PDF of Swahili

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 1

Kiama Cha Mkopaji

Hapo zamani za kale palikuwa na mzee mmoja aitwae Kanyawi ambaye alihamia kijiji cha
Ntenga kutoka Usambaani. Mzee huyu alikuwa anapenda sana kunywa pombe na hata
alipomaliza fedha zake zote aliamua kuweka rehani chochote alichonacho. Hakika mzee
huyu alikuwa kero sana kwa familia yake kwani kila aliyekopwa alifika nyumbani kwake na
kudai deni lao. Kutokana na heshima waliyokuwa nayo watoto wake na mke wake;
walilazimika kulipa madeni mara kwa mara. Ilifikia wakati ambapo mke na watoto wote
ilibidi kubuni miradi mbalimbali ili waweze kulipa madeni na kusomeshana. Mtoto mkubwa
aliyeitwa Mwasu alibuni mradi wa kufuga nyuki na hivyo kuchonga mizinga ya nyuki mizuri
sana pale kijijini.

Siku moja kama ilivyokuwa kawaida ya Mzee Kanyawi; alikopa tena pombe ya dengelua
yenye thamani ya shilingi elfu tatu. Baada ya kudaiwa alimuambia aliyemkopesha kuwa afike
nyumbani kwake kesho yake ili ampe fedha zake. Keshoye yule aliyemkopesha alimpigia
mzee Kanyawi simu kuwa yupo njiani kwenda kuchukua fedha zake.

Mzee kanyawi kusikia hivyo aliangalia juu ya mti uliokuwa karibu na nyumba yake na kuona
mzinga mpya wa nyuki ambao bado haujaingliwa na nyuki na kumwambia mke wake kuwa
kuna watu wanakuja kumuua na hivyo ataingia ndani ya ule mzinga na afungiwe mle ili wale
wanaomdai wasimuone. Kutokana na upendo mkubwa kwa mumewe alikubali ombi lile na
kumfungia mumewe ndani ya mzinga wa nyuki. Punde si punde Yule mzee Mwasu alifika na
kuulizia alipokuwa mzee Kanyawi. Mke wake alimtetea na kusema kasafiri ghafla hadi wiki
ijayo. Mzee Mwasu alisononeka sana na kuamua kuchukua ule mzinga uliokuwa juu bila
kujua kuwa yule mzee alikuwa ndani yake na kuondoka nao hadi nyumbani kwake.

Alipofika kwake Mzee Mwasu aliulizwa na mkewe iwapo alifanikiwa kupata fedha zile na
kumwambiwa kuwa hakumkuta lakini aliamua kuchukua mzinga wake mpya ili waupasue na
kupata kuni za kupikia kwani yule mzee sio mlipaji. Mzee Mwasu alimtaka kijana wake wa
kazi achukue shoka na kupasua ule mzinga ili wapate kuni za kupikia chakula. Hadi hapo
yule mzee Kanyawi alikuwa kimya ndani ya mzinga akisubiri jioni ili atoke na kurudi kwake.
Kijana yule wa “miraba minne” alichuka shoka na kulishushia kewnye mzinga ule na
“ghafla” damu zilitapakaa kila mahali. Walipoangalia vizuri waliona kuwa ni yule mzee
Kanyawi kapasuliiwa kichwa. AMA KWELI KIAMA CHA MKOPAJI KILIMTOA ROHO
BILA KUOMBA MAJI.

You might also like