Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 12

MAMBO YA KUFUATA KATIKA KUPOKEA VITU

KUTOKA KWA MUNGU.

Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao


watashibishwa. Mt 5:6 SUV

1) NENO/ UJUMBE SAUTI


2) MAOMBI – Ufunuo – Ujum
3) KUINGIZA – Kumiliki – Kumilikisha
4) MAWASILIANO – Kutamka
5)KUTENDA – Matendo
6) MATOKEO - Mazao

ØMaombi; wengi wetu tunafanya hatua ya kwanza


kwa ufanisi, tena kwa hali ya juu, tunakesha,
tunafunga na kuomba.
Ø Halafu tunasubiri kwenye hatua ya tano.
ØMatokeo yake ni kukosa yote tuliyoyaomba au
kupokea kwenye maombi.

1. NENO UJUMBE:
ØUnaweza kupokea wakati wowote.
ØKabla ya kuomba, wakati wa maombi, Baada ya
maombi

2. MAOMBI

üUkiwa na orodha ya mahitaji. Maombi


Uliyoyapata kupitia sauti, Neno.
üBila orodha. Ukitarajia Mungu akupe ujumbe.
üBaada ya kupokea simamia Neno ulilopewa
üKeep on asking and it will be given you;
ükeep on seeking and you will find;
ükeep on knocking [reverently-kwa heshima-]
and [the door] will be opened to you. (Matthew
7:7 AMP)
üKuomba kwake mwenye haki kwafaa sana,
akiomba kwa bidii. (YAK. 5:16 SUV)
ü Ikawa baada ya siku nyingi, neno la BWANA
likamjia Eliya, katika mwaka wa tatu, kusema,
Enenda, ukajionyeshe kwa Ahabu; nami nitaleta
mvua juu ya nchi. Basi Ahabu akainuka ili ale na
kunywa. Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha
Karmeli; akasujudu kifudifudi, akainama uso mpaka
magotini. Akamwambia mtumishi wake, Kwea
sasa, utazame upande wa bahari. Akakwea,
akatazama, na kusema, Hakuna kitu. Naye
akanena, Enenda tena mara saba. Ikawa mara ya
saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika
bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu.
Akanena, Enenda, umwambie Ahabu, Tandika,
ushuke, mvua isikuzuie. Ikawa, muda si muda,
mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo,
ikanyesha mvua nyingi. Ahabu akapanda garini,
akaenda zake Yezreeli. 1 Fal 18:1, 42-45
Jua Muda wako wa kuomba…
Jua Style Yako… Mkao wako.
 Kupiga magoti.
 Kukaa.
 Kusimama
 Kutembea
 Kulala kifudifudi.

Ambatanisha sadaka ktk maombi yako..


o Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. ' Zab 20:3
o Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, akiwa na chetezo cha dhahabu,
akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya
dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi. Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu

pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika. ' Ufunuo 8:3-4 .
o mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka
nyingi, na kumwomba Mungu daima. Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini,
Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za
Mungu. ' Mdo 10:2,4

üusikimbile kwenye hatua ya tano ya kusubiri


matokeo au kuona matunda ya kile ulichokiomba
bali fuata hatua ya pili ambayo ni kumiliki au
kuingiza.
3. KUMILIKI – KUINGIZA
üHii ni hatua muhimu sana, kwani hapa ndipo
unapokipokea na kukimiliki kile ulichokipata
katika ulimwengu wa kiroho.
üKwa mfano Mungu anakuambia nataka
unitumikie, basi hapa ndipo unapoanza
kujipanga ndani mwako katika kumtumikia
Mungu.
üAu unamuomba Mungu ili ambadilishe mtu
wako wa karibu mwenye matendo yasiyo mema,
basi anza kuona huyo mtu yuko kama
ulivyoomba.
üHatua hii ni muhimu sana vinginevyo kunaweza
kuwa na upungufu wa matokeo,
üWatu wanaweza kukubali kufunga lakini kama
haujafanikiwa kuyaingiza maono yako sawa
sawa, ndani ya mioyo yao, nao wakajiona ni
sehemu ya maono hayo, basi si wote
watakaofunga.
üUgumu wa hatua hii unachochewa na upungufu
wa Imani na uelewa.
üPia kuna mtu mwingine ambaye Mungu
alimuahidi gari, naye akaanza kusomea udereva
na kuangalia mahali pa kupaki gari yake hata
kabla hajapata fedha za kununua gari.
üNi hali ya kutoa kitu katika ulimwengu wa roho
na kukiingiza nafsini kwako au kwa watu
kadhaa.
üNi hatua ya kubadilisha maono yako na
kuyafanya yawe halisi.
üNi kuyafanya maono uliyoyapata ili yawe maono
ya wenzako.
üHata kama ni kwenye miradi yako bila
kuyaingiza maono yako kwa wafanyakazi wako,
utendaji wao utakuwa duni na hawatatenda kama
ulivyotaka wewe.

4. MAWASILIANO – KUTAMKA
ØKama nilivyoanza kuelezea hapo juu, hatua hii
inasumbua, hasa pale ambapo mazingira
yanapingana na ombi lako.
ØKwa mfano unamuomba Mungu uponyaji lakini
bado hali iko Vilevile.
Ø Tamka kile ulichokiomba waza kile
ulichokiomba.
ØChunga sana maneno ya namna gani
unayotamka baada ya kusema amina.
ØLabda unamuombea mume / mke mlevi ili aache
ulevi, halafu siku moja anarudi amelewa zaidi
ØMawasiliano pia ni kuwaambia wenzako juu ya
jambo unalolitarajia kutoka kwa Mungu. Liseme
kwa wahusika au wale walio karibu nawe.
ØJiambie hata wewe mwenyewe.
ØKama ni ahadi iliyoambatana na Neno lake
litamke kila wakati lisome na uliandike halafu
ulibandike kila mahali unapoweza kuliona,
jikoni, chumbani, ofisini, kwenye gari, n.k.
Jikumbushe na wakumbushe wahusika ili
waendelee kutarajia.
ØPale unapotamka mara kwa mara pia
kunaifanya imani yako ikue,
Ø na Mungu pia analiumba lile ulilotamka kwa
kuwa amesema
Ø"Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani,
amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye
aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya.
Taz ISA. 57:19
ØHatua hii inaambatana na kuwaza, kwa hiyo
yawaze yale uliyoyaomba ndipo
utakapoyatamka kwa kuwa "ajionavyo
(ajiwazavyo) mtu nafsini mwake ndivyo alivyo".
ØKumbuka tatizo si tatizo ulilonalo bali tatizo ni
mawazo uliyonayo juu ya tatizo ulilonalo.

5. KUTENDA
"Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba
anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani
yaweza kumwokoa? Lakini mtu atasema, Wewe
unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe
imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha
imani yangu kwa njia ya matendo yangu. Wewe
waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema.
Mashetani nao waamini na kutetemeka. Lakini
wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu,
kwamba imani pasipo matendo haizai? Je! Baba
yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa
matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya
madhabahu? Waona kwamba imani ilitenda kazi
pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile
ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale. Taz YAK.
2:14, 18-22

Tofauti ya imani ya mkristo na imani ya shetani ni


matendo.

Sisi tunatakiwa kuamini na kutenda.


Bila matendo hakuna ushindi.

Wakati Yoshua alipoambiwa auzunguke ukuta wa


Yeriko kama wasingelitenda hakika hakuna jambo
lolote ambalo lingetokea.
Mimi nimeona mara nyingi sana katika maisha
yangu ya utumishi, Mungu hafanyi kitu isipokuwa
pale ninapothubutu kutenda kile alichoniagiza.
Kwa mfano umemuomba Mungu akupe kazi,

Muombe na utafute biashara ya kufanya, ukipata na


ikipata kibali basi anza hata kwa senti ndogo uliyo
nayo – unakumbuka Yule mjane alitumia yale
mafuta kidogo aliyokuwa nayo Taz 2Fal 4:1-7.

Kama mjane huyu asingemimina mafuta kidogo


aliyokuwa nayo, wala yasingeongezeka, na
angebaki katika shida zake.
Fanyia kazi kile kidogo ulichonacho. Bahati mbaya
ni kwamba watu wengine wamekuwa wakisubiri ili
Bwana afanye na Bwana naye amekuwa akisubiri ili
wafanye.
Acha kukaa na kulia amka na utende jambo.
Fanya hata kama kila kitu kinapingana nawe, wewe
fanya.

Ukiambiwa panda mbegu ya sadaka ili upate basi


wewe panda. Usisubiri upate kwanza ndipo
upande.
6. MATOKEO – MAZAO

1)Hii ni hatua ya mwisho nayo ni kupata kile


ulichokiomba, iwapo uliomba gari basi unakuwa
umepata gari na unaanza kulitumia. Iwapo
uliomba uponyaji, unakuwa umepona.
2)Kwa watu wengine baada ya kukaa na tatizo
kwa muda mrefu wanashindwa kupokea au
kujua pale wanapoondolewa tatizo lao.
3)Kwa mfano kuna ugonjwa fulani (siukumbuki
jina) ugonjwa huu unatokana na mtu kuugua
muda mrefu halafu akapona.
4)Hali hii pia ipo kiroho unakuta mtu amezoea
tatizo lake kiasi kwamba linapoondoka haamini
au anashindwa kupokea.
5)Nimeona watu kadhaa ambao walikuwa
wanasumbuliwa na mapepo. Baada ya
kuhudumiwa na kufunguka,

You might also like