Professional Documents
Culture Documents
UCHAMBUZI WA KITABU "The 21 Irrefutable Laws of Leadership-JOHN MAXWELL
UCHAMBUZI WA KITABU "The 21 Irrefutable Laws of Leadership-JOHN MAXWELL
UCHAMBUZI WA KITABU "The 21 Irrefutable Laws of Leadership-JOHN MAXWELL
Kuna watu wanafikiri kuwa kiongozi mpaka upate nafasi fulani mahali fulani, ndio
ukipata nafasi fulani mahali Fulani ni nafasi ya kuonyesha una uwezo kiasi gani
kama kiongozi kadiri ya kukubalika kwako na mambo utakayofanikisha katika huo
uongozi wako. Lakini unaweza kuanza kuwa kiongozi hapo hapo ulipo kwanza
kwa kujiongoza mwenyewe vyema na kujisimamia katika mambo ambayo
umeshajiahidi utafanya. Lakini pia kama unazungumza na watu wanakusikiliza na
kukuamini na kukukubali na kufuata/kufanyia kazi mambo unayowaambia na
kuhitaji muongozo wako tena na tena basi wewe unaanza kuonyesha dalili nzuri
kwamba wewe ni kiongozi kwa watu hao, sasa kadiri utaendelea kusaidia na
kukubalika zaidi na kadiri utaendelea kukubalika na wengi zaidi na ukawa gumzo
zaidi kwa watu wengi wanaozikubali juhudi zako au mawazo yako basi wewe ni
kiongozi kwao, iwe ni kazini kwako, iwe ni shuleni kwako, iwe ni nyumbani,
kanisani, mtaani au hata hapa hapa facebook, utapendwa utaheshimiwa na
kuaminiwa na kadiri unavyowagusa au kuweza kuwashiwishi wengi ndivyo hata
unaweza kuwashawishi wafanya kitu fulani au wafautilia jambo fulani au
wenyewe kwa hiari yao wanaweza kufanya hivyo na ambavyo kwalo wewe
unaweza kunufaika na kupata mafanikio makubwa na wao pia wakafanikiwa.
Sasa twende pamoja tuzichambue kanuni hizi 21 zisizopingika za Uongozi,
ambazo mwandishi Dr. John C. Maxwell ametumia miaka mingi sana kujifunza,
kufundisha na baadaye kutuandikia kitabu hiki bora sana na kilichouzika kwa
mamilioni ya nakala duniani kote. Kupitia uchambuzi huu na wewe upate kujipima
na kuwapima wale wote waliopewa nafasi mbalimbali za Uongozi kama
wanaendana na kanuni hizi au wanazivunja na matokeo yake wanaweza kuanguka
au kushindwa kuendelea kuongoza kutokana na kuvunja kanuni hizi zisizopingika.
-Sasa kwa mtu mwenye uwezo mkubwa wa uongozi ataweza kutanuka zaidi akawa
na mbinu bora na za uhakika za kuweza kufungua matawi na kuzidi kutanuka
kidogo kidogo huku akiendelea kutoa huduma yenye ubora ule ule kama ule
mgahawa wa mwanzo na kuzidi kukua mpaka kuenea mji mzima, kisha nchi nzima
mpaka nchi jirani na dunia kwa ujumla, yote hii inatokana na uwezo mkubwa wa
kuongoza watu wengi na kutengeneza namna ambazo wataendelea kukua zaidi na
zaidi kwa ubora huo huo.
-Kwa hiyo kadiri uwezo wako wa kiuongozi unavyozidi kuwa mkubwa ndivyo
kadiri unavyoweza kufanikisha mambo makubwa katika kile unachokiongoza
lakini kadiri uwezo wako wa kiuongozi unavyokuwa finyu ndivyo kadiri
utakavyokosa ushawishi na kuwa na mafanikio kiduchu sana na kushindwa kutatua
changamoto nyingi unazokutana nazo katika uongozi wako.
6. Sheria/Kanuni Ya Iliyojichimbia Chini Kabisa Ardhini. (The Law of The Solid Ground)
“Imani Kwa Kiongozi Ndio Msingi Wa Uongozi”
-Linapokuja suala la uongozi, huwezi tu kupita njia za mkato kupelekesha watu, ni
lazima upitie mchakato mzima wa kuwaelewesha lengo na umuhimu wa kila
utakachofanya, tofauti na hapo watakosa imani na wewe, kukubeza na mwisho
kukupuza na kukataa kukusikiliza. Kujenga imani kiongozi lazima aonyeshe
mfano kwa kuwa mahiri, kujenga mahusiano na mwenye sifa njema. Ni vigumu
kwa kiongozi kufika mbali zaidi ya zile tabia au hulka zake.
-Ni kwa namna gani viongozi huheshimika? Ni kwa kufanya maamuzi sahihi,
kukubali makosa na kuyapa kipaumbele maslahi ya wafuasi wao na taasisi au jamii
kuliko ajenda zao binafsi. “Kitu pekee kinachotoka nje ya kaburi na kuungana na
waombolezaji na kukataa kuzikwa ni sifa au tabia za mtu huyo”. Sifa bora za
kiongozi hujenga imani kwa wanaongozwa. Kwanza watu hujenga imani na
kiongozi ndipo humuunga mkono. Na kiongozi yeyote anapovunja imani kwa
wafuasi wake ni lazima atalipa gharama kubwa sana kuirudisha imani hiyo.
7. Sheria/Kanuni Ya Heshima, (The Law of Respect) “Kwa Asili Watu Hufuata Viongozi
Imara Kuliko Wao”
-Kwa asili kabisa mtu akiwa kiongozi bora zaidi watu ambao ni bora kuliko wao
hujikuta wanamfuata bila kujali cheo chake, rangi, au hata kiwango cha elimu,
anaweza kuwa hata ni mfanyakazi wa ndani, mkulima, mwanafunzi au hata
mhudumu wa mgahawa lakini kama ameonyesha kuwa kiongozi imara watu
hujikuta wanamfuata na kumheshimu kuliko hata viongozi wakuu wa nchi endapo
viongozi hao wameonyesha udhaifu katiak uongozi wao.
-Watu wanapomheshimu mtu kama mtu, huvutiwa naye. Wanapomheshimu kama
rafiki, humpenda. Wanapomheshimu kama kiongozi humfuata. Kadiri mtu
anapokuwa na uwezo mkubwa wa kuongoza ndipo kadiri anapoweza kuona
kiwango cha uwezo wa kuongoza kwa wetu wengine.
-Kiongozi ni lazima awe anajua, na anatakiwa awe anajua kwamba anajua, na
anatakiwa awe ana uwezo wa kudhihirisha na kuwaonyesha watu vizuri kabisa
kwamba anajua. Kipimo cha kujua kama kiongozi anaheshimika kiasi gani ni pale
atakapokuwa anafanya mabadiliko makubwa katika uongozi wake.
9. Sheria/Kanuni Ya Sumaku (The Law of Magnetism), “Namna Vile Ulivyo Wewe Ndio
Aina Ya Watu Utakaowavutia”.
-Kila mtu anapenda kufanya kazi na watu wa tabia fulani fulani au aina fulani
Fulani, mtu atakwambia mimi napenda kufanya kazi na mtu mchangamfu, mtu
bora, napenda kufanya kazi na watu wazima zaidi sipendi vijana, mwingine
atakwambia mimi napenda zaidi kufanya kazi na vijana au mtu msafi lakini huwa
hajiangalii yeye ni mtu namna gani. Sheria namba tisa ya uongozi inakwambia
namna ulivyo ndio aina ya watu utakaowavutia kufanya kazi na wewe.
-Yule utakayempata kufanya naye kazi hatokani na nini unataka, atatokana na vile
ulivyo wewe. Kama wewe ni kiongozi wa shirika au taasisi fulani na ni mtu
unayependa kufanya kazi kwa haraka basi baada ya muda fulani utajikuta una
umezungukwa na watu wengi wanaopenda kufanya kazi kwa haraka. n.k., Watu
wenye kufanana na wewe watakutafuta kufanya kazi na wewe. Inawezekana
kiongozi akatafuta watu wa kufanya naye kazi asiofanana nao tabia lakini kwa asili
hatakuwa anawavutia sana yeye kama kiongozi.
-Kama unafikiri watu wako wana mitazamo hasi, basi ni vizuri kujiangalia upya
vizuri wewe una sifa gani. Hata kama kuna mambo mnatofautiana lakini utakuta
kuna mambo mengi sana mnaendana. Mara nyingi utakuta mnafanana mitazamo,
umri unaoendana, pengine mliishi mazingira ya pamoja kama mtaani au shuleni,
tabia kama vile labda wote ni waovu au walevi au wenye kupenda hulka fulani au
watu wa namna fulani, saa nyingine ni wacheshi au wahuni, wapenda ibada sana.
-Pia kadiri unavyokuwa kiongozi bora ndivyo kadiri unavyoweza kuvutia viongozi
bora kufanya nao kazi. Kama unafikiri watu unaowavutia wanatakiwa kuwa bora
basi ni muda wa kujiboresha wewe binafsi kuzidi viwango unavyotaka watu
unaotaka kufanya nao kazi wawe wamefikia.
10. Sheria Kujiunganisha (The Law of Connection), “Viongozi Hugusa Mioyo Ya Watu
Kabla Hawajaomba Kuungwa Mkono”
-Huwezi kuwafanya watu waingie kwenye vitendo kama hujaingia mioyoni mwao
na kuwagusa hisia zao. Mioyo hutanglia kabla hata ya akili kichwani . Kadiri
mahusiano na ukaribu vinavyokuwa imara ndivyo kadiri mfuasi anavyokuwa tayari
kutaka kumsaidia kiongozi. Ukitaka kujiunganisha na watu katika kundi jitahidi
kujenga mahusiano nao kama mmoja mmoja.
-Baadhi ya viongozi hufikiri kazi ya kujiunganisha na kujenga mahusiano ni kazi
ya wafuasi wake. Ni jukumu la kiongozi kujiunganisha na kuimarisha mahusiano
yake na watu. Jitahidi kuimarisha mahusiano na mmoja kwa kujitahidi kujua
majina yao mengi kadiri unavyoweza na kuwaita kwa majina yao moja kwa moja,
pia jitahidi kusalimiana nao kwa kushikana mikono na kila mmoja kadiri
unavyoweza. Watu hawajali unafahamu kiasi gani mpaka wajue unawajali kiasi
gani. Kujiongoza mwenyewe unaweza kutumia kichwa chako, lakini kuongoza
wengine unapaswa kutumia moyo.
11. Sheria/Kanuni Ya Watu Wa Karibu Wanaokuzunguka (The Law Of The Inner Circle),
“Ubora au Umahiri Wa Kiongozi Unatokana Na Wale Walioko Karibu Naye”.
-Hata ujitahidi kujituma na kujihangaisha kiasi gani kuna watu hawawezi
kukuvusha kutoka chini kupanda juu zaidi. Unapokuwa na watu sahihi unaofanya
nao kazi, mafanikio na matazamio yanakwenda juu sana. Hakuna kiongozi wa
peke yake, kama wewe ni kiongozi wa peke yake maana yake hakuna
unachoongoza. Angalia mtu yeyote ambaye anaonekana ni kiongozi mahiri na
utaona watu wengi bora anaofanya nao kazi wamemzunguka. Kila taasisi yenye
mafanikio ina watu bora wanaoifanya ipige hatua kubwa hizo.
-Unapaswa ujitahidi kuajiri watu bora kadiri utakavyopata, jitahidi kuwakuza na
kuwaendeleza kadiri utakavyoweza, na uwakabidhi majukumu yote kadiri
utakavyoona inafaa.
14. Sheria/Kanuni Ya Kumkubali (The Law of Buy In), “Watu humkubali kwanza
kiongozi, ndipo hukubali maono yake”
-Kiongozi huwa na ndoto kwanza ndipo hutafuta watu, ila watu hutafuta kiongozi
kwanza ndipo huwa na ndoto. Kama kiongozi unatakiwa kwanza kutafuta
ushawishi na kukubalika ndipo uje na ndoto au maono kuwashikrikisha watu na
wakubali kushirikiana na wewe katika kuyatimiza.
-Kiongozi ni kama ujumbe, ujumbe wowote watu wanaoupokea hutegemea na
mjumbe anayeufikisha, kama mjumbe huyo ni mtu mwenye kuaminika na
kukubalika basi watu huamini ujumbe huo una thamani, nah ii ndio sababu utakuta
makampuni makubwa huwatumia watu mashuhuri katika kufikisha ujumbe wa
matangazo yao ya bidhaa na huduma mbalimbali. Watu wanaweza kununua labda
pepsi kwa sababu wanamkubali Lionel Messi waliyemuona akinywa pepsi hiyo.
-Ni vigumu kumtenganisha kiongozi na kile anachokipigania au kukisimamia,
yaani iko hivyo kiongozi awe mtu anayefaa kwanza ndio kile anachokipigania au
kukisimamia kitapewa nafasi.
Kwa mfano;-
1. Kama kiongozi hafai, na anapigania jambo lisilokuwa muhimu na lisilo na
manufaa sana kwa watu hapo watu watatafuta kiongozi mwingine.
2. Kama kiongozi hafai, lakini anapigania jambo muhimu na lenye manufaa sana
kwa watu, bado watu watatafuta kiongozi mwingine.
3. Kama kiongozi anafaa, lakini anapigania jambo lisilo muhimu na lisilo na
manufaa sana kwa watu, watu watatafuta jambo lingine.
4. Kama kiongozi anafaa, na anapigania jambo muhimu na lenye manufaa sana
kwa watu, watu watakuwa nyuma yake kumuunga mkono.
-Unahitaji kuwa kiongozi bora ili watu waunge mkono agenda yako, haijalisha
kama una agenda muhimu na iliyo bora kiasi gani, kama wewe mwenyewe sio
kiongozi watu hawatahangaika kujali unabeba ujumbe, maoni/ndoto au agenda
bora kiasi gani.
15. Sheria/Kanuni Ya Ushindi (The Law of Vision), “Kiongozi Hutafuta Njia Ya Timu
Kushinda”
-Viongozi halisi huwa hawakubaliani na swala la kushindwa au kufeli, kiongozi
halisi huhisi swala la kushindwa ni jambo lisilokubalika kabisa na hufanya kila
linalowezekana na kwa namna zote kuweza kupata ushindi. Kiongozi halisi
huamini ushindi ndio kitu cha kwanza, ushindi kwa gharama yoyote bila kujali
itachukua muda gani na safari itakuwa ngumu kiasi gani.
-Wakati mambo yanapochachamaa sana viongozi bora huonyesha uwezo wao wa
juu kabisa kwani chochote bora kilichopo ndani yao huonekana. Viongozi ambao
wanaiishi hii sheria ya ushindi huwa hawana mpango mwingine wa pili tofauti na
ushindi.
18. Sheria/Kanuni Ya Kujitoa (The Law of Sacrifice), “Kiongozi Lazima Ajitoe Sana Ili
Kwenda Juu”
-Kiongozi ni lazima awe mtu wa kujitoa sana, kuanzia muda wake, hapaswi kuwa
mtu wa kujifikiria yeye muda mwingi anafikiria anaowaongoza na
anachokiongoza, wanasema unapokuwa kiongozi unapoteza haki ya kujifikiria
mwenyewe sana. Kiongozi ni mtu anajikuta anakubaliana na usumbufu mwingi na
kufanya kazi kwa moyo sana, na hiyo ndio gharama ya mafanikio ya kiuongozi.
Hii sheria ya kujitoa inasisitiza kwamba kujitoa mara moja ni mara chache sana
inaweza kuleta mafanikio, kiongozi anapaswa kujitoa na kujitoa zaidi na zaidi
mpaka kufanikisha lile analoliazimia. Uongozi unamaanisha kuwa mfano,
ukijikuta katika nafasi ya uongozi watu hufuata kila unachofanya.
-Kujitoa ni jambo endelevu sio swala la mara moja tu. Kama viongozi wanapaswa
kujitoa waende juu, basi wanapaswa kujitoa zaidi ili wabakie juu. Kadiri
unavyoenda juu zaidi ndivyo kadiri unavyojitoa zaidi na zaidi. “Kwa kila kitu
ulichokosa kuna ambacho umepata, na kwa kila ulichopata kuna ambacho
umekosa” alisema Ralph Waldo Emerson. Ukifuatilia viongozi wakubwa wengi
wamejitoa sana maeneo mengi ya maisha yao na kadiri mafanikio yao yanakuwa
makubwa zaidi wanazidi kujitoa zaidi.
-Kadiri kiwango chako cha uongozi kinavyozidi kwenda juu ndivyo kadiri
unavyotakiwa kujitoa zaidi.
19. Sheria/Kanuni Ya Muda Muafaka (The Law of Timing) “Muda wa Kuongoza Una
Umuhimu Sawa Na Nini Cha Kufanya Au Wapi Pa Kwenda”
-Pale kiongozi anapoonekana anafanya maamuzi ya hovyo hata katika vitu vidogo
watu wanaanza kufikiri kwamba yeye kuwa kiongozi wao yalifanyika makosa
makubwa.
-Muda muafaka ni kila kitu,kiongozi yeyote hufahamu hilo na ndio maana mara
zote unapofanya jambo litakuletea matokeo ya aina nne tofauti kama ifuatavyo;-
(i) Ukifanya jambo lisilo sahihi katika muda usio sahihi itapelekea majanga.
(ii) Ukifanya jambo sahihi katika muda usio sahihi litapata upinzani.
(iii) Ukifanya jambo lisilo sahihi katika muda sahihi litakuwa ni kosa
(iv) Ukifanya jambo sahihi katika muda sahihi litapelekea mafanikio.
-Kiongozi sahihi na muda muafaka vinapokutana mambo makubwa hutokea
20. Sheria/Kanuni Ya Kukua Kwa Kasi Na Haraka (The Law of Explosive Growth)
“Kujumlisha Ukuaji Ongoza Wafuasi, Kuzidisha Ukuaju Ongoza Viongozi”
-Ni jukumu la kiongozi kujenga watu ambao wataenda kuijenga
taasisi/kampuni/shirika.
-Kiongozi anayeifanyia kazi sheria hii ya kukua kwa kasi na kwa haraka huacha
kuongoza wafuasi na kuanza kuongoza viongozi. Unapoongoza viongozi ukuaji
unakuwa wa kasi haraka na wa ubora sana, hii hupelekea uwezo wa kampuni kuwa
mkubwa na mambo kufanyika katika ubora wa hali ya juu hata kama kiongozi
Mkuu ana dharura. Ni jukumu la kiongozi kuwajenga wafuasi kuwa viongozi kwa
kuzingatia sheria hizi za uongozi au kutafuta watu ambao tayari wana uwezo
mkubwa wa kuongoza na kuwapa majukumu.
-Tuangalie tofauti kati ya kiongozi anayeongoza wafuasi na kiongozi anayeongoza
viongozi;-
(i).Wakati kiongozi anayeongoza wafuasi anahitaji kuhitajika, kiongozi
anayeongoza viongozi anataka kurithiwa au mtu mwingine kuweza kusimama
kwenye nafasi yake kwa uhakika kabisa.
(ii).Wakati kiongozi anayeongoza wafuasi huangalia zaidi madhaifu katika wale
anaowaongoza, kiongozi anayeongoza viongozi huangalia zaidi uimara wa wale
anaowaongoza
(iii).Wakati kiongozi anayeongoza wafuasi huwachukulia anaowaongoza kwa
usawa, kiongozi anayeongoza viongozi huwachukulia viongozi anaowaongoza
kama watu anaowategemea walete matokeo makubwa kwa nafasi walizopo.
(v).Wakati kiongozi anayeongoza wafuasi hutumia muda wake kukaa na watu,
kiongozi anayeongoza viongozi huwekeza muda kwa watu.
(vi).Wakati kiongozi anayeongoza wafuasi hukua kwa kujumlisha, kiongozi
anayeongoza viongozi hukua kwa kuzidisha.
(vii).Wakati kiongozi anayeongoza wafuasi huwa na madhara kwa watu hao
anaowaongoza peke yake, kiongozi anayeongoza viongozi huwezi kuwafikia
mpaka watu walioko mbali kabisa hata asiowafahamu.
(ix).Wakati kiongozi anayeongoza wafuasi huweza kuwagusa watu yeye
mwenyewe moja kwa moja, kiongozi anayeongoza viongozi huwagusa mpaka
watu walioko mbali asio na ukaribu nao
(x).Wakati kiongozi anayeongoza wafuasi huhangaika kuwaendeleza wale watu wa
chini, kiongozi anayeongoza viongozi huendeleza wale viongozi wa juu na
kuhakikisha wamekuwa bora sana ambapo na wao huendeleza wa chini yao na wa
chini zaidi mpaka taasisi nzima kuwa imejaa viongozi wenye uwezo mzuri.
-Baadhi ya viongozi hupenda kutengeneza wafuasi, lakini viongozi bora hutaka
kutengeneza viongozi, na sio tu kutengeneza viongozi bali kutengeneza viongozi
wa viongozi. Kisha kutengeneza viongozi wa viongozi wa viongozi.
-Njia pekee ya kukua kwa kasi, kwa haraka na kwa ubora ni kufanya hisabati,
hisabati ya viongozi, tengeneza viongozi wa viongozi wa viongozi wa viongozi.