Safari - Nov 6, 2022 at 12:33

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 1

Habari Michezo Video Vipindi vya R

Afya yako: Jitibu


mwenyewe kwa tiba
hizi za nyumbani ,ila
usizidishe kiwango
6 Machi 2021

ISTOCK

Vyakula vinavyoweza kukupatia nguvu mwilini ili


kujenga kinga yako na kudhibiti magonjwa

Wakati mwingine umeziskia hizi tiba za


nyumbani ili kutuliza maumivu ya kichwa na
hata kuweza kupata usingizi .

Mara nyingi tiba hizi umezipata kwa wazee wetu


wa zamani ama hata kuzisoma mitandaoni na
unajiuliza je, zinafanya kazi ama ni kupoteza
muda tu?

Habari njema ni kwamba baadhi ya tiba hizo


zimethibitishwa kwa njia za kisayansi kwamba
zinafanya kazi .

Imebainika wazi sasa kwamba kuna mimea na


mazao yanayotokana na miti mbali mbali yenye
viungo vyenye tiba na hapa tunakupakulia baadhi
ya tiba hizi za nyumbani unazoweza kuzitegema .

Pilipili kutibu maumivu


Pilipili ina kiungo ambacho kina umuhimu mkubwa
wa tiba tangu jadi na sasa matumizi yake
yameanza kukubalika na wengi sio tu kupitia
chakula lakini pia kama dawa .

Ina kiungo kijulikanacho kama capsaicin ambacho


kinatumiwa kuweza kudhibiti maumivu ama
uchungu .Inafanya kazi kwa kuwasha sehemu ya
ngozi kwa kuipa joto na ukali kabla ya kufikisha
ganzi baadaye .

Leo unaweza kuandikiwa dozi ya apsaicin kwa


jina Qutenza ambayo inatumiwa sana kudhibiti
uchungu .

Jitengezee Krimu ya capsaicin


na mafuta ya nazi
1. Changanya vijiko 3 vidogo vya poda ya
cayenne na kikombe 1 cha mafuta ya nazi.

2.Pasha moto mafuta kwa joto la wastani hadi


iyeyuke.

3.Koroga mchanganganyiko huo kwa dakika 5.

4.Ondoa kuoka motoni kisha ipoe na kuweza


kuganda.

5.Jikande kwenye ngozi baada ya kupoa.

6.Ili kuifanya nyororo ongeza mafuta ya nazi


uweze kutumia vizuri kwenye ngozi bila kujikwaza
.

7. Ni vizuri kufanya majaribio ya athari zake kwa


ngozi yake kabla ya kuitumia kikamilifu .

Usiitumie krimu hii karuibu na uso au macho yako


na hakikisha unavalia glavu kabla ya kujipaka
unapotaka kupata afueni

Tangawizi kutibu maumivu na


kichefuchefu

Ni kama ada kutumia tangawizi ukijipata na mafua


au koo lako linakoroma na matumizi yake sio ya
kubahataisha kwani imebainika kwamba tiba hii
inafanya kazi na ina uwezo mkubwa sana wa
kukupa afueni .

Pia chai ya tangawizi itakusaidia kuzuia kuhisi


kichefuchefu . Kuitengeza dawa ya tangawizi ni
rahisi kama kusukutua kwani unachohitaji ni
kuiponda ama kuitumia iliyosagwa na kuitumia
katika chai .

Tangawizi pia ina viungo vya kutuliza maumivu na


mara nyingi hata dawa za homa na mafua
zimetegezwa kwa baadhi ya viungo vya tangawizi
.

Uyoga wa Shiitake kuzuia


kansa ya matiti

GETTY IMAGES

Lentinan, al maarufu kama AHCC ni kiungo


kinachotoka kwenye uyoga wa Shiitake ambaco
huzua uvimbe wa seli na husaidia kabisa
mchipuko wa uvimbe unaoweza kusbabisha
kansa .

Iwapo utafurahishwa na supu ya mifupa wakati


unapoitumia basi usisahau kutupa ndani aina hii
ya uyoga ili kuiboresha tiba hiyo hata Zaidi .

Mafuta ya Mikaratusi/
Eucalyptus kupunguza
uchungu

GETTY IMAGES

Aina tofauti ya mmea wa Mafuta ya Mikaratusi

Mafuta ya mikaratusi yana kiungo kwa jina 1,8-


cineole, ambacho kupunguza uchungu.

Kiungo hicho kina athari kama ya morphine na


kimefantywa uchunguzi na kugunduliwa kuwa na
uwezo mkubwa wa kukupa afueni unapopitia
maumivu .

Hata hivyo matumizi ya mafuta ya eucalyptus sio


ya kila mtu .Mafuta haya yanaweza kuchochea
Asthma na pia kudhuru wanyama wa nyumbani .

Lavender kuumwa na kichwa


na uchovu
Maumivu ya kichwa wakati mwengine yanaweza
kukuathiri ghafla bila kuwa na dawa za kupunguza
makali yake

Iwapo utakumbwa na maumivu haya basi


usichelee endapo una lavender au majani yake.

Pia tiba hii ya nyumbani husaidia kupunguza


uchovu na matatizo ya kifikira endapo umechoka
kupindukia

Mnanaa/Mint kwa maumivu ya


misuli

Mnanaa

Mint, inajulikana na wengi na ina manufaa mengi


ikiwemo kufungua mkondo wa kupumua iwapo
umesakamwa au hata kupunguza maumivu ya
misuli .

Kwa uchungu wa misuli tafuta yenye kiungo cha


methyl salicylate, iliyo na athari ya capsaicin.
Kuitumia kutakupa hisia kama ya 'kuchomwa' na
inapooza.

Aina nyingine ya mint inayotumika sana ni


peppermint. Kiungo hiki kinatumika sana kutibu
maradhi ya koo au kutoa fueni wakati
unapokabwa na mafua .

Kando na matatizo ya tumbo mafuta ya


peppermint au chai ya peppermint inaweza
kusaidia kupunguza maumivu ya kichwa .

Vyakula vyenye Magnesium


kwa kila kitu
Iwapo kuna kiungo kinachoweza kukupa afueni ya
matatizo mengi nyumbani basi ni vyakula vyote
vyenye madini ya magnesium .

Iwapo utapatwa na matatizo kama uchovu,


kuumwa na kichwa na maumivu ya misuli basi tiba
hii ya nyumbani itakupa afueni .

Mboga na matunda yenye magnesium ni kama


Spinachi, avocado, na hata chokolati nyeusi .

Vyakula vyenye magnesium


•Maharagwe ,mbaazi

•tofu

•Nafaka

•samaki wa mafuta kama chache

•Ndizi

Hakikisha unazitumia ifaavyo tiba za nyumbani

Ingawaje nyingi ya tiba hizi hazina madhara ya


pembeni kunazo zenye athari kama hizo
zikitumiwa kwa wingi kupindukia .

Watu wengine huenda wakajipata mashakani kwa


kupitisha kiasi cha tiba hizo na wakati wote unafaa
kufahamu kiasi na njia ifaayo ya kuitumia tiba
yoyote kati ya hizi .

Iwapo mwili wako haustahimili matumizi ya vitu


kama protini basi pia kuwa mwangalifu na uepuke
tiba zenye viungo vya protini .

Mada zinazohusiana

Afya ya kiakili Afya Afya ya Wanawake

Shirika la Afya Duniani (WHO)

Habari kuu
Ndege ya abiria yaanguka Ziwa Victoria nchini
Tanzania
Saa 1 iliyopita

T​etesi za soka Ulaya Jumapili 06.11.2022


Saa 2 zilizopita

Moja kwa moja Vita vya Ukraine: Iran yakiri


kupatia Urusi ndege zisizo na rubani

Gumzo mitandaoni

Simulizi ya kijana aliyemuokoa Waziri Mkuu wa


zamani wa Pakistan Imran Khan kuuawa

4 Novemba 2022

Wanyama watano werevu zaidi duniani

4 Novemba 2022

Giligilani: Kiungo chenye ushujaa katika vyakula


vya Kihindi

4 Novemba 2022

''​Uso wa pili wa Dubai: Jinsi nyota wa Instagram


wanafanya biashara ya ngono kufadhili maisha ya
anasa"

4 Novemba 2022

Fahamu Israel ilivyohamisha maji ya Mto Nile hadi


Ukanda wa Gaza miaka 35 iliyopita

4 Novemba 2022

Wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa Kenya


warejesha begi lenye $19,000 kwa mtalii wa
Uingereza

4 Novemba 2022

Wanyama wanane walioangamia mikononi mwa


binadamu

3 Novemba 2022

Hakutakuwa na barafu Mlima Kilimanjaro ifikapo


2050

3 Novemba 2022

Ni washirika gani wa Putin wanaokosoa vita vya


Urusi nchini Ukraine?

3 Novemba 2022

Iliyosomwa zaidi

1 Ndege ya abiria yaanguka Ziwa Victoria


nchini Tanzania

2 Majengo ya siku za usoni ambapo maisha


yatakua ndani ya uzio

3 T​etesi za soka Ulaya Jumapili 06.11.2022

4 Zifahamu faida 5 bora za kiafya za viazi


vitamu

5 Kwanini wanyama hawa watano ni


werevu zaidi duniani

Kwanini unaweza kuiamini BBC News

Sheria ya matumizi Cookies

Kuhusu BBC Wasiliana na BBC

Sera ya faragha AdChoices / Do Not Sell


My Info

© 2022 BBC. BBC haihusiki na taarifa za kutoka


mitandao ya nje. Soma kuhusu mtazamo wetu wa
viambatanishi vya nje.

You might also like