Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 34

MKATE WA SEMBE

1. Unga wa ngano glass 1,


2. Unga wa sembe glass
3. Maziwa glass 1
4. Mayai 4
5. Sukari glass 1
6. Mafuta ½ glass
7. Baking powder vijiko viwili vya chakula

JINSI YA KUPIKA
1. Vunja mayai uchanganye na sukar, uchukue mchapo (whisk} upige huo mchanganyiko
bila kuachia mkono, mpaka uvimbe uje juu, kisha tia mafuta endelea kupiga na baadae
tia mafuta endelea kupiga na baadae tia maziwa, kisha endelea kupiga kama dk 3 kisha
tia unga wa sembe na wa ngano ambao umeuchanganya na ile Baking powder
uchanganye vizur kwa kutumia mwiko.

2. Weka mchanganyiko katika sufuria ambayo umeipaka mafuta kisha choma kwa oven au
mkaa hakikisha moto umeshakorea

3. Choma mpaka uwe na rangi ya gold, uchome na kijiti kirefu ktk mkate, kama kijiti
kitatoka kisafi hakina mnato hapo mkate wako tayari, utoe katika sufuria uache upoe
kisha ukate

PICCALILI SQUA
5lb chicken breast cubed Green

KEKI YA NDIZI : Nusu kg

MAHITAJI
1. Ndiz mbivu 2
2. Unga wa ngano 2
3. Baking powder, kijiko 1 kikubwa
4. Cocoa
5. Maziwa kikombe 1
6. Sukar kikombe 1
7. Compound chokulete
8. Mafuta nusu
9. Ark kijiko 1

MAANDALIZI
Weka ndizi ndani ya Blender weka sukar Pamoja na mafuta kisha saga
Mimina katika bakuli kisha chukua unga wa ngano changanya na kokoa au chokuleti ya ungu,
wengine wanaweka kahawa, weka na Baking Powder weka kwenye chujio. Halafu chukua
mchanganyiko wanye dizi changanya na unga kisha changanya kwa mwiko au kijiko kikubwa.
Hapo utakuwa mzito sana
Chukua maziwa yako, mimina, kisha changanya vizuri kwa mwiko weka na Arki yako
Mchanganyiko ½ weka chokolet kisha weka kwenye Oven

JINSI YA KUPIKA DAGAAA


 Kaanga dagaa
 Weka zichuuje mafuta
 Mafuta kiasi
 Kitunguu maji
 Nyanya chungu, zikaange kiasi
 Weka swaumu na tangawizi
 Nyanya,funika kwa dk3, kisha weka bamia
 Weka dagaa
 Weka karoti
 Weka hoho
 Weka fishi masala
 Weka Chumvi kiasi
 Weka maziwa mgando
 Weka tui la nazi
 Weka maji kiasi
 Kisha funika kwa dk5 kisha epua tali kwa kula

TEMBELE
 Loweka tembele
 Weka mafuta kiasi
 Weka vitunguu maji
 Nyanya 2
 Weka tembele
 Chumvi kidogo
 Mchuz mix /carpoda
 Karoti
 Hoho
 Tui
 Limao

SAMAKI WA KUOKA
 Limao
 Fish masala
 Pilipili nyeupe
 BBQ masala
 Chumvi
 Mafuta
 Tangawizi & swaumu
 Koroga, nap aka Samaki

VITUMBUA
Loweka mchele usiku kucha

ASUBUHI
 Utoe weka kwenye blender
 Weka sukar kiasi
 Weka hiliki
 Weka amira
 Weka vanira
 Weka tuli la nazi
 Saga mpaka ulainike, funika kwa mda wasaa moja, kisha changanya
 Tayari kwa kuchomwa

NDIZI ZILIZOIVA SANA


 Ndsizi 3 ziponde,
 Ongeza mayai mawili
 Iliki nusu
 Vanilla nusu
1
Changanya mchanganyiko weka Baking powder kijiko kimoja,kisha weka ngano 1 kg,
2
changanya kisha tumbukiza kijiko kwenye mafuta ili kisishike unga anza kuchoma
Halafu pitisha kwenye makapi ya nazi makavu.

MAIN ROST
 Mafuta
 Maini
 Chumvi
Acha yachemke mpaka yaive kisha weka
 Limao
 Saum
 Beef masala
 Viazi mviringo
Vitunguu maji changanya hoho, sweet chich, nyanya ya kusaga funika hoho, karoti,na
pilipili mbuzi, Tuli la nazi
1.MAPISHI YA VITAFUNWA MBALIMBAL
1. Mapishi ya chapati
2. Mapishi ya chapati za maji
3. Mapishi ya Maandazi ya kawaida
4. Mapishi ya Maandazi ya kuoka
5. Mapishi ya Half Keki
6. Mapishi ya Kachori
7.Mapishi ya skonsi
8. Mapishi ya vitumbua
9.Mapishi ya sambusa za nyama
10.Mapishi ya sambusa za viazi
11.Mapishi ya bagia dengu
12. Mapishi ya mikate ya mchele/mikate ya kumimina
13. Mapishi ya bagia za kunde
14. Mapishi ya mkate wa ndizi mbivu
15. Mapishi ya kababu
16. Mapishi ya Egg chop
17. Mapishi ya Donuts
18. Mapishi ya ubuyu wa Zanzibar
19. Mapishi ya chocolate
20. Mapishi ya katlesi za Samaki
21. Mapishi ya biskuti
22. Mapishi ya kashata za chocolate
23.Mapishi ya kalimati
24. Mapishi ya kashata nzima
25.Mapishi ya keki za vikombe
26.Mapishi ya keki za kuganda
27.Mapishi ya shawarma
28.Mapishi ya chauro
29.Mapishi ya jalebi
30.Mapishi ya pizza za Zanzibar – Mikate ya nyama
31. Mapishi ya vitumbua vya maembe
32. Mapishi ya biskut
1.MAPISHI YA CHAPATI (NJIA YA KWANZA)
MAHITAJI
1. Ngano kilo moja
2. Mafuta ya kupikia kwa ajili ya kukandia robo tatu ya kikombe kidogo (yaani
kikombe kijae na kuacha nafasi kidogo) au siagi (blueband au margarine) vijiko
vitatu vya chakula au samli nusu kikombe cha chai
3. Chumvi kijiko kimoja na nusu cha chai
4. Sukari kijiko kimoja cha chakula
5. Maji ya uvuguvugu
6. Mafuta ya kupaka chapati na ya kuchomea chapati.
I. Kikombe kinachozungumziwa hapa ni kikombe cha robo lita – 250 mls *Kama
unatumia siagi au samli pasha moto kwanza ili ziyeyuke.

MAPISHI KUKANDA CHAPATI NA KUKUNJA


1. Mimina ngano katika beseni,mimina humo chumvi na sukari kisha changanya
2. Mwagia mafuta ya kukandia pande zote za ngano kisha changanya vizuri
3. Anza kumwagia maji ya uvugu vugu huku ukichanganya unga na maji
taratibu,hakikisha huzidishi maji.
4. Ngano ikishalowa maji anza kukanda, kanda ngano kwa dakika chache kama 15
kisha iache na ifunike kwa muda wa dakika 15
5. Funua ngano kisha kanda tena kwa dakika 10, ifunike tena kwa muda wa dakika
10
6. Funua ngano kisha tengeneza madonge madonge ya kiasi cha chapati
unachohitaji – Kwngano kilo moja unaweza kutengeneza madonge 5 hadi 20
inategemea unahitaji chapati za kula nyumbani au biashara.
7. Andaa mafuta katika kibakuli na kijiko cha kuchotea mafuta, sukuma donge moja
kutengeneza chapati kisha kwa kutumia tumbo la kijiko pakaa mafuta kwa juu
hadi mafuta yaenee, kisha kunja chapati kama unavyokunja mkeka, kisha
zungusha hiyo chapati kama unavyozungusha kamba ili kutengeneza kama kiota
cha kutagia kuku au ndege,mwisho wa kuzungusha pachika ile ngano kwa chini
ili isijifungue, kisha weka katika sinia,
8. Endelea kuzungusha madonge yaliyobaki.
9. Anza kusukuma hayo madonge ulozungusha katika kibao cha chapati, kumbuka
kunyunyuzia unga na kupaka msukumio unga endapo chapati itanata katika
kibao.
Hakikisha unasukuma chapati kuanzia pembeni kuja kati ili kupata duara zuri, pia
usisukume sana kati ili chapati isiwe nyembamba katikati na kusababisha iwe
ngumu wakati wa kuchoma.
KUCHOMA CHAPATI
1. Moto wa kuchomea chapati unatakiwa usiwe mkali sana wala mdogo sana, yaani
iwe kati na kati kuelekea kwenye ukali.
2. Weka kikaango cha chapati jikoni kisha weka chapati uliyosukuma, iache ipate
moto hadi utakapoona inaanza kuinuka kwa kutoa vipulizo pulizo, hapo iegeuze
upande wa pili, paka mafuta pande zote kwa tumbo la kijiko upande uliogeuza
kisha pindua tena choma upande uliopaka mafuta, huku ukipaka mafuta upande
usio na mafuta, hakikisha unaizungusha zunguusha chapati kwa kijiko na
unaifunua funua kuona kama imeiva. Ukiona upande wa chini umebadirika rangi
na kuwa kahawia, geuza chapati upande huu ambao nao umeupaka mafuta,
kisha choma kwa kuzunguusha zunguusha na kwa kufunua funua hadi uone nao
umebadirika rangi na kuwa kahawia.
3. Toa chapati hifadhi katika sahani au hotpot na funika ili zilainike zaidi.
4. Endelea kuchoma chapati nyingine.

MAPISHI YA CHAPATI (NJIA YA PILI) – NJIA NYEPESI/NJIA


YA BIASHARA
Njia hii ni njia nyepesi na inafaa kwa wafanya biashara wa chakula wanaohitaji kupika
chapati nyingi kwa wakati mmoja, kwa maana hauhitaji kukunja chapati zako. Tofauti
hapa ni kwamba mafuta ya kukandia ni mengi, pia utaikanda ngano kidogo na
utaifunika kwa muda wa saa 1 ili ilainike, na utaikanda tena kidogo kama dakika 10 ili
kuiweka vizuri.

MAHITAJI
I. Ngano kilo moja
II. Mafuta ya kupikia kwa ajili ya kukandia kikombe kimoja na nusu au siagi
(blueband au margarine) vijiko vinne vya chakula au samli kikombe kimoja.
III. Chumvi kijiko kimoja na nusu cha chai
IV. Sukari kijiko kimoja cha chakula
V. Maji ya uvuguvugu
VI. Mafuta ya kupaka chapati na ya kuchomea chapati. *Kama unatumia siagi au
samli pasha moto kwanza ili ziyeyuke.

MAPISHI KUKANDA CHAPATI NA KUSUKUMA


1. Mimina ngano katika beseni,mimina humo chumvi na sukari kisha changanya
2. Mwagia mafuta ya kukandia pande zote za ngano kisha changanya vizuri
3. Anza kumwagia maji ya uvugu vugu huku ukichanganya unga na maji
taratibu,hakikisha huzidishi maji.
4. Ngano ikishalowa maji anza kukanda, kanda ngano kwa dakika chache kama
15 kisha iache na ifunike kwa muda wa saa nzima.
5. Funua ngano kisha kanda tena kwa dakika 10.
6. Funua ngano kisha tengeneza madonge madonge ya kiasi cha chapati
unachohitaji – Kwa ngano kilo moja unaweza kutengeneza madonge 5 hadi
20 inategemea unahitaji chapati za kula nyumbani au biashara.
7. Sukuma chapati moja kwa moja bila kukunja na anza kuchoma. Utaratibu wa
kuchoma ni ule ule. *Tumia kikaango kizito au non-stick pan ili kupata
matokeo mazuri ya chapati.

2.MAPISHI YA CHAPATI ZA MAJI MAHITAJI


MAHITAJI
a) Unga wa ngano nusu kilo
b) Mayai mawili
c) Maziwa robo kikombe cha chai
d) Hiriki ya unga nusu kijiko cha chai
e) Blueband au margarine kijiko kimoja cha chakula
f) Sukari kijiko kimoja cha chai
g) Chumvi kijiko kimoja na nusu cha chakula
h) Karoti saizi ya kati moja
i) Hoho saizi ya kati moja
j) Kitunguu maji kimoja
k) Maji
l) Mafuta ya kupikia

MAPISHI
1. Katakata kitunguu maji na hoho katika vipande vidogo dogo sana kisha saga karoti
2. Katika bakuli kubwa mimina unga wa ngano kisha mimina viungo vyote
3. Mimina maziwa
4. Mimina ute wa mayai
5. Mimina chumvi na sukari
6. Yeyusha blueband au margarine kwa kuipasha kisha mimina humo
7. Anza kumimina maji huku unachanganya na mixer ya mkono au ya umeme
8. Mchanganyiko wako unatakiwa uwe mzito kiasi na usiwe na mabuja buja ya unga
9. Weka kikaango cha chapati jikoni katika moto wa wastani kisha acha kikaango
kipate moto kiasi.
10. Mimina mafuta ya kupikia kiasi cha nusu kijiko cha chakula kisha yatandaze
11. Chota uji uji wa chapati kwa kikombe au upawa kisha tandaza katika kikaango
12. Acha chapati ikauke kisha igeuze upande wa pili,upande wa juu miminia mafuta
kidogo na tandaza na pembeni ya kikaango mimina mafuta kiasi, ikandamize
kandamize chapati yako huku unasambaza mafuta kwa tumbo la kijiko.
13. Pindua tena chapati acha kwa sekunde chache kisha itoe, hakikisha chapati
imekuwa na rangi ya brown (kahawia)
14. Endelea hivi kwa uji wa chapati uliobakia. *6* Kama hauna margarine au blueband
mimina mafuta kijiko kimoja cha chakula katika bakuli wakati wa kuchanganya *9*
Tumia non-stick frying pan kwa matokeo bora ya chapati zako *Unaweza usiweke
maziwa,karoti,hoho,na blueband kama hauna vitu hivyo *Unaweza ukatumia tui la
nazi kama hauna maziwa kutengeneza chapati zako kwa ladha bora zaidi

3.MAPISHI YA MAANDAZI – (MAANDAZI YA NAZI NA


KAWAIDA)
MAHITAJI
a) Unga wa ngano kilo mbili
b) Nazi kubwa moja
c) Hamira kijiko kimoja cha chakula
d) Sukari nusu
e) Hiriki kijiko kimoja cha chai
f) Baking powder kijiko kimoja cha chakula
g) Mafuta ya kupikia kikombe kimoja cha robo lita

MAPISHI
1. Weka unga wa ngano katika sufuria kubwa au beseni
2. Mimina sukari,hiriki,hamira na baking powder kisha changanya kwa pamoja na
unga wa ngano.
3. Chemsha mafuta ya kupikia katika sufuria ndogo hadi yawe ya moto.
4. Kwa uangalifu miminia mafuta ya moto katika unga wa ngano huku unachanganya
na unga wa ngano kwa mwiko.
5. Chukua tui la nazi miminia kwenye ngano ukiwa unakanda hiyo ngano, unamimina
kidogo kidogo hadi utakapoona ngano ni laini
6. Ukimaliza kukanda funika ngano yako na ungo au kitambaa kisha weka sehemu
yenye joto kidogo acha kwa muda wa kama saa mbili hivi hadi ngano yako iumuke.
7. Funua ngano yako kisha fanya kama unaikandamiza na ngumi ili upepo utoke kisha
ikusanye vizuri kama duara.Ikate kate kisha tengeneza maduara kadhaa (mfano
maduara 10) ili usipate shida wakati wa kukata vipande 8.
Sukuma hayo maduara kama chapati nene na katakata vipande vipande kisha
anza kuchoma maandazi yako kwa kuanzia vile vipande vya mwanzo kukatwa
8. Hakikisha moto si mkali sana ili maandazi yaive vizuri.
9. Hakikisha maandazi yanakuwa na rangi ya kahawia kwa nje (Choma upande moja
kwa dakika 3 hadi 4 kabla ya kumalizia kuchoma upande mwingine)
4.MAPISHI YA MAANDAZI YA KUOKA
Mahitaji na hatua za kukanda maandazi ya kuoka ni kama vile maandazi ya
kawaida, tofauti hapa ni kwamba maandazi hauyakaangi katika mafuta bali
unayaoka katika oven au jiko la mkaa

NAMNA YA KUOKA MAANDAZI


A.KWA KUTUMIA OVEN
1. Washa oven nusu saa kabla set joto la oven katika digrii 120 C au 248 F
2. Paka mafuta trei la kuokea vitu, kisha panga maandazi katika trei kisha weka trei
humo katika
oven na acha maandazi kwa muda wa nusu saa hakikisha yamebadirika
rangiFungua oven kisha toa trei na acha maandazi yapoe.

B.KWA KUTUMIA JIKO LA MKAA


1. Chukua sufuria kubwa, kisha tandika foil ndani yake, kisha paka mafuta foil kisha
panga maandazi humo
2. Washa jiko kisha punguza makaa ya moto yabaki kidogo sana, kisha weka
sufuria yenye maandazi ifunike na mfuniko wa bati kisha weka makaa ya moto
kwa juu kiasi kisha acha kwa muda wa nusu saa.
3. Funua sufuria, toa mandazi.

5.MAPISHI YA HALF KEKI MAHITAJI


1. Unga wa ngano kilo moja
2. Sukari kikombe kimoja 3
3. .Baking powder kijiko kimoja na nusu cha chai
4. Baking soda nusu kijiko cha chai
5. Hiriki ya unga robo kijiko cha chai
6. Maziwa fresh kikombe kimoja (ukihitaji)
7. Siagi vijiko 3 vya chakula au mafuta ya kupikia vijiko vitatu vya chakula
8. Vanilla kijiko kimoja cha chai (ukihitaji)
9. Mayai mawili (ukihitaji
10. Chumvi kijiko kimoja na nusu cha chai
11. Maji ya uvuguvugu
12. Mafuta ya kupikia *Vitu kama maziwa,mayai hivyo ni vya kuongezea, unaweza
usiweke kutokana na bajeti yako.

MAPISHI
1. Katika beseni au bakuli kubwa mimina unga wa ngano,sukari,chumvi,hiriki,baking
powder,baking soda, kisha changanya vizuri.
2. Tengeneza kama shimo katika unga wa ngano kisha mimina siagi,mimina maziwa
mimina vanilla na mimina ute wa yai kisha changanya vizuri na unga.
3. Anza kukanda unga wa ngano kwa maji ya uvuguvugu hadi uwe mgumu mgumu
lakini sio sana na usinate kwenye chombo wala kwenye mikono.Ngano ya half
keki haitakiwi kuwa laini kama ya mandazi
4. 4.Tengeneza duara kubwa kisha lipake mafuta na paka mafuta kwa pembeni
katika chombo cha kukandia.
5. Funika ngano kwa muda wa dakika 40 hadi saa 1 6.Funua ngano kisha ikate
katika madonge makubwa kiasi kama kabichi dogo
6. Sukuma madonge hayo kama chapati nene kiasi kisha anza kukata vipande vya
half cake.
7. Weka kikaango katika moto wa wastani kisha kaanga half keki zako hadi ziwe na
rangi ya kahawia kwa nje, na geuza upande wa pili.
8. Toa half keki katika kikaango kisha ziweke katika chujio au tissue ili zichuje
mafuta
9. Half keki zipo tayari

6.MAPISHI YA KACHORI ZA NGANO MAHITAJI


1. Viazi mbatata sado moja na nusu
2. .Vitunguu thomu punje tano kubwa
3. Kitunguu maji kikubwa kimoja
4. Pilipili moja kubwa
5. Limao kubwa moja na kipande
6. Ngano nusu kilo
7. Chumvi kiasi Ongeza vitu hivi katika viazi wakati unavichemsha ukihitaji
kutokana na bajeti yako:- -Manjano:- nusu kijiko cha chai -Tangawizi
iliyopondwa:- Kijiko kimoja cha chai -Pilipilimanga ya unga:- nusu kijiko cha chai
huwekwa viazi vikishaiva -Binzari nyembamba ya unga nusu kijiko cha chai -
Karoti ya kusaga huwekwa wakati wa kuponda viazi -Garam masala:- Kijiko
kimoja cha chai

MAPISHI
I. Menya viazi kisha kata vipande vipande vya nusu kwa nusu
II. Menya vitunguu saum na vitunguu maji kisha vikate katika vipande vidogo
vidogo kisha pasua pilipili na toa mbegu zake na katakata pilipili katika vipande
vipande Pilipili tunaiweka kwa ajili ya ladha tu na si kwa ajili ya kuwasha, ndio
maana tunaitoa mbegu zake.Hivyo usihofu kuwa kachori zitawasha.
III. Weka viazi katika sufuria mwagia chumvi ya kutosha kisha chemsha hadi
mvuke uanze kutokea
IV. Mwagia vipande vya kitunguu maji na vitunguu saum na pilipili humo kwenye
viazi kisha funika.
V. Viazi vikishaiva funua kisha mwaga viazi katika beseni pamoja na viungo vyote
ulivyoweka na anza kuponda ponda vizuri. Viazi visiive sana, yaani viive lakini
viwe vigumu kama vina kiini kwa mbali. Kama viazi vimeshaiva na bado sufuria
ina maji, hakikisha unabana sufuria kwa mfuniko kwa mikono miwili kisha
mwaga maji yaliyobaki, usitoe kiazi kimoja kimoja kwa sababu vitapondeka
pondeka.
VI. Tengeneza vidonge donge vya duara
VII. Chukua sufuria ya wastani weka maji kidogo mwagia rangi ya manjano katika
maji kisha mwagia ngano humo na chumvi kiasi na tengeneza rojo la ngano
zito, ongeza maji kiasi kama rojo la ngano ni zito sana, rojo la ngano linatakiwa
liwe zito ili wakati wa kukaanga kachori zisipasuke pasuke.Tumia blenda au
mixer kutengeneneza rojo la ngano, kama huna tumia mwiko au kijiko,ongeza
rangi kama utahitaji
VIII. Weka kikaango chenye mafuta jikoni kisha acha mafuta yapate moto sana
IX. Unatakiwa uwe na upawa wa kuchanganyia madonge katika rojo la ngano
ambao pia utatumia kutumbukiza madonge yako katika mafuta
yanayochemka,pia unatakiwa uwe na jaro kwa ajili ya kugeuzia kachori katika
mafuta, pia uwe na mwiko wa kusupport wakati unageuza kwa sababu kachori
huwa zinagandana.Kama kachori zimegandana usizitenganishe wakati
unazichoma zichome hivyo hivyo na uzigeuze kwa pamoja. (Chovya madonge
ya viazi katika ngano kisha yachome katika mafuta upande wa kwanza hadi
yakauke,pindua upande wa pili kisha choma upande huo hadi ukauke) Kachori
zikiiva zitoe katika mafuta na ziweke katika chujio ili zichuje mafuta.

[
7.MAPISHI YA SKONZI
1. Unga wa ngano nusu kilo
2. Sukari kijiko kimoja cha chakula
3. Chumvi kijiko kimoja cha chai
4. Maziwa fresh kikombe kimoja cha chai
5. Hamira kijiko kimoja cha chai
6. Siagi vijiko vitatu vya chakula
7. Maji ya uvuguvugu

MAPISHI
1. Chukua bakuli kubwa changanya sukari,chumvi,hamira, na maji kiasi ya
uvuguvugu kisha funika acha kwa dakika 5
2. Pasha siagi kidogo ilainike
3. Katika bakuli lenye mchanganyiko wa namba 1, mimina ngano,siagi,na maziwa
kisha changanya vizuri
4. Endelea kukanda ngano huku unamimina maji ya uvuguvugu na kuongezea
ngano kidogo taratibu taratibu hadi ngano iwe laini na hainati mikononi.
5. Funika kwa kitambaa ngano yako acha iumuke kwa dakika 30
6. Funua ngano yako kisha ibinye kwa ngumi ili itoe upepo, kata madonge ya saizi
unayotaka
7. Chukua sufuria nyepesi pana ya kuokea kisha ipake siagi au mafuta sehemu zote
na panga madonge yako uyaachie nafasi kidogo
8. Funika madonge yako kisha acha yaumuke tena kwa dakika 15.
9. Funua madonge yaki kisha yapake siagi au mafuta kwa juu kwa kutumia brush
maalum ya kupakia au kwa kiganja chako kwa taratibu bila kuzibinya.
10. Washa oven kisha ingiza sufuria yako au chombo cha kuokea weka moto wa
digrii 200, kisha oka skonsi zako kwa dakika 25 AU:- Kwa jiko la mkaa chukua
sufuria kubwa ijaze michanga kiasi kisha weka sufuria yako yenye madonge ya
skonsi humo kisha funika hiyo sufuria kubwa kwa sinia gumu, kwa juu weka
makaa ya moto ya kutosha na kwa chini weka makaa ya moto kiasi, acha kwa
nusu saa. AU Chukua sufuria kubwa iweke foil ndani yake, paka mafuta na panga
skonsi kwa ndani kisha weka sufuria jikoni makaa yawe machache kisha funika
na weka makaa kwa juu ya kutosha.
11. Skonsi zipo tayari kwa kula

9.MAPISHI YA VITUMBUA
MAHITAJI
1. Mchele vikombe vitano vya robo lita
2. Unga wa ngano kikombe kimoja cha robo lita
3. Tui la nazi vikombe viwili vya robo lita
4. Mayai matano
5. Hamira kijiko kimoja cha chakula
6. Sukari vikombe Viwili vya robo lita
7. Hiriki vijiko viwili vya chai
8. Mafuta ya kupikia.

MAPISHI
1. Loweka mchele usiku kucha au saa 8
2. Changanya hamira na tui la nazi.
3. Mimina mchele,ngano,ute wa mayai,hiriki, tui la nazi katika blenda kisha saga
hadi vitu vyote vichanganyike vizuri AU:- Mchele ulioloweka anika juani kisha
saga unga wa kutosha kwa ajili ya vitumbua, hivyo badala ya kusaga mchele
katika blenda utakuwa unatumia huo unga unachanganya na vitu vingine
4. Chukua maji ya uvuguvugu au ya baridi kiasi kidogo kisha changanya na sukari
hadi iyeyuke kidogo.
5. Mimina ute wa sukari ndani ya mchanganyiko kisha saga tena ili sukari
ichanganyike.
6. Mimina mchanganyiko katika chombo kikubwa funika na weka mahali penye
joto kisha acha mchanganyiko uumuke.
7. Baada ya mchanganyiko kuumuka weka kikaango cha vitumbua kwenye moto
8. Mimina mafuta kiasi kwenye kikaango cha vitumbua kisha mimina rojo la
vitumbua.
9. Vitumbua vikiiva upande mmoja geuza upande wa pili pia mwagia mafuta hadi
kiive.
10. Vitumbua tayari kwa kula.

10.MAPISHI YA SAMBUSA ZA NYAMA NA VIAZI


Utengenezaji wa sambusa unahitaji ujuzi tu wa kutengeneza manda Hivyo
angalia namna ya kutengeneza manda

NAMNA YA KUTENGENEZA MANDA ZA SAMBUSA


MAHITAJI
1. Ngano nusu kilo:- ½ Kg. Wheat flour
2. Maji ya uvugu vugu:- Warm water
3. Mafuta ya kupikia kijiko kimoja cha chakula:- 1 tbsp cooking oil
4. Hiriki ya unga theluthi ya kijiko cha chai:- ⅓ tsp cardamom powder
5. Chumvi kiasi:- A pinch of salt

MAANDALIZI
 Kwenye chombo kikubwa mimina unga wa ngano kisha mimina maji
kiasi,hiriki,mafuta kiasi na chumvi kiasi kisha kanda hadi ngano iwe laini kisha
ifunike endelea na hatua zinazofuata.
 Chukua ngano yako uliyokanda kisha igawanye katika madonge kumi kisha
sukuma kutengeneza chapati ndogo ndogo, chukua chapati moja ipake
mafuta juu kisha nyunyuzia ngano kidogo na sambaza kisha weka chapati
nyingine juu yake nayo ipake mafuta na nyunyuzia ngano kidogo na sambaza
kisha weka chapati nyingine juu,endelea hadi zifike chapati tano zisukume
kwa pamoja kutengeneza chapati moja kubwa, kandamiza kidogo kwa
kiganja kwa juu kisha
 Weka chuma cha kukaangia chapati jikoni bila kuweka mafuta kisha weka
chapati hizo na zibabue pande zote mbili hadi ziive bila kubadirika rangi wala
kukauka. Endelea hivi kwa madonge matano mengine.
 Bandua hizo chapati kisha chukua chapati moja moja weka kwenye kibao cha
chapati kisha kata sehemu nne sawa
 Tengeneza uji wa kugandishia kwa kuchanganya vijiko vitatu vya chakula na
maji kiasi
 Katika kila kipande tengeneza umbo la koni kwa kufunga upande mmoja kwa
ute wa ngano.

MAHITAJI YA UTENGENEZAJI WA SAMBUSA ZA NYAMA


1. Nyama ya kusaga nusu kilo
2. Kitunguu maji kilichokatwa katika vipande vidogo vidogo mfano wa voboxi
3. Karoti iliyosagwa
4. Majani ya giligilani yaliyosagwa kiasi
5 .Kitunguu saum nusu kijiko cha chai
6.Pilipili mbichi iliyopondwa kiasi – itoe mbegu na kata kipande tu ndio usage
kutokana na wingi wa nyama.
7. Garam masala au beef masala nusu kijiko cha chai
8. Manda za sambusa
9. Mafuta ya kuchomea sambusa

MAPISHI
1. Chukua nyama mbichi ya kusaga kisha weka katika sufuria, kamulia limao
weka na tangawizi iliyosagwa na pilipilimanga ya unga kidogo na chumvi na
maji kiasi kisha chemsha hadi iive.
2. Weka sufuria au kikaango jikoni kisha mimina mafuta ya kupikia kiasi acha
yapate moto na mimina vipande vya kitunguu maji,kaanga hadi vianze
kulainika kisha mimina thomu iliyosagwa endelea kukoroga kisha mimina
majani ya giligilani yaliyopondwa kiasi kidogo sana kisha mimina nyama na
changanya vyema kisha mimina pilipili iliyosagwa changanya, nyunyuzia
garam masala kisha changanya vyema, hakikisha moto ni wa wastani,
kamulia tena limao kiasi kidogo weka chumvi kiasi changanya na funika.
3. Funua epua acha ipoe.
4. Chukua manda za sambusa jaza nyama uliyopika humo na anza kuchoma
sambusa.
5. Katika kuchoma hakikiasha sambusa zimekuwa brown zitoe na zichuje
mafuta.
6. Sambusa zipo tayari. Ukihitaji kutengeneza sambusa za viazi, unachofanya
ni kukata kata viazi katika vipande vidogo vidogo kisha utavichemsha ndani
yake utaweka viungo mbalimbali kama vile vitunguu maji kidogo,thomu,pilipili
na vinginevyo. Vikiiva utajaza viazi hivyo katika manda za sambusa na
utachoma.
11.MAPISHI YA BAGIA DENGU MAHITAJI
1. Unga wa dengu kikombe kimoja au robo kilo
2. Manjano robo kijiko cha chai
3. Binzari nyembamba ya unga nusu kijiko cha chai
4. Kitunguu saum kilichosagwa robo kijiko cha chai
5. Baking powder nusu kijiko cha chai
6. Kitunguu maji kimoja
7. Hoho moja dogo
8. Pilipili mbichi kiasi
9. Pilipilimanga robo kijiko cha chai
10. Chumvi kiasi
11. Mafuta ya kupikia

MAPISHI
1. Katakata pilipili mbichi na kitunguu maji na hoho katika vipande vidogo vidogo
sana.
2. Katika bakuli kubwa mimina unga wa dengu,manjano,pilipilimanga,chumvi na
baking powder na maji kiasi kisha changanya
3. Mimina viungo vyote vilivyobaki katika bakuli kisha changanya vizuri
4. Mimina maji kidogo kidogo huku unachanganya mchanganyiko (Tumia mwiko
au kipekecho cha mkono au kipekecho cha umeme (mixer) au blenda)
5. Hakikisha mchanganyiko unakuwa uji uji mzito na si mwepesi sana ambao
hauna madonge.
6. Funika uji uji na acha kwa dakika 20
7. Weka kikaango jikoni kisha mimina mafuta ya kupikia na acha yapate moto
wa wastani
8. Chukua kijiko cha chakula kisha chota uji uji wa bagia dengu na mimina
katika kikaango, chota michoto kadhaa kutokana na ukubwa wa kikaango
chako.
9. Choma bagia zako na hadi ziwe kahawia upande mmoja na uzigeuze upande
wa pili 10.Ziweke bagia zako katika chujio lililo juu ya sufuria au juu ya tissue
ili zichuje mafuta 11.Bajia za dengu zipo tayari

12.MAPISHI YA MKATE WA MCHELE/MKATE WA KUMIMINA


MAHITAJI
I. Unga wa mchele vikombe vitatu vya chai (Kikombe cha robo lita - 250 mls)
II. Sukari kikombe kimoja na nusu
III. Hamira kijiko kimoja cha chai
IV. Yai moja
V. Tui la nazi vikombe viwili vya chai (Tui zito na jepesi)
VI. Hiriki kijiko kimoja cha chai

MAPISHI
a) Kama hauna unga wa mchele, chukua mchele vikombe vitatu vya chai kisha
loweka katika maji usiku kucha.
b) Weka hamira katika tui zito kisha koroga hadi hamira upate mchanganyiko
mzito
c) Chukua blenda kisha weka mchele (unga wa mchele),hiriki,hamira na tui la
nazi kisha saga hadi vichanganyike vizuri, lakini zibakie chenga chenga kidogo
za mchele. Kama hauna blenda weka unga katika chombo kikubwa kisha
changanya na vitu vingine humo na koroga na mwiko.
d) Mimina mchanganyiko katika chombo kikubwa kisha funika na acha uumuke
kwa dakika 40.
e) Funua chombo chako kisha mimina sukari na ute wa yai kisha koroga vizuri.
f) Chukua sufuria au chombo cha kuokea kisha pake mafuta pande zote.
g) Mimina mchanganyiko katika chombo cha kuokea.
h) Washa oven kisha set moto wa oven katika digrii 350 C au 572 F
i) Acha mkate kwa dakika 40 hadi uwe na rangi ya kahawia kwa juu.
j) Toa chombo cha kuokea katika oven kisha acha mkate upoe halafu ukatekate
vipande. Kama unaoka kwa jiko la gesi au mkaa, unahitajika uwe na sufuria
kubwa ambayo ndani yake utaweka chombo chako cha kuokea, kisha washa
moto uwe mkali na funika kwa juu weka makaa ya moto kidogo kwa muda wa
dakika 40. Mkate wa kumimina tayari kwa kula.

13.MAPISHI YA BAGIA ZA KUNDE


MAHITAJI
I. Kunde vikombe viwili vyrobo lita
II. Kitunguu maji kimoja
III. Pilipili mbichi kiasi
IV. Juisi ya limao vijiko viwili vya chakula
V. Baking powder kijiko kimoja cha chai
VI. Kitunguu saum kilichosagwa kijiko kimoja cha chai
VII. Tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja cha chai
VIII. Curry powder kijiko kimoja cha chai
IX. Chumvi kiasi
X. Mafuta ya kupikia

MAPISHI
a) Osha na loweka kunde kwenye maji ya moto kwa masaa 8 au usiku mzima
b) Katakata kitunguu maji na pilipili mbichi katika vipande vidogo vidogo
c) Chuja maji katika kunde
d) Mimina kunde tangawizi,kitunguu saum,curry powder,pilipili, na maji ya limao
kwenye mashine ya kusagia chakula au blender kisha saga na zisilainike sana
au twanga vitu vyote kwenye kinu.
e) Kunde zikilainika ongeza vipande vya kitunguu maji kisha saga kiasi na
vitunguu visisagike sana.
f) Weka mchanganyiko kwenye bakuli kubwa.
g) Ongeza chumvi na baking powder, changanya vizuri
h) Tengeneza bagia katika maumbo ya duara
i) Weka kikaango jikoni kisha mimina mafuta na acha yapate moto kiasi
j) Anza kukaanga bagia zako hadi zibadirike rangi na kuwa kahawia.
k) Weka bagia zilizoiva katika chombo chenye tishu au chujio ili kuchuja mafuta.
12.Bagia za kunde zipo tayari kwa kula

14.MAPISHI YA MKATE WA NDIZI


MAHITAJI
1. Unga wa ngano nusu kilo:- ½ Kg Wheat flour
2. Sukari robo kilo:- ¼ Kg. sugar
3. Mayai mawili:- Two eggs
4. Siagi vijiko viwili vya chakula:- 2 tbsp butter
5. Ndizi mbivu tatu:- 3 banana
6. Karanga au korosho za kukaanga
7. Chumvi nusu kijiko cha chai:- 1 tsp salt
8. Baking soda kijiko kimoja cha chai:- 1 tsp baking soda 9.Baking powder robo
kijiko cha chai:- ¼ baking powder

MAPISHI
a) Pasha siagi moto hadi iyeyuke
b) Katika chombo kikubwa mimina sukari,mimina siagi kisha changanya vizuri
hadi sukari iwe rojo rojo
c) Pasulia mayai humo kisha koroga vizuri
d) Kwenye chombo hicho hicho mimina unga wa ngano,baking powder na
baking soda kisha changanya vizuri.
e) Saga ndizi kwa maji kiasi katika blenda
f) Mimina rojo la ndizi mbivu kwenye bakuli yenye mchanganyiko wa vitu vyote
kisha koroga vizuri
g) Funika mchanganyiko wako na acha uumuke kwa muda wa dakika 30
h) Paka mafuta au siagi chombo cha kuokea mkate
i) Mimina mchanganyiko wako katika chombo cha kuokea mkate tupia karanga
au korosho za kukaanga kwa juu kisha ingiza katika oven
j) Joto la oven linatakiwa liwe 180 C au 350 F, kama unatumia mkaa weka
chombo cha kuokea katika sufuria kubwa funika kisha weka jikoni katika moto
wa wastani.
k) Oka mkate wako kwa muda wa dakika 30 hadi saa 1, choma kijiti katika
mkate na kikitoka kikiwa kikavu mkate unakuwa umeiva.
l) Mkate wa ndizi mbivu upo tayari

15.MAPISHI YA KABABU
MAHITAJI
1. Nyama ya kusaga kilo moja
2. Vipande vya mkate vitatu
3. Mayai matatu
4. Unga wa binzari nyembamba kijiko kimoja cha chai au binzari ya kababu
nusu paketi
5. Binzari ya manjano kijiko kimoja cha chai
6. Kitunguu saum kilichosagwa kijiko kimoja cha chai
7. Tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja cha chai
8. Pilipili mbichi iliyosagwa kijiko kimoja cha chai
9. Pilipili manga nusu kijiko cha chai
10. Ndimu kipande kimoja au juisi ya limao kidogo
11. Chumvi kiasi
12.Mafuta ya kupikia

MAPISHI
1. Chukua bakuli kubwa weka nyama ya kusaga iliyochemshwa.
2. Loweka vipande vya mkate katika maji kisha fanya kama una vikamua kisha
vikatekate vipande vipande na changanya na nyama ya kusaga.
3. Mimina viungo vyote na mayai mabichi katika bakuli,kamulia ndimu na
changanya vizuri.
4. Loweka chumvi kwenye maji kidogo kisha mimina kwenye mchanganyiko na
changanya vizuri.
5. Tengeneza kababu zako katika maumbo ya viduara au maumbo ya karoti.
6. Weka kababu zako katika sinia kisha ziache kwa muda kama saa moja
iliviungo vikolee vizuri.
7. Mimina mafuta ya kupikia katika kikaango acha yapate moto vizuri.
8. Anza kukaanga kababu zako hadi ziive upande mmoja kisha zipindue upande
wa pili.
9. Toa kababu zako na ziweke kwenye chujio ili zichuje mafuta.
10. Kababu zako zipo tayari kwa kula.
16.MAPISHI YA EGG CHOP
Ili kutengeneza egg chop, utafuata hatua zile zile za utengenezaji wa kababu, cha
kuongeza ni mayai ya kuchemshwa ambayo utayapasua na utayafunika na nyama ya
kusaga ambayo umeichanganya kwa viungo na utatengeneza duara kisha utachoma
katika mafuta.

17.MAPISHI YA DONUTS MAHITAJI


1. Unga wa ngano kilo moja
2. Mayai matatu
3. Mayai mawili ya kutengenezea kastadi
4. Maziwa fresh lita moja
5. Siagi (blueband) vijiko vinne vya chakula
6. Sukari robo kilo
7. Sukari robo kilo ya kutengenezea kastadi
8. Hamira vijiko viwili vya chai
9. Hiriki ya unga kijiko kimoja cha chai
10. Baking powder kijiko kimoja cha chai
11. Vanilla vijiko viwili vya chai
12. Chumvi kijiko kimoja cha chai
13. Maziwa ya unga robo
14. Mafuta ya kupikia

MAPISH
1. Chemsha maziwa fresh nusu lita kisha yahifadhi kwenye chombo yapate
uvugu vugu
2. Mimina hamira katika maziwa ya uvuguvugu kisha changanya vizuri acha
mchanganyiko kwa dakika 5 hadi yatokee mapovu.
3. Yeyusha siagi yako hadi iwe kimiminika
4. Chukua blenda kisha mimina maziwa yenye hamira,mimina siagi
iliyoyeyushwa,mimina sukari,chumvi,mayai,hamira,vanilla na baking powder
kisha saga hadi vichanganyike kama una mixer utaweka ngano yako kisha
utamimina hivi vitu vyote humo na utakanda ngano yako kwa mixer.
5. Weka ngano katika bakuli kubwa kisha minina huo mchanganyiko wa
kwenye blenda katika ngano kisha anza kukanda hadi ilainike na isinate
mikononi utakuwa unaongezea unga wa ngano kidogo ili ngano yako iweze
kubalance kati ya ugumu kidogo na ulaini kidogo na isinate mikononi.
6. Ipake mafuta ngano yako kwa juu na chini pia paka mafuta chombo cha
kuumulia kisha funika ngano yako na iache kwa saa 1 hadi iumuke
7. Funua ngano yako kisha ikandamize kwa ngumi ili itoe upepo kisha anza
kukata madonge madogo kama 6
8. Sukuma hayo madonge kupata chapati nene kiasi kisha kwa kutumia
chombo chenye shepu ya donati kandamiza kwenye chapati ili kutoa donati
zako.
9. Ziache ziumuke tena kwa muda wa dakika 45
10. Weka mafuta kwenye kikaango hakikisha moto ni wa wastani acha mafuta
yapate joto kisha anza kukaanga donati zako hadi ziwe kahawia.
11. Andaa kastadi kwa kuchemsha maziwa fresh kisha mimina sukari robo
lita,kisha mimina viini vya mayai mawili kisha utachemsha huku unakoroga
hadi mchanganyiko uwe mzito kiasi kama uji.
12. Acha kastadi ipoe kisha chukua donati zako tumbukiza katika kastadi kisha
tumbukiza katika maziwa ya unga kwa pande zote ili kupata donati zenye
utando mweupe kwa nje.
13. Donati zako zipo tayari

18.MAPISHI YA UBUYU WA ZANZIBAR MAHITAJI


1.Ubuyu wa mbegu vikombe vine
2.Sukari vikombe 2
3.Maji vikombe 2
4. Unga wa ubuyu nusu kikombe
5. Pilipili ya unga robo kijiko cha chai
6. Pilipilimanga ya unga nusu kijiko cha chai
7. Chumvi robo kijiko cha chai
8. Hiriki robo kijiko cha chai
9. Rangi nyekundu ya chakula au rangi yoyote ya chakula - kiasi (Anza na nusu
kijiko cha chai)
10. Ladha ya vanilla au vimto kijiko cha chai kisijae

1.MATAYARISHO
1. Katika sufuria,weka maji,sukari,hiriki, chumvi,pilipilimanga,pili pili ya unga na
rangi. Moto uwe juu kiasi na changanya vyote hivyo vichanganye vizuri hadi
sukari iyeyuke.
2. Acha mchanganyiko uchemke hadi mapovu yaanze kutokea kwa juu.
3. Anza kukoroga na endelea kukoroga hadi mchanganyiko (shira) uwe mzito na
mapovu kupungua
4. Gusa mabaki ya shira katika mwiko kuona kama yananata, ikiwa shira inanata
inakuwa tayari imeshaiva.
5. Epua shira kutoka jikoni acha ipoe kiasi
6. Weka ubuyu wa mbegu katika beseni au sufuria kubwa kisha mimina shira kwa
kunyunyuzia sehemu zote na changanya kwa mikono (Unaweza kuvaa gloves ili
kujikinga na joto la shira)
7. Chukua unga wa ubuyu anza kunyunyuzia juu ya mbegu za ubuyu ambazo
umezimwagia shira - Hakikisha unga wa ubuyu unaenea sehemu zote na kuwa
makini unga wa ubuyu usimeze shira katika mbegu za ubuyu - Hakikisha rangi
inaonekana.
8. Anika ubuyu juani ili uwe mkavu
9. Hifadhi ubuyu katika chombo chenye mfuniko au weka ubuyu katika vifungasha
vilivyozibwa tayari kwa kuuza au kwa kula
*Kikombe kinachotumika ni cha kipimo cha robo lita (250 mls)

19.MAPISHI YA CHOCOLATE (Vipande 20)


MAHITAJI
1. Cocoa powder:- vijiko 10 vya chakula
2. Sukari:- vikombe 3
3. Maziwa fresh:- kikombe kimoja na nusu
4. Siagi (Butter):- vijiko vinne vya chakula
5. Vanilla:- kijiko kimoja cha chai
6. Silicon tray ya kuwekea chocolate – Inapatikana supermarket
[[

MAPISHI
1. Andaa bakuli la bati la umbo la mstatiri (ikiwa ni bakuli la bati ni vizuri zaidi) kisha
lipake mafuta - Au chukua bakuli la plastiki kisha weka foil humo iweze kukaa
katika umbo la mstatiri (box) au tumia silicon tray special kwa ajili ya
kutengenezea chocolate.
2. Mimina unga wa cocoa katika sufuria, kisha mimina sukari,kisha mimina maziwa
kisha anza kuchemsha katika moto wa wastani huku unakoroga hadi malighafi
(ingridients) zichanganyike vizuri.
3. Baada ya vitu vyote kuchanganyika acha kukoroga na acha mchanganyiko
uchemke na uwe kama uji mzito
4. Epua sufuria kutoka jikoni kisha weka siagi na vanilla katika mchanganyiko bila
kuchanganya.
5. Acha mchanganyiko upoe kiasi na uwe vuguvugu
6. Chukua kifaa cha kuchanganyia (mixer) kisha changanya mchanganyiko hadi
uwe mzito.
7. Mimina mchanganyiko katika chombo ulichokipaka mafuta kisha acha
mchanganyiko ugande kabisa au hifadhi katika fridge au freezer kwa saa 1 au 2.
8. Katakata vipande vidogo vidogo vya mraba vya chocolate.
9. Chocolate ipo tayari.
10. Hifadhi chocolate katika fridge Chocolate inaweza kukaa hadi miezi mitatu bila
kuharibika

20.MAPISHI YA KATLESI ZA SAMAKI


MAHITAJI
1.Viazi mbatata robo kilo
2.Samaki vibua au samaki yoyote mwenye minofu nusu kilo:- Samaki mbichi
3.Ngano nusu kikombe
4.Mayai matatu
5.Ndimu moja
6.Kitunguu saum kilichopondwa nusu kijiko cha chai
7.Kitunguu maji kidogo
8.Pilipili mbichi moja
9.Karoti moja ndogo
10.Chumvi
11.Mafuta ya kupikia
12.Pilipilimanga ya unga kijiko kimoja cha chai kisijae sana

MAPISHI
1. Chukua pilipili mbichi ikate nusu na ondoa mbegu zake zote, chukua nusu yake
ikate kate vipande vidogo dogo sana
2. Menya viazi mbatat kisha vikate vipande vipande
3. Safisha samaki vyema, kisha kamulia ndimu,weka kitunguu thomu na tangawizi na
chumvi kiasi anza kuchemsha hadi maji yakauke, waive lakini wasilainike sana.
4. Weka viazi katika sufuria kisha mimina vipande vya kitunguu maji na vipande vya
pilipili mbichi kisha chemsha kwa maji kiasi hadi viazi viive lakini visiive sana.
5. Epua viazi na viponde ponde ndani ya beseni kwa kutumia chupa au mchi hadi
vipondeke vyote.
6. Chambua miba na mifupa katika samaki kupata minofu (hakikisha miba na mifupa
yote imeisha) kisha chambua nyama ya samaki tena kupata vipande vipande
vidogo vidogo
7. Mimina vipande vya samaki katika bakuli lenye viazi vilivyopondwa,mimina karoti
zilizosagwa na nyunyuzia pilipilimanga kisha changanya vizuri kwa mwiko.
8. Mimina ngano katika bakuli,mimina maji koroga kupata rojo zito
9. Pasua mayai kisha koroga yachanganyike
10. Changanya rojo la mayai na ngano kwa pamoja kisha koroga vizuri weka chumvi
kiasi.
11. Weka kikaango jikoni,mimina mafuta ya kupikia na acha yapate moto vizuri
12. Chukua mchanganyiko wa samaki na viazi kisha tengeneza viduara kama vya
kachori kisha toweza katika rojo la mayai na ngano na anza kuchoma katika
mafuta, hakikisha upande wa chini umekauka kabla ya kugeuza upande mwingine.
13. Hakikisha katlesi zimekuwa na rangi ya hudhurungi au kahawia au brown

21.MAPISHI YA BISKUTI [ Idadi:- Biskuti 12]


MAHITAJI
1. Unga wa ngano aina ya (Plain flour) gramu 150 au kikombe kimoja
2. Bicarbonate of soda au baking powder nusu kijiko cha chai
3. Corn flour vijiko 3 na robo vya chakula
4. Sukari kikombe kimoja (ukipata sukari ya unga ni vizuri zaidi)
5. Siagi Vijiko 10 na nusu vya chakula - (Yeyusha siagi na ipoe)
6. Vanilla nusu kijiko cha chai
7. Yai moja lililopasuliwa na kuchanganywa
8. Chumvi kiasi *Siagi unaweza kutumia blueband au margarine *Kikombe cha
vipimo ni kikombe kidogo cha robo lita ( 250 mls)

MAPISHI
1. Washa oven katika joto la digrii 180 (C) au 350 (F)
2. Paka mafuta vifaa vya kuokea kisha weka karatasi ya kuokea
3. Pasua yai katika bakuli na lichanganye kiasi
4. Weka ngano katika bakuli kubwa kisha changanya na bicarbonate of soda
5. Mimina sukari,mimina siagi au margarine iliyoyeyushwa,ute wa yai na vanilla
kisha changanya vyema.
6. Kanda ngano hadi iwe laini kiasi na isinate mikononi, ifunike katika bakuli katika
muda wa saa
7. Baada ya saa 1 ikande ngano tena kidogo kisha kwa kutumia msukumio wa
ngano (roller) sukuma ngano iwe kama chapati, mwagia unga kidogo juu ya
ngano na weka unga kidogo kwenye sehemu ya kusukumia ili ngano isinate.
8. Chukua kisu kisha kata ngano vipande vipande kisha weka katika chombo cha
kuokea
9. Weka chombo cha kuokea katika oven
10. .Oka kwa dakika 12 hadi 15 mpaka biskuti ziwe kahawia
11. Zitoe biskuti na ziache zipoe kisha zihifadhi katika chombo chenye mfuniko
zitumie ndani ya wiki mbili
12. Kumbuka kuzima oven

22.MAPISHI YA KASHATA ZA CHOCOLATE


MAHITAJI
1. Unga wa Cocoa (Cocoa powder) - nusu kikombe
2. Maziwa fresh vikombe viwili
3. Sukari nusu kikombe
4. Corn flour kijiko kimoja cha chai
5. Blueband,margarine au siagi yoyote vijiko viwili vya chakula
6. Karanga za kukaanga zilizotolewa maganda kikombe kimoja
7. Chumvi kijiko kimoja cha chai
8. Vanilla nusu kijiko cha chai

MAPISHI
1. Weka sufuria jikoni kisha mimina maziwa na anza kuyachemsha, yakiaanza
kuchemka mimina sukari,cocoa na siagi kisha koroga hadi vitu hivyo viyeyuke.
2. Mimina corn flour humo kisha endelea kukoroga hadi upate uji uji mzito.
3. Mimina karanga humo kisha changanya vyema kwa kutumia mwiko
4. Chukua trei ya pembe nne ya kuokea vitu au kifaa chochote kipana kisha paka
mafuta na mwagia humo mchanganyiko na sambaza vizuri katika unene
unaohitaji
5. Acha huo mchanganyiko upoe na uwe mgumu, unaweza ukahifadhi katika
freezer au fridge 6.Toa trei yako kisha bandua sheet ya kashata ya chocolate na
anza kukata vipande kwa kutumia kisu au kifaa maalumu cha kukatia
6. Kashata za chocolate zipo tayari.

23.MAPISHI YA KALIMATI
MAHITAJI
1. Unga wa ngano robo kilo
2. Hamira kijiko kimoja na nusu cha chai
3. Mtindi nusu kikombe au tui la nazi au maziwa fresh.
4. Blueband kijiko kimoja cha chakula
5. Maji
6. Mafuta ya kupikia
7. Sukari vikombe vitatu
8. Hiriki robo kijiko cha chai
9. Vanilla au ladha yoyoye kidogo kama robo ya kijiko cha chai

MAPISHI
1. Yeyusha blueband
2. Chukua bakuli kisha mimina unga wa ngano,mimina blueband,mtindi, mafuta
kijiko kimoja cha chakula na hamira kisha mimina maji kiasi na koroga hadi uji
uwe mzito kiasi na usiwe na mabuja buja
3. Funika unga kwa muda wa nusu saa ili uumuke
4. Weka kikaango jikoni kisha mafuta ya kupikia yaache yapate moto kiasi
5. .Chota uji wa kalimati kwa kijiko cha chakula na mimina katika mafuta kisha
choma kalimati zako hadi upande mmoja uwe kahawia na geuza upande wa pili
nao uwe kahawia kisha toa kalimati zako ziweke katika chujio au tissue ili zichuje
mafuta.
6. Andaa shira kwa kuweka sufuria jikoni mimina maji kikombe kimoja, mimina
sukari koroga hadi sukari iwe nzito na inayonata ukiishika kwa vidole viwili.
7. Mimina hiriki na rose essense au vanilla kisha koroga
8. Epua sufuria ya shira acha ipoe kiasi
9. Weka kalimati katika bakuli kubwa kisha miminia shira humo na changanya na
kalimati zote kwa mwiko au kupeta kama mchele.
10. Kalimati zipo tayari

24.MAPISHI YA KASHATA ZA KARANGA NZIMA MAHITAJI


1. Karanga kilo moja na nusu
2. Sukari kilo moja

MAPISHI
1. Chambua karanga kutoa uchafu
2. Osha karanga vizuri na zianike juani zikauke maji
3. Zikaange karanga kwa moto wa wastani hakikisha haziungui
4. Acha zipoe
5. Pukuchua karanga kutoa maganda
6. Weka sufuria jikoni katika moto mkali, mimina sukari humo kisha koroga hadi
iyeyuke kisha mimina karanga humo na koroga kuchanganya karanga na shira
7. Paka mafuta meza au sinia kubwa kisha mimina mchanganyiko wa karanga na
shira hapo na sambaza msukumio wa chapati.
8. Anza kukata kashata zako katika umbo unalohitaji
9. Kashata zipo tayari

25.MAPISHI YA KEKI ZA VIKOMBE - CUP CAKES


MAHITAJI
1. Unga wa ngano nusu kilo
2. Mayai sita
3. Maziwa kikombe kimoja
4. Sukari kikombe kimoja
5. Siagi (Blueband) kikombe kimoja au kopo dogo moja
6. Baking powder vijiko viwili vya chai
7. Vanilla kijiko kimoja cha chai
8. Rose essence robo kijiko cha chai
9. Chumvi nusu kijiko cha chai

MAPISHI
1. Kwa kutumia mixer ya chakula au kipekecho mimina sukari na chumvi katika
chombo kikubwa kisha yeyusha siagi na mimina katika chombo chenye sukari
kisha changanya vizuri.
2. Pasulia mayai kwenye hicho chombo kisha mimina vanilla na rose essence na
changanya vizuri
3. Mimina unga wa ngano changanya vizuri na mchanganyiko
4. Mimina maziwa kisha changaya vizuri upate uji mzito
5. Uji usipokuwa mzito mimina maji kiasi
6. Mimina baking powder na changanya vizuri
7. Acha mchanganyiko kwa dakika 20
8. Washa oven katika joto la 350 F kwa dakika 3
9. Chukua trey maalum la kuokea keki hizi kisha weka karatasi za kuokea keki hizi
humo na chota uji wa keki mimina humo hadi karibia na kujaa
10. Ingiza trey lako katika oven kisha oka keki zako kwa muda wa dakika 25
11. Zitoe keki zako zipange katika sahani tayari kwa kula. Kama hauna oven tumia
panga vikaratasi vya kuokea katika sinia mimina uji wa keki humo kisha weka
sinia katika sufuria kubwa, weka sufuria katika jiko la mkaa, kwa chini makaa
yawe kidogo na funika kwa mfuniko wa chuma au bati kwa juu kisha weka
makaa kiasi na endelea kuoka kwa dakika 25 hadi 30.

26.MAPISHI YA KEKI YA KUGANDA MAHITAJI


1. Vipande vya biskuti vilivyovunjwa vunjwa vikombe vitatu
2. Siagi (Margarine au Blueband) - Vijiko 10
3. Vipande vya chocolate vikombe vitatu
4. Zabibu za kukaushwa - Vijiko 5 vya chakula
5. Asali vijiko viwili vya chakula
6. Almond au korosho za kukaangwa (zikatwe katwe nusu vipande) - Vijiko 6 vya
chakula

MAANDALIZI
1. Weka vipande vya biskuti ndani ya mfuko wa plastiki kisha pondaponda na
msukumio wa chapati au kitu chochote kizito, hakikisha hazipondeki sana
2. Weka chocolate,siagi na asali katika bakuli ya glass au ya plastiki kisha weka
bakuli juu ya sufuria yenye maji makali ya moto kisha acha viyeyuke na
kutengeneza ujiuji na changanya vizuri
3. Baada ya mchanganyiko kupoa, mimina vipande vya biskuti,vipande vya
korosho na zabibu zilizokaushwa kisha kwa kutumia mwiko changanya vizuri
4. Chukua bakuli kubwa la umbo la mstatiri weka foil kwa ndani iendane na umbo
la hiyo bakuli kisha mimina huo mchanganyiko humo chukua mfuniko wa bapa
au kifaa maalum cha kukandamizia kisha kandamiza kwa juu ili ipatikane
msawazo.
5. Weka hiyo bakuli katika fridge kwa saa 1 hadi 2 na zaidi ili mchanganyiko
ugande vizuri
6. Baada ya kuganda toa bakuli kisha toa keki yako na ikate katika vipande
vipande Keki ya baridi ipo tayari *Ukiwa na chocolate ya kutosha iyeyushe na
mwagia juu ya mchanganyiko kabla ya kuweka katika fridge

27.MAPISHI YA SHAWARMA
MAHITAJI
1. Minofu ya kuku isiyo na mifupa:- Chicken fillets
2. Karoti moja:- Carrot
3. Hoho moja:- Capsium
4. Kitunguu maji kimoja:- Onion
5. Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko kimoja cha chai:- 1 tsp garlic paste 1
6. Tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja cha chai:- 1 tsp ginger paste
7. Pilipili manga ya unga kijiko kimoja cha chai:- 1 tsp blackpepper powder
8. Pilipili mbichi au ya unga:- Chilli or chilli powder :- Ukihitaji (Optional)
9. Ndimu au limao kipande au unaweza kutumia vinegar kiasi:- Lime or vinegar
10. Chicken masala kijiko kimoja cha chakula
11. Mafuta ya kupikia:- Cooking oil
12. Chumvi:- Salt
13. Tortilla au chapati

MAPISHI ****Andaa tortilla

((MAPISHI YA TORTILLA
MAHITAJI
1. Ngano vikombe vitatu
2. Baking powder kijiko kimoja cha chai
3. Mafuta ya kupikia vijiko 2 vya chakula (Tumia mafuta ya maituni au sunflower
kwa matokeo bora zaidi)
4. Siagi (Blueband au Margarine) iliyoyeyushwa kijiko kimoja cha chakula
5. Maji ya moto kikombe kimoja
6. Chumvi kijiko kimoja cha chai

MAPISHI
1. Changanya unga na baking powder katika bakuli kwa kutumia mwiko
2. Changanya chumvi na maji ya moto
3. Tengeneza shimo katikati ya unga kisha mimina mafuta na maji ya moto
yenye chumvi kisha changanya na unga kisha kanda hadi ngano iwe laini
4. Hamishia katika sehemu ya kukandia ngano iliyowekwa unga kiasi kisha
kanda ngano hadi iwe laini
5. Funika ngano kwa nusu saa hadi saa moja
6. Kata kata ngano katika madonge inayofanana kiasi kama tonge linalojaa
katika kiganja cha mkono
7. Chukua msukimio wa chapati kisha sukuma donge mojawapo katika mduara
mwembamba
8. Weka kikaango jikoni katika moto wa wastani acha kipate moto kiasi, tumia
kikaango kizito ambacho ni non-stick au kama hauna hicho kikaango weka
mafuta kiasi, ila hakuna ulazima wa kutumia mafuta katika kuchoma tortilla
9. Weka tortilla yako katika kikaango kisha choma kwa sekunde kama 30 hadi 45
hadi uone kama inajaa kwa juu na imekuwa kahawia kwa chini, pindua upande
wa pili choma kwa sekunde 15 hadi iwe kahawia
10. Sukuma tortilla nyingine kisha choma
11. Hifadhi tortilla katika hotpot yenye mfuniko ili ziwe laini
12. Kumbuka kupunguza au kuzidisha moto kila unapoona inahitajika kufanya
hivyo, moto unatakiwa kuwa wa wastani.
***Tumia non stick pan kwa matokeo bora zaidi
***Hatutumii mafuta katika kuchoma tortilla
***Unaweza kuzihifadhi tortilla katika friji kwa matumizi ya baadae, na zinaweza
kuhifadhiwa hadi wiki moja
***Tortilla hutumika kutengeneza Shawarma au unaweza kula kama chapati)))

ENDELEA NA HATUA ZINAZOFUATA


1. Muoshe kuku kisha kata vipande vidogo vidogo sana.
2. Weka vipande vya nyama katika bakuli kisha mimina kitunguu
saum,tangawizi,pilipili manga,pilipili iliyosagwa au pilipili ya unga,mtindi,
kamulia limao changanya, nyunyuzia chumvi kisha changanya tena
3. Andaa pilipili hoho, kitunguu maji na karoti. Menya kisha kata vipande vidogo
vya karoti na kitunguu,pilipili hoho kata vipande virefu na vipana.
4. Bandika kikaango jikoni, acha kipate moto kiasi,weka mafuta kiasi. Acha hadi
yapate moto. Weka nyama, tandaza vizuri. Acha iive kisha geuza ili iive vizuri
upande wa pili. Endelea kugeuza mara kwa mara hadi nyama ikauke kiasi na
kubadirika rangi.
5. Weka kikaango jikoni, kikipata moto weka mafuta ya kupikia kisha weka
kitunguu maji. Kaanga vizuri hadi kianze kubadilika rangi. Weka pilipili hoho
na karoti, koroga vizuri. Baada ya dakika 3 weka nyama ya kuku. Koroga
pamoja vizuri. Vikichanganyika vizuri, weka chicken masala koroga vizuri,
kisha epua weka pembeni.
6. Weka tortilla katika kibao au sinia kisha kwa kutumia kijiko chota
mchanganyiko wa kuku na mboga mboga weka katika tortilla, mimina sosi ya
jibini au tomato sauce au sosi yoyote, mimina majani ya giligilani au ya
mnanaa, majani ya saladi (letuce),weka kwa juu vipande vya nyanya, kisha
funga kunja tortilla vizuri kama unavyokunja chapati 7.Shawarma ipo tayari
kwa kula

28. MAPISHI YA CHAURO


MAHITAJI
1. Vimchele (Poha/Pawa):- Kilo 1
2. Crips za viazi (Za kununua au za kutengeneza):- Kiasi chochote kuanzia
bakuli au sufuria kubwa la lita 3
3. Karanga kavu:- robo kilo
4. Korosho zilizokaangwa:- robo kilo
5. Zabibu kavu:- Kikombe kimoja
6. Dengu za vipande za manjano:- Nusu kilo
7. Ndimu ya unga vijiko viwili vya chai
8. Pilipili ya unga kiasi kidogo
9. Majani ya mchuzi (Curry leaves):- Kiasi
10. Manjano kijiko kimoja cha chai
11. Sukari:- Robo kikombe
12. Chumvi kiasi
13. Mafuta ya kupikia

MAPISHI
1. Osha na roweka dengu hadi siku ya pili
2. Weka kikaango jikoni mimina mafuta ya kupikia ya kutosha acha yapate mot
3. 3.Mimina dengu kaanga hadi ziive na zikauke zitoe na zikaushe mafuta katika
chujio
4. Kaanga karanga hadi ziive na zikauke, zitoe zichuje mafuta katika chujio
5. Kaanga vimchele kwa muda kidogo tu vitoe na vichuje mafuta
6. Kaanga zabibu kavu kidogo
7. Weka mafuta kidogo katika frying pan, mimina majani ya mchuzi yakaange
hadi yatoe harufu na yakauke kisha mimina manjano na koroga vizuri hadi
usikie harufu ya manjano.
8. Vunja vunja crips ziwe katika vipande vidogo vidogo
9. Chukua bakuli kubwa kisha mimina vitu vyote humo, kisha mimina
chumvi,sukari, ndimu ya unga na pilipili ya unga na changanya kwa pamoja
hadi vitu vyote vichanganyike kwa pamoja.
10. Chauro ipo tayari. *Mahitaji yote yanapatikana sokoni

29. MAPISHI YA JALEBI


MAHITAJI
1. Ngano vikombe vitatu
2. Unga wa dengu nusu kikombe
3. Baking soda nusu kijiko cha chai
4. Sukari vikombe vitatu
5. Maji vikombe vitatu
6. Hiriki ya unga nusu kijiko cha chai
7. Manjano nusu kijiko cha chai
8. Limao moja au ndimu
9. Mafuta ya kupikia

MAPISHI
1. Chukua bakuli kubwa mimina unga wa ngano, unga wa dengu, baking soda
kisha changanya vizuri kwa kutumia mwiko
2. Mimina maji katika mchanganyiko na changanya kwa kukoroga vizuri hadi
rojo liwe zito kiasi na jepesi kiasi, hakikisha rojo halina madonge.
3. Funika bakuli kisha hifadhi sehemu yenye joto kwa saa 8, na kama upo
sehemu yenye baridi hifadhi mchanganyiko kwa siku nzima.
4. Tengeneza shira kwa kufuata hatua hizi:-
5. Chukua sufuria kisha mimina sukari vikombe vitatu,hiriki na manjano kisha
mimina maji vikombe vitatu na weka jikoni
6. Koroga mchanganyiko hadi sukari iyeyuke, endelea kukoroga hadi yatokee
mapovu na rojo la sukari liwe zito kiasi na linalonata ukishika kati ya vidole
viwili, kabla ya kushika rojo hakikisha unatoa kiasi kidogo unapoza ndipo
unashika.Kamulia limao kidogo kisha koroga.
7. Funua mchanganyiko wa kutengenezea jalebi na andaa chupa yenye kizibo
ambacho kina kitobo, mimina mchanganyiko kwenye chupa
8. Weka kikaango jikoni kisha mimina mafuta ya kupikia acha yapate moto
kiasi, kisha minya chupa yenye rojo la jalebi katika mafuta ya moto na
tengeneza miduara michache ya jalebi kwa kuanzia ndani kwenda nje
9. Choma upande mmoja wa jalebi hadi uwe kahawia na mkavu kisha geuza
na choma upande mwingine
10. Toa jalebi kadhaa katika mafuta kisha ziingize katika shira acha kwa dakika
3 kisha zitoe na weka katika sinia au sahani

30. MAPISHI YA PIZZA ZA ZANZIBAR (MIKATE YA NYAMA)


MAHITAJI
1.Ngano nusu kilo
2.Nyanya tatu
3.Karoti moja kubwa
4.Hoho moja kubwa
5.Nyama ya kusaga iliyochemshwa nusu kilo
6.Mayai matano
7.Manjano kijiko kimoja cha chai
8.Kitunguu saum kilichopondwa kijiko kimoja cha chai
9.Vitunguu maji
10.Majani ya giligilani kiasi

MAPISHI
1. Katakata kitunguu maji,nyanya,karoti,na hoho katika vipande vidogo vidogo
sana
2. Weka kikaango jikoni kisha mimina mafuta ya kupikia kiasi kisha acha yapate
moto kiasi
3. Pasua mayai weka chumvi kiasi kisha changanya vizuri kupata rojo
4. Mimina vipande vya kitunguu maji koroga hadi viwe kahawia,mimina vitunguu
saum koroga hadi vibadirike rangi kiasi,mimina karoti,hoho na vipande vya
nyanya kisha endelea kukoroga kiasi,mimina manjano, mimina chumvi kidogo
koroga, mimina majani ya giligilani kisha changanya tena, epua mchanganyiko
na acha upoe kidogo.
5. Mimina rojo la mayai katika mchanganyiko na koroga vizuri
6. Kanda ngano kama unavyokanda ngano ya kupika chapati, kisha ifunike kwa
nusu saa
7. Andaa madonge kadhaa
8. Chukua madonge kisha sukuma na tengeneza chapati nyepesi sana
9. Kwa kutumia kijiko chota mchanganyiko wa mayai na viungo kisha weka
katika chapati na fungasha chapati kama vile box lenye unene kiasi,
tengeneza rojo la ngano zito kaisi kwa kuchanganya ngano na maji kiasi kisha
tumia kama gundi katika kufunga hiko kibox cha ngano
10. .Weka kikaango cha chapati jikoni kisha weka mafuta kiasi acha yapate moto,
beba kibox chenye mchanganyiko wa nyama na viungo kwa kutumia mshikio
bapa wa kupindulia chapati kibox kisha kiweke kwenye kikaango na kichome
kama chapati pande zote mbili hadi kiwe kahawia
11. Epua kibox weka katika tissue au chujio ili kichuje mafuta
12. .Andaa sosi ya pilipili na juisi au chai ya maziwa na hizi piza, kula na ufurahie.

31. MAPISHI YA VITUMBUA VYA MAEMBE


MAHITAJI
1. Unga wa mchele kikombe kimoja
2. Unga wa ngano vijiko viwili vya chakula
3. Rojo la embe mbivu zilizosagwa kikombe kimoja na nusu
4. Maziwa nusu kikombe
5. Sukari nusu kikombe
6. Hiriki ya unga nusu kijiko cha chai
7. Baking soda kiasi kidogo kama robo kijiko cha chai
8. Chumvi kijiko kimoja cha chai
9. Mafuta ya kupikia au siagi au samli

MAANDALIZI NA MAPISHI
1. Chukua sufuria kisha pasha rojo la maembe kwa kukoroga hadi mvuke uanze
kutoka
2. .Katika bakuli kubwa mimina maziwa changanya na sukari kisha koroga vizuri
hadi sukari iyeyuke kisha mimina unga wa mchele na unga wa ngano
changanya kupata ujiuji au rojo
3. Ongeza hiriki ya unga na baking soda kisha changanya vizuri hadi vitu vyote
vichanganyike vizuri
4. Mimina chumvi kiasi kisha koroga tena
5. Funika mchanganyiko kwa muda wa nusu saa
6. Katika moto wa wastani weka kikaango cha vitumbua jikoni kisha mwagia
mafuta kiasi katika kila tundu na acha yachemke kiasi.
7. Kwa kutumia upawa mwagia rojo katika kila tundu, kaanga vitumbua hadi
upande wa chini uwe kahawia na kukauka kidogo kisha kwa kutumia kitu cha
ncha kali pindua vitumbua upande wa pili taratibu kisha kaanga tena hadi viwe
kahawia na vikavu kiasi. 8.Vitumbua vya maembe vipo tayari

32. NAMNA YA KUTENGENEZA BISKUTI ZA TANGAWIZI


MAHITAJI
1. Unga wa ngano aina ya (
i. a (Plain flour) vikombe viwili
2. Tangawizi ya unga vijiko viwili vya chai
3. Bicarbonate of soda au baking powder kijiko kimoja cha chai
4. Siagi vijiko nane na nusu vya chakula (Siagi kama blueband au magarine)
5. Sukari nusu kikombe na vijiko vinne vya chakula
6. Asali vijiko vinne vya chakula au golden syrup
7. Yai moja
8. Chumvi kiasi *Kikombe kinachotumika ni kikombe cha robo lita (250 mls)

MAPISHI
1. Washa oven katika joto la 180 (C) digrii au 350 (F) digrii
2. Weka tangawizi na bicarbonate of soda katika unga kisha changanya vizuri
3. Changanya siagi katika unga hadi unga uwe kama umeachana achana kisha
mimina sukari
4. Pasua yai na likoroge katika bakuli pembeni kisha mimina katika bakuli lenye
unga, kisha mimina asali na changanya vizuri kisha anza kukanda
5. Chukua kifaa cha kusukuma ngano kisha sukuma ngano katika unene wa
chapati nzito6
6. Chukua kisu kisha katakata vipande vinavyolingana
7. Weka vipande hivyo katika trei la kuokea ambalo kwa juu umeweka karatasi
maalum ya kuokea au foili
8. Ingiza trei katika oven kisha oka biskuti kwa dakika 10 hakikisha zimekuwa na
rangi ya kahawia.
9.Toa biskuti katika trei kisha acha zipoe
10.Kumbuka kuzima oven

KARIBU UJIPATIE VITABU VYETU


VINGINE

You might also like