Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 11

UNAC FOR APAC BUSSNESS PLAN

(UNION OF AGRICULTURALS COURSES FOR AGO-PRODUCTS AND


CONSULTANTS ENTERPRISES)

Confidentiality Agreement

The undersigned reader acknowledges that the information provided by


_________________________ in this business plan is confidential; therefore, reader
Agrees not to disclose it without the express written permission of
_________________________.
It is acknowledged by reader that information to be furnished in this business plan is in
All respects confidential in nature, other than information which is in the public domain
Through other means and that any disclosure or use of same by reader, may cause serious harm
or damage to _________________________.
Upon request, this document is to be immediately returned to
_________________________.
___________________
Signature
___________________
Name (typed or printed)
___________________
Date

This is a business plan. It does not imply an offering of securities.


WAZO BIASHARA

UNAC imefikiria kuja na wazo la kibiashara ambalo linajumuisha Huduma mbalimbali juu ya
kilimo na ufugaji. Lakini pia huduma ya ushauri kama msingi wa wazo kuu la biashara hii,
Ushauri kwa wakulima na wafugaji katika madaraja mbalimbali iwe daraja la juu ama la chini.
UNAC pia imefikiria kuja na wazo juu ya uzalishaji mbalimbali ikiwemo bidhaa na ufugaji kwaa
ajili ya kutanua wigo wa huduma zetu za ushauri juu ya sekta ya kilimo ma ufugaji ili
kuwawezesha wakulima na wafugaji kujionea na kushuhudia mifano hai na thabiti kutoka kwa
wataalamu ili kuwezesha mvuto kwa wakulima hii itapelekea kuendelea ama maendeleo ya
kilimo na ufugaji katika jamii inayotuzunguka pia jamii ilioko mbali nasi pia.

Shughuli hizi zinaangaziwa kufanyika katika mji mdogo wa Tarime ambapo ndipo ofisi zetu za
UNAC zitapatikana mda wote, hii ni kutokana na takwimu kuonesha uhitaji wa huduma zetu
kanda ya ziwa na Tanzania kwa ijumla hivyo imepelekea UNAC kuchagua Tarime kama
mwanzo mzuri wa ofisi zao kabla ya ufunguzi wa matawi kwingine Tanzania.

Wazo kuu ni kuhakikisha wakulima na wafugaji wa eneo hilo, kanda ya ziwa na Tanzania kwa
ujumla kupiga hatua za kitaalamu katika sekta ya kilimo na ufugaji.

MPANGO SOKO

UNAC imedhamilia kuwa na soko la huduma zake ndani ya jamii inayotuzunguka pia jamii ya
mbali ikiwa na maana kuwa nje ya kanda ya ziwa, kwa kusema hivo UNAC itaandaa semina
mbalimbali juu ya sekta ya kilimo na ufugaji, Kwanzia kwenye utayalishaji wa mashamba,
mbegu bora na matumizi sahihi ya mbolea na madawa mbalimbali hii itatolewa kwa njia ya
ushauri bora na wa kitaalamu kwa matokeo chanya zaidi nay a kimaendeleo. UNAC ili kupenya
soko la ushindani itaanza kwa kutoa huduma zetu za ushauri kwa kujitolea kwenda maeneo
mbalimbali ambapo tutawasaidia wakulima na wafugaji hivyo kupelekea kuacha alama ya uhitaji
wa huduma zetu za kitaalamu zinazoendeshwa na UNAC.
Hivyo basi kupitia njia ya kujitolea, semina, vipeperushi na matangazo mbalimbali yatakayo
wekwa mitandao ya kijamii kama vile youtube, instagram, whatsap, tweeter, facebook na pia
kupitia matangazo ya radio hii itapelekea ama kusaidia kutambulika na kupata wateja wa
huduma zetu, na pia itambulike kuwa huduma hizi za ushauri toka kwa UNAC zitaambatana na
uzalishaji na ufugaji toka kwenye ushirika pia bidhaa mbalimbali ambazo zitapokelewa kwa
urahisi kutokana na ufanyaji mzuri wake katika huduma za ushauri na hii itatusaidia UNAC
kuwa na sehemu ya mfano kwa vitendo ambapo wakulima na wafugaji watakua wakioneshwa
kama mfano hai ili kuwapa moyo na nguvu kwenye shughuli zao za uzalishaji. Bei za bidhaa
zetu ama huduma za ushauri wetu zitatolewa kwa bei ya kawaida ile hali kujali zaidi wakulima
na wafugaji pia jamii ya hali ya chini ambapo wataweza nunua huduma za ushauri ama bidhaa
zetu .

Huduma juu ya sekta ya kilimo na ufugaji ni tatizo kubwa ndani ya jamii yetu (Tanzania) hivyo
huduma zetu zinahitajika kwa asilimia nyingi na jamii ya kanda ya ziwa na Tanzania kwa
ujumla. UNAC ambayo itakua na makao yake ya ofisi wilayani Tarime, Mara ambapo itatoa
huduma mbalimbali kama vile;

 Usanifishaji wa muonekano wa mashamba ya samaki.


 Usanifishaji wa muonekano wa mabanda ya kuku.
 Ushauri juu ya vyakula bora kwa matokeo bora na mazuri (samaki na kuku) ya ufugaji
kwa ujumla.
 Ushauri juu ya viwango halisi juu ya uchanganyaji wa vyakula vya mifugo.
 Utunzaji wa parameta za maji katika mashamba ya samaki pia utunzaji wa parameta
tunapokuwa na kilimo mseto.
 Uzuiaji wa milipuko ya magonjwa katika mifugo na hata kilimo.
 Ushauri wa mambo mbalimbali juu ya kilimo na ufugaji kwa hatua za maendeleo zaidi
juu ya sekta izo ili kutoa malighafi zenye ubora wa kimasoko ndani na nje ya nchi.
 Usanifishaji wa udongo bora kwa kilimo endelevu.
 Usanifishaji wa mbegu bora kwa kilimo chenye mafanikio ya mavuno stahiki.
 Uzalishaji na uuzaji wa bidhaa mbalimbali (uzalishaji wa vifaranga wa kuku, mayai,
ufugaji samaki pia bidhaa kama juice nk)
AINA YA BIASHARA

UNAC ni ushirika wa kibiashara unaotokana ama kuundwa na Wataalamu wa taaluma


mbalimbali waliobobea katika taaluma hizo, hivyo basi UNAC itakuwa kwenye aina ya
USHIRIKA yaani mfumo wa ushirika wa kibiashara toka kwa vijana walio amua kusaidia jamii
kwa kujihusisha na kujituma katika kutoa huduma za kitaalamu kutoka kwenye utaalamu walio
pata toka kipindi chao cha mafunzo mbalimbali chuoni kwao. Ushirika, hii ni aina ya mfumo wa
biashara unao onesha mfumo halisi wa UNAC. Ushirika huu utaundwa na wataalamu wa
taaluma hizi;

MPANGO NAFASI

Mkoa wa mara, Kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla inakua ama imeanza kupiga hatua
kutoka kwenye kilimo duni kwenda kwenye kilimo cha kitaalamu kukizi au kuendana na
mipango ya serikali kuhusu mfumo wa viwanda hivyo uhitaji wa malighafi zilizo na ubora
utakao pelekea ukuaji wa soko la ndani na nje ya Tanzania, Zaidi ya makazi laki moja na zaidi
pia wakulima na wafugaji mia tano na zaidi wanaozunguka eneo la ofisi zetu wanahitaji huduma
zetu za kitaalamu kutoka katika uzalishaji mdogo na usio na kiwango. UNAC imetazama nafasi
ya semina kama nyezo kubwa kuwafikia watu wengi kwa mda mfupi pia uchunguzi toka kwa
UNAC unaonesha asilimia 80% ya wakulima wilayani Tarime hupata huduma za ushauri toka
nchi jilani ya Kenya kitu ambacho kinawezekana kutoka kwa wataalamu toka nchini ketu.
Makazi hayo wengi wao ni familia ya watoto watatu au zaidi na uzalishaji katika kilimo na
ufugaji ni asilimia zaidi ya 80%.

Ukuaji katika eneo hili linapelekea uhitaji wa ushauri wa kitaalamu juu ya kilimo na ufugaji kwa
matokeo chanya. Hivyo wateja na wahitaji wa huduma inatarajiwa kuwa wakulima na wafugaji
wa kawaida pia wateja wa mahitaji na miradi mikubwa.

Ufafanuzi wa mgawanyiko wa wateja katika madaraja matatu ambayo ni daraja la chini, kati na
daraja la juu yaani miradi midogo au ya kawaida, miradi ya kati na miradi mikubwa.
mgawanyiko wa wateja

wateja wa miradi midogo


wateja wa miradi mikubwa
wateja wa miradi mingine

KAMPUNI MAELEZO

 Ushirika huu utatambulika kwa jina la UNAC (UNAC FOR APAC) Yaani Union of
Agricultural couses - for Agro production and Consultants, Hivyo itatambulika kama
ushirika wa UNAC. UNAC utakuwa ushirika ambao unatumia mfumo ama muundo wa
USHIRIKA (partinership) kama muundo sheria katika shirika. Hivyo hii itapelekea
UNAC kufata taratibu na misingi kamili ya muundo huu wa ushirika.

Wafanya kazi

Uongozi wa UNAC ambao unaundwa na vijana walio bobea katika taaluma mbalimbali hivyo
ufanyaji kazi chini ya ushirika wa UNAC utahitaji wafanyakazi walio wachapakazi, wajuzi,
walio na heshima na nidhamu kwa wateja pia baina ya wafanyakazi wenyewe kwa wenyewe.
Ufanyaji kazi utazingatia vigezo mbalimbali ambavyo vitawekwa na uongozi wa UNAC ili
kuweza kufanikisha ufanisi wa hali ya juu katika huduma na uzalishaji wa shirika hivyo kuinua
shirika na kuwajengea wateja uaminifu na uhuru kufata huduma zetu na kuzipata kwa uhakika na
wakati.
Matarajio

 Kuwavuta wateja kuona umuhimu wetu katika ukuzaji wa sekta ya kilimo


 Kutoa huduma bora kwa wateja wetu kwa bei inayokidhi ama kubalika kwa wateja pia
kuwezesha kujiamini kwa wateja na malalamiko ya wateja kuwa chini ya asilimia moja
(1%).
 Kutengeneza mzunguko chanya juu ya kipato kutoka kwenye huduma ama bidhaa
zitolewazo na kiwango cha chini cha faida kuwa ni 10%.

Ufunguo wa mafanikio

 Ubora wa bidhaa na huduma zetu kwa kujenga na kuendeleza uaminifu wa wateja juu ya
huduma zetu.
 Eneo la biashara ama ofisi litakalokuwa likifikika kwa urahisi na kupeleka wateja kuja
kwa wingi kupata huduma.
 Uongozi na usimamizi uliopitishwa na kukubalika na wanajuiya wa UNAC na wenye
uwezo wa juu kusimamia biashara ya ushirika.
 Uchapakazi wetu juu ya kuendeleza ongezeko na jumla ya ubora wa huduma zetu.

Misheni

Hapa UNAC imejipanga kutoa bidhaa na huduma bora za ushauri, mfano juu ya ufugaji na
uzalishaji bora wa vifaranga vya samaki na samaki wa uzito mkubwa, ushauri juu ya
uchanganyaji wa chakula kwa ajili ya mifugo mbalimbali kama kuku, na samaki, ushauri juu ya
hatua bora za kilimo kwa ajili ya uzalishaji wa kiwango cha juu pia huduma za usanifishaji
mbalimbali kama vile mabwawa na mabanda. UNAC tutatoa huduma na bidhaa zenye ubora na
zenye vigezo jamii inayohitaji.
UNAC itatumia mbinu , wafanyakazi na shirika kwa ujumla kutoa huduma zitakazo wawezesha
wateja kujiamini, kuwafikia walipo, kuyajua mazingira kitu kitakacho wafanya au wasukuma
kufikia ama kupanua matarajio yao.
Vision (Maono yetu)

Maono ama Matarajio yetu ni kuwa chaguo la kwanza la utoaji huduma bora katika jamii
inayotuzunguka pia kuwafikia walioko mbali nasi na kutufanya kuwa shirika linaloheshimiwa
kwa vipimo vya wateja, wafanyakazi, wadhamini, walio na Ubia pia jamii tuliyopo.

“UWEPO WETU NI MAFANIKIO YAKO”

Ni msingi imara wa UNAC ambao unaelezea sisi ni nani na kututenganisha na washindani wetu,
uwepo wa kauli mbiu hiyo itawezesha uchaguzi sahihi toka kwa wateja kwa kutuchagua kama
shirika stahiki kwa mahitaji yao mbalimbali hivyo kutenganisha ubora wa shirika letu na
washindani wetu.

Ushirika wa UNAC unaundwa na thamani kuu tatu ambazo ni misingi sahihi katika kuimalika
kwake na thamani hizo ni zifuatazo;

 Utendaji kazi; Tunafanya kama wamiliki halali wa ushirika siku zote kufikia ama
kupanua matarajio yetu.
 Umoja; Kwa umoja wetu, kuaminiana kwetu, kuunganishwa kwa kuaminiana na
kushirikiana kwa uaminifu, nidhamu na heshima kati yetu.
 Uadilifu; Kuhudumiana kati yetu na washikadau wetu kwa hadhi, uadilifu na heshima.
Uaminifu, maadili ya tabia na uadilifu ni sifa muhimu katika biashara ya ushirika wetu.

Moto wa ushirika

“UNAC, KWA MATUMIZI BORA YA SHUGHULI ZA KILIMO, UFUGAJI NA


UZALISHAJI”

“UWEPO WETU NI MAFANIKIO YAKO”

Nguvu ya ushirika

 Ujuzi kwenye sekta ya kilimo na ufugaji, kitu ambacho kitakua kama nguvu kazi kwetu
kwa kuwa rasilimali watu itatoka kwetu bila kumtegemea mtu wa nje ya ushirika.
 Uendeshaji wa ushirikiano huu wa UNAC na uangalizi wake kwa ujumla utakuwa chini
ya washirika wa UNAC.
 Ushindani mdogo katika mkoa wa mara na kanda ya ziwa kwa ujmla juu ya huduma za
ushauri katika kilimo na ufugaji ambazo zimeonekana kukosekana katika jamii tajwa.
 Ubora wa huduma zetu za kitaalamu ambazo tutao kwa wateja wetu ambapo upatikanaji
wake ni mdogo katika jamii husika.
 Uhitaji wa utaalamu kwa jamii katika sekta ya kilimo na ufugaji kulingana na mabadiliko
ya teknolojia ambayo tunaweza kuyamudu.

Udhaifu wa shirika (Changamoto)

 Ukosefu ama upungufu wa mtaji


 Ugeni wa ushirika la UNAC kwenye jamii hivyo kuwia ngumu kupata uaminifu katika
jamii.
 Uelewa na upokeaji wa huduma zetu kwenye jamii kutoka na huduma hizi kuwa za
kitaalamu tofauti na mifumo waliozoea.

Nafasi

UNAC imeangalia kwa jicho la tatu nafisi yake katika jamii kutokana na uhalisia kuwa asilimia
za uzalishaji wa kisasa ni mdogo na pia ubora wa uzalishaji umekua ukisuasua kwenye kufanya
vizuri hata masoko ya nje ya nchi, hivyo UNAC imekuja kuhakiki inapata nafasi kwa kujenga
uaminifu kwa wateja wake na kuibuka kuwa ushirika unatoa taaluma ya utaalamu kwa vitendo
ili kutoa mifano dhahili kwa ajili ya sekta ya kilimo na ufugaji kupiga hatua. Kuwa sambamba na
mabadiliko ya teknolojia kunaipa UNAC nafasi ya kufanya vizuri kutoka na utaalamu utakao
tolewa na wataalamu wetu.
Menejimenti na Uongozi

Uongozi unatarajia kutumia vyanzo vyetu vizuri na kwa busara kuendesha kwa faida na kulipa
madeni na kufuata maelekezo na sheria zilizowekwa. Philosophia ya uongozi wetu inatoka au
imejengwa na umoja wetu, uchapa kazi na heshima kati yetu, watu ambao watafanya kazi ndani
ya ushirika wa UNAC watatamani kuwa moja kati ya umoja wetu wa kwa sababu tunafanya kazi
kwa mazingira ambayo yanahamasisha ujuzi, uvumbuzu, ubunifu, ushirikiano, ukuaji yaani
maendeleo, mgawanyiko wa kazi na uchapakazi.

Msimamizi na kiongozi wa ushirika wa UNAC atatokana na uteuzi sahihi na halali kutokana na


katiba ya ushirika ambapo atateuliwa na wanajumuiya wa UNAC kwa kuzingatia ujuzi wa
kitaalamu katika swala zima la sekta ya kilimo na ufugaji kwa ujumla.

MPANGO FEDHA

Kutokana na matarajio na makadilio yetu (UNAC) inatarajia kuhakikisha kuendeleza swala zima
mpango fedha chanya kwa miaka mitano ijayo, mipango hii inaonesha kukua kwa mpango fedha
huu wa ushirika.
Biashara inatarajiwa kuanza kwa mkopo na kudhaminiwa kifedha kwa miaka mitano na shirika
lolote la kifedha litakalo kidhi hitaji la kifedha la ushirika wa UNAC. Pia biashara itaanza kwa
mtaji utakao toka kwa wanajumuiya wanaoitengeneza UNAC huku kila mtu akichangia
500,000/= na pia udhamini wa mtaji toka kwa muwekezaji ama washika dau. Chanzo cha kulipa
mkopo kitakua ni kipato kinachotengenezwa na ushirika wa UNAC huku likiwa sambamba na
uwezeshaji wa kukuza kipato cha ushirika kutoka katika mzunguko wa mapato.
Baada ya kipindi cha mwanzo kwa miaka mitano ushirika utaweza kupanuka kimapato zaidi kwa
kipindi hicho mkopo wowote utatumika kushughulikia maendeleo mapya kwa kuwezesha
upatikanaji wa kipato. Mpango au mfumo ama mchakato wa mfumo wa kifedha umeandaliwa
kwa kufuata misingi na taratibu za mgawanyo wa fedha.
Kutokana na matarajio na makadilio yetu UNAC inatarajia kuendeleza mpango fedha chanya
kwa miaka mitano ijayo. Ushirika unatarajia kukaribia ama kufikia kiwango cha uwekezaji ndani
ya miezi mitatu ya shughuli zake.
Pia tunatarajia kupata faida kwenye mwaka wa kwanza wa shughuli zetu, uongezekaji huo wa
faida utafatia miaka mi nne ifatayo kwa kuanzisha na kuongeza mihimili ya wateja. Lengo
kamili ni kuwa na kiasi cha fedha kinachohitajika kwenye mikono yetu kufikia ulipaji wetu na
kujiandaa kwa matumizi yasiyo rasmi. Kwa utunzaji wa mradi wetu inaonesha kuwa biashara
yetu inauwezo wa kuzalisha mizunguko chanya ya fedha ama kipato na utumiaji salama wa
akiba.
Mchanganuo wa uwiano unaonesha wazi kuwa nafasi ya mapato ya UNAC yatabaki kuwa imara
kama ilivyo onekana kwenye utatuzi na ukusanyaji wa mapato. Faida ya ushirika kama
ilivopimwa kwa uwiano wa faida ni mzuri na itaongezeka taratibu kwa miaka mitano.
Uchapakazi utapongezwa kwa bei ya juu ya soko pale ambapo ushirika umeamua kutambulika
kwenye jamii kwa ujumla.

You might also like