Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 142

Mgodi 2.

0
Geuza Maandishi Kuwa Pesa Mtandaoni

Amosi Nyanda
TARATIBU ZA KISHERIA

Kitabu hiki kimeandikwa na “Amosi Nyanda”, haki zote


zipo chini ya Amosi Nyanda.

Haki zote zimehifadhiwa, huruhusiwi kunakili, kudurufu au


kutumia sehemu ya kitabu hiki bila idhini ya mwandishi.

Kufanya hivyo itakuwa ni ukiukwaji wa haki za mwandishi,


na ukiukwaji wa taratibu hii unaweza kupelekea
mashitaka toka kwa waandaji wa kazi hii.

Kimesanifiwa na Kupangwa na Andrew Rwela


0743 200 738
rwelaandrew@gmail.com
Dar es salaam, Tanzania
UTANGULIZI

“Kutoka Katika Dawati La


Amosi Nyanda”

Arusha, Tanzania
September 2021

Rafiki Mpendwa…
Kitabu hiki nimekiandika Kama mwendelezo wa kitabu
cha Kwanza cha Copywriting skills kinachoitwa MGODI,
na hii imetokana na matokeo makubwa zaidi ya kitabu
cha kwanza baada ya kupokea Mvua ya shuhuda za kila
aina kutoka kwa wasomaji makini na wenye kiu ya
mafanikio kama wewe…

…kwahiyo Kama hujasoma kitabu cha kwanza, tafadhali


kakisome kwanza na kama umekisoma cha kwanza na
leo umekipata hiki cha pili basi lazima washindani wako
wataimba haleluyah!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | i


Hivi Inawezekana Kuuza Bidhaa/huduma yako Bila
Kufungua Mdomo?...

…Baada ya kusoma kitabu hiki, utagundua ni jinsi gani


ilivyo rahisi kumfanya mtu yeyote afanye maamuzi ya
kununua kile unachokiuza kwa kutumia Maandishi Tu
(Kwa Kucheza na maneno Tu)

Ukisoma mpaka mwisho wa kitabu hiki, utakuwa na


uwezo wa kuandika tangazo lolote lenye kuchapisha
(kuprint) Pesa mtandaoni katika soko lolote kwa kutumia
maandishi ya ajabu yaliyofichwa ndani ya kitabu hiki…
kwasababu utajua jinsi ya kuwasaliana (sio kuongea) na
wateja kwa kutumia maandishi na kuwafanya wachukue
hatua unayoitaka

Yaani utajua Siri ya kugeuza Maandishi kuwa pesa


mtandaoni…

…LAKINI kabla ya kufungua sura ya kwanza ya kitabu hiki


nataka Mimi na wewe tukubaliane kitu kimoja kwanza,
Naomba useme maneno yafuatayo kimoyomoyo…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | ii


“Mimi… (Jina lako) naahidi kwamba sitozitumia Siri hizi
Kuumiza wengine bali nitazitumia kwa lengo la kuwasaidia
kutatatua changamoto zao kwasababu ndio kitu sahihi
kwao”

Tayari?... Okay vizuri Sana nakuamini, sitaki nikuchoshe


Sana tuingie mgodini sasa au sio?...

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | iii


SURA YA KWANZA

“SIRI yenye Umri wa Zama za


Pilato Kwenye Biashara”…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 1


Karibu katika Ulimwengu wenye faida na uwezo wa
kukupa kila kitu unachotaka ambao watu wengi bado
hawajashtukia uwepo wake…

Kila kitu unachokitaka katika maisha yako Pesa za


kutosha, heshima kutoka Kwa wale wanaokudharau Kwa
sasa, mafuriko na mvua ya wateja, nyumba Kali, Mwanzo
mpya, asali wa moyo wako yaani karibia kila kitu…
utavipata vyote hivyo kwa kujenga uwezo wa KUUZA
(Salesmanship)

…na ukitumia huo uwezo wa kuuza vizuri katika


matangazo yako basi dunia itakujua tu hata kama unaishi
buza kwa mpalange

Katika kitabu hiki—nitakufundisha kila kitu nilichojifunza


ndani ya miaka mtano Kama Copywriter wa Kitanzania na
itakuchukua siku au masaa kadhaa tu ya kusoma kitabu
hiki na kitaenda kubadilisha maisha pamoja na biashara
yako moja kwa moja

Kama bado hauna bidhaa yoyote ya kuuza mtandaoni,


basi nitakuonesha jinsi ya kutengeneza ndani ya wikiendi
moja tu

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 2


Kama tayari una biashara basi nitaenda kukuonesha jinsi
ya kuongeza mauzo yako mara 10 zaidi ya washindani
wako ndani ya usiku mmoja tu

Kama unaogopa kuuza basi nitaenda kukugeuza mashine


ya kuuza ndani ya wiki moja tu

Ninachoenda kukufundisha katika kitabu hiki ni SIRI za


Juu zaidi za Kutangaza na kuuza chochote kwa njia ya
maandishi ambazo hazijawahi kubadilika tangu enzi za
Romania (ancient rome) na Babiloni (Babylon)

Kitabu hiki nimekiita “MGODI” Kwasababu sio maalumu


Kwa ajili ya wajasiriamali wenye pesa za kupoteza na
kuchezea katika matangazo yao bali ni…Maalumu na
EXCLUSIVE kwa ajili ya wajasiriamali wanaotaka
kuandika/kutengeneza matangazo yenye kuchapisha
(kuprint) pesa Mtandaoni watakazopeleka benki kesho
yake asubuhi

Hii ndio Ahadi pekee ninayoihitaji Kutoka Kwako


—“Naenda kukupa ufunguo wa uhuru wako, SIRI hizi
zinaenda kuyabadilisha maisha yako kwa namna ambayo
hujawahi kuwaza hata siku moja, kitu pekee

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 3


ninachokuomba ni hiki hapa, niahidi kwamba hutozitumia
siri hizi kutapeli na kuibia watu kwasababu siri hizi hizi
hutumiwa na nguli wa matangazo duniani vile vile
hutumiwa na matapeli nguli duniani

…sema kimoyo moyo na apa kwamba hutofanya hivyo—


Najua umeshasema hivyo kule mwanzoni ila nilitaka tu
kujihakikishia?..

Nakuahidi kwamba ukizitumia mbinu hizi Kwa njia halali


zitakuwezesha kutengeneza pesa nyingi, kuwa na jina
sokoni, na usiku utalala kwa amani kama mtoto mchanga
Ukweli ni kwamba katika biashara yako pesa hazipo
katika kile unachokiuza aidha ni bidhaa/huduma, pesa
zipo kwenye uwezo wako wa kuuza hiyo bidhaa/huduma
Mentor wangu wa pili (John Carlton) aliwahi kuniambia
hivi….

“Tangazo zuri linaweza kuuza bidhaa/huduma ambayo


haipo na tangazo baya haliwezi kuuza hata Dhahabu ya
BURE”

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 4


Siri ya kuuza kwenye maandishi ambayo haijawahi
kubadilika tangu enzi za Romania na babiloni ni —
Kutumia Saikolojia ambayo haijawahi kubadilika ya sisi
kuwa wanadamu

…na Hii ndio SIRI na Saikolojia ya Kuuza Chochote aidha


ni Kibaya au Kizuri inayotumika enzi na enzi

“Tengeneza Uaminifu (Trust) Kwa walengwa wako,


Simulia Story inayoaminika na yenye kuendana na hali
yao (ambatanisha na shuhuda kabisa), halalisha gharama
zozote za kile unachokiuza kwa kuwapa sababu ya
Kwanini umeweka hiyo gharama au bei, kisha ahidi
kuwasaidia walengwa wako kutoka kwenye maumivu na
kutimiza hitaji linalowanyima usingizi kila siku usiku kwa
kutumia kile unachotaka kuwauzia aidha ni
bidhaa/huduma then booom”

Ila pesa hazipo kwenye hiyo siri, pesa zipo kwenye jinsi
utakavyoitumia hiyo siri na hii ndio sababu ya mimi
kuwepo hapa ili nikuongoze hatua kwa hatua na muda sio
mrefu tutaanza kuchimba madini hatua kwa hatua!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 5


SURA YA PILI

PESA Katika Tangazo Lako


Zipo Kwenye Maneno Haya…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 6


Watu wengi wanapima uzuri wa tangazo kwa kuangalia
urembo wake badala ya uwezo wake wa kuleta wateja na
kuuza bidhaa/huduma zao…

Watu hawanunui kile unachouza kwasababu umeremba


vizuri tangazo lako

Watu hawanunui kile unachouza kwasababu unajua zaidi


na una akili nyingi kuliko wao

Watu hawanunui kile unachouza kwasababu


umewaambia wewe ni mtaalamu

Na Watu hawanunui kile unachokiuza kwasababu


bidhaa/huduma yako ni nzuri

Watu wananunua kwasababu tangazo lako limewaonesha


kwamba limewaelewa zaidi ya wanavyojielewa wao—watu
huwa hawanunui vitu kwasababu ni vizuri au
wamevipenda watu huwa wananunua vitu kwasababu
wamehisi wameeleweka kwa muuzaji au mwandishi wa
tangazo.

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 7


Ndio maana ukienda mtaani au mtandaoni utaona kuna
rundo la bidhaa/huduma nzuri kibao na hazina wateja
shida sio bidhaa, shida ni uwezo wa kuuza wa mwenye
hizo bidhaa

Usisahau kwamba tangazo lako ni mtu wako wa mauzo


Siri ambayo watalaamu wachache sana wa matangazo
wanaijua ni kwamba—binadamu ni kiumbe mbinafsi mno
linapokuja swala la kununua kitu huwa hajali wala kuwaza
chochote wakati wa kununua bidhaa zaidi yake yeye
mwenyewe tu

..na ukitaka kumuuzia mtu kitu chochote lazima atapinga


kwasababu hakuna mtu anayependa kuuziwa ila kila mtu
anapenda kununua

Leo nataka nikupe SIRI ya Kumfanya Mteja wako afungue


waleti yake na anunue chochote unachokiuza na mapigo
yake ya moyo yaende mbio baada ya kuona tangazo lako
popote Inayoitwa—“The Function Of Seduction”

Mbinu ya “The Function of Seduction” inasema hivi….

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 8


Kama nitajaribu kukuuzia chochote lazima
Utapinga/utajizuia kununua…LAKINI… Kama nitaiteka

ATTENTION yako kwanza kupitia kichwa cha habari cha


tangazo (Headline)…

…kisha nikakuahidi kukupa SOLUTION ya tatizo lako


linalokunyima usingizi kila siku usiku
Halafu nikaielezea hiyo SOLUTION kiasi kwamba ukaona
huna cha kupoteza zaidi ya kupata Faida

Na nikakwambia naelewa jinsi unavyojisikia pamoja na


kukuondolea hofu na kujibu vipingamizi vyote
ulivyonavyo kichwani mwako kwa kulielezea tatizo lako
vizuri zaidi ya unavyoweza kulielezea wewe mwenyewe

Halafu nikakujengea picha ya jinsi utakavyokuwa


kifedha, kiafya na kimahusiano kwa muda mfupi zaidi
baada ya kutumia kile ninachokiuza…

Na mwisho nikarahisisha jinsi ya kukipata kile


ninachokiuza (CTA) —Basi Kwa 100% lazima utanunua
kile ninachokiuza”

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 9


Je umegundua Siri gani iliyopo nyuma ya mbinu inayoitwa
—The Function of Seduction?

Ukweli ni kwamba—hakuna sehemu yoyote


palipotangazwa bidhaa, bali ni maelezo ya jinsi ya kumtoa
mteja kutoka kwenye maumivu aliyonayo na kumuingiza
kwenye raha, maelezo yote ni kuhusu mteja pamoja na
solution na sio kuhusu bidhaa/huduma kama wengi
wanavyofanya

Acha washindani wako watangaze bidhaa/huduma zao


wewe Tangaza solution Kwa wateja wako utofauti
utaonekana kwenye akaunti zenu za benki

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 10


SURA YA TATU

Jinsi Ya Kulifanya Tangazo


Lako Lisomwe Zaidi…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 11


Watu wanakutana na utitiri wa matangazo kuanzia
wanapoamka mpaka wanapolala na hakuna mtu mwenye
hamu ya kuona wala kusoma tangazo lako kwasababu
kiasili watu wanachukia matangazo (watu huwa
hawapendi kutangaziwa vitu kwasababu wanachukia
kuuziwa ila wanapenda kununua)

…swali la kila mjasiriamali wa mtandao kwa sasa ni


—“Nawazaje kuwafanya watu wasome tangazo langu na
sio kuona tangazo langu?”, kwasababu kuna tofauti kati
ya tangazo lako kuonekana na tangazo lako kusomwa,
pesa kwenye tangazo lako zipo kwenye kusomwa sio
kuonekana

Kuna Siri Kuu 2 za Kulifanya Tangazo lako lisomwe zaidi


kuliko washindani wako….

…na Siri hizi nilijifunza kutoka kwa nguli wawili wa


Copywriting duniani ambao ni John Carlton na Gary
Bencivenga

Upo tayari kuziona?...Okay Good!

Hizi Hapa…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 12


Siri # 1: Lifanye Tangazo Lako Lisionekana Kama ni
Tangazo Bali ni “Habari MPYA” (Make your Ad Look Like
NEWS…NOT an Ad)…

Moja ya kosa kubwa zaidi linalofanywa na watu wengi


wanapoandika matangazo yao ni kuyafanya matangazo
yao yaonekane kama matangazo

…lifanye tangazo lako lionekana Kama Makala tu yenye


habari mpya zenye faida au manufaa Kwa mlengwa wako
ili alisome kwasababu watu huwa wanayakwepa
matangazo kila wanapohisi ni matangazo kutokana na
hofu ya kuporwa hela zao au kuuziwa vitu

Ukifanya kosa la kuandika tangazo lako likaonekana


Kama ni tangazo walengwa/wateja wako wataliona
sawa…LAKINI…Hawatalisoma (watu hununua vitu baada
ya kusoma tangazo na sio baada ya kuona tangazo)

…KWAHIYO punguza mbwe mbwe zinazoonesha Kama


hili ni tangazo mfano achana kabisa na maneno kama
Ofa, Ofa, Ofa, au Tangazo, Tangazo, nk Muda wote
kumbuka watu wanayachukia na kuyakwepa matangazo
kama ukoma!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 13


Siri # 2: Lifanye Tangazo Lako Kama Jinsi Lilivyo
Lionekane Lina FAIDA/Manufaa Kwa Walengwa wako
(Make your Ad itself look, feel and actually be Valuable to
your Target audiences)

Andika tangazo lenye kutoa uthamani Kwa walengwa


wako kabla halijataja bidhaa/huduma yako kiasi kwamba
mteja akiamua kutumia zile tu taarifa zilizopo kwenye
tangazo lako anaweza akatatua nusu ya changamoto
yake…

Unatangaza Kwa kutoa uthamani bure wenye kutatua


changamoto inayotatuliwa na bidhaa/huduma yako lakini
usizidishe uthamani kiasi kwamba mteja akakosa ulazima
wa kununua bidhaa/huduma yako—hapa unatoa uthamani
kidogo ili kutengeneza kiu kisha unauza maji baadae

Mfano kama kuna hatua 5 za kufuata ili kutatua


changamoto Fulani ya mteja wako basi wewe kwenye
tangazo unazitaja angalau 2 kisha zilizobaki zitamfanya
mteja afungue waleti yake kununua bidhaa/huduma yako
ili apate zile hatua 3 za mwisho—umepata picha?...okay
vizuri sana

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 14


Kwa kifupi tengeneza tangazo kiasi kwamba hata Hilo
tangazo lenyewe tu linakuwa na Faida au manufaa kwa
msomaji kabla halijatangaza bidhaa/huduma yako
mwishoni (Tangazo libebe Uthamani Fulani kwa walengwa
wako kabla ya kuuza bidhaa/huduma yako)

Mfano…

Miaka ya 90’s nguli wa copywriting Duniani David Ogilvy


aliandika Copy yenye Sifa 47 za tangazo lenye kuuza
zaidi, baada ya hapo ndipo mwishoni akatangaza kitabu
chake cha Copywriting skills—hata kama ungekuwa ni
wewe ungeacha kununua kitabu chake wakati tayari
ameshakupa Siri 47 BURE zitakazokusaidia kuandika
matangazo yako?...

P. S. Kumbuka Vitu Vifuatavyo Kila Unapoandika Tangazo


Lako…

Kazi Kubwa Zaidi ya Tangazo lako Sio Kuuza


Bidhaa/huduma Yako ni Kuuza “KUBOFYA” (clicks) …
KWASABABU ni ngumu sana kumuuzia mtu
bidhaa/huduma moja kwa moja kutoka kwenye
tangazo lako kazi ya tangazo ni kuwafanya watu

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 15


wachukue hatua aidha ni kupiga simu, kubofya link, au
kuja inbox (Dm) anayeuza ni WEWE!

Na Lengo kubwa zaidi la tangazo lako ni kuteka


ATTENTION ya wateja wako na kuwafanya wachukue
hatua aidha wabofye link, waje inbox, wapige simu,
watazame video, watembelee website nk na sio
Kununua Kile Unachokiuza moja kwa moja

Siri hii nilijifunza kutoka Kwa Sabri Suby mwandishi wa


kitabu cha “Sell Like Crazy”

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 16


SURA YA NNE

Jinsi ya Kuandika HEADLINE Yenye


Sumaku Kwa Walengwa Wako…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 17


Kichwa cha Habari (Headline) cha tangazo lako ndicho
kipengele muhimu zaidi katika tangazo lako kuliko
kipengele chochote kile katika tangazo zima kwasababu
60% ya watu husoma kichwa cha habari pekee

Nguli wakubwa wa matangazo duniani (Savvy


Copywriters) hutumia 90% ya muda wao kuandika
Headline tu pindi wanapoandika Tangazo lolote…

…na HEADLINE ya Tangazo lako lazima ifanye kazi kubwa


mbili tu ambazo ni…

1) . Kuteka ATTENTION nzima ya walengwa wako (Target


audiences)…na…

2) Kuwaleta Walengwa Wako Kwenye Tangazo

Njia ya mkato ya kupata attention ya mtu yeyote Kwa


haraka zaidi ni kuita au kutaja jina lake

Swali ni je utawezaje kujua jina la kila mtu


mtandaoni?...Jibu ni Hauwezi wala haina haja

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 18


Ila mbadala wa jina ni kutumia maneno yatakayowalenga
na kuwabagua wahusika wa kile unachokiuza moja kwa
moja baada tu ya kukutana/kuona Tangazo Lako…kiasi
kwamba baada tu ya kuona Headline mlengwa anajua
kabisa tangazo hili amaeandikiwa yeye kutokana na
maneno yalitumika kwasababu umewaita moja kwa moja

….angalia mifano hapa chini..

MFANO #1: “Tiba MPYA Ya Kitambi Yagunduliwa na


Mwanasayansi wa Kitanzania”—(Headline Hii imewaita
kina nani?..ndio upo sahihi ni wenye Vitambi)

Mfano # 2: “Soma Hii Kabla Hujauza Gari Yako”—


(Headline hii imewaita wenye magari na wanaotaka kuuza
magari yao)

Mfano # 3: “Ujumbe Mfupi Kwa Watu Waliopo Single Tu”—


(Headline Hii imewaita waliopo single tu)

Mfano # 4: “Attention WEBSITE Owners!”— (Headline hii


imewaita wenye website tu)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 19


Mfano # 5: “Je wewe ni Mjasiriamali Mwenye Changamoto
Hii?”— (Headline hii imewaita Wajasiriamali wote)

Umepata Concept sasa?...

Okay vizuri sana!

Vilevile… HEADLINE.. ya tangazo lako lazima iwe imebeba


Kitu Kimojawapo kati ya Hivi hapa…

1) Habari MPYA (News) ambazo zinawagusa walengwa


wako moja kwa moja

Mfano; Tiba MPYA ya Kupunguza Uzito bila Kujinyima Kula


wala Kufanya Mazoezi

2) Ahadi Yenye FAIDA (Benefits) Kwa Walengwa Wako


moja kwa moja

Mfano: Dawa MPYA Ya Asali Itakayofanya Kuonekana


Kijana mara 20 zaidi ya hapo ulipo!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 20


3) Iibue UDADISI (Curiosity) kichwani kwa Walengwa
wako

Mfano: Kwanini hutakiwi Kula Vyakula Vya Aina Hii Kama


Unataka Kutokomeza Kitambi?

LAKINI… Hii hapa Formula ya SIRI ya Kuandika Headline


yenye Kuwanasa Walengwa wako Moja Kwa moja Chini
ya dkk 5 Tu…

Formula hii nilijifunza kutoka Kwa miongoni mwa nguli wa


Copywriting anayeitwa “John Carlton” inasema hivi…

“Soma Hii Kama Unataka… [Weka MATOKEO


Wanayoyataka Walengwa Wako]”…

…angalia Mifano yake hapa chini…

Soma Hii Kama Unataka Kupunguza Uzito…

Soma Hii Kama Unataka Kuandika Matangazo


mazuri…

Soma Hii Kama Unataka Kujiajiri….nk

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 21


Umeona jinsi ilivyokuwa rahisi kutumia Formula hii?..Okay
kazi kwako!

Ooh Kabla sijasahau ngoja nikupe Hii Formula ya Mwisho


ya Kupata HEADLINE Kali na haraka Zaidi Niliyojifunza
kutoka Kwa Russel Brunson Inayosema hivi…

“Jinsi ya… [Kupata Matokeo Wanayoyataka Zaidi]…Bila…


[Kufanya Kitu Wanachokihofia, Kukiogoapa na kukichukia
Zaidi]…

…angali mfano hapa chini…

Jinsi ya Kupunguza Uzito Bila Kujinyima Kula…

Jinsi Kupunguza Kitambi bila Kufanya Mazoezi…

Jinsi ya Kupata Kazi Bila Kufanya Usaili (interview)…

Umeona jinsi Formula hii inavyofanya kazi?...yaani


unaweka jinsi ya kukipata kitu wanachokitaka zaidi
walengwa wako bila kufanya kitu wanachokichukia na
kukihofia au kukiogopa zaidi then boom!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 22


KWAHIYO..Kama unataka kuandika Headline
Itakayowafanya Walengwa wako Waache chochote
wanachokifanya na wasome tangazo lako hakikisha
umetumia Formula Moja au umegusa kipengele
kimojawapo kati ya hivyo hapo juu

Kumbuka kazi ya HEADLINE ya Tangazo sio Kuuza Wala


kutangaza Bidhaa/huduma yako—kazi ya HEADLINE ni
Moja tu ambayo ni Kuteka “ATTENTION” (umakini) ya
walengwa wako ili waache chochote wanachokifanya na
wasome tangazo lako!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 23


SURA YA TANO

Formula Kuu Tatu (3) za Kufungua


Tangazo Lako Baada ya… HEADLINE
(Opening paraghraph)…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 24


Baada ya Headline ya tangazo lako kipengele kingine cha
muhimu zaidi kwenye tangazo lako ni jinsi unavyolifungua
baada ya headline…KWASABABU hapa ndipo
unamuandaa na kumpa mteja wako sababu ya kuendelea
kusoma tangazo lako au aendelee na mishe zake

…na hapa ndipo watu wengi wanapowapoteza wateja


kibao licha ya kuwa na Headline nzuri

Tayari Headline yako imeshamleta mteja wako mpaka


mlangoni na ameshaacha kila kitu anachokifanya tayari
kwa kukusikiliza na kazi iliyobaki ni ufunguzi wako
kumfanya mteja akae na asikilize kile ulichomhaidi
kwenye Headline yako

Kuna SIRI kuu 3 unazoweza kuzitumia ili kufungua


tangazo lako lenye kumfanya mteja wako asome mpaka
mwisho

Upo tayari kwa Madini?..Okay Good!...tuzame mgodini…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 25


Siri # 1: “Kama…Basi… (If…Then..Introduction)”
Angalia mfano wa Jinsi ya kufungua tangazo lako kwa
kutumia Siri Hii inayoitwa—“Kama…Basi”

Headline: “Jinsi Ya Kupunguza Uzito Ndani Ya Siku 21 Bila


Kujinyima Kula”…

Opening Paragraph (Ufunguzi): “Kama” Umekuwa


Ukitafuta Njia rahisi ya Kupunguza uzito bila kujinyima
Kula…”Basi” Soma Mpaka mwisho…

…KWAHIYO tangazo lako litasomeka Kama Ifuatavyo….

“Jinsi Ya Kupunguza Uzito Ndani Ya Siku 21 Bila


Kujinyima Kula…

Kama Umekuwa ukitafuta njia rahisi ya kupunguza uzito


bila kujinyima kula…Basi soma mpaka mwisho…”

Umeona uhusiano (connection) uliyopo kati ya Headline


ya tangazo na ufunguzi wa tangazo lako?...

Siri ni kwamba lazima kuwe na mwendelezo wa Ahadi ya


kwenye Headline kwenye ufunguzi wa tangazo lako—we

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 26


usifanye kosa la kuweka mada mbili tofauti kati ya
headline na ufunguzi wa headline kosa hili pekee
limewagharimu watu wengi sana mauzo kwa kuwa na
ufunguzi ambao hauna uhusiano (connection) na
Headline

Siri # 2: “Jitambulishe wewe ni nani pamoja na Kile


Unachokifanya… (Mbinu hii inaitwa— Niambie Wewe ni
Nani na kwanini umeandika hii kwa ajili yangu)

Unaweza ukaona ni kitu kidogo lakini kina maana kubwa


sana kwa walengwa wako hasa hasa kwenye matangazo
ya kulipia…KWASABABU wengi hawakujui na wala
hawajawahi kukusikia popote kwahiyo ukifanya hivyo
utakuwa umewarahisishia kazi ya kukujua pamoja na
kuwapa sababu ya kusoma tangazo lako

…angalia mfano hapa chini wa jinsi ya kufungua tangazo


lako kwa kutumia mbinu hii ya kujitambulisha…

Headline: Jinsi Ya Kupunguza Uzito Ndani Ya Siku 21 Bila


Kufanya Mazoezi…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 27


Ufunguzi (Opening paragraph): Jina langu ni Shamanonga
shukia, Nawasaidia wenye uzito mkubwa kupunguza uzito
kwa kutumia Formula maalumu ya “HAFK” na ndani ya
miaka 3 hiki ndicho nilichokigundua….( Anza Kutiririka
sasa)

…KWAHIYO kwa kutumia siri hii Tangazo lako litasomeka


kama ifuatavyo…

“Jinsi ya Kupunguza Uzito Ndani Ya Siku 21 Bila Kufanya


Mazoezi…

…Jina langu ni shamanonga shukia, Nawasaidia wenye


Uzito Mkubwa kupunguza uzito kwa kutumia Formula
Maalumu ya HAFK na ndani ya miaka 3 hiki ndicho
nilichokigundua

Siri # 3: “Hata…Kama” (Even…If…Introduction)…

Hii ni moja ya silaha zangu za siri kila ninapoandika


tangazo lolote na sababu ni moja tu –wateja wanajua
umewaelewa na kusoma akili zao kwasababu mbinu hii
inajibu swali ambalo tayari wanaliwaza kichwani muda
wote na kama tunavyojua kwamba wateja hawanunui

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 28


kwasababu wameielewa bidhaa/huduma, hununua
kwasababu wamehisi wameeleweka kwa muuzaji wa
bidhaa/huduma

…na jinsi ya kuitumia mbinu hii katika tangazo lako ni


kuanza kwa kujiuliza ni kipingamizi gani mteja wako
atakuwa nacho kichwani mwake kuhusu bidhaa/huduma
yako?

Tuchukulie mfano Kama unataka kuuza program ya


kupunguza uzito…unadhani ni kipingamizi gani mtu
anayetaka kupunguza uzito atakuwa nacho kichwani
mwake?

Tuseme ni hiki hapa—“Nilishajaribu program nyingi nyuma


lakini sikuona matokeo yoyote”

…KWAHIYO kwa kutumia siri hii ya “Hata..Kama” ufunguzi


wa tangazo lako utasomeka kama ifuatavyo…

Mfano….

Headline: Jinsi ya Kupunguza Uzito Ndani ya Siku 21 Bila


Kufanya Mazoezi…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 29


Ufunguzi (Opening paragraph): Hata Kama umeshajaribu
program zingine kipindi cha nyuma bila mafanikio soma
mpaka mwisho ili kugundua utofauti wa program hii na
zingine… (Mpaka hapo tayari umejibu swali la mteja wako
kichwani mwake kisha endelea kutirirka Kama kawaida)
…na tangazo lako litaonekana hivi…

Jinsi ya Kupunguza Uzito Ndani ya Siku 21 Bila Kufanya


Mazoezi…

…Hata Kama umeshajaribu program zingine kipindi cha


nyumba bila mafanikio soma mpaka mwisho ili kugundua
utofauti wa program hii na zingine…

Kazi kwako sasa kuchagua ufunguzi wa tangazo lako


utakaokupendeza zaidi ila siri zote tatu ni za moto na
zinafanya kazi kama uchawi—ila tu usitumie zote kwa
pamoja katika tangazo moja kila siri inajitegemea hapo
chagua moja tembea nayo kwenye tangazo lako then
booom!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 30


SURA YA SITA

Saikolojia ya Juu Zaidi ya


Kuuza Kwenye Maandishi
(Siri kuu Tisa za Kuuza Kwenye
maandishi)…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 31


Wateja hufanya maamuzi ya kununua vitu Kwa kutumia
hisia (Emotions) halafu wanahalalisha maamuzi yao kwa
kutumia mantiki (logic)—Ili kuuza kitu chochote unatakiwa
kuijua saikolojia ambayo haijawahi kubadilika
inayowafanya watu kununua vitu

…ukweli ni kwamba hakuna bidhaa/huduma inayofeli


sokoni kwasababu ya bidhaa/huduma yenyewe bali inafeli
kwasababu ya uwezo wa kuuza wa muuzaji

Hii ndio Saikolojia Inayowafanya watu wafungue pochi


zao na mapigo ya moyo kwenda mbio kila wanaposoma
tangazo lako…

Watu ni wagumu kutoa pesa ili kuzuia Tatizo


Lisitokee…ila watakausha akaunti zao za benki ili
kujitoe kwenye hilo Tatizo baada ya kutokea…

Mfano hakuna mtu anayefanya diet ili kuzuia asinenepe


ila kila mtu anahangaika kufanya diet ili kupunguza unene
kwasababu tayari ameshaonja machungu ya kunenepa
ndio maana kuna rundo la dawa za kupunguza unene
kuliko kuzuia unene (Ukiuza dawa za kuzuia unene soko
lazima likuchumu)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 32


Siri ni Hapa—Watu hununua Zaidi Vitu ili kutoka kwenye
maumivu kuliko Kuingia kwenye raha…KWAHIYO
waambie kwenye tangazo lako kile unachokiuza
kitawatoa kwenye maumivu gani ambayo tayari wanayo
kuliko kuwaambia watapata kitu fulani kutoka kwenye
bidhaa/huduma yako ambacho hawajawahi kukipata

Njia rahisi na ya haraka zaidi ya kujenga uhusiano na


mtu yeyote ni kumuonesha kwamba upo upande
wake na mnapigana na adui mmoja…

…kwahiyo waambie wateja kwenye tangazo lako kwamba


upo upande wao na kile wanachokitaka wao ndicho
unachokitaka pia na kile wanachokichukia wao nawewe
unakichukia pia—ukifanya hivyo watakuona mwenzao na
upo kwa ajili ya maslahi yao sio yako binafsi …KWAHIYO…
watakupenda, na watakuamini then boom!

Epuka Sana Kutumia Sentensi ambazo zitatengeneza


picha hasi Kichwani Kwa mteja pindi anaposoma
tangazo lako…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 33


Kama utatumia sentensi yoyote katika tangazo lako tumia
ile ambayo ina ahidi manufaa zaidi kwa mteja wako zaidi
ya maumivu, andika vitu vitakavyomfanya ajione yeye
bora zaidi baada ya kutumia bidhaa/huduma yako

…Mfano…Epuka Sana kutumia sentensi Kama…

“Usipofanya hivi utapata madhara haya—badala yake tumia


sentensi Kama…”Ukifanya hivi utapata faida zifuatazo…”

Wote Tunataka Zaidi Vitu Ambavyo Hatuwezi Kuvipata…


Hakuna mtu ambae huwa anaridhika na kile alichonacho
ndio maana kila siku watu wananunua matoleo mapya ya
magari, nguo viatu, simu, nk wakati tayari wanavyo hivyo
vitu

…cha ajabu zaidi ni kwamba binadamu huwa anakitaka


zaidi kile kitu ambacho mtu mwingine anakihitaji hata
kama mwanzo hakuona umuhimu wake—ukweli ni
kwamba kadri unavyomnyima mtu kitu ndivyo
anavyokitaka zaidi na hii ndio sababu ya mbinu inayoitwa
“Take Away” kuwa ndio silaha ya siri kwenye matangazo
mengi

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 34


Kama unataka watu wengi zaidi wakutafute kununua
bidhaa/huduma yako tumia zaidi kauli hii hapa kwenye
tangazo lako…

“Bidhaa/huduma Hii inaweza isiwe Kwa ajili yako…


Kwasababu haikutengenezwa Kwa ajili ya kila mtu”…
utaona jinsi watu wengi watakavyokutafuta ili
wakuonesha kwamba na wao wanataka kuwa miongoni
mwa watu wachache ambao bidhaa yako ni kwa ajili yao

Hata siku moja usiseme kile unachokiuza ni kwa ajili ya


kila mtu kwasababu hutouza kwa mtu yeyote kwasababu
hakuna mtu anayetaka kufanana na kila mtu na bidhaa
yako sio kwa ajili ya kila mtu—kadri unavyomsukuma mtu
ndivyo anavyokuhitaji zaidi na kadri unavyomwitaji zaidi
mtu ndivyo anavyokusuma zaidi huwa ipo hivyo!

Wote Tunataka Kujihisi SPECIAL…

Kila mtu anapenda attention, kila anapenda kuonekana


wa kipekee (Exclusive), kila mtu anapenda kuheshimiwa,
kila mtu anapenda kutamaniwa na kuonewa wivu na
wengine kwasababu ana kitu cha kipekee…KWAHIYO
waambie wateja wako kile unachokiuza kitawapa vitu
vyote hivyo…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 35


kwasababu hii ni kiu ya kila mtu na mbinu hii wanaitumia
sana kampuni ya Apple kuuza bidhaa zao kama Iphones
(Mbinu hii Inaitwa—EXCLUSIVITY)

Hivi ukimuona mtu anatumia simu ya iphone au Laptop ya


Apple (macbook) kichwani kwako inakuja picha gani?...

Watu wengi Hawajawahi Kujihisi Washindi Kwenye


Kitu Chochote…

Wafanye wajihisi ni washindi endapo watanunua


bidhaa/huduma yako…kwasababu kumiliki kile
unachokiuza ni bonge moja la dili mtaani kwa sasa—
unaweza ukaona ni kitu cha kawaida lakini kitakuuzia
bidhaa yako balaa

Kinachowafanya Watu Kununua Vitu ni HISIA


(Emotions)

Watu huwa hawanunui Bidhaa za Urembo Kwasababu ni


Nzuri…Huwa wananunua kwasababu ndani ya vichwa
vyao wanahisi watakuwa wazuri baada ya kuvaa huo
urembo

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 36


…ukweli ni kwamba wote huwa hatununui vitu kama jinsi
tunavyodhani tunanunua, huwa tunajinunua sisi wenyewe
kutokana na picha tunayoijenga kichwani tutakavyokuwa

baada ya kumiliki hiyo bidhaa yaani kwa kifupi huwa


tunajinunua sisi bora zaidi baada ya kutumia
bidhaa/huduma (We buy better version of ourselves)
Kwahiyo unapoandika tangazo lako elezea jinsi mteja
wako atakavyokuwa baada ya kununua bidhaa yako na
sio bidhaa kama jinsi ilivyo yaani wape wateja wako
sababu ya kununua kwa kuwajengea picha ya jinsi
watakavyokuwa baada ya kumiliki kile unachokiuza then
booom!

Mara ya kwanza naisikia kauli hii kutoka kwa mentor


wangu nilijisikia vibaya ila baadae nikaja kuamini ni
kweli, inasema kwamba—Sisi ni Kama KONDOO
Linapokuja swala la kufanya maamuzi ya Kununua
Vitu…

Watu huwa wanahitaji uthibitisho wa watu wengine


kwanza juu ya kile wanachotaka kukukinunua kabla ya
kukinunua hata kama hawakitaki hicho kitu
Ukweli ni huu hapa…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 37


Kuna vitu watu hununua sio kwasababu wanavihitaji,
hununua tu kwasababu wameona watu wengine
wananunua

Watu hununua vitu Kwa hofu ya kukosa au kuachwa


nyuma (FOMO) au kuwa sehemu ya wengi Mfano…kuna
watu wengi Sana walinunua kitabu cha mgodi 1.0 na
mpaka leo hawajawahi kukisoma—ukweli ni kwamba
hawakununua kwasababu wanahitaji kitabu au ujuzi huu
walinunua kwasababu waliona watu wengi wananunua na
shuhuda nyingi zinatoka

Au mfano mwingine huu hapa…

“Movies nyingi za Blockbusters haziitwi Blockbusters…


kwasababu ni nzuri ila zinaitwa blockbusters kwasababu
Watu WENGI..Wanaenda Kuziangalia—ukweli ni kwamba
Movies nyingi tu za Blockbusters ni mbovu”

…Kwasababu watu huwa wana hofu ya kufanya makosa


ya kununua vitu…Kwahiyo waoneshe kwamba wao sio wa
kwanza kununua wala wamwisho ndio maana ni muhimu
kuwaambia maneno yafuatayo kwenye tangazo lako…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 38


Hawatakuwa peke yao endapo watanunua
bidhaa/huduma yako leo—kuna wenzao wengi
walishanunua

Wataachwa pekee yao au watabaki peke yao endapo


hawatanunua bidhaa/huduma yako leo

Ndio maana katika matangazo mengi kuna misemo


Kama…

“Ungana na wateja wetu wengine 100 ambao tayari


wanafurahia huduma/bidhaa zetu

“OFA Ilikuwa kwa watu 50 tu na tayari nafasi 25 za kwanza


zimeshachukuliwa”

Watu Wanapenda Kusikia STORY za Kuhamasisha na


za Kishujaa zinazoitwa—Heroes journey…

Watu wanapitia nyakati mbali mbali katika maisha yao


kila siku, nyakati nzuri na ngumu pia

…kwahiyo watu wengi wanahitaji story za kuhamasisha na


kutia moyo ndio maana Story za kishujaa zinauza zaidi

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 39


(Na hii ndio siri ya movies za marvels kuuza zaidi)

Mfano wa Story za Kuandika kwenye tangazo lako ni zile


ambazo zipo katika mfumo huu hapa chini…

“Nilikuwa sina chochote mwaka 2002 na mambo yalikuwa


magumu sana upande wangu, kuna kipindi nilikosa mpaka
hela ya kulipa kodi, na nilijaribu kila kibiashara lakini
niliambulia patupu, lakini 2015 nikagundua siri ambayo
ndani ya miaka 3 tu ikaniwezesha kupata utajiri huu
nilionao, hali ngumu unayopitia sasahivi ni ya muda
mchache tu, kwasababu nilishakuwa huko na naelewa jinsi
unavyohisi kwa sasa lakini usichoke kupambana wala
usikate tamaa siku yako ipo, mimi nakuamini sana”

…hizi zinaitwa inspirational stories watu wanazipenda


mno kwasababu zinawatia moyo, zinawafariji na
kuwaaminisha kwamba hata wao siku moja watatusua tu
na wanajenga imani kwako pia kwamba hata wewe
ulikuwa kama wao kwahiyo unawaelewa kwasababu
ulishawahi kuvaa viatu vyao…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 40


Kwahiyo watanunua chochote unachowauzia (Watu
hununua vitu sio kwasababu wamevielewa, hununua
kwasababu wamehisi wameeleweka kwa muuzaji)

Kwahiyo simulia story ya jinsi ulivyoanza, changamoto


ulizopitia, na jinsi ulivyofika hapo ulipo—watu wanapenda
kusikia hizo story kwasababu wengi wanatamani kufika
hapo ulipo wewe kwa sasa na hiyo maana ya “safari ya
shujaa” kwasababu wewe ni shujaa wao!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 41


SURA YA SABA

Tumia Neno Hili Unapoelezea


Vipengele Vya Bidhaa Yako Ili
Kutengeneza Picha ya FAIDA
Kichwani Kwa Mteja Wako…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 42


Moja ya siri muhimu zaidi inayotumiwa na wataalamu wa
Copywriting ni uwezo wa kutumia maneno yanayojenga
picha ya faida ya kile kinachouzwa kichwani kwa mteja
pindi anaposoma tangazo lako…

..na KOSA kubwa linalowagharimu watu wengi sana


mauzo kwenye matangazo yao ni kuuza Vipengele
(feautures) vya Bidhaa Badala ya FAIDA (benefits) za
hivyo vipengele kwa mteja

Kuuza Vipengele vya bidhaa pekee yake ni kosa


kwasababu unamuacha mteja na maswali mengi
kichwani bila majibu juu ya kile kinachouzwa na kama
tunavyojua mteja akiwa na maswali yasio na majibu
kichwani mwake juu ya bidhaa/huduma yako hawezi
kununua hata kwa dawa

Hakikisha unapotaja kipengele cha bidhaa/huduma yako


kiwe kimejibu hili swali kichwani kwa mteja
wako….“KWAHIYO?” (So What?)

…angalia mfano hapa chini…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 43


Tufanye unauza simu ya “SAMSUNG Galaxy” halafu
ukaandika vipengele vyake kwenye tangazo lako Kama
hivi…

Ina screen kubwa

Ina camera mega pixel 20

Ina kaa na charge masaa 12

Ina ukubwa wa Gb 16

…Hapo hujauza chochote zaidi ya kutaja vipengele vya


Simu yako..na kwa bahati mbaya 80% ya matangazo ya
simu mtandaoni yapo hivyo (Hapo hujauza simu yako bali
umeonesha na kuielezea tu jinsi ilivyo)

Hakikisha umetaja Faida ya hivyo vipengele vya simu yako


Kwa mteja wako hapo ndipo utakuwa umeuza hiyo simu…
kwasababu utakuwa umejibu swali la kila mteja
linalosema “KWAHIYO?’

Ukisema simu yako Ina ukubwa wa Gb 16 mteja kichwani


mwake atajiuliza—Kwahiyo?

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 44


Ukisema simu yako Ina mega pixel 20 mteja atajiliuliza—
Kwahiyo?

…LAKINI..Vipi Kama unauza Samsung Galaxy yako na


Ukaandika tangazo lako kama hivi hapa chini?...

Ina secreen kubwa—Kwahiyo itakuwezesha kuona


picha na video kwa ubora na kiwango wa HD (clear
zaidi)

Ina camera mega pixel 20—Kwahiyo utaweza kupiga


picha zenye ubora zaidi na utaokoa hela za kumlipa
cameraman

In ukubwa wa Gb 16—Kwahiyo itakusaidia kutunza vitu


vingi zaidi bila simu yako kujaa (videos & picha)

Hembu kuwa mkweli ungekuwa unatafuta simu ya


kununua hasa hasa Samsung halafu ukakutana na hayo
matangazo mawili ungenunua wapi?—(nadhani majibu
unayo)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 45


Umeona nilichokifanya hapo?...ni Kujibu tu swali lililopo
kichwani kwa mteja anaposoma vipengele vya kile
ninachokiuza na njia sahihi ya kuelezea vipengele vya
bidhaa/huduma ni kutumia—Bullets points

…Ooh kabla sijasahu kuna FORMULA ya siri ya kuandika


Vipengele vya bidhaa/huduma yako niliyojifunza kutoka
Kwa Sean Volser (7 Figure Marketing Copy) inayosema
hivi….

“Vipengele vya bidhaa/huduma yako (Features) + Faida ya


hivyo vipengele vya bidhaa/huduma Kwa mteja wako
(Benefits) + Faida ya Hizo Faida Kwa mteja wako (Benefit
of the Benefit)

…kwahiyo unapoelezea vipengele vya bidhaa/huduma


yako hakikisha unatumia hizo Formula hapo juu na
utakuwa miles 1,000 mbele zaidi ya washindani wako
sokoni na katika lugha yangu ya kuzaliwa (Kingereza
haha...)

Formula hii itasomeka kama ifuatavyo….

“FEATURES + BENEFITS + BENEFITS OF THE BENEFITS”

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 46


SURA YA NANE

Huu Ndio Ufunguo wa Uhakika


Uliofichwa wa Kuingia Mfukoni
Kwa Mteja Yeyote Kupitia
Matangazo yako…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 47


Nakumbuka mwaka 2018 wakati najifunza ujuzi wa Kuuza
unaoitwa Closing skills mentor wangu (Danlok) aliwahi
kuniambia kwamba—Wauzaji wazuri ni walimu wazuri
(Kuuza ni Kufundisha na Kufundisha ni Kuuza) maana yake
ni kwamba Unawafundisha watu jinsi ya kuvua samaki
halafu baadae Unawauzia Ndoani…(Hii ndio njia ya mkato
zaidi ya kuuza chochote)

…LAKINI swali kubwa zaidi ni Hili hapa—Kuna SIRI gani


Kubwa Zaidi inayowatenganisha kati ya wauzaji nguli na
wale wa kawaida linapokuja swala la kuuza kwenye
maandishi na kwenye maneno?...

Okay kabla sijakupa jibu ngoja tuangalie hawa wazee wa


madini “Harvard University” (Harvard Business Review)
wanasemaje kuhusu hili?...

Harvard Business Review walifanya utafiti kwa


kuwachukua nguli wa mauzo duniani na kuwauliza
kuhusu SIRI wanayoitumia ili kuwa na uhakika wa kuuza
chochote kwa 100% na hiki ndicho walichokigundua na hii
ndio kauli yao ya mwisho…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 48


“Watu Wengi Wanadhani Kwamba Wauzaji Hatari Zaidi
Duniani ni Wale Wenye Mbinu Nyingi Zaidi za Kuuza
pamoja na Uwezo Mkubwa wa Kujenga Uhusiano na
Wateja Wao ambapo Kiuhalisia ni kweli..Kwasababu Kadri
Unavyojenga uhusiano mzuri na wateja wako ndivyo
unavyojiongezea nafasi zaidi ya kuuza bidhaa/huduma
yako…

…LAKINI..Siri waliyoigundua Harvard Business Review


iliyopo nyuma ya wauzaji hatari zaidi duniani ni hii Hapa…

“Wauzaji Hatari Zaidi Duniani ni Wale wanao-CHALLENGE


Mtazamo wa Wateja wao Kuhusu Tatizo au Solution ya
Tatizo…Kisha Wanatoa Tatizo mbadala pamoja na
Solution ya KWELI Kuhusu Hilo Tatizo” (Najua
nimekuvuruga au sio? hahaha…usijali hata mimi nilikuwaga
naugua ghafla kwenye kipindi cha mwalimu wa Kiswahili—
utaelewa fresh kwenye mfano hapo chini)

Angalia Mfano Wake hapa Chini…

Chukulia Mfano unataka kutengenezewa Website Kwa ajili


ya biashara yako na una uelewa kiasi juu ya vitu ambavyo
websites za kawaida huwa zinakuwa navyo…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 49


halafu ukawafuata wataalamu kadhaa wa kutengeneza
website na wakakutajia bei zao tofauti tofauti, wakati bado
unaendelea kufikiria umpe nani kazi yako mara akatokea
Mtaalamu mwingine wa kutengeneza Website na
akakwambia (akaku-challenge) maneno haya hapa chini….

Uhitaji Website, Unahitaji kitu kinachoitwa “Online Lead


Generation Funnel”, Kisha akakuelezea juu ya hiyo online
Lead Genaration Funnel, jinsi inavyofanya kazi na jinsi
itakavyokutengenezea faida katika biashara yako kila
mwezi then?...(malizia mwenyewe hahaha)

Umeona jinsi mbinu hii inavyofanya kazi?—Wewe ulifikiria


tatizo katika biashara yako lipo kwenye Website lakini
akaja mtaalamu akaku-challenge kuhusu kitu ulichodhani
kuwa ndio tatizo na ukakupa mbadala wa tatizo kwamba ni
Online Lead Generation Funnel na sio Website kama
ulivyodhani kisha akakuuzia Solution ya Kweli ambayo ni
matokeo endapo utakuwa na Hiyo Online Lead Generation
Funnel then booom (Hata kama ungekuwa ni wewe
usingechomoka huyu jamaa yupo hovyo mno kwenye
kuuza haha…)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 50


…KWAHIYO ukiwa unaandika Tangazo lako Jiulize kwanza
swali hili—Je ni Kitu gani Nikiandika Kitamfanya Mlengwa
Wangu Afikirie Tofauti Kuhusu Tatizo analodhani
analo?...SIRI hii katika ulimwengu wa Copywriting inaitwa

“Eureka Moment” na mara nyingi huzama moja kwa moja


mpaka mfukoni kwa mteja wako na kukuletea mpunga!

P.S. Na Kama Unataka kuchimba zaidi hii report ya


Harvard Business Review Zama hapa
(http://link.sean.co/hbr)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 51


SURA YA TISA

Jinsi ya Kutumia Formula Hatari zaidi


inayoitwa “CONTRAST PRINCIPLE”
Katika Matangazo yako…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 52


“Constrast Princple” inasema kwamba—Ukitaka kumuuzia
mtu kitu chenye bei kubwa anza kwa kumuonesha
kwanza kile chenye bei kubwa zaidi ya kile unachotaka
kumuuzia kinyume na hapo kila kitu atakiona ni ghali
kwake (Nimekuvuruga au sio?...haha.. Usijali utaelewa
zaidi kwenye mifano)

Angali Mfano wake hapa chini…


Kama mteja ameingia dukani kwako Kwa lengo la
kununua suti baada ya kununua suti ya Tshs 300,000
atanunua chochote Kwa bei kubwa hata ukimwambia
soksi za Tshs 5,000 ni Tshs 30,000…LAKINI akianza kwa
kununua soksi za Tshs 5K kwanza Ukimwambia suti ni
Tshs 300K kichwani mwake ataona kama ni Million moja!
Swali ni je tutawezaje kuitumia Formula hii katika
Matangazo yetu?...

Jibu ni kwamba—utaweza kuitumia Formula hii katika


matangazo yako kwa kulinganisha bei ya bidhaa/huduma
unayoiuza na kitu ambacho mteja wako anakijua kina
thamani kubwa

…au Kwa kumuonesha jinsi itakavyomgharimu Kama


hutonunua bidhaa/huduma yako Kwa bei hiyo

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 53


Mfano kuna siku moja niliandika tangazo la kuuza ebook
yangu ya Mgodi 1.0 Kwa kutumia Contrast Principle na
nilipata mvua ya wateja kwasababu niliandika hivi kwenye
OFA…

Thamani ya kitabu hiki ni Tshs 50,000...LAKINI sasahivi


unakipata kwa OFA ya Tshs 9,999 Tu

Gharama za kuandikiwa tangazo ni zaidi ya Tshs


200,000…LAKINI kwa gharama ya Tshs 9,999 tu utakuwa
na uwezo wa kuandika tangazo lako mwenyewe na
utakuwa umeokoa zaidi ya Tshs 199K

SIRI ya Formula hii ni kumtengenezea mteja picha


kichwani mwake aone kwamba anachokinunua kina
THAMANI kubwa kuliko Bei inayotajwa…Kwasababu kuna
tofauti kubwa kati ya bei na thamani kichwani kwa wateja
na kinachowafanya wanunue ni Uthamani sio bei
(Thamani > Bei)

P.S. Usiweke bei pekee kwenye tangazo lako bila


kuonesha uthamani wa kile unachokiuza (Value Vs Price)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 54


SURA YA KUMI

DHAHABU Tano (5) za Lazima


Kuwepo Katika Tangazo Lako…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 55


Kama tunavyojua kwamba tangazo lako ni sawa na mtu
wako wa mauzo…

…Kwahiyo Kama unataka tangazo lako likuetee matokeo


unayoyataka basi hakikisha umejumuisha vitu hivi Vitano
(5) katika tangazo lako ambavyo ni…

1) Walengwa pamoja na Tatizo Unalolitatua…

Kitu cha kwanza kabisa lazima uwaelezee walengwa


wako kwenye tangazo lako mpaka wajihisi unawaelewa
zaidi ya wanavyojielewa wao na hii ni kwasababu watu
hawanunui kwasababu wameielewa bidhaa/huduma
hununua kwasababu wamehisi wameeleweka kwa
muuzaji

Usiandike tangazo Kwa ajili ya kila mtu kwasababu


ukifanya hivyo hutouza Kwa mtu yeyote—hakikisha
tangazo lako linaongea na kundi la watu Fulani tu

Kadri unavyowaelezea walengwa wako vizuri ndivyo


unavyowavutia zaidi kununua kile unachokiuza
Baada ya hapo Anza kuelezea kuhusu Tatizo la walengwa
wako—waambie jinsi utakavyowasaidia kulitatua na

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 56


kuwatoa kwenye maumivu waambie madhara ya
kutolitatua hilo tatizo, kwa kifupi kielezee vizuri zaidi ya
wanavyoweza kukielezea kile kitu kinachowanyima
usingizi usiku

Na hii ndio maana ya kuingia kwenye viatu vya wateja


wako (wajue nje ndani) kwasababu 80% ya tangazo ni
Utafiti juu ya walengwa wako (research) na 20% tu
kuandika tangazo (writing copy) na hakuna kitu
kinachowafanya wateja wanunue vitu zaidi ya Ahadi ya
kuwatoa kwenye maumivu Fulani

Kila unapotaka kuandika tangazo lako jiulize hili swali


hapa chini…

P.S. “Je Hii bidhaa/huduma ni kwa ajili ya kina nani? Na


inawasaidia hao watu kutatua changamoto gani?— halafu
majibu ya hayo maswali yaandike kwenye tangazo lako
then boom!”

P.P.S. Watu Hununua Zaidi Vitu Vinavyowatoa Kwenye


Maumivu kuliko Vinavyowaingiza kwenye raha
(Pain > Pleasure)— Danlok!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 57


2) Ahadi ya Kipekee…

Unatakiwa uwape wateja wako sababu ya kwanini


wanunue kwako na sio kwa mtu mwingine yeyote
ikiwemo na kutokununua kabisa…

Kuna njia mbili ambazo unaweza kuzitumia kwenye


tangazo lako ili kuwapa wateja wako sababu ya kununua
kwako badala ya washindani wako ambazo ni….

Wape Guarantee yenye kutoa kabisa RISK upande


wao—wateja huwa wana hofu ya kufanya makosa ya
kununua vitu na njia pekee ya kuwatolea hiyo hofu ni
kuwapa guarantee ya muda mrefu kuliko washindani
wako hii inaitwa “Risk Reversal”

Mfano: Kama hujapata matokeo unayoyahitaji ndani ya


miezi 3 utarudishiwa pesa yako bila kuulizwa swali lolote
na bidhaa unabaki nayo—kwahiyo hakuna RISK yoyote
upande wako

Jaza BONUS kwa mteja wako Kisha Linganisha na ofa


za washindani wako

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 58


Muda mwingine wateja hununua kwasababu ya bonus
hata sio kile kinachouzwa kwahiyo waoneshe kwanza
thamani ya bonus kisha wape FREE baada ya kununua
kutoka kwako na lazima iendane na kile kinachouzwa

…Kwahiyo unapotaka kuweka ahadi jiulize hili swali


kwanza –“Kwanini wanunue kwangu na sio kwingine?,
halafu jibu lake andika kwenye tangazo lako!

3) Shuhuda za Matokeo ya waliotumia bidhaa/huduma


yako

Kuweka shuda ni sawa na kuwambia wateja wako


kwamba—sio wenyewe tu wanaonunua na wasiponunua
watabaki pekee yao kwenye hiyo changamoto yao (Watu
hawapendi kuachwa nyuma)

Watu hununua zaidi vile vitu ambavyo wengine


wanavihitaji na kuvinunua kutokana na hofu ya kukosa
(Fomo) vile vile kisaikolojia watu hufanya maamuzi kwa
kuangalia wengine wanafanyaje (social proof) hii
kitaalamu inaitwa “Bandwagon au Halo effect”

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 59


…na shuhuda sio zile za wateja tu hata Story yako pia ya
jinsi kile unachokiuza kilivyokusaidia kutoka kwenye
maumivu Fulani waambie—shuhda ni njia ya mkato ya
kuuza bidhaa/huduma yako bila wewe kuhusika moja kwa
moja..Kwahiyo zitumie kwa faida na zikusanye za kutosha

Na shuhuda nyingine yenye nguvu zaidi ni Kutoa Sample


ya kile unachokiuza BURE au kuonesha jinsi kinavyofanya
kazi mfano kama unauza Brenda ya juice tengeneza
Video fupi inayoonesha jinsi inavyosaga juice then boom!

Shuhuda huwa zinajibu haya maswali hapa kichwani Kwa


mteja wako…

“Nitakuaminije?, nitaaminije kama hiki unachokiuza


kitanisaidia?,Nani mwingine aliwahi kutumia hii
bidhaa/huduma na akafanikiwa?”

4) OFA Ambayo Hawawezi Kuikataa (Irresistible offer)…

Usiwape ugumu wowote wateja wako kununua


bidhaa/huduma yako (usiichezesha bidhaa yako mchezo
unaoitwa—Hard to get)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 60


Nguli wa Copywriting anayeitwa Claude Hopkins aliwahi
kusema—“Tenegeneza OFA ya moto (nzuri) kiasi kwamba
mpaka mteja ajione Fala (mjinga) asiponunua”

Ili OFA yako imfanye mteja ajione mjinga asiponunua


hakikisha unajumuisha vitu Vifuatavyo…

Jenga Uthamani wa kile unachokiuza (Build Value)

Mfano: Ndani ya masaa 24 utaipata bidhaa/huduma hii


Kwa OFA ya Tshs 50,000 Tu (Thamani yake ni Tshs
100,000)

Toa SABABU ya OFA yako—Waambie kwanini umetoa


OFA hiyo?

Na hii ni kwasabu watu hawanunui bila kuwapa Sababu—


SABABU ya Ofa inauza zaidi kuliko ofa yenyewe

Watu hawanunui Kwasababu unauza kitu, wananunua


kutokana na Sababu ya kwanini unauza kitu (meza dini
hili)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 61


Mfano: sababu ya OFA inaweza ikawa ni siku ya kuzaliwa
kwako, wazazi wako, mtoto wako, Anniversary ya ndoa au
biashara yako, kufuata mzigo mpya nk…

Toa RISK yoyote upande wa mteja wako endapo lolote


likitoa na jitwishe kila kitu wewe (Risk reversal)

Ukifanya hivyo mteja wako ataona hana cha kupoteza


endapo atanunua bidhaa/huduma yako kwasababu
kinachowazuia watu kununua vitu ni hofu ya kufanya
makosa endapo kitu kibaya kikitokea

Jibu lile swali ambalo wateja wako huwa wanauliza


mara kwa mara wanapotaka kununua bidhaa/huduma
yako, utakuwa umemaliza mchezo kipindi cha kwanza
kabisa

Mfano: swali ambalo huwa naulizwa Sana na wateja wangu


wa ebooks ni –Vipi nikununua ebook halafu nikapoteza
simu itakuwaje?—Kwahiyo kwenye OFA yangu huwa
nawaambia kabisa ukipoteza ebook bahati mbaya
unatumiwa tena FREE!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 62


…kwahiyo kila unapotaka kuandika OFA yako jiulize swali
hili hapa…

“Niweke kitu gani kitakachomfanya mteja asikie maumivu


zaidi Kama asiponunua?—jibu lake weka kwenye tangazo
lako”

5) Sababu ya Kuchukua Hatua SASAHIVI (Reason to Act


Now)…

Kadri unavyompa mteja wako muda mrefu wa kufikiri juu


ya kile unachokiuza ndivyo unavyozidi kumkosa…

Ni sawa na mteja akwambie ngoja nifikirie kwanza


nitarudi siku nyingine halafu nawewe ukasema sawa
haina shida—hutokaaga umuone tena kwasababu mambo
ni mengi watu wanasahau mapema mno

…KWAHIYO Kama unahitaji mteja wako anunue


bidhaa/huduma yako muda huo huo hakikisha unaweka
vitu hivi kwenye tangazo lako…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 63


Ukomo wa Muda (Time Limit)

Kuweka ukomo wa muda kunampa mteja wako sababu ya


kuchukua hatua muda huo huo ili kununua
bidhaa/huduma yako kwasababu ya kuepuka hofu ya
kukosa (Fomo)

Mfano: Ndani ya masaa 6 tu natoa 90% Discount—mwisho


wa Ofa ni leo saa sita kamili usiku!

Ukomo wa Idadi (Quantity Limit)

Watu wanapenda kuwa sehemu ya watu wengine na


hawapendi kuachwa peke yao ndio maana mbinu hi
inafanya kazi kwasababu kila mtu anataka kuwa miongoni
mwa watu kadhaa..

Mfano: Natoa 90% Discount Kwa watu 10 Tu—Mwisho wa


OFA ni leo saa sita kamili usiku!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 64


ONYO: Moja ya kosa kubwa ninaloona linafanywa na watu
wengi kwenye matangazo yao ikiwemo mpaka makapuni
makubwa ni kutoa OFA ambazo zipo wazi hazina ukomo
wa muda wala ukomo wa idadi—wape wateja wako sababu
ya kuchukua hatua kwa kuweka ukomo wa muda au idadi
kwenye ofa yako!

P.S. Hofu ya kukosa ni kama upupu ikitumika vizuri


inamuwasha mteja mpaka anachomoa mpunga muda huo
huo ananunua bidhaa/huduma yako (FOMO—Fear Of
Missing Out)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 65


SURA YA KUMI NA MOJA

Tumia SILAHA Hii ya Siri


Unapokwama Kabisa Kimauzo…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 66


Mbinu hii ya siri niliigundua Kama zali tu baada ya njia
zote kubuma…

…nakumbuka 12/01/2021 niliandika post kwenye


instagram yangu yenye kichwa cha habari (Headline)
Kinachosema hivi…

“NAONDOKA…Instagram!”

Baada ya hapo nikatoa sababu za kwanini naondoka


Instagram na moja ya sababu ilikuwa ni kugundua
kwamba soko langu kubwa lipo Twitter zaidi kuliko
Instagram na Facebook (80/20 rule)…

Baada ya hayo maelezo mwisho nikasema natoa OFA ya


Mwisho kabla sijaondoka moja kwa moja hapa Instagram,
kwa wale wote wanaotaka kupata kitabu cha Copywriting
skills kinachoitwa Mgodi na wale wanaotaka kupata
kitabu cha Closing skills kinachoitwa Hela basi ndani ya
masaa 24 watakipata kila kitabu kwa Discount ya 50%....

Kwahiyo kama unataka kuwa miongoni mwa watu wa


mwisho kupata hii …EXCLUSIVE OFA nitumie neno
“Mgodi” kwenda 0767-912-157 sasahivi…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 67


…aisee sikuamini nilichokiona, watu walimiminika kwenye
WhatsApp inbox sijawahi kuona—Kwa kifupi nilipata
mafuriko ya wateja ambayo sijawahi kuyapata hata
kwenye matangazo ya kulipia…

Nakumbuka kipindi hicho Account yangu ya facebook ya


matangazo ya kulipia (Ad Account) ilifungwa (Disabled)
Kwa muda…kwahiyo sikuweza kurun matangazo
(Sponsored Ads) yoyote zaidi ya kutegemea post za
kawaida (organic post) Kwa zaidi ya miezi 3 na kibaya
zaidi mwezi unaofuata (wa pili) ilitakiwa nilipe kodi ya
nyumba zaidi ya Tshs 600,000…

Nilichanganyaikiwa mno mpaka nikawa najisemea


kimoyo moyo—“Siku ya kuumbuka imefika..Haha”
…LAKINI…huwezi kuamini ndani ya masaa 24 tu niliweza
kuingiza zaidi ya Tshs 330,000

Halafu baada ya ile OFA ya masaa 24 (50% discount)


kuisha kesho yake tena nikarudi Instagram na ujumbe
mwingine wenye Kichwa cha habari (Headline)
kinachosema…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 68


“I’m SORRY!” (Samahani…)
Halafu chini nikaandika maneno yafuatayo…

“Nimepokea Message nyingi sana kuhusu ujumbe wangu


wa jana wa KUONDOKA hapa Instagram na sikutegemea
kama kuna watu wengi sana wanaofuatilia na kufaidika
na masomo yangu…

Wengi wameonesha kukerwa Sana na kitendo cha mimi


kutaka kuaondoka hapa Instagram

Na nilifanya hivyo nikiamini kwamba Twitter ndio sehemu


yenye wahitaji na wafuasi wengi zaidi wa ujuzi huu wa
Copywriting skills lakini kumbe Nilikosea na kutokana na
kauli hiyo basi naomba niseme—“I’m SORRY”
(samahani…) sitaondoka tena Instagram

…na KWASABABU hiyo leo tena natoa 60% Discount kwa


wale wote waliokerwa na kauli yangu ya jana kuhusu
kuondoka Instagram—Ili kupata OFA hii tuma neno
“Mgodi” kwenda WhatsApp 0767-912 xxxx Sasahivi (OFA
hii itadumu kwa masaa 6 tu)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 69


Gues whaat?...ndani ya masaa 6 tu nilipiga zaidi ya Tshs
470,000 Kwahiyo ndani ya masaa 30 kijana wako tayari
nilishatengeneza Tshs 800,000 (unaweza usiamini lakini
hizi sio story za abunuasi nakiishi ninachokifundisha)

…mwezi wa tano (5) mwaka 2021 nikaja kujifunza kuhusu


mbinu hii kutoka kwa mtaalamu wa Copywriting
anayeitwa John Carlton na ndipo nilipojua kumbe inaitwa
—“Piss Everyone Off…And Then Apologize Strategy”

Yaani Mkere (mzingue) kila mtu halafu omba msamaha


(radhi)..Hahaha ila watu!
Na nilipouliza kwanini mbinu hii inafanya kazi kwenye
matangazo kama uchawi?, nikaambiwa…

“Ni bora zaidi kufanya kitu na kuomba msamaha kuliko


kuomba ruhusa kabla ya kufanya kitu” (peleka benki hiyo)

Na mbinu hii inatumiwa Sana na makapuni kama KFC na


McDonalds na ndio silaha yao ya siri soko linapobuma
(ukiulizwa nani kakwambia na ukanitaja mimi nakuruka
mchana kweupe haha)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 70


P.S. KWAHIYO ukitaka kuitumia SIRI hii katika biashara
yako fikiria Tukio unalohisi litawashtua Watu kisha Toa
OFA yako ndani ya muda Fulani—Halafu huo muda wa ofa
ukiisha rudi omba msahama kwa uliowakwaza kisha toa
Ofa nyingine tena na utakuwa umeuza mara mbili then
booom, SIRI ya mbinu hii imejificha kwenye SABABU ya
ofa na sio ofa

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 71


SURA YA KUMI NA MBILI

FUNNEL Kuu Mbili (2) Zilizobeba


Hela Zako Mtandaoni…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 72


Kama wewe ni msomaji mzuri wa vitabu vya Marketing na
mfuatiliaji wa mambo ya biashara za mtandaoni nina
uhakika umeshawahi kusikia kuhusu hili neno FUNNEL…
…na kama hujawahi kusikia au umesikia lakini hukuelewa
maana yake basi maana yake ni hii hapa chini…

FUNNEL—Ni Mfumo wa mauzo wa kimtandao unaomchuja


mteja wako kutoka kwenye hatua ya kwanza anapoona
tangazo lako mpaka hatua ya mwisho anaponunua
bidhaa/huduma yako bila ushiriki/uwepo wako wa moja
kwa moja katika huo mfumo wa mauzo

Hili ni kama chujio la kimtandao linalochuja kati ya


wazinguaji na wateja halisi au wanunuzi wa
bidhaa/huduma yako mtandaoni pia ni kipashio cha
wateja kuanzia wale wa baridi (cold traffic) ambao
hawakujui, hawakupendi wala hawakuamini na kuwa wa
moto (hot traffic) wanaokujua, kukupenda na kukuamini…

Leo nitakupa Funnel kuu mbili (2) za Siri zilizohakikiwa na


kuthibitishwa kuleta matokeo makubwa Kimauzo katika
biashara yoyote inayofanyika Mtandaoni…

Upo tayari?...okay Good tuzame mgodini au sio?...

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 73


Funnel # 1: WhatsApp Automated Funnel (WhatsApp
Automated Sales System)…

Tunatumia Funnel hii ikiwa WhatsApp yako itatumika


Kama chombo au kifaa cha kuuzia bidhaa/huduma yako
(Conversion tool) na hapa tunaongelea WhatsApp
Business sio WhatsApp messanger kwasababu
WhatsApp business ina vipengele (features) vingi kuliko
WhatsApp ya kawaida (messanger)

Fuata Hatua Zifuatazo Ili Kutengeneza Mfumo wako wa


kuuza kupitia WhatsApp yako bila kupoteza muda wako
kuchati na kila mteja…

Hatua # 1: Tambua Wateja wako Wengi wanatoka katika


Mitandao (Platforms) gani zaidi kati ya hii—Facebook,
Instagram, Twitter, Youtube, Linkedlin etc…

Kwasababu sio kila mtandao utakufaa kulingana na aina


ya biashara yako—kwahiyo anza kwanza kwa kutambua
wateja wako wa kuwapeleka WhatsApp utawatoa katika
platforms zipi kati ya hizo hapo juu? Na hii haijalishi
watatokana na matangazo ya kulipia (Paid Ads) au post
za kawaida (Organic post)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 74


Hatua # 2: Tengeneza Chambo itakayowanasa walengwa
wako kutoka kwenye hizo Platforms aidha ni kutoka
Facebook, Instagram, Twitter nk na kuwapeleka moja kwa
moja kwenye WhatsApp yako…

Najua utakuwa unajiuliza Utapataje/utatengenezaje


chambo?—Swali zuri Sana, njia rahisi ya kutengeneza
chambo yenye kuwanasa wateja wako ni hii hapa…

“Tafuta Swali la Muhimu zaidi ambalo walengwa wa


bidhaa/huduma yako huwa wanajiuliza mara kwa mara bila
Majibu kisha Ahidi Kuwapa Majibu yake BURE”….

Tunaahidi kuwapa majibu bure ili watujue, watuamini na


watupende na kisha watuone kama wataalamu
(Specialist/Expert) na sio wauzaji kama wauzaji wengine
pia hakuna binadamu anayeweza kujizuia katika neno
BURE

— kwahiyo tunafanya kitu kinachoitwa “Positioning” yaani


tunajiweka sokoni kama wataalamu na sio wauzaji kwa
kutoa kitu chenye uthamani kwa walengwa wetu BURE
kabisa kwasababu kinawasaidia kutatua changamoto yao

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 75


Baada ya tayari umeshapata chambo yako utakayoitumia
kuwanasa walengwa wako basi ingia katika hatua
inayofuata hapa chini…

Hatua # 3: Tengeneza Video Fupi yenye Mtiririko wa Vitu


Vifuatavyo ndani yake (Usiruke hatua hata moja)…

Hii video sio lazima sura yako ionekane unaweza kuandaa


presentation kwenye Power point au Canva kisha
ukarecord Screen Kwa kutumia Software za BURE Kama
Screencast-0-matic au Camtasia wakati unaelezea hizi
contents zako hapa chini…

Tuchukulie mfano unauza bidhaa za kupunguza uzito na


Video yako itakuwa kama Ifuatavyo…

Jitambulishe kutokana na tatizo unalolitatua na sio


kile unachokiuza…

Mfano: Naitwa Kelvin John nawasaidia wakina mama


wenye uzito mkubwa kupunguza uzito ndani ya siku 21
Kwa kutumia mchanganyiko maalumu wa matunda asilia—
na sio naitwa Kelvin John nauza bidhaa za kupunguza
uzito

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 76


Wape sababu ya kukusikiliza kwa kuwapa Story fupi
sana juu ya jinsi kile unachokiuza kilivyokusaidia
wewe binafsi au mteja wako kutatua changamoto
Fulani, hiyo itawafanya wateja wako wajione wao
kwenye hiyo story yako kwahiyo watajua unawaelewa
vyema (They will connect with you emotionally)

Wape majibu ya kwenye chambo uliowaahidi kuwapa


BURE…

Kwasababu wateja wengi wanaotokana na matangazo ya


kulipia hawakujui, hawakuamini wala hawakupendi Kwa
kuwapa haya madini bure utawafanya wakujue,
wakuamini, wakupende na wawe tayari kununua chochote
kutoka kwako kabla hata haujatangaza kile unachokiuza

Baada ya tayari umeshawapa madini uliwaahidi


kwenye chambo yako tumia mbinu ya kuuza inayoitwa
—“Stealth Close” kutangaza OFA ya bidhaa/huduma
yako Kwa kusema maneno yafuatayo (Script)…

Mfano: “BY THE WAY”—Kama unachangamoto ya uzito


mkubwa na unataka kupunguza uzito ndani ya siku 21 bila
kufanya mazoezi basi leo nina habari njema sana kwako…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 77


Nina supplements maalumu zitokanazo na mchanganyiko
wa matunda asilia ambazo zitakusaidia kupungua uzito
bila kutumia madawa ya hospitalini ndani ya siku 21 Tu,
ambapo ndani ya masaa 24 utajinyakulia bidhaa yako kwa
OFA ya Tshs 55,000 (Thamani yake ni Tshs 85,000—
utaokoa Tshs 30,000 nzima)

Ili kuwahi OFA yako ndani ya masaa 24 Lipia sasahivi


Kupitia namba hizi hapa chini kisha nitumie uthibitisho wa
muamala kwenye WhatsApp yangu (weka namba za
malipo hapo chini)

Baada ya tayari umeshatoa OFA yako hatua inayofuata ni


hii hapa…

Weka/ambatanisha shuhuda za matokeo ya wateja


wako au zako mwenyewe baada ya kutumia
bidhaa/huduma yako…

Shuhuda huwa zinajibu swali kichwani kwa mteja


linalosema—Nitaaminije kama hii bidhaa/huduma yako
inafanya kazi?

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 78


Kumbuka wateja huwa hawataki kuachwa pekee yao au
kuwa wao ndio wa kwanza pia watu hufanya maamuzi ya
kununua vitu kwa kuangalia wengine (Social proof &
Testimonials)

Mfano: hawa pia walikuwa na changamoto kama yako


lakini angalia jinsi wanavyosema sasahivi baada ya
kutumia bidhaa/huduma hii kisha— weka/ambatanisha
Screenshot za shuhuda za wateja wako hapa!

…baada ya shuhuda wakumbushe tena OFA kisha wape


maalekezo ya kulipia then booom!

Hatua # 4: Fungua Youtube Account (Channel) Halafu


Pakia (Upload) Hiyo Video Kwenye Hiyo Account…

Baada ya kupakia hiyo video unaweza ukaiweka


Unlisted/Private ili isionekane popote mpaka utume Link
au ukaiweka Public ionekane na kila mtu vyovyote ni sawa
ila mimi yangu niliiweka Unlisted

…baada ya tayari umeshapakia hiyo video yako kwenye


Youtube channel yako njoo sasa kwenye hatua ya mwisho
kabisa ambayo ni….

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 79


Hatua # 5: Copy Link ya Hiyo Video Halafu Nenda Kapest
Kwenye WhatsApp Yako…

Katika WhatsApp Business kuna vipengele vya kuweka


“Auto Reply” yaani mtu akikutumia ujumbe kwenye
WhatsApp inajijibu yenyewe umeshawahi kuona
unamtumia mtu message WhatsApp unakutana na
ujumbe unaosema “Samahani kwa sasa hatupo online
tutakutafuta haraka iwezekanovyo punde tutakaporudi
online”?

Okay—hiyo inaitwa “Auto Reply”

….KWAHIYO Link yako ya Video unaenda kuipest Kwenye


Sehemu Inayoitwa “Away Message” Ili mtu yeyote
anayetoka Facebook, Instagram au twitter baada ya
kuona tangazo lako lenye chambo ya BURE
anakaribishwa na Link ya video na akibofya hiyo link
inampeleka moja kwa moja Youtube kusikiliza video
yenye kukuuzia bidhaa/huduma yako bila uwepo wako

Utabakiwa na kazi mbili tu kurun matangazo yenye


kuwapeleka watu WhatsApp ili wakasikilize Video na
kupokea message za M-pesa, Tigo pesa au Bank

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 80


notifications then booooom!. (Halafu nakuona kabisa
unatabasamu au sio?..Hahaha)

P.S. By the way Kama unataka Kuona Mfano wa Video


yangu wakati nafanya majaribio ya hii FUNNEL Bofya Hii
Link hapa … (https://youtu.be/CyiEgL3TyN4) na hii
hapa.... (https://youtu.be/gCJv-ZJ9avE)

Funnel # 2: Client Acquisition Methodology…

Funnel hii nilijifunza kutoka Kwa mentor wangu anaitwa


Sam ovens, huyu jamaa ni miongoni mwa wataalamu
ambao wapo Hovyo (Zaidi ya Vizuri) sana linapokuja
swala la kunasa wateja mtandaoni…

…Na Funnel hii inaenda Kama Ifuatavyo…


(Facebook + Instagram+Twitter… Ads) Value Video
. Call Customer (Boom)!...

Maelezo ya hii Funnel na jinsi utakavyoitumia katika


biashara yako ni haya hapa chini…

“Unatengeneza Tangazo lako aidha ni la kulipia (paid Ads)


au post ya kawaida (organic post) kisha unaliweka

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 81


(Facebook, Instagram au Twitter) Halafu Wote wanaoona
tangazo lako linawapeleka Kwenye Video inayotoa
Uthamani BURE kwa walengwa wako juu ya tatizo lao
(Value Video) halafu baada ya kuona Video mwishoni
unawaalika wakupigie simu (Call) wale wote wanaotaka
Ushauri BURE ndani ya Dkk 5 juu ya tatizo lao na hapo
ndipo unapouza bidhaa/huduma yako (Customer)—
Kwahiyo mauzo yanafanyika kwenye simu sio kwenye
Funnel kama ile ya kwanza”

..Na Kama tunavyojua pesa huwa hazipo kwenye


bidhaa/huduma yako, zipo kwenye uwezo wako wa kuuza
hiyo bidhaa/huduma na hapa ndipo unakuja umuhimu wa
ujuzi unaoitwa Closing skills na bahati nzuri kila kitu
kuhusu ujuzi huu nimeshakuwekea kwenye ebook
inayoitwa “HELA”

Funnel hii inafanya kazi Kama uchawi Kwa sababu


zifuatazo….

Utakuwa umetumia Formula ya Siri inayoitwa “Natural


Selection” kuchuja wateja wenye nia tu ya kununua
bidhaa/huduma yako na sio wazinguaji na wapoteza

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 82


muda…kwasababu asiye mteja hawezi kupoteza Tshs
1,000 ya vocha yake kupiga simu na kama hawezi
kutumia Tshs 1,000 kupiga simu ni wazi kabisa hawezi
kununua bidhaa/huduma yako ya Tshs 10,000 au sio?..
(Hili ni chujio makini sana)

Ni rahisi zaidi kuuza kwa mteja aliyekupigia simu


wewe kuliko yule uliyempigia simu wewe kwasababu
mteja akikupigia simu, wewe ni Mtaalamu (Expert)
Lakini wewe ukimpigia simu mteja ni Muuzaji
(salesperson)

Baada ya kuangalia video yenye kumpa uthamani


BURE tayari atakuwa ameshakujua,
ameshakupenda,na ameshakuamini na utakuwa
umeshauza bidhaa/huduma yako kabla hata ya
kuongea nae kwenye simu…

kwahiyo Funnel hii inawapasha pia wateja wa baridi (Cold


Traffic) kuwa wa moto (Hot Traffic) wanaotokana na
matagangazo ya kulipia (Paid Ads)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 83


Nakumbuka mentor wangu Danlok aliwahi kusema hii
kauli hapa chini ambayo imebeba maana nzima ya hii
Funnel…

“I Don’t Talk to Anybody Unless They Know I’m


Someboday—Yaani Siongei na Mtu yeyote Isipokuwa yule
tu anayejua Mimi ni Mtu Fulani”

Kwanini?...kwasababu ni Vigumu sana kuuza kwa mtu


asiyekujua na ni rahisi sana kuuza kwa mtu anayekujua
ndio maana tunatoa kwanza Video ya BURE yenye
uthamani kwao ili watujue, watupende na kutuamini kabla
ya kuongea na sisi kwenye simu kwahiyo ile video haipo
pale kwa bahati mbaya ipo pale kwa dhumuni maalumu la
kututambulisha sisi na kile tunachokifanya kabla ya
kuongea na wateja wetu

P.S. Kuuza Zaidi Mtandaoni Haijalishi Wewe Unamjua


nani Bali ni Nani Anakujua Wewe! (Peleka benki hili dini)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 84


SURA YA KUMI NA TATU

Jinsi ya Kuigeuza Bio Yako Kuwa


SUMAKU Ya Kunasa Wateja Wako
Mtandaoni 24/7…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 85


Kitu cha kwanza kabisa anachokiangalia mteja baada ya
kufika kwenye ukurasa wako wa Biashara aidha ni
facebook, Instagram, au twitter ni Bio yako…

Bio yako itamwambia kila kitu kuhusu wewe pamoja na


kile unachokifanya na hiyo itampa sababu ya kuendelea
kusoma kilichomo ndani au aendelee na mishi zake

..Moja ya kosa kubwa ambalo watu wengi wanalifanya


pindi wanapoandika bio zao katika kurasa zao za biashara
mtandaoni ni Kujiongelea wao binafsi…

Ndio maana bio nyingi utazikuta zina maneno yafuatayo…

• Business Consultant

• Life Coach

• Business coach

• Entrepreneur

• Business Man nk…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 86


Hili ni kosa kubwa kwasababu Mteja hawezi
kukutofautisha na watu wengine kwasababu wote
mmeandika kitu kimoja na kibaya zaidi mmejiongelea
wenyewe na hakuna chochote kwa ajili ya mteja katika
huo ujumbe …kwahiyo ili kujitofautisha na washindani
wako Bio yako inatakiwa ielezee aidha kuhusu tatizo
linalowanyima usingizi walengwa wako au matokeo
wanayoyatafuta lakini bado hawajui watayapata wapi
lengo likiwa ni kupata attention yao kwa 100%

Ndio maana leo nataka nikupe Formula ya SIRI ya


kuandika Bio yenye kukunasia wateja wako mtandaoni
24/7 inayoitwa—“The Message Equation”

The Message Equation Formula inasema hivi….

“Nawasaidia… (Walengwa wako)…Kupata… (Matokeo


wanayoyataka)…Kwa Kutumia… (Bidhaa/huduma yako)”

…au Kwa Lugha ya Kindengereko tunasema…

“I Help… (NICHE)…To Get… (RESULTS)…By Using… (YOUR


OFFER)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 87


Angalia Mifano hapa chini…

Nawasaidia Wajasirimali Kuongeza Mauzo yao


mtandaoni kwa kutumia Formula maalumu ya KFK!

Nawasaidia Wanawake Wenye Uzito Mkubwa


Kupunguza Uzito wao kwa kutumia Virutubisho
(Supplements) maalumu vitokanazo na matunda asilia

I Help Business owners & Entreprenuers bulid six figure


Monthly revenue by showing them the simple 3 Steps
“CAS” Formula

Mifano ni mingi mno nikisema niendelee kutiririka


tutakesha hapa lakini si umepata picha kupitia hiyo
mifano michache?...okay vizuri sana!

Kwahiyo tumia Formula (The Message Equation) hiyo


kuandika Bio yako waache washindani wako waendelee
kujiongelea wao na kupiga miayo wakisubiri wateja
mtandaoni wakati huo wewe umekunja nne huku wateja
wakimimika wenyewe DM wakiomba kununua
bidhaa/huduma yako!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 88


SURA YA KUMI NA NNE

Jinsi ya Kupata Wazo la


Bidhaa ya Kuuza Mtandaoni
Ndani ya Masaa 24 Tu…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 89


Kama bado hauna bidhaa au kitu cha kuuza mtandaoni ili
kupiga mpunga basi kipengele hiki ni zaidi ya mchongo
kwako…

…lakini kabla hatujaendelea mbele zaidi ngoja nikwambie


kitu hiki hapa ambacho kimewazuia watu wengi
kutengeneza pesa mtandaoni…

“Uhitaji Vyeti ili kuitwa mtaalamu/Expert wa kitu Fulani


unachohitaji ni kitu kimoja tu—Kujua Vitu Vingi Zaidi ya
Wale Unaowalenga au kuwa hatua moja mbele zaidi ya
wateja wako”

Unachohitaji pekee ni uwezo wa kuwaletea matokeo wale


unaowalenga zaidi ya wanavyoweza kujiletea wenyewe…
kwahiyo katika soko la sasa kinachokupa michongo
mtandaoni sio vyeti bali ni uwezo wako wa kuleta
matokeo mezani kwa walengwa…

Hakuna kinachonishangaza tena, umeona bana, kujifunza


ujuzi wa kuuza aidha ni kwenye maandishi au kwenye
maneno ni bonge moja la uwekezaji kwasababu ni ujuzi
wa ajabu sana unaofanya kazi kama uchawi…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 90


KWASABABU unaweza kutumia siri hizi kuuza bidhaa,
huduma, mawazo, hata kujiuza mwenyewe pia..

…na nina uhahika lengo lako kubwa ni kutengeneza Pesa


ya maana ili kuwa na uhuru wa kifedha kwasababu pesa
inatatua matatizo mengi yaliyoletwa na kutokuwa na pesa
na ili kupata hizo pesa lazima uuze kitu Fulani au sio?..

Naona nimechonga Sana sasa ni muda wa kuingia


Mgodini au sio...okay vizuri twende zetu…

Hatua # 1: Usianze Kwa Kutafuta Kitu cha Kuuza


Kwanza…Hapana…hiyo itakuja baadae unachohitaji
Kutafuta Kwanza ni—SOKO Lenye KIU (A Hungry Crowd/
An Audience to Sell to...)

Kujichanganya kwenye hii hatua ya kwanza kumewafanya


wengi (watoto wa mjini) warudishe mpira Kwa kipa—
wengi wanaanza kwa kutafuta bidhaa ya kuuza ili wauze
kwa kila mtu na kama tunavyojua ukimlenga kila mtu
tafasiri yake ni kwamba hauna mteja hata mmoja
(haumlengi mtu yeyote)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 91


…sahau kabisa kuhusu bidhaa yoyote Kwa sasa—katika
hatua ya kwanza anza kwanza kwa kutafuta soko lenye
kiu, lenye tatizo na lenye uwezo wa kununua Solution ya
tatizo

Na Siri ya kuingia katika soko la mtandaoni Kwa gharama


ndogo zaidi baada ya kulijua soko lenye Kiu sio Kwa
kuuza bidhaa ya kushikika (Physical product) ni kwa kuuza
—TAARIFA za Kipekee (Unique Informations) zenye
kutatua tatizo la hao walengwa

Najua utakuwa unajisemea kimoyomoyo—sasa utapataje


hizo Taarifa za kipekee?...usiwe na wasi wasi
nitakuonesha muda sio mrefu kuwa na subira kidogo tu…
Ngoja kwanza tuangalie hatua inayofuata inasemaje…

Hatua # 2: Uza Kile Unachokipenda…

Ukweli ni kwamba mauzo ya kwanza ni wewe kujiuza au


kujiuzia kile unachotaka kukiuza…kwasababu ni ngumu
sana kuuza kitu ambacho hauna hisia za kukimiliki

Mfano…Kama unachukia mbwa halafu ukafungua biashara


ya kuwafundisha wamiliki wa mbwa online jinsi

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 92


ya kuongea na mbwa wao lazima upate shida sana kwenye
kufundisha hata kama unatengeneza pesa nzuri

…kwahiyo chagua kufanya kitu ambacho kipo kwenye


PASSION yako na hili utalijua Mapema tu pindi
utakapoanza kuandika hizo taarifa ukiona huchoki na
unapata hamasa ya kuongea na walengwa wa hicho kitu
bila kuchoka basi upo sehemu sahihi…mfano mimi
ninapoanza kuandika kuhusu Copywriting skills huwa
nasahau mpaka kula yani hahaha..

Baada ya hatua hii ya pili sasa tunapata ruhusa ya


kuzifungisha ndoa kati ya hatua ya kwanza na hatua ya
pili kwa nderemo na vifijo kama ifuatavyo…

Hatua # 3: Weka Nguvu Kubwa Kwenye Shauku (Passion)


Unayochangia na wale unaotaka kuwalenga (soko lenye
kiu)…

Najua nitakuwa nimekuacha kidogo si ndio?.. Usijali


angalia maelezo yake hapa chini….

Mfano Kama unapenda zaidi mambo ya Fashion na


ukatafuta soko lenye kiu na uhitaji wa mambo ya fashion

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 93


pia basi ukifanya biashara ya kuuza taarifa katika soko
hilo lazima utoboe…kwasababu unafanya kitu ambacho
kipo katika interest yako binafsi pamoja na wale
unaowalenga (Soko lenye kiu na njaa)

…Na Kama unapenda mambo ya vyakula na Diet


ukijifunza na kuuza Taarifa za mambo ya kupunguza uzito
(Loss weight) utafanikiwa zaidi kwasababu utakuwa
unachezea uwanja wa nyumbani

Vipi umeanza kupata picha?...okay vizuri sana sasa ni


muda wa kujiandaa kwasababu tunataka tukaanze
Kutafuta Taarifa Zenye Uthamani au madini kwa ajili ya
soko letu lenye kiu na ndipo mpunga ulipo…

Mpaka hapo tayari utakuwa umeshalijua Soko lako lenye


kiu, umeshajua shauku mnayochangia ambayo
itawasukuma walipie hizo taarifa…na sasa ni muda
maalumu wa kutengeneza hiyo bidhaa yenye hizo taarifa
kwa kuangalia hatua ya 4 inavyosema…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 94


Hatua # 4: Sasa ni muda wa Kuwa Mtaalamu (Expert)…

Amini usiamini ni rahisi sana kuwa mtaalamu wa kitu


Fulani, na sitojali unajua kuhusu kitu Fulani au haujui
kabisa kuhusu kitu Fulani ila mpaka mwisho wa wiki
tayari utakuwa mtaalamu kwenye kitu Fulani…
Unachotakiwa kufanya ni kuzingatia kile utakachokisikia
ndani ya hii hatua ya nne

Ukweli ni kwamba ni ngumu Sana kuuza katika soko


ambalo halijui Kama lina tatizo kuliko katika soko ambalo
tayari linatafuta solution (Soko lenye kiu)

Oya kiini cha kuwa mtaalamu wa kitu fulani ni hili swali


hapa —Hivi unajua Kitu Kinachowatenganisha Kati ya
Wataalamu (Experts) wa vitu Fulani na Wasio
wataalamu?...

…ndio upo sahihi ni TAARIFA (Informations)


Mtu yeyote mwenye Taarifa nyingi na anayejua vitu vingi
zaidi kuliko wewe kuhusu kitu Fulani tayari huyo ni
Mtaalamu wako

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 95


Na taarifa zinapatikana wapi?..Ndio upo sahihi ni kwenye
Vitabu na Courses kutoka kwa wataalamu mbali mbali…
Kwahiyo kazi pekee iliyobaki sasahivi kwako ni kupiga
msuli wa maana ili kuzitafuta hizo Taarifa
zitakazokufanya uitwe Mtaalamu kuhusu tatizo unalotaka
kulitatua kwa walengwa wako

Tuchukulie mfano Umechagua Soko la wanaotaka


kupunguza Vitambi (Loss weight niche)

Unachotakiwa kufanya ni Kununua Vitabu au Kozi


zinazohusu mambo ya kupunguza uzito tu kisha Tafuta
Taarifa Zilizopuuzwa lakini zina matokeo makubwa kwa
walengwa wako halafu ziite SIRI!

Jifunze na kusoma kwa makini huku unachukua notes zile


taarifa zote za kipekee (Unique information) ambazo watu
wengi hawazijui na wengine wanazijua lakini wanazipuuza
kwasababu hapo ndipo pesa zilipo

Baada ya siku kadhaa tu za kusoma na kuchukua notes


tayari utakuwa na Taarifa za Kutosha kuhusu mambo ya
Kupunguza vitambi kutoka katika vyanzo vya Wataalamu
mbali mbali wa mambo hayo

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 96


…na baada ya Hapo Hongera sana tayari wewe ni—
MTAALAMU (Expert)

Wataalamu wengi wakubwa unaowaona hawaitwi


Wataalamu kwasababu wanafanya vile vitu, wanaitwa
Wataalamu kwasababu wanamiliki Taarifa Nyingi na nzito
kuhusu hivyo vitu na ndio maana kuna makocha wakubwa
lakini hawajawahi kuwa wachezaji kitu pekee
walichonacho ni Taarifa!

Peleka benki hii siri hapa chini…

“Mtu Haitwi Mtaalamu Kwasababu Anajua Kitu Fulani, bali


anaitwa Mtaalamu Kwasababu ameandika Kitabu Kuhusu
Hicho Kitu”

…na hii inatuingiza katika hatua ya mwisho inayosema…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 97


Hatua # 5: Tangaza Utatuzi wa Tatizo Kwenye soko lako
Kama Mtaalamu wa kile Kinachowanyima usingizi usiku
ambacho tayari umeshakisoma na kukielewa vyema…

Mpaka hapa tayari mchezo umeshaisha kwasababu


umeshalijua soko lako, umeshajifunza kuhusu kile
wanachokihitaji na tayari upo Hovyo kuliko mtu wa
kawaida (expert), na sasa ni muda wa kuja na kile
wanachohitaji kukilipia ili wakipate ambacho ni bidhaa
yenyewe sasa

…na ili kupata bidhaa ambayo itauza kama wazimu basi


pitia humu…

Chuja zile Taarifa Zilizopuuzwa (overlooked) kuhusu


tatizo lao kisha ziite—SIRI (Secrets)

Chukua Taarifa zile tu zenye kuleta matokeo ya haraka


na ni rahisi kuzitumia

Halafu hakikisha matokeo ya hizo Taarifa yawe ni


magumu kuaminika kwa walengwa kiasi kwamba
yalete mshangao kwao (Too good to be true)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 98


Kisha andika hizo taarifa zote na ziweke kwenye kitabu
(ebook) au Kozi then booom tayari una bidhaa ya kuuza
mtandaoni na usiwaze kuhusu lugha ya uandishi wewe
andika kama jinsi unavyoongea kama mimi nilivyofanya
kwenye kitabu hiki na vingine vyote!

P. S. Kitu pekee cha Kukumbuka hapa ni kwamba Bidhaa


yako lazima iwe katika mfumo wa TAARIFA (Information
based product) kwasababu mtaji wake ni mdogo mno
sawa na sifuri

Kitu kikubwa zaidi nilichojifunz kutoka Kwa mentor wangu


wa Consulting skills Sam ovens ni kwamba –Soko ndio
maabara ya kweli hakikisha kila bidhaa unayotaka kuuza
msukumo wake lazima utoke sokoni na sio kwako!

Na hapa ndipo watoto wa mjini wanaporudisha mpira kwa


kipa kwa kuanza kujiwaza wao na kufirikia kwanza kitu
cha kuuza badala ya kuambiwa na soko lenyewe! (Muda
wote unapotaka kuanzisha biashara yoyote hakikisha
unaanzia sokoni, wauzie wanachotaka kununua sio kile
unachotaka kuuza kwasababu unataka hela zao)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 99


SUMMARY Yake ni Hii Hapa Chini…

1. Litambue Soko lenye Kiu au Soko lenye Tatizo ambalo


lipo tayari kulipia utatuzi wa tatizo lao—ambalo hilo soko
ndilo litakalokupa Mrejesho (feedbacks) wa Solution yako
(Bidhaa/huduma)

2. Walengwa wako wanataka Matokeo Gani?—kupata


majibu ya hili swali ni muhimu sana kwasababu utawaletea
kitu wanachotaka sio wanachohitaji na kama tunavyojua
kwamba watu hununua vitu wanavyovitaka na sio vile
wanavyovihitaji….

3. Chombo gani Utakachowaletea ambacho kitawatoa pale


walipo na kuwapeleka kule kwenye Matokeo
wanayoyataka?—na chombo chenyewe ndio
bidhaa/huduma yako

4. Wape Hicho Chombo kitakachowasaidia kupata


matokeo yao BURE kwanza kabla ya kuwaomba hela—
lengo ni kufanya uthibitisho kwao kwamba bidhaa/huduma
yako itawapa matokeo wanayoyataka hii kitaalamu inaitwa
“Validation of an Idea”

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 100


Na hayo matokeo ndio yatakayokuuzia bidhaa/huduma
yako kirahisi zaidi

Ili kupata bidhaa itakayouza zaidi Mtandaoni usijiulize


swali la wengi linalosema—Nitauzaje bidhaa zangu kwa
wingi? Bali jiulize, Nitawezaje kuwasaidia watu wengi zaidi
kutatua changamoto yao kwa kutumia bidhaa yangu?
Kwasababu haupo kwenye soko la bidhaa/huduma, upo
kwenye soko la watu, wanaonunua bidhaa ni watu na
bidhaa haiwezi kujinunua hata siku moja

Tembea na haya maswali hapa chini muda wowote…

Nitawezaje Kuwathibitishia walengwa wangu kwamba


bidhaa/huduma yangu inafanya kazi na itaweza
kuwapa matokeo wanayoyataka?

Nitawezaje kumsaidia mtu Fulani kupata matokeo


anayoyataka?

Hayo matokeo ndio yatakayoenda kuiuza bidhaa/huduma


yako!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 101


Na Formula hii inafanya kazi kwenye aina yoyote ya
biashara aidha ni bidhaa za kawaida nje ya mtandao au
mtandaoni ni ebooks, consulting, coaching programs etc

— Toa BURE Kwanza kile unachokiuza kwa walengwa


wako, Pata matokeo yao, chukua shuhuda na stories za
matokeo yao, kisha tumia hizo shuhuda, matokeo na
stories kuwapata wateja kama wao wengi zaidi na zaidi
then boom!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 1O2


SURA YA KUMI NA TANO

Sentensi Moja Iliyobeba SIRI Kuu 5


Za Ushawishi Duniani na Jinsi ya
kuzitumua Katika Matangazo
yako…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 1O3


Haya ni maneno hatari sana kuyatumia katika matangazo
yako kwasababu yatamfanya mtu yeyote afanye chochote
aidha ni kibaya au kizuri kwake, kwahiyo usizitumie mbinu
hizi kuumiza (kutapeli) wengine bali zitumie kushawishi
walengwa wako kununua bidhaa/huduma yako
kwasababu ndio solution ya matatizo yao na ndio kitu
sahihi kwao—sawa? (Najua umesema sawa)

Mara ya kwanza niliyasikia maneno haya ilikuwa ni kutoka


kwenye kitabu cha mtaalamu wa Ushawishi Dunia
anayeitwa “Blair Warren” kwenye kitabu kinachoitwa
—“The One Sentence Persuasion Course” halafu Russel
Brunson akapigilia nyundo kwenye kitabu chake
kinachoitwa—“Expert Secrets”

Kama huamini maneno yangu jaribu kuchunguza


matangazo yote yanayofanya vizuri Kwa sasa na
yaliofanya vizuri zamani kama hayajatumia neno moja
kati ya haya matano utakayoenda kuyagundua muda
mchache ujao…

…na maneno hayo hatari zaidi ya ushawishi yapo katika


Sentensi moja inayosema…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 1O4


“Watu Watafanya Kitu Chochote Kwa Wale Wanawatia
Moyo na Kuwahimiza Kuhusu Ndoto Zao, Wanaohalalisha
Makosa yao, Wanaowapunguzia Hofu yao,
Wanaothibitisha Tuhuma Zao, na Wale wanaowasaidia
Kuwarushia Mawe maadui zao”

Hiyo ni sentensi moja ila imebeba SIRI kuu 5 Za Ushawishi


Duniani ambazo ni…

• Watie Moyo na Kuwahimiza walengwa wako (wateja)


kuhusu ndoto zao

• Halalisha Makosa yao

• Wapunguzie na Kuwatua mzigo wa Hofu yao

• Zithibitishe tuhuma zao

• Wasaidie Kuwarushia Mawe Maadui zao

Najua nimekuchanganya kiasi au sio? Haha usijali haya


hapa chini maelezo yake…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 1O5


Siri # 1: Watie Moyo na Kuwahimiza Walengwa wako
(wateja wako) Kuhusu Ndoto Zao…

Moja ya kitu cha muhimu zaidi pindi unapotaka kuandika


tangazo lolote ni kuwajua walengwa wako nje ndani
ikiwemo kuzijua ndoto zao, kuijua hofu yao, malengo yao
nk kisha waambie jinsi watakavyotimiza hizo ndoto zao
kwa kutumia kile unachowauzia (bidhaa/huduma yako)

Wazazi huwa wanawakatisha tamaa watoto kuhusu ndoto


zao na kuwaongoza kule wanakodhani wao ni sahihi kwa
mtoto na watoto huwa wanatii wakiamini ni kawaida
mpaka pale anapotokea mtu kutoka kusikojulikana
(ambaye ni wewe sasa) na kuwaambia anaamini katika
ndoto zao na yupo kwa ajili ya kuwasaidia bega kwa bega
kuzifikia hizo ndoto zao/malengo yao…

Kinapotokea kitendo hiki unadhani nani atakuwa na nguvu


zaidi kati ya mtu asiyejulikana mwenye kuamini katika
ndoto zao au mzazi anayetaka mtoto amtii yeye... (Majibu
unayo)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 1O6


Siri # 2: Halalisha Makosa Yao…

Wateja wengi unaotaka kuwauzia bidhaa/huduma yako


tayari walishafanya makosa ya kununua vitu mbali mbali
zamani kutoka kwa watu mbali mbali na wewe hautakuwa
mtu wa kwanza kuwauzia kitu na kutokana na sababu
mbali mbali huenda hawakupata matokeo walioahidiwa
wangeyapata na hawana imani na mtu yeyote kwa sasa…

kwahiyo unachotakiwa kufanya ili kuwashawishi ni—


Kuhalalisha makosa yao kwa kuwaambia kwamba sio
makosa yao ni ya wale waliowauzia bidhaa/huduma
kipindi cha nyuma

Wauzaji wengi wakiwa wanawalaumu wateja kwa kufanya


makosa hayo mwanzo, wewe watue mzigo kwa
kuhalalisha makosa yao kwa kuwaambia hawahusiki kwa
lolote katika hayo makosa kwa kufanya hivyo utakuwa na
nguvu na ushawishi wa hatari katika soko ulilopo kuliko
washindani wako…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 1O7


Siri # 3: Wapunguzie na Kuwatua Mzigo wa Hofu yao
Kuu…

Kama utawapunguzia wateja wako hofu na kuwapa


tumani jipya basi watakufuata mpaka mwisho wa dunia
na kurudi haha..

Tukiwa katika hofu au uwoga ni vigumu sana kuweka


umakini katika jambo lolote lile!

Hivi unadhani mtu akiwa katika uwoga na hofu njia ya


kumfanya atulie ni kumwambia asiogope?...jibu ni hapana
kwasababu kumwambia mtu asiogope au anyamaze kulia
ni njia ya uhakika ya kumchochea aogope au alie zaidi…

Siri pekee ya kumtolea mtu yeyote hofu na uwoga


inayotumiwa na 1% ya wataalamu katika matangazo yao
sio kukwambia usiwe na hofu wala uoga bali ni….

Kukuonesha shuhuda za matokeo ya wengine waliokuwa


na changamoto kama yako, wanaahidi kukushika mkono
hatua kwa hatua, wanakusimulia Stories mbali mbali, je
ungekuwa ni wewe una Hofu ungependa kukaa na mtu
yupi?...

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 1O8


Siri # 4: Thibitisha Tuhuma Zao…

Wateja wako tayari hawana imani na wewe pamoja na


wengine wote katika soko ulilopo, wanahitaji kubadili hali
zao za sasa lakini hawana imani juu ya nani sahihi wa
kuwafikisha kule wanakokutaka na kupatamani…

Ukiweza kuthibitisha kwao Kwa kutumia story ya kwamba


hata wewe ulikuwa na tuhuma kama za kwao kuhusu kile
unachokiuza na ukaelezea jinsi ulivyozishinda hizo
tuhuma wote watakuamini na kufanya chochote
unachowaambia katika tangazo lako

Neno ambalo kila mtu huwa anapenda kulisema ni


—“Nilijua tu” hakuna kitu kizuri kama kuthibitisha tuhuma
zetu kwa wengine mfano kama unahisi mchumba wako
anakusaliti halafu baadae akathibitisha basi utajiona ni
bonge moja la Genius au sio? Hahaha…

Kwahiyo kazi yako hapa ni ndogo tu ni wewe kuthibitisha


kwao ya kwamba hata wewe ulikuwa na tuhuma kama
zao kuhusu kile unachokiuza kwa kutumia story, kwa
kifupi waambie kile wanachotaka kukisia then booom!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 1O9


Siri # 5: Wasaidie Walengwa Wako Kuwarushia mawe
Maadui Zao…

Moja ya njia ya uhakika ya kutengeneza wafuasi wengi


katika soko ulilopo ni kutengeneza mazingira ya “SISI Vs
WAO” yaani uwe na kitu unachokiamini na kile
usichokiamini na Kitu gani unapingana nacho katika soko
ulilopo na kwanini unachokifanya kipo tofauti na
wengine?...

…hakuna kitu kinachowaunganisha watu zaidi ya kuwa na


Adui mmoja, kama inavyosemekana ya kwamba kila mtu
huwa anapigana vita usioijua kwa kifupi ni kwamba kila
mtu ana adui

Na ile vita ambayo kila mtu huwa anapigana nayo ndio


Adui mwenyewe huyo, na adui sio lazima awe ni mtu, adui
anaweza kuwa ni kikundi Fulani, Magonjwa Fulani, Dini
fulani, changamoto Fulani za kurudisha nyuma katika
jambo Fulani, hasara kibiashara nk –Kitu chochote
kinachosimama kati kati na kutuzuia kupata kile
tunachokitaka huyo ni Adui!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 110


Watu huwa wanatafuta watu wa kuwaunga mkono katika
mapambano yao kwahiyo kuwa mtu huyo wa kuwaunga
mkono na watafanya chochote unachowaambia!

Je ni Kitu Gani Kinakosekana Katika Hii Sentensi Moja


Iliyobeba SIRI Kuu 5 za Ushawishi Duniani?...

Kuna kitu kimoja kinakosekana katika sentensi hii


ambacho wengi wanaamini ni cha muhimu zaidi katika
hatua za ushawishi kwa mtu yeyote…

Hembu Somo tena hii Sentensi Hapa chini tuone Kama


unaweza kuligundua Hilo neno Moja linalokosekana…

“Watu Watafanya Kitu Chochote Kwa Wale Wanawatia


Moyo na Kuwahimiza Kuhusu Ndoto Zao, Wanaohalalisha
Makosa yao, Wanaowapunguzia Hofu yao,
Wanaothibitisha Tuhuma Zao, na Wale wanaowasaidia
Kuwarushia Mawe maadui zao”

Vipi umegundua kitu?...kama jibu lako ni ndio basi tayari


upo mbele ya mchezo katika soko ulilopo na Neno
Linalokosekana ni…. “WEWE”…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 111


Hakuna neno hata moja kwenye hiyo Sentensi kuhusu
WEWE, mahitaji yako, malengo yako, hofu yako,
bidhaa/huduma yako au kuhusu kile unachokifikiri wewe
—“Kila Kitu ni Kuhusu Mlengwa Wako (Mteja wako)”

Kwanini?...Kwasababu hakuna mtu anayejali kuhusu


Wewe, watu huwa wanajijali wao wenyewe na hununua
vitu kwa sababu zao wenyewe na sio za muuzaji (Hata
wewe uongo?)

Nguvu yako ya ushawishi itabadilika endapo tu utajitoa


kabisa wewe kwenye mfumo mzima wa kuuza na
kumuweka mbele mteja wako au yule unayemlenga

P.S. Watu Hujinunua WAO Bora Zaidi Baada ya Kumiliki


Kile Unachokiuza na hakuna mtu anayejali kuhusu wewe
mpaka pale watapojua ni kiasi gani unajali kuhusu wao!

Angalia Mifano Mbali mbali ya jinsi unavyoweza


Kuzitumia hizo Siri 5 Katika Matangazo yako…

Mfano wa Kuhalalisha Makosa yao: Kama umeshajaribu


kupunguza uzito bila mafanikio hayo sio makosa yako bali
makosa yapo katika mfumo wa mmeng’enyo wa

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 112


chakula…

Mfano wa Kuthibitisha Tuhuma Zao: Kutumia bidhaa


nyingi za kupunguza uzito bila mafanikio inakera sana…

Mfano wa kuwapunguzia Hofu yao Kuu: Kama


umeshajaribu kila njia ya kupunguza uzito bila mafanikio
basi usiwe na wasi wasi ondoa hofu na relax kitu pekee
unachotakiwa kufanya ili kumaliza kabisa hiyo
changamoto ni hiki hapa…

Mfano wa kuwarushia mawe maadui zao: Uhitaji Kutumia


dawa za Mahosipitali ili kupunguza uzito tiba halisi ipo
kwenye virutubisho asilia…

Mfano wa kuwatia moyo katika ndoto zao: unachohitaji ili


kuyafikia malengo yako ni kupata plan ya kupunguza kg 5
tu kila wiki kwa week 4 mfululizo kwa kutumia Formula hii
nilichokuandalia leo…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 113


SURA YA KUMI NA SITA

Jinsi ya Kuuza Kwa Kutumia


STORY Mtandaoni
(STORYSELLING FORMULA)…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 114


Katika soko hili lenye kelele na miluzi mingi Kitu pekee
kitakachokuokoa na kukutenga na ushindani ni STORY!..

Story ndio silaha yako ya Siri ya kuuza katika soko Jipya


kwasababu Mtu haoni Kama anauziwa chochote na kama
tunavyojua kwamba watu huwa hawapendi kuuziwa ila
wanapenda kununua, kwahiyo wale watakaokuwa na
uwezo mzuri wa kusimulia story ndio watakaokuwa
wafalme wa soko la mtandao

Nadhani umeshawahi kusikia huu msemo wa—“Story


sells, Fact Tells” yaani story zinauza na mantiki zinasema
hii ni kweli kwasababu watu wananunua vitu kwa kutumia
hisia (emotions) kisha wanahalalisha maamuzi yao kwa
kutumia mantiki (Logic)

Leo nataka nikupe Formula ya Siri ya kuandika Story


yenye kukuuzia bidhaa/huduma yako mtandaoni ambayo
inatumiwa na 1% ya Copywriters…

…Na mpaka mwisho wa sura hii utakuwa na uwezo wa


kujua story itakayouza zaidi ndani ya sekunde 4 tu, na ipi
itakayobuma na utajua kwanini stories nyingi haziuzi
mtandaoni, na formula hii itakuweka miles 1,000 mbele

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 115


zaidi ya washindani wako Ngoja tuanze na hiki hapa…

Vitu Vinne (4) Vya Lazima Kuwepo Kwenye Story yako


(Sifa Kuu 4 Za Story Yenye Nguvu zaidi)…

1. Kuwe na mhusika au shujaa wa kwenye story yako

2. Kuwe na Hisia za Kweli

3. Kuwe na Wakati Maalumu

4. Kuwe na Taarifa Zinazoendana na walengwa wako

Haya hapa chini maelezo yake…

• Mhusika au shujaa wa kwenye tangazo Lako…

Moja ya kosa kubwa ambalo watu wengi wanalifanya


wanapoandika story zao ni kuweka mbele kile
wanachokiuza aidha ni bidhaa/huduma badala ya yule
wanaesimulia story yake kwa walengwa…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 116


Story yako lazima iwe na mhusika au shujaa ambae wale
unaowasimulia story watajiona ndani ya huyo shujaa au
mhusika pindi wanaposoma story yako na watajisemea
kimoyo moyo huyu ni kama mimi kabisa

Weka kabisa taarifa zote muhimu za huyo shujaa au


mhusika wa story yako kama, jina, umri, sifa yake,
ikiwezekana weka mpaka rangi ya nguo aliyovaa
kwasababu lengo ni kujenga picha ya huyo
shujaa/mhusika kichwani kwa msomaji

Usiandike chochote kuhusu bidhaa, huduma au kampuni


yako kwasababu lengo hapa ni kumtambulisha shujaa
kwa walengwa wako na sio kuuza bidhaa/huduma yako

• Hisia za Kweli…

Waambie kwenye tangazo lako huyo shujaa/mhusika


alijihisi vipi kutokana na changamoto iliyokuwa ikimyima
usingizi usiku, aidha ni Maumivu, uwoga, hasira,
mshangao, mateso nk

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 117


Kupitia hizo hisia wale wanaosoma story yako watajiona
ndani ya huyo shujaa wako, kadri unavyoweka hisia
ndivyo wanavyoipenda zaidi story yako kwasababu
watajua inawahusu wao

• Wakati Maalumu…

Lazima kwenye story yako kuwe na Muda maalumu


pamoja na sehemu maalumu…

Hapa namaanisha mwaka, Saa, pamoja na eneo husika


(nchi, mkoa, mtaa nk)

Kadri unavyojumuisha taarifa ndogo zaidi za eneo ndivyo


story yako inavyowagusa zaidi mfano usiseme tu ilikuwa
ni nchini Tanzania sema kabisa Tanzania ndani ya mji
gani na kama ni Arusha weka mpaka mtaa kabisa…

Story nyingi hazina muda maalumu, hazina eneo


maalumu kwa kifupi hazina taarifa zenye kumfanya
msomaji atengeneze picha ya eneo na wakati maalumu
kichwani mwake

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 118


• Taarifa Zinazoendana na waalengwa wako (wasomaji)…

Ni muhimu Sana kuwajua walengwa wako nje ndani ili


kwenye story yako uweke taarifa zinazoendana na
uhalisia wa maisha yao kwa 100%...

Story yako hata ikiwa nzuri kiasi gani lakini Kama


umeweka taarifa zisizoendana na walengwa wako
itageuka kero kwao na watajua haiwahusu na
hawatanunua kile unachokiuza kwenye story yako,

kwahiyo weka taarifa zinazoendana moja kwa moja na


zile za wasomaji wako mfano kama walengwa wako ni
matajiri basi weka taarifa za kitajiri na kama ni masikini
weka taarifa zinazoendana na uhalisia wa maisha yao
kwa 100%, umepata picha?... okay vizuri sana!

Vipengele Vitatu (3) Vya Story yenye Kuteka Hisia za


Walengwa wako (Story-selling framework)…

Ili story yako iguse hisia za wasomaji na kukufanyia


mauzo ya bidhaa/huduma yako lazima iwe imegewanyika
katika hivi vupengele vitatu muhimu ambavyo story nyingi
za washindani wako hazitakuwa navyo…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 119


Kwahiyo andika story yako kwa kufuata MTIRIRIKO Huu
hapa chini….

1. Maisha ya Kawaida ya shujaa/mhusika wa story yako!

Na hapa ndipo story yako inapoanzia Kwa kuelezea


maisha ya kawaida ya shujaa wa kwenye story yako, hapa
namaanisha uelezee vitu vifuatavyo kwenye story yako…

Shujaa/mhusika alikuwa na changamoto gani

Alikuwa anapitia katika maumivu gani hasa

Kipi hasa kilichokuwa kinamnyima usingizi usiku

Hiyo changamoto iliyaathiri vipi maisha ya mhusika

2. Mlipuko!

Hiki ndicho kipengele cha kuinadi bidhaa/huduma yako


kupitia story yako Kwa kuweka vitu vifuatavyo….

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 120


Elezea jinsi bidhaa/huduma yako ilivyomsaidia kutatua
changamoto ya huyo mhusika au shujaa wa kwenye
tangazo lako

Jinsi bidhaa/huduma yako ilivyoyabadilisha maisha ya


mhusika

Hisia gani alipata mhusika baada ya kutumia


bidhaa/huduma yako

3. Maisha Mapya ya shujaa/mhusika baada ya Kutumia


bidhaa/huduma yako!

Hii ndio hatua ya kuwatengenezea picha kichwani mwao


wasomaji wako ya jinsi watakavyokuwa Kwa kuelezea
maisha ya mhusika yalivyokuwa baada ya kutatua
changamoto yake Kwa kutumia bidhaa/huduma yako

Kumbuka watu hujinunua wao bora zaidi baada ya


kutumia bidhaa/huduma yako na hapa ndipo
unapoonesha jinsi mhusika wa story alivyokuwa bora
zaidi baada ya kutumia bidhaa/huduma yako kwa kuweka
vitu vifuatavyo…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 121


Elezea jinsi maisha ya mhusika yalivyo tofauti kwa
sasa baada ya kutumia bidhaa/huduma yako

Kipi hasa kimebadilika katika maisha ya


mhusika/shujaa

Anajihisi vipi kwa sasa baada ya kuingia katika maisha


mapya

Maumivu gani hasa yamemalizwa na bidhaa/huduma


yako?

Na baada ya kipengele cha Tatu (3) hatua ya mwisho na


ya muhimu zaidi ni kuwaambia jinsi ya kuipata
bidhaa/huduma yako au kuwafanya wachukue hatua kwa
lugha nyingine tunasema unaweka—“Call to Action”
kwasababu pesa zipo kwenye Call to Action sio kwenye
story yako!

Na huo ndio utofauti kati ya Storytelling na storyselling—


Storytelling ni kitendo cha kusimulia story kwa lengo la
story na Story-selling ni kitendo cha kusimulia story kwa
lengo la kuuza

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 122


Aina Tatu (3) Za STORY Zilizobeba pesa Zako
Mtandaoni…

Story za Uthamani (The Value Story)—hizi ni story


zinazoonesha uthamani wa bidhaa/huduma kwa
mteja kupitia story ya Mteja mwenzao ambaye sisi
tunamwita shujaa/mhusika (Story nyingi mtandaoni
zipo kwenye kundi hili)

Story za Uanzilishi (The Founder story)—hizi ni story


unazosimulia kuonesha jinsi ulivyoanzisha biashara
na jinsi ulivyopata wazo la biashara yako na kwanini
unafanya unachokifanya, story hizi zina nguvu sana
kwasababu watu hawanunui bidhaa/huduma
kwasababu unauza, wananunua juu ya sababu ya
KWANINI (Why) unafanya unachokifanya au unauza
unachokiuza (hizi husimuliwa na wajasiriamali
wenyewe na ndio silaha yao ya siri ya kujitenga na
washindani kwasababu bidhaa/huduma zinaweza
kufanana lakini story kamwe haziwezi kufanana na
watu hununua story iliyopo nyuma ya bidhaa/huduma
sio bidhaa/huduma)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 123


Story za Wateja (Customer story)—hizi ni story
zinazoonesha Uthamani wa bidhaa/huduma yako
lakini zinasimuliwa na mteja mwenyewe na sio
muuzaji tofauti na tulivyoona kwenye Story za
Uthamani, na hizi zinafanya kazi kama shuhuda!

Kwahiyo ukitaka kujihakikishia ushindi zaidi katika soko


ulilopo hakikisha una aina zote tatu za story kuhusu kile
unachokiuza mtandaoni

Hizi ndizo Siri Ambazo Hawatakwambia Kuhusu Kuuza


Kwa Kutumia Story (SIRI za Juu zaidi za Kuuza Kwenye
Story)…

Watu hununua story iliyopo nyuma ya bidhaa/huduma


na sio bidhaa/huduma kwahiyo kitu unachokiuza
hakikisha kina story yake kisha uza story sio
bidhaa/huduma

Tengeneza Story ya kwanini unafanya unachokifanya


kwasababu ndicho kinachonunuliwa na sio kile
unachokifanya

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 124


Kipengele cha mateso ya mhusika/shujaa wa story
yako juu ya changamoto yake ndipo penye hela
kwenye story yako kwahiyo hakikisha unatia chumvi
kwenye kidonda hasa

Utamu wa story upo kwenye kumtengenezea


mazingira magumu mhusika/shujaa wa story yako
kupata Solution ya changamoto yake (Tengeneza
mlima mkubwa kati ya changamoto na solution kwa
shujaa wa story yako)

Hata siku moja usiifanye bidhaa/huduma yako kuwa


ndio SHUJAA wa kwenye story yako—Shujaa wa
kwenye Story yako muda wote ni Mhusika wa kwenye
story au Mteja wako (kosa hili pekee limewakosesha
wengi mauzo kwenye story zao)

Siri ya Kupata story inayoendana na OFA yako ni


kuanza kwanza kuwaza kuhusu OFA na sio kuanza
Story kisha OFA na hii ndio sababu wengi wanakuwa
na story lakini haziendani na OFA zao mwishoni—
Kwahiyo waza KINYUME NYUME yaani Anzia kwenye
OFA ndipo uje kwenye story then booom (Thamani ya
siri hii pekee ni $ 10,000 kataa ukubali)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 125


Huu Ndio Muundo wa STORY Inayouza Zaidi (Proven
Story Structure)…

1. Chambo (Hook)—Andika Headline yenye kutengeneza


kiu ya kilichomo kwenye story yako kwa msomaji pamoja
na kuteka attention yake ili umlete kwenye story (hapa
ndipo hela zako zilipo tumia 90% ya muda wako kwenye
headline)

2. Muktadha (Context) —hapa ndipo unapotakiwa


kuitambulisha story yako Kwa wasomaji Kwa kuweka
taarifa zifuatazo…

Ilikuwa wapi (mahali story yako ilipotokea—eneo


husika)

Ilikuwa lini (weka mwaka au mwezi)

Mtambulishe shujaa/mhusika wa kwenye story yako


(weka jina pamoja na taarifa zingine muhimu za
mhusika)

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 126


3. Changamoto za Shujaa/mhusika wa kwenye story
yako (Conflicts)—katika kipengele hiki ndio kiini cha story
yako, elezea changamoto alizipitia mhusika kabla ya
kupata solution, kuza tatizo, Tia chumvi kwenye kidonda
hasa kiasi kwamba msomaji aone msoto aliopitia
mhusika, tengeneza mazingira msomaji aone kwamba
shujaa hakupata solution kirahisi

4. Maisha mapya ya shujaa baada ya kutumia


bidhaa/huduma yako (New life)—elezea maisha mapya ya
shujaa yalivyokuwa baada ya kutumia bidhaa/huduma
yako, jinsi anavyohisi, na hiki ndicho kipengele cha
kumtengenezea msomaji picha ya jinsi atakavyokuwa
baada ya kumaliza changamoto yake ambayo inafanana
na ile ya shujaa wa kwenye story yako kwasababu watu
hujinunua wao bora zaidi baada ya kutumia
bidhaa/huduma yako (Hiki ndicho kipengele cha kuinadi
na kuiuza bidhaa/huduma yako)

5. Fundisho la story yako kwa msomaji (Lesson)—


waambie wasomaji kile ulichojifunza kutoka kwa
shujaa/mhusika wa story yako na hakikisha hicho kitu
kiwe kinatengeneza kiu ya bidhaa/huduma yako kwa
msomaji wa story yako (na hapa ndipo

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 127


unapomtambulisha shujaa wako ambaye ni mteja wako
badala ya bidhaa/huduma yako)

6. Waambie wasomaji wako wachukue hatua


(Recommended Action)—hii ndio hatua ya mwisho kabisa
ya story yako, unachotakiwa kufanya ni kuwaambia
wasomaji wa story yako jinsi ya kuipata hiyo
bidhaa/huduma yako aidha wapige simu, wabofye link,
watume ujumbe nk, Then boooom!

Ngoja nikupe mfano mmoja wa story zangu zilizofanya


vizuri mno wakati nazindua Kozi mpya ya kuuza kupitia

WhatsApp status inatoitwa—“WhatsApp-ship”…

Jinsi ya Kutumia WhatsApp Status Yako Kuuza


Bidhaa/huduma BURE…

Sitosahau ilikuwa ni 17/03/2021 baada tu ya kurudi


mazoezini (Jogging) mida ya 6:30pm maeneo ya moshono
Arusha….

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 128


…Kama kawaida baada ya kutoka bafuni nikapata kifungua
kinywa kisha nikawasha Laptop yangu (Sony) nikaingia
mtandaoni Kwa ajili ya kuseti tangazo la kulipia yaani—
Paid/sponosored Ad

Lengo ilikuwa ni kuuza vitabu vyangu (Mgodi & Hela)


Baada tu ya kuingia kwenye business manager account
yangu nilikutana na ujumbe wa rangi nyekundu ulionipa
mshtuko kidogo nidondoshe laptop yangu chini kwenye
Tairiz…

Ujumbe ulikuwa unasomeka hivi—“Your Ad Account is


Disabled’ yaani akaunti yangu ya matangazo imefungwa
Umeona…Sijui Kama umeshawahi kukutana na huu msala,
kama bado usiombe kukutana nao kwasababu hisia zake

ni zaidi ya message ya—it’s over between us


Hasa hasa biashara yako ikiwa mtandaoni na inategemea
matangazo ya kulipia

Kusema ukweli niliishiwa nguvu kabisa na kibaya zaidi kodi


ya nyumba ilikuwa inaisha wiki inayofuata…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 129


Nilijaribu kuuza kwenye post za kawaida Instagram pamoja
na twitter mauzo yaliwepo lakini sio kama jinsi nilivyozoea
kwenye matangazo ya kulipia—kwahiyo sikuwa na uhakika
wa kuinusuru biashara yangu pamoja na kuepuka fedhea
ya kushindwa kulipa kodi ya nyumba

…nakumbuka ilikuwa ni siku ya jumamosi mida ya 5:30pm


nikiwa nimekaa kwenye restaurant moja hivi hapa Arusha
maeneo stand ndogo inaitwa—“Marc restaurant” huku
nakunywa kahawa (Cuppocino) kupunguza mawazo

Wakati nikiwa nimejikatia tamaa nikaingia kwenye


WhatsApp status yangu baada ya kuangalia VIEWS
nikakuta wameview zaidi ya watu 299+…

…nikajisemea kimoyo moyo—Vipi kama ningetangaza


bidhaa yangu kwa hawa watu walioview status yangu

ningeuza kwa watu wangapi leo?...


Nakumbuka usiku huo sikulala kabisa nilikesha kuandaa—
Captions za kuuza bidhaa yangu kwenye—WhatsApp
status yangu…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 130


Kesho yake mapema nikapost OFA za vitabu kwenye
Status yangu—OMG! Formula hii ilifanya kazi Kama uchawi
vile, mara mteja wa 1,2,3,4 aisee biashara ikapamba moto
sikuona tena hata haja ya kulipia matangazo facebook &
Instagram

Ndani ya siku 7 niliweza kutengeneza zaidi ya 479,000+


kupitia –WhatsApp Status yangu….

Kwanza sikuamini nilidhani labda nimebahatisha huku


nikijisemea kimoyo moyo—Haiwezekani yaani kirahisi
rahisi tu hivi?”

Baada ya mwezi mmoja kupita rafiki yangu Stanley ana


duka la kuuza jeans—akaniomba nimfundishe jinsi ya
kuuza kwenye WhatsApp status yake sikuwa na imani
kama mbinu hizi zingefanya kazi kwake ila kwasababa
aliomba nikaamua tu kumfundisha hivyo hivyo
Tukaanza Coaching mdogo mdogo…

Ndani ya siku 7 sikuamini macho yangu—kutoka kwenye


watu kuview tu status za Stanley bila kuuliza chochote
mpaka mauzo ya Tshs 753,000 kidogo nidondoke kwenye
kiti baada ya habari hizo…

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 131


Yaani Stanley katoka kwenye kutokujua chochote kuhusu
kuuza kwenye—WhatsApp status yake mpaka mauzo ya
Tshs 753,000 ndani ya siku 7 tu

Na huo ndio ukawa mwanzo na sababu ya kutengeneza


KOZI Maalumu yenye mbinu za Kuuza bidhaa/huduma
BURE Kupitia WhatsApp Status inayoitwa—“WhatsApp-
ship”

…kozi hii sio kwa ajili ya kila mtu ni maalumu kwa wale tu
wanaotaka kutumia WhatsApp status zao kuongeza mauzo
ya bidhaa/huduma zao mara 10 zaidi…

Kozi hii haijatoka rasmi na itakapotoka Thamani yake


itakuwa ni Tshs 79,000…LAKINI leo nataka niitoe kwa watu
30 tu wa kwanza kwa Exclusive OFA ya Tshs 30,000 Tu

Kwahiyo Kama unataka kuwa miongoni mwa watu 30 wa


kwanza kupata kozi hii kwa ofa ya Tshs 30K Tu (Badala ya
Tshs 79K) basi nitumie ujumbe DM au WhatsApp kwenda
0767-912-157 sasahivi!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 132


HITIMISHO

Nataka nikuuulize kitu muhimu Sana sasahivi ambacho


ningependa ukichukulie Kwa uzito mkubwa mno….

“Unadhani Kitu Gani Kingetokea Kwako na Kwenye


Biashara yako Mtandaoni, Endapo Kama Ungetumia
Mbinu Zote Hizi Ulizozigundua Leo Katika Kitabu Hiki?”
Ingekuwaje yani, hembu jaribu kufikiria kuhusu Hilo Kwa
Dakika kadhaa tu…

Tayari nimeshakupa ramani ya kukufikisha kule


unakokutaka na mpira upo mguuni mwako, ingia
uwanjani, jitokeze sokoni, ingiza kwenye vitendo kila kitu
ulichojifunza, Wasaidie watu kutatua changamoto zao,
Tumia hizi mbinu ulizojifunza humu na kamwe huwezi
kuwaza kuhusu mshindani yeyote atayejitokeza mbele
yako katika soko ulilopo!

Je ni Kwa Namna Gani Ungependa Kulitawala Soko


Ulilopo na Kupata Mbinu MPYA za Kuuza Mtandaoni kwa
njia ya Maandishi Zenye Thamani ya Tshs 2,300,000+
($1,000) BURE?...

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 133


Je ni kwa namna Gani ungependa kulitawala soko
ulilopo?...

Ni Kwa namna gani ungependa kuwa miles 1,000 mbele


zaidi ya washindani wako katika soko ulilopo?
Ni Kwa namna gani ungependa kuwa na mbinu za
kuandika matangazo yako mtandaoni yenye kukupa
uhakika wa kwamba, ukiweka $1 inazaa $20?...

…..Leo Nina Habari Njema Sana Kwa ajili yako….

Kwa Muda Maalumu na Kwa Watu wachache sana


nimekuwa nikifanya Private 1 On 1 Coaching ya
Copywriting skills na kuwashika mkono watu serious
kama wewe hatua kwa hatua ndani ya wiki nne (mwezi
mmoja) na kuwageuza mashine za kuchapisha pesa
mtandaoni pamoja na kuliteka soko walilipo
(unafundishwa kwa muda wako bila kuharibu ratiba yako
ya kila siku)

Na sikwambii hivyo Kama njia ya kutaka kukuuzia


chochote Bali ni njia ya kukwambia tu kwamba kuna
Uthamani mkubwa zaidi utaukosa endapo hautafanya
maamuzi yoyote baada ya kumaliza kusoma kitabu hiki

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 134


leo

…Kama utaona Hujapata Madini yenye Thamani ya Tshs


2,300,000+ Baada ya Mwezi Mmoja wa 1 On 1 Coaching
na mimi basi Niambie Kwenye Group na Nitakupa Tshs
100,000 ya Usumbufu wa kukupotezea muda wako –
Kwahiyo Hakuna RISK yoyote upande wako…

Kwasababu Nafasi huwa ni chache sana na watu wengi


wanahitaji huduma hii kama unataka kulipeleka jina lako
pamoja na biashara yako katika viwango vya kimataifa
kupitia EXCLUSIVE na PRIVATE 1 on 1 coaching ya mwezi
mmoja basi nitumie ujumbe WhatsApp 0767-912-157
Sasahivi ili tuone kama utakidhi vigezo vyake!

Kwa ajili ya Mafanikio yako!

Amosi Nyanda (The Sukuma Dragon) & Team nzima ya


MGODI 2.0!

Mgodi 2.0 | Amosi Nyanda | 135

You might also like