Jukwaa La Majadiliano Ya Mada Ya Kwanza

You might also like

Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 10

JUKWAA LA MAJADILIANO YA MADA YA KWANZA

Mjadala kuhusu nafasi ya moduli hii katika kumsaidia mjifunzaji kutekeleza

majukumu yake ya sasa na ya baadaye

 Settings 
 ◄ Uhakiki wa matini za kifasihi

Display mode                                                                        
The due date for posting to this forum was Friday, 2 July 2021, 6:51 AM.

Mjadala kuhusu nafasi ya moduli hii katika kumsaidia mjifunzaji kutekeleza

majukumu yake ya sasa na ya baadaye

by Dr. Wallace Mlaga - Sunday, 6 September 2020, 6:58 AM

Number of replies: 10
Kwa mifano bayana, jadili uhusiano uliopo baina ya uhakiki wa kifasihi, nadharia ya fasihi, na
nadharia ya uhakiki wa fasihi?

PermalinkReply

In reply to Dr. Wallace Mlaga

Re: Mjadala kuhusu nafasi ya moduli hii katika kumsaidia mjifunzaji kutekeleza
majukumu yake ya sasa na ya baadaye

by FAUSTIN NDIKUBWIMANA - Thursday, 27 May 2021, 10:26 AM

Uhusiano uliopo baina ya uhakiki wa kifasihi,nadharia ya fasihi, na nadharia ya uhakiki wa fasihi ni
kuwa istilahi hizi zote zinategemeana. Mhakiki anahakiki na kuzichambua kazi za kifasihi ka kuwa
anaelewa nadharia ya fasihi na muundo unaojumuisha kazi hiyo ya fasihi. Pia mhakiki hana budi
kuelewa ndharia ya uhakiki inayoongoza kazi fulani ya kifasihi. Wakati wa uhakiki,mchambuzi
lazima aelewe nadharia inayoongoza kazi anayoichammbua ili apate uamuzi wa jinsi ya kuhusisha
mawazo yanayopatikana katika hiyo. Kabla ya hayo mhakiki anapohakiki lazima aelewe kuwa kazi
hiyo anayoichambua inahusu nini, ni aina gani ya fasihi? Hivyo vyote kuvielewa vitampa mwelekeo
fulani wa kuhakiki kila kazi anayoitaka.
PermalinkShow parentReply

In reply to FAUSTIN NDIKUBWIMANA

Re: Mjadala kuhusu nafasi ya moduli hii katika kumsaidia mjifunzaji kutekeleza
majukumu yake ya sasa na ya baadaye

by VINCENT BUCYEDUSENGE - Thursday, 27 May 2021, 4:48 PM

Asante sana ndugu Faustin umeeleza vizuri uhusiano uliopo baina ya uhakiki wa kifasihi,nadharia ya
fasihi, na nadharia ya uhakiki wa fasihi.
PermalinkShow parentReply

In reply to Dr. Wallace Mlaga

Re: Mjadala kuhusu nafasi ya moduli hii katika kumsaidia mjifunzaji kutekeleza
majukumu yake ya sasa na ya baadaye

by VINCENT BUCYEDUSENGE - Thursday, 27 May 2021, 5:43 PM

Kwa upande wangu pia kuna uhusiano baina ya istilahi hizi kwani nadharia ya fasihi ni kama
mpango kazi wa kutekeleza kazi ya fasihi, wakati uhakiki wa kifasihi ni kama mchakato wa
kuchambua kazi ya fasihi kitaalamu ili kutafuta na kupata uhahika wa jambo husika na uhakiki wa
kazi yoyote ya fasihi lazima ufanywe kwa kuegemea nadharia fulani. Kwa mfano ili kuelewa wimbo
wa Rugamba Cyprien '' ICYIFUZO'' pale anaposema ''Ningekuwa na nguvu kuzidi za urusi na za
marekani ningeadhibu wajeuri kama afrika kusini…"(tafsiri yangu) ni lazima kutumia nadharia
inayozingatia mtunzi na hadhira yake kwani ujumbe wa wimbo huu si rahisi kuupata bila kuzigatia
historia ya kipindi kile msanii alipoutunga wimbo ni lazima kuzingatia mtunzi aliitunga ktk kipindi
gani? Afrika ya Kusini kulitokea nini katika kipindi hicho? kwa nini alisema nguvu za Urusi na
Marekani?nk. Mhakiki asipochunguza kipindi cha sanaa hiyo historia haitaihakua rahisi kupata
uhakika wa wimbo huu.
Kwa muhtasari, Kazi yoyote huwa na ukweli ndani mwake unaoelezwa na nadharia yake. Ili kupata
ukweli huo, mhakiki lazima afanye uchunguzi wa kitaaluma kwa kuegemea kwenye nadharia fulani.
Ni vizuri kujua kuwa unapoihakiki kazi moja kwakuegemea nadharia mbili tofauti unaweza kupata
tofauti kati ya ukweli unaoupata. Kwa hiyo uchaguzi wa nadharia itakayokuongoza usifanywe
ovyoovyo bali kitaalamu.
PermalinkShow parentReply

In reply to Dr. Wallace Mlaga

Re: Mjadala kuhusu nafasi ya moduli hii katika kumsaidia mjifunzaji kutekeleza
majukumu yake ya sasa na ya baadaye

by LEON NSENGIMANA - Sunday, 30 May 2021, 12:09 PM

Uhakiki wa kifasihi ni namna ya kuchambua kazi ya kifasihi kwa undani, yaani namna ya
kutathimini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida
maalum, pamoja na vipengele mbalimbali vinavyofanyiwa uhakiki katika kazi ya fasihi kama vile
kuonyesha mambo yanayojitokeza katika kazi ya fasihi kama vile, mtindo, dhamira, nadharia ya
kifasihi iliyoegemezwa, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo, msimamo n.k
Kwa mfano: Riwaya “Siku ya watenzi wote” ilifanyiwa uhakiki kuhusu mtindo uliotumiwa na
mwandishi wake ambaye ni Shabaan Robert. Mhakiki wa kazi hii ya fasihi ambaye ni Musa
Muhamed, amezama katika matumizi ya uwili, matumizi ya ushairi na matumizi ya vilugha kama
vipengele vilivyotumiwa na Shabaan Robert kudhihirisha maudhui yake.
Katika uhakiki wa kifasihi, mhakiki pia huchambua nadharia ya uhakiki wa fasihi iliyoegemewa
katika uandishi wa kazi hiyo ya kifasihi.
Nadharia ya fasihi ni nadharia ambayo iliegemewa wakati wa kuandika kazi fulani ya kifasihi.
Wakati wa kuandika kazi ya kifasihi mwandishi anaegemea kwenye nadharia moja au zaidi ya moja
zinazomuongoza katika uandishi wa kazi yake ya kifasihi.
Kwa mfano: katika uhakiki wa Makala “Mizimu katika Ngano za Kiafrika” iliyoandikwa na Angelus
Mnenuka, tunapohakiki Makala hii ya kifasihi inadhihirika kwamba mwandishi aliegemea kwenye
nadharia ya Ontolojia ya kiafrika
Nadharia ya uhakiki wa kifasihi ni mbinu tofauti za kuhakiki nadharia fulani iliyoegemewa katia kazi
fulani ya kifasihi. Ni maoni tofauti ya watu tofauti kuhusu nadharia iliyoegemewa na mwandishi wa
kazi ya kifasihi ambayo mwandishi anaona ndiyo inayofaa kulingana na kazi ya kifasihi inayohusika.
Kwa mfano katika Makala “Nadharia ya fasihi na fasihi ya Kiswahili ya majaribio” iliyoandikwa na
F.E.M.K. Senkoro, anatoa maoni tofauti ya wahakiki tofauti kuhusu nadharia tatu ambazo ni
Umundo, Finominolojia na Hemetiki kama zilivyotumiwa na waandishi wa kazi za kifasihi
mbalimbali.
Kwa ujumla kuna uhusiano wa karibu pamoja na mwingiliano kati ya uhakiki wa kifasihi, nadharia
ya fasihi, na nadharia ya uhakiki wa fasihi kutokana na jinsi haya yote huweza kujitokeza katika kazi
moja ya kifasihi.
PermalinkShow parentReply

In reply to Dr. Wallace Mlaga

Re: Mjadala kuhusu nafasi ya moduli hii katika kumsaidia mjifunzaji kutekeleza
majukumu yake ya sasa na ya baadaye

by LEON NSENGIMANA - Sunday, 30 May 2021, 3:58 PM

Uhakiki wa kifasihi ni namna ya kuchambua kazi ya kifasihi kwa undani, yaani namna ya
kutathimini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida
maalum, pamoja na vipengele mbalimbali vinavyofanyiwa uhakiki katika kazi ya fasihi kama vile
kuonyesha mambo yanayojitokeza katika kazi ya fasihi kama vile, mtindo, dhamira, nadharia ya
kifasihi iliyoegemezwa, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo, msimamo n.k
Kwa mfano: Riwaya “Siku ya watenzi wote” Robert. S. (1968) ilifanyiwa uhakiki kuhusu mtindo
uliotumiwa na mwandishi wake ambaye ni Shabaan Robert. Mhakiki wa kazi hii ya fasihi ambaye ni
Musa Muhamed, amezama katika matumizi ya uwili, matumizi ya ushairi na matumizi ya vilugha
kama vipengele vilivyotumiwa na Shabaan Robert kudhihirisha maudhui yake.
Katika uhakiki wa kifasihi, mhakiki pia huchambua nadharia ya uhakiki wa fasihi iliyoegemewa
katika uandishi wa kazi hiyo ya kifasihi.
Nadharia ya fasihi ni nadharia ambayo iliegemewa wakati wa kuandika kazi fulani ya kifasihi.
Wakati wa kuandika kazi ya kifasihi mwandishi anaegemea kwenye nadharia moja au zaidi ya moja
zinazomuongoza katika uandishi wa kazi yake ya kifasihi.
Kwa mfano: katika uhakiki wa Makala “Mizimu katika Ngano za Kiafrika” iliyoandikwa na
Angelus. M (2020), tunapohakiki Makala hii ya kifasihi inadhihirika kwamba mwandishi aliegemea
kwenye nadharia ya Ontolojia ya kiafrika
Nadharia ya uhakiki wa kifasihi ni mbinu tofauti za kuhakiki nadharia fulani iliyoegemewa katia kazi
fulani ya kifasihi. Ni maoni tofauti ya watu tofauti kuhusu nadharia iliyoegemewa na mwandishi wa
kazi ya kifasihi ambayo mwandishi anaona ndiyo inayofaa kulingana na kazi ya kifasihi inayohusika.
Kwa mfano katika Makala “Nadharia ya fasihi na fasihi ya Kiswahili ya majaribio” iliyoandikwa na
Senkoro F.E.M.K. (1992), anatoa maoni tofauti ya wahakiki tofauti kuhusu nadharia tatu ambazo ni
Umundo, Finominolojia na Hemetiki kama zilivyotumiwa na waandishi wa kazi za kifasihi
mbalimbali.
Kwa ujumla kuna uhusiano wa karibu pamoja na mwingiliano kati ya uhakiki wa kifasihi, nadharia
ya fasihi, na nadharia ya uhakiki wa fasihi kutokana na jinsi haya yote huweza kujitokeza katika kazi
moja ya kifasihi.

Marejeleo
Angelus, M. (2020). Mizimu katika Ngano za Kiafrika: Uchambuzi wa Ngano teule
Senkoro, F.E.M.K. (1992). Nadharia ya fasihi na fasihi ya Kiswahili ya majaribio
Robert, S. (1968). Siku ya Watenzi Wote
PermalinkShow parentReply

In reply to Dr. Wallace Mlaga

Re: Mjadala kuhusu nafasi ya moduli hii katika kumsaidia mjifunzaji kutekeleza
majukumu yake ya sasa na ya baadaye

by VEDASTE MUDAHERANWA - Sunday, 30 May 2021, 10:08 PM

Uhakiki wa Fasihi ninauelewa kama kazi yenyewe ya uchanganuzi ama uchambuzi wa kazi yoyote
ya fasihi. Kwa mfano, mhakiki anapoanza kujiuliza juu ya lugha iliyotumiwa, falsafa ya mwandishi,
migogoro iliyoibuliwa, mbinu za kiuandishi na vipengele vingine vya fani na maudhui; huwa
anahakiki kazi ya fasihi yaani uhakiki wa fasihi.

Kwa upande mwingine, nadharia ya fasihi ni misingi, kanuni na miongozo iliyopo inayomuongoza si
tu mwandishi katika utunzi wa kazi ya fasihi bali pia msomaji katika kushughulikia ama kusoma kazi
ya fasihi.

Nayo nadharia ya uhakiki wa fasihi ni misingi na kanuni zilizopo ambazo zinaongoza uchambuzi wa
kazi ya fasihi. kwa maneno mengine, nadharia ya uhakiki wa fasihi humuongoza ama hutoa misingi
ya uhakiki wa kazi ya fasihi.

Hapa ni lazima pia nidhihirishe kwamba kwa mjibu wa Wafula (2015, uk: 4-5) aliashiria kwamba
kuna mkanganyiko katika kusema kwamba kuna misingi na miongozo inayoongoza uchambuzi wa
kazi ya fasihi. Katika kuzungumzia mkanganyiko huu alipinga hoja za wataalamu kama Werrek na
Wallen walioibuka katika miaka ya 1920 hadi 1960 ambao waliona kwamba dhana ya uhakiki wa
fasihi ni moja. Pamoja na mwelekeo wao walijikuta wakibagua ama wakipuuza kazi nyingine
ambazo hazizingatii moja kwa moja misingi waliyoiweka hasa hasa fasihi simulizi za kienyeji za
Kiafrika. Mawazo haya yalikuja kurekebishwa na baada na waasisi wa umuundo, uhakiki mpya na
umaumbo ingawa nao kwa kiasi fulani walitofautiana.

Kulingana na ushahidi huu uliotolewa hapo juu, ni dhahili kwamba pia suala la nadharia za uhakiki
wa fasihi ni dhana ambayo inaweza kuhojiwa, kwa sababu nadharia zenyewe haziwezi kufikiriwa
kwamba ni hizo na haziwezi kuongezeka ama kuondolewa.

Kwa kutamatisha juu ya mjadala huu, dhana hizi tatu zinaingiliana kwa sababu ifuatayo: katika
kuhakiki kazi ya fasihi, hatuna budi kutumia nadharia, na nadharia inayotumiwa inapaswa kuangukia
katika kundi la nadharia za uhakiki wa fasihi.
PermalinkShow parentReply
In reply to Dr. Wallace Mlaga
Re: Mjadala kuhusu nafasi ya moduli hii katika kumsaidia mjifunzaji kutekeleza
majukumu yake ya sasa na ya baadaye

by FAUSTIN NDIKUBWIMANA - Saturday, 26 June 2021, 8:45 PM

Uhakiki wa Fasihi

Ntarangwi( 2004) uhakiki wa fasihi ni kitendo cha kutathimini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni
juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalumu. Wamitila (2002) kwa mujibu wake,
uhakiki ni uchunguzi wa kazi ya kifasihi kwa makini na kwa utaalamu. Uchunguzi wa aina hii
huchunguza uchanganuzi, fasiri, uelezaji, ufafanuzi, tathimini na utoaji wa kauli ya kijumla.(Peck &
Coyle)

Uhakiki ni utathmini, ufasili na uainishi wa kazi za fasihi, lakini haumaanishi kutafuta makosa ya
kazi hiyo. Kwa hiyo, Uhakiki ni kitendo cha kuchambua, kutathmini na kuainisha kazi ya fasihi ili
kuona ubora na udhaifu wa kazi hiyo kwa kutumia vigezo husika vya fani na maudhui kwa
kuegemea kwenye uzoefu binafsi wa mtu, nadharia fulani, au vionjo vya mtu binafsi vya kiujumi.

Mulokozi (2017) anabainisha kuwa uhakiki (wa fasihi) ni mchakato wa kitaaluma unaojumuisha
fasili, uchambuzi na tathimini ya kazi ya fasihi.Mlaga (2017) naye anabainisha kuwa uhakiki wa
fasihi ni uchambuzi na ufafanuzi wa vipengele vya fani na maudhui katika kazi ya fasihi.

Nadharia za Uhakiki

Castle (2007) anafafanua nadharia ya uhakiki kuwa ni kanuni na dhana, mikakati na mbinu
zinazohitajika kuongoza zoezi la kihakiki. Mlaga (2017) anafafanua nadharia za uhakiki kama
miongozo ya usomaji na ufafanuzi wa kazi za fasihi. Yeye anataka kumaanisha kwamba kazi moja
ya fasihi inaweza kusomwa na kufafanuliwa kwa namna zaidi ya moja kutokana na nadharia
zilizotumiwa kwa kuhakiki kazi hiyo. Wafula na

Njogu (2007) wanafafanua na kupambanua nadharia za uhakiki kuwa ni jumla ya maelekezo

yanayomsaidia msomaji au mhakiki kuifahamu kazi ya fasihi kwa kufuata utaratibu maalumu.
Wanadokeza zaidi kuwa dhana hii hurejelea istilahi ya kijumla inayomaanisha mwongozo
unaomwelekeza msomaji wa kazi ya fasihi kuifahamu kazi hiyo vizuri katika vipengele mbalimbali
vya kazi ya fasihi na namna vinaunganika kuleta umoja katika kazi husika. Wamitila (2003) anaeleza
kuwa nadharia za uhakiki hutumiwa kumaanisha kauli za kijumla au kaida zinazomwongoza
msomaji katika ufasiri wa maana iliopo katika fasihi. Kwa mfano, katika kuelewa maudhui katika
kazi ile ya fasihi.

Uhusiano uliopo baina ya uhakiki wa kifasihi,nadharia ya fasihi, na nadharia ya uhakiki wa fasihi ni

kuwa istilahi hizi zote zinategemeana. Mhakiki anahakiki na kuzichambua kazi za kifasihi ka kuwa
anaelewa nadharia ya fasihi na muundo unaojumuisha kazi hiyo ya fasihi.

Pia mhakiki hana budi kuelewa ndharia ya uhakiki inayoongoza kazi fulani ya kifasihi. Wakati wa
uhakiki,mchambuzi lazima aelewe nadharia inayoongoza kazi anayoichammbua ili apate uamuzi wa
jinsi ya kuhusisha mawazo yanayopatikana katika hiyo. Kabla ya hayo mhakiki anapohakiki lazima
aelewe kuwa kazi hiyo anayoichambua inahusu nini, ni aina gani ya fasihi? Hivyo vyote kuvielewa
vitampa mwelekeo fulani wa kuhakiki kila kazi anayoitaka.

Kwa hiyo istilahi hizi zote hazina budi kutegemeana katika kazi zote za kifasihi.

Marejeleo

Castle, G. (2007). The Blackwell Guide to Literary Theory. Blackwell Publishing: USA.

Mlaga, K.W. (2017). Msingi ya Ufundishaji na Ujifunzaji wa Fasihi, Karne Ya 21. Heko

Mulokozi, M.M. (2017) Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili: Kozi za fasihi vyuoni na vyuo vikuu.

Njogu, K, na R.M Wafula (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. The Jommo Kenyatta Foundation.
Nairobi.

Ntarangwi, M. (2004). Uhakiki wa kazi za Fasihi. Augustana College, Rock Island, IL612

PermalinkShow parentReply

In reply to FAUSTIN NDIKUBWIMANA

Re: Mjadala kuhusu nafasi ya moduli hii katika kumsaidia mjifunzaji kutekeleza
majukumu yake ya sasa na ya baadaye

by Dr. Wallace Mlaga - Sunday, 27 June 2021, 6:18 PM

Faustin, hongera kwa kuboresha kazi yako. Pamoja na hayo, sijaona popote ulipofafanua kuhusu
nadharia ya fasihi.

Aidha, unapotoa ufafanuzi kutoka kwa wataalamu kadhaa kuhusu suala moja, ni muhimu uoneshe
muunganiko. Baada ya kueleza mtaalamu wa kwanza anasema nini, bora utumie maneno, Mlaga
(2017) naye anasema au anaeleza.
Baada ya hapo, toa sasa ufafanuzi wako kama hitimisho au tafsiri ya kile kinachoelezwa na
wataalamu hao kina maana gani sasa? Ussishie tu kusema fulani kasema hivi na fulani kasema hivi.
Piga hatua moja zaidi.
PermalinkShow parentReply

In reply to Dr. Wallace Mlaga

Re: Mjadala kuhusu nafasi ya moduli hii katika kumsaidia mjifunzaji kutekeleza
majukumu yake ya sasa na ya baadaye

by FAUSTIN NDIKUBWIMANA - Sunday, 27 June 2021, 2:39 PM

Uhakiki wa Fasihi

Ntarangwi( 2004) uhakiki wa fasihi ni kitendo cha kutathimini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni
juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalumu. Wamitila (2002) kwa mujibu wake,
uhakiki ni uchunguzi wa kazi ya kifasihi kwa makini na kwa utaalamu. Uchunguzi wa aina hii
huchunguza uchanganuzi, fasiri, uelezaji, ufafanuzi, tathimini na utoaji wa kauli ya kijumla.(Peck &
Coyle)

Uhakiki ni utathmini, ufasili na uainishi wa kazi za fasihi, lakini haumaanishi kutafuta makosa ya
kazi hiyo. Kwa hiyo, Uhakiki ni kitendo cha kuchambua, kutathmini na kuainisha kazi ya fasihi ili
kuona ubora na udhaifu wa kazi hiyo kwa kutumia vigezo husika vya fani na maudhui kwa
kuegemea kwenye uzoefu binafsi wa mtu, nadharia fulani, au vionjo vya mtu binafsi vya kiujumi.

Mulokozi (2017) anabainisha kuwa uhakiki (wa fasihi) ni mchakato wa kitaaluma unaojumuisha
fasili, uchambuzi na tathimini ya kazi ya fasihi.Mlaga (2017) naye anabainisha kuwa uhakiki wa
fasihi ni uchambuzi na ufafanuzi wa vipengele vya fani na maudhui katika kazi ya fasihi.

Nadharia za Uhakiki

Castle (2007) anafafanua nadharia ya uhakiki kuwa ni kanuni na dhana, mikakati na mbinu
zinazohitajika kuongoza zoezi la kihakiki. Mlaga (2017) anafafanua nadharia za uhakiki kama
miongozo ya usomaji na ufafanuzi wa kazi za fasihi. Yeye anataka kumaanisha kwamba kazi moja
ya fasihi inaweza kusomwa na kufafanuliwa kwa namna zaidi ya moja kutokana na nadharia
zilizotumiwa kwa kuhakiki kazi hiyo. Wafula na

Njogu (2007) wanafafanua na kupambanua nadharia za uhakiki kuwa ni jumla ya maelekezo

yanayomsaidia msomaji au mhakiki kuifahamu kazi ya fasihi kwa kufuata utaratibu maalumu.
Wanadokeza zaidi kuwa dhana hii hurejelea istilahi ya kijumla inayomaanisha mwongozo
unaomwelekeza msomaji wa kazi ya fasihi kuifahamu kazi hiyo vizuri katika vipengele mbalimbali
vya kazi ya fasihi na namna vinaunganika kuleta umoja katika kazi husika. Wamitila (2003) anaeleza
kuwa nadharia za uhakiki hutumiwa kumaanisha kauli za kijumla au kaida zinazomwongoza
msomaji katika ufasiri wa maana iliopo katika fasihi. Kwa mfano, katika kuelewa maudhui katika
kazi ile ya fasihi.

Uhusiano uliopo baina ya uhakiki wa kifasihi,nadharia ya fasihi, na nadharia ya uhakiki wa fasihi ni

kuwa istilahi hizi zote zinategemeana. Mhakiki anahakiki na kuzichambua kazi za kifasihi ka kuwa
anaelewa nadharia ya fasihi na muundo unaojumuisha kazi hiyo ya fasihi.

Pia mhakiki hana budi kuelewa ndharia ya uhakiki inayoongoza kazi fulani ya kifasihi. Wakati wa
uhakiki,mchambuzi lazima aelewe nadharia inayoongoza kazi anayoichambua ili apate uamuzi wa
jinsi ya kuhusisha mawazo yanayopatikana katika kazi hiyo. Kabla ya hayo mhakiki anapohakiki
lazima aelewe kuwa kazi hiyo anayoichambua inahusu nini, ni aina gani ya fasihi? Hivyo vyote
kuvielewa vitampa mwelekeo fulani wa kuhakiki kila kazi anayoitaka.

Kwa hiyo istilahi hizi zote hazina budi kutegemeana katika kazi zote za kifasihi.

Marejeleo
Castle, G. (2007). The Blackwell Guide to Literary Theory. Blackwell Publishing: USA.

Mlaga, K.W. (2017). Msingi ya Ufundishaji na Ujifunzaji wa Fasihi, Karne Ya 21. Heko

Mulokozi, M.M. (2017) Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili: Kozi za fasihi vyuoni na vyuo vikuu.

Njogu, K, na R.M Wafula (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. The Jommo Kenyatta Foundation.
Nairobi.

Ntarangwi, M. (2004). Uhakiki wa kazi za Fasihi. Augustana College, Rock Island, IL612
PermalinkShow parentReply

In reply to Dr. Wallace Mlaga

Re: Mjadala kuhusu nafasi ya moduli hii katika kumsaidia mjifunzaji kutekeleza
majukumu yake ya sasa na ya baadaye

by FAUSTIN NDIKUBWIMANA - Monday, 28 June 2021, 1:55 PM

Uhakiki wa Fasihi

Ntarangwi( 2004) uhakiki wa fasihi ni kitendo cha kutathimini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni
juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalumu. Uhakiki
ni uchambuzi na kueleza kazi fulani ya kifasihi.Wamitila (2002) kwa mujibu wake, uhakiki ni
uchunguzi wa kazi ya kifasihi kwa makini na kwa utaalamu.Ni kufasili kazi ya kifasihi na kueleweka
zaidi kwa msomaji. Uchunguzi wa aina hii huchunguza uchanganuzi, fasiri, uelezaji, ufafanuzi,
tathimini na utoaji wa kauli ya kijumla.(Peck & Coyle)

Uhakiki ni utathmini, ufasili na uainishi wa kazi za fasihi, lakini haumaanishi kutafuta makosa ya
kazi hiyo. Kwa hiyo, Uhakiki ni kitendo cha kuchambua, kutathmini na kuainisha kazi ya fasihi ili
kuona ubora na udhaifu wa kazi hiyo kwa kutumia vigezo husika vya fani na maudhui kwa
kuegemea kwenye uzoefu binafsi wa mtu, nadharia fulani, au vionjo vya mtu binafsi vya kiujumi.

Mulokozi (2017) anabainisha kuwa uhakiki (wa fasihi) ni mchakato wa kitaaluma unaojumuisha
fasili, uchambuzi na tathimini ya kazi ya fasihi. Mlaga (2017) naye anabainisha kuwa uhakiki wa
fasihi ni uchambuzi na ufafanuzi wa vipengele vya fani na maudhui katika kazi ya fasihi. Ina maana
kuwa mchambuzi anafuata vipengele vya uchambuzi kama vile maudhui na fani vinavyopatikana
kazi anayoichambua.

Nadharia za Uhakiki

Castle (2007) anafafanua nadharia ya uhakiki kuwa ni kanuni na dhana, mikakati na mbinu
zinazohitajika kuongoza zoezi la kihakiki. Hii ina maana kuwa nadharia za uhakiki ni kaida maalum
zinazoongoza uhakiki. Mlaga (2017) anafafanua nadharia za uhakiki kama miongozo ya usomaji na
ufafanuzi wa kazi za fasihi. Yeye anataka kumaanisha kwamba kazi moja ya fasihi inaweza
kusomwa na kufafanuliwa kwa namna zaidi ya moja kutokana na nadharia zilizotumiwa kwa
kuhakiki kazi hiyo. Wafula na

Njogu (2007) wanafafanua na kupambanua nadharia za uhakiki kuwa ni jumla ya maelekezo

yanayomsaidia msomaji au mhakiki kuifahamu kazi ya fasihi kwa kufuata utaratibu maalumu.
Wanadokeza zaidi kuwa dhana hii hurejelea istilahi ya kijumla inayomaanisha mwongozo
unaomwelekeza msomaji wa kazi ya fasihi kuifahamu kazi hiyo vizuri katika vipengele mbalimbali
vya kazi ya fasihi na namna vinaunganika kuleta umoja katika kazi husika. Wamitila (2003) anaeleza
kuwa nadharia za uhakiki hutumiwa kumaanisha kauli za kijumla au kaida zinazomwongoza
msomaji katika ufasiri wa maana iliopo katika fasihi. Kwa mfano, katika kuelewa maudhui katika
kazi ile ya fasihi.

Nadharia ya Fasihi

Kuna waandishi tofautitofauti ambao walielezea juu ya naharia ya fasihi kama ifuatavyo;
Fasihi ni sanaa yaani mkusanyiko wa kazi mbalimbali zilizosanifiwa kwa kutumia lugha itumiayo
zaidi maneno na kujishughulisha na jinsi binadamu anavyojitambua mwenyewe binafsi, pia
anavyoathiriwa na binadamu wenzake aidha na viumbe vingine aina kwa aina katika mazingira
mbalimbali ya maisha(Nkwera, Fr.F.V,2003:94) . Fasihi ni kazi ya sanaa inayotumia lugha
kuwasilisha ujumbe kwa hadhira au jamii iliyokusudiwa.

Fasihi ni sanaa ya lugha inayoshughulikia masuala yanayomhusu binadamu matatizo yake ,ndoto
zake,matumaini yake,migogoro yake na jinsi anavyoingiliana na mazingira yake.(Wamitila,2004:19).
Fasihi ni kazi ya sanaa inayotumia lugha kuwasilisha ujumbe au fikra za fanani. Fasihi ni kitu
chochote kilicho kwenye maandishi. Hii fasili ina mapungufu sana, kwani fasihi si lazima yawe
maandishi, masimulizi pia yanaweza kuwa ni fasihi, lakini piasi chochote kilichokwenye maandishi
ni fasihi kwani fasihi ni lazima kuwa matumizi ya lugha ya kisanaa.

Fasihi ni sanaa itoayo maudhui yake kwa kutumia lugha ya maneno ambayo hutamkwa ama
kuandikwa.(Senkoro F.E.M.K,2011:11). Fasihi hutoa ujumbe kupitia maandishi na masimulizi.
Tigiti Sengo na Kiango wanasema, fasihi ni mwamvuli wa mtu na jamii na utu na maisha wa hadhi
na taadhima.Fasihi yaweza kuelezwa kwamba, hutegemea msanii ambaye huiumba kwa maneno
katika tukio maalum (Finnegan, 1970).Ni fasihi inayotegemea mdomo katika kutolewa na kuenezwa
kwake (M.L.Matteru, 1979).Ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa,
kuwasilishwa na kusambazwa kwa waasikilizaji na watumiaji waake (Balisidya, 1983).

Fasihi ni maandishi yanayohusu nchi au bara fulani, maandishi hayo sharti yawe ya kubuni.
Ukiangalia fasili hii ina upungufu kwani fasihi si lazima yawe maandishi inaweza kuwa ni
masimulizi, na si lazima yahusu nchi ama bara fulani, hivyo fasili hii inapotosha ukweli kuhusu
fasihi.

Kwa mtazamo wangu kutokana na maana za waandishi tofautitofauti ambao wametoa maana ya
fasihi mimi nimeona kuwa fasihi ni kazi ya sanaa inayotumia lugha katika njia masimulizi au
maandishi kwa kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa jamii husika katika kuikabili mazingira yake
katika nyanja mbalimbali za maisha kamavile siasa uchumi, na utamaduni.