIS
Hii ni sehemu ya chini inayoshikilia hizi sehemu mbili. Ina
beba body na Engine ya gari.
Jifunzegari

Kuna mifumo mbali mbali ya gari na kila mifumo ina mifu-


mo ndani yake. Kwenye kitabu hiki tutaongelea mifumo
mikuu ambayo ipo kwenye kila gari inayotumia mafuta. Mifu-
mo hii ni.
1. MFUMO WA ULAINISHAJI
2. MFUMO WA UPOZAJI
3. MFUMO WA MAFUTA
4. MFUMO WA BREAK
5. MFUMO WA USUKANI
6. MFUMO WA UPELESHI
7. MFUMO WA UMEME
Tutaangalia mfumo mmoja mmoja na namna ya kuutunza
kwa usalama na namna unavyosaidia gari kuishi muda mrefu.

Huu ni mfumo wenye kazi ya kulainisha sehemu tofauti


tofauti za gari ili kupunguza msuguano, joto na ulikaji wa vyu-
ma. Mfumo huu hutumia vilainishi (Lubricant) ambavyo
huchanganywa na dawa ili vifanye kazi kwa ufanisi Zaidi.
Baadhi ya vilainishi vinavyotumika ni pamoja na:-

1. OIL 2. HYDRAULIC

3. GREACE 4. BREAK FLUID


Jifunzegari

Ni mafuta ya kwenye engine yanayotumika kufanya yafu-


atayo.
a. Inasaidia kulainisha vyombo ili kupunguza msuguano.
b. Hupooza bearing na piston
c. Huongeza mgandamizi kwenye silinda kwa kukaakati kati
ya piston na kuta za cylinder.
d. Husaidia katika gear box kupunguza msuguano gear in-
apokua inazunguka.

AINA ZA OIL KWENYE ENGINE


SAE no. 30-40 ambayo inatumika kwenye engine
SAE no. 90 ambayo inatumika kwenye Gear box
SAE no. 140 ambayo inatumika kwenye Final drive
(Differential)
SAE kwa kirefu ni Society of Automotive Engineering ambayo
ni taasisi ya ubora katika vifaa vya usafirishaji.

Oil ikitumika muda mrefu hupungua ujazo na kiwango cha


ubora kutokana na joto ambalo husababishwa na oxidation
(ukaangaji), uchafu ambao hutoka kwenye mfumo wa grease,
moshi n.k
Hivyo ni muhimu kuibadili au kuijazia kila baada ya muda ka-
ma ifuatavyo.
a. Oil ya kwenye Engine hubadilishwa kila baada ya
kutembea km 3,0000 hadi 10,000 kutegemea na aina au
baada ya miezi mitatu.
b. Oil ya kwenye gear box hubadilishwa kila baada ya
kutembea km 50,0000 kwa gari ya manual na km 100,000
kwa gari ya automatic.
c. Oil ya kwenye Differential hubadilishwa kila baada ya
kutembea km 60,0000.
Jifunzegari

Kwa kawaida gari hubadili oil kufuatana na umbali gari lime-


tembea ila kuna special cases gari litahitaji kubadilishiwa oil
Hata kabla ya muda huo kufika. Zifuatazo ni dalili zitakazo-
kuonesha gari lako linahitaji service ya engine oil.
1. Oil inapomaliza miezi mitatu hadi minne hata kama hu-
jafikia kilometer husika badilisha tu oil.
2. Ukiona alama za check engine na oil level. Hizi alama hu-
onesha oil imepungua sana au engine haina mkandamizo
wakutosha. Oil kuisha inawezasababishwa na uvujaji au
wingi wa joto kwenye engine.
3. Mikwaruzo na kelele kwenye engine: Oil ina kazi ya kuwe-
ka layer kati ya vyuma na vyuma kuzuia msuguano na hivyo
kuzuia kelele. Ukisikia kelele ujue hali ya oil si nzuri.
4. Uchafu na weusi kwenye oil: Oil huwa ina rangi ya dhaha-
bu ila ikichafuka inakua nyeusi. Hali hii hutokea oil inapo-
changanyika na uchafu na vipande vya chuma vinavyotoka
kwenye engine. Hii hali sio salama hivyo unahitaji kubadili
oil haraka sana.
5. Harufu ya oil kwenye gari: Hii inamaanisha oil inavuja
hivyo jitahidi ufanye service unapoona hiyo dalili.
6. Moshi mweusi kwenye exaust: Ukiona moshi mweusi
kwenye exaust kuna hatari oil inavuja au inachanganyika na
mafuta. Kagua oil yako na uibadili.
NB: Ukiona hizi dalili wasiliana na fundi wako aikague engine
Kujua kama kuna tatizo jingine linalopelekea kuharibika kwa
oil kabla ya muda maana bila kutatua hilo..tatizo litajirudia.
Pia hakikisha unapima oil walau mara mbili kwa week.
1. Ni aina gani ya oil inatumika kwenye gari langu?
Kuna aina tofauti tofauti za oil ambazo zimegawanyika kufu-
atana na ubora na muda wa kubadili. Ni muhimu kujua ni ipi
unataka na brand gani ni bora kwa gari lako. Huwa tunashauri
upate synthetic oil ya kampuni ya Gastrol na Total ila ni bora
kupata ushauri wa fundi wako au kama gari limekuja na
recomndation tumia hiyo.

2. Ni oil kiasi gani inaingia kwenye engine yako?


Engine ya gari huchukua lita 3 hadi 7 na kama imeishiwa
kabisa hadi lita 12. ni muhimu kufahamu ni kiasi gani cha oil
kinaingia kwenye gari lako, oil ikizidi inawezaleta shida.
3. Huduma gani inaenda na service ya oil?
Huduma hii inaendana na kubadili oil filter na kusafidha au
kubadili air filter. Wengine hukagua matairi, betri na coolant.

4. Kwa nini ni muhimu kunadili oil yote badala ya kuongezea?


Ukichanganya oil mpya na ya zamani unaiongezea stress oil
yako kitu kinachoiongezea stress engine na hivyo kutofanya
kazi vizuri. Ukiongeza iwe ni kwa dharula ila jiandae kuibadili.
5. Nawezabadili brand ya oil wakati wa service?
Ndio, unawezabadili brand ila iwe ni grade na kiwango
kinachotakiwa na engine yako na kilichoelekezwa kwenye
manual book.
6. Oil filter ina kazi gani na kwa nini ni muhimu kubadili?
Ili oil ifanye kazi yake vizuri inabidi iwe safi. Na kazi ya oil fil-
ter ni kuchuja uchafu unaokuwa ndani ya oil. Baada ya muda
hizi filter zinachafuka na hivyo kushindwa kuchuja oil na hyo
ndo sababu inabidi ibadilishwe mara kwa mara.
Hiki ni kilainishi kwenye gari kinachotumika kwenye gearbox
ya gari za automatic (transmission) na kwenye mfumo wa
usukani. Kilainishi hiki kina uwezo wa kubanwa kwenye
vipande vya Dipc plate za gearbox ya automatic na kutoa
nguvu ya mgandamizo ili gari iingie kwenye gear.

Hydraulic haitakiwi kuchafuka wala kupungua na inabidi


ibadilishwe kila miaka minne. Gari iwe imetumika au haija-
tumika.

Ni mafuta mazito yanayotumika sehemu mbali mbali za gari


sana sana sehemu ya joint na vioo. Inakaa kati kati ya vyuma
Kuzuia uishiliaji wa vyuma.

Ni mafuta maalumu ya kulainisha upatikanaji break na na ku-


rainisha uingizaji gia kupitia clutch.

Hii haiishi kirahisi kwa hiyo unashauriwa kuikagua kila


ukienda kubadili oil kisha fundi wako atakushauri ni muda ga-
ni utafaa kuibadili.
MUHIMU
Mfumo wa ulainishi ndo mfumo muhimu Zaidi, sana sana upande wa engine oil.
Hakikisha unaibadili wa wakati na unapima oil walau mara tatu kwa week.
Mfumo huu una kazi ya kubalance joto kwenye engine. Joto
halitakiwi kuzidi au kupungua kiwango kinachotakiwa.
VIFAA VINAVYOUNDA MFUMO HUU.
Rejeta: Huifadhi maji (COOLANT) ambayo hutumika kupoza
engine pia hupoza maji hayo yakitoka kupoza engine.
Pump: Hupandisha maji kwenye ngine na kuyatoa.
Feni: Hufungwa nyuma ya rejeta kupoza maji.
Mpira wa maji. Kuhamisha maji toka rejeta kwenda kwenye
engine na kurudi.
Thermostat: Hufungwa kwenye mpira kati ya rejeta na
engine. Kazi yake ni kuzuia maji yasiingie kwenye rejeta hadi
engine ipoe kabisa.
Mfuniko wa rejeta: Huzuia maji ya kwenye rejeta yasim-
wamgike hovyo wakati wa kuendesha.
Temperature gauge: Hiki ni kipimajoto. Kinatuma majibu
kwenye dashboard.

a. Hakikisha rejeta ina maji/coolant ya kutosha


b. Weka mfuniko sahihi wa rejeta na hakikisha umefungwa
vizuri.
c. Hakikisha rejeta haivuji na ikivuja usiweke vitu ndani
itaziba matundu, izibe tu vizuri na mipira ya maji ifungwe
vizuri.
d. Mkanda wa feni ukaguliwe mara kwa mara na ubadilish
we ukichoka tu.
Engine kuchemka hutokana na sababu tofauti ila kubwa ni
kutopozwa, ikichemka ikaonesha kwenye dash board.
Simamisha gari sehemu salama. Fungua boneti ya gari. Kagua
mkanda wa feni, kiwango cha oil na kiwango cha maji. Kama
huoni shida jikokote taratibu uende kwa fundi au kama una-
weza kumuita faya hvyo.

Tahadhari: Usifungue mfuniko wa rejeta gari likiwa la moto.


Zima gari iache engine kwanza ipoe.

Ni mfumo wa kusafirisha mafuta kutoka kwenye tank kwenda


kwene engine. Kuna njia mbili za usafirishaji mafuta:
a. Grant feed system:- Hapa tank la mafuta linafungwa juu
na mafuta yanasafirishwa kupitia njia maalumu.
b. Pressure feed system: hapa inafungwa pump ya kusukuma
mafuta.
VIFAA VYA KWENYE MFUMO WA MAFUTA

a. Tank la mafuta
b. Mirija ya mafuta
c. Chujio la mafuta
d. Pump ya mafuta
e. Carburettor /Injector pump
a. Hakikisha unajua aina ya mafuta gari lako linatumia kama
ni diesel au petrol na ujue tank lako linabeba mafuta kiasi
gani.
b. Zima gari lako unapokuwa unaweka mafuta kwenye kituo.
c. Jitahidi kujaza mafuta kwenye kituo kimoja ili ikitokea
umejaza mafuta machafu ujue tatizo liko wapi na epuka
mafuta ya kununua tu mitaani au vibaba.
d. Usitembelee mafuta ya ziada (kijagi) na usiache gari lako
liishiwe mafuta kabisa.
e. Kama kuna shida yoyote irekebishe mapema, fanya
matengenezo kwa wakati na tunza kumbukumbu za ujazaji
mafuta.

Huu ni mfumo unaokumruhusu dereva kupunguza mwendo


au kusimama. Mfumo wa break unaweza kuwa toauti kati ya
maisha na kifo, hivyo ni muhimu sana kwenye gari na inabidi
uwe unafanya kazi vizuri muda wote.
Kuna aina tatu za brake, Drum brake, Disk brake na mchang-
anyiko wa zote.
Brake hutumia nguvu za mafuta (break fluid) kusimamisha
gari. Mafuta haya husafiri kutoka katika mtungi wa mafuta,
kutokana na msukumo wa piston ndani ya break mastercylin-
der. Unapokanyaga pedeli ya brake, mafuta hutembea katika
miguu yote ya gari na kuleta msukumo katika lining ya break
na disk break na hivyo drum ama sahani ya chuma ambavyo
vyote huzunguka na tairi hubanwa kulifanya tairi lipunguze
mwendo.
Break hazidumu milele katika gari hivyo ni vyema kujua dalili
zinapoisha.
a. Kuongezeka kwa kiasi cha ukanyagaji break.
b. Kuwepo kwa kelele kwenye matairi unposimamisha gari
c. Baadhi ya matairi kupungua mwendo mengine yana-
zunguka
d. Gari kwenda upande unaposhika break.

a. Fanya ukaguzi mara kwa mara ili ugundue mapungufu


mapema.
b. Hakikisha mafuta ya break yapo muda wote.
c. Hakikisha unaweka mafuta masafi ili kuepuka tatizo la
break
d. Hakikisha gari lako halivuji sehemu yeyote.
e. Badili lining na disc kila baada ya km 100,000

Ni mfumo wa kusafirisha nguvu ya engine kwenda kwenye


matairi.
MFUMO HUU UMEGAWANYIKA SEHEMU MBILI
a. Manual transmission system: hii inamtegemea dereva
kuchagua gia ya mzunguko ili gari liweze kutembea au ku-
badili speed.
b. Automatic transmission: gari halimtegemei dereva kupan-
ga gia kwa sababu zinajipanga zenyewe automatic.
Mfumo upo katika sehemu mbili upeleshi wa tairi mbili
(2WD) na upeleshi wa tairi nne (4WD)
Jifunzegari

Huu ni mfumo wenye kazi ya kuzalisha umeme, kuutunza na


kuupeleka sehemu zote ambako unahitajika kwa muda
muafaka na kwa muda wote. Chanzo cha umeme katika gari
ni betri ambalo huchajiwa, hutunza umeme na kuusambaza
sehemu zote za gari.
Mfumo huu umegawanyika katika mifumo midogo midogo
ambapo na kila mfumo una kazi maalumu. Hii sehemu tuta-
ongelea sehemu moja moja na utunzaji wake.

Huu ni mfumo uwashaji gari. Gari linahitaji umeme ambao


unatolewa kwenye betri mara tu (muendeshaji anapozun-
gusha ufunguo au kupush start) kuelekea kwenye starter
motor ambayo inazungusha engine na hapo gari linawaka.
UTUNZAJI WA MFUMO HUU
a. Usishikilie ufunguo kwa nguvu unapowasha gari.
b. Usiwashe gari kwa muda mrefu..likikataa subiri sekunde
10 alafu jaribu tena.
c. Gari likiwaka achia ufunguo mara moja ili usifanye uharibi-
fu kwenye self starter.
d. Kama gari limekataa kuwawaka na mwanga kwenye dash-
board unafifia huna budi kutafuta betri.
e. Kama gari betri iko sawa na ina mafuta yakutosha lakini
linasumbua kuwaka angalia self starter au tafuta watu wa-
kusukume ili wakubust ulistue likiwa kwenye mwendo.
Jifunzegari

Ignition System (Uchomaji): huu ni mfumo wa uchomaji ma-


futa hasa kwenye gari za petrol. Unatoa umeme kwenye betri
na kuukuza kutoka V+12 mpaka 1500-3000 (DC) na kuugawa
umeme huo katika cylinder na engine.
Umeme huu hutumika kuwasha mchanganyiko wa mafuta na
hewa katika chumba cha muwako. (Combustion chamber)

Huu ni mfumo wa kuzalisha umeme mwingine wa kuhifadhi


kwenye betri. Kazi yake ni kuchaji betri ambapo hufanyika
gari likiwa limewaka.
Betri ni muhimu kuwa na chaji muda wote ila hutokea kuto-
kana na ubovu wa betri au matumizi mabaya ya umeme, be-
tri zinaisha umeme hivyo kumlazimu mtumiaji kutumia betri
jingine kuwashia gari (kuboost):
MAMBO YANAYOWEZA KUPELEKEA BETRI LAKO
KUISHIWA MOTO/KUTOFANYA KAZI
a. Kuacha taa za mbele zinawaka, hii hutokea sana wakati wa
mchana ambapo mtu haoni mwanga hivyo cheki mara mbili
kabla hujazima gari kama taa zinawaka au iset kwenye auto.
b. Uwashaji wa vitu vya ziada, Unapozima gari betri huwa
linaendelea kutumika kwenye maeneo kama funguo, alarm,
sensor N.K na altenator haiwezi kulichaji. Hivyo likikaa siku
nyingi betri itaisha.
c. Kuloose kwa nyaya za betri: kama tunavyojua betri
limeunganishwa na nyaya ambazo husambaza umeme na
kuchaji betri. Hizi nyaya zikilegea betri halifanyi kazi.
Jifunzegari
D. Joto aubaridi kali: Joto na baridi kali vinaharibu betri hasa
kwa betri zilizotumika sana.

E. Betri likiwa halichajiwi wakati wa kuendesha: Kama


tulivyojadili mwanzo kwamba altenator inachaji betri gari liki-
wa linawaka. Sasa ikitokea imepata shida betri halitochajiwa
na hivyo betri itakufa.
F. Uzee wa betri: Betri linavyotumika ndivyo linavyoisha
nguvu.Betri likiwa zee linakua halikai na moto mda mrefu
hivyo kupelekea betri kuzima hata ukiacha vitaa vinawaka
muda mfupi.

MAMBO YAKUZINGATIA UNAPOBOOST GARI BETRI


IKIWA HAINA MOTO
a. Betri zote unashauriwa ziwe na nguvu moja.
b. Jump cable ziwe nzima na zisiwe zinaachia achia.
c. Kuwa makini usichanganye sehemu ya negative na
positive.
d. Uwe makini nyaya zisigusane wakati wa kuunga na baada
ya kuwasha gari toa nyaya haraka.
e. Jitahidi magari yasigusane na inapendeza Zaidi kama uta
weza toa betri kwenye gari moja ukalitumiakuwashia
jingine.

NB: Hakikisha unatembea na vifaa kama jump cable, gloves,


Toach na vingine vitakavyokusaidia ikitokea gari
limekuzimikia
Jifunzegari

Huu ni mfumo wa umeme unaotumia kuwasha taa za mbele,


indicator, taa za break, taa za kurudi nyuma, taa za msaada
(Hazard), taa za ndani ya gari na dashboard.

Mfumo huu husaidia kuendesha shughuli za ziada ambazo


hazina uhusiano wa moja kwa moja na uendeshaji gari ila
bado ni muhimu sana.
Kwenye huu mfumo umeme hutumika kwenye speed meter,
ODO meter, fuel gauge, temperature gauge, tacho meter, trip
meter na trip meter reset button.
Hizi ni alama znazokupa taarifa juu ya kinachoendelea
kwenye mifumo yako, zinatoa onyo na taarifa mbali mbali.

1. Taa za mbele zinawaka. 2.Power steering ina shida


3. Taa za nyuma zinawaka 4. Maji ya kioo yamepungua
5. Break pad zina shida 6. Cruise control imewashwa
7. Ishara za muelekeo 8. Sensor za mvua na mwanga
9. Mfumo wa mabarafu 10 Alama ya taarifa
11 Diesel haijachomwa 12 Onyo la uwepo wa mabarafu
13 Tatizo la ignition switch 14 Ufunguo haupo kwenye gari
15 Betri ya ufunguo iko chini 16 Umekaribia sana gari jingine
17 Kanyaga clutch 18 Kanyaga break
19 Onyo ya usukani kujifunga 20 Umewasha mwanga mkali
21 Upepo wa tairi uko chini 22 Taarifa za mfumo
Jifunzegari

23 Kuna taa haifanyi kazi 24 Brake ina shida


25 Filter ya Diesel ina shida
26 Sehemu ya kuunga tera ina shida
27 Air suspension ina shida 28 Onyo la kuacha msitari wako
29 Kifaa cha kuchuja moshi kina shida
30 Hujafunga mkanda
31 Gari lipo kwenya Parking 32 Betri/Altenator ina shida
33 Mfumo wa kusaidia kupaki 34 Unahitaji kufanya service
35 Mwanga unajibadili kutegemea mazingira
36 Mwanga utaangalia chini ukiwa unateremka na utajiad
just tena ukirudi tambalale.
37 Tatizo kwenye Air spoiler
38 Tatizo kwenye paa la kujifungua
39 Onyo la airbag 40 Umeweka handbreak
41 Maji kwenye filter 42 Airbag hazifanyi kazi
43 Kifaa hakifanyi kazi vizuri
44 Mwanga mkali usiosumbua waendeshaji wengine
45 Air Filter chafu 46 Mfumo wa ECO
47 Mfumo wa kusaidia kushikilia gari ukiwa unashuka mlima
48 Joto kali kwenye engine 49 ABS ina shida
50 Filter ya mafuta ina shida 51 Milango imefunguliwa
52 Bonnet limefunguliwa 53 Mafuta yapo kidogo
54 Gearbox kenye gari la automatic ina shida
55 Speed limiter 56 Suspension dampers
57 Oil imepungua sana 58 Wind screen defrost
59 Buti limefunguliwa 60 Stability control imezimwa
61 Sensor ya mvua 62 Engine ina shida
63 Mfumo wa kuondoa ukungu kwenye kioo
64 Mfumo wa kusafisha vioo automatic
Jifunzegari

DALILI TATIZO
1 Gari kunuka harufu ya mafuta. -Tank la mafuta linavuja
-Injection ya mafuta, mpira
Au filter inavuja

2 Usukani kuwa mgumu, kukataa --Mkanda wa usukani


umeisha.
kuzunguka unaposimama.
3 Gari kubadili muungurumo, Engine -Air filter imezidi uchafu
-Gari aina masega
Kuishiwa nguvu na kuongeza ulaji
Mafuta.
4 Gari kutetemeka linapofikia speed -Matairi halingani/
hayabance.
ya kati ya 50km/h hadi 60km/h
5 Gari kutoa moshi mweupe -Head gasket imeharibika
-Cylinder head imeharibika
-Ukuta wa engine una kreki

6 Gari kukataa kuwaka, dashboard -Betri limekufa

Haioneshi kitu na taa zinafifia.


7 Mafuta kuacha kupanda kwenye -Oil pump ina shida au pipe
Imeachia.
Engine, mafuta kumwagika.
Jifunzegari

Dalili ni nyingi sana na kuna muda mwingine dalili moja in-


amaanisha kitu kingine, kwa dalili nyingine soma post zetu
hasa kwenye sehemu ya maswali na majibu. Ila kwa kumal-
izia tuone ni vitu gani au ni utaratibu gani mtu afanye ili aishi
na gari lake milele.
MAMBO YA KUFANYA ILI GARI LAKO LIISHI MILELE.
1. Fuata kanuni za service: Kwa sasa hivi utakua ushajua kila
aina ya service gari linahitaji na muda muafaka wa kuzifan-
ya, sasa hakikisha gari lako linafanyiwa hizo service kwa
wakati.
2. Tumia oil zenye ubora: Hii ni muhimu sana hasa kwa watu
wenye mizunguko mingi na safari za mbali, hakikisha una-
pata oil yenye ubora na mileage kubwa. Itakusaidia kutun-
za gari lako muda mrefu Zaidi.
3. Fanya ukaguzi walau mara moja kila miezi minne: Un-
apoenda kufanya service jitahidi walau mara moja kila
miezi minne unakagua mifumo yako ya gari kama betri,
AC, Mfumo wa upozaji, break N.K. itakusaidia kuyaona
matatizo kabla hayajawa makubwa yakakugharimu Zaidi.
Ukaguzi huu ni TSH 20,000 hadi 40,000/=
4. Safisha gari lako: Hii ni muhimu..hakikisha gari lako ni safi
kote nje, ndani na engine muda wote. Hii itapunguza
vumbi kuingia na kukwama kwenye mifumo na pia kuwa
na hewa safi ndani ya gari ni muhimu kwa afya yako.
5. Punguza kuazimisha watu hasa ambao hawana record
nzuri barabarani, watumia vilevi na wasiojali. Wa-
takuchukia kwa muda ila wataelewa tu.
6. Simamia mafundi wakati wote: Usiache gari lako na fundi
peke yake hasa garage zenye wanafunzi. Fundi wako ana-
weza awe muaminifu ila akamuachia mwinginw hiyo kazi.
Kama uko busy subiri au tuma mtu unaemuamini.
Jifunzegari

Kwanza tunashukuru kwa kuchukua muda kusoma kitabu


hiki, ni furaha kuona umeona umuhimu na umechukua hatua
ya kwanza kwenye utunzaji gari. Najua utakua unahisi kuso-
ma kitabu hiki inatosha lakini ukweli ni kwamba elimu ni
hatua moja tu. Hatua ya pili ni wewe kuchukua hatua.
Jitahidi kuliangalia na kulitunza vyema gari lako na lenyewe
litakutunza kila utakapolihitaji. Kumbuka gari linaweza kuwa
furaha kwako au stress na utunzaji wake ndo kitu kina-
tofautisha haya mawili.
Jifunze gari ipo muda wote na siku zote kuhakikisha unapata
msaada wa elimu unaohitaji ili kukupa experience iliobora ya
gari lako.
Tunatanguliza shukrani kwa kutuamini na kutusikiliza,
Wako
Jifunze gari.

You might also like