Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

RICHARD JOHN MWALUKO

S.L.P 1249

DODOMA

Phone: 0754092430

09/11/2021

BODI YA MKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

S.L.P 76068

DAR ES SALAAM.

K.K

OFISI YA MTAA NZUGUNI “C”

S.L.P 1249

NZUGUNI – DODOMA.

Ndugu,

YAH: RUFAA YA MAOMBI YA MKOPO MWAKA WA KWANZA WA MASOMO 2021/22

NDUGU MARIETHA RICHARD JOHN.

Husika na kichwa cha habari tajwa hapo juu.Mimi ni baba wa mwanafunzi anayeitwa MARIETHA
RICHARD JOHN ambaye alichaguliwakujiunga na elimu ya juu mwaka wa masomo 2021/22 ngazi ya
shahada ya awali ya Usimamizi wa Rasilimali watu katika Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es salaam.
Sisi wazazi wake ni wakulima na kipato chetu ni kidogo hatuna uwezo wa kukidhi gharama za masomo
yake.
Historia ya elimu yake MARIETHA RICHARD JOHN ipo kama ifuatavyo,alimaliza kidato cha nne
(Form Four) mwaka 2015 Nzuguni Secondary School na namba ya mtahiniwa (Form Four Index
Number) S2897.0026.2015.Alipata ufaulu wa daraja la nne ,alama ambazo hazikumwezesha kuendelea na
masomo ya kidato cha tano.
Baada ya hapo alianza kujisomea masomo ya ziada yaani tuition na kujisajili kama mtahiniwa binafsi
(Private candidate) kwa ajili ya kufanya mtihani wa kidato nne (Form Four) mwaka 2018 ALFA
CENTRE na namba ya mtahiniwa (Form Form Index Number) P2517.0399.2018 alifaulu.
Baadae alijiunga na Masomo ya Tuition kwa kidato cha tano na sita mtaani,mwaka 2021 alijisajili katika
kituo cha kufanyia mtihani kama mtahiniwa binafsi (private candidate) kidato cha sita hapo PERFECT
VISION SEC SCHOOL CENTER namba ya mtahiniwa(form six index number) P1475.0535.2021
Kwa kipindi chote cha elimu yake kuanzia kidato cha nne (Form Four) na kidato cha sita (Form Six)
Amekuwa akitumia mfumo wa kusoma masomo ya ziada yaani Tuition pekee kama mtahiniwa binafsi
bila kujiunga na masomo ya darasa shuleni .Hii ni kutokana na hali ya kipato kidogo cha wazazi wake
ambao ni wakulima.

1
Mwaka 2021 baada ya kupata ufaulu wa daraja la pili (Division two) alichaguliwa na kujiunga masomo
ya elimu ya juu katika chuo kikuu cha Tumaini Dar es salaam, gharama za masomo zikiwa kama
ifuatavyo katika Pesa za Kitanzania (TZS);
1. Tuition Fee…………………………… 1,850,000/=
2. Registration and other cost ……………220,000/=
3. Student Union Fee,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,25,000/=
4. Medical / NHIF Fee………………………50,400/=
Mpaka sasa tumeweza kumudu gharama za usajili pekee (Registration cost) 220,000/= tunategemea
mkopo aliomba ili umsaidie kutimiza ndoto kulingana na juhudi zote ambazo amezifanya katika masomo
ili kufikia malengo na kujikomboa kama mtoto wa kike pia kutimiza ndoto zake.
Tunaomba Bodi ya Mkopo na Serikali ya Mheshimiwa Samia Suluhu iunge mkono Juhudi za
kumuwezesha binti yetu kuendelea na masomo,pia ikiwa ni moja ya sera za kuwawezesha wanawake
kutimiza malengo yao katika masomo na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Wazazi wake kulingana na gharama kuwa na kiwango cha juu,uwezo wetu ni mdogo tunaomba msaada
wa serikali. Gharama zinazotakiwa kumsaidia binti yetu ili afanikishe masomo yake kwa mwaka 2021/22
ni kama ifuatavyo;
1. Tuition Fee…………………………… 1,850,000/=
2. Student Union Fee,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,25,000/=
3. Medical / NHIF Fee………………………50,400/=
4. Hostel Cost ……………………………...600,000/=
5. Food Support…………………………,.2,040,000/=
Jumla ya gharama zote ni …………………… 4,565,000/=
Hii ni Kulingana na kwamba binti huyo anaishi Dodoma na wazazi wake,lakini yuko Dar es salaam baada
ya kuchaguliwa kujiunga na chuo ambacho kiko Dar es salaam.Kwa kipichi chote cha masomo atakuwa
akihitaji gharama ya chakula na mahala pa kuishi kipindi cha masomo.
Kwa Pamoja sisi wazazi,tunatanguliza shukrani za dhati na kuomba maombi yake ya mkopo yapitiwe
kwa mara nyingine tena kwani tunakubali na kutambua jukumu kubwa ambalo mnaendelea nalo la
kusaidia jamii ya watanzania wenye uhitaji.

Wako Mtiifu
……………………………
Richard Mwaluko.

You might also like