Hafidh JR

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 4

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

WIZARA YA AFYA

TAARIFA YA TAHADHARI KWA UMMA KUHUSU MAJI YA CHEMCHEM


YAILIYOPO PEMBENI MWA BAHARI YA HINDI KATIKA SHEHIA YA MSUKA,
MASHARIKI, WILAYA YA MICHEWENI MKOA WA KASKAZINI PEMBA

TAREHE: 05/04/2023
Ndugu wananchi, Hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii
zilisambaa taarifa za kuwepo Chemchem inayotoa maji ambayo
ukinywa maji hayo ni tiba ya magonjwa mbali mbali.

Maji haya yanapatikana katika chemchem iliyopo ndani ya bahari


katika Shehia ya Msuka Mashariki Wilaya ya Micheweni Mkoa wa
Kaskazini Pemba.

Ndugu wananchi, wamejitokeza watu mbali mbali kutoka Kisiwa


cha Pemba na nje ya Kisiwa hicho ambao hufika kwa wingi katika
eneo lenye chemchem hiyo na kuchukua maji hayo katika vyombo
tofauti ikiwemo Madumu, Chupa na Ndoo na kunywa maji hayo
wakiamini kwamba maji hayo ni tiba ya magonjwa mbali mbali.

Ndugu wananchi, Baada kupata taarifa hiyo, Wizara ya Afya ilituma


wataalamu wake kwenda kuchukua sampuli ya maji hayo kwa lengo
la kuyafanyia uchunguzi ili iweze kuthibisha kwamba maji hayo ni
tiba kama inavyoaminika katika jamii. Sampuli zilizochuliwa
zilipelekwa kwa Mkenia Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kwa ajili ya uchunguzi wa maabara ili tuweze kuthibisha madai ya
kuwa maji haya ni tiba kwa magonjwa mbali mbali na yapo salama
kunywewa.

Ndugu wananchi, Baada ya uchunguzi na uchambuzi wa kina wa


maji hayo, uchunguzi umebainisha mambo yafuatayo;-
1. Uwepo wa vimelea vinavyosababisha magonjwa ya kuharisha
(bacteria wa E. Coli) wa idadi kubwa kati ya mia mbili na
ishirini hadi elfu moja na mia nane kwa kila lita mia moja (220
hadi 1800 kwa kila lita 100), kwa kawaida maji ya kunywa
hayatakiwi kuwepo na hata kimelea kimoja cha aina hiyo.
2. Pia uchunguzi umebaini kuwepo vimelea vinavyosababisha
ugonjwa wa kuharisha aina ya “Coliforms” wa zaidi ya elfu
moja mia nane kwa kila lita moja za maji (1800 kwa kila lita
100) , Kwa kawaida vimeilea hivi vinahitajika viwemo kwenye
maji ya kunywa, lakini isiwe zaidi ya watatu kwa lita mia moja
kwa kila lita mia moja ya maji..
3. Uchunguzi huu vile vile umebaini uwepo wa Chloride kwa
kiwango kikubwa ambapo wataalamu wetu wemebaini kiasi
cha upimo wa kuanzia elfu moja mia nne na tisiini
milligram kwa kila lita hadi mpaka elfu mbili na khamsini
na tisa milligram kwa lita moja (1490.88 mg/L hadi 2059.36
mg/L). kiwango kinachokubalika ni kipimo kisichozidi mia mbili
na khamsini milligram kwa kila lita moja. (250 mg/L)
4. Kiwango cha Chumvi chumvi (Salinity) kimebainika kwa
kiwango cha kupima ukali wa chumvi cha baina ya mbili
nukta nane na tatu nukta nane (2.827 hadi 3.827 psu)
ambapo ni zaidi ya kiwango kinachokubalika katika maji ya
kunywa cha sufuri, (0 psu)

Ndugu wananchi, Kutokana na matokeo hayo yatuthibitishia


kwamba maji haya yamechafuliwa na kinyeshi cha viumbe hai na
pia kuna kiwango kikubwa cha Kemikali ambazo sio salama
katika mwili wa binadamu. Kwa maana hio maji haya sio salama
kwa kunywa na kama tukiendekea kuyatumia yanaweza kuathiri
Afya zetu na kupelekea matatizo ya kiafya yafuatayo:-
1. Magonjwa ya kuharisha ikiwemo Kipindupindu, kutapika na
kupoteza maji mengi mwilini
2. Kupata maumivu makali ya tumbo na baadae unaweza
kupata vidonda vya tumbo hapo baadae

Ndugu wananchi, Napenda kuchukua fursa hii kuwaomba


Wazanzibari wenzangu kwamba taarifa zilizosambaa katika
mitandao ya kijamii hapa nchi kwamba maji yanayopatikana katika
Chemchem iliyopo katika Bahari ya Hindi katika Shehia ya Msuka
Mashariki, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba
hayawezi kutibu ugonjwa wowote na tuzipuuze taarifa hizi kwa
hazina ukweli wowote.

Ndugu wananchi, Aidha, napenda niwasihi wananchi wote kwamba


mtu yoyote mwenye matatizo ya kiafya afike katika Kituo cha Afya
au Hospitali iliyokaribu kwa ajili uchunguzi na matibabu na tuache
kutumia maji haya kama tiba kwani yanaweza kutuletea athari zaidi
katika Afya zetu.

Ndugu wananchi, Mwisho kabisa nitoe wito wangu kwa


Wanzanzibari wenzangu kwa tuache kuyatumia maji haya tukiamini
ni tiba ya magonjwa mbali mbali kwani athari yake inaweza kuwa
kubwa na kusabisha matatizo ya kichumi na kijamii

Ahsanteni kwa kunisikiliza

NASSOR AHMED MAZRUI


WAZIRI WA AFYA
ZANZIBAR

You might also like