Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 10

ZEKARIA

Utangulizi
Zekaria alianza huduma yake mnamo mwezi wa nane wa mwaka wa pili wa Dario (520 K.K.), miezi miwili
baada ya ujumbe wa kwanza wa Hagai. Maana ya jina Zekaria ni “BWANA amekumbuka.” Haijulikani kwa
uhakika Zekaria aliendelea kufanya huduma hiyo kwa muda gani.Kwa kadiri ionekanavyo alikuwa kijana (2:4)
wakati alipoanza huduma yake. Ido, ambaye ni babu yake (Zek 1:1) alikuwa miongoni mwa wale waliorudi kutoka
uhamishoni mwaka 538 K.K.
Katika ujumbe wake wa kwanza (1:1-6) Zekaria anawaonya watu ambao ndio kwanza tu walikuwa
wameanza kujenga upya hekalu kwamba inawapasa kusikiliza ujumbe wa Mungu kupitia manabii na kudumisha
uhusiano wa muhimu na Mungu, wasije wakaharakisha hukumu ya Mungu. Mfululizo wa maono ya usiku (1:7-
6:8) yanatia moyo wajenzi ule wakati mgumu katika hatua ya kukata tamaa.Ule utaratibu wa ujenzi ulikuwa
umesababisha maafisa wa Kiajemi kufanya uchunguzi na kuandika taarifa ya malalamiko kwa Dario (Ezr 5-6).
Huenda Wayahudi walikuwa wakingojea hukumu ya Dario wakati Zekaria akitoa ujumbe wake uliowekewa msingi
katika haya maono ya usiku. Mtazamo wa jumla wa mfululizo wa maono haya manane yanawahakikishia wajenzi
kwamba Mungu anao mpango wa muda mrefu kwa ajili ya Israeli.
Miaka miwili baadaye, (518 K.K.) suala la kutia katika matendo kutii kufunga liliibuka (7:1-8:23). Zekaria kwa
mara nyingine anaangaliza watu kwamba njia ya kudumisha uhusiano sahihi na Mungu ni utii. Kule kufunga ili tu
kwamba mtu amefunga ni ubatili.Utaratibu wa kushika sheria kamwe hauwezi kutumika kama njia mbadala ya
kuonyesha upendo wa Mungu katika maisha ya kila siku. Sehemu ya mwisho ya ujumbe wa Zekaria (9-14)
haukuonyeshwa tarehe. Uwezekano mkubwa ni kwamba ulitolewa baadaye, huenda mnamo mwaka 480 K.K.
Hapa mkazo uko katika mpango wa maendeleo wa muda mrefu ukionyesha kusimamishwa kwa ufalme wa
mwisho. Mfalme anatambulishwa kama anayekuja kwa tabia ya unyenyekevu akileta wokovu lakini akikataliwa na
watu wake mwenyewe, yaani, Waisraeli, ambao baadaye wanaachwa kwenye hukumu ya mataifa. Mataifa
yatakapokusanyika kwa ajili ya vita dhidi ya Yerusalemu, Waisreli watamtambua Yeye “Yule waliomchoma mkuki”
(Zek.12:10) na wataibuka na ushindi. Ndipo mataifa yote yatakuja Yerusalemu kumwabudu Mfalme, Bwana wa
Majeshi.
Wazo Kuu
Zekaria anaonyesha kwamba Mungu ana mpango wa muda mrefu na Israeli, hivyo anaita mwito wa
utii.Anaonyesha jinsi ambavyo watu wanaweza kufanya mambo “ Si kwa nguvu wala kwa uwezo bali kwa Roho
Yangu ”asema.( 4:6).. Kuwapa watu wa Mungu matumaini kwa kuwajulisha watu mpango wa Mungu wa baadaye
wa ukombozi kupitia kwa Masiya.
.
Mambo Muhimu
Huu ujumbe wa mwanzoni unafuatiliwa na maono ambayo yaliwatia moyo wajenzi ambao Zekaria aliwatia
moyo kwa kuwaambia kwamba Mungu alikuwa na mpango mrefu kwa ajili ya Israeli.
Katika sura ya 7 na 8 Zekaria aliwataka watu wamtii Mungu, hii ikiwa ni njia ya kila mtu kumjali na kumhurumia
mwenzake. Mungu alitaka utii kwao katika kuhusiana naye.
Sura ya 9 mpaka 14 inazungumzia habari za miezi inayokuja, hukumu ya mwisho na kukua kwa muda mrefu
kwa ufalme wa mwisho.
Mwandishi
Zekaria
Mahali
Yerusalemu
Tarehe
520-470 K.K.
Wahusika
Hagai, Zerubabeli, Yoshua na waliorudi kutoka uhamishoni.
.
Mgawanyo
• Wito wa kuwa watiifu. (1:1-6)
• Maono. (1:7-6:15)
• Hukumu dhidi ya maadui wa Israeli. (9:1-8)

1
ZEKARIA
Wito Wa Kumrudia BWANA ndivyo BWANA Mwenye Nguvu asemavyo:
Katika mwezi wa nane wa mwaka wa pili ‘Geukeni, mziache njia zenu mbaya na matendo
1 wa utawala wa mfalme Dario, neno la yenu maovu.’ Lakini hawakunisikiliza wala
BWANA lilimjia nabii Zekaria mwana wa kufuata maelekezo yangu, asema BWANA.
Berekia, mwana wa Iddo, kusema: 5Wako wapi baba zako sasa? Nao manabii, je,
2“BWANA aliwakasirikia sana baba zako wa wanaishi milele? 6Je, maneno yangu na amri
zamani. 3Kwa hiyo waambie watu: Hivi ndivyo zangu nilizowaagiza manabii watumishi wangu,
BWANA Mwenye Nguvu asemavyo: ‘Nirudieni hayakuwapata baba zenu?’’
mimi,’ asema BWANA Mwenye Nguvu, ‘Nami “Kisha walitubu na kusema, ‘BWANA
nitawarudia ninyi,’ asema BWANA Mwenye Mwenye Nguvu ametutenda sawasawa na njia
Nguvu. 4Msiwe kama baba zenu, ambao zetu na matendo yetu yalivyostahili, kama
manabii waliotangulia waliwatangazia: Hivi alivyokusudia kufanya.’ ’’
‘Nitairudia Yerusalemu kwa rehema na huko
Maono Ya Kwanza: nyumba yangu itajengwa tena. Nayo kamba ya
Mtu Katikati Ya Miti Ya Mihadasi kupimia itanyooshwa Yerusalemu,’ asema
7Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa BWANA Mwenye Nguvu.
kumi na moja,yaani mwezi uitwao Shebati, 17“Endelea kutangaza zaidi kwamba: Hivi

katika mwaka wa pili wa kutawala kwake mfalme ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu: ‘Miji
Dario, neno la BWANA lilimjia nabii Zekaria yangu itafurika tena usitawi na BWANA
mwana wa Berekia mwana wa Iddo. atamfariji tena Sayuni na kumchagua
8Wakati wa usiku nilipata maono, mbele Yerusalemu.’ ’’
yangu alikuwepo mtu akiendesha farasi
mwekundu! Alikuwa amesimama katikati ya miti Maono Ya Pili:
ya mihadasi kwenye bonde. Nyuma yake Pembe Nne Na Mafundi Wanne
walikuwepo farasi wekundu, wa kikahawia na 18Kisha nikatazama juu, na pale mbele

weupe. yangu nikaona pembe nne! 19Nikamwuliza yule


9Nikauliza, ‘‘Hivi ni vitu gani bwana wangu?’’ malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Ni nini
Malaika aliyekuwa akizungumza na mimi hivi?’’
akanijibu, ‘‘Nitakuonyesha kuwa ni nini.’’ Akanijibu, “Hizi ni zile pembe
10Kisha yule mtu aliyesimama katikati ya miti zilizowatawanya Yuda, Israeli na Yerusalemu.’’
ya mihadasi akaeleza, ‘‘Ni wale ambao BWANA 20Kisha BWANA akanionyesha mafundi

amewatuma waende duniani kote.’’ wanne. 21Nikauliza, “Hawa wanakuja kufanya


11Nao wakatoa taarifa kwa yule malaika wa nini?’’
BWANA, aliyekuwa amesimama katikati ya miti Akanijibu, “Hizi ndizo pembe
ya mihadasi, ‘‘Tumepita duniani kote na kukuta zilizowatawanya Yuda ili asiwepo atakayeweza
ulimwengu wote umepumzika kwa amani.’’ kuinua kichwa chake, lakini mafundi wamekuja
kuzitia hofu na kuzitupa chini hizi pembe za
12Kisha malaika wa BWANA akasema, mataifa ambayo yaliinua pembe zao dhidi ya
‘‘BWANA Mwenye Nguvu, utazuia mpaka lini nchi ya Yuda na kuwatawanya watu wake.’’
rehema kutoka Yerusalemu na miji ya Yuda,
ambayo umeikasirikia kwa miaka hii sabini?’’ Maono Ya Tatu:
13Kwa hiyo BWANA akazungumza maneno ya Mtu Mwenye Kamba Ya Kupimia
upole na ya kufariji kwa malaika aliyezungumza
nami. 2 Kisha nikatazama juu, pale mbele yangu
alikuwepo mtu mwenye kamba ya kupimia
14Kisha malaika yule aliyekuwa mkononi mwake! 2Nikamwuliza, “Unakwenda
akizungumza nami akasema, ‘‘Tangaza neno wapi?’’
hili: Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu asemalo: Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata
‘Nina wivu sana kwa ajili ya Yerusalemu na urefu na upana wake.’’
Sayuni, 15lakini nimeyakasirikia sana mataifa 3Kisha malaika aliyekuwa akizungumza

yanayojisikia kuwa yako salama. Nilikuwa nami akaondoka, malaika mwingine akaja
nimewakasirikia Israeli kidogo tu, lakini mataifa kukutana naye 4na kumwambia: “Kimbia,
hayo yaliwazidishia maafa.’ umwambie yule kijana, ‘Yerusalemu utakuwa mji
16‘‘Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo BWANA: usio na kuta kwa sababu ya wingi wa watu na

2
ZEKARIA
mifugo iliyomo. 5Mimi mwenyewe nitakuwa 6Malaika wa BWANA akamwamuru Yoshua:
ukuta wa moto kuuzunguka,’ asema BWANA, 7“Hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye
‘nami nitakuwa utukufu wake ndani yake.’ Nguvu: ‘Ikiwa utakwenda katika njia zangu na
6“Njoni! Njoni! Kimbieni mtoke katika nchi ya kushika masharti yangu, basi utaitawala nyumba
kaskazini,’’ asema BWANA, “Kwa kuwa yangu na kuwa na amri juu ya nyua zangu, nami
nimewatawanya kwenye pande nne za mbingu,’’ nitakupa nafasi miongoni mwa hawa
asema BWANA. wasimamao hapa.
7“Njoo, Ee Sayuni! Kimbia, wewe uishiye 8‘‘ ‘Sikiliza, Ee Yoshua kuhani mkuu, pamoja

ndani ya Binti Babeli!’’ 8Kwa kuwa hivi ndivyo na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni
asemavyo BWANA Mwenye Nguvu: “Baada ya watu ishara ya mambo yatakayokuja:
yeye kuniheshimu na kunituma mimi dhidi ya Ninakwenda kumleta mtumishi wangu, Tawi.
mataifa yaliyokuteka wewe nyara, kwa kuwa ye 9Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua!

yote awagusaye ninyi, anaigusa mboni ya jicho Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami
lake, 9hakika nitauinua mkono wangu dhidi yao nitachora maandishi juu yake,’ asema BWANA
ili watumwa wao wawateke nyara. Ndipo Mwenye Nguvu, ‘nami nitaiondoa dhambi ya
mtakapojua ya kwamba BWANA Mwenye nchi hii kwa siku moja.
Nguvu amenituma. 10“ ‘Katika siku hiyo kila mmoja wenu
10“Piga kelele na ufurahie, Ee Binti Sayuni, atamwalika jirani yake akae chini ya mzabibu
kwa maana ninakuja, nami nitaishi miongoni wake na mtini wake,’ asema BWANA Mwenye
mwenu,’’ asema BWANA. 11“Mataifa mengi Nguvu.’
yataunganishwa na BWANA siku hiyo, nao
watakuwa watu wangu. Nitaishi miongoni Maono Ya Tano:
mwenu nanyi mtajua kwamba BWANA Mwenye Kinara Cha Taa Cha Dhahabu Na Mizeituni
Nguvu amenituma kwenu. 12BWANA atairithi Miwili
Yuda kama fungu lake katika nchi takatifu na
atachagua tena Yerusalemu. 13Tulieni mbele za 4 Kisha malaika aliyezungumza nami
akarudi na kuniamsha, kama mtu
BWANA, enyi watu wote, kwa sababu ameinuka aamshwavyo kutoka katika usingizi wake.
kutoka makao yake matakatifu.” 2Akaniuliza, “Unaona nini?’’

Nikajibu, “Ninaona kinara cha taa cha


Maono Ya Nne: dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake na taa
Mavazi Safi Kwa Ajili Ya Kuhani Mkuu zake saba juu yake, tena iko mirija saba ya

3 Kisha akanionyesha Yoshua kuhani mkuu


akiwa amesimama mbele ya malaika wa
kuleta mafuta, kwenye taa zote zilizo juu yake.
3Pia kuna mizeituni miwili karibu yake, mmoja

BWANA, naye Shetani amesimama upande upande wa kuume wa bakuli na mwingine


wake wa kuume ili amshitaki. 2BWANA upande wa kushoto.’’
akamwambia Shetani, “BWANA akukemee 4Nikamuuliza malaika aliyezungumza nami,

Shetani! BWANA, ambaye ameichagua “Hivi ni vitu gani, bwana wangu?’’


Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo 5Akanijibu, “Hujui kuwa hivi ni vitu gani?’’

kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye Nikajibu, “Hapana, bwana wangu.’’


moto?’’ 6Kisha akaniambia, “Hili ni neno la BWANA
3Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa nguo kwa Zerubabeli: ‘Si kwa nguvu, wala si kwa
chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika. uwezo, bali ni kwa Roho yangu,’ asema BWANA
4Malaika akawaambia wale waliokuwa Mwenye Nguvu.
wamesimama mbele yake, ‘‘Mvueni nguo zake 7‘‘Wewe ni kitu gani, Ee mlima mkubwa

chafu.’’ sana? Mbele ya Zerubabeli wewe utakuwa ardhi


Kisha akamwambia Yoshua, ‘‘Tazama, tambarare. Kisha ataweka jiwe la juu kabisa la
nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mwisho na watu wakipiga kelele wakisema,
mavazi ya kitajiri.’’ ‘Mungu libariki! Mungu libariki!’’
5Kisha nikasema, “Mvike kilemba kilicho safi 8Kisha neno la BWANA likanijia: 9‘‘Mikono

kichwani mwake.’’ Kwa hiyo wakamvika kilemba ya Zerubabeli iliweka msingi wa hekalu hili,
safi kichwani na kumvika yale mavazi mengine, mikono yake pia italimalizia. Kisha mtajua ya
wakati malaika wa BWANA akiwa amesimama kuwa BWANA Mwenye Nguvu amenituma mimi
karibu. kwenu.

3
ZEKARIA
10‘‘Ninani anayeidharau siku ya mambo 9Kisha nikatazama juu na mbele yangu,
madogo? Watu watashangilia watakapoona walikuwepo wanawake wawili, wakiwa na upepo
timazi mkononi mwa Zerubabeli. katika mabawa yao! Walikuwa na mabawa kama
“(Hizi saba ni macho ya BWANA ambayo ya korongo, nao wakainua kile kikapu na kuruka
huzunguka duniani kote.)’’ nacho kati ya mbingu na nchi.
11Kisha nikamwuliza yule malaika, “Hii 10Nikamwuliza yule malaika aliyekuwa
mizeituni miwili iliyoko upande wa kuume na wa akizungumza nami, ‘‘Wanakipeleka wapi hicho
kushoto wa kinara cha taa ni nini?” kikapu?’’
12Tena nikamwuliza, “Haya matawi mawili 11Akanijibu, ‘‘Wanakipeleka katika nchi ya

ya mizeituni karibu na hiyo mirija miwili ya Babeli na kujenga nyumba kwa ajili yake.
dhahabu inayomimina mafuta ya dhahabu ni Itakapokuwa tayari, kikapu kitawekwa pale
nini?’’ mahali pake.’’
13Akajibu, “Hujui kuwa haya ni nini?’’

Nikamjibu, “Hapana, bwana wangu.’’ Maono Ya Nane: Magari Manne Ya Vita

6
14Kwa hiyo akasema, “Hawa ni wawili Nikatazama juu tena, nikaona mbele yangu
ambao wamepakwa mafuta ili kumtumikia magari manne ya vita yakija kutoka kati ya
Bwana wa dunia yote.’’ milima miwili, milima ya shaba! 2Gari la kwanza
lilivutwa na farasi wekundu, la pili lilivutwa na
Maono Ya Sita: Gombo Linaloruka farasi weusi, 3la tatu lilivutwa na farasi weupe na

5 Nikatazama tena, mbele yangu kulikuwa


na kitabu kilichoruka!
2Akaniuliza, “Unaona nini?’’
gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya
kijivu, wote wenye nguvu. 4Nikamwuliza malaika
aliyekuwa akizungumza nami, ‘‘Hawa ni nani
Nikamjibu, “Naona kitabu kinachoruka bwana wangu?’’
chenye,urefu wa dhiraa ishirini a na upana wa 5Malaika akanijibu, ‘‘Hizi ni roho nne za

dhiraa kumi b .’’ mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa


3Akaniambia, “Hii ni laana inayotoka kwenda Bwana wa dunia yote, zinatoka kwenda kufanya
juu ya nchi yote, kwa kuwa kufuatana na yale kazi yake. 6Gari linalovutwa na farasi weusi
yaliyoandikwa katika upande mmoja, kila mwizi linaelekea katika nchi ya kaskazini, la farasi
atahamishwa, pia kufuatana na yaliyo upande weupe linaelekea magharibi na la farasi wa
wa pili, kila aapaye kwa uongo atahamishwa. madoadoa ya kijivu linaelekea kusini.’’
4BWANA Mwenye Nguvu asema, ‘Nitaituma 7Wakati hao farasi wenye nguvu walipokuwa

hiyo laana, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi wakitoka, walikuwa wakijitahidi kwenda duniani
na nyumba ya huyo aapaye kwa uongo kwa jina kote. Akasema, ‘‘Nenda duniani kote!’’ kwa hiyo
langu. Itabaki katika nyumba yake na kuiharibu, wakaenda duniani kote.
pamoja na mbao zake na mawe yake.’ ’’ 8Kisha akaniita, “Tazama, wale
wanaokwenda kuelekea nchi ya kaskazini
Maono Ya Saba: Mwanamke Ndani Ya Kikapu wamepumzisha Roho yangu katika nchi ya
5Kisha yule malaika aliyekuwa akizungumza kaskazini.’’
nami akanijia na kuniambia, “Tazama juu uone
ni nini kile kinachojitokeza.’’ Taji Kwa Ajili Ya Yoshua.
6Nikamwuliza, “Ni kitu gani?’’ Akanijibu, ‘‘Ni 9Neno la BWANA likanijia kusema:
kikapu cha kupimia.’’ Kisha akaongeza kusema, 10‘‘Chukua fedha na dhahabu kutoka kwa watu

‘‘Huu ni uovu wa watu katika nchi nzima.’’ waliohamishwa yaani Heldai, Tobia na Yedaya
7Kisha kifuniko kilichotengenezwa kwa ambao wamefika kutoka Babeli. Siku iyo hiyo
madini ya risasi kilichokuwa kimefunika kile nenda nyumbani kwa Yosia mwana wa Sefania.
kikapu, kiliinuliwa na ndani ya kile kikapu 11Chukua fedha na dhahabu utengeneze taji,

alikuweko mwanamke ameketi! 8Akasema, ‘‘Huu nawe uiweke kichwani mwa kuhani mkuu
ni uovu,’’ akamsukumia ndani ya kikapu na Yoshua, mwana wa Yehosadiki. 12Umwambie,
kushindilia kifuniko juu ya mdomo wa kikapu. hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu:
‘Huyu ndiye mtu ambaye jina lake ni Tawi, naye
atachipua kutoka mahali pake na kujenga
a2 ‘‘dhiraa ishirini’’ ni sawa na mita 9. hekalu la BWANA. 13Ni yeye atakayejenga
b2 ‘‘dhiraa kumi’’ ni sawa na mita 4.5 hekalu la BWANA, naye atavikwa utukufu na

4
ZEKARIA
ataketi kumiliki katika kiti cha enzi naye atakuwa walikuwa wageni. Nchi ikaachwa ukiwa nyuma
kuhani katika kiti chake cha enzi. Hapo yao kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuingia au
patakuwa amani kati ya hao wawili.’ 14Taji kutoka. Hivi ndivyo walivyoifanya ile nchi
itatolewa kwa Heldai, Tobia, Yedaya na Heni iliyokuwa imependeza kuwa ukiwa.’ ’’
mwana wa Sefania kama kumbukumbu ndani ya
hekalu la BWANA. 15Wale walio mbali sana BWANA Anaahidi Kuibariki
watakuja na kusaidia kulijenga hekalu la Yerusalemu
BWANA, nanyi mtajua ya kwamba BWANA
Mwenye Nguvu amenituma kwenu. Hili litatokea 8 Neno la BWANA Mwenye Nguvu likanijia
tena. 2Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye
ikiwa mtamtii BWANA, Mungu wenu kwa bidii.’’ Nguvu: “Nina wivu sana kwa ajili ya Sayuni,
ninawaka wivu kwa ajili yake.”
Haki Na Rehema, Sio Kufunga 3Hiii ndilo asemalo BWANA: “Nitarudi

7 Katika mwaka wa nne wa utawala wa


mfalme Dario, neno la BWANA lilimjia
Sayuni na kufanya makao Yerusalemu. Kisha
Yerusalemu utaitwa mji wa kweli, mlima wa
Zekaria siku ya nne ya mwezi wa tisa, mwezi wa BWANA Mwenye Nguvu utaitwa Mlima
Kisleu. 2Watu wa Betheli walikuwa wamemtuma Mtakatifu.’’
Shareza na Regam-meleki pamoja na watu wao, 4Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu:

kumsihi BWANA 3kwa kuwauliza makuhani wa “Kwa mara nyingine tena wazee wanaume kwa
nyumba ya BWANA Mwenye Nguvu na manabii, wanawake walioshiba umri wataketi katika
“Je, imempasa kuomboleza na kufunga katika barabara za Yerusalemu, kila mmoja akiwa na
mwezi wa tano, kama ambavyo nimekuwa mkongojo wake mkononi kwa sababu ya umri
nikifanya kwa miaka mingi?” wake. 5Barabara za mji zitajaa wavulana na
4Kisha neno la BWANA Mwenye Nguvu wasichana wanaocheza humo.’’
likanijia kusema: 5“Waulize watu wote wa nchi 6Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu:

na makuhani, ‘Je, mlipofunga na kuomboleza “Mambo haya yanaweza kuonekana ya ajabu


katika mwezi wa tano na wa saba kwa miaka kwa mabaki ya watu wakati huo, lakini yaweza
sabini iliyopita, mlifunga kweli kwa ajili yangu? kuwa ya ajabu kwangu?’’ asema BWANA
6Na mlipokuwa mkila na kunywa, je, hamkuwa Mwenye Nguvu.
mnasheherekea kwa ajili ya nafsi zenu? 7Je, 7Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu:

haya sio maneno ya BWANA aliyosema kupitia “Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi za
manabii waliotangulia, wakati Yerusalemu mashariki na magharibi. 8Nitawarudisha waje
pamoja na miji inayoizunguka ilipokuwa katika kuishi Yerusalemu, watakuwa watu wangu nami
hali ya utulivu na ya mafanikio, wakati Negebu nitakuwa mwaminifu na wa haki kwao kama
na Shefala zikiwa zimekaliwa na watu?’ ’’ Mungu wao.’’
8Neno la BWANA likamjia tena Zekaria: 9Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu:
9“Hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye “Ninyi ambao sasa mnasikia maneno haya
Nguvu: ‘Fanyeni hukumu za haki, onyesheni yanayozungumzwa na manabii ambao
rehema na huruma ninyi kwa ninyi. walikuwepo wakati wa kuwekwa kwa msingi wa
10Msimwonee mjane wala yatima, mgeni wala nyumba ya BWANA Mwenye Nguvu, mikono
maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu yenu na iwe na nguvu ili hekalu liweze
ninyi kwa ninyi.’ kujengwa. 10Kabla ya wakati huo, hapakuwepo
11“Lakini wakakataa kusikiliza, wakanipa na ujira kwa mtu wala mnyama. Hakuna mtu
kisogo kwa ukaidi na kuziba masikio yao. aliyeweza kufanya shughuli yake kwa usalama
12Wakaifanya mioyo yao migumu kama jiwe kwa sababu ya adui yake, kwa kuwa nilikuwa
gumu na hawakuisikiliza sheria au maneno nimemfanya kila mtu adui wa jirani yake.
ambayo BWANA Mwenye Nguvu aliyatuma kwa 11Lakini sasa sitawatendea mabaki ya watu

njia ya Roho wake kupitia manabii waliotangulia. hawa kama nilivyowatenda zamani,’’ asema
Kwa hiyo BWANA Mwenye Nguvu alikasirika BWANA Mwenye Nguvu.
sana. 12“Mbegu itakua vizuri, mzabibu utazaa
13‘Wakati nilipoita, hawakusikiliza, kwa hiyo matunda yake, ardhi itatoa mazao yake, na
walipoita, sikusikiliza,’ asema BWANA Mwenye mbingu zitadondosha umande wake. Vitu hivi
Nguvu. 14‘Niliwatawanya kwa upepo wa kisulisuli vyote nitawapa mabaki ya watu kama urithi wao.
miongoni mwa mataifa yote, mahali ambapo 13Jinsi mlivyokuwa kitu cha laana katikati ya

5
ZEKARIA
mataifa, Ee Yuda na Israeli, ndivyo naye atateketezwa kwa moto.
nitakavyowaokoa, nanyi mtakuwa baraka. 5Ashkeloni ataona hili na kuogopa,
Msiogope, bali iacheni mikono yenu iwe na Gaza atagaagaa kwa maumivu makali,
nguvu.’’ pia Ekroni, kwa sababu matumaini yake
14Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye yatanyauka.
Nguvu: “Kama nilivyokuwa nimekusudia kuleta Gaza atampoteza mfalme wake na
maangamizi juu yenu, wakati baba zenu Ashkeloni
waliponikasirisha na sikuonyesha huruma,’’ ataachwa pweke.
asema BWANA Mwenye Nguvu, 15“Hivyo sasa 6Wageni watakalia mji wa Ashdodi,

nimeazimia kufanya mema tena kwa nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti.
Yerusalemu na Yuda. Msiogope. 16Haya ndiyo 7Nitaondoa damu vinywani mwao,

mtakayoyafanya: Semeni kweli kila mtu kwa chakula kile walichokatazwa kati ya meno
mwenzake, mtoe hukumu ya kweli na haki yao.
kwenye mahakama zenu, 17usipange mabaya Mabaki yao yatakuwa mali ya Mungu wetu,
dhidi ya jirani yako, msipende kuapa kwa uongo, nao watakuwa viongozi katika Yuda,
nayachukia yote haya,’’ asema BWANA. naye Ekroni atakuwa kama Wayebusi.
18Neno la BWANA Mwenye Nguvu likanijia 8Lakini nitailinda nyumba yangu dhidi ya majeshi

tena. 19Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye ya wanyang’anyi.


Nguvu: “Saumu za miezi ya nne, tano, saba na Kamwe mdhalimu hatashambulia watu
kumi itakuwa sikukuu za furaha na za shangwe wangu tena,
kwa Yuda. Kwa hiyo uipende kweli na amani.’’ kwa maana sasa ninawachunga.
20Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye

Nguvu: “Mataifa mengi na wakazi wa miji mingi Kuja Kwa Mfalme Wa Sayuni
watakuja, 21na wenyeji wa mji mmoja 9Shangilia sana, Ee Binti Sayuni!
watakwenda kwenye mji mwingine na kusema, Piga kelele, Binti Yerusalemu!
‘Twende mara moja na tukamsihi BWANA, na Tazama, mfalme wako anakuja kwako,
kumtafuta BWANA Mwenye Nguvu. Mimi ni mwenye haki naye ana wokovu,
mwenyewe ninakwenda.’ 22Pia watu wa kabila mpole naye amepanda punda,
nyingi na mataifa yenye nguvu yatakuja mwana punda, mtoto wa punda.
Yerusalemu kumtafuta BWANA Mwenye Nguvu 10Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu na

na kumsihi.’’ farasi wa vita kutoka Yerusalemu,


23Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye nao upinde wa vita utavunjwa.
Nguvu: “Katika siku hizo watu kumi kutoka lugha Atatangaza amani kwa mataifa.
zote na mataifa, watang’ang’ania upindo wa Utawala wake utaenea kutoka bahari
joho la Myahudi mmoja na kusema, ‘Twende hadi bahari na kutoka mto Eufrati hadi
pamoja nawe kwa sababu tumesikia kwamba mwisho wa dunia.
Mungu yu pamoja nawe.’ ’’
11Kwako wewe, kwa sababu ya damu ya agano
Hukumu Juu Ya Adui Za Israeli langu nawe,
(Neno) nitawaacha huru wafungwa wako watoke

9 Neno la BWANA liko kinyume na


nchi ya Hadraki
kwenye shimo lisilo na maji.
12Rudieni ngome yenu, Enyi wafungwa wa

na Dameski itakuwa mahali pa kupumzika, tumaini,


kwa kuwa macho ya watu na ya kabila zote hata sasa ninatangaza kwamba
za Israeli yako kwa BWANA, nitawarejesheeni mara dufu.
2pia juu ya Hamathi inayopakana nayo, 13Nitampinda Yuda kama nipindavyo upindi

juu ya Tiro na Sidoni, wangu,


ingawa wana ujuzi mwingi sana. nitamfanya Efraimu mshale wangu.
3Tiro amejijengea ngome imara, Nitawainua wana wako, Ee Sayuni,
amelundika fedha kama mavumbi dhidi ya wana wako,
na dhahabu kama taka za mitaani. Ee Uyunani na kukufanya kama upanga wa
4Lakini Bwana atamwondolea mali zake shujaa wa vita.
na kuuangamiza uwezo wake wa baharini,

6
ZEKARIA
BWANA Atatokea farasi.
14Kisha BWANA atawatokea,

mshale wake utamulika kama umeme wa 6“Nitaiimarisha nyumba ya Yuda


radi. na kuiokoa nyumba ya Yosefu.
BWANA Mwenyezi atapiga tarumbeta, Nitawarejesha kwa sababu nina huruma juu
naye atatembea katika tufani za kusini, yao.
15BWANA Mwenye Nguvu atawalinda, Watakuwa kama watu ambao sijawahi
wataangamiza na kushinda kwa mawe kuwakataa kwa sababu mimi ndimi
ya kutupa kwa kombeo. BWANA,
Watakunywa na kunguruma kama waliolewa Mungu wao, nami nitawajibu.
mvinyo, 7Waefraimu watakuwa kama mashujaa,

watajaa kama bakuli linalotumika mioyo yao itafurahi kama kwamba ni kwa
kunyunyizia divai.
kwenye pembe za madhabahu. Watoto wao wataona na kushangilia,
16BWANA Mungu wao atawaokoa siku mioyo yao itafurahi katika BWANA.
hiyo kama kundi la watu wake. 8Nitawapa ishara na kuwakusanya ndani.

Watang’ara katika nchi yake kama vito vya Hakika nitawakomboa,


thamani kwenye taji. nao watakuwa wengi kama walivyo
I7Jinsi gani watavutia na kuwa wazuri! kuwa mwanzoni.
Nafaka itawastawisha vijana wanaume, 9Ijapokuwa niliwatawanya miongoni mwa

nayo divai mpya vijana wanawake. mataifa,


hata hivyo wakiwa katika nchi za mbali
BWANA Ataitunza Yuda watanikumbuka mimi.

10
Mwombe BWANA mvua wakati Wao na watoto wao watasalimika
wa vuli, ni BWANA atengenezaye katika hatari nao watarudi.
mawingu ya tufani. 10Nitawarudisha kutoka Misri

Huwapa watu manyunyu ya mvua, na kuwakusanya toka Ashuru.


pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila Nitawaleta katika nchi ya Giliadi na
mtu. Lebanon,
2Sanamu huzungumza udanganyifu, napo hapatakuwa na nafasi ya kuwatosha.
waaguzi huona maono ya uongo, 11Watapita katika bahari ya mateso,

husimulia ndoto ambazo si za kweli, bahari iliyochafuka itatulizwa


wanatoa faraja batili. na vilindi vyote vya mto Nile vitakauka.
Kwa hiyo watu wanatangatanga kama Kiburi cha Ashuru kitashushwa na fimbo ya
kondoo walioonewa kwa kukosa utawala ya Misri itatoweka.
mchungaji. 12Nitawaimarisha katika BWANA

na katika jina lake watatembea,’’


3“Hasirayangu inawaka dhidi ya wachungaji, asema BWANA.
nami nitawaadhibu viongozi,
kwa kuwa BWANA Mwenye Nguvu
atalichunga kundi lake, 11 Fungua milango yako, Ee Lebanoni,
ili moto uteketeze mierezi yako!
nyumba ya Yuda, 2Piga yowe, Ee mti wa msonobari kwa kuwa

naye atawafanya kuwa kama farasi mwenye mwerezi umeanguka,


kiburi akiwa vitani. miti ya fahari imeharibiwa!
4Kutoka Yuda litatokea Jiwe la pembeni, Piga yowe, enyi mialoni ya Bashani,
kutoka kwake vigingi vya hema, msitu mnene umefyekwa!
kutoka kwake upinde wa vita, 3Sikiliza yowe ya wachungaji:

kutoka kwake kila mtawala. malisho yao manono yameharibiwa!


5Kwa pamoja watakuwa kama mashujaa Sikia ngurumo za simba,
wanaokanyaga kichaka kilichostawi sana cha Yordani
barabara za matope wakati wa vita. kimeharibiwa!
Kwa sababu BWANA yu pamoja nao,
watapigana na kuwashinda wapanda

7
ZEKARIA
Wachungaji Wawili Wa Kondoo jicho lake la kuume lipofuke kabisa!”
4Hili ndilo asemalo BWANA Mungu wangu:

“Lilishe kundi lililokusudiwa kuchinjwa. Maadui Wa Yerusalemu Kuangamizwa


5Wanunuzi wake huwachinja na kuondoka (Neno)
pasipo kuadhibiwa. Wale wanaowauza husema,
‘BWANA asifiwe, mimi ni tajiri!’ Wachungaji wao 12 Hili ni neno la BWANA kuhusu Israeli.
BWANA, Yeye azitandaye mbingu,
wenyewe hawawahurumii. 6Kwa kuwa awekaye misingi ya dunia na aiumbaye roho ya
sitawahurumia tena watu wa nchi,’’ asema mwanadamu ndani yake, asema: 2‘‘Nitakwenda
BWANA. “Nitawakabidhi kila mtu mkononi mwa kufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha
jirani yake na mfalme wake. Wataitenda jeuri kulewalewa kwa mataifa yote yanayoizunguka.
nchi, nami sitawaokoa kutoka mikononi mwao.’’ Yuda utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia.
7Kwa hiyo nikalilisha kundi lililotiwa alama 3Katika siku hiyo, wakati mataifa yote ya dunia

kwa kuchinjwa, hasa kundi lililoonewa sana. yatakapokusanyika dhidi yake, nitaufanya
Kisha nikachukua fimbo mbili moja nikaiita Yerusalemu kuwa jabali lisilosogezwa kwa
Fadhili na nyingine Umoja, nami nikalilisha mataifa yote. Wote watakaojaribu kulisogeza
kundi. 8Katika mwezi mmoja nikawaondoa watajiumiza wenyewe. 4Katika siku hiyo
wachungaji watatu. nitampiga kila farasi kwa hofu ya ghafula, naye
Kundi la kondoo likanichukia, nami ampandaye kwa uenda wazimu,’’ asema
nikachoshwa nao 9nikasema, “Sitakuwa BWANA. 5Kisha viongozi wa Yuda watasema
mchungaji wenu. Waache wanaokufa wafe na mioyoni mwao, ‘Watu wa Yerusalemu wana
wanaoangamia waangamie. Wale waliobakia nguvu kwa sababu BWANA Mwenye Nguvu ni
kila mmoja na ale nyama ya mwenzake.’’ Mungu wao.’
10Kisha nikachukua fimbo yangu inayoitwa 6“Katika siku hiyo nitawafanya viongozi wa

Fadhili nikaivunja, kutangua agano nililofanya na Yuda kuwa kama kigae cha moto ndani ya lundo
mataifa yote. 11Likatanguka siku hiyo, kwa hiyo la kuni, kama mwenge uwakao kati ya miganda.
waliodhurika katika kundi waliokuwa Watateketeza kulia na kushoto mataifa yote
wakiniangalia wakajua kuwa hilo lilikuwa neno la yanayowazunguka, lakini Yerusalemu utabaki
BWANA. salama mahali pake.
12Nikawaambia, “Mkiona kuwa ni vema, 7“BWANA atayaokoa makao ya Yuda

nipeni ujira wangu, la sivyo, basi msinipe.’’ Kwa kwanza, ili heshima ya nyumba ya Daudi na
hiyo wakanilipa vipande thelathini vya fedha. wakazi wa Yerusalemu isiwe kubwa zaidi kuliko
13Naye BWANA akaniambia, “Mtupie ile ya Yuda. 8Katika siku hiyo, BWANA
mfinyanzi,’’ hiyo bei nzuri waliyonithaminia! Kwa atawakinga wale waishio Yerusalemu, ili
hiyo nikachukua hivyo vipande thelathini vya kwamba aliye dhaifu kupita wote miongoni
fedha na kumtupia huyo mfinyanzi katika mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi
nyumba ya BWANA. itakuwa kama Mungu, kama Malaika wa
14Kisha nikaivunja fimbo yangu ya pili BWANA akiwatangulia. Katika siku hiyo nitatoka
iitwayo Umoja, kuvunja udugu kati ya Yuda na kuangamiza mataifa yote yatakayoushambulia
Israeli! Yerusalemu.
15Kisha BWANA akaniambia, “Vitwae tena

vifaa vya mchungaji mpumbavu. 16Kwa maana Kumwombolezea Yule Aliyechomwa Mkuki
ninakwenda kumwinua mchungaji juu ya nchi 10“Nami nitamiminia roho ya neema na

ambaye hatamjali aliyepotea, wala kuwatafuta maombi juu ya nyumba ya Daudi na wakazi wa
wale wachanga au kuwaponya waliojeruhiwa, Yerusalemu. Watanitazama mimi, yule
wala kuwalisha wenye afya, lakini atakula waliyemchoma, nao watamwombolezea kama
nyama ya kondoo wanono na kuzirarua kwato mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee
zao. na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia
mzaliwa wake wa kwanza wa kiume. 11Katika
17“Olewa mchungaji asiyefaa, siku hiyo kilio kitakuwa kikubwa Yerusalemu,
anayeliacha kundi! kama kilio cha Hadadrimoni katika tambarare ya
Upanga na uupige mkono wake na jicho Megido. 12Nchi itaomboleza, kila ukoo peke
lake la kuume! yake, nao wake zao peke yao. Ukoo wa nyumba
Mkono wake na unyauke kabisa, ya Daudi na wake zao, ukoo wa nyumba ya

8
ZEKARIA
Nathani na wake zao, 13ukoo wa nyumba ya machoni penu.
Lawi na wake zao, ukoo wa Shimei na wake 2Nitayakusanya mataifa yote huko
zao, 14na koo zote zilizobaki na wake zao. Yerusalemu kupigana dhidi yake, mji utatekwa,
nyumba zitapekuliwa na wanawake
Kutakaswa Dhambi watanajisiwa. Nusu ya mji watakwenda

13 Katika siku hiyo, chemchemi


itafunguliwa kwa nyumba ya Daudi na
uhamishoni, lakini watakaobaki hawataondolewa
kutoka mjini.
wakazi wa Yerusalemu, kuwatakasa dhambi na 3Kisha BWANA atatoka na kupigana dhidi

unajisi. ya watu wa yale mataifa, kama apiganavyo siku


2“Katika siku hiyo, nitayakatilia mbali majina ya vita. 4Siku hiyo miguu yake itasimama juu ya
ya sanamu kutoka nchi, nayo hayatakumbukwa Mlima wa Mzeituni, mashariki mwa Yerusalemu,
tena,” asema BWANA Mwenye Nguvu. nao Mlima wa Mizeituni utagawanyika mara
“Nitaondoa manabii wao pamoja na roho ya mbili kuanzia mashariki hadi magharibi, ukifanya
uchafu katika nchi. 3Ikiwa yupo ye yote bonde kubwa, nusu ya mlima ukisogea kuelekea
atakayeendelea kutabiri, baba yake na mama kaskazini na nusu kuelekea kusini. 5Nanyi
yake waliomzaa watamwambia, ‘ni lazima ufe, mtakimbia kupitia katika bonde hilo la mlima
kwa sababu umesema uongo kwa jina la wangu kwa kuwa litaenea hadi Aseli. Mtakimbia
BWANA.’ Atakapotabiri, wazazi wake kama mlivyokimbia tetemeko la ardhi katika siku
mwenyewe watampasua tumbo. za Uzia mfalme wa Yuda. Kisha BWANA Mungu
4“Katika siku hiyo, kila nabii ataaibika kwa wangu atakuja, nao watakatifu wote pamoja
maono ya unabii wake. Hatavaa vazi la kinabii la naye.
nywele ili apate kudanganya watu. 5Atasema, 6Siku hiyo hakutakuwepo nuru, baridi wala

‘Mimi sio nabii. Mimi ni mkulima, ardhi imekuwa theluji. 7Itakuwa siku ya kipekee, isiyo na
kazi yangu tangu ujana wangu.’ 6Ikiwa mtu mchana wala usiku, siku ijulikanayo na BWANA.
atamwuliza, ‘Majeraha haya yaliyo mwilini Jioni inapofika nuru itakuwepo.
mwako ni ya nini?’ Atajibu, ‘Ni majeraha 8Siku hiyo, maji yaliyo hai yatatiririka kutoka

niliyoyapata katika nyumba ya rafiki zangu. Yerusalemu, nusu kwenda kwenye bahari ya
mashariki na nusu kwenda kwenye bahari ya
Mchungaji Apigwa, Kondoo Watawanyika. magharibi, wakati wa kiangazi na wakati wa
7“Amka, Ee upanga, dhidi ya mchungaji masika.
wangu, 9BWANA atakuwa mfalme juu ya dunia yote.

dhidi ya mtu aliye karibu nami!” Katika siku hiyo atakuwepo BWANA mmoja na
asema BWANA Mwenye Nguvu. jina lake litakuwa jina pekee.
“Mpige mchungaji, 10Nchi yote kuanzia Geba, kaskazini mwa

nao kondoo watatawanyika, Yuda, hadi Rimoni, kusini mwa Yerusalemu,


nami nitageuza mkono wangu dhidi ya walio itakuwa kama Araba a . Lakini Yerusalemu
wadogo, utainuliwa juu na kubaki mahali pake, toka
8katika nchi yote,’’ asema BWANA, Lango la Benyamini hadi mahali pa Lango la
“Theluthi mbili watapigwa na Kwanza, mpaka kwenye Lango la Pembeni na
kuangamia, kutoka Mnara wa Hananeli hadi kwenye
hata hivyo theluthi moja watabakia mashinikizo ya divai ya mfalme. 11Utakaliwa na
ndani yake. watu, kamwe hautaharibiwa tena, Yerusalemu
9Hii theluthi moja nitaileta katika moto, utakaa salama.
nitawasafisha kama fedha isafishwavyo 12Hii ndiyo tauni ambayo BWANA atapiga

na kuwajaribu kama dhahabu. nayo mataifa yote ambayo yalipigana dhidi ya


Wataliitia jina langu nami nitawajibu, Yerusalemu: Nyama ya miili yao itaoza wangali
nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’ wamesimama kwa miguu yao, macho yao
nao watasema, ‘BWANA ni yataoza kwenye matundu yake na ndimi zao
Mungu wetu.’ ’’ zitaoza vinywani mwao. 13Katika siku hiyo
BWANA atawatia wanaume hofu kuu. Kila
BWANA Yuaja Kutawala mwanaume atakamata mkono wa mwenzake

14 Siku ya BWANA inakuja ambayo nyara


zilizotekwa kwenu zitagawanywa
a10 Araba maana yake nchi tambarare
9
ZEKARIA
nao watashambuliana. 14Yuda pia atapigana itawapiga mataifa yale ambayo hayatakwenda
katika Yerusalemu. Utajiri wa mataifa yote kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. 19Hii itakuwa
yanayoizunguka Yerusalemu utakusanywa, adhabu ya Misri na adhabu ya mataifa yote yale
wingi wa dhahabu, fedha na nguo. 15Tauni ya ambayo hayatakwenda Yerusalemu
aina iyo hiyo itapiga farasi na nyumbu, ngamia kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.
na punda nao wanyama wote walio kwenye 20Katika siku hiyo, kengele zilizofungwa

kambi za adui. kwenye farasi zitaandikwa maneno haya: SIKU


16Kisha walionusurika katika mataifa yote TAKATIFU KWA BWANA, navyo vyungu vya
ambayo yaliushambulia Yerusalemu watakuwa kupikia katika nyumba ya BWANA vitakuwa
wakipanda Yerusalemu kila mwaka kumwabudu kama bakuli takatifu mbele ya madhabahu.
Mfalme, BWANA Mwenye Nguvu na 21Kila chungu kilichoko Yerusalemu na Yuda

kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. 17Ikiwa taifa lo kitakuwa kitakatifu kwa BWANA Mwenye Nguvu
lote la dunia hawatakwenda Yerusalemu na wote wanaokuja kutoa dhabihu watachukua
kumwabudu Mfalme, BWANA Mwenye Nguvu, baadhi ya vyungu hivyo na kupikia. Katika siku
hawatapata mvua. 18Ikiwa watu wa Misri nao hiyo hatakuwepo tena mfanyibiashara katika
hawatakwenda kushiriki, hawatapata mvua. nyumba ya BWANA Mwenye Nguvu.
BWANA ataleta juu yao tauni ile ambayo

10

You might also like