Namna Ya Kuishinda Roho Ya Hofu Na Ya Woga

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 17

NAMNA YA KUISHINDA ROHO YA HOFU NA YA WOGA---1

Wakristo wengi leo hii wanateseka kwa sababu ya hofu na woga, lakini Neno la Mungu limetuasa kwamba
hatupaswi kuogopa wala kuwa na hofu kwa sababu aliye ndani yetu ana nguvu kuliko aliye duniani
Hofu ni jambo ambalo linaleta woga au kitisho kwa mtu au kikundi cha watu, hofu ni kisababishi cha muingio
wa woga kwa mtu au makundi ya watu
Kabla ya woga kuna hofu, hivyo hofu hupelekea mtu kuwa na woga juu ya jambo fulani, hofu ni roho halisi
kama woga ulivyo roho halisi
Hofu inakaa kwenye akili na kusababisha mfadhaiko wa akili, ni rahisi sana kukabiliana na hofu kuliko
kukabiliana na woga kwa sababu woga upo katika moyo wa mtu
Adui (Shetani) anatumia silaha ya kumpa mtu hofu ili aweze kuuwa matumaini yake na hatimaye aweze
kumtawala, anayetoa hofu kwenda hatua ya woga ni binadamu mwenyewe kwa kuamua kuamini
Hofu inamaanisha mambo yafuatayo;

Moja, Haujakamilishwa katika upendo,


1Yohana4:18 "Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina
adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo."
Mungu ni pendo, apenda watu kupitia kuokoka tunafanywa kuwa watoto wa Mungu lakini ni muhimu kujifunza
zaidi neno ili upendo wa Mungu ukamilike ndani yetu na uitupe nje hofu inayoletwa na adui
Tunapotembea katika upendo tunakuwa kitu kimoja na Mungu, hatutikisiki wala hatutishiwi na kitu chochote
kwa sababu Mungu ni muweza wa yote na anayetushindia kila kitu

Mbili, Kuna taarifa muhimu ambazo hauzifahamu kuhusiana na unachohofia, hakuna mtu ambaye
anahofia jambo ambalo analifahamu kwa mapana na urefu
Hosea 4:6 "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa,
mimi nami nitakukataa wewe..."

Kadiri unapojifunza na kupata maarifa mapya na mapana kuhusu jambo ambalo unalihofia ndivyo hofu
inavyoondoka katika akili yako
Neno la Mungu linatuita wanafunzi kwa sababu linatuhitaji tuendelee kujifunza kila wakati, Mungu anajua
kwamba kuna mambo mengi ambayo hatuyafahamu kiundani anatarajia tujifunze na hofu tulizonazo ziweze
kuondolewa
Habari ya Daudi na Goliathi inatufundisha namna ambavyo adui anaweza kumpa mtu hofu na hatimaye akaweza
kumtawala na kumfanya mtumwa wake
Goliathi aliwatia hofu wana wa Israeli pamoja na mfalme kwa maneno na muonekano wake na wana wa Israeli
waliruhusu hofu waliyoipata ikaenda hatua nyingine ya woga kwa sababu maneno yalitoka akilini mwao
yakaingia moyoni

1Samweli 17:8 Naye akasimama, akawapigia kelele majeshi ya Israeli akawaambia, Mbona mmetoka
kupanga vita? Je! Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Jichagulieni mtu, akanishukie mimi.
9 Kama akiweza kupigana nami na kuniua, sisi tutakuwa watumwa wenu; nami nikimshinda yeye na
kumwua, ninyi mtakuwa watumwa wetu, na kututumikia.
10 Yule Mfilisti akasema, Nayatukana leo majeshi ya Israeli; nipeni mtu tupigane.
11 Basi Sauli na Israeli wote waliposikia maneno hayo ya Mfilisti, wakafadhaika na kuogopa sana.

Lakini kulikuwa na mwanaume mmoja ambaye alijua siri ya nguvu ya maneno katika kutia mtu hofu na aliyejua
kumsifu na kumshukuru Mungu kwa shuhuda na matendo makuu aliyomfanyia

Daudi hakuhofia jambo lolote, alijua mbinu ya adui kwamba tayari alikuwa ameshawapa hofu na hatimaye
wameshafadhaika mioyo yao ndiyo maana akasema

1Samweli 17:32 "Daudi akamwambia Sauli, Asizimie moyo mtu ye yote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi
wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu"
Tunaona mbeleni kwamba kila mara Goliathi alipokuwa akijaribu kumtamkia Daudi maneno ya kumuingizia
roho ya hofu na hatimaye woga umuingie Daudi hakukaa kimya naye alitamka maneno ya kumtia Goliathi hofu
na hatimaye alishinda vita

Sikia na ufahamu leo kwamba adui anaweza kukutia hofu lakini anayeitoa hofu kwenda kwenye hatua ya woga
ni wewe peke yako kama utashindwa kujitia nguvu katika neno la Mungu

NAMNA YA KUISHINDA ROHO YA HOFU NA YA WOGA-------2

Tatu, Hofu inamaanisha hauongozwi na Roho Mtakatifu, inawezekana unajiongoza mwenyewe au


unaongozwa na adui
Mathayo 10:19 "Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa
ile mtakayosema.20 Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu"

Neno la Mungu limetuasa tusitegemee akili zetu wenyewe kwa sababu hazina uwezo wa kutufanya tuwe na
uhuru ambao Roho wa Bwana anatupatia
Mithali 3:5 "Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe"
Hii haimaanishi haupaswi kutumia akili zako, unazitumia lakini matumaini yako yanapaswa kuwa kwa Bwana,
akili zetu zina kikomo katika kufikiri na kupambanua mambo ndiyo maana zinafikwa na hofu lakini akili ya
Kristo haina kikomo wala kizuizi
Baada ya kuokoka tunapewa akili mpya ya Kristo kupitia kujifunza neno lake ambayo inatufanya tuwe na fikra
na ufahamu mpya unaotuwezesha kuondoa hofu ndani yetu

1Kor 2:16 "Maana, Ni nani aliyeifahamu nia (akili) ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya
Kristo" [EM]
Tunapofikia hatua ya kuongozwa na Roho Mtakatifu ndipo tunapokuwa wana wa Mungu, kusudi la kuokoka ni
ili tuweze kuenenda katika roho na hauwezi kuenenda kiroho kama hauongozwi na Roho Mtakatifu

Warumi 8:14 "Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu."
Roho wa Bwana akikuongoza kamwe huwezi kuwa na hofu kwa sababu kazi yake ni kukupatia amani ambayo
huleta uhuru ndani ya moyo wako
2Kor 3:17 "Basi “Bwana” ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru."
Tunapoongozwa na Mungu hatuwezi kuwa na hofu yoyote kwa sababu Mungu hufanya mambo yafuatayo pindi
tunapomkubali atuongoze;
Moja, Mungu humtangulia anayemwongoza, hufanya hivi ili kusafisha mazingira, kuondoa vizuizi vyote
na kumwandalia njia kumbuka moja ya sifa za Mungu ni yupo sehemu zote kwa wakati wote
Mungu akikutangulia katika suala lolote hauwezi kuwa na hofu kwa sababu ya uhakika wa uongozi wake

Yohana 10:4 "Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa
maana waijua sauti yake"
Mbili, Mungu huenda na anayemwongoza, haishii kwenye kukutangulia bali anakwenda na wewe hii ni kwa
sababu una ushirika naye hivyo hawezi kukuacha peke yako anataka uwe na amani wakati wote
Kama unatembea na Mungu kamwe huwezi kuwa na hofu ndani yako kwa sababu uwepo wake hutowesha hofu
Mathayo 28:20 "na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja
nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari"

Tatu, Mungu humlinda anayemwongoza, ulinzi wa Mungu ni zaidi ya kulindwa na majasusi wa dunia nzima,
Mungu hutulinda pande zote na kila mahali, halali wala hasinzii kama binadamu anakuwa macho ili
kuwaangamiza maadui wataotaka kukudhuru
Ukiwa unaongozwa na Mungu na una ulinzi wa namna hii kamwe hauwezi kuwa na hofu kwa sababu hakuna
jambo lolote litakalokushinda
Kutoka 23:20 "Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka
mpaka mahali pale nilipokutengezea"

NAMNA YA KUISHINDA ROHO YA HOFU NA YA WOGA...... 3


Nne, Mungu anapokuongoza anafanya kazi pamoja na wewe, hii inamaanisha mnashirikiana kufanya kazi na
anakupatia hekima na maarifa

Wakati mwingine hofu ni matokeo ya kufikiria nitafanyaje peke yangu, nitaendaje peke yangu, msaada wangu
utatoka wapi? Nikikwama nani atanisaidia?

Nikupe faraja leo Mungu anasema hivi katika neno lake, Warumi 8:31 "Basi, tuseme nini juu ya hayo?
Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?

Hivyo ukikubali kuongozwa na Mungu kamwe huwezi kuwa na hofu maishani mwako kwa sababu yupo upande
wako na anashirikina na wewe
Tano, Mungu hufanya kazi kwa ajili ya anayemwongoza, haishii kwenye kushirikiana na wewe anaenda
hatua ya ziada anakufanyia kazi ili kukurahisishia mambo
Yohana 14:10 "Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno
niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake."
Kama Mungu anakufanyia kazi huwezi kamwe kuwa na hofu ndio maana ni muhimu sana kukubali kuongozwa
na Roho Mtakatifu ili uweze kuona haya yakidhihirika maishani mwako

Sita, Mungu humfundisha anayemwongoza kwa ajili ya kupata faida


Wakati mwingine tuna hofu kwa sababu hatujui namna ya kufanya jambo fulani lakini Mungu ni mbobezi katika
kufundisha na kutupa maarifa
Unapaswa kuondoa hiyo hofu na ukubali akuongoze ili akufundishe kwa ajili ya faida yako mwenyewe
Isaya 48:17 "BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu
wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata"

Saba, Mungu humneemesha anayemwongoza kwa ajili ya utimilifu kamili


Neema ndiyo inayotupatia nguvu ya kutenda kazi ya Bwana, Mtume Paulo alifanya kazi kupita wote kwa sababu
ya neema kubwa iliyokuwa juu yake
1Kor 15:10 "Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si
bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja
nami"
Neema ya Mungu huitupa hofu nje na kukupatia nguvu maradufu ya kuifanya kazi ya Bwana, hivyo ni muhimu
sana kukubali kuongozwa na Roho Mtakatifu

KWA NINI HAUPASWI KUWA NA HOFU?


i/Bwana Yesu ndiye ngome yako,
Ngome ni ni jengo kubwa lililoimarishwa kwa shabaha ya kujihami dhidi ya maadui na kujitetea dhidi ya
mashambulio
Bwana Yesu anapokuwa ngome yako huwezi kuwa na hofu kwa sababu anaikinga na anakusitiri hivyo kamwe
adui hapati nafasi ya kukushambulia

Zaburi 27:1 "BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima
wangu, Nimhofu nani?5 Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya
hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba."
Yesu anapokuwa ngome yako hata unapokuwa umelala hutakuwa na hofu utalala kama mtoto mchanga kwa
sababu upo ndani
ya ulinzi wa ngome imara
Mithali 3:24 "Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu"
Wengi wanaweweseka usiku katika vitanda vyao kwa sababu ya hofu hawajamruhusu Yesu Kristo aliye ngome
ya kweli na ya uzima aliwalindena kuwaokoa

ii/Bwana anaponya hofu


Unapopatwa na hofu jua kuna tiba yake maalumu ambayo ni Yesu Kristo, leo hii mtafute maadamu anapatikana
Jikabidhi kwake naye atakuponya na hofu yako pasipo malipo au majuto ya aina yoyote ile
Zaburi 34:4 "Nalimtafuta BWANA akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote"

NAMNA YA KUISHINDA ROHO YA HOFU NA YA WOGA -----4


Neno la Mungu limetofautisha wazi wazi aina za hofu na katika somo la leo tutajifunza aina hizo kiundani, ili
hofu inapokujia upate kujua ni aina gani ya hofu
Isaya 8:12 "Msiseme, Ni fitina, katika habari za mambo yote ambayo watu hawa watasema, Ni fitina;
msihofu kwa hofu yao, wala msiogope."

Soma tena kwa makini mstari huo unasema , "msihofu kwa hofu yao.." inamaanisha kuna aina ya hofu
ambayo hatupaswi kabisa kuwa nayo kama wana wa Mungu
Hii inamaanisha kuna hofu ya kidunia ambayo husababishwa na adui na hupelekea mambo mabaya kutokea
katika maisha yetu ndiyo maana Mungu akawahusia wana wa Israeli kupitia kinywa cha nabii Isaya kwamba
hawapaswi kuhofia
Tulijifunza tokea awali kwamba hofu hukaa kwenye akili na kulingana na Neno la Mungu akili ya binadamu ina
sumaku, inanasa na kuvutia mazingira, matukio, watu na hali zinazoendana na kile kilichopo ndani yake
Hii ndiyo maana neno limesema wazi kwamba, Mithali 23:7 "Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo
alivyo...."
Tunapokuwa na aina hii ya hofu maisha yetu yanakuwa ya kufikwa au kuvutia mambo mabaya, hata kama
lisipotokea jambo kama lililopo akilini mwako lakini ni hakika litatokea linalofanana na hilo
Ukiwa na hofu ya jambo baya jua kabisa litakutokea katika maisha yako kulingana na Neno la Mungu, watu
ambao wana hofu ya ugonjwa au kufikwa na matatizo fulani ndio wanaoishia kuumwa
Ayubu 3:25 "Maana jambo hilo nichalo hunipata, Nalo linitialo hofu hunijilia."

Watu wengi leo hii wanateseka sana na wengine wapo kwenye vifungo vya aina mbalimbali kwa sababu ya hofu
walizo nazo, laiti wangaliondoa hofu wangalikuwa huru
Mazingira ya matatizo na vifungo wameyatengeneza wenyewe kupitia hofu zao, mfano wa hofu hizo ni
kama hizi zifuatazo;

i/ Hujaoa au hujaolewa lakini una hofu ya kutokupata mimba au ndoa kuvunjika, matokeo yake haupati
mwenza au ukija kupata hautapata uzao na ndoa itavunjika, hakuna sababu ya kuhofia kutokuoa au
kutokuolewa
Unapaswa kuamini kwamba utaoa au utaolewa kwa wakati na uzao ni haki yako kiungu na utadumu katika ndoa
yenye furaha na amani
ii/Haujamaliza masomo lakini unahofia kutokupata kazi, ukiwa namna hii kamwe ajira hutaweza kupata kwa
sababu hofu ni sawa na unabii wa akili badala yake amini kwamba utamaliza masomo vizuri na utapata kazi
iii/Haujasafiri lakini una hofu ya kupata ajali, maana yake ni kwamba unatengeneza mazingira ya ajali siku
ukisafiri na adui anavyopenda fursa siku ukisafiri atahakikisha unapata ajali
iv/Hujaanzisha biashara lakini tayari una hofu ya kupata hasara, watu wengi hawafanyi biashara sababu ya hofu
na wengine ni wafanyabiashara wa kimataifa lakini hofu imewatawala wameshaanza kupata hasara kabla hata ya
uwekezaji
v/Hujaolewa lakini tayari akilini mwako una hofu ya kuachika, ukiwa namna hii adui atahakikisha ya kwamba
unaachika unapoingia kwenye ndoa, hivyo hatuna budi kuishinda roho ya hofu kama tunataka kuishi maisha ya
amani na mafanikio

Aina nyingine ya pili ya hofu ni kuwa na Hofu ya Mungu, Isaya 8:13 "BWANA wa majeshi ndiye
mtakayemtakasa; na awe yeye hofu yenu, na awe yeye utisho wenu."
Kumhofu Mungu kunapelekea sisi kama viumbe wake kutenda mapenzi yake na vile ambavyo vinampendeza
pekee
Neno la Mungu linasema tumpende Bwana Mungu kwa moyo, roho na akili yetu yote
Mathayo 22:37 "Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako
yote, na kwa akili zako zote."

Haiwezekani kumpenda Mungu kwa akili zako zote kama hauna hofu ya Mungu ndani yako, kumbuka tuliona
kwamba hofu inakaa kwenye akili, unahitaji hofu ya Mungu ili tuweze kumpenda na kumtumikia vyema
Utumishi pasipo hofu ya Mungu hauwezi kuleta matunda mazuri yanayodumu, tofauti na hofu ya kidunia hofu
ya Mungu hutuchochea kutendea kazi neno la Mungu kila wakati

Hofu ya Mungu ndiyo inayosababisha tuweze kuishi maisha ya utakatifu kila wakati kwa sababu inatufanya
tuichukie dhambi huku ikitukumbusha kwamba watenda dhambi makazi yao yatakuwa lile iwa la moto wa milele
Hofu hii hutusaidia kutokumuhuzunisha Roho Mtakatifu kwa sababu hutufanya tulijali hekalu lake (miili yetu)
na kuhakikisha hatulichafui kwa zinaa au uasherati hivyo anaendelea kukaa ndani yetu

Hofu ya Mungu inajenga utayari ndani yetu kwa ajili ya mambo ya Mungu, watu wasioenda kanisani,
wasiopenda kufunga na kuomba, wasiosaidia na kujali wengine hawana hofu ya Mungu
Pale ambapo unakuwa na hofu ya Mungu ni hakika itakufanya upende anachopenda Mungu na kuchukia
anachochukia Mungu kwa sababu unakuwa kitu kimoja na Mungu

Hofu ya Mungu huchochea mambo yafuatayo katika akili na fikra za mtu;


Moja, Huchochea uinjilisti, hii ni kushuhudia wengine habari za Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa
maisha yao

Mbili, Huchochea kuombea Kanisa la Mungu, mtu mwenye hofu ya Mungu haoni shida kufunga na kuomba
kwa ajili ya kanisa la Bwana, anaombea amani kanisa, anaombea wachungaji na watendakazi wa kanisa n.k

Tatu, Huchochea mtu kupenda mambo ya ufalme wa Mungu kila wakati, Mathayo 6:33 "Bali utafuteni
kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa."

Omba ombi hili kwa kumaanisha:


Baba katika Jina la Yesu nijaze roho ya hofu yako ili nipate kulipenda neno lako na kukutumikia daima katika
Jina la Yesu Kristo
Sijui una hofu ya kitu gani maishani mwako, lakini yuko mwanaume mmoja anayetowesha hofu zote katika
maisha yetu

NAMNA YA KUISHINDA ROHO YA HOFU NA YA WOGA-----5


Bwana Yesu asifiwe!
Mtu mwenye hofu ni mtu ambaye ana roho ya utumwa ndani yake kwa sababu hofu hutufanya kuwa watumwa
wa kile ambacho tunakihofia
Warumi 8:15 "Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya
kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba."

Mtumwa ni mtu asiyekuwa na uhuru, ni mtu ambaye anaishi maisha ya kuonewa, kuteseka, anayegandamizwa na
asiyeweza kujitetea kabisa
Mtumwa ni tofauti na mfanyakazi kwa sababu mfanyakazi ana haki ambazo zinamlinda na ana mkataba au
makubaliano maalumu ya malipo kutokana na anachokifanya
Lakini sote tunatambua kwamba kupitia ukombozi Bwana Yesu Kristo ametutenga na utumwa wa kila namna na
kutufanya kuwa viumbe huru ndani yake
Tulikuwa tukiteseka na utumwa wa dhambi na matokeo yake tuliadhibiwa kwa sababu mshahara wa dhambi ni
mauti

Yesu Kristo alikuja kuvunja kazi zote za Ibilisi na kutuondoa katika mateso ya Shetani ndiyo maana kila mara
tunapokuwa na hofu anachukizwa sana tunamfadhaisha kana kwamba kazi aliyoifanya pale msalabani ilikuwa ni
ya bure
Kupitia ukombozi Yesu Kristo alituokoa na maadui zetu hivyo hatupaswi kabisa kuwa na hofu ya aina yoyote ile,
hata hivyo tumeketi naye juu mawinguni katika ulimwengu wa roho
Waefeso 2:6 "Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo
Yesu;"
Kama umeketi pamoja na Kristo Yesu haupaswi kabisa kuwa na hofu, hakuna mtoto anayehofu pale anapokuwa
na mzazi wake anza kujiona upo na Yesu Kristo hiyo itakuondolea hofu zako zote
Kupitia Yesu Kristo Mungu ametukomboa na maasi yote, kama kuna maasi uliyafanya kipindi cha nyuma hata
kama uliuwa na sasa umeokoka acha kuwa na hofu kwa sababu umeshasamehewa na mbele za Mungu huna
dhambi yoyote
Tito 2:14 "ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu
wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema."
Ukombozi umetutoa kutoka kwenye utumwa wa kuhofia nguvu ya kaburi na mauti ndiyo maana Mtume Paulo
akasema
Wafilipi 1:21 "Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida."
Mungu hapendi tunapokuwa na hofu kwa sababu Yesu Kristo alitujulisha mambo yote ambayo Mungu
anayapenda hivyo alitufanya kuwa marafiki zake
Mtumwa hafahamu ni nini Bwana wake anafanya lakini sisi tunafahamu kila kitu ambacho Bwana wetu anafanya
na anayetufunulia ni Roho Mtakatifu

Yohana 15:15 "Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi
nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu."
Unapokuwa mtumwa hauwezi kamwe kuwa mrithi wa baraka kutoka kwa Mungu ndiyo maana ni lazima
uhakikishe unaipinga roho ya hofu kawa nguvu na moyo wako wote
Kupitia kuokoka tumewezeshwa kubarikiwa na baraka zote katika ulimwengu wa roho lakini kama una hofu
hauwezi kupata baraka yoyote kwa sababu utashindwa kuzifanyia kazi au kuzichukulia hatua

Waefeso 1:3 "Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za
rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;"
Hii ndiyo maana neno la Mungu linasema hofu ina adhabu kama Mungu amekupatia kila kitu lakini bado una
hofu jua fika kwamba hofu itakuadhibu na Mungu naye atakuadhibu
1Yohana 4:18 ".....kwa maana hofu ina adhabu;....."

NAMNA YA KUISHINDA ROHO YA HOFU NA YA WOGA-------6


Mungu hataki tuwe na hofu kwa sababu anajua kwamba hofu ina madhara mengi sana, yafuatayo ni madhara
ya hofu
Moja:
Hofu hufungua mlango wa kunaswa na mitego ya adui na pia husababisha kutumbukia shimoni
Isaya 24:17 "Hofu, na shimo, na mtego, vi juu yako, Ee mwenye kukaa duniani.
18 Itakuwa kila akimbiaye sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na kila apandaye na kutoka shimoni
atanaswa na mtego; kwa maana madirisha yaliyo juu yamewekwa wazi, na misingi ya dunia inatikisika."

Adui kamwe hawezi kupata mpenyo kwa mtu kama hana hofu, tunafahamu habari ya Ayubu kwamba Mungu
alimruhusu Shetani amjaribu na hii ni kweli lakini Mungu aliruhusu kwa sababu ndani ya akili ya Ayubu
kulikuwa tayari kuna hofu
Hili tunaliona katika
Ayubu 3:25 "Maana jambo hilo nichalo hunipata, Nalo linitialo hofu hunijilia." hii ina maana Ayubu
alikuwa tayari ana hofu ya kupatwa na mambo mabaya na adui alitumia fursa hiyo kumnasa Ayubu kwenye
mtego wake akapiga mali na familia yake yote
Biblia inaposema kutumbukia kwenye shimo inamaanisha hofu inaweza kusababisha ukafanya jambo ambalo
litaharibu maisha yako au litakugharimu sana
Kutumbukia shimoni ni kuingia ndani ya shimo unatoka katika hali ya juu uliyopo na unaenda chini au unafanya
uamuzi ambao utasababisha kujuta mbeleni kwa sababu ya hofu uliyonayo

Mbili:
Hofu inasababisha mtu kukosa cha kusema mbele za watu, inasababisha hata kile unachokifahamu
unashindwa kukisema
Marko 9:6 "Maana, hakujua la kunena, kwa kuwa waliingiwa na hofu nyingi."
Watu wanaoshindwa kuongea mbele za watu huwa wanazuiwa na hofu, mara nyingi aibu, wasiwasi na mashaka
ni mazao ya hofu
Kama unahofia kuongea mbele za watu unachopaswa kufanya ni kuanza kufanya majaribio kuongea mpaka
utakapokuwa na uhuru wa kuongea
Tunaweza kuishinda hofu ya kitu kwa kukifanya na siyo kukikimbia, sijui unahofia kitu gani maishani mwako
ninamuomba Mungu atoweshe hofu hiyo katika Jina la Yesu
Tatu:
Hofu inaiba amani
Adui anapokuletea hofu kusudi lake ni ili afanye mambo makuu matatu ambayo ni aibe, kuharibu au achinje na
mambo yote haya huiba amani ya mtu
Yohana 10:10 "Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu;......"
Lakini Yesu Kristo alikuja ili apate kuturejeshea amani yetu pamoja na uzima tele kupitia kumwamini yeye kama
Bwana na mwokozi wa maisha yetu

Yohana 10:10 ".......mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele."
Tunaona hata baada ya kifo cha Yesu Kristo hofu ilitanda kwa wanafunzi wake wote na hata baada ya kupaa
walijawa na hofu kwamba Wayahudi wangewatesa na kuwasulubisha lakini Yesu Kristo aliwatokea tena kuwapa
matumaini na ujumbe wa faraja wa kuwatakia amani
Yohana 20:19 "Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango
imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu."

NAMNA YA KUISHINDA ROHO YA HOFU NA YA WOGA-------7


Nne:
Hofu huathiri maamuzi yetu, tunashindwa kufanya maamuzi sahihi kwa wakati
Ayubu 31:34 "Kwa sababu niliwaogopa mkutano mkubwa, Na dharau la jamaa lilinitia hofu, Hata
nilinyamaa kimya, nisitoke mlangoni-"

Watu wengi Mungu amesema nao vitu vya kufanya, wengine kawapa mawazo ya biashara, wengine kawaambia
sehemu za kwenda, wengine kawaambia kazi za kufanya lakini hawataki kufanya sababu ya hofu
Mungu anapokuambia fanya kitu fulani ondoa hofu akilini mwako amini ya kwamba kitafanikiwa kwa sababu
atakufundisha na kukupa njia maalumu za kukifanikisha
Siyo kila mtu aliyeajiriwa alipaswa kuajiriwa, wengine ni watu waliopaswa kufungua makampuni yao na
wakaajiri mamia ya watu lakini sababu ya hofu hawajafanya hivyo
Hofu humzuia mtu kupiga hatua ndio maana neno limesema ".....nisitoke mlangoni" maana yake la kufanya
unaliona lakini ule utayari wa kuliendea unazuiwa na hofu uliyonayo

Tano;
Hofu huweza kusababisha tukapoteza miujiza yetu ambayo Mungu ametutendea
Mathayo 14:26 "Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli;
wakapiga yowe kwa hofu."
Yesu alikuwa akitembea juu ya maji na wanafunzi wake waliingiwa na hofu, lakini Petro alimwambia Yesu
Kristo amruhusu amfuate na alipofanya hivyo alianza kutembea vizuri

Lakini alipoona upepo alianza kuzama kwa sababu hofu ilimuingia na hatimaye woga ukamtawala
moyoni hata akaanza kupiga yowe
Mathayo 14:30 "Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana,
niokoe."
Maisha ya watu wengi leo hii hayatofautiani na ya Petro, wanawenda kwenye maombezi wanaombewa na
wanapokea, lakini wakirudi nyumbani hofu inatanda na wanapoteza walichopokea
Jambo hili linawatesa wengi wanapokea na kupoteza miujiza yao, unaweza kumwombea mtu leo akapona kabisa
lakini baada ya muda sababu ya hofu adui anamrudishia tena kilichokuwa kinamtesa
Ninakuapiza kwa Jina la Yesu kuanzia leo kila muujiza utakaopata utadumu maishani mwako na hofu
haitaupoteza tena katika Jina kuu la Yesu Kristo

Sita;
Hofu inaambukiza, tuliona tangia mwanzo kwamba hofu ni roho na hivyo huambukiza
Kumb 20:8 "Tena maakida na waseme zaidi na watu, wawaambie, Ni mtu gani aliye hapa tena mwenye
hofu na moyo mnyonge? Aende akarudi nyumbani kwake, isije mioyo ya nduguze ikayeyuka mfano wa
moyo wake."
Unapokaa kati ya watu wenye hofu ni rahisi na wewe kuambukizwa na hofu yao, ni sawa na mtu mwenye imani
anavyoweza kumuambukiza asiye na imani
Hivyo usipende kukaa na watu wenye hofu, vutiwa na watu wenye roho ya Imani kwa sababu imani hutowesha
hofu na kila mtu anapokea kulingana na kiwango chake cha imani

NAMNA YA KUISHINDA ROHO YA HOFU NA YA WOGA --------8

Woga maana yake Ni hali ya kuwa na hofu ya kufikwa na jambo la kutisha.” Hii ni maana ya kwanza, maana
nyingine ya woga “Ni hali ya kutoweza kustahimili vitisho.”
Woga ni mfumo na siyo kitendo ndiyo maana kuna neno hali, woga siyo kitu kinachotokea chenyewe, woga
husababishwa na hofu, baada ya hofu kuna woga
Woga ni hofu iliyokomaa, mtu anapokuwa na hofu ya jambo fulani kwa muda mrefu pasipo kulipatia ufumbuzi
hofu juu ya jambo hilo hugeuka na kuwa woga
Hivyo woga ni matokeo ya kutokupata majibu juu ya jambo ambalo limekutatiza kwa muda mrefu, tofauti na
hofu woga hukaa katika moyo wa mtu
Woga kibiblia unaweza kuutafsiri kama matokeo ya kuangalia mambo katika ulimwengu wa mwili na kuyapa
tafsiri kimwili badala ya kiroho

Mfano Mfalme wa Shamu alipofanya vita na Israeli mtumishi wa Elisha alipotoka nje na kuona jeshi kubwa la
watu, farasi na magari, wameuzunguka mji aliogopa

1Wafalme 6:15 "Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda
nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia,
Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje?
Maana yake ni kwamba alitoa tafsiri kwenye ulimwengu wa mwili kwamba kwa sababu kuna jeshi kubwa sana
la Shamu basi wana wa Israeli watapigwa katika vita
Lakini Nabii Elisha alipoona ameogopa sana akamuomba Mungu amfungue macho yake na aone jeshi
linalowazunguka katika ulimwengu wa roho

2Wafalme 6:16 "Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.
17 Elisha akaomba, akasema, Ee BWANA, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. BWANA
akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na
magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote."
Kila jambo linalotutatiza ni lazima tuanze kulitafuta katika ulimwengu wa roho kabla ya wa mwili ili
tuweze kupata majibu yake kiufasaha, kwa sababu mambo yanayoonekana yalitokana na mambo
yasiyoonekana

Waebrania 11:3 "Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu
vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri."
Woga ni roho halisi kama hofu na tuliona kwamba maneno ni roho,
Ezekieli 2:2 "Naye aliposema nami, roho ikaniingia, ikanisimamisha; nikamsikia yeye aliyesema nami."
Tunapaswa kujifunza kukataa maneno ambayo yapo kinyume na hatma zetu kwa sababu kila mara unapoambiwa
maneno ya namna hiyo roho hukuingia na baada ya muda hudhihirika
Huu ni wakati wa kukiri na kuamini kile ambacho neno la Mungu linasema juu yako, kama mtu anakutamkia
maneno mabaya na ya kukukatisha tamaa kwa lengo la kukudhoofisha yapinge kwa Jina la Yesu na damu ya
Yesu Kristo
Neno la Mungu linathibitisha wazi kwamba woga ni roho halisi katika kitabu cha

2Tim 1:7 "Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi."
Hii inamaanisha kila mara unapopatwa na woga ni hakika kwamba ni adui anasababisha, Mungu kamwe hawezi
kukupa woga bali nguvu, upendo na kiasi
Kila mara mtu anapokutamikia maneno roho ya hayo maneno hukuingia, vivyo hivyo maneno yanaweza
kusababisha woga kama yanavyosababisha hofu
Goliathi aliwasababishia woga wana wa Israeli pamoja na mfalme Sauli kwa maneno aliyotamka pamoja na
vitisho alivyowapa huku akiyatukana majeshi ya Israeli
1Samw 17: 10 "Yule Mfilisti akasema, Nayatukana leo majeshi ya Israeli; nipeni mtu tupigane.
11 Basi Sauli na Israeli wote waliposikia maneno hayo ya Mfilisti, wakafadhaika na kuogopa sana."

NAMNA YA KUISHINDA ROHO YA HOFU NA YA WOGA-------9


Woga husababisha masumbuko moyoni na hivyo tunahangaikia vitu vingine na kumsahau Mwenyezi Mungu
au kwa namna nyingine ni kwamba woga husababisha mtu kuweka mlengo kwenye kitu ambacho si cha msingi
Mathayo 6:25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala
miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?

30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je!
Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Tafadhali somo kifungu chote Mathayo 6:25-34 ili kuweza kupata ujumbe wote, katika mafundisho hayo Bwana
Yesu alikuwa akiwaonesha watu kwamba hawapaswi kuangaikia vitu visivyo vya msingi
Bali walipaswa kuutafuta ufalme wa mbinguni kwanza na mengine watazidishiwa
Woga husababisha watu watafute miujiza badala ya kumtafuta Yesu mtenda miujiza na kusudi la Mungu
siyo tuishi kwa miujiza bali kwa kuwa na mahusiano naye
Mafundisho hayo hayamaanishi kwamba chakula, kuvaa na kunywa kunapaswa kupuuziwa bali juhudi zako za
kumtafuta Yesu Kristo na ufalme wake zinapaswa kuzidi juhudi za kutafuta vitu hivyo
Yesu Kristo anapokuwa kipaumbele chako woga juu ya vitu tajwa katika somo hilo unaondoka kwa sababu
ukimpata Yesu umepata vyote kwani Yesu Kristo hukupatia yafuatayo;

Moja
Hutoa kibali ambacho hukuwezesha kufanikisha kila kitu, unaweza kuwa na mawazo mazuri, unaweza kuwa
na mtaji lakini ukikosa kibali hutafanikiwa kamwe hata biashara yako itakufa baada ya muda na hata kazi
uliyoajiriwa unaweza kufukuzwa ndiyo maana ni muhimu kumpata Yesu kwanza
Kutoka 11:3 "BWANA akawapa watu hao kibali machoni pa Wamisri. Zaidi ya hayo, huyo Musa alikuwa
ni mkuu sana katika nchi ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake."

Mbili;
Mungu ndiye anayekupatia nguvu za kupata utajiri, utajiri hauji wenyewe bali ni lazima uwe na nguvu za
kiroho na kimwili za kuupata
Haitoshi tu kusema nitakuwa tajiri jee umewezeshwa kiungu kuupata? Unaweza kustahimili vitisho vya watu?
Upo tayari kuufanyia kazi na kujifunza zaidi kila siku?
Mambo yote haya yanahitaji nguvu za kiroho na kimwili ndiyo maana ni muhimu sana kumtafuta Mungu zaidi
ya mahitaji yetu ya kila siku
Kumb 8:18 "Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri;
ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo."

Tatu;
Mungu ndiye anayebariki kazi za mikono yako, kufanya kazi pasipo baraka ni kujichosha, inahitajika
baraka ili kuweza kufanikiwa katika maisha
Mungu ameshatubariki na baraka zote za rohoni ambazo ndio huleta mafanikio katika ulimwengu wa mwili,
lakini hatuwezi kuzipata kama hatuna mahusiano mazuri na Yesu Kristo

Waefeso 1:3 "Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za
rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;"

Nne;
Mungu ndiye hutupatia hekima ya kufanya kazi na hata kufanikiwa, hekima ni kitu cha msingi sana katika
maisha yetu
Biashara zimekufa, ndoa zimevunjika, huduma zinayumba na nyingine kufa kwa sababu hekima ya uongozi
haipo kabisa, ni jambo moja kuanzisha kitu na ni jambo jingine kukiendeleza
Maono hutuonesha mwisho utakuwaje lakini hekima hutuonesha hatua za kuchukua siku hata siku hata kufikia
maono yetu
Maono pasipo hekima ni kupoteza muda na kamwe hayawezi kutimia kama Mungu alivyokusudia kwa mtu
Mfalme Suleimani alifanikisha sana uongozi wake kwa sababu alimuomba Mungu hekima ya uongozi na
akapatiwa
Tunaona katika utawala wake Israeli iliishi kipindi cha raha na hakuna vita ambavyo vilitokea kwa sababu
alikuwa na hekima ya kuongoza na kutatua migogoro yote
Unahitaji hekima ili uweze kufanikiwa katika maisha yako, kupitia neno la Mungu tunafahamu kwamba Yesu
Kristo ndiye hekima ya Mungu, hivyo ukijenga mahusiano na Yesu Kristo utapata hekima ya Mungu
1Kor 1:24 "bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya
Mungu."

NAMNA YA KUISHINDA ROHO YA HOFU NA YA WOGA---------10


Neno la Kristo, woga huja kwa kusikia neno la adui
Unapopokea taarifa mbaya na ikapata nafasi na kupenyeza ndani ya moyo wako ni lazima woga utakuingia hii
inaleta umuhimu wa sisi kuwa makini na taarifa tunazopokea
Taarifa zinaweza kukujenga kama ni za masuala ya imani, na zinaweza kukubomoa kama ni za masuala

Habari za Wapelelezi waliotumwa na Musa nchi ya ahadi inathibitisha hili kiundani, wale kumi waliokuja na
taarifa mbaya waliwatia woga Waisraeli wote
Hesabu 13:31 "Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu
hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi.
32 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita
kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu
warefu mno.
33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu
kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi."
Kutoka 14:1 "Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule.

2 Kisha wana wa Israeli wote wakamnung’unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia,
Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa
hili."
Katika Neno hilo tunajifunza mambo mengi sana ambayo ni muhimu tukayazingatia kiundani, nilikuwa
ninajiuliza kwa nini Mungu aliwaadhibu wapelelezi wote kumi walioleta taarifa mbaya hata wakafa?

Jibu lake ni kwa sababu;


Moja;
Walileta taarifa mbaya za kukatisha tamaa kwa wana wa Israeli na kumbuka woga ni roho halisi ndio maana
baada ya Israeli kusikia taarifa hiyo walianza kulia na kunung'unika kana kwamba tayari wameanza kupigwa na
Wanefeli
Mbili;
Walikuwa wanaenenda kwa mwili, tuliona woga ni matokeo ya kutoa tafsiri kimwili badala ya kiroho,
wapelelezi waliwaona Wanefeli ni wakubwa mno na matokeo yake wakajiona wao ni mapanzi mbele yao
Maana yake woga uliwafanya watengeneze taswira tofauti na jinsi Mungu alivyowaumba, Mungu aliwaumba
kwa sura na mfano wake lakini leo wanajiona wanafanana na mapanzi hii ilikuwa ni kumdharau Mungu
Tatu;
Hawakuamini nguvu na uweza wa Mungu kwenye kuwashindia vita, japokuwa Mungu alikuwa ameshatenda
ishara nyingi na maajabu bado hawa watu walikuwa hawamuamini hata kidogo, aliwalisha chakula jangwani,
waliona Farao na jeshi likiangamia bahari ya Shamu, waliona wingu likiwaongoza lakini bado hawakuwa na
imani kwa Mungu

Jambo hili lilikuwa ni sawa na kumuasi Bwana, haupaswi kamwe kuogopa wakati unaye Mungu muweza wa
yote, ndio maana Yoshua alirarua mavazi yake na kutamka maneno haya
Hesabu 14:9 "Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula
kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye BWANA yu pamoja nasi; msiwaogope."
Woga ukimuingia mtu anakata tamaa na hataki kusikia taarifa za matumaini, inahitajika nguvu ya ziada,
Yoshua alikua anaeleza kile ambacho Mungu anaweza kuwatendea na aliwaambia kwamba kinga juu yao
imeondolewa lakini wakataka kumuuwa mpaka Mungu alipoamua kuingilia kati
Hesabu 14:10 "Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo utukufu wa BWANA
ukaonekana katika hema ya kukutania, mbele ya wana wa Israeli wote."

Swali jingine nililokuwa ninajiuliza hapa ni kwa nini watu wote walikufa isipokuwa Yoshua na Kaleb
Jibu lake pia tunalipata katika habari hiyo;
Woga ndio ilikuwa sababu ya wao kufa na kutokufika nchi ya ahadi, walioianza safari tokea Misri hata nchi ya
ahadi ni wawili tu wengine wote walikufa jangwani na kizazi kingine kilichozaliwa jangwani ndio kilifika

Katika habari hiyo woga ulipowavaa wana wa Israeli walichagua kufia jangwani na Mungu aliheshimu wazo lao
akawaacha wafe wote jangwani kwa sababu ndio uchaguzi walioufanya, asingaliweza kuwarudisha tena Misri
ndio maana uchaguzi wa Misri hakuwapa
Hesabu 14:2 "Kisha wana wa Israeli wote wakamnung’unikia Musa na Haruni; mkutano wote
wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama
tungalikufa katika jangwa hili."

NAMNA YA KUISHINDA ROHO YA HOFU NA YA WOGA--------------11


Woga unaweza kusababishwa na kushindwa jambo fulani mara nyingi au kupitia hali fulani na ikakujengea
uzoefu fulani wa kushindwa

Wana wa Israeli walivyoteseka utumwani kuna picha fulani ya mateso, manyanyaso, maumivu, kukosa raha na
amani ambayo ilijengeka ndani ya mioyo yao na hii iliwajengea woga dhidi ya jeshi la Farao
Picha hii inapojengeka ndani ya moyo wako kila mara unapomuona yule ambaye anakutesa unasononeka
moyoni na uchungu unajengeka ndani yako kwa sababu inakukumbusha yale ambayo anakufanyia

Woga ukishajengeka moyoni unashindwa kujua ni nini unapaswa kufanya dhidi ya adui yako au
mpinzani wako kwa wakati fulani hivyo unaumia ndani kwa ndani
Lakini Mungu hataki utizame woga kwa namna hiyo kwa sababu anajua hutaweza kuuepuka anataka katikati ya
huo woga uone fursa ya kwenda mbele na moyo wako uwe na utayari wa kufanya hivyo ndio maana anasema
nenda mbele
Kutoka 14:15 "BWANA akamwambia Musa, Mbona unanililia mimi? Waambie wana wa Israeli
waendelee mbele."
Wakati Mungu amewatoa wana wa Israeli kutoka utumwani na wakafika sehemu wako katikati mbele ni bahari
ya Shamu na nyuma jeshi la Farao linakuja kwa spidi walianza kuwaza bora wangebaki Misri waendelee kuwa
watumwa
Kutoka 14:12 "Neno hili silo tulilokuambia huko Misri, tukisema, Tuache tuwatumikie Wamisri? Maana
ni afadhali kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani."
Walisema hivyo kwa sababu ya woga, hivyo woga unaweza kukufanya ukubali kuendelea kutumikia shida, taabu
na mateso kwenye maisha
Hiyo bahari ya mateso unayoona kama hutaweza kuivuka Mungu kwa uweza wake atakupigania na utaivuka
salama pasipo matatizo yoyote, ondoa woga uone namna ambavyo Mungu atakupigania nawe unyamaze kimya

Kutoka 14:14 "BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya."


Mungu yupo tayari kukushirikiana na wewe hata ushinde vita dhidi ya kile ambacho kinakutatiza, lakini kila
akitizama moyo wako anaona umejaa woga na hauna matumaini kwake ndio maana umeendelea kuwa katika
changamoto hiyo kwa muda mrefu
Wengine wanaogopa kuanzisha biashara leo kwa sababu wana uzoefu wa kushindwa na ndani ya mioyo yao
wanaogopa wanajisemea kwamba wameshapoteza fedha mara tatu haiwezekani tena
Alfa na Omega anasema hivi hao Wamisri unayemuogopa mpaka umefikia sehemu umekosa amani, sikia neno la
Bwana kutoka kwa Mtumishi wake kwamba hutawaona tena Wamisri maishani mwako katika Jina la Yesu
Kutoka 14:13 "Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA
atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele."

Hata kwenye maisha yetu ya kila siku timu za mpira/au mabondia wanapopigana zinapocheza na moja
ikafanikiwa kuifunga nyingine, iliyofungwa ikiogopa siku ya marudiano itafungwa zaidi au itakimbia uwanjani
Lakini jiulize ni mara ngapi timu inafunga timu nyingine na kwenye marudiano aliyefunga anafungwa tena
magoli mengi ya kutosha au bondia aliyepigwa kwenye madudiano anampiga maradufu aliyempiga?

NAMNA YA KUISHINDA ROHO YA HOFU NA YA WOGA------------12


BNeno usiogope katika Biblia takatifu limeandikwa mara mia tatu na sitini na tano maana yake ni kwamba
kila mara unapolala na kuamka sauti ya Mungu inakuambia usiogope nipo pamoja nawe
Hasara kubwa kuliko zote ya woga ni kwamba husababisha mtu kushindwa kumshuhudia Yesu Kristo

Yohana 7:13 "Walakini hakuna mtu aliyemtaja waziwazi, kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi."
Siyo kila mtu alikuwa anapinga Injili ya Yesu Kristo wapo wengi ambao walimkubali na kuona kile ambacho
alikiwa anafanya ni chema lakini woga uliwazuia kuongea mbele za Mafarisayo na Makuhani
Unapokuwa na woga unaenda kinyume na agizo kuu la Mungu kwa kila aliyempokea la kufanya watu wengine
kuwa wanafunzi, kwa sababu hautaweza kwenda kumtangaza Yesu Kristo ulimwenguni
Mathayo 28:19 "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la
Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;"

Baada ya kuokoka na kukaa chini kujifunza neno huwa unavikwa uweza na Roho Mtakatifu, uweza huu siyo kwa
ajili ya kuombea mambo yako binafsi, zaidi sana huwa unakupatia ujasiri wa kumtangaza Kristo uliyempokea
kwa watu wengine wasiomfahamu
Usipomshuhudia Yesu Kristo hauna tofauti na yule ambaye anayemkana kwa sababu ni lazima udhihirishe imani
yako kwa kunena na kutenda
Petro alimkana Yesu Kristo kwa kunena, lakini leo hii unaweza kumkana Yesu Kristo kwa kutokumshuhudia na
kutokufanya lolote ambalo anakuagiza
Yesu Kristo ni wako binafsi pale ambapo umempokea, unapokuwa unamwabudu na unapokuwa unaongozwa
naye baada ya hapa unapaswa kumtangaza kwa watu wengine wapate kumfahamu na kumpokea
Usipomshuhudia Yesu Kristo inamaanisha;
Moja;
Unapenda utukufu wa wanadamu kuliko wa Mungu
Tupo kwenye dunia inayomchukia Yesu Kristo ndiyo maana alivyokuja kwa walio wake hawakumpokea hii ni
kwa sababu ya dhambi na uovu
Aliyeokoka anaonekana mshamba, anayekunywa pombe na kwenda disko anaonekana wa mjini lakini
hivi ni vipimo vya binadamu
Mungu hatuoni namna hiyo anahuzunika na kusikitika tunapoangamia, haupaswi kufanya vitu ili upewe sifa na
wanadamu bali unapaswa kumpendeza Mungu
Ukiupenda utukufu wa wanadamu kamwe huwezi kumpendeza Mungu, utaacha kutendea kazi neno la Mungu ili
uwafurahishe watu fulani na Mungu atachukizwa nawe
Yohana 12:42 "Walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya
Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi.43 Kwa maana walipenda utukufu wa
wanadamu kuliko utukufu wa Mungu."

Utukufu wa Mungu ni wake peke yake hataki kumshirikisha mwingine, Mungu anataka kusifiwa na kutangazwa
kuliko kitu kingine chochote kile
Isaya 43:21 "watu wale niliojiumbia nafsi yangu, ili wazitangaze sifa zangu"

Mbili;
Hauthamini kazi aliyoifanya Yesu Kristo
Kama umeelewa vyema alichokifanya Yesu Kristo ni kwa ajili ya kila mtu ni lazima utakithamini na
kukishirikisha kwa wengine
Kazi ya msalaba haikuwa rahisi, kuvaa dhambi na makosa yetu wote, kukubali kuteswa na kusulubishwa pamoja
nasi ilikuwa ni jukumu zito na alituhurumia sana

Hauna budi kumshuhudia kwa wengine, hivyo thamini kazi ya Yesu Kristo kwa kutangaza habari zako kote kote

Tatu;
Umefanya kuokoka kwako ni jambo la siri
Yesu Kristo hakufa sirini alisulubiwa hadharani kila mtu akiona, aliteswa na hata kuvuliwa nguo watu
wakiona
Kwa nini wewe unataka kumhubiri chumbani mwako kwa kuweka picha tu na ukitoka nje unajifanya
haumfahamu?
Ukitaka ajulikane kamtangaze nje kwa watu wengine, kuokoka siyo siri ni uamuzi wa busara kuliko
uamuzi mwingine wowote ule
Chukua jukumu kuanzia leo usinde huo woga kwa kumtangaza Yesu Kristo mtoe huko chumbani kwako n
mpeleke nje kama alivyokuagiza

Nne;
Hautaki Yesu Kristo arudi mapema kuja kulichukua Kanisa lake
Yesu alisema kwamba hatorudi mpaka Injili ihubiriwe pande zote za dunia na mataifa wapate kumfahamu ndipo
hapo ule mwisho utakapokuja
Mathayo 24:14 "Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa
mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja."
Usiruhusu woga kukuzuia kumtangaza Yesu Krito, kumbuka Yesu alisema atakayemkana mbele ya
wanadamu naye atamkana mbele ya Baba yake juu mbinguni

NAMNA YA KUISHINDA ROHO YA HOFU NA YA WOGA--------------13


Bwana Yesu asifiwe!
Leo kipekee tutajifunza juu ya tabia ambazo zinaambatana na mtu mwenye roho ya woga, jikague kiundani pindi
unapojifunza ili ujue kama ni mhanga na uchukue hatua au laa
Tabia ya kwanza;
Woga husababisha mtu ashindwe kuchukua hatua katika maisha yake
Mathayo 25: 25 "basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako."
Tunapojifunza habari za hawa watumwa watatu ambao bwana wao alisafiri na akawapatia talanta kila mmoja
kadiri ya uwezo wake, tunaona madhara ya woga katika maisha yetu
Tafadhali soma habari hii kitabu cha Mathayo 25:14-30 ili upate kuihusisha na somo hili vyema
Katika habari hii mtumwa aliyepewa talanta tano alifanya biashara na kupata faida ya talanta tano zaidi kadhalika
na wa talanta mbili alipata faida ya mbili lakini wa talanta moja hakufanya biashara alifukia chini talanta yake
Maana yake ni kwamba hakuchukua hatua ya kutaka kufanya biashara kwa sababu ya roho ya woga iliyokuwa
inamsumbua
Wakati mwingine kwenye maisha yetu mtaji siyo tatizo kuna watu wana mitaji kama ilivyokuwa kwa huyu
mtumwa lakini woga unawazuia kuchukua hatua ya kuanza kufanya biashara
Hii ni kwa sababu woga humletea mtu uvivu na ulegevu

Mathayo 25:26 "Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa
navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;"

Usipochukua hatua maana yake;


Moja;
Hakuna mabadiliko yatakayotokea katika maisha yako,
Mabadiliko ni zao la hatua kama una hali ngumu ya kifedha na ukaruhusu woga kukuzuia kuchukua hatua ya
kuomba kazi au kuanza biashara maana yake utabakia na mateso na mahangaiko yako ya kifedha pasipo msaada
wowote
Mbili;
Utanyang'anywa ulichonacho na atapewa mtu mwingine
Mungu anapokuamini na kukupa wazo fulani, mtaji au kazi fulani anatarajia utaifanya vyema na italeta faida
katika ufalme wake, Mungu hapendi hasara anataka faida ndio maana alimwambia Abrahamu atazidisha uzao
wake
Kila ambacho kimewekwa mikononi mwako unatarajia ukizalishe maradufu ndio maana neno linasema uendelee
kukifanyia biashara hata Bwana atakapokuja
Luka 19:13 "Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni
biashara hata nitakapokuja."

Lakini kama ukikiuka neno la Mungu na kuamua kutokufanyia biashara na kuongeza ulichopewa Mungu
atakunyang'anya alichokupatia na kumpa mwingine aliye na juhudi katika kukifanyia kazi
Mathayo 25:28 "Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi."

Tatu;
Unapoteza uaminifu wako kwa watu na Mungu pia
Katika maisha unapotegemewa kwamba utafanikisha jambo fulani na familia yako, jamaa zako au marafiki na
ukashindwa kufanya hivyo uaminifu wako hupotea kwao
Hautaaminika wakati mwingine, kama umepewa mtaji na haujaufanyia kazi, umepewa huduma na Mungu
hujaitendea kazi, umepewa karama hutaki kuitumia ni dhahiri uaminifu wako utapotea

Tabia ya pili;
Woga humfanya mtu kuwa na visingizio katika kila jambo
Vijana wengi ukiwauliza watakuambia wanaamini kwamba wao ni wafanyabiashara wakubwa lakini hawataki
kabisa kuanza biashara kwa mtaji mdogo
Hivyo watasingizia hawajaanza kwa sababu ya mtaji au wakati mwingine watasema hali ya uchumi haivutii kwa
sasa, hivi vyote ni visingizio vinavyoletwa na woga wa kuanza biashara kwa kile walichonacho
Wengine Mungu kawapa na ishara, kanena nao kwa ndoto wafungue kampuni lakini bado wameruhusu woga
kuzuia kile Mungu alichoweka ndani yao
Ndivyo ilivyokuwa kwa huyu mtumwa alitafuta visingizio vya kutokufanya biashara sababu ya woga aliokuwa
nao ndio maana alisema hivi
Mathayo 25:24 "Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u
mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;"
Leo nakutabiria kama nabii wa Bwana aliye hai ile kampuni yako kaianzishe katika Jina la Yesu, ile biashara
yako kaifungue maana ni hakika utafanikiwa katika Jina la Yesu, ile kazi uliyoikatia tamaa iombe tena Bwana
wangu atakupatia katika Jina la Yesu
Omba ombi hili kwa homa kali ya kiroho
Ewe roho ya woga! Unayenizuia nisichukue hatua na nitafute visingizio vya kila jambo, Ninakuteketeza kwa
moto wa Roho Mtakatifu katika Jina la Yesu!

NAMNA YA KUISHINDA ROHO YA HOFU NA YA WOGA---------------14


Tabia ya tatu;
Woga humfanya mtu ashindwe kufikiri vyema juu ya jambo analopaswa kufanya
Kabla ya kufanya maamuzi yoyote katika maisha yetu tunapaswa kutumia akili ya Kristo tuliyopewa ili tuweze
kufanya uamuzi sahihi
Mtu mwenye woga hawezi kutulia na hivyo mara zote hushindwa kuitumia akili aliyonayo kufikiri vyema na
matokeo yake anaweza kufanya maamuzi yasiyo na busara au asifanye maamuzi kabisa
Mathayo 25:27 "basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo
yangu na faida yake."
Mtumwa huyu hakufanya alilopaswa kufanya kwa sababu hakuweza kufikiri vyema kama alivyopaswa kufikiri
ndio maana hakufanya biashara akaficha talanta aliyopewa

Tabia ya nne;
Woga husababisha mtu kushindwa kukemea maovu yanapojitokeza
Neno la Mungu halituambii tukumbatie uovu na dhambi, japokuwa inatupaswa kuvumilia lakini mtu anapokosea
tunapaswa kumkemea kulingana na neno la Mungu
Mara nyingi Watumishi huogopa kukemea na kuonya watu na matokeo yake maovu na dhambi huendelea
kuchanua katika mwili wa Kristo na hata kulichafua Kanisa la Mungu
2Tim 4:2 "lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa
uvumilivu wote na mafundisho."

Hatuna budi kumrejesha mtu anapokosea kwa kumkemea na kumuonya kwa upole
ili tuweze kuiokoa nafsi yake na aweze kuingia kwenye uzima wa milele
Tunapaswa kutambua ya kwamba woga utahukumiwa siku ya mwisho na Bwana wetu Yesu Kristo na hukumu
yake ni ziwa la moto wa milele kwa sababu ukiwa na woga kamwe huwezi kuitenda kazi ya Bwana

Mathayo 25:30 "Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na
kusaga meno."

Neno la Mungu limeweka msisitizo zaidi katika kitabu cha Ufunuo juu ya hukumu kwa watu wenye roho
ya woga
Ufununuo 21:8 "Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao
waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo
mauti ya pili."

Mungu anachukia woga kwa sababu husababisha mtu kusema uwongo na hili linaweza kusababisha familia
kusambaratika
Kusudi la Mungu kuweka ndoa ni ili idumu na isitenganishwe na kitu chochote isipokuwa kifo

Baba yetu Abramu alitaka kuisambaratisha familia yake mwenyewe sababu ya woga wakati alipoenda Misri pale
aliposema mke wake ni dada yake hata akachukuliwa na Farao kwa sababu ya uzuri wake
Unaweza kusoma habari hii kiundani kitabu cha (Mwanzo 12:11-20), lakini roho ya woga aliyokuwa nayo
Abramu alimuambukiza mwanaye Isaka naye akataka kuisambaratisha familia yake kwa sababu ya woga
Mwanzo 26:7 "Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni ndugu yangu huyu
maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa maana
alikuwa mzuri wa uso."
Hivyo woga unaweza kusababisha tukawakana wenza wetu mbele ya maadui zetu ndio maana ni lazima
ukatae roho ya woga kwa nguvu zako zote
Familia inapovunjika ina maana Kanisa linaharibika kwa sababu siku zote Kanisa huanzia nyumbani
Familia inapovunjika huweza kupelekea kuwepo kwa watoto wa mitaani na kuwepo kwa watoto wanaolelewa na
upande mmoja jambo ambalo halimpendezi Mungu na siyo zuri kwa malezi ya mtoto

Familia inapovunjika inasababisha mfadhaiko kwa watoto, wanakosa furaha na amani wakati wote

Familia inapovunjika inaweza kusababisha kusudi kutokufanyika vyema, Mungubalikusudia mke na mume
wasaidiane ili kuweza kufanikisha kusudi la maisha yao

NAMNA YA KUISHINDA ROHO YA HOFU NA YA WOGA-----------15


Bwana Yesu asifiwe
Ninakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, heri ya mwanzo mpya wa mwezi wa kumi, kwa kuwa
umeuona utaumaliza katika Jina la Yesu

Tunaendelea na somo letu kipekee kabisa leo tutajifunza aina za woga

Neno la Mungublimetofautisha aina mbili kuu za woga, ni muhimu kujifunza aina hizi ili unapokuwa na woga
upate kujua ni woga unaotokana na nini

Aina ya kwanza ni Kumuogopa Mungu


Tunapaswa kumuogopa Mungu kwa sababu ndiye aliyetuumba na kuumba kila ambacho tunakiona
Mungu hazoeleki ila anafurahi tukiwa marafiki zake, kiu kikubwa cha Mungu ni sisi kuwa na mahusiano ya
karibu na yeye kila wakati
Isaya 59:19 "Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua;
maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya BWANA."

Tunapomuogopa Mungu inatusaidia kuutafuta uso wake kwa bidii kila wakati
2Nyak 20:3 "Yehoshafati akaogopa, akauelekeza uso wake amtafute BWANA; akatangaza mbiu ya watu
kufunga katika Yuda yote."
Tunapokuogopa Mungu hutuchochea kufanya yale ambayo yanampendeza,
Tunamuogopa Mungu kwa sababu ya ukuu wake utishao, uweza wake, hukumu zake na wingi wa haki zake

Ayubu 37:22 "Kaskazini hutokea umemetufu wa dhahabu; Mungu huvikwa ukuu utishao.
23 yeye Mwenyezi hamwezi kumwona; Yeye ni mkuu mwenye uweza; Tena mwenye hukumu, na mwingi
wa haki, hataonea.
24 Kwa hiyo watu humwogopa; Yeye hawaangalii walio na hekima mioyoni."
Tunamuogopa Mungu kwa sababu hutusamehe dhambi zetu, kuna wakati mtu anaweza akawa amefanya dhambi
mpaka akajihukumu mwenyewe kwamba hastahili msamaha, lakini Mungu hutusamehe hata yale ambayo
tunaona hayapaswi kusamehewa
Zaburi 130:4 "Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe."

Neno la Mungu linatufundisha kwamba Mungu anao uwezo wa kuuwa mwili pamoja na roho kwa sababu hiyo
anapaswa kuogopwa
Mathayo 10:28 "Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye
kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum."

Faida za kuliogopa Jina la Bwana


Moja;
Unapatiwa urithi, ni kweli kupitia ukombozi tumefanywa kuwa warithi wa baraka kupitia Yesu Kristo,
lakini wale ambao wanaoweza kuzirithi ni wanaoliogopa Jina la Bwana
Zaburi 61:5 "Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu. Umewapa urithi wao waliogopao jina
lako."

Mbili;
Unapatiwa bendera, Mungu anapokupa bendera ni ishara ya uwakilishi, maana yake unauwakilisha ufalme wake
hapa duniani, pia ishara ya kwamba umepata ushindi katika jambo fulani linalokutatiza, ni ishara ya uhuru wako
Zaburi 60:4 "Umewapa wakuogopao bendera, Ili itwekwe kwa ajili ya kweli."

Tatu;
Ukiziogopa amri za Bwana unapatiwa thawabu na Mungu, thawabu ni baraka na kila mtu anahitaji baraka ili
maisha yake yaweze kubadilika

Mithali 13:13 "Kila alidharauye neno hujiletea uharibifu; Bali yeye aiogopaye amri atapewa thawabu."
Swali ni kwamba nitajuaje kama woga wangu ni mzuri yaani unaotokana na Bwana?

Jibu;
Woga unaotokana na Bwana siku zote utakuchochea kufanya mambo ya Mungu tena yale ambayo
yanayompendeza, unapohisi hali kama hii jua ni woga wa Bwana unakugusa ndani ya moyo wako
Woga wa Bwana huchochea utii ndani yako wa kufanya kila ambacho Bwana anataka ukifanye kwa wakati

Aina ya Pili ya woga ni Kuogopa wanadamu


Wakati mwingine watu hawamuogopi Mungu kwa sababu hawamuoni kwa macho ya nyama lakini
wanawaogopa binadamu
Mathayo 10:26 "Basi, msiwaogope, kwa maana hakuna neno lililositirika, ambalo halitafunuliwa; wala
lililofichwa, ambalo halitajulikana."

Hiyo ilikuwa ni hotuba ya Yesu na alikuwa akisisitiza watu wasiwaogope Mafarisayo na Waandishi hata
washindwe kusema kile anachofundisha
Kipindi cha nyuma walikuwa wanaogopwa kwa sababu walikuwa na uwezo wa kumtenga mtu na sinagogi hata
asiweze kusali kwa sababu hiyo wengi walijua kweli lakini waliogopa kusema sababu wangetengwa
Hatupaswi kamwe katika maisha yetu kuwaogopa binadamu wenzetu kwa sababu tutaangukia mtegoni
Mithali 29:25 "Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama."
Tutaendelea na somo hili kwenye kitabu kitakachotoka hivi karibuni kumbuka tumebakisha vipengele muhimu
kama; --
Kwa nini haupaswi kuogopa

Mbinu za kuushinda woga

Kuhusisha hofu na woga nk

You might also like