Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 3

KATIBA

UMOJA WA TUNAJALIANA
1. JINA LA KIKUNDI
Jina la kikundi ni TUNAJALIANA.

2. UANACHAMA
Kila familia itatambulika kama mwanachama mmoja.

3. MADHUMUNI YA KIKUNDI
I. Kusaidiana katika SHIDA na RAHA;
II. Kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi za kikundi (kuinua uchumi wa wanachama
kama kikundi).

4. SIFA ZA MWANACHAMA
I. Kulipa Ada ya uanachama kama ilivyoainishwa, pamoja na michango mingine ya kila
mwaka kama itakavyo ainishwa kwenye KANUNI;
II. Ada hiyo inapaswa kulipwa mara moja baada ya anapojiunga na chama;
III. Aidha mwanachama MPYA anapaswa kulipa ongezeko la thamani ya mwanachama
kwa mujibu wa KANUNI za chama;
IV. Mwanachama kufanya Majeresho ya michango iliyotolewa na Chama kwa niaba
yake ndani ya Mwezi (1) Mmoja;
V. Mwanachama anapaswa kuhudhuria kila kikao kinachoitishwa. Asipohudhuria vikao
(3) vitatu mfululizo, anapoteza uanachama wake na haki zake zote, isipokuwa kama
ana sababu za msingi kama:- Kuwa nje ya mji, kuugua/kuuguza, kufiwa;
VI. Mwanachama anapaswa kutoa taarifa rasmi ya kutokuhudhuria kikao chochote kwa
njia sahihi;
VII. Mwanachama anapaswa kuhudhuria shughuli zinazohusu chama au za
mwanachama mwenzake;
VIII. Mwanachama anapaswa kutii KATIBA na KANUNI za chama.

5. KUJITOA UANACHAMA
Endapo Mwanachama ataamua kujitoa kwenye chama, atapoteza haki zake zote.

6. SHUGHULI ZA KIUCHUMI
I. Kukopeshana kwa riba ya ASILIMIA 10 (sio zaidi ya miezi mitatu na sio zaidi ya
KIWANGO kitakachowekwa na CHAMA kwa mujibu wa KANUNI ndogo ndogo za
CHAMA) kwa mwanachama mmoja;
II. Aidha kutakuwa na shughuli nyingine za kiuchumi zitakazoamuliwa na CHAMA kwa
mujibu wa VIKAO halali.

7. KUSAIDIANA WAKATI WA SHIDA


I. Mwanachama akipoteza maisha Chama kitatoa kiasi cha fedha kwa mujibu wa
KANUNI halali za CHAMA kwa familia;
II. Tegemezi wa mwanachama akipoteza maisha Chama kitatoa kiasi cha fedha kwa
mujibu wa KANUNI halali za CHAMA kwa mwanachama;
III. Mwanachama akilazwa zaidi ya siku (3) tatu anapatiwa kiasi fulani cha fedha kwa
mujibu wa kanuni halali za Chama kama sehemu ya kumfariji;

1
IV. Tegemezi wa mwanachama akilazwa zaidi ya siku (3) tatu anapatiwa kiasi fulani cha
fedha kwa mujibu wa kanuni halali za Chama kama sehemu ya kumfariji;
V. Ni LAZIMA kwa kila mwanachama kushiriki tukio la SHIDA la mwanachama au
wategemezi wake.

8. RAHA
I. Mwanachama AKIOA/OLEWA anapatiwa na Chama kiasi cha fedha kwa mujibu wa
KANUNI halali za CHAMA kama sehemu ya ZAWADI;
II. Tegemezi wa mwanachama AKIOA/OLEWA anapatiwa na Chama kiasi cha fedha kwa
mujibu wa KANUNI halali za CHAMA kama sehemu ya ZAWADI;
III. Mwanachama AKIOA/OLEWA atachangiwa kiasi fulani cha fedha toka kwa kila
Mwanachama kwa mujibu wa KANUNI halali za CHAMA ili kufanikisha ndoa/harusi
hiyo.
IV. Tegemezi wa mwanachama AKIOA/OLEWA atachangiwa kiasi fulani cha fedha toka
kwa kila Mwanachama kwa mujibu wa KANUNI halali za CHAMA ili kufanikisha
ndoa/harusi hiyo;
V. Shughuli nyingine zinazohusu wanachama/wategemezi kwa mfano:- Kipaimara,
Maulid, Komunio, Kujifungua ambapo kila Mwanachama atapaswa kuchangia kiasi
fulani cha fedha kwa mujibu wa KANUNI halali za CHAMA;
VI. Ni LAZIMA kwa kila mwanachama kushiriki tukio la RAHA la mwanachama au
wategemezi wake;
VII. Ni wajibu kwa kila Mwanachama kutoa taarifa ya shughuli yake walau wiki moja
kabla kama angependa wanachama wenzake washiriki.

9. WATEGEMEZI
Kwa mujibu wa KATIBA hii na katika Umoja huu wategemezi wanaotambulika rasmi ni hawa
wafuatao:-
I. Mtoto, Baba/Mama Mzazi, Baba/Mama mkwe;
II. Msichana/mvulana wa Kazi;
III. Au mtoto yeyote anayeishi nyumbani kwa mmoja wa Mwanachama.

10. MAWASILIANO
Mwanachama anawajibika kutoa TAARIFA ya TUKIO lolote liwe la SHIDA ama RAHA kupitia njia
rasmi za mawasiliano.

11. MICHANGO NA UREJESHAJI WA FEDHA ZA KIKUNDI


I. Kutakuwa na Ada ya kiingilio kwa kila mwanachama kwa kiwango kitakachoamuliwa
na CHAMA kama sehemu ya KANUNI;
II. Mwanachama anapaswa ndani ya miezi (3) mitatu kukamilisha mchango wake wa
LAZIMA;
III. Kila linapotokea TUKIO liwe la SHIDA ama RAHA pesa itatolewa mara MOJA kwenye
KIKUNDI halafu ITARUDISHWA na wanachama si zaidi ya mwezi MMOJA baada ya
TUKIO kutokea;
IV. Mwanachama atafaidika na mafao yaliyotajwa hapo juu endapo tu atakuwa
amekamilisha Ada yake ya uanachama.

12. FAIDA MWISHO WA MWAKA


I. Kila mwisho wa mwaka kila mwanachama atapewa faida ya mfuko wa chama
(kutokana na faida za riba na shughuli zingine za kiuchumi);
II. Aidha pesa ya msingi (ukiondoa faida) itabaki kwenye chama.

2
13. WANACHAMA WAPYA
I. Kila mwanachama MPYA atapaswa kulipa kiingilio kwa mujubu wa KANUNI halali za
CHAMA;
II. Mwanachama Mpya pia atapaswa kulipa nyongeza ya thamani ya Mwanachama
mmoja katika Chama kwa wakati huo.
-
14. MUUNDO WA UONGOZI
I. Kutakuwa viongozi wafuatao katika CHAMA kama ifuatavyo:
 Mwenyekiti
 Makamu Mwenyekiti
 Katibu
 Mweka Hazina
 Mwabarishaji

II. Aidha viongozi hao watakuwa sehemu ya sekretariet ya CHAMA na watawajibika


kuwasilisha jambo au suala lolote kwenye mikutano ya CHAMA ya kila mwezi au
ya dharura;
III. Vikao na mikutano yote vya CHAMA itaongozwa na MWENYEKITI. Kama
MWENYEKITI hayupo MAKAMU MWENYEKITI ataongoza kwa niaba ya
MWENYEKITI.

15. MUDA WA UONGOZI MADARAKANI


I. Viongozi wa CHAMA watakaa katika uongozi kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu (3);
II. Aidha kila baada ya miaka mitatu (3) kutakuwa na uchaguzi wa VIONGOZI wapya.

16. MKUTANO WA WANACHAMA WOTE


I. Kutakuwa na Mkutano wa Wanachama wote mara moja kwa Mwezi, Mkutano huo
utafanyika kila Wiki ya Mwisho wa Mwezi;
II. Mkutano Mkuu wa Uchaguzi kila baada ya miaka mitatu (3);
III. Kwenye uchaguzi kila mtu ni kura moja (1), ingawaje familia ni watu wawili (2);
IV. Mkutano wa dharura unaweza kuitishwa wakati wowote kama kuna jambo la
dharura linalohusu Umoja limetokea.

You might also like