Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 1

SWAHILI PRESS RELEASE: MHE.

MAKAMBA NA CEOrt KUJADILI USHIRIKI WA SEKTA


BINAFSI NDANI YA TASNIA YA NISHATI

Dar es Salaam 18 Agosti 2022: Kulingana na kuongezeka kwa mikakati ya maendeleo ya


sekta ya nishati nchini Tanzania, leo jioni CEO Roundtable - Tanzania (CEOrt) inawakutanisha
viongozi wafanyabiashara kwa ajili ya majadiliano kuhusu “Kuendesha Ushiriki wa Sekta Binafsi
kwenye Sekta ya Nishati”.

Taarifa za hivi karibuni katika sekta ya nishati nchini ni pamoja na mipango kuhusu bomba la
EACOP, maendeleo ya mitambo ya gesi ng’ambo, makubaliano katika mradi wa gesi asilia
iliyosindikwa (LNG) na mapendekezo kadhaa ya mradi wa nishati mbadala. Katika wakati
ambapo mabadiliko ndani ya sekta ya nishati yanaendelea duniani, washikadau wanatilia
maanani matokeo yake kwa fursa zinazoibuka barani na pia maamuzi ya uwekezaji
yanayopaswa kufanywa. Awamu inayofuata katika sekta ya nishati nchini Tanzania inatarajiwa
kujikita katika kukuza uwekezaji na ukuaji, hivyo basi kuwafanya viongozi wa sekta binafsi kuwa
kipengele muhimu kwa kutegemea michango yao ya kimkakati na ushiriki wao katika kufungua
fursa chipukizi nchini.

CEOrt ina heshima kubwa kumkaribisha Mhe. January Makamba, Waziri wa Nishati wa
Tanzania, akiwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo. Mhe. Makamba amesisitiza azma ya Serikali ya
kuweka uwiano wa maendeleo ya nishati vijijini na mijini, na kutaja vipaumbele kuwa ni pamoja
na kuboresha ufanisi wa nishati sambamba na kuongeza utegemezi wa sekta hiyo, na kuhimiza
ushiriki wa sekta binafsi ya ndani katika mnyororo wa thamani wa nishati mbalimbali nchini.
Madhumuni mengine muhimu ya sekta hii ni kupunguza ukataji miti, lengo ambalo CEOrt
inakusudia kusaidia kulifanikisha kwa vile linaendana na msimamo wa jukwaa hilo wa kuchukua
hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Ikiwa imedhamiria kuboresha ushirikiano na Serikali, CEOrt inatazamia kuwezesha


mazungumzo haya kati ya Waziri wa Nishati na viongozi wa sekta binafsi ili kuchunguza zaidi
jukumu la Nishati katika kuleta maendeleo endelevu na mafanikio ya nchi.

Kuhusu CEO Roundtable - Tanzania


Shirika linawakilisha Wakurugenzi Wakuu kutoka kampuni zaidi ya 160 zinazoongoza nchini
Tanzania kutoka sekta mbalimbali za uchumi kwa madhumuni ya pamoja ya kuongeza matokeo
katika uongozi na ustawi endelevu wa jamii na uchumi wa nchi. Kwa pamoja, wanachama wa
CEOrt huchangia katika uchumi wa Tanzania kupitia ukusanyaji wa kodi, ajira, kujenga uwezo,
kuhamisha teknolojia na kuongeza ujuzi.

You might also like